Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo siku-za-mwisho. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo siku-za-mwisho. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 5 Aprili 2019

Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?

Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?

Watu wengi hawaelewi ni kwa nini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu katika siku za mwisho, Bwana Yesu anaitwa Mwenyezi Mungu wakati Anapokuja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa nini haendelei kuitwa Bwana Yesu? Kwa kweli, Mungu ana jina jipya kila wakati Anapofanya hatua moja ya kazi Yake. Jina hili jipya linachukuliwa na Mungu Mwenyewe kama inavyofaa kazi hii–siyo kitu ambacho watu humuita Yeye kama wanavyotaka. Jina analolichukua Mungu katika kila hatua ya kazi lina msingi wake katika Biblia. Jina la Bwana Yesu aliyerejea wa siku za mwisho lilitabiriwa zamani katika Biblia. Isaya alisema “Na Watu wa Mataifa wataiona haki yako, nao wafalme wote watauona utukufu wako; na wewe utaitwa kwa jina jipya, jina ambalo kinywa cha Yehova kitalitamka” (Isaya 62: 2). Katika Kitabu cha Ufunuo, ilisemwa pia kuwa “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika…. Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, na nitaliandika jina la Mungu wangu juu yake, na jina la mji wa Mungu wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu: na nitaliandika juu yake jina langu jipya” (Ufunuo 3: 7, 12). “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, Akasema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi” (Ufunuo 1: 8). “Na nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu Mwenyezi humiliki” (Ufu 19: 6). Jina la Mwenyezi Mungu wa Enzi ya Ufalme ni utimizaji kamili waunabii wa kitabu cha Ufunuo. Jina ambalo Mungu huchukua katika kila enzi lina umuhimi mkubwa na limeshikamana kwa undani na kazi ya Mungu wakati wa enzi hiyo. Mwenyezi Mungu alifichua mafumbo yanayohusiana na hili Aliposema, “Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha tabia ya Mungu wakati wa enzi fulani na linahitaji tu kuwakilisha kazi yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima. Bila kujali iwapo ni enzi ya Yehova, au ni enzi ya Yesu, kila enzi inawakilishwa kwa jina” (“Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“‘Yehova’ ni jina ambalo Nilichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, na linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Lina maana Mungu Anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. ‘Yesu’ ni Imanueli, na lina maana sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, na Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, na Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja tu ya mpango wa usimamizi. Hivyo ni kusema, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wa Uyahudi waliochaguliwa, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa na Mungu wa Wayahudi wote. Na sasa katika enzi hii, Wayahudi wote isipokuwa kabila la Uyahudi wanamwabudu Yehova. Wanatoa kafara Kwake kwa madhabahu, na kumtumikia wakivaa mavazi ya kikuhani hekaluni. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Ambayo ni kusema, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, na kuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu liliwepo ili kuwezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, na ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hivyo jina Yesu linawakilisha kazi ya wokovu, na kuashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliwi bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. ‘Yehova’ Anawakilisha Enzi ya Sheria, na ni jina la heshima kwa Mungu Aliyeabudiwa na Wayahudi. ‘Yesu’ Anawakilisha Enzi ya Neema, na ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kufika kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anatarajia Afike na picha Aliyokuwa nayo kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, na usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, na enzi isingefikishwa kikomo. Hii ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni wa ukombozi na wokovu wa mwanadamu peke yake. Nilichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, na silo jina ambalo nitatumia kuleta wanadamu wote kufika kikomo. Ingawa Yehova, Yesu, na Masiha yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria wakati tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, na hayauwakilishi ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Kwa hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, na wala sio Masiha, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitaleta enzi nzima kufikia tamati. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Niliitwa pia Masiha, na watu wakaniita Yesu Mwokozi pia wakati mmoja kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi sio Yehova au Yesu Ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu Ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu Ambaye ataleta enzi kufika mwisho. Mimi ni Mungu Mwenyewe Ambaye Anainuka katika kingo za dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu” (“Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Mwenyezi Mungu alisema kwa dhahiri kwamba kuna umuhimu mwakilishi kwa jina ambalo Mungu huchukua katika kila enzi: Kila moja huwakilisha kazi ya Mungu na tabia Anayoonyesha katika enzi hiyo. Wakati wa Enzi ya Sheria, Mungu alitumia jina la Yehova kutangaza sheria na amri Zake na kuyaongoza maisha ya wanadamu duniani; wakati wa Enzi ya Neema, Mungu alitumia jina la Yesu kufanya kazi ya ukombozi wa wanadamu; na wakati wa Enzi ya Ufalme, Mungu anaitwa Mwenyezi Mungu, Yeye hufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu kumtakasa, kumbadilisha, na kumwokoa mwanadamu. Mungu hubadilisha enzi akitumia jina Lake, na hutumia jina hili kuwakilisha kazi ya enzi. Wakati Yehova Mungu alifanya kazi ya Enzi ya Sheria, ni kwa kuomba tu kwa jina la Yehova na kutii sheria na amri Zake ndipo watu wangeweza kubarikiwa na kulindwa na Mungu. Kwa kuwasili kwa Enzi ya Neema, Mungu alitumia jina la Yesu kufanya kazi ya ukombozi, na watu hawakuwa na budi ila kumkubali Bwana Yesu kama Mwokozi, na kuombea toba kwa jina la Bwana, kusamehewa dhambi zao na kufurahia ukweli na neema iliyotolewa na Bwana Yesu. Ikiwa watu bado walishikilia jina la Bwana na kukataa kumkubali Bwana Yesu, basi walipoteza utunzaji na ulinzi wa Mungu, na walianguka katika giza, wakilaaniwa na kuadhibiwa na Mungu kama Mafarisayo Wayahudi. Pamoja na ujio wa siku za mwisho, Mungu hutumia jina la Mwenyezi Mungu kutekeleza kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Ni kwa kukubali jina la Mwenyezi Mungu tu, kwenda sambamba na hatua za kazi ya Mungu, na kufanyiwa hukumu na kuadibiwa kwa Mwenyezi Mungu, ndipo watu wanaweza kuelewa na kupata ukweli, kujitenga na dhambi, kutakaswa, na kupokea wokovu wa Mungu. Wote wanaokataa kulikubali jina la Mwenyezi Mungu na kukataa kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho hawawezi kujitoa wenyewe kutoka kwa utumwa wa dhambi, na milele hawatakuwa na sifa kamili kuingia katika ufalme wa mbinguni.

Alhamisi, 28 Februari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya "Wingu Jeupe"

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya "Wingu Jeupe"

Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe katika siku za mwisho (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho.”
Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani aweze kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamemtamani sana na kumwonea shauku kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, kwa Yesu Mwokozi kuwarudia watu ambao Amekuwa mbali nao kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumai kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atazisamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Anatamani Yesu Mwokozi awe jinsi Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi ambaye anapendeka, mwema na wa heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe katika siku za mwisho (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu hafahamu jambo hili: Ingawa Mwokozi Yesu mtakatifu Amejawa na upendo na mapenzi kwa mwanadamu, Angewezaje kufanya kazi katika “mahekalu” yaliyomilikiwa na uchafu na pepo wachafu? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Angewezaje kuwaonekania wale wanaokula mwili wa wasio na haki, kunywa damu ya wasio na haki, kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini lakini hawamfahamu, na wanaompokonya kila wakati? Mwanadamu anajua tu kuwa Yesu Mwokozi amejawa na upendo na huruma, naye ni sadaka ya dhambi iliyojawa na ukombozi. Lakini mwanadamu hana habari kwamba Yeye pia ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, uadhama, ghadhabu, na hukumu, na Aliye na mamlaka na kujawa na hadhi. Kwa hiyo ingawa mwanadamu anazamia kwa hamu na kuonea shauku kurudi kwa Mkombozi, na hata Mbingu inaguswa kwa maombi ya mwanadamu, Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.
“Yehova” ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. “Yesu” ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Uyahudi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa Wayahudi wote. Na hivyo katika enzi ya sasa, Wayahudi wote isipokuwa kabila la Yuda wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu, na kumtumikia wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani katika hekalu. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, nalo lilikuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataitamatisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka katika miisho ya dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.
Mwokozi atakapofika katika siku za mwisho, kama bado angeitwa Yesu, na kuzaliwa mara nyingine katika Uyahudi, na kufanya kazi Yake katika Uyahudi, basi hii ingethibitisha kuwa Niliumba Wayahudi peke yao na kuwakomboa Wayahudi peke yao, na kuwa Sina uhusiano wowote na Mataifa. Je, hii haitakuwa kinyume cha maneno Yangu kwamba “Mimi ni Bwana aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote”? Nilitoka Uyahudi nami Nafanya kazi Yangu kati ya Mataifa kwa sababu Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, ila Mungu wa viumbe vyote. Ninaonekana kati ya Mataifa katika siku za mwisho kwa sababu Mimi si Yehova, Mungu wa Wayahudi tu, lakini, zaidi ya hayo, kwa sababu Mimi ni Muumba wa wateule Wangu wote kati ya Mataifa. Sikuumba Uyahudi, Misri, na Lebanoni pekee, bali pia Niliumba Mataifa yote mbali na Israeli. Na kwa sababu hiyo, Mimi ni Bwana wa viumbe vyote. Nilitumia Uyahudi tu kama hatua ya kwanza ya kazi Yangu, Nikayatumia Uyahudi na Galilaya kama ngome za kazi Yangu ya ukombozi, nami Natumia Mataifa kama msingi ambao Nitatumia kuitamatisha enzi nzima. Nilifanya hatua mbili za kazi katika Uyahudi (hatua mbili za kazi ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema), nami Nimekuwa Nikitekeleza hatua mbili zaidi za kazi (Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme) katika nchi nyingine zote zaidi ya Uyahudi. Nitafanya kazi ya kushinda kati ya Mataifa, na hivyo kuikamilisha enzi. Mwanadamu akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa Nimeianza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa shauku kuwasili kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao wale wasioniamini. Wao ni watu ambao hawanijui, na imani yao Kwangu ni ya bandia. Je, watu kama hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja si kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani maangamizo Yangu ya dunia hii nzee yenye uchafu, lakini badala yake wanatamani kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili, ndipo watakapokombolewa; wanamtazamia Yesu kuwakomboa wanadamu wote mara nyingine kutoka nchi hii iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu kama hao watawezaje kuwa wale wanaoikamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Matamanio ya mwanadamu hayawezi kufikia mapenzi Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu hutamani au kuthamini tu kazi ambayo Nimeifanya hapo awali, naye hajui kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya siku zote na si mzee kamwe. Mwanadamu anajua tu kuwa Mimi ni Yehova, na Yesu, naye hana fununu kuwa Mimi ni Mwisho, Yule ambaye Atawaangamiza wanadamu. Mwanadamu anachotamani na kujua tu ni kuhusu dhana yake mwenyewe, nayo ni yale tu ambayo anaweza kuyaona kwa macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayoifanya, bali hayatangamani nayo. Kama kazi Yangu ingefanywa kulingana na mawazo ya mwanadamu, basi ingeisha lini? Mwanadamu angeingia katika pumziko lini? Nami Ningewezaje kuingia katika siku ya saba, Sabato? Nafanya kazi kulingana na mpango Wangu, kulingana na lengo Langu, na sio kulingana na nia ya mwanadamu.

Ijumaa, 1 Februari 2019

Filamu za Injili | "Nimewahi Treni ya Mwisho" | Entering the Ark of the Last Days

Filamu za Injili | "Nimewahi Treni ya Mwisho" | Entering the Ark of the Last Days

Chen Peng alikuwa mchungaji katika kanisa la nyumba fulani. Alikuwa akimtumikia Bwana kwa bidii, na mara nyingi alifanya kazi kama mhubiri, akiwasaidia wafuasi wake, na kulibebea kanisa mizigo mizito. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kanisa lilizidi kuwa tupu zaidi na zaidi. Waumini walikuwa na roho dhaifu na wavivu, wakikosa mkutano baada ya mkutano. Na hivyo Mchungaji Chen aliona giza likiangukia nafsi yake, kana kwamba kisima cha roho yake kilikuwa kikavu, na hakuweza kuhisi uwepo wa Bwana. Katika mikutano, aligundua kwamba hakuwa na kitu alichoweza kuhubiri. ... Alifanya kila kitu alichoweza kufikiria ili kuimarisha kanisa, lakini jitihada zake zote zilikuwa bure. ... Chen Peng alikuwa amesitikika, amepotea, na hakuweza kuelewa kwa nini kanisa lake lilikuwa linajawa na ukiwa sana, na kwa nini walikuwa wamepoteza uwepo wa Bwana.
Hadi siku moja, kwa bahati, aliposikia injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu. Baada ya kupitia mjadala mkali, Chen Peng hatimaye aligundua sababu ya kanisa lake kuwa na ukiwa, na akaamini kwamba Mungu alikuwa tayari amekuwa mwili na kuwa Mwana wa Adamu: Mwenyezi Mungu, anayehukumiwa na kutelekezawa na ulimwengu wa kidini, ambaye anasema ukweli na kufanya kazi ya hukumu katika zile siku za mwisho! Ni wale tu ambao wanakubali kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu, Kristo wa zile siku za mwisho, na kufuata nyayo za Mwana-Kondoo wataweza kunyakuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kufikia kunyunyuziwa na kupewa maji ya uzima. Kwa sababu ya hilo, Chen Peng aliwahi treni ya mwisho na kukubali kwa furaha kazi ya Mungu katika zile siku za mwisho.

Jumapili, 20 Januari 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu"


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu."

Alhamisi, 29 Novemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli"

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli"

Mwenyezi Mungu anasema, "Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake."
Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri shahiri kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, ujaji tukufu wa Bwana Yesu, kwa mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kwa kuonekana kwa ufalme, na kwa kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: Bwana anafika, na analeta maafa, na kuwazawadia walio wema na kuwaadhibu walio waovu, na anawachukua wale wote wanaomfuata na kukaribisha kurudi Kwake angani kumlaki. Kila wakati tunawaza kuhusu haya, hatuna budi ila kujawa na hisia. Tunashukuru kwa kuwa tulizaliwa nyakati za mwisho na tuna bahati ya kutosha ya kushuhudia kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, yote ni kwa ajili ya malipo ya “utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa”; hii ni baraka iliyoje! Hamu hii yote na neema inayopewa na Bwana mara kwa mara hutufanya kuingia kwenye maombi, na hutuleta pamoja kila mara. Labda mwaka ujao, labda kesho, au labda hata mapema wakati mwanadamu hatarajii, Bwana atarejea ghafla, na atatokea kati ya kundi la watu ambao wamekuwa wakimsubiri kwa umakinifu. Sote tunashindana kati yetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, ili kuwa kundi la kwanza la kutazama kuonekana kwa Bwana, na kuwa mmoja ya wale watakaochukuliwa kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya kuwadia kwa siku hii. Baadhi yetu wameacha kazi zao, wengine wameachana na familia zao, wengine kukana ndoa zao, na baadhi yao hata wamepeana akiba zao zote. Ni upendo usio na ubinafsi wa aina gani huu! Uaminifu na utiifu kama huu lazima uwe unashinda ule wa watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anavyompa neema yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumrehemu yeyote ambaye Yeye anataka, kujitolea kwetu na matumizi yetu, na matumizi yetu, tunaamini, tayari yametazamika machoni pake. Kwa hivyo, pia, sala zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana atatuzawadia kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu aliturehemu kabla hajauumba ulimwengu, na hakuna atakayenyakua baraka na ahadi Zake kutoka kwetu. Sote tunapanga kuhusu siku za usoni, na kupuuza kwamba kujitolea kwetu na kugharamia ni mambo tunayoweza kutumia ili kuchukuliwa kwenda mbinguni kukutana na Bwana. Pia, bila kusita hata kidogo, sisi tunajiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye, tukitawala mataifa na watu wote kwa jumla, ama tunatawala kama wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu kinachotarajiwa.
kutoka kwa Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Jumapili, 25 Novemba 2018

Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Matamshi ya Kristo

Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kufahamu madhumuni ya kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mwanadamu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu. Siku itakapofika utakapomtazama Mungu kwa kweli na kutambua hekima ya Mungu; utakapotazama matendo yote ya Mungu na kutambua kile Mungu Alicho na kile Alicho nacho; utakapotazama wingi Wake, hekima, ajabu Yake, na kazi Yake yote kwa mwanadamu, basi hapo ndipo utakuwa umefikia imani ya mafanikio kwa Mungu. Mungu anaposemekana kuwa Anayejumuisha yote na mwenye wingi, ni nini kinachomaanishwa na kujumuisha yote? Na nini kinachomaanishwa na utele? Iwapo huelewi haya, basi huwezi kuchukuliwa kuwa muumini wa Mungu. Mbona Nasema wale walio katika dunia ya kidini hawaamini katika Mungu na ni waovu, walio sawa na ibilisi? Ninaposema ni watenda maovu, ni kwa sababu hawaelewi matakwa ya Mungu, wala kuona hekima Yake. Hakuna wakati wowote ambao Mungu anadhihirisha kazi Yake kwao; ni vipofu, wasioona matendo ya Mungu. Wao ndio walioachwa na Mungu na hawamiliki kabisa utunzaji na ulinzi wa Mungu, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu. Wale wasio na kazi ya Mungu ni watenda maovu na humpinga Mungu. Wale Ninaosema wanampinga Mungu ni wale wasiomjua Mungu, wale wanaokiri Mungu na maneno matupu ilhali hawamjui, wale wanaomfuata Mungu lakini hawamtii, na wale wanaofurahia neema ya Mungu lakini hawawezi kumshuhudia. Bila ufahamu wa madhumuni ya kazi ya Mungu na kazi ya Mungu kwa mwanadamu, mwanadamu hawezi kuwa katika ulinganifu na moyo wa Mungu, na hawezi kumshuhudia Mungu. Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu. Kwa muda kabla ya Mungu kuwa mwili, kipimo cha kama mwanadamu alimpinga Mungu kilikuwa iwapo alishika amri zilizotolewa na Mungu mbinguni. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, wowote ambao hawakushika sheria za Yehova walikuwa ndio wale waliompinga Mungu; wowote walioiba sadaka ya Yehova, na wowote waliosimama dhidi ya wale waliofadhiliwa na Yehova walikuwa wale waliompinga Mungu na wale ambao wangepigwa mawe hadi kufa; wowote ambao hawakuwaheshimu mama na baba zao, na wowote waliompiga ama kumlaani mwingine ni wale ambao hawakufuata sheria. Na wote ambao hawakufuata sheria za Yehova walikuwa wale waliosimama dhidi Yake. Hii haikuwa hivyo tena katika Enzi ya Neema, wakati wale waliosimama dhidi ya Yesu walikuwa wale waliosimama dhidi ya Mungu, na wowote ambao hawakutii maneno yaliyotamkwa na Yesu ni wale waliosimama dhidi ya Mungu. Katika enzi hii, makusudio ya “upinzani kwa Mungu” yalifafanuliwa zaidi na kuwa halisi. Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa “upinzani kwa Mungu” wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu. Kwa hivyo, vile mwanadamu alivyomwamini Mungu katika mawazo yake, Mungu hakumlaumu mwanadamu ama kuulizia mengi kutoka kwa mwanadamu, kwani mwanadamu hangemwona Mungu hata kidogo. Mungu anapopata mwili na kuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, wote wanamtazama Mungu na kusikia maneno Yake, na wote wanaona vitendo vya Mungu katika mwili. Wakati huo, dhana zote za mwanadamu zinafutwa na kubaki povu tu. Kwa wale wanaomwona Mungu anayejitokeza katika mwili, wote walio na utiifu ndani ya mioyo yao hawalaaniwi, ilhali wanaosimama dhidi Yake kimakusudi watachukuliwa kuwa wapinzani wa Mungu. Wanadamu kama hao ni maadui wa Kristo na ni maadui wanaosimama dhidi ya Mungu kimakusudi. Wale walio na dhana kumhusu Mungu lakini bado wanatii kwa furaha hawatalaaniwa. Mungu anamlaani mwanadamu kulingana na nia yake na vitendo vyake, kamwe sio kwa mawazo na fikira zake. Iwapo mwanadamu angelaaniwa kwa misingi hiyo, basi hakuna mmoja ambaye angeweza kutoroka kutoka katika mikono ya Mungu ya ghadhabu. Wale wanaosimama makusudi dhidi ya Mungu mwenye mwili wataadhibiwa kwa sababu ya kutotii kwao. Upinzani wao wa makusudi unatokana na dhana zao kumhusu, ambao unasababisha usumbufu wao kwa kazi ya Mungu. Wanadamu kama hao wanapinga na kuiharibu kazi ya Mungu wakijua. Hawana tu dhana za Mungu, lakini wanafanya kile kinachosumbua kazi Yake, na ni kwa sababu hii ndiyo wanadamu kama hao watahukumiwa. Wale wasioshiriki katika usumbufu wa kazi kimakusudi huwatahukumiwa kama wenye dhambi, kwani wanaweza kutii kwa makusudi na kutosababisha vurugu na usumbufu. Wanadamu kama hao hawatahukumiwa. Hata hivyo, wakati wanadamu wamepata uzoefu wa miaka mingi ya kazi ya Mungu, kama bado wanaficha dhana zao za Mungu na kubaki wasioweza kujua kazi ya Mungu mwenye mwili, na licha ya miaka mingi ya uzoefu, wanaendelea kushikilia dhana nyingi za Mungu na bado hawawezi kuja kumjua Mungu, basi hata kama hawasababishi shida yoyote kukiwa na dhana nyingi za Mungu ndani ya mioyo yao, na hata kama dhana kama hizi hazionekani, wanadamu kama hao hawana huduma yoyote kwa kazi ya Mungu. Hawawezi kuhubiri injili wala kumshuhudia Mungu; wanadamu kama hao hawana manufaa na ni wapumbavu. Kwa sababu hawamjui Mungu na hawawezi kuondoa dhana zao za Mungu, wamelaaniwa. Inaweza kusemwa hivi: Si jambo geni kwa wanafunzi wa kidini kuwa na dhana za Mungu ama kutojua chochote kumhusu, lakini sio kawaida kwa wale walioamini kwa miaka mingi na kuwa na uzoefu mwingi wa kazi Yake kushikilia dhana kama hizi, na hata zaidi kwa wanadamu kama hao kutokuwa na ufahamu wa Mungu. Ni kwa sababu ya hali kama hii isiyo ya kawaida ndio wanadamu kama hao wanalaaniwa. Wanadamu wasio wa kawaida kama hao hawana manufaa; ni wale wanaompinga Mungu zaidi na waliofurahia neema ya Mungu bure. Wanadamu wote kama hao wataondolewa mwishoni!

Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza? Wale wanaojiheshimu mbele ya Mungu ni wanadamu wa chini kabisa, ilhali wanaojinyenyekeza ndio wa heshima zaidi. Na wale wanaojifikiria kujua kazi ya Mungu na kutangaza neno la Mungu kwa wengine kwa kishindo na tarumbeta nyingi wakati macho yao yako Kwake—hawa ndio wajinga zaidi kati ya wanadamu. Wanadamu kama hao ni wale wasio na ushahidi wa Mungu, na wale walio na kiburi na majivuno. Wale wanaoamini kwamba wana ufahamu mdogo wa Mungu licha ya uzoefu wao halisi na ufahamu wa vitendo ni wale Anaowapenda zaidi. Ni wanadamu kama hawa ndio walio na ushahidi wa kweli na wanaweza kweli kukamilishwa na Mungu. Wale wasioelewa mapenzi ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale wanaoelewa mapenzi ya Mungu lakini bado hawauweki ukweli katika vitendo ni wapinzani wa Mungu; wale wanaokula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado wanaenda dhidi ya kiini cha maneno ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale walio na dhana za Mungu mwenye mwili na wanaasi makusudi ni wapinzani wa Mungu; wale wanaomhukumu Mungu ni wapinzani wa Mungu; na yeyote asiyeweza kumjua Mungu na kumshuhudia ni mpinzani wa Mungu. Kwa hivyo sikiliza ushawishi Wangu: Kama kweli una imani ya kutembea njia hii, basi zidi kuifuata. Iwapo huwezi kuepuka upinzani kwa Mungu, basi ni bora kwenda zako kabla hujachelewa. Vinginevyo, inaashiria mabaya badala ya mazuri, kwani asili yenu ni potovu sana. Huna uaminifu ama utii hata kidogo, ama moyo ulio na kiu ya haki na ukweli. Na wala huna upendo hata kidogo kwa Mungu. Inaweza kusemwa kuwa hali yako mbele ya Mungu imesambaratika kabisa. Huwezi kushika unachopaswa wala kusema unachopaswa. Huwezi kuweka katika vitendo kile ambacho unapaswa, na huwezi kutekeleza kazi unayopaswa. Huna uaminifu, dhamiri, utii ama azimio unalopasa. Hujavumilia mateso unayopaswa kuwa umevumilia, na huna imani unayopaswa kuwa nayo. Huna sifa yoyote kabisa; una heshima binafsi ya kuendelea kuishi? Nakuhimiza kwamba ni bora kufunga macho kwa mapumziko ya milele, hivyo kumtoa Mungu katika kujishughulisha nawe na kuvumilia mateso kwa ajili yako. Unaamini katika Mungu lakini bado hujui mapenzi Yake; unakula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado huwezi kukidhi mahitaji Yake. Unaamini katika Mungu lakini bado humjui, na kuishi ingawa huna lengo la kujaribu kufikia. Huna maadili na huna madhumuni. Unaishi kama mwanadamu lakini huna dhamiri, uadilifu wowote wala hata uaminifu kidogo. Unafikiriwaje kuwa wanadamu? Unaamini katika Mungu lakini unamdanganya. Zaidi ya hayo, unachukua pesa za Mungu na kula sadaka Yake, na bado, mwishowe, huonyeshi fikira kwa hisia za Mungu ama dhamiri kwa Mungu. Huwezi hata kukidhi mahitaji ya Mungu ya chini zaidi. Kwa hivyo unawezaje kufikiriwa kuwa mwanadamu? Chakula unachokula na hewa unayopumua vimetoka kwa Mungu, unafurahia neema Yake, na bado mwishowe, huna hata ufahamu mdogo wa Mungu. Kinyume na hayo, umekuwa mtu asiye na maana anayempinga Mungu. Si basi wewe ni mnyama asiye bora kuliko mbwa? Kuna mnyama yeyote aliye mkatili kukuliko wewe?

Hao wahubiri na wazee wanaosimama katika mimbari ya juu wakimfundisha mwanadamu ni wapinzani wa Mungu na wako katika muungano na Shetani; wale kati yenu wasiosimama katika mimbari ya juu wakimfundisha mwanadamu hawatakuwa hata wapinzani wakubwa zaidi wa Mungu? Juu ya hayo, huna ushirikiano basi na Shetani? Wale wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu hawajui kuwa na makubaliano na moyo wa Mungu. Bila shaka, haiwezi kuwa ukweli kwa wale wanaoyaelewa madhumuni ya kazi Yake? Kazi ya Mungu kamwe haina makosa; badala yake, ni kufuatilia kwa mwanadamu kuliko na dosari. Wale waliosawijika wanaompinga Mungu makusudi sio waovu zaidi na mahasidi kuliko hao wahubiri na wazee? Wanaompinga Mungu ni wengi, na miongoni mwa wanadamu hao wengi, kuna aina mbalimbali ya upinzani dhidi ya Mungu. Kwa kuwa kuna kila aina ya waumini, hivyo pia kuna kila aina ya wale wanaompinga Mungu kila tofauti na mwingine. Hakuna mmoja kati ya wale wasiotambua wazi madhumuni ya kazi ya Mungu anayeweza kuokolewa. Bila kujali jinsi mwanadamu anaweza kuwa alimpinga Mungu zamani, mwanadamu ajapo kufahamu madhumuni ya kazi ya Mungu na kujitolea juhudi zake ili kumridhisha Mungu, dhambi zake za awali zitafutiliwa mbali na Mungu. Bora tu mwanadamu anatafuta ukweli na kuuweka ukweli katika vitendo, Mungu hataweka akilini kile ambacho amefanya. Badala yake, ni kwa msingi wa kutenda ukweli kwa mwandamu ndiyo Mungu anamtetea mwanadamu. Hii ndiyo haki ya Mungu. Kabla ya mwanadamu kumwona Mungu ama kuwa na uzoefu wa kazi Yake, bila kujali jinsi mwanadamu anamtendea Mungu, Haliweki hili akilini. Hata hivyo, mara tu mwanadamu amwonapo Mungu, na kuwa na uzoefu wa kazi Yake, matendo yote na vitendo vyote vya mwanadamu vinaandikwa chini ndani ya “rekodi” na Mungu, kwani mwanadamu amemwona Mungu na kuishi ndani ya kazi Yake.

Wakati mwanadamu ameona kwa kweli kile Mungu alicho nacho na kile Alicho, aonapo ukuu Wake, na kweli amekuja kujua kazi ya Mungu, na zaidi ya hayo, tabia ya awali ya mwanadamu inabadilika, basi mwanadamu atakuwa ameitupilia mbali kabisa tabia yake ya uasi inayompinga Mungu. Inaweza kusemwa kwamba kila mwanadamu amempinga Mungu wakati mmoja na kila mwanadamu ameasi dhidi ya Mungu. Hata hivyo, kama unamtii Mungu mwenye mwili kwa makusudi, na kwa hivyo kuuridhisha moyo wa Mungu kwa uaminifu wako, unaweka katika vitendo ukweli unaopaswa, kutekeleza jukumu lako unavyopaswa, na kufuata kanuni unazopaswa, basi wewe ni mtu aliye tayari kutupilia mbali uasi wake kumridhisha Mungu na mtu anayeweza kukamilishwa na Mungu. Iwapo utakataa kutambua makosa yako na huna moyo wa kutubu; ukiendelea katika njia zako za uasi na huna kabisa moyo wa kufanya kazi na Mungu na kumridhisha Mungu, basi mjinga mkaidi kama wewe kwa hakika ataadhibiwa na hatawahi kuwa mmoja wa kukamilishwa na Mungu. Iwapo hivyo, wewe ni adui wa Mungu leo na kesho, na hivyo pia utabaki adui wa Mungu siku ifuatayo; utakuwa milele mpinzani wa Mungu na adui wa Mungu. Mungu atakuachaje? Ni asili ya mwanadamu kumpinga Mungu, lakini mwanadamu hawezi kwa makusudi kutafuta “siri” za kumpinga Mungu kwa sababu kubadili asili yake ni kazi isiyoshindika. Kama hali ni hiyo, basi ni bora uende zako kabla hujachelewa, isiwe kuadibu kwako wakati ujao kukawa kali zaidi, na isiwe asili yako kama ya mnyama ikaibuka na kuwa isiyotawalika mpaka mwili wako unaondolewa na Mungu mwishowe. Unaamini katika Mungu ili ubarikiwe; ikiwa mwishowe, balaa tu ndiyo itakayokupata, hiyo haitakuwa na thamani. Nawahimiza kuunda mpango mwingine; zoezi jingine litakuwa bora kuliko imani yenu kwa Mungu. Hakika kuna mengi kuliko njia hii moja? Hamngeweza kuendelea kuishi vile vile bila kutafuta ukweli? Mbona kuishi katika ukinzani na Mungu kwa namna hii?

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Alhamisi, 22 Novemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Ufalme wa Milenia Umewasili"

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Ufalme wa Milenia Umewasili"

Mwenyezi Mungu anasema, "kuwasili kwa Ufalme wa Milenia duniani ni kuwasili kwa neno la Mungu duniani. Kushuka kwa Yerusalemu mpya kutoka mbinguni ni kuwasili kwa maneno ya Mungu kuishi miongoni mwa mwanadamu, kuenenda na kila tendo la mwanadamu, na mawazo yake yote ya ndani. Huu pia ni ukweli kwamba Mungu atatimiza, na mandhari mazuri kabisa ya Ufalme wa Milenia. Huu ndio mpango uliowekwa na Mungu: Maneno Yake yataonekana duniani kwa miaka elfu moja, na yatashuhudia matendo yake yote, na kukamilisha kazi Yake yote duniani, ambapo baada ya hatua hii mwanadamu atakuwa amefikia kikomo."

Ijumaa, 12 Oktoba 2018

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (3) - Je, Hakuna Maneno au Kazi ya Mungu Nje ya Biblia?

Dondoo za Filamu za Injili "Sauti Nzuri Ajabu" (3) - Je, Hakuna Maneno au Kazi ya Mungu Nje ya Biblia?

Watu wengi katika ulimwengu wa kidini wanasadiki kwamba maneno yote ya Mungu yako ndani ya Biblia, na chochote kilicho nje ya Biblia hakina kazi Yake na maneno. Hawatafuti nje ya Biblia matamko Yake katika kurudi Kwake. Je, wataweza kukaribisha kurudi kwa Bwana kama wataendelea kushikilia wazo hili? Je, Mungu angeweza kuzuiliwa tu kwa kuongea maneno yaliyo ndani ya Biblia? Biblia inasema: "Na pia kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya, ambayo, yote yakiandikwa, ninafikiri kwamba hata dunia yenyewe haingetosha vitabu hivyo ambavyo vitaandikwa" (Yohana 21:25). Mungu anasema: "Yote yaliyoandikwa katika Biblia ni machache na hayawezi kuwakilisha kazi yote ya Mungu" (Neno Laonekana katika Mwili).
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Video.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maneno ya Mungu

Jumanne, 9 Oktoba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Yudea. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyoondoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Waisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Waisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Yudea, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi pekee, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Waisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaowakomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Waisraeli pekee, na Yeye si Mungu wa Wayahudi pekee; Yeye ni Mungu wa viumbe vyote. Hatua mbili za awali za kazi Yake zilifanyika Israeli, na kwa njia hii, dhana zingine zimejitokeza ndani ya watu. Watu wanafikiri kuwa Yehova alikuwa akifanya kazi Israeli na Yesu Mwenyewe alitekeleza kazi Yake Yudea—zaidi ya hayo, ilikuwa kupitia kupata mwili ambapo Alikuwa akifanya kazi Yudea—na kwa vyovyote, kazi hii haikuenea zaidi ya Israeli. Hakuwa akifanya kazi na Wamisri; Hakuwa akifanya kazi na Wahindi; Alikuwa tu akifanya kazi na Waisraeli. Watu basi wanaunda dhana mbalimbali; aidha, wanapanga kazi ya Mungu ndani ya eneo fulani. Wanasema kwamba wakati Mungu anafanya kazi, ni lazima ifanywe miongoni mwa wateule na ndani ya Israeli; mbali na Waisraeli, Mungu hana mpokeaji mwingine wa kazi Yake, wala Hana eneo lingine la kazi Yake; ni wakali hasa katika “kumfundisha nidhamu” Mungu mwenye mwili, kutomruhusu kuenda zaidi ya eneo la Israeli. Je, hizi zote si dhana za binadamu? Mungu aliunda mbingu na dunia yote na vitu vyote, na kuumba viumbe vyote; Angewezaje kuzuia kazi Yake ndani ya Israeli peke yake? Katika hali hiyo, kungekuwa na haja gani ya Yeye kuumba viumbe Vyake vyote? Aliiumba dunia nzima; Ametekeleza mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita sio tu ndani ya Israeli lakini pia na kila mtu ulimwenguni. Bila kujali kama anaishi Uchina, Amerika, Uingereza ama Urusi, kila mtu ni wa ukoo wa Adamu; wote wameumbwa na Mungu. Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuondoka katika mawanda ya viumbe wa Mungu, na hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuepuka utambulisho wa “ukoo wa Adamu.” Wote ni viumbe wa Mungu, na wote ni wa ukoo wa Adamu; pia ni wazawa wapotovu wa Adamu na Hawa. Sio tu Waisraeli ambao ni viumbe wa Mungu, lakini ni watu wote; hata hivyo, wengine miongoni mwa viumbe wamelaaniwa, na wengine wamebarikiwa. Kuna mambo mengi ya kupendeza kuwahusu Waisraeli; Mungu awali alikuwa akifanya kazi nao kwa sababu walikuwa watu wapotovu kwa kiasi kidogo zaidi. Wachina ni dhaifu wakilinganishwa nao, na hawawezi hata kutumaini kulingana nao; hivyo, Mungu awali alifanya kazi miongoni mwa watu wa Israeli, na hatua ya pili ya kazi Yake ilifanywa tu Yudea. Kwa sababu hii, watu huunda dhana nyingi na kanuni nyingi. Kwa kweli, iwapo Angetenda kulingana na dhana za binadamu, Mungu angekuwa tu Mungu wa Waisraeli; kwa njia hii Asingeweza kupanua kazi Yake katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, kwa sababu Angekuwa tu Mungu wa Waisraeli badala ya Mungu wa viumbe vyote. Unabii ulisema kuwa jina la Yehova lingekuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na kuwa jina la Yehova lingeenezwa kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi—mbona ulisema hivi? Iwapo Mungu angekuwa Mungu wa Waisraeli tu, basi Angefanya kazi tu Israeli. Zaidi ya hayo, Asingepanua kazi hii, na Asingefanya huu unabii. Kwa sababu Alifanya huu unabii, Angehitaji kuipanua kazi Yake hadi mataifa yasiyo ya Kiyahudi na hadi kila taifa na mahali. Kwa sababu Alisema hili, basi Angefanya hivyo. Huu ndio mpango Wake, kwani Yeye ndiye Bwana aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote, na Mungu wa viumbe vyote. Bila kujali iwapo Anafanya kazi na Waisraeli ama katika Yudea nzima, kazi Anayoifanya ni kazi ya ulimwengu mzima na kazi ya binadamu wote. Kazi Anayoifanya leo katika taifa la joka kubwa jekundu—katika taifa lisilo la Kiyahudi—bado ni kazi ya binadamu wote. Israeli inaweza kuwa kituo cha kazi Yake duniani; vivyo hivyo, Uchina pia inaweza kuwa kituo cha kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Je, sasa Hajatimiza unabii kwamba “jina la Yehova litakuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi”? Hatua ya kwanza ya kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi inahusu kazi hii Anayoifanya katika taifa la joka kuu jekundu. Kwa Mungu mwenye mwili kufanya kazi katika nchi hii na kufanya kazi miongoni mwa hawa watu waliolaaniwa hasa inaenda kinyume na dhana za binadamu; hawa watu ni wa chini zaidi na wasio na thamani yoyote. Hawa wote ni watu ambao Yehova alikuwa amewaacha mwanzoni. Watu wanaweza kuachwa na watu wengine, lakini wakiachwa na Mungu, hawa watu hawatakuwa na hadhi, na watakuwa na thamani ya kiwango cha chini zaidi. Kama sehemu ya viumbe, kumilikiwa na Shetani ama kuachwa na watu wengine yote mawili ni mambo machungu, lakini sehemu ya viumbe ikiachwa na Bwana wa viumbe, hii inaashiria kwamba hadhi yake iko katika kiwango cha chini kabisa. Wazawa wa Moabu walilaaniwa, na walizaliwa ndani ya nchi hii isiyo na maendeleo; bila shaka, wazawa wa Moabu ni watu walio na hadhi ya chini zaidi chini ya ushawishi wa giza. Kwa sababu hawa watu walimiliki hadhi ya chini zaidi zamani, kazi inayofanywa miongoni mwao inaweza kabisa kuzivunja dhana za binadamu, na pia ni kazi yenye faida kubwa zaidi kwa mpango Wake mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita. Ili Afanye kazi miongoni mwa watu hawa ni kitendo kinachoweza zaidi kuzivunja dhana za binadamu; Akiwa na hili Anazindua enzi; na hili Anavunja dhana zote za binadamu; Akiwa na hili Anatamatisha kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kazi Yake ya awali ilifanywa Yudea, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uzinduzi wa enzi hata kidogo. Hatua ya mwisho ya kazi Yake haifanywi tu miongoni mwa watu wa mataifa yasiyo ya Kiyahudi; hata zaidi ya hayo, inafanywa miongoni mwa watu waliolaaniwa. Jambo hili moja ndio ushahidi unaoweza zaidi kumwaibisha Shetani; hivyo, Mungu “anakuwa” Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni na kuwa Bwana wa vitu vyote, Anayeabudiwa na kila kiumbe mwenye uhai.

      Kwa sasa bado kuna watu wengine wasioelewa ni aina gani ya kazi mpya ambayo Mungu amezindua. Mungu amefanya mwanzo mpya katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na Ameanza enzi nyingine na kuzindua kazi nyingine, na Anafanya kazi miongoni mwa ukoo wa Moabu. Je, hii si kazi Yake mpya kabisa? Hakuna yeyote katika enzi zote aliyeipitia kazi hii, wala hakuna aliyeisikia, sembuse kuithamini. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, kutoeleweka kwa Mungu, ukubwa wa Mungu, utakatifu wa Mungu vinategemea hatua hii ya kazi katika siku za mwisho, ili kuibuka wazi. Je, hii si kazi mpya inayovunja dhana za binadamu? Bado kuna wale wanaofikiria hivi: “Kwa sababu Mungu alimlaani Moabu na kusema kuwa Angewaacha wazawa wa Moabu, Angeweza kuwaokoaje sasa?” Hao ni wale watu kutoka mataifa yasiyo ya Kiyahudi waliolaaniwa na kulazimishwa nje ya Israeli; Waisraeli waliwaita “mbwa wasio wa Kiyahudi.” Kwa mtazamo wa kila mtu, wao sio mbwa wasio wa Kiyahudi pekee, lakini mbaya hata zaidi, ni wana wa maangamizi; kwa maneno mengine, wao si wateule wa Mungu. Ingawa awali walikuwa wamezaliwa ndani ya eneo la Israeli, wao siyo sehemu ya watu wa Israeli; wao pia walifukuzwa kwenda kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Wao ndio watu wa chini zaidi. Ni kwa sababu hasa wao ni watu wa chini zaidi miongoni mwa binadamu ndio Mungu anatekeleza kazi Yake ya kuzindua enzi mpya miongoni mwao. Kwa sababu wao ni wawakilishi wa binadamu wapotovu na kazi ya Mungu haikosi uchaguzi ama madhumuni, kazi Anayoifanya miongoni mwa watu hawa leo pia ni kazi inayofanywa miongoni mwa viumbe. Nuhu alikuwa sehemu ya viumbe, kama walivyo wazawa wake. Yeyote duniani aliye na mwili na damu ni sehemu ya viumbe. Kazi ya Mungu imeelekezwa kwa viumbe wote; haitekelezwi kulingana na kama mtu amelaaniwa baada ya kuumbwa. Kazi Yake ya usimamizi imeelekezwa kwa viumbe wote, sio wale wateule wasiolaaniwa. Kwa sababu Mungu anataka kutekeleza kazi Yake miongoni mwa viumbe Vyake, kwa hakika Ataifanya hadi kukamilika kwa mafanikio; Atafanya kazi miongoni mwa hao watu walio na manufaa kwa kazi Yake. Kwa hivyo, Anavunja mikataba yote ya kufanya kazi miongoni mwa watu; Kwake, maneno “kulaaniwa,” “kuadibu” na “kubarikiwa” hayana maana! Wayahudi ni wazuri hasa, na wateule wa Israeli sio wabaya pia; ni watu wenye ubora mzuri wa tabia na ubinadamu mzuri. Awali Yehova alizindua kazi Yake miongoni mwao na Akafanya kazi Yake ya awali, lakini ingekuwa bila maana kama Angewatumia kama wapokeaji wa kazi Yake ya ushindi sasa. Ingawa wao pia ni sehemu ya viumbe na wana vipengele vingi vyema, ingekuwa bila maana kutekeleza hatua hii ya kazi miongoni mwao. Asingeweza kumshinda yeyote, wala Asingeweza kushawishi viumbe wote. Huu ndio umuhimu wa uhamisho wa kazi Yake kwa watu hawa wa taifa la joka kubwa jekundu. Maana ya ndani zaidi hapa ni ya uzinduzi Wake wa enzi, ya kuvunja Kwake kwa kanuni zote na dhana zote za mwanadamu na pia kwa kumaliza Kwake kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kama kazi Yake ya sasa ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, ikifika wakati ambao mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilika, kila mtu angeamini kuwa Mungu ni Mungu tu wa Waisraeli, kuwa Waisraeli tu ndio wateule wa Mungu, kuwa Waisraeli tu ndio wanaostahili kurithi baraka na ahadi za Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anapata mwili katika taifa lisilo la Kiyahudi la joka kubwa jekundu; Ametimiza kazi ya Mungu kama Mungu wa viumbe wote; Amekamilisha kazi Yake yote ya usimamizi, na Atamaliza sehemu kuu ya kazi Yake kwa taifa la joka kubwa jekundu. Kiini cha hatua hizi tatu za kazi ni wokovu wa mwanadamu—ambao ni, kufanya viumbe wote vimwabudu Bwana wa viumbe. Hivyo basi, kila hatua ya kazi hii ni muhimu sana; Mungu hatafanya chochote kisicho na maana ama thamani. Kwa upande mmoja, hatua hii ya kazi inajumuisha kuzindua enzi na kukamilisha enzi mbili za awali; kwa upande mwingine inajumuisha kuvunja dhana zote za mwanadamu na njia ya zamani ya imani ya mwanadamu na maarifa. Kazi ya enzi mbili za awali ilifanywa kulingana na dhana tofauti za binadamu; hatua hii, hata hivyo, inafuta kabisa dhana za binadamu, na hivyo kuwashinda binadamu kikamilifu. Kwa kutumia ushindi wa ukoo wa Moabu na kutumia kazi iliyotekelezwa miongoni mwa ukoo wa Moabu, Mungu atawashinda binadamu wote katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa kina zaidi wa hatua hii ya kazi Yake, na ndicho kipengele cha thamani ya hatua hii ya kazi Yake. Hata kama sasa unajua kuwa hadhi yako ni ya chini na kuwa una thamani ya chini, bado utahisi kwamba umekutana na jambo linalofurahisha sana: Umerithi baraka kubwa, ukapata ahadi kubwa, na unaweza kamilisha hii kazi kubwa ya Mungu, na unaweza kuuona uso wa kweli wa Mungu, kujua tabia Yake ya asili, na kufanya mapenzi ya Mungu. Hatua mbili za awali za kazi ya Mungu zilifanywa Israeli. Iwapo hatua hii ya kazi Yake katika siku za mwisho bado ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, viumbe wote havingeamini kwamba Waisraeli tu ndio waliokuwa wateule, lakini pia mpango wa usimamizi wa Mungu wote haungefikia athari iliyotaka. Wakati ambapo hatua hizi mbili za kazi Yake zilifanywa Israeli, hakuna kazi yoyote mpya iliyokuwa imefanywa na hakuna kazi yoyote ya Mungu ya kuzindua enzi ilikuwa imewahi kufanywa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hatua hii ya kazi ya kuzindua enzi inafanywa kwanza katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, na zaidi ya hayo, inafanywa kwanza miongoni mwa ukoo wa Moabu; hii imezindua enzi mpya. Mungu amevunja maarifa yoyote yaliyo ndani ya dhana za binadamu na hajaruhusu yoyote yaendelee kuwa hai. Katika kazi Yake ya kushinda Amevunja dhana za binadamu, hiyo njia ya zamani, ya maarifa ya binadamu, Anaruhusu watu waone kuwa kwa Mungu hakuna kanuni, kwamba hakuna kitu kizee kumhusu Mungu, kwamba kazi Anayoifanya ni ya uhuru kabisa, ni huru kabisa, kwamba Yeye yuko sahihi katika chochote Anachofanya. Ni lazima utii kikamilifu kazi yoyote Anayoifanya miongoni mwa viumbe. Kazi yoyote Anayoifanya ni ya maana na inafanywa kulingana na mtazamo Wake na maarifa Yake na sio kulingana na chaguo za watu na dhana za watu. Anafanya yale mambo yaliyo na manufaa kwa kazi Yake; kama kitu hakina manufaa kwa kazi Yake, Hatakifanya, hata kiwe kizuri vipi! Anafanya kazi na kuchagua mpokeaji na eneo la kazi Yake kulingana na maana na madhumuni ya kazi Yake. Hafuati kanuni za zamani, wala Hafuati fomula nzee; badala yake, Anapanga kazi Yake kulingana na umuhimu wa kazi; mwishowe, Anataka kufikia matokeo yake ya kweli na madhumuni yanayotarajiwa. Iwapo huelewi mambo haya sasa, kazi hii haitatimiza matokeo yoyote kwako.
Sikiliza zaidi: Umeme wa Mashariki VITABU 

Jumanne, 4 Septemba 2018

Swahili Christian Movie "Kutamani Sana" (5) - Ni Mahali Gani Ambapo Bwana Ametutayarishia?

Swahili Christian Movie "Kutamani Sana" (5) - Ni Mahali Gani Ambapo Bwana Ametutayarishia?

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu aliahidi, "Naenda kuwatayarishia mahali. Na nikienda kuwatayarishia mahali, nitarudi tena na kuwapokea kwangu; ili mahali nipo, muweze kuwa pia" (Yohana 14:2-3). Watu wengi wanasadiki kwamba Bwana alirudi mbinguni, hivyo ni yakini kwamba Anatutayarishia mahali sisi kule mbinguni. Je, ufahamu huu unaenda sambamba na maneno ya Bwana? Je, ni mafumbo yapi yanapatikana kwenye ahadi hii?
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kurudi kwa Yesu mara ya pili

Alhamisi, 16 Agosti 2018

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (9) - Ushuhuda kutoka kwa Kupitia Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (9) - Ushuhuda kutoka kwa Kupitia Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho

Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli nchini China na anafanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu. Alishinda na kuokoa kundi la watu, na wao ndio ambao wamepata njia ya uzima wa milele. Je, unataka kujua jinsi ambavyo wamepitia hukumu na kuadibiwa kwa Mungu? Je, unataka kujua ni mabadiliko gani ambayo wamepitia kwa kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu? Unaweza kusikia kutoka kwao ukiitazama hii video fupi.
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Hukumu na Kuadibu

Jumamosi, 11 Agosti 2018

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (4) - Kwa nini Mungu Anatekeleza Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho?

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (4) - Kwa nini Mungu Anatekeleza Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho?

Hata ingawa dhambi zetu husamehewa mara tunapokiri imani yetu katika Bwana, mara nyingi bado sisi hutenda dhambi. Hili ni tatizo ambalo huwakanganya waumini wote. Bila kujali tumeamini katika Bwana kwa miaka mingapi, na bila kujali jinsi tunavyotenda maneno ya Bwana au jinsi tunavyotegemea utashi wetu kujizuia, wakati wote bado hatuwezi kujiweka huru kutokana na udhibiti wa asili yetu ya dhambi. Katika mioyo yetu sote tunateseka sana. Tunaweza kufanya nini ili hatimaye kujiweka huru kutokana na udhibiti wa asili yetu ya kishetani na kufikia wokovu wa kweli? Hii video fupi itakusaidia kujibu swali hilo.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,  kutenda ukweli

Alhamisi, 12 Julai 2018

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(3): Wakiacha Wema na Kufuata Uovu

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(3): Wakiacha Wema na Kufuata Uovu

Katika ulimwengu huu wa mioyo mibaya ambapo pesa ni mfalme, ni machaguo yapi ambayo Xiaozhen aliye safi na mzuri aliyafanya, ya maisha na ya kuendelea kuishi …
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wafuasi wa Kristo

Jumapili, 17 Juni 2018

"Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari" (3) - Kufichua Fumbo la Kupata Mwili

"Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari" (3) - Kufichua Fumbo la Kupata Mwili

Ingawa watu wanaomwamini Bwana wote wanajua kwamba Bwana Yesu ni Mungu aliyepata mwili, hata hivyo hakuna kweli anayeweza kuelewa ukweli wa kupata mwili. Imetabiriwa katika Biblia kwamba Bwana atakuja tena katika mwili kuzungumza na kufanya kazi katika siku za mwisho. Kama hatumjui Mungu mwenye mwili, basi hatuna namna ya kukaribisha kuja kwa mara ya pili kwa Bwana. Hivyo, kumjua Mungu mwenye mwili ni muhimu katika kukaribisha kurudi kwa Bwana. Tunapaswaje basi kumjua Mungu mwenye mwili?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Ijumaa, 15 Juni 2018

"Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari" (1) - Umeme wa Mashariki Laitikisa Dunia ya Kidini

"Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari" (1) - Umeme wa Mashariki Laitikisa Dunia ya Kidini

Umeme wa Mashariki—kuonekana na kazi ya Mungu katika siku za mwisho limetikisa makundi na madhehebu yote, na kila aina ya wanadamu wamefichuliwa. Kondoo wengi wazuri katika kanisa wangependelea kuteseka kukamatwa kusikodhibitiwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China ili tu kutafuta na kuchunguza Umeme wa Mashariki. Watu wengine, hata hivyo, wanaamini maneno ya wachungaji na wazee wa kanisa na wanasisitiza kutochunguza Umeme wa Mashariki, huku wengine, licha ya kujua kikamilifu kwamba Umeme wa Mashariki linashuhudia ukweli, hawathubutu kutafuta wala kulichunguza kwa hofu ya kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China. Kwa nini kondoo wazuri kanisani wanaweza kuchunguza Umeme wa Mashariki? Je, wale watu ambao hawawezi kutafuta na kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni hata hivyo? Video hii fupi inakuletea msukumo.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kazi ya Mungu
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Alhamisi, 24 Mei 2018

"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (2) - Namna ya Kumfahamu Mungu Mwenye Mwili

"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (2) - Namna ya Kumfahamu Mungu Mwenye Mwili

Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili kufanya kazi ili kumwokoa mwanadamu. Lakini kwa sababu hatufahamu ukweli wa kupata mwili, tunamchukulia Mungu mwenye mwili kuwa sawa na mwanadamu wa kawaida, hatuwezi kuitambua sauti ya Mungu na tunajua hata kidogo zaidi jinsi ya kumkaribisha Bwana—kufikia kiwango ambacho hata tunaweza kufuata ulimwengu wa dini na nguvu zinazotawala kumkana na kumshutumu Mungu—hali haiwi tofauti na wakati ambapo Mungu alipata mwili kama Bwana Yesu kufanya kazi Yake ya Enzi ya Neema. Kwa hivyo, inaonekana kwamba, kuufahamu ukweli wa kupata mwili ni muhimu sana katika sisi kumjua Mungu. Kwa hiyo kupata mwili ni nini hasa? Ni nini kiini cha kupata mwili?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.