Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maisha-ya-Kanisa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maisha-ya-Kanisa. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 16 Septemba 2018

Filamu za Kikristo "Wokovu" | Does Forgiveness of Sins Mean Full Salvation?

Filamu za Kikristo "Wokovu" | Does Forgiveness of Sins Mean Full Salvation?

Wokovu ni nini? Wale wanaoamini katika Bwana Yesu hufikiria kwamba ikiwa wataomba kwa dhati kwa Bwana, waungame dhambi zao, na kutubu, dhambi zao zitasamehewa, na watapewa wokovu, na Bwana Atakapokuja, wao watainuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni. Lakini je, wokovu kweli ni rahisi hivyo?
Shujaa katika filamu, Xu Zhiqian, ameamini katika Mungu kwa miaka mingi, akijitolea kwa shauku kwa Mungu, na kuacha kila kitu ili kutenda wajibu wake. Kwa ajili ya hili, alikamatwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China. Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, aliendelea kutekeleza wajibu wake, alipata uzoefu kidogo wa vitendo, na mahubiri yake na kazi ilitatua matatizo ya matendo kwa ndugu zake. Baadaye, mkewe pia alikamatwa, lakini hakulalamika, kuwa hasi, au kusambaratika.... Yote haya yalimshindia pongezi na sifa kutoka kwa ndugu zake. Xu Zhiqian anaamini kwamba ana uhalisi wa ukweli na kwamba hakuna tatizo kuingia katika ufalme wa mbinguni. Lakini punde tu, jaribio lisilotarajiwa lilimjia—mkewe anakufa chini ya mateso ya polisi wa CCP. Xu Zhiqian, akiwa na wasiwasi, ana dhana, kutoelewana, na malalamishi kuhusu Mungu, vilevile mawazo ya maasi dhidi ya na usaliti kwa Mungu.... Baadaye, wakati anapogundua anamsaliti Mungu, anaanza kutafakari, na kustaajabu kama watu ambao, kama yeye, hupitia majaribio na kisha kulalamika, hukosa kumwelewa Mugu, na humsaliti Mungu hakika huokolewa. Je, wao kweli wanastahili kuingia katika ufalme wa Mungu?
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video

Alhamisi, 23 Agosti 2018

Latest Swahili Christian Video "Kufungulia Moyo Minyororo" | Are We Really in Control of Our Own Fate?

Latest Swahili Christian Video "Kufungulia Moyo Minyororo" | Are We Really in Control of Our Own Fate?

Chen Zhi alizaliwa katika familia iliyokuwa masikini. Shuleni, "Maarifa yanaweza kubadilisha majaliwa yako" na "Majaliwa ya mtu yako mikononi mwake" kama alivyofundishwa na shule ikawa wito wake. Aliamini kuwa almuradi angefanya kazi kwa bidii siku zote, angeweza kuwa bora kuliko wenzake, na kujipatia sifa na umaarufu. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, Chen Zhi alipata kazi iliyolipa vizuri sana katika biashara ya nchi za nje. Hata hivyo, hakuridhika na hali aliyokuwa kwa wakati huo hata kidogo. Ili kutimiza njozi yake ya kuwa bora kuliko wengine, aliacha kazi yake na kuanzisha kampuni yake ya kuuza bidhaa. Lakini nyakati nzuri hazikudumu kwa muda mrefu. Kwa vile operesheni haikuendeshwa vizuri, wateja wakawa wachache, na biashara ya kampuni hiyo ikapungua. Hatimaye, kampuni haikuweza kuendelea kufanya kazi. Baada ya kampuni hiyo kufilisika, Chen Zhi hakuwa na nia ya kukubali kushindwa hata kidogo. Aliamini kwamba kwa kutegemea akili na uwezo wake, alimuradi angevumilia angeweza kurudi. Baadaye, Chen Zhi alianzisha tovuti ya mauzo ya mtandaoni na kuanzisha biashara kwenye Mtandao. Baada ya kujishughulisha kwa miaka kadhaa, hakufaulu bado. Chen Zhi akatumbukia katika lindi kuu la huzuni kubwa na kutojiweza ...
Mnamo mwaka wa 2016, familia ya Chen Zhi ilienda Marekani kuishi. Kwa msaada wa mkewe, alikubali kazi ya siku za mwisho za Mwenyezi Mungu. Kupitia kusoma maneno ya Mungu, Chen Zhi hatimaye alielewa kwamba Mungu anadhibiti majaliwa ya wanadamu, na kwamba mtu hawezi kabisa kubadili hatima yake mwenyewe kutegemea uwezo wake mwenyewe. Alijua pia chanzo cha dhiki ya mwanadamu maishani mwake, na jinsi Shetani amewapotosha wanadamu. Alijua kwamba ikiwa mtu ataishi maisha yenye maana, basi lazima aje mbele za Mungu, akubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu ili kupata utakaso, na kuishi kwa kutegemea maneno ya Mungu, na ni hapo tu ndio atapata sifa ya Mungu . Chen Zhi alielewa ukweli fulani katika maneno ya Mwenyezi Mungu, akaanzisha mtazamo sahihi juu ya maisha, alimwaminia Mungu maisha yake yote, akatii udhibiti wa Mungu na mipangilio Yake, na hatimaye kujiondoa jozi katika nafsi yake ya "Majaliwa ya mtu yako mikononi mwake, "na kupata ufunguliwaji na uhuru. Kutoka wakati huo kuendelea alitembea kwenye njia angavu na sahihi ya maisha.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Maisha ya Kanisa

Jumatano, 4 Julai 2018

Swahili Christian Video 2018 | "Ni Vizuri Sana Kutupa Mbali Pingu za Hadhi" | Wokovu wa Mungu

Swahili Christian Video 2018 | "Ni Vizuri Sana Kutupa Mbali Pingu za Hadhi" | Wokovu wa Mungu

Baada ya Liang Zhi kumwamini Mungu, bila kukoma alitafuta kwa shauku, na kujitosa katika kutimiza wajibu wake. Baada ya miaka kadhaa, alichaguliwa kama kiongozi wa kanisa. Wakati alipokuwa akitekeleza wajibu wake kama kiongozi wa kanisa, aligundua kwamba baadhi ya ndugu walikuwa na uwezo zaidi kumliko, ambayo ilimfanya asiwe na furaha kwa kiasi kwamba alikuwa na wivu kwao. Ili kuokoa uso na kulinda hali yake, alishindana nao kwa siri ili kuona ni nani aliyekuwa bora, na alikimbilia umaarufu na hadhi. Umaarufu na hadhi vilionekana kama pingu zisizoonekana zilizomfunga sana, kumnyima uhuru, kumsababisha afanye mambo kinyume na ukweli na kupinga Mungu. Kwa sababu kutekeleza wajibu wake kulikuwa tu kwa ajili ya umaarufu na hadhi, na si kwa kufuatilia ukweli, matokeo yake ni kwamba alipoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Hakuweza kufanya kazi ya vitendo, na aliondolewa kwenye kazi zake za uongozi na kubadilishwa. Aliteseka sana kama matokeo, na akaja mbele ya Mungu kutafakari juu yake mwenyewe. Baada ya kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, alikuja kutambua kwamba ufuatiliaji wa umaarufu na hadhi uliletwa kabisa na tabia yake ya kishetani ya kiburi na majivuno, na kuabudu mamlaka na ushawishi na hadhi. Alifahamu kuwa kiini cha kutafuta umaarufu na hadhi kilikuwa kufuata njia ya mpinga Kristo. Kama hangetubu na kurekebisha njia zake kote, matokeo ya mwisho yalikuwa kwamba alikusudiwa kuzama ndani ya utupu. Wakati huo huo aliona wazi kwamba imani katika Mungu ilihitaji kutembea kwenye njia ya ufuatiliaji wa ukweli na kutekeleza wajibu wake kwa kujitolea. Baada ya hapo, katika kutekeleza wajibu wake aliambatanisha umuhimu katika ufuatiliaji wa ukweli na kutenda ukweli. Kila wakati ambapo tabia potovu ya kukimbilia umaarufu na hadhi ilitokea, hapo basi alimwomba Mungu akitafuta ukweli na, akikubali hukumu na adabu ya maneno ya Mungu, kulingana na neno la Mungu alifanya mazoezi ya kuutelekeza mwili, na kuweka kwa mpangilio nia yake kutimiza wajibu wake mwenyewe. Bila kujali kama alikuwa na hadhi au la, aliweza kabisa kutekeleza majukumu yake. Pole pole alitupa mbali pingu za hadhi ambazo zilimfunga na hakufuatilia tena umaarufu na hadhi, baada ya kutembea kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu ya kutafuta ukweli na kupokea wokovu.

Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wafuasi wa Kristo

Jumatano, 27 Juni 2018

Gospel Video Swahili (2018) | "Nuru ya Mapambazuko"

Gospel Video Swahili (2018) | "Nuru ya Mapambazuko"

Kama mtoto, Yangwang aliwafuata wazazi wake katika imani yao kwa Bwana, na kama mtu mzima alihudumia Bwana kanisani. Mnamo 2013, kanisa lake lilijiunga na Baraza la Makanisa Ulimwenguni ambalo hutetea uunganishwaji wa kanisa kote ulimwenguni na wingi wa dini. Akisadiki kwamba kusisitiza kwa wachungaji na baraza la wazee wake katika kujiunga na Baraza kulikuwa kuondoka kwa njia ya Bwana na hakuwiani na moyo wa Bwana, hatimaye aliliacha dhehebu lake na kuanza kulitafuta kanisa lililo na kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini, baada ya kuyatembelea makanisa mbalimbali, aligundua kwamba madhehebu yote yalikuwa na ukiwa, na kwamba hakukuwa na nuru katika mahubiri ya wachungaji na mabaraza yao ya wazee. Hakuweza kupata utoaji wa uzima, na roho yake ilikuwa ikinyauka na kugeuka kuwa giza. Kwa maumivu yake, mara nyingi angemuita Bwana, akimwomba Bwana arudiharaka. … Siku moja, alienda mtandaoni kutafutataarifa kuhusu kurudi kwa Bwana, pale alipoiona video ambayo maneno ya Mwenyezi Mungu yalisomwa. Maneno ya Mwenyezi Mungu yaliishtua nafsi yake. Alihisi yalikuwa na mamlaka na nguvu na yalionekana kama sauti ya Mungu. Ili kuamua kama Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, alianza kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kupitia kwa kulisoma neno la Mwenyezi Mungu na kusikia ushirika wa watoaji ushuhuda, aliutatua mkanganyo wake. Aligundua kwamba neno lote la Mwenyezi Mungu ni la ukweli, kwamba kwa hakika ni sauti ya Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu ambaye kurudi kwake alikuwa akisubiri kwa miaka mingi akiutamani. Kwa kuwa, amelisoma neno la Mungu kila siku, hivyo basi kuilisha nafsi yake yenye kiu, na kupokea kwa kweli maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Maisha ya Kanisa

Ijumaa, 22 Juni 2018

Latest Swahili Christian Video "Nuru ya Kweli Yaonekana" | The Good News From God

Latest Swahili Christian Video "Nuru ya Kweli Yaonekana" | The Good News From God

Gangqiang ni Mkristo. Aliona namna upendo wa Bwana na huruma Yake kwa binadamu vilivyo vikubwa, na akaamua mara nyingi kwamba angempenda Bwana, kumridhisha Bwana, kutekeleza neno la Bwana, na kuwa na mwenendo wake binafsi kama mtu anayesifiwa na Bwana. Lakini alipotoa athari ya kimatendo kwa neno la Bwana, aligundua kwamba kwake yeye mwenyewe kulikuwa na mambo mengi potovu na ya uasi-ubinafsi, kiburi, udanganifu, na ulaghai na kadhalika. Tabia hizi potovu zilikuwa zinamrudisha nyuma, na hakuwa na nguvu kamwe za kuyatekeleza maneno ya Bwana. Kwa sababu hii, alikuwa na mfadhaiko kabisa, na mara nyingi alimwita Bwana kwa usadizi. Gangqiang baadaye alienda Marekani kufanya kazi na huko akafahamiana na Dada Zhao wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kupitia kwa mawasiliano ya Dada Zhao na kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na kwa kuyasoma baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu, Gangqiang alipata kujua kwamba Bwana Yesu alikuwa tayari Amerudi, na kwamba Alikuwa ametekeleza kazi ya kuhukumu na kutakasa binadamu, Akimwelekeza binadamu katika njia ya kuitatua asili yake yenye dhambi. Moyo wa Gangqiang ulikuwa umepata nuru, na alikubali kwa furaha kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na akaja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kwa kulisoma neno la Mwenyezi Mungu, aliuelewa ukweli fulani, na maisha yake ya huzuni yaliangazwa na maneno ya Mungu …
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kuonekana kwa Mungu
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.