Jumatatu, 8 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II” Sehemu ya Nne

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: “Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi.” Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.” Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, kwamba Anaweza kuangalia kwenye akili ya binadamu, na yanathibitisha kwamba kuidhinisha kwake kwa Ayubu hakuna kosa, kwamba binadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.” Maneno haya ni ushuhuda wa Ayubu kwa Mungu. ... Katika yote haya Ayubu hakutenda dhambi na midomo yake. Hakutenda dhambi kwa kutumia mdomo wake tu, lakini ndani ya moyo wake hakulalamika katu kuhusu Mungu. Hakusema maneno mabaya kuhusu Mungu, wala hakutenda dhambi dhidi ya Mungu. Kinywa chake hakikubariki tu jina la Mungu, lakini ndani ya moyo wake alibariki pia jina la Mungu; mdomo na moyo wake ulikuwa kitu kimoja. Huyu ndiye aliyekuwa Ayubu wa kweli aliyeonekana na Mungu, na hii ndiyo iliyokuwa sababu ya kweli kwa nini Mungu alimthamini sana Ayubu.”
Mbinu ambazo Shetani anatumia kuwapotosha watu zinaletea nini binadamu? Kuna chochote chema kuzihusu? (La.) Kwanza, mwanadamu anaweza kutofautisha kati ya mema na mabaya? Unaona, katika dunia hii, awe ni mtu fulani mkubwa ama jarida fulani, yote yatasema kwamba hiki ama kile ni chema ama kibaya, si hayo ni barabara? Si hayo ni sahihi? (La.) Tathmini zao za matukio na watu ni za haki? Kuna ukweli ndani ya tathmini hizi? (La.) Je, dunia hii ama binadamu huu unatathmini vitu vyema na hasi kulingana na kiwango cha ukweli? (La.) Mbona watu hawana uwezo huo? Watu wamesoma maarifa mengi na wanajua mengi kuhusu sayansi, uwezo wao si mkubwa kutosha? Mbona hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi? Mbona hivi? (Kwa sababu watu hawana ukweli; sayansi na maarifa si ukweli.) Kila kitu Shetani anauletea binadamu ni uovu na upotovu na hakina ukweli, uhai, na njia. Na uovu na upotovu ambao Shetani anamletea mwanadamu, unaweza kusema kwamba Shetani ana upendo? Unaweza kusema kwamba mwanadamu ana upendo? Watu wengine wanaweza kusema: “Huko sahihi, kuna watu wengi duniani kote wanaosaidia maskini na watu wasio na makazi. Si hao ni watu wazuri? Pia kuna mashirika ya hisani ambayo yanafanya kazi nzuri, si kazi yote wanayofanya ni ya uzuri?” Kwa hivyo tunasema nini kuhusu hayo? Shetani anatumia mbinu na nadharia mbalimbali kumpotosha mwanadamu; huu upotovu wa mwanadamu ni dhana isiyo dhahiri? La, siyo dhahiri. Shetani pia anafanya vitu vingine vya utendaji, na pia anakuza mtazamo au nadharia katika dunia hii na katika jamii. Katika kila nasaba na katika kila kipindi cha historia anakuza nadharia na kuingiza baadhi ya fikira ndani ya wanadamu. Fikira na nadharia hizi polepole zinakita mizizi katika mioyo ya watu, na kisha watu wanaanza kuishi kwa nadharia na fikira hizi; si wanakuwa Shetani bila kusudi? Si watu wako kitu kimoja na Shetani? Wakati watu wamekuwa kitu kimoja na Shetani, ni nini mtazamo wao kwa Mungu mwishowe? Si ni mtazamo sawa ambao Shetani anao kwa Mungu? Hakuna anayethubutu kukubali haya, siyo? Ni ya kutisha sana! Mbona Nasema kwamba asili ya Shetani ni ovu? Hii inaamuliwa na kuchambuliwa kulingana na kile Shetani amefanya na vitu ambavyo Shetani amefichua; si bila ustahili kusema kwamba Shetani ni mwovu. Iwapo Ningesema tu kwamba Shetani ni mwovu, mngefikiri nini? Mngefikiri, “Bila shaka Shetani ni mwovu.” Hivyo nitakuuliza: “Ni kipengele kipi cha Shetani ni ovu?” Ukisema: “Shetani kumpinga Mungu ni uovu,” bado hutakuwa ukizungumza kwa uwazi. Sasa tumesema mambo maalum kwa njia hii; je, mna uelewa kuhusu maudhui maalum ya kiini cha uovu wa Shetani? (Ndiyo.) Sasa kwa kuwa mmekuwa na huu uelewa wa asili ovu ya Shetani, ni kiasi gani mnaelewa kuhusu nyinyi wenyewe? Je, mambo haya yanahusiana? (Ndiyo.) Je, uhusiano huu unawaumiza? (La.) Ni wenye msaada kwenu? (Ndiyo.) Ni wenye msaada vipi? (Msaada mkubwa sana!) Hebu tuzungumzie mambo maalum; Sitasikia maneno yenye maana nyingi. Ni kwa kiasi kipi “mkubwa sana” kinarejelea? (Tunajua vitu ambavyo Mungu anachukia, vitu vipi vinaenda kinyume na Mungu; mioyo yetu inaelewa kiasi kuhusu vitu hivi.) Kuna kitu kingine cha kuongezea? Ninaposhiriki kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, ni muhimu Niwe na ushirika kuhusu kiini ovu cha shetani, ni nini maoni yako? (Ndiyo, ni muhimu.) Mbona? (Uovu wa Shetani unauweka utakatifu wa Mungu katika heshima ya juu.) Je, ndivyo ilivyo? Hii ni sahihi kidogo kwa sababu bila uovu wa Shetani, watu hawatajua kuhusu utakatifu wa Mungu; hii ni sahihi. Hata hivyo, ukisema kwamba utakatifu wa Mungu upo tu kwa sababu ya tofauti yake na uovu wa Shetani, hii ni sahihi? Hii hoja si sahihi. Utakatifu wa Mungu ni kiini kiasilia cha Mungu; hata ingawa Mungu anaufichua kupitia matendo Yake, hili bado ni onyesho asili la kiini cha Mungu na ni kiini kiasilia cha Mungu; daima kimekuwepo na ni cha Mungu Mwenyewe lakini mwanadamu hawezi kukiona. Hii ni kwa sababu mwanadamu anaishi katikati ya tabia potovu ya Shetani na chini ya ushawishi wa Shetani, na hawajui kuhusu utakatifu, sembuse maudhui maalum ya utakatifu wa Mungu. Hivyo, ni muhimu kweli kwamba tushiriki kwanza kuhusu kiini ovu cha Shetani? (Ndiyo, ni muhimu.) Unaona, tumeshiriki kuhusu vipengele vingi vya upekee wa Mungu na hatukutaja kiini cha Shetani, siyo? Watu wengine wanaweza kuonyesha baadhi ya shaka kama, “Unashiriki kuhusu Mungu Mwenyewe, mbona Unazungumza daima kuhusu jinsi Shetani anawapotosha watu na jinsi asili ya Shetani ni ovu?” Umeyaweka mapumzikoni mashaka haya? (Ndiyo.) Uliyawekaje mapumzikoni? (Kupitia ushirika wa Mungu, tulitofautisha kile ambacho ni ovu.) Wakati watu wana utambuzi wa uovu na wakati wana ufafanuzi sahihi wa uovu, wakati watu wanaweza kuona wazi maudhui maalum na udhihirisho wa uovu, chanzo na kiini cha uovu—wakati utakatifu wa Mungu unajadiliwa sasa—watu basi watatambua wazi, ama kuufahamu wazi kama utakatifu wa Mungu, kama utakatifu wa kweli. Nisipojadili uovu wa Shetani, watu wengine wataamini kimakosa kwamba kitu fulani ambacho watu wanafanya katika jamii ama miongoni mwa watu—ama kitu fulani katika dunia hii—kinaweza kuhusiana na utakatifu. Si mtazamo huu ni wa makosa? (Ndiyo.)
Hivi, Nimeshiriki kuhusu kiini cha Shetani. Mmefikia uelewa upi wa utakatifu wa Mungu kupitia uzoefu wenu wa miaka ya hivi karibuni, kutokana na nyinyi kuona neno la Mungu na kutokana na kupitia kazi Yake? Endelea, na uuzungumzie. Si lazima utumie maneno yanayofurahisha sikio, zungumza tu kutoka kwa uzoefu wako mwenyewe, utakatifu wa Mungu ni upendo Wake tu? Ni upendo wa Mungu tu tunaoelezea kama utakatifu? Huo utakuwa wa upande mmoja sana, siyo? Si huo utakuwa wa upande mmoja? (Ndiyo.) Mbali na upendo wa Mungu, kuna vipengele vingine vya kiini cha Mungu ambavyo mmeona? (Ndiyo.) Mmeona nini? (Mungu anachukia tamasha na likizo, mila, na ushirikina; huu ni utakatifu wa Mungu.) Ulisema tu kwamba Mungu anachukia mambo fulani; Mungu ni mtakatifu kwa hivyo Anachukia vitu, inamaanisha hivyo? (Ndiyo.) Katika mizizi ya hayo, ni nini utakatifu wa Mungu? Utakatifu wa Mungu hauna maudhui makubwa, ni kwamba tu Anachukia vitu? Katika akili zenu mnafikiria, “Kwa sababu Mungu anachukia vitu hivi ovu, hivyo mtu anaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu”? Si huu ni uvumi hapa? Si hii ni aina ya dhana na hukumu? Ni nini mwiko mkubwa zaidi inapokuja kwa kuelewa kiini cha Mungu? (Kuacha ukweli nyuma.) Ni wakati tunaacha ukweli nyuma kuzungumza kuhusu mafundisho ya kidini, huu ni mwiko mkubwa sana kufanya. Kitu kingine? (Uvumi na ubunifu.) Uvumi na ubunifu, huu pia ni mwiko wa nguvu sana. Mbona uvumi na ubunifu si wa manufaa? Vitu unavyobashiri kuhusu na kufikiria vitu ambavyo kweli unaweza kuona? (La.) Ni kiini cha kweli cha Mungu? (La.) Nini tena ni mwiko? Ni mwiko kuhesabu tu kifungu cha maneno yanayosikika kuwa mazuri kueleza kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Si huku ni kujigamba na upuuzi? Hukumu na uvumi ni upuuzi, kama tu kuchukua maneno yanayosikika kuwa mazuri. Sifa tupu pia ni upuuzi, siyo? (Ndiyo.) Je, Mungu anafurahia kusikiza watu wakisema upuuzi wa aina hii? (La, hafurahii.) Ni nini kisawe cha “kutofurahia” kitu? (Kuhisi kutostareheka.) Anahisi kutostareheka kusikia huu upuuzi! Mungu anaongoza na kuokoa kundi la watu, na baada ya kundi hili la watu kusikia maneno Yake hawaelewi Anachomaanisha. Mtu anaweza kuuliza: “Mungu ni mwema?” na wangejibu, “Mwema!” “Mwema vipi?” “Mwema sana sana!” “Mungu anampenda mwanadamu?” “Ndiyo!” “Kiasi gani?” “Sana, sana zaidi!” “Unaweza kuelezea upendo wa Mungu?” “Ni wa kina zaidi kuliko bahari, wa juu zaidi kuliko anga!” Si huu ni upuuzi? Si huu upuuzi ni sawa na kile mlichotoka kusema kuhusu, “Mungu anachukia tabia potovu ya Shetani, hivyo Mungu ni mtakatifu”? (Ndiyo.) Si kile mlichotoka kusema ni upuuzi? Mengi ya haya mambo ya upuuzi yanayosemwa yanatoka wapi? (Shetani.) Yanatoka kwa Shetani. Mambo ya upuuzi yanayosemwa kimsingi yanatoka kwa kutowajibika kwa watu na kutomheshimu Mungu. Tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Hukuwa na uelewa wowote lakini bado uliongea upuuzi, si huku ni kutowajibika? Si ni kutomheshimu Mungu? Umesoma kiasi kidogo cha maarifa, umeelewa kiasi kidogo cha kufikiria, na kiasi kidogo cha mantiki, ambayo umetumia hapa na, zaidi, umefanya hivyo ukimjua Mungu. Unafikiri Mungu anahisi kutostareheka kuyasikia hayo? Mnawezaje kumjua Mungu mkitumia mbinu hizi? Je, si hayo yanasikika kuwa ya