Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neema-ya-mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neema-ya-mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 10 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Nne

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema: “Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwa madhara na udhibiti wa Shetani. Kando na Mungu, hakuna mtu au kitu kinaweza kukuokoa kutoka kwa bahari ya mateso, ili usiteseke tena: Hili linaamuliwa na kiini cha Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu hukuokoa bila ubinafsi wowote, ni Mungu pekee anayehusika na maisha yako ya baadaye, na hatima yako na maisha yako, na Yeye anapanga mambo yote kwa ajili yako. Hili ni jambo ambalo hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kinaweza kutimiza. Kwa sababu hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kina kiini cha Mungu kama hiki, hakuna mtu au kitu kina uwezo wa kukuokoa au kukuongoza wewe. Huu ndio umuhimu wa kiini cha Mungu kwa mwanadamu.”
Wakati wowote Shetani anampotosha mwanadamu ama anashughulika na madhara yasiyodhibitiwa, Mungu hasimami bila kazi, wala haweki kando ama kupuuza wale ambao amechagua. Yote ambayo Shetani anafanya ni wazi kabisa na yanaeleweka na Mungu. Haijalishi anachofanya Shetani, haijalishi mwenendo anaosababisha kuibuka, Mungu anajua yote ambayo Shetani anajaribu kufanya, na Mungu hawawachi wale ambao amechagua. Badala yake, bila kuvuta macho hata kidogo, kwa siri, kwa ukimya, Mungu anafanya yote yanayohitajika. Anapoanza kufanya kazi kwa mtu, wakati amemchagua mtu, Haambii yeyote, wala Hamwambii Shetani, wala hata kufanya maonyesho makubwa. Anafanya tu kwa ukimya, kwa asili kile ambacho kinahitajika. Kwanza, Anakuchagulia familia; usuli ambao hiyo familia inao, wazazi wako ni nani, mababu zako ni nani—haya yote tayari yaliamuliwa na Mungu. Kwa maneno mengine, haya hayakuwa uamuzi wa mvuto wa ghafla yaliyofanywa na Yeye, lakini badala yake hii ilikuwa kazi iliyoanza kitambo. Baada ya Mungu kukuchagulia familia, pia Anachagua tarehe ambayo utazaliwa. Kwa sasa, Mungu anaangalia unapozaliwa katika dunia hii ukilia, Anatazama kuzaliwa kwako, Anatazama unapotamka maneno yako ya kwanza, Anatazama unapoanguka na kutembea hatua zako za kwanza, ukijifunza kutembea. Kwanza unachukua hatua moja na kisha unachukua nyingine… sasa unaweza kukimbia, sasa unaweza kuruka, sasa unaweza kuongea, sasa unaweza kuonyesha hisia zako. Wakati huu, unapokua, macho ya Shetani yamewekwa kwa kila mmoja wenu, kama chui mkubwa mwenye milia anavyomwangalia nyara wake. Lakini kwa kufanya kazi Yake, Mungu hajawahi kuteseka mapungufu yoyote ya watu, matukio ama mambo, ya nafasi ama wakati; Anafanya kile anachopaswa kufanya na Anafanya kile Anacholazimika kufanya. Katika mchakato wa kukua, unaweza kukutana na mambo mengi ambayo hupendi, kukutana na magonjwa na kuvunjika moyo. Lakini unapotembea njia hii, maisha yako na bahati zako ziko chini ya ulinzi wa Mungu kabisa. Mungu anakupa hakikisho halisi litakalodumu maisha yako yote, kwani Yeye yuko kando yako, anakulinda na kukutunza. Bila kujua haya, unakua. Unaanza kukutana na mambo mapya na unaanza kujua dunia hii na wanadamu hawa. Kila kitu ni kipya kwako. Unapenda kufanya mambo yako na unapenda kufanya kile unachopenda. Unaishi katika ubinadamu wako mwenyewe, unaishi katika nafasi yako ya kuishi na huna hata kiasi kidogo cha mtazamo kuhusu kuwepo kwa Mungu. Lakini Mungu anakulinda katika kila hatua ya njia unapokua, na Anakutazama unapoweka kila hatua mbele. Hata unapojifunza maarifa, ama kusoma sayansi, Mungu hajawahi toka upande wako kwa hatua hata moja. Wewe ni sawa na watu wengine kwamba, katika harakati za kuja kujua na kukutana na dunia, umeanzisha maadili yako mwenyewe, una mambo yako mwenyewe ya kupitisha muda, mambo unayopenda mwenyewe, na pia unayo matamanio ya juu. Wakati mwingi unafikiria siku zako za baadaye, wakati mwingi ukichora muhtasari wa jinsi siku zako za baadaye zinapaswa kuwa. Lakini haijalishi kitakachofanyika njiani, Mungu anaona vyote na macho wazi. Labda wewe mwenyewe umesahau siku zako za nyuma, lakini kwa Mungu, hakuna anayeweza kukuelewa bora kumliko Yeye. Unaishi chini ya macho ya Mungu, unakua, unapevuka. Wakati huu, jukumu muhimu la Mungu ni kitu ambacho hakuna yeyote kamwe hufahamu, kitu ambacho hakuna yeyote anajua. Mungu hakika hakuambii kukihusu. Kwa hivyo hiki kitu muhimu ni nini? Je, mnajua? (Kuleta watu mbele Yake.) Kwa hivyo Mungu anafanya nini kuleta watu mbele Yake? Analeta watu mbele Yake wakati upi? Je, mnajua? Hii ni kazi muhimu zaidi ya Mungu? Hiki ni kitu muhimu zaidi ambacho Mungu anafanya? Tunaweza kusema kwamba ni hakikisho kwamba Mungu atamwokoa mtu. Hii inamaanisha kwamba Mungu anataka kumwokoa mtu huyu, kwa hivyo lazima Afanye hivi, na kazi hii ni muhimu sana kwa mwanadamu na Mungu. Je, mnajua hili? Inaonekana kwamba hamna hisia yoyote kuhusu hili, ama dhana yoyote kuhusu hili, kwa hivyo nitawaambia. Kutoka ulipozaliwa hadi sasa, Mungu amefanya kazi nyingi sana kwako, lakini Hakukwambia kila wakati Alifanya kitu. Haikuwa ujue, kwa hivyo hukuambiwa, sivyo? (Ndiyo.) Kwa mwanadamu, kila kitu anachofanya Mungu ni muhimu. Kwa Mungu, ni kitu ambacho lazima Afanye. Lakini katika moyo wake kuna kitu muhimu Anapaswa kufanya ambacho kinazidi yoyote ya mambo haya. Ni nini hicho? Yaani, kutoka ulipozaliwa hadi sasa, Mungu lazima ahakikishe usalama wa kila mmoja wenu. Mnaweza kuhisi kana kwamba hamwelewi kikamilifu, kusema “usalama huu ni muhimu sana?” Kwa hivyo ni nini maana halisi ya “usalama”? Labda mnauelewa kumaanisha amani ama pengine mnauelewa kumaanisha kutopitia maafa ama msiba wowote, kuishi vyema, kuishi maisha ya kawaida. Lakini katika mioyo yenu lazima mjue kwamba si rahisi hivyo. Kwa hivyo ni nini hasa kitu hiki ambacho Nimekuwa nikizungumzia, ambacho Mungu anapaswa kufanya? Kinamaanisha nini kwa Mungu? Kuna hakikisho lolote la usalama wenu? Kama sasa hivi? La. Kwa hivyo ni nini hiki ambacho Mungu anafanya? Usalama huu unamaanisha humezwi na Shetani. Je, jambo hili ni muhimu? Wewe humezwi na Shetani, kwa hivyo hili linahusisha usalama wako, au la? Hili linahusisha usalama wako binafsi, na hakuwezi kuwa na lolote muhimu zaidi. Baada ya wewe kumezwa na Shetani, nafsi yako wala mwili wako si vya Mungu tena. Mungu hatakuokoa tena. Mungu huacha nafsi kama hiyo na huacha watu kama hao. Kwa hivyo Nasema kitu muhimu sana ambacho Mungu anapaswa kufanya ni kuhakikishia usalama wako, kuhakikisha kwamba hutamezwa na Shetani. Hili ni muhimu kiasi, silo? Kwa hivyo mbona hamwezi kujibu? Inaonekana kwamba hamwezi kuhisi wema mkubwa wa Mungu!
Mungu anafanya mengi kando na kuhakikisha usalama wa watu, kuhakikisha kwamba hawatamezwa na Shetani; pia hufanya kazi nyingi sana kwa kutayarisha kumchagua mtu na kumwokoa. Kwanza, una tabia gani, utazaliwa kwa familia ya aina gani, wazazi wako ni nani, una kaka na dada wangapi, hali na hadhi ya kiuchumi ya familia yako ni gani, hali ya familia yako ni gani—haya yote yanapangiwa wewe kwa uangalifu na Mungu. Je, unajua ni familia ya aina gani watu waliochaguliwa na Mungu wanazaliwa ndani mara nyingi, kama inavyohusu watu wengi? Ni familia mashuhuri? Kunaweza kuwa na nyingine. Hatuwezi sema kwa uhakika hakuna yoyote, lakini kuna chache sana. Ni familia za utajiru wa kupindukia, kama yenye mabilioni ama yenye mamilioni nyingi? Mara nyingi huwa si aina hii ya familia. Kwa hivyo Mungu anapangia watu familia za aina gani zaidi? (Familia za kawaida.) Kwa hivyo familia za kawaida ni zipi? Sanasana ni familia zinazofanya kazi na familia za ukulima. Wafanyakazi wanategemea mishahara yao kuishi na wanaweza kumudu mahitaji ya kimsingi. Hawatakuruhusu kwenda njaa wakati wowote, lakini huwezi kutarajia mahitaji yote ya mwili kutoshelezwa. Wakulima wanategemea kupanda mazao kwa chakula yao, na wana nafaka za kula, na kwa vyovyote vile, hutakuwa na njaa, lakini huwezi kuwa na nguo nzuri sana. Tena kuna familia zingine ambazo zinashughulika katika biashara ama zinazoendesha biashara ndogondogo, na zingine ambazo wazazi ni wenye akili, na hizi zinaweza kuhesabika kama familia za kawaida. Kuna baadhi ya wazazi ambao ni wafanyakazi wa ofisi ama maafisa wadogo wa serikali kwa kiwango zaidi, ambazo haziwezi kuhesabika kama familia mashuhuri pia. Watu wengi zaidi wanazaliwa katika familia za kawaida, na haya yote yanapangiliwa na Mungu. Kusema kwamba, kwanza kabisa mazingira haya unayoishi si familia ya uwezo mkubwa ambayo unaweza kufikiria, lakini badala yake ni familia uliyoamuliwa na Mungu, na watu wengi wataishi katika mipaka ya aina hii ya familia; hatutazungumza mambo ya pekee hapa. Kwa hivyo je, hadhi ya kijamii? Hali ya uchumi ya wengi wa wazazi ni wastani na hawana hadhi ya juu ya kijamii—kwao ni vizuri tu kuwa na kazi. Kuna wowote walio magavana? Kuna wowote walio maraisi? (La.) Kwa zaidi ni watu kama mameneja wa biashara ndogo ama wakubwa wa muda mfupi, wote wakiwa na hadhi wastani ya kijamii, wote wakiishi katika hali wastani ya uchumi. Sababu nyingine ni mazingira ya kuishi ya familia. Kwanza kabisa, hakuna wazazi ambao wanaweza kushawishi kwa wazi watoto wao kutembea njia ya uaguzi na kupiga ramli; hawa pia ni wachache. Wazazi wengi ni wa kawaida kiasi na ni wa hali moja na nyinyi. Mungu anaweka mazingira ya aina hii kwa ajili ya watu wakati sawa na kuwachagua, na ni kwa manufaa sana ya kazi Yake ya kuokoa watu. Kwa nje, inaonekana kwamba Mungu hajafanya chochote kuu kwa mwanadamu; Anafanya kila kitu kwa siri tu, kwa unyenykevu na kwa kimya. Lakini kwa hakika, vyote ambavyo Mungu anafanya vinafanywa kuweka msingi wa wokovu wako, kuandaa njia mbeleni na kuandaa hali zote muhimu za wokovu wako. Mara moja wakati maalum wa kila mtu, Mungu anawarudisha mbele Yake—wakati unapofika kwako kusikia sauti ya Mungu, huo ndio wakati unapokuja mbele Yake. Wakati hili linafanyika, watu wengine wamekuwa wazazi tayari wenyewe, ilhali wengine ni watoto wa mtu tu. Kwa maneno mengine, watu wengine wameoa na kupata watoto ilhali wengine bado hawajaoa, na hawajaanza bado familia zao. Lakini licha ya hali za watu, Mungu tayari ameweka nyakati utakapochaguliwa na injili na maneno Yake yatakapokufikia. Mungu ameweka hali, ameamulia mtu fulani ama muktadha fulani ambamo injili itapitishwa kwako, ili uweze kusikia maneno ya Mungu. Mungu tayari amekuandalia hali zote muhimu ili, bila kujua, unakuja mbele Yake na unarudishwa kwa familia ya Mungu. Pia, bila kujua, unafuata Mungu na kuingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua, kuingia katika njia ya Mungu ya kazi ambayo, hatua kwa hatua amekuandalia. Mungu angalau anafanya na anampa mwanadamu wakati huu kwanza na kabisa utunzaji na ulinzi ambayo mwanadamu anafurahia, na hii bila shaka ni kweli. Kwa hivyo Mungu anatumia njia za aina gani? Mungu anaweka watu na vitu mbalimbali ili mwanadamu aweze kuona kuwepo Kwake na matendo Yake miongoni mwao. Kwa mfano, kuna watu wengine wanaomwamini Mungu kwa sababu mtu katika familia yao ni mgonjwa, na wanasema “Mmoja wa familia yangu ni mgonjwa, nitafanya nini? Watu wengine kisha wanasema “Mwamini Yesu!” Kwa hivyo wanaanza kumwamini Mungu, na imani hii kwa Mungu imekuja kwa sababu ya hali hii. Kwa hivyo ni nani aliyepangilia hali hii? (Mungu.) Kwa njia ya hali hii wanamwendea Mungu. Kuna familia zingine kama hii ambamo wote ni waumini, vijana na wazee, ilhali kuna zingine ambamo imani ni ya kibinafsi. Kwa hivyo Niambie, ni nini muumini anapata kutoka kwa Mungu? Inavyoonekana, ugonjwa unakuja, lakini kwa hakika ni hali aliyopewa yeye ili aje mbele ya Mungu—huu ni wema wa Mungu. Kwa sababu maisha ya familia ya watu wengine ni magumu na hawawezi kupata amani yoyote, fursa ya bahati inakuja ambapo mtu atapitisha injili na kusema “Familia yako ina magumu. Mwamini Yesu. Mwamini Yesu na utakuwa na amani.” Bila fahamu, mtu huyu basi anakuja kumwamini Mungu katika hali asili, kwa hivyo hii si aina ya hali? (Ndiyo.) Na je, familia yake kuwa na amani si neema aliyopewa na Mungu? (Ndiyo.) Kisha kuna wengine wanaokuja kumwamini Mungu kwa sababu zingine, lakini licha ya sababu inakuleta kumwamini Yeye, yote hakika yamepangwa na kuongozwa na Mungu, bila shaka.
Mwanzoni, Mungu alitumia njia mbalimbali kukuchagua na kukuleta katika familia Yake. Hili ni jambo la kwanza Anafanya na ni neema anampa kila mtu. Sasa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, Hampi tena mwanadamu neema na baraka tu kama Alivyofanya mwanzoni, wala halazimishi watu kwenda mbele—hii ni kwa sababu ya msingi wa kazi katika enzi ya Neema. Wakati wa kazi ya siku hizi za mwisho, ni nini mwanadamu ameona kutoka kwa vipengele hivi vyote vya kazi ya Mungu ambavyo wamepitia? Hawajaona tu upendo wa Mungu, lakini pia hukumu na kuadibu kwa Mungu. Kwa wakati huu, Mungu zaidi ya hayo, anamtegemeza, tia nuru, na kumwongoza mwanadamu, ili aje kujua nia Zake polepole, kujua maneno Anayozungumza na ukweli Anaompa mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati amevunjika roho, wakati hana popote pa kugeukia, Mungu atatumia maneno Yake kufariji, kushauri na kuwatia moyo, ili mwanadamu wa kimo ndogo aweze kupata nguvu polepole, kuinuka kwa wema na kuwa radhi kushirikiana na Mungu. Lakini wakati mwanadamu hamtii Mungu ama anampinga Yeye, ama anapofichua upotovu wake na kumpinga Mungu, Mungu hataonyesha huruma kumrudi yeye na kumfundisha nidhamu. Kwa ujinga, kutojua, unyonge, na uchanga wa mwanadamu, hata hivyo, Mungu ataonyesha uvumilivu na ustahimilivu. Kwa njia hii, kupitia kazi yote Mungu anamfanyia mwanadamu, mwanadamu anapevuka, anakua na anakuja kujua nia za Mungu polepole, kujua baadhi ya ukweli, kujua ni nini mambo mema na ni nini mambo hasi, kujua uovu ni nini na kujua giza ni nini. Mungu hamrudi na kumfundisha nidhamu mwanadamu siku zote wala Haonyeshi uvumilivu na ustahimilivu siku zote. Badala yake anampa kila mtu kwa njia tofauti, katika hatua zao tofauti na kulingana na kimo na ubora wa tabia yao tofauti. Anamfanyia mwanadamu mambo mengi na kwa gharama kubwa; mwanadamu hafahamu lolote la gharama hii ama mambo haya Mungu anafanya, ilhali yote ambayo anafanya kwa kweli inafanywa kwa kila mtu. Upendo wa Mungu ni wa kweli: Kupitia neema ya Mungu mwanadamu anaepuka janga moja baada ya jingine, ilhali kwa unyonge wa mwanadamu, Mungu anaonyesha ustahimili wake muda baada ya muda. Hukumu na kuadibu kwa Mungu yanaruhusu watu kuja kutambua upotovu wa wanadamu polepole na kiini chao potovu cha kishetani. Kile ambacho Mungu anapeana, kutia nuru Kwake kwa mwanadamu na uongozi Wake yote yanawaruhusu wanadamu kujua zaidi na zaidi kiini cha ukweli, na kujua zaidi kile ambacho watu wanahitaji, njia wanayopaswa kuchukua, kile wanachoishia, thamani na maana ya maisha yao, na jinsi ya kutembea njia iliyo mbele. Haya mambo yote ambayo Mungu anafanya hayatengwi na lengo Lake la awali. Ni nini, basi lengo hili? Je, mnajua? Mbona Mungu anatumia njia hizi kufanya kazi Yake kwa mwanadamu? Anataka kutimiza matokeo gani? Kwa maneno mengine, ni nini ambacho anataka kuona kwa mwanadamu na kupata kutoka kwake? Kile ambacho Mungu anataka kuona ni kwamba moyo wa mwanadamu unaweza kufufuliwa. Kwa maneno mengine, njia hizi ambazo anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu ni za kuamsha bila kikomo moyo wa mwanadamu, kuamsha roho ya mwanadamu, kumwacha mtu kujua alipotoka, ni nani anayemwongoza, kumsaidia, kumkimu, na ni nani ambaye amemruhusu mwanadamu kuishi hadi sasa; ni ya kuwacha mwanadamu kujua ni nani Muumbaji, ni nani wanapaswa kuabudu, ni njia gani wanapaswa kutembelea, na mwanadamu anapaswa kuja mbele ya Mungu kwa njia gani; yanatumika kufufua moyo wa mwanadamu polepole, ili mwanadamu ajue moyo wa Mungu, aelewe moyo wa Mungu, na aelewe utunzaji mkuu na wazo nyuma ya kazi Yake kumwokoa mwanadamu. Wakati moyo wa mwanadamu umefufuliwa, hataki tena kuishi maisha ya msherati, tabia potovu, lakini badala yake kutaka kutafuta ukweli kwa kuridhishwa kwa Mungu. Wakati moyo wa mwanadamu umeamshwa, anaweza basi kujinusuru kutoka kwa Shetani, kutoathiriwa tena na Shetani, kutodhibitiwa na kudanganywa na yeye. Badala yake, mwanadamu anaweza kushiriki katika kazi ya Mungu na katika maneno Yake kwa njia njema kuridhisha moyo wa Mungu, na hivyo kupata kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Hili ndilo lengo la awali la kazi ya Mungu.

Ijumaa, 19 Aprili 2019

Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

4. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii hasa kwamba mwili wa mwanadamu umepotoshwa ndiyo maana Mungu amemfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mlengwa wa upotovu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa pekee wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, ni lazima Mungu awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi. Mungu lazima awe mwili ili Aweze kufanya kazi Yake kwa ufanisi kwa sababu mwanadamu ni wa mwili, na hana uwezo wa kushinda dhambi au kujivua mwili. Ingawa kiini na utambulisho wa Mungu unatofautiana kwa kiasi kikubwa na kiini na utambulisho wa mwanadamu, bado kuonekana Kwake kunafanana na kuonekana kwa mwanadamu, Ana umbo la mwanadamu wa kawaida, na Anaishi maisha ya mwanadamu wa kawaida, na wale wanaomwona hawawezi kuona tofauti na mtu wa kawaida. Kuonekana huku kwa kawaida na ubinadamu wa kawaida vinatosha Kwake kwa ajili ya kufanya kazi Yake ya kiungu katika ubinadamu wa kawaida. Mwili Wake unamruhusu kufanya kazi Yake katika ubinadamu wa kawaida, na unamsaidia kufanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu, na ubinadamu Wake wa kawaida, aidha, humsaidia kufanya kazi ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Ingawa ubinadamu Wake wa kawaida umeleta msukosuko miongoni mwa wanadamu, msukosuko huo haujaathiri matokeo ya kawaida ya kazi Yake. Kwa ufupi, kazi ya ubinadamu Wake wa kawaida ni ya manufaa makubwa kwa mwanadamu. Ingawa watu wengi hawakubali ubinadamu Wake wa kawaida, kazi Yake bado inaweza kuwa ya ufanisi, na matokeo haya yanapatikana kutokana na ubinadamu Wake wa kawaida. Kuhusu hili hakuna shaka. Kutokana na kazi Yake ya mwili, mwanadamu anapata vitu mara kumi au dazeni kadhaa zaidi kuliko mitazamo iliyopo miongoni mwa mwanadamu kuhusu ubinadamu Wake wa kawaida, na mitazamo hiyo hatimaye itamezwa na kazi Yake. Na matokeo ambayo kazi Yake imefanikiwa, ambayo ni kusema, maarifa ambayo mwanadamu anayo juu Yake, yanazidi kwa mbali sana dhana za mwanadamu kumhusu. Hakuna namna ya kufikiri au kupima kazi Anayofanya katika mwili, maana mwili Wake si kama wa mwanadamu; ingawa sura za nje zinafanana kiini chao si sawa. Mwili Wake unatoa mitazamo mingi kuhusu Mungu miongoni mwa mwanadamu, bado mwili Wake unaweza pia kumruhusu mwanadamu kuwa na maarifa mengi, na anaweza hata kumshinda mwanadamu yeyote mwenye ganda la sawa nje. Maana Yeye si mwanadamu wa kawaida tu, bali ni Mungu mwenye umbo la nje kama la mwanadamu, na hakuna anayeweza kumwelewa au kumfahamu kikamilifu. Mungu asiyeonekana na kushikika anapendwa na kukaribishwa na wote. Kama Mungu ni Roho tu ambayo haionekani kwa mwanadamu, ni rahisi sana kwa mwanadamu kumwamini Mungu. Mwanadamu anaweza kuzipa uhuru fikra zake mwenyewe, anaweza kuchagua taswira yoyote anayotaka kama taswira ya Mungu ili kujifurahisha mwenyewe na kujifanya mwenyewe awe na furaha. Kwa njia hii, mwanadamu anaweza kufanya chochote kile kinachomfurahisha Mungu wake, na kile ambacho Mungu huyu yuko tayari kukifanya bila aibu yoyote. Aidha, mwanadamu huyu anaamini kwamba hakuna ambaye ni mwaminifu zaidi anayejitolea kwa Mungu kuliko yeye, na kwamba wengine wote ni mbwa wa Mataifa, na wasiokuwa waaminifu kwa Mungu. Inaweza kusemekana kwamba hiki ndicho kinachotafutwa na wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya kidhahania na ambayo imejikita katika mafundisho; wanavyovitafuta vinafanana, tofauti ikiwa ndogo tu. Ni kwamba tu taswira za Mungu katika fikra zao ni tofauti, lakini viini vyao kimsingi vinafanana.
