Jumatatu, 11 Februari 2019

2018 Gospel Music "Mungu Kuwatawala na Kuwakimu Wanadamu na Vitu Vyote" (Swahili Subtitles)

2018 Gospel Music "Mungu Kuwatawala na Kuwakimu Wanadamu na Vitu Vyote" (Swahili Subtitles)

Chini ya mbingu, milima, mito, na maziwa vyote vina mipaka yavyo, na viumbe vyote huishi na kuzaana wakati wa misimu yote minne kulingana na sheria za maisha…. Ungependa kujua ni nani huwatawala na kuwakimu wanadamu na vitu v yote? Tazama dondoo hii ya filamu ya Kikristo ili kujua zaidi kuhusu mamlaka ya pekee ya Mungu.
Mwenyezi Mungu alisema, Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Ilikuwa kwa sababu ya upotovu wa binadamu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake, na ilikuwa pia kwa sababu ya uasi wa malaika mkuu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake. Iwapo Mungu hatamshinda Shetani na kuokoa binadamu, ambao wamepotoshwa, Mungu hatawahi tena kuweza kuingia rahani. Mungu anakosa pumziko akosavyo mwanadamu. Wakati Mungu ataingia rahani tena, mwanadamu pia ataingia rahani. Maisha ya pumziko ni yale bila vita, bila uchafu, bila udhalimu unaoendelea. Hii ni kusema kwamba hayana unyanyasaji wa Shetani (hapa “Shetani” inamaanisha nguvu za uhasama), upotovu wa Shetani, na pia uvamizi wa nguvu yoyote inayompinga Mungu. Kila kitu kinafuata aina yake na kuabudu Bwana wa uumbaji. Mbingu na dunia ni shwari kabisa. Haya ni maisha matulivu ya binadamu. Mungu aingiapo rahani, hakuna udhalimu wowote utakaoendelea duniani, na hakutakuwa na uvamizi wowote wa nguvu za uhasama. Binadamu pia wataingia ulimwengu mpya; hawatakuwa tena binadamu waliopotoshwa na Shetani, lakini badala yake binadamu ambao wameokolewa baada ya kupotoshwa na Shetani. Siku ya pumziko ya binadamu pia ni siku ya pumziko ya Mungu. Mungu alipoteza pumziko Lake kwa sababu wanadamu hawakuweza kuingia rahani; haikuwa kwamba Hakuweza awali kupumzika. Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu. Binadamu kuingia rahani kunamaanisha kwamba binadamu wote wataishi ndani ya mwangaza wa Mungu na chini ya baraka Zake; hakutakuwa na upotovu wowote wa Shetani, wala maovu yoyote kutokea. Binadamu wataishi kama kawaida duniani, na wataishi chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba binadamu wameokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi miongoni mwa mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo. Mungu atarudia nafasi yake ya awali, na kila mtu atarudia nafasi yake husika. Hizi ndizo hatima ambazo Mungu na mwanadamu wataishi ndani kwa utaratibu huu baada ya mwisho wa usimamizi wote wa Mungu. Mungu ana hatima ya Mungu na mwanadamu ana hatima ya mwanadamu. Apumzikapo, Mungu ataendelea kuwaongoza binadamu wote kwa maisha yao duniani. Akiwa kwa mwangaza wa Mungu, mwanadamu atamwabudu Mungu wa kweli aliye mbinguni. Mungu hataishi tena miongoni mwa binadamu, na mwanadamu pia hataweza kuishi na Mungu katika hitimisho la Mungu. Mungu na mwanadamu hawawezi kuishi ndani ya ulimwengu sawa; badala yake, wote wawili wana njia zao binafsi za kuishi. Mungu ndiye anayeongoza binadamu wote, wakati binadamu wote ni matokeo ya kazi ya Mungu ya usimamizi. Ni binadamu wanaoongozwa; kuhusu kiini, binadamu si sawa na Mungu. Kuingia rahani kunamaanisha kurudi pahali pa awali pa mtu. Kwa hivyo, Mungu aingiapo rahani, kunamaanisha kwamba Mungu amerudi pahali Pake pa awali. Mungu hataishi tena duniani ama kushiriki kwa furaha na mateso ya binadamu wakati yupo miongoni mwa binadamu. Binadamu wanapoingia rahani, kunamaanisha kwamba mwanadamu amekuwa kiumbe halisi; binadamu watamwabudu Mungu wakiwa duniani na kuwa na maisha ya kawaida ya wanadamu. Watu hawatakuwa tena wasiomtii Mungu ama kumpinga Mungu; watarudia maisha asili ya Adamu na Hawa. Haya ndiyo maisha na hatima binafsi ya Mungu na binadamu baada ya kuingia rahani. Kushindwa kwa Shetani ni mwelekeo usioepukika katika vita kati ya Mungu na Shetani. Kwa njia hii, kuingia kwa Mungu rahani baada ya kukamilika kwa kazi Yake ya usimamizi na wokovu kamili wa mwanadamu na kuingia rahani pia kunakuwa mielekeo isiyoepukika. Pahali pa pumziko pa mwanadamu ni duniani, na pahali pa Mungu pa pumziko ni mbinguni. Mwanadamu anapomwabudu Mungu katika pumziko, ataishi duniani, na Mungu anapoongoza sehemu iliyobaki ya binadamu katika pumziko, Atawaongoza kutoka mbinguni, sio kutoka duniani. Mungu bado atakuwa Roho, wakati mwanadamu bado atakuwa mwili. Mungu na mwanadamu wote wawili wana njia zao tofauti za kupumzika. Mungu anapopumzika, Atakuja na kujitokeza miongoni mwa mwanadamu, mwanadamu anapopumzika, ataongozwa na Mungu kutembea mbinguni na pia kufurahia maisha mbinguni. Baada ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, Shetani hatakuweko tena, na kama Shetani, wale watu waovu pia hawatakuweko tena. Kabla ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, wale watu waovu waliomtesa Mungu wakati mmoja duniani na adui waliokuwa hawamtii duniani watakuwa tayari wameangamizwa; watakuwa wameangamizwa na majanga makubwa ya siku za mwisho. Baada ya hao watu waovu kuangamizwa kabisa, dunia haitajua tena unyanyasaji wa Shetani. Binadamu watapata wokovu kamili, na hapo tu ndipo kazi ya Mungu itaisha kabisa. Haya ndiyo masharti ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani.
Kukaribia kwa mwisho wa kila kitu kunaonyesha mwisho wa kazi ya Mungu na kunaonyesha mwisho wa maendeleo ya binadamu. Hii inamaanisha kwamba binadamu kama walivyopotoshwa na Shetani wamefika mwisho wake wa maendeleo, na kwamba vizazi vya Adamu na Hawa vimeenea hadi mwisho wao binafsi, na pia inamaanisha kwamba haiwezekani kwa binadamu kama hawa, baada ya kupotoshwa na Shetani, kuendelea kustawi. Adamu na Hawa wa mwanzoni hawakuwa wamepotoshwa, lakini Adamu na Hawa waliofukuzwa kutoka Bustani ya Edeni walivurugwa na Shetani. Wakati Mungu na mwanadamu wanaingia rahani pamoja, Adamu na Hawa—waliofukuzwa kutoka Bustani ya Edeni—na vizazi vyao hatimaye watafika mwisho; binadamu wa baadaye bado watakuwa na vizazi vya Adamu na Hawa, lakini hawatakuwa watu wanaomilikiwa na Shetani. Badala yake, watakuwa watu waliookolewa na kutakaswa. Hawa watakuwa binadamu ambao wamehukumiwa na kuadibiwa, na walio watakatifu. Hawa watu hawatakuwa sawa na jamii ya binadamu kama ilivyokuwa awali; mtu anaweza kusema kwamba hao ni watu wa aina tofauti kabisa na Adamu na Hawa wa awali. Hawa watu watakuwa wamechaguliwa kutoka miongoni mwa wote waliopotoshwa na Shetani, na watakuwa ndio watu ambao hatimaye wamesimama imara wakati wa hukumu na kuadibu kwa Mungu, watakuwa kundi la mwisho la watu miongoni mwa wanadamu potovu. Kundi hili la watu ndilo tu litaweza kuingia katika raha ya mwisho pamoja na Mungu. Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaobaki watatakaswa na kufurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani waingiapo ulimwengu wa juu wa binadamu; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. Walikuwa wamekombolewa wakati mmoja, na pia walikuwa wamehukumiwa na kuadibiwa; walikuwa pia wamemhudumia Mungu wakati mmoja, lakini siku ya mwisho itakapofika, bado wataondolewa na kuangamizwa kwa sababu ya uovu wao na kwa sababu ya kutotii na kutokombolewa kwao. Hawatakuwa tena katika ulimwengu wa baadaye, na hawatakuweko tena miongoni mwa jamii ya binadamu ya baadaye. Watenda maovu wote na yeyote na wote ambao hawajaokolewa wataangamizwa wakati watakatifu miongoni mwa binadamu wataingia rahani, bila kujali kama wao ni roho za wafu ama wale wanaoishi bado katika mwili. Bila kujali enzi ya hizi roho zitendazo maovu na watu watenda maovu, ama roho za watu wenye haki na watu wanaofanya haki wako, mtenda maovu yeyote ataangamizwa, na yeyote mwenye haki ataishi. Iwapo mtu ama roho inapokea wokovu haiamuliwi kabisa kulingana na kazi ya enzi ya mwisho, lakini inaamuliwa kulingana na iwapo wamempinga ama kutomtii Mungu. Kama watu wa enzi ya awali walifanya maovu na hawangeweza kuokolewa, bila shaka wangekuwa walengwa wa adhabu. Kama watu wa enzi hii wanafanya maovu na hawawezi kuokolewa, hakika wao pia ni walengwa wa adhabu. Watu wanatengwa kwa msingi wa mema na mabaya, sio kwa msingi wa enzi. Baada ya kutengwa kwa msingi wa mema na mabaya, watu hawaadhibiwi ama kutuzwa mara moja; badala yake, Mungu atafanya tu kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wema baada ya kufanya kazi Yake ya ushindi katika siku za mwisho. Kwa kweli, Amekuwa akitumia mema na mabaya kutenga binadamu tangu Afanye kazi Yake miongoni mwa binadamu. Atawatuza tu wenye haki na kuwaadhibu waovu baada ya kukamilika kwa kazi Yake, badala ya kuwatenga waovu na wenye haki baada ya kukamilika kwa kazi Yake mwishowe na kisha kufanya kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wazuri mara moja. Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi. Kama Mungu hangewaangamiza waovu lakini badala yake kuwaacha wabakie, basi binadamu wote bado hawangeweza kuingia rahani, na Mungu hangeweza kuleta binadamu katika ulimwengu bora. Kazi ya aina hii haingekuwa imekamilika kabisa. Atakapomaliza kazi Yake, binadamu wote watakuwa watakatifu kabisa. Mungu anaweza kuishi kwa amani rahani kwa namna hii pekee.
kutoka kwa Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

0 评论:

Chapisha Maoni