Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumamosi, 8 Juni 2019

Lazima Mjue Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

2. Lazima Mjue Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu.

Maneno Husika ya Mungu:
Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu. …
…………
… Wakati ambapo usimamizi mzima wa Mungu utakaribia kufika mwisho, Mungu ataweka vitu vyote kulingana na aina. Mwanadamu aliumbwa kwa mikono ya Muumba, na mwishowe lazima kabisa amrudishe mwanadamu chini ya utawala Wake; huu ndio mwisho wa hatua tatu za kazi. …
… Hatua tatu za kazi zitakapofikia tamati, patafanyika kundi la watu wanaomshuhudia Mungu, kundi la wale wanaomjua Mungu. Watu hawa wote watamjua Mungu na wataweza kuonyesha ukweli kwa matendo. Watakuwa na utu na hisia, na wote watajua hatua tatu za kazi ya wokovu ya Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo itatekelezwa mwishowe, na watu hawa ndio dhihirisho la kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi, na ndio ushuhuda wenye nguvu zaidi kwa kushindwa kwa Shetani.
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufunua ubovu wa Shetani. Aidha, ni kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kufanya tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, ukuu na udogo, wazi kama mchana. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wanaweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Muumba—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Naweza kuwapa mambo kwa ajili ya raha; na wapate kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na kwamba Shetani ni mmoja tu wa viumbe Vyangu, ambaye baadaye alinigeuka.
kutoka kwa "Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu wa usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha kazi yote ya Mungu ya usimamizi, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, ambayo ni kusema kuwa mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kuwa katika mateka ya Shetani. Shetani anashindwa kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye amechukuliwa mateka, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu ameachiliwa kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, baada ya kuwa kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.
kutoka kwa "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Huu ni mfano wa usimamizi wa Mungu: kuwakabidhi wanadamu kwa Shetani—wanadamu ambao hawajui kile Mungu Alicho, Muumba ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na ni kwa nini inafaa kujitoa kwa Mungu—na kutoa utawala huru kwa uovu wa Shetani. Hatua baada ya hatua, Mungu Anamtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani, hadi mwanadamu amwabudu Mungu kikamilifu na kumkataa Shetani. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Hili linasikika kama hadithi ya visasili na hii ni kwa sababu hawana fununu kuhusu yaliyomtokea mwanadamu katika maelfu ya miaka iliyopita, hata hawajui ni hadithi ngapi ambazo zimetokea katika huu ulimwengu. Na zaidi ya hayo, hii ni kwa sababu hawawezi kufahamu kinachostaajabisha sana, dunia inayoibua hofu zaidi ambayo iko zaidi ya dunia yakinifu, lakini ambayo macho yao ya mwili yanawazuia kuiona. Inasikika ya kutofahamika kwa mwanadamu. Na hii ni kwa sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Hujua kisichopendeza na jinsi kinavyotofautiana na kile kilicho kitakatifu, na hutambua ukubwa wa Mungu na uovu wa Shetani. Wanadamu kama hawa hawatamfanyia Shetani kazi tena, au kumwabudu Shetani, au kumsetiri Shetani. Hii ni kwa sababu wao ni kikundi cha watu ambao wamemilikiwa na Mungu. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuwasimamia wanadamu. …
…………
Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado Anafanya Kazi bila kuchoka na Anapania kuikamilisha. Haijalishi ni kwa kiasi gani watu wanaelewa usimamizi wa Mungu, manufaa na usaidizi wa Kazi inayofanywa na Mungu unaweza kukubalika na kila mtu. Labda, leo, hujahisi upendo wowote au maisha yaliyowezeshwa na Mungu, lakini bora tu humwachi Mungu, na hupotezi matumaini yako ya kutafuta ukweli, basi kutakuwa na siku ambapo tabasamu la Mungu litafichuliwa kwako. Kwa kuwa dhumuni la kazi ya usimamizi wa Mungu ni kuwatoa wanadamu anayemilikiwa na Shetani, sio kuwaacha wanadamu waliopotoshwa na Shetani na kumpinga Mungu
kutoka kwa "Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote, Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Uangamizi wa mwisho wa wale wana wa kutotii pia utafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani. Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani utatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.
kutoka kwa "Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati mwanadamu ataingia kwenye hatima ya milele, mwanadamu atamwabudu Muumba, na kwa sababu mwanadamu amepata wokovu na kuingia ahera, mwanadamu hawezi kimbiza malengo yoyote, wala, zaidi ya hayo, yeye hatakuwa na haja ya kuhangaika kuwa atazingirwa na Shetani. Kwa wakati huu, mwanadamu atajua nafasi yake, na atatekeleza wajibu wake, na hata kama hataadibiwa au kuhukumiwa, kila mtu atatekeleza jukumu lake. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa kiumbe katika sura na hadhi pia. Hakutakuwepo tena na tofauti ya juu na chini; kila mtu atatekeleza tu kazi tofauti. Bado mwanadamu ataishi katika hatima ya wanadamu yenye utaratibu na ifaayo, mwanadamu atatekeleza wajibu wake kwa ajili ya kumwabudu Muumba, na wanadamu kama hawa ni wanadamu wa milele. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa amepata maisha yaliangaziwa na Mungu, maisha chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, na maisha pamoja na Mungu. Wanadamu wataishi maisha ya kawaida duniani, na wanadamu wote wataingia katika njia sahihi. Mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 utakuwa umemshinda shetani kabisa, ambayo ina maana kuwa Mungu atakuwa amerejesha sura ya awali ya mwanadamu kufuatia kuumbwa kwake, na kwa hivyo, nia ya awali ya Mungu itakuwa imetimizwa.
kutoka kwa "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ulikuwa hata umeshaamuliwa kabla zaidi Nilipoiumba dunia. Watu hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho, na pia hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini Nilikuwa Nimeshamwambia adui Yangu lilipokuwa linapambana na Mimi kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kwa muda mrefu walikuwa watoto wa Shetani, na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake. … Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa akitenda kwa mfano wa Shetani—hata kuwa na mwili wake. Wao ni ushahidi wa kuwa shahidi wa Shetani, wa uwazi. Aina hii ya Mwanadamu, uchafu kama huu, au watoto wa familia hii ya binadamu potovu, ni jinsi gani wangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Shahidi Wangu yuko wapi? Adui ambaye anasimama dhidi Yangu na kuwapotosha wanadamu tayari amewachafua wanadamu, viumbe Wangu, waliojawa na utukufu Wangu na wanaoishi kulingana na Mimi. Ameiba utukufu Wangu, na kujaza binadamu na sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. … Nami Nitauchukua tena utukufu Wangu, ushuhuda Wangu miongoni mwa wanadamu na vyote vilivyokuwa mali Yangu, Niliyokuwa Nimewapa wanadamu hapo zamani—na kumshinda mwanadamu kikamilifu. Hata hivyo unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hapo awali hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na sumu yake. Hivyo, Naliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kilichoumbwa na mkono Wangu, Wapendwa Wangu walio watakatifu ambao kamwe hawajawahi kumilikiwa na mwingine yoyote. Aidha, Mimi nitakuwa na furaha nao, na kuwaona kama utukufu Wangu. Hata hivyo, Ninachotaka sio mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ni wa Shetani leo, ambaye si kiumbe Changu tena. Kwa sababu Ninataka kuchukua tena utukufu Wangu katika dunia ya wanadamu, Nitashinda kikamilifu manusura waliobaki kwa wanadamu, kama ushahidi wa utukufu Wangu katika ushindi Wangu dhidi ya Shetani. Mimi huchukua tu ushahidi Wangu kama udhihirisho wa nafsi Yangu, kama kitu cha starehe Yangu. Hii ndiyo nia Yangu.
kutoka kwa "Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Baada ya kutekeleza kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua vitendo Vyake vingi, kimsingi kumshinda Shetani na kuwaokoa binadamu wote. Anatumia fursa hii kuruhusu kila kitu mbinguni, kila kitu kilicho duniani, kila kitu kinachopatikana baharini pamoja na kila kifaa cha mwisho ambacho Mungu aliumba ulimwenguni kuweza kuona uweza wa Mungu na kushuhudia vitendo vyote vya Mungu. Huchukua fursa ya kumshinda Shetani ili kufichua vitendo Vyake kwa binadamu na kuwaruhusu watu kuweza kumsifu Yeye na kuitukuza hekima Yake kwa kumshinda Shetani. Kila kitu nchini, mbinguni na ndani ya bahari humletea utukufu, huusifu uweza Wake, kinasifu vitendo Vyake vyote na kutamka kwa sauti jina Lake takatifu. Hii ni ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani; hii ni ithibati ya Yeye kumshinda Shetani; na la muhimu zaidi, ni ithibati ya wokovu Wake kwa binadamu. Uumbaji wote wa Mungu humletea utukufu, humsifu Yeye kwa kumshinda adui Wake na kurudi kwa ushindi na humsifu Yeye kama Mfalme mkubwa mwenye ushindi. Kusudio lake si kumshinda Shetani tu, na hivyo basi kazi Yake imeendelea kwa miaka 6,000. Anatumia kushindwa kwa Shetani kuwaokoa binadamu; Anakutumia kushindwa kwa Shetani kufichua vitendo Vyake vyote na kufichua utukufu Wake wote. Atapata utukufu, na umati wote wa malaika utaweza pia kushuhudia utukufu Wake wote. Wajumbe walio mbinguni, wanadamu walio nchini na uumbaji wote ulio nchini utauona utukufu wa Muumba. Hii ndiyo kazi Aifanyayo. Viumbe vyake kule mbinguni na nchini wote utauona utukufu Wake, na atarudi kwa vifijo na nderemo baada ya kumshinda Shetani kabisa na kuruhusu binadamu kumsifu Yeye. Ataweza hivyo basi kutimiza kwa ufanisi vipengele hivi viwili. Mwishowe binadamu wote watashindwa na Yeye, na atamwondoa yeyote yule anayepinga au kuasi, hivi ni kusema, Atawaondoa wale wote wanaomilikiwa na Shetani.
kutoka kwa "Wafaa Kujua Namna Ambavyo Ubinadamu Wote Umeendelea Hadi Siku ya Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwanadamu ni bwana wa vitu vyote, lakini wote ambao wamepatwa watakuwa matunda ya vita dhidi ya Shetani. Shetani ndiye mpotoshaji wa vitu vyote, na ndiye mshindwa katika mwisho wa vita vyote, na pia ndiye atakayeadhibiwa kufuatia vita hivi. Miongoni mwa Mungu, mwanadamu na Shetani, ni Shetani pekee ndiye atachukiwa na kukataliwa. Wale waliopatwa na Shetani lakini hawarejeshwi na Mungu, wakati huo huo, watakuwa wale ambao watapokea adhabu kwa niaba ya Shetani. Kati ya hawa watatu, Mungu pekee ndiye anapaswa kuabudiwa na vitu vyote. Wale waliopotoshwa na Shetani lakini wanarejeshwa na Mungu na wale wanaofuata njia ya Mungu, wakati huo huo, wanakuwa wale ambao watapokea ahadi ya Mungu na kuhukumu wale waovu kwa niaba ya Mungu. Bila shaka Mungu atakuwa mshindi na Shetani bila shaka atashindwa, lakini miongoni mwa wanadamu kuna wale watakaoshinda na wale watakaoshindwa. Wale ambao watashinda ni wale wa Mshindi na wale ambao watashindwa ni wale wa mshindwa; huu ni uainishaji wa kila mmoja kufuatana na aina, na ni matokeo ya mwisho ya kazi yote ya Mungu, na pia ni lengo la kazi yote ya Mungu, na kamwe haitabadilika. Msingi wa kazi kuu wa mpango wa usimamizi wa Mungu unalenga wokovu wa mwanadamu, na Mungu anakuwa mwili kimsingi kwa ajili ya msingi huu, kwa ajili ya kazi hii, na ili kumshinda Shetani.
kutoka kwa "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama watu, wanaotembea na Mimi hadi leo, hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na ningali nafanya hivyo sasa. Ingawaje kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio lake linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawaje nimejazwa na hukumu na adabu kwake binadamu, bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, ili niweze kueneza kwa njia bora zaidi injili Yangu na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili. Kwa hiyo sasa, kwa wakati ambapo watu wengi tayari wametamauka pakubwa, ninaendelea na kazi Yangu, nikiendeleza kazi ambayo lazima nifanye ili kuhukumu na kuadibu binadamu. Licha ya ukweli kwamba binadamu amechoshwa na kile ninachosema na licha ya ukweli kwamba hana tamanio la kujali kuhusu kazi Yangu, ningali natekeleza wajibu Wangu kwa sababu kusudio la kazi Yangu halijabadilika na mpango Wangu asilia hautabadilika. Kazi ya hukumu Yangu ni kumfanya binadamu kunitii Mimi kwa njia bora zaidi, na kazi ya adabu Yangu ni kuruhusu binadamu kuwa na mabadiliko bora zaidi. Ingawaje kile ninachofanya ni kwa minajili ya usimamizi Wangu, sijawahi kufanya chochote ambacho hakikufaidi binadamu. Hiyo ndiyo maana ninataka kufanya mataifa yote nje ya Israeli kuwa matiifu tu kama Waisraeli na kuwabadilisha kuwa binadamu halisi, ili niwe na mahali pa usalama katika nchi zilizo nje ya Israeli. Huu ndio usimamizi Wangu; ndiyo kazi ninayotimiza katika nchi za Mataifa. Hata sasa, watu wengi bado hawauelewi usimamizi Wangu kwa sababu hawajautilia maanani, badala yake wanafikiria tu kuhusu mustakabali na hatima yao. Haijalishi ni nini ninachosema, watu hawajali kazi Yangu, badala yake wanalenga tu hatima zao za baadaye. Kwa hiyo kama hilo litaendelea, kazi Yangu itapanuliwa vipi? Injili Yangu itaenezwa vipi kotekote ulimwenguni? Lazima mjue kwamba wakati kazi Yangu inapanuka, nitawatawanya, Nitawaadhibu kama vile tu Yehova alivyoyaadhibu makabila ya Israeli. Haya yote yatafanywa ili injili Yangu iweze kuongezeka kotekote kwenye ulimwengu mzima, ili kazi Yangu iweze kuenezwa kwa Mataifa. Kwa hiyo, jina Langu litasifiwa na watu wazima na watoto kwa pamoja na jina Langu takatifu litatukuzwa kwa vinywa vya watu kutoka makabila na mataifa yote. Katika enzi ya mwisho, Nitafanya jina Langu litukuzwe miongoni mwa Mataifa, kufanya matendo Yangu kuonekana na mataifa mengine ili waniite Mwenyezi, na kuyafanya maneno Yangu kutimika karibuni. Nitawafanya watu wote kujua kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote kuona kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya kutimizwa tu katika siku za mwisho.
kutoka kwa "Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia" katika Neno Laonekana katika Mwili

