Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sifa-na-Ibada. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sifa-na-Ibada. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 16 Aprili 2019

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake. Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu. Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya. Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake. Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana. Tunatafakari, kufikiri maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatuangazia. Tunaondolewa vizuizi na ubaguzi wetu, tunaishi ndani ya upendo wa Mungu. Tunaelewa ukweli na kuwekwa huru, mioyo yetu ni tamu kama asali. Tunapendana, hakuna umbali kati yetu. Tunaelewa moyo wa Mungu, sisi si hasi tena. Tukiishi ndani ya maneno ya Mungu, tunaona uzuri Wake. Tumechukua njia ya nuru maishani, haya yote ni mwongozo wa Mungu. Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu, tunacheza na kucheza. Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme, mioyo yetu kweli ni ya furaha. Ni Mungu aliyetuokoa, tumekuwa watu wa Mungu. Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni furaha isiyo na kifani. Maneno ya Mungu ni yenye thamani sana, yote ni ukweli kabisa. Tunapokubali hukumu ya maneno ya Mungu, upotovu wetu unafunuliwa kabisa. Kwa tabia fidhuli, tunakosa mantiki kweli. Maneno ya Mungu hutupogoa na kutushughulikia, tumekuja kujijua wenyewe. Tunajitafakaria, kujielewa, na kuwa na toba ya kweli. Kupitia hukumu na kuadibu, upotovu wetu unatakaswa. Tunatupa tabia zetu potovu, tunakuwa wanadamu wapya. Tunaweza kutekeleza wajibu wetu vizuri kulipa upendo wa Mungu. Kila mmoja wetu anafanya sehemu yake, tunajitolea kwa Mungu. Tunasimama imara katika ushuhuda kutimiza mapenzi ya Mungu. Kila mmoja anatoa mwanga wake mwenyewe, mwali wake mwenyewe, kumtangaza na kumshuhudia Mungu. Upendo safi na aminifu kwa Mungu ni wenye furaha na mtamu. Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu, tunacheza na kucheza. Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme, mioyo yetu kweli ni ya furaha. Ni Mungu aliyetuokoa, tumekuwa watu wa Mungu. Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni furaha isiyo na kifani. Sisi huunga mioyo na mikono kushuhudia kwa Mungu. Tunaeneza injili ya ufalme, tusiogope kamwe ugumu au uchovu. Katika mateso na majaribu, tunamwomba na kumtegemea Mungu. Njia ni yenye mabonde na milima, lakini Mungu hufungua njia. Tunapoelewa ukweli wa maneno ya Mungu, mioyo yetu hupata nguvu. Maneno ya Mungu yanatuhimiza, tunazidi kwenda mbele milele. Sako kwa bako, mkono kwa mkono tunamshuhudia Mungu, tunajitoa Kwake mwili na akili. Haijalishi ukubwa wa mateso yetu, tuko tayari sana. Kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, tunamshinda Shetani. Tunampenda Mungu kweli, hatutajua kamwe. Tumeliacha kabisa joka kuu jekundu, sisi ni askari washindi. Tunashuhudia katika njia yetu ya upendo kwa Mungu, hatutarudi nyuma kamwe. Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu, tunacheza na kucheza. Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme, mioyo yetu kweli ni ya furaha. Ni Mungu aliyetuokoa, tumekuwa watu wa Mungu. Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni furaha isiyo na kifani. Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu, tunacheza na kucheza. Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme, mioyo yetu kweli ni ya furaha. Ni Mungu aliyetuokoa, tumekuwa watu wa Mungu. Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni furaha isiyo na kifani.
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Alhamisi, 24 Januari 2019

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)

Kote katika ulimwengu mkubwa mno, sayari zote ya mbingu husogea kwa usahihi katika mizunguko yazo zenyewe. Chini ya mbingu, milima, mito, na maziwa vyote vina mipaka yavyo, na viumbe vyote huishi na kuzaana wakati wa misimu yote minne kulingana na sheria za maisha…. Hili lote limepangwa vizuri sana—je, kuna Mwenye Uwezo Mmoja anayepanga na kutawala yote haya? Tangu tuje katika ulimwengu huu tukilia tumeanza kutekeleza majukumu tofauti katika maisha. Sisi husogea kutoka kuzaliwa mpaka uzee mpaka kuugua hadi kifo, sisi husogea kati ya furaha na huzuni…. Wanadamu kwa kweli hutoka wapi, na kwa kweli tutaenda wapi? Ni nani huitawala jaala yetu? Kutoka nyakati za kale hadi siku za kisasa, mataifa makubwa yameibuka, nasaba za wafalme zimekuja na kwenda, na nchi na watu wamesitawi na kuangamia katika mikondo ya historia…. Kama tu sheria za asili, sheria za maendeleo ya wanadamu zina mafumbo yasiyo na kikomo. Ungependa kujua majibu kuyahusu? Filamu iitwayo Yule Ambaye Hushikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu itakuongoza kufikia kiini cha jambo hili, ili kufichua mafumbo yote haya!
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video

Jumatatu, 26 Novemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia Yote Pamoja na Wewe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo za Sifa

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia Yote Pamoja na Wewe

I
Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini. Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza. Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako, nina amani kabisa. Unanibariki, Unatoa maneno Yako ya hukumu. Bado sijui jinsi ninavyokosa kuithamini neema Yako. Kila mara nikiasi, kwa namna fulani nikiuumiza moyo Wako. Na bado Hunitendei kulingana na dhambi zangu lakini Unafanya kazi kwa ajili ya wokovu wangu. Ninapokuwa mbali, Unaniita nirudi kutoka hatarini. Ninapoasi, Unauficha uso Wako, giza likinifunika. Ninaporudi Kwako, Unaonyesha neema, Unatabasamu ili kukumbatia. Shetani anaponipiga, Unatibu vidonda vyangu, Unaupa joto moyo wangu. Shetani anaponiumiza, Uko nami kuanzia mwanzo hadi mwisho wa majaribu. Alfajiri itafika karibuni, na anga itang’aa samawati kama awali, wakati Uko nami. Alfajiri itafika karibuni, anga itang’aa samawati kama awali, wakati Uko nami.
II
Wewe ni uhai wangu, Wewe ni Bwana wangu. Mwenzi wa kila siku, kivuli cha karibu kando yangu. Ukinifunza jinsi ya kuwa binadamu na kunipa ukweli na uhai. Pamoja na Wewe maisha yangu yanasonga mbele kwa utukufu. Bila chaguo langu, natii amri Yako. Kuwa kiumbe wa kweli, narudi upande Wako. Kuishi katika uwepo Wako, nazungumza na Wewe na kusikia sauti Yako. Hutangoja tena katika umbali mpweke. Pamoja na Wewe, hakuna kuogopa dhoruba. Usiku unaponifunika, siko pekee yangu tena. Pamoja na Wewe kando yangu, hatari au matatizo, naweza kuvikabili. Pamoja na Wewe, safari hazitakuwa ngumu sana. Njia zenye mabonde zinapita katika matatizo, zinafungua njia kwenda kwa chemichemi ya kupendeza. Alfajiri itafika karibuni, anga itang’aa samawati kama awali, wakati Uko nami. Pamoja na Wewe, hakuna kuogopa dhoruba tena. Usiku unaponifunika, siko pekee yangu tena. Pamoja na Wewe kando yangu, hatari na matatizo, naweza kuvikumba. Pamoja na Wewe, safari haziwezi kuwa ngumu sana. Njia zenye mabonde zinapita katika matatizo, zinafungua njia kwenda kwa chemichemi ya kupendeza. Alfajiri itafika karibuni, anga itang’aa samawati kama awali. Niko pamoja na Wewe.
kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Uimbe Nyimbo Mpya

Soma Zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatatu, 16 Julai 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Watu! Furahini!

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, utukufu kwa Mungu,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Watu! Furahini!

Mwenyezi Mungu alisema, Katika nuru Yangu, watu wanaona nuru tena. Katika neno Langu, watu wanapata vitu vya raha. Nimekuja kutoka Mashariki nami Natoka huko. Wakati ambapo utukufu Wangu unang'aa, mataifa yote yanaangaziwa, vitu vyote vinaletwa katika nuru, hakuna kitu kinachobaki katika giza. Katika ufalme, maisha ya watu wa Mungu pamoja na Mungu ni ya furaha isiyolinganishwa. Maji yanacheza kwa ajili ya maisha ya watu yaliyobarikiwa, milima inafurahia utele Wangu pamoja na watu. Wanadamu wote wanajitahidi, wakifanya kazi kwa bidii, wakionyesha uaminifu wao katika ufalme Wangu. Katika ufalme, hakuna uasi tena, hakuna upinzani tena; mbingu na dunia vinategemeana, Mimi na mwanadamu tuko karibu nasi tunahisi kwa kina, kupitia furaha kuu za maisha, tukiegemeana.... Wakati huu, Naanza rasmi maisha ya mbinguni. Kuingilia kwa Shetani hakuko tena, na watu wanaingia katika pumziko. Kotekote katika ulimwengu, wateule Wangu wanaishi katika utukufu Wangu, wamebarikiwa kwa kiwango kisichonganishika, si kama watu wanaoishi kati ya watu, bali kama watu wanaoishi na Mungu. Kila mtu amepitia upotovu wa Shetani, ameonja uchungu na utamu wa maisha. Sasa akiishi katika nuru Yangu, mtu anawezaje kukosa kushangilia? Mtu anawezaje kuuacha tu wakati huu mzuri na kuuacha upite? Watu! Sasa imbeni nyimbo zilizo ndani ya mioyo yenu na mnichezee! Sasa inueni mioyo yenu ya kweli na kuipeana Kwangu! Sasa pigeni ngoma zenu na kunichezea! Naangaza furaha juu ya ulimwengu wote! Nawaonyesha watu uso Wangu wa utukufu! Nitanguruma! Nitaupita sana ulimwengu! Tayari Natawala kati ya watu! Nainuliwa na watu! Nachukuliwa katika mbingu za samawati na watu wanaenda na Mimi. Natembea kati ya watu na watu Wangu wananizunguka! Mioyo ya watu ni yenye furaha, nyimbo zao zatetemesha ulimwengu, Nikifanya upenyu katika mbingu! Ulimwengu haujafunikwa kwa ukungu tena; hakuna matope tena, hakuna mkusanyiko wa maji taka tena. Watu watakatifu wa ulimwengu! Chini ya ukaguzi Wangu uso wenu halisi unafichuliwa. Ninyi sio watu waliofunikwa na uchafu, bali watakatifu safi kama jiwe la thamani, wapendwa Wangu wote, wote wanaonifurahisha! Vitu vyote vinafufuka! Watakatifu wote wamerudi mbinguni wakinihudumia, wakiingia katika kumbatio Langu la joto, hawalii tena, hawana wasiwasi tena, wakijitoa Kwangu, wakirudi nyumbani Kwangu, na katika nchi yao watanipenda milele! Hawabadiliki! Huzuni uko wapi! Machozi yako wapi! Mwili uko wapi! Dunia haipo tena; mbingu ni za milele. Ninaonekana kwa watu wote, na watu wote wananisifu. Uzima huu, uzuri huu, tangu wakati wa zamani na hata milele, havitabadilika. Huu ndio uzima katika ufalme.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 3 Julai 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Zhang Jin, Beijing
Agosti 16, 2012
Mimi ni dada mzee mwenye miguu miwili yenye kasoro. Hata wakati hali ya hewa ni nzuri nje, nina shida kutembea, lakini wakati maji ya mafuriko yalipokuwa karibu kunimeza, Mungu aliniruhusu kutoroka hatari kimiujiza.
Ilikuwa Julai 21, mwaka wa 2012. Siku hiyo mvua ya mfoko ilinyesha, na nilikuwa tu nje nikitimiza wajibu wangu. Baada ya saa 10:00 mchana, mvua ilikuwa bado haijaisha. Wakati mkutano wetu ulipomalizika, niliikabili mvua bila woga na kupanda basi kwelekea nyumbani. Wakati nikisafiri, mvua ikawa nzito zaidi na zaidi, na wakati basi lilipofika kituo cha basi kabla ya changu, dereva alituambia sisi sote abiria, "Basi hili haliwezi kwendelea zaidi; barabara imeporomoka huko mbele." Hakukuwa na kitu ambacho kingeweza kufanywa, kwa hivyo sikukuwa na chaguo ila kushuka kutoka kwenye basi na kutembea njia yote. Bila kudhubutu kumwacha Mungu, nilikuwa ninaendelea kuomba moyoni mwangu. Kutokana na nguvu ya gharika, maji yalikuwa yamemeza barabara kabisa. Nilijaribu kuendelea kwa kushikilia nguzo za saruji zilizosimama kwa safu kando ya barabara, nikisonga mbele hatua kwa hatua. Wakati huo, nikasikia mtu akipiga ukelele nyuma yangu, "Acha kusonga mbele! Haraka; geuka na kurudi! Huwezi kupita; maji hayo yana uketo na mkondo una kasi sana. Ukikusomba, sitaweza kukuokoa!" Wakati huo, hata hivyo, singesonga mbele wala kurudi nyuma, kwa sababu maji yalikuwa tayari yamefika kifuani mwangu. Sikudhubutu kutembea zaidi, hivyo yote niliyoweza kufanya ni kumwomba Mungu na kumsihi Yeye afungue njia yangu kupitia: "Mungu! Umeyaruhusu mazingira haya kunifika, na ikiwa nitaishi au kufa iko mikononi Mwako sasa. Kama kiwango cha maji kingeshuka kwa nusu futi tu, ningeendelea kutembea mbele. Mungu, fanya Unavyotaka; Niko tayari kuaminisha maisha yangu Kwako!" Baada ya kufanya sala hii, nilijihisi mnyamavu na mtulivu. Nilikumbuka mojawapo ya maneno ya Mungu: "Mbingu na ardhi na vitu vyote vimeasisiwa na kukamilishwa na maneno ya kinywa Changu na na Mimi chochote kinaweza kufanikishwa" (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). Maneno ya Mungu yalinipa imani na ujasiri. Kwa kuwa mbingu na ardhi na vitu vyote viko mikononi mwa Mungu, nilijua kwamba bila kujali jinsi gharika hiyo ilivyokuwa katili, haingeepuka mpango wa Mungu. Hakuna yeyote ambaye angetegemewa tena; mwanangu wa kiume, binti yangu … hakuna yeyote ambaye angeweza kumtunza mwenzake. Niliamini kuwa mradi nilimtegemea Mungu, hakukuwa na shida ambayo singeweza kuipita. Wakati ule ule, muujiza ukafanyika. Mkondo ukapungua zaidi na zaidi mpaka haukuwa tena mkali kama ilivyokuwa wakati mfupi awali, na nguzo za saruji zilizosimama kwa safu kando ya barabara zimefichuliwa hatua kwa hatua. Kwa hakika, kiwango cha maji kilishuka kwa nusu futi kutoka kiwango cha kifua changu. Na hivyo tu, niliondoka mahali hapo, hatua kwa hatua, chini ya uongozi wa Mungu. Isingekuwa kwa sababu ya huruma na ulinzi wa Mungu, sijui ambako gharika ingenipeleka. Kutoka kwa kina cha moyo wangu, nilionyesha shukrani yangu na sifa, nikimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa ya pili katika maisha.
Baadaye, nikasikia maelezo ya mtoto wangu kuhusu mvua hiyo: Siku hiyo, baada ya kurudi nyumbani kutoka kutimiza wajibu wake, alikwenda msalani kwanza. Mara tu alipotoka chooni na kurudi kwenye chumba chake alisikia sauti kubwa nje. Alipotoka nje kwenda kuangalia, aliona kwamba jengo zima la choo lilikuwa limeanguka kabisa chini ya maji. Isingekuwa kwa ulinzi wa Mungu, angekufa. Ilikuwa hasa kama Mungu alivyosema katika mojawapo ya maneno Yake: "vitu vyote, vilivyo hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, vitafanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu" ("Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili). Msisimko wa kuzidi kiasi niliouhisi ndani ya moyo wangu hakika hauwezi kuelezwa kwa maneno.
Kupitia matukio haya mawili, imani yangu imekuwa imara hata zaidi. Siku hiyo, Mungu alikuwa ameniruhusu kuokoka maafa hasa kuniruhusu mimi kutoa ushahidi kwa ajili Yake. Siwezi kupuuza dhamiri yangu. Ninapoangalia nyuma juu ya jinsi nilivyokuwa na ubinafsi, ukatili, na hali ya kujidai nilivyokuwa awali kwa kawaida nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, ninatambua kuwa sikuhisi kamwe busara ya Mungu ya umuhimu au kushiriki mawazo ya Mungu. Kuanzia sasa kwendelea, napenda kutubu na kubadilika. Nitatumia uzoefu wangu binafsi kuwaleta watu zaidi mbele ya Mungu, na kufanya wajibu wangu katika kazi ya kueneza injili.
kutoka kwa Vita Baina ya Haki na Uovu

Jumanne, 26 Desemba 2017

Wimbo wa Uzoefu wa Maisha Nitampenda Mungu Milele

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Wimbo wa Uzoefu wa Maisha Nitampenda Mungu Milele

I Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako. Nakubali mafunzo katika ufalme Wako mchana na usiku. Majaribio mengi na maumivu, mateso mengi sana. Mara nyingi nilimwaga machozi na kuhisi huzuni, na mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani. Lakini Hujawahi kuniacha. Uliniongoza kupitia matatizo mengi, Umeniweka kupitia hatari nyingi. Sasa najua ya kuwa Wewe Umenipenda.
II Ee Mungu! Waniongoza kwa maisha mapya. Nikifurahia Maneno yako, Nimeelewa mapenzi yako. Maneno yako hunihukumu na kuniadibu, na kutakasa upotovu wangu. Kupitia majaribio nimejifunza kukutii Wewe. Kukua katika neno la Mungu, nimekuja kumjua Mungu. Niko tayari kufanya wajibu wangu kwa shahidi Wako na utukufu. Nitakupenda Wewe kwa muda wote. Kama kubarikiwa au kulaaniwa, mimi nitafurahi kuwa katika huruma Yako. Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Umeme wa Mashariki , Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Jumatatu, 25 Desemba 2017

Mungu Amekuja Mungu Ametawala | “Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18”

Mungu Amekuja Mungu Ametawala | “Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18”

Kwaya za Injili:
1.Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho
2.Mwenyezi Mungu Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi
1.Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji). Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo. Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.Ha! Ha! Ha! Ha! Kila wakati Yeye Mwenyewe Anapofanya kazi miongoni mwa mwanadamu, ni mwanzo wa mapigano mapya. Bila mwanzo wa kazi mpya, kwa kawaida hakungekuwa na kikomo kwa enzi ya kale. Na bila kikomo kwa enzi ya kale ni thibitisho kuwa vita na Shetani, vita na Shetani havijafika mwisho. (Ha!)
Ni kama tu Mungu Mwenyewe Anakuja miongoni mwa mwanadamu na kutenda kazi mpya ndipo mwanadamu atakapoweza kujitoa kutoka katika miliki ya Shetani, miliki ya Shetani, na kupata maisha mapya, maisha mapya na mwanzo mpya. Vinginevyo, mwanadamu ataishi milele katika enzi ya kale na milele kuishi katika ushawishi wa kale wa Shetani, katika ushawishi wa kale wa Shetani. Ha! Ha! Ha! Ha! Katika kila enzi inayoongozwa na Mungu, sehemu ya mwanadamu huwekwa huru, na hivyo, mwanadamu huendelea na kazi ya Mungu kuelekea enzi mpya. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale wote ambao humfuata Yeye. Ushindi wa Mungu in ushindi, ushindi kwa wale wote wanaomfuata Yeye. Katika kila enzi inayoongozwa na Mungu, sehemu ya mwanadamu huwekwa huru, na hivyo, mwanadamu huendelea na kazi ya Mungu kuelekea enzi mpya. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale wote ambao humfuata Yeye. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale wote ambao humfuata Yeye. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho, Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Umeme wa Mashariki, nyimbo za injili,  Kanisa la Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.