Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo mapenzi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo mapenzi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 4 Juni 2019

Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Njia za Kweli na za Uongo, na Makanisa ya Kweli na ya Uongo

4. Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Njia za Kweli na za Uongo, na Makanisa ya Kweli na ya Uongo?

Maneno Husika ya Mungu:
Kanuni ya msingi kabisa katika kuutafuta ukweli ni nini? Unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu au la, iwapo maneno haya ni udhihirishaji wa ukweli, yanamshuhudia nani, na ni kitu gani yanaweza kukupatia. Kutofautisha kati ya njia ya kweli na hizi njia za uongo kunahitaji njia kadhaa za maarifa ya msingi, ya msingi kabisa kati ya zote ni kusema iwapo kuna Kazi ya Roho Mtakatifu au la. Maana kiini cha imani ya mwanadamu kwa Mungu ni imani katika Roho Mtakatifu. Hata imani yake kwa Mungu mwenye mwili ni kwa sababu mwili huu ni mfano halisi wa Roho wa Mungu, ikiwa na maana kwamba imani hiyo bado ni imani katika Roho. Kuna tofauti kati ya Roho na mwili, lakini kwa kuwa mwili unatokana na Roho, na ndio Neno linakuwa mwili, hivyo kile ambacho mwanadamu anaamini katika ni uungu halisi wa Mungu. Na hivyo, katika kutofautisha kama ni njia sahihi au la, zaidi ya yote unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu, na baada ya hapo unapaswa kuangalia kama kuna ukweli katika njia hii. Ukweli huu ni silika ya maisha ya mwanadamu wa kawaida, ni sawa na kusema, kile ambacho Mungu alikitaka kwa mwanadamu alipomuumba hapo mwanzo, yaani, ubinadamu wote wa kawaida (ikiwa ni pamoja na hisia za kibinadamu, umaizi, hekima, na maarifa ya msingi ya kuwa mwanadamu). Yaani, unapaswa kuangalia iwapo njia hii inampeleka mwanadamu katika maisha ya mwanadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli uliozungumzwa unahitajika kulingana na uhalisia wa ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli huu ni wa kiutendaji au hali, na iwapo ni wa wakati muafaka au la. Ikiwa kuna ukweli, basi unaweza kumpeleka mwanadamu katika uzoefu wa kawaida na halisi; aidha, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, hisia za kawaida za kibinadamu zinakuwa kamili zaidi, maisha ya mwanadamu katika mwili na maisha ya kiroho yanakuwa katika mpangilio mzuri zaidi, na mihemko ya mwanadamu inakuwa ya kawaida kabisa. Hii ni kanuni ya pili. Kuna kanuni nyingine moja zaidi, ambayo ni kama mwanadamu ana maarifa mengi juu ya Mungu, kama unapitia uzoefu wa kazi hiyo na ukweli unaweza kuchochea upendo wa Mungu ndani yake au la, na kumsogeza karibu zaidi na Mungu. Katika hili inaweza kupimwa kama ni njia sahihi au la. Kanuni ya msingi ni iwapo njia hii ni ya uhalisia badala ya kuwa ya kimiujiza, na iwapo inaweza kutoa maisha ya mwanadamu. Kama hukubaliana na kanuni hizi, hitimisho linaweza kuwekwa kwamba njia hii ni njia ya kweli. … Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida kabisa, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake, ambayo yameharibiwa na Shetani, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Ni sawa na, kusema, maisha ya mwanadamu yanakuwa na kukua, na Atabia ya upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maishi ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha atabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa uelewa wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu. Umeamini katika Mungu kwa miaka yote hii, halafu bado huna uwezo wa kutofautisha kati ya njia ya kweli na njia ya uongo au kuweza kuitafuta njia ya kweli. Watu wengi hawapendi hata kusikia masuala haya; wanakwenda tu kule ambapo wengi wanakwenda, na wanarudia kile ambacho watu wengi wanasema. Ni kwa njia gani mtu huyu ni mtu anayetafuta njia ya kweli? Na ni kwa njia gani watu kama hao wanaweza kuipata njia ya kweli? Ikiwa utaelewa kanuni hizi muhimu, basi chochote kitakachotokea hutaweza kudanganywa.
kutoka kwa "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wote walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikishwa na uwepo na adabu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo kwenye mkondo huu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale walioikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na vibaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee huduma na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanadhibitiwa na Roho Mtakatifu na huenda wakaadhibiwa. Bila kujali ni aina gani ya watu, ili mradi tu wamo kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake. Wale wanaolitukuza jina Lake na wako radhi kuweka maneno Yake katika vitendo watapokea Baraka Zake; wale wasiomtii na kuyaweka maneno Yake katika vitendo watapokea adhabu Yake. … Sio hivyo na watu wasioikubali kazi mpya: Wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na adhabu na lawama ya Roho Mtakatifu haitumiki kwao. Kila siku hawa watu wanaishi katika mwili, wanaishi katika mitazamo yao, na yote wayafanyayo ni kulingana na mafundisho ya kidini yaliyozalishwa na uchanganuzi pamoja na utafiti wa bongo zao. Si matakwa ya kazi mpya ya Roho Mtakatifu wala sio ushirika na Mungu. Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu wanajinyima uwepo wa Mungu na zaidi wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Mengi ya maneno na matendo yao yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini tu na wala si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kitu cha pekee kinachowaleta pamoja ni dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mikutano ya wote walio miongoni mwao haiwezi kuitwa kanisa bali mkutano mkubwa wa watu wa dini. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya. Ikiwa imesimama juu ya msingi wake asili, kazi ya Roho Mtakatifu imepiga hatua kadhaa kwa kina. Na bado watu hao wamebaki katika hatua ya asili ya kazi ya Mungu na bado wanapenyeza katikati ya vitendo na mwangaza wa zamani. Kazi ya Mungu yaweza kubadilika pakubwa kwa miaka mitatu au mitano, hivyo si mabadiliko hata makubwa zaidi yaweza kuja kwa kipindi cha miaka zaidi ya 2000? Ikiwa mwanadamu hana vitendo vipya ama mwangaza mpya, inamaanisha hajaenda sawia na kazi ya Roho Mtakatifu. Hili ni anguko la mwanadamu; uwepo wa kazi mpya ya Mungu hauwezi kukanwa kwa sababu, leo hii, wale walio na kazi asili ya Roho Mtakatifu bado wanashikilia vitendo vilivyopitwa na wakati. Kazi ya Roho Mtakatifu daima inasonga mbele, na wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanafaa waendelee mbele na kubadilika, hatua kwa hatua. Hawapaswi kukwama katika hatua moja. Ni wale tu wasioifahamu kazi ya Roho Mtakatifu ndio wanaweza kubaki katika hatua ya kazi ya Mungu ya awali na wasikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Ni wale tu walio waasi ndio watakosa uwezo wa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa vitendo vya mwanadamu haviendani na mwendo wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, basi vitendo vya mwanadamu hakika vimetengana na kazi ya leo na kwa hakika havilingani na kazi ya leo. Watu waliopitwa na wakati kama hawa hawawezi kutimiza mapenzi ya Mungu, na zaidi hawawezi kuwa wale watu wa mwisho ambao watamshuhudia Mungu. Aidha, kazi nzima ya usimamizi haiwezi kutimilika miongoni mwa kundi la watu kama hao. Kwa wale walioshikilia sheria za Yehova kipindi fulani, na wale walioumia wakati fulani chini ya msalaba, ikiwa hawawezi kukubali hatua ya kazi ya siku za mwisho, basi yale yote waliyofanya ni bure na yasiyofaa. … Ikiwa mwanadamu atasalia amekwama katika hatua moja tu, basi hili linaonyesha kuwa haendi sawia na kazi ya Mungu na mwangaza mpya; haimaanishi kuwa mpango wa usimamizi wa Mungu haujabadilika. Walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu daima hudhani wako sahihi, lakini kwa hakika, kazi ya Mungu ndani yao ilisita zamani na kazi ya Roho Mtakatifu haimo ndani yao. Kazi ya Mungu imeshahamishiwa kwa kundi jingine la watu, kundi ambalo kwalo Anapania kukamilishia kazi Yake mpya. Kwani walio kwenye dini hawawezi kuikubali kazi mpya ya Mungu, na kushikilia tu kazi kongwe za zamani, hivyo Mungu amewaacha watu hawa na anafanya kazi Yake mpya kwa watu wanaoikubali kazi hii mpya. Hawa ni watu wanaoshiriki katika kazi Yake mpya, na usimamizi Wake utatimilika kwa njia hii tu. Usimamizi wa Mungu daima unasonga mbele na vitendo vya mwanadamu daima vinapanda juu. Mungu daima anafanya kazi na mwanadamu mara zote ni mhitaji ili kwamba wote wanafikia upeo wao, Mungu na mwanadamu wamo katika muungano kikamilifu. Haya ni maonyesho ya kutimilika kwa kazi ya Mungu, na ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi nzima ya usimamizi.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Njia ya kweli ni njia ambayo inaweza kuwaokoa watu, kuwabadilisha watu, na kuwawezesha kufanikisha kukubaliwa na Mungu na kuingia katika hatima ya kweli. Hii tu ndiyo njia ya kweli. Iwapo watu wanadhani kuwa wao wanaamini katika njia ya kweli, lakini malengo haya na matokeo haya hayajapatikana, basi inaweza kusemwa kwamba yao ni njia ya uongo, kwamba si njia ya kweli. Watu wengine husema: "Je, nitawezaje kutambua tofauti kati ya mazuri na mabaya?" Hili linakamilishwa kulingana na maneno ya Mungu. Yote yanayokubaliwa na Mungu, yote Anayomhitaji mwanadamu kumiliki, na kila ambacho Mungu Anapenda mwanadamu afanye ni kizuri; yote ambayo Mungu Anataka wanadamu wayakatae na kuyaacha, na yote yanayoshutumiwa na Mungu, ni mabaya. Kutathmini mazuri na mabaya huamuliwa hivyo, kulingana na maneno ya Mungu; Maneno ya Mungu ni kipimo ambacho huthibitisha iwapo kitu chochote ni cha kweli au cha uongo, na ndicho kiwango pekee cha kupima iwapo kitu chochote ni kweli au uongo. Unatathmini vipi njia gani ni ya kweli, na gani ni ya uongo? Njia inayoweza kukuletea maisha ya kweli, inayoweza kukufanya uone mwanga, inayoweza kukuruhusu ujiondolee upotovu na ushawishi wa Shetani, na kukuwezesha kupata kibali na baraka ya Mungu—hii ndiyo njia ya kweli. Je, huo si ukweli? Je, hukumu na kuadibu kwa Mungu kumetuletea nini? Kumetuletea ukweli wote ambao watu wapotovu lazima wamiliki ili kupata wokovu, kumeleta njia ya kweli ya maisha, kumeturuhusu kuuona mwanga wa maisha, kumetupa wokovu mkuu zaidi, na wokovu wa kweli, ambao ulipangiwa awali na Mungu katika uumbaji wa dunia, na kumetubadilisha sisi kutoka kwa watu ambao walipotoshwa na Shetani, na kumilikiwa na Shetani, na kuwa watu halisi ambao kwa hakika wametakaswa na Mungu na wamejawa na ukweli na ubinadamu. Haya yote ndiyo matokeo yaliyofanikishwa na hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Bila hukumu na kuadibu kwa Mungu, hatungeweza kupata ukweli, upotovu wetu ungebaki bila kutatuliwa, kamwe hatungeweza kuona mwanga wa maisha, na kamwe hatungepata kibali cha Mungu. Hivyo, baraka zote ambazo tumepokea leo zinatokana na kupitia na kutii hukumu na kuadibu kwa Mungu.
…………
Baadhi ya watu husema: "Hebu, iwapo hii ni njia ya kweli, kwa nini watu wachache tu ndio waliojiunga nayo? Kwa kuwa ni njia ya kweli, si inapaswa kuwa na waumini wengi? Si binadamu wote wanapaswa kuamini kwayo?" Watu wanaosema mambo kama hayo hawaelewi ukweli, wao ni wapumbavu. Upotovu wa binadamu wote umefikia hatua fulani; watu wachache zaidi na zaidi ndio wanapenda ukweli, watu wengi zaidi na zaidi wanafuatilia maslahi yao wenyewe, na bila kujali ni imani gani watakubali, wao kwanza huangalia kama ni ya faida kwao—ambayo ina maana kwamba wale ambao wanaamini katika njia ya kweli kwa hakika ni wachache, na wale ambao wanaamini katika njia za uongo, na njia ambazo zinatoa neema na faida, kwa hakika ni wengi. Baada ya kusikia maelezo yangu, utaweza kuona ndani kwenye kiini cha suala. Njia tunayoamini kwayo haiponyi watu, wala kujaza matumbo yao kwa mkate, au kuwapa neema, au kupunga pepo waovu kutoka kwao. Lakini tukiongeza kitu kimoja zaidi kwa njia tunayoamini kwayo—kwamba waumini hawatakufa wakati maafa yoyote yatawasibu—basi watu wote wa dunia wataamini ndani yake. Leo, hili halijahusishwa katika njia yetu. Mungu hajasema, "Naahidi kwamba wote ambao wanaamini katika jina la Mwenyezi Mungu hawatakufa." Hivyo, unapoeneza injili una tahadhari. Watu huuliza, "Kwa hivyo sitakufa nikiamini katika Mwenyezi Mungu?" "Mimi sijui." "Kama Hawezi kunizuia kufa, basi hakuna haja ya kuamini katika Yeye." Watu pia watauliza, "Nitafaidi nini kutoka kwa kuamini katika Mwenyezi Mungu?" "Unaweza kupata ukweli." "Kupata ukweli kutanipatia nini?" "Utanusurika" "Ni nani amewahi kuona hili?" "Nani anayeweza kulithibitisha? Kupata ukweli kunamaanisha nini?" "Mimi Sijui." "Hakuna jinsi ninavyoweza kuamini." Hivyo, ni vigumu kwetu kumshuhudia Mwenyezi Mungu na kueneza injili, kwa kuwa wale wanaopenda ukweli ni wachache sana. Huu ni ukweli. Ilhali baada ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu, jinsi tunavyoamini zaidi, ndivyo tunavyohisi kuwa ni halisi zaidi, na ndivyo imani yetu inavyokuwa na nguvu zaidi. Ni kwa nini vile? Haya ni matokeo ya kuuelewa ukweli. Zaidi mtu anavyoelewa ukweli, ndivyo wanavyohisi zaidi kuwa ni njia ya kweli, na kazi ya Mungu. Zaidi wanavyoulewa ukweli, zaidi wanavyojiambia wenyewe, "Ah, wokovu wa Mungu wa binadamu kwa njia hii ni halisi sana, kuelewa ukweli hakika kunaweza kuniokoa, kusababisha mabadiliko katika tabia yangu, kunifanya mimi kuwa binadamu wa kweli, na kuniruhusu niishi maisha halisi ya ubinadamu wa kawaida—na kwa hivyo njia hii ina maana." Wanahisi kwamba kuupata ukweli kuna maana zaidi, kunastahili, na kwenye thamani zaidi ya faida yoyote, au uponyaji wa wagonjwa, au kujaza matumbo ya watu na chakula. Kwa sababu hiyo, wale ambao wameamini katika Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa huhisi kwamba hakuna kitu cha thamani kuhusu neema yoyote wanayoweza kupewa, kwamba kupata ukweli tu ni kwa thamani—na katika hili, wameona njia ya kweli. Tazama, kuna wowote wa wale wanaoamini katika Mwenyezi Mungu wametoroka? Ingawa baadhi ya watu hawautafuti ukweli, mradi wao wamesikiliza mahubiri kwa miaka michache, je watataka kuondoka? Hakuna hata mmoja angetaka. Na kwa nini wasitake? Wanachojua ni kwamba "Hii ndiyo njia ya kweli. Bora tu nifanye kazi kwa bidii, na kufanya wajibu wangu vizuri, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba nitaishi, kwamba mwisho wangu hautakuwa kifo. Kutokufa ni kwa thamani mno." Leo, watu hawajui ni nini kinahitajika ili kuepuka kifo. Punde tu wangejua, basi kila mtu angekuwa muumini, na imani yao ingekuwa imara.
kutoka kwa "Mafunzo Manne muhimu Ambayo Lazima Yaingiwe ili Kuitii Kazi ya Mungu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (VI)
Iwapo jamii ya kidini nzima haingekuwa na uhasama na kuipinga, basi hii haingekuwa njia ya kweli. Kumbuka: Njia ya kweli lazima ipingwe na watu wengi, hata na duniani. Wakati Bwana Yesu Alikuja mara ya kwanza kufanya kazi na kuhubiri, je, Uyahudi mzima haukumpinga Yeye? Kila wakati Mungu anapoanza kazi mpya, ubinadamu mpotovu unapata ugumu mkubwa katika kuikubali, kwa kuwa kazi ya Mungu inakinzana na na inakanusha dhana za watu; watu hawana uwezo wa kuelewa, na hawana uwezo wa kuupenya ulimwengu wa kiroho, na kama sio kazi ya Roho Mtakatifu, hawangeweza kukubali njia ya kweli. Ikiaminiwa kuwa ni kazi ya Mungu, lakini haipingwi na jamii za kidini, na inakosa upinzani na uhasama wa dunia, basi hii inathibitisha kwamba kazi hii ya Mungu ni ya uongo. Kwa nini wanadamu hawawezi kuukubali ukweli? Kwanza, mwanadamu ni wa mwili, yeye ni wa dutu ya kimwili. Mambo ya kimwili hayawezi kupenya ulimwengu wa kiroho. Inamaanisha nini kwamba "hayawezi kupenya ulimwengu wa kiroho"? Hii ina maana ya kushindwa kuona roho, shughuli za roho na ulimwengu wa kiroho, kuwa asiyeona Anayofanya na kusema Mungu. Watu wangekuwa vipofu katika ulimwengu wa kiroho. Ukifunga macho yako katika ulimwengu wa kimwili, huoni chochote. Ukiyafungua, unaweza kuona nini? Dunia ya asili. Je, unaweza kuona ni roho yupi anafanya kazi gani ndani ya watu? Je, unaweza kuona kile ambacho Roho wa Mungu amekuja kufanya na kusema? Huwezi. Wakati mwingine unaweza kusikia sauti Yake, na kusoma maneno ya Mungu yaliyoandikwa kwenye kitabu, lakini bado hujui ni vipi au lini Mungu Alinena maneno haya. Unaweza kusikia sauti Yake, lakini hujui inakotoka; unayaona maneno ya Mungu yamechapishwa kwenye ukurasa, lakini hujui ni nini maana yake. Watu hawawezi kupenya ulimwengu wa kiroho, au kushika chanzo cha maneno ya Mungu, na hivyo wanahitaji kupata nuru na kuangaziwa kwa Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu, ili kupata matokeo. Pili, ubinadamu umekuwa mpotovu kwa undani sana, na ndani yake imejazwa na sumu nyingi ya Shetani na ufahamu mwingi; akitathmini kila kitu kwa kutumia falsafa mbalimbali za kishetani na maarifa, basi kamwe hataweza kusadikisha ukweli ni upi. Bila kupata nuru na kuangaziwa kwa Roho Mtakatifu, mwanadamu hangekuwa na uwezo wa kuelewa ukweli. Binadamu mpotovu kwa silika hawezi kupenya ulimwengu wa kiroho. Amejazwa na falsafa za kishetani na maarifa, na hawezi kuutambua ukweli. Na hivyo njia ya kweli bila kuepukika inakabiliwa na mateso na kukataliwa kwa mwanadamu. Kwa nini ni rahisi kwa watu kukubali maarifa na falsafa za Shetani? Kwanza, iko sambamba na dhana zao na maslahi ya miili yao, na ni ya manufaa kwa miili yao. Wanajiambia wenyewe, "Kukubali maarifa kama haya yananisaidia: Yatanipa kuongezwa cheo, yatanifanya niwe mwenye mafanikio, na kuniruhusu kufanikisha mambo. Na maarifa kama haya watu wataniheshimu." Tazama jinsi vinavyowafaa watu viko sambamba na dhana zao. ... Kuwa wapotovu kwa kiasi hiki, na kushindwa kupenya ulimwengu wa kiroho, watu wanaweza tu kumpinga Mungu, na hivyo kuwasili kwa kazi ya Mungu kumekutana na kukataliwa na mwanadamu, upinzani, na hukumu. Je, si hili linatarajiwa? Kama kuwasili kwa kazi ya Mungu hakungekutana na hukumu na upinzani wa dunia na wanadamu, basi hili lingethibitisha kuwa sio ukweli. Iwapo yote yaliyosemwa na Mungu yangekuwa sambamba na dhana ya watu, je, wangeyashutumu? Je, wangeyapinga? Bila shaka hawangefanya hivyo.
kutoka kwa "Ushirika na Mahubiri ya wa Juu Kuhusu Kueneza Injili"
Ni kanisa tu ambalo liko na kazi ya Roho Mtakatifu ndilo kanisa la Mungu, na kama tu lina watu ambao hakika wanafuatilia ukweli na kutii kazi ya Mungu ndipo kanisa linaweza kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu; Mungu anatambua makanisa ambayo yako na kazi ya Roho Mtakatifu, na hayatambui makanisa yasiyo na kazi ya Roho Mtakatifu. Hili linapaswa kueleweka kwa wateule wa Mungu.
…………
Kanisa halisi linajumuisha wale ambao hakika wanaamini katika Mungu na wanapenda ukweli, na ni mkusanyiko wa wote wanaomcha Mungu. Hapo tu ndipo linaweza kuitwa kanisa. ... Ni tu mkusanyiko wa wale ambao wameamuliwa kabla na waliochaguliwa na Mungu na wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu ndio kanisa.
kutoka kwa "Jinsi ya Kukabili na Kutatua Vurugu Kati ya Makanisa ya Mitaani" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (II)
Kanisa linajumuisha wale ambao hakika wameamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu—linajumuisha wale wanaopenda ukweli, wanaotafuta ukweli, na wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Ni wakati tu watu hawa wanakusanyika ili kula na kunywa neno la Mungu, kuishi maisha ya kanisa, kupitia kazi ya Mungu, na kufanya wajibu wao kama viumbe wa Mungu ndio linaweza kuwa kanisa. Umati wenye zogo ukisema kwa kweli unaamini katika Mungu, lakini haupendi au kuutafuta ukweli, na hauna kazi ya Roho Mtakatifu, na unafanya sherehe za kidini, na kuomba, na kusoma maneno ya Mungu, basi hili sio kanisa. Kwa usahihi, makanisa yasiyo na kazi ya Roho Mtakatifu si makanisa; hayo ni kumbi za kidini na watu ambao hufanya sherehe za kidini tu. Wao si watu ambao kwa kweli wanamtii Mungu na kupitia kazi ya Mungu.
…………
Kanisa ni mkusanyiko wa watu ambao wanaamini katika Mungu kwa kweli na kufuatilia ukweli, na halishirikishi waovu kabisa—wao si wa kanisa. Iwapo kundi la watu ambao hawakutafuta ukweli na wala kufanya kitu chochote kuuweka ukweli katika vitendo wangekusanyika pamoja, je, hili lingekuwa kanisa? Je, mkusanyiko huu ungekuwa nini? Ungekuwa ukumbi wa kidini, au umati wenye zogo. Kanisa lazima liundwe na watu ambao kwa kweli wanaamini katika Mungu na kuufuatilia ukweli, wanaokula na kunywa maneno ya Mungu, na kumwabudu Mungu, kufanya wajibu wao, na kupitia kazi ya Mungu na wamepata kazi ya Roho Mtakatifu. Hili tu ndilo kanisa. Hivyo, unapotathmini kanisa, lazima kwanza uangalie ni aina gani ya watu linao. Pili, lazima uangalie iwapo wana kazi ya Roho Mtakatifu au la; kama mkutano wao hauna kazi ya Roho Mtakatifu, hilo si kanisa, na kama si mkusanyiko wa wale wanaofuatilia ukweli, basi sio kanisa. Iwapo kanisa halina mtu yeyote anayefuatilia ukweli, na liko bila kazi ya Roho Mtakatifu kabisa, basi kama kuna mtu ndani lake aliye na nia ya kuufuatilia ukweli, na wanabakia katika kanisa kama lile, je, mtu huyo anaweza kuokolewa? Hawezi, na anapaswa kuuacha umati huo wenye zogo na kutafuta kanisa haraka awezavyo. Iwapo, ndani ya kanisa, kuna watu watatu au watano ambao huufuatilia ukweli, na watu 30 au 50 ambao ni umati wenye zogo, basi wale watu watatu au watano ambao wanaamini katika Mungu kwa kweli na kuufuatilia ukweli lazima waje pamoja; wakija pamoja mkutano wao bado ni kanisa, kanisa la wanachama wachache zaidi, lakini lililo safi.
kutoka kwa "Kuelewa Maana ya Kweli ya Kanisa na Kufanya Kazi kulingana na Kanuni Tano za Kazi ya Kanisa Kuna Umuhimu MkubwaSana Wakati wa Mwisho" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (VII)
Watu wengi wanaamini katika Mungu lakini wanaabudu makanisa makuu ya dayosisi na kusadiki kipofu katika wachungaji—na matokeo kwamba, baada ya kuamini katika Mungu kwa miaka mingi, bado hawajaelewa ukweli au kuingia katika hali halisi, wamepata tu baadhi ya mafundisho ya dini na sherehe za kidini na mazoea, na hawamjui Mungu kwa kweli. Katika matokeo, hakuna mabadiliko hata kidogo katika tabia ya maisha yao. Si ajabu, basi, kwamba viongozi hao wa dini na wachungaji hutumia maisha yao yote kwa kuamini katika Mungu na kuhubiri, ilhali hakuna hata mmoja wao anayemjua Mungu kwa kweli, au hata kuwa na moyo unaomcha Mungu; wao hubaki kama Mafarisayo kutoka nyakati za kale, kufanya wawezayo kumpinga Kristo, kuhukumu njia ya kweli, na kuwatega na kuwadhibiti watu wa Mungu waliochaguliwa kwa ajili ya hali zao wenyewe na kuendesha maisha yao. Sababu yao kutoa mfano wa kupenda na kuthamini kundi la wanakondoo wa Mungu kimsingi ni kwa sababu ya kulinda maisha yao wenyewe, kama vile wafanyabiashara wanavyowatendea wateja wao kama miungu ili wapate pesa na kupata utajiri. Kila kitu ambacho jamii ya kidini inafanya ni udhihirisho wa upinzani wake kwa Mungu; si chochote ila sherehe za kidini, na haina uhalisi wa ukweli hata kidogo, na zaidi hakuna dalili yoyote ya kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa dhahiri, jamii ya kidini haimwabudu Mungu wa kweli, ila Mungu asiye dhahiri na Mungu wa kubuniwa tu. Inahubiri mafundisho ya kidini, na elimu halisi ya Biblia, na haina kabisa kupata nuru na mwanga wa Roho Mtakatifu. Hivyo, jamii ya kidini kimsingi haiwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, haiwezi kuwaongoza kwenye njia sahihi ya kuamini katika Mungu, na, zaidi ya hayo, haiwezi kuchukua watu hadi katika hali halisi ya ukweli, au kuwasaidia waokolewe. Hiyo ni kwa sababu viongozi wake na wachungaji hawajafanywa wakamilifu na kujengwa na Roho Mtakatifu wanapopitia kazi ya Mungu, lakini badala yake wamekuwa viongozi na wachungaji katika jamii ya kidini baada ya kufuzu kutoka katika seminari na kupewa cheti cha diploma. Hawana kazi na uthibitisho wa Roho Mtakatifu, hawana ufahamu wa kweli wa Mungu hata kidogo, na midomo yao haiwezi kuzungumza kuhusu kitu kingine ila maarifa ya kitheolojia na nadharia. Wao kwa kweli hawana uzoefu wa kitu chochote. Watu kama hao hawajafuzu kabisa kutumiwa na Mungu; watawezaje kumwongoza mwanadamu kwenda mbele za Mungu? Kwa kiburi hushikilia kuhitimu kutoka chuo seminari kama ushahidi wa haki yao wenyewe, wanafanya kila wawezalo ili kuonyesha kwa majivuno maarifa yao ya Biblia, ni wenye kiburi kisichostahimilika—na kwa sababu hii, wanahukumiwa na Mungu, na kuchukiwa na Mungu, na wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Kuhusu hili hakuna shaka. Kwa nini jamii ya kidini imekuwa adui mkubwa wa Kristo ni swali la kuchochea fikira nyingi sana. Inaonyesha nini kuwa, katika Enzi ya Neema, Uyahudi ulimpiga Yesu Kristo msalabani? Katika Enzi ya Ufalme wa siku za mwisho, jamii za kidini zimeungana na kuweka juhudi zake zote katika kupinga na kuhukumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, zinamkana na kumkataa Kristo mwenye mwili wa siku za mwisho, zimeunda uvumi mbalimbali kuhusu, na kushambulia, kusingizia na kukufuru dhidi ya Mungu mwenye mwili na kanisa la Mungu, na kwa muda mrefu sasa zimempiga misumari Yesu Aliyerudi, Kristo wa siku za mwisho, msalabani. Hii inathibitisha kuwa jamii za kidini kwa muda mrefu sasa zimepotoka na kuwa majeshi ya Shetani yanayopinga na kuasi dhidi ya Mungu. Jamii ya kidini haitawaliwi na Mungu, wala kutawaliwa na ukweli kweli; inatawaliwa kikamilifu na binadamu wapotovu, na zaidi ya hayo, na wapinga Kristo.
Watu wanapoamini katika Mungu kwenye ukumbi wa dini kama huu—ambao ni mali ya Shetani na unatawaliwa na kudhibitiwa na mapepo na wapinga Kristo—wanaweza tu kuelewa mafundisho ya dini, wanaweza tu kufuata sherehe za kidini na kanuni, na kamwe hawatawahi kuuelewa ukweli, kamwe hawatawahi kuipitia kazi ya Mungu, na kwa kikamilifu hawawezi kuokolewa. Hii ni bila shaka. Kwa kuwa hakuna jambo lolote la kazi ya Roho Mtakatifu katika kumbi za kidini, na ni maeneo ambayo yanamkera Mungu, ambayo yanachukiwa na Mungu, na yanashutumiwa na kulaaniwa na Yeye. Mungu hajawahi kuitambua dini, wala hajawahi kuisifu, na kutoka wakati wa Yesu jamii ya kidini imekuwa ikishutumiwa na Mungu. Hivyo, unapoamini katika Mungu lazima upate mahali palipo na kazi ya Roho Mtakatifu; haya tu ndiyo makanisa ya kweli, na ni katika makanisa ya kweli pekee ndiyo utaweza kusikia sauti ya Mungu, na kugundua nyayo za kazi ya Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo njia ambayo Mungu Anatafutwa.
kutoka kwa "Athari za Kuelewa Ukweli kwa Uhalisi" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (I)

Jumatatu, 27 Mei 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa “Maonyo Matatu” | How to Be a Loyal Servant of God

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa “Maonyo Matatu” | How to Be a Loyal Servant of God

Mwenyezi Mungu anasema, “Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla ya kuuamua mwisho wenu, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu. ... Katika maisha yenu, Naona mengi ambayo mnafanya ambayo hayana uhusiano na ukweli, kwa hivyo Nawaambia moja kwa moja muwe watumishi wa ukweli na wala si kutawaliwa na maovu na ubaya. Msikanyage ukweli na kuchafua sehemu yoyote ya nyumba ya Mungu. Hili ndilo onyo Langu kwenu.”
Kwanza, kwa minajili ya majaliwa yenu, mnastahili kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu mnatambua kwamba nyinyi mmehesabiwa miongoni mwa wale walio katika nyumba ya Mungu, basi mnastahili kumletea Mungu utulivu wa akili katika mambo yote na kumtosheleza katika kila jambo. Kwa maneno mengine, lazima muwe wenye maadili katika matendo yenu na kutii ukweli katika mambo kama hayo. Kama hali hii inazidi uwezo wako, basi utachukiwa na kukataliwa na Mungu na vilevile kukataliwa kwa dharau na kila mwanadamu. Punde utakapokuwa katika hali mbaya kama hii, basi hauwezi kuhesabiwa miongoni mwa wale walio kwenye nyumba ya Mungu. Hii ndiyo maana ya kutoidhinishwa na Mungu.
Pili, mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. Kile Ninachoongea ni rahisi sana lakini ni kigumu maradufu kwenu. Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu. Si ajabu kwamba Nina matendo mengine kwa wale ambao si waaminifu. Bila shaka, Ninaelewa ugumu mkuu mnaokumbana nao kwa kuwa binadamu waaminifu. Nyinyi wote ni werevu sana na stadi katika kupima uungwana wa mtu kwa kipimio chenu wenyewe; kwa hiyo kazi Yangu inakuwa rahisi zaidi. Na kwa sababu nyinyi mnaficha siri katika mioyo yenu, basi, Nitawatumeni, mmoja baada ya mwingine, katika janga kupitia “jaribio” la moto, ili baadaye mtajitolea kabisa katika kuamini maneno Yangu. Hatimaye, Nitapokonya maneno “Mungu ni Mungu wa uaminifu,” kutoka kwa vinywa vyenu na kisha ndipo mtakapojigamba na kujitanua kifua na kulalama, “Ujanja ndio moyo wa binadamu!” Hali za akili zenu zitakuwa zipi wakati huu? Ninafikiri hamtajisahau sana na majivuno kama mlivyo sasa. Na sembuse hamtakuwa “wa maana sana kiasi cha kutoeleweka” kama mlivyo sasa. Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme. Unafaa kujua kama kunayo imani ya kweli na uaminifu wa kweli ndani yako, kama una rekodi ya kuteseka kwa ajili ya Mungu, na kama umemtii Mungu kikamilifu. Kama unakosa hivi Nilivyotaja, basi ndani yako kunabaki kutotii, udanganyifu, ulafi, na kutotosheka. Kwa vile moyo wako si mwaminifu, hujawahi kupokea utambuzi mzuri kutoka kwa Mungu na hujawahi kuishi katika mwangaza. Kile ambacho jaala ya mtu kitakuwa hutegemea kama anao moyo wa uaminifu na wa kweli, na kama anayo nafsi isiyo na doa. Kama wewe ni mtu asiye mwaminifu sana, mtu mwenye moyo wa kijicho na nafsi isiyo safi, basi rekodi ya majaliwa yako bila shaka ipo pale ambapo binadamu huadhibiwa. Kama unadai kwamba wewe ni mwaminifu sana, na bado kamwe hutendi kulingana na ukweli au kuongea neno la ukweli, basi bado unatarajia Mungu kukutuza? Bado unatumai Mungu akuchukue kama kipenzi Chake? Je, kufikiria huku si kwa upuzi? Unamdanganya Mungu katika mambo yote, hivyo nyumba ya Bwana inawezaje kumpa nafasi mtu kama wewe, ambaye mikono yake si safi?
Jambo la tatu Ninalotaka kuwaambia ni hili: Kila mwanadamu, katika kuishi maisha yake ya imani katika Mungu, amemkataa na kumdanganya Mungu wakati fulani. Baadhi ya matendo mabaya hayahitaji kurekodiwa kama kosa, lakini mengine hayasameheki; kwani mengi ni yale yanayokiuka amri za utawala, yaani, yanaikosea tabia ya Mungu. Wengi ambao wanajali majaliwa yao binafsi wanaweza kuuliza matendo haya ni yapi. Lazima mjue kwamba nyinyi mna kiburi na wenye majivuno kiasili, na hamko radhi kutii ukweli. Kwa sababu hii, Nitawaambia kidogo kidogo baada ya nyinyi kutafakari kujihusu. Ninawashawishi kuwa na ufahamu bora zaidi wa yaliyomo katika amri za utawala na kujua tabia ya Mungu. Vinginevyo, mtapata ugumu sana kuendelea kufunga vinywa vyenu na kufyata ndimi zenu dhidi ya kuropokwa bila kizuizi kwa mazungumzo ya mbwembwe, na bila kujua mtaikosea tabia ya Mungu na kujipata kwenye giza, mkipoteza uwepo wa Roho Mtakatifu na mwangaza. Kwa sababu nyinyi hamna maadili katika matendo yenu, kufanya na kutenda kile ambacho hufai kufanya hivyo, basi utapokea adhabu inayokufaa. Lazima ujue kwamba ingawa wewe ni mpotovu katika maneno yako na matendo yako, Mungu ni mwenye maadili sana katika hali hizi zote. Sababu ya wewe kupokea adhabu ni kwa sababu umemkosea Mungu na wala si binadamu. Kama, katika maisha yako, wewe hutenda makosa mengi dhidi ya tabia ya Mungu, basi huna budi ila kuwa mtoto wa kuzimu. Kwa binadamu inaweza kuonekana kwamba umetenda matendo machache tu yasiyolingana na ukweli na si chochote zaidi. Je, una habari, hata hivyo, kwamba katika macho ya Mungu, tayari wewe ni mmoja ambaye kwake hakuna tena sadaka ya dhambi? Kwani umevunja amri za utawala za Mungu zaidi ya mara moja na hujaonyesha ishara yoyote ya kutubu, kwa hivyo huna chaguo lolote ila kutumbukia kuzimu pale ambapo Mungu anamwadhibu mwanadamu. Katika wakati wao wa kufuata Mungu, idadi ndogo ya watu ilitenda matendo yaliyoenda kinyume na kanuni, lakini baada ya kushughulikiwa na kuongozwa, waligundua polepole upotovu wao, na kisha wakachukua njia iliyo sawa ya uhalisi, na leo wanabaki wenye msingi imara katika njia ya Bwana. Binadamu kama hawa ndio watakaobakia mwisho. Ni wale walio waaminifu ndio Ninaowatafuta; kama wewe ni mtu mwaminifu na unayetenda kwa maadili, basi unaweza kuwa msiri wa Mungu. Kama katika matendo yako huikosei tabia ya Mungu, na unatafuta mapenzi ya Mungu na unao moyo wa kumcha Mungu, basi imani yako ni ya kiwango kilichowekwa. Yeyote asiyemcha Mungu na asiye na moyo unaotetema kwa woga atakiuka amri za utawala za Mungu kwa urahisi. Wengi humhudumia Mungu kwa misingi ya hisia kali, na hawajui katu amri za utawala za Mungu, sembuse kuelewa athari za neno Lake. Na kwa hivyo, na nia zao nzuri, mara nyingi wanaishia kufanya vitu vinavyokatiza usimamizi wa Mungu. Kwa hali za uzito sana, wanatupwa nje na kunyang’anywa fursa yoyote zaidi ya kumfuata, na wanatupwa kuzimu bila ya kuwa na uhusiano wowote mwingine na nyumba ya Mungu unakoma. Watu hawa hufanya kazi katika nyumba ya Mungu wakiwa na nia nzuri zisizojua na wanaishia kuikasirisha tabia ya Mungu. Watu huleta njia zao za kuwahudumia wakuu na mabwana katika nyumba ya Mungu na kujaribu kufanya yatumike, wakidhania kwa kiburi kwamba njia kama hizo zinaweza kutumika hapa bila jitihada. Hawakuwahi kufikiria kwamba Mungu hana ile tabia ya mwanakondoo bali ile ya simba. Kwa hiyo, wanaojihusisha na Mungu kwa mara ya kwanza wanashindwa kuwasiliana na Yeye, kwani moyo wa Mungu ni tofauti na ule wa binadamu. Ni baada tu ya kuelewa ukweli mwingi ndipo unapoweza kujua siku zote kumhusu Mungu. Maarifa haya si mafungu wala mafundisho, lakini yanaweza kutumika kama hazina ya kuingia katika matumaini ya karibu na Mungu, na ithibati kwamba Anafurahishwa na wewe. Kama unakosa uhalisi wa maarifa na hujajiandaa ukweli, basi huduma yako ya shauku itakuletea tu hali ya chuki ya kupindukia na kuchukizwa sana kwa Mungu. Sasa unafaa kuelewa kwamba imani katika Mungu si masomo tu ya teolojia.
Ingawa maneno Ninayotumia kuwaonya ni mafupi, vyote Nilivyovifafanua hapa ndivyo vinavyokosekana zaidi ndani yenu. Lazima mjue kwamba kile Ninachozungumzia sasa ni kwa minajili ya kazi Yangu ya mwisho miongoni mwa binadamu, kwa ajili ya kuamua hatima ya binadamu. Sipendelei kufanya kazi nyingi zaidi isiyo na maana, na wala Sipendelei kuendelea kuwaongoza wale binadamu wasio na matumaini kama mti uliooza, sembuse wale walio na nia mbaya kisiri. Pengine siku moja mtaelewa nia za dhati zinazoyasukuma maneno Yangu na michango ambayo Nimemfanyia mwanadamu. Pengine siku moja mtafahamu kanuni inayowawezesha kuamua hatima yenu binafsi.

Jumanne, 9 Aprili 2019

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.
“Hukumu” katika maneno yaliyonenwa awali—hukumu itaanza na nyumba ya Mungu—inarejelea hukumu ambayo Mungu anatoa leo kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi katika siku za mwisho. Pengine kuna wale wanaoamini katika mawazo ya kimiujiza kama yale, siku za mwisho zitakapowadia, Mungu ataandaa meza kubwa mbinguni, ambako kitambaa cheupe kitatandikwa, kisha, Mungu ataketi kwenye kiti kikuu cha enzi na wanadamu wote wakipiga magoti ardhini, Atafichua dhambi za kila mwanadamu na hivyo kubainisha iwapo atapaa juu mbinguni ama atatupwa chini kwenye ziwa la moto wa jehanamu. Haijalishi mawazo ya mwanadamu yalivyo, kiini cha kazi ya Mungu hakiwezi kubadilishwa. Mawazo ya mwanadamu ni miundo ya fikra za mwanadamu tu na yanatoka kwenye ubongo wa mwanadamu, na yametungwa na kuunganishwa kutokana na mambo aliyoyaona na kuyasikia. Kwa hivyo Nasema, kwa vyovyote vile hata picha zilizowazwa ziwe za hali ya juu kiasi gani, bado ni kama mchoro tu na haziwezi kubadilishwa na mpango wa kazi ya Mungu. Hata hivyo, mwanadamu amepotoshwa na Shetani, sasa atawezaje kuyaelewa mawazo ya Mungu? Mwanadamu huiona kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu mno. Mwanadamu anaamini kwamba kwa sababu ni Mungu Mwenyewe anayefanya kazi ya kuhukumu, basi lazima iwe ni ya kiwango cha juu zaidi na isiyoeleweka kwa wanadamu wenye mwili wa kufa, na lazima inasikika katika mbingu yote na kutetemesha dunia; vinginevyo itakuwaje kazi ya hukumu ya Mungu? Mwanadamu anaamini kuwa, kwa maana hii ni kazi ya hukumu, basi lazima Mungu ni wa kuvutia na mwadhimu Anapofanya kazi, na wale wanaohukumiwa lazima wawe wanalia kwa sauti wakitoa machozi wakiwa kwenye magoti wakiomba msamaha. Onyesho hili lazima ni la kustaajabisha sana na la kusisimua mno.… Kila mtu hudhani kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu isiyo ya kawaida. Je, unajua, hata hivyo, kwamba Mungu alianza kazi ya kuhukumu miongoni mwa wanadamu kitambo sana na wakati huu wote wewe bado uko katika hali ya kutotambua? Kwamba, wakati ambao unadhani kuwa kazi ya hukumu ya Mungu inaanza rasmi, tayari umewadia wakati ambapo Mungu kuzifanya upya mbingu na nchi? Wakati huo, pengine utakuwa tu umeelewa maana ya maisha, lakini kazi ya adhabu ya Mungu isiyo na huruma itakuleta kuzimu, ukiwa bado usingizini. Hapo tu ndipo kwa ghafla utafahamu kuwa kazi ya hukumu ya Mungu itakuwa imeshahitimika.
Tusipoteze muda wa thamani, na tusizungumzie tena mada hizi za kuchukiza na za karaha. Badala yake, tuzungumzie kinachofanyiza hukumu. Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu. Usipouchukulia ukweli huu kuwa muhimu na kila mara kufikiria kuuepuka au kutafuta njia nyingine isipokuwa ukweli, basi ninasema kuwa wewe ni mtenda dhambi mkubwa. Iwapo una imani kwa Mungu, lakini hutafuti ukweli au mapenzi ya Mungu, wala hupendi njia inayokuleta karibu na Mungu, basi nakwambia kuwa wewe ni yule anayejaribu kuepuka hukumu, na kwamba wewe ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu hatawasamehe waasi wowote wanaotoroka machoni Pake. Wanadamu wa aina hii watapokea adhabu kali zaidi. Wale wanaokuja mbele za Mungu ili wahukumiwe, na zaidi ya hayo wametakaswa, wataishi milele katika ufalme wa Mungu. Bila shaka, hili ni jambo ambalo liko katika siku za usoni.
Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu. Wengi wana hisia mbaya kuhusu kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, kwa maana mwanadamu huona vigumu kuamini ya kwamba Mungu angefanya kazi ya hukumu akiwa na mwili. Hata hivyo, lazima Nikueleze kwamba mara nyingi kazi ya Mungu huzidi sana matarajio ya mwanadamu na ni vigumu kwa mawazo yao kukubali. Kwa maana wanadamu ni mabuu tu kwenye ardhi, ilhali Mungu ni mkuu Anayejaza ulimwengu mzima; mawazo ya mwanadamu ni kama shimo la maji machafu ambayo yanazalisha mabuu peke yake, ilhali kila hatua ya kazi inayoelekezwa na mawazo ya Mungu ni utoneshaji wa hekima ya Mungu. Mwanadamu hutaka kila wakati kushindana na Mungu, ambalo kwalo Nasema ni wazi nani atapata hasara mwishowe. Nawasihi nyote msijichukulie kuwa wa maana zaidi kushinda dhahabu. Ikiwa wengine wanaweza kukubali hukumu ya Mungu, ni kwa nini wewe usiikubali? Ni vipi ambavyo ninyi ni bora zaidi kuliko wengine? Iwapo wengine wanaweza kuinamisha vichwa vyao mbele ya ukweli, ni kwa nini usifanye vile pia? Mwelekeo mkuu wa kazi ya Mungu hauwezi kukomeshwa. Hatarudia kazi ya hukumu tena kwa sababu ya “kustahili” kwako, na utajawa na majuto mengi kwa kupoteza nafasi nzuri kama hiyo. Usipoyaamini maneno Yangu, basi kingoje tu kiti cheupe kikuu cha enzi kilicho angani kipitishe hukumu juu yako! Lazima ujue kwamba Waisraeli wote walimkataa kwa dharau na kumkana Yesu, ilhali uhakika wa ukombozi wa Yesu kwa wanadamu ulizidi kusambaa mpaka mwisho wa ulimwengu. Je, hili silo jambo ambalo Mungu tayari Amelitimiza? Iwapo bado unangoja Yesu aje kukupeleka mbinguni, basi Nasema kuwa wewe ni kipande sugu cha mti mkavu[a]. Yesu hatamkubali mfuasi bandia kama wewe asiye mwaminifu kwa ukweli na anayetafuta baraka pekee. Hasha, Hataonyesha huruma Anapokutupa kwenye ziwa la moto uungue kwa makumi ya maelfu ya miaka.
Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.

Jumamosi, 9 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.”
Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawa Nimejazwa na hukumu na adabu kwa binadamu, kila ninachofanya bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, kwa ajili ya kueneza injili Yangu kwa njia bora zaidi na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili. Kwa hiyo leo, katika wakati ambapo watu wengi tayari wametamauka pakubwa, Naendelea na kazi Yangu, Nikiendeleza kazi ambayo lazima Nifanye ili kuhukumu na kuadibu binadamu. Licha ya ukweli kwamba binadamu amechoshwa na kile Ninachosema na licha ya ukweli kwamba hana tamanio la kujali kuhusu kazi Yangu, Ningali natekeleza wajibu Wangu kwa sababu kusudio la kazi Yangu halijabadilika na mpango Wangu asilia hautabadilika. Kazi ya hukumu Yangu ni kumfanya binadamu anitii Mimi kwa njia bora zaidi, na kazi ya kuadibu Kwangu ni kuruhusu binadamu awe na mabadiliko bora zaidi. Ingawa kile Ninachofanya ni kwa minajili ya usimamizi Wangu, Sijawahi kufanya chochote ambacho hakikufaidi binadamu. Hiyo ndiyo maana Nataka kufanya mataifa yote nje ya Israeli kuwa matiifu tu kama Waisraeli na kuwabadilisha kuwa binadamu halisi, ili Niwe na mahali pa usalama katika nchi zilizo nje ya Israeli. Huu ndio usimamizi Wangu; ndiyo kazi Ninayotimiza katika nchi za Mataifa. Hata sasa, watu wengi bado hawauelewi usimamizi Wangu kwa sababu hawajautilia maanani, badala yake wanafikiria tu kuhusu mustakabali na hatima zao. Haijalishi ni nini Ninachosema, watu hawajali kazi Yangu, badala yake wanalenga tu hatima zao za baadaye. Mambo yakiendelea kwa namna hii, kazi Yangu itapanuliwa vipi? Injili Yangu itaenezwa vipi kotekote ulimwenguni? Lazima mjue kwamba wakati kazi Yangu inapanuka, Nitawatawanya, Nitawaadhibu kama vile tu Yehova alivyoyaadhibu makabila ya Israeli. Haya yote yatafanywa ili injili Yangu iweze kuenea kotekote kwenye ulimwengu mzima, ili kazi Yangu iweze kuenezwa kwa Mataifa, ili kwamba jina Langu litukuzwe na watu wazima na watoto kwa pamoja na jina Langu takatifu litatukuzwa katika vinywa vya watu kutoka makabila na mataifa yote. Katika enzi hii ya mwisho, Nitafanya jina Langu litukuzwe miongoni mwa Mataifa, kufanya matendo Yangu kuonekana na mataifa mengine ili waniite Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kuyafanya maneno Yangu kutimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.
Kazi ambayo Nimekuwa nikisimamia kwa maelfu ya miaka inafichuliwa kabisa tu kwa binadamu katika siku za mwisho. Ni sasa tu ndipo Nimelifumbua fumbo kamili la usimamizi Wangu kwa mwanadamu. Binadamu anajua kusudio la kazi Yangu na zaidi ya yote anapata uelewa wa mafumbo Yangu yote. Na Nimemwambia binadamu kila kitu kuhusu hatima ambayo amekuwa akijali kuhusu. Tayari Nimemfichulia binadamu mafumbo yote yaliyofichwa kwa zaidi ya miaka 5,900. Yehova ni nani? Masiha ni nani? Yesu ni nani? Mnafaa kuyajua haya yote. Mabadiliko makubwa ya kazi Yangu yamo katika majina haya. Je, mmeelewa haya? Jina Langu takatifu linafaa kutangazwa vipi? Jina Langu linafaa kuenezwaje katika taifa lolote ambalo limeniita kwa jina Langu lolote? Kazi Yangu tayari imeanza kupanuka, na Nitaeneza ukamilifu wake katika mataifa yote. Kwa sababu kazi Yangu imetekelezwa ndani yenu, Nitawapiga kama vile Yehova alivyowapiga wale wachungaji wa nyumba ya Daudi kule Israeli, na kuwasababisha kutawanyika miongoni mwa mataifa yote. Kwani katika siku za mwisho, Nitapondaponda mataifa yote kuwa vipande vidogo vidogo na kusababisha watu wao kuenezwa upya. Nitakaporudi tena, mataifa yatakuwa tayari yamegawanywa kwa mipaka iliyowekwa na mwako wa moto Wangu utakaokuwa ukichoma. Katika wakati huo, Nitajionyesha upya kwa binadamu kama jua linalochoma, Nikijionyesha kwao hadharani kwa taswira ya yule Aliye Mtakatifu ambaye hawajawahi kumwona, Nikitembea miongoni mwa mataifa yote, kama vile tu Mimi, Yehova, Nilivyotembea miongoni mwa makabila ya Wayahudi. Kuanzia hapo kuendelea, Nitawaongoza watu huku wakiishi ulimwenguni. Hakika watauona utukufu Wangu hapo na hakika wataona pia nguzo ya wingu hewani ili uwaongoze, kwani Nitaonekana katika sehemu takatifu. Binadamu ataiona siku Yangu ya haki na pia maonyesho Yangu ya utukufu. Hilo litafanyika Nitakapoutawala ulimwengu mzima na kuwaleta wana wengi katika utukufu. Kila pahali duniani, watu watainama, nalo hema Langu takatifu litaundwa miongoni mwao juu ya mwamba wa kazi ambayo Natekeleza sasa. Watu watanihudumia pia hekaluni. Madhabahu, yaliyojaa mambo machafu na ya kuchukiza, Nitayavunjavunja vipandevipande na Nitajenga upya mengine. Madhabahu matakatifu yatarundikwa wanakondoo na ndama waliozaliwa karibuni. Nitaangusha hekalu lililopo leo na kujenga jingine upya. Hekalu lililopo sasa na lililojaa watu wenye chuki litaporomoka na lile Nitakalojenga litajaa watumishi watiifu Kwangu. Kwa mara nyingine watasimama na kunihudumia Mimi kwa utukufu wa hekalu Langu. Kwa hakika mtaiona siku ambayo Nitapokea utukufu mkuu na hakika mtaiona siku ambayo Nitaliangusha hekalu na kujenga lingine upya. Pia, hakika mtaona siku ya kuletwa kwa hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu. Huku Nikilibomoa hekalu, ndivyo Nitakavyoleta hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu; itakuwa kama vile tu ambavyo watu wanavyoniona Nikishuka. Baada ya kuangamiza mataifa yote, Nitayakusanya pamoja upya, Nikilijenga hekalu Langu na kuandaa madhabahu Yangu, ili wote waweze kutoa kafara zao Kwangu, kunihudumia Mimi hapo, na kujitolea kwa uaminifu katika kazi Yangu kwenye mataifa mengineyo. Itafanywa namna tu ambavyo wana wa Israeli wanavyofanya sasa, na joho la kuhani na taji la mfalme, utukufu Wangu, Yehova, ukiwa miongoni mwao na uadhama Wangu ukivinjari juu yao na ukiwa nao. Kazi Yangu katika Mataifa itatekelezwa pia katika njia hiyo. Kama vile kazi Yangu kule Israeli ilivyokuwa, ndivyo kazi Yangu katika Mataifa itakavyokuwa kwa sababu Nitaongeza kazi Yangu kule Israeli na kuieneza katika mataifa yale mengine.
Sasa ndio wakati ambao Roho Wangu anafanya kazi pakubwa, na wakati Ninapofanya kazi miongoni mwa Mataifa. Hata zaidi, ndio wakati ambapo Naainisha viumbe wote na kuweka kila kiumbe katika kundi lenye uhusiano, ili kazi Yangu iweze kuendelea haraka zaidi na kwa njia ya kufaa zaidi. Kwa hiyo, bado Nahitaji kwamba mjitoe mzimamzima kwa minajili ya kazi Yangu yote; aidha, mnafaa kutambua waziwazi na kuwa na hakika ya kazi ile yote ambayo Nimefanya ndani yako, na kuweka nguvu zako zote katika kazi Yangu ili iweze kuwa ya matokeo bora zaidi. Hilo ndilo ambalo lazima uelewe. Msipigane tena wenyewe kwa wenyewe, kutafuta mbinu za usuluhishi, au kutafuta raha za mwili, mambo ambayo yanaweza kuchelewesha kazi Yangu na kuharibu mustakabali wako mzuri. Kufanya hivyo, mbali na kuweza kukupa ulinzi, litakuletea maangamizo. Je, sii huu utakuwa ujinga kwa upande wako? Kile ambacho unafurahia leo kwa tamaa ndicho kile kile ambacho kinaharibu mustakabali wako, huku yale maumivu unayopitia leo ndiyo yaleyale ambayo yanakulinda. Lazima ufahamu waziwazi kuhusu jambo hilo, ili uepuke majaribio ambayo yatakuwa magumu kujinasua kutoka na kuepuka kuingia kwenye ukungu mzito unaozuia jua katika maisha yako. Wakati ukungu huu mzito utakapotoweka, utajipata katika hukumu ya siku kuu. Kufikia wakati huo, siku Yangu itakuwa imekaribia binadamu. Utatorokaje hukumu Yangu? Utawezaje kuvumilia joto kali la jua? Ninapompa binadamu wingi Wangu, haufurahii kwa dhati, lakini badala yake anautupa nje kwenye sehemu zisizotambulika. Wakati siku Yangu itawadia, binadamu hataweza tena kugundua wingi Wangu au kupata ukweli mkali Niliompa zamani sana. Ataomboleza na kulia, kwa sababu amepoteza mwangaza anaofuata na kuingia katika giza totoro. Kile mnachoona leo ni upanga tu mkali wa kinywa Changu. Bado hamjakiona kiboko kilicho katika mkono Wangu au moto Ninaotumia kumchoma binadamu, na ndiyo maana bado mna kiburi na msio na kadiri mbele Yangu. Ndiyo maana bado mnapigana na Mimi katika nyumba Yangu, huku mkipinga kwa ulimi wa mwanadamu kile ambacho Nimenena na kinywa Changu. Binadamu haniogopi Mimi. Akiwa bado katika uhasama na Mimi hadi leo, bado haniogopi kamwe. Mnao ulimi na meno ya wale wasio na haki vinywani mwenu. Maneno na matendo yenu ni kama yale ya yule nyoka aliyemshawishi Hawa na kumfanya kutenda dhambi. Mnadai nyinyi kwa nyinyi kulipiza kisasi, na mnashindana mbele Yangu kwa ajili ya nafasi, umaarufu, na faida kwa ajili yenu wenyewe, ilhali hamjui kwamba Natazama maneno na matendo yenu kwa siri. Kabla hata ya nyinyi kuja mbele Yangu, Nimejua vina vya nyoyo zenu kabisa. Siku zote binadamu hutamani kutoroka kutoka mfumbato Wangu na kuepuka uangalizi wa macho Yangu, lakini Sijawahi kuepuka maneno au matamshi yake. Badala yake, kwa kusudio kuu huwa Nayaruhusu maneno na matendo hayo yaingie katika macho Yangu, ili Niweze kuadibu udhalimu wake na kuhukumu uasi wake. Kwa hiyo, maneno na matendo fiche ya binadamu siku zote yanawekwa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na hukumu Yangu haijawahi kumtoka binadamu, kwa sababu uasi wake ni mwingi mno. Kazi Yangu ni kuteketeza na kusafisha maneno na matendo yote ya binadamu yaliyotamkwa na kufanywa mbele ya Roho Wangu. Kwa njia hiyo, baada ya Mimi kuondoka ulimwenguni, binadamu wataweza bado kuendeleza utiifu Kwangu, na bado watanihudumia kama vile watumishi Wangu watakatifu wanavyofanya katika kazi Yangu, wakiruhusu kazi Yangu hapa ulimwenguni iendelee mpaka siku itakapokamilika.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Ijumaa, 1 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa

Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa. Ingawa Yeye huvumilia shida ambazo watu wanaweza kupata ugumu kuvumilia, ingawa Yeye kama Mungu mkuu ana unyenyekevu wa kuwa mtu wa kawaida, hakuna kipengele cha kazi Yake kimecheleweshwa, na mpango Wake haujatupwa katika mchafuko hata kidogo. Anafanya kazi kulingana na mpango Wake wa awali. Mojawapo ya madhumuni ya kupata mwili huku ni kuwashinda watu. Mengine ni kuwakamilisha watu Anaowapenda. Yeye hutamani kuwaona kwa macho Yake mwenyewe watu Anaowakamilisha, na Yeye hutaka kujionea Mwenyewe jinsi watu Anaowakamilisha humshuhudia. Sio mtu mmoja ambaye hukamilishwa, na sio wawili. Hata hivyo, ni kikundi cha watu wachache sana. Kikundi hiki cha watu huja kutoka nchi mbalimbali za dunia, na kutoka kwa makabila mbalimbali ya ulimwengu. Kusudi la kufanya kazi hii nyingi ni kukipata kikundi hiki cha watu, kupata ushuhuda ambao kikundi hiki cha watu humtolea, na kupata utukufu ambao Yeye hupata kupitia kwa kikundi hiki cha watu. Yeye hafanyi kazi ambayo haina umuhimu, wala hafanyi kazi ambayo haina thamani. Inaweza kusemwa kuwa, kwa kufanya kazi nyingi sana, lengo la Mungu ni kuwakamilisha watu wote ambao Yeye anataka kuwakamilisha. Katika wakati wowote wa ziada Alio nao nje ya hili, Atawaondosha wale walio waovu. Jua kwamba Haifanyi kazi hii kubwa kwa sababu ya wale walio waovu; kwa kinyume, Yeye hufanya kadri Awezavyo kwa sababu ya idadi hiyo ndogo ya watu ambao hawana budi kukamilishwa na Yeye. Kazi ambayo Yeye hufanya, maneno ambayo Yeye hunena, siri ambayo Yeye hufichua, na hukumu Yake na adhabu zote ni kwa ajili ya idadi hiyo ndogo ya watu. Yeye hakupata mwili kwa sababu ya wale walio waovu, sembuse wao kuchochea ghadhabu kubwa ndani Yake. Yeye husema ukweli, na huzungumzia kuingia, kwa sababu ya wale watakaokamilishwa, Alipata mwili kwa sababu yao, na ni kwa sababu yao Yeye hutoa ahadi na baraka Zake. Ukweli, kuingia, na maisha katika ubinadamu ambayo Yeye huzungumzia si kwa ajili ya wale walio waovu. Yeye hutaka kuepuka kuzungumza na wale walio waovu, na hutaka kuwapa wale ambao watakamilishwa ukweli wote. Lakini kazi Yake inahitaji kwamba, kwa sasa, wale walio waovu waruhusiwe kufurahia baadhi ya utajiri Wake. Wale ambao hawatekelezi ukweli, ambao hawamridhishi Mungu, na ambao hukatiza kazi Yake wote ni waovu. Hawawezi kukamilishwa, na wanachukiwa kabisa na kukataliwa na Mungu. Kwa kinyume, watu ambao hutia ukweli katika vitendo na wanaweza kumridhisha Mungu na ambao hujitolea wenyewe kabisa katika kazi ya Mungu ndio watu ambao watakamilishwa na Mungu. Wale ambao Mungu hutaka kuwakamilisha sio wengine bali ni kikundi hiki cha watu, na kazi ambayo Mungu hufanya ni kwa ajili ya watu hawa. Ukweli ambao Yeye huzungumzia unaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kuutia katika vitendo. Yeye huwa hazungumzi na watu ambao hawatii ukweli katika vitendo. Ongezeko la umaizi na ukuaji wa utambuzi ambao Yeye huzungumzia umelengwa kwa watu ambao wanaweza kutekeleza ukweli. Anapozungumza juu ya wale ambao watakamilishwa Yeye anazungumzia watu hawa. Kazi ya Roho Mtakatifu inaelekezwa kwa watu ambao wanaweza kutenda ukweli. Mambo kama kumiliki hekima na kuwa na ubinadamu yanaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kutia ukweli katika vitendo. Wale ambao hawatekelezi ukweli wanaweza kuusikia ukweli mwingi na wanaweza kuuelewa ukweli mwingi, lakini kwa sababu wao ni miongoni mwa watu waovu, ukweli ambao wao huuelewa huja kuwa tu mafundisho na maneno, na hauna umuhimu kwa mabadiliko yao ya tabia au kwa maisha yao. Hakuna hata mmoja wao aliye mwaminifu kwa Mungu; wao wote ni watu wanaomwona Mungu lakini hawawezi kumpata, na wote wamehukumiwa na Mungu.
Roho Mtakatifu ana njia ya kutembea katika kila mtu, na humpa kila mtu fursa za kukamilishwa. Kupitia uhasi wako unajulishwa upotovu wako mwenyewe, na kisha kwa njia ya kuacha uhasi utapata njia ya kutenda, na huku ndiko kukamilishwa kwako. Aidha, kwa njia ya mwongozo na mwangaza wa siku zote wa mambo fulani chanya ndani yako, utatimiza shughuli yako kwa kuamili na kukua katika umaizi na kupata utambuzi. Wakati hali zako ni nzuri, uko tayari hasa kusoma neno la Mungu, na hasa tayari kumwomba Mungu, na unaweza kuyahusisha mahubiri unayoyasikia na hali zako mwenyewe. Kwa nyakati kama hizo Mungu hukupatia nuru na kukuangaza ndani, na kukufanya utambue mambo fulani ya kipengele chanya. Huku ni kukamilishwa kwako katika kipengele chanya. Katika hali hasi, wewe ni dhaifu na hasi, na huhisi kuwa huna Mungu, lakini Mungu hukuangaza, akikusaidia kupata njia ya kutenda. Kutoka nje ya hili ni kupata ukamilisho katika hali chanya. Mungu anaweza kumkamilisha mwanadamu katika vipengele hasi na chanya. Inategemea kama unaweza kupata uzoefu, na kama wewe hufuatilia kukamilishwa na Mungu. Kama kwa hakika unatafuta kukamilishwa na Mungu, basi kilicho hasi hakiwezi kukufanya upoteze, lakini kinaweza kukuletea mambo ambayo ni halisi zaidi, na kinaweza kukufanya uweze zaidi kujua kile kilichopunguka ndani yako, uweze zaidi kufahamu sana hali zako halisi, na kuona kwamba mtu hana kitu, wala si kitu; kama hupitii majaribio, hujui, na daima utahisi kuwa wewe ni wa hadhi ya juu kuliko wengine na bora kuliko kila mtu mwingine. Kwa njia hii yote utaona kwamba yote yaliyotangulia yalifanywa na Mungu na kulindwa na Mungu. Kuingia katika majaribio hukuacha bila upendo au imani, huna sala, na huwezi kuimba nyimbo—na, bila kulitambua, katikati ya hili unakuja kujijua. Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua “siri” katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo.
Ni nini mnachokitafuta sasa? Labda ni kukamilishwa na Mungu, kumjua Mungu, kumpata Mungu, au ni mtindo wa Petro wa miaka ya tisini, ama kuwa na imani kubwa zaidi ya ile ya Ayubu. Mnaweza kutafuta mengi, iwe ni kutafuta kuitwa wenye haki na Mungu na kufika mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, au kuweza kumdhihirisha Mungu duniani na kuwa na ushuhuda wa nguvu na mkubwa sana kwa Mungu. Bila kujali mnachokitafuta, kwa jumla, ni kwa ajili ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Haijalishi kama unatafuta kuwa mtu mwenye haki, au unatafuta mtindo wa Petro, ama imani ya Ayubu, au kukamilishwa na Mungu, chochote unachokitafuta, kwa muhtasari, yote ni kazi ya Mungu. Hivyo ni kusema, bila kujali unachokitafuta, yote ni kwa ajili ya kukamilishwa na Mungu, yote ni kwa ajili ya kupitia neno la Mungu, ili kuuridhisha moyo wa Mungu; yote ni kwa ajili ya kugundua uzuri wa Mungu, yote ni kwa ajili ya kutafuta njia ya kutenda katika uzoefu halisi kwa lengo la kuweza kuiacha tabia yako ya uasi, kufanikisha hali ya kawaida ndani yako mwenyewe, kuweza kufuata kabisa mapenzi ya Mungu, kuwa mtu sahihi, na kuwa na nia sahihi katika kila kitu unachokifanya. Sababu ya wewe kupitia vitu hivi vyote ni kufikia kumjua Mungu na kufanikisha ukuaji wa maisha. Ingawa kile unachokipitia ni neno la Mungu, na kile unachokipitia ni matukio halisi, watu, mambo, na vitu katika mazingira yako, hatimaye unaweza kumjua Mungu na kukamilishwa na Mungu. Kutafuta kuitembea njia ya mtu mwenye haki au kutafuta kutia neno la Mungu katika vitendo, hizi ndizo njia. Kumjua Mungu na kukamilishwa na Mungu ndiyo hatima. Kama unatafuta sasa kukamilishwa na Mungu, au kumshuhudia Mungu, kwa ujumla, hatimaye ni ili kumjua Mungu; ni ili kwamba kazi Anayoifanya ndani yako sio ya bure, ili hatimaye uje kuujua uhalisi wa Mungu, kujua ukuu Wake, vivyo hivyo hata zaidi kuujua unyenyekevu wa Mungu na hali Yake ya kutoonekana, na kujua kazi nyingi ambazo Mungu hufanya ndani yako. Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani, kufanya kazi Yake katika watu hawa wachafu na wapotovu, na kukikamilisha kikundi hiki cha watu. Mungu hakupata mwili tu ili kuishi na kula kati ya watu, kuwalisha watu, kutoa wanachohitaji watu. Jambo muhimu zaidi ni kwamba Yeye hufanya kazi Yake kubwa ya wokovu na ushindi kwa watu hawa walio na upotovu usiovumilika. Alikuja katika kiini cha joka kubwa jekundu ili kuwafanyia kazi watu hawa wapotovu mno, ili watu wote waweze kubadilishwa na kufanywa wapya. Tatizo kubwa ambalo Mungu huvumilia siyo tu shida ambayo Mungu mwenye mwili huvumilia, lakini hasa ni kwamba Roho wa Mungu hupitia udhalilishaji uliokithiri—Yeye hujinyenyekeza na kujificha Mwenyewe sana kiasi kwamba Yeye huwa mtu wa kawaida. Mungu alipata mwili na kuchukua mfano wa mwili ili watu waone kwamba Ana maisha ya kawaida ya binadamu, na kwamba ana mahitaji ya kawaida ya binadamu. Hili linatosha kuthibitisha kwamba Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani. Roho wa Mungu hufanyika katika mwili. Roho Wake ni wa juu sana na mkuu, lakini Yeye huchukua mfano wa mwanadamu wa kawaida, wa mwanadamu asiye muhimu ili kufanya kazi ya Roho Wake. Ubora wa tabia, umaizi, hisi, ubinadamu, na maisha ya kila mmoja wenu vinaonyesha kwamba hamfai kweli kupokea kazi ya Mungu ya aina hii. Hakika hamfai kumruhusu Mungu kuvumilia shida kama hiyo kwa ajili yenu. Mungu ni mkubwa sana. Yeye ni mkuu sana, na watu ni duni sana na wa hali ya chini, lakini Yeye bado huwafanyia kazi. Yeye hakupata mwili tu ili kuwaruzuku watu, kuzungumza na watu, Yeye hata huishi pamoja na watu. Mungu ni mnyenyekevu sana, wa hupendeka sana. Ikiwa punde upendo wa Mungu unapotajwa, mara tu neema ya Mungu inapotajwa, unatoa machozi unapotamka sifa kubwa, ukifika katika hali hii, basi una maarifa ya kweli ya Mungu.
Kuna kuchepuka katika kutafuta kwa watu siku hizi; wao hutafuta tu kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu, lakini hawana maarifa yoyote juu ya Mungu, na wametelekeza nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu ndani yao. Hawana maarifa ya kweli ya Mungu kama msingi. Kwa njia hii wanapoteza nguvu wakati uzoefu wao unapoendelea. Wale wote wanaotafuta kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu, ingawa wakati wa zamani hawakuwa katika hali nzuri, walielekea kwa uhasi na udhaifu, na mara nyingi walitoa machozi, wakaingia katika kukata tamaa, na wakavunjika moyo; sasa hali zao zinakuwa bora kwa kukithiri wanapopata uzoefu zaidi. Baada ya uzoefu wa kushughulikiwa na kuvunjwa, au kupitia kisa cha kusafishwa, wamekuwa na maendeleo makubwa. Hali kama hizo hazionekani zikiwafika tena, tabia zao zimebadilika, na upendo wa Mungu unaishi kwa kudhihirika ndani yao. Kuna kanuni kwa kukamilishwa kwa watu na Mungu, ambayo ni kwamba Yeye hukupa nuru kwa kutumia sehemu yako inayofaa ili uwe na njia ya kutenda na unaweza kujitenga na hali zote hasi, ikisaidia roho yako kupata uhuru, na ikikufanya uweze kumpenda zaidi. Kwa njia hii, unaweza kuiacha tabia potovu ya Shetani. Wewe huna hila na uko wazi, ukiwa tayari kujijua, na ukiwa tayari kutia ukweli katika vitendo. Mungu huona kwamba uko tayari kujijua na uko tayari kutia ukweli katika vitendo, kwa hiyo unapokuwa dhaifu na hasi, Yeye hukupa nuru maradufu, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa tayari kujitubia, na kuweza zaidi kutenda mambo ambayo unapaswa kuyatenda. Ni kwa njia hii tu ambapo moyo wako unahisi amani na utulivu. Mtu ambaye kwa kawaida huzingatia kumjua Mungu, ambaye huzingatia kujijua, ambaye huzingatia vitendo vyake mwenyewe ataweza kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, mara kwa mara kupokea mwongozo na nuru kutoka kwa Mungu. Hata ingawa yuko katika hali hasi, anaweza kugeuka mara moja, iwe ni kwa sababu ya matendo ya dhamiri au kwa sababu ya nuru kutoka kwa neno la Mungu. Mabadiliko ya tabia ya mtu hufanikishwa daima anapojua hali yake mwenyewe halisi na kujua tabia na kazi ya Mungu. Mtu ambaye yuko tayari kujijua na yuko tayari kuwasiliana ataweza kutekeleza ukweli. Aina hii ya mtu ni mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, na mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu ana ufahamu wa Mungu, uwe ni wa kina au wa juu juu, haba au maridhawa. Hii ni haki ya Mungu, na ni kitu ambacho watu hupata, ni faida yao wenyewe. Mtu ambaye ana maarifa ya Mungu ni yule ambaye ana msingi, ambaye ana maono. Mtu wa aina hii ana hakika kuhusu mwili wa Mungu, ana hakika kuhusu neno la Mungu, na ana hakika kuhusu kazi ya Mungu. Bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi au kuzungumza, au jinsi watu wengine husababisha vurugu, anaweza kushikilia msimamo wake, na kuwa shahidi kwa Mungu. Kadiri mtu alivyo katika njia hii ndivyo anavyoweza kutekeleza zaidi ukweli anaouelewa. Kwa sababu daima anatenda neno la Mungu, yeye hupata ufahamu zaidi wa Mungu, na analo azimio la kuwa shahidi kwa Mungu milele.
Kuwa na utambuzi, kuwa na utii, na kuwa na uwezo wa kubaini mambo ili uwe hodari katika roho ina maana kuwa maneno ya Mungu yanakuangaza na kukupa nuru ndani mara tu unapokabiliwa na kitu fulani. Huku ni kuwa hodari katika roho. Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya kusaidia kufufua roho za watu. Kwa nini Mungu daima husema kuwa watu ni wa kujijali na wajinga? Ni kwa sababu roho za watu zimekufa, na wamekuwa wa kutojali kiasi kwamba hawajui kabisa mambo ya roho. Kazi ya Mungu ni kuyafanya maisha ya watu yaendelee na ni kusaidia roho za watu zichangamke, ili waweze kubaini mambo ya roho, na daima waweze kumpenda Mungu, kumridhisha Mungu. Ufikaji mahali hapa huonyesha kwamba roho ya mtu imefufuliwa, na wakati mwingine atakapokabiliwa na kitu fulani, anaweza kuonyesha hisia mara moja. Yeye huitikia mahubiri, na kuonyesha hisia haraka kwa hali mbalimbali. Huku ndiko kufanikisha uhodari wa roho. Kuna watu wengi ambao wana majibizo ya haraka kwa tukio la nje, lakini mara tu kuingia katika uhalisi au mambo kinaganaga ya roho yanapotajwa, wao huwa wa kutojali na wajinga. Wao huelewa kitu tu kikiwa ni dhahiri. Hizi zote ni ishara za kuwa wa kutojali kiroho na mjinga, za kuwa na uzoefu kidogo wa mambo ya roho. Watu wengine ni hodari wa roho na wana utambuzi. Mara tu wanaposikia kitu kinachoelekezwa kwa hali zao hawapotezi muda kukiandika. Wanakitumia kwa uzoefu wao wa baadaye, na kwa kujibadilisha. Huyu ni mtu ambaye ni hodari katika roho. Na kwa nini anaweza kuonyesha hisia haraka sana? Kwa sababu yeye hulenga vipengele hivi katika maisha ya kila siku, na mara tu mojawapo ya vipengele hivi kinapotajwa, kinatokea kufanana na hali yake ya ndani, na anaweza kukipokea mara moja. Ni sawa na kumpa mtu mwenye njaa chakula; anaweza kula mara moja. Ukimpa chakula mtu asiye na njaa, hana haraka kuonyesha hisia. Daima wewe humwomba Mungu, na kisha unaweza kuonyesha hisia mara moja unapokabiliwa na kitu fulani: kile Mungu huhitaji katika jambo hili, na jinsi unavyopaswa kutenda. Mungu alikuongoza juu ya suala hili mara ya mwisho; unapokabiliwa na kitu cha aina hii leo unajua jinsi ya kuingia katika hali hii, kuuridhisha moyo wa Mungu. Daima ukitenda kwa njia hii na daima upate uzoefu kwa njia hii, wakati fulani utakuwa stadi kwayo. Wakati unasoma neno la Mungu unajua ni mtu wa aina gani Mungu anamzungumzia, unajua ni aina gani ya hali za roho Anayozungumzia, na unaweza kuelewa jambo muhimu na kulitia katika vitendo; hii inaonyesha kuwa unaweza kupata uzoefu. Kwa nini watu wengine hawana jambo hili? Ni kwa sababu hawaweki jitihada nyingi katika kipengele cha kutenda. Ingawa wako tayari kutia ukweli katika vitendo, hawana umaizi wa kweli katika utondoti wa huduma, katika utondoti wa ukweli katika maisha yao. Wanachanganyikiwa jambo linapotokea. Kwa njia hii, unaweza kupotoshwa nabii wa uongo au mtume wa uongo anapokuja. Haikubaliki kupuuza utambuzi. Ni lazima uzingatie mambo ya roho daima: jinsi Mungu hufanya kazi, kile Mungu husema, yale yaliyo matakwa Yake kwa watu, ni watu wa namna gani unapaswa kuwasiliana nao, na ni watu wa aina gani unapaswa kuwaepuka. Ni lazima usisitize mambo haya wakati wa kula na kunywa neno la Mungu na wakati wa uzoefu. Daima ukiwa na uzoefu wa mambo kwa njia hii, utaelewa vizuri vitu vingi, na utakuwa na utambuzi pia. Ni nini kufundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu, ni nini lawama inayotokana na nia ya mwanadamu, ni nini mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini mpango wa mazingira, ni nini maneno ya Mungu yanatolea nuru ndani, kama huna uhakika juu ya mambo haya, hutakuwa na utambuzi. Unapaswa kujua kile ambacho huja kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini tabia ya uasi, jinsi ya kulitii neno la Mungu, na jinsi ya kuacha uasi wa mtu mwenyewe; unapaswa kuelewa utondoti wa ukweli huu wote, ili jambo linapotukia, una ukweli unaofaa wa kulinganisha nalo, una maono yanayofaa kama msingi, una kanuni katika kila jambo na unaweza kutenda kulingana na ukweli. Halafu maisha yako yatajazwa na nuru ya Mungu, yatajazwa na baraka za Mungu. Mungu hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye humtafuta kwa kweli. Hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye huishi kwa kumdhihirisha na ambaye hushuhudia kwa ajili Yake, na hatamlaani mtu yeyote ambaye kwa kweli anaweza kuona kiu ya ukweli. Ikiwa, unapokula na kunywa maneno ya Mungu, unaweza kuzingatia hali yako mwenyewe ya kweli, kuzingatia vitendo vyako mwenyewe, na kuzingatia ufahamu wako mwenyewe, basi, unapokabiliwa na tatizo, utapokea nuru na utapata ufahamu wa utendaji. Kisha utakuwa na njia ya kutenda na utakuwa na utambuzi kwa kila kitu. Mtu aliye na ukweli si rahisi kudanganywa, na rahisi kutenda kwa vurugu au kutenda kwa kupita kiasi. Kwa sababu ya ukweli amelindwa, na pia kwa sababu ya ukweli yeye hupata ufahamu zaidi. Kwa sababu ya ukweli ana njia zaidi za kutenda, hupata fursa zaidi za Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yake, na hupata fursa zaidi za kukamilishwa.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 19 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli. Wataweza tu kuzifundisha roho zao, kuifanya mioyo yao iweze kusonga kwa kawaida karibu na Mungu, na kupata kila mara furaha nyingi mno katika kuwa na Mungu. Watakuwa wamejiwekea mipaka kwa ulimwengu mdogo wa kuwa na mshikamano na Mungu, wasiweze kuelewa kile kilicho katika vina vya ndani kabisa. Watu ambao huishi katika mipaka hii pekee hawana uwezo wa kupiga hatua yoyote kubwa. Wakati wowote, wanaweza kulia, “Aa! Bwana Yesu. Amina!” Wanapokula, wao hulia, “Ee Mungu! Nala na Wewe unakula....” Na ni hivi karibu kila siku. Huu ni utendaji wa nyakati zilizopita, ni utendaji wa kuishi ndani ya roho kila wakati. Huo sio utovu wa adabu? Leo, kama ni wakati wa kutafakari juu ya maneno ya Mungu, unapaswa kuyatafakari, kama ni wakati wa kutia ukweli katika vitendo unapaswa kuuweka katika vitendo, na wakati ni muda wa kutekeleza wajibu wako, unapaswa kuutekeleza. Kufanya utendaji hivyo ni huru kabisa, kunakufungua wewe. Sio kama vile wazee wa dini huomba na kusema neema. Bila shaka, hapo awali, hivi ndivyo watu walioamini katika Mungu walitakiwa kutenda—lakini kutenda kwa njia hii kila mara ni kuliko nyuma kimaendeleo kabisa. Utendaji wa wakati uliopita ni msingi wa utendaji wa leo. Ikiwa kungekuwa na njia kwa utendaji wa nyakati zilizopita, utendaji wa leo utakuwa rahisi zaidi. Kwa hiyo, leo, tunapozungumza juu ya “kumleta Mungu katika maisha halisi,” ni hali gani ya utendaji inatajwa? “Maisha halisi” hasa yanahitaji watu wawe na ubinadamu wa kawaida; kile ambacho watu wanapaswa kuwa nacho ni kile ambacho Mungu anataka kutoka kwao leo. Kuyaleta maneno ya Mungu katika maisha halisi ndiyo maana halisi ya “kumleta Mungu katika maisha halisi.” Leo, watu wanapaswa hasa kujiandaa wenyewe na yafuatayo: Kuhusu suala moja, lazima waendeleze uhodari wao, wafunzwe, waongeze msamiati wao, na kuendeleza ustadi wao wa kusoma; na katika lingine, lazima waishi maisha ya watu wa kawaida. Umerudi tu mbele ya Mungu kutoka ulimwenguni, na lazima kwanza uifunze roho yako, kuufunza moyo wako kuwa na amani mbele ya Mungu. Hili ndilo la msingi kabisa, na pia ni hatua ya kwanza katika kutimiza mabadiliko. Watu wengine ni wepesi kubadilika katika utendaji wao; wao hutafakari ukweli huku wakifua nguo zao, wakielewa ukweli wanaopaswa kuelewa na kanuni wanazopaswa kuweka katika vitendo kwa uhalisi. Katika suala moja, lazima uwe na maisha ya kawaida ya ubinadamu, na katika lingine lazima kuwe na kuingia katika ukweli. Huu ni utendaji bora zaidi kwa maisha halisi.
Zamani, watu walipitia magumu mengi sana, lakini mengine yalikuwa yasiohitajika kwa kweli, kwani mengine yalikuwa mambo ambayo hayakuhitajika kutendwa na mwanadamu. Wanapomleta Mungu katika maisha yao halisi, Mungu kimsingi anahitaji kwamba watu wamwabudu Mungu, wafuatilie ufahamu wa Mungu, na kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu katikati ya ubinadamu wa kawaida. Hawahitajiki kumwomba Mungu mara tu wanapoanza kufagia sakafu, wakihisi ni wadeni Wake wasipofanya hivyo. Utendaji wa leo sio hivyo; ni uliolegezwa na rahisi! Watu hawaambiwi watii mafundisho ya dini. Kila mmoja anapaswa kutenda kulingana na kimo chake mwenyewe: Ikiwa mume wako haamini, mchukulie kama mtu asiyemwamini Mungu, na ikiwa yeye huamini mchukulie kama muumini. Usisisitize kuhusu upendo na uvumilivu, bali kuhusu hekima. Watu wengine huenda kununua mboga, na wanapokuwa wakitembea wao hunong’ona: Ee Mungu! Ni mboga gani ambazo unanikubalia ninunue leo? Naomba usaidizi Wako. Je, nichague ninaponunua? Kisha wao hufikiria: Sitachagua; Mungu ananiambia kwamba nimtukuze Yeye, kwamba nilitukuze jina Lake katika mambo yote, na kwamba watu wote wawe na ushuhuda, kwa hiyo muuzaji akinipa kitu fulani cha kitambo na kilichokauka, bado nitampa Mungu shukrani—nitavumilia! Sisi tuaminio katika Mungu hatuchagui ni mboga gani za kununua. Unafikiri kwamba kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na baada ya kutumia yuan[a] moja kununua mboga ya kitambo iliyo na kuvu, bado unaomba na kusema: Ee Mungu! Bado nitaila mboga hii iliyooza—maadamu Unikubali, nitaila. Je, utendaji kama huu sio wa kipumbavu? Je, huko sio kufuata mafundisho ya dini? Hapo awali, watu walizifundisha roho zao na waliishi ndani ya roho kila wakati, na hili lilihusiana na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Neema. Uchaji Mungu, unyenyekevu, upendo, uvumilivu, kutoa shukrani kwa mambo yote—haya ndiyo yaliyotakiwa kutoka kwa kila muumini katika Enzi ya Neema. Wakati huo, watu walimwomba Mungu katika mambo yote; wangeomba waliponunua nguo, na walipofahamishwa juu ya mkutano, pia wangeomba na kusema: Ee Mungu! Je, Unanikubalia niende au la? Ikiwa unanikubalia kwenda, basi nitayarishie njia iliyonyooka, acha kila kitu kifanyike kwa urahisi. Na ikiwa hunikubalii kwenda, basi nifanye nianguke chini. Walipoomba, walimsihi Mungu. Baada ya kuomba walihisi wasio na utulivu, na hawakuenda. Pia kulikuwa na dada ambao, kwa vile waliogopa kupigwa na waume wao wasiomwamini Mungu wakati ambapo wangerudi, walihisi wasio na utulivu walipoomba—na kwa vile walihisi wasio na utulivu, hawakuenda kwa mkutano. Waliamini hayo yalikuwa mapenzi ya Mungu, ilhali kweli ni kwamba, iwapo wangeenda, hakuna chochote ambacho kingefanyika. Matokeo ni kwamba walikosa mkutano. Haya yote yalisababishwa na ujinga wa watu wenyewe. Watu wanaofanya utendaji kwa njia hii huishi kwa hisia zao wenyewe. Njia hii ya utendaji ina kosa na ni ya kipumbavu, haina udhahiri, na hisia na mawazo yao wenyewe kwa wingi sana. Ukiambiwa kuhusu mkutano, basi nenda, na usipoambiwa, basi usiende; unapoambiwa kuuhusu, hakuna haja ya kumwomba Mungu. Je, hili si rahisi? Ikiwa, leo, unahitaji kununua kipande fulani cha mavazi, basi nenda ukafanye hivyo. Usimwombe Mungu na kusema: Ee Mungu! Leo napaswa kununua kipande fulani cha mavazi, je, Unanikubalia niende au la? Ni aina gani ya mavazi ninayopaswa kununua? Je dada mmoja akija hapa nikiwa nimeenda? Kwa kuomba na kutafakari, unajiambia mwenyewe: “Sitaki kwenda leo, huenda dada fulani akaja hapa.” Ilhali matokeo ni kwamba, kufikia jioni, hakuna aliyekuja hapo, na umekosa mengi. Hata katika Enzi ya Neema, njia hii ya utendaji ilikuwa na makosa na isiyo sahihi. Kwa hiyo, ikiwa watu watafanya utendaji kama katika nyakati zilizopita, hakutakuwa na mabadiliko katika maisha yao. Watakuwa tu watiifu, na hawatatilia maanani upambanuzi, na hawatafanya lolote ila kutii na kuvumilia pasipo kufikiria. Katika wakati huo, watu walisisitiza kuhusu kumtukuza Mungu—lakini Mungu hakupata utukufu wowote kutoka kwao, kwani hawakuwa wameishi kwa kudhihirisha lolote, na hawakuwa wamebadilika. Walijitiisha tu na kujiwekea mipaka wenyewe kulingana na dhana zao wenyewe, na hata miaka mingi ya utendaji haikuleta mabadiliko katika maisha yao; walijua tu kuvumilia, kuwa wanyenyekevu, kupenda, na kusamehe, na hawakupata nuru hata kidogo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Wangemjuaje Mungu?
Watu wataingia tu kwa njia sahihi ya imani katika Mungu ikiwa watamleta Mungu ndani ya maisha yao halisi, na katika maisha yao ya kawaida ya ubinadamu. Leo, maneno ya Mungu yanawaongoza ninyi, na hakuna haja ya kutafuta na kupapasa kama nyakati zilizopita. Wakati ambapo unaweza kutenda kulingana na maneno haya, na unaweza kujichunguza na kujitathmini mwenyewe kulingana na hali ambazo Nimetaja, basi utaweza kubadilika. Haya siyo mafundisho ya dini, lakini kile ambacho Mungu anamtaka mwanadamu afanye. Leo, Nakwambia kiini cha jambo: Jishughulishe tu na kutenda kulingana na maneno Yangu. Matakwa Yangu kwako ni kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, na Nimekwambia hilo tayari; ikiwa unasisitiza kabisa kutenda kwa njia hii, utaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Siku hii ndio wakati wa kuishi katika maneno ya Mungu: Maneno ya Mungu yameeleza yote, yote yamefafanuliwa wazi, na maadamu unaishi kwa maneno ya Mungu, utaishi maisha yaliyo huru kabisa na yaliyokombolewa. Hapo awali, ulipomleta Mungu katika maisha yako halisi, ulipitia mafundisho ya dini na sherehe nyingi sana, ulimwomba Mungu hata katika mambo madogo sana, uliyaweka maneno dhahiri upande mmoja, kutoyasoma, na ukajitolea juhudi zako zote kwa kutafuta—na matokeo kwamba hakukuwa na athari. Chukua mfano wa, kile ulichovaa: Wakati ambapo uliomba, uliliweka jambo hili mikononi mwa Mungu, ukiomba kwamba Mungu achague kitu kinachofaa kwa wewe kuvaa. Mungu aliyasikia maneno haya na kusema: “Unaniomba Nijishughulishe Mimi na tondoti hafifu kama hizi? Ubinadamu wa kawaida na urazini Nilivyokuumbia vimeenda wapi?” Wakati mwingine, mtu fulani atafanya makosa katika matendo yake, na ataamini kwamba amemkosea Mungu, naye huanza kufungwa. Hali za watu wengine ni nzuri sana, lakini wanapofanya kitu fulani kidogo kwa njia isiyo sahihi wao huamini kwamba Mungu anawaadibu. Kwa kweli, hii si kazi ya Mungu, lakini ya akili za watu wenyewe. Wakati mwingine, huwa hakuna kosa lolote na vile unavyopitia tukio, laini wengine husema kwamba unapitia tukio kwa njia isiyo sahihi, na hivyo unategwa—unakuwa mbaya, na mwenye giza ndani. Mara kwa mara, watu wakiwa baridi kwa njia hii, wao huamini kwamba wanaadibiwa na Mungu, lakini Mungu husema: “Sifanyi kazi ya kuadibu ndani yako, ungenilaumuje Mimi hivyo?” Watu ni wabaya sana. Wao pia ni wepesi kuhisi sana mara kwa mara na wao hulalamika kuhusu Mungu mara kwa mara. Mungu hakutaki wewe uteseke, ilhali wewe unajiacha uingie katika hali hiyo. Hakuna thamani katika kuteseka kwa aina hii. Kwa sababu watu hawajui kazi inayofanywa na Mungu, katika mambo mengi wao ni wajinga, na hawawezi kuona kwa dhahiri. Katika nyakati kama hizo, wao hunaswa katika mawazo yao wenyewe, wakiendelea kutegwa zaidi milele. Watu wengine husema kwamba vitu vyote na mambo yote yamo mikononi mwa Mungu—kwa hiyo Mungu hangejua watu wanapokuwa wabaya? bila shaka Mungu hujua. Wakati ambapo unategwa katika dhana za binadamu, Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi ndani yako. Wakati mwingi, watu wengine hutegwa katika hali mbaya, lakini Mimi bado huendelea na kazi Yangu. Kama wewe ni mbaya au mtendaji, Mimi sizuiliwi na wewe—lakini unapaswa kujua kwamba maneno mengi Ninenayo, na kiasi kikubwa sana cha kazi Nifanyayo, huja kwa wingi na haraka kulingana na hali ya watu. Wakati ambapo wewe ni mbaya, hili halizuii kazi ya Roho Mtakatifu. Katika nyakati za kuadibu na kifo, watu wote walitegwa ndani ya hali mbaya, lakini hili halikuizuia kazi Yangu; ulipokuwa mbaya, Roho Mtakatifu aliendelea kufanya kilichohitajika kufanywa ndani ya wengine. Unaweza kuendelea kusimama kwa mwezi mmoja, lakini Naendelea kufanya kazi—chochote ufanyacho katika siku za baadaye au sasa, hakiwezi kuizuia kazi ya Roho Mtakatifu. Hali nyingine mbaya hutokana na udhaifu wa binadamu; wakati ambapo watu hawawezi kweli kufanya jambo au kulielewa, wao huwa wabaya. Kwa mfano, katika nyakati za kuadibu, maneno ya Mungu yalizungumza kuhusu kumpenda Mungu kwa kiwango fulani wakati wa kuadibu—lakini wewe uliamini kwamba huwezi. Wakati wa hali hii watu walihisi hasa wenye huzuni na wakaomboleza, walisikitika kwamba miili yao ilikuwa imepotoshwa vikali na Shetani, na kwamba uhodari wao ulikuwa mbaya sana, walihisi kwamba ilisikitisha kuwa walizaliwa katika mazingira haya. Watu wengine walihisi kwamba wakati ulikuwa umepita sana wa kuamini katika Mungu na kumjua Mungu, na kwamba walikuwa hawastahili kufanywa wakamilifu. Hizi zote ni hali za kawaida.
Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za kutotii, ni mchafu ya kusikitisha, ni kitu kichafu. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi, kuna maonyesho mengi sana ya mwili, na kwa hiyo Mungu hudharau mwili kwa kiwango fulani. Watu wanapoacha uchafu, mambo potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini wakibaki bila kuweza kuachana na uchafu na upotovu, basi bado watamilikiwa na Shetani. Kula njama, udanganyifu, na uhalifu wa watu ni mambo ya Shetani; kwa kukuokoa wewe, Mungu hukutenganisha na mambo haya na kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa, na yote ni kwa sababu ya kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unaishi ukimilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na hutapokea urithi wa Mungu. Mara tu umetakaswa na kufanywa kamili, utakuwa mtakatifu, na utakuwa wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na wa kufurahisha kwa Mungu. Kazi inayofanywa na Mungu leo ni wokovu, na, zaidi ya hayo, ni hukumu, kuadibu, na laana. Ina hali nyingi. Je, maneno mengine ya Mungu sio hukumu na kuadibu tu, bali pia laana? Nazungumza ili kutimiza athari fulani, kuwafanya watu wajijue wenyewe, na sio kuwafisha watu; Moyo Wangu ni kwa ajili yenu. Kuzungumza ni mbinu mmojawapo ambayo Mimi hufanyia kazi, Natumia maneno kuonyesha tabia ya Mungu, na kukuruhusu wewe kuelewa mapenzi ya Mungu. Mwili wako waweze kufa, lakini una roho na nafsi. Kama watu wangekuwa na mwili tu, basi hakungekuwa na maana ya wao kuamini katika Mungu, wala hakungekuwa na maana kwa kazi hii yote ambayo Nimefanya. Leo, Nazungumza juu ya jambo moja na kisha lingine, wakati mmoja Ninachukia mno watu, na wakati mwingine Ninapenda kwa hali ya juu; Nafanya hili kuzibadilisha tabia zako, na kuzigeuza dhana zako.
Siku za mwisho zimefika, na nchi nyingi kutoka upande mmoja wa ulimwengu hadi mwingine ziko katika machafuko, kuna vurugu ya kisiasa, njaa, ndwele, mafuriko, na ukame unaonekana kila mahali, kuna maangamizi katika ulimwengu wa mwanadamu, na Mbingu imetuma msiba hapa chini. Hizi ni ishara za siku za mwisho. Lakini kwa watu, unaonekana kama ulimwengu wa uchangamfu na fahari, ambao unaendelea kuwa hivyo zaidi na zaidi. Watu wanapotazama ulimwengu, mioyo yao inavutiwa nao, na wengine hawawezi kujinasua kutoka kwa ulimwengu; idadi kubwa itadanganywa na wale wanaoshiriki katika hila na uchawi. Usipojitahidi ili kuendelea mbele, na huna maadili, utapeperushwa na wimbi hili lenye dhambi. China ni nchi iliyo nyuma sana kimaendeleo kuliko zote, ni nchi ambayo joka kuu jekundu limelala likiwa limejiviringisha, ina watu wengi zaidi wanaoabudu sanamu na kushiriki katika uchawi, hekalu nyingi zaidi, na ni mahali ambapo pepo wachafu huishi. Ulizaliwa ndani yake, unafurahia manufaa yake, na unapotoshwa na kuteswa nalo, lakini baada ya kupitia kujichungua unaachana nalo na unapatwa kabisa na Mungu. Huu ni utukufu wa Mungu, na kwa hiyo hatua hii ya kazi ina umuhimu mkubwa. Mungu amefanya kazi ya kiwango kikubwa hivi, amenena maneno mengi sana, na hatimaye Atawapata ninyi kabisa—hii ni sehemu moja ya kazi ya usimamizi wa Mungu, na ni “mateka ya ushindi” ya vita dhidi ya Shetani. Kadri watu hawa wanavyokuwa bora na kadri maisha ya kanisa yanavyokuwa thabiti, ndivyo joka kuu jekundu linavyotiishwa. Haya ni mambo ya ulimwengu wa kiroho, ni vita vya ulimwengu wa kiroho, na Mungu anapokuwa mshindi, Shetani ataaibishwa na kuanguka chini. Hatua hii ya kazi ya Mungu ina umuhimu wa ajabu. Kazi ya kiwango kikubwa hivyo huokoa kabisa kikundi hiki cha watu; unaponyoka kutoka kwa ushawishi wa Shetani, unaishi katika nchi takatifu, unaishi katika nuru ya Mungu, na hapo kuna uongozi na mwongozo wa nuru, na kisha kuna maana katika kuwa kwako hai. Mnachokula na kuvaa ni tofauti na wao; mnafurahia maneno ya Mungu, na kuishi maisha yenye maana—na wao hufurahia nini? Wao hufurahia tu urithi wa babu zao na “roho ya kitaifa.” Hawana hata dalili ndogo kabisa ya ubinadamu! Mavazi, maneno, na matendo yenu vyote ni tofauti na vyao. Hatimaye, mtaacha kabisa uchafu, hamtategwa tena na ushawishi wa Shetani, na mtapata upaji wa Mungu wa kila siku. Mnapaswa kila mara kuwa waangalifu. Ingawa mnaishi mahali pachafu hamjawekwa mawaa na uchafu na mnaweza kuishi ubavuni mwa Mungu, mkipokea ulinzi Wake mkuu. Mmechaguliwa miongoni mwa wote walio katika nchi hii ya manjano. Je, ninyi sio watu waliobarikiwa zaidi? Kama kiumbe aliyeumbwa, unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu na uishi katika mwili mchafu, basi wewe siye mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kama binadamu, unapaswa kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso. Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu, kama Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kinachotolewa na ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya Shetani, na kukanyagiwa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au njia ya kweli, basi ni nini maana ya maisha yako? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale wanaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?