Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Ijumaa, 24 Mei 2019

Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu

Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu

(1) Mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Mafundisho ya Ukristo yanatoka kwa Biblia, na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanatoka kwa ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu tangu wakati wa uumbaji wakati wa kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hiyo ni kusema, Agano la Kale, Agano Jipya, na Biblia ya Enzi ya Ufalme–Neno Laonekana Katika Mwili–zilizoonyeshwa Bwana Yesu aliyekurudi wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ni imani za msingi na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Agano la Kale linarekodi kazi ya Yehova Mungu ya kuagiza sheria na amri na kuyaongoza maisha ya mwanadamu wakati wa Enzi ya Sheria; Agano Jipya linarekodi kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu wakati wa Enzi ya Neema; na Neno Laonekana Katika Mwili yote ni ukweli kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu wakati wa Enzi ya Ufalme, pamoja na maelezo ya kazi ya hukumu ya Mungu wakati wa siku za mwisho. Biblia ya kweli ni matamko yote ya Mungu wakati wa hatua tatu za kazi, na imani za msingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu ni matamko yote ya Mungu wakati wa hatua tatu za kazi, yaani, ukweli wote ulioonyesha na Mungu wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Maandiko matatu Matakatifu ndiyo imani za msingi na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu.
Ukristo ulizaliwa na kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, lakini Bwana Yesu Kristo unaomwamini alifanya tu kazi ya ukombozi tu katika Enzi ya Neema. Kwa sababu Bwana Yesu mwenye mwili alisulubiwa na alitumika kama sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kumwokoa mtu kutoka kwa mikono ya Shetani na kumtoa kutoka kwa hukumu na laana ya sheria, mtu alikuwa aje tu mbele ya Mungu na kukiri dhambi zake na kutubu ili kusamehewa dhambi zake na kufurahia neema karimu na baraka nyingi zilizofadhiliwa na Mungu. Hii ilikuwa kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu. Ingawa dhambi za mwanadamu zilisamehewa na ukombozi wa Bwana Yesu, mtu hakufutiwa asili yake ya dhambi, alikuwa bado amefungwa na kudhibitiwa nayo, na hangeweza kuepuka kufanya dhambi na kumpinga Mungu kwa kuwa mwenye kiburi na majivuno, akijitahidi kuwa na umaarufu na pato, kuwa na wivu na mgomvi, kusema uongo na kuwadanganya watu, kufuata mienendo miovu ya ulimwengu, na kadhalika. Mwanadamu hakuwa amejikomboa kutoka kwa utumwa wa dhambi na kuwa mtakatifu, na hivyo Bwana Yesu alitabiri mara nyingi kwamba angekuja tena kutekeleza kazi ya hukumu ya siku za mwisho, akisema: “Tazama, Naja upesi” (Ufunuo 22:12). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48). Pia imeandikwa katika Waraka wa Kwanza wa Petro kwamba “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17). Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, ni Bwana Yesu aliyerejea. Yeye ameonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa binadamu, Ametekeleza kazi ya hukumu akianzia kwa nyumba ya Mungu, na Ametimiza kikamilifu unabii wa Biblia. Neno Laonekana Katika Mwili kilivyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni “neno ambalo Roho aliyaambia makanisa” (Ufunuo 2:7) iliyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo, na ni maelezo ya kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Kazi ya hukumu inayofanywa na Mwenyezi Mungu ni hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu ya wokovu wa wanadamu, na pia ni hatua yake ya msingi na muhimu. Kama mtu anataka kuokolewa na Mungu na kuingia katika ufalme wa mbinguni, ni lazima akubali kazi ya Mungu ya hukumu, na katika hili kumetimizwa maneno ya Bwana Yesu: “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha” (Mathayo 25:6). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20). Ni kama tu mtu anakubali na kupitia hukumu na kuadibiwa kwa maneno ya Mungu anapoweza kufahamu utakatifu na haki ya Mungu, kujua kiini na asili ya upotovu wa mwanadamu na Shetani na ukweli wake wa kweli, kwa kweli kutubu mbele ya Mungu, kujiondolea mwenyewe dhambi zote, kufanikisha utakatifu, kuwa yule anayemtii Mungu na kumwabudu Mungu, na kuchumwa na Mungu. Ni hapo tu atakapokuwa na sifa kamili kuzirithi ahadi na baraka za Mungu, na kupata hatima nzuri.
Mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanatoka kwa ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu katika hatua Zake tatu za kazi, ambayo ina maana kwamba yanatoka kwa maneno ya Mungu yaliyoandikwa katika Biblia na kutoka Neno Laonekana Katika Mwili. Mungu alianza kazi ya kumwokoa mwanadamu kufuatia kuumba Kwake dunia, na mpango wa usimamizi Wake kwa wokovu wa binadamu hautakamilika hadi Yeye amalize kazi ya hukumu kuanzia kwa nyumba ya Mungu katika siku za mwisho. Kutoka kwa maneno na ukweli wote ambao Mungu ameuelezea katika hatua tatu za kazi, tunaweza kikamiifu kuona kwamba, iwe ni kazi ya Mungu kufanyika kwa kutumia mtu hapo mwanzo wakati wa Enzi ya Sheria, au kazi Yake Alipokuwa mwili mara mbili katika Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme, yote ni matamko na maonyesho ya ukweli ya Roho mmoja; katika kiini, ni Mungu mmoja ambaye hunena na kufanya kazi. Kwa hiyo, mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanatoka kwa Biblia na kutoka Neno Laonekana Katika Mwili.
(2) Kuhusu Neno Laonekana Katika Mwili
Neno Laonekana Katika Mwili ni matamshi ya kibinafsi ya Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, na ni ukweli wote ambao Mungu ameuonyesha ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu wakati wa kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho. Ukweli huu ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu, ufunuo wa maisha na kiini cha Mungu, na maonyesho ya tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho. Ndizo njia ya pekee ambayo mtu anaweza kupitia ili kumjua Mungu na kutakaswa na kuokolewa. Maneno yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni kanuni kuu ya vitendo vya mtu na mwenendo, na hakuna methali za juu zaidi kwa maisha ya mwanadamu.
Wakristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu husoma maneno ya Mungu katika Neno Laonekana Katika Mwili kila siku, kama vile tu Wakristo wa Ukristo husoma Biblia. Wakristo wote huchukua maneno ya Mungu kama mwongozo wa maisha yao na kama methali ya juu mno kuliko zote katika maisha. Katika Enzi ya Neema, Wakristo wote walisoma Biblia na kusikiliza mahubiri ya Biblia. Mabadiliko yalitokea hatua kwa hatua katika tabia za watu, na walifanya dhambi chache zaidina zaidi. Kadhalika, kupitia kusoma kwa maneno ya Mwenyezi Mungu na ushirika wa maneno ya Mungu, Wakristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu hatua kwa hatua huelewa ukweli na kuachana na utumwa wa dhambi, hawatendi tena dhambi na kumpinga Mungu, na kuwa wa ulingano na Mungu. Ukweli unathibitisha kwamba ni kwa kusoma maneno Mungu tu ndipo mtu anapoweza kutakaswa na kubadilishwa na kuishi kwa kudhihirisha picha ya mtu halisi. Huu ni ukweli ambao hakuna yeyote anayeweza kuukana. Maneno ya Mungu yaliyoandikwa katika Biblia yalionyeshwa Mungu alipofanya kazi katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, wakati Neno Laonekana Katika Mwili ni maneno yanayoonyeshwa na Mungu katika kazi ya siku za mwisho. Chanzo cha yote mawili ni kutoka kwa Roho Mtakatifu. Maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu zimetimiza unabii katika Biblia kikamilifu, na Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, kama vile tu Bwana Yesu alivyosema: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13). Hiyo, pia, ilitabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo kwamba, “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa” (Ufunuo 2:7). “Na nikaona katika mkono wa kuume wa yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu ambacho kiliandikwa ndani na nyuma, kilichofungwa kwa mihuri saba. … tazama, Simba wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na kuifungua ile mihuri saba” (Ufunuo 5:1, 5).
Leo, sisi sote tumeona ukweli mmoja: Maneno yote yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, na yana mamlaka na nguvu–ni sauti ya Mungu. Hakuna anayeweza kukana au kubadilisha hili. Neno Laonekana Katika Mwili chapatikana bila vizuizi kwenye mtandao kwa watu wa nchi na maeneo yote kutafuta na kuchunguza. Hakuna yeyote ambaye huthubutu kukataa kwamba hayo ni maneno ya Mungu, au kwamba ni ya ukweli. Maneno ya Mungu yanaendesha ubinadamu mzima kuendelea mbele, watu wameanza hatua kwa hatua kuamka katikati ya maneno ya Mungu, na wao wanaendelea hatua kwa hatua kuelekea kuukubali ukweli na maarifa ya ukweli. Enzi ya Ufalme ni enzi ambapo maneno ya Mwenyezi Mungu hutawala duniani. Kila moja ya maneno ya Mungu litatimizwa na kukamilishwa. Kama tu vile waumini wote katika Mungu hukiri Biblia leo, watu ambao wanaamini katika Mungu watakiri hivi karibuni kwamba Neno Laonekana Katika Mwili ni maneno ya Mungu katika siku za mwisho. Leo, Neno Laonekana Katika Mwili ni msingi wa imani za Kanisa la Mwenyezi Mungu, na kwa hakika utakuwa msingi wa kuwepo kwa wanadamu wote katika enzi ijayo.
(3) Kuhusu Majina ya Mungu na Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
Kufuatia upotovu wake na Shetani, mwanadamu huishi chini ya miliki ya Shetani na upotovu wake umeongezeka kwa kina kuliko wakati uliopita. Mwanadamu hawezi kujiokoa, na huhitaji wokovu wa Mungu. Kwa mujibu wa mahitaji ya wanadamu wapotovu, Mungu amefanya hatua tatu za kazi katika Enzi ya Sheria, katika Enzi ya Neema, na katika Enzi ya Ufalme. Katika Enzi ya Sheria, Mungu alifanya kazi ya kuagiza sheria na amri na kuongoza maisha ya mwanadamu. Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili, juu ya msingi wa kazi Yake katika Enzi ya Sheria, akatekeleza kazi ya kusulubiwa na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu kwa mara nyingine tena amepata mwili na, juu ya msingi wa kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, hutekeleza kazi ya hukumu kuanzia kwa nyumba ya Mungu, huonyesha ukweli wote wa kwa ajili ya utakaso na wokovu wa mwanadamu, na hutuletea njia pekee kwa ajili ya ufuatiliaji wa utakaso na wokovu. Ni kama tu tukichuma hali halisi ya ukweli kama maisha yetu, tukiwa wale ambao humtii na kumwabudu Mungu, tutakapokuwa na sifa kamili kuongozwa katika ufalme wa Mungu na kupokea ahadi na baraka za Mungu. Hatua tatu za kazi ya Mungu ya wokovu wa mwanadamu zimeunganika kwa karibu, kila hatua ni ya lazima, kila moja huenda juu mno na kuwa na kina zaidi ya ile ya mwisho, zote ni kazi ya Mungu mmoja, na ni hatua hizo tatu tu za kazi ya Mungu ambazo ni kazi kamili ya wokovu wa wanadamu.
Majina matatu–Yehova, Yesu, na Mwenyezi Mungu–ni majina tofauti ambayo Mungu ameyachukua katika Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Mungu huchukua majina tofauti kwa sababu kazi Yake inatofautiana katika enzi tofauti. Mungu hutumia jina jipya kuanza enzi mpya na kuwakilisha kazi ya enzi hiyo. Jina la Mungu lilikuwa Yehova katika Enzi ya Sheria, na Yesu katika Enzi ya Neema. Mungu hutumia jina jipya–Mwenyezi Mungu–katika Enzi ya Ufalme, akitimiza unabii katika Kitabu cha Ufunuo: “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika… Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, na nitaliandika jina la Mungu wangu juu yake, na jina la mji wa Mungu wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu: na nitaliandika juu yake jina langu jipya” (Ufunuo 3:7, 12). “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi” (Ufunuo 1:8). Ingawa majina ya Mungu na kazi katika enzi hizo tatu ni tofauti, kuna Mungu mmoja tu katika kiini, na chanzo ni kimoja.
Kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu hasa hushirikisha hatua tatu za kazi. Yeye ametumia majina tofauti katika kila enzi, lakini kiini cha Mungu hakibadiliki kamwe. Hatua tatu za kazi hufanywa na Mungu mmoja; hivyo, Yehova, Yesu, na Mwenyezi Mungu ni Mungu yule yule mmoja. Yesu alikuwa ni kuonekana kwa Yehova, na Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, na hivyo Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli ambaye aliziumba mbingu na ardhi na vitu vyote, huamrisha vitu vyote, na hushikilia ukuu juu ya kila kitu, na Yeye ndiye yule wa milele na Muumba pekee.
Katika hatua tatu za kazi ya kumwokoa mwanadamu, Mungu ameifichua tabia Yake yote kwa mwanadamu, akituruhusu tuone kwamba tabia ya Mungu si huruma na upendo tu, lakini pia haki, uadhama, na ghadhabu, kwamba kiini Chake ni utakatifu na haki, na ni ukweli na upendo, kwamba tabia ya Mungu na mamlaka na nguvu za Mungu hazimilikiwi na kiumbe chochote kilichoumbwa au kisichoumbwa. Tunaamini kuwa maneno yote ambayo Mungu ameyasema tangu wakati wa uumbaji hadi mwisho wa dunia ni ukweli. Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno ya Mungu kamwe hayatatoweka, na kila mojawapo litatimizwa!

