Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kufuata-Mapenzi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kufuata-Mapenzi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 10 Oktoba 2019

Neno la Mungu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Tisa” (Dondoo 1)

Neno la Mungu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Tisa” (Dondoo 1)

Mwenyezi Mungu anasema, “Mimi Natawala katika ufalme, na zaidi ya hapo, Ninatawala katika ulimwengu mzima; Mimi ni Mfalme wa ufalme na pia Mkuu wa ulimwengu. Kutoka wakati huu na kuendelea, Nitawakusanya wote wasio wateule na Nitaanza kufanya kazi Yangu katika mataifa, Na Nitatangaza amri Yangu ya utawala kwa ulimwengu mzima, ili kwa mafanikio Niweze kuingia katika hatua ifuatayo ya Kazi Yangu. Mimi nitatumia kuadibu ili kueneza kazi Yangu katika Mataifa, ambayo ni kusema, Nitatumia nguvu dhidi ya wale wote walio watu wa Mataifa. Kwa kawaida, kazi hii itafanyika kwa wakati mmoja na ile Kazi Yangu miongoni mwa wale waliochaguliwa. Wakati watu Wangu wanatawala na kushika madaraka duniani ndio pia itakuwa siku ambayo watu wote duniani watakuwa wameshindwa, na zaidi ya hayo, utakuwa wakati Wangu wa mapumziko—na hapo tu ndipo Nitawaonekania wale walioshindwa. Mimi huonekana kwa ufalme mtakatifu, na kujificha kutoka kwa nchi ya uchafu. Wote walioshindwa na kuwa watiifu mbele Yangu wana uwezo wa kuuona uso Wangu kwa macho yao wenyewe, na uwezo wa kusikia sauti Yangu kwa masikio yao wenyewe. Hii ni baraka ya wale waliozaliwa katika siku za mwisho, hii ni baraka Niliyoamua kabla, na hii haiwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Leo, Ninafanya kazi kwa namna hii kwa ajili ya kazi ya baadaye. Kazi Zangu zote zinahusiana, katika yote kuna wito na mwitikio: Kamwe hakuna hatua yoyote iliyokoma kwa ghafla, na kamwe hakuna hatua yoyote iliyofanywa kwa kujitegemea kivyake. Je, hivi sivyo ilivyo? Je, kazi ya siku za nyuma siyo msingi wa kazi ya leo? Je, maneno ya zamani si utangulizi wa maneno leo? Je, hatua za zamani si asili ya hatua za leo? Wakati Ninafungua rasmi hati ya kukunjwa ndio wakati watu ulimwenguni kote wanaadibiwa, wakati watu wote duniani wanakabiliwa na majaribu, na ndicho kilele cha Kazi Yangu; watu wote wanaishi katika nchi bila mwanga, na watu wote wanaishi huku kukiwa na tishio la mazingira yao. Kwa maneno mengine, ni maisha ambayo mwanadamu hajawahi kupitia kutoka wakati wa uumbaji mpaka siku ya leo, na hakuna yeyote katika enzi zote aliyeweza ‘kustarehe’ na aina hii ya maisha, na hivyo Ninasema kwamba Ninafanya kazi ambayo haijawahi kufanyika mbeleni. Hii ndiyo hali halisi ya mambo, na hii ni maana ya ndani. Kwa sababu siku Yangu inakaribia kwa wanadamu wote, kwa sababu haionekani kuwa mbali, lakini iko mbele ya macho ya mwanadamu, ni nani asiyeweza kuwa na uoga kwa sababu ya jambo hili? Ni nani asiyekuwa na furaha katika hili? Mji mchafu wa Babeli hatimaye umefika mwisho wake; mwanadamu amekutana na dunia mpya kabisa, na mbingu na dunia zimebadilishwa na kufanywa mpya.”

Jumatatu, 30 Septemba 2019

Ni Lazima Muielewe Kazi; Msifuate kwa Rabsha

Ni Lazima Muielewe Kazi; Msifuate kwa Rabsha!

Kwa sasa kuna watu wengi ambao huamini kwa njia ya rabsha. Udadisi wenu ni mkubwa mno, tamaa yenu ya kufuatilia baraka ni kubwa mno, na hamu yenu ya kufuatilia maisha ni ndogo mno. Waumini katika Yesu siku hizi wamejaa shauku. Yesu atawakaribisha katika nyumba ya mbinguni–je, wao hawawezi kuamini? Watu wengine ni waumini katika maisha yao yote, wameamini kwa miaka arobaini au hamsini, na hawachoki kamwe kusoma Biblia. Hii ni kwa sababu bila kujali kinachotokea, mradi wao wanaamini, wataingia mbinguni. Mmemfuata Mungu kwa njia hii kwa miaka michache tu, lakini tayari mnajitahidi sana na hamna uvumilivu tena. Hii ni kwa sababu hamu yenu ya kupata baraka ina nguvu mno. Nyinyi kuitembea njia hii ya kweli kunadhibitiwa na hamu yenu ya kupata baraka na nyoyo zenu chunguzi. Hamna ufahamu mwingi wa hatua hii ya kazi. Mengi ya yale Ninayoyasema leo siyo kuongea kwa wale watu wanaoamini katika Yesu; hayaongewi hata kidogo kurudisha pigo dhidi ya dhana zao. Kwa kweli, hizi dhana zinazofichuliwa ni dhana zile zile ambazo zipo kati yenu, kwa sababu hamuelewi ni kwa nini Biblia imewekwa chini, kwa nini Ninasema kuwa kazi ya Yehova imezeeka, na kwa nini Ninasema kuwa kazi ya Yesu imezeeka. Kwa kweli, mna dhana nyingi ambazo hamjazipa sauti. Mna dhana nyingi ambazo zimefungiwa ndani ya mioyo yenu, na nyinyi mnafuata umati tu. Je, mnadhani kuwa dhana zenu ni chache? Ni kwamba tu kuwa hamzizungumzii, na hakuna cha ziada! Kwa kweli, mnafuata tu kwa uzembe, hamtafuti njia ya kweli kamwe, na kwa makusudi hamji kupata uzima. Mna mtazamo wa kutaka tu kuona kitakachotokea. Kwa sababu hamjaziacha dhana zenu za zamani, hakuna yeyote kati yenu ambaye ameweza kujitoa mwenyewe kikamilifu. Baada ya kufika wakati huu, nyote mna wasiwasi kuhusu majaliwa yenu wenyewe, mkifikiri mchana na usiku, msiweze kuyaweka chini kamwe. Je, unafikiri kuwa Mafarisayo ambao Mimi nawaongelea ni “wazee” katika dini? Je, si nyinyi ni wawakilishi wa Mafarisayo wa kuendelea mbele zaidi wa enzi ya sasa? Je, unafikiri kwamba wale watu Ninaowataja wanaoniangalia Mimi kwa makini dhidi ya Biblia wanarejelea tu wale wataalamu wa Biblia wa nyanja za kidini? Je, unadhani kwamba Ninapozungumza juu ya wale ambao kwa mara nyingine wanamtundika Mungu msalabani Nazungumzia viongozi wa jamii za kidini? Je, si nyinyi ni wahusika bora kabisa ambao mnaigiza wajibu huu? Je, unafikiri kwamba katika maneno yote Ninayoyanena kurudisha pigo dhidi ya dhana za watu ni mzaha kwa wachungaji na wazee wa dini? Si nyinyi pia mmeshiriki katika mambo haya yote? Je, mnafikiri kuwa mna dhana chache tu? Ni kwamba tu nyote mmejifunza kuwa mahiri sana sasa. Hamzungumzii mambo ambayo hamyafahamu ama kusaliti hisia zenu kuyahusu, lakini mioyo yenu ya heshima na mioyo yenu ya utii haipo tu. Kama mnavyoona, kusoma, kuzingatia, na kusubiri ni matendo yenu makuu ya leo. Mmejifunza kuwa mahiri mno. Je! mnajua, hata hivyo, kwamba hii ni aina yenu ya saikolojia ya ujanja? Je, mnafikiri kuwa wakati wa mahiri kwa upande wenu utawasaidia kuepuka kuadibiwa kwa milele? Mmejifunza kuwa wenye “busara” mno! Na baadhi ya watu huniuliza Mimi mambo kama: “Siku moja, wakati watu wa kidini huniuliza, nini, ‘Mbona Mungu wako hajatenda muujiza hata mmoja?’ Ninafaa kuelezea vipi?” Sasa, siyo tu kwamba watu wa dini watauliza mambo kama hayo. Badala yake, ni kwamba huielewi kazi ya leo, na una dhana nyingi mno. Je, bado hujui ni nani Ninayemrejelea Ninapotaja maafisa wa kidini? Unajua Ninawaelezea nani Biblia? Je, hujui ni kwa nani Ninazungumzia wakati Ninapoeleza kwa mifano hatua tatu za kazi? Je, Singesema vitu hivi, mngeridhishwa kwa urahisi hivyo? Je, mngenyenyekea kwa urahisi hivyo? Je, ni rahisi kwenu kushusha hizo dhana za zamani? Hasa wale “watu halisi” ambao hawajawahi kumtii yeyote–je, wangeweza kutii kwa urahisi sana? Najua kwamba ingawa mna daraja ya chini ya ubinadamu, mna ubora duni sana wa tabia, mna akili ambazo hazijakua sana, na hamna historia ndefu za kumwamini Mungu, kwa kweli mna dhana nyingi kabisa, na asili yenu ya kawaida ni ya kutomnyenyekea yeyote kwa wepesi. Leo, hata hivyo, mnaweza kunyenyekea kwa sababu mnalazimishwa na hamjiwezi; Ninyi ni chui-milia katika kizimba cha chuma, bila uwezo wa kutumia ujuzi wenu. Ingekuwa vigumu kuruka hata kama mngekuwa na mabawa. Ingawa hamjapewa baraka, mnataka kufuata unyounyo. Hata hivyo, hii si roho yenu ya “mtu mzuri”, ila ni kwamba mmeangushwa kabisa, na mnataka kuchanganyikiwa. Ni kwamba kazi yote hii imewaangusha kabisa. Ikiwa kungekuwa na chochote ambacho mngeweza kufikia, hamngekuwa watiifu kama mlivyo leo, kwa sababu awali, nyote mlikuwa punda mwitu nyikani. Hivyo kinachosemwa leo hakielekezwi tu kwa watu wa dini na madhehebu mbalimbali, na siyo kurudisha pigo dhidi ya dhana zao; badala yake ni kurudisha pigo dhidi ya dhana zenu.
Hukumu ya haki imeanza. Je, Mungu bado atatumikia kama sadaka ya dhambi kwa watu? Je, Mungu atachukua nafasi ya daktari mkuu kwa watu tena? Je, Mungu hana mamlaka zaidi ya hivi? Kundi la watu tayari limefanywa kamilifu, na tayari wamenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi. Je, Yeye bado atawafukuza pepo na kuwaponya wagonjwa? Si hili ni jambo la kale? Je, ushuhuda utawezekana kwa kwendelea jinsi hii? Mungu ametundikwa msalabani mara moja, hivyo Atasulubishwa milele? Baada ya kuwafukuza pepo mara moja, Atawafukuza milele? Je, si hili ni sawa na udhalilishaji? Ni wakati tu hatua hii ya kazi inapokuwa juu zaidi kuliko ile ya awali ndipo enzi husonga mbele. Kisha siku za mwisho zitafikiwa, na wakati utakuja ambapo enzi itahitimishwa. Watu wanaofuatilia ukweli kwa hiyo wanapaswa kuzingatia kuwa dhahiri juu ya maono. Huu ndio msingi. Kila wakati Ninapofanya ushirika nanyi kuhusu maono, daima Mimi huona vigubiko vya jicho vya baadhi ya watu vikinyong’onyea na wakianza kushikwa na usingizi, bila kutaka kusikiliza. Wengine huuliza: “Ni kwa nini wewe husikilizi?” Yeye husema, “Hili halisaidii maisha yangu au kuingia kwangu katika hali halisi. Tunachotaka ni njia za matendo.” Wakati Mimi siongei juu ya njia za matendo, na Ninaongea juu ya kazi, anasema, “Punde unapoongea juu ya kazi mimi huanza kushikwa na usingizi.” Sasa Ninaanza kuzungumza juu ya njia za matendo, na anaanza kuchukua muhtasari. Ninaanza tena kuzungumza juu ya kazi hiyo, na anarejelea kutosikiliza. Je, mnajua ni nini mnachopaswa kujiandaa nacho? Jambo moja ni maono juu ya kazi, na jambo jingine ni matendo yako. Lazima ufahamu mambo yote mawili. Kama huna maono katika jitihada zako za kufanya maendeleo katika maisha, basi huna msingi. Kama una njia za matendo tu na huna maono hata kidogo, na huna ufahamu wowote wa kazi ya mpango mzima wa usimamizi, basi wewe ni bure. Lazima uelewe ukweli wa kipengele cha njozi, na kwa ukweli kuhusu matendo, unahitaji kupata njia mwafaka za kutenda mara unapozielewa; unahitaji kutenda kulingana na maneno, na uingie kulingana na hali zako. Maono ndiyo msingi, na usipozingatia hili, hutaweza kufuata hadi mwisho. Unapopitia njia hii, ama utapotea au kuanguka chini na kushindwa. Hakutakuwa na njia ya kufanikiwa! Watu ambao hawana maono makubwa kama msingi wao wanaweza tu kushindwa na si kufanikiwa. Huwezi kusimama imara! Je, unajua kuamini katika Mungu ni nini? Je, unajua kumfuata Mungu ni nini? Bila maono, ni njia gani ungeitembea? Katika kazi ya leo, kama huna maono hutaweza kufanywa mkamilifu kamwe. Unaamini katika nani? Kwa nini unamwamini Yeye? Mbona unamfuata Yeye? Je, unaamini kama aina ya mchezo? Je, unashughulikia maisha yako kama aina ya mtu anayechezewa? Mungu wa leo ndiye maono makubwa zaidi. Je, ni kiasi gani Chake unachokijua? Je, ni kiasi gani Chake ambacho umekiona? Je, baada ya kumwona Mungu wa leo, msingi wa imani yako katika Mungu u salama? Je, unafikiri kwamba mradi unafuata katika njia hii iliyovurugika, utapata wokovu? Unafikiri unaweza kuvua samaki katika maji yenye tope? Je, ni rahisi hivyo? Je, ni maoni mangapi yako kuhusu kile ambacho Mungu wa leo anasema umeweka chini? Je, una maono ya Mungu wa leo? Ufahamu wako wa Mungu wa leo umesimamia wapi? Daima wewe huamini kuwa kwa kufuata unaweza kumpata Yeye, kwamba kwa kumuona Yeye unaweza kumpata,[a] na kwamba hakuna yeyote anayeweza kukukwepa. Usifikiri kwamba kumfuata Mungu ni rahisi sana. Cha muhimu ni kwamba ni lazima umjue Yeye, lazima uijue kazi Yake, na lazima uwe na nia ya kuvumilia shida kwa ajili Yake, uwe na nia ya kutoa maisha yako kwa ajili Yake, na uwe na nia ya kukamilishwa na Yeye. Haya ndiyo maono ambayo unapaswa kuwa nayo. Haitafaidi kama wewe daima unafikiria kufurahia neema. Usifikiri kwamba Mungu yupo tu kwa ajili ya starehe za watu, na kukirimu neema kwa watu. Wewe ulifikiri vibaya! Kama mtu hawezi kuhatarisha maisha yake ili kufuata, ama mtu hawezi kuacha kila mali ya dunia ili kufuata, basi kwa uhalisi hataweza kufuata hadi mwisho. Lazima uwe na maono kama msingi wako. Kama siku ya kupatwa kwako na maafa itakapokuja, unapaswa kufanya nini? Bado ungeweza kufuata? Usiseme kwa wepesi kama utaweza kufuata hadi mwisho. Ni bora kwanza ufungue macho yako wazi kabisa ili uone wakati wa sasa ni upi. Ingawa sasa mnaweza kuwa kama nguzo za hekalu, wakati utakuja ambapo nguzo hizi zote zitatafunwa na funza, na kusababisha hekalu kuanguka, kwa sababu kwa sasa kuna maono mengi sana ambayo mmekosa. Mnachozingatia tu ni dunia zenu wenyewe ndogo, na hamjui njia iliyo ya kutegemewa kabisa, njia iliyo mwafaka zaidi ya kutafuta ni ipi. Hamtilii maanani maono ya kazi ya leo, na hamyashikilii mambo haya mioyoni mwenu. Je, mmefikiria kwamba siku moja Mungu atawaweka katika mahali pasipojulikana? Je, mnaweza kuwazia siku ambayo huenda Nikawapokonya kila kitu, ni kipi kingewakumba? Nguvu yenu siku hiyo ingekuwa vile ilivyo sasa? Je, imani yenu ingejitokeza tena? Katika kumfuata Mungu, lazima myajue maono haya makubwa ambayo ni “Mungu.” Hili ndilo suala muhimu zaidi. Pia, msidhani kwamba katika kuachana na watu wa kidunia ili kuwa watakatifu kwamba nyinyi ni familia ya Mungu. Leo ni Mungu Mwenyewe ambaye anafanya kazi miongoni mwa uumbaji. Ni Mungu aliyekuja miongoni mwa watu kufanya kazi Yake mwenyewe, si kutekeleza kampeni. Miongoni mwenu, hakuna hata wachache ambao wanaweza kujua kwamba kazi ya leo ni kazi ya Mungu aliye mbinguni ambaye amekuwa mwili. Siyo juu ya nyinyi kufanywa watu waliojipambanua wenye vipaji. Badala yake, ni kuwasaidia kujua umuhimu wa maisha ya binadamu, kujua hatima ya binadamu, na kuwasaidia kumjua Mungu na uzima Wake. Unapaswa kujua kwamba wewe ni uumbaji mikononi mwa Muumba. Unachopaswa kufahamu, unachopaswa kufanya, na unavyopaswa kumfuata Mungu—je, huu si ni ukweli unaopaswa kuuelewa? Je, haya si ni maono ambayo unapaswa kuyaona?
Wakati ambapo mtu ana maono ana msingi. Unapotenda kwa msingi wa kanuni hii, itakuwa rahisi zaidi kuingia ndani. Kwa njia hii hutakuwa na wasiwasi juu ya msingi wa kuingia ndani, na itakuwa rahisi sana kwako kuingia ndani. Kipengele hiki cha kuyaelewa maono, cha kuielewa kazi ni muhimu. Lazima muwe mmejiandaa na kipengele hiki. Kama hujajiandaa na kipengele hiki cha ukweli, na wewe huongea tu juu ya njia za matendo, hii ni kasoro kubwa. Nimegundua kwamba wengi wenu hamsisitizi kipengele hiki, na wakati unaposikiliza kipengele hiki cha ukweli ni kama tu kusikiliza maneno ya mafundisho. Siku moja huenda ukapoteza. Kuna baadhi ya maneno sasa ambayo huyafahamu na hujapata maarifa; kwa hiyo unapaswa kutafuta kwa uvumilivu, na siku itakuja utakapoelewa. Jiandae kidogo kidogo. Hata kama unaelewa mafundisho machache tu ya kiroho, ni bora kuliko kutoyazingatia. Ni bora kuliko kutoelewa mafundisho yoyote kamwe. Haya yote ni ya kusaidia kwa kuingia kwako, na yataondoa mashaka hayo yako. Ni bora kuliko kujazwa kwako na dhana. Ni bora zaidi kuwa na maono haya kama msingi. Bila kuwa na wasiwasi kamwe, inawezekana kuingia ndani kwa mikogo na majivuno. Kwa nini kujisumbua daima ukifuata kwa kukanganyikiwa kwa njia ya shaka? Je, hiyo si ni kama kuziba masikio yako wakati unaiba kengele? Ni jambo zuri kama nini kuingia katika ufalme kwa mikogo na majivuno! Kwa nini ujawe wasiwasi? Je, si huku hasa kungekuwa ni kupitia mateso? Unapokuwa na ufahamu wa kazi ya Yehova, wa kazi ya Yesu, na wa hatua hii ya kazi, basi utakuwa na msingi. Sasa unaweza kufikiri kwamba ni rahisi sana. Baadhi ya watu husema, “Wakati Roho Mtakatifu anapoanza kazi hii kubwa, nitakuwa na maneno yote. Ukweli kwamba kwa kweli sielewi sasa ni kwa sababu Roho Mtakatifu hajanipatia nuru sana.” Si rahisi sana; sio kwamba huko tayari kuikubali sasa, na kisha wakati utakapowadia utaitumia kwa ustadi. Si lazima iwe hivyo! Unaamini kuwa sasa umejiandaa vizuri sana, na kwamba haingekuwa shida kuwajibu wale watu wa kidini na wanadhaharia wakuu zaidi, na hata kuwakanusha. Je, ungeweza kweli kufanya hivyo? Je, ni ufahamu upi unaoweza kuuzungumzia na huo uzoefu wako duni tu? Kuwa umejiandaa na ukweli, kupigana vita ya ukweli, na kutoa ushuhuda kwa jina la Mungu si kile unachofikiri ndicho–kwamba mradi Mungu yuko kazini yote yatakamilishwa. Wakati huo labda utatatizwa na swali fulani, na utafadhaishwa. Cha muhimu ni kama uko dhahiri kuhusu hatua hii ya kazi au la, na ni kiasi gani unaielewa. Ikiwa huwezi kuyashinda majeshi ya adui, na wala kuyashinda majeshi ya kidini, basi si wewe ungekuwa bure? Kama umepata uzoefu wa kazi ya leo, ukaiona kwa macho yako mwenyewe na kuisikia kwa masikio yako mwenyewe, lakini mwishowe unashindwa kushuhudia, bado unathubutu kuendelea kuishi? Ungeweza kukabiliana na nani? Usifikiri kwa kawaida sana sasa. Kazi baadaye haitakuwa rahisi kama unavyofikiri itakuwa. Kupigana vita vya ukweli si rahisi au kawaida sana. Sasa unahitaji kujiandaa. Usipokuwa umejiandaa kwa ukweli sasa, wakati utakapowadia na Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa njia ya mwujiza, basi utakuwa umechanganyikiwa.

Jumatano, 25 Septemba 2019

Sura ya 8 Miisho ya Aina Mbalimbali za Watu na Ahadi ya Mungu kwa Mwanadamu

Sura ya 8 Miisho ya Aina Mbalimbali za Watu na Ahadi ya Mungu kwa Mwanadamu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi Yangu inadumu kwa miaka elfu sita tu, na Mimi niliahidi kwamba udhibiti wa yule mwovu juu ya wanadamu wote utakuwa pia si zaidi ya miaka elfu sita. Na kwa hivyo, wakati umeisha. Nami wala Sitaendelea wala kuchelewa tena: Katika siku za mwisho Nitamshinda Shetani, nami Nitaumiliki tena utukufu Wangu wote, na kurudisha nafsi zile zote zilizo Zangu duniani ili nyoyo hizi za dhiki ziweze kutoroka kutoka bahari ya mateso, na hivyo Nitakuwa nimetimiza kazi Yangu nzima duniani. Kutoka siku hii na kuendelea, kamwe Sitawahi kuwa mwili duniani, na kamwe Roho Wangu wa kudhibiti yote Hatafanya kazi tena duniani. Lakini Nitafanya jambo moja duniani: Nitamfanya tena mwanadamu, mwanadamu aliye mtakatifu, na aliye mji Wangu mwaminifu duniani. Lakini ujue kwamba Sitaiangamiza dunia nzima, wala kuangamiza ubinadamu mzima. Nitahifadhi theluthi moja iliyobaki—theluthi moja inayonipenda na imeshindwa kabisa na Mimi, na Nitaifanya theluthi hii iwe yenye kuzaa matunda na kuongezeka duniani kama Israeli walivyofanya chini ya sheria, kuwalisha kwa kondoo wengi mno na mifugo, na utajiri wote wa dunia. Mwanadamu huyu atabaki na Mimi milele, hata hivyo si mwanadamu mchafu wa kusikitisha wa leo, lakini mwanadamu ambaye ni mkusanyiko wa wale wote ambao wamepatwa na Mimi. Mwanadamu wa aina hii hataharibiwa, kusumbuliwa, au kuzungukwa na Shetani, na atakuwa mwanadamu wa pekee anayepatikana duniani baada ya ushindi Wangu juu ya Shetani. Ni wanadamu ambao leo wameshindwa na Mimi na wamepata ahadi Yangu. Na hivyo, wanadamu ambao wameshindwa katika siku za mwisho pia ndio watakaosamehewa na kupata baraka Zangu za milele. Huu utakuwa ushahidi wa pekee wa ushindi Wangu dhidi ya Shetani, na nyara za pekee za vita Vyangu na Shetani. Hizi nyara za vita zimeokolewa nami kutoka utawala wa Shetani, na ni thibitisho la pekee na matunda ya mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita.
kutoka katika “Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wanaomfuata Mungu kiukweli wana uwezo wa kuhimili majaribu ya kazi yao, ilhali wale wasiomfuata hawawezi kuhimili majaribu yoyote ya Mungu. Karibuni au baadaye watatimuliwa, huku washindi wakisalia kwenye ufalme. Mwanadamu amtafute au asimtafute Mungu kwa ukweli itapimwa kulingana na kazi yake, yaani, kupitia kwa majaribu ya Mungu na hayahusiani na uamuzi wa mwanadamu mwenyewe. Mungu hamkatai mtu yeyote kwa wazo la ghafla; yote ambayo Yeye hufanya yanaweza kumshawishi binadamu kikamilifuHafanyi lolote ambalo halionekani kwa mwanadamu ama kazi yoyote ambayo haiwezi kumthibitishia mwanadamu. Iwapo imani ya mwanadamu ni ya ukweli au sio huthibitishwa na ushahidi, na haiwezi kuamuliwa na mwanadamu. Kwamba “ngano haiwezi kufanywa magugu, na magugu hayawezi kufanywa ngano” ni jambo lililo wazi. Wale wote wanaompenda Mungu kwa dhati hatimaye watasalia katika ufalme, na Mungu hatamtesa yeyote ambaye Yeye anampenda kwa kweli. Kwa misingi ya kazi zao na shuhuda zao tofauti, washindi katika ufalme watatumika kama makuhani au wafuasi, na wale wote watakaoshinda taabu watakuwa mwili wa makuhani katika ufalme. Baraza la makuhani litaundwa wakati kazi ya injili ulimwenguni kote itafikia kikomo. Wakati huo ukitimia, yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu yatakuwa jukumu lake ndani ya ufalme wa Mungu, na kuishi kwake pamoja na Mungu katika ufalme. Katika baraza la makuhani, patakuwepo makuhani wakuu na makuhani, na watakaosalia watakuwa wana na watu wa Mungu. Haya yote huamuliwa na ushuhuda wao kwa Mungu wakati wa majaribu; sio nyadhifa zinazopeanwa kwa wazo la ghafla. Wakati hadhi ya mwanadamu itakuwa imeianzishwa, kazi ya Mungu itamalizika, kwa kuwa kila mojawapo imewekwa kulingana na aina yake na kurejeshwa katika hali yake halisia, na hii ndiyo alama ya ukamilisho wa kazi ya Mungu, na haya ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi ya Mungu na matendo ya mwanadamu, na ndiko kubainika kwa yale maono ya kazi ya Mungu na ushirikiano wa mwanadamu. Mwishowe, mwanadamu atapata pumziko katika ufalme wa Mungu, na, Mungu pia, atarejea kwenye makazi Yake kupumzika. Haya ndiyo yatakayokuwa matokeo ya miaka 6,000 ya ushirikiano wa mwisho kati ya Mungu na mwanadamu.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.
kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale ambao wanafikiri tu juu ya miili yao na wanapenda starehe, wale ambao imani yao ni tata, wale wanaoshiriki katika tiba ya uchawi na usihiri, wale ambao ni wazinzi, na waliovaa matambara na wasio sawa, wale wanaoiba dhabihu kwa Yehova na mali Yake, wale ambao wanapenda rushwa, wale wanaoota kwa uzembe kwenda mbinguni, wale ambao wana kiburi na wenye majivuno, na wanajitahidi tu kwa ajili ya umaarufu wa kibinafsi na utajiri, wale ambao hueneza maneno yasiyofaa, wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe, wale ambao hawafanyi lolote ila kumhukumu na kumkashifu Mungu Mwenyewe, wale wanaokusanyika na wengine na kujaribu kujitegemea, wale wanaojitukuza juu zaidi kuliko Mungu, wale wanaume na wanawake wapuuzi, na wanaume na wanawake wenye umri wa kati na wazee ambao wametegwa katika uovu, wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu wa kibinafsi na utajiri na kufuata hadhi ya kibinafsi kati ya watu wengine, wale watu wasio na toba ambao wamenaswa katika dhambi—je, si wao wote hawawezi kuokolewa? Ufisadi, hali ya kuwa mwenye dhambi, tiba ya uchawi, usihiri, mwenendo chafu, na maneno mafidhuli hufanya fujo kati yenu, maneno ya kweli na uhai hukanyagwa kati yenu, na lugha takatifu inanajisiwa kati yenu. Ninyi Mataifa, mliojawa na uchafu na kutotii! Mtaishia wapi? Je, wale wanaopenda mwili, ambao wanafanya matendo maovu ya mwili, na ambao wametegwa katika uasherati wanawezaje kuthubutu kuendelea kuishi? Je, hujui kwamba watu kama nyinyi ni mabuu ambao hawawezi kuokolewa? Ni nini kinachowapa sifa inayostahili ya kudai hili na lile? Hadi leo, hakujakuwa na mabadiliko hata kidogo kwa wale ambao hawapendi ukweli na wanapenda tu mwili—hivyo watu hawa wanaweza kuokolewaje? Hata leo, wale ambao hawapendi njia ya uzima, ambao hawamtukuzi Mungu na kumshuhudia Yeye, ambao hupanga njama kwa ajili ya hali yao wenyewe, ambao wanajisifu wenyewe sana—je, wao bado si sawa? Iko wapi thamani ya kuwaokoa? Kama mnaweza kuokolewa hakutegemei jinsi ulivyo na sifa za kustahili, au ni umefanya kazi kwa miaka ngapi, sembuse idadi ya sifa ambazo unazo. Kunategemea na ikiwa kumekuwa na matokeo yoyote katika kufuatilia kwako. Unapaswa kujua kwamba wale ambao wameokolewa ni miti ambayo huzaa matunda, si miti ambayo ina majani ya kustawi sana na maua mengi lakini haizai matunda. Hata kama umetumia miaka mingi kuzurura mitaani, ina maana gani? Ushahidi wako uko wapi? Uchaji wako kwa Mungu ni mdogo sana kuliko upendo wako wa wewe na hamu zako za tamaa—mtu kama huyu si mpotovu? Ungewezaje kuwa mfano na kielelezo cha wokovu? Asili yako haibadiliki, wewe ni muasi sana, huwezi kuokolewa! Watu kama hao hawataondolewa? Je, wakati ambapo kazi Yangu inamalizika si wakati ambapo siku yako ya mwisho itakuja? Nimefanya kazi nyingi sana na kusema maneno mengi kati yenu—ni kiasi gani cha hayo kilichoingia ndani ya masikio yenu? Ni kiasi gani cha hayo ambacho mmewahi kutii? Wakati kazi Yangu itaisha ndio pia utakuwa wakati unapoacha kunipinga na kusimama dhidi Yangu. Wakati wa kazi Yangu, daima nyinyi hutenda dhidi Yangu, hamyatii maneno Yangu kamwe. Ninafanya kazi Yangu, na wewe unafanya kazi yako mwenyewe, unatengeneza ufalme wako mdogo mwenyewe—nyinyi kundi la mbweha na mbwa, kila kitu mnachofanya ni dhidi Yangu! Nyinyi daima mnajaribu kuwaleta wale wanaowapenda tu katika kumbatio lenu—uko wapi uchaji wenu? Kila kitu mnachofanya ni kidanganyifu! Hamna utii au uchaji, kila kitu mnachofanya ni udanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hao wanaweza kuokolewa? Wanaume zinzi, wa kiasherati daima hutaka kuwavuta kwao wale makahaba wabembe kwa ajili ya raha yao wenyewe. Sitawaokoa mapepo wenye uasherati kama hao, Nawachukia ninyi mapepo wachafu, uasherati wenu na kupiga bemba kwenu kumewatumbukiza kuzimu—mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi pepo mchafu na roho wabaya ni waovu sana! Nyinyi ni wa kuchukiza! Takataka kama nyinyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi bado wanaweza kuokolewa? Ukweli huu, njia hii, na maisha haya hayapendezi kwenu; mnavutiwa na dhambi, pesa, hadhi, umaarufu na faida, ridhaa za mwili, maumbile mazuri ya wanaume na ubembe wa wanawake. Ni nini kinachowapa sifa zinazostahili kuingia katika ufalme Wangu? Taswira yenu ni kubwa zaidi kuliko Mungu, hali yenu ni ya juu zaidi kuliko Mungu, kutosema chochote cha sifa yenu kati ya wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hamjabadilika kuwa malaika mkuu? Wakati mwisho wa watu unafichuliwa, ambao pia ni wakati kazi ya wokovu inafikia kikomo, wengi wenu mtakuwa maiti ya maiti ambayo haiwezi kuokolewa na lazima muondolewe. Wakati wa kazi ya wokovu, Mimi ni mwenye huruma na mwema kwa watu wote. Wakati kazi inamalizika, mwisho wa watu wa aina tofauti utafichuliwa, na wakati huo Sitakuwa mpole na mwema, kwa maana mwisho wa watu utakuwa umefichuliwa, kila mmoja atakuwa ameainishwa kulingana na aina, na hakutakuwa na maana katika kufanya kazi yoyote zaidi ya wokovu. Ni hasa kwa sababu enzi ya wokovu itakuwa imepita; kwa kuwa itakuwa imepita, haitarudi tena.
kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:
Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.
kutoka katika “Sura ya 26” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawakumbuka, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kuzitafuta ahadi mlizofanyiwa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.
kutoka katika “Sura ya 19” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Inuka na ushirikiane na Mimi! Hakika Sitawatendea vibaya watu wanaotumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu. Wale wanaojitoa Kwangu kwa dhati, Nitawapa baraka Zangu zote. Jitoe kabisa Kwangu! Kile unachokula, kile unachovaa, na mustakabali wako yote yako mikononi Mwangu, Nitayapanga vizuri kabisa, kwa ajili ya furaha yako isiyokuwa na mwisho, isiyoisha, kwa maana Nimesema, “Kwa wale wanaotumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu, hakika Nitakubariki kwa wingi.” Baraka zote huja kwa kila mtu anayetumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu.
kutoka katika “Sura ya 70” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Kile ambacho Nimewaandalia nyinyi, yaani, hazina nadra za thamani kutoka duniani kote, zote mtapewa nyinyi. Nyinyi hamuwezi kufahamu kuhusu wala hamuwezi kufikiri yote haya kwa sasa, na hakuna mwanadamu aliyefurahia hili hapo kabla. Wakati baraka hizi zitawajia, nyinyi mtajawa na furaha bila kikomo, lakini msisahau kwamba hizi zote ni nguvu Zangu, matendo Yangu, haki Yangu na hata zaidi, uadhama Wangu. (Nitawapa neema wale ambao Nitaamua kuwapa neema, na Nitawahurumia wale ambao Nitaamua kuwahurumia). Wakati huo, ninyi hamtakuwa na wazazi, wala hakutakuwa na mahusiano ya damu. Nyinyi nyote ni watu ambao Nawapenda, wana Wangu wapendwa. Hakuna mtu atakayethubutu kuwakandamiza nyinyi kutoka wakati huo na kuendelea. Utakuwa wakati wenu wa kukua na kuwa watu wazima, na wakati wenu wa kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma! Ni nani anayethubutu kuwazuia Wana wangu wapendwa? Ni nani anayethubutu kuwashambulia wana Wangu wapendwa? Wote watawaheshimu wana Wangu wapendwa kwa sababu Baba ametukuzwa. Vitu vyote ambavyo hakuna mtu angeweza kufikiria daima vitaonekana mbele ya macho yenu. Vitakuwa havina kikomo, wasivyoisha, visivyo na mwisho. Kabla ya muda mrefu, nyinyi hakika hamtahitaji tena kuunguzwa na jua na kuvumilia joto linalotesa. Wala hamtalazimika kuteseka na baridi, wala mvua, theluji au upepo havitawafikia. Hii ni kwa sababu Nawapenda, na yote itakuwa ni dunia ya upendo Wangu. Nitawapa kila kitu mnachotaka, nami Nitawaandaa kwa ajili ya kila kitu ambacho mnahitaji. Nani anathubutu kusema kuwa Mimi si mwenye haki? Nitakuua mara moja, kwa sababu Nimewaambia kabla ya kuwa ghadhabu Yangu (dhidi ya waovu) itaendelea milele, nami Sitaachilia hata kidogo. Hata hivyo, upendo Wangu (kwa wana Wangu wapendwa) pia utaendelea milele; Sitauzuia hata kidogo.
kutoka katika “Sura ya 84” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri. Itakuwa mwanzo wa maisha ya mwanadamu na Mungu duniani. Nguzo ya maisha mema kama haya ni lazima iwe hivyo, hivi kwamba baada ya mwanadamu kutakaswa na kushindwa, anajiwasilisha mbele za Muumba. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu kabla ya wanadamu kuingia katika hatima ya ajabu. Maisha kama haya ni maisha ya baadaye ya mwanadamu duniani, ni maisha yanayopendeza zaidi duniani, aina ya maisha ambayo mwanadamu ametamania, aina ambayo mwanadamu hajawahi kamwe kutimiza katika historia ya ulimwengu. Ni matukio ya mwisho ya miaka 6,000 ya kazi ya usimamizi, na ndicho wanadamu wanatamani sana, na pia ni ahadi ya Mungu kwa mwanadamu. Lakini ahadi hii haiwezi timika mara moja: Mwanadamu ataingia katika hatima ya mbeleni punde tu kazi ya siku za mwisho zitakapokuwa zimemalizika na yeye amekwisha kushindwa kikamilifu, yaani, punde tu Shetani atakapokuwa ameshindwa kabisa. Mwanadamu atakuwa hana asili ya kutenda dhambi baada ya kusafishwa, kwa sababu Mungu atakuwa amemshinda Shetani, ambayo ina maana kuwa hakutakuwepo na kuvamiwa na vikosi vya uhasama, na hakuna vikosi vya uhasama ambavyo vinaweza kushambulia mwili wa mwanadamu. Na kwa hivyo mwanadamu atakuwa huru, na mtakatifu—yeye atakuwa ameingia ahera.
kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.
kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni wale tu ambao wanampenda Mungu wanaweza kumshuhudia Mungu, ndio tu mashahidi wa Mungu, ndio tu wamebarikiwa na Mungu, na ndio tu wanaweza kupokea ahadi za Mungu. Wanaompenda Mungu ni wandani wa Mungu, ndio watu ambao wamependwa na Mungu, na wanaweza kufurahia baraka pamoja na Mungu. Ni watu hawa tu ambao wataishi milele, na ni wao tu wataishi milele katika utunzaji na ulinzi wa Mungu. Mungu yuko kwa ajili ya kupendwa na watu, na anastahili upendo wa watu wote, lakini si watu wote ambao wanaweza kumpenda Mungu, na si watu wote wanaweza kumshuhudia Mungu na kushiriki mamlaka pamoja na Mungu. Kwa sababu wanaweza kumshuhudia Mungu, na kutoa juhudi zao zote kwa kazi ya Mungu, wanaompenda Mungu kwa kweli wanaweza kutembea mahala popote chini ya mbingu bila ya mtu yeyote kujaribu kuwapinga, na wanaweza kushika mamlaka na kutawala watu wote wa Mungu. Hawa watu wanakusanyika pamoja kutoka pembe zote za dunia, wanazungumza lugha tofauti na ni wa rangi tofauti, lakini kuishi kwao kuna maana sawa, wote wana moyo unaompenda Mungu, wote wana ushuhuda sawa, na wana maazimio sawa, na mapenzi sawa. Wale ambao wanampenda Mungu wanaweza kutembea ulimwenguni kote wakiwa huru, wanaomshuhudia Mungu wanaweza kusafiri duniani kote. Watu hawa wamependwa wa Mungu, wamebarikiwa na Mungu, na wataishi milele katika mwangaza Wake.
kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu. Binadamu wa aina hii tu ndiye anayestahili kurithi baraka hizi alizofadhiliwa na Mungu:
1. Kupokea upendo mzima wa Mungu.
2. Kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu katika kila kitu.
3. Kupokea mwongozo wa Mungu, kuishi chini ya mwangaza wa Mungu, na kupatiwa nuru na Mungu.
4. Kuishi kwa kudhihirisha taswira inayopendwa na Mungu hapa ulimwenguni; kumpenda Mungu kwa kweli kama vile Petro alivyofanya, kusulubishwa kwa sababu ya Mungu na kustahili kufa kwa kuufidia upendo wa Mungu; kuwa na utukufu sawa na Petro.
5. Kupendwa, kuheshimiwa, na kuvutiwa na wote ulimwenguni.
6. Kushinda utumwa wote wa kifo na Kuzimu, kutoipatia fursa yoyote kazi ya Shetani, kumilikiwa na Mungu, kuishi ndani ya roho safi na changamfu, na kutokuwa na hisia zozote za uchovu.
7. Kuwa na hisia isiyoelezeka ya msisimko na furaha siku zote katika maisha yako yote, ni kana kwamba ameona kuja kwa siku ya utukufu wa Mungu.
8. Kupokea utukufu pamoja na Mungu, na kuwa na sura inayofanana na watakatifu wapendwa wa Mungu.
9. Kuwa kile ambacho Mungu anapenda zaidi ulimwenguni, yaani, mwana mpendwa wa Mungu.
10. Kubadilisha maumbile na kupaa juu pamoja na Baba kwenye mbingu ya tatu, na kuuzidi mwili.
Wale tu wanaoweza kurithi baraka za Mungu ni wale waliokamilishwa na Mungu na kupatwa na Mungu. Je, umefaidi chochote? Mungu amekukamilisha hadi kiwango gani? Mungu hamkamilishi binadamu bila mpango. Kunayo masharti na matokeo dhahiri yanayoweza kuonekana na binadamu. Si jinsi mwanadamu anavyoamini, kwamba mradi tu awe na imani katika Mungu, anaweza kukamilishwa na kupatwa na Mungu, na anaweza kupokea hapa ulimwenguni baraka na urithi wa Mungu. Mambo kama haya ni magumu mno, na hata zaidi inapohusu kubadilika kwa taratibu. Kwa sasa, kile ambacho mnafaa kutafuta kimsingi ni kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, na kukamilishwa na Mungu kupitia kwa watu wote, mambo yote na vitu vyote ambavyo mnakumbwa navyo, ili mambo zaidi ya kile Mungu Alicho yatashirikishwa ndani yenu. Lazima kwanza mpokee urithi wa Mungu ulimwenguni kabla ya kustahili kurithi baraka nyingi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu. Mambo yote haya ndiyo ambayo mnafaa kutafuta na ambayo kwanza mnafaa kuelewa.
kutoka katika “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu

Ijumaa, 12 Julai 2019

Sura ya 35. Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro

Sura ya 35. Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro

Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi zaidi na muhimu zaidi ya utendaji. Hili ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu hupata matokeo bora zaidi. Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu hasa kunamaanisha kutafuta ukweli, kutafuta nia ya Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka kwa maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini na hata alikuwa anazingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alikuwa anazingatia kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na kuelewa asili potovu ya mwanadamu na dosari halisi za mwanadamu, akitimiza kila hali yote ya madai anayotaka Mungu kutoka kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. Alikuwa na utendaji mwingi sahihi ndani ya maneno ya Mungu; hili linalingana sana na mapenzi ya Mungu, na ni ushirikiano bora zaidi wa mwanadamu katika uzoefu wake wa kazi ya Mungu. Wakati ambapo alipitia mamia ya majaribio kutoka kwa Mungu, alijichunguza kabisa dhidi ya kila neno la hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kila neno la ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, na kila neno la madai Yake kwa mwanadamu, na akajaribu kufikia maana ya maneno ya Mungu. Alijaribu kwa bidii kutafakari na kukariri kila neno ambalo Yesu alimwambia, na alitimiza matokeo mazuri sana. Kupitia njia hii ya utendaji aliweza kutimiza kujifahamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na hakuja tu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu, lakini pia alikuja kuelewa kiini cha mwanadamu, asili ya mwanadamu, na aina mbalimbali za dosari ambazo mwanadamu anazo—huku ni kujifahamu kwa kweli. Kutoka kwa maneno ya Mungu, hakutimiza tu kujifahamu kwa kweli, lakini kutokana na mambo yaliyoonyeshwa katika neno la Mungu—tabia ya Mungu yenye haki, kile Anacho na alicho, mapenzi ya Mungu kwa kazi Yake, mahitaji Yake kwa wanadamu—kutoka kwa maneno haya alikuja kumjua Mungu kabisa. Alikuja kujua tabia ya Mungu, na asili yake; alikuja kujua na kuelewa kile Mungu anacho na Alicho, uzuri wa Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu. Hata ingawa wakati huo Mungu hakuzungumza sana kama Anavyofanya leo, matunda yalipatikana ndani ya Petro katika hali hizi. Hili lilikuwa jambo adimu na la thamani. Petro alipitia mamia ya majaribio lakini hakuteseka bure. Hakuja kujielewa tu kutokana na maneno na kazi ya Mungu, lakini pia alikuja kumjua Mungu. Pia alizingatia hasa matakwa ya Mungu kwa wanadamu ndani ya maneno Yake, na ni katika hali gani mwanadamu anapaswa kumridhisha Mungu ili kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Alifanya juhudi kubwa katika hali hii na akatimiza uwazi kamili; hili lilikuwa la manufaa sana kwa kuingia kwake mwenyewe. Haijalishi kile ambacho Mungu alizungumzia, maadamu maneno hayo yangeweza kuwa maisha yake na yalikuwa ya ukweli, aliweza kufanikiwa kuyaweka ndani ya moyo wake kuyatafakari mara nyingi na kuyaelewa. Baada ya kuyasikia maneno ya Yesu aliweza kuathiriwa nayo, ambalo linaonyesha kuwa alikuwa akizingatia hasa maneno ya Mungu, na alitimiza matokeo mwishowe kwa kweli. Yaani, aliweza kuyatia maneno ya Mungu katika vitendo kwa uhuru, kutenda kwa usahihi ukweli na kukubaliana na mapenzi ya Mungu, kutenda kikamilifu kwa mujibu wa nia ya Mungu, na kuacha maoni na mawazo yake mwenyewe. Kwa njia hii aliingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Huduma ya Petro ilikubaliana na mapenzi ya Mungu hasa kwa sababu alifanya hili.
Ikiwa mtu anaweza kweli kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu kutokana na mambo na maneno yanayohitajika na Yeye, basi atakuwa mtu aliyekamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yanafaa kabisa kwa mtu huyu, kwamba maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake, anapata ukweli, na anaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili asili ya mwili wake, yaani, msingi wa kuwepo kwake kwa asili, utatikisika na kuanguka. Baada ya mtu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yake anakuwa mtu mpya. Maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake; maono ya kazi ya Mungu, matakwa yake kwa mwanadamu, ufunuo wake kwa mwanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anahitaji mwanadamu kutimiza vinakuwa maisha yake—anaishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, na mtu huyu anageuka kukamilishwa na maneno ya Mungu. Anapitia kuzaliwa upya na anakuwa mtu mpya kupitia maneno Yake. Hii ni njia ambayo Petro aliitumia kuufuatilia ukweli; Ilikuwa njia ya kukamilishwa, kukamilishwa na maneno ya Mungu, na kupata uzima kutoka kwa maneno ya Mungu. Ukweli ulioonyeshwa na maneno ya Mungu ulikuwa maisha yake, na wakati huo tu ndipo alikuwa mtu aliyepata ukweli. Sote tunajua kwamba karibu wakati wa kupaa kwa Yesu, Petro alikuwa na fikira nyingi, kutotii, na udhaifu. Kwa nini yalibadilika kabisa baada ya hilo? Hili lina uhusiano wa moja kwa moja na ufuatiliaji wake wa ukweli. Kuelewa tu mafundisho ya dini hakuna maana; hakuwezi kuleta mabadiliko katika maisha. Kuelewa tu maana halisi ya neno la Mungu si sawa na kuelewa ukweli; yale mambo muhimu ambayo yanaelezwa kwa mifano katika maneno ya Mungu ndiyo ukweli. Kila sentensi ya maneno ya Mungu ina ukweli, lakini watu huenda wasiuelewe. Kwa mfano, neno la Mungu linasema, "Lazima muwe watu waaminifu": Kuna ukweli katika kauli hii. "Lazima muwe watu wanaomtii Mungu, wanaompenda Mungu, na wanaomwabudu Mungu." "Lazima mfanye wajibu wenu vizuri kama wanadamu." Kauli hizi zina ukweli hata zaidi. Kila sentensi ya maneno ya Mungu ina ukweli mwingi, na maneno mengi yanahitajika ili kufafanua kiini cha kila kauli ya ukweli; wakati kiwango hiki kinafikiwa tu ndipo kitafikiriwa kuwa ufahamu wa ukweli. Ikiwa unaelewa tu maana halisi na kuelezea maneno ya Mungu kulingana na maana halisi ya maneno hayo, huu sio ufahamu wa ukweli—huku ni kucheza tu na mafundisho ya dini.
Zamani, wakati maneno ya Mungu hayakuwa maisha ya watu, ilikuwa ni asili ya Shetani iliyotwaa madaraka na kutawala ndani yao. Ni mambo gani maalum yalikuwa ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini lazima ulinde nafasi yako mwenyewe? Kwa nini hisia zako ni kali sana? Kwa nini unapenda mambo hayo dhalimu, na kwa nini unapenda maovu hayo? Asili ya mambo haya ni nini? Yanatoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali mambo haya? Hivi sasa nyote mmeelewa kuwa hili hasa ni kwa sababu ya sumu ya Shetani iliyo ndani ya mambo haya. Kile sumu ya Shetani kilicho kinaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini wanafanya kitu. Watasema: “Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine.” Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida: Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu, na haijalishi wanachofanya, kama ni kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, wanajifanyia tu. Watu wote hudhani kwamba "Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine," Haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya mwanadamu. "Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine," kauli hii ya Shetani ni sumu yake hasa, na inapowekwa moyoni na mwanadamu inakua asili ya mwanadamu. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia kwa kauli hii; inamwakilisha kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya mwanadamu na inakuwa msingi wa kuwepo kwake; wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na hii kwa maelfu ya miaka. Kila kitu ambacho Shetani hufanya ni kwa ajili yake. Anataka kumpita Mungu, kujiondoa kwa Mungu na kushika mamlaka mwenyewe, na kumiliki vitu vyote ambavyo Mungu ameumba; Kwa hivyo, asili ya mwanadamu ni asili ya Shetani. Kwa kweli, wito wa watu wengi unaweza kuwakilisha na kuakisi asili yao. Haijalishi jinsi mwanadamu anavyoificha, katika kila kitu afanyacho na kila kitu asemacho, hawezi kuificha asili yake. Kuna baadhi ya watu ambao huwa hawasemi ukweli kamwe na wanajua sana kujifanya, lakini baada ya wengine kuingiliana nao kwa muda, asili yao ya udanganyifu na wao kutokuwa waaminifu kabisa kutagunduliwa. Muda utafichua yote. Baada ya kuwajua kwa muda, asili yao itagunduliwa. Mwishowe hitimisho litafanywa: Yeye kamwe huwa hasemi neno lolote la ukweli, na yeye ni mdanganyifu. Kauli hii ni ukweli wa asili yake; ni ushahidi na kielezo chake. Kwa hivyo, falsafa yake ya maisha ni kutomwambia yeyote ukweli, na pia kutomwamini mtu yeyote. Je, hili haliwakilishi asili yake? Asili ya mwanadamu ya kishetani ina kiwango kikubwa cha falsafa ndani yake. Wakati mwingine wewe mwenyewe huelewi vizuri, lakini unaishi kwa kutegemea hilo kila wakati. Unafikiri kuwa ni sahihi sana, yenye mantiki sana, na isiyo kosea. Falsafa ya Shetani inageuka kuwa ukweli wa mwanadamu, na watu wanaishi kwa mujibu wa falsafa yake kabisa bila ukinzani hata kidogo. Kwa hivyo, mwanadamu daima na kila mahali hufichua asili ya Shetani katika maisha, na daima huishi kwa falsafa ya shetani. Asili ya Shetani ni maisha ya mwanadamu. Kuhusu asili ni nini, hili linaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa kuifupisha kwa maneno. Katika asili ya mwanadamu kuna kiburi na ufuatiliaji wa kuwa bora zaidi na wa kipekee; kuna pia tamaa ya kutaka faida tu bila kuyajali maisha; kuna hila, uhalifu, na kuwadanganya watu kila upande; na kuna uovu na uchafu visivyovumilika. Huu ni muhtasari wa asili ya mwanadamu. Kwa hivyo, ikiwa unaweza kuja kujua mambo mengi katika asili ya mwanadamu, basi una ufahamu wa asili yako mwenyewe. Ikiwa hujagundua kitu chochote katika asili yako mwenyewe, basi huna ufahamu wowote wa hilo. Petro alitafuta ndani ya usafishaji wa maneno ya Mungu na ndani ya majaribio mbalimbali ambayo Mungu alimtolea ili aje kujijua, kuona kile alichofichua. Mwishowe alipokuja kujifahamu kweli, aligundua mwanadamu ni mpotovu sana, na hana thamani na hastahili kumtumikia Mungu, na kwamba mwanadamu hastahili kuishi mbele za Mungu. Alianguka chini mbele za Mungu. Mwishowe alihisi: "Kumjua Mungu ni jambo la thamani zaidi! Kama singeweza kumjua Mungu, kifo changu kingekuwa cha aibu mno. Nahisi kwamba kumjua Mungu ndilo jambo muhimu sana, la maana sana. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu basi hastahili kuishi—basi hakuna uzima." Wakati uzoefu wa Petro ulikuwa umefikia kiwango hiki, alikuwa na ufahamu kiasi wa asili yake mwenyewe. Aliielewa vizuri kiasi, na ingawa hangeweza kutumia lugha kuielezea vizuri kabisa kulingana na fikira za wanadamu za sasa, alifikia eneo hili. Kwa hivyo, ufuatiliaji wa njia ya uzima ili kukamilishwa na Mungu ni kuelewa zaidi asili ya mtu mwenyewe ndani ya maneno ya Mungu na kuelewa mambo yaliyo ndani ya asili ya mtu. Kuufupisha kwa maneno, kuelewa kabisa maisha ya mtu ya kale—maisha ya asili ya kale ya shetani—huku ni kuweza kutimiza matokeo yaliyohitajika na Mungu. Ikiwa ufahamu wako haujafikia kiwango hiki lakini unasema unajielewa na kwamba umepata uzima, je, huku sio kujisifu tu? Hujijui, na hujui ulicho mbele za Mungu, kama umepata kiwango cha mwanadamu kweli, au ni vitu vingapi vya Shetani ambavyo bado unavyo. Huelewi vizuri wewe ni wa nani na hata hujifahamu—basi unawezaje kuwa na sababu mbele za Mungu? Wakati Petro alikuwa akiufuatilia uzima, katikati ya majaribio yake alizingatia kujielewa na kubadilisha tabia yake. Alijitahidi kumwelewa Mungu, na mwishowe akahisi: "Mwanadamu lazima afuatilie kumfahamu Mungu maishani; kumfahamu Mungu ndilo jambo muhimu sana; ikiwa simjui Mungu basi siwezi kupumzika kwa amani nitakapokufa. Mungu anaponifanya nife baada ya kumjua, nitahisi kwamba ni jambo la kupendeza zaidi, sitalalamika hata kidogo, na maisha yangu yote yatatimizwa."Petro hakuweza kupata ufahamu huu na kufikia kiwango hiki punde baada ya kuanza kumwamini Mungu—alipaswa kupitia majaribio mengi kwanza. Uzoefu wake ulipaswa kufikia kiwango fulani na alipaswa kujifahamu kabisa kabla ya kuweza kuhisi thamani ya kumjua Mungu. Kwa hivyo, njia aliyoishika ilikuwa njia ya uzima na ya kukamilishwa; utendaji wake maalum ulizingatia hali hii hasa.
Je, nyote mnaishika njia gani sasa? Ikiwa hamjafikia ufuatiliaji wa maisha, wa kujifahamu, au kumfahamu Mungu kama Petro, basi hiyo bado si njia ya Petro. Hivi sasa watu wengi wako katika aina hii ya hali: "Ili kupata baraka ni lazima nijitumie kwa ajili ya Mungu na kulipa gharama kwa ajili Yake. Ili kupata baraka ni lazima niache kila kitu kwa ajili ya Mungu; lazima nikamilishe kile ambacho ameniaminia na kutekeleza wajibu wangu vizuri." Hili linatawaliwa na nia ya kubarikiwa; ni kutumika kwa kusudi la kupata thawabu za Mungu, kwa ajili ya kupata taji. mtu wa aina hii hana ukweli ndani ya moyo wake, na hakika anaelewa tu maneno fulani ya mafundisho ya dini ambayo anaringia kila mahali. Njia yake ni njia ya Paulo. Kumwamini Mungu kwa mtu wa aina hii ni kitendo cha kazi ya siku zote, na katika akili yake anahisi kuwa kadri anavyofanya, ndivyo itakavyothibitisha zaidi kuwa ni mwaminifu kwa Mungu, kwamba kadri anavyofanya ndivyo Mungu ataridhika zaidi, na kwamba kadri anavyofanya ndivyo anavyopaswa zaidi kupata taji mbele za Mungu, na hakika atapata baraka kubwa zaidi katika nyumba ya Mungu. Anahisi kwamba kama anaweza kuvumilia mateso, kuhubiri, na kufa kwa ajili ya Kristo, kama anaweza kuyadharau maisha yake mwenyewe, na kama anaweza kukamilisha wajibu wote ambao Mungu alimwaminia nao, basi atakuwa mtu mwenye kubarikiwa zaidi na Mungu, yule anayepata baraka nyingi zaidi, na hakika atapokea taji. Hili ndilo hasa alilowaza Paulo alilofikiri na kile alichofuatilia; hii ndiyo hasa njia ambayo Paulo alitembea, na ilikuwa chini ya uongozi wa mawazo haya ndio Paulo alifanya kazi kumhudumia Mungu. Je, mawazo na madhumuni kama hayo hayatoki kwa asili ya Shetani? Kama tu watu wa dunia, hapa duniani lazima nifuatilie maarifa, na baada ya kupata maarifa tu ndio ninaweza kufanikiwa, kuwa afisa, na kuwa na cheo. Mara baada ya kupata cheo ninaweza kufikia lengo langu na kuifikisha nyumba yangu na biashara kwa viwango fulani. Je, wasioamini wote huwa hawaifuati njia hii? Wale ambao wanatawaliwa na asili hii ya shetani wanaweza tu kuwa kama Paulo baada ya kumwamini Mungu: "Ni lazima niache kila kitu ili nijitumie kwa ajili ya Mungu, lazima niwe mwaminifu mbele za Mungu, na mwishowe nitapokea taji kubwa zaidi na baraka kubwa zaidi." Hii ni sawa na watu wa dunia wanaofuatilia vitu vya dunia, hakuna tofauti kabisa, na wanapaswa kutii asili hiyo. Watu wana asili ya shetani, kwa hiyo ulimwenguni watafuatilia maarifa, hadhi, kujifunza, na mafanikio ya dunia; nyumbani mwa Mungu, watatafuta kujitumia kwa ajili ya Mungu, kuwa waaminifu, na hatimaye watapokea taji na baraka nyingi. Kama watu hawana ukweli baada ya kumwamini Mungu na hawajakuwa na mabadiliko katika tabia yao, basi bila shaka watakuwa kwenye njia hii—huu ni ukweli ambao hakuna mtu anayeweza kuupinga, na ni wenye kupinga kabisa njia ya Petro. Nyote mnaishika njia gani sasa? Ingawa huwezi kupanga kuishika njia ya Paulo, asili yako inakutawala kwa njia hii, na unaelekea upande huo bila kupenda. Ingawa unataka kuishika njia ya Petro, ikiwa hufahamu vizuri jinsi ya kulifanya hilo, basi bado utaishika njia ya Paulo bila kupenda—huu ni ukweli wa hali hiyo.
Kwa hiyo mnawezaje hasa kuishika njia ya Petro? Kama huwezi kubainisha kati ya njia ya Petro na njia ya Paulo, au huzijui kabisa, basi hata ukisema unapaswa kuishika njia ya Petro hayo yatakuwa maneno matupu. Unahitaji kwanza kufahamu katika mawazo yako njia ya Petro ni gani na njia ya Paulo ni gani. Kama kweli unaelewa kwamba njia ya Petro ni njia ya uzima na njia pekee ya kukamilishwa, wakati huo tu ndipo utaweza kujua na kufahamu ukweli na njia maalum za kuishika njia yake. Ikiwa huifahamu njia ya Petro, basi njia unayoishika bila shaka itakuwa ya Paulo kwa sababu hakutakuwa na njia nyingine—hutakuwa na budi. Kama huna ukweli na huna hamu za kupata kitu basi ni vigumu kuishika njia ya Petro. Inaweza kusemekana kwamba Mungu amewafichulia sasa njia ya kuokolewa naye na ya kukamilishwa. Hii ni neema ya Mungu na kutia moyo na ni Yeye anayewaongoza kwenye njia ya Petro. Bila uongozi na kupata nuru kutoka kwa Mungu hakuna ambaye angeweza kuishika njia ya Petro; chaguo la pekee lingekuwa kuelekea kwa njia ya Paulo, kuzifuata nyayo za Paulo kuelekea kwa uharibifu. Wakati huo, Paulo hakuhisi kwamba haikuwa sahihi kutembea kwenye njia hiyo. Aliamini kwa ukamilifu kwamba ilikuwa sahihi, lakini hakuwa na ukweli na hasa hakuwa na mabadiliko katika tabia. Alijiamini kupita kiasi na akahisi kwamba hakukuwa na ubaya wowote kuishika njia hiyo. Aliendelea akiwa amejaa imani na kwa kujihakikishia kabisa. Kufikia mwisho, hakupata fahamu, bado alifikiria kwamba kwake kuishi ilikuwa ni Kristo. Aliendelea kuishika njia hiyo hadi mwisho, na alipoadhibiwa mwishowe, yote ilikuwa imekwisha. Njia ya Paulo haikuhusisha kujijua au ufuatiliaji wa mabadiliko katika tabia. Hakuchangua kamwe asili yake mwenyewe na hakuwa na ufahamu wa kile alichokuwa; alijua tu kwamba alikuwa mkosaji mkuu katika kumtesa Yesu. Hakuwa amepata ufahamu hata kidogo wa asili yake mwenyewe, na baada ya kumaliza kazi yake alihisi kwamba alikuwa Kristo na anapaswa kupewa thawabu. Kazi ambayo Paulo alifanya ilikuwa tu kutoa huduma kwa Mungu. Kwake mwenyewe, ingawa alipokea ufunuo kiasi kutoka kwa Roho Mtakatifu, hakuwa na ukweli au uzima hata hivyo. Hakuokolewa na Mungu—aliadhibiwa. Kwa nini inasemekana kwamba njia ya Petro ni njia ya kukamilishwa? Kwa sababu katika utendaji wake alizingatia hasa uzima, alifuatilia ufahamu wa Mungu, na akazingatia kujifahamu. Kupitia uzoefu wake wa kazi ya Mungu alikuja kujijua, alipata ufahamu wa hali potovu za mwanadamu, alijua kasoro zake, na ni jambo gani lilikuwa muhimu sana kwa mwanadamu kulifuatilia. Aliweza kumpenda Mungu kwa dhati, alijua jinsi ya kumlipa Mungu, alipata ukweli kiasi, na alikuwa na ukweli ambao Mungu huhitaji. Kutoka kwa vitu vyote alivyosema wakati wa majaribio yake, inaweza kuonekana kwamba Petro alikuwa kweli mwenye ufahamu zaidi wa Mungu. Kwa sababu alielewa ukweli mwingi sana kutoka kwa maneno ya Mungu, njia yake ikawa yenye kung'aa zaidi na zaidi na kuzidi kufungamana na mapenzi ya Mungu. Kama hangekuwa amepata ukweli huu, basi hangeweza kuendelea kuishika njia sahihi kama hiyo.
Hivi sasa bado kuna swali hili: Kama unajua njia ya Petro ilikuwa gani, je, unaweza kuishika? Hili ni swali halisi. Lazima uweze kubainisha wazi ni mtu wa aina gani anaweza kuishika njia ya Petro na mtu wa aina gani hawezi. Wakati watu ni wakosefu hawawezi kukamilishwa na Mungu. Wale ambao wanashika njia ya Petro lazima wawe bila kosa; kama wewe ni mtu asiye na kosa tu ndipo unaweza kukamilishwa. Wale walio kama Paulo hawawezi kuishika njia ya Petro. Aina fulani ya mtu ataishika aina fulani ya njia; hii linaamuliwa kabisa na asili yake. Haijalishi jinsi unavyomwelezea Shetani kwa dhahiri njia ya Petro, hawezi kuitembea. Hata kama angetaka, hangeweza kuishika. Asili yake imeamua kwamba hawezi kuishika njia hiyo. Ni wale tu wanaopenda ukweli ndio wanaweza kuishika njia ya Petro. Mito na milima inaweza kubadilishwa lakini ni vigumu kubadilisha asili ya mwanadamu; kama hakuna dalili za kuupenda ukweli ndani ya asili yako, basi hustahili kwenda kwenye njia ya Petro. Kama wewe ni mtu anayependa ukweli, kama unaweza kukubali ukweli licha ya tabia yako potovu, unaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu na unaweza kuelewa mapenzi ya Mungu, kwa njia hii utaweza kuunyima mwili na kutii mpango wa Mungu. Wakati una mabadiliko katika tabia yako baada ya kupitia majaribio kiasi, hili linamaanisha kuwa polepole unakanyaga kwenye njia ya Petro ya kukamilishwa.
Baadhi ya Makala: Ni Tofauti Gani Iliyopo Kati Ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?