Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumanne, 30 Aprili 2019

Adabu Takatifu Ambayo Waumini wa Mungu Wanapasa Kuwa Nayo

4. Adabu Takatifu Ambayo Waumini wa Mungu Wanapasa Kuwa Nayo

Maneno Husika ya Mungu:
Ni nini kinashirikishwa ndani ya ubinadamu wa kawaida? Utambuzi, hisia, dhamiri na tabia. Iwapo unaweza kufanikisha ukawaida katika kila mojawapo ya vipengele hivi, ubinadamu wako uko katika kiwango kinachostahili. Unapaswa kuwa na mfanano wa binadamu wa kawaida na utende kama anayemwamini Mungu. Sio lazima ufikie viwango vya juu zaidi au kujishughulisha na diplomasia. Unapaswa tu kuwa mwanadamu wa kawaida, na hisia za kawaida za mtu, uweze kung’amua vitu, na kwa kiwango cha chini uonekane kama mwanadamu wa kawaida. Hiyo itakuwa imetosha. Kila kitu kinachohitajika kwako leo kiko katika uwezo wako, na huku si kukulazimisha ufanye kadri ya uwezo wako hata kidogo. Hakuna maneno yasiyo na maana au kazi isiyofaa yatakayotekelezwa kwako. Uovu wote ulioonyeshwa au kufichuliwa katika maisha yako lazima uondolewe. Ninyi mmepotoshwa na Shetani na mna sumu nyingi sana za Shetani. Yote ambayo yanahitajika kwako ni kuiepuka tabia hii potovu ya kishetani, si wewe kuwa mtu mwenye cheo cha juu, au mtu maarufu au mkuu. Hii haina maana. Kazi ambayo imefanyika kwenu inaafikiana na kile ambacho ni cha asili kwenu. Kuna mipaka ya kile Ninachohitaji kutoka kwa watu. Ikiwa watu wa leo wote wangeombwa kutenda kama watu wa kada za Kichina, na kujizoeza toni ya sauti ya kada za Kichina, kujifunza katika namna ya kuzungumza ya viongozi wa serikali wenye cheo cha juu, au kujifunza kwa namna na sauti ya kuzungumza ya waandishi wa insha na waandishi wa riwaya, basi hili halingekubalika pia. Halingeweza kufikiwa. Kwa mujibu wa ubora wa tabia zenu, mnapaswa angalau kuweza kuzungumza kwa hekima na busara na kuelezea mambo wazi. Ni wakati huo ndipo mtakapoyatosheleza mahitaji. Kwa kiwango kidogo sana, utambuzi na hisia vinapaswa kufikiwa. Kwa sasa jambo kuu ni kuitupilia mbali tabia potovu ya kishetani. Lazima uutupilie mbali uovu unaouonyesha. Ikiwa hujavitupilia mbali hivi, unawezaje kugusia hisia na utambuzi wenye mamlaka mkubwa kabisa? Watu wengi wanaona kwamba enzi imebadilika. Hivyo hawajizoezi unyenyekevu au uvumilivu wowote, na pengine pia hawana upendo wowote au mwenendo mwema wa kitakatifu pia. Watu hawa ni wajinga mno! Je, wana kiwango chochote cha ubinadamu wa kawaida? Je, wanao ushuhuda wowote wa kuzungumziwa? Hawana utambuzi na hisia zozote kamwe. Bila shaka, vipengele fulani vya utendaji wa watu vilivyopotoka na vyenye makosa vinapaswa kurekebishwa. Kama vile maisha ya watu ya kiroho yasiyopindika ya zamani au mwonekano wao wenye ganzi na upumbavu—vitu hivi vyote vinapaswa kubadilika. Mabadiliko hayamaanishi kukuruhusu uwe mpotovu au kujiingiza katika mwili, kusema chochote utakacho. Kuzungumza kiholela hakuwezi kukubalika. Kutenda kama mwanadamu wa kawaida ni kuzungumza kwa kueleweka. Ndiyo inamaanisha ndiyo, na la inamaanisha la. Kuwa mwenye ukweli kwa uhakika na uzungumze inavyofaa. Usilaghai, usidanganye. Inapaswa kujulikana ni mipaka gani mtu wa kawaida anaweza kufikia kuhusu mabadiliko ya tabia. Ikiwa hiyo haijulikani, hutaweza kuingia katika uhalisi.
kutoka katika “Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika tabia za watu wa kawaida hakuna uhalifu au udanganyifu, watu wana uhusiano wa kawaida kati yao, hawafanyi mambo pekee yao, na maisha yao si duni wala ya kufifia. Kwa hiyo, vilevile, Mungu huinuliwa miongoni mwa wote, maneno Yake hupenya miongoni mwa wanadamu, watu huishi katika amani kati yao na chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, dunia imejaa upatanifu, bila kuingilia kwa Shetani, na utukufu wa Mungu huwa na umuhimu mkuu sana miongoni mwa wanadamu. Watu kama hao ni kama malaika: watakatifu, wa kusisimua, wasiolalamika kamwe kuhusu Mungu, na hutoa juhudi zao zote kwa utukufu wa Mungu duniani pekee.
kutoka katika “Sura ya 16” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Nina matamanio mengi. Natamani mweze kutenda kwa njia inayofaa na yenye mwenendo mzuri, muwe waaminifu kutimiza wajibu wenu, muwe na ukweli na ubinadamu, muwe watu ambao wanaweza kuacha vitu vyote na kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu, na mengineyo. Matumaini haya yote yanatokana na upungufu wenu na upotovu na kutotii kwenu.
kutoka katika “Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu ambao Mungu hutumia huonekana kwa nje kama watu wasio na akili na huonekana kama wasio na uhusiano wa kawaida na wengine, ingawa wao huzungumza na adabu, hawazungumzi kiholela, na wanaweza daima kuwa na moyo uliotulia mbele ya Mungu. Lakini ni mtu wa aina hiyo tu ndiye anatosha kutumiwa na Roho Mtakatifu. Mtu huyu asiye na akili anayezungumziwa na Mungu anaonekana kama asiye na uhusiano wa kawaida na wengine, na hana upendo wa kuelekea nje au matendo ya juu juu, lakini anapokuwa akieleza mambo ya kiroho anaweza kufungua roho yake na kwa kujinyima awatolee wengine mwangaza na nuru ambayo amepata kutoka kwa uzoefu wake wa hakika mbele za Mungu. Hivi ndivyo anavyodhihirisha upendo wake kwa Mungu na kuridhisha mapenzi ya Mungu. Wengine wote wanapokuwa wanamkashifu na kumdhihaki, ana uwezo wa kutoelekezwa na watu wa nje, matukio, au vitu, na bado anaweza kutulia mbele za Mungu. Mtu wa aina hii inavyooneka yuko na utambuzi wake mwenyewe wa pekee. Bila kujali wengine, moyo wake kamwe haumwachi Mungu. Wengine wanapokuwa wakizungumza kwa furaha na kwa vichekesho, moyo wake bado unasalia mbele za Mungu, kutafakari neno la Mungu au kusali kwa kimya kwa Mungu aliye moyoni mwake, akitafuta makusudi ya Mungu. Kamwe hafanyi udumishaji wa uhusiano wao na wengine lengo lake la msingi. Mtu wa aina hii inavyoonekana hana falsafa ya maisha. Kwa nje, mtu huyu ni mchangamfu, anayependwa, asiye na hatia, lakini pia anamiliki hisia ya utulivu. Huu ni mfano wa mtu ambaye Mungu anamtumia. Mambo kama falsafa ya maisha au “mantiki ya kawaida” hayawezi kupenya kwa mtu wa aina hii; mtu wa aina hii ameutoa moyo wake wote kwa neno la Mungu, ambaye anaonekana kuwa na Mungu tu katika moyo wake. Hii ni aina ya mtu ambaye Mungu anamrejelea kama mtu “bila mantiki,” naye tu ni mtu ambaye anatumiwa na Mungu. Alama ya mtu ambaye anatumiwa na Mungu ni: Haijalishi ni lini au wapi, moyo wake daima uko mbele za Mungu, na haijalishi jinsi gani wengine ni wenye anasa, jinsi gani wanavyoshiriki katika tamaa, wanajiingiza katika anasa za kimwili—moyo wake kamwe haumwachi Mungu, naye hafuatani na umati. Aina hii ya mtu pekee ndiye anafaa kwa ajili ya matumizi ya Mungu, naye hasa ni yule ambaye amekamilika na Roho Mtakatifu. Ikiwa huwezi kufikia hatua hii, basi hustahili kupatwa na Mungu, ili kukamilishwa na Roho Mtakatifu.
kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kufaa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu ambao wana ukweli ni wale ambao, katika matukio wanayopitia ya kweli, wanaweza kusimama imara katika ushuhuda wao, kusimama imara katika nafasi zao, kusimama katika upande wa Mungu, bila kurudi nyuma, na ambao wanaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na watu wanaompenda Mungu, wale ambao, mambo yakishawatokea, wanaweza kumtii Mungu kabisa, na wanaweza kumtii Mungu hadi kifo. Matendo na ufunuo wako katika maisha halisi ndio ushuhuda wa Mungu, ni kuishi kwa kudhihirisha maisha ya mwanadamu na ushuhuda wa Mungu, na huku ni kufurahia upendo wa Mungu; unapopitia hadi kiwango hiki, matukio unayopitia yatakuwa yamekuwa na athari. Watu ambao wameuona upendo wa Mungu kwa kweli ni wale ambao wanaishi kwa kudhihirisha kwa kweli, ambao kila matendo yao yanapongezwa na wengine, ambao sura yao haipendezi lakini wanaoishi kwa kudhihirisha maisha ya utiifu wa hali ya juu, ambao wanawasiliana kwa karibu maneno ya Mungu na huelekezwa na Mungu, na kupata nuru kutoka kwa Mungu, ambao huweza kuongea mapenzi ya Mungu katika maneno yao, na wanawasiliana kwa karibu uhalisi, ambao huelewa zaidi kuhusu kuhudumu katika Roho, wanaongea kwa wazi, ambao ni wenye heshima na kuaminika, ambao hawakabiliki na wana tabia nzuri, ambao wanaweza kutii mipango ya Mungu na kusimama imara katika ushuhuda wakati mambo yanapowatokea, ambao wana utulivu bila kujali wanachokumbana nacho. Watu wengine wangali wachanga, lakini wanatenda kama mtu mzima; wamekomaa, wana ukweli, wanapendwa na wengine—na hawa ndio watu ambao wana ushuhuda, na ndio udhihirisho wa Mungu.
kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Mtu anayemwamini Mungu kwa hakika atatekeleza angalau vipengele hivi vitano vya maisha ya kiroho kila siku: kusoma neno la Mungu, kumwomba Mungu, kuwa na ushirika kuhusu ukweli, kuimba nyimbo na sifa, na kutafuta ukweli katika kila kitu. Ikiwa pia una maisha ya mikutano, utakuwa na furaha kuu zaidi. Mtu akiwa na uwezo wa jumla wa kupokea, kumaanisha anaweza kuelewa dhamira za Mungu baada ya kusoma maneno ya Mungu yeye mwenyewe, ataweza kuelewa ukweli, na kujua jinsi ya kutenda kulingana na ukweli, basi inaweza kusemwa kwamba mtu wa aina hii atafaulu katika imani yake. Iwapo mtu hana maisha ya kiroho ya aina hii, au iwapo maisha yake ya kiroho ni yasiyofaa kupindukia na yanaonekana tu mara chache sana, basi mtu huyo ni muumini aliyechanganyikiwa. Waumini waliochanganyikiwa hawawezi kupata matokeo mazuri kutoka kutimiza jukumu lao. Kuamini katika Mungu bila kuishi maisha ya kiroho ni kuwa na imani kwa maneno pekee; kwa watu kama hao, hakuna Mungu mioyoni mwao, sembuse uchaji wowote wa Mungu. Wanawezaje kuwa na mfano wa binadamu wa kufaa?
…………
Kuna vitu 10 vya kuzingatiwa na kuingiwa inapofikia kwa jinsi mtu wa kufaa anastahili kuwa:
1. Fuata adabu, jua masharti, na uwaheshimu wazee na kuwajali wadogo.
2. Kuwa na hali ya maisha inayofaa; iliyo na manufaa kwako mwenyewe na kwa wengine.
3. Valia kwa namna ya heshima na nyoofu; mavazi ya ajabu au ya urembo yamepigwa marufuku.
4. Usiwahi, kwa sababu yoyote ile, kuomba pesa kutoka kwa ndugu, na usitumie vitu vya watu wengine kama ni jambo la kawaida tu.
5. Kukutana na watu wa jinsia tofauti lazima kuwe na mipaka; vitendo vinahitajika kuwa vya heshima na vinyoofu.
6. Usibishane na watu; jifunze kuwasikiliza wengine kwa uvumilivu.
7. Dumisha usafi mzuri, lakini kwa kuzingatia hali halisi.
8. Jihusishe katika ushirika na uhusiano wa kufaa na wengine, jifunze kuwaheshimu na kuwa mwenye kuwajali watu, na pendaneni.
9. Fanya kila uwezalo kuwasaidia wale walio na mahitaji; usiitishe au kukubali vitu kutoka kwa watu wengine.
10. Usiwaruhusu wengine wakuhudumie; usiwaruhusu wengine wafanye kazi unayofaa kuwa ukifanya mwenyewe.
Masharti kumi ya hapo juu yanafaa kuwa ya msingi yanayofuatwa na waumini wote katika maisha yao, yeyote anayevunja masharti haya ni wa tabia duni. Unaweza kusema kuwa haya ni masharti ya nyumba ya Mungu na wale wanaoyaasi mara kwa mara bila shaka watatupwa kando.
Wale wote wanaoutafuta ukweli pia wanahitaji kufuata mienendo kumi mizuri ya watakatifu wa kale. Watu wanaoweka katika vitendo mara kwa mara na kudumisha haya bila shaka watapata thawabu kubwa za binafsi. Ni yenye manufaa makubwa mno kwa wanadamu.

Kanuni kumi za kuambatana na adabu takatifu:

1. Fanya ibada za kiroho kila asubuhi kwa kusali na kusoma neno la Mungu kwa takriban nusu saa.

2. Tafuta madhumuni ya Mungu katika kila kitu kila siku ili uweze kuuweka ukweli katika matendo kwa usahihi zaidi.

3. Kuwa na ushirika na kila unayekutana naye, mkifunzana kutoka kwa uwezo wa kila mmoja ili nyote muweze kuendelea.

4. Kuwa na mtazamo wa matumaini kuhusu maisha, huku mara nyingi ikiimba nyimbo na sifa na utoe shukrani kwa ajili ya neema ya Mungu.

5. Usitegwe na dunia ya kilimwengu; jongea karibu na Mungu moyoni mwako kwa kawaida na usiingilie mambo ya wengine.

6. Weka hekima moyoni mwako na ukae mbali na uovu na sehemu zenye hatari.

7. Usibishane na watu, kuwa na ushirika kuhusu ukweli, na uelewane na wengine.

8. Kuwa radhi kufanya kila uwezalo kuwasaidia wengine, watulizie mashaka yao, na uwasaidie kutatua ugumu wao katika kuingia katika kumwamini Mungu.

9. Jifunze jinsi ya kutii wengine, usiwatawale watu na kuwalazimisha; waruhusu watu wapate faida kiasi katika kila kitu.

10. Mara nyingi mwabudu Mungu moyoni mwako, ukimwacha Awe na ukuu katika kila kitu na kumridhisha Yeye katika kila kitu.

Kanuni kumi za hapa juu za maisha na namna kumi za kuambatana na adabu takatifu yote ni vitu ambavyo watu wana uwezo wa kuvifanya. Watu wanaweza kuweka vitu hivi katika vitendo alimradi vinaeleweka na makosa ya mara kwa mara si magumu kusuluhisha. Bila shaka, watu fulani ambao ubinadamu wao ni mbaya zaidi wameondolewa katika hili.

kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ubinadamu wa kufaa huashiria hasa kuwa na dhamiri, mantiki, unyoofu na heshima. Dhamiri na mantiki zinajumuisha kuonyesha ustahimilivu, kuwa na uvumilivu kwa wengine, kuwa mwaminifu, kutendea watu kwa hekima, na kuwa na upendo wa kweli kwa ndugu. Hizi ndizo sifa tano ambazo binadamu wa kufaa lazima wawe nazo.

Sifa ya kwanza ni kuwa na moyo wa ustahimilivu. Unamaanisha haijalishi dosari tunazoona ndani ya ndugu zetu, tunafaa kuwatendea vema, tukionyesha uvumilivu na uelewa. Hatupaswi kuwatenga au kuwashambulia kwa maneno. Tunapoona dosari au upotovu ukijifichua ndani ya watu wengine, tunafaa kukumbuka kuwa huu ni wakati wa kazi ya Mungu ya wokovu, kwa hivyo ni jambo la kawaida kwa wateule wa Mungu kufichua upotovu, na tunapaswa kuelewa. Mbali na hayo, tunahitaji kuangalia upotovu wetu sisi wenyewe, si lazima kuwa tunafichua upotovu wa kiwango cha chini kuliko wa watu wengine. Tunapaswa kuchukulia jinsi wengine wanavyofichua upotovu jinsi tunavyochukulia wetu kabisa. Kwa njia hiyo, tunaweza kuwastahimili wengine. Iwapo huwezi kustahimili watu wengine inamaanisha kuna shida na mantiki yako; inathibitisha kwamba huelewi ukweli na hujui kazi ya Mungu. Kutojua kazi ya Mungu kunamaanisha nini? Ni kutojua kwamba kazi ya Mungu bado haijakamilika na kwamba binadamu bado anaishi katika wakati wa kazi ya Mungu ya wokovu—bado hatujafanywa kuwa kamili. Kwa hivyo, kila mtu bila kuzuilika atafichua upotovu. Sasa kila mtu anaufuatilia ukweli kwa njia inayofaa, akipata kuelewa upotovu wake mwenyewe, na kupitia neno la Mungu. Kila mtu yuko kwenye kipindi cha kuingia katika ukweli na bado hajapata ukweli kikamilifu. Ni wakati tu watu wanapopata ukweli ndio tabia ya maisha yao itaanza kubadilika. Watu wanapoelewa jambo hili watakuwa na busara ya mtu wa kawaida, na basi watawatendea wengine na busara pia. Ikiwa watu hawana busara hawatawatendea wengine kwa busara.

Sifa ya pili ni kuonyesha uvumilivu kwa wengine. Kuwa mstahimilivu tu hakutoshi; lazima pia uwe mvumilivu. Wakati mwingine unaweza kuwa mstahimilivu na mwenye kuelewa tu, lakini haiwezekani kuepuka ndugu fulani kufanya jambo linaloweza kukusononesha au kukukosea. Katika hali kama hizo ni rahisi kwa tabia potovu ya binadamu kulipuka, kwa sababu sote tunapenda kupigana na kulinda fahari yetu, na sisi sote ni wenye ubinafsi na bure. Hivyo mtu akisema kitu kinachokusononesha au kufanya kitu kinachokukosea, unafaa kuwa mvumilivu. Uvumilivu pia unajumuishwa katika mawanda ya busara. Watu watakuza uvumilivu tu ikiwa wana busara. Lakini tunawezaje kuwa wavumilivu? Ukitaka kuwa mvumilivu kwa wengine, unahitaji kwanza kuwaelewa, “kumaanisha bila kujali anayesema kitu kinachokusononesha, unafaa kutambua hili: Maneno yake yamenisononesha. Alichosema kilionekana kufunua udhaifu wangu na kilionekana kunilenga mimi. Ikiwa maneno yake yananilenga mimi, anamaanisha nini anapoyasema? Je, anajaribu kunidhuru? Je, ananiona mimi kama adui yake? Je, ananichukia? Je, analipiza kisasi dhidi yangu? Mimi sijamkosea, kwa hivyo majibu ya maswali haya hayawezi kuwa ndiyo.” Kwa kuwa hiyo ndiyo hali, basi haijalishi kile alichosema ndugu huyu, yeye hakuwa na madhumuni ya kukusononesha au kukutendea kama adui yake. Hilo ni bila shaka. Aliposema maneno haya alikuwa anadhihirisha tu yale ambayo binadamu wa kawaida hufikiri, alikuwa anashiriki juu ya ukweli, kujadili maarifa, kufichua upotovu wa watu, au kukubali hali yake mwenyewe ya upotovu; bila shaka hakuwa anamlenga mtu yeyote yule kwa kujua. Kwanza unamwelewa, kisha hasira yako inaweza kutoweka, halafu unaweza kupata uvumilivu. Wengine watauliza: “Mtu akinishambulia kwa kujua na anilenge, na aseme mambo haya kwa makusudi ya kufanikisha kusudi fulani, basi nitawezaje kuwa mvumilivu?” Unapaswa kuwa mvumilivu jinsi hii: “Hata mtu akinishambulia kwa makusudi, bado nafaa kuwa mvumilivu. Hii ni kwa sababu yeye ni ndugu yangu na sio adui yangu, na bila shaka sio ibilisi, Shetani. Haiwezi kuepukika kwamba ndugu watafichua upotovu kiasi na kuwa na makusudi fulani katika mioyo yao. Hii ni kawaida. Napaswa kuelewa, na ninafaa kuhisi maono yake na kuwa mvumilivu.” Unapaswa kuwaza kwa njia hii, kisha usali kwa Mungu na kusema: “Mungu, mtu fulani ametoka kuumiza fahari yangu. Siwezi kukubali aibu hii; kila mara nataka kuwa mwenye hasira na kumshambulia. Huu kwa hakika ni ufichuzi wa upotovu. Nilikuwa nikidhani kuwa nilikuwa na upendo kwa wengine, lakini sasa kwa kuwa maneno ya mtu fulani yamenichoma moyoni siwezi kuvumilia. Nataka kumrudishia pia. Nataka kulipiza kisasi. Uko wapi upendo wangu? Je, hii yote si ni chuki tu? Bado niko na chuki moyoni mwangu! Mungu, jinsi Ulivyo na huruma kwetu na kutusamehe sisi dhambi zetu ndio jinsi tunavyofaa kuwa na huruma kwa wengine. Hatufai kuwa na kisasi dhidi ya wengine. Mungu, tafadhali nikinge, Usiache asili yangu ilipuke. Natamani kukutii Wewe na niishi kwenye upendo Wako. Tunampinga na kumkataa Kristo na Mungu sana katika kila kitu tukifanyacho, lakini Kristo bado Anakuwa mvumilivu nasi. Mungu anafanya hatua hii ya kazi Yake kwa uvumilivu mkubwa na upendo. Je, Kristo Alilazimika kuvumilia mateso, fedheha na kashfa kiasi gani? Ikiwa Kristo Alivumilia hayo, basi kiasi kidogo cha uvumilivu tunaofaa kuwa nao si kitu! Uvumilivu wetu umepungukiwa sana ukilinganishwa na ule wa Kristo….” Mara unapoomba kwa njia hii utajisikia ni kama wewe ni mpotovu mno, asiye wa maana kabisa, aliyepungukiwa katika kimo kabisa, na huo ndio wakati ambapo hasira yako itazimwa. Hivyo ndivyo unavyoweza kufikia uvumilivu.

Sifa ya tatu ni kuwatendea watu kwa uaminifu. Kuwa waaminifu kwa watu kuna maana kwamba bila kujali tunachofanya, iwe ni kuwasaidia wengine au kutoa huduma kwa ndugu zetu au kushiriki kuhusu ukweli, lazima tuzungumze kutoka moyoni. Zaidi ya hayo, usihubiri kile ambacho hujafanya. Wakati wowote ndugu wanahitaji msaada wetu tunapaswa kuwasaidia. Tunapaswa kutimiza wajibu wowote tunaohitaji kuutimiza. Kuwa mwaminifu, wala si muongo au wa kujidai. … Bila shaka, kuwa mtu mwaminifu kunahitaji hekima kiasi wakati unaposhughulika na watu fulani. Ukiona kwamba mtu fulani si wa kutegemewa kwa sababu upotovu wake ni wa kina kabisa, kama huwezi kumbaini na hujui anachoweza kufanya, basi unahitaji kuwa mwenye hekima na uepuke kumweleza kila kitu. Kuwa mtu mwaminifu kunahitaji maadili. Usizungumze kwa upofu kuhusu mambo usiyofaa kuwa ukizungumzia. Zaidi ya hayo, kuwa mtu mwaminifu kunahitaji kuongea na mantiki na usahihi. Watu wengine wanasisitiza kutenda uaminifu na kumfungulia mtu moyo licha ya shughuli nyingi alizo nazo. Huko ni kuwa mtu mwaminifu vipi? Je, huu sio upumbavu? Kuwa mtu wa kweli ni kutokuwa mjinga. Kunahusu kuwa mwerevu, wa kawaida na wazi, na usiyedanganya. Lazima uwe wa heshima na mwenye busara. Uaminifu hujengwa juu ya msingi wa busara. Hii ndiyo maana ya kuwa mwaminifu wakati unaposhughulika na watu, na kuwa mtu mwaminifu. Bila shaka, jambo muhimu sana kuhusu kuwa mtu mwaminifu ni kuwa mwaminifu kwa Mungu. Je, si lingekuwa tatizo kubwa kama wewe ni mtu mwaminifu mbele ya watu wengine tu, lakini wewe si mwaminifu mbele ya Mungu na umdanganye Yeye? Mkitafuta kuwa watu waaminifu mbele ya Mungu, basi kwa kawaida mtakuwa waaminifu mbele ya wengine. Iwapo huwezi kufanya hivyo mbele ya Mungu, basi kwa kweli huwezi kufanya hivyo mbele ya watu wengine. Haijalishi ni kipengele kipi cha ukweli au ni kitu kipi chema ambacho unaingia, lazima kwanza ukifanye mbele ya Mungu. Punde ambapo umepata matokeo mbele ya Mungu, kwa kiasili utaweza kuishi kwa kukidhihirisha mbele ya watu wengine. Usijichoshe kufanya hiki au kile mbele ya wengine, lakini kisha bila kujali ufanye chochote unachotaka mbele ya Mungu. Hili halitakuwa sawa. Jambo muhimu zaidi ni kulifanya mbele ya Mungu, ambaye huwajaribu binadamu na kuchunguza mioyo yao. Una uhalisi kwa hakika ikiwa unaweza kupita jaribio hili mbele ya Mungu. Huna uhalisi ikiwa huwezi kupita jaribio hili mbele ya Mungu—hii ndiyo kanuni ya kutenda ukweli.

Sifa ya nne ni kutendea watu kwa hekima. Baadhi ya watu husema: “Je, kuelewana na ndugu kunahitaji hekima?” Ndiyo, kunahitaji, kwa sababu kutumia hekima hutoa hata manufaa makubwa zaidi kwa ndugu zako. Baadhi watauliza: “Je, si kutumia hekima kwa ndugu ni kuwa mwenye hila?” Hekima si hila. Badala yake, ni kinyume kabisa na hila. Kutumia hekima kuna maana ya kuwa makini kwa jinsi unavyozungumza na ndugu wakati kimo chao ni kidogo, ikija kuwa wao wasiweze kukubali kile unachosema. Pia, kwa watu wenye kimo kidogo, hasa wale ambao hawana ukweli, wanaofichua upotovu fulani na kuwa na tabia fulani za upotovu, kama wewe ni wa kawaida na wazi sana na uwaambie kila kitu, inaweza kuwa rahisi kwao kuwa na kitu dhidi yako au kukutumia vibaya. Hivyo, ni lazima kwa kadiri uchukue tahadhari kiasi na uwe na mbinu fulani unapozungumza. Hata hivyo, kuwa na tahadhari dhidi ya watu hakumaanishi kutowasaidia au kutokuwa na upendo kwao—kunamaanisha tu kutowaambia mara moja baadhi ya mambo muhimu kuhusu nyumba ya Mungu, na kushiriki tu ukweli kwao. Kama wanahitaji msaada wa kiroho katika maisha, kama wanahitaji ruzuku ya na ukweli, lazima tufanye kila kitu tuwezalo ili kuwakidhi katika suala hili. Lakini iwapo wanauliza kuhusu hili na lile kuhusu nyumba ya Mungu, au hili na lile kuhusu viongozi na wafanyakazi wake, basi hakuna haja ya kuwaambia. Ukiwaambia, kuna uwezekano watafichua habari hii na hii itaathiri kazi ya nyumba ya Mungu. Kwa maneno mengine, ikiwa ni kitu ambacho hawafai kujua au kitu ambacho hawana haja ya kujua, basi usiwaruhusu kujua kukihusu. Kama ni kitu ambacho wanapaswa kujua, basi fanya kila uwezalo kuwafanya wajue kukihusu, kwa uthabiti na bila shaka. Kwa hivyo ni mambo yapi wanayopaswa kujua? Ufuatiliaji wa ukweli ndio watu wanapaswa kujua: Ni ukweli upi wanaopaswa kuwa nao, ni vipengele vipi vya ukweli wanafaa kuelewa, ni majukumu yapi wanapaswa kutimiza, ni majukumu yapi yanawafaa wao kutimiza, ni jinsi gani wanafaa kutimiza majukumu hayo, jinsi ya kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, jinsi ya kuishi maisha ya kanisa—haya yote ni mambo ambayo watu wanapaswa kujua. Kwa upande mwingine, masharti na kanuni za nyumba ya Mungu, kazi ya kanisa na hali za ndugu zako haviwezi kuwekwa wazi kwa kawaida kwa watu wa nje wala wasioamini katika familia yako. Hii ni kanuni ambayo ni lazima ifuatwe tunapotumia hekima. Kwa mfano, hupaswi kamwe kuzungumza kuhusu majina ya viongozi wako au wanapoishi. Ukizungumza kuhusu mambo haya, huwezi kujua wakati habari hii inaweza kufikia masikio ya watu wa nje, na mambo yanaweza kuwa ya taabu sana kama yatapishwa kwa baadhi ya wapelelezi wabaya au maajenti wa siri. Hili linahitaji hekima, na hii ndiyo maana nasema kuwa na hekima ni muhimu. Zaidi ya hayo, unapokuwa wa kawaida na wazi, kuna mambo fulani ya binafsi ambayo huwezi tu kumwambia mtu yeyote. Unafaa kupima kimo cha ndugu zako ili uone kama, baada ya kuwaeleza, wanaweza kuwa waovu na wafanye utani kuhusu kile unachosema, wakikusababishia matatizo baada ya hayo mambo kusambazwa, na hili likaharibu heshima yako. Hii ndiyo maana kuwa wa kawaida na wazi pia kunahitaji hekima. Hicho ndicho kiwango cha nne ambacho binadamu sawa lazima wamiliki—kutendea watu kwa hekima.

Sifa ya tano ni kuwa na upendo wa kweli kwa ndugu ambao hakika wanaamini katika Mungu. Hii inahusisha utunzaji kiasi, msaada halisi, na roho ya huduma. Tunapaswa hasa kuwa na ushirika zaidi na hao ndugu wanaofuatilia ukweli, na kuwapa ruzuku zaidi. Haijalishi kama wao ni waumini wapya au wamekuwa waumini kwa miaka kadhaa. Kuna kanuni moja hasa ya maisha ya kanisa: Watunze hasa wale ambao wanafuatilia ukweli. Shiriki na wao zaidi, wape ruzuku zaidi, na uwanyunyizie zaidi ili waweze kusaidiwa kuinuka haraka iwezekanavyo, kuwasaidia wakue katika maisha yao haraka wawezavyo. Kwa wale ambao hawafuatilii ukweli, kama itakuwa wazi kuwa hawaupendi ukweli baada ya kipindi cha unyunyizaji, basi hakuna haja ya kuweka juhudi kubwa kwao. Si lazima kwa sababu tayari umeshafanya kila kitu kiwezekanacho kwa mwanadamu. Inatosha kuwa umetimiza wajibu wako. … Unahitaji kuona ni nani unapaswa kulenga kazi yako kwake. Je, Mungu atawakamilisha wale wasiofuatilia ukweli? Kama Roho Mtakatifu hatafanya hivyo, basi kwa nini watu waendelee kufanya hilo kwa upofu? Huelewi kazi ya Roho Mtakatifu ilhali daima umejiamini sana—je, huo si upumbavu na ujinga wa binadamu? Hivyo, toa usaidizi zaidi kwa ndugu ambao kwa kweli wanaufuatilia ukweli, kwa sababu wao ni vyombo vya wokovu wa Mungu na wateule Wake walioamuliwa kabla. Tukishiriki kuhusu ukweli mara nyingi na watu hawa kwa moyo mmoja na mawazo na kusaidiana na kupeana ruzuku, mwishowe sisi wote tutapata wokovu. Wewe unayasaliti mapenzi ya Mungu usipojiunga na watu hawa. … Wale walio ndani ya kanisa walio na ubinadamu unaofaa wanapaswa kujiweka miongoni mwa wale ambao wanafuatilia ukweli, waingiliane kwa amani na watu hawa, na kwa njia ya ufuatiliaji wa ukweli hatua kwa hatua kujitumia kwa ajili ya Mungu kwa moyo na mawazo sawa. Kwa njia hiyo, wale wanaofuatilia ukweli wataokolewa na wewe pia utaokolewa, kwa sababu Roho Mtakatifu anafanya kazi kati ya wale wanaofuatilia ukweli. …

Ushirika ambao tumetoka kuwa nao ni juu ya vipengele vitano ambavyo binadamu wa kawaida lazima wamiliki. Kama una sifa hizi zote tano, utaweza kuingiliana kwa amani na ndugu zako, utapata nafasi yako katika kanisa, na utatimiza wajibu wako kwa njia bora zaidi kadri ya uwezo wako.


kutoka katika “Jinsi ya Kujenga Maisha ya Kanisa na Maana ya Kujenga Maisha ya Kanisa” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha I

Jumatatu, 29 Aprili 2019

Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

6. Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Maneno Husika ya Mungu:

Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu! Mungu ana hamu ya mwanadamu kumpenda Yeye, lakini kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo kuteseka kwa mwanadamu huwa kwingi zaidi, na kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo majaribio ya mwanadamu huwa makubwa zaidi. Ikiwa unampenda Yeye, basi kila aina ya mateso yatakufika—na ikiwa humpendi, basi labda kila kitu kitaendelea kwa urahisi kwako, na kila kitu kinachokuzunguka kitakuwa kitulivu kwako. Unapompenda Mungu, utahisi kwamba mengi kandokando yako hayawezi kushindikana, na kwa sababu kimo chako ni kidogo sana utasafishwa; aidha, huwezi kumridhisha Mungu, na daima utahisi kwamba mapenzi ya Mungu ni ya juu sana, kwamba hayawezi kufikiwa na mwanadamu. Kwa sababu ya haya yote utasafishwa—kwa sababu kuna udhaifu mwingi ndani yako, na mengi yasiyoweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, utasafishwa ndani. Lakini lazima muone kwa dhahiri kwamba utakaso hutimizwa tu kupitia usafishaji. Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana.

kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Usivunjike moyo, usiwe dhaifu, Nitakufichulia. Njia ya kwenda kwa ufalme sio laini hivyo, hakuna kitu kilicho rahisi hivyo! Unataka baraka zije kwa urahisi rahisi, sivyo? Leo kila mtu atakuwa na majaribio machungu ya kukumbana nayo, vinginevyo moyo wa upendo ulio nao Kwangu hautakuwa wenye nguvu zaidi na hutakuwa na upendo wa kweli Kwangu. Hata kama ni hali ndogo tu, kila mtu lazima azipitie, ni kwamba tu zinatofautiana kwa kiwango fulani. Hali hiyo ni moja ya baraka Zangu, ni wangapi hupiga magoti mbele Yangu mara kwa mara kuomba baraka Yangu? Watoto wapumbavu! Wewe daima huhisi kwamba maneno machache ya bahati huhesabika kama baraka Yangu, lakini huhisi kuwa uchungu ni moja ya baraka Zangu. Wale wanaoshiriki katika uchungu Wangu bila shaka watashiriki utamu Wangu. Hiyo ni ahadi Yangu na baraka Zangu kwenu.

kutoka katika “Sura ya 41” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Wakati Mungu anafanya kazi ili kumsafisha mwanadamu, mwanadamu huteseka. Kadiri usafishaji wake ulivyo mkubwa, ndivyo upendo wake kwa Mungu ulivyo mkubwa zaidi na ndivyo nguvu za Mungu zinafichuliwa zaidi kwake. Kadiri usafishaji wa mwanadamu ulivyo wa kiwango cha chini, ndivyo upendo wake kwa Mungu ulivyo wa kiwango cha chini, na ndivyo nguvu za Mungu zinafichuliwa kwake kwa kiwango cha chini. Kadiri usafishaji wake na uchungu wake ulivyo mkubwa na zaidi yalivyo mateso yake, ndivyo upendo wake wa kweli kwa Mungu utakavyokuwa, ndivyo imani yake kwa Mungu itakavyokuwa ya kweli, na ndivyo maarifa yake ya Mungu yatakuwa ya kina. Katika uzoefu wako utaona kwamba wale ambao wanakabiliwa na usafishaji mkubwa na uchungu, na kushughulikiwa sana na kufundishwa nidhamu, wana upendo mkubwa kwa Mungu, na maarifa ya kina na elekevu ya Mungu. Wale ambao hawajapitia kushughulikiwa wanayo maarifa ya juu juu tu, na wanaweza tu kusema: “Mungu ni mzuri sana, Yeye huwapa watu neema ili waweze kumfurahia Yeye.” Kama watu wamepitia kushughulikiwa na kufundishwa nidhamu, basi hao wanaweza kuyazungumza maarifa ya kweli ya Mungu. Hivyo kazi ya Mungu katika mwanadamu ilivyo ya ajabu zaidi, ndivyo ilivyo ya thamani zaidi na ni muhimu zaidi. Kadiri inavyokosa kupenyeza kwako zaidi na kadiri isivyolingana na mawazo yako, ndivyo kazi ya Mungu inavyoweza kukushinda, kukupata, na kukufanya mkamilifu. Umuhimu wa kazi ya Mungu ni mkubwa sana! Kama Hangemsafisha mwanadamu kwa njia hii, kama Hangefanya kazi kulingana na njia hii, basi kazi ya Mungu haingekuwa na ufanisi na ingekuwa isiyo na maana. Hii ndiyo sababu ya umuhimu wa ajabu wa uteuzi Wake wa kundi la watu katika siku za mwisho. Hapo awali ilisemwa kuwa Mungu angelichagua na kulipata kundi hili. Kadiri ilivyo kuu kazi Anayofanya ndani yenu, ndivyo ulivyo mkubwa na safi upendo wenu kwa Mungu. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi, ndivyo mwanadamu anavyoweza kuonja hekima Yake na ndivyo maarifa ya mwanadamu Kwake yalivyo ya kina zaidi.

kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Lazima uvumilie mateso kwa ajili ya ukweli, lazima ujitoe kwa ajili ya ukweli, lazima uvumilie udhalilishaji kwa ajili ya ukweli, na kupata ukweli zaidi lazima upate mateso zaidi. Hili ndilo unalopaswa kufanya. Msitupilie mbali ukweli kwa ajili ya maisha ya amani ya familia, na lazima msiipoteze heshima na uadilifu wa maisha kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Unapaswa kufuata yote ambayo ni ya kupendeza na mema, na unapaswa kufuata njia katika maisha ambayo ni ya maana zaidi. Kama wewe unaishi maisha ya kishenzi, na wala hufuati malengo yoyote, je, si huko ni kupoteza maisha Yako? Ni nini unachoweza kupata kutoka kwa maisha ya aina hii? Unapaswa kuziacha starehe zote za mwili kwa ajili ya ukweli mmoja, na hupaswi kutupilia mbali ukweli wote kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Watu kama hawa hawana uadilifu au heshima; hakuna maana ya kuwepo kwao!

kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wakati ambapo tunapokea hukumu ya maneno ya Mungu, hatupaswi kuogopa mateso, wala hatupaswi kuogopa maumivu; sembuse kuogopa kwamba maneno ya Mungu yataumiza mioyo yetu. Tunapaswa kusoma matamshi Yake zaidi kuhusu jinsi Anavyotuhukumu na kutuadibu na kufichua asili zetu potovu, na tunapokuwa tukisoma maneno ya Mungu, tunapaswa kujilinganisha mara kwa mara dhidi ya maneno hayo. Tuna upotovu huu wote; sote tunaweza kulingana nao. … Kwanza lazima tujue kuwa haijalishi ikiwa maneno yoyote Yake yanavutia kuyasikia, ikiwa yanatufanya tuhisi uchungu au utamu—lazima tuyakubali yote. Tunapaswa kuwa na mtazamo huu juu ya maneno ya Mungu. Mtazamo huu ni wa aina gani? Je, ni mtazamo wa kumcha Mungu? Wa uvumilivu? Au, ni mtazamo wa kuteseka? Nitawaambia, si wowote kati ya hii. Katika imani yetu, lazima tusisitize kwa uthabiti kwamba maneno ya Mungu ndiyo ukweli. Kwa kuwa kweli ndiyo ukweli, tunapaswa kuyakubali kwa busara. Bila kujali ikiwa tunaweza kutambua au kukubali au la, mtazamo wetu wa kwanza kuelekea maneno ya Mungu unapaswa kuwa ule wa kukubali kabisa.

kutoka katika “Umuhimu na Njia ya Kufuatilia Ukweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Kumpenda Mungu kunahitaji utafutaji wa mapenzi ya Mungu katika mambo yote, na kwamba ujisaili wewe mwenyewe kwa kina jambo lolote likikutokea, kujaribu kujua mapenzi ya Mungu na kujaribu kuona mapenzi ya Mungu ni yapi katika suala hili, Anataka ufanikishe nini, na ni jinsi gani utayajali mapenzi Yake? Kwa mfano: jambo fulani linafanyika linalokutaka uvumilie hali ngumu, wakati huo unapaswa ufahamu ni nini mapenzi ya Mungu, na ni jinsi gani unapaswa kuyajali mapenzi ya Mungu. Usijiridhishe mwenyewe: Jiweke kando kwanza. Hakuna kitu kilicho duni kuliko mwili. Ni lazima udhamirie kumridhisha Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako. Katika mawazo kama hayo, Mungu atakupa nuru ya kipekee katika jambo hili, na moyo wako pia utapata faraja. Jambo lolote likikutendekea, liwe dogo au kubwa, ni sharti kwanza ujiweke pembeni na kuuona mwili kama kitu duni zaidi kuliko vitu vyote. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo unavyochukua uhuru zaidi; ukiuridhisha mara hii, wakati mwingine utataka zaidi, na jinsi hili linaendelea, ndivyo unapata kuupenda mwili hata zaidi. Mwili mara zote una tamaa kupita kiasi, mara zote mwili unakutaka uuridhishe, na kwamba uutosheleze kwa ndani, iwe ni katika chakula unachokula, unachokivaa, au kuwa na hasira katika matendo yako, au kuushawishi udhaifu na uzembe wako…. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo tamaa yake inaongezeka, na jinsi mwili unavyopotoka zaidi, hadi kufikia kiwango ambacho miili ya watu inahodhi dhana nzito, na kutomtii Mungu, na kujiinua, na kuanza kuishuku kazi ya Mungu. … Hivyo unafaa kuuasi mwili na usiutosheleze: “Mume wangu(mke), watoto, matarajio, ndoa, familia—hakuna hata moja kati ya haya ambalo ni la thamani! Moyoni mwangu mna Mungu pekee na nitajaribu kumridhisha Mungu kadiri ya uwezo wangu, na si kuuridhisha mwili.” Lazima uwe na azimio hili. Daima ukiwa na azimio hili, basi ukiuweka ukweli katika vitendo, na kujiweka kando, utaweza kufanya hivyo kwa juhudi kidogo.

kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iwapo utapata uzima mbele za Mungu, na namna hatima yako itakavyokuwa, inategemea uasi wako dhidi ya mwili utakuwa wa namna gani. Mungu amekuokoa, na kukuteua na kukuamulia kabla, bado ikiwa leo hauko radhi kumridhisha, hauko radhi kuuweka ukweli katika vitendo, hauko radhi kuuasi mwili wako kwa moyo umpendao Mungu kwa dhati, hatimaye utajiangamiza mwenyewe, na kwa hivyo utapitia mateso mengi. Ikiwa mara zote unautosheleza mwili, Shetani atakumeza hatua kwa hatua, na kukuacha bila uzima, au upako wa Roho, hadi siku itafika ambayo ndani utakuwa giza. Ukiishi katika giza, utakuwa umetekwa nyara na Shetani, hutakuwa na Mungu tena moyoni mwako, na wakati ule utaukataa uwepo wa Mungu na kumwacha. Kwa hivyo, ikiwa unataka kumpenda Mungu, ni lazima ulipe gharama ya uchungu na kupitia shida. Hakuna haja ya hamasa za nje na shida, kusoma zaidi na kuzungukazunguka zaidi; badala yake, unafaa kuweka kando vitu vilivyomo ndani yako: mawazo kupita kiasi, maslahi ya kibinafsi, na masuala yako binafsi, dhana, na motisha. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.

kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu huwagusa watu ndani ya mioyo yao, na kuwapa nuru na mwangaza. Kwa hivyo katika tukio lolote katika vita: Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie. Kwa sababu motisha nyingi ndani ya watu zina makosa, ama kwa sababu kazi kubwa ya Mungu inakinzana na dhana zao, watu wakiuweka ukweli katika vitendo vita vikali huzuka kisirisiri. Baada ya kuuweka huu ukweli katika vitendo, kisirisiri watu watakuwa wamemwaga machozi mengi sana ya huzuni kabla ya kuamua kumridhisha Mungu. Ni kwa sababu ya vita hivi watu huvumilia shida na usafishaji; huku ni kuteseka kwa kweli. Vita vikikukabili, kama unaweza kusimama kweli upande wa Mungu, utaweza kumridhisha. Kuteseka katika harakati ya kutenda ukweli hakuepukiki; ikiwa, wanapoweka ukweli katika vitendo, kila kitu ndani yao kingekuwa sawa, basi wasingehitaji kufanywa wakamilifu na Mungu, na kusingekuwa na vita, na hawangeteseka. Ni kwa sababu kuna mambo mengi ndani ya watu ndipo hawafai kutumiwa na Mungu, na tabia nyingi za uasi wa mwili, ndipo watu wanapaswa kujifunza funzo la kuasi dhidi ya mwili kwa kina zaidi. Huku ndiko Mungu anaita kuteseka ambako Alimtaka mwanadamu kushiriki Naye.

kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika imani yao kwa Mungu, kile ambacho watu hutafuta ni kupata baraka kwa ajili ya siku zijazo; hili ndilo lengo lao katika imani yao. Watu wote wana kusudi na tumaini hili, lakini upotovu ulio katika asili yao lazima uondolewe kupitia majaribu. Katika hali ambazo bado hujatakaswa, hizi ndizo hali ambamo lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili uweze kujua upotovu wako mwenyewe. Hatimaye, unafika hatua ambapo unaona heri kufa na kuziacha njama na tamaa zako, na kutii mamlaka na mipango ya Mungu. Kwa hiyo, kwa yeyote ambaye hana miaka kadhaa ya usafishaji na hajapitia kiwango fulani cha mateso, hataweza kujiondolea vifungo vya upotovu wa mwili katika mawazo na mioyo yake. Katika hali zozote zile ambazo bado ungali mtumwa wa Shetani, na katika hali zozote zile ambazo bado ungali na tamaa zako mwenyewe na matakwa yako mwenyewe, hizi ndizo hali ambamo unapaswa kuteseka. Ni kupitia mateso tu ndio watu wanaweza kupata mafunzo, kupata ukweli, na kuelewa mapenzi ya Mungu. Kwa kweli, ukweli mwingi unafahamika kwa kupitia majaribu makali. Hakuna anayeweza kufahamu mapenzi ya Mungu, kutambua uweza na busara ya Mungu, wala kuiona tabia ya haki ya Mungu anapokuwa katika mazingira ya utulivu na rahisi au wakati hali ni nzuri. Hilo halingewezekana!

kutoka katika “Namna ya Kumridhisha Mungu Katikati ya Majaribu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Mungu hufanya kazi ndani ya kila mtu, na bila kujali mbinu Yake ni ipi, Anawatumia watu, vitu na mambo ya aina gani kufanya huduma, au maneno Yake yana sauti ya aina gani, Ana lengo moja tu la mwisho: kukuokoa. Kukuokoa kunamaanisha kukugeuza, na hivyo utakosaje kuteseka kidogo? Ni lazima upate kuteseka. Kuteseka huku kunaweza kuhusisha mambo mengi. Wakati mwingine, Mungu huibua watu, mambo, na vitu ambavyo viko karibu nawe ili kukufunua, kukuwezesha kujitambua, vinginevyo Yeye hukushughulikia moja kwa moja, kukupogoa, na kukufichua. Kama vile tu mtu aliye juu ya meza ya upasuaji–lazima upitie maumivu kiasi kwa ajili ya matokeo mazuri. Kama kila wakati Mungu anapokupogoa na kukushughulikia na kila wakati Anaibua watu, mambo, na vitu, hilo huchochea hisia zako na kukuongezea nguvu, basi kupitia hayo kwa njia hii ni sahihi, na utakuwa na kimo na utaingia katika uhalisi wa ukweli. Ikiwa, kila wakati unapopogolewa na kushughulikiwa, na kila wakati Mungu anapoinua mazingira yako, wewe huhisi maumivu au usumbufu wowote, na huhisi chochote kabisa, na kama huji mbele za Mungu kuelewa mapenzi Yake, wala huombi au kutafuta ukweli, basi wewe kweli ni mtu asiyejali kabisa! Watu ambao hawajali kabisa kamwe si hawatambui kiroho; kwa hiyo, Mungu hana njia ya kufanya kazi kwao. Mungu atasema: “Mtu huyu hajali kabisa na amepotoshwa sana. Nimemfanyia mambo mengi, nimetia bidii nyingi, lakini bado Siwezi kuuita moyo wake na Siwezi kuamsha roho yake. Jambo hili ni sumbufu na gumu sana.” Mungu akipanga mazingira, watu, vitu, na mambo fulani kwa ajili yako, Akikupogoa na kukushughulikia na ukijifunza kutokana na hili, ikiwa umejifunza kuja mbele za Mungu kutafuta ukweli, na, bila kujua, umetiwa nuru na kuangaziwa na kupata ukweli, ikiwa umepitia mabadiliko katika mazingira haya, umepata thawabu, na kupiga hatua, ukianza kuwa na ufahamu mdogo kuhusu mapenzi ya Mungu na kuacha kulalamika, basi yote haya yatamaanisha kuwa umesimama imara katikati ya majaribio ya mazingira haya, na umestahimili jaribio. Kwa hiyo, utakuwa umeshinda majaribu haya.

kutoka katika “Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Jumapili, 28 Aprili 2019

Waumini katika Mungu Wanapasa Kujiandaa kwa Ajili ya Hatima Yao kwa Matendo Mema ya Kutosha

7. Waumini katika Mungu Wanapasa Kujiandaa kwa Ajili ya Hatima Yao kwa Matendo Mema ya Kutosha

Maneno Husika ya Mungu:

Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika mamilioni ya miaka, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga. Na wale wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu pekee watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya wanadamu na kuchukia matendo yao maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu, Nikisubiri tu nafasi kutoa adhabu kwa hao na kufurahia kuona hilo. Siku Yangu hatimaye imefika na siwezi kusubiri zaidi!

Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

kutoka katika “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili

Natarajia tu kuwa katika hatua ya mwisho ya kazi Yangu, mnaweza kutekeleza kwa kujitokeza, kujitoa kikamilifu, na wala sio shingo upande tena. Bila shaka, Natarajia pia kuwa nyote muwe na hatima nzuri. Hata hivyo, bado Nina mahitaji Yangu ambayo ni kwenu nyinyi mfanye uamuzi bora kabisa katika kujitoa Kwangu pekee na moyo wa ibada ya mwisho. Kama mtu hana moyo huo wa ibada pekee, mtu huyo hakika atakwenda kuwa thamani ya Shetani, na Mimi Sitaendelea kumtumia. Nitamtuma nyumbani akatunzwe na wazazi wake.

kutoka katika “Juu ya Hatima” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mnapaswa kufanya wajibu wenu wenyewe kwa kadri ya uwezo wenu kwa mioyo iliyo wazi na wima, na muwe tayari kufanya chochote kitakachohitajika. Kama mlivyosema, wakati siku itakuja, Mungu Hatamtendea mtu yeyote vibaya ambaye aliteseka au kulipa gharama kwa ajili Yake. Aina hii ya imani ni yenye thamani kuishikilia, na hampaswi kuisahau kamwe. Ni tu kwa njia hii Ninaweza kutuliza akili Yangu kuwahusu. Vinginevyo, Sitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu, na milele mtakuwa malengo ya chuki Yangu. Kama nyote mnaweza kufuata dhamiri zenu na kutoa yote kwa ajili Yangu, msiwache jitihada zozote kwa ajili ya kazi Yangu, na kutenga maisha ya jitihada za kazi ya injili Yangu, basi si moyo Wangu mara kwa mara utaruka kwa furaha kwa ajili yenu? Si Mimi Nitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu?

kutoka katika “Juu ya Hatima” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme.

kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Matendo mema ni ushahidi kwamba tumepata wokovu, na ni dhihirisho la kuingia kwetu katika ukweli na uhalisi wa neno la Mungu. Kama tumetayarisha matendo mengi mema, hilo linamaanisha kwamba tumekuwa watu wapya mbele za Mungu na kwamba tuna ushahidi wa kweli katika kipengele cha kuwa binadamu halisi. Matendo yetu mema ndiyo yanayoonyesha hasa kwamba tumetubu kwa kweli; ikiwa tumetayarisha matendo mengi mema, hili linamaanisha kuwa tuna mfano wa kweli wa mtu. Ikiwa umemwamini Mungu kwa miaka mingi lakini umefanya matendo mema machache, basi una mfano wa binadamu? Je, una dhamiri na mantiki? Je, wewe ni mtu anayelipiza upendo wa Mungu? Iko wapi imani yako ya kweli? Uko wapi moyo wako wa upendo na utii kwa Mungu? Ni uhalisi upi umeingia ndani? Huna chochote kati ya haya. Kwa hiyo, mtu asiyefanya matendo mema ni mtu asiyepokea chochote kutoka kwa imani yake kwa Mungu. Yeye ni mtu ambaye hajapata kabisa wokovu kutoka kwa Mungu, mtu ambaye upotovu wake ni wa kina sana na ambaye hajabadilika hata kidogo. Matendo mema kweli yanafafanua hili.

kutoka katika “Maana Muhimu ya Kuandaa Matendo Mema” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha II

Matendo mema ya kutosha ni yapi? Tunaweza kusema kwamba wajibu wowote ambao mtu anaweza au anapaswa kuutimiza katika uzoefu wake wa kazi ya Mungu, na kitu chochote ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa mwanadamu—kama mwanadamu anaweza kufanya vitu hivi na anaweza kumridhisha Mungu, basi haya yote ni matendo mema Kama unaweza kuyatosheleza mahitaji ya Mungu, basi ni tendo jema. Kama una moyo wa ibada kwa Mungu wakati unapotimiza wajibu wako, basi ni tendo jema. Kama mambo unayoyafanya ni ya manufaa kwa watu waliochaguliwa na Mungu na kila mtu anafikiria kwamba unayoyafanya ni mazuri, basi ni tendo jema. Mambo yote ambayo dhamiri na mantiki ya mwanadamu huamini kuwa ni kulingana na madhumuni ya Mungu ni matendo mema. Mambo ambayo yanaweza kumridhisha Mungu na yana manufaa kwa watu wateule wa Mungu pia ni matendo mema. Kama mtu anaweza kufanya kila kitu ili kuyatayarisha haya matendo mema ambayo tumetoka kuzungumzia, hatimaye ataweza kuyatimiza, na hilo litamaanisha kuwa amekamilisha matendo mema ya kutosha. … Kila mtu sasa hutaka kutekeleza kazi yake na kufuatilia wokovu, lakini haitoshi tu kuwa na azimio na shauku. Mtu lazima aonyeshe tabia za utendaji na kuchukua hatua ya utendaji. Ni wajibu gani umetekeleza kwa ajili ya kuingia katika maisha ya watu wa Mungu wateule? Umefanya nini na ni thamani gani umelipa ili kuyaridhia matakwa ya Mungu? Umefanya nini ili kumridhisha Mungu na kulipa upendo Wake? Haya yote ni mambo ambayo inakubidi kuyatafakaria. Kama umefanya mambo mengi na kulipa thamani kubwa kwa ajili ya kuyaridhia matakwa ya Mungu na kwa ajili ya kuingia katika maisha na ukuaji wa watu wa Mungu wateule, basi inaweza kusemwa kuwa umeandaa matendo mema ya kutosha.

kutoka katika “Maana Muhimu ya Kuandaa Matendo Mema” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha II

Kwa kiwango cha chini, kutimiza kazi kiasi haitoshi peke yake kufanyiza kiasi cha kuridhisha cha matendo mema. Hivyo ni kusema, kutekeleza tu kiasi kidogo cha wajibu wako hakufikiriwi kuwa matendo mema ya kuridhisha hata kidogo. Matendo mema ya kuridhisha bila shaka sio rahisi kama watu wafikiriavyo. Kuandaa kiasi cha kuridhisha cha matendo mema huhitaji kujitumia kabisa kwa ajili ya Mungu. Aidha, kunahitaji kulipa kila thamani, na kuwa mwaminifu kwa agizo la Mungu tangu mwanzo hadi mwisho kwa imani nzuri; hii ndiyo njia ya pekee ya kuyaridhia matarajio ya Mungu.

Katika kutimiza wajibu wao kuna watu ambao kweli wamelipa thamani, wakafanya mambo ambayo yamesifiwa na Mungu, ambao wametekeleza wajibu wao kwa njia ambazo ni nzuri kabisa, za ajabu, za kupendeza na za kufanikiwa sana kiasi kwamba wanaweza kufikiriwa kuwa wametekeleza matendo mema. Baadhi ya ndugu na dada wamekwenda jela kwa sababu ya kutekeleza wajibu wao, ambao wamepitia maumivu mengi makali bila kumtii Shetani, na wamekuwa mashahidi. Kisha kuna watu ambao huthubutu kujiingiza hatarini bila kujali usalama wa kibinafsi au manufaa, ambao wamejitolea kufanya kazi za hatari kwa roho ya kufanya lililo la haki kwa ujasiri. Na kuna wale ndugu na dada ambao wanaweza kujitolea kwa kazi ya injili, na wanaweza kuvumilia fedheha katika kuhubiri injili ili kuwaokoa watu. Pia kuna wale wenye bidii katika kazi ya injili, wakivumilia shida bila malalamiko, wakiweka kando mambo ya kibinafsi na ya familia huku mawazo yao yakijawa na jinsi wanavyoweza kueneza injili ili kuwaleta watu zaidi mbele ya Mungu na kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Wote ambao wamejitolea kujitumia kabisa ili kumridhisha Mungu ni wale watu ambao tayari wamefanya matendo mema. Lakini bado wana umbali fulani kutoka kwa “matendo mema ya kuridhisha” ambayo Mungu hutaka. Watu wengi wameandaa tu matendo mema kiasi na hawajayaridhia kabisa matakwa ya Mungu. Hilo linatuhitaji kufanya tunaloweza ili kutimiza wajibu wetu na tuwe na bidii katika kuingia ndani kabisa ya ukweli ili kutekeleza matendo mema ya kuridhisha. Hili linatuhitaji tutafute kufanikisha matokeo bora sana ili kuuridhisha moyo wa Mungu, bila kujali ni wajibu gani tunaoutimiza. Hasa katika kueneza injili, bila kujali jinsi fedheha tunayopitia ilivyo kubwa au ni mateso kiasi gani tunayoyavumilia, mradi tunaweza kuwaleta watu zaidi kupata wokovu, ni lazima tuuchukue kama wajibu bila kujali gharama za kibinafsi. Huku tu ndio kutekeleza tendo bora sana. Kama watu wanaweza kutekeleza matendo zaidi yaliyo mema kama hili, hayo yanaweza kufikiriwa kuwa matendo mema ya kuridhisha. Hilo ndilo humletea Mungu furaha na shangwe mno, na watu kama hao kwa hakika watapokea sifa za Mungu. Mbali na hili, katika kutimiza wajibu wetu ni lazima pia tuwe makini na waangalifu sana, daima tukitafuta kujiboresha, na kutojiruhusu kuzembea hata kidogo. Ili kujitumia kwa ajili ya Mungu, ni lazima tuwe na kujitolea kwa uaminifu kabla tuweze kuyaridhisha mapenzi ya Mungu kabisa.

kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Chanzo: Tushughulikie Vipi Umeme wa Mashariki kwa Njia Inayolingana na Mapenzi ya Bwana?

Ijumaa, 26 Aprili 2019

Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

5. Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Maneno Husika ya Mungu:

Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu. Wale wanaotumia upendo kwa Mungu kusitawisha maisha yao yasiyopendeza na kujaza utupu katika mioyo yao ni wale ambao wanataka kuishi katika raha, si wale ambao kweli wanatafuta kumpenda Mungu. Upendo wa aina hii ni kinyume na matakwa ya mtu, harakati ya ridhaa ya hisia, na Mungu hahitaji upendo wa aina hii. Upendo wako, basi, ni upendo wa aina gani? Ni kwa ajili gani unampenda Mungu? Je, ni kiasi gani cha upendo wa kweli, ulicho nacho kwa Mungu sasa? Upendo wa watu wengi kati yenu ni kama uliotajwa hapo awali. Upendo wa aina hii unaweza tu kudumisha hali kama ilivyo; hauwezi kufikia uthabiti wa milele, wala kuchukua mizizi katika mtu. Aina hii ya upendo ni ule wa ua ambalo halizai matunda baada ya kuchanuka na hatimaye kunyauka. Kwa maneno mengine, baada ya wewe kumpenda Mungu mara moja kwa jinsi hii na hakuna mtu wa kukuongoza kwa njia ya mbele, basi utaanguka. Kama unaweza tu kumpenda Mungu katika nyakati za kumpenda Mungu na kutofanya mabadiliko katika tabia ya maisha yako baadaye, basi utaendelea kufunikwa na ushawishi wa giza, bila uwezo wa kutoroka, na bila uwezo wa kujinasua kwa kufungwa na kupumbazwa na Shetani. Hakuna mtu kama huyu anayeweza kukubaliwa na Mungu; mwishowe, roho zao, nafsi na mwili bado ni mali ya Shetani. Hili ni bila ya shaka. Wale wote ambao hawawezi kukubaliwa kikamilifu na Mungu watarudi mahali pao pa awali, yaani, kwa Shetani, na watakwenda chini kwa ziwa liwakalo moto wa jahanamu kukubali hatua ya pili ya adhabu kutoka kwa Mungu. Wale wanaokubaliwa na Mungu ni wale ambao wanamkataa shetani na kutoroka kutoka kwa miliki ya Shetani. Watu kama wale watahesabiwa rasmi miongoni mwa watu wa ufalme. Hivi ndivyo watu wa ufalme huja kuwa.


kutoka katika “Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini” katika Neno Laonekana katika Mwili

Leo, lazima uwe katika njia sahihi kwani unaamini katika Mungu wa vitendo. Kwa kuwa una imani katika Mungu, hupaswi tu kutafuta baraka, lakini pia kutafuta kumpenda Mungu na kumjua Mungu. Kupitia kwa kupata nuru kutoka Kwake na harakati yako mwenyewe, unaweza kula na kunywa neno Lake, kukuza ufahamu wa kweli kuhusu Mungu, na kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu unaotoka moyoni mwako. Kwa maneno mengine, upendo wako kwa Mungu ni wa kweli zaidi, ambapo hakuna yeyote anayeweza kuharibu au kukuzuia kuonyesha upendo wako Kwake. Basi uko kwa njia ya kweli ya imani kwa Mungu. Inathibitisha kwamba wewe unamilikiwa na Mungu, kwani moyo wako umemilikiwa na Mungu na wala huwezi kumilikiwa na kitu kingine. Kutokana na tajriba yako, malipo uliyolipa, na kazi ya Mungu, wewe una uwezo wa kuendeleza upendo usioamriwa kwa Mungu. Kisha unawekwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa neno la Mungu. Ni wakati tu ambao umekuwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza ndipo unaweza kuchukuliwa kuwa umempata Mungu. Katika imani yako kwa Mungu, lazima utafute lengo hili. Huu ni wajibu wa kila mmoja wenu. Hakuna anayelazimika kutosheka na mambo jinsi yalivyo. Hamuwezi kuwa na fikira aina mbili kwa kazi ya Mungu au uichukulie kwa wepesi. Mnapaswa kumfikiria Mungu katika mambo yako yote na wakati wote, na kufanya mambo yote kwa ajili yake. Na wakati mnasema au kufanya mambo, mnapaswa kutilia maanani maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza. Ni hii tu ndio inayolingana na mapenzi ya Mungu.


kutoka katika “Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Sasa, watu wote wameona kuwa mtu anayemtumikia Mungu lazima asijue jinsi ya kuteseka kwa ajili yake tu, lakini hata zaidi, anapaswa kuelewa kwamba kuamini katika Mungu ni kwa ajili ya kutafuta kumpenda. Mungu kukutumia wewe si kwa ajili ya kukusafisha wewe tu au kukufanya uteseke, lakini ni kukufanya ujue matendo Yake, kujua umuhimu halisi wa maisha ya binadamu, na hasa kukufanya ujue kwamba kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Kupata uzoefu wa kazi ya Mungu hakuhusu kufurahia neema Yake, lakini zaidi kuhusu kuteseka kwa sababu ya upendo wako Kwake. Kwa kuwa unafurahia neema ya Mungu, lazima pia ufurahie kuadibu Kwake—lazima upitie haya mambo yote. Unaweza kupata uzoefu wa nuru ya Mungu ndani yako, na unaweza pia kupitia ushughulikiaji Wake kwako na hukumu Yake. Kwa njia hiyo, unakuwa na uzoefu wa pande zote. Mungu amefanya kazi ya hukumu kwako, na Yeye pia amefanya kazi ya kuadibu kwako. Neno la Mungu limekushughulikia, lakini pia limekupa nuru, limekuangazia. Wakati unataka kukimbia, mkono wa Mungu bado unakuvuta kwa nguvu. Hizi kazi zote ni kukufahamisha kwamba kila kitu kuhusu mwanadamu kinadhibitiwa na Mungu. Unaweza kufikiri kuamini katika Mungu ni kuhusu mateso, au kufanya mambo mengi kwa ajili Yake, au kwa ajili ya amani ya mwili wako, au ni kwa ajili ya kila jambo kwenda vyema kwako, kwa ajili ya kila jambo kuwa la kustarehesha—lakini hakuna kati ya haya ambayo ni madhumuni ambayo watu wanapaswa kuwa nayo kwa ajili ya kuamini katika Mungu. Kama hayo ndiyo unayoamini, basi mtazamo wako si sahihi na huwezi kukamilishwa kabisa. Matendo ya Mungu, tabia ya Mungu ya haki, hekima Yake, maneno Yake, na maajabu Yake na kutoeleweka kwa kina Kwake yote ni mambo ambayo watu wanapaswa kuelewa. Tumia uelewa huu kuachana na maombi ya kibinafsi na pia matumaini ya mtu binafsi na dhana zilizo moyoni mwako. Ni kwa kuondoa haya tu ndiyo unaweza kukidhi masharti yanayotakiwa na Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio unaweza kuwa na uzima na kumridhisha Mungu. Kumwamini Mungu ni kwa ajili ya kumridhisha Yeye na kuishi kwa kudhihirisha tabia ambayo Yeye anahitaji, ili matendo na utukufu Wake viweze kudhihirishwa kupitia kundi hili la watu wasiostahili. Huo ndio mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu, na pia lengo unalopaswa kutafuta. Unapaswa kuwa na mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu na kutafuta kupata maneno ya Mungu. Unahitaji kula na kunywa maneno ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli, na hasa kuona matendo Yake ya utendaji, kuona matendo Yake ya ajabu kotekote katika ulimwengu mzima, pamoja na kazi ya vitendo Yeye hufanya katika mwili. Kwa njia ya uzoefu wao halisi, watu wanaweza kufahamu ni jinsi gani hasa Mungu hufanya kazi Yake kwao na mapenzi Yake kwao ni yapi. Haya yote ni ili kuondoa tabia yao potovu ya kishetani. Jiondolee uchafu na udhalimu ndani yako, ondoa nia zako mbaya, na unaweza kuendeleza imani ya kweli katika Mungu. Kwa kuwa tu na imani ya kweli ndiyo unaweza kweli kumpenda Mungu. Unaweza tu kweli kumpenda Mungu kwa msingi wa imani yako Kwake. Je, unaweza kufanikisha kumpenda Mungu bila kumwamini? Kwa kuwa unaamini katika Mungu, huwezi kukanganyika kuhusu jambo hilo. Baadhi ya watu hujawa na nguvu mara tu wanapoona kwamba imani katika Mungu itawaletea baraka, lakini hupoteza nguvu zote mara tu wanapoona wanafaa kupitia kusafishwa. Je, huko ni kuamini katika Mungu? Mwishowe, lazima upate utiifu kamili na mzima mbele ya Mungu katika imani yako. Unaamini katika Mungu lakini bado una madai Kwake, una mawazo mengi ya kidini ambayo huwezi kuyapuuza, maslahi ya kibinafsi huwezi kuacha, na bado unatafuta baraka za mwili na unataka Mungu auokoe mwili wako, kuiokoa nafsi yako—haya yote ni maonyesho ya watu wenye mtazamo usio sahihi. Hata kama watu wenye imani za kidini wana imani katika Mungu, hawatafuti mabadiliko ya tabia, hawafuatilii maarifa ya Mungu, na wanatafuta tu maslahi ya miili yao. Wengi kati yenu wana imani ambazo ni za kikundi cha kusadiki kidini. Hiyo siyo imani ya kweli katika Mungu. Kuamini katika Mungu lazima watu wamiliki moyo wa kuteseka kwa ajili Yake na radhi ya kujitoa wenyewe. Isipokuwa wakikidhi haya masharti mawili haihesabiki kama imani katika Mungu, na hawatakuwa na uwezo wa kufikia mabadiliko ya tabia. Ni watu tu wanaotafuta ukweli kwa kweli, wanaotafuta maarifa ya Mungu, na kufuatilia maisha ndio wale ambao kweli wanaamini katika Mungu.


kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Je sasa mnaelewa imani kwa Mungu ni nini? Je kuamini Mungu ni kuona ishara na maajabu? Je ni kupanda mbinguni? Kuamini Mungu sio rahisi hata kidogo. Zile desturi za kidini lazima zitakaswe; kufuata uponyaji wa wagonjwa na kukemea mapepo, kusisitiza ishara na maajabu, kutamani zaidi neema, amani na furaha ya Mungu, kufuata mandhari na raha za mwili—haya ni matendo ya kidini, na matendo haya ya aina hii ya kidini ni aina ya imani isiyo dhahiri. Leo, imani ya kweli kwa Mungu ni nini? Ni kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha yako na kumjua Mungu kutoka kwa neno Lake ili uufikie upendo wa kweli Kwake. Kuondoa tashwishi: Imani katika Mungu ni ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii Mungu. Unapomjua tu Mungu ndipo unapoweza kupenda Mungu, na kupatikana kwa lengo hili ndilo lengo la pekee mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.


kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea? Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa? Unachofuata ni cha kukuwezesha kupata amani baada ya kumwamini Mungu—watoto wako wawe huru kutokana na magonjwa, ili mme wako apate kazi nzuri, ili mwana wako apate mke mwema, binti wako apate mme anayeheshimika, ili ndume na farasi wako walime shamba vizuri, kwa mwaka wa hali ya anga nzuri kwa mimea yako. Hili ndilo unalolitafuta. Harakati yako ni kuishi kwa starehe, ili ajali isipate familia yako, ili upepo ukupite, ili uso wako usiguswe na changarawe, ili mazao ya familia yako yasipate mafuriko, ili usiguswe na majanga yoyote, kuishi katika mikono ya Mungu, kuishi kwenye kiota chenye joto. Mwoga kama wewe, anafuata mwili kila wakati—je, una moyo, una roho? Si wewe ni mnyama? Nakupa njia ya ukweli bila kukuuliza chochote, ilhali hauifuati. Je, wewe ni wale wamwaminio Mungu? Nahifadhi uhai wa ukweli wa binadamu juu yako, ila hauufuati. Je, una tofauti kati ya nguruwe na mbwa? Nguruwe hawafuati maisha ya binadamu, hawafuati kutakaswa, na hawaelewi maana ya maisha. Kila siku wanapokula na kushiba, wanalala. Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini? Maisha yako ni ya kudharauliwa na kutoheshimika, unaishi huku ukiwa na uchafu na uzinzi, na hufuati lengo lolote; je, si maisha yako ni ya kutoheshimika kwa yote? Je, una ujasiri wa kumtazamia Mungu? Ukiendelea kuwa na uzoefu wa haya, je, si utakosa kupata chochote? Umepewa njia ya ukweli, lakini kama utaipata ama hapana inategemea na kutafuta kwako.


kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mungu anapowasili duniani, yote ambayo Amefanya ndani ya mwanadamu na kumkubalia mwanadamu kuona ni ili mwanadamu atampenda na kumjua Yeye kweli. Kwamba mwanadamu anaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu na ameweza kufikia umbali huu ni, kuhusiana na jambo moja, kwa sababu ya upendo wa Mungu, na kuhusiana na jambo lingine, ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu; zaidi ya hayo, ni kwa sababu ya kazi ya hukumu na kuadibu ambayo Mungu ametekeleza ndani ya mwanadamu. Kama hamna hukumu, kuadibu, na majaribio ya Mungu, na kama Mungu hajawafanya mteseke, basi, kusema ukweli, ninyi hammpendi Mungu kweli. Kadri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi ndani ya mwanadamu, na kadri mateso ya mwanadamu yalivyo makuu zaidi, ndivyo inavyoweza kuonyesha zaidi hasa vile kazi ya Mungu ilivyo ya maana, na ndivyo moyo wa mwanadamu unavyoweza kumpenda Mungu kweli zaidi. Unajifunzaje jinsi ya kumpenda Mungu? Bila mateso makali na usafishaji, bila majaribio ya kuumiza—na kama, zaidi ya hayo, yote ambayo Mungu alimpa mwanadamu ingekuwa neema, upendo, na rehema—je, ungeweza kufikia upendo wa kweli kwa Mungu? Kwa upande mmoja, wakati wa majaribio ya Mungu mwanadamu huja kujua kasoro zake, na huona kwamba yeye ni mdogo, wa kudharauliwa, na duni, kwamba hana chochote, na si kitu; kwa upande mwingine, wakati wa majaribio Yake Mungu humuumbia mwanadamu mazingira tofauti yanayomfanya mwanadamu aweze zaidi kupitia kupendeza kwa Mungu. Ingawa maumivu ni makubwa, na wakati mwingine yasiyoshindika—na hata hufikia kiwango cha huzuni ya kuseta—baada ya kuyapitia, mwanadamu huona vile kazi ya Mungu ndani yake ni ya kupendeza, na ni juu ya msingi huu tu ndiyo ndani ya mwanadamu huzaliwa upendo wa kweli kwa Mungu. Leo mwanadamu huona kwamba na neema, upendo na rehema ya Mungu pekee, hana uwezo wa kujijua mwenyewe kweli, sembuse kuweza kujua kiini cha mwanadamu. Ni kupitia tu usafishaji na hukumu ya Mungu, ni wakati tu wa usafishaji kama huo ndiyo mwanadamu anaweza kujua kasoro zake, na kujua kwamba hana chochote. Hivyo, upendo wa mwanadamu kwa Mungu umejengwa juu ya msingi wa usafishaji na hukumu ya Mungu. Kama wewe hufurahia tu neema ya Mungu, na maisha ya familia yenye amani au baraka yakinifu, basi hujampata Mungu, na imani yako kwa Mungu haijafaulu. Mungu tayari ametekeleza hatua moja ya kazi ya neema katika mwili, na tayari amempa mwanadamu baraka yakinifu—lakini mwanadamu hawezi kufanywa mkamilifu na neema, upendo, na rehema pekee. Katika uzoefu wa mwanadamu yeye hukabiliwa na baadhi ya upendo wa Mungu, na huuona upendo na rehema ya Mungu, lakini baada ya kupitia kwa kipindi fulani cha wakati, yeye huona kwamba neema ya Mungu na upendo na rehema Yake hayawezi kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na hayana uwezo wa kufichua kile ambacho ni potovu ndani ya mwanadamu, wala hayawezi kumwondolea mwanadamu tabia yake potovu, au kufanya kuwa kamilifu upendo na imani yake. Kazi ya Mungu ya neema ilikuwa kazi ya kipindi kimoja, na mwanadamu hawezi kutegemea kufurahia neema ya Mungu ili kumjua Mungu.


kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu: kupata baraka, na ni wazembe sana kuhudhuria chochote ambacho hakihusiani na nia hii. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, acha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia yao, hata hivyo, inastahili sana sisi kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila kukubali na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.

Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi. Hata kama watu watafahamu jinsi walivyo wa kuhurumiwa, wenye chuki na walivyo ovyo, ni wangapi hapo ambao wanaweza kuachana na ukamilifu na matumaini yao? Na ni nani anayeweza kusimamisha hatua zake na kuacha kujifikiria yeye mwenyewe? Mungu Anawahitaji wale watakaojihusisha kwa karibu Naye kukamilisha usimamizi Wake. Anawahitaji wale ambao watatoa mawazo yao na mwili kwa ajili ya kazi Yake ya usimamizi ili kujitoa Kwake; Hawahitaji wale watakaoinua mikono yao na kuomba kutoka Kwake kila siku, na hata wale wanaotoa kidogo na kusubiri kulipwa kwa hilo tendo la kutoa. Mungu Anawadharau wale wanaotoa michango kidogo na kuridhika. Anawachukia wenye roho katili ambao hukataa kazi ya usimamizi Wake na hutaka tu kuongea kuhusu kwenda mbinguni na kupata baraka. Anachukia hata zaidi na wale ambao hufaidika na fursa inayowezeshwa na kazi Anayoifanya katika kuokoa wanadamu. Hii ni kwa sababu hawa watu hawajawahi kushughulishwa na Anachotarajia kupata Mungu kutokana na kazi Yake ya usimamizi. Wanashughulishwa tu na jinsi wanavyoweza kutumia hiyo fursa iliyowezeshwa na kazi ya Mungu ili kupata baraka. Hawajali roho Yake Mungu, kwa kuwa wanajishughulisha na mustakabali na hatima yao. Wale ambao wanakataa kazi ya usimamizi wa Mungu na hawana hata tamanio dogo katika jinsi Mungu Anavyowaokoa wanadamu na mapenzi Yake, wote wanafanya wapendavyo kando na kazi ya usimamizi wa Mungu. Tabia yao haikumbukwi na Mungu, na haikubaliwi na Mungu, na hata haiangaliwi kwa fadhila ya Mungu.


kutoka katika “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee” katika Neno Laonekana katika Mwili

Je, ni nini unachopaswa kufuatilia sasa? Unachopaswa kufuatilia ni kama wewe una uwezo wa kuonyesha matendo ya Mungu, kama unaweza kuwa onyesho na udhihirisho wa Mungu, na kama wewe unastahili kutumiwa na Yeye. Ni kiasi gani cha kazi ambacho Mungu hakika amefanya kwako? Ni kiasi gani ambacho umeona, ni kiasi gani ambacho umegusa? Umepitia kiasi gani, na kuonja kiasi gani? Kama Mungu amekujaribu, kukushughulikia, au kukuadhibu—haijalishi chochote, matendo Yake na kazi Yake vimetekelezwa juu yako, lakini kama muumini katika Mungu, kama mtu ambaye ana nia ya kufuatilia kukamilishwa na Yeye, je, una uwezo wa kuonyesha matendo ya Mungu kwa njia ya uzoefu wako mwenyewe wa utendaji? Je, unaweza kuishi kwa kumdhihirisha Mungu kupitia kwa hili? Je, unaweza kuwakimu wengine kupitia uzoefu wako mwenyewe wa utendaji, na kugharimika mwenyewe kwa ajili ya kazi ya Mungu? Ili kuwa na ushuhuda kwa ajili ya matendo ya Mungu lazima uweze kueleza matendo Yake ni nini, na hili linafanywa kupitia uzoefu wako, maarifa, na mateso ambayo umevumilia. Je, wewe ni mtu ambaye huwa na ushuhuda kwa ajili ya matendo ya Mungu? Je, una matamanio haya? Kama unaweza kuwa na ushuhuda kwa ajili ya jina Lake, na hata zaidi, matendo Yake, pamoja na kuishi kwa kudhihirisha sura ambayo Yeye anataka kutoka kwa watu Wake, basi wewe ni shahidi wa Mungu. Je, unashuhudia kwa ajili ya Mungu vipi kwa hakika? Kutafuta na kuwa na hamu sana ya kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, kuwa na ushahidi kupitia kwa maneno yako, kuwaruhusu watu kujua na kuona matendo Yake—kama kweli unatafuta yote haya, Mungu atakukamilisha. Ikiwa yote unayotafuta ni kukamilishwa na Mungu na kubarikiwa mwishoni kabisa, basi mtazamo wa imani yako katika Mungu si safi. Unapaswa kuwa ukifuatilia jinsi ya kuona matendo ya Mungu katika maisha ya kweli, jinsi ya kumridhisha Yeye wakati anafichua mapenzi Yake kwako, kutafuta jinsi ya kutoa ushuhuda kwa maajabu Yake na hekima, na jinsi ya kuonyesha nidhamu na ushughulikiaji Wake kwako. Haya yote ni mambo unayopaswa kuwa ukijaribu kuelewa sasa. Kama upendo wako kwa Mungu ni ili tu uweze kushiriki katika utukufu wa Mungu baada ya Yeye kukukamilisha, bado hautoshi na hauwezi kukidhi mahitaji ya Mungu. Unahitaji kuwa na uwezo wa kuwa na ushuhuda kwa matendo ya Mungu, kutosheleza mahitaji Yake, na kuwa na uzoefu wa kazi ambayo Amefanya kwa watu kwa njia ya utendaji. Iwe ni maumivu, machozi, au huzuni, lazima uyapitie yote kwa vitendo. Haya yote ni ili uweze kuwa shahidi wa Mungu. Je, ni chini ya utawala wa nini hasa sasa ndiyo unateseka na kutafuta ukamilifu? Je, ni kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu? Je, ni kwa ajili ya baraka za mwili au kwa ajili ya matarajio ya baadaye? Dhamira zako zote, motisha, na malengo ya kibinafsi ya kufuatilia lazima yarekebishwe na hayawezi kuongozwa na mapenzi yako mwenyewe.


kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili