Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo wafuasi-wa-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo wafuasi-wa-Kristo. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 9 Juni 2019

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji.

4. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji.

Maneno Husika ya Mungu:
Majaribu haya yanailenga hali gani ya ndani ya watu? Yanalenga tabia ya uasi ndani ya watu ambayo haiwezi kumridhisha Mungu. Kuna mengi ambayo ni machafu ndani ya watu, na mengi ambayo ni ya unafiki, na kwa hivyo Mungu anawatia katika majaribu ili kuwasafisha. …
… Upendo wa kweli wa Mungu ni tabia Yake kamili, na tabia kamili ya Mungu ikionyeshwa kwako, hili linakuletea nini mwilini mwako? Tabia ya haki ya Mungu ikionyeshwa kwako, bila shaka mwili wako utapata uchungu mkubwa. Iwapo hutapata haya maumivu, basi huwezi kufanywa mkamilifu na Mungu, wala huwezi kumpa Mungu mapenzi ya kweli. Mungu akikufanya mkamilifu kwa hakika atakuonyesha tabia Yake kamili. Tangu uumbaji hadi leo, Mungu hajawahi kuonyesha tabia Yake kamili—ila katika siku za mwisho Anaifichua kwa hili kundi la watu ambao Aliwateua awali na kuwachagua, na kwa kuwafanya watu wakamilifu, Anaiweka wazi tabia Yake, na kupitia kwayo Analifanya kamili kundi la watu. Huo ndio upendo wa kweli wa Mungu kwa watu. Kuyapitia mapenzi ya kweli ya Mungu kunawapasa watu wastahimili uchungu mkali, na kulipa gharama kubwa. Ni baada tu ya hili ndipo watapatikana na Mungu na waweze kutoa tena mapenzi ya kweli kwa Mungu, na ni hapo tu ndipo Moyo wa Mungu utaridhishwa. Ikiwa watu wanataka wafanywe wakamilifu na Mungu, na kama wanataka kutenda kulingana na mapenzi Yake, na kumpa Mungu mapenzi yao ya dhati kikamilifu, ni sharti wapitie mateso mengi na maumivu makali kutokana na hali hizo, kupata uchungu mkali kuliko mauti, hatimaye watashurutishwa kuirejesha mioyo yao ya kweli kwa Mungu. Ikiwa mtu anampenda Mungu kwa dhati au la, itafichuliwa wakati wa shida na usafishaji. Mungu hutakasa mapenzi ya watu, na hili vilevile hupatikana tu ndani ya shida na usafishaji.
kutoka kwa "Kumpenda Mungu Tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Anapokabiliwa na hali ya mwanadamu na mtazamo wake kwa Mungu, Mungu amefanya kazi mpya, Akimruhusu mwanadamu kuwa na ufahamu Wake na utiifu Kwake, na upendo pia na ushahidi. Hivyo, mwanadamu lazima apitie usafishaji wa Mungu kwake, na pia hukumu, ushughulikiaji na upogoaji Wake kwake, ambazo pasi nazo mwanadamu hangewahi kumjua Mungu, na hangewahi kuwa na uwezo wa kumpenda kwa kweli na kuwa na ushuhuda Kwake. Usafishaji wa Mungu kwa mwanadamu sio tu kwa ajili ya athari inayoegemea upande mmoja, bali kwa ajili ya athari inayogusia pande nyingi. Ni kwa jinsi hii tu ndiyo Mungu hufanya kazi ya usafishaji kwa wale ambao wako tayari kutafuta ukweli, ili upendo na uamuzi wa mwanadamu yafanywe timilifu na Mungu. Kwa wale walio tayari kuutafuta ukweli na wanaomtamani Mungu, hakuna kilicho cha maana zaidi, au cha usaidizi zaidi, kuliko usafishaji kama huu. Tabia ya Mungu haijulikani wala kueleweka kwa urahisi sana na mwanadamu, kwani Mungu, hatimaye, ni Mungu. Mwishowe, haiwezekani kwa Mungu kuwa na tabia sawa na mwanadamu, na hivyo si rahisi kwa mwanadamu kujua tabia Yake. Ukweli haumilikiwi kwa asili na mwanadamu, na hauleweki kwa urahisi na wale ambao wamepotoshwa na Shetani; mwanadamu hana ukweli na hana azimio la kutia ukweli katika vitendo, na asipoteseka, na asisafishwe au kuhukumiwa, basi uamuzi wake hautawahi kufanywa timilifu. Kwa watu wote, usafishaji ni wa kutesa sana na ni mgumu sana kukubali—ilhali ni katika usafishaji ndipo Mungu huweka wazi tabia Yake ya haki kwa mwanadamu, na Huweka hadharani mahitaji Yake kwa mwanadamu, na Hutoa nuru zaidi, na upogoaji na ushughulikiaji halisi zaidi; kwa kulinganisha mambo ya hakika na ukweli, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi kujihusu na ukweli, na Humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu, hivyo kumruhusu mwanadamu kuwa na upendo wa kweli zaidi na safi zaidi wa Mungu. Haya ndiyo malengo ya Mungu katika kutekeleza usafishaji. Kazi yote Afanyayo Mungu kwa mwanadamu ina malengo yake na maana yake; Mungu hafanyi kazi isiyo na maana, wala Hafanyi kazi isiyo na manufaa kwa mwanadamu. Usafishaji haumaanishi kuondoa watu kutoka mbele ya Mungu, wala haumaanishi kuwaangamiza katika kuzimu. Unamaanisha kubadilisha tabia ya mwanadamu wakati wa usafishaji, kubadilisha motisha zake, mitazamo yake ya kale, kubadilisha upendo wake kwa Mungu, na kubadilisha maisha yake yote. Usafishaji ni jaribio la kweli la mwanadamu, na aina ya mafunzo halisi na ni wakati wa usafishaji tu ndipo upendo wake unaweza kutimiza wajibu wake wa asili.
kutoka kwa "Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kumpenda Mungu kwa Kweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anaweza kumfanya mwanadamu kuwa mtimilifu kwa hali chanya na hata hasi. Inategemea na kama unaweza kupitia, na kama unafuatilia kufanywa na Mungu kuwa mtimilifu. Kama unatafuta kwa kweli kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu, basi yale mambo mabaya hayawezi kuchukua chochote kutoka kwako, lakini yanaweza kukuletea mambo ambayo ni halisi zaidi, na yanaweza kukufanya kuweza kujua zaidi kile ambacho kinakosekana ndani yako, kukufanya kuweza kuelewa zaidi hali yako halisi, na kuhakikisha kwamba mwanadamu hana chochote, na hana thamani yoyote; kama hutapitia majaribio, huyajui haya, na siku zote utahisi kwamba unawazidi wengine na kwamba wewe ni bora zaidi ya kila mtu mwingine. Kupitia haya yote utatambua kwamba yale yote uliyoyapitia awali yalifanywa na Mungu na kulindwa na Mungu. Kuingia katika majaribu hukuwacha bila upendo au imani, unakosa maombi, na huwezi kuimba nyimbo za kuabudu—na, bila ya kutambua, katikati ya haya yote unakuja kujijua. Mungu anazo mbinu nyingi za kumfanya binadamu kuwa mtimilifu. Yeye hutumia namna zote za mazingira ili kushughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia mambo mbalimbali ya kumweka mwanadamu wazi; kwa njia moja Anamshughulikia binadamu, kwa njia nyingine Anamweka mwanadamu wazi, na kwa njia nyingine Anamfichua mwanadamu, Akichunguza na kufichua "siri" zilizomo katika kina cha moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kufichua hali zake nyingi. Mungu humfanya mwanadamu kuwa mtimilifu kupitia mbinu nyingi—kupitia kwa ufunuo, kumshughulikia, utakasaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa matendo.
kutoka kwa "Ni Wale tu Wanaolenga Vitendo Ndio Wanaweza Kufanywa kuwa Watimilifu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Bila kujali ni sehemu gani ya kazi ya Mungu, yote ni isiyoeleweka kwa mwanadamu. Ikiwa ungeweza kuifahamu, basi kazi ya Mungu ingekuwa isiyo na maana au thamani. Kazi inayofanywa na Mungu ni isiyoeleweka: inakinzana pakubwa na mawazo yako, na zaidi isivyopatana na mawazo yako, ndivyo inaonyesha zaidi kwamba kazi ya Mungu ni ya maana; ingekuwa inalingana na mawazo yako, basi ingekuwa isiyo maana. Leo, unahisi kwamba kazi ya Mungu ni ya ajabu mno, na zaidi ilivyo ya ajabu, ndivyo unahisi kwamba Mungu ni asiyeeleweka, na kuona jinsi matendo ya Mungu yalivyo makubwa. Kama Angefanya tu kazi fulani ya juu juu ya kutimiza wajibu kumshinda mwanadamu na Awachie hapo, basi mwanadamu hangeweza kuona umuhimu wa kazi ya Mungu. Ingawa unapokea usafishaji kidogo sasa, ni wa faida kubwa sana kwa ukuaji wa maisha yako—na hivyo ugumu wa aina hii ni wenye umuhimu mkubwa sana kwako. Leo, unapokea usafishaji kidogo, lakini baadaye utaweza kwa kweli kuyaona matendo ya Mungu, na hatimaye utasema: "Matendo ya Mungu ni ya ajabu mno!" Haya ndiyo yatakuwa maneno moyoni mwako. Baada ya kupitia usafishaji wa Mungu kwa muda (majaribu ya[a] watenda huduma na wakati wa kuadibu), baadhi ya watu hatimaye walisema: "Kuamini katika Mungu ni kugumu kweli kweli!" "Kugumu" huku kunaonyesha kwamba matendo ya Mungu ni yasiyoeleweka, kuwa kazi ya Mungu ni yenye umuhimu mkubwa na thamani, na ni yenye kustahili sana kuthaminiwa na mwanadamu. Ikiwa, baada ya Mimi kufanya kazi nyingi hivi, hukuwa na maarifa hata kidogo, basi kazi yangu ingeweza kuwa na thamani bado? Itakufanya useme: "Huduma kwa Mungu ni ngumu kweli kweli, matendo ya Mungu ni ya ajabu mno, Mungu kweli ni mwenye hekima! Yeye ni mwenye kupendeza kweli kweli!" Kama, baada ya kupitia kipindi cha uzoefu, una uwezo wa kusema maneno kama haya, basi hii inathibitisha kuwa umepata kazi ya Mungu ndani yako.
kutoka kwa "Ni Lazima Wale Wanaofaa Kufanywa Wakamilifu Wapitie Usafishaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati Mungu anafanya kazi ili kumsafisha mwanadamu, mwanadamu huteseka, upendo wake kwa Mungu unakuwa mkubwa zaidi, na zaidi ya nguvu za Mungu zinafichuliwa kwake. Kadri usafishaji wa mwanadamu ulivyo wa kiwango cha chini, ndivyo upendo wake kwa Mungu ulivyo wa kiwango cha chini, na ndivyo nguvu za Mungu zinafichuliwa kwake kwa kiwango cha chini. Kadri usafishaji wake na uchungu wake ulivyo mkubwa na zaidi yalivyo mateso yake, ndivyo upendo wake wa kweli kwa Mungu utakavyokuwa, ndivyo imani yake kwa Mungu itakavyokuwa ya kweli, na ndivyo maarifa yake ya Mungu yatakuwa ya kina. Katika uzoefu wako utaona kwamba wale ambao wanakabiliwa na usafishaji mkubwa na uchungu, na kushughulikiwa sana na nidhamu, wana upendo mkubwa kwa Mungu, na maarifa ya kina na elekevu ya Mungu. Wale ambao hawajapitia kushughulikiwa wanayo maarifa ya juu juu tu, na wanaweza tu kusema: "Mungu ni mzuri sana, Yeye huwapa watu neema ili waweze kumfurahia Yeye." Kama watu wamepitia kushughulikiwa na kufundishwa nidhamu, basi hao wanaweza kuyazungumza maarifa ya kweli ya Mungu. Hivyo kazi ya Mungu katika mwanadamu ilivyo ya ajabu zaidi, ndivyo ilivyo ya thamani zaidi na ni muhimu zaidi. Zaidi inavyokosa kupenyeza kwako na zaidi isivyolingana na mawazo yako, ndivyo kazi ya Mungu inavyoweza kukushinda wewe, kukupata wewe, na kukufanya mkamilifu. Umuhimu wa kazi ya Mungu ni mkubwa sana! Kama Hangemsafisha mwanadamu kwa njia hii, ikiwa Hangefanya kazi kulingana na njia hii, basi kazi ya Mungu haingekuwa na ufanisi na ingekuwa isiyo na maana. Hii ndiyo sababu ya umuhimu wa ajabu wa uteuzi Wake wa kundi la watu katika siku za mwisho. Hapo awali ilisemwa kuwa Mungu angelichagua na kulipata kundi hili. Zaidi ilivyo kuu kazi Anayofanya ndani yenu, ndivyo ulivyo mkubwa na safi upendo wenu. Kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi, ndivyo zaidi mwanadamu anavyoweza kupenda hekima Yake na ndivyo maarifa ya mwanadamu Kwake yalivyo ya kina zaidi.
kutoka kwa "Ni Lazima Wale Wanaofaa Kufanywa Wakamilifu Wapitie Usafishaji" katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumamosi, 1 Juni 2019

Swahili Gospel Video "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (7) - Je, Kufanya Kazi Ngumu Kunamaanisha Tunafuata Mapenzi ya Baba wa Mbinguni?

Swahili Gospel Video "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (7) - Je, Kufanya Kazi Ngumu Kunamaanisha Tunafuata Mapenzi ya Baba wa Mbinguni?

Waumini wengine wa Bwana hufikiria kwamba yote tunayohitaji kufanya ni kuteseka na kulipa gharama ya kueneza injili ya Bwana, kubeba msalaba ili kumfuata Bwana, na kutenda unyenyekevu, subira na uvumilivu, na kwamba kwa kufanya mambo haya yote tunafuata mapenzi ya Baba wa mbinguni, na pia wao huamini kwamba kila mara tukifuatilia imani yetu kwa njia hii, basi hatimaye tutaokolewa na Mungu na kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele. Lakini je, ni sahihi kuwa na ufahamu wa aina hii na kutenda kwa njia hii? Bwana Yesu alisema, "Wengi wataniita siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujafanya unabii kwa jina lako? na kwa jina lako kutoa pepo? na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Halafu nitasema wazi kwao, Sikuwajua nyinyi kamwe: ondokeni mbele yangu, nyinyi watenda maovu" (Mathayo 7:22-23). Kwa nini watu hawa ambao huhubiri na kufanya kazi kwa bidii kwa jina la Bwana hawataingia katika ufalme wa mbinguni pekee, lakini pia wataadhibiwa na Bwana?
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Jumapili, 14 Aprili 2019

Nilipitia Wokovu wa Mungu

Nilipitia Wokovu wa Mungu

Cheng Hao Mji wa Yongzhou, Mkoa wa Hunan
Wajibu ambao mimi na mke wangu tunatimiza kanisani ni kuhubiri injili. Muda mfupi uliopita, mke wangu alipandishwa cheo kuwa mkuu wa kundi la injili, huku mimi, kutokana na kiburi changu mwenyewe na utukutu wangu, nilipoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kupelekwa nyumbani kutafakari juu ya matendo yangu. Kutokana na kwamba mimi na mke wangu tulianza kutimiza wajibu wetu wakati mmoja, lilikuwa jambo gumu kukubali kumuona akipandishwa cheo wakati nilifukuzwa kutoka kwa wajibu wangu. Machozi yalidondoka machoni mwangu nilipofikiri: “Mungu anatenganisha kila mmoja kwa jinsi yake na, kuzingatia kuwa nimefukuzwa, hii ni hakika kwamba nimefichuliwa na kuondoshwa. Aa! Nani angefikiri kwamba baada ya miaka yote hii, maisha yangu kama muumini yangeishia kwa kutofaulu kabisa. Yote ninayoweza kufanya sasa ni kusubiri adhabu yangu.” Kisha nikaenda nyumbani na moyo mzito. Kuanzia wakati huo kwendelea nikawa nimetatizika katika kushindwa na kujawa na suitafahamu na lawama kwa Mungu. Nilikuwa nimetumbukia katika giza bila matumaini.
Siku moja, nikapata vifungu viwili vinavyofuata vya neno la Mungu kwa bahati: “Sijawahi kusema kuwa hamkuwa na mategemeo, sembuse kwamba mlipaswa kuangamizwa au kupotea; je, Nimetangaza hadharani jambo hilo? Wewe husema kuwa huna tumaini, lakini si hili ni hitimisho lako? Je, si hii ni athari ya mawazo yako mwenyewe? Je, hitimisho lako lina maana?” (“Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Huoni tabia ya Mungu yenye haki, na daima unamwelewa Mungu visivyo na kugeuza nia Zake, ambayo hukufanya daima uwe bila rajua na kupoteza matumaini. Je, hili si la kujiadhibu? … Huelewi kazi ya Mungu na huyaelewi mapenzi ya Mungu katu; hata zaidi, huelewi nia nzuri ambazo Mungu ameweka katika miaka Yake 6,000 za kazi ya usimamizi” (“Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nikisoma vifungu hivi, nilitambua kwa mshangao: Mungu hazungumzi juu yangu? Mara tu nilipoarifiwa kwamba kanisa lilikuwa limenifukuza, nilikisia na kuhitimisha kuwa nilikuwa nimefichuliwa na kuondoshwa na kupoteza imani katika kutafuta ukweli. Niliishi katika hali ya kudumu ya uhasi na kutoelewana, kama nimekubali bila kulalamika kabisa kushindwa kwangu mwenyewe. Wakati huo, nilitazama moyoni mwangu, nikiuliza: “Je, unaelewa kwa kweli ni kwa nini umekutana na balaa hii? Je! Unaelewa kwa kweli mapenzi ya Mungu? Bila shaka hapana! Sielewi! Basi kwa nini nifanye makisio ya kishenzi na ufafanuzi kwa maneno usio na msingi? Je, si huku kulikuwa ni kuwa na kiburi sana, udanganyifu mno? Je, si nilikuwa nimejishusha katika mahali hapa pa mateso ya giza? Upumbavu jinsi gani, jinsi nilivyokuwa na upuuzi!” Kwa hiyo, nilikwenda mbele ya Mungu kwa sala, nikiomba nuru Yake ili nipate kufichua mapenzi Yake katika ufunuo huu wa hivi karibuni. Baadaye, niliona kifungu hiki cha neno la Mungu: “Yote Ayafanyayo ni mapenzi ya dhati kwako; Hana nia mbaya. Anawahukumu kwa sababu ya dhambi zenu, ili kwamba mweze kujichunguza wenyewe na kupokea wokovu mkubwa. Haya yote hufanywa kumfinyanga mwanadamu. Tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu amekuwa Akifanya kila Awezalo kumwokoa mwanadamu, na hakika hayuko tayari kuwaangamiza kabisa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Sasa Amekuja miongoni mwenu kufanya kazi; je, huu si wokovu zaidi? Je, Angalikuchukia, Angaliendelea kufanya kazi ya kiwango hicho cha juu ili kukuongoza wewe Mwenyewe? Ni kwa nini Ateseke hivyo? Mungu hawachukii wala hana nia mbaya juu yenu. Mnapaswa kufahamu kuwa mapenzi ya Mungu ndiyo mapenzi ya kweli zaidi. Anawaokoa kupitia hukumu kwa sababu tu ya uasi wa mwanadamu; la sivyo, hawangepata wokovu. … Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo. Hili ndilo kusudi kuu la kufanya kazi ya kushinda miongoni mwenu—ni kwa ajili ya wokovu tu” (“Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu ya dhati yaliufurahisha moyo wangu na kuniamsha kutoka kwa kuishiwa imani kwangu kulikokuwa kumetiwa ganzi. Kama ilivyobainika, ingawa hali yangu ilionekana kuwa ya kutia hofu kwa ukaguzi wa kwanza, ilikuwa ni Mungu kwa kweli akiniletea upendo Wake, na akinipa wokovu Wake. Haikuwa, kama nilivyofikiria, kwamba ningeondoshwa. Nilikuwa mwenye kiburi na mgumu—nikitimiza wajibu wangu kwa kuzembea na utundu bila kuwa na subira. Mungu hangevumilia kuniona nikiendelea kukanyagwa na Shetani. Hakuweza kuvumilia kuniona nikizidi kuzama chini zaidi na Yeye hasa hakuweza kuvumilia kuniona nikikabiliwa na adhabu kwa kuikosea tabia ya Mungu kupitia vitendo vya kiburi kisichozuilika. Hivyo, kupitia hukumu na kuadibiwa, Aliniletea wokovu, akanibariki kwa neema Yake ya kuokoa na kunisaidia kuyatoroka mishiko ya upotovu wa Shetani. Kufukuzwa kwa kanisa kulikuwa, kweli, wokovu mkuu mno wa Mungu. Jinsi nilivyozidi kuwa na kiburi, ndivyo Mungu alivyozidi kutengeneza mazingira ili kukabiliana na makosa yangu. Aliruhusu tamaa zangu kubaki bila kutimizwa ili moyo wangu uliokufa ganzi uanze kuhisi maumivu. Alitenda kupitia maumivu haya ili kunifanya kutafakari juu ya matendo yangu, kuelewa kiini cha asili yangu potovu na kutafuta ukweli ili kufanikisha mabadiliko katika tabia yangu. Hii ndiyo ile kazi halisi ya wokovu ambayo Mungu aliniletea. Yote aliyoyafanya yalikuwa ni utunzaji na upendo kwangu. Vinginevyo, bado ningekuwa naishi katika dhambi bila kujua isiyojali, bado nikitenda kwa uzembe, nikikatiza na kuingiliza kati kazi ya injili. Mwishowe, vitendo vyangu vingekuwa vimeikosea tabia ya Mungu na ningekuwa nimeondoshwa na Mungu. Wakati huu, nilikuja kuona kwamba wokovu wa Mungu ulikuwa halisi. Hakuna kitu cha uongo au kitupu kuhusu upendo wa Mungu—ni kweli na halisi. Mimi, hata hivyo, nilikosa kuona kazi ya Mungu na wokovu Wake. Nilikosa kutafuta nia yenye ari katika wokovu wa Mungu, badala yake nilijifafanua kupita kiasi mara kwa mara huku nikimwelewa Mungu visivyo na kumlaumu na kuishi kwa uzembe bila rajua. Nilikosa busara kiasi gani! Nilikuwa mtu asiyefaa kupokea hukumu ya Mungu na kuadibiwa.
Mungu mpendwa, asante! Kupitia uzoefu huu, ninatambua kwamba wokovu Wako ni wa kweli na hukumu Yako na kuadibu vimejaa upendo. Bila hukumu Yako na kuadibu, singewahi kamwe kujitazama kwa kweli. Ningendelea kuishi katika upotovu, hali yangu ikiendelea kuharibika, kukanyagwa na Shetani na hatimaye kubebwa naye. Kupitia uzoefu huu, nilitambua pia kuwa kiini Chako ni upendo na kwamba matendo Yako yote yanalenga kuwaokoa wanadamu. Mungu, ninaapa kujiwekeza kikamilifu katika kutafuta ukweli na kuanza upya. Bila kujali matokeo ni yapi, ninaapa kutimiza wajibu wangu wa kiumbe ili kuyaridhisha mapenzi Yako. Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!

