Alhamisi, 27 Desemba 2018

"Wimbo wa Ushindi" (1) - Je, Bwana Atatokeaje na Kufanya Kazi Yake Wakati Atakaporudi?

"Wimbo wa Ushindi" (1) - Je, Bwana Atatokeaje na Kufanya Kazi Yake Wakati Atakaporudi?

Ishara ya maafa makubwa wakati wa siku za mwisho- miezi minne ya damu imetokea na nyota za angani zimechukua kuonekana kwa ajabu; maafa makubwa yanakaribia, na wengi wa wale walio na imani katika Bwana wamepata hisia ya kurudi Kwake kwa pili au kwamba tayari Amewasili. Wakati wote wanasubiri kuja kwa mara ya pili kwa Bwana kwa hamu kubwa, labda tumefikiria juu ya maswali yafuatayo: Je, Bwana ataonekanaje kwa mwanadamu Atakaporudi katika siku za mwisho? Je, ni kazi gani ambayo Bwana atafanya wakati Atakapokuja tena? Je, unabii wa hukumu ya kiti kikuu cheupe cha enzi kutoka Kitabu cha Ufunuo utatimizwaje hasa? Video hii fupi itafunua majibu kwako!
Mwenyezi Mungu alisema, Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaelekea kikomo, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnasubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? Wale wote wanaosubiri kuonekana kwa Mungu wanakumbana na maswali kama haya. Nyinyi nyote mmewahi kuyafikiria zaidi ya mara moja—ila matokeo ni gani? Mungu hujidhihirisha wapi? Nyayo za Mungu zipo wapi? Mmepata majibu? Majibu ya watu wengi yangekuwa: Mungu hudhihirika miongoni mwa wale wanaomfuata na nyayo Zake zimo miongoni mwetu; ni rahisi hivyo! Mtu yeyote anaweza kutoa jibu kwa kutumia mbinu fulani, lakini je, mnafahamu kuonekana kwa Mungu ni nini, na nyayo za Mungu ni nini? Kuonekana kwa Mungu hurejelea kuwasili Kwake duniani kufanya kazi Yake. Akiwa na utambulisho na tabia Yake, na katika mbinu Yake ya asili, Yeye hushuka miongoni mwa wanadamu kufanya kazi ya kuanzisha enzi mpya na kukamilisha enzi nyingine. Kuonekana kwa aina hii si aina fulani ya sherehe. Si ishara, picha, muujiza, au ono kuu, na hata zaidi si mchakato fulani wa kidini. Ni ukweli halisi ambao waweza kushikwa na kuonekana. Kuonekana kama huku si kwa ajili ya kufuata taratibu, au kwa ajili ya shughuli ya muda mfupi; ni, badala yake, kwa ajili ya hatua ya kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Kuonekana kwa Mungu daima ni kwenye maana na daima huenda pamoja na mpango wa usimamizi. Kuonekana huku ni tofauti kabisa na udhihirisho wa uongozi wa Mungu, utawala na kupata nuru kwa mwanadamu. Mungu hufanya kazi kubwa kila mara Anapojifunua. Kazi hii ni tofauti na enzi yoyote nyingine. Haiwezi kufikirika na mwanadamu na haijawahi na mwanadamu hana uzoefu huu. Ni kazi ambayo huanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya awali, na ni aina mpya ya kazi na iliyoboreshwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu; aidha, ni kazi ya kuleta wanadamu katika enzi mpya. Huo ndio umuhimu wa kuonekana kwa Mungu.
kutoka kwa Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

0 评论:

Chapisha Maoni