Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo unabii-wa-Biblia. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo unabii-wa-Biblia. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 7 Januari 2019

Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

9. Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; na atatufunza kuhusu njia zake, nasi tutatembea kwa njia zake: kwani sheria itatoka Zayuni, na neno la Mungu litatoka Yerusalemu. Naye atahukumu miongoni mwa mataifa, na atawakemea watu wengi: nao wata, nao watafua panga zao ili ziwe majembe, na mikuki yao ili iwe mundu: hakuna taifa litakaloinua upanga dhidi ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena. Enyi wa nyumba ya Yakobo, njooni, tutembee katika nuru ya Yehova" (ISA 2:2-5).
Maneno Husika ya Mungu:
Ujio wa Mungu katika mwili wa siku za mwisho umehitimisha Enzi ya Neema. Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, kutumia maneno ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, kumwangazia na kumpa nuru mwanadamu, na kumwondoa Mungu asiye yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii sio hatua ya kazi ambayo Yesu Aliifanya Alipokuja. Yesu Alipokuja, Alifanya miujiza mingi, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alifanya kazi ya wokovu ya msalaba. Na matokeo yake ni kwamba, katika dhana za mwanadamu, mwanadamu anaamini kwamba hivi ndivyo Mungu Anapaswa kuwa. Maana Yesu Alipokuja, hakufanya kazi ya kuondoa taswira ya Mungu asiye yakini moyoni mwa mwanadamu; Alipokuja, Alisulubishwa, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni. Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho.
kutoka kwa "Kuijua Kazi ya Mungu Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni leo tu, Nikujapo binafsi miongoni mwa mwanadamu na kuongea maneno Yangu, ndipo mwanadamu anapata maarifa kidogo kunihusu, kutoa nafasi "Yangu" ndani ya mawazo yao, badala yake kutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya fahamu zake. Mwanadamu ana dhana na amejawa na udadisi; ni nani ambaye hangetaka kumwona Mungu? Ni nani ambaye hangetamani kukutana na Mungu? Lakini bado kitu pekee kilicho na nafasi ya uhakika ndani ya moyo wa mwanadamu ni Mungu ambaye mwanadamu anahisi kuwa dhahania na asiye dhahiri. Nani angetambua haya kama Singewaeleza wazi? Nani angeamini kwa kweli Mimi nipo? Kwa hakika bila shaka yoyote? Kuna tofauti kubwa kati ya "Mimi" aliye ndani ya mwanadamu na "Mimi" wa ukweli, na hakuna anayeweza kuwalinganisha. Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi Nijua, na hata angekuja kunijua, je, maarifa kama hayo bado hayangekuwa dhana? …
… Kwa sababu mwanadamu amejaribiwa na kupotoshwa na Shetani, kwa sababu amechukuliwa na kufikiria kwa dhana, Nimekuwa mwili ili kuwashinda binafsi wanadamu wote, kufichua dhana zote za mwanadamu, na kupasua mawazo ya mwanadamu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu hajionyeshi mbele Yangu tena, na hanitumikii tena akitumia dhana zake mwenyewe, na hivyo, "Mimi" katika dhana za mwanadamu ameondoka kabisa.
kutoka kwa "Tamko la Kumi na Moja" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika ujenzi wa ufalme Ninatenda moja kwa moja katika hali ya uungu Wangu, na kuruhusu watu wote kujua kile Nilicho nacho na nilicho nimejiweka msingi juu ya maarifa ya maneno Yangu, hatimaye kuwaruhusu kupata ufahamu Wangu Mimi Niliye katika mwili. Hivyo hukomesha harakati zote za wanadamu kutafuta Mungu asiye dhahiri, na hukomesha nafasi ya "Mungu mbinguni" katika moyo wa mwanadamu, ambayo ni kusema, unaruhusu mwanadamu kujua matendo Yangu katika mwili Wangu, na hivyo unahitimisha wakati Wangu duniani.
kutoka kwa "Tamko la Nane" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha silika zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza inapaswa iondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanahitajika kutupilia mbali silika yao iliyopotoka, kwanza wanapaswa kujua silika yao iliyopotoka. Ikiwa mwanadamu anafanya kazi ili kuondoa taswira za Miungu wasio dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu wasio dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kuwekwa hadharani, kutupwa, au kufukuzwa kabisa kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu ndiyo inayoweza kuchukua nafasi ya vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza ili kuwaruhusu watu kuvielewa taratibu, na ni kwa njia hii pekee ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. Mwanadamu anatambua kwamba Mungu aliyekuwa anamtafuta huko nyuma ni asiye dhahiri na wa kimiujiza. Kile ambacho kinaweza kufanikiwa hapa sio uongozi wa moja kwa moja wa Roho, na wala sio mafundisho ya mtu fulani, bali ni Mungu mwenye mwili. Mitazamo ya mwanadamu inakuwa wazi pale ambapo Mungu mwenye mwili atafanya kazi Yake rasmi, kwa sababu ukawaida na uhalisi wa Mungu mwenye mwili ni kinyume na nadharia za Mungu asiye dhahiri na wa kufikirika katika fikra za mwanadamu. Mitazamo asilia ya mwanadamu inaweza tu kudhihirishwa kupitia tofauti zao na Mungu mwenye mwili. Bila ulinganisho na Mungu mwenye mwili, mitazamo ya mwanadamu isingefunuliwa; kwa maneno mengine, bila tofauti ya uhalisi vitu visivyo dhahiri visingefunuliwa. Hakuna anayeweza kutumia maneno ili kufanya kazi hii, na hakuna anayeweza kuizungumzia kazi hii kwa kutumia maneno. Ni Mungu Mwenyewe Pekee Ndiye anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni pevu kiasi gani, hawezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza kumjua Mungu zaidi kwa matendo, na anaweza kumwona kwa uwazi ziadi, ikiwa Mungu anafanya kazi miongoni mwanadamu na anaonyesha kikamilifu sura Yake na uungu Wake. Athari hizi haziwezi kupatwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili. Bila shaka, Roho wa Mungu pia hawezi kupata matokeo haya.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili wake, wale wanaofuata wanakuwa hawatafuti tena vitu hivyo visivyo yakini, na wanaacha kukisia mapenzi ya Munguasiye yakini. ... Mwanadamu hawezi kumgusa Roho, na wala hawezi kumwona, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Hata hivyo picha anazozijenga mwanadamu kumhusu Mungu, sio halisi na haziwezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; silika ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigizwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekena na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye Yeye binafsi anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia halisi ambayo Mungu anaonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwangalia Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wote watakapokuwa na ufahamu mkubwa zaidi kuhusu Mimi baada ya kukubali matamshi Yangu ni wakati ambapo watu Wangu kuishi kulingana na Mimi, ni wakati ambapo kazi Yangu katika mwili imekamilika, na wakati ambapo uungu Wangu unaishi kwa kudhihirishwa kabisa katika mwili. Wakati huu, watu wote watajaribu kunijua Mimi katika mwili, na kweli wataweza kusema kwamba Mungu huonekana katika mwili, na hili litakuwa ndilo tunda. ... Hatimaye, watu wa Mungu wataweza kumpatia Mungu sifa ambayo ni ya kweli, si ya kulazimishwa, na ambayo inatoka mioyoni mwao. Hiki ndicho kipo katika kiini cha mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000. Yaani, ni udhihirisho wa mpango huu wa usimamizi wa miaka 6,000: kuwafanya watu wote kujua umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu—kuwafanya kumjua Mungu kupata mwili kwa vitendo, ambayo ni kusema, matendo ya Mungu katika mwili—ili kwamba wamkane Mungu asiye yakini, na kumjua Mungu ambaye ni wa leo na pia wa jana, na zaidi ya hilo, Mungu wa kesho, ambaye kwa kweli Ameishi toka milele hadi milele. Ni baada ya hapo tu, ndipo Mungu ataingia pumzikoni!