Ijumaa, 22 Machi 2019

Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna yeyote anayemchukua Kristo kama binadamu wa nyama na mwili aliye na kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao hufanya wanavyopenda wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa "Kristo wa kweli." Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.
Kabla ya kuwasiliana na Kristo, unaweza kuamini kwamba tabia yako imebadilishwa kabisa, kwamba wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo, na kwamba wewe unastahili kupokea baraka za Kristo zaidi. Pia kwamba, kwa kuwa umesafiri njia nyingi, umefanya kazi nyingi, na kuleta matunda mengi, hivyo ni lazima utakuwa mtu anayepata taji mwishowe. Hata hivyo kuna ukweli ambao hujui: Tabia potovu na uasi na upinzani wa mwanadamu huonekana wazi mara tu anapomwona Kristo, na uasi na upinzani unaoonekana wakati huu kwa hakika na kamilifu kuliko wakati mwingine wote. Ni kwa sababu Kristo ni Mwana wa Adamu—Mwana wa Adamu aliye na ubinadamu wa kawaida—kwamba mwanadamu hamwogopi wala kumheshimu. Ni kwa sababu Mungu anaishi katika mwili ndio maana uasi wa mwanadamu hufichuliwa kikamilifu na kwa uwazi sana. Kwa hivyo Nasema kwamba kuja kwake Kristo kumechimbua uasi wote wa wanadamu na kutupa asili ya mwanadamu katika afueni ya ghafla. Huku kunaitwa "kumvuta chui mkubwa kutoka mlimani" na "kumvuta mbwa mwitu kutoka pangoni pake." Je, unathubutu kusema kwamba wewe ni mwaminifu kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe huonyesha utiifu kamili kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe si muasi? Wengine watasema: Kila wakati ambao Mungu ananiweka katika mazingira mapya, mimi daima hutii na silalamiki na aidha siweki fikra zozote juu ya Mungu. Wengine watasema: Kazi zozote nilizopewa na Mungu mimi hufanya kadri ya uwezo wangu na kamwe mimi si mvivu. Kama ndivyo hali, Nawauliza hivi: Je, mnaweza kulingana na Kristo wakati mnaishi pamoja naye? Na ni kwa muda gani nyinyi mnaweza kulingana na Yeye? Siku moja? Siku mbili? Saa moja? Saa mbili? Imani yenu inaweza kuwa ya kustahili sifa, lakini hamna uthabiti wa kutosha. Wakati unaishi na Kristo kwa kweli, kujidai kwako na kujigamba kwako kutawekwa wazi kwa maneno na matendo yako kidogo kidogo, na hivyo ndivyo tamaa yako ya kupindukia na uasi na kutoridhika kwako kutafichuka kwa kawaida. Mwishowe, kiburi chako kitakuwa kikubwa zaidi, hadi wakati wewe utazozana sana na Kristo kama maji na moto, na basi asili yako itawekwa wazi kabisa. Wakati huo, fikra zako haziwezi kufichika tena, malalamiko yako, pia, yataonekana kwa ghafla, na ubinadamu wako duni utakuwa wazi kabisa. Hata hivyo, hata wakati huo, utaendelea kukana uasi wako mwenyewe, ukiamini kwamba badala yake kwamba Kristo kama huyu si rahisi kukubaliwa na mwanadamu, ni mwingi wa madai kwa binadamu, na ungetii kikamilifu kwake kama yeye angekuwa tu Kristo mwenye huruma zaidi. Mnaamini kwamba daima kuna sababu ya haki ya uasi wenu, na kwamba nyinyi mnamwasi tu baada ya Kristo amewafikisha hatua fulani. Kamwe hamjawahi kufikiri kwamba mmekosa kumchukulia Kristo kama Mungu na katika nia ya kumtii. Badala yake, wewe kwa ukaidi unasisitiza Kristo afanye kazi Yake kulingana na matakwa yako, na punde ambapo kuna jambo lolote ambamo Hafanyi hivyo, basi unaamini kwamba Yeye si Mungu bali ni mwanadamu. Je, si kuna wengi kati yenu ambao wameridhika na Yeye katika hali hii? Ni nani huyo mnayemwamini hata hivyo? Na ni jinsi gani mnatafuta?
Kila mara mnataka kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijipandishe hadhi hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, wakati unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa. Ushirika wako na ndugu (au dada) huenda usionyeshe mengi kukuhusu wewe, lakini si rahisi hivyo unaposhiriki na Kristo. Wakati wowote, fikira zako zinaweza kukita mizizi, kiburi chako kianze kuchipuka, na uasi wako kuzaa mitini. Unawezaje kufaa kushiriki na Kristo na ubinadamu kama huo? Je, kweli unaweza kumchukua Yeye kama Mungu kila wakati wa kila siku? Je, kweli utakuwa na hali halisi ya utiifu kwa Mungu? Mnamuabudu Mungu mkubwa ndani ya mioyo yenu kama Yehova wakati mnamchukua Kristo anayeonekana kama mwanadamu. Hisia zenu ni duni mno na ubinadamu wenu ni wa hali ya chini! Hamwezi kumfikiria Kristo kama Mungu milele; ni mara chache tu, mnapotaka, ndio mnamshika na kumwabudu kama Mungu. Hii ndiyo sababu Ninasema nyinyi si waumini wa Mungu, lakini kikundi cha washirika ambao wanapigana dhidi ya Kristo. Hata watu ambao huonyesha wema kwa wengine hulipwa, lakini Kristo, ambaye amefanya kazi ya namna hiyo kati yenu, hajapokea upendo wa Mungu au fidia na utii wake. Je, hili si ni jambo la kusikitisha mno?
Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kufanya tendo mbaya, lakini katika ushirika wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kwa uaminifu, au kutii neno la Kristo; basi, Ninasema kwamba wewe ni mtu mbaya na mwovu zaidi katika dunia. Unaweza kuwa mkunjufu na mwaminifu mno kwa jamaa zako, marafiki, mke (au mume), wanao na mabinti, na wazazi, na kamwe huwatumii wengine vibaya, lakini kama huwezi kulingana na kupatana na Kristo, basi hata ukitumia vitu vyako vyote kuwasaidia majirani zako au kulinda vizuri baba yako, mama, na wanakaya, Ningesema kwamba wewe bado ni mwovu, na zidi ya hayo aliyejaa hila za ujanja. Usifikiri, kwamba wewe unalingana na Kristo kwa sababu tu unapatana na wengine au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unafikiri kwamba nia yako ya huruma inaweza kupata baraka kutoka Mbinguni kwa udanganyifu? Je, unafikiri kwamba matendo machache mema yanaweza kubadilishwa na utii wako? Hakuna hata mmoja yenu anaweza kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, na wote wanaona vigumu kukubali ubinadamu wa kawaida wa Kristo, hata hivyo siku zote mnatangaza utiifu wenu kwa Mungu. Imani kama yenu italeta adhabu ya kufaa. Wacheni kujihusisha katika ndoto za ajabu na kutaka kumwona Kristo, kwa maana nyinyi ni wadogo sana katika kimo, kiasi kwamba nyinyi hata hamstahili kumwona. Wakati umeuwacha kabisa uasi wako na unaweza kupatana na Kristo, wakati huo Mungu Atakuonekania kwa kawaida. Iwapo utaenda kumwona Mungu kabla ya kupogolewa au kupitia hukumu, basi bila shaka utakuwa mpinzani wa Mungu na utakuwa katika njia ya kuangamizwa. Asili ya mwanadamu kwa kawaida ina uhasama kwa Mungu, kwa kuwa watu wote wamepotoshwa kabisa na shetani. Hakuna kizuri kinachoweza kupatikana kwa mtu kujaribu kushirikiana na Mungu kutokana na upotovu wake, vitendo na maneno yake kwa hakika vitafichua upotovu wake kila wakati; na katika kushirikiana na Mungu, uasi wake utafichuka katika vipengele vyote. Binadamu, kwa kutojua anakuja anampinga Kristo, kumdanganya Kristo, na kumtelekeza Kristo; hili litakapofanyika, mwanadamu atakuwa katika hali ya hatari zaidi na, hili likiendelea, atapata adhabu.
Baadhi ya watu wanaweza kuamini kwamba, kama kushirikiana na Mungu ni hatari sana, basi huenda likawa jambo la busara zaidi kukaa mbali na Mungu. Ni nini watu kama hawa wanaweza kupokea? Je, wanaweza kuwa waaminifu kwa Mungu? Hakika, kushirikiana na Mungu ni kugumu sana, lakini hiyo hasa ni kwa sababu mwanadamu amepotoka na si kwa sababu Mungu hawezi kushiriki naye. Ingekuwa bora kwenu kuweka juhudi zaidi kwa ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata fadhili kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu ni chukizo sana Kwake? Kwa nini maneno yenu yanachochea chuki Yake? Punde ambapo mmeonyesha uaminifu kidogo, nyinyi mnajisifu wenyewe, na mnadai malipo kwa ajili ya mchango mdogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kumdharau Mungu baada ya kufanya kazi ndogo. Mnataka utajiri, zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kutendewa kwa heshima. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Kuna chochote kinachostahili sifa katika maneno na matendo yenu? Wale ambao wanatekeleza wajibu wao na wale wasiofanya; wale ambao huongoza na wale ambao hufuata; wale wanaompokea Mungu na wale wasiompokea; wale wanaotoa na wale wasiotoa; wale wanaohubiri na wale ambao hupokea neno, na kadhalika; watu wote kama hawa hujisifu wenyewe. Je, hamuoni hili likiwa la kuchekesha? Mkijua vyema kwamba mnamwamini Mungu, hata hivyo ninyi hamwezi kulingana na Mungu. Mkijua vyema kutostahili kwenu, mnaendelea bado kujigamba. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imepunguka kiasi kwamba hamwezi tena kujizuia? Na hisia kama hii, mnastahili vipi kushirikiana na Mungu? Je, kufikia hapa nyinyi hamjionei hofu? Tabia yenu tayari imepunguka kiasi kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Hali ikiwa hivi, je, imani yenu si ya kuchekesha? Imani yenu si ya kipuuzi? Ni jinsi gani utashughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kutembelea?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu,

Jumatatu, 18 Machi 2019

Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii moyoni mwake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni zozote, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi Anayofanya daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya utendaji kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake. Maarifa ya mwanadamu ya maisha yanakua hata juu zaidi, na vivyo hivyo kazi ya Mungu pia inakuwa juu zaidi. Mwanadamu anaweza kufikia ukamilifu kwa njia hii tu na kufaa kwa matumizi ya Mungu. Kwa upande mmoja, Mungu anafanya kazi hivi ili kupinga na kubadilisha fikira za mwanadamu, na kwa upande mwingine, kumwongoza mwanadamu katika hali ya juu zaidi na kweli zaidi, hadi katika ulimwengu wa juu zaidi wa imani katika Mungu, ili mwishowe, mapenzi ya Mungu yaweze kufanyika. Wote walio na asili isiyotii wanaopinga kwa kusudi wataachwa nyuma na hatua hii ya kazi ya Mungu ya haraka na yenye kusonga mbele kwa nguvu; wale tu walio na moyo mtiifu na wako tayari kuwa wanyonge wataendelea hadi mwisho wa njia. Katika kazi kama hii, nyote mnapaswa kujua jinsi ya kutii na kuweka kando fikira zenu. Mnapaswa kuwa waangalifu katika kila hatua mnayochukua. Kama wewe ni mzembe, hakika utakuwa mmoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na yule anayemkatiza Mungu katika kazi Yake. Kabla ya kufanyiwa hatua hii ya kazi, kanuni na sheria za mwanadamu za zamani zilikuwa nyingi sana hadi akawa na msisimko zaidi, na mwishowe, akawa mwenye majivuno na kujisahau. Hivi vyote ni vikwazo vinavyomzuia mwanadamu kuikubali kazi mpya ya Mungu; vinakuwa pingamizi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Iwapo mwanadamu hana utii katika moyo wake wala tamaa ya ukweli, basi atakuwa hatarini. Ukitii tu kazi na maneno yaliyo rahisi, na huwezi kukubali yoyote yaliyo na ugumu zaidi, basi wewe ni yule anayeendelea na njia za zamani na hawezi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa katika awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu ambaye ni mtiifu kwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima katika utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haikubaliki na Mungu. Kama huwezi kwenda sambamba na kazi mpya Ninayoshiriki na uendelee kuyashikilia maneno ya zamani, basi kutakuaje na ukuaji katika maisha yako? Kazi ya Mungu ni kukuruzuku kupitia neno Lake. Unapotii na kulikubali neno Lake, basi Roho Mtakatifu hakika atafanya kazi ndani yako. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa njia Ninayozungumza kabisa. Fanya Nilivyosema, na Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako mara moja. Natoa mwangaza mpya ili muweze kuona na kuwaleta kwa mwangaza wa wakati wa sasa. Unapotembea katika mwangaza huu, Roho Mtakatifu ataanza kazi ndani yako mara moja. Kuna wengine wanaoweza kuwa wakaidi na kusema, “Sitafanya tu usemavyo.” Basi Nakwambia kwamba sasa umefika mwisho wa njia umenyauka na huna maisha zaidi. Hivyo, kwa kupitia mabadiliko ya tabia yako, ni muhimu kabisa kwenda sambamba na mwangaza wa sasa. Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi ndani ya mtu mwingine ajaye. Fanya hima ufuate; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndivyo maisha yako yanaweza kuzidi kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Kwa kufanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu kwa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui ni kupitia kwa mtu wa aina gani ndiyo Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo ndiyo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani. Ukiweza kutembea kwenye njia hii sawa, hii inaonyesha kwamba kuna matumaini makubwa kwako kukamilishwa na Mungu. Kama huwezi kufanya hivyo, inaonyesha kwamba maisha yako ya baadaye ni ya dhalili na giza. Mara unapoendenda kwenye njia iliyo sahihi, utapata ufunuo katika mambo yote. Bila kujali yale ambayo Roho Mtakatifu atafichua kwa wengine, ukiendelea kupitia mambo wewe mwenyewe kwa msingi wa maarifa yao, basi uzoefu huu utakuwa sehemu ya maisha yako, na utaweza kuwakimu wengine kwa sababu ya huu uzoefu. Wale wanaowakimu wengine kwa kuyarudia maneno ni wale wasio na uzoefu wowote; lazima ujifunze kupata, kupitia mwangaza na nuru ya wengine, njia ya kutenda kabla ya kuzungumza kuhusu uzoefu na maarifa yako halisi. Hii itakuwa ya manufaa zaidi kwa maisha yako binafsi. Unapaswa kuwa na uzoefu kwa njia hii, kutii yote yatokayo kwa Mungu. Unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu katika vitu vyote na kujifunza masomo katika vitu vyote, ukijenga ukuaji kwa maisha yako. Vitendo vya aina hii huleta ukuaji wa haraka zaidi.
Roho Mtakatifu anakupa nuru kupitia uzoefu wa vitendo vyako na kukukamilisha kupitia imani yako. Uko tayari kweli kukamilishwa? Kama kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu, basi utakuwa na ujasiri kuweka kando mwili wako, na utaweza kutekeleza maneno ya Mungu na kutokuwa mtu anayekaa tu ama mnyonge. Utaweza kutii yote yatokayo kwa Mungu, na vitendo vyako vyote, viwe vimefanywa hadharani au faraghani, vitastahiki kwa Mungu. Kama wewe ni mtu mwaminifu, na unatenda ukweli katika mambo yote, basi utakamilishwa. Wale wanadamu wadanganyifu wanaotenda njia moja mbele ya wengine na nyingine nyuma yao hawako tayari kukamilishwa. Wote ni wana wa maangamizo na uharibifu; wao si wa Mungu lakini ni wa Shetani. Hao si aina ya wanadamu waliochaguliwa na Mungu! Kama vitendo na tabia yako haviwezi kustahiki mbele ya Mungu ama kufikiriwa na Roho wa Mungu, hii ni thibitisho kwamba wewe una shida. Ukikubali tu hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kuweka umuhimu katika mabadiliko ya tabia yako ndipo utafika kwenye njia ya kukamilishwa. Ikiwa kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu na kufanya mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kutii kazi yote ya Mungu na kutotoa neno lolote la kulalamika, wala hupaswi kutathmini ama kuhukumu kazi ya Mungu utakavyo. Haya ni masharti ya msingi kabisa ya kukamilishwa na Mungu. Mahitaji ya lazima kwa wale wanaotaka kukamilishwa na Mungu ni haya: fanya mambo yote kwa moyo unaompenda Mungu. Inamaanisha nini “kufanya mambo kwa moyo unaompenda Mungu”? Inamaanisha kwamba vitendo na tabia yako yote inaweza kuletwa mbele ya Mungu. Kwa sababu una nia sawa, iwapo vitendo vyako ni sawa ama vibaya, huogopi vikionyeshwa kwa Mungu ama kwa ndugu zako; unathubutu kuapa mbele ya Mungu. Kwamba kila nia, fikra, na wazo lako linaweza kufaa kuchunguzwa mbele ya Mungu: ukitenda na kuingia kwa njia hii, basi maendeleo katika maisha yako yatakuwa mepesi.
Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu? Hata wale walio tu na moyo nusu wa utii hawawezi kutembea hadi mwisho, sembuse hawa wadhalimu wasio na utii hata kidogo kwa mioyo yao. Kazi ya Mungu haipatwi virahisi na mwanadamu. Hata mwanadamu akitumia nguvu yake yote, ataweza kupata kipande tu na kufikia ukamilifu mwishowe. Na vipi basi kuhusu watoto wa malaika mkuu wanaotaka kuharibu kazi ya Mungu? Je, hawana hata matumaini madogo zaidi ya kupatwa na Mungu? Madhumuni Yangu katika kufanya kazi ya ushindi si tu kushinda kwa sababu ya ushindi, lakini kushinda ili kufichua haki na udhalimu, kupata ushahidi kwa ajili ya adhabu ya mwanadamu, kulaani waovu, na hata zaidi, kushinda kwa sababu ya kuwakamilisha wale walio radhi kutii. Mwishowe, wote watatengwa kulingana na aina, na mawazo ya wale wote waliokamilishwa yatajazwa na utii. Hii ndiyo kazi itakayokamilishwa mwishowe. Lakini waliojawa na uasi wataadhibiwa, kutumwa kuchomeka motoni na milele kulaaniwa. Wakati huo utakapofika, wale “mashujaa wakubwa wasioshindwa” wa awali watakuwa “waoga wanyonge na wasio na maana” wa chini zaidi na wanaoepukwa zaidi. Hii tu ndiyo inaweza kuonyesha kila kipengele cha haki ya Mungu na kufichua tabia Yake ambayo hairuhusu kosa lolote. Hili tu ndilo linaloweza kutuliza chuki iliyo moyoni Mwangu. Je, hamkubali kwamba hili ni la busara sana?
Sio wote walio na uzoefu wa kazi ya Roho Mtakatifu wanaweza kupata uzima, na sio wote katika mkondo huu wanaweza kupata uzima. Uzima sio mali ya kawaida inayoshirikisha binadamu wote, na mabadiliko ya tabia ni kitu ambacho hakifikiwi na wote kwa urahisi. Kujisalimisha kwa kazi ya Mungu lazima kugusike na kuishi kwa kudhihirishwa. Kujisalimisha kwa kiwango cha juu juu hakuwezi kupokea idhini ya Mungu, na kutii tu vipengele vya juujuu vya neno la Mungu bila kutaka mgeuzo wa tabia ya mtu, hakutaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Utiifu kwa Mungu na kujinyenyekeza kwa kazi ya Mungu ni kitu kimoja. Wale wanaomtii Mungu tu lakini hawatii kazi Yake hawawezi kudhaniwa kuwa watiifu, sembuse wale wasiotii kwa kweli na kwa nje hao ni wa kujipendekeza. Wale ambao kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu wote wanaweza kufaidika kutokana na kazi na kupata ufahamu wa tabia na kazi ya Mungu. Wanadamu kama hawa tu ndio kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu. Wanadamu kama hawa wanaweza kupata maarifa mapya kutokana na kazi mpya na kuwa na uzoefu wa mabadiliko mapya kutoka hayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wana idhini ya Mungu; mwanadamu wa aina hii tu ndiye amekamilishwa, ndiye amepitia mabadiliko ya tabia yake. Wale wanaopokea idhini ya Mungu ni wale wanaojisalimisha kwa Mungu kwa furaha, na pia kwa neno na kazi Yake. Mwanadamu wa aina hii tu ndiye yuko sahihi; mwanadamu wa aina hii tu ndiye kweli anamtamani Mungu, na anamtafuta Mungu kwa dhati. Na kwa wale wanaozungumzia tu imani yao kwa Mungu kwa vinywa vyao lakini kwa hakika wanamlaani, ni wanadamu waliovaa barakoa, walio na sumu ya nyoka, ni wanadamu wasaliti zaidi. Siku moja hawa waovu watavuliwa barakoa zao mbovu. Je, hiyo si kazi inayofanywa leo? Wanadamu waovu daima watakuwa waovu na hawataepuka kamwe siku ya adhabu. Wanadamu wazuri daima watakuwa wazuri na watafichuliwa kazi itakapoisha. Hakuna hata mmoja wa waovu atakayedhaniwa kuwa wenye haki, wala yeyote mwenye haki atakayedhaniwa kuwa mwovu. Je, Ningemruhusu yeyote ashtakiwe kimakosa?
Maisha yako yanapoendelea, lazima daima uwe na kiingilio kipya na ufahamu mpya na wa juu zaidi, unaokua kwa kina na kila hatua. Hiki ndicho wanadamu wote wanapaswa kuingia ndani. Kupitia kuwasiliana, kusikiliza ujumbe, kusoma neno la Mungu, ama kushughulikia suala, utapata ufahamu mpya na kupata nuru upya. Huishi ndani ya kanuni za zamani na nyakati za zamani. Unaishi daima ndani ya mwangaza mpya, na hupotei mbali na neno la Mungu. Huku ndiko kunaitwa kwenda katika njia sahihi. Kulipa tu gharama ya juu juu hakutakubalika. Siku baada ya siku, neno la Mungu linaingia katika ulimwengu wa juu zaidi na mambo mapya yanajitokeza kila siku. Ni muhimu pia kwa mwanadamu kuingia upya kila siku. Mungu anavyozungumza, ndivyo Anavyotimiza yote ambayo Amezungumza; kama huwezi kwenda sambamba, basi unabaki nyuma. Lazima uende kwa kina zaidi katika maombi yako; kula na kunywa neno la Mungu hakuwezikuwa kunakosa mfululizo. Imarisha nuru na mwangaza unayopokea, ufunuo unaopokea, na dhana zako na fikira zako lazima zipungue hatua kwa hatua. Lazima pia uimarishe hekima yako, na chochote unachopitia, lazima uwe na mawazo yako kukihusu na uwe na mtazamo wako.Kwa kuelewa mambo fulani katika roho, lazima upate ufahamu wa mambo ya nje na kuelewa kiini cha suala lolote. Kama hujajiandaa na mambo haya, utawezaje kuliongoza kanisa? Iwapo unazungumzia tu barua na mafundisho ya dini bila uhalisi wowote na bila njia ya kutenda, unaweza tu kuendelea kwa muda mfupi. Inaweza kukubalika kidogo kwa waumini wapya, lakini baada ya muda, wakati waumini wapya wanapata tajriba halisi, basi hutaweza tena kuwakimu. Basi unafaa vipi kwa matumizi ya Mungu? Bila kupata nuru upya, huwezi kufanya kazi. Walio bila nuru upya ni wale wasiojua jinsi ya kuwa na uzoefu, na wanadamu kama hao kamwe hawapati maarifa mapya ama tajriba. Na katika suala la kuleta maisha, hawawezi kamwe kufanya jukumu lao la kusambaza uhai, wala hawawezi kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu. Mwanadamu kama huyu ni dhaifu na hana maana. Kwa kweli, wanadamu kama hawa hawawezi kufanya jukumu lao kabisa kwa kazi na wote hawana faida. Wanashindwa kufanya jukumu lao na pia kwa kweli wanaweka mzigo mwingi usiohitajika juu ya kanisa. Nawahimiza hawa “wanaume wazee” kuharakisha na kuondoka kanisani ili wengine wasilazimishwe kuwaona tena. Wanadamu kama hawa hawaelewi kazi mpya lakini wamejawa na fikira zisizokoma. Hawafanyi chochote kanisani; badala yake, wanachochea na kusambaza uhasi kila pahali, hata kushiriki katika kila namna ya utovu wa nidhamu na vurugu kanisani, na hivyo kuwarusha wale wasiobagua katika vurugu na machafuko. Haya ibilisi wanaoishi, hawa mapepo mabaya wanapaswa kuondoka kanisani haraka iwezekanavyo, kanisa lisije likaharibiwa kwa sababu yako. Labda huogopi kazi ya leo, lakini huogopi adhabu ya haki ya kesho? Kuna idadi kubwa ya watu kanisani ambao ni vimelea, na pia kuna idadi kubwa ya mbwa mwitu wanaotafuta kuvuruga kazi ya kawaida ya Mungu. Vitu hivi vyote ni mapepo yaliyotumwa na Ibilisi, ni mbwa mwitu wakali wanaotafuta kuwala kondoo wasio na hatia. Iwapo wanadamu kama hawa hawatafukuzwa, basi wanakuwa vimelea kwa kanisa na nondo wanaokula sadaka. Hawa mabuu wenye kudharauliwa wajinga, duni, na wenye kuchukiza wataadhibiwa siku moja karibuni!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumamosi, 16 Machi 2019

Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

Mwenyezi Mungu alisema, Mnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu. Ikiwa unamwamini tu Mungu lakini humpendi, hujapata ufahamu wa Mungu, na hujawahi kumpenda Mungu kwa upendo wa kweli utokao moyoni mwako, basi imani yako kwa Mungu ni bure; kama katika imani yako kwa Mungu humpendi Mungu, basi unaishi bure, na maisha yako yote ndiyo ya duni zaidi kwa maisha yote. Ikiwa katika maisha yako yote hujawahi kumpenda au kumtosheleza Mungu, basi kuna haja gani ya kuishi? Kuna haja gani ya imani yako kwa Mungu? Huku si kuharibu nguvu? Hii ni kusema, kama watu wanataka kuamini na kumpenda Mungu, ni sharti wagharamike. Badala ya kujaribu kuenenda kwa namna fulani kwa nje tu, wanapaswa watafute utambuzi wa kweli kutoka ndani ya mioyo yao. Ikiwa unapenda sana kuimba na kucheza lakini huwezi kuonyesha ukweli katika vitendo, unaweza kusemekana kwamba unampenda Mungu? Kumpenda Mungu kunahitaji utafutaji wa mapenzi ya Mungu katika mambo yote, na kwamba ujisaili wewe mwenyewe kwa kina jambo lolote likikutokea, kujaribu kujua mapenzi ya Mungu na kujaribu kuona mapenzi ya Mungu ni yapi katika suala hili, Anataka ufanikishe nini, na ni jinsi gani utayajali mapenzi Yake? Kwa mfano: jambo fulani linafanyika linalokutaka uvumilie hali ngumu, wakati huo unapaswa ufahamu ni nini mapenzi ya Mungu, na ni jinsi gani unapaswa kuyajali mapenzi ya Mungu. Usijiridhishe mwenyewe: Jiweke kando kwanza. Hakuna kitu kilicho duni kuliko mwili. Ni lazima udhamirie kumridhisha Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako. Katika mawazo kama hayo, Mungu atakupa nuru ya kipekee katika jambo hili, na moyo wako pia utapata faraja. Jambo lolote likikutendekea, liwe dogo au kubwa, ni sharti kwanza ujiweke pembeni na kuuona mwili kama kitu duni zaidi kuliko vitu vyote. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo unavyochukua uhuru zaidi; ukiuridhisha mara hii, wakati mwingine utataka zaidi, na jinsi hili linaendelea, ndivyo unapata kuupenda mwili hata zaidi. Mwili mara zote una tamaa kupita kiasi, mara zote mwili unakutaka uuridhishe, na kwamba uutosheleze kwa ndani, iwe ni katika chakula unachokula, unachokivaa, au kuwa na hasira katika matendo yako, au kuushawishi udhaifu na uzembe wako… Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo tamaa yake inaongezeka, na jinsi mwili unavyopotoka zaidi, hadi kufikia kiwango ambacho miili ya watu inahodhi dhana nzito, na kutomtii Mungu, na kujiinua, na kuanza kuishuku kazi ya Mungu. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo udhaifu wa mwili unavyokuwa mkubwa; daima utahisi kuwa hakuna anayekuonea huruma kwa udhaifu wako, daima utaamini kuwa Mungu amezidi sana, na utasema: Mungu anawezaje kuwa mkali namna hii? Ni kwa nini Hawezi kuwapa watu nafasi? Watu wakiudekeza sana mwili, na kuupenda kupindukia, basi watajiponza wao wenyewe. Ikiwa unampenda Mungu kwa dhati, na huuridhishi mwili, basi utaona kuwa kila anachokifanya Mungu ni chenye haki sana, na kizuri sana, na kwamba laana Yake kwa uasi wako na hukumu ya udhalimu wako ni haki. Zitakuwepo nyakati ambapo Mungu atakurudi na kukufundisha nidhamu, na kuanzisha mazingira ya kukukasirisha, na kukushurutisha uje mbele Zake—na daima utahisi kuwa anachokifanya Mungu ni cha ajabu. Hivyo utahisi kana kwamba hakuna uchungu mwingi, na kwamba Mungu anapendeza. Ukifuata udhaifu wa mwili, na kusema kwamba Mungu amezidi, basi daima utahisi uchungu na daima utahuzunika, na utakosa uwazi kuhusu kazi yote ya Mungu na itaonekana kana kwamba Mungu hana huruma kwa udhaifu wa mwanadamu, na Hatambui shida za mwanadamu. Hivyo utajihisi mnyonge na mpweke, kana kwamba umekumbwa na dhuluma kubwa, na wakati huo utaanza kulalama. Kadiri unavyoutosheleza udhaifu wa mwili, ndivyo unavyohisi kuwa Mungu anazidi, hadi inakuwa mbaya kiasi kwamba unaikana kazi ya Mungu, na kuanza kumpinga Mungu na kujaa uasi. Hivyo unafaa kuuasi mwili na usiutosheleze: “Mume wangu(mke), watoto, matarajio, ndoa, familia—hakuna hata moja kati ya haya ambalo ni la thamani! Moyoni mwangu mna Mungu pekee na nitajaribu kumridhisha Mungu kadiri ya uwezo wangu, na si kuuridhisha mwili.” Lazima uwe na azimio hili. Daima ukiwa na azimio hili, basi ukiuweka ukweli katika vitendo, na kujiweka kando, utaweza kufanya hivyo kwa juhudi kidogo. Inasemekana kuwa kulikuwepo na mkulima aliyeona nyoka barabarani aliyekuwa ameganda. Huyu mkulima alimchukua yule nyoka na kumweka kifuani mwake, na baada ya yule nyoka kuamka alimuuma yule mkulima hadi akafa. Miili ya wanadamu ni kama yule nyoka: asili yake ni kuyadhuru maisha yao—na ikipata mbinu yake kikamilifu, maisha yako yanapotea. Mwili ni wa Shetani. Kuna tamaa kupita kiasi ndani yake, hujithamini wenyewe, unafurahia faraja, na kushangilia burudani, kujiachilia katika uvivu na uzembe, na baada ya kuuridhisha kwa kiwango fulani mwishowe utakuangamiza. Hivi ni kusema, ukiuridhisha sasa, wakati mwingine utakuomba zaidi. Daima mwili una tamaa na matakwa kupita kiasi, na unajinufaisha kutokana na wewe kuutosheleza mwili na kukufanya uufurahie hata zaidi na kuishi katika starehe zake—na ikiwa hutaushinda, mwishowe utajipotosha. Iwapo utapata uzima mbele za Mungu, na namna hatima yako itakavyokuwa, inategemea uasi wako dhidi ya mwili utakuwa wa namna gani. Mungu amekuokoa, na kukuteua na kukuamulia kabla, bado ikiwa leo hauko radhi kumridhisha, hauko radhi kuuweka ukweli katika vitendo, hauko radhi kuuasi mwili wako kwa moyo umpendao Mungu kwa dhati, hatimaye utajiangamiza mwenyewe, na kwa hivyo utapitia mateso mengi. Ikiwa mara zote unautosheleza mwili, Shetani atakumeza hatua kwa hatua, na kukuacha bila uzima, au upako wa Roho, hadi siku itafika ambayo ndani utakuwa giza. Ukiishi katika giza, utakuwa umetekwa nyara na Shetani, hutakuwa na Mungu tena moyoni mwako, na wakati ule utaukataa uwepo wa Mungu na kumwacha. Kwa hivyo, ikiwa unataka kumpenda Mungu, ni lazima ulipe gharama ya uchungu na kupitia shida. Hakuna haja ya hamasa za nje na shida, kusoma zaidi na kuzungukazunguka zaidi; badala yake, unafaa kuweka kando vitu vilivyomo ndani yako: mawazo kupita kiasi, maslahi ya kibinafsi, na masuala yako binafsi, dhana, na motisha. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.
Ushughulikiaji wa Mungu juu ya tabia za nje za watu ni sehemu moja ya kazi Yake; kwa mfano, kushughulikia ubinadamu wa watu wa nje, usiokuwa wa kawaida, au maisha na tabia zao, njia na desturi zao, na vilevile vitendo vyao vya nje, na hamasa zao. Lakini Anapowataka watu wauweke ukweli katika vitendo na wabadilishe tabia zao, kimsingi kinachoshughulikiwa hapa ni motisha na mawazo yaliyo ndani yao. Kushughulikia tabia zako za nje tu si kugumu; ni sawa na kukukataza kula vitu uvipendavyo, jambo ambalo ni rahisi. Kinachogusia dhana zilizo ndani yako, hata hivyo, si rahisi kukiachia: inakuhitaji uuasi mwili wako, na kulipa gharama, na kuteseka mbele za Mungu. Hii ndiyo hali hasa katika motisha za watu. Tangu wakati wa imani yao kwa Mungu mpaka leo, watu wamekuwa na motisha ambazo si sahihi. Wakati ambapo huweki ukweli katika vitendo, unahisi kuwa motisha zako ni sahihi, lakini jambo likikutokea, utaona kuwa kuna motisha nyingi ndani zisizo sahihi. Hivyo, Mungu akiwafanya watu kuwa wakamilifu, Anawafanya kugundua kuwa kuna dhana nyingi ndani yao ambazo zinawazuia kumfahamu Mungu. Ukitambua kuwa motisha zako zina makosa, kama unaweza kuacha kutenda kulingana na motisha na dhana zako, na unaweza kuwa na ushuhuda wa Mungu na kusimama imara katika msimamo wako kwa kila lifanyikalo kwako, hili linathibitisha kuwa umeuasi mwili wako. Ukiasi dhidi ya mwili wako, bila shaka kutakuwa na vita ndani yako. Shetani atajaribu kufanya watu kuifuata, atajaribu kuwafanya wafuate dhana za kimwili na kutekeleza maslahi ya kimwili—ila maneno ya Mungu yatawapa nuru watu na kuwaangazia kwa ndani, na wakati huu itakuwa juu yako ikiwa utamfuata Mungu au utamfuata Shetani. Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu huwagusa watu ndani ya mioyo yao, na kuwapa nuru na mwangaza. Kwa hivyo katika tukio lolote katika vita: Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie. Kwa sababu motisha nyingi ndani ya watu zina makosa, ama kwa sababu kazi kubwa ya Mungu inakinzana na dhana zao, watu wakiuweka ukweli katika vitendo vita vikali huzuka kisirisiri. Baada ya kuuweka huu ukweli katika vitendo, kisirisiri watu watakuwa wamemwaga machozi mengi sana ya huzuni kabla ya kuamua kumridhisha Mungu. Ni kwa sababu ya vita hivi watu huvumilia shida na usafishaji; huku ni kuteseka kwa kweli. Vita vikikukabili, kama unaweza kusimama kweli upande wa Mungu, utaweza kumridhisha. Kuteseka katika harakati ya kutenda ukweli hakuepukiki; ikiwa, wanapoweka ukweli katika vitendo, kila kitu ndani yao kingekuwa sawa, basi wasingehitaji kufanywa wakamilifu na Mungu, na kusingekuwa na vita, na hawangeteseka. Ni kwa sababu kuna mambo mengi ndani ya watu ndipo hawafai kutumiwa na Mungu, na tabia nyingi za uasi wa mwili, ndipo watu wanapaswa kujifunza funzo la kuasi dhidi ya mwili kwa kina zaidi. Huku ndiko Mungu anaita kuteseka ambako Alimtaka mwanadamu kushiriki Naye. Ukikumbana na shida, fanya hima na umwombe Mungu: Ee Mungu! Ninataka kukuridhisha, ninataka kustahimili mateso ya mwisho ili kuuridhisha moyo Wako, na bila kujali kuwa vikwazo ninavyokumbana navyo ni vikubwa kiasi gani, bado ni sharti nikuridhishe. Hata ikiwa ni kuyatoa maisha yangu yote, bado ni sharti nikuridhishe! Ukiomba na hili azimio utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako. Kila wawekapo ukweli katika vitendo, kila wapitiapo usafishaji, kila wanapojaribiwa, na kila wakati kazi ya Mungu inapowashukia, watu wanapitia mateso makubwa. Haya yote ni mtihani wa watu, na kwa hivyo ndani yao wote mna vita. Hii ndiyo gharama hasa wanayolipa. Kusoma zaidi neno la Mungu na kuzungukazunguka zaidi, kwa namna fulani ni gharama. Ndiyo watu wanapaswa kufanya, ndio wajibu wao, na jukumu ambalo ni sharti walitimize, lakini ni lazima watu waweke kando yale yanayofaa kuwekwa kando. Ikiwa hamwezi, basi haijalishi mateso yako yatakuwa makubwa kiasi gani, na utazunguka kiasi gani, yote yatakuwa bure! Hivi ni kusema, ni mabadiliko ndani yako tu yanaweza kuamua iwapo mateso yako ya nje yana thamani. Tabia yako ya ndani ikibadilika na ikiwa umeweka ukweli katika vitendo, basi mateso yako yote ya nje yatapata kibali cha Mungu; ikiwa hakujakuwa na mabadiliko katika tabia yako ya ndani, basi haijalishi unateseka kiasi gani au unazungukazunguka kiasi gani nje, hakutakuwa na kibali kutoka kwa Mungu—na mateso ambayo hayajaidhinishwa na Mungu ni bure! Hivyo, kama gharama ambayo umelipa imedhinishwa na Mungu inaamuliwa na kama umekuwa na mabadiliko ndani yako au la, na kama unatia ukweli katika vitendo na kuasi dhidi ya motisha na dhana zako mwenyewe ili kupata ridhaa ya mapenzi ya Mungu, ufahamu wa Mungu, na uaminifu kwa Mungu. Haijalishi unazungukazunguka kiasi gani, ikiwa hujawahi kujua kuasi dhidi ya motisha zako, unatafuta tu matendo na hamasa za nje, na usitilie maanani maisha yako, basi taabu zako zitakuwa zimepita bure. Ikiwa una kitu unachotaka kusema katika mazingira fulani, ila kwa ndani huhisi ni sawa, kwamba hakina faida kwa ndugu na dada zako, na kinaweza kuwadhuru, basi na usikiseme, uchague kuumia kwa ndani, kwa kuwa haya maneno hayawezi kuridhisha mapenzi ya Mungu. Wakati huu, kutakuwa na vita ndani yako, lakini utakuwa tayari kuumia na kuviacha uvipendavyo, utakuwa radhi kustahimili haya mateso ili kumridhisha Mungu na ingawa utaumia kwa ndani, hutautosheleza mwili, na moyo wa Mungu utakuwa umeridhishwa, hivyo utafarijika kwa ndani. Kwa hakika huku ni kulipa gharama, na ndiyo gharama inayotakiwa na Mungu. Ukitenda kwa njia hii, kwa hakika Mungu atakubariki; ikiwa huwezi kulifanikisha hili, basi haijalishi unaelewa kiasi gani, au unaweza kunena vyema kiasi gani, yote haya hayatafaa kitu! Katika njia ya kumpenda Mungu, ikiwa unaweza kusimama upande wa Mungu anapopigana na Shetani, na usimgeukie Shetani, basi utakuwa umefanikisha mapenzi ya Mungu, na utakuwa umesimama imara katika ushuhuda wako.
Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. Kwa mfano, ikiwa unawabagua ndugu na dada zako, utakuwa na maneno ambayo unataka kusema—maneno unayohisi huenda yasimpendeze Mungu—lakini usipoyasema, utahisi kutoridhika ndani, na kwa wakati huu vita vitazuka ndani yako: “Niseme au nisiseme?” Hivi ndivyo vita. Kwa hivyo, katika kila jambo unalopitia kuna vita, na wakati kuna vita ndani yako, kutokana na ushirikiano wako na kuteseka kwako, Mungu anafanya kazi ndani yako. Hatimaye unaweza kuliweka kando jambo lenyewe na ghadhabu yako inazimika. Hiyo ndiyo athari ya ushirika wako na Mungu. Kila kitu wafanyacho watu kinawahitaji kulipa gharama fulani katika juhudi zao. Bila taabu ya kweli, hawawezi kumridhisha Mungu, hata hawakaribii kumridhisha Mungu, na wanarusha tu maneno matupu! Je, haya maneno matupu yaweza kumridhisha Mungu? Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda. Kwa nje yataonekana kama mambo madogo; lakini haya mambo yakitendeka huonyesha kama unampenda Mungu au la. Ikiwa unampenda, utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako Kwake, na ikiwa hujaweka upendo Wake katika vitendo, hili linaonyesha kuwa wewe si Mtu ambaye anapenda kuuweka ukweli katika vitendo, kwamba huna ukweli, huna uzima, kuwa wewe ni makapi! Mambo huwatokea watu wakati Mungu anawataka wasimame imara katika ushuhuda wao Kwake. Hakuna kubwa lililokutendekea kwa sasa, na huna ushuhuda mkubwa, lakini kila chembe ya maisha yako ya kila siku inahusiana na ushuhuda kwa Mungu. Ikiwa utawavutia ndugu na dada zako, wanafamilia, na kila aliye karibu nawe; ikiwa siku moja wasioamini watakuja na wavutiwe na yote unenayo na utendayo, na kuona kuwa yote afanyayo Mungu ni ya ajabu, basi utakuwa umekuwa na ushuhuda. Ijapokuwa huna ufahamu na wewe si mwerevu sasa, kupitia kwa kufanywa mkamilifu na Mungu, unaweza kumridhisha na kuzingatia mapenzi Yake. Wengine wataona kazi Yake kubwa miongoni mwa wasio werevu. Watu huja kumjua Mungu na huwa washindi mbele ya Shetani na waaminifu kwa Mungu kwa kiwango fulani. Hakuna atakayekuwa na uthabiti kuliko hili kundi la watu. Huu utakuwa ushuhuda mkubwa zaidi. Ijapokuwa huwezi kufanya kazi kubwa, unaweza kumridhisha Mungu. Wengine hawawezi kuyaacha mawazo yao, ila wewe unaweza; wengine hawawezi kuwa na ushuhuda kwa Mungu wakati wa mapito yao ya kweli, ila unaweza kutumia hadhi na matendo yako ya kweli kulipia mapenzi ya Mungu na kuwa na ushuhuda mkubwa Kwake. Hili ndilo huhesabika kama mapenzi ya kweli kwa Mungu. Ikiwa huliwezi hili, basi hutoi ushuhuda miongoni mwa jamaa zako, miongoni mwa ndugu zako, miongoni mwa dada zako, au mbele ya walimwengu. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda mbele ya Shetani, Shetani atakucheka, atakuchukulia kama mzaha, mwanasesere, mara kwa mara atakuchezea na kukughadhibisha. Majaribu mengi yatakupata siku za usoni—lakini ikiwa leo unampenda Mungu kwa moyo wa dhati, na ikiwa haijalishi ukubwa wa majaribu yaliyo mbele, bila kujali unachokipitia, unaweza kusimama imara katika ushuhuda wako, na kuweza kumridhisha Mungu, basi moyo wako utafarijiwa, na utakuwa jasiri hata majaribu utakayokabiliana nayo siku za usoni yawe makubwa kiasi gani. Hamwezi kuona ni nini kitatendeka siku za usoni; mnaweza tu kuridhisha Mungu katika hali ya leo. Hamwezi kufanya kazi yoyote kubwa, na unafaa kulenga kumridhisha Mungu kwa kuyapitia maneno yake katika maisha halisi, na kuwa na ushuhuda thabiti na mzito ambao unamtia aibu Shetani. Japo mwili wako hautaridhishwa na utateseka, utakuwa umemridhisha Mungu na kumletea aibu Shetani. Ikiwa daima unatenda hivi, Mungu atakufungulia njia mbele yako. Na siku moja, jaribio kubwa likija, wengine wataanguka chini, ila utaweza kuendelea kusimama imara: kwa sababu ya gharama uliyolipa, Mungu atakulinda ili usimame imara na usianguke. Kwa kawaida, ikiwa unaweza kuweka ukweli katika vitendo na kumridhisha Mungu kwa moyo ambao unampenda kweli, kwa hakika Mungu atakulinda wakati wa majaribu ya siku zijazo. Japokuwa wewe ni mpumbavu na mwenye kimo cha chini na usiye mwerevu, Mungu hatakubagua. Inategemea iwapo motisha zako ni za haki. Unaweza kumridhisha Mungu leo, iwapo uko makini na masuala madogo, unamridhisha Mungu kwa mambo yote, una moyo unaompenda Mungu kwa dhati, unampa Mungu moyo wa dhati, na japokuwa kuna baadhi ya mambo ambayo huwezi kuelewa, unaweza kwenda mbele za Mungu kurekebisha motisha zako, na kuyafuata mapenzi ya Mungu, na kufanya kila lipaswalo kumridhisha Mungu. Pengine ndugu na dada zako wataachana nawe, lakini moyo wako utakuwa unamridhisha Mungu, na hutatamani raha za mwili. Ikiwa daima unatenda kwa namna hii, utalindwa majaribu yakikusibu.
Majaribu haya yanailenga hali gani ya ndani ya watu? Yanalenga tabia ya uasi ndani ya watu ambayo haiwezi kumridhisha Mungu. Kuna mengi ambayo ni machafu ndani ya watu, na mengi ambayo ni ya unafiki, na kwa hivyo Mungu anawatia katika majaribu ili kuwasafisha. Lakini, ikiwa leo unaweza kumridhisha, basi majaribu ya siku zijazo yatakuwa ukamilifu kwako. Ikiwa leo, huwezi kumridhisha Mungu, basi majaribu ya siku za usoni yatakushawishi, na utaanguka bila kujua, na wakati huo hutaweza kujisaidia mwenyewe, kwani huendani na kazi ya Mungu, na huna kimo halisi. Na kwa hivyo, kama unataka kuweza kusimama imara katika siku za usoni, kumridhisha vyema Mungu, na kumfuata hadi mwisho, unapaswa kujenga msingi thabiti leo, unafaa kumridhisha Mungu kwa kutia ukweli katika vitendo kwa kila jambo, na kuzingatia mapenzi Yake. Iwapo daima unatenda kwa namna hii, kutakuwa na msingi ndani yako, na Mungu atahamasisha ndani yako moyo unaompenda, na Atakupa imani. Siku moja ambapo majaribu yatakuwa yamekukumba kwa kweli, ijapo utaumia, na kuhisi umedhulumiwa kwa kiwango fulani, na kuwa na huzuni kubwa, kana kwamba ulikuwa umekufa—ila mapenzi yako kwa Mungu hayatabadilika, na yataongezeka zaidi. Hizo ni baraka za Mungu. Ikiwa unaweza kumkubali Mungu na yote asemayo na atendayo leo kwa moyo mtiifu, basi kwa hakika utabarikiwa na Mungu, na kwa hivyo utakuwa mtu aliyebarikiwa na Mungu, na anayepokea ahadi Yake. Ikiwa leo hutendi, siku ambayo majaribu yatakukumba utakosa imani au moyo wenye mapenzi, na wakati huo jaribu litakuwa kishawishi; utatoswa ndani ya kishawishi cha Shetani na hutapata namna ya kuponyoka. Leo, unaweza kusimama imara jaribio dogo likikukabili, ila huenda usiweze kusimama imara siku ambayo jaribio kubwa litakukumba. Baadhi ya watu hujivuna, na kufikiri kwamba wako karibu na ukamilifu. Ikiwa huzami zaidi wakati huo, na kuridhika, basi utakuwa hatarini. Leo, Mungu hafanyi kazi ya majaribu makubwa, kwa kuonekana, kila kitu kiko salama, ila Mungu atakapokujaribu, utagundua kuwa umepungukiwa sana, kwani kimo chako ni kidogo mno, na huna uwezo wa kustahimili majaribu mazito. Ikiwa leo, hutasonga mbele, ukibaki katika hatua ile ile, basi dhoruba nzito ikija utaanguka. Mara nyingi inafaa mtazame udogo wa kimo chenu; mtapiga hatua kwa njia hii tu. Ikiwa unauona udogo wa ukomavu wako wakati wa majaribu tu, kwamba kimo chako ni dhaifu, kwamba kuna kidogo sana ndani yako ambacho ni halisi, na kwamba hutoshi kwa mapenzi ya Mungu—na kama utagundua haya wakati wa majaribu tu, utakuwa umechelewa mno.
Ikiwa hujui tabia ya Mungu, bila shaka utaanguka wakati wa majaribu, kwa kuwa hufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu kuwa wakamilifu, na ni kwa njia gani Huwafanya wakamilifu, na majaribu ya Mungu yakikushukia na yasilingane na mawazo yako, utashindwa kusimama imara. Upendo wa kweli wa Mungu ni tabia Yake kamili, na tabia kamili ya Mungu ikionyeshwa kwako, hili linakuletea nini mwilini mwako? Tabia ya haki ya Mungu ikionyeshwa kwako, bila shaka mwili wako utapata uchungu mkubwa. Iwapo hutapata haya maumivu, basi huwezi kufanywa mkamilifu na Mungu, wala huwezi kumpa Mungu mapenzi ya kweli. Mungu akikufanya mkamilifu kwa hakika atakuonyesha tabia Yake kamili. Tangu uumbaji hadi leo, Mungu hajawahi kuonyesha tabia Yake kamili—ila katika siku za mwisho Anaifichua kwa hili kundi la watu ambao Aliwateua awali na kuwachagua, na kwa kuwafanya watu wakamilifu, Anaiweka wazi tabia Yake, na kupitia kwayo Analifanya kamili kundi la watu. Huo ndio upendo wa kweli wa Mungu kwa watu. Kuyapitia mapenzi ya kweli ya Mungu kunawapasa watu wastahimili uchungu mkali, na kulipa gharama kubwa. Ni baada tu ya hili ndipo watapatikana na Mungu na waweze kutoa tena mapenzi ya kweli kwa Mungu, na ni hapo tu ndipo Moyo wa Mungu utaridhishwa. Ikiwa watu wanataka wafanywe wakamilifu na Mungu, na kama wanataka kufanya na mapenzi Yake, na kumpa Mungu mapenzi yao ya dhati kikamilifu, ni sharti wapitie mateso mengi na maumivu makali kutokana na hali hizo, kupata uchungu mkali kuliko mauti, hatimaye watashurutishwa kuirejesha mioyo yao ya kweli kwa Mungu. Ikiwa mtu anampenda Mungu kwa dhati au la, itafichuliwa wakati wa shida na usafishaji. Mungu hutakasa mapenzi ya watu, na hili vilevile hupatikana tu ndani ya shida na usafishaji.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 19 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli. Wataweza tu kuzifundisha roho zao, kuifanya mioyo yao iweze kusonga kwa kawaida karibu na Mungu, na kupata kila mara furaha nyingi mno katika kuwa na Mungu. Watakuwa wamejiwekea mipaka kwa ulimwengu mdogo wa kuwa na mshikamano na Mungu, wasiweze kuelewa kile kilicho katika vina vya ndani kabisa. Watu ambao huishi katika mipaka hii pekee hawana uwezo wa kupiga hatua yoyote kubwa. Wakati wowote, wanaweza kulia, “Aa! Bwana Yesu. Amina!” Wanapokula, wao hulia, “Ee Mungu! Nala na Wewe unakula....” Na ni hivi karibu kila siku. Huu ni utendaji wa nyakati zilizopita, ni utendaji wa kuishi ndani ya roho kila wakati. Huo sio utovu wa adabu? Leo, kama ni wakati wa kutafakari juu ya maneno ya Mungu, unapaswa kuyatafakari, kama ni wakati wa kutia ukweli katika vitendo unapaswa kuuweka katika vitendo, na wakati ni muda wa kutekeleza wajibu wako, unapaswa kuutekeleza. Kufanya utendaji hivyo ni huru kabisa, kunakufungua wewe. Sio kama vile wazee wa dini huomba na kusema neema. Bila shaka, hapo awali, hivi ndivyo watu walioamini katika Mungu walitakiwa kutenda—lakini kutenda kwa njia hii kila mara ni kuliko nyuma kimaendeleo kabisa. Utendaji wa wakati uliopita ni msingi wa utendaji wa leo. Ikiwa kungekuwa na njia kwa utendaji wa nyakati zilizopita, utendaji wa leo utakuwa rahisi zaidi. Kwa hiyo, leo, tunapozungumza juu ya “kumleta Mungu katika maisha halisi,” ni hali gani ya utendaji inatajwa? “Maisha halisi” hasa yanahitaji watu wawe na ubinadamu wa kawaida; kile ambacho watu wanapaswa kuwa nacho ni kile ambacho Mungu anataka kutoka kwao leo. Kuyaleta maneno ya Mungu katika maisha halisi ndiyo maana halisi ya “kumleta Mungu katika maisha halisi.” Leo, watu wanapaswa hasa kujiandaa wenyewe na yafuatayo: Kuhusu suala moja, lazima waendeleze uhodari wao, wafunzwe, waongeze msamiati wao, na kuendeleza ustadi wao wa kusoma; na katika lingine, lazima waishi maisha ya watu wa kawaida. Umerudi tu mbele ya Mungu kutoka ulimwenguni, na lazima kwanza uifunze roho yako, kuufunza moyo wako kuwa na amani mbele ya Mungu. Hili ndilo la msingi kabisa, na pia ni hatua ya kwanza katika kutimiza mabadiliko. Watu wengine ni wepesi kubadilika katika utendaji wao; wao hutafakari ukweli huku wakifua nguo zao, wakielewa ukweli wanaopaswa kuelewa na kanuni wanazopaswa kuweka katika vitendo kwa uhalisi. Katika suala moja, lazima uwe na maisha ya kawaida ya ubinadamu, na katika lingine lazima kuwe na kuingia katika ukweli. Huu ni utendaji bora zaidi kwa maisha halisi.
Zamani, watu walipitia magumu mengi sana, lakini mengine yalikuwa yasiohitajika kwa kweli, kwani mengine yalikuwa mambo ambayo hayakuhitajika kutendwa na mwanadamu. Wanapomleta Mungu katika maisha yao halisi, Mungu kimsingi anahitaji kwamba watu wamwabudu Mungu, wafuatilie ufahamu wa Mungu, na kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu katikati ya ubinadamu wa kawaida. Hawahitajiki kumwomba Mungu mara tu wanapoanza kufagia sakafu, wakihisi ni wadeni Wake wasipofanya hivyo. Utendaji wa leo sio hivyo; ni uliolegezwa na rahisi! Watu hawaambiwi watii mafundisho ya dini. Kila mmoja anapaswa kutenda kulingana na kimo chake mwenyewe: Ikiwa mume wako haamini, mchukulie kama mtu asiyemwamini Mungu, na ikiwa yeye huamini mchukulie kama muumini. Usisisitize kuhusu upendo na uvumilivu, bali kuhusu hekima. Watu wengine huenda kununua mboga, na wanapokuwa wakitembea wao hunong’ona: Ee Mungu! Ni mboga gani ambazo unanikubalia ninunue leo? Naomba usaidizi Wako. Je, nichague ninaponunua? Kisha wao hufikiria: Sitachagua; Mungu ananiambia kwamba nimtukuze Yeye, kwamba nilitukuze jina Lake katika mambo yote, na kwamba watu wote wawe na ushuhuda, kwa hiyo muuzaji akinipa kitu fulani cha kitambo na kilichokauka, bado nitampa Mungu shukrani—nitavumilia! Sisi tuaminio katika Mungu hatuchagui ni mboga gani za kununua. Unafikiri kwamba kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na baada ya kutumia yuan[a] moja kununua mboga ya kitambo iliyo na kuvu, bado unaomba na kusema: Ee Mungu! Bado nitaila mboga hii iliyooza—maadamu Unikubali, nitaila. Je, utendaji kama huu sio wa kipumbavu? Je, huko sio kufuata mafundisho ya dini? Hapo awali, watu walizifundisha roho zao na waliishi ndani ya roho kila wakati, na hili lilihusiana na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Neema. Uchaji Mungu, unyenyekevu, upendo, uvumilivu, kutoa shukrani kwa mambo yote—haya ndiyo yaliyotakiwa kutoka kwa kila muumini katika Enzi ya Neema. Wakati huo, watu walimwomba Mungu katika mambo yote; wangeomba waliponunua nguo, na walipofahamishwa juu ya mkutano, pia wangeomba na kusema: Ee Mungu! Je, Unanikubalia niende au la? Ikiwa unanikubalia kwenda, basi nitayarishie njia iliyonyooka, acha kila kitu kifanyike kwa urahisi. Na ikiwa hunikubalii kwenda, basi nifanye nianguke chini. Walipoomba, walimsihi Mungu. Baada ya kuomba walihisi wasio na utulivu, na hawakuenda. Pia kulikuwa na dada ambao, kwa vile waliogopa kupigwa na waume wao wasiomwamini Mungu wakati ambapo wangerudi, walihisi wasio na utulivu walipoomba—na kwa vile walihisi wasio na utulivu, hawakuenda kwa mkutano. Waliamini hayo yalikuwa mapenzi ya Mungu, ilhali kweli ni kwamba, iwapo wangeenda, hakuna chochote ambacho kingefanyika. Matokeo ni kwamba walikosa mkutano. Haya yote yalisababishwa na ujinga wa watu wenyewe. Watu wanaofanya utendaji kwa njia hii huishi kwa hisia zao wenyewe. Njia hii ya utendaji ina kosa na ni ya kipumbavu, haina udhahiri, na hisia na mawazo yao wenyewe kwa wingi sana. Ukiambiwa kuhusu mkutano, basi nenda, na usipoambiwa, basi usiende; unapoambiwa kuuhusu, hakuna haja ya kumwomba Mungu. Je, hili si rahisi? Ikiwa, leo, unahitaji kununua kipande fulani cha mavazi, basi nenda ukafanye hivyo. Usimwombe Mungu na kusema: Ee Mungu! Leo napaswa kununua kipande fulani cha mavazi, je, Unanikubalia niende au la? Ni aina gani ya mavazi ninayopaswa kununua? Je dada mmoja akija hapa nikiwa nimeenda? Kwa kuomba na kutafakari, unajiambia mwenyewe: “Sitaki kwenda leo, huenda dada fulani akaja hapa.” Ilhali matokeo ni kwamba, kufikia jioni, hakuna aliyekuja hapo, na umekosa mengi. Hata katika Enzi ya Neema, njia hii ya utendaji ilikuwa na makosa na isiyo sahihi. Kwa hiyo, ikiwa watu watafanya utendaji kama katika nyakati zilizopita, hakutakuwa na mabadiliko katika maisha yao. Watakuwa tu watiifu, na hawatatilia maanani upambanuzi, na hawatafanya lolote ila kutii na kuvumilia pasipo kufikiria. Katika wakati huo, watu walisisitiza kuhusu kumtukuza Mungu—lakini Mungu hakupata utukufu wowote kutoka kwao, kwani hawakuwa wameishi kwa kudhihirisha lolote, na hawakuwa wamebadilika. Walijitiisha tu na kujiwekea mipaka wenyewe kulingana na dhana zao wenyewe, na hata miaka mingi ya utendaji haikuleta mabadiliko katika maisha yao; walijua tu kuvumilia, kuwa wanyenyekevu, kupenda, na kusamehe, na hawakupata nuru hata kidogo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Wangemjuaje Mungu?
Watu wataingia tu kwa njia sahihi ya imani katika Mungu ikiwa watamleta Mungu ndani ya maisha yao halisi, na katika maisha yao ya kawaida ya ubinadamu. Leo, maneno ya Mungu yanawaongoza ninyi, na hakuna haja ya kutafuta na kupapasa kama nyakati zilizopita. Wakati ambapo unaweza kutenda kulingana na maneno haya, na unaweza kujichunguza na kujitathmini mwenyewe kulingana na hali ambazo Nimetaja, basi utaweza kubadilika. Haya siyo mafundisho ya dini, lakini kile ambacho Mungu anamtaka mwanadamu afanye. Leo, Nakwambia kiini cha jambo: Jishughulishe tu na kutenda kulingana na maneno Yangu. Matakwa Yangu kwako ni kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, na Nimekwambia hilo tayari; ikiwa unasisitiza kabisa kutenda kwa njia hii, utaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Siku hii ndio wakati wa kuishi katika maneno ya Mungu: Maneno ya Mungu yameeleza yote, yote yamefafanuliwa wazi, na maadamu unaishi kwa maneno ya Mungu, utaishi maisha yaliyo huru kabisa na yaliyokombolewa. Hapo awali, ulipomleta Mungu katika maisha yako halisi, ulipitia mafundisho ya dini na sherehe nyingi sana, ulimwomba Mungu hata katika mambo madogo sana, uliyaweka maneno dhahiri upande mmoja, kutoyasoma, na ukajitolea juhudi zako zote kwa kutafuta—na matokeo kwamba hakukuwa na athari. Chukua mfano wa, kile ulichovaa: Wakati ambapo uliomba, uliliweka jambo hili mikononi mwa Mungu, ukiomba kwamba Mungu achague kitu kinachofaa kwa wewe kuvaa. Mungu aliyasikia maneno haya na kusema: “Unaniomba Nijishughulishe Mimi na tondoti hafifu kama hizi? Ubinadamu wa kawaida na urazini Nilivyokuumbia vimeenda wapi?” Wakati mwingine, mtu fulani atafanya makosa katika matendo yake, na ataamini kwamba amemkosea Mungu, naye huanza kufungwa. Hali za watu wengine ni nzuri sana, lakini wanapofanya kitu fulani kidogo kwa njia isiyo sahihi wao huamini kwamba Mungu anawaadibu. Kwa kweli, hii si kazi ya Mungu, lakini ya akili za watu wenyewe. Wakati mwingine, huwa hakuna kosa lolote na vile unavyopitia tukio, laini wengine husema kwamba unapitia tukio kwa njia isiyo sahihi, na hivyo unategwa—unakuwa mbaya, na mwenye giza ndani. Mara kwa mara, watu wakiwa baridi kwa njia hii, wao huamini kwamba wanaadibiwa na Mungu, lakini Mungu husema: “Sifanyi kazi ya kuadibu ndani yako, ungenilaumuje Mimi hivyo?” Watu ni wabaya sana. Wao pia ni wepesi kuhisi sana mara kwa mara na wao hulalamika kuhusu Mungu mara kwa mara. Mungu hakutaki wewe uteseke, ilhali wewe unajiacha uingie katika hali hiyo. Hakuna thamani katika kuteseka kwa aina hii. Kwa sababu watu hawajui kazi inayofanywa na Mungu, katika mambo mengi wao ni wajinga, na hawawezi kuona kwa dhahiri. Katika nyakati kama hizo, wao hunaswa katika mawazo yao wenyewe, wakiendelea kutegwa zaidi milele. Watu wengine husema kwamba vitu vyote na mambo yote yamo mikononi mwa Mungu—kwa hiyo Mungu hangejua watu wanapokuwa wabaya? bila shaka Mungu hujua. Wakati ambapo unategwa katika dhana za binadamu, Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi ndani yako. Wakati mwingi, watu wengine hutegwa katika hali mbaya, lakini Mimi bado huendelea na kazi Yangu. Kama wewe ni mbaya au mtendaji, Mimi sizuiliwi na wewe—lakini unapaswa kujua kwamba maneno mengi Ninenayo, na kiasi kikubwa sana cha kazi Nifanyayo, huja kwa wingi na haraka kulingana na hali ya watu. Wakati ambapo wewe ni mbaya, hili halizuii kazi ya Roho Mtakatifu. Katika nyakati za kuadibu na kifo, watu wote walitegwa ndani ya hali mbaya, lakini hili halikuizuia kazi Yangu; ulipokuwa mbaya, Roho Mtakatifu aliendelea kufanya kilichohitajika kufanywa ndani ya wengine. Unaweza kuendelea kusimama kwa mwezi mmoja, lakini Naendelea kufanya kazi—chochote ufanyacho katika siku za baadaye au sasa, hakiwezi kuizuia kazi ya Roho Mtakatifu. Hali nyingine mbaya hutokana na udhaifu wa binadamu; wakati ambapo watu hawawezi kweli kufanya jambo au kulielewa, wao huwa wabaya. Kwa mfano, katika nyakati za kuadibu, maneno ya Mungu yalizungumza kuhusu kumpenda Mungu kwa kiwango fulani wakati wa kuadibu—lakini wewe uliamini kwamba huwezi. Wakati wa hali hii watu walihisi hasa wenye huzuni na wakaomboleza, walisikitika kwamba miili yao ilikuwa imepotoshwa vikali na Shetani, na kwamba uhodari wao ulikuwa mbaya sana, walihisi kwamba ilisikitisha kuwa walizaliwa katika mazingira haya. Watu wengine walihisi kwamba wakati ulikuwa umepita sana wa kuamini katika Mungu na kumjua Mungu, na kwamba walikuwa hawastahili kufanywa wakamilifu. Hizi zote ni hali za kawaida.
Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za kutotii, ni mchafu ya kusikitisha, ni kitu kichafu. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi, kuna maonyesho mengi sana ya mwili, na kwa hiyo Mungu hudharau mwili kwa kiwango fulani. Watu wanapoacha uchafu, mambo potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini wakibaki bila kuweza kuachana na uchafu na upotovu, basi bado watamilikiwa na Shetani. Kula njama, udanganyifu, na uhalifu wa watu ni mambo ya Shetani; kwa kukuokoa wewe, Mungu hukutenganisha na mambo haya na kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa, na yote ni kwa sababu ya kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unaishi ukimilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na hutapokea urithi wa Mungu. Mara tu umetakaswa na kufanywa kamili, utakuwa mtakatifu, na utakuwa wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na wa kufurahisha kwa Mungu. Kazi inayofanywa na Mungu leo ni wokovu, na, zaidi ya hayo, ni hukumu, kuadibu, na laana. Ina hali nyingi. Je, maneno mengine ya Mungu sio hukumu na kuadibu tu, bali pia laana? Nazungumza ili kutimiza athari fulani, kuwafanya watu wajijue wenyewe, na sio kuwafisha watu; Moyo Wangu ni kwa ajili yenu. Kuzungumza ni mbinu mmojawapo ambayo Mimi hufanyia kazi, Natumia maneno kuonyesha tabia ya Mungu, na kukuruhusu wewe kuelewa mapenzi ya Mungu. Mwili wako waweze kufa, lakini una roho na nafsi. Kama watu wangekuwa na mwili tu, basi hakungekuwa na maana ya wao kuamini katika Mungu, wala hakungekuwa na maana kwa kazi hii yote ambayo Nimefanya. Leo, Nazungumza juu ya jambo moja na kisha lingine, wakati mmoja Ninachukia mno watu, na wakati mwingine Ninapenda kwa hali ya juu; Nafanya hili kuzibadilisha tabia zako, na kuzigeuza dhana zako.
Siku za mwisho zimefika, na nchi nyingi kutoka upande mmoja wa ulimwengu hadi mwingine ziko katika machafuko, kuna vurugu ya kisiasa, njaa, ndwele, mafuriko, na ukame unaonekana kila mahali, kuna maangamizi katika ulimwengu wa mwanadamu, na Mbingu imetuma msiba hapa chini. Hizi ni ishara za siku za mwisho. Lakini kwa watu, unaonekana kama ulimwengu wa uchangamfu na fahari, ambao unaendelea kuwa hivyo zaidi na zaidi. Watu wanapotazama ulimwengu, mioyo yao inavutiwa nao, na wengine hawawezi kujinasua kutoka kwa ulimwengu; idadi kubwa itadanganywa na wale wanaoshiriki katika hila na uchawi. Usipojitahidi ili kuendelea mbele, na huna maadili, utapeperushwa na wimbi hili lenye dhambi. China ni nchi iliyo nyuma sana kimaendeleo kuliko zote, ni nchi ambayo joka kuu jekundu limelala likiwa limejiviringisha, ina watu wengi zaidi wanaoabudu sanamu na kushiriki katika uchawi, hekalu nyingi zaidi, na ni mahali ambapo pepo wachafu huishi. Ulizaliwa ndani yake, unafurahia manufaa yake, na unapotoshwa na kuteswa nalo, lakini baada ya kupitia kujichungua unaachana nalo na unapatwa kabisa na Mungu. Huu ni utukufu wa Mungu, na kwa hiyo hatua hii ya kazi ina umuhimu mkubwa. Mungu amefanya kazi ya kiwango kikubwa hivi, amenena maneno mengi sana, na hatimaye Atawapata ninyi kabisa—hii ni sehemu moja ya kazi ya usimamizi wa Mungu, na ni “mateka ya ushindi” ya vita dhidi ya Shetani. Kadri watu hawa wanavyokuwa bora na kadri maisha ya kanisa yanavyokuwa thabiti, ndivyo joka kuu jekundu linavyotiishwa. Haya ni mambo ya ulimwengu wa kiroho, ni vita vya ulimwengu wa kiroho, na Mungu anapokuwa mshindi, Shetani ataaibishwa na kuanguka chini. Hatua hii ya kazi ya Mungu ina umuhimu wa ajabu. Kazi ya kiwango kikubwa hivyo huokoa kabisa kikundi hiki cha watu; unaponyoka kutoka kwa ushawishi wa Shetani, unaishi katika nchi takatifu, unaishi katika nuru ya Mungu, na hapo kuna uongozi na mwongozo wa nuru, na kisha kuna maana katika kuwa kwako hai. Mnachokula na kuvaa ni tofauti na wao; mnafurahia maneno ya Mungu, na kuishi maisha yenye maana—na wao hufurahia nini? Wao hufurahia tu urithi wa babu zao na “roho ya kitaifa.” Hawana hata dalili ndogo kabisa ya ubinadamu! Mavazi, maneno, na matendo yenu vyote ni tofauti na vyao. Hatimaye, mtaacha kabisa uchafu, hamtategwa tena na ushawishi wa Shetani, na mtapata upaji wa Mungu wa kila siku. Mnapaswa kila mara kuwa waangalifu. Ingawa mnaishi mahali pachafu hamjawekwa mawaa na uchafu na mnaweza kuishi ubavuni mwa Mungu, mkipokea ulinzi Wake mkuu. Mmechaguliwa miongoni mwa wote walio katika nchi hii ya manjano. Je, ninyi sio watu waliobarikiwa zaidi? Kama kiumbe aliyeumbwa, unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu na uishi katika mwili mchafu, basi wewe siye mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kama binadamu, unapaswa kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso. Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu, kama Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kinachotolewa na ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya Shetani, na kukanyagiwa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au njia ya kweli, basi ni nini maana ya maisha yako? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale wanaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?