Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 15 Julai 2019

Sura ya 13. Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao

Sura ya 13. Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao

1. Hakuna Ambaye Angeokolewa iwapo Mungu Angeangalia Tu Maonyesho ya Asili ya Watu
Kwa sasa, utendaji wa watu unaamua matokeo yao, lakini huu utendaji ni upi? Je, unaujua? Nyinyi mnaweza kufikiri kwamba hili linarejelea tabia ya watu iliyopotoka ikijionyesha kazini mwao, lakini halimaanishi lile. Utendaji huu unanena kuhusu ikiwa unaweza kuweka ukweli kwenye vitendo au la na ikiwa unaweza kusalia mwaminifu na kujizatiti unapotenda wajibu wako au la, na vilevile mtazamo wako wa kumwamini Mungu, msimamo wako kwa Mungu, uamuzi wako wa kuteseka kwa ajili ya ugumu, mtazamo wako kwa kukubali hukumu na kupogolewa, kiwango chako cha mabadiliko na idadi ya dhambi kubwa. Haya yote yanachangia katika utendaji wako. Utendaji huu haumaanishi kiwango cha mwisho cha kufichua tabia yako iliyopotoshwa, lakini badala yake umefanikiwa kwa kiasi gani katika imani yako kwa Mungu. Iwapo matokeo ya watu yangeamuliwa kulingana na maonyesho ya asili yao, basi hakuna mtu ambaye angeokolewa. Je, hii ingekuwaje haki ya Mungu? Ikiwa wewe ni kiongozi, asili yako itajionyesha zaidi, na yeyote ambaye atajionyesha zaidi hatakuwa na uhakika sana wa kusalia. Kama hii ingeamua matokeo ya watu, basi kadiri watu wangezidi kutenda kazi katika kiwango cha juu, ndivyo wangezidi kumalizika haraka; kadiri wangezidi kuwa katika kiwango cha juu, ndivyo wangezidi kuonyesha asili yao katika kiasi kikubwa. Kama hali ingekuwa hivi, basi ni nani ambaye angethubutu kutekeleza wajibu wake? Kwa njia hii, je, haingekuwa kwamba wale ambao hawatekelezi wajibu wao wangeokolewa wote?
Utendaji huu unahusiana na ikiwa wewe ni mwaminifu na umejitoa kwa Mungu au la, ikiwa una upendo kwake au la, ikiwa unaweka ukweli kwenye matendo au la na vilevile ni katika kiwango gani ambacho umebadilika. Ni kulingana na utendaji huu kwamba hukumu yako inaamuliwa; si kulingana na kiwango cha upotovu wa tabia yako kinachojionyesha. Ukifikiria jinsi hii, umetafsiri vibaya mapenzi ya Mungu. Asili yote ya wanadamu ni sawa, ni vile tu kuna ubaya na uzuri wa ubinadamu. Hata usipoonyesha, asili yako bado ni sawa na yule anayeonyesha. Mungu Anajua vyema kilicho katika undani wa mwanadamu. Huhitaji kuficha chochote — Mungu huchunguza mioyo ya watu na mawazo. Ikiwa upotovu wako mwingi unafichuliwa wakati unapofanya kazi katika kiwango cha juu, Mungu atauona; ikiwa hutafanya kazi na usifichuliwe, je, Mungu hajui kuuhusu? Je, huku si kuamini uongo wako? Ukweli ni kwamba Mungu Anajua asili yako nje na ndani, bila kujali ulipo. Mungu Anajua vyema wale wote wanaofanya kazi yao, lakini je, si pia Ajua wale wasiofanya? Watu wengine hudhani kuwa hao viongozi walio kwenye hadhi ya juu wanachimba makaburi yao tu, kwa sababu upotovu wao mwingi utajifichua na kuonekana na Mungu pasi na kuepuka. Je, ungefichuliwa sana vile iwapo hawangeifanya kazi? Kufikiria kwa jinsi hii ni kwa upuzi! Ikiwa Mungu hauoni, basi si Hataweza kuuhukumu? Kama hali ingekuwa ile, je, haingekuwa kwamba wale ambao hawafanyi kazi wangesalia wote? Kulingana na kuelewa kwa mwanadamu, Mungu hangeona mabadiliko ya wale ambao hufanya kazi, bila kujali mabadiliko hayo ni makuu kiasi gani; Mungu Angewahukumu tu kulingana na maonyesho yao ya upotovu. Kinyume na hayo, Mungu hangewahukumu wale ambao wanaonyesha machache, licha ya kubadilika kwa kiasi kidogo. Je, unaamini kuwa hii ni haki ya Mungu? Je, mtu yeyote anaweza kusema kuwa Mungu ni mwenye haki iwapo Angefanya hili? Je, huku sio kutafasiri kubaya kwako ambako kunapelekea kuelewa kwa Mungu kubaya? Basi, je, imani yako kwa Mungu si ni ya uongo? Je, huku si kuamini kuwa Mungu sio mwenye haki daima? Je, si imani kama ile ni kufuru kwa Mungu? Ikiwa huna kitu chochote kilicho hasi na lolote jema halifichuliwi pia, bado huwezi kuokolewa. Jambo kuu ambalo huamua matokeo ya watu ni utendaji wao mwema. Lakini, hakuwezi kuwa na kitu hasi sana vilevile—kama ni kikuu kiasi cha kuleta maafa au adhabu, basi wote wataangamizwa. Kama kungekuwa jinsi mnavyofikiria, wale walio wafuasi wa kiwango cha chini wangepata wokovu mwishowe, na wale ambao ni viongozi wangekwisha. Una wajibu ambao lazima uutekeleze; lakini unapoutekeleza wajibu huo, utafichua upotovu wako licha yako mwenyewe, ni kama unakwenda kwa gilotini. Kama matokeo ya watu yangeamuliwa na asili yao, hakuna yeyote ambaye angeokolewa—kama hali kweli ingekuwa hii, basi, je, haki ya Mungu ingekuwa wapi? Haingeonekana kabisa. Nyinyi nyote mmeelewa mapenzi ya Mungu visivyo.
2. Utendaji Huu ni Kwa Ajili ya Kazi ya Mungu kwa Watu
Acheni niwape mfano: Katika shamba la miti ya matunda, mwenyewe hunyunyuzia maji na kutia mbolea, kisha husubiri matunda. Miti ambayo inazaa matunda ni mizuri na inahifahdiwa; ile ambayo haizai matunda bila shaka ni mibaya na haitahifadhiwa. Fikiria hali hii: Mti unazaa matunda, lakini una ugonjwa, na baadhi ya matawi mabaya yanahitaji kupogolewa. Je, mtu huu unapaswa kuhifadhiwa? Unapaswa kuhifadhiwa, na utakuwa mzuri baada ya kupogolewa na kutibiwa. Fikiria hali nyingine: Mti hauna maradhi, lakini hauna matunda—mti kama huu haufai kuhifadhiwa. Je, huku “kuzaa matunda” kunamaanisha nini? Kuna maana ya kazi ya Mungu kuwa na athari. Mungu anapofanya kazi kwa watu, asili yao haina vingine ila kujionyesha, na kwa ajili ya upotovu wa Shetani hawataepuka kuwa na dhambi, lakini katikati ya haya kazi ya Mungu ndani yao itazaa matunda. Ikiwa Mungu haoni hivyo, lakini Anaona tu asili ya mwanadamu ikionyeshwa, basi ule hautaitwa wokovu wa mwanadamu. Tunda la watu kuokolewa linadhihirishwa hasa katika kutekeleza wajibu kwao na kuweka ukweli kwenye matendo. Mungu huangalia kiwango cha watu cha mafanikio katika sehemu hizo na pia ukubwa wa dhambi zao. Hali hizi mbili zinachangia katika kuamua matokeo yao na ikiwa watasalia au la. Mathalani, watu wengine walikuwa wapotovu sana, wakijitolea kabisa kwa miili yao, na wala sio kwa familia ya Mungu. Hawakutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu hata kidogo, lakini sasa wanatekeleza wajibu wao kwa shauku na wako na moyo mmoja na Mungu—kwa huu matazamo, je, kumekuwa na mabadiliko? Haya ni mabadiliko. Ni mabadiliko haya ambayo Mungu Anataka. Pia, watu wengine walipenda kusambaza mawazo walipokuwa nayo, lakini sasa wanapokuwa na mawazo mengine, wanaweza kuwa watiifu na kufuatilia ukweli, bila kuyasambaza au kufanya kinyume na Mungu. je, kumekuwa na mabadiliko? Naam! Watu wengine wanaweza kuwa wamepinga wakati mmoja waliposhughulikiwa na kupogolewa tena, lakini sasa wanapopogolewa na kushughulikiwa, wanaweza kujifahamu. Baada ya kuyakubali, wanapitia mabadiliko ya kweli—je, hii si athari? Naam! Hata hivyo, bila kujali mabadiliko yako ni makuu kiasi gani, asili yako haiwezi kubadilishwa kwa mara moja. Haiwezekani kutofichua dhambi zozote, lakini ikiwa kuingia kwako kutafanywa kwa kawaida, hata kwa uasi mwingine, utakuwa na ufahamu wake wakati huo. Ufahamu huu unaweza kukuletea mabadiliko ya mara moja na hali yako itaimarika na kuwa nzuri zaidi na zaidi. Unaweza kuwa na dhambi mara moja au mbili, lakini sio kila mara. Haya ni mabadiliko. Haimaanishi kwamba mtu aliyebadilika kwa kitengo fulani hana dhambi zozote tena; huo sio ukweli. Aina hii ya mabadiliko ina maana kuwa mtu aliyepitia kazi ya Mungu anaweza kuweka ukweli mwingi kweye vitendo na anaweza kutenda baadhi ya yale ambayo Mungu anahitaji. Dhambi zao zitapungua na kuwa chache zaidi na zaidi na matukio ya kuasi yatakuwa machache na madogo. Unaweza kuona kutokana na haya kuwa kazi ya Mungu imekuwa na athari; kile ambacho Mungu anataka ni kujionyesha kama huku ambako matokeo haya yamefanikishwa kwa watu. Hivyo, jinsi ambavyo Mungu Anashughulikia matokeo ya watu na Anavyomtendea mtu ni yenye haki kabisa, mwafaka na isiyo na mapendeleo. Unahitaji tu kutia bidii katika kutumia rasilmali yako kwa ajili ya Mungu, kuweka moyo wako wote katika kutenda ukweli ambayo unapaswa bila kusita, na Mungu hawezi kukutendea isiyo haki. Ebu fikiria: je, wale wanaoweka ukweli kwenye vitendo wanaweza kuadhibiwa na Mungu? Watu wengi wanashuku tabia ya Mungu yenye haki na wanachelea kuwa bado wataadhibiwa ikiwa wataweka ukweli kwenye vitendo; wanaogopa kuwa Mungu hataona uaminifu wao na kujitolea kwao. Watu wengine wanakuwa wa kutoonyesha hisia baada ya kupogolewa na kushughulikiwa; wanahisi wanyonge kiasi cha kutotekeleza wajibu wao na wanapoteza uaminifu wao na kujitolea kwao. Kwanini hivi? Hili kwa kiasi ni kwa ajili ya watu kukosa ufahamu kuhusu kiini cha matendo yao ambayo hupelekea kutokubali kupogolewa na kushughulikiwa. Pia kwa kiasi ni kwa ajili ya watu kutoelewa umuhimu wa kushughulikiwa na kupogolewa, wakiamini hilo kuwa ishara ya kuamuliwa kwa matokeo yao. Kwa sababu hiyo, kimakosa watu huamini kuwa wakiwa na uaminifu fulani na kujitolea kwa Mungu, basi hawawezi kushughulikiwa na kupogolewa; wakishughulikiwa, haiwezi kuwa haki ya Mungu. Kutoelewa kama huku kunawafanya wengi kutoaminika na kutojitolea kwa Mungu. Hakika, yote ni kwa sababu watu ni waongo sana; hawataki kupitia ugumu—wanataka kupata baraka kwa njia rahisi. Hawana ufahamu wa haki ya Mungu. Si kwamba Mungu hajafanya lolote la haki ama kwamba hatafanya lolote la haki, ni tu kwamba watu daima hawafikiri kwamba Anayofanya Mungu ni haki. Machoni pa wanadamu, kama kazi ya Mungu haipatani na mapenzi ya mwanadamu ama kama si matarajio yao, ina maana kuwa Yeye si mwenye haki. Watu kamwe hawatambui wakati kile wanachofanya si sahihi ama haiambatani na ukweli; katu hawatambui kwamba wanampinga Mungu. Kama Mungu hangewashughulikia ama kuwapogoa watu kwa ajili ya dhambi zao na wala kuwakaripia kwa sababu ya makosa yao, lakini daima angekuwa mtulivu, kamwe bila kuwakasirisha, daima bila kuwakosea, na daima bila kufunua makovu yao, lakini angewakubalia kula na kuwa na wakati mzuri na Yeye, basi watu hawangelalamika kuwa Mungu sio mwenye haki. Wangesema kuwa Mungu ni mwenye haki kwa unafiki. Kwa hivyo, watu bado hawaamini kuwa kile ambacho Mungu Anahitaji ni utendaji wao baada ya kubadilishwa kwao. Je, Mungu angekuwa vipi na uhakika kama wangeendelea na hayo? Kama Mungu angewasuta watu kidogo, hawangeamini tena kuwa Yeye huona utendaji wao baada ya mabadiliko. Wangeacha kuamini kuwa Yeye ni mwenye haki, na hawangekuwa na radhi kubadilishwa. Kama watu wangeendelea na hali hii, wangehadaiwa na mawazo yao wenyewe.
Soma Zaidi: Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ijumaa, 12 Julai 2019

