Jumanne, 12 Juni 2018

"Kubisha Hodi Mlangoni" (3) - Wakristo Wameamka Baada ya Kumsikia Bwana Akizungumza Wakati wa Kurudi Kwake


"Kubisha Hodi Mlangoni" (3) - Wakristo Wameamka Baada ya Kumsikia Bwana Akizungumza Wakati wa Kurudi Kwake

Bwana Yesu alisema, "Tazama, nasimama mlangoni, na kubisha: mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja na yeye, na yeye pamoja na mimi" (Ufunuo 3:20). Kwa miaka hii yote, Kanisa la Mwenyezi Mungu limeshuhudia kwa uthabiti kuwa Bwana Yesu amerudi, na kwamba amesema maneno ya kufanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho. Wachungaji na wazee wa jamii za kidini, hata hivyo, kwa kisingizio cha kuwalinda kondoo, hufanya kila wanaloweza ili kuwazuia waumini kuchunguza njia ya kweli na kusikia sauti ya Mungu. Wakristo watafanya uchaguzi gani wanapojongelea jambo hili?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ujio wa pili wa Yesu
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

0 评论:

Chapisha Maoni