Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo sauti-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo sauti-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 20 Septemba 2019

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda

2. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda

Maneno Husika ya Mungu:
Wanadamu kwa ajili ya kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi. Wanadamu watashindwa vipi hasa? Watapata kushindwa kwa kutumia hii kazi ya maneno kumshawishi mwanadamu kwa dhati; kwa kutumia toba, hukumu, kuadibu, na laana isiyo na huruma dhibiti kabisa; na kwa kuweka wazi uasi wa mwanadamu na kwa kuhukumu upinzani wake ili ajue udhalimu wa mwanadamu na uchafu wake, mambo ambayo yatatumiwa kuangazia tabia ya haki ya Mungu. Kwa kiwango kikubwa, ni matumizi ya maneno haya yatakayomshinda mwanadamu na kumshawishi kabisa. Maneno ndiyo njia ya kuwashinda wanadamu na wote wanaokubali ushindi lazima wakubali mapigo na hukumu ya maneno. Mchakato wa sasa wa kunena ni mchakato wa kushinda. Ni kwa njia gani watu wanapaswa hasa kushirikiana? Ni kwa kula na kunywa haya maneno ipasavyo na kuyafahamu. Watu hawawezi kujipatia ushindi wao wenyewe. Ni lazima, kwa kula na kunywa haya matamshi, upate kufahamu uovu na uchafu wako, uasi na udhalimu wako, na uanguke chini mbele ya Mungu. Ikiwa waweza kufahamu mapenzi ya Mungu kisha uyatie katika vitendo, na zaidi, uwe na maono, na ikiwa waweza kuyatii maneno haya kabisa na usitende kulingana na mapenzi yako, basi utakuwa umeshindwa. Na itakuwa ni haya maneno yamekuwezesha kushindwa. Ni kwa nini wanadamu walipoteza ushuhuda? Ni kwa sababu hakuna aliye na imani kwa Mungu au anamshikilia Mungu rohoni mwake. Kuwashinda wanadamu kunamaanisha watu wairudie hii imani. Watu daima wanauegemea ulimwengu, wakiwa na matumaini mengi sana, wakitaka kujua mengi sana kwa ajili ya maisha yao ya usoni, na wakiwa na mahitaji mengi ya kupita kiasi. Wanaifikiria na kuipangia miili yao kila mara wala hawatamani kutafuta njia ya kumwamini Mungu. Roho zao zimetekwa na Shetani, wameacha kumheshimu Mungu, na wanatoa mioyo yao kwa Shetani. Ila mwanadamu aliumbwa na Mungu. Hivyo, mwanadamu amepoteza ushuhuda, kumaanisha amepoteza utukufu wa Mungu. Kusudi la kumshinda mwanadamu ni kuurejesha utukufu wa mwanadamu wa kumheshimu Mungu.

kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kazi ya sasa ya kushinda ni kazi inayokusudiwa kuweka wazi hatima ya mwanadamu itakuwaje. Ni kwa nini Ninasema kuwa kuadibu na hukumu ni hukumu mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe cha siku za mwisho? Hulioni hili? Ni kwa nini kazi ya kushinda ni hatua ya mwisho? Je, si kudhihirisha kwa usahihi hatima ya kila tabaka la wanadamu? Si kumruhusu kila mtu, katika harakati ya kazi ya kushinda ya kuadibu na hukumu, kuonyesha tabia zake halisi na kisha kuwekwa katika aina yake baadaye? Badala ya kusema kuwa huku ni kuwashinda wanadamu, inaweza bora kusema kuwa huku ni kuonyesha hatima ya kila aina ya mwanadamu. Yaani, huku ni kuhukumu dhambi zao halafu kuonyesha matabaka mbalimbali ya wanadamu, na kwa njia hiyo kubaini kama ni waovu au ni wenye haki. Baada ya kazi ya kushinda, kazi ya kutuza mazuri na kuadhibu maovu inafuata: watu wanaotii kabisa, yaani walioshindwa kabisa, watawekwa katika hatua nyingine ya kusambaza kazi ulimwenguni kote; wasioshindwa watawekwa gizani na watapatwa na majanga. Hivyo mwanadamu ataainishwa kulingana na aina yake, watenda maovu watawekwa pamoja na maovu, wasiuone mwangaza tena, na wenye haki watawekwa pamoja na mazuri, ili kupokea mwangaza na kuishi milele katika mwangaza. Mwisho wa vitu vyote u karibu, mwisho wa mwanadamu umebainishwa wazi machoni mwake, na vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina yake. Ni vipi basi wanadamu wataepuka kuathiriwa na kuanisha huku? Kufichua mwisho kwa kila jamii ya mwanadamu kutafanywa hatima ya kila kitu ikikaribia, na kutafanywa wakati wa kazi ya kushinda ulimwengu mzima (ikiwemo kazi yote ya kushinda kuanzia kazi ya sasa). Huku kufichua mwisho wa wanadamu kunafanywa mbele ya kiti cha hukumu, katika harakati ya kuadibu, na harakati ya kazi ya kushinda ya siku za mwisho. … Hatua ya mwisho ya kushinda ni ya kukomboa watu na vilevile kufichua mwisho wa kila mtu. Inaweka wazi upotevu wa watu kupitia hukumu na kwa njia hiyo kuwafanya watubu, waamke, na kufuatilia uzima na njia ya haki ya maisha ya mwanadamu. Ni ya kuamsha mioyo ya waliolala na wapumbavu na kuonyesha, kwa njia ya hukumu, uasi wao wa ndani. Hata hivyo, ikiwa watu bado hawawezi kutubu, bado hawawezi kufuata njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na hawawezi kuutupa upotovu huu, basi watakuwa vyombo visivyoweza kukombolewa vya kumezwa na Shetani. Hii ndiyo maana ya kushinda—kuwakomboa watu na vilevile kuwaonyesha mwisho wao. Mwisho mzuri, mwisho mbaya—yote yanafichuliwa na kazi ya kushinda. Kama watu watakombolewa au kulaaniwa yote yanafichuliwa wakati wa kazi ya kushinda.

Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia kushinda. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maneno mengine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. La sivyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, watu wa kila mataifa vilevile watapitia kazi ya kushinda. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake?

kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Jinsi ambavyo mwenendoama mwili wa mwanadamu hubadilika haiamui ikiwa ameshindwa. Badala yake, ni wakati ambapo fikira, ufahamu, na utambuzi wa mwanadamu unabadilika—yaani, ni wakati mielekeo yako yote ya kifikira inabadilika—ndipo huwa umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa. Katika ulimwengu wa dini, watu wengi huteseka pakubwa maishani mwao mwote, kwa kuihini miili yao au kuubeba msalaba wao, au hata kuteseka na kustahimili hadi pumzi zao za mwisho! Wengine huwa wanafunga hadi siku ya kifo chao. Katika maisha yao yote wanajinyima chakula kizuri na mavazi mazuri, wakisisitiza mateso tu. Wanaweza kuihini miili yao na kuinyima miili yao. Uwezo wao wa kustahimili mateso unastahili sifa. Ila fikira zao, mawazo yao, mielekeo yao ya kiakili, na kwa hakika asili yao ya kale—hakuna kati yavyo kilichoshughulikiwa hata kidogo. Hawajifahamu. Picha ya Mungu akilini mwao ni ya kijadi na ya kidhahania, Mungu asiye yakini. Uamuzi wao wa kuteseka kwa ajili ya Mungu unaletwa na azma na asili yao chanya. Hata ikiwa wanamwamini Mungu, hawamfahamu Mungu wala kuyafahamu mapenzi Yake. Wanamfanyia Mungu kazi na kumtesekea Mungu kama vipofu. Hawawekei utambuzi thamani yoyote na hawajishughulishi na jinsi ambayo huduma yao inatimiza mapenzi ya Mungu kwa kweli. Aidha hawajui jinsi ya kutimiza ufahamu kuhusu Mungu. Mungu wanayemhudumia si Mungu katika sura Yake ya asili, ila ni Mungu waliyejifikiria, Mungu waliyemsikia, au Mungu wa kihadithi wanayemsoma katika maandiko. Kisha wanatumia mawazo yao dhahiri na mioyo yao ya kiungu kumtesekea Mungu na kuifanya kazi ambayo Mungu anapaswa kufanya. Huduma yao haiko sahihi, kiasi kwamba hakuna anayemhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi Yake. Haijalishi wako radhi kiasi gani kuteseka, mitazamo yao asilia ya huduma na picha ya Mungu akilini mwao havibadiliki kwani hawajapitia hukumu ya Mungu na kuadibu na usafishaji Wake na ukamilifu, na kwa sababu hakuna yeyote aliyewaongoza na ukweli. Japo wanasadiki kwa Yesu Mwokozi, hamna kati yao aliyewahi kumwona Mwokozi. Wamemsikia tu kwa hadithi na uvumi. Hivyo huduma yao ni sawa na kuhudumu mara mojamoja macho yao yakiwa yamefungwa kama kipofu anayemhudumia baba yake. Ni nini kinaweza kupatikana kutokana na huduma kama hiyo? Na ni nani anaweza kuikubali? Huduma yao haibadiliki kamwe toka mwanzo hadi mwisho. Wanapokea mafunzo ya kibinadamu na kukita huduma yao katika uasili wao na kile wanachokipenda wao. Hili laweza kuzalisha faida gani? Hata Petro, aliyemwona Yesu, hakujua jinsi ya kumhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi ya Mungu. Ni katika uzee wake ndipo alipopata ufahamu. Hili linaonyesha nini kuhusu wanadamu vipofu ambao hawajapitia ushughulikiaji na hawana upogoaji na ambao hawajawahi kupata yeyote wa kuwaongoza? Je, si huduma ya wengi miongoni mwenu leo ni kama ile ya vipofu? Wale wote ambao hawajapokea hukumu, hawajapokea upogoaji na ushughulikiaji, na hawana mabadiliko—je, wao si waliokosa kushindwa kabisa? Wana manufaa gani watu kama hao? Ikiwa fikira zako, ufahamu wako wa maisha, na ufahamu wako wa Mungu hauonyeshi mabadiliko mapya na hautoi faida hata kidogo, hutatimiza chochote kizuri katika huduma yako. Bila maono na bila ufahamu mpya wa kazi ya Mungu, huwezi kuwa mtu aliyeshindwa. Njia yako ya kumfuata Mungu itakuwa kama ile ya wale wanaoteseka na kufunga—itakuwa ya thamani ndogo! Hii ni kwa sababu kuna ushuhuda kidogo katika yale wayafanyayo ndipo Nasema huduma yao ni bure! Kotekote katika maisha yao, hao watu huteseka, hukaa gerezani kwa muda, na kwa kila wakati, hustahimili, husisitiza mapenzi na ukarimu, na kubeba msalaba wao. Wanatukanwa na kukataliwa na ulimwengu na hupitia kila ugumu. Wanatii hadi mwisho ila bado hawapati ushindi na hawawezi kutoa ushuhuda wa kutwaliwa. Wameteseka si haba, ila kwa ndani hawamfahamu Mungu kabisa. Hakuna fikira zao za zamani, mawazo ya zamani, vitendo vyao, uelewa wa wanadamu, na mawazo ya wanadamu yaliyoshughulikiwa. Kamwe hakuna uelewa mpya ndani yao. Hakuna hata chembe ya ufahamu wao wa Mungu ambao ni wa kweli au ni sahihi. Wamekosa kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Je, huku kwaweza kuwa kumhudumia Mungu? Japo ulimfahamu Mungu zamani, tuseme umeudumisha ufahamu huo hadi leo na kuendelea kukita ufahamu wako kuhusu Mungu kwenye fikira na mawazo yako bila kujali Mungu anafanya nini. Yaani, ikiwa huna ufahamu mpya na wa kweli kuhusu Mungu na ukose kutambua sura na tabia ya kweli ya Mungu. Ikiwa ufahamu wako wa Mungu bado unaongozwa na fikira za uhasama na ushirikina na bado una mawazo na fikira za mwanadamu. Ikiwa hii ndiyo hali, basi hujashindwa. Lengo langu la kukwambia maneno haya yote sasa ni kukupa fursa ya kufahamu na kutumia utambuzi huu kukuongoza katika ufahamu sahihi na mpya. Aidha yanalengwa kukuondolea mawazo ya zamani na utambuzi wa zamani ulio nao ili uweze kuwa na ufahamu mpya. Ikiwa unakula na kunywa matamshi Yangu kweli, basi ufahamu wako utabadilika kwa kiwango kikubwa. Bora tu udumishe moyo mtiifu kwa kula na kunywa matamshi ya Mungu, mtazamo wako utabadilika. Bora tu unaweza kukubali kuadibu kwa kila mara, fikira zako za zamani zitabadilika taratibu. Bora tu fikira zako za zamani zimebadilishwa kabisa na kuwa mpya, vitendo vyako vitabadilika ipasavyo. Kwa njia hii, huduma yako itaendelea kuwa yenye malengo zaidi, na itaweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Ukibadilisha maisha yako, ufahamu wako wa maisha, na mawazo yako mengi kuhusu Mungu, basi uasili wako utadidimia taratibu. Hili, na hakuna jingine ila hili, ndilo tokeo baada ya Mungu kumshinda mwanadamu; haya ndiyo mabadiliko yatakayoonekana ndani ya mwanadamu.

kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kazi ya Yehova ilikuwa uumbaji wa ulimwengu, ilikuwa mwanzo; awamu hii ya kazi ni mwisho wa kazi, na ni hitimisho. Hapo mwanzo, kazi ya Mungu ilifanyika miongoni mwa wateule wa Israeli, na ilikuwa mapambazuko ya kipindi kipya katika pahali patakatifu zaidi ya popote. Awamu ya mwisho ya kazi inafanywa katika nchi ambayo ni chafu zaidi ya zote, kuhukumu ulimwengu na kuleta enzi kwenye kikomo. Katika awamu ya kwanza kazi ya Mungu ilifanyika katika maeneo yenye kung’aa kuliko maeneo yote, na awamu ya mwisho inafanyika katika maeneo yaliyo katika giza kuliko maeneo yote, na giza hili litaondolewa, na mwanga kufunguliwa, na watu wote kushindwa. Wakati watu wa maeneo haya yaliyo chafu kuliko yote na yaliyo na giza watakuwa wameshindwa na idadi yote ya watu wametambua kuwa Mungu yupo, na ya kuwa ni Mungu wa kweli, na kila mtu Amemwamini kabisa, basi ukweli huu utatumika kutekeleza kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima. Awamu hii ya kazi ni ya ishara: Punde tu kazi ya kipindi hiki itakapomalizika, kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi itafikia mwisho kabisa. Mara baada ya wale walioko katika maeneo yaliyo na giza kuliko yote watakapokuwa wameshindwa, bila shaka itakuwa hivyo pia kila mahali pengine. Kwa hivyo, kazi ya ushindi tu katika China inabeba ishara ya maana. China inajumuisha nguvu zote za giza, na watu wa China wanawakilisha wale wote ambao ni wa mwili, wa Shetani, na wa mwili na damu. Ni watu wa China ndio wamepotoshwa sana na joka kubwa jekundu, ambao wana upinzani wenye nguvu dhidi ya Mungu, ambao wana ubinadamu ulio mbovu zaidi na ulio mchafu, na kwa hivyo hao ni umbo asili la wanadamu wote wenye matendo maovu. Hii si kusema kwamba nchi nyingine hazina shida kabisa; dhana za mwanadamu ni sawa zote, na ingawa watu wa nchi hizi wanaweza kuwa na uhodari mzuri, ikiwa hawamjui Mungu, basi ni lazima iwe kwamba wanampinga. Kwa nini Wayahudi pia walimpinga na kumwasi Mungu? Kwa nini Mafarisayo pia walimpinga? Kwa nini Yuda alimsaliti Yesu? Wakati huo, wengi wa wanafunzi hawakumjua Yesu. Kwa nini, baada ya Yesu kusulubiwa na kufufuliwa tena, watu bado hawakumwamini? Je, uasi wa mwanadamu sio sawa wote? Ni tu kwamba watu wa China wamefanyika mfano, na watakaposhindwa watakuwa mfano na kielelezo, na watatumika kama kumbukumbu kwa wengine. Kwa nini mimi daima Nimesema yakuwa nyinyi ni kiungo cha mpango wangu wa usimamizi? Ni katika watu wa China ambapo upotovu, uchafu, udhalimu, upinzani, na uasi unadhihirishwa kikamilifu zaidi na kufichuliwa kwa hali zao mbalimbali. Kwa upande mmoja, wao ni wa kimo cha umaskini, na kwa upande mwingine, maisha yao na mawazo yao ni ya nyuma kimaendeleo, na tabia zao, mazingira ya kijamii, familia ya kuzaliwa—yote ni ya umaskini na ya nyuma kimaendeleo kuliko yote. Hadhi yao, pia, ni ya chini. Kazi katika eneo hili ni ya ishara, na baada ya kazi hii ya majaribio hufanywa kwa ukamilifu wake, na kazi yake inayofuata itakwenda vizuri zaidi. Kama awamu hii ya kazi inaweza kukamilika, basi kazi inayofuata itakamilika bila shaka. Mara baada ya awamu ya kazi hii kutimizwa, na mafanikio makubwa kufikiwa kikamilifu, kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima itakua imefikia kikomo kamili. Kwa kweli, mara baada ya kazi miongoni mwenu imekuwa ya mafanikio, hii itakuwa sawa na mafanikio katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa sababu Yangu kuwafanya mfano wa kuigwa na kielelezo. Uasi, upinzani, uchafu, udhalimu—yote haya hupatikana kwa watu hawa, na ndani yao pamewakilishwa uasi wote wa wanadamu. Wao ni wa kushangaza kweli. Hivyo, wanafanywa kuwa mfano wa ushindi, na punde tu watakaposhindwa watakuwa kama ilivyo kawaida kielelezo na mfano wa kuigwa na wengine.

kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mwanadamu anajali tu kuhusu hatima ya siku zijazo, hatima, na kama kuna ama hamna kitu kizuri cha kutumainia. Iwapo mwanadamu angepewa matumaini mazuri wakati wa kazi ya ushindi, na kama, kabla ya kushindwa kwa mwanadamu, yeye angepewa hatima ifaayo ya kufuata, basi kushindwa kwa mwanadamu kusingekosa kuwa na athari tu, bali athari za kushindwa zingeshawishika pia. Hivi ni kusema kwamba, kazi ya ushindi inafanikisha mazao yake kwa kuchukua hatima na matarajio ya mwanadamu na kuhukumu na kuadibu uasi wa tabia ya mwanadamu. Haifanikishwi kwa kufanya mpango na mwanadamu, yaani, kwa kumpa mwanadamu baraka na neema, lakini ni kwa kufichua uaminifu wa mwanadamu kwa kumnyang’anya “uhuru” wake na kukomesha matarajio yake. Hiki ni kiini cha kazi ya ushindi. Kama mtu angepewa matumaini mazuri hapo mwanzoni sana, na kazi ya kuadibu na hukumu zingefanywa baadaye, basi mwanadamu angekubali kuadibu huku na hukumu kwa msingi kwamba alikuwa na matarajio, na mwishowe, utiifu na ibada ya Muumba isiyo na masharti ya viumbe vyote vyake haingetimizika; kungekuwepo tu na utiifu wenye upofu na wa ujinga, au pengine mwanadamu angetoa madai yasiyo na msingi kwa Mungu, na ingekuwa ni vigumu kushinda moyo wa mwanadamu. Kwa hivyo, kazi kama hii ya ushindi haingekuwa na uwezo wa kumpata mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, ya kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Viumbe kama hawa hawangeweza kutekeleza jukumu lao, na wangeweza tu kufikia makubaliano na Mungu; hii haitakuwa ushindi, lakini huruma na baraka. Tatizo kubwa mno kwa mwanadamu ni kuwa yeye hufikiria tu kuhusu hatima yake na matarajio, na kuyaabudu. Mwanadamu humfuata Mungu kwa ajili ya hatima yake na matarajio; yeye hamwabudu Mungu kwa sababu ya upendo wake kwake. Na kwa hivyo, katika ushindi kwa mwanadamu, ubinafsi wa mwanadamu, uroho na vitu ambavyo sana sana huzuia ibada yake kwa Mungu ni sharti viondolewe. Kwa kufanya hivyo, matokeo ya ushindi kwa mwanadamu yatatimizwa. Hivyo, katika ushindi wa kwanza wa mwanadamu ni muhimu kwanza kuondoa matarajio makubwa ya mwanadamu na udhaifu unaohuzunisha kabisa, na, kupitia hili, kufichua upendo wa mwanadamu kwa Mungu, na kubadilisha maarifa yake kuhusu maisha ya binadamu, mtazamo wake kwa Mungu, na maana ya kuwepo kwake. Kwa njia hii, upendo wa mwanadamu kwa Mungu unatakaswa, ambapo ni kusema, moyo wa binadamu unashindwa. Lakini katika mtazamo wake wa viumbe vyote, Mungu hashindi kwa sababu ya kushinda; badala yake, Yeye anashinda ili kumpata mtu, kwa sababu ya utukufu wake mwenyewe, na ili kuokoa ufanano wa kwanza wa awali wa mwanadamu. Kama angeshinda kwa ajili ya kushinda, basi umuhimu wa kazi ya ushindi ungepotea. Hiyo ni kusema kuwa ikiwa, baada ya kumshinda mwanadamu, Mungu alikata tamaa kwa ajili ya mwanadamu, na hakuzingatia maisha au kifo chake, basi hii haitakuwa usimamizi wa mwanadamu, wala kumshinda mwanadamu haitakuwa ni kwa ajili ya wokovu wake. Ni upato wa mwanadamu tu kufuatia ushindi wake na ujio wake wa mwisho katika hatima ya ajabu ndiyo yaliyomo katika kiini cha kazi yote ya wokovu, na ni hii tu ndio inayoweza kufikia lengo la wokovu wa mwanadamu. Kwa maneno mengine, ni ufikaji wa mwanadamu katika hatima nzuri na kuingia kwake katika mapumziko tu ndiyo matarajio ambayo yanatakiwa yamilikiwe na viumbe vyote, na kazi ambayo lazima ifanywe na Muumba.

kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hatua ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni hatua ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na hatua ya mwisho katika kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na wanadamu kamwe hawangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilishwa kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu ya usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha usimamizi wote wa Mungu, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, yaani mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kutekwa nyara na Shetani. Hivyo, Shetani lazima ashindwe kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani, mabadiliko ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye ametekwa nyara, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, na baada ya hapo kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.

kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kazi ya kushinda inayofanywa kwenu nyie ni ya umuhimu mkubwa sana: Kwa upande mmoja, kusudi la hii kazi ni kukikamilisha kikundi cha watu, yaani, kuwakamilisha na kuwa kundi la washindi, kama kundi la kwanza la watu waliofanywa wakamilifu, yaani matunda ya kwanza. Kwa upande wa pili, ni kuruhusu viumbe wa Mungu kufurahia mapenzi ya Mungu, kupokea wokovu mkubwa wa Mungu, na kupokea wokovu kamili wa Mungu. Kile Mungu anamkubali mwanadamu kufurahia si tu huruma na wema, ila muhimu zaidi ni kuadibu na hukumu. Tangu uumbaji wa dunia hadi sasa, yote ambayo Mungu amefanya katika kazi Yake ni upendo, bila chuki yoyote kwa mwanadamu. Hata kuadibu na hukumu uliyoiona ni mapenzi pia, upendo wa kweli na wa dhati zaidi; upendo huu huwaongoza wanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu. Kwa upande wa tatu, ni kushuhudia mbele ya Shetani. Kwa upande wa nne, ni kuweka msingi wa kueneza kazi ya baadaye ya injili. Kazi yote Aliyoifanya ni kumwongoza mwanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya wanadamu, ili kwamba wawe na maisha ya kawaida ya wanadamu, kwani mwanadamu hajui jinsi ya kuishi. Bila uongozi kama huo, utaishi maisha tupu yasiyo na maana wala thamani, na kamwe hutajua jinsi ya kuwa mwanadamu wa kawaida. Huu ndio umuhimu mkuu wa kumshinda mwanadamu.

kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 16 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”

Mwenyezi Mungu anasema: “Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata uzoefu wa maisha ya binadamu, Nikichunguza kwa karibu matendo yote ya mwanadamu. Hakuna aliyewahi kujitolea Kwangu kwa kweli. Hakuna aliyewahi kufuata ukweli. Hakuna aliyewahi kuwa mwangalifu Kwangu. Hakuna aliyewahi kufanya maazimio mbele Yangu na kufanya wajibu wake. Hakuna aliyewahi kuniruhusu kuishi ndani yake. Hakuna aliyewahi kunithamini kama afanyavyo maisha yake. Hakuna aliyewahi kuona kwa vitendo vya ukweli uzima wote wa uungu Wangu. Hakuna aliyewahi kutamani kuwasiliana na Mungu wa vitendo Mwenyewe.”
Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa ufalme. Ingawa chini ya nuru ya Roho Wangu watu wengi wametabiri uzuri wa ufalme, wanajua tu nje ya ufalme, sio umuhimu wa ndani. Leo, ufalme ujapo kuwepo rasmi duniani, binadamu wote bado hujui kinachopaswa kukamilishwa, ulimwengu ambao binadamu hatimaye ataletwa ndani, wakati wa Enzi ya Ufalme. Kuhusu haya, Naogopa watu wote wako katika hali ya mkanganyiko. Kwa sababu siku ya utambuzi kamili wa ufalme bado haijafika kabisa, wanadamu wote wamechanganyikiwa, hawawezi kuiona vizuri. Kazi Yangu ya uungu inaanza rasmi na Enzi ya Ufalme. Ni katika mwanzo rasmi wa Enzi ya Ufalme kwamba tabia Yangu inaanza kuendelea kudhihirika kwa mwanadamu. Hivyo kwa muda huu tarumbeta takatifu inaanza rasmi kutoa sauti na kutangaza kwa wote. Nichukuapo kirasmi mamlaka Yangu na kutawala kama Mfalme katika ufalme, watu Wangu wote watakamilishwa na Mimi baada ya muda. Wakati mataifa yote ya dunia yatavurugwa, hapo ndipo hasa ufalme Wangu utaanzishwa na kupata umbo na pia Nitabadilika na kurejea kwa ulimwengu mzima. Wakati huo, watu wote watauona uso Wangu tukufu, watauona uso Wangu wa kweli. Tangu kuumbwa kwa dunia hadi sasa, binadamu umepotoshwa na Shetani hadi kiasi kilicho leo. Kwa ufisadi wa mwanadamu, Nimefichwa zaidi na zaidi kutoka kwake na Nikazidi kutoeleweka na wao. Mwanadamu hajawahi kuuona uso Wangu wa kweli, hajawahi kuathiriana na Mimi moja kwa moja. Ni kwa tetesi na hadithi tu ndipo kumekuwa na “Mimi” kwa ubunifu wa mwanadamu. Kwa hivyo Nakubaliana na ubunifu wa binadamu, kwamba, ni dhana za binadamu, kukabiliana na “Mimi” kwa akili za wanadamu, kwamba Naweza kubadilisha hali ya “Mimi” ambayo wameweka kwa miaka mingi. Hii ni kanuni ya kazi Yangu. Hakuna mtu hata mmoja ameweza kuijua vizuri sana. Ingawa wanadamu wamejilaza na kuja mbele Yangu kuniabudu, Sifurahii matendo kama haya ya wanadamu kwa sababu kwa mioyo yao hawajashikilia mfano Wangu, lakini mfano Wangu wa nje. Kwa hivyo, akili zao zinapokosa tabia Yangu, hawajui chochote kuhusu uso Wangu wa kweli. Kwa hivyo, wakati wameamini wamenipinga ama kukosea amri Zangu za kiutawala, Nitajifanya kwamba sioni. Na hivyo, kwa kumbukumbu zao, Mimi ni Mungu anayeonyesha huruma kwa wanadamu badala ya kuwaadibu, ama Mimi ni Mungu Mwenyewe asiyemaanisha Anachokisema. Haya yote ni mawazo yanayotokana na fikira za wanadamu na sio kwa mujibu na ukweli.
Najificha wakati wanadamu wana kazi nyingi na kujifichua wakati wao wa burudani. Binadamu unanidhania kuwa Anayejua yote na kuwa Mungu Mwenyewe anayekubali maombi yote. Wote basi wanakuja mbele Yangu kutafuta tu msaada wa Mungu, bila kuwa na tamaa ya kunijua. Wakiwa katika maumivu ya magonjwa, wanadamu wananiomba msaada. Wakiwa na shida, wananiambia matatizo yao kwa nguvu zao zote ili kumwaga mateso yao. Na bado hakuna mwanadamu hata mmoja ameweza kunipenda pia akiwa na faraja. Hakuna mtu hata mmoja amenitafuta wakati wa amani na furaha ili Nishiriki furaha yake. Wakati familia yao ya karibu ina furaha na iko sawa, wanadamu tayari wananiweka kando ama kunifungia mlango, kunikataza kuingia, na hivyo kufurahia furaha heri ya familia. Akili ya binadamu ni nyembamba sana, nyembamba sana hata kumshikilia Mungu, apendaye, mwenye huruma, na mkunjufu kama Mimi. Nimekataliwa mara ngapi na wanadamu wakati wao wa kicheko na furaha, Nimetegemewa kama gongo mara ngapi na wanadamu wakati wanaanguka; Ni mara ngapi Nimelazimishwa kuwa daktari wa wanadamu wanaougua magonjwa. Mwanadamu ni katili jinsi gani! Hawana akili na ni wabaya kabisa. Hawana hata hisia zinazopatikana kwa binadamu. Nusura hawana ubinadamu hata kidogo. Fikiria siku za nyuma na linganisha na sasa. Kuna mabadiliko yanayofanyika ndani zenu? Kuna siku kidogo za zamani sasa? Ama zamani bado haijabadilishwa?
Juu ya mlima na chini ya bonde Nimepitia, na kuwa na uzoefu wa panda shuka za dunia. Nimetembea na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi, lakini bado inaonekana tabia ya binadamu imebadilika kidogo. Na ni kama asili ya zamani ya mwanadamu imeeneza mizizi na kuota ndani yao. Hawawezi kamwe kubadili hiyo asili ya zamani, kuiboresha tu kwa msingi wa kwanza. Wasemavyo wanadamu, kiini hakijabadilika, lakini umbo limebadilika sana. Kila mtu, inaonekana, anajaribu kunidanganya, kunipofusha, ili aweze kuingia na kupata shukrani Yangu. Sipendi wala kutia maanani udanganyifu wa watu. Badala ya kukasirika, Nachukua mtazamo wa kuangalia lakini si kuona. Napanga kuupa binadamu kiwango fulani cha uhuru, na hivyo, kushughulikia wanadamu wote kama kitu kimoja. Kwa sababu wanadamu wote hawajiheshimu na ni maskini wasio na faida, wasiojithamini, watawezaje kunihitaji kuonyesha huruma na mapenzi mapya? Wanadamu wote hawajijui, na hawajui uzito wao. Wanapaswa kujipima uzito. Binadamu haunitambui, hivyo Nami pia siutilii maanani. Wanadamu hawanitambui, kwa hivyo Mimi pia Siweki juhudi kwao. Je, hii ni bora? Je, hii haiwazungumzii, watu Wangu? Nani amefanya maazimio mbele Yangu na kukosa kuyatupilia mbali baadaye? Nani amefanya maazimio ya muda mrefu mbele Yangu badala ya kutatua mara nyingi juu ya hii na hiyo? Daima, wanadamu hufanya maazimio mbele Yangu wakati wa raha na kuyafuta kabisa wakati wa shida. Baadaye, wanachukua uamuzi wao na kuuweka mbele Yangu. Je, Mimi si wa kuheshimika hadi Naweza kubali kwa kawaida taka iliyookotwa na mwanadamu kutoka pipani? Wanadamu wachache hushikilia maazimio yao, wachache ni safi, na wachache wanatoa yenye thamani kubwa zaidi kama sadaka Kwangu. Je, nyinyi wote si sawa kwa njia hii? Iwapo, kama mmoja wa watu Wangu kwenye ufalme, huwezi kufanya wajibu wenu, mtachukiwa na kukataliwa na Mimi!

Jumanne, 7 Mei 2019

Tofauti Kati Ya Kumfuata Mungu na Kuwafuata Watu

5. Tofauti Kati Ya Kumfuata Mungu na Kuwafuata Watu

Maneno Husika ya Mungu:
Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno ya Mungu leo. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno ya Mungu leo, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake. Haijalishi vile ulichoelewa awali ni cha ajabu na safi, Mungu hakitaki, na kama huwezi kuweka kando vitu hivyo, basi vitakuwa kizuizi kikubwa mno kwa kuingia kwako katika siku za baadaye. Wale wote ambao wanaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Watu wa enzi zilizopita pia walifuata nyayo za Mungu, ilhali hawangeweza kufuata mpaka leo; hii ndiyo baraka ya watu wa siku za mwisho. Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu.

kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa huchukuliwa kama wenye dharau. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.

Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuchukua mtazamo ambapo unaona kazi ya Kristo kuwa ngumu sana kukubali na huko tayari kuikubali. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa ulilazimishwa. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.

kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Kumfuata Mungu humaanisha kumsikiliza Mungu katika kila kitu, kuitii mipango yote ya Mungu, kutenda kulingana na maneno ya Mungu, na kuyakubali yote yatokayo kwa Mungu. Kama unamwamini Mungu, basi unapaswa kumfuata Mungu; lakini, bila kulitambua, wakati wanapomwamini Mungu watu wengi huwafuata watu, ambalo ni jambo la mzaha na la kuhuzunisha. Kusema kwa kweli, yeyote watu wanayemfuata ni yule wanayemwamini. Ingawa watu wengine humwamini Mungu kwa jina tu, mioyoni mwao hakuna Mungu; katika mioyo yao, wao huwaabudu viongozi wao. Kuwasikiliza viongozi wa fulani, na kwenda hata kiasi cha kuikataa mipango ya Mungu, ni onyesho la kumwamini Mungu lakini kuwafuata watu. Kabla ya hawajapata ukweli, imani ya kila mtu imevurugika na kuchanganyikiwa kama hili. Wao hata hawajui kabisa maana ya kumfuata Mungu, na wanashindwa kusema tofauti kati ya kumfuata Mungu na kuwafuata watu. Wao huamini tu kwamba yeyote anayesema mafundisho mema, na ya juu, ni baba au mama yao; kwao, yeyote aliye na maziwa ni mama yao, na yeyote aliye na nguvu ni baba yao. Hivyo ndivyo jinsi wanavyosikitisha. Inaweza kusemwa kuwa, kwa hatua tofauti tofauti, hii ndiyo hali ya kiroho ya watu wengi.

Inamaanisha nini kumfuata Mungu? Na unawezaje kutia hilo katika vitendo? Kumfuata Mungu hakuhusishi tu kumwomba Mungu na kumsifu Mungu; kilicho muhimu zaidi ni kula na kunywa maneno ya Mungu na kuishi kulingana na maneno ya Mungu, kutenda kulingana na ukweli, kutafuta njia ya kupata uzoefu wa maisha katikati ya maneno ya Mungu, kukubali agizo la Mungu, kutekeleza kila moja ya wajibu wako vizuri, na kuitembea njia iliyo mbele yako kama unavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Hasa, katika nyakati muhimu, wakati matatizo makuu yanapokufika, kuna hata haja kubwa zaidi ya kutafuta maana ya Mungu, kuwa na hadhari ya kudanganywa na mafundisho ya mwanadamu, na kutokuwa chini ya udhibiti wa mtu yeyote. “Kile kitokacho kwa Mungu mimi hukitii na kukifuata, lakini ikiwa kinatoka kwa mapenzi ya mwanadamu mimi hukikataa kwa uthabiti; wakati kile kinachohubiriwa na viongozi au wafanyakazi kina mgongano na mipango ya Mungu, basi mimi bila shaka humfuata Mungu na kuwakataa watu. Kama kina makubaliano kamili na mipango na mapenzi ya Mungu, basi naweza kukisikiliza.”

