Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Alhamisi, 1 Novemba 2018

Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo | Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Nguzo inapopandishwa kidogo, mnaweza kupiga hatua kidogo. Si jambo baya kuwa na mahitaji ya juu kutoka kwenu na wala si jambo baya kuwauliza maswali magumu. Lengo ni kuwafanya muwe na ufahamu zaidi juu ya elimu na maarifa ya kawaida ya kipengele cha weledi cha wajibu wenu.[a] Huenda labda nyinyi bado hulalamika katika nyoyo zenu, mkisema: "Tumejifunza mambo mengi mazuri lakini Mungu huwa hayataji kamwe au kuturuhusu kuyatumia. Kwa hiyo hatuthubutu kuyataja au kuyatumia. Je, na kama yakikanushwa mara tu tunapoyatumia? Na je, tukikosolewa? "Sasa Nawaambieni kwamba mnaweza kuyatumia mambo haya kwa ujasiri. Lakini ni lazima mpitie ukaguzi wa ndugu zenu wa kiume na wa kike. Usiwe wa kujidai, na kusema: "Mungu amesema wakati huu tunaweza kutumia mambo haya kwa ujasiri, kwa hiyo tutatumia mambo haya kwa ujasiri." Kuwa na ujasiri sio kuenea pote au kuwa wenye dharau. Lazima kuwe na mipaka ya kuwa na ujasiri, ni lazima kukubaliane na kanuni, na ndugu wa kiume na wa kike wanapaswa kulifikiria kuwa linafaa. Mtu fulani akisema, "Hili halikubaliki," basi si unahitaji kulibadilisha? Je, watu wakaidi ni watu wema? (Hapana.) Haishauriwi kuwa hivyo. Ni lazima usikilize maoni ya wengine, na unapowasikia wakisema hivi, unasema, "Uko sawa. Ni lazima nilibadilishe." Baada ya kulibadilisha, watu wengine husema: "Uko karibu hapo, nahisi vyema kuhusu hili. Liko sawa, limefaulu." Safi sana! Kwa kufanya mambo kwa njia hii, kipengele kimoja ni kwamba mnaweza kuingia kwa kina katika kipengele cha weledi, na muwe wakomavu na wenye uzoefu; kipengele kingine ni kwamba nyinyi pia mna uwezo wa kujifunza mambo mengi; na bado kipengele kingine ni kwamba mmejifunza somo. Unapokabiliwa na masuala, hupaswi kujidai, ukifikiri, "Nina kauli ya mwisho. Hamna sifa ya kuzungumza. Ninaelewa kanuni, nyinyi mnaelewa nini? Hamuelewi, ninaelewa!" Huku ni kujidai. Kuwa wa kujidai ni tabia potovu ya kishetani; si kitu kilicho ndani ya ubinadamu wa kawaida. Kwa hiyo, ni nini maana ya kutokuwa wa kujidai? (Kupata mapendekezo kutoka kwa kila mtu, na kila mtu kuyapima pamoja.) Wakati kila mtu anapoliidhinisha, na kila mtu anapokubaliana nalo, basi mmefanya kazi nzuri. Mradi baadhi ya watu au kikundi cha watu hudakiza kipingamizi, basi ni lazima muwe mahsusi zaidi kuhusu kipengele cha weledi. Ni lazima msijifanye kutotambua na kusema: "Nani? Aliyedakiza nini? Ni nini kinachoendelea? Je, wewe ndiye unayelielewa hili au ni mimi? Je, unaelewa hili vyema kuniliko? Unaelewa nini? Huelewi!" Hii ni tabia mbaya, sivyo? Ijapokuwa aliyedakiza kipingamizi huenda asielewe vizuri sana na anaweza kuwa mlei, na unaweza kuwa na haki na kile ulichokifanya kinaweza kuwa sahihi, tatizo hapa ni tabia yako. Kwa hiyo ni nini maonyesho na vitendo sahihi vinavyokubaliana na kanuni na kukubaliana na ukweli? Unasema: "Tatizo ni nini? Acha niangalie. Sio mimi tu, lakini kila mtu anaangalia. Wale ambao wana mapendekezo fulani kuhusu kipengele hiki au utambuzi fulani ndani yake, au ambao wana uzoefu fulani katika kipengele hiki, hebu sote tuangalie pamoja na tuweze kuzungumza juu yake. "Ikiwa kila mtu huamini kweli kuwa kufanya kitu kwa njia hii ni vibaya, kwamba kuna shida kidogo hapa, na unatazama mara moja na huwezi kuona tatizo, unatazama mara mbili na bado huwezi kuliona, kisha unaangalia mara tatu au mara nne na unavyozidi kuangalia ndivyo unavyozidi kuona kuna shida, basi hili kwa kweli ni tatizo. Na lazima ulisahihishe, lifanye liwe zuri na uombe mawazo ya kila mtu. Je, hili ni jambo jema au jambo baya? (Ni jambo jema.) Unaomba mawazo ya kila mtu, kila mtu analizungumzia, unashirikiana pamoja na Roho Mtakatifu anakupa nuru; unafuata hilo, na tatizo linarekebishwa ipasavyo. Kila mtu huangalia na kusema, "Hilo ni sawa, na ni bora zaidi kuliko hapo awali!" Je, si huu ni mwongozo wa Mungu? Hili ni jambo kubwa! Unapofanya mambo kwa njia hii, kama wewe hujidai, unapoacha mawazo yako mwenyewe na fikira zako mwenyewe, na unapotenda ukweli, unanyenyekea na kusikiliza mawazo ya wengine, kisha ni nini hutokea? Wewe hupata fursa ya Roho Mtakatifu kufanya kazi kwako na Roho Mtakatifu hukupatia nuru. Nini hutokea wakati Roho Mtakatifu anapokupatia nuru? Umejifunza kitu kingine cha weledi. Je, si hiki ni kitu chema?
Mara unapokuwa umepitia hili, wewe hufikiri, "Ninapokabiliwa na masuala, ni lazima nisijidai. Kila mtu hunichukia ninapojidai." Wakati kila mtu anapomchukia mtu fulani, Mungu humchukia? (Ndiyo, Yeye humchukia.) Unajifunza somo, kweli? Unapotenda kwa njia hii daima, kipengele kimoja ni kwamba utaona maendeleo katika hali ya weledi ya wajibu wako, na Mungu atakupa nuru na kukubariki; kipengele kingine ni kwamba utakuwa na njia ya kufuata katika kutenda ukweli, utajua jinsi ya kutenda ukweli, hatua kwa hatua utakuja kuelewa kanuni na kupata njia, utajua jinsi ya kufanya mambo kwa namna ambayo itasababisha kupata nuru ya Mungu na uongozi, ni njia zipi za kufanya mambo ambazo humsababisha Mungu kukupuuza au kukuchukia, na jinsi ya kufanya mambo kwa njia ambayo inaweza kubarikiwa na Mungu. Watu wanapopata baraka za Mungu na nuru, kuna furaha au huzuni ndani ya mioyo yao? Kuna furaha. Unapokuja kuwajibika kwa kile ambacho umekifanya mbele ya Mungu, utapata furaha na utafikiri, "Nilikifanya vizuri." Ndani yako utajisikia mwenye amani na furaha. Hisia hii ya amani na furaha hutolewa kwako na Mungu, na ni kuchochea ulikopewa na Roho Mtakatifu. Ikiwa hutendi hili lakini daima huhimili kwa njia zako mwenyewe, ukisema, "Sitamsikiliza mtu yeyote. Hata nikisikiliza, nitaonekana tu kusikiliza na sitabadilika. Nitafanya mambo kwa njia hii, ninahisi niko sawa na nahisi nimethibitishwa kabisa, "ni nini kitakachotokea? Huenda kuwa umethibitishwa na huenda kusiwe na kosa katika kile ufanyacho, huenda hujafanya makosa yoyote na huenda ukaelewa kipengele cha weledi vyema zaidi kuliko wengine, lakini mara unapofanya aina hizi za maonyesho na kutenda kwa njia hii, wengine wataona na watasema: "Tabia ya mtu huyu si nzuri. Unapokabiliwa na masuala, huwa hawakubali lakini hupinga kitu chochote mtu mwingine yeyote anachosema, kama kiko sahihi au la. Mtu huyu huwa hakubali ukweli." Watu wanaposema wewe hukubali ukweli, Mungu atafikiri nini? Je, Mungu anaweza kuona maonyesho haya yako? Bila shaka, Mungu anaweza kuyaona. Mungu hachunguzi tu chokomeani mwa moyo wa mwanadamu, Yeye pia huangalia kila kitu usemacho na kufanya wakati wote na mahali pote. Na Anapoona mambo haya, Yeye hufanya nini? Yeye husema: "Wewe umefanywa mgumu. Uko jinsi hii katika hali ambapo wewe uko sawa, na uko jinsi hii pia katika hali ambapo umekosea. Bila kujali uko katika hali gani, kila kitu unachofichua na kuonyesha ni kupingana na upinzani. Hukubali hata kidogo mawazo au mapendekezo ya mtu yeyote mwingine. Moyo wako unapingana kabisa, kukataa na kutokubali mawazo ya wengine. Wewe ni mgumu sana!" Ni kwa njia gani unakuwa mgumu? Kuwa kwako mgumu ni kwamba maonyesho yako sio njia mbaya ya kufanya mambo au tabia mbaya, lakini kwa usahihi zaidi ni ufichuzi wa tabia yako. Je, tabia yako imefichua nini? Unauchukia ukweli na una uhasama mintarafu ya ukweli. Na wakati umefafanuliwa kama mtu ambaye ana uhasama mintarafu ya ukweli, machoni mwa Mungu uko katika shida. Si zaidi ya haya, kila mtu atasema, "Mtu huyu ana tabia mbaya, yeye ni mkaidi na mwenye kiburi. Mtu huyu ni vigumu kukubaliana naye, hana matendo ya ukweli na hapendi ukweli. Hajawahi kuukubali ukweli." Si zaidi ya haya, kila mtu atakutathmini kwa njia hii; lakini tathmini hii inaweza kuamua jaala yako? Watu hufanya tathmini yako, lakini hili haliwezi kuamua jaala yako. Lakini kuna jambo moja ambalo hupaswi kulisahau: Mungu huuchunguza moyo wa mwanadamu, na wakati huo huo Yeye huangalia kila kitu ambacho mtu husema na kufanya. Mungu akimfafanua mtu kwa kusema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," Yeye hamfafanui tu kwa kusema, "Mtu huyu ana tabia potovu kidogo na kwa kiasi kidogo si mtiifu," bali kwa usahihi zaidi Yeye anasema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," hii ni hoja kubwa au hoja ndogo? (Ni hoja kubwa.) Na hili husababisha shida? (Ndiyo.) Je, hili huleta shida gani? Shida hii haiko katika jinsi watu wengine hukuona au jinsi wanavyokutathmini, lakini liko katika jinsi Mungu anavyoona tabia yako potovu ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli. Hivyo ni vipi basi Mungu huona tabia yako ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, unajua? Mungu husema, "Ana uhasama mintarafu ya ukweli na hapendi ukweli." Je, Mungu huliona kwa jinsi gani? Ukweli hutoka wapi? Ukweli humwakilisha nani? (Humwakilisha Mungu.) Hivyo fikiria hili: Mungu anapaswa kuonaje tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, Yeye atalionaje? (Mungu huliona kuwa na uhasama kwelekea Kwake na kama adui Yake.) Na hili ni jambo zito? Mtu aliye na uhasama mintarafu ya ukweli ana uhasama mintarafu ya Mungu. Kwa nini Ninasema kuwa ana uhasama mintarafu ya Mungu? Je, huwa anamtukana Mungu? La. Huwa anampinga Mungu bayana? La. Je, huwa anamshushia Yeye hadhi kisiri? La. Hivyo kufichua tabia ya jinsi hii huwaje uhasama mintarafu ya Mungu? Je, si huu wote ni msukosuko wa bure? Kuna kitu ndani yake, sivyo? Unajua ni kitu gani? Mtu fulani ana tabia hii na hufichua aina hii ya tabia wakati wote na katika maeneo yote na, zaidi ya hayo, yeye huitegemea ili kuishi na haachi kamwe njia hii ambayo kwayo yeye huishi na kufanya mambo, na haitupi kamwe. Wewe hutegemea mambo na tabia hii ili kuishi, na wakati hakuna kitu kinachotokea, ikiwa mtu atasema kuwa una uhasama mintarafu ya Mungu, unaweza kukubaliana naye? Huwezi kukubaliana naye. Hata hivyo, matatizo yanapochipuka, unapokuwa na aina hii ya tabia, wewe huifichua wakati wote na mahali pote? Kwa hiyo hii ni tabia gani? Ni tabia ambayo ni uhasama mintarafu ya Mungu na uhasama mintarafu ya ukweli. Unayasaili maneno ya Mungu, unayachangua, unayachambua na kuyatilia shaka. Inamaanisha nini unapofanya mambo haya? Inamaanisha kwamba unaposikia maneno ya Mungu, wewe hufikiria, "Je, haya ni maneno ya Mungu? Sifikiri huu ni ukweli na sifikiri yote ni lazima yawe ni sahihi." Tabia yako imefichuliwa, ni kweli? Je, una uwezo wa kutii wakati unapofikiria jinsi hii? Hakika huna uwezo. Na kama huna uwezo wa kutii, Mungu bado ni Mungu wako? Hapana, Yeye si Mungu wako. Je, wewe basi humuona Mungu kama nini? Kama chombo cha kujifunza na cha shaka, na hata kama tu mtu wa kawaida, kama mtu mwenye tabia potovu kama tu mtu. Je, si hili linaletwa na tabia potovu ya mtu?
Wakati mtu amekwenda mbali hivyo na wakati ana uhusiano wa aina hii na Mungu, ni uhusiano gani uliopo kati ya mtu huyu na Mungu? Ni wa uhasama na yeye amekuwa mpinzani wa Mungu, sivyo? Ikiwa unamwamini Mungu lakini huwezi kuupata ukweli au kuukubali ukweli, Mungu si Mungu wako. Mungu hakuoni kama adui lakini wewe unamwona Mungu kama mpinzani wako na huwezi kukubali kwamba Yeye ni ukweli wako na njia yako, basi tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa jinsi gani? Unapokabiliwa na maswala unapaswa kwanza kufikiria, "Hali ni ipi hapa? Siielewi vizuri sana, na haiko dhahiri kwangu. "Bila kujali suala ni nini, hufafanui suala hilo kwanza, badala yake kwanza ni lazima uone kile maneno ya Mungu yanachosema juu yake. Unaweza kushindwa kupata maneno husika ya Mungu, na huenda pia usijue ni ukweli gani suala hili linahusisha, lakini unang'amua kanuni—ni kutii, kwanza kabisa. Kwanza kabisa, endelea kutii, tuliza moyo wako na usubiri, usiwe na mawazo au fikira za binafsi, subiri kwa muda na uone jinsi Mungu anavyopanga kukabiliana nalo na kile ambacho Mungu atafanya. Hili ni katika hali ambapo huelewi kabisa. Na je, wakati ambapo huelewi? Kwa mfano, mtu anatoa maoni; unashughulikiaje suala hili? Je, unalishughulikiaje kwa njia inayopatana na ukweli? Kwanza unalikubali; unasikiliza na kusema, "Haya yote ni nini? Aa, kuna shida kwangu kulifanya kwa njia hii? Ikiwa kuna shida, basi hebu tuangalie." Usiichukulie hoja hiyo kwa wepesi; inahusisha mambo katika upeo wa wajibu wako, kwa hiyo unapaswa kulitazama kwa uangalifu. Huu ndio mtazamo sahihi wa kuchukua na hali sahihi ya kuwemo. Unapokuwa katika hali sahihi, wewe hufichua tabia ambayo imechoshwa na ukweli? (Hapana.) Hufichui tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli, na unapotenda kwa njia hii tabia yako ya upotovu inabadilishwa; unatenda ukweli. Unapotenda ukweli kwa njia hii, ni matokeo gani yanayofanikishwa? (Roho Mtakatifu hutuongoza.) Mwongozo wa Roho Mtakatifu ni kipengele kimoja. Kwa Mungu, unatenda ukweli. Wakati mwingine una mwongozo wa Roho Mtakatifu na tatizo linarekebishwa; wakati mwingine baada ya kusikia juu ya suala hili, unalielewa kwa urahisi, na unaliona likiwa rahisi sana. Hicho ni kitu ambacho akili ya mwanadamu inaweza kufanikisha na unahitaji tu kukirekebisha. Hii ni hoja ndogo. Na hoja kubwa ni ipi? Unapotenda kwa njia hii, Mungu hukuona kama mtu anayetenda ukweli na kama mtu anayependa ukweli, na Yeye huona kwamba wewe si mtu anayeuchukia ukweli au ana uhasama mintarafu ya ukweli. Wakati huo huo Mungu anapoona moyo wako, Yeye pia huona tabia yako. Hii ni hoja kubwa. Yaani, unalolifanya mbele za Mungu, unaloishi kwa kudhihirisha mbele ya Mungu na unachokifichua mbele ya Mungu, na vilevile mtazamo unaouchukua, mawazo uliyo nayo na hali uliyomo katika kila kitu unachokifanya—maonyesho haya yote unayo mbele ya Mungu—haya ndiyo mambo muhimu zaidi.
Watu daima wanalalamika juu ya watu na masuala, na hili ni tatizo kubwa. Je, wao daima hufikiri nini? Wanafikiri kuwa ni watu wengine ambao ni wakatili kwao, au kwamba wengine huyafanya mambo kuwa magumu kwa makusudi, au huyapata makosa tu na watu wengine. Je, mtazamo huu ni sahihi? (Hapana, si sahihi.) Kwa nini unasema hapana? Ni kosa kabisa kulalamika daima juu ya masuala na watu. Hawafanyi jitihada na ukweli, na wao wanajaribu daima kuepuka aibu na kutafuta uthibitisho mbele ya wengine au miongoni mwa watu wengine, na wao daima hutaka kutumia njia za kibinadamu kuzitatua hoja hizi zote. Hiki ndicho kikwazo kikubwa mno kwa kuingia kwa maisha. Kwa kufanya kwa njia hii, kutenda kwa njia hii na kumwamini Mungu kwa njia hii, hutaweza kamwe kupata ukweli, kwa kuwa kamwe huji mbele ya Mungu. Huji kamwe mbele ya Mungu kukubali vitu vyote ambavyo Mungu hupanga kwa ajili yako, hutumii kamwe ukweli ili kutatua mambo haya yote, na daima wewe hutaka kutumia mbinu za kibinadamu kuyatatua. Hivyo machoni pa Mungu, umeenda mbali sana na Yeye na sio tu kwamba moyo wako umekwenda mbali sana na Mungu, lakini mawazo yako yote, nia zako zote na hali yako yote havijawahi kuwa mbele ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu huwaona wale ambao hulalamika juu ya masuala na watu. Kwa hiyo, watu wengine ambao wana kipaji cha kuzungumza na ni wepesi kung'amua, hufikiria, "Nina ufasaha, na wakati ninapokuwa na watu wengine, wote hunihusudu na kunipenda. Wao hunitukuza, na watu wengi sana huridhishwa nami. "Je, hili ni la manufaa yoyote? Sifa yako njema miongoni mwa watu wengine imeanzishwa, lakini mbele ya Mungu, Amekupuuza daima, na anasema kuwa wewe ni mtu asiyemwamini Mungu na kwamba una uhasama mintarafu ya ukweli. Miongoni mwa wengine wewe hutenda kwa njia ambayo ni laini na ya hila, unaweza kumshughulikia mtu yeyote, una uwezo mkubwa wa kushughulikia hoja, na unaweza kukubaliana na mtu yeyote. Lakini mwishowe, kwa tathmini moja kutoka kwa Mungu utakwisha, utafika mwisho mbaya, na jaala yako itapangwa. Mungu atasema: "Huyu ni mtu asiyeamini, akipeperusha bendera ya imani katika Mungu ili kupata baraka. Huyu mtu ana uhasama mintarafu ya ukweli, hajawahi kamwe kufanya jitihada na ukweli, na hajawahi kuukubali ukweli." Mnafikiria nini juu ya aina hii ya tathmini? Je, hii ndiyo tathmini mnayoitaka? (Hapana.) Bila shaka sicho kile mnachokitaka. Labda watu wengine hawajali, na wao husema, "Sijali. Hatuwezi kumwona Mungu kwa njia yoyote. Suala la kweli zaidi ambalo tunalo ni kuwa tunapaswa kukubaliana na watu walio nasi. Ikiwa hatuwezi kufanya mahusiano haya yafaulu basi tunawezaje kuishi miongoni mwa watu hawa? Maisha yetu yangekuwa magumu sana. Angalau sana tunapaswa kukubaliana na watu hawa na kushughulikia mahusiano vizuri. Chochote kingine kinaweza kusubiri." Ni watu wa aina gani hawa? Je, hawa bado ni watu ambao wanamwamini Mungu? (Hapana.) Mtu ni lazima aishi mbele ya Mungu nyakati zote na ni lazima aje mbele ya Mungu na kutafuta ukweli nyakati zote na kwa hoja zote, ili mwishowe Mungu atasema: "Wewe ni mtu anayeupenda ukweli na Mungu anafurahishwa nawe, Mungu anakukubali. Mungu huuona moyo wako na huiona tabia yako. "Unafikiria nini kuhusu tathmini hii? Hii ina maana kwamba wewe ni salama, sivyo?
Je, nyinyi kwa kawaida huzingatia hoja hizi? Hebu niwaambie, mnapomwamini Mungu, bila kujali kama unafanya wajibu wa nje, au unafanya wajibu unaohusiana na kazi yoyote au kipengele chochote cha kazi ya weledi ndani ya familia ya Mungu—bila kujali ni wajibu gani unaoufanya—ikiwa huwezi daima kuja mbele ya Mungu, ikiwa huwezi kuishi mbele ya Mungu, basi wewe si muumini na hakuna tofauti kati yako na mtu asiyeamini. Je, hili linasikika sahihi kwako? Je, mnaweza kufahamu jambo hili? Labda kuna baadhi ya watu sasa ambao hawawezi kufanya wajibu wao kwa sababu ya mazingira yasiyofaa, na wanaishi miongoni mwa wasioamini, lakini daima wanaweza kupata nuru na mwongozo wa Mungu—hivyo hali ni ipi hapa? Mnajua? (Ni kwa sababu daima wao huja mbele ya Mungu.) Ndiyo, hili huamua jinsi hali ya kiroho ya mtu ilivyo. Ikiwa, ndani yako mwenyewe, daima huwezi kumhisi Mungu, ikiwa daima u mdhaifu, daima u hasi, au wewe daima ni mwasherati, au daima hubebi mzigo katika wajibu wako na moyo wako siku zote unaboronga bila lengo lolote, basi hii ni hali nzuri au hali mbaya kuwemo? Je, ni hali ambapo unaishi mbele ya Mungu? Au ni hali ambapo huishi kamwe mbele ya Mungu? (Ni hali ambapo hatuishi mbele ya Mungu.) Basi fikirieni hili kwa makini—katika hali nyingi, huwa mnaishi mbele ya Mungu au hamuishi mbele ya Mungu? Je, mnafahamu vyema juu ya hili ndani ya mioyo yenu? Je, nyinyi huishi mbele ya Mungu wakati mwingi, au ni kwa nyakati chache tu? (Ni kwa nyakati chache tu.) Hili ni sumbufu kwenu. Kama mtu ni mchezaji, mwimbaji, mwandishi au mtengenezaji filamu, ikiwa moyo wake haujishughulishi kamwe na kufanya wajibu wowote unaofaa, ikiwa yeye ni mpotovu na hastahimiliki, ikiwa huwa daima anavurugika anapokabiliwa na masuala, hana wazo lolote ni hoja ipi inayohusisha kipengele kipi cha ukweli, wala hana wazo lolote kama kile anachokifanya kina athari yoyote, ikiwa hajui mambo gani anayoyafanya kila siku yanayomchukiza Mungu, ni mambo gani ambayo Mungu anaweza kuyakubali au ni mambo gani Mungu huyachukia, na wao huendelea tu siku baada ya siku katika kiwewe, basi ni hali aina gani hii ya kuwemo? Je, wale wanaoishi katika hali hii wana moyo wa kumuogopa Mungu ndani yao? Je, wana uwezo wa kutenda na kanuni? Je, wana uwezo wa kufanya chochote cha maana? (Hapana.) Wanapofanya wajibu wao, wanaweza kusema, "Ni lazima nivumilie vikwazo fulani, ni lazima nifanye kazi kwa bidii, kwa moyo wangu wote na kwa nguvu zangu zote, na kuwa mwaminifu"? Je, ana uwezo wa kuwa na uaminifu wowote? (Hapana.) Basi mnafanya nini hapa kwa kweli mnapofanya wajibu wenu? (Mkitumia nguvu.) Mko sawa; Mnatumia nguvu. Nyinyi ni wenye uwezo wa kazi, sivyo? Chakula chenu na nyumba zenu zote zimeshughulikwa, na halafu nyinyi hufanya kazi hapa. Ingawa hamchumi fedha hapa, mnahisi ni sawa mnapopata chakula, kinywaji na mahali pa kuishi. Lakini nyinyi huchuma ukweli? (Hapana.) Basi nyinyi hupoteza sana. Nyinyi ni wapumbavu mno! Mmemwamini Mungu kwa miaka mingi sasa, hazijakuwa siku chache tu. Mmesikia ukweli mwingi sana na hamjui mnamwamini Mungu kwa minajili gani, mnachohitaji kufanya, mnachopaswa kupata, au ni kitu gani cha muhimu zaidi kupata. Mnajua kidogo sasa? (Ndiyo.) Mnajua nini? Niambieni. (Kwa kumwamini Mungu, kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi.) Kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi? Kweli au uongo? (Kweli.) Bila shaka ni kweli. Lakini labda huenda msiwe na maarifa halisi ndani ya mioyo yenu hivi sasa, na huenda hamjalitambua kwa kiwango hiki.
Je, mmekisoma Kitabu cha Ayubu? (Ndiyo.) Na mlipokisoma Kitabu cha Ayubu, mioyo yenu ilisisimka? (Ndiyo.) Hivyo mlipata fikira za shauku, na kutaka kuwa mtu kama Ayubu? (Ndiyo.) Ni kwa muda gani mliweza kuendeleza hali hiyo na hisia hiyo? Nusu siku, siku mbili, juma moja? Au kwa mwezi mmoja au miwili, au mwaka mmoja au miwili? (Labda siku mbili hadi tatu.) Hisia hiyo iliondoka baada ya siku tatu? Wakati hisia hiyo inapoondoka, wewe huendelea kusoma, na unapoendelea kusoma unaweza kuiendeleza kwa siku zingine tatu. Lakini hivyo sivyo ilivyo, au ndivyo? Unaposoma kitabu hicho na unahisi msisimko, unapaswa kuomba, kindani fanya uamuzi wako kuwa unataka kuwa kama Ayubu, mtu ambaye anaweza kumjua Mungu, ambaye anaweza kupata ukweli, na anayeweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unasali kwa Mungu afanye vivyo hivyo kwako, na kwamba Mungu akuongoze na kukupangia mazingira, kukutolea nguvu, kukukinga katika mazingira yoyote ambayo unaweza kukabiliana nayo ili uweze kusimama imara, ili usimuasi Mungu, na unaweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Unahitaji daima kumsihi Mungu kwa lengo hili na kwa kile unachokitamani sana na unachotaka kukipata moyoni mwako, unahitaji kusihi na kuomba kwa ajili yalo, na wakati Mungu anapouona moyo wako wa kweli Yeye atalifanya. Huhitaji kuogopa Mungu akifanya jambo hili, kwa maana Mungu hawezi kuufanya mwili wako kufunikwa na vidonda kama wakati Alipomjaribu Ayubu na kukunyang'anya kila kitu ulicho nacho; Mungu hatakufanyia hivyo. Hatua kwa hatua Atafanya kazi Yake kwako kwa mujibu wa kimo chako. Ni lazima usihi kwa uaminifu; usilisome tu leo, ujihisi kusisimka na kumsihi Mungu, na kisha baada ya siku mbili usifanye chochote, na yawe yameisha mara unapogeuka. Watu husema, "Ayubu ni nani?" "Nani? Ayubu? Ayubu ni nani? Je, nawezaje kutojua? Huenda nimesikia kumhusu." Hili ni sumbufu! Usilisome kwa siku tatu na lote limesahaulika, limetoka moyoni mwako. Ukiwahusudu watu kama Ayubu na ungependa kuwa mtu kama huyo, moyoni mwako unapaswa kuwa na njia ya jinsi ya kuwa mtu kama huyo, lazima uweke moyo wako mbele ya Mungu, kisha ni lazima uombe kuihusu, omba kuihusu mara nyingi, chukua hoja hii kutoka moyoni mwako na kuitafakari mara nyingi, soma vitabu, soma makala kuhusu Ayubu na maneno ya Mungu yanayohusiana na Ayubu, itafakari daima na tena na tena, fanya ushirika pamoja na watu ambao wana aina hii ya maarifa, uzoefu au azimio , na lazima ufanye kazi kwa bidii mintarafu ya lengo hilo. Unapaswa vipi kufanya kazi kwa bidii? Kusoma tu kwa kweli sio kufanya kazi kwa bidii. Unahitaji kufanya jitihada na hoja hii, utoe maombi yako na kuiweka katika matendo, huku wakati huo huo ukiwa na azimio la kuvumilia mateso na kuwa na moyo wa shauku na hamu. Kisha unarairai, utoe maombi yako na kumwomba Mungu afanye hivi. Ikiwa Mungu haifanyi, itakuwa bure bila kujali ni jitihada kiasi gani unayoiweka, na jitihada zako ni za bure. Mungu huifanyaje? Yeye huanza kwa kuweka na kupanga mambo kwa ajili yako kulingana na kimo chako. Kwa mfano, unakaribia kuchukua mtihani wa kuingia chuo cha elimu, na unasema, "Ninataka alama ili kuingia katika Chuo Kikuu cha Tsinghua." Unaanza kuweka jitihada ili kufanikisha hili, unapitia upya masomo yako, unatafuta vifaa vya kujifunza juu ya chochote na kila kitu na unatafuta walimu kukufundisha. Kisha unawaambia wazazi wako na wanasema, "Mtoto wetu ana azimio zuri. Yeye huanza jambo kwa dhati, ana azimio na hajakosa ustadi." Kwa hiyo, wazazi wako watafanya nini? Wote wawili wataandaa ada yako ya masomo na kukupatia mwalimu. Watafanya mipango sahihi ya maisha yako, wakati unapopaswa kupumzika, na masomo yako, wakupeleke shuleni na kukuchukua baadaye, na watalifanya ili kwamba, wakati huu, usipate uchovu, au njaa, au kukosa chakula cha kutosha. Watakusaidia kwa kushughulikia na kusimamia mambo katika ulimwengu wa nje ili usichanganyikiwe. Watakufanyia mipango sahihi katika vipengele vyote. Kwa njia hii, utakuwa na wakati wa kutosha wa kupitia upya, kusoma na kufanikisha ndoto yako. Kuhusu kumwamini Mungu, chochote unacholenga au uamuzi wowote ulio nao, unapaswa kuzungumza na Mungu. Unahitaji kuomba juu ya hoja hii na kusihi sana juu yalo; itachukua muda mrefu! Itakuwa bure kuwa na moyo usio mwaminifu. Ikiwa unasali mara kadhaa tu mara kwa mara na kisha unapoona kwamba Mungu hajakufanyia chochote, unasema, "Lisahau. Sijali. Liwe liwalo, nitaacha tu mambo yatokee kama kawaida yake, na nitachukua mambo kama yanavyokuja," basi hili litakuwa bure, na moyo wako si mwaminifu. Je, Mungu atakufanyia chochote ikiwa una dakika kadhaa tu za shauku? Je, Mungu atapanga mazingira kwa ajili yako? Je, hilo linakubalika? Kwa kweli Mungu hafanyi kazi kwa njia hiyo. Mungu anataka kuona uaminifu wako na Anataka kuona ni kwa muda gani uaminifu wako na bidii ya moyo wako vinaweza kudumishwa, na kama moyo wako ni kweli au uongo. Mungu atangoja; Yeye husikiliza sala zako na kile unachorairai, na Yeye husikia maazimio yako na shauku zako, lakini Yeye bado hajaona maazimio yako ya kuvumilia mateso, kwa hivyo Yeye hatakufanyia chochote. Ikiwa wewe husema maneno machache na kisha kwenda, Mungu atakufanyia chochote? Hakika hapana. Lazima uendelee kurairai, endelea kuomba, jitahidi na kulitafakari, kisha uonje mazingira ambayo Mungu hukupangia—yatakujia kidogo kidogo, na Mungu ataanza kutenda. Bila moyo wa kweli, ni bure. Wewe husema, "kwa kweli mimi humhusudu Ayubu na kwa kweli mimi humhusudu Petro." Ni haja gani kuwahusudu? Huwezi kuwa wao bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, na bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, Mungu hatakufanyia kazi sawa na ile Aliwafanyia. Kwa nini hivyo? Kwa sababu wewe si aina moja ya mtu kama walivyokuwa. Humiliki azimio lao, au ubinadamu wao, na humiliki moyo wao wa shauku uliotafuta ukweli. Wakati utakapokuja utakapomiliki vitu hivi, ni hapo tu ndipo Mungu atakapokufanyia zaidi. Unaelewa?
Je, wengi wenu sasa wana azimio la kuelewa ukweli, kupata ukweli na kukamilishwa mwishowe? (Ndiyo.) Azimio lako ni kubwa kiasi gani? Je, unaweza kufanya liendelee kwa muda gani? Unajua? (Nina azimio hili wakati niko katika hali nzuri. Wakati mambo yanapotokea ambayo hayakubaliani na mwili wangu au kupatana na dhana zangu, na ninapopatwa na usafishaji au matatizo ndani yangu, basi imani yangu hupotea, mimi hukwama kwa namna ya hali hasi, na azimio nililokuwa nalo mwanzo hupungua hatua kwa hatua.) Hili halitaweza. Huku ni kuwa dhaifu sana. Lazima ufikie hatua ambapo azimio lako halibadiliki bila kujali ni mazingira gani unayoyakabili; huku tu ndiko kuwa mwaminifu, na huo ndio upendo halisi wa ukweli na shauku halisi ya kuwa aina hii ya mtu. Itakuwa bure kujikunyata wakati hoja fulani ndogo au shida inapotokea, au kuwa hasi, kusononeka na kuacha azimio lako mwenyewe wakati unapokabiliwa na shida ndogo. Unahitaji kuwa na nguvu ya mtu anayechagua kuhatarisha maisha yake, na kusema, "Bila kujali kinachotokea, hata kama ni lazima nife sitaacha azimio langu au kuachana na lengo hili." Halafu hakutakuwa na shida ambayo inaweza kukuzuia, na Mungu atakufanyia jambo hili. Aidha, lazima uwe na mtazamo wa aina hii na ufahamu jambo linapotokea, na kusema, "Bila kujali kinachofanyika, yote ni sehemu ya kufanikisha lengo langu, na ni shughuli ya Mungu. Kuna udhaifu ndani yangu, lakini mimi si hasi. Ninamshukuru Mungu kwa upendo Anaonipa na kwa kunipangia aina hii ya mazingira. Ni lazima nisisalimu amri. Kusalimu amri kwangu kungekuwa sawa na kufanya masikilizano na Shetani, na ni sawa na kujiangamiza. Kusalimu amri juu ya shauku na azimio langu kutakuwa sawa na kumsaliti Mungu. "Hii ni aina ya moyo ambao ni lazima uwe nao. Suala lolote dogo unalokabiliana nalo ni pumziko dogo katika mfanyiko tendani wa kufanya maendeleo katika maisha, na ni sharti usiruhusu lizuie kwendelea kwako au kuzuia mwelekeo wako wa mbele. Ni vyema kwako kuchukua pumziko dogo au upumzike kwa muda, lakini mwelekeo wako haupaswi kubadilika, na ni lazima usikome kabisa kwa hali yoyote; hii ndiyo aina ya azimio na uamuzi unayopaswa kuwa nayo. Bila kujali wengine wanavyosema au jinsi walivyo, na bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, azimio lako halipaswi kubadilika. Mungu asema, "Sikutaki tena," nawe unasema, "Mungu hanitaki tena, kwa hivyo nitasahau tu kulihusu." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Au Mungu asema, "Wewe umepotoka sana, na Ninakuchukia," nawe unasema, "Mungu ananichukia, nitaishi kwa sababu gani tena? Nitatafuta kamba ili kujinyonga." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Hutafanikisha lengo lako jinsi hii. Kwa mintarafu ya hadhi yenu ya sasa, hakuna hata mmoja wenu ambaye ameweza kujaribiwa na Mungu bado, na kusema, "Mungu, tafadhali nijaribu." Huna hadhi hii. Je, mna uwezo wa kufanya nini tu? Ni lazima muombe: "Ee Mungu, tafadhali niongoze, nipe nuru, nipe bidii ya kuendelea na unipe bidii ili niweze kuitembea njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa mujibu wa shauku zangu. Bila kujali namna gani ya mateso ninayoyapitia, Wewe hunipa nguvu na Wewe hunilinda. Ingawa ninaweza kuwa dhaifu na ingawa kimo changu ni kichanga, ninakuomba Unipe nguvu, kunilinda na kunionyesha wema. Sitasalimu amri." Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba, na ni lazima daima mje mbele ya Mungu kuomba. Wakati wengine wanacheka na kufanya mzaha na kujiendekeza, ombea hili; wakati wengine wanapojifurahisha, ombea hili; wakati wengine ni hasi, ombea hili; wakati wengine wanalala fofofo, au kuchelewa kuamka, wewe tayari unaliombea hili; wakati wengine wanatembea njia ya ulimwengu na kwa ulafi kufurahia anasa za kimwili, au kufuata mienendo ya kidunia, ombea hili. Wakati unapoweza kuishi mbele ya Mungu katika mambo yote na unaweza kujiweka katika mipaka fulani, wakati unapoweza kujiweka ukiishi mbele ya Mungu na kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi Mungu anaweza kuliona hili. Wakati Mungu anapouona moyo wa mtu, Yeye hayatumii tu macho Yake; Yeye hupanga mazingira kwa ajili yako na Yeye hugusa moyo wako kwa mikono Yake. Kwa nini Nasema hili? Wakati Mungu anapokupangia mazingira, Yeye hutazama kuona kama moyo wako unachafuliwa nayo, unayachukia, unayapenda au ni mtiifu, au kama husubiri kwa utulivu, au hutafuta ukweli—Yeye huona jinsi moyo wako unavyobadilika na ni katika mwelekeo gani huenda. Mabadiliko katika moyo wako, kila badiliko la fikira na mawazo ndani ya moyo wako kuhusu watu, hoja, na mambo ambayo Mungu hupanga kwa ajili yenu, na kila badiliko ya hali ya moyo uliyo nayo—Mungu anaweza kuyahisi yote. Ingawa huenda hujamwambia yeyote na huenda hujaomba, badala yake kufikiria tu mawazo haya kwa moyo wako mwenyewe au katika ulimwengu wako mwenyewe, lakini kwa Mungu ni wazi kabisa na Yeye huliona wazi kwa tazamo moja. Watu hutumia macho yao kukuona, na Mungu hutumia moyo Wake kuugusa moyo wako—Yeye yu karibu hivi nawe. Na kama unaweza kuuhisi uchunguzi wa Mungu, basi unaishi mbele ya Mungu. Kama huwezi kuuhisi kabisa na unaishi ndani ya ulimwengu wako, basi uko katika shida. Wewe huishi mbele ya Mungu, wewe uko mbali na Mungu na mbali sana kutoka Kwake, huendi karibu Yake kwa moyo wako au moyo wako uukaribie moyo Wake, na hukubali uchunguzi wa Mungu. Na Mungu anajua hili! Mungu anaweza kabisa kuhisi yote haya. Kwa hivyo, wakati una azimio na lengo la kukamilishwa na Mungu, kuwa mtu anayetekeleza mapenzi ya Mungu, mtu anayemcha Mungu na aepukanaye na maovu, unapoweza kuomba mara nyingi juu ya hoja hii na kusihi kwa ajili yalo, unapoweza kuishi mbele ya Mungu, kutokwenda mbali na Mungu au kumwacha Mungu, basi wewe unalielewa hili, na Mungu anajua kuhusu hilo pia. Watu wengine wanasema: "Mimi ni dhahiri kulihusu, lakini sijui kama Mungu anajua kulihusu." Hili si jambo la busara. Kwa hiyo hali ni gani hapa? Kama wewe mwenyewe u dhahiri kulihusu, na hujui kama Mungu anajua kulihusu, basi huna uhusiano na Mungu. Umeelewa? Kwa nini Nasema wewe huna uhusiano na Mungu? Wewe huishi mbele ya Mungu, kwa hivyo unashindwa kuhisi kama Mungu yu pamoja nawe, kama Mungu anakuongoza au kukulinda, na kama Mungu anakushutumu wakati unapofanya jambo baya. Huwezi kuhisi jambo lolote kati ya haya, kwa hiyo hili linamaanisha kwamba huishi mbele ya Mungu. Wewe hufikiria tu mwenyewe na kuleweshwa na mawazo yako mwenyewe; huko ni kuishi katika ulimwengu wako mwenyewe na sio kuishi mbele ya Mungu, na hakuna uhusiano kati yako na Mungu.
Mtu anawezaje kuudumisha uhusiano wake na Mungu? Ni kwa njia gani anaweza kuudumisha? Kwa njia ya kusihi, kuomba na kuwa na ushirikiano na Mungu katika moyo wake. Aina hii ya uhusiano itakuwezesha kuishi daima mbele ya Mungu, na kwa hiyo utakuwa mtu mwenye amani sana. Watu wengine daima hufanya mambo ya nje na hujihusisha na mashauri ya nje. Baada ya siku moja au mbili bila kushiriki katika maisha ya kiroho, moyo wao hauna utambuzi, na baada ya siku tatu, au siku tano, bado hauna utambuzi, au bado hauna utambuzi baada ya mwezi mmoja au miwili. Hili lina maana kwamba hawaombi au kurairai chochote, na hawajishughulishi na ushirikiano wa kiroho. Kusihi ni wakati unapokabiliwa na masuala, unamwomba Mungu akusaidie, akuongoze, akukimu, akupe nuru, akuruhusu ujue mapenzi ya Mungu na kujua ukweli ni nini. Kuomba kuna mawanda mapana kiasi. Wakati mwingine ni kusema maneno ndani ya moyo wako, kuzungumza na Mungu wakati unapokabiliwa na shida na kusema maneno yaliyo moyoni mwako kwa Mungu wakati unapokuwa hasi na dhaifu. Unaweza pia kumwomba Mungu unapokuwa mwasi, au unasema na Mungu juu ya masuala yanayokukabili kila siku, yote kuhusu yale ambayo unaweza kuyabaini na yale ambayo huwezi kuyabaini. Huku ni kuomba. Mawanda ya kuomba kimsingi ni kuwa na mazungumzo na Mungu, wakati mwingine kwa nyakati zilizopangwa na wakati mwingine kwa nyakati zisizoratibiwa, na yanaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Ushirikiano wa kiroho kwa kweli haushikilii muundo fulani. Labda kuna suala, labda hakuna; wakati mwingine kutakuwa na kitu cha kusema, na wakati mwingine hakutakuwa. Huu ni ushirikiano wa kiroho. Wakati kuna suala maalum la kuzungumzia na Mungu, basi unaweza kuomba. Wakati hakuna suala lolote, unafikiri tu juu ya Mungu, "Mungu humpendaje mwanadamu? Mungu anamtunzaje mwanadamu? Mungu humshutumuje mwanadamu?" "Ee Mungu, ninahisi nimefanya jambo hili vibaya. Kama kwa kweli nimefanya jambo hili vibaya, basi nishutumu na unifanye nifahamu." Huu ni ushirika wa kiroho, na unaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Wakati mwingine uko barabarani na unafikiria kuhusu kitu ambacho huufanya moyo wako uhisi huzuni kweli. Huna haja ya kupiga magoti au kuyafunga macho yako, lakini badala yake unasema mara moja kwa Mungu moyoni mwako: "Ee Mungu, naomba Uniongoze na suala hili. Mimi ni dhaifu na siwezi kulishinda. "Moyo wako umesisimuliwa, na kwa maneno haya machache rahisi Mungu anajua yote kulihusu. Wakati mwingine unafikiria kuhusu familia yako, na unaweza kusema: "Ee Mungu, kwa kweli nimeikosa familia yangu …." Humkosi mtu yeyote hasa, unahisi tu vibaya, hivyo unaongea na Mungu. Usizungumze na watu wengine kulihusu, kwa kuwa hilo halina maana. Unapozungumza na mtu mwingine kulihusu, huenda ikawa kwamba anaikosa familia yake hata zaidi ya wewe, basi hili linakuathiri na unaishia kuikosa yako hata zaidi, na hili halikuletei faida yoyote kamwe. Unapozungumza na Mungu kulihusu, basi Mungu atakufariji, Akufurahishe tena na kukupisha katika wakati huu mgumu na kupita hali hii ndogo. Hali hii, jiwe hili dogo njiani mwako halitakukwaa, halitakuzuia au kuathiri utekelezaji wa wajibu wako. Wakati mwingine, unapozungumza au kufanya ushirika na wengine, moyo wako unaweza ghafla kuwa na hisia ya kuvunjika kidogo au kujisikia mwenye wasiwasi sana, hivyo unafanya haraka kumwomba Mungu, na unaweza kufanya hivi wakati wowote na katika mahali popote. Kunaweza kuwa hakuna chochote unachokisihi, au chochote unachotaka Mungu akufanyie au akunurishie, unaongea tu na Mungu na kuzungumza Naye wakati wowote na katika mahali popote. Ni hisia gani unayopaswa uwe nayo wakati wote? Ni hii: Mungu huwa hatoki kandoni mwangu kamwe, Yeye yu pamoja nami kandoni mwangu wakati wote, Yeye hajawahi kuniacha, na ninaweza kuhisi hili. Bila kujali ni mahali gani nipo, bila kujali ninafanya nini, kama ninapumzika au kulala, kula chakula, au kwa mkutano, au kama sisemi chochote mchana kutwa ninapotekeleza wajibu wangu, najua moyoni mwangu kwamba Mungu ananiongoza kwa mkono, na kwamba Yeye hajawahi kuniacha. Wakati mwingine, wewe hufikiria jinsi umefaulu kwa miaka hii michache iliyopita, mwezi baada ya mwezi, na unahisi moyoni mwako kwamba kimo chako kimekomaa na kwamba ni Mungu anayekuongoza, na kwamba ni upendo wa Mungu ambao unakulinda daima. Unapofikiri hivi, unaomba moyoni mwako: "Nakushukuru Wewe, Mungu!" Na wewe unatoa shukrani zako, na kusema: "Mimi ni dhaifu sana, mwenye woga sana, na mpotovu kwa kina sana. Kama Hukuniongoza kwa njia hii, mimi mwenyewe singeweza kufanikiwa hadi leo. Asante Mungu!" Je, si huu ni ushirika wa kiroho? Kama ungekuwa jinsi hii, basi si ungekuwa na mengi ya kumwambia Mungu? Hungeishi siku baada ya siku bila kuwa na kitu cha kumwambia Mungu. Ikiwa huna chochote cha kumwambia Mungu, basi inamaanisha kwamba Mungu hayuko ndani ya moyo wako. Kama una Mungu ndani ya moyo wako, basi unaweza kumwambia Mungu mambo unayoweza kusema kwa wandani wako—Mungu ni msiri wako wa karibu zaidi. Unapomruhusu Mungu kuwa msiri wako wa karibu zaidi, rafiki yako wa karibu zaidi, familia unayoweza kuitegemea zaidi, kuiegemea zaidi, na Aliye mwaminifu zaidi, Aliye mwandani sana na wa karibu, basi itakuwa vigumu kutokuwa na mambo ya kusema Kwake. Wakati daima una mambo ya kumwambia Mungu, si basi utaweza kuishi daima mbele ya Mungu? Unapoweza kuishi mbele ya Mungu daima, basi wakati wote utaweza kutambua jinsi Mungu anavyokuongoza, jinsi Mungu anavyokulinda, jinsi Anavyokutunza, jinsi Anavyokuwa amani yako na furaha, Anavyokupa baraka na nuru, jinsi Mungu anavyokushutumu, kukufundisha nidhamu, kukuadhibu, kukuhukumu na kukuadibu. Wakati unapoishi mbele ya Mungu daima, moyo wako utajua kwa dhahiri sana kile Mungu anachofanya ndani yako. Hutakuwa na siku ambapo utakuwa mpumbavu kabisa na kutojua chochote, ukisema tu maneno "Ninamwamini Mungu, mimi hutekeleza wajibu wangu, mimi huhudhuria mikutano, mimi husoma kila siku na huomba kila siku." Huwezi tu kupitia mifanyiko tendani hii yote au kuwa tu na aina hii ya tabia ya nje.
Mnapaswa kujua sasa, kwa hiyo ni nini kitu muhimu zaidi katika kumwamini Mungu? Unapomwamini Mungu, kama Mungu hayuko ndani ya moyo wako na Yeye hakuhusu, na kama humwoni Mungu kama mwandani wako sana, wako wa karibu sana, familia na msiri mwaminifu sana na wa kutegemewa sana, basi Mungu si Mungu wako. Sawa, kwa hiyo sasa nendeni na mtende kwa muda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema, na muone kama hali yenu ya ndani itabadilika au la. Tenda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema na hakika utaishi mbele ya Mungu, utaishi katika tabia ya kawaida na kuwa katika hali ya kawaida. Wakati hali ya mtu ni ya kawaida, ni hapo tu ambapo mambo anayoyaonyesha na kuyafichua kwa kila hatua, au miongoni mwa watu tofauti, masuala, na mambo, au katika mazingira tofauti, yatakuwa ya kawaida. Ni kwa njia hii tu ambapo maisha yake yanaweza kukomaa na anaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli kidogo kidogo. Unaelewa? (Ndiyo.)
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatano, 31 Oktoba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Je, Umekuwa Hai Tena?"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Je, Umekuwa Hai Tena?"

Mwenyezi Mungu anasema, "Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Baada ya hapo ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi."
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumanne, 30 Oktoba 2018

Mashahidi wa Kristo wa Siku za Mwisho | Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hekima ya Mungu

Mashahidi wa Kristo wa Siku za Mwisho | 8. Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu
8. Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?
Aya za Biblia za Kurejelea:
"Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Hivyo ndivyo alivyokuwa mwanzoni na Mungu" (YN. 1:1-2).
"Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli" (YN. 1:14).
"Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu" (YN. 14:6).
"Maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai" (YN. 6:63).
Maneno Husika ya Mungu:
Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu.
kutoka kwa "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea" katika Neno Laonekana katika Mwili
"Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili." Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili.
kutoka kwa "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia kwenye neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani chake. Kupitia neno, kazi yote ambayo Mungu hupenda kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa. Kupitia neno, binadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Binadamu ameliona neno, amelisikia neno, na akapata habari ya uwepo wa neno. Kutokana na haya, binadamu anaamini katika uwepo wa Mungu; binadamu anaamini katika uwezo na hekima za Mungu, pamoja na moyo wa upendo wa Mungu kwa binadamu na tamanio Lake la kumwokoa binadamu. Ingawa neno "neno" ni rahisi na kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu kuwa mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Baadaye, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, akichungwa na kujazwa na neno; wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata zaidi kuishi chini ya na hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kutimiza mapenzi ya Mungu, kubadilisha sura asilia wa ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa.
kutoka kwa "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo Mungu Amekuwa mwili kimsingi ili kukamilisha kazi ya "Neno kuonekana katika mwili," kutumia neno kumfanya mwanadamu kamili, na kumfanya mwanadamu kukubali ushughulikiaji wa neno na usafishaji wa neno. Katika maneno Yake, anakufanya kupata kupewa na kupata uzima; katika maneno Yake, unaona kazi Yake na matendo. Mungu Anatumia neno kukuadibu na kukutakasa, na hivyo ukipata ugumu wa maisha, ni pia kwa sababu ya neno la Mungu. Leo, Mungu hafanyi kazi kwa kutumia mambo ya hakika, ila ni kwa maneno. Baada tu ya neno Lake kuja juu yako ndipo Roho Mtakatifu Atafanya kazi ndani yako na kukufanya upate uchungu ama uhisi utamu. Ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukuleta katika hali halisi, na ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukufanya mkamilifu. Kwa hivyo, angalau lazima uelewe kuwa kazi inayofanywa na Mungu katika siku za mwisho kimsingi ni kutumia neno Lake kumfanya kila mwanadamu kamili na kumwongoza mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ni kupitia kwa neno; Hatumii ukweli kuadibu. … Kwa hivyo, katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi. Katika maneno Yake pekee ndipo unaweza kuona kile Alicho; ni katika maneno Yake pekee ndiyo unaweza kuona kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe. Mungu katika mwili Anapokuja duniani, hafanyi kazi nyingine ila kuongea maneno—hivyo basi hakuna haja ya kutumia uhakika; maneno yanatosha. Hii ni kwa sababu Amekuja kimsingi kufanya kazi hii, kumruhusu mwanadamu aone nguvu Zake na ukuu ulio kwenye neno Lake, kumruhusu mwanadamu kuona kupitia kwa maneno Yake jinsi Alivyojificha kwa unyenyekevu, na kumruhusu mwanadamu kujua ukamilifu Wake kupitia kwa maneno Yake. Kila kitu Alicho nacho na kile Alicho kiko katika maneno Yake, hekima Yake na ajabu yako katika maneno Yake. Katika hii ndipo unapofanywa kuona mbinu nyingi ambazo Mungu anatumia kuongea maneno Yake. … Leo Mungu wa kweli Mwenyewe wa mwili Anaongea tu, na hatendi. Huu ni ukweli! Anatumia maneno kukufanya mkamilifu, na Anatumia maneno kukulisha na kukunyunyizia. Pia Anatumia maneno kufanya kazi, na Anatumia maneno badala ya uhakika kukufanya ujue ukweli Wake. Kama una uwezo wa kutazama ukweli huu wa kazi ya Mungu, basi itakuwa vigumu kuwa wa kutoonyesha hisia.
kutoka kwa "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Na bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu, wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye tu, anafanya kazi anayotarajia kufanya, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa na aibu na wanyonge. …
Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua baada ya hatua ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, na hukabiliwa na kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunajifunza haki ya Mungu na adhama ya tabia Yake, na kufurahia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua asili na kiini cha Mungu, tunakuja kufahamu mapenzi ya Mungu, tunakuja kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno yake hutufanya sisi tufe, na kutufanya kuzaliwa upya; maneno yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa kwenye mikononi Yake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho yake na kufurahia upendo wake na huba yake; wakati mwingine sisi ni kama adui wake, waliofanywa majivu na ghadhabu yake katika macho yake. Sisi ni wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao Yeye hufikiria kuhusu kuwapata mchana na usiku. Yeye ni mwenye huruma kwetu, anatudharau, yeye hutuinua, yeye hutufariji na kutuhimiza, yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Yeye hujitia wasiwasi usiku na mchana kwa ajili yetu, Yeye hutulinda na kututunza usiku na mchana, na hatuachi kamwe, na Yeye hutoa utunzaji Wake wote kwetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa maneno ya mwili huu mdogo na wa kawaida, tumefurahia ukamilifu wa Mungu, na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. …
Matamshi ya mungu yanaendelea, na Yeye hutumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya na kutuelekeza tutakachofanya na kueleza sauti ya moyo Wake. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, na hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuwa na hamu ya sauti ya moyo wa huyu mwanadamu asiye wa ajabu. Yeye hufanya juhudi za mchwa kwa ajili yetu, anapoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na moyo Wake huvuja damu na kulia kwa ajili ya uasi na kufa ganzi kwetu. Utu kama huu na umiliki Wake haupo kwa upeo wa binadamu wa kawaida, na hauwezi kumilikiwa na yeyote aliyepotoka. Ana uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake haumilikiwi na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu ama kiini chetu, ama kuhukumu uasi wetu na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu wa mbinguni. Hakuna mtu ila Yeye anayeweza kumiliki mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho yametoka, kwa ukamilifu wao, kutoka Kwake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana utumwa wa shetani ama upotovu wa tabia yetu potovu Yeye huwakilisha Mungu, na kuonyesha sauti ya moyo wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu, yote ambayo huelekezwa kwa mwanadamu. Ameanza enzi mpya, nyakati mpya, na akaleta mbingu na nchi mpya, kazi mpya, na ametuletea matumaini, na akamaliza maisha ambayo si dhahiri, na akatuwezesha kikamilifu kuona njia ya wokovu. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zinapata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na kwa muda amekuwa akikataliwa na sisi—Je, si Yeye ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye Kweli! Yeye ni Mungu wetu. Yeye ndiye kweli, njia, na uzima! Yeye ameturuhusu kuishi tena, na kuona nuru, na kusimamisha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso wake, na tumeona barabara iliyo mbele.
kutoka kwa "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake" katika Neno Laonekana katika Mwili
Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele. Mimi Ndiye msambazaji wa binadamu na kiongozi wa pekee wa mwanadamu. Thamani na maana ya maneno Yangu haibainishwi na kama yanakubaliwa au kutambuliwa na mwanadamu, ila ni kwa kiini cha maneno yenyewe. Hata kama hakuna mtu hata mmoja duniani anaweza kupokea maneno Yangu, thamani ya maneno Yangu na usaidizi wake kwa mwanadamu hayapimiki na mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, Ninapokumbwa na wanadamu wengi wanaoasi, kukataa au kudharau kabisa maneno Yangu, msimamo Wangu ni huu tu: Wacha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai. Wacha vionyeshe kuwa yote Niliyosema ni ya ukweli, na kuwa ni yale ambayo mwanadamu lazima apewe, na, zaidi ya yote, yale ambayo mwanadamu anafaa akubali. Nitawaruhusu wote wanaonifuata wajue ukweli huu: Wote wasioyakubali maneno Yangu kikamilifu, wale wasioyaweka maneno Yangu katika vitendo, wale wasiopata sababu ndani ya maneno Yangu, na wale wasiopata wokovu kwa sababu ya maneno Yangu, ni wale ambao wamehukumiwa na maneno Yangu na, zaidi ya hayo, wamepoteza wokovu Wangu, na fimbo Yangu haitaondoka kamwe miongoni mwao.
kutoka kwa "Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Neno limepata mwili na Roho wa kweli amepatikana katika mwili—kwamba ukweli wote, uzima, na njia umekuja katika mwili, na Roho amewasili duniani na katika mwili kwa kweli. Ingawa, kijuujuu, hili linaonekana ni tofauti na utungaji mimba kwa Roho Mtakatifu, katika kazi hii mnaweza kuona kwa dhahiri zaidi kwamba Roho tayari amepatikana katika mwili, na, zaidi ya hayo, kwamba Neno limepata mwili, na Neno limeonekana katika mwili, na unaweza kufahamu maana ya kweli ya maneno haya: Hapo mwanzo kulikuwako na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Zaidi ya hayo, lazima ufahamu maneno ya leo ni Mungu, na lazima utazame maneno yakipata mwili. Huu ni ushuhuda bora zaidi unaoweza kuwa nao. Hili linathibitisha kwamba una ufahamu wa kweli wa Mungu kupata mwili—wewe huwezi tu kumjua na kumchambua Yeye, lakini pia unajua kwamba njia unayoifuata leo ni njia ya uzima, na njia ya ukweli. Yesu alifanya hatua ya kazi ambayo ilitimiza tu kiini cha "Neno alikuwako kwa Mungu": Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka Kwake, yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa aliyepata mwili wa kwanza wa Mungu. Hatua hii ya kazi ilitimiza maana ya ndani ya "Neno lapata mwili," ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya "naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu," na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno haya kwamba "Hapo mwanzo kulikuwako na Neno." Ambalo ni kusema, wakati wa uumbaji Mungu alikuwa na maneno, Maneno Yake yalikuwa na Yeye na yasiyotenganishwa kutoka Kwake, na enzi ya mwisho inafanya nguvu na mamlaka ya maneno Yake yawe hata wazi zaidi, na kumkubalia mwanadamu kuyaona maneno Yake yote—kuyasikia maneno Yake yote. Hiyo ndiyo kazi ya enzi ya mwisho. Lazima uyajue mambo haya yote kabisa. Si suala la kuujua mwili, bali la kuujua mwili na Neno. Hiki ndicho kile unachotakiwa kushuhudia, kile ambacho kila mtu lazima akijue. Kwa sababu hii ni kazi ya kupata mwili kwa pili—na mara ya mwisho ambapo Mungu anapata mwili—inakamilisha kwa ukamilifu umuhimu wa kupata mwili, inatekeleza kabisa na kutoa kazi yote ya Mungu katika mwili, na kumaliza enzi ya Mungu kuwa katika mwili.
kutoka kwa "Utendaji (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele
Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha si rahisi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung'aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Maisha ya Mungu, huishi milele bila kubadilika katika kusumbuka kwa mbingu na nchi. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.
Pengine, sasa, unataka kupokea maisha, au labda unataka kupata ukweli. Vyovyote vilivyo, unataka kumpata Mungu, kumpata Mungu unayeweza kutegemea, na ambaye anaweza kukupa uzima wa milele. Ukitaka kupata uzima wa milele, lazima kwanza uelewe chanzo cha uzima wa milele, na lazima kwanza ujue Mungu yuko wapi. Tayari nilishasema Mungu pekee ndiye maisha yasiyobadilika, na Mungu tu ndiye aliye na njia ya maisha. Kwa kuwa maisha Yake ni imara, hivyo ni ya milele; kwa kuwa Mungu tu ndiye njia ya maisha, basi Mungu Mwenyewe ni njia ya uzima wa milele. Kwa hivyo, lazima kwanza uelewe aliko Mungu, na jinsi ya kupata njia hii ya uzima wa milele. Hebu sasa tushiriki kwa masuala haya mawili tofauti.
Kama kweli unataka kupata njia ya uzima wa milele, na kama wewe unayo tamaa katika utafutaji wako kwa ajili yake, basi kwanza ulijibu swali hili: Mungu yuko wapi leo? Labda utajibu kwamba Mungu anaishi mbinguni, bila shaka—Hangeishi katika nyumba yako? Labda unaweza kusema, kawaida Mungu anaishi kati ya mambo yote. Au unaweza kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa kila mtu, au kwamba Mungu yuko katika ulimwengu wa kiroho. Mimi sipingi lolote kati ya haya, lakini lazima nifafanue suala hilo. Sio sahihi kabisa kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa mwanadamu, wala si makosa kabisa. Hiyo ni kwa sababu, miongoni mwa waumini katika Mungu, kuna wale ambao imani yao ni ya kweli na wale ambao imani yao ni uongo, kuna wale ambao Mungu anawakubali na wale ambao hawakubali, kuna wale ambao humfurahisha na wale ambao ni chukizo, na kuna wale ambao Yeye huwafanya kamili na wale ambao hupunguza. Na hivyo mimi Nasema kwamba Mungu Anaishi tu katika nyoyo za watu wachache, na watu hawa bila shaka ni wale ambao kweli wanaamini katika Mungu, wale ambao Mungu anawakubali, wale ambao humpendeza, na wale ambao Yeye huwafanya kamili. Wao ni wale wanaoongozwa na Mungu. Kwa kuwa wanaongozwa na Mungu, kwa hivyo ni watu ambao tayari wamesikia na kuona njia ya Mungu ya uzima wa milele. Wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya uongo, wale ambao hawajaidhinishwa na Mungu, wale ambao wanadharauliwa na Mungu, wale ambao wamechujwa na Mungu—wamefungwa katika kukataliwa na Mungu, wamefungwa kubaki bila njia ya maisha, na wamefungwa kubaki wajinga wa kujua aliko Mungu. Kwa upande mwingine, wale ambao Mungu anaishi katika nyoyo zao wanajua aliko Mungu. Wao ni watu wale ambao Mungu huwapa njia ya uzima wa milele, na ni wale wanaomfuata Mungu. Je, unajua, sasa, aliko Mungu? Mungu yupo katika moyo wa mtu na upande wa mtu. Hayupo tu katika ulimwengu wa kiroho, na juu ya mambo yote, lakini hata zaidi Yupo duniani ambapo mwanadamu huishi. Na hivyo kufika kwa siku za mwisho kumechukua hatua ya kazi ya Mungu katika sehemu mpya. Mungu ana ukuu juu ya mambo yote katika ulimwengu, na Yeye ni uti wa mgongo wa mwanadamu katika moyo wake, na zaidi ya hayo, Yeye yuko miongoni mwa wanadamu. Ni kwa njia hii pekee Anaweza kuleta njia ya maisha kwa binadamu, na kumleta mwanadamu katika njia ya maisha. Mungu amekuja duniani, na Anaishi kati ya wanadamu, ili wanadamu wanaweza kupata njia ya maisha, na hivyo binadamu anaweza kuwepo. Wakati huo huo, Mungu pia huamuru mambo yote katika ulimwengu, ili wapate kushirikiana na usimamizi Wake miongoni mwa wanadamu. Na hivyo, kama wewe unakiri tu kwamba Mungu yuko mbinguni na katika moyo wa mwanadamu, lakini usikiri ukweli wa kuwepo kwa Mungu miongoni mwa watu, basi kamwe hutapata uzima, na kamwe hutapata njia ya kweli.
Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!
Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, Kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, badala yake, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale Kristo bandia wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe. Kwa njia hii, kama kweli unataka kutafuta njia ya maisha, lazima kwanza ukiri kuwa ni kwa kuja duniani ndipo Anazirejesha njia za maisha kwa binadamu, na lazima kukiri ni katika siku za mwisho Yeye anakuja duniani kuhifadhia njia ya maisha kwa mwanadamu. Haya sio ya wakati wa nyuma; yanatendeka leo.
Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, wala njia inayoweza kukuongoza kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.
Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.
kutoka kwa "Neno Laonekana katika Mwili"
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatatu, 29 Oktoba 2018

Neno la Mungu | "Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana"

Neno la Mungu | "Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana"

Mwenyezi Mungu anasema, "Wale waliofanywa kuwa watimilifu hawawezi tu kuwa watiifu baada ya kushindwa, lakini wanaweza pia kuwa na maarifa na kubadilisha tabia yao. Wanamjua Mungu, wamepitia njia ya Mungu mwenye upendo, na wamejazwa na ukweli. Wanajua namna ya kupitia kazi ya Mungu, wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu, na wanayo mapenzi yao wenyewe. … Kufanywa kuwa watimilifu kunarejelea wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanaweza kufuatilia ukweli na kufaidika kutoka kwa Mungu. Kunaashiria wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanasimama imara katika majaribio na wanaishi kwa kudhihirisha ukweli."
Soma Zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumapili, 28 Oktoba 2018

Swahili Christian Video "Bwana Anakuja Kwa Namna Gani Hasa?" | The Son of Man Has Come to Earth

Swahili Christian Video "Bwana Anakuja Kwa Namna Gani Hasa?" | The Son of Man Has Come to Earth

Katika siku za mwisho, hali ya moyo ya Wakristo wanaongoja kurudi kwa Bwana Yesu inakuwa kali sana, lakini ni kwa vipi, hasa, Bwana atarudi? Baadhi wanasema, "Bwana Yesu atakuja na mawingu." Wengine wanasema, "Unabii unaotabiri kurudi Kwake nao unasema, 'Tazama, mimi nakuja kama mwizi' (Ufu 16:15). 'Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki' (Luka 17:25). 'Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha' (Mat 25:6). Kama anakuja na mawingu kwa kila mmoja kumwona, tunaelezaje fumbo la Yeye kuja kwa siri, kuteseka, na kukataliwa, pamoja na kusema kwamba wengine watashuhudia kuhusu kurudi Kwake?" Bwana atatokeaje kwetu? Mchezo wa kuchekesha Bwana Anakujaje Hasa unajaribu kusuluhisha mashaka yetu kuhusu jambo hili.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumamosi, 27 Oktoba 2018

Filamu za Kikristo | "Mazungumzo" | Christian Testimony of Overcoming Satan

Filamu za Kikristo | "Mazungumzo" | Christian Testimony of Overcoming Satan

Jiang Xinyi na Wakristo wengine walikamatwa na serikali ya CCP; wao huwatesa Wakristo kwa ukatili ili kutwaa fedha za kanisa na kuwakamata viongozi zaidi wa kanisa. Kisha, ili kuwalazimisha kuikataa imani yao, wao huzindua kampenii moja baada ya nyingine ya kuwatia kasumba, lakini kwa uongozi wa maneno ya Mungu, wao huweza kuyashinda mateso na udanganyifu wote wa Shetani. Wao hutegemea ukweli kushiriki katika vita vikali na serikali ya CCP …
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Ijumaa, 26 Oktoba 2018

Swahili Gospel Movie Segment "Mungu Anashikilia Ukuu Juu Ya Majaliwa ya Kila Nchi na Watu Wote"

Swahili Gospel Movie Segment "Mungu Anashikilia Ukuu Juu Ya Majaliwa ya Kila Nchi na Watu Wote"

Milki ya kale ya Kirumi na Milki ya zamani ya Uingereza zilikuwa na mafanikio na nguvu kwa haraka sana na kisha kufifia kuelekea kudhoofika na uharibifu. Sasa, Marekani limekuwa taifa kubwa lisilobishaniwa la ulimwengu na pia lina jukumu lisilofidika la kudumisha na kuimarisha hali ya ulimwengu. Ni mafumbo ya aina gani hasa yaliyofichika kuhusiana na kuinuka na kuanguka kwa mataifa? Ni nani aliye na mamlaka juu ya majaliwa ya kila nchi na watu wote? Sehemu hii ya ajabu kutoka kwa filamu ya Kikristo, "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu", itakufichulia majibu haya.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Alhamisi, 25 Oktoba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ujana Uliotumiwa Bila Majuto

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukatili Mateso

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ujana Uliotumiwa Bila Majuto

Xiaowen, Chongqing
"Upendo ni hisia safi, safi bila ya dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vikwazo au umbali. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Ukipenda hudanganyi, kunung'unika, kutelekeza, kutarajia kupata malipo" ("Upendo safi bila Dosari" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wimbo huu wa neno la Mungu siku moja ulinisaidia kupitia maumivu ya maisha ya muda mrefu yaliorefuka bure gerezani ambao ulidumu miaka 7 na miezi 4. Ingawa serikali ya CCP ilininyang'anya miaka mizuri zaidi ya ujana wangu, nimepata ukweli halisi na wa thamani zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwa hiyo sina malalamiko au majuto.
Mnamo mwaka wa 1996 nilipokea kukuzwa na Mungu na kukubali wokovu wa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kupitia kusoma maneno ya Mungu na kukusanyika katika ushirika, nilidhihirisha kwamba yote ambayo Mungu amesema ni ukweli, ambayo ni tofauti kabisa na maarifa na nadharia zote za dunia hii mbovu. Neno la Mwenyezi Mungu ni methali ya juu zaidi kwa maisha. Kilichofanya nisisimke zaidi kilikuwa kwamba ningeweza kuwa wa kawaida na wazi na kuzungumza kwa uhuru juu ya chochote na ndugu wa kiume na wa kike. Sikuwa na haja hata kidogo ya kujilinda dhidi ya lawama au kushindwa kwa akili na watu wakati wa kuingiliana nao. Nilihisi faraja na furaha ambayo sikuwahi kuhisi awali; kwa kweli niliipenda familia hii. Hata hivyo, si muda mrefu ulipita kabla sijasikia kwamba nchi hii haikuwaruhusu watu kumwamini Mwenyezi Mungu. Jambo hili lilinifanya kuchanganyikiwa kabisa, kwa sababu neno Lake liliwaruhusu watu kumwabudu Mungu na kuitembea njia sahihi ya maisha; liliwaruhusu watu kuwa waaminifu. Kama kila mtu angemwamini Mwenyezi Mungu, basi ulimwengu wote ungekuwa na amani. Kwa kweli sifahamu: Kumwamini Mungu kulikuwa ndiko shughuli ya haki zaidi; kwa nini serikali ya CCP ilitaka kutesa na kupinga kumwamini Mwenyezi Mungu kiasi kwamba ingewakamata waumini Wake? Niliwaza: Bila kujali ni vipi serikali ya CCP inatutesa au ni jinsi gani maoni ya umma ya kijamii ni makubwa, nimeamua kuwa hii ndiyo njia sahihi ya maisha na mimi kwa hakika nitaitembelea hadi mwisho!
Baada ya haya, nilianza kutekeleza wajibu wangu katika kanisa wa kusambaza vitabu vya neno la Mungu. Nilijua kwamba kutimiza wajibu huu katika nchi hii ambayo ilimpinga Mungu ilikuwa hatari sana na ningeweza kukamatwa wakati wowote. Lakini nilijua pia kuwa kama sehemu ya uumbaji wote, ulikuwa ni misheni yangu katika maisha wa kutumia kila kitu kwa ajili ya Mungu na kutimiza wajibu wangu; lilikuwa ni jukumu ambalo sikuweza kulikwepa. Nilipokuwa tu nikianza kushirikiana na Mungu kwa imani, siku moja mnamo Septemba mwaka wa 2003, nilikuwa njiani kuwapelekea ndugu fulani wa kiume na wa kike vitabu vya neno la Mungu na nilikamatwa na watu kutoka kwa Ofisi ya Usalama wa Taifa ya mjini.
Katika Ofisi ya Usalama wa Taifa, nilihojiwa tena na tena na sikujua jinsi ya kujibu; nilimlilia Mungu kwa haraka: "Ee Mwenyezi Mungu, nakuuliza Wewe unipe hekima Yako, na unipe maneno ambayo napaswa kuzungumza ili nisikusaliti Wewe na niweze kuwa shahidi kwa ajili Yako." Wakati huo, nilimlilia Mungu kila siku; Sikuthubutu kumwacha Mungu, nilimwomba tu Mungu anipe akili na hekima ili niweze shughulikia polisi hao waovu. Shukrani kwa Mungu kwa kunichunga na kunilinda; kila wakati nilipohojiwa, ama nilikuwa nikitema mate, au nilikuwa na kwikwi mfululizo na sikuweza kuzungumza. Katika kuona kazi ya ajabu ya Mungu, nikaamua kwa dhati: Kuwa waziwazi! Wanaweza kuchukua kichwa changu, wanaweza kuchukua maisha yangu, lakini kabisa hawatanifanya kumsaliti Mungu leo kamwe! Ninapoweka azimio langu kwamba ningependa kuhatarisha maisha yangu kuliko kumsaliti Mungu kama Yuda, Mungu alinipa "endelea" kwa kila namna: Kila wakati nilipohojiwa, Mungu angenilinda na kuniruhusu nipitie majaribu. Ingawa sikusema chochote, serikali ya CCP ilinishtaki kwa "kutumia dhehebu bovu kuangamiza utekelezaji wa sheria" na kunihukumu kifungo cha miaka 9 katika jela! Niliposikia hukumu ya mahakama, sikuwa na huzuni kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, wala sikuwaogopa; badala yake, niliwadharau. Wakati watu hao walikuwa wakitangaza hukumu, nilisema kwa sauti ya chini: "Huu ni ushahidi kwamba serikali ya CCP inampinga Mungu!" Baadaye, maafisa wa usalama wa umma walikuja tu kuchunguza jinsi mtazamo wangu ulivyokuwa, na nikawaambia kwa utulivu: "Miaka tisa ni nini? Wakati utakapofika kwangu kutoka, bado nitakuwa mshiriki wa Kanisa la Mwenyezi Mungu; ikiwa huniamini, subiri tu na kuona! Lakini unapaswa kukumbuka, kesi hii wakati mmoja ilikuwa katika mikono yenu!" Mtazamo wangu kwa kweli uliwashangaza; waliinua vidole gumba vyao juu na kusema tena na tena: "Umekuwa mahiri sana! Tunakustahi! Wewe ni mjeuri kuliko Dada Jiang! [a] Hebu tukutane wakati utakapotoka, na tutakupa chakula cha jioni!" Wakati huo, nilihisi kwamba Mungu alipata utukufu na moyo wangu ulipendezwa. Mwaka huo nilipohukumiwa, nilikuwa na umri wa miaka 31 tu.
Jela za China ni kuzimu duniani, na maisha ya muda mrefu ya gereza yalinifanya kuona kabisa unyama wa kweli wa Shetani na kiini chake cha kishetani ambacho kimekuwa adui kwa Mungu. Polisi wa China huwa hawafuati utawala wa sheria, lakini badala yake hufuata utawala wa uovu. Gerezani, polisi binafsi huwa hawawashughulikii watu, lakini huwachochea wafungwa kufanya vurugu ili kutiisha wafungwa wengine. Hawa polisi waovu pia hutumia mbinu za aina zote kuyafungia mawazo ya watu; kwa mfano, kila mtu anayeingia anapaswa kuvaa sare sawa za mfungwa zilizo na nambari maalum ya mfululizo, ni sharti anyolewe nywele zao kulingana na matakwa ya gereza, ni lazima avae viatu vilivyoidhinishwa na jela, anapaswa kutembelea vijia ambavyo gereza limemruhusu kutembelea, na anapaswa kutembea mwendo wa askari kwa kasi iliyoruhusiwa na gereza. Bila kujali kama ni majira ya kuchipua, majira ya joto, majira ya kupukutika kwa majani au majira ya baridi, ikiwa kuna mvua au kuna jua, au kama ni siku ya baridi kali, wafungwa wote wanapaswa kufanya kama walivyoamriwa bila ya uchaguzi wowote. Kila siku tulihitajika kukusanyika angalau mara 15 kupangwa na kuimba nyimbo za sifa kwa serikali ya CCP angalau mara tano; tulikuwa pia na kazi za kisiasa, yaani, walitufanya tujifunze sheria za gereza na katiba, na walitufanya kufanya mtihani kila baada ya miezi sita. Kusudi la hili lilikuwa ni kututia kasumba. Pia wangeyapima bila mpango maalum maarifa yetu ya masomo na sheria za jela. Polisi wa gereza walitutesa sio kiakili tu, wao pia walituharibu kimwili kwa unyama kamili: nilipaswa kufanya kazi ngumu kwa zaidi ya saa kumi kwa siku, kama tumesokomezwa pamoja na watu wengine mia kadhaa katika kiwanda chembamba tukifanya kazi za mikono. Kwa sababu kulikuwa watu wengi sana katika nafasi ndogo kiasi hicho, na kwa sababu kelele ya kutatanisha ya mashine ilikuwa kila mahali, bila kujali mtu alikuwa na afya kiasi gani, mwili wake ungepata uharibifu mkubwa kama angekaa hapo kwa muda. Nyuma yangu kulikuwa na mashine ya kutoboa matundu na kila siku ilitoboa mashimo mfululizo. Sauti ya kunguruma iliyopitisha ilikuwa isiyovumilika na baada ya miaka michache, nilipata ugonjwa hatari wa kutosikia. Hata leo hii sijapata nafuu. Kitu kilichokuwa kibaya zaidi kwa watu kilikuwa vumbi na uchafuzi wa mazingira katika kiwanda hicho. Baada ya kuchunguzwa, watu wengi walipatikana wakiwa wameambukizwa kifua kikuu na uvimbe wa koromeo. Aidha, kutokana na muda mrefu wa kukaa kitako hapo kufanya kazi ya mikono, ilikuwa haiwezekani kusogea hapa na pale na watu wengi waliambukizwa ugonjwa hatari wa bawasiri. Serikali ya CCP iliwachukulia wafungwa kama mashine za kutengeneza pesa; hawakuwa na mazingatio hata kidogo ya kama mtu aliishi au alikufa. Waliwafanya watu kufanya kazi tangu asubuhi na mapema mpaka usiku kabisa. Mara nyingi nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba sikuweza kuendelea kimwili. Haikuwa hii tu, nilipaswa pia nishughulike na aina zote za mitihani ya nasibu bali na kazi zangu za kila wiki za kisiasa, kazi za mikono, na kazi za umma, nk. Kwa hiyo, kila siku nilikuwa katika hali ya wasiwasi wa hali ya juu; hali yangu ya kiakili ilikuwa ikinyoshwa daima, na nilikuwa na wasiwasi zaidi kwamba singeweza kuwafikia wengine kama ningezembea hata kidogo, na kwa hiyo ningeadhibiwa na polisi wa gereza. Katika mazingira ya aina hiyo, kumaliza siku moja salama haikuwa kazi rahisi kufanya.
Nilipoanza tu kumaliza kifungo changu, sikuweza kustahimili aina hii ya kuharibiwa kikatili na polisi wa gereza. Aina zote za kazi ngumu ya mikono na shinikizo la kiitikadi lilifanya kupumua kuwe kugumu, sembuse kuwa ilibidi niwe na mawasiliano ya aina yote na wafungwa. Nilibidi pia kuvumilia dhuluma na matusi ya polisi wa kishetani wa gereza na wafungwa …. Niliteswa mara kwa mara na kuwekwa taabuni. Mara kadhaa, nilizama katika hali ya kukata tamaa, hasa nilipofikiria urefu wa hukumu yangu ya miaka tisa, nilihisi mshindo wa kutojiweza kwa kuhuzunisha na sikujua ni mara ngapi nililia—kiasi kwamba nilifikiria kujiua ili kujiweka huru kutoka kwa maumivu niliyokuwa nayo. Kila wakati nilipokuwa na huzuni kupita kiasi na sikuweza kujifadhili, ningeomba kwa haraka na kumlilia Mungu na Mungu angenipatia nuru na kuniongoza: “Bado huwezi kufa. Sharti ukaze ngumi yako na kuendelea kuishi kwa ari; lazima uishi maisha kwa ajili ya Mungu. Watu wanapokuwa na ukweli ndani yao basi wanakuwa na azimio hili na kamwe hawatamani kufa tena; kifo kinapokutisha, utasema, ‘Ee Mungu, siko radhi kufa; bado sikufahamu! Bado sijalipiza upendo Wako! … Lazima niwe na ushuhuda mzuri wa Mungu. Lazima nilipize upendo wa Mungu. Baada ya hapo, haijalishi jinsi nitakavyokufa. Kisha, nitakuwa nimeishi maisha ya kutosheleza. Bila kujali ni nani mwengine anayekufa, sitakufa sasa; lazima niendelee kuishi kwa ushupavu’” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalikuwa kama maono laini na latifu ya mama yangu akiutuliza moyo wangu mpweke. Yalikuwa pia kama baba yangu akitumia mikono miwili kuyafuta kwa uangalifu machozi kutoka kwa uso wangu kwa upendo. Moja kwa moja, mkondo wa vuguvugu na nguvu zilikurupuka kupitia moyo wangu. Ingawa nilikuwa nikiteseka kimwili katika jela la giza, kujaribu kujiua hakukuwa mapenzi ya Mungu. Singeweza kumshuhudia Mungu na pia ningekuwa kichekesho cha Shetani. Ingekuwa ushuhuda kama ningetoka hai kutoka gereza hili lenye pepo baada ya miaka tisa. Maneno ya Mungu yalinipa ujasiri wa kuendelea na maisha yangu na nikafanya azimio moyoni mwangu: Haijalishi matatizo gani yaliyo mbele yangu, kwa uangalifu nitaendelea kuishi; nitaishi kwa ujasiri na nguvu na hakika nitashuhudia kuridhika kwa Mungu.
Mwaka nenda mwaka rudi, kazi ya kuzidi kiasi ilisababisha mwili wangu kudhoofika hatua kwa hatua. Baada ya kukaa kitako kwa muda mrefu katika kiwanda ningeanza kutoa jasho maridhawa na bawasiri zangu zingevuja damu zilipokuwa kali vya kutosha. Kutokana na upungufu wangu mkali wa damu, mara kwa mara ningehisi kizunguzungu. Lakini gerezani, kumwona daktari si jambo rahisi kufanya; kama polisi wa gereza walikuwa wamefurahi, wangenipa dawa za bei nafuu. Kama hawakuwa na furaha, wangesema nilikuwa nikijifanya mgonjwa ili kuepuka kazi. Ningevumilia mateso ya ugonjwa huu na kuyazuilia machozi yangu. Baada ya kazi ya siku kutwa ningekuwa nimechoka kabisa. Niliukokota mwili wangu mchovu hadi kwa chumba changu kidogo cha gereza na nilitaka kupata mapumziko, lakini sikuwa hata na chembe ya ya nguvu ya kupata usingizi madhubuti: Ama polisi wa gereza walikuwa wakiniita katikati ya usiku kufanya kitu fulani, au niliamshwa na kelele ya kunguruma iliyopigwa na polisi wa gereza. … Mara kwa mara nilichezewachezewa nao na kuteseka vibaya sana. Aidha, nililazimika kustahimili kutendewa kinyama na polisi hawa wa gereza. Nilikuwa kama mkimbizi nikilala sakafuni au ushorobani, au hata kando ya choo. Nguo nilizoziosha hazikuwa kavu, lakini zilikuwa zimefungwa pamoja na nguo za wafungwa wengine ili kukaushwa. Kuosha nguo katika majira ya baridi kulikuwa kwa kukatisha tamaa hasa, na watu wengi waliambukizwa ugonjwa wa baridi yabisi kwa sababu ya kuvaa mavazi manyevu kwa vipindi virefu vya wakati. Gerezani, haikuchukua muda mrefu kwa watu wenye afya kuwa goigoi na bozi, wadhaifu kimwili au kujawa magonjwa. Mara kwa mara tulikula majani ya mboga ya zamani, yaliyokaushwa na ambayo yalikuwa yamepitwa na msimu. Kama ulitaka kula kitu bora zaidi, basi ulilazimika kununua chakula ghali huko gerezani. Ingawa watu walifanywa kujifunza sheria gerezani, hakukuwa na sheria huko; polisi wa gereza ndio waliokuwa sheria na kama mtu yeyote angewaudhi, walipata sababu ya kukuadhibu—hata kwa kiasi kwamba waliweza kukuadhibu bila sababu yoyote. Hata la kudharauliwa zaidi ni kwamba walichukulia waumini wa Mwenyezi Mungu kuwa wahalifu wa kisiasa, wakisema kuwa uhalifu wetu ulikuwa mbaya zaidi kuliko mauaji na kuchoma mali. Kwa hiyo, walinichukia hasa na walinidhibiti kikamilifu, na kunitesa kikatili sana. Aina hii ya tabia mbovu ni ushahidi usiobadilika wa tabia potovu ya madikteta, upinzani kwa Mbinguni, na kuwa na uadui na Mungu! Baada ya kuvumilia mateso ya kikatili ya gereza, moyo wangu mara kwa mara ulijazwa na hasira ya haki: Ni sheria gani kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu hukiuka? Ni uhalifu gani kumfuata Mungu na kuitembea njia sahihi ya maisha? Wanadamu waliumbwa na mikono ya Mungu na kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu ni sheria ya mbingu na dunia; ni sababu gani serikali ya CCP iliyo nayo ya kuzuia kwa nguvu na kusumbua hili? Kwa dhahiri ni tabia yake potovu na upinzani kwa Mbingu; huwa inajiweka yenyewe dhidi ya Mungu katika kila kipengele, huwa inashikiza kitambulisho cha kupinga maendeleo kwa waumini wa Mwenyezi Mungu na hututesa kwa ukali na kutuharibu. Huwa inajaribu kuwaondosha waumini wote wa Mwenyezi Mungu kwa dharuba moja kali. Si huku ni kubadilisha weusi na weupe na kuwa mpinga maendeleo kikamilifu? Kwa hasira huipinga Mbingu na ina uhasama na Mungu; hatimaye ni lazima ipitie adhabu ya haki ya Mungu! Kila mahali kuna upotovu, lazima kuwe na hukumu; kila mahali kuna dhambi, lazima kuwe na adhabu. Hii ni sheria ya Mungu ya mbinguni iliyoamuliwa kabla, hakuna mtu anayeweza kuitoroka. Uhalifu muovu wa serikali CCP umepanda kwa anga, na itapitia maangamizo ya Mungu. Kama tu Mungu alivyosema: “Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga mwovu huyu, joka wa zamani mwenye chuki, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote; Mungu hatamhurumia hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote, Atamharibu kabisa” (“Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Katika gereza hili la pepo, nilikuwa duni kuliko mbwa wa kutangatanga machoni mwa polisi hawa maovu; hawakunipiga na kunikemea tu, lakini polisi hawa waovu mara kwa mara na kwa ghafla wangeingia kwa vishindo na kutawanya matandiko yangu na vitu vyangu vya kibinafsi kuwa takataka. Pia, wakati wowote ambapo ghasia fulani zilifanyika katika ulimwengu wa nje, watu walio gerezani ambao ni wasimamizi wa masuala ya kisiasa wangenitafuta na kudadisi maoni yangu kuhusu matukio haya na kwa kawaida wangenishambulia kuhusu ni kwa nini niliitembea njia ya kumwamini Mungu. Kila wakati nilipokabiliwa na aina hii ya kuhojiwa, ningekuwa na wasiwasi, kwa sababu sikujua mpango upi muovu waliokuwa nao kwangu. Moyo wangu daima ulikuwa ukimwomba Mungu kwa haraka na kulilia msaada na mwongozo kupitia wakati wa kilele cha hatari hii. Siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, dhuluma, unyonywaji, na ukandamizwaji viliniumiza kwa mateso yasiyosemeka: Kila siku nilipewa kazi ya mikono iliyozidi na majukumu ya kisiasa ya kuchusha, ya kuchosha, nilisumbuliwa pia na ugonjwa wangu na juu ya yote, nilidhoofika akili. Lilinifikisha kwenye ukingo wa kusambaratika. Hasa wakati nilipoona mfungwa wa makamo wa kike amejinyonga kutoka kwa dirisha usiku wa manane kwa sababu hakuweza kuvumilia mateso ya kinyama ya polisi hawa waovu, na mfungwa mwingine mzee wa kike aliyekufa kutokana matibabu ya ugonjwa wake yaliyocheleweshwa, nilizama katika shida zile zile zilizosonga na tena nikaanza kutafakari kujiua. Nilihisi kuwa kifo kilikuwa ndiyo aina bora ya faraja. Lakini nilijua kwamba huko kungekuwa kumsaliti Mungu na singeweza kufanya hivyo. Sikuwa na chaguo jingine lolote ila kuvumilia maumivu yote na kuitii mipango ya Mungu. Lakini mara tu nilipofikiri juu ya hukumu yangu ndefu, na kufikiri juu ya nilivyokuwa mbali na kupata uhuru, nilihisi kuwa hakuna maneno yaliyoweza kuelezea maumivu yangu na kukata tamaa kwangu; nilihisi kuwa sikuweza kuendelea kuhimili hili na kwamba sikujua ni muda gani ningeweza kusimama imara. Ni mara ngapi sikuweza kufanya chochote ila kujifunika kwa mfarishi wangu usiku wa manane na kulia, nikimuomba na kumsihi Mwenyezi Mungu na kumwambia Yeye kuhusu maumivu yote yaliyokuwa kwa mawazo yangu. Katika wakati wa maumivu yangu mengi na kutojiweza, niliwaza: Mimi ninateseka leo ili nipate kujitenga na upotovu na kupokea wokovu wa Mungu. Shida hizi ndizo ninazopaswa kupitia, na ambazo ni lazima nipitie. Mara tu nilipofikiria hili, sikuhisi uchungu tena; Badala yake, nilihisi kuwa kulazimishwa kuingia gerezani kwa sababu ya imani yangu kwa Mungu, na kupitia shida ili kupata wokovu lilikuwa jambo la thamani na umuhimu mkubwa mno; mateso haya yalikuwa ya thamani sana! Bila kujua, dhiki ya moyo wangu ilibadilika kuwa furaha na sikuweza kuzuia hisia zangu; nilianza kuimba bila kufungua mdomo wimbo wa uzoefu niliokuwa na uzoefu nao moyoni mwangu uitwao "Maisha Yetu si ya Bure": "Maisha yetu si ya bure", mateso yetu yana maana. Maisha yetu si ya bure, hatutakubali kughairi bila kujali ni jinsi gani maisha yalivyo magumu. Maisha yetu si ya bure, sisi hupata fursa nzuri ya kumjua Mungu. Maisha yetu si ya bure, sisi tunaweza kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu mkuu. Ni nani aliyebarikiwa kutuliko? Ni nani mwenye bahati kutuliko? Ee, kile ambacho Mungu hutupa kinazidi vyote vya vizazi vilivyopita; tunapaswa kuishi kwa ajili ya Mungu na tunapaswa kumlipa Mungu kwa sababu ya upendo Wake mkubwa." Niliurudia wimbo huo ndani ya moyo wangu na nilivyozidi kuimba ndani ya moyo wangu, ndivyo nilivyozidi kutiwa moyo; nilivyozidi kuimba, ndivyo nilivyozidi kuhisi kuwa nilikuwa na nguvu na furaha. Sikuweza kujizuia kuapa mbele ya Mungu: "Ee, Mwenyezi Mungu, ninakushukuru Wewe kwa faraja Yako na kunitumainisha ambavyo vimenisababisha kuwa tena na imani na ujasiri wa kuendelea kuishi. Umeniruhusu kujisikia kwamba Wewe kweli ni Bwana wa maisha yangu na Wewe ni nguvu ya maisha yangu. Ingawa nimefungwa mahali hapa pa kusikitisha sana, siko peke yangu, kwa sababu Umekuwa pamoja nami daima kupitia siku hizi za giza; Umenipa imani tena na tena na umenipa motisha kuendelea. Ee Mungu, kama ninaweza kutoka nje ya hapa siku moja na kuishi kwa uhuru, basi nitatimiza wajibu wangu na sitauumiza moyo Wako tena wala kujifanyia mipango mwenyewe. Ee Mungu, bila kujali jinsi siku zijazo zilivyo ngumu au zilivyo za shida, niko radhi kukutegemea Wewe kwendelea kuishi na nguvu!"
Gerezani, mara kwa mara nilikumbuka siku za nyuma tukiwa na ndugu zangu wa kiume na wa kike; huo ulikuwa wakati mzuri sana! Kila mtu alishangilia na kucheka, na pia tulikuwa na migogoro, lakini yote haya yalikuwa kumbukumbu nzuri. Lakini kila wakati nilipotafakari juu ya nyakati ambapo kwa uzembe nilifanya kazi zangu za zamani, nilihisi kuwa na hatia sana na mwenye kuwiwa. Nilifikiri juu ya migogoro niliyokuwa nayo na ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa sababu ya tabia yangu ya kiburi; nilihisi kuwa na wasiwasi hasa na mwenye kujuta. Kila wakati hili lilipotokea, ningeangua kilio na kimya kimya ningeimba wimbo mashuhuri katika moyo wangu: “Ninajuta sana, Ninajuta sana, nimepoteza muda mwingi sana wa thamani. Muda husonga mbele milele na ni majuto tu ambayo hubaki. … Kwa ajili ya kuwiwa kwangu kwa zamani na nitaanza upya na imani na kujivunia. Mungu anipa fursa nyingine, na kwa uvumilivu Wake nitafanya uchaguzi wangu mpya. Nitafurahia siku hii hasa, kutenda ukweli, kutekeleza wajibu wangu vizuri inavyowezekana, na hivyo kumridhisha Mungu. Moyo wa Mungu una wasiwasi, umejaa matarajio. Kwa hiyo sitavunja moyo Wake tena" ("Ninajuta sana" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Katika maumivu yangu na kujilaumu, mara kwa mara nilimwomba Mungu moyoni mwangu: Ee Mungu! Kwa hakika nimepungukiwa na Wewe mno; kama Utaliruhusu, niko radhi kutafuta kukupenda Wewe. Baada ya kuondoka gerezani, bado nitakuwa tayari kutimiza wajibu wangu na nitakuwa radhi kuanza tena! Nitaufidia upungufu wangu wa zamani! Wakati wa muda wangu gerezani, nilikuwa nimewakosa hasa wale ndugu wa kiume na wa kike niliokuwa nikiwasiliana nao asubuhi na usiku; kwa kweli nilitaka kuwaona, lakini katika gereza hili la pepo ambalo nilikuwa nimefungiwa, tamaa hii ilikuwa ombi lisilowezekana. Hata hivyo, mara kwa mara ningewaona ndugu hawa wa kiume na wa kike katika ndoto zangu; niliota kwamba tulikuwa tunasoma neno la Mungu pamoja na kuwasiliana ukweli pamoja. Tulikuwa na furaha na wachangamfu.
Wakati wa tetemeko kubwa la ardhi la Wenchuan la mwaka wa 2008, gereza tulimokuwa tulifungiwa ndani lilitetemeshwa na mimi nilikuwa mtu wa mwisho kuhama eneo hilo wakati huo. Katika siku hizo kulikuwa na mitikisiko midogo baada ya tetemeko ambayo haikusita. Wafungwa wote na polisi wa gereza waliogopa sana na kuwa na wasiwasi kiasi kwamba hawakuweza kuendelea. Lakini moyo wangu ulikuwa hasa mtulivu na imara, kwa sababu nilijua kwamba hili lilikuwa ni neno la Mungu likitimia; kulikuwa ni kuwasili kwa ghadhabu kali ya Mungu. Wakati wa tetemeko hilo moja katika miaka mia, neno la Mungu liliulinda moyo wangu daima; ninaamini kwamba maisha na kifo cha mwanadamu vyote vi mikononi mwa Mungu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya hivyo, niko radhi kuitii mipango ya Mungu. Hata hivyo, kitu cha pekee kilichonifanya kuhuzunika ni kama ningekufa, basi singepata tena fursa ya kutimiza wajibu wangu kwa Bwana wa viumbe, singekuwa na fursa tena ya kuufidia upendo wa Mungu, na singeweza kuwaona ndugu zangu wa kiume na wa kike. Lakini, wasiwasi wangu ulikuwa uliozidi; Mungu alikuwa nami daima na alinipa ulinzi mkubwa sana, ambao uliniruhusu kuendelea kuishi baada ya tetemeko la ardhi na kuishi kwa amani wakati wa tetemeko!
Mnamo Januari ya mwaka wa 2011, niliachiliwa mapema, ambako hatimaye kulimaliza maisha yangu ya utumwa gerezani. Katika kupata uhuru wangu, moyo wangu ulikuwa na msisimko mkubwa: Ninaweza kurudi kanisani! Ninaweza kuwa pamoja na ndugu zangu wa kiume na wa kike! Maneno hayakuweza kuelezea hali yangu ya kihisia ya akili. Kile ambacho sikutarajia ni kwamba baada ya kurudi nyumbani, binti yangu hakunijua, na jamaa na marafiki zangu walinitazama kwa mtazamo wa pekee; wote walijitenga nami na hawangeingiliana nami. Watu waliokuwa karibu nami hawakunielewa au kunikaribisha. Wakati huu, ingawa sikuwa gerezani nikidhulumiwa na kuteswa, mitazamo ya dharau, dhihaka, na kuachwa vilifanya kuwe vigumu kustahimili. Nilikuwa dhaifu na hasi. Sikuweza kujizuia kutafakari juu ya siku za nyuma: wakati tukio lilipotendeka, nilikuwa na umri wa miaka thelathini na mmoja tu; wakati nilipotoka gerezani, majira nane ya baridi na majira saba ya joto yalikuwa yamepita. Ni mara ngapi ambapo Mungu alikuwa amepanga watu, mambo na vitu wakati wa upweke wangu na kutojiweza ili kunisaidia; ni mara ngapi maneno ya Mungu yalinifariji katika maumivu yangu na kukata tamaa kwangu; ni mara ngapi nilipotaka kufa Mungu alinipa uwezo wa kuwa na ujasiri wa kuendelea kuishi …. Katika kipindi hicho cha miaka mirefu ya mchungu, ni Mungu aliyeniongoza hatua kwa hatua nje ya bonde la kivuli cha mauti hadi kuendelea kuishi kwa ushupavu. Katika kukabili shida hii sasa, nilikuwa hasi na dhaifu na nilikuwa nimemsikitisha Mungu. Kwa kweli nilikuwa mwoga na mtu asiyeweza ambaye alikuwa alikuwa na asante ya punda! Katika kufikiria hili, moyo wangu ulishutumiwa vikali; sikuweza kujizuia kufikiri juu ya kiapo nilichofanya na Mungu wakati nilipokuwa gerezani: "Kama ninaweza kutoka nje ya hapa siku moja na kuishi kwa uhuru, basi bado nitatimiza wajibu wangu. Siko tayari kuumiza tena moyo wa Mungu na sitajifanyia mipango mwenyewe tena!" Niliwazia kiapo hiki na kutafakari juu ya hali niliyokuwa nayo wakati nilipofanya kiapo kwa Mungu. Machozi yaliyatia ukungu kuona kwangu na polepole nikaimba wimbo mmoja wa neno la Mungu:
Kwa hiari yangu mwenyewe mimi humfuata Mungu. Sijali kama Yeye ananitaka au la. Natafuta kumpenda Yeye, kwa udhabiti kumfuata Yeye. Nitampata Yeye, na kutoa maisha yangu Kwake.
I. Mapenzi ya Mungu yatimizwe. Moyo wangu utolewe kwa Mungu kikamilifu. Bila kujali Mungu anafanya nini au Anachonipangia, nitaendelea kufuata, nikitafuta kumpata Yeye. Kwa hiari yangu mwenyewe ninamfuata Mungu. Sijali kama Yeye ananitaka au la. Natafuta kumpenda Yeye, kwa udhabiti kumfuata Yeye. Mimi nitampata, na kutoa maisha yangu kwake.
II. Ukitamani kusimama na kutimiza mapenzi ya Mungu, ukitaka kumfuata Yeye mpaka mwisho, kuweka msingi imara, tenda ukweli katika vitu vyote. Hili humpendeza Mungu na Yeye ataimarisha upendo wako. Kwa hiari yangu mwenyewe mimi humfuata Mungu. Sijali kama Yeye ananitaka au la. Natafuta kumpenda Yeye, kwa udhabiti kumfuata Yeye. Nitampata Yeye, na kutoa maisha yangu Kwake.
III. Unapokabiliwa na majaribu, unahuzunika na kuteseka. Lakini, kwa ajili ya kumpenda Mungu, ungevumilia kila shida, kuacha maisha yako na kila kitu. Kwa hiari yangu mwenyewe mimi humfuata Mungu. Sijali kama Yeye ananitaka au la. Natafuta kumpenda Yeye, kwa udhabiti kumfuata Yeye. Nitampata Yeye, na kutoa maisha yangu Kwake. ("Sitapumzika Mpaka Nimpate Mungu" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya)
Baada ya muda wa ibada za kiroho na urekebishaji, kwa haraka nilitoka nje ya uhasi wangu chini ya kunurishwa kwa Mungu na nikajirudisha kwenye safu za kutimiza wajibu wangu.
Hata kama miaka bora zaidi ya ujana wangu ilitumika gerezani; katika miaka hii saba na miezi minne nilipopitia shida kwa sababu ya imani yangu katika Mungu, sina malalamiko na sina majuto, kwa sababu ninaelewa ukweli fulani na nimepitia upendo wa Mungu. Nahisi kuwa kuna maana na thamani kwa mateso yangu; hili ni jambo la pekee la utukufu na neema ambazo Mungu alinitengenezea, hili ni pendeleo langu! Hata kama jamaa na marafiki zangu hawanielewi, na hata kama binti yangu hanijui, hakuna mtu, jambo au kitu kitakachoweza kunitenga na uhusiano wangu na Mungu; hata kama nikifa, siwezi kumwacha Mungu.
Upendo Safi Bila Dosari ndio wimbo niliopenda sana kuuimba gerezani; sasa, nataka kutumia matendo yangu halisi kutoa upendo safi zaidi kwa Mungu!
kutoka kwa Ushuhuda wa Washindi
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.