Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 25 Septemba 2019

Sura ya 8 Miisho ya Aina Mbalimbali za Watu na Ahadi ya Mungu kwa Mwanadamu

Sura ya 8 Miisho ya Aina Mbalimbali za Watu na Ahadi ya Mungu kwa Mwanadamu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi Yangu inadumu kwa miaka elfu sita tu, na Mimi niliahidi kwamba udhibiti wa yule mwovu juu ya wanadamu wote utakuwa pia si zaidi ya miaka elfu sita. Na kwa hivyo, wakati umeisha. Nami wala Sitaendelea wala kuchelewa tena: Katika siku za mwisho Nitamshinda Shetani, nami Nitaumiliki tena utukufu Wangu wote, na kurudisha nafsi zile zote zilizo Zangu duniani ili nyoyo hizi za dhiki ziweze kutoroka kutoka bahari ya mateso, na hivyo Nitakuwa nimetimiza kazi Yangu nzima duniani. Kutoka siku hii na kuendelea, kamwe Sitawahi kuwa mwili duniani, na kamwe Roho Wangu wa kudhibiti yote Hatafanya kazi tena duniani. Lakini Nitafanya jambo moja duniani: Nitamfanya tena mwanadamu, mwanadamu aliye mtakatifu, na aliye mji Wangu mwaminifu duniani. Lakini ujue kwamba Sitaiangamiza dunia nzima, wala kuangamiza ubinadamu mzima. Nitahifadhi theluthi moja iliyobaki—theluthi moja inayonipenda na imeshindwa kabisa na Mimi, na Nitaifanya theluthi hii iwe yenye kuzaa matunda na kuongezeka duniani kama Israeli walivyofanya chini ya sheria, kuwalisha kwa kondoo wengi mno na mifugo, na utajiri wote wa dunia. Mwanadamu huyu atabaki na Mimi milele, hata hivyo si mwanadamu mchafu wa kusikitisha wa leo, lakini mwanadamu ambaye ni mkusanyiko wa wale wote ambao wamepatwa na Mimi. Mwanadamu wa aina hii hataharibiwa, kusumbuliwa, au kuzungukwa na Shetani, na atakuwa mwanadamu wa pekee anayepatikana duniani baada ya ushindi Wangu juu ya Shetani. Ni wanadamu ambao leo wameshindwa na Mimi na wamepata ahadi Yangu. Na hivyo, wanadamu ambao wameshindwa katika siku za mwisho pia ndio watakaosamehewa na kupata baraka Zangu za milele. Huu utakuwa ushahidi wa pekee wa ushindi Wangu dhidi ya Shetani, na nyara za pekee za vita Vyangu na Shetani. Hizi nyara za vita zimeokolewa nami kutoka utawala wa Shetani, na ni thibitisho la pekee na matunda ya mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita.
kutoka katika “Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wanaomfuata Mungu kiukweli wana uwezo wa kuhimili majaribu ya kazi yao, ilhali wale wasiomfuata hawawezi kuhimili majaribu yoyote ya Mungu. Karibuni au baadaye watatimuliwa, huku washindi wakisalia kwenye ufalme. Mwanadamu amtafute au asimtafute Mungu kwa ukweli itapimwa kulingana na kazi yake, yaani, kupitia kwa majaribu ya Mungu na hayahusiani na uamuzi wa mwanadamu mwenyewe. Mungu hamkatai mtu yeyote kwa wazo la ghafla; yote ambayo Yeye hufanya yanaweza kumshawishi binadamu kikamilifuHafanyi lolote ambalo halionekani kwa mwanadamu ama kazi yoyote ambayo haiwezi kumthibitishia mwanadamu. Iwapo imani ya mwanadamu ni ya ukweli au sio huthibitishwa na ushahidi, na haiwezi kuamuliwa na mwanadamu. Kwamba “ngano haiwezi kufanywa magugu, na magugu hayawezi kufanywa ngano” ni jambo lililo wazi. Wale wote wanaompenda Mungu kwa dhati hatimaye watasalia katika ufalme, na Mungu hatamtesa yeyote ambaye Yeye anampenda kwa kweli. Kwa misingi ya kazi zao na shuhuda zao tofauti, washindi katika ufalme watatumika kama makuhani au wafuasi, na wale wote watakaoshinda taabu watakuwa mwili wa makuhani katika ufalme. Baraza la makuhani litaundwa wakati kazi ya injili ulimwenguni kote itafikia kikomo. Wakati huo ukitimia, yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu yatakuwa jukumu lake ndani ya ufalme wa Mungu, na kuishi kwake pamoja na Mungu katika ufalme. Katika baraza la makuhani, patakuwepo makuhani wakuu na makuhani, na watakaosalia watakuwa wana na watu wa Mungu. Haya yote huamuliwa na ushuhuda wao kwa Mungu wakati wa majaribu; sio nyadhifa zinazopeanwa kwa wazo la ghafla. Wakati hadhi ya mwanadamu itakuwa imeianzishwa, kazi ya Mungu itamalizika, kwa kuwa kila mojawapo imewekwa kulingana na aina yake na kurejeshwa katika hali yake halisia, na hii ndiyo alama ya ukamilisho wa kazi ya Mungu, na haya ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi ya Mungu na matendo ya mwanadamu, na ndiko kubainika kwa yale maono ya kazi ya Mungu na ushirikiano wa mwanadamu. Mwishowe, mwanadamu atapata pumziko katika ufalme wa Mungu, na, Mungu pia, atarejea kwenye makazi Yake kupumzika. Haya ndiyo yatakayokuwa matokeo ya miaka 6,000 ya ushirikiano wa mwisho kati ya Mungu na mwanadamu.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.
kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale ambao wanafikiri tu juu ya miili yao na wanapenda starehe, wale ambao imani yao ni tata, wale wanaoshiriki katika tiba ya uchawi na usihiri, wale ambao ni wazinzi, na waliovaa matambara na wasio sawa, wale wanaoiba dhabihu kwa Yehova na mali Yake, wale ambao wanapenda rushwa, wale wanaoota kwa uzembe kwenda mbinguni, wale ambao wana kiburi na wenye majivuno, na wanajitahidi tu kwa ajili ya umaarufu wa kibinafsi na utajiri, wale ambao hueneza maneno yasiyofaa, wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe, wale ambao hawafanyi lolote ila kumhukumu na kumkashifu Mungu Mwenyewe, wale wanaokusanyika na wengine na kujaribu kujitegemea, wale wanaojitukuza juu zaidi kuliko Mungu, wale wanaume na wanawake wapuuzi, na wanaume na wanawake wenye umri wa kati na wazee ambao wametegwa katika uovu, wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu wa kibinafsi na utajiri na kufuata hadhi ya kibinafsi kati ya watu wengine, wale watu wasio na toba ambao wamenaswa katika dhambi—je, si wao wote hawawezi kuokolewa? Ufisadi, hali ya kuwa mwenye dhambi, tiba ya uchawi, usihiri, mwenendo chafu, na maneno mafidhuli hufanya fujo kati yenu, maneno ya kweli na uhai hukanyagwa kati yenu, na lugha takatifu inanajisiwa kati yenu. Ninyi Mataifa, mliojawa na uchafu na kutotii! Mtaishia wapi? Je, wale wanaopenda mwili, ambao wanafanya matendo maovu ya mwili, na ambao wametegwa katika uasherati wanawezaje kuthubutu kuendelea kuishi? Je, hujui kwamba watu kama nyinyi ni mabuu ambao hawawezi kuokolewa? Ni nini kinachowapa sifa inayostahili ya kudai hili na lile? Hadi leo, hakujakuwa na mabadiliko hata kidogo kwa wale ambao hawapendi ukweli na wanapenda tu mwili—hivyo watu hawa wanaweza kuokolewaje? Hata leo, wale ambao hawapendi njia ya uzima, ambao hawamtukuzi Mungu na kumshuhudia Yeye, ambao hupanga njama kwa ajili ya hali yao wenyewe, ambao wanajisifu wenyewe sana—je, wao bado si sawa? Iko wapi thamani ya kuwaokoa? Kama mnaweza kuokolewa hakutegemei jinsi ulivyo na sifa za kustahili, au ni umefanya kazi kwa miaka ngapi, sembuse idadi ya sifa ambazo unazo. Kunategemea na ikiwa kumekuwa na matokeo yoyote katika kufuatilia kwako. Unapaswa kujua kwamba wale ambao wameokolewa ni miti ambayo huzaa matunda, si miti ambayo ina majani ya kustawi sana na maua mengi lakini haizai matunda. Hata kama umetumia miaka mingi kuzurura mitaani, ina maana gani? Ushahidi wako uko wapi? Uchaji wako kwa Mungu ni mdogo sana kuliko upendo wako wa wewe na hamu zako za tamaa—mtu kama huyu si mpotovu? Ungewezaje kuwa mfano na kielelezo cha wokovu? Asili yako haibadiliki, wewe ni muasi sana, huwezi kuokolewa! Watu kama hao hawataondolewa? Je, wakati ambapo kazi Yangu inamalizika si wakati ambapo siku yako ya mwisho itakuja? Nimefanya kazi nyingi sana na kusema maneno mengi kati yenu—ni kiasi gani cha hayo kilichoingia ndani ya masikio yenu? Ni kiasi gani cha hayo ambacho mmewahi kutii? Wakati kazi Yangu itaisha ndio pia utakuwa wakati unapoacha kunipinga na kusimama dhidi Yangu. Wakati wa kazi Yangu, daima nyinyi hutenda dhidi Yangu, hamyatii maneno Yangu kamwe. Ninafanya kazi Yangu, na wewe unafanya kazi yako mwenyewe, unatengeneza ufalme wako mdogo mwenyewe—nyinyi kundi la mbweha na mbwa, kila kitu mnachofanya ni dhidi Yangu! Nyinyi daima mnajaribu kuwaleta wale wanaowapenda tu katika kumbatio lenu—uko wapi uchaji wenu? Kila kitu mnachofanya ni kidanganyifu! Hamna utii au uchaji, kila kitu mnachofanya ni udanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hao wanaweza kuokolewa? Wanaume zinzi, wa kiasherati daima hutaka kuwavuta kwao wale makahaba wabembe kwa ajili ya raha yao wenyewe. Sitawaokoa mapepo wenye uasherati kama hao, Nawachukia ninyi mapepo wachafu, uasherati wenu na kupiga bemba kwenu kumewatumbukiza kuzimu—mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi pepo mchafu na roho wabaya ni waovu sana! Nyinyi ni wa kuchukiza! Takataka kama nyinyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi bado wanaweza kuokolewa? Ukweli huu, njia hii, na maisha haya hayapendezi kwenu; mnavutiwa na dhambi, pesa, hadhi, umaarufu na faida, ridhaa za mwili, maumbile mazuri ya wanaume na ubembe wa wanawake. Ni nini kinachowapa sifa zinazostahili kuingia katika ufalme Wangu? Taswira yenu ni kubwa zaidi kuliko Mungu, hali yenu ni ya juu zaidi kuliko Mungu, kutosema chochote cha sifa yenu kati ya wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hamjabadilika kuwa malaika mkuu? Wakati mwisho wa watu unafichuliwa, ambao pia ni wakati kazi ya wokovu inafikia kikomo, wengi wenu mtakuwa maiti ya maiti ambayo haiwezi kuokolewa na lazima muondolewe. Wakati wa kazi ya wokovu, Mimi ni mwenye huruma na mwema kwa watu wote. Wakati kazi inamalizika, mwisho wa watu wa aina tofauti utafichuliwa, na wakati huo Sitakuwa mpole na mwema, kwa maana mwisho wa watu utakuwa umefichuliwa, kila mmoja atakuwa ameainishwa kulingana na aina, na hakutakuwa na maana katika kufanya kazi yoyote zaidi ya wokovu. Ni hasa kwa sababu enzi ya wokovu itakuwa imepita; kwa kuwa itakuwa imepita, haitarudi tena.
kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:
Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.
kutoka katika “Sura ya 26” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawakumbuka, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kuzitafuta ahadi mlizofanyiwa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.
kutoka katika “Sura ya 19” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Inuka na ushirikiane na Mimi! Hakika Sitawatendea vibaya watu wanaotumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu. Wale wanaojitoa Kwangu kwa dhati, Nitawapa baraka Zangu zote. Jitoe kabisa Kwangu! Kile unachokula, kile unachovaa, na mustakabali wako yote yako mikononi Mwangu, Nitayapanga vizuri kabisa, kwa ajili ya furaha yako isiyokuwa na mwisho, isiyoisha, kwa maana Nimesema, “Kwa wale wanaotumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu, hakika Nitakubariki kwa wingi.” Baraka zote huja kwa kila mtu anayetumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu.
kutoka katika “Sura ya 70” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Kile ambacho Nimewaandalia nyinyi, yaani, hazina nadra za thamani kutoka duniani kote, zote mtapewa nyinyi. Nyinyi hamuwezi kufahamu kuhusu wala hamuwezi kufikiri yote haya kwa sasa, na hakuna mwanadamu aliyefurahia hili hapo kabla. Wakati baraka hizi zitawajia, nyinyi mtajawa na furaha bila kikomo, lakini msisahau kwamba hizi zote ni nguvu Zangu, matendo Yangu, haki Yangu na hata zaidi, uadhama Wangu. (Nitawapa neema wale ambao Nitaamua kuwapa neema, na Nitawahurumia wale ambao Nitaamua kuwahurumia). Wakati huo, ninyi hamtakuwa na wazazi, wala hakutakuwa na mahusiano ya damu. Nyinyi nyote ni watu ambao Nawapenda, wana Wangu wapendwa. Hakuna mtu atakayethubutu kuwakandamiza nyinyi kutoka wakati huo na kuendelea. Utakuwa wakati wenu wa kukua na kuwa watu wazima, na wakati wenu wa kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma! Ni nani anayethubutu kuwazuia Wana wangu wapendwa? Ni nani anayethubutu kuwashambulia wana Wangu wapendwa? Wote watawaheshimu wana Wangu wapendwa kwa sababu Baba ametukuzwa. Vitu vyote ambavyo hakuna mtu angeweza kufikiria daima vitaonekana mbele ya macho yenu. Vitakuwa havina kikomo, wasivyoisha, visivyo na mwisho. Kabla ya muda mrefu, nyinyi hakika hamtahitaji tena kuunguzwa na jua na kuvumilia joto linalotesa. Wala hamtalazimika kuteseka na baridi, wala mvua, theluji au upepo havitawafikia. Hii ni kwa sababu Nawapenda, na yote itakuwa ni dunia ya upendo Wangu. Nitawapa kila kitu mnachotaka, nami Nitawaandaa kwa ajili ya kila kitu ambacho mnahitaji. Nani anathubutu kusema kuwa Mimi si mwenye haki? Nitakuua mara moja, kwa sababu Nimewaambia kabla ya kuwa ghadhabu Yangu (dhidi ya waovu) itaendelea milele, nami Sitaachilia hata kidogo. Hata hivyo, upendo Wangu (kwa wana Wangu wapendwa) pia utaendelea milele; Sitauzuia hata kidogo.
kutoka katika “Sura ya 84” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri. Itakuwa mwanzo wa maisha ya mwanadamu na Mungu duniani. Nguzo ya maisha mema kama haya ni lazima iwe hivyo, hivi kwamba baada ya mwanadamu kutakaswa na kushindwa, anajiwasilisha mbele za Muumba. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu kabla ya wanadamu kuingia katika hatima ya ajabu. Maisha kama haya ni maisha ya baadaye ya mwanadamu duniani, ni maisha yanayopendeza zaidi duniani, aina ya maisha ambayo mwanadamu ametamania, aina ambayo mwanadamu hajawahi kamwe kutimiza katika historia ya ulimwengu. Ni matukio ya mwisho ya miaka 6,000 ya kazi ya usimamizi, na ndicho wanadamu wanatamani sana, na pia ni ahadi ya Mungu kwa mwanadamu. Lakini ahadi hii haiwezi timika mara moja: Mwanadamu ataingia katika hatima ya mbeleni punde tu kazi ya siku za mwisho zitakapokuwa zimemalizika na yeye amekwisha kushindwa kikamilifu, yaani, punde tu Shetani atakapokuwa ameshindwa kabisa. Mwanadamu atakuwa hana asili ya kutenda dhambi baada ya kusafishwa, kwa sababu Mungu atakuwa amemshinda Shetani, ambayo ina maana kuwa hakutakuwepo na kuvamiwa na vikosi vya uhasama, na hakuna vikosi vya uhasama ambavyo vinaweza kushambulia mwili wa mwanadamu. Na kwa hivyo mwanadamu atakuwa huru, na mtakatifu—yeye atakuwa ameingia ahera.
kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.
kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni wale tu ambao wanampenda Mungu wanaweza kumshuhudia Mungu, ndio tu mashahidi wa Mungu, ndio tu wamebarikiwa na Mungu, na ndio tu wanaweza kupokea ahadi za Mungu. Wanaompenda Mungu ni wandani wa Mungu, ndio watu ambao wamependwa na Mungu, na wanaweza kufurahia baraka pamoja na Mungu. Ni watu hawa tu ambao wataishi milele, na ni wao tu wataishi milele katika utunzaji na ulinzi wa Mungu. Mungu yuko kwa ajili ya kupendwa na watu, na anastahili upendo wa watu wote, lakini si watu wote ambao wanaweza kumpenda Mungu, na si watu wote wanaweza kumshuhudia Mungu na kushiriki mamlaka pamoja na Mungu. Kwa sababu wanaweza kumshuhudia Mungu, na kutoa juhudi zao zote kwa kazi ya Mungu, wanaompenda Mungu kwa kweli wanaweza kutembea mahala popote chini ya mbingu bila ya mtu yeyote kujaribu kuwapinga, na wanaweza kushika mamlaka na kutawala watu wote wa Mungu. Hawa watu wanakusanyika pamoja kutoka pembe zote za dunia, wanazungumza lugha tofauti na ni wa rangi tofauti, lakini kuishi kwao kuna maana sawa, wote wana moyo unaompenda Mungu, wote wana ushuhuda sawa, na wana maazimio sawa, na mapenzi sawa. Wale ambao wanampenda Mungu wanaweza kutembea ulimwenguni kote wakiwa huru, wanaomshuhudia Mungu wanaweza kusafiri duniani kote. Watu hawa wamependwa wa Mungu, wamebarikiwa na Mungu, na wataishi milele katika mwangaza Wake.
kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu. Binadamu wa aina hii tu ndiye anayestahili kurithi baraka hizi alizofadhiliwa na Mungu:
1. Kupokea upendo mzima wa Mungu.
2. Kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu katika kila kitu.
3. Kupokea mwongozo wa Mungu, kuishi chini ya mwangaza wa Mungu, na kupatiwa nuru na Mungu.
4. Kuishi kwa kudhihirisha taswira inayopendwa na Mungu hapa ulimwenguni; kumpenda Mungu kwa kweli kama vile Petro alivyofanya, kusulubishwa kwa sababu ya Mungu na kustahili kufa kwa kuufidia upendo wa Mungu; kuwa na utukufu sawa na Petro.
5. Kupendwa, kuheshimiwa, na kuvutiwa na wote ulimwenguni.
6. Kushinda utumwa wote wa kifo na Kuzimu, kutoipatia fursa yoyote kazi ya Shetani, kumilikiwa na Mungu, kuishi ndani ya roho safi na changamfu, na kutokuwa na hisia zozote za uchovu.
7. Kuwa na hisia isiyoelezeka ya msisimko na furaha siku zote katika maisha yako yote, ni kana kwamba ameona kuja kwa siku ya utukufu wa Mungu.
8. Kupokea utukufu pamoja na Mungu, na kuwa na sura inayofanana na watakatifu wapendwa wa Mungu.
9. Kuwa kile ambacho Mungu anapenda zaidi ulimwenguni, yaani, mwana mpendwa wa Mungu.
10. Kubadilisha maumbile na kupaa juu pamoja na Baba kwenye mbingu ya tatu, na kuuzidi mwili.
Wale tu wanaoweza kurithi baraka za Mungu ni wale waliokamilishwa na Mungu na kupatwa na Mungu. Je, umefaidi chochote? Mungu amekukamilisha hadi kiwango gani? Mungu hamkamilishi binadamu bila mpango. Kunayo masharti na matokeo dhahiri yanayoweza kuonekana na binadamu. Si jinsi mwanadamu anavyoamini, kwamba mradi tu awe na imani katika Mungu, anaweza kukamilishwa na kupatwa na Mungu, na anaweza kupokea hapa ulimwenguni baraka na urithi wa Mungu. Mambo kama haya ni magumu mno, na hata zaidi inapohusu kubadilika kwa taratibu. Kwa sasa, kile ambacho mnafaa kutafuta kimsingi ni kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, na kukamilishwa na Mungu kupitia kwa watu wote, mambo yote na vitu vyote ambavyo mnakumbwa navyo, ili mambo zaidi ya kile Mungu Alicho yatashirikishwa ndani yenu. Lazima kwanza mpokee urithi wa Mungu ulimwenguni kabla ya kustahili kurithi baraka nyingi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu. Mambo yote haya ndiyo ambayo mnafaa kutafuta na ambayo kwanza mnafaa kuelewa.
kutoka katika “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu

Jumatatu, 26 Agosti 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Ingawa wale waliozaliwa katika enzi hii wametiishwa chini ya upotovu wa Shetani na mapepo wachafu sana, pia ni kweli kwamba wanaweza kupata wokovu mkuu kutokana na upotovu huu, hata mkubwa kuliko mifugo wanaotanda milima na tambarare na mali nyingi ya familia ambayo Ayubu alipata, na pia ni zaidi ya baraka ambayo Ayubu alipokea ya kumwona Yehova baada ya majaribu yake. Ilikuwa tu baada ya Ayubu kupitia jaribio la kifo ndipo angeweza kuyasikia maneno ya Yehova na angeweza kusikia sauti Yake ya mshindo kutoka mawinguni. Hata hivyo, hakuuona uso wa Yehova na hakujua tabia Yake. Kile Ayubu alipata kilikuwa tu mali ya kimwili ambayo hutoa furaha za mwili na watoto wazuri mno katika miji jirani pamoja na ulinzi kutoka kwa malaika wa mbinguni. Hakuwahi kumwona Yehova, na hata ingawa aliitwa mwenye haki, kamwe hakuijua tabia ya Yehova. Ingawa watu wa leo ni maskini kwa muda katika starehe za kimwili au wanapitia mazingira ya nje ya uhasama, Nimedhihirisha tabia Yangu ambayo Sikuwahi kuifunua kwa wanadamu katika vizazi vilivyopita, ambayo siku zote imekuwa siri, na miujiza Yangu kabla ya enzi kwa watu duni mno ambao pia Nimewapa wokovu mkuu, na hii ni mara ya kwanza ambayo Nimefanya hivyo. Sijawahi kufanya aina ya hii awali, na ingawa ninyi mko chini zaidi kuliko Ayubu, yale mmepata na yale mmeona yamemshinda Ayubu kwa mbali. Ingawa mmepitia kila aina ya mateso na maudhi, mateso hayo si kama majaribu ya Ayubu, lakini ni hukumu na kuadibu ambako watu wamepokea kwa sababu ya uasi na ukinzani wao, na kwa sababu ya tabia Yangu yenye haki. Ni hukumu yenye haki, kuadibu, na laana. Ayubu alikuwa mmoja wa Waisraeli, mmoja wa watu wenye haki aliyepokea upendo na rehema ya ajabu ya Yehova. Hakufanya vitendo viovu na hakumpinga Yehova; badala yake, alijitoa kwa Yehova kwa uaminifu, naye alitiishwa chini ya majaribu kwa sababu ya haki yake, na alipitia majaribu makali kwa sababu alikuwa mtumishi mwaminifu wa Yehova. Watu leo wako chini ya hukumu na laana Yangu kwa sababu ya uchafu na uovu wao. Ingawa mateso yao hayalingani kabisa na kile Ayubu alipitia wakati alipoteza mifugo wake, mali yake, watumishi wake, watoto wake, na wale walio wapendwa kwake wote, kile watu wanapitia ni usafishaji na uteketezaji mkali; kilicho kikubwa zaidi kuliko kile Ayubu alipitia ni kwamba aina hii ya jaribio haipunguzwi wala kuondolewa kwa sababu ya udhaifu wao, badala yake, ni ya muda mrefu hadi siku yao ya mwisho ya maisha. Hii ni adhabu, hukumu, laana—ni ya kuteketea bila huruma, na hata zaidi ni “urithi” wa wanadamu wa haki. Ni kile wanachostahili, na ni mahali pa maonyesho ya tabia Yangu yenye haki. Ni ukweli unaojulikana. Lakini yale watu wamepata yanapita sana yale wamevumilia sasa. Yale ambayo mmepitia ni vipingamizi tu kutokana na upumbavu, lakini mapato yenu ni mara mia zaidi ya mateso yenu. Kwa mujibu wa sheria za Israeli katika Agano la Kale, wale wote wanaonipinga Mimi, wale wote wanaonihukumu waziwazi, na wale wote wasioifuata njia Yangu lakini wanatoa sadaka zenye kukufuru Kwangu kwa ujasiri kwa hakika wataharibiwa kwa moto katika hekalu, au baadhi ya watu waliochaguliwa watawatupia mawe hadi kifo, na hata vizazi vyao vya nyumba yao wenyewe na jamaa zao wengine wa karibu watapitia laana Yangu, na katika dunia ijayo hawatakuwa huru, lakini watakuwa watumwa wa watumwa Wangu, Nami nitawaelekeza hadi uhamishoni miongoni mwa Mataifa nao hawataweza kurudi katika nchi yao. Kulingana na vitendo vyao, tabia zao, mateso yanayovumiliwa na watu leo si makubwa kama adhabu waliyopitia Waisraeli. Kusema kuwa kile mnachopitia sasa ni adhabu si bila sababu, na hii ni kwa sababu mmevuka mpaka kweli, na kama mngekuwa katika Israeli mngekuwa mmoja wa wenye dhambi milele na mngekatwa vipande vipande na Waisraeli muda mrefu uliopita na pia mngeteketezwa kwa moto kutoka mbinguni katika hekalu la Yehova. Na nini ambacho mmepata sasa? Nini ambacho mmepokea, nini ambacho mmefurahia? Nimedhihirisha tabia Yangu yenye haki ndani yenu, lakini muhimu zaidi ni kwamba Nimefunua uvumilivu Wangu kwa ukombozi wa mwanadamu. Mtu angesema kwamba yote ambayo Nimefanya ndani yenu ni kazi na uvumilivu, kwamba ni kwa ajili ya usimamizi Wangu, na hata zaidi ni kwa ajili ya starehe ya wanadamu.
Ingawa Ayubu alipitia majaribu kutoka kwa Yehova, alikuwa tu mtu mwenye haki aliyemwabudu Yehova, na hata alipokuwa akipitia majaribu hayo hakulalamika kumhusu Yeye, lakini alithamini sana kukutana kwake na Yehova. Watu wa leo hawathamini tu uwepo wa Yehova, bali humkataa, humchukia sana, hulalamika kumhusu, na hudhihaki uwepo Wake. Je, hamjapata zaidi ya kidogo? Je, mateso yenu kweli hayajakuwa makubwa sana? Je, baraka zenu hazijakuwa nyingi kuliko zile za Maria na Yakobo? Je, upinzani wenu haujakuwa hafifu? Inawezekana kuwa yale Nimehitaji kwenu, yale Nimeuliza kutoka kwenu yamekuwa makuu mno na mengi sana? Ghadhabu Yangu iliachiliwa huru tu juu ya wale Waisraeli walionipinga Mimi, si moja kwa moja juu yenu, lakini kile ambacho mmepata kimekuwa tu hukumu Yangu isiyo na huruma na mafichuzi pamoja na utakaso mkali usio na huruma. Licha ya haya watu bado wananipinga na kunikana Mimi bila hata chembe ya utii. Na hata kuna baadhi ya watu ambao hujitenga na Mimi na kunikataa; aina hiyo ya mtu si bora zaidi kuliko bendi ya Kora na Dathani wakimpinga Musa. Mioyo ya watu imekuwa migumu sana, na asili zao ni kaidi sana. Kamwe hawatabadili mienendo yao ya zamani. Wamejiweka wazi kama kahaba hadharani kwa matamshi Yangu, na maneno Yangu ni makali sana kwamba “hayana adabu”, yakiweka wazi asili za watu hadharani. Lakini watu huamkia tu kwa vichwa vyao, wanamwaga machozi machache, na kuwa na hisia za kusikitisha kidogo tu. Mara tu inapoisha, ni wakali kama mfalme wa wanyama wa pori katika milima na hawana utambuzi kabisa. Je, watu na aina hii ya tabia wanawezaje kujua kwamba wamefurahia baraka zaidi ya mara mia kuliko zile za Ayubu? Wanawezaje kugundua kwamba kile wanachokifurahia ni baraka ambazo zimeonekana katika enzi zote kwa nadra sana, ambazo hakuna mtu aliyewahi kuzifurahia awali? Dhamiri za watu zinawezaje kuhisi aina hii ya baraka ambayo hubeba adhabu? Kusema ukweli, chote Ninachohitaji kwenu ni ili muweze kuwa mifano kwa kazi Yangu na kuwa mashahidi kwa ajili ya tabia Yangu yote na matendo Yangu yote, na ili muweze kuwekwa huru kutokana na mateso ya Shetani. Lakini wanadamu daima huchukizwa na kazi Yangu na wanakuwa na uhasama kwake kimakusudi. Aina hiyo ya mtu anawezaje kutonichochea Mimi kurejesha sheria za Israeli na kuleta juu yake ghadhabu Yangu kwa ajili ya Israeli? Ingawa kuna wengi miongoni mwenu ambao ni “watiifu” Kwangu, kuna hata zaidi ambao wa namna ya “bendi ya Kora” Mara tu Nitakapoupata utukufu Wangu kamili, Nitachukua moto kutoka mbinguni na kuwateketeza hadi wawe majivu. Mnapaswa kujua kwamba Sitawaadibu watu kwa maneno Yangu tena, lakini kabla ya kuifanya kazi ya Israel, Nitaiteketeza kabisa ile namna ya “bendi ya Kora” wanaonipinga Mimi na ambao Nimewaondoa muda mrefu uliopita. Wanadamu hawatapata tena nafasi ya kunifurahia, lakini yote ambayo wataona yatakuwa ghadhabu na “moto” Wangu kutoka mbinguni. Nitafichua matokeo ya watu wote, na Nitawagawanya watu wote katika makundi mbalimbali. Nitaangalia kila tendo lao lenye uasi, na kisha kuimaliza kazi Yangu, ili matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na uamuzi Wangu wakati wako duniani pamoja na mitazamo yao kunihusu. Wakati huo utakapofika, hakutakuwa na kitu kitakachoweza kubadilisha matokeo yao. Acha watu wafunue matokeo yao wenyewe! Acha Niyakabidhi matokeo ya watu kwa Baba wa mbinguni.
Soma Zaidi :Umeme wa Mashariki Unatoka Wapi?

Jumamosi, 27 Julai 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Tabia ya Mungu iko wazi kwa kila mmoja na haijafichwa, kwa sababu Mungu hajawahi kuepuka kimakusudi mtu yeyote na Hajawahi kimakusudi kujaribu kujificha Mwenyewe ili watu wasiweze kumjua Yeye au kumwelewa Yeye. Tabia ya Mungu siku zote imekuwa wazi na siku zote imekuwa ikitazama kila mtu kwa njia ya uwazi. Katika usimamizi wa Mungu, Mungu hufanya kazi Yake akitazama kila mmoja; na kazi Yake ndiyo inafanywa kwa kila mtu . Anapofanya kazi hii, Anafichua bila kusita tabia Yake, huku Akitumia bila kusita kiini Chake na kile Anacho na alicho kuongoza na kukimu kila mmoja. Katika kila enzi na kila awamu, licha ya kama hali ni nzuri au mbaya, tabia ya Mungu siku zote iko wazi kwa kila mtu binafsi,na vile vitu Anavyomiliki na uwepo Wake siku zote viko wazi kwa kila mtu binafsi, kwa njia sawa kwamba maisha Yake yanamtoshelezea mwanadamu kila wakati na bila kusita na kumsaidia mwanadamu.” Tazama zaidi: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha
Hawanuii kufahamu mapenzi ya Mungu kupitia ushirikiano wa kimakusudi—wanafurahia tu milele na hawachoki kufanya mambo wanayotaka kuyafanya; kusadiki kwa Mungu wanayetaka kusadiki kwake; kusadiki kwa Mungu anayekuwepo tu katika dhana zao, Mungu anayekuwepo tu katika fikira zao, Mungu anayekuwepo tu katika dhana zao; na kusadiki kwa Mungu asiyeweza kutenganishwa na wao katika maisha yao ya kila siku. Na kwake Mungu Mwenyewe wa kweli, wanapuuza kabisa, hawataki kusikia mambo ya Mungu na hawana tamanio la kumwelewa Yeye, kumtilia maanani Yeye, na hata hawana nia kidogo ya kuwa karibu zaidi na Yeye. Wanayatumia tu maneno ambayo Mungu anayaonyesha ili kuweza kujipamba, kujiandaa upya. Kwa wao, hilo tayari linawafanya kuwa waumini wenye mafanikio na watu walio na imani kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Ndani ya mioyo yao, wanaongozwa na kufikiria kwao, dhana zao, na hata ufasili wao binafsi wa Mungu. Mungu Mwenyewe wa kweli, kwa mkono mwingine, hana chochote kuhusiana na wao. Kwa sababu pindi wanapomwelewa Mungu Mwenyewe wa kweli, kuelewa tabia ya Mungu ya kweli, na kuelewa kile Mungu anacho na alicho, hii inamaanisha kwamba vitendo vyao, imani yao, na yale yote wanayoyafuatilia yatashutumiwa. Na ndiyo maana hawako radhi kukielewa kiini cha Mungu, na ndiyo maana wanasitasita na hawako radhi kutafuta kwa bidii au kuomba kumwelewa zaidi Mungu, kupata kujua zaidi kuhusu mapenzi Yake Mungu, na kuelewa kwa njia bora zaidi tabia ya Mungu. Afadhali Mungu kwao awe kitu kilichotungwa, kisicho na chochote na kibaya. Afadhali kwao Mungu awe mtu ambaye yupo hasa vile ambavyo wamemfikiria Yeye, Anayeweza kunyenyekea mbele zao, Asiyeishiwa na ujazo na Anayepatikana siku zote. Wanapotaka kufurahia neema ya Mungu, wanamuomba Mungu kuwa hiyo neema. Wanapohitaji baraka za Mungu, wanamuomba Mungu kuwa baraka hizo. Wanapokabiliwa na dhiki, wanamwomba Mungu kuwatia wao moyo, na kuwa usalama wao. Maarifa ya watu hawa kumhusu Mungu imebakia palepale pa mipaka ya neema na baraka. Uelewa wao wa kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu umezuiliwa pia na kufikiria kwao na vilevile barua na mafundisho ya kidini tu. Lakini wapo baadhi ya watu walio na hamu ya kuielewa tabia ya Mungu, wanaotaka kumwona Mungu Mwenyewe kwa kweli, na kuielewa tabia ya Mungu kwa kweli na kile Anacho na alicho. Watu hawa wanautafuta uhalisia wa ukweli na wokovu wa Mungu na wanatafuta kupokea ushindi, wokovu, na utimilifu wa Mungu. Watu hawa wanaitumia mioyo yao kulisoma neno la Mungu, wanaitumia mioyo yao kuthamini hali na kila mtu, tukio, au kitu ambacho Mungu amewapangia, na kuomba na kutafuta kwa uaminifu. Kile wanachotaka zaidi ni kuyajua mapenzi ya Mungu na kuielewa tabia ya kweli na kiini cha Mungu. Hivi ndivyo ilivyo ili wasiweze tena kumkosea Mungu, na kupitia kwa mambo waliyoyapitia, waweze kuona upendo zaidi wa Mungu na upande Wake wa kweli. Iko hivyo pia ili Mungu halisi na wa kweli ataweza kuwepo ndani ya mioyo yao, na ili Mungu atakuwa na nafasi katika mioyo yao, kiasi cha kwamba hawatakuwa wakiishi tena miongoni mwa kufikiria, dhana, au hali ya kuyaepuka mambo. Kwa watu hawa, sababu inayowafanya kuwa na tamanio kuu la kuielewa tabia ya Mungu na kiini Chake ni kwa sababu tabia ya Mungu na kiini Chake ni mambo ambayo mwanadamu anaweza kuyahitaji wakati wowote katika uzoefu wao, mambo yanayojaza uhai katika maisha yao yote walioishi. Pindi wanapoielewa tabia ya Mungu, wataweza kumheshimu sana kwa njia bora zaidi, kushirikiana kwa njia bora zaidi na kazi ya Mungu, na kuyaweka zaidi katika fikira mapenzi ya Mungu na kutekeleza wajibu wao kwa njia bora zaidi wakitumia uwezo wao. Hawa ndio watu wa aina mbili inapokuja katika mielekeo yao kwa tabia ya Mungu. Watu wa aina ya kwanza hawataki kuielewa tabia ya Mungu. Ingawaje wanasema wanataka kuielewa tabia ya Mungu, kupata kumjua Mungu Mwenyewe, kuona kile Mungu anacho na alicho, na kushukuru kwa dhati mapenzi ya Mungu, ndani yao kabisa wanaona afadhali Mungu asikuwepo. Ni kwa sababu watu wa aina hii wanakosa kumtii Mungu kila wakati na wanampinga; wanapigana na Mungu kwa sababu ya vyeo vilivyo ndani ya mioyo yao na mara nyingi wanashuku na hata kukataa uwepo wa Mungu. Hawataki kuruhusu tabia ya Mungu au kuacha Mungu mwenyewe wa kweli kumiliki mioyo yao. Wanataka tu kutosheleza matamanio, kufikiria, na maono yao binafsi. Hivyo basi, watu hawa wanaweza kumsadiki Mungu, kumfuata Mungu, na hata wanaweza kutupilia mbali familia na kazi zao kwa sababu Yake Yeye, lakini hawasitishi njia zao za maovu. Baadhi yao hata huiba au kubadhiri sadaka au kumlaani Mungu kisirisiri, huku wengine wakiweza kutumia vyeo vyao kushuhudia mara kwa mara kuhusu wao wenyewe, kujiongezea zaidi umaarufu wao, na kushindana na Mungu kwa ajili ya watu na hadhi. Wanatumia mbinu na njia mbalimbali kuwafanya watu kuwaabudu, kujaribu mara kwa mara kuwa na ufuasi mkubwa wa watu na kutaka kuwadhibiti watu hao. Baadhi hata hupotosha kimakusudi watu na kuwafanya kufikiria kwamba wao ni Mungu ili waweze kuchukuliwa kama Mungu. Hawawezi katu kuwaambia watu kwamba wamepotoshwa, kwamba pia wao wamepotoka na wana kiburi, na hivyo basi hawafai kuwaabudu, na kwamba haijalishi watafanya vyema kiasi kipi, haya yote ni kutokana na utukuzaji wa Mungu na kile wanachostahili kufanya kwa kweli. Kwa nini hawasemi mambo haya? Kwa sababu wana hofu kuu ya kupoteza nafasi yao ndani ya mioyo ya watu. Hii ndiyo maana watu kama hao hawamtukuzi Mungu katu na katu hawamshuhudii Mungu, kwani hawajawahi kujaribu kumwelewa Mungu. Wanaweza kumjua Mungu kama hawamwelewi? Haiwezekani! Hivyo, ingawa maneno katika mada “kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu mwenyewe” yanaweza kuwa rahisi, maana yao ni tofauti kwa kila mmoja. Kwa mtu anayekosa kumtii Mungu mara kwa mara, na anampinga Mungu na ni mkatili kwa Mungu, yanamaanisha shutuma; huku kwa mtu anayefuatilia uhalisia wa kweli na mara nyingi anakuja mbele ya Mungu kutafuta mapenzi ya Mungu, maneno hayo bila shaka ni kama samaki na maji. Hivyo miongoni mwenu, wakati baadhi yenu mnaposikiza mazungumzo ya tabia ya Mungu na kazi ya Mungu, wanaanza kuumwa na kichwa, mioyo yao inajaa upinzani, na wanakuwa katika hali isiyo na utulivu kabisa. Lakini kuna wengine miongoni mwenu wanaofikiria: Mada hii ndiyo hasa Ninayohitaji, kwa sababu mada hii ni yenye manufaa sana kwangu. Ni sehemu ambayo haiwezi kukosekana katika uzoefu wangu wa maisha; ni swali ambalo halijapata jibu bado, msingi wa imani kwa Mungu, na jambo ambalo mwanadamu hawezi kufikiria kuliacha. Kwenu nyote, mada hii inaweza kuonekana kuwa karibu na mbali, isiyojulikana ilhali inayozoeleka. Lakini haijalishi ni nini, hii ni mada ambayo kila mmoja aliyeketi hapa lazima aisikilize, aijue, na lazima aielewe. Haijalishi ni vipi utakavyoishughulikia, haijalishi ni vipi utakavyoiangalia au utakavyoipokea, lakini umuhimu wa mada hii huwezi kupuuzwa.
Mungu amekuwa akifanya kazi Yake tangu Alipomuumba mwanadamu. Mwanzoni, kazi ilikuwa rahisi sana, lakini hata hivyo, ingali ilikuwa na maonyesho ya kiini na tabia ya Mungu. Ingawa kazi ya Mungu sasa imepandishwa daraja, na Yeye akitia kiwango kikubwa mno cha kazi thabiti kwa kila mmoja anayemfuata Yeye, na kuonyesha kiwango kikubwa cha neno Lake, kuanzia mwanzo hadi sasa, nafsi ya Mungu imekuwa ikifichwa kutoka kwa mwanadamu. Ingawaje amekuwa mwili mara mbili, kuanzia wakati wa simulizi za biblia hadi kwa siku za kisasa, nani amewahi kuona nafsi halisi ya Mungu? Kutokana na uelewa wenu, yupo mtu amewahi kuona nafsi halisi ya Mungu? La. Hakuna aliyewahi kuona nafsi halisi ya Mungu, kumaanisha hakuna aliyewahi kuona nafsi ya kweli ya Mungu. Hili ni jambo ambalo kila mmoja anakubaliana nalo. Hivi ni kusema, nafsi halisi ya Mungu, au Roho wa Mungu, amefichwa kutoka kwa binadamu wote, wakiwemo Adamu na hawa, ambao Aliwaumba, na akiwemo Ayubu mwenye haki, ambaye alikuwa Amemkubali. Hata wao hawakuona nafsi halisi ya Mungu. Lakini kwa nini Mungu anaficha kimakusudi nafsi Yake halisi? Baadhi ya watu husema: “Mungu anaogopa kuwaogofya watu.” Wengine husema: “Mungu huficha nafsi Yake halisi kwa sababu binadamu ni mdogo sana na Mungu ni mkubwa sana; wanadamu hawaruhusiwi kumwona Yeye, la sivyo watakufa.” Wapo pia wale wanaosema: “Mungu ameshughulika sana akisimamia kazi Yake kila siku, huenda Asiwe na muda wa kuonekana na kuruhusu watu kumwona Yeye.” Haijalishi ni nini mnachosadiki, Ninayo hitimisho hapa. Hitimisho hilo ni nini? Ni kwamba Mungu hataki hata watu kuona nafsi Yake halisi. Akiwa amefichwa kutoka kwa binadamu ni kitu ambacho Mungu anafanya kimakusudi. Kwa maneno mengine, ni nia ya Mungu kwa watu kutoona nafsi Yake halisi. Hili linafaa kuwa wazi kwa wote sasa. Kama Mungu hajawahi kuonyesha nafsi Yake kwa yeyote, basi mnafikiria nafsi ya Mungu ipo? (Ipo.) Bila shaka ipo. Uwepo wa nafsi ya Mungu haupingiki. Lakini kuhusu nafsi ya Mungu ni kubwa vipi au inafanana vipi, haya ni maswali ambayo mwanadamu anafaa kuchunguza? La. Jibu ni la. Kama nafsi ya Mungu si mada ambayo tunafaa kuchunguza, basi ni swali lipi ambalo tunafaa kuchunguza? (Tabia ya Mungu.) (Kazi ya Mungu.) Kabla hatujaanza kuwasiliana mada hii rasmi, hata hivyo, hebu turudi katika kile tulichokuwa tukikizungumzia muda mfupi uliopita: Kwa nini Mungu hajawahi kuonyesha nafsi Yake kwa mwanadamu? Kwa nini Mungu anaficha kimakusudi nafsi Yake kutoka kwa mwanadamu? Kunayo sababu moja tu, nayo ni: Ingawaje binadamu aliyeumbwa amepitia miaka elfu na elfu ya kazi ya Mungu, hakuna hata mtu mmoja anayejua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na kiini cha Mungu. Watu kama hao, mbele ya macho ya Mungu, ni upinzani kwake Yeye, na Mungu hatajionyesha kwa watu walio wakatili kwake Yeye. Hii ndiyo sababu ya pekee mbona Mungu hajawahi kumwonyesha binadamu nafsi Yake na ndiyo sababu anaikinga yeye kimakusudi nafsi Yake dhidi yao. Sasa mnaelewa kuhusu umuhimu wa kujua tabia ya Mungu?
Tangu kuwepo kwa usimamizi wa Mungu, siku zote amejitolea kabisa katika kutekeleza kazi Yake. Licha ya kuficha nafsi Yake kutoka kwao, siku zote Amekuwa katika upande wa binadamu, akiwafanyia kazi, akionyesha tabia Yake, akiongoza binadamu wote na kiini Chake, na kufanya kazi Yake kwa kila mmoja kupitia nguvu Zake, hekima Yake, na mamlaka Yake, hivyo akiileta Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na sasa Enzi ya Ufalme katika uwepo. Ingawaje Mungu huificha nafsi Yake kutoka kwa binadamu, tabia Yake, uwepo Wake na miliki Yake, na mapenzi Yake kwa binadamu yanafichuliwa bila wasiwasi wowote kwa binadamu kwa minajili ya kuona na kupitia hali hiyo. Kwa maneno mengine, ingawaje binadamu hawawezi kumwona au kumgusa Mungu, tabia na kiini cha Mungu ambacho binadamu wamekuwa wakigusana nacho ni maonyesho kabisa ya Mungu Mwenyewe. Je, hayo si kweli? Licha ya ni mbinu gani au ni kutoka katika mtazamo gani Mungu hufanya kazi Yake, siku zote Anawakaribisha watu kulingana na utambulisho Wake wa kweli, akifanya kile ambacho Anafaa kufanya na kusema kile Anachofaa kusema. Haijalishi ni nafasi gani Mungu anazungumzia kutoka—Anaweza kuwa amesimama kwenye mbingu ya tatu, au amesimama akiwa mwili Wake, au hata kama mtu wa kawaida—siku zote Anaongea kwa binadamu kwa moyo Wake wote na kwa akili Zake zote, bila uongo na bila ufichaji wowote. Wakati Anapotekeleza kazi Yake, Mungu huonyesha neno Lake na tabia Yake, na huonyesha kile Anacho na alicho, bila kuficha chochote. Anamwongoza mwanadamu na maisha Yake na uwepo Wake na miliki yake. Hivi ndivyo binadamu alivyoishi katika Enzi ya Sheria—enzi asilia ya binadamu—akiongozwa na Mungu asiyeonekana na asiyegusika.
Mungu alipata mwili kwa mara ya kwanza baada ya Enzi ya Sheria, hali ya kupata mwili iliyodumu kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Kwa mwanadamu, miaka thelathini na mitatu na nusu ni muda mrefu? (Si mrefu sana.) Kwa sababu urefu wa maisha ya mwanadamu ni mirefu kuliko miaka thelathini na fulani, huu si muda mrefu kwa mwanadamu. Lakini kwa Mungu mwenye mwili, miaka hii thelathini na mitatu na nusu ilikuwa mirefu mno. Aligeuka na kuwa mtu—mtu wa kawaida aliyetekeleza kazi na agizo la Mungu. Hii ilimaanisha kwamba lazima angefanya kazi ambayo mtu wa kawaida asingeweza kufanya, huku akivumilia mateso ambayo binadamu wa kawaida hawezi kuvumilia. Kiwango cha mateso aliyovumilia Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, kuanzia mwanzo wa kazi Yake hadi wakati Aliposulubishwa kwenye msalaba, huenda kisiwe ni kitu watu wa leo wangeweza kushuhudia wao binafsi, lakini mnaweza angaa kutambua kiasi kupitia hadithi zilizo kwenye Biblia? Licha ya ni maelezo mangapi yaliyopo kwenye ukweli huu uliorekodiwa, kwa ujumla, kazi ya Mungu katika kipindi hiki kilijaa ugumu na mateso. Kwa mwanadamu aliyepotoka muda wa miaka thelathini na mitatu na nusu si mrefu; mateso kidogo si jambo la kutisha. Lakini kwa Mungu mtakatifu asiye na doa, ambaye lazima avumilie dhambi zote za binadamu, na kula, kulala na kuishi na watenda dhambi, maumivu haya ni mengi mno. Yeye ndiye Muumba, Bwana wa viumbe vyote na Mtawala wa vitu vyote, lakini Alipokuja duniani alilazimika kuvumilia unyanyasaji na ukatili wa wanadamu waliopotoka. Ili kuikamilisha kazi Yake na kuokoa binadamu kutoka kwa taabu, Alilazimika kushutumiwa na binadamu, na kuvumilia dhambi za wanadamu wote. Kiwango cha mateso aliyopitia hakiwezi kwa kweli kueleweka au kutambulika na watu wa kawaida. Mateso haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu. Yanasimamia udhalilishaji Alioteseka na gharama Aliyolipia kwa sababu ya wokovu wa binadamu, kukomboa dhambi zake, na kukamilisha awamu hii ya kazi Yake. Yanamaanisha binadamu angekombolewa kutoka katika msalaba na Mungu. Hii ndiyo gharama iliyolipwa kwa damu, kwa maisha, gharama ambayo viumbe walioumbwa hawawezi kumudu. Ni kwa sababu Anacho kiini cha Mungu na Amejihami na kile Mungu anacho na alicho, ndiyo maana Anaweza kuvumilia aina hii ya mateso na aina hii ya kazi. Hili ni jambo ambalo hakuna kiumbe aliyeumbwa anaweza kufanya badala Yake. Hii ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema na ufunuo wa tabia Yake. Je, hii inafichua chochote kuhusu kile Mungu anacho na alicho? Je, wanadamu wanastahili kuijua?

Jumapili, 21 Julai 2019

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili.

5. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Maneno Husika ya Mungu:
Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. Ni mpaka siku za mwisho tu ambapo Mungu Ametakasa binadamu kikamilifu kwa kufanya kazi ya hukumu na kuadibu mwanadamu kwa kuwa muasi, ndipo Mungu atakamilisha kazi Yake ya wokovu na kupumzika. Kwa hivyo, katika hatua tatu za kazi, ni mara mbili tu ndipo Mungu Alikuwa mwili ili kufanya kazi Yake kati ya mwanadamu Mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu moja tu kati ya hatua tatu za kazi ni kuwaongoza wanadamu katika maisha yao, ilhali zingine mbili ni kazi ya wokovu. Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Katika hali hii tu ndipo Ataweza kumpatia mwanadamu wa uumbaji Wake neno la matendo wanalohitaji. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki na mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa maneno yote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili. Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili. Baada ya hapo, kazi ya Mungu mwenye mwili itakuwa imefika mwisho kabisa. Baada ya kupata mwili mara ya pili, hatakuwa mwili tena kwa kazi Yake. Kwani usimamizi Wake wote utakuwa umefika mwisho. Katika siku za mwisho, mwili Wake utakuwa umepata watu Wake teule kabisa, na yote mwanadamu katika siku za mwisho watakuwa wamegawanywa kulingana na aina yao. Hatafanya kazi ya wokovu tena, wala Hatarudi kuwa mwili ili kutekeleza kazi yoyote.

kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mwanadamu angeishi katika huo msingi, alichukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, hii ina maana kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia ya kuielekea tabia iliyobadilika; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii inamfanya mwanadamu kuwa safi kupitia neno ili kumpatia mwanadamu njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.

kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mungu mwenye mwili wa kwanza Hakukamilisha kazi ya kupata mwili; Alikamilisha tu hatua ya kwanza ya kazi iliyokuwa lazima kwa Mungu kuifanya katika mwili. Kwa hivyo, ili kuimaliza kazi ya kupata mwili, Mungu Amerudi katika mwili kwa mara nyingine tena, Akiishi kulingana na ukawaida na uhalisia wote wa mwili, yaani, kuifanya kazi ya Mungu ijitokeze katika mwili wa kawaida kabisa, na kwa njia hiyo Anahitimisha kazi Aliyoiacha bila kukamilisha katika mwili. Mwili wa pili uliopatikana kimsingi ni sawa na ule wa kwanza, lakini ni halisi zaidi, wa kawaida kabisa kuliko ule wa kwanza. Kwa sababu hiyo, mateso unayoyapitia mwili wa pili uliopatikana ni makubwa kuliko yale ya ule wa kwanza, ila mateso haya ni kwa sababu ya huduma Yake katika mwili, ambayo ni tofauti na mateso ya mwanadamu mwovu. Vilevile yanachipuka kutokana na ukawaida na uhalisi wa mwili Wake. Kwa kuwa Anatekeleza huduma Yake katika mwili wa kawaida na halisi kabisa, mwili ni sharti upitie mateso mazito. Kadiri mwili ulivyo wa kawaida na halisi, ndivyo unateseka zaidi katika utekelezaji wa huduma Yake. Kazi ya Mungu inaonyeshwa katika mwili wa kawaida sana, mwili ambao si wa rohoni kamwe. Kwa kuwa mwili Wake ni wa kawaida, na ni lazima ubebe kazi ya kumwokoa mwanadamu, Anateseka hata zaidi kuliko ambavyo mwili wa rohoni unaweza kuteseka—mateso haya yote yanatokana na uhalisi na ukawaida wa mwili Wake. Kutokana na mateso yaliyopitiwa na hii miili miwili iliyopatikana wakati wa kutekeleza huduma Zao, mtu anaweza kuona kiini cha mwili uliopatikana. Kadiri mwili ulivyo wa kawaida, ndivyo Anapata mateso mazito Afanyapo kazi, kadri mwili unaofanya kazi unavyokuwa wa kweli, ndivyo maoni ya watu yanaendelea kuwa makali, na hatari zinazomkabili zinaendelea kuongezeka. Lakini, kadiri mwili ulivyo halisi, kadiri mwili unavyokuwa na hali kamili ya binadamu wa kawaida, ndivyo Anaweza zaidi kuifanya kazi ya Mungu katika mwili. Ulikuwa mwili wa Yesu ulioangikwa msalabani, mwili Wake Alioutoa kama kafara kwa dhambi; ni kupitia kwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida ndipo Aliweza kumshinda Shetani na kumkomboa kabisa mwanadamu kutoka msalabani. Ni kupitia mwili kamili ndipo Mungu katika mwili mara ya pili Anatekeleza kazi ya ushindi na kumshinda Shetani. Ni mwili tu wa kawaida na halisi kabisa unaoweza kutekeleza kazi ya ushindi kwa ukamilifu wake na kutoa ushuhuda wa nguvu. Hii ni sawa na kusema kwamba kazi ya[a] kumshinda mwanadamu inafanywa kuwa bora kupitia uhalisia na ukawaida wa mwili wa Mungu, si kupitia miujiza mikuu na ufunuo. Huduma ya huyu Mungu mwenye mwili ni ya kunena na kwa njia hiyo inamshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu; kwa maneno mengine, kazi ya Roho Aliyejitokeza katika mwili, wajibu wa mwili, ni kunena na kupitia kwa hili kumshinda, kumfichua, kumfanya kuwa kamilifu, na kumwondoa mwanadamu kabisa. Kwa hivyo, ni katika kazi ya kushinda ambapo kazi ya Mungu katika mwili itatimiziwa kwa ukamilifu. Kazi ya ukombozi ya kwanza ilikuwa mwanzo tu wa kazi ya kupata mwili kwa Yesu; mwili unaofanya kazi ya kushinda utaikamilisha kazi nzima ya kupata mwili kwa Yesu. Kijinsia, mmoja ni mwanamke na mwingine ni mwanamume; kwa hili, maana ya kupata mwili kwa Mungu imekamilishwa. Mawazo mabaya ya mwanadamu kumhusu Mungu yameondolewa: Mungu Anaweza kuwa mwanamke na mwanamume, na kimsingi Mungu mwenye mwili Hana jinsia. Alimuumba mwanamume na mwanamke, na Hatofautishi kati ya hizi jinsia. Katika hatua hii ya kazi, Mungu Hafanyi ishara na miujiza, ili kwamba kazi iweze kutimiza matokeo yake kupitia kwa maneno. Sababu ya jambo hili, aidha, ni kwa maana kazi ya Mungu mwenye mwili mara hii si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, ila kumshinda mwanadamu kupitia kunena, ikiwa na maana kwamba uwezo asili uliomo kwenye huu mwili uliopatikana wa Mungu ni kunena maneno na kumshinda mwanadamu, si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo. Kazi Yake katika ubinadamu wa kawaida si kutenda miujiza, si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, ila ni kunena, na kwa hivyo Yesu kupata mwili kwa mara ya pili kunaonekana kwa watu kuwa kawaida zaidi ya mara ya kwanza. Watu wanaona kuwa Mungu kupata mwili si uongo; lakini huyu Mungu mwenye mwili ni tofauti na Yesu Aliyekuwa mwili, na japo wote ni Mungu wenye mwili, Hawako sawa kabisa. Yesu Alikuwa na ubinadamu wa desturi, ubinadamu wa kawaida, lakini Aliambatana na ishara nyingi na miujiza. Katika huyu Mungu mwenye mwili, macho ya mwanadamu hayataona ishara au miujiza, wala kuponya wagonjwa au kufukuza mapepo, wala kutembea juu ya bahari, wala kufunga kwa siku arobaini… Hafanyi kazi sawa na Aliyoifanya Yesu, si kwa kuwa mwili Wake kimsingi ni tofauti na ule wa Yesu, ila ni kwa sababu si huduma Yake kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo. Haharibu kazi Yake mwenyewe, Havurugi kazi Yake mwenyewe. Kwa kuwa anamshinda mwanadamu kwa maneno Yake halisi, haina haja ya kumhini kwa miujiza, na kwa hivyo hii hatua ni kukamilisha kazi ya kupata mwili.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kwa nini Ninasema kuwa maana ya kupata mwili haikukamilishwa katika kazi ya Yesu? Ni kwa sababu Neno halikuwa Mwili kikamilifu. Kilichofanywa na Yesu kilikuwa tu sehemu moja ya kazi ya Mungu katika mwili; Alifanya tu kazi ya ukombozi na Hakufanya kazi ya kumpata mwanadamu kikamilifu. Kwa sababu hii, Mungu Amekuwa mwili mara nyingine tena katika siku za mwisho. Hatua hii ya kazi, pia inafanywa katika mwili wa kawaida, ikifanywa na mwanadamu wa kawaida kabisa, ambaye ubinadamu wake haupiti mipaka ya ubinadamu. Kwa maneno mengine, Mungu Amekuwa mwanadamu kamili, na ni mtu ambaye utambulisho wake ni ule wa Mungu, mwanadamu kamili, mwili kamili, Ambaye Anatekeleza kazi. Katika jicho la mwanadamu, Yeye ni mwili tu ambao haujapita mipaka ya ubinadamu hata kidogo, mwanadamu wa kawaida kabisa Anayeweza kuzungumza lugha ya mbinguni, Ambaye Haonyeshi ishara za kimiujiza, Hafanyi miujiza, sembuse kuweka wazi ukweli wa ndani kuhusu dini katika kumbi kuu za mikutano. Kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili inaonekana kwa wanadamu kuwa tofauti kabisa na ile ya kwanza, kiasi kwamba kazi hizi mbili zinaonekana kutokuwa na uhusiano wowote, na hakuna chochote katika kazi ya kwanza kinachoweza kuonekana wakati huu. Japo kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili ni tofauti na ile ya kwanza, hili halithibitishi kuwa chanzo Chao si kimoja na sawa. Iwapo chanzo Chao ni kimoja inategemea aina ya kazi iliyofanywa na miili na si katika maumbo Yao ya nje. Katika hatua tatu za kazi Yake, Mungu Amekuwa mwili mara mbili, na mara zote kazi ya Mungu kuwa mwili inaanzisha enzi mpya, inaanzisha kazi mpya; kuwa mwili kwa mara ya kwanza na pili kunakamilishana. Macho ya wanadamu hayawezi kugundua kuwa hii miili miwili kwa kweli imetokana na chanzo kimoja. Ni wazi kwamba hili liko nje ya uwezo wa macho ya wanadamu au akili za wanadamu. Ila katika kiini Chao, ni miili sawa, kwani kazi Yao inatokana na Roho mmoja. Iwapo hii miili miwili inatokana na chanzo kimoja haiwezi kuamuliwa kutokana na enzi na sehemu Ilipozaliwa, au vigezo vingine kama hivyo, ila kwa kazi ya uungu iliyoonyeshwa Nayo. Kupata mwili wa pili hakufanyi kazi yoyote iliyofanywa na Yesu, kwani kazi ya Mungu haifuati makubaliano, lakini kila wakati inafungua njia mpya. Kupata mwili wa pili hakulengi kuongeza au kuimarisha maono ya kupata mwili wa kwanza katika akili za watu, ila kuutimiza na kuukamilisha, kuongeza kina cha wanadamu kumwelewa Mungu, kuvunja sheria zote ambazo zipo katika mioyo ya watu, na kufuta picha za uongo kuhusu Mungu mioyoni mwao. Ni wazi kuwa hakuna hatua yoyote ya kazi ya Mungu mwenyewe inaweza kumpa mwanadamu ufahamu kamili wa Mungu; kila mojawapo inatoa kwa sehemu tu, si ufahamu mzima. Japo Mungu Ameonyesha tabia Yake kikamilifu, kwa sababu ya upungufu wa ufahamu wa wanadamu, ufahamu wake kuhusu Mungu si kamili. Haiwezekani, kutumia lugha ya wanadamu, kueleza tabia nzima ya Mungu; basi hatua moja tu ya kazi Yake itamwelezaje Mungu kikamilifu? Anafanya kazi katika mwili kwa kujisetiri katika ubinadamu Wake wa kawaida, na mtu anaweza kumjua tu kupitia kwa maonyesho ya uungu Wake, si kupitia kwa umbo Lake la kimwili. Mungu Anakuja katika mwili kumruhusu mwanadamu Amjue kupitia kazi Zake mbalimbali, na hakuna hatua mbili za kazi Yake zinafanana. Ni kwa njia hii tu mwanadamu anaweza kuwa na ufahamu kamili wa kazi ya Mungu katika mwili, si kwa kujifunga katika kipengele kimoja tu.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Yesu alifanya hatua ya kazi ambayo ilitimiza tu kiini cha “Neno alikuwako kwa Mungu”: Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka Kwake, yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa aliyepata mwili wa kwanza wa Mungu. Hatua hii ya kazi ilitimiza maana ya ndani ya “Neno lapata mwili,” ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya “naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,” na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno haya kwamba “Hapo mwanzo kulikuwako na Neno.” Ambalo ni kusema, wakati wa uumbaji Mungu alikuwa na maneno, Maneno Yake yalikuwa na Yeye na yasiyotenganishwa kutoka Kwake, na enzi ya mwisho inafanya nguvu na mamlaka ya maneno Yake yawe hata wazi zaidi, na kumkubalia mwanadamu kuyaona maneno Yake yote—kuyasikia maneno Yake yote. Hiyo ndiyo kazi ya enzi ya mwisho. Lazima uyajue mambo haya yote kabisa. Si suala la kuujua mwili, bali la kuujua mwili na Neno. Hiki ndicho kile unachotakiwa kushuhudia, kile ambacho kila mtu lazima akijue. Kwa sababu hii ni kazi ya kupata mwili kwa pili—na mara ya mwisho ambapo Mungu anapata mwili—inakamilisha kwa ukamilifu umuhimu wa kupata mwili, inatekeleza kabisa na kutoa kazi yote ya Mungu katika mwili, na kumaliza enzi ya Mungu kuwa katika mwili.

kutoka katika “Utendaji (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ikiwa katika hii hatua Mungu mwenye mwili Anapitia ugumu au Anatekeleza huduma Yake, Anafanya hivyo ili kukamilisha maana ya kupata mwili, kwani huku ndiko Mungu kupata mwili kwa mara ya mwisho. Mungu Anaweza kuwa mwili mara mbili tu. Hakuwezi kuwepo mara ya tatu. Kuwa mwili kwa mara ya kwanza Alikuwa ni wa kiume, wa pili ni wa kike, na kwa hivyo sura ya mwili wa Mungu imekamilika katika akili za mwanadamu; aidha, huku kuwa mwili mara mbili tayari kumemaliza kazi ya Mungu katika mwili. Mara ya kwanza, Mungu mwenye mwili Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, ili kukamilisha maana ya kupata mwili. Mara hii vilevile Ana ubinadamu wa kawaida ila maana ya huku kupata mwili ni tofauti: ni kwa kina, na kazi Yake ni ya umuhimu mkubwa. Sababu ya Mungu kuwa mwili tena ni kukamilisha maana ya kupata mwili. Mungu Akiikamilisha kabisa hii hatua ya kazi Yake, maana nzima ya kupata mwili, yaani, kazi ya Mungu katika mwili, itakuwa imekamilika, na hakutakuwa na kazi nyingine ya kufanywa katika mwili. Yaani, tangu sasa Mungu Hatawahi tena kuja katika mwili kufanya kazi Yake.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu wake mkubwa. Yesu alipokuja zamani, Alikuwa mwanaume, lakini Mungu anapokuja wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili huo unaweza kumwakilisha Yeye. Uwe wa kiume au kike, unaweza kumwakilisha Mungu alimradi tu ni mwili Wake wa nyama. Kama Yesu angeonekana kama kike alipokuja, kwa maneno mengine, iwapo mtoto wa kike, sio wa kiume, angezaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, hatua hiyo ya kazi ingekuwa imekamilika pia. Kama hali ingekuwa hivyo, basi hatua ya leo ya kazi ingelazimika kukamilishwa badala yake na mwanaume, lakini kazi ingekamilika pia. Kazi inayofanywa katika hatua hizi zote ni muhimu kwa kiwango sawa; hakuna hatua yoyote ya kazi inayojirudia au kupingana na nyingine. Wakati huo, Yesu alipokuwa akifanya kazi Yake aliitwa Mwana wa pekee, na “Mwana” inaashiria jinsia ya kiume. Basi kwa nini Mwana wa pekee halikutajwa katika hatua hii? Hii ni kwa sababu mahitaji ya kazi yamelazimisha badiliko la jinsia ambayo ni tofauti na ile ya Yesu. Kwa Mungu hakuna tofauti ya jinsia. Kazi Yake inafanywa kama Anavyotaka na katika kufanya kazi Yake hazuiliwi na kitu chochote kile, lakini hasa yupo huru. Hata hivyo, kila hatua ya kazi ina umuhimu wake mkubwa. Mungu alipata mwili mara mbili, na ni dhahiri kwamba kupata mwili Kwake katika siku za mwisho ni mara ya mwisho. Amekuja kufichua matendo Yake yote. Ikiwa katika hatua hii Hakupata mwili ili Yeye binafsi afanye kazi kwa ajili ya mwanadamu kushuhudia, mwanadamu milele angeshikilia fikra kwamba Mungu ni wa kuime tu, na si wa kike. Kabla ya hili, wanadamu wote waliamini kwamba Mungu angeweza kuwa tu mwanaume na kwamba mwanamke hawezi kuitwa Mungu, maana wanadamu wote walimchukulia mwanamume kuwa na mamlaka juu ya mwanamke. Waliamini kwamba hakuna mwanamke anayeweza kuchukua mamlaka, bali ni mwanamume tu. Aidha hata walisema kwamba mwanamume alikuwa ni mkuu wa mwanamke na kwamba mwanamke anapaswa kumtii mwanaume na asimshinde. Iliposemwa hapo nyuma kwamba mwanamume alikuwa mkuu wa mwanamke, ilielekezwa kwa Adamu na Hawa ambao walikuwa wamedanganywa na yule nyoka, na wala sio kwa mwanamume na mwanamke kama walivyoumbwa na Yehova hapo mwanzo. Bila shaka, mwanamke anapaswa kumtii na kumpenda mume wake, na mume anapaswa kujifunza kuilisha na kuiruzuku familia yake. Hizi ni sheria na kanuni zilizowekwa na Yehova ambazo kwazo wanadamu wanapaswa kuzifuata katika maisha yao ya hapa duniani. Yehova alimwambia mwanamke “Ashiki yako itakuwa kwa mume wako, na atatawala juu yako.” Alisema hivyo tu ili kwamba wanadamu (yaani, mwanamume na mwanamke) waweze kuishi maisha ya kawaida chini ya utawala wa Yehova, na tu ili kwamba maisha ya wanadamu yaweze kuwa na mfumo na yasipoteze mwelekeo. Kwa hivyo, Yehova alitengeneza kanuni zinazofaa ya namna ambavyo mwanamume na mwanamke wanavyopaswa kutenda, lakini hili lilihusu tu viumbe wote wanaoishi duniani na halikuhusiana na mwili wa Mungu wa nyama. Inawezekanaje Mungu awe sawa na viumbe Wake? Maneno Yake yalielekezwa tu kwa wanadamu wa viumbe Wake; Alianzishia mwanamume na mwanamke kanuni ili wanadamu waweze kuishi maisha ya kawaida. Hapo mwanzo, Yehova alipoumba wanadamu, Aliwaumba wanadamu wa aina mbili, mwanamume na mwanamke; na kwa hiyo, kuna mgawanyo wa kike na kiume katika miili Yake. Hakuamua juu ya kazi Yake kulingana na maneno aliyozungumza kwa Adamu na Hawa. Mara mbili Alipopata mwili kuliamuliwa kwa kuzingatia kabisa mawazo Yake alipowaumba wanadamu kwa mara ya kwanza, yaani, Alikamilisha kazi ya kupata Kwake mwili mara mbili, kwa msingi wa mwanamke na mwanamume kabla ya wao kupotoshwa. Ikiwa wanadamu wangechukua maneno yaliyozungumzwa na Yehova kwa Adamu na Hawa, ambao walikuwa wamedanganywa na yule nyoka, na kuyatumia katika kazi ya mwili wa Mungu, je, si Yesu pia angepaswa kumpenda mke Wake kama Alivyotakiwa? Je, kwa njia hii, Mungu bado ni Mungu? Na ikiwa ni hivyo, je, bado Angeweza kukamilisha kazi Yake? Ikiwa ni vibaya kwa mwili wa Mungu kuwa mwanamke, je, basi lisingekuwa kosa kubwa sana pia kwa Mungu kumuumba mwanamke? Ikiwa mwanadamu bado anaamini kwamba Mungu kupata mwili kama mwanamke ni vibaya, je, basi Yesu, ambaye hakuoa na hivyo hakuweza kumpenda mke Wake, angekuwa na makosa kama kupata mwili wa sasa? Kwa kuwa unatumia maneno yaliyozungumzwa na Yehova kwa Hawa ili kupima ukweli wa Mungu kupata mwili leo, basi unapaswa kutumia maneno ya Yehova kwa Adamu kumhukumu Bwana Yesu ambaye alipata mwili katika Enzi ya Neema. Je, hawa wawili sio sawa? Kwa kuwa unampima Bwana Yesu kulingana na mwanamume ambaye hakuwa amedanganywa na yule nyoka, basi hupaswi kuhukumu ukweli wa kupata mwili leo hii kulingana na mwanamke ambaye alikuwa amedanganywa na yule nyoka. Hili si haki! Ikiwa umefanya hukumu ya namna hiyo, inathibitisha kukosa urazini kwako. Yehova alipopata mwili mara mbili, jinsia ya mwili Wake ilikuwa inahusiana na mwanamume na mwanamke ambaye hakuwa amedanganywa na yule nyoka; Alipata mwili mara mbili kulingana na mwanamume na mwanamke ambaye hakuwa amedanganywa na yule nyoka. Usifikiri kwamba uanaume wa Yesu ulikuwa sawa na uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa na yule nyoka. Hahusiani naye kabisa, na ni wanaume wawili wa asili tofauti. Hakika haiwezi kuwa kwamba uanaume wa Yesu unathibitisha Yeye ni mkuu wa wanawake wote lakini sio mkuu wa wanaume wote? Je, Yeye si Mfalme wa Wayahudi wote (ikiwa ni pamoja na wanaume na wanawake)? Yeye ni Mungu Mwenyewe, sio tu mkuu wa mwanamke bali mkuu wa mwanamume pia. Yeye ni Bwana wa viumbe vyote, na mkuu wa viumbe vyote. Unawezaje kuamua uanaume wa Yesu kuwa ishara ya mkuu wa mwanamke? Huku si kukufuru? Yesu ni mwanamume ambaye hajapotoshwa. Yeye ni Mungu; Yeye ni Kristo; Yeye ni Bwana. Anawezaje kuwa mwanamume kama Adamu ambaye alipotoshwa? Yesu ni mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu aliye mtakatifu sana. Unawezaje kusema kuwa Yeye ni Mungu aliye na uanaume wa Adamu? Kama ni hivyo, kazi yote ya Mungu haingekuwa si sahihi? Je, Yehova angeweza kuuweka ndani ya Yesu uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa na yule nyoka? Je, si kupata mwili kwa wakati huu ni tukio jingine la kazi ya Mungu mwenye mwili ambaye ni tofauti kijinsia na Yesu lakini aliye kama Yeye katika asili? Bado unathubutu kusema kwamba Mungu mwenye mwili hawezi kuwa mwanamke kwa kuwa mwanamke ndiye aliyedanganywa kwanza na yule nyoka? Bado unathubutu kusema kwamba, kwa kuwa mwanamke ndiye mwenye najisi sana na ni chanzo cha upotovu wa wanadamu, Mungu hawezi kabisa kupata mwili kama mwanamke? Bado unathubutu kuendelea kusema kwamba “mwanamke siku zote atamtii mwanamume na hawezi kamwe kudhihirisha au kumwakilisha Mungu moja kwa moja”? Hukuelewa hapo nyuma; lakini sasa bado unaweza kuendelea kukufuru kazi ya Mungu, hususan mwili wa nyama wa Mungu? Kama huwezi kuona hili kwa uwazi kabisa, ni vizuri zaidi ukawa makini na ulimi wako, la sivyo upumbavu na ujinga wako ufichuliwe na ubaya wako uwekwe wazi. Usidhani kwamba unaelewa kila kitu. Nakueleza kwamba yote uliyokwishayaona na kuyapitia hayakutoshelezi wewe kuelewa hata sehemu ndogo kabisa ya mpango Wangu wa usimamizi. Hivyo kwa nini basi unakuwa mwenye kiburi sana? Talanta ndogo hiyo uliyonayo na maarifa kidogo hayo uliyonayo hayatoshelezi kutumika na Yesu hata katika sekunde moja ya kazi Yake! Je, una uzoefu kiasi gani hasa? Yale uliyoyaona na yote uliyoyasikia katika maisha yako yote na yale uliyoyafikiria ni kidogo kuliko kazi Ninayoifanya kwa muda mfupi sana! Ni bora usichambue na kutafuta kosa. Haijalishi una kiburi kiasi gani, wewe bado ni kuimbe tu mdogo kuliko mchwa! Vyote vilivyomo katika tumbo lako ni vichache zaidi ya vile vilivyomo katika tumbo la mchwa! Usifikiri kwamba kwa kuwa tu umepata uzoefu na ukubwa kiasi, unaweza kuashiria kwa shauku na kuzungumza kwa majivuno. Je, uzoefu wako na ukubwa wako sio matokeo ya maneno Niliyoyazungumza? Je, unaamini kwamba yalikuwa mbadala wa kufanya kwako kazi kwa bidii na kutokwa jasho? Siku hii, unaona kuwa nimepata mwili, na kwa sababu ya hili pekee unajawa na dhana nyingi hizo, na kutoka kwalo unakuwa na fikira nyingi isiyohesabika. Isingekuwa kwa kupata mwili Kwangu, bila kujali talanta ulizo nazo ni za ajabu kiasi gani, usingekuwa na dhana hizi nyingi; na. Si fikira zako zinatoka hapa? Kama si kupata mwili kwa Yesu mara hiyo ya kwanza, je, hata ungejua kuhusu kupata mwili? Je, si kwa sababu ya maarifa yako kutoka kwa kupata mwili mara ya kwanza ndio una ufidhuli kuthubutu kuhukumu kupata mwili kwa mara ya pili? Kwa nini ukuchunguze badala ya kuwa mfuasi mtiifu? Wakati umeingia katika mkondo huu na kuja mbele ya Mungu mwenye mwili, je, Angekuruhusu kuchunguza hili? Ni sawa kwako kuchunguza historia ya familia yako, lakini ukijaribu kuchunguza “historia ya familia” ya Mungu, inawezekanaje Mungu wa leo akuruhusu kufanya uchunguzi kama huo? Je, wewe si kipofu? Je, hujiletei dharau kwako mwenyewe?

Ikiwa tu kazi ya Yesu ingefanywa bila kukamilishwa na kazi katika hatua hii ya siku za mwisho, basi mwanadamu milele angeshikilia fikira kwamba Yesu tu ndiye Mwana wa pekee wa Mungu, yaani, Mungu ana mwana mmoja tu, na kwamba yeyote anayekuja baada yake akiwa na jina jingine hawezi kuwa Mwana pekee wa Mungu, sembuse Mungu Mwenyewe. Mwanadamu ana fikira kwamba yeyote ambaye anajitoa sadaka kwa ajili ya dhambi au yule ambaye anachukua mamlaka kwa niaba ya Mungu na anayewakomboa wanadamu wote ni Mwana wa Mungu wa pekee. Kuna baadhi ambao wanaamini kwamba alimradi Yeye anayekuja ni mwanamume, Anaweza kuchukuliwa kuwa ni Mwana wa Mungu wa pekee na mwakilishi wa Mungu, na hata kuna wale wanaosema kwamba Yesu ni Mwana wa Yehova, Mwana Wake wa pekee. Je, hii kweli siyo tu fikira iliyopita kiasi ya mwanadamu? Ikiwa hatua hii ya kazi haingefanywa katika enzi ya mwisho, basi wanadamu wote wangekuwa gizani sana kumhusu Mungu. Ingekuwa ni hivyo, mwanamume angejidhania kuwa ni wa juu sana kuliko mwanamke, na wanawake hawangeweza kamwe kuinua vichwa vyao juu na hivyo, hakuna mwanamke angeweza kuokolewa. Watu siku zote wanaamini kwamba Mungu ni mwanamume, na aidha kwamba siku zote Amemchukia mwanamke na asingempa wokovu. Ingekuwa ni hivyo, isingekuwa ukweli kwamba wanawake wote walioumbwa na Yehova na pia ambao wamepotoshwa, wasingeweza kuwa na fursa ya kuokolewa? Je, basi isingekuwa bure kwa Yehova kumuumba mwanamke, yaani, kumuumba Hawa? Na je, mwanamke asingeangamia milele? Kwa hiyo, hatua ya kazi katika siku za mwisho inafanywa ili kuwaokoa wanadamu wote, sio mwanamke tu Ikiwa kunaye anayefikiria kwamba ikiwa Mungu angepata mwili kama kike, ingekuwa kwa ajili ya kumwokoa mwanamke pekee, basi mtu huyo bila shaka angekuwa mpumbavu!

Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imeisha, kazi ya Mungu imeendelea mbele. Kwa nini Ninasema mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya siku hii ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na maendeleo ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata kwa karibu. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya ile iliyofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingejengwa juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi kusulubiwa kwingine kufanyike katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kiwango cha kazi kimewekwa juu kabisa kuliko kilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na kwenye mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii inajengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita. Kazi ya hatua hii inafanywa kwa msingi wa kazi ya Enzi ya Neema. Ikiwa hatua hizi mbili za kazi hazikuhusiana, kwa nini basi kusulubiwa hakurudiwi katika hatua hii? Kwa nini Sibebi dhambi za mwanadamu, lakini badala yake Naja kumhukumu na kumwadibu mwanadamu moja kwa moja? Ikiwa kazi Yangu ya kumhukumu na kumwadibu mwanadamu na kuja Kwangu saa hii si kwa njia ya Roho Mtakatifu na hakukufuata kusulubiwa, basi Nisingekuwa na sifa zinazostahili kumhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kazi katika hatua inajenga kabisa juu ya kazi katika hatua iliyotangulia. Hiyo ndiyo maana ni kazi kama hii tu ndiyo inaweza kumleta mwanadamu katika wokovu hatua kwa hatua. Yesu pamoja na Mimi tunatoka kwa Roho Mmoja. Ingawa miili Yetu haina uhusiano, Roho Zetu ni moja; ingawa kile Tunachofanya na kazi Tulizo nazo hazifanani, kwa asili Tunafanana; Miili Yetu ina maumbo tofauti, lakini hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya enzi na mahitaji tofauti ya kazi Yetu; huduma Zetu hazifanani, hivyo kazi Tunayoileta na tabia Tunayoifichua kwa mwanadamu pia ni tofauti. Ndiyo maana kile ambacho mwanadamu anakiona na kukielewa leo hii si kama kile cha wakati uliopita; ni hivyo kwa sababu ya mabadiliko ya enzi. Ingawa jinsia na maumbo ya miili Yao ni tofauti, na kwamba hawakuzaliwa katika familia moja, sembuse katika kipindi kimoja, hata hivyo Roho Zao ni moja. Ingawa miili Yao haina uhusiano wa damu au kimwili kwa namna yoyote ile, haipingiki kwamba Wao ni Mungu kupata mwili katika vipindi viwili tofauti vya nyakati. Ni ukweli usiopingika kwamba Wao ni miili ya nyama ya Mungu, ingawa hawatoki katika ukoo mmoja na hawatumii lugha moja ya binadamu (mmoja alikuwa mwanamume aliyezungumza lugha ya Wayahudi na mwingine ni mwanamke anayezungumza Kichina pekee). Ni kwa sababu hizi ndiyo Wameishi katika nchi tofauti kufanya kazi ambayo inampasa kila mmoja kufanya, na katika nyakati tofauti vilevile. Licha ya ukweli kwamba Wao ni Roho moja, wakiwa na asili inayofanana, hakuna mfanano wa wazi kabisa kati ya ngozi za nje za miili Yao. Wanashiriki tu ubinadamu sawa, lakini sura ya nje ya miili Yao na kuzaliwa Kwao hakufanani. Mambo haya hayana athari katika kazi Zao au maarifa aliyonayo mwanadamu juu Yao, maana, kimsingi, Wao ni Roho moja na hakuna anayeweza kuwatenganisha. Ingawa Hawana uhusiano wa damu, nafsi Zao zote zinaongoza Roho Zao, ambazo zinawapa kazi tofauti katika nyakati tofauti, na miili Yao kwa ukoo tofauti. Roho wa Yehova si baba wa Roho wa Yesu na Roho wa Yesu si mwana wa Roho wa Yehova: Ni Roho moja. Vile vile Kama vile Mungu mwenye mwili wa leo na Yesu. Ingawa Hawahusiani kwa damu, ni Wamoja; hii ni kwa sababu Roho Zao ni moja. Mungu anaweza kufanya kazi ya rehema na wema, vilevile na ile kazi ya hukumu ya haki na kumwadibu mwanadamu, na ile ya kuleta laana kwa mwanadamu; na hatimaye, Anaweza kufanya kazi ya kuuharibu ulimwengu na kuwaadhibu waovu. Je, hafanyi haya yote Mwenyewe? Je, hii si kudura ya Mungu? Aliweza kutangaza sheria kwa ajili ya mwanadamu na kumpa amri, na aliweza pia kuwaongoza Waisraeli wa awali katika kuishi maisha yao duniani na kuwaongoza kujenga hekalu na madhabahu, Akiwatawala Waisraeli wote. Kwa kutegemea mamlaka Yake, Aliishi pamoja na Waisraeli duniani kwa miaka elfu mbili. Waisraeli hawakuthubutu kumwasi; wote walimheshimu Yehova na walifuata amri Zake. Hii ilikuwa Kazi iliyofanywa kwa kutegemea mamlaka Yake na kudura Yake. Kisha, katika Enzi ya Neema, Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote walioanguka (sio Waisraeli pekee). Alionyesha rehema na wema kwa mwanadamu. Yesu ambaye mwanadamu alimwona katika Enzi ya Neema Alikuwa amejazwa na wema na siku zote Alikuwa mwenye upendo kwa mwanadamu, maana Alikuwa amekuja kuwakomboa wanadamu kutoka dhambini. Aliweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao hadi pale ambapo kusulubiwa Kwake kuliwakomboa wanadamu kutoka dhambini kabisa. Wakati huo, Mungu alionekana kwa mwanadamu kwa rehema na wema; yaani, Alijitoa sadaka kwa ajili ya mwanadamu na Alisulubiwa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ili kwamba ziweze kusamehewa milele. Alikuwa mwenye rehema, mwenye huruma, mwenye upendo na mstahimilivu. Na wale wote waliomfuata Yesu katika Enzi ya Neema nao pia walitafuta kuwa wastahimilivu na wenye upendo katika mambo yote. Walistahimili mateso kwa muda mrefu, na hawakuwahi kulipiza kisasi hata walipopigwa, kulaaniwa au kupigwa mawe. Lakini haya hayawezi kuwa hivyo tena katika hatua ya mwisho. Vivyo hivyo, hata ingawa Roho Zao zilikuwa moja, kazi ya Yesu na Yehova hazikufanana kabisa. Kazi ya Yehova haikuwa kwa ajili ya kukamilisha enzi bali kuiongoza, kukaribisha maisha ya wanadamu duniani. Hata hivyo, kazi sasa ni kuwashinda wale walio katika mataifa yasiyo ya Wayahudi na ambao wamepotoshwa sana, kuongoza sio tu familia ya China bali ulimwengu mzima. Inaweza kuonekana kwako kwamba kazi hii inafanywa Uchina pekee, lakini kwa kweli imekwishaanza kusambaa katika nchi za ughaibuni. Ni kwa nini wageni mara kwa mara wanatafuta njia ya kweli? Hiyo ni kwa sababu Roho tayari amekwishaanza kazi, na maneno yanayonenwa sasa yanaelekezwa kwa watu ulimwenguni kote. Na hili, nusu ya kazi tayari inafanywa. Kutoka kuumbwa kwa dunia hadi sasa, Roho wa Mungu ameendeleza hii kazi kubwa, na aidha Amefanya kazi tofauti katika enzi tofauti, na katika mataifa tofauti. Watu wa kila enzi wanaiona tabia Yake tofauti, ambayo kwa asili inafichuliwa kupitia kazi tofauti Anazozifanya. Yeye ni Mungu, aliye mwingi wa rehema na wema; Yeye ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mwanadamu na mchungaji wa mwanadamu; lakini pia Yeye ni hukumu, kuadibu, na laana kwa mwanadamu. Angeweza kumwongoza mwanadamu kuishi duniani kwa miaka elfu mbili na pia Angeweza kuwaokoa wanadamu waliopotoka kutoka dhambi. Leo, pia Anaweza kuwashinda wanadamu ambao hawamjui na kuwafanya wawe chini ya miliki Yake, ili kwamba wote wajinyenyekeze kwake kikamilifu. Mwishowe, Atachoma yote ambayo si safi na ambayo ni dhalimu ndani ya wanadamu katika ulimwengu mzima, ili kuwaonyesha kwamba Yeye si Mungu wa Rehema, na upendo tu, si Mungu wa hekima, na maajabu tu, si Mungu mtakatifu tu, bali, hata zaidi ni Mungu anayemhukumu mwanadamu. Kwa waovu miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwenye kuchoma, kuhukumu na kuadhibu; kwa wale ambao wanapaswa kukamilishwa, Yeye ni mateso, usafishaji, na majaribu, na vilevile faraja, ruzuku, utoaji wa maneno, kushughulika na kupogoa. Na kwa wale ambao wanaondolewa, Yeye ni adhabu na vilevile malipo. Niambie, je, Mungu si mwenye enzi? Anaweza kufanya kazi yoyote na yote, sio tu kusulubiwa kama ulivyokuwa ukifikiri. Unamfikiria Mungu kuwa ni wa chini sana! Je, unaamini kwamba chote Anachoweza kufanya ni kukomboa wanadamu wote kupitia kusulubiwa kwako pekee? Na baada ya hilo, utamfuata mbinguni kula tunda kutoka mti wa uzima na kunywa kutoka mto wa uzima? … Je, inaweza kuwa rahisi hivyo? Niambie, umekamilisha nini? Je, una uzima wa Yesu? Ni kweli ulikombolewa naye, lakini kusulubiwa kulikuwa ni kazi ya Yesu Mwenyewe. Ni wajibu gani umeukamilisha kama mwanadamu? Una uchaji Mungu wa nje pekee lakini huielewi njia Yake. Hivyo ndivyo unavyomdhihirisha? Ikiwa hujapata maisha ya Mungu au kuona tabia Yake yote ya haki, basi huwezi kudai kuwa mtu aliye na uzima, na hustahili kupitia katika lango la ufalme wa mbinguni.

Mungu si Roho pekee, Anaweza pia kuwa mwili: aidha, Yeye ni mwili wa utukufu. Yesu, ingawa hamjamwona, alishuhudiwa na Waisraeli, yaani, Wayahudi wa wakati huo. Mwanzoni alikuwa mwili wa nyama, lakini baada ya kusulubiwa, Aligeuka mwili wa utukufu. Yeye ni Roho anayezunguka mambo yote na Anaweza kufanya kazi katika kila mahali. Anaweza kuwa Yehova, au Yesu au Masihi; hatimaye, Anaweza pia kuwa Mwenyezi Mungu. Yeye ni haki, hukumu, na kuadibu; Yeye ni laana na ghadhabu, lakini pia Yeye ni rehema na wema. Kazi zote ambazo Amezifanya zinaweza kumwakilisha. Unasema Yeye ni Mungu ni wa aina gani? Hutaweza kuelezea kabisa. Yote unayoweza kusema ni: “Kuhusu Mungu ni wa aina gani, siwezi kuelezea.” Usihitimishe kwamba Mungu milele ni Mungu wa rehema na wema, kwa sababu tu Yeye alifanya kazi ya ukombozi katika hatua moja. Je, unaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye ni Mungu wa rehema na upendo pekee? Ikiwa Yeye ni Mungu wa rehema na mwenye upendo, kwa nini Ataikomesha enzi katika siku za mwisho? Kwa nini Ataleta chini majanga mengi sana? Ikiwa ni kama unavyofikiri, kwamba Yeye ni Mungu wa rehema na upendo kwa mwanadamu hadi mwisho kabisa, hata hadi katika enzi ya mwisho, basi kwa nini atatuma chini majanga kutoka mbinguni? Ikiwa Anampenda mwanadamu kama Anavyojipenda na kama Anavyompenda Mwanawe wa pekee, basi kwa nini Atatuma chini mapigo na mvua ya mawe kutoka mbinguni? Kwa nini Anamruhusu mwanadamu kuteseka na njaa na ndwele ya kufisha? Kwa nini anamruhusu mwanadamu kuteseka majanga haya? Hakuna yeyote kati wenu anayethubutu kusema Yeye ni Mungu wa aina gani, na hakuna anayeweza kuelezea. Je, unaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye ni Roho? Je, unathubutu kusema kuwa Yeye ni mwili wa Yesu pekee? Na unathubutu kusema kuwa Yeye ni Mungu ambaye milele atasulubiwa kwa ajili ya mwanadamu?

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili