Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumanne, 19 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli. Wataweza tu kuzifundisha roho zao, kuifanya mioyo yao iweze kusonga kwa kawaida karibu na Mungu, na kupata kila mara furaha nyingi mno katika kuwa na Mungu. Watakuwa wamejiwekea mipaka kwa ulimwengu mdogo wa kuwa na mshikamano na Mungu, wasiweze kuelewa kile kilicho katika vina vya ndani kabisa. Watu ambao huishi katika mipaka hii pekee hawana uwezo wa kupiga hatua yoyote kubwa. Wakati wowote, wanaweza kulia, “Aa! Bwana Yesu. Amina!” Wanapokula, wao hulia, “Ee Mungu! Nala na Wewe unakula....” Na ni hivi karibu kila siku. Huu ni utendaji wa nyakati zilizopita, ni utendaji wa kuishi ndani ya roho kila wakati. Huo sio utovu wa adabu? Leo, kama ni wakati wa kutafakari juu ya maneno ya Mungu, unapaswa kuyatafakari, kama ni wakati wa kutia ukweli katika vitendo unapaswa kuuweka katika vitendo, na wakati ni muda wa kutekeleza wajibu wako, unapaswa kuutekeleza. Kufanya utendaji hivyo ni huru kabisa, kunakufungua wewe. Sio kama vile wazee wa dini huomba na kusema neema. Bila shaka, hapo awali, hivi ndivyo watu walioamini katika Mungu walitakiwa kutenda—lakini kutenda kwa njia hii kila mara ni kuliko nyuma kimaendeleo kabisa. Utendaji wa wakati uliopita ni msingi wa utendaji wa leo. Ikiwa kungekuwa na njia kwa utendaji wa nyakati zilizopita, utendaji wa leo utakuwa rahisi zaidi. Kwa hiyo, leo, tunapozungumza juu ya “kumleta Mungu katika maisha halisi,” ni hali gani ya utendaji inatajwa? “Maisha halisi” hasa yanahitaji watu wawe na ubinadamu wa kawaida; kile ambacho watu wanapaswa kuwa nacho ni kile ambacho Mungu anataka kutoka kwao leo. Kuyaleta maneno ya Mungu katika maisha halisi ndiyo maana halisi ya “kumleta Mungu katika maisha halisi.” Leo, watu wanapaswa hasa kujiandaa wenyewe na yafuatayo: Kuhusu suala moja, lazima waendeleze uhodari wao, wafunzwe, waongeze msamiati wao, na kuendeleza ustadi wao wa kusoma; na katika lingine, lazima waishi maisha ya watu wa kawaida. Umerudi tu mbele ya Mungu kutoka ulimwenguni, na lazima kwanza uifunze roho yako, kuufunza moyo wako kuwa na amani mbele ya Mungu. Hili ndilo la msingi kabisa, na pia ni hatua ya kwanza katika kutimiza mabadiliko. Watu wengine ni wepesi kubadilika katika utendaji wao; wao hutafakari ukweli huku wakifua nguo zao, wakielewa ukweli wanaopaswa kuelewa na kanuni wanazopaswa kuweka katika vitendo kwa uhalisi. Katika suala moja, lazima uwe na maisha ya kawaida ya ubinadamu, na katika lingine lazima kuwe na kuingia katika ukweli. Huu ni utendaji bora zaidi kwa maisha halisi.
Zamani, watu walipitia magumu mengi sana, lakini mengine yalikuwa yasiohitajika kwa kweli, kwani mengine yalikuwa mambo ambayo hayakuhitajika kutendwa na mwanadamu. Wanapomleta Mungu katika maisha yao halisi, Mungu kimsingi anahitaji kwamba watu wamwabudu Mungu, wafuatilie ufahamu wa Mungu, na kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu katikati ya ubinadamu wa kawaida. Hawahitajiki kumwomba Mungu mara tu wanapoanza kufagia sakafu, wakihisi ni wadeni Wake wasipofanya hivyo. Utendaji wa leo sio hivyo; ni uliolegezwa na rahisi! Watu hawaambiwi watii mafundisho ya dini. Kila mmoja anapaswa kutenda kulingana na kimo chake mwenyewe: Ikiwa mume wako haamini, mchukulie kama mtu asiyemwamini Mungu, na ikiwa yeye huamini mchukulie kama muumini. Usisisitize kuhusu upendo na uvumilivu, bali kuhusu hekima. Watu wengine huenda kununua mboga, na wanapokuwa wakitembea wao hunong’ona: Ee Mungu! Ni mboga gani ambazo unanikubalia ninunue leo? Naomba usaidizi Wako. Je, nichague ninaponunua? Kisha wao hufikiria: Sitachagua; Mungu ananiambia kwamba nimtukuze Yeye, kwamba nilitukuze jina Lake katika mambo yote, na kwamba watu wote wawe na ushuhuda, kwa hiyo muuzaji akinipa kitu fulani cha kitambo na kilichokauka, bado nitampa Mungu shukrani—nitavumilia! Sisi tuaminio katika Mungu hatuchagui ni mboga gani za kununua. Unafikiri kwamba kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na baada ya kutumia yuan[a] moja kununua mboga ya kitambo iliyo na kuvu, bado unaomba na kusema: Ee Mungu! Bado nitaila mboga hii iliyooza—maadamu Unikubali, nitaila. Je, utendaji kama huu sio wa kipumbavu? Je, huko sio kufuata mafundisho ya dini? Hapo awali, watu walizifundisha roho zao na waliishi ndani ya roho kila wakati, na hili lilihusiana na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Neema. Uchaji Mungu, unyenyekevu, upendo, uvumilivu, kutoa shukrani kwa mambo yote—haya ndiyo yaliyotakiwa kutoka kwa kila muumini katika Enzi ya Neema. Wakati huo, watu walimwomba Mungu katika mambo yote; wangeomba waliponunua nguo, na walipofahamishwa juu ya mkutano, pia wangeomba na kusema: Ee Mungu! Je, Unanikubalia niende au la? Ikiwa unanikubalia kwenda, basi nitayarishie njia iliyonyooka, acha kila kitu kifanyike kwa urahisi. Na ikiwa hunikubalii kwenda, basi nifanye nianguke chini. Walipoomba, walimsihi Mungu. Baada ya kuomba walihisi wasio na utulivu, na hawakuenda. Pia kulikuwa na dada ambao, kwa vile waliogopa kupigwa na waume wao wasiomwamini Mungu wakati ambapo wangerudi, walihisi wasio na utulivu walipoomba—na kwa vile walihisi wasio na utulivu, hawakuenda kwa mkutano. Waliamini hayo yalikuwa mapenzi ya Mungu, ilhali kweli ni kwamba, iwapo wangeenda, hakuna chochote ambacho kingefanyika. Matokeo ni kwamba walikosa mkutano. Haya yote yalisababishwa na ujinga wa watu wenyewe. Watu wanaofanya utendaji kwa njia hii huishi kwa hisia zao wenyewe. Njia hii ya utendaji ina kosa na ni ya kipumbavu, haina udhahiri, na hisia na mawazo yao wenyewe kwa wingi sana. Ukiambiwa kuhusu mkutano, basi nenda, na usipoambiwa, basi usiende; unapoambiwa kuuhusu, hakuna haja ya kumwomba Mungu. Je, hili si rahisi? Ikiwa, leo, unahitaji kununua kipande fulani cha mavazi, basi nenda ukafanye hivyo. Usimwombe Mungu na kusema: Ee Mungu! Leo napaswa kununua kipande fulani cha mavazi, je, Unanikubalia niende au la? Ni aina gani ya mavazi ninayopaswa kununua? Je dada mmoja akija hapa nikiwa nimeenda? Kwa kuomba na kutafakari, unajiambia mwenyewe: “Sitaki kwenda leo, huenda dada fulani akaja hapa.” Ilhali matokeo ni kwamba, kufikia jioni, hakuna aliyekuja hapo, na umekosa mengi. Hata katika Enzi ya Neema, njia hii ya utendaji ilikuwa na makosa na isiyo sahihi. Kwa hiyo, ikiwa watu watafanya utendaji kama katika nyakati zilizopita, hakutakuwa na mabadiliko katika maisha yao. Watakuwa tu watiifu, na hawatatilia maanani upambanuzi, na hawatafanya lolote ila kutii na kuvumilia pasipo kufikiria. Katika wakati huo, watu walisisitiza kuhusu kumtukuza Mungu—lakini Mungu hakupata utukufu wowote kutoka kwao, kwani hawakuwa wameishi kwa kudhihirisha lolote, na hawakuwa wamebadilika. Walijitiisha tu na kujiwekea mipaka wenyewe kulingana na dhana zao wenyewe, na hata miaka mingi ya utendaji haikuleta mabadiliko katika maisha yao; walijua tu kuvumilia, kuwa wanyenyekevu, kupenda, na kusamehe, na hawakupata nuru hata kidogo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Wangemjuaje Mungu?
Watu wataingia tu kwa njia sahihi ya imani katika Mungu ikiwa watamleta Mungu ndani ya maisha yao halisi, na katika maisha yao ya kawaida ya ubinadamu. Leo, maneno ya Mungu yanawaongoza ninyi, na hakuna haja ya kutafuta na kupapasa kama nyakati zilizopita. Wakati ambapo unaweza kutenda kulingana na maneno haya, na unaweza kujichunguza na kujitathmini mwenyewe kulingana na hali ambazo Nimetaja, basi utaweza kubadilika. Haya siyo mafundisho ya dini, lakini kile ambacho Mungu anamtaka mwanadamu afanye. Leo, Nakwambia kiini cha jambo: Jishughulishe tu na kutenda kulingana na maneno Yangu. Matakwa Yangu kwako ni kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, na Nimekwambia hilo tayari; ikiwa unasisitiza kabisa kutenda kwa njia hii, utaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Siku hii ndio wakati wa kuishi katika maneno ya Mungu: Maneno ya Mungu yameeleza yote, yote yamefafanuliwa wazi, na maadamu unaishi kwa maneno ya Mungu, utaishi maisha yaliyo huru kabisa na yaliyokombolewa. Hapo awali, ulipomleta Mungu katika maisha yako halisi, ulipitia mafundisho ya dini na sherehe nyingi sana, ulimwomba Mungu hata katika mambo madogo sana, uliyaweka maneno dhahiri upande mmoja, kutoyasoma, na ukajitolea juhudi zako zote kwa kutafuta—na matokeo kwamba hakukuwa na athari. Chukua mfano wa, kile ulichovaa: Wakati ambapo uliomba, uliliweka jambo hili mikononi mwa Mungu, ukiomba kwamba Mungu achague kitu kinachofaa kwa wewe kuvaa. Mungu aliyasikia maneno haya na kusema: “Unaniomba Nijishughulishe Mimi na tondoti hafifu kama hizi? Ubinadamu wa kawaida na urazini Nilivyokuumbia vimeenda wapi?” Wakati mwingine, mtu fulani atafanya makosa katika matendo yake, na ataamini kwamba amemkosea Mungu, naye huanza kufungwa. Hali za watu wengine ni nzuri sana, lakini wanapofanya kitu fulani kidogo kwa njia isiyo sahihi wao huamini kwamba Mungu anawaadibu. Kwa kweli, hii si kazi ya Mungu, lakini ya akili za watu wenyewe. Wakati mwingine, huwa hakuna kosa lolote na vile unavyopitia tukio, laini wengine husema kwamba unapitia tukio kwa njia isiyo sahihi, na hivyo unategwa—unakuwa mbaya, na mwenye giza ndani. Mara kwa mara, watu wakiwa baridi kwa njia hii, wao huamini kwamba wanaadibiwa na Mungu, lakini Mungu husema: “Sifanyi kazi ya kuadibu ndani yako, ungenilaumuje Mimi hivyo?” Watu ni wabaya sana. Wao pia ni wepesi kuhisi sana mara kwa mara na wao hulalamika kuhusu Mungu mara kwa mara. Mungu hakutaki wewe uteseke, ilhali wewe unajiacha uingie katika hali hiyo. Hakuna thamani katika kuteseka kwa aina hii. Kwa sababu watu hawajui kazi inayofanywa na Mungu, katika mambo mengi wao ni wajinga, na hawawezi kuona kwa dhahiri. Katika nyakati kama hizo, wao hunaswa katika mawazo yao wenyewe, wakiendelea kutegwa zaidi milele. Watu wengine husema kwamba vitu vyote na mambo yote yamo mikononi mwa Mungu—kwa hiyo Mungu hangejua watu wanapokuwa wabaya? bila shaka Mungu hujua. Wakati ambapo unategwa katika dhana za binadamu, Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi ndani yako. Wakati mwingi, watu wengine hutegwa katika hali mbaya, lakini Mimi bado huendelea na kazi Yangu. Kama wewe ni mbaya au mtendaji, Mimi sizuiliwi na wewe—lakini unapaswa kujua kwamba maneno mengi Ninenayo, na kiasi kikubwa sana cha kazi Nifanyayo, huja kwa wingi na haraka kulingana na hali ya watu. Wakati ambapo wewe ni mbaya, hili halizuii kazi ya Roho Mtakatifu. Katika nyakati za kuadibu na kifo, watu wote walitegwa ndani ya hali mbaya, lakini hili halikuizuia kazi Yangu; ulipokuwa mbaya, Roho Mtakatifu aliendelea kufanya kilichohitajika kufanywa ndani ya wengine. Unaweza kuendelea kusimama kwa mwezi mmoja, lakini Naendelea kufanya kazi—chochote ufanyacho katika siku za baadaye au sasa, hakiwezi kuizuia kazi ya Roho Mtakatifu. Hali nyingine mbaya hutokana na udhaifu wa binadamu; wakati ambapo watu hawawezi kweli kufanya jambo au kulielewa, wao huwa wabaya. Kwa mfano, katika nyakati za kuadibu, maneno ya Mungu yalizungumza kuhusu kumpenda Mungu kwa kiwango fulani wakati wa kuadibu—lakini wewe uliamini kwamba huwezi. Wakati wa hali hii watu walihisi hasa wenye huzuni na wakaomboleza, walisikitika kwamba miili yao ilikuwa imepotoshwa vikali na Shetani, na kwamba uhodari wao ulikuwa mbaya sana, walihisi kwamba ilisikitisha kuwa walizaliwa katika mazingira haya. Watu wengine walihisi kwamba wakati ulikuwa umepita sana wa kuamini katika Mungu na kumjua Mungu, na kwamba walikuwa hawastahili kufanywa wakamilifu. Hizi zote ni hali za kawaida.
Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za kutotii, ni mchafu ya kusikitisha, ni kitu kichafu. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi, kuna maonyesho mengi sana ya mwili, na kwa hiyo Mungu hudharau mwili kwa kiwango fulani. Watu wanapoacha uchafu, mambo potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini wakibaki bila kuweza kuachana na uchafu na upotovu, basi bado watamilikiwa na Shetani. Kula njama, udanganyifu, na uhalifu wa watu ni mambo ya Shetani; kwa kukuokoa wewe, Mungu hukutenganisha na mambo haya na kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa, na yote ni kwa sababu ya kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unaishi ukimilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na hutapokea urithi wa Mungu. Mara tu umetakaswa na kufanywa kamili, utakuwa mtakatifu, na utakuwa wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na wa kufurahisha kwa Mungu. Kazi inayofanywa na Mungu leo ni wokovu, na, zaidi ya hayo, ni hukumu, kuadibu, na laana. Ina hali nyingi. Je, maneno mengine ya Mungu sio hukumu na kuadibu tu, bali pia laana? Nazungumza ili kutimiza athari fulani, kuwafanya watu wajijue wenyewe, na sio kuwafisha watu; Moyo Wangu ni kwa ajili yenu. Kuzungumza ni mbinu mmojawapo ambayo Mimi hufanyia kazi, Natumia maneno kuonyesha tabia ya Mungu, na kukuruhusu wewe kuelewa mapenzi ya Mungu. Mwili wako waweze kufa, lakini una roho na nafsi. Kama watu wangekuwa na mwili tu, basi hakungekuwa na maana ya wao kuamini katika Mungu, wala hakungekuwa na maana kwa kazi hii yote ambayo Nimefanya. Leo, Nazungumza juu ya jambo moja na kisha lingine, wakati mmoja Ninachukia mno watu, na wakati mwingine Ninapenda kwa hali ya juu; Nafanya hili kuzibadilisha tabia zako, na kuzigeuza dhana zako.
Siku za mwisho zimefika, na nchi nyingi kutoka upande mmoja wa ulimwengu hadi mwingine ziko katika machafuko, kuna vurugu ya kisiasa, njaa, ndwele, mafuriko, na ukame unaonekana kila mahali, kuna maangamizi katika ulimwengu wa mwanadamu, na Mbingu imetuma msiba hapa chini. Hizi ni ishara za siku za mwisho. Lakini kwa watu, unaonekana kama ulimwengu wa uchangamfu na fahari, ambao unaendelea kuwa hivyo zaidi na zaidi. Watu wanapotazama ulimwengu, mioyo yao inavutiwa nao, na wengine hawawezi kujinasua kutoka kwa ulimwengu; idadi kubwa itadanganywa na wale wanaoshiriki katika hila na uchawi. Usipojitahidi ili kuendelea mbele, na huna maadili, utapeperushwa na wimbi hili lenye dhambi. China ni nchi iliyo nyuma sana kimaendeleo kuliko zote, ni nchi ambayo joka kuu jekundu limelala likiwa limejiviringisha, ina watu wengi zaidi wanaoabudu sanamu na kushiriki katika uchawi, hekalu nyingi zaidi, na ni mahali ambapo pepo wachafu huishi. Ulizaliwa ndani yake, unafurahia manufaa yake, na unapotoshwa na kuteswa nalo, lakini baada ya kupitia kujichungua unaachana nalo na unapatwa kabisa na Mungu. Huu ni utukufu wa Mungu, na kwa hiyo hatua hii ya kazi ina umuhimu mkubwa. Mungu amefanya kazi ya kiwango kikubwa hivi, amenena maneno mengi sana, na hatimaye Atawapata ninyi kabisa—hii ni sehemu moja ya kazi ya usimamizi wa Mungu, na ni “mateka ya ushindi” ya vita dhidi ya Shetani. Kadri watu hawa wanavyokuwa bora na kadri maisha ya kanisa yanavyokuwa thabiti, ndivyo joka kuu jekundu linavyotiishwa. Haya ni mambo ya ulimwengu wa kiroho, ni vita vya ulimwengu wa kiroho, na Mungu anapokuwa mshindi, Shetani ataaibishwa na kuanguka chini. Hatua hii ya kazi ya Mungu ina umuhimu wa ajabu. Kazi ya kiwango kikubwa hivyo huokoa kabisa kikundi hiki cha watu; unaponyoka kutoka kwa ushawishi wa Shetani, unaishi katika nchi takatifu, unaishi katika nuru ya Mungu, na hapo kuna uongozi na mwongozo wa nuru, na kisha kuna maana katika kuwa kwako hai. Mnachokula na kuvaa ni tofauti na wao; mnafurahia maneno ya Mungu, na kuishi maisha yenye maana—na wao hufurahia nini? Wao hufurahia tu urithi wa babu zao na “roho ya kitaifa.” Hawana hata dalili ndogo kabisa ya ubinadamu! Mavazi, maneno, na matendo yenu vyote ni tofauti na vyao. Hatimaye, mtaacha kabisa uchafu, hamtategwa tena na ushawishi wa Shetani, na mtapata upaji wa Mungu wa kila siku. Mnapaswa kila mara kuwa waangalifu. Ingawa mnaishi mahali pachafu hamjawekwa mawaa na uchafu na mnaweza kuishi ubavuni mwa Mungu, mkipokea ulinzi Wake mkuu. Mmechaguliwa miongoni mwa wote walio katika nchi hii ya manjano. Je, ninyi sio watu waliobarikiwa zaidi? Kama kiumbe aliyeumbwa, unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu na uishi katika mwili mchafu, basi wewe siye mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kama binadamu, unapaswa kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso. Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu, kama Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kinachotolewa na ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya Shetani, na kukanyagiwa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au njia ya kweli, basi ni nini maana ya maisha yako? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale wanaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatatu, 18 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (4)

Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? Kauli ile imeshatimia? Kukubali kwao injili ni kwa mujibu wa Biblia; wao huhubiri injili kulingana na Biblia. Wao huyategemea maneno ya Biblia kumwamini Mungu; bila Biblia, wao hawatamwamini Mungu. Hii ndiyo njia ambayo wao huishi, kuichunguza Biblia hivyo. Wakati ambapo wao huchunguza Biblia tena na kukuuliza wewe kuhusu ufafanuzi, unaweza kusema, “Kwanza, hebu tusithibitishe kila kauli. Badala yake, hebu tuangalie vile Roho Mtakatifu hufanya kazi. Hebu tulinganishe dhidi ya ukweli ili tuone kama njia tunayotembea inakubaliana na kazi ya Roho Mtakatifu, na tutumie kazi ya Roho Mtakatifu kuangalia kwa makini kama njia hiyo ni sahihi. Kuhusu kama kauli hii au kauli ile imeshatimia, sisi binadamu hatupaswi kuingilia. Ni bora kwetu badala yake kuzungumza kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya karibuni zaidi ambayo Mungu anafanya sasa. Biblia ina maneno ya Mungu yaliyonenwa na manabii na maneno yaliyoandikwa na wanadamu waliotumiwa na Mungu wakati huo; ni Mungu Mwenyewe tu ndiye anaweza kueleza maneno hayo, Roho Mtakatifu pekee ndiye anaweza kutambulisha maana ya maneno hayo, na Mungu Mwenyewe tu ndiye anaweza kuivunja mihuri saba na kukifungua kitabu. Wewe si Mungu, na wala Mimi si Mungu, kwa hiyo nani anathubutu kueleza kwa hiari maneno ya Mungu? Je, wewe unathubutu kueleza maneno hayo? Hata kama manabii Yeremia, Yohana na Eliya wangekuwa hapa, hawangethubutu, kwani wao si Mwanakondoo. Ni Mwanakondoo pekee ndiye anaweza kuivunja mihuri saba na kufungua kitabu, na hakuna mwingine awezaye kuyaeleza maneno Yake. Sithubutu kunyang’anya jina la Mungu, seuze kujaribu kuyaeleza maneno ya Mungu. Naweza tu kuwa yule ambaye humtii Mungu. Je, wewe ni Mungu? Hakuna viumbe wa Mungu ambao huthubutu kufungua kitabu au kuyafafanua maneno hayo, na hivyo Sithubutu kuyaeleza pia. Ni bora usijaribu kuyaeleza. Hakuna kati yetu atakayeeleza. Hebu tuzungumze kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu; hili ndilo mwanadamu anaweza kufanya. Najua machache kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, lakini kwa vile Sina uzoefu Wangu binafsi na kazi hiyo, Naweza tu kuizungumzia kwa kiasi kidogo. Kuhusu maneno yaliyonenwa na Isaya au Yesu wakati huo, Sitafanya ufafanuzi. Sijifunzi Biblia; badala yake, Mimi hufuata kazi ya sasa ya Mungu. Wewe kwa kweli unaichukulia Biblia kuwa kitabu kidogo, lakini siyo kweli kwamba kinaweza tu kufunguliwa na Mwanakondoo. Isipokuwa Mwanakondoo, nani mwingine anaweza kufanya hivyo? Wewe si Mwanakondoo, na wala Mimi sithubutu kudai kuwa Mungu Mwenyewe, kwa hiyo hebu tusichambue au kuichunguza Biblia. Bora kujadili kazi ambayo hufanywa na Roho Mtakatifu, yaani, kazi ya sasa ambayo hufanywa na Mungu Mwenyewe. Hebu tuangalie kanuni na kiini cha kazi ya Mungu, kisha tuyaangalie kwa makini dhidi ya hayo kuona kama njia tunayotembea siku hii ni ya kweli. Hebu tulinganishe na hili kama kiwango.” Kama ninyi huhubiri injili, hasa kwa wale walio katika ulimwengu wa kidini, lazima muelewe Biblia na muwe na ujuzi wa hadithi yake ya ndani, la sivyo, hutaweza kuhubiri injili. Mara tu unapopata utambuzi wa taswira kubwa, usiyachunguze maneno ya Biblia yaliyopitwa na wakati, na zungumza tu kuhusu kazi ya Mungu na ukweli wa maisha, kisha utaweza kuwapata wale wanaotafuta kwa roho ya kweli.
Mnafaa kuelewa kazi ya Yehova, sheria Alizoweka, na kanuni ambazo kwazo Aliyaongoza maisha ya mwanadamu, yaliyomo kwenye kazi Aliyofanya kwenye Enzi ya Sheria, kusudio lililomfanya Yeye kuweka wazi zile sheria, umuhimu wa kazi Yake katika Enzi ya Neema, na kazi anayofanya Mungu kwenye awamu hii ya mwisho. Hatua ya kwanza ni kazi ya Enzi ya Sheria, hatua ya pili ni kazi ya Enzi ya Neema, na hatua ya tatu ni kazi ya siku za mwisho. Lazima muelewe awamu hizi za kazi ya Mungu. Tangu mwanzo hadi mwisho, kuna hatua tatu kwa jumla. Ni nini kiini cha kila hatua ya kazi? Ni hatua ngapi hutekelezwa katika kazi ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita? Kila hatua hutekelezwa vipi, na kwa nini kila mojawapo hutekelezwa kwa njia hii? Haya yote ni maswali ya maana sana. Kazi ya kila enzi ni wakilishi. Yehova alitekeleza kazi gani? Mbona Alifanya hivyo? Mbona Aliitwa Yehova? Yesu alitekeleza kazi gani katika Enzi ya Neema, na Alifanyaje hivyo? Ni hali gani za tabia ya Mungu huwakilishwa na kila hatua ya kazi na kila enzi? Ni hali zipi za tabia Yake zilijitokeza katika Enzi ya Sheria? Na katika Enzi ya Neema? Na kisha katika enzi ya mwisho? Haya maswali halisi ni yale ambayo ni lazima myaelewe. Tabia yote ya Mungu imefichuliwa katika mpango wote wa uongozi wa miaka elfu sita. Haikufichuliwa tu katika Enzi ya Neema, ni katika Enzi ya Sheria tu, na zaidi ya hayo, ni katika wakati huu wa siku za mwisho. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inawakilisha hukumu, ghadhabu na kuadibu. Kazi ifanywayo katika siku za mwisho haiwezi kuwekwa mbadala wa kazi ya Enzi ya Sheria ama ile ya Enzi ya Neema. Ingawa, hatua zote tatu zinaungana kuwa kitu kimoja na yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kawaida, utekelezaji wa kazi hizi umegawanyishwa katika enzi tofauti. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inaleta kila kitu mpaka tamati; ile iliyofanywa katika Enzi ya Sheria ni ya mwanzo; na ile iliyofanywa katika Enzi ya Neema ni ya ukombozi. Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita, hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa. Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati. Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, ambayo haiwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafichuliwa kwenu. Mafumbo kama hayo hayawezi kufichuliwa na mwanadamu yeyote. Haijalishi mwanadamu ana maarifa makubwa ya Biblia vipi, yanabaki tu kuwa maneno na si kitu zaidi, kwani mwanadamu haelewi kiini cha Biblia. Mwanadamu anaposoma Biblia, anaweza kupokea baadhi ya ukweli, kueleza baadhi ya maneno ama kuchunguza vifungu maarufu na nukuu, lakini hatawahi kuwa na uwezo wa kunasua maana iliyoko katika maneno hayo, kwani yote aonayo mwanadamu ni maneno yaliyokufa pekee, sio matendo ya kazi ya Yehova na Yesu, na mwanadamu hawezi kufumbua mafumbo ya kazi ya aina hiyo. Kwa hivyo, fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ni fumbo kuu, iliyofichwa zaidi na isiyoshawishika kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuelewa moja kwa moja mapenzi ya Mungu, ama, Yeye Mwenyewe Aeleze na kumfungulia mwanadamu, vinginevyo, yatabaki kuwa mafumbo milele kwa mwanadamu na kubaki mafumbo yaliyofungwa milele. Usiwajali wale walio katika ulimwengu wa kidini; kama hamngeambiwa leo, pia nyinyi hamngeweza kuelewa. Kazi hii ya miaka elfu sita ni ya fumbo zaidi kuliko unabii wote wa manabii. Ni fumbo kuu zaidi tangu uumbaji, na hakuna nabii wa awali ambaye amewahi kuweza kulielewa, kwani fumbo hili hufumbuliwa tu katika enzi ya mwisho na kamwe halijawahi kufichuliwa hapo awali. Mkielewa fumbo hili na muweze kulipokea kwa ukamilifu, wale watu wote wa kidini watashindwa kwa fumbo hili. Hili pekee ndilo kuu zaidi ya maono, lile ambalo mwanadamu hutamani sana kulielewa lakini pia lile ambalo si wazi zaidi kwake. Mlipokuwa katika Enzi ya Neema, hamkujua kazi ambayo ilifanywa na Yesu wala ile ambayo ilifanywa na Yehova. Watu hawakuelewa chochote kuhusu kwa nini Yehova alitangaza sheria, kwa nini Aliwaambia watu wazitii sheria au kwa nini ilikuwa lazima kwa hekalu kujengwa, na sembuse watu kuelewa kwa nini Waisraeli waliongozwa kutoka Misri hadi jangwani na kisha hadi Kanaani. Ni mpaka siku hii ndipo mambo haya yamefichuliwa.
Kazi katika siku za mwisho ni hatua ya mwisho kati ya hizo tatu. Ni kazi ya enzi nyingine mpya na haiwakilishi kazi ya usimamizi mzima. Mpango wa miaka elfu sita umegawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya yote. Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Aliyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja. Kwa hivyo, kama Mungu Alifanya kazi katika Enzi ya Sheria pekee, mwanadamu angemfafanua Mungu na kusema, “Mungu ni Mungu Aliye hekaluni. Ili kumtumikia Mungu, lazima tuvae mavazi ya kikuhani na tuingie hekaluni.” Iwapo kazi katika Enzi ya Neema haingetekelezwa na Enzi ya Sheria ingeendelea mpaka wakati huu wa sasa, mwanadamu hangefahamu kuwa Mungu pia ni mwenye huruma na upendo. Iwapo kazi katika Enzi ya Sheria haingefanywa, na badala yake kazi katika Enzi ya Neema pekee , basi yote ambayo mwanadamu angefahamu ni kwamba Mungu Anakomboa tu mwanadamu na kumsamehe dhambi zake. Wangefahamu tu kuwa Yeye ni mtakatifu na asiye na hatia, kwamba Anaweza kujitoa kafara na kusulubishwa kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu angejua tu kuhusu haya na asiwe na ufahamu wa mambo mengine yoyote. Kwa hivyo kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu. Enzi ya Sheria inawakilisha vipengele vingine, Enzi ya Neema vipengele vingine na enzi hii vipengele vingine. Tabia ya Mungu inaweza tu kuonekana kwa mchanganyiko wa hatua zote tatu. Ni wakati tu mwanadamu anajua hatua hizi tatu ndipo anaweza kuipokea kikamilifu. Hakuna hatua kati ya hizo tatu ambayo inaweza kuachwa. Utaiona tu tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake mara tu utakapozijua hatua hizi tatu za kazi. Ukweli kamba Mungu alikamilisha kazi yake katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kwamba Yeye ni Mungu chini ya sheria tu, na ukweli kamba alikamilisha kazi Yake ya ukombozi haimaanishi kuwa Mungu Atamkomboa mwanadamu milele. Hizi zote ni hitimisho zilizofanywa na mwanadamu kuhusu jambo hilo. Enzi ya Neema ikiwa imefika mwisho, huwezi basi kusema kuwa Mungu ni wa msalaba tu na kuwa msalaba pekee unawakilisha wokovu wa Mungu. Ukifanya hivyo, basi utakuwa unamfasili Mungu. Katika hatua hii, Mungu Anafanya zaidi kazi ya Neno, lakini huwezi kusema kuwa Mungu hajawahi kuwa Mwenye huruma kwa mwanadamu na kwamba yote Aliyoleta ni kuadibu na hukumu. Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu lazima yaelezwe ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kugawanywa kulinga na aina zao. Baada tu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilishwa ndipo mwanadamu atapata kuelewa tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake, kwani usimamizi Wake utakuwa umefika mwisho. Kwa kuwa mmeipitia kazi ya Mungu katika enzi ya mwisho, tabia ya Mungu ni gani? Je, wewe unathubutu kusema kwamba Mungu ni Mungu ambaye hunena maneno tu? Hungeweza kuthubutu kufanya uamuzi huu. Wengine husema kwamba Mungu ni Mungu ambaye hufumbua mafumbo, kwamba Mungu ni Mwanakondoo na Ambaye huvunja mihuri saba. Hakuna ambaye huthubutu kufanya uamuzi huu. Na kuna wengine ambao husema kwamba Mungu ni aliyepata mwili. Hili bado si sahihi. Wengine husema kwamba Mungu mwenye mwili hunena maneno tu na Hafanyi ishara na maajabu. Wala hungeweza kuthubutu kunena kwa njia hii, kwani Yesu alipata mwili na Alifanya ishara na maajabu, kwa hiyo wewe huthubutu kumfafanua Mungu kwa urahisi. Kazi yote iliyofanyika katika mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita imefika mwisho sasa. Ni baada tu ya kazi hii kubainika wazi kwa mwanadamu na kutekelezwa miongoni mwa wanadamu ndipo watakapofahamu tabia Yake na mali Yake na uwepo. Kazi za enzi hizi zitakapokamilika, mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu yatakuwa yamebainika, ukweli wote ambao haukuwa unaeleweka utawekwa wazi, na mwanadamu atakuwa ameambiwa njia na hatima ya baadaye. Hii ndio kazi yote inayopaswa kufanyika katika hatua hii. Ingawa njia ambayo mwanadamu hutembea leo pia ni njia ya msalaba na ya kuteseka, kile ambacho mwanadamu wa leo hutenda, hula, hunywa na hufurahia ni tofauti zaidi na yale ya mwanadamu aliyekuwa chini ya sheria na katika Enzi ya Neema. Kinachohitajika kutoka kwa mwanadamu wakati huu sio kama ilivyokuwa kitambo na zaidi sio kama kilichohitajika kutoka kwake katika Enzi ya Sheria. Na ni kipi kilichoulizwa kwa mwanadamu chini ya Sheria kazi ilipofanya Israeli? Hawakuulizwa chochote zaidi ya kuiheshimu Sabato na Sheria za Yehova. Lakini si hivyo katika wakati huu. Siku ya Sabato, mwanadamu anafanya kazi, hukusanyika na kuomba kama kawaida, na hakuna vizuizi vinavyowekwa. Wale katika Enzi ya Neema ilibidi wabatizwe, na pia zaidi walitarajiwa kufunga, kuvunja mkate, kunywa divai, kufunika vichwa vyao na kuwaoshea wengine miguu yao. Sasa, sheria hizi zimefutwa na mahitaji makuu yanaulizwa kutoka kwa mwanadamu, kwani kazi ya Mungu inaendelea kuimarika na kuingia kwa mwanadamu kunafika kiwango cha juu. Zamani, Yesu Aliweka mikono Yake juu ya mwanadamu na kuomba, lakini sasa kwamba kila kitu kimesemwa, kuwekelea mikono kuna maana gani? Maneno pekee yanaweza kupata matokeo. Alipowekelea mikono Yake juu ya mwanadamu hapo awali, ilikuwa ni kwa ajili ya kumbariki na kumponya mwanadamu. Hivyo ndivyo Roho Mtakatifu Alivyofanya kazi wakati huo, lakini sio hivyo wakati huu. Wakati huu, Roho Mtakatifu Anatumia maneno katika kazi Yake ili kupata matokeo. Ameyafanya maneno Yake wazi kwenu, na mnapaswa tu kuyaweka katika matendo. Maneno Yake ni mapenzi Yake na yanaonyesha kazi Atakayofanya. Kupitia kwa maneno Yake, utaweza kuelewa mapenzi Yake na yale ambayo Anauliza upate. Unayaweka tu maneno Yake katika matendo moja kwa moja bila haja ya kuwekelea mikono. Wengine wanaweza kusema, “Wekelea mikono Yako juu yangu! Wekelea mikono yako juu yangu ili niweze kupokea baraka zako na kushiriki kwako.” Haya yote ni mazoezi yaliyopitwa na wakati na ambayo yanakataliwa katika wakati huu, kwani enzi zimebadilika. Roho Mtakatifu Anafanya kazi kulingana na enzi, sio tu katika mapenzi Yake ama kulingana na masharti. Enzi zimebadilika, na enzi mpya lazima ilete kazi mpya. Huu ni ukweli wa kila hatua ya kazi, na hivyo kazi Yake haiwezi kurudiwa. Katika Enzi ya Neema, Yesu Alifanya nyingi ya kazi hiyo, kama kuponya magonjwa, kukemea mapepo, kuwekelea mikono Yake juu ya wanadamu, na kumbariki mwanadamu. Hata hivyo, kuendelea kufanya hivyo hakutasaidia chochote katika wakati huu. Roho Mtakatifu Alifanya kazi hivyo katika huo wakati, kwani ilikuwa Enzi ya Neema, na mwanadamu alipewa neema ya kutosha ili afurahie. Mwanadamu hakuhitajika kulipa gharama yoyote na angepokea neema mradi tu angekuwa na imani. Kila mtu alitendewa kwa neema kubwa. Sasa, enzi imebadilika, na kazi ya Mungu imeendelea zaidi; kupitia kuadibu na hukumu Yake, uasi wa mwanadamu na vitu vichafu katika mwanadamu vitatupiliwa mbali. Jinsi ilivyokuwa hatua ya wokovu, ilimbidi Mungu kufanya kazi hiyo, Akimwonyesha mwanadamu neema ya kutosha ili mwanadamu afurahie, ili Amkomboe mwanadamu kutoka kwa dhambi, na kwa neema amsamehe mwanadamu dhambi zake. Hatua hii ya sasa ni ya kufichua udhalimu ulio ndani ya mwanadamu kwa njia ya kuadibu, hukumu, kupigwa na maneno, na vile vile nidhamu na ufunuo wa maneno, ili baadaye binadamu waweze kuokolewa. Hii ni kazi ya undani zaidi kuliko ukombozi. Katika Enzi ya Neema, mwanadamu alifurahia neema ya kutosha na amezoea neema hii, kwa hivyo sio ya kufurahiwa na mwanadamu tena. Kazi kama hii imepitwa na wakati sasa na haitafanyika tena. Sasa, mwanadamu anaokolewa kupitia hukumu ya neno. Baada ya mwanadamu kuhukumiwa, kuadibiwa na kusafishwa, tabia yake basi inabadilika. Je sio kwa sababu ya maneno ambayo Nimenena? Kila hatua ya kazi inafanywa kulingana na maendeleo ya binadamu wote na kwa enzi. Kazi yote ina umuhimu wake; inafanywa kwa ajili ya wokovu wa mwisho, ili binadamu awe na hatima nzuri baadaye, na kwa mwanadamu kugawanywa kulingana na aina Yake mwishowe.
Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini haimaanishi kuwa mwanadamu hana dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia potovu za zamani za kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mwanadamu angeishi katika huo msingi, alichukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, hii ina maana kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia ya kuielekea tabia iliyobadilika; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii inamfanya mwanadamu kuwa safi kupitia neno ili kumpatia mwanadamu njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.
Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu atasikia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili. Kama Mungu hangegeuka na kupata mwili, hakuna mwanadamu mwenye mwili ambaye angepokea wokovu huo mkuu, wala hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwanadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu. Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. Ni mpaka siku za mwisho tu ambapo Mungu Ametakasa binadamu kikamilifu kwa kufanya kazi ya hukumu na kuadibu mwanadamu kwa kuwa muasi, ndipo Mungu atakamilisha kazi Yake ya wokovu na kupumzika. Kwa hivyo, katika hatua tatu za kazi, ni mara mbili tu ndipo Mungu Alikuwa mwili ili kufanya kazi Yake kati ya mwanadamu Mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu moja tu kati ya hatua tatu za kazi ni kuwaongoza wanadamu katika maisha yao, ilhali zingine mbili ni kazi ya wokovu. Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Katika hali hii tu ndipo Ataweza kumpatia mwanadamu wa uumbaji Wake neno la matendo wanalohitaji. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki na mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa maneno yote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili. Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili. Baada ya hapo, kazi ya Mungu mwenye mwili itakuwa imefika mwisho kabisa. Baada ya kupata mwili mara ya pili, hatakuwa mwili tena kwa kazi Yake. Kwani usimamizi Wake wote utakuwa umefika mwisho. Katika siku za mwisho, mwili Wake utakuwa umepata watu Wake teule kabisa, na yote mwanadamu katika siku za mwisho watakuwa wamegawanywa kulingana na aina yao. Hatafanya kazi ya wokovu tena, wala Hatarudi kuwa mwili ili kutekeleza kazi yoyote. Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua binafsi wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado ni ya dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo atakapotwaliwa na Mungu na kutakaswa. Wakati mapepo yalikemewa kutoka kwa mwanadamu na alikombolewa, hii ilimaanisha tu kwamba alipokonywa kutoka kwa mikono ya Shetani na kurudishwa kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi, lakini mwanadamu hana maarifa kumhusu na bado anamkataa na kumsaliti Mungu. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuutupa nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivyo, hata kama sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. Kwa mfano, wakati ambapo watu walijua kwamba walitoka kwa Moabu, walitoa maneno ya malalamiko, hawakutafuta tena uzima, na wakawa baridi kabisa. Je, hili halionyeshi kwamba bado hawawezi kutii kwa ukamilifu kutawaliwa na Mungu? Je, hii siyo tabia ya kishetani ya upotovu kabisa? Ulipokuwa hupitii kuadibu, mikono yako iliinuliwa juu zaidi ya wengine wote, hata ile ya Yesu. Na ulilia kwa sauti kubwa: Kuwa mwana mpendwa wa Mungu! Kuwa mwandani wa Mungu! Ni heri tufe kuliko kumtii Shetani! Muasi Shetani wa zamani! Liasi joka kuu jekundu! Acha joka kuu jekundu lianguke kabisa kutoka mamlakani! Acha Mungu atufanye kamili! Vilio vyako vilikuwa vikubwa zaidi ya wengine. Lakini kisha zikaja nyakati za kuadibu na, mara tena, tabia ya upotovu ya watu ilifichuliwa. Kisha, vilio vyao vikakoma, na hawakuwa tena na azimio. Huu ni upotovu wa mwanadamu; unaingia ndani zaidi kuliko dhambi, ulipandwa na Shetani na umekita mizizi ndani zaidi ya mwanadamu. Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea. Mwanadamu alipiga kelele hivyo wakati uliopita kwa sababu mwanadamu hakuwa na ufahamu wa tabia yake potovu ya asili. Huo ndio uchafu ulio ndani ya mwanadamu. Kotekote katika kipindi kirefu hivyo cha hukumu na kuadibu, mwanadamu aliishi katika mazingira ya mvutano. Je, haya yote hayakutimizwa kupitia kwa neno? Wewe pia hukulia kwa sauti ya juu kabla ya majaribio ya watendaji huduma? Ingia katika ufalme! Wale wote ambao wanalikubali jina hili wataingia katika ufalme! Wote watashiriki Mungu! Wakati ambapo majaribio ya watendaji huduma yalikuja, hukulia tena. Mwanzoni, wote walilia, “Mungu! Popote Uniwekapo, nitatii kuongozwa na Wewe.” Baada ya kusoma maneno ya Mungu, “Nani atakuwa Paulo Wangu?” mwanadamu alisema, “Niko radhi!” Kisha akayaona maneno, “Na kuhusu imani ya Ayubu?” Kwa hiyo akasema, “Niko radhi kuichukua imani ya Ayubu. Mungu, tafadhali nijaribu!” Majaribio ya watendaji huduma yalipokuja, alizirai mara moja na nusura angekosa kusimama tena. Baada ya hilo, uchafu ndani ya moyo wa mwanadamu ulipungua polepole. Je, hili halikutimizwa kupitia kwa neno? Kwa hiyo, kile ambacho mmepitia wakati wa sasa ni matokeo ambayo hutimizwa kupitia kwa neno, hata makuu zaidi ya yale ambayo hutimizwa kupitia kwa Yesu kufanya ishara na maajabu. Utukufu wa Mungu na mamlaka ya Mungu Mwenyewe ambayo ninyi huona hayaonekani tu kupitia kwa usulubishaji, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo, lakini zaidi kupitia kwa hukumu Yake kwa neno. Hili hukuonyesha wewe kwamba sio tu ufanyaji wa ishara, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo ndiyo mamlaka na nguvu za Mungu, bali hukumu kwa neno unaweza kuwakilisha bora mamlaka ya Mungu na kufichua uweza Wake.
Kile ambacho mwanadamu amepata sasa—kimo cha mwanadamu leo, maarifa yao, upendo, uaminifu, utiifu, na pia kuona kwao—ni matokeo yanayopatikana kupitia hukumu kwa neno. Kwamba unaweza kuwa na uaminifu na kubaki umesimama mpaka siku hii ipatikane kwa kupita neno. Hivi sasa mwanadamu anaona kuwa kazi ya Mungu kupata mwili ni ya ajabu kweli. Kuna mengi ambayo hayawezi kupatikana na mwanadamu; ni mafumbo na maajabu. Kwa hivyo, wengi wamejiwasilisha. Wengine hawajawahi kujiwasilisha kwa mwanadamu yeyote kutoka siku za kuzaliwa kwao, ilhali wanapoyaona maneno ya Mungu siku hii, wanajiwasilisha kikamilifu bila kujua wamefanya vile, na hawajaribu kuchunguza au kusema chochote kingine. Binadamu wameanguka chini ya neno na wamesujudu chini ya hukumu kwa neno. Kama Roho wa Mungu angemwongelesha mwanadamu moja kwa moja, wote wangejiwasilisha kwa sauti hiyo, na kuanguka chini bila maneno ya ufunuo, vile Paulo alivyoanguka chini kukiwa na nuru alipokuwa akisafiri kwenda Damaski. Mungu angeendelea kufanya kazi kwa njia hii, mwanadamu hangeweza kutambua upotovu wake kupitia kwa hukumu katika neno na kupata wokovu. Ni kwa kupata mwili pekee ndiyo Ataweza kuwasilisha maneno Yake Mwenyewe kwa masikio ya wale wote ambao wana masikio waweze kuyasikia maneno Yake na kupokea kazi Yake ya hukumu kupitia kwa neno. Hayo tu ndio matokeo yanayopokewa na neno Lake, badala ya kutokea kwa Roho ikimtisha mwanadamu kuwasilisha. Ni kupitia tu kwa kazi ya vitendo na ya ajabu ndio tabia ya mwanadamu, iliyofichika ndani zaidi kwa enzi nyingi, ifichuliwe kabisa ili mwanadamu aitambue na kuibadilisha. Hili ndiyo kazi ya vitendo ya Mungu mwenye mwili wa Mungu; Ananena na kutekeleza hukumu juu ya mwanadamu kupitia kwa neno. Haya ndiyo mamlaka ya Mungu mwenye mwili na umuhimu wa Mungu kupata mwili. Inafanyika kuonyesha mamlaka ya Mungu mwenye mwili, matokeo yanayopatikana na kazi ya neno, na kwamba Roho Amekuja kwa mwili; Anaonyesha mamlaka Yake kupitia hukumu juu ya mwanadamu kwa neno. Ingawa mwili Wake ni hali ya nje ya mwanadamu wa kawaida, ni matokeo ambayo neno Lake linapokea ndiyo yanamwonyesha mwanadamu kuwa Amejaa mamlaka, kwama ni Mungu Mwenyewe na kwamba maneno Yake ni maonyesho ya Mungu Mwenyewe. Hii inaonyesha wanadamu wote kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe Aliyekuwa mwili, na kwamba Asikosewe na yeyote. Hakuna anayeweza kuepuka hukumu Yake kupitia kwa neno, na hakuna nguvu ya giza inayoweza kutamalaki juu ya mamlaka Yake. Mwanadamu anamtii Yeye kabisa kwa sababu Yeye ni Neno aliyepata mwili, kwa sababu ya mamlaka Yake, na kwa sababu ya hukumu Yake kwa neno. Kazi iliyoletwa na mwili Wake uliokuwa mwili ni mamlaka ambayo Anamiliki. Anakuwa mwili kwani mwili pia unaweza kuwa na mamlaka, na Anaweza kutekeleza kazi kati ya wanadamu katika halii ya njia halisi, inayoonekana na kuguswa na mwanadamu. Kazi kama hii ni ya ukweli kuliko kazi ingine yoyote ifanywayo moja kwa moja na Roho wa Mungu Aliye na mamlaka yote, na matokeo Yake ni dhahiri pia. Hii ni kwa sababu mwili Wake unaweza kuongea na kufanya kazi kwa njia halisi; hali ya nje ya mwili Wake haina mamlaka yoyote na inaweza kukaribiwa na mwanadamu. Dutu Yake inabeba mamlaka, lakini mamlaka Yake hayaonekani kwa yeyote. Anaponena na kufanya kazi, mwanadamu hana uwezo wa kutambua uwepo wa mamlaka Yake; hili ni nzuri kwa kazi Yake hata zaidi. Na kazi yote kama hiyo inaweza kupata matokeo. Ingawa hakuna mwanadamu anayefahamu kuwa Anayo mamlaka ama kuona kuwa Hastahili kukosewa ama kuona hasira Yake, kupitia mamlaka Yake yaliyofichika na hasira na hotuba ya uma, Anapata matokeo yaliyotarajiwa ya neno Lake. Kwa maneno mengine, kupitia kwa tani ya sauti Yake, ukali wa hotuba Yake, na hekima ya maneno Yake, mwanadamu anashawishika kabisa. Kwa njia hii, mwanadamu anawasilisha kwa neno la Mungu mwenye mwili wa Mungu, ambaye anaonekana kutokuwa na mamlaka, hivyo kufikia lengo Lake la wokovu kwa mwanadamu. Huu ndio umuhimu mwingine wa kuingia Kwake katika mwili: kuongea na ukweli zaidi na kukubali ukweli wa neno Lake kuwa na athari juu ya mwanadamu ili kushuhudia nguvu ya neno la Mungu. Kwa hivyo kazi hii, isipofanywa kupitia kupata mwili, haitakuwa na matokeo hata kidogo na haitaweza kuokoa watenda dhambi kikamilifu. Mungu Asipokuwa mwili, Atabaki kama Roho bila kuonekana au kuguswa na mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe wa mwili, na mwanadamu na Mungu ni wa dunia mbili tofauti na ni tofauti kwa asili. Roho wa Mungu hana uwiano na mwili wa mwanadamu, na hakuna uhusiano unaoweza kuwepo kati yao; pia, mwanadamu hawezi kuwa roho. Hivyo, Roho wa Mungu lazima ageuke mmoja wa viumbe na kufanya kazi yake ya asili. Mungu anaweza kujipandisha mahali pa juu zaidi na pia aweze kunyenyekea na kuwa mwanadamu aliyeumbwa, kufanya kazi na kuishi kati ya wanadamu, laikini mwanadamu hawezi kupanda juu na kuwa roho na pia kuteremka chini. Kwa hivyo, Mungu lazima awe mwili ili atekeleze kazi Yake. Kama ilivyokuwa wakati wa kuingia katika mwili mara ya kwanza, mwili wa Mungu mwenye mwili pekee ndio unaoweza kumkomboa mwanadamu kupitia kusulubiwa, ilhali hakuna uwezo wa Roho wa Mungu kusulubiwa kama sadaka ya dhambi kwa mwanadamu. Mungu Angekuwa mwili moja kwa moja ili kuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu, lakini mwanadamu hangepanda mbinguni moja kwa moja kuchukua sadaka ambayo Mungu alikuwa amewaandalia. Hivyo, lazima Mungu asafiri kwenda na kurudi kati ya mbingu na nchi, badala ya kumwacha mwanadamu apande mbinguni kuchukua wokovu huu, kwani mwanadamu alikuwa ameanguka na hangepanda mbinguni, ama hata kupata sadaka ya dhambi. Kwa hivyo, ilikuwa lazima kwa Yesu kuja kati ya wanadamu na binafsi kufanya kazi ambayo mwanadamu hangeweza kukamilisha. Kila wakati ambapo Mungu aligeuka kuwa mwili, ilikuwa lazima kabisa Afanye hivyo. Iwapo hatua yoyote ingetekelezwa moja kwa moja na Roho wa Mungu, Hangevumilia ukosefu wa hadhi unaoambatana na kupata mwili.
Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na, mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumia kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na kujua dutu yao. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote. Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno? Katika hatua ya awali, Yesu Alifanya ishara na maajabu, lakini sio hivyo katika hatua hii. Je si kuelewa kwako kwa nini Hafanyi hivyo pia kulipatikana kupitia neno? Kwa hivyo, maneno yanenwayo katika hatua hii, yanashinda kazi iliyofanywa na mitume na manabii wa vizazi vilivyopita. Hata unabii uliotabiriwa na manabii haungeweza kupata matokeo haya. Manabii waliongelea unabii pekee, ya kile kitakachotendeka hapo baadaye, lakini sio kazi ambayo Mungu angefanya katika wakati huo. Hawakuongea kuongoza mwanadamu katika maisha yao, kuhifadhi ukweli juu ya mwanadamu ama kumfichulia mwanadamu mafumbo, ama hata kutawaza maisha. Kwa maneno yaliyonenwa katika hatua hii, kuna unabii na ukweli, lakini hasa yanafanya kazi ya kutawaza maisha juu ya mwanadamu. Maneno ya wakati huu sio kama unabii wa manabii. Hii ni hatua ya kazi isiyo ya unabii ila ya maisha ya mwanadamu, kubadili tabia ya maisha ya mwanadamu. Hatua ya kwanza ilikuwa kazi ya Yehova kutengeneza njia ya mwanadamu kuabudu Mungu duniani. Ilikuwa kazi ya kuanzisha kutafuta chanzo cha kazi duniani. Wakati huo, Yehova aliwafunza Waisraeli kuiheshimu Sabato, kuwaheshimu wazazi wao na kuishi kwa amani na wengine. Hii ilikuwa kwa sababu wanadamu wa wakati huo hawakuwa wanaelewa kiini cha mwanadamu, wala hawakuelewa wanavyopaswa kuishi duniani. Ilikuwa lazima Kwake katika hatua ya kwanza ya kazi kuwaongoza wanadamu katika maisha yao. Yote yale Yehova aliwazungumzia hayakuwa yamewahi kujulikana kwa binadamu ama kuwa katika umiliki wao. Wakati huo, manabii wengi walisimamishwa kuongelea unabii, yote kutengenezwa chini ya uongozi wa Yehova. Hii ilikuwa sehemu ya kazi hiyo. Katika hatua ya kwanza, Mungu hakuwa mwili, hivyo Alizungumza na makabila yote na mataifa kupitia kwa manabii. Yesu alipofanya kazi Yake katika huo wakati, Hakuzungumza sana kama wakati huu wa leo. Kazi hii ya neno katika siku za mwisho haijafanyika katika enzi na vizazi vilivyopita. Ingawa Isaya, Danieli na Yohana walitabiri utabiri mwingi, unabii huo ulikuwa tofauti kabisa na maneno yazungumzwayo sasa. Walichoongelea ulikuwa unabii pekee, lakini maneno ya sasa sio unabii. Iwapo Ningebadilisha Ninayoongea sasa yawe unabii, je mngeweza kuyaelewa? Iwapo ningezungumzia mambo baada ya Mimi kuondoka, utawezaje kupata kuelewa? Kazi ya neno haikuwahi kufanyika wakati wa Yesu ama Enzi ya Sheria. Labda wengine wanaweza kusema, “Je Yehova hakuzungumza maneno pia katika wakati wa kazi Yake? Juu yaa kuponya magonjwa, kukemea mapepo na kufanya ishara na maajabu, je Yesu hakuzungumza katika wakati huo?” Kuna tofauti katika vile maneno yananenwa. Ni nini ndiyo ilikuwa dutu ya maneno yaliyonenwa na Yehova? Alikuwa tu anawaongoza wanadamu katika maisha yao duniani, ambayo hayakuwa yanahusiana na mambo ya kiroho katika maisha. Ni kwa nini inasemekana kuwa maneno ya Yehova yalitangazwa katika sehemu zote? Neno “kufundisha” linamaanisha kuwaambia waziwazi na kuamrisha moja kwa moja. Hakupa mwanadamu maisha; ila, Alimchukua mwanadamu kwa mkono na kumfunza jinsi ya kumheshimu sana. Hakukuwa na mafumbo. Kazi ya Yehova katika Israeli haikuwa kushughulika na ama kumwadhibu mwanadamu ama kutoa hukumu na kuadibu; ilikuwa kuongoza. Yehova alimwambia Musa awaeleze watu Wake wakusanye mana jangwani. Kila asubuhi kabla ya jua kuchomoza, walikuwa wakusanye mana, iliyotosha tu kuliwa siku hiyo. Mana haingewekwa hadi siku inayofuata, kwani ingeoza. Hakuwafunza wanadamu kufichua asili zao, na Hakufichua mawazo yao na fikira. Hakuwabadilisha wanadamu ila tu aliwaongoza katika maisha yao. Katika wakati huo, mwanadamu alikuwa kama mtoto; mwanadamu hakuelewa chochote na angefanya hatua za kuelekezwa; kwa hivyo, Yehova aliamuru tu sheria kuongoza watu.
Iwapo unataka kueneza injili ili wale wote wanaotafuta kwa moyo wa kweli wapate maarifa ya kazi inayofanywa katika siku hii na kushawishika kabisa, lazima uielewe hadithi ya ndani, dutu na umuhimu wa kazi iliyofanywa katika kila hatua. Kwa kusikia ushirika wako, wataelewa kazi ya Yehova na kazi ya Yesu na, zaidi ya hayo, kazi yote ya Mungu wa leo, na vilevile uhusiano na tofauti kati ya hatua hizo tatu za kazi, ili kwamba, baada ya wao kusikiza, wataona kuwa hakuna hatua yoyote kati ya hizo tatu inahitilafiana na nyingine. Kwa hakika, yote yamefanywa na Roho mmoja. Ingawa Wanafanya kazi katika enzi tofauti , maudhui ya kazi Wanayotekeleza ni tofauti, na maneno Wanayozungumza pia ni tafauti, kanuni ambazo Wanafanya kazi nazo ni sawa. Haya ndiyo maono makuu zaidi ambayo watu wote wanapaswa kuelewa.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 17 Februari 2019

Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda

Hatua ya kazi ya watenda-huduma ni hatua ya kwanza ya kazi ya ushindi; kwa sasa hii ni hatua ya pili ya kazi ya ushindi. Kwa nini ukamilifu unajadiliwa katika kazi ya ushindi? Ni kuujenga msingi kwa ajili ya siku za baadaye—kwa sasa hii ni hatua ya mwisho katika kazi ya kushinda, na baada ya hii, kazi ya kuwakamilisha watu itaanza rasmi wakati watakuwa wanapitia dhiki kuu. Jambo la msingi sasa ni ushindi; hata hivyo, hii pia ni hatua ya kwanza ya kukamilisha, kukamilisha ufahamu na utii wa watu, ambayo kwa kweli bado yanajenga msingi wa kazi ya kushinda. Kama unataka kukamilishwa, lazima uwe na uwezo wa kusimama imara katikati ya mateso ya siku za baadaye na uziweke nguvu zako zote katika kupanua hatua yenye kufuata ya kazi. Huku ni kukamilishwa, na huo ndio wakati ambao watu watakuwa wamepatwa na Mungu kabisa. Kile kinachojadiliwa hivi sasa ni kushindwa, ambako pia ni kukamilishwa; hata hivyo, kile kinachofanywa sasa ni msingi wa kukamilishwa katika siku za baadaye. Ili kufanywa mkamilifu, lazima watu wapitie mashaka, na lazima wayapitie juu ya msingi wa kushindwa. Kama watu hawana msingi huu wa sasa, kama hawajashindwa kikamilifu, basi itakuwa vigumu kwao kusimama hadi hatua inayofuata. Kushindwa tu si kufikia lengo la mwisho—ni kushuhudia kwa Mungu tu mbele ya Shetani. Kukamilishwa ni lengo la mwisho, na kama bado hujakamilishwa, basi utahesabiwa kama asiyefaa. Wanapokabiliwa na mashaka katika siku za baadaye, ndipo tu kimo halisi cha watu kitaonekana, yaani, usafi halisi wa upendo wako kwa Mungu utaonekana. Sasa, watu wote husema: “Haidhuru kile Mungu anachofanya sisi tutatii, nasi tuko tayari kuwa foili, kuchochea ukuu wa Mungu, tabia ya Mungu. Haidhuru kama Anaifadhili neema Yake juu yetu au la ama kama Anatulaani au Anatuhukumu, tutatoa shukrani Kwake.” Wewe kusema hili sasa ni ufahamu kiasi tu, lakini kama linaweza kutumika kwa hali halisi linategemea kama ufahamu wako kweli ni wa kweli. Kwamba watu sasa wameona na kueleweka mambo haya ni mafanikio ya kazi ya ushindi; kama unaweza kukamilishwa au la itaonekana hasa wakati mashaka yanakuja juu yako. Wakati huo itaonekana kama una upendo wa kweli kwa Mungu katika moyo wako au la, na kama kweli unao upendo safi kwa ajili Yake, utasema: “Sisi ni foili tu; sisi ni viumbe katika mikono ya Mungu.” Na wakati unapoieneza injili kwa mataifa mengine, utasema: “Mimi ni mtendaji-huduma tu na ni kwa sababu ya tabia zetu potovu ndiyo Mungu alinena sana kiasi kwamba tumeiona tabia Yake ya haki. Kama Mungu hangesema mambo hayo hatungeweza kumwona Yeye, hatungeweza kuionja hekima Yake, na hatungeweza kuupata wokovu mkuu mno, baraka kubwa mno. ”Kama kweli unayo maoni hayo, basi unafanya vizuri. Sasa umesema mambo mengi bila kufikiri na daima unasema wito kwa sauti kubwa: "Sisi ni foili na watenda-huduma; tuko tayari kushindwa na kuwa mashahidi wakubwa sana wa Mungu…” Huwezi tu kupaaza sauti na umalize bila kulifikiria tena, na uthibitishe kwamba wewe ni mtu mwenye kimo. Lazima uwe na ufahamu wa kweli, na ufahamu wako unapaswa kujaribiwa.
Tafakari uzoefu katika kipindi hiki cha wakati na uangalie tena mambo haya ambayo Nimeyasema, kisha uyalinganishe kile unachofanya. Ni kweli kabisa kwamba wewe ni foili kabisa! Ni kiwango gani cha ufahamu ulicho nacho sasa? Mawazo yako, fikra, tabia, maneno na matendo yako, kila kitu ambacho unaishi kwa kudhihirisha—si yot tu ni foili kwa haki na utakatifu wa Mungu? Si kila kitu ambacho kinafunuliwa kiko katika maneno ya sasa ya Mungu kuhusu tabia potovu ya wanadamu? Tabia ya Mungu yenye haki na utakatifu vinaonyesha kupitia mawazo yako na nia zako, na kupitia kwa yale unayoyafunua. Yeye, pia Akiishi katika nchi ya uchafu, hajatiwa waa na uchafu hata kidogo. Anaishi katika dunia ile ile chafu kama wewe, lakini Anamiliki mantiki na umaizi; Anachukia uchafu. Wewe mwenyewe huwezi kuona mambo machafu katika maneno na matendo yako mwenyewe lakini Yeye Anaweza—Anaweza kukuonyesha. Mambo hayo yako ya zamani—ukosefu wako wa kukuza, umaizi, na hisia, maisha yako ya kuelekea nyuma—yote yamefunuliwa kupitia kwa kufichua Kwake kwa mambo hayo sasa. Mungu Amekuja duniani kufanya kazi kwa namna hii, ili watu wauone utakatifu Wake na tabia Yake ya haki. Anakuhukumu na Kukuadibu na Kukufanya ujielewe. Wakati mwingine asili yako yenye pepo mbaya huonekana na Anaweza kukuonyesha. Anakijua kiini cha wanadamu sana. Anaishi kama wewe unavyoishi, Anakula chakula sawa na wewe, Anaishi katika aina ya nyumba kama wewe, lakini Anajua mengi zaidi kukuliko. Lakini kile Anachochukia hasa ni maisha ya filosofia ya watu na upotovu na udanganyifu wao. Anavichukia vitu hivi na Yeye hana nia ya kuvitambua. Yeye hasa anachukia maathiriano ya kimwili ya watu. Ingawa Haelewi kabisa baadhi ya maarifa ya jumla ya maathiriano wa binadamu, Anafahamu kikamilifu wakati ambapo watu wanafichua baadhi ya tabia zao potovu. Katika kazi Yake, Ananena na kuwafundisha watu kupitia mambo haya ndani yao, na kupitia haya Yeye huwahukumu watu na kufichua tabia yake yenye haki na takatifu. Hivi ndivyo watu wanakuwa foili kwa ajili ya kazi Yake. Ni Mungu mwenye mwili tu ambaye Anaweza kufichua kila aina ya tabia potovu za mwanadamu na nyuso zote mbaya za Shetani. Yeye hakuadhibu, Angeweza tu kukufanya wewe uwe foili kwa utakatifu wa Mungu. Huwezi kusimama imara mwenyewe kwa sababu wewe ni mchafu sana. Anaongea kupitia mambo yale ambayo watu wanadhihirisha na Yeye huyafunua ili watu waweze wajue jinsi Mungu ni mtakatifu. Hataacha uchafu hata kidogo ndani ya binadamu, sio hata wazo dogo zaidi chafu katika mioyo yao au maneno na matendo ambayo si sambamba na mapenzi Yake. Kupitia kwa maneno Yake, hakuna uchafu na hakuna kitu ndani ya mtu kitabaki—vyote vitawekwa wazi. Ni hapo tu ndipo utakapoona ya kwamba Yeye kweli yuko tofauti na watu. Anachukizwa kabisa na uchafu hata kidogo zaidi katika wanadamu. Wakati mwingine watu hata hawaelewi, na wanasema: “Kwa nini Wewe una hasira kila mara? Mungu, kwa nini Huujali udhaifu wa wanadamu? Kwa nini Huna msamaha kidogo kwa wanadamu? Kwa nini Hujali hisia za mwanadamu? Unajua jinsi watu walivyo wapotovu, hivyo kwa nini bado Unawatendea watu kwa njia hii?” Anachukizwa na dhambi; Anachukia dhambi. Yeye anachukizwa hasa na uasi wowote unaoweza kuwa ndani yako. Wakati ambapo unafichua tabia ya uasi Anachukizwa kupita kadiri. Ni kwa kupitia mambo haya ambapo tabia Yake na asili vinaweza kuonyeshwa. Unaipolinganisha na wewe mwenyewe, utaona kwamba ingawa Anakula chakula sawa, Anavaa mavazi sawa, na Ana starehe sawa na watu, ingawa Anaishi kandokando na pamoja na watu, Yeye si sawa. Je, hii si maana halisi ya kuwa foili? Ni kupitia mambo haya kwa watu ndiyo maana nguvu kuu ya Mungu inaonekana kwa urahisi sana; ni giza ambalo huchochea kuwepo kwa mwanga wa thamani.
Bila shaka Yeye hawatumii ninyi kwa makusudi kama foili, lakini wakati ambapo kazi hii inaonyesha matokeo, inaonyesha uasi wa wanadamu kama foili kwa ajili ya tabia ya Mungu yenye haki. Ni kwa sababu mmetenda kama foili ndiyo maana mna nafasi ya kujua maonyesho asili ya tabia ya Mungu yenye haki. Ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo maana mmepatwa na hukumu na kuadibu mara kwa mara; lakini pia ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo manaa mmetenda kama foili na mmepata neema kubwa sana ambayo Mungu amewakirimu. Ni uasi wenu ambao ni foili kwa uenyezi na hekima ya Mungu, na ni kwa sababu yake ndipo mmepata wokovu mkuu mno, baraka kubwa mno. Ingawa mmepokea hukumu Yangu mara kwa mara, pia mmepata wokovu mkuu ambao wale waliokuwa mbele yenu hawakuwahi kuupata. Kazi hii ni yenye maana ya ajabu sana kwenu. “Foili” hii kwa kweli ni yenye thamani sana kwenu—ni kwa sababu ya kutenda kama foili ndipo mmepata wokovu na neema. Je, si kuwa aina hii ya foili ya thamani sana? Je, si ni ya maana sana? Ni kwa sababu mnaishi katika ulimwengu sawa na Mungu, kwa sababu mnaishi naye katika nchi chafu ndipo mmekuwa foili Wake na mmepata wokovu wa ajabu sana. Kama Hangekuwa mwili, nani angekuwa na huruma kwenu, na nani angewatunza ninyi watu duni? Nani angewajali ninyi? Kama Mungu mwenye mwili hangekuwa anafanya kazi miongoni mwenu, ni wakati gani ambapo mngeweza kuupata wokovu huu ambao hakuna mtu yeyote amewahi kuupata awali? Kama Nisingekuwa mwili Niwajali na kuzihukumu dhambi zenu, si mgekuwa mmeanguka Kuzimuni muda mrefu uliopita? Kama Nisingekuwa mwili kujinyenyekeza miongoni mwenu, mngekuwa na haki gani kuwa foili kwa tabia ya Mungu yenye haki? Je, hamtendi kama foili kwa sababu Nimekuwa mwili kati yenu ili kwamba muweze kuupata wokovu mkuu mno? Si hiyo kabisa ni kwa sababu Nilikuwa mwili? Kama isingekuwa kwa ajili ya Mungu mwenye mwili akiishi miongoni mwenu, je, mngeweza kugundua kwamba mnaishi katika kuzimu duniani, vibaya zaidi kuliko nguruwe au mbwa? Je, si hukumu na kuadibu ambako mmepata kumekuwa kwa sababu ninyi ni foili kwa ajili ya kazi Yangu katika mwili? Kazi ya kuwa foili inafaa sana kwenu kwa kuwa mmeupata wokovu wa hukumu ya Mungu kwa sababu ya hii. Je, hamhisi kuwa ni baraka ya maisha yenu kuweza kutenda kama foili wenye sifa? Yote ambayo mmeyafanya ni kazi ya kuwa foili, lakini mmepata wokovu ambao hamjawahi kuupata au kufikiri kabla. Kuwa foili ni wajibu wenu sasa, na baraka za milele mtakazozifurahia wakati ujao zitakuwa zawadi mnayostahili. Wokovu mnaoupata si ufahamu wa mara moja au maarifa leo, lakini ni baraka zaidi, mwendelezo wa milele wa maisha. Ingawa ni kupitia kuwa foili ndiyo mnashindwa, mnapaswa kujua kwamba wokovu huu, baraka hii ni kuwapata ninyi kabisa; ni ushindi na pia ili kuwaokoa bora zaidi. Kuwa foili ni ukweli, lakini ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo ninyi ni foili na mmepata baraka ambazo hakuna aliyewahi kuzipata. Leo, mnaona na kusikia, na kesho mtapata, na mtapokea baraka kubwa hata zaidi. Hivyo si kuwa aina hii ya foili jambo muhimu sana? Ni kupitia kwa foili ya tabia zenu za uasi ndiyo kazi ya sasa ya kushinda huzaa matunda, ambayo ni, kilele cha kuadibu na hukumu ya pili ni kuufanya uchafu na uasi wenu kuwa foili ili muweze kuiona tabia ya haki ya Mungu. Wakati mtakapokuwa watiifu kwa mara nyingine tena katika kuadibu na hukumu ya pili, tabia Yake yenye haki yote itafunuliwa wazi kwenu. Hiyo ni, wakati ambapo kukubali kwenu kazi ya ushindi kumefika mwisho utakuwa wakati ambapo mmetimiza wajibu wenu wa kuwa foili. Si kuamua jambo kuwahusu bila kujali kuwajua, lakini ni kuikamilisha kazi ya kwanza ya kushinda kupitia kwa wajibu wenu kama watenda-huduma, ikifichua tabia yenye haki ya Mungu, isiyokosewa. Kupitia kwa kutenda kwenu kama foili, kupitia kwa uasi wenu kama foili, matunda ya kazi ya pili ya ushindi yamepatikana. Tabia Yake yenye haki ambayo haikuwa imefunuliwa kwenu kikamilifu mara ya kwanza sasa imefunguliwa yote juu yenu ili muweze kuiona tabia Yake yote yenye haki, muone yote ambayo Yeye aliye, ambayo ni ya hekima ya kazi Yake, ajabu, na utakatifu na usafi. Matunda haya ya kazi Yake yamefanikishwa kupitia kwa vipindi tofauti vya ushindi pamoja na hatua mbalimbali za hukumu. Kadri hukumu Yake inavyofikia kilele chake, ndivyo Yeye anavyoweza kufichua tabia za uasi za watu na ndivyo Yeye anaweza kufikia matokeo ya ushindi. Tabia Yake yote ya haki imedhihirishwa kutoka miongoni mwa aina hii ya kazi ya kushinda. Kazi ya ushindi imetengwa katika hatua mbili ambazo zinatekelezwa katika nyakati tofauti na ziko katika viwango mbalimbali. Na bila shaka matokeo yanayopatikana pia ni tofauti; ambayo ni, kiwango cha utii wa watu kinakuwa cha kina zaidi na zaidi. Tangu wakati huu kuendelea hatimaye itawezekana kuwaleta watu kwenye njia sahihi ya kukamilishwa. Baada ya kazi yote ya ushindi kukamilika (wakati ambapo hukumu ya pili imepata matokeo yake ya mwisho) hatimaye Mungu hatawahukumu wanadamu tena, lakini atawataka waingie katika njia sahihi ya kupitia maisha. Hii ni kwa sababu hukumu inawakilisha ushindi, na aina ya ushindi ni hukumu na kuadibu.
Ni kwa Mungu kuwa mwili tu katika mahali palipo nyuma mno kimaendeleo na pachafu mno ndiyo Yeye anaweza kudhihirisha ukamilifu wote wa tabia Yake takatifu na yenye haki. Na kupitia kwa nini ndiyo tabia Yake yenye haki inadhihirishwa? Kupitia kwa hukumu ya dhambi za watu, hukumu ya Shetani, karaha kuelekea dhambi, na chuki kwa maadui Zake ambao wanaasi dhidi Yake na kumpinga Yeye. Kile ambacho Nasema leo ni kuhukumu dhambi za watu na maovu yao; ni kulaani uasi wa watu. Udanganyifu na upotovu wao, na maneno na matendo yao, mambo yote ambayo hayako sambamba na mapenzi Yake yatapitia hukumu, na uasi wa watu unaamuliwa kuwa wenye dhambi. Ananena kulingana na kanuni za hukumu, naye anadhihirisha tabia Yake yenye haki kwa kuhukumu maovu yao, kulaani uasi wao, na kufichua nyuso zao zote mbaya. Utakatifu unawakilisha tabia Yake ya haki; utakatifu Wake kwa kweli ni tabia Yake ya haki. Msingi wa maneno Yangu leo ni kuzungumza, kuhukumu, na kufanya kazi ya ushindi kutokana na tabia zenu potovu. Hii pekee ni kazi halisi, na hii pekee ndiyo inaweza kabisa kuufanya utakatifu wa Mungu uonekane kwa urahisi sana. Kama hukuwa na tabia potovu hata kidogo, Mungu hangekuhukumu, pia hungeweza kuiona tabia Yake ya haki. Kwa kuwa una tabia potovu, Mungu hatakuachilia. Ni kupitia kwa hili ndiyo utakatifu wake unafunuliwa. Kama uchafu na uasi wa watu ni mkubwa mno na Aliuona lakini hakusema neno na wala Hakukuhumu wala kukuadibu kwa maovu yako, ingeonyesha kuwa Yeye hakuwa Mungu hata kidogo kwa sababu Yeye hangechukia dhambi, lakini angekuwa tu mchafu kama wanadamu walivyo. Hukumu Yangu kwako leo ni kwa sababu ya uchafu wako; kuadibu Kwangu kwako leo ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako. Si kwa ajili ya kupata mamlaka na ufahari kati yenu wala kuwadhulumu kimakusudi, lakini ni kwa sababu ninyi mnaoishi katika nchi ya uchafu mmepakwa matope na uchafu mwingi sana. Mmepoteza tu uadilifu wenu, ubinadamu wenu, na hamko tofauti na nguruwe wanaoishi katika maeneo maovu mno. Ni kwa sababu ya mambo haya ndani yenu ndiyo mnahukumiwa na kwamba hasira Yake imepatiliziwa juu yenu. Ni kwa sababu ya hukumu hizi ndiyo mmeweza kuona kwamba Mungu ni Mungu mwenye haki, kwamba Mungu ni Mungu mtakatifu. Ni kwa sababu ya utakatifu na haki yake ndiyo Amewahukumu kuwapatilizia hasira Zake juu yenu. Kwa sababu Yeye anaweza kudhihirisha tabia yake ya haki anapotazama uasi wa wanadamu, na kwa sababu Anaweza kudhihirisha utakatifu Wake anapotazama uchafu wa wanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na bila doa, lakini pia Anaishi katika nchi ya uchafu. Kama Yeye angekuwa mtu Anayejitia matope pamoja na watu na kama Asingekuwa na dalili zozote za utakatifu au tabia ya haki, Asingekuwa na sifa kuhukumu uovu wa wanadamu au kuwa hakimu wa wanadamu. Kama mwanadamu angemhukumu mwanadamu, isingekuwa kama kuzaba kofi uso wake wenyewe? Mtu anawezaje kuwa na haki ya kuhukumu aina sawa ya mtu, ambaye ni mchafu tu kama yeye? Yule tu ambaye anaweza kuwahukumu wanadamu wote wachafu ni Mungu mtakatifu Mwenyewe, na mwanadamu angewezaje kuzihukumu dhambi za mwanadamu? Mwanadamu angewezaje kuona dhambi za mwanadamu, na angewezaje kuwa na sifa zinazostahili kumshutumu mwanadamu? Kama Mungu hangekuwa na haki ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, basi Angewezaje kuwa Mungu mwenye haki mwenyewe? Wakati ambapo tabia potovu za watu zinadhihirishwa, Yeye ananena kuwahukumu, na ni wakati huo tu ndipo wanaweza kuona kwamba Yeye ni mtakatifu. Hukumu, kuadibiwa, na mfichuo wa dhambi za wanadamu—hakuna mtu mmoja au kitu kinaweza kuepuka hukumu hii. Yote ambayo ni machafu yanahukumiwa na Yeye. Ni kwa kupitia hili tu ndiyo tabia Yake inasemekana kuwa yenye haki. Vinginevyo, inawezaje kusemwa kwamba ninyi mnastahili kuitwa foili?
Kazi iliyofanywa katika Israeli ni tofauti kabisa na kazi ya leo. Yehova aliyaongoza maisha yao lakini hakuwahukumu wala kuwaadibu almradi inavyofanyika sasa kwa sababu wakati huo, watu walielewa kidogo mno kuhusu mambo ya dunia na walikuwa na tabia chache potovu. Wakati huo, Waisraeli walikuwa wanyenyekevu kwa Yehova katika kila namna. Wakati Alipowaamuru kujenga madhabahu wangeharakisha kufanya hivyo, na Alipowaamuru kuvaa mavazi ya makuhani wangetii. Wakati huo Yehova alikuwa tu kama mchungaji wao akiliongoza kundi la kondoo duniani, na kondoo wote walifuata mahali mchungaji aliwaongoza kula nyasi katika malisho. Yehova Aliyaongoza maisha yao; Alikuwa mwongozo kwa ajili ya chakula chao, mavazi, malazi, na usafiri. Huo haukuwa wakati wa kufichua tabia ya Mungu kwa sababu watu wa wakati huo walikuwa watoto wachanga, na kisha kulikuwa na watu wachache sana ambao walikuwa waasi au wapinzani, nao hawakuwa wametiwa matope mno. Hivyo hawangeweza kuwa foili kwa ajili ya tabia ya Mungu. Utakatifu wa Mungu unafichuliwa kwa watu katika nchi ya uchafu. Na sasa ni uchafu unaofichuliwa na watu katika nchi ya uchafu ambao Mungu huuhukumu. Kwa njia hii, kile Alicho kinaonyeshwa chote katika hukumu Yake. Na kwa nini Yeye huhukumu? Ni kwa sababu Anachukizwa na dhambi, na hivyo Yeye ana uwezo wa kutoa maneno ya hukumu. Kama Yeye hangechukizwa na uasi wa mwanadamu, Angekuwa mwenye ghadhabu sana? Kama hakungekuwa na maudhi, hakuna chuki ndani Yake, ikiwa watu ni waasi lakini hakuwajali, hiyo ingeonyesha kwamba Yeye alikuwa mchafu tu kama wachafu kama wanadamu. Sababu amabyo Yeye ana uwezo wa kuhukumu na kuwaadibu wanadamu ni kwamba Anakuchukizwa na uchafu. Kila kitu ambacho Anachukizwa nacho ni kile Yeye mwenyewe hamiliki. Kama Yeye pia angekuwa na upinzani na uasi ndani ya nafsi Yake, hangechukizwa na watu wapinzani na waasi. Kama Kazi Yake katika siku za mwisho ingekuwa bado inafanywa katika Israeli haingekuwa na umuhimu hata kidogo. Kwa nini kazi ya siku za mwisho inafanywa nchini China, mahali penye giza sana, iliyo nyuma zaidi kimaendeleo? Ni kufichua utakatifu na haki ya Mungu. Kwa ufupi, jinsi mahali palivyo penye giza zaidi ndipo panapoweza kutoa mwanga bora kwa utakatifu Wake. Ukweli ni kwamba kufanya yote haya ni kwa ajili ya kazi ya Mungu. Mnajua tu sasa kwamba Mungu aliye mbinguni ameshuka duniani na anasimama katikati yenu, na Amepewa umuhimu dhidi ya uchafu na uasi wenu, ili muanze kuwa na ufahamu wa Mungu—je, si hili linatia moyo pakubwa? Ukweli ni kwamba ninyi ni kundi la watu nchini China ambao mmechaguliwa, na kwa sababu watu hawa wamechaguliwa na wamefurahia neema ya Mungu, na kwa sababu watu hawa hawafai kufurahia neema Yake nyingi, inaonyesha kwamba yote haya yanatia moyo pakubwa kwenu. Mungu Amejidhihirisha na tabia Yake yote takatifu kwenu, na Ametawaza yote hayo juu yenu, Akiwaruhusu kufurahia baraka tele. Hamjaonja tu tabia Yake yenye haki, lakini la muhimu zaidi, mmeonja wokovu Wake pamoja na ukombozi Wake na upendo usio na kikomo, ili ninyi, wachafu zaidi ya watu wote, mmepokea neema kuu mno—si huku ni kubarikiwa? Je, si huku ni kutiwa moyo na Mungu? Ninyi ni wa hadhi ya chini sana na hamkufaa baraka kuu kama hii, lakini Mungu alikuwa na nia ya kukutia moyo. Je, huoni aibu? Kama huwezi kutimiza wajibu wako, mwishowe utajionea aibu kabisa. Utajiadibu. Kwa sasa Yeye hakuchapi wala kukuadhibu; mwili yako uko salama salimini, lakini mwishowe maneno Yake yatakuletea aibu kwako mwenyewe. Hadi sasa Sijawahi kumwadibu mtu yeyote hadharani. Nimenena kwa ukali, lakini Nimekuwaje kuwaelekea watu? Nimekuwa mwenye faraja, Nimewahimiza, na pia Nimewaonya. Hii haijakuwa kwa lengo lingine zaidi ila kuwaokoa. Inawezekana kuwa kwamba hamueilewi nia Yangu kwa kweli? Ninaposema hivi nyote mnapaswa kuelewa na mnapaswa kutiwa moyo kwa maneno haya. Kunao wengi ambao hatimaye wameelewa hili sasa: Je, baraka hii si kutenda kama kama foili? Je, si kuwa foili jambo lenye baraka kuliko mambo yote? Mwishowe, mtaeneza injili ifuatayo: “Sisi ni foili wa mfano hasa. Watawauliza: “Ni nini maana ya kuwa na foili wa mfano hasa?” Na kisha mtasema: “Sisi ambao tunaikamilisha kazi ya Mungu na kutumika kama foili kwa nguvu za Mungu—ni kupitia kwa uasi wetu ndiyo tunatumika kama foili kwa ajili ya tabia Yake yote yenye haki. Sisi ni vyombo vya huduma na viungo kwa kazi ya mwisho ya Mungu—sisi ni vifaa. “Wanaposikia hivyo, watavutiwa sana. Kisha mtasema: “Sisi pia ni vielelezo na mifano kwa ajili ya kuikamilisha kazi ya ulimwengu mzima, na kuwashinda wanadamu wote. Bila kujali kama ninyi ni watakatifu au wachafu, tumebarikiwa zaidi kuwaliko, kwa sababu tumemwona Mungu. Nguvu ya Mungu imechochewa kupitia nafasi Yake kutushinda sisi, na ni kwa sababu ya uchafu wetu ndipo tabia yake yenye haki imechochewa. Je, mna uwezo wa hilo? Hamna haki! Hii kabisa ni sisi kutiwa moyo na Yeye! Ingawa sisi si wenye kiburi, tuna fahari ya kumtukuza Mungu kwa sababu hakuna mtu mwingine yeyote anaweza kushuhudia ahadi hiyo kubwa mno, na hakuna mtu mwingine yeyote anaweza kufurahia baraka kubwa kama hiyo. Ni ajabu kwamba watu wachafu jinsi hii kweli wanaweza kufanya kazi ya foili katika usimamizi wa Mungu, na kwa kweli tunashukuru zaidi ya maneno yanavyoweza kueleza. Watauliza: “Kwa hiyo basi, kielelezo na mfano ni nini?” Nanyi mtasema: “Sisi ni waasi zaidi miongoni mwa wanadamu wote pamoja na kuwa wachafu mno. Sisi ni wale walio wapotovu kwa undani zaidi na Shetani na wenye maendeleo kidogo mno na binadamu duni kabisa ambao ni wa mwili. Sisi ni wa mfano hasa wenye taswira ya kutumiwa na Shetani. Sasa tumechaguliwa na Mungu kuwa wale ambao wameshindwa kwanza kati ya wanadamu. Tumeiona tabia ya Mungu yenye haki, tumeirithi ahadi Yake, na Yeye atawashinda watu zaidi kupitia kwetu. Hii ndiyo sababu sisi ni vielelezo na mifano kwa wale ambao wameshindwa kati ya wanadamu.” Huu ni ushuhuda wenu bora kabisa, na huu ni uzoefu wenu bora kabisa.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu

Jumamosi, 16 Februari 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (3)

Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, maneno mengi ya Mungu yameshindwa kuanza kustawi. Kuna sababu mbalimbali za huu ubora duni wa tabia, kama vile uharibifu wa mawazo na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeweka maovu mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu; maarifa ya juujuu ya utamaduni, na takribani asilimia tisini na nane ya watu ambao hawana elimu ya utamaduni na, aidha, watu wachache sana wanaopata viwango vya juu vya elimu ya utamaduni, hivyo kimsingi watu hawajui ni nini maana ya Mungu au Roho, bali wana taswira hafifu ya Mungu na isiyoeleweka vizuri kama iliyopatikana kutoka kwa imani ya usihiri; ushawishi wenye madhara ambao maelfu ya miaka ya “roho wa juu sana wa utaifa” umeacha ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu pamoja na fikira za kikabaila ambazo watu wamefungwa nazo na kutiwa minyororo, bila uhuru wowote, na kusababisha watu kutokuwa na hamasa au ustahimilivu, hawana shauku ya kusonga mbele, lakini badala yake wanakuwa baridi na kurudi nyuma, wakiwa na akili ya utumwa ambayo ina nguvu sana. Na kadhalika. Sababu hizi zimetengeneza taswira chafu na mbaya kwa mitazamo ya njozi, mawazo, maadili, na tabia ya binadamu. Inaonekana, wanadamu wanaishi katika dunia ya giza la kutisha, na hakuna anayetafuta kusonga mbele miongoni mwao, hakuna anayefikiria kwenda katika ulimwengu ulio bora. badala yake, wanaridhika na waliyo nayo maishani,[1] kutumia siku zao kuzaa na kuwalea watoto, wakikazana, wakitoka jasho, wakifanya kazi zao, wakiwa na njozi ya kuwa na familia ya raha na yenye furaha, ya upendo wa ndoa, ya watoto wenye upendo, ya maisha yenye furaha katika miaka yao ya uzeeni wanapoishi kwa kudhihirisha maisha yao kwa amani. … Kwa makumi, maelfu, makumi ya maelfu ya miaka hadi sasa, watu wamekuwa wakipoteza muda wao kwa njia hii, hakuna anayetengeneza maisha makamilifu, wanapigana tu wenyewe kwa wenyewe katika ulimwengu huu wa giza, wakipambana kupata umaarufu na utajiri, na kufanyiana njama wao kwa wao. Nani amewahi kutafuta mapenzi ya Mungu? Kuna mtu yeyote aliyewahi kutilia maanani kazi ya Mungu? Sehemu hizi zote za binadamu zinazomilikiwa na ushawishi wa giza zimekuwa asili ya mwanadamu tangu zamani, kwa hiyo ni vigumu sana kutekeleza kazi ya Mungu na hata watu hawana moyo wa kuzingatia kile ambacho Mungu amewaaminia leo. Vyovyote vile, Ninaamini kwamba watu hawatajali Ninapotamka maneno haya kwa vile kile Ninachokisema ni historia ya maelfu ya miaka. Kuzungumza juu ya historia kuna maana ya ukweli na, zaidi ya hayo, kashfa zinazojulikana kwa wote, sasa kuna maana gani kuzungumza kitu ambacho ni kinyume na ukweli? Lakini pia Naamini kwamba watu wenye akili, wanapoona maneno haya, wataamka na kujitahidi kwa ajili ya kuendelea mbele. Mungu hutumaini kwamba wanadamu wanaweza kuishi na kufanya kazi kwa amani na kuridhika huku wakati ule ule wakiweza kumpenda Mungu. Ni mapenzi ya Mungu kwamba binadamu wote waweze kuingia katika raha; zaidi ya hili, kuijaza nchi yote na utukufu wa Mungu ni shauku kubwa ya Mungu. Ni aibu tu kwamba wanadamu husalia washenzi na wasiotambua mambo, waliopotoshwa vibaya sana na Shetani hivi kwamba leo hawafanani tena na binadamu. Kwa hiyo mawazo ya binadamu, uadilifu na elimu huunda kiungo muhimu, pamoja na mafunzo katika kujua kusoma na kuandika utamaduni yakiunda kiungo cha pili, bora zaidi ya kuinua ubora wa tabia wa utamadani wa binadamu na kubadilisha mtazamo wao wa kiroho.
Kwa kweli, Mungu hahitaji mengi kutoka kwa binadamu, lakini kwa sababu pengo kati ya uhodari wa watu na kiwango anachohitaji Mungu ni kikubwa sana, watu wengi sana hutazama tu upande wa matakwa ya Mungu lakini hukosa uwezo wa kuyatimiza. Kipaji cha watu cha asili, pamoja na kile wanachojiandaa nacho baada ya kuzaliwa, kiko mbali sana na kutimiza matakwa ya Mungu. Bali kutambua tu wazo hili si suluhisho la hakika kufanikiwa. Maji ya mbali hayawezi kukata kiu ya sasa hivi. Hata watu wakijifahamu kuwa duni kuliko vumbi, kama hawana azimio la kuuridhisha moyo wa Mungu, sembuse kuifuata njia iliyoko mbele ili kutimiza matakwa ya Mungu, basi maarifa ya aina hiyo yana thamani gani? Je, si kama kuchota maji na chungio—juhudi isiyo na maana? Kiini cha kile Nisemacho kinahusu kuingia; hiyo ndiyo mada kuu.
Wakati wa kuingia kwa mwanadamu, maisha huwa ya kuchosha daima, yaliyojaa sifa za lazima zisizobadilika za maisha ya kiroho, kama vile kufanya maombi, kula na kunywa maneno ya Mungu kiasi, au kufanya mikusanyiko, ili watu wahisi daima kwamba kumwamini Mungu hakuleti raha kuu. Shughuli za kiroho kama hizo kila mara hutekelezwa kwa msingi wa tabia ya asili ya binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani. Ingawa wakati mwingine watu wanaweza kupokea nuru ya Roho Mtakatifu, kufikiri kwao kwa asili, tabia, mitindo ya maisha na mienendo bado imekita mizizi, na kwa hiyo asili yao husalia isiyobadilika. Shughuli za kishirikina ambazo watu wanashughulika nazo ndizo Mungu anazichukia sana. lakini watu wengi bado hawawezi kuachana nazo, wakifikiri kwamba shughuli hizi za kishirikina zimeamriwa na Mungu, na hata leo bado hawajaziacha kabisa. Mambo kama mipango ambayo vijana hufanya kwa ajili ya sherehe za arusi au mahari, zawadi za pesa, dhifa, na maneno mengine na virai vinavyohusiana na matukio ya sherehe; maneno ya zamani ambayo yamerithishwa; shughuli zote za kishirikina zisizokuwa na maana zinazofanywa kwa niaba ya wafu na taratibu za mazishi; yote haya yanachukiwa sana na Mungu. Hata Jumapili (Sabato, kama inavoadhimishwa na Wayahudi) pia inachukiwa naye; mahusiano ya kijamii na mawasiliano ya kidunia kati ya mwanamme na mwanamme pia yanachukiwa na kukataliwa zaidi na Mungu. Hata Sikukuu ya Machipuko na Siku ya Krismasi, ambazo zinajulikana kwa kila mtu, haziamriwi na Mungu, sembuse wanasesere na mapambo (mashairi, keki ya Mwaka Mpya, mafataki, kandili, zawadi za Krismasi, sherehe za Krismasi, na Ushirika Matakatifu) ya sikukuu hizi—je, sio sanamu katika akili za wanadamu? Kumega mkate siku ya Sabato, mvinyo, na kitani nyembamba navyo ni sanamu zaidi. Siku zote za sherehe za kijadi ambazo ni maarufu sana nchini China, kama vile Siku ya kuinua Vichwa vya Joka, Sikukuu ya Mashua ya Joka, Sikukuu ya Majira ya Kati ya Kupukutika, Sikukuu ya Laba, na Siku ya Mwaka Mpya, na sikukuu zisizothibitika katika ulimwengu wa kidini, kama vile Pasaka, Siku ya Ubatizo, na Siku ya Krismasi, zote hizi zimepangwa na kurithishwa kwa watu wengi tangu zama za kale hadi leo, zote hazilingani kabisa na binadamu aliyeumbwa na Mungu. Ni uwezo mkubwa wa fikra za binadamu na dhana bunifu ambazo zimewaruhusu kurithishwa hadi leo. Zinaonekana kuwa hazina kasoro, lakini kwa kweli ni hila ambazo Shetani alifanya kwa binadamu. Kadri Shetani wanavyoishi katika eneo fulani, na kadri eneo hilo lilivyo nyuma kimaendeleo na kutofaa, ndivyo desturi zake za kikabaila zinakuwa nyingi zaidi. Vitu hivi vinawafunga watu kwa nguvu, bila kutoa nafasi kwa ajili ya maendeleo. Sikukuu nyingi katika ulimwengu wa kidini zinaonekana kuonyesha ubunifu mkubwa na zinaonekana kujenga daraja kwa kazi ya Mungu, lakini kweli ni vifungo visivyoshikika ambavyo Shetani hutumia kuwafunga watu ili wasije kumjua Mungu—hizi zote ni hila za ujanja za Shetani. Kwa kweli, hatua ya kazi ya Mungu inapomalizika, tayari Amekwishaharibu zana na mtindo wa wakati huo, bila kuacha alama yoyote. Hata hivyo, “waumini wasalihina” bado wanaabudu vitu hivyo vya kushikika; wakati huo huo wanaacha kile Alicho nacho Mungu, bila hata kukichunguza zaidi, wakionekana wamejawa na upendo wa Mungu lakini kwa uhalisi walimtoa ndani ya nyumba zamani sana na kumweka Shetani mezani kwa ajili ya kumwabudu. Sanamu ya Yesu, Msalaba, Maria, Ubatizo wa Yesu na Karamu ya Mwisho—watu wanavichukulia hivi kama Bwana wa Mbinguni, wanaviabudu wakati wote wakilia kwa sauti kwa kurudiarudia “Mungu Baba.” Je, huu sio utani? Hadi leo, misemo mingi ya kimapokeo kama hiyo iliyorithishwa miongoni mwa wanadamu ni chukizo kwa Mungu; inazuia kabisa njia ya kuendelea mbele kwa Mungu na, zaidi ya hayo, inasababisha vipingamizi vikubwa kwa kuingia kwa mwanadamu. Mbali na kiwango ambacho Shetani amemharibu mwanadamu, sheria ya Witness Lee, uzoefu wa Lawrence, uchunguzi wa Watchman Nee, na kazi ya Paulo, haya yote yameuteka moyo wa mwanadamu. Mungu hana namna ya kufanya kazi kwa wanadamu, kwa sababu ndani yao kuna ubinafsi mwingi, sheria, kanuni, taratibu na mifumo, na vitu kama hivi; vitu hivi, ukiongezea vitendo vya watu vya imani za kishirikina, vimewakamata na kuwaharibu wanadamu. Ni kana kwamba mawazo ya watu ni filamu ya ajabu ya kichimbakazi katika rangi kamili, ikiwa na watu wa ajabu wakiendesha mawingu, ya kubuni sana kiasi cha kuwastaajabisha watu, ikiwaacha watu wametunduwazwa na kupigwa butwaa. Kusema kweli, kazi ambayo Mungu huja kufanya leo ni hasa kushughulikia na kuondoa sifa za ushirikina za binadamu na kugeuza kabisa mtazamo wao wa akili. Kazi ya Mungu sio kile ambacho kimepitishwa kwa vizazi na kuhifadhiwa mpaka leo na binadamu; ni kazi kama ilivyoanzishwa na Yeye binafsi na kukamilishwa na Yeye, bila haja yoyote ya kuurithi urithi wa mwanadamu fulani mkuu wa kiroho, au kurithi kazi yoyote ya asili ya uwakilishi iliyofanywa na Mungu katika enzi nyingine fulani. Binadamu hawahitaji kujishughulisha na jambo lolote kati ya haya. Mungu ana mtindo mwingine leo wa kuzungumza na wa kufanya kazi, kwa hiyo mbona binadamu wajisumbue? Kama wanadamu watatembea njia ya leo katika mkondo wa sasa huku wakiendeleza urithi wa “babu” zao, hawatafikia hatima yao. Mungu huhisi kinyaa sana kwa hali hii hasa ya tabia ya mwanadamu, jinsi Anavyoichukia mno miaka, miezi na siku za ulimwengu wa binadamu.
Njia bora zaidi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu ni kuondoa vitu hivi vyenye sumu kubwa katika mioyo ya wanadamu, kuwaruhusu watu kuanza kubadilisha fikira na maadili yao. Kwanza kabisa, watu wanatakiwa kuona waziwazi kwamba kaida zote hizi za kidini, shughuli za kidini, miaka na miezi, na sikukuu zote ni za kumchukiza Mungu. Wanatakiwa kuwa huru kutoka kwa vifungo hivi vya fikira za kishirikina na kuondoa kila alama ya kishirikina iliyozama kabisa ndani. Mambo haya yote ni sehemu ya kuingia kwa mwanadamu. Mnatakiwa kuelewa kwa nini Mungu huwatoa watu katika ulimwengu usiokuwa na dini, na pia kwa nini Huwatoa katika desturi na kanuni. Hili ndilo lango la kuingia kwenu, na ingawa halina uhusiano na uzoefu wenu wa kiroho, hivi ni vizuizi vikubwa vinavyowazuia kuingia, vinavyowazuia kumjua Mungu. Vinatengeza wavu unaowakamata watu. Watu wengi husoma Biblia sana na wanaweza hata kukariri mafungu mengi kutoka katika Biblia. Katika kuingia kwao leo, watu bila kujua wanaitumia Biblia kupima kazi ya Mungu, kana kwamba msingi wa hatua hii katika kazi ya Mungu ni Biblia na chanzo chake ni Biblia. Kazi ya Mungu inapokuwa sambamba na Biblia, watu huiunga mkono kazi ya Mungu kwa nguvu zote na kumwangalia Mungu kwa taadhima mpya; kazi ya Mungu inapokuwa haifanani na Biblia, watu huwa na dukuduku sana kiasi cha kuanza kutokwa jasho, wakitafuta ndani yake msingi wa kazi ya Mungu; kama kazi ya Mungu haikutajwa katika Biblia, watu watampuuza Mungu. Inaweza kusemwa kwamba, watu wengi wanaikubali kwa hadhari sana, wanatii kwa kusita, na hawajali kuhusu kuijua kazi ya Mungu; na kuhusu mambo yaliyopita, wanashikilia nusu moja na kuacha nusu nyingine. Je, huku kunaweza kuitwa kuingia? Kushikilia vitabu vya wengine kama hazina, na kuvichukulia kama ufunguo wa dhahabu wa kufungua lango la ufalme, watu hawaonyeshi kuvutiwa na matakwa ya Mungu ya leo. Aidha, “wataalamu wengi wenye akili” katika mkono wao wa kushoto wanashikilia maneno ya Mungu, huku katika mkono wa kulia wanashikilia “kazi kuu” za wengine, kana kwamba wanataka kutafuta msingi wa maneno ya Mungu kutoka kwa kazi hizi kuu ili kuthibitisha kwa ukamilifu kwamba maneno ya Mungu ni sahihi, na hata wanatoa ufafanuzi kwa wengine kwa kuunganisha na kazi kuu, kana kwamba walikuwa wanafanya kazi. Kusema kweli, kuna “watafiti wa kisayansi” wengi miongoni mwa wanadamu ambao hawajawahi heshimu mafanikio makubwa ya kisayansi ya leo, mafanikio ya kisayansi ambayo hayana kigezo (yaani, kazi ya Mungu, maneno ya Mungu, na njia ya kuingia uzimani), hivyo watu wote “wanajitegemea,” “wakihubiri” mbali sana wakitegemea sana ufasaha wao, wakiringia “jina zuri la Mungu.” Wakati huo huo, kuingia kwao kuko hatarini na umbali wa matakwa ya Mungu unaonekana kuwa mbali sana jinsi uumbaji ulivyo mbali na wakati huu. Ni rahisi kiasi gani kufanya kazi ya Mungu? Inaonekana kwamba watu wamekwishaamua kuacha nusu yao kwa mambo ya zamani na kuleta nusu yao kwa wakati wa leo, kuwasilisha nusu kwa Shetani na kukabidhi nusu kwa Mungu, kana kwamba hii ndiyo njia ya kutuliza dhamiri yao na kuweza kuwa na hisia ya utulivu fulani. Mioyo ya watu inadhuru sana kwa siri, wanaogopa sio tu kupoteza kesho bali pia wanahofia kupoteza jana, wanaogopa sana kumkosea Shetani na kumkosea Mungu wa leo, Anayeonekana kuwa na bado kutokuwa. Kwa sababu watu wameshindwa kukuza vizuri fikira na maadili yao, wanakosa utambuzi kabisa, na kimsingi hawajui kama kazi ya leo ni ile ya Mungu au siyo. Pengine ni kwa sababu fikra za kishirikina za watu zimekita mizizi sana kiasi kwamba ushirikina na ukweli, Mungu na sanamu, vimewekwa katika kundi moja; wala hawajali kuvibainisha vitu hivi, na inaonekana kama wametesa bongo zao lakini bado mambo hayo hayajawa wazi. Na hiyo ndio maana wanadamu wamesimama katika njia zao na hawasongi mbele tena. Haya yote yanatokea kwa sababu watu hawana elimu ya itikadi ambayo ni sahihi, kitu ambacho husababisha ugumu katika kuingia kwao. Na matokeo yake, watu wanapoteza mvuto kabisa katika kazi ya Mungu wa kweli, bali wanashikilia kwa kung’ang’ania[2] kazi ya mwanadamu (kama vile watu wanaotazamwa kuwa ni watu wakubwa) kana kwamba imepigwa muhuri. Je, hizi si mada mpya kabisa ambazo wanadamu wanapaswa kuingia ndani?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili