Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushuhuda-wa-Washindi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushuhuda-wa-Washindi. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 15 Desemba 2018

Upendo wa Mungu Ulikuwa Nami Katika Gereza la Giza la Ibilisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Upendo wa Mungu

Upendo wa Mungu Ulikuwa Nami Katika Gereza la Giza la Ibilisi

Yang Yi, Mkoa wa Jiangsu
Mimi ni Mkristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nimekuwa mfuasi wa Mwenyezi Mungu kwa zaidi ya miaka kumi. Katika wakati huu, kitu kimoja ambacho sitawahi kusahau ni taabu mbaya sana nilipokamatwa na polisi wa CCP muongo mmoja uliopita. Wakati huo, licha ya mimi kuteswa na kukandamizwa na ibilisi waovu, na kuwa ukingoni mwa kifo mara kadhaa, Mwenyezi Mungu alitumia mkono Wake wa nguvu kuniongoza na kunilinda, kunirudisha kwa uhai, na kunipeleka kwa usalama…. Kupitia hili, kwa kweli nilipitia uvukaji mipaka na ukuu wa nguvu ya uhai wa Mungu, na kupata utajiri wa thamani wa maisha niliyotunikiwa na Mungu.
Ilikuwa Januari 23, 2004 (siku ya pili ya Mwaka Mpya wa Kichina). Nilihitaji kuenda kumtembelea dada fulani kutoka kwa kanisa; alikuwa katika shida na alihitaji msaada kwa dharura. Kwa kuwa aliishi mbali sana, ilinibidi nirauke mapema ili kupata teksi ili niweze kurudi siku hiyo hiyo. Niliondoka nyumbani wakati tu mwanga ulichomoka. Kulikuwa na watu wachache sana barabarani, wafanyikazi wa kusafisha taka pekee. Kwa wasiwasi nilitafuta teksi, lakini hakukuwa na yoyote hapo. Nilienda kwa stesheni ya teksi kusubiri, na nikasongea kwa barabara kusimamisha moja nilipoiona ikija—lakini ikatokea kuwa gari la Shirika la Kulinda Mazingira. Waliniuliza mbona niliwasimamisha. “Naomba radhi, ilikuwa makosa, nilidhani mlikuwa teksi,” nilisema. “Tunafikiri ulikuwa ukitundika mabango yasiyo halali,” walijibu. “Je, mliniona? Yako wapi mabango niliyokuwa nikitundika?” nilisema. Bila kunipa fursa ya kujitetea, wao watatu walikimbia mbele na kwa nguvu walichunguza mfuko wangu. Walipekua kila kitu katika mfuko wangu—nakala ya mahubiri, kitabu cha kuandikia, pochi, simu ya rununu na bipa iliyoondolewa uwezo, na kadhalika. Kisha walichunguza kwa makini nakala hiyo ya mahubiri na kitabu cha kuandikia. Kwa kuona kwamba hakukuwa na mabango ndani ya mfuko wangu, waliinua nakala hiyo ya mahubiri na kusema: “Yaweza kuwa hukuwa ukitundika mabango yasiyo halali, lakini unamwamini Mwenyezi Mungu.” Kisha, walipigia simu Divisheni ya Dini ya Kikosi cha Usalama wa Taifa. Punde baadaye, watu wanne kutoka kwa Kikosi cha Usalama wa Taifa waliwasili. Walijua kwamba nilikuwa muumini wa Mwenyezi Mungu punde walipoona vitu ndani ya mfuko wangu. Bila kuniruhusu kusema lolote, walinitupa ovyo katika gari lao, kisha walifunga mlango kwa ufunguo ili kunikomesha kuhepa.
Tulipowasili katika Shirika la Usalama wa Umma, polisi waliniongoza kuingia katika chumba. Mmoja wao alichezacheza na bipa na simu yangu ya rununu, akitafuta dokezo. Aliwasha simu lakini ikaonyesha kwamba ilikuwa na betri ya chini, kisha ikasema betri ilikuwa tupu kabisa. Ingawa alijaribu sana, hangeweza kuiwasha. Akishika simu, alionekana kuwa na wasiwasi. Nilikanganywa pia—nilikuwa nimechaji simu hiyo asubuhi hiyo. Inawezekanaje iwe haina chaji? Ghafla nilitambua kwamba Mungu alikuwa amepanga hili kwa miujiza ili kuzuia polisi kupata taarifa yoyote kuhusu ndugu wengine. Pia nilielewa maneno yaliyonenwa na Mungu: “vitu vyote, vilivyo hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, vitafanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu anavyotawala juu ya kila kitu” (Kutoka kwa “Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Hili lilinipa ufahamu wa kweli wa ukuu na mpango wa Mungu wa mambo yote, na kuimarisha imani yangu katika ushirikiano wa baadaye. Akiashiria vitu ndani ya mfuko wangu, afisa wa polisi aliuliza kwa shutuma: “Haya yanaonyesha kwamba kwa kweli wewe si mshirika wa kawaida wa kanisa. Lazima uwe mmoja wa uongozi mkubwa, mtu ambaye ni muhimu. Kwa maana viongozi wadogo hawana bipa ama simu za rununu. Niko sahihi?” “Sielewi unachosema,” nilijibu. “Unajifanya huelewi!” alisema kwa sauti kubwa, kisha akaniamuru kuchuchumaa nilipozungumza. “Huku akiona kwamba singeshirikiana, walinizingira na kuanza kunipiga ngumu na kunipiga teke—kiasi cha kutosha kuniua. Uso wangu ukiwa umejaa damu na kuvimba, mwili wangu mzima ukiuma kiasi cha kutovumilika, nilianguka sakafuni. Nilikasirishwa. Nilitaka kuzungumza maana kwao, kutoa sababu ya kuthibitisha hali yangu: Nimekosea wapi? Mbona mlinichapa hivyo? Lakini sikuwa na njia ya kuongea maana nao, kwa sababu serikali ya CCP haiongei maana. Nilikanganyikiwa, lakini sikutaka kukubali vipigo vyao. Nilipokuwa tu sijui la kufanya, ghafla nilifikiri jinsi, kwa kuwa hawa maofisa waovu wa serikali ya CCP walikuwa wapuuzi sana, kwa kuwa hawakuwa wakiniruhusu kuzungumza maneno yoyote ya maana, sikuhitaji kuwaambia chochote. Ilikuwa ni heri nibaki kimya—kwa njia hiyo singekuwa na manufaa yoyote kwao. Nilipofikiri hili, niliacha kutia maanani walichokuwa wakisema.
Huku wakiona kuwa mtazamo huu haukuwa na athari yoyote kwangu, polisi hao waovu walikasirika sana na wakawa katili hata zaidi: Waligeukia mateso ili kutoa ili kunifanya nikiri. Walinitia pingu kwa kiti cha chuma kilichokazwa kwa skrubu sakafuni kwa njia ambayo singechuchumaa wala kusimama. Mmoja wao aliweka mkono wangu ambao hukuwa umetiwa pingu kwa kiti na kuupiga kwa kiatu, akikomesha tu wakati upande wa nyuma wa mkono wangu ulikuwa umegeuka rangi kuwa mweusi na samawati: mwingine aliponda vidole vyangu vya miguu chini ya kiatu chake cha ngozi. Ni hapo tu ndipo nilipitia kwamba uchungu katika vidole huenda moja kwa moja hadi moyoni. Baada ya hapo, polisi wasita ama saba walichukua zamu kwangu. Mmoja wao alilenga viungo vyangu, na kuvichuna kwa nguvu sana kiasi kwamba mwezi mmoja baadaye bado singeweza kuupinda mkono wangu. Mwingine alinyakua nywele zangu na kutingisha kichwa changu upande mmoja kuelekea upande mwingine, kisha akakivuta kwa ghafla nyuma ili nilikuwa nikiangalia juu. “Tazama anga na kuona iwapo kuna Mungu!” alisema kwa ukali. Waliendelea hadi usiku. Wakiona kwamba hawangepata chochote kutoka kwangu, na kwa sababu ilikuwa Mwaka Mpya wa Kichina, walinituma moja kwa moja hadi katika kituo cha kuzuia.
Nilipowasili katika kituo cha kuzuia, mlinzi alimwamuru mfungwa wa kike kunivua nguo zote na kuzirusha katika pipa la takataka. Kisha walinifanya nivae sare chafu ya gereza, iliyokuwa ikinuka vibaya. Walinzi waliniweka katika seli na kisha wakawadanganya wafungwa wengine, wakisema: “Yeye hasa alivunja familia za watu. Familia nyingi zimeharibiwa na yeye. Yeye ni mwongo, huwadanganya watu waaminifu, na kuvuruga utulivu wa umma….” “Mbona anafanana na punguani?” mmoja wa wafungwa aliuliza. Kwa hilo walinzi walijibu: “Anajifanya kuepuka kuhukumiwa. Ni nani kati yenu aliye mwerevu hivyo? Yeyote anayefikiri yeye ni mpumbavu ni mjinga kabisa kwa wote.” Hivyo wakiwa wamedanganywa na walinzi hao, wafungwa wengine wote walisema nilikuwa nikisamehewa kwa urahisi sana, na kwamba kitu kizuri pekee kwa mtu ambaye ni mbaya kama mimi kilikuwa kikosi cha wauaji! Kusikia hili kulinikasirisha—lakini hakukuwa na chochote ambacho ningeweza kufanya. Majaribio yangu ya upinzani yalikuwa bure, yalileta tu mateso na ukatili zaidi. Katika kituo cha kuzuia, walinzi waliwafanya wafungwa kukariri amri kila siku: “Kiri uhalifu wako na kutii sheria. Kuwashawishi wengine kutenda uhalifu hakukubaliwi. Kuunda magenge hakukubaliwi. Kupigana hakukubaliwi. Kuwadhulumu wengine hakukubaliwi. Kutoa mashtaka yasiyo kweli dhidi ya wengine hakukubaliwi. Kunyakua chakula ama mali ya wengine hakukubaliwi. Kufanya hila kwa wengine hakukubaliwi. Wadhalimu wa gerezani wanapaswa kuchukuliwa hatua kali. Ukiukaji wowote wa sheria unapaswa kuripotiwa kwa wasimamizi ama polisi wenye madaraka mara moja. Unapaswa kutoficha ukweli ama kujaribu kulinda wale wafungwa ambao wamekiuka sheria na kufuatia kunapaswa kuwa kwa kwenye huruma. …” Kwa kweli, walinzi waliwatia moyo wafungwa wengine kunitesa, wakiwaruhusu kunitendea hila kila siku: Wakati ambapo halijoto ilikuwa digrii 8 ama 9 chini ya sufuri, walilowa viatu vyangu: kwa siri walimwaga maji kwenye chakula changu: jioni, nilipokuwa nikilala, walirowesha jaketi langu lililojazwa pamba: walinifanya nilale kando ya choo, mara kwa mara walivuta mfarishi wangu usiku, walivuta nywele zangu, ili kunizuia kulala; walininyang’anya andazi langu lilikopikwa kwa mvuke, walinilazimisha kusafisha choo, na kuingiza kwa nguvu dawa zao zilizosalia ndani ya mdomo wangu, hawakuniacha nikojoe…. Wakati sikufanya walichosema, wangechangia na kunipiga—na mara nyingi wakati kama huu wasimamizi ama polisi walio na mamlaka wangetoroka wasionekane ama kujifanya hawajaona chochote; wakati mwingine wangejificha mbali na kutazama. Iwapo wafungwa wangekaa siku chache bila kunitesa, wasimamizi na polisi wenye mamlaka wangewauliza: “Yule mwanamke mjinga ameerevuka siku hizi chache, siyo? Wakati huo, ninyi mmekuwa wajinga. Yeyote atakayembadilisha huyo mwanamke mjinga atapata msamaha.” Mateso ya kikatili ya hao walinzi yalinijaza na chuki kwao. Leo, iwapo singeona hili na macho yangu mwenyewe na kulipitia mimi binafsi, kamwe singeamini kwamba serikali ya CCP, ambayo inapaswa kuwa imejaa ukarimu na maadili, ingeweza kuwa ovu, ya kuogofya na mbaya—singewahi kuona sura yake ya kweli, sura ambayo ni danganyifu na yenye unafiki. Mazungumzo yake yote ya “kuhudumia watu, kutengeneza jamii iliyostaarabika na ya upatanifu”—huu ni uongo ulioundwa kuwadanganya na kuwahadaa watu, ilikuwa njia, hila, ya kujipendekeza na kupata heshima haifai kupata. Wakati huo, nilifikiri kuhusu maneno ya Mungu: “Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo mashetani hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa mashetani anayeua watu kwa kufumba na kufumbua, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, na hawana hata chembe ya wema, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi!” (Kutoka kwa “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nikilinganisha maneno ya CCP na uhalisi, niliona asili ovu na mbaya ya serikali ya CCP ya shetani kwa ubayana kamili. Kudumisha mamlaka yake ovu, inaweka mshiko uliobanwa kwa watu wake, na kufanya kila kitu kuwalaghai na kuwadanganya. Kwa juu juu, inadai kutoa uhuru wa dini—lakini kwa siri, inawakamata, kuwakandamiza, kuwatesa, na kuwaua watu kutoka kila pande zote za nchi ambao wanamwamini Mungu. Hata inajaribu kuwaua wote. Jinsi gani ibilisi alivyo mjanja, katili, na asiyependa maendeleo! Uhuru uko wapi? Haki za binadamu ziko wapi? Je, si zote ni hila za kutumia kuwadanganya watu? Je, watu wanaweza kuona mara moja matumaini ama mwanga wowote wakiishi chini ya utawala wake muovu? Wanawezaje kuwa huru kumwamini Mungu na kufuatilia ukweli? Hapo tu ndipo nilitambua kwamba Mungu alikuwa ameruhusu mateso na majaribu haya kunifikia, kwamba Alikuwa ameitumia kunionyesha ubaya na ukatili wa serikali ya CCP, ili kunionyesha asili yake ya shetani ambayo ina uadui na ukweli na ya uhasama kwa Mungu, na kunionyesha kwamba polisi wa watu, ambao serikali kwa nguvu huwajenga na kuwatangaza kama wanaoadhibu uovu, kutetea wema, na kukuza haki, ni washirika na watumishi imelea kwa uangalifu, kundi la wauaji ambao wana sura za wanaume lakini mioyo ya wanyama, na ambao wangeua kufumba kufumbua. Ili kujaribu kupiga marufuku na kukomesha kazi ya Mungu, na kunilazimisha kukataa na kumsaliti Mungu na kukubali nguvu yake ya dikteta, serikali ya CCP ilifanya kila kitu kunitesa na kuniangamiza—ilhali haikujua hata kidogo kwamba kadiri ilivyonitesa, ndivyo niliona sura yake ya ibilisi kwa wazi kabisa, na ndivyo nilivyoidharau na kuikataa zaidi kutoka kwa vina vya moyo wangu, kunifanya kumtamani sana Mungu kwa kweli na kumwamini Mungu. Hata zaidi, ilikuwa hasa kwa sababu ya mateso ya walinzi ndipo bila kutambua nilikuja kuelewa kinachomaanisha kweli kupenda anachopenda Mungu na kuchukia anachochukia Mungu, kinachomaanisha kumkwepa Shetani na kugeuza moyo wa mtu kwa Mungu, kinachomaanisha kuwa katili, nguvu za giza ni nini, na zaidi ya hayo, kinachomaanisha kuwa mbaya sana na mwenye kudhuru kwa siri, na mwongo na mdanganyifu. Nilimshukuru Mungu kwa kuniruhusu nipitie hali hii, kwa kuniruhusu kujua sahihi kutoka kwa isiyo sahihi na kuona njia sahihi ya maisha ambayo napaswa kuchukua. Moyo wangu—ambao ulikuwa umedanganywa na Shetani kwa muda mrefu sana—hatimaye uliamshwa na upendo wa Mungu. Nilihisi kwamba kulikuwa na maana kuu katika mimi kuwa na bahati ya kupitia jaribio na majaribu haya, kwamba kwa kweli nilikuwa nimeonyeshwa fadhili maalum.
Baada ya kujaribu kila kitu kingine, polisi waovu waliunda mpango mwingine: Walimpata mchungaji kutoka kwa kanisa la Nafsi Tatu ambaye alinijua kunifichua. Alisema nilimwamini Mwenyezi Mungu na wakati mmoja nilijaribu kueneza injili kwake—lakini alikuwa amekataa. Na pia alijaribu kunifanya nimkwepe Mungu. Kwa kuona huyu mtumishi mwovu ambaye alikuwa amewaripoti ndugu wengi ambao walieneza injili, na kwa kusikia maneno yote mabaya yaliyotoka mdomoni mwake—maneno yaliyosingizia, kukashifu, na kukufuru dhidi ya Mungu—moyo wangu ulijawa na ghadhabu. Nilitaka kumpigia kelele, kuuliza mbona alikuwa na uhasama kwa Mungu mno. Kwa nini iwe kwamba alifurahia sana neema ya Mungu, ilhali alikuwa ameshirikiana na ibilisi waovu kuwatesa wateule wa Mungu? Katika moyo wangu, kulikuwa na huzuni na uchungu usioelezeka. Nilihisi pia hisia kubwa ya huzuni na mwenye deni; kwa kweli nilijichukia kwa jinsi, zamani, sikuwa nimejaribu kufuatilia ukweli, na sikuwahi kujua lolote isipokuwa furaha ya neema na baraka za Mungu kama mtoto mjinga, nisitilie maanani uchungu na fedheha ambayo Mungu alikuwa amestahimili kwa ajili ya wokovu wetu. Ni sasa tu, nilipokuwa ndani sana ya pango la ibilisi, ndipo nilihisi jinsi ilivyokuwa vigumu kwa Mungu kufanya kazi katika nchi hii chafu, potovu, na jinsi uchungu Aliokuwa amepitia ulivyokuwa mkubwa! Kwa kweli, upendo wa Mungu kwa mwanadamu hubeba uchungu mkubwa. Anafanya kazi ya kumwokoa mwanadamu huku Akivumilia usaliti wa mwanadamu. Usaliti wa mwanadamu umemletea Yeye uchungu na maumivu pekee. Si ajabu Mungu alisema wakati mmoja: “Hata kama ni kwa muda wa usiku mmoja tu, wao watatoka katika hali ya tabasamu, watu wenye “mioyo mikunjufu” hadi wenye sura mbovu na wauaji wakatili, ghafla wakiwatendea wafadhili wao wa jana kana kwamba ni adui wa milele, bila chanzo wala sababu” (Kutoka kwa “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Leo, ingawa nilikuwa nimetumbukia katika mishiko ya ibilisi, singemsaliti Mungu bila kujali chochote. Bila kujali taabu kubwa niliyopitia, singekuwa Yuda kwa ajili ya kujiokoa. Singemsababishia Mungu uchungu na huzuni. Kwa ajili ya mimi kusalitiwa na huyu mchungaji kutoka kwa jamii ya dini, polisi waovu waliongeza mateso yao. Yeye, wakati huo, alisimama upande mmoja na kusema: “Hujui kutofautisha mazuri kutoka kwa mabaya. Unastahili hili! Huthamini ukarimu wangu. Unastahili kuteswa hadi kufa!” Kusikia maneno haya mabaya, maovu kulinikasirisha—lakini pia nilihisi hisia isiyoelezeka ya huzuni. Nilitaka kulia, lakini nilijua haikunipasa kufanya hivyo. Moyoni mwangu, niliomba kwa siri: Ee Mungu! Ningependa upate moyo wangu. Ingawa siwezi kukufanyia lolote wakati huu, nataka kukutolea ushuhuda wa ushindi mbele ya Shetani na mtu huyu mwovu, kuwaaibisha kabisa, na kupitia hili kuleta faraja kwa moyo Wako. Ee Mungu! Ningependa ulinde moyo Wangu, na kunifanya kuwa mwenye nguvu zaidi. Iwapo nina machozi, naomba yatiririke kwa ndani—siwezi kuwaruhusu waone machozi yangu. Napaswa kuwa na furaha kwa sababu naelewa ukweli, kwani umeng’arisha macho yangu, Ukinipa uwezo wa kutofautisha, na kuona kwa dhahiri asili na kiini cha Shetani, ambacho ni kukupinga, kukusaliti, na kuvunja kazi Yako. Katikati ya usafishaji, nimeona pia jinsi mkono Wako wenye hekima hupanga yote. Nataka kuendelea kushirikiana na Wewe, hadi ushindi uwe Wako. Baada ya kuomba, moyoni mwangu kulikuwa na nguvu ya kutopumzika hadi nilipomaliza ushuhuda wangu kwa Mungu. Nilijua kwamba hili lilikuwa limepewa kwangu na Mungu, kwamba Mungu alikuwa amenipa ulinzi mkubwa na kunisisimua sana. Polisi waovu walitaka kutumia mtu mwovu kunifanya kumsaliti Mungu, lakini Mungu ni Mungu mwenye hekima, na Alitumia mtu huyo mwovu kama mfano unaopinga kunionyesha asili ya uasi ya wanadamu wapotovu, Akichangamsha azimio na imani yangu kumridhisha Mungu. Hata zaidi, nilikuwa na ufahamu fulani wa kazi ya hekima ya Mungu, niliona kwamba Mungu hutawala na kushawishi yote yaliyo katika huduma kukamilisha watu wa Mungu. Huu ni ukweli dhabiti wa utumizi wa Mungu wa hekima kumshinda Shetani.
Kwa kuona kuwa hawangeniruhusu kusema chochote nilichotaka, walitumia kila gharama—iwe ikama, ama vifaa na rasilmali za fedha—kufanya juu chini kuuliza dhibitisho kwamba nilikuwa muumini wa Mungu. Baada ya miezi mitatu, kuharakisha kote kwao huku na kule hakukuwa kumezaa matunda. Mwishowe, walijaribu kupiku: Walimpata mhojaji stadi. Ilisemekana kwamba kila mtu aliyeletwa kwake alipitia aina zake tatu za mateso, na hakuna mbaye hakuwahi kukiri. Siku moja, maafisa wanne wa polisi walikuja na kuniambia: “Leo, tunakupeleka nyumbani mpya.” Kisha, walinisukuma kwa gari la kusafirisha wafungwa, kufunga pingu mikono yangu nyuma ya mgongo wangu, na kuweka kifuniko kichwani mwangu. Hali ilinifanya nifikiri walikuwa wakinipeleka kuniua kwa siri. Moyoni mwangu, sikuweza kujizuia kuwa na hofu. Lakini baadaye, nilifikiri kuhusu wimbo ambao nilikuwa nikiimba nilipomwamini Yesu: “Tangu nyakati za awali kabisa za kanisa, wale ambao humfuata Bwana wamelazimika kulipa gharama ya juu. Makumi ya maelfu ya jamaa wa kiroho wamejitoa kwa injili, na hivyo wamepata uzima wa milele. Kifo cha kishahidi kwa ajili ya Bwana, niko tayari kufa shahidi kwa ajili ya Bwana.” Siku hiyo, hatimaye nilielewa wimbo huo: Wale wanaomfuata Bwana lazima walipe gharama ya juu. Mimi pia nilikuwa tayari kufa kwa ajili ya Mungu. Kustaajabika, baada ya kuingia kwa gari, bila kuwa mwangalifu nilisikia bila kusudia mazungumzo baina ya polisi waovu. Ilionekana walikuwa wakinipeleka mahali pengine kuhojiwa. Aa! Hawakuwa wakinipeleka kuuawa—na nilikuwa nimejitayarisha kufa shahidi kwa ajili ya Mungu! Nilipokuwa tu nikifikiria hili, kwa sababu fulani zisizojulikana mmoja wa polisi alikaza kamba za ukaya kichwani mwangu. Punde baadaye, nilianza kuhisi kutotulia–ilihisi kana kwamba nilikuwa nikisongwa. Nilijipata nikijiuliza iwapo kwa kweli wangenitesa hadi nife. Wakati huo, nilifikiri kuhusu jinsi wanafunzi wa Yesu walikuwa wamejitoa kueneza injili. Singekuwa mwoga. Hata iwapo ningekufa, singewasihi wailegeze, hata zaidi singekubali kushindwa. Lakini sikuweza kujidhibiti: Nilizirai na kuwaangukia. Huku wakiona kilichokuwa kikitendeka, polisi kwa haraka walilegeza kifuniko. Nilianza kutoa povu mdomoni, kisha sikuweza kuacha kutapika. Ilihisi kana kwamba ningetapika mpaka matumbo yangu yatoke nje. Nilihisi kizunguzungu, kichwa changu kilikuwa kitupu, na singeweza kufungua macho yangu. Sikuwa na nguvu popote mwilini mwangu kana kwamba nilikuwa nimepooza. Ilihisi kana kwamba kulikuwa na kitu cha kunata mdomoni mwangu ambacho singeweza kutoa. Daima nilikuwa dhaifu, na baada ya kuteswa namna hii nilihisi kwamba nilikuwa taabani, kwamba ningeacha kupumua wakati wowote. Katikati ya uchungu, nilimwomba Mungu: “Ee Mungu! Iwapo Unataka nishuhudie kifo Kwako, kwa furaha nakutii, na kwa furaha kutumia kifo kukuridhisha. Najua kwamba wale wanaokufa kwa jina la Mungu hawakufi, ila wanalala. Naamini kwamba chochote Unachofanya, ni cha haki, na ningependa kwamba Uulinde moyo wangu, ili kwamba niweze kustahi yote ambayo Unapanga na kuweka kwa utaratibu.” Wakati mwingine baadaye, gari liliwasili kwa hoteli fulani. Wakati huo, mwili wangu wote ulihisi mnyonge na singeweza kufungua macho yangu. Walinibeba hadi kwa chumba kilichofungwa kabisa. Yote ambayo ningesikia ilikuwa sauti ya watumishi wengi wa serikali ya CCP waliokuwa wamesimama wakinizingira wakinijadili, wakisema kwamba kuniona kulikuwa kama kuona jinsi Liu Hulan alivyokuwa. Ilikuwa kitu kilichozindua, cha kuvutia sana! Yeye hata ni sugu kuliko jinsi Liu Hulan alivyokuwa! Kwa kusikia hili, moyo wangu ulifura kwa msisimko. Niliona kwamba Mwenyezi Mungu alilazimika kuwa mshindi, kwamba Shetani alikuwa chini ya miguu ya Mungu! Nilimshukuru na kumsifu Mungu kwa kunipa imani na utiifu. Wakati huu, nilisahau uchungu. Nilihisi kufurahishwa pakubwa mno kutukuzwa na Mungu.
Punde baadaye, “mtaalamu wa mahojiano” ambaye polisi walimzungumzia aliwasili. Punde alipoingia, alipaza sauti: “Yuko wapi huyo mwanamke mjinga? Acha nimwone!” Alitembea mbele yangu na kunishika kwa nguvu. Bada ya kunizaba makofi mara kadhaa usoni, alinipiga ngumi za nguvu mara kadhaa kifuani na mgongoni, kisha akaondoa kiatu chake moja cha ngozi na kunipiga usoni nacho. Baada ya kuchapwa naye hivi, nilipoteza hisia kwamba kulikuwa na kitu ambacho singeondoa mdomoni ama tumboni mwangu. Kuchanganyikiwa kuliacha kichwa changu na ningeweza kufungua macho yangu. Hisia polepole ilirudi katika viungo vyangu, na nguvu ilianza kurudi mwilini mwangu. Kisha, kwa ukali alinyakua mabega yangu na kunisukuma nyuma dhidi ya ukuta, akiniamuru nimwangalie na kujibu maswali yake. Kuona kwamba sikuwa namzingatia hata kidogo kulimfanya akasirike sana, na alijaribu kupata mjibizo kutoka kwangu kupitia kutukana, kukashifu na kumkufuru Mungu. Alitumia mbinu duni, za kustahili dharau kabisa kuniambika, na kusema kwa kuogofya: “Kwa makusudi nakutesa kwa kutumia kile kisichovumilika na mwili na nafsi yako, ili kukufanya upitie uchungu ambao hakuna mtu wa kawaida angeweza kupitia—utatamani heri ufe. Mwishowe, utaniomba nikuache uende na hapo ndipo utazungumza maana, na kusema kwamba majaliwa yako hayako mikononi mwa Mungu—yako mikononi mwangu. Nikitaka ufe, itafanyika mara moja; nikitaka uishi, utaishi; na taabu yoyote nyingine ninayotaka upitie, hiyo ndiyo utapitia. Mwenyezi Mungu wako hawezi kukuokoa—utaishi tu ukituomba tukuokoe.” Nikiwa nimekabiliwa na hawa wauaji, wanyama mwitu, ibilisi waovu wenye kustahili dharau, wasio na aibu na walio duni, nilitaka sana kupigana nao. Wakati huo nilifikiri kuhusu wimbo wa uzoefu wa maisha: “Mbingu na dunia na kila kitu ndani yavyo viliumbwa na Mungu, na ni asili na haki kwa Mungu kuvifurahia. Mfalme wa ibilisi huvimiliki bila aibu; Shetani ana hatia ya uhalifu mbaya sana kabisa; makumi ya maelfu ya jamaa wa kiroho lazima waibuke” (“Kukimbia Kuelekea kwenye Njia Ng’avu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilikuwa nimefanya nini kuibuka? Kwa kutosema hata chochote kuwakanusha, kuwaacha tu wanitese kwa njia yoyote ambayo walitaka—katika hili, je, nilikuwa mnyonge sana? Moyo wangu ulijawa na ghadhabu. Nilihisi kana kwamba singeweza kuidhibiti, nilitaka kupiga yowe, kurudisha pigo, kuwatangazia: “Mwanadamu kamwe hawezi kuomba huruma kutoka kwa mbwa!” Niliamini kwamba hii ilikuwa hisia ya haki—lakini kwa mshangao wangu, kadiri nilivyofikiri zaidi kwa njia hii, ndivyo nilikuwa mwenye giza zaidi ndani. Nilijipata bila maneno ya maombi, nisiweze kufikiri nyimbo zozote. Mawazo yangu yalianza kukanganyikiwa, na sikujua cha kufanya, na wakati huo nilianza kuhisi mwenye woga kiasi. Kwa haraka nilijituliza mbele ya Mungu. Nilifikiri kujihusu, na kujaribu kujijua, na wakati huo maneno ya Mungu ya hukumu yalinijia: “Unachopendezwa nacho sio kujishusha kwa Kristo…. Haupendi wosia au kependeza kwa Kristo …” (Kutoka kwa “Je, Wewe ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Je, kufuata tamaa zako mwenyewe kunafichua mlingano Wangu? Je, hilo litaridhisha moyo Wangu? Je, wewe ni mtu ambaye kwa uaminifu amefuata dhamira Zangu? Je, wewe ni mtu ambaye kwa kweli amejaribu kuelewa moyo Wangu? Je, kwa hakika umejitoa Kwangu? Je, kwa kweli umejitumia kwa ajili Yangu. Je, umeyatafakari maneno Yangu?” (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). Kila neno la hukumu ya Mungu liliudunga moyo wangu. Ndiyo—nilikuwa nimemwona Kristo kama mdogo sana, nilikuwa nimependa nguvu na uwezo, sio unyenyekevu wa Kristo, hata zaidi nilikuwa nimetamani hekima ya kazi fiche ya Mungu. Mungu hutumia hekima Yake kumshinda Shetani, Yeye hutumia unyenyekevu na ufiche Wake kufichua sura ya kweli ya Shetani, na kukusanya ushahidi kuwaadhibu waovu. Mimi, wakati huo, nilitegemea falsafa za kishetani kuheshimu kazi ya Kristo, daima nikijaribu kulipiza kisasi kuamini kwamba kuwa mzuri ni kudanganywa, kwamba watu wote huweka mizigo juu ya farasi aliye radhi. Mbona, wakati ambapo tunateswa, tunapaswa kuwaacha polisi waovu wafanye watakavyo? Je, ni bahati nasibu ya wale wanaomwamini Mungu kudhulumiwa, kandamizwa, na kutiwa uchungu? Kama matokeo ya asili yangu ya kiburi, sikuwa tayari kustahimili fedheha, sembuse dhuluma na ukandamizaji. Hili lilikuwa limenifanya niidharau kazi ya hekima ya Kristo na kutothamini unyenyekevu na ufiche wa Kristo. Badala yake, niliamini kwamba hisia ya haki, nguvu ya sifa, na heshima ilikuwa katika kupigana nao. Sikujua kabisa kwamba Shetani alitaka kunichochea ili nipigane dhidi yao, kunilazimisha kukiri ukweli wa imani yangu kwa Mungu ili kunitia hatiani. Iwapo kweli ningepigana nao na ujasiri wa msukumo, singeshikwa na njama zao danganyifu? Kwa kweli nilimshukuru Mungu kwa ajili ya kuadibu na hukumu Yake kwangu kwa wakati ufaao, ambayo ilinipa ulinzi katikati ya uasi wangu, ili kwamba nilibaini njama danganyifu za Shetani, na kutambua sumu za Shetani ndani yangu, na kupata maarifa kiasi ya kile alicho Mungu na asili ya uhai wa Mungu iliyo nyenyekevu na fiche. Nilifikiri juu ya jinsi Kristo alikabiliwa na kuteswa, kuwindwa, na kuuwawa na ibilisi CCP, na jinsi wanadamu wote walimhukumu, na kumshutumu, na kumkashifu, na kumwacha. Wakati huo wote, Alivumilia haya yote kwa ukimya, Akistahimili uchungu huu wote kutekeleza kazi Yake ya wokovu, kamwe kutopigana, na kamwe kutolalamika. Niliona jinsi tu tabia ya Mungu ilivyo karimu, na nzuri na ya heshima! Wakati huo, mimi—mtu mchafu, mpotovu—nilikuwa nimetaka kupigana nilipoteswa na ibilisi waovu, nilikuwa nimetaka kutumia ujasiri wangu wa msukumo kutetea heshima yangu ya kudhaniwa, kupigana kwa ajili ya haki yangu mwenyewe kulingana na mapenzi yangu mwenyewe. Hisia ya haki ilikuwa wapi ndani ya hili? Na nguvu ya sifa na heshima ilikuwa wapi? Katika hili, sikuwa nikionyesha sura yangu mbaya ya shetani? Sikuwa nikifichua asili yangu ya kiburi? Je, kulikuwa na ukweli wowote katika hili? Nikifikiri hili, moyo wangu ulijawa na huzuni. Niliamua kumwiga Kristo. Nilikuwa tayari kuvumilia hali hii na kujaribu kadri nilivyoweza kushirikiana na Mungu, nisimwachie Shetani fursa yoyote.
Moyo wangu ulianza kuwa mtulivu, na kwa kimya nilisubiri zamu iliyofuata ya mapambano haya na ibilisi. Kukataa kwangu kukiri kulikuwa kumemwaibisha sana huyo aliyedhaniwa mtaalamu. Kwa hasira alipinda mkono wangu mmoja nyuma ya mgongo wangu na kuvuta huo mwingine nyuma ya mabega yangu, kisha alitia pingu mikono yangu na kuibana pamoja. Baada ya chini ya nusu saa, matone makubwa ya jasho yalikuwa yakitiririka usoni pangu, yakinizuia kuweza kufungua macho yangu. Huku akiona kwamba bado singejibu maswali yake, alinirusha sakafuni, kisha aliniinua kwa pingu nyuma ya mgongo wangu. Mikono yangu mara moja ilihisi uchungu mwingi, kana kwamba ilikuwa imevunjwa. Ilitia uchungu sana kiasi kwamba nilipumua kwa shida. Kisha, alinirusha dhidi ya ukuta na kunifanya nisimame dhidi yake. Jasho ilikuwa ikitia waa macho yangu. Nilihisi uchungu sana kiasi kwamba mwili wangu wote ulijawa na jasho—hata viatu vyangu vililowa. Daima nilikuwa dhaifu, na wakati huu nilianguka. Yote ambayo ningefanya tu ilikuwa kuhema kupitia mdomo wangu. Ibilisi alisimama kwa upande mmoja akinitazama. Sikujua alichoona—pengine aliogopa angelaumiwa iwapo ningekufa—kwa haraka alichukua kiasi kidogo cha karatasi ya shashi na kupanguza jasho yangu, kisha akaninywesha kikombe cha maji. Alifanya hivi kila wakati chini ya nusu saa ilikuwa imepita. Sijui nilifanana vipi wakati huo. Nadhani lazima ilikuwa inaogofya sana, kwa sababu ningehema tu mdomo wangu ukiwa wazi: ilionekana nilikuwa nimepoteza uwezo wangu kupumua kupitia pua langu. Midomo yangu ilikuwa imekauka na kufanya upenyu na ilichukua nguvu yote niliyokuwa nayo kupumua tu. Nilihisi kifo kikikaribia tena—pengine wakati huu kwa kweli ningekufa. Lakini wakati huo, Roho Mtakatifu alinitia nuru. Nilimfikiria Luka, mmoja wa wanafunzi wa Mungu, na uzoefu wake wa kuangikwa akiwa hai. Moyoni mwangu, nilipata tena nguvu yangu kwa hiari, na kuendelea kusema kitu kile kile tena na tena kujikumbusha: “Luka alikufa kwa kuangikwa akiwa hai. Mimi, pia, lazima niwe Luka, lazima niwe Luka, niwe Luka … Mungu atawasafisha watu kabisa; lakini mimi ni mnyonge sana, siwezi kushuhudia kabisa—na sasa niko karibu kufa. Hata nikifa kweli, kwa hiari ninatii utaratibu na mipango ya Mungu, nataka kuwa mwaminifu kwa Mungu hadi kufa kama Luka.” Wakati ule ule maumivu yalipokuwa hayawezi kuvumilika na nilikuwa ukingoni mwa kifo, ghafla nilisikia polisi mmoja mwovu kisema kwamba ndugu kadhaa waliomwamini Mwenyezi Mungu walikuwa wamekamatwa. Moyoni mwangu, nilishtuka: Ndugu wengine kadhaa watateswa. Lazima watakuwa wagumu hasa kwa kaka. Moyo wangu ulijawa na wasiwasi. Niliendelea kuwaombea kwa ukimya, nikimwomba Mungu awalinde na kuwaruhusu wawe na ushuhuda wa ushindi mbele ya Shetani na kutowahi kumsaliti Mungu, kwani sikutaka ndugu wowote wengine kuteseka kama nilivyoteseka. Pengine niliguswa na Roho Mtakatifu; niliomba bila kukoma, na kadiri nilivyoomba zaidi ndivyo nilivyotiwa moyo zaidi. Nilisahau uchungu wangu bila kufahamu. Nilijua vizuri sana kwamba hii ilikuwa mipango ya hekima ya Mungu; Mungu alijali udhaifu wangu, na alikuwa akiniongoza kupitia wakati wangu wa uchungu zaidi. Usiku huo, sikujali tena jinsi polisi waovu walivyonitendea, na sikutia maanani hata kidogo maswali yao. Huku wakiona kilichokuwa kikitendeka, polisi waovu walitumia ngumi zao kuupiga uso wangu kwa ukatili, kisha wakapinda nywele kwa panja langu vidoleni vyao na kuzivuta kwa ghafla. Masikio yangu yalikuwa yamevimba kwa ajili ya kupindwa, uso wangu ulikuwa usiotambulika, pande za juu na chini za miguu yangu zilikuwa zimeachwa na majeraha, na kuchunuka waliponichapa na kipande kinene cha mbao, na vidole vyangu vya miguu, pia, vilikuwa vimeachwa vyeusi na samawati baada ya kupondwa na kipande cha mbao. Baada ya kuniangika juu kwa pingu kwa saa sita, wakati polisi waovu walifungua pingu, zilikuwa zimeondoa nyama kutoka kwa kidole changu gumba cha kushoto—kulisalia tu safu nyembamba kabla ya mfupa. Pingu pia zilikuwa zimeacha vifundo vyangu vikiwa vimefunikwa na lengelenge ya njano, na hakukuwa na njia ya kuirudisha. Wakati huo, polisi wa kike aliyeonekana mwenye madaraka makubwa aliingia. Alinitazama juu na chini, kisha akawaambia: “Hamwezi kumchapa huyu tena—yuko karibu kufa.”
Polisi walinifungia katika chumba kimoja hotelini. Mapazia yake yalikuwa yamefungwa kwa kubanwa usiku kucha na mchana kutwa. Mtu fulani alipewa jukumu la kulinda mlango, na hakuna kati ya watumishi wa huduma aliyeruhusiwa kuingia, wala hakuna aliyeruhusiwa kuona matukio ya wao kunitesa na kunishambulia kikatili kule ndani. Walichukua zamu kunihoji bila pumziko. Kwa siku na usiku tano, hawakuniruhusu kulala, hawakuniruhusu kukaa wala kuchuchumaa, wala hawakuniruhusu kula chakula changu hadi kushiba. Niliruhusiwa tu kusimama nikiegemea dhidi ya ukuta. Siku moja, afisa mmoja alikuja kunihoji. Huku akiona kwamba nilikuwa nikimpuuza, alishikwa na hasira na kunipiga teke lililonirusha chini ya meza. Kisha, alinivuta kutoka hapo na kunipiga ngumi, akisababisha damu kububujika kutoka kwa kona ya mdomo wangu. Ili kuficha ukatili wake, kwa haraka alifunga mlango kuzuia yeyote kuingia. Kisha alirarua kiasi kidogo cha karatasi ya shashi na kupanguza damu yangu, akisafisha damu kutoka usoni pangu kwa maji na kusafisha damu kutoka kwenye sakafu. Niliacha damu kiasi kwa sweta yangu nyeupe kwa makusudi. Niliporudi katika kituo cha kuzuia, hata hivyo, polisi waovu waliwaambia wafungwa wengine kwamba damu kwenye mavazi yangu ilitokana na wakati nilipokuwa nikithibitishwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili, na kusema kwamba hapo ndipo nilipokuwa siku kadhaa zilizopita. Majeraha na damu mwilini mwangu yalikuwa yamesababishwa na wagonjwa, wao, polisi, hawakuwa wamenigusa…. Ukweli huu katili ulinionyesha ukatili, ujanja wenye kudhuru kwa siri, na unyama wa “polisi wa watu,” na nilihisi kutojiweza na huzuni ya wale wanaoanguka mikononi mwao. Wakati huo huo, nilipata ufahamu wa kina wa haki, utakatifu, uchangamfu, na uzuri wa Mungu, na kuhisi kwamba kila kitu kinachotoka kwa Mungu ni upendo, ulinzi, nuru, ugavi, faraja, na msaada. Kila wakati uchungu wangu ulipofika kiwango mbaya kabisa, Mungu daima angeendelea kunitia nuru na kuniongoza, Akiongeza imani na nguvu yangu, Akiniruhusu kuiga roho ya watakatifu ambao walikuwa wamekufa shahidi kwa ajili ya Mungu kotekote katika enzi, kunipa ujasiri wa kutetea ukweli. Wakati ambapo ukatili wa polisi waovu uliniacha karibu na kifo, Mungu aliniruhusu kusikia habari ya kukamatwa kwa ndugu, kutumia hili kunisisimua zaidi kuwaombea, ili kwamba nilisahau uchungu wangu na bila kujua kushinda vikwazo vya kifo. Kwa sababu ya utumbuizo wa Shetani mwovu, mkatili, niliona kwamba Mungu pekee ndiye ukweli, njia, na uhai, na kwamba Mungu pekee ndiye ishara ya mamlaka ya juu, ya haki, na ishara ambayo haiwezi kushindwa ama kuingiliwa na uovu na nguvu yoyote ya uhasama. Mungu pekee ndiye hutawala vitu vyote, na hupanga kila kitu, na Yeye hutumia nguvu Yake kuu na hekima kuongoza kila hatua yangu katika kushinda mizinga ya umati wa ibilisi, katika kushinda udhaifu wa mwili na vikwazo vya kifo, kuniruhusu kwa kunata kuokoka katika pango hili ovu. Nilipokuwa nikifikiri kuhusu upendo na wokovu wa Mungu, nilihisi kutiwa moyo sana, na nikaamua kupigana na Shetani hadi mwisho kabisa. Hata ningedhoofika gerezani, ningesimama imara katika ushuhuda wangu na kumridhisha Mungu.
Siku moja, polisi wengi waovu ambao sikuwa nimewahi kuwaona awali walikuja kuniangalia na kujadili kesi yangu. Bila kutaka, nilisikia bila kusudia mtaalamu—akisema: “Kwa mahojiano yote ambayo nimefanya, sijawahi kuwa mgumu kwa mtu yeyote kama huyo mwanamke mjinga. Nilimfanya atundikwe kwa pingu kwa saa nane (kwa kweli ilikuwa saa sita, lakini alitaka kujionyesha, akiogopa kwamba wasimamizi wake wangesema alikuwa bure) na bado hakukiri.” Nilisikia sauti ya kike ikisema, “Mbona ulimchapa mwanamke huyo vibaya hivyo? Wewe ni mkatili.” Ilitukia kwamba miongoni mwa kila mtu ambaye alikuwa amekamatwa, nilikuwa nimeteseka zaidi. Mbona nilikuwa nimeteseka sana hivyo? Je, nilikuwa mpotovu kuliko watu wengine? Je, kile nilichopitia kilikuwa adhabu ya Mungu kwangu? Pengine kulikuwa na upotovu mwingi sana ndani yangu, na tayari nilikuwa nimefika kiwango cha adhabu? Nikifikiri hili, singeweza kuzuia machozi yangu. Nilijua kwamba lazima nisilie. Singeacha Shetani aone machozi yangu—kama angeona, angeamini kwamba nilikuwa nimeshindwa. Ilhali sikuweza kudhibiti hisia ya huzuni moyoni mwangu, na machozi yalitiririka kupita udhibiti wangu. Katikati ya kukata tamaa kwangu, ningemwita tu Mungu: “Ee Mungu! Wakati huu, nahisi kusikitika sana. Naendelea kutaka kulia. Tafadhali nilinde, nizuie dhidi ya kuinamisha kichwa changu mbele ya Shetani—siwezi ruhusu aone machozi yangu. Najua kwamba hali niliyomo si sahihi. Natoa madai Kwako, na kulalamika. Na najua kwamba bila kujali kile Ufanyacho, ni bora zaidi—lakini kimo changu ni kidogo sana, tabia yangu ya uasi ni kubwa sana, na sina uwezo wa kukubali ukweli huu kwa furaha, wala sijui kile ninachopaswa kufanya kutoka katika hali hii mbaya. Ningependa Uniongoze, na kuniruhusu kutii utaratibu na mipango Yako, na kutokufahamu visivyo tena ama kulalamika kuhusu Wewe.” Nilipokuwa nikiomba, fungu la maneno ya Mungu yalinijia akilini: “Lazima pia unywe kutoka kwenye kikombe kikali nilichonywea Mimi (hili ndilo alilomwambia baada ya kufufuka), lazima utembee njia niliyotembea Mimi, lazima uyapoteze maisha yako kwa ajili Yangu” (Kutoka kwa “Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Machozi yangu yalikoma mara moja. Mateso ya Kristo yalikuwa yasiyoweza kufananishwa na yale ya kiumbe yeyote aliyeumbwa, wala hayakuweza kuvumilika na kiumbe aliyeumbwa—ilhali nilikuwa hapa nikihisi nimekosewa na nikilalamika kwa Mungu kwamba haikuwa haki baada ya kupitia taabu kidogo. Dhamiri na mantiki ilikuwa wapi katika hili? Nilifaa vipi kuitwa binadamu? Baada ya hiyo, nilifikiri kuhusu kile Mungu alisema: “Hata hivyo, upotovu ndani ya asili ya binadamu ni lazima uondolewe kupit majaribu. Katika hali yoyote usiyoipita, ni katika hizi hali ambamo ni lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili ujue upotovu wako mwenyewe” (Kutoka kwa “Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nikitafakari maneno ya Mungu na kufikiri kujihusu, nilielewa kwamba kile kilichopangwa na Mungu kililenga upotovu na upungufu wangu—na kilikuwa hasa kile ambacho maisha yangu yalihitaji. Kwa sababu nilikuwa nimepofishwa sana na kutiwa sumu na serikali ya CCP, moyo wangu daima ulikuwa umejaa imani na tegemeo mintaarafu yake, na hata ingawa nilikuwa nimeona makosa yake kiasi, hiyo haikuwa imebadili maoni yangu kuihusu. Leo, Mungu alikuwa ameunda hali hii maalum kwangu, Akiniruhusu kutofautisha kati ya Mungu na Shetani, kuweza kujua ni nani huniokoa na ni nani hunipotosha, nani ambaye napaswa kuabudu na nani ambaye napaswa kulaani, na ni kwa sababu ya hili tu ndipo niliona mwanga wa ukweli, na kumtazama Mungu wa kweli, na kuja kujua tofauti kati ya mwanga na giza. Iwapo singepitia taabu ambayo ilikuwa nyingi na kali ya kutosha, maarifa yangu na maoni ya serikali ya CCP hayangekuwa yamebadilika—wala, moyoni mwangu, singeutekeleza kwa kweli, na kwa kweli kumgeukia Mungu. Taabu hii ilikuwa upendo wa Mungu kwangu, ilikuwa baraka Yake maalum kwangu. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, moyo wangu mara moja ulihisi dhahiri na mchangamfu. Suitafahamu yangu ya Mungu ilitoweka. Nilihisi kulikuwa na thamani kubwa na maana katika mimi kuweza kupitia taabu hiyo siku!
Baada ya kujaribu kila kitu walichoweza, polisi waovu hawakuwa wamepata chochote kutoka kwangu. Mwishowe, walisema kwa kusadiki sana: “Wakomunisti wametengenezwa kwa chuma, lakini wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu wametengenezwa kwa almasi—wako katika kiwango cha juu zaidi kuliko wakomunisti katika kila hali.” Baada ya kusikia maneno haya, moyoni mwangu singeweza kujizuia kufurahia na kumsifu Mungu: Ee Mungu, nakushukuru na kukusifu! Kwa uweza na hekima Yako Umemshinda Shetani na kushinda maadui Wako. Wewe ni mamlaka ya juu zaidi, na naomba utukufu uwe Wako! Ni wakati huu tu ndio niliona: Je, Chama cha Kikomunisti kina maana gani? Na je, utawala wote wa siasa duniani una maana gani? Vitu vyote mbinguni na duniani huja chini ya utawala wa Mungu. Lazima visiwe na chaguo lingine sembuse Shetani mdogo, asiye na maana ibilisi ambaye ni utumbuizo tu.
Siku moja, polisi waovu walikuja kunihoji mara nyingine tena. Wakati huu, wote walionekana kuwa wa ajabu kidogo. Waliniangalia walipozungumza, lakini haikuonekana kama walikuwa wakinizungumzia. Walionekana kujadili kitu. Kama nyakati za awali, mahojiano haya yaliishia katika kushindwa. Baadaye, polisi waovu walinirudisha kwa seli. Njiani, nilisikia ghafla wakisema kwamba ilionekana kuwa ningeachiliwa siku ya kwanza ya mwezi ujao. Kwa kusikia hili, moyo wangu karibu ulipasuka kwa msisimko: Hili inamaanisha nitaondoka katika siku tatu! Hatimaye naweza kuondoka katika jahanamu hii ya shetani! Kwa kukandamiza furaha iliyokuwa moyoni mwangu, nilitarajia na kusubiri kila sekunde ilipokuwa ikipita. Siku tatu zilihisi zaidi kama miaka mitatu. Mwishowe, siku ya kwanza ya mwezi iliwadia! Siku hiyo, niliendelea kukodolea mlango macho, nikisubiri mtu aite jina langu. Asubuhi ilipita, na hakuna kilichofanyika, niliweka matumaini yangu yote katika kuondoka alasiri—lakini jioni ilipofika, bado hakuna kilichofanyika. Wakati ambapo ilikuwa wakati wa chakula cha jioni, sikuhisi kula. Moyoni mwangu, nilikuwa na hisia ya hasara; wakati huo, ilikuwa kana kwamba moyo wangu ulikuwa umeanguka kutoka mbinguni hadi jahanamu. “Mbona hali?” mlinzi aliuliza wafungwa wengine. “Hajala sana tangu aliporudi kutoka kwa mahojiano siku ile,” mfungwa mmoja alijibu. “Gusa panja lake; je, yeye ni mgonjwa?” mlinzi alisema. Mfungwa alikuja na kugusa panja langu. Alisema lilikuwa na joto sana, kwamba nilikuwa na homa. Kwa kweli nilikuwa na homa. Ugonjwa huo ulikuwa umekuja ghafla sana, na ulikuwa mkali sana. Wakati huo, nilianguka. Kwa kipindi cha saa mbili, homa ikawa mbaya na mbaya zaidi. Nililia! Wote, akiwemo mlinzi, walinitazama nikilia. Wote waliduwaza: Maoni yao kunihusu yalikuwa kama mtu ambaye hakushawishika kwa kivutio wala kuogopeshwa kwa vitisho, ambaye hakuwahi kutoa chozi hata moja kila wakati alipokabiliwa na mateso ya kuhuzunisha, ambaye alikuwa ameangikwa juu kwa pingu kwa saa sita bila kupiga kite. Ilhali, leo, bila mateso yoyote, nililia. Hawakujua machozi yangu yalitoka wapi—walifikiri tu kwamba lazima niwe mgonjwa sana. Kwa kweli, mimi na Mungu tu ndio tulijua sababu. Haya yote yalikuwa kwa sababu ya uasi na kutotii kwangu. Machozi haya yalitiririka kwa sababu nilihisi kukata tamaa wakati ambapo matarajio yangu yaliambulia patupu na matumaini yangu yalikuwa yamevunjika. Yalikuwa machozi ya uasi na lalamiko. Wakati huo, sikutaka tena kuweka azimio langu kumshuhudia Mungu. Hata sikuwa na ujasiri kujaribiwa hivi tena. Jioni hiyo, nililia machozi ya taabu, kwa sababu nilikuwa nimechoshwa na maisha gerezani, niliwadharau pepo hawa—na hata zaidi ya hilo, nilichukia kuwa mahali hapa pa pepo. Sikutaka kukaa sekunde nyingine hapo. Kadiri nilivyofikiri kuhusu hilo, ndivyo nilivyovunjika moya zaidi, na ndivyo nilivyohisi hisia kubwa ya taabu, ya huzuni, na upweke zaidi. Nilihisi kana kwamba nilikuwa mashua pweke juu ya bahari, moja ambayo ingemezwa na maji wakati wowote; zaidi ya hayo, nilihisi wale walionizunguka walikuwa wenye kudhuru kwa siri sana na wabaya sana kiasi kwamba wangetoa hasira yao kwangu wakati wowote. Singeweza kujizuia kulia kwa sauti: “Ee Mungu! Nakuomba uniokoe. Niko karibu kuanguka, ninaweza kukusaliti wakati wowote na mahali popote. Ningependa uushike moyo wangu na uniwezeshe kurudi mbele Yako tena, ningependa Unihurumie mara moja nyingine, na kuniruhusu nikubali utaratibu na mipango Yako. Ingawa siwezi kuelewa kile Unachofanya sasa, najua kwamba yote Unayofanya ni mema, na ningetaka Uniokoe mara nyingine, na kuruhusu moyo wangu ukugeukie.” Baada ya kuomba, niliacha kuhisi kuogopa, nilianza kutulia na kufikiri kujihusu, na wakati huo maneno ya Mungu ya hukumu na ufunuo yalinijia: “Unataka mwili ama ukweli? Unataka hukumu, ama faraja? Baada ya kupitia na kuiona kazi nyingi ya Mungu, na baada ya kuuona utakatifu na haki ya Mungu, unafaa kumfuata vipi? Unapaswa kutembea vipi katika njia hii? Utahitajika kuweka mapenzi ya Mungu katika matendo kivipi? Je, adabu na hukumu ya Mungu zimekuwa na athari yoyote kwako? Kama una maarifa ya adabu na hukumu ya Mungu itategemea jinsi unavyoishi kwa kudhihirisha, na kiwango gani unapenda Mungu! Kinywa chako kinasema unampenda Mungu, ilhali unachoishi kwa kudhihirisha ni tabia nzee, zilizo potovu; humchi Mungu, na zaidi ya yote huna dhamiri. Je, watu wa aina hii wanampenda Mungu? Je, watu wa aina hii ni waaminifu kwa Mungu? … Mtu kama huyu anaweza kuwa Petro? Wale walio kama Petro wana maarifa, lakini je, wanaishi kulingana nayo?” (Kutoka kwa “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila neno la Mungu la hukumu lilikuwa kama upanga ukatao kuwili likiugonga udhaifu wangu, likirundika lawama juu yangu: Ndiyo, kulikuwa na nyakati nyingi ambapo nilitoa viapo vya dhati mbele ya Mungu, nikisema kwamba ningetelekeza kila kitu na kustahimili kila taabu kwa ajili ya ukweli. Ilhali leo, wakati ambapo Mungu alitumia ukweli kuniomba jambo, wakati Alinihitaji kwa kweli kuteseka na kulipa gharama ili kumridhisha, sikuwa nimechagua ukweli ama uzima, lakini kwa upofu nilikuwa nimejawa na wasiwasi, dhiki na masumbuko kwa sababu ya maslahi na matazamio ya mwili. Sikuwa hata na imani hata kidogo kwa Mungu. Katika hili, ningewezaje kuridhisha mapenzi ya Mungu? Mungu alitaka kile nilichoishi kwa kudhihirisha kuzaa matunda. Hakutaka viapo vya madoido, vitupu. Ilhali mbele ya Mungu nilikuwa na maarifa lakini sikuwa na uhalisi wowote, na kuelekea kwa Mungu, sikuwa na uaminifu ama upendo wa kweli, sembuse kuwa na utiifu wowote; sikuishi kwa kudhihirisha chochote ila udanganyifu, uasi, na upinzani. Katika hili, je, si nilikuwa mtu ambaye alimsaliti Mungu? Je, sikuwa mtu aliyeuvunja moyo wa Mungu? Wakati huo, nilifikiri kuhusu wakati Bwana Yesu alipokamatwa na kupigwa misumari msalabani. Mmoja baada ya mwingine, wale ambao mara nyingi walikuwa wamefurahia neema Yake walimwacha. Moyoni mwangu, singeweza kujizuia kujawa na majuto. Nilichukia uasi wangu, nilichukia ukosefu wangu wa ubinadamu, nilitaka kwa mara nyingine kusimama, kutumia vitendo vya ukweli kufanya ahadi zangu kwa Mungu kuwa uhalisi. Hata kama ningedhoofika gerezani, singeuumiza tena moyo wa Mungu. Singesaliti tena gharama ya damu ambayo Mungu alikuwa amelipa kwangu. Niliacha kulia, na moyoni mwangu nilimwomba Mungu kwa kimya: Ee Mungu, ahsante kwa kunitia nuru na kuniongoza, kuniruhusu kuelewa mapenzi Yako. Naona kwamba kimo changu ni kidogo sana, na kwamba sina upendo ama utiifu hata kidogo Kwako. Ee Mungu, sasa hivi nataka kujitoa kikamilifu Kwako. Hata nikiishi maisha yangu yote gerezani, kamwe singemkubali Shetani. Nataka tu kutumia vitendo vyangu vya ukweli kukuridhisha.
Baada ya muda, kulikuwa na uvumi zaidi kwamba ningeachiliwa. Walisema kwamba ingekuwa siku chache tu. Kwa sababu ya masomo niliyofunzwa wakati uliopita, wakati huu nilikuwa razini na mtulivu kiasi. Ingawa nilihisi mwenye kusisimka sana, nilitaka kuomba na kutafuta mbele ya Mungu, kutokuwa tena na chaguo langu mwenyewe. Ningemwomba Mungu tu anilinde ili niweze kutii utaratibu na mipango Yake yote. Baada ya siku chache, uvumi mara nyingine ulikuwa bure. Zaidi ya hayo, nilimsikia mlinzi akisema kwamba hata kama ningekufa gerezani, hawangeniachilia, sababu ikiwa kwamba singewaambia anwani yangu ya nyumbani na jina—hivyo ningetiwa gerezani milele. Kusikia hili kulikuwa kugumu sana, lakini nilijua kwamba huu ulikuwa uchungu niliopaswa kupitia. Mungu alitaka niwe na ushuhuda huu Kwake, na nilikuwa tayari kumtii Mungu, na kutii mapenzi ya Mungu, na niliamini kwamba mambo na vitu vyote vimo mikononi mwa Mungu. Hii ilikuwa neema maalum ya Mungu na kuniinua. Awali, ingawa nilikuwa nimesema ningedhoofika gerezani, hiyo ilikuwa tu hamu yangu na tamaa zangu—sikuwa na uhalisi huu. Leo, nilikuwa tayari kuwa na ushuhuda huu kupitia kuishi kwangu kulingana na matendo na kumruhusu Mungu kupata faraja kwangu. Wakati nilijawa na chuki kwa ajili ya Shetani, na nikaamua kufanya mapigano na Shetani hadi mwishoni kabisa, kwa kweli kuwa na ushuhuda wa kweli ya kudhoofikia gerezani, niliona kudura na matendo ya muujiza ya Mungu. Mnamo Desemba 6, 2005, gari la gerezani lilinichukua kutoka kituo cha kuzuia na kuniacha kando ya barabara. Kutoka wakati huo kuendelea, maisha yangu ya miaka miwili gerezani yaliisha.
Baada ya kupitia majaribu haya mabaya, ingawa mwili wangu ulikuwa umevumilia taabu kiasi, nilikuwa nimepata mara mia moja—mara elfu moja—zaidi: sikuwa tu nimekuza umaizi na utofautishaji, na kweli kuona kwamba serikali ya CCP ni mfano halisi wa Shetani ibilisi, kundi la wauaji ambao wangewaua watu kufumba kufumbua, lakini pia nilikuja kuelewa kudura na maarifa ya Mungu, na vilevile haki na utakatifu Wake, nilikuwa nimekuja kufahamu nia nzuri za Mungu katika kuniokoa, na utunzaji Wake na ulinzi Wake kwangu, Akiniruhusu, katika ukatili wa Shetani, kumshinda Shetani hatua kwa hatua, na kusimama imara katika ushuhuda wangu. Kutoka siku hiyo kuendelea, nilitaka kutoa nafsi yangu yote kwa Mungu kikamilifu. Kwa uthabiti ningemfuata Mungu, kwamba ningeweza kupatwa na Yeye mapema.
kutoka kwa Ushuhuda wa Washindi

Alhamisi, 25 Oktoba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ujana Uliotumiwa Bila Majuto

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukatili Mateso

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ujana Uliotumiwa Bila Majuto

Xiaowen, Chongqing
"Upendo ni hisia safi, safi bila ya dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vikwazo au umbali. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Ukipenda hudanganyi, kunung'unika, kutelekeza, kutarajia kupata malipo" ("Upendo safi bila Dosari" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wimbo huu wa neno la Mungu siku moja ulinisaidia kupitia maumivu ya maisha ya muda mrefu yaliorefuka bure gerezani ambao ulidumu miaka 7 na miezi 4. Ingawa serikali ya CCP ilininyang'anya miaka mizuri zaidi ya ujana wangu, nimepata ukweli halisi na wa thamani zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwa hiyo sina malalamiko au majuto.
Mnamo mwaka wa 1996 nilipokea kukuzwa na Mungu na kukubali wokovu wa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kupitia kusoma maneno ya Mungu na kukusanyika katika ushirika, nilidhihirisha kwamba yote ambayo Mungu amesema ni ukweli, ambayo ni tofauti kabisa na maarifa na nadharia zote za dunia hii mbovu. Neno la Mwenyezi Mungu ni methali ya juu zaidi kwa maisha. Kilichofanya nisisimke zaidi kilikuwa kwamba ningeweza kuwa wa kawaida na wazi na kuzungumza kwa uhuru juu ya chochote na ndugu wa kiume na wa kike. Sikuwa na haja hata kidogo ya kujilinda dhidi ya lawama au kushindwa kwa akili na watu wakati wa kuingiliana nao. Nilihisi faraja na furaha ambayo sikuwahi kuhisi awali; kwa kweli niliipenda familia hii. Hata hivyo, si muda mrefu ulipita kabla sijasikia kwamba nchi hii haikuwaruhusu watu kumwamini Mwenyezi Mungu. Jambo hili lilinifanya kuchanganyikiwa kabisa, kwa sababu neno Lake liliwaruhusu watu kumwabudu Mungu na kuitembea njia sahihi ya maisha; liliwaruhusu watu kuwa waaminifu. Kama kila mtu angemwamini Mwenyezi Mungu, basi ulimwengu wote ungekuwa na amani. Kwa kweli sifahamu: Kumwamini Mungu kulikuwa ndiko shughuli ya haki zaidi; kwa nini serikali ya CCP ilitaka kutesa na kupinga kumwamini Mwenyezi Mungu kiasi kwamba ingewakamata waumini Wake? Niliwaza: Bila kujali ni vipi serikali ya CCP inatutesa au ni jinsi gani maoni ya umma ya kijamii ni makubwa, nimeamua kuwa hii ndiyo njia sahihi ya maisha na mimi kwa hakika nitaitembelea hadi mwisho!
Baada ya haya, nilianza kutekeleza wajibu wangu katika kanisa wa kusambaza vitabu vya neno la Mungu. Nilijua kwamba kutimiza wajibu huu katika nchi hii ambayo ilimpinga Mungu ilikuwa hatari sana na ningeweza kukamatwa wakati wowote. Lakini nilijua pia kuwa kama sehemu ya uumbaji wote, ulikuwa ni misheni yangu katika maisha wa kutumia kila kitu kwa ajili ya Mungu na kutimiza wajibu wangu; lilikuwa ni jukumu ambalo sikuweza kulikwepa. Nilipokuwa tu nikianza kushirikiana na Mungu kwa imani, siku moja mnamo Septemba mwaka wa 2003, nilikuwa njiani kuwapelekea ndugu fulani wa kiume na wa kike vitabu vya neno la Mungu na nilikamatwa na watu kutoka kwa Ofisi ya Usalama wa Taifa ya mjini.
Katika Ofisi ya Usalama wa Taifa, nilihojiwa tena na tena na sikujua jinsi ya kujibu; nilimlilia Mungu kwa haraka: "Ee Mwenyezi Mungu, nakuuliza Wewe unipe hekima Yako, na unipe maneno ambayo napaswa kuzungumza ili nisikusaliti Wewe na niweze kuwa shahidi kwa ajili Yako." Wakati huo, nilimlilia Mungu kila siku; Sikuthubutu kumwacha Mungu, nilimwomba tu Mungu anipe akili na hekima ili niweze shughulikia polisi hao waovu. Shukrani kwa Mungu kwa kunichunga na kunilinda; kila wakati nilipohojiwa, ama nilikuwa nikitema mate, au nilikuwa na kwikwi mfululizo na sikuweza kuzungumza. Katika kuona kazi ya ajabu ya Mungu, nikaamua kwa dhati: Kuwa waziwazi! Wanaweza kuchukua kichwa changu, wanaweza kuchukua maisha yangu, lakini kabisa hawatanifanya kumsaliti Mungu leo kamwe! Ninapoweka azimio langu kwamba ningependa kuhatarisha maisha yangu kuliko kumsaliti Mungu kama Yuda, Mungu alinipa "endelea" kwa kila namna: Kila wakati nilipohojiwa, Mungu angenilinda na kuniruhusu nipitie majaribu. Ingawa sikusema chochote, serikali ya CCP ilinishtaki kwa "kutumia dhehebu bovu kuangamiza utekelezaji wa sheria" na kunihukumu kifungo cha miaka 9 katika jela! Niliposikia hukumu ya mahakama, sikuwa na huzuni kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, wala sikuwaogopa; badala yake, niliwadharau. Wakati watu hao walikuwa wakitangaza hukumu, nilisema kwa sauti ya chini: "Huu ni ushahidi kwamba serikali ya CCP inampinga Mungu!" Baadaye, maafisa wa usalama wa umma walikuja tu kuchunguza jinsi mtazamo wangu ulivyokuwa, na nikawaambia kwa utulivu: "Miaka tisa ni nini? Wakati utakapofika kwangu kutoka, bado nitakuwa mshiriki wa Kanisa la Mwenyezi Mungu; ikiwa huniamini, subiri tu na kuona! Lakini unapaswa kukumbuka, kesi hii wakati mmoja ilikuwa katika mikono yenu!" Mtazamo wangu kwa kweli uliwashangaza; waliinua vidole gumba vyao juu na kusema tena na tena: "Umekuwa mahiri sana! Tunakustahi! Wewe ni mjeuri kuliko Dada Jiang! [a] Hebu tukutane wakati utakapotoka, na tutakupa chakula cha jioni!" Wakati huo, nilihisi kwamba Mungu alipata utukufu na moyo wangu ulipendezwa. Mwaka huo nilipohukumiwa, nilikuwa na umri wa miaka 31 tu.
Jela za China ni kuzimu duniani, na maisha ya muda mrefu ya gereza yalinifanya kuona kabisa unyama wa kweli wa Shetani na kiini chake cha kishetani ambacho kimekuwa adui kwa Mungu. Polisi wa China huwa hawafuati utawala wa sheria, lakini badala yake hufuata utawala wa uovu. Gerezani, polisi binafsi huwa hawawashughulikii watu, lakini huwachochea wafungwa kufanya vurugu ili kutiisha wafungwa wengine. Hawa polisi waovu pia hutumia mbinu za aina zote kuyafungia mawazo ya watu; kwa mfano, kila mtu anayeingia anapaswa kuvaa sare sawa za mfungwa zilizo na nambari maalum ya mfululizo, ni sharti anyolewe nywele zao kulingana na matakwa ya gereza, ni lazima avae viatu vilivyoidhinishwa na jela, anapaswa kutembelea vijia ambavyo gereza limemruhusu kutembelea, na anapaswa kutembea mwendo wa askari kwa kasi iliyoruhusiwa na gereza. Bila kujali kama ni majira ya kuchipua, majira ya joto, majira ya kupukutika kwa majani au majira ya baridi, ikiwa kuna mvua au kuna jua, au kama ni siku ya baridi kali, wafungwa wote wanapaswa kufanya kama walivyoamriwa bila ya uchaguzi wowote. Kila siku tulihitajika kukusanyika angalau mara 15 kupangwa na kuimba nyimbo za sifa kwa serikali ya CCP angalau mara tano; tulikuwa pia na kazi za kisiasa, yaani, walitufanya tujifunze sheria za gereza na katiba, na walitufanya kufanya mtihani kila baada ya miezi sita. Kusudi la hili lilikuwa ni kututia kasumba. Pia wangeyapima bila mpango maalum maarifa yetu ya masomo na sheria za jela. Polisi wa gereza walitutesa sio kiakili tu, wao pia walituharibu kimwili kwa unyama kamili: nilipaswa kufanya kazi ngumu kwa zaidi ya saa kumi kwa siku, kama tumesokomezwa pamoja na watu wengine mia kadhaa katika kiwanda chembamba tukifanya kazi za mikono. Kwa sababu kulikuwa watu wengi sana katika nafasi ndogo kiasi hicho, na kwa sababu kelele ya kutatanisha ya mashine ilikuwa kila mahali, bila kujali mtu alikuwa na afya kiasi gani, mwili wake ungepata uharibifu mkubwa kama angekaa hapo kwa muda. Nyuma yangu kulikuwa na mashine ya kutoboa matundu na kila siku ilitoboa mashimo mfululizo. Sauti ya kunguruma iliyopitisha ilikuwa isiyovumilika na baada ya miaka michache, nilipata ugonjwa hatari wa kutosikia. Hata leo hii sijapata nafuu. Kitu kilichokuwa kibaya zaidi kwa watu kilikuwa vumbi na uchafuzi wa mazingira katika kiwanda hicho. Baada ya kuchunguzwa, watu wengi walipatikana wakiwa wameambukizwa kifua kikuu na uvimbe wa koromeo. Aidha, kutokana na muda mrefu wa kukaa kitako hapo kufanya kazi ya mikono, ilikuwa haiwezekani kusogea hapa na pale na watu wengi waliambukizwa ugonjwa hatari wa bawasiri. Serikali ya CCP iliwachukulia wafungwa kama mashine za kutengeneza pesa; hawakuwa na mazingatio hata kidogo ya kama mtu aliishi au alikufa. Waliwafanya watu kufanya kazi tangu asubuhi na mapema mpaka usiku kabisa. Mara nyingi nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba sikuweza kuendelea kimwili. Haikuwa hii tu, nilipaswa pia nishughulike na aina zote za mitihani ya nasibu bali na kazi zangu za kila wiki za kisiasa, kazi za mikono, na kazi za umma, nk. Kwa hiyo, kila siku nilikuwa katika hali ya wasiwasi wa hali ya juu; hali yangu ya kiakili ilikuwa ikinyoshwa daima, na nilikuwa na wasiwasi zaidi kwamba singeweza kuwafikia wengine kama ningezembea hata kidogo, na kwa hiyo ningeadhibiwa na polisi wa gereza. Katika mazingira ya aina hiyo, kumaliza siku moja salama haikuwa kazi rahisi kufanya.
Nilipoanza tu kumaliza kifungo changu, sikuweza kustahimili aina hii ya kuharibiwa kikatili na polisi wa gereza. Aina zote za kazi ngumu ya mikono na shinikizo la kiitikadi lilifanya kupumua kuwe kugumu, sembuse kuwa ilibidi niwe na mawasiliano ya aina yote na wafungwa. Nilibidi pia kuvumilia dhuluma na matusi ya polisi wa kishetani wa gereza na wafungwa …. Niliteswa mara kwa mara na kuwekwa taabuni. Mara kadhaa, nilizama katika hali ya kukata tamaa, hasa nilipofikiria urefu wa hukumu yangu ya miaka tisa, nilihisi mshindo wa kutojiweza kwa kuhuzunisha na sikujua ni mara ngapi nililia—kiasi kwamba nilifikiria kujiua ili kujiweka huru kutoka kwa maumivu niliyokuwa nayo. Kila wakati nilipokuwa na huzuni kupita kiasi na sikuweza kujifadhili, ningeomba kwa haraka na kumlilia Mungu na Mungu angenipatia nuru na kuniongoza: “Bado huwezi kufa. Sharti ukaze ngumi yako na kuendelea kuishi kwa ari; lazima uishi maisha kwa ajili ya Mungu. Watu wanapokuwa na ukweli ndani yao basi wanakuwa na azimio hili na kamwe hawatamani kufa tena; kifo kinapokutisha, utasema, ‘Ee Mungu, siko radhi kufa; bado sikufahamu! Bado sijalipiza upendo Wako! … Lazima niwe na ushuhuda mzuri wa Mungu. Lazima nilipize upendo wa Mungu. Baada ya hapo, haijalishi jinsi nitakavyokufa. Kisha, nitakuwa nimeishi maisha ya kutosheleza. Bila kujali ni nani mwengine anayekufa, sitakufa sasa; lazima niendelee kuishi kwa ushupavu’” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalikuwa kama maono laini na latifu ya mama yangu akiutuliza moyo wangu mpweke. Yalikuwa pia kama baba yangu akitumia mikono miwili kuyafuta kwa uangalifu machozi kutoka kwa uso wangu kwa upendo. Moja kwa moja, mkondo wa vuguvugu na nguvu zilikurupuka kupitia moyo wangu. Ingawa nilikuwa nikiteseka kimwili katika jela la giza, kujaribu kujiua hakukuwa mapenzi ya Mungu. Singeweza kumshuhudia Mungu na pia ningekuwa kichekesho cha Shetani. Ingekuwa ushuhuda kama ningetoka hai kutoka gereza hili lenye pepo baada ya miaka tisa. Maneno ya Mungu yalinipa ujasiri wa kuendelea na maisha yangu na nikafanya azimio moyoni mwangu: Haijalishi matatizo gani yaliyo mbele yangu, kwa uangalifu nitaendelea kuishi; nitaishi kwa ujasiri na nguvu na hakika nitashuhudia kuridhika kwa Mungu.
Mwaka nenda mwaka rudi, kazi ya kuzidi kiasi ilisababisha mwili wangu kudhoofika hatua kwa hatua. Baada ya kukaa kitako kwa muda mrefu katika kiwanda ningeanza kutoa jasho maridhawa na bawasiri zangu zingevuja damu zilipokuwa kali vya kutosha. Kutokana na upungufu wangu mkali wa damu, mara kwa mara ningehisi kizunguzungu. Lakini gerezani, kumwona daktari si jambo rahisi kufanya; kama polisi wa gereza walikuwa wamefurahi, wangenipa dawa za bei nafuu. Kama hawakuwa na furaha, wangesema nilikuwa nikijifanya mgonjwa ili kuepuka kazi. Ningevumilia mateso ya ugonjwa huu na kuyazuilia machozi yangu. Baada ya kazi ya siku kutwa ningekuwa nimechoka kabisa. Niliukokota mwili wangu mchovu hadi kwa chumba changu kidogo cha gereza na nilitaka kupata mapumziko, lakini sikuwa hata na chembe ya ya nguvu ya kupata usingizi madhubuti: Ama polisi wa gereza walikuwa wakiniita katikati ya usiku kufanya kitu fulani, au niliamshwa na kelele ya kunguruma iliyopigwa na polisi wa gereza. … Mara kwa mara nilichezewachezewa nao na kuteseka vibaya sana. Aidha, nililazimika kustahimili kutendewa kinyama na polisi hawa wa gereza. Nilikuwa kama mkimbizi nikilala sakafuni au ushorobani, au hata kando ya choo. Nguo nilizoziosha hazikuwa kavu, lakini zilikuwa zimefungwa pamoja na nguo za wafungwa wengine ili kukaushwa. Kuosha nguo katika majira ya baridi kulikuwa kwa kukatisha tamaa hasa, na watu wengi waliambukizwa ugonjwa wa baridi yabisi kwa sababu ya kuvaa mavazi manyevu kwa vipindi virefu vya wakati. Gerezani, haikuchukua muda mrefu kwa watu wenye afya kuwa goigoi na bozi, wadhaifu kimwili au kujawa magonjwa. Mara kwa mara tulikula majani ya mboga ya zamani, yaliyokaushwa na ambayo yalikuwa yamepitwa na msimu. Kama ulitaka kula kitu bora zaidi, basi ulilazimika kununua chakula ghali huko gerezani. Ingawa watu walifanywa kujifunza sheria gerezani, hakukuwa na sheria huko; polisi wa gereza ndio waliokuwa sheria na kama mtu yeyote angewaudhi, walipata sababu ya kukuadhibu—hata kwa kiasi kwamba waliweza kukuadhibu bila sababu yoyote. Hata la kudharauliwa zaidi ni kwamba walichukulia waumini wa Mwenyezi Mungu kuwa wahalifu wa kisiasa, wakisema kuwa uhalifu wetu ulikuwa mbaya zaidi kuliko mauaji na kuchoma mali. Kwa hiyo, walinichukia hasa na walinidhibiti kikamilifu, na kunitesa kikatili sana. Aina hii ya tabia mbovu ni ushahidi usiobadilika wa tabia potovu ya madikteta, upinzani kwa Mbinguni, na kuwa na uadui na Mungu! Baada ya kuvumilia mateso ya kikatili ya gereza, moyo wangu mara kwa mara ulijazwa na hasira ya haki: Ni sheria gani kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu hukiuka? Ni uhalifu gani kumfuata Mungu na kuitembea njia sahihi ya maisha? Wanadamu waliumbwa na mikono ya Mungu na kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu ni sheria ya mbingu na dunia; ni sababu gani serikali ya CCP iliyo nayo ya kuzuia kwa nguvu na kusumbua hili? Kwa dhahiri ni tabia yake potovu na upinzani kwa Mbingu; huwa inajiweka yenyewe dhidi ya Mungu katika kila kipengele, huwa inashikiza kitambulisho cha kupinga maendeleo kwa waumini wa Mwenyezi Mungu na hututesa kwa ukali na kutuharibu. Huwa inajaribu kuwaondosha waumini wote wa Mwenyezi Mungu kwa dharuba moja kali. Si huku ni kubadilisha weusi na weupe na kuwa mpinga maendeleo kikamilifu? Kwa hasira huipinga Mbingu na ina uhasama na Mungu; hatimaye ni lazima ipitie adhabu ya haki ya Mungu! Kila mahali kuna upotovu, lazima kuwe na hukumu; kila mahali kuna dhambi, lazima kuwe na adhabu. Hii ni sheria ya Mungu ya mbinguni iliyoamuliwa kabla, hakuna mtu anayeweza kuitoroka. Uhalifu muovu wa serikali CCP umepanda kwa anga, na itapitia maangamizo ya Mungu. Kama tu Mungu alivyosema: “Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga mwovu huyu, joka wa zamani mwenye chuki, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote; Mungu hatamhurumia hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote, Atamharibu kabisa” (“Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Katika gereza hili la pepo, nilikuwa duni kuliko mbwa wa kutangatanga machoni mwa polisi hawa maovu; hawakunipiga na kunikemea tu, lakini polisi hawa waovu mara kwa mara na kwa ghafla wangeingia kwa vishindo na kutawanya matandiko yangu na vitu vyangu vya kibinafsi kuwa takataka. Pia, wakati wowote ambapo ghasia fulani zilifanyika katika ulimwengu wa nje, watu walio gerezani ambao ni wasimamizi wa masuala ya kisiasa wangenitafuta na kudadisi maoni yangu kuhusu matukio haya na kwa kawaida wangenishambulia kuhusu ni kwa nini niliitembea njia ya kumwamini Mungu. Kila wakati nilipokabiliwa na aina hii ya kuhojiwa, ningekuwa na wasiwasi, kwa sababu sikujua mpango upi muovu waliokuwa nao kwangu. Moyo wangu daima ulikuwa ukimwomba Mungu kwa haraka na kulilia msaada na mwongozo kupitia wakati wa kilele cha hatari hii. Siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, dhuluma, unyonywaji, na ukandamizwaji viliniumiza kwa mateso yasiyosemeka: Kila siku nilipewa kazi ya mikono iliyozidi na majukumu ya kisiasa ya kuchusha, ya kuchosha, nilisumbuliwa pia na ugonjwa wangu na juu ya yote, nilidhoofika akili. Lilinifikisha kwenye ukingo wa kusambaratika. Hasa wakati nilipoona mfungwa wa makamo wa kike amejinyonga kutoka kwa dirisha usiku wa manane kwa sababu hakuweza kuvumilia mateso ya kinyama ya polisi hawa waovu, na mfungwa mwingine mzee wa kike aliyekufa kutokana matibabu ya ugonjwa wake yaliyocheleweshwa, nilizama katika shida zile zile zilizosonga na tena nikaanza kutafakari kujiua. Nilihisi kuwa kifo kilikuwa ndiyo aina bora ya faraja. Lakini nilijua kwamba huko kungekuwa kumsaliti Mungu na singeweza kufanya hivyo. Sikuwa na chaguo jingine lolote ila kuvumilia maumivu yote na kuitii mipango ya Mungu. Lakini mara tu nilipofikiri juu ya hukumu yangu ndefu, na kufikiri juu ya nilivyokuwa mbali na kupata uhuru, nilihisi kuwa hakuna maneno yaliyoweza kuelezea maumivu yangu na kukata tamaa kwangu; nilihisi kuwa sikuweza kuendelea kuhimili hili na kwamba sikujua ni muda gani ningeweza kusimama imara. Ni mara ngapi sikuweza kufanya chochote ila kujifunika kwa mfarishi wangu usiku wa manane na kulia, nikimuomba na kumsihi Mwenyezi Mungu na kumwambia Yeye kuhusu maumivu yote yaliyokuwa kwa mawazo yangu. Katika wakati wa maumivu yangu mengi na kutojiweza, niliwaza: Mimi ninateseka leo ili nipate kujitenga na upotovu na kupokea wokovu wa Mungu. Shida hizi ndizo ninazopaswa kupitia, na ambazo ni lazima nipitie. Mara tu nilipofikiria hili, sikuhisi uchungu tena; Badala yake, nilihisi kuwa kulazimishwa kuingia gerezani kwa sababu ya imani yangu kwa Mungu, na kupitia shida ili kupata wokovu lilikuwa jambo la thamani na umuhimu mkubwa mno; mateso haya yalikuwa ya thamani sana! Bila kujua, dhiki ya moyo wangu ilibadilika kuwa furaha na sikuweza kuzuia hisia zangu; nilianza kuimba bila kufungua mdomo wimbo wa uzoefu niliokuwa na uzoefu nao moyoni mwangu uitwao "Maisha Yetu si ya Bure": "Maisha yetu si ya bure", mateso yetu yana maana. Maisha yetu si ya bure, hatutakubali kughairi bila kujali ni jinsi gani maisha yalivyo magumu. Maisha yetu si ya bure, sisi hupata fursa nzuri ya kumjua Mungu. Maisha yetu si ya bure, sisi tunaweza kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu mkuu. Ni nani aliyebarikiwa kutuliko? Ni nani mwenye bahati kutuliko? Ee, kile ambacho Mungu hutupa kinazidi vyote vya vizazi vilivyopita; tunapaswa kuishi kwa ajili ya Mungu na tunapaswa kumlipa Mungu kwa sababu ya upendo Wake mkubwa." Niliurudia wimbo huo ndani ya moyo wangu na nilivyozidi kuimba ndani ya moyo wangu, ndivyo nilivyozidi kutiwa moyo; nilivyozidi kuimba, ndivyo nilivyozidi kuhisi kuwa nilikuwa na nguvu na furaha. Sikuweza kujizuia kuapa mbele ya Mungu: "Ee, Mwenyezi Mungu, ninakushukuru Wewe kwa faraja Yako na kunitumainisha ambavyo vimenisababisha kuwa tena na imani na ujasiri wa kuendelea kuishi. Umeniruhusu kujisikia kwamba Wewe kweli ni Bwana wa maisha yangu na Wewe ni nguvu ya maisha yangu. Ingawa nimefungwa mahali hapa pa kusikitisha sana, siko peke yangu, kwa sababu Umekuwa pamoja nami daima kupitia siku hizi za giza; Umenipa imani tena na tena na umenipa motisha kuendelea. Ee Mungu, kama ninaweza kutoka nje ya hapa siku moja na kuishi kwa uhuru, basi nitatimiza wajibu wangu na sitauumiza moyo Wako tena wala kujifanyia mipango mwenyewe. Ee Mungu, bila kujali jinsi siku zijazo zilivyo ngumu au zilivyo za shida, niko radhi kukutegemea Wewe kwendelea kuishi na nguvu!"
Gerezani, mara kwa mara nilikumbuka siku za nyuma tukiwa na ndugu zangu wa kiume na wa kike; huo ulikuwa wakati mzuri sana! Kila mtu alishangilia na kucheka, na pia tulikuwa na migogoro, lakini yote haya yalikuwa kumbukumbu nzuri. Lakini kila wakati nilipotafakari juu ya nyakati ambapo kwa uzembe nilifanya kazi zangu za zamani, nilihisi kuwa na hatia sana na mwenye kuwiwa. Nilifikiri juu ya migogoro niliyokuwa nayo na ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa sababu ya tabia yangu ya kiburi; nilihisi kuwa na wasiwasi hasa na mwenye kujuta. Kila wakati hili lilipotokea, ningeangua kilio na kimya kimya ningeimba wimbo mashuhuri katika moyo wangu: “Ninajuta sana, Ninajuta sana, nimepoteza muda mwingi sana wa thamani. Muda husonga mbele milele na ni majuto tu ambayo hubaki. … Kwa ajili ya kuwiwa kwangu kwa zamani na nitaanza upya na imani na kujivunia. Mungu anipa fursa nyingine, na kwa uvumilivu Wake nitafanya uchaguzi wangu mpya. Nitafurahia siku hii hasa, kutenda ukweli, kutekeleza wajibu wangu vizuri inavyowezekana, na hivyo kumridhisha Mungu. Moyo wa Mungu una wasiwasi, umejaa matarajio. Kwa hiyo sitavunja moyo Wake tena" ("Ninajuta sana" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Katika maumivu yangu na kujilaumu, mara kwa mara nilimwomba Mungu moyoni mwangu: Ee Mungu! Kwa hakika nimepungukiwa na Wewe mno; kama Utaliruhusu, niko radhi kutafuta kukupenda Wewe. Baada ya kuondoka gerezani, bado nitakuwa tayari kutimiza wajibu wangu na nitakuwa radhi kuanza tena! Nitaufidia upungufu wangu wa zamani! Wakati wa muda wangu gerezani, nilikuwa nimewakosa hasa wale ndugu wa kiume na wa kike niliokuwa nikiwasiliana nao asubuhi na usiku; kwa kweli nilitaka kuwaona, lakini katika gereza hili la pepo ambalo nilikuwa nimefungiwa, tamaa hii ilikuwa ombi lisilowezekana. Hata hivyo, mara kwa mara ningewaona ndugu hawa wa kiume na wa kike katika ndoto zangu; niliota kwamba tulikuwa tunasoma neno la Mungu pamoja na kuwasiliana ukweli pamoja. Tulikuwa na furaha na wachangamfu.
Wakati wa tetemeko kubwa la ardhi la Wenchuan la mwaka wa 2008, gereza tulimokuwa tulifungiwa ndani lilitetemeshwa na mimi nilikuwa mtu wa mwisho kuhama eneo hilo wakati huo. Katika siku hizo kulikuwa na mitikisiko midogo baada ya tetemeko ambayo haikusita. Wafungwa wote na polisi wa gereza waliogopa sana na kuwa na wasiwasi kiasi kwamba hawakuweza kuendelea. Lakini moyo wangu ulikuwa hasa mtulivu na imara, kwa sababu nilijua kwamba hili lilikuwa ni neno la Mungu likitimia; kulikuwa ni kuwasili kwa ghadhabu kali ya Mungu. Wakati wa tetemeko hilo moja katika miaka mia, neno la Mungu liliulinda moyo wangu daima; ninaamini kwamba maisha na kifo cha mwanadamu vyote vi mikononi mwa Mungu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya hivyo, niko radhi kuitii mipango ya Mungu. Hata hivyo, kitu cha pekee kilichonifanya kuhuzunika ni kama ningekufa, basi singepata tena fursa ya kutimiza wajibu wangu kwa Bwana wa viumbe, singekuwa na fursa tena ya kuufidia upendo wa Mungu, na singeweza kuwaona ndugu zangu wa kiume na wa kike. Lakini, wasiwasi wangu ulikuwa uliozidi; Mungu alikuwa nami daima na alinipa ulinzi mkubwa sana, ambao uliniruhusu kuendelea kuishi baada ya tetemeko la ardhi na kuishi kwa amani wakati wa tetemeko!
Mnamo Januari ya mwaka wa 2011, niliachiliwa mapema, ambako hatimaye kulimaliza maisha yangu ya utumwa gerezani. Katika kupata uhuru wangu, moyo wangu ulikuwa na msisimko mkubwa: Ninaweza kurudi kanisani! Ninaweza kuwa pamoja na ndugu zangu wa kiume na wa kike! Maneno hayakuweza kuelezea hali yangu ya kihisia ya akili. Kile ambacho sikutarajia ni kwamba baada ya kurudi nyumbani, binti yangu hakunijua, na jamaa na marafiki zangu walinitazama kwa mtazamo wa pekee; wote walijitenga nami na hawangeingiliana nami. Watu waliokuwa karibu nami hawakunielewa au kunikaribisha. Wakati huu, ingawa sikuwa gerezani nikidhulumiwa na kuteswa, mitazamo ya dharau, dhihaka, na kuachwa vilifanya kuwe vigumu kustahimili. Nilikuwa dhaifu na hasi. Sikuweza kujizuia kutafakari juu ya siku za nyuma: wakati tukio lilipotendeka, nilikuwa na umri wa miaka thelathini na mmoja tu; wakati nilipotoka gerezani, majira nane ya baridi na majira saba ya joto yalikuwa yamepita. Ni mara ngapi ambapo Mungu alikuwa amepanga watu, mambo na vitu wakati wa upweke wangu na kutojiweza ili kunisaidia; ni mara ngapi maneno ya Mungu yalinifariji katika maumivu yangu na kukata tamaa kwangu; ni mara ngapi nilipotaka kufa Mungu alinipa uwezo wa kuwa na ujasiri wa kuendelea kuishi …. Katika kipindi hicho cha miaka mirefu ya mchungu, ni Mungu aliyeniongoza hatua kwa hatua nje ya bonde la kivuli cha mauti hadi kuendelea kuishi kwa ushupavu. Katika kukabili shida hii sasa, nilikuwa hasi na dhaifu na nilikuwa nimemsikitisha Mungu. Kwa kweli nilikuwa mwoga na mtu asiyeweza ambaye alikuwa alikuwa na asante ya punda! Katika kufikiria hili, moyo wangu ulishutumiwa vikali; sikuweza kujizuia kufikiri juu ya kiapo nilichofanya na Mungu wakati nilipokuwa gerezani: "Kama ninaweza kutoka nje ya hapa siku moja na kuishi kwa uhuru, basi bado nitatimiza wajibu wangu. Siko tayari kuumiza tena moyo wa Mungu na sitajifanyia mipango mwenyewe tena!" Niliwazia kiapo hiki na kutafakari juu ya hali niliyokuwa nayo wakati nilipofanya kiapo kwa Mungu. Machozi yaliyatia ukungu kuona kwangu na polepole nikaimba wimbo mmoja wa neno la Mungu:
Kwa hiari yangu mwenyewe mimi humfuata Mungu. Sijali kama Yeye ananitaka au la. Natafuta kumpenda Yeye, kwa udhabiti kumfuata Yeye. Nitampata Yeye, na kutoa maisha yangu Kwake.
I. Mapenzi ya Mungu yatimizwe. Moyo wangu utolewe kwa Mungu kikamilifu. Bila kujali Mungu anafanya nini au Anachonipangia, nitaendelea kufuata, nikitafuta kumpata Yeye. Kwa hiari yangu mwenyewe ninamfuata Mungu. Sijali kama Yeye ananitaka au la. Natafuta kumpenda Yeye, kwa udhabiti kumfuata Yeye. Mimi nitampata, na kutoa maisha yangu kwake.
II. Ukitamani kusimama na kutimiza mapenzi ya Mungu, ukitaka kumfuata Yeye mpaka mwisho, kuweka msingi imara, tenda ukweli katika vitu vyote. Hili humpendeza Mungu na Yeye ataimarisha upendo wako. Kwa hiari yangu mwenyewe mimi humfuata Mungu. Sijali kama Yeye ananitaka au la. Natafuta kumpenda Yeye, kwa udhabiti kumfuata Yeye. Nitampata Yeye, na kutoa maisha yangu Kwake.
III. Unapokabiliwa na majaribu, unahuzunika na kuteseka. Lakini, kwa ajili ya kumpenda Mungu, ungevumilia kila shida, kuacha maisha yako na kila kitu. Kwa hiari yangu mwenyewe mimi humfuata Mungu. Sijali kama Yeye ananitaka au la. Natafuta kumpenda Yeye, kwa udhabiti kumfuata Yeye. Nitampata Yeye, na kutoa maisha yangu Kwake. ("Sitapumzika Mpaka Nimpate Mungu" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya)
Baada ya muda wa ibada za kiroho na urekebishaji, kwa haraka nilitoka nje ya uhasi wangu chini ya kunurishwa kwa Mungu na nikajirudisha kwenye safu za kutimiza wajibu wangu.
Hata kama miaka bora zaidi ya ujana wangu ilitumika gerezani; katika miaka hii saba na miezi minne nilipopitia shida kwa sababu ya imani yangu katika Mungu, sina malalamiko na sina majuto, kwa sababu ninaelewa ukweli fulani na nimepitia upendo wa Mungu. Nahisi kuwa kuna maana na thamani kwa mateso yangu; hili ni jambo la pekee la utukufu na neema ambazo Mungu alinitengenezea, hili ni pendeleo langu! Hata kama jamaa na marafiki zangu hawanielewi, na hata kama binti yangu hanijui, hakuna mtu, jambo au kitu kitakachoweza kunitenga na uhusiano wangu na Mungu; hata kama nikifa, siwezi kumwacha Mungu.
Upendo Safi Bila Dosari ndio wimbo niliopenda sana kuuimba gerezani; sasa, nataka kutumia matendo yangu halisi kutoa upendo safi zaidi kwa Mungu!
kutoka kwa Ushuhuda wa Washindi
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.

Jumatano, 24 Oktoba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 2.Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe

Dong Mei, Mkoa wa Henan
Mimi ni mtu wa kawaida. Niliishi maisha ya kawaida. Kama wengi wanaotamani sana mwanga, nilijaribu njia nyingi kutafuta maana ya kweli ya uwepo wa wanadamu, nikijaribu kuyapa maisha yangu umuhimu zaidi. Mwishowe, juhudi zangu zote zilikuwa bure. Lakini baada ya kuwa na bahati ya kutosha kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, mabadiliko ya muujiza yalitokea katika maisha yangu. Yalileta rangi zaidi katika maisha yangu, na nilikuja kuelewa kwamba ni Mungu pekee ni Mtoa wa kweli wa roho na maisha ya wanadamu. Nilikuwa na furaha kwamba hatimaye nilikuwa nimepata njia sahihi ya maisha. Hata hivyo, huku nikitekeleza wajibu wangu wakati mmoja nilikamatwa kiharamu na kuteswa kikatili na serikali ya CCP. Kutoka kwa hili, safari ya maisha yangu ilipata uzoefu ambao kamwe sitasahau ...
Siku moja mnamo Desemba 2011 takribani saa moja asubuhi, mimi na kiongozi mwingine wa kanisa ulikuwa tukitekeleza hesabu ya mali ya kanisa wakati zaidi ya maafisa kumi wa polisi ghafla waliingia. Mmoja wa hawa polisi waovu alitukurupia na kusema kwa kelele: “Msisonge!” Baada ya kuona kilichokuwa kikitokea, kichwa changu kilishtuka. Kisha, polisi waovu walituchungquza kama magaidi waliokuwa wakitekeleza wizi. Pia walipekua kila chumba, walivigeuza shelabela kwa haraka sana. Mwishowe, walipata mali fulani ya kanisa, kadi tatu za benki, risiti za kuweka pesa, kompyuta, simu za rununu, na kadhalika. Waliyachukua yote ngawira, na kisha walituchukua sisi wanne kwa kituo cha polisi.
Alasiri, polisi waovu waliwaleta ndani dada wengine watatu ambao walikuwa wamewakamata. Walitufungia sisi saba katika chumba na hawakuacha tuzungumze, wala hawakuturuhusu tulale usiku ulipofika. Baada ya kuona dada wakifungiwa ndani na mimi, na kufikiri kuhusu ni kiasi gani cha pesa ambacho kanisa lilipoteza, nilikuwa nimezuzuliwa na wasiwasi. Yote ambayo ningefanya ni kuomba kwa dharura kwa Mungu: Ee Mungu! Huku nikikabiliwa na hali ya aina hii, sijui la kufanya. Tafadhali linda moyo wangu na kuufanya mtulivu. Baada ya kuomba, nilifikiri maneno ya Mungu: “Usiogope, mambo kama haya yanapofanyika katika kanisa, yote yanaruhusiwa na Mimi. Simama na kuwa sauti Yangu. Kuwa na imani kwamba mambo na vitu vyote vinaruhusiwa na kiti Changu cha enzi na vyote vina nia zangu ndani yavyo” (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). “Unapaswa kujua kwamba vitu vyote katika mazingira yaliyokuzunguka yako hapo kwa ruhusa Yangu, Napanga yote. Ona kwa dhahiri na kuridhisha moyo Wangu katika mazingira ambayo Nimekupa” (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). Maneno ya Mungu yalizima hofu kubwa moyoni mwangu. Nilitambua kwamba, leo, hii hali imenipata kwa ruhusa ya Mungu, na kwamba wakati ulikuwa umewadia ambapo Mungu alitaka nimshuhudie. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, nilimwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Nataka kutii utaratibu na mipango Yako na kusimama imara katika ushuhuda Kwako—lakini mimi ni wa kimo kidogo, na naomba kwamba Unipe imani na nguvu, na kunilinda katika kusimama imara.”
Asubuhi iliyofuata, walitutenga na kutuhoji. “Najua wewe ni kiongozi wa kanisa. Tumekuwa tukiwafuatia ninyi watu kwa miezi mitano,” alisema mmoja wa polisi waovu kwa maringo. Nilipomsikia akieleza kwa utondoti kila kitu ambacho walikuwa wamefanya kunifuatia, nilitetemeka kwaa woga. Katika akili yangu, nilifikiri, Polisi waovu kweli waliweka matayarisho mengi katika kutukamata. Kwa kuwa tayari wanajua mimi ni kiongozi wa kanisa, hakuna jinsi wataniacha niende. Mara moja niliweka azimio langu mbele ya Mungu: Afadhali nife badala ya kumsaliti Mungu na kuwa Yuda. Baada ya kuona kuwa kuhoji kwao hakukuwa kunazaa matunda yoyote, walimpa mtu kazi ya kunitazama na kutoniacha nilale.
Katika siku ya tatu ya mahojiano, mkuu wa polisi waovu aliwasha kompyuta na kunifanya nisome taarifa zilizomsingizia Mungu. Kwa kuona kwamba sikuguswa, baada ya hapo alinihoji kwa makini kuhusu fedha za kanisa. Niligeuza kichwa changu kwa upande mmoja na kumpuuza. Hili lilimfanya kukasirika sana na alianza kutukana. “Haijalishi usiposema lolote—tunaweza kukuzuia bila mwisho, na kukutesa wakati wowote ule tunaotaka,” alinitisha kwa ukali. Katikati ya usiku huo, polisi walianza mateso yao. Walivuta mkono wangu mmoja nyuma ya bega langu na mwingine juu kutoka kwa mgongo wangu. Walifinya mgongo wangu na miguu yao, kwa nguvu walitia pingu vifundo pamoja. Ilikuwa uchungu sana kiasi kwamba nilipiga yowe kwa maumivu—mifupa na nyama katika mabega yangu zilihizi kana kwamba zingepasuka. Ningeweza tu kupiga magoti bila kusonga na kichwa changu kikiwa sakafuni. Nilifikiri mayowe yangu yangewafanya watulize makali kwangu, lakini badala yake waliweka kikombe cha chai kati ya pingu na mgongo wangu, jambo ambalo lilizidisha tena maumivu. Mifupa katika mwili wangu wa juu ilihisi kana kwamba ilikuwa imevunjwa nusu. Nilihisi uchungu sana hivi kwamba sikuthubutu kupumua nje na jasho baridi ilitiririka usoni pangu. Punde tu nilipohisi kwamba singevumilia uchungu tena, mmoja wa polisi waovu alichukua fursa hii kuniambia: “Tupe tu jina na tutakuachilia uende mara moja.” Wakati huo, nilimwita Mungu aulinde moyo wangu. Mara moja nilifikiri maneno ya wimbo wa uzoefu wa maisha: “Mungu mwenye mwili hupitia maumivu. Je, mimi, mtu huyu mpotovu, napaswa kuteseka kiasi gani zaidi? Nikikubali ushawishi wa giza, nawezaje kukutana na Mungu? ...Afadhali nivumilie taabu zote, na kufidia huzuni kubwa ya Mungu” (“Kusubiri Habari Njema Kutoka kwa Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wimbo ulinipa nguvu. Ndiyo—Mungu mwenye mwili amepitia uchungu huo wote kwa ajili ya wokovu wetu, nami, mtu huyu aliyepotoshwa kwa kina na Shetani, lazima niteseke hata zaidi. Iwapo ningekubali kushindwa na Shetani kwa sababu singeweza kuvumilia uchungu, ningewezaje kukabiliana na Mungu wakati wowote tena? Kufikiri hili kulinipa nguvu, na nikakua mgumu mara nyingine tena. Polisi waovu walinitesa kwa takriban saa moja. Walipoondoa pingu, mwili wangu mzima ulianguka bila nguvu sakafuni. “Usipoongea tutafanya hilo tena!” walinipigia kelele. Niliwatazama na kutosema chochote. Moyo wangu ulijawa na chuki kwa polisi hawa waovu. Mmoja wa polisi waovu alisonga mbele kutia pingu tena. Huku nikifikiri uchungu mkali sana ambao nilikuwa nimeupita karibuni, niliendelea kumwomba Mungu moyoni mwangu. Kwa mshangao wangu, alipojaribu kuvuta mikono yangu nyuma ya mgongo wangu hangeweza kuisogeza. Haikuwa uchungu sana, pia. Alikuwa akijaribu kwa nguvu sana hivi kwamba kichwa chake chote kilikuwa kimejaa jasho—lakini bado hangeweza kutia pingu. “Una nguvu mwingi!” alitweta kwa hasira. Nilijua kwamba huyu alikuwa Mungu akinijali, kwamba Mungu alikuwa akinipa nguvu. Shukrani iwe kwa Mungu!
Kufika alfajiri kulikuwa vigumu. Bado nilikuwa na kiwewe nilipofikiri nyuma jinsi polisi waovu walikuwa wamenitesa. Pia walinitisha, wakiniambia kwamba iwapo singesema chochote, wangelazimika kunipeleka ndani sana ya milimani na kuniua. Baadaye, walipokamata waumini wengine, wangesema nililisaliti kanisa—wangechafua jina langu, na kuwafanya ndugu wengine wa kanisa wanichukie na kunikana. Kufikiri hilo, moyo wangu ulizidiwa na mawimbi ya majonzi na kutojiweza. Nilijipata nikihisi mwoga na mnyonge. Akilini mwangu nilifikiri: Afadhali nife. Kwa njia hiyo sitakuwa Yuda na kumsaliti Mungu, wala sitakanwa na ndugu zangu. Pia nitaepuka uchungu wa mateso ya mwili. Kwa hivyo nilingoja hadi wakati ambapo polisi waovu waliokuwa wakinilinda hawakuwa wakitia makini na kuupiga kichwa changu kwa nguvu sana dhidi ya ukuta—lakini yote yaliyotokea ilikuwa kwamba kichwa changu kiliona kizunguzungu, sikufa. Wakati huo, maneno ya Mungu yalinipa nuru kutoka ndani: “katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kwa rehema ya Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana” (Kutoka kwa “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Wengine wanapokuelewa vibaya, unaweza kumwomba Mungu na kusema: ‘Ee Mungu! Siombi kwamba wengine wanivumilie, wala kwamba wanisamehe. Naomba tu kwamba niweze kukupenda moyoni mwangu, kwamba niwe na uhakika moyoni mwangu, na kwamba dhamiri yangu ni safi. Siombi kwamba wengine wanisifu, au kuniheshimu, ninatafuta tu kukuridhisha kutoka moyoni mwangu’” (Kutoka kwa “Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kumpenda Mungu kwa Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yaliondoa huzuni kutoka kwa moyo wangu. Ndiyo—Mungu huwataka watu wenye azimio, watu ambao wanaweza kumshuhudia Mungu mbele ya Shetani, watu ambao wanaweza kustahimili hadi mwisho kabisa na kufuata mipango yote ya Mungu bila kujali jinsi taabu wanayopitia ilivyo kubwa. Hata zaidi, Mungu huona mioyo ya ndani kabisa ya watu. Iwapo polisi wakinisingizia, hata kama ndugu wengine kwa kweli wanielewe visivyo na kunikataa kwa sababu hawajui kile kilichotendeka kwa kweli, naamini kwamba nia za Mungu ni nzuri; Mungu anajaribu imani na upendo wangu Kwake, na napaswa kufuatilia kumfanya Mungu kuridhika. Baada ya kubaini njama janja za Shetani, ghafla nilihisi mwenye fedheha na aibu. Niliona kwamba imani yangu kwa Mungu ilikuwa ndogo sana. Sikuwa nimeweza kusimama imara baada ya kupitia uchungu kidogo, na nilikuwa nimefikiri kutoroka na kuepuke mipango ya Mungu kupitia kifo. Watu wanapomwacha Mungu, wanaishi katika giza. Lengo la polisi waovu katika kuzungumza maneno haya ya tishio lilikuwa kunifanya nimkane Mungu. Na isingekuwa ulinzi wa Mungu, ningedanganywa na njama zao janja. Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, moyo wangu ulijawa na mwanga. Sikutaka tena kufa, ila kuishi maisha mazuri, na kutumia kile ambacho kweli niliishi kwa kudhihirisha kumshuhudia Mungu na kumletea Shetani aibu.
Polisi hao wawili waovu waliopewa kazi ya kunilinda waliuliza mbona nilikuwa nimegongesha kichwa changu dhidi ya ukuta. Nilisema kwa sababu polisi hao wengine walikuwa wamenipiga. “Kimsingi tunafanya kazi kupitia elimu. Usijali—sitawaacha wakupige tena,” mmoja wao alisema kwa tabasamu. Baada ya kusikia maneno yake ya faraja, nilifikiri: Hawa watu wawili si wabaya; tangu nikamatwe wamekuwa wazuri kabisa kwangu. Kwa hilo, nililegeza tahadhari yangu. Lakini wakati huo, maneno ya Mungu yalikuja ghafla moyoni mwangu: “Nyakati zote, watu Wangu wanapaswa kujihadhari dhidi ya hila danganyifu za Shetani, walinde lango la nyumba Yangu kwa ajili Yangu, … kitu ambacho kitawazuia kuingia katika mtego wa Shetani, wakati mtakapokuwa na majuto ya kuchelewa sana” (“Tamko la Tatu” la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa kumbusho la wakati wa kufaa, yakinionyesha kwamba njama janja za ibilisi ni nyingi, na napaswa kuwa hadhari dhidi ya ibilisi hawa wakati wote. Sikutarajia hata kidogo kwamba punde wangefichua tabia zao halisi. Mmoja wa polisi waovu alianza kumkashifu Mungu, huku mwingine aliketi chini kando yangu alinipapasa mguu wangu, akinitazama kwa jicho la husuda na kuuliza kuhusu fedha za kanisa. Jioni, alipoona kwamba nilikuwa nikisinzia, alianza kupapasa kifua changu. Baada ya kuona kwamba walikuwa wamefichua tabia yao halisi, nilijawa na hasira. Ni sasa tu nilipoona waliodhaniwa polisi wa watu walikuwa tu wahuni na wadhalimu. Haya yalikuwa mambo mabaya yenye kustahili dharau, ambayo wangeweza kufanya. Kama matokeo, niliweza tu kumwomba Mungu kwa dharura ili anilinde kutokana na madhara yao.
Katika siku kadhaa zilizofuata, polisi waovu hawakunihoji tu kwa makini kuhusu kanisa, lakini pia walichukua zamu kunitazama ili kwamba nisilale. Baadaye, walipoona jinsi sikuwa nimewapa chochote, polisi hao wawili waovu waliokuwa wakinihoji walizidi kwa ghadhabu. Mmoja wao alinishambulia vikali, akinizaba kofi usoni, akinipiga kwa vishindo mara kadhaa. Uso wangu uliwasha, ulianza kuvimba, na mwishowe ukawa wenye ganzi sana kiasi kwamba singehisi chochote. Kwa sababu maswali yao hayakuwa yamezaa matunda yoyote kutoka kwangu, jioni moja mkuu wa polisi waovu alinipigia unyende na kusema, “Unahitaji kuanza kufungua mdomo wako. Unajaribu subira yangu—siamini kwamba hakuna chochote tunaweza kufanya na wewe. Nimekutana na watu wengi wagumu zaidi kukuliko. Tusipokuwa wakali kwako, hutatii katu!!” Alitoa amri na polisi waovu kadhaa walianza kunitesa. Jioni, chumba cha mahojiano kilikuwa cha huzuni na cha kuogofya—nilihisi kana kwamba nilikuwa jahanamu. Walinifanya nichutame sakafuni na kufunga mikono yangu katikati ya magoti na miguu yangu. Kisha, waliingiza kifimbo cha mbao katikati ya mapindi ya mikono yangu na nyuma ya magoti yangu, wakilazimisha mwili wangu wote kupinda juu. Kisha walikiinua kifimbo na kukiweka katikati ya meza mbili, wakiuacha mwili wangu wote ukining’inia hewani na kichwa changu kikiwa juu chini. Punde waliponiinua juu, kichwa changu kilipata kizunguzungu na niliona vigumu kupumua. Ilihisi kana kwamba nilikuwa nikisongwa. Kwa sababu nilikuwa nilining’inishwa hewani juu chini uzito wangu wote ulikuwa ukiangukia vifundo vyangu. Mwanzoni, ili kukomesha pingu kuukata mwili wangu, nilifumbata mikono yangu pamoja kwa kukaza, nikaupinda mwili wangu, na kujaribu kwa nguvu kadiri nilivyoweza kubaki katika hali hiyo. Lakini nguvu yangu ilipungua polepole. Mikono yangu iliteleza kutoka kwa vifundo vya miguu hadi kwa magoti yangu, na pingu ilikata kwa kina katika mwili wangu, ikiniacha na uchungu mkubwa sana. Baada ya kuning’inia hivi kwa takribani nusu saa, ilihisi kana kwamba damu yote katika mwili wangu ilikuwa imejikusanya kichwani mwangu. Uvimbe mchungu katika kichwa changu na macho ulifanya yahisi kana kwamba yalikuwa karibu kulipuka. Makato ya kina yalikuwa yamechimbwa katika vifundo vyangu, na mikono yangu ilikuwa imevimba sana kiasi kwamba ilionekana kama mikate miwili. Nilihisi nilikuwa ukingoni mwa kifo. “Siwezi kuvumilia tena, niweke chini!” nilipaza sauti kwa kukata tamaa. “Hakuna anayeweza kukuokoa ila wewe mwenyewe. Tuambie tu jina na tutakuacha uteremke chini,” alisema mmoja wa polisi waovu kwa ukali. Mwishowe, waliona kwa kweli nilikuwa katika taabu na waliniweka chini. Walinilisha glukosi kiasi na kuanza kunihoji tena. Nililala bila nguvu kama matope ardhini, macho yangu yakifumbwa kwa kukaza, nikiwa siwatilii makini. Bila kutarajia, polisi waovu waliniinua hewani tena. Bila nguvu ya kushikilia kwa mikono yangu, sikuwa na lingine ila kuacha pingu ijitie ndani katika vifundo vyangu, makali yaliyochongoka yakikata mwili wangu. Wakati huo, ilikuwa uchungu sana nilitoa yowe la kuhuzunisha sana. Sikuwa na nguvu ya kuendelea kupigana na kupumua kwangu kulikuwa kumekua kwa kina kifupi sana. Ilionekana kana kwamba wakati ulikuwa umesimama. Nilihisi kwamba nilikuwa nikiyumbayumba ukingoni mwa kifo. Nilipofikiri kwamba wakati huu kweli ningekufa, nilitaka kumwambia Mungu maneno yaliyokuwa moyoni mwangu kabla ya maisha yangu kuisha: “Ee Mungu! Wakati huu, ambapo kweli niko ukingoni mwa kifo, nahisi woga— lakini hata kama kweli nikifa leo, bado nitasifu haki Yako. Ee Mungu! Katika safari yangu fupi ya maisha, nakushukuru kwa kunichagua nirudi nyumbani kutoka kwa dunia hii ya dhambi, kunizuia kuzurura, nikiwa nimepotea, na kuniruhusu kuishi milele katika kumbatio Lako kunjufu. Ee Mungu, nimefurahia upendo Wako sana—na ilhali sasa tu, wakati maisha yangu yako karibu kuisha, ndipo nagundua kwamba sijatunza upendo Wako. Nyakati nyingi nimekufanya kuwa na huzuni na masikitiko; mimi ni kama mtoto mjinga anayejua tu kufurahia upendo wa mama yake, ilhali hajawahi kufikiria kuulipiza. Sasa tu ambapo niko karibu kupoteza maisha yangu ndipo naelewa kwamba ni lazima nitunze upendo Wako, na ni sasa tu ndipo najuta kukosa nyakati nyingi nzuri. Sasa, ninachojuta zaidi ni kwamba sijaweza kukufanyia lolote na unanidai mengi sana, na kama bado naweza kuishi, kwa hakika nitafanya kila niwezalo kutekeleza wajibu wangu, kufidia kile Unachonidai. Wakati huu, naomba tu kwamba Unipe nguvu, kuniruhusu kutowahi tena kuogopa kifo, na kuwa mwenye nguvu katika kile ninachokabili....” Tone baada ya tone la machozi lilianguka kutoka kwa paji la uso wangu. Usiku ulikuwa kimya kiasi cha kuogofya. Sauti ya pekee ilikuwa saa kubwa ikipiga ta-ta, kana kwamba kuhesabu sekunde ambazo zilisalia za maisha yangu. Hapo ndipo kitu cha muujiza kilifanyika: Nilihisi kana kwamba mwanga wa jua wa vuguvugu ulikuwa ukiniangazia, na polepole niliacha kuhisi uchungu mwilini mwangu. Maneno ya Mungu nguruma akilini mwangu: “Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo” (Kutoka kwa “Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ndiyo—Mungu ndiye chanzo cha maisha yangu, Mungu hutawala kudura yangu, na lazima nijiachilie mikononi mwa Mungu na kujiweka katika matumizi Yake. Kutafakari maneno ya Mungu kulinipa hisia ya kufurahisha, tulivu moyoni mwangu, kana kwamba nilikuwa nikijinyoosha katika kumbatio kunjufu la Mungu. Nilijipata nikilala. Wakiwa na woga kwamba ningekufa, polisi waovu waliniweka chini na kwa haraka walinipa glukosi kiasi na maji. Katika kukaribia kwangu kifo, nilikuwa nimetazama matendo ya muujiza ya Mungu.
Siku iliyofuata, polisi waovu walishinda jioni nzima wakiniinua juu tena na tena. Walinihoji kuhusu mahali ambapo pesa za risiti ambazo walikuwa wamechukua ngariwa zilikuwa. Wakati huo wote, sikusema chochote—ilhali bado hawakukata tamaa. Ili kupata pesa za kanisa, walitumia kila njia yenye kustahili dharau kunitesa. Wakati huo, maneno ya Mungu yalirudia rudia moyoni mwangu: “Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo–inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake, usimwache kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa Shetani huyu wa zamani” (Kutoka kwa “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa nguvu na imani kubwa. Ningepigana hadi kufa na Shetani, na hata kama ningekufa, ningesimama imara katika ushuhuda wangu kwa Mungu. Nikitiwa msukumo na maneno ya Mungu, bila kujua nilisahau uchungu. Kwa njia hii, kila wakati waliniinua juu, maneno ya Mungu yalinitia msukumo na kunipa motisha, na hivyo kadiri walivyonibeba juu mara nyingi, ndivyo nilivyoweza kubaini asili yao zaidi—ambayo ilikuwa ya ibilisi waovu—na ndivyo azimio langu kusimama imara katika ushuhuda wangu na kumridhisha Mungu lilivyokuwa kubwa zaidi. Mwishowe, wote walichoshwa na mimi. “Watu wengi sana hawawezi kuvumilia kutundikwa hivi kwa nusu saa, lakini amevumilia wakati huu wote—kwa kweli yeye ni sugu!” Niliwasikia wakitoa mawazo. Kwa kusikia maneno haya, nilijawa na msisimko. Akilini mwangu, nilifikiri: Mungu msaada wangu, huwezi kunivunja moyo. Mbali na mateso ya mwili, wakati wa siku na usiku zangu tisa katika kituo cha polisi polisi waovu pia walininyima usingizi. Kila wakati nilipofunga macho yangu na kuanza kusinzia, wangepiga vifimbo vyao dhidi ya meza, au sivyo wangenifanya nisimame na kukimbia huku na kule, au sivyo kunipigia kelele tu, wakijaribu kunihuzunisha na kuvunja akili yangu. Baada ya siku tisa, wakiona kwamba hawakuwa wamefikia lengo lao, polisi bado hawakukata tamaa. Walinipeleka katika hoteli, ambapo walitia pingu mikono yangu mbele ya miguu yangu, kisha wakaingiza kifimbo cha mbao katikati ya mapindi ya mikono na miguu yangu, nikilazimika kuketi mwili wangu ukiwa umepinda juu sakafuni. Walinifanya nibaki katika hali hii nikiketi sakafuni kwa siku kadhaa zilizofuata, ambayo ilisababisha pingu kuukata mwili wangu. Mikono na vifundo vyangu vilivimba na kubadilika rangi kuwa zambarau, na kikalio changu kilihisi uchungu sana sikuthubutu kukisugua ama kukishika; ilihisi kama nilikuwa nikikalia sindano. Siku moja, mmoja wa viongozi wa polisi waovu, akiona kwamba mahojiano yangu hayakuwa yamezaa matunda, alitembea kunifikia akiwa amekasirika sana na kunizaba kofi kwa nguvu usoni—kwa nguvu kiasi cha kutosha kulegeza meno yangu mbili.
Mwishowe, wakuu wawili kutoka kwa Idara ya Usalama wa Umma ya Mkoa walikuja. Punde walipowasili, waliondoa pingu, wakanisaidia kwenda kwa kochi, na kunipa kikombe cha maji. “Umekuwa na wakati mgumu kwa siku chache zilizopita—lakini usilitilie moyoni, walikuwa wakifuata tu amri,” walisema kwa unafiki. Unafiki wao ulinifanya niwachukie sana kiasi kwamba nilisaga meno yangu. Pia walijaribu kutumia Biblia kunileta upande wao, na kuwasha kompyuta na kunionyesha ushahidi usio kweli. Walisema maneno mengi ambayo yalishutumu na kufukuru dhidi ya Mungu. Moyoni mwangu, nilihisi kukasirishwa. Nilitaka kubishana nao, lakini nilijua kwamba kufanya hivyo kungewafanya tu kukufuru dhidi ya Mungu kwa wayowayo hata zaidi. Wakati huu, nilihisi kweli jinsi taabu aliyopitia Mungu mwenye mwili ilivyokuwa kubwa, na jinsi Mungu alivyovumilia fedheha nyingi kwa ajili ya kumwokoa mwanadamu. Kilicho zaidi, niliona uhafifu na kustahili dharau kwa ibilisi hawa waovu. Moyoni mwangu, kwa siri niliapa kwamba ningejiondoa kabisa kwa Shetani na milele kuwa mwaminifu kwa Mungu. Baadaye, bila kujali jinsi walivyojaribu kunidanganya, niliendelea kufunga mdomo wangu na sikusema chochote. Baada ya kuona kuwa maneno yao hayakuwa na athari yoyote, wakuu hao wawili waliondoka tu kwa hasira.
Katika kipindi cha siku na usiku kumi katika hoteli, waliendelea kunitia pingu, wakinifanya kuchuchumaa sakafuni nikishika miguu yangu. Nikikumbuka tangu nilipokamatwa, nilikuwa nimeishi siku na usiku kumi na tisa katika kituo cha polisi na hoteli. Ulinzi wa upendo wa Mungu ulikuwa umeniruhusu nilale kidogo, lakini polisi waovu hawakuwa wameniruhusu kulala wakati huo wote; ningefunga macho tu kwa muda na wangefanya chochote kilichohitajika kuniweka macho—kupiga meza, kunipiga teke kwa nguvu, kunipigia kelele, kuniamuru nikimbie huku na kule, na kadhalika. Kila wakati ningeshtuliwa, moyo wangu ungetwanga kifuani mwangu, na ningehisi woga sana. Hilo, likiongezwa kwa mateso ya mara kwa mara ya polisi waovu, na nguvu yangu iliishia kupunguka kabisa, mwili wangu wote ulikuwa umevimba na usiotulia, na niliona kila kitu vikiwa mbili mbili. Ningejua kulikuwa na watu mbele yangu wakiongea, lakini sauti ya milio yao ingeonekana kana kwamba ilikuwa ikitoka mbali sana. Zaidi ya hayo, mijibizo yangu ilianza kuwa ya polepole sana. Kwa mimi kustahimili hili kwa kiasi fulani kulikuwa yote kwa sababu ya nguvu kuu ya Mungu! Kama alivyosema Mungu: “Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu…. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha si rahisi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui” (Kutoka kwa “Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili). Moyoni mwangu, nilitoa shukrani na sifa ya uaminifu kwa Mungu: Ee Mungu! Unatawala vitu vyote, matendo Yako ni yasiyokadirika, Wewe pekee ni mwenyezi, Wewe ni nguvu ya maisha isiyozimika, Wewe ni chemichemi ya maji hai kwa maisha yangu. Katika hali hii maalum, nimetazama nguvu Yako maalum na mamlaka. Mwishowe, polisi waovu hawakupata majibu kwa maswali yao kutoka kwangu, na walinituma hadi katika kituo cha kuzuia.
Njiani kuelekea katika kituo cha kuzuia, polisi wawili waliniambia: “Umefanya vizuri sana. Ninyi watu huenda mkawa katika kituo cha kuzuia, lakini ninyi ni watu wazuri. Kuna aina nyingi hapo: wauza madawa, wauaji, malaya—utaona utakapowasili.” “Kwa kuwa unajua sisi ni watu wazuri, mbona mnatukamata? Je, serikali haiongei kuhusu uhuru wa dini?” niliuliza. “Hiyo ni Chama cha Kikomunisti inawadanganya. Chama hicho hutupa riziki yetu, kwa hivyo lazima tufanye kinachosema. Hatuna chuki kwako ama kuwa na kitu chochote dhidi yako. Tulikukamata tu kwa sababu unamwamini Mungu,” mmoja wa polisi alisema. Baada ya kusikia hili, nilikumbuka kila kitu nilichokuwa nimepitia. Singeweza kuzuia kukumbuka maneno ya Mungu: “Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi!” (Kutoka kwa “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yaliulenga kiini cha suala, yakiniruhusu kuona kwa kweli sura ya kweli ya serikali ya CCP na jinsi inavyojaribu kupata heshima ambayo haistahili; kwa juu juu, inapeperusha bendera ya uhuru wa dini, lakini kwa siri inakamata, kukandamiza, na kushambulia wale wanaomwamini Mungu pande zote za nchi na kupora pesa za kanisa—yote ambayo huweka wazi asili yake ya yenye dhambi ya kuchukiza, ya shetani.
Nikiwa katika kituo cha kuzuia, kulikuwa na nyakati ambapo nilikuwa dhaifu na katika maumivu. Lakini maneno ya Mungu yaliendelea kunipa moyo, kunipa nguvu na imani, kuniruhusu kuelewa kwamba ingawa Shetani alikuwa ameniondolea uhuru wa mwili, mateso yalikuwa yameniongeza, yakinifundisha kumtegemea Mungu wakati wa mateso ya hao ibilisi waovu, kuniruhusu kuelewa maana ya kweli ya ukweli mwingi, kuona thamani ya ukweli, na kuongeza azimio langu na motisha ya kufuatilia ukweli. Nilikuwa tayari kuendelea kumtii Mungu, na kupitia yote ambayo Mungu alikuwa amenipangia. Kama matokeo, nilipokuwa nikifanya kazi katika kituo cha kuzuia, niliimba nyimbo na kwa kimya nilifikiri kuhusu upendo wa Mungu. Nilihisi kwamba moyo wangu ulikuwa umekuja karibu na Mungu, na sikuona tena siku zikiwa chungu ama za kudhikisha sana.
Wakati wa kipindi hiki, polisi waovu walinihoji mara mingi zaidi. Nilimshukuru Mungu kwa kuniongoza katika kushinda mateso yao mara kwa mara tena. Baadaye polisi waovu waliondoa pesa zote kutoka kwa kadi zangu tatu za benki. Kutazama bila kujiweza peza za kanisa zikichukuliwa na polisi waovu kuliuvunja moyo wangu. Moyo wangu ulijawa na chuki kwa hili kundi lafi, ovu la ibilisi, na nilitamani sana ufalme wa Kristo kuwasili punde. Mwishowe, licha ya kutokuwa na ushahidi wowote, walinihukumu mwaka mmoja na miezi mitatu ya kuelimishwa tena kupitia kazi kwa ajili ya “kuvuruga utulivu wa umma.”
Baada ya kuteswa kikatili na serikali ya CCP, kwa kweli nilikuwa nimeonja upendo na wokovu wa Mungu kwangu, na nilikuja kufahamu ukuu na uweza wa Mungu na matendo Yake ya muujiza, nilikuwa nimeona mamlaka na nguvu ya maneno ya Mungu. Aidha kwa kweli nilikuwa nimemdharau Shetani. Katika kipindi hicho cha mateso, maneno ya Mungu yalikuwa yameandamana na mimi kupitia mchana na usiku za kudhikisha, maneno ya Mungu yalikuwa yameniruhusu kubaini njama janja za Shetani na kutoa ulinzi wa wakati wa kufaa. Maneno ya Mungu yalikuwa yamenifanya kuwa mwenye nguvu na ujasiri, yakiniruhusu kushinda mateso yao katili mara kwa mara tena. Maneno ya Mungu yalikuwa yamenipa nguvu na imani, yalikuwa yamenipa ujasiri wa kupigana na Shetani hadi mwisho kabisa.... Shukrani ziwe kwa Mungu! Mwenyezi Mungu ndiye ukweli, njia na uzima! Daima nitamfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho kabisa!
kutoka kwa Ushuhuda wa Washindi