Sura ya 35. Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro

Sura ya 35. Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro

Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi zaidi na muhimu zaidi ya utendaji. Hili ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu hupata matokeo bora zaidi. Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu hasa kunamaanisha kutafuta ukweli, kutafuta nia ya Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka kwa maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini na hata alikuwa anazingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alikuwa anazingatia kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na kuelewa asili potovu ya mwanadamu na dosari halisi za mwanadamu, akitimiza kila hali yote ya madai anayotaka Mungu kutoka kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. Alikuwa na utendaji mwingi sahihi ndani ya maneno ya Mungu; hili linalingana sana na mapenzi ya Mungu, na ni ushirikiano bora zaidi wa mwanadamu katika uzoefu wake wa kazi ya Mungu. Wakati ambapo alipitia mamia ya majaribio kutoka kwa Mungu, alijichunguza kabisa dhidi ya kila neno la hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kila neno la ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, na kila neno la madai Yake kwa mwanadamu, na akajaribu kufikia maana ya maneno ya Mungu. Alijaribu kwa bidii kutafakari na kukariri kila neno ambalo Yesu alimwambia, na alitimiza matokeo mazuri sana. Kupitia njia hii ya utendaji aliweza kutimiza kujifahamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na hakuja tu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu, lakini pia alikuja kuelewa kiini cha mwanadamu, asili ya mwanadamu, na aina mbalimbali za dosari ambazo mwanadamu anazo—huku ni kujifahamu kwa kweli. Kutoka kwa maneno ya Mungu, hakutimiza tu kujifahamu kwa kweli, lakini kutokana na mambo yaliyoonyeshwa katika neno la Mungu—tabia ya Mungu yenye haki, kile Anacho na alicho, mapenzi ya Mungu kwa kazi Yake, mahitaji Yake kwa wanadamu—kutoka kwa maneno haya alikuja kumjua Mungu kabisa. Alikuja kujua tabia ya Mungu, na asili yake; alikuja kujua na kuelewa kile Mungu anacho na Alicho, uzuri wa Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu. Hata ingawa wakati huo Mungu hakuzungumza sana kama Anavyofanya leo, matunda yalipatikana ndani ya Petro katika hali hizi. Hili lilikuwa jambo adimu na la thamani. Petro alipitia mamia ya majaribio lakini hakuteseka bure. Hakuja kujielewa tu kutokana na maneno na kazi ya Mungu, lakini pia alikuja kumjua Mungu. Pia alizingatia hasa matakwa ya Mungu kwa wanadamu ndani ya maneno Yake, na ni katika hali gani mwanadamu anapaswa kumridhisha Mungu ili kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Alifanya juhudi kubwa katika hali hii na akatimiza uwazi kamili; hili lilikuwa la manufaa sana kwa kuingia kwake mwenyewe. Haijalishi kile ambacho Mungu alizungumzia, maadamu maneno hayo yangeweza kuwa maisha yake na yalikuwa ya ukweli, aliweza kufanikiwa kuyaweka ndani ya moyo wake kuyatafakari mara nyingi na kuyaelewa. Baada ya kuyasikia maneno ya Yesu aliweza kuathiriwa nayo, ambalo linaonyesha kuwa alikuwa akizingatia hasa maneno ya Mungu, na alitimiza matokeo mwishowe kwa kweli. Yaani, aliweza kuyatia maneno ya Mungu katika vitendo kwa uhuru, kutenda kwa usahihi ukweli na kukubaliana na mapenzi ya Mungu, kutenda kikamilifu kwa mujibu wa nia ya Mungu, na kuacha maoni na mawazo yake mwenyewe. Kwa njia hii aliingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Huduma ya Petro ilikubaliana na mapenzi ya Mungu hasa kwa sababu alifanya hili.
Ikiwa mtu anaweza kweli kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu kutokana na mambo na maneno yanayohitajika na Yeye, basi atakuwa mtu aliyekamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yanafaa kabisa kwa mtu huyu, kwamba maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake, anapata ukweli, na anaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili asili ya mwili wake, yaani, msingi wa kuwepo kwake kwa asili, utatikisika na kuanguka. Baada ya mtu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yake anakuwa mtu mpya. Maneno ya Mungu yanakuwa maisha yake; maono ya kazi ya Mungu, matakwa yake kwa mwanadamu, ufunuo wake kwa mwanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anahitaji mwanadamu kutimiza vinakuwa maisha yake—anaishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, na mtu huyu anageuka kukamilishwa na maneno ya Mungu. Anapitia kuzaliwa upya na anakuwa mtu mpya kupitia maneno Yake. Hii ni njia ambayo Petro aliitumia kuufuatilia ukweli; Ilikuwa njia ya kukamilishwa, kukamilishwa na maneno ya Mungu, na kupata uzima kutoka kwa maneno ya Mungu. Ukweli ulioonyeshwa na maneno ya Mungu ulikuwa maisha yake, na wakati huo tu ndipo alikuwa mtu aliyepata ukweli. Sote tunajua kwamba karibu wakati wa kupaa kwa Yesu, Petro alikuwa na fikira nyingi, kutotii, na udhaifu. Kwa nini yalibadilika kabisa baada ya hilo? Hili lina uhusiano wa moja kwa moja na ufuatiliaji wake wa ukweli. Kuelewa tu mafundisho ya dini hakuna maana; hakuwezi kuleta mabadiliko katika maisha. Kuelewa tu maana halisi ya neno la Mungu si sawa na kuelewa ukweli; yale mambo muhimu ambayo yanaelezwa kwa mifano katika maneno ya Mungu ndiyo ukweli. Kila sentensi ya maneno ya Mungu ina ukweli, lakini watu huenda wasiuelewe. Kwa mfano, neno la Mungu linasema, "Lazima muwe watu waaminifu": Kuna ukweli katika kauli hii. "Lazima muwe watu wanaomtii Mungu, wanaompenda Mungu, na wanaomwabudu Mungu." "Lazima mfanye wajibu wenu vizuri kama wanadamu." Kauli hizi zina ukweli hata zaidi. Kila sentensi ya maneno ya Mungu ina ukweli mwingi, na maneno mengi yanahitajika ili kufafanua kiini cha kila kauli ya ukweli; wakati kiwango hiki kinafikiwa tu ndipo kitafikiriwa kuwa ufahamu wa ukweli. Ikiwa unaelewa tu maana halisi na kuelezea maneno ya Mungu kulingana na maana halisi ya maneno hayo, huu sio ufahamu wa ukweli—huku ni kucheza tu na mafundisho ya dini.
Zamani, wakati maneno ya Mungu hayakuwa maisha ya watu, ilikuwa ni asili ya Shetani iliyotwaa madaraka na kutawala ndani yao. Ni mambo gani maalum yalikuwa ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini lazima ulinde nafasi yako mwenyewe? Kwa nini hisia zako ni kali sana? Kwa nini unapenda mambo hayo dhalimu, na kwa nini unapenda maovu hayo? Asili ya mambo haya ni nini? Yanatoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali mambo haya? Hivi sasa nyote mmeelewa kuwa hili hasa ni kwa sababu ya sumu ya Shetani iliyo ndani ya mambo haya. Kile sumu ya Shetani kilicho kinaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini wanafanya kitu. Watasema: “Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine.” Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida: Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu, na haijalishi wanachofanya, kama ni kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, wanajifanyia tu. Watu wote hudhani kwamba "Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine," Haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya mwanadamu. "Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine," kauli hii ya Shetani ni sumu yake hasa, na inapowekwa moyoni na mwanadamu inakua asili ya mwanadamu. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia kwa kauli hii; inamwakilisha kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya mwanadamu na inakuwa msingi wa kuwepo kwake; wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na hii kwa maelfu ya miaka. Kila kitu ambacho Shetani hufanya ni kwa ajili yake. Anataka kumpita Mungu, kujiondoa kwa Mungu na kushika mamlaka mwenyewe, na kumiliki vitu vyote ambavyo Mungu ameumba; Kwa hivyo, asili ya mwanadamu ni asili ya Shetani. Kwa kweli, wito wa watu wengi unaweza kuwakilisha na kuakisi asili yao. Haijalishi jinsi mwanadamu anavyoificha, katika kila kitu afanyacho na kila kitu asemacho, hawezi kuificha asili yake. Kuna baadhi ya watu ambao huwa hawasemi ukweli kamwe na wanajua sana kujifanya, lakini baada ya wengine kuingiliana nao kwa muda, asili yao ya udanganyifu na wao kutokuwa waaminifu kabisa kutagunduliwa. Muda utafichua yote. Baada ya kuwajua kwa muda, asili yao itagunduliwa. Mwishowe hitimisho litafanywa: Yeye kamwe huwa hasemi neno lolote la ukweli, na yeye ni mdanganyifu. Kauli hii ni ukweli wa asili yake; ni ushahidi na kielezo chake. Kwa hivyo, falsafa yake ya maisha ni kutomwambia yeyote ukweli, na pia kutomwamini mtu yeyote. Je, hili haliwakilishi asili yake? Asili ya mwanadamu ya kishetani ina kiwango kikubwa cha falsafa ndani yake. Wakati mwingine wewe mwenyewe huelewi vizuri, lakini unaishi kwa kutegemea hilo kila wakati. Unafikiri kuwa ni sahihi sana, yenye mantiki sana, na isiyo kosea. Falsafa ya Shetani inageuka kuwa ukweli wa mwanadamu, na watu wanaishi kwa mujibu wa falsafa yake kabisa bila ukinzani hata kidogo. Kwa hivyo, mwanadamu daima na kila mahali hufichua asili ya Shetani katika maisha, na daima huishi kwa falsafa ya shetani. Asili ya Shetani ni maisha ya mwanadamu. Kuhusu asili ni nini, hili linaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa kuifupisha kwa maneno. Katika asili ya mwanadamu kuna kiburi na ufuatiliaji wa kuwa bora zaidi na wa kipekee; kuna pia tamaa ya kutaka faida tu bila kuyajali maisha; kuna hila, uhalifu, na kuwadanganya watu kila upande; na kuna uovu na uchafu visivyovumilika. Huu ni muhtasari wa asili ya mwanadamu. Kwa hivyo, ikiwa unaweza kuja kujua mambo mengi katika asili ya mwanadamu, basi una ufahamu wa asili yako mwenyewe. Ikiwa hujagundua kitu chochote katika asili yako mwenyewe, basi huna ufahamu wowote wa hilo. Petro alitafuta ndani ya usafishaji wa maneno ya Mungu na ndani ya majaribio mbalimbali ambayo Mungu alimtolea ili aje kujijua, kuona kile alichofichua. Mwishowe alipokuja kujifahamu kweli, aligundua mwanadamu ni mpotovu sana, na hana thamani na hastahili kumtumikia Mungu, na kwamba mwanadamu hastahili kuishi mbele za Mungu. Alianguka chini mbele za Mungu. Mwishowe alihisi: "Kumjua Mungu ni jambo la thamani zaidi! Kama singeweza kumjua Mungu, kifo changu kingekuwa cha aibu mno. Nahisi kwamba kumjua Mungu ndilo jambo muhimu sana, la maana sana. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu basi hastahili kuishi—basi hakuna uzima." Wakati uzoefu wa Petro ulikuwa umefikia kiwango hiki, alikuwa na ufahamu kiasi wa asili yake mwenyewe. Aliielewa vizuri kiasi, na ingawa hangeweza kutumia lugha kuielezea vizuri kabisa kulingana na fikira za wanadamu za sasa, alifikia eneo hili. Kwa hivyo, ufuatiliaji wa njia ya uzima ili kukamilishwa na Mungu ni kuelewa zaidi asili ya mtu mwenyewe ndani ya maneno ya Mungu na kuelewa mambo yaliyo ndani ya asili ya mtu. Kuufupisha kwa maneno, kuelewa kabisa maisha ya mtu ya kale—maisha ya asili ya kale ya shetani—huku ni kuweza kutimiza matokeo yaliyohitajika na Mungu. Ikiwa ufahamu wako haujafikia kiwango hiki lakini unasema unajielewa na kwamba umepata uzima, je, huku sio kujisifu tu? Hujijui, na hujui ulicho mbele za Mungu, kama umepata kiwango cha mwanadamu kweli, au ni vitu vingapi vya Shetani ambavyo bado unavyo. Huelewi vizuri wewe ni wa nani na hata hujifahamu—basi unawezaje kuwa na sababu mbele za Mungu? Wakati Petro alikuwa akiufuatilia uzima, katikati ya majaribio yake alizingatia kujielewa na kubadilisha tabia yake. Alijitahidi kumwelewa Mungu, na mwishowe akahisi: "Mwanadamu lazima afuatilie kumfahamu Mungu maishani; kumfahamu Mungu ndilo jambo muhimu sana; ikiwa simjui Mungu basi siwezi kupumzika kwa amani nitakapokufa. Mungu anaponifanya nife baada ya kumjua, nitahisi kwamba ni jambo la kupendeza zaidi, sitalalamika hata kidogo, na maisha yangu yote yatatimizwa."Petro hakuweza kupata ufahamu huu na kufikia kiwango hiki punde baada ya kuanza kumwamini Mungu—alipaswa kupitia majaribio mengi kwanza. Uzoefu wake ulipaswa kufikia kiwango fulani na alipaswa kujifahamu kabisa kabla ya kuweza kuhisi thamani ya kumjua Mungu. Kwa hivyo, njia aliyoishika ilikuwa njia ya uzima na ya kukamilishwa; utendaji wake maalum ulizingatia hali hii hasa.
Je, nyote mnaishika njia gani sasa? Ikiwa hamjafikia ufuatiliaji wa maisha, wa kujifahamu, au kumfahamu Mungu kama Petro, basi hiyo bado si njia ya Petro. Hivi sasa watu wengi wako katika aina hii ya hali: "Ili kupata baraka ni lazima nijitumie kwa ajili ya Mungu na kulipa gharama kwa ajili Yake. Ili kupata baraka ni lazima niache kila kitu kwa ajili ya Mungu; lazima nikamilishe kile ambacho ameniaminia na kutekeleza wajibu wangu vizuri." Hili linatawaliwa na nia ya kubarikiwa; ni kutumika kwa kusudi la kupata thawabu za Mungu, kwa ajili ya kupata taji. mtu wa aina hii hana ukweli ndani ya moyo wake, na hakika anaelewa tu maneno fulani ya mafundisho ya dini ambayo anaringia kila mahali. Njia yake ni njia ya Paulo. Kumwamini Mungu kwa mtu wa aina hii ni kitendo cha kazi ya siku zote, na katika akili yake anahisi kuwa kadri anavyofanya, ndivyo itakavyothibitisha zaidi kuwa ni mwaminifu kwa Mungu, kwamba kadri anavyofanya ndivyo Mungu ataridhika zaidi, na kwamba kadri anavyofanya ndivyo anavyopaswa zaidi kupata taji mbele za Mungu, na hakika atapata baraka kubwa zaidi katika nyumba ya Mungu. Anahisi kwamba kama anaweza kuvumilia mateso, kuhubiri, na kufa kwa ajili ya Kristo, kama anaweza kuyadharau maisha yake mwenyewe, na kama anaweza kukamilisha wajibu wote ambao Mungu alimwaminia nao, basi atakuwa mtu mwenye kubarikiwa zaidi na Mungu, yule anayepata baraka nyingi zaidi, na hakika atapokea taji. Hili ndilo hasa alilowaza Paulo alilofikiri na kile alichofuatilia; hii ndiyo hasa njia ambayo Paulo alitembea, na ilikuwa chini ya uongozi wa mawazo haya ndio Paulo alifanya kazi kumhudumia Mungu. Je, mawazo na madhumuni kama hayo hayatoki kwa asili ya Shetani? Kama tu watu wa dunia, hapa duniani lazima nifuatilie maarifa, na baada ya kupata maarifa tu ndio ninaweza kufanikiwa, kuwa afisa, na kuwa na cheo. Mara baada ya kupata cheo ninaweza kufikia lengo langu na kuifikisha nyumba yangu na biashara kwa viwango fulani. Je, wasioamini wote huwa hawaifuati njia hii? Wale ambao wanatawaliwa na asili hii ya shetani wanaweza tu kuwa kama Paulo baada ya kumwamini Mungu: "Ni lazima niache kila kitu ili nijitumie kwa ajili ya Mungu, lazima niwe mwaminifu mbele za Mungu, na mwishowe nitapokea taji kubwa zaidi na baraka kubwa zaidi." Hii ni sawa na watu wa dunia wanaofuatilia vitu vya dunia, hakuna tofauti kabisa, na wanapaswa kutii asili hiyo. Watu wana asili ya shetani, kwa hiyo ulimwenguni watafuatilia maarifa, hadhi, kujifunza, na mafanikio ya dunia; nyumbani mwa Mungu, watatafuta kujitumia kwa ajili ya Mungu, kuwa waaminifu, na hatimaye watapokea taji na baraka nyingi. Kama watu hawana ukweli baada ya kumwamini Mungu na hawajakuwa na mabadiliko katika tabia yao, basi bila shaka watakuwa kwenye njia hii—huu ni ukweli ambao hakuna mtu anayeweza kuupinga, na ni wenye kupinga kabisa njia ya Petro. Nyote mnaishika njia gani sasa? Ingawa huwezi kupanga kuishika njia ya Paulo, asili yako inakutawala kwa njia hii, na unaelekea upande huo bila kupenda. Ingawa unataka kuishika njia ya Petro, ikiwa hufahamu vizuri jinsi ya kulifanya hilo, basi bado utaishika njia ya Paulo bila kupenda—huu ni ukweli wa hali hiyo.
Kwa hiyo mnawezaje hasa kuishika njia ya Petro? Kama huwezi kubainisha kati ya njia ya Petro na njia ya Paulo, au huzijui kabisa, basi hata ukisema unapaswa kuishika njia ya Petro hayo yatakuwa maneno matupu. Unahitaji kwanza kufahamu katika mawazo yako njia ya Petro ni gani na njia ya Paulo ni gani. Kama kweli unaelewa kwamba njia ya Petro ni njia ya uzima na njia pekee ya kukamilishwa, wakati huo tu ndipo utaweza kujua na kufahamu ukweli na njia maalum za kuishika njia yake. Ikiwa huifahamu njia ya Petro, basi njia unayoishika bila shaka itakuwa ya Paulo kwa sababu hakutakuwa na njia nyingine—hutakuwa na budi. Kama huna ukweli na huna hamu za kupata kitu basi ni vigumu kuishika njia ya Petro. Inaweza kusemekana kwamba Mungu amewafichulia sasa njia ya kuokolewa naye na ya kukamilishwa. Hii ni neema ya Mungu na kutia moyo na ni Yeye anayewaongoza kwenye njia ya Petro. Bila uongozi na kupata nuru kutoka kwa Mungu hakuna ambaye angeweza kuishika njia ya Petro; chaguo la pekee lingekuwa kuelekea kwa njia ya Paulo, kuzifuata nyayo za Paulo kuelekea kwa uharibifu. Wakati huo, Paulo hakuhisi kwamba haikuwa sahihi kutembea kwenye njia hiyo. Aliamini kwa ukamilifu kwamba ilikuwa sahihi, lakini hakuwa na ukweli na hasa hakuwa na mabadiliko katika tabia. Alijiamini kupita kiasi na akahisi kwamba hakukuwa na ubaya wowote kuishika njia hiyo. Aliendelea akiwa amejaa imani na kwa kujihakikishia kabisa. Kufikia mwisho, hakupata fahamu, bado alifikiria kwamba kwake kuishi ilikuwa ni Kristo. Aliendelea kuishika njia hiyo hadi mwisho, na alipoadhibiwa mwishowe, yote ilikuwa imekwisha. Njia ya Paulo haikuhusisha kujijua au ufuatiliaji wa mabadiliko katika tabia. Hakuchangua kamwe asili yake mwenyewe na hakuwa na ufahamu wa kile alichokuwa; alijua tu kwamba alikuwa mkosaji mkuu katika kumtesa Yesu. Hakuwa amepata ufahamu hata kidogo wa asili yake mwenyewe, na baada ya kumaliza kazi yake alihisi kwamba alikuwa Kristo na anapaswa kupewa thawabu. Kazi ambayo Paulo alifanya ilikuwa tu kutoa huduma kwa Mungu. Kwake mwenyewe, ingawa alipokea ufunuo kiasi kutoka kwa Roho Mtakatifu, hakuwa na ukweli au uzima hata hivyo. Hakuokolewa na Mungu—aliadhibiwa. Kwa nini inasemekana kwamba njia ya Petro ni njia ya kukamilishwa? Kwa sababu katika utendaji wake alizingatia hasa uzima, alifuatilia ufahamu wa Mungu, na akazingatia kujifahamu. Kupitia uzoefu wake wa kazi ya Mungu alikuja kujijua, alipata ufahamu wa hali potovu za mwanadamu, alijua kasoro zake, na ni jambo gani lilikuwa muhimu sana kwa mwanadamu kulifuatilia. Aliweza kumpenda Mungu kwa dhati, alijua jinsi ya kumlipa Mungu, alipata ukweli kiasi, na alikuwa na ukweli ambao Mungu huhitaji. Kutoka kwa vitu vyote alivyosema wakati wa majaribio yake, inaweza kuonekana kwamba Petro alikuwa kweli mwenye ufahamu zaidi wa Mungu. Kwa sababu alielewa ukweli mwingi sana kutoka kwa maneno ya Mungu, njia yake ikawa yenye kung'aa zaidi na zaidi na kuzidi kufungamana na mapenzi ya Mungu. Kama hangekuwa amepata ukweli huu, basi hangeweza kuendelea kuishika njia sahihi kama hiyo.
Hivi sasa bado kuna swali hili: Kama unajua njia ya Petro ilikuwa gani, je, unaweza kuishika? Hili ni swali halisi. Lazima uweze kubainisha wazi ni mtu wa aina gani anaweza kuishika njia ya Petro na mtu wa aina gani hawezi. Wakati watu ni wakosefu hawawezi kukamilishwa na Mungu. Wale ambao wanashika njia ya Petro lazima wawe bila kosa; kama wewe ni mtu asiye na kosa tu ndipo unaweza kukamilishwa. Wale walio kama Paulo hawawezi kuishika njia ya Petro. Aina fulani ya mtu ataishika aina fulani ya njia; hii linaamuliwa kabisa na asili yake. Haijalishi jinsi unavyomwelezea Shetani kwa dhahiri njia ya Petro, hawezi kuitembea. Hata kama angetaka, hangeweza kuishika. Asili yake imeamua kwamba hawezi kuishika njia hiyo. Ni wale tu wanaopenda ukweli ndio wanaweza kuishika njia ya Petro. Mito na milima inaweza kubadilishwa lakini ni vigumu kubadilisha asili ya mwanadamu; kama hakuna dalili za kuupenda ukweli ndani ya asili yako, basi hustahili kwenda kwenye njia ya Petro. Kama wewe ni mtu anayependa ukweli, kama unaweza kukubali ukweli licha ya tabia yako potovu, unaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu na unaweza kuelewa mapenzi ya Mungu, kwa njia hii utaweza kuunyima mwili na kutii mpango wa Mungu. Wakati una mabadiliko katika tabia yako baada ya kupitia majaribio kiasi, hili linamaanisha kuwa polepole unakanyaga kwenye njia ya Petro ya kukamilishwa.
Baadhi ya Makala: Ni Tofauti Gani Iliyopo Kati Ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Jumanne, 9 Julai 2019

Sura ya 12. Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana

Sura ya 12. Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana

1. Usijishughulishe na Ikiwa Umejaaliwa na Mungu, bali Ujishughulishe na Ufuatiliaji Wako
Watu wengi hawaelewi mapenzi ya Mungu; wanafikiri kuwa kila mtu ambaye ameamuliwa na Mungu ataokolewa bila kuepuka na wanafikiri kuwa kila mtu asiyeamuliwa na Mungu hataokolewa hata wakiyafanya mambo vyema zaidi. Wanafikiri kwamba Mungu hataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji na tabia yao. Iwapo unafikiri hivi, basi unamwelewa Mungu visivyo kabisa. Iwapo Mungu angefanya hili kweli, basi Mungu angekuwa mwenye haki? Mungu huamua matokeo ya watu kulingana na kanuni: Mwishowe matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na utendaji wao wa kibinafsi na tabia. Huoni tabia ya Mungu yenye haki, na daima unamwelewa Mungu visivyo na kugeuza nia Zake, ambayo hukufanya daima uwe bila rajua na kupoteza matumaini. Je, hili si la kujiadhibu? Kwa kweli, unaelewa kweli, na una uhakika wa nia za Mungu? Daima umetumia “Majaaliwa ya Mungu” kusawiri na kukana maneno ya Mungu. Huku ni kumuelewa Mungu visivyo kukuu! Huelewi kazi ya Mungu na huyaelewi mapenzi ya Mungu katu; hata zaidi, huelewi nia nzuri ambazo Mungu ameweka katika miaka Yake 6,000 za kazi ya usimamizi! Unakuwa na moyo wa kukata tamaa, kubahatisha na kuwa na shaka na Mungu; unaogopa kwa kina kuwa mtendaji-huduma, ukifikiri, “Hakuna jambo kuu kunihusu; mbona nimepandishwa daraja ili kuifanya kazi hii? Je, Mungu ananitumia? Je, ni kwamba Ananifanya nitoe huduma na kisha kunifukuza wakati ambapo sina faida tena?” Je, si maoni haya yanambainisha Yeye na wale walio mamlakani? Daima umemwelewa Mungu visivyo; umewaza maovu kumhusu Mungu na kumchukia. Hujawahi kuyaamini maneno ya Mungu na kusema Kwake ukweli, umeanza mwenyewe kutafuta kuwa mtendaji-huduma, umeanza mwenyewe kutembea katika njia ya watendaji-huduma, lakini hujatafuta kubadili tabia yako wala hujapitia dhiki ili kuuweka ukweli kwenye vitendo. Mwishowe, umeyasukuma majukumu yako kwa Mungu, ukisema kuwa hukuwa umejaaliwa na Mungu, na kwamba Mungu hajakuwa wazi nawe. Je, tatizo ni lipi? Unayaelewa visivyo madhumuni ya Mungu, huyaamini maneno ya Mungu, huuweki ukweli kwenye vitendo wala kujitolea unapotimiza wajibu wako. Je, unawezaje kuyaridhisha mapenzi ya Mungu? Kwa huu mwelekeo wa matendo, hujahitimu hata kidogo kuwa mtendaji-huduma, hivyo unawezaje kuhitimu kujadiliana na Mungu? Ikiwa unafikiri kuwa Mungu si mwenye haki, basi kwanini unamwamini? Daima umetaka kusikia Mungu akikuambia, “Nyinyi ni watu wa ufalme na hili halitawahi kubadilika” kabla ya hamjajitahidi kwa ajili ya familia ya Mungu. Mungu asingesema hili, basi usingepeana moyo wako wa kweli kwa Mungu. Mtu wa aina hii ni mkaidi kiasi gani! Nimewaona watu wengi ambao hawajawahi kulenga kubadilisha tabia zao, hata zaidi hawajalenga kuuweka ukweli kwenye vitendo. Wao tu hutilia maanani kuuliza ikiwa watapata hatima nzuri ya mwisho, jinsi Mungu atakavyowashughulikia, ikiwa Ana majaaliwa yao kuwa watu Wake na mambo mengine ya uvumi. Je, watu hawa ambao hawajashughulika na kazi ya kweli wanawezaje kupata uzima wa milele? Je, wanawezaje kusalia katika familia ya Mungu? Sasa Ninawaambia kwa taadhima: Mtu aliyejaaliwa na Mungu asipouweka ukweli katika vitendo, basi ataondolewa mwishowe; na mtu anayetumia rasilmali yake na kufanya vyema ili kuuweka ukweli katika vitendo—hata ikiwa watu humwona kama mtu asiyejaaliwa kusalia—atakuwa na hatima nzuri zaidi kuwaliko wale wanaoitwa watu waliojaaliwa ambao hawajakuwa na kujitolea, kwa sababu ya tabia ya Mungu yenye haki. Je, unayaamini maneno haya? Iwapo huna uwezo wa kuyaamini maneno haya na unaendela na shughuli zako kwa njia mbaya, basi Ninakuambia kuwa hutaweza kusalia, kwa sababu humtaki Mungu kwa kweli na hujauzoea ukweli. Kwa vile ni hivi, kudura ya Mungu kwa watu si ya maana. Ninasema hili kwa sababu mwishowe, Mungu ataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji wao na mienendo; hata hivyo, tukizungumza bila upendeleo, majaaliwa ya Mungu yana kazi ndogo tu na hayana umuhimu mkubwa. Je, unayaelewa maneno haya?
2. Kazi ya Mungu katika Siku za Mwisho si kwa Madhumuni ya Kuwahukumu Watu, lakini badala yake Kuwaokoa Watu
Watu wengine husema: “Asili yangu si nzuri, yaache mambo yalivyo!” Je, huna uwezo wa kuunyima mwili? Je, huna moyo na akili? Je, mnaombaje kila siku? “Mwili, toka nje! Yaache mambo yalivyo, Mungu ameujaalia; sihitaji kufanya lolote.” Je, hili ndilo ombi lako? La! Basi kwanini hufanyi kazi na Mungu? Baadhi ya watu ambao wamelifanya kosa dogo watasema: Je, nitaangushwa na Mungu? Mungu hakuja wakati huu ili kuwaangusha watu, lakini badala yake kuwaokoa watu kwa kiwango kikubwa kiwezekanacho. Je, ni nani asiyefanya makosa kabisa? Je, kila mtu akiangushwa, basi unawezaje kuitwa wokovu? Makosa mengine hufanywa kimakusudi na makosa mengine kufanywa bila kupenda. Kwa mambo ya bila kupenda, unaweza kubadilika baada ya kuyatambua, hivyo Mungu angekugonga kabla hujabadilika? Je, hivi ndivyo Mungu huwaokoa watu? Si hivyo! Bila kujali iwapo unakosea bila kupenda ama kutokana na asili ya uasi, kumbuka tu: Harakisha na uuzindukie uhalisi! Endelea kwa bidii; bila kujali ni hali gani inayotokea, lazima uendelee kwa bidii. Mungu anafanya kazi ili kuwaokoa watu na Hatawagonga watu Anaotaka kuwaokoa bila taratibu. Bila kujali kiasi chako cha mgeuzo, hata kama Mungu angekuangusha mwishowe, basi Mungu angefanya hivyo kwa uhaki; wakati huo utakapofika, Atakufanya uelewe. Sasa hivi jukumu lako la pekee ni kuendelea kwa bidii, kutafuta kubadilishwa na kutafuta kumridhisha Mungu; unapaswa kujali tu kuhusu kuutimiza wajibu wako kulingana na mapenzi ya Mungu. Hapana kosa katika hili! Mwishowe, bila kujali jinsi Mungu anavyokushughulikia, hilo daima hufanywa katika uhaki; hupaswi kushuku hili au kuwa na wasiwasi nalo; hata kama huwezi kuelewa uhaki wa Mungu hivi sasa, kutakuwa na siku ambayo utaridhishwa. Hakika Mungu si kama mkuu wa serikali ama mfalme wa ibilisi! Mkijaribu kuelewa kipengele hiki kwa makini, basi mwishowe mtaamini kwa udhabiti kuwa kazi ya Mungu ni kuwaokoa watu na kubadilisha tabia za watu. Kwa kuwa ni kazi ya kuzibadilisha tabia za watu, watu wasipofichua tabia zao, basi hakuna linaloweza kufanywa na hakutakuwa na matokeo yoyote. Lakini baada ya kufichua tabia yako, kuendelea hivyo kutakuwa kwa taabu, kutakosea amri za utawala na kumkosea Mungu. Mungu atatoa adhabu za kiasi tofauti, na utalipa gharama kwa dhambi zako. Mara chache wewe hupotoka bila kufahamu na Mungu hukuonyesha, hukupogoa, na kukushughulikia; ukifanya vyema, Mungu hatakulaumu. Hii ndio namna ya kawaida ya mgeuzo; umuhimu wa kweli wa kazi ya wokovu unajitokeza katika mchakato huu. Huu ndio ufunguo! Chukua kwa mfano mipaka kati ya wanaume na wanawake; leo unatenda kwa ajili ya raghba ya kuushika mkono wa mtu, lakini unaporudi unatafakari: Je, hii sio tabia potovu? Je, hii sio dhambi? Je, hii sio tahayari kwa Mungu wakati ambapo mipaka kati ya wanaume na wanawake hauzingatiwi? Je, ninawezaje kufanya kitu cha aina hii? Kisha unakuja mbele za Mungu na kuomba: “Ee Mungu! Nimekosa tena; jambo hili halipatani na ukweli na nauchukia mwili uliopotoka.” Baadaye, unaweka azimio la kutowashika au kuwakaribia sana. Je, huu si mgeuzo? Ikiwa una mbadiliko wa aina hii, je, Mungu bado atakuhukumu kwa kuwashika mkono? Ikiwa uliishika mikono yao na hukuhisi vyema kuhusu hilo, na usiikiri dhambi yako kwa Mungu, ukifkiri kuwa halikuwa jambo la aibu, na hujidharau, kuwa mwangalifu, ama kuwa na azimio, basi baadaye hutaishika mikono yao tu, utawakumbatia! Mambo yatakuwa mazito zaidi na zaidi na yatakupelekea kufanya dhambi, na katika kufanya hivyo, Mungu atakuhukumu kwa dhambi zako; utafanya dhambi tena na tena, haina tiba. Kama kwa kweli ungefichua sehemu ndogo ya tabia iliyopotoka pasipo kutaka, ukiweza kutubu, basi Mungu hatakuhukumu na bado unaweza kuokolewa. Mungu anataka kuwaokoa watu, na haiwezekani kwa asili za watu kutofichuliwa kwa kiasi fulani; hata hivyo, unapaswa kuzingatia kutubu na kubadilika kwa haraka. Je, hili halingeridhisha mapenzi ya Mungu? Watu wengine hawaamini haya na daima wanakuwa na mtazamo wa kujihadhari kumhusu Mungu; mtu wa aina hii atateseka siku moja.
Imetajwa hapo awali: Matukio yaliyopita yanaweza kufutwa kwa alama ya kalamu; siku za baadaye zaweza kuchukua nafasi ya yaliyopita; uvumilivu wa Mungu hauna mipaka. Lakini maneno haya yana kanuni ndani yake; si kweli kwamba bila kujali umetenda dhambi kuu kiasi gani mwishowe, Mungu anaweza kuifuta kwa alama moja; kazi yote ya Mungu ina kanuni. Zamani kulikuwa na aina hii ya amri ya utawala: Yule ambaye alifanya dhambi fulani kabla ya kulikubali jina la Mungu, mwache ajiunge; akifanya dhambi hiyo tena baada ya kuingia, mshughulikie kwa njia fulani; akirudia kufanya dhambi iyo hiyo tena, basi mfukuze. Mungu daima amewasamehe watu kwa kiwango kikubwa sana kinachowezekana katika kazi Yake; kutoka kwa mtazamo huu, inaweza kuonekana kuwa kazi hii kweli ni kazi ya kuwaokoa watu. Lakini katika hatua hii ya mwisho ukifanya dhambi isiyosameheka bado, hutaweza kuponywa ama kuweza kubadilika. Mungu ana mchakato wa kubadilisha tabia za watu na wa kuwaokoa watu. Kupitia kwa mchakato wa watu kufichua tabia zao, Mungu atawabadilisha; kupitia njia ya watu kufichua na kubadilisha tabia zao siku zote, Mungu hupata lengo Lake la wokovu. Baadhi ya watu hufikiri: Kwa kuwa ni asili yangu, basi nitaionyesha zaidi iwezekanavyo! Baadaye, nitaitambua na kuuweka ukweli kwenye vitendo. Je, huu mchakato ni wa lazima? Ikiwa kwa kweli wewe ni mtu unayeuweka ukweli kwenye vitendo, na ukiona kwamba pia una matatizo ambayo wengine wanayo, basi utafanya bidii kuepuka kuyafanya mambo hayo. Je, huu si mgeuzo usio wa moja kwa moja? Wakati mwingine, unafikiri kufanya namna ile, lakini kabla ya kufanya, unafahamu na kuiacha. Je, hili halipati matokeo ya wokovu? Kuna mchakato wa kuuweka ukweli wote kwenye vitendo; ni vigumu kwako kuwa mtimilifu na kutokuwa na mawazo ya kighushi unapoanza kutenda. Bado kuna vitu kadha ambavyo kwavyo unategemea mawazo yako mwenyewe kabisa, lakini baada ya kushughulikiwa na kupogolewa, mwishowe utatenda kulingana na nia na maneno ya Mungu kikamilifu. Haya ni mbadiliko na mgeuzo.
Zaidi:Kanisa la Mwenyezi Mungu Lilikujaje Kuwepo?

Jumamosi, 6 Julai 2019

Sura ya 30. Kumtumikia Mungu Mtu Anapaswa Kutembea Njia ya Petro

Sura ya 30. Kumtumikia Mungu Mtu Anapaswa Kutembea Njia ya Petro

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi hawawezi kuainisha ni watu gani wana ukweli, watu gani hawana ukweli na watu gani husema mambo yaliyo na ukweli. Unapoulizwa kueleza ni nini maana ya "ukweli," huwezi kueleza kwa wazi. Lakini mara tu mtu anaposema kitu, unasema: “Mtazamo wake ni wa kweli. Maneno ayasemayo yanaonyesha ufahamu wa utendaji uliopatikana kupitia kwa uzoefu.” Unaelewa mara tu unapowasikia wakizungumza. Kwa ninyi hapa mlio wapya, Nikiwauliza ni nini maana ya 'uhalisi,' hamtaweza tu kunijibu, lakini pia hamtaweza kueleza tofauti kati ya mtu anayezungumza uhalisi na mtu anayezungumza mafundisho ya dini. Hili halisemwi kuwadunisha ninyi, ni tu kwamba hamna uzoefu. Tazama wale wakongwe wa kanisa; ingawa washawishi wengine wa kufanya mengi huenda wakawakanganya na vitu wasivyoweza haswa kutambua sababu sahihi, bado wanajua kwamba wanachosema watu hao si sahihi. Wanaweza kutambua ni watu gani wanazungumza mafundisho ya dini, na watu gani wanazungumza uhalisi. Ninyi, kwa hali yoyote, hata bado hamjababia. Hili halisemwi kuwashushia hadhi, kwa hivyo msione vibaya kwa sababu ya hili. Hii ni njia ya kawaida ya uzoefu ambayo kila mtu ni lazima apitie. Kila mtu ni lazima apitie miaka mingi ya kunyunyiziwa maji, kufanyiwa uchunguji, kusikiliza, kuhisi, kutambua na kupitia kabla ya kufahamu polepole lakini kwa kina uzoefu wa maisha, kabla ya kuvuka lango na kufungua macho yao. Ukizungumza tu mafundisho ya dini na kusikia mafundisho ya dini, ikiwa huwezi kutambua masuala yanayohusu uhalisi na usiwe na utambuzi, basi macho yako hayajafunguliwa; bado tu hayajafunguliwa. Ni nini maana ya "macho yako hayajafunguliwa"? Inamaanisha bado hujavuka lango, na huo ni ukweli. Inamaanisha kwamba hujavuka lango panapohusiana na ukweli. Jitazameni sasa. Labda unaweza kufanya kazi ya uchungaji, kuwasaidia wengine, kutoa msaada na kutumia, au kufanya mambo mengine ya desturi katika familia ya Mungu. Lakini wewe hasa huna uhalisi, wala hutakuwa hasa na utambuzi wowote wa kufikia uhalisi au kufikia nyaraka na mafundisho ya dini. Labda hamjaridhishwa na hili, mpaka siku moja mtu fulani aje anayezungumza mafundisho ya dini, aliye na maneno ya kushawishi, na kisha huenda mtamkweza. Na wakati mtu yule aliye na uhalisi wa kweli ajapo, aliye kimya, asiyetoa sauti, basi huenda mtamdharau. Mara mnapofanya hivi, wakati huo mtajua kimo chenu wenyewe kiko wapi. Ndio, kimo cha mwanadamu, ufahamu wa mtu kuhusu uhalisi na wa mtu mwenyewe, uzoefu wa mtu kuhusu kweli, ufahamu wa mtu kuhusu Mungu—mambo haya yote hutokana na uzoefu, hutokana na kuishi siku baada ya siku, hili ni wazi na dhahiri. Vitu hivi bila shaka havitokani na kusoma wala kutoka kwa mambo mangapi uliyoyasikia. "Nina mambo haya, nimeyasikia na ninayakumbuka. Kiwango changu cha maarifa kiko juu sana, mimi ni mwanafunzi wa chuo, ninafanya kazi fulani, ninachunguza jambo fulani, na mimi huyajua mambo mara tu niyasikiapo." Unaweza kutumia maarifa uliyojifunza kusikia falsafa, siasa au fasihi. Lakini huwezi kuyatumia hapa, hayana maana! Tuna nini hapa, basi? Maarifa uliyojifunza huenda yakakusaidia kujua maneno yaliyoandikwa ya ukweli au kuhusu vile yameelezwa vizuri zaidi kuliko wengine, lakini wewe si bora kuliko wengine inapohusu wewe kuupitia ukweli; huna heri kuhusiano na hilo. Mnalikubali hili, sivyo? Hamchunguzi masuala ya uzoefu wa maisha na mnakosa mambo mengi sana. Lakini kwa ninyi ambao mna maarifa fulani, ambao sasa mko katika nafasi ya heri ya kuwa kiongozi juu ya watu wengine, ambao mko kazini mara kwa mara na ambao hukutana na wakongwe wa kanisa walio katika viwango vya juu, na ambao hufanya kazi fulani maalum, mnaweza kuendelea haraka zaidi. Mnaweza kuendelea haraka sana kuliko vile wale wakongwe wa kanisa wangeweza hapo awali, haraka na ufahamu wenu wa uhalisi, na hali yoyote ya ukweli na kwa kujifahamu wenyewe. Labda hamtatembea katika njia inayopinda au labda ninyi pia mtahitajika kupatwa na vipingamizi fulani. Hali ya kila mtu ni tofauti, hali zao ni tofauti. Watu wengine wanahitajika kupatwa na vipingamizi fulani kabla ya kuweza kupitia mabadiliko makuu. Na kisha kuna watu wengine ambao hawahitaji kupatwa na vipingamizi vikubwa, lakini hugundua njia wanayopaswa kutembea na upotovu wao wenyewe katika mambo yanayotendeka kandokando yao, na wao hupata ujuzi fulani katika watu, mambo na vitu vilivyo kandokando yao—huyu ni mtu anayeendelea upesi sana kwa kulinganisha.
Hivyo mnapaswa kuzingatia nini sasa? Ikiwa mtazingatia tu kuyafanyia kazi na kujishughulisha na mambo ya ukingoni, basi maendeleo yenu yatacheleweshwa. Mnapoamini katika Mungu, maendeleo yenu binafsi maishani ni muhimu zaidi na ni ya maana zaidi. Huenda ukajiandaa tu na mafundisho ya dini, au na uwezo wa kufanya kazi, au huenda ukafanya jambo fulani kwa kutumia mbinu fulani nzuri sana, au kwa hekima; mambo haya yote ni ya kufuata, ingawa bado huwezi kuendelea bila hayo. Suala kuu la imani yako kwa Mungu ni kwamba lazima uujue ukweli kabisa, upitie ukweli na uwe na ufahamu fulani wa ukweli, na uweze kuwa na moyo mtiifu na kutosheleza mapenzi ya Mungu mbele Yake. Iwapo unaamini katika Mungu lakini kadri unavyoamini, ndivyo uhusiano wako na Mungu unaenda mrama, ndivyo unavyosonga mbali zaidi na Mungu na ndivyo unavyokuwa na sehemu nyingi ndani yako zinazopingana na ukweli, basi hilo linathibitisha kwamba imani yako haikuongozi kuendelea, kwamba Roho Mtakatifu hajakushughulikia, na kwamba umepotea na umevuka mipaka. Iwapo unaamini kwa kipindi fulani na kisha unakuwa na ufahamu fulani wa uhalisi, kujifahamu kwa kiasi fulani, na ufikirie umeelewa mambo fulani ya uhalisi, basi hili linathibitisha kwamba unafahamu mambo ya kiroho, macho yako yamefunguka na unatembea katika njia sahihi. Kuna wakongwe wengine sasa ambao wamefuata kwa miaka miwili au mitatu, ambao hata hawajababia, ambao ni waasi na wasiozuiwa na ambao hujitayarisha kupokea baraka, ambao wanajitayarisha kufurahia utajiri wao mzuri baada ya kazi kukamilishwa. Hata bado hawajababia kulingana na uzoefu wa maisha, na hawana uhusiano wenye upatanifu na Mungu hata kidogo. Ni vyema kuwa nao kwa kipindi kifupi, na watatii shingo upande, na hawatathubutu kutoa sauti ikiwa wana dhana. Lakini baada ya muda fulani kupita, mara tu wanapoanza kupinga, wanakuwa vyombo vya kuangamia. Kila mtu yuko juu ya ardhi hatari, na hili ni jambo la kuogofya. Ikiwa unamwamini Mungu na unatembea kwenye njia sahihi, basi imani yako ni muafaka na utapata baraka. Ikiwa utaenda kombo, ukitembea kwenye njia isiyo sahihi au njia isiyonyooka, usipoendelea mbele, usipoendelea mbele kwa uwezo wako wote, basi utaangamia na utapata adhabu.
Watu wana njia mbili za imani katika Mungu: Moja ni kuweza kumwamini Mungu kabisa; na nyengine ni kumuasi Mungu na kumpinga Yeye. Hizi ndizo njia mbili pekee. Haiwezekani kwamba humpingi Mungu lakini pia humtii Yeye; hili haliwezekani. Ikiwa humtii Mungu na huna ufahamu halisi, basi unaweza tu kuwa mkaidi na muasi. Huenda usionyeshe uasi kwa mambo unayosema, na huenda usimpinge Yeye waziwazi kwa silaha zilizochukuliwa, lakini bado moyo wako ni mkaidi. Au iwapo huulizwi kufanya jambo, huenda ukahisi umejawa na upendo kwa Mungu na kuhisi uko karibu sana na Mungu. Lakini mara tu unapoulizwa kufanya jambo, basi ukaidi wako, kiburi chako, kujidai kwako na mambo yako ya Shetani hufichuliwa; mara tu yanapofichuliwa, basi ukaidi wako unakuwa wa kweli. Je, si hivyo? Huenda ukaichukulia imani yako kwa Mungu kama tu "Mimi nimebarikiwa kwa kuamini katika Mungu na baadaye nitakuwa chombo cha baraka Zake. Mimi ni mshirika wa familia ya Mungu na mimi nimeinuliwa na Mungu; mimi ni mtu aliyekwezwa na Mungu. Nimebarikiwa na Mungu ni mwema kwangu." Lakini ikiwa unliona kwa njia hii, kuna maana gani? Kuna maana gani kupiga makelele kwa maneno haya matupu yanayorudiwarudiwa? Jambo kuu sasa ni iwapo unaweza kuokolewa au la, iwapo unatembea kwa njia sahihi ya maisha au la, iwapo Mungu anakusifu katika imani yako au la, iwapo Mungu anakubali kuwa kwako mshirika wa familia ya Mungu au la, na iwapo Mungu anakukubali au la; ni hayo tu ndiyo yanaweza kuchukuliwa kama kuwa makini katika imani yako kwa Mungu. Imani ya kipumbavu, kama vile "Ah, Mungu ni mwema kwangu, Mungu hunifadhili, nimebarikiwa na mimi hufanikiwa kila mahali. Tazama, Mungu ameniinua na kunifanya kuwa kiongozi katika familia Yake. Nimekuwa na bahati sana na nyota yangu imekuwa ikiinuka tangu nilipokuja katika familia ya Mungu." Kuringia tu jambo la aina hii hakuna maana. Ni tupu; lisilo na maana! Ikiwa umepewa nafasi lakini huishikilii upesi, basi ilitolewa bure, na hakutakuwa na maana hata ukipewa nafasi nyingi kiasi gani. Shikilia upesi mambo fulani ya kweli, na halisi. Baadhi ya waumini wakongwe husema: "Ah, nimebarikiwa! Mimi nimebarikiwa na mimi ni mtu aliyebarikiwa zaidi katika dunia yote, katika ulimwengu wote!" Haingekusaidia hata ungekuwa malaika; huwezi tu kusema mambo ya aina hii, ni lazima ushikilie upesi mambo ya kweli. Hasa ninyi ambao mumeamini katika Mungu kwa muda mfupi tu na mmepata uzoefu kidogo kutokana na kufanya mambo, ambao hamkupitia zile hatua za kazi hapa mwanzo, na ambao mlikuja mwisho kabisa—je, uko tayari kuwa na uhakika kabisa ili baadaye uweze kuokolewa? Je, uko tayari? Huko tayari, sivyo? Ikiwa huko tayari kuwa na uhakika kabisa kuhusu jambo hilo, basi uko katika nafasi hatari!
Ikiwa huelewi ni nini maana ya kumhudumia Mungu au nini maana ya kutii Mungu, na unaelewa kidogo sana namna ya kumwabudu Mungu au jinsi watu wanapaswa kuamini katika Mungu; iwapo hujashikilia mambo haya na huyafahamu katika moyo wako, basi utaenda mrama kwa urahisi sana na utamuasi Mungu kwa urahisi sana. Kama wale walioanguka hapa awali waliosema: "Roho Mtakatifu na atufunulie mambo haya!" Ninyi nyote sasa mnaona jambo hili kwa dhahiri. Wakati huo hawakuwa na nia yoyote ya kufanya chochote kibaya na kumuasi Mungu, na walijua kwmba Mungu alikuwa amewainua na kwamba ni lazima wafanye kazi kwa bidii. Ilhali hawakutembea kwenye njia sahihi, wakifikiria tu kwamba Mungu alikuwa amewainua, kwamba walitaka kufanya kazi kwa bidii, na kufanya kazi nzuri ya kuwa wachungaji wa wale waliokuwa chini yao kanisani; walidhani chochote kile ambacho waliokuwa juu yao waliwataka wafanye, wangefanya. Hawakuwa wameshika mambo ya utendaji na hakika walikuwa wanafanya mambo bila kutambua, wakitegemea ushupavu wao wenyewe. Walipokuwa hawatumiwi tena, walikasirika sana na kusema: "Mungu ni mwenye haki. Roho na afichue hili! Imani yangu haiko katika mwanadamu, iko katika Mungu." Hawakupanga awali kusema maneno haya, hivyo yalisemwa bila hiari? Sababu yake ilikuwa gani? Ilikuwa ni kwa sababu mwanadamu hamchi Mungu na hamfahamu Yeye. Unaona kwamba watu wengine husema mambo mengine ambayo ni ya upumbavu na ujinga, na wao husamehewa. Wao husamehewa kwa ajili ya ujinga wao na kile ambacho wajibu wao ulikuwa hakichunguzwi. Mbona hali si hiyo kwa watu wengine? Kwa sababu walisema mambo yaliyokuwa mazito sana: "Wewe ni Mungu, lakini bado sitakutii Wewe." Watu hawa ni wapinga Kristo; wao humuasi Mungu na hawakubali ukweli. Watu wengine ni wapumbavu na wajinga. Ni sawa kuonyesha upumbavu wako na ujinga mara moja au mara mbili; lakini ukikosea amri za Mungu za usimamizi au ukikosea tabia ya Mungu, basi utakuwa matatani. Tazama njia ambayo Petro alitembea. Alipata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu hapo mwanzo na alizungumza na Yesu, akisema: "Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aishiye." Mara tu Roho Mtakatifu alipokuwa amempa nuru, wakati huo alipata ujuzi fulani na moyo wake ulijazwa nuru. Hata kama wakati huo hakuwa na ufahamu wa kina, lakini alitafuta kumfahamu Mungu, na akatembea kwenye njia sahihi ya kumhudumia Mungu. Kumhudumia Mungu ni jambo la hatari zaidi, na pia ni jambo la utukufu zaidi. Kwa sababu wanadamu ni wakaidi na wapotovu, mara tu wanapopotea, wao humalizika. Watu humhudumia Mungu, sio watu wengine; kumhudumia Mungu ni jambo la hatari. Petro alitembea katika njia hiyo na alikuwa na imani hii. Na je, kuhusu Paulo? Hakukubali kwamba Yesu alikuwa Kristo. Alimuwinda bila kukoma na, baada ya kuangushwa chini, bado Paulo hakutambua kwamba Mungu alikuwa Bwana wa vitu vyote, wala vile wanadamu wanapaswa kumtii Yeye. Hakuwa na akili ya kawaida ya kufikiria, lakini kuanzia mwanzo hadi mwisho alihodhi fikira za kiburi: "Ninakupa Wewe kiasi hiki kwa hivyo unapaswa kunipa kiasi hicho; ninatumia rasilimali kiashi hiki, kwa hivyo Wewe unapaswa kunituza kiasi hicho na kunipa kiasi hicho cha mshahara." Kazi yake ilikuwa chini ya utawala wa fikira za aina hii wakati huo wote. Hivyo hakuwahi kuwa na moyo wa kumheshimu Mungu, hakuwahi kuwa na moyo wa kumcha Mungu. Angalia toni ya maneno yake: "Nimepigana vita"—Nimepigana vita Ulivyonifanya nipigane; "Nimemaliza kazi yangu"—Nimekimbia kwenye njia uliyoniambia nikimbie; "Nimeidumisha imani"—je, hukunifanya niidumishe?" Nimeidumisha, kwa hivyo taji ya utukufu haipaswi kuhifadhiwa kwa ajili yangu? Je, hakunena na toni ya aina hii? Bila shaka hangeweza kuzungumza waziwazi namna hii katika waraka. Alizungumza kitasifida na kimafumbo, lakini maneno yake yalianza kutoka kwa dhana hizi. Ni nini kilifanyika mwishowe? Yeye bado aliadhibiwa, au sivyo? Mnatakiwa kuona dhahiri vile wanadamu wanapaswa kuchagua kwenye njia ya kumhudumia Mungu, kwenye njia ya kuamini katika Mungu. Ni njia zipi za kumhudumia Mungu ni za njia za Paulo? Ni njia zipi za kuamini ni za njia ya Paulo? Ni jinsi gani njia ya kumcha Mungu ya kumhudumia Mungu kama ya Petro inaweza kutimizwa? Kuna njia ambayo viumbe wa Mungu wanapaswa kutembea ili kumwabudu Yeye; njia hiyo ni lazima ichaguliwe sawasawa na malengo yenu ni lazima yawe dhahiri. Usiwe mpumbavu, lakini tembea kwa bidii na kusimama juu ya ardhi imara, na maono yaliyo dhahiri kikamilifu. Ni hatari wewe kutembea kwenda mbele katika njia ya kipumbavu na ina hakikisha kwamba siku moja utakosea amri za usimamizi za Mungu au kuanza kunung'unika.
