Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wakristo-wa-China. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wakristo-wa-China. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 23 Machi 2019

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Mchezo mfupi Mipaka ya Meya wa Kijiji inaeleza hadithi ya kweli ya mume na mke Wakristo ambao wanalazimishwa kutoroka kwa sababu ya mateso ya serilaki ya CCP.
Mkristo Liu Ming'en anahukumiwa na CCP miaka saba gerezani kwa kuamini katika Mungu. Hata baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, anabakia kuwa wakulengwa na uchunguzi mkali wa CCP. Meya wa kijiji anatumia mfumo wa wajibu wa kaya-tano , kamera za usalama, ziara za nyumba, na njia nyingine kumzuia Liu Ming'en na mkewe kuamini katika Mungu, lakini hakuna inayoleta na matokeo yanayotakiwa. Wakati huu, meya anapokea taarifa za kipaumbele kutoka Kamati Kuu ya Chama, baada ya hapo anajaribu kutafuta njia za kumlazimisha Liu Ming'en na mkewe kuweka saini barua ya kuahidi kuacha kuamini katika Mungu. Baada ya hila yake kushindwa, polisi tena wanakuja kuwakamata waumini hawa wawili. Kuepuka kukamatwa na kuendelea kumfuata Mungu na kuamini katika Mungu, Liu Ming'en na mkewe wanalazimishwa kutoroka nyumbani kwao.
Mwenyezi Mungu alisema, Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kupotea kutoka kwa Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamwasi Mungu na kulaani Mbingu. Na hivyo, bila kujulikana kwa mwanadamu, majaliwa ya nchi yataletwa kwa uharibifu. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na anaweza hata kuzifuta kutoka uso wa dunia. Kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa kunategemea kama viongozi wao wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wao karibu na Mungu na kumwabudu. Lakini, kwa hii enzi ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli na kumwabudu wanazidi kuwa wachache, Mungu anaweka fadhili ya pekee juu ya nchi ambapo Ukristo ni dini ya serikali. Anazikusanya pamoja kuunda kambi ya haki kiasi ya dunia, wakati nchi zikanazo Mungu ama zile zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu mahali miongoni mwa wanadamu pa kufanyia kazi Yake, lakini pia Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, ili kulazimisha mipaka na vikwazo kwa nchi hizo zinazompinga Mungu. Lakini licha ya hayo, bado hakuna watu zaidi wanaokuja mbele kumwabudu Mungu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na Mungu hajakuwa kwa mawazo ya mwanadamu kwa muda mrefu. Kunabakia tu duniani nchi zinazotumia haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ni mbali na matakwa ya Mungu, kwani hakuna kiongozi wa nchi yoyote atamruhusu Mungu kuongoza watu wake, na hakuna chama cha kisiasa kitakachokusanya pamoja watu wake kumwabudu Mungu; Mungu amepoteza mahala Pake halali kwa mioyo ya nchi zote, taifa, chama tawala, na hata kwa moyo wa kila mtu. Ingawa nguvu za haki ziko kwa dunia hii, utawala ambapo Mungu hana mahali kwa moyo wa mwanadamu ni dhaifu. Bila baraka ya Mungu, uwanja wa kisiasa utaanguka katika vurugu na wenye kuweza kudhuriwa na mashambulizi. Kwa mwanadamu, kuwa bila baraka ya Mungu ni kama kukosa mwanga wa jua. Bila kujali jinsi viongozi wanafanya mchango kwa watu wao kwa uangalifu, bila kujali idadi ya mikutano ya haki wanadamu wanafanya pamoja, hakuna kati ya hii itakayorejesha mambo ama kubadilisha majaliwa ya mwanadamu. Mwanadamu anaamini kuwa nchi ambapo watu wanalishwa na kuvalishwa nguo, ambapo watu wanaishi kwa amani, ni nchi nzuri, na iliyo na uongozi mzuri. Lakini Mungu hafikirii hivyo. Anaamini kuwa nchi ambapo hakuna mtu anayemwabudu ndiyo Atakayoiangamiza. Njia ya mwanadamu ya kufikiria ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kwa hiyvo, kama mkuu wa nchi hamwabudu Mungu, basi majaliwa ya nchi hii itakuwa ya kutisha, na nchi haitakuwa na majaliwa.
Mungu hashiriki katika siasa za mwanadamu, lakini majaliwa ya nchi ama taifa inadhibitiwa na Mungu, Mungu anadhibiti dunia hii na ulimwengu mzima. Majaliwa ya mwanadamu na mpango wa Mungu yanashikamana kwa undani, na hakuna mwanadamu, nchi ama taifa limetolewa kwa mamlaka ya Mungu. Iwapo mwanadamu anatamani kujua majaliwa yake, basi lazima aje mbele ya Mungu. Mungu atawafanya wanaomfuata na kumwabudu kufanikiwa, na Atashusha na kuwaangamiza wale wanaompinga na kumkataa.
Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Loti alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma jinsi watu wa Ninawi walitubu dhambi zao kwa gunia na majivu, na kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.
Leo, Mungu amerudi duniani kufanya kazi Yake. Atasimama kwanza kwa mkutano mkubwa wa viongozi madikteta: Uchina, ngome kali ya ukanaji Mungu. Mungu amepata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Wakati huu, Anawindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso makubwa, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na kutoweza kupata makazi. Licha ya haya, Mungu bado anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Anatamka sauti Yake na kueneza injili. Hakuna anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu zaidi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu anafanya yote Awezayo kuokoa kila mshiriki wa ubinadamu. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo. Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama tu ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni.
Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.

Alhamisi, 31 Januari 2019

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Mchezo mfupi Mipaka ya Meya wa Kijiji inaeleza hadithi ya kweli ya mume na mke Wakristo ambao wanalazimishwa kutoroka kwa sababu ya mateso ya serilaki ya CCP. Mkristo Liu Ming'en anahukumiwa na CCP miaka saba gerezani kwa kuamini katika Mungu. Hata baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, anabakia kuwa wakulengwa na uchunguzi mkali wa CCP. Meya wa kijiji anatumia mfumo wa wajibu wa kaya-tano , kamera za usalama, ziara za nyumba, na njia nyingine kumzuia Liu Ming'en na mkewe kuamini katika Mungu, lakini hakuna inayoleta na matokeo yanayotakiwa. Wakati huu, meya anapokea taarifa za kipaumbele kutoka Kamati Kuu ya Chama, baada ya hapo anajaribu kutafuta njia za kumlazimisha Liu Ming'en na mkewe kuweka saini barua ya kuahidi kuacha kuamini katika Mungu. Baada ya hila yake kushindwa, polisi tena wanakuja kuwakamata waumini hawa wawili. Kuepuka kukamatwa na kuendelea kumfuata Mungu na kuamini katika Mungu, Liu Ming'en na mkewe wanalazimishwa kutoroka nyumbani kwao.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatatu, 19 Novemba 2018

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (4): Kuitii Serikali Inayotawala Sio Sawa na Kumtii Mungu

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (4): Kuitii Serikali Inayotawala Sio Sawa na Kumtii Mungu

Ili kumdanganya na kumjaribu Mkristo mmoja kumtelekeza Mungu, CCP kilimwita mchungaji mmoja wa Kanisa la Utatu kumtia kasumba, na Mkristo huyu na mchungaji wakazua mjadala mzuri juu ya maneno ya Paulo: "Acha kila nafsi itii mamlaka ya juu zaidi. Kwani hakuna mamlaka isipokuwa ya Mungu: mamlaka yaliyoko yameamriwa na Mungu" (Warumi 13:1). Fasiri zao tofauti ni zipi za maneno haya? Mchungaji wa Utatu yuko chini ya CCP na huchukua njia ya Kanisa la Utatu—kwa kweli ni kusudi gani la siri liko hapo? Mkristo atakanaje hoja hii ya mchungaji "kuwa chini ya mamlaka ya juu"?
Mwenyezi Mungu alisema, Kuanzia leo, Mungu ataweza kuwafanya watu wasiokuwa na fikira za kidini kuwa watimilifu kwa njia rasmi, ambao wako tayari kuweka pembeni nafsi zao za kale, na ambao wanamtii tu Mungu, pamoja na kuwafanya kuwa watimilifu wale wanaotamani neno la Mungu. Watu hawa wanafaa kusimama na kumhudumia Mungu. Kwake Mungu kunayo na hekima nyingi na isiyoisha. Kazi yake ya kustaajabisha na matamshi yake yenye thamani ni vitu ambavyo vipo ili watu wengi zaidi kuweza kufurahia. Kama ilivyo sasa, vitu hivi vipya haviwezi kukubaliwa na wale walio na fikira za kidini, wanaochukua hali ya ukubwa, na wale ambao hawaweki pembeni nafsi zao za kale. Roho Mtakatifu hana fursa ya kuwafanya watu kama hao kuwa watimilifu. Kama mtu hana hamu ya kutii, na hana kiu cha neno la Mungu, basi mtu huyo hataweza kupokea mambo mapya. Wataendelea tu kuasi zaidi na zaidi, kuwa wajanja zaidi na zaidi, na hatimaye kujipata kwenye njia mbaya. Katika kazi ya Mungu ya sasa, Atawainua watu zaidi wanaompenda Yeye kwa kweli na wanaoweza kukubali mwangaza mpya. Na Atakatiza kabisa maafisa wa kidini wanaoonyesha ukubwa wao. Hataki mtu hata mmoja anayekataa mabadiliko. Je, unataka kuwa mmoja wa watu hao? Je, unatekeleza huduma yako kulingana na mapendeleo yako, au unafanya kile Mungu anachotaka? Hili ni jambo ambalo lazima ujijulie mwenyewe. Je, wewe ni mmojawapo wa maafisa wa kidini, au wewe ni mtoto mchanga aliyezaliwa na anayefanywa kuwa mtimilifu na Mungu? Je, ni kiwango kipi cha huduma yako ambacho kinapongezwa na Roho Mtakatifu? Kati ya kiwango hiki ni kipi ambacho Mungu hatakumbuka? Baada ya miaka mingi ya huduma, umeleta mabadiliko kiasi kipi katika maisha yako? Je, uko wazi kuhusu mambo haya yote? Kama unayo imani ya kweli, basi utaweka pembeni fikira zako za kale za kidini na utahudumia Mungu kwa njia bora zaidi na kwa njia mpya. Kama utajitahidi zaidi sasa, hujachelewa sana. Fikira za kale za kidini zitamnyima mtu maisha mazuri. Uzoefu ambao anapata utamwongoza mbali na Mungu, kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe. Kama hutatupilia mbali vitu hivi, vitakuwa kikwazo katika kukua kwa maisha yako. Mungu siku zote amewafanya wote wanaomhudumia Yeye kuwa watimilifu. Hawatupilii mbali vivihivi tu. Kutakuwa na mustakabali kwako kama tu utakubali kwa kweli hukumu na vilevile kuadibiwa kwa neno la Mungu, kama unaweza kuweka pembeni matendo na mafundisho ya kidini yako ya kale ya kidini , na kuepuka kutumia fikira za kale za kidini kama kipimo cha neno la Mungu hii leo. Lakini kama utashikilia vitu vya kale, kama bado unavithamini, basi huwezi kupata wokovu. Mungu hatawatambua watu kama hao. Kama kweli unataka kufanywa kuwa mtimilifu, basi lazima uamue kutupilia mbali kabisa kila kitu cha kale. Hata kama kile kilichokuwa kimefanywa awali kilikuwa sahihi, hata kama ilikuwa ni kazi ya Mungu, utaiweka pembeni; hufai kuishikilia. Hata kama ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu iliyo wazi, iliyofanywa moja kwa moja na Roho Mtakatifu, leo lazima uiweke pembeni. Hufai kuishikilia. Hivi ndivyo Mungu anavyotuamuru. Kila kitu lazima kipate upya wake. Katika kazi ya Mungu na neno la Mungu, Mungu harejelei vitu vya kale ambavyo vilishapita, na vilevile hafukui historia ya kale. Mungu siku zote ni mpya na hajawahi kuwa mzee. Hashikilii hata maneno Yake mwenyewe aliyoyasema kale. Hii inaonyesha kwamba Mungu hafuati mafundisho ya dini yoyote. Katika hali hii, kama mwanadamu, kama siku zote unashikilia kabisa vitu vya kale na kuvitumia vivyohivyo fomula huku naye Mungu hafanyi kazi tena katika njia Alizokuwa akifanya awali, basi maneno yako na matendo yako hayakatizi? Je, hujawa adui wa Mungu? Je, uko radhi kuyaharibu maisha yako yote kwa sababu ya mambo haya ya kale? Mambo haya ya kale yanakufanya kuwa mtu anayezuia kazi ya Mungu. Je, mtu kama huyu ndiye wewe unataka kuwa? Kama kweli hutaki hivyo, basi acha mara moja kile unachofanya na ubadilike; anza tena upya. Mungu hakumbuki huduma yako ya kale.

Jumamosi, 17 Novemba 2018

Swahili Christian Video "Mazungumzo"(3): Upingaji wa Wakristo wa Kushangaza kwa Uvumi na Kashfa za CCP

Swahili Christian Video "Mazungumzo"(3): Upingaji wa Wakristo wa Kushangaza kwa Uvumi na Kashfa za CCP

Ili kuwadanganya Wakristo kumsaliti Mungu na kuiacha imani yao, CCP kimemsaliti Kristo wa siku za mwisho na Bwana Yesu hadharani, kikisema kuwa wote wawili ni watu wa kawaida na sio Mungu mwenye mwili. CCP kimewakashifu Wakristo kama wanaomwamini mtu tu na sio Mungu. Pia kimeeneza uvumi kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu liliundwa na mtu kwa kuwa tu mtu ambaye hutumiwa na Mungu ndiye anayeyaendesha mambo yote ya utawala ya kanisa. Kupata mwili kwa kweli ni nini? Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzwaje, na ni nani aliyelianzisha? Wakristo wanautumiaje ukweli na mambo ya hakika kukanusha uvumi na kashfa za umma ambazo CCP kinaeneza kuhusu Kristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Jumatano, 24 Oktoba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 2.Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe

Dong Mei, Mkoa wa Henan
Mimi ni mtu wa kawaida. Niliishi maisha ya kawaida. Kama wengi wanaotamani sana mwanga, nilijaribu njia nyingi kutafuta maana ya kweli ya uwepo wa wanadamu, nikijaribu kuyapa maisha yangu umuhimu zaidi. Mwishowe, juhudi zangu zote zilikuwa bure. Lakini baada ya kuwa na bahati ya kutosha kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, mabadiliko ya muujiza yalitokea katika maisha yangu. Yalileta rangi zaidi katika maisha yangu, na nilikuja kuelewa kwamba ni Mungu pekee ni Mtoa wa kweli wa roho na maisha ya wanadamu. Nilikuwa na furaha kwamba hatimaye nilikuwa nimepata njia sahihi ya maisha. Hata hivyo, huku nikitekeleza wajibu wangu wakati mmoja nilikamatwa kiharamu na kuteswa kikatili na serikali ya CCP. Kutoka kwa hili, safari ya maisha yangu ilipata uzoefu ambao kamwe sitasahau ...
Siku moja mnamo Desemba 2011 takribani saa moja asubuhi, mimi na kiongozi mwingine wa kanisa ulikuwa tukitekeleza hesabu ya mali ya kanisa wakati zaidi ya maafisa kumi wa polisi ghafla waliingia. Mmoja wa hawa polisi waovu alitukurupia na kusema kwa kelele: “Msisonge!” Baada ya kuona kilichokuwa kikitokea, kichwa changu kilishtuka. Kisha, polisi waovu walituchungquza kama magaidi waliokuwa wakitekeleza wizi. Pia walipekua kila chumba, walivigeuza shelabela kwa haraka sana. Mwishowe, walipata mali fulani ya kanisa, kadi tatu za benki, risiti za kuweka pesa, kompyuta, simu za rununu, na kadhalika. Waliyachukua yote ngawira, na kisha walituchukua sisi wanne kwa kituo cha polisi.
Alasiri, polisi waovu waliwaleta ndani dada wengine watatu ambao walikuwa wamewakamata. Walitufungia sisi saba katika chumba na hawakuacha tuzungumze, wala hawakuturuhusu tulale usiku ulipofika. Baada ya kuona dada wakifungiwa ndani na mimi, na kufikiri kuhusu ni kiasi gani cha pesa ambacho kanisa lilipoteza, nilikuwa nimezuzuliwa na wasiwasi. Yote ambayo ningefanya ni kuomba kwa dharura kwa Mungu: Ee Mungu! Huku nikikabiliwa na hali ya aina hii, sijui la kufanya. Tafadhali linda moyo wangu na kuufanya mtulivu. Baada ya kuomba, nilifikiri maneno ya Mungu: “Usiogope, mambo kama haya yanapofanyika katika kanisa, yote yanaruhusiwa na Mimi. Simama na kuwa sauti Yangu. Kuwa na imani kwamba mambo na vitu vyote vinaruhusiwa na kiti Changu cha enzi na vyote vina nia zangu ndani yavyo” (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). “Unapaswa kujua kwamba vitu vyote katika mazingira yaliyokuzunguka yako hapo kwa ruhusa Yangu, Napanga yote. Ona kwa dhahiri na kuridhisha moyo Wangu katika mazingira ambayo Nimekupa” (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). Maneno ya Mungu yalizima hofu kubwa moyoni mwangu. Nilitambua kwamba, leo, hii hali imenipata kwa ruhusa ya Mungu, na kwamba wakati ulikuwa umewadia ambapo Mungu alitaka nimshuhudie. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, nilimwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Nataka kutii utaratibu na mipango Yako na kusimama imara katika ushuhuda Kwako—lakini mimi ni wa kimo kidogo, na naomba kwamba Unipe imani na nguvu, na kunilinda katika kusimama imara.”
Asubuhi iliyofuata, walitutenga na kutuhoji. “Najua wewe ni kiongozi wa kanisa. Tumekuwa tukiwafuatia ninyi watu kwa miezi mitano,” alisema mmoja wa polisi waovu kwa maringo. Nilipomsikia akieleza kwa utondoti kila kitu ambacho walikuwa wamefanya kunifuatia, nilitetemeka kwaa woga. Katika akili yangu, nilifikiri, Polisi waovu kweli waliweka matayarisho mengi katika kutukamata. Kwa kuwa tayari wanajua mimi ni kiongozi wa kanisa, hakuna jinsi wataniacha niende. Mara moja niliweka azimio langu mbele ya Mungu: Afadhali nife badala ya kumsaliti Mungu na kuwa Yuda. Baada ya kuona kuwa kuhoji kwao hakukuwa kunazaa matunda yoyote, walimpa mtu kazi ya kunitazama na kutoniacha nilale.
Katika siku ya tatu ya mahojiano, mkuu wa polisi waovu aliwasha kompyuta na kunifanya nisome taarifa zilizomsingizia Mungu. Kwa kuona kwamba sikuguswa, baada ya hapo alinihoji kwa makini kuhusu fedha za kanisa. Niligeuza kichwa changu kwa upande mmoja na kumpuuza. Hili lilimfanya kukasirika sana na alianza kutukana. “Haijalishi usiposema lolote—tunaweza kukuzuia bila mwisho, na kukutesa wakati wowote ule tunaotaka,” alinitisha kwa ukali. Katikati ya usiku huo, polisi walianza mateso yao. Walivuta mkono wangu mmoja nyuma ya bega langu na mwingine juu kutoka kwa mgongo wangu. Walifinya mgongo wangu na miguu yao, kwa nguvu walitia pingu vifundo pamoja. Ilikuwa uchungu sana kiasi kwamba nilipiga yowe kwa maumivu—mifupa na nyama katika mabega yangu zilihizi kana kwamba zingepasuka. Ningeweza tu kupiga magoti bila kusonga na kichwa changu kikiwa sakafuni. Nilifikiri mayowe yangu yangewafanya watulize makali kwangu, lakini badala yake waliweka kikombe cha chai kati ya pingu na mgongo wangu, jambo ambalo lilizidisha tena maumivu. Mifupa katika mwili wangu wa juu ilihisi kana kwamba ilikuwa imevunjwa nusu. Nilihisi uchungu sana hivi kwamba sikuthubutu kupumua nje na jasho baridi ilitiririka usoni pangu. Punde tu nilipohisi kwamba singevumilia uchungu tena, mmoja wa polisi waovu alichukua fursa hii kuniambia: “Tupe tu jina na tutakuachilia uende mara moja.” Wakati huo, nilimwita Mungu aulinde moyo wangu. Mara moja nilifikiri maneno ya wimbo wa uzoefu wa maisha: “Mungu mwenye mwili hupitia maumivu. Je, mimi, mtu huyu mpotovu, napaswa kuteseka kiasi gani zaidi? Nikikubali ushawishi wa giza, nawezaje kukutana na Mungu? ...Afadhali nivumilie taabu zote, na kufidia huzuni kubwa ya Mungu” (“Kusubiri Habari Njema Kutoka kwa Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wimbo ulinipa nguvu. Ndiyo—Mungu mwenye mwili amepitia uchungu huo wote kwa ajili ya wokovu wetu, nami, mtu huyu aliyepotoshwa kwa kina na Shetani, lazima niteseke hata zaidi. Iwapo ningekubali kushindwa na Shetani kwa sababu singeweza kuvumilia uchungu, ningewezaje kukabiliana na Mungu wakati wowote tena? Kufikiri hili kulinipa nguvu, na nikakua mgumu mara nyingine tena. Polisi waovu walinitesa kwa takriban saa moja. Walipoondoa pingu, mwili wangu mzima ulianguka bila nguvu sakafuni. “Usipoongea tutafanya hilo tena!” walinipigia kelele. Niliwatazama na kutosema chochote. Moyo wangu ulijawa na chuki kwa polisi hawa waovu. Mmoja wa polisi waovu alisonga mbele kutia pingu tena. Huku nikifikiri uchungu mkali sana ambao nilikuwa nimeupita karibuni, niliendelea kumwomba Mungu moyoni mwangu. Kwa mshangao wangu, alipojaribu kuvuta mikono yangu nyuma ya mgongo wangu hangeweza kuisogeza. Haikuwa uchungu sana, pia. Alikuwa akijaribu kwa nguvu sana hivi kwamba kichwa chake chote kilikuwa kimejaa jasho—lakini bado hangeweza kutia pingu. “Una nguvu mwingi!” alitweta kwa hasira. Nilijua kwamba huyu alikuwa Mungu akinijali, kwamba Mungu alikuwa akinipa nguvu. Shukrani iwe kwa Mungu!
Kufika alfajiri kulikuwa vigumu. Bado nilikuwa na kiwewe nilipofikiri nyuma jinsi polisi waovu walikuwa wamenitesa. Pia walinitisha, wakiniambia kwamba iwapo singesema chochote, wangelazimika kunipeleka ndani sana ya milimani na kuniua. Baadaye, walipokamata waumini wengine, wangesema nililisaliti kanisa—wangechafua jina langu, na kuwafanya ndugu wengine wa kanisa wanichukie na kunikana. Kufikiri hilo, moyo wangu ulizidiwa na mawimbi ya majonzi na kutojiweza. Nilijipata nikihisi mwoga na mnyonge. Akilini mwangu nilifikiri: Afadhali nife. Kwa njia hiyo sitakuwa Yuda na kumsaliti Mungu, wala sitakanwa na ndugu zangu. Pia nitaepuka uchungu wa mateso ya mwili. Kwa hivyo nilingoja hadi wakati ambapo polisi waovu waliokuwa wakinilinda hawakuwa wakitia makini na kuupiga kichwa changu kwa nguvu sana dhidi ya ukuta—lakini yote yaliyotokea ilikuwa kwamba kichwa changu kiliona kizunguzungu, sikufa. Wakati huo, maneno ya Mungu yalinipa nuru kutoka ndani: “katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kwa rehema ya Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana” (Kutoka kwa “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Wengine wanapokuelewa vibaya, unaweza kumwomba Mungu na kusema: ‘Ee Mungu! Siombi kwamba wengine wanivumilie, wala kwamba wanisamehe. Naomba tu kwamba niweze kukupenda moyoni mwangu, kwamba niwe na uhakika moyoni mwangu, na kwamba dhamiri yangu ni safi. Siombi kwamba wengine wanisifu, au kuniheshimu, ninatafuta tu kukuridhisha kutoka moyoni mwangu’” (Kutoka kwa “Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kumpenda Mungu kwa Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yaliondoa huzuni kutoka kwa moyo wangu. Ndiyo—Mungu huwataka watu wenye azimio, watu ambao wanaweza kumshuhudia Mungu mbele ya Shetani, watu ambao wanaweza kustahimili hadi mwisho kabisa na kufuata mipango yote ya Mungu bila kujali jinsi taabu wanayopitia ilivyo kubwa. Hata zaidi, Mungu huona mioyo ya ndani kabisa ya watu. Iwapo polisi wakinisingizia, hata kama ndugu wengine kwa kweli wanielewe visivyo na kunikataa kwa sababu hawajui kile kilichotendeka kwa kweli, naamini kwamba nia za Mungu ni nzuri; Mungu anajaribu imani na upendo wangu Kwake, na napaswa kufuatilia kumfanya Mungu kuridhika. Baada ya kubaini njama janja za Shetani, ghafla nilihisi mwenye fedheha na aibu. Niliona kwamba imani yangu kwa Mungu ilikuwa ndogo sana. Sikuwa nimeweza kusimama imara baada ya kupitia uchungu kidogo, na nilikuwa nimefikiri kutoroka na kuepuke mipango ya Mungu kupitia kifo. Watu wanapomwacha Mungu, wanaishi katika giza. Lengo la polisi waovu katika kuzungumza maneno haya ya tishio lilikuwa kunifanya nimkane Mungu. Na isingekuwa ulinzi wa Mungu, ningedanganywa na njama zao janja. Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, moyo wangu ulijawa na mwanga. Sikutaka tena kufa, ila kuishi maisha mazuri, na kutumia kile ambacho kweli niliishi kwa kudhihirisha kumshuhudia Mungu na kumletea Shetani aibu.
Polisi hao wawili waovu waliopewa kazi ya kunilinda waliuliza mbona nilikuwa nimegongesha kichwa changu dhidi ya ukuta. Nilisema kwa sababu polisi hao wengine walikuwa wamenipiga. “Kimsingi tunafanya kazi kupitia elimu. Usijali—sitawaacha wakupige tena,” mmoja wao alisema kwa tabasamu. Baada ya kusikia maneno yake ya faraja, nilifikiri: Hawa watu wawili si wabaya; tangu nikamatwe wamekuwa wazuri kabisa kwangu. Kwa hilo, nililegeza tahadhari yangu. Lakini wakati huo, maneno ya Mungu yalikuja ghafla moyoni mwangu: “Nyakati zote, watu Wangu wanapaswa kujihadhari dhidi ya hila danganyifu za Shetani, walinde lango la nyumba Yangu kwa ajili Yangu, … kitu ambacho kitawazuia kuingia katika mtego wa Shetani, wakati mtakapokuwa na majuto ya kuchelewa sana” (“Tamko la Tatu” la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa kumbusho la wakati wa kufaa, yakinionyesha kwamba njama janja za ibilisi ni nyingi, na napaswa kuwa hadhari dhidi ya ibilisi hawa wakati wote. Sikutarajia hata kidogo kwamba punde wangefichua tabia zao halisi. Mmoja wa polisi waovu alianza kumkashifu Mungu, huku mwingine aliketi chini kando yangu alinipapasa mguu wangu, akinitazama kwa jicho la husuda na kuuliza kuhusu fedha za kanisa. Jioni, alipoona kwamba nilikuwa nikisinzia, alianza kupapasa kifua changu. Baada ya kuona kwamba walikuwa wamefichua tabia yao halisi, nilijawa na hasira. Ni sasa tu nilipoona waliodhaniwa polisi wa watu walikuwa tu wahuni na wadhalimu. Haya yalikuwa mambo mabaya yenye kustahili dharau, ambayo wangeweza kufanya. Kama matokeo, niliweza tu kumwomba Mungu kwa dharura ili anilinde kutokana na madhara yao.
Katika siku kadhaa zilizofuata, polisi waovu hawakunihoji tu kwa makini kuhusu kanisa, lakini pia walichukua zamu kunitazama ili kwamba nisilale. Baadaye, walipoona jinsi sikuwa nimewapa chochote, polisi hao wawili waovu waliokuwa wakinihoji walizidi kwa ghadhabu. Mmoja wao alinishambulia vikali, akinizaba kofi usoni, akinipiga kwa vishindo mara kadhaa. Uso wangu uliwasha, ulianza kuvimba, na mwishowe ukawa wenye ganzi sana kiasi kwamba singehisi chochote. Kwa sababu maswali yao hayakuwa yamezaa matunda yoyote kutoka kwangu, jioni moja mkuu wa polisi waovu alinipigia unyende na kusema, “Unahitaji kuanza kufungua mdomo wako. Unajaribu subira yangu—siamini kwamba hakuna chochote tunaweza kufanya na wewe. Nimekutana na watu wengi wagumu zaidi kukuliko. Tusipokuwa wakali kwako, hutatii katu!!” Alitoa amri na polisi waovu kadhaa walianza kunitesa. Jioni, chumba cha mahojiano kilikuwa cha huzuni na cha kuogofya—nilihisi kana kwamba nilikuwa jahanamu. Walinifanya nichutame sakafuni na kufunga mikono yangu katikati ya magoti na miguu yangu. Kisha, waliingiza kifimbo cha mbao katikati ya mapindi ya mikono yangu na nyuma ya magoti yangu, wakilazimisha mwili wangu wote kupinda juu. Kisha walikiinua kifimbo na kukiweka katikati ya meza mbili, wakiuacha mwili wangu wote ukining’inia hewani na kichwa changu kikiwa juu chini. Punde waliponiinua juu, kichwa changu kilipata kizunguzungu na niliona vigumu kupumua. Ilihisi kana kwamba nilikuwa nikisongwa. Kwa sababu nilikuwa nilining’inishwa hewani juu chini uzito wangu wote ulikuwa ukiangukia vifundo vyangu. Mwanzoni, ili kukomesha pingu kuukata mwili wangu, nilifumbata mikono yangu pamoja kwa kukaza, nikaupinda mwili wangu, na kujaribu kwa nguvu kadiri nilivyoweza kubaki katika hali hiyo. Lakini nguvu yangu ilipungua polepole. Mikono yangu iliteleza kutoka kwa vifundo vya miguu hadi kwa magoti yangu, na pingu ilikata kwa kina katika mwili wangu, ikiniacha na uchungu mkubwa sana. Baada ya kuning’inia hivi kwa takribani nusu saa, ilihisi kana kwamba damu yote katika mwili wangu ilikuwa imejikusanya kichwani mwangu. Uvimbe mchungu katika kichwa changu na macho ulifanya yahisi kana kwamba yalikuwa karibu kulipuka. Makato ya kina yalikuwa yamechimbwa katika vifundo vyangu, na mikono yangu ilikuwa imevimba sana kiasi kwamba ilionekana kama mikate miwili. Nilihisi nilikuwa ukingoni mwa kifo. “Siwezi kuvumilia tena, niweke chini!” nilipaza sauti kwa kukata tamaa. “Hakuna anayeweza kukuokoa ila wewe mwenyewe. Tuambie tu jina na tutakuacha uteremke chini,” alisema mmoja wa polisi waovu kwa ukali. Mwishowe, waliona kwa kweli nilikuwa katika taabu na waliniweka chini. Walinilisha glukosi kiasi na kuanza kunihoji tena. Nililala bila nguvu kama matope ardhini, macho yangu yakifumbwa kwa kukaza, nikiwa siwatilii makini. Bila kutarajia, polisi waovu waliniinua hewani tena. Bila nguvu ya kushikilia kwa mikono yangu, sikuwa na lingine ila kuacha pingu ijitie ndani katika vifundo vyangu, makali yaliyochongoka yakikata mwili wangu. Wakati huo, ilikuwa uchungu sana nilitoa yowe la kuhuzunisha sana. Sikuwa na nguvu ya kuendelea kupigana na kupumua kwangu kulikuwa kumekua kwa kina kifupi sana. Ilionekana kana kwamba wakati ulikuwa umesimama. Nilihisi kwamba nilikuwa nikiyumbayumba ukingoni mwa kifo. Nilipofikiri kwamba wakati huu kweli ningekufa, nilitaka kumwambia Mungu maneno yaliyokuwa moyoni mwangu kabla ya maisha yangu kuisha: “Ee Mungu! Wakati huu, ambapo kweli niko ukingoni mwa kifo, nahisi woga— lakini hata kama kweli nikifa leo, bado nitasifu haki Yako. Ee Mungu! Katika safari yangu fupi ya maisha, nakushukuru kwa kunichagua nirudi nyumbani kutoka kwa dunia hii ya dhambi, kunizuia kuzurura, nikiwa nimepotea, na kuniruhusu kuishi milele katika kumbatio Lako kunjufu. Ee Mungu, nimefurahia upendo Wako sana—na ilhali sasa tu, wakati maisha yangu yako karibu kuisha, ndipo nagundua kwamba sijatunza upendo Wako. Nyakati nyingi nimekufanya kuwa na huzuni na masikitiko; mimi ni kama mtoto mjinga anayejua tu kufurahia upendo wa mama yake, ilhali hajawahi kufikiria kuulipiza. Sasa tu ambapo niko karibu kupoteza maisha yangu ndipo naelewa kwamba ni lazima nitunze upendo Wako, na ni sasa tu ndipo najuta kukosa nyakati nyingi nzuri. Sasa, ninachojuta zaidi ni kwamba sijaweza kukufanyia lolote na unanidai mengi sana, na kama bado naweza kuishi, kwa hakika nitafanya kila niwezalo kutekeleza wajibu wangu, kufidia kile Unachonidai. Wakati huu, naomba tu kwamba Unipe nguvu, kuniruhusu kutowahi tena kuogopa kifo, na kuwa mwenye nguvu katika kile ninachokabili....” Tone baada ya tone la machozi lilianguka kutoka kwa paji la uso wangu. Usiku ulikuwa kimya kiasi cha kuogofya. Sauti ya pekee ilikuwa saa kubwa ikipiga ta-ta, kana kwamba kuhesabu sekunde ambazo zilisalia za maisha yangu. Hapo ndipo kitu cha muujiza kilifanyika: Nilihisi kana kwamba mwanga wa jua wa vuguvugu ulikuwa ukiniangazia, na polepole niliacha kuhisi uchungu mwilini mwangu. Maneno ya Mungu nguruma akilini mwangu: “Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo” (Kutoka kwa “Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ndiyo—Mungu ndiye chanzo cha maisha yangu, Mungu hutawala kudura yangu, na lazima nijiachilie mikononi mwa Mungu na kujiweka katika matumizi Yake. Kutafakari maneno ya Mungu kulinipa hisia ya kufurahisha, tulivu moyoni mwangu, kana kwamba nilikuwa nikijinyoosha katika kumbatio kunjufu la Mungu. Nilijipata nikilala. Wakiwa na woga kwamba ningekufa, polisi waovu waliniweka chini na kwa haraka walinipa glukosi kiasi na maji. Katika kukaribia kwangu kifo, nilikuwa nimetazama matendo ya muujiza ya Mungu.
Siku iliyofuata, polisi waovu walishinda jioni nzima wakiniinua juu tena na tena. Walinihoji kuhusu mahali ambapo pesa za risiti ambazo walikuwa wamechukua ngariwa zilikuwa. Wakati huo wote, sikusema chochote—ilhali bado hawakukata tamaa. Ili kupata pesa za kanisa, walitumia kila njia yenye kustahili dharau kunitesa. Wakati huo, maneno ya Mungu yalirudia rudia moyoni mwangu: “Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo–inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake, usimwache kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa Shetani huyu wa zamani” (Kutoka kwa “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa nguvu na imani kubwa. Ningepigana hadi kufa na Shetani, na hata kama ningekufa, ningesimama imara katika ushuhuda wangu kwa Mungu. Nikitiwa msukumo na maneno ya Mungu, bila kujua nilisahau uchungu. Kwa njia hii, kila wakati waliniinua juu, maneno ya Mungu yalinitia msukumo na kunipa motisha, na hivyo kadiri walivyonibeba juu mara nyingi, ndivyo nilivyoweza kubaini asili yao zaidi—ambayo ilikuwa ya ibilisi waovu—na ndivyo azimio langu kusimama imara katika ushuhuda wangu na kumridhisha Mungu lilivyokuwa kubwa zaidi. Mwishowe, wote walichoshwa na mimi. “Watu wengi sana hawawezi kuvumilia kutundikwa hivi kwa nusu saa, lakini amevumilia wakati huu wote—kwa kweli yeye ni sugu!” Niliwasikia wakitoa mawazo. Kwa kusikia maneno haya, nilijawa na msisimko. Akilini mwangu, nilifikiri: Mungu msaada wangu, huwezi kunivunja moyo. Mbali na mateso ya mwili, wakati wa siku na usiku zangu tisa katika kituo cha polisi polisi waovu pia walininyima usingizi. Kila wakati nilipofunga macho yangu na kuanza kusinzia, wangepiga vifimbo vyao dhidi ya meza, au sivyo wangenifanya nisimame na kukimbia huku na kule, au sivyo kunipigia kelele tu, wakijaribu kunihuzunisha na kuvunja akili yangu. Baada ya siku tisa, wakiona kwamba hawakuwa wamefikia lengo lao, polisi bado hawakukata tamaa. Walinipeleka katika hoteli, ambapo walitia pingu mikono yangu mbele ya miguu yangu, kisha wakaingiza kifimbo cha mbao katikati ya mapindi ya mikono na miguu yangu, nikilazimika kuketi mwili wangu ukiwa umepinda juu sakafuni. Walinifanya nibaki katika hali hii nikiketi sakafuni kwa siku kadhaa zilizofuata, ambayo ilisababisha pingu kuukata mwili wangu. Mikono na vifundo vyangu vilivimba na kubadilika rangi kuwa zambarau, na kikalio changu kilihisi uchungu sana sikuthubutu kukisugua ama kukishika; ilihisi kama nilikuwa nikikalia sindano. Siku moja, mmoja wa viongozi wa polisi waovu, akiona kwamba mahojiano yangu hayakuwa yamezaa matunda, alitembea kunifikia akiwa amekasirika sana na kunizaba kofi kwa nguvu usoni—kwa nguvu kiasi cha kutosha kulegeza meno yangu mbili.
Mwishowe, wakuu wawili kutoka kwa Idara ya Usalama wa Umma ya Mkoa walikuja. Punde walipowasili, waliondoa pingu, wakanisaidia kwenda kwa kochi, na kunipa kikombe cha maji. “Umekuwa na wakati mgumu kwa siku chache zilizopita—lakini usilitilie moyoni, walikuwa wakifuata tu amri,” walisema kwa unafiki. Unafiki wao ulinifanya niwachukie sana kiasi kwamba nilisaga meno yangu. Pia walijaribu kutumia Biblia kunileta upande wao, na kuwasha kompyuta na kunionyesha ushahidi usio kweli. Walisema maneno mengi ambayo yalishutumu na kufukuru dhidi ya Mungu. Moyoni mwangu, nilihisi kukasirishwa. Nilitaka kubishana nao, lakini nilijua kwamba kufanya hivyo kungewafanya tu kukufuru dhidi ya Mungu kwa wayowayo hata zaidi. Wakati huu, nilihisi kweli jinsi taabu aliyopitia Mungu mwenye mwili ilivyokuwa kubwa, na jinsi Mungu alivyovumilia fedheha nyingi kwa ajili ya kumwokoa mwanadamu. Kilicho zaidi, niliona uhafifu na kustahili dharau kwa ibilisi hawa waovu. Moyoni mwangu, kwa siri niliapa kwamba ningejiondoa kabisa kwa Shetani na milele kuwa mwaminifu kwa Mungu. Baadaye, bila kujali jinsi walivyojaribu kunidanganya, niliendelea kufunga mdomo wangu na sikusema chochote. Baada ya kuona kuwa maneno yao hayakuwa na athari yoyote, wakuu hao wawili waliondoka tu kwa hasira.
Katika kipindi cha siku na usiku kumi katika hoteli, waliendelea kunitia pingu, wakinifanya kuchuchumaa sakafuni nikishika miguu yangu. Nikikumbuka tangu nilipokamatwa, nilikuwa nimeishi siku na usiku kumi na tisa katika kituo cha polisi na hoteli. Ulinzi wa upendo wa Mungu ulikuwa umeniruhusu nilale kidogo, lakini polisi waovu hawakuwa wameniruhusu kulala wakati huo wote; ningefunga macho tu kwa muda na wangefanya chochote kilichohitajika kuniweka macho—kupiga meza, kunipiga teke kwa nguvu, kunipigia kelele, kuniamuru nikimbie huku na kule, na kadhalika. Kila wakati ningeshtuliwa, moyo wangu ungetwanga kifuani mwangu, na ningehisi woga sana. Hilo, likiongezwa kwa mateso ya mara kwa mara ya polisi waovu, na nguvu yangu iliishia kupunguka kabisa, mwili wangu wote ulikuwa umevimba na usiotulia, na niliona kila kitu vikiwa mbili mbili. Ningejua kulikuwa na watu mbele yangu wakiongea, lakini sauti ya milio yao ingeonekana kana kwamba ilikuwa ikitoka mbali sana. Zaidi ya hayo, mijibizo yangu ilianza kuwa ya polepole sana. Kwa mimi kustahimili hili kwa kiasi fulani kulikuwa yote kwa sababu ya nguvu kuu ya Mungu! Kama alivyosema Mungu: “Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu…. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha si rahisi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui” (Kutoka kwa “Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili). Moyoni mwangu, nilitoa shukrani na sifa ya uaminifu kwa Mungu: Ee Mungu! Unatawala vitu vyote, matendo Yako ni yasiyokadirika, Wewe pekee ni mwenyezi, Wewe ni nguvu ya maisha isiyozimika, Wewe ni chemichemi ya maji hai kwa maisha yangu. Katika hali hii maalum, nimetazama nguvu Yako maalum na mamlaka. Mwishowe, polisi waovu hawakupata majibu kwa maswali yao kutoka kwangu, na walinituma hadi katika kituo cha kuzuia.
Njiani kuelekea katika kituo cha kuzuia, polisi wawili waliniambia: “Umefanya vizuri sana. Ninyi watu huenda mkawa katika kituo cha kuzuia, lakini ninyi ni watu wazuri. Kuna aina nyingi hapo: wauza madawa, wauaji, malaya—utaona utakapowasili.” “Kwa kuwa unajua sisi ni watu wazuri, mbona mnatukamata? Je, serikali haiongei kuhusu uhuru wa dini?” niliuliza. “Hiyo ni Chama cha Kikomunisti inawadanganya. Chama hicho hutupa riziki yetu, kwa hivyo lazima tufanye kinachosema. Hatuna chuki kwako ama kuwa na kitu chochote dhidi yako. Tulikukamata tu kwa sababu unamwamini Mungu,” mmoja wa polisi alisema. Baada ya kusikia hili, nilikumbuka kila kitu nilichokuwa nimepitia. Singeweza kuzuia kukumbuka maneno ya Mungu: “Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi!” (Kutoka kwa “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yaliulenga kiini cha suala, yakiniruhusu kuona kwa kweli sura ya kweli ya serikali ya CCP na jinsi inavyojaribu kupata heshima ambayo haistahili; kwa juu juu, inapeperusha bendera ya uhuru wa dini, lakini kwa siri inakamata, kukandamiza, na kushambulia wale wanaomwamini Mungu pande zote za nchi na kupora pesa za kanisa—yote ambayo huweka wazi asili yake ya yenye dhambi ya kuchukiza, ya shetani.
Nikiwa katika kituo cha kuzuia, kulikuwa na nyakati ambapo nilikuwa dhaifu na katika maumivu. Lakini maneno ya Mungu yaliendelea kunipa moyo, kunipa nguvu na imani, kuniruhusu kuelewa kwamba ingawa Shetani alikuwa ameniondolea uhuru wa mwili, mateso yalikuwa yameniongeza, yakinifundisha kumtegemea Mungu wakati wa mateso ya hao ibilisi waovu, kuniruhusu kuelewa maana ya kweli ya ukweli mwingi, kuona thamani ya ukweli, na kuongeza azimio langu na motisha ya kufuatilia ukweli. Nilikuwa tayari kuendelea kumtii Mungu, na kupitia yote ambayo Mungu alikuwa amenipangia. Kama matokeo, nilipokuwa nikifanya kazi katika kituo cha kuzuia, niliimba nyimbo na kwa kimya nilifikiri kuhusu upendo wa Mungu. Nilihisi kwamba moyo wangu ulikuwa umekuja karibu na Mungu, na sikuona tena siku zikiwa chungu ama za kudhikisha sana.
Wakati wa kipindi hiki, polisi waovu walinihoji mara mingi zaidi. Nilimshukuru Mungu kwa kuniongoza katika kushinda mateso yao mara kwa mara tena. Baadaye polisi waovu waliondoa pesa zote kutoka kwa kadi zangu tatu za benki. Kutazama bila kujiweza peza za kanisa zikichukuliwa na polisi waovu kuliuvunja moyo wangu. Moyo wangu ulijawa na chuki kwa hili kundi lafi, ovu la ibilisi, na nilitamani sana ufalme wa Kristo kuwasili punde. Mwishowe, licha ya kutokuwa na ushahidi wowote, walinihukumu mwaka mmoja na miezi mitatu ya kuelimishwa tena kupitia kazi kwa ajili ya “kuvuruga utulivu wa umma.”
Baada ya kuteswa kikatili na serikali ya CCP, kwa kweli nilikuwa nimeonja upendo na wokovu wa Mungu kwangu, na nilikuja kufahamu ukuu na uweza wa Mungu na matendo Yake ya muujiza, nilikuwa nimeona mamlaka na nguvu ya maneno ya Mungu. Aidha kwa kweli nilikuwa nimemdharau Shetani. Katika kipindi hicho cha mateso, maneno ya Mungu yalikuwa yameandamana na mimi kupitia mchana na usiku za kudhikisha, maneno ya Mungu yalikuwa yameniruhusu kubaini njama janja za Shetani na kutoa ulinzi wa wakati wa kufaa. Maneno ya Mungu yalikuwa yamenifanya kuwa mwenye nguvu na ujasiri, yakiniruhusu kushinda mateso yao katili mara kwa mara tena. Maneno ya Mungu yalikuwa yamenipa nguvu na imani, yalikuwa yamenipa ujasiri wa kupigana na Shetani hadi mwisho kabisa.... Shukrani ziwe kwa Mungu! Mwenyezi Mungu ndiye ukweli, njia na uzima! Daima nitamfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho kabisa!
kutoka kwa Ushuhuda wa Washindi

Jumanne, 7 Agosti 2018

Swahili Christian Video | Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China | "Ni Nani Aliyemlazimisha Kuyatamatisha Maisha Yake"


Swahili Christian Video | Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China | "Ni Nani Aliyemlazimisha Kuyatamatisha Maisha Yake"

Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii inasimulia hadithi ya Gao Yufeng, Mkristo katika China Bara, ambaye alikamatwa na polisi wa CCP na kupewa mateso ya kikatili ya aina zote ambayo hatimaye yalimfanya kujiua katika kambi ya kazi kwa kumwamini Mungu na kutimiza wajibu wake. Filamu hii inaonyesha udhalimu mbaya sana na mateso ya kikatili yaliyowafika Wakristo waliozuiliwa baada ya kukamatwa chini ya utawala muovu wa CCP, ikionyesha asili ya pepo ya chuki ya CCP kwa Mungu na kuuawa kwa Wakristo.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kufichua Ukweli

Ijumaa, 16 Februari 2018

Swahili Christian Testimony Video "Utamu katika Shida" | Mungu Ndiye Nguvu Wangu

Swahili Christian Testimony Video "Utamu katika Shida" | Mungu Ndiye Nguvu Wangu

Han Lu ni kiongozi wa Kanisa la Mwenyezi Mungu katika China bara. Ameamini katika Mungu kwa zaidi ya muongo mmoja na amepitia kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Anaelewa baadhi ya ukweli na anajua kwamba ni kupitia tu Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ndiyo mwanadamu ataweza kuwekwa huru kutoka dhambini na kuishi maisha yenye maana. Ametupa mbali kila kitu kumfuata Mwenyezi Mungu, na ametembea huku na huku na kushuhudia kuonekana kwa Mungu na kazi katika siku za mwisho. Hata hivyo, nchini China ambako chama cha kisiasa kikanamungu cha CCP kiko mamlakani, hakuna uhuru wa imani ya dini kwa vyovyote. Serikali ya CCP imetoa hati za siri ikipiga marufuku kabisa makanisa yote ya nyumbani, na wamewakamata kwa hasira na kuwatesa Wakristo. Han Lu na wengine walichunguzwa na kufuatwa na maafisa wa polisi wa CCP, ambayo ilisababisha kukamatwa kwao. Maafisa hao wa polisi wa CCP wamemtesa kikatili Han Lu kujaribu kuliibia kanisa mali lake na kuwashika wakuu zaidi wa kanisa, na pia wametumia uvumi na uongo kumtia kasumba, wakatumia familia yake kujaribu kumshurutisha, na njia zingine za kudharauliwa kujaribu kumtishia katika jaribio la kumshurutisha amkane Mungu na kumsaliti Mungu. … Katika uchungu na udhaifu wake, Han Lu amemtegemea Mungu na kumwomba Mungu, na chini ya uongozi wa neno la Mungu, ameweza kubaini ujanja wote wa Shetani. Ameweza kustahimili mahojiano mengi chini ya mateso na ameweza kwa nguvu kukana uvumi na uongo kadhaa wa CCP. Ndani ya mazingira machungu ya utesaji wa CCP, ushuhuda wa kupendeza na wa nguvu umefanywa …
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mateso ya Kidini
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.