Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kristo-wa-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kristo-wa-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 29 Machi 2019

Muujiza katika Msiba | Video ya Injili "Mungu Abariki"


Muujiza katika Msiba | Video ya Injili "Mungu Abariki"

Watu mara nyingi husema kwamba "Dhoruba hukusanyika bila tahadhari na balaa huwafika watu kwa ghafula sana." Katika enzi yetu iliyopo ya kupanua kwa haraka kwa sayansi, uchukuzi wa kisasa na utajiri wa mali, maafa yanayotokea pande zote zinazotuzunguka huongeza kila siku. Tunapoligeuza na kulifungua gazeti au kuwasha TV, tunayoyaona hasa ni: vita, matetemeko ya ardhi, sunami, tufani, moto, mafuriko, ajali za ndege, maafa ya kuchimba madini, msukosuko wa kijamii, mgongano mkali sana, mashambulizi ya kigaidi nk. Yote tunayoona ni maafa ya kiasili na maafa yaliyotengenezwa na mtu. Maafa haya yanatokea mara kwa mara na yanazidi kuwa makali zaidi. Shambulizi hili la maafa huleta mateso, damu, kulemazwa na kifo. Misiba hutokea pande zote zinazotuzunguka wakati wote, ikisisitiza ufupi na udhaifu wa maisha. Hatuna njia ya kutabiri ni aina gani ya maafa tutakayokutana nayo katika siku zijazo. Aidha, hatujui ni mkondo gani wa hatua tunaopaswa kuchukua. Kama wanajumuiya wa wanadamu, tunapaswa kufanya nini ili kuondokana na maafa haya? Katika programu hii, utapata jibu. Utapata njia ya pekee ya kupokea ulinzi wa Mungu ili kwamba uweze kunusurika maafa yanayokaribia.
Mwenyezi Mungu alisema, Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, wala njia inayoweza kukuongoza kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.
Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

Jumatatu, 18 Machi 2019

Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii moyoni mwake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni zozote, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi Anayofanya daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya utendaji kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake. Maarifa ya mwanadamu ya maisha yanakua hata juu zaidi, na vivyo hivyo kazi ya Mungu pia inakuwa juu zaidi. Mwanadamu anaweza kufikia ukamilifu kwa njia hii tu na kufaa kwa matumizi ya Mungu. Kwa upande mmoja, Mungu anafanya kazi hivi ili kupinga na kubadilisha fikira za mwanadamu, na kwa upande mwingine, kumwongoza mwanadamu katika hali ya juu zaidi na kweli zaidi, hadi katika ulimwengu wa juu zaidi wa imani katika Mungu, ili mwishowe, mapenzi ya Mungu yaweze kufanyika. Wote walio na asili isiyotii wanaopinga kwa kusudi wataachwa nyuma na hatua hii ya kazi ya Mungu ya haraka na yenye kusonga mbele kwa nguvu; wale tu walio na moyo mtiifu na wako tayari kuwa wanyonge wataendelea hadi mwisho wa njia. Katika kazi kama hii, nyote mnapaswa kujua jinsi ya kutii na kuweka kando fikira zenu. Mnapaswa kuwa waangalifu katika kila hatua mnayochukua. Kama wewe ni mzembe, hakika utakuwa mmoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na yule anayemkatiza Mungu katika kazi Yake. Kabla ya kufanyiwa hatua hii ya kazi, kanuni na sheria za mwanadamu za zamani zilikuwa nyingi sana hadi akawa na msisimko zaidi, na mwishowe, akawa mwenye majivuno na kujisahau. Hivi vyote ni vikwazo vinavyomzuia mwanadamu kuikubali kazi mpya ya Mungu; vinakuwa pingamizi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Iwapo mwanadamu hana utii katika moyo wake wala tamaa ya ukweli, basi atakuwa hatarini. Ukitii tu kazi na maneno yaliyo rahisi, na huwezi kukubali yoyote yaliyo na ugumu zaidi, basi wewe ni yule anayeendelea na njia za zamani na hawezi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa katika awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu ambaye ni mtiifu kwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima katika utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haikubaliki na Mungu. Kama huwezi kwenda sambamba na kazi mpya Ninayoshiriki na uendelee kuyashikilia maneno ya zamani, basi kutakuaje na ukuaji katika maisha yako? Kazi ya Mungu ni kukuruzuku kupitia neno Lake. Unapotii na kulikubali neno Lake, basi Roho Mtakatifu hakika atafanya kazi ndani yako. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa njia Ninayozungumza kabisa. Fanya Nilivyosema, na Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako mara moja. Natoa mwangaza mpya ili muweze kuona na kuwaleta kwa mwangaza wa wakati wa sasa. Unapotembea katika mwangaza huu, Roho Mtakatifu ataanza kazi ndani yako mara moja. Kuna wengine wanaoweza kuwa wakaidi na kusema, “Sitafanya tu usemavyo.” Basi Nakwambia kwamba sasa umefika mwisho wa njia umenyauka na huna maisha zaidi. Hivyo, kwa kupitia mabadiliko ya tabia yako, ni muhimu kabisa kwenda sambamba na mwangaza wa sasa. Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi ndani ya mtu mwingine ajaye. Fanya hima ufuate; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndivyo maisha yako yanaweza kuzidi kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Kwa kufanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu kwa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui ni kupitia kwa mtu wa aina gani ndiyo Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo ndiyo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani. Ukiweza kutembea kwenye njia hii sawa, hii inaonyesha kwamba kuna matumaini makubwa kwako kukamilishwa na Mungu. Kama huwezi kufanya hivyo, inaonyesha kwamba maisha yako ya baadaye ni ya dhalili na giza. Mara unapoendenda kwenye njia iliyo sahihi, utapata ufunuo katika mambo yote. Bila kujali yale ambayo Roho Mtakatifu atafichua kwa wengine, ukiendelea kupitia mambo wewe mwenyewe kwa msingi wa maarifa yao, basi uzoefu huu utakuwa sehemu ya maisha yako, na utaweza kuwakimu wengine kwa sababu ya huu uzoefu. Wale wanaowakimu wengine kwa kuyarudia maneno ni wale wasio na uzoefu wowote; lazima ujifunze kupata, kupitia mwangaza na nuru ya wengine, njia ya kutenda kabla ya kuzungumza kuhusu uzoefu na maarifa yako halisi. Hii itakuwa ya manufaa zaidi kwa maisha yako binafsi. Unapaswa kuwa na uzoefu kwa njia hii, kutii yote yatokayo kwa Mungu. Unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu katika vitu vyote na kujifunza masomo katika vitu vyote, ukijenga ukuaji kwa maisha yako. Vitendo vya aina hii huleta ukuaji wa haraka zaidi.
