Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumanne, 18 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”

Mwenyezi Mungu anasema, “Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu.”
Ni njia gani ambayo Mungu hutumia kumkamilisha mwanadamu? Ni vipengele vipi vinavyojumuishwa? Je, uko tayari kukamilishwa na Mungu? Je, uko tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu? Unajua nini kuhusu maswali haya? Kama huwezi kuzungumzia maarifa kama haya, basi hii inaonyesha kwamba bado huijui kazi ya Mungu na hujapatiwa nuru katu na Roho Mtakatifu. Binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa. Wanaweza tu kupokea kiasi kidogo cha neema ili kufurahia kwa muda mfupi na haiwezi kuendelezwa kwa kipindi kirefu. Kama mtu hufurahia tu neema ya Mungu, hawezi kukamilishwa na Mungu. Baadhi wanaweza kutoshelezwa na amani na furaha ya mwili, maisha yenye furaha bila ya dhiki au msiba, huku wakiishi kwa amani na familia zao bila ya mapigano au ugomvi. Wanaweza hata kuamini kwamba hii ni baraka ya Mungu, lakini kwa kweli, ni neema ya Mungu tu. Hamwezi kutosheka tu kwa kufurahia neema ya Mungu. Kufikiria kwa aina hii ni kuchafu mno. Hata ukisoma neno la Mungu kila siku, uombe kila siku, na roho yako ihisi furaha na amani halisi, ilhali mwishowe huwezi kuzungumzia maarifa yoyote ya Mungu na kazi Yake au hujapata uzoefu wa mambo kama hayo, na haijalishi ni kiasi gani cha neno la Mungu ambacho umekula na kunywa, ukihisi tu amani na furaha katika roho yako na kwamba neno la Mungu ni tamu mno kiasi kwamba haliwezi kulinganishwa na kingine chochote, kana kwamba huwezi kulifurahia ukatosheka, lakini huna uzoefu halisi na huna hakika yoyote na neno la Mungu, basi ni nini unachoweza kupokea kutoka kwa aina hii ya imani katika Mungu? Kama huwezi kuishi kwa kudhihirisha kiini cha neno la Mungu, kula na kunywa kwako kwa maneno ya Mungu na maombi vyote vinahusu dini. Basi binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa na hawezi kupatwa na Mungu. Wale wote waliopatwa na Mungu ni wale wanaofuatilia ukweli. Kile ambacho Mungu hufaidi si mwili wa binadamu wala miliki zake, lakini sehemu iliyo ndani yake inayomilikiwa na Mungu. Kwa hivyo, Mungu huukamilisha moyo wa binadamu wala si mwili wake, ili moyo wa binadamu uweze kupatwa na Mungu. Kwa maneno mengine, kiini cha kusema kwamba Mungu humkamilisha mwanadamu ni kwamba Mungu huukamilisha moyo wa mwanadamu ili uweze kumgeukia Mungu na kumpenda Yeye.
Wale tu wanaoweza kurithi baraka za Mungu ni wale waliokamilishwa na Mungu na kupatwa na Mungu. Je, umefaidi chochote? Mungu amekukamilisha hadi kiwango gani? Mungu hamkamilishi binadamu bila mpango. Kunayo masharti na matokeo dhahiri yanayoweza kuonekana na binadamu. Si jinsi mwanadamu anavyoamini, kwamba mradi tu awe na imani katika Mungu, anaweza kukamilishwa na kupatwa na Mungu, na anaweza kupokea hapa ulimwenguni baraka na urithi wa Mungu. Mambo kama haya ni magumu mno, na hata zaidi inapohusu kubadilika kwa taratibu. Kwa sasa, kile ambacho mnafaa kutafuta kimsingi ni kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, na kukamilishwa na Mungu kupitia kwa watu wote, mambo yote na vitu vyote ambavyo mnakumbwa navyo, ili mambo zaidi ya kile Mungu Alicho yatashirikishwa ndani yenu. Lazima kwanza mpokee urithi wa Mungu ulimwenguni kabla ya kustahili kurithi baraka nyingi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu. Mambo yote haya ndiyo ambayo mnafaa kutafuta na ambayo kwanza mnafaa kuelewa. Zaidi unavyotafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, ndivyo utakavyoweza kuona mkono wa Mungu zaidi katika mambo yote, na hivyo kutafuta kwa bidii kuingia katika hali ya neno la Mungu na uhalisia wa neno Lake kupitia mitazamo tofauti na katika mambo tofauti. Huwezi kutosheka na hali hasi kama kutotenda dhambi tu, au kutokuwa na dhana, kutokuwa na filosofia ya maisha, na kutokuwa na hiari ya binadamu. Mungu humkamilisha mwanadamu kwa njia tofauti, na inawezekana katika mambo yote kwako kukamilishwa hatimaye. Huwezi tu kukamilishwa kwa kuzingatia mambo halisi, lakini pia mambo hasi, na hivyo kuboresha kile unachopata. Kila siku kunazo fursa za kukamilishwa na muda wa kupatwa na Mungu. Baada ya kipindi cha kupitia mambo kama haya, utabadilika pakubwa. Utaweza sasa kimaumbile kufaidi utambuzi katika mambo mengi ambayo hukuyaelewa awali; bila ya kuhitaji wengine kukufunza, bila kujua, utaweza kufahamishwa na Mungu, ili uweze kuwa na fahamisho katika mambo yote na mambo yote utakayopitia yatakuwa mengi. Mungu atakuongoza wewe ili usije ukapotoka kwa vyovyote vile. Kisha utawekwa wazi kwenye njia ya kufanywa kuwa mtimilifu na Yeye.

Jumatatu, 17 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Mwenyezi Mungu anasema, “Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka shtaka rasmi lililoandikwa; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika enzi zote, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga. Na wale wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu pekee watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya wanadamu na kuchukia matendo yao maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu, Nikisubiri tu nafasi kutoa adhabu kwa hao na kufurahia kuona hilo. Siku Yangu hatimaye imefika na siwezi kusubiri zaidi!”
Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimetamka mengi pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele katika mpango Wangu mpya, katika kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya katika kazi Yangu ili wale ambao wanaoniona watajipiga kifuani na kuulilia na kuombolezea uwepo Wangu bila kukoma. Kwani Ninaleta mwisho wa wanadamu duniani, na baada ya hapo kuendelea, Ninaweka wazi tabia Yangu yote mbele ya wanadamu, ili wote wanijuao na wasionijua watayashibisha macho yao na kuona kwamba kweli, nimekuja ulimwenguni, nimekuja duniani ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, ni “kukiri” Kwangu kwa pekee tangu Niwaumbe wanadamu. Matilaba yangu ni kuona mnafuatilia kwa moyo wenu wote kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinamkaribia wanadamu tena, karibu na wale wote wanaonipinga.
Pamoja na mbingu, Ninaanza kazi ambayo ni lazima Niifanye. Kwa hivyo Mimi husafiri kati ya misururu ya watu na kupita kati ya mbingu na ardhi, bila ya yeyote kutambua mienendo Yangu au kuyatambua maneno Yangu. Kwa hivyo, mpango Wangu bado unaendelea kwa urahisi. Ni vile tu hisia zenu zote zimekuwa nzito kiasi kwamba hamjui hatua za kazi Yangu hata kidogo. Hata hivyo, siku moja hakika mtakuja kutambua kusudio Langu. Leo hii, Ninaishi miongoni mwenu na Ninasumbuka pamoja nanyi. Kwa muda mrefu Nimeelewa mtazamo walio nao wanadamu juu Yangu. Nisingependa kueleza wazi zaidi, sembuse kutoa mifano zaidi ya kile kinachoniumiza ili kuwaaibisha. Ombi Langu la pekee ni kwamba myaweke moyoni yale yote mliyoyafanya kwa ajili ya kulinganisha maelezo yetu siku tutakapokutana tena. Nisingependa kumshutumu yeyote miongoni mwenu kwa njia isiyo ya kweli, kwa sababu daima Nimekuwa Nikifanya mambo kwa njia ya haki, bila upendeleo, na kwa heshima. Bila shaka, Ningependa pia kwamba nyinyi mngeweza kuwa wazi na wakarimu na kutofanya lolote lililo kinyume na mbingu na ardhi na dhamiri yenu. Haya pekee ndiyo Ninayowauliza. Watu wengi huhisi kusumbuka na hawana amani kwa sababu wametenda makosa mabaya, na wengi wanaona aibu kwa sababu hawajawahi kutenda tendo lolote zuri. Tena wapo pia wengi ambao, mbali na kutahayari kutokana na dhambi zao, wanakuwa wabaya zaidi, wakizitoa kabisa barakoa inayoficha sura zao mbaya—ambayo ilikuwa bado haijaonyeshwa kikamilifu—ili kujaribu tabia Yangu. Huwa Sijali wala sitilii maanani sana matendo ya mtu yeyote. Badala yake, Mimi hufanya kazi Ninayopaswa kufanya, iwe kukusanya habari, kuzungukazunguka katika nchi au kufanya lile ambalo linanipendeza. Katika nyakati muhimu, Mimi nitaendelea na kazi Yangu miongoni mwa wanadamu kama Nilivyopanga awali, bila kuchelewa au kuwa mapema hata kidogo, na kwa urahisi na kwa makini. Hata hivyo, kuna watu wengine ambao wanawekwa pembeni kwa kila hatua katika kazi Yangu, kwa sababu Ninadharau hali yao ya kujipendekeza na hali ya kujifanya wanyenyekevu. Wale wanaochukiza Kwangu hakika watatelekezwa, iwe ni kwa kupenda au kwa kutopenda. Kwa ufupi, Ninataka wale wote Ninaowadharau kuwa mbali sana Nami. Ni dhahiri kwamba, Sitawahurumia wale waovu ambao wamebaki katika makao Yangu. Kwa kuwa siku ya adhabu ya mwanadamu inakaribia, Sina haraka ya kuzitupa nje zile nyoyo zote zinazostahili dharau, kwa kuwa Nina mpango Wangu Mwenyewe.
Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, wala si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo yote ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya nyingine, na vilevile njia zao katika kunifuata, sifa zao asilia, na utendakazi wao wa mwisho. Kwa njia hii, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu na kila mmoja atakuwa wa aina yake kama Nilivyowaweka. Ninaamua hatima ya kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu. Sijafanya mabadiliko yoyote katika mpango Wangu tangu kuuanzisha. Ni vile tu, kwa binadamu, wale ambao kwao Mimi huelekeza maneno Yangu wanaonekana kupungua kwa idadi, na vile vile wale Ninaowakubali kwa kweli. Hata hivyo, Ninasisitiza kwamba mpango Wangu haujawahi kubadilika; badala yake, ni imani na upendo wa mwanadamu ambao hubadilika daima, kufifia daima, kiasi kwamba upo uwezekano wa kila mwanadamu kubadilika kutoka kujipendekeza Kwangu hadi kufikia hali ya kunidharau au hata kunitupa nje. Mtazamo Wangu kwenu hautakuwa baridi wala moto, hadi pale Nitakapohisi kuchukizwa na kuchafuliwa moyo, na hatimaye kutoa adhabu. Hata hivyo, katika siku ya adhabu yenu, bado Nitawaona lakini nyinyi hamtaweza kuniona tena. Tayari Kwa kuwa maisha miongoni mwenu yamekuwa ya kuchosha na ya taabu tayari Kwangu, kwa hivyo ni wazi kuwa, Nimechagua mazingira tofauti Yangu kuishi, ili Niepuke vizuri kuumizwa na maneno yenu mabovu na kuwa mbali na tabia zenu hafifu sana, ili msinipumbaze au kunitendea kwa namna ya uzembe. Kabla Sijawaacha, lazima bado Ninawasihi mjiepushe kufanya yale ambayo hayaambatani na ukweli. Badala yake, mnafaa kufanya yale ambayo yanawapendeza watu wote, na yale ambayo yana manufaa kwa binadamu wote, na yale yanayofaidi hatima yenu wenyewe, la sivyo, yule atakayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe.
Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Jumapili, 16 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”

Mwenyezi Mungu anasema: “Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata uzoefu wa maisha ya binadamu, Nikichunguza kwa karibu matendo yote ya mwanadamu. Hakuna aliyewahi kujitolea Kwangu kwa kweli. Hakuna aliyewahi kufuata ukweli. Hakuna aliyewahi kuwa mwangalifu Kwangu. Hakuna aliyewahi kufanya maazimio mbele Yangu na kufanya wajibu wake. Hakuna aliyewahi kuniruhusu kuishi ndani yake. Hakuna aliyewahi kunithamini kama afanyavyo maisha yake. Hakuna aliyewahi kuona kwa vitendo vya ukweli uzima wote wa uungu Wangu. Hakuna aliyewahi kutamani kuwasiliana na Mungu wa vitendo Mwenyewe.”
Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa ufalme. Ingawa chini ya nuru ya Roho Wangu watu wengi wametabiri uzuri wa ufalme, wanajua tu nje ya ufalme, sio umuhimu wa ndani. Leo, ufalme ujapo kuwepo rasmi duniani, binadamu wote bado hujui kinachopaswa kukamilishwa, ulimwengu ambao binadamu hatimaye ataletwa ndani, wakati wa Enzi ya Ufalme. Kuhusu haya, Naogopa watu wote wako katika hali ya mkanganyiko. Kwa sababu siku ya utambuzi kamili wa ufalme bado haijafika kabisa, wanadamu wote wamechanganyikiwa, hawawezi kuiona vizuri. Kazi Yangu ya uungu inaanza rasmi na Enzi ya Ufalme. Ni katika mwanzo rasmi wa Enzi ya Ufalme kwamba tabia Yangu inaanza kuendelea kudhihirika kwa mwanadamu. Hivyo kwa muda huu tarumbeta takatifu inaanza rasmi kutoa sauti na kutangaza kwa wote. Nichukuapo kirasmi mamlaka Yangu na kutawala kama Mfalme katika ufalme, watu Wangu wote watakamilishwa na Mimi baada ya muda. Wakati mataifa yote ya dunia yatavurugwa, hapo ndipo hasa ufalme Wangu utaanzishwa na kupata umbo na pia Nitabadilika na kurejea kwa ulimwengu mzima. Wakati huo, watu wote watauona uso Wangu tukufu, watauona uso Wangu wa kweli. Tangu kuumbwa kwa dunia hadi sasa, binadamu umepotoshwa na Shetani hadi kiasi kilicho leo. Kwa ufisadi wa mwanadamu, Nimefichwa zaidi na zaidi kutoka kwake na Nikazidi kutoeleweka na wao. Mwanadamu hajawahi kuuona uso Wangu wa kweli, hajawahi kuathiriana na Mimi moja kwa moja. Ni kwa tetesi na hadithi tu ndipo kumekuwa na “Mimi” kwa ubunifu wa mwanadamu. Kwa hivyo Nakubaliana na ubunifu wa binadamu, kwamba, ni dhana za binadamu, kukabiliana na “Mimi” kwa akili za wanadamu, kwamba Naweza kubadilisha hali ya “Mimi” ambayo wameweka kwa miaka mingi. Hii ni kanuni ya kazi Yangu. Hakuna mtu hata mmoja ameweza kuijua vizuri sana. Ingawa wanadamu wamejilaza na kuja mbele Yangu kuniabudu, Sifurahii matendo kama haya ya wanadamu kwa sababu kwa mioyo yao hawajashikilia mfano Wangu, lakini mfano Wangu wa nje. Kwa hivyo, akili zao zinapokosa tabia Yangu, hawajui chochote kuhusu uso Wangu wa kweli. Kwa hivyo, wakati wameamini wamenipinga ama kukosea amri Zangu za kiutawala, Nitajifanya kwamba sioni. Na hivyo, kwa kumbukumbu zao, Mimi ni Mungu anayeonyesha huruma kwa wanadamu badala ya kuwaadibu, ama Mimi ni Mungu Mwenyewe asiyemaanisha Anachokisema. Haya yote ni mawazo yanayotokana na fikira za wanadamu na sio kwa mujibu na ukweli.
Najificha wakati wanadamu wana kazi nyingi na kujifichua wakati wao wa burudani. Binadamu unanidhania kuwa Anayejua yote na kuwa Mungu Mwenyewe anayekubali maombi yote. Wote basi wanakuja mbele Yangu kutafuta tu msaada wa Mungu, bila kuwa na tamaa ya kunijua. Wakiwa katika maumivu ya magonjwa, wanadamu wananiomba msaada. Wakiwa na shida, wananiambia matatizo yao kwa nguvu zao zote ili kumwaga mateso yao. Na bado hakuna mwanadamu hata mmoja ameweza kunipenda pia akiwa na faraja. Hakuna mtu hata mmoja amenitafuta wakati wa amani na furaha ili Nishiriki furaha yake. Wakati familia yao ya karibu ina furaha na iko sawa, wanadamu tayari wananiweka kando ama kunifungia mlango, kunikataza kuingia, na hivyo kufurahia furaha heri ya familia. Akili ya binadamu ni nyembamba sana, nyembamba sana hata kumshikilia Mungu, apendaye, mwenye huruma, na mkunjufu kama Mimi. Nimekataliwa mara ngapi na wanadamu wakati wao wa kicheko na furaha, Nimetegemewa kama gongo mara ngapi na wanadamu wakati wanaanguka; Ni mara ngapi Nimelazimishwa kuwa daktari wa wanadamu wanaougua magonjwa. Mwanadamu ni katili jinsi gani! Hawana akili na ni wabaya kabisa. Hawana hata hisia zinazopatikana kwa binadamu. Nusura hawana ubinadamu hata kidogo. Fikiria siku za nyuma na linganisha na sasa. Kuna mabadiliko yanayofanyika ndani zenu? Kuna siku kidogo za zamani sasa? Ama zamani bado haijabadilishwa?
Juu ya mlima na chini ya bonde Nimepitia, na kuwa na uzoefu wa panda shuka za dunia. Nimetembea na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi, lakini bado inaonekana tabia ya binadamu imebadilika kidogo. Na ni kama asili ya zamani ya mwanadamu imeeneza mizizi na kuota ndani yao. Hawawezi kamwe kubadili hiyo asili ya zamani, kuiboresha tu kwa msingi wa kwanza. Wasemavyo wanadamu, kiini hakijabadilika, lakini umbo limebadilika sana. Kila mtu, inaonekana, anajaribu kunidanganya, kunipofusha, ili aweze kuingia na kupata shukrani Yangu. Sipendi wala kutia maanani udanganyifu wa watu. Badala ya kukasirika, Nachukua mtazamo wa kuangalia lakini si kuona. Napanga kuupa binadamu kiwango fulani cha uhuru, na hivyo, kushughulikia wanadamu wote kama kitu kimoja. Kwa sababu wanadamu wote hawajiheshimu na ni maskini wasio na faida, wasiojithamini, watawezaje kunihitaji kuonyesha huruma na mapenzi mapya? Wanadamu wote hawajijui, na hawajui uzito wao. Wanapaswa kujipima uzito. Binadamu haunitambui, hivyo Nami pia siutilii maanani. Wanadamu hawanitambui, kwa hivyo Mimi pia Siweki juhudi kwao. Je, hii ni bora? Je, hii haiwazungumzii, watu Wangu? Nani amefanya maazimio mbele Yangu na kukosa kuyatupilia mbali baadaye? Nani amefanya maazimio ya muda mrefu mbele Yangu badala ya kutatua mara nyingi juu ya hii na hiyo? Daima, wanadamu hufanya maazimio mbele Yangu wakati wa raha na kuyafuta kabisa wakati wa shida. Baadaye, wanachukua uamuzi wao na kuuweka mbele Yangu. Je, Mimi si wa kuheshimika hadi Naweza kubali kwa kawaida taka iliyookotwa na mwanadamu kutoka pipani? Wanadamu wachache hushikilia maazimio yao, wachache ni safi, na wachache wanatoa yenye thamani kubwa zaidi kama sadaka Kwangu. Je, nyinyi wote si sawa kwa njia hii? Iwapo, kama mmoja wa watu Wangu kwenye ufalme, huwezi kufanya wajibu wenu, mtachukiwa na kukataliwa na Mimi!

Ijumaa, 14 Juni 2019

Unafaa Utofautishe Vipi Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Pepo Wabaya?

2. Unafaa Utofautishe Vipi Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Pepo Wabaya?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhusu kuwasaidia watu kupata faida; ni kuwaadilisha watu; hakuna kazi ambayo haiwanufaishi watu. Haijalishi kama ukweli ni wa kina au usio wa kina, na haijalishi tabia ya wale wanaopokea ukweli huo ilivyo, chochote ambacho Roho Mtakatifu Anafanya, yote hayo huwanufaisha watu.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu. Wakati watu wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndani yao ni watakatifu hasa. Wale ambao wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu huishi kwa kudhihirisha upendo wa Mungu, upendo wa kaka na dada zao, na kufurahia vitu ambavyo Mungu hufurahia na kuchukia vitu ambavyo Mungu huchukia. Watu ambao wanaguswa na kazi ya Roho Mtakatifu wana ubinadamu wa kawaida, na wanamiliki ubinadamu na daima hufuatilia ukweli. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya watu, hali zao huwa nzuri zaidi na zaidi, na ubinadamu wao unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi, na ingawa ushirikiano wao mwingine unaweza kuwa mpumbavu, motisha zao ziko sahihi, kuingia kwao ni kwa hali nzuri, hawajaribu kukatiza, na hakuna nia mbaya ndani yao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida na ya kweli, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa mwanadamu kulingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na Yeye huwapa nuru na kuongoza watu kulingana na ufuatiliaji halisi wa watu wa kawaida. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa watu, Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, Anawakimu kwa msingi wa mahitaji yao, na Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kwa hali nzuri kwa msingi wa kile ambacho wanakosa, na kwa upungufu wao; wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, kazi hii inalingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na ni katika maisha halisi pekee ndio watu wanaweza kuona kazi ya Roho Mtakatifu. Iwapo, katika maisha yao ya kila siku, watu wako katika hali nzuri na wana maisha ya kawaida ya kiroho, basi wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali kama hiyo, wakati wanakula na kunywa maneno ya Mungu wana imani, wakati wanaomba wanatiwa moyo, wakati kitu kinawafanyikia wao si baridi, na wakati kinawafanyikia wanaweza kuona masomo ambayo Mungu anawahitaji kujifunza, na hawako baridi, ama dhaifu, na ingawa wana ugumu wa kweli, wako tayari kukubali mipango yote ya Mungu.
…………
Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia katindani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuwa na hali za kawaida mbele ya Mungu. Ambayo ni kusema, punde tu kuna kazi ya Shetani ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba. Kazi ya roho waovu huharibu uhusiano wa kawaida kati ya mwanadamu na Mungu, na huvuruga maono ya awali ya watu na njia ambayo maisha yao yameingia, katika mioyo yao hawawezi kamwe kumkaribia Mungu, daima mambo hufanyika ambayo huwasababishia vurugu na kuwatia pingu, na mioyo yao haiwezi kupata amani, kuacha upendo wao wa Mungu bila nguvu, na kuwafanya kusononeka. Hayo ndiyo maonyesho ya kazi ya Shetani. Kazi ya Shetani inadhihirishwa katika yafuatayo: kutoweza kushikilia msimamo na kuwa na ushuhuda, kukusababisha kuwa mtu ambaye ana makosa mbele ya Mungu, na ambaye hana uaminifu kwa Mungu. Kwa kuingilia kwa Shetani, unapoteza upendo na uaminifu kwa Mungu ndani yako, unaondolewa uhusiano wa kawaida na Mungu, hufuatilii ukweli, ama kujiendeleza, unarudi nyuma, na kuwa baridi, unajipendeza, unaachia uenezaji wa dhambi, na huchukii dhambi; zaidi ya hayo, kuingilia kwa Shetani kunakufanya mpotovu, kunasababisha mguso wa Mungu kutoweka ndani yako, na kunakufanya kulalamika kuhusu Mungu na kumpinga Yeye, kukufanya uwe na shaka na Mungu, na hata kuna hatari ya wewe kumwacha Mungu. Hii yote ni kazi ya Shetani.
kutoka kwa "Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida kabisa, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake, ambayo yameharibiwa na Shetani, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Ni sawa na, kusema, maisha ya mwanadamu yanakuwa na kukua, na Atabia ya upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maishi ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha atabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa uelewa wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu.
kutoka kwa "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mambo yanayotokana na Mungu hukusababisha kuwa wazi zaidi kuhusu maono, na hukusababisha kusogea karibu na karibu zaidi na Mungu, ukishiriki upendo na ndugu kwa bidii; unakuwa na uwezo wa kutilia maanani mzigo wa Mungu, na moyo wako umpendao Mungu haupungui; kuna njia mbele yako kuitembea. Mambo ambayo hutokana na Shetani hukusababisha kupoteza maono na vyote ulivyokuwa navyo awali vimetoweka; unajitenga na Mungu, huna upendo kwa ndugu nawe una moyo wa chuki. Unakuwa mwenye kukata tamaa, hutaki tena kuishi maisha ya kanisa, na moyo wako umpendao Mungu hauko tena. Hii ni kazi ya Shetani na pia ni matokeo ambayo yameletwa na kazi ya roho mbaya.
kutoka kwa Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni
Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ili kuwapa watu nuru, Yeye kwa ujumla kuwapa ufahamu wa kazi ya Mungu, na ya kuingia kwao ya kweli na hali ya ukweli, na pia Huwapa azimio, huwaruhusu kuelewa kusudi la hamu la Mungu na mahitaji yake kwa ajili ya mtu leo, Huwapa azimio la kufungua njia zote. Hata wakati ambapo watu wanapitia umwagaji damu na sadaka ni lazima watende kwa ajili ya Mungu, na hata kama wanakumbana na mateso na dhiki, lazima bado wampende Mungu, na wasiwe na majuto, na lazima wawe shahidi kwa Mungu. Azimio la aina hii ni misisimko ya Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu—lakini jua kwamba hujamilikiwa na misismko kama hii kila wakati.
kutoka kwa "Utendaji (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine husema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao nyakati zote. Hili haliwezekani. Ikiwa wangesema kwamba Roho Mtakatifu yuko nao kila mara, hilo lingekuwa la kweli. Ikiwa wangesema kwamba fikira na hisi zao ni za kawaida nyakati zote, hilo pia lingekuwa la kweli, na lingeonyesha kwamba Roho Mtakatifu yuko nao. Ikiwa unasema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako kila mara, kwamba unapata nuru kutoka kwa Mungu na kuguswa na Roho Mtakatifu kila wakati, na unapata ufahamu mpya kila wakati, basi hili si la kawaida. Ni la rohoni kabisa! Bila tashwishi yoyote, watu hao ni pepo wabaya! Hata wakati ambapo Roho wa Mungu huja ndani ya mwili, kuna nyakati ambapo lazima Apumzike, na lazima Ale—sembuse wewe. Wale ambao wamemilikiwa na pepo wabaya huonekana kutokuwa na udhaifu wa mwili. Wanaweza kutelekeza na kuacha kila kitu, wao ni wasiohemkwa, wenye uwezo wa kustahimili mateso, wao hawahisi uchovu hata kidogo sana, kana kwamba wamevuka mipaka ya mwili. Je, hili silo la rohoni kabisa? Kazi ya pepo mwovu ni ya rohoni, na mambo haya ni yasiyofikiwa na mwanadamu. Wale wasioweza kutofautisha huwa na wivu wanapoona watu kama hao, na husema kwamba imani yao katika Mungu ni thabiti sana, na nzuri sana, na kwamba wao huwa si wadhaifu kamwe. Kwa kweli, hili ni dhihirisho la kazi ya pepo mwovu. Hiyo ni kwa sababu watu wenye hali ya kawaida huwa na udhaifu wa binadamu usioepukika; hii ni hali ya kawaida ya wale walio na kuwepo kwa Roho Mtakatifu.
kutoka kwa "Utendaji (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wanaweza kuzungumza kutoka ndani mwako au ndani ya sikio lako, au la sivyo wanaweza kuyachanganya mawazo na akili yako, wanazuia kuguswa kwa Roho Mtakatifu ili usiweze kuuhisi, na baada ya hapo wanaanza kukuingilia, kuzifanya fikira zako ziwe zilizochanganyikiwa na akilia yako iwe iliyovurugika, na kukufanya usiyekuwa na utulivu na usiye thabiti. Hivyo ndivyo ilivyo kazi ya roho wabaya.
