Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo maneno-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo maneno-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 24 Julai 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote”

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote”

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Waisraeli pekee, na Yeye si Mungu wa Wayahudi pekee; Yeye ni Mungu wa viumbe vyote. … Kazi Yake ya awali ilifanywa Yudea, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uzinduzi wa enzi hata kidogo. Hatua ya mwisho ya kazi Yake haifanywi tu miongoni mwa watu wa mataifa yasiyo ya Kiyahudi; hata zaidi ya hayo, inafanywa miongoni mwa watu waliolaaniwa. Jambo hili moja ndio ushahidi unaoweza zaidi kumwaibisha Shetani; hivyo, Mungu “anakuwa” Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni na kuwa Bwana wa vitu vyote, Anayeabudiwa na kila kiumbe mwenye uhai .” Tazama zaidi: Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu"| Musical Documentary (Swahili Subtitles)
Je, hizi zote si dhana za binadamu? Mungu aliunda mbingu na dunia yote na vitu vyote, na kuumba viumbe vyote; Angewezaje kuzuia kazi Yake ndani ya Israeli peke yake? Katika hali hiyo, kungekuwa na haja gani ya Yeye kuumba viumbe Vyake vyote? Aliiumba dunia nzima; Ametekeleza mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita sio tu ndani ya Israeli lakini pia na kila mtu ulimwenguni. Bila kujali kama anaishi Uchina, Amerika, Uingereza ama Urusi, kila mtu ni wa ukoo wa Adamu; wote wameumbwa na Mungu. Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuondoka katika mawanda ya viumbe wa Mungu, na hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuepuka utambulisho wa “ukoo wa Adamu.” Wote ni viumbe wa Mungu, na wote ni wa ukoo wa Adamu; pia ni wazawa wapotovu wa Adamu na Hawa. Sio tu Waisraeli ambao ni viumbe wa Mungu, lakini ni watu wote; hata hivyo, wengine miongoni mwa viumbe wamelaaniwa, na wengine wamebarikiwa. Kuna mambo mengi ya kupendeza kuwahusu Waisraeli; Mungu awali alikuwa akifanya kazi nao kwa sababu walikuwa watu wapotovu kwa kiasi kidogo zaidi. Wachina ni dhaifu wakilinganishwa nao, na hawawezi hata kutumaini kulingana nao; hivyo, Mungu awali alifanya kazi miongoni mwa watu wa Israeli, na hatua ya pili ya kazi Yake ilifanywa tu Yudea. Kwa sababu hii, watu huunda dhana nyingi na kanuni nyingi. Kwa kweli, iwapo Angetenda kulingana na dhana za binadamu, Mungu angekuwa tu Mungu wa Waisraeli; kwa njia hii Asingeweza kupanua kazi Yake katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, kwa sababu Angekuwa tu Mungu wa Waisraeli badala ya Mungu wa viumbe vyote. Unabii ulisema kuwa jina la Yehova lingekuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na kuwa jina la Yehova lingeenezwa kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi—mbona ulisema hivi? Iwapo Mungu angekuwa Mungu wa Waisraeli tu, basi Angefanya kazi tu Israeli. Zaidi ya hayo, Asingepanua kazi hii, na Asingefanya huu unabii. Kwa sababu Alifanya huu unabii, Angehitaji kuipanua kazi Yake hadi mataifa yasiyo ya Kiyahudi na hadi kila taifa na mahali. Kwa sababu Alisema hili, basi Angefanya hivyo. Huu ndio mpango Wake, kwani Yeye ndiye Bwana aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote, na Mungu wa viumbe vyote. Bila kujali iwapo Anafanya kazi na Waisraeli ama katika Yudea nzima, kazi Anayoifanya ni kazi ya ulimwengu mzima na kazi ya binadamu wote. Kazi Anayoifanya leo katika taifa la joka kubwa jekundu—katika taifa lisilo la Kiyahudi—bado ni kazi ya binadamu wote. Israeli inaweza kuwa kituo cha kazi Yake duniani; vivyo hivyo, Uchina pia inaweza kuwa kituo cha kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Je, sasa Hajatimiza unabii kwamba “jina la Yehova litakuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi”? Hatua ya kwanza ya kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi inahusu kazi hii Anayoifanya katika taifa la joka kuu jekundu. Kwa Mungu mwenye mwili kufanya kazi katika nchi hii na kufanya kazi miongoni mwa hawa watu waliolaaniwa hasa inaenda kinyume na dhana za binadamu; hawa watu ni wa chini zaidi na wasio na thamani yoyote. Hawa wote ni watu ambao Yehova alikuwa amewaacha mwanzoni. Watu wanaweza kuachwa na watu wengine, lakini wakiachwa na Mungu, hawa watu hawatakuwa na hadhi, na watakuwa na thamani ya kiwango cha chini zaidi. Kama sehemu ya viumbe, kumilikiwa na Shetani ama kuachwa na watu wengine yote mawili ni mambo machungu, lakini sehemu ya viumbe ikiachwa na Bwana wa viumbe, hii inaashiria kwamba hadhi yake iko katika kiwango cha chini kabisa. Wazawa wa Moabu walilaaniwa, na walizaliwa ndani ya nchi hii isiyo na maendeleo; bila shaka, wazawa wa Moabu ni watu walio na hadhi ya chini zaidi chini ya ushawishi wa giza. Kwa sababu hawa watu walimiliki hadhi ya chini zaidi zamani, kazi inayofanywa miongoni mwao inaweza kabisa kuzivunja dhana za binadamu, na pia ni kazi yenye faida kubwa zaidi kwa mpango Wake mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita. Ili Afanye kazi miongoni mwa watu hawa ni kitendo kinachoweza zaidi kuzivunja dhana za binadamu; Akiwa na hili Anazindua enzi; na hili Anavunja dhana zote za binadamu; Akiwa na hili Anatamatisha kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kazi Yake ya awali ilifanywa Yudea, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uzinduzi wa enzi hata kidogo. Hatua ya mwisho ya kazi Yake haifanywi tu miongoni mwa watu wa mataifa yasiyo ya Kiyahudi; hata zaidi ya hayo, inafanywa miongoni mwa watu waliolaaniwa. Jambo hili moja ndio ushahidi unaoweza zaidi kumwaibisha Shetani; hivyo, Mungu “anakuwa” Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni na kuwa Bwana wa vitu vyote, Anayeabudiwa na kila kiumbe mwenye uhai.
Kwa sasa bado kuna watu wengine wasioelewa ni aina gani ya kazi mpya ambayo Mungu amezindua. Mungu amefanya mwanzo mpya katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na Ameanza enzi nyingine na kuzindua kazi nyingine, na Anafanya kazi miongoni mwa ukoo wa Moabu. Je, hii si kazi Yake mpya kabisa? Hakuna yeyote katika enzi zote aliyeipitia kazi hii, wala hakuna aliyeisikia, sembuse kuithamini. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, kutoeleweka kwa Mungu, ukubwa wa Mungu, utakatifu wa Mungu vinategemea hatua hii ya kazi katika siku za mwisho, ili kuibuka wazi. Je, hii si kazi mpya inayovunja dhana za binadamu? Bado kuna wale wanaofikiria hivi: “Kwa sababu Mungu alimlaani Moabu na kusema kuwa Angewaacha wazawa wa Moabu, Angeweza kuwaokoaje sasa?” Hao ni wale watu kutoka mataifa yasiyo ya Kiyahudi waliolaaniwa na kulazimishwa nje ya Israeli; Waisraeli waliwaita “mbwa wasio wa Kiyahudi.” Kwa mtazamo wa kila mtu, wao sio mbwa wasio wa Kiyahudi pekee, lakini mbaya hata zaidi, ni wana wa maangamizi; kwa maneno mengine, wao si wateule wa Mungu. Ingawa awali walikuwa wamezaliwa ndani ya eneo la Israeli, wao siyo sehemu ya watu wa Israeli; wao pia walifukuzwa kwenda kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Wao ndio watu wa chini zaidi. Ni kwa sababu hasa wao ni watu wa chini zaidi miongoni mwa binadamu ndio Mungu anatekeleza kazi Yake ya kuzindua enzi mpya miongoni mwao, kwani wao ni wawakilishi wa binadamu wapotovu. Kazi ya Mungu haikosi uchaguzi ama madhumuni, kazi Anayoifanya miongoni mwa watu hawa leo pia ni kazi inayofanywa miongoni mwa viumbe. Nuhu alikuwa sehemu ya viumbe, kama walivyo wazawa wake. Yeyote duniani aliye na mwili na damu ni sehemu ya viumbe. Kazi ya Mungu imeelekezwa kwa viumbe wote; haitekelezwi kulingana na kama mtu amelaaniwa baada ya kuumbwa. Kazi Yake ya usimamizi imeelekezwa kwa viumbe wote, sio wale wateule wasiolaaniwa. Kwa sababu Mungu anataka kutekeleza kazi Yake miongoni mwa viumbe Vyake, kwa hakika Ataifanya hadi kukamilika kwa mafanikio; Atafanya kazi miongoni mwa hao watu walio na manufaa kwa kazi Yake. Kwa hivyo, Anavunja mikataba yote ya kufanya kazi miongoni mwa watu; Kwake, maneno “kulaaniwa,” “kuadibu” na “kubarikiwa” hayana maana! Wayahudi ni wazuri hasa, na wateule wa Israeli sio wabaya pia; ni watu wenye ubora mzuri wa tabia na ubinadamu mzuri. Awali Yehova alizindua kazi Yake miongoni mwao na Akafanya kazi Yake ya awali, lakini ingekuwa bila maana kama Angewatumia kama wapokeaji wa kazi Yake ya ushindi sasa. Ingawa wao pia ni sehemu ya viumbe na wana vipengele vingi vyema, ingekuwa bila maana kutekeleza hatua hii ya kazi miongoni mwao. Asingeweza kumshinda yeyote, wala Asingeweza kushawishi viumbe wote. Huu ndio umuhimu wa uhamisho wa kazi Yake kwa watu hawa wa taifa la joka kubwa jekundu. Maana ya ndani zaidi hapa ni ya uzinduzi Wake wa enzi, ya kuvunja Kwake kwa kanuni zote na dhana zote za mwanadamu na pia kwa kumaliza Kwake kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kama kazi Yake ya sasa ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, ikifika wakati ambao mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilika, kila mtu angeamini kuwa Mungu ni Mungu tu wa Waisraeli, kuwa Waisraeli tu ndio wateule wa Mungu, kuwa Waisraeli tu ndio wanaostahili kurithi baraka na ahadi za Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anapata mwili katika taifa lisilo la Kiyahudi la joka kubwa jekundu; Ametimiza kazi ya Mungu kama Mungu wa viumbe wote; Amekamilisha kazi Yake yote ya usimamizi, na Atamaliza sehemu kuu ya kazi Yake kwa taifa la joka kubwa jekundu. Kiini cha hatua hizi tatu za kazi ni wokovu wa mwanadamu—ambao ni, kufanya viumbe wote vimwabudu Bwana wa viumbe. Hivyo basi, kila hatua ya kazi hii ni muhimu sana; Mungu hatafanya chochote kisicho na maana ama thamani. Kwa upande mmoja, hatua hii ya kazi inajumuisha kuzindua enzi na kukamilisha enzi mbili za awali; kwa upande mwingine inajumuisha kuvunja dhana zote za mwanadamu na njia ya zamani ya imani ya mwanadamu na maarifa. Kazi ya enzi mbili za awali ilifanywa kulingana na dhana tofauti za binadamu; hatua hii, hata hivyo, inafuta kabisa dhana za binadamu, na hivyo kuwashinda binadamu kikamilifu. Kwa kutumia ushindi wa ukoo wa Moabu na kutumia kazi iliyotekelezwa miongoni mwa ukoo wa Moabu, Mungu atawashinda binadamu wote katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa kina zaidi wa hatua hii ya kazi Yake, na ndicho kipengele cha thamani ya hatua hii ya kazi Yake. Hata kama sasa unajua kuwa hadhi yako ni ya chini na kuwa una thamani ya chini, bado utahisi kwamba umekutana na jambo linalofurahisha sana: Umerithi baraka kubwa, ukapata ahadi kubwa, na unaweza kamilisha hii kazi kubwa ya Mungu, na unaweza kuuona uso wa kweli wa Mungu, kujua tabia Yake ya asili, na kufanya mapenzi ya Mungu. Hatua mbili za awali za kazi ya Mungu zilifanywa Israeli. Iwapo hatua hii ya kazi Yake katika siku za mwisho bado ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, viumbe wote havingeamini kwamba Waisraeli tu ndio waliokuwa wateule, lakini pia mpango wa usimamizi wa Mungu wote haungefikia athari iliyotaka. Wakati ambapo hatua hizi mbili za kazi Yake zilifanywa Israeli, hakuna kazi yoyote mpya iliyokuwa imefanywa na hakuna kazi yoyote ya Mungu ya kuzindua enzi ilikuwa imewahi kufanywa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hatua hii ya kazi ya kuzindua enzi inafanywa kwanza katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, na zaidi ya hayo, inafanywa kwanza miongoni mwa ukoo wa Moabu; hii imezindua enzi mpya. Mungu amevunja maarifa yoyote yaliyo ndani ya dhana za binadamu na hajaruhusu yoyote yaendelee kuwa hai. Katika kazi Yake ya kushinda Amevunja dhana za binadamu, hiyo njia ya zamani, ya maarifa ya binadamu, Anaruhusu watu waone kuwa kwa Mungu hakuna kanuni, kwamba hakuna kitu kizee kumhusu Mungu, kwamba kazi Anayoifanya ni ya uhuru kabisa, ni huru kabisa, kwamba Yeye yuko sahihi katika chochote Anachofanya. Ni lazima utii kikamilifu kazi yoyote Anayoifanya miongoni mwa viumbe. Kazi yoyote Anayoifanya ni ya maana na inafanywa kulingana na mtazamo Wake na maarifa Yake na sio kulingana na chaguo za watu na dhana za watu. Anafanya yale mambo yaliyo na manufaa kwa kazi Yake; kama kitu hakina manufaa kwa kazi Yake, Hatakifanya, hata kiwe kizuri vipi! Anafanya kazi na kuchagua mpokeaji na eneo la kazi Yake kulingana na maana na madhumuni ya kazi Yake. Hafuati kanuni za zamani, wala Hafuati fomula nzee; badala yake, Anapanga kazi Yake kulingana na umuhimu wa kazi; mwishowe, Anataka kufikia matokeo yake ya kweli na madhumuni yanayotarajiwa. Iwapo huelewi mambo haya sasa, kazi hii haitatimiza matokeo yoyote kwako.

Jumapili, 23 Juni 2019

Neno la Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza

Neno la Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii:
Hakuna Awezaye Kuzuia Kazi Ambayo Mungu Anaamua Kufanya Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Wanadamu Yaanza na Ibrahimu Kumtoa Isaka Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli Binadamu Anapata Baraka za Mungu kwa Sababu ya Uaminifu na Utii Wake Kuwapata Wale Wanaomjua Mungu na Wanaoweza Kumshuhudia Ndilo Tamanio la Mungu Lisilobadilika
Mwenyezi Mungu alisema, Maneno na tabia iliyowasilishwa mbele na kufichuliwa na Mungu inawakilisha mapenzi Yake, na pia inawakilisha kiini Chake halisi. Wakati Mungu anapojihusisha na binadamu, haijalishi ni nini Anachosema au kufanya, au tabia gani Anayofichua, na haijalishi ni nini binadamu anaona kuhusu kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho, vyote vinawasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Licha ya kiwango ambacho binadamu anaweza kutambua, kufahamu, au kuelewa, vyote hivi vinawakilisha mapenzi ya Mungu—mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Hili ni bila shaka! Mapenzi ya Mungu kwa binadamu ni vile Anavyohitaji watu kuwa, kile Anachohitaji wao kufanya, namna Anavyohitaji wao kuishi, na vile Anavyowahitaji kuweza kukamilisha kutimia kwa mapenzi ya Mungu. Je, mambo haya hayawezi kutenganishwa na kiini cha Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu huwasilisha mbele tabia Yake na chote Alicho nacho na alicho wakati huohuo Akimtolea madai binadamu. Hakuna uongo, hakuna kusingizia, hakuna ufichaji, na wala hakuna kupiga chuku. Ilhali kwa nini binadamu hawezi kujua na kwa nini hajawahi kuweza kutambua waziwazi tabia ya Mungu? Na kwa nini hajawahi kutambua mapenzi ya Mungu? Kile ambacho kimefichuliwa na kuwasilishwa mbele na Mungu ndicho kile Mungu anacho Mwenyewe na maana yake, na kinaonyesha kila kipengele cha tabia Yake ya kweli—hivyo kwa nini binadamu hawezi kuona? Kwa nini binadamu hana uwezo wa kuwa na maarifa ya kina? Kunayo sababu muhimu ya haya. Na sababu yenyewe ni ipi? Tangu wakati wa uumbaji, binadamu hajawahi kumchukulia Mungu kama Mungu. Kwenye nyakati zile za mwanzo kabisa, haikujalisha ni nini Mungu alifanya kuhusiana na binadamu, yule binadamu ambaye ndiye tu alikuwa ameumbwa, binadamu alimchukulia yeye kuwa mwandani wake tu na wala si zaidi ya hapo, kama mtu wa kutegemewa, na hakuwa na maarifa yoyote wala uelewa wa Mungu. Hivi ni kusema, hakujua kwamba kile kilichowasilishwa mbele na Kiumbe huyu—Kiumbe huyu ambaye yeye alitegemea na kumwona kuwa mwandani wake—alikuwa kiini cha Mungu, na wala hakujua kwamba Kiumbe huyu ndiye anayetawala viumbe wote. Nikisema kwa urahisi, watu wa wakati huo hawakuwa na maarifa hata kidogo kumhusu Mungu. Hawakujua kwamba mbingu na nchi na mambo yote yalikuwa yameumbwa na Yeye na wala hawakujua ni wapi Alipotokea, na, zaidi hawakujua Yeye Alikuwa nani. Bila shaka, wakati huo Mungu hakumhitaji binadamu kumjua Yeye au kumfahamu Yeye au kuelewa kila kitu Alichofanya, au kufahamishwa kuhusu mapenzi Yake, kwani hizi zilikuwa nyakati za mapema zaidi baada ya uumbwaji wa wanadamu. Wakati Mungu alipoanza matayarisho ya kazi ya Enzi ya Sheria, Mungu alifanya mambo fulani kwa binadamu na pia Akaanza kutolea binadamu madai fulani, Akimwambia namna ya kutolea Mungu sadaka na namna ya kumwabudu. Ni wakati huo ndipo binadamu alipopata mawazo machache mepesi kuhusu Mungu, ni hapo tu ndipo alipojua tofauti kati ya binadamu na Mungu na kwamba Mungu Ndiye aliyewaumba wanadamu. Wakati binadamu alipojua kwamba Mungu alikuwa Mungu na binadamu alikuwa binadamu kukawa umbali fulani kati ya Yeye na Mungu, bado Mungu hakuhitaji kwamba binadamu awe na maarifa makuu au uelewa wa kina kumhusu Yeye. Hivyo basi, Mungu anayatoa mahitaji tofauti kwa binadamu kutokana na awamu na hali za kazi Yake. Mnaona nini katika haya? Ni kipengele kipi cha tabia ya Mungu unayoitambua? Je, Mungu ni wa kweli? Yale mahitaji ambayo Mungu anampa binadamu yanastahili? Kwenye nyakati za mapema kabisa kufuatia uumbaji wa wanadamu na Mungu, wakati ambao Mungu alikuwa bado hajatekeleza kazi ya ushindi na utimilifu wa binadamu, na Alikuwa hata bado hajaongea yale maneno mengi sana kwake, Alihitaji kidogo sana kutoka kwa binadamu. Licha ya kile ambacho binadamu alifanya na namna alivyotenda—hata kama alifanya mambo fulani yaliyomkosea Mungu—Mungu alimsamehe hayo yote, na akayapuuza. Kwa sababu Mungu Alijua kile Alichokuwa Amempa binadamu, na Alijua kile kilichokuwa ndani ya binadamu, basi Alijua kiwango cha mahitaji ambayo anafaa kudai kutoka kwa binadamu. Ingawaje kiwango cha mahitaji Yake kilikuwa cha chini sana wakati huo, hii haimaanishi kwamba tabia Yake haikuwa kuu, au kwamba hekima na uweza Wake yalikuwa si yoyote ila maneno matupu. Kwa binadamu, kunayo njia moja tu ya kujua tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe: kwa kufuata hatua za kazi ya usimamizi ya Mungu na wokovu wa wanadamu, na kuyakubali maneno ambayo Mungu anaongea akiyaelekeza kwa wanadamu. Kujua kile Mungu anacho na alicho, na kujua tabia ya Mungu, bado binadamu angemuuliza Mungu kumwonyesha nafsi Yake halisi? Binadamu hatafanya hivyo, na hathubutu kufanya hivyo, kwa kuweza kuifahamu tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho, tayari binadamu atakuwa amemwona Mungu Mwenyewe wa kweli, na atakuwa tayari ameona nafsi Yake halisi. Haya ndiyo matokeo yasiyoepukika.
Kazi na mpango wa Mungu ulipokuwa ukiendelea mbele bila kusia, na baada ya Mungu kuanzisha agano la upinde wa mvua na binadamu kama ishara kwamba Hangewahi tena kuuangamiza ulimwengu kwa kutumia gharika, Mungu alikuwa na tamanio lililokuwa likiongezeka na kumsukuma kuwapata wale ambao wangeweza kuwa katika akili moja na Yeye. Hivyo, pia, Alikuwa na tamanio la haraka zaidi la kupata wale waliokuwa na uwezo wa kufanya mapenzi Yake duniani, na, isitoshe, kupata kundi la watu ambao wangeweza kuwa huru dhidi ya nguvu za giza, na kutoweza kuwa watumwa wa Shetani, na kuweza kuwa na ushuhuda kwake Yeye duniani. Kupata kundi la watu kama hawa kulikuwa ni tamanio la Mungu kwa muda mrefu, Alichokuwa akisubiria tangu wakati wa uumbaji. Hivyo basi, licha ya matumizi ya gharika na Mungu ili kuuangamiza ulimwengu, au agano Lake na binadamu, mapenzi ya Mungu, hali yake ya akili, mpango, na matumaini yote yalibakia yaleyale. Kile Alichotaka kufanya, ambacho Alikuwa ametamani kwa muda mrefu kabla ya uumbaji, kilikuwa kupata wale walio miongoni mwa wanadamu ambao Alitamani kuwapata—Kupata watu wa kundi hili ambao walioweza kufahamu na kujua tabia Yake, na kuyaelewa mapenzi Yake, kundi ambalo lingeweza kumwabudu Yeye. Watu kwenye kundi kama hili wanaweza kweli kuwa na ushuhuda kwake, na wao ndio, yaweza kusemekana, wasiri Wake.