Roho Mtakatifu anakupa nuru kupitia uzoefu wa vitendo vyako na kukukamilisha kupitia imani yako. Uko tayari kweli kukamilishwa? Kama kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu, basi utakuwa na ujasiri kuweka kando mwili wako, na utaweza kutekeleza maneno ya Mungu na kutokuwa mtu anayekaa tu ama mnyonge. Utaweza kutii yote yatokayo kwa Mungu, na vitendo vyako vyote, viwe vimefanywa hadharani au faraghani, vitastahiki kwa Mungu. Kama wewe ni mtu mwaminifu, na unatenda ukweli katika mambo yote, basi utakamilishwa. Wale wanadamu wadanganyifu wanaotenda njia moja mbele ya wengine na nyingine nyuma yao hawako tayari kukamilishwa. Wote ni wana wa maangamizo na uharibifu; wao si wa Mungu lakini ni wa Shetani. Hao si aina ya wanadamu waliochaguliwa na Mungu! Kama vitendo na tabia yako haviwezi kustahiki mbele ya Mungu ama kufikiriwa na Roho wa Mungu, hii ni thibitisho kwamba wewe una shida. Ukikubali tu hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kuweka umuhimu katika mabadiliko ya tabia yako ndipo utafika kwenye njia ya kukamilishwa. Ikiwa kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu na kufanya mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kutii kazi yote ya Mungu na kutotoa neno lolote la kulalamika, wala hupaswi kutathmini ama kuhukumu kazi ya Mungu utakavyo. Haya ni masharti ya msingi kabisa ya kukamilishwa na Mungu. Mahitaji ya lazima kwa wale wanaotaka kukamilishwa na Mungu ni haya: fanya mambo yote kwa moyo unaompenda Mungu. Inamaanisha nini “kufanya mambo kwa moyo unaompenda Mungu”? Inamaanisha kwamba vitendo na tabia yako yote inaweza kuletwa mbele ya Mungu. Kwa sababu una nia sawa, iwapo vitendo vyako ni sawa ama vibaya, huogopi vikionyeshwa kwa Mungu ama kwa ndugu zako; unathubutu kuapa mbele ya Mungu. Kwamba kila nia, fikra, na wazo lako linaweza kufaa kuchunguzwa mbele ya Mungu: ukitenda na kuingia kwa njia hii, basi maendeleo katika maisha yako yatakuwa mepesi.
Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu? Hata wale walio tu na moyo nusu wa utii hawawezi kutembea hadi mwisho, sembuse hawa wadhalimu wasio na utii hata kidogo kwa mioyo yao. Kazi ya Mungu haipatwi virahisi na mwanadamu. Hata mwanadamu akitumia nguvu yake yote, ataweza kupata kipande tu na kufikia ukamilifu mwishowe. Na vipi basi kuhusu watoto wa malaika mkuu wanaotaka kuharibu kazi ya Mungu? Je, hawana hata matumaini madogo zaidi ya kupatwa na Mungu? Madhumuni Yangu katika kufanya kazi ya ushindi si tu kushinda kwa sababu ya ushindi, lakini kushinda ili kufichua haki na udhalimu, kupata ushahidi kwa ajili ya adhabu ya mwanadamu, kulaani waovu, na hata zaidi, kushinda kwa sababu ya kuwakamilisha wale walio radhi kutii. Mwishowe, wote watatengwa kulingana na aina, na mawazo ya wale wote waliokamilishwa yatajazwa na utii. Hii ndiyo kazi itakayokamilishwa mwishowe. Lakini waliojawa na uasi wataadhibiwa, kutumwa kuchomeka motoni na milele kulaaniwa. Wakati huo utakapofika, wale “mashujaa wakubwa wasioshindwa” wa awali watakuwa “waoga wanyonge na wasio na maana” wa chini zaidi na wanaoepukwa zaidi. Hii tu ndiyo inaweza kuonyesha kila kipengele cha haki ya Mungu na kufichua tabia Yake ambayo hairuhusu kosa lolote. Hili tu ndilo linaloweza kutuliza chuki iliyo moyoni Mwangu. Je, hamkubali kwamba hili ni la busara sana?
Sio wote walio na uzoefu wa kazi ya Roho Mtakatifu wanaweza kupata uzima, na sio wote katika mkondo huu wanaweza kupata uzima. Uzima sio mali ya kawaida inayoshirikisha binadamu wote, na mabadiliko ya tabia ni kitu ambacho hakifikiwi na wote kwa urahisi. Kujisalimisha kwa kazi ya Mungu lazima kugusike na kuishi kwa kudhihirishwa. Kujisalimisha kwa kiwango cha juu juu hakuwezi kupokea idhini ya Mungu, na kutii tu vipengele vya juujuu vya neno la Mungu bila kutaka mgeuzo wa tabia ya mtu, hakutaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Utiifu kwa Mungu na kujinyenyekeza kwa kazi ya Mungu ni kitu kimoja. Wale wanaomtii Mungu tu lakini hawatii kazi Yake hawawezi kudhaniwa kuwa watiifu, sembuse wale wasiotii kwa kweli na kwa nje hao ni wa kujipendekeza. Wale ambao kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu wote wanaweza kufaidika kutokana na kazi na kupata ufahamu wa tabia na kazi ya Mungu. Wanadamu kama hawa tu ndio kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu. Wanadamu kama hawa wanaweza kupata maarifa mapya kutokana na kazi mpya na kuwa na uzoefu wa mabadiliko mapya kutoka hayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wana idhini ya Mungu; mwanadamu wa aina hii tu ndiye amekamilishwa, ndiye amepitia mabadiliko ya tabia yake. Wale wanaopokea idhini ya Mungu ni wale wanaojisalimisha kwa Mungu kwa furaha, na pia kwa neno na kazi Yake. Mwanadamu wa aina hii tu ndiye yuko sahihi; mwanadamu wa aina hii tu ndiye kweli anamtamani Mungu, na anamtafuta Mungu kwa dhati. Na kwa wale wanaozungumzia tu imani yao kwa Mungu kwa vinywa vyao lakini kwa hakika wanamlaani, ni wanadamu waliovaa barakoa, walio na sumu ya nyoka, ni wanadamu wasaliti zaidi. Siku moja hawa waovu watavuliwa barakoa zao mbovu. Je, hiyo si kazi inayofanywa leo? Wanadamu waovu daima watakuwa waovu na hawataepuka kamwe siku ya adhabu. Wanadamu wazuri daima watakuwa wazuri na watafichuliwa kazi itakapoisha. Hakuna hata mmoja wa waovu atakayedhaniwa kuwa wenye haki, wala yeyote mwenye haki atakayedhaniwa kuwa mwovu. Je, Ningemruhusu yeyote ashtakiwe kimakosa?
Maisha yako yanapoendelea, lazima daima uwe na kiingilio kipya na ufahamu mpya na wa juu zaidi, unaokua kwa kina na kila hatua. Hiki ndicho wanadamu wote wanapaswa kuingia ndani. Kupitia kuwasiliana, kusikiliza ujumbe, kusoma neno la Mungu, ama kushughulikia suala, utapata ufahamu mpya na kupata nuru upya. Huishi ndani ya kanuni za zamani na nyakati za zamani. Unaishi daima ndani ya mwangaza mpya, na hupotei mbali na neno la Mungu. Huku ndiko kunaitwa kwenda katika njia sahihi. Kulipa tu gharama ya juu juu hakutakubalika. Siku baada ya siku, neno la Mungu linaingia katika ulimwengu wa juu zaidi na mambo mapya yanajitokeza kila siku. Ni muhimu pia kwa mwanadamu kuingia upya kila siku. Mungu anavyozungumza, ndivyo Anavyotimiza yote ambayo Amezungumza; kama huwezi kwenda sambamba, basi unabaki nyuma. Lazima uende kwa kina zaidi katika maombi yako; kula na kunywa neno la Mungu hakuwezikuwa kunakosa mfululizo. Imarisha nuru na mwangaza unayopokea, ufunuo unaopokea, na dhana zako na fikira zako lazima zipungue hatua kwa hatua. Lazima pia uimarishe hekima yako, na chochote unachopitia, lazima uwe na mawazo yako kukihusu na uwe na mtazamo wako.Kwa kuelewa mambo fulani katika roho, lazima upate ufahamu wa mambo ya nje na kuelewa kiini cha suala lolote. Kama hujajiandaa na mambo haya, utawezaje kuliongoza kanisa? Iwapo unazungumzia tu barua na mafundisho ya dini bila uhalisi wowote na bila njia ya kutenda, unaweza tu kuendelea kwa muda mfupi. Inaweza kukubalika kidogo kwa waumini wapya, lakini baada ya muda, wakati waumini wapya wanapata tajriba halisi, basi hutaweza tena kuwakimu. Basi unafaa vipi kwa matumizi ya Mungu? Bila kupata nuru upya, huwezi kufanya kazi. Walio bila nuru upya ni wale wasiojua jinsi ya kuwa na uzoefu, na wanadamu kama hao kamwe hawapati maarifa mapya ama tajriba. Na katika suala la kuleta maisha, hawawezi kamwe kufanya jukumu lao la kusambaza uhai, wala hawawezi kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu. Mwanadamu kama huyu ni dhaifu na hana maana. Kwa kweli, wanadamu kama hawa hawawezi kufanya jukumu lao kabisa kwa kazi na wote hawana faida. Wanashindwa kufanya jukumu lao na pia kwa kweli wanaweka mzigo mwingi usiohitajika juu ya kanisa. Nawahimiza hawa “wanaume wazee” kuharakisha na kuondoka kanisani ili wengine wasilazimishwe kuwaona tena. Wanadamu kama hawa hawaelewi kazi mpya lakini wamejawa na fikira zisizokoma. Hawafanyi chochote kanisani; badala yake, wanachochea na kusambaza uhasi kila pahali, hata kushiriki katika kila namna ya utovu wa nidhamu na vurugu kanisani, na hivyo kuwarusha wale wasiobagua katika vurugu na machafuko. Haya ibilisi wanaoishi, hawa mapepo mabaya wanapaswa kuondoka kanisani haraka iwezekanavyo, kanisa lisije likaharibiwa kwa sababu yako. Labda huogopi kazi ya leo, lakini huogopi adhabu ya haki ya kesho? Kuna idadi kubwa ya watu kanisani ambao ni vimelea, na pia kuna idadi kubwa ya mbwa mwitu wanaotafuta kuvuruga kazi ya kawaida ya Mungu. Vitu hivi vyote ni mapepo yaliyotumwa na Ibilisi, ni mbwa mwitu wakali wanaotafuta kuwala kondoo wasio na hatia. Iwapo wanadamu kama hawa hawatafukuzwa, basi wanakuwa vimelea kwa kanisa na nondo wanaokula sadaka. Hawa mabuu wenye kudharauliwa wajinga, duni, na wenye kuchukiza wataadhibiwa siku moja karibuni!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 24 Februari 2019

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Mwenyezi Mungu alisema, Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi. Watu, ambao wamepotoshwa, wote huishi katika mtego wa Shetani, wao kuishi katika mwili, kuishi katika tamaa za ubinafsi, na hakuna hata mmoja kati yao anayelingana na Mimi. Kuna wale ambao wanasema kwamba wao wanalingana na Mimi, lakini ambao wote huabudu sanamu zisizo yakini. Ingawa wanakubali jina Langu kama takatifu, wao hutembea kwenye njia ambazo huenda kinyume na Yangu, na maneno yao yamejaa kiburi na kujiamini, kwa sababu, katika mizizi, wote wananipinga na hawalingani Nami. Kila siku wao hutafuta dalili Yangu katika Biblia, na kupata vifungu "vinavyofaa" hapa na pale wanavyovisoma bila kukoma, na ambavyo wao hukariri kama maandiko. Hawajui jinsi ya kulingana na Mimi, hawajui maana ya kuwa katika uadui na Mimi, na wanasoma tu maandiko kwa upofu. Wao huzuia ndani ya Biblia na Mungu asiye yakini ambaye hawajawahi kumwona, na hawana uwezo wa kumwona, na wao huitoa tu na kuiangazia wakati wao wa ziada. Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswikufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo? Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu waliofuata maneno ya Maandiko kwa uimara; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?
Na je watu leo? Kristo amekuja kutoa ukweli, lakini wanaona ni afadhali wao kumfukuza Yeye kutoka kati ya wanadamu ili wapate kuingia mbinguni na kupokea neema. Wanaona ni afadhali kabisa kukataa kuja kwa ukweli, ili kulinda maslahi ya Biblia, na ni afadhali kumtundika Kristo ambaye Alirudi kwa mwili kwa misumari msalabani tena ili kuhakikisha kuwepo kwa Biblia milele. Jinsi gani mwanadamu anaweza kupokea wokovu Wangu, wakati moyo wake una nia mbaya namna hiyo, na asili yake inanipinga Mimi? Mimi huishi miongoni mwa wanadamu, ilhali bado wanadamu hawajui kuhusu kuwepo Kwangu. Ninapoangaza mwanga Wangu juu ya wanadamu, bado yeye hana ufahamu kuhusu kuwepo Kwangu. Wakati Ninatoa ghadhabu Yangu juu ya wanadamu, wao hukanusha kuwepo Kwangu kwa nguvu kubwa zaidi. Binadamu hutafuta uwiano na maneno, na Biblia, ilhali bado hakuna mwanadamu hata mmoja huja Kwangu kutafuta njia ya uwiano na ukweli. Binadamu huniheshimu sana Nikiwa mbinguni, na kujishughulisha hasa na kuwepo Kwangu mbinguni, ilhali hakuna anayenijali Nikiwa katika mwili, kwa maana Mimi Ninayeishi miongoni mwa wanadamu sina umuhimu kwao hata kidogo. Wale ambao hutafuta tu uwiano na maneno ya Biblia, na ambao hutafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, mbele Yangu ni fidhuli. Hiyo ni kwa sababu wanachokiabudu ni maneno yaliyokufa, na Mungu Aliye na uwezo wa kuwapa hazina isiyoambilika. Wanachoabudu ni mungu anayedhibitiwa na mtu, na ambaye hayuko. Ni nini, basi, ambacho watu wa namna hiyo wanaweza kupokea kutoka Kwangu? Mwanadamu ni kiumbe duni sana kiasi kwamba maneno hayawezi kueleza hali yake. Wale wanaonipinga, wanaofanya madai yasiyo na kipimo dhidi Yangu, wasio na upendo kwa ukweli, wanaoniasi—wangewezaje kulingana na Mimi?
Wale wanaonipinga ni wale ambao hawalingani na Mimi. Vile vile wale wasiopenda ukweli, na wale wanaoniasi ndio walio wapinzani Wangu zaidi na hawalingani na Mimi. Wale wote ambao hawalingani na Mimi Nawawasilisha mikononi mwa yule mwovu. Ninawaacha wao kwa upotovu wa yule mwovu, Nawaachilia huru ili wafichue maovu yao, na hatimaye kuwakabidhi kwa yule mwovu ili waliwe. Mimi Sijali ni watu wangapi wananiabudu, ambayo ni kusema, Sijali ni watu wangapi wanaamini ndani Yangu. Kinachonijalisha ni watu wangapi wanalingana na Mimi. Hiyo ni kwa sababu wote wasiolingana na Mimi ni wale waovu wanaonisaliti; wao ni adui Zangu, Nami "Sitawatunza" adui Zangu katika nyumba Yangu. Wale ambao wanalingana na Mimi watanitumikia milele katika nyumba Yangu, na wale wanaojiweka katika uadui na Mimi watateseka milele katika adhabu Yangu. Wale wanaojali tu kuhusu maneno ya Biblia, wasiojali kuhusu ukweli au kutafuta nyayo Zangu—wao wananipinga, kwa kuwa wao wananizuilia Mimi kulingana na Biblia, na kuniwekea vizuizi ndani ya na Biblia, na hivyo ni wa kukufuru pakubwa dhidi Yangu. Jinsi gani watu wa aina hii wanaweza kuja mbele Zangu? Wao hawatilii maanani matendo Yangu, au mapenzi Yangu, au ukweli, badala yake wanashikilia maneno, maneno yanayoua. Jinsi gani watu kama hao wanaweza kulingana na Mimi?
Nimeeleza maneno mengi sana, na pia nimeeleza mapenzi Yangu na tabia, lakini hata hivyo, bado watu hawana uwezo wa kunijua Mimi na kuniamini. Au, inaweza kusemwa, bado hawana uwezo wa kunitii. Wale wanaoishi katika Biblia, wale wanaoishi katika sheria, wale wanaoishi juu ya msalaba, wale ambao wanaishi kwa mujibu wa mafundisho, wale wanaoishi miongoni mwa kazi Ninayofanya leo—yupi kati yao analingana na Mimi? Ninyi mnafikiria tu kupokea baraka na tuzo, na hamjawahi kamwe kufikiria jinsi ya kulingana na Mimi, au jinsi ya kujizuia wenyewe kutoka katika uadui na Mimi. Nimeaibishwa sana na nyinyi, kwa kuwa Nimewapa mengi sana, ilhali Mimi Nimepokea kidogo sana kutoka kwenu. Udanganyifu wenu, kiburi chenu, tamaa yenu, tamaa yenu yenye fujo, usaliti wenu, kuasi—lipi kati ya haya linaweza kujificha kutoka kwa macho Yangu? Mnafanya mzaha na Mimi, mnanidanganya Mimi, mnanitusi, mnanilaghai, mnanilazimisha, mnapata sadaka kutoka Kwangu kwa nguvu—ni jinsi gani tabia ya kudhuru kama hii itaepuka ghadhabu Yangu? Udhalimu wenu ni thibitisho la uadui wako Kwangu, na ni thibitisho la uwiano wenu na Mimi. Kila mmoja wenu anaamini mwenyewe akilingana na Mimi, lakini ikiwa ni hivyo, basi ni kwa nani ushahidi huu dhahiri unatumika? Mnaamini wenyewe kwamba mnao ukweli wa juu sana na uaminifu Kwangu. Mnafikiri kwamba nyinyi ni wema sana, wenye huruma sana, na mmetoa sana Kwangu. Mnafikiri kwamba mmefanya vya kutosha kwa ajili Yangu. Bado hamjawahi kulinganisha imani hizi dhidi ya tabia zenu wenyewe? Nasema mmejaa mengi ya kiburi, tamaa nyingi, wingi wa uzembe; hila mnayotumia kunidanganya ni janja sana, na mna mengi ya nia ya kudharau na mbinu ya kudharau. Uaminifu wenu pia ni mdogo, bidii yenu pia ni ndogo, na dhamiri yako hata haipo zaidi. Kuna mabaya mengi sana katika nyoyo zenu, na hakuna mtu atakayesamehewa kutoka kwa hayo, hata Mimi mwenyewe. Mnanifungia nje kwa ajili ya watoto wenu, au waume wenu, au kwa ajili ya hifadhi zenu wenyewe. Badala ya kunijali, mnajali familia zenu, watoto wenu, hali yenu, maisha yenu ya baadaye, na kujitosheleza wenyewe. Ni lini mmewahi kuniwaza Mimi mnapozungumza au kutenda? Wakati hali ya hewa ni baridi, mawazo yenu hurejea kwa watoto wenu, waume wenu, wake wenu, au wazazi wenu. Wakati hali ya hewa ni ya joto, hata Siwezi kupata nafasi katika mawazo yenu pia. Unapotekeleza wajibu wako, wewe huwaza tu kuhusu maslahi yako mwenyewe, ya usalama wako mwenyewe binafsi, ya watu wa familia yako. Ni nini umewahi kufanya kwa ajili Yangu? Ni lini umeweza kuwaza kunihusu Mimi? Ni lini umewahi kujitoa mwenyewe, kwa gharama yoyote, kwa ajili Yangu na kazi Yangu? Uko wapi ushahidi wa uwiano wako na Mimi? Uko wapi ukweli wa uaminifu wako kwa ajili Yangu? Uko wapi ukweli wa utiifu wako Kwangu? Ni lini mujibu wako hujakuwa kwa sababu ya kupokea baraka Zangu? Mnanilaghai na kunidanganya Mimi, mnacheza na ukweli na kuficha kuwepo kwa kweli, na kuisaliti dutu ya ukweli, na mnajiweka wenyewe kwa uadui kama huu na Mimi. Basi, ni nini kinawangoja katika siku za usoni? Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Wakati uo huo, mtagundua kuwa hakuna mtu yeyote asiyelingana na Kristo atakayeepuka siku ya ghadhabu, na mtagundua ni aina gani ya adhabu italetwa juu ya wale walio katika uadui na Kristo. Siku hiyo itakapofika, ndoto yenu ya kubarikiwa kwa imani yenu katika Mungu na kupata kuingia mbinguni, yote itakatizwa. Lakini, hata hivyo, si hivyo kwa wale ambao wanalingana na Kristo. Ingawa wao wamepoteza sana, ingawa wamekabiliwa na mengi ya ugumu wa maisha, watapokea urithi wote ambao Nimeutoa kwa ajili ya mwanadamu. Hatimaye, mtaelewa kwamba Mimi tu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba ni Mimi tu Niliye na uwezo wa kuwachukua binadamu mpaka kwenye hatima yao yenye kupendeza.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatano, 30 Januari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna yeyote anayemchukua Kristo kama binadamu wa nyama na mwili aliye na kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao hufanya wanavyopenda wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa "Kristo wa kweli." Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.”

Jumamosi, 29 Septemba 2018

Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God


Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God

Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu, na Anatawala vitu vyote kutoka juu. Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia. Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati, kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya.
Mungu anamjua mwanadamu kama kiganja cha mkono Wake. Mahali pa siri ni makao ya Mungu, anga ndicho kitanda Mungu akilaliacho. Nguvu ya Shetani haiwezi kumfikia Mungu, kwani Yeye amejawa na utukufu, haki, na hukumu.
Mungu amekanyaga vitu vyote na miguu Yake, Yeye ananyosha mtazamo Wake juu ya ulimwengu. Na Mungu ametembea kati ya wanadamu, ameonja utamu na uchungu, ladha zote za dunia ya mwanadamu; lakini wanadamu, kamwe hawakumtambua Mungu kweli, wala hawakumwona Mungu alipokuwa akitembea ughaibuni. Kwa sababu Mungu alikuwa kimya, na hakufanya matendo yasiyo ya kawaida, hivyo, hakuna aliyemwona kweli. Vitu haviko vilivyokuwa awali: Mungu anaenda kufanya vitu ambavyo, katika enzi zote, ulimwengu haujawahi kuona, Mungu anaenda kunena maneno ambayo, katika enzi zote, wanadamu hawajawahi kusikia, kwa sababu Yeye anawataka binadamu wote waje kumjua Mungu katika mwili. kwa sababu Yeye anawataka binadamu wote waje kumjua Mungu katika mwili.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kazi ya Mungu

Jumamosi, 4 Agosti 2018

Sinema za Injili "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" | Roho wa Ukweli Amekuja!


Sinema za Injili "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" | Roho wa Ukweli Amekuja!

Tao Wei alikuwa mhubiri kutoka kanisa la nyumba. Kanisa lake lilipokuwa na ukiwa zaidi na zaidi siku baada ya siku, wafuasi wake wote wakawa walegevu na wenye roho dhaifu, na roho yake mwenyewe ilikuwa na giza. Yeye hakuweza tena kuhisi uwepo wa Bwana, na Tao Wei alichanganyikiwa, bila kujua la kufanya. Ulimwengu wa dini ulikuwa umepotezaje kazi ya Roho Mtakatifu? Inaweza kuwa kwamba Bwana alikuwa tayari amerudi, na alikuwa ameonekana ili kufanya kazi mahali pengine? ... Tao Wei alipotafuta haraka majibu ya maswali haya, alitamani zaidi na zaidi kufikia utoaji wa hai maji ya uzima kutoka kwa Mungu. Yeye na ndugu zake walitafuta kazi ya Mungu na kuonekana Kwake kwa pamoja, na hatimaye walikuja katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, ambapo walianza kuwasiliana na kujadiliana na wahubiri wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. ... Je, wataweza kupata chanzo cha maji yaliyo hai ya uzima katika Kanisa la Mwenyezi Mungu? Je, wataweza kufikia maji ya uzima kutoka kwa mto unaobubujika kutoka katika kiti cha enzi?
Soma Zaidi:  Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kristo wa Siku za Mwisho