kutoka kwa "Ufafanuzi wa Tamko la Tatu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kitu kizuri kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ya kusihi, na mapenzi Yake kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwa na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambayo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya matendo zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, anamfunulia mwamadamu Mungu ambaye ni halisia na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili badala ya Roho wa Mungu.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa maelfu ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu, Atabadilisha namna wanavyomfahamu na mitazamo yao Kwake, ili kwamba maarifa yao juu ya Mungu, yaweze kuanza katika rekodi safi, na mioyo yao itakuwa imesafishwa upya na kubadilishwa. Kushughulika na nidhamu ni njia, na ushindi na kufanya upya ni malengo. Kuondoa mawazo ya kishirikina aliyonayo mwanadamu kuhusu Mungu asiye dhahiri ndilo limekuwa kusudi la Mungu milele, na hivi karibuni limekuwa suala la haraka kwake. Ni matumaini Yangu kwamba watu wote watalifikiria hili zaidi.
kutoka kwa "Kazi na Kuingia (7)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kimsingi, Ujio wa Mungu katika mwili ni kuwawezesha watu kuona matendo halisi ya Mungu, kumfanya Roho asiye na umbo kuwa bayana katika mwili, na kuwapa watu fursa ya kumwona na kumgusa. Kwa njia hii, wanaokamilishwa Naye wataishi kwa kumfuata Yeye, watamfaidi na kuupendeza moyo Wake. Mungu angalinena kutoka mbinguni tu, na hakika asije duniani, basi bado watu hawangeweza kumjua, wangeweza tu kuyahubiri matendo ya Mungu kwa kutumia nadharia tupu, na hawangekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Mungu amekuja duniani kimsingi kuwa mfano na kielelezo kwa wale ambao wamepatwa na Mungu; ni kwa njia hii pekee ndio watu wanaweza kumjua Mungu kwa hakika, na kumgusa Mungu, na kumwona, na hapo ndipo wanaweza kupatikana na Mungu kwa kweli.
kutoka kwa "Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwanadamu atakuwa hana asili ya kutenda dhambi baada ya kusafishwa, kwa sababu Mungu atakuwa amemshinda Shetani, ambayo ina maana kuwa hakutakuwepo na kuvamiwa na vikosi vya uhasama, na hakuna vikosi vya uhasama ambavyo vinaweza kushambulia mwili wa mwanadamu. Na kwa hivyo mwanadamu atakuwa huru, na mtakatifu—yeye atakuwa ameingia ahera. Ni kama tu vikosi vya uhasama wa giza vitakuwa vimefungwa ndipo mwanadamu atakuwa huru kokote aendako, na bila uasi au upinzani. Shetani ni sharti awe amefungwa ili mwanadamu awe sawa; leo, hayuko sawa kwa sababu[a] Shetani bado huchochea shida kila mahali hapa duniani, na kwa sababu kazi nzima ya usimamizi wa Mungu bado haijafika mwisho wake. Punde tu shetani anaposhindwa, mwanadamu atakuwa amekombolewa kikamilifu; wakati mwanadamu anampata Mungu na anatoka katika kumilikiwa na Shetani, atatazama jua ya haki. Maisha atakayolipwa mwanadamu wa kawaida yatarejeshwa; yote yale ambayo ni lazima yamilikiwe na mwanadamu wa kawaida—kama uwezo wa kupambanua mema na mabaya, na kufahamu jinsi ya kula na kujivisha mwenyewe, na uwezo wa kuishi kama kawaida—yote haya yatarejeshwa. Hata kama Hawa hakuwa amejaribiwa na nyoka, mwanadamu ni lazima angekuwa na maisha kama haya ambayo ni ya kawaida baada ya kuumbwa hapo mwanzo. Ni lazima angekula, angevishwa, na kuendelea na maisha ya mwanadamu wa kawaida hapa duniani. Ila baada ya mwanadamu kupotoshwa, maisha haya yakakuwa ndoto, na hata leo mwanadamu hathubutu kufikiri mambo kama haya. Kwa kweli, maisha haya ya kupendeza ambayo mwanadamu anatamani ni haja yake: Iwapo mwanadamu angekuwa hana hatima kama hii, basi maisha yake ya duniani yaliyopotoshwa kamwe hayangekoma, na kama hakungekuwepo na maisha yakupendeza kama haya, basi hakungekuwa na hitimisho la majaliwa ya Shetani au kwa enzi ambayo Shetani ana utawala duniani kote. Mwanadamu ni sharti awasili kwenye ufalme ambao huwezi kufikiwa na nguvu za giza, na wakati atawasili, hii itathibitisha ya kwamba Shetani amekwisha shindwa. Kwa njia hii, punde tu hakuna usumbufu wa Shetani, Mungu mwenyewe atamdhibiti mwanadamu, na Yeye ataamuru na kudhibiti maisha yote ya mwanadamu; hii tu ndiyo itahesabika kama kushindwa kwa Shetani.
kutoka kwa "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kufuatia kukamilika kwa maneno Yangu, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata tena maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu. Naenda Nikipitia dunia nzima, Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika Wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na kamwe hakuna tena anayenung’unika kuwa ana shida Kwangu.
kutoka kwa "Tamko la Ishirini" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati ambapo watu wote watakuwa wamefanywa kamili na mataifa yote ya dunia kugeuka kuwa ufalme wa Kristo, basi huo utakuwa wakati ambapo radi saba zitanguruma. Siku ya sasa ni hatua ndefu ya kwenda mbele katika mwelekeo wa hatua hiyo, shambulio limeachiliwa huru kwa muda ujao. Huu ni mpango wa Mungu—hivi karibuni utafanikishwa. Hata hivyo, Mungu tayari amefanikisha yote ambayo Amesema. Hivyo, ni dhahiri kwamba mataifa ya dunia ni makasri tu yaliyo mchangani yanayotetemeka bamvua linapokaribia: Siku ya mwisho iko karibu sana na joka kubwa jekundu litaanguka chini ya neno la Mungu. Ili kuhakikisha kwamba mpango wa Mungu unatekelezwa kwa ufanisi, malaika wa mbinguni wameshuka juu ya dunia, wakifanya kila wanaloweza kumridhisha Mungu. Mungu Mwenyewe mwenye mwili Amejipanga katika uwanja wa vita kupigana na adui. Po pote ambapo Aliyepata mwili huonekana, adui anaangamiziwa mahali hapo. Uchina ni ya kwanza kuangamizwa, kuharibiwa kabisa kwa mkono wa Mungu. Mungu haipi Uchina upande wowote kabisa. Thibitisho la kuendelea kuanguka kwa joka kubwa jekundu linaweza kuonekana katika ukomavu wa watu unaoendelea. Hili linaweza kuonekana wazi na mtu yeyote. Ukomavu wa watu ni ishara ya kifo cha adui. Huu ni ufafanuzi kidogo wa kile kinachomaanishwa na "kufanya vita."
kutoka kwa "Ufafanuzi wa Tamko la Kumi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi hii lazima itekelezwe kwa njia ya Mungu kusababisha mabaa mbalimbali duniani. Lakini Mungu hataonekana; kwa sababu, wakati huu, nchi ya joka kubwa jekundu bado itakuwa ni nchi ya uchafu, Mungu hataonekana, lakini ataibuka tu kwa njia ya kuadibu. Hiyo ndiyo tabia ya Mungu yenye haki, na hakuna anayeweza kuiepuka. Katika wakati huu, vyote vinavyoishi katika taifa la joka kubwa jekundu vitapitia maafa, ambavyo kwa kawaida ni pamoja na ufalme ulio duniani (kanisa). Huu ndio hasa wakati ambao ukweli hujitokeza, na kwa hiyo unapitiwa na watu wote, na hakuna anayeweza kuepuka. Hili limejaaliwa na Mungu. Ni kwa sababu ya hatua hii ya kazi hasa ndio Mungu asema, "Huu ndio wakati wa mtu kutumia vizuri sana vipaji vyake." Kwa sababu, katika siku za baadaye, hakutakuwa na kanisa duniani, na kwa ajili ya majilio ya machafuko, watu hawawezi kufikiria kuhusu kitu chochote kingine, na ni vigumu kwao kumfurahia Mungu katikati ya machafuko, hivyo, watu wanatakiwa kumpenda Mungu kwa moyo wao wote katika wakati huu wa ajabu, ili wasikose nafasi. Ukweli huu unapopita, Mungu amelishinda kabisa joka kubwa jekundu, na hivyo kazi ya ushuhuda wa watu wa Mungu imefika mwisho; baadaye Mungu ataanza hatua inayofuata ya kazi, Akifanya uharibifu kwa nchi ya joka kubwa jekundu, na hatimaye kuwagongomelea watu juu chini msalabani kotekote katika ulimwengu, baadaye Atawaangamiza wanadamu wote—hizi ni hatua za siku za baadaye za kazi ya Mungu.
kutoka kwa "Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Mbili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Nichukuapo kirasmi mamlaka Yangu na kutawala kama Mfalme katika ufalme, watu Wangu wote watakamilishwa na Mimi baada ya muda. Wakati mataifa yote ya dunia yatavurugwa, hapo ndipo hasa ufalme Wangu utaanzishwa na kupata umbo na pia Nitabadilika na kurejea kwa ulimwengu mzima. Wakati huo, watu wote watauona uso Wangu tukufu, watauona uso Wangu wa kweli.
kutoka kwa "Tamko la Kumi na Nne" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikipitisha wazi amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayeyakiuka:
Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa viwango tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Ubinadamu wote utafuata aina yake, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.
kutoka kwa "Tamko la Ishirini na Sita" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumapili, 30 Desemba 2018

Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

1. Bwana Yesu Mwenyewe alitabiri ya kwamba Mungu angepata mwili katika siku za mwisho na kuonekana kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi.

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja" (LK. 12:40).
"Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki" (LK. 17:24-25).
"Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha" (MT. 25:6).
"Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na mimi" (UFU. 3:20).
"Tazama, mimi nakuja kama mwizi. Amebarikiwa yeye anayekesha, na kuzihifadhi nguo zake, asije akatembea uchi, na wao waione haya yake" (UFU. 16:15).
"Na nikapinduka ili kuiona sauti hiyo iliyonizungumzia. Na baada ya kupinduka, nikatazama vinara saba vya taa vilivyokuwa vya dhahabu; Na hapo katikati ya hivyo vinara saba vya taa nilimwona mtu aliyefanana na Mwana wa Adamu, aliyekuwa amevalia nguo iliyofika katika miguu yake, na kifuani alikuwa amefungwa kanda ya dhahabu. Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye" (UFU. 1:12-16).
Maneno Husika ya Mungu:
Yesu alisema kwamba Angewasili kama Alivyoondoka, lakini unajua maana halisi ya maneno Yake? Je, angeweza kwa kweli kukwambia? Unajua tu kwamba Atawasili kama Alivyoondoka juu ya wingu, lakini unajua hasa jinsi Mungu Mwenyewe hufanya kazi Yake? Ikiwa ungeweza kuona kweli, basi maneno ya Yesu yanapaswa kuelezwa vipi? Alisema, "Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika siku za mwisho, Yeye Mwenyewe hatajua, malaika hawatajua, wajumbe wa mbinguni hawatajua, na watu wote hawatajua. Baba tu ndiye atakayejua, yaani, Roho pekee ndiye atajua." Ikiwa una uwezo wa kujua na kuona, basi haya si maneno matupu? Hata Mwana wa Adamu Mwenyewe hajui, lakini wewe unaweza kuona na kujua? Ikiwa umeona na macho yako mwenyewe, je, maneno hayo hayakusemwa bure? Na Yesu alisema nini wakati huo? "Lakini kuhusu siku ile na saa ile hakuna mwanadamu aijuaye, hata malaika wa mbinguni, ila Baba yangu peke yake. Lakini kama vile zilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kuja kwake Mwana wa Adamu kutakavyokuwa. ... Basi ninyi pia muwe tayari: kwani katika saa msiyofikiria Mwana wa Adamu atakuja." Wakati siku hiyo itakapofika, Mwana wa Adamu Mwenyewe hataijua. Mwana wa Adamu inahusu umbo la Mungu lililopata mwili wa Mungu, ambaye atakuwa mtu wa kawaida. Hata Yeye mwenyewe hajui, kwa hiyo wewe ungejuaje?
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuna wale ambao husema kwamba Mungu mwenyewe Alisema kuwa Atawasili kwa wingu. Ni ukweli kuwa Mungu mwenyewe Alisema hivyo, lakini, je, wajua kuwa siri za Mungu haziwezi kueleweka na mwanadamu? Je, unajua kuwa maneno ya Mungu hayawezi kuelezwa na mwanadamu? Na wewe una hakika kuwa ulipewa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu? Je, Roho Mtakatifu Alikuonyesha moja kwa moja kwa namna hii? Je, haya ni maelekezo ya Roho Mtakatifu, au ni dhana zako? Walisema, "Haya yalisemwa na Mungu mwenyewe." Lakini hatuwezi kutumia dhana zetu na akili zetu kupima maneno ya Mungu. Na kuhusu maneno ya Isaya, je, unaweza kueleza maneno yake kwa kujiamini kikamilifu? Je, wewe unathubutu kueleza maneno yake? Kwa sababu huthubutu kueleza maneno ya Isaya, mbona unathubutu kueleza maneno ya Yesu? Nani ameinuliwa kuliko mwingine, Yesu au Isaya? Kwa vile jibu ni Yesu, kwa nini unaeleza maneno yaliyosemwa na Yesu? Je, Mungu Angeweza kukwambia kuhusu kazi yake mapema? Hakuna kiumbe kinachoweza kufahamu, wala hata wajumbe walio mbinguni, wala hata Mwana wa Adamu, kwa hivyo wewe ungejuaje?
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho anasema kwa makanisa." … Kuna wanadamu wajinga wanaoamini kwamba maneno ya Roho Mtakatifu yanapaswa kuja chini kutoka mbinguni hadi kwa masikio ya mwanadamu. Yeyote anayefikiria hivi hajui kazi ya Mungu. Kwa kweli, matamshi yaliyosemwa na Roho Mtakatifu ni yale yaliyosemwa na Mungu aliyekuwa mwili. Roho Mtakatifu hawezi kuongea moja kwa moja na mwanadamu, na Yehova hakuongea moja kwa moja na watu, hata kwa Enzi ya Sheria. Si ungekuwa uwezekano wa chini zaidi kwamba Angefanya hivyo kwa enzi ya leo? Kwa Mungu kunena matamshi ili kutekeleza kazi, lazima Awe mwili, la sivyo kazi yake haiwezi kukamilisha malengo Yake. Wanaomkataa Mungu ni wale wasiojua Roho ama kanuni ambazo Mungu hufanya kazi.
kutoka kwa "Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani kuweza kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamengoja na kumtamani kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, ili Yesu Mwokozi Arudi kwa watu ambao wamekuwa mbali Naye kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumaini kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atasamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Wanatamani Yesu Mwokozi Awe Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi Ambaye Anapendeka, wa kirafiki na heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu Aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa na neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi Anawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea ghafla kwa Yesu Kristo, kutimiza maneno ya Yesu Akiwa duniani: "Nitarejea tu jinsi Nilivyoondoka." Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu Alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kulia wa Yule Aliye Juu. Vilevile, mwanadamu anatazamia kuwa Yesu Atashuka, tena juu ya wingu jeupe (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu Alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kuwa Atachukua mwonekano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atafadhili chakula kwa sababu yao, na kufanya maji ya uzima kuwamwagika kwa ajili yao, na Ataishi miongoni mwa wanadamu, Akiwa amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na wa hakika. Na mengine. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya haya; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alikuwa anatazamia. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, na hakutokea kwa wanadamu wote Akitumia wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, na kubaki mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Yake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote ambayo Yeye ni), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu hafahamu haya: Ingawa Mwokozi Mtakatifu Yesu Amejawa na upendo na mapenzi kwa mwanadamu, Atafanya kazi vipi katika "hekalu" ambalo limejaa uchafu na roho wasio safi? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Atawaonekania vipi wale wanaokula mwili wa wale wasio na haki, kunywa damu ya wasio na haki, kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini lakini hawamfahamu, na wanaompokonya kila wakati? Mwanadamu anajua tu kuwa Yesu Mwokozi Amejawa na upendo na huruma, na ni sadaka ya dhambi iliyojawa na ukombozi. Lakini mwanadamu hana habari kwamba Yeye pia ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, utukufu, ghadhabu, na hukumu, na kuwa na mamlaka na kujawa na hadhi. Kwa hivyo ingawa mwanadamu anayo hamu na kutamani kurudi kwa Mkombozi, na hata Mbingu inaguswa na maombi ya mwanadamu, Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.
kutoka kwa "Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimamishwa. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango wake. Usimamizi wake huendelea kimya kimya, bila madhara ilhali nyayo zake, daima hukaribia binadamu, na kiti chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, yaani, tukio hilo ni uwakilishaji wa mandhari kwa makini na wa kuonyesha Mungu ni mkuu. Kama njiwa na kama simba anayenguruma, Roho anawasili kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya, na huwasili na mamlaka akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuja Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya mwanadamu inabaki ilivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa kawaida, kama mfuasi asiye na maana na pia kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na vile vile, ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini wa kawaida asiye na maana.
kutoka kwa "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu Amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu Alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, bado hakuna mtu yeyote aliyejua. Hata leo hii, hakuna mtu anayetambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua. Haijalishi ni kwa kiwango kikubwa kiasi gani Roho Mtakatifu Anafanya kazi, siku zote Mungu yupo katika hali ya utulivu, kamwe Hajiachilii mbali. Mtu anaweza kusema kwamba inaonekana kama hatua hii ya kazi Yake inafanyika mbinguni. Ingawa ipo wazi kabisa kwa kila mtu, hakuna anayeitambua. Mungu Atakapomaliza hatua hii ya kazi Yake, kila mtu atazinduka kutoka katika ndoto yake na kugeuza mitazamo yao ya zamani[1]. … Wakati wa mapambazuko, bila kujulikana kwa mtu yeyote, Mungu Alikuja duniani na Akaanza maisha Yake katika mwili. Watu hawakujua kipindi hiki. Pengine wote walikuwa wamelala, pengine wengi waliokuwa wanakesha walikuwa wanasubiri, na pengine wengi walikuwa wanamwomba Mungu wa mbinguni kimyakimya. Lakini miongoni mwa watu hawa wote, hakuna hata mmoja aliyejua kuwa Mungu tayari Amekwishawasili duniani. Mungu Alifanya hivi ili Aifanye kazi Yake kwa urahisi na kupata matokeo bora zaidi, na pia ilikuwa ni kwa sababu ya kuepuka majaribu zaidi. Mwanadamu anapoamka kutoka usingizini, kazi ya Mungu itakuwa imekwishakamilika zamani sana na Ataondoka, na kufunga maisha Yake ya kutembeatembea na kusafiri duniani.
kutoka kwa "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiyo anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, liyevaa vazi lililofika kwa miguu, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti Yake kama sauti ya maji mengi. Ana nyota saba katika mkono Wake wa kuume, upanga wenye makali kuwili uko katika kinywa Chake na uso Wake ni kama jua liking'aa kwa nguvu zake!
kutoka kwa "Tamko la Kumi na Tano" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni asili ya watu ambayo itaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia raha ya ulimwengu wa mbinguni, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupata ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, kisha mnazikiri, wakati baada ya mwingine? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?
kutoka kwa "Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kiwango ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, kizazi cha malaika mkuu, kiwango ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeitwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Itaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna uashirio wa ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo kutakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatiao la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba "Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo" watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Anashughulika nao tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wamejaa kiburi. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na msimkufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndio mtapata kufaidika.
kutoka kwa "Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni matumaini yangu kuwa ndugu wanaotafuta kuonekana kwa Mungu hawatarudia tanzia ya kihistoria. Hampaswi kuwa Mafarisayo wa wakati huu na kumsulubisha Mungu msalabani tena. Mnafaa kufikiria kwa makini jinsi ya kukaribisha kurudi kwa Mungu, na kuwa na mawazo dhahiri ya jinsi ya kuwa mtu anayetii ukweli. Hili ni jukumu la kila mtu anayengoja Yesu arudi na mawingu. Tunafaa kufumbua macho yetu ya kiroho, na tusiwe waathiriwa wa maneno yaliyojaa mambo ya kufurahisha macho. Tunafaa kuwaza juu ya kazi ya Mungu ya matendo, na tunafaa kuangalia upande wa hakika wa Mungu. Msijisahau ama kupotelea ndotoni, mkitazamia daima ile siku ambayo Yesu atashuka kwa ghafla juu ya mawingu kuwachukua nyinyi ambao hamjawahi kumjua wala kumwona Yeye, na msiojua kutenda mapenzi Yake. Ni vyema kufikiri juu ya mambo ya kiutendaji!
kutoka kwa "Dibaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Alhamisi, 15 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unajua Nini Kuhusu Imani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unajua Nini Kuhusu Imani?

Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamumwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo. Kwani kazi Ninayoifanya ni yake binadamu kunijia Mimi na kunijia Mimi, wala si kwa binadamu kuvutiwa na kuniangalia Mimi kwa njia mpya kwa sababu ya kazi Yangu. Awali Nilijionyesha katika ishara na maajabu mengi na kufanya miujiza mingi. Waisraeli wakati huo waliniangalia Mimi kwa tamanio kuu na walistahi pakubwa uwezo Wangu wa kipekee wa kuponya wagonjwa na kupunga mapepo. Wakati huo, Wayahudi walifikiri nguvu Zangu za uponyaji zilikuwa za kistadi na zisizo za kawaida. Kwa matendo Yangu mengi kama hayo, wote walinichukulia Mimi kwa heshima; waliweza kuhisi tamanio kuu katika nguvu Zangu zote. Kwa hiyo yeyote aliyeniona Mimi nikifanya miujiza alinifuatilia Mimi kwa karibu kiasi kwamba maelfu ya watu walinizunguka ili kunitazama nikiwaponya wagonjwa. Nilionyesha ishara na maajabu mengi, ilhali binadamu alinichukulia Mimi kama daktari stadi; Niliongea maneno mengi ya mafunzo kwa watu hao wakati huo, ilhali wote walinichukulia Mimi tu kama mwalimu aliyekuwa na mamlaka zaidi kwa wanafunzi wake! Hadi siku ya leo, baada ya binadamu kuona rekodi za kihistoria za kazi Yangu, ufasiri wao unaendelea kuwa kwamba Mimi ni daktari mkuu anayeponya wagonjwa na mwalimu kwa wasiojua. Na wameniita Mimi Bwana Yesu Kristo Mwenye huruma. Wale wanaofasiri maandiko huenda walizidi mbinu Zangu katika uponyaji, au huenda pengine wakawa wanafunzi ambao tayari wamempita mwalimu wao, ilhali binadamu kama hao wanaofahamika sana ambao majina yao yanajulikana kote ulimwenguni wananichukulia Mimi kwa kiwango cha chini sana cha kuwa daktari tu! Matendo Yangu ni mengi zaidi kwa kuhesabiwa kuliko chembechembe za changarawe kwenye ufuo na hekima Yangu kubwa zaidi kuliko ile ya watoto wote wa kiume wa Suleimani, ilhali binadamu wanafikiria kwamba Mimi ni daktari tu asiye na mengi kumhusu na mwalimu wa binadamu asiyejulikana! Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupata uponyaji? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu niweze kutumia nguvu Zangu kupunga roho chafu kutoka kwenye miili yao? Na ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu waweze kupokea amani na furaha kutoka Kwangu? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili kuhitaji kutoka Kwangu utajiri mwingi zaidi wa dunia, na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuishi maisha hayo kwa usalama na kuwa salama salimini katika maisha yajayo? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuepuka tu mateso ya kuzimu na kupokea baraka za mbinguni? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili wapate tulizo lakini hawatafuti kupata chochote kutoka kwa ulimwengu ujao? Niliposhushia hasira Zangu binadamu na kuchukua furaha na amani yote aliyokuwa nayo mwanzo, binadamu akaanza kuwa na shaka. Nilipomkabidhi binadamu mateso ya kuzimu na kuchukua tena baraka za mbinguni, aibu ya binadamu iligeuka na kuwa hasira. Wakati binadamu aliponiomba Mimi kumponya, bado Sikumtambua na vilevile nilimchukia pakubwa, binadamu alienda mbali sana na Mimi na akatafuta njia za waganga na wachawi. Nilipochukua kila kitu ambacho binadamu alitaka kutoka Kwangu, kisha kila kitu kilitoweka bila kuonekana tena. Kwa hivyo, Ninasema kwamba binadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata. Wayahudi waliniamini Mimi kwa neema Yangu, na wakanifuata Mimi popote Nilipoenda. Binadamu hawa wasiojua wenye maarifa na uzoefu finyu walitafuta tu kuona ishara na maajabu ambayo nilionyesha. Walinichukulia Mimi kuwa mkuu wa nyumba ya Wayahudi ambaye angeweza kutekeleza miujiza mikubwa zaidi. Kwa hivyo, Nilipopunga mapepo kutoka kwa binadamu walijizungumzia miongoni mwao kwa mkanganyo mkubwa wakisema Mimi ni Eliya, kwamba Mimi ni Musa, kwamba Mimi ndimi nabii wa kale zaidi kati ya wote, kwamba Mimi ndimi daktari mkuu zaidi kuliko wote. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Mimi ndimi maisha, njia na ukweli, hakuna yeyote angejua uwepo Wangu au utambulisho Wangu. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba mbingu ndipo ambapo Baba Yangu anapoishi, hakuna aliyejua kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu, na tena Mungu Mwenyewe. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Nitaleta ukombozi kwa wanadamu wote na kulipia mwanadamu fidia, hakuna aliyejua Mimi ni Mkombozi wa mwanadamu; binadamu alinijua tu Mimi kama mtu mkarimu na mwenye huruma. Na mbali na Mimi Mwenyewe kuweza kufafanua kila kitu kuhusu Mimi, hakuna aliyeweza kunitambua Mimi, hakuna aliyeamini kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai. Binadamu pia anayo imani kama hii Kwangu Mimi, na ananidanganya Mimi kwa njia hii. Binadamu anawezaje kunitolea Mimi ushuhuda wakati anayo mitazamo kama hii kunihusu Mimi?
Binadamu anayo imani Kwangu Mimi lakini hawezi kunitolea ushuhuda Mimi; kabla ya Mimi Mwenyewe kujitambulisha, binadamu hawezi kunitolea ushuhuda Mimi. Binadamu anaona tu kwamba Mimi ninazidi viumbe na binadamu wote wengine watakatifu, na anaona kwamba kazi ninayofanya haiwezi kufanywa na binadamu wengine. Kwa hivyo, kuanzia kwaWayahudi hadi kwa binadamu wa siku ya leo, yeyote ambaye ameyaona matendo Yangu yenye utukufu anajawa tu na uchu wa kudadisi mengi kuhusu Mimi, ilhali hakuna kinywa cha kiumbe kimoja ambacho kingeweza kunitolea ushuhuda. Baba Yangu tu ndiye Aliyenitolea ushuhuda Mimi; Alinitengenezea njia Mimi miongoni mwa viumbe vyote. Kwani, haijalishi ni namna gani Nilivyofanya kazi, binadamu asingewahi kujua Mimi ndimi Bwana wa viumbe, binadamu anajua tu kuchukua, na hajui kuwa na imani ndani Yangu Mimi kwa sababu ya kazi Yangu Mimi. Binadamu ananijua Mimi tu kwa sababu Mimi sina hatia wala si mtenda dhambi kwa vyovyote vile, kwa sababu Ninaweza kufafanua mafumbo mengi, kwa sababu Mimi niko juu ya wengine wote, au kwa sababu binadamu amefaidi pakubwa kutoka Kwangu. Ilhali wachache ndio wanaoamini kwamba Mimi ndimi Bwana wa viumbe. Hii ndiyo maana Ninasema ya kwamba binadamu hajui ni kwa nini anayo imani Kwangu mimi; hajui kusudio au umuhimu wa kuwa na imani Kwangu mimi. Uhalisia wa binadamu umekosekana, kiasi cha kwamba karibu hana thamani tena ya kuweza kunitolea ushuhuda Mimi. Unayo imani ya kweli ndogo sana na umefaidi kidogo sana, kwa hivyo una ushuhuda mdogo. Aidha, unaelewa mambo machache sana na unapungukiwa na mambo mengi sana kiasi kwamba hufai kushuhudia matendo Yangu. Azimio lako kwa hakika linaeleweka, lakini je una hakika kwamba utaweza kunitolea ushuhuda kwa ufanisi kuhusu hali halisi ya Mungu? Kile ambacho umepitia na kuona kinazidi kile ambacho watakatifu na manabii wengine wa awali walivyoshuhudia, lakini je unaweza kutoa ushuhuda mkubwa zaidi kuliko maneno ya hawa watakatifu na manabii waliotangulia? Kile Ninachokupa wewe sasa kinazidi kile Nilichompa Musa na ni kikubwa zaidi kuliko kile nilichompa Daudi, kwa hivyo vilevile Ninakuomba ushuhuda wako uzidi ule wa Musa na kwamba maneno yako yawe makubwa zaidi kuliko yale ya Daudi. Ninakupa vyote hivi mara mia moja, kwa hivyo vilevile ninakuomba nawe unilipe tena vivyo hivyo. Lazima ujue kwamba Mimi Ndimi ninayempa maisha mwanadamu, na kwamba wewe ndiwe unayepokea maisha kutoka Kwangu na lazima unitolee ushuhuda Mimi. Huu ndio wajibu wako, ambao Ninashusha kwako na ambao unastahili kunifanyia Mimi. Nimekupa utukufu Wangu wote, na kukupatia maisha ambayo watu wateule, Waisraeli, hawakuwahi kupokea. Bila kukosea, unastahili kunitolea ushuhuda, na kuutoa ujana wako kwa ajili Yangu na kuyatoa maisha yako. Yeyote yule ninayempa Mimi utukufu Wangu ataweza kunitolea Mimi ushuhuda na kunipatia maisha yake. Haya yote yametabiriwa mapema. Ni utajiri wako wewe ambao Ninawekea utukufu Wangu kwako wewe na wajibu wako ni kuutolea ushuhuda utukufu Wangu. Kama unaniamini tu Mimi ili kupata utajiri, basi kazi Yangu haitakuwa yenye umuhimu, na hutakuwa unatimiza wajibu wako. Waisraeli waliona tu huruma Yangu, upendo Wangu na ukubwa Wangu nao Wayahudi walitoa tu ushuhuda wa subira Yangu na ukombozi Wangu. Waliona kazi kidogo sana ya Roho Yangu; huenda ikawa kwamba kiwango chao cha uelewa kilikuwa sehemu ndogo sana ya ile ambayo wewe umesikia na kuona. Kile ulichoona kinazidi hata kile ambacho makuhani wakuu waliona miongoni mwao. Siku hii, ukweli ambao umeelewa umezidi wao; kile ambacho umeona siku hii kinazidi kile kilichoonwa kwenye Enzi ya Sheria pamoja na Enzi ya Neema na kile ambacho umepitia kinazidi hata kile ambacho Musa na Eliya walipitia. Kile ambacho Waisraeli walielewa kilikuwa tu sheria ya Yehova na kile ambacho waliona kilikuwa tu ni mgongo wake Yehova; kile ambacho Wayahudi walielewa kilikuwa tu ukombozi wa Yesu, kile walichopokea kilikuwa neema waliyowekewa na Yesu, na kile walichoona kilikuwa ni taswira ya Yesu ndani ya nyumba ya Wayahudi. Kile utakachoona siku hii ni utukufu wa Yehova, ukombozi wa Yesu na matendo Yangu yote ya siku hii. Umesikia pia maneno ya Roho Yangu, hekima Yangu teule, na ukaja kujua kuhusu maajabu Yangu, na umeweza kujifunza kuhusu tabia Yangu. Nimeweza pia kukuambia kuhusu mpango Wangu wa usimamizi. Kile ambacho umeona si tu Mungu mwenye upendo na huruma, lakini yule aliyejawa na haki. Umeiona kazi Yangu ya maajabu na kujua kwamba Nimejawa na hasira na adhama. Aidha, umejua kwamba Niliwahi kuzishusha hasira Zangu katika nyumba ya Israeli, na kwamba leo hii, umeshushiwa wewe. Umeelewa zaidi kuhusu mafumbo Yangu kule mbinguni kuliko vile alivyoelewa Isaya pamoja na Yohana; unajua zaidi kuhusu uzuri Wangu na kustahiwa Kwangu kuliko watakatifu wote wa vizazi viilivyotangulia. Kile ulichopokea si ukweli Wangu tu, njia Yangu, maisha Yangu, lakini maono na ufunuo ambavyo ni vikubwa zaidi kuliko vile vya Yohana. Umeelewa mafumbo mengine mengi zaidi na pia umeona sura Yangu kamili; umekubali mengi kuhusu hukumu Yangu na tabia Yangu ya haki. Kwa hivyo, ingawaje ulizaliwa kwenye siku za mwisho, uelewa wako ni ule wa siku za awali na za kale; umeweza pia kupitia ni nini kilichomo kwenye siku hii, na kile kilichotimizwa na mkono Wangu. Kile Ninachokuomba kinawezekana, kwani kile Nilichokupa ni kingi mno na ni mengi ambayo umeona Kwangu mimi. Kwa hivyo, Ninakuomba kunishuhudia Mimi kama vile watakatifu wa awali walivyofanya na hili ndilo tamanio tu la moyo Wangu.
Ni Baba Yangu ambaye amekuwa akinishuhudia Mimi, lakini Natafuta kupokea utukufu mkubwa zaidi na kwa maneno ya ushuhuda kutoka kwenye vinywa vya viumbe. Kwa hiyo Ninakupa kila kitu chote Changu kwa kusudi la wewe kuweza kutimiza wajibu wako na kuhitimisha kazi Yangu miongoni mwa binadamu. Unastahili kuelewa ni kwa nini una imani Kwangu Mimi. Ukinifuata Mimi tu ili uwe mwanafunzi Wangu au mgonjwa Wangu, au kuwa mojawapo wa watakatifu Wangu mbinguni, basi jitihada zako zitakuwa bure. Kunifuata Mimi kwa njia kama hiyo ni sawa tu na kuharibu jitihada zako; kuwa na imani kama hiyo Kwangu mimi ni kuishi tu ukiharibu siku zako na kutomakinikia ujana wako. Na mwisho hutapokea chochote. Huku si ni kufanya kazi bure? Ni muda mrefu tangu Nimetoka miongoni mwa Wayahudi na mimi si daktari tena wa binadamu au dawa ya binadamu. Mimi si mnyama tena wa kumbebea mizigo binadamu ili aniendeshe au kunichinja akipenda; badala yake Nimekuja miongoni mwa binadamu ili kuhukumu na kuadibu binadamu, na kwa binadamu kunijua Mimi. Unafaa kujua kwamba Niliwahi kufanya kazi ya ukombozi; Niliwahi kuwa Yesu, lakini Nisingebakia kuwa Yesu milele, licha ya kwamba Niliwahi kuwa Yehova lakini baadaye nikawa Yesu. Mimi ndimi Mungu wa mwanadamu, Bwana wa viumbe, lakini Siwezi kubakia Yesu milele au kubakia Yehova milele. Nimekuwa kile ambacho binadamu aliona ni daktari, lakini haiwezi kusemekana kwamba Mungu ni daktari tu wa mwanadamu. Kwa hiyo kama utakuwa na mtazamo huo wa kale katika imani yako Kwangu mimi, basi hutapata chochote. Haijalishi ni vipi utakavyonisifu siku hii: “Tazama Mungu alivyo na upendo kwa binadamu; Ananiponya mimi na kunipa baraka, amani na furaha. Ni vipi ambavyo Mungu atakavyokuwa mzuri kwa binadamu; kama tutakuwa na imani tu Kwake Yeye, basi hatutahitajika kuwa na wasiwasi wa pesa na utajiri…,” Siwezi bado kutatiza kazi Yangu asilia. Kama utaniamini Mimi siku hii, utapokea tu utukufu Wangu na kustahili kunitolea ushuhuda, na kila kitu kingine kitafuata. Hili lazima ulijue wazi.
Sasa unajua kweli ni kwa nini unaniamini Mimi? Kweli unajua kusudi na umuhimu wa kazi Yangu? Kweli unajua wajibu wako? Kweli unaujua ushuhuda Wangu? Kama unaniamini Mimi tu, ilhali si utukufu Wangu wala ushuhuda Wangu vinaweza kuonekana ndani yako, basi Nimekutupa nje kitambo kirefu. Kwa wale wanaoona wanajua kila kitu, wao ni miiba zaidi katika macho Yangu, na katika nyumba Yangu, wao ni vizuizi tu Kwangu. Wao ndio magugu yanayopaswa kupepetwa kabisa na kuondolewa kwenye kazi Yangu, bila ya jitihada hata kidogo na bila ya uzito wowote; Nimevichukia kitambo kirefu. Na kwa wale bila ya ushuhuda, hasira Yangu siku zote iko juu yao, na kiboko Changu hakijawahi kutoka kwao. Kitambo kirefu Nimewakabidhi kwenye mikono ya yule mwovu, na hawana tena baraka Zangu zozote. Na siku hiyo ikifika, adhabu yao itakuwa mbaya zaidi kuliko ile ya wanawake wajinga. Sasa hivi Ninafanya kazi ile ambayo ndiyo wajibu Wangu kufanya; Nitakusanya pamoja ngano yote, pamoja na magugu. Hii ndiyo kazi Yangu sasa. Magugu haya yataweza kupepetwa na kuondolewa wakati wa kupepeta Kwangu, kisha nafaka za ngano zitakusanywa kwenye ghala, na magugu ambayo yatakuwa yamepepetwa yatawekwa motoni na kuchomwa hadi kugeuka jivu. Kazi Yangu sasa ni kuwaweka tu binadamu wote kwa pamoja, yani, kuweza kuwashinda wote kabisa. Kisha Nitaanza upepetaji wa kufichua mwisho wa binadamu wote. Kwa hiyo unastahili kujua namna ya kunitosheleza Mimi sasa na namna unavyostahili kuwa kwenye njia iliyo sawa katika imani yako Kwangu. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako. Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. Wajibu wa imani Yako Kwangu mimi ni kunishuhudia Mimi, kuwa mwaminifu Kwangu mimi na si mwengine yeyote, na kuwa mtiifu hadi mwisho. Kabla Sijaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu, utawezaje kunishuhudia Mimi? Utawezaje kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi? Je, unajitolea uaminifu wako wote katika utendakazi au utakata tamaa tu? Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa? Ninakuadibu ili uweze kunishuhudia Mimi, na kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi. Pia, kuadibu huku kwa sasa kunalenga katika kufichua hatua inayofuata ya kazi Yangu na kuruhusu kazi hiyo kuendelea bila kutatizwa. Hivyo basi Nakushawishi wewe kuwa mwenye hekima na kutochukulia maisha yako au umuhimu wa kuwepo kwako kuwa ule ambao hauna manufaa kamwe. Unaweza kujua haswa kazi Yangu ijayo itakuwa ipi? Je, unajua namna Nitakavyofanya kazi katika siku zijazo na namna ambavyo kazi Yangu itakavyobadilika? Unafaa kujua umuhimu wa kile ambacho umepitia katika kazi Yangu, na zaidi, umuhimu wa imani yako Kwangu mimi. Nimefanya mengi kweli; iweje Nikate tamaa Nikiwa katikati kama unavyofikiria? Nimefanya kazi kubwa kweli; ninawezaje kuiharibu? Kwa hakika, Nimekuja kuhitimisha enzi hii. Hii ni kweli, lakini zaidi, lazima ujue kwamba Ninafaa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na, zaidi ya yote, kueneza injili ya ufalme. Kwa hivyo unafaa kujua kwamba kazi ya sasa inalenga katika kuanzisha tu enzi mpya, na kuweka msingi wa kueneza injili na kuihitimisha enzi ya sasa katika wakati ujao. Kazi Yangu si rahisi sana kama unavyofikiria, wala si kwamba haina manufaa au maana kama unavyoweza kutaka kuamini. Kwa hivyo, Ninakuambia kama awali: Unastahili kujitolea maisha Yako katika kazi Yangu, na zaidi, unastahili kujitolea wewe mwenyewe katika utukufu Wangu. Aidha, wewe kunishuhudia ndicho kile kitu ambacho Nimetamani kwa muda mrefu, na kingine ambacho Nimetamani hata zaidi ni wewe kueneza injili Yangu. Unastahili kuelewa kile kilichomo ndani ya moyo Wangu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.

Jumatano, 7 Novemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo; lazima mle na mnywe maneno Yangu zaidi na, muhimu zaidi, lazima mweze kuyala na kuyanywa nyinyi wenyewe. Jiandaeni wenyewe na ukweli wote, njooni mbele Yangu ili nifungue macho yenu ya kiroho na kuwaruhusu kuona siri zote zilizo rohoni.... Wakati kanisa linaingia awamu yake ya ujenzi, vita vya watakatifu dhidi ya Shetani[a] vinaanza. Vipengele mbalimbali vya Shetani vya kutisha Vinawekwa mbele yenu; je, mnaacha na kurudi nyuma au mnainuka na kuendelea mkinitegemea Mimi? Weka hadharani vipengele vya Shetani vyenye upotovu na viovu, bila hisia wala huruma! Pambana na Shetani hadi kifo! Mimi ni msaada wenu na ni lazima muwe na roho ya mwana wa kiume! Shetani yuko katika hekaheka zake za kifo cha mwisho lakini bado hataweza kuhepa hukumu Yangu. Shetani yuko chini ya miguu Yangu na pia anakanyagwa chini ya miguu yenu—ni ukweli!
Wale wapinga dini wote na wale ambao hubomoa ujenzi wa kanisa hawafai kuvumiliwa hata kidogo na nitawahukumu mara moja. Weka Shetani hadharani, mkanyagie chini ya miguu, muangamize kabisa na usimuachie pa kujificha. Kila aina ya mapepo na vizuka hakika wataonyesha maumbile yao ya kweli mbele Yangu na Nitawatupa wote kuzimu ambamo hawatawahi kuwa huru; wote wako chini ya miguu yetu. Kama unataka kupigana vita vizuri kwa ajili ya ukweli, basi kwanza kabisa, usimpe Shetani nafasi ya kufanya kazi, na ili kufanya hivi mtastahili kuwa na nia moja na muweze kutumika katika kushirikiana, acheni dhana zenu za kibinafsi, maoni, mitazamo na njia za kufanya mambo, tuliza moyo wako ndani Yangu, zingatia sauti ya Roho Mtakatifu, kuwa makini na kazi ya Roho Mtakatifu na uwe na uzoefu wa maneno ya Mungu kwa kina. Lazima uwe na nia moja tu, ambayo ni kwamba mapenzi Yangu yaweze kutendeka. Hupaswi kuwa na nia nyingine. Lazima uangalie Kwangu kwa moyo wako wote, angalia hatua Zangu na Ninavyotenda mambo kwa karibu, na wala usiwe mzembe kabisa. Roho yako lazima iwe amilifu, macho yako yakiwa wazi. Kwa kawaida, wale ambao nia na malengo yao si sahihi, wale ambao wanapenda kuonekana na wengine, wenye hamu ya kutenda mambo, wenye tabia ya kukatiza, walio imara katika mafundisho ya dini, watumishi wa Shetani, nk., watu hawa wanapoinuka wanakuwa ugumu kwa kanisa na kula na kunywa kwa ndugu kunakuwa si kitu; unapompata mtu wa aina hii jifanye kisha mpige marufuku mara moja. Kama muda baada ya muda hawabadiliki basi watateseka sana. Kama wale wanaoendelea katika njia zao kwa ukaidi wanajitetea na kujaribu kufunika dhambi zao, kanisa linapaswa kuwaondoa mara moja na kutowaachia nafasi ya kuendelea. Usipoteze mengi kwa kujaribu kuokoa machache, na uzingatie makubwa.
Macho yako ya kiroho lazima sasa yafunguke, na kutofautisha aina kadhaa za watu kanisani:
Je, ni mtu wa ina gani anaelewa masuala ya kiroho na anajua roho?
Je, ni mtu wa ina gani haelewi masuala ya kiroho?
Je, ni mtu wa ina gani ana roho waovu ndani yake?
Je, ni mtu wa ina gani ana Shetani anafanya kazi juu yake?
Je, ni mtu wa ina gani ambaye ana tabia ya kukatiza?
Je, ni mtu wa ina gani ambaye Roho Mtakatifu anatenda kazi kwake?
Je, ni mtu wa ina gani huonyesha kuzingatia kuelekea mzigo wa Mungu?
Je, ni mtu wa ina gani anaweza kutenda mapenzi Yangu?
Je, ni nani shahidi Wangu mwaminifu?
Jua ya kwamba nuru ambayo Roho mtakatifu hupatia makanisa yote ni maono ya leo ya juu zaidi. Msichanganyikiwe kuhusu mambo haya, lakini badala yake lazima mchukuwe muda wa kuyafikiria kabisa—hii ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya maisha yenu! Kama huelewi mambo haya yaliyo machoni pako basi hutakuwa na uwezo wa kusonga mbele, utakuwa katika hatari ya majaribu na ufungwa wakati wowote, na huenda ukavamiwa. Jambo kuu sasa ni kuzingatia kuweza kuwa karibu na Mimi moyoni mwako, kufanya ushirika zaidi na Mimi, na chochote unachokosa au kutafuta utafidiwa kupitia kuwa karibu na Mimi na kufanya ushirika na Mimi. Maisha yako hakika yatashughulikiwa na utakuwa na nuru mpya. Mimi kamwe siangalii jinsi mlikuwa wajinga awali na siyakumbuki makosa yenu. Mimi huangalia jinsi mnavyonipenda: Je, mnaweza kunipenda zaidi ya mambo mengine yote? Naangalia kuona iwapo mnaweza kugeuka nyuma na kunitegemea kuondoa ujinga wenu au la. Baadhi ya watu husimama Kwangu, kunipinga hadharani, na kuhukumu watu wengine; hawajui maneno Yangu, na hata uwezekano wao wa kuona uso Wangu uko chini. Wote wale walio mbele Yangu ambao hunifuata kwa dhati, ambao wana mioyo yenye njaa na kiu cha haki, Nitawapa nuru, kuwafichulia, kuwaruhusu kuniona kwa macho yenu na kugusa mapenzi Yangu wenyewe; hakika moyo Wangu utafichuliwa kwenu, ili mpate kuelewa. Lazima muweze kutenda yale ambayo naangaza ndani yenu kulingana na maneno Yangu, vinginevyo mtahukumiwa. Fuata mapenzi Yangu na hamtapotea
Kwa wote wale wanaotafuta kuingia ndani ya maneno Yangu, neema na baraka vitaongezeka mara mbili juu yenu, mtapata nuru mpya kila siku, ufahamu mpya kila siku na kujisikia mpya katika kula na kunywa maneno Yangu kila siku; utayaonja kwa kinywa chako mwenyewe: Ni tamu jinsi gani! … Lazima uwe makini, na usitosheke unapokuwa na ufahamu kiasi na ladha kiasi ya utamu—cha msingi ni kuendelea kutafuta mbele! Baadhi ya watu hufikiria ya kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kweli ajabu na halisi—huyu kweli ni mtu wa Mwenyezi Mungu anafichuliwa wazi, na ishara na maajabu kubwa zaidi viko mbele. Kuwa makini na macho wakati wote, angalia kabisa kwenye chanzo, kuwa mtulivu mbele Yangu, zingatia na usikilize kwa makini, na kuwa na uhakika kuhusu maneno Yangu. Haiwezekani kuwa na utata; kama una shaka hata kidogo basi Nina hofu kuwa utapotea zaidi ya malango. Kuwa na maono wazi, simama kwenye sakafu ngumu, fuata mkondo huu wa maisha na uufuate popote ufikapo; usisite hata kidogo kabisa. Kula, kunywa na kutoa sifa tu, tafuta kwa moyo mtakatifu na usikate tamaa. Leta chochote usichokielewa mbele Yangu zaidi na hakikisha usiwe na moyo wa mashaka ili uepuke kupata hasara kubwa. Endelea! Endelea! Kaa karibu! Jikwamue kutoka kwa vizuizi na usijichafue. Endelea kwa moyo wote na usirudi nyuma. Lazima utoe moyo wako wakati wote na kamwe usiwahi kuupoteze muda wowote. Roho Mtakatifu daima ana kazi mpya ya kutenda, hutenda mambo mapya na ana nuru mpya kila siku; “kugeuka sura mlimani”—mwili mtakatifu wa kiroho wa Mungu umeonekana! Jua lenye haki hutoa nuru na huangaza, mataifa yote na watu wote wameona uso Wako mtakatifu. Nuru Yangu itaangaza juu ya wale wote wanaokuja mbele Yangu. Maneno yangu ni nuru, yakiwaongoza mbele. Hamtageuka kushoto au kulia mnapotembea lakini mtatembea ndani ya nuru Yangu, na kukimbia kwenu hakutakuwa kazi isiyo na matunda. Lazima muone kazi ya Roho Mtakatifu kwa uwazi na mapenzi Yangu yako pale ndani yake. Siri zote zimefichwa na zitafunuliwa kwenu hatua kwa hatua. Wekeni maneno Yangu akilini wakati wote na mje mbele Yangu kufanya ushirika zaidi na Mimi. Kazi ya Roho Mtakatifu huendelea. Tembeeni katika nyayo Zangu; maajabu makuu yako mbele na yatafunuliwa kwenu moja baada ya lingine. Ni wale tu ambao wanajali, wanaosubiri na ambao wako macho watayaona. Hakikisha usiwe mlegevu. Mpango wa usimamizi wa Mungu unakaribia hatua yake ya mwisho, ujenzi wa kanisa utafanikiwa, idadi ya washindi tayari imewekwa, mwana wa kiume mshindi atafanyika na wataingia katika ufalme na Mimi, kuchukua ufalme Nami, kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kuwa katika utukufu pamoja!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatano, 10 Oktoba 2018

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (1) - Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia?

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (1) - Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia?

Watu wengi katika ulimwengu wa kidini hufuata unabii unaosema kwamba Bwana atashuka akiwa juu ya wingu na wanamsubiria Yeye kuja kwa njia hiyo kisha kuwanyakua hadi kwenye ufalme wa mbinguni, lakini wanapuuza unabii mbalimbali wa Bwana kuhusu kuja kwa siri: "Tazama, mimi nakuja kama mwizi" (Ufunuo 16:15). "Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha" (Mathayo 25:6). Hivyo unabii huu mbalimbali wa kurudi kwa Bwana unatimizwa vipi? Na tunafaa kuwa vipi wanawali wenye hekima ambao wanakaribisha kurudi kwa Bwana?
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, unabii wa Biblia

Ijumaa, 10 Agosti 2018

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (3) - Ili Kuchunguza Kurudi kwa Bwana Tunapaswa Kusikiliza Sauti ya Mungu


Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (3) - Ili Kuchunguza Kurudi kwa Bwana Tunapaswa Kusikiliza Sauti ya Mungu

Kimsingi unabii wote uliotajwa katika Biblia kuhusiana na kurudi kwa Bwana tayari umetokea. Watu wengi wamehisi kwamba Bwana tayari amerudi, hivyo, tunapaswa kuchunguza vipi ili kuhakikisha kuhusu suala la ikiwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi au la? Tunapaswa kufanya uamuzi wetu kulingana na unabii wa Biblia au tunapaswa kuchunguza moja kwa moja neno na kazi ya Mwenyezi Mungu? Tunapaswa kuchukua fursa hii adimu sana na kujadiliana kurudi kwa Bwana wetu vipi? Mwenyezi Mungu anasema, "Unachopaswa kufanya ni kukubali, bila haja ya kuthibitisha zaidi kutoka kwa Biblia, kazi yoyote iwapo tu ni ya Roho Mtakatifu, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushahidi zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu" (Neno Laonekana katika Mwili).
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, unabii wa Biblia

Jumapili, 22 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (3) - Je, Inamaanisha Nini katika Ufunuo Inaposema Mtu Asiongeze kwa Unabii?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (3) - Je, Inamaanisha Nini katika Ufunuo Inaposema Mtu Asiongeze kwa Unabii?

Ufunuo sura ya 22, mstari wa 18 "Kwa kuwa namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Iwapo mtu yeyote ataongeza kwa mambo haya, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki." Je, ungependa kujua maana halisi ya maneno haya? Video hii itakuonyesha jibu.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maandiko ya Biblia

Ijumaa, 20 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (1) - Imefichuliwa: Je, Kuna Maneno Yoyote au Kazi ya Mungu Mbali na Yaliyo katika Biblia?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (1) - Imefichuliwa: Je, Kuna Maneno Yoyote au Kazi ya Mungu Mbali na Yaliyo katika Biblia?

Wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini mara nyingi huwafundisha watu kwamba hakuna maneno na kazi ya Mungu nje ya Biblia, na hivyo kwenda zaidi ya Biblia ni uzushi. Je, wazo hili linastahili kuchunguzwa? Je, linalingana na ukweli wa kazi ya Mungu? Kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema haijaandikwa tu katika Agano la Kale na inakwenda zaidi ya Agano la Kale. Ikiwa kwenda zaidi ya Biblia ni uzushi, je, si basi sisi pia tunahukumu kazi ya Bwana? Hivyo kuna maneno au kazi ya Mungu isipokuwa yale yaliyo katika Biblia, au hakuna? Video hii itakufichulia jibu.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Dondoo za Video ,

Jumapili, 1 Julai 2018

Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia

Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia

Feng Jiahui na wazazi wake waliamini katika Bwana tangu alipokuwa mdogo. Alipokuwa na umri wa miaka 18 aliingia katika shule ya seminari, na katika miaka yake ya 30 akawa mhubiri katika kanisa la nyumba huko Shanxi, Uchina. Kwa miaka mingi, Feng Jiahui alidumisha imani madhubuti ya kuwa Biblia ilitiwa msukumo na Mungu, na kwamba lazima tuamini katika Mungu kwa mujibu wa Biblia. Aliamini kuwa hakukuwa na maneno yaliyonenwa na Mungu nje ya Biblia, na kwamba kuondoka kutoka kwa Biblia kutakuwa uzushi. Biblia ilikuwa imepata nafasi takatifu moyoni mwake, mahali pa mamlaka ya juu na isiyoweza kushindwa. Hata hivyo, katika kipindi cha miaka michache iliyopita, kanisa lake lilianza kuwa tupu siku baada ya siku, na Feng Jiahui na wafanyakazi wenzake walianza kuhisi giza likiingia ndani ya roho zao, na hawakuweza kuhisi uwepo wa Bwana miongoni mwao.... Aliwaalika wahubiri kutoka katika makanisa mengine ili kusaidia kurejesha kanisa, lakini bila mafanikio …
Wakati mmoja, Ndugu Yuan, mfanyakazi mwenzake Feng Jiahui alimwalika shahidi kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu aje kanisani. Shahidi alipokuwa akifanya ushirika juu ya ukweli kuhusu Biblia, kila kitu alichosema kilikuwa cha utendaji, wazi sana, na waumini waliona kuwa ya faida sana kwao. Hata hivyo, Feng Jiahui aliendelea kushikilia Biblia, akisisitiza kwa uthabiti kwamba imani katika Mungu lazima iwe na msingi katika Biblia, na kuondoka kwa Biblia kulikuwa uzushi. Baadaye, baada ya kuwa na mjadala mkubwa, Feng Jiahui hatimaye alielewa... undani wa Biblia na kiini cha kweli cha Biblia: Biblia ni kumbukumbu tu ya hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu, na Biblia haiwezi kumwakilisha Mungu, sembuse kufanya kazi ya Mungu ya wokovu kwa ajili Yake. Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima kwa mwanadamu, na Mungu pekee ndiye anaweza kufanya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, sisi ambao tunamwamini Mungu lazima tufuate nyayo za Mungu, na wakati huo tu ndiyo tutaweza kufikia njia ya uzima wa milele. Hatimaye, Feng Jiahui aliweza kwenda zaidi ya Biblia, kukubali kazi ya Mungu ya siku zile za mwisho, na kuwaongoza waumini katika kanisa lake kurudi kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Filamu za Injili