Leo, hebu tuendelee kuzifuata nyayo za Mungu na kufuata nyayo za kazi Yake, ili tuweze kufichua fikira na mawazo ya Mungu, na kila kitu kinachomhusu Mungu, vyote ambavyo “vimehifadhiwa kwenye ghala” kwa muda mrefu. Kupitia mambo haya tutajua hatimaye tabia ya Mungu, kukielewa kiini cha Mungu, tutamruhusu Mungu kuingia kwenye mioyo yetu, na kila mmoja wetu ataweza kukaribia Mungu kwa utaratibu, na kupunguza umbali wetu na Mungu.
Sehemu ya kile tulichozungumzia wakati wa mwisho ilihusiana na kwa nini Mungu alianzisha agano na binadamu. Wakati huu, tutakuwa na ushirika kuhusu vifungo vya maandiko vilivyo hapa chini. Hebu tuanze kwa kuyasoma maandiko.

Jumatatu, 6 Mei 2019

Unawezaje Kutofautisha Kati ya Viongozi wa Kweli na wa Uongo, na Wachungaji wa Kweli na wa Uongo

6. Unawezaje Kutofautisha Kati ya Viongozi wa Kweli na wa Uongo, na Wachungaji wa Kweli na wa Uongo?

Maneno Husika ya Mungu:
Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno halisi ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno halisi ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi halisi ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana, na huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga. Huduma hiyo huenda kinyume na Mungu, na hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu. "Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu" kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu.
kutoka kwa "Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasioona mbali, wanaojaribu kuonyesha tu jinsi walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha "wasomi" wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Je, watu hawa wana mantiki yoyote ya kuzungumzia? Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki?
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mtu kama huyu daima anakuwa na uadui dhidi ya kazi mpya ya Mungu, haonyeshi nia ya kujisalimisha, na hajawahi kutii ama kujinyenyekea kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe hajisalimishi kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi kwa kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi hazina anazomiliki, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiriwa kwa wengine, na kutumiwa kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni "mashujaa wasioshindwa," kizazi baada ya kizazi kinakaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanafikiria kuhubiri neno (mafundisho ya dini) ni wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wanatekeleza kwa nguvu wajibu wao "mtakatifu na usiokiukwa". Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna anayethubutu kuwapinga kwa uwazi. Walikuwa "mfalme" kwa nyumba ya Mungu, wakitenda kama dikteta kupitia enzi nyingi.
kutoka kwa "Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi , unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi, na kazi yako inaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe. Kwa hakika, utakuwa msumbufu zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hii ni uzoefu na mafunzo ya kibinadamu. Ni filosofia ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa wanapatikana miongoni mwa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini.
kutoka kwa "Sitisha Huduma ya Kidini" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali utu wa watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua mitazamo yao, achilia mbali kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokidhihirisha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambayo ni nje ya mguso wa uhalisia na kuwapatia watu uzima. Kimsingi, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga wa bahari, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Katika hili, je huwadanganyi watu? Je, wewe si mtu wa maneno matupu bila vitendo? Kutenda kwa namna hii ni hatari kwa watu! Kadri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisia, na ndivyo inavyokosa uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisia; kadri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya kumuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisia, maana watu hawa hawajawa na uzoefu binafsi nazo, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kumwongoza mwanadamu katika njia nzuri, na watawapotosha tu watu. Je, hii si hatari kwa watu? Kwa kiwango cha chini kabisa, unapaswa uweze kutatua shida za sasa na kuwaruhusu watu kupata kuingia; hii tu ndiyo inahesabika kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno mazuri, ya kibunifu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo mazuri, na kutaongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuwaongoza watu namna hii kutazalisha taratibu nyingi, ambazo zitafanya watu wakuchukie. Huu ndio udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli hauvumiliki.
kutoka kwa "Sisitiza Zaidi Kwa Uhalisia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Maarifa yenu yanaweza kuwakimu watu kwa muda tu. Wakati unapoendelea, ukiendelea kusema kitu kile kile, watu kadhaa wataweza kutambua; watasema wewe ni mtu wa juu juu sana, aliyekosa kina sana. Hutakuwa na budi ila kujaribu kuwadanganya watu kwa kuongea mafundisho, na kama wewe daima huendelea hivi, wale walio chini yako watafuata namna yako, nyayo, na mfano wa kumwamini Mungu na kupitia, na watatia maneno na mafundisho hayo katika vitendo, na hatimaye, unapoongea katika njia hii, watakutumia kama mfano. Unachukua mwongozo kuongea mafundisho, na wale walio chini yako watajifunza mafundisho kutoka kwako, na vitu vinapoendelea utakuwa umechukua njia ambayo si sawa. Wale walio chini yako wanafuata njia yako … Tazama viongozi wa kila madhehebu na faraka. Wote ni wa kujigamba na kujisifu, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ujuzi fulani, na wanaweza kuongea mafundisho kiasi, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa, ambao kupitia kwake wamewaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu—lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na wale wanaohubiri njia ya kweli, baadhi yao wangesema, "Lazima tutafute ushauri kwake kuhusu imani yetu katika Mungu." Tazama jinsi wanavyohitaji ridhaa ya mtu ili kumwamini Mungu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?
kutoka kwa "Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kutoa kwenu "muhtasari kuhusu ukweli" hakufanywi ili kuwawezesha watu kupata maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunafanywa ili watu waweze kuwa weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka kwa ukweli. Wao huonekana kana kwamba wanaelewa lengo lililokusudiwa katika kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno ya mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli, na si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia. Wewe unakusanya vitabu hivi au vifaa hivyo, na hivyo unapata umiliki wa kipengele hiki cha mafundisho au kipengele kile cha ujuzi. Wewe ni msemaji wa kiwango cha juu wa mafundisho—lakini huwaje unapomaliza kusema? Watu basi hawana uwezo wa kupitia, hawana ufahamu wa kazi ya Mungu na hawana ufahamu wao wenyewe pia. Mwishowe, vitu vyote watakavyokuwa wamepata ni fomyula na sheria … Kwa kuuliza swali baada ya swali kuhusu maneno hayo, kisha kujibu, kufanya muhtasari, unadhani kuwa wale walio chini wanaweza kuelewa kwa urahisi. Mbali na kuwa rahisi kukumbuka, wao wana uhakika juu ya maswali haya kwa tazamo la haraka, na unafikiri ni vizuri kufanya mambo kwa njia hii. Lakini kile wanachokielewa siyo maana iliyokusudiwa ya ukweli; inatofautiana na ukweli na ni maneno ya mafundisho tu. Hivyo ingekuwa bora zaidi kama wewe hungefanya mambo haya hata kidogo. Unafanya mambo haya kuwaongoza watu kuelewa ujuzi na weledi wa elimu. Wewe huwaleta wengine katika mafundisho, katika dini, na kuwafanya wamfuate Mungu na kumwamini Mungu ndani ya mafundisho ya dini. Je, si wewe ni sawa tu na Paulo? … Mwishowe wao wangeletwa mahali ambapo hawawezi kupata ukweli na hawawezi kupitia neno la Mungu, mahali ambapo wanaweza kujiandaa tu na kujadili mafundisho na ni mahali ambapo hawawezi kumwelewa Mungu. Yote ambayo wangeweza kuzungumza yangekuwa mafundisho yenye kupendeza, mafundisho sahihi, lakini hakungekuwa na uhalisi ndani yao na hawangekuwa na njia ya kutembelea. Aina hii ya kuongoza kweli hufanya madhara makubwa!
kutoka kwa "Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine wanajihami tu na ukweli fulani kwa wakati wa dharura ama kujitelekeza wenyewe na kuwasaidia wengine, sio kutatua shida zao wenyewe; tunawaita "watu wasio na ubinafsi." Wanawaona wengine kama vikaragosi wa ukweli na wenyewe kama mabwana wa ukweli, wakiwafunza wengine kuushikilia ukweli na wasiwe wasiojihususha, ilhali wao wenyewe ni watazamaji kando kando mwa uwanja—hao ni watu wa aina gani? Wakiwa wamejihami na baadhi ya maneno ya ukweli ili kuwahubiria wengine tu, wakikosa kufanya chochote kujizuia kutokana na kuangamia kwao wenyewe—inasikitishaje! Kama maneno yao yanaweza kuwasaidia wengine, mbona wasijisaidie wenyewe? Tunafaa kuwaita wanafiki wasio na ukweli. Wanatoa maneno ya ukweli kwa wengine na kuwaambia wengine wayaweke katika matendo, lakini hawafanyi juhudi yoyote kuyatenda wenyewe—je sio wa kudharauliwa? Kwa hakika hawawezi kulifanya wenyewe, ilhali wanawalazimisha wengine kuweka maneno ya ukweli katika matendo—hii ni njia ya ukatili iliyoje! Hawatumii ukweli kuwasaidia wengine; hawawatolei wengine kwa moyo wa upendo wa mama; wanawadanyanya tu watu na kuwapotosha watu. Hili likiendelea—na kila mtu akipitisha maneno ya ukweli kwa anayefuata—je kila mmoja mwishowe hatakuwa na uelewa tu wa maandishi ya ukweli wakikosa uwezo wa kuyatenda?
kutoka kwa "Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Wale wanaosoma Biblia kwa makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu wabovu, kila mmoja akisimama juu kumfundisha Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga makusudi. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, mapepo yanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Ingawa wenye "mwili imara," wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni maadui wa Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?
kutoka kwa "Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mbona Nasema wale walio katika dunia ya kidini hawaamini katika Mungu na ni waovu, walio sawa na ibilisi? Ninaposema ni watenda maovu, ni kwa sababu hawaelewi matakwa ya Mungu, wala kuona hekima Yake. Hakuna wakati ambao Mungu anadhihirisha kazi Yake kwao; ni vipofu, wasioona matendo ya Mungu. Wao ndio walioachwa na Mungu na hawamiliki kabisa utunzaji na ulinzi wa Mungu, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu. Wale walio bila kazi ya Mungu ni watenda maovu na humpinga Mungu.
kutoka kwa "Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Wajibu wa wafanyakazi ni kutenda kazi yao na kuyaongoza makanisa kulingana na mapenzi ya Mungu na kwa mujibu wa mahitaji na mipango ya Mungu. Kazi kama hii hubarikiwa na Mungu. Ikiwa wafanyakazi hawana urazini kama huo, na hukiuka mapenzi ya Mungu kwa kufanya mambo kwa njia yao wenyewe, wakichukua nafasi ya mchungaji na kuwafundisha watu jinsi wanavyopenda, wakitoa dhana zao, mawazo, na mafundisho na kuwafanya wengine kuyakubali, basi wafanyakazi kama hawa wamekuwa wachungaji wa uongo. Kuna mifano mingi ya wafanyakazi kuwa wachungaji wa uongo, na idadi kubwa wameondoshwa na Mungu katika kila hatua ya kazi Yake. Mungu wakati mmoja Alisema kuwa katika kila enzi kuna watu wengi wanaomtumikia Mungu na bado pia humpinga, hata hatimaye huwafanya wengine wawatii na kuwaabudu kama wao ni Mungu. Hili ni dhihirisho la "wachungaji wa uongo." Sote tunapaswa kuchukua hili kama onyo; wafanyakazi wanapaswa kuzingatia mabadiliko katika tabia, na ikiwa watazembea na kutokuwa waangalifu kwa hili, basi ni rahisi mno kwao kuwa wachungaji wa uongo. Kazi ya wachungaji wa uongo ina mkazo maalum juu ya kuwaongoza watu kulingana na maana ya wachungaji wa uongo wenyewe. Yote wanayofanya, kusema, na kutafuta ni ya mpango wao wenyewe, na hulichukulia hili kama ukweli safi mno kuliko ukweli wote, na wao hudhani kuwa wanaweza kuwafundisha watu kuwa wanadamu na kuwaruhusu watu kupata ukweli kulingana na mpango wao wenyewe. Haya ni maonyesho ya kiburi cha juu kabisa na hali ya kujidai ya wachungaji wa uwongo. Kwa wale ambao kweli ni wa busara, wanapoamini kuwa wako sahihi hasa wangetafuta na kuwasiliana ukweli kwa karibu , na kutenga uangalifu wao kwa kusikia maoni na maarifa tofauti ya wengine ili kuthibitisha kama yote waliyoyaelewa ni sahihi. Wale wote ambao wamepitia kupogolewa na kushughulikiwa kwa Mungu wanapaswa kuweza kuweka kando baadhi ya hali zao za kujidai na majisifu. Wanapofanya kazi, wao ni waangalifu katika hatua zao ili kuepuka kukiuka mapenzi ya Mungu na kuchukua njia mbaya. Matokeo yao kuwa wachungaji wa uongo hayawezi kufikiriwa. Kila mfanyakazi ana matendo yake mwenyewe, wote wana nadharia zao wenyewe ambazo wao hutumia kunyunyizia watu; kwa kweli, hakuna yeyote anayeweza kufahamu kabisa ni kiasi gani cha ukweli au thamani njia yao wenyewe inacho. Watu wamekosa hali ya kujitambua, hawana bidii au tafakari ya kina sana katika maarifa yao ya ukweli, na wao huchukua kiholela vitu visivyo na maana na kuvichukulia kama hazina za kutolewa kwa wengine. Si matendo kama hayo yanaashiria mchungaji wa uwongo? Si hili linawadhuru wengine pamoja na wao wenyewe? Bila kujali ni kazi kiasi gani wachungaji wa uwongo hufanya, hawana uwezo kabisa wa kuwaleta watu mbele ya Mungu na kuwaruhusu wamjue na kumtii Mungu. Yote yanayofunguliwa na wachungaji wa uongo ni maneno na mafundisho tu, na mawazo na fikra, na hakuna kitu ambacho huzuia kazi ya Mungu au kumpinga Yeye zaidi.
kutoka kwa "Maana ya 'Wachungaji Kondoo wa Uongo'" katika Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu
Huduma kulingana na mbinu za kidini inamaanisha kufanya kila kitu kulingana na njia za desturi za dini na utaratibu wa huduma, kuzingatia kwa imara sherehe mbalimbali za kidini, na kuwaongoza watu tu kulingana na maarifa ya Biblia. Kwa kuonekana, yaelekea kuwa yenye bidii na nguvu, inaashiria dini, inafaa barabara kwa mawazo ya watu, na hawana vipingamizi. Lakini haina kabisa kazi ya Roho Mtakatifu, kinachohubiriwa si kitu ila mafundisho ya kidini na elimu ya Biblia, imejaa mawazo ya kidini, haina chochote kuhusu upataji wa nuru ya Roho Mtakatifu, na mikutano imetuama na kukosa uhai. Kwa huduma kama hii, miaka inavyoendelea watu waliochaguliwa wa Mungu bado wanabaki bila ukweli, hawana maarifa ya Mungu au utii kwa Mungu, na hawajaingia kwenye njia sahihi ya imani kwa Mungu–kwa kuwa kile watu hufuatilia sio wokovu bali ni neema na baraka, kiasi kwamba hakuna dalili za mabadiliko katika tabia ya maisha yao. Baada ya kuhudumu kwa miaka kadhaa, hawa watu bado wako mikono mitupu, bila ushahidi wa kitu walichopata wenyewe. Haya ndiyo matokeo ya huduma kulingana na mbinu za kidini. Ni dhahiri kuwa, watu kama hawa wanaomtumikia Mungu hawajui kazi ya Mungu, hawaelewi mapenzi ya Mungu, na hawajui maana ya kushirikiana na kazi ya Roho Mtakatifu. Ni jambo dhahiri la vipofu wakiwaongoza vipofu, huwapotosha watu waliochaguliwa wa Mungu , kama Mafarisayo humwamini Mungu na bado humpinga Mungu, hawamjui Mungu, na kimsingi hawawezi kufanikisha wokovu wa Mungu.
kutoka kwa "Wale tu Wanaoingia Kwenye Njia Sahihi ya Imani katika Mungu Ndio Wanaweza Kuchukua njia Sahihi ya Huduma kwa Mungu" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (I)
Wachungaji wa jamii ya kidini hutumia kila fursa ya kutangaza kiwango cha maarifa yao na kutoa sura ya uchaji Mungu. Lengo lao ni kuwafanya watu wawastahi na kuwaabudu, na wao hutumia taswira yao wenyewe kuwavuta watu kwao ili wawatii na kuwafuata, matokeo yakiwa ni wao kuwaongoza watu kuabudu maarifa ya Biblia, kuabudu hadhi na nguvu, na kuabudu ustadi katika kuhubiri. Kwa njia hii, kwa kila hatua huwaongoza watu katika njia ya kumpinga Mungu. Wale wanaoongozwa na wapinga Kristo humwamini Mungu asiye yakini, wao ni wazuri kwa kuzungumzia mafundisho matupu na yasiyo na maana, na wenye ujuzi katika unafiki, na wao wote humwamini Mungu na bado humpinga na kumwasi Mungu. Hakuna shaka kwamba njia ambayo viongozi wa uongo na wapinga Kristo hufanyia kazi–ile ambayo wao hutumia kumtumikia Mungu na bado kumpinga Yeye–ni ya kuwadhuru watu sana.
kutoka kwa "Kulinda Dhidi ya Wapinga Kristo na Njia ya Wapinga Kristo Ni ya Umuhimu Mkuu" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (II)

Jumatano, 24 Aprili 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa. Kwa maneno mengine, usimamizi wa Mungu wa mwanadamu ulianza kutokana na kazi ya kumwokoa mwanadamu, na wala haukutokana na kazi ya kuiumba dunia. Hakungekuwa na kazi ya kumsimamia mwanadamu pasipo kuwepo na tabia potovu ya mwanadamu, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu ina sehemu tatu, badala ya hatua nne, au enzi nne. Hii tu ndio njia sahihi ya kutaja kazi ya Mungu ya usimamizi wa mwanadamu. Enzi ya mwisho itakapofikia kikomo, kazi ya kusimamia mwanadamu itakuwa imekamilika. Hitimisho la kazi ya usimamizi lina maana kuwa kazi ya kuwaokoa wanadamu wote imemalizika kabisa, na kwamba mwanadamu amefika mwisho wa safari yake. Pasipo kazi ya kuwaokoa wanadamu wote, kazi ya usimamizi wa wanadamu haingekuwapo, wala hakungekuwa na hatua tatu za kazi. Ilikuwa ni hasa kwa ajili ya upotovu wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu alihitaji wokovu kwa dharura, ndipo Yehova alikamilisha uumbaji wa dunia na kuanza kazi ya Enzi ya Sheria. Hapo tu ndipo kazi ya kumsimamia mwanadamu ilipoanza, kumaanisha kwamba hapo tu ndipo kazi ya kumwokoa mwanadamu ilipoanza. "Kumsimamia mwanadamu" haimaanishi kuongoza maisha ya mwanadamu aliyeumbwa upya duniani (ambapo ni kusema, mwanadamu ambaye bado hakuwa amepotoshwa). Badala yake, ni wokovu wa ubinadamu ambao umepotoshwa na Shetani, ambapo ni kusema kwamba, ni kubadilishwa kwa mwanadamu aliyepotoshwa. Hii ndiyo maana ya kumsimamia mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu haihusishi kazi ya kuiumba dunia, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu haijumuishi kazi ya kuumba ulimwengu, na inahusisha tu hatua tatu za kazi zilizo tofauti na uumbaji wa ulimwengu. Ili kuelewa kazi ya kumsimamia mwanadamu, ni muhimu kuwa na ufahamu wa historia ya hatua tatu za kazi—hili ndilo kila mtu anapaswa kulifahamu ili kuokolewa. Kama viumbe wa Mungu, mnapaswa kutambua kuwa mwanadamu aliumbwa na Mungu, na kufahamu chanzo cha upotovu wa mwanadamu, na, vilevile, kufahamu mchakato wa wokovu wa mwanadamu. Iwapo mnafahamu tu jinsi ya kutenda kulingana na mafundisho ili kupata neema ya Mungu, lakini hamna fununu jinsi Mungu anavyomwokoa mwanadamu, au ya chanzo cha upotovu wa mwanadamu, basi hili ndilo mnalokosa kama viumbe wa Mungu. Hupaswi kutoshelezwa tu na kuelewa kwa ukweli unaoweza kuwekwa katika vitendo, huku ukibakia kutojua upeo mpana wa kazi ya usimamizi ya Mungu—kama hivi ndivyo ilivyo, basi wewe ni mwenye kulazimisha kauli sana. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo hadithi ya ndani ya usimamizi wa Mungu wa mwanadamu, ujio wa injili ya dunia nzima, fumbo kubwa zaidi kati ya wanadamu, na pia ni msingi wa kueneza injili. Ukizingatia tu kuelewa ukweli sahili unaohusiana na maisha yako, na usijue lolote kuhusu hili, maajabu makuu zaidi na maono, basi maisha yako si ni sawa na bidhaa yenye kasoro, yasio na maana isipokuwa kuangaliwa?
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya usimamizi ilikuja tu kwa ajili ya wanadamu, yaani ilitolewa kwa ajili ya uwepo wa wanadamu. Usimamizi haukuwepo kabla ya uwepo wa wanadamu au mwanzo wakati mbingu na nchi na vilivyomo vilipoumbwa. Iwapo, katika kazi nzima ya Mungu, hakungekuwa na vitendo vinavyomfaidi mwanadamu, yaani kama Mungu asingeweka matakwa maalum kwa mwanadamu aliyepotoka (ikiwa kazi ifanywayo na Mungu haikuwa na njia nzuri ya vitendo vya mwanaadamu), basi kazi hii isingeitwa usimamizi wa Mungu. Iwapo kazi nzima ya Mungu ingehusisha tu kuwaambia wanadamu waliopotoka jinsi ya kuendeleza vitendo vyao, na Mungu hakuendeleza kazi yoyote ya mipango Yake, na Hakuonyesha uwepo wake wa daima au busara, basi bila kujali ni jinsi gani matakwa ya Mungu kwa mwanadamu yangewekwa juu, bila kujali Mungu aliishi muda mrefu kiasi gani miongoni mwa wanadamu, mwanadamu asingejua chochote juu ya tabia ya Mungu; kama ingekuwa hivyo, basi kazi hii isingeweza kukaribia kuitwa usimamizi wa Mungu. Kwa ufupi, kazi ya usimamizi wa Mungu ni kazi iliyofanywa na Mungu na kazi zote zilizofanywa chini ya uongozi wa Mungu na wale ambao wamepatikana na Mungu. Kazi kama hiyo inaweza kuchukuliwa kwa ufupisho kama usimamizi, na inaelezea kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu na vilevile ni ushirikiano Wake na wale wanaomfuata; kwa ujumla, hayo yote yanaweza kuitwa usimamizi. Hapa kazi ya Mungu inaitwa maono na ushirikianao wa mwanadamu unaitwa vitendo. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo juu (yaani kadiri maono yalivyo juu), ndivyo tabia za Mungu zinakuwa wazi kwa mwanadamu, na kutoafikiana na mawazo ya mwanadamu, na ndivyo vitendo na ushirikiano wa mwanadamu huwa vya juu. Kadiri matakwa kwa mwanadamu yanavyokuwa ya juu, ndivyo kazi ya Mungu inavyotofautiana mawazo ya mwanadamu, matokeo yake yakiwa majaribu ya mwanadamu, na viwango anavyotarajiwa kuwa navyo, vilevile vinakuwa vya juu. Katika hatima ya kazi hii, maono yote yatakuwa yametimizwa, na yale yote mwanadamu anapaswa kuweka katika vitendo yatakuwa yamefikia kilele cha ukamilifu. Huu ndio wakati pia ambapo kila kitu kitawekwa katika kundi lake kwani kile kinachopaswa kufahamika na mwanadamu kitakuwa kimebainishwa kwake. Kwa hivyo maono yatakapofikia upeo wa juu, vivyo hivyo kazi nayo itakaribia hatima yake na vitendo vya mwanadamu vitakuwa vimefikia ufanisi wake. Vitendo vya mwanadamu vimekitwa katika kazi ya Mungu, na usimamizi wa Mungu unadhihirika tu kupitia vitendo na ushirikiano wa mwanadamu. Mwanadamu ni mfano wa kazi ya Mungu, na mlengwa wa kazi ya usimamizi mzima wa Mungu, na pia mazao ya kazi ya usimamizi wote wa Mungu. Iwapo Mungu angefanya kazi peke yake bila ushirika wa mwanadamu, basi pasingekuwepo na kitu cha kudhihirisha kazi Yake nzima na kwa hali hiyo kusingekuwa na umuhimu hata kidogo wa usimamizi wa Mungu. Ni kwa kuchagua tu chombo kifaacho kilicho nje ya kazi ya Mungu, na kinachoweza kudhihirisha kazi hii, na kuthibitisha kudura na busara zake, je, inawezekana kufikia dhumuni la usimamizi wa Mungu na kufikia dhumuni la kutumia kazi hii yote ili kumshinda kabisa Shetani. Na kwa hivyo mwanadamu ni sehemu muhimu katika kazi ya usimamizi ya Mungu, na mwanadamu ndiye pekee anayeweza kuifanya kazi ya usimamizi ya Mungu izae matunda na kufikia lengo Lake kuu; mbali na mwanadamu, hakuna kiumbe kingine chenye uhai kinachoweza kuchukua nafasi hiyo. Ikiwa mwanadamu atakuwa dhihirisho kamili la kazi ya usimamizi, basi uasi wa wanadamu wenye maovu lazima utokomezwe. Hii inahitaji kuwa mwanadamu apewe utendaji ufaao kwa kila muktadha, na kwamba Mungu afanye kazi inayotangamana miongoni mwa wanadamu. Ni kwa njia hii tu ndipo kutakuwa na kundi la watu waliokubaliwa ambao ni dhihirisho la kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu haiwezi kuwa ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe kupitia kazi ya Mungu peke yake; ushuhuda huo vilevile unahitaji wanadamu ambao wanafaa ili kazi yake iafikiwe. Mwanzo Mungu atawatayarisha watu hawa ambao kupitia kwao kazi Yake itadhihirika na ushuhuda Wake utachukuliwa miongoni mwa viumbe. Kwa hili, Mungu atakuwa ameafiki lengo la kazi Yake. Mungu hafanyi kazi peke Yake kumshinda Shetani kwa sababu Mungu hawezi kujishuhudia Mwenyewe moja kwa moja miongoni mwa viumbe wote. Angefanya hivyo, ingekuwa vigumu kumshawishi mwanadamu, kwa hivyo Mungu lazima Afanye kazi kwa mwanadamu ili kumshinda na ndipo Atakapoweza kupata ushuhuda miongoni mwa viumbe vyote. Mungu angefanya kazi peke Yake bila kushirikiana na mwanadamu, au kama mwanadamu asingetakiwa kushirikiana, basi mwanadamu asingeitambua tabia ya Mungu na daima asingefahamu nia ya Mungu; na kwa hali hii haiwezi kuitwa usimamizi wa Mungu. Mwanadamu mwenyewe angejizatiti, na kutafuta, na kufanya bidii, bila kuifahamu kazi ya Mungu, basi mwanadamu angekuwa anafanya mizaha. Bila kazi ya Roho Mtakatifu, akifanyacho mwanadamu ni cha Shetani, ni muasi na mtenda maovu; Shetani anadhihirika katika yote yafanywayo na mwanadamu mwenye maovu na hamna kinachoafikiana na Mungu, na yote ni dalili ya Shetani. Hakuna kati ya vilivyozungumziwa kisichokuwa na maono na vitendo. Katika msingi wa maono, mwanadamu hupata vitendo, anapata njia ya utiifu, ili kwamba aweze kuweka kando mawazo yake ili apate vile ambavyo hajawahi kuwa navyo hapo awali. Mungu huhitaji mwanadamu ashirikiane naye, kwamba mwanadamu asikilize matakwa Yake, na mwanadamu ashikilie kazi ifanywayo na Mungu Mwenyewe na kuupitia uwezo mkubwa wa Mungu na kuifahamu tabia ya Mungu. Kwa kifupi, haya ndiyo usimamizi wa Mungu. Ushirika wa Mungu na mwanadamu ndio usimamizi, na ni usimamizi mkuu zaidi.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 22 Aprili 2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini? Baada ya Mungu kuumba vitu vyote na baada ya kuwepo wanadamu, Mungu alichagua kundi la watu ambao walimfuata, na wanaitwa tu “wateule wa Mungu.” Kuna mipaka maalum na umuhimu katika uchaguzi wa Mungu wa watu hawa. Mipaka ni kwamba kila wakati Mungu anafanya kazi muhimu ni lazima waje—ambacho ni kitu cha kwanza kati ya vinavyowafanya maalum. Na umuhimu wao ni gani? Kuchaguliwa kwao na Mungu kunamaanisha kuwa wana umuhimu mkubwa. Yaani, Mungu angelipenda kuwafanya hawa watu timilifu, na kuwafanya wakamilifu, na baada ya kazi Yake ya usimamizi kuisha, Atawachukua watu hawa. Je, umuhimu huu si mkubwa? Kwa hiyo, hawa wateule ni wa umuhimu mkubwa kwa Mungu, kwa kuwa ni wale ambao Mungu anakusudia kuwapata. Lakini watendaji huduma—vyema, hebu tuachane na uamuzi uliokwisha kufanywa na Mungu, na kwanza tuzungumzie asili yao. Maana ya kawaida ya “mtendaji huduma” ni mtu anayehudumu. Wanaohudumu ni wa kupita; hawahudumu kwa muda mrefu, au milele, ila wanaajiriwa au kuandikwa kwa muda mfupi. Wengi wao wanachaguliwa kutoka miongoni mwa wasioamini. Wajapo duniani ndipo inapoamriwa kwamba watachukua nafasi ya watendaji huduma katika kazi ya Mungu. Wanaweza kuwa walikuwa mnyama katika maisha yao yaliyopita, lakini pia wanaweza kuwa walikuwa mmoja wa wasioamini. Hiyo ndiyo asili ya watendaji huduma.
Hebu turejee kwa wateule wa Mungu. Wanapokufa, wateule wa Mungu huenda sehemu fulani tofauti kabisa na wasioamini na watu mbalimbali wenye imani. Ni sehemu ambayo wanaambatana na malaika na wajumbe wa Mungu, na ambayo inaendeshwa na Mungu binafsi. Japo katika sehemu hii, wateule wa Mungu hawawezi kumwona Mungu kwa macho yao wenyewe, si kama sehemu nyingine yoyote katika milki ya kiroho; ni sehemu ambayo hili kundi la watu huenda baada ya kufa. Wakifa, wao pia hupitia uchunguzi mkali kutoka kwa wajumbe wa Mungu. Na ni nini kinachochunguzwa? Wajumbe wa Mungu huchunguza njia zilizopitiwa na hawa watu katika maisha yao yote katika imani yao kwa Mungu, ikiwa waliwahi au hawakuwahi kumpinga Mungu wakati huo, au kumlaani, na ikiwa walitenda au hawakutenda dhambi mbaya au maovu. Uchunguzi huu unajibu swali la ikiwa mtu fulani ataondoka au atabaki. “Kuondoka” kunarejelea nini? Na “kubaki” kunarejelea nini? “Kuondoka” kunarejelea ikiwa, kulingana na mienendo yao, watabaki miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu. “Kubaki” kunarejelea kuwa wanaweza kubaki miongoni mwa watu ambao wanafanywa na Mungu kuwa kamili katika siku za mwisho. Mungu ana mipango maalum kwa wale wanaobaki. Katika kila kipindi cha kazi Yake, Mungu atatuma watu kufanya kazi kama mitume au kufanya kazi ya kuyaamsha makanisa, au kuyahudumia. Lakini watu ambao wana uwezo wa kazi kama hizo hawapati miili mara kwa mara kama wasioamini, ambao wanazaliwa upya tena na tena; badala yake, wanarudishwa duniani kulingana na mahitaji na hatua ya kazi ya Mungu, na si wale wapatao mwili mara kwa mara. Je, kuna amri kuhusu ni lini wapate mwili? Je, wanakuja mara moja baada ya kila miaka michache? Je, wanakuja na hiyo haraka? Hawafanyi hivyo. Hii inategemea nini? Inategemea kazi ya Mungu, hatua ya kazi ya Mungu, na mahitaji Yake, na hakuna amri. Amri moja tu ni kwamba Mungu akifanya hatua ya mwisho ya kazi Yake katika siku za mwisho, wateule hawa wote watakuja. Wakija wote, hii itakuwa mara ya mwisho ambapo wanapata mwili. Na kwa nini hivyo? Hii inategemea matokeo yatakayopatikana katika hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu—kwani katika hatua hii ya mwisho ya kazi, Mungu atawafanya wateule hawa kuwa kamili kabisa. Hili linamaanisha nini? Ikiwa, katika hii awamu ya mwisho, watu hawa watafanywa kuwa kamili, na kufanywa wakamilifu, basi hawatapata mwili kama awali; mchakato wa kuwa wanadamu utakamilika kabisa, sawa na mchakato wa kupata mwili. Hili linawahusu wale watakaobaki. Je, wale ambao hawawezi kubaki huenda wapi? Wasioweza kubaki wanakuwa na sehemu mwafaka ya kwenda. Kwanza kabisa kwa sababu ya maovu yao, makosa waliyofanya, na dhambi walizofanya, wao pia wanaadhibiwa. Baada ya kuadhibiwa, Mungu anawatuma miongoni mwa wasioamini; kulingana na hali ilivyo, Atafanya mpango wawe miongoni mwa wasioamini, vinginevyo miongoni mwa watu mbalimbali wenye imani. Yaani, wana chaguzi mbili: Moja ni labda waishi miongoni mwa watu wa dini fulani baada ya adhabu, na nyingine ni wawe wasioamini. Kama watakuwa wasioamini, basi watapoteza kila fursa. Lakini wakiwa watu wa imani—kwa mfano, wakiwa Wakristo—bado wangali na nafasi ya kurudi miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu; kwa hili kuna uhusiano changamano sana. Kwa ufupi, ikiwa mmoja wa wateule wa Mungu atafanya kitu kitakachomkosea Mungu, wataadhibiwa sawa tu na watu wengine. Chukulia Paulo, kwa mfano, ambaye tulizungumzia awali. Paulo ni mfano wa wale wanaoadhibiwa. Je, mnapata picha ya yale ninayozungumzia? Je, mipaka ya wateule wa Mungu ni ya kudumu? (Kwa kiasi kikubwa ni ya kudumu.) Kiasi kikubwa chake ni cha kudumu, lakini sehemu ndogo si ya kudumu. Kwa nini hivyo? (Kwa sababu wametenda maovu.) Nimerejelea hapa mfano mmoja dhahiri: kutenda maovu. Wanapotenda maovu, Mungu hawataki, na wakati Mungu hawataki, anawatupa miongoni mwa makabila na aina mbalimbali za watu, kitu ambacho kinawaacha bila tegemeo na kufanya kurudi kwao kuwe kugumu. Haya yote yanahusu mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wa Mungu.
Kinachofuata ni mzunguko wa uhai na mauti wa watendaji huduma. Tulisema asili za watendaji huduma ni gani? (Wengine walikuwa wasioamini, wengine walikuwa wanyama.) Hawa watendaji huduma walipata mwili baada ya kuwa wasioamini au wanyama. Na ujio wa hatua ya mwisho ya kazi, Mungu amechagua kundi la watu hawa kutoka kwa wasioamini, na ni kundi ambalo ni maalum. Nia ya Mungu ya kuchagua watu hawa ni kuhudumia kazi Yake. “Huduma” si neno la jamala kutamka, wala si kitu ambacho mtu yeyote angependa, lakini tunapaswa kuona ambao linawalenga. Kuna umuhimu maalum katika uwepo wa watendaji huduma wa Mungu. Hamna mwingine awezaye kuchukua nafasi yao, kwa kuwa walichaguliwa na Mungu. Na ni ipi nafasi ya watendaji huduma? Kuwahudumia wateule wa Mungu. Kwa ujumla, kazi yao ni kuihudumia kazi ya Mungu, kushirikiana na kazi ya Mungu, na kushirikiana na ukamilisho wa Mungu wa wateule Wake. Haijalishi kama wanafanya kazi ngumu, wanafanya kazi fulani, au wanajiandaa kufanya kazi fulani, ni yapi mahitaji ya Mungu kwa hawa watu? Je, anawadai sana kwa masharti Yake kwao? (La, Mungu anawataka wawe waaminifu.) Watendaji huduma pia wanapaswa kuwa waaminifu. Haijalishi asili zako, au kwa nini Mungu alikuchagua, ni lazima uwe mwaminifu: Ni lazima uwe mwaminifu kwa Mungu, kwa kile anachokuagiza, na vilevile kazi unayoiwajibikia na jukumu unalolifanya. Ikiwa watendaji huduma wanaweza kuwa waaminifu, na kumridhisha Mungu, basi hatima yao itakuwaje? Wataweza kubaki. Je, ni baraka kuwa mtendaji huduma anayebaki? Kubaki kunamaanisha nini? Hii baraka inamaanisha nini? Kihadhi, hawafanani na wateule wa Mungu, wanaonekana tofauti. Kwa hakika, hata hivyo, wakipatacho katika maisha haya siyo sawa na wakipatacho wateule wa Mungu? Angalau, katika haya maisha ni sawa. Hamlipingi hili, naam? Matamko ya Mungu, neema ya Mungu, riziki ya Mungu, baraka za Mungu—ni nani hafurahii vitu hivi? Kila mtu anafurahia wingi wa haya. Kitambulisho cha mtendaji huduma ni mtendaji huduma, lakini kwa Mungu, ni miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba—tofauti ni kwamba tu nafasi yao ni ile ya watendaji huduma. Kama mmoja wa viumbe wa Mungu, kuna tofauti kati ya watendaji huduma na wateule wa Mungu? Kwa hakika, hakuna. Kwa mazungumzo ya kawaida, kuna tofauti, katika kiini kuna tofauti, kwa kurejelea nafasi wanazoshika kuna tofauti, ila Mungu hawabagui hawa watu. Hivyo ni kwa nini hawa watu wanatambuliwa kama watendaji huduma? Unapaswa kuelewa hili. Watendaji huduma wanatokana na wasioamini. Kutaja wasioamini kunatuambia kuwa maisha yao ya awali ni mabaya: Wote ni wakana Mungu, katika maisha yao ya nyuma walikuwa wakana Mungu, hawakumwamini Mungu, na walikuwa mahasimu wa Mungu, wa ukweli, na vitu vizuri. Hawakumwamini Mungu, hawakuamini kuwa kuna Mungu, hivi wana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu? Ni haki kusema kwamba, kwa kiwango kikubwa, hawana. Sawa tu na wanyama wasivyo na uwezo wa kuelewa maneno ya mwanadamu, watendaji huduma hawaelewi Mungu anasema nini, Anahitaji nini, kwa nini Ana mahitaji kama hayo—hawaelewi, hivi vitu havieleweki kwao, wanabaki bila nuru. Na kwa sababu hii, watu hawa hawana uhai tuliouzungumzia. Je, bila uhai, watu wanaweza kuelewa ukweli? Je, wana ukweli? Je, wana uzoefu na ufahamu wa maneno ya Mungu? (La.) Hizo ndizo asili za watendaji huduma. Lakini kwa kuwa Mungu anawafanya hawa watu watendaji huduma, bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo; Hawadharau, na Hawachukulii kwa uzembe. Japo hawaelewi maneno yake, na hawana uhai, bado Mungu ni mwema kwao, na bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo. Mmevizungumzia hivi viwango hivi karibuni: Kuwa mwaminifu kwa Mungu, na kufanya Asemacho. Katika huduma yako ni lazima uhudumu unapohitajika, na ni lazima uhudumu hadi mwisho. Kama unaweza kuhudumu hadi mwisho, ikiwa unaweza kuwa mtendaji huduma mwaminifu, unaweza kuhudumu hadi mwisho, na unaweza kukamilisha kazi upewayo na Mungu kikamilifu, basi utaishi maisha ya thamani, na utaweza kubaki. Ukitia bidii kidogo, ukijaribu kwa nguvu, ukiongeza maradufu jitihada zako za kumjua Mungu, ukiweza kuongea kidogo kuhusu ufahamu wa Mungu, ukiweza kumshuhudia Mungu, na zaidi, ukielewa kitu kuhusu mapenzi ya Mungu, ukiweza kushirikiana katika kazi ya Mungu, na ukiyazingatia kidogo mapenzi ya Mungu, basi wewe, mtendaji huduma, utapata bahati. Na hili litakuwa badiliko gani katika bahati? Hutaweza kubaki tu. Kutegemea tabia yako na malengo na juhudi zako binafsi, Mungu atakufanya mmoja wa wateule. Hii itakuwa bahati yako. Kwa watendaji huduma, ni nini kizuri kuhusu hili? Ni kwamba unaweza kuwa mmoja wa wateule wa Mungu. Inamaanisha nini ukiwa mmoja wa wateule wa Mungu? Inamaanisha kuwa hawatapata tena mwili kama wanyama au wasioamini. Je, hiyo ni habari njema? Ndiyo, na ni habari njema. Inamaanisha, watendaji huduma wanaweza kufinyangwa. Si kwamba kwa mtendaji huduma, Mungu akimpangia awali kuhudumu, daima atahudumu; si lazima iwe hivyo. Kutegemea tabia yake binafsi, Mungu atamtendea tofauti, na kumjibu tofauti.
Lakini kuna watendaji huduma ambao hawana uwezo wa kumtumikia Mungu hadi mwisho; wakati wa huduma yao, kuna wale ambao wanajitoa nusu na kutelekeza Mungu, kuna wale ambao hufanya mambo mengi mabaya, na hata wale ambao wanasababisha madhara makubwa na kufanya uharibifu mkubwa kwa Kazi ya Mungu, kuna hata watendaji huduma ambao humlaani Mungu, na kadhalika—na ni nini maana ya matokeo haya yasiyorekebishika? Matendo maovu yoyote kama hayo humaanisha kufikia mwisho kwa huduma yao. Kwa sababu matendo yako wakati wa huduma yamekuwa maovu sana, kwa sababu umevuka mipaka yako, wakati Mungu anaona huduma yako haijafikia kiwango Atakutoa ustahiki wa kutoa huduma, Hatakubali ufanye huduma, Atakutoa mbele ya macho Yake, na kutoka katika nyumba ya Mungu. Au ni kwamba hutaki kufanya huduma? Je, siku zote hutamani kufanya maovu? Je, siku zote wewe si mwaminifu? Sawa basi, kuna suluhisho rahisi: Utanyang'anywa ustahiki wako wa kuhudumu. Kwa Mungu, kunyang'anya mtendaji huduma ustahiki wa kufanya huduma kuna maana kuwa mwisho wa mtendaji huduma huyu umetangazwa, na hatakuwa anastahili kufanya huduma kwa Mungu tena, Mungu hahitaji huduma zake tena, na haijalishi ni vitu vipi vizuri atasema, maneno haya yatabaki ya bure. Mambo yanapofikia kiwango hiki, hii hali itakuwa isiyorekebishika; watendaji huduma kama hawa hawana njia ya kurudi nyuma. Na Mungu huwafanyia nini watendaji huduma kama hawa? Anawaachisha tu kutoa huduma? La! Je, Anawazuia tu wasibaki? Au anawaweka katika upande mmoja. Na kuwangoja wabadilike? Hafanyi hivyo. Kwa kweli Mungu hana upendo sana kwa watendaji huduma. Iwapo mtu ana aina hii ya mwelekeo katika huduma yake kwa Mungu, Mungu, kutokana na matokeo ya mwelekeo huu, Atawanyang’anya ustahiki wao wa kutoa huduma, na kwa mara nyingine kuwatupa tena miongoni mwa wasioamini. Na ni ipi hatima ya watendaji huduma waliorudishwa tena kati ya wasioamini? Ni sawa na ile ya wasioamini; kupata mwili kama wanyama na kupokea adhabu ya wasioamini katika ulimwengu wa kiroho. Na Mungu hatakuwa na maslahi ya kibinafsi katika adhabu yao, kwa kuwa hawana umuhimu wowote tena katika kazi ya Mungu. Huu si mwisho tu wa maisha yao ya imani kwa Mungu, ila mwisho wa hatima yao pia, kutangazwa kwa hatima yao. Kwa hiyo watendaji huduma wakihudumu vibaya, watapata matokeo wao wenyewe. Kama mtendaji huduma hana uwezo wa kufanya huduma hadi mwisho kabisa, au amenyang’anywa ustahiki wake wa kutoa huduma katikati ya njia, basi watatupwa miongoni mwa wasioamini—na kama watatupwa miongoni mwa wasioamini watashughulikiwa sawa na jinsi mifugo wanavyoshughulikiwa, sawa na watu wasio na akili au urazini. Ninapoielezea namna hiyo, unaelewa, naam?
Hivyo ndivyo Mungu anavyoushughulikia mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wake na watendaji huduma. Mnajihisi vipi baada ya kusikia haya? Nimewahi kuzungumza kuhusu mada ambayo Nimeitaja sasa hivi, mada ya wateule wa Mungu na watendaji huduma? Kwa kweli Nimewahi, lakini hamkumbuki. Mungu ni mwenye haki kwa wateule wake na watendaji huduma. Kwa vyovyote vile Yeye ni mwenye haki, siyo? Kuna mahali popote unaweza kupata makosa? Wapo watu ambao watasema: “Kwa nini Mungu ni mvumilivu sana kwa wateule? Na kwa nini anawavumilia kidogo sana watendaji huduma?” Kuna yeyote angependa kuwatetea watendaji huduma? “Je, Mungu anaweza kuwapa watendaji huduma muda zaidi, na kuwa mstahimilivu na mvumilivu zaidi kwao?” Haya maneno yako sahihi? (Hapana, hayapo sahihi.) Na ni kwa nini hayapo sahihi? (Kwa kuwa tumeonyeshwa neema kweli kwa kufanywa kuwa watendaji huduma.) Watendaji huduma wameonyeshwa neema kwa kuruhusiwa kufanya huduma! Bila ya dhana “watendaji huduma,” na bila Kazi ya watendaji huduma, hawa watendaji huduma wangekuwa wapi? Miongoni mwa wasioamini, wakiishi na kufa pamoja na mifugo. Ni neema iliyoje wanayoifurahia leo, kuruhusiwa kuja mbele za Mungu, na kuja katika nyumba ya Mungu! Hii ni neema kubwa! Kama Mungu hakukupa nafasi ya kutoa huduma, usingekuwa na nafasi ya kuja mbele za Mungu. Kwa kusema machache, hata kama wewe ni Mbudha na umepata maisha ya milele, sanasana wewe ni mtumwa katika ulimwengu wa kiroho; hutaweza kamwe kumwona Mungu, au kusikia sauti Yake, au kusikia maneno Yake, au kuhisi upendo Wake na baraka Zake kwako, na hata isingewezekana kamwe kuonana na Yeye uso kwa uso. Kilicho tu mbele ya wafuasi wa Budha ni kazi rahisi. Hawawezi kamwe kumjua Mungu, na wanaitikia na kutii kiupofu tu, wakati ambapo watendaji huduma wanafaidi mengi sana katika hatua hii ya kazi. Kwanza, wanaweza kuonana na Mungu uso kwa uso, kusikia sauti Yake, kuyasikia maneno Yake, na kupitia neema na baraka Anazowapa watu. Zaidi ya hayo, wanaweza kufurahia maneno na ukweli unaotolewa na Mungu. Wanapata mengi zaidi! Mengi zaidi! Hivyo, kama mtendaji huduma, huwezi hata kufanya juhudi zilizo za kweli, je, Mungu bado atakuweka? Hawezi kukuweka. Hataki mengi kutoka kwako lakini hufanyi chochote Anachotaka vizuri, hujawajibika ipasavyo—na kwa hivyo, bila shaka, Mungu hawezi kukuweka. Hiyo ndiyo tabia ya haki ya Mungu. Mungu hakudekezi, lakini wala Hakubagui. Mungu anafanya kazi na kanuni hizo. Mungu hutekeleza mambo jinsi hii kwa watu na viumbe wote.
Inapokuja katika ulimwengu wa kiroho, kama viumbe mbalimbali waliomo watafanya kitu kibaya, kama hawafanyi kazi yao inavyostahili, Mungu pia ana sheria za peponi na amri zifaazo kuwashughulikia—hili halipingwi. Basi, katika maelfu kadhaa ya miaka ya kazi ya usimamizi ya Mungu, wasimamizi wengine ambao walifanya maovu wameangamizwa, wengine, leo, wangali wanazuiliwa na kuadhibiwa. Hili ndilo linafaa kukabiliwa na kila kiumbe aliye katika ulimwengu wa kiroho. Kama watafanya kitu kibaya au kutenda maovu, wanaadhibiwa—ambayo ni sawa na jinsi Mungu anatenda kwa wateule Wake na watendaji huduma. Na kwa hivyo, iwe ni katika ulimwengu wa kiroho au ulimwengu yakinifu, kanuni ambazo Mungu hutekeleza matendo hazibadiliki. Bila kujali kama unaweza kuona matendo ya Mungu au la, kanuni zao hazibadiliki. Daima, Mungu amekuwa na kanuni sawa kwa jinsi Anavyotekeleza matendo kwa vitu vyote na kuvishughulikia vitu vyote. Hili halibadiliki. Mungu atakuwa mkarimu kwa wale walio miongoni mwa wasioamini ambao angalau wanaishi ipasavyo, na kuwapa nafasi wale walio katika kila dini ambao wana tabia nzuri na hawatendi maovu, kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao katika vitu vyote vinavyosimamiwa na Mungu, na kufanya kile ambacho wanafaa kufanya. Vivyo hivyo, kati ya wale wanaomfuata Mungu, kati ya wateule Wake, Mungu habagui mtu yeyote kulingana na kanuni Zake hizi. Ni mwema kwa kila mtu anayeweza kumfuata kwa dhati, na kupenda kila mtu anayemfuata kwa dhati. Ni kwamba tu kwa aina hizi mbalimbali za watu—wasioamini, aina tofauti za watu wenye imani, na wateule wa Mungu—anachowazawadia wao ni tofauti. Chukulia wasioamini: hata kama hawamwamini Mungu, na Mungu huwaona kama mifugo, miongoni mwa kila kitu kila mmoja wao ana chakula, mahali pao wenyewe, na mzunguko wa kawaida wa uhai na mauti. Wanaotenda maovu wanaadhibiwa, na wanaofanya mazuri wanabarikiwa na hupokea wema wa Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo? Kwa watu wenye imani, kama wanaweza kutii hasa maadili ya kidini, kizazi baada ya kizazi, basi baada ya hivi vizazi vyote Mungu hatimaye atatoa uamuzi Wake kwao. Vivyohivyo, kwa wewe leo, awe mmoja wa wateule wa Mungu au mtendaji huduma, Mungu vilevile atakuwazisha na kuamua mwisho wako kulingana na kanuni na amri za utawala ambazo Ameziweka. Miongoni mwa aina hizi kadhaa za watu—aina tofauti za watu wa imani, walio katika dini tofauti—je, Mungu amewapa nafasi ya kuishi? Uko wapi Uyahudi? Mungu ameingilia katika imani yao? Hajaingilia, siyo? Na vipi kuhusu Ukristo? Hajaingilia pia? Anawaruhusu kufuata mipangilio yao wenyewe, na Hasemi nao, au kuwapa nuru yoyote, na, zaidi ya hayo, Hawafichulii kitu chochote: “Kama unafikiria ni sahihi, basi amini hivyo!” Wakatoliki wanamwamini Maria, na kwamba ni kupitia kwa Maria ambapo habari zilimfikia Bwana Yesu; hiyo ndiyo aina yao ya imani. Na Mungu amewahi kurekebisha imani yao? Mungu huwapa uhuru, Mungu hawasikizi, na huwapa sehemu fulani ambapo wataishi. Na kwa Waisilamu na wafuasi wa Budha, je, Yuko hivyo pia? Ameweka mipaka kwa ajili yao, pia, na kuwaruhusu kuwa na mahali pao wenyewe pa kuishi, bila ya kuingilia imani zao. Yote yamepangwa vizuri. Na unaona nini katika haya yote? Kwamba Mungu ana mamlaka, lakini hatumii vibaya mamlaka Yake. Mungu hupanga vitu vyote katika mpangilio taratibu, na ni mwenye utaratibu, na katika hili busara na kudura Zake vinadhihirika.
Leo tumezungumzia mada mpya na maalum, ambayo inahusu masuala ya ulimwengu wa kiroho, ambayo ni sehemu mojawapo ya uendeshaji na utawala wa Mungu juu ya ulimwengu wa kiroho. Mlipokuwa hamyaelewi mambo haya, huenda mlisema; “Chochote kinachohusiana na haya ni mafumbo, na hayahusiani na kuingia kwetu katika uhai; mambo haya yametenganishwa na jinsi watu wanaishi hasa, na hatutaki kuyaelewa, wala hatutamani kuyasikia. Hayana uhusiano wowote na kumfahamu Mungu.” Sasa, mnafikiria kuna shida na aina hiyo ya mawazo? Ni sahihi? (La.) Mawazo kama hayo sio sahihi, na yana matatizo makubwa. Hii ni kwa sababu, kama unatamani kujua jinsi Mungu anatawala juu ya vitu vyote, huwezi tu kuelewa kile ambacho unaweza kuona na kile unachokipata kutoka kwa mawazo yako. Ni lazima pia ufahamu ya ulimwengu ule mwingine ambao hauonekani kwako, ambao umeunganishwa kwa njia isiyochanganulika na huu ulimwengu ambao unaweza kuuona. Haya yanahusu ukuu wa Mungu, yanahusu mada ya “Mungu ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote”; ni taarifa kuhusu hayo. Bila ya hii taarifa, kungekuwepo na dosari na upungufu katika ufahamu kuhusu jinsi Mungu alivyo chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Hivyo, kile ambacho tumeongea leo kinaweza kusemwa kuwa kimetamatisha yale tuliyoyaongelea kabla, pamoja na maudhui ya “Mungu ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote.” Baada ya kuelewa haya, mna uwezo wa kumjua Mungu kupitia maudhui haya? Na kilicho muhimu zaidi ni kwamba leo, Nimewapitisha ujumbe muhimu sana: kuhusu watendaji huduma. Ninajua mnapenda sana kusikia mada kama hizi, kwamba mnayatilia maanani sana mambo haya, basi mnahisi mmeridhika na yale Nimezungumzia leo? (Ndiyo, tumeridhika.) Mwaweza kuwa hamvutiwi sana na vitu vingine, lakini haswa mnavutiwa na mazungumzo kuhusu watendaji huduma, kwa kuwa hii mada inagusia kila moyo wa mmoja wenu.

Jumapili, 31 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu I” Sehemu ya Tano

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu I” Sehemu ya Tano

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio Mungu Pekee, Ambaye Anao Utambulisho wa Muumba, Anamiliki Mamlaka ya Kipekee Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hufai Kufuata lile Wazo la Imani ya Kuabudu Miungu Wengi Ingawaje Binadamu Amepotoka, Angali Anaishi Chini ya Ukuu wa Mamlaka ya Muumba
Mwenyezi Mungu alisema, Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho? La, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo! Hii ni kwa sababu vikao hivi vya ushirika vilitupa tu ufahamu wa sehemu ya tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho—na wala si kila kitu, au uzima Wake wote. Vikao hivi vya ushirika vilikuwezesha wewe kuelewa sehemu ya kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na kupitia kwa hayo uliweza kuielewa tabia ya Mungu, na kile Anacho, na alicho, pamoja na mtazamo na kufikiria kuliko kila kitu ambacho Amefanya. Hata hivyo huu ni ufahamu tu wa moja kwa moja, wa matamshi, na katika moyo wako, unabakia kutojua ni kiwango kipi haswa ambacho ni kweli. Ni nini hasa huamua kama kunao uhalisia wowote katika ufahamu wako wa mambo kama haya? Yanaamuliwa na kiwango kipi cha maneno na tabia ya Mungu ambayo kwa kweli umepitia kwenye yale yote ya kweli ambayo wewe umepitia, na kiwango kipi ambacho umeweza kuona na kujua kwenye hali hizi halisi ambazo ulipitia. “Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vilituruhusu kuelewa mambo yanayofanywa na Mungu, fikira za Mungu, na, zaidi ya yote, mtazamo wa Mungu kwa mwanadamu na msingi wa hatua Zake, pamoja na kanuni za vitendo Vyake. Na kwa hivyo tumekuja kuelewa tabia ya Mungu, na kujua Mungu kwa uzima Wake.” Je, kunaye aliyesema maneno haya? Ni sahihi kusema hivi? Kwa kweli ni wazi kwamba si sahihi. Na kwa nini Nasema kwamba si sahihi? Tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho, vyote vinaonyeshwa katika mambo ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye ametamka. Binadamu anaweza kuelewa kile Anacho na alicho kupitia kwa kazi ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye ameongea, lakini hii ni kusema tu kwamba ile kazi na maneno humwezesha binadamu kuelewa sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya kile Anacho na alicho. Kama binadamu atataka kufaidi ufahamu mwingi zaidi na ulio wazi kuhusu Mungu, basi binadamu lazima apitie maneno na kazi nyingi zaidi za Mungu. Ingawaje binadamu hufaidi tu ufahamu kiasi wa Mungu wakati anapokuwa akipitia sehemu ya maneno au kazi ya Mungu, je, ufahamu huu wa kiasi unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu? Je, unawakilisha hali halisi ya Mungu? Bila shaka unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu, na hali halisi ya Mungu, hapo hapana shaka. Haijalishi ni lini au wapi, au ni kwa njia gani ambayo Mungu hufanya kazi Yake, au ni umbo gani ambalo humwonekania binadamu, au ni kwa njia gani Anaonyesha mapenzi Yake, kila kitu Anachofichua na kuonyesha huwakilisha Mungu Mwenyewe, hali halisi ya Mungu na kile Anacho na alicho. Mungu hutekeleza kazi Yake na kile Anacho na alicho, na katika utambulisho Wake wa kweli; Huu ni ukweli mtupu. Ilhali, leo, watu wanao ufahamu kiasi tu wa Mungu kupitia maneno Yake, na kupitia kile wanachosikia wanaposikiliza mahubiri, na kwa hivyo hadi kufikia kiwango fulani, ufahamu huu unaweza kusemwa tu kuwa maarifa ya kinadharia. Kwa mtazamo wa hali zenu halisi, mnaweza kuthibitisha tu ufahamu au maarifa ya Mungu ambayo mmesikia, kuona, au kujua na kuelewa katika moyo wako leo kama kila mmoja wenu atashuhudia haya kupitia kwa yale yote halisi aliyoyapitia, na anakuja kuyajua kidogokidogo. Kama Singeweza kushiriki maneno haya na wewe, je, ungeweza kutimiza maarifa ya kweli ya Mungu ukiwa pekee kupitia kwa yale yote uliyoyapitia? Kufanya hivyo, Naogopa, kunaweza kuwa vigumu sana. Hiyo ni kwa sababu lazima watu wawe kwanza na maneno ya Mungu ili kujua namna ya kuyapitia. Hata hivyo wingi wa maneno ya Mungu ambayo watu hushiriki, hicho ndicho kiwango wanachoweza kupitia. Maneno ya Mungu huongoza njia iliyo mbele, na humpa binadamu mwongozo katika yale yote anayoyapitia. Kwa ufupi, kwa wale walio na baadhi ya mambo ya kweli waliyoyapitia, vikao hivi mbalimbali vya mwisho vitawasaidia kutimiza ufahamu wa kina wa kweli, na hali yenye uhalisia zaidi kuhusu maarifa ya Mungu. Lakini kwa wale wasiokuwa na hali yoyote ya kweli ya waliyoipitia, au ambao wameanza tu hali yao wanayopitia, au wameanza tu kugusia uhalisia wa mambo, huu ni mtihani mkubwa.
Yale maudhui makuu ya vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika yalihusu “tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe.” Ni nini ulichoona kwenye sehemu zile muhimu na kuu kati ya kila kitu Nilichoongea? Kupitia kwenye vikao hivi vya ushirika, unaweza kutambua kwamba Yule aliyefanya kazi, na Akaweza kufichua tabia hizi, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye na ukuu juu ya mambo yote? Kama jibu lako ni ndiyo, basi ni nini kinachokuongoza katika hitimisho kama hilo? Ni katika dhana zipi uliweza kufikia hitimisho hili? Je, kunaye yeyote anayeweza kuniambia Mimi? Ninajua kwamba vikao vya mwisho vya ushirika vilikuathiri kwa undani, na vilikupa mwanzo mpya katika moyo wako kwa minajili ya maarifa yako kwa Mungu, jambo ambalo ni kuu. Lakini ingawaje umeweza kuchukua hatua kubwa katika ufahamu wako wa Mungu ukilinganishwa na awali, ufafanuzi wako wa utambulisho wa Mungu bado unahitaji hatua zaidi ya majina ya Yehova Mungu wa Enzi ya Sheria, Bwana Yesu wa Enzi ya Neema, na Mwenyezi Mungu wa Enzi ya Ufalme. Hivi ni kusema kwamba, ingawaje vikao hivi vya ushirika kuhusu “tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” viliweza kukupa ufahamu fulani wa maneno yaliyowahi kuzungumzwa na Mungu, na kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na uwepo na vinavyomilikiwa vilivyowahi kufichuliwa na Mungu, huwezi kutoa ufafanuzi wa ukweli na mpangilio sahihi wa neno “Mungu.” Na wala huna mpangilio wa kweli na sahihi na maarifa ya hali na utambulisho wa Mungu Mwenyewe, hii ni kusema, katika hadhi ya Mungu miongoni mwa mambo yote na kotekote kwenye ulimwengu mzima. Hii ni kwa sababu, kwenye vikao vya ushirika vya awali kuhusu Mungu Mwenyewe na tabia ya Mungu, maudhui yote yalitokana na maonyesho na ufunuo mbalimbali wa awali kuhusu Mungu uliorekodiwa kwenye Biblia. Ilhali ni vigumu kwa binadamu kugundua uwepo na miliki ambazo zinamilikiwa na kuonyeshwa na Mungu wakati wa, au nje ya, usimamizi na wokovu Wake kwa mwanadamu. Kwa hivyo, hata kama utaelewa nafsi na miliki za Mungu ambazo zilifichuliwa kwenye kazi Aliyowahi kufanya, ufafanuzi wako wa utambulisho na hadhi ya Mungu ungali mbali sana na ule wa Mungu wa kipekee, Yule anayeshikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na ni tofauti na ule wa Muumba. Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vilifanya kila mmoja kuhisi kwa njia moja: Binadamu angejuaje fikira za Mungu? Kama kweli mtu angejua, basi mtu huyo bila shaka angekuwa Mungu, kwa maana Mungu Mwenyewe ndiye anayejua fikira Zake, na Mungu Mwenyewe tu ndiye anayejua msingi na mtazamo wa kila kitu Anachofanya. Yaonekana ya kueleweka na ya mantiki kwako wewe kutambua utambulisho wa Mungu kwa njia kama hiyo, lakini ni nani anayeweza kujua kutoka kwenye tabia na kazi ya Mungu kwamba kwa kweli hii ni kazi ya Mungu Mwenyewe, na wala si kazi ya binadamu, kazi ambayo haiwezi kufanywa kwa niaba ya Mungu na binadamu? Nani anayeweza kuona kwamba kazi hii inapatikana katika uongozi wa ukuu wa Yule aliye na hali halisi na nguvu za Mungu? Hii ni kusema kwamba, kupitia sifa au hali halisi gani ndipo unapotambua kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe, aliye na utambulisho wa Mungu, na Ndiye aliye na ukuu juu ya viumbe vyote? Umewahi kufikiria hivi? Kama hujawahi, basi hii inathibitisha hoja moja: Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vimeweza kukupa tu ufahamu fulani wa kipande cha historia ambapo Mungu alifanya kazi Yake, na mtazamo, maonyesho, na ufunuo wa Mungu kwenye kipindi cha kufanyika kwa kazi hiyo. Ingawaje ufahamu kama huo unafanya kila mmoja wenu kutambua bila ya shaka yoyote kwamba Yule aliyetekeleza awamu hizi mbili za kazi ni Mungu Mwenyewe ambaye tunamsadiki na kumfuata, na Ndiye lazima siku zote tumfuate, tungali hatuna uwezo wa kutambua kwamba Yeye ni Mungu aliyekuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, na Atakayeendelea kuwepo milele hadi milele, na wala hatuwezi kutambua kwamba Yeye Ndiye anayetuongoza na Anayeshikilia utawala juu ya wanadamu wote. Kwa kweli hujawahi kufikiria kuhusu tatizo hili. Awe ni Yehova Mungu au Bwana Yesu, ni kupitia kwa dhana zipi za hali halisi na maonyesho husika ndipo unaweza kutambua kwamba Yeye si Mungu tu ambaye lazima umfuate, lakini pia Ndiye anayeamuru mwanadamu na Anayeshikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu, ambaye, vilevile, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee anayeshikilia ukuu dhidi ya mbingu na ardhi na viumbe vyote? Ni kupitia kwenye njia gani ndipo unapotambua kwamba Yule unayemsadiki na kumfuata ni Mungu Mwenyewe anayeshikilia ukuu juu ya viumbe vyote? Ni kupitia kwenye njia gani ndipo unapounganisha Mungu unayemsadiki na Mungu anayeshikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu? Ni nini kinachokuruhusu kutambua kwamba Mungu unayemsadiki ndiye yule Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye mbinguni na ulimwenguni, na miongoni mwa viumbe vyote? Hili ndilo tatizo ambalo Nitatatua kwenye sehemu ijayo.
Matatizo ambayo hujawahi kufikiria kuhusu au huwezi kufikiria kuhusu ndiyo yayo hayo ambayo yanaweza kuwa muhimu zaidi kwa kumjua Mungu, na ambayo kwayo unaweza kutafuta ukweli usioweza kufikirika kwa mwanadamu. Wakati matatizo haya yanapokukumba, na lazima wewe ndiwe unayefaa kuyakabili, na unahitajika kufanya uamuzi, kama hutaweza kuyatatua kikamilifu kwa sababu ya ujinga au kutojua kwako, au kwa sababu yale yote uliyopitia wewe ni ya juujuu sana na unakosa maarifa ya kweli ya Mungu, basi yatakuwa kizuizi kikubwa zaidi na changamoto kubwa zaidi kwenye njia yako ya kumsadiki Mungu. Na kwa hivyo Nahisi kwamba tunahitajika kabisa kushiriki pamoja nanyi mada hii. Je, unajua tatizo lako ni nini sasa? Je, unatambua matatizo Ninayoyazungumzia? Je, matatizo haya ndiyo utakayokabiliana nayo? Je, haya ndiyo matatizo usiyoyaelewa? Je, haya ndiyo matatizo ambayo hayajawahi kukutokea? Je, matatizo haya ni muhimu kwako? Je, ni matatizo kweli? Suala hili ni chanzo cha mkanganyo mkuu kwako, na hivyo inaonekana kwamba huna ufahamu wa kweli wa Mungu unayemsadiki, na kwamba humchukulii Yeye kwa umakinifu. Baadhi ya watu husema, “Ninajua Yeye ni Mungu, na kwa hivyo ninamfuata Yeye kwa sababu maneno Yake ni maonyesho ya Mungu. Hayo yanatosha. Thibitisho lipi zaidi linahitajika? Kwa kweli hatuhitaji kuibua shaka kuhusu Mungu? Kwa kweli hatupaswi kumjaribu Mungu? Kwa kweli hatuhitaji kuulizia hali halisi ya Mungu na utambulisho wa Mungu Mwenyewe?” Bila kujali kama unafikiria kwa njia hii, huwa Siyaulizi maswali fulani ili kukukanganya kuhusu Mungu, au kukufanya umjaribu Mungu, na isitoshe ili kukupa shaka kuhusu utambulisho na hali halisi ya Mungu. Badala yake, Ninafanya hivi ili kuhimiza ndani yenu ufahamu mkubwa zaidi wa hali halisi ya Mungu, na uhakika na imani kubwa zaidi kuhusu hadhi ya Mungu, ili Mungu awe Ndiye wa pekee katika mioyo ya wale wote wanaomfuata Mungu, na ili ile hadhi ya asili ya Mungu—kama Muumba, Kiongozi wa viumbe vyote, Mungu Mwenyewe wa kipekee—iweze kurejeshwa katika mioyo ya kila kiumbe. Hii pia ndiyo mada itakayohusu ushirika wetu.