Alhamisi, 5 Septemba 2019

Neno la Mungu | “Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni”

Neno la Mungu | “Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni”

Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati nuru ya Mashariki inapong'aa polepole tu ndipo giza kote duniani litaanza kugeuka na kuwa nuru, na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba Nilishatoka Israeli zamani na Nimeanza kuchomoza upya Mashariki. Niliwahi kushuka Israeli na baadaye Niliondoka kutoka huko, Siwezi tena kuzaliwa Israeli kwa mara nyingine, kwa kuwa kazi Yangu inauongoza ulimwengu mzima na, zaidi ya hilo, umeme unamulika moja kwa moja kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hii ndiyo sababu Nimeshuka Mashariki na kuwaletea watu wa Mashariki Kanaani. Ningependa kuwaleta watu kutoka dunia nzima waje katika nchi ya Kanaani, na kwa hiyo Naendelea kutoa maneno Yangu katika nchi ya Kanaani ili kuudhibiti ulimwengu mzima. Kwa wakati huu,hakuna nuru katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani, na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi. Niliipa Israeli utukufu Wangu kisha Nikauchukua na baadaye Nikawaleta Waisraeli Mashariki, na vilevile ubinadamu wote Mashariki. Nimewaleta wote kwenye nuru ili waweze kuungana tena nayo, na kushirikiana na nuru , na wasilazimike kuitafuta tena.” Tazama zaidi: Maonyesho ya Mungu | "Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu"
Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika wanadamu yakitawanyika hapa na pale, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa. Kuanzia wakati huu kuendelea, Nimeingia katika enzi mpya, kuwaleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Niliporudi katika “nchi Yangu,” Nilianza sehemu nyingine tena ya kazi katika mpango Wangu wa asili, ili mwanadamu aje kunijua zaidi. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, kwa hiyo Naharakisha mbele na nyuma kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu. Hii ni enzi mpya, hata hivyo, na Nimeleta kazi mpya ili Niwachukue watu wapya wengi zaidi katika enzi mpya na kuachana na wengi wa wale Nitakaowaondoa. Katika taifa la joka kubwa jekundu, Nimetekeleza hatua ya kazi isiyoeleweka kwa wanadamu, kuwafanya kuyumba katika upepo, ambapo baadaye wengi wanabebwa kwa siri na upepo unaovuma. Kweli, huu ni “uwanja wa kupura” Ninaotaka kuusafisha; ni kile Ninachotamani na pia ni mpango Wangu. Kwa maana wengi waovu wameingia ndani kimya wakati Niko kazini, lakini Sina haraka ya kuwafukuza. Badala yake, Nitawatawanya wakati utakapofika. Ni baada ya hapo tu ndipo Nitakuwa chemchemi ya uzima, kuwakubalia wanaonipenda kweli wapokee kutoka Kwangu tunda la mtini na harufu ya yungiyungi. Katika nchi ambako Shetani huishi, nchi ya vumbi, hakuna dhahabu safi iliyobaki, ila ni mchanga tu, na kwa hiyo, Nikikabiliwa na hali hizi, Nafanya hatua hiyo ya kazi. Lazima ujue kwamba Ninachopata ni dhahabu safi, iliyosafishwa, wala si mchanga. Ni jinsi gani waovu wanaweza kubaki katika nyumba Yangu? Ninawezaje kuruhusu Mbweha kuwa vimelea ndani ya paradiso Yangu? Natumia kila mbinu inayoweza kufikiriwa kuvifukuza vitu hivi. Kabla ya mapenzi Yangu kufichuliwa, hakuna anayefahamu Ninachotaka kufanya. Nikichukua fursa hii, Ninawafukuza wale waovu, na wanalazimika kuondoka machoni Pangu. Hili ndilo Mimi huwafanyia waovu, lakini bado kutakuwa na siku ya wao kunifanyia huduma. Hamu ya watu kupata baraka ni kubwa mno; Kwa hivyo Ninageuza mwili Wangu na kuonyesha uso Wangu wa utukufu kwa nchi za Mataifa, ili watu wote waishi katika dunia yao wenyewe na kujihukumu, huku Naendelea kusema maneno ambayo Napaswa kuyasema na kuwaruzuku wanadamu wanachohitaji. Wakati wanadamu wanapata fahamu, Nitakuwa Nimeeneza kazi Yangu kitambo. Kisha Nitawaonyesha wanadamu mapenzi Yangu, na kuanza sehemu ya pili ya kazi Yangu juu ya wanadamu, kuwaruhusu watu wote wanifuate kwa karibu ili waambatane na kazi Yangu, na kuwaruhusu watu kufanya kila wawezalo kutekeleza nami kazi Ninayopaswa kufanya.
Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Kama mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni, wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye “Mlima wa Mizeituni” wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni “mtoto mchanga” Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!

0 评论:

Chapisha Maoni