Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Njia-ya-Kumjua-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Njia-ya-Kumjua-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 30 Septemba 2019

Ni Lazima Muielewe Kazi; Msifuate kwa Rabsha

Ni Lazima Muielewe Kazi; Msifuate kwa Rabsha!

Kwa sasa kuna watu wengi ambao huamini kwa njia ya rabsha. Udadisi wenu ni mkubwa mno, tamaa yenu ya kufuatilia baraka ni kubwa mno, na hamu yenu ya kufuatilia maisha ni ndogo mno. Waumini katika Yesu siku hizi wamejaa shauku. Yesu atawakaribisha katika nyumba ya mbinguni–je, wao hawawezi kuamini? Watu wengine ni waumini katika maisha yao yote, wameamini kwa miaka arobaini au hamsini, na hawachoki kamwe kusoma Biblia. Hii ni kwa sababu bila kujali kinachotokea, mradi wao wanaamini, wataingia mbinguni. Mmemfuata Mungu kwa njia hii kwa miaka michache tu, lakini tayari mnajitahidi sana na hamna uvumilivu tena. Hii ni kwa sababu hamu yenu ya kupata baraka ina nguvu mno. Nyinyi kuitembea njia hii ya kweli kunadhibitiwa na hamu yenu ya kupata baraka na nyoyo zenu chunguzi. Hamna ufahamu mwingi wa hatua hii ya kazi. Mengi ya yale Ninayoyasema leo siyo kuongea kwa wale watu wanaoamini katika Yesu; hayaongewi hata kidogo kurudisha pigo dhidi ya dhana zao. Kwa kweli, hizi dhana zinazofichuliwa ni dhana zile zile ambazo zipo kati yenu, kwa sababu hamuelewi ni kwa nini Biblia imewekwa chini, kwa nini Ninasema kuwa kazi ya Yehova imezeeka, na kwa nini Ninasema kuwa kazi ya Yesu imezeeka. Kwa kweli, mna dhana nyingi ambazo hamjazipa sauti. Mna dhana nyingi ambazo zimefungiwa ndani ya mioyo yenu, na nyinyi mnafuata umati tu. Je, mnadhani kuwa dhana zenu ni chache? Ni kwamba tu kuwa hamzizungumzii, na hakuna cha ziada! Kwa kweli, mnafuata tu kwa uzembe, hamtafuti njia ya kweli kamwe, na kwa makusudi hamji kupata uzima. Mna mtazamo wa kutaka tu kuona kitakachotokea. Kwa sababu hamjaziacha dhana zenu za zamani, hakuna yeyote kati yenu ambaye ameweza kujitoa mwenyewe kikamilifu. Baada ya kufika wakati huu, nyote mna wasiwasi kuhusu majaliwa yenu wenyewe, mkifikiri mchana na usiku, msiweze kuyaweka chini kamwe. Je, unafikiri kuwa Mafarisayo ambao Mimi nawaongelea ni “wazee” katika dini? Je, si nyinyi ni wawakilishi wa Mafarisayo wa kuendelea mbele zaidi wa enzi ya sasa? Je, unafikiri kwamba wale watu Ninaowataja wanaoniangalia Mimi kwa makini dhidi ya Biblia wanarejelea tu wale wataalamu wa Biblia wa nyanja za kidini? Je, unadhani kwamba Ninapozungumza juu ya wale ambao kwa mara nyingine wanamtundika Mungu msalabani Nazungumzia viongozi wa jamii za kidini? Je, si nyinyi ni wahusika bora kabisa ambao mnaigiza wajibu huu? Je, unafikiri kwamba katika maneno yote Ninayoyanena kurudisha pigo dhidi ya dhana za watu ni mzaha kwa wachungaji na wazee wa dini? Si nyinyi pia mmeshiriki katika mambo haya yote? Je, mnafikiri kuwa mna dhana chache tu? Ni kwamba tu nyote mmejifunza kuwa mahiri sana sasa. Hamzungumzii mambo ambayo hamyafahamu ama kusaliti hisia zenu kuyahusu, lakini mioyo yenu ya heshima na mioyo yenu ya utii haipo tu. Kama mnavyoona, kusoma, kuzingatia, na kusubiri ni matendo yenu makuu ya leo. Mmejifunza kuwa mahiri mno. Je! mnajua, hata hivyo, kwamba hii ni aina yenu ya saikolojia ya ujanja? Je, mnafikiri kuwa wakati wa mahiri kwa upande wenu utawasaidia kuepuka kuadibiwa kwa milele? Mmejifunza kuwa wenye “busara” mno! Na baadhi ya watu huniuliza Mimi mambo kama: “Siku moja, wakati watu wa kidini huniuliza, nini, ‘Mbona Mungu wako hajatenda muujiza hata mmoja?’ Ninafaa kuelezea vipi?” Sasa, siyo tu kwamba watu wa dini watauliza mambo kama hayo. Badala yake, ni kwamba huielewi kazi ya leo, na una dhana nyingi mno. Je, bado hujui ni nani Ninayemrejelea Ninapotaja maafisa wa kidini? Unajua Ninawaelezea nani Biblia? Je, hujui ni kwa nani Ninazungumzia wakati Ninapoeleza kwa mifano hatua tatu za kazi? Je, Singesema vitu hivi, mngeridhishwa kwa urahisi hivyo? Je, mngenyenyekea kwa urahisi hivyo? Je, ni rahisi kwenu kushusha hizo dhana za zamani? Hasa wale “watu halisi” ambao hawajawahi kumtii yeyote–je, wangeweza kutii kwa urahisi sana? Najua kwamba ingawa mna daraja ya chini ya ubinadamu, mna ubora duni sana wa tabia, mna akili ambazo hazijakua sana, na hamna historia ndefu za kumwamini Mungu, kwa kweli mna dhana nyingi kabisa, na asili yenu ya kawaida ni ya kutomnyenyekea yeyote kwa wepesi. Leo, hata hivyo, mnaweza kunyenyekea kwa sababu mnalazimishwa na hamjiwezi; Ninyi ni chui-milia katika kizimba cha chuma, bila uwezo wa kutumia ujuzi wenu. Ingekuwa vigumu kuruka hata kama mngekuwa na mabawa. Ingawa hamjapewa baraka, mnataka kufuata unyounyo. Hata hivyo, hii si roho yenu ya “mtu mzuri”, ila ni kwamba mmeangushwa kabisa, na mnataka kuchanganyikiwa. Ni kwamba kazi yote hii imewaangusha kabisa. Ikiwa kungekuwa na chochote ambacho mngeweza kufikia, hamngekuwa watiifu kama mlivyo leo, kwa sababu awali, nyote mlikuwa punda mwitu nyikani. Hivyo kinachosemwa leo hakielekezwi tu kwa watu wa dini na madhehebu mbalimbali, na siyo kurudisha pigo dhidi ya dhana zao; badala yake ni kurudisha pigo dhidi ya dhana zenu.
Hukumu ya haki imeanza. Je, Mungu bado atatumikia kama sadaka ya dhambi kwa watu? Je, Mungu atachukua nafasi ya daktari mkuu kwa watu tena? Je, Mungu hana mamlaka zaidi ya hivi? Kundi la watu tayari limefanywa kamilifu, na tayari wamenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi. Je, Yeye bado atawafukuza pepo na kuwaponya wagonjwa? Si hili ni jambo la kale? Je, ushuhuda utawezekana kwa kwendelea jinsi hii? Mungu ametundikwa msalabani mara moja, hivyo Atasulubishwa milele? Baada ya kuwafukuza pepo mara moja, Atawafukuza milele? Je, si hili ni sawa na udhalilishaji? Ni wakati tu hatua hii ya kazi inapokuwa juu zaidi kuliko ile ya awali ndipo enzi husonga mbele. Kisha siku za mwisho zitafikiwa, na wakati utakuja ambapo enzi itahitimishwa. Watu wanaofuatilia ukweli kwa hiyo wanapaswa kuzingatia kuwa dhahiri juu ya maono. Huu ndio msingi. Kila wakati Ninapofanya ushirika nanyi kuhusu maono, daima Mimi huona vigubiko vya jicho vya baadhi ya watu vikinyong’onyea na wakianza kushikwa na usingizi, bila kutaka kusikiliza. Wengine huuliza: “Ni kwa nini wewe husikilizi?” Yeye husema, “Hili halisaidii maisha yangu au kuingia kwangu katika hali halisi. Tunachotaka ni njia za matendo.” Wakati Mimi siongei juu ya njia za matendo, na Ninaongea juu ya kazi, anasema, “Punde unapoongea juu ya kazi mimi huanza kushikwa na usingizi.” Sasa Ninaanza kuzungumza juu ya njia za matendo, na anaanza kuchukua muhtasari. Ninaanza tena kuzungumza juu ya kazi hiyo, na anarejelea kutosikiliza. Je, mnajua ni nini mnachopaswa kujiandaa nacho? Jambo moja ni maono juu ya kazi, na jambo jingine ni matendo yako. Lazima ufahamu mambo yote mawili. Kama huna maono katika jitihada zako za kufanya maendeleo katika maisha, basi huna msingi. Kama una njia za matendo tu na huna maono hata kidogo, na huna ufahamu wowote wa kazi ya mpango mzima wa usimamizi, basi wewe ni bure. Lazima uelewe ukweli wa kipengele cha njozi, na kwa ukweli kuhusu matendo, unahitaji kupata njia mwafaka za kutenda mara unapozielewa; unahitaji kutenda kulingana na maneno, na uingie kulingana na hali zako. Maono ndiyo msingi, na usipozingatia hili, hutaweza kufuata hadi mwisho. Unapopitia njia hii, ama utapotea au kuanguka chini na kushindwa. Hakutakuwa na njia ya kufanikiwa! Watu ambao hawana maono makubwa kama msingi wao wanaweza tu kushindwa na si kufanikiwa. Huwezi kusimama imara! Je, unajua kuamini katika Mungu ni nini? Je, unajua kumfuata Mungu ni nini? Bila maono, ni njia gani ungeitembea? Katika kazi ya leo, kama huna maono hutaweza kufanywa mkamilifu kamwe. Unaamini katika nani? Kwa nini unamwamini Yeye? Mbona unamfuata Yeye? Je, unaamini kama aina ya mchezo? Je, unashughulikia maisha yako kama aina ya mtu anayechezewa? Mungu wa leo ndiye maono makubwa zaidi. Je, ni kiasi gani Chake unachokijua? Je, ni kiasi gani Chake ambacho umekiona? Je, baada ya kumwona Mungu wa leo, msingi wa imani yako katika Mungu u salama? Je, unafikiri kwamba mradi unafuata katika njia hii iliyovurugika, utapata wokovu? Unafikiri unaweza kuvua samaki katika maji yenye tope? Je, ni rahisi hivyo? Je, ni maoni mangapi yako kuhusu kile ambacho Mungu wa leo anasema umeweka chini? Je, una maono ya Mungu wa leo? Ufahamu wako wa Mungu wa leo umesimamia wapi? Daima wewe huamini kuwa kwa kufuata unaweza kumpata Yeye, kwamba kwa kumuona Yeye unaweza kumpata,[a] na kwamba hakuna yeyote anayeweza kukukwepa. Usifikiri kwamba kumfuata Mungu ni rahisi sana. Cha muhimu ni kwamba ni lazima umjue Yeye, lazima uijue kazi Yake, na lazima uwe na nia ya kuvumilia shida kwa ajili Yake, uwe na nia ya kutoa maisha yako kwa ajili Yake, na uwe na nia ya kukamilishwa na Yeye. Haya ndiyo maono ambayo unapaswa kuwa nayo. Haitafaidi kama wewe daima unafikiria kufurahia neema. Usifikiri kwamba Mungu yupo tu kwa ajili ya starehe za watu, na kukirimu neema kwa watu. Wewe ulifikiri vibaya! Kama mtu hawezi kuhatarisha maisha yake ili kufuata, ama mtu hawezi kuacha kila mali ya dunia ili kufuata, basi kwa uhalisi hataweza kufuata hadi mwisho. Lazima uwe na maono kama msingi wako. Kama siku ya kupatwa kwako na maafa itakapokuja, unapaswa kufanya nini? Bado ungeweza kufuata? Usiseme kwa wepesi kama utaweza kufuata hadi mwisho. Ni bora kwanza ufungue macho yako wazi kabisa ili uone wakati wa sasa ni upi. Ingawa sasa mnaweza kuwa kama nguzo za hekalu, wakati utakuja ambapo nguzo hizi zote zitatafunwa na funza, na kusababisha hekalu kuanguka, kwa sababu kwa sasa kuna maono mengi sana ambayo mmekosa. Mnachozingatia tu ni dunia zenu wenyewe ndogo, na hamjui njia iliyo ya kutegemewa kabisa, njia iliyo mwafaka zaidi ya kutafuta ni ipi. Hamtilii maanani maono ya kazi ya leo, na hamyashikilii mambo haya mioyoni mwenu. Je, mmefikiria kwamba siku moja Mungu atawaweka katika mahali pasipojulikana? Je, mnaweza kuwazia siku ambayo huenda Nikawapokonya kila kitu, ni kipi kingewakumba? Nguvu yenu siku hiyo ingekuwa vile ilivyo sasa? Je, imani yenu ingejitokeza tena? Katika kumfuata Mungu, lazima myajue maono haya makubwa ambayo ni “Mungu.” Hili ndilo suala muhimu zaidi. Pia, msidhani kwamba katika kuachana na watu wa kidunia ili kuwa watakatifu kwamba nyinyi ni familia ya Mungu. Leo ni Mungu Mwenyewe ambaye anafanya kazi miongoni mwa uumbaji. Ni Mungu aliyekuja miongoni mwa watu kufanya kazi Yake mwenyewe, si kutekeleza kampeni. Miongoni mwenu, hakuna hata wachache ambao wanaweza kujua kwamba kazi ya leo ni kazi ya Mungu aliye mbinguni ambaye amekuwa mwili. Siyo juu ya nyinyi kufanywa watu waliojipambanua wenye vipaji. Badala yake, ni kuwasaidia kujua umuhimu wa maisha ya binadamu, kujua hatima ya binadamu, na kuwasaidia kumjua Mungu na uzima Wake. Unapaswa kujua kwamba wewe ni uumbaji mikononi mwa Muumba. Unachopaswa kufahamu, unachopaswa kufanya, na unavyopaswa kumfuata Mungu—je, huu si ni ukweli unaopaswa kuuelewa? Je, haya si ni maono ambayo unapaswa kuyaona?
Wakati ambapo mtu ana maono ana msingi. Unapotenda kwa msingi wa kanuni hii, itakuwa rahisi zaidi kuingia ndani. Kwa njia hii hutakuwa na wasiwasi juu ya msingi wa kuingia ndani, na itakuwa rahisi sana kwako kuingia ndani. Kipengele hiki cha kuyaelewa maono, cha kuielewa kazi ni muhimu. Lazima muwe mmejiandaa na kipengele hiki. Kama hujajiandaa na kipengele hiki cha ukweli, na wewe huongea tu juu ya njia za matendo, hii ni kasoro kubwa. Nimegundua kwamba wengi wenu hamsisitizi kipengele hiki, na wakati unaposikiliza kipengele hiki cha ukweli ni kama tu kusikiliza maneno ya mafundisho. Siku moja huenda ukapoteza. Kuna baadhi ya maneno sasa ambayo huyafahamu na hujapata maarifa; kwa hiyo unapaswa kutafuta kwa uvumilivu, na siku itakuja utakapoelewa. Jiandae kidogo kidogo. Hata kama unaelewa mafundisho machache tu ya kiroho, ni bora kuliko kutoyazingatia. Ni bora kuliko kutoelewa mafundisho yoyote kamwe. Haya yote ni ya kusaidia kwa kuingia kwako, na yataondoa mashaka hayo yako. Ni bora kuliko kujazwa kwako na dhana. Ni bora zaidi kuwa na maono haya kama msingi. Bila kuwa na wasiwasi kamwe, inawezekana kuingia ndani kwa mikogo na majivuno. Kwa nini kujisumbua daima ukifuata kwa kukanganyikiwa kwa njia ya shaka? Je, hiyo si ni kama kuziba masikio yako wakati unaiba kengele? Ni jambo zuri kama nini kuingia katika ufalme kwa mikogo na majivuno! Kwa nini ujawe wasiwasi? Je, si huku hasa kungekuwa ni kupitia mateso? Unapokuwa na ufahamu wa kazi ya Yehova, wa kazi ya Yesu, na wa hatua hii ya kazi, basi utakuwa na msingi. Sasa unaweza kufikiri kwamba ni rahisi sana. Baadhi ya watu husema, “Wakati Roho Mtakatifu anapoanza kazi hii kubwa, nitakuwa na maneno yote. Ukweli kwamba kwa kweli sielewi sasa ni kwa sababu Roho Mtakatifu hajanipatia nuru sana.” Si rahisi sana; sio kwamba huko tayari kuikubali sasa, na kisha wakati utakapowadia utaitumia kwa ustadi. Si lazima iwe hivyo! Unaamini kuwa sasa umejiandaa vizuri sana, na kwamba haingekuwa shida kuwajibu wale watu wa kidini na wanadhaharia wakuu zaidi, na hata kuwakanusha. Je, ungeweza kweli kufanya hivyo? Je, ni ufahamu upi unaoweza kuuzungumzia na huo uzoefu wako duni tu? Kuwa umejiandaa na ukweli, kupigana vita ya ukweli, na kutoa ushuhuda kwa jina la Mungu si kile unachofikiri ndicho–kwamba mradi Mungu yuko kazini yote yatakamilishwa. Wakati huo labda utatatizwa na swali fulani, na utafadhaishwa. Cha muhimu ni kama uko dhahiri kuhusu hatua hii ya kazi au la, na ni kiasi gani unaielewa. Ikiwa huwezi kuyashinda majeshi ya adui, na wala kuyashinda majeshi ya kidini, basi si wewe ungekuwa bure? Kama umepata uzoefu wa kazi ya leo, ukaiona kwa macho yako mwenyewe na kuisikia kwa masikio yako mwenyewe, lakini mwishowe unashindwa kushuhudia, bado unathubutu kuendelea kuishi? Ungeweza kukabiliana na nani? Usifikiri kwa kawaida sana sasa. Kazi baadaye haitakuwa rahisi kama unavyofikiri itakuwa. Kupigana vita vya ukweli si rahisi au kawaida sana. Sasa unahitaji kujiandaa. Usipokuwa umejiandaa kwa ukweli sasa, wakati utakapowadia na Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa njia ya mwujiza, basi utakuwa umechanganyikiwa.

Jumatatu, 24 Juni 2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Tatu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu alifanya kazi katika siri. Kabla ya mwanadamu kuingia katika ulimwengu huu, kabla ya kukutana na wanadamu hawa, Mungu alikuwa tayari ameviumba vitu hivi vyote. Kila kitu alichofanya kilikuwa kwa ajili ya wanadamu, kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao, na kwa ajili ya kufikiria juu ya kuwepo kwa wanadamu, ili wanadamu waweze kuishi kwa furaha katika ulimwengu huu yakinifu wa ufahari na wingi ambao Mungu aliwatayarishia, bila kuwa na wasiwasi kuhusu chakula au nguo, na bila kukosa chochote. Wanadamu wanaendelea kuzaa na kuendelea kuishi katika mazingira hayo.” Tazama zaidi: Maonyesho ya Mungu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu"
Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia. Watu wengi huuliza: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? (Kuku.) Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai. Baada ya kuatamiza mayai kwa siku 21, kuku huangua. Kisha kuku huyo hutaga mayai, na kuku huanguliwa tena kutoka kwa mayai. Hivyo kuku alitangulia au yai lilitangulia? Mnajibu "kuku" kwa uhakika. Kwa nini? (Biblia inasema Mungu aliumba ndege na wanyama wa mwitu.) Hiyo ina msingi katika Biblia. Ninataka mzungumze kuhusu maarifa yenu wenyewe kuona iwapo mna maarifa ya kweli ya matendo ya Mungu. Je, mna hakika kuhusu jibu lenu au la? (Kwa sababu vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu vinaimarishana na kuzuiana, na kutegemeana vyenyewe. Mungu aliumba kuku, anayeweza kutaga mayai, na kuku anahitaji kuatamiza mayai. Kuna haja hiyo na hali ya utendaji.) Baadhi ya ndugu na dada walicheka. Mbona msizungumze kuhusu jambo hilo? (Mungu aliumba kuku, halafu akampa uwezo wa kuzaa uhai—uwezo wa kuatamiza mayai, na uwezo wa kufanya maisha yaendelee.) Maelezo haya yanakaribia ukweli. Je, ndugu au dada wengine wana maoni? Zungumza kwa huru na kuwasiliana. Hii ni nyumba ya Mungu. Ni kanisa. Ikiwa mna kitu cha kusema, semeni. (Hivi ndivyo ninavyofikiria: Mungu aliumba vitu vyote, na kila kitu alichoumba ni kizuri na kamili. Kuku ni kiumbe hai na ana kazi ya kuzaa na kuatamiza mayai. Hili ni kamili. Kwa hiyo, kuku alitangulia, na kisha yai. Hiyo ndiyo taratibu.) Hili ni hakika. Si fumbo la maana sana, lakini watu wa dunia huliona kuwa la maana sana na hutumia falsafa kwa utoaji hoja. Mwishowe, bado huwa hawana hitimisho. Jambo hili ni kama tu watu kutojua kwamba kuku aliumbwa na Mungu. Watu hawajui kanuni hii, wala hawana uhakika kuhusu iwapo yai au kuku anapaswa kutangulia. Hawajui ni nini kinapaswa kutangulia, hivyo kila mara wao hushindwa kupata jibu. Ni kawaida kabisa kwamba kuku alitangulia. Ikiwa yai lingetangulia kabla ya kuku, basi hiyo haingekuwa kawaida! Bila shaka kuku alitangulia. Hiki ni kitu rahisi sana. Hakiwahitaji nyinyi kuwa wenye maarifa mengi. Mungu aliumba hivi vyote. Kusudi lake la mwanzo lilikuwa ni mwanadamu kuvifurahia. Kuku akiwepo tu yai litakuja kwa kawaida. Je, hilo si dhahiri? Ikiwa yai lingeumbwa kwanza, je, halingehitaji kuku kuliatamiza? Kuumba kuku moja kwa moja ni rahisi kabisa. Kuku angeweza kutaga mayai na pia kuatamiza vifaranga wadogo, huku mwanadamu akiweza kula kuku pia. Je, hilo si la kufaa zaidi. Vile Mungu afanyavyo mambo ni kwa maneno machache ya wazi na sio kwa usumbufu. Yai linatoka wapi? Linatoka kwa kuku. Hakuna yai bila kuku. Alichoumba Mungu ni kiumbe chenye uhai! Wanadamu ni wa upuuzi na wa dhihaka, kila mara wanajitatanisha katika mambo haya rahisi, na mwishowe hata wanafikia kifungu kizima cha hoja za uwongo. Hayo ni ya kitoto! Uhusiano kati ya yai na kuku ni dhahiri: Kuku alitangulia. Hayo ndiyo maelezo sahihi kabisa, njia sahihi kabisa ya kulielewa, na jibu sahihi kabisa. Hii ni ya kweli.
Tumetoka kuzungumzia nini? Hapo mwanzo, tulizungumza kuhusu mazingira ya kuishi ya wanadamu na kile Mungu alifanya, alitayarisha, na kushughulikia kwa ajili ya mazingira haya, na vilevile mahusiano kati ya vitu vyote ambavyo Mungu aliwatayarishia wanadamu na jinsi Mungu alishughulikia mahusiano haya yote kuzuia vitu vyote kuleta madhara kwa wanadamu. Mungu pia alitatua athari hasi katika mazingira ya wanadamu zilizosababishwa na vitu mbalimbali vya asili ambavyo vinaletwa na mambo yote, Akaruhusu vitu vyote kuongeza hadi upeo shughuli za vitu hivyo, na Akawaletea wanadamu mazingira ya kufaa na vitu vyote vya asili vyenye manufaa, kuwawezesha wanadamu kuwa wepesi kubadilika kwa mazingira hayo na kuendelea na mfuatano wa kuzaa na wa maisha kwa kawaida. Kilichofuata kilikuwa chakula kilichohitajika na mwili wa mwanadamu—chakula cha kila siku na kinywaji. Hii pia ni hali muhimu ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Hiyo ni kusema, mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi tu kwa kupumua, kuwa na mwangaza wa jua au upepo pekee, au halijoto za kufaa tu. Wanahitaji pia kujaza matumbo yao. Vitu hivi vya kujaza matumbo yao vyote vimetayarishwa pia na Mungu kwa ajili ya wanadamu—hiki ni chanzo cha chakula cha wanadamu. Baada ya kuona mazao haya ya fahari na mengi—vyanzo vya chakula cha wanadamu na kinywaji—unaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha kupeana wanadamu na vitu vyote? (Ndiyo.) Ikiwa Mungu angeumba tu miti na nyasi au hata viumbe mbalimbali vyenye uhai Alipoumba vitu vyote, na wanadamu hawangekula chochote kati ya hivyo, je, wanadamu wangeweza kuendelea kuishi hadi wakati huu? Na je, viumbe mbalimbali vyenye uhai na mimea miongoni mwa vitu vyote ambavyo Mungu aliumbe vingekuwa vya ng’ombe na kondoo kula, au vya pundamilia, paa na aina nyingine mbalimbali za wanyama—kwa mfano, simba wale chakula kama pundamilia na paa, chui wakubwa wenye milia wale chakula kama wanakondoo na nguruwe—lakini kusiwe na hata kitu kimoja cha kufaa wanadamu kula? Je, hilo lingefaulu? Halingefaulu. Wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi. Na je, wanadamu wangekula tu majani ya miti? Hilo lingefaulu? Matumbo ya wanadamu hayangeweza kustahimili. Huwezi kujua usipojaribu, lakini mara unapofanya hivyo utajua vizuri sana. Basi ungeweza kula nyasi ambayo kondoo hutayarishiwa? Huenda ikawa sawa ukijaribu kidogo tu, lakini ukiendelea kula kwa muda mrefu, hutadumu kwa muda mrefu. Na hata kuna vitu vingine ambavyo vinaweza kuliwa na wanyama, lakini wanadamu wakivila watapata sumu. Kuna vitu vingine vyenye sumu ambavyo wanyama wanaweza kuvila bila kuathiriwa, lakini wanadamu hawawezi kufanya vivyo hivyo. Kwa maneno mengine, Mungu aliwaumba wanadamu, hivyo Mungu anajua vizuri sana kanuni na muundo wa mwili wa mwanadamu na wanachohitaji wanadamu. Mungu ana hakika kamili kuhusu sehemu na vijenzi vyake, na inachohitaji, vilevile jinsi sehemu za ndani ya mwili wa mwanadamu hufanya kazi, hufyonza, huondosha, na kuvunjavunja kemikali mwilini. Watu hawana hakika kuhusu hili na wakati mwingine hula na kujaliza bila kujua. Wao hujaliza kupita kiasi na mwisho husababisha kutolingana nguvu. Ukila na kufurahia vitu hivi alivyokutayarishia Mungu kwa kawaida, hutakuwa na shida yoyote. Hata kama wakati mwingine una hali mbaya ya moyo na una ukwamaji wa damu, haidhuru. Unahitaji tu kula aina fulani ya mmea na ukwamaji utatatuliwa. Mungu ametayarisha vitu hivi vyote. Kwa hivyo, machoni mwa Mungu, wanadamu wako juu zaidi ya kiumbe chengine chote chenye uhai. Mungu alitayarishia kila aina ya mimea mazingira ya kuishi na Akatayarishia kila aina ya wanyama chakula na mazingira ya kuishi, lakini mahitaji ya wanadamu pekee kwa mazingira yao ya kuishi ndiyo makali zaidi na yasiyostahamili kutotunzwa. La sivyo, wanadamu hawangeweza kuendelea kukua na kuzaa na kuishi kwa kawaida. Mungu anajua hili vizuri zaidi moyoni Mwake. Mungu alipofanya hili, alilipa umuhimu zaidi kuliko kitu chengine chochote. Labda huwezi kuhisi umuhimu wa kitu fulani kisicho na maana unachokiona na kufurahia au kitu unachohisi ulizaliwa nacho na unaweza kufurahia, lakini Mungu alikuwa tayari amekutayarishia zamani sana kwa hekima Yake. Mungu ameondoa na kutatua kwa kiwango kikubwa zaidi iwezekanavyo vipengele vyote hasi visivyofaa kwa wanadamu na vinavyoweza kudhuru mwili wa mwanadamu. Nini ambacho hiki kinaweka wazi? Je, kinahakikisha mtazamo wa Mungu kwa wanadamu Alipowaumba wakati huu? Mtazamo huo ulikuwa upi? Mtazamo wa Mungu ulikuwa wa msimamo na maana kubwa, na Hakustahimili kuingilia kati kwa vipengele au hali au nguvu zozote za adui isipokuwa Mungu. Kutokana na hili, unaweza kuona mtazamo wa Mungu alipoumba wanadamu na katika usimamizi Wake wa wanadamu wakati huu. Mtazamo wa Mungu ni upi? Kupitia kwa mazingira ya kuishi na kuendelea kuishi ambayo wanadamu wanafurahia pamoja na chakula chao cha kila siku na kinywaji na mahitaji ya kila siku, tunaweza kuona mtazamo wa Mungu wa wajibu kwao wanadamu ambao Anao tangu Awaumbe, na vilevile uamuzi wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu wakati huu. Je, tunaweza kuona uhalisi wa Mungu kupitia kwa haya yote? Tunaweza kuona ustaajabishaji wa Mungu? Tunaweza kuona kutoweza kueleweka kwa Mungu? Tunaweza kuona kudura ya Mungu? Mungu anatumia tu njia Zake za uweza na hekima kuwapa wanadamu wote, na vilevile kuvipa vitu vyote. Licha ya hayo, baada ya Mimi kusema mengi sana, mnaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo.) Hili ni hakika. Je, mna shaka yoyote? (La.) Upeanaji wa Mungu wa vitu vyote ni wa kutosha kuonyesha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, kwa sababu Yeye ni chanzo cha upeanaji ambao umewezesha vitu vyote kuwepo, kuishi, kuzaa, na kuendelea. Mbali na Mungu hakuna mwingine. Mungu hupeana mahitaji yote ya vitu vyote na mahitaji yote ya wanadamu, bila kujali iwapo ni hitaji la msingi kabisa, wanachohitaji watu kila siku, au upeanaji wa ukweli kwa roho za watu. Kutokana na mitazamo yote, inapofikia utambulisho wa Mungu na hadhi Yake kwa wanadamu, ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Hili ni sahihi? (Ndiyo.) Yaani, Mungu ni Mtawala, Bwana, na Mpaji wa dunia hii yakinifu ambayo watu wanaweza kuona kwa macho yao na kuhisi. Kwa wanadamu, je, huu si utambulisho wa Mungu? Hii ni kweli kabisa. Hivyo unapoona ndege wakiruka angani, unapaswa kujua kwamba Mungu aliumba vitu vinavyoweza kuruka. Lakini kuna viumbe vyenye uhai vinavyoogelea majini, navyo pia huendelea kuishi kwa njia mbalimbali. Miti na mimea inayoishi ndani ya udongo huchipuka katika majira ya kuchipuka na huzaa matunda na kupoteza majani katika majira ya kupukutika kwa majani, na ifikapo wakati wa majira ya baridi majani yote huwa yameanguka na kupitia katika majira ya baridi. Hiyo ni njia yao ya kuendelea kuishi. Mungu aliumba vitu vyote, na kila kimojawapo huishi kupitia taratibu mbalimbali na njia mbalimbali na hutumia mbinu mbalimbali kuonyesha nguvu zake na taratibu ya maisha. Haijalishi ni mbinu gani, yote iko chini ya utawala wa Mungu. Ni nini kusudi la Mungu la kutawala taratibu zote mbalimbali za maisha na viumbe vyenye uhai? Je, ni kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu? (Ndiyo.) Anadhibiti sheria zote za maisha kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hii inaonyesha hasa vile kuendelea kuishi kwa wanadamu ni muhimu kwa Mungu.
Wanadamu kuweza kuendelea kuishi na kuzaa kwa kawaida ni jambo la muhimu zaidi kwa Mungu. Kwa hiyo, Mungu daima huwapa wanadamu na vitu vyote. Anapeana vitu vyote kwa njia mbalimbali, na chini ya hali za kudumisha kuendelea kuishi kwa vitu vyote, Anawawezesha wanadamu kuendelea kusonga mbele ili Aweze kudumisha kuwepo kwa kawaida kwa wanadamu. Hivi ndivyo vipengele viwili tunavyowasiliana leo. Vipengele hivi ni vipi? (Kutokana na mtazamo mkubwa, Mungu aliwaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Hicho ni kipengele cha kwanza. Pia, Mungu alitayarisha hivi vitu yakinifu ambavyo wanadamu wanahitaji na wanaweza kuona na kugusa.) Tumewasilisha mada yetu kuu kupitia vipengele hivi viwili. Mada yetu kuu ni gani? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Mnapaswa sasa kuwa na ufahamu fulani wa mbona Niliwasilisha maudhui haya chini ya mada hii. Je, kumekuwa na majadiliano yoyote yasiyohusiana na mada kuu? Hakuna, sivyo? Labda baada ya kusikia mambo haya, wengine wenu wanaweza kupata ufahamu fulani na kuhisi kwamba maneno haya ni muhimu sana, lakini wengine huenda wakapata tu ufahamu kidogo wa kawaida na kuhisi kwamba maneno haya hayana maana. Haijalishi vile nyinyi mnaelewa hili wakati huu, mnapoendelea kupitia matukio itafika siku ambayo ufahamu wenu utafikia kiwango fulani, yaani, wakati maarifa yenu ya matendo ya Mungu na Mungu Mwenyewe yatafikia kiwango fulani, mtatumia maneno yenu wenyewe ya kiutendaji kuwasilisha ushuhuda wa maana na wa kweli kuhusu matendo ya Mungu.
Ninafikiri ufahamu wenu sasa bado ni sahili na wa kawaida, lakini mnaweza angaa, baada ya kunisikiliza Nikiwasilisha vipengele hivi viwili, kutambua ni mbinu zipi Mungu hutumia kuwapa wanadamu au ni vitu vipi Mungu huwapa wanadamu? Je, mna wazo la msingi na vilevile ufahamu wa msingi? (Ndiyo.) Lakini vipengele hivi viwili Nilivyowasilisha vinahusiana na Biblia? (La.) Vinahusiana na hukumu na kuadibu kwa Mungu katika Enzi ya Ufalme? (La.) Basi kwa nini Niliwasilisha vipengele hivi? Je, ni kwa sababu watu ni lazima wavielewe ili kumjua Mungu? (Ndiyo.) Ni muhimu sana kuvijua na pia ni muhimu sana kuvielewa. Usizuiwe tu kwa Biblia, na usizuiwe tu kwa Mungu kuhukumu na kuadibu wanadamu ili kuelewa kila kitu kuhusu Mungu. Ni nini kusudi la Mimi kusema hili? Ni ili kuwafanya watu wajue kwamba Mungu si Mungu wa watu Wake waliochaguliwa pekee. Wewe sasa unamfuata Mungu, na Yeye ni Mungu wako, lakini kwa wale walio nje ya watu wanaomfuata Mungu, je, Mungu ni Mungu wao? Je, Mungu ni Mungu wa watu wote walio nje ya wale wanaomfuata Yeye? (Ndiyo.) Basi Mungu ni Mungu wa vitu vyote? (Ndiyo.) Basi Mungu hutenda kazi Yake na kutekeleza matendo Yake kwa wale tu wanaomfuata Yeye? (La.) Eneo lake ni ulimwengu mzima. Kutoka kwa mtazamo mdogo, eneo lake ni wanadamu wote na miongoni mwa vitu vyote. Kutokana na mtazamo mkubwa, ni ulimwengu mzima. Hivyo tunaweza kusema kwamba Mungu hufanya kazi Yake na kutekeleza matendo Yake miongoni mwa wanadamu wote. Hili ni la kutosha kuwafanya watu wajue yote kuhusu Mungu Mwenyewe. Ikiwa unataka kumjua Mungu na upate kweli kumjua na kumfahamu Yeye, basi usizuiwe tu katika hatua tatu za kazi ya Mungu, na usizuiwe tu katika hadithi za kazi ambayo Mungu alitekeleza wakati mmoja. Ukijaribu kumjua hivyo, basi unajaribu kumzuilia Mungu kwa mipaka fulani. Unamwona Mungu kama asiye na maana sana. Ni athari gani ungepata kutoka kwa matokeo kama hayo? Hungeweza kujua maajabu na mamlaka ya juu kabisa ya Mungu, na hungeweza kamwe kujua nguvu za Mungu na kudura na eneo la mamlaka Yake. Ufahamu kama huo ungeathiri uwezo wako wa kukubali ukweli kwamba Mungu ni Mtawala wa vitu vyote, na vilevile maarifa yako ya utambulisho wa kweli na hadhi ya Mungu. Kwa maneno mengine, iwapo ufahamu wako wa Mungu umewekewa mipaka katika eneo, unachoweza kupokea pia kimewekewa mipaka. Ndiyo maana ni lazima upanue eneo na kufungua upeo wa macho yako. Iwe ni eneo la kazi ya Mungu, usimamizi wa Mungu, na utawala wa Mungu, au vitu vyote vinavyotawaliwa na kusimamiwa na Mungu, unapaswa kujua yote na kupata kujua matendo ya Mungu yaliyo ndani. Kupitia njia hii ya ufahamu, utahisi bila kujua kwamba Mungu anatawala, anasimamia na kupeana vitu vyote miongoni mwao. Wakati huo huo, utahisi kweli kwamba wewe ni sehemu ya vitu vyote, na kiungo cha vitu vyote. Mungu anapovipa vitu vyote, wewe pia unakubali utawala na upeanaji wa Mungu. Huu ni ukweli usioweza kupingwa na yeyote. Vitu vyote viko chini ya mamlaka ya sheria zao, ambazo ziko chini ya utawala wa Mungu, na vitu vyote vina sheria zao za kuendelea kuishi, ambazo pia ziko chini ya utawala wa Mungu, huku majaliwa ya wanadamu na wanachohitaji pia vikihusiana kwa karibu na utawala wa Mungu na upeanaji Wake. Ndiyo maana, chini ya utawala wa Mungu na uongozi, wanadamu na vitu vyote vinahusiana, vinategemeana, na vinafumana. Hili ni kusudi na thamani ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote. Unaelewa hili sasa? (Ndiyo.) Iwapo unaelewa basi acha tumalizie mawasiliano yetu hapa siku hii. Kwaheri! (Mshukuru Mungu!)