Je, mna hakika kuhusu asili gani au hali gani ndani ya wanadamu huwaongoza kwa urahisi sana katika uangamiaji, bila kujali ikiwa ni kiongozi au mfuasi? Je, unajua kuhusu asili ya kawaida ya wanadamu? Ukawaida wa asili ya wanadamu ni kumsaliti Mungu; kila mtu na watu wote wanaweza kumsaliti Mungu. Je, kutoamini pekee sio kumsaliti Mungu? Je, kumsaliti Mungu ni nini? Ni mambo gani yanamaanisha kumsaliti Mungu? Ni lazima ufahamu kiini cha wanadamu kimeumbwa na nini; ni lazima uelewe hili na kufahamu mzizi wa mambo hayo. Udhaifu wako wa mauti, hasira, njia mbaya, tabia mbaya au adabu mbaya—mambo haya yote ni ya juujuu. Ukiyashika tu mambo haya kwa kukaza na kiini chako kibakie kisichofumbuliwa, basi bado utatembea kwenye njia isiyonyooka na bado utamuasi Mungu. Je, sivyo? Ninyi bado kila mara tu mnababia na kukamata utondoti hafifu. Mwanadamu anaweza kumsaliti Mungu wakati wowote au mahali popote na hili ni tatizo kubwa. Labda wakati huu unaweza kumpenda Mungu kwa kiwango kikubwa, kutumia rasilimali nyingi kwa ajili ya Mungu, kuwa mwaminifu hasa; labda wakati huu unaweza kuwa wa akili hasa na kuwa na dhamiri. Lakini huenda kukaja na wakati na mahali ambapo kitu fulani kitakuongoza kumsaliti Mungu. Tuseme kwamba mtu fulani ni wa akili hasa wakati huu; Roho Mtakatifu anamshughulikia, ana uzoefu fulani wa utendaji, amebeba mzigo, yeye hutekeleza jukumu lake kwa uaminifu na ana imani thabiti sana. Basi tuseme Mungu angefanya jambo fulani la kumsikitisha, jambo alilodhani si sahihi. Dhana zingeinuka ndani yake wakati huo, mara moja angekuwa mbaya, na angepoteza shauku na kuwa ovyoovyo katika kazi yake, na angeachana na maombi, akisema, "Ni nini ambacho ninaombea? Mungu hapaswi kufanya jambo hili! Ninawezaje kuomba?" Nguvu zake zingeisha na shauku yake ya maombi ingeipotea. Hii inaitwa nini? Je, hili sio dhihirisho la usaliti? Katika wakati wowote au mahali popote, mwanadamu anaweza kumwacha Mungu, kumkana Mungu na kumshutumu Mungu—je, haya yote si usaliti? Hili ni jambo la kuogofya. Tazama, unadhani kwamba sasa huna dhana zozote na unaweza kumtii Mungu wakati mwingi, kwamba unaposhughulikiwa na kupogolewa hutamwacha Mungu. Ilhali unaweza bado kumsaliti Mungu wakati wowote au mahali popote. Ni lazima ufahamu vilivyo asili ya mwanadamu. Bila shaka, baadhi ya watu wakati mwingine watakuwa na dhamiri fulani, na hao watakuwa watu ambao asili zao ni nzuri kwa kulinganisha. Wengine watakuwa na ubinadamu wa uovu, na asili zao zitakuwa mbaya. Lakini haijalishi iwapo mtu yeyote anasema ubinadamu wako ni mzuri au mbaya, au iwapo ubora wako ni mzuri au mbaya, asili ya kawaida ni kwamba unaweza kumsaliti Mungu. Asili ya mwanadamu ni kumsaliti Mungu, hivyo watu wangeweza kumsaliti Mungu kama hawangekuwa wamepotoshwa? Bado mnafikiri sasa: "Asili za watu ambao wamepotoshwa na Shetani zitamsaliti Mungu kwa hivyo hakuna ninachoweza kufanya. Nitahitajika tu kubadilika polepole." Je, bado mnawaza kwa njia hii? Basi Niambieni, je, watu wangeweza kumsaliti Mungu ikiwa hawangekuwa wamepotoshwa? Watu wangeweza pia kumsaliti Mungu ikiwa hawangekuwa wamepotoshwa. Wanadamu walipoumbwa walipewa hiari, walikuwa wadhaifu sana, na hawakuwa na moyo ambao ungeweza kumfikia Mungu kwa kweli au uliogeuka kumwelekea Mungu kwa kweli: Mungu ni Muumba wetu na sisi ni viumbe Wake. Wanadamu hakuwa na moyo huu. Wanadamu hawakuwa na ukweli ndani yao wala chochote ambacho kingeweza kuwasaidia kumwabudu Mungu. Mungu aliwapa hiari ili kwamba wanadamu waweze kufikiria, lakini wanadamu hawakujua Mungu ni nani na hawakufahamu jinsi ya kumwabudu Mungu. Hawakuwa na kitu kama hiki ndani yao. Hata kama hungepotoshwa, bado ungeweza tu kumsaliti Mungu. Kwa nini ni hivi? Shetani hukushawishi ili umfuate yeye na kumsaliti Mungu. Wewe uliumbwa na Mungu lakini humfuati Yeye. Badala yake unamfuata Shetani. Je, wewe si msaliti basi? Wasaliti husaliti. Wewe unafahamu kwelikweli kiini hiki, au sivyo? Hivyo wanadamu wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na katika mahali popote. Ni wakati tu wanadamu watakapoishi kikamilifu ndani ya ufalme wa Mungu na ndani ya nuru ya Mungu, wakati Shetani atakuwa ameangamizwa na hakuna tena ushawishi wowote, hapo tu ndipo wanadamu hawataweza tena kumsaliti Mungu. Wakati bado kuna ushawishi, wanadamu badow wanaweza kumsaliti Mungu; hivyo inasemekana kwamba wanadamu hawana thamani. Bado unafikiria: "Sasa nimepata mambo fulani. Nina mambo fulani ambayo hayamsaliti Mungu, lakini yaliyo na upatanifu na Mungu. Siwezi kufikiriwa kuwa kioo kinachong'aa, lakini angalau kama chupa ya udongo. Siwezi kufikiriwa kuwa dhahabu, lakini labda shaba nyekundu." Unajistahi mwenyewe kwa hali ya juu sana. Je, unajua mwanadamu ni kitu cha aina gani? Mwanadamu anaweza kumsaliti Mungu wakati wowote au mahali popote na hafikii hata thamani ya peni moja. Kama tu alivyosema Mungu: "Rundo la mavi ya mbwa, wakatili na mafidhuli." Watu hufikiria: "Mimi si fidhuli! Mimi si fidhuli kamwe! Kwa nini nisiweze kuelewa jambo hili? Kwa nini sijalipitia? Ikiwa sijapotoshwa, basi siwezi kumsaliti Mungu." Kuna mifano ya hili, na kuna ukweli. Ninachowaambia sasa hakikosi msingi. Mambo haya yote ni kuwaonyesha ninyi, kuwaridhisha ninyi; ni kwa njia hii pekee ndio mnaweza kufikia ufahamu wa upotovu wenu wenyewe na kutatua tatizo la usaliti. Hakutakuwa tena na usaliti wowote ndani ya wanadamu katika ufalme, wanadamu wataishi chini ya utawala wa Mungu na Shetani hatakuwa na utawala juu yao, na wanadamu wataishi huru na hawatahitaji kuwa na wasiwasi, wakidhani, "Je, naweza kumsaliti Mungu?" Hakutakuwa na haja ya kuwa na wasiwasi; haitakuwa na maana! Baadaye, inaweza kutangazwa kwamba humtakuwa na chochote ndani yenu kinachomsaliti Mungu. Lakini sasa, mambo hayajakuwa sawa, kwani kiini cha wanadamu ni kile kinachoweza kumsaliti Mungu wakati wowote na katika mahali popote. Sio kwamba utamsaliti Mungu kwa sababu ya hali fulani mbaya, au kwamba bila hali yoyote mbaya au bila mtu yeyote kukulazimisha basi hutamsaliti Mungu. Unaweza bado kumsaliti Mungu hata iwapo hakuna anayekulazimisha; hili ni tatizo la kiini potovu cha wanadamu, na ni tatizo la asili yao. Ona jinsi unavyopumua tu sasa, jinsi hujafanya chochote, hujasonga, hujafikiria chochote, na ilhali hiyo asili inayomsaliti Mungu iko ndani yako—je, hii ni sahihi? Kwa nini? Kwa sababu wanadamu wana usaliti ndani yao na Mungu hayuko ndani yao. Roho ya wanadamu na nafsi ya wanadamu havina sehemu ya Mungu ndani yao. Hivyo, unaweza kumsaliti Mungu wakati wowote au katika mahali popote. Angalia, malaika ni tofauti. Hawana tabia ya Mungu, wala hawana kiini cha Mungu. Lakini wanaweza kumtii Mungu kikamilifu kwa sababu waliumbwa na Mungu sanasana kumhudumia Yeye na wao hutumwa kila mahali; wao ni mali ya Mungu. Wanadamu, kwa hali yoyote, waliumbwa kuishi duniani na hawakuumbwa na akili ya kumwabudu Mungu. Wanadamu wana uwezo wa kumsaliti Mungu na ni vyombo vinavyoweza kutumiwa au kupiganiwa na mtu yeyote. Wao ni wa thamani duni! Kwamba wanadamu wana asili hii imefichuliwa ili watu waweze kupata ufahamu wa jambo hili na wao wenyewe. Kutokana na hali hii, watu wanaweza kuanza kubadilika, na kuanzia hapa wanaweza kutafuta njia ya utendaji. Kufahamu ni katika mambo gani unaweza kumsaliti Mungu na ni kasoro gani unahitaji kurekebisha ili usimsaliti Mungu, utafikia hatua ambapo hutamsaliti tena Mungu katika hali nyingi na utaepuka kumsaliti Yeye katika nyingi ya hali hizo. Iwapo baadaye utamsaliti Mungu au la haitakuwa juu yako. Safari yako ya maisha itafikia mwisho wake, na itafikia wakati huo ambapo kazi ya Mungu itafanyika, lakini iwapo baadaye utamsaliti Mungu au la hautakuwa wajibu wako. Kwa nini hilo lilisemwa wakati huu tu? Kabla ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, alikuja na akawashawishi wanadamu, na hapo basi waliweza kumsaliti Mungu. Baada ya Shetani kuangamizwa, je, wanadamu wakati huo hawatamsaliti Mungu tena? Wakati huo haujafika bado. Kwa hivyo wanadamu bado wana tabia potovu ya kishetani ndani yao, na wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote. Mara tu uzoefu wako wa maisha unapofikia hatua fulani, vitu vingi ndani yako vinavyomsaliti Mungu vitatupiliwa mbali. Wewe wakati huo utakuwa na vitu vingi vizuri, utaweza kutekeleza kujizuia na utaweza kujitawala mwenyewe. Hutakuwa na uwezo wa kumsaliti Mungu tena kwa wingi wa wakati huo, na baada ya Shetani kuangamia utapitia mabadiliko kamili. Hatua hii ya kazi ni kutatua sasa usaliti wa wanadamu na kutatua ukaidi wa wanadamu. Baadaye watu hawatamsaliti Mungu kwani Shetani atakuwa ameangamizwa, na hili haliwahusu wanadamu hata kidogo. Je, unafahamu? Kufahamu asili ya wanadamu ya kusaliti kunaanzia hapa: Ni mambo gani ni ya asili inayomsaliti Mungu, ni mambo gani ni sehemu ya kuonyesha usaliti, jinsi wanadamu wanapaswa kuingia na jinsi wanapaswa kufahamu. Kiini hiki cha wanadamu bado kiko ndani yao, wao bado wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote au mahali popote, na bado wanaweza kufanya mambo ambayo hawafikirii kuwa ni ya kumsaliti Mungu. Wanadamu wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote, hiyo ni kusema kwamba wanadamu hawana hali ya kujitawala, kwani Shetani amewamiliki. Unaweza bado kumsaliti Mungu hata kama hujapotoshwa, achilia mbali wakati huu ambapo umejazwa na tabia potovu ya kishetani. Wewe unaweza hata zaidi kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote. Sasa unahitajika kutupilia mbali tabia potovu, ili kwamba hayo mambo yaliyo ndani yako yanayomsaliti Mungu yatapungua zaidi na zaidi, na utakuwa na nafasi nyingi zaidi mbele ya Mungu kumruhusu Yeye kukukamilisha na kukukubali. Ikiwa utapata uzoefu mwingi kuhusu wokovu wa Mungu katika mambo yote, utakamilishwa wakati wa hatua hii. Hivyo, ikiwa kitu fulani cha Shetani, au pepo mchafu, atakuja kukudanganya na kukusumbua, unaweza basi kutumia utambuzi wako, au sivyo? Kwa njia hii, tabia yako ya usaliti itapungua, na hiki ni kitu ambacho kitahemshwa ndani yako katika siku za baadaye. Wanadamu walipoumbwa kwa mara ya kwanza, hawakuwa na akili hii, wala hawakufahamu ibada ya Mungu, jinsi ya kumtii Mungu au usaliti wa Mungu ni nini. Shetani alikuja kuwashawishi wanadamu na wakamfuata, walimsaliti Mungu, na wakawa wasaliti kwa Mungu. Hii ni kwa sababu wanadamu hawakuwa na uwezo wa kutambua mema na mabaya, hawakuwa na akili ya kumwabudu Mungu, wala hawakuwa na ufahamu wowote kwamba Mungu alikuwa Muumba au ufahamu wowote wa jinsi wanadamu wanapaswa kumwabudu Mungu. Katika siku za baadaye, Mungu kuwafinyanga wanadamu sasa ni kufanya kweli hizi (ufahamu wa kiini cha Mungu na tabia Yake...) ndani ya wanadamu, ili kwamba waweze kufahamu hali hizi na wawe kiwango fulani cha kujitawala na hali hizi. Yaani, kadiri uzoefu wako unavyokuwa wa kina, ndivyo utakavyomfahamu Mungu na ndivyo utapunguza kuwa na mambo yanayomsaliti Mungu. Kadiri unavyokuwa na mambo yanayopatana na Mungu, ndivyo utakavyoweza kumshinda Shetani, kadiri unavyokuwa na hali ya kujitawala, ndivyo utakavyoweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kweli. Baadhi ya watu huuliza: "Wanadamu wana kiini cha upotovu ndani yao na wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote; ni vipi ambavyo Mungu anaweza kusema bado Amewafanya wanadamu kuwa wakamilifu?" Kufanywa mkamilifu ni kumfahamu Mungu kupitia kwa uzoefu, na pia ni kufahamu asili yao wenyewe, kujua jinsi ya kumwabudu Mungu na kumtii Mungu, kuweza kutambua kati ya kazi ya Mungu na kazi ya wanadamu, na kutambua tofauti kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya pepo wachafu kupitia kwa uzoefu. Pia ni kuwa na ufahamu wa jinsi Shetani ibilisi humuasi Mungu, jinsi wanadamu humuasi Mungu, uumbaji ni nini na Muumba ni nani. Ninyi mnafahamu mambo haya, au sivyo? Haya yote ni mambo waliyopewa wanadamu kupitia kwa kazi ya Mungu katika siku za baadaye. Hivyo, wale watakaofanywa wakamilifu mwishowe watabeba uzito zaidi na watakuwa na thamani zaidi kuliko wale wa hapo mwanzo ambao hawakuwa wamepitia upotovu. Kwa sababu kuna mambo mengine ambayo yameongezwa ndani ya wanadamu na mambo mengine ambayoyamehemshwa ndani yao, watu wanaofanywa wakamilifu mwishowe watakuwa na hali ya kujitwala kuliko Adamu na Hawa wa wakati huo, na watafahamu ukweli zaidi wa jinsi ya kumwabudu Mungu na kumtii Yeye; watafahamu zaidi jinsi ya kuwa binadamu. Adamu na Hawa hawakujua mambo haya na nyoka alikuja kuwashawishi na wakala tunda kutoka kwa mti wa kufahamu mema na mabaya. Mwishowe walijua aibu, na wakaendelea kutojua jinsi ya kumwabudu Mungu, na wakawa wapotovu zaidi na zaidi, hadi wakati huu. Hili ni jambo la kina kabisa, na hakuna yeyote katika ubinadamu potovu anayeweza kulifahamu kabisa. Wanadamu bado wanaweza kumsaliti Mungu wakati wowote na mahali popote kwa sababu ya silika za mwili wao. Ilhali, mwishowe, Mungu atawakamilisha wanadamu na kuwaingiza katika hatua inayofuata; hili ni jambo ambalo watu huona ni vigumu kulifahamu.
Kwa nini wanadamu wanahitajika kumfahamu Mungu? Ikiwa wanadamu hawatamfahamu Mungu au hawatafahamu hali hii ya ukweli, basi watatumiwa kwa urahisi sana na kudanganywa na pepo wachafu. Mara tu wanapofahamu ukweli, basi haitakuwa rahisi kwao kudanganywa na kutumiwa na pepo wachafu. Lakini ikiwa, baada ya wewe kupata ufahamu huu, na ukaendelea kufanya jambo unalojua kwamba ni kukosea amri za usimamizi za Mungu au linafanywa kwa kuasi Mungu, basi hutaweza kukombolewa. Wewe uko katika hali gani wakati huu? Maadamu sasa mna tumaini moja, bila kujali iwapo Mungu anakumbuka mambo ya zamani au la, mnapaswa kudumisha fikira hizi: Ni lazima nitafute badiliko katika tabia yangu, nitafute kumfahamu Mungu, kutodanganywa na Shetani tena na kutofanya chochote kinacholeta aibu kwa jina la Mungu. Ni sehemu gani kuu huamua iwapo mtu sasa ana thamani yoyote, iwapo ataokolewa au la na iwapo ana tumaini yoyote au la? Nazo ni, baada ya wewe kusikia mahubiri, iwapo unaweza kupokea ukweli au la, iwapo unaweza kutekeleza ukweli huo au la na iwapo unaweza kubadilika au la. Hizi ni sehemu muhimu. Ikiwa utahisi tu majuto, ikiwa utaenda tu kufanya mambo na kuendelea kufikiria kwa njia hiyo hiyo ya zamani, na ukose kuwa na ufahamu wowote kabisa kuhusu jambo hili lakini badala yake uwe mbaya zaidi na zaidi, basi utakosa tumaini na unapaswa kutangazwa kuwa asiye na thamani. Kadiri unavyomfahamu Mungu, na kadiri unavyojifahamu, basi ndivyo utakavyoweza kujitawala mwenyewe. Kadiri unavyoweza kupenya katika asili yako mwenyewe kwa ufahamu, ndivyo utakavyoweza kujitawala mwenyewe. Baada ya wewe kujumlisha uzoefu wako, hutawahi tena kushindwa katika jambo hili. Kwa kweli kabisa, kila mtu ana madoa fulani juu yake ambayo hayajachunguzwa tu. Kila mtu anayo, wengine wana madogo, wengine wana makubwa; wengine huongea waziwazi, na wengine huficha nia zao na kufanya kazi kwa siri. Kila mtu anayo; Baadhi ya watu hufanya mambo ambayo watu wengine wanajua kuyahusu na baadhi ya watu hufanya mambo ambayo watu wengine hawajui kuyahusu. Kuna mawaa juu ya kila mtu na yote yanafichua tabia fulani za upotovu, kama vile kiburi au majivuno, au wao hufanya dhambi fulani, au makosa fulani au kupotoka katika kazi zao, au wanaonyesha kiasi kidogo cha ukaidi. Haya yote ni mambo ya kusamehewa kwani ni mambo ambayo mtu yeyote aliyepotoka hawezi kuepuka. Ilhali yanapaswa kuepukika mara tu unapofahamu ukweli. Na hakutakuwa tena na haja ya wewe kusumbuliwa mara kwa mara na mambo yaliyofanyika katika siku za zamani. Badala yake, inafaa kuhofiwa kwamba bado hutabadilika hata baada ya kupata kufahamu, eti utajua kwamba si sahihi kufanya kitu na bado uendelee kukifanya, na kwamba utaendelea kufanya kitu fulani hata baada ya kuambiwa kwamba ni kibaya. Watu hawa hawawezi kukombolewa.

Jumatano, 3 Julai 2019

Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Mwenyezi Mungu alisema, Nguzo inapopandishwa kidogo, mnaweza kupiga hatua kidogo. Si jambo baya kuwa na mahitaji ya juu kutoka kwenu na wala si jambo baya kuwauliza maswali magumu. Lengo ni kuwafanya muwe na ufahamu zaidi juu ya elimu na maarifa ya kawaida ya kipengele cha weledi cha wajibu wenu.[a] Huenda labda nyinyi bado hulalamika katika nyoyo zenu, mkisema: "Tumejifunza mambo mengi mazuri lakini Mungu huwa hayataji kamwe au kuturuhusu kuyatumia. Kwa hiyo hatuthubutu kuyataja au kuyatumia. Je, na kama yakikanushwa mara tu tunapoyatumia? Na je, tukikosolewa? "Sasa Nawaambieni kwamba mnaweza kuyatumia mambo haya kwa ujasiri. Lakini ni lazima mpitie ukaguzi wa ndugu zenu wa kiume na wa kike. Usiwe wa kujidai, na kusema: "Mungu amesema wakati huu tunaweza kutumia mambo haya kwa ujasiri, kwa hiyo tutatumia mambo haya kwa ujasiri." Kuwa na ujasiri sio kuenea pote au kuwa wenye dharau. Lazima kuwe na mipaka ya kuwa na ujasiri, ni lazima kukubaliane na kanuni, na ndugu wa kiume na wa kike wanapaswa kulifikiria kuwa linafaa. Mtu fulani akisema, "Hili halikubaliki," basi si unahitaji kulibadilisha? Je, watu wakaidi ni watu wema? (Hapana.) Haishauriwi kuwa hivyo. Ni lazima usikilize maoni ya wengine, na unapowasikia wakisema hivi, unasema, "Uko sawa. Ni lazima nilibadilishe." Baada ya kulibadilisha, watu wengine husema: "Uko karibu hapo, nahisi vyema kuhusu hili. Liko sawa, limefaulu." Safi sana! Kwa kufanya mambo kwa njia hii, kipengele kimoja ni kwamba mnaweza kuingia kwa kina katika kipengele cha weledi, na muwe wakomavu na wenye uzoefu; kipengele kingine ni kwamba nyinyi pia mna uwezo wa kujifunza mambo mengi; na bado kipengele kingine ni kwamba mmejifunza somo. Unapokabiliwa na masuala, hupaswi kujidai, ukifikiri, "Nina kauli ya mwisho. Hamna sifa ya kuzungumza. Ninaelewa kanuni, nyinyi mnaelewa nini? Hamuelewi, ninaelewa!" Huku ni kujidai. Kuwa wa kujidai ni tabia potovu ya kishetani; si kitu kilicho ndani ya ubinadamu wa kawaida. Kwa hiyo, ni nini maana ya kutokuwa wa kujidai? (Kupata mapendekezo kutoka kwa kila mtu, na kila mtu kuyapima pamoja.) Wakati kila mtu anapoliidhinisha, na kila mtu anapokubaliana nalo, basi mmefanya kazi nzuri. Mradi baadhi ya watu au kikundi cha watu hudakiza kipingamizi, basi ni lazima muwe mahsusi zaidi kuhusu kipengele cha weledi. Ni lazima msijifanye kutotambua na kusema: "Nani? Aliyedakiza nini? Ni nini kinachoendelea? Je, wewe ndiye unayelielewa hili au ni mimi? Je, unaelewa hili vyema kuniliko? Unaelewa nini? Huelewi!" Hii ni tabia mbaya, sivyo? Ijapokuwa aliyedakiza kipingamizi huenda asielewe vizuri sana na anaweza kuwa mlei, na unaweza kuwa na haki na kile ulichokifanya kinaweza kuwa sahihi, tatizo hapa ni tabia yako. Kwa hiyo ni nini maonyesho na vitendo sahihi vinavyokubaliana na kanuni na kukubaliana na ukweli? Unasema: "Tatizo ni nini? Acha niangalie. Sio mimi tu, lakini kila mtu anaangalia. Wale ambao wana mapendekezo fulani kuhusu kipengele hiki au utambuzi fulani ndani yake, au ambao wana uzoefu fulani katika kipengele hiki, hebu sote tuangalie pamoja na tuweze kuzungumza juu yake. "Ikiwa kila mtu huamini kweli kuwa kufanya kitu kwa njia hii ni vibaya, kwamba kuna shida kidogo hapa, na unatazama mara moja na huwezi kuona tatizo, unatazama mara mbili na bado huwezi kuliona, kisha unaangalia mara tatu au mara nne na unavyozidi kuangalia ndivyo unavyozidi kuona kuna shida, basi hili kwa kweli ni tatizo. Na lazima ulisahihishe, lifanye liwe zuri na uombe mawazo ya kila mtu. Je, hili ni jambo jema au jambo baya? (Ni jambo jema.) Unaomba mawazo ya kila mtu, kila mtu analizungumzia, unashirikiana pamoja na Roho Mtakatifu anakupa nuru; unafuata hilo, na tatizo linarekebishwa ipasavyo. Kila mtu huangalia na kusema, "Hilo ni sawa, na ni bora zaidi kuliko hapo awali!" Je, si huu ni mwongozo wa Mungu? Hili ni jambo kubwa! Unapofanya mambo kwa njia hii, kama wewe hujidai, unapoacha mawazo yako mwenyewe na fikira zako mwenyewe, na unapotenda ukweli, unanyenyekea na kusikiliza mawazo ya wengine, kisha ni nini hutokea? Wewe hupata fursa ya Roho Mtakatifu kufanya kazi kwako na Roho Mtakatifu hukupatia nuru. Nini hutokea wakati Roho Mtakatifu anapokupatia nuru? Umejifunza kitu kingine cha weledi. Je, si hiki ni kitu chema?
Mara unapokuwa umepitia hili, wewe hufikiri, "Ninapokabiliwa na masuala, ni lazima nisijidai. Kila mtu hunichukia ninapojidai." Wakati kila mtu anapomchukia mtu fulani, Mungu humchukia? (Ndiyo, Yeye humchukia.) Unajifunza somo, kweli? Unapotenda kwa njia hii daima, kipengele kimoja ni kwamba utaona maendeleo katika hali ya weledi ya wajibu wako, na Mungu atakupa nuru na kukubariki; kipengele kingine ni kwamba utakuwa na njia ya kufuata katika kutenda ukweli, utajua jinsi ya kutenda ukweli, hatua kwa hatua utakuja kuelewa kanuni na kupata njia, utajua jinsi ya kufanya mambo kwa namna ambayo itasababisha kupata nuru ya Mungu na uongozi, ni njia zipi za kufanya mambo ambazo humsababisha Mungu kukupuuza au kukuchukia, na jinsi ya kufanya mambo kwa njia ambayo inaweza kubarikiwa na Mungu. Watu wanapopata baraka za Mungu na nuru, kuna furaha au huzuni ndani ya mioyo yao? Kuna furaha. Unapokuja kuwajibika kwa kile ambacho umekifanya mbele ya Mungu, utapata furaha na utafikiri, "Nilikifanya vizuri." Ndani yako utajisikia mwenye amani na furaha. Hisia hii ya amani na furaha hutolewa kwako na Mungu, na ni kuchochea ulikopewa na Roho Mtakatifu. Ikiwa hutendi hili lakini daima huhimili kwa njia zako mwenyewe, ukisema, "Sitamsikiliza mtu yeyote. Hata nikisikiliza, nitaonekana tu kusikiliza na sitabadilika. Nitafanya mambo kwa njia hii, ninahisi niko sawa na nahisi nimethibitishwa kabisa, "ni nini kitakachotokea? Huenda kuwa umethibitishwa na huenda kusiwe na kosa katika kile ufanyacho, huenda hujafanya makosa yoyote na huenda ukaelewa kipengele cha weledi vyema zaidi kuliko wengine, lakini mara unapofanya aina hizi za maonyesho na kutenda kwa njia hii, wengine wataona na watasema: "Tabia ya mtu huyu si nzuri. Unapokabiliwa na masuala, huwa hawakubali lakini hupinga kitu chochote mtu mwingine yeyote anachosema, kama kiko sahihi au la. Mtu huyu huwa hakubali ukweli." Watu wanaposema wewe hukubali ukweli, Mungu atafikiri nini? Je, Mungu anaweza kuona maonyesho haya yako? Bila shaka, Mungu anaweza kuyaona. Mungu hachunguzi tu chokomeani mwa moyo wa mwanadamu, Yeye pia huangalia kila kitu usemacho na kufanya wakati wote na mahali pote. Na Anapoona mambo haya, Yeye hufanya nini? Yeye husema: "Wewe umefanywa mgumu. Uko jinsi hii katika hali ambapo wewe uko sawa, na uko jinsi hii pia katika hali ambapo umekosea. Bila kujali uko katika hali gani, kila kitu unachofichua na kuonyesha ni kupingana na upinzani. Hukubali hata kidogo mawazo au mapendekezo ya mtu yeyote mwingine. Moyo wako unapingana kabisa, kukataa na kutokubali mawazo ya wengine. Wewe ni mgumu sana!" Ni kwa njia gani unakuwa mgumu? Kuwa kwako mgumu ni kwamba maonyesho yako sio njia mbaya ya kufanya mambo au tabia mbaya, lakini kwa usahihi zaidi ni ufichuzi wa tabia yako. Je, tabia yako imefichua nini? Unauchukia ukweli na una uhasama mintarafu ya ukweli. Na wakati umefafanuliwa kama mtu ambaye ana uhasama mintarafu ya ukweli, machoni mwa Mungu uko katika shida. Si zaidi ya haya, kila mtu atasema, "Mtu huyu ana tabia mbaya, yeye ni mkaidi na mwenye kiburi. Mtu huyu ni vigumu kukubaliana naye, hana matendo ya ukweli na hapendi ukweli. Hajawahi kuukubali ukweli." Si zaidi ya haya, kila mtu atakutathmini kwa njia hii; lakini tathmini hii inaweza kuamua jaala yako? Watu hufanya tathmini yako, lakini hili haliwezi kuamua jaala yako. Lakini kuna jambo moja ambalo hupaswi kulisahau: Mungu huuchunguza moyo wa mwanadamu, na wakati huo huo Yeye huangalia kila kitu ambacho mtu husema na kufanya. Mungu akimfafanua mtu kwa kusema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," Yeye hamfafanui tu kwa kusema, "Mtu huyu ana tabia potovu kidogo na kwa kiasi kidogo si mtiifu," bali kwa usahihi zaidi Yeye anasema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," hii ni hoja kubwa au hoja ndogo? (Ni hoja kubwa.) Na hili husababisha shida? (Ndiyo.) Je, hili huleta shida gani? Shida hii haiko katika jinsi watu wengine hukuona au jinsi wanavyokutathmini, lakini liko katika jinsi Mungu anavyoona tabia yako potovu ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli. Hivyo ni vipi basi Mungu huona tabia yako ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, unajua? Mungu husema, "Ana uhasama mintarafu ya ukweli na hapendi ukweli." Je, Mungu huliona kwa jinsi gani? Ukweli hutoka wapi? Ukweli humwakilisha nani? (Humwakilisha Mungu.) Hivyo fikiria hili: Mungu anapaswa kuonaje tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, Yeye atalionaje? (Mungu huliona kuwa na uhasama kwelekea Kwake na kama adui Yake.) Na hili ni jambo zito? Mtu aliye na uhasama mintarafu ya ukweli ana uhasama mintarafu ya Mungu. Kwa nini Ninasema kuwa ana uhasama mintarafu ya Mungu? Je, huwa anamtukana Mungu? La. Huwa anampinga Mungu bayana? La. Je, huwa anamshushia Yeye hadhi kisiri? La. Hivyo kufichua tabia ya jinsi hii huwaje uhasama mintarafu ya Mungu? Je, si huu wote ni msukosuko wa bure? Kuna kitu ndani yake, sivyo? Unajua ni kitu gani? Mtu fulani ana tabia hii na hufichua aina hii ya tabia wakati wote na katika maeneo yote na, zaidi ya hayo, yeye huitegemea ili kuishi na haachi kamwe njia hii ambayo kwayo yeye huishi na kufanya mambo, na haitupi kamwe. Wewe hutegemea mambo na tabia hii ili kuishi, na wakati hakuna kitu kinachotokea, ikiwa mtu atasema kuwa una uhasama mintarafu ya Mungu, unaweza kukubaliana naye? Huwezi kukubaliana naye. Hata hivyo, matatizo yanapochipuka, unapokuwa na aina hii ya tabia, wewe huifichua wakati wote na mahali pote? Kwa hiyo hii ni tabia gani? Ni tabia ambayo ni uhasama mintarafu ya Mungu na uhasama mintarafu ya ukweli. Unayasaili maneno ya Mungu, unayachangua, unayachambua na kuyatilia shaka. Inamaanisha nini unapofanya mambo haya? Inamaanisha kwamba unaposikia maneno ya Mungu, wewe hufikiria, "Je, haya ni maneno ya Mungu? Sifikiri huu ni ukweli na sifikiri yote ni lazima yawe ni sahihi." Tabia yako imefichuliwa, ni kweli? Je, una uwezo wa kutii wakati unapofikiria jinsi hii? Hakika huna uwezo. Na kama huna uwezo wa kutii, Mungu bado ni Mungu wako? Hapana, Yeye si Mungu wako. Je, wewe basi humuona Mungu kama nini? Kama chombo cha kujifunza na cha shaka, na hata kama tu mtu wa kawaida, kama mtu mwenye tabia potovu kama tu mtu. Je, si hili linaletwa na tabia potovu ya mtu?
Wakati mtu amekwenda mbali hivyo na wakati ana uhusiano wa aina hii na Mungu, ni uhusiano gani uliopo kati ya mtu huyu na Mungu? Ni wa uhasama na yeye amekuwa mpinzani wa Mungu, sivyo? Ikiwa unamwamini Mungu lakini huwezi kuupata ukweli au kuukubali ukweli, Mungu si Mungu wako. Mungu hakuoni kama adui lakini wewe unamwona Mungu kama mpinzani wako na huwezi kukubali kwamba Yeye ni ukweli wako na njia yako, basi tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa jinsi gani? Unapokabiliwa na maswala unapaswa kwanza kufikiria, "Hali ni ipi hapa? Siielewi vizuri sana, na haiko dhahiri kwangu. "Bila kujali suala ni nini, hufafanui suala hilo kwanza, badala yake kwanza ni lazima uone kile maneno ya Mungu yanachosema juu yake. Unaweza kushindwa kupata maneno husika ya Mungu, na huenda pia usijue ni ukweli gani suala hili linahusisha, lakini unang'amua kanuni—ni kutii, kwanza kabisa. Kwanza kabisa, endelea kutii, tuliza moyo wako na usubiri, usiwe na mawazo au fikira za binafsi, subiri kwa muda na uone jinsi Mungu anavyopanga kukabiliana nalo na kile ambacho Mungu atafanya. Hili ni katika hali ambapo huelewi kabisa. Na je, wakati ambapo huelewi? Kwa mfano, mtu anatoa maoni; unashughulikiaje suala hili? Je, unalishughulikiaje kwa njia inayopatana na ukweli? Kwanza unalikubali; unasikiliza na kusema, "Haya yote ni nini? Aa, kuna shida kwangu kulifanya kwa njia hii? Ikiwa kuna shida, basi hebu tuangalie." Usiichukulie hoja hiyo kwa wepesi; inahusisha mambo katika upeo wa wajibu wako, kwa hiyo unapaswa kulitazama kwa uangalifu. Huu ndio mtazamo sahihi wa kuchukua na hali sahihi ya kuwemo. Unapokuwa katika hali sahihi, wewe hufichua tabia ambayo imechoshwa na ukweli? (Hapana.) Hufichui tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli, na unapotenda kwa njia hii tabia yako ya upotovu inabadilishwa; unatenda ukweli. Unapotenda ukweli kwa njia hii, ni matokeo gani yanayofanikishwa? (Roho Mtakatifu hutuongoza.) Mwongozo wa Roho Mtakatifu ni kipengele kimoja. Kwa Mungu, unatenda ukweli. Wakati mwingine una mwongozo wa Roho Mtakatifu na tatizo linarekebishwa; wakati mwingine baada ya kusikia juu ya suala hili, unalielewa kwa urahisi, na unaliona likiwa rahisi sana. Hicho ni kitu ambacho akili ya mwanadamu inaweza kufanikisha na unahitaji tu kukirekebisha. Hii ni hoja ndogo. Na hoja kubwa ni ipi? Unapotenda kwa njia hii, Mungu hukuona kama mtu anayetenda ukweli na kama mtu anayependa ukweli, na Yeye huona kwamba wewe si mtu anayeuchukia ukweli au ana uhasama mintarafu ya ukweli. Wakati huo huo Mungu anapoona moyo wako, Yeye pia huona tabia yako. Hii ni hoja kubwa. Yaani, unalolifanya mbele za Mungu, unaloishi kwa kudhihirisha mbele ya Mungu na unachokifichua mbele ya Mungu, na vilevile mtazamo unaouchukua, mawazo uliyo nayo na hali uliyomo katika kila kitu unachokifanya—maonyesho haya yote unayo mbele ya Mungu—haya ndiyo mambo muhimu zaidi.
Watu daima wanalalamika juu ya watu na masuala, na hili ni tatizo kubwa. Je, wao daima hufikiri nini? Wanafikiri kuwa ni watu wengine ambao ni wakatili kwao, au kwamba wengine huyafanya mambo kuwa magumu kwa makusudi, au huyapata makosa tu na watu wengine. Je, mtazamo huu ni sahihi? (Hapana, si sahihi.) Kwa nini unasema hapana? Ni kosa kabisa kulalamika daima juu ya masuala na watu. Hawafanyi jitihada na ukweli, na wao wanajaribu daima kuepuka aibu na kutafuta uthibitisho mbele ya wengine au miongoni mwa watu wengine, na wao daima hutaka kutumia njia za kibinadamu kuzitatua hoja hizi zote. Hiki ndicho kikwazo kikubwa mno kwa kuingia kwa maisha. Kwa kufanya kwa njia hii, kutenda kwa njia hii na kumwamini Mungu kwa njia hii, hutaweza kamwe kupata ukweli, kwa kuwa kamwe huji mbele ya Mungu. Huji kamwe mbele ya Mungu kukubali vitu vyote ambavyo Mungu hupanga kwa ajili yako, hutumii kamwe ukweli ili kutatua mambo haya yote, na daima wewe hutaka kutumia mbinu za kibinadamu kuyatatua. Hivyo machoni pa Mungu, umeenda mbali sana na Yeye na sio tu kwamba moyo wako umekwenda mbali sana na Mungu, lakini mawazo yako yote, nia zako zote na hali yako yote havijawahi kuwa mbele ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu huwaona wale ambao hulalamika juu ya masuala na watu. Kwa hiyo, watu wengine ambao wana kipaji cha kuzungumza na ni wepesi kung'amua, hufikiria, "Nina ufasaha, na wakati ninapokuwa na watu wengine, wote hunihusudu na kunipenda. Wao hunitukuza, na watu wengi sana huridhishwa nami. "Je, hili ni la manufaa yoyote? Sifa yako njema miongoni mwa watu wengine imeanzishwa, lakini mbele ya Mungu, Amekupuuza daima, na anasema kuwa wewe ni mtu asiyemwamini Mungu na kwamba una uhasama mintarafu ya ukweli. Miongoni mwa wengine wewe hutenda kwa njia ambayo ni laini na ya hila, unaweza kumshughulikia mtu yeyote, una uwezo mkubwa wa kushughulikia hoja, na unaweza kukubaliana na mtu yeyote. Lakini mwishowe, kwa tathmini moja kutoka kwa Mungu utakwisha, utafika mwisho mbaya, na jaala yako itapangwa. Mungu atasema: "Huyu ni mtu asiyeamini, akipeperusha bendera ya imani katika Mungu ili kupata baraka. Huyu mtu ana uhasama mintarafu ya ukweli, hajawahi kamwe kufanya jitihada na ukweli, na hajawahi kuukubali ukweli." Mnafikiria nini juu ya aina hii ya tathmini? Je, hii ndiyo tathmini mnayoitaka? (Hapana.) Bila shaka sicho kile mnachokitaka. Labda watu wengine hawajali, na wao husema, "Sijali. Hatuwezi kumwona Mungu kwa njia yoyote. Suala la kweli zaidi ambalo tunalo ni kuwa tunapaswa kukubaliana na watu walio nasi. Ikiwa hatuwezi kufanya mahusiano haya yafaulu basi tunawezaje kuishi miongoni mwa watu hawa? Maisha yetu yangekuwa magumu sana. Angalau sana tunapaswa kukubaliana na watu hawa na kushughulikia mahusiano vizuri. Chochote kingine kinaweza kusubiri." Ni watu wa aina gani hawa? Je, hawa bado ni watu ambao wanamwamini Mungu? (Hapana.) Mtu ni lazima aishi mbele ya Mungu nyakati zote na ni lazima aje mbele ya Mungu na kutafuta ukweli nyakati zote na kwa hoja zote, ili mwishowe Mungu atasema: "Wewe ni mtu anayeupenda ukweli na Mungu anafurahishwa nawe, Mungu anakukubali. Mungu huuona moyo wako na huiona tabia yako. "Unafikiria nini kuhusu tathmini hii? Hii ina maana kwamba wewe ni salama, sivyo?
Je, nyinyi kwa kawaida huzingatia hoja hizi? Hebu niwaambie, mnapomwamini Mungu, bila kujali kama unafanya wajibu wa nje, au unafanya wajibu unaohusiana na kazi yoyote au kipengele chochote cha kazi ya weledi ndani ya familia ya Mungu—bila kujali ni wajibu gani unaoufanya—ikiwa huwezi daima kuja mbele ya Mungu, ikiwa huwezi kuishi mbele ya Mungu, basi wewe si muumini na hakuna tofauti kati yako na mtu asiyeamini. Je, hili linasikika sahihi kwako? Je, mnaweza kufahamu jambo hili? Labda kuna baadhi ya watu sasa ambao hawawezi kufanya wajibu wao kwa sababu ya mazingira yasiyofaa, na wanaishi miongoni mwa wasioamini, lakini daima wanaweza kupata nuru na mwongozo wa Mungu—hivyo hali ni ipi hapa? Mnajua? (Ni kwa sababu daima wao huja mbele ya Mungu.) Ndiyo, hili huamua jinsi hali ya kiroho ya mtu ilivyo. Ikiwa, ndani yako mwenyewe, daima huwezi kumhisi Mungu, ikiwa daima u mdhaifu, daima u hasi, au wewe daima ni mwasherati, au daima hubebi mzigo katika wajibu wako na moyo wako siku zote unaboronga bila lengo lolote, basi hii ni hali nzuri au hali mbaya kuwemo? Je, ni hali ambapo unaishi mbele ya Mungu? Au ni hali ambapo huishi kamwe mbele ya Mungu? (Ni hali ambapo hatuishi mbele ya Mungu.) Basi fikirieni hili kwa makini—katika hali nyingi, huwa mnaishi mbele ya Mungu au hamuishi mbele ya Mungu? Je, mnafahamu vyema juu ya hili ndani ya mioyo yenu? Je, nyinyi huishi mbele ya Mungu wakati mwingi, au ni kwa nyakati chache tu? (Ni kwa nyakati chache tu.) Hili ni sumbufu kwenu. Kama mtu ni mchezaji, mwimbaji, mwandishi au mtengenezaji filamu, ikiwa moyo wake haujishughulishi kamwe na kufanya wajibu wowote unaofaa, ikiwa yeye ni mpotovu na hastahimiliki, ikiwa huwa daima anavurugika anapokabiliwa na masuala, hana wazo lolote ni hoja ipi inayohusisha kipengele kipi cha ukweli, wala hana wazo lolote kama kile anachokifanya kina athari yoyote, ikiwa hajui mambo gani anayoyafanya kila siku yanayomchukiza Mungu, ni mambo gani ambayo Mungu anaweza kuyakubali au ni mambo gani Mungu huyachukia, na wao huendelea tu siku baada ya siku katika kiwewe, basi ni hali aina gani hii ya kuwemo? Je, wale wanaoishi katika hali hii wana moyo wa kumuogopa Mungu ndani yao? Je, wana uwezo wa kutenda na kanuni? Je, wana uwezo wa kufanya chochote cha maana? (Hapana.) Wanapofanya wajibu wao, wanaweza kusema, "Ni lazima nivumilie vikwazo fulani, ni lazima nifanye kazi kwa bidii, kwa moyo wangu wote na kwa nguvu zangu zote, na kuwa mwaminifu"? Je, ana uwezo wa kuwa na uaminifu wowote? (Hapana.) Basi mnafanya nini hapa kwa kweli mnapofanya wajibu wenu? (Mkitumia nguvu.) Mko sawa; Mnatumia nguvu. Nyinyi ni wenye uwezo wa kazi, sivyo? Chakula chenu na nyumba zenu zote zimeshughulikwa, na halafu nyinyi hufanya kazi hapa. Ingawa hamchumi fedha hapa, mnahisi ni sawa mnapopata chakula, kinywaji na mahali pa kuishi. Lakini nyinyi huchuma ukweli? (Hapana.) Basi nyinyi hupoteza sana. Nyinyi ni wapumbavu mno! Mmemwamini Mungu kwa miaka mingi sasa, hazijakuwa siku chache tu. Mmesikia ukweli mwingi sana na hamjui mnamwamini Mungu kwa minajili gani, mnachohitaji kufanya, mnachopaswa kupata, au ni kitu gani cha muhimu zaidi kupata. Mnajua kidogo sasa? (Ndiyo.) Mnajua nini? Niambieni. (Kwa kumwamini Mungu, kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi.) Kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi? Kweli au uongo? (Kweli.) Bila shaka ni kweli. Lakini labda huenda msiwe na maarifa halisi ndani ya mioyo yenu hivi sasa, na huenda hamjalitambua kwa kiwango hiki.
Je, mmekisoma Kitabu cha Ayubu? (Ndiyo.) Na mlipokisoma Kitabu cha Ayubu, mioyo yenu ilisisimka? (Ndiyo.) Hivyo mlipata fikira za shauku, na kutaka kuwa mtu kama Ayubu? (Ndiyo.) Ni kwa muda gani mliweza kuendeleza hali hiyo na hisia hiyo? Nusu siku, siku mbili, juma moja? Au kwa mwezi mmoja au miwili, au mwaka mmoja au miwili? (Labda siku mbili hadi tatu.) Hisia hiyo iliondoka baada ya siku tatu? Wakati hisia hiyo inapoondoka, wewe huendelea kusoma, na unapoendelea kusoma unaweza kuiendeleza kwa siku zingine tatu. Lakini hivyo sivyo ilivyo, au ndivyo? Unaposoma kitabu hicho na unahisi msisimko, unapaswa kuomba, kindani fanya uamuzi wako kuwa unataka kuwa kama Ayubu, mtu ambaye anaweza kumjua Mungu, ambaye anaweza kupata ukweli, na anayeweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unasali kwa Mungu afanye vivyo hivyo kwako, na kwamba Mungu akuongoze na kukupangia mazingira, kukutolea nguvu, kukukinga katika mazingira yoyote ambayo unaweza kukabiliana nayo ili uweze kusimama imara, ili usimuasi Mungu, na unaweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Unahitaji daima kumsihi Mungu kwa lengo hili na kwa kile unachokitamani sana na unachotaka kukipata moyoni mwako, unahitaji kusihi na kuomba kwa ajili yalo, na wakati Mungu anapouona moyo wako wa kweli Yeye atalifanya. Huhitaji kuogopa Mungu akifanya jambo hili, kwa maana Mungu hawezi kuufanya mwili wako kufunikwa na vidonda kama wakati Alipomjaribu Ayubu na kukunyang'anya kila kitu ulicho nacho; Mungu hatakufanyia hivyo. Hatua kwa hatua Atafanya kazi Yake kwako kwa mujibu wa kimo chako. Ni lazima usihi kwa uaminifu; usilisome tu leo, ujihisi kusisimka na kumsihi Mungu, na kisha baada ya siku mbili usifanye chochote, na yawe yameisha mara unapogeuka. Watu husema, "Ayubu ni nani?" "Nani? Ayubu? Ayubu ni nani? Je, nawezaje kutojua? Huenda nimesikia kumhusu." Hili ni sumbufu! Usilisome kwa siku tatu na lote limesahaulika, limetoka moyoni mwako. Ukiwahusudu watu kama Ayubu na ungependa kuwa mtu kama huyo, moyoni mwako unapaswa kuwa na njia ya jinsi ya kuwa mtu kama huyo, lazima uweke moyo wako mbele ya Mungu, kisha ni lazima uombe kuihusu, omba kuihusu mara nyingi, chukua hoja hii kutoka moyoni mwako na kuitafakari mara nyingi, soma vitabu, soma makala kuhusu Ayubu na maneno ya Mungu yanayohusiana na Ayubu, itafakari daima na tena na tena, fanya ushirika pamoja na watu ambao wana aina hii ya maarifa, uzoefu au azimio , na lazima ufanye kazi kwa bidii mintarafu ya lengo hilo. Unapaswa vipi kufanya kazi kwa bidii? Kusoma tu kwa kweli sio kufanya kazi kwa bidii. Unahitaji kufanya jitihada na hoja hii, utoe maombi yako na kuiweka katika matendo, huku wakati huo huo ukiwa na azimio la kuvumilia mateso na kuwa na moyo wa shauku na hamu. Kisha unarairai, utoe maombi yako na kumwomba Mungu afanye hivi. Ikiwa Mungu haifanyi, itakuwa bure bila kujali ni jitihada kiasi gani unayoiweka, na jitihada zako ni za bure. Mungu huifanyaje? Yeye huanza kwa kuweka na kupanga mambo kwa ajili yako kulingana na kimo chako. Kwa mfano, unakaribia kuchukua mtihani wa kuingia chuo cha elimu, na unasema, "Ninataka alama ili kuingia katika Chuo Kikuu cha Tsinghua." Unaanza kuweka jitihada ili kufanikisha hili, unapitia upya masomo yako, unatafuta vifaa vya kujifunza juu ya chochote na kila kitu na unatafuta walimu kukufundisha. Kisha unawaambia wazazi wako na wanasema, "Mtoto wetu ana azimio zuri. Yeye huanza jambo kwa dhati, ana azimio na hajakosa ustadi." Kwa hiyo, wazazi wako watafanya nini? Wote wawili wataandaa ada yako ya masomo na kukupatia mwalimu. Watafanya mipango sahihi ya maisha yako, wakati unapopaswa kupumzika, na masomo yako, wakupeleke shuleni na kukuchukua baadaye, na watalifanya ili kwamba, wakati huu, usipate uchovu, au njaa, au kukosa chakula cha kutosha. Watakusaidia kwa kushughulikia na kusimamia mambo katika ulimwengu wa nje ili usichanganyikiwe. Watakufanyia mipango sahihi katika vipengele vyote. Kwa njia hii, utakuwa na wakati wa kutosha wa kupitia upya, kusoma na kufanikisha ndoto yako. Kuhusu kumwamini Mungu, chochote unacholenga au uamuzi wowote ulio nao, unapaswa kuzungumza na Mungu. Unahitaji kuomba juu ya hoja hii na kusihi sana juu yalo; itachukua muda mrefu! Itakuwa bure kuwa na moyo usio mwaminifu. Ikiwa unasali mara kadhaa tu mara kwa mara na kisha unapoona kwamba Mungu hajakufanyia chochote, unasema, "Lisahau. Sijali. Liwe liwalo, nitaacha tu mambo yatokee kama kawaida yake, na nitachukua mambo kama yanavyokuja," basi hili litakuwa bure, na moyo wako si mwaminifu. Je, Mungu atakufanyia chochote ikiwa una dakika kadhaa tu za shauku? Je, Mungu atapanga mazingira kwa ajili yako? Je, hilo linakubalika? Kwa kweli Mungu hafanyi kazi kwa njia hiyo. Mungu anataka kuona uaminifu wako na Anataka kuona ni kwa muda gani uaminifu wako na bidii ya moyo wako vinaweza kudumishwa, na kama moyo wako ni kweli au uongo. Mungu atangoja; Yeye husikiliza sala zako na kile unachorairai, na Yeye husikia maazimio yako na shauku zako, lakini Yeye bado hajaona maazimio yako ya kuvumilia mateso, kwa hivyo Yeye hatakufanyia chochote. Ikiwa wewe husema maneno machache na kisha kwenda, Mungu atakufanyia chochote? Hakika hapana. Lazima uendelee kurairai, endelea kuomba, jitahidi na kulitafakari, kisha uonje mazingira ambayo Mungu hukupangia—yatakujia kidogo kidogo, na Mungu ataanza kutenda. Bila moyo wa kweli, ni bure. Wewe husema, "kwa kweli mimi humhusudu Ayubu na kwa kweli mimi humhusudu Petro." Ni haja gani kuwahusudu? Huwezi kuwa wao bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, na bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, Mungu hatakufanyia kazi sawa na ile Aliwafanyia. Kwa nini hivyo? Kwa sababu wewe si aina moja ya mtu kama walivyokuwa. Humiliki azimio lao, au ubinadamu wao, na humiliki moyo wao wa shauku uliotafuta ukweli. Wakati utakapokuja utakapomiliki vitu hivi, ni hapo tu ndipo Mungu atakapokufanyia zaidi. Unaelewa?
Je, wengi wenu sasa wana azimio la kuelewa ukweli, kupata ukweli na kukamilishwa mwishowe? (Ndiyo.) Azimio lako ni kubwa kiasi gani? Je, unaweza kufanya liendelee kwa muda gani? Unajua? (Nina azimio hili wakati niko katika hali nzuri. Wakati mambo yanapotokea ambayo hayakubaliani na mwili wangu au kupatana na dhana zangu, na ninapopatwa na usafishaji au matatizo ndani yangu, basi imani yangu hupotea, mimi hukwama kwa namna ya hali hasi, na azimio nililokuwa nalo mwanzo hupungua hatua kwa hatua.) Hili halitaweza. Huku ni kuwa dhaifu sana. Lazima ufikie hatua ambapo azimio lako halibadiliki bila kujali ni mazingira gani unayoyakabili; huku tu ndiko kuwa mwaminifu, na huo ndio upendo halisi wa ukweli na shauku halisi ya kuwa aina hii ya mtu. Itakuwa bure kujikunyata wakati hoja fulani ndogo au shida inapotokea, au kuwa hasi, kusononeka na kuacha azimio lako mwenyewe wakati unapokabiliwa na shida ndogo. Unahitaji kuwa na nguvu ya mtu anayechagua kuhatarisha maisha yake, na kusema, "Bila kujali kinachotokea, hata kama ni lazima nife sitaacha azimio langu au kuachana na lengo hili." Halafu hakutakuwa na shida ambayo inaweza kukuzuia, na Mungu atakufanyia jambo hili. Aidha, lazima uwe na mtazamo wa aina hii na ufahamu jambo linapotokea, na kusema, "Bila kujali kinachofanyika, yote ni sehemu ya kufanikisha lengo langu, na ni shughuli ya Mungu. Kuna udhaifu ndani yangu, lakini mimi si hasi. Ninamshukuru Mungu kwa upendo Anaonipa na kwa kunipangia aina hii ya mazingira. Ni lazima nisisalimu amri. Kusalimu amri kwangu kungekuwa sawa na kufanya masikilizano na Shetani, na ni sawa na kujiangamiza. Kusalimu amri juu ya shauku na azimio langu kutakuwa sawa na kumsaliti Mungu. "Hii ni aina ya moyo ambao ni lazima uwe nao. Suala lolote dogo unalokabiliana nalo ni pumziko dogo katika mfanyiko tendani wa kufanya maendeleo katika maisha, na ni sharti usiruhusu lizuie kwendelea kwako au kuzuia mwelekeo wako wa mbele. Ni vyema kwako kuchukua pumziko dogo au upumzike kwa muda, lakini mwelekeo wako haupaswi kubadilika, na ni lazima usikome kabisa kwa hali yoyote; hii ndiyo aina ya azimio na uamuzi unayopaswa kuwa nayo. Bila kujali wengine wanavyosema au jinsi walivyo, na bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, azimio lako halipaswi kubadilika. Mungu asema, "Sikutaki tena," nawe unasema, "Mungu hanitaki tena, kwa hivyo nitasahau tu kulihusu." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Au Mungu asema, "Wewe umepotoka sana, na Ninakuchukia," nawe unasema, "Mungu ananichukia, nitaishi kwa sababu gani tena? Nitatafuta kamba ili kujinyonga." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Hutafanikisha lengo lako jinsi hii. Kwa mintarafu ya hadhi yenu ya sasa, hakuna hata mmoja wenu ambaye ameweza kujaribiwa na Mungu bado, na kusema, "Mungu, tafadhali nijaribu." Huna hadhi hii. Je, mna uwezo wa kufanya nini tu? Ni lazima muombe: "Ee Mungu, tafadhali niongoze, nipe nuru, nipe bidii ya kuendelea na unipe bidii ili niweze kuitembea njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa mujibu wa shauku zangu. Bila kujali namna gani ya mateso ninayoyapitia, Wewe hunipa nguvu na Wewe hunilinda. Ingawa ninaweza kuwa dhaifu na ingawa kimo changu ni kichanga, ninakuomba Unipe nguvu, kunilinda na kunionyesha wema. Sitasalimu amri." Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba, na ni lazima daima mje mbele ya Mungu kuomba. Wakati wengine wanacheka na kufanya mzaha na kujiendekeza, ombea hili; wakati wengine wanapojifurahisha, ombea hili; wakati wengine ni hasi, ombea hili; wakati wengine wanalala fofofo, au kuchelewa kuamka, wewe tayari unaliombea hili; wakati wengine wanatembea njia ya ulimwengu na kwa ulafi kufurahia anasa za kimwili, au kufuata mienendo ya kidunia, ombea hili. Wakati unapoweza kuishi mbele ya Mungu katika mambo yote na unaweza kujiweka katika mipaka fulani, wakati unapoweza kujiweka ukiishi mbele ya Mungu na kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi Mungu anaweza kuliona hili. Wakati Mungu anapouona moyo wa mtu, Yeye hayatumii tu macho Yake; Yeye hupanga mazingira kwa ajili yako na Yeye hugusa moyo wako kwa mikono Yake. Kwa nini Nasema hili? Wakati Mungu anapokupangia mazingira, Yeye hutazama kuona kama moyo wako unachafuliwa nayo, unayachukia, unayapenda au ni mtiifu, au kama husubiri kwa utulivu, au hutafuta ukweli—Yeye huona jinsi moyo wako unavyobadilika na ni katika mwelekeo gani huenda. Mabadiliko katika moyo wako, kila badiliko la fikira na mawazo ndani ya moyo wako kuhusu watu, hoja, na mambo ambayo Mungu hupanga kwa ajili yenu, na kila badiliko ya hali ya moyo uliyo nayo—Mungu anaweza kuyahisi yote. Ingawa huenda hujamwambia yeyote na huenda hujaomba, badala yake kufikiria tu mawazo haya kwa moyo wako mwenyewe au katika ulimwengu wako mwenyewe, lakini kwa Mungu ni wazi kabisa na Yeye huliona wazi kwa tazamo moja. Watu hutumia macho yao kukuona, na Mungu hutumia moyo Wake kuugusa moyo wako—Yeye yu karibu hivi nawe. Na kama unaweza kuuhisi uchunguzi wa Mungu, basi unaishi mbele ya Mungu. Kama huwezi kuuhisi kabisa na unaishi ndani ya ulimwengu wako, basi uko katika shida. Wewe huishi mbele ya Mungu, wewe uko mbali na Mungu na mbali sana kutoka Kwake, huendi karibu Yake kwa moyo wako au moyo wako uukaribie moyo Wake, na hukubali uchunguzi wa Mungu. Na Mungu anajua hili! Mungu anaweza kabisa kuhisi yote haya. Kwa hivyo, wakati una azimio na lengo la kukamilishwa na Mungu, kuwa mtu anayetekeleza mapenzi ya Mungu, mtu anayemcha Mungu na aepukanaye na maovu, unapoweza kuomba mara nyingi juu ya hoja hii na kusihi kwa ajili yalo, unapoweza kuishi mbele ya Mungu, kutokwenda mbali na Mungu au kumwacha Mungu, basi wewe unalielewa hili, na Mungu anajua kuhusu hilo pia. Watu wengine wanasema: "Mimi ni dhahiri kulihusu, lakini sijui kama Mungu anajua kulihusu." Hili si jambo la busara. Kwa hiyo hali ni gani hapa? Kama wewe mwenyewe u dhahiri kulihusu, na hujui kama Mungu anajua kulihusu, basi huna uhusiano na Mungu. Umeelewa? Kwa nini Nasema wewe huna uhusiano na Mungu? Wewe huishi mbele ya Mungu, kwa hivyo unashindwa kuhisi kama Mungu yu pamoja nawe, kama Mungu anakuongoza au kukulinda, na kama Mungu anakushutumu wakati unapofanya jambo baya. Huwezi kuhisi jambo lolote kati ya haya, kwa hiyo hili linamaanisha kwamba huishi mbele ya Mungu. Wewe hufikiria tu mwenyewe na kuleweshwa na mawazo yako mwenyewe; huko ni kuishi katika ulimwengu wako mwenyewe na sio kuishi mbele ya Mungu, na hakuna uhusiano kati yako na Mungu.
Mtu anawezaje kuudumisha uhusiano wake na Mungu? Ni kwa njia gani anaweza kuudumisha? Kwa njia ya kusihi, kuomba na kuwa na ushirikiano na Mungu katika moyo wake. Aina hii ya uhusiano itakuwezesha kuishi daima mbele ya Mungu, na kwa hiyo utakuwa mtu mwenye amani sana. Watu wengine daima hufanya mambo ya nje na hujihusisha na mashauri ya nje. Baada ya siku moja au mbili bila kushiriki katika maisha ya kiroho, moyo wao hauna utambuzi, na baada ya siku tatu, au siku tano, bado hauna utambuzi, au bado hauna utambuzi baada ya mwezi mmoja au miwili. Hili lina maana kwamba hawaombi au kurairai chochote, na hawajishughulishi na ushirikiano wa kiroho. Kusihi ni wakati unapokabiliwa na masuala, unamwomba Mungu akusaidie, akuongoze, akukimu, akupe nuru, akuruhusu ujue mapenzi ya Mungu na kujua ukweli ni nini. Kuomba kuna mawanda mapana kiasi. Wakati mwingine ni kusema maneno ndani ya moyo wako, kuzungumza na Mungu wakati unapokabiliwa na shida na kusema maneno yaliyo moyoni mwako kwa Mungu wakati unapokuwa hasi na dhaifu. Unaweza pia kumwomba Mungu unapokuwa mwasi, au unasema na Mungu juu ya masuala yanayokukabili kila siku, yote kuhusu yale ambayo unaweza kuyabaini na yale ambayo huwezi kuyabaini. Huku ni kuomba. Mawanda ya kuomba kimsingi ni kuwa na mazungumzo na Mungu, wakati mwingine kwa nyakati zilizopangwa na wakati mwingine kwa nyakati zisizoratibiwa, na yanaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Ushirikiano wa kiroho kwa kweli haushikilii muundo fulani. Labda kuna suala, labda hakuna; wakati mwingine kutakuwa na kitu cha kusema, na wakati mwingine hakutakuwa. Huu ni ushirikiano wa kiroho. Wakati kuna suala maalum la kuzungumzia na Mungu, basi unaweza kuomba. Wakati hakuna suala lolote, unafikiri tu juu ya Mungu, "Mungu humpendaje mwanadamu? Mungu anamtunzaje mwanadamu? Mungu humshutumuje mwanadamu?" "Ee Mungu, ninahisi nimefanya jambo hili vibaya. Kama kwa kweli nimefanya jambo hili vibaya, basi nishutumu na unifanye nifahamu." Huu ni ushirika wa kiroho, na unaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Wakati mwingine uko barabarani na unafikiria kuhusu kitu ambacho huufanya moyo wako uhisi huzuni kweli. Huna haja ya kupiga magoti au kuyafunga macho yako, lakini badala yake unasema mara moja kwa Mungu moyoni mwako: "Ee Mungu, naomba Uniongoze na suala hili. Mimi ni dhaifu na siwezi kulishinda. "Moyo wako umesisimuliwa, na kwa maneno haya machache rahisi Mungu anajua yote kulihusu. Wakati mwingine unafikiria kuhusu familia yako, na unaweza kusema: "Ee Mungu, kwa kweli nimeikosa familia yangu …." Humkosi mtu yeyote hasa, unahisi tu vibaya, hivyo unaongea na Mungu. Usizungumze na watu wengine kulihusu, kwa kuwa hilo halina maana. Unapozungumza na mtu mwingine kulihusu, huenda ikawa kwamba anaikosa familia yake hata zaidi ya wewe, basi hili linakuathiri na unaishia kuikosa yako hata zaidi, na hili halikuletei faida yoyote kamwe. Unapozungumza na Mungu kulihusu, basi Mungu atakufariji, Akufurahishe tena na kukupisha katika wakati huu mgumu na kupita hali hii ndogo. Hali hii, jiwe hili dogo njiani mwako halitakukwaa, halitakuzuia au kuathiri utekelezaji wa wajibu wako. Wakati mwingine, unapozungumza au kufanya ushirika na wengine, moyo wako unaweza ghafla kuwa na hisia ya kuvunjika kidogo au kujisikia mwenye wasiwasi sana, hivyo unafanya haraka kumwomba Mungu, na unaweza kufanya hivi wakati wowote na katika mahali popote. Kunaweza kuwa hakuna chochote unachokisihi, au chochote unachotaka Mungu akufanyie au akunurishie, unaongea tu na Mungu na kuzungumza Naye wakati wowote na katika mahali popote. Ni hisia gani unayopaswa uwe nayo wakati wote? Ni hii: Mungu huwa hatoki kandoni mwangu kamwe, Yeye yu pamoja nami kandoni mwangu wakati wote, Yeye hajawahi kuniacha, na ninaweza kuhisi hili. Bila kujali ni mahali gani nipo, bila kujali ninafanya nini, kama ninapumzika au kulala, kula chakula, au kwa mkutano, au kama sisemi chochote mchana kutwa ninapotekeleza wajibu wangu, najua moyoni mwangu kwamba Mungu ananiongoza kwa mkono, na kwamba Yeye hajawahi kuniacha. Wakati mwingine, wewe hufikiria jinsi umefaulu kwa miaka hii michache iliyopita, mwezi baada ya mwezi, na unahisi moyoni mwako kwamba kimo chako kimekomaa na kwamba ni Mungu anayekuongoza, na kwamba ni upendo wa Mungu ambao unakulinda daima. Unapofikiri hivi, unaomba moyoni mwako: "Nakushukuru Wewe, Mungu!" Na wewe unatoa shukrani zako, na kusema: "Mimi ni dhaifu sana, mwenye woga sana, na mpotovu kwa kina sana. Kama Hukuniongoza kwa njia hii, mimi mwenyewe singeweza kufanikiwa hadi leo. Asante Mungu!" Je, si huu ni ushirika wa kiroho? Kama ungekuwa jinsi hii, basi si ungekuwa na mengi ya kumwambia Mungu? Hungeishi siku baada ya siku bila kuwa na kitu cha kumwambia Mungu. Ikiwa huna chochote cha kumwambia Mungu, basi inamaanisha kwamba Mungu hayuko ndani ya moyo wako. Kama una Mungu ndani ya moyo wako, basi unaweza kumwambia Mungu mambo unayoweza kusema kwa wandani wako—Mungu ni msiri wako wa karibu zaidi. Unapomruhusu Mungu kuwa msiri wako wa karibu zaidi, rafiki yako wa karibu zaidi, familia unayoweza kuitegemea zaidi, kuiegemea zaidi, na Aliye mwaminifu zaidi, Aliye mwandani sana na wa karibu, basi itakuwa vigumu kutokuwa na mambo ya kusema Kwake. Wakati daima una mambo ya kumwambia Mungu, si basi utaweza kuishi daima mbele ya Mungu? Unapoweza kuishi mbele ya Mungu daima, basi wakati wote utaweza kutambua jinsi Mungu anavyokuongoza, jinsi Mungu anavyokulinda, jinsi Anavyokutunza, jinsi Anavyokuwa amani yako na furaha, Anavyokupa baraka na nuru, jinsi Mungu anavyokushutumu, kukufundisha nidhamu, kukuadhibu, kukuhukumu na kukuadibu. Wakati unapoishi mbele ya Mungu daima, moyo wako utajua kwa dhahiri sana kile Mungu anachofanya ndani yako. Hutakuwa na siku ambapo utakuwa mpumbavu kabisa na kutojua chochote, ukisema tu maneno "Ninamwamini Mungu, mimi hutekeleza wajibu wangu, mimi huhudhuria mikutano, mimi husoma kila siku na huomba kila siku." Huwezi tu kupitia mifanyiko tendani hii yote au kuwa tu na aina hii ya tabia ya nje.
Mnapaswa kujua sasa, kwa hiyo ni nini kitu muhimu zaidi katika kumwamini Mungu? Unapomwamini Mungu, kama Mungu hayuko ndani ya moyo wako na Yeye hakuhusu, na kama humwoni Mungu kama mwandani wako sana, wako wa karibu sana, familia na msiri mwaminifu sana na wa kutegemewa sana, basi Mungu si Mungu wako. Sawa, kwa hiyo sasa nendeni na mtende kwa muda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema, na muone kama hali yenu ya ndani itabadilika au la. Tenda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema na hakika utaishi mbele ya Mungu, utaishi katika tabia ya kawaida na kuwa katika hali ya kawaida. Wakati hali ya mtu ni ya kawaida, ni hapo tu ambapo mambo anayoyaonyesha na kuyafichua kwa kila hatua, au miongoni mwa watu tofauti, masuala, na mambo, au katika mazingira tofauti, yatakuwa ya kawaida. Ni kwa njia hii tu ambapo maisha yake yanaweza kukomaa na anaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli kidogo kidogo. Unaelewa? (Ndiyo.)