kufedhehesha? Kwa hivyo, inapokuja kwa maarifa ya Mungu, mtu lazima awe makini sana; mahali unapojua Mungu, zungumza tu kuhusu hayo. Zungumza kwa uaminifu na kivitendo na usipambe maneno yako na pongezi za kawaida na usitumie sifa isiyostahilika; Mungu haihitaji na kitu kama hiki kinatoka kwa Shetani. Tabia ya Shetani ni ya kiburi na Shetani anapenda kupewa sifa isiyostahilika na kusikia maneno mazuri. Shetani ataridhishwa na kufurahia iwapo watu watataja maneno yote mazuri ambayo wamejifunza na kutumia maneno haya kwa Shetani. Lakini Mungu hahitaji hii; Mungu hahitaji kuvishwa kilemba cha ukoka ama sifa isiyostahilika na Hahitaji kwamba watu wazungumze upuuzi na kumsifu kwa upofu. Mungu anachukizwa sana na hata Hatasikiza sifa ambayo haiko sambamba na ukweli. Hivyo, wakati watu wengine wanamsifu Mungu kwa upofu na kile wanachosema hakilingani na kile kiko katika mioyo yao na wanapofanya viapo kwa upofu na kumwomba ovyo ovyo, Mungu hasikizi hata kidogo. Lazima uwajibike kwa kile unachosema. Ikiwa hujui jambo, sema tu; ikiwa unajua jambo, onyesha hivyo kwa njia ya kitendo. Sasa, kwa maudhui halisi ya utakatifu wa Mungu, mna uelewa maalum kuuhusu? (Nilipofichua uasi, nilipokuwa na makosa, nilipokea hukumu na kuadibu kwa Mungu, na hapo niliona utakatifu wa Mungu. Na nilipokabiliana na mazingira ambayo hayakukubaliana na matarajio yangu, niliomba kuhusu mambo haya na kutafuta nia za Mungu na Mungu aliponipa nuru na kuniongoza na maneno Yake, niliona utakatifu wa Mungu.) Haya yametoka kwa uzoefu wako mwenyewe, siyo? (Nimeona kwa kile Mungu amezungumzia kwamba mwanadamu amepotoshwa na kudhuriwa na Shetani hivi. Hata hivyo, Mungu ametoa yote kutuokoa na kutokana na haya naona utakatifu wa Mungu.) Hii ni njia ya kweli ya kuzungumza na ni maarifa ya kweli. Kuna maoni mengine tofauti na haya? (Sijui iwapo uelewa wangu ni sahihi au la. Naona uovu wa Shetani kutoka kwa maneno alisema ili kumlaghai Hawa kutenda dhambi na ushawishi wake wa Bwana Yesu. Kutoka kwa maneno ambayo kwayo Mungu aliwaambia Adamu na Hawa kile walichoweza na wasichoweza kula, naona kwamba maneno ya Mungu ni wazi na safi na kwamba ni ya kuaminiwa; kutoka kwa haya naona utakatifu wa Mungu.) Kwa kile mmesikia watu hawa wakisema, mnasema Amina zaidi kwa maneno ya nani? Matamshi ya nani, ushirika wa nani ulikuwa karibu zaidi na ushirika wa mada yetu leo, ya nani ilikuwa ya kweli zaidi? Ushirika wa dada wa mwisho ulikuwa vipi? (Mzuri.) Unasema Amina kwa kile alichosema, ni nini alichosema kilichokuwa sahihi kwa lengo? Unaweza kuwa wazi, sema unachotaka kusema na usijali kuhusu kutokuwa sahihi. (Katika maneno ambayo ndugu alizungumza hivi karibuni, nilisikia kwamba neno la Mungu linaeleweka kwa urahisi na ni wazi sana, si kama maneno ya Shetani yasiyo ya moja kwa moja. Niliona utakatifu wa Mungu kwa haya.) Hii ni sehemu ya hayo. Je, nyote mlisikia kilichosemwa hivi karibuni? (Ndiyo.) Kilikuwa sahihi? (Ndiyo.) Hebu tumpigie dada makofi. Vizuri sana. Naona kwamba mmepata kitu katika shirika hizi mbili za hivi karibuni, lakini lazima nyinyi mwendelee kufanya kazi kwa bidii. Ni lazima mfanye kazi kwa sababu kuelewa kiini cha Mungu ni somo kubwa sana; si kitu ambacho mtu anaweza kuelewa mara moja ama anaweza kuzungumza wazi kwa maneno machache tu.
Kila kipengele cha tabia potovu ya Kishetani ya watu, maarifa, filosofia, fikira na mitazamo ya watu, na vipengele binafsi vinawazuia pakubwa kujua kiini cha Mungu; hivyo mnapozisikia mada hizi, mada zingine zinaweza kuwa mbali kwenu kufikia, mada zingine pengine hamtaelewa, ilhali mada zingine pengine kimsingi hamtalingana nazo na hali halisi. Licha ya hayo, Nimesikia kuhusu uelewa wenu wa utakatifu wa Mungu na Najua kwamba katika mioyo yenu mmeanza kukubali kile Nilichosema na kushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu. Najua kwamba katika mioyo yenu hamu yenu ya kuelewa kiini cha utakatifu wa Mungu imeanza kuchipuka. Lakini ni nini kinachonifanya kuwa na furaha zaidi? Ni kwamba wengine wenu tayari wanaweza kutumia maneno rahisi sana kuelezea maarifa yenu ya utakatifu wa Mungu. Ingawa hiki ni kitu rahisi kusema na Nimekisema awali, katika mioyo ya wengi wenu hii bado haijakubaliwa ama kuweka alama. Hata hivyo, wengine wenu wameweka maneno haya moyoni na ni vizuri kabisa na huu ni mwanzo mzuri sana. Natumai kwamba kwa mada ambazo mnafikiri kuwa za maana sana—ama kwa mada ambazo ziko mbali kwenu kufikia—mtaendelea kutafakari, na kufanya ushirika zaidi na zaidi. Kwa yale masuala ambayo yako mbali kwenu kufikia kutakuwa na mtu wa kuwapa mwongozo zaidi. Mkishiriki katika ushirika zaidi kuhusu maeneo ambayo mnaweza kufikia sasa, Roho Mtakatifu atafanya kazi Yake na mtakuwa na uelewa mkubwa zaidi. Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kinapeana msaada usioweza kupimika kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo; kwa sababu kumjua Mungu ni msingi muhimu na msingi wa imani ya mwanadamu kwa Mungu na ufuatiliaji wa mwanadamu wa ukweli na wokovu na kitu ambacho hakifai kuachiliwa. Iwapo mwanadamu anamwamini Mungu lakini hamjui Mungu, na iwapo mwanadamu anaishi miongoni mwa baadhi ya barua na mafundisho ya kidini, hutawahi kufikia wokovu hata kama utatenda na kuishi kulingana na maana ya juujuu ya ukweli. Hiyo ni kusema, iwapo imani yako kwa Mungu haitokani na kumjua, basi imani yako haimaanishi chochote. Unaelewa, sivyo? (Ndiyo, tunaelewa.) Ushirika wetu utaishia hapa kwa leo. (Mshukuru Mungu!)
Januari 4, 2014

0 评论:

Chapisha Maoni