Inamaanisha nini kuwafuata watu? Kuwafuata watu inamaanisha mtu huwafuata wafanyakazi au viongozi anaowaabudu. Mungu hana nafasi kubwa katika mioyo yaomoyo wake; yeye hutundika kidokezo akisema anamwamini Mungu, na katika kila kitu anachofanya yeye ni kujifananisha na watu au kuwaiga. Hasa wakati ni jambo kuu, anawaacha watu kuamua, anawaacha watu waongoze jaala yao, yeye mwenyewe hatafuti maana ya Mungu, na anashindwa kutambua maneno yanayosemwa na watu. Mradi anachokisikia kinaonekana kuwa cha maana, basi bila kujali kama kinapatana na ukweli bado yeye hukikubali na kukisikiliza. Haya ni maonyesho ya kuwafuata watu. Imani ya watu kama hao katika Mungu haina kanuni, hakuna ukweli katika matendo yao, wao husikiliza mtu yeyote anayesema jambo la maana, na hata vijimungu vyao vikichukua njia mbaya, wao huvifuata mpaka mwisho. Mungu Akivilaani vijimungu vyao, basi watakuwa na dhana juu ya Mungu, na kushikilia kikiki vijimungu vyao. Sababu zao ni kwamba “tunapaswa kumsikiliza yeyote aliye na madaraka juu yetu; nguvu ya karibu ni bora kuliko nguvu ya juu.” Hii ni mantiki duni, upumbavu mtupu, lakini huo ndio upumbavu wa hao ambao huwafuata watu. Wale wanaowafuata watu hawana ukweli. Ni wale tu ambao humfuata Mungu wanaoamini kweli katika Mungu; Wale wanaowafuata watu huabudu sanamu, wamekuwa wakidanganywa na watu, na katika mioyo yao hakuna Mungu wala ukweli.

kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Watu wengi humwamini Mungu lakini hawajui ni nini maana ya kumtii Mungu, na hufikiri kwamba kuwasikiliza viongozi wao katika vitu vyote ni sawa na kumtii Mungu. Maoni kama haya ni ya upuuzi kabisa, kwa sababu chanzo cha utii wao si sahihi. Wao hudhukuru kuwasikiliza viongozi wao kuwa ni kumtii Mungu. Kumwamini Mungu kulingana na maoni haya ni kumwamini Mungu kwa jina tu; kwa uhakika, watu hawa huwaamini watu. …

Tunapomwamini Mungu, Mungu anapaswa kushikilia mahali pa kuongoza katika mioyo yetu, tunapaswa kusalimisha uongozi kwa Mungu katika mambo yote, tunapaswa kutafuta maana ya Mungu katika kila kitu, vitendo vyetu vinapaswa kulingana na maneno ya Mungu, na kwa mujibu wa mwongozo wa Roho Mtakatifu, na tunapaswa kutii yote yatokayo kwa Mungu. Ukiwasikiliza watu, basi hili linathibitisha kwamba Mungu hana mahali moyoni mwako, kwamba ni watu pekee walio na mahali katika moyo wako. Hakuna kilicho muhimu zaidi kwa watu kuliko kufuatilia ukweli na kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Ikiwa huzingatii kuyatafuta malengo ya Mungu na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, basi wako si utii wa kweli. Haijalishi ni sahihi jinsi gani wanavyosikika, ikiwa daima wewe huwasikiliza watu, basi kwa kiini wewe huwasikiliza watu–ambako si sawa na kumtii Mungu. Kwa kweli, kama wale wanaomwamini Mungu wanaweza kuelewa maana ya Mungu moja kwa moja kutoka kwa maneno Yake, ikiwa wanaweza kupata njia yao wenyewe ya kutenda katika maneno Yake, na huwasiliana ukweli kwa karibu, na kuuelewa ukweli, kwa maneno Yake, baada ya hayo wao waiweke katika vitendo, na ikiwa kwa wakati muhimu, wanaweza kuomba zaidi, na kutafuta uongozi wa Roho Mtakatifu, na kutii malengo ya Roho Mtakatifu, hivi kweli ni kumtii Mungu. Wale wanaomtii Mungu hutafuta njia katika maneno ya Mungu, matatizo yao hutatuliwa katika maneno ya Mungu, na wao hufanya kazi katikati ya uongozi wa Roho Mtakatifu; hivi kweli ni kumtii Mungu. Wale ambao husikiliza viongozi wao katika kila kitu wana hakika ya kupotea mbali na Mungu katika mioyo yao. Zaidi ya hayo, hawana amani mbele ya Mungu, sio wale wanaoishi mbele ya Mungu na kutafuta ukweli, hawana uhusiano na Mungu, na kanuni ya matendo yao ni kumsikiliza yeyote anayesema mambo halisi–mradi ni kiongozi, watatii. Vitendo kama hivyo ni vya dhihaka. Hawana ukweli wala uwezo wa kutofautisha, na wanaweza tu kudhibitisha kilicho sawa au kibaya kulingana na mawazo yao au akili, kwa hiyo jinsi gani wanaweza kujua kama kinafanana na ukweli? Kama wao huamini Mungu kulingana na maoni hayo, basi katika maisha yao yote hawatauelewa ukweli au kumjua Mungu. Aina hizo za imani zinaweza kusemwa kuwa kuamini katika ubongo wao wenyewe na kuitembea njia yao wenyewe, na hawana uhusiano na Mungu wa vitendo.

kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Jumamosi, 4 Mei 2019

1. Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

1. Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu.
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Kwa imani yao, yote yanayohitajika kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kuhifadhi sheria, na iwapo watatubu na kukiri dhambi zao, dhamira ya Mungu milele itaridhika. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?
kutoka katika “Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu kazi ya Mungu mara zote huwa na masuala mapya, hivyo pana kazi mpya, na hivyo basi kuwepo na kazi iliyopitwa na wakati. Hapana ukinzani kati ya kazi mpya na ya zamani, ila zinatoshelezana, kila hatua ikifuata iliyotangulia. Kwa kuwa kuna kazi mpya, mambo ya zamani, kwa hakika, ni sharti yaondolewe. Kwa mfano, baadhi ya vitendo vilivyokita mizizi na misemo ya mwanadamu iliyozoeleka, kuongeza juu miaka mingi ya mazoea na mafundisho ya mwanadamu, ilimuumbia mwanadamu kila aina ya dhana. Maelezo ya mwanadamu kuhusu dhana kama hizi ni kwamba bado Mungu hajafichua uso Wake halisi na tabia Yake asili kwa mwanadamu, pamoja na kuenea kwa nadharia za kale kwa miaka mingi. Ni haki kusema kuwa katika kipindi cha imani ya mwanadamu kwa Mungu, ushawishi wa dhana mbalimbali umesababisha kutengenezwa na kubadilika kwa ufahamu kwa mwanadamu ambapo mwanadamu ana kila aina ya dhana kumhusu Mungu—na matokeo yake ni kuwa wengi wa watu wa kidini wanaomhudumia Mungu wamegeuka kuwa adui Zake. Kwa hivyo, kadiri dhana za watu ya kidini zinavyokuwa thabiti, ndivyo wanavyozidi kumpinga Mungu, na ndivyo wanavyozidi kuwa maadui wa Mungu. Kazi ya Mungu daima huwa mpya, si kongwe na huwa haitengenezi mafundisho ya kidini na badala yake inabadilika kila mara na kuwa mpya kwa kiwango fulani. Kazi hii ni onyesho la tabia ya asili ya Mungu Mwenyewe. Vilevile ni kanuni ya asili ya kazi ya Mungu na mojawapo ya njia ambazo Mungu hutimiza usimamizi Wake. Iwapo Mungu asingefanya kazi kwa njia hii, mwanadamu asingebadilika au kuweza kumfahamu Mungu, na Shetani asingeshindwa. Hivyo basi, kila mara katika kazi Yake, kunatokea mabadiliko ambayo yanaonekana hayatabiriki, ila ambayo, kwa hakika, yana kipindi chake. Njia mwanadamu anavyomwamini Mungu hata hivyo ni tofauti. Anashikilia mifumo ya zamani ya kidini na kadiri yalivyo ya zamani, ndivyo yanavyokuwa ya kupendeza kwake. Akili ya kipumbavu ya mwanadamu, akili isiyobadilika kama mawe inawezaje kukubali kazi nyingi isiyoeleweka mpya na maneno ya Mungu? Mwanadamu anamchukia Mungu ambaye ni mpya kila siku na si wa zamani; anampenda Mungu wa zamani ambaye Amejaa mvi na Asiyepiga hatua. Hivyo, kwa sababu Mungu na mwanadamu kila mmoja analo alipendalo, mwanadamu amekuwa adui wa Mungu. Kwa kiwango kikubwa, huu utata upo hata leo, wakati ambao Mungu amekuwa akifanya kazi mpya kwa takribani miaka 6000. Hawawezi kusaidika. … Madhumuni ya Mungu mara zote ni kuona kazi Yake ikiwa mpya na hai, si kongwe na iliyokufa, na kile Anachotaka mwanadamu ashikilie kwa nguvu kinabadilika kulingana na enzi na kipindi, na si cha kudumu milele na kisichobadilika. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu ambaye husababisha mwanadamu kuishi na kuwa mpya, tofauti na ibilisi anayemsababishia mwanadamu kufa na kuwa mzee. Je, bado hamlielewi hili? Una dhana kuhusu Mungu na umeshindwa kuziacha kwa kuwa hutafakari. Si kwamba kuna maana kidogo sana katika kazi ya Mungu, au kwa sababu kazi ya Mungu hailingani na matakwa ya binadamu—wala kwamba Mungu mara zote ni “mzembe katika wajibu Wake.” Huwezi kuacha dhana zako kwa kuwa umepungukiwa na utiifu, na huna sifa hata kidogo za kiumbe wa Mungu, na si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu. Yote haya umejisababishia na hayana uhusiano na Mungu; mateso na misukosuko yote husababishwa na mwanadamu. Dhamira za Mungu mara zote huwa nzuri: hakusudii kukufanya uzitoe dhana, ila angependa ubadilike na uwe mpya kadiri enzi zinavyopita. Ila bado huwezi kutofautisha chokaa na jibini na kila mara ama unachunguza au unachanganua. Si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu, ila ni kuwa humheshimu Mungu na uasi wako umezidi. Kiumbe mdogo anathubutu kuchukua sehemu ndogo ya kile alichopewa mwanzo na Mungu na kukitumia ili kumvamia Mungu—je, huu si uasi wa mwanadamu? Ni haki kusema kuwa mwanadamu hana sifa kabisa za kutoa maoni yake mbele za Mungu, sembuse kubuni apendavyo kanuni zozote zile zisizo na thamani, za kuchukiza na zilizooza—bila kutaja chochote kuhusu hizo dhana zilizooza. Haina maana?
kutoka katika “Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako wa zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.
kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?
kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu. …
Chanzo cha ufunuo wa upotovu wa tabia ya mwanadamu ni dhamiri yake iliyofifia, asili yake mbovu na akili yake isiyo timamu; kama dhamiri ya mwanadamu na hisia vinaweza kurudi kawaida, basi atafaa kwa matumizi mbele ya Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa dhamiri ya mwanadamu daima imekuwa isiyosikia, akili ya mwanadamu haijawahi kuwa timamu, na inazidi kuwa hafifu ndio mwanadamu amezidisha uasi wake kwa Mungu, hata akampiga Yesu misumari juu ya msalaba na kumkataa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kuingia katika nyumba yake, na analaani mwili wa Mungu, na anaona mwili wa Mungu kuwa ya kuchukiza na wa hali ya chini. Kama mwanadamu angekuwa na ubinadamu kidogo, hangekuwa mkatili kiasi hicho katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na akili hata kidogo tu, hangekuwa hivyo katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na dhamiri hata kidogo, hangekuwa mwenye “shukrani” kwa Mungu mwenye mwili kwa njia hii. Mwanadamu anaishi katika enzi ya Mungu kuwa katika mwili, lakini yeye hawezi kumshukuru Mungu kwa kumpatia nafasi nzuri kiasi hicho, na badala yake analaani kuja kwa Mungu, au kupuuza kabisa ukweli wa Mungu aliyepata mwili, na inaonekana anapinga hali hii na anachoshwa nayo. Haijalishi jinsi mwanadamu anachukua kuja kwa Mungu, Mungu, kwa ufupi, daima ameendeleza kazi yake bila kujali—hata kama mwanadamu hajawahi kumkaribisha, na bila kujua yeye hufanya maombi kwa Mungu. Tabia ya mwanadamu imekuwa mbaya zaidi, akili yake imekuwa hafifu zaidi, na dhamiri yake imekanyagwa kabisa na yule muovu na kwa muda mrefu imekoma kuwa dhamiri ya awali ya mwanadamu.
kutoka katika “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Jumapili, 28 Aprili 2019

Waumini katika Mungu Wanapasa Kujiandaa kwa Ajili ya Hatima Yao kwa Matendo Mema ya Kutosha

7. Waumini katika Mungu Wanapasa Kujiandaa kwa Ajili ya Hatima Yao kwa Matendo Mema ya Kutosha

Maneno Husika ya Mungu:

Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika mamilioni ya miaka, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga. Na wale wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu pekee watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya wanadamu na kuchukia matendo yao maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu, Nikisubiri tu nafasi kutoa adhabu kwa hao na kufurahia kuona hilo. Siku Yangu hatimaye imefika na siwezi kusubiri zaidi!

Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

kutoka katika “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili

Natarajia tu kuwa katika hatua ya mwisho ya kazi Yangu, mnaweza kutekeleza kwa kujitokeza, kujitoa kikamilifu, na wala sio shingo upande tena. Bila shaka, Natarajia pia kuwa nyote muwe na hatima nzuri. Hata hivyo, bado Nina mahitaji Yangu ambayo ni kwenu nyinyi mfanye uamuzi bora kabisa katika kujitoa Kwangu pekee na moyo wa ibada ya mwisho. Kama mtu hana moyo huo wa ibada pekee, mtu huyo hakika atakwenda kuwa thamani ya Shetani, na Mimi Sitaendelea kumtumia. Nitamtuma nyumbani akatunzwe na wazazi wake.

kutoka katika “Juu ya Hatima” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mnapaswa kufanya wajibu wenu wenyewe kwa kadri ya uwezo wenu kwa mioyo iliyo wazi na wima, na muwe tayari kufanya chochote kitakachohitajika. Kama mlivyosema, wakati siku itakuja, Mungu Hatamtendea mtu yeyote vibaya ambaye aliteseka au kulipa gharama kwa ajili Yake. Aina hii ya imani ni yenye thamani kuishikilia, na hampaswi kuisahau kamwe. Ni tu kwa njia hii Ninaweza kutuliza akili Yangu kuwahusu. Vinginevyo, Sitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu, na milele mtakuwa malengo ya chuki Yangu. Kama nyote mnaweza kufuata dhamiri zenu na kutoa yote kwa ajili Yangu, msiwache jitihada zozote kwa ajili ya kazi Yangu, na kutenga maisha ya jitihada za kazi ya injili Yangu, basi si moyo Wangu mara kwa mara utaruka kwa furaha kwa ajili yenu? Si Mimi Nitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu?

kutoka katika “Juu ya Hatima” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme.

kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Matendo mema ni ushahidi kwamba tumepata wokovu, na ni dhihirisho la kuingia kwetu katika ukweli na uhalisi wa neno la Mungu. Kama tumetayarisha matendo mengi mema, hilo linamaanisha kwamba tumekuwa watu wapya mbele za Mungu na kwamba tuna ushahidi wa kweli katika kipengele cha kuwa binadamu halisi. Matendo yetu mema ndiyo yanayoonyesha hasa kwamba tumetubu kwa kweli; ikiwa tumetayarisha matendo mengi mema, hili linamaanisha kuwa tuna mfano wa kweli wa mtu. Ikiwa umemwamini Mungu kwa miaka mingi lakini umefanya matendo mema machache, basi una mfano wa binadamu? Je, una dhamiri na mantiki? Je, wewe ni mtu anayelipiza upendo wa Mungu? Iko wapi imani yako ya kweli? Uko wapi moyo wako wa upendo na utii kwa Mungu? Ni uhalisi upi umeingia ndani? Huna chochote kati ya haya. Kwa hiyo, mtu asiyefanya matendo mema ni mtu asiyepokea chochote kutoka kwa imani yake kwa Mungu. Yeye ni mtu ambaye hajapata kabisa wokovu kutoka kwa Mungu, mtu ambaye upotovu wake ni wa kina sana na ambaye hajabadilika hata kidogo. Matendo mema kweli yanafafanua hili.

kutoka katika “Maana Muhimu ya Kuandaa Matendo Mema” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha II

Matendo mema ya kutosha ni yapi? Tunaweza kusema kwamba wajibu wowote ambao mtu anaweza au anapaswa kuutimiza katika uzoefu wake wa kazi ya Mungu, na kitu chochote ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa mwanadamu—kama mwanadamu anaweza kufanya vitu hivi na anaweza kumridhisha Mungu, basi haya yote ni matendo mema Kama unaweza kuyatosheleza mahitaji ya Mungu, basi ni tendo jema. Kama una moyo wa ibada kwa Mungu wakati unapotimiza wajibu wako, basi ni tendo jema. Kama mambo unayoyafanya ni ya manufaa kwa watu waliochaguliwa na Mungu na kila mtu anafikiria kwamba unayoyafanya ni mazuri, basi ni tendo jema. Mambo yote ambayo dhamiri na mantiki ya mwanadamu huamini kuwa ni kulingana na madhumuni ya Mungu ni matendo mema. Mambo ambayo yanaweza kumridhisha Mungu na yana manufaa kwa watu wateule wa Mungu pia ni matendo mema. Kama mtu anaweza kufanya kila kitu ili kuyatayarisha haya matendo mema ambayo tumetoka kuzungumzia, hatimaye ataweza kuyatimiza, na hilo litamaanisha kuwa amekamilisha matendo mema ya kutosha. … Kila mtu sasa hutaka kutekeleza kazi yake na kufuatilia wokovu, lakini haitoshi tu kuwa na azimio na shauku. Mtu lazima aonyeshe tabia za utendaji na kuchukua hatua ya utendaji. Ni wajibu gani umetekeleza kwa ajili ya kuingia katika maisha ya watu wa Mungu wateule? Umefanya nini na ni thamani gani umelipa ili kuyaridhia matakwa ya Mungu? Umefanya nini ili kumridhisha Mungu na kulipa upendo Wake? Haya yote ni mambo ambayo inakubidi kuyatafakaria. Kama umefanya mambo mengi na kulipa thamani kubwa kwa ajili ya kuyaridhia matakwa ya Mungu na kwa ajili ya kuingia katika maisha na ukuaji wa watu wa Mungu wateule, basi inaweza kusemwa kuwa umeandaa matendo mema ya kutosha.

kutoka katika “Maana Muhimu ya Kuandaa Matendo Mema” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha II

Kwa kiwango cha chini, kutimiza kazi kiasi haitoshi peke yake kufanyiza kiasi cha kuridhisha cha matendo mema. Hivyo ni kusema, kutekeleza tu kiasi kidogo cha wajibu wako hakufikiriwi kuwa matendo mema ya kuridhisha hata kidogo. Matendo mema ya kuridhisha bila shaka sio rahisi kama watu wafikiriavyo. Kuandaa kiasi cha kuridhisha cha matendo mema huhitaji kujitumia kabisa kwa ajili ya Mungu. Aidha, kunahitaji kulipa kila thamani, na kuwa mwaminifu kwa agizo la Mungu tangu mwanzo hadi mwisho kwa imani nzuri; hii ndiyo njia ya pekee ya kuyaridhia matarajio ya Mungu.

Katika kutimiza wajibu wao kuna watu ambao kweli wamelipa thamani, wakafanya mambo ambayo yamesifiwa na Mungu, ambao wametekeleza wajibu wao kwa njia ambazo ni nzuri kabisa, za ajabu, za kupendeza na za kufanikiwa sana kiasi kwamba wanaweza kufikiriwa kuwa wametekeleza matendo mema. Baadhi ya ndugu na dada wamekwenda jela kwa sababu ya kutekeleza wajibu wao, ambao wamepitia maumivu mengi makali bila kumtii Shetani, na wamekuwa mashahidi. Kisha kuna watu ambao huthubutu kujiingiza hatarini bila kujali usalama wa kibinafsi au manufaa, ambao wamejitolea kufanya kazi za hatari kwa roho ya kufanya lililo la haki kwa ujasiri. Na kuna wale ndugu na dada ambao wanaweza kujitolea kwa kazi ya injili, na wanaweza kuvumilia fedheha katika kuhubiri injili ili kuwaokoa watu. Pia kuna wale wenye bidii katika kazi ya injili, wakivumilia shida bila malalamiko, wakiweka kando mambo ya kibinafsi na ya familia huku mawazo yao yakijawa na jinsi wanavyoweza kueneza injili ili kuwaleta watu zaidi mbele ya Mungu na kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Wote ambao wamejitolea kujitumia kabisa ili kumridhisha Mungu ni wale watu ambao tayari wamefanya matendo mema. Lakini bado wana umbali fulani kutoka kwa “matendo mema ya kuridhisha” ambayo Mungu hutaka. Watu wengi wameandaa tu matendo mema kiasi na hawajayaridhia kabisa matakwa ya Mungu. Hilo linatuhitaji kufanya tunaloweza ili kutimiza wajibu wetu na tuwe na bidii katika kuingia ndani kabisa ya ukweli ili kutekeleza matendo mema ya kuridhisha. Hili linatuhitaji tutafute kufanikisha matokeo bora sana ili kuuridhisha moyo wa Mungu, bila kujali ni wajibu gani tunaoutimiza. Hasa katika kueneza injili, bila kujali jinsi fedheha tunayopitia ilivyo kubwa au ni mateso kiasi gani tunayoyavumilia, mradi tunaweza kuwaleta watu zaidi kupata wokovu, ni lazima tuuchukue kama wajibu bila kujali gharama za kibinafsi. Huku tu ndio kutekeleza tendo bora sana. Kama watu wanaweza kutekeleza matendo zaidi yaliyo mema kama hili, hayo yanaweza kufikiriwa kuwa matendo mema ya kuridhisha. Hilo ndilo humletea Mungu furaha na shangwe mno, na watu kama hao kwa hakika watapokea sifa za Mungu. Mbali na hili, katika kutimiza wajibu wetu ni lazima pia tuwe makini na waangalifu sana, daima tukitafuta kujiboresha, na kutojiruhusu kuzembea hata kidogo. Ili kujitumia kwa ajili ya Mungu, ni lazima tuwe na kujitolea kwa uaminifu kabla tuweze kuyaridhisha mapenzi ya Mungu kabisa.

kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Chanzo: Tushughulikie Vipi Umeme wa Mashariki kwa Njia Inayolingana na Mapenzi ya Bwana?

Jumamosi, 13 Aprili 2019

Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme

Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme

1. Mwanadamu hapasi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.
2. Unapaswa kufanya lolote ambalo lina manufaa kwa kazi ya Mungu, na hupasi kufanya chochote ambacho kitaleta madhara kwa manufaa ya kazi ya Mungu. Unapaswa kutetea jina la Mungu, ushahidi Wake, na kazi ya Mungu.
3. Pesa, vitu vya dunia, na mali yote ambayo yako katika kaya ya Mungu ni sadaka ambazo zinapasa kutolewa na binadamu. Sadaka hizi hazifai kufurahiwa na binadamu yeyote ila kasisi na Mungu Mwenyewe, kwani sadaka zinazotolewa na binadamu ni za kufurahiwa na Mungu, Mungu pekee ndiye Anayeweza kumgawia kasisi sadaka hizi, na hakuna mwengine yeyote aliyehitimu wala kuwa na haki ya kufurahia sehemu yoyote ya sadaka hizi. Sadaka zote zinazotolewa na mwanadamu (ikiwemo pesa na vitu vinavyoweza kufurahiwa kimwili) vinapewa Mungu, na sio kwa mwanadamu. Na hivyo, vitu hivi havipaswi kufurahiwa na mwanadamu; iwapo mwanadamu angevifurahia vitu hivi, basi angekuwa anaiba sadaka. Yeyote yule atakayefanya hili ni msaliti kama Yuda, kwa kuwa, zaidi ya yuda kuwa msaliti. Yuda alijitwalia vilivyokuwa katika mfuko wa hela.
4. Mwanadamu anayo tabia ya upotovu na, zaidi ya hayo, amejawa na hisia. Kwa hivyo, ni marufuku kabisa kwa watu wa jinsia mbili tofauti kufanya pamoja kazi wakati wa kumtumikia Mungu. Yeyote yule atakayepatikana na kosa hili atatupiliwa mbali, bila ubaguzi—na hakuna atakayeepuka hili.
5. Hupasi kumhukumu Mungu, au kujadili kwa kawaida mambo yanayomuhusu Mungu. Unapaswa kutenda vile mwanadamu anavyopaswa kutenda, na kuzungumza jinsi mwanadamu anapasa kuzungumza, na hupasi kuvuka upeo wako wala kuvuka mipaka yako. Uchunge ulimi wako na uwe mwangalifu na hatua zako. Yote haya yatakuzuia kufanya jambo lolote linaloweza kukosea tabia ya Mungu.
6. Unapaswa kufanya yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu, na kutenda wajibu wako, na kutimiza majukumu yako, na kushikilia jukumu lako. Kwa sababu unaamini katika Mungu, unapasa kutoa mchango wako kwa kazi ya Mungu; kama huwezi, basi wewe hufai kula na kunywa maneno ya Mungu, na hufai kuishi katika nyumba ya Mungu.
7. Katika kazi na mambo yanayohusiana na kanisa, kando na kumtii Mungu, katika kila kitu unapaswa kufuata maagizo ya mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata kosa lolote hata liwe dogo kivipi halikubaliwi. Lazima uwe mkamilifu katika kutii kwako, na hupasi kuchunguza kati ya mazuri na mabaya; yaliyo mazuri au mabaya hayakuhusu. Unapaswa kujishughulisha tu na utiifu kamili.
8. Watu wanaoamini katika Mungu wanapaswa kumtii na kumwabudu. Hupasi kusifu au kumwabudu mtu yeyote; hupaswi kumpa Mungu nafasi ya kwanza, binadamu unayemheshimu nafasi ya pili, kisha wewe mwenyewe nafasi ya tatu. Mtu yeyote asishikilie nafasi yoyote moyoni mwako, na hufai kuzingatia watu—hasa wale unaowaenzi—kuwa katika kiwango sawa na Mungu, kuwa sawa na Yeye. Mungu hawezi kustahimili hili.
9. Mawazo yako yanapasa kuwa ya kazi ya kanisa. Unapaswa kuweka kando matarajio ya mwili wako, uwe na msimamo dhabiti kuhusu mambo ya kifamilia, na ujitoe kwa moyo wako wote kwa kazi ya Mungu, na uiweke kazi ya Mungu kwanza kisha maisha yako katika nafasi ya pili. Huu ndio mwenendo mwema wa utakatifu.
10. Jamaa zako (watoto, mke au mume, dada zako au wazazi wako na kadhalika) wasio wa imani yako hawapaswi kulazimishwa kuja kanisani. Nyumba ya Mungu haina ukosefu wa washirika, na hakuna haja ya kuijaza na watu wasiokuwa na maana katika nyumba Yake. Wale wote wasioamini kwa moyo mchangamfu, hawapaswi kuongozwa kuingia kanisani. Amri hii inaelekezwa kwa kila mwanadamu. Kuhusu hili jambo mnapaswa kuchunguza, mfuatilie na mkumbushane, na hakuna anayepasa kukiuka amri hii. Hata jamaa wako wasio wa imani yako wanapoingia kanisani shingo upande, hawapaswi kupatiwa jina mpya wala kupewa vitabu vya kanisa; watu kama hao si wa kaya ya Mungu, na kuingia kwao kanisani kunapaswa kukomeshwa kwa udi na uvumba. Iwapo matatizo yataletwa kanisani kwa sababu ya uvamizi wa mapepo, basi wewe mwenyewe utafukuzwa au kuwekewa vikwazo. Kwa ufupi, kila mmoja anayo jukumu katika hili jambo, lakini pia hupasi kuwa asiyejali, wala kutumia jambo hili kulipiza kisasi cha kibinafsi.
Soma Zaidi: Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Alhamisi, 4 Aprili 2019

Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Mwenyezi Mungu alisema, Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaelekea kikomo, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnasubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? Wale wote wanaosubiri kuonekana kwa Mungu wanakumbana na maswali kama haya. Nyinyi nyote mmewahi kuyafikiria zaidi ya mara moja—ila matokeo ni gani? Mungu hujidhihirisha wapi? Nyayo za Mungu zipo wapi? Mmepata majibu? Majibu ya watu wengi yangekuwa: Mungu hudhihirika miongoni mwa wale wanaomfuata na nyayo Zake zimo miongoni mwetu; ni rahisi hivyo! Mtu yeyote anaweza kutoa jibu kwa kutumia mbinu fulani, lakini je, mnafahamu kuonekana kwa Mungu ni nini, na nyayo za Mungu ni nini? Kuonekana kwa Mungu hurejelea kuwasili Kwake duniani kufanya kazi Yake. Akiwa na utambulisho na tabia Yake, na katika mbinu Yake ya asili, Yeye hushuka miongoni mwa wanadamu kufanya kazi ya kuanzisha enzi mpya na kukamilisha enzi nyingine. Kuonekana kwa aina hii si aina fulani ya sherehe. Si ishara, picha, muujiza, au ono kuu, na hata zaidi si mchakato fulani wa kidini. Ni ukweli halisi ambao waweza kushikwa na kuonekana. Kuonekana kama huku si kwa ajili ya kufuata taratibu, au kwa ajili ya shughuli ya muda mfupi; ni, badala yake, kwa ajili ya hatua ya kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Kuonekana kwa Mungu daima ni kwenye maana na daima huenda pamoja na mpango wa usimamizi. Kuonekana huku ni tofauti kabisa na udhihirisho wa uongozi wa Mungu, utawala na kupata nuru kwa mwanadamu. Mungu hufanya kazi kubwa kila mara Anapojifunua. Kazi hii ni tofauti na enzi yoyote nyingine. Haiwezi kufikirika na mwanadamu na haijawahi na mwanadamu hana uzoefu huu. Ni kazi ambayo huanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya awali, na ni aina mpya ya kazi na iliyoboreshwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu; aidha, ni kazi ya kuleta wanadamu katika enzi mpya. Huo ndio umuhimu wa kuonekana kwa Mungu.
Katika wakati uo huo wa kuelewa kuonekana kwa Mungu, mnapaswa kutafuta nyayo za Mungu vipi? Swali hili si gumu kueleza: Palipo na kuonekana kwa Mungu; mtapata nyayo za Mungu. Maelezo kama haya yanaonekana yapo wazi, ila si rahisi kuelezea kwani watu wengi hawafahamu pale Mungu anapojidhihirisha, wala pale ambapo Angependa kujidhihirishia ama iwapo Anapaswa kujidhihirisha. Wengine kwa msukumo huamini kuwa palipo na kazi ya Roho Mtakatifu kuna kuonekana kwa Mungu. Ama sivyo watu huamini kuwa palipo na watu mashuhuri wa kiroho ndipo Mungu huonekana. Vinginevyo, wanaamini kuwa palipo na watu wanaojulikana vyema ndipo Mungu huonekana. Kwa sasa tusishauriane ikiwa imani hizi ni sahihi au la. Kujibu swali kama hilo, kwanza ni lazima tuwe wazi kuhusu lengo: tunazitafuta nyayo za Mungu. Hatutafuti viongozi wa kiroho, wala kutafuta watu mashuhuri; tunafuata nyayo za Mungu. Kwa hivyo, kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa “Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.” Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani! Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulinganishwa na fikira za mwanadamu, sembuse Mungu kuonekana kwa amri ya mwanadamu. Mungu hufanya uamuzi Wake mwenyewe na huwa na mipango Yake Afanyapo kazi; aidha, Ana malengo Yake, na mbinu Zake. Si lazima Ajadiliane kazi Azifanyazo na mwanadamu au Atafute ushauri wa mwanadamu, au hata kumfahamisha kila mtu kuhusu kazi Yake. Hii ndiyo tabia ya Mungu na zaidi inafaa kutambuliwa na kila mmoja. Kama mnatamani kushuhudia kuonekana kwa Mungu, kama mnatamani kufuata nyayo za Mungu, basi kwanza ni sharti mzishinde dhana zenu. Ni sharti muache kudai kuwa Mungu afanye hiki au kile sembuse kumweka Yeye ndani ya mipaka yenu wenyewe na kumwekea upeo kwa dhana zenu. Badala yake, mnafaa kujua ni vipi mtazitafuta nyayo za Mungu, na vipi mnapaswa kukubali kuonekana kwa Mungu na ni vipi mnapaswa kutii kazi mpya ya Mungu; hiki ndicho kinapaswa kufanywa na mwanadamu. Kwa kuwa mwanadamu si ukweli, na hamiliki ukweli, mwanadamu anafaa kutafuta, kukubali na kutii.
Bila kujali kama wewe ni Mmarekani, Mwingereza, au mtu wa taifa jingine, ni lazima utoke nje ya mipaka yako, ni lazima ujipite, na ni sharti uione kazi ya Mungu kama kiumbe wa Mungu. Kwa njia hii, hutaweka vikwazo katika nyayo za Mungu. Kwa sababu, leo, watu hufikiri kuwa haiwezekani Mungu kudhihirika katika nchi au taifa fulani. Umuhimu wa kazi ya Mungu una undani kiasi gani, na kuonekana kwa Mungu kuna maana ilioje! Vinawezaje kupimwa kwa dhana na fikira za mwanadamu? Na ndiyo maana Ninasema kuwa unafaa kujiondoa katika mawazo ya uraia wako au kabila lako unapokutafuta kuonekana kwa Mungu. Kwa njia hii, hutafungwa na dhana zako mwenyewe; kwa njia hii, utahitimu kukaribisha kuonekana kwa Mungu. Vinginevyo, daima utakuwa gizani na hutapata kibali cha Mungu.
Mungu ni Mungu wa wanadamu wote. Hawi mali binafsi ya nchi au taifa lolote na hufanya kazi ya mpango Wake bila kuzuiwa na mfumo wowote, nchi au taifa. Labda hujawahi kuwazia mfumo huu, au labda wewe hukana uwepo wake, au labda nchi au taifa ambapo Mungu huonekana limebaguliwa na lina maendeleo duni sana duniani. Na bado Mungu ana busara Yake. Na uwezo Wake kupitia ukweli na tabia Zake kwa hakika Amepata kundi la watu wenye mawazo sawa na Yeye. Na Amepata kundi la watu ambao alitaka kutengeneza: kundi lililoshindwa Naye, watu ambao wameyavumilia majaribu machungu na aina zote za mateso na wanaweza kumfuata mpaka mwisho. Malengo ya kuonekana kwa Mungu, bila vizuizi vya nchi yoyote, ni kumruhusu Akamilishe kazi ya mpango Wake. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kutimiza kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kuwa mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu na hatimaye ikawa ni kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, na vilevile kukushutumu kuonekana huku; “kutowezekana” kwao kwa mara nyingine kunabana kuonekana kwa Mungu katika mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakicheka na kuanguka baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kukufuru kwa Wayahudi? Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli hata kidogo. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama hauwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? Mahali Mungu anajitokeza, kuna maonyesho ya kweli, na kuna sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Weka dhana zako kando. Tafakari na kusoma maneno haya kwa makini. Ukitamani ukweli, Mungu atakupa nuru ya kuyafahamu mapenzi Yake na maneno Yake. Weka kando mitazamo yenu ya “haiwezekani”! Kadiri watu wanavyoamini kuwa jambo fulani haliwezekani, ndivyo uwezekano wa utukiaji wake unavyoendelea kujiri, kwani ufahamu wa Mungu hupaa juu kuliko mbingu, mawazo ya Mungu yako juu ya yale ya mwanadamu, na kazi ya Mungu inapita mipaka ya fikira za mwanadamu. Kadiri kitu kinavyokuwa hakiwezekani, ndivyo kunavyokuwepo na ukweli wa kutafutwa; kadiri kitu kilivyo nje ya mipaka ya mawazo na fikira za mwanaadamu, ndivyo kinavyozidi kuwa na mapenzi ya Mungu. Kwani bila kujali Mungu anajidhihirishia wapi, Mungu bado ni Mungu, na kiini chake hakitawahi kubadilika kwa sababu ya mahali ama namna ya kuonekana Kwake. Tabia ya Mungu hubaki kuwa vilevile bila kujali nyayo Zake ziko wapi. Bila kujali nyayo za Mungu zilipo, Yeye ndiye Mungu wa wanadamu wote. Kwa mfano, Bwana Yesu si Mungu tu wa Waisraeli, lakini vilevile ni Mungu wa watu wote wa Asia, Ulaya, na Marekani, na hata zaidi, ndiye Mungu pekee wa ulimwengu mzima. Hivyo basi, tuyatafute mapenzi ya Mungu na tugundue kuonekana Kwake kutoka kwa matamshi Yake na tufuate nyayo Zake. Mungu ndiye ukweli, njia na uzima. Maneno Yake na kuonekana Kwake yanakuwepo sawia, na tabia na nyayo Zake daima zitafikika na wanadamu. Ndugu wapendwa, natumaini kwamba mnaweza kuona kuonekana kwa Mungu katika maneno haya, na kwamba mtaanza kuzifuata nyayo Zake kuelekea enzi mpya, na hadi katika mbingu mpya yenye kupendeza na dunia mpya iliyoandaliwa kwa wale wanaosubiri kuonekana kwa Mungu.