Alhamisi, 23 Mei 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu. Binadamu kuingia rahani kunamaanisha kwamba binadamu wote wataishi ndani ya mwangaza wa Mungu na chini ya baraka Zake; hakutakuwa na upotovu wowote wa Shetani, wala maovu yoyote kutokea. Binadamu wataishi kama kawaida duniani, na wataishi chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba binadamu wameokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi miongoni mwa mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo.“
Kukaribia kwa mwisho wa kila kitu kunaonyesha mwisho wa kazi ya Mungu na kunaonyesha mwisho wa maendeleo ya binadamu. Hii inamaanisha kwamba binadamu kama walivyopotoshwa na Shetani wamefika mwisho wake wa maendeleo, na kwamba vizazi vya Adamu na Hawa vimeenea hadi mwisho wao binafsi, na pia inamaanisha kwamba haiwezekani kwa binadamu kama hawa, baada ya kupotoshwa na Shetani, kuendelea kustawi. Adamu na Hawa wa mwanzoni hawakuwa wamepotoshwa, lakini Adamu na Hawa waliofukuzwa kutoka Bustani ya Edeni walivurugwa na Shetani. Wakati Mungu na mwanadamu wanaingia rahani pamoja, Adamu na Hawa—waliofukuzwa kutoka Bustani ya Edeni—na vizazi vyao hatimaye watafika mwisho; binadamu wa baadaye bado watakuwa na vizazi vya Adamu na Hawa, lakini hawatakuwa watu wanaomilikiwa na Shetani. Badala yake, watakuwa watu waliookolewa na kutakaswa. Hawa watakuwa binadamu ambao wamehukumiwa na kuadibiwa, na walio watakatifu. Hawa watu hawatakuwa sawa na jamii ya binadamu kama ilivyokuwa awali; mtu anaweza kusema kwamba hao ni watu wa aina tofauti kabisa na Adamu na Hawa wa awali. Hawa watu watakuwa wamechaguliwa kutoka miongoni mwa wote waliopotoshwa na Shetani, na watakuwa ndio watu ambao hatimaye wamesimama imara wakati wa hukumu na kuadibu kwa Mungu, watakuwa kundi la mwisho la watu miongoni mwa wanadamu potovu. Kundi hili la watu ndilo tu litaweza kuingia katika raha ya mwisho pamoja na Mungu. Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaobaki watatakaswa na kufurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani waingiapo ulimwengu wa juu wa binadamu; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. Walikuwa wamekombolewa wakati mmoja, na pia walikuwa wamehukumiwa na kuadibiwa; walikuwa pia wamemhudumia Mungu wakati mmoja, lakini siku ya mwisho itakapofika, bado wataondolewa na kuangamizwa kwa sababu ya uovu wao na kwa sababu ya kutotii na kutokombolewa kwao. Hawatakuwa tena katika ulimwengu wa baadaye, na hawatakuweko tena miongoni mwa jamii ya binadamu ya baadaye. Watenda maovu wote na yeyote na wote ambao hawajaokolewa wataangamizwa wakati watakatifu miongoni mwa binadamu wataingia rahani, bila kujali kama wao ni roho za wafu ama wale wanaoishi bado katika mwili. Bila kujali enzi ya hizi roho zitendazo maovu na watu watenda maovu, ama roho za watu wenye haki na watu wanaofanya haki wako, mtenda maovu yeyote ataangamizwa, na yeyote mwenye haki ataishi. Iwapo mtu ama roho inapokea wokovu haiamuliwi kabisa kulingana na kazi ya enzi ya mwisho, lakini inaamuliwa kulingana na iwapo wamempinga ama kutomtii Mungu. Kama watu wa enzi ya awali walifanya maovu na hawangeweza kuokolewa, bila shaka wangekuwa walengwa wa adhabu. Kama watu wa enzi hii wanafanya maovu na hawawezi kuokolewa, hakika wao pia ni walengwa wa adhabu. Watu wanatengwa kwa msingi wa mema na mabaya, sio kwa msingi wa enzi. Baada ya kutengwa kwa msingi wa mema na mabaya, watu hawaadhibiwi ama kutuzwa mara moja; badala yake, Mungu atafanya tu kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wema baada ya kufanya kazi Yake ya ushindi katika siku za mwisho. Kwa kweli, Amekuwa akitumia mema na mabaya kutenga binadamu tangu Afanye kazi Yake miongoni mwa binadamu. Atawatuza tu wenye haki na kuwaadhibu waovu baada ya kukamilika kwa kazi Yake, badala ya kuwatenga waovu na wenye haki baada ya kukamilika kwa kazi Yake mwishowe na kisha kufanya kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wazuri mara moja. Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi. Kama Mungu hangewaangamiza waovu lakini badala yake kuwaacha wabakie, basi binadamu wote bado hawangeweza kuingia rahani, na Mungu hangeweza kuleta binadamu katika ulimwengu bora. Kazi ya aina hii haingekuwa imekamilika kabisa. Atakapomaliza kazi Yake, binadamu wote watakuwa watakatifu kabisa. Mungu anaweza kuishi kwa amani rahani kwa namna hii pekee.
Watu leo hawawezi kutengana na mambo ya mwili; hawawezi kuacha starehe za mwili, wala hawawezi kuiacha dunia, pesa, ama tabia yao potovu. Watu wengi wanaendelea na shughuli zao kwa hali ya uzembe. Kwa kweli, hawa watu hawana Mungu mioyoni mwao hata kidogo; zaidi ya hayo, hawamchi Mungu. Hawana Mungu mioyoni mwao, na hivyo hawawezi kutambua yote anayofanya Mungu, na hawawezi kabisa kuamini maneno Azungumzayo kwa mdomo Wake. Watu hawa ni wa mwili sana, wamepotoshwa sana na hawana ukweli wowote, zaidi ya hayo, hawaamini kwamba Mungu anaweza kuwa mwili. Yeyote asiyemwamini Mungu wa mwili—yaani, yeyote asiyeamini kazi na hotuba ya Mungu anayeonekana na haamini Mungu anayeonekana lakini badala yake anaabudu Mungu asiyeonekana mbinguni—hana Mungu katika moyo wake. Ni watu wasiomtii na wanaompinga Mungu. Watu hawa hawana ubinadamu na fahamu, kusema chochote kuhusu ukweli. Kwa watu hawa Mungu anayeonekana na kushikika hawezi kuaminika zaidi, lakini Mungu asiyeonekana wala kushikika ni Mungu wa kuaminika na pia Anayefurahisha nyoyo zao. Wanachotafuta si ukweli wa uhalisi, wala si kiini cha kweli cha uhai, wala nia za Mungu; badala yake, wanatafuta msisimko. Mambo yoyote yanayoweza kuwaruhusu kufikia tamaa zao ni, bila shaka, imani na shughuli zao. Wamwamini Mungu tu ili kuridhisha tamaa zao, si kutafuta ukweli. Hawa watu si watenda maovu? Wanajiamini sana, na hawaamini kwamba Mungu aliye mbinguni atawaangamiza, hawa “watu wazuri.” Badala yake, wanaamini kwamba Mungu atawaruhusu kubaki na, zaidi ya hayo, Atawatuza vizuri sana, kwani wamemfanyia Mungu mambo mengi na kuonyesha kiwango kikubwa cha “uaminifu” Kwake. Kama wangemtafuta Mungu anayeonekana, wangelipiza kisasi mara moja dhidi ya Mungu na kukasirika wakati hawatapata tamaa zao. Hawa ni watu waovu wanaotaka kuridhisha tamaa zao; si watu wa uadilifu wanaosaka ukweli. Watu kama hao ni wale wanaojulikana kama waovu wanaomfuata Kristo. Wale watu wasioutafuta ukweli hawawezi kuamini ukweli. Hawawezi kabisa kutambua matokeo ya baadaye ya binadamu, kwani hawaamini kazi ama hotuba yoyote ya Mungu anayeonekana, na hawawezi kuamini hitimisho la baadaye la binadamu. Hivyo, hata wakimfuata Mungu anayeonekana, bado wanatenda maovu na hawatafuti ukweli, wala hawatendi ukweli Ninaohitaji. Wale watu wasioamini kwamba wataangamizwa kinyume ni kwamba ni wale watu watakaoangamizwa. Wote wanajiamini kuwa wajanja sana, na wanaamini kwamba wao wenyewe ndio wanaotenda ukweli. Wanafikiria mwenendo wao mbovu kuwa ukweli na hivyo wanauthamini. Hawa watu waovu wanajiamini sana; wanachukua ukweli kuwa mafundisho ya dini, na kuchukua vitendo vyao vibovu kuwa ukweli, na mwishowe watavuna tu walichopanda. Watu wanapojiamini zaidi na wanapokuwa na kiburi zaidi, ndipo hawawezi zaidi kupata ukweli; watu wanapomwamini Mungu wa mbinguni zaidi, ndipo wanampinga Mungu zaidi. Hawa ndio watu watakaoadhibiwa. Kabla ya binadamu kuingia rahani, iwapo kila aina ya mtu ataadhibiwa ama kutuzwa kutaamuliwa kulingana na iwapo wanatafuta ukweli, iwapo wanamjua Mungu, iwapo wanaweza kumtii Mungu anayeonekana. Waliomhudumia Mungu anayeonekana lakini bado hawamjui wala kumtii hawana ukweli. Watu hawa ni watenda maovu, na watenda maovu bila shaka wataadhibiwa; zaidi ya hapo, wataadhibiwa kulingana na mienendo yao mibovu. Mungu ni wa mwanadamu kumwamini, na pia Anastahili utii wa mwanadamu. Wale wanaomwamini tu Mungu asiye yakini na asiyeonekana ni wale wasiomwamini Mungu; zaidi ya hapo, hawawezi kumtii Mungu. Kama hawa watu bado hawawezi kumwamini Mungu anayeonekana wakati kazi Yake ya ushindi inakamilika, na pia wanaendelea kutomtii na kumpinga Mungu anayeonekana katika mwili, hawa wanaoamini isiyo yakini bila shaka, wataangamizwa. Ni kama ilivyo na wale miongoni mwenu—yeyote anayemtambua Mungu Aliyepata mwili kwa maneno lakini bado hatendi ukweli wa utii kwa Mungu Aliyepata mwili hatimaye ataondolewa na kuangamizwa, na yeyote anayemtambua Mungu anayeonekana na pia kula na kunywa ukweli ulioonyeshwa na Mungu anayeonekana lakini bado anamtafuta Mungu asiye yakini na asiyeonekana pia yeye ataangamizwa baadaye. Hakuna hata mmoja wa watu hawa anayeweza kubaki hadi wakati wa pumziko baada ya kazi ya Mungu kukamilika; hakuwezi kuwa yeyote kama watu hawa atakayebakia hadi wakati wa pumziko. Watu wenye pepo ni wale wasiotenda ukweli; asili yao ni ile inayompinga na kutomtii Mungu, na hawana nia hata kidogo za kumtii Mungu. Watu wote kama hao wataangamizwa. Iwapo una ukweli na iwapo unampinga Mungu hayo yanaamuliwa kulingana na asili yako, si kulingana na sura yako ama hotuba na mwenendo wako wa mara kwa mara. Asili ya kila mtu inaamua iwapo ataangamizwa; hii inaamuliwa kulingana na asili iliyofichuliwa na mienendo yao na kutafuta kwao ukweli. Miongoni mwa watu wanaofanya kazi sawa na pia kufanya kiasi sawa cha kazi, wale ambao asili yao ni nzuri na wanaomiliki ukweli ni watu wanaoweza kubaki, lakini wale ambao asili yao ya ubinadamu ni mbovu na wasiomtii Mungu anayeonekana ni wale watakaoangamizwa. Kazi ama maneno yoyote ya Mungu yanayoelekezwa kwa hatima ya binadamu yanahusiana na binadamu ipasavyo kulingana na asili ya kila mtu; hakutakuwa na ajali yoyote, na hakika hakutakuwa na kosa hata kidogo. Mtu anapofanya kazi tu ndipo hisia za binadamu ama maana itachanganywa ndani. Kazi anayofanya Mungu ndiyo inayofaa zaidi; hakika Hataleta madai ya uongo dhidi ya kiumbe yeyote. Sasa kuna watu wengi wasioweza kutambua hatima ya baadaye ya binadamu na ambao pia hawaamini maneno Nisemayo; wote wasioamini, pamoja na wasiotenda ukweli, ni mapepo!
Wanaotafuta na wasiotafuta sasa ni aina mbili tofauti ya watu, na wao ni aina mbili ya watu na hatima mbili tofauti. Wanaotafuta maarifa ya ukweli na kutenda ukweli ni watu ambao Mungu ataokoa. Wale wasiojua njia ya ukweli ni mapepo na adui; ni vizazi vya malaika mkuu na wataangamizwa. Hata wacha Mungu wanaomwamini Mungu asiye yakini—je, si mapepo pia? Watu wanaomiliki dhamiri nzuri lakini hawakubali njia ya ukweli ni mapepo; asili yao ni ile inayompinga Mungu. Wale wasiokubali njia ya ukweli ni wale wanaompinga Mungu, na hata kama watu hawa wanavumilia taabu nyingi, bado wataangamizwa. Wasio tayari kuiwacha dunia, wasioweza kuvumilia kutengana na wazazi wao, wasioweza kuvumilia kujiondolea raha zao za mwili, wote hawamtii Mungu na wote wataangamizwa. Yeyote asiyemwamini Mungu aliyepata mwili ni pepo; zaidi ya hayo, wataangamizwa. Wanaoamini lakini hawatendi ukweli, wasiomwamini Mungu aliyepata mwili, na wale ambao hawaamini kabisa kuwepo kwa Mungu wataangamizwa. Yeyote anayeweza kubaki ni mtu ambaye amepitia uchungu wa usafishaji na kusimama imara; huyu ni mtu ambaye kweli amepitia majaribio. Yeyote asiyemtambua Mungu ni adui; yaani, yeyote aliye ndani ama nje ya mkondo huu ambaye hamtambui Mungu aliyepata mwili ni adui wa Kristo! Shetani ni nani, mapepo ni nani, na nani ni maadui wa Mungu kama si wapinzani wasiomwamini Mungu? Wao si watu wasiomtii Mungu? Wao si watu wanaodai kwa maneno kuamini lakini hawana ukweli? Wao si wale watu wanaofuata tu kupata kwa baraka lakini hawawezi kumshuhudia Mungu? Bado unaweza kushiriki na wale mapepo leo na kusisitiza dhamiri na mapenzi na hawa mapepo; je, hii haichukuliwi kuwa kueneza nia nzuri kwa Shetani? Haichukuliwi kuwa kushiriki na mapepo? Kama watu bado hawawezi kutofautisha kati ya mazuri na maovu leo, na bado wanasisitiza kwa upofu mapenzi na huruma bila kwa njia yoyote kutamani kutafuta matakwa ya Mungu, na hawawezi kwa njia yoyote kuwa na moyo wa Mungu kama wao, mwisho wao utakuwa dhalili zaidi. Yeyote asiyemwamini Mungu wa mwili ni adui wa Mungu. Kama unaweza kusisitiza dhamiri na mapenzi kwa adui, je, hujakosa hisia ya haki? Kama unalingana na wale Ninaowachukia na kutokubaliana nao, na bado unasisitiza mapenzi na hisia za binafsi nao, basi wewe si asiyetii? Humpingi Mungu kimakusudi? Je, mtu kama huyu anamiliki ukweli? Ikiwa watu wanasisitiza dhamiri kwa adui, kusisitiza upendo kwa mapepo na kusisitiza huruma kwa Shetani, hawakatizi kazi ya Mungu kimakusudi? Wale watu wanaomwamini Yesu tu na hawamwamini Mungu aliyepata mwili wakati wa siku za mwisho na wale wanaodai kwa maneno kumwamini Mungu aliyepata mwili lakini wanafanya maovu wote ni adui wa Kristo, sembuse wale watu wasiomwamini Mungu. Hawa watu wote wataangamizwa. Kiwango ambacho mwanadamu anamhukumu mwanadamu kinatokana na tabia zake; aliye na mwenendo mzuri ni mtu mwenye haki, na aliye na mwenendo wa kuchukiza ni mwovu. Kiwango ambacho Mungu anamhukumu mwanadamu kinatokana na iwapo asili ya mtu inamtii Yeye; anayemtii Mungu ni mtu mwenye haki, na asiyemtii Mungu ni adui na mtu mwovu, bila kujali iwapo tabia ya mtu huyu ni nzuri ama mbaya, na bila kujali iwapo hotuba ya mtu huyu ni sahihi ama si sahihi. Watu wengine wanatamani kutumia matendo mazuri kupata hatima nzuri ya baadaye, na watu wengine wanataka kutumia hotuba nzuri kununua hatima nzuri. Watu wanaamini kimakosa kwamba Mungu anaamua matokeo ya mwanadamu kulingana na tabia ama hotuba yake, na kwa hivyo watu wengi watataka kutumia haya kupata fadhila ya muda mfupi kupitia udanganyifu. Watu ambao baadaye watasalimika kupitia pumziko wote watakuwa wamevumilia siku ya dhiki na pia kumshuhudia Mungu; wote watakuwa watu ambao wamefanya jukumu lao na wana nia ya kumtii Mungu. Wanaotaka tu kutumia fursa kufanya huduma ili kuepuka kutenda ukweli hawataweza kubaki. Mungu ana viwango sahihi vya mipangilio ya matokeo ya kila mtu; Hafanyi tu maamuzi haya kulingana na maneno na mwenendo wa mtu, wala Hayafanyi kulingana na tabia zao wakati wa kipindi kimoja cha muda. Hakika Hatakuwa na huruma na mwenendo wowote mbaya wa mtu kwa sababu ya huduma ya mtu ya zamani kwa Mungu, wala Hatamnusuru mtu kutokana na kifo kwa sababu ya gharama kwa Mungu ya mara moja. Hakuna anayeweza kuepuka adhabu ya uovu wake, na hakuna anayeweza kuficha tabia zake mbovu na hivyo kuepuka adhabu ya maangamizi. Kama mtu anaweza kweli kufanya jukumu lake, basi inamaanisha kwamba ni mwaminifu milele kwa Mungu na hatafuti tuzo, bila kujali iwapo anapokea baraka ama bahati mbaya. Kama watu wana uaminifu kwa Mungu waonapo baraka lakini wanapoteza uaminifu wao wasipoweza kuona baraka na mwishowe bado wasiweze kumshuhudia Mungu na bado wasiweze kufanya jukumu lao kama wapasavyo, hawa watu waliomhudumia Mungu wakati mmoja kwa uaminifu bado wataangamizwa. Kwa ufupi, watu waovu hawawezi kuishi milele, wala hawawezi kuingia rahani; watu wenye haki tu ndio mabwana wa pumziko. Baada ya binadamu kuingia katika njia sawa, watu watakuwa na maisha ya kawaida ya binadamu. Wote watafanya jukumu lao husika na kuwa waaminifu kabisa kwa Mungu. Watatoa kabisa kutotii kwao na tabia yao iliyopotoshwa, na wataishi kwa ajili ya Mungu na kwa sababu ya Mungu. Watakosa uasi na upinzani. Wataweza kabisa kumtii Mungu. Haya ndiyo maisha ya Mungu na mwanadamu na maisha ya ufalme, na ni maisha ya pumziko.
kutoka kwa Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Alhamisi, 16 Mei 2019

Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

1. Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili. Kwanza ni maisha Anayoishi kabla ya kuanza kutekeleza huduma Yake. Anaishi katika familia ya kawaida ya binadamu, katika ubinadamu wa kawaida kabisa, Akifuata maadili na sheria za maisha ya wanadamu, Akiwa na mahitaji ya kawaida ya binadamu (chakula, nguo, makazi, na usingizi), na udhaifu wa kawaida wa binadamu na hisia za kawaida za binadamu. Kwa maneno mengine, katika hatua hii ya kwanza Anaishi maisha yasiyo na uungu, ubinadamu wa kawaida kabisa, Akijishughulisha na shughuli zote za wanadamu. Hatua ya pili ni ya maisha Anayoishi baada ya kuanza kutekeleza huduma Yake. Bado Yumo katika ubinadamu wa kawaida Akiwa na umbo la nje la binadamu bila kuonyesha ishara isiyo ya kawaida kwa nje. Lakini kimsingi Anaishi kwa ajili ya huduma Yake, na wakati huu ubinadamu Wake wa kawaida upo kikamilifu kuhudumia kazi ya kawaida ya uungu Wake; kwani wakati huo, ubinadamu Wake wa kawaida umekomaa kiasi cha kuweza kutekeleza huduma Yake. Kwa hivyo hatua ya pili ya maisha Yake ni ya kutekeleza huduma Yake katika ubinadamu Wake wa kawaida, ni maisha ya ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Sababu ya kuishi katika maisha ya kawaida kabisa ya ubinadamu katika hatua ya kwanza ya maisha Yake ni kwamba ubinadamu Wake bado ulikuwa haujalingana na ukamilifu wa kazi ya uungu, bado haujakomaa; ni baada tu ya kukomaa kwa ubinadamu Wake na kuwa na uwezo wa kustahimili huduma Yake, ndipo Anaweza kuanza kutekeleza huduma Yake. Kwa kuwa Yeye, kama mwili, Anahitaji kukua na kukomaa, hatua ya kwanza ya maisha Yake ni ile ya ubinadamu wa kawaida, ilhali katika hatua ya pili, kwa kuwa ubinadamu Wake una uwezo wa kuanza kazi Yake na kutekeleza huduma Yake, maisha ambayo Mungu mwenye mwili Anaishi katika kipindi cha huduma Yake ni ya ubinadamu na ya uungu kamili. Iwapo Mungu mwenye mwili Angeanza huduma Yake kwa dhati tangu kuzaliwa kwake, na kufanya ishara na maajabu ya mwujiza, basi Asingekuwa na kiini cha kimwili. Kwa hivyo, ubinadamu Wake upo kwa sababu ya kiini chake cha Kimwili; hakuwezi kuwepo na mwili bila ubinadamu, na mtu bila ubinadamu si mwanadamu. Kwa njia hii, ubinadamu wa mwili wa Mungu ni sifa ya ndani ya mwili wa Mungu. Kusema kwamba “Mungu Anapokuwa mwili Anakuwa na uungu kamili, kwa vyovyote vile si ubinadamu,” ni kufuru, kwa sababu huu ni msimamo usioweza kuchukuliwa, msimamo unaokinzana na kanuni ya Yesu kuupata mwili. Hata baada ya kuanza kutekeleza huduma Yake, uungu Wake bado unaishi ndani ya umbo la nje la binadamu Anapofanya kazi Yake; ni kwamba tu wakati huo, ubinadamu Wake una kusudi la pekee la kuuwezesha uungu Wake kutekeleza kazi katika mwili wa kawaida. Kwa hivyo wakala wa kazi ni uungu unaosetiriwa katika ubinadamu Wake. Ni uungu na wala si ubinadamu Wake unaofanya kazi, lakini ni uungu uliojificha katika ubinadamu Wake; kimsingi kazi Yake inafanywa na uungu Wake kikamilifu, haifanywi na ubinadamu Wake. Ila mtekelezaji wa kazi ni mwili Wake. Mtu anaweza kusema kuwa Yeye ni mwanadamu na vilevile Mungu, kwani Mungu Anakuwa Mungu Anayeishi katika mwili, mwenye umbo la mwanadamu na kiini cha binadamu lakini pia na kiini cha Mungu. Kwa sababu ni mwanadamu mwenye kiini cha Mungu, Yuko juu ya wanadamu wote walioumbwa, juu ya mwanadamu yeyote anayeweza kutekeleza kazi ya Mungu. Kwa hivyo, miongoni mwa wale wote walio na umbo la binadamu kama Lake, miongoni mwa wale wote walio na ubinadamu, Yeye pekee ndiye Mungu mwenye mwili Mwenyewe—wengine wote ni wanadamu walioumbwa. Japokuwa wote wana ubinadamu, wanadamu walioumbwa hawana chochote ila ubinadamu, ilhali Mungu mwenye mwili ni tofauti: katika mwili Wake, si tu kwamba ana ubinadamu ila pia muhimu zaidi Ana uungu. Ubinadamu Wake waweza kuonekana katika mwonekano wa nje wa Mwili Wake na katika maisha Yake ya kila siku; ila uungu Wake ni vigumu kuonekana. Kwa kuwa uungu Wake huonyeshwa pale tu Anapokuwa na ubinadamu, na si wa kimuujiza kama watu wanavyoukisia kuwa, ni vigumu sana kwa watu kuuona. Hata leo hii ni vigumu sana kwa watu kuelewa kiini cha kweli cha Mungu mwenye mwili. Kwa kweli, hata baada ya Mimi kulizungumzia kwa mapana, Natarajia bado liwe fumbo kwa wengi wenu. Suala hili ni rahisi sana: kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, kiini Chake ni muungano wa ubinadamu na uungu. Muungano huu unaitwa Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe duniani.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maisha Aliyoishi Yesu duniani yalikuwa maisha ya kimwili ya kawaida. Aliishi katika ubinadamu wa kawaida wa mwili Wake. Mamlaka Yake—kufanya kazi Yake na kuzungumza neno Lake, au kuwaponya wagonjwa au kufukuza mapepo, kufanya hiyo kazi isiyo ya kawaida—hayakujitokeza, kwa kiasi kikubwa, hadi Alipoanza huduma Yake. Maisha Yake kabla ya umri wa miaka ishirini na tisa, kabla ya Yeye kuanza kutekeleza huduma Yake, yalikuwa uthibitisho tosha kuwa Alikuwa mwili wa kawaida. Kwa sababu ya hili, na kwa kuwa Alikuwa bado Hajaanza kutekeleza huduma Yake, watu hawakuona chochote cha uungu ndani Yake, hawakuona chochote zaidi ya ubinadamu wa kawaida, mwanadamu wa kawaida—kama vile wakati ule baadhi ya watu walimwamini kuwa mwana wa Yosefu. Watu walidhani kuwa Alikuwa mwana wa mwanadamu wa kawaida, hawakuwa na njia ya kugundua kuwa Alikuwa mwili wa Mungu; hata wakati Alipotenda miujiza mingi katika harakati za kutekeleza huduma Yake, watu wengi bado walisema Alikuwa mwana wa Yosefu, kwani Alikuwa Kristo mwenye umbo la nje la ubinadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake wa kawaida pamoja na kazi yake vyote vilikuwepo ili kutimiza umuhimu wa kupata mwili kwa mara ya kwanza, kuthibitisha kuwa Mungu Alikuwa Amekuja katika mwili kwa ukamilifu, kuwa mwanadamu wa kawaida kabisa. Kuwa na ubinadamu wa kawaida kabla ya kuanza kazi Yake ulikuwa uthibitisho kuwa Alikuwa mwili wa kawaida; na kwa kuwa Alifanya kazi baadaye lilithibitisha pia kuwa Alikuwa mwili wa kawaida, kwa kuwa Alifanya ishara na miujiza, kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo katika mwili na ubinadamu wa kawaida. Sababu za kufanya miujiza ilikuwa kwamba mwili Wake ulikuwa umebeba mamlaka ya Mungu, ulikuwa mwili ambamo Roho wa Mungu Alikuwa Amesetiriwa. Alikuwa na mamlaka haya kwa sababu ya Roho wa Mungu, na haikumaanishi kuwa Hakuwa Mwili. Kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo ilikuwa kazi Aliyopaswa kutekeleza katika huduma Yake, onyesho la uungu Wake uliojificha ndani ya ubinadamu Wake, na haijalishi ni ishara za aina gani Alionyesha au Alidhihirisha vipi mamlaka Yake, bado Aliishi katika ubinadamu wa kawaida na bado Alikuwa mwili wa kawaida. Aliishi katika mwili wa kawaida mpaka wakati Alipofufuliwa baada ya kufa msalabani. Aliishi katika mwili wa kawaida. Akitoa neema, Akiwaponya wagonjwa, na kufukuza mapepo hayo yote yalikuwa sehemu ya huduma Yake, hiyo yote ilikuwa kazi Aliyotekeleza katika mwili Wake wa kawaida. Kabla ya kwenda msalabani, Hakuuacha mwili Wake wa kawaida, haijalishi Alikuwa Anafanya nini. Alikuwa Mungu Mwenyewe, Akifanya kazi ya Mungu, lakini kwa sababu Alikuwa Mwili wa Mungu, Alikula chakula na kuvaa nguo, Alikuwa na mahitaji ya kawaida ya binadamu, Alikuwa na fikira za kawaida za binadamu na akili za kawaida. Haya yote yalikuwa uthibitisho kwamba Alikuwa mwanadamu wa kawaida, ambayo yalithibitisha kuwa mwili wa Mungu ulikuwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida, haukuwa wa rohoni. Kazi Yake ilikuwa kukamilisha kazi ya Mungu kupata mwili mara ya kwanza, kutimiza huduma ya kupata mwili mara ya kwanza. Umuhimu wa kupata mwili ni kwamba mtu wa kawaida Anatekeleza kazi ya Mungu Mwenyewe; yaani, kwamba Mungu Anatekeleza kazi Yake ya uungu katika ubinadamu na hivyo kumshinda Shetani. Kupata mwili kunamaanisha kwamba Roho wa Mungu Anakuwa Mwili, yaani, Mungu Anakuwa mwili; kazi Anayoifanya katika mwili ni kazi ya Roho, inayothibitika katika mwili, na kuonyeshwa kwa mwili. Hakuna mwingine ila tu mwili wa Mungu Anayeweza kutimiza huduma ya Mungu mwenye mwili; yaani, mwili wa Mungu kuwa mwili pekee, ubinadamu huu wa kawaida—na hakuna mwingine yeyote—anayeweza kuonyesha kazi ya uungu.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ubinadamu wa Mungu kuwa mwili huwepo kudumisha kazi ya kawaida ya uungu katika mwili; fikira Zake za kawaida za binadamu zinadumisha ubinadamu Wake wa kawaida na shughuli Zake zote za kimwili. Mtu anaweza kusema kuwa fikira zake za kawaida za binadamu zipo ili kudumisha kazi yote ya Mungu katika mwili. Kama mwili huu usingekuwa na akili ya mwanadamu wa kawaida, basi Mungu Asingefanya kazi katika mwili, na Anachopaswa kufanya kimwili kisingetimilika. Japo Mungu mwenye mwili Ana akili ya mwanadamu wa kawaida, kazi Yake haijatiwa doa na mawazo ya binadamu; Anafanya kazi katika ubinadamu na akili ya kawaida chini ya masharti ya awali kuwa atakuwa na ubinadamu na akili ya kawaida, na si na mawazo ya kawaida ya binadamu. Haijalishi mawazo ya mwili Wake ni bora kiasi gani, kazi Yake haionyeshi alama ya mantiki au kufikiria. Kwa maneno mengine, kazi Yake haiwazwi na akili ya mwili Wake, ila ni onyesho la moja kwa moja la kazi ya uungu katika ubinadamu Wake. Kazi Yake yote ni huduma Anayostahili kutimiza, na haiwazwi hata chembe kwa akili Zake. Kwa mfano, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kusulubishwa hayakuwa mazao ya akili Zake za binadamu, yasingeweza kutimizwa na mwanadamu yeyote mwenye akili za binadamu. Vivyo hivyo, kazi ya ushindi ya leo ni huduma ambayo ni sharti itekelezwe na Mungu mwenye mwili, lakini si kazi ya mapenzi ya mwanadamu, ni kazi ambayo uungu Wake unapaswa kufanya, kazi ambayo hakuna mwanadamu wa mwili anaiweza. Kwa hivyo, Mungu mwenye mwili ni lazima Awe na akili za binadamu, ni lazima Awe na ubinadamu wa kawaida, kwa sababu ni lazima Atekeleze kazi Yake katika ubinadamu akiwa na akili za kawaida. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Mungu mwenye Mwili, kiini chenyewe cha Mungu mwenye mwili.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kabla Yesu Hajatekeleza kazi yake, Aliishi tu katika ubinadamu Wake wa kawaida. Hakuna mtu ambaye angeweza kutambua kuwa Alikuwa Mungu, hakuna aliyegundua kuwa Alikuwa Mungu mwenye mwili; watu walimjua tu kama mwanadamu wa kawaida kabisa. Ubinadamu Wake wa kawaida ulikuwa uthibitisho kuwa Mungu Alipata mwili, na kwamba Enzi ya Neema ilikuwa enzi ya kazi ya Mungu mwenye mwili, si enzi ya kazi ya Roho. Ilikuwa uthibitisho kuwa Roho wa Mungu Alipatikana kikamilifu katika mwili, kwamba katika enzi ya kupata mwili kwa Mungu mwili Wake ungetekeleza kazi yote ya Roho. Kristo mwenye ubinadamu wa kawaida ni mwili ambao kwao Roho Hupatikana, Akiwa na ubinadamu wa kawaida, ufahamu wa kawaida, na fikira za wanadamu. “Kupatikana” kunamaanisha Mungu kuwa mwanadamu, Roho kuwa mwili; kuiweka wazi, ni wakati ambapo Mungu Mwenyewe Anaishi katika mwili wenye ubinadamu wa kawaida, na kupitia kwenye huo mwili, Anaonyesha kazi yake ya uungu—hii ndiyo maana ya kupatikana, au kupata mwili.

kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika kipindi cha Muda ambacho Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi, watu wangeweza kuona kwamba Mungu alikuwa na maonyesho mengi ya kibinadamu. Kwa mfano, Aliweza kucheza, Aliweza kuhudhuria harusi, Aliweza kuwasiliana kwa karibu na watu, kuongea na wao, na kujadili mambo pamoja nao. Aidha, Bwana Yesu aliweza pia kukamilisha kazi nyingi zilizowakilisha uungu Wake, na bila shaka kazi Yake yote ilikuwa ni maonyesho na ufichuzi wa tabia ya Mungu. Katika kipindi hiki, wakati uungu wa Mungu ulitambuliwa kupitia kwa mwili wa kawaida ambao watu wangeweza kuona na kugusa, hawakuhisi tena kwamba Alikuwa akionekana na kutoweka, na kwamba wangeweza kumkaribia. Kinyume cha mambo ni kwamba, wangejaribu kuelewa mapenzi ya Mungu au kuuelewa uungu Wake kupitia kila hatua, maneno, na kazi ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu. Hata ingawa kazi iliyokamilishwa na Bwana Yesu, njia Zake za kufanya kazi, na mitazamo ambayo kutoka kwayo Aliongea ilitofautiana na ile ya nafsi halisi ya Mungu katika ulimwengu wa kiroho, kila kitu kumhusu kilimwakilisha kwa kweli Mungu Mwenyewe ambaye binadamu walikuwa hawajawahi kumwona awali—hili haliwezi kukataliwa! Hivi ni kusema, haijalishi ni kwa umbo gani ambalo Mungu huonekana, haijalishi huongea kutoka katika mtazamo upi, au Yeye hukabiliana na binadamu kupitia kwa taswira gani, Mungu hawakilishi chochote isipokuwa Yeye Mwenyewe. Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote—Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote aliyepotoka. Mungu ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kukataliwa.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ingawa kuonekana kwa Mungu mwenye mwili ni kama mwanadamu, Anajifunza maarifa ya mwanadamu na kuongea lugha ya mwanadamu, na wakati mwingine Anaonyesha hata mawazo Yake kwa jinsi na hisia za mwanadamu, namna Anavyowaona wanadamu, kiini cha vitu, na namna ambavyo watu waliopotoka wanavyomwona mwanadamu na kiini cha vitu kwa hakika si sawa kabisa. Mtazamo Wake na kimo Anachosimamia ni jambo ambalo halifikiwi na mtu aliyepotoka. Hii ni kwa sababu Mungu ni ukweli, mwili Anaouvalia unamiliki pia kiini cha Mungu, na fikira Zake na kile ambacho kinadhihirishwa na ubinadamu Wake pia ni ukweli. Kwa watu waliopotoka, kile Anachoeleza katika mwili ni matoleo ya ukweli na maisha. Matoleo haya si ya mtu mmoja tu lakini kwa wanadamu wote. Kwa mtu yeyote aliyepotoka, katika moyo wake kunao tu wale watu wachache ambao wanahusiana na yeye. Kunao tu hao watu kadhaa ambao anawatunza ambao anajali kuwahusu. Wakati janga linakaribia, anafikiria kwanza kuhusu watoto wake binafsi, mume au mke au wazazi, na mtu mwenye moyo wa kujitoa zaidi kuhusu mwanadamu angefikiria zaidi kuhusu baadhi ya watu wa ukoo au rafiki mzuri; je yeye huwafikiria wengine? La hasha! Kwa sababu binadamu ni, kwa hakika, binadamu, na wanaweza tu kuangalia kila kitu kutoka kwa mtazamo na kutoka katika kimo cha mtu. Hata hivyo, Mungu mwenye mwili ni tofauti kabisa na mtu aliyepotoka. Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha madaraka Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na akili ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka. Watu wanapowaangalia wanadamu, wanawaangalia kwa mtazamo wa binadamu, na wanatumia mambo kama vile maarifa ya binadamu na masharti na nadharia za binadamu kama kipimo. Hali hii imo ndani ya mawanda ya kile ambacho watu wanaweza kuona kwa macho yao; ni ndani ya upana ambao watu waliopotoka wanaweza kutimiza. Mungu anapowatazama wanadamu, Anawatazama kwa macho ya kiungu, na Anatumia kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho kama kipimo. Mawanda haya yanajumuisha mambo ambayo watu hawawezi kuona, na hapo ndipo Mungu mwenye mwili na wanadamu waliopotoka walivyo tofauti kabisa. Tofauti hii inaamuliwa na viini tofauti vya wanadamu na vya Mungu na ndivyo vinavyoamua utambulisho na nafasi zao pamoja na mtazamo na kimo ambacho wanaona mambo.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu ni mwili wa Mungu mwenyewe. Roho wa Mungu ni mkubwa, Yeye ni mwenyezi, mtakatifu, na mwenye haki—na vilevile ndivyo ambavyo mwili Wake ulivyo pia mkubwa, wenye uwezo, mtakatifu, na wenye haki. Mwili kama huo unaweza kufanya tu kile ambacho ni chenye haki na manufaa kwa mwanadamu, kile ambacho ni kitakatifu, chenye utukufu, na uweza, na hakiwezi kukifanya chochote ambacho kinakiuka ukweli au uadilifu na haki, isitoshe hata kile ambacho kinaasi dhidi ya Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni mtakatifu, na hivyo basi mwili Wake hauwezi kuharibiwa na Shetani; mwili Wake una kiini tofauti na ule mwili wa mwanadamu. Kwani ni mwanadamu, wala si Mungu, ambaye anaharibiwa na Shetani, na mwili wa Mungu usingeweza kuharibiwa na Shetani.

kutoka katika “Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo wa kweli sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale wanaojifanya kuwa Kristo wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.

kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)

Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili kamwe hangefanya kazi yoyote ambayo inasumbua usimamizi Wake Mwenyewe. Hili ndilo ambalo binadamu wote wanapaswa kuelewa. Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya usimamizi wa Mungu Mwenyewe. Vile vile, kazi ya Kristo ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Kutokana na kwamba Mungu Anapata mwili, Anatambua dutu Yake ndani ya mwili Wake, kama kwamba mwili Wake ni wa kutosha kufanya kazi Yake. Kwa hivyo, kazi zote za Roho wa Mungu zinabadilishwa na kazi ya Kristo wakati wa kupata mwili, na kwenye msingi wa kazi zote wakati wa kupata mwili ni kazi ya Kristo. Haiwezi kuchanganyika na kazi yoyote ile kutoka enzi nyingine yoyote. Na kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, Yeye Anafanya kazi katika utambulisho wa mwili Wake; kwa kuwa Yeye hukuja katika mwili, kisha Yeye humaliza katika mwili kazi hiyo Anayoazimia kufanya. Iwe ni Roho wa Mungu au ni Kristo, wote ni Mungu Mwenyewe, na Anafanya kazi hiyo Anayoazimia kufanya na hufanya huduma hiyo Anayopaswa kufanya.

Dutu ya Mungu yenyewe hushika na kutumia mamlaka, lakini Yeye Anao uwezo wa kuwasilisha kwa ukamilifu mamlaka ambayo hutoka Kwake. Iwe ni kazi ya Roho au kazi ya mwili, hakuna ambayo itazozana na nyingine. Roho wa Mungu ndiyo mamlaka juu ya viumbe vyote. Mwili na dutu ya Mungu pia inayo mamlaka, bali Mungu katika mwili Anaweza kufanya kazi yote inayotii mapenzi ya Baba wa mbinguni. Hii haiwezi kupatikana au kufanyika na binadamu yeyote. Mungu Mwenyewe ni mamlaka, lakini mwili Wake unaweza kunyenyekea kwa mamlaka Yake. Hii ndiyo maana ya ndani ya maneno: “Kristo hutii mapenzi ya Mungu Baba.” Mungu ni Roho na Anaweza kufanya kazi ya wokovu, kama vile Mungu Anavyoweza kuwa mwanadamu. Hata hivyo, Mungu Mwenyewe Anafanya kazi Yake Mwenyewe; Yeye wala hazuii wala kuathiri, wala kufanya kazi inayozipinganisha pande zote mbili, kwa kuwa kiini cha kazi iliyofanywa na Roho na mwili yote ni sawa. Iwe ni Roho au mwili, vyote hufanya kazi kutimiza nia moja na kusimamia kazi sawa. Ingawa Roho na mwili huwa na sifa mbili tofauti, dutu yao ni sawa; zote zina dutu ya Mungu Mwenyewe, na utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Mungu Mwenyewe hana mambo ya kuasi; dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote. Hata katika mwili, Mungu hafanyi lolote linalomuasi Mungu Baba. Hata kwa gharama ya kutoa sadaka maisha Yake, Angekuwa kwa ukamilifu tayari na kutofanya uchaguzi mwingine. Mungu hana mambo ya ukamilifu wa kibinafsi na umuhimu wa kibinafsi, au yale wa kujiona na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na ile ya Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelaghaiwa na kufinyangwa Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani. Haijalishi ugumu wa kazi, au udhaifu wa mwili, Mungu, wakati Anapoishi katika mwili, kamwe hatafanya kitu chochote kitakachopinga kazi ya Mungu Mwenyewe, wala kuacha mapenzi ya Mungu Baba kwa njia ya uasi. Ni afadhali Ateseke maumivu ya mwili kuliko kwenda kinyume na matakwa ya Mungu Baba; ni kama vile Yesu Alisema katika sala, “Baba, kama inawezekana, kikombe hiki kiniondokee: hata hivyo si kama Mimi Nipendavyo, bali kama Wewe upendavyo.” Wanadamu watachagua, bali Kristo hawezi. Ingawa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe, bado Yeye Anatafuta mapenzi ya Mungu Baba, na Anatimiza kile Alichokabidhiwa na Mungu Baba, kutoka kwa mtazamo wa mwili. Hili ni jambo ambalo haliwezi kupatikana kwa binadamu. Hilo ambalo huja kutoka kwa Shetani haliwezi kuwa na dutu ya Mungu, bali mojawapo ya yale ambayo hukosa kutii na kumpinga Mungu. Haliwezi kumtii Mungu kikamilifu, wala kutii mapenzi ya Mungu kwa hiari. Wanadamu wote isipokuwa Kristo wanaweza kufanya yaliyo ya kumpinga Mungu, na hakuna anayeweza moja kwa moja kufanya kazi aliyoaminiwa na Mungu; hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuzingatia usimamizi wa Mungu kama wajibu wake wenyewe kutekeleza. Kuwasilisha mapenzi ya Mungu Baba ni kiini cha Kristo; uasi dhidi ya Mungu ni tabia ya shetani. Sifa hizo mbili hazipatani, na yeyote aliye na sifa za shetani hawezi kuitwa Kristo. Sababu ambayo binadamu hawezi kufanya kazi ya Mungu kwa niaba Yake ni kwa sababu mwanadamu hana kiini chochote cha Mungu. Binadamu humfanyia Mungu kazi kwa ajili ya maslahi binafsi ya binadamu na ya matarajio Yake ya baadaye, lakini Kristo Anafanya kazi ya kufanya mapenzi ya Mungu Baba.

Ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake. Ingawa yuko katika mwili, ubinadamu Wake si kama ule wa binadamu wa mwili kabisa. Anao upekee wa tabia Yake Mwenyewe, na hii pia huongozwa na uungu Wake. Uungu Wake hauna udhaifu; udhaifu wa Kristo unaelezea ule wa ubinadamu Wake. Kwa kiasi fulani, udhaifu huu huzuia uungu Wake, lakini mipaka hiyo ipo tu kati ya wigo fulani na wakati, na sio zisizo na mipaka. Linapokuja suala la muda wa kufanya kazi ya uungu Wake, hufanyika bila kujali ubinadamu Wake. Ubinadamu wa Kristo kabisa huongozwa na uungu Wake. Mbali na maisha ya kawaida ya ubinadamu Wake, matendo mengine yote ya ubinadamu Wake ni ya kushawishiwa, inayoathirika na kuelekezwa na uungu Wake. Ingawa Kristo Anao ubinadamu, haukatizi kazi ya uungu Wake. Hii hasa ni kwa sababu ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake; ingawa ubinadamu Wake haujakomaa katika mwenendo Wake mbele ya wengine, hauathiri kazi ya kawaida ya uungu Wake. Ninaposema kwamba ubinadamu Wake haujapotoshwa, Ninamaanisha kwamba ubinadamu wa Kristo unaweza moja kwa moja kuongozwa na uungu Wake, na kwamba Yeye ni mwenye hisia kubwa kuliko ile ya mwanadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake unafaa zaidi kwa kuongozwa na uungu katika kazi Yake; ubinadamu Wake una uwezo wa kuonyesha kazi ya uungu, kama vile unao uwezo wa kutii kazi kama hiyo. Mungu Anapofanya kazi katika mwili, hajawahi kamwe kupoteza maono ya wajibu wa mwanadamu katika mwili Anaopaswa kutimiza; Anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli. Anayo dutu ya Mungu, na utambulisho Wake ni mfano wa Mungu Mwenyewe. Ni kwamba tu Amekuja duniani na kuwa kiumbe aliyeumbwa, na ganda la nje la kiumbe, na sasa Amemiliki ubinadamu ambao hakuwa nao mwanzo; Yeye anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni. Hiki ni kiumbe cha Mungu Mwenyewe na hakiigwi na binadamu. Utambulisho Wake ni Mungu Mwenyewe. Ni kutokana na mtazamo wa mwili ndio Yeye huabudu Mungu; Kwa hivyo, maneno “Kristo huabudu Mungu mbinguni” si kwa makosa. Kile Anachouliza binadamu hasa ni nafsi Yake Mwenyewe; Yeye tayari Ameshafanikisha yote Anayotarajia kutoka kwa binadamu kabla ya kuwauliza wafanye hayo. Asingeweza kudai wengine wakati Yeye Mwenyewe Anapata kwao bure, kwa kuwa haya yote yanayotengeneza nafsi Yake. Bila kujali jinsi Yeye hufanya kazi Yake, wala Naye hangewahi kutenda kwa namna inayomuasi Mungu. Haijalishi Analomuuliza mwanadamu, hakuna mahitaji Yake yanayozidi uwezo wa mwanadamu kupata. Yote Afanyayo ni kutenda mapenzi ya Mungu na ni kwa ajili ya usimamizi Wake. Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote, kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa. Mamlaka haya ni uungu Wake, yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe, ambayo huamua utambulisho Wake. Kwa hiyo, haijalishi jinsi ubinadamu Wake ni wa kawaida ni wazi kuwa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe; haijalishi upande Anaosimama Akiongea na kwa vyovyote vile Yeye hutii mapenzi ya Mungu, haiwezi kusemwa kwamba Yeye si Mungu Mwenyewe. Wanadamu wajinga na wapumbavu mara nyingi huchukua ubinadamu wa kawaida wa Kristo kama dosari. Haijalishi jinsi Anavyofichua na kuonyesha nafsi ya uungu Wake, mwanadamu bado hawezi kukiri kwamba Yeye ni Kristo. Na zaidi kwamba Kristo Anaonyesha utii Wake na unyenyekevu, ndivyo wanadamu wengi wajinga humchukua Kristo kwa mzaha. Kuna hata wale ambao huelekeza Kwake mtizamo wa kutengwa na dharau, ilhali kuweka wale “wanadamu wakubwa” wa picha ya kujidai juu ya meza na kuwaabudu. Upinzani wa binadamu dhidi ya, na uasi wa Mungu huja kutokana na ukweli kwamba kiini cha Mungu mwenye mwili hutii mapenzi ya Mungu, vile vile kutokana ubinadamu wa kawaida wa Kristo; hapa ndipo kuna chanzo cha upinzani wa binadamu na uasi wake kwa Mungu. Kama Kristo hangekuwa mwenye umbo la ubinadamu wala nia ya kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe aliyeumbwa, lakini badala yake kumiliki ubinadamu mkuu, basi kuna uwezekano hakungekuwa na uasi katika mwanadamu yeyote. Sababu ya binadamu kuwa tayari kuamini katika Mungu Asiyeonekana mbinguni ni kwa sababu Mungu mbinguni hana ubinadamu na Yeye hana sifa ya kiumbe hata moja. Hivyo binadamu siku zote humchukua Yeye kwa heshima kubwa, lakini anayo tabia ya dharau kwa Kristo.

Ingawa Kristo duniani Anaweza kufanya kazi kwa niaba ya Mungu Mwenyewe, hajakuja na nia ya kuonyesha watu wote mfano Wake katika mwili. Yeye hajakuja kwa watu wote kumwona; Anakuja kwa ajili ya kuwaruhusu binadamu kuongozwa na mkono Wake, na hivyo kuingia katika enzi mpya. Kazi ya mwili wa Kristo ni kwa ajili ya kazi ya Mungu Mwenyewe, yaani, kwa ajili ya kazi ya Mungu katika mwili, na si ili kuwawezesha binadamu kuelewa kikamilifu kiini cha mwili Wake. Haijalishi jinsi Anavyofanya kazi, haiwezi kuzidi yanayoweza kupatwa na mwili. Haijalishi jinsi Anavyofanya kazi, anafanya hivyo katika mwili na ubinadamu wa kawaida, na wala hafichui kwa kikamilifu kwa mwanadamu uso wa kweli wa Mungu. Zaidi ya hayo, kazi Yake katika mwili kamwe sio isiyo ya kawaida au isiyokadirika kama mwanadamu anavyodhani. Japokuwa Kristo Anamwakilisha Mungu Mwenyewe katika mwili na hufanya binafsi ambayo Mungu Mwenyewe Anapaswa kufanya, Yeye hakani kuwepo kwa Mungu mbinguni, wala kuyatangaza matendo Yake Mwenyewe kwa msisimko. Badala yake, Yeye kwa unyenyekevu Hubaki kwa siri ndani ya mwili Wake. Mbali na Kristo, wale ambao wanadai kwa udanganyifu kuwa Kristo hawana sifa Zake. Wakiwekwa sambamba dhidi ya tabia za kiburi na kujiinua za Kristo wa uongo, inakuwa dhahiri aina gani ya mwili ndiye Kristo wa kweli. Walivyo waongo zaidi, ndivyo Kristo wa uongo wanavyojionyesha wenyewe, na ndivyo wanavyoweza zaidi kufanya kazi za ishara na maajabu ya kuwahadaa binadamu. Kristo wa uongo hawana sifa za Mungu; Kristo hajachafuliwa na kipengele chochote cha dutu ya Kristo wa uongo. Mungu hupata mwili tu kukamilisha kazi ya mwili, na sio tu kuwaruhusu watu wote kumwona. Badala yake, Yeye huacha kazi Yake ithibitishe utambulisho Wake, na kuruhusu Anachofichua kushuhudia dutu Yake. Dutu Yake haikosi msingi; utambulisho Wake haukukamatwa na mkono Wake; huamuliwa kwa kazi Yake na dutu Yake. Ingawa Anacho kiini cha Mungu Mwenyewe na uwezo wa kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, Yeye bado, hata hivyo, mwili ambao sio kama Roho. Yeye si Mungu na sifa za Roho; Yeye ni Mungu na ganda la mwili. Kwa hivyo, haijalishi jinsi ya ukawaida Wake na Alivyo mdhaifu, na vyovyote vile Anavyotafuta mapenzi ya Mungu Baba, uungu Wake ni usioweza kupingwa. Katika mwili wa Mungu haupo tu ubinadamu wa kawaida na udhaifu Wake; kunao hata zaidi uzuri na mambo yasiyoeleweka ya uungu Wake, na vile vile matendo Yake yote katika mwili. Kwa hiyo, ubinadamu na uungu kwa kweli vipo kwa matendo ndani ya Kristo. Hili sio jambo tupu au lisilo la kawaida kwa vyovyote vile. Yeye huja duniani na lengo kuu la kufanya kazi; ni muhimu kumiliki ubinadamu wa kawaida kutekeleza kazi duniani; la sivyo, haijalishi ukubwa wa nguvu ya uungu Wake, kazi Yake ya awali haiwezi kutiwa katika utumizi mzuri. Ingawa ubinadamu Wake ni wa umuhimu mkubwa, sio dutu Yake. Dutu Yake ni uungu; Kwa hiyo, wakati Anapoanza kufanya huduma Yake hapa duniani ndio wakati Yeye huanza kuonyesha nafsi ya uungu Wake. Ubinadamu Wake uko kwa ajili tu ya kuendeleza maisha ya kawaida ya mwili Wake ili uungu Wake uweze kufanya kazi kama kawaida katika mwili; ni uungu ndio unaoongoza kazi Yake kwa ukamilifu. Wakati Anapomaliza kazi Yake, Atakuwa Ametimiza mujibu wa huduma Yake. Wanachopaswa kujua wanadamuni ni ukamilifu wa kazi Yake, na ni kwa njia ya kazi Yake kuwa Yeye Humwezesha binadamu kumjua Yeye. Katika kipindi cha kazi Yake, Yeye huonyesha kikamilifu kabisa nafsi ya uungu Wake, ambayo si tabia iliyochafuliwa na ubinadamu, au nafsi iliyochafuliwa na mawazo na tabia za binadamu. Wakati utakapokuja ambapo huduma Yake yote imefika mwisho, Atakuwa tayari kwa kikamilifu na kikamilifu Amekwishaonyesha tabia hiyo Anayopaswa kueleza. Kazi Yake haifundishwi na mwanadamu yeyote; maonyesho ya tabia Yake pia ni huru kabisa, haudhibitiwi na akili au kutengenezwa na mawazo, bali hujitokeza kiasili. Hili haliwezi kutimizwa na binadamu yeyote. Hata kama mazingira ni magumu au hali haziruhusu, Yeye Anao uwezo wa kuonyesha tabia Yake kwa wakati muafaka. Yule Ambaye ni Kristo Anaonyesha nafsi ya Kristo, ilhali wale ambao sio hawana tabia za Kristo. Kwa hivyo, hata kama wote watampinga Yeye au kuwa na fikira Kwake, hakuna anayeweza kukana kwa misingi ya fikira ya mwanadamu kwamba tabia iliyoonyeshwa na Kristo ni ile ya Mungu. Wale wote ambao humfuata Kristo kwa moyo wa kweli au kumtafuta Mungu kwa nia watakubali kwamba Yeye ni Kristo kulingana na maonyesho ya uungu Wake. Wao kamwe hawangewahi kumkataa Kristo kwa misingi ya kipengele chochote Chake ambacho hakipatani na fikira za mwanadamu. Ingawa binadamu ni wapumbavu sana, wote wanajua hasa ni nini mapenzi ya binadamu na kile kitokacho kwa Mungu. Ni kwamba tu watu wengi kwa makusudi humpinga Kristo kutokana na makusudi yao wenyewe. Kama si kwa ajili ya haya, hakuna hata mwanadamu mmoja angekuwa na sababu ya kukataa kuwepo kwa Kristo, kwa kuwa uungu uliodhihirishwa na Kristo kwa hakika upo, na kazi Yake inaweza kushuhudiwa kwa macho ya wote.

Kazi na maonyesho ya Kristo huamua dutu Yake. Yeye Anaweza kukamilisha kwa moyo wa kweli kile Alichoaminiwa kufanya. Anaweza kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli, na kwa moyo wa kweli Atafute mapenzi ya Mungu Baba. Yote haya yanaamuliwa na dutu Yake. Na vile vile ufunuo Wake wa asili pia unaamuliwa na dutu Yake; sababu ya ufunuo Wake wa asili kuitwa hivyo ni kwa sababu ya maonyesho Yake siyo maigizo, au matokeo ya elimu na mwanadamu, au matokeo ya miaka mingi ya kukuzwa na mwanadamu. Hakujifunza au kujivika nayo Yeye Mwenyewe; badala yake, ni asili ndani Yake. Mwanadamu anaweza kukataa kazi Yake, maonyesho Yake, ubinadamu Wake, na maisha yote ya ubinadamu Wake wa kawaida, lakini hakuna hata mmoja anayeweza kukana kwamba Yeye humwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli; hakuna anayeweza kukana kwamba Amekuja kutimiza mapenzi ya Baba wa mbinguni, na hakuna anayeweza kukana uaminifu Alio nao Anapomtafuta Mungu Baba. Ingawa mfano Wake si wa kupendeza hisia, ingawa hotuba Yake haujajawa na hewa ya ajabu, na kazi Yake sio ya kutikisa ulimwengu au mbingu vile mwanadamu anavyofikiria, Yeye hakika ni Kristo, Anayetimiza mapenzi ya Baba wa mbinguni kwa moyo wa kweli, Ananyenyekea kikamilifu kwa Baba wa mbinguni, na ni mtiifu mpaka wakati kifo. Hii ni kwa sababu dutu Yake ni dutu ya Kristo. Ukweli huu ni mgumu kwa mwanadamu kuamini lakini kwa kweli upo. Wakati huduma ya Kristo imetimia kikamilifu, mwanadamu ataweza kuona kutokana na kazi Zake kwamba tabia Yake na nafsi Yake yanawakilisha tabia na nafsi ya Mungu huko mbinguni. Wakati huo, ujumla wa kazi Zake zote utaweza kuthibitisha kwamba Yeye kweli ni Neno linalogeuka mwili, na si sawa na ule wa mwili na damu ya mwanadamu. Kila hatua ya kazi ya Kristo duniani ina umuhimu wakilishi Wake, lakini mwanadamu anayepitia kazi halisi ya kila hatua hawezi kufahamu umuhimu wa kazi Yake. Hii hasa ni vile katika hatua kadhaa za kazi zilizofanywa na Mungu mwenye mwili mara ya pili. Wengi wa wale ambao wamesikia tu au kuona maneno ya Kristo tu lakini bado hawajawahi kumwona hawana fikira ya kazi Yake; wale ambao wamemwona Kristo na kusikia maneno Yake, na vile vile kupitia kazi Yake, huona ugumu kuikubali kazi Yake. Je, hii si kwa sababu ya kwamba kuonekana na ubinadamu wa kawaida kwa Kristo hakulingani na matarajio ya binadamu? Wale wanaokubali kazi Yake baada ya Kristo kwenda hawatakuwa na matatizo kama hayo, kwa kuwa wao wanaikubali kazi Yake na wala hawapati kukutana na ubinadamu wa kawaida wa Kristo. Mwanadamu hawezi kuacha fikira zake kuhusu Mungu na badala yake humchunguza kwa mkazo; hii ni kutokana na ukweli kwamba mwanadamu analenga tu juu ya kuonekana Kwake na anashindwa kutambua dutu Yake kwa kuzingatia kazi Yake na maneno Yake. Iwapo mwanadamu ataufumbia macho kuonekana kwa Kristo au kuepuka kujadili ubinadamu wa Kristo, na aongee tu juu ya uungu Wake, Ambao kazi Yake na maneno hayawezi kufikiwa na mwanadamu yeyote, basi fikira ya binadamu itapungua kwa nusu, hata kwa kiasi kwamba matatizo yote ya mwanadamu yatatatuliwa. Wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, mwanadamu hawezi kumvumilia na amejaa wingi wa fikira mbalimbali kumhusu, na matukio ya upinzani na uasi ni kawaida. Binadamu hawezi kuvumilia kuwepo kwa Mungu, kuonyesha “upole” kwa unyenyekevu na kujificha kwa Kristo, au “kuisamehe” dutu ya Kristo inayomtii Baba wa mbinguni. Kwa hivyo, Hawezi kukaa na mwanadamu milele baada ya kumaliza kazi Yake, kwa kuwa mwanadamu hana nia ya kumruhusu kuishi pamoja nao. Iwapo mwanadamu hawawezi “kuonyesha upole” Kwake katika kipindi Chake cha kazi, basi, ni jinsi gani wangeweza kumvumilia Yeye kuishi nao baada ya kumaliza kutekeleza shughuli Zake, kuwaangalia hatua kwa hatua na wakipitia maneno Yake? Je, si wengi kisha wangeanguka kwa ajili Yake? Mwanadamu anamruhusu tu kufanya kazi duniani; hiki ndicho kiasi kikubwa zaidi cha upole wa mwanadamu. Kama si kwa sababu ya kazi Yake, mwanadamu angekuwa ameshamtupa nje ya dunia, hivyo kwa kiasi gani kidogo wangeweza kumwonyesha upole mara kazi Yake inapokamilika? Basi si mwanadamu angemuua na kumtesa hadi kufa? Iwapo Yeye hangekuwa Anaitwa Kristo, basi kuna uwezekano hangewahi kufanya kazi miongoni mwa wanadamu; iwapo hangefanya kazi na utambulisho wa Mungu Mwenyewe, na badala yake Afanye kazi tu kama mwanadamu wa kawaida, basi mwanadamu hangevumilia sentensi hata moja kutamkwa Naye, wala kuvumilia hata kiasi kidogo cha kazi Yake. Basi Anaweza kubeba tu utambulisho huu pamoja Naye katika kazi Yake. Kwa njia hii, kazi Yake ni ya nguvu zaidi kuliko kama hangefanya hivyo, kwa kuwa binadamu wote wako tayari kutii hadhi na utambulisho mkubwa. Iwapo Yeye hangekuwa na utambulisho wa Mungu Mwenyewe Alipokuwa akifanya kazi ama kuonekana kama Mungu Mwenyewe, basi hangekuwa na nafasi ya kufanya kazi hata kidogo. Ingawa Yeye Anayo dutu ya Mungu na nafsi ya Kristo, mwanadamu hangelegea na kumruhusu kufanya kazi kwa urahisi miongoni mwa wanadamu. Yeye hubeba utambulisho wa Mungu Mwenyewe katika kazi Yake; ingawa kazi hiyo ina nguvu mara kadhaa zaidi kuliko ile hufanyika bila utambulisho huo, bado wanadamu sio watiifu Kwake kikamilifu, kwa kuwa binadamu hunyenyekea tu kwa msimamo Wake wala si dutu Yake. Kama ni hivyo, wakati labda siku moja Kristo aamue kujiuzulu kutoka katika wadhifa Wake, inawezekana mwanadamu amruhusu kubaki hai hata kwa siku moja? Mungu yuko tayari kuishi duniani na binadamu ili Aweze kuona matokeo ambayo kazi ya mikono Yake italeta katika miaka itakayofuata. Hata hivyo, binadamu wanashindwa kuvumilia kukaa Kwake duniani hata siku moja, hivyo inamfanya kukata tamaa. Tayari ni kiasi kikubwa cha upole na neema ya mwanadamu kumruhusu Mungu kutenda kazi Anayopaswa kufanya miongoni mwa wanadamu na kutimiza huduma Yake. Ingawa wale ambao wameshindwa kibinafsi na Yeye wanamwonyesha neema kuu, bado tu wamempa kibali cha kuwepo tu kwa ajili ya kutimiza kazi Yake na si hata saa moja zaidi baada ya kukamilisha kazi hiyo. Iwapo ni hivyo, je itakuwaje na wale ambao bado hawajashindwa na yeye? Je, sababu ambayo mwanadamu anamtendea Mungu mwenye mwili kwa njia hii ni kwa sababu Yeye ni Kristo na ganda la binadamu wa kawaida? Iwapo Angekuwa tu na uungu na sio ubinadamu wa kawaida, basi si matatizo ya binadamu yangetatuliwa kwa urahisi mno? Binadamu kishingo upande anatambua uungu Wake na haonyeshi haja yoyote katika ganda Lake la ubinadamu wa kawaida, licha ya ukweli kwamba dutu Yake ni sawa hasa kama vile ile ya Kristo inayonyenyekea kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kwa sababu hii, Aliweza tu kuikomesha kazi Yake ya kuwa miongoni mwa wanadamu kushiriki pamoja nao katika furaha na huzuni, kwa kuwa mwanadamu hangeweza tena kuvumilia uwepo Wake.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumatano, 15 Mei 2019

Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili

2. Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili

Maneno Husika ya Mungu:
Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu ni mwanadamu hata zaidi ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyepotoka, ambaye anaishi pamoja na Yeye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuweza kumpata mwanadamu kabisa. Kwa sababu hii, ingawa mwili huu ni wa kawaida, mchango Wake kwa wanadamu na umuhimu Wake katika uwepo wa mwanadamu kunamfanya Awe wa thamani zaidi, na thamani halisi na umuhimu wa mwili huu hauwezi kupimwa na mwanadamu yeyote. Ingawa mwili huu hauwezi kumwangamiza Shetani moja kwa moja, Anaweza kutumia kazi Yake kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, na kumfanya Shetani kutii kikamilifu katika utawala Wake. Ni kwa sababu Mungu amepata mwili ili kwamba Aweze kumshinda Shetani na aweze kumwokoa binadamu. Hamwangamizi Shetani moja kwa moja, bali Anakuwa mwili ili kuweza kufanya kazi ya kumshinda binadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Kwa njia hii, Anakuwa na uwezo zaidi wa kuwa ushuhuda Kwake Mwenyewe miongoni mwa viumbe, na Anakuwa na uwezo zaidi wa kumwokoa mwanadamu aliyepotea. Ushindi wa Mungu mwenye mwili dhidi ya Shetani unabeba ushuhuda mkubwa, na una ushawishi mkubwa, kuliko uangamizaji wa Shetani wa moja kwa moja na Roho wa Mungu. Mungu katika mwili Ana uwezo zaidi wa kumsaidia mwanadamu kumjua Muumba, na Ana uwezo zaidi wa kuwa na ushuhuda Wake mwenyewe miongoni mwa viumbe.

kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kitu kizuri zaidi kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ya kusihi, na mapenzi Yake kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi Wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwepo na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambapo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya utendaji zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, Anamfunulia mwanadamu Mungu ambaye ni halisi na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonyesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, Anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, Anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na Anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili badala ya Roho wa Mungu. Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili Wake, wale wanaofuata wanakuwa hawatafuti tena vitu hivyo visivyo yakini, na wanaacha kukisia mapenzi ya Mungu asiye yakini. Mungu anapoeneza kazi Yake katika mwili, wale wanaomfuata wataieneza kazi ambayo Ameifanya katika mwili kwa dini na madhehebu yote, na watazungumza maneno Yake yote katika masikio ya wanadamu wote. Yote yale yanayosikizwa na wale wanaoipokea injili Yake yatakuwa ni ukweli wa kazi Yake, yatakuwa mambo ambayo mwanadamu ameyashuhudia na kuyaona binafsi, na utakuwa ukweli na sio uvumi. Ukweli huu ni ushahidi ambao Anauenezea kazi na pia ni zana ambazo Anazitumia katika kueneza kazi. Bila uwepo wa ukweli, injili Yake isingeweza kuenea katika nchi zote na maeneo yote; bila ukweli bali kwa fikira tu za mwanadamu, Asingeweza kufanya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Roho hagusiki na mwanadamu, na wala haonekani kuonekana na mwanadamu, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Mawazo ya mwanadamu, hata hivyo, ni matupu, na hayawezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; tabia ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekana na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye binafsi Anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia halisi ambayo Mungu anaonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwona Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili.

kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na hata Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote. Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu; bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu itapungukiwa na mwangaza, dunia itakuwa vurugu, na wanadamu wote wataishi katika njaa na mabaa. Atawaonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima mngekuwa viongozi wa wenye dhambi na maiti milele. Mnapaswa kujua kwamba bila kuwepo kwa mwili huu, wanadamu wote wangetazamia msiba usioepukika na kupata kuwa ngumu kuponyoka adhabu kali zaidi ya Mungu katika siku za mwisho. Bila kuzaliwa kwa mwili huu wa kawaida, nyinyi nyote mngekuwa katika hali ambayo uhai wala kifo havitakuja bila kujali jinsi mtakavyovitafuta; bila kuwepo kwa mwili huu, basi siku hii hamngeweza kupokea ukweli na kuja mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Badala yake, mngeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zenu zinazohuzunisha. Je, mnajua? Kama sio kwa kurudi kwa Mungu kwa mwili, hakuna ambaye angepata nafasi ya wokovu; na isipokuwa kwa kuja kwa mwili huu, Mungu angekuwa ameimaliza kitambo enzi ya zamani. Hivyo basi, mnaweza bado kuukataa kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu? Sababu mnaweza kufaidika sana kutoka kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi mbona hamumkubali kwa urahisi?

Kazi ya Mungu ni ile usiyoweza kuelewa. Kama huwezi kufahamu kama uamuzi wako ni sahihi wala kujua kama kazi ya Mungu inaweza kufaulu, basi mbona usijaribu bahati yako na kuona iwapo huyu mwanadamu wa kawaida ni wa msaada mkubwa kwako, na iwapo Mungu amefanya kazi kubwa. Hata hivyo, lazima Nikuelezee kuwa wakati wa Nuhu, wanadamu walikuwa wamekula na kunywa, wakifunga ndoa na kupeana katika ndoa hadi kiwango ambacho Mungu asingevumilia kushuhudia, hivyo, Alituma chini mafuriko makubwa kuangamiza wanadamu na kuacha tu nyuma familia ya Nuhu ya watu wanane na aina yote ya ndege na wanyama. Katika siku za mwisho, hata hivyo, wale waliohifadhiwa na Mungu ni wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake hadi mwisho. Ingawa nyakati zote mbili zilikuwa za upotovu mkubwa Asizoweza kuvumilia kushuhudia Mungu, na mwanadamu katika enzi zote mbili alikuwa mpotovu kiasi cha kumkana Mungu kama Bwana, watu wote katika wakati wa Nuhu waliangamizwa na Mungu. Mwanadamu katika enzi zote mbili amemhuzunisha Mungu sana, lakini Mungu bado Amebakia mvumilivu na wanadamu katika siku za mwisho hadi sasa. Mbona hivi? Hamjawahi kufikiria haya? Kama kweli hamjui, basi wacha Niwaelezee. Sababu Mungu anaweza kushughulika na wanadamu kwa neema siku za mwisho si kwamba ni wapotovu kidogo zaidi kuliko wanadamu katika wakati wa Nuhu ama kwamba wamemwonyesha Mungu toba, sembuse si kwamba Mungu hawezi kuvumilia kuwaangamiza wanadamu katika siku za mwisho ambapo teknolojia imeendelea. Badala yake, ni kwamba Mungu ana kazi ya kufanya kwa kundi la wanadamu katika siku za mwisho na hii itafanywa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Zaidi ya hayo, Mungu atachagua sehemu ya kundi hili kama vyombo Vyake vya wokovu, tunda la mpango Wake wa usimamizi, na kuleta wanadamu kama hawa naye katika enzi ifuatayo. Kwa hivyo, bila kujali, hii gharama iliyolipwa na Mungu yote imekuwa katika maandalizi ya kazi ya kupata mwili Kwake katika siku za mwisho. Yote mliyonayo siku hii ni kwa sababu ya huu mwili. Ni kwa sababu Mungu huishi ndani ya mwili ndiyo mna nafasi ya kuishi. Hii bahati yote nzuri imepatwa kwa sababu ya huyu mwanadamu wa kawaida. Siyo haya tu, lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu. Kwa sababu ni Yeye aliyeleta ukweli, uhai, na njia ya kuwaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya Mungu na mwanadamu, kuleta Mungu na mwanadamu pamoja karibu zaidi na kuwasilisha mawazo kati ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye ambaye Ameleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi yenu na nyinyi kumshikilia? Mkiukataa ukweli unaotamkwa kutoka mdomo Wake na pia kuchukia kuwepo Kwake miongoni mwenu, basi nini itakuwa majaliwa yenu?

Kazi yote ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kupitia huyu mwanadamu wa kawaida. Atakupa kila kitu, na juu ya hayo, Anaweza kuamua kila kitu kukuhusu. Mtu kama huyu anaweza kuwa mnavyoamini: mtu wa kawaida sana kiasi cha kutostahili kutajwa? Ukweli Wake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ushuhuda wa vitendo Vyake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ama ni kuwa njia Anayowaongozea haistahili nyinyi kuifuata? Ni nini kinachowasababisha kumchukia na kumtupilia mbali na kumwepuka? Ni Yeye anayeonyesha ukweli, ni Yeye anayetoa ukweli, na ni Yeye anayewawezesha kuwa na njia ya kusafiri. Inaweza kuwa kwamba bado hamwezi pata chembe cha kazi ya Mungu ndani ya ukweli huu? Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu.

kutoka katika “Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili