Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumamosi, 31 Agosti 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno” (Dondoo1)

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno” (Dondoo1)

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumkamilisha binadamu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani yake. Kupitia katika neno, kazi yote ambayo Mungu angependa kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa. Kupitia katika neno, binadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Binadamu ameliona neno, amelisikia neno, na akapata habari ya uwepo wa neno. Kutokana na haya, binadamu anaamini katika uwepo wa Mungu; binadamu anaamini katika uwezo na hekima za Mungu, pamoja na moyo wa upendo wa Mungu kwa binadamu na tamanio Lake la kumwokoa binadamu. Ingawa neno ‘neno’ ni rahisi na la kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Kuanzia wakati huu kuendelea, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, wakichungwa na kuruzukiwa na neno. Binadamu wote wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata kuna binadamu zaidi wanaoishi chini ya hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kwa minajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa minajili ya kubadilisha sura asilia ya ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, na pia hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia neno kufanya kazi Yake na kutimiza matokeo ya kazi Yake; Hafanyi maajabu au kutenda miujiza; Anafanya tu kazi Yake kupitia kwa neno. Kwa sababu ya neno, binadamu anastawishwa na kuruzukiwa; kwa sababu ya neno, binadamu hupokea maarifa na kupata uzoefu wa kweli. Binadamu katika Enzi ya Neno amepokea kwa kweli baraka za kipekee. Binadamu huwa hapati maumivu ya mwili na hufurahia tu ruzuku nyingi ya neno la Mungu; hawahitaji tena kutafuta au kushika safari, na kwa utulivu huona kuonekana kwa Mungu, wanamsikia Yeye akiongea binafsi, wanapokea ujazo Wake, na kumwona Yeye binafsi akifanya kazi Yake. Haya ndiyo mambo ambayo binadamu katika enzi zilizopita hawakuweza kufurahia, na hizi ndizo baraka ambazo wasingewahi kupokea.”

Jumatatu, 26 Agosti 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Ingawa wale waliozaliwa katika enzi hii wametiishwa chini ya upotovu wa Shetani na mapepo wachafu sana, pia ni kweli kwamba wanaweza kupata wokovu mkuu kutokana na upotovu huu, hata mkubwa kuliko mifugo wanaotanda milima na tambarare na mali nyingi ya familia ambayo Ayubu alipata, na pia ni zaidi ya baraka ambayo Ayubu alipokea ya kumwona Yehova baada ya majaribu yake. Ilikuwa tu baada ya Ayubu kupitia jaribio la kifo ndipo angeweza kuyasikia maneno ya Yehova na angeweza kusikia sauti Yake ya mshindo kutoka mawinguni. Hata hivyo, hakuuona uso wa Yehova na hakujua tabia Yake. Kile Ayubu alipata kilikuwa tu mali ya kimwili ambayo hutoa furaha za mwili na watoto wazuri mno katika miji jirani pamoja na ulinzi kutoka kwa malaika wa mbinguni. Hakuwahi kumwona Yehova, na hata ingawa aliitwa mwenye haki, kamwe hakuijua tabia ya Yehova. Ingawa watu wa leo ni maskini kwa muda katika starehe za kimwili au wanapitia mazingira ya nje ya uhasama, Nimedhihirisha tabia Yangu ambayo Sikuwahi kuifunua kwa wanadamu katika vizazi vilivyopita, ambayo siku zote imekuwa siri, na miujiza Yangu kabla ya enzi kwa watu duni mno ambao pia Nimewapa wokovu mkuu, na hii ni mara ya kwanza ambayo Nimefanya hivyo. Sijawahi kufanya aina ya hii awali, na ingawa ninyi mko chini zaidi kuliko Ayubu, yale mmepata na yale mmeona yamemshinda Ayubu kwa mbali. Ingawa mmepitia kila aina ya mateso na maudhi, mateso hayo si kama majaribu ya Ayubu, lakini ni hukumu na kuadibu ambako watu wamepokea kwa sababu ya uasi na ukinzani wao, na kwa sababu ya tabia Yangu yenye haki. Ni hukumu yenye haki, kuadibu, na laana. Ayubu alikuwa mmoja wa Waisraeli, mmoja wa watu wenye haki aliyepokea upendo na rehema ya ajabu ya Yehova. Hakufanya vitendo viovu na hakumpinga Yehova; badala yake, alijitoa kwa Yehova kwa uaminifu, naye alitiishwa chini ya majaribu kwa sababu ya haki yake, na alipitia majaribu makali kwa sababu alikuwa mtumishi mwaminifu wa Yehova. Watu leo wako chini ya hukumu na laana Yangu kwa sababu ya uchafu na uovu wao. Ingawa mateso yao hayalingani kabisa na kile Ayubu alipitia wakati alipoteza mifugo wake, mali yake, watumishi wake, watoto wake, na wale walio wapendwa kwake wote, kile watu wanapitia ni usafishaji na uteketezaji mkali; kilicho kikubwa zaidi kuliko kile Ayubu alipitia ni kwamba aina hii ya jaribio haipunguzwi wala kuondolewa kwa sababu ya udhaifu wao, badala yake, ni ya muda mrefu hadi siku yao ya mwisho ya maisha. Hii ni adhabu, hukumu, laana—ni ya kuteketea bila huruma, na hata zaidi ni “urithi” wa wanadamu wa haki. Ni kile wanachostahili, na ni mahali pa maonyesho ya tabia Yangu yenye haki. Ni ukweli unaojulikana. Lakini yale watu wamepata yanapita sana yale wamevumilia sasa. Yale ambayo mmepitia ni vipingamizi tu kutokana na upumbavu, lakini mapato yenu ni mara mia zaidi ya mateso yenu. Kwa mujibu wa sheria za Israeli katika Agano la Kale, wale wote wanaonipinga Mimi, wale wote wanaonihukumu waziwazi, na wale wote wasioifuata njia Yangu lakini wanatoa sadaka zenye kukufuru Kwangu kwa ujasiri kwa hakika wataharibiwa kwa moto katika hekalu, au baadhi ya watu waliochaguliwa watawatupia mawe hadi kifo, na hata vizazi vyao vya nyumba yao wenyewe na jamaa zao wengine wa karibu watapitia laana Yangu, na katika dunia ijayo hawatakuwa huru, lakini watakuwa watumwa wa watumwa Wangu, Nami nitawaelekeza hadi uhamishoni miongoni mwa Mataifa nao hawataweza kurudi katika nchi yao. Kulingana na vitendo vyao, tabia zao, mateso yanayovumiliwa na watu leo si makubwa kama adhabu waliyopitia Waisraeli. Kusema kuwa kile mnachopitia sasa ni adhabu si bila sababu, na hii ni kwa sababu mmevuka mpaka kweli, na kama mngekuwa katika Israeli mngekuwa mmoja wa wenye dhambi milele na mngekatwa vipande vipande na Waisraeli muda mrefu uliopita na pia mngeteketezwa kwa moto kutoka mbinguni katika hekalu la Yehova. Na nini ambacho mmepata sasa? Nini ambacho mmepokea, nini ambacho mmefurahia? Nimedhihirisha tabia Yangu yenye haki ndani yenu, lakini muhimu zaidi ni kwamba Nimefunua uvumilivu Wangu kwa ukombozi wa mwanadamu. Mtu angesema kwamba yote ambayo Nimefanya ndani yenu ni kazi na uvumilivu, kwamba ni kwa ajili ya usimamizi Wangu, na hata zaidi ni kwa ajili ya starehe ya wanadamu.
Ingawa Ayubu alipitia majaribu kutoka kwa Yehova, alikuwa tu mtu mwenye haki aliyemwabudu Yehova, na hata alipokuwa akipitia majaribu hayo hakulalamika kumhusu Yeye, lakini alithamini sana kukutana kwake na Yehova. Watu wa leo hawathamini tu uwepo wa Yehova, bali humkataa, humchukia sana, hulalamika kumhusu, na hudhihaki uwepo Wake. Je, hamjapata zaidi ya kidogo? Je, mateso yenu kweli hayajakuwa makubwa sana? Je, baraka zenu hazijakuwa nyingi kuliko zile za Maria na Yakobo? Je, upinzani wenu haujakuwa hafifu? Inawezekana kuwa yale Nimehitaji kwenu, yale Nimeuliza kutoka kwenu yamekuwa makuu mno na mengi sana? Ghadhabu Yangu iliachiliwa huru tu juu ya wale Waisraeli walionipinga Mimi, si moja kwa moja juu yenu, lakini kile ambacho mmepata kimekuwa tu hukumu Yangu isiyo na huruma na mafichuzi pamoja na utakaso mkali usio na huruma. Licha ya haya watu bado wananipinga na kunikana Mimi bila hata chembe ya utii. Na hata kuna baadhi ya watu ambao hujitenga na Mimi na kunikataa; aina hiyo ya mtu si bora zaidi kuliko bendi ya Kora na Dathani wakimpinga Musa. Mioyo ya watu imekuwa migumu sana, na asili zao ni kaidi sana. Kamwe hawatabadili mienendo yao ya zamani. Wamejiweka wazi kama kahaba hadharani kwa matamshi Yangu, na maneno Yangu ni makali sana kwamba “hayana adabu”, yakiweka wazi asili za watu hadharani. Lakini watu huamkia tu kwa vichwa vyao, wanamwaga machozi machache, na kuwa na hisia za kusikitisha kidogo tu. Mara tu inapoisha, ni wakali kama mfalme wa wanyama wa pori katika milima na hawana utambuzi kabisa. Je, watu na aina hii ya tabia wanawezaje kujua kwamba wamefurahia baraka zaidi ya mara mia kuliko zile za Ayubu? Wanawezaje kugundua kwamba kile wanachokifurahia ni baraka ambazo zimeonekana katika enzi zote kwa nadra sana, ambazo hakuna mtu aliyewahi kuzifurahia awali? Dhamiri za watu zinawezaje kuhisi aina hii ya baraka ambayo hubeba adhabu? Kusema ukweli, chote Ninachohitaji kwenu ni ili muweze kuwa mifano kwa kazi Yangu na kuwa mashahidi kwa ajili ya tabia Yangu yote na matendo Yangu yote, na ili muweze kuwekwa huru kutokana na mateso ya Shetani. Lakini wanadamu daima huchukizwa na kazi Yangu na wanakuwa na uhasama kwake kimakusudi. Aina hiyo ya mtu anawezaje kutonichochea Mimi kurejesha sheria za Israeli na kuleta juu yake ghadhabu Yangu kwa ajili ya Israeli? Ingawa kuna wengi miongoni mwenu ambao ni “watiifu” Kwangu, kuna hata zaidi ambao wa namna ya “bendi ya Kora” Mara tu Nitakapoupata utukufu Wangu kamili, Nitachukua moto kutoka mbinguni na kuwateketeza hadi wawe majivu. Mnapaswa kujua kwamba Sitawaadibu watu kwa maneno Yangu tena, lakini kabla ya kuifanya kazi ya Israel, Nitaiteketeza kabisa ile namna ya “bendi ya Kora” wanaonipinga Mimi na ambao Nimewaondoa muda mrefu uliopita. Wanadamu hawatapata tena nafasi ya kunifurahia, lakini yote ambayo wataona yatakuwa ghadhabu na “moto” Wangu kutoka mbinguni. Nitafichua matokeo ya watu wote, na Nitawagawanya watu wote katika makundi mbalimbali. Nitaangalia kila tendo lao lenye uasi, na kisha kuimaliza kazi Yangu, ili matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na uamuzi Wangu wakati wako duniani pamoja na mitazamo yao kunihusu. Wakati huo utakapofika, hakutakuwa na kitu kitakachoweza kubadilisha matokeo yao. Acha watu wafunue matokeo yao wenyewe! Acha Niyakabidhi matokeo ya watu kwa Baba wa mbinguni.
Soma Zaidi :Umeme wa Mashariki Unatoka Wapi?

Jumatano, 21 Agosti 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini”


Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini”

Mwenyezi Mungu anasema, “Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako? Ni mara ngapi umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, huku ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Vitendo kama hivi pekee ndivyo humridhisha Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli.”

Video Husika: Wimbo Mpya wa Dini | "Mungu Anapata Mwili ili tu Kumshinda Shetani na Kuwaokoa Binadamu"

Ijumaa, 2 Agosti 2019

Wimbo Mpya wa Dini 2019 | "Upendo Safi Bila Dosari" (Lyrics Video)

Wimbo wa Kuabudu | "Upendo Safi Bila Dosari" (Lyrics Video)

I Upendo ni hisia safi, safi bila dosari. Tumia moyo, tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Ukipenda hudanganyi, hulalamiki, hugeuki, hutazamii kupata kitu, cha malipo. Ukipenda utajitolea, ukubali taabu, kuwa kimoja, Mungu katika mapatano.
II Upendo hauna shauku, ujanja wala uongo. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Upendo haujitengi, upendo hauna dosari. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Ukipenda hudanganyi, hulalamiki, hugeuki, hutazamii kupata kitu cha malipo. Ukipenda utajitolea, ukubali taabu, kuwa kimoja, Mungu katika mapatano .
III Utatoa familia, ujana wako na siku za usoni. Utoe ndoa yako kwa Mungu, toa vyote kwake. Utatoa familia,ujana na siku za usoni. Utoe ndoa yako kwa Mungu, toa vyote kwake. Ama upendo wako si upendo kabisa, bali uongo, usaliti kwa Mungu.
IV Upendo ni hisia safi, safi bila dosari. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga. Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.
Tazama Zaidi: Nyimbo za Injili za Kanisa la Mwenyezi Mungu: nyimbo za kusifu, kumjua Mungu na uzoefu wa maisha, na mengine. Sikiliza mtandaoni! Pakua bure!