Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 19 Desemba 2017

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Nino Laonekana katika Mwili , Hukumu, Kristo,

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.

“Hukumu” katika maneno yaliyonenwa awali—hukumu itaanza na nyumba ya Mungu—inarejelea hukumu ambayo Mungu anatoa leo kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi katika siku za mwisho. Pengine kuna wale wanaoamini katika mawazo ya kimiujiza kama yale, siku za mwisho zitakapowadia, Mungu ataandaa meza kubwa mbinguni, ambako kitambaa cheupe kitatandikwa, kisha, Mungu ataketi kwenye kiti kikuu cha enzi na wanadamu wote wakipiga magoti ardhini, Atafichua dhambi za kila mwanadamu na hivyo kubainisha iwapo atapaa juu mbinguni ama atatupwa chini kwenye ziwa la moto wa jehanamu. Haijalishi mawazo ya mwanadamu yalivyo, kiini cha kazi ya Mungu hakiwezi kubadilishwa. Mawazo ya mwanadamu ni miundo ya fikra za mwanadamu tu na yanatoka kwenye ubongo wa mwanadamu, na yametungwa na kuunganishwa kutokana na mambo aliyoyaona na kuyasikia. Kwa hivyo Nasema, kwa vyovyote vile hata picha zilizowazwa ziwe za hali ya juu kiasi gani, bado ni kama mchoro tu na haziwezi kubadilishwa na mpango wa kazi ya Mungu. Hata hivyo, mwanadamu amepotoshwa na Shetani, sasa atawezaje kuyaelewa mawazo ya Mungu? Mwanadamu huiona kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu mno. Mwanadamu anaamini kwamba kwa sababu ni Mungu Mwenyewe anayefanya kazi ya kuhukumu, basi lazima iwe ni ya kiwango cha juu zaidi na isiyoeleweka kwa wanadamu wenye mwili wa kufa, na lazima inasikika katika mbingu yote na kutetemesha dunia; vinginevyo itakuwaje kazi ya hukumu ya Mungu? Mwanadamu anaamini kuwa, kwa maana hii ni kazi ya hukumu, basi lazima Mungu ni wa kuvutia na mwadhimu Anapofanya kazi, na wale wanaohukumiwa lazima wawe wanalia kwa sauti wakitoa machozi wakiwa kwenye magoti wakiomba msamaha. Onyesho hili lazima ni la kustaajabisha sana na la kusisimua mno.… Kila mtu hudhani kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu isiyo ya kawaida. Je, unajua, hata hivyo, kwamba Mungu alianza kazi ya kuhukumu miongoni mwa wanadamu kitambo sana na wakati huu wote wewe bado uko katika hali ya kutotambua? Kwamba, wakati ambao unadhani kuwa kazi ya hukumu ya Mungu inaanza rasmi, tayari umewadia wakati ambapo Mungu kuzifanya upya mbingu na nchi? Wakati huo, pengine utakuwa tu umeelewa maana ya maisha, lakini kazi ya adhabu ya Mungu isiyo na huruma itakuleta kuzimu, ukiwa bado usingizini. Hapo tu ndipo kwa ghafla utafahamu kuwa kazi ya hukumu ya Mungu itakuwa imeshahitimika.

Tusipoteze muda wa thamani, na tusizungumzie tena mada hizi za kuchukiza na za karaha. Badala yake, tuzungumzie kinachofanyiza hukumu. Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu. Usipouchukulia ukweli huu kuwa muhimu na kila mara kufikiria kuuepuka au kutafuta njia nyingine isipokuwa ukweli, basi ninasema kuwa wewe ni mtenda dhambi mkubwa. Iwapo una imani kwa Mungu, lakini hutafuti ukweli au mapenzi ya Mungu, wala hupendi njia inayokuleta karibu na Mungu, basi nakwambia kuwa wewe ni yule anayejaribu kuepuka hukumu, na kwamba wewe ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu hatawasamehe waasi wowote wanaotoroka machoni Pake. Wanadamu wa aina hii watapokea adhabu kali zaidi. Wale wanaokuja mbele za Mungu ili wahukumiwe, na zaidi ya hayo wametakaswa, wataishi milele katika ufalme wa Mungu. Bila shaka, hili ni jambo ambalo liko katika siku za usoni.

Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu. Wengi wana hisia mbaya kuhusu kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, kwa maana mwanadamu huona vigumu kuamini ya kwamba Mungu angefanya kazi ya hukumu akiwa na mwili. Hata hivyo, lazima Nikueleze kwamba mara nyingi kazi ya Mungu huzidi sana matarajio ya mwanadamu na ni vigumu kwa mawazo yao kukubali. Kwa maana wanadamu ni mabuu tu kwenye ardhi, ilhali Mungu ni mkuu Anayejaza ulimwengu mzima; mawazo ya mwanadamu ni kama shimo la maji machafu ambayo yanazalisha mabuu peke yake, ilhali kila hatua ya kazi inayoelekezwa na mawazo ya Mungu ni utoneshaji wa hekima ya Mungu. Mwanadamu hutaka kila wakati kushindana na Mungu, ambalo kwalo Nasema ni wazi nani atapata hasara mwishowe. Nawasihi nyote msijichukulie kuwa wa maana zaidi kushinda dhahabu. Ikiwa wengine wanaweza kukubali hukumu ya Mungu, ni kwa nini wewe usiikubali? Ni vipi ambavyo ninyi ni bora zaidi kuliko wengine? Iwapo wengine wanaweza kuinamisha vichwa vyao mbele ya ukweli, ni kwa nini usifanye vile pia? Mwelekeo mkuu wa kazi ya Mungu hauwezi kukomeshwa. Hatarudia kazi ya hukumu tena kwa sababu ya “kustahili” kwako, na utajawa na majuto mengi kwa kupoteza nafasi nzuri kama hiyo. Usipoyaamini maneno Yangu, basi kingoje tu kiti cheupe kikuu cha enzi kilicho angani kipitishe hukumu juu yako! Lazima ujue kwamba Waisraeli wote walimkataa kwa dharau na kumkana Yesu, ilhali uhakika wa ukombozi wa Yesu kwa wanadamu ulizidi kusambaa mpaka mwisho wa ulimwengu. Je, hili silo jambo ambalo Mungu tayari Amelitimiza? Iwapo bado unangoja Yesu aje kukupeleka mbinguni, basi Nasema kuwa wewe ni kipande sugu cha mti mkavu[a]. Yesu hatamkubali mfuasi bandia kama wewe asiye mwaminifu kwa ukweli na anayetafuta baraka pekee. Hasha, Hataonyesha huruma Anapokutupa kwenye ziwa la moto uungue kwa makumi ya maelfu ya miaka.

Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.

kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Jumatatu, 18 Desemba 2017

Upendo wa Mungu na wokovu | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Upendo wa Mungu na wokovu | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Mwenyezi Mungu alisema, "Mwanadamu, ambaye aliacha kupokea uzima wake kutoka kwa Mwenye Uweza, hajui ni kwa nini anaishi, na bado anaogopa kifo. Hukuna usaidizi, wala msaada, lakini mwanadamu bado anasita kufumba macho yake, akiyakabili yote bila woga, kuishi katika maisha yasiyokuwa na maana katika ulimwengu ndani ya miili isiyokuwa na utambuzi wa roho. Unaishi hivyo, pasipo tumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na malengo. Kuna Mmoja tu aliye Mtakatifu katika hadithi hii ambaye atakuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa kuumia na wanasubiri kwa shauku kubwa kuja Kwake. Imani hii haiwezi kutambulika kufikia sasa kwa watu ambao hawana utambuzi. Hata hivyo, watu watu bado wanaitaka sana. Mwenye Uweza ana rehema kwa watu hawa wanaoteseka sana. Wakati huo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na utambuzi, maana lazima Asubiri sana jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kuchunguza, kuuchunguza moyo na roho yako. Anataka kukuletea chakula na maji na kukuamsha, ili usipate kiu na kupata njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote."
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Ijumaa, 15 Desemba 2017

Mungu ni upendo | "Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu" | Best Swahili Gospel Worship Song

Mungu ni upendo | "Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu" | Best Swahili Gospel Worship Song

Sasa kwa kushangilia sana, utakatifu wa Mungu na haki vinakua ulimwenguni kote, ikitukuka sana kati ya wanadamu wote. Miji ya mbinguni inacheka, falme za dunia zinacheza. Ni nani asiyesherehekea? Ni nani asiyetoa machozi? Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde; jua linaaangaza kotekote. wakiishi katika mwanga wa Mungu, wakiwa na amani na kila mmoja. Dunia ni ya mbingu, mbingu inaungana na dunia. Mwanadamu ndiye ukamba unaounganisha mbingu na dunia. Kwa sababu ya utakatifu wa mwanadamu, kwa sababu ya upya wake, mbingu haijifichi kutoka kwa dunia tena, dunia haiinyamazii mbingu tena. Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde; hawaliabishi jina la Mungu, wakiishi katika mwanga wa Mungu, wakiwa na amani na kila mmoja. Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde; hawaliabishi jina la Mungu, wakiishi katika mwanga wa Mungu, wakiwa na amani na kila mmoja. Hewa ni changamfu, ukungu mzito umetoweka, jua linaangaza kotekote. Hewa ni changamfu, ukungu mzito umetoweka, jua linaangaza kotekote. Hewa ni changamfu, ukungu mzito umetoweka, jua linaangaza kotekote. Hewa ni changamfu, ukungu mzito umetoweka, jua linaangaza kotekote. Nyuso za ubinadamu zimezingirwa na tabasamu. Ukiwa umejificha mioyoni mwao, utamu unaenda kwa mwendo mrefu. Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde; hawaliabishi jina la Mungu, wakiishi katika mwanga wa Mungu, wakiwa na amani na kila mmoja. Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde; hawaliabishi jina la Mungu, wakiishi katika mwanga wa Mungu, wakiwa na amani na kila mmoja, wakiwa na amani na kila mmoja, wakiwa na amani na kila mmoja.
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Gospel, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Jumanne, 12 Desemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Matunda Machungu ya Kiburi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,

17. Matunda Machungu ya Kiburi | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hu Qing Jijini Suzhou, Mkoani Anhui
Nilipoona maneno ya Mungu yakisema: “Wale miongoni mwenu ambao huhudumu kama viongozi daima hutaka kuwa na ubunifu mkubwa, kuwa wazuri kuliko wengine, kupata hila mpya ili Mungu aweze kuona jinsi kweli mlivyo viongozi wakuu. … Nyinyi daima hutaka kuringa; si huu ni ufunuo kwa usahihi wa asili ya kiburi?” (“Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo), Nilifikiri mwenyewe: Nani ana ujasiri kama huo kujaribu kupata ujanja mpya ya ubunifu?

Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mmoja anapaswa kuchunguza maisha yake upya ya kumwamini Mungu ili kuona iwapo, katika kumtafuta Mungu, ameelewa kwa dhati, amefahamukwa dhati, na kuja kumjua Mungukwa dhati, iwapo anajua kweli ni mawazo gani Mungu Anayo kwa aina tofauti za binadamu, na iwapo kweli anaelewa kile ambacho Mungu Anafanya juu yake na jinsi Mungu Anaeleza kila tendo lake. Huyu Mungu, Ambaye yuko kando yako, Akiongoza mwelekeo wa kuendelea kwako, Akiamuru hatima yako, na kukupa mahitaji yako—ni kiasi gani ambacho, katika uchambuzi wako, unaelewa nani kiasi gani ambacho kweli unajua kumhusu Yeye? Je, unajua Anachofanyia kazi kwako kila siku? Je, unajua kanuni na makusudi Anayozingatia katika matendo Yake yote? Unajua jinsi Anavyokuongoza? Unajua mbinu Anazotumia kukupa mahitaji yako? Unajua mbinu ambazo Anatumia kukuongoza? Je, unajua kile Anachotaka kupata kutoka kwako na kile Anachotaka kutimiza kwako? Je, unajua mtazamo Anaochukua katika namna nyingi ambazo unatenda? Unajua iwapo wewe ni mtu Anayependwa na Yeye? Unajua chanzo cha furaha, hasira, huzuni na uchangamfu Wake, fikira na dhana zinazohusiana na hayo, na kiini Chake? Unajua, hatimaye, huyu Mungu ni Mungu wa aina gani ambaye unamwamini? Je, maswali haya na mengine ya aina hii kitu ambacho hujawahi kuelewa ama kuwaza kuyahusu? Katika kufuata imani yako kwa Mungu, umewahi, katika ufahamu halisi na kuyatambua maneno ya Mungu, umeondoa hali za kutomwelewa? Je, baada ya kupokea adhabu na kurudi kwa Mungu, umefikia unyenyekevu halisi na kujali kwa kweli? Je, wakati wa kuadibu kwa Mungu na hukumu, umepata kutambua uasi na asili ya kishetani ya mwanadamu na kupata kiasi kidogo cha kuelewa kuhusu utakatifu wa Mungu? Je, chini ya uongozi na kupata nuru kwa maneno ya Mungu, umeanza kuwa na mtazamo mpya wa maisha? Katika majaribu yaliyotumwa na Mungu, umepata kuhisi kutovumilia Kwake makosa ya mwanadamu na pia kile Anachohitaji kutoka kwako na vile Anavyokuokoa? Iwapo hujui kutomwelewa Mungu ni nini, au jinsi ya kumaliza kutoelewa huku, basi mtu anaweza kusema hujawahi kuingia katika ushirika wa kweli na Mungu na hujawahi kumwelewa Mungu, ama angalau mtu anaweza kusema kuwa hujawahi kuwa na nia ya Kumwelewa. Iwapo hujui nidhamu ya Mungu na kuadibu ni nini, basi kwa hakika hujui kujiwasilisha na kujali ni nini, ama angalau hujawahi kujiwasilisha kwa Mungu kwa kweli au kumjali. Iwapo hujawahi kupitia kuadibu kwa Mungu na hukumu, basi kwa kweli hutajua utakatifu Wake ni nini, na utakuwa hata na ufahamu dhahiri kiasi kidogo kwa mintarafu ya uasi wa mwanadamu ni nini. Iwapo hujawahi kuwa na mtazamo sahihi wa maisha, au lengo sahihi katika maisha, bali bado uko katika hali ya mshangao na kutokuwa na uamuzi kuhusu njia yako ya maisha ya baadaye, hata kwa kiwango cha kusita kuenda mbele, basi ni dhahiri kuwa hujawahi kupokea nuru na uongozi wa Mungu kwa kweli, na mtu anaweza tu kusema kuwa hujawahi kupewa au kujazwa tena na maneno ya Mungu kwa kweli. Iwapo bado hujapitia majaribu ya Mungu, basi ni hakika kuwa bila shaka hutajua kutovumilia kwa Mungu makosa ya mwanadamu ni nini, wala hutaelewa kile ambacho Mungu Anahitaji hatimaye kutoka kwako, ama hata kidogo zaidi, hatimaye, kazi Yake ya kumsimamia na kumwokoa mwanadamu ni nini. Haijalishi ni kwa miaka mingapi mwanadamu ameamini katika Mungu, iwapo hajawahi kupitia ama kutambua chochote katika maneno ya Mungu, basi kwa hakika hatembei katika njia ya kuelekea wokovu, imani yake katika Mungu kwa hakika haina chochote, maarifa yake kumhusu Mungu pia kwa hakika ni sufuri, na ni hakika kuwa hana ufahamu wowote kuhusu ni nini kumcha Mungu.

Miliki na uwepo wa Mungu, kiini cha Mungu, tabia ya Mungu—yote yamewekwa wazi katika maneno Yake kwa binadamu. Anapopitia maneno ya Mungu, katika mchakato wa kuyatekeleza mwanadamu atapata kuelewa kusudi la maneno Anayonena Mungu, na kuelewa chemichemi na usuli wa maneno ya Mungu, na kuelewa na kufahamu matokeo yaliotarajiwa ya maneno ya Mungu. Kwa binadamu, haya ni mambo yote ambayo mwanadamu lazima ayapitie, ayatambue, na kuyafikia ili kuufikia ukweli na uzima, kutambua nia ya Mungu, kubadilishwa katika tabia yake, na kuweza kutii mamlaka ya Mungu na mipango. Katika wakati huo ambao mwanadamu anapitia, anafahamu, na kuvifikia vitu hivi, atakuwa kupata kumwelewa Mungu polepole, na katika wakati huu atakuwa pia amepata viwango tofauti vya ufahamu kumhusu Yeye. Kuelewa huku na maarifa havitoki katika kitu ambacho mwanadamu amefikiria ama kutengeneza, ila kutoka kwa kile ambacho anafahamu, anapitia, anahisi, na anashuhudia ndani yake mwenyewe. Ni baada tu ya kufahamu, kupitia, kuhisi, na kushuhudia vitu hivi ndipo ufahamu wa mwanadamu kumhusu Mungu utapata ujazo, ni maarifa anayopata katika wakati huu pekee ndio ulio halisi, wa kweli na sahihi, na mchakato huu—wa kupata kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu kwa kuelewa, uzoefu, kuhisi, na kushuhudia maneno Yake—sio kingine ila ushirika wa kweli kati ya mwanadamu na Mungu. Katikati ya aina hii ya ushirika, mwanadamu anakuja kuelewa kwa dhati na kufahamu nia za Mungu, anakuja kuelewa kwa dhati na kujua miliki na uwepo wa Mungu, anakuja na kuelewa kujua kwa kweli kiini cha Mungu, anakuja kuelewa na kujua tabia ya Mungu polepole, anafikia uhakika wa kweli kuhusu, na ufafanuzi sahihi wa, ukweli wa mamlaka ya Mungu juu ya vitu vyote vilivyoumbwa, na kupata mkondo kamili kwa na ufahamu wa utambulisho wa Mungu na nafasi Yake. Katika aina hii ya ushirika, mwanadamu anabadilika, hatua kwa hatua, mawazo yakekuhusu Mungu, bila kumwaza pasi na msingi, ama kuipa nafasi tashwishi yake kumhusu Yeye, ama kutomwelewa, ama kumshutumu, ama kupitisha hukumu Kwake, ama kuwa na shaka Naye. Kwa sababu hii, mwanadamu atakuwa na mijadala michache na Mungu, atakuwa na uhasama kiasi kidogo na Mungu, na kutakuwa na matukio machache ambapo atamuasi Mungu. Kwa upande mwingine, kujali kwa mwanadamu na utii kwa Mungu kutakua kwa kiasi kikubwa, na uchaji wake Mungu utakuwa wa kweli zaidi na pia mkubwa zaidi. Katika ya aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kupewa ukweli pekee na ubatizo wa uzima, bali wakati uo huo pia atapata maarifa ya kweli ya Mungu. Katika aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kubadilishwa kwa tabia yake na kupata wokovu pekee, bali pia kwa wakati huo atafikia uchaji na ibada ya kweli ya kiumbe aliyeumbwa kwa Mungu. Baada ya kuwa na aina hii ya ushirika, imani ya mwanadamu katika Mungu haitakuwa tena ukurasa tupu wa karatasi, ama ahadi ya maneno matupu, ama harakati na tamanio lisilo na lengo na kuabudu kama mungu; katika aina hii ya ushirika pekee ndio maisha ya mwanadamu yatakua kuelekea ukomavu siku baada ya siku, na ni wakati huu ndio tabia yake itabadilika polepole, na imani yake kwa Mungu, hatua kwa hatua, itatoka kwenye imani ya wasiwasi na kutoeleweka na imani isiyo ya hakika mpaka katika utii wa kweli na kujali, na kuwa katika uchaji Mungu wa kweli; mwanadamu pia katika kumfuata Mungu, ataendelea polepole kutoka kuwa mtazamaji na kuwa na hali ya utendaji, kutoka yule anayeshughulikwa na kuwa anayechukua nafasi ya kutenda; kwa aina hii ya ushirika pekee ndipo mwanadamu atafikia kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu, kwa ufahamu wa kweli wa Mungu. Kwa sababu watu wengi hawajawahi kuiingia katika ushirika wa kweli na Mungu, ufahamu wao wa Mungu unakomea kiwango cha nadharia, katika kiwango cha barua na kanuni. Hivyo ni kusema, watu wengi, haijalishi ni miaka mingapi wamemwamini Mungu, ikija kwa kumjua Mungu bado wako mahali walipoanzia, wamekwama katika msingi wa aina za heshima, na mitego yao ya hadhi na kabailaza kishirikina. Kwamba maarifa ya mwanadamu kumhusu Mungu yanapaswa kukomea yalipoanzia ina maana kwamba hayapo kabisa. Mbali na uthibitisho wa mwanadamu kuhusu nafasi ya Mungu na utambulisho, imani ya mwanadamu kwa Mungu bado iko katika hali ya kutoeleweka na kutokuwa na uhakika. Hii ikiwa hivyo, ni kiasi gani ambacho mwanadamu anaweza kuwa nacho kuhusu uchaji Mungu wa kweli?

Haijalishi kiwango cha imani yako katika uwepo Wake, hili haliwezi kuchukua mahali pa ufahamu wako wa Mungu, wala uchaji wako wa Mungu. Haijalishi kiwango ambacho umefurahia baraka Zake na neema Yake, hii haiwezi kuchukua nafasi ya ufahamu wako wa Mungu. Haijalishi ni kiwango gani unataka na kutamani kuweka wakfu kila kitu chako na kugharimika kwa ajili Yake, hii haiwezi kuchukua nafasi ya maarifa yako kuhusu Mungu. Ama labda umeyazoea sana maneno ambayo Amenena mpaka unayajua kimoyomoyo na unaweza kuyasema upesi kinyumenyume; hata hivyo, hii haiwezi kuchukua nafasi ya maarifa yako kuhusu Mungu. Haijalishi kiwango cha dhamira ya mwanadamu katika kumfuata Mungu, iwapo hajawahi kuwa na ushirika wa kweli na Mungu, ama kuwa na uzoefu wa kweli wa maneno ya Mungu, basi ufahamu wake wa Mungu utakuwa utupu tu au ndoto isiyo na mwisho; kwa kuwa yote yale unaweza kuwa “umekumbana” na Mungu kwa kupita, au kukutana Naye uso kwa uso, ufahamu wako wa Mungu bado utakuwa sufuri, na uchaji wako wa Mungu utakuwa tu kidahizo ama njozi.

Watu wengi huyashika maneno ya Mungu kuyasoma siku baada ya siku, kiasi kwamba wanaviweka akilini vifungu vyote maarufu humo kama vitu vyao vyenye thamani zaidi, na zaidi kuyahubiri maneno ya Mungu kila mahali, wakiwatolea na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno Yake. Wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, kuwa na ushuhuda kwa maneno Yake, kwamba kufanya hivi ni kufuata njia ya Mungu; wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuishi kulingana na maneno ya Mungu, kwamba kufanya hivi ni kuleta maneno Yake katika maisha yao halisi, kuwa kufanya hivi kutawawezesha kupokea pongezi ya Mungu, na kuokolewa na kukamilika. Lakini, hata wanapohubiri maneno ya Mungu, hawazingatii maneno ya Mungu katika matendo, ama kujaribu kujileta sambamba na yale yanayofichuliwa katika maneno ya Mungu. Badala yake, wanayatumia maneno ya Mungu kupata upendo na imani ya wengine kwa hila, kuingia katika usimamizi wao wenyewe, na kubadhiri na kuiba sifa za Mungu. Wanatarajia, kwa ubatili, kutumia nafasi waliyopata kwa kueneza maneno ya Mungu ili kupewa kazi ya Mungu na pongezi Yake. Miaka mingapi imepita, lakini hao watu hawajaweza tu kupata pongezi ya Mungu katika hatua ya kuyahubiri maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kugundua njia ambayo wanafaa kufuata katika hatua ya kushuhudia maneno ya Mungu, na hawajajisaidia tu ama kujipatia wenyewe katika hatua ya kuwapa na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kumjua Mungu, ama kuamsha ndani yao uchaji wa kweli wa Mungu, katika hatua ya kufanya haya yote; kwa upande mwingine, kutoelewa kwao kuhusu Mungu kunakuwa hata wenye kina zaidi, kutokuwa na imani kwao kwa Mungu kunazidi kuwa na mashaka, na mawazo yao kumhusu yanatiwa chumvi zaidi. Wakijazwa na kuongozwa na mawazo yao kuhusu maneno ya Mungu, wanaonekana kuwa katika haki yao kamili, kana kwamba wanapitia ujuzi wao bila juhudi, kana kwamba wamepata kusudi lao katika maisha, wito wao, na kana kwamba wameshinda maisha mapya na kuokolewa, kana kwamba, maneno ya Mungu yakibiringika kutoka kwenye ulimi kwa kukariri, wameupata ukweli, kushika nia za Mungu, na kugundua njia ya kumjua Mungu, kana kwamba, katika wakati wa kuhubiri maneno ya Mungu, wanakuja kila wakati uso kwa uso na Mungu, pia, wana “sukumwa” kila wakati mpaka kiwango cha kilio, na kila wakati kuongozwa na “Mungu” katika maneno ya Mungu, wanaonekana kushika bila kukoma wasiwasi Wake wenye ari na nia njema, na wakati uo huo kushika wokovu wa Mungu kwa mwanadamu na usimamizi Wake, kuja kujua kiini Chake, na kuelewa tabia Yake ya haki. Msingi huu ukizingatiwa, wanaoneka kuamini hata zaidi katika uwepo wa Mungu, kujua zaidi hali ya utukufu Wake, na kuhisi hata kwa kina zaidi ukuu Wake na kuvuka mipaka Kwake. Wakiwa wameinuka katika ufahamu wao wa kijuujuu wa maneno ya Mungu, itaonekana kuwa imani yao imekua, kuamua kwao kupitia mateso kumetiwa nguvu, na maarifa yao kwa Mungu yamekuwa na kina. Ila hawajui kwamba, hadi watakapopitia maneno ya Mungu kwa kweli, maarifa yao yote kuhusu Mungu na mawazo yao kumhusu Yeye yanatoka kwa mawazo yao wenyewe ya kufikiri kwa ubunifu na kukisia. Imani yao haiwezi kusimama jaribio lolote kutoka kwa Mungu, wanachoita kiroho na kimo haviwezi kusimama chini ya majaribu ya Mungu na ukaguzi, uamuzi wao ni ngome tu iliyojengwa juu ya changarawe, na wanachoita maarifa juu ya Mungu pia sio zaidi ya ubunifu wa mawazo yao. Kwa hakika, watu hawa, ambao, ilivyokuwa, wameweka juhudi kubwa katika maneno ya Mungu, hawajawahi kutambua imani ya kweli ni nini, kujiwasilisha kwa kweli ni nini, kujali kwa kweli ni nini, ama maarifa ya kweli ya Mungu ni nini. Wanachukua nadharia, mawazo, maarifa, zawadi, utamaduni, ushirikina na hata tabia nzuri za binadamu, na kuyafanya kuwa “uwekezaji wa msingi” na “zana za kijeshi” za kumwamini Mungu na kumfuata, hata kuyafanya kuwa misingi ya imani yao kwa Mungu na katika kumfuata Yeye. Wakati uo huo, pia wanachukua uwekezaji msingi huu na silaha na kuyafanya kuwa hirizi ya uchawi kwa kumjua Mungu, ya kukutana na kubishana na ukaguzi wa Mungu, majaribu, kuadibu, na hukumu. Mwishowe, wanachopata bado hakijumlishi chochote zaidi ya hitimisho kumhusu Mungu zinazoegemea hisia za kidini, katika kabaila za ushirikina, na kwa yote yaliyo ya kimapenzi, ya kustaajabisha, na yenye ugumu kuelewa, na njia yao ya kujua na kumweleza Mungu imepigwa muhuri katika muundo sawa na wa wale watu wanaomini katika Mbingu iliyo Juu pekee, ama Mtu Mzee aliye Mawinguni, wakati ukweli wa Mungu, kiini Chake, tabia Zake, miliki Zake na asili, na kadhalika, yote yanayomhusu Mungu wa kweli Mwenyewe, ni vitu ambavyo kuvijua kumekosa mshiko, havina uhusiano kabisa na viko mbali kabis. Katika njia hii, ingawa wanaishi chini ya upaji na ustawishaji wa maneno ya Mungu, hawawezi hata hivyo kutembea kwa kweli katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Sababu ya hakika ya hii ni kwamba hawajawahi kupata kujuana na Mungu, wala hawajawahi kuwa na mawasiliano ya kweli ama ushirika Naye, kwa hivyo haiwezekani kufikia maelewano ya pamoja na Mungu, ama kuamsha ndani mwao imani halisi katika, kufuata, ama ibada ya Mungu. Kwamba wanafaa kuyahusisha maneno ya Mungu, kwamba wanafaa kumhusisha Mungu—mwelekeo huu na tabia imewahukumu kurudi mkono mtupu kutoka kwa jitihada zao, imewahukumu katika maisha yote wasiweze kutembea katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Lengo wanalolengea, na mwelekeo wanaoelekea, inamaanisha kuwa ni maadui wa Mungu milele, na kwamba hata milele hawatawahi kuweza kupokea wokovu.

Iwapo, katika tukio la mwanadamu ambaye amemfuata Mungu kwa miaka mingi na kufurahia kupewa maneno Yake kwa miaka mingi, ufafanuzi wake kuhusu Mungu ni, katika kiini chake, sawa na ule wa mtu anayejisujudu kwa heshima mbele ya sanamu, basi hii itamaanisha kuwa huyu mtu hajapata ukweli wa maneno ya Mungu. Kwa kutazama katika chanzo cha hii, mtu anaona kuwa tu hajaingia katika ukweli wa maneno ya Mungu, na kwa sababu hii hali halisi, ukweli, nia, na matarajio juu ya binadamu, yote ambayo yana asili kwa maneno ya Mungu, hayana uhusiano wowote na yeye. Hivyo ni kusema, haijalishi ni kiwango gani mwanadamu wa aina hii anaweza kufanya bidii katika maana ya juu ya maneno ya Mungu, yote ni bure: kwani yale anayofuata ni maneno tu, kwa hivyo yale atakayopata yatakuwa pia ni maneno tu. Kama maneno yanayonenwa na Mungu ni, katika mwonekano wa nje, wazi ama magumu kuelewa, yote ni ukweli ulio lazima kwa mwanadamu anapoingia katika uzima; ni chemichemi ya maji ya uzima yanayomwezesha kuishi katika roho na mwili. Yanatosheleza kile ambacho mwanadamu anahitaji ili awe hai; kanuni na imani ya kufanya maisha yake ya kila siku; njia, lengo, na mwelekeo ambao lazima apitie ili kupokea wokovu; kila ukweli ambao anapaswa awe nao kama kiumbe aliyeumbwa mbele za Mungu; na kila ukweli jinsi mwanadamu anavyotii na kumwabudu Mungu. Ni uhakika ambao unahakikisha kuishi kwa mwanadamu, ni mkate wa kila siku wa mwanadamu, na pia ni nguzo ya msaada inayowezesha mwanadamu kuwa na nguvu na kusimama. Yamejaa utajiri wa ukweli wa ubinadamu wa kawaida anavyoishi binadamu aliyeumbwa, yamejaa ukweli ambao mwanadamu anatumia kutoka kwa upotovu na kuepuka mitego ya Shetani, yamejaa mafunzo bila kuchoka, kuonya, kuhamasisha na furaha ambayo Muumba anampa binadamu aliyeumbwa. Ni ishara ambayo inawaongoza na kuwaelimisha wanadamu kuelewa yale yote yaliyo mazuri, hakika inayohakikisha kuwa wanadamu wataishi kwa kudhihirisha na kumiliki yale yote yaliyo ya haki na mema, kigezo ambacho watu, matukio, na vitu vyote vinapimwa, na pia alama ya usafiri inayowaongoza wanadamu kuelekea wokovu na njia ya mwanga. Katika uzoefu wa kweli wa maneno ya Mungu tu ndipo mwanadamu anapewa ukweli na uzima; humu pekee ndimo anakuja kupata kuelewa ubinadamu wa kawaida ni nini, maisha yenye umuhimu ni nini, kiumbe halisi ni nini, utiifu wa kweli kwa Mungu ni nini; humu pekee ndimo anakuja kuelewa anavyofaa kumjali Mungu, jinsi ya kutimiza wajibu ya kiumbe aliyeumbwa, na jinsi ya kumiliki mfano wa mwanadamu wa kweli; humu tu ndimo anapata kuelewa maana ya imani halisi na ibada halisi; humu tu ndimo anaelewa nani ndiye Mtawala wa mbingu na nchi na vitu vyote; humu tu ndimo anakuja kuelewa njia ambayo Yule ambaye ni Bwana wa uumbaji wote Anatawala, anaongoza, na kuutosheleza uumbaji; na hapa pekee ndipo anakuja kuelewa na kushika njia ambayo Yule aliye Bwana wa uumbaji wote Anakuwa, Anadhihirishwa na kufanya kazi.… Akitenganishwa na uzoefu wa kweli wa maneno ya Mungu, mwanadamu hana maarifa ya kweli ama ufahamu katika maneno ya Mungu na ukweli. Mwanadamu wa aina hii ni maiti inayoishi tu, ganda lililoisha, na ufahamu wote unaohusiana na Muumba hauna chochote kingine kumhusu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu kama huyo hajawahi kumwamini, ama kuwahi kumfuata, na hivyo Mungu hamtambui yeye kama mwumini Wake wala mfuasi Wake, ama hata kama kiumbe halisi aliyeumbwa.

Ili kuwa kiumbe halisi aliyeumbwa, sharti ujue Muumba ni nani, uumbaji wa mwanadamu ni wa umuhimu gani, jinsi ya kutekeleza majukumu ya kiumbe, na jinsi ya kumwabudu Bwana wa uumbaji wote, lazima aelewe, ashike, ajue, na kujali kuhusu nia za Muumba, mapenzi Yake, na madai Yake, na lazima atende kulingana na njia ya Muumba—kumcha Mungu na kuepuka maovu.

Kumcha Mungu kuna maana gani? Na mtu anawezaje kuepuka maovu?

“Kumcha Mungu” hakumaanishi woga na hofu isiyotajika, wala kukwepa, wala kuweka umbali, wala si kuabudu kama mungu ama ushirikina. Ila, ni kutazama na kupendezwa, sifa, imani, kuelewa, kujali, kutii, kuweka wakfu, upendo, na pia ibada isiyo na vikwazo au malalamishi, malipo na kujisalimisha. Bila ya ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na kupendezwa halisi, imani halisi, kuelewa halisi, kujali halisi ama utiifu, ila tu hofu na kukosa utulivu, shaka pekee, kutoelewa, kukwepa, na kuepuka; bila maarifa halisi ya Mungu, binadamu hawatakuwa na kuwakfishwa halisi na malipo; bila ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na ibada halisi na kujisalimisha, uabudu kama mungu upofu tu na ushirikina; bila maarifa halisi juu ya Mungu, binadamu hawawezi kutenda kulingana na njia ya Mungu, ama kumcha Mungu, ama kuepuka maovu. Badala yake, kila tendo na tabia ambayo mwanadamu anashiriki litajaa uasi na kutotii, na kumbukumbu zinazokashifu na hukumu ya usengenyaji kumhusu Yeye, na mienendo miovu inayokwenda kinyume na ukweli na maana ya kweli ya maneno ya Mungu.

Kuwa na imani ya kweli kwa Mungu, binadamu watajua kweli jinsi ya kumfuata Mungu na kumtegemea; kwa imani ya kweli pekee na tegemeo kwa Mungu ndipo binadamu watakuwa na kuelewa kwa kina na ufahamu; pamoja na ufahamu wa kweli wa Mungu inakuja kumjali Kwake kwa kweli; ni kwa kumjali Mungu kwa kweli pekee ndipo binadamu watakuwa na utiifu wa kweli kwa Mungu; na ni kwa utiifu wa Mungu kwa kweli pekee ndipo binadamu watakuwa na uwekaji wakfu wa kweli; na ni kwa uwekaji wakfu wa kweli kwa Mungu pekee ndipo binadamu watakuwa na malipo yasiyo na kiwango na kulalamika; ni kwa imani na msimamo wa kweli, kuelewa na kujali kwa kweli, utiifu wa kweli, uwakfishaji wa kweli na malipo, ndipo binadamu watakuja kujua kwa kweli tabia na kiini cha Mungu, na kujua utambulisho wa Muumba; Watakapopata kumjua Muumba ndipo binadamu wataamsha ndani yao ibada ya kweli na kujisalimisha; watakapokuwa na ibada ya kweli na kujisalimisha kwa Muumba tu ndipo binadamu wataweza kwa kweli kuweka kando njia zao za uovu, hivyo ni kusema, kuepuka maovu.

Hii inajumlisha hatua yote ya “kumcha Mungu na kuepuka maovu” na pia ni maudhui katika kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa ujumla, na pia njia ambayo ni lazima kupitia ili kufikia kumcha Mungu na kuepuka maovu.

“Kumwogopa Mungu na kuepuka maovu” na kumjua Mungu ni uhusiano usiogawanyishwa na uliounganishwa kwa nyuzi zisizohesabika, na uhusiano kati yao ni dhahiri. Iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kuepuka maovu, lazima kwanza amche Mungu kwa kweli; iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kumcha Mungu kwa kweli, lazima awe na maarifa ya kweli kuhusu Mungu; Iwapo mtu anataka kupata maarifa ya Mungu, lazima kwanza ayapitie maneno ya Mungu, aingie katika ukweli wa maneno ya Mungu, apitie kuadibu na nidhamu ya Mungu, kuadibu Kwake na hukumu; iwapo mtu anataka kupitia maneno ya Mungu, lazima aje ana kwa ana na maneno ya Mungu, aje ana kwa ana na Mungu, na kumwomba Mungu Ampe fursa ya kupitia maneno ya Mungu katika hali ya aina yote ya mazingira inayowahusisha watu, matukio na vitu; iwapo mtu anataka kuja ana kwa ana na Mungu na maneno ya Mungu, lazima kwanza amiliki moyo wa kweli na mwaminifu, awe tayari kuukubali ukweli, kukubali kupitia mateso, uamuzi na ujasiri wa kuepuka uovu, na azimio la kuwa kiumbe halisi…Kwa njia hii, kuendelea mbele hatua kwa hatua, utamkaribia Mungu zaidi, moyo wako utakuwa safi zaidi, na maisha yako na thamani ya kuwa hai, pamoja na maarifa yako kumhusu Mungu, yatakuwa ya maana zaidi na yatakuwa hata ya kupevuka zaidi. Mpaka siku moja, utahisi kuwa Muumba sio fumbo tena, kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka kwako, kwamba Muumba hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako, kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata kidogo, kwamba Muumba siye yule unayemtamania katika mawazo yako lakini kwamba huwezi kumfikia na hisia zako, kwamba Anasimama kwa kweli kama mlinzi kulia na kushoto kwako, Akiruzuku maisha yako, na kudhibiti majaliwa yako. Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho. Mungu kama huyo Anakukubali umpende kutoka moyoni, umshikilie, umweke karibu, umtamani, uhofu kumpoteza, na kutotaka kumkataa tena, kutomtii tena, ama kumwepuka tena ama kumweka mbali. Kile unachotaka ni kumjali tu, kumtii, kulipia kila kitu Anachokupa, na kujisalimisha katika himaya Yake. Hukatai tena kuongozwa, kupewa, kuangaliwa, na kuwekwa na Yeye, hukatai tena Anachoamuru na kukitawaza kwako. Unachotaka tu ni kumfuata, kutembea kando Yake katika kushoto ama kulia Kwake, kile utakacho ni kumkubali kama maisha yako ya pekee, kumkubali kama Bwana wako mmoja na wa pekee, Mungu wako mmoja na wa pekee.
Agosti 18, 2014

Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Video za Kikristo | Kuelezea Wazi Uhusiano Kati ya Biblia na Mungu | "Biblia na Mungu" (Swahili Subtitles)


Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.” Moyoni mwake, Biblia ni kuu. Kwa sababu ya upendo na imani yake pofu katika Biblia, hajawahi kutafuta au kuitazama kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hadi siku moja, alipowazuia waumini kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu mtandaoni, akawa na fursa ya kukutana na wahubiri kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Baada ya kupitia majadiliano makali kuhusu ukweli, aliweza hatimaye kuona wazi uhusiano kati ya Biblia na Mungu? Je, aliweza kusonga mbali na Biblia kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima? Je, atachukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Jumatatu, 11 Desemba 2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ufalme wa Milenia Umewasili

Ufalme wa Milenia Umewasili | Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. Kutoka mbinguni Mungu alituma chakula, maji, na mana ili watu waweze kuvifurahia, na leo bado ni hivyo: Mungu mwenyewe ametuma vitu chini kwa ajili ya kula na kunywa ili watu wafurahi, na yeye mwenyewe ametuma laana ili kuwaadibu watu. Na hivyo kila hatua ya kazi Yake inafanywa na Mungu Mwenyewe. Leo, watu wanatamani utokeaji wa kweli, wanajaribu kuona ishara na maajabu, na kuna uwezekano mkubwa watu wa namna hiyo kutelekezwa, maana kazi ya Mungu inazidi kuwa halisi. Hakuna anayejua kwamba Mungu ameshuka kutoka mbinguni, bado hawajui kwamba Mungu ametuma chini chakula na maji ya kutia nguvu kutoka mbinguni, lakini Mungu kimsingi yupo, na mazingira mazuri ya Ufalme wa Milenia ambao watu wanaufikiria pia ni matamshi ya Mungu Mwenyewe. Huu ni ukweli, ni huu tu ndio unaotawala pamoja na Mungu duniani. Kutawala na Mungu duniani kunarejelea mwili. Kile ambacho si cha mwili hakipo duniani, na hivyo wale wote wanaojikita katika kusonga mbele katika mbingu ya tatu wanafanya hivyo bure. Siku moja, ambapo ulimwengu mzima utarudi kwa Mungu, kitovu cha kazi Yake katika ulimwengu wote kitafuata sauti ya Mungu; kwingineko watu watapiga simu, wengine watapanda ndege, wengine watapanda boti na kupita baharini, na wengine watatumia leza kupokea matamshi ya Mungu. Kila mmoja atakuwa anatamani na mwenye shauku, wote watakuja karibu na Mungu, na kukusanyika kwa Mungu, na wote watamwabudu Mungu—na yote haya yatakuwa matendo ya Mungu. Kumbuka hili! Mungu hawezi kuanza tena kwingineko. Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini inakufa kwa njaa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea. Huo ndio utakuwa muda ambapo matendo ya Mungu yatafichuliwa, na Mungu atatukuzwa; watu wote katika ulimwengu wote watakuja na kumwabudu "mtu" asiyekuwa wa kawaida. Je, hii haitakuwa siku ya utukufu wa Mungu? Siku moja, wachungaji wa zamani watatuma ujumbe wakitafuta maji kutoka katika chemchemi za maji ya uzima. Watakuwa wazee, lakini watakuja kumwabudu mtu huyu ambaye walimdharau. Katika vinywa vyao watakiri na katika mioyo yao wataamini—je, hii si ishara na maajabu? Siku ambapo ufalme wote utafurahia ni siku ya utukufu wa Mungu, na mtu yeyote atakayewajia, na kupokea habari njema za Mungu atabarikiwa na Mungu, na nchi hizi na watu hawa watabarikiwa na kulindwa na Mungu. Mwelekeo wa maisha yajayo utakuwa hivi: Wale ambao watapata matamshi kutoka katika kinywa cha Mungu watakuwa na njia ya kutembea duniani, na wawe wafanya biashara au wanasayansi, au waelimishaji au wataalamu wa viwandani, wale ambao hawana maneno ya Mungu watakuwa na wakati mgumu wa kuchukua hata hatua moja, na watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Hiki ndicho kinamaanishwa na, "Ukiwa na ukweli utatembea ulimwengu mzima; bila ukweli, hutafika popote." Ukweli ni huu: Mungu atatumia Njia (ikiwa na maana kwamba maneno Yake yote) kuuamuru ulimwengu wote na kumwongoza na kumshinda mwanadamu. Watu siku zote wanatarajia kuwa na mabadiliko makubwa katika namna ambayo Mungu anafanya kazi. Kuzungumza kwa wazi, ni kupitia maneno ndipo Mungu anawadhibiti watu, na unapaswa kufanya kile Anachokisema[a] haijalishi kama unataka au hutaki; huu ni ukweli halisi, na unapaswa kutiiwa na watu wote, na hivyo haubadiliki, na kujulikana kwa wote.

Roho Mtakatifu anawapatia watu hisia. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, katika mioyo yao wamesimama imara, na wana amani, wakati wale ambao hawapati maneno ya Mungu wanajihisi watupu. Hiyo ni nguvu ya maneno ya Mungu—watu wanapaswa kuyasoma, baada ya kuyasoma wananawirishwa, na hawawezi kufanya chochote bila hayo. Ni kama ambapo watu wanatumia afyuni: Inawapatia nguvu, bila hiyo wanahisi kukanganyikiwa, na wanakosa nguvu. Hayo ndiyo mazoea miongoni mwa watu leo. Kusoma maneno ya Mungu kunawapatia watu nguvu. Ikiwa hawayasomi, wanajiona hawana nguvu, lakini baada ya kuyasoma, wanainuka mara moja kutoka katika kitanda cha mgonjwa. Hii ndiyo maana ya utawala wa Mungu (Neno) duniani. Baadhi ya watu wanataka kuacha au wamechoshwa na kazi ya Mungu. Licha ya kwamba hawawezi kujitenga na maneno ya Mungu; bila kujali ni wadhaifu kiasi gani, bado ni lazima wategemee maneno ya Mungu ili waishi, na haijalishi ni watu wa uasi kiasi gani, lakini bado hawathubutu kuacha maneno ya Mungu. Pale ambapo maneno ya Mungu yanaonyesha ukuu wao ndipo ambapo Mungu anatawala na kuchukua nguvu, na hivi ndivyo Mungu anavyofanya kazi. Hata hivyo, hii ndiyo njia ambayo kwayo Mungu anafanya kazi, na hakuna anayeweza kuiacha. Maneno ya Mungu yataenea katika nyumba zisizohesabika, yatafahamika kwa wote, na wakati huo tu ndipo kazi yake itaenea ulimwenguni kote. Ambapo ni sawa na kusema, ikiwa kazi ya Mungu itaenea ulimwenguni kote, basi maneno Yake ni lazima yaenee. Katika siku ya utukufu wa Mungu, maneno ya Mungu yataonesha nguvu yake na mamlaka. Kila neno Lake kuanzia wakati huo hadi leo litatimizwa na kuwa la kweli. Kwa njia hii, utukufu utakuwa wa Mungu duniani—ambavyo ni sawa na kusema, kazi yake itatawala duniani. Wote ambao ni waovu wataadibiwa na maneno katika kinywa cha Mungu, wale wote ambao ni wa haki watabarikiwa na maneno katika kinywa Chake, na wote watathibitishwa na kukamilishwa na maneno katika kinywa Chake. Wala hataonyesha ishara zozote na maajabu; yote yatakamilishwa na maneno Yake, na maneno Yake yatazalisha ukweli. Kila mtu duniani atasherehekea maneno ya Mungu, ama ni watu wazima au watoto, wanaume, wanawake, wazee, au vijana, watu wote watajinyenyekeza katika maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu yataonekana katika mwili, na yataonekana waziwazi na kufanana na maisha ya watu duniani. Hii ndiyo maana ya Neno kufanyika mwili. Mungu amekuja duniani kwa lengo la kukamilisha ukweli wa "Neno kufanyika mwili," ni sawa na kusema, Amekuja ili kwamba maneno Yake yaweze kutolewa kutoka katika mwili (sio kama wakati wa Musa katika Agano la Kale, ambapo Mungu alizungumza moja kwa moja kutoka mbinguni). Baada ya hapo, kila neno Lake litatimizwa wakati wa Enzi ya Ufalme wa Milenia, zitakuwa ni kweli ambazo zitaonekana katika macho ya watu, na watu watazitazama kwa kutumia macho bila tofauti hata kidogo. Hii ndiyo maana kuu ya Mungu kupata mwili. Ni sawa na kusema, kazi ya Roho imetimizwa kupitia mwili, na kupitia maneno. Hii ndiyo maana ya kweli ya "Neno kufanyika mwili" na "Neno Laonekana katika mwili." Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuzungumza mapenzi ya Roho, na ni Mungu pekee katika mwili ndiye anayeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho; maneno ya Mungu yamewekwa wazi katika Mungu kupata mwili, na kila mtu anaongozwa nayo. Hakuna aliyeachwa, wote wanakuwa ndani ya mawanda haya. Ni kutoka tu katika matamshi haya ndipo watu wanaweza kujua; wale ambao hawatapata njia hii wanaota ndoto za mchana ikiwa wanadhani wanaweza kupata matamshi kutoka mbinguni. Hayo ndiyo mamlaka yaliyooneshwa katika mwili wa Mungu uliopata mwili: kuwafanya wote kuamini. Hata wataalamu wa kuheshimiwa sana na wachungaji hawawezi kuzungumza maneno haya. Wote ni lazima wajinyenyekeze chini yao, na hakuna anayeweza kuanza mwanzo mpya. Mungu atatumia maneno kuushinda ulimwengu. Atafanya hivi si kwa kupata kwake mwili, lakini kwa kutumia matamshi kutoka kwa Mungu katika mwili kushinda watu wote duniani; Namna hii tu ndiye Mungu katika mwili, na huu tu ndio kuonekana kwa Mungu katika mwili. Labda kwa watu, inaonekana kana kwamba Mungu hajafanya kazi kubwa—lakini Mungu analazimika kutamka maneno Yake ili watu washawishike kabisa, na wao kutishika kabisa. Bila kweli, watu wanapiga makelele na kupiga mayowe; kwa maneno ya Mungu, wote wananyamaza kimya. Mungu hakika atakamilisha ukweli huu, maana huu ni mpango ulioanzishwa na Mungu: kukamilisha ukweli wa Neno kuwasili duniani. Kimsingi, sina haja ya kuelezea—kuwasili kwa Ufalme wa Milenia duniani ni kuwasili kwa neno la Mungu duniani. Kushuka kwa Yerusalemu mpya kutoka mbinguni ni kuwasili kwa maneno ya Mungu kuishi miongoni mwa mwanadamu, kuenenda na kila tendo la mwanadamu, na mawazo yake yote ya ndani. Huu pia ni ukweli kwamba Mungu atatimiza, na mandhari mazuri kabisa ya Ufalme wa Milenia. Huu ndio mpango uliowekwa na Mungu: Maneno Yake yataonekana duniani kwa miaka elfu moja, na yatashuhudia matendo yake yote, na kukamilisha kazi Yake yote duniani, ambapo baada ya hatua hii mwanadamu atakuwa amefikia kikomo.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 10 Desemba 2017

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana | Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu

Ha … nyimbo ni nyingi na ngoma ni za madaha; ulimwengu na miisho ya dunia zinakuwa bahari inayosisimka. Ha … mbingu ni mpya na dunia ni mpya. Eneo kubwa la ulimwengu limejaa kusifu; tunapiga ukelele na kuruka kwa shangwe. Milima yajiunga na milima na maji mengi kujiunga na maji mengi, ndugu wote wa kiume na kike ni wandani. Twamsifu Mungu bila kukoma. Viumbe wampenda Mungu, wakija, mbele ya kiti chake cha enzi kwa furaha kuabudu pamoja. Mungu Amefichua katika Sayuni kwa ulimwengu uadilifu Wake na utakatifu Wake. Watu wote wa Mungu wanachangamka kwa furaha, wakimtukuza Mungu bila kukoma. Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya! Msifuni Mungu, msifuni Mungu!
Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu. Sauti inayosifu yapasua mbingu. Acha sisi, waume kwa wake, wazee kwa vijana, tuwahi pamoja. Watoa nyimbo nami natoa ngoma, uimbe nami nishirikiane. Aliyetiwa aibu ni shetani—joka kubwa jekundu; lililotukuzwa ni jina la Mwenyezi Mungu wa kweli. Tumeona tabia adilifu ya Mungu kutoka kwa kazi Yake. Mwenyezi Mungu ni Mungu mwadilifu. Watu wote wa Mungu wameiona sura Yake tukufu. Sisi sote hufuata kumpenda na kumtosheleza Mungu, tukipenda kuwa waaminifu Kwake milele. Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Haleluya! Msifuni Mungu, msifuni Mungu! Njooni! Hebu tumsifu Mungu! Njooni! Hebu tumsifu Mungu! Kuja!
Milima inashangilia na maji mengi yanacheka, mataifa yote na watu wote wanacheka kwa furaha. Mtazamo mpya ulioje! Hiyo mbingu mpya, dunia mpya, na ufalme mpya! Tunacheza na kuimba nyimbo mpya kwa Mungu; tumefurahi sana! Nyimbo nzuri sana zaimbiwa Mungu, ngoma za madaha zaidi zawasilishwa kwa Mungu. Moyo mnyofu umeinuliwa juu kwa Mungu, moyo wa kweli umetolewa juu kwa Mungu. Watu wote wa Mungu na vitu vyote watamsifu Yeye milele bila kukoma. Ha! Lo! Sayuni ni tukufu sana! Makao ya Mungu hung'aa kwa miale ya mwanga. Utukufu wake hung'aa kotekote ulimwengu mzima. Mwenyezi Mungu huvaa tabasamu, na hukalia enzi Yake akitazama umbo jipya la ulimwengu mzima. Ala!
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Ijumaa, 8 Desemba 2017

Neno Laonekana katika Mwili | Je, Utatu Mtakatifu Upo?

Je, Utatu Mtakatifu Upo?

Ni baada tu ya ukweli wa Yesu kuwa mwili kutokea ndipo mwanadamu alipogundua hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ni sehemu hizo tatu pekee ambazo zimefanywa moja ambazo ni Mungu kamili. Bila Baba Mtakatifu, Mungu asingekuwa mkamilifu. Vivyo hivyo, wala Mungu asingekuwa mkamilifu bila Mwana au Roho Mtakatifu. Katika mawazo yao, wanaamini kuwa Baba au Mwana pekee hawezi kuwa Mungu. Ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu tu kwa pamoja wanaoweza kuwa Mungu Mwenyewe. Sasa, waumini wote wa kidini, akiwemo kila mfuasi miongoni mwenu, anashikilia hii imani. Ilhali, ikiwa hii imani ni sahihi, hakuna anayeweza kuelezea, kwani daima mmechanganyikiwa kuhusu masuala ya Mungu Mwenyewe. Japo hizi ni fikra tu, hamjui kama ni sawa au mbaya, kwani mmeathiriwa vibaya na mawazo ya kidini. Mmeyakubali kwa kina haya mawazo ya kidini yaliyozoeleka, na hii sumu imezama kwa kina ndani yenu. Hivyo basi, hata kwa hili mmeanguka katika huu ushawishi wenye madhara, kwani Utatu haupo. Yaani, Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haupo. Hizi zote ni fikra za kawaida za mwanadamu, na imani za uongo za mwanadamu. Kwa karne nyingi, mwanadamu ameamini katika huu Utatu, ambao umebuniwa na mawazo katika akili za mwanadamu, ukatengenezwa na mwanadamu, na ambao haujawahi kuonekana na mwanadamu. Kwa miaka mingi, kumekuwa na watu maarufu wa kiroho ambao wameeleza “maana ya kweli” ya Utatu, ila maelezo hayo ya Utatu kama nafsi tatu dhahiri yamekuwa si yakini na hayapo wazi na yote yamepumbazwa na “ujenzi” wa Mungu. Hakuna mtu maarufu yeyote aliyewahi kutoa maelezo kamili; maelezo mengi yanafaa katika masuala ya mjadala na katika maandishi, ila hakuna hata mtu mmoja ambaye ana ufahamu kamili na wa wazi kuhusu maana ya Utatu. Hii ni kwa sababu huu Utatu huu mkuu ambao mwanadamu anashikilia moyoni kwa hakika haupo. Kwani hakuna aliyewahi kuiona sura ya Mungu au kubahatika kumtembelea katika makao Yake ili kuchunguza ni vitu gani vipo mahali ambapo Mungu anakaa, kubainisha wazi ni makumi mangapi ya maelfu, au mamia ya mamilioni ya vizazi yako katika “nyumba ya Mungu” au hata kuchunguza ni sehemu ngapi zimeuunga mwili wa asili wa Mungu Kinachofaa hasa kuchunguzwa ni: enzi ya Baba na Mwana, na vilevile Roho Mtakatifu; umbo la kila mmoja; hasa ni vipi Wanajitenganisha, na ni vipi Wanafanywa kuwa kitu kimoja. Kwa bahati mbaya, katika miaka hii yote, hakuna hata mtu mmoja ambaye ameweza kugundua ukweli wa haya mambo. Wote wanabuni tu, kwani hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kwenda mbinguni kwa matembezi na kurejea na “ripoti ya uchunguzi” kwa wanadamu wote ili kuripoti kuhusu ukweli wa mambo kwa wale waumini wote wa kidini wenye bidii na wacha Mungu wanaojishughulisha sana na Utatu Mtakatifu. Bila shaka, mwanadamu hawezi kulaumiwa kwa kubuni na fikra hizo, maana kwa nini Yehova Baba hakuambatana na Yesu Mwana alipomuumba mwanadamu? Ingekuwa hapo mwanzoni kuwa wote waliitwa Yehova, ingekuwa bora zaidi. Ikiwa kuna wa kulaumiwa, wacha lawama iwe kwa kuteleza kwa muda kwa Yehova Mungu, ambaye hakuwaita Mwana na Roho Mtakatifu mbele Zake wakati wa uumbaji, ila badala yake Akafanya kazi Yake peke Yake. Ikiwa Wote Wangefanya kazi wakati mmoja, basi wasingekuwa kitu kimoja? Ikiwa, tangu mwanzo kabisa hadi mwisho, kungekuwa na jina moja tu Yehova pasipo jina la Yesu tangu Enzi ya Neema, au ikiwa Angeitwa bado Yehova, je, Mungu asingeepushiwa na wanadamu taabu ya huu utengano? Kwa hakika, Yehova hawezi kulaumiwa kwa haya yote; kama ni lawama, hebu na iwekwe kwa Roho Mtakatifu, ambaye kwa maelfu ya miaka Aliendelea na kazi yake kwa jina la Yehova, la Yesu, na hata la Roho Mtakatifu, Akiwachanganya na kuwakanganya wanadamu kiasi kwamba wanadamu wakashindwa kufahamu Mungu ni nani hasa. Iwapo Roho Mtakatifu angefanya kazi bila umbo au sura, aidha, bila jina kama vile Yesu, na mwanadamu asingemgusa wala kumuona, ila kusikia tu ngurumo za radi, basi si kazi hiyo ingekuwa ya manufaa zaidi kwa mwanadamu? Hivyo nini kinaweza kufanywa sasa? Fikra za mwanadamu zimerundikana juu kama mlima na kuenea kama bahari, kiasi kwamba Mungu wa sasa hawezi kuzistahimili kamwe na hajui la kufanya. Hapo nyuma wakati kulikuwa tu na Yehova, Yesu, na Roho Mtakatifu katikati ya hao wawili, mwanadamu tayari alikuwa amechanganyikiwa na jinsi ya kuvumilia, na sasa kuna ongezeko la mwenye Uweza, ambaye hata anasemekana kuwa sehemu ya Mungu. Ni nani anajua Yeye ni nani na Ameingiliana au kujificha kwa nani katika Utatu Mtakatifu kwa miaka mingapi? Mwanadamu anawezaje kulistahimili hili? Utatu Mtakatifu pekee ulitosha kumchukua mwanadamu milele kuueleza, lakini sasa kuna “Mungu mmoja katika nafsi nne.” Hili linaweza kuelezewa vipi? Unaweza kulieleza? Ndugu! Mmeaminije katika Mungu huyu mpaka leo? Ninawavulia kofia. Utatu uliweza kuvumilika, na bado mnaendelea kuwa na imani isiyotikisika kwa huyu Mungu mmoja katika nafsi nne. Mmehimizwa muondoke na bado mnakataa. Ajabu iliyoje! Nyinyi ni watu wa ajabu! Mtu kweli anaweza kuendelea kuamini Mungu wanne na asiwaelewe; hamuoni kuwa huu ni muujiza? Sikujua kwamba mlikuwa na uwezo wa kutenda muujiza mkubwa kiasi hiki! Hebu Niwaambie hilo, kwa hakika, Utatu Mtakatifu haupo popote katika dunia hii. Mungu hana Baba wala Mwana, vivyo hivyo hakuna dhana ya chombo kitumiwacho kwa pamoja na Baba na Mwana: Roho Mtakatifu. Huu wote ni uongo mkubwa zaidi na haupo kabisa katika dunia hii! Hata hivyo uongo huu una asili yake na haukosi msingi kabisa, kwani akili zenu si punguani, na mawazo yenu hayakosi mantiki. Badala yake, ziko sawa na yenye ubunifu kwa kiasi kikubwa, kwamba haziwezi kuzuiwa hata na Shetani yeyote. La kusikitisha ni kwamba mawazo haya ni uongo mtupu na hayapo kabisa! Hamjaona ukweli halisi haswa; mnabuni na kujiundia dhana, na kuzitengeneza kuwa hadithi ili kuteka imani ya wengine kwa uongo na kupata mamlaka miongoni mwa wanadamu wapumbavu wasio na busara, ili kwamba waamini katika “mafundisho yenu ya kitaaluma” makuu na mashuhuri. Je, huu ni ukweli? Je, hii ndiyo njia ya uzima ambayo wanadamu wanafaa kupokea? Huu ni upuuzi! Hakuna hata neno moja linafaa! Katika miaka hii yote, nyinyi mmegawanya Mungu namna hii, na kuendelea kugawanywa zaidi katika kila kizazi kiasi kwamba Mungu mmoja amegawanywa kuwa Mungu watatu. Na sasa haiwezekani kabisa kwa mwanadamu kumuunganisha Mungu kuwa mmoja kwani mmemgawanya zaidi. Ingekuwa si kazi yangu ya upesiupesi kabla ya muda kuyoyoma, haijulikani mngeishi hivi kwa muda gani! Kuendelea kumgawanya Mungu namna hii, Anawezaje kuendelea kuwa Mungu wenu? Je, bado mngeendelea kumtambua Mungu? Je, bado mngemrudia? Ningechelewa hata kidogo, inaonekana kwamba mngewarudisha “Baba na Mwana,” Yehova na Yesu kwenda Israeli na mdai kwamba nyinyi wenyewe ni sehemu ya Mungu. Kwa bahati nzuri, sasa ni siku za mwisho. Hatimaye, siku Niliyoitarajia kwa hamu imewadia, na ni baada tu ya kuifanya hatua hii ya kazi kwa mikono Yangu ndipo kumgawanya kwenu Mungu Mwenyewe kumesitishwa. Isingekuwa hivi, mngezidisha, hadi kuwaweka Mashetani wote miongoni mwenu kwenye madhabahu kwa ibada. Hii ndiyo njama yenu! Mbinu yenu ya kumgawanya Mungu! Je, mtaendelea kufanya hivyo sasa? Hebu Niwaulize: Kuna Mungu Wangapi? Ni Mungu Yupi atawaletea wokovu? Je, ni Mungu wa kwanza, wa pili au wa tatu mnayemwomba? Ni nani kati Yao mnayemwamini? Je, ni Baba? Au ni Mwana? Au ni Roho? Niambie ni nani unayemwamini. Ijapokuwa kwa kila neno unasema unamwamini Mungu, mnachokiamini hasa ni akili zenu! Hamna Mungu mioyoni mwenu kabisa! Na bado akilini mwenu mna “Utatu Mtakatifu” kadhaa. Hamkubaliani na hili?

Ikiwa hatua tatu za kazi zitakadiriwa kulingana na dhana hii ya Utatu, basi ni lazima kuwe na Mungu watatu kwani kazi iliyofanywa na kila mmoja si sawa. Ikiwa yeyote miongoni mwenu anasema kwamba hakika Utatu upo, basi eleza huyu Mungu mmoja katika nafsi tatu ni nini hasa. Baba Mtakatifu ni nini? Mwana ni nini? Roho Mtakatifu ni nini? Je, Yehova ni Baba Mtakatifu? Je, Yesu ni Mwana? Basi, Roho Mtakatifu je? Je, Baba si Roho? Je, kiini cha Mwana vilevile si Roho? Je, kazi ya Yesu haikuwa ya Roho Mtakatifu? Je, kazi ya Yehova haikufanywa wakati ule na Roho sawa tu na kazi ya Yesu? Mungu Anaweza kuwa na Roho wangapi? Kulingana na maelezo yako hizi nafsi tatu, yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni mmoja; kama ni hivyo, kuna Roho watatu lakini kuwa na Roho watatu kunamaanisha kuwa kuna Mungu Watatu. Hii inamaanisha kuwa hakuna Mungu Mmoja wa kweli; Mungu wa aina hii anawezaje kuwa kiini asili cha Mungu? Kama unakubali kuwa kuna Mungu mmoja tu, basi Anawezaje kuwa na Mwana na awe Baba? Je, hizi si fikra zako mwenyewe? Kuna Mungu Mmoja tu, nafsi moja katika Mungu huyu, na Roho mmoja tu wa Mungu sawa tu na ilivyoandikwa katika Bibliay kwamba “Kuna tu Roho Mtakatifu mmoja na Mungu mmoja tu.” Haijalishi kama Baba na Mwana unaowazungumzia wapo, kuna Mungu mmoja tu, na kiini cha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu mnaowaamini ni kiini cha Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, Mungu ni Roho, ila Ana uwezo wa kupata Mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu na vilevile kuwa juu ya vitu vyote. Roho Wake anajumuisha kila kitu na Anapatikana kila mahala. Anaweza kuwa katika mwili na wakati ule ule akawa kote duniani. Kwa kuwa watu wanasema kwamba Mungu ndiye tu Mungu wa kweli, basi kuna Mungu mmoja, ambaye hawezi kugawanywa kwa mapenzi ya awaye yote! Mungu ni Roho mmoja tu, na nafsi moja; na huyo ni Roho wa Mungu. Ikiwa ni kama usemavyo, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, basi Hawa si watatu? Roho Mtakatifu ni kitu kimoja, Mwana ni kingine, na Baba vilevile ni kingine. Ni nafsi tatu tofauti zenye viini tofauti, iweje basi ziwe kila moja sehemu ya Mungu mmoja? Roho Mtakatifu ni Roho; hili ni rahisi kueleweka kwa wanadamu. Ikiwa ni hivyo basi, Baba ni Roho zaidi. Hajawahi kushuka kuja duniani na Hajawahi kupata mwili; Yeye ni Yehova Mungu katika mioyo ya mwanadamu, na kwa hakika Yeye vilevile ni Roho. Basi kuna uhusiano gani kati Yake na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Baba na Mwana? Au ni uhusiano kati ya Roho Mtakatifu na Roho wa Mungu? Je, kiini cha kila Roho ni sawa? Au Roho Mtakatifu ni chombo cha Baba? Hili linaweza kuelezwaje? Aidha kuna uhusiano gani kati ya Mwana na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Roho wawili au ni uhusiano kati ya mwanadamu na Roho? Haya yote ni masuala ambayo hayawezi kuelezewa! Ikiwa Wote ni Roho mmoja, basi hapawezi kuwepo na mjadala kuhusu nafsi tatu, kwani zote zinamilikiwa na Roho mmoja. Kama Zingekuwa nafsi tofauti, basi Roho Zao Zingetofautiana katika nguvu zao na kamwe hawangekuwa Roho mmoja. Hii dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni upuuzi mtupu! Hili linamweka Mungu katika vitengo na kumgawanya kuwa nafsi tatu, kila moja ikiwa na hadhi na Roho; basi Atawezaje kuwa Roho mmoja na Mungu mmoja? Hebu niambie, je, mbingu na dunia na vyote vilivyomo viliumbwa na Baba, Mwana, au na Roho Mtakatifu? Wengine husema Waliviumba kwa pamoja. Basi ni nani alimkomboa mwanadamu? Alikuwa Roho Mtakatifu, Mwana, au Baba? Wengine husema ni Mwana aliyewakomboa wanadamu. Basi Mwana ni nani katika kiini? Siye kupata mwili kwa Roho wa Mungu? Mungu aliyepata mwili anamwita Mungu aliye Mbinguni Baba katika mtazamo wa mwanadamu aliyeumbwa. Je, hufahamu kuwa Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba kupitia Roho Mtakatifu. Ndani yake mna Roho Mtakatifu; lolote usemalo, Yeye bado ni mmoja na Mungu wa Mbinguni, kwani Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu. Hili wazo la Mwana si kweli Kabisa. Ni Roho mmoja anayefanya Kazi yote; Mungu Mwenyewe pekee, yaani, Roho wa Mungu anafanya kazi Yake. Roho wa Mungu ni nani? Je, si Roho Mtakatifu? Je, si Roho Mtakatifu anayefanya kazi ndani ya Yesu? Ingekuwa kazi haikufanywa na Roho Mtakatifu (yaani Roho wa Mungu), je, kazi Yake ingemwakilisha Mungu Mwenyewe? Yesu alipomwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba alipokuwa akiomba, hili lilifanywa katika mitazamo ya mwanadamu aliyeumbwa, kwa sababu Roho wa Mungu alikuwa amejivisha kama mwanadamu wa kawaida na Alikuwa na umbile la nje la mwanadamu aliyeumbwa. Hata ikiwa ndani yake mlikuwa na Roho wa Mungu, umbo Lake la nje bado lilikuwa lile la mwanadamu wa kawaida; kwa maana nyingine, Alikuwa “Mwana wa Adamu” jambo ambalo watu wote, akiwemo Yesu Mwenyewe, walilizungumzia. Na kwa sababu Anaitwa Mwana wa Adamu, Yeye ni mtu (Mwanamke au mwanamume, kwa vyovyote vile mwenye umbo la nje la mwanadamu) aliyezaliwa katika familia ya kawaida ya watu wa kawaida. Kwa hivyo, Yesu kumwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba kulikuwa sawa na mlivyomwita mara ya kwanza Baba; Alifanya hivyo kutokana na mtazamo wa Mwanadamu aliyeumbwa. Je, mnakumbuka Sala ya Bwana ambayo Yesu aliwafundisha kukariri? “Baba Yetu Uliye mbinguni….” Aliwaambia wanadamu wote wamwite Mungu wa Mbinguni kwa jina la Baba. Na kwa kuwa Naye pia alimwita Baba, alifanya hivyo kutoka kwa mtazamo wa mtu aliye katika daraja moja nanyi nyote. Kwa kuwa mlimuita Mungu wa mbinguni Baba, hili linaonyesha kuwa Yesu alijichukulia kuwa katika daraja sawa nanyi, kama mwanadamu duniani aliyeteuliwa na Mungu (yaani, Mwana wa Mungu). Kama mnamwita Mungu “Baba,” je, hii si kwa sababu nyinyi ni wanadamu walioumbwa? Haijalishi Yesu alikuwa na mamlaka makubwa kiasi gani duniani, kabla ya kusulubiwa, Alikuwa tu Mwana wa Adamu, akiongozwa na Roho Mtakatifu (yaani, Mungu), Akiwa miongoni mwa viumbe wa duniani, kwani bado Alikuwa hajaikamilisha kazi Yake. Kwa hivyo, kumwita kwake Mungu wa mbinguni Baba kulikuwa tu unyenyekevu na utiifu Wake. Yeye kumwita Mungu (yaani, Roho aliye mbinguni) kwa namna ile, hata hivyo, hakudhibitishi kuwa Yeye ni Mwana wa Roho wa Mungu aliye mbinguni. Badala yake, ni kuwa mtazamo wake ni tofauti, si kwamba ni nafsi tofauti. Uwepo wa nafsi tofauti ni uongo. Kabla ya kusulubiwa kwake, Yesu alikuwa Mwana wa Adamu aliyefungwa katika udhaifu wa kimwili, na Hakuwa na mamlaka kamilifu ya Roho. Hiyo ndiyo maana Angeweza tu kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe. Ni kama tu Alivyoomba mara tatu huko Gethsemane: “Si kama Nitakavyo, bali kama utakavyo.” Kabla Atundikwe msalabani, Hakuwa zaidi ya Mfalme wa Wayahudi; alikuwa Kristo, Mwana wa Adamu, na wala si mwenye utukufu. Hiyo ndiyo maana, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, Alimwita Mungu Baba. Sasa, huwezi kusema kuwa wote wamwitao Mungu Baba ni Wana. Ingekuwa kweli, basi wote si mngekuwa Mwana punde Yesu alipowafundisha Sala ya Bwana? Ikiwa bado hamjaridhika, basi niambieni hili, ni nani mmwitaye Baba? Ikiwa mnamrejelea Yesu, je, Baba ya Yesu ni nani kwenu? Baada ya Yesu kurudi mbinguni, hii dhana ya Baba na Mwana ilikoma. Hii dhana ilifaa tu kipindi ambacho Yesu alikuwa mwili; katika mazingira mengine yoyote, uhusiano ni ule wa kati ya Bwana wa uumbaji na kiumbe mnapomwita Mungu Baba. Hakuna wakati ambapo wazo hili la Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu linaweza kuwa na mashiko; ni uongo ambao ni nadra kuonekana na halipo!

Hili laweza kuwakumbusha watu maneno ya Mungu kutoka katika kitabu cha Mwanzo: “Na tumuumbe mwanadamu katika sura yetu, kwa mfanano wetu.” Ikichukuliwa kuwa Mungu anasema “na tumtengeneze” mtu kwa mfano “wetu,” basi “tu-” inaashiria wawili au wengi; na kwa kuwa anataja “tu-” basi hakuna tu Mungu mmoja. Kwa njia hii, mwanadamu alianza kufikiria udhahania wa nafsi bayana, na kutokana na maneno haya kulitokea dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Basi, Baba anafananaje? Je, Mwana anafananaje? Na Roho Mtakatifu anafananaje? Yawezekana kuwa mwanadamu wa leo aliumbwa kwa mfano wa mtu mmoja aliyeunganishwa pamoja kutoka kwa nafsi tatu? Je, sura ya mwanadamu inafanana na ile ya Baba, Mwana, au Roho Mtakatifu? Mwanadamu ni mfano wa nani katika nafsi za Mungu? Mawazo ya mwanadamu ni ya kimakosa na upuuzi! Yanaweza tu Kumgawanya Mungu kuwa Mungu kadhaa. Wakati Musa aliandika kitabu cha Mwanzo, ni baada ya wanadamu kuumbwa baada ya uumbaji wa dunia. Mwanzo kabisa, dunia ilipoanza, Musa hakuwepo. Ni hadi baadaye kabisa ndipo Musa aliandika Biblia, basi angejuaje alichokinena Mungu kutoka mbinguni? Hakuwa na ufahamu wowote jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu. Katika Agano la Kale la Biblia, hapakutajwa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ni Mungu mmoja tu wa kweli, Yehova, akiifanya kazi yake nchini Israeli. Anaitwa majina tofauti kadri enzi zinavyobadilika, ila hili haliwezi kuthibitisha kuwa kila jina linarejelea mtu tofauti. Ingekuwa hivi, basi je, si kungekuwa na nafsi nyingi sana katika Mungu? Kilichoandikwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova, hatua ya kazi ya Mungu Mwenyewe tangu mwanzo wa Enzi ya Sheria. Ilikuwa ni kazi ya Mungu, ambapo Alinena, ilikuwa, na Alipoamuru, ilitendeka. Hakuna hata wakati mmoja ambapo Yehova alisema kuwa alikuwa Baba aliyekuja kufanya kazi, wala Hakutabiri kuja kwa Mwana kuwakomboa wanadamu. Wakati wa Yesu ulipowadia, ilisemekana tu kwamba Mungu alikuwa Ameupata mwili kuwakomboa wanadamu, si kwamba ni Mwana aliyekuwa amekuja. Kwa sababu enzi hazifanani na kazi ambayo Mungu Mwenyewe hufanya vilevile inatofautiana, Anapaswa kufanya kazi Yake katika milki tofauti, kwa njia hii utambulisho Alionao vilevile unatofautiana. Mwanadamu anaamini kwamba Yehova ndiye Baba ya Yesu, ila hili halijakiriwa na Yesu ambaye alisema: “Hatukubainishwa kamwe kama Baba na Mwana; Mimi na Baba aliye Mbinguni ni kitu kimoja. Baba yu ndani Yangu Nami ni ndani Yake; wanadamu wanapomwona Mwana, wanamwona Baba.” Baada ya yote kusemwa, iwe Baba au Mwana, Wao ni Roho mmoja, Hawajagawanywa kuwa nafsi tofautitofauti. Mara tu wanadamu wanapojaribu kueleza, mambo hutatizwa na wazo la nafsi tofauti, na vilevile na uhusiano kati ya Baba, Mwana na Roho. Mwanadamu akizungumzia nafsi tofauti, je, hili halimfanyi Mungu kuwa kitu? Mwanadamu hata zaidi huziorodhesha nafsi hizi kama nafsi ya kwanza, ya pili, na ya tatu; haya yote ni mawazo ya mwanadamu yasiyofaa kurejelewa, hayana uhalisi kabisa! Ukimwuliza: “Kuna Mungu wangapi?” atasema kuwa Mungu ni Utatu Mtakatifu wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu: Yule mmoja wa kweli. Ukiuliza tena: “Baba ni nani?” atasema: “Baba ni Roho wa Mungu aliye mbinguni; anatawala kila kitu, na kiongozi wa mbinguni.” “Je, Yehova ni Roho?” Atasema: “Ndiyo!” Ukimuuliza tena, “Mwana ni nani?” atasema kuwa Yesu ndiye Mwana, bila shaka. “Basi kisa cha Yesu ni kipi? Alitoka wapi?” Atasema: “Yesu alizaliwa na Maria kupitia kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu.” “Je, kiini Chake si Roho vilevile? Je, kazi Yake si kiwakilishi cha Roho Mtakatifu? Yehova ni Roho, vivyo hivyo na kiini cha Yesu. Sasa katika siku za mwisho, bila shaka ni Roho Anayeendelea kufanya Kazi[a]; Wangewezaje kuwa nafsi tofauti? Je, si Roho wa Mungu anafanya kazi ya Roho kutoka katika mitazamo tofauti?” Kwa hivyo, hakuna tofauti bayana kati ya nafsi. Yesu alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu, na bila shaka, Kazi Yake hasa ilikuwa ile ya Roho Mtakatifu. Katika hatua ya kwanza ya kazi iliyofanywa na Yehova, Hakuwa mwili au kuonekana kwa mwanadamu. Kwa hivyo mwanadamu hakuona uso Wake. Haijalishi Alikuwa mashuhuri au mrefu kiasi gani, bado Alikuwa Roho, Mungu Mwenyewe aliyemuumba mwanadamu mwanzoni. Yaani, alikuwa Roho wa Mungu. Aliponena na wanadamu kutoka mawinguni, alikuwa Roho tu. Hakuna hata mmoja aliyeuona Uso wake; ni katika Enzi ya Neema tu ambapo Roho wa Mungu alikuwa mwili na Alipata mwili kule Uyahudi ndipo mwanadamu aliona sura ya kupata mwili kama Myahudi. Hisia ya Yehova haingeweza kuhisika. Hata hivyo, Alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu, yaani, Alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho wa Yehova Mwenyewe, na Yesu bado alizaliwa kama mfano halisi wa Roho wa Mungu. Alichokiona mwanadamu mwanzoni kilikuwa ni Roho Mtakatifu Akimshukia Yesu kama njiwa; Hakuwa Roho mwenye upekee kwa Yesu tu, badala yake alikuwa Roho Mtakatifu. Basi roho wa Yesu anaweza kutenganishwa na Roho Mtakatifu? Ikiwa Yesu ni Yesu, Mwana, na Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, basi wangewezaje kuwa kitu kimoja? Ingekuwa hivyo kazi isingefanywa. Roho ndani ya Yesu, Roho aliye mbinguni, na Roho wa Yehova wote ni mmoja. Anaweza kuitwa Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho aliyezidishwa mara saba, na Roho mwenye vyote. Roho wa Mungu mwenyewe anaweza kufanya kazi nyingi. Ana uwezo wa kuumba na kuiangamiza dunia kwa kuleta mafuriko duniani; Anaweza kuwakomboa wanadamu, aidha, kuwashinda na kuwaangamiza wanadamu wote. Kazi hii yote inafanywa na Mungu Mwenyewe na haiwezi kufanywa na yeyote katika nafsi za Mungu kwa niaba Yake. Roho Wake anaweza kuitwa Yehova na Yesu, na vilevile mwenye Uweza. Yeye ni Bwana na Kristo. Anaweza pia kuwa Mwana wa Adamu. Yuko mbinguni na vilevile duniani; Yuko juu ya dunia na pia miongoni mwa umati. Yeye tu ndiye Bwana wa Mbingu na dunia! Tangu wakati wa uumbaji hadi sasa, kazi hii imekuwa ikifanywa na Roho wa Mungu Mwenyewe. Iwe ni kazi mbinguni au katika mwili, yote hufanywa na Roho Wake Mwenyewe. Viumbe wote, wawe mbinguni au duniani, wamo katika kiganja cha mkono Wake wenye nguvu; yote hii ni kazi ya Mungu na haiwezi kufanywa na yeyote kwa niaba Yake. Mbinguni Yeye ni Roho na vilevile Mungu Mwenyewe; miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwili ila anaendelea kuwa Mungu Mwenyewe. Japo Anaweza kuitwa mamia ya maelfu ya majina, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, na kazi yote[b] ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Wake. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubiwa Kwake ilikuwa kazi ya moja kwa moja ya Roho Wake, na vilevile tangazo kwa mataifa yote na nchi zote wakati wa siku za mwisho. Wakati wote Mungu anaweza kuitwa mwenye uweza na Mungu mmoja wa kweli, Mungu Mwenyewe mwenye vyote. Nafsi bayana hazipo, aidha dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haipo! Kuna Mungu mmoja mbinguni na duniani!

Mpango wa usimamizi wa Mungu umeenea katika miaka elfu sita na umegawanyika katika enzi tatu kutegemea tofauti katika kazi Yake: Enzi ya kwanza ni Enzi ya Sheria ya Agano la Kale; ya pili ni Enzi ya Neema; na ya tatu ni ile ya siku za mwisho—Enzi ya Ufalme. Katika kila enzi utambulisho tofauti huwasilishwa. Hili linafanywa kwa sababu ya utofauti wa kazi, yaani, mahitaji ya kazi. Hatua ya kwanza ya kazi ilifanyiwa nchini Israeli, na hatua ya pili ya kuhitimisha kazi ya ukombozi ilifanyiwa Uyahudi. Kwa kazi ya ukombozi, Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba wa Roho Mtakatifu na kama Mwana wa pekee. Haya yote yalitokana na mahitaji ya kazi. Katika siku za mwisho, Mungu anadhamiria kupanua kazi Yake katika watu wa Mataifa, na kuwashinda watu wa huko, ili kwamba jina lake liweze kuwa maarufu miongoni mwao. Anadhamiria kumwongoza mwanadamu katika kuzielewa njia zote za uzima wa mwanadamu, pamoja na ukweli na njia ya uzima. Kazi hii yote inafanywa na Roho mmoja. Ijapokuwa Anaweza kufanya hivyo kutoka mitazamo tofautitofauti, asili na kanuni za kazi zinabaki zile zile. Mara tu ukizifuata kanuni na asili ya kazi Waliyoifanya, basi utagundua kuwa ilikuwa kazi ya Roho mmoja. Hata hivyo, wengine wanaweza kusema: “Baba ni Baba; Mwana ni Mwana; Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, na mwishowe, Watafanywa kitu kimoja.” Je, Utawafanyaje kitu kimoja? Baba na Roho Mtakatifu Wawezaje kufanywa kitu kimoja? Ikiwa Walikuwa wawili kiasili, haijalishi Wamewekwa pamoja kwa namna gani, je, Hawataendelea kuwa sehemu mbili? Unaposema kuwa kuwafanya kuwa kitu kimoja, huko si kuunganisha sehemu mbili kutengeneza kitu kamili? Je, Hawakuwa sehemu mbili kabla ya kufanywa kitu kizima? Kila Roho ana kiini kinachotofautiana, na Roho wawili Hawawezi kufanywa kuwa kitu kimoja. Roho si chombo cha kutengenezwa, si kama chombo chochote katika ulimwengu. Kulingana na mitazamo ya wanadamu, Baba ni Roho mmoja, Mwana ni mwingine, na Roho Mtakatifu tena ni mwingine, halafu Roho Hawa huchanganyika sawa na glasi tatu za maji kuunda kitu kimoja kizima. Je, hizo si sehemu tatu zimefanywa kuwa kitu kimoja? Haya ni maelezo ya kimakosa! Je, huku si kumgawa Mungu? Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wanawezaje kufanywa kuwa kitu kimoja? Je, Wao si sehemu tatu zenye asili tofauti? Aidha kuna wale wasemao, je, si Mungu alitaja wazi kuwa Yesu ni Mwanawe mpendwa? Maneno “Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa Naye” bila shaka yalitamkwa na Mungu Mwenyewe. Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, “Baba Yu ndani Yangu Nami ni ndani Yake,” hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe. Kutokana na kubadilika kwa enzi, mahitaji ya kazi, na hatua mbalimbali za mpango Wake wa usimamizi, vilevile jina wamwitalo wanadamu hubadilika. Alipokuja kufanya hatua ya kwanza ya kazi, Angeweza kuitwa tu Yehova, mchungaji wa Waisraeli. Katika hatua ya pili, Mungu mwenye mwili Angeweza kuitwa tu Bwana, na Kristo. Lakini wakati huo, Roho aliye mbinguni alikariri tu kwamba Alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu, bila kutaja kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu. Hili halikufanyika kabisa. Mungu angewezaje kuwa na Mwana wa pekee? Basi, Mungu asingekuwa mwanadamu? Kwa kuwa Alikuwa Mwili, Aliitwa Mwana mpendwa wa Mungu na kutokana na hili, kukazuka uhusiano wa Baba na Mwana. Ni kwa sababu tu ya utengano kati ya mbingu na dunia. Yesu aliomba kutokana na msimamo wa mwili. Kwa sababu Alikuwa Amepata mwili wa ubinadamu wa kawaida, ni kutokana na msimamo wa mwili ndipo Alisema: “Umbo Langu la nje ni la kiumbe. Kwa sababu Nilijivisha mwili kuja duniani, sasa Niko mbali, mbali sana na mbinguni.” Kwa sababu hii, Angeomba tu kwa Baba kutokana na msimamo wa mwili. Huu ulikuwa wajibu Wake, ambao ni sharti Roho wa Mungu aliyepata mwili anapaswa kupewa. Haiwezekani kusema kwamba Hawezi kuwa Mungu kwa sababu tu Anamwomba Baba kutokana na msimamo wa mwili. Ijapokuwa Anaitwa Mwana mpendwa wa Mungu, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, ni vile tu Yeye ni mwili wa Roho, na kiini chake bado ni Roho. Kama wanavyoona wanadamu, wanashangaa ni kwa nini Anaomba ikiwa yeye ni Mungu Mwenyewe. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu mwenye mwili, Mungu aishiye mwilini, bali si Roho aliye mbinguni. Kama anavyoona mwanadamu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wote ni Mungu. Ni kwamba tu wote watatu wanafanywa kuwa kitu kimoja na kudhaniwa kuwa Mungu wa Kweli, na kwa njia hii, uwezo Wake unakuwa mkuu kupindukia. Kuna wanaosema kuwa ni kwa njia hii tu anakuwa Roho aliyezidishwa mara saba. Mwana alipoomba baada ya kuja Kwake, alimwomba Roho. Kwa hakika, alikuwa Akiomba kutokana na msimamo wa kiumbe. Kwa kuwa mwili si kamili, na Hakuwa mkamilifu na pia Alikuwa na udhaifu mwingi Alipokuja katika mwili. Vivyo hivyo Alisumbuka sana Alipoifanya kazi Yake katika mwili. Hii ndiyo maana Alimwomba Mungu Baba mara tatu kabla ya kusulubiwa Kwake, na hata mara nyingi zaidi kabla ya hapo. Aliomba miongoni mwa wanafunzi Wake; Aliomba peke Yake juu mlimani; Aliomba Akiwa Ameabiri dau la uvuvi; Aliomba Akiwa katika umati; Aliomba akiwa anaumega mkate; na kuomba akiwa Anawabariki wengine. Kwa nini Alifanya hivyo? Ilikuwa ni Roho Aliyemwomba; Alikuwa Akimwomba Roho, Alimwomba Mungu aliye mbinguni; kutokana na msimamo wa mwili. Hivyo basi kutoka katika msimamo wa mwanadamu, Yesu alikuwa Mwana katika hatua ile ya kazi. Katika hatua hii hata hivyo, Haombi. Kwa nini? Hii ni kwa sababu Anachokileta ni kazi ya neno, na hukumu na kuadibu kutumia neno. Hana haja ya maombi kwani huduma Yake ni ya kunena. Hajawekwa msalabani, na hashitakiwi na wanadamu kwa wale walio madarakani. Anafanya tu kazi Yake na yote yanakuwa sawa. Wakati Yesu alipoomba, Alikuwa akimwomba Mungu Baba ili ufalme wa mbinguni ushuke, ili mapenzi ya Baba yatimizwe, na ili kazi ifike. Katika hatua hii, ufalme wa mbinguni umeshuka, basi, Ana haja ya kuendelea kuomba? Kazi Yake ni kuihitimisha enzi, na hakuna tena enzi mpya, basi, kuna haja ya kuombea hatua inayofuata? Ninasikitika hakuna haja!

Kuna ukinzani mwingi katika maelezo ya mwanadamu. Kweli, haya ni mawazo ya mwanadamu; bila uchunguzi zaidi, ambayo nyote mngeamini kuwa yako sahihi. Je, hamjui hii dhana ya Mungu kama Utatu Mtakatifu ni mawazo ya mwanadamu tu? Hakuna ufahamu wa mwanadamu ulio mzima na kamili. Mara zote kuna madoa, na mwanadamu ana mawazo mengi mno; hili linaonyesha kuwa kiumbe hawezi kuieleza kazi ya Mungu. Kuna mengi sana katika akili ya mwanadamu, yote yakitokana na mantiki na tafakari, ambayo hukinzana na ukweli. Je, mantiki yako yaweza kuichangua kazi ya Mungu? Je, waweza kupata utambuzi wa kazi yote ya Yehova? Je, ni wewe mwanadamu uwezaye kuona kila kitu, au ni Mungu Mwenyewe awezaye kuona kutoka milele hadi milele? Je, ni wewe mwanadamu uwezaye kuona tangu milele ya zamani sana hadi milele ijayo, au Mungu ndiye Ana uwezo wa kufanya hivyo? Unasema nini? Unafaa vipi kumweleza Mungu? Maelezo yako yametegemezwa katika misingi gani? Wewe ni Mungu? Mbingu na dunia, na vyote vilivyomo viliumbwa na Mungu Mwenyewe. Si wewe uliyelifanya hili, basi ni kwa nini unatoa maelezo yasiyo sahihi? Sasa, unaendelea kuamini katika utatu mtakatifu? Hufikirii kuwa huu ni mzigo mkubwa kwa njia hii? Itakuwa bora kwako kuamini katika Mungu mmoja, si watatu. Ni bora zaidi kuwa mwepesi, kwani “mzigo wa Bwana ni mwepesi.”