Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumamosi, 22 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho? Hakuna kati yenu aliye wazi sana juu ya hili. Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu. Bila kujali kama kuna matokeo yoyote, au kama kuna kuelewa kwa kweli, watu hawa hulenga tu kufanya mambo yasiyo ya dhati kwa nje, na hawalengi matokeo ni watu wanaoishi ndani ya mila za dini, na si watu wanaoishi ndani ya kanisa, na hata zaidi wao si watu wa ufalme. Sala za mtu wa aina hii, nyimbo zake, na kula na kunywa kwake maneno ya Mungu yote yanafuata amri, wanalazimika kufanya hayo, na yanafanyika katika kufuata mitindo, hayafanyiki kwa hiari wala kufanyika kutoka moyoni. Haijalishi ni kiasi gani watu hawa wanaomba au kuimba, hakutakuwa na matokeo kamwe, kwa sababu yote wanayofanya ni amri na mila za kidini, na wao hawatendi neno la Mungu. Kwa kulenga tu mbinu, na kuchukua maneno ya Mungu kama amri ya kuhifadhi, mtu wa aina hii hatendi neno la Mungu, bali tu anaridhisha mwili, na anafanya vitu ili kujionyesha kwa wengine. Aina hii ya matambiko ya dini na amri yanatoka kwa mwanadamu, si kwa Mungu. Mungu hahifadhi sheria, Hazingatii sheria yoyote; Anafanya mambo mapya kila siku na Anafanya kazi ya vitendo. Kama watu katika Kanisa la Nafsi Tatu ambao wamewekewa mipaka kwa ulinzi wa kila asubuhi, sala ya jioni, kutoa shukrani kabla ya kula, kuonyesha shukrani katika kila kitu, na matendo mengine kama haya, haijalishi ni kiasi gani watu hawa wanafanya, au muda wanatenda, hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama watu huishi ndani ya amri, na mioyo yao ikiwa katika vitendo, basi Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi, kwa sababu mioyo ya watu inachukuliwa na amri, inachukuliwa na dhana za kibinadamu; kwa hiyo Mungu hana njia ya kufanya kazi; watu daima watakuwa wakiishi tu chini ya utawala wa sheria, mtu wa aina hii kamwe hataweza kupokea sifa za Mungu.
Maisha ya kawaida ya kiroho ni kuishi maisha mbele ya Mungu. Wakati wa kuomba mtu anaweza kutuliza moyo wake mbele ya Mungu, na kwa njia ya sala anaweza kutafuta kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, kuelewa maneno ya Mungu, na anaweza kuelewa mapenzi ya Mungu. Wakati wa kula na kunywa maneno ya Mungu mtu anaweza kuelewa zaidi na kuwa udhahiri zaidi juu ya ni nini Mungu anataka kufanya sasa hivi, na mtu anaweza kuwa na njia mpya ya matendo na asiwe wa kushikilia ukale, ili matendo ya mtu yote ni kwa lengo la kufanikisha maendeleo katika maisha. Kwa mfano, sala ya mtu si kwa ajili ya kusema baadhi ya maneno mazuri, au kupiga kelele mbele ya Mungu kuonyesha deni ya mtu, bali ni kwa kufanya mazoezi ya kutumia roho ya mtu, kutuliza moyo wa mtu mbele ya Mungu, kufanya mazoezi ya kutafuta uongozi kwa vyote vile, kufanya moyo wa mtu uwe moyo wa kuvutiwa na mwanga mpya kila siku, kutokuwa wa kukaa tu wala mvivu, na kuingia kwenye njia sahihi ya kutenda maneno ya Mungu. Kwa sasa watu wengi wanalenga mbinu, na hawajaribu kufuata ukweli ili kufikia maendeleo katika maisha; hapa ndipo watu hupotoka. Pia kuna baadhi ya watu ambao, hata kama wao wana uwezo wa kupokea mwanga mpya, taratibu zao hazibadiliki, wao huunganisha fikra za dini za zamani ili kupokea neno la Mungu leo, na wanayoingiza bado ni kanuni ambayo hubeba fikra za dini kwa pamoja, na hawaingiziwi mwanga wa leo kabisa. Kwa hivyo, matendo yao ni machafu wanafanya matendo yale yale kwa jina jipya, na haijalishi matendo yao ni mazuri kiwango gani, bado ni ya unafiki. Mungu huongoza watu kufanya mambo mapya kila siku, na Anahitaji watu kuwa na umaizi mpya na ufahamu mpya kila siku, na si kuwa na mienendo ya zamani au wasiobadilika. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, ila mbinu zako hazijabadilika kamwe, kama bado wewe ni wa shauku na mwenye shughuli nyingi kwa nje, na wala huji mbele za Mungu kufurahia maneno Yake kwa moyo mtulivu, basi hutaweza kupata chochote. Wakati wa kupokea kazi mpya wa Mungu, kama hutaunda mpango mpya, kama hutatenda katika njia mpya, kama hutatafuta ufahamu mpya, lakini badala yake kushikilia mambo mazee ya zamani na kupokea kiasi kidogo tu cha mwanga mpya bila kubadili jinsi unavyotenda, basi mtu wa aina hii ingawa yu ndani ya mkondo huu kwa kawaida kwa kweli ni Mfarisayo wa dini nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu.
Kama unataka kuishi maisha ya kawaida ya kiroho, unahitaji kupata mwanga mpya kila kuchao, kutafuta ufahamu wa kweli wa maneno ya Mungu, na kufikia udhahiri kuelekea ukweli. Unahitaji kuwa na njia ya kufanya matendo kwa vyote vile, na kwa kusoma maneno ya Mungu kila siku unaweza kupata maswali mapya na kugundua upungufu wako mwenyewe. Hili litaleta moyo ulio na kiu na unaotafuta, ambao utaweka nafsi yako yote katika mwendo, na wewe utakuwa na uwezo wa kuwa kimya mbele ya Mungu wakati wowote, na kuwa na hofu kubwa ya kuachwa nyuma. Kama mtu anaweza kuwa na huu moyo wa kiu, huu moyo wa kutafuta, na pia awe na nia ya kuingia ndani kwa kuendelea, basi yupo katika njia sahihi kwa ajili ya maisha ya kiroho. Wale wote ambao wanaweza kukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu, ambao wanatamani kufanya maendeleo, ambao wako radhi kutafuta kukamilishwa na Mungu, wale ambao wanatamani kuelewa kwa undani maneno ya Mungu, na ambao hawatafuti vitu visivyo vya kawaida lakini wanalipa gharama ya vitendo, kuonyesha kwa vitendo kufikiria mapenzi ya Mungu, kuingia ndani kwa vitendo, kufanya uzoefu wao kuwa wa kweli zaidi na halisi zaidi, ambao hawatafuti maneno matupu ya kanuni, na ambao pia hawatafuti hisia isiyo ya kawaida, wala kumwabudu mtu yeyote mkubwa mtu wa aina hii ameingia katika maisha ya kawaida ya kiroho, na kila kitu anachofanya ni kwa lengo la kufanikisha maendeleo zaidi katika maisha, kufanya upya roho yake na wala si palepale, na daima awe na uwezo wa kuingia ndani kwa wema. Kwa mfano, aombapo kabla ya kula, halazimishwi kufanya hivyo, lakini badala yake anatuliza moyo wake mbele ya Mungu, kumshukuru Mungu katika moyo wake, yuko tayari kuishi kwa ajili ya Mungu, kuweka muda wake katika mikono ya Mungu, na yuko tayari kushirikiana na Mungu na kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu. Kama moyo wake hauwezi kuwa kimya mbele ya Mungu, ni afadhali asile bali azidi kutenda, basi hii si kufuata sheria, lakini ni kutenda neno la Mungu. Baadhi ya watu, wanapoomba kabla ya kula, kwa kujua wao hujifanya ili kuweka matendo ya kujionyesha, ambayo yanaweza kuonekana kama kumcha Mungu, lakini akili zao huwaza: "Kwa nini nahitaji kufanya matendo kwa njia hii? Si mambo ni mazuri bila kuomba? Mambo yangali vile baada ya kuomba, hivyo kwa nini kujisumbua?" Mtu wa aina hii hufuata amri, na ingawa maneno yake yanasema kwamba yuko tayari kumridhisha Mungu, moyo wake haujaja mbele za Mungu. Haombi namna hii ili afanye mazoezi ya kutuliza moyo wake mbele ya Mungu, bali hufanya hivyo ili kuwadanganya watu wengine na ili watu wengine waone. Mtu wa aina hii ni mnafiki kabisa, kama mchungaji wa dini ambaye anaweza kuombea tu wengine lakini hawezi mwenyewe kuingia ndani; mtu wa aina hii ni ofisa wa kidini, kabisa! Kila siku Mungu ananena mambo mapya, Anafanya mambo mapya, lakini wewe unafuata amri kila siku, ukijaribu kumdanganya Mungu, kushughulikia Mungu bila uangalifu, hivyo si wewe ni mtu ambaye anamwasi Mungu? Je, unaweza kupokea baraka wakati unazingatia amri na kumwasi Mungu? Si wewe utaadibiwa na Mungu?
Kazi ya Mungu kwa kasi inaendelea ikitupa vikundi vidogo mbalimbali vya watu wenye dini na "watu mashuhuri" wanaoshikilia misa ya kanisa kwa umbali sana, na pia kutawanya kwa pande zote nne wale "wataalamu" kati yenu ambao hasa hupenda kufuata kanuni. Kazi ya Mungu haisubiri, haitegemei kitu chochote nawala haizembei. Haivuti au kuburuta mtu yeyote; kama huwezi kustahimili basi utaachwa, bila kujali ni miaka ngapi umefuata. Haijalishi wewe ni mkongwe anayestahili kiasi kipi, kama wewe hufuata amri basi lazima uondolewe. Ninamshauri mtu wa aina hii kuwa na maarifa fulani ya kibinafsi, kwa hiari kuchukua kiti cha nyuma, na kutoshikilia kilicho cha kale; kuwalazimu wengine kutenda neno la Mungu kwa mujibu wa kanuni zako za vitendo si hii ni kujaribu kushinda mioyo ya watu? Utendaji wako ni kufuata sheria, kuwafundisha watu kufuata ibada ya kanisa, na mara zote kuwafanya watu wafanye mambo kulingana na matakwa yako, hivyo huku si kutengeneza vikundi? Hivyo huku si kugawanya kanisa? Basi wewe una ujasiri wa kusema kuwa unafikiria mapenzi ya Mungu vipi? Ni kipi kinakuwezesha kusema kwamba hili ni kuwakamilisha wengine? Ukiendelea kuongoza kwa njia hii, si hii ni kuwaongoza watu ndani ya matambiko ya kidini? Kama mtu ana maisha ya kawaida ya kiroho, kama anapata ufunguliaji na uhuru katika roho zao kila siku, basi anaweza kutenda maneno ya Mungu bila kuzuiwa kumridhisha na, hata anapoomba hapitii tu kanuni au kufuata mchakato, na anao uwezo wa kustahimili mwanga mpya kila siku. Wakati anafanya mazoezi ya kutuliza moyo wake mbele za Mungu, anaweza kufanya moyo wake kweli uwe tulivu mbele ya Mungu na hakuna mtu anayeweza kumvuruga, na hakuna mtu au kitu kinaweza kuzuia maisha yake ya kawaida ya kiroho. Aina hii ya matendo ni kwa lengo la kufanikisha matokeo, si tu kuwapa watu kanuni fulani za kuzingatia. Aina hii ya matendo si kufuata sheria, ila kuendeleza maendeleo ya watu katika maisha. Kama wewe ni mfuataji amri tu, basi maisha yako kamwe hayatabadilika, ingawa wengine wanaweza kufanya matendo kwa njia hii, kama wewe ufanyavyo, mwishowe, wengine wanaweza kustahimili kasi za kazi ya Roho Mtakatifu, wakati utaondolewa kutoka kwa mkondo wa Roho Mtakatifu. Hivyo basi je, hujidanganyi? Madhumuni ya maneno haya ni kuwaruhusu watu watulize mioyo yao mbele ya Mungu na kurejea kwa Mungu, kuruhusu kazi ya Mungu kutekelezwa kwa watu bila kizuizi, na ili itimize matokeo.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Alhamisi, 20 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Mwenyezi Mungu anasema, "Nyie watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda-shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwakomboa? Ni mara ngapi mmeanguka katika mitego ya Shetani? Ni mara ngapi mmejiingiza katika vishawishi vya wanadamu? Na tena, ni mara ngapi mmejikuta katika ugomvi usio na kikomo kati yenu kwa kukosa kuziachilia nafsi zenu? Ni mara ngapi miili yenu imekuwa katika nyumba Yangu ila roho zenu zikiwa kusikojulikana? Licha ya hayo, ni mara ngapi Nimewanyooshea mkono Wangu wa ukombozi; ni mara ngapi Nimewaonea huruma; ni mara ngapi Nimekosa uvumilivu wa kuziona hali zenu za kuhuzunisha za mateso? Ni mara ngapi … hamfahamu?"
Lakini leo kwa ulinzi Wangu, hatimaye mmezishinda shida zote na kuingia katika furaha pamoja Nami; hili ndilo dhihirisho la busara Yangu. Hata hivyo, likumbuke hili vyema! Ni nani kati yenu amewahi kuanguka na akaendelea kuwa thabiti? Ni nani kati yenu amewahi kuwa thabiti bila kuwa na nyakati za unyonge? Miongoni mwa wanadamu, ni nani amewahi kupokea baraka ambazo hazikutoka Kwangu? Ni nani kapitia misukosuko isiyotoka Kwangu? Inawezekana kuwa wale wote wanaonipenda hupokea baraka peke yake? Inawezekana kwamba misukosuko ilimpata Ayubu kwa kukosa kunipenda ila akanikana Mimi? Inawezekana kwamba Paulo aliweza kunihudumia kwa utiifu mbele Yangu kwa sababu aliweza kunipenda kwa dhati? Ijapokuwa mnaweza kushikilia ushuhuda Wangu, lakini je, kuna mtu kati yenu aliye na ushuhuda safi kama dhahabu ambayo haijatiwa najisi? Je, mwanadamu anaweza kuwa na uaminifu halisi? Ushuhuda wenu kuniletea furaha hakukinzani na “uaminfu” kwa sababu Sijawahi kumtarajia mtu yeyote kutoa zaidi. Kwa kufuata dhamira asilia ya mpango Wangu, nyinyi nyote mngekuwa “bidhaa duni—zisizokidhi kiwango.” Je, huu si ni mfano Niliowaambia “kuwaonea huruma”? Je, mnachoona si ni ukombozi Wangu?
Nyinyi nyote mnafaa kuvuta kumbukumbu zenu: Tangu mrejee katika nyumba Yangu, kuna yeyote kati yenu, bila kutafakari faida na hasara, amenifahamu sawa na Petro alivyonifahamu? Mmekariri Biblia kikamilifu, lakini je, mlijifunza chochote cha asili yake? Japo hivyo, bado mmeshikilia “mtaji” wenu, mkikataa kuziachilia nafsi zenu. Ninapotoa tamko, Nikiwazungumzia ana kwa ana, Ni nani kati yenu amewahi kuweka chini “nyaraka” zilizofunikwa kupokea maneno ya uzima ambayo Nimeyaweka wazi? Hamyajali maneno Yangu na wala hamyapendi. Badala yake, mnatumia maneno Yangu kama bombomu dhidi ya maadui wenu ili kudumisha nafasi zenu; hamjaribu hata kidogo kuyakubali maoni Yangu ili mnifahamu. Kila mmoja wenu anamwangazia sana mtu mwingine, nyinyi nyote ni “wasio bahili,” nyote “mnawajali wengine” katika kila hali; je, haya siyo mliyokuwa mnafanya jana? Na leo je? “Utiifu” wenu umepanda juu kwa alama kidogo, nyote mmekuwa wazoefu kiasi, mmekomaa kidogo na kwa sababu ya haya, “uoga” wenu Kwangu umeongezeka kwa njia fulani, na hamna hata mmoja “anayethubutu kutenda kwa wepesi.” Kwa nini mnaishi katika hali ya ubaridi wa kudumu? Ni kwa nini sifa nzuri hazipatikani kwenu? Enyi watu Wangu! Ya zamani yalipita kitambo; msiendelee kuyashikilia zaidi. Zamani mlishikilia msimamo wenu, leo mnapaswa kunipa utiifu wenu wa dhati, na zaidi mnafaa kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu siku za usoni, na mtarithi baraka Zangu hapo baadaye. Hili ndilo mnapaswa kufahamu.
Februari 28, 1992

Jumanne, 18 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”

Mwenyezi Mungu anasema, “Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu.”
Ni njia gani ambayo Mungu hutumia kumkamilisha mwanadamu? Ni vipengele vipi vinavyojumuishwa? Je, uko tayari kukamilishwa na Mungu? Je, uko tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu? Unajua nini kuhusu maswali haya? Kama huwezi kuzungumzia maarifa kama haya, basi hii inaonyesha kwamba bado huijui kazi ya Mungu na hujapatiwa nuru katu na Roho Mtakatifu. Binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa. Wanaweza tu kupokea kiasi kidogo cha neema ili kufurahia kwa muda mfupi na haiwezi kuendelezwa kwa kipindi kirefu. Kama mtu hufurahia tu neema ya Mungu, hawezi kukamilishwa na Mungu. Baadhi wanaweza kutoshelezwa na amani na furaha ya mwili, maisha yenye furaha bila ya dhiki au msiba, huku wakiishi kwa amani na familia zao bila ya mapigano au ugomvi. Wanaweza hata kuamini kwamba hii ni baraka ya Mungu, lakini kwa kweli, ni neema ya Mungu tu. Hamwezi kutosheka tu kwa kufurahia neema ya Mungu. Kufikiria kwa aina hii ni kuchafu mno. Hata ukisoma neno la Mungu kila siku, uombe kila siku, na roho yako ihisi furaha na amani halisi, ilhali mwishowe huwezi kuzungumzia maarifa yoyote ya Mungu na kazi Yake au hujapata uzoefu wa mambo kama hayo, na haijalishi ni kiasi gani cha neno la Mungu ambacho umekula na kunywa, ukihisi tu amani na furaha katika roho yako na kwamba neno la Mungu ni tamu mno kiasi kwamba haliwezi kulinganishwa na kingine chochote, kana kwamba huwezi kulifurahia ukatosheka, lakini huna uzoefu halisi na huna hakika yoyote na neno la Mungu, basi ni nini unachoweza kupokea kutoka kwa aina hii ya imani katika Mungu? Kama huwezi kuishi kwa kudhihirisha kiini cha neno la Mungu, kula na kunywa kwako kwa maneno ya Mungu na maombi vyote vinahusu dini. Basi binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa na hawezi kupatwa na Mungu. Wale wote waliopatwa na Mungu ni wale wanaofuatilia ukweli. Kile ambacho Mungu hufaidi si mwili wa binadamu wala miliki zake, lakini sehemu iliyo ndani yake inayomilikiwa na Mungu. Kwa hivyo, Mungu huukamilisha moyo wa binadamu wala si mwili wake, ili moyo wa binadamu uweze kupatwa na Mungu. Kwa maneno mengine, kiini cha kusema kwamba Mungu humkamilisha mwanadamu ni kwamba Mungu huukamilisha moyo wa mwanadamu ili uweze kumgeukia Mungu na kumpenda Yeye.
Wale tu wanaoweza kurithi baraka za Mungu ni wale waliokamilishwa na Mungu na kupatwa na Mungu. Je, umefaidi chochote? Mungu amekukamilisha hadi kiwango gani? Mungu hamkamilishi binadamu bila mpango. Kunayo masharti na matokeo dhahiri yanayoweza kuonekana na binadamu. Si jinsi mwanadamu anavyoamini, kwamba mradi tu awe na imani katika Mungu, anaweza kukamilishwa na kupatwa na Mungu, na anaweza kupokea hapa ulimwenguni baraka na urithi wa Mungu. Mambo kama haya ni magumu mno, na hata zaidi inapohusu kubadilika kwa taratibu. Kwa sasa, kile ambacho mnafaa kutafuta kimsingi ni kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, na kukamilishwa na Mungu kupitia kwa watu wote, mambo yote na vitu vyote ambavyo mnakumbwa navyo, ili mambo zaidi ya kile Mungu Alicho yatashirikishwa ndani yenu. Lazima kwanza mpokee urithi wa Mungu ulimwenguni kabla ya kustahili kurithi baraka nyingi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu. Mambo yote haya ndiyo ambayo mnafaa kutafuta na ambayo kwanza mnafaa kuelewa. Zaidi unavyotafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, ndivyo utakavyoweza kuona mkono wa Mungu zaidi katika mambo yote, na hivyo kutafuta kwa bidii kuingia katika hali ya neno la Mungu na uhalisia wa neno Lake kupitia mitazamo tofauti na katika mambo tofauti. Huwezi kutosheka na hali hasi kama kutotenda dhambi tu, au kutokuwa na dhana, kutokuwa na filosofia ya maisha, na kutokuwa na hiari ya binadamu. Mungu humkamilisha mwanadamu kwa njia tofauti, na inawezekana katika mambo yote kwako kukamilishwa hatimaye. Huwezi tu kukamilishwa kwa kuzingatia mambo halisi, lakini pia mambo hasi, na hivyo kuboresha kile unachopata. Kila siku kunazo fursa za kukamilishwa na muda wa kupatwa na Mungu. Baada ya kipindi cha kupitia mambo kama haya, utabadilika pakubwa. Utaweza sasa kimaumbile kufaidi utambuzi katika mambo mengi ambayo hukuyaelewa awali; bila ya kuhitaji wengine kukufunza, bila kujua, utaweza kufahamishwa na Mungu, ili uweze kuwa na fahamisho katika mambo yote na mambo yote utakayopitia yatakuwa mengi. Mungu atakuongoza wewe ili usije ukapotoka kwa vyovyote vile. Kisha utawekwa wazi kwenye njia ya kufanywa kuwa mtimilifu na Yeye.

Jumatatu, 17 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Mwenyezi Mungu anasema, “Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka shtaka rasmi lililoandikwa; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika enzi zote, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga. Na wale wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu pekee watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya wanadamu na kuchukia matendo yao maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu, Nikisubiri tu nafasi kutoa adhabu kwa hao na kufurahia kuona hilo. Siku Yangu hatimaye imefika na siwezi kusubiri zaidi!”
Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimetamka mengi pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele katika mpango Wangu mpya, katika kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya katika kazi Yangu ili wale ambao wanaoniona watajipiga kifuani na kuulilia na kuombolezea uwepo Wangu bila kukoma. Kwani Ninaleta mwisho wa wanadamu duniani, na baada ya hapo kuendelea, Ninaweka wazi tabia Yangu yote mbele ya wanadamu, ili wote wanijuao na wasionijua watayashibisha macho yao na kuona kwamba kweli, nimekuja ulimwenguni, nimekuja duniani ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, ni “kukiri” Kwangu kwa pekee tangu Niwaumbe wanadamu. Matilaba yangu ni kuona mnafuatilia kwa moyo wenu wote kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinamkaribia wanadamu tena, karibu na wale wote wanaonipinga.
Pamoja na mbingu, Ninaanza kazi ambayo ni lazima Niifanye. Kwa hivyo Mimi husafiri kati ya misururu ya watu na kupita kati ya mbingu na ardhi, bila ya yeyote kutambua mienendo Yangu au kuyatambua maneno Yangu. Kwa hivyo, mpango Wangu bado unaendelea kwa urahisi. Ni vile tu hisia zenu zote zimekuwa nzito kiasi kwamba hamjui hatua za kazi Yangu hata kidogo. Hata hivyo, siku moja hakika mtakuja kutambua kusudio Langu. Leo hii, Ninaishi miongoni mwenu na Ninasumbuka pamoja nanyi. Kwa muda mrefu Nimeelewa mtazamo walio nao wanadamu juu Yangu. Nisingependa kueleza wazi zaidi, sembuse kutoa mifano zaidi ya kile kinachoniumiza ili kuwaaibisha. Ombi Langu la pekee ni kwamba myaweke moyoni yale yote mliyoyafanya kwa ajili ya kulinganisha maelezo yetu siku tutakapokutana tena. Nisingependa kumshutumu yeyote miongoni mwenu kwa njia isiyo ya kweli, kwa sababu daima Nimekuwa Nikifanya mambo kwa njia ya haki, bila upendeleo, na kwa heshima. Bila shaka, Ningependa pia kwamba nyinyi mngeweza kuwa wazi na wakarimu na kutofanya lolote lililo kinyume na mbingu na ardhi na dhamiri yenu. Haya pekee ndiyo Ninayowauliza. Watu wengi huhisi kusumbuka na hawana amani kwa sababu wametenda makosa mabaya, na wengi wanaona aibu kwa sababu hawajawahi kutenda tendo lolote zuri. Tena wapo pia wengi ambao, mbali na kutahayari kutokana na dhambi zao, wanakuwa wabaya zaidi, wakizitoa kabisa barakoa inayoficha sura zao mbaya—ambayo ilikuwa bado haijaonyeshwa kikamilifu—ili kujaribu tabia Yangu. Huwa Sijali wala sitilii maanani sana matendo ya mtu yeyote. Badala yake, Mimi hufanya kazi Ninayopaswa kufanya, iwe kukusanya habari, kuzungukazunguka katika nchi au kufanya lile ambalo linanipendeza. Katika nyakati muhimu, Mimi nitaendelea na kazi Yangu miongoni mwa wanadamu kama Nilivyopanga awali, bila kuchelewa au kuwa mapema hata kidogo, na kwa urahisi na kwa makini. Hata hivyo, kuna watu wengine ambao wanawekwa pembeni kwa kila hatua katika kazi Yangu, kwa sababu Ninadharau hali yao ya kujipendekeza na hali ya kujifanya wanyenyekevu. Wale wanaochukiza Kwangu hakika watatelekezwa, iwe ni kwa kupenda au kwa kutopenda. Kwa ufupi, Ninataka wale wote Ninaowadharau kuwa mbali sana Nami. Ni dhahiri kwamba, Sitawahurumia wale waovu ambao wamebaki katika makao Yangu. Kwa kuwa siku ya adhabu ya mwanadamu inakaribia, Sina haraka ya kuzitupa nje zile nyoyo zote zinazostahili dharau, kwa kuwa Nina mpango Wangu Mwenyewe.
Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, wala si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo yote ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya nyingine, na vilevile njia zao katika kunifuata, sifa zao asilia, na utendakazi wao wa mwisho. Kwa njia hii, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu na kila mmoja atakuwa wa aina yake kama Nilivyowaweka. Ninaamua hatima ya kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu. Sijafanya mabadiliko yoyote katika mpango Wangu tangu kuuanzisha. Ni vile tu, kwa binadamu, wale ambao kwao Mimi huelekeza maneno Yangu wanaonekana kupungua kwa idadi, na vile vile wale Ninaowakubali kwa kweli. Hata hivyo, Ninasisitiza kwamba mpango Wangu haujawahi kubadilika; badala yake, ni imani na upendo wa mwanadamu ambao hubadilika daima, kufifia daima, kiasi kwamba upo uwezekano wa kila mwanadamu kubadilika kutoka kujipendekeza Kwangu hadi kufikia hali ya kunidharau au hata kunitupa nje. Mtazamo Wangu kwenu hautakuwa baridi wala moto, hadi pale Nitakapohisi kuchukizwa na kuchafuliwa moyo, na hatimaye kutoa adhabu. Hata hivyo, katika siku ya adhabu yenu, bado Nitawaona lakini nyinyi hamtaweza kuniona tena. Tayari Kwa kuwa maisha miongoni mwenu yamekuwa ya kuchosha na ya taabu tayari Kwangu, kwa hivyo ni wazi kuwa, Nimechagua mazingira tofauti Yangu kuishi, ili Niepuke vizuri kuumizwa na maneno yenu mabovu na kuwa mbali na tabia zenu hafifu sana, ili msinipumbaze au kunitendea kwa namna ya uzembe. Kabla Sijawaacha, lazima bado Ninawasihi mjiepushe kufanya yale ambayo hayaambatani na ukweli. Badala yake, mnafaa kufanya yale ambayo yanawapendeza watu wote, na yale ambayo yana manufaa kwa binadamu wote, na yale yanayofaidi hatima yenu wenyewe, la sivyo, yule atakayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe.
Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Jumapili, 16 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”

Mwenyezi Mungu anasema: “Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata uzoefu wa maisha ya binadamu, Nikichunguza kwa karibu matendo yote ya mwanadamu. Hakuna aliyewahi kujitolea Kwangu kwa kweli. Hakuna aliyewahi kufuata ukweli. Hakuna aliyewahi kuwa mwangalifu Kwangu. Hakuna aliyewahi kufanya maazimio mbele Yangu na kufanya wajibu wake. Hakuna aliyewahi kuniruhusu kuishi ndani yake. Hakuna aliyewahi kunithamini kama afanyavyo maisha yake. Hakuna aliyewahi kuona kwa vitendo vya ukweli uzima wote wa uungu Wangu. Hakuna aliyewahi kutamani kuwasiliana na Mungu wa vitendo Mwenyewe.”
Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa ufalme. Ingawa chini ya nuru ya Roho Wangu watu wengi wametabiri uzuri wa ufalme, wanajua tu nje ya ufalme, sio umuhimu wa ndani. Leo, ufalme ujapo kuwepo rasmi duniani, binadamu wote bado hujui kinachopaswa kukamilishwa, ulimwengu ambao binadamu hatimaye ataletwa ndani, wakati wa Enzi ya Ufalme. Kuhusu haya, Naogopa watu wote wako katika hali ya mkanganyiko. Kwa sababu siku ya utambuzi kamili wa ufalme bado haijafika kabisa, wanadamu wote wamechanganyikiwa, hawawezi kuiona vizuri. Kazi Yangu ya uungu inaanza rasmi na Enzi ya Ufalme. Ni katika mwanzo rasmi wa Enzi ya Ufalme kwamba tabia Yangu inaanza kuendelea kudhihirika kwa mwanadamu. Hivyo kwa muda huu tarumbeta takatifu inaanza rasmi kutoa sauti na kutangaza kwa wote. Nichukuapo kirasmi mamlaka Yangu na kutawala kama Mfalme katika ufalme, watu Wangu wote watakamilishwa na Mimi baada ya muda. Wakati mataifa yote ya dunia yatavurugwa, hapo ndipo hasa ufalme Wangu utaanzishwa na kupata umbo na pia Nitabadilika na kurejea kwa ulimwengu mzima. Wakati huo, watu wote watauona uso Wangu tukufu, watauona uso Wangu wa kweli. Tangu kuumbwa kwa dunia hadi sasa, binadamu umepotoshwa na Shetani hadi kiasi kilicho leo. Kwa ufisadi wa mwanadamu, Nimefichwa zaidi na zaidi kutoka kwake na Nikazidi kutoeleweka na wao. Mwanadamu hajawahi kuuona uso Wangu wa kweli, hajawahi kuathiriana na Mimi moja kwa moja. Ni kwa tetesi na hadithi tu ndipo kumekuwa na “Mimi” kwa ubunifu wa mwanadamu. Kwa hivyo Nakubaliana na ubunifu wa binadamu, kwamba, ni dhana za binadamu, kukabiliana na “Mimi” kwa akili za wanadamu, kwamba Naweza kubadilisha hali ya “Mimi” ambayo wameweka kwa miaka mingi. Hii ni kanuni ya kazi Yangu. Hakuna mtu hata mmoja ameweza kuijua vizuri sana. Ingawa wanadamu wamejilaza na kuja mbele Yangu kuniabudu, Sifurahii matendo kama haya ya wanadamu kwa sababu kwa mioyo yao hawajashikilia mfano Wangu, lakini mfano Wangu wa nje. Kwa hivyo, akili zao zinapokosa tabia Yangu, hawajui chochote kuhusu uso Wangu wa kweli. Kwa hivyo, wakati wameamini wamenipinga ama kukosea amri Zangu za kiutawala, Nitajifanya kwamba sioni. Na hivyo, kwa kumbukumbu zao, Mimi ni Mungu anayeonyesha huruma kwa wanadamu badala ya kuwaadibu, ama Mimi ni Mungu Mwenyewe asiyemaanisha Anachokisema. Haya yote ni mawazo yanayotokana na fikira za wanadamu na sio kwa mujibu na ukweli.
Najificha wakati wanadamu wana kazi nyingi na kujifichua wakati wao wa burudani. Binadamu unanidhania kuwa Anayejua yote na kuwa Mungu Mwenyewe anayekubali maombi yote. Wote basi wanakuja mbele Yangu kutafuta tu msaada wa Mungu, bila kuwa na tamaa ya kunijua. Wakiwa katika maumivu ya magonjwa, wanadamu wananiomba msaada. Wakiwa na shida, wananiambia matatizo yao kwa nguvu zao zote ili kumwaga mateso yao. Na bado hakuna mwanadamu hata mmoja ameweza kunipenda pia akiwa na faraja. Hakuna mtu hata mmoja amenitafuta wakati wa amani na furaha ili Nishiriki furaha yake. Wakati familia yao ya karibu ina furaha na iko sawa, wanadamu tayari wananiweka kando ama kunifungia mlango, kunikataza kuingia, na hivyo kufurahia furaha heri ya familia. Akili ya binadamu ni nyembamba sana, nyembamba sana hata kumshikilia Mungu, apendaye, mwenye huruma, na mkunjufu kama Mimi. Nimekataliwa mara ngapi na wanadamu wakati wao wa kicheko na furaha, Nimetegemewa kama gongo mara ngapi na wanadamu wakati wanaanguka; Ni mara ngapi Nimelazimishwa kuwa daktari wa wanadamu wanaougua magonjwa. Mwanadamu ni katili jinsi gani! Hawana akili na ni wabaya kabisa. Hawana hata hisia zinazopatikana kwa binadamu. Nusura hawana ubinadamu hata kidogo. Fikiria siku za nyuma na linganisha na sasa. Kuna mabadiliko yanayofanyika ndani zenu? Kuna siku kidogo za zamani sasa? Ama zamani bado haijabadilishwa?
Juu ya mlima na chini ya bonde Nimepitia, na kuwa na uzoefu wa panda shuka za dunia. Nimetembea na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi, lakini bado inaonekana tabia ya binadamu imebadilika kidogo. Na ni kama asili ya zamani ya mwanadamu imeeneza mizizi na kuota ndani yao. Hawawezi kamwe kubadili hiyo asili ya zamani, kuiboresha tu kwa msingi wa kwanza. Wasemavyo wanadamu, kiini hakijabadilika, lakini umbo limebadilika sana. Kila mtu, inaonekana, anajaribu kunidanganya, kunipofusha, ili aweze kuingia na kupata shukrani Yangu. Sipendi wala kutia maanani udanganyifu wa watu. Badala ya kukasirika, Nachukua mtazamo wa kuangalia lakini si kuona. Napanga kuupa binadamu kiwango fulani cha uhuru, na hivyo, kushughulikia wanadamu wote kama kitu kimoja. Kwa sababu wanadamu wote hawajiheshimu na ni maskini wasio na faida, wasiojithamini, watawezaje kunihitaji kuonyesha huruma na mapenzi mapya? Wanadamu wote hawajijui, na hawajui uzito wao. Wanapaswa kujipima uzito. Binadamu haunitambui, hivyo Nami pia siutilii maanani. Wanadamu hawanitambui, kwa hivyo Mimi pia Siweki juhudi kwao. Je, hii ni bora? Je, hii haiwazungumzii, watu Wangu? Nani amefanya maazimio mbele Yangu na kukosa kuyatupilia mbali baadaye? Nani amefanya maazimio ya muda mrefu mbele Yangu badala ya kutatua mara nyingi juu ya hii na hiyo? Daima, wanadamu hufanya maazimio mbele Yangu wakati wa raha na kuyafuta kabisa wakati wa shida. Baadaye, wanachukua uamuzi wao na kuuweka mbele Yangu. Je, Mimi si wa kuheshimika hadi Naweza kubali kwa kawaida taka iliyookotwa na mwanadamu kutoka pipani? Wanadamu wachache hushikilia maazimio yao, wachache ni safi, na wachache wanatoa yenye thamani kubwa zaidi kama sadaka Kwangu. Je, nyinyi wote si sawa kwa njia hii? Iwapo, kama mmoja wa watu Wangu kwenye ufalme, huwezi kufanya wajibu wenu, mtachukiwa na kukataliwa na Mimi!

Ijumaa, 14 Juni 2019

Unafaa Utofautishe Vipi Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Pepo Wabaya?

2. Unafaa Utofautishe Vipi Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Pepo Wabaya?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhusu kuwasaidia watu kupata faida; ni kuwaadilisha watu; hakuna kazi ambayo haiwanufaishi watu. Haijalishi kama ukweli ni wa kina au usio wa kina, na haijalishi tabia ya wale wanaopokea ukweli huo ilivyo, chochote ambacho Roho Mtakatifu Anafanya, yote hayo huwanufaisha watu.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu. Wakati watu wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndani yao ni watakatifu hasa. Wale ambao wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu huishi kwa kudhihirisha upendo wa Mungu, upendo wa kaka na dada zao, na kufurahia vitu ambavyo Mungu hufurahia na kuchukia vitu ambavyo Mungu huchukia. Watu ambao wanaguswa na kazi ya Roho Mtakatifu wana ubinadamu wa kawaida, na wanamiliki ubinadamu na daima hufuatilia ukweli. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya watu, hali zao huwa nzuri zaidi na zaidi, na ubinadamu wao unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi, na ingawa ushirikiano wao mwingine unaweza kuwa mpumbavu, motisha zao ziko sahihi, kuingia kwao ni kwa hali nzuri, hawajaribu kukatiza, na hakuna nia mbaya ndani yao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida na ya kweli, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa mwanadamu kulingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na Yeye huwapa nuru na kuongoza watu kulingana na ufuatiliaji halisi wa watu wa kawaida. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa watu, Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, Anawakimu kwa msingi wa mahitaji yao, na Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kwa hali nzuri kwa msingi wa kile ambacho wanakosa, na kwa upungufu wao; wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, kazi hii inalingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na ni katika maisha halisi pekee ndio watu wanaweza kuona kazi ya Roho Mtakatifu. Iwapo, katika maisha yao ya kila siku, watu wako katika hali nzuri na wana maisha ya kawaida ya kiroho, basi wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali kama hiyo, wakati wanakula na kunywa maneno ya Mungu wana imani, wakati wanaomba wanatiwa moyo, wakati kitu kinawafanyikia wao si baridi, na wakati kinawafanyikia wanaweza kuona masomo ambayo Mungu anawahitaji kujifunza, na hawako baridi, ama dhaifu, na ingawa wana ugumu wa kweli, wako tayari kukubali mipango yote ya Mungu.
…………
Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia katindani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuwa na hali za kawaida mbele ya Mungu. Ambayo ni kusema, punde tu kuna kazi ya Shetani ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba. Kazi ya roho waovu huharibu uhusiano wa kawaida kati ya mwanadamu na Mungu, na huvuruga maono ya awali ya watu na njia ambayo maisha yao yameingia, katika mioyo yao hawawezi kamwe kumkaribia Mungu, daima mambo hufanyika ambayo huwasababishia vurugu na kuwatia pingu, na mioyo yao haiwezi kupata amani, kuacha upendo wao wa Mungu bila nguvu, na kuwafanya kusononeka. Hayo ndiyo maonyesho ya kazi ya Shetani. Kazi ya Shetani inadhihirishwa katika yafuatayo: kutoweza kushikilia msimamo na kuwa na ushuhuda, kukusababisha kuwa mtu ambaye ana makosa mbele ya Mungu, na ambaye hana uaminifu kwa Mungu. Kwa kuingilia kwa Shetani, unapoteza upendo na uaminifu kwa Mungu ndani yako, unaondolewa uhusiano wa kawaida na Mungu, hufuatilii ukweli, ama kujiendeleza, unarudi nyuma, na kuwa baridi, unajipendeza, unaachia uenezaji wa dhambi, na huchukii dhambi; zaidi ya hayo, kuingilia kwa Shetani kunakufanya mpotovu, kunasababisha mguso wa Mungu kutoweka ndani yako, na kunakufanya kulalamika kuhusu Mungu na kumpinga Yeye, kukufanya uwe na shaka na Mungu, na hata kuna hatari ya wewe kumwacha Mungu. Hii yote ni kazi ya Shetani.
kutoka kwa "Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida kabisa, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake, ambayo yameharibiwa na Shetani, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Ni sawa na, kusema, maisha ya mwanadamu yanakuwa na kukua, na Atabia ya upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maishi ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha atabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa uelewa wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu.
kutoka kwa "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mambo yanayotokana na Mungu hukusababisha kuwa wazi zaidi kuhusu maono, na hukusababisha kusogea karibu na karibu zaidi na Mungu, ukishiriki upendo na ndugu kwa bidii; unakuwa na uwezo wa kutilia maanani mzigo wa Mungu, na moyo wako umpendao Mungu haupungui; kuna njia mbele yako kuitembea. Mambo ambayo hutokana na Shetani hukusababisha kupoteza maono na vyote ulivyokuwa navyo awali vimetoweka; unajitenga na Mungu, huna upendo kwa ndugu nawe una moyo wa chuki. Unakuwa mwenye kukata tamaa, hutaki tena kuishi maisha ya kanisa, na moyo wako umpendao Mungu hauko tena. Hii ni kazi ya Shetani na pia ni matokeo ambayo yameletwa na kazi ya roho mbaya.
kutoka kwa Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni
Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ili kuwapa watu nuru, Yeye kwa ujumla kuwapa ufahamu wa kazi ya Mungu, na ya kuingia kwao ya kweli na hali ya ukweli, na pia Huwapa azimio, huwaruhusu kuelewa kusudi la hamu la Mungu na mahitaji yake kwa ajili ya mtu leo, Huwapa azimio la kufungua njia zote. Hata wakati ambapo watu wanapitia umwagaji damu na sadaka ni lazima watende kwa ajili ya Mungu, na hata kama wanakumbana na mateso na dhiki, lazima bado wampende Mungu, na wasiwe na majuto, na lazima wawe shahidi kwa Mungu. Azimio la aina hii ni misisimko ya Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu—lakini jua kwamba hujamilikiwa na misismko kama hii kila wakati.
kutoka kwa "Utendaji (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine husema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao nyakati zote. Hili haliwezekani. Ikiwa wangesema kwamba Roho Mtakatifu yuko nao kila mara, hilo lingekuwa la kweli. Ikiwa wangesema kwamba fikira na hisi zao ni za kawaida nyakati zote, hilo pia lingekuwa la kweli, na lingeonyesha kwamba Roho Mtakatifu yuko nao. Ikiwa unasema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako kila mara, kwamba unapata nuru kutoka kwa Mungu na kuguswa na Roho Mtakatifu kila wakati, na unapata ufahamu mpya kila wakati, basi hili si la kawaida. Ni la rohoni kabisa! Bila tashwishi yoyote, watu hao ni pepo wabaya! Hata wakati ambapo Roho wa Mungu huja ndani ya mwili, kuna nyakati ambapo lazima Apumzike, na lazima Ale—sembuse wewe. Wale ambao wamemilikiwa na pepo wabaya huonekana kutokuwa na udhaifu wa mwili. Wanaweza kutelekeza na kuacha kila kitu, wao ni wasiohemkwa, wenye uwezo wa kustahimili mateso, wao hawahisi uchovu hata kidogo sana, kana kwamba wamevuka mipaka ya mwili. Je, hili silo la rohoni kabisa? Kazi ya pepo mwovu ni ya rohoni, na mambo haya ni yasiyofikiwa na mwanadamu. Wale wasioweza kutofautisha huwa na wivu wanapoona watu kama hao, na husema kwamba imani yao katika Mungu ni thabiti sana, na nzuri sana, na kwamba wao huwa si wadhaifu kamwe. Kwa kweli, hili ni dhihirisho la kazi ya pepo mwovu. Hiyo ni kwa sababu watu wenye hali ya kawaida huwa na udhaifu wa binadamu usioepukika; hii ni hali ya kawaida ya wale walio na kuwepo kwa Roho Mtakatifu.
kutoka kwa "Utendaji (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wanaweza kuzungumza kutoka ndani mwako au ndani ya sikio lako, au la sivyo wanaweza kuyachanganya mawazo na akili yako, wanazuia kuguswa kwa Roho Mtakatifu ili usiweze kuuhisi, na baada ya hapo wanaanza kukuingilia, kuzifanya fikira zako ziwe zilizochanganyikiwa na akilia yako iwe iliyovurugika, na kukufanya usiyekuwa na utulivu na usiye thabiti. Hivyo ndivyo ilivyo kazi ya roho wabaya.
Wanaweza kuzungumza kutoka ndani mwako au ndani ya sikio lako, au la sivyo wanaweza kuyachanganya mawazo na akili yako, wanazuia kuguswa kwa Roho Mtakatifu ili usiweze kuuhisi, na baada ya hapo wanaanza kukuingilia, kuzifanya fikira zako ziwe zilizochanganyikiwa na akilia yako iwe iliyovurugika, na kukufanya usiyekuwa na utulivu na usiye thabiti. Hivyo ndivyo ilivyo kazi ya roho wabaya.
kutoka kwa "Maana ya Mungu Kuupitia Uchungu wa Dunia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Unaweza kuhisi roho yako mwenyewe? Unaweza kugusa roho yako? Unaweza kuhisi roho yako inafanya nini? Hujui, siyo? Ikiwa unaweza kuhisi na kugusa vitu fulani kama hiki, basi ni roho nyingine ndani yako inafanya kitu kwa nguvu—ikidhibiti vitendo na maneno yako. Ni kitu kisichohusiana na wewe, kisicho cha wewe. Wale wenye roho ovu wana uzoefu wa kina na hili.
kutoka kwa "Jinsi ya kuelewa Umoja wa Mwili wa Mungu na Roho" katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo kunao baadhi ya pepo wabaya wanaofanya kazi kupitia kwa mambo yasiyo ya ulimwenguni humu ili kumpotosha mwanadamu; hilo si chochote bali ni uigaji kwa upande wao, kumpotosha mwanadamu kupitia kwa kazi ambayo kwa sasa haifanywi na Roho Mtakatifu. Pepo wengi wabaya huiga ufanyaji wa miujiza na uponyaji wa magonjwa; si chochote ila kazi ya pepo wabaya, kwani Roho Mtakatifu hafanyi tena kazi kama hiyo leo. Wale wote wanaokuja baadaye na wanaoiga kazi ya Roho Mtakatifu—ni pepo wabaya.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Kazi ya Roho Mtakatifu huwaruhusu watu kuuelewa ukweli, huwaruhusu kujua kiini potovu cha Shetani, na huwapa maarifa ya kweli kuhusu kile Mungu anacho na Alicho. Athari zake zote ni nzuri kwa ujumla. Leo, tunajua ukweli ni nini, kwamba ukweli unatoka kwa Mungu, kwamba mambo mazuri yanatoka kwa Mungu, kile kinachofaa kumilikiwa na watu wenye ubinadamu wa kawaida, kile ambacho ni mapenzi ya Mungu, na kile ambacho ni maisha ya kweli. Mambo haya yote ni mazuri, na uhalisi wa mambo mazuri ni ukweli. Hivi ndivyo athari ya kazi ya Mungu ilivyo, na tunaielewa tu kutokana na kupata nuru na uangazaji wa Roho Mtakatifu. Kazi ya pepo wabaya haiwezi kuwapa watu maarifa ya mambo mazuri. Unafaa kuwa wazi na kujua kwamba watu ambao pepo wabaya hufanya kazi ndani yao hawaelewi wala kuufahamu ukweli wowote. Kazi ya pepo wabaya inaweza tu kuwafanya watu kuwa waovu zaidi na zaidi, inaweza kuleta tu giza zaidi na zaidi ndani ya mioyo yao, kuzifanya tabia zao kuwa potovu zaidi na zaidi, na hali yao kuzoroteka zaidi na zaidi, na hatimaye kuishia katika kuteseka milele na kuangamia. Kazi ya Roho Mtakatifu huwafanya watu kuwa wa kawaida zaidi na zaidi, huwapa ufahamu mkubwa zaidi wa ukweli na siku zote huwapa imani kubwa zaidi kwa Mungu, na wanaweza kumtii Mungu zaidi na zaidi. Hatimaye, huwaruhusu kumjua kabisa Mungu na kumwabudu Mungu. Hii ndiyo athari ya kazi ya Roho Mtakatifu, na ni kinyume kabisa cha kazi ya pepo wabaya.
kutoka kwa "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)
Hapa chini, hebu tuangalie baadhi ya utofauti mwingine waziwazi kati ya kazi mbalimbali za pepo wabaya na kazi ya Roho Mtakatifu, na namna ambavyo zinaonyeshwa kwa njia mahususi. Roho Mtakatifu huwachagua watu wanaofuatilia ukweli, na walio na dhamiri na mwelekeo, na wanaomiliki uadilifu. Hawa ndio aina ya watu ambao Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao. Pepo wabaya huchagua watu ambao ni wajanja na wa kipuuzi, wasiopenda ukweli, na wasio na dhamiri wala mwelekeo. Watu kama hao ndio pepo wabaya hufanya kazi ndani yao. Ni nini tunachoona tunapolinganisha wale waliochaguliwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu, na wale waliochaguliwa kwa kazi ile ya pepo wabaya? Tunaweza kuona kwamba Mungu ni mtakatifu, na mwenye haki, kwamba wale wanaochaguliwa na Mungu huutafuta ukweli, na wanayo dhamiri na mwelekeo, kwamba wanao uadilifu na wanapenda kile ambacho ni haki. Wale wanaochaguliwa na pepo wabaya ni wajanja, ni wachoyo na wenye dharau, hawaupendi ukweli, hawana dhamiri na mwelekeo, na hawautafuti ukweli. Pepo wabaya huchagua tu mambo mabaya na wale watu ambao si wa kweli, ambapo tunaona ya kwamba pepo wabaya wanapenda uovu na giza, kwamba wanawakimbia wale wanaoutafuta ukweli, na ni wepesi wa kuwamiliki wale ambao wako kombo na ni wajanja, wale ambao wanavutiwa na udhalimu, na wanaorogwa kwa urahisi. Wale ambao pepo wabaya huchagua kufanyia kazi ndani yao hawawezi kuokolewa, na wanaondolewa na Mungu. Ni lini, na ni katika mazingira gani, ndipo pepo wabaya hufanya kazi? Wao hufanya kazi wakati watu wamesonga mbali na Mungu na kuasi dhidi ya Mungu. Kazi ya pepo wabaya huwaroga watu, na hufanya hivyo kwa kuchukua fursa ile wanapotenda dhambi. Wakati watu wako katika hali yao dhaifu zaidi, hasa wanapokuwa katika maumivu makuu ndani ya mioyo yao, wakati wanapohisi vibaya na wakiwa wamechanganyikiwa, pepo mbaya huchukua fursa hii kujiingiza ndani polepole ili kuwaroga na kuwapotosha, kuleta kutoelewana kati yao na Mungu. Kunao wakati wa kazi ya Roho Mtakatifu: Wakati watu wanapomwita Mungu, wakati mioyo yao inapomgeukia Mungu, wanapomhitaji Mungu, wanapotubu kwa Mungu, na wanapoutafuta ukweli, basi ndipo Roho Mtakatifu huanza kufanya kazi ndani yao. Tazama namna ambavyo kila dhana ya kazi ya Roho Mtakatifu ilivyo ili kumwokoa mwanadamu, namna Anavyotafuta fursa za kumwokoa mwanadamu, ilhali pepo wabaya hutafuta fursa za kuwapotosha na kuwalaghai watu. Pepo wabaya wanayo dharau na ni waovu, ni wenye kudhuru kwa siri na wabaya, kila kitu wanachofanya kinalenga katika kumpotosha mwanadamu, na kumdhuru mwanadamu, na kumteketeza yeye. Wakati watu wanapohitaji msaada, wanapomtafuta Mungu kwa dharura, wanapohitaji wokovu wa Mungu, na wanapotaka kusonga karibu na Mungu ndani ya mioyo yao, Roho Mtakatifu hujitokeza kwao na kufanya kazi ya wokovu. Mungu ni upendo, na pepo wabaya ni chuki—hili liko wazi kwako, sivyo? Kile tu ambacho pepo wabaya hufanya ni ili kuwezesha kumteketeza na kumpotosha mwanadamu, na kile tu ambacho Roho Mtakatifu hufanya ni kwa upendo na wokovu wa mwanadamu. Athari ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwatakasa watu, kuwaokoa dhidi ya kupotoka kwao, kuwaruhusu kujijua na kumjua Shetani, kuweza kuasi dhidi ya Shetani, kuweza kuufuatilia ukweli, na hatimaye kuishi kwa kudhihirisha mfanano wa mwanadamu. Pepo wabaya hupotosha, hutia najisi, na kuwafunga watu, huwaweka ndani zaidi ya dhambi, na kuwasababishia maumivu makubwa zaidi katika maisha yao, na hivyo wakati pepo wabaya wanapofanya kazi ndani ya watu, watu hao wamo hatarini; hatimaye, wanateketezwa na Shetani, jambo ambalo ni matokeo ya kazi ya pepo wabaya. Athari ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuweza hatimaye kuwaokoa watu, kuwafanya kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kuwa huru na kukombolewa kabisa, na kupokea baraka za Mungu. Tazama: Pepo wabaya humweka mwanadamu katika giza, humpeleka kwenye shimo la kuzimu; Roho Mtakatifu humchukua mwanadamu kutoka kwenye giza, na kumpeleka kwenye mwangaza, na hadi kwenye uhuru. Kazi ya Roho Mtakatifu huwapa watu nuru na kuwaongoza watu, Huwapa fursa mbalimbali, na wanapokuwa wanyonge na dhambi Yeye huwapa faraja. Huwaruhusu watu kujijua, huwaruhusu kuufuatilia ukweli, na Halazimishi watu kufanya mambo, lakini Huwaacha kujichagulia njia yao wao wenyewe, na hatimaye Huwapeleka kwenye mwangaza. Pepo wabaya huwalazimisha watu kufanya mambo na kuwaamrisha hapa na pale. Kila kitu wanachosema ni uongo na kinawaroga watu, kuwadanganya na kuwafunga; pepo wabaya hawawapatii watu uhuru, hawawaruhusu kuchagua, huwalazimisha kufuata barabara ya maangamio, na hatimaye kuwaingiza ndani ya dhambi zaidi na zaidi, na kuwasababishia kifo. Hebu tazama watu hao waovu, wale watu waovu: Wanawakokota wengine hadi kwenye uharibifu, wanawavuta kwenye uhalifu, na kuwavuta kwa ghafla kwenye maeneo ya kuchezea kamari. Hatimaye, baada ya wao kuziharibu familia za watu na kuwafarakanisha na dunia, wanafurahi, kazi yao imekamilika, na wametimiza nia yao. Je, hawa ni mashetani, sivyo? Ilhali wale ambao ni wazuri kwa kweli na wanamcha Mungu wanawaongoza watu kuwa karibu zaidi na Mungu, na kuwaongoza katika imani ya Mungu, katika ufahamu wa ukweli, katika kuyafuatilia maisha halisi, na hatimaye kuwafanya kuishi kwa kudhihirisha mfanano wa mwanadamu. Utofautishi kati ya mambo haya mazuri na mabaya ni wazi vipi! Katika kulinganisha kanuni, mbinu, na athari ya mwisho ya kazi ya Roho Mtakatifu na ile ya pepo wabaya, tunaona kwamba Mungu humwokoa mwanadamu, humpenda mwanadamu, na humpa mwanadamu ukweli, kwamba Yeye humchukua mwanadamu na kumweka kwenye mwangaza, na hatimaye humruhusu mwanadamu kubarikiwa na kuwa mtu halisi na kuishi kwa kudhihirisha maisha ya ukweli. Shetani humpotosha mwanadamu, humfunga mwanadamu, hujaribu kumteketeza mwanadamu, na hatimaye humwongoza mwanadamu katika kuteseka milele na kuangamia. Kupitia kujua kazi ya Roho Mtakatifu, tunaweza kutambua kazi ya pepo wabaya na kuujua ukweli wa upotoshwaji wa mwanadamu na Shetani. Leo, katika imani yetu kwa Mungu tunafahamu kile tunachofaa kufuatilia, kwamba Mungu ni mzuri, na kwamba tunafaa kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kumtii Mungu. Tunayo malengo katika maisha yetu, na tunalo tumaini la wokovu. Hizi ndizo athari za kazi ya Roho Mtakatifu. Leo, kama ungeulizwa kusema Shetani ni nini, ungeweza kusema? Tabia potovu ya Shetani inaonyeshwa kwa njia gani? Tabia ya Shetani ni yenye maovu, yenye kudhuru kwa siri, yenye makosa, mbovu, yenye dharau, yenye kushikilia maovu yote, na yenye sumu kabisa. Kila kitu ambacho Mungu anacho na Alicho ni nini? Ni hali ya kuwa mwenye haki, utakatifu, heshima, kudura, hekima, na rehema na upendo. Ile hisia ambayo Shetani huwapatia watu ni ya kuchukiza na iliyolaaniwa. Ile hisia ambayo Mungu huwapatia watu ni ya kukaribishwa, uzuri na kuheshimiwa.
kutoka kwa "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)
Ni nini athari ya kazi ya Roho Mtakatifu kwa mwanadamu? Humruhusu mwanadamu kuyaelewa maneno ya Mungu, na ukweli, na humruhusu mwanadamu kumjua Mungu na kujijua. Ukweli unao athari maradufu. Kwa upande mmoja, kuufahamu ukweli huwapatia watu maarifa ya Mungu, kwani ukweli ndio kiini cha maisha ya Mungu, ni kile Mungu anacho na Alicho, ni uhalisi wa mambo mazuri, na unawakilisha tabia na maisha ya Mungu—na hivyo basi ni sahihi kabisa kusema kwamba, kwa kuuelewa ukweli, tunafaidi ufahamu fulani wa Mungu. Wakati uo huo, ukweli unaweka pia wazi kupotoka kwetu, na hivyo basi wale wote wanaouelewa ukweli wanayo maarifa ya kweli kujihusu, na wameona wazi kabisa picha yao ya kweli na picha ya kweli ya Shetani. Kila kitu kinawekwa wazi kwa ukweli. Ni nini athari ya ufahamu wa ukweli kupitia kazi ya Roho Mtakatifu? Kwa upande mmoja, tunakijua kiini chetu potovu, tunamwona kwamba mwanadamu ni maskini, wa kuhurumiwa, kipofu, aliye na uchi, aliyepotoka, mwovu, mchoyo na mwenye dharau, kwamba hana mfanano hata kidogo wa mwanadamu wa kweli, kwamba hayuko tofauti hata kidogo na Shetani, kwamba asili yake na kiini chake vyote viko sawa na Shetani. Je, hii si athari ya ufahamu wa ukweli? Hakuna chochote ambacho si sahihi kuhusu haya. Isitoshe, kwa mtazamo huu tuko wazi kabisa kuhusu athari za kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi ya Roho Mtakatifu inayo pia athari nyingine nyingi. Kazi ya Roho Mtakatifu inaweza kuwapa watu imani ya kweli: Kila mojawapo ya maombi yetu kwa Mungu hutufanya kuhisi kwamba imani yetu kwa Mungu imeongezeka, na kwamba ni kweli zaidi. … Si ukweli hata kidogo kusema kwamba kunazo sehemu nyingi katika kazi ya Roho Mtakatifu, na mitazamo mingi ya athari zake. … kazi ya Roho Mtakatifu hutupatia maarifa ya kweli ya tabia ya Mungu, ya kudura na hekima ya Mungu, ya uchanganuzi Wake wa kina wa mioyo yetu, na hutupatia maarifa ya matendo ya ajabu na hali isiyofikirika kuhusu Mungu. Hivyo, pia, ndivyo inavyoturuhusu kujua na kushikilia kudura ya Mungu na utawala wake dhidi ya vyote.
kutoka kwa "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)
Wale ambao pepo wabaya hufanya kazi ndani yao hugeuka na kuwa wabaya na wazi na wenye kufanya jeuri wakati wanapoongea na kuwaambia watu ni nini cha kufanya. Baadhi yao hata hukiuka tabia njema na maadili ya ubinadamu wa kawaida. Maneno yao na vitendo vyao huroga na kuingilia kati watu, asili ya maneno hayo na vitendo hivyo ni mbovu na ya kuchukiza, na wanapotosha watu, na kuwadhuru watu, na hawana manufaa yoyote kwao. Punde tu pepo mbaya anapoonekana ndani ya mtu, wanahisi woga na wasiwasi, na kunakuwa na dharura kuu katika vitendo vyao, ni kana kwamba wanalipuka kwa kutokuwa wastahimilivu. Kuonekana kwake huwafanya watu kuhisi hasa kwa njia isiyo ya kawaida, na hakuna manufaa yoyote hata kidogo kwa wengine. Maonyesho makuu ya kazi ya pepo wabaya: Onyesho la kwanza ni kuwaelekeza watu kufanya hivi au vile, kuwaambia kufanya mambo, au kuwaelekeza kuongea unabii wa uongo. Onyesho la pili ni kuongea kwa mbinu ile ijulikanayo kama ya "ndimi" ambayo hakuna anayeielewa; hata wasemaji wenyewe hawawezi kuelewa kile wanachosema, na baadhi yao wanaweza "kuifasiri." Onyesho la tatu ni pale ambapo watu siku zote wanaupokea ufunuo, unaofanyika kwa uradidi fulani. Kwa wakati mmoja wataelekezwa kufanya kitu kimoja, na kwa wakati mwingine wataambiwa kufanya kitu kingine, na wanaishi katika wasiwasi usioisha. Onyesho la nne: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao wanayo hamu ya kufanya hiki au kile, na hawawezi kusubiri—licha ya kama kitu hicho kinakubaliwa katika mazingira yao au la. Huwa hata wanatoka nje kwenye giza la usiku; mwenendo wao si wa kawaida kamwe. Onyesho la tano: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao huwa hasa wenye majivuno na kiburi, kila kitu wanachosema ni cha kushusha hadhi na kuamrisha, hawawezi kuuongea ukweli wowote, anawaacha watu wakiwa wamekasirika, na kuwalazimisha watu kuingia kwenye taabu kama pepo. Onyesho la sita: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao hawana ufahamu kiasi kidogo cha mipangilio kutoka juu, isitoshe hawaelewi kanuni za kazi; wanamkenulia Mungu, wanajaribu kuwadanganya watu, na matendo yao mabaya yanatatiza mpangilio wa kawaida wa kanisa. Onyesho la saba: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao mara nyingi hujifanya kuwa watu wengine bila sababu, au vinginevyo wametumwa na mtu, kuwafanya watu kuyasikiliza maneno yao, na hakuna anayeweza kujua namna walivyofikia hapo. Onyesho la nane: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao mara nyingi hawana urazini, na hawauelewi ukweli; kwa kawaida, wanakosa welekevu wa kuelewa, na hawana kule kupewa nuru na Roho Mtakatifu. Watu hugundua kwamba kile wanachoelewa hasa si cha kawaida, na si sahihi kabisa. Onyesho la tisa: watu ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao ni wenye makuu kabisa na wasio na urazini, hawamtukuzi Mungu wala kumtolea ushuhuda kamwe, hawawezi kuuongea ukweli wowote, na kile wanachofanya na kusema tu huwa kinawashambulia watu, kinawafunga, na kuwawekea mipaka, mpaka pale ambapo mioyo yao imeshughulikiwa, na wao kupigwa na kugeuzwa kuwa wabaya na wasioweza kujiokoa, huku nao wakiwa na furaha kisirisiri—ambayo ndiyo nia kuu ya kazi ya pepo wabaya. Onyesho la kumi: watu ambao wamepagawa na pepo wabaya—maisha yao yana kasoro kabisa, mtazamo wao mkali, na maneno yao hasa hayana urafiki, ni kana kwamba wao ni pepo ambaye ameingia ulimwenguni humu. Hakuna nidhamu katika maisha yao ya kila siku, hawana uthabiti kabisa, wao hawatabiriki kama vile wale wanyama wasiofugwa, wanyama mwitu, na watu wanawaona kuwa wanaweza kupingika kabisa. Hayo ndiyo maonyesho ya watu waliofungwa na mashetani. Watu ambao wamepagawa na pepo wabaya mara nyingi hasa wanakuwa wenye chuki na kujitenga na wale ambao Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao na wanaoweza kuuongea ukweli. Ndivyo inavyokuwa mara nyingi kwamba watu wanapokuwa bora zaidi, ndipo wanapotaka kuwashambulia na kuwashutumu, ilhali watu wanapokosa mwelekeo na kuchanganyikiwa zaidi, ndipo wanapofanya kadri wanachoweza kuwalaghai na kuwavisha kilemba cha ukoka, na hasa wao kuwa radhi kujihusisha nao. Kazi ya pepo wabaya hugeuza nyeusi ikawa nyeupe, na kuyafanya mazuri kuwa mabaya na mabaya kuwa mazuri. Hayo ndiyo matendo ya pepo wabaya.
kutoka kwa "Maonyesho Makuu ya Kazi ya Pepo Wabaya" katika Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu
Roho yoyote ambayo kazi yake inajionyesha katika hali isiyo ya ulimwenguni humu ni pepo mbaya, na kazi na matamko ya roho yoyote inayotekeleza kazi isiyo ya ulimwenguni humu ndani ya watu ni kazi ya pepo mbaya; mbinu hizi zote ndizo ambazo pepo wabaya hufanya kazi na si za kawaida na za humu ulimwenguni, na zinaonyeshwa kimsingi kwa njia sita zifuatazo:
1. Udhibiti wa moja kwa moja wa uneni wa watu, jambo ambalo linaonyesha waziwazi kwamba pepo mbaya anazungumza, na wala si watu wenyewe wanaozungumza kwa kawaida;
2. Hisia kwamba pepo mbaya anawaelekeza watu na kuwaamuru kufanya hiki na kile;
3. Watu ambao, wakati wakiwa kwenye chumba, wanaweza kujua wakati mtu yuko karibu kuingia ndani;
4. Watu ambao mara nyingi wanazisikia sauti zikiwazungumzia na ambazo wengine hawawezi kuzisikia;
5. Watu ambao wanaweza kuona na kusikia mambo ambayo wengine hawawezi;
6. Watu ambao siku zote wanafadhaishwa, na wanajizungumzia wenyewe, na hawawezi kuwa katika mazungumzo ya kawaida au utangamano na watu.
Wale wote ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao bila kuepukika wanayo maonyesho haya sita. Wao hawana urazini, siku zote wako katika hali ya taharuki, hawawezi kutangamana na watu kwa njia ya kawaida, ni kana kwamba wao hawashawishiki kwa lolote lile, na kuna jambo lililojitenga na lisilo lao. Watu kama hao wamepagawa na pepo mbaya au wanaye pepo mbaya anayefanya kazi ndani yao, na kazi yote ya pepo wabaya inajionyesha na si ya ulimwenguni humu. Hii ndiyo kazi inayotambulika kwa haraka zaidi kuhusu pepo wabaya. Wakati pepo mbaya anapompagaa mtu, anacheza nao kiasi cha kwamba wanaathirika kabisa. Wanakosa urazini, kama zuzu, hali ambayo inathibitisha kwamba kiini cha mambo ni kuwa, pepo wabaya ni pepo waovu wanaopotosha na kuteketeza watu. Matamko ya pepo wabaya ni rahisi kuyatambua: Matamko yao yanaonyesha kikamilifu kiini chao cha uovu, yapo palepale, yamevurugika, na yananuka, yanarishai harufu ya kifo. Kwa watu walio na uhodari mzuri, maneno ya pepo wabaya huwafanya kuhisi utupu na kutovutiwa, yasiyorekebisha maadili, yasiyo na chochote ila uongo na maneno yasiyo na maana, wanahisi wakiwa wamevurugika na wanaona ugumu kuelewa yote haya, kama zigo la upuuzi. Huu ni baadhi ya upuuzi unaotambulika kwa haraka zaidi kuhusu pepo wabaya. Kuwaroga watu, baadhi ya wale pepo wabaya wa "kiwango cha juu" hujifanya kuwa Mungu au Kristo wanapoongea, huku wengine wakijifanya kuwa malaika au watu maarufu. Wanapoongea, pepo hawa wabaya ni stadi katika kuiga maneno au kauli fulani za Mungu, au sauti ya Mungu, na watu wasiouelewa ukweli wanadanganywa kwa urahisi na pepo kama hawa wabaya wa "kiwango cha juu." Watu wa Mungu waliochaguliwa lazima wawe wazi kwamba, kiini cha mambo ni kwamba, pepo wabaya ni waovu na wasio na aibu, na hata kama wao ni pepo wabaya wa "kiwango cha juu," wao hawana ukweli kabisa. Pepo wabaya, zaidi ya yote, ni pepo wabaya, kiini cha pepo wabaya ni uovu, na wenye sampuli moja na Shetani.
kutoka kwa "Jinsi ya Kutambua Upumbavu na Uongo wa Roho Waovu, Makristo wa Uongo, na Wapinga Kristo" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (II)
Kila kitu ambacho pepo wabaya hufanya si cha ulimwenguni humu kabisa, wao huelekeza moja kwa moja watu kufanya hiki au kile, huwaamuru moja kwa moja kufanya hiki na kile, huwalazimisha kwa njia ya moja kwa moja kufanya mambo—haya ndiyo maonyesho ya kazi ya pepo wabaya. Kazi ya Roho Mtakatifu haijawahi kuwalazimisha watu kufanya hiki au kile, haijawahi kuwaamuru watu huku na kule, haijawahi kukosa kuwa ya ulimwenguni humu, haijawahi kutumia mbinu zisizo za ulimwenguni humu kuwaelekeza watu kufanya mambo, siku zote imefichwa ndani kabisa ya watu, na inawagusa kupitia kwa dhamiri yao ili kuwafanya kuuelewa ukweli na maneno ya Mungu, na baadaye hutumia dhamiri kuwafanya kuuweka ukweli ule katika matendo. Hii ndiyo mbinu ambayo Roho Mtakatifu hufanyia kazi. Roho Mtakatifu hajawahi kuwalazimisha wala kuwashurutisha watu, Hajawahi kufanya chochote kisicho cha ulimwenguni humu au chenye maonyesho, na Haelekezi watu waziwazi. Tunajua nini kutoka kwa haya? Tunajua kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni nyenyekevu na fiche, na hasa fiche, na hakuna yoyote yake imefichuliwa. Mungu ni mwenye kudura na anashikilia utawala dhidi ya vitu vyote, lakini Roho Mtakatifu hamwambii mwanadamu kwa njia ya moja kwa moja, "Aisee, unafaa kufanya hivi au vile." Roho Mtakatifu hajawahi kuchukua hatua namna hii; Yeye hukugusa, kwa kutumia upendo Yeye hukugusa, na Yeye ni mtulivu sana, kiasi cha kwamba huhisi kama mtu anakugusa—lakini kwenye kina cha moyo wako unahisi kwamba unafaa kuchukua hatua kwa njia fulani, na kwamba ni sahihi na bora kufanya hivyo. Tazama namna ambavyo Mungu alivyo mzuri! Tazama tena sura mbovu na ya kuhurumiwa ya wale waliopagawa na pepo wabaya, tazama ambavyo, pindi wanapokutana na watu, wanasema, "Leo roho amenielekeza kusema hivi, ameniambia kufanya vile, amenifanya kufanya hivi," angalia namna ambavyo wakati mwingine wanavyoamka kwenye usiku wa giza kueneza injili, au kuomba, au kusema namna ambavyo wameguswa na lazima watimize wajibu wao. Tazama namna, punde watu wanapofungwa na pepo mbaya, yeye huwasababishia mateso mabaya, na kuwafanya kusambaratika, tazama namna ambavyo hawajui ni lini watakula au kufanya mambo, namna ambavyo maisha yao yamebadilika na kuwa kombo. Wakati ambapo pepo wabaya wanafanya kazi ndani ya watu, wao huwazungusha huku na kule, na kuwaacha wakiwa wamechoka na hoi. Hatimaye, wanaambulia patupu: Hakuna mabadiliko katika tabia yao ya maisha, wangali bado wamepotoka kama walivyokuwa awali, wale ambao kwa kawaida walikuwa na majivuno na makuu wangali bado na majivuno na makuu, na wale waliokuwa wajanja na wakujitia mapuuza wangali wajanja na walewale wa kujitia mapuuza. Kazi ya pepo wabaya huwapotosha watu, na kuwaacha wakiwa si wa kawaida kiakili. Kutoka kwenye utaratibu wa utendaji wa pepo wabaya, tunaona tu namna ambavyo wana dharau, uovu, mapuuza, na ujinga. Hafanyi chochote ila kuwanyanyasa na kuwapotosha watu, kwa sababu ya haya wanachukiwa na kulaaniwa na watu, wanaosema kwamba wao ni wabaya. Hivyo, kazi ya pepo wabaya inamwakilisha Shetani—hakuna kosa katika haya. Yeyote aliyewaona watu ambao pepo wabaya hufanya kazi ndani yao, au wale waliopagawa na Shetani, anajua tu namna wanavyochukiza, walivyo na mapuuza, uovu, na walivyojaa upotovu. Je, mnayaona haya? Je, mnayaona baadhi yake, sivyo? Je, mmeona kwamba pepo wabaya wanaumiliki ukweli? Je, pepo wabaya wanao upendo wowote kwa wanadamu? Kutoka kwenye kazi ya pepo wabaya, inaweza kuonekana kwamba hawana ukweli hata kidogo, na kwamba asili yao ni ya uovu kabisa. Baada ya kuona namna ambavyo pepo wabaya wanavyowapotosha watu, umeona namna ambavyo Shetani hupotosha watu—ni ukweli kabisa. Kwa sababu pepo wote wabaya wanashirikiana na Shetani, kwani wote wanamfuata Shetani, na ndio washiriki, marafiki, na washirikishi wa Shetani, wamekuwa na Shetani tangu hapo zama za kale. Shetani aliwaongoza pepo hawa wote wabaya katika kuasi dhidi ya Mungu na akaangushwa hapa ulimwenguni. Je, pepo mbaya angeweza—pepo mbaya asiye na ukweli na mwenye kuasi kabisa Mungu katika asili yake—kuuleta ukweli wowote kwa mtu anapompagaa? Anaweza kuyaleta mabadiliko katika tabia zao? Bila shaka, la.
kutoka kwa "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)

Alhamisi, 13 Juni 2019

Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

2. Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu na mwanadamu hawawezi kuzungumziwa kama wa kulingana. Dutu ya Mungu na kazi Yake ni vitu visivyoeleweka na kufahamika kwa mwanadamu. Ikiwa Mungu hawezi kufanya kazi Yake binafsi na kuzungumza maneno Yake katika ulimwengu wa mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kuelewa mapenzi ya Mungu, na kwa hivyo, hata wale waliotoa maisha yao yote kwa ajili ya Mungu hawataweza kupata idhini ya Mungu. Bila kazi ya Mungu, haijalishi jinsi gani mwanadamu anatenda mema, haitahesabika kama chochote, kwa maana fikira za Mungu daima zitakuwa juu ya fikira za mwanadamu, na hekima ya Mungu haieleweki kwa mwanadamu. Na kwa hivyo Nasema kwamba wale ambao “wanaona kwa wazi” Mungu na kazi Yake ni wasioweza kufanikisha chochote, wao wote ni wenye kiburi na wapumbavu. Mwanadamu hafai kufafanua kazi ya Mungu; zaidi ya hayo, mwanadamu hawezi kufafanua kazi ya Mungu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu ni mdogo kushinda mchwa, kwa hivyo mwanadamu atawezaje kuelewa kazi ya Mungu? Wale wasemao daima, “Mungu hafanyi kazi kwa njia hii ama ile” au “Mungu yuko hivi ama vile”—je hawa wote si wenye kiburi? Tunafaa sote kujua kwamba watu, ambao ni wa mwili, wote wamepotoshwa na Shetani. Ni katika hali yao asili kumuasi Mungu, na hawako katika usawa na Mungu, sembuse kuweza kutoa mawaidha kwa kazi ya Mungu. Jinsi Mungu anavyomwelekeza mwanadamu ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mwanadamu anafaa kunyenyekea, na hafai kuwa na wazo hili ama lile, kwani mwanadamu ni mchanga tu. Kwa sababu tunajaribu kumtafuta Mungu, hatufai kuwekelea dhana zetu katika kazi ya Mungu ili Mungu Aziwaze, na zaidi hatufai kutumia tabia zetu potovu kwa kupinga kazi ya Mungu kwa makusudi. Je hili halitatufanya wapinga Kristo? Je, watu kama hawa watawezaje kusema kuwa wanamwamini Mungu? Kwa maana tunaamini kuwa kuna Mungu, na kwa maana tunatamani kumtosheleza na kumwona, tunapaswa kutafuta njia ya ukweli, na tunapaswa kutafuta njia ya kulingana na Mungu. Hatupaswi kuwa katika upinzani sugu kwa Mungu; Matendo kama haya yatakuwa na matokeo gani mazuri?
Leo hii, Mungu Anayo kazi mpya. Unaweza kuyakataa maneno haya, yanaweza kuhisi yasiyo ya kawaida kwako, lakini Nakushauri usifichue asili yako halisi, kwa maana wale tu walio na njaa ya kweli na kiu cha haki mbele za Mungu ndio wanaweza kupata ukweli, na wale wanaomcha Mungu kwa ukweli tu ndio wanaweza kupata nuru na kuongozwa na Mungu. Hakuna litakalotoka kwa kutafuta ukweli kupitia ugomvi. Ni kwa kutafuta kwa utulivu ndio tunaweza kupata matokeo. Ninaposema kwamba “Leo, Mungu Anayo kazi mpya,” Ninaashiria Mungu kurudi katika mwili. Pengine huyajali maneno haya, pengine unayachukia, au pengine una haja kubwa sana nayo. Haijalishi ni hali gani, Natumai kuwa wote walio na tamaa ya kweli ya kuonekana kwa Mungu wataweza kuukabili ukweli huu na kutafakari juu yake kwa makini. Ni vyema usiamue jambo upesi bila kuzingatia suala zima. Hivi ndivyo watu wenye hekima wanapaswa kutenda.
kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili
Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe kawaida na wenye kutojali katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?
kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa “Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.” Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani! Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulinganishwa na fikira za mwanadamu, sembuse Mungu kuonekana kwa amri ya mwanadamu. Mungu hufanya uamuzi Wake mwenyewe na huwa na mipango Yake Afanyapo kazi; aidha, Ana malengo Yake, na mbinu Zake. Si lazima Ajadiliane kazi Azifanyazo na mwanadamu au Atafute ushauri wa mwanadamu, sembuse kumfahamisha kila mtu kuhusu kazi Yake. Hii ndiyo tabia ya Mungu na, zaidi ya hayo, inafaa kutambuliwa na kila mmoja. Kama mnatamani kushuhudia kuonekana kwa Mungu, kama mnatamani kufuata nyayo za Mungu, basi kwanza ni sharti mzishinde dhana zenu. Ni sharti muache kudai kuwa Mungu afanye hiki au kile sembuse kumweka Yeye ndani ya mipaka yenu wenyewe na kumwekea upeo kwa dhana zenu. Badala yake, mnafaa kujua ni vipi mtazitafuta nyayo za Mungu, na vipi mnapaswa kukubali kuonekana kwa Mungu na ni vipi mnapaswa kutii kazi mpya ya Mungu; hiki ndicho kinapaswa kufanywa na mwanadamu. Kwa kuwa mwanadamu si ukweli, na hamiliki ukweli, mwanadamu anafaa kutafuta, kukubali na kutii.
Bila kujali kama wewe ni Mmarekani, Mwingereza, au mtu wa taifa jingine, ni lazima utoke nje ya mipaka yako, ni lazima ujipite, na ni sharti uione kazi ya Mungu kama kiumbe wa Mungu. Kwa njia hii, hutaweka vikwazo katika nyayo za Mungu. Kwa sababu, leo, watu hufikiri kuwa haiwezekani Mungu kudhihirika katika nchi au taifa fulani. Umuhimu wa kazi ya Mungu una undani kiasi gani, na kuonekana kwa Mungu kuna maana ilioje! Vinawezaje kupimwa kwa dhana na fikira za mwanadamu? Na ndiyo maana Ninasema kuwa unafaa kujiondoa katika dhana za uraia wako au kabila lako unapokutafuta kuonekana kwa Mungu. Kwa njia hii, hutafungwa na dhana zako mwenyewe; kwa njia hii, utahitimu kukaribisha kuonekana kwa Mungu. Vinginevyo, daima utakuwa gizani na hutapata kibali cha Mungu.
kutoka katika “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu ni Mungu wa wanadamu wote. Hawi mali binafsi ya nchi au taifa lolote na hufanya kazi ya mpango Wake bila kuzuiwa na mfumo wowote, nchi au taifa. Labda hujawahi kuwazia mfumo huu, au labda wewe hukana kuwepo kwake, au labda nchi au taifa ambapo Mungu huonekana limebaguliwa na lina maendeleo duni sana duniani. Na bado Mungu ana busara Yake. Na uwezo Wake kupitia ukweli na tabia Zake kwa hakika Amepata kundi la watu wenye mawazo sawa na Yeye. Na Amepata kundi la watu ambao alitaka kutengeneza: kundi lililoshindwa Naye, watu ambao wameyavumilia majaribu machungu na aina zote za mateso na wanaweza kumfuata mpaka mwisho. Malengo ya kuonekana kwa Mungu, bila vizuizi vya nchi yoyote, ni kumruhusu Akamilishe kazi ya mpango Wake. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kutimiza kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kuwa mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu na hatimaye ikawa kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, na vilevile kukushutumu kuonekana huku; “kutowezekana” kwao kwa mara nyingine kunabana kuonekana kwa Mungu katika mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakicheka na kuanguka baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kukufuru kwa Wayahudi? Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama huwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? Mahali ambapo Mungu anajitokeza, kuna maonyesho ya kweli, na kuna sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Weka dhana zako kando. Tafakari na kusoma maneno haya kwa makini. Ukitamani ukweli, Mungu atakupa nuru ya kuyafahamu mapenzi Yake na maneno Yake. Wekeni kando mitazamo yenu ya “haiwezekani”! Kadiri watu wanavyozidi kuamini kuwa jambo fulani haliwezekani, ndivyo uwezekano wa utukiaji wake unavyoendelea kujiri, kwani ufahamu wa Mungu hupaa juu kuliko mbingu, mawazo ya Mungu yako juu ya yale ya mwanadamu, na kazi ya Mungu inapita mipaka ya fikira za mwanadamu. Kadiri kitu kinavyokuwa hakiwezekani, ndivyo kunavyokuwepo na ukweli wa kutafutwa; kadiri kitu kilivyo nje ya mipaka ya dhana na fikira za mwanaadamu, ndivyo kinavyozidi kuwa na mapenzi ya Mungu. Kwani bila kujali Mungu anajidhihirishia wapi, Mungu bado ni Mungu, na kiini chake hakitawahi kubadilika kwa sababu ya mahali ama namna ya kuonekana Kwake. Tabia ya Mungu hubaki kuwa vilevile bila kujali nyayo Zake ziko wapi. Bila kujali nyayo za Mungu zilipo, Yeye ndiye Mungu wa wanadamu wote. Kwa mfano, Bwana Yesu si Mungu tu wa Waisraeli, lakini vilevile ni Mungu wa watu wote wa Asia, Ulaya, na Marekani, na hata zaidi, ndiye Mungu pekee wa ulimwengu mzima. Hivyo basi, tuyatafute mapenzi ya Mungu na tugundue kuonekana Kwake kutoka kwa matamshi Yake na tufuate nyayo Zake. Mungu ndiye ukweli, njia na uzima. Maneno Yake na kuonekana Kwake yanakuwepo sawia, na tabia na nyayo Zake daima zitapatikana na wanadamu. Ndugu wapendwa, natumaini kwamba mnaweza kuona kuonekana kwa Mungu katika maneno haya, na kwamba mtaanza kuzifuata nyayo Zake kuelekea enzi mpya, na hadi katika mbingu mpya yenye kupendeza na dunia mpya iliyoandaliwa kwa wale wanaosubiri kuonekana kwa Mungu.
kutoka katika “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili