Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumapili, 7 Januari 2018

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema , Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe. Huzuni iliyoje! Kuokolewa kwa mwanadamu hakuwezi kutenganishwa na usimamizi wa Mungu, aidha hakuwezi kutenganishwa na mipango ya Mungu. Na bado mwanadamu hafikirii chochote kuhusu usimamizi wa Mungu, na hivyo anaendelea kujitenga mbali na Mungu. Kutokana na hayo, idadi ya watu wanaomfuata Mungu inaendelea kuongezeka bila kujua mambo yanayohusiana na kuokolewa kwa mwanadamu kama vile uumbaji ni nini, kuamini kwa Mungu ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na kadhalika. Kufikia sasa, basi, lazima tuzungumze kuhusu usimamizi wa Mungu, ndiposa kila mfuasi ajue wazi umuhimu wa kumfuata Mungu na kumwamini. Watakuwa na uwezo wa kuchagua njia watakayoifuata ipasavyo, badala ya kumfuata Mungu tu ili kupata baraka, au kuepukana na majanga, au kuwa na mafanikio.

Japo usimamizi wa Mungu waweza kuonekana mkubwa kwa mwanadamu, si jambo la kutofahamika kwa mwanadamu, kwa kuwa kazi yote ya Mungu imefungamanishwa na usimamizi wake, inahusiana na Kazi ya kuokoa mwanadamu, na inajishughulisha na maisha, kuishi, na hatima ya wanadamu. Kazi ambayo Mungu Anaifanya kati ya na kwa mwanadamu, yaweza kusemwa kuwa, ni ya utendaji na yenye maana kubwa. Inaweza kuonekana na mwanadamu, kuhusishwa na mwanadamu, na iko mbali na dhahania. Kama mwanadamu hana uwezo wa kukubali kazi zote Anazozifanya Mungu, basi ni upi umuhimu wa kazi hii? Na ni vipi usimamizi huu unaweza kusababisha kuokolewa kwa mwanadamu? Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu: kupata baraka, na ni wazembe sana kuhudhuria chochote ambacho hakihusiani na nia hii. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, wacha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia zao, hata hivyo, ni muhimu sana kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila kukubali na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.

Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi. Hata kama watu watafahamu jinsi walivyo wa kuhurumiwa, wenye chuki na walivyo ovyo, ni wangapi hapo ambao wanaweza kuachana na ukamilifu na matumaini yao? Na ni nani anayeweza kusimamisha hatua zake na kuacha kujifikiri yeye mwenyewe? Mungu Anawahitaji wale watakaojihusisha kwa karibu Naye na kukamilisha usimamizi Wake. Anawahitaji wale ambao watatoa mawazo yao na mwili kwa ajili ya kazi Yake ya usimamizi ili kujitoa Kwake; Hawahitaji wale watakaoinua mikono yao na kuomba kutoka Kwake kila siku, na hata wale wanaotoa kidogo na kusubiri kulipwa kwa hilo tendo la kutoa. Mungu Anawadharau wale wanaotoa michango kidogo na kuridhika. Anawachukia wenye roho katili ambao hukataa kazi ya usimamizi Wake na hutaka tu kuongea kuhusu kwenda mbinguni na kupata baraka. Anachukia hata zaidi na wale ambao hufaidika na fursa inayowezeshwa na kazi Anayoifanya katika kuokoa wanadamu. Hii ni kwa sababu hawa watu hawajawahi kushughulishwa na Anachotarajia kupata Mungu kutokana na kazi Yake ya usimamizi. Wanashughulishwa tu na jinsi wanavyoweza kutumia hiyo fursa iliyowezeshwa na kazi ya Mungu ili kupata baraka. Hawajali roho Yake Mungu, kwa kuwa wanajishughulisha na mustakabali na hatima yao. Wale ambao wanakataa kazi ya usimamizi wa Mungu na hawana hata tamanio dogo katika jinsi Mungu Anavyowaokoa wanadamu na mapenzi Yake, wote wanafanya wapendavyo kando na kazi ya usimamizi wa Mungu. Tabia yao haitawaliwi na Mungu, na haikubaliwi na Mungu, na hata haiangaliwi kwa fadhila ya Mungu.

Ni viumbe wangapi wanaoishi na kuzaana katika ulimwengu mpana, wakifuata sheria ya maisha tena na tena, wakifuata sheria isiyobadilika. Wanaokufa huenda na hadithi za walio hai, na walio hai hurudia historia hii yenye huzuni ya wale waliokufa. Na kwa hivyo wanadamu hawawezi kujizuia ila kujiuliza wenyewe; Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii? Na ni nani muumbaji wa mwanadamu? Je, kweli wanadamu waliumbwa na mazingira asilia? Je, kweli wanadamu wana uamuzi juu ya hatima yao?... Kwa maelfu ya miaka wanadamu wameyauliza haya maswali, tena na tena. Kwa bahati mbaya, jinsi wanadamu wanavyopagawa na haya maswali, ndivyo kiu yao ya sayansi huendelea kukua. Sayansi hupatiana kutosheleza kwa muda na raha ya muda ya mwili, ila haitoshi kumpa mwanadamu uhuru kutokana na upweke, ukiwa, na hofu isiyodhihirika na kutosaidika ndani ya moyo wake. Wanadamu hutumia ujuzi wa kisayansi unaoweza kuonekana kwa macho na ambao akili zaweza kuufahamu kutuliza moyo wake. Na bado ujuzi wa kisayansi kama huu hauwezi kuwazuia wanadamu kutafiti yasiyofahamika. Wanadamu hawajui ni nani Mkuu wa kila kitu katika ulimwengu huu, aidha hajui mwanzo na mustakabali wa wanadamu. Wanadamu wanaishi tu, bila budi, katikati ya hii sheria. Hakuna anayeweza kuiepuka wala kuibadilisha kwani katika vitu vyote na katika mbingu kuna Mmoja kutoka milele hadi milele ambaye ni Mkuu wa kila kitu. Ni Yeye ambaye Hajawahi kuonekana na mwanadamu, ambaye wanadamu hawajawahi kumjua, ambaye wanadamu hawajawahi kuamini kuwepo Kwake, na bado ni Yeye Aliyewapulizia pumzi mababu wa wanadamu na kuwapa wanadamu uhai. Ni Yeye ndiye Huruzuku na kustawisha wanadamu kwa kuishi kwao, na huwaongoza wanadamu hadi siku ya leo. Aidha, Yeye na Yeye pekee ni wa kutegemewa na wanadamu ili kuendelea kuishi. Ni Mkuu wa kila kitu na Hutawala viumbe vyote vyenye uhai chini ya dunia. Huamrisha misimu yote minne, na ni Yeye huita upepo, jalidi, theluji na mvua. Huwapa wanadamu mwangaza wa jua na huleta machweo ya jioni. Ni Yeye Aliyeumba mbingu na ardhi, Akampa mwanadamu milima, maziwa na mito na kila kitu kilicho na uhai ndani yake. Matendo Yake yamo kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. Kila mojawapo ya hizi sheria na kanuni ni mfano mzuri wa matendo Yake, na kila mojawapo inafichua hekima na mamlaka Yake. Nani anayeweza kujiondoa kutoka kwa ukuu Wake? Na ni nani anayeweza kujitoa mwenyewe katika njia Zake? Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma. Bila kujali kama unaweza kutambua vitendo vya Mungu, bila kujali kama unaamini katika kuwepo kwa Mungu, hakuna shaka kuwa hatima yako inaegemea katika mipango ya Mungu, na hakuna shaka kuwa Mungu atakuwa na ukuu juu ya kila kitu. Uwepo na utawala Wake haviwezi kutabiriwa ikiwa vinatambulika na kufahamika na binadamu au la. Ni Yeye pekee Anayejua kuhusu yaliyopita ya mwanadamu, yaliyomo na yanayojiri, na Yeye pekee ndiye mwamuzi wa hatima ya wanadamu. Haijalishi kama unaukubali huu ukweli, haitachukua muda mrefu kabla mwanadamu kushuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe, na huu ni ukweli ambao hivi karibu Mungu Ataudhihirisha. Wanadamu huishi na hufa chini ya macho yake Mungu. Wanadamu huishi kwa usimamizi wa Mungu, na wakati macho Yake yatafumbika kwa mara ya mwisho, hio pia ni kwa usimamizi Wake. Tena na tena, mwanadamu huja na kwenda, nyuma na mbele. Bila mapendeleo, yote ni sehemu ya ukuu na michoro ya Mungu. Usimamizi wa Mungu ungali unaendelea mbele na haujawahi kusimama. Atawafanya wanadamu wafahamu uwepo Wake, waamini katika ukuu Wake, watazame matendo Yake, na warudi katika ufalme Wake. Huu ni mpango Wake, na kazi ambayo Amekuwa Akiitekeleza kwa maelefu ya miaka.

Kazi ya usimamizi wa Mungu ilianza Alipoumba ulimwengu, na mwanadamu ni kiini cha kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa kila kitu, unaweza kusemwa, ni kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu Kazi ya usimamizi Wake imesambaa katika maelfu ya miaka, na haijatekelezwa katika dakika na sekunde tu, ama kufumba na kufumbua, ama katika mwaka mmoja au miwili, ilimbidi Aumbe vitu vingine zaidi kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, kama vile jua, mwezi, na aina zote za viumbe walio hai, na chakula na mazingira kwa ajili ya wanadamu. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa usimamizi wa Mungu.

Baada ya hapo, Mungu Alimkabidhi mwanadamu kwa Shetani, mwanadamu aliishi chini ya miliki ya Shetani, na hili taratibu lilisababisha kazi ya Mungu ya enzi ya kwanza: hadithi ya Enzi ya Sheria.... Kipindi cha miaka elfu kadhaa za Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wazoefu wa maelekezo ya Enzi ya Sheria, na wakaanza kupuuza, na taratibu wakaacha ulinzi wa Mungu. Na hivyo, pamoja na kushikilia sheria, walimwabudu Mungu na kutenda matendo maovu. Walikuwa bila ulinzi wa Yehova, na waliishi tu mbele ya madhabahu ndani ya hekalu. Kwa kweli, Kazi ya Mungu ilikuwa imejitenga nao kitambo sana, na hata kama Waisraeli walijikita katika sheria, na kulitaja jina la Yehova, na kwa majivuno kuamini kuwa wao pekee ndio walikuwa watu wa Yehova na walikuwa wamechaguliwa na Yehova, utukufu wa Mungu uliwaacha kimyakimya…

Mungu Anapofanya kazi Yake, huacha sehemu moja na taratibu hutekeleza kazi Yake katika sehemu nyingine mpya. Hii huonekana ya kiajabu sana kwa watu ambao wamepooza. Watu wameishi kukithamini cha zamani na kukirejelea kipya, vitu visivyofahamika kwa uhasama, au hata kuonekana kama bughudha. Aidha, kazi yoyote mpya Aifanyayo Mungu, kutoka mwanzo hadi mwisho, mwanadamu ndiye huwa wa mwisho kufahamu kuihusu miongoni mwa kila kitu.

Kama ilivyokuwa kawaida, baada ya kazi ya Yehova katika Enzi ya Sheria, Mungu Alianza kazi yake ya hatua ya pili: kwa kuutwaa mwili, kuwa na mwili kama binadamu kwa miaka kumi, ishirini, na kuongea na kufanya kazi Yake Kati ya waumini. Na bado bila mapendeleo, hakuna aliyejua, na ni idadi ndogo tu ya watu walitambua kuwa Alikuwa Mungu Aliyepata mwili baada ya Yesu Kristo kupigiliwa misumari msalabani na kufufuka. Kwa taabu, palitokea mmoja aliyeitwa Paulo, aliyejitolea kuwa adui wa kuua watu wa Mungu. Hata kama aliangushwa chini na kuwa mtume, hali yake ya zamani haikubadilika, na akaandika barua nyingi. Kwa bahati mbaya, baadaye vizazi vilichukua barua zake kama neno la Mungu la kufurahiwa, kiasi kwamba ziliwekwa ndani ya Agano Jipya na kutatizana na maneno yaliyosemwa na Mungu. Hii kwa kweli ni aibu kubwa tangu majilio ya Maandiko Matakatifu. Je, hili kosa halikutendwa na mwanadamu kutokana na upumbavu wake? Hawakujua kuwa, katika rekodi za kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema, barua na maandiko matakatifu ya mwanadamu hayafai kuwa hapo kuiga kazi na maneno ya Mungu. Lakini hii ni kando na hoja, wacha turejelee mada ya awali. Baada tu ya kazi ya Mungu katika hatua ya pili kukamilika—baada ya kusulubishwa—kazi ya Mungu ya kutoa mwanadamu kwenye dhambi (ambayo ni kusema, kumtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani) ilitimilika. Na hivyo, kutoka wakati huo kuendelea mbele, wanadamu walipaswa tu kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi ili dhambi zao ziweze kusamehewa. Yaani, dhambi za wanadamu hazikuwa tena kizuizi cha kuufikia wokovu wake na kuja mbele za Mungu na hazikuwa tena nguvu za kushawishi ambazo Shetani alitumia kumlaumu mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe Alikuwa Amefanya kazi halisi, na kuwa katika mfano na limbuko la mwili wenye dhambi, na Mungu mwenyewe Alikuwa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, mwanadamu alishuka kutoka msalabani, akiwa amekombolewa na mwili wa Mungu, mfano wa huu mwili wa dhambi. Na hivyo, baada ya kushikwa mateka na Shetani, mwanadamu alikuja hatua moja mbele karibu na kukubali wokovu mbele za Mungu. Kwa hakika, huu ulingo wa kazi ndio ulikuwa usimamizi wa Mungu ambao ulikuwa hatua moja mbali na Enzi ya sheria, na wa kiwango cha ndani kuliko Enzi ya Sheria.

Huu ni mfano wa usimamizi wa Mungu: kuwakabidhi wanadamu kwa Shetani—wanadamu ambao hawajui kile Mungu Alicho, Muumba ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na ni kwa nini inafaa kujitoa kwa Mungu—na kutoa utawala huru kwa uovu wa Shetani. Hatua baada ya hatua, Mungu Anamtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani, hadi mwanadamu amwabudu Mungu kikamilifu na kumkataa Shetani. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Hili linasikika kama hadithi ya visasili na hii ni kwa sababu hawana fununu kuhusu yaliyomtokea mwanadamu katika maelfu ya miaka iliyopita, hata hawajui ni hadithi ngapi ambazo zimetokea katika huu ulimwengu. Na zaidi ya hayo, hii ni kwa sababu hawawezi kufahamu kinachostaajabisha sana, dunia inayoibua hofu zaidi ambayo iko zaidi ya dunia yakinifu, lakini ambayo macho yao ya mwili yanawazuia kuiona. Inasikika ya kutofahamika kwa mwanadamu. Na hii ni kwa sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Hujua kisichopendeza na jinsi kinavyotofautiana na kile kilicho kitakatifu, na hutambua ukubwa wa Mungu na uovu wa Shetani. Wanadamu kama hawa hawatamfanyia Shetani kazi tena, au kumwabudu Shetani, au kumsetiri Shetani. Hii ni kwa sababu wao ni kikundi cha watu ambao wamemilikiwa na Mungu. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuwasimamia wanadamu. Katika kazi ya usimamizi wa Mungu wa wakati huu, wanadamu ndio chombo cha maovu ya Shetani, na kwa wakati uo huo ni chombo cha ukombozi wa Mungu, aidha ni sababu ya vita dhidi ya Mungu na Shetani. Wakati sawia na wakati wa kutekeleza kazi Yake, Mungu taratibu Humtoa mwanadamu kutoka mikononi mwa Shetani, na hivyo mwanadamu anakuja karibu zaidi na Mungu...

Baadaye kukaja Enzi ya Ufalme, ambayo ni hatua ya utendaji zaidi na bado ni ngumu zaidi kukubalika na mwanadamu. Hii ni kwa sababu jinsi mwanadamu ajavyo karibu na Mungu, ndivyo afikapo karibu na kiboko cha Mungu, na ndivyo uso wa Mungu unavyokuwa wazi mbele ya mwanadamu. Kwa kufuatia kukombolewa kwa wanadamu, mwanadamu kirasmi anarejelea familia ya Mungu. Mwanadamu alifikiria kuwa huu ndio wakati wa kufurahia, bado ameegemezwa kwa shambulizi la Mungu na mifano ya yale bado hayajaonekana na yeyote. Inavyokuwa, huu ni ubatizo ambao watu wa Mungu wanapaswa "kuufurahia." Katika muktadha huo, watu hawana lingine ila kuacha na kujifikiria wao wenyewe, Mimi ndimi mwanakondoo, aliyepotea kwa miaka mingi, ambaye Mungu Amegharamika kumnunua, sasa kwa nini Mungu Ananitendea hivi? Ama ni njia ya Mungu kunicheka, na kunifichua?... Baada ya miaka mingi kupita, mwanadamu amedhoofika, kwa kuupitia ugumu wa usafishaji na kuadibu. Ijapokuwa mwanadamu amepoteza "utukufu" na "mapenzi" ya wakati uliopita, bila ya kufahamu amekuja kuelewa ukweli wa kuwa mwanadamu, na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu. Taratibu mwanadamu anaanza kuchukia ushenzi wake mwenyewe. Anaanza kuchukia jinsi alivyo mkali, na lawama kuelekea kwa Mungu, na mahitaji yote yasiyokuwa na mwelekeo aliyodai kutoka Kwake. Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma, matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu, na maneno na upendo wa Mungu vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya. Majeraha ya mwanadamu hupona siku baada ya siku, nguvu humrudia, na akasimama na kutazamia uso Wake mwenye Uweza...ndipo anagundua kuwa daima Ameishi kando yangu, na kwamba tabasamu Lake na sura Yake ya kupendeza bado zinasisimua. Moyo Wake bado unawajali wanadamu Aliowaumba, na mikono Yake bado ina joto na nguvu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni. Ni kama mwanadamu alirudi kwenye bustani ya Edeni, lakini wakati huu mwanadamu hasikizi ushawishi wa nyoka, na hatazami kando na uso wa Yehova. Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu, na kutazama uso Wake wenye tabasamu, na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado Anafanya Kazi bila kuchoka na Anapania kuikamilisha. Haijalishi ni kwa kiasi gani watu wanaelewa usimamizi wa Mungu, manufaa na usaidizi wa Kazi inayofanywa na Mungu unaweza kukubalika na kila mtu. Labda, leo, hujahisi upendo wowote au maisha yaliyowezeshwa na Mungu, lakini bora tu humwachi Mungu, na hupotezi matumaini yako ya kutafuta ukweli, basi kutakuwa na siku ambapo tabasamu la Mungu litafichuliwa kwako. Kwa kuwa dhumuni la kazi ya usimamizi wa Mungu ni kuwatoa wanadamu anayemilikiwa na Shetani, sio kuwaacha wanadamu waliopotoshwa na Shetani na kumpinga Mungu.

Yalisimuliwa mnamo Septemba 23, 2005

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumamosi, 6 Januari 2018

Ishini Katika Upendo wa Mungu | "Wimbo wa Mapenzi Matamu" | Best Swahili Christian Worship Song

Ishini Katika Upendo wa Mungu | "Wimbo wa Mapenzi Matamu" | Best Swahili Christian Worship Song

Kinani mwa moyo wangu, ni mapenzi Yako. Ni matamu sana, nakaa karibu yako. Kukutunza hukoleza moyo wangu; kukutumikia na mawazo yangu yote. Kuongoza moyo wangu, ni mapenzi Yako; mimi hufuata nyayo zako za mapenzi. Mimi hujisogeza kulingana na macho Yako; mapenzi yanaonyesha furaha ya moyo wangu. Mapenzi yanaonyesha furaha ya moyo wangu. Sasa mimi huishi katika ulimwengu mwingine, hakuna yeyote isipokuwa wewe uko nami. Unanipenda, ninakupenda; hakuna huzuni wala sikitiko hutusumbua. Hakuna huzuni wala sikitiko hutusumbua. Kumbukumbu chungu hutokomea. Kumbukumbu chungu hutokomea.
Kukufuata katika mapenzi, niko karibu Yako; furaha hutujaa Wewe na mimi. Kuelewa mapenzi Yako, mimi hukutii tu, bila kutaka kutokukutii Wewe. Nitaishi mbele Yako kuliko wakati wowote, siwezi kuwa mbali na Wewe tena. Nikiyawaza na kuyaonja maneno Yako, napenda Ulicho nacho, kile Ulicho. Napenda Ulicho nacho, kile Ulicho. Nataka Uwe maisha yangu. Nitakuruhusu Uchukue moyo wangu. Ah! Nakupenda, nakupenda. Mapenzi Yako yamenishinda, kwa hivyo nina bahati kukamilishwa ili niutosheleze moyo Wako. Haleluya! Haleluya! Haleluya! Mungu asifiwe! Haleluya! Haleluya! Haleluya! Mungu asifiwe! Haleluya! Haleluya! Haleluya! Mungu asifiwe! Haleluya! Haleluya! Haleluya! Mungu asifiwe!
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Ijumaa, 5 Januari 2018

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kanisa la Mwenyezi Mungu , Umeme wa Mashariki , Yesu, Kristo,

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Mwenyezi Mungu alisema, Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, ujaji wa Bwana Yesu kwa utukufu, kwa mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kwa kuonekana kwa ufalme, na kwa kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: Bwana anafika, na analeta maafa, na kuwazawadia walio wema na kuwaadhibu walio waovu, na Anawachukua wale wote wanaomfuata na kukaribisha kurudi Kwake angani kumlaki. Kila wakati tunapowaza kuhusu haya, hatuna budi ila kujawa na hisia. Tunashukuru kwa kuwa tulizaliwa siku za mwisho na tuna bahati ya kutosha ya kushuhudia kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, yote ni kwa ajili ya malipo ya “utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa”; hiyo ni baraka kweli! Hamu hii yote na neema inayopewa na Bwana mara kwa mara hutufanya kuingia kwenye maombi, na hutuleta pamoja mara kwa mara zaidi. Labda mwaka ujao, labda kesho, au labda hata mapema zaidi wakati mwanadamu hatarajii, Bwana atarejea ghafla, na ataonekana kati ya kundi la watu ambao wamekuwa wakimsubiri kwa umakinifu. Sote tunashindana kati yetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, ili kuwa kundi la kwanza la kutazama kuonekana kwa Bwana, na kuwa mmoja wa wale watakaonyakuliwa kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya kuwadia kwa siku hii. Baadhi yetu wameacha kazi zao, wengine wameachana na familia zao, wengine wamekana ndoa zao, na baadhi yao hata wamepeana akiba zao zote. Ni upendo usio na ubinafsi wa aina gani huu! Uaminifu na utiifu kama huu lazima uwe hata unashinda ule wa watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anampa neema yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumrehemu yeyote ambaye Yeye anataka, kujitolea kwetu na matumizi yetu, tunaamini, tayari yametazamika machoni Pake. Kwa hivyo, pia, sala zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana atatuzawadia kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu aliturehemu kabla hajauumba ulimwengu, na hakuna atakayenyakua baraka na ahadi Zake kwetu. Sote tunapanga kuhusu siku za usoni, na kupuuza kwamba kujitolea kwetu na kugharamia ni mambo tunayoweza kutumia ili kuchukuliwa kwenda mbinguni kukutana na Bwana. Kuongezea, bila kusita hata kidogo, sisi tunajiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye, tukitawala mataifa na watu wote kwa jumla, ama tunatawala kama wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu kinachotarajiwa.

Tunadharau wale wote walio kinyume na Bwana Yesu; na mwishowe, wote wataangamizwa. Nani aliwaambia wasiamini kwamba Bwana Yesu ni Mwokozi? Bila shaka, kuna nyakati ambapo tunajifunza kutoka kwa Bwana Yesu na tunakuwa na huruma kwa dunia, kwa kuwa hawaelewi, na tunapaswa kuwa wavumilivu na kuwasamehe. Kila kitu tufanyacho ni kwa mujibu wa maneno ya Biblia, kwani kila kitu ambacho hakifuatani na Biblia ni uzushi, na madhehebu maovu. Imani kama hiyo imehifadhiwa ndani sana ya akili zetu. Bwana wetu yumo katika Biblia, na tusipoondoka kwenye Biblia basi hatutaondoka kwa Bwana; tukitii kanuni hii, basi tutaokolewa. Sisi husaidiana na kuchochea kila mmoja wetu, na kila wakati tunapokusanyika pamoja ni matumaini yetu kwamba kila kitu tunachosema na kutenda kinaambatana na matakwa ya Bwana na kuwa kinaweza kukubaliwa na Bwana. Licha ya uhasama mkali ulioko kwenye mazingira yetu, mioyo yetu imejaa furaha. Tunapowaza kuhusu baraka hizi tunazoweza kupata kwa urahisi, je, kuna kitu ambacho hatuwezi kukiacha? Je, kuna kitu ambacho hatuwezi kuvumilia kutengana nacho? Yote haya ni thabiti, na haya yote yanatazamwa na macho ya Mungu. Sisi, walio wachache wa maskini ambao tumeinuliwa kutoka jaani, ni sawa na wafuasi wa Bwana Yesu wa kawaida: Tunaota kuhusu kunyakuliwa, na kubarikiwa, na kutawala mataifa yote. Upotovu wetu umeanikwa peupe machoni pa Mungu, na tamaa zetu na uchoyo zinahukumiwa machoni pa Mungu. Bado, yote haya hutokea bila ajabu kabisa, yenye mantiki sana, na hakuna hata mmoja kati yetu ambaye hushangaa kama hamu yetu ni ya haki, sembuse yeyote kati yetu ambaye anashuku usahihi wa yote yale ambayo sisi hushikilia. Nani anayeweza kujua mapenzi ya Mungu? Hatujui jinsi ya kutafuta, au kuchunguza, au hata kujishughulisha na njia ambayo mwanadamu hupitia. Kwa maana sisi hujali tu kuhusu kama tutaweza kunyakuliwa, kama tunaweza kubarikiwa, kama kuna pahali tumetengewa katika ufalme wa mbinguni, na kama sisi tutaweza kupata mgawo wa maji ya mto wa uzima na matunda ya mti wa uzima. Je, sisi hatumwamini Bwana, na je, sisi sio wafuasi wake Bwana, kwa ajili ya kupata vitu hivi? Dhambi zetu zimesamehewa, tumetubu dhambi zetu, tumekunywa kikombe cha mvinyo ambao ni mchungu, na tumeuweka msalaba migongoni mwetu. Nani anayeweza kusema kuwa gharama ambayo tumelipia haitakubalika na Bwana? Nani anayeweza kusema kuwa hatujatayarisha mafuta yanayotosha? Hatutaki kuwa wale mabikira wapumbavu, ama mmoja wa wale ambao wameachwa. Aidha, tunaomba mara nyingi, na kumwomba Bwana atuepushe kutokana na kudanganywa na Kristo wa uongo, kwa maana imeandikwa kwenye Biblia kuwa “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24:23-24). Sisi sote tumeweka mistari hii ya Biblia kwenye kumbukumbu, tunaijua vyema sana, na tunaiona kama hazina ya thamani, kama maisha, na kama vitambulisho vyetu vya wokovu wetu na kunyakuliwa kwetu …

Kwa maelfu ya miaka, wanaoishi wamefariki, wakichukua tamaa zao na ndoto zao, na hakuna anayejua kwa kweli iwapo wameenda kwa ufalme wa mbinguni. Wafu wanarudi, na wamesahau hadithi zote zilizowahi kutokea wakati mmoja, na bado wanafuata mafundisho na njia za babu zetu. Na kwa hivyo, miaka inavyopita na siku zinavyosonga, hakuna anayejua iwapo Bwana Yesu, Mungu wetu, kwa kweli hukubali yote tunayoyafanya. Tunangojea tu matokeo na kubashiri kuhusu yale yote ambayo yatatokea. Bado Mungu yu kimya siku zote, na hajawahi kutuonekania, wala kusema nasi. Na kwa hivyo, kwa hiari yetu tunahukumu mapenzi ya Mungu na tabia kwa mujibu wa Biblia na ishara. Sisi tumezoea kimya cha Mungu; tumekuwa na mazoea ya kupima usahihi na makosa ya tabia zetu kutumia njia zetu wenyewe za mawazo: tumekuwa na mazoea ya kutumia elimu yetu, dhana, na maadili yetu na kuyafanya yachukue nafasi ya matakwa ya Mungu kwetu sisi; tumekuwa na mazoea ya kufurahia neema ya Mungu; tumekuwa na mazoea ya Mungu kutoa msaada wakati sisi tunahitaji msaada huo; tumekuwa na mazoea ya kunyosha mikono yetu kwa Mungu ili tupate mambo yote, na kumuagiza Mungu; na pia tumekuwa na mazoea ya kufuata mafundisho ya dini, kutotilia maanani jinsi Roho Mtakatifu hutuongoza; zaidi ya hayo, tumekuwa na mazoea ya siku ambazo sisi ni bwana zetu wenyewe. Tunamwamini Mungu wa namna hii, ambaye hatujawahi kukutana naye. Maswali kama namna tabia Yake ilivyo, asili Yake na mali Zake ni zipi, mfano Wake ulivyo, kama tutamjua ama hatutamjua wakati Atakaporudi, na kadhalika—haya yote hayana umuhimu. Jambo muhimu ni kuwa Yeye yumo mioyoni mwetu, na kuwa tunamsubiri, na kuwa tunaweza kufikiria jinsi Alivyo. Tunathamini imani yetu, na kuthamini hali yetu ya kiroho. Tunaona kila kitu ni kama samadi, na kukanyaga vimbo vyote kwa nyayo zetu. Kwa sababu sisi ni wafuasi wa Bwana mwenye utukufu, bila kujali jinsi safari yetu ilivyo ndefu na ngumu, bila kujali shida na hatari zinazotukumba, hakuna kitu kitakachosimamisha nyayo zetu tunapomfuata Bwana. “Mto safi wa maji ya uhai, ung’aao kama kioo, uliondoka katika kiti cha Mungu cha enzi na cha Mwanakondoo. Na katika kila upande wa ule mto, ulikuwapo ule mti wa uhai unaozaa matunda ya jinsi kumi na mbili, na kuyatoa hayo matunda yake kila mwezi: na majani yake mti huu yalikuwa ya ajili ya kuyaponya mataifa. Na laana haitakuwepo tena: ila kiti cha Mungu cha enzi na cha Mwanakondoo kitakuwa ndani yake; na watumishi wake watamhudumia: Na wao wataona uso wake; nayo mapaji ya nyuso zao yatakuwa na jina lake. Na hakutakuwa na usiku pale; wala hawahitaji mshumaa, wala mwanga wa jua; kwa sababu Bwana Mungu huwapa mwanga: na wao watatawala daima na milele” (Ufunuo 22:1-5). Kila wakati sisi hukariri maneno hayo, mioyo yetu hujawa na furaha isiyo na kifani na maridhio, na machozi hutiririka kutoka machoni mwetu. Shukrani ni kwa Bwana kwa kutuchagua, shukrani ni kwa Bwana kwax neema Yake. Ametupa mara mia sasa, Yeye ametupa uzima wa milele kwa ulimwengu ujao, na kama angetuomba tufe sasa, tungetii hiyo bila kusita hata kidogo. Bwana! Tafadhali njoo hivi karibuni! Usikawie hata dakika moja tena, kwa kuwa sisi tunakutamani sana na tumeacha kila kitu kwa ajili Yako.

Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimama. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi Wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango Wake. Usimamizi Wake huendelea kimya kimya, bila madhara ya kutia shauku ilhali nyayo Zake, daima hukaribia binadamu, na kiti Chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti Chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, tukio hilo ni mandhari ya adhimu na yenye taadhima. Kama njiwa, na kama simba anayenguruma, Roho anawasili kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya akiwa na mamlaka na akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuwasili Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya mwanadamu yanabaki yalivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa kawaida, kama mfuasi asiye na maana kabisa na kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na zaidi, Ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini asiye wa maana. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu yote yanawekwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye hutilia maanani uwepo Wake, hamna aliye na mawazo yoyote ya kazi Yake, na zaidi ya hayo, hakuna mtu aliye na tuhuma yoyote kuhusu Yeye ni nani. Sisi huendelea na kazi yetu tu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi …

Kwa bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia” Kwake, na ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa sana, tunatambua kuwa hilo ni tamko la Mungu, na tunaukubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya, ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hatuwezi kuyakana. Tamko linalofuata linaweza kuwa kupitia kwangu, au kwako, ama linaweza kupitia yeye. Bila kujali ni nani, yote ni neema ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu huyo ni nani, hatufai kumwabudu, kwa kuwa bila kuzingatia chochote kingine, hawezi kuwa Mungu; hatuwezi kwa njia yoyote kumchagua mtu wa kawaida kama huyu kuwa ndiye Mungu wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika sana; Anawezaje kuwakilishwa na binadamu asiye na umuhimu hivyo? Zaidi ya hayo, sisi sote tunasubiri ujaji wa Mungu kuturudisha kwa ufalme wa mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu hivyo anawezaje kustahili kufanya kazi ngumu na muhimu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima iwe juu ya wingu jeupe, linaloonekana na wote. Huo utakuwa wa adhimu namna gani! Itakuwaje Ajifiche kwa ukimya kati ya kundi la watu wa kawaida?

Na bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu, wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa na aibu na fedheha. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anatarajia kufanya. Labda tunaweza tu kunyakuliwa baada ya kuvumilia maumivu kama hayo? Vichwani mwetu tunafanya hesabu … kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili na hutenda kazi kati yetu. Japokuwa Amekuwa pamoja nasi kwa muda mrefu, ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado hatuko tayari kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa mustakabali wetu, wala hatuna nia ya kumwaminisha mtu asiye na maana udhibiti wa mustakabali na hatima yetu. Kutoka Kwake, tunafurahia ugavi usioisha wa maji ya uhai, na kwa sababu Yake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Sisi tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Yeye bado, kwa unyenyekevu, hufanya kazi akiwa amefichwa ndani ya mwili, akionyesha sauti ya moyo Wake, akionekana kama hafahamu kukataliwa Kwake na binadamu, inavyoonekana yeye milele kusamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele kuvumilia mwanadamu kutomheshimu.

Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua baada ya hatua ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, na hukabiliwa na kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, tunakuja kufahamu mapenzi ya Mungu, tunakuja kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi tufe, na kutufanya kuzaliwa upya; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake na huba Yake; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, waliofanywa majivu na ghadhabu Yake katika macho Yake. Sisi ni wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao Yeye hufikiria kuhusu kuwapata mchana na usiku. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Yeye hujitia wasiwasi usiku na mchana kwa ajili yetu, Yeye hutulinda na kututunza usiku na mchana, na Hatuachi kamwe, na Yeye hutoa utunzaji Wake wote kwetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa maneno ya mwili huu mdogo na wa kawaida, tumefurahia ukamilifu wa Mungu, na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Ila, licha ya haya, majivuno yangali mioyoni mwetu, na sisi bado hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana nyingi sana, nyingi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambalo linaweza kunyakua nafasi ya Bwana katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum na hadhi ya huyu mwanadamu kwa kusita sana. Kama Yeye haneni kwa nguvu na kutufanya kukiri kwamba Yeye ni Mungu, basi sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu ambaye yuko karibu kuja ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu sana.

Matamshi ya mungu yanaendelea, na Yeye hutumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya tutakachofanya na kuonyesha sauti ya moyo Wake. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, na hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na sauti ya moyo ya huyu mwanadamu asiye wa ajabu. Yeye hufanya juhudi za mchwa kwa ajili yetu, anapoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na moyo Wake huvuja damu na kulia kwa ajili ya uasi na kufa ganzi kwetu. Asili kama hii na mali Zake zimeshinda za binadamu wa kawaida, na haziwezi kumilikiwa au kupatwa na yeyote aliyepotoka. Ana uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake haumilikiwi na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu wa mbinguni. Hakuna mtu ila Yeye anayeweza kumiliki mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, kutoka Kwake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu, na kuonyesha sauti ya moyo ya Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu ambayo huelekezwa kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na akaleta mbingu na nchi mpya, kazi mpya, na Ametuletea matumaini, na akamaliza maisha yetu ambayo hayakuwa dhahiri, na Akatuwezesha kikamilifu kuona njia ya wokovu. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zinapata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, si Yeye ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu. Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ameturuhusu kuishi tena, kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele. Wakati huo, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, wala hatupingi tena kazi na neno Lake, na tunasujudu, kabisa, mbele Yake. Hakuna tunachotaka ila kufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila Yake, na kulipa upendo Wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio Yake, na kushirikiana na kazi Yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile Anachotuaminia.

Kushindwa na Mungu ni kama mashindano ya kareti.

Kila neno la Mungu hugonga eneo letu la ubinadamu, na hutuacha tukiwa tumejawa na huzuni na hofu. Yeye hufichua fikra zetu, hufichua mawazo yetu, na hufichua tabia zetu potovu. Kupitia kwa yale yote sisi husema na kuyatenda, na kila wazo na fikra zetu, asili na kiini zinafichuliwa kwa neno Lake, na kutuacha na fedheha, tukitetemeka kwa hofu. Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, na hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa hadharani kabisa, na hata zaidi kuhisi tumeshawishika vikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba hatuna thamani machoni Pake, na kuwa sisi ni Shetani aishiye. Matumaini yetu yanavunjika, na kamwe hatuthubutu kumpa madai yoyote yasiyo na msingi au kumjaribu, na hata ndoto zetu hupotelea mara moja. Huu ni ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na ambao hakuna yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Kwa muda, akili zetu hukosa msimamo, na hatujui tutakavyoendelea kwa njia iliyo mbele wala hatujui jinsi ambavyo tutaendelea katika imani zetu. Inaonekana kama imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na ya kuwa hatujawahi kukutana na kufahamiana na Bwana Yesu. Kila kitu machoni petu hutushangaza, na kutufanya tuhisi ni kama tumetupwa mbali. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu kuna hasira ambayo haiwezi kufichika na pia kuna aibu. Tunajaribu kujieleza, kupata suluhisho, na, hali kadhalika, sisi hujaribu kuendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, na kujieleza kwa dhati mbele Yake. Ingawa kuna wakati mwingine ambao hatuna kiburi wala unyenyekevu kwa kutazamwa kwa nje, mioyoni mwetu tunateseka na hisia ya hasara kuliko ile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaweza kuonekana ni kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, ndani yetu tunavumilia bahari ya mateso inayopanda na kushuka. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimechukua matumaini na ndoto zetu zote, na kutuacha bila tamaa zetu kuu na kutokuwa tayari kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu na anayeweza kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kubwa kati yetu na Yeye na hakuna aliye tayari hata kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni mara ya kwanza ambapo sisi tunateseka kwa kupata pingamizi kubwa hivi na udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo. Hukumu na kuadibu Kwake zimetuwezesha kwa kweli kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia Kwake kosa la binadamu, ambazo tukilinganishwa nazo, sisi ni watu wa hadhi ya chini na najisi sana. Hukumu Yake na kuadibu zimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hataweza kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi tena katika tabia potovu kama hiyo, na zimetufanya tutamani kuacha asili kama hiyo na kiini kama hicho haraka iwezekanavyo, na kutochukiwa tena Naye wala tusimchafue moyo. Hukumu na kuadibu kwake zimetufanya tufurahie kutii maneno Yake, na hatumo tayari tena kwenda kinyume na matayarisho na mipangilio Yake. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kutafuta uzima, na zimetuwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu ... Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, tumetoka kuzimu, tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti.… Mwenyezi Mungu ametupata, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na kuwashinda adui Zake zote!

Sisi ni kundi la watu wa kawaida tu waliomilikiwa na tabia potovu ya kishetani, sisi ndio watu waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na sisi ndio maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati tulipomkataa na kumshutumu Mungu, ila sasa tumeshindwa na Yeye. Tumepokea uzima na kupokea njia ya uzima wa milele kutoka kwa Mungu. Bila kujali mahali ambapo tupo hapa duniani, licha ya mateso na dhiki, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu pekee!

Upendo wa Mungu unaenea mbele kama maji ya chemichemi, na unapewa wewe, na mimi pia, na kwake, na kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli kwa kweli na kungoja kuonekana kwa Mungu.

Kama vile mwezi hufuata jua daima, kazi ya Mungu haikomi kamwe, na inatekelezwa kwako, kwangu, kwake, na kwa wale wote ambao hufuata nyayo za Mungu na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu.

Ilielezewa Machi 23, 2010
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Alhamisi, 4 Januari 2018

Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Mwenyezi Mungu alisema , Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha si rahisi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung'aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Maisha ya Mungu, huishi milele bila kubadilika katika kusumbuka kwa mbingu na nchi. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.

Pengine, sasa, unataka kupokea maisha, au labda unataka kupata ukweli. Vyovyote vilivyo, unataka kumpata Mungu, kumpata Mungu unayeweza kutegemea, na ambaye anaweza kukupa uzima wa milele. Ukitaka kupata uzima wa milele, lazima kwanza uelewe chanzo cha uzima wa milele, na lazima kwanza ujue Mungu yuko wapi. Tayari nilishasema Mungu pekee ndiye maisha yasiyobadilika, na Mungu tu ndiye aliye na njia ya maisha. Kwa kuwa maisha Yake ni imara, hivyo ni ya milele; kwa kuwa Mungu tu ndiye njia ya maisha, basi Mungu Mwenyewe ni njia ya uzima wa milele. Kwa hivyo, lazima kwanza uelewe aliko Mungu, na jinsi ya kupata njia hii ya uzima wa milele. Hebu sasa tushiriki kwa masuala haya mawili tofauti.

Kama kweli unataka kupata njia ya uzima wa milele, na kama wewe unayo tamaa katika utafutaji wako kwa ajili yake, basi kwanza ulijibu swali hili: Mungu yuko wapi leo? Labda utajibu kwamba Mungu anaishi mbinguni, bila shaka—Hangeishi katika nyumba yako? Labda unaweza kusema, kawaida Mungu anaishi kati ya mambo yote. Au unaweza kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa kila mtu, au kwamba Mungu yuko katika ulimwengu wa kiroho. Mimi sipingi lolote kati ya haya, lakini lazima nifafanue suala hilo. Sio sahihi kabisa kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa mwanadamu, wala si makosa kabisa. Hiyo ni kwa sababu, miongoni mwa waumini katika Mungu, kuna wale ambao imani yao ni ya kweli na wale ambao imani yao ni uongo, kuna wale ambao Mungu anawakubali na wale ambao hawakubali, kuna wale ambao humfurahisha na wale ambao ni chukizo, na kuna wale ambao Yeye huwafanya kamili na wale ambao hupunguza. Na hivyo mimi Nasema kwamba Mungu Anaishi tu katika nyoyo za watu wachache, na watu hawa bila shaka ni wale ambao kweli wanaamini katika Mungu, wale ambao Mungu anawakubali, wale ambao humpendeza, na wale ambao Yeye huwafanya kamili. Wao ni wale wanaoongozwa na Mungu. Kwa kuwa wanaongozwa na Mungu, kwa hivyo ni watu ambao tayari wamesikia na kuona njia ya Mungu ya uzima wa milele. Wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya uongo, wale ambao hawajaidhinishwa na Mungu, wale ambao wanadharauliwa na Mungu, wale ambao wamechujwa na Mungu—wamefungwa katika kukataliwa na Mungu, wamefungwa kubaki bila njia ya maisha, na wamefungwa kubaki wajinga wa kujua aliko Mungu. Kwa upande mwingine, wale ambao Mungu anaishi katika nyoyo zao wanajua aliko Mungu. Wao ni watu wale ambao Mungu huwapa njia ya uzima wa milele, na ni wale wanaomfuata Mungu. Je, unajua, sasa, aliko Mungu? Mungu yupo katika moyo wa mtu na upande wa mtu. Hayupo tu katika ulimwengu wa kiroho, na juu ya mambo yote, lakini hata zaidi Yupo duniani ambapo mwanadamu huishi. Na hivyo kufika kwa siku za mwisho kumechukua hatua ya kazi ya Mungu katika sehemu mpya. Mungu ana ukuu juu ya mambo yote katika ulimwengu, na Yeye ni uti wa mgongo wa mwanadamu katika moyo wake, na zaidi ya hayo, Yeye yuko miongoni mwa wanadamu. Ni kwa njia hii pekee Anaweza kuleta njia ya maisha kwa binadamu, na kumleta mwanadamu katika njia ya maisha. Mungu amekuja duniani, na Anaishi kati ya wanadamu, ili wanadamu wanaweza kupata njia ya maisha, na hivyo binadamu anaweza kuwepo. Wakati huo huo, Mungu pia huamuru mambo yote katika ulimwengu, ili wapate kushirikiana na usimamizi Wake miongoni mwa wanadamu. Na hivyo, kama wewe unakiri tu kwamba Mungu yuko mbinguni na katika moyo wa mwanadamu, lakini usikiri ukweli wa kuwepo kwa Mungu miongoni mwa watu, basi kamwe hutapata uzima, na kamwe hutapata njia ya kweli.

Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!

Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, Kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, badala yake, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale Kristo bandia wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe. Kwa njia hii, kama kweli unataka kutafuta njia ya maisha, lazima kwanza ukiri kuwa ni kwa kuja duniani ndipo Anazirejesha njia za maisha kwa binadamu, na lazima kukiri ni katika siku za mwisho Yeye anakuja duniani kuhifadhia njia ya maisha kwa mwanadamu. Haya sio ya wakati wa nyuma; yanatendeka leo.

Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, wala njia inayoweza kukuongoza kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.

Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Jumatano, 3 Januari 2018

Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu , Kanisa la Mwenyezi Mungu ,Umeme wa Mashariki

Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema , Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa thabiti katika kazi Yake, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na harakati ya mambo yote. Kama kila kiumbe, mwanadamu bila kujua anapata lishe ya utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yote ya mwanadamu yanatunzwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, vilivyo hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu anavyotawala juu ya kila kitu.

Usiku uingiapo kwa utulivu, mwanadamu huwa hafahamu, kwani moyo wa mwanadamu hauwezi kujua jinsi giza linapokaribia au linakotoka. Usiku unapotoweka polepole, mwanadamu anakaribisha mwanga wa mchana, lakini moyo wa mwanadamu haufahamu ilikotoka nuru hii na jinsi gani nuru yenyewe imeliondoa giza la usiku. Mabadiliko kama haya ya kawaida ya mchana na usiku humpitisha mwanadamu katika kipindi kimoja baada ya kingine, kupita katika nyakati, wakati huu wote ikihakikisha kwamba kazi ya Mungu na mpango wake unafanywa wakati wa kila kipindi na katika nyakati zote. Mwanadamu alitembea kwa enzi nyingi na Mungu, lakini bado mwanadamu hafahamu kwamba Mungu ndiye kiongozi wa hatima ya mambo yote na viumbe hai au jinsi Mungu hupanga na kuelekeza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Na juu ya ni kwa sababu ipi, sio kwa sababu njia za Mungu hazifahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu. Kwa hivyo, hata ingawa mwanadamu Anamfuata Mungu, bila kujua yeye hubaki katika huduma ya Shetani. Hakuna anayetafuta kwa ukamilifu nyayo au nafsi ya Mungu, na hakuna anayetaka kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani na yule mwovu ili kubadilishwa na dunia hii na kanuni za maisha ambazo watu waovu hufuata. Katika nafasi hii, moyo na roho za mwanadamu hutolewa kafara kwa shetani na kuwa riziki yake. Aidha, moyo wa binadamu na roho yake huwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na kuufanya uwanja wake wa kuchezea. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni ya kuwa binadamu, na wa thamani na madhumuni ya kuwepo kwa binadamu. Sheria kutoka kwa Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu mpaka mwishowe mwanadamu hawezi tena kuomba au kufuata na kumsikiza Mungu. Wakati upitapo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu au kutambua kwamba yote hayo ni kutoka kwa Mungu. Mwanadamu huanza kupinga sheria na amri kutoka kwa Mungu; moyo na roho ya mwanadamu hufishwa. ... Mungu humpoteza mwanadamu Aliyemuumba pale mwanzo, na mwanadamu hupoteza mizizi ya mwanzo wake. Hii ni huzuni ya uanadamu. Kwa uhakika, tangu mwanzo mpaka sasa, Mungu alilifanya janga la wanadamu ambalo mwanadamu ni mhusika mkuu na mwaathiriwa, na hakuna hata mmoja anayeweza kupata jibu kuhusu nani ndiye mwelekezi wa hadithi hii ya janga.

Katika dunia hii kubwa, mabadiliko yasiyo hesabika yamefanyika, tena na tena. Hapana aliye na uwezo wa kuongoza binadamu isipokuwa Yeye ambaye Anatawala juu ya kila kitu katika ulimwengu. Hakuna yeyote hodari kwa kazi au kufanya maandalizi kwa ajili ya binadamu, wala aliye na uwezo wa kuwaongoza wanadamu kurejelea mwanga na ukombozi kutokana na ukosefu wa haki duniani. Mungu Analalamikia wakati ujao wa wanadamu, na Anahuzunishwa na kuanguka kwa mwanadamu. Anahisi huzuni kwa kuangamia kwa mwanadamu polepole na kwenda katika njia isiyo na upande wa kurudi. Mwanadamu ameuvunja moyo wa Mungu, akamkana na kumfuata yule mwovu. Hakuna waliowahi kuwa na mawazo kuhusu mwelekeo ambao mwanadamu wa aina hii atafuata. Ni kwa sababu hii haswa ndio kwamba hakuna ambaye ameona hasira ya Mungu. Hakuna anayetafuta njia ya kumpendeza Mungu au kujaribu kuwa karibu na Mungu. Kadhalika, hakuna anayetafuta kufahamu huzuni na maumivu ya Mungu. Hata baada ya kusikia sauti ya Mungu, binadamu anaendelea tu kwenye njia yake mbali na Mungu, kukwepa neema na huduma ya Mungu, na kuepuka ukweli wa Mungu, akiona ni afadhali auuze mwili wake kwa Shetani, adui wa Mungu. Na ni nani amewahi kuwa na mawazo yoyote ya jinsi gani Mungu atamtendea mwanadamu asiyetubu na ambaye amempuuza? Hakuna anayejua kwamba ukumbusho wa mara kwa mara na nasaha za Mungu ni kwa sababu Yeye anayo katika mikono yake maafa Aliyowaandalia yasiyokuwa ya kawaida, maafa ambayo yatakuwa magumu kwa mwili na nafsi ya mwanadamu kustahimili. Janga hili sio tu adhabu ya mwili bali ya roho pia. Lazima ujue hili: Mpango wa Mungu unapokataliwa na wakati kuwakumbusha kwake na nasaha hazileti mabadiliko, Atakuwa na hasira ya aina gani? Hii itakuwa kama kitu ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo awali au hata kusikika na viumbe vyovyote. Na hivyo Nasema, janga hili ni kubwa mno na kamwe hayatawahi kurudiwa. Hii ni kwa sababu uumbaji mmoja tu na wokovu mmoja wa mwanadamu ndio ulio ndani ya mpango wa Mungu. Hii ni mara ya kwanza na pia ni ya mwisho. Kwa hivyo, hakuna anayeweza kuelewa nia ya huruma na hamu ya Mungu kwa matarajio yake ya kuwaokoa wanadamu.

Mungu aliumba dunia hii na kuleta mwanadamu, kiumbe hai ambacho alitia uhai ndani yake. Baadaye, mwanadamu akaja kuwa na wazazi na jamaa na hakuwa mpweke tena. Tangu mwanadamu alipotua macho kwa mara ya kwanza katika dunia hii tunayoishi, ilibainika kuwa angeishi ndani ya utaratibu wa Mungu. Ni pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ndiyo hustawisha kila kiumbe hai katika ukuaji wake hadi kinapokomaa. Wakati wa mchakato huu, hakuna hata mmoja anayeamini kwamba mwanadamu huishi na kukua chini ya uangalizi wa Mungu. Badala yake, anashikilia kwamba mwanadamu hukua chini ya upendo na utunzaji wa wazazi wake, na kwamba ukuaji wake unaongozwa na silika ya maisha. Hii ni kwa sababu mwanadamu hajui aliyeleta maisha au kulikotoka maisha hayo, pia hafahamu jinsi silika ya maisha husababisha miujiza. Mwanadamu anajua tu kwamba chakula ndicho msingi wa kuendelea kwa maisha, kwamba uvumilivu ni chanzo cha kuwepo kwa maisha, na kwamba imani iliyomo akilini mwake ni utajiri wa maisha yake. Mwanadamu haihisi neema na riziki itokayo kwa Mungu. Mwanadamu huyatumia kwa uharibifu maisha aliyopewa na Mungu. ... Hapana hata mwanadamu mmoja ambaye Mungu Anamwangazia usiku na mchana amechukua jukumu la kuanza Kumwabudu. Mungu Anaendelea kufanya kazi kama Alivyopanga juu ya mwanadamu Akiwa hana matarajio yoyote kutoka kwa mwanadamu. Anafanya hivyo kwa matumaini kwamba siku moja, mwanadamu ataamka kutoka katika ndoto yake na ghafla kuelewa thamani na madhumuni ya maisha, kuelewa gharama Aliyopitia Mungu ili Ampe mwanadamu kila kitu alicho nacho, na kujua jinsi Mungu anavyotamani kwa ari mwanadamu ageuke na Kumrudia. Hakuna yeyote amewahi kufikiria juu ya siri ya asili na endelezo la maisha ya mwanadamu. Na bila shaka, Mungu tu Ambaye Anaelewa yote haya na kwa kimya huvumilia mapigo na maumivu kutoka kwa binadamu, ambaye alipokea kila kitu kutoka kwa Mungu bila shukurani. Binadamu huchukulia kila kitu kinacholetwa na maisha kimzaha, na tena kama "kama jambo lisilo na shaka," Mungu amesalitiwa, amesahaulika, na kukataliwa na binadamu. Je, mpango wa Mungu ni wa maana namna hii? Je mwanadamu, kiumbe hai ambaye alitoka katika mkono wa Mungu, ni wa maana namna hiyo? Mpango wa Mungu ni wa umuhimu kabisa; hata hivyo, maisha ya viumbe vya mkono wa Mungu vipo kwa ajili ya mpango Wake. Kwa hivyo, Mungu hawezi kuuharibu mpango wake kwa sababu ya chuki Yake kwa mwanadamu. Ni kwa ajili ya mpango Wake na pumzi aliyotoa ndiyo maana Mungu Hustahimili mateso yote, siyo kwa ajili ya mwili wa mwanadamu ila ni kwa sababu ya uhai wa mwanadamu. Mungu ana hamu ya kuchukua pumzi aliyopuliza ndani mwa mwanadamu, wala sio nyama za mwili. Huu ndio mpango wake.

Wote wanaokuja duniani lazima wapitie maisha na kifo, na wengi wamepitia mzunguko wa kifo na kuzaliwa upya. Wale wanaoishi watakufa hivi karibuni na wafu watarejea karibuni. Yote haya ni mwendo wa maisha uliopangwa na Mungu kwa kila kiumbe hai. Hata hivyo, njia hii na mzunguko huu ni ukweli ambao Mungu Anataka binadamu aone, kwamba maisha aliyopewa na Mungu hayana kikomo na hayazuiliwi na mwili, wakati, au nafasi. Hii ni siri ya maisha aliyopewa binadamu na Mungu na dhihirisho kwamba maisha yalikuja kutoka Kwake. Ingawa watu wengi wanaweza kosa kuamini kwamba maisha yalitoka kwa Mungu, binadamu bila ya kufahamu wanafurahia yote yatokayo kwa Mungu, iwe wanaamini au wanakana uwepo Wake. Iwapo siku moja Mungu kwa ghafla Atabadili moyo na Atake kurudisha yote yaliyomo duniani na kuchukua maisha Aliyotoa, basi yote duniani yataisha. Mungu Hutumia maisha Yake kukimu vitu vyote vilivyo hai na visivyo na uhai, na kuleta yote kwa utaratibu mzuri kwa mujibu wa madaraka na mamlaka Yake. Huu ni ukweli ambao hakuna anayeweza kuufahamu au kuuelewa kwa urahisi, na kweli hizi zisizoeleweka kwa fikira zetu ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha. Sasa hebu nikupe siri: Ukuu na nguvu ya uhai wa Mungu hauwezi kueleweka na kiumbe chochote. Hii ilikuwa hivyo awali, iko hivyo wakati huu, na itakuwa hivyo wakati ujao. Siri ya pili Nitakayotoa ni hii: chanzo cha uhai hutoka kwa Mungu, kwa viumbe vyote, haijalishi tofauti katika maumbile au muundo. Hata uwe kiumbe hai cha aina gani, huwezi kwenda kinyume na njia ya maisha ambayo Mungu ameweka. Katika hali yoyote, kile Napenda ni kuwa mwanadamu aelewe kwamba bila huduma, utunzaji, na utoaji wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, haijalishi juhudi au mapambano yake. Bila ruzuku ya uhai kutoka kwa Mungu, mwanadamu hupoteza maana ya thamani katika maisha na kupoteza madhumuni ya kusudi katika maisha. Mungu angewezaje kuruhusu mwanadamu anayepoteza thamani ya uhai wake kuishi hivyo bila ya kujali? Kisha tena, usisahau kwamba Mungu Ndiye chanzo cha maisha yako. Iwapo mwanadamu atashindwa kuthamini yote ambayo Mungu Amemfanyia, Mungu Hatachukua kile Alichotoa pekee, lakini zaidi ya hayo, mwanadamu atalipa mara mbili kufanya fidia kwa yote ambayo Mungu Ametumia.

Mei 26, 2003

Jumanne, 2 Januari 2018

Ngurumo Saba Zatoa Sauti— Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Ngurumo Saba Zatoa Sauti— Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Mwenyezi Mungu alisema , Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika mtawanyiko wa wanadamu, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa.

Jumatatu, 1 Januari 2018

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Chini ya mbingu ya usiku yenye nyota, tulivu na kimya, kundi la Wakristo wanasubiri kwa ari kurudi kwa Mwokozi wakiimba na kucheza kwa muziki mchangamfu.Wanaposikia habari za furaha "Mungu amerejea" na "Mungu ametamka maneno mapya", wanashangaa na kusisimka. Wanafikiri: "Mungu ameonekana? Tayari ametokea?" Kwa udadisi na kutokuwa na uhakika, mmoja baada ya mwingine, wanaingia katika safari ya kuyatafuta maneno mapya ya Mungu. Katika kutafuta kwao kugumu, baadhi ya watu wanauliza maswali hali wengine wanalikubali tu. baadhi ya watu wanaangalia bila kutoa maoni, wakati wengine wanafanya mapendekezo na kutafuta majibu katika Biblia–wanaangalia lakini mwishowe kuangalia huku hakuzai matunda .... Wakati tu wanapokata tamaa, shahidi mmoja anawaletea nakala ya Biblia ya Enzi ya Ufalme, na wanavutiwa kwa kina na maneno yaliyomo katika kitabu. Hiki ni kitabu cha aina gani kweli? Je, kwa kweli wamepata maneno mapya ambayo Mungu ameyanena katika kitabu hiki? Je, wamekaribisha kwa furaha kuonekana kwa Mungu?
Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo
1 Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na hata Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya.
2 Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote.
3 Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu; bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu itapungukiwa na mwangaza, dunia itakuwa vurugu, na wanadamu wote wataishi katika njaa na mabaa. Atawaonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima mngekuwa viongozi wa wenye dhambi na maiti milele.
...
“Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu”katika Neno Laonekana katika Mwili
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.