Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo maandiko-ya-Biblia. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo maandiko-ya-Biblia. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 6 Aprili 2019

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Wanadamu walipopotoshwa na Shetani, Mungu alianza mpango Wake wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria na kuyaongoza maisha ya wanadamu, Akiwafanya watu kujua kwamba wanapaswa kumwabudu Mungu, na kuwafanya wajue dhambi ni nini. Lakini kutokana na ujio wa hatua za mwisho za Enzi ya Sheria, upotovu wa wanadamu ukawa hata wa kina zaidi, na watu mara nyingi walikiuka sheria na kutenda dhambi dhidi ya Yehova. Walikabiliwa na hatari ya kuhukumiwa na kuuawa kwa sababu ya ukiukaji wao. Hivyo, kwa kujibu mahitaji ya wanadamu, wakati wa Enzi ya Neema Mungu alichukua umbo la kibinadamu na akawa Bwana Yesu. Yeye, Alitundikwa msalabani kwa ajili ya wanadamu, na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi, kuwawezesha watu kuja mbele ya Mungu na kuomba kwa Mungu, kukiri dhambi na kutubu, kusamehewa dhambi zao, na kuishi chini ya utajiri wa neema na baraka za Mungu. Lakini kwa sababu asili ya dhambi ya watu ilikuwa bado haijatatuliwa, na bado mara nyingi walitenda dhambi na kumuasi Mungu, katika Enzi ya Ufalme Mungu mara nyingine akawa mwili, kwa kutumia jina la Mwenyezi Mungu kuonyesha ukweli wote kwa ajili ya wokovu na utakaso wa wanadamu juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, kufuta asili ya dhambi ya wanadamu, kusababisha wanadamu kusitisha uasi wake kwa Mungu na kumpinga Mungu, kuwaruhusu watu kwa hakika kumtii Mungu na kumwabudu Mungu, na hatimaye kuwaongoza wanadamu kwenye hatima nzuri. Ingawa kazi ambayo Mungu amefanya katika Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme imekuwa tofauti, na majina Aliyoyachukua na tabia ambayo Ameonyesha yamekuwa tofauti, kiini na malengo ya kazi Yake ni sawa–yote ni ili kuwaokoa wanadamu, na kazi yote inafanywa na Mungu Mwenyewe. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema, “Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu” (“Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Kwa maelfu ya miaka, watu wachache wamejua kwa hakika kwamba Bwana Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe, kwamba Yeye ni kuonekana kwa Mungu, na kwamba Bwana Yesu ni kupata mwili kwa Bwana. Kwa kweli, Biblia tayari imetabiri kwa dhahiri kitambo. Katika Kitabu cha Isaya, ilinenwa kwamba “Hata hivyo Yehova alikuwa na ridhaa kumchubua; amempa huzuni: wakati utafanya nafsi yake kuwa sadaka ya dhambi (ama: wakati atajitoa mwenyewe kama sadaka ya dhambi)” (Isa 53:10). Kutoka kwa kifungu hiki cha Biblia inaweza kuonekana kwamba kwa Bwana Yesu kutumika kama sadaka ya dhambi ina maana kwamba Yehova alijitoa nafsi kama toleo la dhambi, na kwamba Bwana Yesu alikuwa Yehova. “yule ambaye ameniona mimi amemwona Baba” (Yohana 14:9). “Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake” (Yohana 10:38). “Mimi na Baba yangu tu mmoja” (Yohana 10:30). Wakati Bwana Yesu alisema kwamba “Mimi na Baba yangu tu mmoja.” Alikuwa akisema kwamba Yeye na Yehova ni roho mmoja naye. Maneno yanayosemwa na Bwana Yesu na yale yanayosemwa na Yehova ni sawa–wote wawili ni ukweli, ni matamshi ya Roho mmoja, na chanzo ni sawa; yaani, Bwana Yesu na Yehova ni Mungu mmoja. Vivyo hivyo, chanzo cha maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho na yale ya Bwana Yesu ni sawa, ni matamshi ya Roho Mtakatifu, ni ukweli, na ni sauti ya Mungu. Wale wanaomwamini Bwana wote wanajua kwamba idadi kubwa ya unabii katika Biblia inahusu kurudi kwa Bwana na kazi ya hukumu ya Mungu wa siku za mwisho. Kama Bwana Yesu alivyosema, “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo” (Yohana 14:3) “Na tazama, ninakuja upesi” (Ufunuo. 22:12). “Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija katika wingu akiwa na nguvu na utukufu mwingi” (Luk 21:27). “Tazama, nitakuja kama mwizi” (Ufunuo 16:15). “Yeye anikataaye mimi, na hayakubali maneno yangu, anaye amhukumuye: neno hilo nililolinena, ndilo hilo litakalomhukumu siku ya mwisho” (Yohana 12:48). Katika Waraka wa Kwanza wa Petro pia ilisemwa kuwa, “Kwa maana wakati umefika ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1Pet 4:17). Ilizungumzwa kwa dhahiri sana katika maandiko haya kwamba Bwana Yesu angerejea wakati wa siku za mwisho, na angeonyesha maneno na kufanya kazi ya hukumu. Wakati Mwenyezi Mungu anapokuja wakati wa siku za mwisho, Yeye hufanya kazi ya hukumu akianza kwa nyumba ya Mungu juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, na huonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu. Ingawa kazi ya Mwenyezi Mungu na ile ya Bwana Yesu ni tofauti, chanzo chao ni sawa– Mungu Aliye mmoja! Hili hutimiza kikamilifu unabii wa Bwana Yesu: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambia, lakini hivi sasa hamwezi kuyastahimili. Hata hivyo, yeye, Roho wa kweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwa ukweli wote: kwa maana hatanena juu yake mwenyewe; bali yote atakayoyasikia, hayo ndiyo atakayoyanena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16: 12-13). Mwenyezi Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho ni mfano halisi wa Roho wa kweli; Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu.

Jumapili, 30 Desemba 2018

Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

1. Bwana Yesu Mwenyewe alitabiri ya kwamba Mungu angepata mwili katika siku za mwisho na kuonekana kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi.

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja" (LK. 12:40).
"Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki" (LK. 17:24-25).
"Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha" (MT. 25:6).
"Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na mimi" (UFU. 3:20).
"Tazama, mimi nakuja kama mwizi. Amebarikiwa yeye anayekesha, na kuzihifadhi nguo zake, asije akatembea uchi, na wao waione haya yake" (UFU. 16:15).
"Na nikapinduka ili kuiona sauti hiyo iliyonizungumzia. Na baada ya kupinduka, nikatazama vinara saba vya taa vilivyokuwa vya dhahabu; Na hapo katikati ya hivyo vinara saba vya taa nilimwona mtu aliyefanana na Mwana wa Adamu, aliyekuwa amevalia nguo iliyofika katika miguu yake, na kifuani alikuwa amefungwa kanda ya dhahabu. Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye" (UFU. 1:12-16).
Maneno Husika ya Mungu:
Yesu alisema kwamba Angewasili kama Alivyoondoka, lakini unajua maana halisi ya maneno Yake? Je, angeweza kwa kweli kukwambia? Unajua tu kwamba Atawasili kama Alivyoondoka juu ya wingu, lakini unajua hasa jinsi Mungu Mwenyewe hufanya kazi Yake? Ikiwa ungeweza kuona kweli, basi maneno ya Yesu yanapaswa kuelezwa vipi? Alisema, "Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika siku za mwisho, Yeye Mwenyewe hatajua, malaika hawatajua, wajumbe wa mbinguni hawatajua, na watu wote hawatajua. Baba tu ndiye atakayejua, yaani, Roho pekee ndiye atajua." Ikiwa una uwezo wa kujua na kuona, basi haya si maneno matupu? Hata Mwana wa Adamu Mwenyewe hajui, lakini wewe unaweza kuona na kujua? Ikiwa umeona na macho yako mwenyewe, je, maneno hayo hayakusemwa bure? Na Yesu alisema nini wakati huo? "Lakini kuhusu siku ile na saa ile hakuna mwanadamu aijuaye, hata malaika wa mbinguni, ila Baba yangu peke yake. Lakini kama vile zilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kuja kwake Mwana wa Adamu kutakavyokuwa. ... Basi ninyi pia muwe tayari: kwani katika saa msiyofikiria Mwana wa Adamu atakuja." Wakati siku hiyo itakapofika, Mwana wa Adamu Mwenyewe hataijua. Mwana wa Adamu inahusu umbo la Mungu lililopata mwili wa Mungu, ambaye atakuwa mtu wa kawaida. Hata Yeye mwenyewe hajui, kwa hiyo wewe ungejuaje?
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuna wale ambao husema kwamba Mungu mwenyewe Alisema kuwa Atawasili kwa wingu. Ni ukweli kuwa Mungu mwenyewe Alisema hivyo, lakini, je, wajua kuwa siri za Mungu haziwezi kueleweka na mwanadamu? Je, unajua kuwa maneno ya Mungu hayawezi kuelezwa na mwanadamu? Na wewe una hakika kuwa ulipewa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu? Je, Roho Mtakatifu Alikuonyesha moja kwa moja kwa namna hii? Je, haya ni maelekezo ya Roho Mtakatifu, au ni dhana zako? Walisema, "Haya yalisemwa na Mungu mwenyewe." Lakini hatuwezi kutumia dhana zetu na akili zetu kupima maneno ya Mungu. Na kuhusu maneno ya Isaya, je, unaweza kueleza maneno yake kwa kujiamini kikamilifu? Je, wewe unathubutu kueleza maneno yake? Kwa sababu huthubutu kueleza maneno ya Isaya, mbona unathubutu kueleza maneno ya Yesu? Nani ameinuliwa kuliko mwingine, Yesu au Isaya? Kwa vile jibu ni Yesu, kwa nini unaeleza maneno yaliyosemwa na Yesu? Je, Mungu Angeweza kukwambia kuhusu kazi yake mapema? Hakuna kiumbe kinachoweza kufahamu, wala hata wajumbe walio mbinguni, wala hata Mwana wa Adamu, kwa hivyo wewe ungejuaje?
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho anasema kwa makanisa." … Kuna wanadamu wajinga wanaoamini kwamba maneno ya Roho Mtakatifu yanapaswa kuja chini kutoka mbinguni hadi kwa masikio ya mwanadamu. Yeyote anayefikiria hivi hajui kazi ya Mungu. Kwa kweli, matamshi yaliyosemwa na Roho Mtakatifu ni yale yaliyosemwa na Mungu aliyekuwa mwili. Roho Mtakatifu hawezi kuongea moja kwa moja na mwanadamu, na Yehova hakuongea moja kwa moja na watu, hata kwa Enzi ya Sheria. Si ungekuwa uwezekano wa chini zaidi kwamba Angefanya hivyo kwa enzi ya leo? Kwa Mungu kunena matamshi ili kutekeleza kazi, lazima Awe mwili, la sivyo kazi yake haiwezi kukamilisha malengo Yake. Wanaomkataa Mungu ni wale wasiojua Roho ama kanuni ambazo Mungu hufanya kazi.
kutoka kwa "Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani kuweza kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamengoja na kumtamani kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, ili Yesu Mwokozi Arudi kwa watu ambao wamekuwa mbali Naye kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumaini kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atasamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Wanatamani Yesu Mwokozi Awe Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi Ambaye Anapendeka, wa kirafiki na heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu Aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa na neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi Anawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea ghafla kwa Yesu Kristo, kutimiza maneno ya Yesu Akiwa duniani: "Nitarejea tu jinsi Nilivyoondoka." Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu Alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kulia wa Yule Aliye Juu. Vilevile, mwanadamu anatazamia kuwa Yesu Atashuka, tena juu ya wingu jeupe (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu Alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kuwa Atachukua mwonekano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atafadhili chakula kwa sababu yao, na kufanya maji ya uzima kuwamwagika kwa ajili yao, na Ataishi miongoni mwa wanadamu, Akiwa amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na wa hakika. Na mengine. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya haya; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alikuwa anatazamia. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, na hakutokea kwa wanadamu wote Akitumia wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, na kubaki mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Yake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote ambayo Yeye ni), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu hafahamu haya: Ingawa Mwokozi Mtakatifu Yesu Amejawa na upendo na mapenzi kwa mwanadamu, Atafanya kazi vipi katika "hekalu" ambalo limejaa uchafu na roho wasio safi? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Atawaonekania vipi wale wanaokula mwili wa wale wasio na haki, kunywa damu ya wasio na haki, kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini lakini hawamfahamu, na wanaompokonya kila wakati? Mwanadamu anajua tu kuwa Yesu Mwokozi Amejawa na upendo na huruma, na ni sadaka ya dhambi iliyojawa na ukombozi. Lakini mwanadamu hana habari kwamba Yeye pia ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, utukufu, ghadhabu, na hukumu, na kuwa na mamlaka na kujawa na hadhi. Kwa hivyo ingawa mwanadamu anayo hamu na kutamani kurudi kwa Mkombozi, na hata Mbingu inaguswa na maombi ya mwanadamu, Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.
kutoka kwa "Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimamishwa. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango wake. Usimamizi wake huendelea kimya kimya, bila madhara ilhali nyayo zake, daima hukaribia binadamu, na kiti chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, yaani, tukio hilo ni uwakilishaji wa mandhari kwa makini na wa kuonyesha Mungu ni mkuu. Kama njiwa na kama simba anayenguruma, Roho anawasili kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya, na huwasili na mamlaka akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuja Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya mwanadamu inabaki ilivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa kawaida, kama mfuasi asiye na maana na pia kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na vile vile, ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini wa kawaida asiye na maana.
kutoka kwa "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu Amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu Alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, bado hakuna mtu yeyote aliyejua. Hata leo hii, hakuna mtu anayetambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua. Haijalishi ni kwa kiwango kikubwa kiasi gani Roho Mtakatifu Anafanya kazi, siku zote Mungu yupo katika hali ya utulivu, kamwe Hajiachilii mbali. Mtu anaweza kusema kwamba inaonekana kama hatua hii ya kazi Yake inafanyika mbinguni. Ingawa ipo wazi kabisa kwa kila mtu, hakuna anayeitambua. Mungu Atakapomaliza hatua hii ya kazi Yake, kila mtu atazinduka kutoka katika ndoto yake na kugeuza mitazamo yao ya zamani[1]. … Wakati wa mapambazuko, bila kujulikana kwa mtu yeyote, Mungu Alikuja duniani na Akaanza maisha Yake katika mwili. Watu hawakujua kipindi hiki. Pengine wote walikuwa wamelala, pengine wengi waliokuwa wanakesha walikuwa wanasubiri, na pengine wengi walikuwa wanamwomba Mungu wa mbinguni kimyakimya. Lakini miongoni mwa watu hawa wote, hakuna hata mmoja aliyejua kuwa Mungu tayari Amekwishawasili duniani. Mungu Alifanya hivi ili Aifanye kazi Yake kwa urahisi na kupata matokeo bora zaidi, na pia ilikuwa ni kwa sababu ya kuepuka majaribu zaidi. Mwanadamu anapoamka kutoka usingizini, kazi ya Mungu itakuwa imekwishakamilika zamani sana na Ataondoka, na kufunga maisha Yake ya kutembeatembea na kusafiri duniani.
kutoka kwa "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiyo anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, liyevaa vazi lililofika kwa miguu, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti Yake kama sauti ya maji mengi. Ana nyota saba katika mkono Wake wa kuume, upanga wenye makali kuwili uko katika kinywa Chake na uso Wake ni kama jua liking'aa kwa nguvu zake!
kutoka kwa "Tamko la Kumi na Tano" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni asili ya watu ambayo itaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia raha ya ulimwengu wa mbinguni, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupata ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, kisha mnazikiri, wakati baada ya mwingine? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?
kutoka kwa "Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kiwango ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, kizazi cha malaika mkuu, kiwango ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeitwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Itaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna uashirio wa ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo kutakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatiao la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba "Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo" watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Anashughulika nao tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wamejaa kiburi. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na msimkufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndio mtapata kufaidika.
kutoka kwa "Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni matumaini yangu kuwa ndugu wanaotafuta kuonekana kwa Mungu hawatarudia tanzia ya kihistoria. Hampaswi kuwa Mafarisayo wa wakati huu na kumsulubisha Mungu msalabani tena. Mnafaa kufikiria kwa makini jinsi ya kukaribisha kurudi kwa Mungu, na kuwa na mawazo dhahiri ya jinsi ya kuwa mtu anayetii ukweli. Hili ni jukumu la kila mtu anayengoja Yesu arudi na mawingu. Tunafaa kufumbua macho yetu ya kiroho, na tusiwe waathiriwa wa maneno yaliyojaa mambo ya kufurahisha macho. Tunafaa kuwaza juu ya kazi ya Mungu ya matendo, na tunafaa kuangalia upande wa hakika wa Mungu. Msijisahau ama kupotelea ndotoni, mkitazamia daima ile siku ambayo Yesu atashuka kwa ghafla juu ya mawingu kuwachukua nyinyi ambao hamjawahi kumjua wala kumwona Yeye, na msiojua kutenda mapenzi Yake. Ni vyema kufikiri juu ya mambo ya kiutendaji!
kutoka kwa "Dibaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumatatu, 24 Desemba 2018

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (2) :Kurudi kwa Bwana katika Mwili Kunatimiza Unabii wa Biblia

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (2) :Kurudi kwa Bwana katika Mwili Kunatimiza Unabii wa Biblia

Kwa maana Bwana atarudi katika zile siku za mwisho, Bwana Yesu akasema, “Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja” (Luka 12:40)."Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17: 24-25). Ni maana gani inayodokezwa na "Mwana wa Adamu atakuja" na "ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa katika siku yake" kama ilivyoelezwa katika maandiko haya? Ikiwa Bwana anarudi kuja na mawingu, "kupata mateso mengi" na "kukataliwa na kizazi hiki," hii inaelewekaje?
Mwenyezi Mungu alisema Biblia ni kitabu cha aina gani? Agano la Kale ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria. Agano la Kale la Biblia linarekodi kazi yote ya Yehova wakati wa Enzi ya Sheria na kazi Yake ya uumbaji. Lote linarekodi kazi iliyofanywa na Yehova, na hatimaye linahitimisha maelezo ya kazi ya Yehova kwa kitabu cha Malaki. Agano la Kale linarekodi kazi mbili zilizofanywa na Mungu: Moja ni kazi ya uumbaji, na nyingine ni kuamrisha sheria. Zote ni kazi zilizofanywa na Yehova. Enzi ya Sheria inawakilisha kazi ya Mungu chini ya jina la Yehova; ni ujumla wa kazi iliyofanywa kimsingi chini ya jina la Yehova. Hivyo, Agano la Kale linarekodi kazi ya Yehova, na Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu, kazi ambayo kimsingi ilifanywa chini ya jina la Yesu. Umuhimu mkubwa wa jina la Yesu na kazi Aliyoifanya imerekodiwa katika Agano Jipya. Katika wakati wa Agano la Kale, Yehova alijenga hekalu na madhabahu katika Israeli, Aliongoza maisha ya Wanaisraeli duniani, kuzingatia kwamba walikuwa watu Wake, kundi la kwanza la watu ambalo alilichagua duniani na ambao walikuwa wanautafuta moyo Wake, kundi la kwanza ambalo Yeye Mwenyewe aliliongoza; ni sawa na kusema, makabila kumi na mawili ya Israeli walikuwa ni wateule wa kwanza wa Yehova, na hivyo Mungu siku zote Alifanya kazi ndani yao, hadi ambapo kazi ya Yehova ya Enzi ya Sheria ilihitimishwa. Hatua ya pili ya kazi ilikuwa ni kazi ya Enzi ya Neema ya Agano Jipya, na ilifanyika katika kabila la Yuda, moja ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Kwamba mawanda ya kazi yalikuwa madogo ilikuwa kwa sababu Yesu alikuwa Mungu alifanyika mwili. Yesu alifanya kazi katika eneo lote la Yudea pekee, na Alifanya tu kazi ya miaka mitatu na nusu; hivyo, kile kilichorekodiwa katika Agano la Kale kiko mbali zaidi kupitiliza kiwango cha kazi kilichorekodiwa katika Agano la Kale. Kazi ya Yesu ya Enzi ya Neema kimsingi imerekodiwa katika Injili Nne. Njia iliyopitiwa na watu wa Enzi ya Neema ilikuwa ile mabadiliko ya juu juu katika tabia yao ya maisha, nyingi zaidi ambayo imerekodiwa katika nyaraka. Nyaraka zinaonyesha jinsi ambavyo Roho Mtakatifu alifanya kazi wakati huo. (Ni kweli, licha ya ama Paulo aliadibiwa au alikutana na majanga, katika kazi aliyofanya alikuwa ameelekezwa na Roho Mtakatifu, alikuwa ni mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu wakati huo; Petro pia, alitumiwa na Roho Mtakatifu, lakini hakufanya kazi kubwa kama aliyofanya Paulo. Kwa kuangalia nyaraka zilizoandikwa na Paulo, inaweza kuonekana ni jinsi gani Roho Mtakatifu alifanya kazi wakati huo; njia ambayo Paulo aliiongoza ilikuwa njia njema, ilikuwa ni sahihi, na ilikuwa ni njia ya Roho Mtakatifu.)
kutoka kwa Kuhusu Biblia (1)

Jumapili, 28 Oktoba 2018

Swahili Christian Video "Bwana Anakuja Kwa Namna Gani Hasa?" | The Son of Man Has Come to Earth

Swahili Christian Video "Bwana Anakuja Kwa Namna Gani Hasa?" | The Son of Man Has Come to Earth

Katika siku za mwisho, hali ya moyo ya Wakristo wanaongoja kurudi kwa Bwana Yesu inakuwa kali sana, lakini ni kwa vipi, hasa, Bwana atarudi? Baadhi wanasema, "Bwana Yesu atakuja na mawingu." Wengine wanasema, "Unabii unaotabiri kurudi Kwake nao unasema, 'Tazama, mimi nakuja kama mwizi' (Ufu 16:15). 'Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki' (Luka 17:25). 'Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha' (Mat 25:6). Kama anakuja na mawingu kwa kila mmoja kumwona, tunaelezaje fumbo la Yeye kuja kwa siri, kuteseka, na kukataliwa, pamoja na kusema kwamba wengine watashuhudia kuhusu kurudi Kwake?" Bwana atatokeaje kwetu? Mchezo wa kuchekesha Bwana Anakujaje Hasa unajaribu kusuluhisha mashaka yetu kuhusu jambo hili.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Ijumaa, 5 Oktoba 2018

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Je, Kuamini katika Biblia Kunaweza Kuwakilisha Kumwamini Mungu?

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Je, Kuamini katika Biblia Kunaweza Kuwakilisha Kumwamini Mungu?

Wachungaji na wazee wa ulimwengu wa dini hushikilia maneno ya Paulo katika Biblia yanayosema "Maandiko yote yametolewa kwa msukumo wa Mungu," wakiamini kwamba Biblia ni maneno ya Mungu kabisa na kufanya yote wanayoweza kuiinua Biblia na kuishuhudia, na kuifanya Biblia na Mungu kuwa visawe. Wanaamini kwamba Biblia inamwakilisha Bwana na kwamba imani katika Bwana ni imani katika Biblia. Je, Biblia nzima kweli imetolewa kwa msukumo wa Mungu? Je, Bwana, Mungu, yuko ndani ya Biblia? Je, ni kazi ya Mungu ambayo imetoa Biblia, au Biblia ambayo imetoa kazi ya Mungu? Je, Biblia inaweza kweli kumwakilisha Bwana? Video hii fupi itakuonyesha njia sahihi.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumwamini Mungu

Alhamisi, 13 Septemba 2018

Filamu za Kikristo "Kumbukumbu Chungu" | Majadiliano Kuhusu Wokovu na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni

Filamu za Kikristo "Kumbukumbu Chungu" | Majadiliano Kuhusu Wokovu na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni

Hasa ni mtu aina gani anayeweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni? Baadhi ya watu hufikiria dhambi zetu zinasamehewa pindi tunaposadiki Bwana, kwamba pindi tunapookolewa basi tunaokolewa milele, na kwamba mtu aina hii anaweza kunyakuliwa na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni. Kisha kuna wale wanaosadiki kwamba, ingawa dhambi zetu zinasamehewa pindi tunaposadiki Bwana, bado tunafanya dhambi mara kwa mara na hatujafikia utakatifu, na kwa sababu Biblia inasema kwamba wale ambao si watakatifu hawawezi kumwona Bwana, basi ni vipi tunaweza kunyakuliwa na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni wakati hatujafikia utakatifu? Hivyo ni nani aliye sahihi na nani asiye sahihi kutokana na mitazamo hii miwili? Tafadhali tazama pande zote mbili zikishiriki katika majadiliano makali!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maandiko ya Biblia

Jumatano, 29 Agosti 2018

Swahili Christian Movie "Kutamani Sana" (1) - Hivyo Hivi Ndivyo Bwana Anavyorudi

Swahili Christian Movie "Kutamani Sana" (1) - Hivyo Hivi Ndivyo Bwana Anavyorudi

Waumini wengi ndani ya Bwana wameusoma unabii ufuatao wa kibiblia: "Wao watamwona yule Mwana wa Adamu akifika kwa mawingu ya mbinguni akiwa na nguvu na utukufu mkubwa" (Mathayo 24:30). Wanasadiki kwamba wakati Bwana atakaporudi, ni yakini kwamba Atashuka akiwa juu ya wingu, lakini kuna unabii mwingine katika Biblia unaosema: "Tazama, mimi nakuja kama mwizi" (Ufunuo 16:15). "Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha" (Mathayo 25:6). Ni wazi kwamba kunao unabii kwamba Bwana atakuja kwa siri mbali na ule unabii kwamba Atakuja waziwazi akiwa juu ya wingu. Hivyo ukweli ni upi kuhusu kurudi Kwake?
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ujio wa pili wa Yesu

Jumatatu, 23 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (4) - Je, Biblia Nzima Imetiwa Msukumo na Mungu Kweli?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (4) - Je, Biblia Nzima Imetiwa Msukumo na Mungu Kweli?

Watu wengi katika ulimwengu wa dini wanaamini kwamba "Kila andiko limetolewa kwa msukumo wa Mungu," yote katika Biblia ni neno la Mungu. Je, kauli ya aina hii inakubaliana na ukweli? Biblia ni ushahidi wa Mungu pekee, rekodi ya kazi ya Mungu tu, na haijaundwa kwa matamshi ya Mungu kikamilifu. Ndani ya Biblia, ni maneno yaliyonenwa na Yehova Mungu, maneno ya Bwana Yesu, unabii wa Ufunuo na maneno ya manabii yaliyotolewa kwa msukumo wa Mungu pekee, ndiyo neno la Mungu. Mbali na hayo, mengi ya yaliyosalia yanahusiana na rekodi za kihistoria na ushuhuda wa uzoefu wa mwanadamu. Ikiwa ungependa kujua undani wa Biblia, basi tafadhali angalia video hii!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Dondoo za Video ,

Jumapili, 22 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (3) - Je, Inamaanisha Nini katika Ufunuo Inaposema Mtu Asiongeze kwa Unabii?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (3) - Je, Inamaanisha Nini katika Ufunuo Inaposema Mtu Asiongeze kwa Unabii?

Ufunuo sura ya 22, mstari wa 18 "Kwa kuwa namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Iwapo mtu yeyote ataongeza kwa mambo haya, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki." Je, ungependa kujua maana halisi ya maneno haya? Video hii itakuonyesha jibu.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maandiko ya Biblia

Alhamisi, 17 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu

"Yehova" na "Yesu" yalikuwa ni majina ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, na imetabiriwa katika Ufunuo kuwa Mungu atakuwa na jina jipya katika siku za mwisho. Ni kwa nini Mungu anaitwa kwa majina tofauti katika enzi mbalimbali? Majina haya mawili ya "Yehova" na "Yesu" yana umuhimu gani? Video hii fupi itakusaidia kukutatulia fumbo hili.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Jina la Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Jumatano, 16 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (1) - Je, Kuna Maneno Mengine ya Mungu Kando ya Yale Yaliyo kwenye Biblia?

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (1) - Je, Kuna Maneno Mengine ya Mungu Kando ya Yale Yaliyo kwenye Biblia?

Biblia inasema, "Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kilichofungwa kwa mihuri saba" (Ufunuo 5:1). "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa; Kwa yule ashindaye nitampa mana iliyofichwa aile" (Ufunuo 2:17). Kulingana na Biblia, Bwana atakaporudi katika siku za mwisho Atafungua kitabu, afungue mihuri saba na ampe mwanadamu mana iliyofichwa. Lakini wachungaji na wazee wengine wa ulimwengu wa kidini wanaamini kuwa maneno yote ya Mungu yameandikwa katika Biblia na kuwa hakuna maneno mengine ya Mungu kando ya yale yaliyo kwenye Biblia. Je, mtazamo wa aina hiiunalinganana ukweli? Je, kwa kweli hakuna maneno mengine ya Mungu kando ya yale yaliyo kwenye Biblia? Video hii fupi itakuangazia maswali haya.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Jina la Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Jumatano, 21 Machi 2018

"Vunja Pingu na Ukimbie" (4) - Jifungue Kutoka kwa Utumwa wa Mafarisayo wa Kidini na Kurudi Kwa Mungu

"Vunja Pingu na Ukimbie" (4) - Jifungue Kutoka kwa Utumwa wa Mafarisayo wa Kidini na Kurudi Kwa Mungu

Katika jumuiya ya kidini, wachungaji wanajua Biblia kwa kina na mara nyingi huelezea vifungu kutoka kwa Biblia kwa watu. Kutoka kwa macho yetu, inaonekana kuwa wote wanamjua Mungu, lakini kwa nini kuna watu wengi katika ulimwengu wa kidini ambao huilaumu na kuipinga kazi ya Mungu mwenye mwili ya siku za mwisho? Mwenyezi Mungu anasema, "Wale wanaosoma Biblia kwa makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu wabovu, kila mmoja akisimama juu kumfundisha Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga makusudi" (Neno Laonekana katika Mwili).
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Alhamisi, 28 Desemba 2017

Kuhusu Biblia (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kuhusu Biblia (2)

Mwenyezi Mungu alisema , Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, wajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika “Agano Jipya” linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao.