Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yesu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yesu. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 30 Januari 2018

Kuhusu Biblia (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kuhusu Biblia (3)

Mwenyezi Mungu alisema, Sio kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote.

Jumapili, 21 Januari 2018

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki , Mwenyezi Mungu,

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Mwenyezi Mungu alisema, Katika kipindi kile ambacho Petro alikuwa na Yesu, aliona sifa nyingi za kupendeza ndani ya Yesu, hali nyingi zenye za kustahili kuigwa, na nyingi ambazo zilimkimu. Ingawa Petro aliona nafsi ya Mungu ndani ya Yesu katika njia nyingi, na kuona sifa nyingi za kupendeza, mara ya kwanza hakumjua Yesu. Petro alianza kumfuata Yesu alipokuwa na umri wa miaka 20, na akaendelea kufanya hivyo kwa miaka sita. Katika kipindi hiki cha muda, hakuwahi kupata kumjua Yesu, lakini alikuwa radhi kumfuata kutokana na kuvutiwa na Yeye tu. Wakati Yesu alipomwita kwanza kwenye ufuko wa Bahari ya Galilaya, Aliuliza: “Simioni, mwana wa Yona, je, utanifuata?” Petro akasema: “Lazima nimfuate yeye aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu. Nitakufuata.” Wakati huo, Petro alikuwa amesikia kuhusu mwanamume mmoja aliyeitwa Yesu, nabii mkubwa zaidi kuliko wote, Mwana mpendwa wa Mungu, na Petro alikuwa akitumai kila wakati kumpata, akitumai kupata fursa ya kumwona Yeye (kwa sababu hivyo ndivyo alivyoongozwa wakati huo na Roho Mtakatifu). Ingawa alikuwa hajawahi kumwona Yeye na alikuwa amesikia tu uvumi kuhusu Yeye, kwa utaratibu tamanio na kivutio cha kumwabudu Yesu vyote vikaongezeka katika moyo wake, na mara nyingi alitamani siku ile atakayomtazama Yesu. Na Yesu alimwitaje Petro? Yeye pia alikuwa amesikia habari za mwanamume aliyeitwa Petro, na si kwamba Roho Mtakatifu alimwagiza: “Nenda katika Bahari ya Galilaya, pale ambapo kunaye bwana mmoja anayeitwa Simioni, mwana wa Yona.” Yesu alimsikia mtu akisema kwamba kulikuwa na bwana mmoja aliyeitwa Simioni, mwana wa Yona, na kwamba watu walikuwa wamesikia mahubiri yake, kwamba yeye pia alihubiri injili ya ufalme wa mbinguni, na kwamba watu waliomsikiliza waliguswa kiasi cha wote kutokwa na machozi. Baada ya kusikia haya, Yesu alimfuata mtu huyu, na kuelekea kwenye Bahari ya Galilaya; wakati Petro alipoukubali mwito wa Yesu, alimfuata.
Katika kipindi hiki akimfuata Yesu, alikuwa na maoni mengi kuhusu Yeye na siku zote Alimhukumu kutokana na mtazamo wake. Ingawa alikuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa Roho Mtakatifu, Petro hakuwa ametiwa nuru sana, na haya yanaonekana katika maneno yake aliposema: “Lazima nimfuate yeye aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu.” Hakuelewa mambo yale ambayo Yesu alifanya na wala hakupata nuru yoyote. Baada ya kumfuata kwa muda fulani alivutiwa kwa kile alichofanya Yeye na kusema, na kwa Yesu Mwenyewe. Alikuja kuhisi kwamba Yesu alivutia upendo na heshima; alipenda kujihusisha na Yeye na kuwa kando Yake, na kusikiliza maneno Yake Yesu kulimpa ruzuku na msaada. Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. Aliona kwamba ingawa Yesu hakuwa na kimo kikubwa wala ubinadamu usio wa kawaida, Alikuwa na umbo la ajabu na lisilo la kawaida kwa kweli. Ingawa Petro hakuweza kuyafafanua kabisa, aliweza kuona kwamba Yesu alikuwa na mwenendo tofauti na kila mtu mwingine, kwani Aliyafanya mambo yaliyokuwa tofauti kabisa na yale yaliyofanywa na binadamu wa kawaida. Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi cha kwamba aligeuka na kuwa mwepesi na mchangamfu kama njiwa, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyeathirika na hali ya hewa. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayenguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.
Petro alikuwa ni binadamu mwenye akili, aliyekuwa na akili za asili, ilhali aliyafanya mambo mengi ya kijinga alipokuwa akimfuata Yesu. Mwanzoni kabisa, alikuwa na fikira fulani kuhusu Yesu. Aliuliza: “Watu wanasema kuwa Wewe ni nabii, kwa hiyo ulipokuwa na umri wa miaka minane na mkomavu vya kutosha kutambua mambo, je ulijua kuwa Wewe ni Mungu? Je ulijua kwamba mimba Yako ilitungwa na Roho Mtakatifu?” Yesu alijibu: “La, Sikujua! Kwani Sionekani kama mtu wa kawaida tu kwako? Mimi niko sawa na mtu yeyote mwingine yule. Yule mtu Baba hutuma ni mtu wa kawaida, na wala si mtu asiyekuwa wa kawaida. Na Ingawa kazi Ninayofanya inawakilisha Baba Yangu wa mbinguni, taswira Yangu, hulka Yangu na mwili Wangu haviwezi kuwakilisha kikamilifu Baba Yangu wa mbinguni, ni sehemu moja tu Yake. Ingawa Nilitoka kwenye Roho, Mimi Ningali mtu wa kawaida, naye Baba Yangu alinituma Mimi hapa ulimwenguni kama mtu wa kawaida, wala si mtu asiyekuwa wa kawaida.” Ni wakati tu Petro aliposikia haya ndipo alipopata ufahamu kidogo kuhusu Yesu. Na ilikuwa tu baada ya kupitia saa nyingi zisizohesabika za kazi ya Yesu, mafunzo Yake, uchungaji Wake, na ruzuku Yake, ndipo alipopata ufahamu wa kina zaidi. Katika mwaka Wake wa 30, Yesu alimwambia Petro kuhusu kusulubishwa Kwake kujako, kwamba Alikuwa amekuja kufanya kazi ya kusulubishwa ili kukomboa wanadamu wote. Alimwambia pia kwamba siku tatu baada ya kusulubishwa Kwake, Mwana wa Adamu angefufuka tena, na baada ya kufufuka Angeonekana kwa watu kwa siku 40. Petro alikuwa na huzuni baada ya kusikia maneno haya, lakini akawa karibu zaidi na Yesu huku akiathiriwa na maneno Yake.
Baada ya kushuhudia mambo haya kwa muda fulani, Petro alikuja kutambua kwamba kila kitu Yesu alichofanya kilitokana na nafsi ya Mungu, na akaja kufikiria kwamba Yesu alikuwa wa kupendeka ajabu. Pale tu alipokuja kuwa na uelewa huu ndipo Roho Mtakatifu alimtia nuru kutoka ndani yake. Kisha Yesu akawageukia wanafunzi wake na wafuasi wengine na kusema: “Yohana, wewe unasema Mimi ni nani?” Yohana akajibu: “Wewe ni Musa.” Kisha akamgeukia Luka: “Na wewe, Luka, wewe unasema Mimi ni nani?” Luka akajibu: “Wewe ndiwe mkubwa zaidi kati ya manabii.” Kisha akamwuliza mtawa: “Wewe nawe unasema Mimi ni nani?” Mtawa akajibu: “Wewe ndiwe nabii mkubwa zaidi anayeongea maneno mengi kutoka milele hadi milele. Hakuna unabii wa yeyote yule mwingine ambao ni mkubwa kama Wako, wala hekima ya yeyote yule mwingine kubwa kama Yako; Wewe ni nabii.” Kisha Yesu akamgeukia Petro na kuuliza: “Petro, wewe nawe unasema Mimi ni nani?” Petro akajibu: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Aliye hai. Unatoka mbinguni, Wewe si wa ulimwenguni, Wewe si sawa na viumbe wa Mungu. Sisi tuko ulimwenguni na Wewe u pamoja nasi hapa, lakini Wewe ni wa mbinguni, Wewe si wa ulimwengu, na Wewe si wa ulimwengu.” Ni kupitia katika uzoefu wake ndipo Roho Mtakatifu alipomtia nuru, hali iliyomwezesha kuwa na uelewa huu. Baada ya nuru hii, alivutiwa na kila kitu ambacho Yesu alikuwa amefanya hata zaidi, alimfikiria Yeye kuwa wa kupendeka hata zaidi, na siku zote alikuwa moyoni mwake asitake kutengana na Yesu. Kwa hiyo, mara ya kwanza Yesu alipojifichua kwake Petro baada ya kusulubishwa na kufufuka Petro alilia kwa furaha ya kipekee: “Bwana! Umefufuka!” Kisha, huku akilia, alimvua samaki mkubwa ajabu, akampika na kumpakulia Yesu. Yesu alitabasamu, lakini hakuongea. Ingawa Petro alijua Yesu alikuwa amefufuka, hakuelewa fumbo hilo. Alipompa Yesu samaki yule kumla, Yesu hakukataa na ilhali hakuongea wala kuketi chini kula, lakini badala yake alitoweka ghafla. Huu ulikuwa ni mshtuko wa ajabu kwake Petro, na hapo tu ndipo alipoelewa ya kwamba yule Yesu aliyefufuka alikuwa tofauti na yule Yesu wa awali. Baada ya kutambua hili, Petro alihuzunika, lakini pia akapata tulizo kwa kujua kwamba Bwana alikuwa amekamilisha kazi Yake. Alijua kwamba Yesu alikuwa amekamilisha kazi Yake, kwamba muda Wake wa kukaa na binadamu ulikuwa umeisha, na kwamba binadamu angelazimika kutembea kwa njia yake mwenyewe kuanzia hapo kuendelea. Yesu aliwahi kumwambia: “Lazima pia unywe kutoka kwenye kikombe kikali nilichonywea Mimi (hili ndilo alilomwambia baada ya kufufuka), lazima wewe pia utembee njia niliyotembea Mimi, lazima uyapoteze maisha yako kwa ajili Yangu.” Tofauti na sasa, kazi wakati huo haikuchukua mfumo wa mazungumzo ya uso kwa uso. Katika Enzi ya Neema, kazi ya Roho Mtakatifu ilikuwa fiche sana, naye Petro aliteseka katika ugumu mwingi, na wakati mwingine angefikia kiwango cha kumaka: “Mungu! Sina chochote ila maisha haya. Ingawa hayana thamani nyingi Kwako, ningependa kuyatoa Kwako. Ingawa binadamu hawastahili kukupenda, na upendo wao na mioyo yao haina thamani, naamini kwamba unaweza kuona nia iliyomo ndani ya mioyo ya binadamu. Na hata ingawa miili ya binadamu haifikii ridhaa Yako, ningependa Wewe uweze kuukubali moyo wangu.” Baada ya kutamka maombi haya angetiwa moyo, haswa wakati alipoomba: “Nitautoa moyo wangu wote kwa Mungu. Ingawa siwezi kumfanyia Mungu chochote, nitamtosheleza Mungu kwa utiifu na kujitolea Kwake kwa moyo wangu wote. Ninaamini Mungu lazima auangalie moyo wangu.” Alisema: “Siombi chochote katika maisha yangu ila fikira zangu za upendo kwa Mungu na tamanio la moyo wangu kuweza kukubaliwa na Mungu. Nilikuwa naye Bwana Yesu kwa muda mrefu, ilhali sikuwahi kumpenda Yeye, hili ndilo deni langu kubwa zaidi. Ingawa niliishi na Yeye, sikumjua, na hata nilizungumza maneno yasiyofaa kama Hayupo. Kufikiria kuhusu mambo haya kunanifanya kuhisi ni kana kwamba napaswa kumshukuru zaidi Bwana Yesu.” Siku zote aliomba kwa njia hii. Alisema: “Mimi ni duni kuliko vumbi. Siwezi kufanya chochote ila kuutoa moyo huu mtiifu kwa Mungu.”
Kulikuwepo na kilele katika yale Petro alipitia, wakati mwili wake ulikuwa karibu kunyenyekea kabisa, lakini Yesu akamtia moyo ndani. Na akajitokeza kwake mara moja. Wakati Petro alikuwa katika mateso makuu na alisikitika, Yesu alimwelekeza: “Ulikuwa na Mimi ulimwenguni, na Nilikuwa na wewe hapa. Na Ingawa awali tulikuwa pamoja mbinguni, hata hivyo, ni ya ulimwengu wa kiroho. Sasa Nimerudi katika ulimwengu wa kiroho, na wewe umo ulimwenguni. Kwani Mimi si wa ulimwengu, na Ingawa wewe pia si wa ulimwengu, lazima utimize kazi yako hapa ulimwenguni. Kwani wewe ni mtumishi, lazima uwajibike kwa njia bora zaidi uwezayo.” Petro alipata tulizo, kwa kusikia kwamba angeweza kurudi kwa upande wa Mungu. Wakati Petro alipokuwa katika masumbuko hayo kiasi kwamba karibu awe mahututi kitandani, alisikitika kiasi cha kusema hivi: “Nimepotoka kwelikweli, siwezi kumtosheleza Mungu.” Yesu alijitokeza kwake na kusema: “Petro, huenda ikawa umesahau azimio ulilowahi kutoa mbele Yangu? Je, kwa kweli umesahau kila kitu Nilichosema? Umesahau azimio ulilonitolea?” Petro aliona kwamba alikuwa Yesu na akainuka kutoka kitandani, naye Yesu akamfariji : “Mimi si wa ulimwengu, tayari Nimekuambia wewe—hili lazima uelewe, lakini umesahau kitu kingine Nilichokuambia? ‘Wewe pia si wa ulimwengu, si wa dunia.’ Sasa hivi kunayo kazi unayohitaji kufanya, huwezi kuhuzunika namna hivi, huwezi kuteseka hivi. Ingawa binadamu na Mungu hawawezi kuishi pamoja katika ulimwengu mmoja, Ninayo kazi Yangu na wewe unayo yako, na siku moja wakati kazi yako imekamilika, tutakuwa pamoja katika himaya moja, nami Nitakuongoza wewe kuwa pamoja Nami milele na milele.” Petro alipata tulizo na hakikisho baada ya kuyasikia maneno hayo. Alijua kwamba kuteseka huku kulikuwa ni jambo ambalo lazima angevumilia na kupitia, na akatiwa msukumo kuanzia hapo kuendelea. Yesu alijitokeza haswa kwake katika kila muda muhimu, akimpa nuru na mwongozo maalum, na akifanya kazi nyingi ndani yake. Na ni nini ambacho Petro alijutia zaidi? Yesu alimwuliza Petro swali jingine (ingawa haijarekodiwa katika Biblia kwa njia hii) si kipindi kirefu baadaye Petro alikuwa amesema “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu aliye hai,” nalo swali lenyewe lilikuwa: “Petro! Umewahi kunipenda?” Petro alielewa kile alichomaanisha, na kusema: “Bwana! Niliwahi kumpenda Baba wa mbinguni, lakini nakubali sijawahi kukupenda Wewe.” Yesu naye akasema: “Kama watu hawampendi Baba wa mbinguni, watawezaje kumpenda Mwana hapa ulimwenguni? Na kama watu hawampendi Mwana aliyetumwa na Mungu, Baba, wanawezaje kumpenda Baba aliye mbinguni? Kama kweli watu wanampenda Mwana aliye ulimwenguni, basi kwa kweli wanampenda Baba aliye mbinguni.” Wakati Petro alipoyasikia maneno haya aligundua upungufu wake. Siku zote alihisi huzuni hadi kiwango cha kulia kutokana na maneno yake “niliwahi kumpenda Baba wa mbinguni, lakini sikuwahi kukupenda Wewe.” Baada ya ufufuo na kupaa angani kwa Yesu alihuzunika na kuwa na simanzi zaidi kwa yale yote yaliyokuwa yamefanyika. Huku akikumbuka kazi yake iliyopita na kimo chake cha sasa, mara nyingi angekuja mbele ya Yesu kwa maombi, siku zote akiwa na hisia za majuto na masikitiko kwa kutoweza kwake kutosheleza tamanio la Mungu, na kutoweza kufikia viwango vya Mungu. Masuala haya yakawa ndiyo mzigo wake mkubwa. Alisema: “Siku moja nitatoa kila kitu nilicho nacho na kila nilicho, nitakupa kile chenye thamani zaidi.” Alisema: “Mungu! Ninayo imani moja tu na upendo mmoja tu. Maisha yangu hayana thamani, na mwili wangu hauna thamani. Ninayo imani moja tu na upendo mmoja tu. Ninayo imani kwako Wewe katika akili yangu na upendo Kwako wewe katika moyo wangu; mambo haya mawili tu ndiyo niliyonayo kukupatia Wewe, na wala sina kingine chochote.” Petro alihimizwa pakubwa na maneno yake Yesu, kwa sababu kabla ya Yesu kusulubishwa alikuwa amemwambia: “Mimi si wa ulimwengu huu, na wewe pia si wa ulimwengu huu.” Baadaye, wakati Petro alipofikia hali ya maumivu makali, Yesu alimkumbusha: “Petro, je, umesahau? Mimi si wa ulimwengu huu, na ni kwa ajili tu ya kazi Yangu ndipo Niliondoka mapema. Wewe pia si wa ulimwengu huu, umesahau? Nimekuambia mara mbili, kwani hukumbuki?” Petro alimsikia na kumwambia: “Sijasahau!” Yesu naye akasema: “Uliwahi kuwa na wakati mzuri ukiwa umekusanyika pamoja na Mimi kule mbinguni na kwa kipindi fulani kando Yangu mimi. Unanidata Mimi, na Mimi ninakudata. Ingawa viumbe hawa hawastahili kutajwa machoni Pangu, ninawezaje kukosa kupenda yule ambaye hana hatia na anapendeka? Je, umesahau ahadi Yangu? Lazima ulikubali agizo Langu hapa ulimwenguni, lazima utimize kazi Niliyokuaminia. Bila shaka siku moja Nitakuongoza kuwa kando Yangu.” Baada ya kuyasikia haya, Petro akahimizwa zaidi, na kupata msukumo mkubwa zaidi, kiasi cha kwamba alipokuwa msalabani, aliweza kusema hivi: “Mungu! Siwezi kukupenda vya kutosha! Hata ukiniomba nife, siwezi bado kukupenda vya kutosha! Popote Utakapotuma nafsi yangu, utimize au ukose kutimiza ahadi Zako, chochote ufanyacho baadaye, ninakupenda na ninakuamini.” Kile alichoshikilia kilikuwa imani yake, na upendo wa kweli.
Jioni moja, wanafunzi mbalimbali, akiwemo Petro, walikuwa kwenye mashua ya kuvulia samaki. Walikuwa pamoja naye Yesu, naye Petro akamwuliza Yesu swali la kijinga sana: “Bwana! kunalo swali ambalo nimekuwa nalo kwa muda mrefu sana ambalo ningependa kukuuliza Wewe.” Yesu akajibu: “Basi uliza tafadhali!” Petro naye akauliza: “Je, kazi iliyofanywa kwenye Enzi ya Sheria ilitokana na Wewe?” Yesu akatabasamu, kana kwamba alikuwa akisema: “Huyu mtoto, jinsi alivyo mjinga!” Kisha akaendelea kwa kusudio: “Haikuwa kazi Yangu hiyo, ilikuwa kazi ya Yehova na Musa.” Petro akasikia haya na kushangaa: “Salaale! Kwa hivyo haikuwa kazi Yako.” Punde tu Petro aliposema hayo, Yesu hakuongea tena. Petro akajiwazia: “Si Wewe uliyefanya kazi hiyo, kwa hiyo ndiyo maana umekuja kuiangamiza sheria, kwani hiyo haikuwa kazi Yako.” Moyo wake ukapata tulizo pia. Baadaye, Yesu akatambua kwamba Petro alikuwa mjinga kiasi, lakini kwa sababu hakuwa na utambuzi wowote wakati huo, Yesu hakusema chochote kingine au kumkemea waziwazi. Siku moja Yesu alihubiri kwenye sinagogi, na watu wengi walikuwepo, akiwemo Petro, ili waweze kumsikiliza akihubiri. Yesu akasema: “Yule atakayekuja kutoka milele hadi milele atafanya kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, kuwakomboa wanadamu wote kutoka kwa dhambi, lakini, hatazuiliwa na taratibu zozote katika kumwongoza binadamu nje ya dhambi. Atatembea kutoka kwa sheria na kuingia katika Enzi ya Neema. Atakomboa wanadamu wote. Atapiga hatua mbele kutoka kwa Enzi ya Sheria hadi kwa ile Enzi ya Neema, ilhali hakuna atakayemjua Yeye, Yule aliyekuja kutoka kwa Yehova. Kazi aliyofanya Musa alipewa na Yehova; Musa aliziandika sheria kwa sababu ya ile kazi ambayo Yehova alikuwa amefanya.” Baada ya kusema hili, aliendelea: “Wale watakaotupilia mbali mafundisho ya Enzi ya Neema katika Enzi ya Neema watakumbana na janga. Lazima wasimame katika hekalu na kupokea maangamizo ya Mungu, nao moto utawajia.” Baada ya Petro kumaliza kusikiliza haya, alikuwa na mwitikio wa aina fulani. Katika kipindi cha kile alichopitia, Yesu alichunga na kumtunza Petro, huku akiongea naye kwa dhati, jambo ambalo lilimpatia Petro ufahamu bora zaidi kiasi kuhusu Yesu. Wakati Petro alipokuwa akifikiria kuhusu mahubiri ya Yesu ya siku hiyo, kisha swali alilowahi kumwuliza Yesu walipokuwa kwenye mashua ya kuvua samaki nalo jibu alilopewa na Yesu, pamoja na vile alivyocheka, ndipo alipoelewa kila kitu. Baadaye, Roho Mtakatifu alimtia nuru Petro, na kupitia kwa haya tu ndipo alipoelewa kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mungu aliye hai. Ufahamu wa Petro ulitokana na kutiwa nuru na Roho Mtakatifu, lakini kulikuwepo na mchakato katika uelewa huu. Ilikuwa kupitia kwa kuuliza maswali, kusikiliza mahubiri ya Yesu, kisha kupitia kupokea ushirika maalum wa Yesu na uchungaji Wake maalum, ndipo Petro alipokuja kutambua Yesu kuwa Mwana wa Mungu Aliye hai. Haya yote hayakufikiwa usiku kucha; ulikuwa ni mchakato, na huu ukawa ni msaada kwake katika yale yote aliyopitia baadaye. Kwa nini Yesu hakufanya kazi ya kukamilisha kwa watu wengine, lakini Petro tu? Kwa sababu Petro tu ndiye aliyeelewa kwamba Yesu ndiye aliyekuwa Mwana wa Mungu aliye hai na hakuna mwingine aliyejua hili. Ingawa kulikuwa na wanafunzi wengi waliojua mengi wakati walipomfuata, maarifa yao yalikuwa ya juujuu tu. Na ndiyo maana Petro alichaguliwa na Yesu kuwa mfano wa kukamilishwa. Kile Yesu alichomwambia Petro wakati huo ndicho anachowaambia watu leo, ambao maarifa yao na kuingia kwao katika maisha lazima yafikie yale ya Petro. Ni kulingana na mahitaji haya na njia hii ndiyo Mungu atakapofanya kila mtu kuwa mkamilifu. Kwa nini watu leo wanahitajika kuwa na imani halisi na upendo wa kweli? Kile Petro alichopitia pia nyinyi lazima mpitie, yale matunda ambayo Petro alipata kutoka kwa yale aliyoyapitia pia lazima yaonyeshwe ndani yenu, na maumivu aliyoteseka Petro, nyinyi pia lazima mtayapitia kwa kweli. Njia mnayotembelea ndiyo ile ile ambayo Petro alitembelea. Maumivu mnayoteseka ndiyo maumivu ambayo Petro aliteseka. Mnapopokea utukufu na mnapoishi kwa kudhihirisha maisha halisi, basi mnaishi kwa kudhihirisha taswira ya Petro. Njia ni ileile, na kulingana na haya ndipo mtu anafanywa kuwa timilifu. Hata hivyo, ubora wa tabia wa watu wa leo kwa kiasi fulani unao upungufu ukilinganishwa na ule wa Petro, kwani nyakati zimebadilika, na ndivyo pia kiwango cha kupotoka. Na pia kwa Yudea kulikuwepo ufalme wa kipindi kirefu uliokuwa na utamaduni wa kale. Kwa hiyo lazima mjaribu kuboresha ubora wenu wa tabia.
Petro alikuwa mtu mwenye akili razini, makini kwa kila kitu alichofanya, na pia mwaminifu kupindukia. Alikumbana na vipingamizi vingi. Alikumbana na jamii akiwa na umri wa miaka 14, huku akihudhuria shule na mara nyingi akienda kwenye sinagogi. Alikuwa na shauku nyingi na siku zote alikuwa radhi kuhudhuria mikutano. Wakati huo, Yesu alikuwa hajaanza rasmi kazi Yake; huu ulikuwa ni mwanzo tu wa Enzi ya Neema. Petro alianza kukumbana na wahusika wa kidini alipokuwa na umri wa miaka 14; kufikia wakati alipokuwa na umri wa 18 aliwasiliana na wajuzi wa kidini, lakini baada ya kushuhudia machafuko ya dini yaliyotendeka kisiri, aliondoka. Kwa kuona watu hao walivyokuwa wenye hila, wajanja, na waliojaa mabishano, aliudhika kabisa (hivi ndivyo Roho Mtakatifu alivyofanya kazi wakati huo, ili kumfanya kuwa mkamilifu. Roho Mtakatifu alimsukuma haswa na akaweza kufanya kazi maalum ndani yake), na hivyo basi akaondoka kwenye sinagogi akiwa na umri wa miaka 18. Wazazi wake walimtesa na wasingemruhusu kuamini (walikuwa wa shetani, na hawakuwa na imani yoyote). Hatimaye, Petro alitoka nyumbani na kusafiri kwa mapenzi yake, huku akivua samaki na kuhubiri kwa miaka miwili, kipindi ambacho aliweza pia kuwaongoza watu wachache kiasi. Sasa unafaa uweze kuona waziwazi njia iliyochukuliwa na Petro. Kama umeiona waziwazi, basi huenda umejua kazi inayofanywa leo, kwa hiyo usingelalamika au kuwa kukaa tu, au kutamani chochote. Unafaa kupitia hali halisi aliyopitia Petro wakati huo: Alikumbwa na huzuni; hakuomba tena kuwa na mustakabali au baraka yoyote. Hakutafuta faida, furaha, umaarufu, au utajiri wa ulimwengu na alitafuta tu kuishi maisha yenye maana zaidi, ambayo yalikuwa ya kulipiza upendo wa Mungu na kujitolea kile alichokuwa nacho cha thamani zaidi kwa Mungu. Kisha angetosheka katika moyo wake. Mara nyingi aliomba kwa Yesu akitumia maneno haya: “Bwana Yesu Kristo, niliwahi kukupenda Wewe, lakini sikukupenda Wewe kwa kweli. Ingawa nilisema nina imani kwako Wewe, sikuwahi kukupenda kwa moyo wa kweli. Nilikuwa nakutazamia Wewe tu, nikikuabudu Wewe, na kukudata Wewe, lakini sikuwahi kukupenda Wewe au kuwa na imani ya kweli kwako Wewe.” Siku zote aliomba ili kutoa azimio lake, alihimizwa kila wakati na maneno Yake Yesu[a] na kuyageuza kuwa motisha. Baadaye, baada ya kipindi cha kile alichopitia, Yesu alimjaribu yeye, akimchochea kumtaka Yeye zaidi. Alisema: “Bwana Yesu Kristo! Ninakudata kweli, na kutamani kukutazamia. Ninakosa mengi mno, na siwezi kufidia upendo Wako. Ninakusihi kunichukua hivi karibuni. Utanihitaji mimi lini? Utanichukua lini? Ni lini nitakapoutazama uso Wako tena? Sitamani kuishi tena katika mwili huu, kuendelea kupotoka, na vilevile sitamani kuasi zaidi ya nilivyoasi. Niko tayari kujitolea vyote nilivyonavyo Kwako punde iwezekanavyo, na sitamani kukuhuzunisha Wewe zaidi ya hivi nilivyofanya.” Hivi ndivyo alivyoomba, lakini hakujua wakati huo kwamba Yesu angemfanya kuwa mkamilifu. Katika makali ya majaribio yake, Yesu alijitokeza kwake tena na kusema: “Petro, Ningependa kukufanya kuwa mkamilifu, ili uwe kipande cha tunda ambacho ni dhihirisho la Mimi kukukamilisha, ambacho Nitafurahia. Unaweza kweli kunishuhudia Mimi? Umefanya kile Nilichokuomba kufanya? Umeishi kwa kudhihirisha yale maneno Niliyoyaongea? Uliwahi kunipenda Mimi, lakini Ingawa ulinipenda Mimi, umeishi kwa kunidhihirisha? Ni nini ulichonifanyia Mimi? Unatambua kwamba wewe hufai upendo Wangu, lakini wewe umenifanyia nini?” Petro aliona kwamba alikuwa hajamfanyia Yesu chochote na akakumbuka kiapo cha awali cha kumpa Mungu maisha yake. Na kwa hiyo, hakulalamika tena, na maombi yake baadaye yakazidi kuwa bora zaidi. Akaomba, akisema: “Bwana Yesu Kristo! Niliwahi kukuacha Wewe, na Wewe pia uliwahi kuniacha mimi. Tumekuwa mbalimbali kwa kipindi cha muda, na muda kiasi tukiwa pia pamoja. Ilhali unanipenda mimi zaidi ya kila kitu kingine. Nimekuasi Wewe mara nyingi na nikakuhuzunisha mara nyingi. Ninawezaje kusahau mambo kama haya? Kazi uliyofanya ndani yangu mimi na kile ambacho umeniaminia nazingatia daima, sikisahau kamwe. Pamoja na kazi uliyonifanyia mimi nimejaribu kadri ya uwezo wangu. Unajua kile ninachoweza kufanya, na unajua zaidi wajibu ninaoweza kutekeleza. Nitafanya lolote utakalo na nitajitolea kila kitu nilichonacho Kwako. Wewe tu ndiwe unayejua kile ninachoweza kukufanyia Wewe. Ingawa Shetani alinidanganya sana na nikakuasi Wewe, ninaamini kwamba Hunikumbuki mimi kwa ajili ya dhambi hizo, kwamba hunichukulii mimi kutokana na hizo dhambi. Ningependa kuyatoa maisha yangu yote kwa ajili Yako wewe. Siombi chochote, na wala sina matumaini au mipango mingine; ningependa tu kuchukua hatua kulingana na nia Zako na kutimiza mapenzi Yako. Nitakunywa kutoka kwenye kikombe Chako kichungu, na mimi ni Wako wa kuamuru.”
Lazima muwe wazi kuhusu njia mnayotembelea; lazima muwe wazi kuhusu njia mtakayotumia katika siku za usoni, ni nini haswa ambacho Mungu atafanya kuwa mkamilifu na ni nini ambacho mmeaminiwa nacho. Siku moja, pengine, mtajaribiwa, na kama wakati huo mtaweza kutiwa msukumo kutoka kwa yale aliyopitia Petro, yatawaonyesha kwamba kwa kweli mnatembea njia ya Petro. Petro alipongezwa na Mungu kwa ajili ya imani na upendo wake wa kweli, na kwa ajili ya utiifu wake kwa Mungu. Na ilikuwa kutokana na uaminifu wake na kutamani kwake Mungu katika moyo wake ndiposa Mungu akamkamilisha kuwa timilifu. Kama kweli unao upendo na imani kama hiyo ya Petro, basi Yesu kwa kweli atakufanya kuwa timilifu.
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Jumatano, 17 Januari 2018

Habari kuu njema za furaha! | Drama yenye Muziki ya Sifa za Ufalme–Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki ,Ngoma za Sifa

Chini ya mbingu ya usiku yenye nyota, tulivu na kimya, kundi la Wakristo wanasubiri kwa ari kurudi kwa Mwokozi wakiimba na kucheza kwa muziki mchangamfu.Wanaposikia habari za furaha "Mungu amerejea" na "Mungu ametamka maneno mapya", wanashangaa na kusisimka.

Jumapili, 14 Januari 2018

Kwa Furaha Ukaribishe Ujio wa Mungu! | Drama yenye Muziki ya Sifa za Ufalme–Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Jina: Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo
Jamii: Drama yenye muziki
UTANGULIZI: Chini ya mbingu ya usiku yenye nyota, tulivu na kimya, kundi la Wakristo wanasubiri kwa ari kurudi kwa Mwokozi wakiimba na kucheza kwa muziki mchangamfu.Wanaposikia habari za furaha "Mungu amerejea" na "Mungu ametamka maneno mapya", wanashangaa na kusisimka. Wanafikiri: "Mungu ameonekana? Tayari ametokea?" Kwa udadisi na kutokuwa na uhakika, mmoja baada ya mwingine, wanaingia katika safari ya kuyatafuta maneno mapya ya Mungu. Katika kutafuta kwao kugumu, baadhi ya watu wanauliza maswali hali wengine wanalikubali tu. baadhi ya watu wanaangalia bila kutoa maoni, wakati wengine wanafanya mapendekezo na kutafuta majibu katika Biblia–wanaangalia lakini mwishowe kuangalia huku hakuzai matunda .... Wakati tu wanapokata tamaa, shahidi mmoja anawaletea nakala ya Biblia ya Enzi ya Ufalme, na wanavutiwa kwa kina na maneno yaliyomo katika kitabu. Hiki ni kitabu cha aina gani kweli? Je, kwa kweli wamepata maneno mapya ambayo Mungu ameyanena katika kitabu hiki? Je, wamekaribisha kwa furaha kuonekana kwa Mungu?

Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo | Msifuni Mwenyezi Mungu

1 Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na hata Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya.
2 Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote.
3 Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu; bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu itapungukiwa na mwangaza, dunia itakuwa vurugu, na wanadamu wote wataishi katika njaa na mabaa. Atawaonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima mngekuwa viongozi wa wenye dhambi na maiti milele.
4 Mnapaswa kujua kwamba bila kuwepo kwa mwili huu, wanadamu wote wangetazamia msiba usioepukika na kupata kuwa ngumu kuponyoka adhabu kali zaidi ya Mungu katika siku za mwisho. Bila kuzaliwa kwa mwili huu wa kawaida, nyinyi nyote mngekuwa katika hali ambayo uhai wala kifo havitakuja bila kujali jinsi mtakavyovitafuta; bila kuwepo kwa mwili huu, basi siku hii hamngeweza kupokea ukweli na kuja mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Badala yake, mngeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zenu zinazohuzunisha. Je, mnajua? Kama sio kwa kurudi kwa Mungu kwa mwili, hakuna ambaye angepata nafasi ya wokovu; na isipokuwa kwa kuja kwa mwili huu, Mungu angekuwa ameimaliza kitambo enzi ya zamani. Hivyo basi, mnaweza bado kuukataa kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu? Sababu mnaweza kufaidika sana kutoka kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi mbona hammkubali kwa urahisi?
5 Lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu. Kwa sababu ni Yeye aliyeleta ukweli, uhai, na njia ya kuwaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya Mungu na mwanadamu, kuleta Mungu na mwanadamu pamoja karibu zaidi na kuwasilisha mawazo kati ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye ambaye Ameleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi yenu na nyinyi kumshikilia?
“Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu”katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumatano, 10 Januari 2018

Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe

Mwenyezi Mungu alisema , Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe.

Ijumaa, 5 Januari 2018

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kanisa la Mwenyezi Mungu , Umeme wa Mashariki , Yesu, Kristo,

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Mwenyezi Mungu alisema, Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, ujaji wa Bwana Yesu kwa utukufu, kwa mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kwa kuonekana kwa ufalme, na kwa kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: Bwana anafika, na analeta maafa, na kuwazawadia walio wema na kuwaadhibu walio waovu, na Anawachukua wale wote wanaomfuata na kukaribisha kurudi Kwake angani kumlaki. Kila wakati tunapowaza kuhusu haya, hatuna budi ila kujawa na hisia. Tunashukuru kwa kuwa tulizaliwa siku za mwisho na tuna bahati ya kutosha ya kushuhudia kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, yote ni kwa ajili ya malipo ya “utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa”; hiyo ni baraka kweli! Hamu hii yote na neema inayopewa na Bwana mara kwa mara hutufanya kuingia kwenye maombi, na hutuleta pamoja mara kwa mara zaidi. Labda mwaka ujao, labda kesho, au labda hata mapema zaidi wakati mwanadamu hatarajii, Bwana atarejea ghafla, na ataonekana kati ya kundi la watu ambao wamekuwa wakimsubiri kwa umakinifu. Sote tunashindana kati yetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, ili kuwa kundi la kwanza la kutazama kuonekana kwa Bwana, na kuwa mmoja wa wale watakaonyakuliwa kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya kuwadia kwa siku hii. Baadhi yetu wameacha kazi zao, wengine wameachana na familia zao, wengine wamekana ndoa zao, na baadhi yao hata wamepeana akiba zao zote. Ni upendo usio na ubinafsi wa aina gani huu! Uaminifu na utiifu kama huu lazima uwe hata unashinda ule wa watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anampa neema yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumrehemu yeyote ambaye Yeye anataka, kujitolea kwetu na matumizi yetu, tunaamini, tayari yametazamika machoni Pake. Kwa hivyo, pia, sala zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana atatuzawadia kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu aliturehemu kabla hajauumba ulimwengu, na hakuna atakayenyakua baraka na ahadi Zake kwetu. Sote tunapanga kuhusu siku za usoni, na kupuuza kwamba kujitolea kwetu na kugharamia ni mambo tunayoweza kutumia ili kuchukuliwa kwenda mbinguni kukutana na Bwana. Kuongezea, bila kusita hata kidogo, sisi tunajiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye, tukitawala mataifa na watu wote kwa jumla, ama tunatawala kama wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu kinachotarajiwa.

Tunadharau wale wote walio kinyume na Bwana Yesu; na mwishowe, wote wataangamizwa. Nani aliwaambia wasiamini kwamba Bwana Yesu ni Mwokozi? Bila shaka, kuna nyakati ambapo tunajifunza kutoka kwa Bwana Yesu na tunakuwa na huruma kwa dunia, kwa kuwa hawaelewi, na tunapaswa kuwa wavumilivu na kuwasamehe. Kila kitu tufanyacho ni kwa mujibu wa maneno ya Biblia, kwani kila kitu ambacho hakifuatani na Biblia ni uzushi, na madhehebu maovu. Imani kama hiyo imehifadhiwa ndani sana ya akili zetu. Bwana wetu yumo katika Biblia, na tusipoondoka kwenye Biblia basi hatutaondoka kwa Bwana; tukitii kanuni hii, basi tutaokolewa. Sisi husaidiana na kuchochea kila mmoja wetu, na kila wakati tunapokusanyika pamoja ni matumaini yetu kwamba kila kitu tunachosema na kutenda kinaambatana na matakwa ya Bwana na kuwa kinaweza kukubaliwa na Bwana. Licha ya uhasama mkali ulioko kwenye mazingira yetu, mioyo yetu imejaa furaha. Tunapowaza kuhusu baraka hizi tunazoweza kupata kwa urahisi, je, kuna kitu ambacho hatuwezi kukiacha? Je, kuna kitu ambacho hatuwezi kuvumilia kutengana nacho? Yote haya ni thabiti, na haya yote yanatazamwa na macho ya Mungu. Sisi, walio wachache wa maskini ambao tumeinuliwa kutoka jaani, ni sawa na wafuasi wa Bwana Yesu wa kawaida: Tunaota kuhusu kunyakuliwa, na kubarikiwa, na kutawala mataifa yote. Upotovu wetu umeanikwa peupe machoni pa Mungu, na tamaa zetu na uchoyo zinahukumiwa machoni pa Mungu. Bado, yote haya hutokea bila ajabu kabisa, yenye mantiki sana, na hakuna hata mmoja kati yetu ambaye hushangaa kama hamu yetu ni ya haki, sembuse yeyote kati yetu ambaye anashuku usahihi wa yote yale ambayo sisi hushikilia. Nani anayeweza kujua mapenzi ya Mungu? Hatujui jinsi ya kutafuta, au kuchunguza, au hata kujishughulisha na njia ambayo mwanadamu hupitia. Kwa maana sisi hujali tu kuhusu kama tutaweza kunyakuliwa, kama tunaweza kubarikiwa, kama kuna pahali tumetengewa katika ufalme wa mbinguni, na kama sisi tutaweza kupata mgawo wa maji ya mto wa uzima na matunda ya mti wa uzima. Je, sisi hatumwamini Bwana, na je, sisi sio wafuasi wake Bwana, kwa ajili ya kupata vitu hivi? Dhambi zetu zimesamehewa, tumetubu dhambi zetu, tumekunywa kikombe cha mvinyo ambao ni mchungu, na tumeuweka msalaba migongoni mwetu. Nani anayeweza kusema kuwa gharama ambayo tumelipia haitakubalika na Bwana? Nani anayeweza kusema kuwa hatujatayarisha mafuta yanayotosha? Hatutaki kuwa wale mabikira wapumbavu, ama mmoja wa wale ambao wameachwa. Aidha, tunaomba mara nyingi, na kumwomba Bwana atuepushe kutokana na kudanganywa na Kristo wa uongo, kwa maana imeandikwa kwenye Biblia kuwa “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24:23-24). Sisi sote tumeweka mistari hii ya Biblia kwenye kumbukumbu, tunaijua vyema sana, na tunaiona kama hazina ya thamani, kama maisha, na kama vitambulisho vyetu vya wokovu wetu na kunyakuliwa kwetu …

Kwa maelfu ya miaka, wanaoishi wamefariki, wakichukua tamaa zao na ndoto zao, na hakuna anayejua kwa kweli iwapo wameenda kwa ufalme wa mbinguni. Wafu wanarudi, na wamesahau hadithi zote zilizowahi kutokea wakati mmoja, na bado wanafuata mafundisho na njia za babu zetu. Na kwa hivyo, miaka inavyopita na siku zinavyosonga, hakuna anayejua iwapo Bwana Yesu, Mungu wetu, kwa kweli hukubali yote tunayoyafanya. Tunangojea tu matokeo na kubashiri kuhusu yale yote ambayo yatatokea. Bado Mungu yu kimya siku zote, na hajawahi kutuonekania, wala kusema nasi. Na kwa hivyo, kwa hiari yetu tunahukumu mapenzi ya Mungu na tabia kwa mujibu wa Biblia na ishara. Sisi tumezoea kimya cha Mungu; tumekuwa na mazoea ya kupima usahihi na makosa ya tabia zetu kutumia njia zetu wenyewe za mawazo: tumekuwa na mazoea ya kutumia elimu yetu, dhana, na maadili yetu na kuyafanya yachukue nafasi ya matakwa ya Mungu kwetu sisi; tumekuwa na mazoea ya kufurahia neema ya Mungu; tumekuwa na mazoea ya Mungu kutoa msaada wakati sisi tunahitaji msaada huo; tumekuwa na mazoea ya kunyosha mikono yetu kwa Mungu ili tupate mambo yote, na kumuagiza Mungu; na pia tumekuwa na mazoea ya kufuata mafundisho ya dini, kutotilia maanani jinsi Roho Mtakatifu hutuongoza; zaidi ya hayo, tumekuwa na mazoea ya siku ambazo sisi ni bwana zetu wenyewe. Tunamwamini Mungu wa namna hii, ambaye hatujawahi kukutana naye. Maswali kama namna tabia Yake ilivyo, asili Yake na mali Zake ni zipi, mfano Wake ulivyo, kama tutamjua ama hatutamjua wakati Atakaporudi, na kadhalika—haya yote hayana umuhimu. Jambo muhimu ni kuwa Yeye yumo mioyoni mwetu, na kuwa tunamsubiri, na kuwa tunaweza kufikiria jinsi Alivyo. Tunathamini imani yetu, na kuthamini hali yetu ya kiroho. Tunaona kila kitu ni kama samadi, na kukanyaga vimbo vyote kwa nyayo zetu. Kwa sababu sisi ni wafuasi wa Bwana mwenye utukufu, bila kujali jinsi safari yetu ilivyo ndefu na ngumu, bila kujali shida na hatari zinazotukumba, hakuna kitu kitakachosimamisha nyayo zetu tunapomfuata Bwana. “Mto safi wa maji ya uhai, ung’aao kama kioo, uliondoka katika kiti cha Mungu cha enzi na cha Mwanakondoo. Na katika kila upande wa ule mto, ulikuwapo ule mti wa uhai unaozaa matunda ya jinsi kumi na mbili, na kuyatoa hayo matunda yake kila mwezi: na majani yake mti huu yalikuwa ya ajili ya kuyaponya mataifa. Na laana haitakuwepo tena: ila kiti cha Mungu cha enzi na cha Mwanakondoo kitakuwa ndani yake; na watumishi wake watamhudumia: Na wao wataona uso wake; nayo mapaji ya nyuso zao yatakuwa na jina lake. Na hakutakuwa na usiku pale; wala hawahitaji mshumaa, wala mwanga wa jua; kwa sababu Bwana Mungu huwapa mwanga: na wao watatawala daima na milele” (Ufunuo 22:1-5). Kila wakati sisi hukariri maneno hayo, mioyo yetu hujawa na furaha isiyo na kifani na maridhio, na machozi hutiririka kutoka machoni mwetu. Shukrani ni kwa Bwana kwa kutuchagua, shukrani ni kwa Bwana kwax neema Yake. Ametupa mara mia sasa, Yeye ametupa uzima wa milele kwa ulimwengu ujao, na kama angetuomba tufe sasa, tungetii hiyo bila kusita hata kidogo. Bwana! Tafadhali njoo hivi karibuni! Usikawie hata dakika moja tena, kwa kuwa sisi tunakutamani sana na tumeacha kila kitu kwa ajili Yako.

Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimama. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi Wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango Wake. Usimamizi Wake huendelea kimya kimya, bila madhara ya kutia shauku ilhali nyayo Zake, daima hukaribia binadamu, na kiti Chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti Chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, tukio hilo ni mandhari ya adhimu na yenye taadhima. Kama njiwa, na kama simba anayenguruma, Roho anawasili kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya akiwa na mamlaka na akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuwasili Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya mwanadamu yanabaki yalivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa kawaida, kama mfuasi asiye na maana kabisa na kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na zaidi, Ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini asiye wa maana. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu yote yanawekwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye hutilia maanani uwepo Wake, hamna aliye na mawazo yoyote ya kazi Yake, na zaidi ya hayo, hakuna mtu aliye na tuhuma yoyote kuhusu Yeye ni nani. Sisi huendelea na kazi yetu tu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi …

Kwa bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia” Kwake, na ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa sana, tunatambua kuwa hilo ni tamko la Mungu, na tunaukubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya, ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hatuwezi kuyakana. Tamko linalofuata linaweza kuwa kupitia kwangu, au kwako, ama linaweza kupitia yeye. Bila kujali ni nani, yote ni neema ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu huyo ni nani, hatufai kumwabudu, kwa kuwa bila kuzingatia chochote kingine, hawezi kuwa Mungu; hatuwezi kwa njia yoyote kumchagua mtu wa kawaida kama huyu kuwa ndiye Mungu wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika sana; Anawezaje kuwakilishwa na binadamu asiye na umuhimu hivyo? Zaidi ya hayo, sisi sote tunasubiri ujaji wa Mungu kuturudisha kwa ufalme wa mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu hivyo anawezaje kustahili kufanya kazi ngumu na muhimu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima iwe juu ya wingu jeupe, linaloonekana na wote. Huo utakuwa wa adhimu namna gani! Itakuwaje Ajifiche kwa ukimya kati ya kundi la watu wa kawaida?

Na bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu, wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa na aibu na fedheha. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anatarajia kufanya. Labda tunaweza tu kunyakuliwa baada ya kuvumilia maumivu kama hayo? Vichwani mwetu tunafanya hesabu … kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili na hutenda kazi kati yetu. Japokuwa Amekuwa pamoja nasi kwa muda mrefu, ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado hatuko tayari kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa mustakabali wetu, wala hatuna nia ya kumwaminisha mtu asiye na maana udhibiti wa mustakabali na hatima yetu. Kutoka Kwake, tunafurahia ugavi usioisha wa maji ya uhai, na kwa sababu Yake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Sisi tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Yeye bado, kwa unyenyekevu, hufanya kazi akiwa amefichwa ndani ya mwili, akionyesha sauti ya moyo Wake, akionekana kama hafahamu kukataliwa Kwake na binadamu, inavyoonekana yeye milele kusamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele kuvumilia mwanadamu kutomheshimu.

Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua baada ya hatua ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, na hukabiliwa na kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, tunakuja kufahamu mapenzi ya Mungu, tunakuja kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi tufe, na kutufanya kuzaliwa upya; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake na huba Yake; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, waliofanywa majivu na ghadhabu Yake katika macho Yake. Sisi ni wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao Yeye hufikiria kuhusu kuwapata mchana na usiku. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Yeye hujitia wasiwasi usiku na mchana kwa ajili yetu, Yeye hutulinda na kututunza usiku na mchana, na Hatuachi kamwe, na Yeye hutoa utunzaji Wake wote kwetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa maneno ya mwili huu mdogo na wa kawaida, tumefurahia ukamilifu wa Mungu, na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Ila, licha ya haya, majivuno yangali mioyoni mwetu, na sisi bado hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana nyingi sana, nyingi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambalo linaweza kunyakua nafasi ya Bwana katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum na hadhi ya huyu mwanadamu kwa kusita sana. Kama Yeye haneni kwa nguvu na kutufanya kukiri kwamba Yeye ni Mungu, basi sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu ambaye yuko karibu kuja ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu sana.

Matamshi ya mungu yanaendelea, na Yeye hutumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya tutakachofanya na kuonyesha sauti ya moyo Wake. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, na hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na sauti ya moyo ya huyu mwanadamu asiye wa ajabu. Yeye hufanya juhudi za mchwa kwa ajili yetu, anapoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na moyo Wake huvuja damu na kulia kwa ajili ya uasi na kufa ganzi kwetu. Asili kama hii na mali Zake zimeshinda za binadamu wa kawaida, na haziwezi kumilikiwa au kupatwa na yeyote aliyepotoka. Ana uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake haumilikiwi na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu wa mbinguni. Hakuna mtu ila Yeye anayeweza kumiliki mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, kutoka Kwake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu, na kuonyesha sauti ya moyo ya Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu ambayo huelekezwa kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na akaleta mbingu na nchi mpya, kazi mpya, na Ametuletea matumaini, na akamaliza maisha yetu ambayo hayakuwa dhahiri, na Akatuwezesha kikamilifu kuona njia ya wokovu. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zinapata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, si Yeye ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu. Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ameturuhusu kuishi tena, kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele. Wakati huo, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, wala hatupingi tena kazi na neno Lake, na tunasujudu, kabisa, mbele Yake. Hakuna tunachotaka ila kufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila Yake, na kulipa upendo Wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio Yake, na kushirikiana na kazi Yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile Anachotuaminia.

Kushindwa na Mungu ni kama mashindano ya kareti.

Kila neno la Mungu hugonga eneo letu la ubinadamu, na hutuacha tukiwa tumejawa na huzuni na hofu. Yeye hufichua fikra zetu, hufichua mawazo yetu, na hufichua tabia zetu potovu. Kupitia kwa yale yote sisi husema na kuyatenda, na kila wazo na fikra zetu, asili na kiini zinafichuliwa kwa neno Lake, na kutuacha na fedheha, tukitetemeka kwa hofu. Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, na hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa hadharani kabisa, na hata zaidi kuhisi tumeshawishika vikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba hatuna thamani machoni Pake, na kuwa sisi ni Shetani aishiye. Matumaini yetu yanavunjika, na kamwe hatuthubutu kumpa madai yoyote yasiyo na msingi au kumjaribu, na hata ndoto zetu hupotelea mara moja. Huu ni ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na ambao hakuna yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Kwa muda, akili zetu hukosa msimamo, na hatujui tutakavyoendelea kwa njia iliyo mbele wala hatujui jinsi ambavyo tutaendelea katika imani zetu. Inaonekana kama imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na ya kuwa hatujawahi kukutana na kufahamiana na Bwana Yesu. Kila kitu machoni petu hutushangaza, na kutufanya tuhisi ni kama tumetupwa mbali. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu kuna hasira ambayo haiwezi kufichika na pia kuna aibu. Tunajaribu kujieleza, kupata suluhisho, na, hali kadhalika, sisi hujaribu kuendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, na kujieleza kwa dhati mbele Yake. Ingawa kuna wakati mwingine ambao hatuna kiburi wala unyenyekevu kwa kutazamwa kwa nje, mioyoni mwetu tunateseka na hisia ya hasara kuliko ile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaweza kuonekana ni kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, ndani yetu tunavumilia bahari ya mateso inayopanda na kushuka. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimechukua matumaini na ndoto zetu zote, na kutuacha bila tamaa zetu kuu na kutokuwa tayari kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu na anayeweza kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kubwa kati yetu na Yeye na hakuna aliye tayari hata kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni mara ya kwanza ambapo sisi tunateseka kwa kupata pingamizi kubwa hivi na udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo. Hukumu na kuadibu Kwake zimetuwezesha kwa kweli kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia Kwake kosa la binadamu, ambazo tukilinganishwa nazo, sisi ni watu wa hadhi ya chini na najisi sana. Hukumu Yake na kuadibu zimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hataweza kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi tena katika tabia potovu kama hiyo, na zimetufanya tutamani kuacha asili kama hiyo na kiini kama hicho haraka iwezekanavyo, na kutochukiwa tena Naye wala tusimchafue moyo. Hukumu na kuadibu kwake zimetufanya tufurahie kutii maneno Yake, na hatumo tayari tena kwenda kinyume na matayarisho na mipangilio Yake. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kutafuta uzima, na zimetuwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu ... Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, tumetoka kuzimu, tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti.… Mwenyezi Mungu ametupata, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na kuwashinda adui Zake zote!

Sisi ni kundi la watu wa kawaida tu waliomilikiwa na tabia potovu ya kishetani, sisi ndio watu waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na sisi ndio maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati tulipomkataa na kumshutumu Mungu, ila sasa tumeshindwa na Yeye. Tumepokea uzima na kupokea njia ya uzima wa milele kutoka kwa Mungu. Bila kujali mahali ambapo tupo hapa duniani, licha ya mateso na dhiki, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu pekee!

Upendo wa Mungu unaenea mbele kama maji ya chemichemi, na unapewa wewe, na mimi pia, na kwake, na kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli kwa kweli na kungoja kuonekana kwa Mungu.

Kama vile mwezi hufuata jua daima, kazi ya Mungu haikomi kamwe, na inatekelezwa kwako, kwangu, kwake, na kwa wale wote ambao hufuata nyayo za Mungu na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu.

Ilielezewa Machi 23, 2010
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumanne, 12 Desemba 2017

Umuhimu na Mazoezi ya Sala | Maneno ya Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Jesus praying at Gethsemane

Sura ya 34. Umuhimu na Mazoezi ya Sala | Maneno ya Mwenyezi Mungu

Je, mnaomba vipi kwa sasa? Ni maendeleo kwa sala za kidini jinsi gani? Mnaelewa nini hasa kuhusu umuhimu wa sala? Je mmechunguza maswali haya? Kila mtu ambaye hafanyi sala ako mbali na Mungu, kila mtu ambaye hasali anafuata mapenzi yake; Kukosekana kwa sala kunaashiria kwenda mbali na Mungu na usaliti wa Mungu. Ni nini uzoefu wenu hasa na sala? Sasa hivi, kazi ya Mungu tayari inakaribia mwisho na uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu unaweza kuonekana kutoka kwa maombi ya mwanadamu.

Ijumaa, 8 Desemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Ubinadamu Wote Umeendelea Hadi Siku ya Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Wafaa Kujua Namna Ambavyo Ubinadamu Wote Umeendelea Hadi Siku ya Leo

Mwenyezi Mungu alisema, Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya ubinadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova hakuwa amepanga bado awamu ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; awamu ya pili ya kazi, ile ya neema; au awamu ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kuanzia hapa Angeweza kushinda ulimwengu mzima.