Mwanadamu hasumbuliwi na imani yake ya kutojali katika Mungu, na anamwamini Mungu kwa namna anavyotaka. Hii ni moja ya “haki na uhuru wa mwanadamu,” ambao hakuna mtu anayeweza kuuingilia kwa sababu mwanadamu anamwamini Mungu wake mwenyewe na wala si Mungu wa mtu yeyote yule; ni mali yake binafsi, na takribani kila mtu anamiliki aina hii ya mali binafsi. Mwanadamu anaichukulia mali hii kama hazina ya thamani, lakini kwa Mungu hakuna kitu ambacho ni duni au hakina thamani zaidi ya hiki, maana hakuna kiashiria cha wazi cha upinzani kwa Mungu kuliko mali hii binafsi ya mwanadamu. Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu mwenye mwili ndiyo Mungu amefanyika mwili ambaye ana umbo la kugusika, na ambaye anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu. Yeye si Roho asiyekuwa na umbo, bali mwili ambao unaweza kuhusiana na kuonekana kwa mwanadamu. Hata hivyo, Miungu mingi ambayo watu wanaamini kwayo ni miungu isiyo na mwili na umbo maalumu, na ambayo haifungwi na umbo maalumu. Kwa njia hii, Mungu mwenye mwili amekuwa adui wa wengi wanaomwamini Mungu, na wale ambao hawawezi kuukubali ukweli wa Mungu mwenye mwili, vilevile, wamekuwa maadui wa Mungu. Mwanadamu amejawa na dhana si kwa sababu ya namna anavyofikiri, au kwa sababu ya uasi wake, bali ni kwa sababu ya mali hii binafsi ya mwanadamu. Ni kwa sababu ya mali hii watu wengi hufa, na ni Mungu huyu asiye dhahiri, ambaye hawezi kuguswa, hawezi kuonwa, na ambaye hayupo hakika ambaye huangamiza maisha ya mwanadamu. Maisha ya mwanadamu yanapotea si kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sembuse na Mungu wa mbinguni, bali ni Mungu wa fikra za mwanadamu mwenyewe. Sababu pekee ambayo Mungu mwenye mwili amefanyika mwili ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu aliyepotoka. Ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu na si ya Mungu, na mateso Yake na sadaka ni kwa ajili ya mwanadamu na si kwa manufaa ya Mungu Mwenyewe. Hakuna faida wala hasara au tuzo kwa Mungu; Hatavuna mavuno yoyote ya baadaye, bali ni kile ambacho hapo awali Aliwiwa. Yote Anayoyafanya na kujitolea kwa ajili mwanadamu si kwa sababu Atapata thawabu kubwa, bali ni kwa ajili ya mwanadamu. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inahusisha ugumu mwingi usiofikirika, matokeo ambayo yanapatikana mwishowe yanazidi kwa mbali sana kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Kazi ya mwili inahusisha taabu nyingi sana, na mwili hauwezi kuwa na utambulisho mkubwa kama wa Roho, hauwezi kufanya matendo ya kimiujiza kama Roho, sembuse kuwa na mamlaka kama ya Roho. Lakini kiini cha kazi inayofanywa na mwili huu usiokuwa wa kawaida ni kuu zaidi kulinganisha na kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na mwili huu Mwenyewe ndio jibu kwa mahitaji yote ya mwanadamu. Kwa wale wanaotaka kuokolewa, thamani ya Roho ipo chini zaidi kulinganisha na ile ya mwili. Kazi ya Roho inaweza kuufikia ulimwengu wote, katika milima yote, mito, maziwa, na bahari, lakini kazi ya mwili kwa ufanisi zaidi inahusiana na kila mtu anayekutana na Yeye. Aidha, mwili wa Mungu katika umbo la kushikika unaweza kueleweka vizuri na kuaminiwa na mwanadamu, na unaweza kuimarisha maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu, na anaweza kumwachia mwanadamu mvuto wa kina wa matendo halisi ya Mungu. Kazi ya Roho imefungwa sirini, ni vigumu kwa viumbe wenye mwili wa kufa kuelewa, na vigumu zaidi kwao kuona, na hivyo wanaweza kutegemea tu vitu vya kufikirika. Hata hivyo, kazi ya mwili ni ya kawaida, na imejikita katika uhalisi, na ina hekima kubwa sana, na ni ukweli unaoweza kuonekana kwa macho ya mwanadamu; mwanadamu anaweza kupitia uzoefu wa hekima ya Mungu, na hana haja ya kuwa na fikira zake kubwa. Huu ndio usahihi na thamani halisi ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Roho anaweza tu kufanya vitu ambavyo havionekani kwa mwanadamu na vigumu kwake kufikiria, kwa mfano nuru ya Roho, mzunguko wa Roho na uongozi wa Roho, lakini kwa mwanadamu mwenye akili, hivi havitoi maana inayoeleweka. Vinatoa maana ya kusonga, au ya jumla tu, na havitoi maelekezo kwa maneno. Hata hivyo, kazi ya Mungu mwenye mwili, ni tofauti sana: Ina mwongozo sahihi wa maneno, ina nia ya wazi, ina malengo ya wazi yanayohitajika. Na hivyo mwanadamu hahitaji kupapasa, au kutumia fikra zake, au kufanya makisio. Huu ndio uwazi wa kazi katika mwili, na tofauti yake kubwa na kazi ya Roho. Kazi ya Roho inafaa tu kwa mawanda finyu, na haiwezi kuchukua kazi ya mwili. Kazi ya mwili inampa mwanadamu malengo halisi zaidi na yanayohitajika na maarifa yaliyo halisi zaidi na yenye thamani kuliko kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi ambayo ina thamani kubwa kwa mwanadamu aliyepotoka ambayo inatoa maneno sahihi, malengo wazi ya kufuata, na ambayo inaweza kuonekana na kuguswa. Ni kazi yenye kuwezekana tu, na uongozi wa wakati ndio unaofaa kwa ladha ya mwanadamu, na kazi halisi ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika tabia yake iliyopotoka na kusawijika. Hii inaweza kufanywa na Mungu mwenye mwili tu; ni Mungu mwenye mwili peke yake ndiye Anayeweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika hali yake ya zamani ya kupotoka. Ingawa Roho ni kiini cha asili ya Mungu, kazi kama hii inaweza tu kufanywa na mwili Wake. Kama Roho angefanya kazi peke Yake, basi haingewezekana kwa kazi Yake kuwa ya ufanisi—huu ni ukweli ulio wazi kabisa. Ingawa watu wengi wamekuwa maadui wa Mungu kwa sababu ya mwili huu, Anapokamilisha kazi Yake, wale ambao wapo kinyume Chake hawataacha tu kuwa maadui Zake, bali kinyume Chake watakuwa mashahidi Wake. Watakuwa mashahidi watakaokuwa wameshindwa naye, mashahidi ambao wana ulinganifu na Yeye na ambao hawatenganishwi naye. Atamsababisha mwanadamu kujua umuhimu wa kazi Yake katika mwili kwa mwanadamu, na mwanadamu atajua umuhimu wa mwili huu katika maana ya uwepo wa mwanadamu, atajua thamani Yake halisi katika ukuaji wa maisha ya mwanadamu, aidha, atajua mwili huu utakuwa chemchemi ya uhai ambayo kwayo mwanadamu hataachana nayo. Ingawa Mungu mwenye mwili anatofautiana sana na utambulisho na nafasi ya Mungu, na anaonekana kwa mwanadamu kuwa hana ulinganifu na hadhi yake halisi, mwili huu, ambao hauna sura halisi ya Mungu, au utambulisho halisi wa Mungu, unaweza kufanya kazi ambayo Roho wa Mungu hawezi kuifanya moja kwa moja. Hiyo ndiyo maana ya kweli na thamani ya Mungu mwenye mwili, na ni umuhimu huu na thamani ambayo mwanadamu hawezi kuithamini na kuikubali. Ingawa wanadamu wote wanamtazamia Roho wa Mungu na wanamdharau Mungu mwenye mwili, bila kujali vile wanavyoona au kufikiri, maana na thamani halisi ya mwili inapita kwa mbali ile ya Roho. Bila shaka, hii ni kwa mujibu wa mwanadamu aliyepotoka. Kwa kuwa kila mtu anayetafuta ukweli na anatamani kumwona Mungu, Kazi ya Roho inaweza kutoa tu kuguswa au ufunuo, na hisia ya kuona maajabu ambayo hayaelezeki na kufikirika, na hisia ambayo ni kuu, ya juu sana kuliko uwezo wa mwanadamu, na inayotamanika, lakini ambayo pia haifikiwi na haipatikani kwa wote. Mwanadamu na Roho wa Mungu wanaweza tu kutazamana kwa mbali, kana kwamba kuna umbali mrefu baina yao, na hawawezi kufanana kamwe, kana kwamba wametenganishwa na kitu kisichoonekana. Kwa hakika, hizi ni fikra za uongo ambazo Roho amempa mwanadamu, ambayo ndiyo sababu Roho na mwanadamu sio wa aina moja, na Roho na mwanadamu hawawezi kuishi pamoja katika ulimwengu mmoja, na kwa sababu Roho hana kitu chochote cha mwanadamu. Kwa hivyo mwanadamu hana haja ya Roho, maana Roho hawezi kufanya kazi inayohitajika sana na mwanadamu moja kwa moja. Kazi ya mwili inampatia mwanadamu malengo halisi ya kufuata, maneno halisi, na hisia kwamba Yeye ni halisi na wa kawaida, kwamba ni mnyenyekevu na wa kawaida. Ingawa mwanadamu anaweza kumwogopa, kwa watu wengi Yeye ni rahisi kuhusiana naye: Mwanadamu anaweza kuuona uso Wake, na kuisikia sauti Yake, na hahitaji kumwangalia kwa kutokea mbali. Mwanadamu anahisi kuwa ni rahisi kuufikia mwili huu, sio wa mbali au usioeleweka, bali unaoonekana na kushikika, maana mwili huu upo katika ulimwengu mmoja na mwanadamu.
Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha tabia zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza inapaswa iondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanahitajika kutupilia mbali tabia yao iliyopotoka, kwanza wanapaswa kujua tabia yao iliyopotoka. Ikiwa mwanadamu anafanya kazi ili kuondoa taswira za Miungu wasio dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu wasio dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kuwekwa hadharani, kutupwa, au kufukuzwa kabisa kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu ndiyo inayoweza kuchukua nafasi ya vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza ili kuwaruhusu watu kuvielewa taratibu, na ni kwa njia hii pekee ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. Mwanadamu anatambua kwamba Mungu aliyekuwa anamtafuta huko nyuma ni asiye dhahiri na wa kimiujiza. Kile ambacho kinaweza kufanikisha matokeo haya sio uongozi wa moja kwa moja wa Roho, sembuse mafundisho ya mtu fulani, bali ni Mungu mwenye mwili. Dhana za mwanadamu zinakuwa wazi pale ambapo Mungu mwenye mwili atafanya kazi Yake rasmi, kwa sababu ukawaida na uhalisi wa Mungu mwenye mwili ni kinyume na nadharia za Mungu asiye dhahiri na wa kufikirika katika fikra za mwanadamu. Dhana asili za mwanadamu zinaweza tu kudhihirishwa kupitia tofauti zao na Mungu mwenye mwili. Bila ulinganisho na Mungu mwenye mwili, dhana za mwanadamu zisingefichuliwa; kwa maneno mengine, bila tofauti ya uhalisi vitu visivyo dhahiri visingefichuliwa. Hakuna anayeweza kutumia maneno ili kufanya kazi hii, na hakuna anayeweza kuizungumzia kazi hii kwa kutumia maneno. Ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni pevu kiasi gani, hawezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kumjua Mungu zaidi kwa utendaji, na anaweza tu kumwona kwa uwazi zaidi, ikiwa Mungu binafsi anafanya kazi miongoni mwanadamu na anaonyesha kikamilifu sura Yake na uungu Wake. Athari hii haiwezi kupatwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili. Bila shaka, Roho wa Mungu pia hawezi kupata matokeo haya. Mungu anaweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika ushawishi wa Shetani, lakini kazi hii haiwezi kukamilishwa moja kwa moja na Roho wa Mungu; badala yake, inaweza kufanywa tu na mwili ambao Roho wa Mungu anauvaa, na mwili wa Mungu mwenye mwili. Mwili huu ni mwanadamu na pia ni Mungu, ni mwanadamu aliye katika ubinadamu wa kawaida na pia ni Mungu ambaye ana uungu wote. Na hivyo, hata kama mwili huu sio Roho wa Mungu, na unatofautiana kwa kiasi kikubwa na Roho, bado ni Mungu mwenye mwili Mwenyewe ambaye Anamwokoa mwanadamu, ambaye ni Roho, pia ni mwili. Haijalishi Anaitwa majina gani, hatimaye bado ni Mungu Mwenyewe anayemwokoa mwanadamu. Maana Roho wa Mungu hatenganishwi na mwili, na kazi ya mwili pia ni kazi ya Roho wa Mungu; ni kwamba tu kazi hii haifanywi kwa kutumia utambulisho wa Roho, lakini inafanywa kwa kutumia utambulisho wa mwili. Kazi inayotakiwa kufanywa moja kwa moja na Roho haihitaji kufanyika mwili, na kazi ambayo inahitaji mwili kuifanya haiwezi kufanywa moja kwa moja na Roho, na inaweza kufanywa tu na Mungu mwenye mwili. Hiki ndicho kinachohitajika kwa kazi hii, na ndicho kinachohitajika na mwanadamu aliyepotoka. Katika hatua tatu za kazi ya Mungu, ni hatua moja tu ndiyo iliyofanywa moja kwa moja na Roho, na hatua mbili zilizobaki zimechukuliwa na Mungu mwenye mwili, na hazifanywi moja kwa moja na Roho. Kazi ya Enzi ya Sheria iliyofanywa na Roho haikuhusisha kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu, na wala haikuwa na uhusiano wowote na maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu. Hata hivyo kazi ya Mungu mwenye mwili katika Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme, inahusisha tabia ya dhambi ya mwanadamu na maarifa yake juu ya Mungu, na ni sehemu ya maana na muhimu ya kazi ya wokovu. Kwa hiyo, mwanadamu aliyepotoka anahitaji zaidi wokovu wa Mungu mwenye mwili, na anahitaji zaidi kazi ya moja kwa moja ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anamhitaji Mungu mwenye mwili ili kumchunga, kumsaidia, kumnywesha maji, kumlisha, kumhukumu na kumwadibu, na anahitaji neema zaidi na wokovu mkubwa kutoka kwa Mungu mwenye mwili. Ni Mungu katika mwili pekee ndiye anayeweza kuwa msiri wa mwanadamu, mchungaji wa mwanadamu, msaada wa mwanadamu uliopo kila mara, na hii yote ni ulazima wa kufanyika mwili leo na katika nyakati za nyuma.