Ijumaa, 7 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”

Mwenyezi Mungu anasema, “Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu.” “Kila siku Naona vitendo vyote vya watu wengi, na kila siku Nachunguza mioyo na akili za watu wengi; hakuna aliyewahi kutoroka hukumu Yangu, na hakuna aliyewahi kuachana na uhalisi wa hukumu Yangu.”
Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu. Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani? Wakati Wanangu na watu Wangu wanarudi katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Ambayo ni kusema, Nianzapo binafsi kazi Yangu duniani, na wakati enzi ya hukumu inakaribia tamati yake, Naanza kuelekeza maneno Yangu kwa ulimwengu mzima, na kutoa sauti ya Roho Wangu kwa dunia nzima. Kupitia maneno Yangu, Nitasafisha wanadamu na mambo yote miongoni mwa yote yaliyo mbinguni na duniani, ili nchi si chafu na fisadi tena, lakini ni ufalme takatifu. Nitatengeneza upya mambo yote, ili yatolewe kwa matumizi Yangu, na yasiwe na pumzi ya dunia tena, na yasichafuliwe na ladha ya ardhi tena. Duniani, mwanadamu ametafuta malengo na asili ya maneno Yangu, na amechunguza matendo Yangu, lakini bado hakuna aliyewahi kujua kwa kweli asili ya maneno Yangu, na hakuna aliyewahi kuona kwa kweli matendo Yangu ya ajabu. Ni leo tu, Nikujapo binafsi miongoni mwa wanadamu na kuongea maneno Yangu, ndipo mwanadamu anapata maarifa kidogo kunihusu, kutoa nafasi “Yangu” ndani ya mawazo yao, badala yake kutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya fahamu zake. Mwanadamu ana dhana na amejawa na udadisi; ni nani ambaye hangetaka kumwona Mungu? Ni nani ambaye hangetamani kukutana na Mungu? Lakini bado kitu pekee kilicho na nafasi ya uhakika ndani ya moyo wa mwanadamu ni Mungu ambaye mwanadamu anahisi kuwa dhahania na asiye dhahiri. Nani angetambua haya kama Singewaeleza wazi? Nani angeamini kwa kweli Mimi nipo? Kwa hakika bila shaka yoyote? Kuna tofauti kubwa kati ya “Mimi” aliye ndani ya mwanadamu na “Mimi” wa ukweli, na hakuna anayeweza kuwalinganisha. Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi Nijua, na hata angekuja kunijua, je, maarifa kama hayo bado hayangekuwa dhana? Kila siku Natembea miongoni mwa watu wengi, na kila siku Nafanya kazi ndani ya kila mtu. Wakati mwanadamu kweli ananiona, ataweza kunijua kwa maneno Yangu, na kuelewa njia Ninazotumia kuzungumza na pia nia Zangu.
Ufalme ufikapo rasmi duniani, ni nini, kati ya mambo yote, sio kimya? Nani, kati ya watu wote, hana hofu? Natembea kila mahali katika ulimwengu dunia wote, na kila kitu kinapangwa na Mimi binafsi. Wakati huu, nani asiyejua vitendo Vyangu ni vya ajabu? Mikono Yangu inashikilia mambo yote, lakini bado Niko juu ya mambo yote. Leo, si kupata mwili Kwangu na kuwepo Kwangu binafsi miongoni mwa wanadamu maana ya ukweli ya unyenyekevu na kujificha Kwangu? Kwa nje, watu wengi wananipongeza kama mzuri, wananisifu kama mzuri, lakini ni nani anayenijua kweli? Leo, mbona Nauliza kuwa mnijue? Lengo Langu sio kuaibisha joka kubwa jekundu? Sitaki kumlazimisha mwanadamu kunisifu, lakini kumfanya anijue kupitia hapo atakuja kunipenda, na hivyo kunisifu. Sifa kama hiyo inastahili jina lake, na si mazungumzo yasiyokuwepo; ni sifa tu kama hii inaweza kufikia kiti Changu cha enzi na kupaa angani. Kwa sababu mwanadamu amejaribiwa na kupotoshwa na Shetani, kwa sababu amechukuliwa na kufikiria kwa dhana, Nimekuwa mwili ili kuwashinda binafsi wanadamu wote, kufichua dhana zote za mwanadamu, na kupasua mawazo ya mwanadamu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu hajionyeshi mbele Yangu tena, na hanitumikii tena akitumia dhana zake mwenyewe, na hivyo, “Mimi” katika dhana za mwanadamu ameondoka kabisa. Ufalme ufikapo, Naanza kwanza hatua hii ya kazi, na Nafanya hivyo miongoni mwa watu Wangu. Sababu nyinyi ni watu Wangu waliozaliwa kwa nchi ya joka kubwa jekundu, kwa hakika hakuna tu hata kidogo, ama kipimo cha sumu ya joka kubwa jekundu ndani yenu. Hivyo, hatua hii ya kazi Yangu hasa inawaangazia, na hiki ni kipengele kimoja cha umuhimu wa kupata mwili Kwangu Uchina. Watu wengi hawawezi kuelewa hata chembe cha maneno Ninayoyasema, na wanapoweza, uelewa wao ni wenye ukungu na ovyo. Hii ni mojawapo ya sehemu muhimu ya mbinu Ninayozungumzia. Iwapo watu wote wangeweza kusoma maneno Yangu na kuelewa maana yao, basi nani miongoni mwa wanadamu angeweza okolewa, na kutupwa kuzimu? Mwanadamu anijuapo na kunitii ndio wakati Nitakapopumzika, na itakuwa wakati hasa ambapo mwanadamu ataweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Leo, kimo chenu ni kidogo sana, karibu kiwe kiwango cha kusikitisha, na hakistahili hata kuinuliwa—sembuse ujuzi wenu kunihusu.

Alhamisi, 6 Juni 2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba vitu vyote kuhusiana, kupatana na kutegemeana. Alitumia njia hii na kanuni hizi kudumisha kuendelea kuishi na uwepo wa vitu vyote na kwa njia hii binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili. Kama kusingekuwa na udhibiti na ukuu wa Mungu, hakuna mwanadamu ambaye angeweza kudumisha na kuweka wiano katika mazingira, hata kama yaliumbwa na Mungu kwanza.”
Mungu anamwacha mwanadamu kusimamia vitu vyote na kuwa na utawala juu yao, lakini mwanadamu anafanya kazi nzuri? (Hapana.) Ni kwa jinsi gani mwanadamu anafanya kazi mbaya? Mwanadamu ana tabia ya uharibifu; mwanadamu sio kwamba tu hawezi kutunza vitu kama Mungu alivyoviumba, kwa kweli ameviharibu. Binadamu ameifanya milima kuwa vifusi, ameijaza bahari kwa mchanga, na amezibadilisha tambarare kuwa majangwa ambapo hakuna kinachoweza kuishi. Halafu katika majangwa hayo mwanadamu amejenga viwanda na kujenga vinu vya nyuklia na uharibifu unaendelea katika pande zote. Mito si mito tena, bahari si bahari tena.... Binadamu anapovunja uwiano na kanuni za maumbile, siku yao ya maafa na kifo haipo mbali na haiepukiki. Maafa yanapokuja, watajua viumbe vya Mungu ni vya thamani kiasi gani jinsi vyote ni muhimu kwa binadamu. Mwanadamu kuishi katika mazingira yenye hali ya hewa nzuri ni sawa na kuwa peponi. Watu hawatambui baraka hii, lakini wakati ambapo wataipoteza yote ndipo watatambua ni jinsi gani yote ni adimu na ya thamani. Ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuirudisha hii yote? Watu wangefanyaje ikiwa Mungu Asingekuwa tayari kuitengeneza tena? Mngefanyaje? (Tusingeweza kufanya chochote.) Kwa kweli, kuna kitu mnachoweza kufanya na ni rahisi sana na Nitakapowaambia ni nini, mara moja mtajua kwamba hiyo inawezekana. Kwa nini mwanadamu amejikuta katika mashaka yake ya kimazingira ya sasa? Je, ni kwa sababu ya tamaa na uharibifu wa mwanadamu? Ikiwa mwanadamu atasitisha uharibifu huu, je, mazingira ya kuishi hayatakuwa sawa taratibu yenyewe? Ikiwa Mungu hafanyi chochote, ikiwa Mungu hatamani tena kufanya kitu chochote kwa ajili ya binadamu—yaani, hataki kuingilia—njia bora zaidi ingekuwa ni binadamu kusitisha uharibifu huu na kurudisha vitu kuwa vile vilivyokuwa. Kusitisha uharibifu huu wote humaanisha kusitisha uporaji na uharibifu wa vitu ambavyo Mungu ameviumba. Hii itaruhusu mazingira ambamo mwanadamu anaishi kuboreka taratibu. Kushindwa kufanya hivyo kutasababisha uharibifu zaidi wa mazingira na hali itakuwa mbaya zaidi. Je, mbinu Yangu ni rahisi? (Ndiyo, ni rahisi.) Ni rahisi na inawezekana, siyo? Ni rahisi kweli, na inawezekana kwa baadhi ya watu, lakini je, hii inawezekana kwa watu walio wengi duniani? (Haiwezekani.) Kwenu nyinyi, angalau inawezekana? (Ndiyo.) Chanzo cha “ndiyo” yenu ni nini? Je, mtu anaweza kusema kuwa inahusisha kuanzisha msingi wa uelewa kuhusu matendo ya Mungu? Je, mtu anaweza kusema inahusisha kushikilia kanuni na mpango wa Mungu? (Ndiyo.) Kuna njia ya kubadilisha haya yote, lakini hiyo siyo mada tunayoijadili sasa. Mungu anawajibika kwa kila uhai wa binadamu na anawajibika hadi mwisho. Mungu Anawakimu, hata kama umeugua kutokana na mazingira yaliyoharibiwa na Shetani, au kuathiriwa na uchafuzi au kupata madhara mengine, haijalishi; Mungu Anakukimu na Atakuacha uendelee kuishi. Je, una imani katika hili? (Ndiyo.) Mungu hachukulii upotevu wa maisha ya binadamu kwa urahisi.
Mmehisi umuhimu wa kumtambua Mungu kama chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo, tumehisi.) Mna hisia gani? Endelea, nitasikiliza. (Hapo awali, hatukufikiria kamwe kuhusisha milima, bahari na maziwa na matendo ya Mungu. Leo, kupitia ushirika wa Mungu, sasa tunaelewa kwamba haya yote siku zote yalikuwa ni matendo ya Mungu na yanatoka kwa hekima Yake, hivyo tunaona kwamba uumbaji wa Mungu wa vitu vyote ulioamuliwa kabla kuanzia mwanzoni kabisa na vyote vinakuwa na mapenzi mema ya Mungu. Vitu vyote vinahusiana na binadamu ndiye anayenufaika mwishowe. Tulichokisikia leo kinaonekana ni kipya na kigeni, na tumehisi jinsi ambavyo matendo ya Mungu ni halisi. Katika uhalisia na katika maisha yetu ya kila siku tunaona kwa kweli vitu kama vilivyo tunapokutana na viumbe hai.) Unaiona kabisa, sio? Mungu kumkimu binadamu sio bila msingi imara, hatamki tu maneno machache na kuishia hapo tu. Mungu anafanya mambo mengi, hata vitu ambavyo huvioni anafanya kwa manufaa yako. Mwanadamu anaishi katika mazingira haya, ulimwengu huu ambao Mungu Aliutengeneza, na ndani yake watu na vitu vingine vinategemeana, kama tu ambavyo gesi inayotoka kwenye mimea inaitakasa hewa na kuwanufaisha watu wanaoivuta. Hata hivyo, baadhi ya mimea ni sumu kwa watu, lakini hakuna mimea mingine ambayo ni kiuasumu kwao? Hili ni moja ya maajabu ya uumbaji wa Mungu! Hatukujadili mada hii leo, badala yake tumejadili kimsingi hali ya kutegemeana ya mwanadamu na vitu vingine, jinsi ambavyo mwanadamu hawezi kuishi bila vitu vingine. Ni nini umuhimu wa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote? Mwanadamu hawezi kuishi bila vitu vingine, kama ambavyo mwanadamu anahitaji hewa kuweza kuishi na namna ambavyo kama ungewekwa kwenye ombwe ungekufa upesi. Hii ni kanuni ya msingi sana kukufanya kuona kwamba mwanadamu anahitaji vitu vingine. Hivyo ni aina gani ya mtazamo ambao mwanadamu anapaswa kuwa nao kwa vitu vyote? (Kuvithamini sana.) Vithamini sana, vitunze, vitumie kwa ufanisi, usiviharibu, usivipoteze, na usivibadilishe kwa ghafula, maana vitu vyote vinatoka kwa Mungu na vinatolewa kwa binadamu na binadamu anapaswa kuvichukulia kwa uangalifu. Leo tumejadili mada hizi mbili, na mtarudi na kuzitafakari kwa kina. Wakati ujao tutajadili vitu vingi zaidi kwa kina. Ushirika wetu utaishia hapa kwa leo. Kwa heri! (Kwa heri!)

Jumatano, 5 Juni 2019

Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo

3. Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo?

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, Kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, badala yake, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale Kristo bandia wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.
kutoka kwa "Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Huwa mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amekuwa mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, Atampa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, itadadisiwa kutoka katika dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini katika dutu Yake (Kazi Yake, Maneno Yake, Tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu.
kutoka kwa "Dibaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe.
…………
… Japokuwa Kristo Anamwakilisha Mungu Mwenyewe katika mwili na hufanya binafsi ambayo Mungu Mwenyewe Anapaswa kufanya, Yeye hakani kuwepo kwa Mungu mbinguni, wala kuyatangaza matendo Yake Mwenyewe kwa msisimko. Badala yake, Yeye kwa unyenyekevu Hubaki kwa siri ndani ya mwili Wake. Mbali na Kristo, wale ambao wanadai kwa udanganyifu kuwa Kristo hawana sifa Zake. Wakiwekwa sambamba dhidi ya tabia za kiburi na kujiinua za Kristo wa uongo, inakuwa dhahiri aina gani ya mwili ndiye Kristo wa kweli. Walivyo waongo zaidi, ndivyo Kristo wa uongo wanavyojionyesha wenyewe, na ndivyo wanavyoweza zaidi kufanya kazi za ishara na maajabu ya kuwahadaa binadamu. Kristo wa uongo hawana sifa za Mungu; Kristo hajachafuliwa na kipengele chochote cha dutu ya Kristo wa uongo. Mungu hupata mwili tu kukamilisha kazi ya mwili, na sio tu kuwaruhusu watu wote kumwona. Badala yake, Yeye huacha kazi Yake ithibitishe utambulisho Wake, na kuruhusu Anachofichua kushuhudia dutu Yake. Dutu Yake haikosi msingi ; utambulisho Wake haukukamatwa na mkono Wake; huamuliwa kwa kazi Yake na dutu Yake. …
Kazi na maonyesho ya Kristo huamua dutu Yake. Yeye Anaweza kukamilisha kwa moyo wa kweli kile Alichoaminiwa kufanya. Anaweza kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli, na kwa moyo wa kweli Atafute mapenzi ya Mungu Baba. Yote haya yanaamuliwa na dutu Yake. Na vile vile ufunuo Wake wa asili pia unaamuliwa na dutu Yake; sababu ya ufunuo Wake wa asili kuitwa hivyo ni kwa sababu ya maonyesho Yake siyo maigizo, au matokeo ya elimu na mwanadamu, au matokeo ya miaka mingi ya kukuzwa na mwanadamu. Hakujifunza au kujivika nayo Yeye Mwenyewe; badala yake, ni asili ndani Yake.
kutoka kwa "Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na ana uwezo wa kutoa mapepo, na kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba haya yote ni ujio wa Yesu, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuigi Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine; mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Unapaswa kuelewa vizuri mambo haya.
kutoka kwa "Kuijua Kazi ya Mungu Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, "Mimi ni Mungu!" Lakini mwishowe, hawawezi wakasimama, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. Mimi sipigi mayowe Nikisema, Mimi ni Mungu, Mimi ni Mwana Mpendwa wa Mungu! Lakini kazi Nifanyayo ni ya Mungu. Kuna haja Nipige mayowe? Hakuna haja ya kujiinua. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na hahitaji mwanadamu kumpa ruhusa ama cheo kubwa, na kazi Yake inatosha kuwakilisha utambulisho Wake na cheo. Kabla ya ubatizo Wake, si Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe? Je, Yeye hakuwa mwili wa Mungu? Hakika haiwezi kusemekana kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu baada ya kushuhudiwa? Je, hakukuwa na mwanadamu jina lake Yesu kitambo kabla Aanze kazi Yake? Huwezi kuleta njia mpya ama kumwakilisha Roho. Huwezi kueleza kazi ya Roho ama maneno Anenayo. Huwezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ama ile ya Roho. Huwezi kuelezea hekima, ajabu na mambo ya Mungu yasiyoeleweka, ama tabia yote ambayo Mungu humwadibu mwanadamu kupitia kwayo. Kwa hivyo madai yako ya kila mara ya kusema kuwa wewe ni Mungu hayajalishi; unalo tu jina lakini huna dutu. Mungu Mwenyewe Amekuja, lakini hakuna anayemtambua, ilhali Anaendelea na kazi Yake na Anafanya hivyo kwa uwakilishi wa Roho. Haijalishi unamwita mwanadamu ama Mungu, Bwana ama Kristo, ama umwite dada, yote ni sawa. Lakini kazi Afanyayo ni ile ya Roho na Anawakilisha kazi ya Mungu Mwenyewe. Hajali ni jina gani mwanadamu anamwita. Je, jina hilo linaweza kuamua kazi Yake? Bila kujali unachomwita, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu; Anawakilisha Roho na amekubaliwa na Yeye. Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake.
kutoka kwa "Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kati ya hao Kristo wa uwongo, manabii waongo na wadanganyifu, hakuna wanaoitwa Mungu pia? Na mbona hao sio Mungu? Kwa sababu hawana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu. Mizizini, wao ni wanadamu, wanaowadanganya watu, sio Mungu, na hivyo hawana utambulisho wa Mungu.
kutoka kwa "Kuhusu Majina na Utambulisho" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Sisi ambao tumepitia kazi ya Mungu ya siku za mwisho sote tumeweza kuona waziwazi ukweli mmoja: Kila wakati Mungu Anapofanya awamu mpya ya kazi, Shetani na roho mbalimbali waovu humfuata Yeye unyo kwa unyo, wakiiga na kuifanya kazi Yake kuonekana ya uongo ili kuwalaghai watu. Yesu Aliponya, na kuyatoa mashetani, na hivyo, ndivyo pia, Shetani na roho wa maovu wanavyofanya kwa kuponya na kutoa mashetani; Roho Mtakatifu alimpa mwanadamu tuzo ya kuongea kwa ndimi, na hivyo, pia, ndivyo pepo wabaya wanavyowafanya watu kuongea "kwa ndimi" ambazo hakuna anayeelewa. Na bado, ingawaje pepo wabaya wanafanya mambo mbalimbali yanayoshawishi mahitaji ya mwanadamu, na kutenda baadhi ya vitendo visivyo vya ulimwenguni humu ili kuweza kumlaghai yeye, kwa sababu si Shetani wala pepo hawa wabaya wameumiliki ukweli hata kidogo zaidi, hawatawahi kuweza kumpatia mwanadamu ukweli. Kuanzia sehemu hii pekee inawezekana kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo.
… Baada ya kupata mwili, Roho wa Mungu hufanya kazi kwa unyenyekevu na kwa siri, na hupitia maumivu yote ya mwanadamu bila ya malalamiko hata kidogo. Kama Kristo, Mungu hajawahi Kujishaua Mwenyewe, au kujigamba, isitoshe Hajawahi jifanya kuhusu nafasi Yake, au kuwa wa kujidai, hali ambayo inaonyesha kabisa uheshima na utakatifu wa Mungu. Hali hii inaonyesha kiini cha heshima chenye ukubwa wa maisha ya Mungu, na inaonyesha kwamba Yeye ndiye mfano halisi wa upendo. Kazi ya Makristo wa uongo na pepo wabaya kwa usahihi ni kinyume cha kazi ya Kristo: Kabla ya kitu chochote kile, pepo wabaya siku zote wanatangaza kwamba wao ni Kristo, na wanasema kwamba kama hutawasikiliza huwezi kuingia kwenye ufalme. Wanafanya kila kitu wanachoweza kuwafanya watu kukutana na wao, wanajigamba, na kujishaua wenyewe, na kujiona, au vinginevyo kutenda baadhi ya ishara na maajabu ili kuwalaghai watu —na baada ya watu hawa kulaghaiwa na kuzikubali kazi zao, wanasambaratika bila watu kuwa na habari kwa sababu kipindi kirefu kimepita tangu walipopewa ukweli. Kunayo mifano mingi, mifano mingi ya haya. Kwa sababu Makristo wa uongo si ukweli, njia, au uzima, hivyo basi hawana njia, na muda mfupi ujao au baadaye wale wanaowafuata watadhalilishwa—lakini wakati huo mambo yatakuwa yameharibika tayari na hayataweza kurekebishwa. Na hivyo, muhimu zaidi ni kutambua kwamba Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima. Makristo wa uongo na pepo wabaya kwa hakika wameondolewa ukweli; haijalishi ni mambo mangapi wanayoyasema, au vitabu vingapi wanavyoviandika, hakuna kati ya hivyo vilivyo na ukweli hata kidogo. Hali hii ni kamili. Kristo pekee ndiye Anayeweza kuuonyesha ukweli, na hii ni muhimu katika kutambua tofauti kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo. Isitoshe, Kristo hajawahi kuwalazimisha watu kumkubali au kumtambua Yeye. Kwa wale wanaomsadiki Yeye, ukweli unazidi kuwa wazi zaidi na zaidi, na namna wanavyotembea inazidi kuwa angavu zaidi na zaidi, na hii ni thibitisho kwamba Kristo pekee ndiye Anayeweza kuwaokoa watu, kwani Kristo ndiye ukweli. Makristo wa uongo wanaweza tu kuiga maneno machache, au kutamka maneno yanayogeuza weusi ukawa weupe. Hawana ukweli, na wanaweza tu kuwaletea watu giza, maangamizo, na kazi ya pepo wabaya.
kutoka kwenye Utangulizi wa Kuchanganua Kesi za Ulaghai na Kristo wa Uongo na Wapinga Kristo
Makristo wa uongo wanawezaje kutambuliwa? Ni rahisi mno. Unawaambia: "Endelea, zungumza. Nini kinachokufanya kuwa Kristo? Sema kitu kuhusu kile Mungu anacho na alicho, na kama huwezi kukisema, kukiandika ni SAWA, pia. Andika baadhi ya maneno yaliyoonyeshwa uungu—endelea, niandikie jambo. Huna tatizo kuiga baadhi ya maneno ya ubinadamu. Hebu sema mengine zaidi, zungumza kwa saa tatu na uone kama unaweza kufanya hivyo. Wasiliana ukweli nami kwa saa tatu, ongea kuhusu Alicho Mungu, na awamu hii ya kazi Yake, nizungumzie waziwazi, jaribu na uone. Na kama huwezi kuongea, basi wewe ni bandia, na ni pepo mbaya. Kristo wa kweli anaweza kuzungumza kwa siku nyingi bila ya matatizo yoyote, Kristo wa kweli Ameonyesha zaidi ya maneno milioni—na angali hajamaliza. Hakuna vipimo kuhusu ni kiwango kipi Anachoweza kuongea, Anaweza kuongea wakati wowote au mahali popote, na maneno Yake yasingeweza kuandikwa na binadamu yeyote kotekote ulimwenguni. Maneno Yake yangeweza kuandikwa na mtu yeyote yule asiyekuwa na uungu? Mtu kama huyo angeweza kuyaongea maneno haya? Nyinyi Makristo wa uongo hamna uungu, na Roho wa Mungu hayumo ndani yenu. Ungewezaje kuyaongea maneno ya Mungu? Unaweza kuyaiga baadhi ya maneno ya Mungu, lakini unaweza kuendelea hivyo kwa muda gani? Mtu yeyote aliye na akili anaweza kukariri maneno machache, kwa hivyo ongea kwa saa moja, wasiliana kwa karibu ukweli kwa saa mbili—jaribu na uone." Ukisisitiza kwao hivyo, watafichuliwa, watapigwa na bumbuazi, na watatoroka hivi karibuni. Je, hali iko hivyo? Nyinyi mnasemaje, mambo yako hivyo? Waambie haya kwao: Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima, hivyo basi onyesha ukweli wa Kristo kwangu mimi ili niweze kusikia, au kusoma. Kama utaweza, basi wewe ndiwe Kristo, na kama hutaweza, basi wewe ni pepo mbaya! Ni rahisi kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo. Makristo wa uongo na wapinga kristo hawana ukweli; yeyote yule ambaye ameumiliki ukweli ni Kristo, na yeyote yule anayekosa ukweli si Kristo. Je, hali iko hivyo? Waambie: "Kama huwezi kuonyesha Kristo ni nani, au kile Mungu Alicho, na unasema kwamba wewe ni Kristo, basi unadanganya. Kristo ndiye ukweli—hebu tuone ni maneno mangapi ya ukweli unayoweza kuonyesha. Kama utaiga sentensi kadhaa, basi huziwasilishi , na unazinakili pekee. Umeziiba, ni mwigo." Hapo sawa—hayo ndiyo yanayohitajika ili kuwatambua Makristo wa uongo. … Hebu tuuzungumzie ukweli: namna ambavyo Mungu Alionekana wakati Alipoonekana. Wakati Mungu Alipoanza kufanya kazi, Hakusema kwamba Yeye ni Mungu, Hakusema hivyo. Mungu Aliyaonyesha maneno mengi, na baada ya Kuyaonyesha mamia ya maelfu ya maneno, bado Hakusema kwamba Yeye ni Mungu. Mamia ya maelfu ya maneno—hicho ni kitabu kizima, takribani kurasa mia tatu au nne—na bado Hakusema kwamba Yeye ni Mungu. Baada ya kuangaziwa na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, baadhi ya watu walisema: "Jameni, haya ndiyo maneno ya Mungu, hii ndiyo sauti ya Roho Mtakatifu!" Mwanzoni, walisadiki kwamba ilikuwa ni sauti ya Roho Mtakatifu; baadaye, walisema kwamba ilikuwa sauti ya Roho wale saba, ya Roho aliyezidi na aliyekuwa mara saba. Waliita "sauti ya Roho saba," au "matamko ya Roho Mtakatifu." Haya ndiyo waliyoyasadiki mwanzoni. Ni baadaye tu, baada ya Mungu kuyatamka maneno mengi, mamia ya maelfu ya maneno, ndipo Alipoanza kushuhudia maana ya kupata mwili, na maana ya kuonekana kwa Neno katika mwili— na hapo tu ndipo watu walianza kujua, wakisema: "Jameni! Mungu amepata mwili! Ni kupata mwili kwa Mungu Anayetuzungumzia sisi!" Hebu tazama namna kazi ya Mungu ilivyo fiche na yenye unyenyekevu. Hatimaye, baada ya Mungu kumaliza kuyaonyesha maneno Yake yote ambayo lazima Angeyaonyesha, bado Hakusema kwamba Yeye ni Mungu Alipofanya kazi na kuhubiri, bado Hakuwahi kusema, "Mimi ni Mungu! Nyinyi lazima mnisikilize Mimi." Hakuwahi kuongea hivyo. Na bado Makristo wa uongo wanasema wao ni Kristo kabla ya hata kutamka maneno machache. Je, hawa wanaweza kukosa kuwa bandia? Mungu wa kweli ni mfiche na mnyenyekevu, na kamwe Hajishaui; Shetani na pepo wabaya, kinyume cha mambo ni kwamba, wanapenda kujishaua, ambayo ni njia nyingineyo ya kuwatambua.
kutoka kwa "Majibu ya Maswali" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (I)
Sasa, kama watu watajaribu kuwalaghai, angalieni kama wanaweza kuionyesha sauti ya Mungu. Hali hii itathibitisha kama wamemiliki au la kiini cha uungu. Kama hawawezi kuzungumzia kuhusu kile Mungu anacho na alicho, na hawawezi kuonyesha mambo na sauti ya Mungu, basi kwa kweli hawana kiini cha Mungu, na hivyo wao ni bandia. Kunao wale wanaosema: Tumewaona baadhi ya watu wakiongea maneno ambayo hakuna mwanadamu angeweza kuyasema. Wanaweza pia kuongea unabii, na kuongea bila ya kutatizwa kwa mambo ambayo hakuna mtu angeyajua wala kuyaona—hivyo basi, wao ni Mungu? Mnawezaje kutofautisha haya mambo hasa kuhusu watu kama hawa? Kama ambavyo imesemwa tu, kama wao ni Mungu, basi lazima waweze kuongea kuhusu kile Mungu anacho na alicho, na kuweza kuzungumzia siri za ufalme wa Mungu; ni mtu kama huyu tu ndiye anayeweza kusemekana kuwa mwili wa Mungu. Kama kunao watu wanaoweza kuongea mambo ambayo wengine hawajui, wanaoweza kuwaambia kuhusu siku zao za usoni, na wanaoweza kusema kile kitakachofanyikia nchi, haya si lazima yawe maneno ya Mungu; pepo wabaya wanaweza pia kusababisha mambo haya. Kwa mfano, kama leo utawaambia: "Ni nini kitakachonifanyikia katika siku za usoni?" watakuambia ni janga aina gani litakalokupata wewe, au watakuambia ni lini utakapokufa, au vinginevyo watakuambia ni nini kitakachofanyikia familia yako. Katika matukio mengi, mambo haya huja kuwa kweli. Lakini kuweza kuzungumzia mambo kama haya si kile Mungu Alicho, wala si sehemu ya kazi ya Mungu. Lazima uwe wazi kuihusu hoja hii. Haya ndiyo mambo madogomadogo ambayo pepo wabaya wanatia fora kwayo; Mungu hajihusishi na mambo kama haya. Tazama ni kazi gani ambayo Mungu Amefanya kila wakati Amepata mwili. Mungu Anafanya kazi ya kumwokoa mwanadamu, Hatabiri kile kitakachowafanyikia watu, wataishi kwa muda gani, ni watoto wangapi watakaowapata, au ni lini janga litakapowapata. Je, Mungu amewahi kuyatabiri mambo kama haya? Hajawahi. Sasa, nyinyi mnasema nini, Mungu Anayajua mambo kama haya? Bila shaka Anayajua, kwani Aliumba mbingu na ardhi na vitu vyote. Mungu tu ndiye Anayevijua kwa njia bora zaidi, ilhali kunayo mipaka kuhusu kile ambacho pepo wabaya wanajua. Pepo wabaya wana uwezo wa kujua nini? Pepo wabaya wanajua hatima ya mtu, au nchi, au taifa. Lakini hawajui chochote kuhusu usimamizi wa Mungu, hawajui hatima ya mwanadamu itakuwa vipi, au ni wapi ambapo mwisho wa kweli wa mwanadamu unapatikana, isitoshe hawajui ni lini ulimwengu utafika mwisho na ufalme wa Mungu kuwasili, au maonyesho mazuri ya ufalme wa mbinguni yatakuwa vipi. Hawajui chochote kuhusu haya yote, hakuna yeyote kati yao anayeyajua. Mungu pekee ndiye Anayejua masuala kama haya, na hivyo Mungu ni Mjua-yote, ilhali kile pepo wabaya wanachojua kinao ufinyu mkubwa sana. Tunajua kwamba manabii wakubwa zaidi wa ulimwengu walikuwa waliongea kuhusu kile kitakachofanyika kwenye siku za mwisho, na leo maneno yao yametimizwa—lakini hawakujua chochote kuhusu kazi ambayo Mungu Anafanya kwenye siku za mwisho, isitoshe hawakujua kile ambacho Mungu Amekuja kutimiza, au namna ambavyo Ufalme wa Milenia utakavyofikiwa, au ni nani atakayeingia kwenye ufalme wa Mungu na kuishi. Wala, na kuongezea hayo, hawakujua chochote kuhusu kile kitakachofanyika baadaye, kwa ufalme wa Mungu. Hakuna pepo mbaya anayejua masuala kama hayo; Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayejua, na hivyo pepo wabaya hawawezi kamwe kujua chochote kinachohusu mpango wa usimamizi wa Mungu. Kama utawaambia, "Hatima yangu ni nini? Nini kitakachofanyikia familia yangu?" baadhi ya pepo wabaya wataweza kukuambia jibu dhahiri. Lakini ukiwaambia, "Kwenye siku za usoni, nitakuwa na hatima katika imani yangu kwa Mungu? Nitaishi?" hawatajua. Pepo wabaya wanao ufinyu mkubwa sana kuhusu kile wanachojua. Kama pepo mbaya anaweza kusema tu mambo machache finyu, anaweza kuwa Mungu? Hawezi kuwa—ni pepo mbaya. Wakati pepo mbaya anaweza kuwaambia watu mambo wasiyoyajua, kuwaambia kuhusu siku zao za usoni, na hata kuwaambia namna ambavyo walikuwa na mambo ambayo wameyafanya, kama kunao wale wanaofikiria kwamba kufanya hivi kunao uungu kwa kweli, je, huoni kwamba watu hao ni wa kukejeliwa? Hii inathibitisha kwamba wewe hujui Mungu kabisa. Unaziona mbinu ndogo za pepo wabaya kuwa zenye uungu kabisa, na kuwachukulia kama Mungu. Je, unajua kuihusu kudura ya Mungu? Hivyo, kama leo tunayo maarifa kuihusu kudura na kazi ya Mungu, hakuna pepo mbaya, haijalishi ni ishara na maajabu gani ambayo wanatenda, anayeweza kutulaghai, kwani kwa hakika lipo jambo japo moja ambalo tuna hakika nalo: Pepo wabaya si ukweli, hawawezi kufanya kazi ya Mungu, wao si Muumba, hawawezi kumwokoa mwanadamu, na wanaweza kumpotosha tu mwanadamu.
kutoka kwa “Utofauti kati ya Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)

Jumanne, 4 Juni 2019

Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Njia za Kweli na za Uongo, na Makanisa ya Kweli na ya Uongo

4. Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Njia za Kweli na za Uongo, na Makanisa ya Kweli na ya Uongo?

Maneno Husika ya Mungu:
Kanuni ya msingi kabisa katika kuutafuta ukweli ni nini? Unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu au la, iwapo maneno haya ni udhihirishaji wa ukweli, yanamshuhudia nani, na ni kitu gani yanaweza kukupatia. Kutofautisha kati ya njia ya kweli na hizi njia za uongo kunahitaji njia kadhaa za maarifa ya msingi, ya msingi kabisa kati ya zote ni kusema iwapo kuna Kazi ya Roho Mtakatifu au la. Maana kiini cha imani ya mwanadamu kwa Mungu ni imani katika Roho Mtakatifu. Hata imani yake kwa Mungu mwenye mwili ni kwa sababu mwili huu ni mfano halisi wa Roho wa Mungu, ikiwa na maana kwamba imani hiyo bado ni imani katika Roho. Kuna tofauti kati ya Roho na mwili, lakini kwa kuwa mwili unatokana na Roho, na ndio Neno linakuwa mwili, hivyo kile ambacho mwanadamu anaamini katika ni uungu halisi wa Mungu. Na hivyo, katika kutofautisha kama ni njia sahihi au la, zaidi ya yote unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu, na baada ya hapo unapaswa kuangalia kama kuna ukweli katika njia hii. Ukweli huu ni silika ya maisha ya mwanadamu wa kawaida, ni sawa na kusema, kile ambacho Mungu alikitaka kwa mwanadamu alipomuumba hapo mwanzo, yaani, ubinadamu wote wa kawaida (ikiwa ni pamoja na hisia za kibinadamu, umaizi, hekima, na maarifa ya msingi ya kuwa mwanadamu). Yaani, unapaswa kuangalia iwapo njia hii inampeleka mwanadamu katika maisha ya mwanadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli uliozungumzwa unahitajika kulingana na uhalisia wa ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli huu ni wa kiutendaji au hali, na iwapo ni wa wakati muafaka au la. Ikiwa kuna ukweli, basi unaweza kumpeleka mwanadamu katika uzoefu wa kawaida na halisi; aidha, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, hisia za kawaida za kibinadamu zinakuwa kamili zaidi, maisha ya mwanadamu katika mwili na maisha ya kiroho yanakuwa katika mpangilio mzuri zaidi, na mihemko ya mwanadamu inakuwa ya kawaida kabisa. Hii ni kanuni ya pili. Kuna kanuni nyingine moja zaidi, ambayo ni kama mwanadamu ana maarifa mengi juu ya Mungu, kama unapitia uzoefu wa kazi hiyo na ukweli unaweza kuchochea upendo wa Mungu ndani yake au la, na kumsogeza karibu zaidi na Mungu. Katika hili inaweza kupimwa kama ni njia sahihi au la. Kanuni ya msingi ni iwapo njia hii ni ya uhalisia badala ya kuwa ya kimiujiza, na iwapo inaweza kutoa maisha ya mwanadamu. Kama hukubaliana na kanuni hizi, hitimisho linaweza kuwekwa kwamba njia hii ni njia ya kweli. … Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida kabisa, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake, ambayo yameharibiwa na Shetani, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Ni sawa na, kusema, maisha ya mwanadamu yanakuwa na kukua, na Atabia ya upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maishi ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha atabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa uelewa wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu. Umeamini katika Mungu kwa miaka yote hii, halafu bado huna uwezo wa kutofautisha kati ya njia ya kweli na njia ya uongo au kuweza kuitafuta njia ya kweli. Watu wengi hawapendi hata kusikia masuala haya; wanakwenda tu kule ambapo wengi wanakwenda, na wanarudia kile ambacho watu wengi wanasema. Ni kwa njia gani mtu huyu ni mtu anayetafuta njia ya kweli? Na ni kwa njia gani watu kama hao wanaweza kuipata njia ya kweli? Ikiwa utaelewa kanuni hizi muhimu, basi chochote kitakachotokea hutaweza kudanganywa.
kutoka kwa "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wote walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikishwa na uwepo na adabu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo kwenye mkondo huu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale walioikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na vibaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee huduma na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanadhibitiwa na Roho Mtakatifu na huenda wakaadhibiwa. Bila kujali ni aina gani ya watu, ili mradi tu wamo kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake. Wale wanaolitukuza jina Lake na wako radhi kuweka maneno Yake katika vitendo watapokea Baraka Zake; wale wasiomtii na kuyaweka maneno Yake katika vitendo watapokea adhabu Yake. … Sio hivyo na watu wasioikubali kazi mpya: Wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na adhabu na lawama ya Roho Mtakatifu haitumiki kwao. Kila siku hawa watu wanaishi katika mwili, wanaishi katika mitazamo yao, na yote wayafanyayo ni kulingana na mafundisho ya kidini yaliyozalishwa na uchanganuzi pamoja na utafiti wa bongo zao. Si matakwa ya kazi mpya ya Roho Mtakatifu wala sio ushirika na Mungu. Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu wanajinyima uwepo wa Mungu na zaidi wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Mengi ya maneno na matendo yao yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini tu na wala si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kitu cha pekee kinachowaleta pamoja ni dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mikutano ya wote walio miongoni mwao haiwezi kuitwa kanisa bali mkutano mkubwa wa watu wa dini. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya. Ikiwa imesimama juu ya msingi wake asili, kazi ya Roho Mtakatifu imepiga hatua kadhaa kwa kina. Na bado watu hao wamebaki katika hatua ya asili ya kazi ya Mungu na bado wanapenyeza katikati ya vitendo na mwangaza wa zamani. Kazi ya Mungu yaweza kubadilika pakubwa kwa miaka mitatu au mitano, hivyo si mabadiliko hata makubwa zaidi yaweza kuja kwa kipindi cha miaka zaidi ya 2000? Ikiwa mwanadamu hana vitendo vipya ama mwangaza mpya, inamaanisha hajaenda sawia na kazi ya Roho Mtakatifu. Hili ni anguko la mwanadamu; uwepo wa kazi mpya ya Mungu hauwezi kukanwa kwa sababu, leo hii, wale walio na kazi asili ya Roho Mtakatifu bado wanashikilia vitendo vilivyopitwa na wakati. Kazi ya Roho Mtakatifu daima inasonga mbele, na wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanafaa waendelee mbele na kubadilika, hatua kwa hatua. Hawapaswi kukwama katika hatua moja. Ni wale tu wasioifahamu kazi ya Roho Mtakatifu ndio wanaweza kubaki katika hatua ya kazi ya Mungu ya awali na wasikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Ni wale tu walio waasi ndio watakosa uwezo wa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa vitendo vya mwanadamu haviendani na mwendo wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, basi vitendo vya mwanadamu hakika vimetengana na kazi ya leo na kwa hakika havilingani na kazi ya leo. Watu waliopitwa na wakati kama hawa hawawezi kutimiza mapenzi ya Mungu, na zaidi hawawezi kuwa wale watu wa mwisho ambao watamshuhudia Mungu. Aidha, kazi nzima ya usimamizi haiwezi kutimilika miongoni mwa kundi la watu kama hao. Kwa wale walioshikilia sheria za Yehova kipindi fulani, na wale walioumia wakati fulani chini ya msalaba, ikiwa hawawezi kukubali hatua ya kazi ya siku za mwisho, basi yale yote waliyofanya ni bure na yasiyofaa. … Ikiwa mwanadamu atasalia amekwama katika hatua moja tu, basi hili linaonyesha kuwa haendi sawia na kazi ya Mungu na mwangaza mpya; haimaanishi kuwa mpango wa usimamizi wa Mungu haujabadilika. Walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu daima hudhani wako sahihi, lakini kwa hakika, kazi ya Mungu ndani yao ilisita zamani na kazi ya Roho Mtakatifu haimo ndani yao. Kazi ya Mungu imeshahamishiwa kwa kundi jingine la watu, kundi ambalo kwalo Anapania kukamilishia kazi Yake mpya. Kwani walio kwenye dini hawawezi kuikubali kazi mpya ya Mungu, na kushikilia tu kazi kongwe za zamani, hivyo Mungu amewaacha watu hawa na anafanya kazi Yake mpya kwa watu wanaoikubali kazi hii mpya. Hawa ni watu wanaoshiriki katika kazi Yake mpya, na usimamizi Wake utatimilika kwa njia hii tu. Usimamizi wa Mungu daima unasonga mbele na vitendo vya mwanadamu daima vinapanda juu. Mungu daima anafanya kazi na mwanadamu mara zote ni mhitaji ili kwamba wote wanafikia upeo wao, Mungu na mwanadamu wamo katika muungano kikamilifu. Haya ni maonyesho ya kutimilika kwa kazi ya Mungu, na ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi nzima ya usimamizi.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Njia ya kweli ni njia ambayo inaweza kuwaokoa watu, kuwabadilisha watu, na kuwawezesha kufanikisha kukubaliwa na Mungu na kuingia katika hatima ya kweli. Hii tu ndiyo njia ya kweli. Iwapo watu wanadhani kuwa wao wanaamini katika njia ya kweli, lakini malengo haya na matokeo haya hayajapatikana, basi inaweza kusemwa kwamba yao ni njia ya uongo, kwamba si njia ya kweli. Watu wengine husema: "Je, nitawezaje kutambua tofauti kati ya mazuri na mabaya?" Hili linakamilishwa kulingana na maneno ya Mungu. Yote yanayokubaliwa na Mungu, yote Anayomhitaji mwanadamu kumiliki, na kila ambacho Mungu Anapenda mwanadamu afanye ni kizuri; yote ambayo Mungu Anataka wanadamu wayakatae na kuyaacha, na yote yanayoshutumiwa na Mungu, ni mabaya. Kutathmini mazuri na mabaya huamuliwa hivyo, kulingana na maneno ya Mungu; Maneno ya Mungu ni kipimo ambacho huthibitisha iwapo kitu chochote ni cha kweli au cha uongo, na ndicho kiwango pekee cha kupima iwapo kitu chochote ni kweli au uongo. Unatathmini vipi njia gani ni ya kweli, na gani ni ya uongo? Njia inayoweza kukuletea maisha ya kweli, inayoweza kukufanya uone mwanga, inayoweza kukuruhusu ujiondolee upotovu na ushawishi wa Shetani, na kukuwezesha kupata kibali na baraka ya Mungu—hii ndiyo njia ya kweli. Je, huo si ukweli? Je, hukumu na kuadibu kwa Mungu kumetuletea nini? Kumetuletea ukweli wote ambao watu wapotovu lazima wamiliki ili kupata wokovu, kumeleta njia ya kweli ya maisha, kumeturuhusu kuuona mwanga wa maisha, kumetupa wokovu mkuu zaidi, na wokovu wa kweli, ambao ulipangiwa awali na Mungu katika uumbaji wa dunia, na kumetubadilisha sisi kutoka kwa watu ambao walipotoshwa na Shetani, na kumilikiwa na Shetani, na kuwa watu halisi ambao kwa hakika wametakaswa na Mungu na wamejawa na ukweli na ubinadamu. Haya yote ndiyo matokeo yaliyofanikishwa na hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Bila hukumu na kuadibu kwa Mungu, hatungeweza kupata ukweli, upotovu wetu ungebaki bila kutatuliwa, kamwe hatungeweza kuona mwanga wa maisha, na kamwe hatungepata kibali cha Mungu. Hivyo, baraka zote ambazo tumepokea leo zinatokana na kupitia na kutii hukumu na kuadibu kwa Mungu.
…………
Baadhi ya watu husema: "Hebu, iwapo hii ni njia ya kweli, kwa nini watu wachache tu ndio waliojiunga nayo? Kwa kuwa ni njia ya kweli, si inapaswa kuwa na waumini wengi? Si binadamu wote wanapaswa kuamini kwayo?" Watu wanaosema mambo kama hayo hawaelewi ukweli, wao ni wapumbavu. Upotovu wa binadamu wote umefikia hatua fulani; watu wachache zaidi na zaidi ndio wanapenda ukweli, watu wengi zaidi na zaidi wanafuatilia maslahi yao wenyewe, na bila kujali ni imani gani watakubali, wao kwanza huangalia kama ni ya faida kwao—ambayo ina maana kwamba wale ambao wanaamini katika njia ya kweli kwa hakika ni wachache, na wale ambao wanaamini katika njia za uongo, na njia ambazo zinatoa neema na faida, kwa hakika ni wengi. Baada ya kusikia maelezo yangu, utaweza kuona ndani kwenye kiini cha suala. Njia tunayoamini kwayo haiponyi watu, wala kujaza matumbo yao kwa mkate, au kuwapa neema, au kupunga pepo waovu kutoka kwao. Lakini tukiongeza kitu kimoja zaidi kwa njia tunayoamini kwayo—kwamba waumini hawatakufa wakati maafa yoyote yatawasibu—basi watu wote wa dunia wataamini ndani yake. Leo, hili halijahusishwa katika njia yetu. Mungu hajasema, "Naahidi kwamba wote ambao wanaamini katika jina la Mwenyezi Mungu hawatakufa." Hivyo, unapoeneza injili una tahadhari. Watu huuliza, "Kwa hivyo sitakufa nikiamini katika Mwenyezi Mungu?" "Mimi sijui." "Kama Hawezi kunizuia kufa, basi hakuna haja ya kuamini katika Yeye." Watu pia watauliza, "Nitafaidi nini kutoka kwa kuamini katika Mwenyezi Mungu?" "Unaweza kupata ukweli." "Kupata ukweli kutanipatia nini?" "Utanusurika" "Ni nani amewahi kuona hili?" "Nani anayeweza kulithibitisha? Kupata ukweli kunamaanisha nini?" "Mimi Sijui." "Hakuna jinsi ninavyoweza kuamini." Hivyo, ni vigumu kwetu kumshuhudia Mwenyezi Mungu na kueneza injili, kwa kuwa wale wanaopenda ukweli ni wachache sana. Huu ni ukweli. Ilhali baada ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu, jinsi tunavyoamini zaidi, ndivyo tunavyohisi kuwa ni halisi zaidi, na ndivyo imani yetu inavyokuwa na nguvu zaidi. Ni kwa nini vile? Haya ni matokeo ya kuuelewa ukweli. Zaidi mtu anavyoelewa ukweli, ndivyo wanavyohisi zaidi kuwa ni njia ya kweli, na kazi ya Mungu. Zaidi wanavyoulewa ukweli, zaidi wanavyojiambia wenyewe, "Ah, wokovu wa Mungu wa binadamu kwa njia hii ni halisi sana, kuelewa ukweli hakika kunaweza kuniokoa, kusababisha mabadiliko katika tabia yangu, kunifanya mimi kuwa binadamu wa kweli, na kuniruhusu niishi maisha halisi ya ubinadamu wa kawaida—na kwa hivyo njia hii ina maana." Wanahisi kwamba kuupata ukweli kuna maana zaidi, kunastahili, na kwenye thamani zaidi ya faida yoyote, au uponyaji wa wagonjwa, au kujaza matumbo ya watu na chakula. Kwa sababu hiyo, wale ambao wameamini katika Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa huhisi kwamba hakuna kitu cha thamani kuhusu neema yoyote wanayoweza kupewa, kwamba kupata ukweli tu ni kwa thamani—na katika hili, wameona njia ya kweli. Tazama, kuna wowote wa wale wanaoamini katika Mwenyezi Mungu wametoroka? Ingawa baadhi ya watu hawautafuti ukweli, mradi wao wamesikiliza mahubiri kwa miaka michache, je watataka kuondoka? Hakuna hata mmoja angetaka. Na kwa nini wasitake? Wanachojua ni kwamba "Hii ndiyo njia ya kweli. Bora tu nifanye kazi kwa bidii, na kufanya wajibu wangu vizuri, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba nitaishi, kwamba mwisho wangu hautakuwa kifo. Kutokufa ni kwa thamani mno." Leo, watu hawajui ni nini kinahitajika ili kuepuka kifo. Punde tu wangejua, basi kila mtu angekuwa muumini, na imani yao ingekuwa imara.
kutoka kwa "Mafunzo Manne muhimu Ambayo Lazima Yaingiwe ili Kuitii Kazi ya Mungu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (VI)
Iwapo jamii ya kidini nzima haingekuwa na uhasama na kuipinga, basi hii haingekuwa njia ya kweli. Kumbuka: Njia ya kweli lazima ipingwe na watu wengi, hata na duniani. Wakati Bwana Yesu Alikuja mara ya kwanza kufanya kazi na kuhubiri, je, Uyahudi mzima haukumpinga Yeye? Kila wakati Mungu anapoanza kazi mpya, ubinadamu mpotovu unapata ugumu mkubwa katika kuikubali, kwa kuwa kazi ya Mungu inakinzana na na inakanusha dhana za watu; watu hawana uwezo wa kuelewa, na hawana uwezo wa kuupenya ulimwengu wa kiroho, na kama sio kazi ya Roho Mtakatifu, hawangeweza kukubali njia ya kweli. Ikiaminiwa kuwa ni kazi ya Mungu, lakini haipingwi na jamii za kidini, na inakosa upinzani na uhasama wa dunia, basi hii inathibitisha kwamba kazi hii ya Mungu ni ya uongo. Kwa nini wanadamu hawawezi kuukubali ukweli? Kwanza, mwanadamu ni wa mwili, yeye ni wa dutu ya kimwili. Mambo ya kimwili hayawezi kupenya ulimwengu wa kiroho. Inamaanisha nini kwamba "hayawezi kupenya ulimwengu wa kiroho"? Hii ina maana ya kushindwa kuona roho, shughuli za roho na ulimwengu wa kiroho, kuwa asiyeona Anayofanya na kusema Mungu. Watu wangekuwa vipofu katika ulimwengu wa kiroho. Ukifunga macho yako katika ulimwengu wa kimwili, huoni chochote. Ukiyafungua, unaweza kuona nini? Dunia ya asili. Je, unaweza kuona ni roho yupi anafanya kazi gani ndani ya watu? Je, unaweza kuona kile ambacho Roho wa Mungu amekuja kufanya na kusema? Huwezi. Wakati mwingine unaweza kusikia sauti Yake, na kusoma maneno ya Mungu yaliyoandikwa kwenye kitabu, lakini bado hujui ni vipi au lini Mungu Alinena maneno haya. Unaweza kusikia sauti Yake, lakini hujui inakotoka; unayaona maneno ya Mungu yamechapishwa kwenye ukurasa, lakini hujui ni nini maana yake. Watu hawawezi kupenya ulimwengu wa kiroho, au kushika chanzo cha maneno ya Mungu, na hivyo wanahitaji kupata nuru na kuangaziwa kwa Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu, ili kupata matokeo. Pili, ubinadamu umekuwa mpotovu kwa undani sana, na ndani yake imejazwa na sumu nyingi ya Shetani na ufahamu mwingi; akitathmini kila kitu kwa kutumia falsafa mbalimbali za kishetani na maarifa, basi kamwe hataweza kusadikisha ukweli ni upi. Bila kupata nuru na kuangaziwa kwa Roho Mtakatifu, mwanadamu hangekuwa na uwezo wa kuelewa ukweli. Binadamu mpotovu kwa silika hawezi kupenya ulimwengu wa kiroho. Amejazwa na falsafa za kishetani na maarifa, na hawezi kuutambua ukweli. Na hivyo njia ya kweli bila kuepukika inakabiliwa na mateso na kukataliwa kwa mwanadamu. Kwa nini ni rahisi kwa watu kukubali maarifa na falsafa za Shetani? Kwanza, iko sambamba na dhana zao na maslahi ya miili yao, na ni ya manufaa kwa miili yao. Wanajiambia wenyewe, "Kukubali maarifa kama haya yananisaidia: Yatanipa kuongezwa cheo, yatanifanya niwe mwenye mafanikio, na kuniruhusu kufanikisha mambo. Na maarifa kama haya watu wataniheshimu." Tazama jinsi vinavyowafaa watu viko sambamba na dhana zao. ... Kuwa wapotovu kwa kiasi hiki, na kushindwa kupenya ulimwengu wa kiroho, watu wanaweza tu kumpinga Mungu, na hivyo kuwasili kwa kazi ya Mungu kumekutana na kukataliwa na mwanadamu, upinzani, na hukumu. Je, si hili linatarajiwa? Kama kuwasili kwa kazi ya Mungu hakungekutana na hukumu na upinzani wa dunia na wanadamu, basi hili lingethibitisha kuwa sio ukweli. Iwapo yote yaliyosemwa na Mungu yangekuwa sambamba na dhana ya watu, je, wangeyashutumu? Je, wangeyapinga? Bila shaka hawangefanya hivyo.
kutoka kwa "Ushirika na Mahubiri ya wa Juu Kuhusu Kueneza Injili"
Ni kanisa tu ambalo liko na kazi ya Roho Mtakatifu ndilo kanisa la Mungu, na kama tu lina watu ambao hakika wanafuatilia ukweli na kutii kazi ya Mungu ndipo kanisa linaweza kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu; Mungu anatambua makanisa ambayo yako na kazi ya Roho Mtakatifu, na hayatambui makanisa yasiyo na kazi ya Roho Mtakatifu. Hili linapaswa kueleweka kwa wateule wa Mungu.
…………
Kanisa halisi linajumuisha wale ambao hakika wanaamini katika Mungu na wanapenda ukweli, na ni mkusanyiko wa wote wanaomcha Mungu. Hapo tu ndipo linaweza kuitwa kanisa. ... Ni tu mkusanyiko wa wale ambao wameamuliwa kabla na waliochaguliwa na Mungu na wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu ndio kanisa.
kutoka kwa "Jinsi ya Kukabili na Kutatua Vurugu Kati ya Makanisa ya Mitaani" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (II)
Kanisa linajumuisha wale ambao hakika wameamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu—linajumuisha wale wanaopenda ukweli, wanaotafuta ukweli, na wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Ni wakati tu watu hawa wanakusanyika ili kula na kunywa neno la Mungu, kuishi maisha ya kanisa, kupitia kazi ya Mungu, na kufanya wajibu wao kama viumbe wa Mungu ndio linaweza kuwa kanisa. Umati wenye zogo ukisema kwa kweli unaamini katika Mungu, lakini haupendi au kuutafuta ukweli, na hauna kazi ya Roho Mtakatifu, na unafanya sherehe za kidini, na kuomba, na kusoma maneno ya Mungu, basi hili sio kanisa. Kwa usahihi, makanisa yasiyo na kazi ya Roho Mtakatifu si makanisa; hayo ni kumbi za kidini na watu ambao hufanya sherehe za kidini tu. Wao si watu ambao kwa kweli wanamtii Mungu na kupitia kazi ya Mungu.
…………
Kanisa ni mkusanyiko wa watu ambao wanaamini katika Mungu kwa kweli na kufuatilia ukweli, na halishirikishi waovu kabisa—wao si wa kanisa. Iwapo kundi la watu ambao hawakutafuta ukweli na wala kufanya kitu chochote kuuweka ukweli katika vitendo wangekusanyika pamoja, je, hili lingekuwa kanisa? Je, mkusanyiko huu ungekuwa nini? Ungekuwa ukumbi wa kidini, au umati wenye zogo. Kanisa lazima liundwe na watu ambao kwa kweli wanaamini katika Mungu na kuufuatilia ukweli, wanaokula na kunywa maneno ya Mungu, na kumwabudu Mungu, kufanya wajibu wao, na kupitia kazi ya Mungu na wamepata kazi ya Roho Mtakatifu. Hili tu ndilo kanisa. Hivyo, unapotathmini kanisa, lazima kwanza uangalie ni aina gani ya watu linao. Pili, lazima uangalie iwapo wana kazi ya Roho Mtakatifu au la; kama mkutano wao hauna kazi ya Roho Mtakatifu, hilo si kanisa, na kama si mkusanyiko wa wale wanaofuatilia ukweli, basi sio kanisa. Iwapo kanisa halina mtu yeyote anayefuatilia ukweli, na liko bila kazi ya Roho Mtakatifu kabisa, basi kama kuna mtu ndani lake aliye na nia ya kuufuatilia ukweli, na wanabakia katika kanisa kama lile, je, mtu huyo anaweza kuokolewa? Hawezi, na anapaswa kuuacha umati huo wenye zogo na kutafuta kanisa haraka awezavyo. Iwapo, ndani ya kanisa, kuna watu watatu au watano ambao huufuatilia ukweli, na watu 30 au 50 ambao ni umati wenye zogo, basi wale watu watatu au watano ambao wanaamini katika Mungu kwa kweli na kuufuatilia ukweli lazima waje pamoja; wakija pamoja mkutano wao bado ni kanisa, kanisa la wanachama wachache zaidi, lakini lililo safi.
kutoka kwa "Kuelewa Maana ya Kweli ya Kanisa na Kufanya Kazi kulingana na Kanuni Tano za Kazi ya Kanisa Kuna Umuhimu MkubwaSana Wakati wa Mwisho" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (VII)
Watu wengi wanaamini katika Mungu lakini wanaabudu makanisa makuu ya dayosisi na kusadiki kipofu katika wachungaji—na matokeo kwamba, baada ya kuamini katika Mungu kwa miaka mingi, bado hawajaelewa ukweli au kuingia katika hali halisi, wamepata tu baadhi ya mafundisho ya dini na sherehe za kidini na mazoea, na hawamjui Mungu kwa kweli. Katika matokeo, hakuna mabadiliko hata kidogo katika tabia ya maisha yao. Si ajabu, basi, kwamba viongozi hao wa dini na wachungaji hutumia maisha yao yote kwa kuamini katika Mungu na kuhubiri, ilhali hakuna hata mmoja wao anayemjua Mungu kwa kweli, au hata kuwa na moyo unaomcha Mungu; wao hubaki kama Mafarisayo kutoka nyakati za kale, kufanya wawezayo kumpinga Kristo, kuhukumu njia ya kweli, na kuwatega na kuwadhibiti watu wa Mungu waliochaguliwa kwa ajili ya hali zao wenyewe na kuendesha maisha yao. Sababu yao kutoa mfano wa kupenda na kuthamini kundi la wanakondoo wa Mungu kimsingi ni kwa sababu ya kulinda maisha yao wenyewe, kama vile wafanyabiashara wanavyowatendea wateja wao kama miungu ili wapate pesa na kupata utajiri. Kila kitu ambacho jamii ya kidini inafanya ni udhihirisho wa upinzani wake kwa Mungu; si chochote ila sherehe za kidini, na haina uhalisi wa ukweli hata kidogo, na zaidi hakuna dalili yoyote ya kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa dhahiri, jamii ya kidini haimwabudu Mungu wa kweli, ila Mungu asiye dhahiri na Mungu wa kubuniwa tu. Inahubiri mafundisho ya kidini, na elimu halisi ya Biblia, na haina kabisa kupata nuru na mwanga wa Roho Mtakatifu. Hivyo, jamii ya kidini kimsingi haiwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, haiwezi kuwaongoza kwenye njia sahihi ya kuamini katika Mungu, na, zaidi ya hayo, haiwezi kuchukua watu hadi katika hali halisi ya ukweli, au kuwasaidia waokolewe. Hiyo ni kwa sababu viongozi wake na wachungaji hawajafanywa wakamilifu na kujengwa na Roho Mtakatifu wanapopitia kazi ya Mungu, lakini badala yake wamekuwa viongozi na wachungaji katika jamii ya kidini baada ya kufuzu kutoka katika seminari na kupewa cheti cha diploma. Hawana kazi na uthibitisho wa Roho Mtakatifu, hawana ufahamu wa kweli wa Mungu hata kidogo, na midomo yao haiwezi kuzungumza kuhusu kitu kingine ila maarifa ya kitheolojia na nadharia. Wao kwa kweli hawana uzoefu wa kitu chochote. Watu kama hao hawajafuzu kabisa kutumiwa na Mungu; watawezaje kumwongoza mwanadamu kwenda mbele za Mungu? Kwa kiburi hushikilia kuhitimu kutoka chuo seminari kama ushahidi wa haki yao wenyewe, wanafanya kila wawezalo ili kuonyesha kwa majivuno maarifa yao ya Biblia, ni wenye kiburi kisichostahimilika—na kwa sababu hii, wanahukumiwa na Mungu, na kuchukiwa na Mungu, na wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Kuhusu hili hakuna shaka. Kwa nini jamii ya kidini imekuwa adui mkubwa wa Kristo ni swali la kuchochea fikira nyingi sana. Inaonyesha nini kuwa, katika Enzi ya Neema, Uyahudi ulimpiga Yesu Kristo msalabani? Katika Enzi ya Ufalme wa siku za mwisho, jamii za kidini zimeungana na kuweka juhudi zake zote katika kupinga na kuhukumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, zinamkana na kumkataa Kristo mwenye mwili wa siku za mwisho, zimeunda uvumi mbalimbali kuhusu, na kushambulia, kusingizia na kukufuru dhidi ya Mungu mwenye mwili na kanisa la Mungu, na kwa muda mrefu sasa zimempiga misumari Yesu Aliyerudi, Kristo wa siku za mwisho, msalabani. Hii inathibitisha kuwa jamii za kidini kwa muda mrefu sasa zimepotoka na kuwa majeshi ya Shetani yanayopinga na kuasi dhidi ya Mungu. Jamii ya kidini haitawaliwi na Mungu, wala kutawaliwa na ukweli kweli; inatawaliwa kikamilifu na binadamu wapotovu, na zaidi ya hayo, na wapinga Kristo.
Watu wanapoamini katika Mungu kwenye ukumbi wa dini kama huu—ambao ni mali ya Shetani na unatawaliwa na kudhibitiwa na mapepo na wapinga Kristo—wanaweza tu kuelewa mafundisho ya dini, wanaweza tu kufuata sherehe za kidini na kanuni, na kamwe hawatawahi kuuelewa ukweli, kamwe hawatawahi kuipitia kazi ya Mungu, na kwa kikamilifu hawawezi kuokolewa. Hii ni bila shaka. Kwa kuwa hakuna jambo lolote la kazi ya Roho Mtakatifu katika kumbi za kidini, na ni maeneo ambayo yanamkera Mungu, ambayo yanachukiwa na Mungu, na yanashutumiwa na kulaaniwa na Yeye. Mungu hajawahi kuitambua dini, wala hajawahi kuisifu, na kutoka wakati wa Yesu jamii ya kidini imekuwa ikishutumiwa na Mungu. Hivyo, unapoamini katika Mungu lazima upate mahali palipo na kazi ya Roho Mtakatifu; haya tu ndiyo makanisa ya kweli, na ni katika makanisa ya kweli pekee ndiyo utaweza kusikia sauti ya Mungu, na kugundua nyayo za kazi ya Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo njia ambayo Mungu Anatafutwa.
kutoka kwa "Athari za Kuelewa Ukweli kwa Uhalisi" katika Kumbukumbu za Kihistoria za Ushirika na Mipangilio ya Kazi ya Kanisa (I)

Jumatatu, 3 Juni 2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya ndani yao ni kule tu kufanya kazi na pamoja na kupanua kile ambacho tayari kimo ndani yao. Wawe ni manabii au binadamu wanaotumiwa na Mungu kutoka kwa enzi zilizopita, hakuna yeyote anayeweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.” “Kwani kiini cha binadamu ni tofauti na kile cha Mungu. Binadamu hawezi kamwe kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, sembuse kuwa Mungu. Kile ambacho Roho Mtakatifu anamwelekeza binadamu kuishi kwa kudhihirisha ni kulingana tu na kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu.”
Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezuiliwa bila ya kuachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo tabia ya binadamu, baada ya kutengenezwa na Shetani, inaendelea kuongezeka kuwa potovu. Mtu anaweza kusema kwamba binadamu huishi daima na tabia yake potovu ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa sababu ya hili, kama binadamu anataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe kujidai kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na tabia ya Shetani. Vinginevyo, upendo wa binadamu ni upendo usio safi, ni upendo wa Shetani, na ule ambao hauwezi kabisa kupokea idhini ya Mungu. Kama binadamu hakamilishwi, kushughulikiwa, kuvunjwa, kupogolewa, kufundishwa nidhamu, kuadibiwa, au kusafishwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja, hakuna yeyote anayeweza kumpenda Mungu kwa kweli. Ukisema kwamba sehemu ya tabia yako inamwakilisha Mungu na hivyo basi unaweza kumpenda Mungu kwa kweli, basi wewe ndiwe unayezungumza maneno ya kiburi na ni binadamu wa upuuzi. Binadamu kama hao ni malaika mkuu! Asili ya ndani ya binadamu haiwezi kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja. Lazima binadamu aiondoe asili yake ya ndani kupitia kwa ukamilifu wa Mungu, na kisha kupitia kutunza na kutosheleza mapenzi ya Mungu tu, na hata zaidi kupitia kwa kazi ya Roho Mtakatifu, ndipo kuishi kwa kudhihirishwa kwake kunaweza kuidhinishwa na Mungu. Hakuna anayeishi katika mwili anayeweza kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja isipokuwa kama yeye ni binadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, hata kama huyu, tabia yake na kile anachoishi kwa kudhihirisha chote hakiwezi kuchukuliwa kwamba kinamwakilisha Mungu kabisa; inaweza kusemekana tu kwamba kile anachoishi kwa kudhihirishwa kinatawaliwa na Roho Mtakatifu. Tabia ya mtu kama huyo haiwezi kumwakilisha Mungu.
Ingawa tabia ya binadamu inaamrishwa na Mungu—hili halina shaka na linaweza kuchukuliwa kama jambo zuri—limetengenezwa na Shetani. Hiyo ndiyo maana tabia zote za binadamu kwa kweli ni tabia ya Shetani. Mtu anaweza kusema kuwa Mungu, katika tabia yake, ni mnyofu katika kutekeleza mambo, na kwamba yeye pia anatenda kwa njia hii; yeye pia an tabia kama hii, na hivyo basi anasema kwamba tabia yake inamwakilisha Mungu. Huyu ni binadamu wa aina gani? Je, tabia potovu ya kishetani inaweza kumwakilisha Mungu? Yeyote yule anayetangaza kwamba tabia yake ni wakilishi kwa Mungu, huyo mtu anamkufuru Mungu na kumtukana Roho Mtakatifu! Tukiangalia namna ambavyo Roho Mtakatifu hufanya kazi, kazi ambayo Mungu anafanya hapa ulimwenguni ni kwa ajili ya kushinda pekee. Hii ndiyo maana, nyingi ya tabia potovu za kishetani za binadamu bado hazijatakaswa, na ndiyo maana mienendo ya maisha ya binadamu bado ni taswira ya Shetani. Ndicho binadamu huamini kuwa chema a na kinawakilisha vitendo vya mwili wa binadamu au kwa usahihi zaidi, kinawakilisha Shetani na hakiwezi kumwakilisha Mungu kabisa. Hata kama binadamu tayari anampenda Mungu hadi kufikia kiwango ambacho anaweza kufurahia maisha ya mbinguni hapa ulimwenguni, anaweza kutamka kauli kama vile: “Eh Mungu! Siwezi kukupenda vya kutosha,” na kwamba amefikia eneo la juu zaidi, huwezi kusema kwamba anaishi kwa kumdhihirisha Mungu au kumwakilisha Mungu, kwani kiini cha binadamu ni tofauti na kile cha Mungu. Binadamu hawezi kamwe kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, sembuse kuwa Mungu. Kile ambacho Roho Mtakatifu anamwelekeza binadamu kuishi kwa kudhihirisha ni kulingana tu na kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu.

Jumamosi, 1 Juni 2019

Swahili Gospel Video "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (7) - Je, Kufanya Kazi Ngumu Kunamaanisha Tunafuata Mapenzi ya Baba wa Mbinguni?

Swahili Gospel Video "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (7) - Je, Kufanya Kazi Ngumu Kunamaanisha Tunafuata Mapenzi ya Baba wa Mbinguni?

Waumini wengine wa Bwana hufikiria kwamba yote tunayohitaji kufanya ni kuteseka na kulipa gharama ya kueneza injili ya Bwana, kubeba msalaba ili kumfuata Bwana, na kutenda unyenyekevu, subira na uvumilivu, na kwamba kwa kufanya mambo haya yote tunafuata mapenzi ya Baba wa mbinguni, na pia wao huamini kwamba kila mara tukifuatilia imani yetu kwa njia hii, basi hatimaye tutaokolewa na Mungu na kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele. Lakini je, ni sahihi kuwa na ufahamu wa aina hii na kutenda kwa njia hii? Bwana Yesu alisema, "Wengi wataniita siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujafanya unabii kwa jina lako? na kwa jina lako kutoa pepo? na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Halafu nitasema wazi kwao, Sikuwajua nyinyi kamwe: ondokeni mbele yangu, nyinyi watenda maovu" (Mathayo 7:22-23). Kwa nini watu hawa ambao huhubiri na kufanya kazi kwa bidii kwa jina la Bwana hawataingia katika ufalme wa mbinguni pekee, lakini pia wataadhibiwa na Bwana?
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Ijumaa, 31 Mei 2019

“Sauti Nzuri Ajabu” – Hukumu ya Mungu ya Siku za Mwisho Ni Wokovu kwa Mwanadamu | Filamu za Injili (Movie Clip 5/5)


“Sauti Nzuri Ajabu” – Hukumu ya Mungu ya Siku za Mwisho Ni Wokovu kwa Mwanadamu | Filamu za Injili (Movie Clip 5/5)

Baadhi ya watu husoma maneno ya Mungu na kuona kwamba kunayo mambo makali ambayo ni hukumu ya wanadamu, na shutuma na laana. Wanafikiria kwamba kama Mungu huhukumu na kulaani watu, nao pia hawatashutumiwa na kuadhibiwa? Inawezaje kusemekana kwamba aina hii ya hukumu ni ya kutakasa na kuokoa wanadamu? Maneno ya Mungu yanasema: "Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu." "Ufichuzi mkali wa neno ni kwa kusudi la kukuongoza kwenye njia sahihi" (Neno Laonekana katika Mwili). Ni njia gani nzuri ya kufahamu kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho?
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.