Jumatano, 29 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarifa na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kudumisha na kupata umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa katika miili ya watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo watu kamwe wanatembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa, wakibeba pingu hizi bila kujua. Kwa ajili ya umaarufu na faida, binadamu hutenganishwa na Mungu na anamsaliti. Kwa kupita kwa kila kizazi, binadamu anakuwa mwovu zaidi na zaidi, mweusi wa moyo zaidi na zaidi, na hivyo kwa njia hii kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani.”
Upotovu wa Shetani wa mwanadamu unadhihirika kimsingi katika vipengele vitano; hivi vipengele vitano ni njia tano ambazo Shetani anampotosha mwanadamu. Ya kwanza kati ya njia hizi tano tulizotaja ni maarifa, kwa hivyo wacha kwanza tuchukue maarifa kama mada ya kushiriki. Shetani hutumia maarifa kama chambo. Sikiza kwa makini: Ni aina tu ya chambo. Watu wanavutiwa “kusoma kwa bidii na kuboreka kila siku,” kujihami kwa maarifa, kama silaha, kisha kutumia maarifa kufungua njia ya sayansi; kwa maneno mengine, kadri unapopata maarifa zaidi, ndivyo utavyoelewa zaidi. Shetani huwaambia watu haya yote. Shetani huwaambia watu kuwa na fikira za juu pia, kwa wakati sawa wanaposoma maarifa, akiwaambia kuwa na matarajio na maadili. Bila kujua kwa watu, Shetani anasambaza ujumbe mwingi kama huu, na kuwafanya watu kuhisi bila kujua kwamba vitu hivi ni sahihi, ama ni vya manufaa. Bila kujua, watu wanatembea njia ya aina hii, bila kujua wanaongozwa mbele na matarajio na maadili yao. Hatua kwa hatua, watu bila kujua wanajifunza kutoka kwa maarifa waliyopewa na Shetani kufikiria kwa watu wakubwa ama maarufu, na kukubali fikira hizi. Wanajifunza pia jambo moja baada ya lingine kutoka kwa matendo ya wengine ambao watu wanachukulia kuwa “mashujaa.” Mnaweza kujua baadhi ya yale ambayo Shetani anatetea kwa mwanadamu katika matendo ya hawa “mashujaa,” ama kile anachotaka kuingiza kwa mwanadamu. Ni kipi ambacho Shetani anaingiza kwa mwanadamu? Mwanadamu lazima awe mzalendo, awe na uadilifu wa kitaifa, na awe shujaa. Ni yapi ambayo mwanadamu anajifunza kutoka kwa baadhi ya hadithi za kihistoria ama kutoka kwa wasifu wa mashujaa? Kuwa na hisia ya uaminifu wa kibinafsi, ama kufanya lolote kwa ajili ya rafiki ya mtu ama kwa rafiki. Miongoni mwa maarifa haya ya Shetani, mwanadamu bila kujua anajifunza mambo mengi, na anajifunza mambo mengi hasi. Katikati ya kutojua huku, mbegu zilizotayarishwa kwa ajili yao na Shetani zinapandwa katika akili zao zisizokomaa. Mbegu hizi zinawafanya kuhisi kwamba wanapaswa kuwa watu wakubwa, wanapaswa kuwa maarufu, wanapaswa kuwa mashujaa, kuwa wazalendo, kuwa watu wanaopenda familia zao, ama kuwa watu wanaoweza kufanya chochote kwa ajili ya rafiki na kuwa na hisia za uaminifu wa kibinafsi. Baada ya kushawishiwa na Shetani, bila kujua wanatembea njia ambayo amewatayarishia. Wanapotembea njia hii, wanalazimika kukubali kanuni za Shetani za kuishi. Bila kujua na bila wao kuwa na uelewa kabisa, wanakuwa na kanuni zao za kuishi, wakati hizi si chochote ila kanuni za Shetani ambazo zimeingizwa kwao kwa nguvu. Wakati wa mchakato wa kujifunza, Shetani anawasababisha kukuza malengo yao wenyewe, kuamua malengo yao ya maisha wenyewe, kanuni za kuishi, na mwelekeo wa maisha, wakati huo wote anawaingizia mambo ya Shetani, kwa kutumia hadithi, kwa kutumia wasifu, kwa kutumia mbinu zote zinazowezekana kuwapata watu, kuchukua chambo polepole. Kwa njia hii, watu wanakuwa na mambo yao ya kupitisha muda na shughuli katika mkondo wa kujifunza kwao: Wengine wanakuja kupenda fasihi, wengine uchumi, wengine unajimu ama jiografia. Kisha kuna wengine wanaokuja kupenda siasa, wengine wanaopenda fizikia, wengine kemia, na hata wengine wanaopenda theolojia. Haya yote ni sehemu ya maarifa na nyote mmepatana nayo. Katika mioyo yenu, kila mmoja wenu anajua yalivyo na mambo haya, kila mmoja amepatana nayo awali. Kuhusiana na maarifa ya aina hii, yeyote anaweza kuzungumza bila kikomo kuhusu moja yao fulani. Na hivyo ni wazi jinsi maarifa haya yameingia kwa kina katika akili ya mwanadamu, inaonyesha nafasi iliyochukuliwa na maarifa haya katika akili ya mwanadamu na jinsi yalivyo na athari ya kina kwa mwanadamu. Punde tu mtu anapenda sehemu ya maarifa, wakati katika moyo wake mtu amependa kwa dhati mojawapo, basi bila kujua anaendeleza maadili: Watu wengine wanataka kuwa watunzi, wengine wanataka kuwa waandishi, wengine wanataka kuwa na kazi kutokana na siasa, na wengine wanataka kushiriki katika uchumi na kuwa wanabiashara. Kisha kuna kundi la watu ambao wanataka kuwa mashujaa, kuwa wakubwa ama maarufu. Bila kujali mtu anataka kuwa mtu wa aina gani, lengo lake ni kuchukua mbinu hii ya kujifunza maarifa na kuitumia kwa ajili yake, kufikia matamanio yake, maadili yake mwenyewe. Haijalishi inasikika kuwa nzuri namna gani—anataka kufikia ndoto yake, asiishi katika maisha haya bure, ama anataka kushiriki katika kazi—anakuza haya maadili na matarajio ya juu lakini, kimsingi, yote ni ya nini? Je, mmeyafikiria haya awali? Mbona Shetani anataka kufanya hivi? Madhumuni ya Shetani ni yapi, kuyaweka mambo haya kwa mwanadamu? Mioyo yenu lazima ielewe vizuri swali hili.
Tumetoka tu kuongea kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu, basi kinachofuata wacha tushiriki kuhusu jinsi Shetani hutumia sayansi kumpotosha mwanadamu. Kwanza, kwa kutumia sayansi kumpotosha mwanadamu, Shetani hutumia jina la sayansi kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu, kuridhisha hamu ya mwanadamu [a] kutafiti sayansi na kuchunguza siri. Pia, katika jina la sayansi, Shetani huridhisha haja ya mwili na mahitaji ya mwanadmu kuendelea kuinua ubora wao wa maisha. Shetani hivyo, katika jina hili, hutumia njia ya sayansi kumpotosha mwanadamu. Je, ni kufikiria tu kwa mwanadamu ama akili za mwanadamu ambazo Shetani anapotosha kwa kutumia njia hii ya sayansi? Miongoni mwa watu na mambo katika mazingira yetu ambayo tunaweza kuona na ambayo tunakutana nayo, ni yapi mengine ambayo Shetani anatumia sayansi kupotosha? (Mazingira ya kiasili.) Mko sahihi. Inaonekana kwamba mmedhuriwa sana na hili, na pia mmeathirika sana na yeye. Mbali na kutumia sayansi kumdanganya mwanadamu, kutumia matokeo yote ya utafiti na mahitimisho mbalimbali ya sayansi kumdanganya mwanadamu, Shetani pia hutumia sayansi kama mbinu ya kutekeleza uangamizi na unyonyaji tele wa mazingira ya kuishi aliyopewa mwanadamu na Mungu. Anafanya hivi chini ya kisingizio kwamba iwapo mwanadamu anatekeleza utafiti wa kisayansi, basi mazingira ya kuishi ya mwanadamu yatakuwa bora na bora zaidi na viwango vya kuishi vya mwanadamu daima vitaboreka, na zaidi ya hayo kwamba maendeleo ya kisayansi yanafanywa ili kuhudumia mahitaji ya mwili ya mwanadamu yanayozidi kila siku na haja ya daima ya kuinua ubora wao wa maisha. Kama sio kwa sababu ya sababu hizi, basi huuliza kile unachofanya hata kuendeleza sayansi. Huu ni msingi wa kidhahania wa maendeleo ya Shetani ya sayansi. Sayansi, hata hivyo, ina matokeo yapi kwa binadamu? Mazingira yetu ya karibu kabisa yana nini? Si hewa ambayo binadamu hupumua imechafuliwa? Maji tunayoyanywa kweli bado ni safi? (La.) Basi, je, chakula tunachokula, kingi chake ni cha kiasili? (La.) Basi ni nini tena? Kinakuzwa kwa kutumia mbolea na kupaliliwa kwa kutumia vinasaba, na pia kuna mabadiliko yanayozalishwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za sayansi, ili kwamba hata mboga na matunda tunayoyala sio ya kiasili tena. Si rahisi sasa kwa watu kupata mazao ya vyakula ambavyo havijabadilishwa kula. Hata mayai hayaonji yalivyokuwa yakionja awali, baada ya kusindikwa na inayoitwa sayansi na Shetani. Kwa kuangalia taswira kubwa, anga nzima imeharibika na kuchafuliwa; milima, maziwa, misitu, mito, bahari, na kila kitu juu na chini ya ardhi vyote vimeharibiwa na inayoitwa mafanikio ya kisayansi. Kwa maneno mengine, ikolojia nzima, mazingira yote ya kuishi yaliyopewa mwanadamu na Mungu yamechafuliwa na kuharibiwa na iitwayo sayansi. Ingawa kuna watu wengi waliopata walichotarajia katika suala la ubora wa maisha wanaotafuta, kuridhisha tamaa na miili yao, mazingira ambayo mwanadamu anaishi kimsingi yameharibiwa na kuangamizwa na “mafanikio” mbalimbali yaliyoletwa na sayansi. Hata nje ama katika nyumba zetu hatuna tena haki ya kupumua pumzi moja ya hewa safi. Wewe niambie, hii ni huzuni ya mwanadamu? Bado kuna furaha yoyote ya kuzungumzia kwa mwanadamu kuishi katika nafasi hii ya kuishi? Mwanadamu anaishi katika nafasi hii ya kuishi na, kutoka mwanzoni, haya mazingira ya kuishi yaliumbwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Maji ambayo watu hunywa, hewa ambayo watu hupumua, chakula ambacho watu hula, mimea, miti, na bahari—haya mazingira ya kuishi yote yalipewa mwanadamu na Mungu; ni asili, na hutekeleza kulingana na amri asili iliyotolewa na Mungu. Kama hakungekuwa na sayansi, na watu wangefurahia alichopewa mwanadamu kulingana na njia ya Mungu, wangekuwa na furaha na wangefurahia kila kitu kikiwa cha asili kabisa. Sasa, hata hivyo, haya yote yameangamizwa na kuharibiwa na Shetani; nafasi ya kimsingi ya kuishi ya mwanadamu haipo tena katika hali yake asili zaidi. Lakini hakuna anayeweza kutambua kilichosababisha matokeo ya aina hii ama jinsi haya yalikuja kuwa, na zaidi ya hapo hata watu zaidi wanaelewa na kukaribia sayansi kwa kutumia mawazo waliyoingiziwa na Shetani, na kwa kutazama sayansi kwa macho ya dunia. Je, hii si ya kuchukiza sana na ya kusikitisha? Kwa kuwa Shetani sasa amechukua nafasi ambamo wanadamu wapo na mazingira yao ya kuishi na kuwapotosha kuwa katika hali hii, na kwa kuwa wanadamu wanaendelea kwa njia hii, kuna haja yoyote ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu hawa duniani ambao wamepotoshwa sana na ambao wamekuwa maadui Wake? Kuna haja ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu? (La.) Iwapo wanadamu watazidi kuendelea kwa njia hii, watachukua mwelekeo upi? (Uharibifu.) Wanadamu wataharibiwa vipi? Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza, mapigo, na ukungu uliosambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo? Sasa kwa sababu mnaelewa hili, iwapo wanadamu hawamfuati Mungu, lakini daima wanamfuata Shetani kwa njia hii—kutumia maarifa daima kujitajirisha, kutumia sayansi kuchunguza bila kikomo siku za baadaye za maisha ya binadamu, kutumia mbinu ya aina hii kuendelea kuishi—mnaweza kutambua hitimisho ya asili ya wanadamu itakuwa vipi? Matokeo ya mwisho asilia yatakuwa yapi? (Uharibifu.) Itakuwa uharibifu: kukaribia uharibifu hatua moja kwa wakati. Kukaribia uharibifu kwa hatua moja kwa wakati! Inaonekana sasa kama sayansi ni aina ya ushombwe ama sumu inayofanya kazi polepole ambayo Shetani amemwandalia mwanadamu, ili wakati mnapojaribu kupambanua mambo mnafanya hivyo katika hali ya ukungu; haijalishi mnaangalia kwa ugumu aje, hamwezi kuona mambo kwa wazi, na haijalishi mnajaribu sana vipi, hamwezi kuyatambua. Shetani, hata hivyo, bado anatumia jina la sayansi kuzidisha hamu yako na kukuongoza kwa pua, mguu mmoja mbele ya mwingine, kuelekea shimo na kuelekea kifo. Sivyo? (Ndiyo.) Hii ndiyo njia ya pili.
Suala la jinsi Shetani hutumia desturi ya kitamaduni kumpotosha mwanadamu pia linahitaji maelezo. Kuna usawa mwingi kati ya desturi ya kitamaduni na ushirikina, ni tu kuwa desturi ya kitamaduni ina hadithi fulani, vidokezo, na vyanzo fulani. Shetani ametunga na kuunda ngano ama hadithi nyingi katika vitabu vya historia, na kuacha watu na hisia za kina za desturi ya kitamaduni ama watu wa kishirikina. Chukua kwa mfano Watu Wanane Wasiokufa Wanaovuka Bahari, Safari ya kwenda Magharibi, Mfalme Mkuu Jade, Nezha Anamshinda Joka Mfalme, na Uchunguzi wa Miungu, zote za Uchina. Haya hayajakita mizizi katika akili za mwanadamu? Hata iwapo watu wengine hawajui maelezo yote, bado wanajua hadithi za jumla, na yaliyomo kwa jumla ndiyo yanayokwama katika moyo wako na yanakwama katika akili yako, na huwezi kuyasahau. Haya ni mambo ambayo Shetani alimwekea mwanadamu kitambo sana, baada ya kusambaza katika nyakati tofauti mawazo yake na filosofia zake mbalimbali za maisha. Haya mambo yanadhuru moja kwa moja na kumomonyoa nafsi za watu na kuweka watu chini ya fingo moja baada ya jingine. Hiyo ni kusema kwamba baada ya wewe kukubali mambo haya yanayotoka kwa desturi ya kitamaduni, hadithi ama ushirikina, baada ya mambo haya kuwekwa kwa akili yako, baada ya hayo kukwama katika moyo wako, ni kama tu apizo—unakamatwa na kushawishika na hizi tamaduni, haya mawazo na hadithi za kitamaduni. Yanashawishi maisha yako, mtazamo wako wa maisha na pia yanashawishi maoni yako ya mambo. Hata zaidi yanashawishi ufuataji wako wa njia sahihi ya maisha: Hii bila shaka ni apizo! Unajaribu lakini huwezi kuyatupilia mbali; unayakatakata lakini huwezi kuyakata chini; unayapiga lakini huwezi kuyapiga chini. Sivyo? (Ndiyo.) Zaidi ya hayo, baada ya mwanadamu bila kujua kuwekwa chini ya aina hii ya apizo, bila kujua, anaanza kumwabudu Shetani, kukuza taswira ya Shetani katika moyo wake. Kwa maneno mengine, anamweka Shetani kama sanamu, kifaa cha yeye kuabudu na kutazamia, hata kwenda mbali zaidi na kuichukulia kwa njia sawa ambayo wangemchukulia Mungu. Bila kujua, mambo haya yako katika mioyo ya watu yakidhibiti maneno na matendo yao. Bila kujua unakubali kuwepo kwa hadithi hizi, kuzitengenezea sanamu halisi, kuzibadili kuwa mambo halisi yaliyopo. Katika kutojua, unapokea haya mawazo bila kufahamu na kuwepo kwa vitu hivi. Pia unapokea bila kufahamu mashetani, Shetani na sanamu ndani ya nyumba yako na ndani ya moyo wako—hii bila shaka ni apizo. Je, mnahisi sawa? (Ndiyo.) Kuna yeyote miongoni mwenu ambao wamechoma ubani na kuabudu Budhaa? (Ndiyo.) Kwa hivyo madhumuni ya kuchoma ubani na kumwabudu Budhaa yalikuwa yapi? (Kuombea amani.) Je ni ujinga kuombea amani kutoka kwa Shetani? Shetani analeta amani? (La.) Kuifikiria sasa, mlikuwa wajinga hapo nyuma? (Ndiyo.) Namna ya aina hiyo ni ya upuuzi, jinga na nyofu, siyo? Shetani hawezi kukupa amani. Mbona? Shetani anafikiria tu jinsi ya kukupotosha na hawezi kukupa amani; anaweza tu kukupa nafasi ya kupumua ya muda mfupi. Lakini lazima uchukue kiapo na ukivunja ahadi yako ama ukivunja kiapo ulichofanya, basi utaona jinsi anavyokuadhibu. Kwa kukufanya uchukue kiapo, kwa kweli anataka kukudhibiti, sivyo? Wakati mlipoombea amani, mlipata amani? (La.) Hamkupata amani, lakini kinyume na hayo alileta bahati mbaya, majanga yasiyoisha na majanga mengi—kweli bahari isiyo na mipaka ya uchungu. Amani haiko miongoni mwa miliki ya Shetani, na hili ni ukweli. Haya ndiyo matokeo kwa wanadamu ya ushirikina wa kikabila na desturi ya kitamaduni.

0 评论:

Chapisha Maoni