Mwanadamu amepotoshwa na Shetani, na yeye ndiye kiumbe wa juu kabisa kuliko viumbe wote wa Mungu, hivyo mwanadamu anahitaji wokovu wa Mungu. Mlengwa wa wokovu wa Mungu ni mwanadamu, si Shetani, na kile kitakachookolewa ni mwili wa mwanadamu, na roho ya mwanadamu, na si mwovu. Shetani ni mlengwa wa uharibifu wa Mungu, mwanadamu ni mlengwa wa wokovu wa Mungu, na mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, kwa hivyo kitu cha kwanza kuokolewa ni mwili wa mwanadamu. Mwili wa mwanadamu umepotoshwa kwa kiasi kikubwa, na umekuwa kitu cha kumpinga Mungu, ambacho kinapinga na kukana waziwazi uwepo wa Mungu. Mwili huu uliopotoka ni vigumu sana kushughulika nao, na hakuna kitu ambacho ni kigumu sana kushughulika nacho au kukibadilisha kuliko tabia potovu ya mwili. Shetani anaingia katika mwili wa mwanadamu ili kuchochea usumbufu, na anatumia mwili wa mwanadamu kuisumbua kazi ya Mungu, na kuharibu mpango wa Mungu, na hivyo mwanadamu amekuwa Shetani, na adui wa Mungu. Ili mwanadamu aweze kuokolewa, kwanza ni lazima achukuliwe mateka. Ni kwa sababu hii ndiyo maana Mungu anainuka na kuingia katika vita na Anaingia katika mwili ili afanye kazi ambayo Amekusudia kufanya, na kupambana na Shetani. Lengo Lake ni wokovu wa mwanadamu, mwanadamu ambaye amepotoshwa, na kushindwa na kuangamizwa kwa Shetani, ambaye ameasi dhidi Yake. Anamshinda Shetani kupitia kazi Yake ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo anamwokoa mwanadamu aliyepotoka. Hivyo, Mungu anatatua matatizo mawili kwa wakati mmoja. Anafanya kazi katika mwili, na Anazungumza katika mwili, na Anafanya kazi zote katika mwili ili aweze kujihusisha vizuri na mwanadamu, na kumdhibiti mwanadamu vizuri. Wakati wa mwisho ambapo Mungu atakuwa mwili, kazi Yake katika siku za mwisho itahitimishwa katika mwili. Atawaainisha wanadamu wote kulingana na aina, na kuhitimisha usimamizi wake wote, na pia kuhitimisha kazi Yake yote katika mwili. Baada ya kazi Yake yote duniani kuisha, Atakuwa mshindi kikamilifu. Kufanya kazi katika mwili, Mungu atakuwa amemshinda mwanadamu kikamilifu na atakuwa amempata mwanadamu kikamilifu. Hii haimaanishi kuwa usimamizi Wake wote utakuwa umekoma? Mungu anapohitimisha kazi Yake katika mwili, ilivyo kwamba Amemshinda Shetani kikamilifu, na Amekuwa mshindi, Shetani hatakuwa na fursa zaidi ya kumpotosha mwanadamu. Kazi ya Mungu mwenye mwili wa kwanza ilikuwa ni wokovu na msamaha wa dhambi za mwanadamu. Sasa ni kazi ya kumshinda na kumpata mwanadamu, ili kwamba Shetani asiweze tena kufanya kazi yake, na atakuwa amepotea kabisa, na Mungu atakuwa ameshinda kabisa. Hii ni kazi ya mwili, na ni kazi inayofanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya awali ya hatua tatu za kazi ya Mungu ilifanywa moja kwa moja na Roho, na wala si mwili. Hata hivyo, kazi ya mwisho ya hatua tatu za kazi ya Mungu, inafanywa na Mungu mwenye mwili, na wala haifanywi moja kwa moja na Roho. Kazi ya ukombozi ya hatua ya katikati pia imefanywa na Mungu mwenye mwili. Katika kazi yote ya usimamizi, kazi muhimu sana ni wokovu kutoka katika ushawishi wa Shetani. Kazi muhimu ni kumshinda kabisa mwanadamu aliyepotoka, na hivyo kurejesha heshima ya awali ya Mungu katika moyo wa mwanadamu, na kumruhusu kufikia maisha ya kawaida, ni sawa na kusema, maisha ya kawaida ya kiumbe wa Mungu. Kazi hii ni muhimu, na ni kiini cha kazi ya usimamizi. Katika hatua tatu za kazi ya wokovu, hatua ya kwanza ya kazi ya Enzi ya Sheria inatofautiana sana na kiini cha kazi ya usimamizi; ilikuwa tu ina kuonekana kwa mbali kwa kazi ya wokovu, na haikuwa mwanzo wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Hatua ya kwanza ya kazi ilifanywa na Roho kwa sababu, chini ya sheria, mwanadamu alijua tu kuzishika sheria, na hakuwa na ukweli zaidi, na kwa sababu kazi katika Enzi ya Sheria haikujihusisha na kubadilisha tabia ya mwanadamu, sembuse haikuwa inajihusisha na kazi ya jinsi ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Roho wa Mungu alikamilisha hatua hii rahisi ya kazi ambayo haikujihusisha na tabia iliyopotoka ya mwanadamu. Hatua hii ya kazi ilikuwa na uhusiano mdogo na kiini cha usimamizi na haikuwa na uhusiano mkubwa na kazi rasmi ya wokovu wa mwanadamu, na kwa hivyo haikumhitaji Mungu ili aweze kuifanya kazi Yake. Kazi inayofanywa na Roho ni mdokezo na haifahamiki, na ya kuogopesha na isiyofikiwa kwa mwanadamu; Roho hafai kikamilifu kwa ajili ya kufanya kazi ya wokovu moja kwa moja, na hafai kikamilifu kwa ajili ya kumpa mwanadamu uzima moja kwa moja. Kinachomfaa zaidi mwanadamu ni kubadilisha kazi ya Roho na kuwa katika hali ambayo inamkaribia mwanadamu, yaani, kile kinachomfaa mwanadamu zaidi ni Mungu kuwa mtu wa kawaida ili kufanya kazi Yake. Hili linahitaji Mungu apate mwili ili kuchukua kazi ya Roho, na kwa mwanadamu, hakuna njia inayofaa zaidi ya Mungu kufanya kazi. Kati ya hatua hizi tatu za kazi, hatua mbili zinafanywa na mwili, na hatua hizi mbili ni awamu muhimu ya kazi ya usimamizi. Kupata mwili huku kuwili kunakamilishana na kuafikiana. Hatua ya kwanza ya Mungu mwenye mwili iliweka msingi kwa ajili ya hatua ya pili, na tunaweza kusema kwamba kupata mwili huku kuwili kwa Mungu kunafanya hatua moja, na zote hazina ulinganifu. Hatua mbili hizi za kazi ya Mungu zinafanywa na Mungu katika utambulisho Wake katika mwili kwa sababu zina umuhimu sana katika kazi nzima ya usimamizi. Inaweza kusemwa kuwa, bila kazi ya Mungu mwenye mwili katika hatua mbili hizi, kazi nzima ya usimamizi ingefikia kikomo kwa ghafla, na kazi ya kumwokoa mwanadamu isingekuwa kitu isipokuwa maneno matupu. Haijalishi kazi hii ni muhimu au si muhimu lakini imejikita katika mahitaji ya mwanadamu, na uhalisi wa upotovu wa mwanadamu, na uzito wa kutotii kwa Shetani na usumbufu wake katika kazi. Mhusika sahihi anayeifanya kazi ametabiriwa na asili ya kazi yake, na umuhimu wa kazi. Unapokuja umuhimu wa kazi hii, kwa misingi ya mbinu ya kutumia—kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, au kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili, au kazi inayofanywa kupitia mwanadamu—ya kwanza kuondolewa ni kazi inayofanywa kupitia mwanadamu, na kulingana na asili ya kazi, na asili ya kazi ya Roho dhidi ya ile ya mwili, hatimaye inaamuliwa kwamba kazi inayofanywa na mwili ni ya manufaa zaidi kwa mwanadamu kuliko kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na inakuwa na manufaa zaidi. Hili ni wazo la Mungu wakati wa kuamua ama kazi ifanywe na Roho au ifanywe na mwili. Kuna umuhimu na msingi katika kila hatua ya kazi. Siyo fikra tu zisizo na msingi, na wala hazifanywi kiholela; kuna hekima fulani ndani yake. Huo ndio ukweli wa kazi zote za Mungu. Hasa, kuna mpango wa Mungu zaidi katika kazi kubwa kama hiyo kwa kuwa Mungu mwenye mwili akifanya kazi miongoni mwa wanadamu. Na kwa hivyo, hekima ya Mungu na uungu Wake wote unaakisiwa katika kila tendo Lake, fikira, na wazo katika kufanya kazi; huu ndio uungu wa Mungu ambao uko imara na wenye mpangilio. Fikira hizi na mawazo pembuzi ni ngumu kwa mwanadamu kuwaza, na mambo magumu kwa mwanadamu kuamini, aidha, magumu kwa mwanadamu kuyafahamu. Kazi inayofanywa na mwanadamu ni kulingana na kanuni ya ujumla, ambayo, kwa mwanadamu, ni ya kuridhisha sana. Lakini ikilinganisha na kazi ya Mungu, kuna tofauti kubwa sana; ingawa matendo ya Mungu ni makuu na kazi ya Mungu ni ya kiwango cha juu sana, nyuma yake kuna mipango na mipangilio midogo ya uhakika ambayo haiwezi kufikirika kwa mwanadamu. Kila hatua ya kazi Yake sio kulingana na kanuni tu, lakini pia inajumuisha vitu vingi ambavyo haviwezi kusemwa kwa lugha ya kibinadamu, na haya ni mambo ambayo hayaonekani kwa mwanadamu. Bila kujali kama ni kazi ya Roho au kazi ya Mungu mwenye mwili, kila kazi inajumuisha mpango wa kazi Yake. Hafanyi kazi bila kuwa na msingi, na hafanyi kazi isiyokuwa na maana. Roho anapofanya kazi moja kwa moja, ni kwa malengo Yake, na Anapokuwa mwanadamu (ambayo ni sawa na kusema, Anapobadilisha ganda Lake la nje) kufanya kazi, ni zaidi hata na lengo Lake. Kwa sababu ipi nyingine Abadilishe utambulisho Wake vivi hivi tu? Kwa sababu ipi nyingine Abadilike awe mtu ambaye anachukuliwa kuwa ni duni na kuteswa?
Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo Atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo hakungekuwa kazi ya hukumu. Je, upotovu wa wanadamu wote si ni sawa? Je, kiini cha wanadamu wote hakifanani? Kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu kilichopotoka, kiini cha mwanadamu kilichopotoshwa na Shetani, na dhambi zote za mwanadamu. Mungu hahukumu makosa madogo madogo ya mwanadamu na yasiyokuwa na umuhimu. Kazi ya hukumu ni ya uwakilishi, na haifanywi mahususi kwa ajili ya mtu fulani. Badala yake, ni kazi ambayo kwayo kundi la watu wanahukumiwa ili kuiwakilisha hukumu ya wanadamu wote. Kwa Yeye mwenyewe kufanya kazi Yake katika kundi la watu, Mungu mwenye mwili anatumia kazi Yake ili kuwakilisha kazi ya wanadamu wote, ambayo inaenea taratibu. Kazi ya hukumu pia iko hivyo. Mungu hahukumu aina fulani ya mtu au kundi fulani la watu, bali anawahukumu wasio na haki wote miongoni mwa wanadamu—upinzani wa mwanadamu kwa Mungu, kwa mfano, au mwanadamu kutomcha Yeye, au kusababisha usumbufu katika kazi ya Mungu, na kadhalika. Kile kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu cha kumpinga Mungu, na kazi hii ni kazi ya ushindi ya siku za mwisho. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili lililoshuhudiwa na mwanadamu ni kazi ya hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi wakati wa siku za mwisho, ambacho kilibuniwa na mwanadamu katika kipindi cha siku za nyuma. Kazi ambayo sasa inafanywa na Mungu mwenye mwili ni hukumu yenyewe mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu mwenye mwili wa leo ni Yule Mungu anayewahukumu wanadamu wote wakati wa siku za mwisho. Mwili huu na kazi, neno, na tabia Yake yote, vyote ni ujumla Wake. Ingawa mawanda ya kazi Yake ni finyu, na hayahusishi moja kwa moja ulimwengu wote, kiini cha kazi ya hukumu ni hukumu ya moja kwa moja kwa wanadamu wote; si kazi inayofanywa kwa ajili ya Uchina tu, au kwa idadi ndogo ya watu. Wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, ingawa mawanda ya kazi hii hayahusishi ulimwengu mzima, inawakilisha kazi ya ulimwengu mzima na, baada ya kuhitimisha kazi ndani ya mawanda ya mwili Wake, Ataipanua kazi hii mara moja katika ulimwengu mzima, kwa namna ile ile, injili ya Yesu ilienea ulimwengu mzima baada ya kufufuka Kwake na kupaa mbinguni. Bila kujali endapo ni kazi ya Roho au ni kazi ya mwili, ni kazi ambayo inafanywa ndani ya mawanda finyu, lakini ambayo inauwakilisha ulimwengu mzima. Wakati wa siku za mwisho, Mungu anaonekana kufanya kazi Yake kwa kutumia utambulisho Wake wa Mungu mwenye mwili, na Mungu mwenye mwili ni Mungu anayemhukumu mwanadamu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Bila kujali endapo ni Roho au mwili, Yule ambaye anafanya kazi ya hukumu ni Mungu anayemhukumu mwanadamu katika siku za mwisho. Hii inafasiliwa kwa kutegemeza kwa kazi Yake, na haifasiliwi kulingana na umbo Lake la nje au sababu nyinginezo. Ingawa mwanadamu ana dhana za maneno haya, hakuna anayeweza kukana ukweli wa hukumu ya Mungu mwenye mwili na kuwashinda wanadamu wote. Bila kujali ni jinsi gani binadamu anafikiri kuuhusu, ukweli ni, baada ya yote, ukweli tu. Hukuna anayeweza kusema “Kazi imefanywa na Mungu lakini mwili si Mungu.” Huu ni upuuzi, maana kazi hii haiwezi kufanywa na mtu yeyote isipokuwa Mungu mwenye mwili. Kwa kuwa kazi hii imekwishakamilika, kufuatia kazi hii, kazi ya hukumu ya Mungu kwa mwanadamu haitatokea kwa mara ya pili; Mungu mwenye mwili amekwishaikamilisha kazi yote ya usimamizi, na hakutakuwa na hatua ya nne ya kazi ya Mungu. Kwa sababu yule anayehukumiwa ni mwanadamu, mwanadamu ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa, na sio roho ya Shetani ambayo inahukumiwa moja kwa moja, kazi ya hukumu haifanywi katika ulimwengu wa roho, bali miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayefaa zaidi na anayestahili, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. Ikiwa hukumu ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, basi isingekuwa inajumuisha wote. Aidha, kazi kama hiyo itakuwa vigumu kwa mwanadamu kuikubali, maana Roho hawezi kukutana uso kwa uso na mwanadamu, na kwa sababu hii, matokeo hayawezi kuwa ya haraka, sembuse mwanadamu hataweza kuona kwa uwazi kabisa tabia ya Mungu isiyokosewa. Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali Yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye anayestahili, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana Ana ukweli, na mwenye haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine. Ikiwa kazi hii ingefanywa na Roho wa Mungu, basi usingekuwa ushindi dhidi ya Shetani. Roho kiasili huwa ameinuliwa sana kuliko viumbe wenye mwili wa kufa, na Roho wa Mungu ni mtakatifu kwa asili, na anaushinda mwili. Ikiwa Roho angefanya kazi hii moja kwa moja, Asingeweza kuhukumu kutotii kote kwa mwanadamu, na asingeweza kufichua hali nzima ya mwanadamu ya kutokuwa na haki. Kwa maana kazi ya hukumu pia inafanywa kwa mitazamo ya mwanadamu juu ya Mungu, na mwanadamu hajawahi kuwa na dhana yoyote juu ya Roho, na hivyo Roho hana uwezo wa kufunua hali ya mwanadamu ya kutokuwa na haki, wala kuweza kuweka wazi kabisa hali hiyo ya kutokuwa na haki. Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana za mwanadamu na kumpinga, Anafunua hali yote ya kutotii ya mwanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtii, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika mitazamo na kuwa na maarifa, na kutoka kukataliwa hadi upendo. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anaokolewa tu kwa kukubali hukumu Yake, bali hatua kwa hatua tu atamwelewa taratibu kupitia neno la mdomo Wake, ametwaliwa na Yeye wakati wa upinzani wake Kwake, na anapata uzima kutoka Kwake wakati wa kukubali kuadibu Kwake. Hii yote ni kazi ya Mungu mwenye mwili, na sio kazi ya Mungu katika utambulisho Wake kama Roho. Kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili ni kazi kubwa sana, na ni kazi ya kina sana, na sehemu muhimu ya hatua tatu za kazi ya Mungu ni hatua mbili za kazi ya kupata mwili. Upotovu wa kina wa mwanadamu ni kikwazo kikubwa sana katika kazi ya Mungu mwenye mwili. Hasa, kazi inayofanywa kwa watu wa siku za mwisho ni ngumu sana, na mazingira ni ya uhasama, na ubora wa tabia ya kila aina ya mwanadamu ni duni sana. Lakini mwishoni mwa kazi hii, bado itapokea matokeo mazuri, bila dosari yoyote; haya ni matokeo ya kazi ya mwili, na matokeo haya yanashawishi sana kuliko kazi ile ya Roho. Hatua tatu za kazi ya Mungu zitahitimishwa katika mwili, na lazima zikamilishwe na Mungu mwenye mwili. Kazi muhimu sana imefanywa katika mwili, na wokovu wa mwanadamu ni lazima ufanywe na Mungu mwenye mwili. Ingawa binadamu wote wanahisi kwamba Mungu katika mwili hahusiani na mwanadamu, kwa kweli ni kuwa mwili huu unahusiana na majaliwa na uwepo wa wanadamu wote.
Kila hatua ya kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote, na inawalenga wanadamu wote. Ingawa ni kazi Yake katika mwili, bado inaelekezwa kwa binadamu wote; Yeye ni Mungu wa binadamu wote, na ni Mungu wa viumbe vyote vilivyoumbwa na ambavyo havijaumbwa. Ingawa kazi Yake katika mwili ipo ndani ya mawanda finyu, na kusudi la kazi hii pia lina mipaka, kila wakati Anapokuwa mwili kufanya kazi Yake, Yeye huchagua chombo cha kazi Yake ambacho ni wakilishi na ambacho kina uakilishi mkubwa; Hachagui kikundi cha watu wa kawaida na wasiosifika kwa ajili ya kuwafanyiza kazi, lakini badala yake huwachagua kama wawakilishi wa kazi Yake kundi la watu wenye uwezo kuwa wahusika wa kazi Yake katika mwili. Kundi hili la watu linachaguliwa kwa sababu ya mawanda ya kazi Yake katika mwili ni finyu, na wamejiandaa mahususi kwa ajili ya Kufanyika Kwake kuwa mwili, na limechaguliwa hasa kwa ajili ya kazi Yake katika mwili. Uchaguzi wa Mungu wa walengwa wa kazi Yake si usio na msingi, bali kulingana na kanuni: Mlengwa wa kazi anapaswa kuwa na manufaa katika kazi ya Mungu mwenye mwili, na anapaswa kuwa na uwezo wa kuwawakilisha wanadamu wote. Kwa mfano, Wayahudi waliweza kuwawakilisha binadamu wote katika kupokea wokovu binafsi wa Yesu, na Wachina wanaweza kuwawakilisha wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu mwenye mwili. Kuna msingi kwa Wayahudi kuwa wawakilishi wa binadamu wote, na kuna msingi kwa uwakilishi wa Wachina wa wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu. Hakuna kinachofichua maana ya ukombozi kuliko kazi ya ukombozi iliyofanywa miongoni mwa Wayahudi, na hakuna kinachofichua uhakika na mafanikio ya kazi ya ushindi kuliko kazi ya ushindi iliyofanywa miongoni mwa Wachina. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili vinaonekana kuelekezwa kwa kikundi kidogo tu cha watu, lakini kwa hakika, kazi Yake miongoni mwa kikundi hiki kidogo ni kazi ya ulimwengu wote, na neno Lake limeelekezwa kwa wanadamu wote. Baada ya kazi Yake katika mwili kufikia kikomo, wale wanaomfuata wataanza kueneza kazi ambayo Amefanya miongoni mwao. Kitu kizuri zaidi kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ya kusihi, na mapenzi Yake kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi Wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwepo na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambapo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya utendaji zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, Anamfunulia mwanadamu Mungu ambaye ni halisi na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonyesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, Anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, Anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na Anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili badala ya Roho wa Mungu. Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili Wake, wale wanaofuata wanakuwa hawatafuti tena vitu hivyo visivyo yakini, na wanaacha kukisia mapenzi ya Mungu asiye yakini. Mungu anapoeneza kazi Yake katika mwili, wale wanaomfuata wataieneza kazi ambayo Ameifanya katika mwili kwa dini na madhehebu yote, na watazungumza maneno Yake yote katika masikio ya wanadamu wote. Yote yale yanayosikizwa na wale wanaoipokea injili Yake yatakuwa ni ukweli wa kazi Yake, yatakuwa mambo ambayo mwanadamu ameyashuhudia na kuyaona binafsi, na utakuwa ukweli na sio uvumi. Ukweli huu ni ushahidi ambao Anauenezea kazi na pia ni zana ambazo Anazitumia katika kueneza kazi. Bila uwepo wa ukweli, injili Yake isingeweza kuenea katika nchi zote na maeneo yote; bila ukweli bali kwa fikira tu za mwanadamu, Asingeweza kufanya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Roho hagusiki na mwanadamu, na wala haonekani kuonekana na mwanadamu, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Mawazo ya mwanadamu, hata hivyo, ni matupu, na hayawezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; tabia ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekana na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye binafsi Anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia halisi ambayo Mungu anaonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwona Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili. Baada ya Mungu kufanya kazi Yake hadi hatua hii, kazi Yake tayari imeshafanikiwa kuwa na matokeo mazuri, na imekuwa ni mafanikio kamili. Kazi binafsi ya Mungu mwenye mwili tayari imekwishakamilisha asilimia tisini ya kazi ya usimamizi Wake mzima. Mwili umetoa mwanzo mzuri katika kazi Yake yote, na muhtasari kwa ajili ya kazi Yake yote, na umetangaza kazi Yake yote na Ameifanya ya mwisho kupitia ujazaji tena wa kazi hii yote. Kuanzia sasa, hakutakuwepo na Mungu mwingine katika mwili kwa ajili ya kufanya hatua ya nne ya kazi ya Mungu, na hakutakuwa na kazi ya miujiza zaidi ya kupata mwili kwa tatu kwa Mungu.
Kila hatua ya kazi ya Mungu katika mwili inawakilisha kazi Yake ya enzi yote, na haiwakilishi kipindi fulani kama kazi ya mwanadamu. Na hivyo mwisho wa kazi ya kufanyika Kwake mwili mara ya mwisho haimaanishi kwamba kazi Yake imefikia mwisho kabisa, kwa maana kazi Yake katika mwili inawakilisha enzi yote, na haiwakilishi kipindi tu ambacho Anafanya kazi Yake katika mwili tu. Ni kwamba tu Anakamilisha kazi Yake ya enzi yote wakati ambapo yupo katika mwili, ambayo baadaye inaenea sehemu zote. Baada ya Mungu mwenye mwili kutimiza huduma yake, atawakabidhi wale wote wanaoifuata kazi Yake ya baadaye. Kwa njia hii kazi Yake ya enzi yote itaendelezwa bila kusitishwa. Kazi ya enzi yote ya kufanyika kuwa mwili itachukuliwa tu kuwa imekamilika baada ya kuenea ulimwenguni kote. Kazi ya Mungu mwenye mwili huanzisha enzi mpya, na wale wanaoiendeleza kazi Yake ni watu wanaotumiwa naye. Kazi inayofanywa na mwanadamu yote ipo ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili, na haina uwezo wa kwenda zaidi ya mawanda haya. Ikiwa Mungu mwenye mwili haji kufanya kazi Yake, mwanadamu hana uwezo wa kuhitimisha enzi ya zamani, na hana uwezo wa kuikaribisha enzi mpya. Kazi inayofanywa na mwanadamu ipo tu ndani ya wajibu wake ambao unawezekana kibinadamu, na haiwakilishi kazi ya Mungu. Ni Mungu mwenye mwili pekee ndiye anayeweza kuja na kukamilisha kazi ambayo Anapaswa kuifanya, na mbali na Yeye, hakuna anayeweza kuifanya kazi hii badala Yake. Bila shaka, kile Ninachozungumzia ni kuhusiana na kazi ya kufanyika mwili. Huyu Mungu mwenye mwili, kwanza anachukua hatua ya kazi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu, baada ya hapo Anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu. Lengo la kazi hii ni kumshinda mwanadamu. Kwa upande mmoja, kupata mwili kwa Mungu hakupatani na dhana za mwanadamu, aidha, Anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na dhana za mwanadamu, na kwa hivyo mwanadamu anakuza mawazo zaidi ya kukosoa kumhusu. Anafanya kazi ya ushindi miongoni mwa wanadamu ambaye ana dhana nyingi sana kumhusu. Bila kujali jinsi wanavyomchukulia, Atakapokuwa amekamilisha huduma Yake, wanadamu wote watakuwa chini ya utawala Wake. Ukweli wa kazi hii hauonekani tu miongoni mwa Wachina, bali wao wanawakilisha namna ambavyo wanadamu wote watakavyoshindwa. Matokeo yanayoonekana kwa watu hawa ni kitangulizi cha matokeo yatakayoonekana kwa wanadamu wote, na matokeo ya kazi Anayofanya wakati ujao yatazidi sana matokeo kwa watu hawa. Kazi ya Mungu katika mwili haihusishi mshindo mkubwa wa tarumbeta, wala haijakita katika mafumbo. Ni halisi na ya kweli, na ni kazi ambayo moja kujumlisha na moja ni sawa sawa na mbili. Hajafichwa kwa mtu yeyote, na wala haimdanganyi mtu yeyote. Kile ambacho watu wanaona ni vitu halisi, na kile ambacho mwanadamu anapata ni ukweli halisi na maarifa. Kazi itakapokamilika, mwanadamu atakuwa na maarifa mapya juu Yake, na wale ambao kweli wanamtafuta Mungu hawatakuwa na dhana zozote juu Yake. Haya siyo tu matokeo ya kazi Yake kwa Wachina, lakini pia inawakilisha matokeo ya kazi Yake katika kuwashinda wanadamu wote, kwa maana hakuna kitu ambacho ni cha manufaa zaidi katika kazi ya kuwashinda watu kuliko mwili huu, na kazi ya mwili huu, na kila kitu cha mwili huu. Vina manufaa katika kazi Yake leo, na vina manufaa katika kazi Yake hapo baadaye. Mwili huu utawashinda wanadamu wote na utawapata wanadamu wote. Hakuna kazi bora zaidi ambayo kwayo wanadamu wote watamwona Mungu, na kumtii Mungu, na kumfahamu Mungu. Kazi inayofanywa na mwanadamu inawakilisha tu mawanda finyu, na Mungu anapofanya kazi Yake hazungumzi na watu fulani, bali Anazungumza na wanadamu wote, na wale wote wanaoikubali kazi Yake. Mwisho Anaoutangaza ni mwisho wa wanadamu wote, na sio mwisho wa mtu fulani tu. Hamtendei mtu yeyote kwa umahususi, wala hampendelei mtu yeyote, na Anafanya kazi kwa ajili ya, na Anazungumza na wanadamu wote. Na kwa hiyo Mungu huyu katika mwili amekwisha waainisha wanadamu wote kulingana na aina yao, tayari amekwisha wauhukumu wanadamu wote, na amekwishapangilia hatima inayofaa kwa wanadamu wote. Ingawa Mungu anafanya kazi Yake China tu, kwa hakika Ameshaamua kazi ya ulimwengu mzima. Hawezi kusubiri hadi kazi Yake itakapoenea miongoni mwa wanadamu wote kabla ya kutoa matamko Yake na kuweka mipango hatua kwa hatua. Hivyo, sio kwamba utakuwa umechelewa sana? Sasa Anaweza kabisa kukamilisha kazi ya wakati ujao kabla ya wakati huo. Kwa sababu Yule anayefanya kazi ni Mungu mwenye mwili, Anafanya kazi isiyokuwa na mipaka ndani ya mawanda yenye mipaka, na baadaye Atamfanya mwanadamu atekeleze jukumu ambalo mwanadamu anapaswa kulitekeleza; hii ni kanuni ya kazi Yake. Anaweza kuishi tu na mwanadamu kwa muda, na hawezi kuambatana na mwanadamu hadi kazi ya enzi zote itakapokamilika. Ni kwa sababu Yeye ni Mungu kwamba Yeye hutabiri kazi Yake ya Wakati ujao kabla ya wakati. Baada ya hapo, Atawaainisha wanadamu wote kulingana na aina kwa maneno Yake, na mwanadamu ataingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua kulingana na neno Lake. Hakuna atakayekwepa, na wote wanapaswa kutenda kulingana na hili. Hivyo, katika wakati ujao, enzi itaongozwa na maneno Yake, na sio kuongozwa na Roho.
Kazi ya Mungu katika mwili ni lazima ifanywe katika mwili. Kama ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu isingeweza kutoa matokeo yoyote. Hata kama ingefanywa na Roho, kazi hii isingekuwa na maana kubwa, na hatimaye isingekuwa na ushawishi. Viumbe vyote vinatamani kujua iwapo kazi ya Muumbaji ina maana, na inawakilisha kitu gani, na ni kwa ajili ya nini, na iwapo kazi ya Mungu ina mamlaka kamili na hekima, na endapo ina thamani na maana ya kina. Kazi Anayofanya ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote, kwa ajili ya kumshinda Shetani, na kwa kuwa na ushuhuda wa Mungu miongoni mwa vitu vyote. Hivyo, kazi Anayoifanya ni lazima iwe ya umuhimu mkubwa. Mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, na wengi wamepofushwa, na kuumizwa sana. Sababu muhimu sana ambayo inamfanya Mungu kufanya kazi katika mwili ni kwa sababu mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, ambaye ni wa mwili, na kwa sababu Shetani pia anatumia mwili wa mwanadamu kusumbua kazi ya Mungu. Vita na Shetani kwa hakika ni kazi ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo mwanadamu pia ni mlengwa wa wokovu wa Mungu. Kwa njia hii, kazi ya Mungu mwenye mwili ni muhimu. Shetani aliupotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu akawa mfano halisi wa Shetani, na akawa mlengwa wa kushindwa na Mungu. Kwa njia hii, kazi ya kupambana na Shetani na kumwokoa mwanadamu inatokea duniani, na Mungu ni lazima awe mwanadamu ili aweze kupambana na mwanadamu. Hii ni kazi yenye utendaji wa hali ya juu. Mungu anapofanya kazi katika mwili, kwa hakika Anapambana na Shetani katika mwili. Anapofanya kazi katika mwili, Anafanya kazi Yake katika ulimwengu wa kiroho, na Anafanya kazi Yake yote katika ufalme wa kiroho ili iwe halisi duniani. Anayeshindaniwa ni mwanadamu, asiye mtiifu Kwake, yule anayeshindwa ni mfano halisi wa Shetani (bila shaka, huyu pia ni mwanadamu), ambaye ana uadui na Yeye, na ambaye ataokolewa hatimaye ni mwanadamu. Kwa namna hii, ni muhimu zaidi Kwake kuwa mwanadamu ambaye ana ganda la nje la kiumbe, ili kwamba Awe na uwezo wa kupambana na Shetani katika uhalisi, kumshinda mwanadamu, ambaye si mtiifu Kwake na ambaye ana kuonekana kwa nje ambako kunafanana na Yeye, na kumwokoa mwanadamu, ambaye ana umbo la nje kama Lake na aliyeumizwa na Shetani. Adui Wake ni mwanadamu, mlengwa wa ushindi Wake ni mwanadamu, na mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, aliyeumbwa na Yeye. Hivyo ni lazima Awe mwanadamu, na kwa njia hii, kazi Yake inakuwa rahisi zaidi. Ana uwezo wa kumshinda Shetani na kumshinda mwanadamu, aidha, anaweza kumwokoa mwanadamu. Ingawa mwili huu ni wa kawaida na halisi, Yeye si mwili wa kawaida. Yeye si mwili ambao ni mwanadamu tu, bali mwili ambao una uanadamu na uungu. Hii ndiyo tofauti Yake na mwanadamu, na ni alama ya utambulisho wa Mungu. Ni mwili tu kama huu ndio unaweza kufanya kazi Anayokusudia kufanya, na kutimiza huduma ya Mungu katika mwili, na kukamilisha kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Isingekuwa hivyo, kazi Yake miongoni mwa wanadamu ingekuwa tupu na yenye dosari. Ingawa Mungu anaweza kupambana na roho wa Shetani na kuibuka mshindi, asili ya zamani ya mwanadamu aliyepotoka haiwezi kuondolewa, na wale ambao sio watiifu Kwake na wanaompinga hawawezi kuwa wahusika katika utawala Wake, ambayo kusema, Hawezi kamwe kumshinda mwanadamu, na hawezi kamwe kuwapata wanadamu wote. Kama kazi Yake duniani haiwezi kutatuliwa, basi usimamizi Wake hautafika mwisho, na wanadamu wote hawataweza kuingia katika pumziko. Kama Mungu hawezi kuingia katika pumziko pamoja na viumbe Wake wote, basi hakutakuwa na matokeo ya usimamizi huo, na utukufu wa Mungu kwa sababu hiyo utatoweka. Ingawa mwili Wake hauna mamlaka, kazi Anayofanya itapokea matokeo yake. Huu ndio mwelekeo usioepukika wa kazi Yake. Haijalishi kama mwili Wake una mamlaka au la, maadamu Ana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, basi Yeye ni Mungu Mwenyewe. Haijalishi mwili huu ni wa kawaida kiasi gani, Anaweza kufanya kazi Anayopaswa kufanya, maana mwili huu ni Mungu na wala si mwanadamu tu. Sababu ambayo mwili huu unaweza kufanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya ni kwamba kiini Chake cha ndani si kama cha mwanadamu yeyote yule, na sababu kuwa Anaweza kumwokoa mwanadamu ni kuwa utambulisho Wake ni tofauti na wa mwanadamu yeyote yule. Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu ni mwanadamu hata zaidi ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyepotoka, ambaye anaishi pamoja na Yeye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuweza kumpata mwanadamu kabisa. Kwa sababu hii, ingawa mwili huu ni wa kawaida, mchango Wake kwa wanadamu na umuhimu Wake katika uwepo wa mwanadamu kunamfanya Awe wa thamani zaidi, na thamani halisi na umuhimu wa mwili huu hauwezi kupimwa na mwanadamu yeyote. Ingawa mwili huu hauwezi kumwangamiza Shetani moja kwa moja, Anaweza kutumia kazi Yake kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, na kumfanya Shetani kutii kikamilifu katika utawala Wake. Ni kwa sababu Mungu amepata mwili ili kwamba Aweze kumshinda Shetani na aweze kumwokoa binadamu. Hamwangamizi Shetani moja kwa moja, bali Anakuwa mwili ili kuweza kufanya kazi ya kumshinda binadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Kwa njia hii, Anakuwa na uwezo zaidi wa kuwa ushuhuda Kwake Mwenyewe miongoni mwa viumbe, na Anakuwa na uwezo zaidi wa kumwokoa mwanadamu aliyepotea. Ushindi wa Mungu mwenye mwili dhidi ya Shetani unabeba ushuhuda mkubwa, na una ushawishi mkubwa, kuliko uangamizaji wa Shetani wa moja kwa moja na Roho wa Mungu. Mungu katika mwili Ana uwezo zaidi wa kumsaidia mwanadamu kumjua Muumba, na Ana uwezo zaidi wa kuwa na ushuhuda Wake mwenyewe miongoni mwa viumbe.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumatano, 3 Aprili 2019

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe. Huzuni iliyoje! Kuokolewa kwa mwanadamu hakuwezi kutenganishwa na usimamizi wa Mungu, aidha hakuwezi kutenganishwa na mipango ya Mungu. Na bado mwanadamu hafikirii chochote kuhusu usimamizi wa Mungu, na hivyo anaendelea kujitenga mbali na Mungu. Kutokana na hayo, idadi ya watu wanaomfuata Mungu inaendelea kuongezeka bila kujua mambo yanayohusiana na kuokolewa kwa mwanadamu kama vile uumbaji ni nini, kuamini kwa Mungu ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na kadhalika. Kufikia sasa, basi, lazima tuzungumze kuhusu usimamizi wa Mungu, ndiposa kila mfuasi ajue wazi umuhimu wa kumfuata Mungu na kumwamini. Watakuwa na uwezo wa kuchagua njia watakayoifuata ipasavyo, badala ya kumfuata Mungu tu ili kupata baraka, au kuepukana na majanga, au kuwa na mafanikio.
Japo usimamizi wa Mungu waweza kuonekana mkubwa kwa mwanadamu, si jambo la kutofahamika kwa mwanadamu, kwa kuwa kazi yote ya Mungu imefungamanishwa na usimamizi wake, inahusiana na Kazi ya kuokoa mwanadamu, na inajishughulisha na maisha, kuishi, na hatima ya wanadamu. Kazi ambayo Mungu Anaifanya kati ya na kwa mwanadamu, yaweza kusemwa kuwa, ni ya utendaji na yenye maana kubwa. Inaweza kuonekana na mwanadamu, kuhusishwa na mwanadamu, na iko mbali na dhahania. Kama mwanadamu hana uwezo wa kukubali kazi zote Anazozifanya Mungu, basi ni upi umuhimu wa kazi hii? Na ni vipi usimamizi huu unaweza kusababisha kuokolewa kwa mwanadamu? Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu: kupata baraka, na ni wazembe sana kuhudhuria chochote ambacho hakihusiani na nia hii. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, acha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia yao, hata hivyo, inastahili sana sisi kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila kukubali na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.
Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi. Hata kama watu watafahamu jinsi walivyo wa kuhurumiwa, wenye chuki na walivyo ovyo, ni wangapi hapo ambao wanaweza kuachana na ukamilifu na matumaini yao? Na ni nani anayeweza kusimamisha hatua zake na kuacha kujifikiria yeye mwenyewe? Mungu Anawahitaji wale watakaojihusisha kwa karibu Naye kukamilisha usimamizi Wake. Anawahitaji wale ambao watatoa mawazo yao na mwili kwa ajili ya kazi Yake ya usimamizi ili kujitoa Kwake; Hawahitaji wale watakaoinua mikono yao na kuomba kutoka Kwake kila siku, na hata wale wanaotoa kidogo na kusubiri kulipwa kwa hilo tendo la kutoa. Mungu Anawadharau wale wanaotoa michango kidogo na kuridhika. Anawachukia wenye roho katili ambao hukataa kazi ya usimamizi Wake na hutaka tu kuongea kuhusu kwenda mbinguni na kupata baraka. Anachukia hata zaidi na wale ambao hufaidika na fursa inayowezeshwa na kazi Anayoifanya katika kuokoa wanadamu. Hii ni kwa sababu hawa watu hawajawahi kushughulishwa na Anachotarajia kupata Mungu kutokana na kazi Yake ya usimamizi. Wanashughulishwa tu na jinsi wanavyoweza kutumia hiyo fursa iliyowezeshwa na kazi ya Mungu ili kupata baraka. Hawajali roho Yake Mungu, kwa kuwa wanajishughulisha na mustakabali na hatima yao. Wale ambao wanakataa kazi ya usimamizi wa Mungu na hawana hata tamanio dogo katika jinsi Mungu Anavyowaokoa wanadamu na mapenzi Yake, wote wanafanya wapendavyo kando na kazi ya usimamizi wa Mungu. Tabia yao haitawaliwi na Mungu, na haikubaliwi na Mungu, na hata haiangaliwi kwa fadhila ya Mungu.
Ni viumbe wangapi wanaoishi na kuzaana katika ulimwengu mpana, wakifuata sheria ya maisha tena na tena, wakifuata sheria isiyobadilika. Wanaokufa huenda na hadithi za walio hai, na walio hai hurudia historia hii yenye huzuni ya wale waliokufa. Na kwa hivyo wanadamu hawawezi kujizuia ila kujiuliza wenyewe; Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii? Na ni nani muumbaji wa mwanadamu? Je, kweli wanadamu waliumbwa na mazingira asilia? Je, kweli wanadamu wana uamuzi juu ya hatima yao? ... Kwa maelfu ya miaka wanadamu wameyauliza haya maswali, tena na tena. Kwa bahati mbaya, jinsi wanadamu wanavyopagawa na haya maswali, ndivyo kiu yao ya sayansi huendelea kukua. Sayansi hupatiana kutosheleza kwa muda na raha ya muda ya mwili, ila haitoshi kumpa mwanadamu uhuru kutokana na upweke, ukiwa, na hofu isiyodhihirika na kutosaidika ndani ya moyo wake. Wanadamu hutumia ujuzi wa kisayansi unaoweza kuonekana kwa macho na ambao akili zaweza kuufahamu kutuliza moyo wake. Na bado ujuzi wa kisayansi kama huu hauwezi kuwazuia wanadamu kutafiti yasiyofahamika. Wanadamu hawajui ni nani Mkuu wa kila kitu katika ulimwengu huu, aidha hajui mwanzo na mustakabali wa wanadamu. Wanadamu wanaishi tu, bila budi, katikati ya hii sheria. Hakuna anayeweza kuiepuka wala kuibadilisha kwani katika vitu vyote na katika mbingu kuna Mmoja kutoka milele hadi milele ambaye ni Mkuu wa kila kitu. Ni Yeye ambaye Hajawahi kuonekana na mwanadamu, ambaye wanadamu hawajawahi kumjua, ambaye wanadamu hawajawahi kuamini kuwepo Kwake, na bado ni Yeye Aliyewapulizia pumzi mababu wa wanadamu na kuwapa wanadamu uhai. Ni Yeye ndiye Huruzuku na kustawisha wanadamu kwa kuishi kwao, na huwaongoza wanadamu hadi siku ya leo. Aidha, Yeye na Yeye pekee ni wa kutegemewa na wanadamu ili kuendelea kuishi. Ni Mkuu wa kila kitu na Hutawala viumbe vyote vyenye uhai chini ya dunia. Huamrisha misimu yote minne, na ni Yeye huita upepo, jalidi, theluji na mvua. Huwapa wanadamu mwangaza wa jua na huleta machweo ya jioni. Ni Yeye Aliyeumba mbingu na ardhi, Akampa mwanadamu milima, maziwa na mito na kila kitu kilicho na uhai ndani yake. Matendo Yake yamo kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. Kila mojawapo ya hizi sheria na kanuni ni mfano mzuri wa matendo Yake, na kila mojawapo inafichua hekima na mamlaka Yake. Nani anayeweza kujiondoa kutoka kwa ukuu Wake? Na ni nani anayeweza kujitoa mwenyewe katika njia Zake? Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma. Bila kujali kama unaweza kutambua vitendo vya Mungu, bila kujali kama unaamini katika kuwepo kwa Mungu, hakuna shaka kuwa hatima yako inaegemea katika mipango ya Mungu, na hakuna shaka kuwa Mungu atakuwa na ukuu juu ya kila kitu. Uwepo na utawala Wake haviwezi kutabiriwa ikiwa vinatambulika na kufahamika na binadamu au la. Ni Yeye pekee Anayejua kuhusu yaliyopita ya mwanadamu, yaliyomo na yanayojiri, na Yeye pekee ndiye mwamuzi wa hatima ya wanadamu. Haijalishi kama unaukubali huu ukweli, haitachukua muda mrefu kabla mwanadamu kushuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe, na huu ni ukweli ambao hivi karibu Mungu Ataudhihirisha. Wanadamu huishi na hufa chini ya macho yake Mungu. Wanadamu huishi kwa usimamizi wa Mungu, na wakati macho Yake yatafumbika kwa mara ya mwisho, hio pia ni kwa usimamizi Wake. Tena na tena, mwanadamu huja na kwenda, nyuma na mbele. Bila mapendeleo, yote ni sehemu ya ukuu na michoro ya Mungu. Usimamizi wa Mungu ungali unaendelea mbele na haujawahi kusimama. Atawafanya wanadamu wafahamu uwepo Wake, waamini katika ukuu Wake, watazame matendo Yake, na warudi katika ufalme Wake. Huu ni mpango Wake, na kazi ambayo Amekuwa Akiitekeleza kwa maelfu ya miaka.
Kazi ya usimamizi wa Mungu ilianza Alipoumba ulimwengu, na mwanadamu ni kiini cha kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa kila kitu, unaweza kusemwa, ni kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu Kazi ya usimamizi Wake imesambaa katika maelfu ya miaka, na haijatekelezwa katika dakika na sekunde tu, ama kufumba na kufumbua, ama katika mwaka mmoja au miwili, ilimbidi Aumbe vitu vingine zaidi kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, kama vile jua, mwezi, na aina zote za viumbe walio hai, na chakula na mazingira kwa ajili ya wanadamu. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa usimamizi wa Mungu.
Baada ya hapo, Mungu Alimkabidhi mwanadamu kwa Shetani, mwanadamu aliishi chini ya miliki ya Shetani, na hili taratibu lilisababisha kazi ya Mungu ya enzi ya kwanza: hadithi ya Enzi ya Sheria.... Kipindi cha miaka elfu kadhaa za Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wazoefu wa maelekezo ya Enzi ya Sheria, na wakaanza kupuuza, na taratibu wakaacha ulinzi wa Mungu. Na hivyo, pamoja na kushikilia sheria, walimwabudu Mungu na kutenda matendo maovu. Walikuwa bila ulinzi wa Yehova, na waliishi tu mbele ya madhabahu ndani ya hekalu. Kwa kweli, Kazi ya Mungu ilikuwa imejitenga nao kitambo sana, na hata kama Waisraeli walijikita katika sheria, na kulitaja jina la Yehova, na kwa majivuno kuamini kuwa wao pekee ndio walikuwa watu wa Yehova na walikuwa wamechaguliwa na Yehova, utukufu wa Mungu uliwaacha kimyakimya …
Mungu Anapofanya kazi Yake, huacha sehemu moja na taratibu hutekeleza kazi Yake katika sehemu nyingine mpya. Hii huonekana ya kiajabu sana kwa watu ambao wamepooza. Watu wameishi kuvithamini vya zamani na kuvirejelea vipya, vitu visivyofahamika kwa uhasama, au hata kuonekana kama bughudha. Aidha, kazi yoyote mpya Aifanyayo Mungu, kutoka mwanzo hadi mwisho, mwanadamu ndiye huwa wa mwisho kufahamu kuihusu miongoni mwa kila kitu.
Kama ilivyokuwa kawaida, baada ya kazi ya Yehova katika Enzi ya Sheria, Mungu Alianza kazi yake ya hatua ya pili: kwa kuutwaa mwili—kuwa na mwili kama binadamu kwa miaka kumi, ishirini—na kuongea na kufanya kazi Yake Kati ya waumini. Na bado bila mapendeleo, hakuna aliyejua, na ni idadi ndogo tu ya watu walitambua kuwa Alikuwa Mungu Aliyepata mwili baada ya Yesu Kristo kupigiliwa misumari msalabani na kufufuka. Kwa taabu, palitokea mmoja aliyeitwa Paulo, aliyejitolea kuwa adui wa kuua watu wa Mungu. Hata baada ya kuangushwa chini na kuwa mtume, hali yake ya zamani haikubadilika, na alitembea njia ya kumpinga Mungu. Wakati alipofanya kazi, Paulo aliandika barua nyingi; kwa bahati mbaya, vizazi vya baadaye vilifurahia barua zake kama maneno ya Mungu, kiasi kwamba ziliwekwa ndani ya Agano Jipya na kutatizana na maneno yaliyosemwa na Mungu. Hii kwa kweli ni aibu kubwa tangu majilio ya Maandiko Matakatifu! Na je, hili kosa halikutendwa na mwanadamu kutokana na upumbavu wake? Hawakujua kuwa, katika rekodi za kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema, barua na maandiko matakatifu ya mwanadamu hayafai kuwa hapo kuiga kazi na maneno ya Mungu. Lakini hii ni kando na hoja, acha turejelee mada ya awali. Baada tu ya kazi ya Mungu katika hatua ya pili kukamilika—baada ya kusulubishwa—kazi ya Mungu ya kutoa mwanadamu kwenye dhambi (ambayo ni kusema, kumtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani) ilitimilika. Na hivyo, kutoka wakati huo kuendelea mbele, wanadamu walipaswa tu kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi ili dhambi zao ziweze kusamehewa. Yaani, dhambi za wanadamu hazikuwa tena kizuizi cha kuufikia wokovu wake na kuja mbele za Mungu na hazikuwa tena nguvu za kushawishi ambazo Shetani alitumia kumlaumu mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe Alikuwa Amefanya kazi halisi, na kuwa katika mfano na limbuko la mwili wenye dhambi, na Mungu mwenyewe Alikuwa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, mwanadamu alishuka kutoka msalabani, akiwa amekombolewa na mwili wa Mungu, mfano wa huu mwili wa dhambi. Na hivyo, baada ya kushikwa mateka na Shetani, mwanadamu alikuja hatua moja mbele karibu na kukubali wokovu mbele za Mungu. Kwa hakika, huu ulingo wa kazi ndio ulikuwa usimamizi wa Mungu ambao ulikuwa hatua moja mbali na Enzi ya sheria, na wa kiwango cha ndani kuliko Enzi ya Sheria.
Huu ni mfano wa usimamizi wa Mungu: kuwakabidhi wanadamu kwa Shetani—wanadamu ambao hawajui kile Mungu Alicho, Muumba ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na ni kwa nini inafaa kujitoa kwa Mungu—na kutoa utawala huru kwa uovu wa Shetani. Hatua baada ya hatua, Mungu Anamtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani, hadi mwanadamu amwabudu Mungu kikamilifu na kumkataa Shetani. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Hili linasikika kama hadithi ya visasili; na inaonekana inatatanisha. Watu wanahisi kwamba ni kama hadithi ya visasili, na hii ni kwa sababu hawana fununu kuhusu yaliyomtokea mwanadamu katika maelfu ya miaka iliyopita, hata hawajui ni hadithi ngapi ambazo zimetokea katika huu ulimwengu. Na zaidi ya hayo, hii ni kwa sababu hawawezi kufahamu kinachostaajabisha sana, dunia inayoibua hofu zaidi ambayo iko zaidi ya dunia yakinifu, lakini ambayo macho yao ya mwili yanawazuia kuiona. Inasikika ya kutofahamika kwa mwanadamu. Na hii ni kwa sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Hujua kisichopendeza na jinsi kinavyotofautiana na kile kilicho kitakatifu, na hutambua ukubwa wa Mungu na uovu wa Shetani. Wanadamu kama hawa hawatamfanyia Shetani kazi tena, au kumwabudu Shetani, au kumsetiri Shetani. Hii ni kwa sababu wao ni kikundi cha watu ambao wamemilikiwa na Mungu. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuwasimamia wanadamu. Katika kazi ya usimamizi wa Mungu wa wakati huu, wanadamu ndio chombo cha maovu ya Shetani, na kwa wakati uo huo ni chombo cha ukombozi wa Mungu, aidha ni sababu ya vita dhidi ya Mungu na Shetani. Wakati sawia na wakati wa kutekeleza kazi Yake, Mungu taratibu Humtoa mwanadamu kutoka mikononi mwa Shetani, na hivyo mwanadamu anakuja karibu zaidi na Mungu ...
Baadaye kukaja Enzi ya Ufalme, ambayo ni hatua ya utendaji zaidi na bado ni ngumu zaidi kukubalika na mwanadamu. Hii ni kwa sababu jinsi mwanadamu ajavyo karibu na Mungu, ndivyo afikapo karibu na kiboko cha Mungu, na ndivyo uso wa Mungu unavyokuwa wazi mbele ya mwanadamu. Kwa kufuatia kukombolewa kwa wanadamu, mwanadamu kirasmi anarejelea familia ya Mungu. Mwanadamu alifikiria kuwa huu ndio wakati wa kufurahia, bado ameegemezwa kwa shambulizi la Mungu na mifano ya yale ambayo bado hayajaonekana na yeyote: Inavyokuwa, huu ni ubatizo ambao watu wa Mungu wanapaswa “kuufurahia.” Katika muktadha huo, watu hawana lingine ila kuacha na kujifikiria wao wenyewe, Mimi ndimi mwanakondoo, aliyepotea kwa miaka mingi, ambaye Mungu Amegharamika kumnunua, sasa kwa nini Mungu Ananitendea hivi? Ama ni njia ya Mungu kunicheka, na kunifichua? ... Baada ya miaka mingi kupita, mwanadamu amedhoofika, kwa kuupitia ugumu wa usafishaji na kuadibu. Ijapokuwa mwanadamu amepoteza “utukufu” na “mapenzi” ya wakati uliopita, bila ya kufahamu amekuja kuelewa ukweli wa kuwa mwanadamu, na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu. Taratibu mwanadamu anaanza kuchukia ushenzi wake mwenyewe. Anaanza kuchukia jinsi alivyo mkali, na lawama kuelekea kwa Mungu, na mahitaji yote yasiyokuwa na mwelekeo aliyodai kutoka Kwake. Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma, matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu, na maneno na upendo wa Mungu vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya. Majeraha ya mwanadamu hupona siku baada ya siku, nguvu humrudia, na akasimama na kutazamia uso Wake mwenye Uweza … ndipo anagundua kuwa daima Ameishi kando yangu, na kwamba tabasamu Lake na sura Yake ya kupendeza bado zinasisimua. Moyo Wake bado unawajali wanadamu Aliowaumba, na mikono Yake bado ina joto na nguvu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni. Ni kama mwanadamu alirudi kwenye bustani ya Edeni, lakini wakati huu mwanadamu hasikizi ushawishi wa nyoka, na hatazami kando na uso wa Yehova. Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu, na kutazama uso Wake wenye tabasamu, na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!
Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado Anafanya Kazi bila kuchoka na Anapania kuikamilisha. Haijalishi ni kwa kiasi gani watu wanaelewa usimamizi wa Mungu, manufaa na usaidizi wa Kazi inayofanywa na Mungu unaweza kukubalika na kila mtu. Labda, leo, hujahisi upendo wowote au maisha yaliyowezeshwa na Mungu, lakini bora tu humwachi Mungu, na hupotezi matumaini yako ya kutafuta ukweli, basi kutakuwa na siku ambapo tabasamu la Mungu litafichuliwa kwako. Kwa kuwa dhumuni la kazi ya usimamizi wa Mungu ni kuwatoa wanadamu wanaomilikiwa na Shetani, sio kuwaacha wanadamu waliopotoshwa na Shetani na kumpinga Mungu.
Septemba 23, 2005

Alhamisi, 21 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”

Mwenyezi Mungu anasema, “Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu.” “Kila siku Naona vitendo vyote vya watu wengi, na kila siku Nachunguza mioyo na akili za watu wengi; hakuna aliyewahi kutoroka hukumu Yangu, na hakuna aliyewahi kuachana na uhalisi wa hukumu Yangu.”
Mwenyezi Mungu anasema, Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu. Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani? Wakati Wanangu na watu Wangu wanarudi katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Ambayo ni kusema, Nianzapo binafsi kazi Yangu duniani, na wakati enzi ya hukumu inakaribia tamati yake, Naanza kuelekeza maneno Yangu kwa ulimwengu mzima, na kutoa sauti ya Roho Wangu kwa dunia nzima. Kupitia maneno Yangu, Nitasafisha wanadamu na mambo yote miongoni mwa yote yaliyo mbinguni na duniani, ili nchi si chafu na fisadi tena, lakini ni ufalme takatifu. Nitatengeneza upya mambo yote, ili yatolewe kwa matumizi Yangu, na yasiwe na pumzi ya dunia tena, na yasichafuliwe na ladha ya ardhi tena. Duniani, mwanadamu ametafuta malengo na asili ya maneno Yangu, na amechunguza matendo Yangu, lakini bado hakuna aliyewahi kujua kwa kweli asili ya maneno Yangu, na hakuna aliyewahi kuona kwa kweli matendo Yangu ya ajabu. Ni leo tu, Nikujapo binafsi miongoni mwa wanadamu na kuongea maneno Yangu, ndipo mwanadamu anapata maarifa kidogo kunihusu, kutoa nafasi “Yangu” ndani ya mawazo yao, badala yake kutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya fahamu zake. Mwanadamu ana dhana na amejawa na udadisi; ni nani ambaye hangetaka kumwona Mungu? Ni nani ambaye hangetamani kukutana na Mungu? Lakini bado kitu pekee kilicho na nafasi ya uhakika ndani ya moyo wa mwanadamu ni Mungu ambaye mwanadamu anahisi kuwa dhahania na asiye dhahiri. Nani angetambua haya kama Singewaeleza wazi? Nani angeamini kwa kweli Mimi nipo? Kwa hakika bila shaka yoyote? Kuna tofauti kubwa kati ya “Mimi” aliye ndani ya mwanadamu na “Mimi” wa ukweli, na hakuna anayeweza kuwalinganisha. Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi Nijua, na hata angekuja kunijua, je, maarifa kama hayo bado hayangekuwa dhana? Kila siku Natembea miongoni mwa watu wengi, na kila siku Nafanya kazi ndani ya kila mtu. Wakati mwanadamu kweli ananiona, ataweza kunijua kwa maneno Yangu, na kuelewa njia Ninazotumia kuzungumza na pia nia Zangu.
Ufalme ufikapo rasmi duniani, ni nini, kati ya mambo yote, sio kimya? Nani, kati ya watu wote, hana hofu? Natembea kila mahali katika ulimwengu dunia wote, na kila kitu kinapangwa na Mimi binafsi. Wakati huu, nani asiyejua vitendo Vyangu ni vya ajabu? Mikono Yangu inashikilia mambo yote, lakini bado Niko juu ya mambo yote. Leo, si kupata mwili Kwangu na kuwepo Kwangu binafsi miongoni mwa wanadamu maana ya ukweli ya unyenyekevu na kujificha Kwangu? Kwa nje, watu wengi wananipongeza kama mzuri, wananisifu kama mzuri, lakini ni nani anayenijua kweli? Leo, mbona Nauliza kuwa mnijue? Lengo Langu sio kuaibisha joka kubwa jekundu? Sitaki kumlazimisha mwanadamu kunisifu, lakini kumfanya anijue kupitia hapo atakuja kunipenda, na hivyo kunisifu. Sifa kama hiyo inastahili jina lake, na si mazungumzo yasiyokuwepo; ni sifa tu kama hii inaweza kufikia kiti Changu cha enzi na kupaa angani. Kwa sababu mwanadamu amejaribiwa na kupotoshwa na Shetani, kwa sababu amechukuliwa na kufikiria kwa dhana, Nimekuwa mwili ili kuwashinda binafsi wanadamu wote, kufichua dhana zote za mwanadamu, na kupasua mawazo ya mwanadamu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu hajionyeshi mbele Yangu tena, na hanitumikii tena akitumia dhana zake mwenyewe, na hivyo, “Mimi” katika dhana za mwanadamu ameondoka kabisa. Ufalme ufikapo, Naanza kwanza hatua hii ya kazi, na Nafanya hivyo miongoni mwa watu Wangu. Sababu nyinyi ni watu Wangu waliozaliwa kwa nchi ya joka kubwa jekundu, kwa hakika hakuna tu hata kidogo, ama kipimo cha sumu ya joka kubwa jekundu ndani yenu. Hivyo, hatua hii ya kazi Yangu hasa inawaangazia, na hiki ni kipengele kimoja cha umuhimu wa kupata mwili Kwangu Uchina. Watu wengi hawawezi kuelewa hata chembe cha maneno Ninayoyasema, na wanapoweza, uelewa wao ni wenye ukungu na ovyo. Hii ni mojawapo ya sehemu muhimu ya mbinu Ninayozungumzia. Iwapo watu wote wangeweza kusoma maneno Yangu na kuelewa maana yao, basi nani miongoni mwa wanadamu angeweza okolewa, na kutupwa kuzimu? Mwanadamu anijuapo na kunitii ndio wakati Nitakapopumzika, na itakuwa wakati hasa ambapo mwanadamu ataweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Leo, kimo chenu ni kidogo sana, karibu kiwe kiwango cha kusikitisha, na hakistahili hata kuinuliwa—sembuse ujuzi wenu kunihusu.
Ingawa Nasema malaika wameanza kutumwa mbele kuchunga wana na watu Wangu, hakuna anayeweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Nikujapo binafsi miongoni mwa binadamu, malaika wanaanza wakati huo huo kazi ya uchungaji, na wakati huo wa uchungaji wa malaika, wana na watu wote hawapati tu majaribio na uchungaji, lakini wanaweza pia kuona, na macho yao, tukio la kila aina ya maono. Kwa sababu Nafanya kazi moja kwa moja kwa uungu, kila kitu kinaingia katika mwanzo mpya, na kwa sababu uungu huu unafanya kazi moja kwa moja, hauzuiliwi hata kidogo na ubinadamu, na unaonekana kwa binadamu kufanya kazi huru chini ya hali isiyo ya kawaida. Lakini bado, Kwangu, yote ni kawaida (mwanadamu anaamini si ya kawaida kwa sababu hajawahi kukutana na uungu moja kwa moja); hauna dhana zozote za mwanadamu, na haujachafuliwa na maana ya binadamu. Watu wataona haya wakati tu wote wataingia katika njia sawa; kwa sababu sasa ndio mwanzo, inapokuja suala la kuingia kwake, mwanadamu ana mapungufu mengi, na makosa kama haya na upofu huwezi ukaepukwa kwa urahisi. Leo, sababu Nimewaongoza hadi hapa, Nimefanya mipango ya kufaa, na Nina malengo Yangu Mwenyewe. Ningewaeleza kuyahusu leo, mngeweza kweli kuyajua? Nayajua vizuri mawazo ya akili ya mwanadamu na matakwa ya moyo wa mwanadamu: Nani hajawahi kutafuta njia ya kujitoa mwenyewe? Nani hajawahi fikiria matarajio yake mwenyewe? Lakini hata kama mwanadamu ana akili tajiri na wa mche nani aliweza kutabiri kwamba, kufuatia enzi, sasa kungekuwa kulivyo? Hili kweli ni tunda la juhudi zako binafsi? Haya ni malipo ya kazi yako ya bidii? Hii ndiyo picha nzuri iliyoonwa na akili yako? Nisingewaongoza wanadamu wote, nani angeweza kujitenga na mipango Yangu na kupata njia nyingine ya kutoka? Ni mawazo na matakwa ya mwanadamu ambayo yamemleta hadi leo? Watu wengi wanaishi maisha yao yote bila kutimiziwa kwa matakwa yao. Kweli hili ni kwa sababu ya kosa katika fikira zao? Maisha ya watu wengi yamejawa na furaha na ridhaa isiyotarajiwa. Kweli ni kwa sababu wanatarajia kidogo sana? Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu. Ingawa Sijitokezi binafsi kumruhusu mwanadamu kunitazama vizuri, watu wengi wanaogopa kuona uso Wangu, wanaogopa sana Nitawapiga chini, kwamba Nitawaangamiza. Mwanadamu kweli ananijua Mimi ama hanijui? Hakuna anayeweza kusema kwa hakika. Sivyo? Mnaniogopa na pia kuadibu Kwangu, lakini bado mnasimama na kunipinga wazi na kunihukumu hadharani. Sivyo? Kwamba mwanadamu hajawahi kunijua ni kwa sababu hajawahi kuuona uso Wangu ama kuisikia sauti Yangu. Hivyo, hata kama Niko ndani ya moyo wa mwanadamu, je, kuna wale ambao Sionekani mwenye ukungu na asiye dhahiri katika mioyo yao? Kuna wale Ninaoonekana vizuri ndani ya mioyo yao? Sitamani wale walio watu Wangu pia kutoniona vizuri, na hivyo Naanza kazi hii kubwa.Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu. Ingawa Sijitokezi binafsi kumruhusu mwanadamu kunitazama vizuri, watu wengi wanaogopa kuona uso Wangu, wanaogopa sana Nitawapiga chini, kwamba Nitawaangamiza. Mwanadamu kweli ananijua Mimi ama hanijui? Hakuna anayeweza kusema kwa hakika. Sivyo? Mnaniogopa na pia kuadibu Kwangu, lakini bado mnasimama na kunipinga wazi na kunihukumu hadharani. Sivyo? Kwamba mwanadamu hajawahi kunijua ni kwa sababu hajawahi kuuona uso Wangu ama kuisikia sauti Yangu. Hivyo, hata kama Niko ndani ya moyo wa mwanadamu, je, kuna wale ambao Sionekani mwenye ukungu na asiye dhahiri katika mioyo yao? Kuna wale Ninaoonekana vizuri ndani ya mioyo yao? Sitamani wale walio watu Wangu pia kutoniona vizuri, na hivyo Naanza kazi hii kubwa.
Nakuja polepole miongoni mwa wanadamu, na Naondoka taratibu. Kuna aliyewahi kuniona? Jua linaweza kuniona kwa sababu ya moto wake unaochoma? Mwezi unaweza kuniona kwa sababu ya uwazi wake unaong’aa? Kundinyota zinaweza kuniona kwa sababu ya mahali zipo angani? Nikujapo, mwanadamu hajui, na mambo yote yanabakia gizani, na Niondokapo, bado mwanadamu hafahamu. Nani anaweza kuwa na ushuhuda Kwangu? Inaweza kuwa sifa ya watu wa dunia? Inaweza kuwa mayungiyungi yanayochanua porini? Inaweza kuwa ndege wanaoruka angani? Inaweza kuwa simba wanaonguruma milimani? Hakuna anayeweza kunishuhudia kikamilifu. Hakuna anayeweza kufanya kazi Nitakayoifanya! Hata kama wangefanya kazi hii, ingekuwa na athari gani? Kila siku Naona vitendo vyote vya watu wengi, na kila siku Nachunguza mioyo na akili za watu wengi; hakuna aliyewahi kutoroka hukumu Yangu, na hakuna aliyewahi kuachana na uhalisi wa hukumu Yangu. Nasimama juu ya mawingu na kuangalia kwa umbali: Nimewaangamiza watu wengi, lakini pia watu wengi wanaishi katika huruma, na wema Wangu. Nyinyi pia hamuishi chini ya hali kama hizi?
Machi 5, 1992
Chanzo: Sura ya 11