Wanaweza kuzungumza kutoka ndani mwako au ndani ya sikio lako, au la sivyo wanaweza kuyachanganya mawazo na akili yako, wanazuia kuguswa kwa Roho Mtakatifu ili usiweze kuuhisi, na baada ya hapo wanaanza kukuingilia, kuzifanya fikira zako ziwe zilizochanganyikiwa na akilia yako iwe iliyovurugika, na kukufanya usiyekuwa na utulivu na usiye thabiti. Hivyo ndivyo ilivyo kazi ya roho wabaya.
kutoka kwa "Maana ya Mungu Kuupitia Uchungu wa Dunia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Unaweza kuhisi roho yako mwenyewe? Unaweza kugusa roho yako? Unaweza kuhisi roho yako inafanya nini? Hujui, siyo? Ikiwa unaweza kuhisi na kugusa vitu fulani kama hiki, basi ni roho nyingine ndani yako inafanya kitu kwa nguvu—ikidhibiti vitendo na maneno yako. Ni kitu kisichohusiana na wewe, kisicho cha wewe. Wale wenye roho ovu wana uzoefu wa kina na hili.
kutoka kwa "Jinsi ya kuelewa Umoja wa Mwili wa Mungu na Roho" katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo kunao baadhi ya pepo wabaya wanaofanya kazi kupitia kwa mambo yasiyo ya ulimwenguni humu ili kumpotosha mwanadamu; hilo si chochote bali ni uigaji kwa upande wao, kumpotosha mwanadamu kupitia kwa kazi ambayo kwa sasa haifanywi na Roho Mtakatifu. Pepo wengi wabaya huiga ufanyaji wa miujiza na uponyaji wa magonjwa; si chochote ila kazi ya pepo wabaya, kwani Roho Mtakatifu hafanyi tena kazi kama hiyo leo. Wale wote wanaokuja baadaye na wanaoiga kazi ya Roho Mtakatifu—ni pepo wabaya.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Kazi ya Roho Mtakatifu huwaruhusu watu kuuelewa ukweli, huwaruhusu kujua kiini potovu cha Shetani, na huwapa maarifa ya kweli kuhusu kile Mungu anacho na Alicho. Athari zake zote ni nzuri kwa ujumla. Leo, tunajua ukweli ni nini, kwamba ukweli unatoka kwa Mungu, kwamba mambo mazuri yanatoka kwa Mungu, kile kinachofaa kumilikiwa na watu wenye ubinadamu wa kawaida, kile ambacho ni mapenzi ya Mungu, na kile ambacho ni maisha ya kweli. Mambo haya yote ni mazuri, na uhalisi wa mambo mazuri ni ukweli. Hivi ndivyo athari ya kazi ya Mungu ilivyo, na tunaielewa tu kutokana na kupata nuru na uangazaji wa Roho Mtakatifu. Kazi ya pepo wabaya haiwezi kuwapa watu maarifa ya mambo mazuri. Unafaa kuwa wazi na kujua kwamba watu ambao pepo wabaya hufanya kazi ndani yao hawaelewi wala kuufahamu ukweli wowote. Kazi ya pepo wabaya inaweza tu kuwafanya watu kuwa waovu zaidi na zaidi, inaweza kuleta tu giza zaidi na zaidi ndani ya mioyo yao, kuzifanya tabia zao kuwa potovu zaidi na zaidi, na hali yao kuzoroteka zaidi na zaidi, na hatimaye kuishia katika kuteseka milele na kuangamia. Kazi ya Roho Mtakatifu huwafanya watu kuwa wa kawaida zaidi na zaidi, huwapa ufahamu mkubwa zaidi wa ukweli na siku zote huwapa imani kubwa zaidi kwa Mungu, na wanaweza kumtii Mungu zaidi na zaidi. Hatimaye, huwaruhusu kumjua kabisa Mungu na kumwabudu Mungu. Hii ndiyo athari ya kazi ya Roho Mtakatifu, na ni kinyume kabisa cha kazi ya pepo wabaya.
kutoka kwa "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)
Hapa chini, hebu tuangalie baadhi ya utofauti mwingine waziwazi kati ya kazi mbalimbali za pepo wabaya na kazi ya Roho Mtakatifu, na namna ambavyo zinaonyeshwa kwa njia mahususi. Roho Mtakatifu huwachagua watu wanaofuatilia ukweli, na walio na dhamiri na mwelekeo, na wanaomiliki uadilifu. Hawa ndio aina ya watu ambao Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao. Pepo wabaya huchagua watu ambao ni wajanja na wa kipuuzi, wasiopenda ukweli, na wasio na dhamiri wala mwelekeo. Watu kama hao ndio pepo wabaya hufanya kazi ndani yao. Ni nini tunachoona tunapolinganisha wale waliochaguliwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu, na wale waliochaguliwa kwa kazi ile ya pepo wabaya? Tunaweza kuona kwamba Mungu ni mtakatifu, na mwenye haki, kwamba wale wanaochaguliwa na Mungu huutafuta ukweli, na wanayo dhamiri na mwelekeo, kwamba wanao uadilifu na wanapenda kile ambacho ni haki. Wale wanaochaguliwa na pepo wabaya ni wajanja, ni wachoyo na wenye dharau, hawaupendi ukweli, hawana dhamiri na mwelekeo, na hawautafuti ukweli. Pepo wabaya huchagua tu mambo mabaya na wale watu ambao si wa kweli, ambapo tunaona ya kwamba pepo wabaya wanapenda uovu na giza, kwamba wanawakimbia wale wanaoutafuta ukweli, na ni wepesi wa kuwamiliki wale ambao wako kombo na ni wajanja, wale ambao wanavutiwa na udhalimu, na wanaorogwa kwa urahisi. Wale ambao pepo wabaya huchagua kufanyia kazi ndani yao hawawezi kuokolewa, na wanaondolewa na Mungu. Ni lini, na ni katika mazingira gani, ndipo pepo wabaya hufanya kazi? Wao hufanya kazi wakati watu wamesonga mbali na Mungu na kuasi dhidi ya Mungu. Kazi ya pepo wabaya huwaroga watu, na hufanya hivyo kwa kuchukua fursa ile wanapotenda dhambi. Wakati watu wako katika hali yao dhaifu zaidi, hasa wanapokuwa katika maumivu makuu ndani ya mioyo yao, wakati wanapohisi vibaya na wakiwa wamechanganyikiwa, pepo mbaya huchukua fursa hii kujiingiza ndani polepole ili kuwaroga na kuwapotosha, kuleta kutoelewana kati yao na Mungu. Kunao wakati wa kazi ya Roho Mtakatifu: Wakati watu wanapomwita Mungu, wakati mioyo yao inapomgeukia Mungu, wanapomhitaji Mungu, wanapotubu kwa Mungu, na wanapoutafuta ukweli, basi ndipo Roho Mtakatifu huanza kufanya kazi ndani yao. Tazama namna ambavyo kila dhana ya kazi ya Roho Mtakatifu ilivyo ili kumwokoa mwanadamu, namna Anavyotafuta fursa za kumwokoa mwanadamu, ilhali pepo wabaya hutafuta fursa za kuwapotosha na kuwalaghai watu. Pepo wabaya wanayo dharau na ni waovu, ni wenye kudhuru kwa siri na wabaya, kila kitu wanachofanya kinalenga katika kumpotosha mwanadamu, na kumdhuru mwanadamu, na kumteketeza yeye. Wakati watu wanapohitaji msaada, wanapomtafuta Mungu kwa dharura, wanapohitaji wokovu wa Mungu, na wanapotaka kusonga karibu na Mungu ndani ya mioyo yao, Roho Mtakatifu hujitokeza kwao na kufanya kazi ya wokovu. Mungu ni upendo, na pepo wabaya ni chuki—hili liko wazi kwako, sivyo? Kile tu ambacho pepo wabaya hufanya ni ili kuwezesha kumteketeza na kumpotosha mwanadamu, na kile tu ambacho Roho Mtakatifu hufanya ni kwa upendo na wokovu wa mwanadamu. Athari ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwatakasa watu, kuwaokoa dhidi ya kupotoka kwao, kuwaruhusu kujijua na kumjua Shetani, kuweza kuasi dhidi ya Shetani, kuweza kuufuatilia ukweli, na hatimaye kuishi kwa kudhihirisha mfanano wa mwanadamu. Pepo wabaya hupotosha, hutia najisi, na kuwafunga watu, huwaweka ndani zaidi ya dhambi, na kuwasababishia maumivu makubwa zaidi katika maisha yao, na hivyo wakati pepo wabaya wanapofanya kazi ndani ya watu, watu hao wamo hatarini; hatimaye, wanateketezwa na Shetani, jambo ambalo ni matokeo ya kazi ya pepo wabaya. Athari ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuweza hatimaye kuwaokoa watu, kuwafanya kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kuwa huru na kukombolewa kabisa, na kupokea baraka za Mungu. Tazama: Pepo wabaya humweka mwanadamu katika giza, humpeleka kwenye shimo la kuzimu; Roho Mtakatifu humchukua mwanadamu kutoka kwenye giza, na kumpeleka kwenye mwangaza, na hadi kwenye uhuru. Kazi ya Roho Mtakatifu huwapa watu nuru na kuwaongoza watu, Huwapa fursa mbalimbali, na wanapokuwa wanyonge na dhambi Yeye huwapa faraja. Huwaruhusu watu kujijua, huwaruhusu kuufuatilia ukweli, na Halazimishi watu kufanya mambo, lakini Huwaacha kujichagulia njia yao wao wenyewe, na hatimaye Huwapeleka kwenye mwangaza. Pepo wabaya huwalazimisha watu kufanya mambo na kuwaamrisha hapa na pale. Kila kitu wanachosema ni uongo na kinawaroga watu, kuwadanganya na kuwafunga; pepo wabaya hawawapatii watu uhuru, hawawaruhusu kuchagua, huwalazimisha kufuata barabara ya maangamio, na hatimaye kuwaingiza ndani ya dhambi zaidi na zaidi, na kuwasababishia kifo. Hebu tazama watu hao waovu, wale watu waovu: Wanawakokota wengine hadi kwenye uharibifu, wanawavuta kwenye uhalifu, na kuwavuta kwa ghafla kwenye maeneo ya kuchezea kamari. Hatimaye, baada ya wao kuziharibu familia za watu na kuwafarakanisha na dunia, wanafurahi, kazi yao imekamilika, na wametimiza nia yao. Je, hawa ni mashetani, sivyo? Ilhali wale ambao ni wazuri kwa kweli na wanamcha Mungu wanawaongoza watu kuwa karibu zaidi na Mungu, na kuwaongoza katika imani ya Mungu, katika ufahamu wa ukweli, katika kuyafuatilia maisha halisi, na hatimaye kuwafanya kuishi kwa kudhihirisha mfanano wa mwanadamu. Utofautishi kati ya mambo haya mazuri na mabaya ni wazi vipi! Katika kulinganisha kanuni, mbinu, na athari ya mwisho ya kazi ya Roho Mtakatifu na ile ya pepo wabaya, tunaona kwamba Mungu humwokoa mwanadamu, humpenda mwanadamu, na humpa mwanadamu ukweli, kwamba Yeye humchukua mwanadamu na kumweka kwenye mwangaza, na hatimaye humruhusu mwanadamu kubarikiwa na kuwa mtu halisi na kuishi kwa kudhihirisha maisha ya ukweli. Shetani humpotosha mwanadamu, humfunga mwanadamu, hujaribu kumteketeza mwanadamu, na hatimaye humwongoza mwanadamu katika kuteseka milele na kuangamia. Kupitia kujua kazi ya Roho Mtakatifu, tunaweza kutambua kazi ya pepo wabaya na kuujua ukweli wa upotoshwaji wa mwanadamu na Shetani. Leo, katika imani yetu kwa Mungu tunafahamu kile tunachofaa kufuatilia, kwamba Mungu ni mzuri, na kwamba tunafaa kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kumtii Mungu. Tunayo malengo katika maisha yetu, na tunalo tumaini la wokovu. Hizi ndizo athari za kazi ya Roho Mtakatifu. Leo, kama ungeulizwa kusema Shetani ni nini, ungeweza kusema? Tabia potovu ya Shetani inaonyeshwa kwa njia gani? Tabia ya Shetani ni yenye maovu, yenye kudhuru kwa siri, yenye makosa, mbovu, yenye dharau, yenye kushikilia maovu yote, na yenye sumu kabisa. Kila kitu ambacho Mungu anacho na Alicho ni nini? Ni hali ya kuwa mwenye haki, utakatifu, heshima, kudura, hekima, na rehema na upendo. Ile hisia ambayo Shetani huwapatia watu ni ya kuchukiza na iliyolaaniwa. Ile hisia ambayo Mungu huwapatia watu ni ya kukaribishwa, uzuri na kuheshimiwa.
kutoka kwa "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)
Ni nini athari ya kazi ya Roho Mtakatifu kwa mwanadamu? Humruhusu mwanadamu kuyaelewa maneno ya Mungu, na ukweli, na humruhusu mwanadamu kumjua Mungu na kujijua. Ukweli unao athari maradufu. Kwa upande mmoja, kuufahamu ukweli huwapatia watu maarifa ya Mungu, kwani ukweli ndio kiini cha maisha ya Mungu, ni kile Mungu anacho na Alicho, ni uhalisi wa mambo mazuri, na unawakilisha tabia na maisha ya Mungu—na hivyo basi ni sahihi kabisa kusema kwamba, kwa kuuelewa ukweli, tunafaidi ufahamu fulani wa Mungu. Wakati uo huo, ukweli unaweka pia wazi kupotoka kwetu, na hivyo basi wale wote wanaouelewa ukweli wanayo maarifa ya kweli kujihusu, na wameona wazi kabisa picha yao ya kweli na picha ya kweli ya Shetani. Kila kitu kinawekwa wazi kwa ukweli. Ni nini athari ya ufahamu wa ukweli kupitia kazi ya Roho Mtakatifu? Kwa upande mmoja, tunakijua kiini chetu potovu, tunamwona kwamba mwanadamu ni maskini, wa kuhurumiwa, kipofu, aliye na uchi, aliyepotoka, mwovu, mchoyo na mwenye dharau, kwamba hana mfanano hata kidogo wa mwanadamu wa kweli, kwamba hayuko tofauti hata kidogo na Shetani, kwamba asili yake na kiini chake vyote viko sawa na Shetani. Je, hii si athari ya ufahamu wa ukweli? Hakuna chochote ambacho si sahihi kuhusu haya. Isitoshe, kwa mtazamo huu tuko wazi kabisa kuhusu athari za kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi ya Roho Mtakatifu inayo pia athari nyingine nyingi. Kazi ya Roho Mtakatifu inaweza kuwapa watu imani ya kweli: Kila mojawapo ya maombi yetu kwa Mungu hutufanya kuhisi kwamba imani yetu kwa Mungu imeongezeka, na kwamba ni kweli zaidi. … Si ukweli hata kidogo kusema kwamba kunazo sehemu nyingi katika kazi ya Roho Mtakatifu, na mitazamo mingi ya athari zake. … kazi ya Roho Mtakatifu hutupatia maarifa ya kweli ya tabia ya Mungu, ya kudura na hekima ya Mungu, ya uchanganuzi Wake wa kina wa mioyo yetu, na hutupatia maarifa ya matendo ya ajabu na hali isiyofikirika kuhusu Mungu. Hivyo, pia, ndivyo inavyoturuhusu kujua na kushikilia kudura ya Mungu na utawala wake dhidi ya vyote.
kutoka kwa "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)
Wale ambao pepo wabaya hufanya kazi ndani yao hugeuka na kuwa wabaya na wazi na wenye kufanya jeuri wakati wanapoongea na kuwaambia watu ni nini cha kufanya. Baadhi yao hata hukiuka tabia njema na maadili ya ubinadamu wa kawaida. Maneno yao na vitendo vyao huroga na kuingilia kati watu, asili ya maneno hayo na vitendo hivyo ni mbovu na ya kuchukiza, na wanapotosha watu, na kuwadhuru watu, na hawana manufaa yoyote kwao. Punde tu pepo mbaya anapoonekana ndani ya mtu, wanahisi woga na wasiwasi, na kunakuwa na dharura kuu katika vitendo vyao, ni kana kwamba wanalipuka kwa kutokuwa wastahimilivu. Kuonekana kwake huwafanya watu kuhisi hasa kwa njia isiyo ya kawaida, na hakuna manufaa yoyote hata kidogo kwa wengine. Maonyesho makuu ya kazi ya pepo wabaya: Onyesho la kwanza ni kuwaelekeza watu kufanya hivi au vile, kuwaambia kufanya mambo, au kuwaelekeza kuongea unabii wa uongo. Onyesho la pili ni kuongea kwa mbinu ile ijulikanayo kama ya "ndimi" ambayo hakuna anayeielewa; hata wasemaji wenyewe hawawezi kuelewa kile wanachosema, na baadhi yao wanaweza "kuifasiri." Onyesho la tatu ni pale ambapo watu siku zote wanaupokea ufunuo, unaofanyika kwa uradidi fulani. Kwa wakati mmoja wataelekezwa kufanya kitu kimoja, na kwa wakati mwingine wataambiwa kufanya kitu kingine, na wanaishi katika wasiwasi usioisha. Onyesho la nne: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao wanayo hamu ya kufanya hiki au kile, na hawawezi kusubiri—licha ya kama kitu hicho kinakubaliwa katika mazingira yao au la. Huwa hata wanatoka nje kwenye giza la usiku; mwenendo wao si wa kawaida kamwe. Onyesho la tano: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao huwa hasa wenye majivuno na kiburi, kila kitu wanachosema ni cha kushusha hadhi na kuamrisha, hawawezi kuuongea ukweli wowote, anawaacha watu wakiwa wamekasirika, na kuwalazimisha watu kuingia kwenye taabu kama pepo. Onyesho la sita: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao hawana ufahamu kiasi kidogo cha mipangilio kutoka juu, isitoshe hawaelewi kanuni za kazi; wanamkenulia Mungu, wanajaribu kuwadanganya watu, na matendo yao mabaya yanatatiza mpangilio wa kawaida wa kanisa. Onyesho la saba: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao mara nyingi hujifanya kuwa watu wengine bila sababu, au vinginevyo wametumwa na mtu, kuwafanya watu kuyasikiliza maneno yao, na hakuna anayeweza kujua namna walivyofikia hapo. Onyesho la nane: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao mara nyingi hawana urazini, na hawauelewi ukweli; kwa kawaida, wanakosa welekevu wa kuelewa, na hawana kule kupewa nuru na Roho Mtakatifu. Watu hugundua kwamba kile wanachoelewa hasa si cha kawaida, na si sahihi kabisa. Onyesho la tisa: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao ni wenye makuu kabisa na wasio na urazini, hawamtukuzi Mungu wala kumtolea ushuhuda kamwe, hawawezi kuuongea ukweli wowote, na kile wanachofanya na kusema tu huwa kinawashambulia watu, kinawafunga, na kuwawekea mipaka, mpaka pale ambapo mioyo yao imeshughulikiwa, na wao kupigwa na kugeuzwa kuwa wabaya na wasioweza kujiokoa, huku nao wakiwa na furaha kisirisiri—ambayo ndiyo nia kuu ya kazi ya pepo wabaya. Onyesho la kumi: watu ambao wamepagawa na pepo wabaya—maisha yao yana kasoro kabisa, mtazamo wao mkali, na maneno yao hasa hayana urafiki, ni kana kwamba wao ni pepo ambaye ameingia ulimwenguni humu. Hakuna nidhamu katika maisha yao ya kila siku, hawana uthabiti kabisa, wao hawatabiriki kama vile wale wanyama wasiofugwa, wanyama mwitu, na watu wanawaona kuwa wanaweza kupingika kabisa. Hayo ndiyo maonyesho ya watu waliofungwa na mashetani. Watu ambao wamepagawa na pepo wabaya mara nyingi hasa wanakuwa wenye chuki na kujitenga na wale ambao Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao na wanaoweza kuuongea ukweli. Ndivyo inavyokuwa mara nyingi kwamba watu wanapokuwa bora zaidi, ndipo wanapotaka kuwashambulia na kuwashutumu, ilhali watu wanapokosa mwelekeo na kuchanganyikiwa zaidi, ndipo wanapofanya kadri wanachoweza kuwalaghai na kuwavisha kilemba cha ukoka, na hasa wao kuwa radhi kujihusisha nao. Kazi ya pepo wabaya hugeuza nyeusi ikawa nyeupe, na kuyafanya mazuri kuwa mabaya na mabaya kuwa mazuri. Hayo ndiyo matendo ya pepo wabaya.
kutoka kwa "Maonyesho Makuu ya Kazi ya Pepo Wabaya" katika Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu
Roho yoyote ambayo kazi yake inajionyesha katika hali isiyo ya ulimwenguni humu ni pepo mbaya, na kazi na matamko ya roho yoyote inayotekeleza kazi isiyo ya ulimwenguni humu ndani ya watu ni kazi ya pepo mbaya; mbinu hizi zote ndizo ambazo pepo wabaya hufanya kazi na si za kawaida na za humu ulimwenguni, na zinaonyeshwa kimsingi kwa njia sita zifuatazo:
1. Udhibiti wa moja kwa moja wa uneni wa watu, jambo ambalo linaonyesha waziwazi kwamba pepo mbaya anazungumza, na wala si watu wenyewe wanaozungumza kwa kawaida;
2. Hisia kwamba pepo mbaya anawaelekeza watu na kuwaamuru kufanya hiki na kile;
3. Watu ambao, wakati wakiwa kwenye chumba, wanaweza kujua wakati mtu yuko karibu kuingia ndani;
4. Watu ambao mara nyingi wanazisikia sauti zikiwazungumzia na ambazo wengine hawawezi kuzisikia;
5. Watu ambao wanaweza kuona na kusikia mambo ambayo wengine hawawezi;
6. Watu ambao siku zote wanafadhaishwa, na wanajizungumzia wenyewe, na hawawezi kuwa katika mazungumzo ya kawaida au utangamano na watu.
Wale wote ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao bila kuepukika wanayo maonyesho haya sita. Wao hawana urazini, siku zote wako katika hali ya taharuki, hawawezi kutangamana na watu kwa njia ya kawaida, ni kana kwamba wao hawashawishiki kwa lolote lile, na kuna jambo lililojitenga na lisilo lao. Watu kama hao wamepagawa na pepo mbaya au wanaye pepo mbaya anayefanya kazi ndani yao, na kazi yote ya pepo wabaya inajionyesha na si ya ulimwenguni humu. Hii ndiyo kazi inayotambulika kwa haraka zaidi kuhusu pepo wabaya. Wakati pepo mbaya anapompagaa mtu, anacheza nao kiasi cha kwamba wanaathirika kabisa. Wanakosa urazini, kama zuzu, hali ambayo inathibitisha kwamba kiini cha mambo ni kuwa, pepo wabaya ni pepo waovu wanaopotosha na kuteketeza watu. Matamko ya pepo wabaya ni rahisi kuyatambua: Matamko yao yanaonyesha kikamilifu kiini chao cha uovu, yapo palepale, yamevurugika, na yananuka, yanarishai harufu ya kifo. Kwa watu walio na uhodari mzuri, maneno ya pepo wabaya huwafanya kuhisi utupu na kutovutiwa, yasiyorekebisha maadili, yasiyo na chochote ila uongo na maneno yasiyo na maana, wanahisi wakiwa wamevurugika na wanaona ugumu kuelewa yote haya, kama zigo la upuuzi. Huu ni baadhi ya upuuzi unaotambulika kwa haraka zaidi kuhusu pepo wabaya. Kuwaroga watu, baadhi ya wale pepo wabaya wa "kiwango cha juu" hujifanya kuwa Mungu au Kristo wanapoongea, huku wengine wakijifanya kuwa malaika au watu maarufu. Wanapoongea, pepo hawa wabaya ni stadi katika kuiga maneno au kauli fulani za Mungu, au sauti ya Mungu, na watu wasiouelewa ukweli wanadanganywa kwa urahisi na pepo kama hawa wabaya wa "kiwango cha juu." Watu wa Mungu waliochaguliwa lazima wawe wazi kwamba, kiini cha mambo ni kwamba, pepo wabaya ni waovu na wasio na aibu, na hata kama wao ni pepo wabaya wa "kiwango cha juu," wao hawana ukweli kabisa. Pepo wabaya, zaidi ya yote, ni pepo wabaya, kiini cha pepo wabaya ni uovu, na wenye sampuli moja na Shetani.
kutoka kwa "Jinsi ya Kutambua Upumbavu na Uongo wa Roho Waovu, Makristo wa Uongo, na Wapinga Kristo" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (II)
Kila kitu ambacho pepo wabaya hufanya si cha ulimwenguni humu kabisa, wao huelekeza moja kwa moja watu kufanya hiki au kile, huwaamuru moja kwa moja kufanya hiki na kile, huwalazimisha kwa njia ya moja kwa moja kufanya mambo—haya ndiyo maonyesho ya kazi ya pepo wabaya. Kazi ya Roho Mtakatifu haijawahi kuwalazimisha watu kufanya hiki au kile, haijawahi kuwaamuru watu huku na kule, haijawahi kukosa kuwa ya ulimwenguni humu, haijawahi kutumia mbinu zisizo za ulimwenguni humu kuwaelekeza watu kufanya mambo, siku zote imefichwa ndani kabisa ya watu, na inawagusa kupitia kwa dhamiri yao ili kuwafanya kuuelewa ukweli na maneno ya Mungu, na baadaye hutumia dhamiri kuwafanya kuuweka ukweli ule katika matendo. Hii ndiyo mbinu ambayo Roho Mtakatifu hufanyia kazi. Roho Mtakatifu hajawahi kuwalazimisha wala kuwashurutisha watu, Hajawahi kufanya chochote kisicho cha ulimwenguni humu au chenye maonyesho, na Haelekezi watu waziwazi. Tunajua nini kutoka kwa haya? Tunajua kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni nyenyekevu na fiche, na hasa fiche, na hakuna yoyote yake imefichuliwa. Mungu ni mwenye kudura na anashikilia utawala dhidi ya vitu vyote, lakini Roho Mtakatifu hamwambii mwanadamu kwa njia ya moja kwa moja, "Aisee, unafaa kufanya hivi au vile." Roho Mtakatifu hajawahi kuchukua hatua namna hii; Yeye hukugusa, kwa kutumia upendo Yeye hukugusa, na Yeye ni mtulivu sana, kiasi cha kwamba huhisi kama mtu anakugusa—lakini kwenye kina cha moyo wako unahisi kwamba unafaa kuchukua hatua kwa njia fulani, na kwamba ni sahihi na bora kufanya hivyo. Tazama namna ambavyo Mungu alivyo mzuri! Tazama tena sura mbovu na ya kuhurumiwa ya wale waliopagawa na pepo wabaya, tazama ambavyo, pindi wanapokutana na watu, wanasema, "Leo roho amenielekeza kusema hivi, ameniambia kufanya vile, amenifanya kufanya hivi," angalia namna ambavyo wakati mwingine wanavyoamka kwenye usiku wa giza kueneza injili, au kuomba, au kusema namna ambavyo wameguswa na lazima watimize wajibu wao. Tazama namna, punde watu wanapofungwa na pepo mbaya, yeye huwasababishia mateso mabaya, na kuwafanya kusambaratika, tazama namna ambavyo hawajui ni lini watakula au kufanya mambo, namna ambavyo maisha yao yamebadilika na kuwa kombo. Wakati ambapo pepo wabaya wanafanya kazi ndani ya watu, wao huwazungusha huku na kule, na kuwaacha wakiwa wamechoka na hoi. Hatimaye, wanaambulia patupu: Hakuna mabadiliko katika tabia yao ya maisha, wangali bado wamepotoka kama walivyokuwa awali, wale ambao kwa kawaida walikuwa na majivuno na makuu wangali bado na majivuno na makuu, na wale waliokuwa wajanja na wakujitia mapuuza wangali wajanja na walewale wa kujitia mapuuza. Kazi ya pepo wabaya huwapotosha watu, na kuwaacha wakiwa si wa kawaida kiakili. Kutoka kwenye utaratibu wa utendaji wa pepo wabaya, tunaona tu namna ambavyo wana dharau, uovu, mapuuza, na ujinga. Hafanyi chochote ila kuwanyanyasa na kuwapotosha watu, kwa sababu ya haya wanachukiwa na kulaaniwa na watu, wanaosema kwamba wao ni wabaya. Hivyo, kazi ya pepo wabaya inamwakilisha Shetani—hakuna kosa katika haya. Yeyote aliyewaona watu ambao pepo wabaya hufanya kazi ndani yao, au wale waliopagawa na Shetani, anajua tu namna wanavyochukiza, walivyo na mapuuza, uovu, na walivyojaa upotovu. Je, mnayaona haya? Je, mnayaona baadhi yake, sivyo? Je, mmeona kwamba pepo wabaya wanaumiliki ukweli? Je, pepo wabaya wanao upendo wowote kwa wanadamu? Kutoka kwenye kazi ya pepo wabaya, inaweza kuonekana kwamba hawana ukweli hata kidogo, na kwamba asili yao ni ya uovu kabisa. Baada ya kuona namna ambavyo pepo wabaya wanavyowapotosha watu, umeona namna ambavyo Shetani hupotosha watu—ni ukweli kabisa. Kwa sababu pepo wote wabaya wanashirikiana na Shetani, kwani wote wanamfuata Shetani, na ndio washiriki, marafiki, na washirikishi wa Shetani, wamekuwa na Shetani tangu hapo zama za kale. Shetani aliwaongoza pepo hawa wote wabaya katika kuasi dhidi ya Mungu na akaangushwa hapa ulimwenguni. Je, pepo mbaya angeweza—pepo mbaya asiye na ukweli na mwenye kuasi kabisa Mungu katika asili yake—kuuleta ukweli wowote kwa mtu anapompagaa? Anaweza kuyaleta mabadiliko katika tabia zao? Bila shaka, la.
kutoka kwa "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)

Alhamisi, 13 Juni 2019

Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

2. Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu na mwanadamu hawawezi kuzungumziwa kama wa kulingana. Dutu ya Mungu na kazi Yake ni vitu visivyoeleweka na kufahamika kwa mwanadamu. Ikiwa Mungu hawezi kufanya kazi Yake binafsi na kuzungumza maneno Yake katika ulimwengu wa mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kuelewa mapenzi ya Mungu, na kwa hivyo, hata wale waliotoa maisha yao yote kwa ajili ya Mungu hawataweza kupata idhini ya Mungu. Bila kazi ya Mungu, haijalishi jinsi gani mwanadamu anatenda mema, haitahesabika kama chochote, kwa maana fikira za Mungu daima zitakuwa juu ya fikira za mwanadamu, na hekima ya Mungu haieleweki kwa mwanadamu. Na kwa hivyo Nasema kwamba wale ambao “wanaona kwa wazi” Mungu na kazi Yake ni wasioweza kufanikisha chochote, wao wote ni wenye kiburi na wapumbavu. Mwanadamu hafai kufafanua kazi ya Mungu; zaidi ya hayo, mwanadamu hawezi kufafanua kazi ya Mungu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu ni mdogo kushinda mchwa, kwa hivyo mwanadamu atawezaje kuelewa kazi ya Mungu? Wale wasemao daima, “Mungu hafanyi kazi kwa njia hii ama ile” au “Mungu yuko hivi ama vile”—je hawa wote si wenye kiburi? Tunafaa sote kujua kwamba watu, ambao ni wa mwili, wote wamepotoshwa na Shetani. Ni katika hali yao asili kumuasi Mungu, na hawako katika usawa na Mungu, sembuse kuweza kutoa mawaidha kwa kazi ya Mungu. Jinsi Mungu anavyomwelekeza mwanadamu ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mwanadamu anafaa kunyenyekea, na hafai kuwa na wazo hili ama lile, kwani mwanadamu ni mchanga tu. Kwa sababu tunajaribu kumtafuta Mungu, hatufai kuwekelea dhana zetu katika kazi ya Mungu ili Mungu Aziwaze, na zaidi hatufai kutumia tabia zetu potovu kwa kupinga kazi ya Mungu kwa makusudi. Je hili halitatufanya wapinga Kristo? Je, watu kama hawa watawezaje kusema kuwa wanamwamini Mungu? Kwa maana tunaamini kuwa kuna Mungu, na kwa maana tunatamani kumtosheleza na kumwona, tunapaswa kutafuta njia ya ukweli, na tunapaswa kutafuta njia ya kulingana na Mungu. Hatupaswi kuwa katika upinzani sugu kwa Mungu; Matendo kama haya yatakuwa na matokeo gani mazuri?
Leo hii, Mungu Anayo kazi mpya. Unaweza kuyakataa maneno haya, yanaweza kuhisi yasiyo ya kawaida kwako, lakini Nakushauri usifichue asili yako halisi, kwa maana wale tu walio na njaa ya kweli na kiu cha haki mbele za Mungu ndio wanaweza kupata ukweli, na wale wanaomcha Mungu kwa ukweli tu ndio wanaweza kupata nuru na kuongozwa na Mungu. Hakuna litakalotoka kwa kutafuta ukweli kupitia ugomvi. Ni kwa kutafuta kwa utulivu ndio tunaweza kupata matokeo. Ninaposema kwamba “Leo, Mungu Anayo kazi mpya,” Ninaashiria Mungu kurudi katika mwili. Pengine huyajali maneno haya, pengine unayachukia, au pengine una haja kubwa sana nayo. Haijalishi ni hali gani, Natumai kuwa wote walio na tamaa ya kweli ya kuonekana kwa Mungu wataweza kuukabili ukweli huu na kutafakari juu yake kwa makini. Ni vyema usiamue jambo upesi bila kuzingatia suala zima. Hivi ndivyo watu wenye hekima wanapaswa kutenda.
kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili
Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe kawaida na wenye kutojali katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?
kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa “Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.” Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani! Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulinganishwa na fikira za mwanadamu, sembuse Mungu kuonekana kwa amri ya mwanadamu. Mungu hufanya uamuzi Wake mwenyewe na huwa na mipango Yake Afanyapo kazi; aidha, Ana malengo Yake, na mbinu Zake. Si lazima Ajadiliane kazi Azifanyazo na mwanadamu au Atafute ushauri wa mwanadamu, sembuse kumfahamisha kila mtu kuhusu kazi Yake. Hii ndiyo tabia ya Mungu na, zaidi ya hayo, inafaa kutambuliwa na kila mmoja. Kama mnatamani kushuhudia kuonekana kwa Mungu, kama mnatamani kufuata nyayo za Mungu, basi kwanza ni sharti mzishinde dhana zenu. Ni sharti muache kudai kuwa Mungu afanye hiki au kile sembuse kumweka Yeye ndani ya mipaka yenu wenyewe na kumwekea upeo kwa dhana zenu. Badala yake, mnafaa kujua ni vipi mtazitafuta nyayo za Mungu, na vipi mnapaswa kukubali kuonekana kwa Mungu na ni vipi mnapaswa kutii kazi mpya ya Mungu; hiki ndicho kinapaswa kufanywa na mwanadamu. Kwa kuwa mwanadamu si ukweli, na hamiliki ukweli, mwanadamu anafaa kutafuta, kukubali na kutii.
Bila kujali kama wewe ni Mmarekani, Mwingereza, au mtu wa taifa jingine, ni lazima utoke nje ya mipaka yako, ni lazima ujipite, na ni sharti uione kazi ya Mungu kama kiumbe wa Mungu. Kwa njia hii, hutaweka vikwazo katika nyayo za Mungu. Kwa sababu, leo, watu hufikiri kuwa haiwezekani Mungu kudhihirika katika nchi au taifa fulani. Umuhimu wa kazi ya Mungu una undani kiasi gani, na kuonekana kwa Mungu kuna maana ilioje! Vinawezaje kupimwa kwa dhana na fikira za mwanadamu? Na ndiyo maana Ninasema kuwa unafaa kujiondoa katika dhana za uraia wako au kabila lako unapokutafuta kuonekana kwa Mungu. Kwa njia hii, hutafungwa na dhana zako mwenyewe; kwa njia hii, utahitimu kukaribisha kuonekana kwa Mungu. Vinginevyo, daima utakuwa gizani na hutapata kibali cha Mungu.
kutoka katika “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu ni Mungu wa wanadamu wote. Hawi mali binafsi ya nchi au taifa lolote na hufanya kazi ya mpango Wake bila kuzuiwa na mfumo wowote, nchi au taifa. Labda hujawahi kuwazia mfumo huu, au labda wewe hukana kuwepo kwake, au labda nchi au taifa ambapo Mungu huonekana limebaguliwa na lina maendeleo duni sana duniani. Na bado Mungu ana busara Yake. Na uwezo Wake kupitia ukweli na tabia Zake kwa hakika Amepata kundi la watu wenye mawazo sawa na Yeye. Na Amepata kundi la watu ambao alitaka kutengeneza: kundi lililoshindwa Naye, watu ambao wameyavumilia majaribu machungu na aina zote za mateso na wanaweza kumfuata mpaka mwisho. Malengo ya kuonekana kwa Mungu, bila vizuizi vya nchi yoyote, ni kumruhusu Akamilishe kazi ya mpango Wake. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kutimiza kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kuwa mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu na hatimaye ikawa kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, na vilevile kukushutumu kuonekana huku; “kutowezekana” kwao kwa mara nyingine kunabana kuonekana kwa Mungu katika mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakicheka na kuanguka baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kukufuru kwa Wayahudi? Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama huwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? Mahali ambapo Mungu anajitokeza, kuna maonyesho ya kweli, na kuna sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Weka dhana zako kando. Tafakari na kusoma maneno haya kwa makini. Ukitamani ukweli, Mungu atakupa nuru ya kuyafahamu mapenzi Yake na maneno Yake. Wekeni kando mitazamo yenu ya “haiwezekani”! Kadiri watu wanavyozidi kuamini kuwa jambo fulani haliwezekani, ndivyo uwezekano wa utukiaji wake unavyoendelea kujiri, kwani ufahamu wa Mungu hupaa juu kuliko mbingu, mawazo ya Mungu yako juu ya yale ya mwanadamu, na kazi ya Mungu inapita mipaka ya fikira za mwanadamu. Kadiri kitu kinavyokuwa hakiwezekani, ndivyo kunavyokuwepo na ukweli wa kutafutwa; kadiri kitu kilivyo nje ya mipaka ya dhana na fikira za mwanaadamu, ndivyo kinavyozidi kuwa na mapenzi ya Mungu. Kwani bila kujali Mungu anajidhihirishia wapi, Mungu bado ni Mungu, na kiini chake hakitawahi kubadilika kwa sababu ya mahali ama namna ya kuonekana Kwake. Tabia ya Mungu hubaki kuwa vilevile bila kujali nyayo Zake ziko wapi. Bila kujali nyayo za Mungu zilipo, Yeye ndiye Mungu wa wanadamu wote. Kwa mfano, Bwana Yesu si Mungu tu wa Waisraeli, lakini vilevile ni Mungu wa watu wote wa Asia, Ulaya, na Marekani, na hata zaidi, ndiye Mungu pekee wa ulimwengu mzima. Hivyo basi, tuyatafute mapenzi ya Mungu na tugundue kuonekana Kwake kutoka kwa matamshi Yake na tufuate nyayo Zake. Mungu ndiye ukweli, njia na uzima. Maneno Yake na kuonekana Kwake yanakuwepo sawia, na tabia na nyayo Zake daima zitapatikana na wanadamu. Ndugu wapendwa, natumaini kwamba mnaweza kuona kuonekana kwa Mungu katika maneno haya, na kwamba mtaanza kuzifuata nyayo Zake kuelekea enzi mpya, na hadi katika mbingu mpya yenye kupendeza na dunia mpya iliyoandaliwa kwa wale wanaosubiri kuonekana kwa Mungu.
kutoka katika “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 11 Juni 2019

Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

5. Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Mwenyezi Mungu alisema,Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa. Kwa maneno mengine, usimamizi wa Mungu wa mwanadamu ulianza kutokana na kazi ya kumwokoa mwanadamu, na wala haukutokana na kazi ya kuiumba dunia. Hakungekuwa na kazi ya kumsimamia mwanadamu pasipo kuwepo na tabia potovu ya mwanadamu, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu ina sehemu tatu, badala ya hatua nne, au enzi nne. Hii tu ndio njia sahihi ya kutaja kazi ya Mungu ya usimamizi wa mwanadamu. Enzi ya mwisho itakapofikia kikomo, kazi ya kusimamia mwanadamu itakuwa imekamilika. Hitimisho la kazi ya usimamizi lina maana kuwa kazi ya kuwaokoa wanadamu wote imemalizika kabisa, na kwamba mwanadamu amefika mwisho wa safari yake. Pasipo kazi ya kuwaokoa wanadamu wote, kazi ya usimamizi wa wanadamu haingekuwapo, wala hakungekuwa na hatua tatu za kazi. Ilikuwa ni hasa kwa ajili ya upotovu wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu alihitaji wokovu kwa dharura, ndipo Yehova alikamilisha uumbaji wa dunia na kuanza kazi ya Enzi ya Sheria. Hapo tu ndipo kazi ya kumsimamia mwanadamu ilipoanza, kumaanisha kwamba hapo tu ndipo kazi ya kumwokoa mwanadamu ilipoanza. "Kumsimamia mwanadamu" haimaanishi kuongoza maisha ya mwanadamu aliyeumbwa upya duniani (ambapo ni kusema, mwanadamu ambaye bado hakuwa amepotoshwa). Badala yake, ni wokovu wa ubinadamu ambao umepotoshwa na Shetani, ambapo ni kusema kwamba, ni kubadilishwa kwa mwanadamu aliyepotoshwa. Hii ndiyo maana ya kumsimamia mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu haihusishi kazi ya kuiumba dunia, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu haijumuishi kazi ya kuumba ulimwengu, na inahusisha tu hatua tatu za kazi zilizo tofauti na uumbaji wa ulimwengu. Ili kuelewa kazi ya kumsimamia mwanadamu, ni muhimu kuwa na ufahamu wa historia ya hatua tatu za kazi—hili ndilo kila mtu anapaswa kulifahamu ili kuokolewa. Kama viumbe wa Mungu, mnapaswa kutambua kuwa mwanadamu aliumbwa na Mungu, na kufahamu chanzo cha upotovu wa mwanadamu, na, vilevile, kufahamu mchakato wa wokovu wa mwanadamu. Iwapo mnafahamu tu jinsi ya kutenda kulingana na mafundisho ili kupata neema ya Mungu, lakini hamna fununu jinsi Mungu anavyomwokoa mwanadamu, au ya chanzo cha upotovu wa mwanadamu, basi hili ndilo mnalokosa kama viumbe wa Mungu. Hupaswi kutoshelezwa tu na kuelewa kwa ukweli unaoweza kuwekwa katika vitendo, huku ukibakia kutojua upeo mpana wa kazi ya usimamizi ya Mungu—kama hivi ndivyo ilivyo, basi wewe ni mwenye kulazimisha kauli sana. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo hadithi ya ndani ya usimamizi wa Mungu wa mwanadamu, ujio wa injili ya dunia nzima, fumbo kubwa zaidi kati ya wanadamu, na pia ni msingi wa kueneza injili. Ukizingatia tu kuelewa ukweli sahili unaohusiana na maisha yako, na usijue lolote kuhusu hili, maajabu makuu zaidi na maono, basi maisha yako si ni sawa na bidhaa yenye kasoro, yasio na maana isipokuwa kuangaliwa?
Ikiwa mwanadamu huzingatia tu matendo, na kuona kazi ya Mungu na hekima ya mwanadamu kama za upili, basi si ni sawa na kuwa mwerevu kwa kiasi kidogo cha pesa na mjinga kwa kiasi kikubwa cha pesa? Lile ambalo sharti ulijue, lazima ulijue, na kile unachostahili kuonyesha kwa vitendo, lazima ukionyeshe kwa vitendo. Ni hapo tu ndipo utakapokuwa mtu anayejua kufuata ukweli. Siku yako ya kueneza injili itakapowadia, ikiwa utaweza kusema tu kuwa Mungu ni Mkuu na Mwenye haki, kuwa ni Mungu Mkuu, Mungu ambaye hapana mwanadamu yeyote mkuu anayeweza kujilinganisha naye, na kuwa hakuna aliye juu zaidi wa kumpiku..., kama waweza tu kusema maneno haya yasiyofaa na ovyo, na kabisa huwezi kunena maneno yenye umuhimu zaidi, na yaliyo na kiini, kama huna lolote la kusema kuhusu kumjua Mungu, ama kazi ya Mungu, na zaidi ya hapo, huwezi kuelezea ukweli, au kutoa kile ambacho kinakosekana kwa mwanadamu, basi mtu kama wewe hana uwezo wa kutekeleza wajibu wake vyema. Kumshuhudia Mungu na kueneza injili ya ufalme si jambo rahisi. Lazima kwanza uwe na ukweli, na maono yatakayoeleweka. Unapokuwa na uwazi wa maono na ukweli wa masuala tofauti tofauti ya kazi ya Mungu, moyoni mwako unapata kujua kazi ya Mungu, na bila kujali anayoyafanya Mungu—iwe ni hukumu ya haki ama kusafishwa kwa mwanadamu—unamiliki maono makuu kama msingi wako, na unamiliki ukweli sahihi wa kuonyesha kwa matendo, basi utaweza kumfuata Mungu hadi mwisho. Lazima ujue kuwa bila kujali kazi ambayo Yeye anatenda, lengo la kazi ya Mungu halibadiliki, kiini cha kazi Yake hakibadiliki, na mapenzi Yake kwa mwanadamu hayabadiliki. Bila kujali maneno Yake ni makali namna gani, haijalishi mazingira ni mabaya kiasi gani, kanuni za kazi Yake, na nia Yake ya kumwokoa mwanadamu hayatabadilika. Mradi tu si ufunuo wa mwisho wa mwadhamu au hatima ya mwanadamu, na si kazi ya awamu ya mwisho, au kazi ya kutamatisha mpango wote wa usimamizi, na mradi tu ni wakati Anapomfinyanga mwanadamu, basi kiini cha kazi Yake hakitabadilika: Daima kitakuwa wokovu wa mwanadamu. Hili linapaswa kuwa msingi wa imani yenu katika Mungu. Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu. Punde unapofahamu lengo la hatua hizi tatu za kazi, basi utafahamu jinsi ya kuthamini umuhimu wa kila hatua ya kazi, na utatambua jinsi ya kutenda ili kutosheleza shauku ya Mungu. Iwapo utaweza kufikia hatua hii, basi hili, ono kubwa kuliko yote, litakuwa msingi wako. Unapaswa kufuata sio tu njia rahisi za matendo, ama ukweli wenye undani, lakini unapaswa kuunganisha maono na matendo, ili kwamba kuwe na ukweli unaoweza kuwekwa kwenye vitendo, na maarifa yaliyo na msingi wa maono. Ni hapo tu ndipo utakapokuwa mtu anayefuatilia ukweli.
Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani ya hatua kuna maelezo ya tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu; wale wanaoshikilia tu imara mafundisho ya dini yanayosalia kutoka katika hatua moja ya kazi ni watu wanaomwekea Mungu mipaka kwa mafundisho ya dini, na wale ambao imani yao kwa Mungu haina udhahiri na uhakika . Watu kama hao kamwe hawawezi kupokea wokovu wa Mungu. Ni hatua tatu tu za Mungu zinazoweza kuonyesha kabisa ukamilifu wa tabia ya Mungu, na kuonyesha kabisa nia ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu wote, na mchakato mzima wa wokovu wa mwanadamu. Hili ni dhibitisho kuwa Yeye amemshinda Shetani na kumpata mwanadamu, ni dhibitisho la ushindi wa Mungu, na ni maonyesho ya tabia kamili ya Mungu. Wale wanaoelewa hatua moja tu kati ya hatua tatu za kazi ya Mungu wanajua tu sehemu ya tabia ya Mungu. Katika dhana ya mwanadamu, ni rahisi kwa hatua hii moja kuwa mafundisho ya kidini, panakuwa na uwezekano zaidi wa mwanadamu kuweka amri kumhusu Mungu, na mwanadamu anatumia hii sehemu moja ya tabia ya Mungu kama dhihirisho la tabia nzima ya Mungu. Zaidi ya hayo, mawazo mengi ya mwanadamu yanachanganywa ndani yake, hivi kwamba anaweka vikwazo imara kwa tabia, nafsi, na hekima ya Mungu, na pia kanuni za kazi ya Mungu ndani ya vigezo vyenye mipaka, akiamini kwamba ikiwa Mungu alikuwa hivi wakati mmoja, basi Yeye atasalia kuwa vile daima, na kamwe hatabadilika. Ni wale tu wanaojua na kuthamini hatua tatu za kazi ndio wanaoweza kumjua Mungu kabisa na kwa usahihi. Angalau, hawatamfafanua Mungu kama Mungu wa Waisraeli, ama Wayahudi, na hawatamwona kama Mungu atakayesulubiwa msalabani milele kwa ajili ya mwanadamu. Kama unapata kumjua Mungu kutokana na hatua moja ya kazi Yake tu, basi maarifa yako ni kidogo, kidogo sana. Maarifa yako ni sawa na tone moja katika bahari. Kama si hivyo, kwa nini wengi wa walinzi wa kidini wa kale walimtundika Mungu msalabani akiwa hai? Je, si kwa ajili mwanadamu humwekea Mungu mipaka kwenye vigezo fulani? Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasioona mbali, wanaojaribu kuonyesha tu jinsi walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha "wasomi" wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Je, watu hawa wana mantiki yoyote ya kuzungumzia? Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki? Leo, mnapaswa kuelewa umuhimu wenu wa kujua hatua tatu za kazi ya Mungu. Maneno Ninayosema yana manufaa kwenu, wala si mazungumzo ya bure. Mkikimbiza mambo, je, si bidii Yangu yote itakuwa kazi bure? Kila mmoja wenu anapaswa kujua asili yake. Wengi wenu wamebobea katika mabishano, majibu ya maswali ya nadharia yanatoka kinywani mwenu, lakini hamna la kusema kwa maswali kuhusu dutu. Hadi leo, bado mnashiriki mazungumzo duni, na hamuwezi kubadilisha asili yenu ya zamani, na wengi wenu hawana nia ya kubadilisha jinsi mnavyofuatilia ili kupata ukweli wa juu, mnaishi tu maisha yenu shingo upande. Je, watu kama hawa wataweza kumfuata Mungu hadi tamati vipi? Hata ikiwa mtafika mwishoni mwa safari, itakuwa na faida gani kwenu? Ni bora mbadili mawazo yenu kabla hamjachelewa, kufuatilia kwa kweli, au kufa moyo mapema. Muda unapokatika utakuwa kimelea doezi—je, mko radhi kutekeleza jukumu kama hili la hali ya chini na lenye aibu?
Hatua tatu za kazi ni rekodi ya kazi nzima ya Mungu, ni rekodi ya wokovu wa Mungu wa mwanadamu, na si porojo tu. Kama kweli mnataka kutafuta kujua tabia nzima ya Mungu, basi sharti mfahamu hatua tatu za kazi inayofanywa na Mungu, na, zaidi, sharti msiache hatua yoyote. Hiki ndicho kiwango cha chini kinachopaswa kufikiwa na wale wanaotafuta kumjua Mungu. Mwanadamu mwenyewe hawezi kuvumbua maarifa ya Mungu. Si kitu ambacho mwanadamu mwenyewe anaweza kufikiria, wala si matokeo ya fadhila za Roho Mtakatifu kwa mtu mmoja. Badala yake, ni maarifa yanayotokea mwanadamu anapopitia kazi ya Mungu, na ni maarifa ya Mungu yanayotokana tu na mwanadamu kupitia ukweli wa kazi ya Mungu. Maarifa kama haya hayawezi kutimizwa kwa ghafla, wala si jambo linaloweza kufundishwa. Inahusiana kabisa na uzoefu wa kibinafsi. Wokovu wa Mungu wa mwanadamu ndiyo kiini cha hatua hizi tatu za kazi, ilhali katika kazi ya wokovu kumejumuishwa mbinu kadhaa za kufanya kazi na namna ambazo tabia ya Mungu imeonyeshwa. Hili ndilo jambo gumu sana kwa mwanadamu kutambua na kwa mwanadamu kuelewa. Mgawanyiko wa enzi, mabadiliko ya kazi ya Mungu, mabadiliko katika eneo la kazi, mabadiliko ya wanaopokea kazi na kadhalika—haya yote yamejumuishwa katika hatua tatu za kazi. Hususan, tofauti katika njia ya utendakazi wa Roho Mtakatifu, na vilevile mabadiliko katika tabia ya Mungu, picha, jina, utambulisho, au mabadiliko mengine, yote ni sehemu ya hatua tatu za kazi. Sehemu moja ya kazi inaweza tu kuwakilisha sehemu moja, na imewekewa mipaka ndani ya wigo fulani. Haihusiani na mgawanyiko wa enzi, ama mabadiliko ya kazi ya Mungu, wala masuala mengine. Huu ni ukweli ulio waziwazi. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo ukamilifu wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu lazima ajue kazi ya Mungu, tabia ya Mungu katika kazi ya wokovu, na bila ukweli huu, maarifa yako kumhusu Mungu yatakuwa tu maneno matupu, ni mahubiri ya starehe tu. Maarifa kama haya hayawezi kumshawishi au kumshinda mtu, maarifa kama haya yako nje ya uhalisi, na si ukweli. Yanaweza kuwa mengi, na mazuri kwa masikio, lakini kama hayaambatani na tabia ya asili ya Mungu, basi Mungu hatakusamehe. Hatakosa kuyasifu maarifa yako tu, bali pia atakuadhibu kwa kuwa mwenye dhambi aliyemkufuru. Maneno ya kumjua Mungu hayazungumzwi kwa mzaha. Ingawa unaweza kuwa na ulimi laini wenye maneno matamu, na maneno yako yaweza kuwafufua wafu, na kuwaua walio hai, bado huna elimu ya kuzungumza kuhusu maarifa ya Mungu. Mungu si mtu ambaye unaweza kuhukumu kwa urahisi, ama kusifu bila mpango, ama kupaka tope bila kujali. Unamsifu mtu yeyote na watu wowote, ilhali unajitahidi kupata maneno sahihi ya kuelezea ukuu wa wema na neema za Mungu—hili ndilo mshindwa yeyote hujifunza. Ingawa kuna wataalam wengi wa lugha wanaoweza kumwelezea Mungu, usahihi wa kile wanachoelezea ni asilimia moja ya ukweli unaozungumzwa na watu wa Mungu na wana misamiati michache tu, ilhali wanamiliki tajriba yenye uzito. Basi inaweza kuonekana kuwa maarifa ya Mungu yapo katika usahihi na uhalisi, na wala si utumiaji mzuri wa maneno au misamiati mingi. Maarifa ya mwanadamu na maarifa ya Mungu kabisa hayahusiani. Somo la kumjua Mungu liko juu zaidi kuliko sayansi za asili za mwanadamu. Ni somo linaloweza kutimizwa tu na idadi ndogo sana ya watu wanaotafuta kumjua Mungu, na haliwezi kutimizwa na mtu yeyote tu mwenye kipaji. Na kwa hivyo lazima msione kumjua Mungu na kufuatilia ukweli kama kwamba kunaweza kupatikana na mtoto mdogo tu. Pengine umekuwa na mafanikio makuu katika maisha yako ya kifamilia, ama kazi yako, ama katika ndoa yako, lakini inapofika kwenye ukweli, na somo la kumjua Mungu, huna lolote la kujivunia, hujatimiza malengo yoyote. Kutia ukweli kwenye vitendo, inaweza kusemwa, ni jambo gumu kwenu, na kumjua Mungu ni tatizo kuu hata zaidi. Hili ni tatizo lenu, na pia ni tatizo linalokabiliwa na wanadamu wote. Kati ya wale wenye mafanikio katika kumjua Mungu, karibu wote hawajafikia kiwango. Mwanadamu hajui maana ya kumjua Mungu, ama kwa nini ni muhimu kumjua Mungu, ama kiasi gani kinahesabiwa kama kumjua Mungu. Hili ndilo linalomshangaza mwanadamu, na ni kitendawili kikubwa zaidi kinachokabiliwa na mwanadamu—na hakuna awezaye kujibu swali hili, ama aliye na hiari kujibu hili swali, kwa sababu, hadi leo, hamna katika wanadamu aliyefanikiwa katika kusomea kazi hii. Pengine, kitendawili cha hatua tatu za kazi kitakapotambulishwa kwa mwanadamu, kutakuwepo katika mfululizo kundi la watu wenye vipaji wanaomjua Mungu. Bila shaka, Natumaini kuwa hivyo ndivyo ilivyo, na, hata zaidi, Niko katika harakati ya kutekeleza kazi hii, na Ninatumaini kuona kujitokeza kwa vipaji zaidi kama hivi katika siku za hivi karibuni. Watakuwa wale wanaoshuhudia ukweli wa hatua hizi tatu za kazi, na, bila shaka, watakuwa pia wa kwanza kushuhudia hizi hatua tatu za kazi. Kama kutakuwa na aliye na vipaji hivi, siku ambayo kazi ya Mungu itafikia kikomo, ama kuwe na wawili ama watatu, na kibinafsi wamekubali kufanywa wakamilifu na Mungu mwenye mwili, basi hakuna jambo la kuhuzunisha na kujutia kama hili—ingawa ni katika hali mbaya zaidi tu. Kwa vyovyote vile, Ninatumai kuwa wale wote wanaotafuta kwa kweli wanaweza kupata baraka hii. Tangu mwanzo wa wakati, hakujawahi kuwa na kazi kama hii, hapo awali hakujawahi kuwa na kazi kama hii katika historia ya ukuaji wa mwanadamu. Kama kweli unaweza kuwa mmoja wa wale wa kwanza wanaomjua Mungu, je, si hii itakuwa heshima ya juu kuliko viumbe wote? Je, kuna kiumbe mwingine kati ya wanadamu anayeweza kusifiwa na Mungu zaidi? Kazi kama hii ni ngumu kutekeleza, lakini mwishowe bado itapokea malipo. Bila kujali jinsia yao ama uraia wao, wale wote wenye uwezo wa kufikia maarifa ya Mungu, mwishowe, watapokea heshima kuu ya Mungu, na watakuwa tu wenye kumiliki mamlaka ya Mungu. Hii ndiyo kazi ya leo, na pia ndiyo kazi ya siku za usoni; ni ya mwisho na ya juu zaidi kuwahi kutekelezwa katika miaka 6000 ya kazi, na ni njia ya kufanya kazi inayodhihirisha kila kundi la mwanadamu. Kupitia kazi ya kumfanya wanadamu kumjua Mungu, daraja tofauti za mwanadamu zinadhihirishwa: Wale wanaomjua Mungu wamehitimu kupokea baraka za Mungu na kukubali ahadi zake, wakati wale wasiomjua Mungu hawajahitimu kupokea baraka za Mungu wala kupokea ahadi zake. Wale wanaomjua Mungu ni wandani wa Mungu, na wale wasiomjua Mungu hawawezi kuitwa wandani wa Mungu; wandani wa Mungu wanaweza kupokea baraka zozote za Mungu, lakini wale wasio wandani wa Mungu hawastahili kazi yoyote Yake. Iwe ni dhiki, usafishaji, ama hukumu, yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu hatimaye kufikia maarifa ya Mungu na ili kwamba mwanadamu amtii Mungu. Hii ndiyo athari pekee itakayofikiwa hatimaye. Hakuna lolote katika hatua tatu za kazi lililofichwa, na hii ni faida kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu, na humsaidia mwanadamu kupata maarifa kamili na mengi ya Mungu. Kazi hii yote ni ya kumfaidi mwanadamu.
Kazi ya Mungu Mwenyewe ni maono ambayo mwanadamu lazima afahamu, kwa kuwa kazi ya Mungu haiwezi kutekelezwa na mwanadamu, wala haimilikiwi na mwanadamu. Hatua tatu za kazi ndizo ukamilifu wa usimamizi wa Mungu, na hakuna ono kuu kuliko hili linalopaswa kufahamika kwa mwanadamu. Kama mwanadamu hafahamu maono haya makuu, basi si rahisi kumjua Mungu, na si rahisi kujua mapenzi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, njia ambayo mwanadamu anapitia inazidi kuwa ngumu. Bila maono, mwanadamu hangeweza kufika umbali huu. Ni maono ambayo yamemlinda mwanadamu hadi leo, na ambayo yamempa mwanadamu ulinzi mkuu. Katika siku za usoni, maarifa yenu lazima yawe ya kina, na sharti mfahamu mapenzi Yake yote na umuhimu wa kazi Yake yenye busara katika hatua tatu za kazi. Hiki tu ndicho kimo chenu cha kipekee. Hatua ya kazi ya mwisho haisimami peke yake, ila ni sehemu ya yote iliyounganishwa pamoja na hatua mbili za awali, ambayo ni kusema kwamba haiwezekani kukamilisha kazi nzima ya wokovu kwa kufanya kazi ya hatua moja pekee. Ingawa hatua ya mwisho ya kazi inaweza kumwokoa mwanadamu kabisa, hii haimaanishi kwamba ni muhimu tu kutekeleza hatua hii pekee, na kwamba hatua mbili za hapo awali hazihitajiki kumwokoa mwanadamu kutokana na ushawishi wa Shetani. Hakuna hatua moja kati ya zote tatu inayoweza kuwekwa kama maono ya kipekee ambayo lazima yajulishwe mwanadamu, kwa kuwa ukamilifu wa kazi ya wokovu ni hatua tatu za kazi, wala si hatua moja kati ya tatu. Ilimradi kazi ya wokovu bado haijakamilishwa, usimamizi wa Mungu utashindwa kufikia kikomo. Nafsi ya Mungu, tabia, na hekima zimeonyeshwa katika ukamilifu wa kazi ya wokovu, wala hazikufichuliwa kwa mwanadamu hapo mwanzo, lakini zimeonyeshwa hatua kwa hatua katika kazi ya wokovu. Kila hatua ya kazi ya wokovu huonyesha sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya nafsi Yake: si kila hatua ya kazi inayoweza moja kwa moja kuonyesha kabisa na kwa ukamilifu nafsi ya Mungu. Kwa hivyo, kazi ya wokovu inaweza tu kuhitimishwa hatua tatu za kazi zitakapokamilika, na kwa hivyo, maarifa ya mwanadamu ya ukamilifu wa Mungu hayawezi kutenganishwa na hatua tatu za kazi ya Mungu. Kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa hatua moja ya kazi ni tabia ya Mungu inayoonyeshwa katika sehemu moja ya kazi yake tu. Haiwezi kuwakilisha tabia na nafsi inayoonyeshwa katika hatua ya awali na ijayo. Hii ni kwa sababu kazi ya kumwokoa mwanadamu haiwezi kumalizika mara moja katika kipindi kimoja, ama katika eneo moja, lakini hukuwa kwa kina hatua kwa hatua kulingana na kiwango cha kukua kwa mwanadamu katika wakati na maeneo tofauti. Ni kazi inayofanywa hatua kwa hatua, na haikamilishwi katika hatua moja. Na kwa hiyo, hekima yote ya Mungu imejumuishwa katika hatua tatu, badala ya hatua moja. Nafsi yake yote na hekima yake yote zimewekwa wazi katika hatua hizi tatu, na kila hatua ina nafsi Yake, na ni rekodi ya hekima ya kazi Yake. Mwanadamu anapasa kujua tabia yote ya Mungu iliyoonyeshwa katika hatua hizi tatu. Nafsi hii ya Mungu ndiyo ina maana zaidi kwa wanadamu wote, na ikiwa watu hawana maarifa haya wanapomwabudu Mungu, basi hawana tofauti na wale wanaoabudu Budha. Kazi ya Mungu kati ya wanadamu haijafichiwa mwanadamu, na inapaswa kujulikana na wale wote wanaomwabudu Mungu. Kwa sababu Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi ya wokovu kati ya wanadamu, mwanadamu anapaswa kujua maonyesho ya kile ambacho anacho na alicho wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Hili ndilo ambalo ni lazima lifanywe na mwanadamu. Kile ambacho Mungu anamfichia mwanadamu ni kile ambacho mwanadamu hawezi kutimiza, na kile ambacho mwanadamu hapaswi kujua, ilhali yale Mungu anayomfunulia mwanadamu ni yale ambayo mwanadamu anapaswa kujua na yale ambayo mwanadamu anapaswa kumiliki. Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, tofauti na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ina kina kuliko iliyopita. Kila hatua inaendelea kutoka kwa msingi wa hatua ya mwisho ambayo haiondolewi. Kwa njia hii, katika kazi Yake ambayo daima huwa mpya na kamwe si kuukuu, Mungu mara kwa mara anaonyesha kipengele cha tabia yake ambayo hayajawahi kuonyeshwa kwa mwanadamu hapo awali, na daima anamfichulia mwanadamu kazi Yake mpya, na nafsi Yake mpya, na hata ikiwa wazoefu wakongwe wa kidini hufanya juu chini kukinzana na hili, na kulipinga waziwazi, Mungu daima hufanya kazi mpya ambayo anakusudia kufanya. Kazi Yake daima hubadilika, na kwa sababu hili, daima inakabiliwa na upinzani wa mwanadamu. Na hivyo, pia, tabia Yake inabadilika daima, na vilevile enzi na wanaopokea kazi Yake. Zaidi ya hayo, kila mara Yeye hufanya kazi ambayo haijawahi kufanywa tena, hata kufanya kazi ambayo huonekana kwa mwanadamu kuhitilafiana na kazi iliyofanywa awali, kuwa kinyume nayo. Mwanadamu anaweza kukubali tu aina moja ya kazi, ama njia moja ya matendo. Ni vigumu kwa wanadamu kukubali kazi ama njia za matendo, ambayo yanakinzana nao, ama yaliyo juu kuwaliko—lakini Roho Mtakatifu daima anafanya kazi mpya, na kwa hivyo kunakuwepo kikundi baada ya kikundi cha wataalamu wa kidini wanaoipinga kazi mpya ya Mungu. Watu hawa wamekuwa wataalamu hasa kwa sababu mwanadamu hana maarifa ya jinsi Mungu huwa mpya wala hazeeki, na zaidi ya hayo, hana maarifa ya kanuni za kazi ya Mungu, na hata zaidi hawana maarifa ya njia nyingi ambazo Mungu humwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, mwanadamu kabisa anashindwa kueleza kama ni kazi inayotoka kwa Roho Mtakatifu, au ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Watu wengi hushikilia mtazamo ambao, kama inalingana na maneno yanayokuja kabla, basi wanaweza kuikubali, na kama kuna tofauti na kazi ya awali, basi wanaipinga na kuikataa. Leo, je, nyote hamjafuata katika kanuni hizi? Hatua tatu za kazi ya wokovu hazijakuwa na athari kubwa kwenu, na kuna wale wanaoamini kuwa hatua mbili zilizopita za kazi ni mzigo usiohitaji kufahamika. Wanafikiria kuwa hatua hizi hazifai kutangazwa kwa umati na zinafaa kufutwa haraka iwezekanavyo, ili watu wasihisi kwamba wamezidiwa na hatua mbili za awali za zile hatua tatu za kazi. Wengi wanaamini kuwa kupeana ufahamu kuhusu hatua mbili zilizopita ni hatua ya mbali sana, wala haina faida katika kumjua Mungu—hivyo ndivyo mnavyofikiria. Leo, nyote mnaamini kuwa ni haki kutenda vile, lakini siku itawadia ambapo mtagundua umuhimu wa kazi Yangu: Mjue kuwa Sifanyi kazi yoyote ambayo haina umuhimu. Kwa sababu Ninawatangazia hatua tatu za kazi, kwa hivyo lazima ziwe na faida kwenu; kwa sababu hatua hizi tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, kwa hivyo lazima ziwe lengo la kila mmoja duniani. Siku moja, nyote mtagundua umuhimu wa kazi hii. Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; utu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, Ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, asili yako ya zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo "mtaji" ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotevu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.
Ni katika kuweka dhana zako za kale kando tu ndipo utakapoweza kupata maarifa mapya, ilhali maarifa ya zamani si lazima yawe dhana za zamani. "Dhana" inamaanisha vitu vinavyodhaniwa na mwanadamu ambavyo viko mbali na uhalisi. Kama maarifa ya zamani yalikuwa yamepitwa na wakati katika enzi ya kale, na yalimzuia mwanadamu kuingia katika kazi mpya, basi maarifa kama yale pia ni dhana. Ikiwa mwanadamu ataweza kuchukua mwelekeo mzuri kwa maarifa kama yale, na anaweza pata kumjua Mungu kutoka kwa vipengele tofauti, kuunganisha ya zamani na mapya, basi maarifa ya kale yatamsaidia mwanadamu, na yatakuwa msingi wa mwanadamu kuingia katika enzi mpya. Funzo la kumjua Mungu linahitaji kwamba uwe stadi wa kanuni nyingi: jinsi ya kuingia kwenye njia ya kumjua Mungu, ukweli gani unapasa kuelewa ili kumjua Mungu, na jinsi ya kufanya dhana zako na asili yako ya asili kutii mipango yote ya kazi mpya ya Mungu. Ukitumia kanuni hizi kama msingi wa kuingia kwenye somo la kumjua Mungu, basi maarifa yako yatakuwa na kina zaidi na zaidi. Kama una maarifa wazi ya hatua tatu za kazi—ambapo ni kusema kwamba, ya mpango mzima wa usimamizi wa Mungu—na ikiwa utaweza kupatanisha hatua mbili za awali na hatua ya sasa, na unaweza kuona kwamba ni kazi iliyofanywa na Mungu Mmoja, basi utakuwa na msingi imara zaidi. Hatua tatu za kazi zilifanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo. Ingawa hatua tatu za kazi ya Mungu zimefanywa katika enzi tofauti na maeneo tofauti, na ingawa kazi ya kila moja ni tofauti, yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kati ya maono yote, hili ndilo kuu zaidi ambalo mwanadamu anapaswa kulijua, na ikiwa litaeleweka kabisa na mwanadamu, basi ataweza kusimama imara. Leo, tatizo kuu linaloyakumba madhehebu yote na vikundi vya dini ni kwamba hayajui kazi ya Roho Mtakatifu, na hayana uwezo wa kutofautisha kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi isiyo ya Roho Mtakatifu—na kwa hivyo hawawezi kueleza kama hatua hii ya kazi, kama hatua mbili za awali, pia zimefanywa na Yehova Mungu. Ingawa watu wanamfuata Mungu, wengi hawawezi kueleza kama ni njia sahihi. Mwanadamu anahofia ikiwa hii ndiyo njia inayoongozwa na Mungu Mwenyewe , na kama Mungu kupata mwili ni jambo la hakika, na watu wengi bado hawana dokezo jinsi ya kupambanua ikifikia maneno kama haya. Wale wanaomfuata Mungu hawawezi kujua njia, na kwa hivyo habari zinazozungumzwa zinaathiri sehemu ndogo tu kati ya watu hawa na hayana uwezo wa kufaa kikamilifu, na kwa hivyo, hili basi linaathiri maisha ya watu kama hawa. Ikiwa mwanadamu anaweza kuona katika hatua tatu za kazi kuwa zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe wakati tofauti, katika maeneo tofauti, na kwa watu tofauti, basi mwanadamu ataona kuwa,[a] ingawa kazi ni tofauti, yote imefanywa na Mungu mmoja. Kwa kuwa ni kazi ambayo imefanywa na Mungu mmoja, basi lazima iwe sawa, na bila dosari, na ingawa halingani na dhana za mwanadamu, hakuna kupinga kuwa ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Ikiwa mwanadamu anaweza kusema kwa hakika kuwa ni kazi ya Mungu mmoja, basi dhana zake zitakuwa duni, na ambazo hazifai kutajwa. Kwa sababu maono ya mwanadamu hayako wazi, na mwanadamu anamjua Mungu tu kama Yehova, na Yesu kama Bwana, na ana mitazamo miwili kumhusu Mungu mwenye mwili wa leo, watu wengi wamejitoa kwa ajili ya kazi ya Yehova na Yesu, na wamezingirwa na dhana kuhusu kazi ya leo, watu wengi daima huwa na shaka na hawachukulii kazi ya leo kwa makini. Mwanadamu hana uelewa kuhusu hatua mbili za mwisho, ambazo hazikuonekana. Hili ni kwa sababu mwanadamu haelewi uhalisi wa hatua mbili za mwisho kazi, na wala hakuzishuhudia binafsi. Ni kwa sababu haziwezi kuonekana ndiyo mwanadamu anawaza jinsi anavyopenda; bila kujali atakayodhania, hakuna ukweli wa kudhibitisha, na yeyote wa kurekebisha. Mwanadamu anaruhusu silika yake ya asili itawale, huku akikosa kujali na kuachilia mawazo yake yaende popote, kwa kuwa hakuna ukweli wa kudhibitisha, na kwa hivyo dhana za mwanadamu zinakuwa "ukweli," bila kujali kama zina dhibitisho. Kwa hivyo mwanadamu anaamini Mungu wake aliyemuwazia akilini mwake, na hamtafuti Mungu wa uhalisi. Ikiwa mtu mmoja ana aina moja ya imani, basi kati ya watu mia moja kuna aina mia moja za imani. Mwanadamu ana imani kama hizi kwa maana hajaona uhalisi wa kazi ya Mungu, kwa sababu amesikia tu kwa masikio yake na hajaona kwa macho yake. Mwanadamu amesikia hekaya na hadithi —lakini amesikia kwa nadra kuhusu maarifa ya ukweli ya kazi ya Mungu. Ni katika dhana zao ndivyo watu ambao wamekuwa waumini kwa mwaka mmoja tu wanaamini Mungu, na hilo ni kweli pia kwa wale ambao wamemwamini Mungu katika maisha yao yote. Wale ambao hawawezi kuona ukweli daima hawawezi kuepuka imani ambayo wana dhana kwazo kumhusu Mungu. Mwanadamu anaamini kuwa amejiweka huru kutokana na vifungo vya dhana zake za kale, na ameingia eneo jipya. Je, mwanadamu hajui kuwa maarifa ya wale wasioweza kuona uso wa kweli wa Mungu kuwa ni dhana na tetesi? Mwanadamu anafikiria kuwa dhana zake ni sawa, na wala hayana kasoro, na hufikiri kuwa hizi dhana zimetoka kwa Mungu. Leo, mwanadamu anaposhuhudia kazi ya Mungu, anaachilia dhana zilizokuwa zimeongezeka kwa miaka mingi. Mawazo na dhana za awali zinakuwa vizuizi vya kazi ya hatua hii, na inakuwa vigumu kwa mwanadamu kuachana na dhana kama hizo na kupinga mawazo kama yale. Dhana kuhusu kazi hii ya hatua kwa hatua ya wengi wa wale wanaomfuata Mungu hadi leo zimekuwa ya kuhuzunisha na watu hawa wamefanya uadui wa kikaidi na Mungu mwenye mwili hatua kwa hatua, na chanzo cha chuki ni mawazo na dhana za mwanadamu. Ni hasa kwa sababu ukweli haumruhusu mwanadamu kuwa na uhuru wa hiari ya mawazo yake, na, zaidi ya hayo, hauwezi kupingwa na mwanadamu kwa urahisi, na mawazo na dhana za mwanadamu hazistahimili uwepo wa ukweli, na hata zaidi ya hayo, kwa sababu mwanadamu hawezi kufikiria kuhusu usahihi na unyofu wa ukweli, na kwa nia moja tu huachilia mawazo yake, na hutumia dhana yake, kwamba dhana na mawazo ya mwanadamu zimekuwa adui wa kazi ya leo, kazi ambayo haiambatani na dhana za mwanadamu. Hili linaweza kusemwa kuwa kasoro ya dhana za mwanadamu, na wala si dosari ya kazi ya Mungu. Mwanadamu anaweza kufikiria lolote atakalo, lakini hawezi teta kwa ajili ya hatua yoyote ya kazi ya Mungu au hata sehemu yoyote; ukweli wa kazi ya Mungu hauwezi kukiukwa na mwanadamu. Unaweza kuruhusu mawazo yako yatawale, na unaweza pia kujumuisha hadithi nzuri kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, lakini kamwe huwezi kupinga ukweli wa kila hatua ya kazi ya Yehova na Yesu; hii ni kanuni, na pia ni amri ya utawala, na mnapaswa kuelewa umuhimu wa masuala haya. Mwanadamu anaamini kuwa hatua hii ya kazi hailingani na dhana za mwanadamu, na hivi sivyo katika hatua mbili zilizopita za kazi. Katika mawazo yake, mwanadamu anaamini kuwa kazi ya hatua mbili zilizopita kwa hakika si sawa na kazi ya leo—lakini je, umewahi kufikiria kuwa kanuni zote za kazi ya Mungu ni sawa, na kuwa kazi Yake huwa vitendo daima, na kuwa, bila kujali enzi, daima kutakuwa na halaiki ya watu wanaokataa na kuupinga ukweli wa kazi Yake? Wale wote ambao leo wanakataa na kuipinga hatua hii ya kazi bila shaka wangempinga Mungu wakati uliopita, kwa kuwa watu kama hawa daima watakuwa adui za Mungu. Watu wanaoujua ukweli wa kazi ya Mungu wataona hatua tatu za kazi kama kazi ya Mungu mmoja, na watatupilia mbali dhana zao. Hawa ni watu wanaomjua Mungu, na watu kama hawa ndio kwa kweli humfuata Mungu. Wakati ambapo usimamizi mzima wa Mungu utakaribia kufika mwisho, Mungu ataweka vitu vyote kulingana na aina. Mwanadamu aliumbwa kwa mikono ya Muumba, na mwishowe lazima kabisa amrudishe mwanadamu chini ya utawala Wake; huu ndio mwisho wa hatua tatu za kazi. Hatua ya kazi ya siku za mwisho, na hatua mbili zilizopitwa katika Israeli na Yudea, ni mpango wa Mungu wa usimamizi katika dunia nzima. Hakuna anayeweza kupinga hili, na ni ukweli wa kazi ya Mungu. Ingawa watu hawajapata uzoefu ama kushuhudia kazi zake nyingi, ukweli unabaki kuwa ukweli, na hauwezi kukanwa na mwanadamu yeyote. Watu wanaomwamini Mungu katika nchi zote duniani watakubali hatua tatu za kazi. Kama wajua tu hatua moja ya kazi, na huelewi hatua nyingine mbili za kazi, na huelewi kazi ya Mungu katika wakati uliopita, basi huwezi kuongea ukweli wa mpango mzima wa usimamizi wa Mungu, na maarifa yako ya Mungu yameegemea upande mmoja, kwa kuwa katika imani yako katika Mungu humfahamu, ama kumwelewa, na kwa hivyo hustahili kutoa ushuhuda wa Mungu. Bila kujali kama maarifa yako ya sasa ya mambo haya yana kina kirefu ama cha juujuu tu, mwishowe, lazima muwe na maarifa, na ushawishike kabisa, na watu wote wataona uzima wa kazi ya Mungu na kunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Mwishoni mwa kazi hii, madhehebu yote yatakuwa moja, viumbe wote watarejea chini ya utawala wa Muumba, viumbe wote watamwabudu Mungu mmoja wa kweli, na madhehebu yote yatakuwa bure, na hayataonekana tena.
Mbona mfululizo huu wa marejeo yanayohusu hatua tatu za kazi? Kupita kwa enzi, maendeleo ya kijamii, na uso wa asili unaobadilika yote hufuata mabadiliko katika hatua tatu za kazi. Mwanadamu hubadilika kwa wakati na kazi ya Mungu, na wala hakui peke yake mwenyewe. Kutajwa kwa hatua tatu za kazi ya Mungu ni kwa ajili ya kuleta viumbe wote, na watu kutoka dini zote, chini ya utawala wa Mungu mmoja. Bila kujali wewe ni wa dini gani, mwishowe nyote mtanyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu anayeweza kufanya kazi hii; haiwezi kufanywa na kiongozi yeyote wa kidini. Kuna dini kadhaa kuu duniani, na kila moja ina kichwa, ama kiongozi, na wafuasi wameenea katika nchi tofauti tofauti na maeneo yote duniani; kila nchi, iwe ndogo au kubwa, ina dini tofauti tofauti ndani yake. Hata hivyo, bila kujali ni dini ngapi zilizo duniani, watu wote wanaoishi duniani mwishowe wanaishi katika uongozi wa Mungu mmoja, na uwepo wao hauongozwi na viongozi wa kidini au vichwa. Ambayo ni kusema kwamba wanadamu hawaongozwi na kiongozi yeyote wa kidini ama kiongozi; badala yake wanadamu wote wanaongozwa na Muumba, aliyeziumba mbingu na nchi, na vitu vyote, na ambaye aliwaumba wanadamu—na huu ni ukweli. Hata ingawa dunia ina dini kadhaa kuu, bila kujali jinsi zilivyo kuu, zote zipo chini ya utawala wa Muumba, na hakuna inayoweza kuzidi wigo wa mamlaka hii. Maendeleo ya wanadamu, maendeleo ya kijamii, maendeleo ya sayansi ya asili—kila moja haitengani na mipango ya Muumba, na kazi hii sio kitu kinachoweza kufanywa na uongozi fulani wa dini. Viongozi wa dini ni viongozi tu wa dini fulani, na hawawezi kuwakilisha Mungu, ama Yule aliyeziumba mbingu na nchi na vitu vyote. Viongozi wa kidini wanaweza kuongoza wale wote walio katika dini yote, lakini hawawezi kuamrisha viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu—huu ni ukweli uliokubalika ulimwenguni. Viongozi wa dini ni viongozi tu, na hawawezi kuwa sawa na Mungu (Muumba). Vitu vyote vi mikononi mwa Muumba, na mwishowe vyote vitarejea mikononi mwa Muumba. Mwanadamu kiasili aliumbwa na Mungu, na haijalishi dini, kila mtu atarejea katika utawala wa Mungu— hili haliwezi kuepukika. Ni Mungu tu Aliye Juu Zaidi kati ya vitu vyote, na mtawala mkuu kati ya viumbe wote lazima pia warejee chini ya utawala Wake. Bila kujali mwanadamu ana hadhi ya juu kiasi gani, hawezi kumfikishwa mwanadamu kwenye hatima inayomfaa, wala hakuna anayeweza kuainisha kila kitu kulingana na aina. Yehova mwenyewe alimuumba mwanadamu na kumwainisha kila mmoja kulingana na aina na siku ya mwisho itakapowadia bado Atafanya kazi Yake Mwenyewe, kuanisha kila kitu kulingana na aina—hili haliwezi kufanywa na mwingine isipokuwa Mungu. Hatua tatu za kazi ambazo zilifanywa tangu mwanzo hadi leo zote zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe, na zilitekelezwa na Mungu mmoja. Ukweli wa hatua tatu za kazi ni ukweli wa uongozi wa Mungu kwa wanadamu wote, ukweli ambao hakuna anayeweza kuupinga. Mwishoni mwa hatua tatu za kazi, vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina na kurejea chini ya utawala wa Mungu, kwa kuwa duniani kote kuna Mungu mmoja tu, na hakuna dini nyingine. Yule asiyeweza kuiumba dunia hataweza kuiangamiza, ilhali Yule aliyeumba dunia hakika ataiangamiza, na kwa hivyo, kama mtu hana uwezo wa kutamatisha enzi na ni wa kumsaidia mwanadamu kukuza akili zake tu, basi hakika hatakuwa Mungu, na hakika hatakuwa Bwana wa mwanadamu. Hataweza kufanya kazi kuu kama hii; kuna mmoja tu anayeweza kufanya kazi kama hii, na wote wasioweza kufanya hii kazi hakika ni adui wala si Mungu. Kama ni madhehebu, basi hawalingani na Mungu, na kama hawaligani na Mungu basi wao ni adui za Mungu. Kazi yote inafanywa na huyu Mungu mmoja wa kweli, na ulimwengu mzima unatawaliwa na huyu Mungu mmoja. Bila kujali kama anafanya kazi Uchina ama Israeli, bila kujali kama kazi inafanywa na Roho ama mwili, yote hufanywa na Mungu Mwenyewe, na haiwezi kufanywa na mwingine yeyote. Ni kabisa kwa sababu Yeye ni Mungu wa wanadamu wote ndiyo kwamba Yeye hufanya kazi kwa njia ya uhuru, pasipo kuwekewa masharti yoyote—na haya ndiyo maono makuu zaidi. Kama kiumbe wa Mungu, kama ungependa kutekeleza jukumu la kiumbe wa Mungu na kuelewa mapenzi ya Mungu, lazima uelewe kazi ya Mungu, lazima uelewe mapenzi ya Mungu kwa viumbe, lazima uelewe mpango wake wa usimamizi, na lazima uelewe umuhimu wote wa kazi Anayofanya. Wale wasioelewa hivi hawajahitimu kuwa viumbe wa Mungu! Kama kiumbe wa Mungu, kama huelewi ulikotoka, huelewi historia ya mwanadamu na kazi yote iliyofanywa na Mungu, na, hata zaidi, huelewi jinsi mwanadamu ameendelea hadi leo, na huelewi ni nani anayeamuru wanadamu wote, basi huna uwezo wa kutekeleza wajibu wako. Mungu amemwongoza mwanadamu hadi leo, na tangu alipomuumba mwanadamu duniani hajawahi kumwacha. Roho Mtakatifu daima haachi kufanya kazi, hajawahi kuacha kumwongoza mwanadamu, na hajawahi kumwacha. Lakini mwanadamu hatambui kuwa kuna Mungu, pia hamjui Mungu, na je, kuna jambo la kufedhehesha zaidi kuliko hili kwa viumbe wote wa Mungu? Mungu binafsi humwongoza mwanadamu, lakini mwanadamu haelewi kazi ya Mungu. Wewe ni kiumbe wa Mungu, ilhali huelewi historia yako mwenyewe, na wala hujui ni nani aliyekuongoza katika safari yako, hutambui kazi iliyofanywa na Mungu, na kwa hivyo huwezi kumjua Mungu. Ikiwa hujui sasa, basi hutawahi kuhitimu kutoa ushuhuda kwa Mungu. Leo, Muumba binafsi huwaongoza watu wote kwa mara nyingine, na kuwafanya watu wote kuona hekima yake, uweza, wokovu, na kustaajabisha kwake. Ilhali bado hujatambua au kuelewa—na kwa hivyo, je, si wewe ndiwe utakayekosa kupokea wokovu? Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa. Wale wasioyaelewa mapenzi ya Mungu na hawaitambui kazi ya Mungu hawawezi kupata maarifa ya Mungu, na watu kama hawa hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu. Kama ungependa kumshuhudia Mungu, basi lazima umjue Mungu, na maarifa ya Mungu yanapatikana kwa kupitia kazi ya Mungu. Kwa ufupi, kama ungependa kumjua Mungu, basi lazima ujue kazi ya Mungu: Kufahamu kazi ya Mungu ndilo jambo la umuhimu kabisa. Hatua tatu za kazi zitakapofikia tamati, patafanyika kundi la watu wanaomshuhudia Mungu, kundi la wale wanaomjua Mungu. Watu hawa wote watamjua Mungu na wataweza kuonyesha ukweli kwa matendo. Watakuwa na utu na hisia, na wote watajua hatua tatu za kazi ya wokovu ya Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo itatekelezwa mwishowe, na watu hawa ndio dhihirisho la kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi, na ndio ushuhuda wenye nguvu zaidi kwa kushindwa kwa Shetani. Wale wanaoweza kumshuhudia Mungu wataweza kupokea ahadi na baraka za Mungu, na litakuwa ndilo kundi litakalosalia pale mwisho kabisa, lile linalomiliki mamlaka ya Mungu na lililo na ushuhuda wa Mungu. Pengine wale kati yenu wanaweza wote kuwa sehemu ya kundi hili, ama pengine nusu tu, ama wachache tu —inategemea radhi yenu na ufuatiliaji wenu.
Kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili