Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Ijumaa, 9 Novemba 2018

2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Ulimwengu" (Swahili Subtitles)

2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Ulimwengu" (Swahili Subtitles)

Ulimwengu ni mkubwa sana na usio na kikomo, na una nyota nyingi mno zisizohesabika katika mzunguko sahihi…. Unatamani kujua aliyeziumba sayari za juu za ulimwengu, na yule ambaye huamuru tao la mtupo angani? Dondoo ya kustaajabisha ya filamu ya Kikristo ya Mungu Kuutawala Ulimwengu itakuonyesha nguvu yenye uwezo ya Muumba.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Alhamisi, 8 Novemba 2018

Muziki wa Injili "Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu" | God Is Salvation to Man

Muziki wa Injili "Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu" | God Is Salvation to Man

Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena. Wanajua ubaya wa Shetani, hivyo wanamkataa. Wanakuja mbele ya Mungu, wanakubali adabu na hukumu. Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu. Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani. Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena. Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu.
Katika usimamizi wa Mungu wa wakati huu, mwanadamu ni lengo la upotovu wa Shetani, yeye ni kasidi cha wokovu wa Mungu na kile ambacho Mungu na Shetani wanapigania. Wakati wa kazi ya Mungu, Anampata tena mwanadamu hatua kwa hatua kutoka Shetani. Kisha mwanadamu anakuwa karibu zaidi na Mungu … Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu. Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani. Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena. Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu. Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu. Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani. Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena. Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video

Jumatano, 7 Novemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo; lazima mle na mnywe maneno Yangu zaidi na, muhimu zaidi, lazima mweze kuyala na kuyanywa nyinyi wenyewe. Jiandaeni wenyewe na ukweli wote, njooni mbele Yangu ili nifungue macho yenu ya kiroho na kuwaruhusu kuona siri zote zilizo rohoni.... Wakati kanisa linaingia awamu yake ya ujenzi, vita vya watakatifu dhidi ya Shetani[a] vinaanza. Vipengele mbalimbali vya Shetani vya kutisha Vinawekwa mbele yenu; je, mnaacha na kurudi nyuma au mnainuka na kuendelea mkinitegemea Mimi? Weka hadharani vipengele vya Shetani vyenye upotovu na viovu, bila hisia wala huruma! Pambana na Shetani hadi kifo! Mimi ni msaada wenu na ni lazima muwe na roho ya mwana wa kiume! Shetani yuko katika hekaheka zake za kifo cha mwisho lakini bado hataweza kuhepa hukumu Yangu. Shetani yuko chini ya miguu Yangu na pia anakanyagwa chini ya miguu yenu—ni ukweli!
Wale wapinga dini wote na wale ambao hubomoa ujenzi wa kanisa hawafai kuvumiliwa hata kidogo na nitawahukumu mara moja. Weka Shetani hadharani, mkanyagie chini ya miguu, muangamize kabisa na usimuachie pa kujificha. Kila aina ya mapepo na vizuka hakika wataonyesha maumbile yao ya kweli mbele Yangu na Nitawatupa wote kuzimu ambamo hawatawahi kuwa huru; wote wako chini ya miguu yetu. Kama unataka kupigana vita vizuri kwa ajili ya ukweli, basi kwanza kabisa, usimpe Shetani nafasi ya kufanya kazi, na ili kufanya hivi mtastahili kuwa na nia moja na muweze kutumika katika kushirikiana, acheni dhana zenu za kibinafsi, maoni, mitazamo na njia za kufanya mambo, tuliza moyo wako ndani Yangu, zingatia sauti ya Roho Mtakatifu, kuwa makini na kazi ya Roho Mtakatifu na uwe na uzoefu wa maneno ya Mungu kwa kina. Lazima uwe na nia moja tu, ambayo ni kwamba mapenzi Yangu yaweze kutendeka. Hupaswi kuwa na nia nyingine. Lazima uangalie Kwangu kwa moyo wako wote, angalia hatua Zangu na Ninavyotenda mambo kwa karibu, na wala usiwe mzembe kabisa. Roho yako lazima iwe amilifu, macho yako yakiwa wazi. Kwa kawaida, wale ambao nia na malengo yao si sahihi, wale ambao wanapenda kuonekana na wengine, wenye hamu ya kutenda mambo, wenye tabia ya kukatiza, walio imara katika mafundisho ya dini, watumishi wa Shetani, nk., watu hawa wanapoinuka wanakuwa ugumu kwa kanisa na kula na kunywa kwa ndugu kunakuwa si kitu; unapompata mtu wa aina hii jifanye kisha mpige marufuku mara moja. Kama muda baada ya muda hawabadiliki basi watateseka sana. Kama wale wanaoendelea katika njia zao kwa ukaidi wanajitetea na kujaribu kufunika dhambi zao, kanisa linapaswa kuwaondoa mara moja na kutowaachia nafasi ya kuendelea. Usipoteze mengi kwa kujaribu kuokoa machache, na uzingatie makubwa.
Macho yako ya kiroho lazima sasa yafunguke, na kutofautisha aina kadhaa za watu kanisani:
Je, ni mtu wa ina gani anaelewa masuala ya kiroho na anajua roho?
Je, ni mtu wa ina gani haelewi masuala ya kiroho?
Je, ni mtu wa ina gani ana roho waovu ndani yake?
Je, ni mtu wa ina gani ana Shetani anafanya kazi juu yake?
Je, ni mtu wa ina gani ambaye ana tabia ya kukatiza?
Je, ni mtu wa ina gani ambaye Roho Mtakatifu anatenda kazi kwake?
Je, ni mtu wa ina gani huonyesha kuzingatia kuelekea mzigo wa Mungu?
Je, ni mtu wa ina gani anaweza kutenda mapenzi Yangu?
Je, ni nani shahidi Wangu mwaminifu?
Jua ya kwamba nuru ambayo Roho mtakatifu hupatia makanisa yote ni maono ya leo ya juu zaidi. Msichanganyikiwe kuhusu mambo haya, lakini badala yake lazima mchukuwe muda wa kuyafikiria kabisa—hii ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya maisha yenu! Kama huelewi mambo haya yaliyo machoni pako basi hutakuwa na uwezo wa kusonga mbele, utakuwa katika hatari ya majaribu na ufungwa wakati wowote, na huenda ukavamiwa. Jambo kuu sasa ni kuzingatia kuweza kuwa karibu na Mimi moyoni mwako, kufanya ushirika zaidi na Mimi, na chochote unachokosa au kutafuta utafidiwa kupitia kuwa karibu na Mimi na kufanya ushirika na Mimi. Maisha yako hakika yatashughulikiwa na utakuwa na nuru mpya. Mimi kamwe siangalii jinsi mlikuwa wajinga awali na siyakumbuki makosa yenu. Mimi huangalia jinsi mnavyonipenda: Je, mnaweza kunipenda zaidi ya mambo mengine yote? Naangalia kuona iwapo mnaweza kugeuka nyuma na kunitegemea kuondoa ujinga wenu au la. Baadhi ya watu husimama Kwangu, kunipinga hadharani, na kuhukumu watu wengine; hawajui maneno Yangu, na hata uwezekano wao wa kuona uso Wangu uko chini. Wote wale walio mbele Yangu ambao hunifuata kwa dhati, ambao wana mioyo yenye njaa na kiu cha haki, Nitawapa nuru, kuwafichulia, kuwaruhusu kuniona kwa macho yenu na kugusa mapenzi Yangu wenyewe; hakika moyo Wangu utafichuliwa kwenu, ili mpate kuelewa. Lazima muweze kutenda yale ambayo naangaza ndani yenu kulingana na maneno Yangu, vinginevyo mtahukumiwa. Fuata mapenzi Yangu na hamtapotea
Kwa wote wale wanaotafuta kuingia ndani ya maneno Yangu, neema na baraka vitaongezeka mara mbili juu yenu, mtapata nuru mpya kila siku, ufahamu mpya kila siku na kujisikia mpya katika kula na kunywa maneno Yangu kila siku; utayaonja kwa kinywa chako mwenyewe: Ni tamu jinsi gani! … Lazima uwe makini, na usitosheke unapokuwa na ufahamu kiasi na ladha kiasi ya utamu—cha msingi ni kuendelea kutafuta mbele! Baadhi ya watu hufikiria ya kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kweli ajabu na halisi—huyu kweli ni mtu wa Mwenyezi Mungu anafichuliwa wazi, na ishara na maajabu kubwa zaidi viko mbele. Kuwa makini na macho wakati wote, angalia kabisa kwenye chanzo, kuwa mtulivu mbele Yangu, zingatia na usikilize kwa makini, na kuwa na uhakika kuhusu maneno Yangu. Haiwezekani kuwa na utata; kama una shaka hata kidogo basi Nina hofu kuwa utapotea zaidi ya malango. Kuwa na maono wazi, simama kwenye sakafu ngumu, fuata mkondo huu wa maisha na uufuate popote ufikapo; usisite hata kidogo kabisa. Kula, kunywa na kutoa sifa tu, tafuta kwa moyo mtakatifu na usikate tamaa. Leta chochote usichokielewa mbele Yangu zaidi na hakikisha usiwe na moyo wa mashaka ili uepuke kupata hasara kubwa. Endelea! Endelea! Kaa karibu! Jikwamue kutoka kwa vizuizi na usijichafue. Endelea kwa moyo wote na usirudi nyuma. Lazima utoe moyo wako wakati wote na kamwe usiwahi kuupoteze muda wowote. Roho Mtakatifu daima ana kazi mpya ya kutenda, hutenda mambo mapya na ana nuru mpya kila siku; “kugeuka sura mlimani”—mwili mtakatifu wa kiroho wa Mungu umeonekana! Jua lenye haki hutoa nuru na huangaza, mataifa yote na watu wote wameona uso Wako mtakatifu. Nuru Yangu itaangaza juu ya wale wote wanaokuja mbele Yangu. Maneno yangu ni nuru, yakiwaongoza mbele. Hamtageuka kushoto au kulia mnapotembea lakini mtatembea ndani ya nuru Yangu, na kukimbia kwenu hakutakuwa kazi isiyo na matunda. Lazima muone kazi ya Roho Mtakatifu kwa uwazi na mapenzi Yangu yako pale ndani yake. Siri zote zimefichwa na zitafunuliwa kwenu hatua kwa hatua. Wekeni maneno Yangu akilini wakati wote na mje mbele Yangu kufanya ushirika zaidi na Mimi. Kazi ya Roho Mtakatifu huendelea. Tembeeni katika nyayo Zangu; maajabu makuu yako mbele na yatafunuliwa kwenu moja baada ya lingine. Ni wale tu ambao wanajali, wanaosubiri na ambao wako macho watayaona. Hakikisha usiwe mlegevu. Mpango wa usimamizi wa Mungu unakaribia hatua yake ya mwisho, ujenzi wa kanisa utafanikiwa, idadi ya washindi tayari imewekwa, mwana wa kiume mshindi atafanyika na wataingia katika ufalme na Mimi, kuchukua ufalme Nami, kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kuwa katika utukufu pamoja!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 6 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utangulizi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utangulizi

Mnamo Februari 11, mwaka wa 1991, Mungu alitoa tamko Lake la kwanza katika kanisa ambalo lilikuwa na athari isiyo ya kawaida kwa kila mmoja wa watu walioishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu wakati huo. Tamko hili lilitaja yafuatayo: “Makazi ya Mungu yameonekana” na “Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—Yeye ni Jua linalong’aa.” Kwa maneno haya ya maana sana, watu hawa wote waliletwa katika ulimwengu mpya. Wale wote waliosoma tamko hili walihisi maelezo ya kazi mpya, kazi kuu ambayo Mungu alikuwa karibu kuanzisha. Lilikuwa ni tamko hili zuri, laini, na lenye habari nyingi katika maelezo machache lililoleta binadamu wote katika kazi mpya ya Mungu na katika enzi mpya, na ambalo liliweka msingi na kuanzisha kazi ya Mungu katika kupata mwili huku. Mtu anaweza kusema kwamba tamko ambalo Mungu alitoa wakati huu ni lile ambalo linaunganisha enzi; kwamba ni wakati wa kwanza tangu mwanzo wa Enzi ya Neema ambapo Mungu amezungumza wazi kwa jamii ya binadamu; zaidi, kwamba ni wakati wa kwanza Amezungumza baada ya kujificha kwa miaka elfu mbili; na, zaidi ya hayo, kwamba ni utangulizi, sehemu muhimu ya kuanzia, kwa kazi ambayo Mungu yuko karibu kufanya katika Enzi ya Ufalme.
Wakati wa kwanza Mungu alitoa tamko, Alifanya hivyo kwa jinsi ya sifa kutoka kwa mtazamo wa nafsi ya tatu, kwa lugha ambayo wakati mmoja ilikuwa ya sanaa na ya ustaarabu na wazi na ya nyumbani, na vile vile ruzuku ya maisha ambayo ingeeleweka kwa urahisi na bila shida. Akiwa na hili, Alichukua kundi hili dogo la watu, waliojua tu jinsi ya kufurahia neema Yake wakingoja kurudi kwa Bwana Yesu kwa hamu, na kuwaleta kwa kimya katika hatua nyingine ya kazi katika mpango wa Mungu wa usimamizi. Katika hali hizi, binadamu hawakujua, sembuse kuthubutu kufikiri, ni aina gani ya kazi Mungu angefanya hatimaye, ama kilichokuwa njiani mbele. Baadaye, Mungu aliendelea kutoa matamko zaidi kuwaleta binadamu katika enzi mpya hatua kwa hatua. La kushangaza, kila tamko la Mungu ni tofauti katika maudhui na aidha hutumia aina tofauti za sifa na njia za maonyesho. Matamko haya, yaliyo sawa kwa sauti lakini ya namna mbalimbali katika maudhui, yamejazwa kila wakati na hisia za Mungu za utunzaji na kujali, na karibu kila moja lina ruzuku za maisha na maudhui tofauti na vile vile maneno ya kukumbusha, kushawishi, na kufariji kutoka kwa Mungu hadi kwa mwanadamu. Katika matamko haya, mafungu kama hili yanaonekana mara kwa mara: “Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote”; “Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu”; “Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake”; na mengineo. Ujumbe unapitishwa katika mafungu haya, ama mtu anaweza kusema kwamba mafungu haya yanapitisha ujumbe kwa jamii ya binadamu: Mungu tayari amekuja katika dunia ya binadamu, Mungu ataanzisha kazi kubwa hata zaidi, ufalme wa Mungu tayari umeshuka katika kundi fulani la watu, na Mungu tayari amepata utukufu na kushinda maadui Wake wengi. Kila tamko la Mungu linaushika moyo wa kila binadamu. Wanadamu wote wanamsubiri Mungu ayape sauti hata maneno mengi zaidi, kwa sababu kila wakati Mungu huzungumza, Anatikisa moyo wa binadamu hadi kwa kina chake, na zaidi Anaongoza na kuweka sawa kila mwendo na kila hisia ya mwanadamu, ili kwamba binadamu waanze kuyategemea na hata zaidi kuyaheshimu maneno ya Mungu…. Kwa njia hii, pasipo kujua, watu wengi sana walikuwa wameisahau Biblia kimsingi, na kuyasikiliza shingo upande mahubiri ya kale na maandishi ya watu wa kiroho, kwa sababu hawakuweza kupata katika maandishi ya zamani msingi wowote wa maneno haya ya Mungu, wala hawakuweza kugundua mahali popote makusudi ya Mungu katika kutoa matamko haya. Kwa sababu hiyo, ilimpasa kwa kiasi gani binadamu kukiri kwamba matamko haya ni sauti ya Mungu ambayo hayajaonwa wala kusikika tangu mwanzo wa wakati, kwamba yako mbali ya uwezo wa mtu yeyote anayemwamini Mungu, na kwamba yanapita matamko yote yaliyotolewa na mtu yeyote wa roho anayeishi katika enzi za zamani au na Mungu zamani. Wakihimizwa na kila moja ya matamko haya, binadamu waliingia bila kujua katika hali ya kuashiria wema wa kazi ya Roho Mtakatifu, kuingia katika maisha kwa safu ya mbele ya enzi mpya. Wakihimizwa na maneno ya Mungu, binadamu, wakiwa wamejawa na matarajio, walionja utamu wa kuongozwa binafsi na maneno ya Mungu. Naamini muda huu mfupi kuwa wakati ambapo kila binadamu ataangalia nyuma kwa kumbukumbu ya kuvumilia, wakati ambapo kwa kweli kile ambacho binadamu walifurahia wakati huu hakikuwa zaidi ya hali ya kuashiria wema wa kazi ya Roho Mtakatifu, au mtu anaweza kukiita ladha tamu ya kudanganya. Hii ni kwa sababu, kutoka hatua hii kuendelea, bado chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, bado katika hali ya kuashiria wema wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, binadamu waliongozwa katika awamu nyingine ya maneno ya Mungu pasipo kujua, ambayo ilikuwa hatua ya kwanza iliyohemshwa na tamko la Mungu katika Enzi ya Ufalme—jaribio la watendaji huduma.
Maneno yaliyotamkwa kabla ya jaribio la watendaji huduma yalikuwa hasa kwa jinsi ya maagizo, ushawishi, lawama, na kufundisha nidhamu, na katika sehemu nyingine yalitumia jinsi nzee ya utambulisho iliyotumiwa katika Enzi ya Neema—kutumia “Wanangu” kwa wale waliomfuata Mungu ili kufanya iwe rahisi kwa binadamu kumkaribia Mungu, au ili binadamu waweze kuchukulia uhusiano wao na Mungu kuwa wa karibu. Kwa njia hii, bila kujali hukumu ambayo Mungu alitoa kwa kujiona, majivuno na tabia nyingine potovu za binadamu, mwanadamu angeweza kushughulikia na kulikubali katika utambulisho wake wa “mwana,” bila kuwa na uhasama kwa matamko ya “Mungu Baba,” ambayo kwa kuongezea ahadi ambayo “Mungu Baba” alitoa kwa “wana” Wake haikuwa ya shaka kamwe. Katika kipindi hiki, binadamu wote walifurahia uwepo ulio huru kutokana na taabu kama wa mtoto mchanga, na hili lilitimiza makusudi ya Mungu, ambayo ni, walipoingia katika utu uzima, Angeanza kutekeleza hukumu kwao. Hili pia liliweka msingi wa kazi ya kuhukumu jamii ya binadamu ambayo Mungu anaanzisha rasmi katika Enzi ya Ufalme. Kwa sababu kazi ya Mungu katika kupata mwili huku hasa ni kuhukumu na kushinda jamii nzima ya binadamu, punde tu mwanadamu alipoweka miguu yake chini kwa uthabiti, Mungu aliingia katika mtindo wa kazi Yake mara moja—katika kazi ambamo kwayo Anamhukumu mwanadamu na kumwadibu. Kwa uwazi, matamko yote kabla ya jaribio la watendaji huduma yalitolewa kwa ajili ya kupitia mageuzi, lengo la kweli likiwa tofauti na lile lilioonekana kuwa. Nia ya hamu ya Mungu ilikuwa kwamba Aweze kuzindua rasmi kazi Yake katika Enzi ya Ufalme punde iwezekanavyo. Hakutaka kwa vyovyote vile kuendelea kumbembeleza binadamu mbele kwa kumpa maneno madogo madanganyifu; badala yake, Alikuwa na hamu kuona uso wa kweli wa kila mwanadamu kabla ya kiti Chake cha hukumu, na hata kwa hamu zaidi Alitaka kuona mtazamo wa kweli ambao binadamu wote wangekuwa nao kuelekea Kwake baada ya kupoteza neema Yake. Alitaka tu kuona matokeo, sio mchakato. Lakini wakati huo hakukuwa na mtu aliyeelewa nia ya Mungu yenye hamu, kwa sababu moyo wa binadamu ulishughulika tu na hatima yake na matarajio yake ya baadaye. Sio ajabu kwamba hukumu ya Mungu ilikuwa imeelekezwa, mara kwa mara, kwa jamii nzima ya binadamu. Ilikuwa tu wakati binadamu, chini ya mwongozo wa Mungu, walianza kuishi maisha ya kawaida ya binadamu ambapo mtazamo wa Mungu kwa binadamu ulibadilika.
Mwaka wa 1991 haukuwa wa kawaida: hebu tuuite mwaka huu “mwaka wa ustawi.” Mungu alianzisha kazi mpya ya Enzi ya Ufalme na kuelekeza matamko Yake kwa jamii yote ya binadamu. Wakati huo huo, binadamu walifurahia wema wa pekee na, hata zaidi, kupitia uchungu unaofuata hukumu ya Mungu ya pekee kwa mwanadamu. Jamii ya binadamu ilionja utamu usiojulikana mpaka sasa na kuhisi pia hukumu na hali ya kutupwa isiyojulikana mpaka sasa kana kwamba ilikuwa imempata Mungu na tena kana kwamba ilikuwa imempoteza Mungu. Kuteseka katika umiliki na kuteseka katika ufukara—hisia hizi zinajulikana tu na wale wanaozipitia wao wenyewe; ni kitu ambacho mwanadamu hana uwezo wala njia ya kueleza. Majeraha ya aina hii ni yale Mungu alimpa kila mtu kama aina ya uzoefu usioshikika na mali. Maudhui ya matamko yaliyotolewa na Mungu katika mwaka huu kweli yamo katika sehemu mbili kuu: Ya kwanza ni sehemu ambapo Mungu alishuka katika dunia ya wanadamu kuwaalika binadamu kuja mbele ya kiti Chake cha enzi kama wageni; ya pili, sehemu ambapo binadamu, baada ya kula na kunywa hadi kushiba, walitumiwa na Mungu kama watendaji huduma. Bila shaka ni dhahiri kwamba sehemu ya kwanza ni matakwa ya binadamu ya thamani nyingi na ari zaidi, hasa kwa kuwa wanadamu wamezoea tangu zamani kufanya kufurahia kila kitu cha Mungu kuwa lengo la imani yao Kwake. Hii ndiyo maana, punde Mungu alipoanza kuyapa matamko Yake sauti, binadamu wote walikuwa tayari kuingia katika ufalme na walisubiri hapo ili Mungu awape thawabu tofauti. Watu katika hali hizi hawakulipa gharama ya kufaa kabisa kwa kubadilisha tabia zao, kutafuta kumridhisha Mungu, kufikiria mapenzi ya Mungu na kadhalika. Kwa mtazamo wa haraka wa juu juu, wanadamu walionekana kushughulika huku na kule siku zote huku wakijitumia na kufanya kazi kwa ajili ya Mungu, wakati kwa kweli walikuwa wakifanya hesabu, katika mahala pa siri zaidi pa vina vya mioyo yao, hatua ifuatayo wanayopaswa kuchukua kupata baraka au kutawala kama wafalme. Mtu anaweza kusema kwamba, wakati moyo wa mwanadamu ulipokuwa ukimfurahia Mungu, ulikuwa ukifanya hila dhidi ya Mungu wakati huo huo. Wanadamu katika hali hii hukutana na chuki ya kina zaidi ya Mungu na karaha; tabia ya Mungu haivumilii binadamu yeyote kumdanganya au kumtumia. Lakini hekima ya Mungu haifikiki kwa mwanadamu yeyote. Ilikuwa katikati ya kuvumilia mateso haya yote ambapo Alisema sehemu ya kwanza ya matamko Yake. Kiasi cha mateso ambayo Mungu alivumilia, na ni kiasi gani cha kujali na fikira Alitumia wakati huu, hakuna mwanadamu anayeweza kuwaza. Lengo la sehemu ya kwanza ya haya matamko ni kufichua aina tofauti za ubaya ambazo mwanadamu huonyesha anapokabiliwa na cheo na faida, na kufichua ulafi na kustahili dharau kwa mwanadamu. Hata ingawa, katika kuzungumza, Mungu huyafuma maneno Yake kwa sauti ya kweli na ya moyo ya mama anayependa, ghadhabu katika kina zaidi ya moyo Wake huwaka kama jua la mchana ambalo Anaelekeza dhidi ya adui Zake. Mungu hataki katika hali yoyote kuzungumza kwa kundi la watu wasio na usawa wa kawaida wa jamii ya binadamu, na hivyo, wakati wowote Anapozungumza, Anazuia ghadhabu iliyo ndani ya moyo Wake ilhali wakati huo huo Akijizuia ili kuonyesha tamko Lake. Zaidi ya hayo Anazungumza kwa jamii ya binadamu isiyo na ubinadamu wa kawaida, isiyo na mantiki, potovu kabisa, na ulafi kugeuka kuwa asili ya pili, na isiyotii na inayomwasi Mungu hadi mwisho kabisa. Vina ambavyo jamii ya mwanadamu imeanguka vinaweza kufikiriwa kwa urahisi, na hata zaidi chuki na karaha ya Mungu kwa jamii ya mwanadamu inaweza kufikiriwa kwa urahisi, lakini jamii ya binadamu ina ugumu kufikiri kwamba maumivu waliyompa Mungu hayawezi kuelezwa na maneno. Lakini ilikuwa hasa katika usuli huu—ambapo hakuna mtu aliweza kugundua jinsi moyo wa Mungu unavyoteseka, na aidha hakuna mtu aliyegundua jinsi jamii ya binadamu isivyo ya akili na isiyorekebishika—kwamba kila mtu, bila aibu yoyote au haya hata kidogo, aliona kuwa jambo la kawaida kwamba alikuwa na haki kama wana wa Mungu kupokea thawabu zote ambazo Alikuwa amemtayarishia mwanadamu, hata kwa kiwango cha kugombana, kusiwe na mtu aliyetaka kubaki nyuma na wote wakiogopa sana kupoteza. Kufikia sasa unapaswa kujua ni nafasi ya aina gani ambayo watu wakati huo walimiliki machoni pa Mungu. Jamii ya wanadamu kama hii inawezaje kupata thawabu za Mungu? Lakini kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa Mungu ni hazina ya thamani sana nyakati zote, na kinyume chake kile ambacho Mungu hupokea kutoka kwa mwanadamu ni uchungu mkubwa kabisa. Tangu mwanzoni mwa uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, hiki ndicho mwanadamu amepokea daima kutoka kwa Mungu na kile ambacho amempa Mungu daima kama malipo.
Hata ingawa Mungu alijaa wasiwasi, Alipoona jamii hii ya binadamu, iliyo potovu kwa kina sana, Hakuwa na chaguo ila kuitupa ndani ya jahanamu ili iweze kusafishwa. Hii ni sehemu ya pili ya tamko la Mungu, ambapo Mungu aliwatumia binadamu kama watendaji huduma Wake. Katika sehemu hii, Mungu alitoka kuwa mpole hadi kuwa mkali, na kutoka machache hadi mengi, kuhusu mbinu na urefu, akitumia nafasi ya “nafsi ya Mungu” kama ubembe kufichua asili potovu ya mwanadamu ilhali wakati huo huo kuweka mbele vikundi tofauti vya[a] watendaji huduma, watu, na wana kwa watu kuchagua kutoka hapo. Bila shaka, kama vile Mungu alivyokuwa ametabiri, hakuna mtu aliyechagua kuwa mtendaji huduma kwa ajili ya Mungu, na badala yake wote walijitahidi kuwa nafsi ya Mungu. Hata ingawa, katika kipindi hiki, ukali ambao kwao Mungu alizungumza kilikuwa kitu ambacho binadamu hawakuwahi kutarajia na sembuse kusikia, hata hivyo, kujali sana kuhusu hadhi, na juu ya hili, kushughulika kwa msisimko mkubwa na kupata baraka, hawakuwa na wakati wa kuunda fikira kuhusu sauti ya Mungu ya kuzungumza na njia Yake ya kuzungumza, badala yake wakinuia kutenda bila hadhari hadhi zao na kile kilichowangoja baadaye. Kwa njia hii, binadamu waliletwa, bila kujua, na tamko la Mungu ndani ya matata mengi Aliyokuwa amewawekea. Wakiwa wameshawishiwa, bila hiari, na mvuto wa siku za mbele na kudura yao, binadamu walijijua hawafai kuwa nafsi ya Mungu, na bado walikuwa wakisita kutenda kama watendaji huduma Wake. Wakiwa wamechanganyikiwa kati ya fikira hizi zinazopingana, bila kujijua walikubali hukumu ya pekee na kuadibu ambako Mungu alikuwa amewapa binadamu. Kwa kawaida, aina hii ya hukumu na usafishaji kilikuwa kitu ambacho binadamu hawakuwa tayari kukubali hata kidogo. Hata hivyo, Mungu tu ndiye aliye na hekima, na ni Yeye tu aliye na uwezo, kutoza unyenyekevu mpole kutoka kwa jamii hii potovu ya wanadamu, ili kwamba, watake au wasitake, wote walikubali mwishowe. Binadamu hawakuwa na mbadala kuchagua kutoka. Ni Mungu tu aliye na uamuzi wa mwisho, na ni Mungu tu anaweza kutumia mbinu kama hii kumpa mwanadamu ukweli na uhai na kumwonyesha mwelekeo. Mbinu hii ni kutoepukika kwa kazi ya Mungu kwa mwanadamu, na pia, bila shaka au ugomvi, ni haja ya lazima ya mwanadamu. Mungu hutumia mbinu kama hii kwa ajili ya kunena na kufanya kazi kupitisha ukweli huu kwa binadamu: Katika kumwokoa binadamu, Mungu hufanya hivyo kutokana na upendo na huruma Yake na kwa ajili ya usimamizi Wake; katika kupokea wokovu wa Mungu, jamii ya binadamu inafanya hivyo kwa sababu imeanguka hadi kwa hatua ambapo Mungu huzungumza Yeye binafsi tu. Mwanadamu anapopokea wokovu wa Mungu, hii ndiyo neema ya juu zaidi, na pia ni fadhila ya pekee, yaani, isingekuwa Mungu kulipa tamko Lake sauti Yeye binafsi, majaliwa ya jamii ya binadamu ingekuwa kutoweka. Wakati huo huo ambapo Anakirihi jamii ya binadamu, Mungu bado yuko tayari na mwenye radhi kulipa gharama yoyote kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Wakati huo, mwanadamu huzungumza kwa kurudiarudia juu ya upendo wake kwa Mungu na jinsi anavyoweka yote wakfu kwa Mungu, anaasi dhidi ya Mungu na kupokonya kila aina ya neema kutoka kwa Mungu, na hata, wakati huo huo, akimwumiza Mungu na kuumiza moyo Wake kwa uchungu mbaya. Hivyo ndivyo ilivyo tofauti dhahiri kati ya asiye na ubinafsi na aliye na ubinafsi katika uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu!
Katika kufanya kazi na kuzungumza, Mungu halazimiki kufuata mbinu yoyote maalum, ila hufanya kufikia matokeo katika upande Wake. Kwa sababu hii, katika “maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa,” Amehakikisha kutoonyesha utambulisho Wake kwa dhahiri, ila tu kufichua maneno machache kama “Kristo wa siku za mwisho,” “Mkuu wa ulimwengu,” na mengineyo. Hili haliathiri hata kidogo huduma ya Kristo au ufahamu wa binadamu wa Mungu, hasa kwa kuwa binadamu katika siku hizo za awali walikuwa wajinga kabisa kuhusu dhana ya “Kristo” na “kupata mwili,” kiasi kwamba Mungu alilazimika kujinyenyekeza Mwenyewe kuwa mtu na “kazi maalum” kuonyesha tamko Lake. Huu ni mfano wa nia ya juhudi ya Mungu, kwa sababu watu wakati huo wangeweza tu kukubali aina hii ya utambulisho. Bila kujali aina ya utambulisho ambao Mungu hutumia, matokeo ya kazi Yake hayaathiriwi, kwa sababu katika yote Anayofanya Mungu hunuia kumwezesha mwanadamu kubadilika, kumwezesha mwanadamu kupata wokovu wa Mungu. Bila kujali Anachokifanya, Mungu daima hufikiria mahitaji ya mwanadamu. Hii ndiyo nia ya Mungu kufanya kazi na kuzungumza. Hata ingawa Mungu yuko mwangalifu kikamilifu katika kufikiria vipengele vyote vya binadamu, na ni mwenye busara kikamilifu katika yote Anayofanya, Naweza kusema hili: Kama Mungu hangejishuhudia Yeye Mwenyewe, hakungekuwa na mmoja miongoni mwa jamii ya binadamu walioumbwa ambaye anayeweza kumtambua Mungu Mwenyewe au kusimama kumshuhudia Mungu Mwenyewe. Kama Mungu angeendelea kutumia “mtu na kazi maalum” kama aina ya utambulisho katika kazi Yake, hakungekuwa na binadamu hata mmoja ambaye angemchukulia Mungu kama Mungu—huu ni huzuni wa binadamu. Yaani, miongoni mwa jamii ya binadamu walioumbwa hakuna mtu anayeweza kumjua Mungu, hakuna wa kumpenda Mungu, kumjali Mungu na kumkaribia Mungu. Imani ya mwanadamu ni kwa ajili ya kupata baraka pekee. Utambulisho wa Mungu kama mtu aliye na kazi maalum imetoa dokezo kwa kila binadamu: Binadamu anaona ikiwa rahisi kumchukulia Mungu kama mmoja miongoni mwa jamii ya wanadamu walioumbwa; uchungu na fedheha ya juu kabisa ambayo binadamu anamwumiza nayo Mungu ni hiyo hasa, Anapoonekana na kufanya kazi kwa wazi, Mungu bado anakataliwa na mwanadamu na hata kusahaulika na yeye. Mungu huvumilia fedheha ya juu zaidi ili kuiokoa jamii ya binadamu; katika kutoa kila kitu, lengo Lake ni kumwokoa binadamu, kupata utambuzi wa binadamu. Gharama ambayo Mungu amelipa kwa ajili ya haya yote ni kitu ambacho kila mtu aliye na dhamiri anapaswa kuweza kuthamini. Jamii ya binadamu imepata kuzungumza na kufanya kazi kwa Mungu, na kupata wokovu wa Mungu. Wakati uo huo, hakuna mtu ambaye amefikiria kuuliza hili: Na ni nini ambacho Mungu amepata kutoka kwa binadamu? Kutoka katika kila tamko la Mungu, binadamu wamepata ukweli, wamefanikiwa kubadilika, wamepata mwelekeo katika maisha; lakini kile ambacho Mungu amekipata si zaidi ya maneno Anayowia na minong’ono dhaifu za sifa. Hakika hii siyo fidia ambayo Mungu anadai kutoka kwa mwanadamu?
Ingawa matamko mengi ya Mungu sasa yameonyeshwa, watu wengi bado wamepumzika kidogo katika hatua inayowakilishwa na “maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa” katika ufahamu na maarifa yao ya Mungu, ambapo kwayo hawajaendelea mbele—hii kweli ni mada chungu. Sehemu hii ya “maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa” ni ufunguo tu wa kufungua moyo wa binadamu; kupumzika kidogo hapa ni kutotimiza nia ya Mungu kabisa. Lengo la Mungu katika kuzungumza sehemu hii ya matamko Yake ni kumleta binadamu kutoka kwa Enzi ya Neema tu hadi katika Enzi ya Ufalme; Hataki hata kidogo binadamu wabaki wakisimama katika sehemu hii ya matamko Yake au hata kuchukua sehemu hii ya matamko Yake kama mwongozo, vinginevyo matamko ya baadaye ya Mungu hayatakuwa muhimu au ya maana. Iwapo kuna yeyote ambaye bado hawezi kuingia katika kile ambacho Mungu anadai kwamba mwanadamu apate katika sehemu hii ya matamko Yake, basi kuingia kwa mtu huyo kunabaki kusikojulikana. Sehemu hii ya matamko ya Mungu inajumuisha mahitaji ya msingi kabisa ambayo Mungu hutaka kutoka kwa mwanadamu katika Enzi ya Ufalme, na ndiyo njia ya pekee ambayo kwayo binadamu ataingia katika njia sahihi. Iwapo wewe ni mtu asiyeelewa chochote, basi ni bora uanze kwa kusoma maneno katika sehemu hii!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumapili, 4 Novemba 2018

Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Matamshi ya Kristo

Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La
Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli. Lakini hivyo ungeweza vipi kufikia kiwango hiki cha kawaida baada ya kusikia ushirika? Mbona ulikuwa na furaha sana baada ya kuusikia ukweli? Wengine wanasema ni kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu. Mbona basi kazi ya Roho Mtakatifu inakoma baada ya takriban siku kumi? Wengine husema ni kwa sababu wanakuwa wazembe na kuacha kusonga mbele na juu. Mbona basi hili linafanyika hata wakati watu wanapojaribu kufanya maendeleo? Mbona Roho Mtakatifu pia hafanyi kazi? Je, hukuwa unajaribu kusonga mbele na juu? Basi mbona Roho Mtakatifu hayuko kazini? Sababu ambazo watu hutoa haziko sambamba na hali ya kweli. Hapa, lazima tuibue hoja ifuatayo: Kama Roho Mtakatifu yuko kazini au la, ushirikiano wa watu binafsi hauwezi kupuuzwa. Watu walio wazi kuhusu ukweli na wanapenda ukweli kila wakati watakuwa na uwezo wa kubaki katika hali ya kawaida, bila kujali kama Roho Mtakatifu yuko kazini ama hapana. Kwa wale wasiopenda ukweli—hata kama ukweli hasa ni wazi kwao na hata kama Roho Mtakatifu anafanya kazi sana—kuna upeo kwa ukweli ambao wanaweza kuweka katika vitendo na kiwango cha muda ambao wanaweza kutenda. Mbali na wakati huo, hawafanyi chochote zaidi ya kudhihirisha asili yao wenyewe na maslahi yao wenyewe. Ipasavyo, kama hali ya mtu itafikia kiwango cha kawaida ama hapana na kama atauweka ukweli katika matendo ama hapana haitegemei tu kama Roho Mtakatifu yuko kazini au hapana, wala haiamuliwi tu na kama yuko wazi kuhusu ukweli ama hapana, ila hutegemea kama yuko tayari kuuweka ukweli katika matendo ama hapana na kama anapenda ukweli ama hapana.
Kwa kawaida, mtu husikia ukweli na, kwa muda, kila kitu huhisi kuwa kawaida kabisa kwake; katika muda huo wa kawaida, ukweli unaziinua hali zako kuwa kawaida. Unakufanya kujua asili yako potovu; moyo wako una furaha na unakuwa huru na hali yako inabadilika kuwa bora. Lakini baada ya muda, jambo laweza kukuchanganya; ukweli ulio ndani yako unakuwa usioonekana na bila kujua unaufanya ukweli huo kama jambo lisilo muhimu sana kwako; hujaribu kumtafuta Mungu katika matendo yako, unatenda kila kitu kwa mapenzi yako mwenyewe na huna nia ya kutenda ukweli kabisa. Wakati unapopita, unapoteza ukweli uliokuwa nao. Daima unadhihirisha asili yako mwenyewe, ukikosa kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya kufanya kazi ndani mwako; hutafuti nia ya Mungu kamwe; hata unapomkaribia Mungu, unapitia tu katika mizunguko. Punde tu unapogundua ukweli wa ugonjwa wako, moyo wako uko mbali sana na Mungu; umemkataa Mungu kwa vitu vingi na kutamka kufuru nyingi. Bado kuna ukombozi kwa wale ambao hawajaenda mbali sana katika njia hii, lakini kwa wale ambao wameenda mbali sana hata kumkufuru Mungu na kujiweka wenyewe dhidi ya Mungu, wakipigania cheo, na chakula na mavazi, hakuna ukombozi. Kusudi la ushurika wazi kuhusu ukweli ni ili kuwafanya watu kutenda ukweli na kubadilisha tabia yao, sio tu kuwafanya wafurahi. Kama unaelewa ukweli lakini hauuweki katika matendo, basi ushirika kuhusu ukweli na ufahamu wa ukweli hautakuwa na maana yoyote. Iwapo unaelewa ukweli lakini hauuweki katika matendo, utapoteza nafasi yako ya kupata ukweli na kupoteza nafasizyote za kuokolewa. Ukiuweka ukweli unaoelewa katika matendo, utapata ukweli wa ndani zaidi; utapata wokovu wa Mungu; utapata kupata nuru, mwangaza na uongozi wa Roho Mtakatifu. Wengi hulalamika tu kuwa Roho Mtakatifu kamwe hawapi nuru, lakini hawagundui kuwa kimsingi hawauweki ukweli katika matendo. Kwa hivyo, hali zao hazitawahi kupata ukawaida na hawatawahi kuyaelewa mapenzi ya Mungu.
2. Unahitaji Tu Kutenda Ukweli na Njia Itafunguka Mbele Yako
Wengine husema kuwa shida zao hazitatatuliwa kwa kutenda ukweli. Wengine huamini kuwa ukweli hauwezi kutatua kikamilifu tabiapotovu za watu. Ukweli ni kwamba shida zote za watu zaweza kutatuliwa; cha muhimu ni kama watu wanaweza kutenda kulingana na ukweli au hapana. Shida zenu za sasa sio saratani ama magonjwa yasiotibika; kama mnaweza kuweka ukweli katika matendo, shida hizi zote zaweza kubadilishwa, ikitegemea kama unaweza kutenda kulingana na ukweli ama hapana. Kama unatembea katika njia sawa, utafanikiwa; kama unatembea katika njia mbaya, utakuwa umemalizika. Kwa mfano, watu wengine hufanya kazi zao bila kufikiria kuhusu jinsi ya kufanya vitu kwa njia ya faida kwa kazi ama kama jinsi wanavyofanya vitu inapatana na mapenzi ya Mungu; kama tokeo, wanafanya mabo mengi ambayo Mungu anachukia. Kama wangetenda kulingana na ukweli katika kila jambo, je hawangekuwa watu ambao wanaupendeza moyo wa Mungu? Watu wengine wanajua ukweli lakini hawauweki katika matendo, wakiamini kuwa ukweli ni hili tu na sio kitu kingine zaidi. Wanaamini kuwa hauwezi kutatua mapenzi yao wenyewe na upotovu wao. Je, mtu wa aina hii sio mmwenye mzaha? Je, yeye sio mpumbavu? Je hajioni mwenyewe kuwa werevu? Watu wakitenda kulingana na ukweli, tabia yao potovu itabadilishwa; watu wakimwamini na kumtumikia Mungu kulingana na tabia zao asili, hakuna kati yao atakayebadilishiwa tabia yake. Watu wengine wanajipata katika shughuli zao wenyewe siku nzima na wanakosa kuchunguza ama kutenda ukweli unaopatikana tayari. Utendaji huu ni wa kipumbavu sana; watu wa aina hii ni watesekaji kiasili, kuwa na baraka lakini hawaifurahii! Njia ipo, kinachofaa kufanywa tu ni wewe kuiweka katika matendo. Kama umeamua kuuweka ukweli katika matendo, unyonge wako na dosari mbaya zinaweza kubadilishwa, lakini lazima kila wakati uchukue tahadhari na kuwa makini na kupitia ugumu zaidi. Kumwamini Mungu kunahitaji moyo wenye busara—unaweza kumwamini Mungu vizuri ukichukua namna hii ya kawaida?
Watu wengine wanajihami tu na ukweli fulani kwa wakati wa dharura ama kujitelekeza wenyewe na kuwasaidia wengine, sio kutatua shida zao wenyewe; tunawaita “watu wasio na ubinafsi.” Wanawaona wengine kama vikaragosi wa ukweli na wenyewe kama mabwana wa ukweli, wakiwafunza wengine kuushikilia ukweli na wasiwe wasiojihususha, ilhali wao wenyewe ni watazamaji kando kando mwa uwanja—hao ni watu wa aina gani? Wakiwa wamejihami na baadhi ya maneno ya ukweli ili kuwahubiria wengine tu, wakikosa kufanya chochote kujizuia kutokana na kuangamia kwao wenyewe—inasikitishaje! Kama maneno yao yanaweza kuwasaidia wengine, mbona wasijisaidie wenyewe? Tunafaa kuwaita wanafiki wasio na ukweli. Wanatoa maneno ya ukweli kwa wengine na kuwaambia wengine wayaweke katika matendo, lakini hawafanyi juhudi yoyote kuyatenda wenyewe—je sio wa kudharauliwa? Kwa hakika hawawezi kulifanya wenyewe, ilhali wanawalazimisha wengine kuweka maneno ya ukweli katika matendo—hii ni njia ya ukatili iliyoje! Hawatumii ukweli kuwasaidia wengine; hawawatolei wengine kwa moyo wa upendo wa mama; wanawadanyanya tu watu na kuwapotosha watu. Hili likiendelea—na kila mtu akipitisha maneno ya ukweli kwa anayefuata—je kila mmoja mwishowe hatakuwa na uelewa tu wa maandishi ya ukweli wakikosa uwezo wa kuyatenda? Watu wa aina hii wanawezaje kubadilishwa? Hawazitambui shida zao wenyewe kabisa; kutaweza vipi kuwa na njia kwa ajili yao?
Kila tatizo lina njia ya kutatuliwa; kwa kila tatizo kila wakati kutakuwa na ukweli ufaao kushauri ili kukupa njia ya kuendelea mbele na kukuwezesha kubadilika. Hata kama mabadiliko hayatafanyika mara moja, sasa unaweza kuitambua hali yako. Kama kweli hizi hazingeweza kutatua matatizo ya watu, basi Mungu hatakuwa Amenena bure? Kwa hivyo, kama uko tayari kuuweka ukweli katika matendo, kila wakati utakua na njia ya kufuata.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumamosi, 3 Novemba 2018

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Mchezo mfupi Mipaka ya Meya wa Kijiji inaeleza hadithi ya kweli ya mume na mke Wakristo ambao wanalazimishwa kutoroka kwa sababu ya mateso ya serilaki ya CCP.
Mkristo Liu Ming'en anahukumiwa na CCP miaka saba gerezani kwa kuamini katika Mungu. Hata baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, anabakia kuwa wakulengwa na uchunguzi mkali wa CCP. Meya wa kijiji anatumia mfumo wa wajibu wa kaya-tano , kamera za usalama, ziara za nyumba, na njia nyingine kumzuia Liu Ming'en na mkewe kuamini katika Mungu, lakini hakuna inayoleta na matokeo yanayotakiwa. Wakati huu, meya anapokea taarifa za kipaumbele kutoka Kamati Kuu ya Chama, baada ya hapo anajaribu kutafuta njia za kumlazimisha Liu Ming'en na mkewe kuweka saini barua ya kuahidi kuacha kuamini katika Mungu. Baada ya hila yake kushindwa, polisi tena wanakuja kuwakamata waumini hawa wawili. Kuepuka kukamatwa na kuendelea kumfuata Mungu na kuamini katika Mungu, Liu Ming'en na mkewe wanalazimishwa kutoroka nyumbani kwao.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Ijumaa, 2 Novemba 2018

Neno la Mungu | "Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya"

Neno la Mungu | "Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya"

Mwenyezi Mungu anasema, "Kuonekana kwa Mungu hurejelea kuwasili Kwake duniani kufanya kazi Yake. Akiwa na utambulisho na tabia Yake, na katika mbinu Yake ya asili, Yeye hushuka miongoni mwa wanadamu kufanya kazi ya kuanzisha enzi mpya na kukamilisha enzi nyingine. Kuonekana kwa aina hii si aina fulani ya sherehe. Si ishara, picha, muujiza, au ono kuu, na hata zaidi si mchakato fulani wa kidini. Ni ukweli halisi ambao waweza kushikwa na kuonekana. Kuonekana kama huku si kwa ajili ya kufuata taratibu, au kwa ajili ya shughuli ya muda mfupi; ni, badala yake, kwa ajili ya hatua ya kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Kuonekana kwa Mungu daima ni kwenye maana na daima huenda pamoja na mpango wa usimamizi. Kuonekana huku ni tofauti kabisa na udhihirisho wa uongozi wa Mungu, utawala na kupata nuru kwa mwanadamu. Mungu hufanya kazi kubwa kila mara Anapojifunua. Kazi hii ni tofauti na enzi yoyote nyingine. Haiwezi kufikirika na mwanadamu na haijawahi na mwanadamu hana uzoefu huu. Ni kazi ambayo huanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya awali, na ni aina mpya ya kazi na iliyoboreshwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu; aidha, ni kazi ya kuleta wanadamu katika enzi mpya. Huo ndio umuhimu wa kuonekana kwa Mungu."
Soma Zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Alhamisi, 1 Novemba 2018

Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo | Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Nguzo inapopandishwa kidogo, mnaweza kupiga hatua kidogo. Si jambo baya kuwa na mahitaji ya juu kutoka kwenu na wala si jambo baya kuwauliza maswali magumu. Lengo ni kuwafanya muwe na ufahamu zaidi juu ya elimu na maarifa ya kawaida ya kipengele cha weledi cha wajibu wenu.[a] Huenda labda nyinyi bado hulalamika katika nyoyo zenu, mkisema: "Tumejifunza mambo mengi mazuri lakini Mungu huwa hayataji kamwe au kuturuhusu kuyatumia. Kwa hiyo hatuthubutu kuyataja au kuyatumia. Je, na kama yakikanushwa mara tu tunapoyatumia? Na je, tukikosolewa? "Sasa Nawaambieni kwamba mnaweza kuyatumia mambo haya kwa ujasiri. Lakini ni lazima mpitie ukaguzi wa ndugu zenu wa kiume na wa kike. Usiwe wa kujidai, na kusema: "Mungu amesema wakati huu tunaweza kutumia mambo haya kwa ujasiri, kwa hiyo tutatumia mambo haya kwa ujasiri." Kuwa na ujasiri sio kuenea pote au kuwa wenye dharau. Lazima kuwe na mipaka ya kuwa na ujasiri, ni lazima kukubaliane na kanuni, na ndugu wa kiume na wa kike wanapaswa kulifikiria kuwa linafaa. Mtu fulani akisema, "Hili halikubaliki," basi si unahitaji kulibadilisha? Je, watu wakaidi ni watu wema? (Hapana.) Haishauriwi kuwa hivyo. Ni lazima usikilize maoni ya wengine, na unapowasikia wakisema hivi, unasema, "Uko sawa. Ni lazima nilibadilishe." Baada ya kulibadilisha, watu wengine husema: "Uko karibu hapo, nahisi vyema kuhusu hili. Liko sawa, limefaulu." Safi sana! Kwa kufanya mambo kwa njia hii, kipengele kimoja ni kwamba mnaweza kuingia kwa kina katika kipengele cha weledi, na muwe wakomavu na wenye uzoefu; kipengele kingine ni kwamba nyinyi pia mna uwezo wa kujifunza mambo mengi; na bado kipengele kingine ni kwamba mmejifunza somo. Unapokabiliwa na masuala, hupaswi kujidai, ukifikiri, "Nina kauli ya mwisho. Hamna sifa ya kuzungumza. Ninaelewa kanuni, nyinyi mnaelewa nini? Hamuelewi, ninaelewa!" Huku ni kujidai. Kuwa wa kujidai ni tabia potovu ya kishetani; si kitu kilicho ndani ya ubinadamu wa kawaida. Kwa hiyo, ni nini maana ya kutokuwa wa kujidai? (Kupata mapendekezo kutoka kwa kila mtu, na kila mtu kuyapima pamoja.) Wakati kila mtu anapoliidhinisha, na kila mtu anapokubaliana nalo, basi mmefanya kazi nzuri. Mradi baadhi ya watu au kikundi cha watu hudakiza kipingamizi, basi ni lazima muwe mahsusi zaidi kuhusu kipengele cha weledi. Ni lazima msijifanye kutotambua na kusema: "Nani? Aliyedakiza nini? Ni nini kinachoendelea? Je, wewe ndiye unayelielewa hili au ni mimi? Je, unaelewa hili vyema kuniliko? Unaelewa nini? Huelewi!" Hii ni tabia mbaya, sivyo? Ijapokuwa aliyedakiza kipingamizi huenda asielewe vizuri sana na anaweza kuwa mlei, na unaweza kuwa na haki na kile ulichokifanya kinaweza kuwa sahihi, tatizo hapa ni tabia yako. Kwa hiyo ni nini maonyesho na vitendo sahihi vinavyokubaliana na kanuni na kukubaliana na ukweli? Unasema: "Tatizo ni nini? Acha niangalie. Sio mimi tu, lakini kila mtu anaangalia. Wale ambao wana mapendekezo fulani kuhusu kipengele hiki au utambuzi fulani ndani yake, au ambao wana uzoefu fulani katika kipengele hiki, hebu sote tuangalie pamoja na tuweze kuzungumza juu yake. "Ikiwa kila mtu huamini kweli kuwa kufanya kitu kwa njia hii ni vibaya, kwamba kuna shida kidogo hapa, na unatazama mara moja na huwezi kuona tatizo, unatazama mara mbili na bado huwezi kuliona, kisha unaangalia mara tatu au mara nne na unavyozidi kuangalia ndivyo unavyozidi kuona kuna shida, basi hili kwa kweli ni tatizo. Na lazima ulisahihishe, lifanye liwe zuri na uombe mawazo ya kila mtu. Je, hili ni jambo jema au jambo baya? (Ni jambo jema.) Unaomba mawazo ya kila mtu, kila mtu analizungumzia, unashirikiana pamoja na Roho Mtakatifu anakupa nuru; unafuata hilo, na tatizo linarekebishwa ipasavyo. Kila mtu huangalia na kusema, "Hilo ni sawa, na ni bora zaidi kuliko hapo awali!" Je, si huu ni mwongozo wa Mungu? Hili ni jambo kubwa! Unapofanya mambo kwa njia hii, kama wewe hujidai, unapoacha mawazo yako mwenyewe na fikira zako mwenyewe, na unapotenda ukweli, unanyenyekea na kusikiliza mawazo ya wengine, kisha ni nini hutokea? Wewe hupata fursa ya Roho Mtakatifu kufanya kazi kwako na Roho Mtakatifu hukupatia nuru. Nini hutokea wakati Roho Mtakatifu anapokupatia nuru? Umejifunza kitu kingine cha weledi. Je, si hiki ni kitu chema?
Mara unapokuwa umepitia hili, wewe hufikiri, "Ninapokabiliwa na masuala, ni lazima nisijidai. Kila mtu hunichukia ninapojidai." Wakati kila mtu anapomchukia mtu fulani, Mungu humchukia? (Ndiyo, Yeye humchukia.) Unajifunza somo, kweli? Unapotenda kwa njia hii daima, kipengele kimoja ni kwamba utaona maendeleo katika hali ya weledi ya wajibu wako, na Mungu atakupa nuru na kukubariki; kipengele kingine ni kwamba utakuwa na njia ya kufuata katika kutenda ukweli, utajua jinsi ya kutenda ukweli, hatua kwa hatua utakuja kuelewa kanuni na kupata njia, utajua jinsi ya kufanya mambo kwa namna ambayo itasababisha kupata nuru ya Mungu na uongozi, ni njia zipi za kufanya mambo ambazo humsababisha Mungu kukupuuza au kukuchukia, na jinsi ya kufanya mambo kwa njia ambayo inaweza kubarikiwa na Mungu. Watu wanapopata baraka za Mungu na nuru, kuna furaha au huzuni ndani ya mioyo yao? Kuna furaha. Unapokuja kuwajibika kwa kile ambacho umekifanya mbele ya Mungu, utapata furaha na utafikiri, "Nilikifanya vizuri." Ndani yako utajisikia mwenye amani na furaha. Hisia hii ya amani na furaha hutolewa kwako na Mungu, na ni kuchochea ulikopewa na Roho Mtakatifu. Ikiwa hutendi hili lakini daima huhimili kwa njia zako mwenyewe, ukisema, "Sitamsikiliza mtu yeyote. Hata nikisikiliza, nitaonekana tu kusikiliza na sitabadilika. Nitafanya mambo kwa njia hii, ninahisi niko sawa na nahisi nimethibitishwa kabisa, "ni nini kitakachotokea? Huenda kuwa umethibitishwa na huenda kusiwe na kosa katika kile ufanyacho, huenda hujafanya makosa yoyote na huenda ukaelewa kipengele cha weledi vyema zaidi kuliko wengine, lakini mara unapofanya aina hizi za maonyesho na kutenda kwa njia hii, wengine wataona na watasema: "Tabia ya mtu huyu si nzuri. Unapokabiliwa na masuala, huwa hawakubali lakini hupinga kitu chochote mtu mwingine yeyote anachosema, kama kiko sahihi au la. Mtu huyu huwa hakubali ukweli." Watu wanaposema wewe hukubali ukweli, Mungu atafikiri nini? Je, Mungu anaweza kuona maonyesho haya yako? Bila shaka, Mungu anaweza kuyaona. Mungu hachunguzi tu chokomeani mwa moyo wa mwanadamu, Yeye pia huangalia kila kitu usemacho na kufanya wakati wote na mahali pote. Na Anapoona mambo haya, Yeye hufanya nini? Yeye husema: "Wewe umefanywa mgumu. Uko jinsi hii katika hali ambapo wewe uko sawa, na uko jinsi hii pia katika hali ambapo umekosea. Bila kujali uko katika hali gani, kila kitu unachofichua na kuonyesha ni kupingana na upinzani. Hukubali hata kidogo mawazo au mapendekezo ya mtu yeyote mwingine. Moyo wako unapingana kabisa, kukataa na kutokubali mawazo ya wengine. Wewe ni mgumu sana!" Ni kwa njia gani unakuwa mgumu? Kuwa kwako mgumu ni kwamba maonyesho yako sio njia mbaya ya kufanya mambo au tabia mbaya, lakini kwa usahihi zaidi ni ufichuzi wa tabia yako. Je, tabia yako imefichua nini? Unauchukia ukweli na una uhasama mintarafu ya ukweli. Na wakati umefafanuliwa kama mtu ambaye ana uhasama mintarafu ya ukweli, machoni mwa Mungu uko katika shida. Si zaidi ya haya, kila mtu atasema, "Mtu huyu ana tabia mbaya, yeye ni mkaidi na mwenye kiburi. Mtu huyu ni vigumu kukubaliana naye, hana matendo ya ukweli na hapendi ukweli. Hajawahi kuukubali ukweli." Si zaidi ya haya, kila mtu atakutathmini kwa njia hii; lakini tathmini hii inaweza kuamua jaala yako? Watu hufanya tathmini yako, lakini hili haliwezi kuamua jaala yako. Lakini kuna jambo moja ambalo hupaswi kulisahau: Mungu huuchunguza moyo wa mwanadamu, na wakati huo huo Yeye huangalia kila kitu ambacho mtu husema na kufanya. Mungu akimfafanua mtu kwa kusema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," Yeye hamfafanui tu kwa kusema, "Mtu huyu ana tabia potovu kidogo na kwa kiasi kidogo si mtiifu," bali kwa usahihi zaidi Yeye anasema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," hii ni hoja kubwa au hoja ndogo? (Ni hoja kubwa.) Na hili husababisha shida? (Ndiyo.) Je, hili huleta shida gani? Shida hii haiko katika jinsi watu wengine hukuona au jinsi wanavyokutathmini, lakini liko katika jinsi Mungu anavyoona tabia yako potovu ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli. Hivyo ni vipi basi Mungu huona tabia yako ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, unajua? Mungu husema, "Ana uhasama mintarafu ya ukweli na hapendi ukweli." Je, Mungu huliona kwa jinsi gani? Ukweli hutoka wapi? Ukweli humwakilisha nani? (Humwakilisha Mungu.) Hivyo fikiria hili: Mungu anapaswa kuonaje tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, Yeye atalionaje? (Mungu huliona kuwa na uhasama kwelekea Kwake na kama adui Yake.) Na hili ni jambo zito? Mtu aliye na uhasama mintarafu ya ukweli ana uhasama mintarafu ya Mungu. Kwa nini Ninasema kuwa ana uhasama mintarafu ya Mungu? Je, huwa anamtukana Mungu? La. Huwa anampinga Mungu bayana? La. Je, huwa anamshushia Yeye hadhi kisiri? La. Hivyo kufichua tabia ya jinsi hii huwaje uhasama mintarafu ya Mungu? Je, si huu wote ni msukosuko wa bure? Kuna kitu ndani yake, sivyo? Unajua ni kitu gani? Mtu fulani ana tabia hii na hufichua aina hii ya tabia wakati wote na katika maeneo yote na, zaidi ya hayo, yeye huitegemea ili kuishi na haachi kamwe njia hii ambayo kwayo yeye huishi na kufanya mambo, na haitupi kamwe. Wewe hutegemea mambo na tabia hii ili kuishi, na wakati hakuna kitu kinachotokea, ikiwa mtu atasema kuwa una uhasama mintarafu ya Mungu, unaweza kukubaliana naye? Huwezi kukubaliana naye. Hata hivyo, matatizo yanapochipuka, unapokuwa na aina hii ya tabia, wewe huifichua wakati wote na mahali pote? Kwa hiyo hii ni tabia gani? Ni tabia ambayo ni uhasama mintarafu ya Mungu na uhasama mintarafu ya ukweli. Unayasaili maneno ya Mungu, unayachangua, unayachambua na kuyatilia shaka. Inamaanisha nini unapofanya mambo haya? Inamaanisha kwamba unaposikia maneno ya Mungu, wewe hufikiria, "Je, haya ni maneno ya Mungu? Sifikiri huu ni ukweli na sifikiri yote ni lazima yawe ni sahihi." Tabia yako imefichuliwa, ni kweli? Je, una uwezo wa kutii wakati unapofikiria jinsi hii? Hakika huna uwezo. Na kama huna uwezo wa kutii, Mungu bado ni Mungu wako? Hapana, Yeye si Mungu wako. Je, wewe basi humuona Mungu kama nini? Kama chombo cha kujifunza na cha shaka, na hata kama tu mtu wa kawaida, kama mtu mwenye tabia potovu kama tu mtu. Je, si hili linaletwa na tabia potovu ya mtu?
Wakati mtu amekwenda mbali hivyo na wakati ana uhusiano wa aina hii na Mungu, ni uhusiano gani uliopo kati ya mtu huyu na Mungu? Ni wa uhasama na yeye amekuwa mpinzani wa Mungu, sivyo? Ikiwa unamwamini Mungu lakini huwezi kuupata ukweli au kuukubali ukweli, Mungu si Mungu wako. Mungu hakuoni kama adui lakini wewe unamwona Mungu kama mpinzani wako na huwezi kukubali kwamba Yeye ni ukweli wako na njia yako, basi tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa jinsi gani? Unapokabiliwa na maswala unapaswa kwanza kufikiria, "Hali ni ipi hapa? Siielewi vizuri sana, na haiko dhahiri kwangu. "Bila kujali suala ni nini, hufafanui suala hilo kwanza, badala yake kwanza ni lazima uone kile maneno ya Mungu yanachosema juu yake. Unaweza kushindwa kupata maneno husika ya Mungu, na huenda pia usijue ni ukweli gani suala hili linahusisha, lakini unang'amua kanuni—ni kutii, kwanza kabisa. Kwanza kabisa, endelea kutii, tuliza moyo wako na usubiri, usiwe na mawazo au fikira za binafsi, subiri kwa muda na uone jinsi Mungu anavyopanga kukabiliana nalo na kile ambacho Mungu atafanya. Hili ni katika hali ambapo huelewi kabisa. Na je, wakati ambapo huelewi? Kwa mfano, mtu anatoa maoni; unashughulikiaje suala hili? Je, unalishughulikiaje kwa njia inayopatana na ukweli? Kwanza unalikubali; unasikiliza na kusema, "Haya yote ni nini? Aa, kuna shida kwangu kulifanya kwa njia hii? Ikiwa kuna shida, basi hebu tuangalie." Usiichukulie hoja hiyo kwa wepesi; inahusisha mambo katika upeo wa wajibu wako, kwa hiyo unapaswa kulitazama kwa uangalifu. Huu ndio mtazamo sahihi wa kuchukua na hali sahihi ya kuwemo. Unapokuwa katika hali sahihi, wewe hufichua tabia ambayo imechoshwa na ukweli? (Hapana.) Hufichui tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli, na unapotenda kwa njia hii tabia yako ya upotovu inabadilishwa; unatenda ukweli. Unapotenda ukweli kwa njia hii, ni matokeo gani yanayofanikishwa? (Roho Mtakatifu hutuongoza.) Mwongozo wa Roho Mtakatifu ni kipengele kimoja. Kwa Mungu, unatenda ukweli. Wakati mwingine una mwongozo wa Roho Mtakatifu na tatizo linarekebishwa; wakati mwingine baada ya kusikia juu ya suala hili, unalielewa kwa urahisi, na unaliona likiwa rahisi sana. Hicho ni kitu ambacho akili ya mwanadamu inaweza kufanikisha na unahitaji tu kukirekebisha. Hii ni hoja ndogo. Na hoja kubwa ni ipi? Unapotenda kwa njia hii, Mungu hukuona kama mtu anayetenda ukweli na kama mtu anayependa ukweli, na Yeye huona kwamba wewe si mtu anayeuchukia ukweli au ana uhasama mintarafu ya ukweli. Wakati huo huo Mungu anapoona moyo wako, Yeye pia huona tabia yako. Hii ni hoja kubwa. Yaani, unalolifanya mbele za Mungu, unaloishi kwa kudhihirisha mbele ya Mungu na unachokifichua mbele ya Mungu, na vilevile mtazamo unaouchukua, mawazo uliyo nayo na hali uliyomo katika kila kitu unachokifanya—maonyesho haya yote unayo mbele ya Mungu—haya ndiyo mambo muhimu zaidi.
Watu daima wanalalamika juu ya watu na masuala, na hili ni tatizo kubwa. Je, wao daima hufikiri nini? Wanafikiri kuwa ni watu wengine ambao ni wakatili kwao, au kwamba wengine huyafanya mambo kuwa magumu kwa makusudi, au huyapata makosa tu na watu wengine. Je, mtazamo huu ni sahihi? (Hapana, si sahihi.) Kwa nini unasema hapana? Ni kosa kabisa kulalamika daima juu ya masuala na watu. Hawafanyi jitihada na ukweli, na wao wanajaribu daima kuepuka aibu na kutafuta uthibitisho mbele ya wengine au miongoni mwa watu wengine, na wao daima hutaka kutumia njia za kibinadamu kuzitatua hoja hizi zote. Hiki ndicho kikwazo kikubwa mno kwa kuingia kwa maisha. Kwa kufanya kwa njia hii, kutenda kwa njia hii na kumwamini Mungu kwa njia hii, hutaweza kamwe kupata ukweli, kwa kuwa kamwe huji mbele ya Mungu. Huji kamwe mbele ya Mungu kukubali vitu vyote ambavyo Mungu hupanga kwa ajili yako, hutumii kamwe ukweli ili kutatua mambo haya yote, na daima wewe hutaka kutumia mbinu za kibinadamu kuyatatua. Hivyo machoni pa Mungu, umeenda mbali sana na Yeye na sio tu kwamba moyo wako umekwenda mbali sana na Mungu, lakini mawazo yako yote, nia zako zote na hali yako yote havijawahi kuwa mbele ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu huwaona wale ambao hulalamika juu ya masuala na watu. Kwa hiyo, watu wengine ambao wana kipaji cha kuzungumza na ni wepesi kung'amua, hufikiria, "Nina ufasaha, na wakati ninapokuwa na watu wengine, wote hunihusudu na kunipenda. Wao hunitukuza, na watu wengi sana huridhishwa nami. "Je, hili ni la manufaa yoyote? Sifa yako njema miongoni mwa watu wengine imeanzishwa, lakini mbele ya Mungu, Amekupuuza daima, na anasema kuwa wewe ni mtu asiyemwamini Mungu na kwamba una uhasama mintarafu ya ukweli. Miongoni mwa wengine wewe hutenda kwa njia ambayo ni laini na ya hila, unaweza kumshughulikia mtu yeyote, una uwezo mkubwa wa kushughulikia hoja, na unaweza kukubaliana na mtu yeyote. Lakini mwishowe, kwa tathmini moja kutoka kwa Mungu utakwisha, utafika mwisho mbaya, na jaala yako itapangwa. Mungu atasema: "Huyu ni mtu asiyeamini, akipeperusha bendera ya imani katika Mungu ili kupata baraka. Huyu mtu ana uhasama mintarafu ya ukweli, hajawahi kamwe kufanya jitihada na ukweli, na hajawahi kuukubali ukweli." Mnafikiria nini juu ya aina hii ya tathmini? Je, hii ndiyo tathmini mnayoitaka? (Hapana.) Bila shaka sicho kile mnachokitaka. Labda watu wengine hawajali, na wao husema, "Sijali. Hatuwezi kumwona Mungu kwa njia yoyote. Suala la kweli zaidi ambalo tunalo ni kuwa tunapaswa kukubaliana na watu walio nasi. Ikiwa hatuwezi kufanya mahusiano haya yafaulu basi tunawezaje kuishi miongoni mwa watu hawa? Maisha yetu yangekuwa magumu sana. Angalau sana tunapaswa kukubaliana na watu hawa na kushughulikia mahusiano vizuri. Chochote kingine kinaweza kusubiri." Ni watu wa aina gani hawa? Je, hawa bado ni watu ambao wanamwamini Mungu? (Hapana.) Mtu ni lazima aishi mbele ya Mungu nyakati zote na ni lazima aje mbele ya Mungu na kutafuta ukweli nyakati zote na kwa hoja zote, ili mwishowe Mungu atasema: "Wewe ni mtu anayeupenda ukweli na Mungu anafurahishwa nawe, Mungu anakukubali. Mungu huuona moyo wako na huiona tabia yako. "Unafikiria nini kuhusu tathmini hii? Hii ina maana kwamba wewe ni salama, sivyo?
Je, nyinyi kwa kawaida huzingatia hoja hizi? Hebu niwaambie, mnapomwamini Mungu, bila kujali kama unafanya wajibu wa nje, au unafanya wajibu unaohusiana na kazi yoyote au kipengele chochote cha kazi ya weledi ndani ya familia ya Mungu—bila kujali ni wajibu gani unaoufanya—ikiwa huwezi daima kuja mbele ya Mungu, ikiwa huwezi kuishi mbele ya Mungu, basi wewe si muumini na hakuna tofauti kati yako na mtu asiyeamini. Je, hili linasikika sahihi kwako? Je, mnaweza kufahamu jambo hili? Labda kuna baadhi ya watu sasa ambao hawawezi kufanya wajibu wao kwa sababu ya mazingira yasiyofaa, na wanaishi miongoni mwa wasioamini, lakini daima wanaweza kupata nuru na mwongozo wa Mungu—hivyo hali ni ipi hapa? Mnajua? (Ni kwa sababu daima wao huja mbele ya Mungu.) Ndiyo, hili huamua jinsi hali ya kiroho ya mtu ilivyo. Ikiwa, ndani yako mwenyewe, daima huwezi kumhisi Mungu, ikiwa daima u mdhaifu, daima u hasi, au wewe daima ni mwasherati, au daima hubebi mzigo katika wajibu wako na moyo wako siku zote unaboronga bila lengo lolote, basi hii ni hali nzuri au hali mbaya kuwemo? Je, ni hali ambapo unaishi mbele ya Mungu? Au ni hali ambapo huishi kamwe mbele ya Mungu? (Ni hali ambapo hatuishi mbele ya Mungu.) Basi fikirieni hili kwa makini—katika hali nyingi, huwa mnaishi mbele ya Mungu au hamuishi mbele ya Mungu? Je, mnafahamu vyema juu ya hili ndani ya mioyo yenu? Je, nyinyi huishi mbele ya Mungu wakati mwingi, au ni kwa nyakati chache tu? (Ni kwa nyakati chache tu.) Hili ni sumbufu kwenu. Kama mtu ni mchezaji, mwimbaji, mwandishi au mtengenezaji filamu, ikiwa moyo wake haujishughulishi kamwe na kufanya wajibu wowote unaofaa, ikiwa yeye ni mpotovu na hastahimiliki, ikiwa huwa daima anavurugika anapokabiliwa na masuala, hana wazo lolote ni hoja ipi inayohusisha kipengele kipi cha ukweli, wala hana wazo lolote kama kile anachokifanya kina athari yoyote, ikiwa hajui mambo gani anayoyafanya kila siku yanayomchukiza Mungu, ni mambo gani ambayo Mungu anaweza kuyakubali au ni mambo gani Mungu huyachukia, na wao huendelea tu siku baada ya siku katika kiwewe, basi ni hali aina gani hii ya kuwemo? Je, wale wanaoishi katika hali hii wana moyo wa kumuogopa Mungu ndani yao? Je, wana uwezo wa kutenda na kanuni? Je, wana uwezo wa kufanya chochote cha maana? (Hapana.) Wanapofanya wajibu wao, wanaweza kusema, "Ni lazima nivumilie vikwazo fulani, ni lazima nifanye kazi kwa bidii, kwa moyo wangu wote na kwa nguvu zangu zote, na kuwa mwaminifu"? Je, ana uwezo wa kuwa na uaminifu wowote? (Hapana.) Basi mnafanya nini hapa kwa kweli mnapofanya wajibu wenu? (Mkitumia nguvu.) Mko sawa; Mnatumia nguvu. Nyinyi ni wenye uwezo wa kazi, sivyo? Chakula chenu na nyumba zenu zote zimeshughulikwa, na halafu nyinyi hufanya kazi hapa. Ingawa hamchumi fedha hapa, mnahisi ni sawa mnapopata chakula, kinywaji na mahali pa kuishi. Lakini nyinyi huchuma ukweli? (Hapana.) Basi nyinyi hupoteza sana. Nyinyi ni wapumbavu mno! Mmemwamini Mungu kwa miaka mingi sasa, hazijakuwa siku chache tu. Mmesikia ukweli mwingi sana na hamjui mnamwamini Mungu kwa minajili gani, mnachohitaji kufanya, mnachopaswa kupata, au ni kitu gani cha muhimu zaidi kupata. Mnajua kidogo sasa? (Ndiyo.) Mnajua nini? Niambieni. (Kwa kumwamini Mungu, kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi.) Kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi? Kweli au uongo? (Kweli.) Bila shaka ni kweli. Lakini labda huenda msiwe na maarifa halisi ndani ya mioyo yenu hivi sasa, na huenda hamjalitambua kwa kiwango hiki.
Je, mmekisoma Kitabu cha Ayubu? (Ndiyo.) Na mlipokisoma Kitabu cha Ayubu, mioyo yenu ilisisimka? (Ndiyo.) Hivyo mlipata fikira za shauku, na kutaka kuwa mtu kama Ayubu? (Ndiyo.) Ni kwa muda gani mliweza kuendeleza hali hiyo na hisia hiyo? Nusu siku, siku mbili, juma moja? Au kwa mwezi mmoja au miwili, au mwaka mmoja au miwili? (Labda siku mbili hadi tatu.) Hisia hiyo iliondoka baada ya siku tatu? Wakati hisia hiyo inapoondoka, wewe huendelea kusoma, na unapoendelea kusoma unaweza kuiendeleza kwa siku zingine tatu. Lakini hivyo sivyo ilivyo, au ndivyo? Unaposoma kitabu hicho na unahisi msisimko, unapaswa kuomba, kindani fanya uamuzi wako kuwa unataka kuwa kama Ayubu, mtu ambaye anaweza kumjua Mungu, ambaye anaweza kupata ukweli, na anayeweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unasali kwa Mungu afanye vivyo hivyo kwako, na kwamba Mungu akuongoze na kukupangia mazingira, kukutolea nguvu, kukukinga katika mazingira yoyote ambayo unaweza kukabiliana nayo ili uweze kusimama imara, ili usimuasi Mungu, na unaweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Unahitaji daima kumsihi Mungu kwa lengo hili na kwa kile unachokitamani sana na unachotaka kukipata moyoni mwako, unahitaji kusihi na kuomba kwa ajili yalo, na wakati Mungu anapouona moyo wako wa kweli Yeye atalifanya. Huhitaji kuogopa Mungu akifanya jambo hili, kwa maana Mungu hawezi kuufanya mwili wako kufunikwa na vidonda kama wakati Alipomjaribu Ayubu na kukunyang'anya kila kitu ulicho nacho; Mungu hatakufanyia hivyo. Hatua kwa hatua Atafanya kazi Yake kwako kwa mujibu wa kimo chako. Ni lazima usihi kwa uaminifu; usilisome tu leo, ujihisi kusisimka na kumsihi Mungu, na kisha baada ya siku mbili usifanye chochote, na yawe yameisha mara unapogeuka. Watu husema, "Ayubu ni nani?" "Nani? Ayubu? Ayubu ni nani? Je, nawezaje kutojua? Huenda nimesikia kumhusu." Hili ni sumbufu! Usilisome kwa siku tatu na lote limesahaulika, limetoka moyoni mwako. Ukiwahusudu watu kama Ayubu na ungependa kuwa mtu kama huyo, moyoni mwako unapaswa kuwa na njia ya jinsi ya kuwa mtu kama huyo, lazima uweke moyo wako mbele ya Mungu, kisha ni lazima uombe kuihusu, omba kuihusu mara nyingi, chukua hoja hii kutoka moyoni mwako na kuitafakari mara nyingi, soma vitabu, soma makala kuhusu Ayubu na maneno ya Mungu yanayohusiana na Ayubu, itafakari daima na tena na tena, fanya ushirika pamoja na watu ambao wana aina hii ya maarifa, uzoefu au azimio , na lazima ufanye kazi kwa bidii mintarafu ya lengo hilo. Unapaswa vipi kufanya kazi kwa bidii? Kusoma tu kwa kweli sio kufanya kazi kwa bidii. Unahitaji kufanya jitihada na hoja hii, utoe maombi yako na kuiweka katika matendo, huku wakati huo huo ukiwa na azimio la kuvumilia mateso na kuwa na moyo wa shauku na hamu. Kisha unarairai, utoe maombi yako na kumwomba Mungu afanye hivi. Ikiwa Mungu haifanyi, itakuwa bure bila kujali ni jitihada kiasi gani unayoiweka, na jitihada zako ni za bure. Mungu huifanyaje? Yeye huanza kwa kuweka na kupanga mambo kwa ajili yako kulingana na kimo chako. Kwa mfano, unakaribia kuchukua mtihani wa kuingia chuo cha elimu, na unasema, "Ninataka alama ili kuingia katika Chuo Kikuu cha Tsinghua." Unaanza kuweka jitihada ili kufanikisha hili, unapitia upya masomo yako, unatafuta vifaa vya kujifunza juu ya chochote na kila kitu na unatafuta walimu kukufundisha. Kisha unawaambia wazazi wako na wanasema, "Mtoto wetu ana azimio zuri. Yeye huanza jambo kwa dhati, ana azimio na hajakosa ustadi." Kwa hiyo, wazazi wako watafanya nini? Wote wawili wataandaa ada yako ya masomo na kukupatia mwalimu. Watafanya mipango sahihi ya maisha yako, wakati unapopaswa kupumzika, na masomo yako, wakupeleke shuleni na kukuchukua baadaye, na watalifanya ili kwamba, wakati huu, usipate uchovu, au njaa, au kukosa chakula cha kutosha. Watakusaidia kwa kushughulikia na kusimamia mambo katika ulimwengu wa nje ili usichanganyikiwe. Watakufanyia mipango sahihi katika vipengele vyote. Kwa njia hii, utakuwa na wakati wa kutosha wa kupitia upya, kusoma na kufanikisha ndoto yako. Kuhusu kumwamini Mungu, chochote unacholenga au uamuzi wowote ulio nao, unapaswa kuzungumza na Mungu. Unahitaji kuomba juu ya hoja hii na kusihi sana juu yalo; itachukua muda mrefu! Itakuwa bure kuwa na moyo usio mwaminifu. Ikiwa unasali mara kadhaa tu mara kwa mara na kisha unapoona kwamba Mungu hajakufanyia chochote, unasema, "Lisahau. Sijali. Liwe liwalo, nitaacha tu mambo yatokee kama kawaida yake, na nitachukua mambo kama yanavyokuja," basi hili litakuwa bure, na moyo wako si mwaminifu. Je, Mungu atakufanyia chochote ikiwa una dakika kadhaa tu za shauku? Je, Mungu atapanga mazingira kwa ajili yako? Je, hilo linakubalika? Kwa kweli Mungu hafanyi kazi kwa njia hiyo. Mungu anataka kuona uaminifu wako na Anataka kuona ni kwa muda gani uaminifu wako na bidii ya moyo wako vinaweza kudumishwa, na kama moyo wako ni kweli au uongo. Mungu atangoja; Yeye husikiliza sala zako na kile unachorairai, na Yeye husikia maazimio yako na shauku zako, lakini Yeye bado hajaona maazimio yako ya kuvumilia mateso, kwa hivyo Yeye hatakufanyia chochote. Ikiwa wewe husema maneno machache na kisha kwenda, Mungu atakufanyia chochote? Hakika hapana. Lazima uendelee kurairai, endelea kuomba, jitahidi na kulitafakari, kisha uonje mazingira ambayo Mungu hukupangia—yatakujia kidogo kidogo, na Mungu ataanza kutenda. Bila moyo wa kweli, ni bure. Wewe husema, "kwa kweli mimi humhusudu Ayubu na kwa kweli mimi humhusudu Petro." Ni haja gani kuwahusudu? Huwezi kuwa wao bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, na bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, Mungu hatakufanyia kazi sawa na ile Aliwafanyia. Kwa nini hivyo? Kwa sababu wewe si aina moja ya mtu kama walivyokuwa. Humiliki azimio lao, au ubinadamu wao, na humiliki moyo wao wa shauku uliotafuta ukweli. Wakati utakapokuja utakapomiliki vitu hivi, ni hapo tu ndipo Mungu atakapokufanyia zaidi. Unaelewa?
Je, wengi wenu sasa wana azimio la kuelewa ukweli, kupata ukweli na kukamilishwa mwishowe? (Ndiyo.) Azimio lako ni kubwa kiasi gani? Je, unaweza kufanya liendelee kwa muda gani? Unajua? (Nina azimio hili wakati niko katika hali nzuri. Wakati mambo yanapotokea ambayo hayakubaliani na mwili wangu au kupatana na dhana zangu, na ninapopatwa na usafishaji au matatizo ndani yangu, basi imani yangu hupotea, mimi hukwama kwa namna ya hali hasi, na azimio nililokuwa nalo mwanzo hupungua hatua kwa hatua.) Hili halitaweza. Huku ni kuwa dhaifu sana. Lazima ufikie hatua ambapo azimio lako halibadiliki bila kujali ni mazingira gani unayoyakabili; huku tu ndiko kuwa mwaminifu, na huo ndio upendo halisi wa ukweli na shauku halisi ya kuwa aina hii ya mtu. Itakuwa bure kujikunyata wakati hoja fulani ndogo au shida inapotokea, au kuwa hasi, kusononeka na kuacha azimio lako mwenyewe wakati unapokabiliwa na shida ndogo. Unahitaji kuwa na nguvu ya mtu anayechagua kuhatarisha maisha yake, na kusema, "Bila kujali kinachotokea, hata kama ni lazima nife sitaacha azimio langu au kuachana na lengo hili." Halafu hakutakuwa na shida ambayo inaweza kukuzuia, na Mungu atakufanyia jambo hili. Aidha, lazima uwe na mtazamo wa aina hii na ufahamu jambo linapotokea, na kusema, "Bila kujali kinachofanyika, yote ni sehemu ya kufanikisha lengo langu, na ni shughuli ya Mungu. Kuna udhaifu ndani yangu, lakini mimi si hasi. Ninamshukuru Mungu kwa upendo Anaonipa na kwa kunipangia aina hii ya mazingira. Ni lazima nisisalimu amri. Kusalimu amri kwangu kungekuwa sawa na kufanya masikilizano na Shetani, na ni sawa na kujiangamiza. Kusalimu amri juu ya shauku na azimio langu kutakuwa sawa na kumsaliti Mungu. "Hii ni aina ya moyo ambao ni lazima uwe nao. Suala lolote dogo unalokabiliana nalo ni pumziko dogo katika mfanyiko tendani wa kufanya maendeleo katika maisha, na ni sharti usiruhusu lizuie kwendelea kwako au kuzuia mwelekeo wako wa mbele. Ni vyema kwako kuchukua pumziko dogo au upumzike kwa muda, lakini mwelekeo wako haupaswi kubadilika, na ni lazima usikome kabisa kwa hali yoyote; hii ndiyo aina ya azimio na uamuzi unayopaswa kuwa nayo. Bila kujali wengine wanavyosema au jinsi walivyo, na bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, azimio lako halipaswi kubadilika. Mungu asema, "Sikutaki tena," nawe unasema, "Mungu hanitaki tena, kwa hivyo nitasahau tu kulihusu." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Au Mungu asema, "Wewe umepotoka sana, na Ninakuchukia," nawe unasema, "Mungu ananichukia, nitaishi kwa sababu gani tena? Nitatafuta kamba ili kujinyonga." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Hutafanikisha lengo lako jinsi hii. Kwa mintarafu ya hadhi yenu ya sasa, hakuna hata mmoja wenu ambaye ameweza kujaribiwa na Mungu bado, na kusema, "Mungu, tafadhali nijaribu." Huna hadhi hii. Je, mna uwezo wa kufanya nini tu? Ni lazima muombe: "Ee Mungu, tafadhali niongoze, nipe nuru, nipe bidii ya kuendelea na unipe bidii ili niweze kuitembea njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa mujibu wa shauku zangu. Bila kujali namna gani ya mateso ninayoyapitia, Wewe hunipa nguvu na Wewe hunilinda. Ingawa ninaweza kuwa dhaifu na ingawa kimo changu ni kichanga, ninakuomba Unipe nguvu, kunilinda na kunionyesha wema. Sitasalimu amri." Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba, na ni lazima daima mje mbele ya Mungu kuomba. Wakati wengine wanacheka na kufanya mzaha na kujiendekeza, ombea hili; wakati wengine wanapojifurahisha, ombea hili; wakati wengine ni hasi, ombea hili; wakati wengine wanalala fofofo, au kuchelewa kuamka, wewe tayari unaliombea hili; wakati wengine wanatembea njia ya ulimwengu na kwa ulafi kufurahia anasa za kimwili, au kufuata mienendo ya kidunia, ombea hili. Wakati unapoweza kuishi mbele ya Mungu katika mambo yote na unaweza kujiweka katika mipaka fulani, wakati unapoweza kujiweka ukiishi mbele ya Mungu na kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi Mungu anaweza kuliona hili. Wakati Mungu anapouona moyo wa mtu, Yeye hayatumii tu macho Yake; Yeye hupanga mazingira kwa ajili yako na Yeye hugusa moyo wako kwa mikono Yake. Kwa nini Nasema hili? Wakati Mungu anapokupangia mazingira, Yeye hutazama kuona kama moyo wako unachafuliwa nayo, unayachukia, unayapenda au ni mtiifu, au kama husubiri kwa utulivu, au hutafuta ukweli—Yeye huona jinsi moyo wako unavyobadilika na ni katika mwelekeo gani huenda. Mabadiliko katika moyo wako, kila badiliko la fikira na mawazo ndani ya moyo wako kuhusu watu, hoja, na mambo ambayo Mungu hupanga kwa ajili yenu, na kila badiliko ya hali ya moyo uliyo nayo—Mungu anaweza kuyahisi yote. Ingawa huenda hujamwambia yeyote na huenda hujaomba, badala yake kufikiria tu mawazo haya kwa moyo wako mwenyewe au katika ulimwengu wako mwenyewe, lakini kwa Mungu ni wazi kabisa na Yeye huliona wazi kwa tazamo moja. Watu hutumia macho yao kukuona, na Mungu hutumia moyo Wake kuugusa moyo wako—Yeye yu karibu hivi nawe. Na kama unaweza kuuhisi uchunguzi wa Mungu, basi unaishi mbele ya Mungu. Kama huwezi kuuhisi kabisa na unaishi ndani ya ulimwengu wako, basi uko katika shida. Wewe huishi mbele ya Mungu, wewe uko mbali na Mungu na mbali sana kutoka Kwake, huendi karibu Yake kwa moyo wako au moyo wako uukaribie moyo Wake, na hukubali uchunguzi wa Mungu. Na Mungu anajua hili! Mungu anaweza kabisa kuhisi yote haya. Kwa hivyo, wakati una azimio na lengo la kukamilishwa na Mungu, kuwa mtu anayetekeleza mapenzi ya Mungu, mtu anayemcha Mungu na aepukanaye na maovu, unapoweza kuomba mara nyingi juu ya hoja hii na kusihi kwa ajili yalo, unapoweza kuishi mbele ya Mungu, kutokwenda mbali na Mungu au kumwacha Mungu, basi wewe unalielewa hili, na Mungu anajua kuhusu hilo pia. Watu wengine wanasema: "Mimi ni dhahiri kulihusu, lakini sijui kama Mungu anajua kulihusu." Hili si jambo la busara. Kwa hiyo hali ni gani hapa? Kama wewe mwenyewe u dhahiri kulihusu, na hujui kama Mungu anajua kulihusu, basi huna uhusiano na Mungu. Umeelewa? Kwa nini Nasema wewe huna uhusiano na Mungu? Wewe huishi mbele ya Mungu, kwa hivyo unashindwa kuhisi kama Mungu yu pamoja nawe, kama Mungu anakuongoza au kukulinda, na kama Mungu anakushutumu wakati unapofanya jambo baya. Huwezi kuhisi jambo lolote kati ya haya, kwa hiyo hili linamaanisha kwamba huishi mbele ya Mungu. Wewe hufikiria tu mwenyewe na kuleweshwa na mawazo yako mwenyewe; huko ni kuishi katika ulimwengu wako mwenyewe na sio kuishi mbele ya Mungu, na hakuna uhusiano kati yako na Mungu.
Mtu anawezaje kuudumisha uhusiano wake na Mungu? Ni kwa njia gani anaweza kuudumisha? Kwa njia ya kusihi, kuomba na kuwa na ushirikiano na Mungu katika moyo wake. Aina hii ya uhusiano itakuwezesha kuishi daima mbele ya Mungu, na kwa hiyo utakuwa mtu mwenye amani sana. Watu wengine daima hufanya mambo ya nje na hujihusisha na mashauri ya nje. Baada ya siku moja au mbili bila kushiriki katika maisha ya kiroho, moyo wao hauna utambuzi, na baada ya siku tatu, au siku tano, bado hauna utambuzi, au bado hauna utambuzi baada ya mwezi mmoja au miwili. Hili lina maana kwamba hawaombi au kurairai chochote, na hawajishughulishi na ushirikiano wa kiroho. Kusihi ni wakati unapokabiliwa na masuala, unamwomba Mungu akusaidie, akuongoze, akukimu, akupe nuru, akuruhusu ujue mapenzi ya Mungu na kujua ukweli ni nini. Kuomba kuna mawanda mapana kiasi. Wakati mwingine ni kusema maneno ndani ya moyo wako, kuzungumza na Mungu wakati unapokabiliwa na shida na kusema maneno yaliyo moyoni mwako kwa Mungu wakati unapokuwa hasi na dhaifu. Unaweza pia kumwomba Mungu unapokuwa mwasi, au unasema na Mungu juu ya masuala yanayokukabili kila siku, yote kuhusu yale ambayo unaweza kuyabaini na yale ambayo huwezi kuyabaini. Huku ni kuomba. Mawanda ya kuomba kimsingi ni kuwa na mazungumzo na Mungu, wakati mwingine kwa nyakati zilizopangwa na wakati mwingine kwa nyakati zisizoratibiwa, na yanaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Ushirikiano wa kiroho kwa kweli haushikilii muundo fulani. Labda kuna suala, labda hakuna; wakati mwingine kutakuwa na kitu cha kusema, na wakati mwingine hakutakuwa. Huu ni ushirikiano wa kiroho. Wakati kuna suala maalum la kuzungumzia na Mungu, basi unaweza kuomba. Wakati hakuna suala lolote, unafikiri tu juu ya Mungu, "Mungu humpendaje mwanadamu? Mungu anamtunzaje mwanadamu? Mungu humshutumuje mwanadamu?" "Ee Mungu, ninahisi nimefanya jambo hili vibaya. Kama kwa kweli nimefanya jambo hili vibaya, basi nishutumu na unifanye nifahamu." Huu ni ushirika wa kiroho, na unaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Wakati mwingine uko barabarani na unafikiria kuhusu kitu ambacho huufanya moyo wako uhisi huzuni kweli. Huna haja ya kupiga magoti au kuyafunga macho yako, lakini badala yake unasema mara moja kwa Mungu moyoni mwako: "Ee Mungu, naomba Uniongoze na suala hili. Mimi ni dhaifu na siwezi kulishinda. "Moyo wako umesisimuliwa, na kwa maneno haya machache rahisi Mungu anajua yote kulihusu. Wakati mwingine unafikiria kuhusu familia yako, na unaweza kusema: "Ee Mungu, kwa kweli nimeikosa familia yangu …." Humkosi mtu yeyote hasa, unahisi tu vibaya, hivyo unaongea na Mungu. Usizungumze na watu wengine kulihusu, kwa kuwa hilo halina maana. Unapozungumza na mtu mwingine kulihusu, huenda ikawa kwamba anaikosa familia yake hata zaidi ya wewe, basi hili linakuathiri na unaishia kuikosa yako hata zaidi, na hili halikuletei faida yoyote kamwe. Unapozungumza na Mungu kulihusu, basi Mungu atakufariji, Akufurahishe tena na kukupisha katika wakati huu mgumu na kupita hali hii ndogo. Hali hii, jiwe hili dogo njiani mwako halitakukwaa, halitakuzuia au kuathiri utekelezaji wa wajibu wako. Wakati mwingine, unapozungumza au kufanya ushirika na wengine, moyo wako unaweza ghafla kuwa na hisia ya kuvunjika kidogo au kujisikia mwenye wasiwasi sana, hivyo unafanya haraka kumwomba Mungu, na unaweza kufanya hivi wakati wowote na katika mahali popote. Kunaweza kuwa hakuna chochote unachokisihi, au chochote unachotaka Mungu akufanyie au akunurishie, unaongea tu na Mungu na kuzungumza Naye wakati wowote na katika mahali popote. Ni hisia gani unayopaswa uwe nayo wakati wote? Ni hii: Mungu huwa hatoki kandoni mwangu kamwe, Yeye yu pamoja nami kandoni mwangu wakati wote, Yeye hajawahi kuniacha, na ninaweza kuhisi hili. Bila kujali ni mahali gani nipo, bila kujali ninafanya nini, kama ninapumzika au kulala, kula chakula, au kwa mkutano, au kama sisemi chochote mchana kutwa ninapotekeleza wajibu wangu, najua moyoni mwangu kwamba Mungu ananiongoza kwa mkono, na kwamba Yeye hajawahi kuniacha. Wakati mwingine, wewe hufikiria jinsi umefaulu kwa miaka hii michache iliyopita, mwezi baada ya mwezi, na unahisi moyoni mwako kwamba kimo chako kimekomaa na kwamba ni Mungu anayekuongoza, na kwamba ni upendo wa Mungu ambao unakulinda daima. Unapofikiri hivi, unaomba moyoni mwako: "Nakushukuru Wewe, Mungu!" Na wewe unatoa shukrani zako, na kusema: "Mimi ni dhaifu sana, mwenye woga sana, na mpotovu kwa kina sana. Kama Hukuniongoza kwa njia hii, mimi mwenyewe singeweza kufanikiwa hadi leo. Asante Mungu!" Je, si huu ni ushirika wa kiroho? Kama ungekuwa jinsi hii, basi si ungekuwa na mengi ya kumwambia Mungu? Hungeishi siku baada ya siku bila kuwa na kitu cha kumwambia Mungu. Ikiwa huna chochote cha kumwambia Mungu, basi inamaanisha kwamba Mungu hayuko ndani ya moyo wako. Kama una Mungu ndani ya moyo wako, basi unaweza kumwambia Mungu mambo unayoweza kusema kwa wandani wako—Mungu ni msiri wako wa karibu zaidi. Unapomruhusu Mungu kuwa msiri wako wa karibu zaidi, rafiki yako wa karibu zaidi, familia unayoweza kuitegemea zaidi, kuiegemea zaidi, na Aliye mwaminifu zaidi, Aliye mwandani sana na wa karibu, basi itakuwa vigumu kutokuwa na mambo ya kusema Kwake. Wakati daima una mambo ya kumwambia Mungu, si basi utaweza kuishi daima mbele ya Mungu? Unapoweza kuishi mbele ya Mungu daima, basi wakati wote utaweza kutambua jinsi Mungu anavyokuongoza, jinsi Mungu anavyokulinda, jinsi Anavyokutunza, jinsi Anavyokuwa amani yako na furaha, Anavyokupa baraka na nuru, jinsi Mungu anavyokushutumu, kukufundisha nidhamu, kukuadhibu, kukuhukumu na kukuadibu. Wakati unapoishi mbele ya Mungu daima, moyo wako utajua kwa dhahiri sana kile Mungu anachofanya ndani yako. Hutakuwa na siku ambapo utakuwa mpumbavu kabisa na kutojua chochote, ukisema tu maneno "Ninamwamini Mungu, mimi hutekeleza wajibu wangu, mimi huhudhuria mikutano, mimi husoma kila siku na huomba kila siku." Huwezi tu kupitia mifanyiko tendani hii yote au kuwa tu na aina hii ya tabia ya nje.
Mnapaswa kujua sasa, kwa hiyo ni nini kitu muhimu zaidi katika kumwamini Mungu? Unapomwamini Mungu, kama Mungu hayuko ndani ya moyo wako na Yeye hakuhusu, na kama humwoni Mungu kama mwandani wako sana, wako wa karibu sana, familia na msiri mwaminifu sana na wa kutegemewa sana, basi Mungu si Mungu wako. Sawa, kwa hiyo sasa nendeni na mtende kwa muda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema, na muone kama hali yenu ya ndani itabadilika au la. Tenda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema na hakika utaishi mbele ya Mungu, utaishi katika tabia ya kawaida na kuwa katika hali ya kawaida. Wakati hali ya mtu ni ya kawaida, ni hapo tu ambapo mambo anayoyaonyesha na kuyafichua kwa kila hatua, au miongoni mwa watu tofauti, masuala, na mambo, au katika mazingira tofauti, yatakuwa ya kawaida. Ni kwa njia hii tu ambapo maisha yake yanaweza kukomaa na anaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli kidogo kidogo. Unaelewa? (Ndiyo.)
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?