Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumcha-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumcha-Mungu. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 20 Septemba 2019

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda

2. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda

Maneno Husika ya Mungu:
Wanadamu kwa ajili ya kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi. Wanadamu watashindwa vipi hasa? Watapata kushindwa kwa kutumia hii kazi ya maneno kumshawishi mwanadamu kwa dhati; kwa kutumia toba, hukumu, kuadibu, na laana isiyo na huruma dhibiti kabisa; na kwa kuweka wazi uasi wa mwanadamu na kwa kuhukumu upinzani wake ili ajue udhalimu wa mwanadamu na uchafu wake, mambo ambayo yatatumiwa kuangazia tabia ya haki ya Mungu. Kwa kiwango kikubwa, ni matumizi ya maneno haya yatakayomshinda mwanadamu na kumshawishi kabisa. Maneno ndiyo njia ya kuwashinda wanadamu na wote wanaokubali ushindi lazima wakubali mapigo na hukumu ya maneno. Mchakato wa sasa wa kunena ni mchakato wa kushinda. Ni kwa njia gani watu wanapaswa hasa kushirikiana? Ni kwa kula na kunywa haya maneno ipasavyo na kuyafahamu. Watu hawawezi kujipatia ushindi wao wenyewe. Ni lazima, kwa kula na kunywa haya matamshi, upate kufahamu uovu na uchafu wako, uasi na udhalimu wako, na uanguke chini mbele ya Mungu. Ikiwa waweza kufahamu mapenzi ya Mungu kisha uyatie katika vitendo, na zaidi, uwe na maono, na ikiwa waweza kuyatii maneno haya kabisa na usitende kulingana na mapenzi yako, basi utakuwa umeshindwa. Na itakuwa ni haya maneno yamekuwezesha kushindwa. Ni kwa nini wanadamu walipoteza ushuhuda? Ni kwa sababu hakuna aliye na imani kwa Mungu au anamshikilia Mungu rohoni mwake. Kuwashinda wanadamu kunamaanisha watu wairudie hii imani. Watu daima wanauegemea ulimwengu, wakiwa na matumaini mengi sana, wakitaka kujua mengi sana kwa ajili ya maisha yao ya usoni, na wakiwa na mahitaji mengi ya kupita kiasi. Wanaifikiria na kuipangia miili yao kila mara wala hawatamani kutafuta njia ya kumwamini Mungu. Roho zao zimetekwa na Shetani, wameacha kumheshimu Mungu, na wanatoa mioyo yao kwa Shetani. Ila mwanadamu aliumbwa na Mungu. Hivyo, mwanadamu amepoteza ushuhuda, kumaanisha amepoteza utukufu wa Mungu. Kusudi la kumshinda mwanadamu ni kuurejesha utukufu wa mwanadamu wa kumheshimu Mungu.

kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kazi ya sasa ya kushinda ni kazi inayokusudiwa kuweka wazi hatima ya mwanadamu itakuwaje. Ni kwa nini Ninasema kuwa kuadibu na hukumu ni hukumu mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe cha siku za mwisho? Hulioni hili? Ni kwa nini kazi ya kushinda ni hatua ya mwisho? Je, si kudhihirisha kwa usahihi hatima ya kila tabaka la wanadamu? Si kumruhusu kila mtu, katika harakati ya kazi ya kushinda ya kuadibu na hukumu, kuonyesha tabia zake halisi na kisha kuwekwa katika aina yake baadaye? Badala ya kusema kuwa huku ni kuwashinda wanadamu, inaweza bora kusema kuwa huku ni kuonyesha hatima ya kila aina ya mwanadamu. Yaani, huku ni kuhukumu dhambi zao halafu kuonyesha matabaka mbalimbali ya wanadamu, na kwa njia hiyo kubaini kama ni waovu au ni wenye haki. Baada ya kazi ya kushinda, kazi ya kutuza mazuri na kuadhibu maovu inafuata: watu wanaotii kabisa, yaani walioshindwa kabisa, watawekwa katika hatua nyingine ya kusambaza kazi ulimwenguni kote; wasioshindwa watawekwa gizani na watapatwa na majanga. Hivyo mwanadamu ataainishwa kulingana na aina yake, watenda maovu watawekwa pamoja na maovu, wasiuone mwangaza tena, na wenye haki watawekwa pamoja na mazuri, ili kupokea mwangaza na kuishi milele katika mwangaza. Mwisho wa vitu vyote u karibu, mwisho wa mwanadamu umebainishwa wazi machoni mwake, na vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina yake. Ni vipi basi wanadamu wataepuka kuathiriwa na kuanisha huku? Kufichua mwisho kwa kila jamii ya mwanadamu kutafanywa hatima ya kila kitu ikikaribia, na kutafanywa wakati wa kazi ya kushinda ulimwengu mzima (ikiwemo kazi yote ya kushinda kuanzia kazi ya sasa). Huku kufichua mwisho wa wanadamu kunafanywa mbele ya kiti cha hukumu, katika harakati ya kuadibu, na harakati ya kazi ya kushinda ya siku za mwisho. … Hatua ya mwisho ya kushinda ni ya kukomboa watu na vilevile kufichua mwisho wa kila mtu. Inaweka wazi upotevu wa watu kupitia hukumu na kwa njia hiyo kuwafanya watubu, waamke, na kufuatilia uzima na njia ya haki ya maisha ya mwanadamu. Ni ya kuamsha mioyo ya waliolala na wapumbavu na kuonyesha, kwa njia ya hukumu, uasi wao wa ndani. Hata hivyo, ikiwa watu bado hawawezi kutubu, bado hawawezi kufuata njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na hawawezi kuutupa upotovu huu, basi watakuwa vyombo visivyoweza kukombolewa vya kumezwa na Shetani. Hii ndiyo maana ya kushinda—kuwakomboa watu na vilevile kuwaonyesha mwisho wao. Mwisho mzuri, mwisho mbaya—yote yanafichuliwa na kazi ya kushinda. Kama watu watakombolewa au kulaaniwa yote yanafichuliwa wakati wa kazi ya kushinda.

Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia kushinda. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maneno mengine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. La sivyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, watu wa kila mataifa vilevile watapitia kazi ya kushinda. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake?

kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Jinsi ambavyo mwenendoama mwili wa mwanadamu hubadilika haiamui ikiwa ameshindwa. Badala yake, ni wakati ambapo fikira, ufahamu, na utambuzi wa mwanadamu unabadilika—yaani, ni wakati mielekeo yako yote ya kifikira inabadilika—ndipo huwa umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa. Katika ulimwengu wa dini, watu wengi huteseka pakubwa maishani mwao mwote, kwa kuihini miili yao au kuubeba msalaba wao, au hata kuteseka na kustahimili hadi pumzi zao za mwisho! Wengine huwa wanafunga hadi siku ya kifo chao. Katika maisha yao yote wanajinyima chakula kizuri na mavazi mazuri, wakisisitiza mateso tu. Wanaweza kuihini miili yao na kuinyima miili yao. Uwezo wao wa kustahimili mateso unastahili sifa. Ila fikira zao, mawazo yao, mielekeo yao ya kiakili, na kwa hakika asili yao ya kale—hakuna kati yavyo kilichoshughulikiwa hata kidogo. Hawajifahamu. Picha ya Mungu akilini mwao ni ya kijadi na ya kidhahania, Mungu asiye yakini. Uamuzi wao wa kuteseka kwa ajili ya Mungu unaletwa na azma na asili yao chanya. Hata ikiwa wanamwamini Mungu, hawamfahamu Mungu wala kuyafahamu mapenzi Yake. Wanamfanyia Mungu kazi na kumtesekea Mungu kama vipofu. Hawawekei utambuzi thamani yoyote na hawajishughulishi na jinsi ambayo huduma yao inatimiza mapenzi ya Mungu kwa kweli. Aidha hawajui jinsi ya kutimiza ufahamu kuhusu Mungu. Mungu wanayemhudumia si Mungu katika sura Yake ya asili, ila ni Mungu waliyejifikiria, Mungu waliyemsikia, au Mungu wa kihadithi wanayemsoma katika maandiko. Kisha wanatumia mawazo yao dhahiri na mioyo yao ya kiungu kumtesekea Mungu na kuifanya kazi ambayo Mungu anapaswa kufanya. Huduma yao haiko sahihi, kiasi kwamba hakuna anayemhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi Yake. Haijalishi wako radhi kiasi gani kuteseka, mitazamo yao asilia ya huduma na picha ya Mungu akilini mwao havibadiliki kwani hawajapitia hukumu ya Mungu na kuadibu na usafishaji Wake na ukamilifu, na kwa sababu hakuna yeyote aliyewaongoza na ukweli. Japo wanasadiki kwa Yesu Mwokozi, hamna kati yao aliyewahi kumwona Mwokozi. Wamemsikia tu kwa hadithi na uvumi. Hivyo huduma yao ni sawa na kuhudumu mara mojamoja macho yao yakiwa yamefungwa kama kipofu anayemhudumia baba yake. Ni nini kinaweza kupatikana kutokana na huduma kama hiyo? Na ni nani anaweza kuikubali? Huduma yao haibadiliki kamwe toka mwanzo hadi mwisho. Wanapokea mafunzo ya kibinadamu na kukita huduma yao katika uasili wao na kile wanachokipenda wao. Hili laweza kuzalisha faida gani? Hata Petro, aliyemwona Yesu, hakujua jinsi ya kumhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi ya Mungu. Ni katika uzee wake ndipo alipopata ufahamu. Hili linaonyesha nini kuhusu wanadamu vipofu ambao hawajapitia ushughulikiaji na hawana upogoaji na ambao hawajawahi kupata yeyote wa kuwaongoza? Je, si huduma ya wengi miongoni mwenu leo ni kama ile ya vipofu? Wale wote ambao hawajapokea hukumu, hawajapokea upogoaji na ushughulikiaji, na hawana mabadiliko—je, wao si waliokosa kushindwa kabisa? Wana manufaa gani watu kama hao? Ikiwa fikira zako, ufahamu wako wa maisha, na ufahamu wako wa Mungu hauonyeshi mabadiliko mapya na hautoi faida hata kidogo, hutatimiza chochote kizuri katika huduma yako. Bila maono na bila ufahamu mpya wa kazi ya Mungu, huwezi kuwa mtu aliyeshindwa. Njia yako ya kumfuata Mungu itakuwa kama ile ya wale wanaoteseka na kufunga—itakuwa ya thamani ndogo! Hii ni kwa sababu kuna ushuhuda kidogo katika yale wayafanyayo ndipo Nasema huduma yao ni bure! Kotekote katika maisha yao, hao watu huteseka, hukaa gerezani kwa muda, na kwa kila wakati, hustahimili, husisitiza mapenzi na ukarimu, na kubeba msalaba wao. Wanatukanwa na kukataliwa na ulimwengu na hupitia kila ugumu. Wanatii hadi mwisho ila bado hawapati ushindi na hawawezi kutoa ushuhuda wa kutwaliwa. Wameteseka si haba, ila kwa ndani hawamfahamu Mungu kabisa. Hakuna fikira zao za zamani, mawazo ya zamani, vitendo vyao, uelewa wa wanadamu, na mawazo ya wanadamu yaliyoshughulikiwa. Kamwe hakuna uelewa mpya ndani yao. Hakuna hata chembe ya ufahamu wao wa Mungu ambao ni wa kweli au ni sahihi. Wamekosa kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Je, huku kwaweza kuwa kumhudumia Mungu? Japo ulimfahamu Mungu zamani, tuseme umeudumisha ufahamu huo hadi leo na kuendelea kukita ufahamu wako kuhusu Mungu kwenye fikira na mawazo yako bila kujali Mungu anafanya nini. Yaani, ikiwa huna ufahamu mpya na wa kweli kuhusu Mungu na ukose kutambua sura na tabia ya kweli ya Mungu. Ikiwa ufahamu wako wa Mungu bado unaongozwa na fikira za uhasama na ushirikina na bado una mawazo na fikira za mwanadamu. Ikiwa hii ndiyo hali, basi hujashindwa. Lengo langu la kukwambia maneno haya yote sasa ni kukupa fursa ya kufahamu na kutumia utambuzi huu kukuongoza katika ufahamu sahihi na mpya. Aidha yanalengwa kukuondolea mawazo ya zamani na utambuzi wa zamani ulio nao ili uweze kuwa na ufahamu mpya. Ikiwa unakula na kunywa matamshi Yangu kweli, basi ufahamu wako utabadilika kwa kiwango kikubwa. Bora tu udumishe moyo mtiifu kwa kula na kunywa matamshi ya Mungu, mtazamo wako utabadilika. Bora tu unaweza kukubali kuadibu kwa kila mara, fikira zako za zamani zitabadilika taratibu. Bora tu fikira zako za zamani zimebadilishwa kabisa na kuwa mpya, vitendo vyako vitabadilika ipasavyo. Kwa njia hii, huduma yako itaendelea kuwa yenye malengo zaidi, na itaweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Ukibadilisha maisha yako, ufahamu wako wa maisha, na mawazo yako mengi kuhusu Mungu, basi uasili wako utadidimia taratibu. Hili, na hakuna jingine ila hili, ndilo tokeo baada ya Mungu kumshinda mwanadamu; haya ndiyo mabadiliko yatakayoonekana ndani ya mwanadamu.

kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kazi ya Yehova ilikuwa uumbaji wa ulimwengu, ilikuwa mwanzo; awamu hii ya kazi ni mwisho wa kazi, na ni hitimisho. Hapo mwanzo, kazi ya Mungu ilifanyika miongoni mwa wateule wa Israeli, na ilikuwa mapambazuko ya kipindi kipya katika pahali patakatifu zaidi ya popote. Awamu ya mwisho ya kazi inafanywa katika nchi ambayo ni chafu zaidi ya zote, kuhukumu ulimwengu na kuleta enzi kwenye kikomo. Katika awamu ya kwanza kazi ya Mungu ilifanyika katika maeneo yenye kung’aa kuliko maeneo yote, na awamu ya mwisho inafanyika katika maeneo yaliyo katika giza kuliko maeneo yote, na giza hili litaondolewa, na mwanga kufunguliwa, na watu wote kushindwa. Wakati watu wa maeneo haya yaliyo chafu kuliko yote na yaliyo na giza watakuwa wameshindwa na idadi yote ya watu wametambua kuwa Mungu yupo, na ya kuwa ni Mungu wa kweli, na kila mtu Amemwamini kabisa, basi ukweli huu utatumika kutekeleza kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima. Awamu hii ya kazi ni ya ishara: Punde tu kazi ya kipindi hiki itakapomalizika, kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi itafikia mwisho kabisa. Mara baada ya wale walioko katika maeneo yaliyo na giza kuliko yote watakapokuwa wameshindwa, bila shaka itakuwa hivyo pia kila mahali pengine. Kwa hivyo, kazi ya ushindi tu katika China inabeba ishara ya maana. China inajumuisha nguvu zote za giza, na watu wa China wanawakilisha wale wote ambao ni wa mwili, wa Shetani, na wa mwili na damu. Ni watu wa China ndio wamepotoshwa sana na joka kubwa jekundu, ambao wana upinzani wenye nguvu dhidi ya Mungu, ambao wana ubinadamu ulio mbovu zaidi na ulio mchafu, na kwa hivyo hao ni umbo asili la wanadamu wote wenye matendo maovu. Hii si kusema kwamba nchi nyingine hazina shida kabisa; dhana za mwanadamu ni sawa zote, na ingawa watu wa nchi hizi wanaweza kuwa na uhodari mzuri, ikiwa hawamjui Mungu, basi ni lazima iwe kwamba wanampinga. Kwa nini Wayahudi pia walimpinga na kumwasi Mungu? Kwa nini Mafarisayo pia walimpinga? Kwa nini Yuda alimsaliti Yesu? Wakati huo, wengi wa wanafunzi hawakumjua Yesu. Kwa nini, baada ya Yesu kusulubiwa na kufufuliwa tena, watu bado hawakumwamini? Je, uasi wa mwanadamu sio sawa wote? Ni tu kwamba watu wa China wamefanyika mfano, na watakaposhindwa watakuwa mfano na kielelezo, na watatumika kama kumbukumbu kwa wengine. Kwa nini mimi daima Nimesema yakuwa nyinyi ni kiungo cha mpango wangu wa usimamizi? Ni katika watu wa China ambapo upotovu, uchafu, udhalimu, upinzani, na uasi unadhihirishwa kikamilifu zaidi na kufichuliwa kwa hali zao mbalimbali. Kwa upande mmoja, wao ni wa kimo cha umaskini, na kwa upande mwingine, maisha yao na mawazo yao ni ya nyuma kimaendeleo, na tabia zao, mazingira ya kijamii, familia ya kuzaliwa—yote ni ya umaskini na ya nyuma kimaendeleo kuliko yote. Hadhi yao, pia, ni ya chini. Kazi katika eneo hili ni ya ishara, na baada ya kazi hii ya majaribio hufanywa kwa ukamilifu wake, na kazi yake inayofuata itakwenda vizuri zaidi. Kama awamu hii ya kazi inaweza kukamilika, basi kazi inayofuata itakamilika bila shaka. Mara baada ya awamu ya kazi hii kutimizwa, na mafanikio makubwa kufikiwa kikamilifu, kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima itakua imefikia kikomo kamili. Kwa kweli, mara baada ya kazi miongoni mwenu imekuwa ya mafanikio, hii itakuwa sawa na mafanikio katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa sababu Yangu kuwafanya mfano wa kuigwa na kielelezo. Uasi, upinzani, uchafu, udhalimu—yote haya hupatikana kwa watu hawa, na ndani yao pamewakilishwa uasi wote wa wanadamu. Wao ni wa kushangaza kweli. Hivyo, wanafanywa kuwa mfano wa ushindi, na punde tu watakaposhindwa watakuwa kama ilivyo kawaida kielelezo na mfano wa kuigwa na wengine.

kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mwanadamu anajali tu kuhusu hatima ya siku zijazo, hatima, na kama kuna ama hamna kitu kizuri cha kutumainia. Iwapo mwanadamu angepewa matumaini mazuri wakati wa kazi ya ushindi, na kama, kabla ya kushindwa kwa mwanadamu, yeye angepewa hatima ifaayo ya kufuata, basi kushindwa kwa mwanadamu kusingekosa kuwa na athari tu, bali athari za kushindwa zingeshawishika pia. Hivi ni kusema kwamba, kazi ya ushindi inafanikisha mazao yake kwa kuchukua hatima na matarajio ya mwanadamu na kuhukumu na kuadibu uasi wa tabia ya mwanadamu. Haifanikishwi kwa kufanya mpango na mwanadamu, yaani, kwa kumpa mwanadamu baraka na neema, lakini ni kwa kufichua uaminifu wa mwanadamu kwa kumnyang’anya “uhuru” wake na kukomesha matarajio yake. Hiki ni kiini cha kazi ya ushindi. Kama mtu angepewa matumaini mazuri hapo mwanzoni sana, na kazi ya kuadibu na hukumu zingefanywa baadaye, basi mwanadamu angekubali kuadibu huku na hukumu kwa msingi kwamba alikuwa na matarajio, na mwishowe, utiifu na ibada ya Muumba isiyo na masharti ya viumbe vyote vyake haingetimizika; kungekuwepo tu na utiifu wenye upofu na wa ujinga, au pengine mwanadamu angetoa madai yasiyo na msingi kwa Mungu, na ingekuwa ni vigumu kushinda moyo wa mwanadamu. Kwa hivyo, kazi kama hii ya ushindi haingekuwa na uwezo wa kumpata mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, ya kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Viumbe kama hawa hawangeweza kutekeleza jukumu lao, na wangeweza tu kufikia makubaliano na Mungu; hii haitakuwa ushindi, lakini huruma na baraka. Tatizo kubwa mno kwa mwanadamu ni kuwa yeye hufikiria tu kuhusu hatima yake na matarajio, na kuyaabudu. Mwanadamu humfuata Mungu kwa ajili ya hatima yake na matarajio; yeye hamwabudu Mungu kwa sababu ya upendo wake kwake. Na kwa hivyo, katika ushindi kwa mwanadamu, ubinafsi wa mwanadamu, uroho na vitu ambavyo sana sana huzuia ibada yake kwa Mungu ni sharti viondolewe. Kwa kufanya hivyo, matokeo ya ushindi kwa mwanadamu yatatimizwa. Hivyo, katika ushindi wa kwanza wa mwanadamu ni muhimu kwanza kuondoa matarajio makubwa ya mwanadamu na udhaifu unaohuzunisha kabisa, na, kupitia hili, kufichua upendo wa mwanadamu kwa Mungu, na kubadilisha maarifa yake kuhusu maisha ya binadamu, mtazamo wake kwa Mungu, na maana ya kuwepo kwake. Kwa njia hii, upendo wa mwanadamu kwa Mungu unatakaswa, ambapo ni kusema, moyo wa binadamu unashindwa. Lakini katika mtazamo wake wa viumbe vyote, Mungu hashindi kwa sababu ya kushinda; badala yake, Yeye anashinda ili kumpata mtu, kwa sababu ya utukufu wake mwenyewe, na ili kuokoa ufanano wa kwanza wa awali wa mwanadamu. Kama angeshinda kwa ajili ya kushinda, basi umuhimu wa kazi ya ushindi ungepotea. Hiyo ni kusema kuwa ikiwa, baada ya kumshinda mwanadamu, Mungu alikata tamaa kwa ajili ya mwanadamu, na hakuzingatia maisha au kifo chake, basi hii haitakuwa usimamizi wa mwanadamu, wala kumshinda mwanadamu haitakuwa ni kwa ajili ya wokovu wake. Ni upato wa mwanadamu tu kufuatia ushindi wake na ujio wake wa mwisho katika hatima ya ajabu ndiyo yaliyomo katika kiini cha kazi yote ya wokovu, na ni hii tu ndio inayoweza kufikia lengo la wokovu wa mwanadamu. Kwa maneno mengine, ni ufikaji wa mwanadamu katika hatima nzuri na kuingia kwake katika mapumziko tu ndiyo matarajio ambayo yanatakiwa yamilikiwe na viumbe vyote, na kazi ambayo lazima ifanywe na Muumba.

kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hatua ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni hatua ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na hatua ya mwisho katika kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na wanadamu kamwe hawangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilishwa kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu ya usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha usimamizi wote wa Mungu, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, yaani mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kutekwa nyara na Shetani. Hivyo, Shetani lazima ashindwe kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani, mabadiliko ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye ametekwa nyara, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, na baada ya hapo kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.

kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kazi ya kushinda inayofanywa kwenu nyie ni ya umuhimu mkubwa sana: Kwa upande mmoja, kusudi la hii kazi ni kukikamilisha kikundi cha watu, yaani, kuwakamilisha na kuwa kundi la washindi, kama kundi la kwanza la watu waliofanywa wakamilifu, yaani matunda ya kwanza. Kwa upande wa pili, ni kuruhusu viumbe wa Mungu kufurahia mapenzi ya Mungu, kupokea wokovu mkubwa wa Mungu, na kupokea wokovu kamili wa Mungu. Kile Mungu anamkubali mwanadamu kufurahia si tu huruma na wema, ila muhimu zaidi ni kuadibu na hukumu. Tangu uumbaji wa dunia hadi sasa, yote ambayo Mungu amefanya katika kazi Yake ni upendo, bila chuki yoyote kwa mwanadamu. Hata kuadibu na hukumu uliyoiona ni mapenzi pia, upendo wa kweli na wa dhati zaidi; upendo huu huwaongoza wanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu. Kwa upande wa tatu, ni kushuhudia mbele ya Shetani. Kwa upande wa nne, ni kuweka msingi wa kueneza kazi ya baadaye ya injili. Kazi yote Aliyoifanya ni kumwongoza mwanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya wanadamu, ili kwamba wawe na maisha ya kawaida ya wanadamu, kwani mwanadamu hajui jinsi ya kuishi. Bila uongozi kama huo, utaishi maisha tupu yasiyo na maana wala thamani, na kamwe hutajua jinsi ya kuwa mwanadamu wa kawaida. Huu ndio umuhimu mkuu wa kumshinda mwanadamu.

kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Alhamisi, 16 Mei 2019

Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

1. Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili. Kwanza ni maisha Anayoishi kabla ya kuanza kutekeleza huduma Yake. Anaishi katika familia ya kawaida ya binadamu, katika ubinadamu wa kawaida kabisa, Akifuata maadili na sheria za maisha ya wanadamu, Akiwa na mahitaji ya kawaida ya binadamu (chakula, nguo, makazi, na usingizi), na udhaifu wa kawaida wa binadamu na hisia za kawaida za binadamu. Kwa maneno mengine, katika hatua hii ya kwanza Anaishi maisha yasiyo na uungu, ubinadamu wa kawaida kabisa, Akijishughulisha na shughuli zote za wanadamu. Hatua ya pili ni ya maisha Anayoishi baada ya kuanza kutekeleza huduma Yake. Bado Yumo katika ubinadamu wa kawaida Akiwa na umbo la nje la binadamu bila kuonyesha ishara isiyo ya kawaida kwa nje. Lakini kimsingi Anaishi kwa ajili ya huduma Yake, na wakati huu ubinadamu Wake wa kawaida upo kikamilifu kuhudumia kazi ya kawaida ya uungu Wake; kwani wakati huo, ubinadamu Wake wa kawaida umekomaa kiasi cha kuweza kutekeleza huduma Yake. Kwa hivyo hatua ya pili ya maisha Yake ni ya kutekeleza huduma Yake katika ubinadamu Wake wa kawaida, ni maisha ya ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Sababu ya kuishi katika maisha ya kawaida kabisa ya ubinadamu katika hatua ya kwanza ya maisha Yake ni kwamba ubinadamu Wake bado ulikuwa haujalingana na ukamilifu wa kazi ya uungu, bado haujakomaa; ni baada tu ya kukomaa kwa ubinadamu Wake na kuwa na uwezo wa kustahimili huduma Yake, ndipo Anaweza kuanza kutekeleza huduma Yake. Kwa kuwa Yeye, kama mwili, Anahitaji kukua na kukomaa, hatua ya kwanza ya maisha Yake ni ile ya ubinadamu wa kawaida, ilhali katika hatua ya pili, kwa kuwa ubinadamu Wake una uwezo wa kuanza kazi Yake na kutekeleza huduma Yake, maisha ambayo Mungu mwenye mwili Anaishi katika kipindi cha huduma Yake ni ya ubinadamu na ya uungu kamili. Iwapo Mungu mwenye mwili Angeanza huduma Yake kwa dhati tangu kuzaliwa kwake, na kufanya ishara na maajabu ya mwujiza, basi Asingekuwa na kiini cha kimwili. Kwa hivyo, ubinadamu Wake upo kwa sababu ya kiini chake cha Kimwili; hakuwezi kuwepo na mwili bila ubinadamu, na mtu bila ubinadamu si mwanadamu. Kwa njia hii, ubinadamu wa mwili wa Mungu ni sifa ya ndani ya mwili wa Mungu. Kusema kwamba “Mungu Anapokuwa mwili Anakuwa na uungu kamili, kwa vyovyote vile si ubinadamu,” ni kufuru, kwa sababu huu ni msimamo usioweza kuchukuliwa, msimamo unaokinzana na kanuni ya Yesu kuupata mwili. Hata baada ya kuanza kutekeleza huduma Yake, uungu Wake bado unaishi ndani ya umbo la nje la binadamu Anapofanya kazi Yake; ni kwamba tu wakati huo, ubinadamu Wake una kusudi la pekee la kuuwezesha uungu Wake kutekeleza kazi katika mwili wa kawaida. Kwa hivyo wakala wa kazi ni uungu unaosetiriwa katika ubinadamu Wake. Ni uungu na wala si ubinadamu Wake unaofanya kazi, lakini ni uungu uliojificha katika ubinadamu Wake; kimsingi kazi Yake inafanywa na uungu Wake kikamilifu, haifanywi na ubinadamu Wake. Ila mtekelezaji wa kazi ni mwili Wake. Mtu anaweza kusema kuwa Yeye ni mwanadamu na vilevile Mungu, kwani Mungu Anakuwa Mungu Anayeishi katika mwili, mwenye umbo la mwanadamu na kiini cha binadamu lakini pia na kiini cha Mungu. Kwa sababu ni mwanadamu mwenye kiini cha Mungu, Yuko juu ya wanadamu wote walioumbwa, juu ya mwanadamu yeyote anayeweza kutekeleza kazi ya Mungu. Kwa hivyo, miongoni mwa wale wote walio na umbo la binadamu kama Lake, miongoni mwa wale wote walio na ubinadamu, Yeye pekee ndiye Mungu mwenye mwili Mwenyewe—wengine wote ni wanadamu walioumbwa. Japokuwa wote wana ubinadamu, wanadamu walioumbwa hawana chochote ila ubinadamu, ilhali Mungu mwenye mwili ni tofauti: katika mwili Wake, si tu kwamba ana ubinadamu ila pia muhimu zaidi Ana uungu. Ubinadamu Wake waweza kuonekana katika mwonekano wa nje wa Mwili Wake na katika maisha Yake ya kila siku; ila uungu Wake ni vigumu kuonekana. Kwa kuwa uungu Wake huonyeshwa pale tu Anapokuwa na ubinadamu, na si wa kimuujiza kama watu wanavyoukisia kuwa, ni vigumu sana kwa watu kuuona. Hata leo hii ni vigumu sana kwa watu kuelewa kiini cha kweli cha Mungu mwenye mwili. Kwa kweli, hata baada ya Mimi kulizungumzia kwa mapana, Natarajia bado liwe fumbo kwa wengi wenu. Suala hili ni rahisi sana: kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, kiini Chake ni muungano wa ubinadamu na uungu. Muungano huu unaitwa Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe duniani.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maisha Aliyoishi Yesu duniani yalikuwa maisha ya kimwili ya kawaida. Aliishi katika ubinadamu wa kawaida wa mwili Wake. Mamlaka Yake—kufanya kazi Yake na kuzungumza neno Lake, au kuwaponya wagonjwa au kufukuza mapepo, kufanya hiyo kazi isiyo ya kawaida—hayakujitokeza, kwa kiasi kikubwa, hadi Alipoanza huduma Yake. Maisha Yake kabla ya umri wa miaka ishirini na tisa, kabla ya Yeye kuanza kutekeleza huduma Yake, yalikuwa uthibitisho tosha kuwa Alikuwa mwili wa kawaida. Kwa sababu ya hili, na kwa kuwa Alikuwa bado Hajaanza kutekeleza huduma Yake, watu hawakuona chochote cha uungu ndani Yake, hawakuona chochote zaidi ya ubinadamu wa kawaida, mwanadamu wa kawaida—kama vile wakati ule baadhi ya watu walimwamini kuwa mwana wa Yosefu. Watu walidhani kuwa Alikuwa mwana wa mwanadamu wa kawaida, hawakuwa na njia ya kugundua kuwa Alikuwa mwili wa Mungu; hata wakati Alipotenda miujiza mingi katika harakati za kutekeleza huduma Yake, watu wengi bado walisema Alikuwa mwana wa Yosefu, kwani Alikuwa Kristo mwenye umbo la nje la ubinadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake wa kawaida pamoja na kazi yake vyote vilikuwepo ili kutimiza umuhimu wa kupata mwili kwa mara ya kwanza, kuthibitisha kuwa Mungu Alikuwa Amekuja katika mwili kwa ukamilifu, kuwa mwanadamu wa kawaida kabisa. Kuwa na ubinadamu wa kawaida kabla ya kuanza kazi Yake ulikuwa uthibitisho kuwa Alikuwa mwili wa kawaida; na kwa kuwa Alifanya kazi baadaye lilithibitisha pia kuwa Alikuwa mwili wa kawaida, kwa kuwa Alifanya ishara na miujiza, kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo katika mwili na ubinadamu wa kawaida. Sababu za kufanya miujiza ilikuwa kwamba mwili Wake ulikuwa umebeba mamlaka ya Mungu, ulikuwa mwili ambamo Roho wa Mungu Alikuwa Amesetiriwa. Alikuwa na mamlaka haya kwa sababu ya Roho wa Mungu, na haikumaanishi kuwa Hakuwa Mwili. Kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo ilikuwa kazi Aliyopaswa kutekeleza katika huduma Yake, onyesho la uungu Wake uliojificha ndani ya ubinadamu Wake, na haijalishi ni ishara za aina gani Alionyesha au Alidhihirisha vipi mamlaka Yake, bado Aliishi katika ubinadamu wa kawaida na bado Alikuwa mwili wa kawaida. Aliishi katika mwili wa kawaida mpaka wakati Alipofufuliwa baada ya kufa msalabani. Aliishi katika mwili wa kawaida. Akitoa neema, Akiwaponya wagonjwa, na kufukuza mapepo hayo yote yalikuwa sehemu ya huduma Yake, hiyo yote ilikuwa kazi Aliyotekeleza katika mwili Wake wa kawaida. Kabla ya kwenda msalabani, Hakuuacha mwili Wake wa kawaida, haijalishi Alikuwa Anafanya nini. Alikuwa Mungu Mwenyewe, Akifanya kazi ya Mungu, lakini kwa sababu Alikuwa Mwili wa Mungu, Alikula chakula na kuvaa nguo, Alikuwa na mahitaji ya kawaida ya binadamu, Alikuwa na fikira za kawaida za binadamu na akili za kawaida. Haya yote yalikuwa uthibitisho kwamba Alikuwa mwanadamu wa kawaida, ambayo yalithibitisha kuwa mwili wa Mungu ulikuwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida, haukuwa wa rohoni. Kazi Yake ilikuwa kukamilisha kazi ya Mungu kupata mwili mara ya kwanza, kutimiza huduma ya kupata mwili mara ya kwanza. Umuhimu wa kupata mwili ni kwamba mtu wa kawaida Anatekeleza kazi ya Mungu Mwenyewe; yaani, kwamba Mungu Anatekeleza kazi Yake ya uungu katika ubinadamu na hivyo kumshinda Shetani. Kupata mwili kunamaanisha kwamba Roho wa Mungu Anakuwa Mwili, yaani, Mungu Anakuwa mwili; kazi Anayoifanya katika mwili ni kazi ya Roho, inayothibitika katika mwili, na kuonyeshwa kwa mwili. Hakuna mwingine ila tu mwili wa Mungu Anayeweza kutimiza huduma ya Mungu mwenye mwili; yaani, mwili wa Mungu kuwa mwili pekee, ubinadamu huu wa kawaida—na hakuna mwingine yeyote—anayeweza kuonyesha kazi ya uungu.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ubinadamu wa Mungu kuwa mwili huwepo kudumisha kazi ya kawaida ya uungu katika mwili; fikira Zake za kawaida za binadamu zinadumisha ubinadamu Wake wa kawaida na shughuli Zake zote za kimwili. Mtu anaweza kusema kuwa fikira zake za kawaida za binadamu zipo ili kudumisha kazi yote ya Mungu katika mwili. Kama mwili huu usingekuwa na akili ya mwanadamu wa kawaida, basi Mungu Asingefanya kazi katika mwili, na Anachopaswa kufanya kimwili kisingetimilika. Japo Mungu mwenye mwili Ana akili ya mwanadamu wa kawaida, kazi Yake haijatiwa doa na mawazo ya binadamu; Anafanya kazi katika ubinadamu na akili ya kawaida chini ya masharti ya awali kuwa atakuwa na ubinadamu na akili ya kawaida, na si na mawazo ya kawaida ya binadamu. Haijalishi mawazo ya mwili Wake ni bora kiasi gani, kazi Yake haionyeshi alama ya mantiki au kufikiria. Kwa maneno mengine, kazi Yake haiwazwi na akili ya mwili Wake, ila ni onyesho la moja kwa moja la kazi ya uungu katika ubinadamu Wake. Kazi Yake yote ni huduma Anayostahili kutimiza, na haiwazwi hata chembe kwa akili Zake. Kwa mfano, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kusulubishwa hayakuwa mazao ya akili Zake za binadamu, yasingeweza kutimizwa na mwanadamu yeyote mwenye akili za binadamu. Vivyo hivyo, kazi ya ushindi ya leo ni huduma ambayo ni sharti itekelezwe na Mungu mwenye mwili, lakini si kazi ya mapenzi ya mwanadamu, ni kazi ambayo uungu Wake unapaswa kufanya, kazi ambayo hakuna mwanadamu wa mwili anaiweza. Kwa hivyo, Mungu mwenye mwili ni lazima Awe na akili za binadamu, ni lazima Awe na ubinadamu wa kawaida, kwa sababu ni lazima Atekeleze kazi Yake katika ubinadamu akiwa na akili za kawaida. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Mungu mwenye Mwili, kiini chenyewe cha Mungu mwenye mwili.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kabla Yesu Hajatekeleza kazi yake, Aliishi tu katika ubinadamu Wake wa kawaida. Hakuna mtu ambaye angeweza kutambua kuwa Alikuwa Mungu, hakuna aliyegundua kuwa Alikuwa Mungu mwenye mwili; watu walimjua tu kama mwanadamu wa kawaida kabisa. Ubinadamu Wake wa kawaida ulikuwa uthibitisho kuwa Mungu Alipata mwili, na kwamba Enzi ya Neema ilikuwa enzi ya kazi ya Mungu mwenye mwili, si enzi ya kazi ya Roho. Ilikuwa uthibitisho kuwa Roho wa Mungu Alipatikana kikamilifu katika mwili, kwamba katika enzi ya kupata mwili kwa Mungu mwili Wake ungetekeleza kazi yote ya Roho. Kristo mwenye ubinadamu wa kawaida ni mwili ambao kwao Roho Hupatikana, Akiwa na ubinadamu wa kawaida, ufahamu wa kawaida, na fikira za wanadamu. “Kupatikana” kunamaanisha Mungu kuwa mwanadamu, Roho kuwa mwili; kuiweka wazi, ni wakati ambapo Mungu Mwenyewe Anaishi katika mwili wenye ubinadamu wa kawaida, na kupitia kwenye huo mwili, Anaonyesha kazi yake ya uungu—hii ndiyo maana ya kupatikana, au kupata mwili.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika kipindi cha Muda ambacho Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi, watu wangeweza kuona kwamba Mungu alikuwa na maonyesho mengi ya kibinadamu. Kwa mfano, Aliweza kucheza, Aliweza kuhudhuria harusi, Aliweza kuwasiliana kwa karibu na watu, kuongea na wao, na kujadili mambo pamoja nao. Aidha, Bwana Yesu aliweza pia kukamilisha kazi nyingi zilizowakilisha uungu Wake, na bila shaka kazi Yake yote ilikuwa ni maonyesho na ufichuzi wa tabia ya Mungu. Katika kipindi hiki, wakati uungu wa Mungu ulitambuliwa kupitia kwa mwili wa kawaida ambao watu wangeweza kuona na kugusa, hawakuhisi tena kwamba Alikuwa akionekana na kutoweka, na kwamba wangeweza kumkaribia. Kinyume cha mambo ni kwamba, wangejaribu kuelewa mapenzi ya Mungu au kuuelewa uungu Wake kupitia kila hatua, maneno, na kazi ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu. Hata ingawa kazi iliyokamilishwa na Bwana Yesu, njia Zake za kufanya kazi, na mitazamo ambayo kutoka kwayo Aliongea ilitofautiana na ile ya nafsi halisi ya Mungu katika ulimwengu wa kiroho, kila kitu kumhusu kilimwakilisha kwa kweli Mungu Mwenyewe ambaye binadamu walikuwa hawajawahi kumwona awali—hili haliwezi kukataliwa! Hivi ni kusema, haijalishi ni kwa umbo gani ambalo Mungu huonekana, haijalishi huongea kutoka katika mtazamo upi, au Yeye hukabiliana na binadamu kupitia kwa taswira gani, Mungu hawakilishi chochote isipokuwa Yeye Mwenyewe. Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote—Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote aliyepotoka. Mungu ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kukataliwa.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ingawa kuonekana kwa Mungu mwenye mwili ni kama mwanadamu, Anajifunza maarifa ya mwanadamu na kuongea lugha ya mwanadamu, na wakati mwingine Anaonyesha hata mawazo Yake kwa jinsi na hisia za mwanadamu, namna Anavyowaona wanadamu, kiini cha vitu, na namna ambavyo watu waliopotoka wanavyomwona mwanadamu na kiini cha vitu kwa hakika si sawa kabisa. Mtazamo Wake na kimo Anachosimamia ni jambo ambalo halifikiwi na mtu aliyepotoka. Hii ni kwa sababu Mungu ni ukweli, mwili Anaouvalia unamiliki pia kiini cha Mungu, na fikira Zake na kile ambacho kinadhihirishwa na ubinadamu Wake pia ni ukweli. Kwa watu waliopotoka, kile Anachoeleza katika mwili ni matoleo ya ukweli na maisha. Matoleo haya si ya mtu mmoja tu lakini kwa wanadamu wote. Kwa mtu yeyote aliyepotoka, katika moyo wake kunao tu wale watu wachache ambao wanahusiana na yeye. Kunao tu hao watu kadhaa ambao anawatunza ambao anajali kuwahusu. Wakati janga linakaribia, anafikiria kwanza kuhusu watoto wake binafsi, mume au mke au wazazi, na mtu mwenye moyo wa kujitoa zaidi kuhusu mwanadamu angefikiria zaidi kuhusu baadhi ya watu wa ukoo au rafiki mzuri; je yeye huwafikiria wengine? La hasha! Kwa sababu binadamu ni, kwa hakika, binadamu, na wanaweza tu kuangalia kila kitu kutoka kwa mtazamo na kutoka katika kimo cha mtu. Hata hivyo, Mungu mwenye mwili ni tofauti kabisa na mtu aliyepotoka. Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha madaraka Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na akili ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka. Watu wanapowaangalia wanadamu, wanawaangalia kwa mtazamo wa binadamu, na wanatumia mambo kama vile maarifa ya binadamu na masharti na nadharia za binadamu kama kipimo. Hali hii imo ndani ya mawanda ya kile ambacho watu wanaweza kuona kwa macho yao; ni ndani ya upana ambao watu waliopotoka wanaweza kutimiza. Mungu anapowatazama wanadamu, Anawatazama kwa macho ya kiungu, na Anatumia kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho kama kipimo. Mawanda haya yanajumuisha mambo ambayo watu hawawezi kuona, na hapo ndipo Mungu mwenye mwili na wanadamu waliopotoka walivyo tofauti kabisa. Tofauti hii inaamuliwa na viini tofauti vya wanadamu na vya Mungu na ndivyo vinavyoamua utambulisho na nafasi zao pamoja na mtazamo na kimo ambacho wanaona mambo.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu ni mwili wa Mungu mwenyewe. Roho wa Mungu ni mkubwa, Yeye ni mwenyezi, mtakatifu, na mwenye haki—na vilevile ndivyo ambavyo mwili Wake ulivyo pia mkubwa, wenye uwezo, mtakatifu, na wenye haki. Mwili kama huo unaweza kufanya tu kile ambacho ni chenye haki na manufaa kwa mwanadamu, kile ambacho ni kitakatifu, chenye utukufu, na uweza, na hakiwezi kukifanya chochote ambacho kinakiuka ukweli au uadilifu na haki, isitoshe hata kile ambacho kinaasi dhidi ya Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni mtakatifu, na hivyo basi mwili Wake hauwezi kuharibiwa na Shetani; mwili Wake una kiini tofauti na ule mwili wa mwanadamu. Kwani ni mwanadamu, wala si Mungu, ambaye anaharibiwa na Shetani, na mwili wa Mungu usingeweza kuharibiwa na Shetani.

kutoka katika “Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo wa kweli sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale wanaojifanya kuwa Kristo wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.

kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)

Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili kamwe hangefanya kazi yoyote ambayo inasumbua usimamizi Wake Mwenyewe. Hili ndilo ambalo binadamu wote wanapaswa kuelewa. Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya usimamizi wa Mungu Mwenyewe. Vile vile, kazi ya Kristo ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Kutokana na kwamba Mungu Anapata mwili, Anatambua dutu Yake ndani ya mwili Wake, kama kwamba mwili Wake ni wa kutosha kufanya kazi Yake. Kwa hivyo, kazi zote za Roho wa Mungu zinabadilishwa na kazi ya Kristo wakati wa kupata mwili, na kwenye msingi wa kazi zote wakati wa kupata mwili ni kazi ya Kristo. Haiwezi kuchanganyika na kazi yoyote ile kutoka enzi nyingine yoyote. Na kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, Yeye Anafanya kazi katika utambulisho wa mwili Wake; kwa kuwa Yeye hukuja katika mwili, kisha Yeye humaliza katika mwili kazi hiyo Anayoazimia kufanya. Iwe ni Roho wa Mungu au ni Kristo, wote ni Mungu Mwenyewe, na Anafanya kazi hiyo Anayoazimia kufanya na hufanya huduma hiyo Anayopaswa kufanya.

Dutu ya Mungu yenyewe hushika na kutumia mamlaka, lakini Yeye Anao uwezo wa kuwasilisha kwa ukamilifu mamlaka ambayo hutoka Kwake. Iwe ni kazi ya Roho au kazi ya mwili, hakuna ambayo itazozana na nyingine. Roho wa Mungu ndiyo mamlaka juu ya viumbe vyote. Mwili na dutu ya Mungu pia inayo mamlaka, bali Mungu katika mwili Anaweza kufanya kazi yote inayotii mapenzi ya Baba wa mbinguni. Hii haiwezi kupatikana au kufanyika na binadamu yeyote. Mungu Mwenyewe ni mamlaka, lakini mwili Wake unaweza kunyenyekea kwa mamlaka Yake. Hii ndiyo maana ya ndani ya maneno: “Kristo hutii mapenzi ya Mungu Baba.” Mungu ni Roho na Anaweza kufanya kazi ya wokovu, kama vile Mungu Anavyoweza kuwa mwanadamu. Hata hivyo, Mungu Mwenyewe Anafanya kazi Yake Mwenyewe; Yeye wala hazuii wala kuathiri, wala kufanya kazi inayozipinganisha pande zote mbili, kwa kuwa kiini cha kazi iliyofanywa na Roho na mwili yote ni sawa. Iwe ni Roho au mwili, vyote hufanya kazi kutimiza nia moja na kusimamia kazi sawa. Ingawa Roho na mwili huwa na sifa mbili tofauti, dutu yao ni sawa; zote zina dutu ya Mungu Mwenyewe, na utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Mungu Mwenyewe hana mambo ya kuasi; dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote. Hata katika mwili, Mungu hafanyi lolote linalomuasi Mungu Baba. Hata kwa gharama ya kutoa sadaka maisha Yake, Angekuwa kwa ukamilifu tayari na kutofanya uchaguzi mwingine. Mungu hana mambo ya ukamilifu wa kibinafsi na umuhimu wa kibinafsi, au yale wa kujiona na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na ile ya Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelaghaiwa na kufinyangwa Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani. Haijalishi ugumu wa kazi, au udhaifu wa mwili, Mungu, wakati Anapoishi katika mwili, kamwe hatafanya kitu chochote kitakachopinga kazi ya Mungu Mwenyewe, wala kuacha mapenzi ya Mungu Baba kwa njia ya uasi. Ni afadhali Ateseke maumivu ya mwili kuliko kwenda kinyume na matakwa ya Mungu Baba; ni kama vile Yesu Alisema katika sala, “Baba, kama inawezekana, kikombe hiki kiniondokee: hata hivyo si kama Mimi Nipendavyo, bali kama Wewe upendavyo.” Wanadamu watachagua, bali Kristo hawezi. Ingawa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe, bado Yeye Anatafuta mapenzi ya Mungu Baba, na Anatimiza kile Alichokabidhiwa na Mungu Baba, kutoka kwa mtazamo wa mwili. Hili ni jambo ambalo haliwezi kupatikana kwa binadamu. Hilo ambalo huja kutoka kwa Shetani haliwezi kuwa na dutu ya Mungu, bali mojawapo ya yale ambayo hukosa kutii na kumpinga Mungu. Haliwezi kumtii Mungu kikamilifu, wala kutii mapenzi ya Mungu kwa hiari. Wanadamu wote isipokuwa Kristo wanaweza kufanya yaliyo ya kumpinga Mungu, na hakuna anayeweza moja kwa moja kufanya kazi aliyoaminiwa na Mungu; hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuzingatia usimamizi wa Mungu kama wajibu wake wenyewe kutekeleza. Kuwasilisha mapenzi ya Mungu Baba ni kiini cha Kristo; uasi dhidi ya Mungu ni tabia ya shetani. Sifa hizo mbili hazipatani, na yeyote aliye na sifa za shetani hawezi kuitwa Kristo. Sababu ambayo binadamu hawezi kufanya kazi ya Mungu kwa niaba Yake ni kwa sababu mwanadamu hana kiini chochote cha Mungu. Binadamu humfanyia Mungu kazi kwa ajili ya maslahi binafsi ya binadamu na ya matarajio Yake ya baadaye, lakini Kristo Anafanya kazi ya kufanya mapenzi ya Mungu Baba.

Ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake. Ingawa yuko katika mwili, ubinadamu Wake si kama ule wa binadamu wa mwili kabisa. Anao upekee wa tabia Yake Mwenyewe, na hii pia huongozwa na uungu Wake. Uungu Wake hauna udhaifu; udhaifu wa Kristo unaelezea ule wa ubinadamu Wake. Kwa kiasi fulani, udhaifu huu huzuia uungu Wake, lakini mipaka hiyo ipo tu kati ya wigo fulani na wakati, na sio zisizo na mipaka. Linapokuja suala la muda wa kufanya kazi ya uungu Wake, hufanyika bila kujali ubinadamu Wake. Ubinadamu wa Kristo kabisa huongozwa na uungu Wake. Mbali na maisha ya kawaida ya ubinadamu Wake, matendo mengine yote ya ubinadamu Wake ni ya kushawishiwa, inayoathirika na kuelekezwa na uungu Wake. Ingawa Kristo Anao ubinadamu, haukatizi kazi ya uungu Wake. Hii hasa ni kwa sababu ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake; ingawa ubinadamu Wake haujakomaa katika mwenendo Wake mbele ya wengine, hauathiri kazi ya kawaida ya uungu Wake. Ninaposema kwamba ubinadamu Wake haujapotoshwa, Ninamaanisha kwamba ubinadamu wa Kristo unaweza moja kwa moja kuongozwa na uungu Wake, na kwamba Yeye ni mwenye hisia kubwa kuliko ile ya mwanadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake unafaa zaidi kwa kuongozwa na uungu katika kazi Yake; ubinadamu Wake una uwezo wa kuonyesha kazi ya uungu, kama vile unao uwezo wa kutii kazi kama hiyo. Mungu Anapofanya kazi katika mwili, hajawahi kamwe kupoteza maono ya wajibu wa mwanadamu katika mwili Anaopaswa kutimiza; Anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli. Anayo dutu ya Mungu, na utambulisho Wake ni mfano wa Mungu Mwenyewe. Ni kwamba tu Amekuja duniani na kuwa kiumbe aliyeumbwa, na ganda la nje la kiumbe, na sasa Amemiliki ubinadamu ambao hakuwa nao mwanzo; Yeye anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni. Hiki ni kiumbe cha Mungu Mwenyewe na hakiigwi na binadamu. Utambulisho Wake ni Mungu Mwenyewe. Ni kutokana na mtazamo wa mwili ndio Yeye huabudu Mungu; Kwa hivyo, maneno “Kristo huabudu Mungu mbinguni” si kwa makosa. Kile Anachouliza binadamu hasa ni nafsi Yake Mwenyewe; Yeye tayari Ameshafanikisha yote Anayotarajia kutoka kwa binadamu kabla ya kuwauliza wafanye hayo. Asingeweza kudai wengine wakati Yeye Mwenyewe Anapata kwao bure, kwa kuwa haya yote yanayotengeneza nafsi Yake. Bila kujali jinsi Yeye hufanya kazi Yake, wala Naye hangewahi kutenda kwa namna inayomuasi Mungu. Haijalishi Analomuuliza mwanadamu, hakuna mahitaji Yake yanayozidi uwezo wa mwanadamu kupata. Yote Afanyayo ni kutenda mapenzi ya Mungu na ni kwa ajili ya usimamizi Wake. Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote, kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa. Mamlaka haya ni uungu Wake, yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe, ambayo huamua utambulisho Wake. Kwa hiyo, haijalishi jinsi ubinadamu Wake ni wa kawaida ni wazi kuwa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe; haijalishi upande Anaosimama Akiongea na kwa vyovyote vile Yeye hutii mapenzi ya Mungu, haiwezi kusemwa kwamba Yeye si Mungu Mwenyewe. Wanadamu wajinga na wapumbavu mara nyingi huchukua ubinadamu wa kawaida wa Kristo kama dosari. Haijalishi jinsi Anavyofichua na kuonyesha nafsi ya uungu Wake, mwanadamu bado hawezi kukiri kwamba Yeye ni Kristo. Na zaidi kwamba Kristo Anaonyesha utii Wake na unyenyekevu, ndivyo wanadamu wengi wajinga humchukua Kristo kwa mzaha. Kuna hata wale ambao huelekeza Kwake mtizamo wa kutengwa na dharau, ilhali kuweka wale “wanadamu wakubwa” wa picha ya kujidai juu ya meza na kuwaabudu. Upinzani wa binadamu dhidi ya, na uasi wa Mungu huja kutokana na ukweli kwamba kiini cha Mungu mwenye mwili hutii mapenzi ya Mungu, vile vile kutokana ubinadamu wa kawaida wa Kristo; hapa ndipo kuna chanzo cha upinzani wa binadamu na uasi wake kwa Mungu. Kama Kristo hangekuwa mwenye umbo la ubinadamu wala nia ya kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe aliyeumbwa, lakini badala yake kumiliki ubinadamu mkuu, basi kuna uwezekano hakungekuwa na uasi katika mwanadamu yeyote. Sababu ya binadamu kuwa tayari kuamini katika Mungu Asiyeonekana mbinguni ni kwa sababu Mungu mbinguni hana ubinadamu na Yeye hana sifa ya kiumbe hata moja. Hivyo binadamu siku zote humchukua Yeye kwa heshima kubwa, lakini anayo tabia ya dharau kwa Kristo.

Ingawa Kristo duniani Anaweza kufanya kazi kwa niaba ya Mungu Mwenyewe, hajakuja na nia ya kuonyesha watu wote mfano Wake katika mwili. Yeye hajakuja kwa watu wote kumwona; Anakuja kwa ajili ya kuwaruhusu binadamu kuongozwa na mkono Wake, na hivyo kuingia katika enzi mpya. Kazi ya mwili wa Kristo ni kwa ajili ya kazi ya Mungu Mwenyewe, yaani, kwa ajili ya kazi ya Mungu katika mwili, na si ili kuwawezesha binadamu kuelewa kikamilifu kiini cha mwili Wake. Haijalishi jinsi Anavyofanya kazi, haiwezi kuzidi yanayoweza kupatwa na mwili. Haijalishi jinsi Anavyofanya kazi, anafanya hivyo katika mwili na ubinadamu wa kawaida, na wala hafichui kwa kikamilifu kwa mwanadamu uso wa kweli wa Mungu. Zaidi ya hayo, kazi Yake katika mwili kamwe sio isiyo ya kawaida au isiyokadirika kama mwanadamu anavyodhani. Japokuwa Kristo Anamwakilisha Mungu Mwenyewe katika mwili na hufanya binafsi ambayo Mungu Mwenyewe Anapaswa kufanya, Yeye hakani kuwepo kwa Mungu mbinguni, wala kuyatangaza matendo Yake Mwenyewe kwa msisimko. Badala yake, Yeye kwa unyenyekevu Hubaki kwa siri ndani ya mwili Wake. Mbali na Kristo, wale ambao wanadai kwa udanganyifu kuwa Kristo hawana sifa Zake. Wakiwekwa sambamba dhidi ya tabia za kiburi na kujiinua za Kristo wa uongo, inakuwa dhahiri aina gani ya mwili ndiye Kristo wa kweli. Walivyo waongo zaidi, ndivyo Kristo wa uongo wanavyojionyesha wenyewe, na ndivyo wanavyoweza zaidi kufanya kazi za ishara na maajabu ya kuwahadaa binadamu. Kristo wa uongo hawana sifa za Mungu; Kristo hajachafuliwa na kipengele chochote cha dutu ya Kristo wa uongo. Mungu hupata mwili tu kukamilisha kazi ya mwili, na sio tu kuwaruhusu watu wote kumwona. Badala yake, Yeye huacha kazi Yake ithibitishe utambulisho Wake, na kuruhusu Anachofichua kushuhudia dutu Yake. Dutu Yake haikosi msingi; utambulisho Wake haukukamatwa na mkono Wake; huamuliwa kwa kazi Yake na dutu Yake. Ingawa Anacho kiini cha Mungu Mwenyewe na uwezo wa kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, Yeye bado, hata hivyo, mwili ambao sio kama Roho. Yeye si Mungu na sifa za Roho; Yeye ni Mungu na ganda la mwili. Kwa hivyo, haijalishi jinsi ya ukawaida Wake na Alivyo mdhaifu, na vyovyote vile Anavyotafuta mapenzi ya Mungu Baba, uungu Wake ni usioweza kupingwa. Katika mwili wa Mungu haupo tu ubinadamu wa kawaida na udhaifu Wake; kunao hata zaidi uzuri na mambo yasiyoeleweka ya uungu Wake, na vile vile matendo Yake yote katika mwili. Kwa hiyo, ubinadamu na uungu kwa kweli vipo kwa matendo ndani ya Kristo. Hili sio jambo tupu au lisilo la kawaida kwa vyovyote vile. Yeye huja duniani na lengo kuu la kufanya kazi; ni muhimu kumiliki ubinadamu wa kawaida kutekeleza kazi duniani; la sivyo, haijalishi ukubwa wa nguvu ya uungu Wake, kazi Yake ya awali haiwezi kutiwa katika utumizi mzuri. Ingawa ubinadamu Wake ni wa umuhimu mkubwa, sio dutu Yake. Dutu Yake ni uungu; Kwa hiyo, wakati Anapoanza kufanya huduma Yake hapa duniani ndio wakati Yeye huanza kuonyesha nafsi ya uungu Wake. Ubinadamu Wake uko kwa ajili tu ya kuendeleza maisha ya kawaida ya mwili Wake ili uungu Wake uweze kufanya kazi kama kawaida katika mwili; ni uungu ndio unaoongoza kazi Yake kwa ukamilifu. Wakati Anapomaliza kazi Yake, Atakuwa Ametimiza mujibu wa huduma Yake. Wanachopaswa kujua wanadamuni ni ukamilifu wa kazi Yake, na ni kwa njia ya kazi Yake kuwa Yeye Humwezesha binadamu kumjua Yeye. Katika kipindi cha kazi Yake, Yeye huonyesha kikamilifu kabisa nafsi ya uungu Wake, ambayo si tabia iliyochafuliwa na ubinadamu, au nafsi iliyochafuliwa na mawazo na tabia za binadamu. Wakati utakapokuja ambapo huduma Yake yote imefika mwisho, Atakuwa tayari kwa kikamilifu na kikamilifu Amekwishaonyesha tabia hiyo Anayopaswa kueleza. Kazi Yake haifundishwi na mwanadamu yeyote; maonyesho ya tabia Yake pia ni huru kabisa, haudhibitiwi na akili au kutengenezwa na mawazo, bali hujitokeza kiasili. Hili haliwezi kutimizwa na binadamu yeyote. Hata kama mazingira ni magumu au hali haziruhusu, Yeye Anao uwezo wa kuonyesha tabia Yake kwa wakati muafaka. Yule Ambaye ni Kristo Anaonyesha nafsi ya Kristo, ilhali wale ambao sio hawana tabia za Kristo. Kwa hivyo, hata kama wote watampinga Yeye au kuwa na fikira Kwake, hakuna anayeweza kukana kwa misingi ya fikira ya mwanadamu kwamba tabia iliyoonyeshwa na Kristo ni ile ya Mungu. Wale wote ambao humfuata Kristo kwa moyo wa kweli au kumtafuta Mungu kwa nia watakubali kwamba Yeye ni Kristo kulingana na maonyesho ya uungu Wake. Wao kamwe hawangewahi kumkataa Kristo kwa misingi ya kipengele chochote Chake ambacho hakipatani na fikira za mwanadamu. Ingawa binadamu ni wapumbavu sana, wote wanajua hasa ni nini mapenzi ya binadamu na kile kitokacho kwa Mungu. Ni kwamba tu watu wengi kwa makusudi humpinga Kristo kutokana na makusudi yao wenyewe. Kama si kwa ajili ya haya, hakuna hata mwanadamu mmoja angekuwa na sababu ya kukataa kuwepo kwa Kristo, kwa kuwa uungu uliodhihirishwa na Kristo kwa hakika upo, na kazi Yake inaweza kushuhudiwa kwa macho ya wote.

Kazi na maonyesho ya Kristo huamua dutu Yake. Yeye Anaweza kukamilisha kwa moyo wa kweli kile Alichoaminiwa kufanya. Anaweza kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli, na kwa moyo wa kweli Atafute mapenzi ya Mungu Baba. Yote haya yanaamuliwa na dutu Yake. Na vile vile ufunuo Wake wa asili pia unaamuliwa na dutu Yake; sababu ya ufunuo Wake wa asili kuitwa hivyo ni kwa sababu ya maonyesho Yake siyo maigizo, au matokeo ya elimu na mwanadamu, au matokeo ya miaka mingi ya kukuzwa na mwanadamu. Hakujifunza au kujivika nayo Yeye Mwenyewe; badala yake, ni asili ndani Yake. Mwanadamu anaweza kukataa kazi Yake, maonyesho Yake, ubinadamu Wake, na maisha yote ya ubinadamu Wake wa kawaida, lakini hakuna hata mmoja anayeweza kukana kwamba Yeye humwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli; hakuna anayeweza kukana kwamba Amekuja kutimiza mapenzi ya Baba wa mbinguni, na hakuna anayeweza kukana uaminifu Alio nao Anapomtafuta Mungu Baba. Ingawa mfano Wake si wa kupendeza hisia, ingawa hotuba Yake haujajawa na hewa ya ajabu, na kazi Yake sio ya kutikisa ulimwengu au mbingu vile mwanadamu anavyofikiria, Yeye hakika ni Kristo, Anayetimiza mapenzi ya Baba wa mbinguni kwa moyo wa kweli, Ananyenyekea kikamilifu kwa Baba wa mbinguni, na ni mtiifu mpaka wakati kifo. Hii ni kwa sababu dutu Yake ni dutu ya Kristo. Ukweli huu ni mgumu kwa mwanadamu kuamini lakini kwa kweli upo. Wakati huduma ya Kristo imetimia kikamilifu, mwanadamu ataweza kuona kutokana na kazi Zake kwamba tabia Yake na nafsi Yake yanawakilisha tabia na nafsi ya Mungu huko mbinguni. Wakati huo, ujumla wa kazi Zake zote utaweza kuthibitisha kwamba Yeye kweli ni Neno linalogeuka mwili, na si sawa na ule wa mwili na damu ya mwanadamu. Kila hatua ya kazi ya Kristo duniani ina umuhimu wakilishi Wake, lakini mwanadamu anayepitia kazi halisi ya kila hatua hawezi kufahamu umuhimu wa kazi Yake. Hii hasa ni vile katika hatua kadhaa za kazi zilizofanywa na Mungu mwenye mwili mara ya pili. Wengi wa wale ambao wamesikia tu au kuona maneno ya Kristo tu lakini bado hawajawahi kumwona hawana fikira ya kazi Yake; wale ambao wamemwona Kristo na kusikia maneno Yake, na vile vile kupitia kazi Yake, huona ugumu kuikubali kazi Yake. Je, hii si kwa sababu ya kwamba kuonekana na ubinadamu wa kawaida kwa Kristo hakulingani na matarajio ya binadamu? Wale wanaokubali kazi Yake baada ya Kristo kwenda hawatakuwa na matatizo kama hayo, kwa kuwa wao wanaikubali kazi Yake na wala hawapati kukutana na ubinadamu wa kawaida wa Kristo. Mwanadamu hawezi kuacha fikira zake kuhusu Mungu na badala yake humchunguza kwa mkazo; hii ni kutokana na ukweli kwamba mwanadamu analenga tu juu ya kuonekana Kwake na anashindwa kutambua dutu Yake kwa kuzingatia kazi Yake na maneno Yake. Iwapo mwanadamu ataufumbia macho kuonekana kwa Kristo au kuepuka kujadili ubinadamu wa Kristo, na aongee tu juu ya uungu Wake, Ambao kazi Yake na maneno hayawezi kufikiwa na mwanadamu yeyote, basi fikira ya binadamu itapungua kwa nusu, hata kwa kiasi kwamba matatizo yote ya mwanadamu yatatatuliwa. Wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, mwanadamu hawezi kumvumilia na amejaa wingi wa fikira mbalimbali kumhusu, na matukio ya upinzani na uasi ni kawaida. Binadamu hawezi kuvumilia kuwepo kwa Mungu, kuonyesha “upole” kwa unyenyekevu na kujificha kwa Kristo, au “kuisamehe” dutu ya Kristo inayomtii Baba wa mbinguni. Kwa hivyo, Hawezi kukaa na mwanadamu milele baada ya kumaliza kazi Yake, kwa kuwa mwanadamu hana nia ya kumruhusu kuishi pamoja nao. Iwapo mwanadamu hawawezi “kuonyesha upole” Kwake katika kipindi Chake cha kazi, basi, ni jinsi gani wangeweza kumvumilia Yeye kuishi nao baada ya kumaliza kutekeleza shughuli Zake, kuwaangalia hatua kwa hatua na wakipitia maneno Yake? Je, si wengi kisha wangeanguka kwa ajili Yake? Mwanadamu anamruhusu tu kufanya kazi duniani; hiki ndicho kiasi kikubwa zaidi cha upole wa mwanadamu. Kama si kwa sababu ya kazi Yake, mwanadamu angekuwa ameshamtupa nje ya dunia, hivyo kwa kiasi gani kidogo wangeweza kumwonyesha upole mara kazi Yake inapokamilika? Basi si mwanadamu angemuua na kumtesa hadi kufa? Iwapo Yeye hangekuwa Anaitwa Kristo, basi kuna uwezekano hangewahi kufanya kazi miongoni mwa wanadamu; iwapo hangefanya kazi na utambulisho wa Mungu Mwenyewe, na badala yake Afanye kazi tu kama mwanadamu wa kawaida, basi mwanadamu hangevumilia sentensi hata moja kutamkwa Naye, wala kuvumilia hata kiasi kidogo cha kazi Yake. Basi Anaweza kubeba tu utambulisho huu pamoja Naye katika kazi Yake. Kwa njia hii, kazi Yake ni ya nguvu zaidi kuliko kama hangefanya hivyo, kwa kuwa binadamu wote wako tayari kutii hadhi na utambulisho mkubwa. Iwapo Yeye hangekuwa na utambulisho wa Mungu Mwenyewe Alipokuwa akifanya kazi ama kuonekana kama Mungu Mwenyewe, basi hangekuwa na nafasi ya kufanya kazi hata kidogo. Ingawa Yeye Anayo dutu ya Mungu na nafsi ya Kristo, mwanadamu hangelegea na kumruhusu kufanya kazi kwa urahisi miongoni mwa wanadamu. Yeye hubeba utambulisho wa Mungu Mwenyewe katika kazi Yake; ingawa kazi hiyo ina nguvu mara kadhaa zaidi kuliko ile hufanyika bila utambulisho huo, bado wanadamu sio watiifu Kwake kikamilifu, kwa kuwa binadamu hunyenyekea tu kwa msimamo Wake wala si dutu Yake. Kama ni hivyo, wakati labda siku moja Kristo aamue kujiuzulu kutoka katika wadhifa Wake, inawezekana mwanadamu amruhusu kubaki hai hata kwa siku moja? Mungu yuko tayari kuishi duniani na binadamu ili Aweze kuona matokeo ambayo kazi ya mikono Yake italeta katika miaka itakayofuata. Hata hivyo, binadamu wanashindwa kuvumilia kukaa Kwake duniani hata siku moja, hivyo inamfanya kukata tamaa. Tayari ni kiasi kikubwa cha upole na neema ya mwanadamu kumruhusu Mungu kutenda kazi Anayopaswa kufanya miongoni mwa wanadamu na kutimiza huduma Yake. Ingawa wale ambao wameshindwa kibinafsi na Yeye wanamwonyesha neema kuu, bado tu wamempa kibali cha kuwepo tu kwa ajili ya kutimiza kazi Yake na si hata saa moja zaidi baada ya kukamilisha kazi hiyo. Iwapo ni hivyo, je itakuwaje na wale ambao bado hawajashindwa na yeye? Je, sababu ambayo mwanadamu anamtendea Mungu mwenye mwili kwa njia hii ni kwa sababu Yeye ni Kristo na ganda la binadamu wa kawaida? Iwapo Angekuwa tu na uungu na sio ubinadamu wa kawaida, basi si matatizo ya binadamu yangetatuliwa kwa urahisi mno? Binadamu kishingo upande anatambua uungu Wake na haonyeshi haja yoyote katika ganda Lake la ubinadamu wa kawaida, licha ya ukweli kwamba dutu Yake ni sawa hasa kama vile ile ya Kristo inayonyenyekea kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kwa sababu hii, Aliweza tu kuikomesha kazi Yake ya kuwa miongoni mwa wanadamu kushiriki pamoja nao katika furaha na huzuni, kwa kuwa mwanadamu hangeweza tena kuvumilia uwepo Wake.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 23 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Kwa Kupinga Mungu kwa Ukaidi, Binadamu Anaangamizwa na Hasira za Mungu
Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu Sodoma Yaangamizwa kwa Kukosea Hasira za Mungu
Baada ya Ukinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Ukatili Wao Dhidi Yake, Mungu Anaufuta Kabisa
Mwenyezi Mungu alisema, Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu
Kwenye usiku huo, Lutu alipokea wajumbe wawili kutoka kwa Mungu na akawatayarishia karamu. Baada ya chajio, kabla hawajalala, watu kutoka kila pahali kwenye mji walizunguka makazi ya Lutu na kumwita nje Lutu. Maandiko yanawarekodi wakisema, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua.” Ni nani aliyesema maneno haya? Alikuwa akiwaambia kina nani? Haya yalikuwa maneno ya watu wa Sodoma, walipiga mayowe nje ya makazi ya Lutu wakinuia kumwita Lutu. Je, unahisi vipi ukiyasikia maneno haya? Unaghadhibishwa? Je, maneno haya yanakuhuzunisha? Je, unabubujikwa na hasira kali? Je, Huoni kwamba maneno haya yananuka Shetani? Kupitia kwa maneno haya, unaweza kuhisi uovu na giza vilivyomo kwenye mji huu? Je, unaweza kuhisi ukatili na ushamba wa tabia za watu hawa kupitia kwa maneno yao? Je, unaweza kuhisi kina cha kupotoka kwao kupitia kwa tabia yao? Kupitia kwa maudhui ya hotuba yao, si vigumu kuona kwamba asili yao ya dhambi na tabia yao iliyopotoka ilikuwa imefikia kiwango kilichokuwa zaidi ya wao kuidhibiti. Isipokuwa Lutu, kila mtu katika mji huu hakuwa tofauti na Shetani; ule mtazamo tu wa mtu mwingine uliwafanya watu hawa kutaka kudhuru na kuwapotosha wao…. Mambo haya hayampatii tu mtu hisia ya asili potovu na ya kutisha ya mji huu, lakini pia yanamwonyesha harufu ya kifo iliyouzunguka mji huu; yanampa pia mtu hisia za dhambi na umwagikaji wa damu.
Alipojipata uso kwa uso na genge la majambazi waliojaa ukatili, watu waliokuwa wamejaa na maono ya kupotosha nafsi, Lutu aliitikia vipi? Kulingana na Maandiko: “Nawaomba … msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu.” Lutu alimaanisha yafuatayo katika maneno yake: Alikuwa radhi kuwatoa binti zake wawili ili kuwalinda wale wajumbe. Kutokana na akili razini, watu hawa wangekubali masharti ya Lutu na kuwaacha wale wajumbe wawili pekee; kwani hata hivyo, wajumbe hao walikuwa watu wageni kabisa kwao, watu ambao hawakuwa na chochote katu kuhusiana na wao; wajumbe hawa wawili walikuwa hawajawahi kudhuru masilahi yao. Hata hivyo, wakiwa na motisha ya asili yao ya dhambi, hawakuliwachia suala hili hapo. Badala yake, walizidisha tu jitihada zao. Hapa mojawapo ya mabishano yao yanaweza bila shaka kumpatia mtu maono zaidi kuhusu asili ya kweli na potovu ya watu hawa; wakati uo huo yanatujuza na kutufanya tuelewe sababu ya Mungu kutaka kuuangamiza mji huu.
Kwa hivyo walisema nini baadaye? Kama vile Biblia inavyosoma: “Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango.” Kwa nini walitaka kuuvunja mlango? Sababu ni kwamba walikuwa na hamu kubwa zaidi ya kuwadhuru wale wajumbe wawili. Wale wajumbe walikuwa wakifanya nini Sodoma? Kusudio lao la kuja hapo lilikuwa ni kumwokoa Lutu na familia yake; hata hivyo, watu wa mji huo walifikiri kimakosa kwamba walikuwa wamekuja kuchukua nyadhifa zao rasmi. Bila ya kuulizia kusudio lao, ilikuwa tu hali ya kujiamulia kufanya mambo kabla ya kujua ukweli wake, iliyoufanya mji huo kutaka kuwadhuru vibaya wajumbe hawa wawili; walitaka kuwadhuru watu wawili ambao hawakuhusiana kwa vyovyote vile na wao. Ni wazi kwamba watu wa mji huu walikuwa wamepoteza kabisa ubinadamu na akili zao razini. Kiwango cha wendawazimu wao na kukosa ustaarabu kwao kilikuwa tayari si tofauti na asili potovu ya Shetani ya kudhuru na kudanganya binadamu.
Walipowaamuru watu hawa watoke kwa Lutu, Lutu alifanya nini? Kutoka kwenye maandishi yanayofuata tunajua kwamba Lutu hakuwakabidhi wajumbe hawa kwa watu hawa. Je, Lutu aliwajua wajumbe hawa wawili wa Mungu? Bila shaka la! Lakini kwa nini aliweza kuwaokoa watu hawa wawili? Je, alijua ni nini walichokuwa wamekuja kufanya? Ingawaje hakujua kuhusu sababu yao ya kuja, alijua kwamba walikuwa ni watumishi wa Mungu, na kwa hivyo aliwapokea. Kwamba aliweza kuwaita watumishi hawa wa Mungu mabwana yaonyesha kwamba Lutu kwa kawaida alikuwa ni mfuasi wa Mungu, tofauti na wale wengine waliokuwa ndani ya Sodoma. Kwa hivyo, wakati wajumbe wa Mungu walipomjia, alihatarisha maisha yake binafsi ili kuwapokea watumishi hao wawili; aidha, aliwakabidhi binti zake wawili badala ya watumishi hao wawili ili kuwalinda watumishi hao. Hiki ndicho kitendo cha haki ya Lutu; vilevile ni onyesho linaloonekana waziwazi kuhusu asili na hali halisi ya Lutu, na ndiyo pia sababu ya Mungu kuwatuma watumishi Wake ili kumwokoa Lutu. Wakati alipokabiliwa na changamoto, Lutu aliwalinda watumishi hawa wawili bila kujali chochote kingine; alijaribu hata kufanya biashara ya kuwabadilisha binti zake wawili mradi tu watumishi hawa wapate usalama. Mbali na Lutu, kulikuwa na mtu yeyote mwingine ndani ya mji ambaye angefanya jambo kama hili? Kama vile hoja zinavyothibitisha—la! Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba kila mtu katika Sodoma, isipokuwa Lutu, alikuwa mlengwa wa kuangamizwa pamoja na mlengwa aliyestahili kuangamizwa.

Jumatano, 27 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Ikiwa watu wanaweza kweli kuielewa kikamilifu njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Wasingetamani tena kuwatumikia wazazi wao ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Je, mategemeo ya baadaye na majaliwa ya mwanadamu si kabisa kile kinachodaiwa nyakati za sasa kuwa “wazazi” wa Petro? Yamekuwa kama tu mwili na damu ya mwanadamu. Je, hatima, mategemeo ya baadaye ya mwili yatakuwa ni kumwona Mungu wakati ukiwa hai, au kwa roho kukutana na Mungu baada ya kifo? Je, mwili kesho utaishia katika tanuu kubwa kama katika taabu, au utakuwa katika kuteketezwa kwa moto? Je, maswali kama haya yanayohusu iwapo mwili wa mwanadamu utahimili taabu au mateso ni habari kubwa sana ambayo kila mtu sasa katika mkondo huu ambaye ana ubongo na akili yake iko sawa anahangaika zaidi nayo? (Hapa, kuhimili mateso hurejelea kupokea baraka; kuteseka humaanisha kwamba majaribu ya siku zijazo ni yenye manufaa kwa hatima ya mwanadamu. Taabu hurejelea kushindwa kusimama imara, au kudanganywa; au, humaanisha kwamba mtu anakabiliana na hali ya hatari ya bahati mbaya katikati ya majanga na maisha yake yanakuwa magumu kuendelea nayo, na kwamba hakuna hatima nzuri kwa roho.) Watu wanajitayarisha na mantiki timamu lakini pengine kile wanachofikiri hakifanani kabisa na kile ambacho mantiki yao inapaswa kutayarishwa nayo. Hii ni kwa sababu ni wajinga kiasi na wanafuata vitu bila kufikiri. Wote wanapaswa kuwa na uelewe wa kina wa kile ambacho wanapaswa kuingia kwacho, na kwa mahususi wanapaswa kutatua kile wanachopaswa kuingia kwacho wakati wa mateso (yaani, wakati wa utakasaji wa tanuu), na kile wanachopaswa kutayarishwa nacho katika jaribu la moto. Usiwatumikie wazazi wako siku zote (kumaanisha mwili) ambao ni sawa na nguruwe na mbwa, na ni wabaya zaidi kuliko chungu na wadudu. Kuna haja gani ya kuteseka juu ya hilo, kufikiri sana, kuutesa ubongo wako? Mwili si wako, bali upo katika mikono ya Mungu ambaye Hakudhibiti wewe pekee bali pia Anamwamuru Shetani. (Kwa asili ilimaanisha kuwa ulikuwa wa Shetani. Kwa kuwa Shetani pia yupo mikononi mwa Mungu, ingeweza kuwekwa hivyo tu. Maana inashawishi zaidi kusema namna hiyo—inamaanisha kuwa wanadamu hawapo chini ya miliki ya Shetani kabisa, bali wapo mikononi mwa Mungu.) Unaishi chini ya mateso ya mwili, lakini je, mwili ni wako? Upo chini ya udhibiti wako? Kwa nini usumbuke kufikiri sana juu ya hilo? Kwa nini usumbuke sana kumsihi Mungu kwa ajili ya mwili wako uliooza ambao umeshahukumiwa zamani sana na kulaaniwa, vilevile kutiwa najisi na roho wachafu? Kwa nini usumbuke siku zote kwa kushikilia washirika wa Shetani karibu na moyo wako? Huna wasiwasi kwamba mwili unaweza kuharibu mategemeo yako halisi ya baadaye, matumaini mazuri, na hatima ya kweli ya maisha yako?
Njia ya leo si rahisi kuitembea. Mtu anaweza kusema kwamba ni vigumu kuipitia na ni adimu sana katika enzi zote. Hata hivyo, nani angeweza kufikiri kuwa mwili wa mwanadamu pekee unatosha kumwangamiza mara moja? Kazi leo hakika ni ya thamani kama vile mvua wakati wa majira ya kuchipua na ni ya thamani kama wema wa Mungu kwa mwanadamu. Hata hivyo, ikiwa mwanadamu hajui kusudi la kazi Yake leo au kuelewa kiini cha mwanadamu, inawezekanaje tunu na thamani yake vizungumziwe? Mwili si wa wanadamu wenyewe, hivyo kwa kweli hakuna mtu anayeweza kuona waziwazi hatima yake itakuwa wapi. Hata hivyo, unapaswa kujua vizuri kwamba Mungu wa uumbaji Atawarudisha binadamu, ambao waliumbwa, katika nafasi yao ya asili, na kurejesha sura yao ya asili kutoka wakati wa kuumbwa kwao. Atachukua tena kikamilifu pumzi Aliyompuliza ndani ya binadamu, na kuchukua tena mifupa na mwili wake na kurudisha vyote kwa Bwana wa viumbe. Atabadilisha na kufanya upya binadamu kikamilifu, na kuchukua tena kutoka binadamu urithi wote ambao kwa asili haukuwa wa binadamu, bali ulikuwa wa Mungu. Hatamkabidhi tena binadamu urithi huo. Maana hakuna hata kitu kimoja kati ya hivyo vilikuwa vya binadamu kwa asili. Atavichukua vyote tena—huu si uporaji usio wa haki, bali unakusudiwa kuirejesha mbingu na dunia katika hali yake ya asili, na kubadilisha na kumfanya upya binadamu. Hii ni hatima inayofaa kwa mwanadamu, ingawa pengine si kuichukua tena baada ya kuuadibu mwili kama watu wanavyofikiri. Mungu hataki mifupa ya mwili baada ya maangamizi yake, bali vitu vya asili katika mwanadamu ambavyo mwanzo vilikuwa vya Mungu. Hivyo, hatawaangamiza binadamu au kuuondoa kabisa mwili wa binadamu, maana mwili wa binadamu si mali binafsi ya mwanadamu. Badala yake, ni kiungo cha Mungu, ambaye anasimamia binadamu. Angewezaje kuuangamiza mwili wa binadamu ili Yeye “afurahi”? Je, wakati huu, kwa kweli umeachana na kila kitu cha huo mwili wako ambao hauna thamani hata ya senti moja? Kama ungeweza kuelewa asilimia thelathini ya kazi ya siku za mwisho (asilimia thelathini tu, yaani, kuifahamu kazi ya Roho Mtakatifu leo, vilevile kazi ya neno Mungu hufanya katika siku za mwisho), basi usingeweza kuendelea “kuutumikia” au “kuwa” na upendo kwa mwili wako kama unavyofanya leo, ambao umepotoka kwa miaka mingi. Unapaswa kuelewa kwa kina kwamba binadamu sasa wameendelea kwa hali ambayo haijawahi kutokea na hawataendelea tena kusonga mbele kama magurudumu ya historia. Mwili wako wa udongo umeshafunikwa na nzi tangu zamani, hivyo unawezaje kuwa na nguvu ya kurudisha nyuma magurudumu ya historia ambayo Mungu ameyawezesha kuendelea hadi siku hii ya leo? Unawezaje kufanya saa ya siku za mwisho ambayo ni kama bubu ipige tena na kuendelea kusogeza mikono yake kwa upande wa kulia? Unawezaje kuubadilisha upya ulimwengu ambao unaonekana kama umefunikwa na ukungu mzito? Je, mwili wako unaweza kufufua milima na mito? Je, mwili wako, ambao una kazi ndogo tu, unaweza kweli kurejesha ulimwengu wa binadamu ambao umekuwa ukiutamani? Unaweza kweli kuwaelimisha wadhuria wako kuwa “binadamu”? Unaelewa sasa? Mwili wako unamilikiwa na nini hasa? Makusudi halisi ya Mungu ya kumfinyanga mwanadamu, ya kumkamilisha mwanadamu, na ya kumbadilisha mwanadamu hayakuwa kukupatia nchi nzuri ya asili au kuleta pumziko la amani kwa mwili wa mwanadamu. Badala yake, ilikuwa ni kwa ajili ya utukufu Wake na ushuhuda Wake, kwa furaha bora ya binadamu hapo baadaye, na ili kwamba hivi karibuni waweze kufurahia pumziko. Bado, si kwa ajili ya mwili wako, maana mwanadamu ni mtaji wa usimamizi wa Mungu na mwili wa mwanadamu ni kiungo tu. (Mwanadamu ni kitu chenye roho na mwili, wakati mwili ni kitu kiharibikacho tu. Hii humaanisha kwamba mwili ni chombo kwa ajili ya mpango wa usimamizi.) Unapaswa kujua kwamba kuwakamilisha wanadamu, kuwatimiza wanadamu, na kuwapata wanadamu hakujaleta kitu chochote zaidi ya mapanga na maangamizi kwa mwili wao, na kumeleta mateso yasiyokoma, kuungua kwa moto, hukumu zisizokuwa na huruma, kuadibu, na laana, na vilevile majaribu yasiyokuwa na mipaka. Hicho ni kisa cha ndani na ukweli wa kazi ya kumsimamia binadamu. Hata hivyo, vitu hivi vyote vimelengwa dhidi ya mwili wa binadamu, na mikuki yote ya uhasama bila huruma inaelekezwa kwenye mwili wa binadamu (maana kwa asili binadamu hakuwa na hatia). Hayo yote ni kwa ajili ya utukufu na ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake. Hii ni kwa sababu kazi Yake si tu kwa ajili ya binadamu, bali ni kwa ajili ya mpango wote na kutimiza mapenzi Yake ya asili Alipomuumba binadamu. Kwa hiyo, pengine asilimia tisini ya kile ambacho watu wanapitia ni mateso na majaribu ya moto, lakini kuna siku chache sana tamu na za furaha au hata hakuna kabisa ambazo mwili wa mwanadamu umekuwa ukitamani, na hata hawawezi kufurahia nyakati za furaha katika mwili wakishinda jioni nzuri pamoja na Mungu. Mwili ni mchafu, hivyo kile ambacho mwili wa mwanadamu unakiona au unakifurahia si chochote bali ni adabu ya Mungu ambayo haipendwi na mwanadamu, na ni kana kwamba ulikuwa unakosa mantiki ya kawaida. Hii ni kwa sababu Atadhihirisha tabia Yake ya haki ambayo haipendwi na mwanadamu, haivumilii makosa ya mwanadamu, na huchukia kabisa maadui. Mungu hufichua waziwazi tabia Yake yote kupitia njia yoyote iwezekanayo, na hivyo Akihitimisha kazi ya vita Vyake na Shetani vya miaka elfu sita—kazi ya wokovu wa binadamu wote na maangamizi ya Shetani wa zamani!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili