Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Ijumaa, 15 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Saba

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Saba

Mwenyezi Mungu anasema,“Kuonekana kwa Bwana Yesu kulifanikisha kujali Kwake kwingi kwa minajili ya wafuasi Wake katika ubinadamu na akakupokeza kwa mwili Wake wa kiroho,au unaweza kusema uungu Wake 。Kuonekana Kwake kuliwaruhusu watu kuwa na hali nyingine waliyopitia na hisia walizopitia zinazohusu kujali na utunzaji wa Mungu huku kukithibitisha kwa uthabiti kwamba Mungu Ndiye anayefungua enzi,anayeiendeleza enzi,na Yeye ndiye anayetamatisha enzi。Kupitia kwa Kuonekana Kwake Aliipatia nguvu imani ya watu wote,na kupitia kwa Kuonekana Kwake alithibitishia ulimwengu hoja kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe。Hali hii iliwapa wafuasi Wake uthibitisho wa milele,na kupitia kwa Kuonekana Kwake pia Aliweza kufungua awamu ya kazi Yake katika enzi mpya。“Tazama zaidi:Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu”
Baada ya kushiriki kuhusu haya yote, je, mnao ufahamu wa kweli wa mapenzi ya Mungu? Mungu anaona tukio hili la usimamizi wa binadamu, wa kuwaokoa wanadamu, kama muhimu sana kuliko chochote kingine. Huyafanya mambo haya yote si kwa kutumia akili Zake tu, wala si kwa kutumia maneno Yake tu, na vilevile Yeye hafanyi hivi hususan kwa juujuu tu—Yeye huyafanya mambo haya yote kwa mpango, kwa viwango, na kwa mapenzi Yake. Ni wazi kwamba kazi hii ya kumwokoa binadamu imeshikilia umuhimu mkubwa kwa Mungu na hata binadamu. Haijalishi kazi ilivyo ngumu, haijalishi changamoto ni kubwa jinsi gani, haijalishi binadamu ni wanyonge jinsi gani, au binadamu amekuwa mwasi wa kweli, hakuna chochote kati ya haya ambacho ni kigumu kwa Mungu. Mungu hujibidiisha Mwenyewe, Akitumia jitihada Zake za bidii za kazi na kusimamia kazi ambayo Yeye Mwenyewe Anataka kutekeleza. Yeye pia Anapanga kila kitu na kuwatawala watu wote na kazi ambayo Anataka kukamilisha—hakuna chochote kati ya haya ambacho kimefanywa awali. Ndiyo mara ya kwanza Mungu ametumia mbinu hizi na kulipa gharama kubwa kwa minajili ya mradi huu mkubwa wa kusimamia na kumwokoa mwanadamu. Huku Mungu akiwa Anatekeleza kazi hii, hatua kwa hatua Anawaonyesha binadamu bila kuficha bidii Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, hekima na uweza, na kila dhana ya tabia Yake. Anafichua bila kuacha chochote haya yote kwa mwanadamu kidogo kidogo, Akifichua na kuonyesha mambo haya kwa namna ambayo Hajawahi kufanya awali. Kwa hivyo, katika ulimwengu mzima, mbali na watu ambao Mungu analenga kuwasimamia na kuwaokoa, hakujawahi kuwepo na viumbe vyovyote vilivyo karibu na Mungu, ambavyo vinao uhusiano wa karibu sana na Yeye. Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipia gharama ya juu na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa bila kukoma na wao, Hakati tamaa na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …
Baada ya kusikia haya yote leo, mnaweza kuhisi kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni kawaida sana. Yaonekana kwamba binadamu siku zote wamehisi mapenzi fulani ya Mungu kwao kutokana na matamshi Yake na pia kazi Yake, lakini siku zote kuna umbali fulani katikati ya hisia zao au maarifa yao na kile ambacho Mungu anafikiria. Kwa hivyo, Nafikiri ni muhimu kuwasiliana na watu wote kuhusu ni kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu, na maelezo zaidi yanayoonyesha tamanio Lake la kuwapata watu aliokuwa Akitumainia. Ni muhimu kushiriki habari hii na kila mmoja, ili kila mmoja aweze kuwa wazi moyoni mwake. Kwa sababu kila fikira na wazo la Mungu, na kila awamu na kila kipindi cha kazi Yake vinafungamana ndani ya, na vyote hivi vimeunganishwa kwa karibu na, usimamizi Wake mzima wa kazi, unapoelewa fikira na mawazo ya Mungu, na mapenzi Yake katika kila hatua ya kazi Yake, ni sawa na ufahamu wa chanzo cha kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Ni katika msingi huu ndipo ufahamu wako wa Mungu unapoanza kuwa wa kina. Ingawa kila kitu ambacho Mungu alifanya Alipoumba kwanza ulimwengu ambacho Nilitaja awali ni taarifa fulani tu kwa watu sasa na yaonekana kwamba hayana umuhimu sana katika utafutaji wa ukweli, katika mkondo wa kile ambacho utapitia kutakuwa na siku ambapo hutafikiria kuwa ni jambo rahisi sana kama mkusanyiko tu wa taarifa, wala kwamba ni kitu rahisi sana kama mafumbo fulani. Kwa kadri maisha yako yanavyoendelea na pale ambapo pana msimamo kidogo wa Mungu katika moyo wako, au unapokuja kuelewa waziwazi na kwa kina mapenzi Yake, utaweza kuelewa kwa kweli umuhimu na haja ya kile Ninachozungumzia leo. Haijalishi ni kwa kiwango kipi umeyakubali haya; ni muhimu kwamba uelewe na ujue mambo haya. Wakati Mungu anapofanya jambo, wakati Anapotekeleza kazi Yake, haijalishi kama amefanya na mawazo Yake au kwa mikono Yake, haijalishi kama ni mara ya kwanza ambapo Amelifanya au kama ni mara ya mwisho—mwishowe, Mungu anao mpango, na makusudio Yake na fikira Zake vyote vimo katika kila kitu Anachokifanya. Makusudio na fikira hizi vinawakilisha tabia ya Mungu, na vinaonyesha kile Alicho nacho na kile Alicho. Vitu hivi viwili—tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho—lazima vieleweke na kila mmoja. Punde mtu anapoelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho, ataanza kuelewa kwa utaratibu ni kwa nini Mungu anafanya kile Anachofanya na kwa nini Anasema kile Anachosema. Kutokana na hayo, anaweza kuwa na imani zaidi ya kumfuata Mungu, kuufuatilia ukweli, na kufuatilia mabadiliko katika tabia. Hivi ni kusema, ufahamu wa binadamu kuhusu Mungu na imani yake katika Mungu ni vitu viwili visivyoteganishwa.
Hata ingawa kile watu wanachosikia kuhusu au kupata ufahamu huo ni tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, kile wanachofaidi ni maisha yanayotoka kwa Mungu. Baada ya maisha haya kuhemshwa ndani yako, uchaji wako wa Mungu utakuwa mkubwa zaidi na zaidi, na kuvuna mavuno haya kunafanyika kwa kawaida sana. Kama hutaki kuelewa au kujua kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake, kama hutaki hata kutafakari juu ya mambo haya au kuyazingatia, Naweza kukuambia kwa hakika kwamba hiyo njia unayoifuatilia katika imani yako kwa Mungu haitawahi kukuruhusu kuyaridhisha mapenzi Yake au kupata sifa Zake. Zaidi ya hayo, huwezi kamwe kufikia wokovu—hizi ndizo athari za mwisho. Wakati watu hawamwelewi Mungu na hawajui tabia Yake, mioyo yao haiwezi kamwe kuwa wazi Kwake. Punde wanapomwelewa Mungu, wataanza kuelewa na kufurahia kile kilicho moyoni Mwake kwa kivutio na imani. Unapoelewa na kufurahia kile kilichomo ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utaanza kwa utaratibu, kidogokidogo, kuwa wazi Kwake. Wakati moyo wako unakuwa wazi Kwake, utahisi namna ambavyo mabadilishano yako na Mungu yatakavyokuwa ya aibu na duni, madai yako kutoka kwa Mungu na matamanio yako mengi binafsi. Moyo wako unapofunguka kwa kweli kwa Mungu, utaona kwamba moyo Wake ni ulimwengu usio na mwisho, na utaingia katika ulimwengu ambao hujawahi kuupitia awali. Katika ulimwengu huu hakuna kudanganya, hakuna udanganyifu, hakuna giza, hakuna maovu. Kunao ukweli wa dhati na uaminifu; kunayo nuru na uadilifu tu; kunayo haki na huruma. Umejaa upendo na utunzaji, umejaa rehema na uvumilivu, na kupitia katika ulimwengu huu utahisi shangwe na furaha ya kuwa hai. Mambo haya ndiyo ambayo Atakufichulia utakapoufungua moyo wako kwa Mungu. Hii dunia isiyo na kikomo imejaa hekima ya Mungu, na imejaa kudura Yake; umejaa pia upendo Wake na mamlaka Yake. Hapa unaweza kuona kila kipengele cha kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, ni nini kinachomletea Yeye shangwe, kwa nini Anakuwa na wasiwasi na kwa nini Anakuwa na huzuni, kwa nini Anakuwa na hasira…. Haya ndiyo ambayo kila mmoja anayeufungua moyo wake na kumruhusu Mungu kuingia ndani anaweza kuona. Mungu anaweza tu kuingia katika moyo wako kama utaufungua kwa ajili Yake. Unaweza kuona tu kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na unaweza kuona tu mapenzi Yake kwako, kama Ameingia katika moyo wako. Wakati huo, utagundua kwamba kila kitu kuhusu Mungu ni chenye thamani, kwamba kile Alicho nacho na kile Alicho kina thamani sana ya kuthaminiwa. Ukilinganisha na hayo, watu wanaokuzunguka, vifaa na matukio katika maisha yako, hata wapendwa wako, mwandani wako, na mambo unayopenda, si muhimu sana. Ni madogo mno, na ni ya kiwango cha chini; utahisi kwamba hakuna chombo chochote cha anasa ambacho kitaweza kukuvutia tena, na vitu hivi haviwezi kukufanya kuvilipia gharama yoyote tena. Kwa unyenyekevu wa Mungu utaona ukubwa Wake na mamlaka Yake ya juu; aidha, katika jambo Alilofanya uliloliamini kuwa dogo mno, utaweza kuiona hekima Yake na uvumilivu Wake usio na mwisho, na utaiona subira Yake, uvumilivu Wake na ufahamu Wake kwako. Hili litazaa ndani yako upendo Kwake. Siku hiyo, utahisi kwamba mwanadamu anaishi katika ulimwengu mchafu, kwamba watu walio upande wako na mambo yanayokufanyikia katika maisha yako, na hata kwa wale unaopenda, upendo wao kwako, na ulinzi wao kama ulivyojulikana au kujali kwao kwako havistahili hata kutajwa—Mungu tu ndiye mpendwa wako na ni Mungu tu unayethamini zaidi. Wakati siku hiyo itawadia, Naamini kwamba kutakuwa na baadhi ya watu watakaosema: Upendo wa Mungu ni mkubwa na kiini Chake ni kitakatifu mno—ndani ya Mungu hakuna udanganyifu, hakuna uovu, hakuna wivu, na hakuna mabishano, lakini ni haki tu na uhalisi, na kila kitu Alicho nacho Mungu na kile Alicho vyote vinafaa kutamaniwa na binadamu. Binadamu wanafaa kujitahidi na kuwa na hamu ya kuvipata. Ni kwa msingi gani ndipo uwezo wa mwanadamu wa kutimiza haya umejengwa? Unajengwa kwa msingi wa ufahamu wa binadamu wa tabia ya Mungu, na ufahamu wao kuhusu kiini cha Mungu. Hivyo basi kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, ni funzo la maisha yote kwa kila mtu na ni lengo la maisha yote linalofuatiliwa na kila mtu anayelenga kubadilisha tabia yake, na kutamani kumjua Mungu.
Tumezungumza tu kuhusu kazi yote ambayo Mungu amekamilisha, misururu ya mambo Aliyoyafanya kwa mara ya kwanza. Kila mojawapo ya mambo haya yanahusiana na mpango wa Mungu wa usimamizi na mapenzi ya Mungu. Yanahusiana pia na tabia binafsi ya Mungu na kiini Chake. Kama tunataka kuelewa bora zaidi kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho, hatuwezi kukoma katika Agano la Kale au katika Enzi ya Sheria, lakini tunahitaji kusonga mbele pamoja na hatua ambazo Mungu alichukua katika kazi Yake. Hivyo basi, Mungu alipotamatisha Enzi ya Sheria na kuanza Enzi ya Neema, hatua zetu binafsi zimefika katika Enzi ya Neema—enzi iliyojaa neema na ukombozi. Katika enzi hii, Mungu tena Alifanya kitu cha muhimu sana kwa mara ya kwanza. Kazi katika enzi hii mpya kwa Mungu na hata kwa mwanadamu ilikuwa sehemu mpya ya kuanzia. Sehemu hii mpya ya kuanzia ilikuwa tena kazi mpya ambayo Mungu alifanya kwa mara ya kwanza. Kazi hii mpya ilikuwa kitu ambacho hakikuwahi kutokea awali ambacho Mungu alitekeleza na hakikufikirika na binadamu na viumbe vyote. Ni kitu ambacho kwa sasa kinajulikana kwa watu wote—hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu aligeuka kuwa binadamu, mara ya kwanza Alianza kazi mpya kwa umbo la binadamu, Akiwa na utambulisho wa mwanamume. Kazi hii mpya ilionyesha kwamba Mungu alikuwa Amekamilisha kazi Yake katika Enzi ya Sheria, kwamba Asingefanya au kusema tena chochote chini ya sheria. Wala Asingewahi tena kuzungumza au kufanya chochote kwa mfano wa sheria au kulingana na kanuni au masharti ya sheria. Yaani, kazi Yake yote inayotokana na sheria ilisitishwa milele na isingeendelezwa, kwa sababu Mungu alitaka kuanza kazi mpya na kufanya mambo mapya, na mpango Wake kwa mara nyingine tena ulikuwa na sehemu mpya ya kuanzia. Hivyo basi, Mungu lazima Angemwongoza binadamu hadi katika enzi inayofuata.

Alhamisi, 14 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Nne

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Nne

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii:
Uzao: Awamu ya Tano 
1. Mtu Hana Udhibiti wa Hatima ya Uzao Wake 
2. Baada ya Kulea Kizazi Kijacho, Watu Hufaidi Ufahamu Mpya wa Hatima Yao 
3. Kusadiki Katika Hatima si Kibadala cha Maarifa ya Ukuu wa Muumba 
4. Wale tu Wanaonyenyekea Ukuu wa Muumba Ndio Wanaweza Kupata Uhuru wa Kweli
Mwenyezi Mungu alisema,Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka. Hivyo ni kusema kwamba, ni Muumba tu—Mungu Yule wa kipekee—ambaye anaonyeshwa kwa njia hii na ndiye aliye na hali halisi hii. Kwa nini tuzungumzie mamlaka ya Mungu? Mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanatofautiana vipi na mamlaka yaliyomo kwenye akili ya binadamu? Ni nini maalum sana kuyahusu? Na kunao umuhimu gani haswa kuyazungumzia hapa? Kila mmoja wenu lazima aweze kutilia maanani kwa umakinifu suala hili. Kwa watu wengi zaidi, “Mamlaka ya Mungu” ni fikira isiyoeleweka, ile ambayo ni ngumu sana kupata kuielewa, na mazungumzo yoyote kuihusu huenda yasizae matunda mazuri. Kwa hivyo lazima kutakuwepo na pengo kati ya maarifa ya mamlaka ya Mungu ambayo binadamu anaweza kumiliki, na hali halisi ya mamlaka ya Mungu. Ili kuliziba pengo hili, mtu lazima kwa utaratibu aweze kuelewa mamlaka ya Mungu kwa njia ya watu halisi-maishani, matukio, vitu au mambo muhimu yanayopatikana katika uwezo wa binadamu, na ambayo binadamu wanaweza kuyaelewa. Ingawaje kauli hii “Mamlaka ya Mungu” inaweza kuonekana kama isiyoeleweka, mamlaka ya Mungu kwa kweli si ya dhahania kamwe. Yeye yupo na binadamu kila dakika ya maisha yake, akimwongoza kila siku. Kwa hivyo, katika maisha ya kila siku ya kila mtu ataweza haswa kuona na kupitia dhana halisi ya mamlaka ya Mungu. Uhalisi huu ni ithibati tosha kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo, na unakuruhusu kabisa kutambua na kuelewa hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya.
Mungu aliumba kila kitu, na baada ya kukiumba, Anao utawala juu ya kila kitu. Kuongezea kuwa na utawala juu ya kila kitu, pia anadhibiti kila kitu. Wazo hili linamaanisha nini “Mungu anadhibiti kila kitu”? Hali hii inaweza kuelezewa vipi? Hali hii inatumika vipi katika maisha halisi? Mnawezaje kuyajua mamlaka ya Mungu kwa kuelewa hoja hii kwamba “Mungu Anadhibiti kila kitu”? Kutoka kwenye kauli ile ile “Mungu anadhibiti kila kitu” tunafaa kuona kwamba kile ambacho Mungu anadhibiti si sehemu ya sayari, sehemu ya uumbaji, wala sehemu ya mwanadamu, lakini kila kitu: kuanzia kwa viumbe vile vikubwa hadi vile vidogovidogo, kuanzia kwa vile vinavyoonekana hadi visivyoonekana, kuanzia kwa nyota ulimwenguni hadi kwenye vitu vilivyo na uhai ulimwenguni, pamoja na viumbe vidogovidogo visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida au viumbe vilivyo katika maumbo mengine. Huu ndio ufafanuzi hakika wa “kila kitu” ambacho Mungu “anadhibiti,” na ndio upana ambao Mungu anaonyesha ukuu Wake, urefu wa utawala na kanuni Yake.
Kabla ya binadamu hawa kujitokeza, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa uwepo wavyo wote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata ruwaza maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data yenye uhakika; njia ambazo zinasafiria, kasi na ruwaza ya mizingo yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa hakika na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kupotoka hata chembe. Hakuna nguvu inaweza kubadilisha au kutatiza mizingo yazo au ruwaza zao ambazo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum zinazotawala mzunguko wazo na data yenye uhakika inayozifafanua iliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu ruwaza fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje binadamu hawakubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na ruwaza zinazoonyesha mzunguko wavyo, vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Hoja hii inampa binadamu mshawasha wa kukubaliana na kutambua kwamba kunaye Mwenyezi aliye miongoni mwa ruwaza hizi za mzunguko, anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei-kimaumbile lakini zinaamrishwa na Bwana na Mungu. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.
Kwenye kiwango cha mambo madogomadogo, milima, mito, maziwa, bahari, na maeneo ya ardhi yote ambayo binadamu anatazama nchini, misimu yote ambayo yeye anapitia, mambo yote yanayopatikana kwenye ulimwengu, kukiwemo mimea, wanyama, vijiumbe na binadamu, vyote viko chini ya ukuu wa Mungu na vinadhibitiwa na Mungu Mwenyewe. Katika ukuu na udhibiti wa Mungu, vitu vyote vinakuwepo au vinatoweka kulingana na fikira Zake, maisha ya vitu hivi yanatawaliwa na sheria fulani, na vinakua na kuzaana kulingana nazo. Hakuna binadamu au kiumbe chochote kilicho juu ya sheria hizi. Kwa nini hali iko hivi? Jibu la pekee tu ni, kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Au, nikijibu kwa njia nyingine, kwa sababu ya fikira za Mungu na matamshi ya Mungu; kwa sababu Mungu Mwenyewe hufanya haya yote. Hivi ni kusema, ni mamlaka ya Mungu na ni akili ya Mungu ambayo iliunda sheria hizi; zitasonga na kubadilika kulingana na fikira Zake, na kusonga huku na mabadiliko haya yote yanafanyika au kutoweka kwa minajili ya mpango Wake. Hebu tuchukulie magonjwa ya mlipuko, kwa mfano. Yanazuka tu bila onyo, hakuna anayejua asili yake, au sababu maalum zinazoelezea ni kwa nini huwa yanafanyika, na kila wakati magonjwa ya mlipuko yanapofika mahali fulani, wale walio na bahati mbaya hawawezi kukwepa maafa. Sayansi ya binadamu inafafanua na kutuelewesha kwamba magonjwa ya mlipuko yanasababishwa na kuenea kwa vijiumbe maradhi vibaya au haribifu, na kasi yao, eneo lao, na mbinu ya kuenea kwake haiwezi kutabiriwa au kudhibitiwa na sayansi ya binadamu. Ingawaje binadamu huvipinga vijiumbe maradhi hivi kwa kila namna inayowezekana, huwa hauwezi kudhibiti ni watu gani au wanyama gani ambao wanaathiriwa kwa vyovyote vile wakati kunapokuwa na mkurupuko wa magonjwa mlipuko. Kitu cha pekee ambacho binadamu wanaweza kufanya ni kujaribu kuyazuia, kuyapinga, na kuyafanyia utafiti. Lakini hakuna anayejua chanzo asilia kinachoelezea mwanzo au mwisho wa magonjwa mlipuko yoyote ya kibinafsi, na hakuna anayeweza kuyadhibiti. Wakiwa wamekabiliwa na ongezeko na kuenea kwa magonjwa mlipuko, suala la kwanza ambalo binadamu hufanya ni kuunda chanjo, lakini mara nyingi magojwa mlipuko hayo hutoweka kabisa kabla ya hata chanjo kuwa tayari. Kwa nini magonjwa mlipuko hutoweka kabisa? Wengine husema kwamba viini vimeweza kudhibitiwa, wengine husema kwamba vimetoweka kabisa kwa sababu ya mabadiliko katika misimu…. Kuhusiana na ikiwa makisio haya ya kuchanganyikiwa ni kweli au la, sayansi haiwezi kutupa ufafanuzi wowote, na wala haitoi jibu lolote lenye uhakika. Kile ambacho binadamu wanakabiliwa nacho si makisio haya tu lakini pia ukosefu wa mwanadamu katika kuelewa na woga wa magonjwa mlipuko haya. Hakuna anayejua, baada ya kila kitu kuchambuliwa, ni kwa nini magonjwa mlipuko haya huanza au ni kwa nini huisha. Kwa sababu binadamu wanayo imani tu katika sayansi, unategemea pakubwa kwa sayansi hiyo, lakini hautambui mamlaka ya Muumba au kuukubali ukuu Wake, hautawahi kuwa na jibu.
Katika ukuu wa Mungu, mambo yote yapo na huangamia kwa sababu ya mamlaka Yake, kwa sababu ya usimamizi Wake. Baadhi ya mambo huja na kwenda polepole, na binadamu hawezi kutambua ni wapi yalitokea au kung’amua sheria ambazo mambo haya hufuata, sisemi hata kuelewa sababu za mambo haya kuja na kwenda. Ingawaje binadamu anaweza kushuhudia, kusikia, au kupitia yote yanayokuja na kuisha miongoni mwa mambo yote; ingawaje mambo haya yanao mwelekeo kwa binadamu, na ingawaje binadamu hung'amua kupitia kwa yaliyofichika akilini mwake, hali isiyokuwa ya kawaida, hali ya mara kwa mara au hata hali ya ajabu ya mambo mbalimbali, bado hajui chochote kuhusu mapenzi ya Muumba na akili Yake ambavyo vinaelezea mambo hayo. Kunazo hadithi nyingi zinazotokana na haya mambo yote, ukweli mwingi uliofichwa. Kwa sababu binadamu amepotoka na kwenda mbali na Muumba, kwa sababu hakubali hoja hii kwamba Mamlaka ya Muumba ndiyo hutawala mambo yote, hatawahi kujua kila kitu kinachofanyika katika ukuu Wake. Kwa sehemu nyingi zaidi, udhibiti na ukuu wa Mungu huzidi mipaka ya fikra ya binadamu, maarifa ya binadamu, kuelewa kwa binadamu, kuhusu kile ambacho sayansi ya binadamu inaweza kutimiza; uwezo wa binadamu walioundwa hauwezi kushindana nao. Baadhi ya watu husema “Kwa sababu hujashuhudia ukuu wa Mungu wewe mwenyewe, unawezaje kusadiki kwamba kila kitu kinatokana na mamlaka Yake?” Kuona si kuamini kila mara; kuona si kutambua na kuelewa kila mara. Kwa hivyo “sadiki” hutokea wapi? Ninaweza kusema kwa uhakika, “Sadiki inatokana na kiwango na kina cha kuelewa kwa watu kwa, na hali wanayopitia wao, uhalisi na chanzo kikuu cha mambo.” Kama unasadiki kwamba Mungu yupo, lakini huwezi kutambua, na wala huwezi kuelewa, hoja ya udhibiti wa Mungu na ukuu wa Mungu katika mambo yote, basi katika moyo wako hutawahi kukubali kwamba Mungu anayo mamlaka kama haya na kwamba mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Hutawahi kukubali kwa kweli Muumba kuwa Bwana wako, Mungu wako.
Sikiliza zaidi:

Jumanne, 12 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tabia Yako Ni Duni Sana!

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tabia Yako Ni Duni Sana!

Ninyi nyote mmeketi katika viti vya kifahari, mkiwafundisha wale wa vizazi vijana ambao ni wa aina yenu, ukiwafanya waketi nawe. Je, mngekosaje kujua kwamba wale “watoto” wenu walikuwa tayari hawana pumzi, na kwamba hawakuwa na kazi Yangu zamani? Utukufu Wangu huangaza kutoka nchi ya Mashariki hadi nchi ya Magharibi, lakini wakati utukufu Wangu huenea mpaka mwisho wa dunia na wakati unapoanza kuinuka na kuangaza, Nitaondoa utukufu wa Mashariki na kuuletea Magharibi ili kwamba watu hawa wa giza katika Mashariki ambao wameniacha Mimi watakuwa bila mwanga unaong’aa kuanzia hapo kwendelea. Wakati huo, mtaishi katika bonde la kivuli. Ingawa watu leo ni wazuri mara mia zaidi kuliko awali, bado hawawezi kuyatosheleza mahitaji Yangu, na bado wao si ushahidi mtukufu Kwangu. Kwamba nyinyi mnaweza kuwa wazuri mara mia zaidi kuliko awali yote ni matokeo ya kazi Yangu—ni tunda la kazi Yangu duniani. Hata hivyo, bado Ninahisi maudhi kwa maneno na matendo yenu, na tabia yenu, na Ninahisi hasira ya ajabu sana kwa matendo yenu mbele Yangu, kwa maana hamna ufahamu wowote Wangu. Kwa hiyo mnawezaje kuwa walio hai kutoka kwa utukufu Wangu, na mnawezaje kuwa waaminifu kabisa kwa kazi Yangu ya baadaye? Imani yenu ni nzuri sana; mnasema kwamba mko radhi kutoa maisha yenu kwa kazi Yangu, kufanya chochote na kila kitu kwa ajili yake, lakini tabia yenu haijabadilika sana. Kumekuwa tu na maneno ya kiburi, na matendo yenu halisi ni duni sana. Inaonekana kwamba ulimi na midomo ya mtu iko mbinguni lakini miguu ya mtu iko mbali sana duniani, hivyo maneno na matendo yake na sifa yake bado yako katika hali mbaya sana. Sifa zenu tayari zimeharibiwa, mwenendo wenu unashuka hadhi, njia yenu ya kuzungumza ni ya chini, maisha yenu ni ya kudharauliwa, na hata ubinadamu wenu wote ni wa chini. Nyinyi ni wa mawazo finyu kwa watu na nyinyi hubishana juu ya kila kitu kidogo. Nyinyi hugombana juu ya sifa zenu na hadhi zenu wenyewe, hata kufikia kiasi kwamba mko radhi kushuka kuzimu, katika ziwa la moto. Maneno na matendo yenu ya sasa yanatosha kiasi kwamba Ninaweza kuamua kuwa nyinyi ni wenye dhambi. Mtazamo wenu juu ya kazi Yangu unatosha Kwangu kutambua kuwa nyinyi ni wale wadhalimu, na tabia zenu zote zinatosha kusema kuwa nyinyi ni roho chafu ambazo zimejaa machukizo. Maonyesho yenu na kile mnachofichua ni tosha kusema kuwa nyinyi ni watu ambao mmekunywa damu ya kutosha ya pepo wachafu. Wakati kuingia katika ufalme kunapozungumzwa hamfichui hisia zenu. Mnaamini kuwa jinsi mlivyo sasa kunatosha kwenu kuingia katika lango la ufalme Wangu wa mbinguni? Je, mnaamini kuwa mnaweza kupata kuingia katika nchi takatifu ya kazi na maneno Yangu bila maneno na vitendo vyenu kupitia majaribio Yangu? Ni nani anayeweza kwa ufanisi kuyadanganya macho Yangu mawili? Je, tabia zenu za mazungumzo ya kudharauliwa na duni, zawezaje kuepuka Mimi kuona? Maisha yenu yameamuliwa na Mimi kama maisha ya kunywa damu ya pepo hizo chafu na kula nyama ya pepo hao wachafu kwa sababu mnachukua sura yao mbele Yangu kila siku. Mbele Yangu tabia zenu zilikuwa mbaya hasa, hivyo, ni vipi Mimi singeweza kuchukizwa? Katika kile mnachosema kuna najisi ya pepo wachafu: Nyinyi hudanganya, huficha, na kujipendekeza kama wale tu wanaofanya uchawi, kama wale wanaodanganya na kunywa damu ya wasio wa haki. Maonyesho yote ya wanadamu ni madhalimu sana, hiyo watu wote wanawezaje kuwekwa katika nchi takatifu ambako wenye haki wapo? Je, unafikiri kwamba tabia hiyo yako ya kudharauliwa inaweza kukubainisha kama mtakatifu dhidi ya wale wadhalimu? Huo ulimi wako unaofanana na nyoka hatimaye utaangamiza mwili wako ambao huleta maangamizi na hufanya machukizo, na mikono yako hiyo ambayo imefunikwa na damu ya pepo wachafu pia itavuta roho yako kuzimu hatimaye, hiyo kwa nini usichukue fursa hii kuitakasa mikono yako iliyofunikwa na uchafu? Na kwa nini huchukui fursa hii kuukata ulimi wako huo ambao husema maneno maovu? Inawezekana kuwa uko radhi kuteseka chini ya moto wa kuzimu kwa sababu ya mikono yako miwili na ulimi wako na midomo? Mimi huilinda mioyo ya watu wote kwa macho Yangu mawili kwa sababu muda mrefu kabla ya kuwaumba wanadamu, Nilikuwa Nimeishika mioyo yao ndani ya mikono Yangu. Zamani Nilibaini moyo wa mwanadamu, kwa hiyo mawazo ya ndani ya moyo wa mwanadamu yanawezaje kuyaepuka macho Yangu? Na wanawezaje kuwepo mapema ili kuepuka kuchomwa kwa Roho Wangu?
Midomo yako ni yenye huruma zaidi kuliko njiwa lakini moyo wako ni mbaya zaidi kuliko nyoka ya kale, hata midomo yako ni mizuri kama mwanamke Mlebanoni, lakini moyo wako si mwema kama ule wa wanawake Walebanoni na hakika hauwezi kulinganishwa na uzuri wa Wakanaani. Moyo wako ni mdanganyifu sana. Ninachochukia ni midomo ya wadhalimu na mioyo ya wadhalimu pekee. Mahitaji Yangu kwa watu si ya juu kuliko watakatifu, ni vile tu kwamba Mimi huhisi chukizo kwa matendo maovu ya wadhalimu na Natumaini kwamba wadhalimu huenda waweze kuondoa kuchafuka kwao na kukimbia kutoka kwa mashaka yao ya sasa ili waweze kutofautishwa na wale wadhalimu, na kuishi na kuwa watakatifu pamoja na wale wenye haki. Nyinyi mko katika hali sawa na Mimi, lakini mmefunikwa na uchafu, hakuna hata mfano kidogo wa wanadamu walioumbwa hapo mwanzo ndani yenu, na kwa sababu kila siku mnaiga mfano wa hao pepo wachafu na mnafanya kile wanachokifanya na kusema kile wanachokisema, kila sehemu zenu na hata ndimi zenu na midomo yenu imelowa katika maji yao mabaya. Ni kwa kiwango ambacho mmefunikwa kabisa na hayo mawaa na hakuna sehemu hata moja ambayo inaweza kutumiwa kwa kazi Yangu. Ni jambo la kusikitisha sana! Mnaishi katika ulimwengu huu wa farasi na ng’ombe lakini bado kwa kweli hamjihisi kuwa na wasiwasi; na mmejaa furaha na nyinyi huishi kwa uhuru na kwa urahisi. Mnaogelea katika maji haya mabaya lakini kwa kweli hamjui kwamba mmeanguka katika mazingira haya. Kila siku unaafikiana na pepo wachafu na una shughuli na “kinyesi.” Uhai wako ni duni sana, lakini hujui kwamba bila shaka huendelei kuishi katika ulimwengu wa kibinadamu na kwamba humo ndani ya ufahamu wako mwenyewe. Je, hujui kwamba maisha yako yalikanyagwa na pepo wachafu zamani, kwamba tabia yako ilivunjiwa hadhi na maji machafu zamani? Je, unadhani kuwa unaishi katika paradiso ya kidunia, kwamba uko katikati ya furaha? Je, hujui kwamba umeishi maisha na pepo wachafu, na kwamba umeishi maisha na kila kitu ambacho wamekuandalia? Je, kuishi kwako kungewezaje kuwa na maana yoyote? Je, maisha yako yangewezaje kuwa na thamani yoyote? Umekuwa ukienda huku na huko kwa ajili ya wazazi wako pepo wachafu, hadi sasa, lakini hujui kwamba wale ambao wanakunasa mtegoni ni hao pepo wachafu, wazazi wako ambao walikuzaa na kukulea. Aidha, hujui kuwa uchafu wako hakika ulipewa wote na wao; yote unayojua ni kwamba wanaweza kukupa “ridhaa,” hawakuadibu, wala hawakuhukumu, na hasa hawakulaani. Hawajawahi kukulipukia kwa ghadhabu, lakini hukutendea kwa bashasha na kwa ukarimu. Maneno yao hulisha moyo wako na kukupendeza mno ili ukanganywe na bila kulitambua, unavutwa ndani na uko radhi kuwa wa huduma kwao, uwe mlango wao na kadhalika mtumishi wao. Huna malalamiko kamwe lakini uko radhi kutumiwa nao—unadanganywa nao. Kwa sababu hii, bila shaka huna majibizo yoyote kwa kazi ambayo Mimi hufanya—si ajabu kwamba wewe daima hutaka kuponyoka kwa siri kutoka kwa mikono Yangu, na si ajabu kwamba wewe daima hutaka kutumia maneno matamu ili kuidanganya fadhila Yangu. Inadhihirika kwamba tayari ulikuwa na mpango mwingine, mpangilio mwingine. Unaweza kuona sehemu ndogo ya vitendo Yangu, vitendo vya Mwenyezi, lakini hujui chembe ya hukumu na kuadibu kwangu. Hujui wakati kuadibu kwangu kulianza; unajua tu jinsi ya kunidanganya Mimi, lakini hujui kuwa Sivumilii ukiukaji na mwanadamu. Kwa kuwa tayari umeweka uamuzi wako kunitumikia Mimi, sitakuacha uende. Mimi ni Mungu mwenye wivu, na Mimi ni Mungu ambaye ana wivu kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umewekelea maneno yako juu ya madhabahu, Sitakuvumilia wewe kuhudumia mabwana wawili. Je, ulifikiri ungepata upendo mwingine baada ya kuweka maneno yako juu ya madhabahu Yangu, baada ya kuyaweka mbele ya macho Yangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo? Je, ulidhani kwamba ungeweza kuweka nadhiri kikawaida, kula kiapo kunielekea Mimi na ulimi wako? Je, ungewezaje kula kiapo kunielekea kiti Changu cha enzi, Aliye Juu Zaidi? Je, ulifikiri kwamba viapo vyako vilikuwa tayari vimekufa? Nawaambia, hata kama miili yenu ikifa, viapo vyenu haviwezi kufa. Hatimaye, Nitawahukumu kwa msingi wa viapo vyenu. Lakini mnadhani kwamba mnaweza kuweka maneno yenu mbele Yangu ili kunivumilia Mimi na kwamba mioyo yenu inaweza kuwatumikia pepo wachafu na pepo wabaya. Je, hasira Yangu ingewezaje kuwavumilia hao watu mithili ya mbwa na nguruwe wanaonidanganya? Lazima Nitekeleze amri Zangu za kiutawala, na kuwapokonya kutoka kwa mikono ya pepo wachafu wale wote wenye fukuto, “wacha Mungu” ambao wanaamini katika Mimi “kunitumikia” Mimi kwa njia ya mpango, kuwa ng’ombe Wangu, kuwa farasi Wangu na kudhibitiwa na Mimi. Nitakufanya ushike uamuzi wako wa awali na kunitumikia Mimi tena. Siwezi kuvumilia kiumbe yeyote kunidanganya Mimi. Je, ulifikiria kwamba ungeweza kufanya maombi tu kiutukutu na kudanganya kiutukutu mbele Yangu? Je, ulifikiri kwamba Mimi sikuwa nimesikia au kuona maneno na matendo yako? Je, maneno yako na matendo yako yangekosaje kuwa katika mtazamo Wangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo?
Nimekuwa miongoni mwenu, Nimeshirikiana nanyi kwa majira kadhaa ya kuchipua na kwa majira kadhaa ya kupukutika, Nimeishi kati yenu kwa muda mrefu—ni kiasi gani cha tabia yenu ya kudharaulika kimeponyoka mbele ya macho Yangu? Maneno yenu hayo ya dhati daima yarudisha mwangwi ndani ya masikio Yangu; mamilioni na mamilioni ya matarajio yenu yamewekwa juu ya madhabahu Yangu—hayawezi hata kuhesabiwa. Lakini kwa kujitolea kwako na kile mnachokitumia, hakuna hata kidogo. Hakuna hata tone dogo la uaminifu wenu kwenye madhabahu Yangu. Yako wapi matunda ya imani yenu Kwangu? Mmepokea neema isiyo na mwisho kutoka Kwangu na mmeona mafumbo yasiyo na mwisho kutoka mbinguni, na Nimewaonyesha hata miale ya mbinguni lakini Sijawahi kuwa na moyo wa kuwachoma, na ni kiasi gani mmenipa Mimi kama malipo? Je, mko radhi kunipa Mimi kiasi gani? Kama umeshikilia chakula Nilichokupa, unageuka na kunitolea Mimi, hata ukisema kuwa ni kitu ambacho umepata kama malipo kwa jasho la kazi yako ngumu, kwamba unatoa yote uliyo nayo Kwangu. Je, unawezaje kukosa kujua kwamba “michango” yako Kwangu ni vitu vyote vilivyoibwa kutoka kwa madhabahu Yangu? Na sasa unavitoa Kwangu—si wewe unanidanganya Mimi? Unawezaje kukosa kujua kuwa vitu Ninavyovifurahia leo ni matoleo yote juu ya madhabahu Yangu, na sicho kile ulichokichuma kama malipo ya kazi yako ngumu halafu ukanitolea Mimi? Kwa kweli mnathubutu kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa hiyo ni kwa jinsi gani Ninaweza kuwasamehe? Ninawezaje kuvumilia hili zaidi? Nimewapa kila kitu. Nimewafungulia kila kitu, Nikakimu mahitaji yenu, na kuyafungua macho yenu, lakini bado mnanidanganya Mimi kwa njia hii, mkipuuza dhamiri yenu. Bila ubinafsi Nimewapa kila kitu, ili kwamba hata kama mnateseka, mmepata kutoka Kwangu kila kitu Nilichokileta kutoka mbinguni. Lakini hamna kujitolea kamwe, na hata kama mna mchango mdogo, mnalipa deni baada ya hapo. Je, si mchango wako utakuwa bure? Kile ambacho umenipa si chochote isipokuwa chembe moja ya mchanga, lakini kile ulichouliza kutoka Kwangu ni tani moja ya dhahabu. Je, si wewe unakuwa muhali? Ninafanya kazi miongoni mwenu. Hakuna kabisa dalili ya asilimia kumi ambayo Ninapaswa kupata, sembuse dhabihu za ziada. Zaidi ya hayo, asilimia kumi inayochangwa na wale ambao ni wacha Mungu inachukuliwa na wale waovu. Je, si nyinyi wote mmetawanyika kutoka Kwangu? Je, si nyinyi nyote mna uhasama na Mimi? Je, si nyinyi nyote mnaharibu madhabahu Yangu? Je, mtu wa aina hii anawezaje kuonekana kama hazina machoni Pangu? Je, si yeye ni nguruwe, mbwa ambao Ninawachukia? Ningewezaje kurejelea uovu wenu kama hazina? Kazi Yangu kwa kweli ni ya nani? Inawezekana kuwa tu ni ya kuwapiga nyinyi nyote ili kufichua mamlaka Yangu? Je, si maisha yenu yameshikiliwa na neno moja kutoka Kwangu? Ni kwa nini Ninatumia maneno tu kuwaagiza na Sijayageuza maneno kuwa ukweli ili kuwapiga haraka iwezekanavyo? Je, maneno Yangu na kazi Yangu ni ya kuwapiga wanadamu tu? Je, Mimi ni Mungu ambaye huwaua wasio na hatia bila ubaguzi? Hivi sasa, ni wangapi wenu ambao wako hapo mbele Yangu ambao wanatafuta njia sahihi ya maisha ya mwanadamu na nafsi zao nzima? Ni miili yenu tu iliyo mbele Yangu, lakini mioyo yenu iko huru, na iko mbali, mbali na Mimi. Kwa sababu hamjui kwa kweli kazi Yangu ni nini, kuna baadhi yenu ambao mnataka kuondoka Kwangu, mnaojitenga na Mimi, na mnataka kuishi katika mahali hapo pa raha ambapo hakuna kuadibu, hakuna hukumu. Je, hili ndilo watu wanatamani katika mioyo yao? Mimi hakika sikulazimishi. Njia yoyote utakayoichukua ni uchaguzi wako mwenyewe, na njia ya leo huenda sambamba na hukumu na laana, lakini nyote mnapaswa kujua kwamba kile Niliyowapa, iwe ni hukumu au kuadibu, zote ni zawadi bora kabisa Ninazoweza kuwapa, na vyote ni vitu ambavyo mnahitaji kwa dharura.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 11 Machi 2019

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)

Kote katika ulimwengu mkubwa mno, sayari zote ya mbingu husogea kwa usahihi katika mizunguko yazo zenyewe. Chini ya mbingu, milima, mito, na maziwa vyote vina mipaka yavyo, na viumbe vyote huishi na kuzaana wakati wa misimu yote minne kulingana na sheria za maisha…. Hili lote limepangwa vizuri sana—je, kuna Mwenye Uwezo Mmoja anayepanga na kutawala yote haya? Tangu tuje katika ulimwengu huu tukilia tumeanza kutekeleza majukumu tofauti katika maisha. Sisi husogea kutoka kuzaliwa mpaka uzee mpaka kuugua hadi kifo, sisi husogea kati ya furaha na huzuni…. Wanadamu kwa kweli hutoka wapi, na kwa kweli tutaenda wapi? Ni nani huitawala jaala yetu? Kutoka nyakati za kale hadi siku za kisasa, mataifa makubwa yameibuka, nasaba za wafalme zimekuja na kwenda, na nchi na watu wamesitawi na kuangamia katika mikondo ya historia…. Kama tu sheria za asili, sheria za maendeleo ya wanadamu zina mafumbo yasiyo na kikomo. Ungependa kujua majibu kuyahusu? Filamu iitwayo Yule Ambaye Hushikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu itakuongoza kufikia kiini cha jambo hili, ili kufichua mafumbo yote haya!
Mwenyezi Mungu alisema, Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa thabiti katika kazi Yake, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na harakati ya mambo yote. Kama kila kiumbe, mwanadamu bila kujua anapata lishe ya utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yote ya mwanadamu yanatunzwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, vilivyo hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu anavyotawala juu ya kila kitu.
Usiku uingiapo kwa utulivu, mwanadamu huwa hafahamu, kwani moyo wa mwanadamu hauwezi kujua jinsi giza linapokaribia au linakotoka. Usiku unapotoweka polepole, mwanadamu anakaribisha mwanga wa mchana, lakini moyo wa mwanadamu haufahamu ilikotoka nuru hii na jinsi gani nuru yenyewe imeliondoa giza la usiku. Mabadiliko kama haya ya kawaida ya mchana na usiku humpitisha mwanadamu katika kipindi kimoja baada ya kingine, kupita katika nyakati, wakati huu wote ikihakikisha kwamba kazi ya Mungu na mpango wake unafanywa wakati wa kila kipindi na katika nyakati zote. Mwanadamu alitembea kwa enzi nyingi na Mungu, lakini bado mwanadamu hafahamu kwamba Mungu ndiye kiongozi wa hatima ya mambo yote na viumbe hai au jinsi Mungu hupanga na kuelekeza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Na juu ya ni kwa sababu ipi, sio kwa sababu njia za Mungu hazifahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu. Kwa hivyo, hata ingawa mwanadamu Anamfuata Mungu, bila kujua yeye hubaki katika huduma ya Shetani. Hakuna anayetafuta kwa ukamilifu nyayo au nafsi ya Mungu, na hakuna anayetaka kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani na yule mwovu ili kubadilishwa na dunia hii na kanuni za maisha ambazo watu waovu hufuata. Katika nafasi hii, moyo na roho za mwanadamu hutolewa kafara kwa shetani na kuwa riziki yake. Aidha, moyo wa binadamu na roho yake huwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na kuufanya uwanja wake wa kuchezea. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni ya kuwa binadamu, na wa thamani na madhumuni ya kuwepo kwa binadamu. Sheria kutoka kwa Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu mpaka mwishowe mwanadamu hawezi tena kuomba au kufuata na kumsikiza Mungu. Wakati upitapo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu au kutambua kwamba yote hayo ni kutoka kwa Mungu. Mwanadamu huanza kupinga sheria na amri kutoka kwa Mungu; moyo na roho ya mwanadamu hufishwa. ... Mungu humpoteza mwanadamu Aliyemuumba pale mwanzo, na mwanadamu hupoteza mizizi ya mwanzo wake. Hii ni huzuni ya uanadamu. Kwa uhakika, tangu mwanzo mpaka sasa, Mungu alilifanya janga la wanadamu ambalo mwanadamu ni mhusika mkuu na mwaathiriwa, na hakuna hata mmoja anayeweza kupata jibu kuhusu nani ndiye mwelekezi wa hadithi hii ya janga.
Katika dunia hii kubwa, mabadiliko yasiyo hesabika yamefanyika, tena na tena. Hapana aliye na uwezo wa kuongoza binadamu isipokuwa Yeye ambaye Anatawala juu ya kila kitu katika ulimwengu. Hakuna yeyote hodari kwa kazi au kufanya maandalizi kwa ajili ya binadamu, wala aliye na uwezo wa kuwaongoza wanadamu kurejelea mwanga na ukombozi kutokana na ukosefu wa haki duniani. Mungu Analalamikia wakati ujao wa wanadamu, na Anahuzunishwa na kuanguka kwa mwanadamu. Anahisi huzuni kwa kuangamia kwa mwanadamu polepole na kwenda katika njia isiyo na upande wa kurudi. Mwanadamu ameuvunja moyo wa Mungu, akamkana na kumfuata yule mwovu. Hakuna waliowahi kuwa na mawazo kuhusu mwelekeo ambao mwanadamu wa aina hii atafuata. Ni kwa sababu hii haswa ndio kwamba hakuna ambaye ameona hasira ya Mungu. Hakuna anayetafuta njia ya kumpendeza Mungu au kujaribu kuwa karibu na Mungu. Kadhalika, hakuna anayetafuta kufahamu huzuni na maumivu ya Mungu. Hata baada ya kusikia sauti ya Mungu, binadamu anaendelea tu kwenye njia yake mbali na Mungu, kukwepa neema na huduma ya Mungu, na kuepuka ukweli wa Mungu, akiona ni afadhali auuze mwili wake kwa Shetani, adui wa Mungu. Na ni nani amewahi kuwa na mawazo yoyote ya jinsi gani Mungu atamtendea mwanadamu asiyetubu na ambaye amempuuza? Hakuna anayejua kwamba ukumbusho wa mara kwa mara na nasaha za Mungu ni kwa sababu Yeye anayo katika mikono yake maafa Aliyowaandalia yasiyokuwa ya kawaida, maafa ambayo yatakuwa magumu kwa mwili na nafsi ya mwanadamu kustahimili. Janga hili sio tu adhabu ya mwili bali ya roho pia. Lazima ujue hili: Mpango wa Mungu unapokataliwa na wakati kuwakumbusha kwake na nasaha hazileti mabadiliko, Atakuwa na hasira ya aina gani? Hii itakuwa kama kitu ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo awali au hata kusikika na viumbe vyovyote. Na hivyo Nasema, janga hili ni kubwa mno na kamwe hayatawahi kurudiwa. Hii ni kwa sababu uumbaji mmoja tu na wokovu mmoja wa mwanadamu ndio ulio ndani ya mpango wa Mungu. Hii ni mara ya kwanza na pia ni ya mwisho. Kwa hivyo, hakuna anayeweza kuelewa nia ya huruma na hamu ya Mungu kwa matarajio yake ya kuwaokoa wanadamu.
Mungu aliumba dunia hii na kuleta mwanadamu, kiumbe hai ambacho alitia uhai ndani yake. Baadaye, mwanadamu akaja kuwa na wazazi na jamaa na hakuwa mpweke tena. Tangu mwanadamu alipotua macho kwa mara ya kwanza katika dunia hii tunayoishi, ilibainika kuwa angeishi ndani ya utaratibu wa Mungu. Ni pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ndiyo hustawisha kila kiumbe hai katika ukuaji wake hadi kinapokomaa. Wakati wa mchakato huu, hakuna hata mmoja anayeamini kwamba mwanadamu huishi na kukua chini ya uangalizi wa Mungu. Badala yake, anashikilia kwamba mwanadamu hukua chini ya upendo na utunzaji wa wazazi wake, na kwamba ukuaji wake unaongozwa na silika ya maisha. Hii ni kwa sababu mwanadamu hajui aliyeleta maisha au kulikotoka maisha hayo, pia hafahamu jinsi silika ya maisha husababisha miujiza. Mwanadamu anajua tu kwamba chakula ndicho msingi wa kuendelea kwa maisha, kwamba uvumilivu ni chanzo cha kuwepo kwa maisha, na kwamba imani iliyomo akilini mwake ni utajiri wa maisha yake. Mwanadamu haihisi neema na riziki itokayo kwa Mungu. Mwanadamu huyatumia kwa uharibifu maisha aliyopewa na Mungu. ... Hapana hata mwanadamu mmoja ambaye Mungu Anamwangazia usiku na mchana amechukua jukumu la kuanza Kumwabudu. Mungu Anaendelea kufanya kazi kama Alivyopanga juu ya mwanadamu Akiwa hana matarajio yoyote kutoka kwa mwanadamu. Anafanya hivyo kwa matumaini kwamba siku moja, mwanadamu ataamka kutoka katika ndoto yake na ghafla kuelewa thamani na madhumuni ya maisha, kuelewa gharama Aliyopitia Mungu ili Ampe mwanadamu kila kitu alicho nacho, na kujua jinsi Mungu anavyotamani kwa ari mwanadamu ageuke na Kumrudia. Hakuna yeyote amewahi kufikiria juu ya siri ya asili na endelezo la maisha ya mwanadamu. Na bila shaka, Mungu tu Ambaye Anaelewa yote haya na kwa kimya huvumilia mapigo na maumivu kutoka kwa binadamu, ambaye alipokea kila kitu kutoka kwa Mungu bila shukurani. Binadamu huchukulia kila kitu kinacholetwa na maisha kimzaha, na tena kama "kama jambo lisilo na shaka," Mungu amesalitiwa, amesahaulika, na kukataliwa na binadamu. Je, mpango wa Mungu ni wa maana namna hii? Je mwanadamu, kiumbe hai ambaye alitoka katika mkono wa Mungu, ni wa maana namna hiyo? Mpango wa Mungu ni wa umuhimu kabisa; hata hivyo, maisha ya viumbe vya mkono wa Mungu vipo kwa ajili ya mpango Wake. Kwa hivyo, Mungu hawezi kuuharibu mpango wake kwa sababu ya chuki Yake kwa mwanadamu. Ni kwa ajili ya mpango Wake na pumzi aliyotoa ndiyo maana Mungu Hustahimili mateso yote, siyo kwa ajili ya mwili wa mwanadamu ila ni kwa sababu ya uhai wa mwanadamu. Mungu ana hamu ya kuchukua pumzi aliyopuliza ndani mwa mwanadamu, wala sio nyama za mwili. Huu ndio mpango wake.
Wote wanaokuja duniani lazima wapitie maisha na kifo, na wengi wamepitia mzunguko wa kifo na kuzaliwa upya. Wale wanaoishi watakufa hivi karibuni na wafu watarejea karibuni. Yote haya ni mwendo wa maisha uliopangwa na Mungu kwa kila kiumbe hai. Hata hivyo, njia hii na mzunguko huu ni ukweli ambao Mungu Anataka binadamu aone, kwamba maisha aliyopewa na Mungu hayana kikomo na hayazuiliwi na mwili, wakati, au nafasi. Hii ni siri ya maisha aliyopewa binadamu na Mungu na dhihirisho kwamba maisha yalikuja kutoka Kwake. Ingawa watu wengi wanaweza kosa kuamini kwamba maisha yalitoka kwa Mungu, binadamu bila ya kufahamu wanafurahia yote yatokayo kwa Mungu, iwe wanaamini au wanakana uwepo Wake. Iwapo siku moja Mungu kwa ghafla Atabadili moyo na Atake kurudisha yote yaliyomo duniani na kuchukua maisha Aliyotoa, basi yote duniani yataisha. Mungu Hutumia maisha Yake kukimu vitu vyote vilivyo hai na visivyo na uhai, na kuleta yote kwa utaratibu mzuri kwa mujibu wa madaraka na mamlaka Yake. Huu ni ukweli ambao hakuna anayeweza kuufahamu au kuuelewa kwa urahisi, na kweli hizi zisizoeleweka kwa fikira zetu ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha. Sasa hebu nikupe siri: Ukuu na nguvu ya uhai wa Mungu hauwezi kueleweka na kiumbe chochote. Hii ilikuwa hivyo awali, iko hivyo wakati huu, na itakuwa hivyo wakati ujao. Siri ya pili Nitakayotoa ni hii: chanzo cha uhai hutoka kwa Mungu, kwa viumbe vyote, haijalishi tofauti katika maumbile au muundo. Hata uwe kiumbe hai cha aina gani, huwezi kwenda kinyume na njia ya maisha ambayo Mungu ameweka. Katika hali yoyote, kile Napenda ni kuwa mwanadamu aelewe kwamba bila huduma, utunzaji, na utoaji wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, haijalishi juhudi au mapambano yake. Bila ruzuku ya uhai kutoka kwa Mungu, mwanadamu hupoteza maana ya thamani katika maisha na kupoteza madhumuni ya kusudi katika maisha. Mungu angewezaje kuruhusu mwanadamu anayepoteza thamani ya uhai wake kuishi hivyo bila ya kujali? Kisha tena, usisahau kwamba Mungu Ndiye chanzo cha maisha yako. Iwapo mwanadamu atashindwa kuthamini yote ambayo Mungu Amemfanyia, Mungu Hatachukua kile Alichotoa pekee, lakini zaidi ya hayo, mwanadamu atalipa mara mbili kufanya fidia kwa yote ambayo Mungu Ametumia.
Mei 26, 2003

Jumapili, 10 Machi 2019

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika. Mambo mengi hayawezi kusemwa kwenu moja kwa moja na athari ya awali haiwezi kutimizwa. Kwa hiyo, kazi za ziada zinapaswa kuongezwa kwa kazi Yangu. Ni muhimu kuzindua kazi hii ya "kuinua ubora wa tabia ya watu" miongoni mwenu kwa sababu uwezo wenu wa kupokea, uwezo wa kuona mambo, na viwango vya maisha yenu ni maskini sana. Huu ndio mwelekeo unaohitajika; hakuna uchaguzi badili, na ni lazima ufanyike kwa namna hii ili sehemu ya matokeo iweze kutimizwa. Vinginevyo, maneno yote Ninayosema hayatafanikiwa, na hamngekumbukwa kama wenye dhambi? Je! Hamngekuwa wapotovu? Je, kazi hii inafanywa kwenu ni nini? Nini kinachohitajika kwenu? Je, hamjui? Mnapaswa kujua ubora wenu wenyewe wa tabia; hauwezi kufikia kile Ninachohitaji kamwe. Je, hii haicheleweshi kazi? Kwa ubora wa tabia na hulka yenu ya sasa, hakuna hata mmoja wenu ambaye anafaa kushuhudia kwa ajili Yangu, na hakuna mtu anayewezana na kazi ya kulichukua jukumu kubwa la kazi Yangu ya baadaye. Je, hamhisi aibu sana kuhusu hili? Itawezekanaje kuyakidhi matakwa Yangu yote kama hili linaendelea kutendeka? Unapaswa kufanya maisha yako yawe kamili na yenye thawabu. Usiruhusu muda upite bure. Hakuna thamani katika kufanya hivyo. Unapaswa kujua mambo ambayo inabidi kujiandaa nayo. Usijione kuwa mjuaji wa kila kitu. Hukaribii hata kidogo! Je! Kuna nini cha kuzungumzia ikiwa huna hata ufahamu wa kimsingi wa ubinadamu? Je, si vyote havingekuwa na maana? Hakuna hata mmoja kati yenu aliye na sifa zinazostahili kabisa kwa mintarafu ya kile Ninachohitaji kwa ubora wa tabia ya kibinadamu. Ni vigumu kupata mtu ambaye anafaa kutumiwa. Mnaamini ninyi ni watu ambao wanaweza kufanya kazi kubwa zaidi kwa ajili Yangu na kujitwika ukabidhi mkubwa kutoka Kwangu. Kwa kweli, hamjui jinsi hata ya kuingia katika masomo mengi mbele yenu, hivyo ingewezekanaje kuingia katika kweli za kina? Lazima kuingia kwenu kuwe kwenye utaratibu. Msifanye hivyo bila mpango. Hili si jambo la manufaa. Ingieni kutoka mwisho wenye kina kifupi—yasome maneno haya mstari kwa mstari hadi mfikie ufahamu na ubayana. Kila ndugu angalau anapaswa aweze kusoma. Usilitazame mara moja tu kwa haraka, na usilifanye kwa namna isiyo ya dhati. Kwa kawaida, unaweza pia kusoma baadhi ya kazi za kumbukumbu (kama vile sarufi au vitabu vya balagha). Hakuna haja ya kusoma vitabu vinavyoichochea akili yako sana (riwaya za mapenzi, ponografia, magazeti, au wasifu za watu mashuhuri), ambavyo husababisha madhara zaidi kuliko mema. Lazima uwe mweledi wa yote unayopaswa kuingia na unapaswa kufahamu. Madhumuni ya kuendeleza ubora wa tabia sio mengine ila kuwasaidia watu kujua asili yao wenyewe, utambulisho, hadhi au thamani. Nini jambo kuu ambalo makanisa hapa chini yanapaswa kuingia? Je, watu hawaongezi ubora wa tabia yao sasa? Ni muhimu kushikilia kuingia huku kwa kugeuka kuwa msomi; hakuwezi kuachiliwa huru! Kipengele kimoja ni kwamba lazima ninyi muelewe kwa nini ubora wa tabia ya watu unapaswa kuendelezwa, jinsi ubora wa tabia unaweza kuendelezwa, na vipengele vipi vya kuingia. Lazima muelewe maana ya ubinadamu wa kawaida, kwa nini kazi hii inapaswa kufanywa, na jinsi inapaswa kuratibiwa. Katika kuelimika, ni vipengele vipi vinayopaswa kufunzwa, na jinsi gani mtu anapaswa kuingia? Nyote mnapaswa kujua lengo la kuelimika ni nini. Je, sio kuyafahamu maneno ya Mungu na kuingia katika ukweli? Hali inayosambaa makanisani sasa ni ipi? Mkimwomba mtu apate kuelimika, anasahau kuhusu furaha ya maneno ya Mungu. Mkizungumza kuhusu ubinadamu wa kawaida, anashughulikia tu kuisafisha nyumba yake, kufagia sakafu au kupika, kusafisha jikoni na kununua vyombo vya kupika. Anajali tu kuhusu mambo haya na hajui jinsi ya kuishi maisha ya kanisa kwa kawaida. Vinginevyo anatafuta tu maneno katika kamusi na kujifunza maneno mapya, lakini hafanyi jambo lingine lolote siku nzima. Umepotoka ikiwa unabaki katika hali ya sasa. Basi kwa nini unaombwa kuingia katika maisha ya kiroho? Yote unayojifunza ni mambo haya ambayo hayawezi kukusaidia kufikia kile kinachohitajika kwako. Jambo la muhimu zaidi bado ni kuingia kwa maisha. Sababu ya kufanya kazi hii ni kutatua shida ambazo watu hukumbana nazo katika uzoefu wao. Kuinua ubora wa tabia kunakuwezesha kujua ubinadamu na kiini cha mwanadamu—kusudi kuu la kuyajua mambo haya ni ili maisha ya watu ya kiroho yaweze kukua na tabia yao iweze kubadilika. Unaweza kujua jinsi ya kuvaa na kupendeza; unaweza kuwa na utambuzi na hekima, na hata hivyo hatimaye, siku inapokuja kwako kuenda kazini, unashindwa kufanya hivyo. Unapaswa kujua, kwa hiyo, kile unapaswa kufanya pia wakati unainua ubora wako wa tabia. Kukubadilisha ni lengo. Kuinua ubora wa tabia ni jambo la ziada. Haitakubalika kama ubora wako wa tabia hauendelezwi. Ni vibaya hata zaidi ikiwa tabia yako haiwezi kubadilishwa. Moja bila ya nyingine haitoshi. Kuwa na ubinadamu wa kawaida hakumaanishi kwamba umekuwa na ushuhuda mkubwa sana. Kile kinachohitajika kwako si rahisi sana.
Wakati ambapo ubora wa tabia ya mtu umeendelea kiasi kwamba ana hisia na mtindo wa maisha ya ubinadamu wa kawaida na pia kuwa na kuingia kwa maisha, ni hapo tu ndipo ataweza kubadilika na kushuhudia. Siku ya kutoa ushuhuda inapofika, pia kuna haja ya kuzungumza kuhusu mabadiliko katika maisha ya binadamu na kuhusu ufahamu wa Mungu ndani. Mchanganyiko wa vipengele hivi viwili tu ndio ushahidi wa kweli na faida yako ya kweli. Haitakubalika ikiwa una mabadiliko tu katika ubinadamu kwa nje na huna ufahamu kwa ndani. Haitakubalika pia ikiwa una ufahamu na ukweli kwa ndani lakini hutilii maanani kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida. Kazi inayofanyika kwako leo sio kuwaonyesha wengine bali kukubadilisha. Unahitaji tu kuzingatia kujibadilisha. Unaweza kuandika na kusikiliza kila siku, lakini haitawezekana ikiwa hushiriki katika maeneo mengine ya maisha yako. Unapaswa kuwa na kuingia katika kila kipengele. Unapaswa kuwa na maisha ya kawaida ya mtakatifu. Akina dada wengi huvaa kama wanawake matajiri na kaka wanavaa kama waungwana matajiri au mabwana, wakipoteza kabisa ustahifu wa watakatifu. Kipengele kimoja ni kuinua ubora wa tabia ya mtu, ambacho kinaweza kufanikishwa kwa kawaida. Kipengele kingine cha umuhimu mkubwa ni kula na kunywa maneno ya Mungu. Je, haingekuwa kupoteza elimu ikiwa ubora wako wa tabia umeinuliwa lakini haukukutumiwa kwa sababu hukula na kunywa maneno ya Mungu? Lazima vipengele vyote viwili viunganishwe. Kwa nini maarifa ya Mungu yanatajwa katika majadiliano ya kile kinachohitajika kwako? Je, hii si kwa ajili ya matokeo ya kazi ya baadaye? Baada yako kushindwa, lazima uweze kushuhudia kutokana na uzoefu wako mwenyewe. Haitakubalika kama sura yako ya nje ni moja ya ubinadamu wa kawaida lakini huwezi kuonyesha uzoefu wako kupitia kinywa chako. Unapokuwa na maisha ya kawaida ya kiroho, unapaswa kufikia ubinadamu wa kawaida, na vipengele vingi vya ubinadamu wa kawaida vitaweza kufunzwa kwa dhahiri. Je, ungesema kwamba kufagia sakafu kunahitaji mafunzo maalum? Ikiwa unahitaji kutumia saa moja kufanya mazoezi jinsi ya kushikilia vijiti kwa kula, hiyo haikubaliki hata zaidi! Ubinadamu wa kawaida unashirikisha vipengele hivi: utambuzi, hisia, dhamiri na tabia. Iwapo unaweza kufanikisha ukawaida katika kila mojawapo ya vipengele hivi, ubinadamu wako uko katika kiwango kinachostahili. Unapaswa kuwa na mfanano wa binadamu wa kawaida na utende kama anayemwamini Mungu. Sio lazima ufikie viwango vya juu zaidi au kujishughulisha na diplomasia. Unapaswa tu kuwa mwanadamu wa kawaida, na hisia za kawaida za mtu, uweze kung’amua vitu, na kwa kiwango cha chini uonekane kama mwanadamu wa kawaida. Hiyo itakuwa imetosha. Kila kitu kinachohitajika kwako leo kiko katika uwezo wako, na huku si kukulazimisha ufanye kadri ya uwezo wako hata kidogo. Hakuna maneno yasiyo na maana au kazi isiyofaa yatatekelezwa kwako. Uovu wote ulioonyeshwa au kufichuliwa katika maisha yako lazima uondolewe. Ninyi mmepotoshwa na Shetani na mna sumu nyingi sana za Shetani. Yote ambayo yanahitajika kwako ni kuiepuka tabia hii potovu ya kishetani, si wewe kuwa mtu mwenye cheo cha juu, au mtu maarufu au mkuu. Hii haina maana. Kazi ambayo imefanyika kwenu inaafikiana na kile ambacho ni cha asili kwenu. Kuna mipaka ya kile Ninachohitaji kutoka kwa watu. Ikiwa watu wa leo wote wangeulizwa kutenda kama watu wa kada za Kichina, na kujizoeza toni ya sauti ya kada za Kichina, kujifunza katika namna ya kuzungumza ya viongozi wa serikali wenye cheo cha juu, au kujifunza kwa namna na sauti ya kuzungumza ya waandishi wa insha na waandishi wa riwaya, basi hili halingekubalika pia. Halingeweza kufikiwa. Kwa mujibu wa ubora wa tabia za watu hawa, wanapaswa angalau kuweza kuzungumza kwa hekima na busara na kuelezea mambo wazi. Ni wakati huo ndipo watakapoyatosheleza mahitaji. Kwa kiwango kidogo sana, utambuzi na hisia vinapaswa kufikiwa. Kwa sasa jambo kuu ni kuitupilia mbali tabia potovu ya kishetani. Lazima uutupilie mbali uovu unaouonyesha. Ikiwa hujavitupilia mbali hivi, unawezaje kugusia hisia na utambuzi wenye mamlaka mkubwa kabisa? Watu wengi wanaona kwamba enzi imebadilika. Hivyo hawajizoezi unyenyekevu au uvumilivu wowote, na pengine pia hawana upendo wowote au mwenendo mwema wa kitakatifu pia. Watu hawa ni wajinga mno! Je, wana kiwango chochote cha ubinadamu wa kawaida? Je, wanao ushuhuda wowote wa kuzungumziwa? Hawana utambuzi na hisia zozote kamwe. Bila shaka, vipengele fulani vya utendaji wa watu vilivyopotoka na vyenye makosa vinapaswa kurekebishwa. Kama vile maisha ya watu ya kiroho yasiyopindika au mwonekano wenye ganzi na upumbavu wa zamani—vitu hivi vyote vinapaswa kubadilika. Mabadiliko hayamaanishi kukuruhusu uwe mpotovu au kujiingiza katika mwili, au kusema chochote utakacho. Kuzungumza kiholela hakuwezi kukubalika! Kutenda kama mwanadamu wa kawaida ni kuzungumza kwa kueleweka. Ndiyo inamaanisha ndiyo, na la inamaanisha la. Kuwa mwenye ukweli kwa uhakika na uzungumze inavyofaa. Usilaghai, usidanganye. Inapaswa kujulikana ni mipaka gani mtu wa kawaida anaweza kufikia kuhusu mabadiliko ya tabia. Ikiwa hiyo haijulikani, hutaweza kuingia katika uhalisi.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumamosi, 9 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.”
Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawa Nimejazwa na hukumu na adabu kwa binadamu, kila ninachofanya bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, kwa ajili ya kueneza injili Yangu kwa njia bora zaidi na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili. Kwa hiyo leo, katika wakati ambapo watu wengi tayari wametamauka pakubwa, Naendelea na kazi Yangu, Nikiendeleza kazi ambayo lazima Nifanye ili kuhukumu na kuadibu binadamu. Licha ya ukweli kwamba binadamu amechoshwa na kile Ninachosema na licha ya ukweli kwamba hana tamanio la kujali kuhusu kazi Yangu, Ningali natekeleza wajibu Wangu kwa sababu kusudio la kazi Yangu halijabadilika na mpango Wangu asilia hautabadilika. Kazi ya hukumu Yangu ni kumfanya binadamu anitii Mimi kwa njia bora zaidi, na kazi ya kuadibu Kwangu ni kuruhusu binadamu awe na mabadiliko bora zaidi. Ingawa kile Ninachofanya ni kwa minajili ya usimamizi Wangu, Sijawahi kufanya chochote ambacho hakikufaidi binadamu. Hiyo ndiyo maana Nataka kufanya mataifa yote nje ya Israeli kuwa matiifu tu kama Waisraeli na kuwabadilisha kuwa binadamu halisi, ili Niwe na mahali pa usalama katika nchi zilizo nje ya Israeli. Huu ndio usimamizi Wangu; ndiyo kazi Ninayotimiza katika nchi za Mataifa. Hata sasa, watu wengi bado hawauelewi usimamizi Wangu kwa sababu hawajautilia maanani, badala yake wanafikiria tu kuhusu mustakabali na hatima zao. Haijalishi ni nini Ninachosema, watu hawajali kazi Yangu, badala yake wanalenga tu hatima zao za baadaye. Mambo yakiendelea kwa namna hii, kazi Yangu itapanuliwa vipi? Injili Yangu itaenezwa vipi kotekote ulimwenguni? Lazima mjue kwamba wakati kazi Yangu inapanuka, Nitawatawanya, Nitawaadhibu kama vile tu Yehova alivyoyaadhibu makabila ya Israeli. Haya yote yatafanywa ili injili Yangu iweze kuenea kotekote kwenye ulimwengu mzima, ili kazi Yangu iweze kuenezwa kwa Mataifa, ili kwamba jina Langu litukuzwe na watu wazima na watoto kwa pamoja na jina Langu takatifu litatukuzwa katika vinywa vya watu kutoka makabila na mataifa yote. Katika enzi hii ya mwisho, Nitafanya jina Langu litukuzwe miongoni mwa Mataifa, kufanya matendo Yangu kuonekana na mataifa mengine ili waniite Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kuyafanya maneno Yangu kutimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.
Kazi ambayo Nimekuwa nikisimamia kwa maelfu ya miaka inafichuliwa kabisa tu kwa binadamu katika siku za mwisho. Ni sasa tu ndipo Nimelifumbua fumbo kamili la usimamizi Wangu kwa mwanadamu. Binadamu anajua kusudio la kazi Yangu na zaidi ya yote anapata uelewa wa mafumbo Yangu yote. Na Nimemwambia binadamu kila kitu kuhusu hatima ambayo amekuwa akijali kuhusu. Tayari Nimemfichulia binadamu mafumbo yote yaliyofichwa kwa zaidi ya miaka 5,900. Yehova ni nani? Masiha ni nani? Yesu ni nani? Mnafaa kuyajua haya yote. Mabadiliko makubwa ya kazi Yangu yamo katika majina haya. Je, mmeelewa haya? Jina Langu takatifu linafaa kutangazwa vipi? Jina Langu linafaa kuenezwaje katika taifa lolote ambalo limeniita kwa jina Langu lolote? Kazi Yangu tayari imeanza kupanuka, na Nitaeneza ukamilifu wake katika mataifa yote. Kwa sababu kazi Yangu imetekelezwa ndani yenu, Nitawapiga kama vile Yehova alivyowapiga wale wachungaji wa nyumba ya Daudi kule Israeli, na kuwasababisha kutawanyika miongoni mwa mataifa yote. Kwani katika siku za mwisho, Nitapondaponda mataifa yote kuwa vipande vidogo vidogo na kusababisha watu wao kuenezwa upya. Nitakaporudi tena, mataifa yatakuwa tayari yamegawanywa kwa mipaka iliyowekwa na mwako wa moto Wangu utakaokuwa ukichoma. Katika wakati huo, Nitajionyesha upya kwa binadamu kama jua linalochoma, Nikijionyesha kwao hadharani kwa taswira ya yule Aliye Mtakatifu ambaye hawajawahi kumwona, Nikitembea miongoni mwa mataifa yote, kama vile tu Mimi, Yehova, Nilivyotembea miongoni mwa makabila ya Wayahudi. Kuanzia hapo kuendelea, Nitawaongoza watu huku wakiishi ulimwenguni. Hakika watauona utukufu Wangu hapo na hakika wataona pia nguzo ya wingu hewani ili uwaongoze, kwani Nitaonekana katika sehemu takatifu. Binadamu ataiona siku Yangu ya haki na pia maonyesho Yangu ya utukufu. Hilo litafanyika Nitakapoutawala ulimwengu mzima na kuwaleta wana wengi katika utukufu. Kila pahali duniani, watu watainama, nalo hema Langu takatifu litaundwa miongoni mwao juu ya mwamba wa kazi ambayo Natekeleza sasa. Watu watanihudumia pia hekaluni. Madhabahu, yaliyojaa mambo machafu na ya kuchukiza, Nitayavunjavunja vipandevipande na Nitajenga upya mengine. Madhabahu matakatifu yatarundikwa wanakondoo na ndama waliozaliwa karibuni. Nitaangusha hekalu lililopo leo na kujenga jingine upya. Hekalu lililopo sasa na lililojaa watu wenye chuki litaporomoka na lile Nitakalojenga litajaa watumishi watiifu Kwangu. Kwa mara nyingine watasimama na kunihudumia Mimi kwa utukufu wa hekalu Langu. Kwa hakika mtaiona siku ambayo Nitapokea utukufu mkuu na hakika mtaiona siku ambayo Nitaliangusha hekalu na kujenga lingine upya. Pia, hakika mtaona siku ya kuletwa kwa hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu. Huku Nikilibomoa hekalu, ndivyo Nitakavyoleta hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu; itakuwa kama vile tu ambavyo watu wanavyoniona Nikishuka. Baada ya kuangamiza mataifa yote, Nitayakusanya pamoja upya, Nikilijenga hekalu Langu na kuandaa madhabahu Yangu, ili wote waweze kutoa kafara zao Kwangu, kunihudumia Mimi hapo, na kujitolea kwa uaminifu katika kazi Yangu kwenye mataifa mengineyo. Itafanywa namna tu ambavyo wana wa Israeli wanavyofanya sasa, na joho la kuhani na taji la mfalme, utukufu Wangu, Yehova, ukiwa miongoni mwao na uadhama Wangu ukivinjari juu yao na ukiwa nao. Kazi Yangu katika Mataifa itatekelezwa pia katika njia hiyo. Kama vile kazi Yangu kule Israeli ilivyokuwa, ndivyo kazi Yangu katika Mataifa itakavyokuwa kwa sababu Nitaongeza kazi Yangu kule Israeli na kuieneza katika mataifa yale mengine.
Sasa ndio wakati ambao Roho Wangu anafanya kazi pakubwa, na wakati Ninapofanya kazi miongoni mwa Mataifa. Hata zaidi, ndio wakati ambapo Naainisha viumbe wote na kuweka kila kiumbe katika kundi lenye uhusiano, ili kazi Yangu iweze kuendelea haraka zaidi na kwa njia ya kufaa zaidi. Kwa hiyo, bado Nahitaji kwamba mjitoe mzimamzima kwa minajili ya kazi Yangu yote; aidha, mnafaa kutambua waziwazi na kuwa na hakika ya kazi ile yote ambayo Nimefanya ndani yako, na kuweka nguvu zako zote katika kazi Yangu ili iweze kuwa ya matokeo bora zaidi. Hilo ndilo ambalo lazima uelewe. Msipigane tena wenyewe kwa wenyewe, kutafuta mbinu za usuluhishi, au kutafuta raha za mwili, mambo ambayo yanaweza kuchelewesha kazi Yangu na kuharibu mustakabali wako mzuri. Kufanya hivyo, mbali na kuweza kukupa ulinzi, litakuletea maangamizo. Je, sii huu utakuwa ujinga kwa upande wako? Kile ambacho unafurahia leo kwa tamaa ndicho kile kile ambacho kinaharibu mustakabali wako, huku yale maumivu unayopitia leo ndiyo yaleyale ambayo yanakulinda. Lazima ufahamu waziwazi kuhusu jambo hilo, ili uepuke majaribio ambayo yatakuwa magumu kujinasua kutoka na kuepuka kuingia kwenye ukungu mzito unaozuia jua katika maisha yako. Wakati ukungu huu mzito utakapotoweka, utajipata katika hukumu ya siku kuu. Kufikia wakati huo, siku Yangu itakuwa imekaribia binadamu. Utatorokaje hukumu Yangu? Utawezaje kuvumilia joto kali la jua? Ninapompa binadamu wingi Wangu, haufurahii kwa dhati, lakini badala yake anautupa nje kwenye sehemu zisizotambulika. Wakati siku Yangu itawadia, binadamu hataweza tena kugundua wingi Wangu au kupata ukweli mkali Niliompa zamani sana. Ataomboleza na kulia, kwa sababu amepoteza mwangaza anaofuata na kuingia katika giza totoro. Kile mnachoona leo ni upanga tu mkali wa kinywa Changu. Bado hamjakiona kiboko kilicho katika mkono Wangu au moto Ninaotumia kumchoma binadamu, na ndiyo maana bado mna kiburi na msio na kadiri mbele Yangu. Ndiyo maana bado mnapigana na Mimi katika nyumba Yangu, huku mkipinga kwa ulimi wa mwanadamu kile ambacho Nimenena na kinywa Changu. Binadamu haniogopi Mimi. Akiwa bado katika uhasama na Mimi hadi leo, bado haniogopi kamwe. Mnao ulimi na meno ya wale wasio na haki vinywani mwenu. Maneno na matendo yenu ni kama yale ya yule nyoka aliyemshawishi Hawa na kumfanya kutenda dhambi. Mnadai nyinyi kwa nyinyi kulipiza kisasi, na mnashindana mbele Yangu kwa ajili ya nafasi, umaarufu, na faida kwa ajili yenu wenyewe, ilhali hamjui kwamba Natazama maneno na matendo yenu kwa siri. Kabla hata ya nyinyi kuja mbele Yangu, Nimejua vina vya nyoyo zenu kabisa. Siku zote binadamu hutamani kutoroka kutoka mfumbato Wangu na kuepuka uangalizi wa macho Yangu, lakini Sijawahi kuepuka maneno au matamshi yake. Badala yake, kwa kusudio kuu huwa Nayaruhusu maneno na matendo hayo yaingie katika macho Yangu, ili Niweze kuadibu udhalimu wake na kuhukumu uasi wake. Kwa hiyo, maneno na matendo fiche ya binadamu siku zote yanawekwa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na hukumu Yangu haijawahi kumtoka binadamu, kwa sababu uasi wake ni mwingi mno. Kazi Yangu ni kuteketeza na kusafisha maneno na matendo yote ya binadamu yaliyotamkwa na kufanywa mbele ya Roho Wangu. Kwa njia hiyo, baada ya Mimi kuondoka ulimwenguni, binadamu wataweza bado kuendeleza utiifu Kwangu, na bado watanihudumia kama vile watumishi Wangu watakatifu wanavyofanya katika kazi Yangu, wakiruhusu kazi Yangu hapa ulimwenguni iendelee mpaka siku itakapokamilika.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Ijumaa, 8 Machi 2019

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Pili

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu ni kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupeana vitu vyote. Mungu ni chanzo cha vitu vyote, na wanadamu hufurahia vitu vyote wakati Mungu anawapa. Hiyo ni kusema, mwanadamu hufurahia vitu vyote anapokubali maisha ambayo Mungu anatoa kwa vitu vyote. Wanadamu hufurahia matokeo ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ilhali Mungu ni Bwana. Kisha kutokana na mtazamo wa vitu vyote, ni nini tofauti kati ya Mungu na wanadamu? Mungu anaweza kuona vizuri mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote, na kudhibiti na kutawala mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote. Yaani, vitu vyote vipo machoni mwa Mungu na katika eneo Lake la ukaguzi. ... Kwa hiyo Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu! Hata mwanadamu akiendelea kuchunguza sayansi na sheria za vitu vyote, ni katika eneo lililowekewa mipaka pekee, ilhali Mungu anadhibiti vitu vyote. Kwa mwanadamu, hiyo ni isiyo na kikomo."
Wanadamu kuweza kuendelea kuishi na kuzaa kwa kawaida ni jambo la muhimu zaidi kwa Mungu. Kwa hiyo, Mungu daima huwapa wanadamu na vitu vyote. Anapeana vitu vyote kwa njia mbalimbali, na chini ya hali za kudumisha kuendelea kuishi kwa vitu vyote, Anawawezesha wanadamu kuendelea kusonga mbele ili Aweze kudumisha kuwepo kwa kawaida kwa wanadamu. Hivi ndivyo vipengele viwili tunavyowasiliana leo. Vipengele hivi ni vipi? (Kutokana na mtazamo mkubwa, Mungu aliwaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Hicho ni kipengele cha kwanza. Pia, Mungu alitayarisha hivi vitu yakinifu ambavyo wanadamu wanahitaji na wanaweza kuona na kugusa.) Tumewasilisha mada yetu kuu kupitia vipengele hivi viwili. Mada yetu kuu ni gani? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Mnapaswa sasa kuwa na ufahamu fulani wa mbona Niliwasilisha maudhui haya chini ya mada hii. Je, kumekuwa na majadiliano yoyote yasiyohusiana na mada kuu? Hakuna, sivyo? Labda baada ya kusikia mambo haya, wengine wenu wanaweza kupata ufahamu fulani na kuhisi kwamba maneno haya ni muhimu sana, lakini wengine huenda wakapata tu ufahamu kidogo wa kawaida na kuhisi kwamba maneno haya hayana maana. Haijalishi vile nyinyi mnaelewa hili wakati huu, mnapoendelea kupitia matukio itafika siku ambayo ufahamu wenu utafikia kiwango fulani, yaani, wakati maarifa yenu ya matendo ya Mungu na Mungu Mwenyewe yatafikia kiwango fulani, mtatumia maneno yenu wenyewe ya kiutendaji kuwasilisha ushuhuda wa maana na wa kweli kuhusu matendo ya Mungu.
Ninafikiri ufahamu wenu sasa bado ni sahili na wa kawaida, lakini mnaweza angaa, baada ya kunisikiliza Nikiwasilisha vipengele hivi viwili, kutambua ni mbinu zipi Mungu hutumia kuwapa wanadamu au ni vitu vipi Mungu huwapa wanadamu? Je, mna wazo la msingi na vilevile ufahamu wa msingi? (Ndiyo.) Lakini vipengele hivi viwili Nilivyowasilisha vinahusiana na Biblia? (La.) Vinahusiana na hukumu na kuadibu kwa Mungu katika Enzi ya Ufalme? (La.) Basi kwa nini Niliwasilisha vipengele hivi? Je, ni kwa sababu watu ni lazima wavielewe ili kumjua Mungu? (Ndiyo.) Ni muhimu sana kuvijua na pia ni muhimu sana kuvielewa. Usizuiwe tu kwa Biblia, na usizuiwe tu kwa Mungu kuhukumu na kuadibu wanadamu ili kuelewa kila kitu kuhusu Mungu. Ni nini kusudi la Mimi kusema hili? Ni ili kuwafanya watu wajue kwamba Mungu si Mungu wa watu Wake waliochaguliwa pekee. Wewe sasa unamfuata Mungu, na Yeye ni Mungu wako, lakini kwa wale walio nje ya watu wanaomfuata Mungu, je, Mungu ni Mungu wao? Je, Mungu ni Mungu wa watu wote walio nje ya wale wanaomfuata Yeye? (Ndiyo.) Basi Mungu ni Mungu wa vitu vyote? (Ndiyo.) Basi Mungu hutenda kazi Yake na kutekeleza matendo Yake kwa wale tu wanaomfuata Yeye? (La.) Eneo lake ni ulimwengu mzima. Kutoka kwa mtazamo mdogo, eneo lake ni wanadamu wote na miongoni mwa vitu vyote. Kutokana na mtazamo mkubwa, ni ulimwengu mzima. Hivyo tunaweza kusema kwamba Mungu hufanya kazi Yake na kutekeleza matendo Yake miongoni mwa wanadamu wote. Hili ni la kutosha kuwafanya watu wajue yote kuhusu Mungu Mwenyewe. Ikiwa unataka kumjua Mungu na upate kweli kumjua na kumfahamu Yeye, basi usizuiwe tu katika hatua tatu za kazi ya Mungu, na usizuiwe tu katika hadithi za kazi ambayo Mungu alitekeleza wakati mmoja. Ukijaribu kumjua hivyo, basi unajaribu kumzuilia Mungu kwa mipaka fulani. Unamwona Mungu kama asiye na maana sana. Ni athari gani ungepata kutoka kwa matokeo kama hayo? Hungeweza kujua maajabu na mamlaka ya juu kabisa ya Mungu, na hungeweza kamwe kujua nguvu za Mungu na kudura na eneo la mamlaka Yake. Ufahamu kama huo ungeathiri uwezo wako wa kukubali ukweli kwamba Mungu ni Mtawala wa vitu vyote, na vilevile maarifa yako ya utambulisho wa kweli na hadhi ya Mungu. Kwa maneno mengine, iwapo ufahamu wako wa Mungu umewekewa mipaka katika eneo, unachoweza kupokea pia kimewekewa mipaka. Ndiyo maana ni lazima upanue eneo na kufungua upeo wa macho yako. Iwe ni eneo la kazi ya Mungu, usimamizi wa Mungu, na utawala wa Mungu, au vitu vyote vinavyotawaliwa na kusimamiwa na Mungu, unapaswa kujua yote na kupata kujua matendo ya Mungu yaliyo ndani. Kupitia njia hii ya ufahamu, utahisi bila kujua kwamba Mungu anatawala, anasimamia na kupeana vitu vyote miongoni mwao. Wakati huo huo, utahisi kweli kwamba wewe ni sehemu ya vitu vyote, na kiungo cha vitu vyote. Mungu anapovipa vitu vyote, wewe pia unakubali utawala na upeanaji wa Mungu. Huu ni ukweli usioweza kupingwa na yeyote. Vitu vyote viko chini ya mamlaka ya sheria zao, ambazo ziko chini ya utawala wa Mungu, na vitu vyote vina sheria zao za kuendelea kuishi, ambazo pia ziko chini ya utawala wa Mungu, huku majaliwa ya wanadamu na wanachohitaji pia vikihusiana kwa karibu na utawala wa Mungu na upeanaji Wake. Ndiyo maana, chini ya utawala wa Mungu na uongozi, wanadamu na vitu vyote vinahusiana, vinategemeana, na vinafumana. Hili ni kusudi na thamani ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote. Unaelewa hili sasa? (Ndiyo.) Iwapo unaelewa basi acha tumalizie mawasiliano yetu hapa siku hii. Kwaheri! (Mshukuru Mungu!)
kutoka kwa Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIIIMungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Alhamisi, 7 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo

Wale miongoni mwa ndugu na dada ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika Imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi hawatashindwa tu kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomuasi Mungu. Wakati mtu anayeamini Mungu hamtii Mungu ama kumcha Mungu lakini badala yake anamwasi Yeye, basi hii ndiyo aibu kuu zaidi kwa muumini. Ikiwa usemi na mwenendo wa muumini daima havina mpango na bila kizuizi kama asiyeamini, basi huyu muumini ni mwovu zaidi kumpiku asiyeamini; yeye ni ibilisi halisi. Wale walio kanisani ambao wanaeneza matamshi yao yenye sumu, wale miongoni mwa ndugu na dada ambao wanasambaza uvumi, kuchochea utengano na kufanya magenge wanapaswa kufukuzwa kutoka kanisani. Lakini watu hawa wamezuiwa kwa kuwa sasa ni enzi tofauti ya kazi ya Mungu, kwa sababu wamehukumiwa kuwa vyombo vya kuondolewa. Wale waliopotoshwa na Shetani wote wana tabia iliyopotoka. Lakini ilhali baadhi ya watu wana tu tabia iliyopotoka kuna wengine wasio jinsi hii, ya kuwa hawana tu tabia za kishetani zilizopotoka, lakini asili zao pia ni mbovu kupita kiasi. Yote anayoyafanya mtu huyu na kusema hayaonyeshi tu tabia yake ya kishetani, bali yeye mwenyewe ni ibilisi Shetani halisi. Anachofanya ni kuvuruga na kukatiza kazi ya Mungu, kuvuruga maisha ya kuingia ya ndugu na dada, na kuharibu maisha ya kawaida ya kanisa. Mbwa mwitu hawa waliovalia ngozi ya kondoo lazima waondolewe nje siku moja, na mtu lazima awe na mtazamo usiojizuia kwa vibaraka hawa wa Shetani; mtu lazima awe na mtazamo wa kuachwa kwao. Ni katika kufanya hili pekee ndipo mtu atakaweza kusimama upande wa Mungu na wale wasioweza kufanya hili wako katika ushirika na Shetani. Mungu daima yumo mioyoni mwa wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na daima wana moyo wa kumcha Mungu, moyo wa kumpenda Mungu. Wale wanaomwamini Mungu lazima wayafanye mambo kwa moyo wa uangalifu na wenye busara, na yote wanayoyafanya yanapasa kulingana na matakwa ya Mungu na yaweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Hawapaswi kuwa wabishi, wakifanya watakavyo, hayo hayafai katika utaratibu mtakatifu. Watu hawawezi kuipunga bendera ya Mungu kwa madaha na kucharuka kila mahali, wakijishau na kutapeli kotekote; kutenda haya ni tendo la uasi la juu zaidi. Familia zina masharti na mataifa yana sheria, hivyo ni kwa kiasi gani zaidi ndiyo familia ya Mungu ina viwango vikali? Je, si pia ina amri za usimamiaji? Watu wana uhuru wa kutenda watakayo, lakini amri za usimamizi za Mungu haziwezi kubadilishwa kwa hiari. Mungu ni Mungu asiyewaruhusu watu kumkosea Yeye na Mungu ni Mungu anayewauwa watu—je, watu hawajui hili tayari?
Kila moja ya kanisa lina watu wanaolivuruga kanisa, watu wanaokatiza kazi ya Mungu. Watu hawa wote ni Shetani wanaojifanya katika familia ya Mungu. Mtu wa aina hii ni mjuzi wa kuiga, akija mbele Yangu kwa heshima, akitikisa vichwa kwa kukubali na kuinama, akitenda kama mbwa wengi walio hafifu, akijitolea “yote” yake ili kufikia malengo yake mwenyewe, lakini akionyesha sura yake mbaya mbele ya ndugu. Anapomwona mtu akiuweka ukweli katika vitendo anamshambulia na kumtenga, na anapomwona mtu mbaya kumpiku yeye mwenyewe, anamsifu mno na kujipendekeza kwake, wakitenda kama viongozi wa kiimla kanisani. Inaweza kusemwa kuwa mengi ya makanisa yana aina hii ya “nyoka mwovu wa ndani,” aina hii ya “mbwa wa kupakata” kati yao. Wanatembea kwa siri kwa pamoja, wakikonyezeana na kuashiriana, na hakuna hata mmoja wao anayeweka ukweli katika vitendo. Yeyote aliye na sumu zaidi ndiye “ibilisi mkuu,” na yeyote aliye na hadhi ya juu zaidi huwaongoza, akipeperusha bendera yao juu zaidi. Watu hawa wanakuwa huru na kufanya wanachotaka kanisani, wakieneza ubaya wao, wakiachilia kifo, wakifanya watakavyo, wakisema wanachopenda, bila anayedhubutu kuwakomesha, wakijawa na tabia za kishetani. Punde tu wanapoanza kusababisha usumbufu, hewa ya kifo inaingia ndani ya kanisa. Wale wanaoweka ukweli katika vitendokatika kanisa wanaachwa na wanashindwa kufikia uwezo wao, ilhali wale wanaovuruga kanisa na kusambaza kifo wanakuwa huru na kufanya wanachotaka kanisani. Cha ziada ni, watu wengi huwafuata. Aina hii ya kanisa iko chini ya udhibiti wa Shetani na ibilisi ni mfalme wao. Iwapo watu wa kanisa hawataamka na kuwafukuza hao ibilisi wakuu, basi pia watakuja kuangamia siku moja. Kuanzia leo na kuendelea hatua lazima zichukuliwe dhidi ya kanisa la aina hii. Ikiwa wale wanaoweza kuuweka ukweli mdogo katika vitendo hawajihusishi na utafutaji, basi kanisa hilo litapigwa marufuku. Ikiwa hakuna mtu yeyote kanisani aliye radhi kuuweka ukweli katika vitendo, hakuna yeyote anayeweza kuwa shahidi kwa Mungu, basi kanisa hilo linapasa kutengwa kabisa, na miunganisho yao na makanisa mengine kukatizwa. Hili linaitwa kuzika kifo, na kumfukuza Shetani. Iwapo kuna nyoka kadhaa waovu wa ndani katika kanisa, na vilevile nzi wadogo wanaowafuata wale wasio na ufahamu kabisa, ikiwa wale wa kanisa bado hawawezi kutoa vifungu na ushawishi wa nyoka hawa baada ya wao kuona ukweli, basi hawa wajinga wataondolewa mwishoni. Ingawa nzi hawa wadogo wanaweza kuwa hawajafanya lolote baya, wao ni wenye hila hata zaidi, wadanganyifu hata zaidi na wenye kukwepa hata zaidi na kila mtu aliye namna hii ataondolewa. Hakuna yeyote atakayeachwa! Wale walio wa Shetani watarudishwa kwa Shetani, ilhali wale walio wa Mungu hakika watakwenda kutafuta ukweli; hili linaamuliwa na asili zao. Acheni wale wote wanaomfuata Shetani waangamie! Hakuna huruma watakayoonyeshwa watu hawa. Acheni wale wanaofuata ukweli wapate utoaji na muwakubalie kufurahia neno la Mungu hadi mioyo yao itosheke. Mungu ni mwenye haki; Yeye hawatendei watu kwa udhalimu. Ikiwa wewe ni ibilisi basi hutakuwa na uwezo wa kuuweka ukweli katika vitendo. Ikiwa wewe ni mtu anayetafuta ukweli basi ni wazi kuwa hutatekwa nyara na Shetani—hili halina tashwishi yoyote.
Wale wasiotafuta kuendelea daima wanataka wengine wawe wabaya na watepetevu kama wao wenyewe, wale wasioweka ukweli katika vitendo wanawaonea gere wale wanaotenda ukweli. Wale wasioweka ukweli katika vitendo daima wanataka kuwadanganya wale wapumbavu na wasio na ufahamu. Mambo ambayo watu hawa wanaeneza yanaweza kukufanya usawijike, kuteleza kwenda chini, kuwa na hali isiyokuwa ya kawaida na kujawa na kiza ndani yako; yanaweza kukufanya usogezwe mbali na Mungu, na yanakufanya uuthamini mwili na kujihusisha na tamaa. Wale ambao hawapendi ukweli, ambao daima humshughulikia Mungu kwa uzembe hawana maarifa ya binafsi, na tabia zao huwashawishi watu kufanya dhambi na kuasi Mungu. Hawaweki ukweli katika vitendo wala kuwaruhusu wengine kutenda ukweli. Wanathamini dhambi na hawana chuki kwao wenyewe. Hawajifahamu wenyewe na huwakomesha wengine kujifahamu wenyewe, na huwakomesha wengine kuwa na matamanio ya kujua ukweli. Wale wanaowadanganya hawawezi kuona mwangaza na huanguka gizani, hawajijui wenyewe, na ukweli kwao si wazi na wanakuwa mbali zaidi na zaidi na Mungu. Hawaweki ukweli katika vitendo na huwakomesha wengine kutenda ukweli, wakiwaleta watu hao wajinga mbele yao. Badala ya kusema kuwa wanamwamini Mungu ingekuwa vyema kusema kuwa wanawaamini mababu zao, kwamba kile wanachoamini ni sanamu zilizo mioyoni mwao. Ingekuwa vyema kwa wale watu wanaosema kuwa wanamfuata Mungu kufungua macho yao watazame vizuri waone ni nani wanayemwamini hasa: Je, ni Mungu unayemwamini hakika, ama Shetani? Ikiwa unajua kuwa unayemwamini si Mungu ila sanamu zako mwenyewe, basi ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Ikiwa hakika hujui unayemwamini ni nani, basi, pia, ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Kusema hivi kutakuwa kukufuru! Hakuna anayekushurutisha umwamini Mungu. Msiseme kuwa mnaniamini Mimi, kwa kuwa Niliyasikia maneno hayo hapo kale wala Sitamani kuyasikia tena, kwa kuwa mnachoamini ni sanamu zilizo katika mioyo yenu na nyoka waovu wa ndani walio miongoni mwenu. Wale wanaotikisa vichwa vyao wanaposikia ukweli, wanaotabasamu sana wanaposikia mazungumzo ya kifo ni watoto wa Shetani, na wote ni vyombo vya kuondolewa. Kuna watu wengi kanisani ambao hawana ufahamu, na jambo la uongo linapotendeka wanasimama tu upande wa Shetani. Wanapoitwa vibaraka wa Shetani wanahisi kuwa wamekosewa sana. Wanasemekana kuwa hawana ufahamu, lakini daima wanasimama upande usiokuwa na ukweli. Hakujakuwa na wakati muhimu ambapo wamesimama upande wa ukweli, hakuna wakati mmoja ambapo wamesimama na kutetea mjadala juu ya ukweli, kwa hivyo je, hawana ufahamu? Kwa nini daima wanasimama upande wa Shetani? Kwa nini hawasemi neno lolote la haki ama lenye maantiki kwa ukweli? Je, hali hii kweli imetokana na kuchanganyikiwa kwao kwa ghafla? Kadri mtu anapokuwa na ufahamu mdogo, ndivyo anavyozidi kushindwa kusimama upande wa ukweli. Je, hili linaonyesha nini? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu wanapenda uovu? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu ni watoto waaminifu wa Shetani? Je, ni kwa nini daima wanaweza kusimama upande wa Shetani na kuzungumza lugha moja naye? Kila neno na tendo lao, na maonyesho yao yanathibitisha vya kutosha kuwa wao sio wapenzi wa ukweli kwa namna yoyote, lakini badala yake wao ni watu wanaochukia ukweli. Kwamba wanaweza kusimama upande wa Shetani kunadhihirisha kuwa hakika Shetani anawapenda ibilisi hawa wadogo wanaopigana kwa ajili ya Shetani katika maisha yao yote. Je, taarifa hizi za kweli si wazi sana? Ikiwa hakika wewe ni mtu unayependa ukweli, basi kwa nini huwezi kuwaheshimu wale wanaotenda ukweli, na mbona unawafuata mara moja wale wasioweka ukweli katika vitendo punde tu wanapokuwa na mabadiliko ya sura? Je, hili ni tatizo la aina gani? Sijali iwapo una ufahamu au la, sijali kwamba umelipa gharama kuu kiasi gani, sijali kuwa nguvu zako ni kuu kiasi gani na sijali ikiwa wewe ni nyoka mwovu wa ndani ama kiongozi anayepeperusha bendera. Ikiwa nguvu zako ni kuu basi ni kwa ajili tu ya usaidizi wa nguvu za Shetani; ikiwa hadhi yako iko juu, basi ni kwa sababu kuna wengi waliokuzunguka wasiotenda ukweli; ikiwa hujafukuzwa basi ni kwa kuwa sasa sio wakati wa kazi ya kufukuza, bali ni wakati wa kazi ya kuondoa. Hakuna haraka ya kukufukuza sasa. Ninahitaji tu kusubiri siku ifike ambayo utakuwa umeshaondolewa ili Nikuadhibu. Yeyote asiyeweka ukweli katika vitendo ataondolewa!
Wale wanaomwamini Mungu kwa kweli ni wale walioradhi kuweka neno la Mungu kwenye matendo, na ni wale walioradhi kutenda ukweli. Wale wanaoweza kwa kweli kuwa shahidi kwa Mungu pia ni wale walioradhi kuweka neno Lake kwenye matendo, na ni wale ambao kwa kweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wanaotumia hila na wale wanaotenda yasio haki wote ni watu wasiokuwa na ukweli na wote huleta aibu kwa Mungu. Wale walio kanisani wanaohusika na mabishano ni vibaraka wa Shetani, na ni mfano mwema wa Shetani. Mtu wa aina hii ni mwovu sana. Wale wasio na ufahamu na wasio na uwezo wa kusimama upande wa ukweli wanahifadhi nia mbovu na kufifisha ukweli. Watu hawa hata zaidi ni mawakilishi kamili wa Shetani; wamepita hali ya ukombozi na ni wazi mno kuwa wao wote ni vitu vya kuondolewa. Wale wasioweka ukweli katika vitendo hawapaswi kuruhusiwa kusalia katika familia ya Mungu, wala wale wanaobomoa kanisa kwa maksudi. Lakini sasa Sifanyi kazi ya kufukuza. Watafichuliwa tu na kuondolewa mwishoni. Hakuna kazi nyingine ya bure itakayofanywa kwa watu hawa; wale walio wa Shetani hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, ilhali wale wanaotafuta ukweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wasioweka ukweli katika vitendo hawastahili kusikia njia ya kweli na hawastahili kuwa na ushuhuda kwa ukweli. Kimsingi ukweli si kwa ajili ya masikio yao lakini badala yake unazungumzwa kwa ajili ya masikio ya wale wanaoutenda. Kabla ya mwisho wa kila mtukufichuliwa, wale wanaovuruga kanisa na kukatiza kazi kwanza wataachwa upande moja. Pindi kazi itakapokamilika, watu hawa watafunuliwa mmoja baada ya mwingine kabla ya kuondolewa. Wakati wa kutoa ukweli, Siwatilii maanani kwa sasa. Ukweli wote unapofichuliwa kwa mwanadamu watu hao wanapasa kuondolewa, kwa kuwa huo pia utakuwa wakati ambapo watu wataainishwa kulingana na aina yao. Kwa sababu ya werevu wao mdogo, wale wasio na ufahamu watakuja kuangamia mikononi mwa watu waovu na watapotoshwa na watu waovu na watashindwa kurudi. Watu hawa wanapasa kushughulikiwa kwa njia hii, kwa kuwa hawaupendi ukweli, kwa sababu hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, kwa sababu wanawafuata watu waovu, wanawaunga mkono watu waovu, na kwa sababu wanashirikiana na watu waovu na kumuasi Mungu. Wanajua vema kuwa watu hao waovu wananururisha uovu lakini wanafanya mioyo yao kuwa migumu na kuwafuata, wakienda kinyume na ukweli. Je, watu hawa wasioweka ukweli katika vitendo lakini wanaofanya mambo ya uharibifu na ya chukizo wote si wanafanya maovu? Ingawa kuna wale miongoni mwao ambao wanajipa mtindo wenyewe kama “wafalme” na wale wanaofuata msururu nyuma yao, je, asili yao ya kuasi Mungu si ni sawa yote? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu hawaokoi? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu si mwenye haki? Je, si ni uovu wao wenyewe ambao umewaangamiza? Je, si ni uasi wao ambao utawavuta hadi jahanamu? Wale wanaoweka ukweli katika vitendo mwishowe wataokolewa na kufanywa wakamilifu kwa kupitia ukweli. Wale wasioweka ukweli katika vitendo mwishowe watakaribisha maangamizi kwa kupitia ukweli. Hii ndio miisho inayowasubiri wale wanaoweka ukweli katika vitendo na wale wasioutenda. Ninawashauri wale ambao hawana mpango wa kuweka ukweli katika vitendo watoke kanisani haraka iwezekanavyo ili kuepuka kutenda dhambi nyingi zaidi. Wakati utakapofika, hata majuto yatakuwa yamechelewa, na hasa wale wanaofanya magenge na kufanya migawanyiko, na wale nyoka waovu wa ndani katika kanisa lazima watoke haraka sana. Watu hawa ambao ni wenye asili ya mbwa mwitu mwovu hawana uwezo wa mabadiliko, ni heri watoke kanisani kwa nafasi inayopatikana mwanzo, wasiweze kuyavuruga maisha mazuri ya ndugu na dada tena, na hivyo kuepuka adhabu ya Mungu. Nyinyi ambao mlienda pamoja nao mtafanya vema kutumia nafasi hii kutafakari juu yenu wenyewe. Je, mtawafuata waovu nje ya kanisa, ama kusalia na kufuata kwa uaminifu wote? Lazima uzingatie jambo hili kwa makini. Ninawapa nafasi moja zaidi ya kuchagua. Ninalisubiri jibu lenu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili