Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumamosi, 20 Aprili 2019

Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Anayetawala Juu ya Vitu Vyote.

1. Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Anayetawala Juu ya Vitu Vyote.

Maneno Husika ya Mungu:
Wanadamu hawajui ni nani Mkuu wa kila kitu katika ulimwengu huu, aidha hajui mwanzo na mustakabali wa wanadamu. Wanadamu wanaishi tu, bila budi, katikati ya hii sheria. Hakuna anayeweza kuiepuka wala kuibadilisha kwani katika vitu vyote na katika mbingu kuna Mmoja kutoka milele hadi milele ambaye ni Mkuu wa kila kitu. Ni Yeye ambaye Hajawahi kuonekana na mwanadamu, ambaye wanadamu hawajawahi kumjua, ambaye wanadamu hawajawahi kuamini kuwepo Kwake, na bado ni Yeye Aliyewapulizia pumzi mababu wa wanadamu na kuwapa wanadamu uhai. Ni Yeye ndiye Huruzuku na kustawisha wanadamu kwa kuishi kwao, na huwaongoza wanadamu hadi siku ya leo. Aidha, Yeye na Yeye pekee ni wa kutegemewa na wanadamu ili kuendelea kuishi. Ni Mkuu wa kila kitu na Hutawala viumbe vyote vyenye uhai chini ya dunia. Huamrisha misimu yote minne, na ni Yeye huita upepo, jalidi, theluji na mvua. Huwapa wanadamu mwangaza wa jua na huleta machweo ya jioni. Ni Yeye Aliyeumba mbingu na ardhi, Akampa mwanadamu milima, maziwa na mito na kila kitu kilicho na uhai ndani yake. Matendo Yake yamo kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. Kila mojawapo ya hizi sheria na kanuni ni mfano mzuri wa matendo Yake, na kila mojawapo inafichua hekima na mamlaka Yake. Nani anayeweza kujiondoa kutoka kwa ukuu Wake? Na ni nani anayeweza kujitoa mwenyewe katika njia Zake? Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma. Bila kujali kama unaweza kutambua vitendo vya Mungu, bila kujali kama unaamini katika kuwepo kwa Mungu, hakuna shaka kuwa hatima yako inaegemea katika mipango ya Mungu, na hakuna shaka kuwa Mungu atakuwa na ukuu juu ya kila kitu. Uwepo na utawala Wake haviwezi kutabiriwa ikiwa vinatambulika na kufahamika na binadamu au la. Ni Yeye pekee Anayejua kuhusu yaliyopita ya mwanadamu, yaliyomo na yanayojiri, na Yeye pekee ndiye mwamuzi wa hatima ya wanadamu. Haijalishi kama unaukubali huu ukweli, haitachukua muda mrefu kabla mwanadamu kushuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe, na huu ni ukweli ambao hivi karibu Mungu Ataudhihirisha.
kutoka kwa "Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha si rahisi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung'aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Maisha ya Mungu, huishi milele bila kubadilika katika kusumbuka kwa mbingu na nchi. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.
kutoka kwa "Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu aliumba dunia hii na kuleta mwanadamu, kiumbe hai ambacho alitia uhai ndani yake. Baadaye, mwanadamu akaja kuwa na wazazi na jamaa na hakuwa mpweke tena. Tangu mwanadamu alipotua macho kwa mara ya kwanza katika dunia hii tunayoishi, ilibainika kuwa angeishi ndani ya utaratibu wa Mungu. Ni pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ndiyo hustawisha kila kiumbe hai katika ukuaji wake hadi kinapokomaa. Wakati wa mchakato huu, hakuna hata mmoja anayeamini kwamba mwanadamu huishi na kukua chini ya uangalizi wa Mungu. Badala yake, anashikilia kwamba mwanadamu hukua chini ya upendo na utunzaji wa wazazi wake, na kwamba ukuaji wake unaongozwa na silika ya maisha. Hii ni kwa sababu mwanadamu hajui aliyeleta maisha au kulikotoka maisha hayo, pia hafahamu jinsi silika ya maisha husababisha miujiza. Mwanadamu anajua tu kwamba chakula ndicho msingi wa kuendelea kwa maisha, kwamba uvumilivu ni chanzo cha kuwepo kwa maisha, na kwamba imani iliyomo akilini mwake ni utajiri wa maisha yake. Mwanadamu haihisi neema na riziki itokayo kwa Mungu. Mwanadamu huyatumia kwa uharibifu maisha aliyopewa na Mungu.
kutoka kwa "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Majaliwa ya mwanadamu inadhibitiwa na mikono ya Mungu. Wewe huna uwezo wa kujidhibiti mwenyewe: Licha ya mwanadamu yeye mwenyewe daima kukimbilia na kujishughulisha, anabakia bila uwezo wa kujidhibiti. Kama ungejua matarajio yako mwenyewe, kama ungeweza kudhibiti majaliwa yako mwenyewe, ingekuwa wewe bado ni kiumbe? Kwa kifupi, bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi, kazi yote yake ni kwa ajili ya mwanadamu. Chukua, kwa mfano, mbingu na nchi na vitu vyote ambavyo Mungu aliviumba ili kumhudumia mwanadamu: mwezi, jua, na nyota ambazo Yeye alimuumbia mwanadamu, wanyama na mimea, majira ya machipuko, majira ya joto, vuli na baridi, na kadhalika—yote ni kwa ajili ya kuwepo kwa mwanadamu.
kutoka kwa "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa thabiti katika kazi Yake, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na harakati ya mambo yote. Kama kila kiumbe, mwanadamu bila kujua anapata lishe ya utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yote ya mwanadamu yanatunzwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, vilivyo hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, vitafanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu anavyotawala juu ya kila kitu.
Usiku uingiapo kwa utulivu, mwanadamu huwa hafahamu, kwani moyo wa mwanadamu hauwezi kujua jinsi giza linapokaribia au linakotoka. Usiku unapotoweka polepole, mwanadamu anakaribisha mwanga wa mchana, lakini moyo wa mwanadamu haufahamu ilikotoka nuru hii na jinsi gani nuru yenyewe imeliondoa giza la usiku. Mabadiliko kama haya ya kawaida ya mchana na usiku humpitisha mwanadamu katika kipindi kimoja baada ya kingine, kupita katika nyakati, wakati huu wote ikihakikisha kwamba kazi ya Mungu na mpango wake unafanywa wakati wa kila kipindi na katika nyakati zote. Mwanadamu alitembea katika enzi nyingi na Mungu, lakini bado mwanadamu hafahamu kwamba Mungu ndiye kiongozi wa hatima ya mambo yote na viumbe hai na pia hafahamu jinsi Mungu hupanga na kuongoza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo.
kutoka kwa "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Tangu wakati wa uumbaji, nilianza uamuzi wa mapema na uteuzi wa kundi hili la watu—lenu nyinyi, kundi hili leo. Tabia yako, uhodari, umbo, ukomavu, familia uliyozaliwa ndani, kazi yako, ndoa—kila kitu chako, hata rangi ya nywele zako, ngozi yako, na tarehe yako ya kuzaliwa—vyote hivi vimepangiliwa kwenye mkono Wangu. Chochote unachofanya na yeyote unayekutana naye kila siku vyote vinategemea mpangilio Wangu, sisemi chochote kuhusu kitakachokuleta mbele yangu Mimi leo, ambacho hasa ni maudhui ya mpangilio Wangu. Usijisababishie mahangaiko wewe mwenyewe, lakini endelea kwa utulivu.
kutoka Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni
Tangu Alipoanza uumbaji wa viumbe vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni njia gani Alitumia, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, viumbe vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwenye muda kabla ya mwanadamu kuumbwa ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba viumbe vyote kwa minajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwenye viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, nuru, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, zikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila mojawapo kilipewa maisha kwa matamshi ya Muumba, na kila kiumbe mojawapo kilizaana kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimojawapo kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawaje hawakupokea pumzi za Muumba, bado walionyesha maisha na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa mifumo na miundo yao mbalimbali; ingawaje hawakupokea uwezo wa kuongea aliopewa mwanadamu na Muumba, kila kimojawapo kilipokea njia ya kuelezea maisha yao ambayo walipewa na Muumba, na ambayo ilitofautiana na ile lugha ya Mwanadamu. Mamlaka ya Muumba hayatoi tu nguvu za maisha kwenye vifaa vinavyoonekana kuwa tuli, ili visiwahi kutoweka, lakini, vilevile, hupatia silika ya kuzaana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, vitaweza kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatilia mkazo mamlaka Yake haikubaliani kwa lazima na mtazamo wa mambo makubwamakubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka ya umbo lolote; Anaweza kuamuru utendaji mambo katika ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya maisha na kifo cha viumbe vyote, na, vilevile, Anaweza kushughulikia viumbe vyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala viumbe vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya pekee ya Muumba miongoni mwa viumbe vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu ya maisha tunayoishi, na hayatawahi kusita, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kubadilisha utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote-ambacho hakikuumbwa.
kutoka kwa "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hatima za binadamu na zile za ulimwengu zimeingiliana kwa ndani na ukuu wa Muumba, zimefungamanishwa na haziwezi kutenganishwa na mipango ya Muumba; na hatimaye, haziwezi kutenganishwa na mamlaka ya Muumba. Kupitia kwenye sheria za mambo yote binadamu huja kuelewa mipango ya Muumba na ukuu Wake; kupitia kwenye sheria za namna ya kuishi ambazo anaona katika utawala wa Muumba; kutoka kwenye hatima za mambo yote anapata hitimisho kuhusu njia ambazo Muumba huonyesha ukuu Wake na kuvidhibiti; na kwenye mzunguko wa maisha ya binadamu na mambo yote ambayo binadamu kwa kweli hupitia ile mipango na mipangilio ya Muumba kwa mambo yote na kwa viumbe vyote vilivyo hai na anashuhudia kwa kweli namna ambavyo mipango na mipangilio hiyo inavyozidi sheria zote za nchi, kanuni, na taasisi, mamlaka na nguvu zote nyingine. Kwa mujibu wa haya, binadamu wanashawishiwa kutambua kwamba, ukuu wa Muumba hauwezi kukiukwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, kwamba hakuna nguvu zinazoweza kuharibu au kubadilisha matukio na mambo yaliyoamuliwa kabla na Muumba. Ni kupitia kwenye sheria na kanuni hizi takatifu ambapo binadamu na viumbe vyote wanaweza kuishi na kuzalisha, kizazi baada ya kizazi. Je, huu si mfano halisi wa mamlaka ya Muumba?
kutoka kwa "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III" katika Neno Laonekana katika Mwili
(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote
Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.
Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.
Angalia nyuma wakati wa safina ya Nuhu: Wanadamu walikuwa wapotovu sana, walikuwa wamepotea kutoka katika baraka za Mungu, hawakuwa wanatunzwa na Mungu tena, na walikuwa wamepoteza ahadi za Mungu. Waliishi gizani, bila mwangaza wa Mungu. Hivyo wakawa waasherati kwa asili, wakajiachilia katika mkengeuko wa kutisha. Watu kama hao hawangeweza tena kupokea ahadi za Mungu; hawakufaa kushuhudia uso wa Mungu, wala kusikia sauti ya Mungu, kwani walikuwa wamemwacha Mungu, kuweka kando yote Aliyowapa, na kusahau mafunzo ya Mungu. Mioyo yao ilipotea mbali zaidi na zaidi na Mungu, na ilivyofanya hivyo, wakawa wapotovu zaidi ya mantiki na ubinadamu wote na wakazidi kuwa waovu. Hivyo walikaribia kifo zaidi, na kukabiliwa na ghadhabu na adhabu ya Mungu. Ni Nuhu tu aliyemwabudu Mungu na kuepukana na uovu, na hivyo aliweza kusikia sauti ya Mungu, na kusikia maelekezo ya Mungu. Alijenga safina kulingana na maelekezo ya neno la Mungu, na kukusanya aina yote ya viumbe hai. Na kwa njia hii, wakati kila kitu kilikuwa kimetayarishwa, Mungu aliangamiza dunia. Nuhu tu na wanachama saba wa familia yake walinusurika maangamizi, kwani Nuhu alimwabudu Yehova na kuepukana na uovu.
Kisha angalia enzi ya sasa: Hawa watu wenye haki kama Nuhu, ambao wangeweza kumwabudu Mungu na kuepuka uovu, wamekoma kuwepo. Lakini bado Mungu ana fadhili kwa mwanadamu huyu, na Anamsamehe mwanadamu wakati huu wa enzi ya mwisho. Mungu anawatafuta wanaomtaka Yeye ajitokeze. Anawatafuta wale wanaoweza kuyasikia maneno Yake, wale ambao hawajasahau agizo Lake na wanatoa mioyo na miili yao Kwake. Anawatafuta wale walio watiifu kama watoto wachanga mbele Yake, na hawampingi. Kama hujazuiliwa na nguvu zozote katika ibada yako Kwake, basi Mungu atakutazama na neema, na kukupea baraka Zake. Kama wewe ni wa daraja la juu, wa sifa ya heshima, aliyemiliki maarifa mengi, mmiliki wa mali nyingi, na kuungwa mkono na watu wengi, lakini mambo haya hayakuzuii kuja mbele za Mungu kuukubali wito Wake na agizo Lake, kufanya kile Mungu anachokuambia ufanye, basi yote unayoyafanya yatakuwa yenye umuhimu zaidi duniani na yenye haki zaidi ya binadamu. Ukiukataa wito wa Mungu kwa sababu ya hadhi yako na malengo yako mwenyewe, yote utakayoyafanya yatalaaniwa na hata kudharauliwa na Mungu. Labda wewe ni rais, ama mwanasayansi, ama mchungaji, ama mzee, lakini bila kujali ukuu wa ofisi yako, ukitegemea maarifa yako na uwezo katika shughuli zako, basi daima utakuwa wa kushindwa na kamwe utanyimwa baraka za Mungu, kwa sababu Mungu hakubali chochote unachofanya, na Hakubali kwamba kazi yako ni yenye haki, wala kukubali kwamba unafanya kazi kwa msaada wa mwanadamu. Atasema yote unayofanya, ni ya kutumia maarifa na nguvu za mwanadamu kumvulia mwanadamu ulinzi wa Mungu na kumnyima baraka za Mungu. Atasema kuwa unamwongoza mwanadamu kuelekea gizani, kuelekea kifo, na kuelekea mwanzo wa kuwepo bila mipaka ambapo mwanadamu amempoteza Mungu na baraka Zake.
Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa imani kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalia kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha. … Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu. Na kwa njia hii, ustaarabu wa ubinadamu bila fahamu ukawa huwezi kukutana na matakwa ya mwanadamu hata zaidi, na hata kuna watu zaidi wanaohisi kwamba, kuishi kwa dunia kama hii, wanayo furaha ya chini kuliko watu walioenda. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa juu wanaeleza malalamiko haya. Kwani bila mwongozo wa Mungu, bila kujali jinsi viongozi na wanasosiolojia wanatafakari kuhifadhi ustaarabu wa binadamu, haina mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu kwa moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uhai wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza udhalimu wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kafara na uchunguzi usio na sababu wa mwanadamu vitamwongoza tu kwa dhiki zaidi. Mwanadamu daima atakuwa katika hali ya hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele. Mwanadamu atakuja hata kuogopa sayansi na elimu, na kuhofia hata zaidi utupu ulio ndani yake sana. Duniani humu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, siri na majaliwa ya mwanadamu. Chini ya hayo, huna uwezo wa kutoroka hisia ya utupu inayotatiza. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasosiolojia, lakini hakuna mtu mkubwa anayeweza kuja mbele kutatua shida kama hizi. Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu utaweza kutatuliwa. Iwapo watu wa nchi ama taifa hawawezi kupokea wokovu na utunzaji wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litatembelea njia inayoelekea uharibifuni, inayoelekea gizani, na litaangamizwa na Mungu.
Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kupotea kutoka kwa Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamwasi Mungu na kulaani Mbingu. Na hivyo majaliwa ya nchi pasipo kujua yataletwa kwa uharibifu. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na anaweza hata kuzifuta kutoka uso wa dunia. Kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa kunategemea kama viongozi wao wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wao karibu na Mungu na kumwabudu. Lakini, kwa hii enzi ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli na kumwabudu wanazidi kuwa wachache, Mungu anaweka fadhili ya pekee juu ya nchi ambapo Ukristo ni dini ya serikali. Anazikusanya pamoja kuunda kambi ya haki kiasi ya dunia, wakati nchi zikanazo Mungu ama zile zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu mahali miongoni mwa wanadamu pa kufanyia kazi Yake, lakini pia Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, ili kulazimisha mipaka na vikwazo kwa nchi hizo zinazompinga Mungu. Lakini licha ya hayo, bado hakuna watu zaidi wanaokuja mbele kumwabudu Mungu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na Mungu hajakuwa kwa mawazo ya mwanadamu kwa muda mrefu. Kunabakia tu duniani nchi zinazotumia haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ni mbali na matakwa ya Mungu, kwani hakuna kiongozi wa nchi yoyote atamruhusu Mungu kuongoza watu wake, na hakuna chama cha kisiasa kitakachokusanya pamoja watu wake kumwabudu Mungu; Mungu amepoteza mahala Pake halali kwa mioyo ya nchi zote, taifa, chama tawala, na hata kwa moyo wa kila mtu. Ingawa nguvu za haki ziko kwa dunia hii, utawala ambapo Mungu hana mahali kwa moyo wa mwanadamu ni dhaifu. Bila baraka ya Mungu, uwanja wa kisiasa utaanguka katika vurugu na wenye kuweza kudhuriwa na mashambulizi. Kwa mwanadamu, kuwa bila baraka ya Mungu ni kama kukosa mwanga wa jua. Bila kujali jinsi viongozi wanafanya mchango kwa watu wao kwa uangalifu, bila kujali idadi ya mikutano ya haki wanadamu wanafanya pamoja, hakuna kati ya hii itakayorejesha mambo ama kubadilisha majaliwa ya mwanadamu. Mwanadamu anaamini kuwa nchi ambapo watu wanalishwa na kuvalishwa nguo, ambapo watu wanaishi kwa amani, ni nchi nzuri, na iliyo na uongozi mzuri. Lakini Mungu hafikirii hivyo. Anaamini kuwa nchi ambapo hakuna mtu anayemwabudu ndiyo Atakayoiangamiza. Njia ya mwanadamu ya kufikiria ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kama mkuu wa nchi hamwabudu Mungu, basi majaliwa ya nchi hii itakuwa ya kutisha, na nchi haitakuwa na majaliwa.
Mungu hashiriki katika siasa za mwanadamu, lakini majaliwa ya nchi ama taifa inadhibitiwa na Mungu, Mungu anadhibiti dunia hii na ulimwengu mzima. Majaliwa ya mwanadamu na mpango wa Mungu yanashikamana kwa undani, na hakuna mwanadamu, nchi ama taifa limetolewa kwa mamlaka ya Mungu. Iwapo mwanadamu anatamani kujua majaliwa yake, basi lazima aje mbele ya Mungu. Mungu atawafanya wanaomfuata na kumwabudu kufanikiwa, na Atashusha na kuwaangamiza wale wanaompinga na kumkataa.
Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Loti alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma jinsi watu wa Ninawi walitubu dhambi zao kwa gunia na majivu, na kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.
Leo, Mungu amerudi duniani kufanya kazi Yake. Atasimama kwanza kwa mkutano mkubwa wa viongozi madikteta: Uchina, ngome kali ya ukanaji Mungu. Mungu amepata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Wakati huu, Anawindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso makubwa, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na kutoweza kupata makazi. Licha ya haya, Mungu bado anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Anatamka sauti Yake na kueneza injili. Hakuna anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu zaidi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu anafanya yote Awezayo kuokoa kila mshiriki wa ubinadamu. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo. Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama tu ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni.
Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Ijumaa, 19 Aprili 2019

Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

4. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii hasa kwamba mwili wa mwanadamu umepotoshwa ndiyo maana Mungu amemfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mlengwa wa upotovu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa pekee wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, ni lazima Mungu awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi. Mungu lazima awe mwili ili Aweze kufanya kazi Yake kwa ufanisi kwa sababu mwanadamu ni wa mwili, na hana uwezo wa kushinda dhambi au kujivua mwili. Ingawa kiini na utambulisho wa Mungu unatofautiana kwa kiasi kikubwa na kiini na utambulisho wa mwanadamu, bado kuonekana Kwake kunafanana na kuonekana kwa mwanadamu, Ana umbo la mwanadamu wa kawaida, na Anaishi maisha ya mwanadamu wa kawaida, na wale wanaomwona hawawezi kuona tofauti na mtu wa kawaida. Kuonekana huku kwa kawaida na ubinadamu wa kawaida vinatosha Kwake kwa ajili ya kufanya kazi Yake ya kiungu katika ubinadamu wa kawaida. Mwili Wake unamruhusu kufanya kazi Yake katika ubinadamu wa kawaida, na unamsaidia kufanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu, na ubinadamu Wake wa kawaida, aidha, humsaidia kufanya kazi ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Ingawa ubinadamu Wake wa kawaida umeleta msukosuko miongoni mwa wanadamu, msukosuko huo haujaathiri matokeo ya kawaida ya kazi Yake. Kwa ufupi, kazi ya ubinadamu Wake wa kawaida ni ya manufaa makubwa kwa mwanadamu. Ingawa watu wengi hawakubali ubinadamu Wake wa kawaida, kazi Yake bado inaweza kuwa ya ufanisi, na matokeo haya yanapatikana kutokana na ubinadamu Wake wa kawaida. Kuhusu hili hakuna shaka. Kutokana na kazi Yake ya mwili, mwanadamu anapata vitu mara kumi au dazeni kadhaa zaidi kuliko mitazamo iliyopo miongoni mwa mwanadamu kuhusu ubinadamu Wake wa kawaida, na mitazamo hiyo hatimaye itamezwa na kazi Yake. Na matokeo ambayo kazi Yake imefanikiwa, ambayo ni kusema, maarifa ambayo mwanadamu anayo juu Yake, yanazidi kwa mbali sana dhana za mwanadamu kumhusu. Hakuna namna ya kufikiri au kupima kazi Anayofanya katika mwili, maana mwili Wake si kama wa mwanadamu; ingawa sura za nje zinafanana kiini chao si sawa. Mwili Wake unatoa mitazamo mingi kuhusu Mungu miongoni mwa mwanadamu, bado mwili Wake unaweza pia kumruhusu mwanadamu kuwa na maarifa mengi, na anaweza hata kumshinda mwanadamu yeyote mwenye ganda la sawa nje. Maana Yeye si mwanadamu wa kawaida tu, bali ni Mungu mwenye umbo la nje kama la mwanadamu, na hakuna anayeweza kumwelewa au kumfahamu kikamilifu. Mungu asiyeonekana na kushikika anapendwa na kukaribishwa na wote. Kama Mungu ni Roho tu ambayo haionekani kwa mwanadamu, ni rahisi sana kwa mwanadamu kumwamini Mungu. Mwanadamu anaweza kuzipa uhuru fikra zake mwenyewe, anaweza kuchagua taswira yoyote anayotaka kama taswira ya Mungu ili kujifurahisha mwenyewe na kujifanya mwenyewe awe na furaha. Kwa njia hii, mwanadamu anaweza kufanya chochote kile kinachomfurahisha Mungu wake, na kile ambacho Mungu huyu yuko tayari kukifanya bila aibu yoyote. Aidha, mwanadamu huyu anaamini kwamba hakuna ambaye ni mwaminifu zaidi anayejitolea kwa Mungu kuliko yeye, na kwamba wengine wote ni mbwa wa Mataifa, na wasiokuwa waaminifu kwa Mungu. Inaweza kusemekana kwamba hiki ndicho kinachotafutwa na wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya kidhahania na ambayo imejikita katika mafundisho; wanavyovitafuta vinafanana, tofauti ikiwa ndogo tu. Ni kwamba tu taswira za Mungu katika fikra zao ni tofauti, lakini viini vyao kimsingi vinafanana.
Mwanadamu hasumbuliwi na imani yake ya kutojali katika Mungu, na anamwamini Mungu kwa namna anavyotaka. Hii ni moja ya “haki na uhuru wa mwanadamu,” ambao hakuna mtu anayeweza kuuingilia kwa sababu mwanadamu anamwamini Mungu wake mwenyewe na wala si Mungu wa mtu yeyote yule; ni mali yake binafsi, na takribani kila mtu anamiliki aina hii ya mali binafsi. Mwanadamu anaichukulia mali hii kama hazina ya thamani, lakini kwa Mungu hakuna kitu ambacho ni duni au hakina thamani zaidi ya hiki, maana hakuna kiashiria cha wazi cha upinzani kwa Mungu kuliko mali hii binafsi ya mwanadamu. Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu mwenye mwili ndiyo Mungu amefanyika mwili ambaye ana umbo la kugusika, na ambaye anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu. Yeye si Roho asiyekuwa na umbo, bali mwili ambao unaweza kuhusiana na kuonekana kwa mwanadamu. Hata hivyo, Miungu mingi ambayo watu wanaamini kwayo ni miungu isiyo na mwili na umbo maalumu, na ambayo haifungwi na umbo maalumu. Kwa njia hii, Mungu mwenye mwili amekuwa adui wa wengi wanaomwamini Mungu, na wale ambao hawawezi kuukubali ukweli wa Mungu mwenye mwili, vilevile, wamekuwa maadui wa Mungu. Mwanadamu amejawa na dhana si kwa sababu ya namna anavyofikiri, au kwa sababu ya uasi wake, bali ni kwa sababu ya mali hii binafsi ya mwanadamu. Ni kwa sababu ya mali hii watu wengi hufa, na ni Mungu huyu asiye dhahiri, ambaye hawezi kuguswa, hawezi kuonwa, na ambaye hayupo hakika ambaye huangamiza maisha ya mwanadamu. Maisha ya mwanadamu yanapotea si kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sembuse na Mungu wa mbinguni, bali ni Mungu wa fikra za mwanadamu mwenyewe. Sababu pekee ambayo Mungu mwenye mwili amefanyika mwili ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu aliyepotoka. Ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu na si ya Mungu, na mateso Yake na sadaka ni kwa ajili ya mwanadamu na si kwa manufaa ya Mungu Mwenyewe. Hakuna faida wala hasara au tuzo kwa Mungu; Hatavuna mavuno yoyote ya baadaye, bali ni kile ambacho hapo awali Aliwiwa. Yote Anayoyafanya na kujitolea kwa ajili mwanadamu si kwa sababu Atapata thawabu kubwa, bali ni kwa ajili ya mwanadamu. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inahusisha ugumu mwingi usiofikirika, matokeo ambayo yanapatikana mwishowe yanazidi kwa mbali sana kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Kazi ya mwili inahusisha taabu nyingi sana, na mwili hauwezi kuwa na utambulisho mkubwa kama wa Roho, hauwezi kufanya matendo ya kimiujiza kama Roho, sembuse kuwa na mamlaka kama ya Roho. Lakini kiini cha kazi inayofanywa na mwili huu usiokuwa wa kawaida ni kuu zaidi kulinganisha na kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na mwili huu Mwenyewe ndio jibu kwa mahitaji yote ya mwanadamu. Kwa wale wanaotaka kuokolewa, thamani ya Roho ipo chini zaidi kulinganisha na ile ya mwili. Kazi ya Roho inaweza kuufikia ulimwengu wote, katika milima yote, mito, maziwa, na bahari, lakini kazi ya mwili kwa ufanisi zaidi inahusiana na kila mtu anayekutana na Yeye. Aidha, mwili wa Mungu katika umbo la kushikika unaweza kueleweka vizuri na kuaminiwa na mwanadamu, na unaweza kuimarisha maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu, na anaweza kumwachia mwanadamu mvuto wa kina wa matendo halisi ya Mungu. Kazi ya Roho imefungwa sirini, ni vigumu kwa viumbe wenye mwili wa kufa kuelewa, na vigumu zaidi kwao kuona, na hivyo wanaweza kutegemea tu vitu vya kufikirika. Hata hivyo, kazi ya mwili ni ya kawaida, na imejikita katika uhalisi, na ina hekima kubwa sana, na ni ukweli unaoweza kuonekana kwa macho ya mwanadamu; mwanadamu anaweza kupitia uzoefu wa hekima ya Mungu, na hana haja ya kuwa na fikira zake kubwa. Huu ndio usahihi na thamani halisi ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Roho anaweza tu kufanya vitu ambavyo havionekani kwa mwanadamu na vigumu kwake kufikiria, kwa mfano nuru ya Roho, mzunguko wa Roho na uongozi wa Roho, lakini kwa mwanadamu mwenye akili, hivi havitoi maana inayoeleweka. Vinatoa maana ya kusonga, au ya jumla tu, na havitoi maelekezo kwa maneno. Hata hivyo, kazi ya Mungu mwenye mwili, ni tofauti sana: Ina mwongozo sahihi wa maneno, ina nia ya wazi, ina malengo ya wazi yanayohitajika. Na hivyo mwanadamu hahitaji kupapasa, au kutumia fikra zake, au kufanya makisio. Huu ndio uwazi wa kazi katika mwili, na tofauti yake kubwa na kazi ya Roho. Kazi ya Roho inafaa tu kwa mawanda finyu, na haiwezi kuchukua kazi ya mwili. Kazi ya mwili inampa mwanadamu malengo halisi zaidi na yanayohitajika na maarifa yaliyo halisi zaidi na yenye thamani kuliko kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi ambayo ina thamani kubwa kwa mwanadamu aliyepotoka ambayo inatoa maneno sahihi, malengo wazi ya kufuata, na ambayo inaweza kuonekana na kuguswa. Ni kazi yenye kuwezekana tu, na uongozi wa wakati ndio unaofaa kwa ladha ya mwanadamu, na kazi halisi ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika tabia yake iliyopotoka na kusawijika. Hii inaweza kufanywa na Mungu mwenye mwili tu; ni Mungu mwenye mwili peke yake ndiye Anayeweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika hali yake ya zamani ya kupotoka. Ingawa Roho ni kiini cha asili ya Mungu, kazi kama hii inaweza tu kufanywa na mwili Wake. Kama Roho angefanya kazi peke Yake, basi haingewezekana kwa kazi Yake kuwa ya ufanisi—huu ni ukweli ulio wazi kabisa. Ingawa watu wengi wamekuwa maadui wa Mungu kwa sababu ya mwili huu, Anapokamilisha kazi Yake, wale ambao wapo kinyume Chake hawataacha tu kuwa maadui Zake, bali kinyume Chake watakuwa mashahidi Wake. Watakuwa mashahidi watakaokuwa wameshindwa naye, mashahidi ambao wana ulinganifu na Yeye na ambao hawatenganishwi naye. Atamsababisha mwanadamu kujua umuhimu wa kazi Yake katika mwili kwa mwanadamu, na mwanadamu atajua umuhimu wa mwili huu katika maana ya uwepo wa mwanadamu, atajua thamani Yake halisi katika ukuaji wa maisha ya mwanadamu, aidha, atajua mwili huu utakuwa chemchemi ya uhai ambayo kwayo mwanadamu hataachana nayo. Ingawa Mungu mwenye mwili anatofautiana sana na utambulisho na nafasi ya Mungu, na anaonekana kwa mwanadamu kuwa hana ulinganifu na hadhi yake halisi, mwili huu, ambao hauna sura halisi ya Mungu, au utambulisho halisi wa Mungu, unaweza kufanya kazi ambayo Roho wa Mungu hawezi kuifanya moja kwa moja. Hiyo ndiyo maana ya kweli na thamani ya Mungu mwenye mwili, na ni umuhimu huu na thamani ambayo mwanadamu hawezi kuithamini na kuikubali. Ingawa wanadamu wote wanamtazamia Roho wa Mungu na wanamdharau Mungu mwenye mwili, bila kujali vile wanavyoona au kufikiri, maana na thamani halisi ya mwili inapita kwa mbali ile ya Roho. Bila shaka, hii ni kwa mujibu wa mwanadamu aliyepotoka. Kwa kuwa kila mtu anayetafuta ukweli na anatamani kumwona Mungu, Kazi ya Roho inaweza kutoa tu kuguswa au ufunuo, na hisia ya kuona maajabu ambayo hayaelezeki na kufikirika, na hisia ambayo ni kuu, ya juu sana kuliko uwezo wa mwanadamu, na inayotamanika, lakini ambayo pia haifikiwi na haipatikani kwa wote. Mwanadamu na Roho wa Mungu wanaweza tu kutazamana kwa mbali, kana kwamba kuna umbali mrefu baina yao, na hawawezi kufanana kamwe, kana kwamba wametenganishwa na kitu kisichoonekana. Kwa hakika, hizi ni fikra za uongo ambazo Roho amempa mwanadamu, ambayo ndiyo sababu Roho na mwanadamu sio wa aina moja, na Roho na mwanadamu hawawezi kuishi pamoja katika ulimwengu mmoja, na kwa sababu Roho hana kitu chochote cha mwanadamu. Kwa hivyo mwanadamu hana haja ya Roho, maana Roho hawezi kufanya kazi inayohitajika sana na mwanadamu moja kwa moja. Kazi ya mwili inampatia mwanadamu malengo halisi ya kufuata, maneno halisi, na hisia kwamba Yeye ni halisi na wa kawaida, kwamba ni mnyenyekevu na wa kawaida. Ingawa mwanadamu anaweza kumwogopa, kwa watu wengi Yeye ni rahisi kuhusiana naye: Mwanadamu anaweza kuuona uso Wake, na kuisikia sauti Yake, na hahitaji kumwangalia kwa kutokea mbali. Mwanadamu anahisi kuwa ni rahisi kuufikia mwili huu, sio wa mbali au usioeleweka, bali unaoonekana na kushikika, maana mwili huu upo katika ulimwengu mmoja na mwanadamu.
Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha tabia zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza inapaswa iondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanahitajika kutupilia mbali tabia yao iliyopotoka, kwanza wanapaswa kujua tabia yao iliyopotoka. Ikiwa mwanadamu anafanya kazi ili kuondoa taswira za Miungu wasio dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu wasio dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kuwekwa hadharani, kutupwa, au kufukuzwa kabisa kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu ndiyo inayoweza kuchukua nafasi ya vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza ili kuwaruhusu watu kuvielewa taratibu, na ni kwa njia hii pekee ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. Mwanadamu anatambua kwamba Mungu aliyekuwa anamtafuta huko nyuma ni asiye dhahiri na wa kimiujiza. Kile ambacho kinaweza kufanikisha matokeo haya sio uongozi wa moja kwa moja wa Roho, sembuse mafundisho ya mtu fulani, bali ni Mungu mwenye mwili. Dhana za mwanadamu zinakuwa wazi pale ambapo Mungu mwenye mwili atafanya kazi Yake rasmi, kwa sababu ukawaida na uhalisi wa Mungu mwenye mwili ni kinyume na nadharia za Mungu asiye dhahiri na wa kufikirika katika fikra za mwanadamu. Dhana asili za mwanadamu zinaweza tu kudhihirishwa kupitia tofauti zao na Mungu mwenye mwili. Bila ulinganisho na Mungu mwenye mwili, dhana za mwanadamu zisingefichuliwa; kwa maneno mengine, bila tofauti ya uhalisi vitu visivyo dhahiri visingefichuliwa. Hakuna anayeweza kutumia maneno ili kufanya kazi hii, na hakuna anayeweza kuizungumzia kazi hii kwa kutumia maneno. Ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni pevu kiasi gani, hawezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kumjua Mungu zaidi kwa utendaji, na anaweza tu kumwona kwa uwazi zaidi, ikiwa Mungu binafsi anafanya kazi miongoni mwanadamu na anaonyesha kikamilifu sura Yake na uungu Wake. Athari hii haiwezi kupatwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili. Bila shaka, Roho wa Mungu pia hawezi kupata matokeo haya. Mungu anaweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika ushawishi wa Shetani, lakini kazi hii haiwezi kukamilishwa moja kwa moja na Roho wa Mungu; badala yake, inaweza kufanywa tu na mwili ambao Roho wa Mungu anauvaa, na mwili wa Mungu mwenye mwili. Mwili huu ni mwanadamu na pia ni Mungu, ni mwanadamu aliye katika ubinadamu wa kawaida na pia ni Mungu ambaye ana uungu wote. Na hivyo, hata kama mwili huu sio Roho wa Mungu, na unatofautiana kwa kiasi kikubwa na Roho, bado ni Mungu mwenye mwili Mwenyewe ambaye Anamwokoa mwanadamu, ambaye ni Roho, pia ni mwili. Haijalishi Anaitwa majina gani, hatimaye bado ni Mungu Mwenyewe anayemwokoa mwanadamu. Maana Roho wa Mungu hatenganishwi na mwili, na kazi ya mwili pia ni kazi ya Roho wa Mungu; ni kwamba tu kazi hii haifanywi kwa kutumia utambulisho wa Roho, lakini inafanywa kwa kutumia utambulisho wa mwili. Kazi inayotakiwa kufanywa moja kwa moja na Roho haihitaji kufanyika mwili, na kazi ambayo inahitaji mwili kuifanya haiwezi kufanywa moja kwa moja na Roho, na inaweza kufanywa tu na Mungu mwenye mwili. Hiki ndicho kinachohitajika kwa kazi hii, na ndicho kinachohitajika na mwanadamu aliyepotoka. Katika hatua tatu za kazi ya Mungu, ni hatua moja tu ndiyo iliyofanywa moja kwa moja na Roho, na hatua mbili zilizobaki zimechukuliwa na Mungu mwenye mwili, na hazifanywi moja kwa moja na Roho. Kazi ya Enzi ya Sheria iliyofanywa na Roho haikuhusisha kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu, na wala haikuwa na uhusiano wowote na maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu. Hata hivyo kazi ya Mungu mwenye mwili katika Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme, inahusisha tabia ya dhambi ya mwanadamu na maarifa yake juu ya Mungu, na ni sehemu ya maana na muhimu ya kazi ya wokovu. Kwa hiyo, mwanadamu aliyepotoka anahitaji zaidi wokovu wa Mungu mwenye mwili, na anahitaji zaidi kazi ya moja kwa moja ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anamhitaji Mungu mwenye mwili ili kumchunga, kumsaidia, kumnywesha maji, kumlisha, kumhukumu na kumwadibu, na anahitaji neema zaidi na wokovu mkubwa kutoka kwa Mungu mwenye mwili. Ni Mungu katika mwili pekee ndiye anayeweza kuwa msiri wa mwanadamu, mchungaji wa mwanadamu, msaada wa mwanadamu uliopo kila mara, na hii yote ni ulazima wa kufanyika mwili leo na katika nyakati za nyuma.
Mwanadamu amepotoshwa na Shetani, na yeye ndiye kiumbe wa juu kabisa kuliko viumbe wote wa Mungu, hivyo mwanadamu anahitaji wokovu wa Mungu. Mlengwa wa wokovu wa Mungu ni mwanadamu, si Shetani, na kile kitakachookolewa ni mwili wa mwanadamu, na roho ya mwanadamu, na si mwovu. Shetani ni mlengwa wa uharibifu wa Mungu, mwanadamu ni mlengwa wa wokovu wa Mungu, na mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, kwa hivyo kitu cha kwanza kuokolewa ni mwili wa mwanadamu. Mwili wa mwanadamu umepotoshwa kwa kiasi kikubwa, na umekuwa kitu cha kumpinga Mungu, ambacho kinapinga na kukana waziwazi uwepo wa Mungu. Mwili huu uliopotoka ni vigumu sana kushughulika nao, na hakuna kitu ambacho ni kigumu sana kushughulika nacho au kukibadilisha kuliko tabia potovu ya mwili. Shetani anaingia katika mwili wa mwanadamu ili kuchochea usumbufu, na anatumia mwili wa mwanadamu kuisumbua kazi ya Mungu, na kuharibu mpango wa Mungu, na hivyo mwanadamu amekuwa Shetani, na adui wa Mungu. Ili mwanadamu aweze kuokolewa, kwanza ni lazima achukuliwe mateka. Ni kwa sababu hii ndiyo maana Mungu anainuka na kuingia katika vita na Anaingia katika mwili ili afanye kazi ambayo Amekusudia kufanya, na kupambana na Shetani. Lengo Lake ni wokovu wa mwanadamu, mwanadamu ambaye amepotoshwa, na kushindwa na kuangamizwa kwa Shetani, ambaye ameasi dhidi Yake. Anamshinda Shetani kupitia kazi Yake ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo anamwokoa mwanadamu aliyepotoka. Hivyo, Mungu anatatua matatizo mawili kwa wakati mmoja. Anafanya kazi katika mwili, na Anazungumza katika mwili, na Anafanya kazi zote katika mwili ili aweze kujihusisha vizuri na mwanadamu, na kumdhibiti mwanadamu vizuri. Wakati wa mwisho ambapo Mungu atakuwa mwili, kazi Yake katika siku za mwisho itahitimishwa katika mwili. Atawaainisha wanadamu wote kulingana na aina, na kuhitimisha usimamizi wake wote, na pia kuhitimisha kazi Yake yote katika mwili. Baada ya kazi Yake yote duniani kuisha, Atakuwa mshindi kikamilifu. Kufanya kazi katika mwili, Mungu atakuwa amemshinda mwanadamu kikamilifu na atakuwa amempata mwanadamu kikamilifu. Hii haimaanishi kuwa usimamizi Wake wote utakuwa umekoma? Mungu anapohitimisha kazi Yake katika mwili, ilivyo kwamba Amemshinda Shetani kikamilifu, na Amekuwa mshindi, Shetani hatakuwa na fursa zaidi ya kumpotosha mwanadamu. Kazi ya Mungu mwenye mwili wa kwanza ilikuwa ni wokovu na msamaha wa dhambi za mwanadamu. Sasa ni kazi ya kumshinda na kumpata mwanadamu, ili kwamba Shetani asiweze tena kufanya kazi yake, na atakuwa amepotea kabisa, na Mungu atakuwa ameshinda kabisa. Hii ni kazi ya mwili, na ni kazi inayofanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya awali ya hatua tatu za kazi ya Mungu ilifanywa moja kwa moja na Roho, na wala si mwili. Hata hivyo, kazi ya mwisho ya hatua tatu za kazi ya Mungu, inafanywa na Mungu mwenye mwili, na wala haifanywi moja kwa moja na Roho. Kazi ya ukombozi ya hatua ya katikati pia imefanywa na Mungu mwenye mwili. Katika kazi yote ya usimamizi, kazi muhimu sana ni wokovu kutoka katika ushawishi wa Shetani. Kazi muhimu ni kumshinda kabisa mwanadamu aliyepotoka, na hivyo kurejesha heshima ya awali ya Mungu katika moyo wa mwanadamu, na kumruhusu kufikia maisha ya kawaida, ni sawa na kusema, maisha ya kawaida ya kiumbe wa Mungu. Kazi hii ni muhimu, na ni kiini cha kazi ya usimamizi. Katika hatua tatu za kazi ya wokovu, hatua ya kwanza ya kazi ya Enzi ya Sheria inatofautiana sana na kiini cha kazi ya usimamizi; ilikuwa tu ina kuonekana kwa mbali kwa kazi ya wokovu, na haikuwa mwanzo wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Hatua ya kwanza ya kazi ilifanywa na Roho kwa sababu, chini ya sheria, mwanadamu alijua tu kuzishika sheria, na hakuwa na ukweli zaidi, na kwa sababu kazi katika Enzi ya Sheria haikujihusisha na kubadilisha tabia ya mwanadamu, sembuse haikuwa inajihusisha na kazi ya jinsi ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Roho wa Mungu alikamilisha hatua hii rahisi ya kazi ambayo haikujihusisha na tabia iliyopotoka ya mwanadamu. Hatua hii ya kazi ilikuwa na uhusiano mdogo na kiini cha usimamizi na haikuwa na uhusiano mkubwa na kazi rasmi ya wokovu wa mwanadamu, na kwa hivyo haikumhitaji Mungu ili aweze kuifanya kazi Yake. Kazi inayofanywa na Roho ni mdokezo na haifahamiki, na ya kuogopesha na isiyofikiwa kwa mwanadamu; Roho hafai kikamilifu kwa ajili ya kufanya kazi ya wokovu moja kwa moja, na hafai kikamilifu kwa ajili ya kumpa mwanadamu uzima moja kwa moja. Kinachomfaa zaidi mwanadamu ni kubadilisha kazi ya Roho na kuwa katika hali ambayo inamkaribia mwanadamu, yaani, kile kinachomfaa mwanadamu zaidi ni Mungu kuwa mtu wa kawaida ili kufanya kazi Yake. Hili linahitaji Mungu apate mwili ili kuchukua kazi ya Roho, na kwa mwanadamu, hakuna njia inayofaa zaidi ya Mungu kufanya kazi. Kati ya hatua hizi tatu za kazi, hatua mbili zinafanywa na mwili, na hatua hizi mbili ni awamu muhimu ya kazi ya usimamizi. Kupata mwili huku kuwili kunakamilishana na kuafikiana. Hatua ya kwanza ya Mungu mwenye mwili iliweka msingi kwa ajili ya hatua ya pili, na tunaweza kusema kwamba kupata mwili huku kuwili kwa Mungu kunafanya hatua moja, na zote hazina ulinganifu. Hatua mbili hizi za kazi ya Mungu zinafanywa na Mungu katika utambulisho Wake katika mwili kwa sababu zina umuhimu sana katika kazi nzima ya usimamizi. Inaweza kusemwa kuwa, bila kazi ya Mungu mwenye mwili katika hatua mbili hizi, kazi nzima ya usimamizi ingefikia kikomo kwa ghafla, na kazi ya kumwokoa mwanadamu isingekuwa kitu isipokuwa maneno matupu. Haijalishi kazi hii ni muhimu au si muhimu lakini imejikita katika mahitaji ya mwanadamu, na uhalisi wa upotovu wa mwanadamu, na uzito wa kutotii kwa Shetani na usumbufu wake katika kazi. Mhusika sahihi anayeifanya kazi ametabiriwa na asili ya kazi yake, na umuhimu wa kazi. Unapokuja umuhimu wa kazi hii, kwa misingi ya mbinu ya kutumia—kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, au kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili, au kazi inayofanywa kupitia mwanadamu—ya kwanza kuondolewa ni kazi inayofanywa kupitia mwanadamu, na kulingana na asili ya kazi, na asili ya kazi ya Roho dhidi ya ile ya mwili, hatimaye inaamuliwa kwamba kazi inayofanywa na mwili ni ya manufaa zaidi kwa mwanadamu kuliko kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na inakuwa na manufaa zaidi. Hili ni wazo la Mungu wakati wa kuamua ama kazi ifanywe na Roho au ifanywe na mwili. Kuna umuhimu na msingi katika kila hatua ya kazi. Siyo fikra tu zisizo na msingi, na wala hazifanywi kiholela; kuna hekima fulani ndani yake. Huo ndio ukweli wa kazi zote za Mungu. Hasa, kuna mpango wa Mungu zaidi katika kazi kubwa kama hiyo kwa kuwa Mungu mwenye mwili akifanya kazi miongoni mwa wanadamu. Na kwa hivyo, hekima ya Mungu na uungu Wake wote unaakisiwa katika kila tendo Lake, fikira, na wazo katika kufanya kazi; huu ndio uungu wa Mungu ambao uko imara na wenye mpangilio. Fikira hizi na mawazo pembuzi ni ngumu kwa mwanadamu kuwaza, na mambo magumu kwa mwanadamu kuamini, aidha, magumu kwa mwanadamu kuyafahamu. Kazi inayofanywa na mwanadamu ni kulingana na kanuni ya ujumla, ambayo, kwa mwanadamu, ni ya kuridhisha sana. Lakini ikilinganisha na kazi ya Mungu, kuna tofauti kubwa sana; ingawa matendo ya Mungu ni makuu na kazi ya Mungu ni ya kiwango cha juu sana, nyuma yake kuna mipango na mipangilio midogo ya uhakika ambayo haiwezi kufikirika kwa mwanadamu. Kila hatua ya kazi Yake sio kulingana na kanuni tu, lakini pia inajumuisha vitu vingi ambavyo haviwezi kusemwa kwa lugha ya kibinadamu, na haya ni mambo ambayo hayaonekani kwa mwanadamu. Bila kujali kama ni kazi ya Roho au kazi ya Mungu mwenye mwili, kila kazi inajumuisha mpango wa kazi Yake. Hafanyi kazi bila kuwa na msingi, na hafanyi kazi isiyokuwa na maana. Roho anapofanya kazi moja kwa moja, ni kwa malengo Yake, na Anapokuwa mwanadamu (ambayo ni sawa na kusema, Anapobadilisha ganda Lake la nje) kufanya kazi, ni zaidi hata na lengo Lake. Kwa sababu ipi nyingine Abadilishe utambulisho Wake vivi hivi tu? Kwa sababu ipi nyingine Abadilike awe mtu ambaye anachukuliwa kuwa ni duni na kuteswa?
Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo Atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo hakungekuwa kazi ya hukumu. Je, upotovu wa wanadamu wote si ni sawa? Je, kiini cha wanadamu wote hakifanani? Kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu kilichopotoka, kiini cha mwanadamu kilichopotoshwa na Shetani, na dhambi zote za mwanadamu. Mungu hahukumu makosa madogo madogo ya mwanadamu na yasiyokuwa na umuhimu. Kazi ya hukumu ni ya uwakilishi, na haifanywi mahususi kwa ajili ya mtu fulani. Badala yake, ni kazi ambayo kwayo kundi la watu wanahukumiwa ili kuiwakilisha hukumu ya wanadamu wote. Kwa Yeye mwenyewe kufanya kazi Yake katika kundi la watu, Mungu mwenye mwili anatumia kazi Yake ili kuwakilisha kazi ya wanadamu wote, ambayo inaenea taratibu. Kazi ya hukumu pia iko hivyo. Mungu hahukumu aina fulani ya mtu au kundi fulani la watu, bali anawahukumu wasio na haki wote miongoni mwa wanadamu—upinzani wa mwanadamu kwa Mungu, kwa mfano, au mwanadamu kutomcha Yeye, au kusababisha usumbufu katika kazi ya Mungu, na kadhalika. Kile kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu cha kumpinga Mungu, na kazi hii ni kazi ya ushindi ya siku za mwisho. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili lililoshuhudiwa na mwanadamu ni kazi ya hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi wakati wa siku za mwisho, ambacho kilibuniwa na mwanadamu katika kipindi cha siku za nyuma. Kazi ambayo sasa inafanywa na Mungu mwenye mwili ni hukumu yenyewe mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu mwenye mwili wa leo ni Yule Mungu anayewahukumu wanadamu wote wakati wa siku za mwisho. Mwili huu na kazi, neno, na tabia Yake yote, vyote ni ujumla Wake. Ingawa mawanda ya kazi Yake ni finyu, na hayahusishi moja kwa moja ulimwengu wote, kiini cha kazi ya hukumu ni hukumu ya moja kwa moja kwa wanadamu wote; si kazi inayofanywa kwa ajili ya Uchina tu, au kwa idadi ndogo ya watu. Wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, ingawa mawanda ya kazi hii hayahusishi ulimwengu mzima, inawakilisha kazi ya ulimwengu mzima na, baada ya kuhitimisha kazi ndani ya mawanda ya mwili Wake, Ataipanua kazi hii mara moja katika ulimwengu mzima, kwa namna ile ile, injili ya Yesu ilienea ulimwengu mzima baada ya kufufuka Kwake na kupaa mbinguni. Bila kujali endapo ni kazi ya Roho au ni kazi ya mwili, ni kazi ambayo inafanywa ndani ya mawanda finyu, lakini ambayo inauwakilisha ulimwengu mzima. Wakati wa siku za mwisho, Mungu anaonekana kufanya kazi Yake kwa kutumia utambulisho Wake wa Mungu mwenye mwili, na Mungu mwenye mwili ni Mungu anayemhukumu mwanadamu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Bila kujali endapo ni Roho au mwili, Yule ambaye anafanya kazi ya hukumu ni Mungu anayemhukumu mwanadamu katika siku za mwisho. Hii inafasiliwa kwa kutegemeza kwa kazi Yake, na haifasiliwi kulingana na umbo Lake la nje au sababu nyinginezo. Ingawa mwanadamu ana dhana za maneno haya, hakuna anayeweza kukana ukweli wa hukumu ya Mungu mwenye mwili na kuwashinda wanadamu wote. Bila kujali ni jinsi gani binadamu anafikiri kuuhusu, ukweli ni, baada ya yote, ukweli tu. Hukuna anayeweza kusema “Kazi imefanywa na Mungu lakini mwili si Mungu.” Huu ni upuuzi, maana kazi hii haiwezi kufanywa na mtu yeyote isipokuwa Mungu mwenye mwili. Kwa kuwa kazi hii imekwishakamilika, kufuatia kazi hii, kazi ya hukumu ya Mungu kwa mwanadamu haitatokea kwa mara ya pili; Mungu mwenye mwili amekwishaikamilisha kazi yote ya usimamizi, na hakutakuwa na hatua ya nne ya kazi ya Mungu. Kwa sababu yule anayehukumiwa ni mwanadamu, mwanadamu ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa, na sio roho ya Shetani ambayo inahukumiwa moja kwa moja, kazi ya hukumu haifanywi katika ulimwengu wa roho, bali miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayefaa zaidi na anayestahili, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. Ikiwa hukumu ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, basi isingekuwa inajumuisha wote. Aidha, kazi kama hiyo itakuwa vigumu kwa mwanadamu kuikubali, maana Roho hawezi kukutana uso kwa uso na mwanadamu, na kwa sababu hii, matokeo hayawezi kuwa ya haraka, sembuse mwanadamu hataweza kuona kwa uwazi kabisa tabia ya Mungu isiyokosewa. Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali Yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye anayestahili, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana Ana ukweli, na mwenye haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine. Ikiwa kazi hii ingefanywa na Roho wa Mungu, basi usingekuwa ushindi dhidi ya Shetani. Roho kiasili huwa ameinuliwa sana kuliko viumbe wenye mwili wa kufa, na Roho wa Mungu ni mtakatifu kwa asili, na anaushinda mwili. Ikiwa Roho angefanya kazi hii moja kwa moja, Asingeweza kuhukumu kutotii kote kwa mwanadamu, na asingeweza kufichua hali nzima ya mwanadamu ya kutokuwa na haki. Kwa maana kazi ya hukumu pia inafanywa kwa mitazamo ya mwanadamu juu ya Mungu, na mwanadamu hajawahi kuwa na dhana yoyote juu ya Roho, na hivyo Roho hana uwezo wa kufunua hali ya mwanadamu ya kutokuwa na haki, wala kuweza kuweka wazi kabisa hali hiyo ya kutokuwa na haki. Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana za mwanadamu na kumpinga, Anafunua hali yote ya kutotii ya mwanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtii, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika mitazamo na kuwa na maarifa, na kutoka kukataliwa hadi upendo. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anaokolewa tu kwa kukubali hukumu Yake, bali hatua kwa hatua tu atamwelewa taratibu kupitia neno la mdomo Wake, ametwaliwa na Yeye wakati wa upinzani wake Kwake, na anapata uzima kutoka Kwake wakati wa kukubali kuadibu Kwake. Hii yote ni kazi ya Mungu mwenye mwili, na sio kazi ya Mungu katika utambulisho Wake kama Roho. Kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili ni kazi kubwa sana, na ni kazi ya kina sana, na sehemu muhimu ya hatua tatu za kazi ya Mungu ni hatua mbili za kazi ya kupata mwili. Upotovu wa kina wa mwanadamu ni kikwazo kikubwa sana katika kazi ya Mungu mwenye mwili. Hasa, kazi inayofanywa kwa watu wa siku za mwisho ni ngumu sana, na mazingira ni ya uhasama, na ubora wa tabia ya kila aina ya mwanadamu ni duni sana. Lakini mwishoni mwa kazi hii, bado itapokea matokeo mazuri, bila dosari yoyote; haya ni matokeo ya kazi ya mwili, na matokeo haya yanashawishi sana kuliko kazi ile ya Roho. Hatua tatu za kazi ya Mungu zitahitimishwa katika mwili, na lazima zikamilishwe na Mungu mwenye mwili. Kazi muhimu sana imefanywa katika mwili, na wokovu wa mwanadamu ni lazima ufanywe na Mungu mwenye mwili. Ingawa binadamu wote wanahisi kwamba Mungu katika mwili hahusiani na mwanadamu, kwa kweli ni kuwa mwili huu unahusiana na majaliwa na uwepo wa wanadamu wote.
Kila hatua ya kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote, na inawalenga wanadamu wote. Ingawa ni kazi Yake katika mwili, bado inaelekezwa kwa binadamu wote; Yeye ni Mungu wa binadamu wote, na ni Mungu wa viumbe vyote vilivyoumbwa na ambavyo havijaumbwa. Ingawa kazi Yake katika mwili ipo ndani ya mawanda finyu, na kusudi la kazi hii pia lina mipaka, kila wakati Anapokuwa mwili kufanya kazi Yake, Yeye huchagua chombo cha kazi Yake ambacho ni wakilishi na ambacho kina uakilishi mkubwa; Hachagui kikundi cha watu wa kawaida na wasiosifika kwa ajili ya kuwafanyiza kazi, lakini badala yake huwachagua kama wawakilishi wa kazi Yake kundi la watu wenye uwezo kuwa wahusika wa kazi Yake katika mwili. Kundi hili la watu linachaguliwa kwa sababu ya mawanda ya kazi Yake katika mwili ni finyu, na wamejiandaa mahususi kwa ajili ya Kufanyika Kwake kuwa mwili, na limechaguliwa hasa kwa ajili ya kazi Yake katika mwili. Uchaguzi wa Mungu wa walengwa wa kazi Yake si usio na msingi, bali kulingana na kanuni: Mlengwa wa kazi anapaswa kuwa na manufaa katika kazi ya Mungu mwenye mwili, na anapaswa kuwa na uwezo wa kuwawakilisha wanadamu wote. Kwa mfano, Wayahudi waliweza kuwawakilisha binadamu wote katika kupokea wokovu binafsi wa Yesu, na Wachina wanaweza kuwawakilisha wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu mwenye mwili. Kuna msingi kwa Wayahudi kuwa wawakilishi wa binadamu wote, na kuna msingi kwa uwakilishi wa Wachina wa wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu. Hakuna kinachofichua maana ya ukombozi kuliko kazi ya ukombozi iliyofanywa miongoni mwa Wayahudi, na hakuna kinachofichua uhakika na mafanikio ya kazi ya ushindi kuliko kazi ya ushindi iliyofanywa miongoni mwa Wachina. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili vinaonekana kuelekezwa kwa kikundi kidogo tu cha watu, lakini kwa hakika, kazi Yake miongoni mwa kikundi hiki kidogo ni kazi ya ulimwengu wote, na neno Lake limeelekezwa kwa wanadamu wote. Baada ya kazi Yake katika mwili kufikia kikomo, wale wanaomfuata wataanza kueneza kazi ambayo Amefanya miongoni mwao. Kitu kizuri zaidi kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ya kusihi, na mapenzi Yake kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi Wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwepo na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambapo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya utendaji zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, Anamfunulia mwanadamu Mungu ambaye ni halisi na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonyesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, Anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, Anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na Anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili badala ya Roho wa Mungu. Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili Wake, wale wanaofuata wanakuwa hawatafuti tena vitu hivyo visivyo yakini, na wanaacha kukisia mapenzi ya Mungu asiye yakini. Mungu anapoeneza kazi Yake katika mwili, wale wanaomfuata wataieneza kazi ambayo Ameifanya katika mwili kwa dini na madhehebu yote, na watazungumza maneno Yake yote katika masikio ya wanadamu wote. Yote yale yanayosikizwa na wale wanaoipokea injili Yake yatakuwa ni ukweli wa kazi Yake, yatakuwa mambo ambayo mwanadamu ameyashuhudia na kuyaona binafsi, na utakuwa ukweli na sio uvumi. Ukweli huu ni ushahidi ambao Anauenezea kazi na pia ni zana ambazo Anazitumia katika kueneza kazi. Bila uwepo wa ukweli, injili Yake isingeweza kuenea katika nchi zote na maeneo yote; bila ukweli bali kwa fikira tu za mwanadamu, Asingeweza kufanya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Roho hagusiki na mwanadamu, na wala haonekani kuonekana na mwanadamu, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Mawazo ya mwanadamu, hata hivyo, ni matupu, na hayawezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; tabia ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekana na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye binafsi Anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia halisi ambayo Mungu anaonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwona Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili. Baada ya Mungu kufanya kazi Yake hadi hatua hii, kazi Yake tayari imeshafanikiwa kuwa na matokeo mazuri, na imekuwa ni mafanikio kamili. Kazi binafsi ya Mungu mwenye mwili tayari imekwishakamilisha asilimia tisini ya kazi ya usimamizi Wake mzima. Mwili umetoa mwanzo mzuri katika kazi Yake yote, na muhtasari kwa ajili ya kazi Yake yote, na umetangaza kazi Yake yote na Ameifanya ya mwisho kupitia ujazaji tena wa kazi hii yote. Kuanzia sasa, hakutakuwepo na Mungu mwingine katika mwili kwa ajili ya kufanya hatua ya nne ya kazi ya Mungu, na hakutakuwa na kazi ya miujiza zaidi ya kupata mwili kwa tatu kwa Mungu.
Kila hatua ya kazi ya Mungu katika mwili inawakilisha kazi Yake ya enzi yote, na haiwakilishi kipindi fulani kama kazi ya mwanadamu. Na hivyo mwisho wa kazi ya kufanyika Kwake mwili mara ya mwisho haimaanishi kwamba kazi Yake imefikia mwisho kabisa, kwa maana kazi Yake katika mwili inawakilisha enzi yote, na haiwakilishi kipindi tu ambacho Anafanya kazi Yake katika mwili tu. Ni kwamba tu Anakamilisha kazi Yake ya enzi yote wakati ambapo yupo katika mwili, ambayo baadaye inaenea sehemu zote. Baada ya Mungu mwenye mwili kutimiza huduma yake, atawakabidhi wale wote wanaoifuata kazi Yake ya baadaye. Kwa njia hii kazi Yake ya enzi yote itaendelezwa bila kusitishwa. Kazi ya enzi yote ya kufanyika kuwa mwili itachukuliwa tu kuwa imekamilika baada ya kuenea ulimwenguni kote. Kazi ya Mungu mwenye mwili huanzisha enzi mpya, na wale wanaoiendeleza kazi Yake ni watu wanaotumiwa naye. Kazi inayofanywa na mwanadamu yote ipo ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili, na haina uwezo wa kwenda zaidi ya mawanda haya. Ikiwa Mungu mwenye mwili haji kufanya kazi Yake, mwanadamu hana uwezo wa kuhitimisha enzi ya zamani, na hana uwezo wa kuikaribisha enzi mpya. Kazi inayofanywa na mwanadamu ipo tu ndani ya wajibu wake ambao unawezekana kibinadamu, na haiwakilishi kazi ya Mungu. Ni Mungu mwenye mwili pekee ndiye anayeweza kuja na kukamilisha kazi ambayo Anapaswa kuifanya, na mbali na Yeye, hakuna anayeweza kuifanya kazi hii badala Yake. Bila shaka, kile Ninachozungumzia ni kuhusiana na kazi ya kufanyika mwili. Huyu Mungu mwenye mwili, kwanza anachukua hatua ya kazi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu, baada ya hapo Anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu. Lengo la kazi hii ni kumshinda mwanadamu. Kwa upande mmoja, kupata mwili kwa Mungu hakupatani na dhana za mwanadamu, aidha, Anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na dhana za mwanadamu, na kwa hivyo mwanadamu anakuza mawazo zaidi ya kukosoa kumhusu. Anafanya kazi ya ushindi miongoni mwa wanadamu ambaye ana dhana nyingi sana kumhusu. Bila kujali jinsi wanavyomchukulia, Atakapokuwa amekamilisha huduma Yake, wanadamu wote watakuwa chini ya utawala Wake. Ukweli wa kazi hii hauonekani tu miongoni mwa Wachina, bali wao wanawakilisha namna ambavyo wanadamu wote watakavyoshindwa. Matokeo yanayoonekana kwa watu hawa ni kitangulizi cha matokeo yatakayoonekana kwa wanadamu wote, na matokeo ya kazi Anayofanya wakati ujao yatazidi sana matokeo kwa watu hawa. Kazi ya Mungu katika mwili haihusishi mshindo mkubwa wa tarumbeta, wala haijakita katika mafumbo. Ni halisi na ya kweli, na ni kazi ambayo moja kujumlisha na moja ni sawa sawa na mbili. Hajafichwa kwa mtu yeyote, na wala haimdanganyi mtu yeyote. Kile ambacho watu wanaona ni vitu halisi, na kile ambacho mwanadamu anapata ni ukweli halisi na maarifa. Kazi itakapokamilika, mwanadamu atakuwa na maarifa mapya juu Yake, na wale ambao kweli wanamtafuta Mungu hawatakuwa na dhana zozote juu Yake. Haya siyo tu matokeo ya kazi Yake kwa Wachina, lakini pia inawakilisha matokeo ya kazi Yake katika kuwashinda wanadamu wote, kwa maana hakuna kitu ambacho ni cha manufaa zaidi katika kazi ya kuwashinda watu kuliko mwili huu, na kazi ya mwili huu, na kila kitu cha mwili huu. Vina manufaa katika kazi Yake leo, na vina manufaa katika kazi Yake hapo baadaye. Mwili huu utawashinda wanadamu wote na utawapata wanadamu wote. Hakuna kazi bora zaidi ambayo kwayo wanadamu wote watamwona Mungu, na kumtii Mungu, na kumfahamu Mungu. Kazi inayofanywa na mwanadamu inawakilisha tu mawanda finyu, na Mungu anapofanya kazi Yake hazungumzi na watu fulani, bali Anazungumza na wanadamu wote, na wale wote wanaoikubali kazi Yake. Mwisho Anaoutangaza ni mwisho wa wanadamu wote, na sio mwisho wa mtu fulani tu. Hamtendei mtu yeyote kwa umahususi, wala hampendelei mtu yeyote, na Anafanya kazi kwa ajili ya, na Anazungumza na wanadamu wote. Na kwa hiyo Mungu huyu katika mwili amekwisha waainisha wanadamu wote kulingana na aina yao, tayari amekwisha wauhukumu wanadamu wote, na amekwishapangilia hatima inayofaa kwa wanadamu wote. Ingawa Mungu anafanya kazi Yake China tu, kwa hakika Ameshaamua kazi ya ulimwengu mzima. Hawezi kusubiri hadi kazi Yake itakapoenea miongoni mwa wanadamu wote kabla ya kutoa matamko Yake na kuweka mipango hatua kwa hatua. Hivyo, sio kwamba utakuwa umechelewa sana? Sasa Anaweza kabisa kukamilisha kazi ya wakati ujao kabla ya wakati huo. Kwa sababu Yule anayefanya kazi ni Mungu mwenye mwili, Anafanya kazi isiyokuwa na mipaka ndani ya mawanda yenye mipaka, na baadaye Atamfanya mwanadamu atekeleze jukumu ambalo mwanadamu anapaswa kulitekeleza; hii ni kanuni ya kazi Yake. Anaweza kuishi tu na mwanadamu kwa muda, na hawezi kuambatana na mwanadamu hadi kazi ya enzi zote itakapokamilika. Ni kwa sababu Yeye ni Mungu kwamba Yeye hutabiri kazi Yake ya Wakati ujao kabla ya wakati. Baada ya hapo, Atawaainisha wanadamu wote kulingana na aina kwa maneno Yake, na mwanadamu ataingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua kulingana na neno Lake. Hakuna atakayekwepa, na wote wanapaswa kutenda kulingana na hili. Hivyo, katika wakati ujao, enzi itaongozwa na maneno Yake, na sio kuongozwa na Roho.
Kazi ya Mungu katika mwili ni lazima ifanywe katika mwili. Kama ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu isingeweza kutoa matokeo yoyote. Hata kama ingefanywa na Roho, kazi hii isingekuwa na maana kubwa, na hatimaye isingekuwa na ushawishi. Viumbe vyote vinatamani kujua iwapo kazi ya Muumbaji ina maana, na inawakilisha kitu gani, na ni kwa ajili ya nini, na iwapo kazi ya Mungu ina mamlaka kamili na hekima, na endapo ina thamani na maana ya kina. Kazi Anayofanya ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote, kwa ajili ya kumshinda Shetani, na kwa kuwa na ushuhuda wa Mungu miongoni mwa vitu vyote. Hivyo, kazi Anayoifanya ni lazima iwe ya umuhimu mkubwa. Mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, na wengi wamepofushwa, na kuumizwa sana. Sababu muhimu sana ambayo inamfanya Mungu kufanya kazi katika mwili ni kwa sababu mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, ambaye ni wa mwili, na kwa sababu Shetani pia anatumia mwili wa mwanadamu kusumbua kazi ya Mungu. Vita na Shetani kwa hakika ni kazi ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo mwanadamu pia ni mlengwa wa wokovu wa Mungu. Kwa njia hii, kazi ya Mungu mwenye mwili ni muhimu. Shetani aliupotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu akawa mfano halisi wa Shetani, na akawa mlengwa wa kushindwa na Mungu. Kwa njia hii, kazi ya kupambana na Shetani na kumwokoa mwanadamu inatokea duniani, na Mungu ni lazima awe mwanadamu ili aweze kupambana na mwanadamu. Hii ni kazi yenye utendaji wa hali ya juu. Mungu anapofanya kazi katika mwili, kwa hakika Anapambana na Shetani katika mwili. Anapofanya kazi katika mwili, Anafanya kazi Yake katika ulimwengu wa kiroho, na Anafanya kazi Yake yote katika ufalme wa kiroho ili iwe halisi duniani. Anayeshindaniwa ni mwanadamu, asiye mtiifu Kwake, yule anayeshindwa ni mfano halisi wa Shetani (bila shaka, huyu pia ni mwanadamu), ambaye ana uadui na Yeye, na ambaye ataokolewa hatimaye ni mwanadamu. Kwa namna hii, ni muhimu zaidi Kwake kuwa mwanadamu ambaye ana ganda la nje la kiumbe, ili kwamba Awe na uwezo wa kupambana na Shetani katika uhalisi, kumshinda mwanadamu, ambaye si mtiifu Kwake na ambaye ana kuonekana kwa nje ambako kunafanana na Yeye, na kumwokoa mwanadamu, ambaye ana umbo la nje kama Lake na aliyeumizwa na Shetani. Adui Wake ni mwanadamu, mlengwa wa ushindi Wake ni mwanadamu, na mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, aliyeumbwa na Yeye. Hivyo ni lazima Awe mwanadamu, na kwa njia hii, kazi Yake inakuwa rahisi zaidi. Ana uwezo wa kumshinda Shetani na kumshinda mwanadamu, aidha, anaweza kumwokoa mwanadamu. Ingawa mwili huu ni wa kawaida na halisi, Yeye si mwili wa kawaida. Yeye si mwili ambao ni mwanadamu tu, bali mwili ambao una uanadamu na uungu. Hii ndiyo tofauti Yake na mwanadamu, na ni alama ya utambulisho wa Mungu. Ni mwili tu kama huu ndio unaweza kufanya kazi Anayokusudia kufanya, na kutimiza huduma ya Mungu katika mwili, na kukamilisha kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Isingekuwa hivyo, kazi Yake miongoni mwa wanadamu ingekuwa tupu na yenye dosari. Ingawa Mungu anaweza kupambana na roho wa Shetani na kuibuka mshindi, asili ya zamani ya mwanadamu aliyepotoka haiwezi kuondolewa, na wale ambao sio watiifu Kwake na wanaompinga hawawezi kuwa wahusika katika utawala Wake, ambayo kusema, Hawezi kamwe kumshinda mwanadamu, na hawezi kamwe kuwapata wanadamu wote. Kama kazi Yake duniani haiwezi kutatuliwa, basi usimamizi Wake hautafika mwisho, na wanadamu wote hawataweza kuingia katika pumziko. Kama Mungu hawezi kuingia katika pumziko pamoja na viumbe Wake wote, basi hakutakuwa na matokeo ya usimamizi huo, na utukufu wa Mungu kwa sababu hiyo utatoweka. Ingawa mwili Wake hauna mamlaka, kazi Anayofanya itapokea matokeo yake. Huu ndio mwelekeo usioepukika wa kazi Yake. Haijalishi kama mwili Wake una mamlaka au la, maadamu Ana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, basi Yeye ni Mungu Mwenyewe. Haijalishi mwili huu ni wa kawaida kiasi gani, Anaweza kufanya kazi Anayopaswa kufanya, maana mwili huu ni Mungu na wala si mwanadamu tu. Sababu ambayo mwili huu unaweza kufanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya ni kwamba kiini Chake cha ndani si kama cha mwanadamu yeyote yule, na sababu kuwa Anaweza kumwokoa mwanadamu ni kuwa utambulisho Wake ni tofauti na wa mwanadamu yeyote yule. Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu ni mwanadamu hata zaidi ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyepotoka, ambaye anaishi pamoja na Yeye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuweza kumpata mwanadamu kabisa. Kwa sababu hii, ingawa mwili huu ni wa kawaida, mchango Wake kwa wanadamu na umuhimu Wake katika uwepo wa mwanadamu kunamfanya Awe wa thamani zaidi, na thamani halisi na umuhimu wa mwili huu hauwezi kupimwa na mwanadamu yeyote. Ingawa mwili huu hauwezi kumwangamiza Shetani moja kwa moja, Anaweza kutumia kazi Yake kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, na kumfanya Shetani kutii kikamilifu katika utawala Wake. Ni kwa sababu Mungu amepata mwili ili kwamba Aweze kumshinda Shetani na aweze kumwokoa binadamu. Hamwangamizi Shetani moja kwa moja, bali Anakuwa mwili ili kuweza kufanya kazi ya kumshinda binadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Kwa njia hii, Anakuwa na uwezo zaidi wa kuwa ushuhuda Kwake Mwenyewe miongoni mwa viumbe, na Anakuwa na uwezo zaidi wa kumwokoa mwanadamu aliyepotea. Ushindi wa Mungu mwenye mwili dhidi ya Shetani unabeba ushuhuda mkubwa, na una ushawishi mkubwa, kuliko uangamizaji wa Shetani wa moja kwa moja na Roho wa Mungu. Mungu katika mwili Ana uwezo zaidi wa kumsaidia mwanadamu kumjua Muumba, na Ana uwezo zaidi wa kuwa na ushuhuda Wake mwenyewe miongoni mwa viumbe.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Alhamisi, 18 Aprili 2019

Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?

Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno "Mungu" na mafungu ya maneno kama "kazi ya Mungu", hawamjui Mungu, na kwa kiwango cha chini zaidi hawaijui kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa makini kwa kuwa kuamini katika Mungu ni jambo geni, jambo lisolo la kawaida sana kwao. Kwa njia hii, hawafikii mahitaji ya Mungu. Kwa maneno mengine, ikiwa watu hawamjui Mungu, hawajui kazi Yake, basi hawafai kwa matumizi na Mungu, na zaidi ya hayo hawawezi kutimiza hamu ya Mungu. "Imani katika Mungu" inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu sio sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni hali ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtakuwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu. Ilhali watu mara nyingi huona kuamini katika Mungu kama jambo rahisi sana na la kipuuzi tu. Imani ya watu wa aina hii haina maana na haitawahi kupata idhini ya Mungu, kwa sababu wanatembea katika njia mbaya. Leo, kuna wale bado wanaamini katika Mungu katika barua, katika mafundisho ya dini yaliyo tupu. Hawana habari kuwa imani yao katika Mungu haina dutu, na hawawezi kupata idhini ya Mungu, na bado wanaomba kupata amani na neema ya kutosha kutoka kwa Mungu. Tunafaa kuweka kituo na kujiuliza wenyewe: Je, kuamini kwa Mungu linaweza kuwa jambo rahisi ya yote duniani? Je, kuamini kwa Mungu hakumaanishi chochote zaidi ya kupokea neema nyingi kutoka kwa Mungu? Je, watu wanaoamini kwa Mungu na hawamjui, na wanaamini kwa Mungu ila wanamuasi; je watu kama hawa wanaweza kutimiza haja za Mungu?
kutoka kwa "Dibaji" kwa Neno Laonekana katika Mwili
Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu. Ingawa ni uamuzi wa watu kama hawa kumfuata Mungu, hawafaidi chochote. Wale wasiopata chochote kwenye mkondo huu ndio watakaotupiliwa mbali, na ni wale watu wanaofanya juhudi za chini zaidi. Haijalishi ni hatua gani ya kazi ya Mungu unayopitia, lazima uandamane na maono makuu. Bila maono kama haya, itakuwa vigumu kwako kukubali kila hatua ya kazi mpya, kwa maana mwanadamu hana uwezo wa kuwaza kuhusu kazi mpya ya Mungu, ni kuu kushinda mawazo ya mwanadamu. Kwa hivyo bila mchungaji kumlinda mwanadamu, bila mchungaji kushirikiana na mwanadamu kuhusu maono hayo, mwanadamu hana uwezo kukubali kazi hii mpya. Iwapo mwanadamu hawezi kupokea maono haya, basi hawezi kupata kazi mpya ya Mungu, na iwapo mwanadamu hawezi kutii kazi mpya ya Mungu, basi mwanadamu hana uwezo wa kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na hivyo ufahamu wake wa Mungu ni bure. Kabla mwanadamu atimilize maneno ya Mungu, lazima ayajue maneno ya Mungu, hivyo ni kusema, aelewe mapenzi ya Mungu; ni kwa njia hii tu ndiyo maneno ya Mungu yanaweza kutekelezwa kwa usahihi na kulingana na moyo wa Mungu. Hili lazima liwe na kila mmoja anayetafuta ukweli, na ndiyo njia ambayo lazima kila mmoja anayejaribu kumjua Mungu aipitie. Njia ya kuyajua maneno ya Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na pia njia ya kuijua kazi ya Mungu. Na hivyo, kujua maono hakuashirii tu kuujua ubinadamu wa Mungu mwenye mwili, lakini pia kunajumuisha kujua maneno na kazi ya Mungu. Kutokana na maneno ya Mungu wanadamu wanapata kuelewa mapenzi ya Mungu, na kutokana na maneno ya Mungu wanapata kuelewa tabia ya Mungu na pia kujua kile Mungu alicho. Imani katika Mungu ndiyo hatua ya kwanza katika kumjua Mungu. Harakati ya kusonga kutoka katika imani ya mwanzo katika Mungu mpaka imani kuu kwa Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na harakati ya kuipitia kazi ya Mungu. Iwapo unaamini kwa Mungu kwa ajili tu ya kuamini kwa Mungu, na huamini kwa Mungu kwa ajili ya kumjua Mungu, basi hakuna ukweli katika imani yako, na haiwezi kuwa safi—kuhusu hili hakuna tashwishi. Iwapo, wakati wa harakati anapopata kumuonja Mungu, mwanadamu anapata kumjua Mungu polepole, basi hatua kwa hatua tabia yake itabadilika pia, na imani yake itaongezeka kuwa ya kweli zaidi. Kwa njia hii, wakati mwanadamu anafaulu katika imani yake kwa Mungu, ataweza kumpata Mungu kwa ukamilifu. Mungu alijitoa pakubwa kuingia katika mwili mara ya pili na kufanya kazi Yake binafsi ili mwanadamu apate kumjua Yeye, na ili mwanadamu aweze kumwona. Kumjua Mungu[a] ndiyo matokeo ya mwisho yanayofikiwa katika mwisho wa kazi ya Mungu; ndilo hitaji la mwisho la Mungu kwa mwanadamu. Anafanya hili kwa ajili ya ushuhuda Wake wa mwisho, na ili kwamba mwanadamu mwishowe na kwa kikamilifu aweze kumgeukia Yeye. Mwanadamu anaweza tu kumpenda Mungu kwa kumjua Mungu, na ili ampende Mungu lazima amjue Mungu. Haijalishi vile anavyotafuta, au kile anachotafuta kupata, lazima aweze kupata ufahamu wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumridhisha Mungu. Ni kwa kumjua Mungu tu ndio mwanadamu anaweza kumwamini Mungu kwa ukweli, na ni kwa kumjua Mungu tu ndio anaweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Wale wasiomjua Mungu hawataweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Kumjua Mungu kunahusisha kujua tabia ya Mungu, kuelewa mapenzi ya Mungu, na kujua kile Mungu alicho. Na haijalishi ni kipengee gani cha kumjua Mungu, kila mojawapo kinamhitaji mwanadamu alipe gharama, na kinahitaji nia ya kutii, ambapo bila hivi hakuna atakayeweza kufuata mpaka mwisho. Kazi ya Mungu hailingani na mawazo ya mwanadamu hata kidogo, tabia ya Mungu na kile Mungu alicho ni vitu vigumu sana kwa mwanadamu kufahamu, na yote Anayosema na kufanya Mungu ni makuu sana yasiyoeleweka na mwanadamu; iwapo mwanadamu anatamani kumfuata Mungu, na hana nia ya kumtii Mungu, basi mwanadamu hatafaidi chochote. Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa, Mungu Amefanya kazi nyingi ambayo haieleweki na mwanadamu na ambayo mwanadamu amepata ugumu kuikubali, na Mungu amesema mengi yanayofanya mawazo ya mwanadamu magumu kupona. Ilhali Hajawahi kukomesha kazi Yake kwa sababu mwanadamu ana ugumu mwingi; Ameendelea kufanya kazi na kuzungumza, na hata ingawa idadi kubwa ya "wanajeshi" wameangamia njiani, Yeye bado Anaendelea na kazi Yake, na bado anateua kundi baada ya kundi la watu walio tayari kukubali kazi Yake mpya. Yeye hawahurumii wale "mashujaa" walioangamia, na badala yake anawathamini wale wanaoikubali kazi Yake mpya na maneno. Lakini ni kwa sababu gani ndiyo Anafanya kazi kwa njia hii, hatua kwa hatua? Ni kwa nini Yeye kila mara huwaondoa na kuchagua watu wengine? Ni kwa nini Yeye hutumia mbinu za aina hii kila mara? Kusudi la kazi Yake ni ile wanadamu wapate kumjua, na ili waweze kutwaliwa na Yeye. Kanuni ya kazi Yake ni kufanya kazi kwa wale wanaoweza kutii kazi Anayofanya leo, na sio kufanya kazi kwa wale wanaotii kazi Yake ya zamani, na wanaipinga kazi Yake ya leo. Hii ndiyo sababu hasa Amewafuta na kuwaangamiza watu wengi.
kutoka kwa "Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni imani katika Mungu ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kutekeleza mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii Mungu. Unapomjua tu Mungu ndipo unapoweza kupenda Mungu, na kupatikana kwa lengo hili ndilo lengo la pekee mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.
kutoka kwa "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu unamsadiki Mungu, lazima ule na kunywa neno Lake, upitie neno Lake, na uishi kwa kudhihirisha neno Lake. Hivi tu ndivyo unavyomsadiki Mungu! Kama unasema umemsadiki Mungu ilhali huwezi kuongea maneno Yake yoyote au kuyatia katika matendo, huchukuliwi kuwa unamsadiki Mungu. Hivi ni "kuutafuta mkate ili kuikabili njaa." … Wanaomwamini Mungu wanafaa kumiliki tabia nzuri kwa nje, angalau, na kilicho na umuhimu mkubwa zaidi ni kuwa na neno la Mungu. Haijalishi ni nini, huwezi kuligeukia neno la Mungu. Maarifa yako katika Mungu na kukamilishwa kwa mapenzi Yake vyote vinatimizwa kupitia kwa neno Lake. Mataifa yote, imani, madhehebu, na sekta zote zitaweza kushindwa kupitia kwa neno kwenye siku za usoni. Mungu ataongea moja kwa moja, na watu wote watashikilia neno la Mungu katika mikono yao; kupitia haya watu watafanywa kuwa watimilifu. Neno la Mungu limeenea kotekote: Watu huongelea neno la Mungu na kutenda kulingana na neno la Mungu, huku likiwa limehifadhiwa ndani bado huwa ni neno la Mungu. Kwa ndani na hata kwa nje, wanarowekwa katika neno la Mungu, na hivyo basi wanafanywa kuwa watimilifu. Wale wanaokamilisha mapenzi ya Mungu na wanaweza kumshuhudia Yeye ndio wale walio na neno la Mungu kama uhalisi.
Kuingia katika Enzi ya Neno, yaani, Enzi ya Ufalme wa Milenia, ndiyo kazi ambayo inakamilishwa sasa. Kuanzia sasa, fanya mazoezi ya kushiriki kuhusu neno la Mungu. Ni kupitia tu kula na kunywa neno Lake na kulipitia ndipo unapoweza kuonyesha neno la Mungu. Ni kupitia tu maneno yako ya uzoefu ndipo wengine wanapoweza kushawishika na wewe. Kama huna neno la Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuongea neno la Mungu. Kama huwezi, hii yaonyesha kwamba Roho Mtakatifu bado hajakufanyia kazi na ungali bado hujafanywa kuwa mtimilifu. Huu ndio umuhimu wa neno la Mungu.
kutoka kwa "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mchakato ambamo watu huyapitia maneno ya Mungu ni sawa na mchakato ambamo wanafahamu kujitokeza kwa maneno ya Mungu katika mwili. Kadiri watu wanavyoyapitia maneno ya Mungu, ndivyo wanavyomjua Roho wa Mungu; kwa kuyapitia maneno ya Mungu, watu wanaelewa kanuni za kazi ya Roho na kupata kumjua Mungu wa vitendo Mwenyewe. Kwa hakika, Mungu akiwafanya watu wakamilifu na kuwachukua, Anawafanya wayajue matendo ya Mungu wa vitendo; Anatumia kazi ya Mungu wa vitendo kuwaonyesha watu umuhimu halisi wa kupata mwili, na kuwaonyesha kuwa Roho wa Mungu hakika ameonekana kwa mwanadamu. Watu wakichukuliwa na kufanywa wakamilifu na Mungu, maonyesho ya Mungu wa vitendo huwa amewashinda, maneno ya Mungu wa vitendo huwa yamewabadilisha, na kutoa uzima Wake ndani yao, kuwajaza na kile Alicho (iwe ni uwepo wake wa binadamu, au ule wa uungu), kuwajaza kwa kiini cha maneno Yake, na kuwafanya watu waishi kwa kudhihirisha maneno Yake. Mungu akiwapata watu, kimsingi Anafanya hivyo kwa kutumia maneno na matamko ya Mungu wa vitendo ili kuushughulikia upungufu wa watu, na kuhukumu na kufichua tabia zao za uasi, kuwafanya wapate wanachokihitaji, na kuwaonyesha kuwa Mungu yuko miongoni mwa wanadamu. Muhimu zaidi, kazi ifanywayo na Mungu wa vitendo ni kumwokoa kila mtu kutoka katika ushawishi wa Shetani, kuwatoa katika nchi ya uchafu, na kuziondoa tabia zao potovu. Umuhimu mkubwa zaidi wa watu kupatikana na Mungu wa vitendo ni kuwa na uwezo wa kumfanya Mungu wa vitendo kielelezo, na kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, kuweza kutenda kulingana na maneno na mahitaji ya Mungu wa vitendo, bila upotofu au kuteleza, kutenda kama Asemavyo, na kuweza kufanikisha lolote Atakalo. Kwa njia hii, utakuwa umepatwa na Mungu.
kutoka kwa "Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kadiri ufahamu wako wa maneno ya Mungu ulivyo mkuu na kadiri unavyoyatia kwenye matendo, ndivyo unavyoweza kuingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu na Mungu haraka. Kupitia kuomba, unaweza kufanywa mtimilifu katikati ya maombi; kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno ya Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, unaweza kufanywa kuwa mtimilifu. Kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu kila siku, unapata kujua kile unachokosa ndani yako, na, zaidi ya hayo, unapata kujua udhaifu wako na upungufu, na unatoa sala kwa Mungu, ambayo kwayo utafanywa mtimilifu polepole. Njia za kufanywa mtimilifu: kuomba, kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno ya Mungu, kuingia katika uzoefu wa maneno ya Mungu, kuja kujua kinachokosa ndani yako, kuitii kazi ya Mungu, kuzingatia mzigo wa Mungu na kuunyima mwili kwa kupitia moyo wako wa upendo, na kuwa na ushirika wa mara kwa mara na ndugu, ambayo yanaboresha uzoefu wako. Iwe ni maisha ya jumuiya au maisha yako binafsi, na iwe ni makusanyiko makubwa au madogo, yote yanaweza kukuwezesha kupata uzoefu na kupata mafunzo ili moyo wako uwe na utulivu mbele ya Mungu na kurudi kwa Mungu. Haya yote ni mchakato wa kufanywa mtimilifu. Kuyapitia maneno ya Mungu ambayo yamesemwa kunamaanisha kuwa na uwezo wa kwa kweli kuyaonja maneno ya Mungu na kuyaruhusu yaweze kuishi kwa kudhihirishwa ndani yako ili uwe na imani kubwa na upendo kwa Mungu. Kupitia njia hii, utaondoa tabia potovu ya kishetani polepole, utaachana na motisha isiyofaa polepole, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kawaida. Kadiri upendo kwa Mungu ndani yako unavyozidi kuwa mkuu—yaani, kadiri unavyozidi kufanywa mtimilifu na Mungu mara nyingi—ndivyo unayopotoshwa na Shetani kwa kiasi kidogo. Kupitia uzoefu wako wa vitendo, utaingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu polepole. Hivyo, ikiwa unataka kufanywa mtimilifu, kuzingatia mapenzi ya Mungu na kuyapitia maneno ya Mungu hasa ni muhimu sana.
kutoka kwa "Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Baada ya hapo ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa.
kutoka kwa "Je, Umekuwa Hai Tena?" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu huwakamilisha watu kupitia utii wao, kupitia kula kwao, kunywa na kufurahia maneno ya Mungu, na kupitia mateso na usafishaji maishani mwao. Ni kupitia tu imani kama hii ndipo tabia za watu zinaweza kubadilika, baada ya hapo tu ndipo wanaweza kuwa na maarifa ya kweli kuhusu Mungu. Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu cha ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka.
kutoka kwa "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni lazima utafute uzima. Leo, wale watakaofanywa wakamilifu ni wa aina sawa na Petro: ni wale ambao hutafuta mabadiliko katika tabia yao wenyewe, na wako tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kutekeleza wajibu wao kama kiumbe wa Mungu. Ni watu kama hawa pekee watakaofanywa wakamilifu. Kama wewe tu unatazamia tuzo, na hutafuti kubadilisha tabia ya maisha yako mwenyewe, basi juhudi zako zote zitakuwa za bure—na huu ni ukweli usiobadilika!
kutoka kwa "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea" katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, "kubadailishwa kwa tabia" ni nini? Lazima uwe mpenzi wa ukweli, uikubali hukumu na kuadibiwa na neno la Mungu unapopitia kazi Yake, na kupitia aina zote za mateso na kusafishwa, ambayo kwayo unatakaswa kutokana na sumu ya kishetani iliyo ndani yako. … Mabadiliko katika tabia yanamaanisha kuwa mtu, kwa sababu anapenda na anaweza kuukubali ukweli, hatimaye huja kujua asili yake ya uasi na ya kumpinga Mungu; anaelewa kuwa upotovu wa mwanadamu ni wenye kina zaidi na kuelewa upumbavu na udanganyifu wa mwanadamu. Anajua uduni wa mwanadamu na kusikitisha kwake, na hatimaye anaelewa kiini cha asili ya mwanadamu. Kwa kujua haya yote, anaweza kujikana na kujinyima kabisa, kuishi kwa neno la Mungu, na kutenda ukweli katika kila kitu. Mtu wa aina hii anamjua Mungu na tabia yake imebadilishwa.
kutoka kwa "Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mgeuzo katika tabia hasa huhusu mgeuzo katika asili yako. Asili si kitu unachoweza kuona kutoka kwa mienendo ya nje; asili inahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuishi kwa watu. Inahusisha moja kwa moja maadili ya maisha ya binadamu, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi, na kiini cha watu. Kama watu hawangeweza kukubali ukweli, basi hawangekuwa na migeuzo katika hali hizi. Ni kama watu wamepitia kazi ya Mungu tu na wameingia kwa ukamilifu katika ukweli, wamebadilisha maadili na mitazamo yao kuhusu kuishi na maisha, wameyatazama mambo kwa njia sawa na Mungu, na wamekuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zao zinaweza kusemekana zimebadilika.
kutoka kwa "Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Baada ya kupitia kwa kiwango fulani, maoni ya maisha ya mtu, umuhimu wa kuwepo, na msingi wa kuwepo utabadilika kabisa. Hiyo ni kwamba mtazaliwa tena, na kuwa watu tofauti kabisa. Hili ni la kushangaza! Haya ni mabadiliko makubwa; ni mabadiliko ambayo hugeuza kila kitu pindu. Utahisi kwamba umaarufu, faida, msimamo, mali, anasa, na utukufu wa dunia havina maana na kwamba una uwezo wa kuviachilia kwa urahisi. Huyu ni mtu katika mfano wa mwanadamu. Wale ambao hatimaye wamekamilishwa watakuwa kikundi kama hiki. Wao wataishi kwa ajili ya ukweli, kwa ajili ya Mungu, na kwa ajili haki. Huu ni mfano wa mtu.
kutoka kwa "Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Ni tu pale ambapo mtu anamjua Mungu na kuwa na ukweli ndipo huishi nuruni; na ni pale tu ambapo maoni yake ya dunia na maoni yake ya maisha yanabadilika ndipo anabadilika kimsingi. Anapokuwa na lengo la maisha na kujiheshimu kulingana na ukweli; anapomtii Mungu kabisa na kuishi kwa neno la Mungu; anapohisi kuhakikishiwa na kuchangamshwa ndani ya moyo wake; moyo wake unapokuwa huru bila giza; na anapoishi kikamilifu na kwa huru na bila kuzuiwa kenye uwepo wa Mungu—hapo tu ndipo atakapoishi maisha ya mwanadamu ya kweli na kuwa mtu anayemiliki ukweli. Aidha, ukweli wote ulio nao unatoka kwa neno la Mungu na kwa Mungu Mwenyewe. Mtawala wa ulimwengu mzima na kila kitu—Mungu Mkuu Zaidi—Anakupenda wewe, kama mwadamu halisi anayeishi maisha ya kweli ya mwanadamu. Je, nini linaweza kuwa la maana zaidi kuliko hili? Mtu wa aina hii ni yule aliye na ukweli.
kutoka kwa "Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo