Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wokovu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wokovu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 29 Juni 2019

Wokovu Unawezekana Tu Kupitia Imani kwa Mwenyezi Mungu

3. Wokovu Unawezekana Tu Kupitia Imani kwa Mwenyezi Mungu.

Maneno Husika ya Mungu:
Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani ilimlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi, lakini pia ilimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uhai.
…………
… Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Huafikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.
kutoka kwa "Dibaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—hauwezi kuwa na bahati hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu.
kutoka kwa "Kuhusu Majina na Utambulisho" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini haimaanishi kuwa mwanadamu hana dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia potovu za zamani za kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na uonekano wa kiungu; kama mwanadamu angeishi katika huo msingi, alichukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, hii ina maana kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia ya kuielekea tabia iliyobadilika; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii inamfanya mwanadamu kuwa safi kupitia neno ili kumpatia mwanadamu njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendeleaa na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupuwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua kivyako wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado ni ya dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo atakapotwaliwa na Mungu na kutakaswa. Lingine lisipofanywa ila kukemea mapepo katika mwanadamu na kumkomboa, huko ni kumshika tu kutoka kwa mikono ya Shetani na kumrudisha kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi, lakini mwanadamu hana maarifa kumhusu na bado anamkataa na kumsaliti Mungu. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuutupa nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivyo, hata kama sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Nyinyi nyote mnaishi mahala pa dhambi na ufisadi; nyinyi nyote ni watu wafisadi na wenye dhambi. Leo hii hamwezi tu kumwona Mungu, ila la muhimu zaidi, mmepokea kuadibu na hukumu, mmepokea wokovu wa kina, yaani, mmepokea upendo mkubwa zaidi wa Mungu. Yote Ayafanyayo ni mapenzi ya dhati kwako; Hana nia mbaya. Anawahukumu kwa sababu ya dhambi zenu, ili kwamba mweze kujichunguza wenyewe na kupokea wokovu mkubwa. Haya yote hufanywa kumfinyanga mwanadamu. Tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu amekuwa Akifanya kila Awezalo kumwokoa mwanadamu, na hakika hayuko tayari kuwaangamiza kabisa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Sasa Amekuja miongoni mwenu kufanya kazi; je, huu si wokovu zaidi? Je, Angalikuchukia, Angaliendelea kufanya kazi ya kiwango hicho cha juu ili kukuongoza wewe Mwenyewe? Ni kwa nini Ateseke hivyo? Mungu hawachukii wala hana nia mbaya juu yenu. Mnapaswa kufahamu kuwa mapenzi ya Mungu ndiyo mapenzi ya kweli zaidi. Anawaokoa kupitia hukumu kwa sababu tu ya uasi wa mwanadamu; la sivyo, hawangepata wokovu. Kwa kuwa hamjui jinsi ya kuishi, na mnaishi katika mahala pa ufisadi na dhambi na ni mapepo wenye ufisadi na uchafu, Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo. Hili ndilo kusudi kuu la kufanya kazi ya kushinda miongoni mwenu—ni kwa ajili ya wokovu tu.
kutoka kwa "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atajua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutahitimu kuingia lango la ufalme wa mbinguni, kwa ajili nyote ni makaragosi na wafungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na barua, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kiti cha enzi. Wale ambao hawajasambaziwa na maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya mchezo wa Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani?
kutoka kwa "Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni dhihirisho la Roho Mtakatifu, udhihirisho wa Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.
kutoka kwa "Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele" katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumatano, 24 Aprili 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa. Kwa maneno mengine, usimamizi wa Mungu wa mwanadamu ulianza kutokana na kazi ya kumwokoa mwanadamu, na wala haukutokana na kazi ya kuiumba dunia. Hakungekuwa na kazi ya kumsimamia mwanadamu pasipo kuwepo na tabia potovu ya mwanadamu, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu ina sehemu tatu, badala ya hatua nne, au enzi nne. Hii tu ndio njia sahihi ya kutaja kazi ya Mungu ya usimamizi wa mwanadamu. Enzi ya mwisho itakapofikia kikomo, kazi ya kusimamia mwanadamu itakuwa imekamilika. Hitimisho la kazi ya usimamizi lina maana kuwa kazi ya kuwaokoa wanadamu wote imemalizika kabisa, na kwamba mwanadamu amefika mwisho wa safari yake. Pasipo kazi ya kuwaokoa wanadamu wote, kazi ya usimamizi wa wanadamu haingekuwapo, wala hakungekuwa na hatua tatu za kazi. Ilikuwa ni hasa kwa ajili ya upotovu wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu alihitaji wokovu kwa dharura, ndipo Yehova alikamilisha uumbaji wa dunia na kuanza kazi ya Enzi ya Sheria. Hapo tu ndipo kazi ya kumsimamia mwanadamu ilipoanza, kumaanisha kwamba hapo tu ndipo kazi ya kumwokoa mwanadamu ilipoanza. "Kumsimamia mwanadamu" haimaanishi kuongoza maisha ya mwanadamu aliyeumbwa upya duniani (ambapo ni kusema, mwanadamu ambaye bado hakuwa amepotoshwa). Badala yake, ni wokovu wa ubinadamu ambao umepotoshwa na Shetani, ambapo ni kusema kwamba, ni kubadilishwa kwa mwanadamu aliyepotoshwa. Hii ndiyo maana ya kumsimamia mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu haihusishi kazi ya kuiumba dunia, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu haijumuishi kazi ya kuumba ulimwengu, na inahusisha tu hatua tatu za kazi zilizo tofauti na uumbaji wa ulimwengu. Ili kuelewa kazi ya kumsimamia mwanadamu, ni muhimu kuwa na ufahamu wa historia ya hatua tatu za kazi—hili ndilo kila mtu anapaswa kulifahamu ili kuokolewa. Kama viumbe wa Mungu, mnapaswa kutambua kuwa mwanadamu aliumbwa na Mungu, na kufahamu chanzo cha upotovu wa mwanadamu, na, vilevile, kufahamu mchakato wa wokovu wa mwanadamu. Iwapo mnafahamu tu jinsi ya kutenda kulingana na mafundisho ili kupata neema ya Mungu, lakini hamna fununu jinsi Mungu anavyomwokoa mwanadamu, au ya chanzo cha upotovu wa mwanadamu, basi hili ndilo mnalokosa kama viumbe wa Mungu. Hupaswi kutoshelezwa tu na kuelewa kwa ukweli unaoweza kuwekwa katika vitendo, huku ukibakia kutojua upeo mpana wa kazi ya usimamizi ya Mungu—kama hivi ndivyo ilivyo, basi wewe ni mwenye kulazimisha kauli sana. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo hadithi ya ndani ya usimamizi wa Mungu wa mwanadamu, ujio wa injili ya dunia nzima, fumbo kubwa zaidi kati ya wanadamu, na pia ni msingi wa kueneza injili. Ukizingatia tu kuelewa ukweli sahili unaohusiana na maisha yako, na usijue lolote kuhusu hili, maajabu makuu zaidi na maono, basi maisha yako si ni sawa na bidhaa yenye kasoro, yasio na maana isipokuwa kuangaliwa?
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya usimamizi ilikuja tu kwa ajili ya wanadamu, yaani ilitolewa kwa ajili ya uwepo wa wanadamu. Usimamizi haukuwepo kabla ya uwepo wa wanadamu au mwanzo wakati mbingu na nchi na vilivyomo vilipoumbwa. Iwapo, katika kazi nzima ya Mungu, hakungekuwa na vitendo vinavyomfaidi mwanadamu, yaani kama Mungu asingeweka matakwa maalum kwa mwanadamu aliyepotoka (ikiwa kazi ifanywayo na Mungu haikuwa na njia nzuri ya vitendo vya mwanaadamu), basi kazi hii isingeitwa usimamizi wa Mungu. Iwapo kazi nzima ya Mungu ingehusisha tu kuwaambia wanadamu waliopotoka jinsi ya kuendeleza vitendo vyao, na Mungu hakuendeleza kazi yoyote ya mipango Yake, na Hakuonyesha uwepo wake wa daima au busara, basi bila kujali ni jinsi gani matakwa ya Mungu kwa mwanadamu yangewekwa juu, bila kujali Mungu aliishi muda mrefu kiasi gani miongoni mwa wanadamu, mwanadamu asingejua chochote juu ya tabia ya Mungu; kama ingekuwa hivyo, basi kazi hii isingeweza kukaribia kuitwa usimamizi wa Mungu. Kwa ufupi, kazi ya usimamizi wa Mungu ni kazi iliyofanywa na Mungu na kazi zote zilizofanywa chini ya uongozi wa Mungu na wale ambao wamepatikana na Mungu. Kazi kama hiyo inaweza kuchukuliwa kwa ufupisho kama usimamizi, na inaelezea kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu na vilevile ni ushirikiano Wake na wale wanaomfuata; kwa ujumla, hayo yote yanaweza kuitwa usimamizi. Hapa kazi ya Mungu inaitwa maono na ushirikianao wa mwanadamu unaitwa vitendo. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo juu (yaani kadiri maono yalivyo juu), ndivyo tabia za Mungu zinakuwa wazi kwa mwanadamu, na kutoafikiana na mawazo ya mwanadamu, na ndivyo vitendo na ushirikiano wa mwanadamu huwa vya juu. Kadiri matakwa kwa mwanadamu yanavyokuwa ya juu, ndivyo kazi ya Mungu inavyotofautiana mawazo ya mwanadamu, matokeo yake yakiwa majaribu ya mwanadamu, na viwango anavyotarajiwa kuwa navyo, vilevile vinakuwa vya juu. Katika hatima ya kazi hii, maono yote yatakuwa yametimizwa, na yale yote mwanadamu anapaswa kuweka katika vitendo yatakuwa yamefikia kilele cha ukamilifu. Huu ndio wakati pia ambapo kila kitu kitawekwa katika kundi lake kwani kile kinachopaswa kufahamika na mwanadamu kitakuwa kimebainishwa kwake. Kwa hivyo maono yatakapofikia upeo wa juu, vivyo hivyo kazi nayo itakaribia hatima yake na vitendo vya mwanadamu vitakuwa vimefikia ufanisi wake. Vitendo vya mwanadamu vimekitwa katika kazi ya Mungu, na usimamizi wa Mungu unadhihirika tu kupitia vitendo na ushirikiano wa mwanadamu. Mwanadamu ni mfano wa kazi ya Mungu, na mlengwa wa kazi ya usimamizi mzima wa Mungu, na pia mazao ya kazi ya usimamizi wote wa Mungu. Iwapo Mungu angefanya kazi peke yake bila ushirika wa mwanadamu, basi pasingekuwepo na kitu cha kudhihirisha kazi Yake nzima na kwa hali hiyo kusingekuwa na umuhimu hata kidogo wa usimamizi wa Mungu. Ni kwa kuchagua tu chombo kifaacho kilicho nje ya kazi ya Mungu, na kinachoweza kudhihirisha kazi hii, na kuthibitisha kudura na busara zake, je, inawezekana kufikia dhumuni la usimamizi wa Mungu na kufikia dhumuni la kutumia kazi hii yote ili kumshinda kabisa Shetani. Na kwa hivyo mwanadamu ni sehemu muhimu katika kazi ya usimamizi ya Mungu, na mwanadamu ndiye pekee anayeweza kuifanya kazi ya usimamizi ya Mungu izae matunda na kufikia lengo Lake kuu; mbali na mwanadamu, hakuna kiumbe kingine chenye uhai kinachoweza kuchukua nafasi hiyo. Ikiwa mwanadamu atakuwa dhihirisho kamili la kazi ya usimamizi, basi uasi wa wanadamu wenye maovu lazima utokomezwe. Hii inahitaji kuwa mwanadamu apewe utendaji ufaao kwa kila muktadha, na kwamba Mungu afanye kazi inayotangamana miongoni mwa wanadamu. Ni kwa njia hii tu ndipo kutakuwa na kundi la watu waliokubaliwa ambao ni dhihirisho la kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu haiwezi kuwa ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe kupitia kazi ya Mungu peke yake; ushuhuda huo vilevile unahitaji wanadamu ambao wanafaa ili kazi yake iafikiwe. Mwanzo Mungu atawatayarisha watu hawa ambao kupitia kwao kazi Yake itadhihirika na ushuhuda Wake utachukuliwa miongoni mwa viumbe. Kwa hili, Mungu atakuwa ameafiki lengo la kazi Yake. Mungu hafanyi kazi peke Yake kumshinda Shetani kwa sababu Mungu hawezi kujishuhudia Mwenyewe moja kwa moja miongoni mwa viumbe wote. Angefanya hivyo, ingekuwa vigumu kumshawishi mwanadamu, kwa hivyo Mungu lazima Afanye kazi kwa mwanadamu ili kumshinda na ndipo Atakapoweza kupata ushuhuda miongoni mwa viumbe vyote. Mungu angefanya kazi peke Yake bila kushirikiana na mwanadamu, au kama mwanadamu asingetakiwa kushirikiana, basi mwanadamu asingeitambua tabia ya Mungu na daima asingefahamu nia ya Mungu; na kwa hali hii haiwezi kuitwa usimamizi wa Mungu. Mwanadamu mwenyewe angejizatiti, na kutafuta, na kufanya bidii, bila kuifahamu kazi ya Mungu, basi mwanadamu angekuwa anafanya mizaha. Bila kazi ya Roho Mtakatifu, akifanyacho mwanadamu ni cha Shetani, ni muasi na mtenda maovu; Shetani anadhihirika katika yote yafanywayo na mwanadamu mwenye maovu na hamna kinachoafikiana na Mungu, na yote ni dalili ya Shetani. Hakuna kati ya vilivyozungumziwa kisichokuwa na maono na vitendo. Katika msingi wa maono, mwanadamu hupata vitendo, anapata njia ya utiifu, ili kwamba aweze kuweka kando mawazo yake ili apate vile ambavyo hajawahi kuwa navyo hapo awali. Mungu huhitaji mwanadamu ashirikiane naye, kwamba mwanadamu asikilize matakwa Yake, na mwanadamu ashikilie kazi ifanywayo na Mungu Mwenyewe na kuupitia uwezo mkubwa wa Mungu na kuifahamu tabia ya Mungu. Kwa kifupi, haya ndiyo usimamizi wa Mungu. Ushirika wa Mungu na mwanadamu ndio usimamizi, na ni usimamizi mkuu zaidi.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Ijumaa, 29 Machi 2019

Muujiza katika Msiba | Video ya Injili "Mungu Abariki"


Muujiza katika Msiba | Video ya Injili "Mungu Abariki"

Watu mara nyingi husema kwamba "Dhoruba hukusanyika bila tahadhari na balaa huwafika watu kwa ghafula sana." Katika enzi yetu iliyopo ya kupanua kwa haraka kwa sayansi, uchukuzi wa kisasa na utajiri wa mali, maafa yanayotokea pande zote zinazotuzunguka huongeza kila siku. Tunapoligeuza na kulifungua gazeti au kuwasha TV, tunayoyaona hasa ni: vita, matetemeko ya ardhi, sunami, tufani, moto, mafuriko, ajali za ndege, maafa ya kuchimba madini, msukosuko wa kijamii, mgongano mkali sana, mashambulizi ya kigaidi nk. Yote tunayoona ni maafa ya kiasili na maafa yaliyotengenezwa na mtu. Maafa haya yanatokea mara kwa mara na yanazidi kuwa makali zaidi. Shambulizi hili la maafa huleta mateso, damu, kulemazwa na kifo. Misiba hutokea pande zote zinazotuzunguka wakati wote, ikisisitiza ufupi na udhaifu wa maisha. Hatuna njia ya kutabiri ni aina gani ya maafa tutakayokutana nayo katika siku zijazo. Aidha, hatujui ni mkondo gani wa hatua tunaopaswa kuchukua. Kama wanajumuiya wa wanadamu, tunapaswa kufanya nini ili kuondokana na maafa haya? Katika programu hii, utapata jibu. Utapata njia ya pekee ya kupokea ulinzi wa Mungu ili kwamba uweze kunusurika maafa yanayokaribia.
Mwenyezi Mungu alisema, Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, wala njia inayoweza kukuongoza kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.
Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

Jumatano, 26 Desemba 2018

Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Upendo wa Mungu

Sura ya 12. Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana

1. Usijishughulishe na Ikiwa Umejaaliwa na Mungu, bali Ujishughulishe na Ufuatiliaji Wako
Watu wengi hawaelewi mapenzi ya Mungu; wanafikiri kuwa kila mtu ambaye ameamuliwa na Mungu ataokolewa bila kuepuka na wanafikiri kuwa kila mtu asiyeamuliwa na Mungu hataokolewa hata wakiyafanya mambo vyema zaidi. Wanafikiri kwamba MunfNyimbogu hataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji na tabia yao. Iwapo unafikiri hivi, basi unamwelewa Mungu visivyo kabisa. Iwapo Mungu angefanya hili kweli, basi Mungu angekuwa mwenye haki? Mungu huamua matokeo ya watu kulingana na kanuni: Mwishowe matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na utendaji wao wa kibinafsi na tabia. Huoni tabia ya Mungu yenye haki, na daima unamwelewa Mungu visivyo na kugeuza nia Zake, ambayo hukufanya daima uwe bila rajua na kupoteza matumaini. Je, hili si la kujiadhibu? Kwa kweli, unaelewa kweli, na una uhakika wa nia za Mungu? Daima umetumia “Majaaliwa ya Mungu” kusawiri na kukana maneno ya Mungu. Huku ni kumuelewa Mungu visivyo kukuu! Huelewi kazi ya Mungu na huyaelewi mapenzi ya Mungu katu; hata zaidi, huelewi nia nzuri ambazo Mungu ameweka katika miaka Yake 6,000 za kazi ya usimamizi! Unakuwa na moyo wa kukata tamaa, kubahatisha na kuwa na shaka na Mungu; unaogopa kwa kina kuwa mtendaji-huduma, ukifikiri, “Hakuna jambo kuu kunihusu; mbona nimepandishwa daraja ili kuifanya kazi hii? Je, Mungu ananitumia? Je, ni kwamba Ananifanya nitoe huduma na kisha kunifukuza wakati ambapo sina faida tena?” Je, si maoni haya yanambainisha Yeye na wale walio mamlakani? Daima umemwelewa Mungu visivyo; umewaza maovu kumhusu Mungu na kumchukia. Hujawahi kuyaamini maneno ya Mungu na kusema Kwake ukweli, umeanza mwenyewe kutafuta kuwa mtendaji-huduma, umeanza mwenyewe kutembea katika njia ya watendaji-huduma, lakini hujatafuta kubadili tabia yako wala hujapitia dhiki ili kuuweka ukweli kwenye vitendo. Mwishowe, umeyasukuma majukumu yako kwa Mungu, ukisema kuwa hukuwa umejaaliwa na Mungu, na kwamba Mungu hajakuwa wazi nawe. Je, tatizo ni lipi? Unayaelewa visivyo madhumuni ya Mungu, huyaamini maneno ya Mungu, huuweki ukweli kwenye vitendo wala kujitolea unapotimiza wajibu wako. Je, unawezaje kuyaridhisha mapenzi ya Mungu? Kwa huu mwelekeo wa matendo, hujahitimu hata kidogo kuwa mtendaji-huduma, hivyo unawezaje kuhitimu kujadiliana na Mungu? Ikiwa unafikiri kuwa Mungu si mwenye haki, basi kwanini unamwamini? Daima umetaka kusikia Mungu akikuambia, “Nyinyi ni watu wa ufalme na hili halitawahi kubadilika” kabla ya hamjajitahidi kwa ajili ya familia ya Mungu. Mungu asingesema hili, basi usingepeana moyo wako wa kweli kwa Mungu. Mtu wa aina hii ni mkaidi kiasi gani! Nimewaona watu wengi ambao hawajawahi kulenga kubadilisha tabia zao, hata zaidi hawajalenga kuuweka ukweli kwenye vitendo. Wao tu hutilia maanani kuuliza ikiwa watapata hatima nzuri ya mwisho, jinsi Mungu atakavyowashughulikia, ikiwa Ana majaaliwa yao kuwa watu Wake na mambo mengine ya uvumi. Je, watu hawa ambao hawajashughulika na kazi ya kweli wanawezaje kupata uzima wa milele? Je, wanawezaje kusalia katika familia ya Mungu? Sasa Ninawaambia kwa taadhima: Mtu aliyejaaliwa na Mungu asipouweka ukweli katika vitendo, basi ataondolewa mwishowe; na mtu anayetumia rasilmali yake na kufanya vyema ili kuuweka ukweli katika vitendo—hata ikiwa watu humwona kama mtu asiyejaaliwa kusalia—atakuwa na hatima nzuri zaidi kuwaliko wale wanaoitwa watu waliojaaliwa ambao hawajakuwa na kujitolea, kwa sababu ya tabia ya Mungu yenye haki. Je, unayaamini maneno haya? Iwapo huna uwezo wa kuyaamini maneno haya na unaendela na shughuli zako kwa njia mbaya, basi Ninakuambia kuwa hutaweza kusalia, kwa sababu humtaki Mungu kwa kweli na hujauzoea ukweli. Kwa vile ni hivi, kudura ya Mungu kwa watu si ya maana. Ninasema hili kwa sababu mwishowe, Mungu ataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji wao na mienendo; hata hivyo, tukizungumza bila upendeleo, majaaliwa ya Mungu yana kazi ndogo tu na hayana umuhimu mkubwa. Je, unayaelewa maneno haya?
2. Kazi ya Mungu katika Siku za Mwisho si kwa Madhumuni ya Kuwahukumu Watu, lakini badala yake Kuwaokoa Watu
Watu wengine husema: “Asili yangu si nzuri, yaache mambo yalivyo!” Je, huna uwezo wa kuunyima mwili? Je, huna moyo na akili? Je, mnaombaje kila siku? “Mwili, toka nje! Yaache mambo yalivyo, Mungu ameujaalia; sihitaji kufanya lolote.” Je, hili ndilo ombi lako? La! Basi kwanini hufanyi kazi na Mungu? Baadhi ya watu ambao wamelifanya kosa dogo watasema: Je, nitaangushwa na Mungu? Mungu hakuja wakati huu ili kuwaangusha watu, lakini badala yake kuwaokoa watu kwa kiwango kikubwa kiwezekanacho. Je, ni nani asiyefanya makosa kabisa? Je, kila mtu akiangushwa, basi unawezaje kuitwa wokovu? Makosa mengine hufanywa kimakusudi na makosa mengine kufanywa bila kupenda. Kwa mambo ya bila kupenda, unaweza kubadilika baada ya kuyatambua, hivyo Mungu angekugonga kabla hujabadilika? Je, hivi ndivyo Mungu huwaokoa watu? Si hivyo! Bila kujali iwapo unakosea bila kupenda ama kutokana na asili ya uasi, kumbuka tu: Harakisha na uuzindukie uhalisi! Endelea kwa bidii; bila kujali ni hali gani inayotokea, lazima uendelee kwa bidii. Mungu anafanya kazi ili kuwaokoa watu na Hatawagonga watu Anaotaka kuwaokoa bila taratibu. Bila kujali kiasi chako cha mgeuzo, hata kama Mungu angekuangusha mwishowe, basi Mungu angefanya hivyo kwa uhaki; wakati huo utakapofika, Atakufanya uelewe. Sasa hivi jukumu lako la pekee ni kuendelea kwa bidii, kutafuta kubadilishwa na kutafuta kumridhisha Mungu; unapaswa kujali tu kuhusu kuutimiza wajibu wako kulingana na mapenzi ya Mungu. Hapana kosa katika hili! Mwishowe, bila kujali jinsi Mungu anavyokushughulikia, hilo daima hufanywa katika uhaki; hupaswi kushuku hili au kuwa na wasiwasi nalo; hata kama huwezi kuelewa uhaki wa Mungu hivi sasa, kutakuwa na siku ambayo utaridhishwa. Hakika Mungu si kama mkuu wa serikali ama mfalme wa ibilisi! Mkijaribu kuelewa kipengele hiki kwa makini, basi mwishowe mtaamini kwa udhabiti kuwa kazi ya Mungu ni kuwaokoa watu na kubadilisha tabia za watu. Kwa kuwa ni kazi ya kuzibadilisha tabia za watu, watu wasipofichua tabia zao, basi hakuna linaloweza kufanywa na hakutakuwa na matokeo yoyote. Lakini baada ya kufichua tabia yako, kuendelea hivyo kutakuwa kwa taabu, kutakosea amri za utawala na kumkosea Mungu. Mungu atatoa adhabu za kiasi tofauti, na utalipa gharama kwa dhambi zako. Mara chache wewe hupotoka bila kufahamu na Mungu hukuonyesha, hukupogoa, na kukushughulikia; ukifanya vyema, Mungu hatakulaumu. Hii ndio namna ya kawaida ya mgeuzo; umuhimu wa kweli wa kazi ya wokovu unajitokeza katika mchakato huu. Huu ndio ufunguo! Chukua kwa mfano mipaka kati ya wanaume na wanawake; leo unatenda kwa ajili ya raghba ya kuushika mkono wa mtu, lakini unaporudi unatafakari: Je, hii sio tabia potovu? Je, hii sio dhambi? Je, hii sio tahayari kwa Mungu wakati ambapo mipaka kati ya wanaume na wanawake hauzingatiwi? Je, ninawezaje kufanya kitu cha aina hii? Kisha unakuja mbele za Mungu na kuomba: “Ee Mungu! Nimekosa tena; jambo hili halipatani na ukweli na nauchukia mwili uliopotoka.” Baadaye, unaweka azimio la kutowashika au kuwakaribia sana. Je, huu si mgeuzo? Ikiwa una mbadiliko wa aina hii, je, Mungu bado atakuhukumu kwa kuwashika mkono? Ikiwa uliishika mikono yao na hukuhisi vyema kuhusu hilo, na usiikiri dhambi yako kwa Mungu, ukifkiri kuwa halikuwa jambo la aibu, na hujidharau, kuwa mwangalifu, ama kuwa na azimio, basi baadaye hutaishika mikono yao tu, utawakumbatia! Mambo yatakuwa mazito zaidi na zaidi na yatakupelekea kufanya dhambi, na katika kufanya hivyo, Mungu atakuhukumu kwa dhambi zako; utafanya dhambi tena na tena, haina tiba. Kama kwa kweli ungefichua sehemu ndogo ya tabia iliyopotoka pasipo kutaka, ukiweza kutubu, basi Mungu hatakuhukumu na bado unaweza kuokolewa. Mungu anataka kuwaokoa watu, na haiwezekani kwa asili za watu kutofichuliwa kwa kiasi fulani; hata hivyo, unapaswa kuzingatia kutubu na kubadilika kwa haraka. Je, hili halingeridhisha mapenzi ya Mungu? Watu wengine hawaamini haya na daima wanakuwa na mtazamo wa kujihadhari kumhusu Mungu; mtu wa aina hii atateseka siku moja.
Imetajwa hapo awali: Matukio yaliyopita yanaweza kufutwa kwa alama ya kalamu; siku za baadaye zaweza kuchukua nafasi ya yaliyopita; uvumilivu wa Mungu hauna mipaka. Lakini maneno haya yana kanuni ndani yake; si kweli kwamba bila kujali umetenda dhambi kuu kiasi gani mwishowe, Mungu anaweza kuifuta kwa alama moja; kazi yote ya Mungu ina kanuni. Zamani kulikuwa na aina hii ya amri ya utawala: Yule ambaye alifanya dhambi fulani kabla ya kulikubali jina la Mungu, mwache ajiunge; akifanya dhambi hiyo tena baada ya kuingia, mshughulikie kwa njia fulani; akirudia kufanya dhambi iyo hiyo tena, basi mfukuze. Mungu daima amewasamehe watu kwa kiwango kikubwa sana kinachowezekana katika kazi Yake; kutoka kwa mtazamo huu, inaweza kuonekana kuwa kazi hii kweli ni kazi ya kuwaokoa watu. Lakini katika hatua hii ya mwisho ukifanya dhambi isiyosameheka bado, hutaweza kuponywa ama kuweza kubadilika. Mungu ana mchakato wa kubadilisha tabia za watu na wa kuwaokoa watu. Kupitia kwa mchakato wa watu kufichua tabia zao, Mungu atawabadilisha; kupitia njia ya watu kufichua na kubadilisha tabia zao siku zote, Mungu hupata lengo Lake la wokovu. Baadhi ya watu hufikiri: Kwa kuwa ni asili yangu, basi nitaionyesha zaidi iwezekanavyo! Baadaye, nitaitambua na kuuweka ukweli kwenye vitendo. Je, huu mchakato ni wa lazima? Ikiwa kwa kweli wewe ni mtu unayeuweka ukweli kwenye vitendo, na ukiona kwamba pia una matatizo ambayo wengine wanayo, basi utafanya bidii kuepuka kuyafanya mambo hayo. Je, huu si mgeuzo usio wa moja kwa moja? Wakati mwingine, unafikiri kufanya namna ile, lakini kabla ya kufanya, unafahamu na kuiacha. Je, hili halipati matokeo ya wokovu? Kuna mchakato wa kuuweka ukweli wote kwenye vitendo; ni vigumu kwako kuwa mtimilifu na kutokuwa na mawazo ya kighushi unapoanza kutenda. Bado kuna vitu kadha ambavyo kwavyo unategemea mawazo yako mwenyewe kabisa, lakini baada ya kushughulikiwa na kupogolewa, mwishowe utatenda kulingana na nia na maneno ya Mungu kikamilifu. Haya ni mbadiliko na mgeuzo.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ijumaa, 8 Juni 2018

Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

1. Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Ndugu wawili wa kawaida, Beijing
Agosti 15, 2012
Julai 21, mwaka wa 2012 ilikuwa siku isiyosahaulika sana kwangu, pamoja na kuwa siku muhimu zaidi ya maisha yangu.
Siku hiyo, mvua kubwa ilikuwa ikinyesha katika Wilaya ya Fangshan jijini Beijing—ilikuwa kubwa kuliko yoyote iliyowahi kuonekana pale katika miaka sitini na mmoja.

Jumatano, 31 Januari 2018

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake;

Alhamisi, 25 Januari 2018

Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu

Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu

Wazazi wa Wenya walitengana alipokuwa na umri wa miaka miwili, na baada ya hapo aliishi na baba yake na mama wa kambo. Mamake wa kambo hakuweza kumvumilia na daima alikuwa akibishana na baba yake. Alikuwa na chaguo dogo — alilazimika kumpeleka Wenya nyumbani kwa mama yake, lakini mama yake alilenga kikamilifu kuendesha biashara yake na hakuwa na muda wa kumtunza Wenya, hivyo mara nyingi alipelekwa nyumbani kwa jamaa na marafiki zake kupata ulezi. Baada ya miaka mingi sana ya maisha ya kutunzwa na walezi, Wenya alihisi upweke na asiyejiweza, na alitamani ukunjufu wa nyumbani. Ni wakati tu ambapo baba yake na mama wa kambo walitangua ndoa ndipo alirudi upande wa baba yake, na kuanzia hapo na kuendelea alikuwa na nyumbani, wakati mzuri au mbaya. Mara Wenya alipokua, alikuwa mwangalifu na mtiifu sana, na alisoma kwa bidii. Lakini wakati ule ule alipokuwa akitia bidii ili kujiandaa kwa ajili ya mitihani yake ya kuingilia chuo, msiba ulimfika: mama yake alikuwa na hemoraji ya ubongo na akapooza na kuwa mgonjwa kitandani. Babake wa kambo alimtelekeza mama yake na hata kuchukua udhibiti juu ya mali yake yote, na kisha babake akapelekwa hospitalini kwa ajili ya saratani ya ini... Wenya hangeweza kabisa kujitwisha mzigo wa kaya, hivyo yote ambayo angeweza kufanya ni kuwasihi jamaa na marafiki, lakini alikataliwa. …
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki ,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.