Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kutenda-ukweli. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kutenda-ukweli. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 6 Mei 2019

Unawezaje Kutofautisha Kati ya Viongozi wa Kweli na wa Uongo, na Wachungaji wa Kweli na wa Uongo

6. Unawezaje Kutofautisha Kati ya Viongozi wa Kweli na wa Uongo, na Wachungaji wa Kweli na wa Uongo?

Maneno Husika ya Mungu:
Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno halisi ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno halisi ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi halisi ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana, na huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga. Huduma hiyo huenda kinyume na Mungu, na hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu. "Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu" kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu.
kutoka kwa "Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasioona mbali, wanaojaribu kuonyesha tu jinsi walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha "wasomi" wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Je, watu hawa wana mantiki yoyote ya kuzungumzia? Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki?
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mtu kama huyu daima anakuwa na uadui dhidi ya kazi mpya ya Mungu, haonyeshi nia ya kujisalimisha, na hajawahi kutii ama kujinyenyekea kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe hajisalimishi kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi kwa kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi hazina anazomiliki, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiriwa kwa wengine, na kutumiwa kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni "mashujaa wasioshindwa," kizazi baada ya kizazi kinakaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanafikiria kuhubiri neno (mafundisho ya dini) ni wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wanatekeleza kwa nguvu wajibu wao "mtakatifu na usiokiukwa". Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna anayethubutu kuwapinga kwa uwazi. Walikuwa "mfalme" kwa nyumba ya Mungu, wakitenda kama dikteta kupitia enzi nyingi.
kutoka kwa "Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi , unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi, na kazi yako inaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe. Kwa hakika, utakuwa msumbufu zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hii ni uzoefu na mafunzo ya kibinadamu. Ni filosofia ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa wanapatikana miongoni mwa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini.
kutoka kwa "Sitisha Huduma ya Kidini" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali utu wa watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua mitazamo yao, achilia mbali kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokidhihirisha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambayo ni nje ya mguso wa uhalisia na kuwapatia watu uzima. Kimsingi, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga wa bahari, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Katika hili, je huwadanganyi watu? Je, wewe si mtu wa maneno matupu bila vitendo? Kutenda kwa namna hii ni hatari kwa watu! Kadri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisia, na ndivyo inavyokosa uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisia; kadri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya kumuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisia, maana watu hawa hawajawa na uzoefu binafsi nazo, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kumwongoza mwanadamu katika njia nzuri, na watawapotosha tu watu. Je, hii si hatari kwa watu? Kwa kiwango cha chini kabisa, unapaswa uweze kutatua shida za sasa na kuwaruhusu watu kupata kuingia; hii tu ndiyo inahesabika kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno mazuri, ya kibunifu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo mazuri, na kutaongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuwaongoza watu namna hii kutazalisha taratibu nyingi, ambazo zitafanya watu wakuchukie. Huu ndio udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli hauvumiliki.
kutoka kwa "Sisitiza Zaidi Kwa Uhalisia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Maarifa yenu yanaweza kuwakimu watu kwa muda tu. Wakati unapoendelea, ukiendelea kusema kitu kile kile, watu kadhaa wataweza kutambua; watasema wewe ni mtu wa juu juu sana, aliyekosa kina sana. Hutakuwa na budi ila kujaribu kuwadanganya watu kwa kuongea mafundisho, na kama wewe daima huendelea hivi, wale walio chini yako watafuata namna yako, nyayo, na mfano wa kumwamini Mungu na kupitia, na watatia maneno na mafundisho hayo katika vitendo, na hatimaye, unapoongea katika njia hii, watakutumia kama mfano. Unachukua mwongozo kuongea mafundisho, na wale walio chini yako watajifunza mafundisho kutoka kwako, na vitu vinapoendelea utakuwa umechukua njia ambayo si sawa. Wale walio chini yako wanafuata njia yako … Tazama viongozi wa kila madhehebu na faraka. Wote ni wa kujigamba na kujisifu, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ujuzi fulani, na wanaweza kuongea mafundisho kiasi, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa, ambao kupitia kwake wamewaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu—lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na wale wanaohubiri njia ya kweli, baadhi yao wangesema, "Lazima tutafute ushauri kwake kuhusu imani yetu katika Mungu." Tazama jinsi wanavyohitaji ridhaa ya mtu ili kumwamini Mungu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?
kutoka kwa "Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kutoa kwenu "muhtasari kuhusu ukweli" hakufanywi ili kuwawezesha watu kupata maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunafanywa ili watu waweze kuwa weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka kwa ukweli. Wao huonekana kana kwamba wanaelewa lengo lililokusudiwa katika kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno ya mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli, na si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia. Wewe unakusanya vitabu hivi au vifaa hivyo, na hivyo unapata umiliki wa kipengele hiki cha mafundisho au kipengele kile cha ujuzi. Wewe ni msemaji wa kiwango cha juu wa mafundisho—lakini huwaje unapomaliza kusema? Watu basi hawana uwezo wa kupitia, hawana ufahamu wa kazi ya Mungu na hawana ufahamu wao wenyewe pia. Mwishowe, vitu vyote watakavyokuwa wamepata ni fomyula na sheria … Kwa kuuliza swali baada ya swali kuhusu maneno hayo, kisha kujibu, kufanya muhtasari, unadhani kuwa wale walio chini wanaweza kuelewa kwa urahisi. Mbali na kuwa rahisi kukumbuka, wao wana uhakika juu ya maswali haya kwa tazamo la haraka, na unafikiri ni vizuri kufanya mambo kwa njia hii. Lakini kile wanachokielewa siyo maana iliyokusudiwa ya ukweli; inatofautiana na ukweli na ni maneno ya mafundisho tu. Hivyo ingekuwa bora zaidi kama wewe hungefanya mambo haya hata kidogo. Unafanya mambo haya kuwaongoza watu kuelewa ujuzi na weledi wa elimu. Wewe huwaleta wengine katika mafundisho, katika dini, na kuwafanya wamfuate Mungu na kumwamini Mungu ndani ya mafundisho ya dini. Je, si wewe ni sawa tu na Paulo? … Mwishowe wao wangeletwa mahali ambapo hawawezi kupata ukweli na hawawezi kupitia neno la Mungu, mahali ambapo wanaweza kujiandaa tu na kujadili mafundisho na ni mahali ambapo hawawezi kumwelewa Mungu. Yote ambayo wangeweza kuzungumza yangekuwa mafundisho yenye kupendeza, mafundisho sahihi, lakini hakungekuwa na uhalisi ndani yao na hawangekuwa na njia ya kutembelea. Aina hii ya kuongoza kweli hufanya madhara makubwa!
kutoka kwa "Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine wanajihami tu na ukweli fulani kwa wakati wa dharura ama kujitelekeza wenyewe na kuwasaidia wengine, sio kutatua shida zao wenyewe; tunawaita "watu wasio na ubinafsi." Wanawaona wengine kama vikaragosi wa ukweli na wenyewe kama mabwana wa ukweli, wakiwafunza wengine kuushikilia ukweli na wasiwe wasiojihususha, ilhali wao wenyewe ni watazamaji kando kando mwa uwanja—hao ni watu wa aina gani? Wakiwa wamejihami na baadhi ya maneno ya ukweli ili kuwahubiria wengine tu, wakikosa kufanya chochote kujizuia kutokana na kuangamia kwao wenyewe—inasikitishaje! Kama maneno yao yanaweza kuwasaidia wengine, mbona wasijisaidie wenyewe? Tunafaa kuwaita wanafiki wasio na ukweli. Wanatoa maneno ya ukweli kwa wengine na kuwaambia wengine wayaweke katika matendo, lakini hawafanyi juhudi yoyote kuyatenda wenyewe—je sio wa kudharauliwa? Kwa hakika hawawezi kulifanya wenyewe, ilhali wanawalazimisha wengine kuweka maneno ya ukweli katika matendo—hii ni njia ya ukatili iliyoje! Hawatumii ukweli kuwasaidia wengine; hawawatolei wengine kwa moyo wa upendo wa mama; wanawadanyanya tu watu na kuwapotosha watu. Hili likiendelea—na kila mtu akipitisha maneno ya ukweli kwa anayefuata—je kila mmoja mwishowe hatakuwa na uelewa tu wa maandishi ya ukweli wakikosa uwezo wa kuyatenda?
kutoka kwa "Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Wale wanaosoma Biblia kwa makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu wabovu, kila mmoja akisimama juu kumfundisha Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga makusudi. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, mapepo yanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Ingawa wenye "mwili imara," wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni maadui wa Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?
kutoka kwa "Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mbona Nasema wale walio katika dunia ya kidini hawaamini katika Mungu na ni waovu, walio sawa na ibilisi? Ninaposema ni watenda maovu, ni kwa sababu hawaelewi matakwa ya Mungu, wala kuona hekima Yake. Hakuna wakati ambao Mungu anadhihirisha kazi Yake kwao; ni vipofu, wasioona matendo ya Mungu. Wao ndio walioachwa na Mungu na hawamiliki kabisa utunzaji na ulinzi wa Mungu, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu. Wale walio bila kazi ya Mungu ni watenda maovu na humpinga Mungu.
kutoka kwa "Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Wajibu wa wafanyakazi ni kutenda kazi yao na kuyaongoza makanisa kulingana na mapenzi ya Mungu na kwa mujibu wa mahitaji na mipango ya Mungu. Kazi kama hii hubarikiwa na Mungu. Ikiwa wafanyakazi hawana urazini kama huo, na hukiuka mapenzi ya Mungu kwa kufanya mambo kwa njia yao wenyewe, wakichukua nafasi ya mchungaji na kuwafundisha watu jinsi wanavyopenda, wakitoa dhana zao, mawazo, na mafundisho na kuwafanya wengine kuyakubali, basi wafanyakazi kama hawa wamekuwa wachungaji wa uongo. Kuna mifano mingi ya wafanyakazi kuwa wachungaji wa uongo, na idadi kubwa wameondoshwa na Mungu katika kila hatua ya kazi Yake. Mungu wakati mmoja Alisema kuwa katika kila enzi kuna watu wengi wanaomtumikia Mungu na bado pia humpinga, hata hatimaye huwafanya wengine wawatii na kuwaabudu kama wao ni Mungu. Hili ni dhihirisho la "wachungaji wa uongo." Sote tunapaswa kuchukua hili kama onyo; wafanyakazi wanapaswa kuzingatia mabadiliko katika tabia, na ikiwa watazembea na kutokuwa waangalifu kwa hili, basi ni rahisi mno kwao kuwa wachungaji wa uongo. Kazi ya wachungaji wa uongo ina mkazo maalum juu ya kuwaongoza watu kulingana na maana ya wachungaji wa uongo wenyewe. Yote wanayofanya, kusema, na kutafuta ni ya mpango wao wenyewe, na hulichukulia hili kama ukweli safi mno kuliko ukweli wote, na wao hudhani kuwa wanaweza kuwafundisha watu kuwa wanadamu na kuwaruhusu watu kupata ukweli kulingana na mpango wao wenyewe. Haya ni maonyesho ya kiburi cha juu kabisa na hali ya kujidai ya wachungaji wa uwongo. Kwa wale ambao kweli ni wa busara, wanapoamini kuwa wako sahihi hasa wangetafuta na kuwasiliana ukweli kwa karibu , na kutenga uangalifu wao kwa kusikia maoni na maarifa tofauti ya wengine ili kuthibitisha kama yote waliyoyaelewa ni sahihi. Wale wote ambao wamepitia kupogolewa na kushughulikiwa kwa Mungu wanapaswa kuweza kuweka kando baadhi ya hali zao za kujidai na majisifu. Wanapofanya kazi, wao ni waangalifu katika hatua zao ili kuepuka kukiuka mapenzi ya Mungu na kuchukua njia mbaya. Matokeo yao kuwa wachungaji wa uongo hayawezi kufikiriwa. Kila mfanyakazi ana matendo yake mwenyewe, wote wana nadharia zao wenyewe ambazo wao hutumia kunyunyizia watu; kwa kweli, hakuna yeyote anayeweza kufahamu kabisa ni kiasi gani cha ukweli au thamani njia yao wenyewe inacho. Watu wamekosa hali ya kujitambua, hawana bidii au tafakari ya kina sana katika maarifa yao ya ukweli, na wao huchukua kiholela vitu visivyo na maana na kuvichukulia kama hazina za kutolewa kwa wengine. Si matendo kama hayo yanaashiria mchungaji wa uwongo? Si hili linawadhuru wengine pamoja na wao wenyewe? Bila kujali ni kazi kiasi gani wachungaji wa uwongo hufanya, hawana uwezo kabisa wa kuwaleta watu mbele ya Mungu na kuwaruhusu wamjue na kumtii Mungu. Yote yanayofunguliwa na wachungaji wa uongo ni maneno na mafundisho tu, na mawazo na fikra, na hakuna kitu ambacho huzuia kazi ya Mungu au kumpinga Yeye zaidi.
kutoka kwa "Maana ya 'Wachungaji Kondoo wa Uongo'" katika Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu
Huduma kulingana na mbinu za kidini inamaanisha kufanya kila kitu kulingana na njia za desturi za dini na utaratibu wa huduma, kuzingatia kwa imara sherehe mbalimbali za kidini, na kuwaongoza watu tu kulingana na maarifa ya Biblia. Kwa kuonekana, yaelekea kuwa yenye bidii na nguvu, inaashiria dini, inafaa barabara kwa mawazo ya watu, na hawana vipingamizi. Lakini haina kabisa kazi ya Roho Mtakatifu, kinachohubiriwa si kitu ila mafundisho ya kidini na elimu ya Biblia, imejaa mawazo ya kidini, haina chochote kuhusu upataji wa nuru ya Roho Mtakatifu, na mikutano imetuama na kukosa uhai. Kwa huduma kama hii, miaka inavyoendelea watu waliochaguliwa wa Mungu bado wanabaki bila ukweli, hawana maarifa ya Mungu au utii kwa Mungu, na hawajaingia kwenye njia sahihi ya imani kwa Mungu–kwa kuwa kile watu hufuatilia sio wokovu bali ni neema na baraka, kiasi kwamba hakuna dalili za mabadiliko katika tabia ya maisha yao. Baada ya kuhudumu kwa miaka kadhaa, hawa watu bado wako mikono mitupu, bila ushahidi wa kitu walichopata wenyewe. Haya ndiyo matokeo ya huduma kulingana na mbinu za kidini. Ni dhahiri kuwa, watu kama hawa wanaomtumikia Mungu hawajui kazi ya Mungu, hawaelewi mapenzi ya Mungu, na hawajui maana ya kushirikiana na kazi ya Roho Mtakatifu. Ni jambo dhahiri la vipofu wakiwaongoza vipofu, huwapotosha watu waliochaguliwa wa Mungu , kama Mafarisayo humwamini Mungu na bado humpinga Mungu, hawamjui Mungu, na kimsingi hawawezi kufanikisha wokovu wa Mungu.
kutoka kwa "Wale tu Wanaoingia Kwenye Njia Sahihi ya Imani katika Mungu Ndio Wanaweza Kuchukua njia Sahihi ya Huduma kwa Mungu" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (I)
Wachungaji wa jamii ya kidini hutumia kila fursa ya kutangaza kiwango cha maarifa yao na kutoa sura ya uchaji Mungu. Lengo lao ni kuwafanya watu wawastahi na kuwaabudu, na wao hutumia taswira yao wenyewe kuwavuta watu kwao ili wawatii na kuwafuata, matokeo yakiwa ni wao kuwaongoza watu kuabudu maarifa ya Biblia, kuabudu hadhi na nguvu, na kuabudu ustadi katika kuhubiri. Kwa njia hii, kwa kila hatua huwaongoza watu katika njia ya kumpinga Mungu. Wale wanaoongozwa na wapinga Kristo humwamini Mungu asiye yakini, wao ni wazuri kwa kuzungumzia mafundisho matupu na yasiyo na maana, na wenye ujuzi katika unafiki, na wao wote humwamini Mungu na bado humpinga na kumwasi Mungu. Hakuna shaka kwamba njia ambayo viongozi wa uongo na wapinga Kristo hufanyia kazi–ile ambayo wao hutumia kumtumikia Mungu na bado kumpinga Yeye–ni ya kuwadhuru watu sana.
kutoka kwa "Kulinda Dhidi ya Wapinga Kristo na Njia ya Wapinga Kristo Ni ya Umuhimu Mkuu" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (II)

Jumatano, 27 Machi 2019

Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yanayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake. Hayo ndiyo binadamu wote wanayaamini. Aina hii ya imani kwa Mungu haitaruhusu binadamu kupatwa na kukamilishwa Naye kwa uhakika. Kwa kweli, si kwamba neno la Mungu ni pungufu, badala yake uwezo wa binadamu wa kupokea neno Lake ni duni mno. Inaweza kusemwa karibu binadamu wote hutenda kulingana na nia za Mungu. Badala yake, imani yao kwa Mungu ni kwa mujibu wa nia zao wenyewe, fikra za kidini zilizowekwa, na desturi. Ni wachache wanaopitia mabadiliko baada ya kulikubali neno la Mungu na kuanza kutenda kwa mujibu wa mapenzi Yake. Badala yake, wanaendelea katika imani yao potovu. Wakati mwanadamu anaanza kuamini katika Mungu, anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za kawaida za dini, na anaishi na kuhusiana na wengine kwa misingi ya falsafa yake ya maisha. Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu tisa kati ya kila watu kumi. Ni wachache sana wanaounda mpango mwingine na kuanza mwanzo mpya baada ya kuanza kumwamini Mungu. Hakuna anayeona au kuweka katika vitendo neno la Mungu kama ukweli.
Chukua imani katika Yesu, kwa mfano. Kama mtu alikuwa mwanafunzi katika imani au alikuwa wa imani hiyo kwa muda mrefu, wote walitumia “vipaji” vyovyote walivyokuwa navyo na kuonyesha “ujuzi” wowote waliokuwa nao. Mwanadamu aliongeza tu “imani katika Mungu,” maneno haya matatu, katika maisha yake ya kawaida, bado hayakufanya mabadiliko katika tabia yake, na imani yao kwa Mungu haikukua hata kidogo. Ukimbizaji wa mwanadamu wa swala hili haukuwa baridi wala moto. Hakusema kwamba hakuamini, lakini pia hakujitoa kikamilifu kwa Mungu. Hakuwahi kumpenda Mungu kwa kweli wala kumtii Mungu. Imani yake kwa Mungu ilikuwa halali na ya kujifanya, na aligeuka na akapuuza na wala hakuwa na bidii kwa kutenda imani yake. Aliendelea katika hali kama hiyo ya kuchanganyikiwa tangu mwanzo hadi wakati wake wa kufa. Ni nini maana ya hili? Leo, lazima uwe katika njia sahihi kwani unaamini katika Mungu wa vitendo. Kwa kuwa una imani katika Mungu, hupaswi tu kutafuta baraka, lakini pia kutafuta kumpenda Mungu na kumjua Mungu. Kupitia kwa kupata nuru kutoka Kwake na harakati yako mwenyewe, unaweza kula na kunywa neno Lake, kukuza ufahamu wa kweli kuhusu Mungu, na kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu unaotoka moyoni mwako. Kwa maneno mengine, upendo wako kwa Mungu ni wa kweli zaidi, ambapo hakuna yeyote anayeweza kuharibu au kukuzuia kuonyesha upendo wako Kwake. Basi uko kwa njia ya kweli ya imani kwa Mungu. Inathibitisha kwamba wewe unamilikiwa na Mungu, kwani moyo wako umemilikiwa na Mungu na wala huwezi kumilikiwa na kitu kingine. Kutokana na tajriba yako, malipo uliyolipa, na kazi ya Mungu, wewe una uwezo wa kuendeleza upendo usioamriwa kwa Mungu. Kisha unawekwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa neno la Mungu. Ni wakati tu ambao umekuwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza ndipo unaweza kuchukuliwa kuwa umempata Mungu. Katika imani yako kwa Mungu, lazima utafute lengo hili. Huu ni wajibu wa kila mmoja wenu. Hakuna anayelazimika kutosheka na mambo jinsi yalivyo. Hamuwezi kuwa na fikira aina mbili kwa kazi ya Mungu au uichukulie kwa wepesi. Mnapaswa kumfikiria Mungu katika mambo yako yote na wakati wote, na kufanya mambo yote kwa ajili yake. Na wakati mnasema au kufanya mambo, mnapaswa kutilia maanani maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza. Ni hii tu ndio inayolingana na mapenzi ya Mungu.
Kosa kubwa sana la binadamu kuwa na imani katika Mungu ni kwamba imani yake ni ya maneno tu, na Mungu hayupo popote katika maisha yake ya utendaji. Watu wote, kwa kweli, wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini Mungu si sehemu ya maisha yao ya kila siku. Maombi mengi kwa Mungu hutoka katika kinywa cha mtu, lakini Mungu amepewa nafasi ndogo sana katika moyo wake, na hivyo Mungu humjaribu binadamu tena na tena. Kwa vile mtu ni mchafu, Mungu hana budi ila kumjaribu mtu, ili aweze kuona aibu na kisha aje kujitambua mwenyewe katika majaribu. La sivyo, mwanadamu atageuka mwana wa malaika mkuu, na kuzidi kuwa mpotovu. Wakati wa imani ya mtu katika Mungu, nia nyingi na malengo ya kibinafsi hutupwa mbali anavyotakaswa na Mungu bila kukoma. La sivyo, hakuna mwanadamu anayeweza kutumiwa na Mungu, na Mungu hana njia ya kufanya ndani ya mtu kazi anayopaswa kufanya. Mungu kwanza humtakasa mwanadamu. Katika mchakato huu, mtu anaweza kuja kujijua mwenyewe na Mungu huenda akambadilisha mwanadamu. Ni baada ya haya ndipo Mungu anaweza kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kwa njia hii pekee ndio moyo wa binadamu unaweza kumgeukia Mungu kwa ukamilifu. Kwa hivyo, kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Katika njia hii, wanadamu wengi wanaweza kusema wana maarifa mengi, lakini katika wakati wao wa kufa, macho yao hujawa machozi, nao hujichukia wenyewe kwa kuharibu maisha yao yote na kuishi maisha yasiyo na mazao hadi uzeeni. Wanaelewa tu mafundisho lakini hawawezi kutia ukweli katika vitendo na kushuhudia kwa Mungu, badala yake wakikimbia huku na kule, wakiwa na kazi kama nyuki; mara wanapochungulia kaburi wao hatimaye huona kwamba hawana ushuhuda wa kweli, kwamba hawamjui Mungu kamwe. Je, si huku ni kuchelewa mno? Kwa nini usichukue nafasi hii na kutafuta ukweli unaoupenda? Kwa nini usubiri hadi kesho? Iwapo katika maisha huwezi kuteseka kwa ajili ya ukweli au kutafuta kuupata, inaweza kuwa kwamba unataka kujuta katika saa yako ya kufa? Ikiwa hivyo, basi kwa nini umwamini Mungu? Kwa kweli, kuna mambo mengi ambayo mtu, iwapo ataweka juhudi kidogo tu, anaweza kuweka ukweli katika vitendo na hivyo kumridhisha Mungu. Moyo wa binadamu daima umepagawa na mapepo na kwa hivyo hawezi kutenda mambo kwa ajili ya Mungu. Badala yake, yeye daima yumo katika safari ya huku na kule kwa sababu ya mwili, na hafaidiki na chochote mwishowe. Ni kwa sababu hizi ndio mtu hupata matatizo ya mara kwa mara na mateso. Je, haya sio mateso ya Shetani? Je, huu sio ufisadi wa mwili? Hufai kumdanganya Mungu kwa maneno ya mdomo. Badala yake, lazima uchukue hatua inayoonekana. Usijidanganye; ni nini maana katika hilo? Ni faida gani utakayopata kutokana na kuishi kwa ajili ya mwili wako na kufanya bidii kwa ajili ya umaarufu na mali ya dunia?

Jumamosi, 9 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.”
Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawa Nimejazwa na hukumu na adabu kwa binadamu, kila ninachofanya bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, kwa ajili ya kueneza injili Yangu kwa njia bora zaidi na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili. Kwa hiyo leo, katika wakati ambapo watu wengi tayari wametamauka pakubwa, Naendelea na kazi Yangu, Nikiendeleza kazi ambayo lazima Nifanye ili kuhukumu na kuadibu binadamu. Licha ya ukweli kwamba binadamu amechoshwa na kile Ninachosema na licha ya ukweli kwamba hana tamanio la kujali kuhusu kazi Yangu, Ningali natekeleza wajibu Wangu kwa sababu kusudio la kazi Yangu halijabadilika na mpango Wangu asilia hautabadilika. Kazi ya hukumu Yangu ni kumfanya binadamu anitii Mimi kwa njia bora zaidi, na kazi ya kuadibu Kwangu ni kuruhusu binadamu awe na mabadiliko bora zaidi. Ingawa kile Ninachofanya ni kwa minajili ya usimamizi Wangu, Sijawahi kufanya chochote ambacho hakikufaidi binadamu. Hiyo ndiyo maana Nataka kufanya mataifa yote nje ya Israeli kuwa matiifu tu kama Waisraeli na kuwabadilisha kuwa binadamu halisi, ili Niwe na mahali pa usalama katika nchi zilizo nje ya Israeli. Huu ndio usimamizi Wangu; ndiyo kazi Ninayotimiza katika nchi za Mataifa. Hata sasa, watu wengi bado hawauelewi usimamizi Wangu kwa sababu hawajautilia maanani, badala yake wanafikiria tu kuhusu mustakabali na hatima zao. Haijalishi ni nini Ninachosema, watu hawajali kazi Yangu, badala yake wanalenga tu hatima zao za baadaye. Mambo yakiendelea kwa namna hii, kazi Yangu itapanuliwa vipi? Injili Yangu itaenezwa vipi kotekote ulimwenguni? Lazima mjue kwamba wakati kazi Yangu inapanuka, Nitawatawanya, Nitawaadhibu kama vile tu Yehova alivyoyaadhibu makabila ya Israeli. Haya yote yatafanywa ili injili Yangu iweze kuenea kotekote kwenye ulimwengu mzima, ili kazi Yangu iweze kuenezwa kwa Mataifa, ili kwamba jina Langu litukuzwe na watu wazima na watoto kwa pamoja na jina Langu takatifu litatukuzwa katika vinywa vya watu kutoka makabila na mataifa yote. Katika enzi hii ya mwisho, Nitafanya jina Langu litukuzwe miongoni mwa Mataifa, kufanya matendo Yangu kuonekana na mataifa mengine ili waniite Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kuyafanya maneno Yangu kutimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.
Kazi ambayo Nimekuwa nikisimamia kwa maelfu ya miaka inafichuliwa kabisa tu kwa binadamu katika siku za mwisho. Ni sasa tu ndipo Nimelifumbua fumbo kamili la usimamizi Wangu kwa mwanadamu. Binadamu anajua kusudio la kazi Yangu na zaidi ya yote anapata uelewa wa mafumbo Yangu yote. Na Nimemwambia binadamu kila kitu kuhusu hatima ambayo amekuwa akijali kuhusu. Tayari Nimemfichulia binadamu mafumbo yote yaliyofichwa kwa zaidi ya miaka 5,900. Yehova ni nani? Masiha ni nani? Yesu ni nani? Mnafaa kuyajua haya yote. Mabadiliko makubwa ya kazi Yangu yamo katika majina haya. Je, mmeelewa haya? Jina Langu takatifu linafaa kutangazwa vipi? Jina Langu linafaa kuenezwaje katika taifa lolote ambalo limeniita kwa jina Langu lolote? Kazi Yangu tayari imeanza kupanuka, na Nitaeneza ukamilifu wake katika mataifa yote. Kwa sababu kazi Yangu imetekelezwa ndani yenu, Nitawapiga kama vile Yehova alivyowapiga wale wachungaji wa nyumba ya Daudi kule Israeli, na kuwasababisha kutawanyika miongoni mwa mataifa yote. Kwani katika siku za mwisho, Nitapondaponda mataifa yote kuwa vipande vidogo vidogo na kusababisha watu wao kuenezwa upya. Nitakaporudi tena, mataifa yatakuwa tayari yamegawanywa kwa mipaka iliyowekwa na mwako wa moto Wangu utakaokuwa ukichoma. Katika wakati huo, Nitajionyesha upya kwa binadamu kama jua linalochoma, Nikijionyesha kwao hadharani kwa taswira ya yule Aliye Mtakatifu ambaye hawajawahi kumwona, Nikitembea miongoni mwa mataifa yote, kama vile tu Mimi, Yehova, Nilivyotembea miongoni mwa makabila ya Wayahudi. Kuanzia hapo kuendelea, Nitawaongoza watu huku wakiishi ulimwenguni. Hakika watauona utukufu Wangu hapo na hakika wataona pia nguzo ya wingu hewani ili uwaongoze, kwani Nitaonekana katika sehemu takatifu. Binadamu ataiona siku Yangu ya haki na pia maonyesho Yangu ya utukufu. Hilo litafanyika Nitakapoutawala ulimwengu mzima na kuwaleta wana wengi katika utukufu. Kila pahali duniani, watu watainama, nalo hema Langu takatifu litaundwa miongoni mwao juu ya mwamba wa kazi ambayo Natekeleza sasa. Watu watanihudumia pia hekaluni. Madhabahu, yaliyojaa mambo machafu na ya kuchukiza, Nitayavunjavunja vipandevipande na Nitajenga upya mengine. Madhabahu matakatifu yatarundikwa wanakondoo na ndama waliozaliwa karibuni. Nitaangusha hekalu lililopo leo na kujenga jingine upya. Hekalu lililopo sasa na lililojaa watu wenye chuki litaporomoka na lile Nitakalojenga litajaa watumishi watiifu Kwangu. Kwa mara nyingine watasimama na kunihudumia Mimi kwa utukufu wa hekalu Langu. Kwa hakika mtaiona siku ambayo Nitapokea utukufu mkuu na hakika mtaiona siku ambayo Nitaliangusha hekalu na kujenga lingine upya. Pia, hakika mtaona siku ya kuletwa kwa hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu. Huku Nikilibomoa hekalu, ndivyo Nitakavyoleta hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu; itakuwa kama vile tu ambavyo watu wanavyoniona Nikishuka. Baada ya kuangamiza mataifa yote, Nitayakusanya pamoja upya, Nikilijenga hekalu Langu na kuandaa madhabahu Yangu, ili wote waweze kutoa kafara zao Kwangu, kunihudumia Mimi hapo, na kujitolea kwa uaminifu katika kazi Yangu kwenye mataifa mengineyo. Itafanywa namna tu ambavyo wana wa Israeli wanavyofanya sasa, na joho la kuhani na taji la mfalme, utukufu Wangu, Yehova, ukiwa miongoni mwao na uadhama Wangu ukivinjari juu yao na ukiwa nao. Kazi Yangu katika Mataifa itatekelezwa pia katika njia hiyo. Kama vile kazi Yangu kule Israeli ilivyokuwa, ndivyo kazi Yangu katika Mataifa itakavyokuwa kwa sababu Nitaongeza kazi Yangu kule Israeli na kuieneza katika mataifa yale mengine.
Sasa ndio wakati ambao Roho Wangu anafanya kazi pakubwa, na wakati Ninapofanya kazi miongoni mwa Mataifa. Hata zaidi, ndio wakati ambapo Naainisha viumbe wote na kuweka kila kiumbe katika kundi lenye uhusiano, ili kazi Yangu iweze kuendelea haraka zaidi na kwa njia ya kufaa zaidi. Kwa hiyo, bado Nahitaji kwamba mjitoe mzimamzima kwa minajili ya kazi Yangu yote; aidha, mnafaa kutambua waziwazi na kuwa na hakika ya kazi ile yote ambayo Nimefanya ndani yako, na kuweka nguvu zako zote katika kazi Yangu ili iweze kuwa ya matokeo bora zaidi. Hilo ndilo ambalo lazima uelewe. Msipigane tena wenyewe kwa wenyewe, kutafuta mbinu za usuluhishi, au kutafuta raha za mwili, mambo ambayo yanaweza kuchelewesha kazi Yangu na kuharibu mustakabali wako mzuri. Kufanya hivyo, mbali na kuweza kukupa ulinzi, litakuletea maangamizo. Je, sii huu utakuwa ujinga kwa upande wako? Kile ambacho unafurahia leo kwa tamaa ndicho kile kile ambacho kinaharibu mustakabali wako, huku yale maumivu unayopitia leo ndiyo yaleyale ambayo yanakulinda. Lazima ufahamu waziwazi kuhusu jambo hilo, ili uepuke majaribio ambayo yatakuwa magumu kujinasua kutoka na kuepuka kuingia kwenye ukungu mzito unaozuia jua katika maisha yako. Wakati ukungu huu mzito utakapotoweka, utajipata katika hukumu ya siku kuu. Kufikia wakati huo, siku Yangu itakuwa imekaribia binadamu. Utatorokaje hukumu Yangu? Utawezaje kuvumilia joto kali la jua? Ninapompa binadamu wingi Wangu, haufurahii kwa dhati, lakini badala yake anautupa nje kwenye sehemu zisizotambulika. Wakati siku Yangu itawadia, binadamu hataweza tena kugundua wingi Wangu au kupata ukweli mkali Niliompa zamani sana. Ataomboleza na kulia, kwa sababu amepoteza mwangaza anaofuata na kuingia katika giza totoro. Kile mnachoona leo ni upanga tu mkali wa kinywa Changu. Bado hamjakiona kiboko kilicho katika mkono Wangu au moto Ninaotumia kumchoma binadamu, na ndiyo maana bado mna kiburi na msio na kadiri mbele Yangu. Ndiyo maana bado mnapigana na Mimi katika nyumba Yangu, huku mkipinga kwa ulimi wa mwanadamu kile ambacho Nimenena na kinywa Changu. Binadamu haniogopi Mimi. Akiwa bado katika uhasama na Mimi hadi leo, bado haniogopi kamwe. Mnao ulimi na meno ya wale wasio na haki vinywani mwenu. Maneno na matendo yenu ni kama yale ya yule nyoka aliyemshawishi Hawa na kumfanya kutenda dhambi. Mnadai nyinyi kwa nyinyi kulipiza kisasi, na mnashindana mbele Yangu kwa ajili ya nafasi, umaarufu, na faida kwa ajili yenu wenyewe, ilhali hamjui kwamba Natazama maneno na matendo yenu kwa siri. Kabla hata ya nyinyi kuja mbele Yangu, Nimejua vina vya nyoyo zenu kabisa. Siku zote binadamu hutamani kutoroka kutoka mfumbato Wangu na kuepuka uangalizi wa macho Yangu, lakini Sijawahi kuepuka maneno au matamshi yake. Badala yake, kwa kusudio kuu huwa Nayaruhusu maneno na matendo hayo yaingie katika macho Yangu, ili Niweze kuadibu udhalimu wake na kuhukumu uasi wake. Kwa hiyo, maneno na matendo fiche ya binadamu siku zote yanawekwa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na hukumu Yangu haijawahi kumtoka binadamu, kwa sababu uasi wake ni mwingi mno. Kazi Yangu ni kuteketeza na kusafisha maneno na matendo yote ya binadamu yaliyotamkwa na kufanywa mbele ya Roho Wangu. Kwa njia hiyo, baada ya Mimi kuondoka ulimwenguni, binadamu wataweza bado kuendeleza utiifu Kwangu, na bado watanihudumia kama vile watumishi Wangu watakatifu wanavyofanya katika kazi Yangu, wakiruhusu kazi Yangu hapa ulimwenguni iendelee mpaka siku itakapokamilika.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 4 Februari 2019

Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli. Lakini hivyo ungeweza vipi kufikia kiwango hiki cha kawaida baada ya kusikia ushirika? Mbona ulikuwa na furaha sana baada ya kuusikia ukweli? Wengine wanasema ni kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu. Mbona basi kazi ya Roho Mtakatifu inakoma baada ya takriban siku kumi? Wengine husema ni kwa sababu wanakuwa wazembe na kuacha kusonga mbele na juu. Mbona basi hili linafanyika hata wakati watu wanapojaribu kufanya maendeleo? Mbona Roho Mtakatifu pia hafanyi kazi? Je, hukuwa unajaribu kusonga mbele na juu? Basi mbona Roho Mtakatifu hayuko kazini? Sababu ambazo watu hutoa haziko sambamba na hali ya kweli. Hapa, lazima tuibue hoja ifuatayo: Kama Roho Mtakatifu yuko kazini au la, ushirikiano wa watu binafsi hauwezi kupuuzwa. Watu walio wazi kuhusu ukweli na wanapenda ukweli kila wakati watakuwa na uwezo wa kubaki katika hali ya kawaida, bila kujali kama Roho Mtakatifu yuko kazini ama hapana. Kwa wale wasiopenda ukweli—hata kama ukweli hasa ni wazi kwao na hata kama Roho Mtakatifu anafanya kazi sana—kuna upeo kwa ukweli ambao wanaweza kuweka katika vitendo na kiwango cha muda ambao wanaweza kutenda. Mbali na wakati huo, hawafanyi chochote zaidi ya kudhihirisha asili yao wenyewe na maslahi yao wenyewe. Ipasavyo, kama hali ya mtu itafikia kiwango cha kawaida ama hapana na kama atauweka ukweli katika matendo ama hapana haitegemei tu kama Roho Mtakatifu yuko kazini au hapana, wala haiamuliwi tu na kama yuko wazi kuhusu ukweli ama hapana, ila hutegemea kama yuko tayari kuuweka ukweli katika matendo ama hapana na kama anapenda ukweli ama hapana.
Kwa kawaida, mtu husikia ukweli na, kwa muda, kila kitu huhisi kuwa kawaida kabisa kwake; katika muda huo wa kawaida, ukweli unaziinua hali zako kuwa kawaida. Unakufanya kujua asili yako potovu; moyo wako una furaha na unakuwa huru na hali yako inabadilika kuwa bora. Lakini baada ya muda, jambo laweza kukuchanganya; ukweli ulio ndani yako unakuwa usioonekana na bila kujua unaufanya ukweli huo kama jambo lisilo muhimu sana kwako; hujaribu kumtafuta Mungu katika matendo yako, unatenda kila kitu kwa mapenzi yako mwenyewe na huna nia ya kutenda ukweli kabisa. Wakati unapopita, unapoteza ukweli uliokuwa nao. Daima unadhihirisha asili yako mwenyewe, ukikosa kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya kufanya kazi ndani mwako; hutafuti nia ya Mungu kamwe; hata unapomkaribia Mungu, unapitia tu katika mizunguko. Punde tu unapogundua ukweli wa ugonjwa wako, moyo wako uko mbali sana na Mungu; umemkataa Mungu kwa vitu vingi na kutamka kufuru nyingi. Bado kuna ukombozi kwa wale ambao hawajaenda mbali sana katika njia hii, lakini kwa wale ambao wameenda mbali sana hata kumkufuru Mungu na kujiweka wenyewe dhidi ya Mungu, wakipigania cheo, na chakula na mavazi, hakuna ukombozi. Kusudi la ushurika wazi kuhusu ukweli ni ili kuwafanya watu kutenda ukweli na kubadilisha tabia yao, sio tu kuwafanya wafurahi. Kama unaelewa ukweli lakini hauuweki katika matendo, basi ushirika kuhusu ukweli na ufahamu wa ukweli hautakuwa na maana yoyote. Iwapo unaelewa ukweli lakini hauuweki katika matendo, utapoteza nafasi yako ya kupata ukweli na kupoteza nafasizyote za kuokolewa. Ukiuweka ukweli unaoelewa katika matendo, utapata ukweli wa ndani zaidi; utapata wokovu wa Mungu; utapata kupata nuru, mwangaza na uongozi wa Roho Mtakatifu. Wengi hulalamika tu kuwa Roho Mtakatifu kamwe hawapi nuru, lakini hawagundui kuwa kimsingi hawauweki ukweli katika matendo. Kwa hivyo, hali zao hazitawahi kupata ukawaida na hawatawahi kuyaelewa mapenzi ya Mungu.
2. Unahitaji Tu Kutenda Ukweli na Njia Itafunguka Mbele Yako
Wengine husema kuwa shida zao hazitatatuliwa kwa kutenda ukweli. Wengine huamini kuwa ukweli hauwezi kutatua kikamilifu tabiapotovu za watu. Ukweli ni kwamba shida zote za watu zaweza kutatuliwa; cha muhimu ni kama watu wanaweza kutenda kulingana na ukweli au hapana. Shida zenu za sasa sio saratani ama magonjwa yasiotibika; kama mnaweza kuweka ukweli katika matendo, shida hizi zote zaweza kubadilishwa, ikitegemea kama unaweza kutenda kulingana na ukweli ama hapana. Kama unatembea katika njia sawa, utafanikiwa; kama unatembea katika njia mbaya, utakuwa umemalizika. Kwa mfano, watu wengine hufanya kazi zao bila kufikiria kuhusu jinsi ya kufanya vitu kwa njia ya faida kwa kazi ama kama jinsi wanavyofanya vitu inapatana na mapenzi ya Mungu; kama tokeo, wanafanya mabo mengi ambayo Mungu anachukia. Kama wangetenda kulingana na ukweli katika kila jambo, je hawangekuwa watu ambao wanaupendeza moyo wa Mungu? Watu wengine wanajua ukweli lakini hawauweki katika matendo, wakiamini kuwa ukweli ni hili tu na sio kitu kingine zaidi. Wanaamini kuwa hauwezi kutatua mapenzi yao wenyewe na upotovu wao. Je, mtu wa aina hii sio mmwenye mzaha? Je, yeye sio mpumbavu? Je hajioni mwenyewe kuwa werevu? Watu wakitenda kulingana na ukweli, tabia yao potovu itabadilishwa; watu wakimwamini na kumtumikia Mungu kulingana na tabia zao asili, hakuna kati yao atakayebadilishiwa tabia yake. Watu wengine wanajipata katika shughuli zao wenyewe siku nzima na wanakosa kuchunguza ama kutenda ukweli unaopatikana tayari. Utendaji huu ni wa kipumbavu sana; watu wa aina hii ni watesekaji kiasili, kuwa na baraka lakini hawaifurahii! Njia ipo, kinachofaa kufanywa tu ni wewe kuiweka katika matendo. Kama umeamua kuuweka ukweli katika matendo, unyonge wako na dosari mbaya zinaweza kubadilishwa, lakini lazima kila wakati uchukue tahadhari na kuwa makini na kupitia ugumu zaidi. Kumwamini Mungu kunahitaji moyo wenye busara—unaweza kumwamini Mungu vizuri ukichukua namna hii ya kawaida?
Watu wengine wanajihami tu na ukweli fulani kwa wakati wa dharura ama kujitelekeza wenyewe na kuwasaidia wengine, sio kutatua shida zao wenyewe; tunawaita “watu wasio na ubinafsi.” Wanawaona wengine kama vikaragosi wa ukweli na wenyewe kama mabwana wa ukweli, wakiwafunza wengine kuushikilia ukweli na wasiwe wasiojihususha, ilhali wao wenyewe ni watazamaji kando kando mwa uwanja—hao ni watu wa aina gani? Wakiwa wamejihami na baadhi ya maneno ya ukweli ili kuwahubiria wengine tu, wakikosa kufanya chochote kujizuia kutokana na kuangamia kwao wenyewe—inasikitishaje! Kama maneno yao yanaweza kuwasaidia wengine, mbona wasijisaidie wenyewe? Tunafaa kuwaita wanafiki wasio na ukweli. Wanatoa maneno ya ukweli kwa wengine na kuwaambia wengine wayaweke katika matendo, lakini hawafanyi juhudi yoyote kuyatenda wenyewe—je sio wa kudharauliwa? Kwa hakika hawawezi kulifanya wenyewe, ilhali wanawalazimisha wengine kuweka maneno ya ukweli katika matendo—hii ni njia ya ukatili iliyoje! Hawatumii ukweli kuwasaidia wengine; hawawatolei wengine kwa moyo wa upendo wa mama; wanawadanyanya tu watu na kuwapotosha watu. Hili likiendelea—na kila mtu akipitisha maneno ya ukweli kwa anayefuata—je kila mmoja mwishowe hatakuwa na uelewa tu wa maandishi ya ukweli wakikosa uwezo wa kuyatenda? Watu wa aina hii wanawezaje kubadilishwa? Hawazitambui shida zao wenyewe kabisa; kutaweza vipi kuwa na njia kwa ajili yao?
Kila tatizo lina njia ya kutatuliwa; kwa kila tatizo kila wakati kutakuwa na ukweli ufaao kushauri ili kukupa njia ya kuendelea mbele na kukuwezesha kubadilika. Hata kama mabadiliko hayatafanyika mara moja, sasa unaweza kuitambua hali yako. Kama kweli hizi hazingeweza kutatua matatizo ya watu, basi Mungu hatakuwa Amenena bure? Kwa hivyo, kama uko tayari kuuweka ukweli katika matendo, kila wakati utakua na njia ya kufuata.

Ijumaa, 25 Januari 2019

Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu

Sura ya 28. Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kutoa kwenu "muhtasari kuhusu ukweli" hakufanywi ili kuwawezesha watu kupata maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunafanywa ili watu waweze kuwa weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka kwa ukweli. Wao huonekana kana kwamba wanaelewa lengo lililokusudiwa katika kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno ya mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli, na si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia. Wewe unakusanya vitabu hivi au vifaa hivyo, na hivyo unapata umiliki wa kipengele hiki cha mafundisho au kipengele kile cha ujuzi. Wewe ni msemaji wa kiwango cha juu wa mafundisho—lakini huwaje unapomaliza kusema? Watu basi hawana uwezo wa kupitia, hawana ufahamu wa kazi ya Mungu na hawana ufahamu wao wenyewe pia. Mwishowe, vitu vyote watakavyokuwa wamepata ni fomyula na sheria, na wanaweza kuzungumza juu ya mambo hayo lakini hakuna kitu kingine, hivyo kama Mungu akifanya jambo jipya, je, mafundisho yote unayoyajua yanaweza kufanana na kile Mungu anachofanya? Kwa hiyo, mambo hayo yako ni sheria tu na wewe unawafanya watu wajifunze theolojia tu: Wewe huwaruhusu kupitia neno la Mungu au kupitia ukweli. Vitabu hivi ambavyo watu hukusanya vinaweza kuwaletea teolojia na ujuzi tu, katika fomyula mpya na katika sheria na mila. Haviwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, au kuwaruhusu watu kuuelewa ukweli au kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Kwa kuuliza swali baada ya swali kuhusu maneno hayo, kisha kujibu, kufanya muhtasari, unadhani kuwa wale walio chini wanaweza kuelewa kwa urahisi. Mbali na kuwa rahisi kukumbuka, wao wana uhakika juu ya maswali haya kwa tazamo la haraka, na unafikiri ni vizuri kufanya mambo kwa njia hii. Lakini kile wanachokielewa siyo maana iliyokusudiwa ya ukweli; inatofautiana na ukweli na ni maneno ya mafundisho tu. Hivyo ingekuwa bora zaidi kama wewe hungefanya mambo haya hata kidogo. Unafanya mambo haya kuwaongoza watu kuelewa ujuzi na weledi wa elimu. Wewe huwaleta wengine katika mafundisho, katika dini, na kuwafanya wamfuate Mungu na kumwamini Mungu ndani ya mafundisho ya dini. Je, si wewe ni sawa tu na Paulo? Ninyi hufikiri kwamba kupata weledi wa ujuzi wa ukweli ni muhimu hasa, na pia kujifunza kwa moyo mafungu mengi ya maneno ya Mungu. Lakini jinsi watu wanavyoelewa neno la Mungu si muhimu hata kidogo. Ninyi hudhani ni muhimu sana kwa watu kuweza kukariri mengi ya maneno ya Mungu, kuweza kuzungumza mafundisho mengi na kugundua fomyula nyingi ndani ya maneno ya Mungu. Kwa hiyo, siku zote ninyi hutaka kuweka katika mfumo vitu hivi ili kila mtu awe akiimba wimbo mmoja na kusema mambo hayo hayo, ili kila mtu aongee mafundisho sawa na wengine, awe na maarifa sawa na huweka sheria sawa—hili ndilo lengo lenu. Ninyi hufanya hivi kana kwamba kuwafanya watu waelewe vizuri zaidi, wakati kwa kinyume chake hamjui kwamba kwa kufanya hivi mnawaingiza watu katikati ya sheria ambazo ziko nje ya ukweli wa maneno ya Mungu. Ili kuwafanya watu wawe na ufahamu halisi wa ukweli, ni lazima ujiunge na uhalisi, jiunge na kazi, na uwalete watu mbele ya Mungu. Ni kwa njia hii tu ambapo watu wanaweza kuwa na weledi wa ukweli. Ikiwa jitihada zako zinaelekezwa tu kwa kutumia fomyula na sheria kwa maneno yaliyoandikwa, basi hutaweza kufikia ufahamu wa kweli, hutaweza kuwaongoza wengine kwa uhalisi, na seuze kuweza kuwaruhusu wengine kupitia mabadiliko zaidi au kujielewa wenyewe zaidi. Kama neno lililoandikwa lingekuwa badala ya watu, basi hamngehitaji kufanya chochote kamwe.
Nyinyi bado hamjagundua sheria za maneno ya Mungu, na watu wengi husema hivi: "Hakuna mantiki kwa maneno ya Mungu. Kila makala ina ya maudhui ya aina zote na kuna maana tofauti katika kila kifungu na kila sentensi hali inayofanya kuwa vigumu kwetu kukumbuka na vigumu kuelewa. Hata siyo rahisi kufupisha wazo la jumla la ibara." Neno la Mungu siyo riwaya, wala si nadhari au kazi ya fasihi. Ni ukweli; ni neno ambalo humpa mtu uzima. Neno silo jambo ambalo linaweza kueleweka kwa kufikiriwa kwa akili zenu, wala sheria zake haziwezi kufupishwa kwa juhudi kidogo. Kwa hiyo bila kujali ni kipengele kipi watu wana ufahamu mdogo wacho au wana ufahamu wa sheria zake, inaweza tu kuwa ufahamu wa upande mmoja, wa juu juu tu, kama tone moja tu katika bahari, na kimsingi hauwezi kufikia kile alichokusudia Mungu awali. Makala yoyote ya maneno ya Mungu itakuwa na vipengele kadhaa vya ukweli. Kwa mfano, makala kuhusu fumbo la Mungu kupata mwili itajumuisha umuhimu wa kupata mwili pamoja na kazi inayofanywa na upataji wa mwili. Na pia itakuwa na jinsi watu wanavyopaswa kuamini katika Mungu, na labda inaweza pia kuwa na jinsi watu wanavyopaswa kumwelewa na kumpenda Mungu; itajumuisha mambo mengi ya ukweli. Kama, kwa mujibu wa mawazo yako, umuhimu wa kupata mwili ulikuwa na vipengele vichache tu na unaweza kujumlishwa katika sentensi chache, ni matokeo yapi ambayo kazi ya Mungu kwa mtu yangeweza kufanikisha? Watu hufanywa kuelewa umuhimu wa kupata mwili ili kuwafanya wamwelewe Mungu. Baada ya mtu kumwelewa Mungu, kwa kawaida anakuwa na moyo ambao humcha Mungu, na hili sasa linahusisha matendo ya mtu. Hivyo hakuna kipengele cha maneno ya Mungu na hakuna kipengele cha ukweli kilicho rahisi kama unavyofikiria. Ikiwa wewe hutazama neno la Mungu na lugha ya Mungu kuwa rahisi, ukifikiri kwamba swali lolote linaweza kujibiwa kwa ibara ya maneno ya Mungu, basi huo si ukweli. Kila makala ina mitazamo mingi ambayo maneno ya Mungu huzungumzwa kwayo na hakuna njia ya watu kufupisha au ya kutoa muhtasari wa maneno Yake. Baada ya kufupisha maneno Yake, unafikiri fungu hili limejibu swali lililo hapo juu, lakini fungu hili pia linahusiana na maswali mengine. Kwa hiyo unasema nini kwa hilo? Ukweli una mambo mengi. Kwa nini husemwa kuwa ukweli ni uzima, kwamba unaweza kuleta starehe kwa mtu, kwamba hauwezi kupitiwa kwa ukamilifu wake kwa aushi kadhaa au miaka mia kadhaa? Kwa mfano ulikuwa uvitolee muhtasari baadhi ya vipengele vya ukweli au kifungu fulani cha maneno ya Mungu, halafu uulize swali kulihusu hilo. Kisha, kuzingatia swali hili, ulikuwa usome kifungu hiki, kisha ingekuwa dhahiri kuwa hiki kifungu kimesomwa kwa kulijibu swali hilo. Kwa hiyo kifungu hiki kimekuwa fomyula, kanuni na mafundisho, na si ukweli. Ingawa hakuna hata moja ya maneno ya awali limebadilika, hiki kwa dhahiri sana ni kipande cha mafundisho, na sio ukweli. Kwa nini? Kwa sababu swali ulilouliza uliliuliza vibaya. Liliwaongoza watu kupotea na kuwaingiza katika mafundisho, likawafanya kufikiri, kuwaza, kufikiria swali hili, na walisoma kifungu hiki kwa mujibu wa mafundisho yako, kukisoma wakitumia mtazamo wako wa mafundisho. Kisha wangekisoma tena na kurudia, wakiona swali moja pekee na bila kuona kitu kingine chochote. Mwishowe wao wangeletwa mahali ambapo hawawezi kupata ukweli na hawawezi kupitia neno la Mungu, mahali ambapo wanaweza kujiandaa tu na kujadili mafundisho na ni mahali ambapo hawawezi kumwelewa Mungu. Yote ambayo wangeweza kuzungumza yangekuwa mafundisho yenye kupendeza, mafundisho sahihi, lakini hakungekuwa na uhalisi ndani yao na hawangekuwa na njia ya kutembelea. Aina hii ya kuongoza kweli hufanya madhara makubwa!
Ni nini mwiko mkubwa katika huduma ya mtu kwa Mungu? Unajua? Wale miongoni mwenu ambao huhudumu kama viongozi daima hutaka kuwa na ubunifu mkubwa, kuwa wazuri kuliko wengine, kupata hila mpya ili Mungu aweze kuona jinsi kweli mlivyo na uwezo. Hata hivyo, nyinyi hamzingatii kufahamu ukweli na kuingia katika uhalisi wa neno la Mungu. Nyinyi daima hutaka kuringa; si huu ni ufunuo kwa usahihi wa asili ya kiburi? Wengine hata husema: "Kwa kufanya hivi nina uhakika kwamba Mungu atafurahi sana; Yeye kweli atapenda sana. Wakati huu nitaacha Mungu aone, kumpa Yeye mshangao mzuri." Kwa sababu yashangao huu unaondolewa! Usifanye tu chochote kijacho akilini mwako bila kufikiri. Je, inawezaje kuwa sawa kutozingatia matokeo hayo? Wakati wale kati yenu ambao huudhi tabia ya Mungu na kuziudhi amri Zake za utawala wataondolewa wakati huo, hakutakuwa na maneno mnayoweza kusema. Bila kujali dhamira yako, bila kujali kama wewe hufanya hivyo kwa makusudi au la, kama wewe huelewi tabia ya Mungu au huyaelewi mapenzi ya Mungu, kwa urahisi utamkosea Mungu na kwa urahisi utaziudhi amri Zake za utawala, hiki ni kitu ambacho kila mtu ni lazima ajichunge dhidi yake. Mara unapoziudhi amri za utawala za Mungu au kuiudhi tabia ya Mungu, Mungu hataangalia kama ulifanya hivyo makusudi au bila kukusudia; hiki ni kitu ambacho ni lazima uone kwa dhahiri. Ikiwa huwezi kuona ukweli halisi wa suala hili, basi unahakikishiwa kuwa na tatizo. Katika kumhudumia Mungu, watu wanataka kupiga hatua kubwa, kufanya mambo makubwa, kusema maneno makubwa, kufanya kazi kubwa, kuchapisha vitabu vikubwa, kufanya mikutano mikubwa na kuwa viongozi wakuu. Kama siku zote una matarajio makuu, basi utaziudhi amri kuu za utawala za Mungu; watu kama hawa watakufa haraka. Kama wewe si mwenye tabia njema, mwenye kumcha Mungu au mwenye busara katika kumhudumia Mungu, ipo siku utaziudhi amri za utawala za Mungu. Kama ukikosea tabia ya Mungu, kuziudhi amri Zake za kiutawala, na hivyo kutenda dhambi dhidi ya Mungu, basi Yeye hataangalia kuona ni kwa sababu gani ulitenda hivi, wala kuona nia zako. Kwa hivyo unafikiri Mungu hana busara? Je, Yeye amekosa huruma kwa mwanadamu? Hapana. Kwa nini Mimi Ninasema hapana? Kwa sababu watu si kiziwi, mjinga au kipofu. Nyote mnaweza kuona na kusikia, na bado mnasababisha kosa. Ni sababu gani unaweza kuizungumzia bado? Hata kama wewe huhifadhi nia zozote, mara unapokosea Mungu, lazima utaangamia na kupata adhabu. Kuna haja ya hali yoyote yako izingatiwe? Hakuna mtu yeyote anayelazimishwa kwa kisu kuzikosea amri za utawala za Mungu au tabia ya Mungu. Hili halifanyiki kamwe. Mtu alikuwekea kisu kooni na kukulazimisha, akisema: "Mlaani Mungu wenu. Baada ya kumlaani Yeye nitakupa pesa na sitakuua." Labda katika hali aina hii ungesema maneno ya kukufuru kwa sababu tu unaogopa kufa. Je, hali ya aina hii inaweza kutokea? Mambo huwa hayafiki kiwango hiki, ama hufika? Kwamba tabia ya Mungu haitaruhusu kosa ina maana yake iliyodokezwa. Hata hivyo adhabu za Mungu zinategemeza hali za watu na asili zao. Hali moja ni pale ambapo mtu hajui kuwa Yeye ni Mungu naye humkosea Yeye. Kujua kwamba Yeye ni Mungu na bado kumkosea Yeye kwa makusudi ni hali nyingine. Ikiwa mtu anafahamu kikamilifu kwamba Yeye ni Mungu na bado humkosea, basi mtu huyo ni lazima aadhibiwe. Mungu huonyesha kiasi cha tabia Yake katika kila hatua ya kazi Yake—watu wanafahamu chochote kwa hili? Katika siku za mwisho, Mungu amefanya kazi kwa miaka mingi, je, watu hawajui tabia Yake na ni vitu vipi ambavyo watu hufanya au kusema ambavyo vinaweza kumchukiza Mungu kwa urahisi? Na vitu ambavyo vimefafanuliwa na amri za utawala za Mungu—kile watu wanapaswa kufanya na kile hawapaswi kufanya—Je, watu hawajui hayo pia? Watu hawawezi kuelewa mambo fulani ambayo yanahusiana na ukweli au na kanuni. Hiyo ni kwa sababu hawajapitia kufikia kiwango hicho, na hivyo hawana njia ya kuelewa. Lakini amri za utawala za Mungu ziko ndani ya mawanda yaliyofafanuliwa na yanastahili kuwa ya sheria. Sio lazima kwa watu kuzielewa kwa njia yoyote, ni kwamba tu wafuate maana yazo halisi. Je, si hili ni jambo ambalo mtu sharti apambane nalo? Wewe huzingatii zaidi kitu chochote na humwogopi Mungu, kwa hiyo ni lazima upate adhabu!
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Jumamosi, 1 Desemba 2018

Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, sauti ya Mungu

Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli

Hapo awali sana, umuhimu wa kuwa na maisha sahihi ya kanisa ulitajwa katika mahubiri. Kwa hivyo ni kwa nini maisha ya kanisa hayajaboreka bado, na bado ni kile kitu kimoja tu cha zamani? Mbona hakuna njia mpya na tofauti kabisa ya maisha? Je, inaweza kuwa sahihi kwa mtu wa miaka ya tisini kuishi kama mfalme wa enzi iliyopita? Ingawa chakula na vinywaji vinaweza kuwa vyakula vitamu vilivyoonjwa mara chache katika enzi zilizopita, hapajakuwa na mabadiliko makubwa katika hali kanisani. Imekuwa kama kuweka divai ya kale katika kiriba kipya. Je, kuna haja gani basi ya Mungu kusema sana? Makanisa katika maeneo mengi hayajabadilika kabisa. Mimi nimeliona kwa macho Yangu na ni wazi katika moyo Wangu; Hata kama sijapata uzoefu wa maisha ya kanisa Mimi Mwenyewe, Nazijua hali za mikusanyiko ya kanisa kama mgongo wa mkono Wangu. Hawajafanya maendeleo mengi. Inarejelea msemo—ni kama kutia divai ya kale katika kiriba kipya. Hakuna kilichobadilika, siyo hata kidogo! Wakati mtu anapowachunga wao huwaka kama moto, lakini wakati hakuna mtu hapo kuwafadhili, wao ni kama pande kubwa la barafu. Si wengi wanaoweza kuzungumza juu ya mambo ya vitendo, na ni mara chache mtu yeyote anaweza kushika usukani. Ingawa mahubiri ni ya juu, imekuwa nadra kwa mtu yeyote kupata kuingia. Watu wachache hutunza neno la Mungu. Wao hujawa na machozi wanapolikubali neno la Mungu na kuwa wachangamfu wanapoliweka kando; Wao husononeka na kuwa wenye huzuni wanapoliondokea. Kwa kusema kweli, nyinyi hamlitunzi neno la Mungu, na hamyaoni kamwe maneno kutoka kinywa Chake mwenyewe kama hazina. Nyinyi huwa na wasiwasi tu mnapolisoma neno Lake, na kuhisi ni lenye kuhitaji nguvu nyingi sana mnapolikariri, na inapofika kuliweka neno Lake katika matendo, ni kama kukabiliana na kazi isiyoweza kukamilika—hamjamotishwa, Nyinyi daima huwa mnachangamka mnaposoma neno la Mungu, lakini mnasahau mnapolitenda. Kwa hakika, maneno haya si lazima yazungumzwe kwa jitihada sana na kurudiwa kwa uvumilivu sana; watu husikiliza tu lakini hawayaweki katika matendo, kwa hiyo kimekuwa kizuizi kwa kazi ya Mungu. Mimi siwezi kukosa kulileta jambo hili kwa mjadala, Mimi siwezi kukosa kulizungumzia. Mimi ninalazimika kufanya hivyo; Siyo kwamba Mimi hufurahia kufunua udhaifu wa wengine. Mnafikiri kwamba matendo yenu yanafaa tu na mnadhani kwamba wakati ufunuo uko kileleni, kwamba mmeingia katika kilele pia? Je, ni rahisi hivyo? Hamchunguzi kamwe msingi ambao uzoefu wenu hatimaye umejengwa juu yake. Kwa wakati huu, mikusanyiko yenu haiwezi kuitwa maisha mazuri ya kanisa kabisa, wala kuwa maisha yafaayo ya kiroho kamwe. Ni mkusanyiko wa kundi la watu ambao hufurahia kuzungumza na kuimba. Kusema kweli, hakuna uhalisi mwingi ndani yake. Kulisema kwa dhahiri zaidi, kama hutendi, u wapi uhalisi? Je, huko siko kujigamba kusema kwamba una uhalisi? Wale ambao daima hufanya kazi ni wa kujigamba na wenye majivuno, wakati ambapo wale ambao hutii daima hutulia na kuinamisha vichwa vyao chini, bila nafasi yoyote ya kutenda. Watu ambao hufanya kazi huwa hawafanyi chochote ila kuzungumza, kuendelea zaidi na zaidi na mazungumzo yao yenye kuvutia, na wafuasi husikiliza tu. Hakuna mabadiliko ya kuzungumzia; Hizi ni njia tu za zamani! Leo, kuweza kwako kunyenyekea na kutothubutu kuingilia au kutenda makusudi ni kutokana na kuwasili kwa amri za kiutawala za Mungu; siyo mabadiliko uliyoyapata kupitia uzoefu. Ukweli kwamba kuna mambo mengi ambayo huwezi kuyafanya leo ambayo ungeweza kuyafanya jana ni kwa sababu kazi ya Mungu ni dhahiri kiasi kwamba imeshinda watu. Acha Nimuulize mtu fulani, ni kiasi gani cha ufanikishaji wako leo kilichopatikana kwa jasho la kazi ngumu yako mwenyewe? Ni kiasi gani ulichoambiwa moja kwa moja na Mungu? Ungejibu vipi? Je, ungepigwa na bumbuwazi na kutoweza kunena? Ungekosa adabu? Ni kwa nini wengine wanaweza kuzungumza juu ya mengi ya uzoefu wao ili kukuruzuku, wakati ambapo unafurahia tu chakula ambacho wengine wamepika? Je, huoni haya? Je, hutahayari?
Mnaweza kutekeleza uchunguzi wa kutafuta ukweli, kuchunguza wale walio katika viwango vya juu ambao yamkini ni bora zaidi: Unaelewa ukweli kiasi gani? Je, ni kiasi gani ambacho wewe hatimaye huweka katika mazoezi? Ni nani unayempenda zaidi, Mungu au wewe mwenyewe? Je, wewe hutoa mara nyingi zaidi, au hupokea mara nyingi zaidi? Je, ni mara ngapi wakati lengo lako lilikuwa lenye kosa umetelekeza nafsi yako ya zamani na kuyaridhisha mapenzi ya Mungu? Maswali haya machache tu yatawakanganya watu wengi. Kwa watu wengi sana, hata kama wakitambua kuwa nia yao si sahihi, bado hufanya makosa makusudi, nao hata hawajakaribia kuinyima miili yao wenyewe. Watu wengi sana huruhusu dhambi kuenea kote ndani yao, wakiruhusu hali ya dhambi kuongoza kila tendo lao. Hawawezi kushinda dhambi zao, na huendelea kuishi katika dhambi. Baada ya kufika kwenye hatua hii ya sasa, ni nani asiyejua ni matendo mangapi mabaya ameyafanya? Ukisema hujui, basi Mimi ningesema kwamba unasema uongo. Kusema ukweli, yote ni kutotaka kutelekeza nafsi yako ya zamani. Je, kuna maana gani ya kusema "maneno mengi kutoka kwa moyo" ya kutubu ambayo hayafai? Je, hili lingekusaidia kukua katika maisha yako? Kujijua mwenyewe ni kazi yako ya kudumu. Mimi huwafanya watu wakamilifu kupitia utii wao na kutenda kwao kwa maneno ya Mungu. Ukivaa tu neno la Mungu kama jinsi ungevaa nguo zako, ili kuwa tu nadhifu na maridadi, je, hujidanganyi mwenyewe na kuwadanganya wengine? Ikiwa yote uliyonayo ni kuongea na kamwe huyaweki katika matendo, ni kitu gani utakachokifikia?
Watu wengi wanaweza kuzungumza kidogo juu ya matendo na wanaweza kuzungumza kuhusu fikira zao za kibinafsi, lakini mengi yayo ni mwanga kutoka kwa maneno ya wengine. Haijumuishi chochote kutoka kwa matendo yao binafsi kamwe, wala kujumuisha kile wanachokiona kutokana na uzoefu wao. Nimechangua suala hili mapema; usifikiri kwamba sijui chochote. Wewe ni tishio la bure tu, na bado unaongea juu ya kumshinda Shetani, juu ya kutoa ushahidi wa ushindi, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa Mungu? Huu wote ni upuuzi! Je, unadhani kwamba maneno yote ambayo Mungu ameyasema leo ni yako kupendezwa nayo? Kinywa chako hunena juu ya kutelekeza nafsi yako ya zamani na kuweka ukweli katika matendo, lakini mikono yako inafanya vitendo vingine na moyo wako unapanga hila zingine—wewe ni mtu wa aina gani? Kwa nini moyo wako na mikono yako si kitu kimoja? Kuhubiri kwingi sana kumekuwa maneno matupu; si hili ni la kuvunja moyo? Ikiwa umeshindwa kuweka neno la Mungu katika matendo, inathibitisha kuwa bado hujaingia katika njia ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi, bado haujapata kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani yako, na bado haujapata mwongozo Wake. Ukisema kuwa unaweza tu kuelewa neno la Mungu lakini umeshindwa kuliweka katika matendo, basi wewe ni mtu asiyependa ukweli. Mungu huwa haji kumwokoa mtu wa aina hii. Yesu alipatwa na maumivu makubwa wakati Yeye aliposulubiwa ili kuwaokoa wenye dhambi, kuwaokoa maskini, kuwaokoa hao watu wanyenyekevu. Kusulubiwa Kwake kulileta sadaka ya dhambi. Ikiwa huwezi kutenda neno la Mungu, basi unapaswa kuondoka haraka unavyoweza; usijikalie pote katika nyumba ya Mungu kama doezi. Watu wengi hata huona vigumu kujizuia kufanya mambo ambayo humpinga Mungu kwa dhahiri. Je, si wanauliza kifo? Wanawezaje kuongea juu ya kuingia katika ufalme wa Mungu? Je, wangekuwa na ujasiri wa kuuona uso Wake? Kula chakula ambacho Yeye hukupa, kufanya mambo ya uhalifu ambayo humpinga Mungu, kuwa mwenye nia mbaya, mwenye kudhuru, na mwenye hila, hata wakati Mungu anakuruhusu kufurahia baraka ambazo Yeye amekupa—je, huzihisi zikiichoma mikono yako unapozipokea? Je, huuhisi uso wako ukigeuka kuwa mwekundu? Baada ya kufanya kitu kinyume na Mungu, baada ya kufanya hila ili "kuwa laghai," huhisi hofu? Kama huhisi chochote, unawezaje kuzungumza juu ya wakati wowote ujao? Kulikuwa tayari hakuna wakati ujao kwako zamani za kale, kwa hiyo ni matarajio yapi makubwa zaidi unaweza kuwa nayo bado? Ukisema kitu bila haya lakini huhisi hatia, na moyo wako hauna ufahamu, basi haimaanishi kwamba tayari umekataliwa na Mungu? Kuzungumza na kutenda kwa kujiachia na bila kuzuiwa imekuwa asili yako; Je, unawezaje kufanywa mkamilifu na Mungu hivi? Ungeweza kutembea ulimwenguni kote? Ni nani angethibitishiwa na wewe? Wale ambao wanaijua asili yako ya kweli watakaa mbali nawe. Je, si hii ni adhabu ya Mungu? Kwa jumla, ikiwa kuna mazungumzo tu bila matendo, hakuna ukuaji. Ingawa Roho Mtakatifu anaweza kuwa anafanya kazi kwako unapozungumza, kama hutendi, Roho Mtakatifu ataacha kufanya kazi. Ukizidi kuendelea kwa njia hii, kunawezaje kuwa na majadiliano yoyote ya wakati ujao au kutoa nafsi yako yote kwa kazi ya Mungu? Wewe husema tu juu ya kutoa nafsi yako yote, na bado humpi Mungu moyo wako ambao kwa hakika humpenda Yeye. Yote ambayo Mungu amepokea ni moyo wa maneno yako, na siyo moyo wa utendaji wako. Je, hiki kinaweza kuwa ndicho kimo chako cha kweli? Ikiwa ungeendelea kwa jinsi hii, ungefanywa mkamilifu na Mungu lini? Je, huhisi wasiwasi juu ya kesho yako ya giza na majonzi? Je, huhisi kwamba Mungu amepoteza tumaini kwako? Je, hujui kwamba Mungu hutamani kuwapa ukamilisho watu wengi na wapya? Je, vitu vya zamani vingeweza kukacha? Wewe huyazingatii maneno ya Mungu leo: Je, unasubiri kesho?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Ijumaa, 30 Novemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Jambo muhimu katika kumtii Mungu ni kuitambua nuru mpya, na kuweza kuikubali na kuiweka katika vitendo. Huu pekee ndio utii wa kweli. ... Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka."

Alhamisi, 23 Agosti 2018

Latest Swahili Christian Video "Kufungulia Moyo Minyororo" | Are We Really in Control of Our Own Fate?

Latest Swahili Christian Video "Kufungulia Moyo Minyororo" | Are We Really in Control of Our Own Fate?

Chen Zhi alizaliwa katika familia iliyokuwa masikini. Shuleni, "Maarifa yanaweza kubadilisha majaliwa yako" na "Majaliwa ya mtu yako mikononi mwake" kama alivyofundishwa na shule ikawa wito wake. Aliamini kuwa almuradi angefanya kazi kwa bidii siku zote, angeweza kuwa bora kuliko wenzake, na kujipatia sifa na umaarufu. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, Chen Zhi alipata kazi iliyolipa vizuri sana katika biashara ya nchi za nje. Hata hivyo, hakuridhika na hali aliyokuwa kwa wakati huo hata kidogo. Ili kutimiza njozi yake ya kuwa bora kuliko wengine, aliacha kazi yake na kuanzisha kampuni yake ya kuuza bidhaa. Lakini nyakati nzuri hazikudumu kwa muda mrefu. Kwa vile operesheni haikuendeshwa vizuri, wateja wakawa wachache, na biashara ya kampuni hiyo ikapungua. Hatimaye, kampuni haikuweza kuendelea kufanya kazi. Baada ya kampuni hiyo kufilisika, Chen Zhi hakuwa na nia ya kukubali kushindwa hata kidogo. Aliamini kwamba kwa kutegemea akili na uwezo wake, alimuradi angevumilia angeweza kurudi. Baadaye, Chen Zhi alianzisha tovuti ya mauzo ya mtandaoni na kuanzisha biashara kwenye Mtandao. Baada ya kujishughulisha kwa miaka kadhaa, hakufaulu bado. Chen Zhi akatumbukia katika lindi kuu la huzuni kubwa na kutojiweza ...
Mnamo mwaka wa 2016, familia ya Chen Zhi ilienda Marekani kuishi. Kwa msaada wa mkewe, alikubali kazi ya siku za mwisho za Mwenyezi Mungu. Kupitia kusoma maneno ya Mungu, Chen Zhi hatimaye alielewa kwamba Mungu anadhibiti majaliwa ya wanadamu, na kwamba mtu hawezi kabisa kubadili hatima yake mwenyewe kutegemea uwezo wake mwenyewe. Alijua pia chanzo cha dhiki ya mwanadamu maishani mwake, na jinsi Shetani amewapotosha wanadamu. Alijua kwamba ikiwa mtu ataishi maisha yenye maana, basi lazima aje mbele za Mungu, akubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu ili kupata utakaso, na kuishi kwa kutegemea maneno ya Mungu, na ni hapo tu ndio atapata sifa ya Mungu . Chen Zhi alielewa ukweli fulani katika maneno ya Mwenyezi Mungu, akaanzisha mtazamo sahihi juu ya maisha, alimwaminia Mungu maisha yake yote, akatii udhibiti wa Mungu na mipangilio Yake, na hatimaye kujiondoa jozi katika nafsi yake ya "Majaliwa ya mtu yako mikononi mwake, "na kupata ufunguliwaji na uhuru. Kutoka wakati huo kuendelea alitembea kwenye njia angavu na sahihi ya maisha.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Maisha ya Kanisa

Jumatatu, 20 Agosti 2018

Sinema Fupi ya Injili "Kuamka Kutoka kwa Ndoto" (2) - Bila Utakatifu Hakuna Mwanadamu Atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni


Sinema Fupi ya Injili "Kuamka Kutoka kwa Ndoto" (2) - Bila Utakatifu Hakuna Mwanadamu Atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni

Wakati dhambi zetu sisi wanaomwamini Bwana zinasamehewa, je, tunapokea utakaso? Ikiwa hatutajitahidi kupata utakaso, na kujali tu kutumika kwa ajili ya Bwana na kufanya kazi ya Bwana kwa uaminifu, je, tutanyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni? Filamu hii ya Kuamka Kutoka kwa Ndoto, itakupa majibu yote!
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kukamilishwa na Mungu

Jumamosi, 11 Agosti 2018

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (4) - Kwa nini Mungu Anatekeleza Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho?

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (4) - Kwa nini Mungu Anatekeleza Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho?

Hata ingawa dhambi zetu husamehewa mara tunapokiri imani yetu katika Bwana, mara nyingi bado sisi hutenda dhambi. Hili ni tatizo ambalo huwakanganya waumini wote. Bila kujali tumeamini katika Bwana kwa miaka mingapi, na bila kujali jinsi tunavyotenda maneno ya Bwana au jinsi tunavyotegemea utashi wetu kujizuia, wakati wote bado hatuwezi kujiweka huru kutokana na udhibiti wa asili yetu ya dhambi. Katika mioyo yetu sote tunateseka sana. Tunaweza kufanya nini ili hatimaye kujiweka huru kutokana na udhibiti wa asili yetu ya kishetani na kufikia wokovu wa kweli? Hii video fupi itakusaidia kujibu swali hilo.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,  kutenda ukweli