Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Alhamisi, 28 Februari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya "Wingu Jeupe"

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya "Wingu Jeupe"

Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe katika siku za mwisho (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho.”
Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani aweze kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamemtamani sana na kumwonea shauku kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, kwa Yesu Mwokozi kuwarudia watu ambao Amekuwa mbali nao kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumai kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atazisamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Anatamani Yesu Mwokozi awe jinsi Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi ambaye anapendeka, mwema na wa heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe katika siku za mwisho (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu hafahamu jambo hili: Ingawa Mwokozi Yesu mtakatifu Amejawa na upendo na mapenzi kwa mwanadamu, Angewezaje kufanya kazi katika “mahekalu” yaliyomilikiwa na uchafu na pepo wachafu? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Angewezaje kuwaonekania wale wanaokula mwili wa wasio na haki, kunywa damu ya wasio na haki, kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini lakini hawamfahamu, na wanaompokonya kila wakati? Mwanadamu anajua tu kuwa Yesu Mwokozi amejawa na upendo na huruma, naye ni sadaka ya dhambi iliyojawa na ukombozi. Lakini mwanadamu hana habari kwamba Yeye pia ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, uadhama, ghadhabu, na hukumu, na Aliye na mamlaka na kujawa na hadhi. Kwa hiyo ingawa mwanadamu anazamia kwa hamu na kuonea shauku kurudi kwa Mkombozi, na hata Mbingu inaguswa kwa maombi ya mwanadamu, Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.
“Yehova” ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. “Yesu” ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Uyahudi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa Wayahudi wote. Na hivyo katika enzi ya sasa, Wayahudi wote isipokuwa kabila la Yuda wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu, na kumtumikia wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani katika hekalu. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, nalo lilikuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataitamatisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka katika miisho ya dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.
Mwokozi atakapofika katika siku za mwisho, kama bado angeitwa Yesu, na kuzaliwa mara nyingine katika Uyahudi, na kufanya kazi Yake katika Uyahudi, basi hii ingethibitisha kuwa Niliumba Wayahudi peke yao na kuwakomboa Wayahudi peke yao, na kuwa Sina uhusiano wowote na Mataifa. Je, hii haitakuwa kinyume cha maneno Yangu kwamba “Mimi ni Bwana aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote”? Nilitoka Uyahudi nami Nafanya kazi Yangu kati ya Mataifa kwa sababu Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, ila Mungu wa viumbe vyote. Ninaonekana kati ya Mataifa katika siku za mwisho kwa sababu Mimi si Yehova, Mungu wa Wayahudi tu, lakini, zaidi ya hayo, kwa sababu Mimi ni Muumba wa wateule Wangu wote kati ya Mataifa. Sikuumba Uyahudi, Misri, na Lebanoni pekee, bali pia Niliumba Mataifa yote mbali na Israeli. Na kwa sababu hiyo, Mimi ni Bwana wa viumbe vyote. Nilitumia Uyahudi tu kama hatua ya kwanza ya kazi Yangu, Nikayatumia Uyahudi na Galilaya kama ngome za kazi Yangu ya ukombozi, nami Natumia Mataifa kama msingi ambao Nitatumia kuitamatisha enzi nzima. Nilifanya hatua mbili za kazi katika Uyahudi (hatua mbili za kazi ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema), nami Nimekuwa Nikitekeleza hatua mbili zaidi za kazi (Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme) katika nchi nyingine zote zaidi ya Uyahudi. Nitafanya kazi ya kushinda kati ya Mataifa, na hivyo kuikamilisha enzi. Mwanadamu akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa Nimeianza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa shauku kuwasili kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao wale wasioniamini. Wao ni watu ambao hawanijui, na imani yao Kwangu ni ya bandia. Je, watu kama hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja si kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani maangamizo Yangu ya dunia hii nzee yenye uchafu, lakini badala yake wanatamani kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili, ndipo watakapokombolewa; wanamtazamia Yesu kuwakomboa wanadamu wote mara nyingine kutoka nchi hii iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu kama hao watawezaje kuwa wale wanaoikamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Matamanio ya mwanadamu hayawezi kufikia mapenzi Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu hutamani au kuthamini tu kazi ambayo Nimeifanya hapo awali, naye hajui kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya siku zote na si mzee kamwe. Mwanadamu anajua tu kuwa Mimi ni Yehova, na Yesu, naye hana fununu kuwa Mimi ni Mwisho, Yule ambaye Atawaangamiza wanadamu. Mwanadamu anachotamani na kujua tu ni kuhusu dhana yake mwenyewe, nayo ni yale tu ambayo anaweza kuyaona kwa macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayoifanya, bali hayatangamani nayo. Kama kazi Yangu ingefanywa kulingana na mawazo ya mwanadamu, basi ingeisha lini? Mwanadamu angeingia katika pumziko lini? Nami Ningewezaje kuingia katika siku ya saba, Sabato? Nafanya kazi kulingana na mpango Wangu, kulingana na lengo Langu, na sio kulingana na nia ya mwanadamu.

Jumatano, 27 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Ikiwa watu wanaweza kweli kuielewa kikamilifu njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Wasingetamani tena kuwatumikia wazazi wao ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Je, mategemeo ya baadaye na majaliwa ya mwanadamu si kabisa kile kinachodaiwa nyakati za sasa kuwa “wazazi” wa Petro? Yamekuwa kama tu mwili na damu ya mwanadamu. Je, hatima, mategemeo ya baadaye ya mwili yatakuwa ni kumwona Mungu wakati ukiwa hai, au kwa roho kukutana na Mungu baada ya kifo? Je, mwili kesho utaishia katika tanuu kubwa kama katika taabu, au utakuwa katika kuteketezwa kwa moto? Je, maswali kama haya yanayohusu iwapo mwili wa mwanadamu utahimili taabu au mateso ni habari kubwa sana ambayo kila mtu sasa katika mkondo huu ambaye ana ubongo na akili yake iko sawa anahangaika zaidi nayo? (Hapa, kuhimili mateso hurejelea kupokea baraka; kuteseka humaanisha kwamba majaribu ya siku zijazo ni yenye manufaa kwa hatima ya mwanadamu. Taabu hurejelea kushindwa kusimama imara, au kudanganywa; au, humaanisha kwamba mtu anakabiliana na hali ya hatari ya bahati mbaya katikati ya majanga na maisha yake yanakuwa magumu kuendelea nayo, na kwamba hakuna hatima nzuri kwa roho.) Watu wanajitayarisha na mantiki timamu lakini pengine kile wanachofikiri hakifanani kabisa na kile ambacho mantiki yao inapaswa kutayarishwa nayo. Hii ni kwa sababu ni wajinga kiasi na wanafuata vitu bila kufikiri. Wote wanapaswa kuwa na uelewe wa kina wa kile ambacho wanapaswa kuingia kwacho, na kwa mahususi wanapaswa kutatua kile wanachopaswa kuingia kwacho wakati wa mateso (yaani, wakati wa utakasaji wa tanuu), na kile wanachopaswa kutayarishwa nacho katika jaribu la moto. Usiwatumikie wazazi wako siku zote (kumaanisha mwili) ambao ni sawa na nguruwe na mbwa, na ni wabaya zaidi kuliko chungu na wadudu. Kuna haja gani ya kuteseka juu ya hilo, kufikiri sana, kuutesa ubongo wako? Mwili si wako, bali upo katika mikono ya Mungu ambaye Hakudhibiti wewe pekee bali pia Anamwamuru Shetani. (Kwa asili ilimaanisha kuwa ulikuwa wa Shetani. Kwa kuwa Shetani pia yupo mikononi mwa Mungu, ingeweza kuwekwa hivyo tu. Maana inashawishi zaidi kusema namna hiyo—inamaanisha kuwa wanadamu hawapo chini ya miliki ya Shetani kabisa, bali wapo mikononi mwa Mungu.) Unaishi chini ya mateso ya mwili, lakini je, mwili ni wako? Upo chini ya udhibiti wako? Kwa nini usumbuke kufikiri sana juu ya hilo? Kwa nini usumbuke sana kumsihi Mungu kwa ajili ya mwili wako uliooza ambao umeshahukumiwa zamani sana na kulaaniwa, vilevile kutiwa najisi na roho wachafu? Kwa nini usumbuke siku zote kwa kushikilia washirika wa Shetani karibu na moyo wako? Huna wasiwasi kwamba mwili unaweza kuharibu mategemeo yako halisi ya baadaye, matumaini mazuri, na hatima ya kweli ya maisha yako?
Njia ya leo si rahisi kuitembea. Mtu anaweza kusema kwamba ni vigumu kuipitia na ni adimu sana katika enzi zote. Hata hivyo, nani angeweza kufikiri kuwa mwili wa mwanadamu pekee unatosha kumwangamiza mara moja? Kazi leo hakika ni ya thamani kama vile mvua wakati wa majira ya kuchipua na ni ya thamani kama wema wa Mungu kwa mwanadamu. Hata hivyo, ikiwa mwanadamu hajui kusudi la kazi Yake leo au kuelewa kiini cha mwanadamu, inawezekanaje tunu na thamani yake vizungumziwe? Mwili si wa wanadamu wenyewe, hivyo kwa kweli hakuna mtu anayeweza kuona waziwazi hatima yake itakuwa wapi. Hata hivyo, unapaswa kujua vizuri kwamba Mungu wa uumbaji Atawarudisha binadamu, ambao waliumbwa, katika nafasi yao ya asili, na kurejesha sura yao ya asili kutoka wakati wa kuumbwa kwao. Atachukua tena kikamilifu pumzi Aliyompuliza ndani ya binadamu, na kuchukua tena mifupa na mwili wake na kurudisha vyote kwa Bwana wa viumbe. Atabadilisha na kufanya upya binadamu kikamilifu, na kuchukua tena kutoka binadamu urithi wote ambao kwa asili haukuwa wa binadamu, bali ulikuwa wa Mungu. Hatamkabidhi tena binadamu urithi huo. Maana hakuna hata kitu kimoja kati ya hivyo vilikuwa vya binadamu kwa asili. Atavichukua vyote tena—huu si uporaji usio wa haki, bali unakusudiwa kuirejesha mbingu na dunia katika hali yake ya asili, na kubadilisha na kumfanya upya binadamu. Hii ni hatima inayofaa kwa mwanadamu, ingawa pengine si kuichukua tena baada ya kuuadibu mwili kama watu wanavyofikiri. Mungu hataki mifupa ya mwili baada ya maangamizi yake, bali vitu vya asili katika mwanadamu ambavyo mwanzo vilikuwa vya Mungu. Hivyo, hatawaangamiza binadamu au kuuondoa kabisa mwili wa binadamu, maana mwili wa binadamu si mali binafsi ya mwanadamu. Badala yake, ni kiungo cha Mungu, ambaye anasimamia binadamu. Angewezaje kuuangamiza mwili wa binadamu ili Yeye “afurahi”? Je, wakati huu, kwa kweli umeachana na kila kitu cha huo mwili wako ambao hauna thamani hata ya senti moja? Kama ungeweza kuelewa asilimia thelathini ya kazi ya siku za mwisho (asilimia thelathini tu, yaani, kuifahamu kazi ya Roho Mtakatifu leo, vilevile kazi ya neno Mungu hufanya katika siku za mwisho), basi usingeweza kuendelea “kuutumikia” au “kuwa” na upendo kwa mwili wako kama unavyofanya leo, ambao umepotoka kwa miaka mingi. Unapaswa kuelewa kwa kina kwamba binadamu sasa wameendelea kwa hali ambayo haijawahi kutokea na hawataendelea tena kusonga mbele kama magurudumu ya historia. Mwili wako wa udongo umeshafunikwa na nzi tangu zamani, hivyo unawezaje kuwa na nguvu ya kurudisha nyuma magurudumu ya historia ambayo Mungu ameyawezesha kuendelea hadi siku hii ya leo? Unawezaje kufanya saa ya siku za mwisho ambayo ni kama bubu ipige tena na kuendelea kusogeza mikono yake kwa upande wa kulia? Unawezaje kuubadilisha upya ulimwengu ambao unaonekana kama umefunikwa na ukungu mzito? Je, mwili wako unaweza kufufua milima na mito? Je, mwili wako, ambao una kazi ndogo tu, unaweza kweli kurejesha ulimwengu wa binadamu ambao umekuwa ukiutamani? Unaweza kweli kuwaelimisha wadhuria wako kuwa “binadamu”? Unaelewa sasa? Mwili wako unamilikiwa na nini hasa? Makusudi halisi ya Mungu ya kumfinyanga mwanadamu, ya kumkamilisha mwanadamu, na ya kumbadilisha mwanadamu hayakuwa kukupatia nchi nzuri ya asili au kuleta pumziko la amani kwa mwili wa mwanadamu. Badala yake, ilikuwa ni kwa ajili ya utukufu Wake na ushuhuda Wake, kwa furaha bora ya binadamu hapo baadaye, na ili kwamba hivi karibuni waweze kufurahia pumziko. Bado, si kwa ajili ya mwili wako, maana mwanadamu ni mtaji wa usimamizi wa Mungu na mwili wa mwanadamu ni kiungo tu. (Mwanadamu ni kitu chenye roho na mwili, wakati mwili ni kitu kiharibikacho tu. Hii humaanisha kwamba mwili ni chombo kwa ajili ya mpango wa usimamizi.) Unapaswa kujua kwamba kuwakamilisha wanadamu, kuwatimiza wanadamu, na kuwapata wanadamu hakujaleta kitu chochote zaidi ya mapanga na maangamizi kwa mwili wao, na kumeleta mateso yasiyokoma, kuungua kwa moto, hukumu zisizokuwa na huruma, kuadibu, na laana, na vilevile majaribu yasiyokuwa na mipaka. Hicho ni kisa cha ndani na ukweli wa kazi ya kumsimamia binadamu. Hata hivyo, vitu hivi vyote vimelengwa dhidi ya mwili wa binadamu, na mikuki yote ya uhasama bila huruma inaelekezwa kwenye mwili wa binadamu (maana kwa asili binadamu hakuwa na hatia). Hayo yote ni kwa ajili ya utukufu na ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake. Hii ni kwa sababu kazi Yake si tu kwa ajili ya binadamu, bali ni kwa ajili ya mpango wote na kutimiza mapenzi Yake ya asili Alipomuumba binadamu. Kwa hiyo, pengine asilimia tisini ya kile ambacho watu wanapitia ni mateso na majaribu ya moto, lakini kuna siku chache sana tamu na za furaha au hata hakuna kabisa ambazo mwili wa mwanadamu umekuwa ukitamani, na hata hawawezi kufurahia nyakati za furaha katika mwili wakishinda jioni nzuri pamoja na Mungu. Mwili ni mchafu, hivyo kile ambacho mwili wa mwanadamu unakiona au unakifurahia si chochote bali ni adabu ya Mungu ambayo haipendwi na mwanadamu, na ni kana kwamba ulikuwa unakosa mantiki ya kawaida. Hii ni kwa sababu Atadhihirisha tabia Yake ya haki ambayo haipendwi na mwanadamu, haivumilii makosa ya mwanadamu, na huchukia kabisa maadui. Mungu hufichua waziwazi tabia Yake yote kupitia njia yoyote iwezekanayo, na hivyo Akihitimisha kazi ya vita Vyake na Shetani vya miaka elfu sita—kazi ya wokovu wa binadamu wote na maangamizi ya Shetani wa zamani!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 26 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili. Kwa hivyo ingawa wale Waisraeli walinipigilia misumari msalabani hadharani, wao, ambao wamekuwa wanamngoja Masiha na Yehova na kumtamani sana Mwokozi Yesu, hawajasahau ahadi Yangu. Hii ni kwa sababu Sijawatelekeza. Hata hivyo, Nilikuwa nimechukua damu kama ushahidi wa agano Nililoanzisha na mwanadamu. Ukweli huu umekuwa "damu ya agano" lililoandikwa katika mioyo ya watu wachanga na wasio na hatia, kana kwamba lilichapiliwa, na kama kuishi kwa pamoja kwa amani kwa mbingu na dunia milele. Sijawahi kuzidanganya nafsi hizo za huzuni Nilizoziokoa, kuzipata, na ambazo hunipenda zaidi ya yule mwovu baada ya Mimi kuzijaalia na kuzichagua. Kwa hiyo, kwa shauku zinatazamia kurudi Kwangu na kwa hamu zinatarajia kukutana na Mimi. Kwa kuwa Sijawahi kufuta agano Nililoanzisha nazo kwa damu, si ajabu kwamba zimekuwa zikisubiri kwa hamu. Nitawateka tena wanakondoo hawa ambao wamepotea kwa miaka, kwa maana siku zote Nimewapenda mwanadamu. Ni kwamba tu dalili za uovu zimeongezwa kwa wema katika wanadamu. Nitazipata zile nafsi hafifu ambazo zinanipenda na ambazo Nimezipenda tayari, lakini Nawezaje kuwaleta wale waovu ambao hawajawahi kunipenda na wametenda kama adui ndani ya nyumba Yangu? Sitawaleta wazawa wa Shetani na nyoka mwenye sumu kali ambao hunichukia, hunipinga, hunikataa, hunishambulia, na kunilaani ndani ya ufalme Wangu, hata ingawa Nimeanzisha agano la damu na mwanadamu. Unapaswa kujua kwa nini na kwa ajili ya nani Ninatekeleza kazi hiyo. Je, ni wema au uovu katika upendo wako? Je, kwa kweli unanijua kama vile walivyonijua Daudi na Musa? Je, kwa kweli unanihudumia kama vile alivyonihudumia Ibrahimu? Ni kweli kwamba unafanywa kamili na Mimi, lakini unapaswa kujua hili: Ni nani utakayemwakilisha? Utakuwa na matokeo sawa na nani? Katika maisha yako, una mavuno ya furaha na mengi katika kupata uzoefu kunihusu? Je, ni mengi na yenye matokeo mazuri? Unapaswa kujichunguza mwenyewe. Kwa miaka umefanya kazi kwa bidii kwa ajili Yangu, lakini umewahi kupata chochote? Umebadili au kupata kitu chochote? Badala ya uzoefu wako katika shida, je, unakuwa kama Petro ambaye alisulubiwa, au kama Paulo ambaye alibwagwa na kupokea mwanga mkubwa? Unapaswa kuwa na ufahamu wa haya. Mimi sizungumzi siku zote juu ya, na kufikiria kuhusu maisha yako ambayo ni madogo kuliko mbegu ya haradali, ambayo ni ukubwa wa punje ya mchanga. Kusema kweli, ni mwanadamu ambaye Ninasimamia. Hata hivyo, Sifikirii maisha ya mwanadamu, ambaye wakati mmoja Nilimchukia lakini baadaye Nikamwinua tena, kama sehemu muhimu ya usimamizi Wangu. Unapaswa kuwa mwenye uhakika juu ya utambulisho wako wa zamani kwa kweli ulikuwa upi, na ni nani mliyemtumikia kama watumwa. Kwa hiyo, Situmii nyuso za wanadamu kama ya Shetani kama mali ghafi kuwasimamia, kwa kuwa wanadamu si vitu vya thamani. Mnapaswa kukumbuka mtazamo Wangu kwenu hapo mwanzoni, na hotuba Yangu kwenu wakati huo ambayo haikuwa bila umuhimu wa utendaji. Unapaswa kujua kwamba zile "kofia" juu ya vichwa vyenu zina msingi. Ninadhani kwamba nyote mnajua kwamba hamkuwa wa Mungu kwa asili, lakini mlikamatwa na Shetani zamani na kutumikia nyumbani kwake kama watumishi waaminifu. Mmenisahau kwa muda mrefu, kwani kwa muda mrefu mmekuwa nje ya nyumba Yangu lakini mikononi mwa yule mwovu. Wale ambao Mimi huokoa ni wale ambao Nimewaamulia kabla zamani na wamekombolewa na Mimi, wakati ninyi ni nafsi hafifu ambazo zimewekwa kati ya wanadamu kama jambo la pekee. Mnapaswa kujua kwamba nyinyi si wa nyumba ya Daudi au Yakobo, lakini ni wa nyumba ya Moabu, ambao ni wanachama wa kabila la Mataifa. Kwa maana Sikuanzisha agano na nyinyi, lakini Nilitekeleza tu kazi na kunena kati yenu, na kuwaongoza. Damu Yangu haikumwagika kwa ajili yenu. Nilitekeleza tu kazi kati yenu kwa ajili ya ushuhuda Wangu. Je, hamjajua hilo? Je, kazi Yangu kweli ni kama Yesu kumwaga damu hadi kufa kwa niaba yenu? Haikuwa na thamani kwamba Nilivumilia fedheha kubwa kwa ajili yenu. Mungu, ambaye hana dhambi kabisa, kwa kweli Alikuja pahali ambapo ni kama pahali pa mbwa na nguruwe, ambapo panachukiza kabisa na kukirihi, na hapawezi kukalika na mwanadamu. Hata hivyo, Nilivumilia hii aibu yote ya ukatili kwa ajili ya utukufu wa Baba Yangu na kwa ajili ya ushuhuda wa milele. Mnapaswa kujua mienendo yenu na kuona kwamba nyinyi si watoto waliozaliwa katika "familia tajiri na yenye nguvu" bali watoto fukara tu wa Shetani. Nyinyi si waanzilishi kati ya wanadamu, na hamna haki za kibinadamu au uhuru. Kwa asili, hamkuwa na mgao wowote kabisa la baraka kutoka kwa binadamu au ufalme wa mbinguni. Hili ni kwa sababu mko chini kabisa ya binadamu katika wanadamu, na Sijawahi kufikiria kuhusu wakati wenu ujao. Kwa hivyo, ingawa ilikuwa sehemu ya asili ya mpango Wangu kwamba leo Ningekuwa na imani kuwakamilisha, ni kazi ya pekee, kwa sababu hadhi yenu ni ya chini sana na kiasili hamkuwa na mgawo katika binadamu. Je, hii si baraka kwa wanadamu?
Wale Ninaowaokoa ni nafsi ambazo Nilizitoa kutoka toharani zamani, na waliochaguliwa ambao Nilitembelea zamani, kwa kuwa wametamani sana kuonekana Kwangu tena kati yao. Wamenipenda, na wameandika agano Langu ambalo Nilianzisha kwa damu katika mioyo yao, kwa sababu Nimewapenda. Wao ni kama kondoo waliopotea ambao wamekuwa wakinitafuta kwa miaka mingi, na wao ni wazuri, na kwa hivyo Ninawaita Waisraeli wazuri na malaika wadogo wanaopendeza. Singepitia aibu kama hii iwapo Ningekuwa miongoni mwao. Ni kwa sababu wananipenda zaidi kuliko wanavyopenda maisha yao wenyewe, na Ninawapenda kama kile ambacho ni kirembo zaidi kati ya vitu vyote. Ni kwa sababu waliumbwa na Mimi na ni Wangu; hawajawahi kunisahau. Upendo wao unazidi upendo wenu, na wananipenda kwa upendo mkubwa zaidi kuliko mnavyopenda maisha yenu wenyewe. Wananitii Mimi kama vile njiwa wadogo weupe hufanyia anga, na kwa upendo mkubwa zaidi kuliko mnavyonifanyia. Na ni kwa sababu wao ni wazawa wa Yakobo, watoto wa Adamu, na ni miongoni mwa wateule Wangu, kwa kuwa Nimewapenda zamani, na hata zaidi kuliko Ninavyowapenda, na kwa sababu nyinyi ni waasi sana, upinzani wenu ni mkubwa sana, mnaniangalia kwa dharau sana, hamnithamini hata kidogo Kwangu, mnanipenda kidogo sana, na mnanichukia sana. Mnadharau kazi Yangu, na kutweza vitendo Vyangu sana. Tofauti na wao, hamjawahi kuona matendo Yangu kuwa kitu cha thamani. Badala yake, mnayadharau na macho mekundu ya wasiwasi, kama tu Shetani. Utiifu wenu uko wapi? Tabia zenu ziko wapi? Upendo wenu uko wapi? Ni lini mmeonyesha wazi dalili ya upendo ndani yenu? Ni lini mmechukua kazi Yangu kwa uzito kabisa? Hurumia wale malaika wa kupendeza ambao kwa wasiwasi wananitazamia na kuteseka sana wakati wanaponisubiri kwa wasiwasi, kwani Ninawapenda kwa dhati. Hata hivyo, kile Ninachokiona leo ni ulimwengu usio wa kibinadamu sana ambao hauhusiani nao. Je, hamfikirii kuwa dhamiri zenu zilikuwa zisizojali na zisizo na huruma muda mrefu uliopita? Je, hamfikirii kuwa nyinyi ndio watu duni mnaozuia kurudiana Kwangu na malaika wa kupendeza? Ni lini hawajakuwa wakisubiri kurudi Kwangu? Ni lini hawajakuwa wakisubiri kuungana tena na Mimi? Je, ni lini hawajatarajia kushinda kwa siku nzuri na kula pamoja na Mimi? Je, mliwahi kutambua kwamba kile mfanyacho leo—yaani, kufanya ghasia ulimwenguni, kupanga njama dhidi ya nyinyi kwa nyinyi, kudanganyana, kutenda kwa uongo, kwa siri na kwa ukavu wa macho, kutojua ukweli, kuwa wasio waaminifu na wadanganyifu, kutenda ubembelezaji, nyinyi kujiona daima kuwa waadilifu na bora zaidi kuliko wengine, kuwa wenye kiburi, na kutenda kikatili kama wanyama wa mwitu milimani na kwa fujo kama mfalme wa wanyama—uko wapi mfano wa mwanadamu? Nyinyi ni fidhuli na wasio na busara. Hamjawahi kuliona neno Langu kuwa hazina, lakini badala yake mmechukua mtazamo wa dharau. Kwa njia hii, mafanikio, maisha ya kweli ya binadamu, na matumaini mazuri yangetoka wapi? Je, wazo lako badhirifu litakuokoa kwa kweli kutoka kwa kinywa cha chui? Kweli litakuokoa kutoka kwa moto unaowaka? Je, ungekuwa umeanguka hadi hapa iwapo kwa kweli ungeiona kazi Yangu kuwa kitu cha thamani kubwa mno? Inaweza kuwa kwamba majaliwa yako kweli hayawezi kubadilishwa? Je, uko tayari kufa na majuto kama haya?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 25 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Katika miaka hii miwili hadi mitatu ya kazi, kile kilichopaswa kutimizwa katika kazi ya hukumu iliyofanyika juu yenu kimetimizwa kimsingi. Watu wengi wamesahau matarajio na kudura yao ya baadaye. Hata hivyo, inapotajwa kuwa ninyi ni uzao wa Moabu, wengi wenu huchukizwa sana—nyuso zenu hubadilika, vinywa vyenu hupinda, na macho yenu hukodolea. Hamuwezi kabisa kuamini kwamba ninyi ni uzao wa Moabu. Moabu ilifukuzwa hadi nchi hii baada ya kulaaniwa. Ukoo wa wana wa Moabu umerithishwa mpaka leo, na ninyi nyote ni uzao wake. Hakuna kitu ambacho Ninaweza kufanya—nani aliyekusababisha uzaliwe katika nyumba ya Moabu? Ninakuhurumia na Siko radhi uwe hivi, lakini ukweli hauwezi kubadilishwa na watu. Wewe ni uzao wa Moabu, na Siwezi kusema kuwa wewe ni uzao wa Daudi. Haijalishi wewe ni uzao wa nani, bado wewe ni mmoja wa viumbe. Ni kwamba tu wewe ni kiumbe wa cheo cha chini—wewe ni kiumbe wa kuzaliwa katika hali duni. Viumbe vyote lazima vipitie kazi yote ya Mungu, vyote ni vyombo vya kushinda Kwake, na lazima vyote viione tabia Yake yenye haki, na kupitia hekima na kudura Yake. Sasa wewe ni uzao wa Moabu na lazima uikubali hukumu hii na kuadibu, hivyo kama hungekuwa uzao wa Moabu, basi pia hungehitaji kukubali hukumu na kuadibu huku? Unapaswa kutambua hili! Kwa kweli, kufanya kazi kwa uzao wa Moabu kwa sasa ni kwa thamani sana na kwenye umuhimu sana. Maadam kazi imefanywa kwenu, ina umuhimu mkubwa mno. Kama kazi ingefanywa kwa uzao wa Hamu haingeweza kuwa muhimu kwa sababu wao hawajazaliwa katika hali duni kama hiyo na kuzaliwa kwao sio sawa na Moabu. Uzao wa mwana wa pili wa Nuhu Hamu umelaaniwa tu—hawakuja kutokana na uasherati. Ni kwamba tu wao ni wa hali ya chini, kwa sababu Nuhu aliwalaani na wao ni watumishi wa watumishi. Wanayo hali ya chini, lakini thamani yao ya asili haikuwa chini. Tukizungumza kuhusu Moabu, watu wanajua kwamba awali alikuwa na hali ya chini kwa sababu alizaliwa kutokana na uasherati. Ingawa nafasi ya Loti ilikuwa ya juu sana, Moabu alizaliwa na Lutu na binti yake. Ingawa Loti alikuwa mtu mwenye haki, Moabu bado alikuwa chombo cha laana. Moabu alikuwa wa thamani ya chini na alikuwa na cheo cha chini, na hata kama hakuwa amelaaniwa alikuwa wa uchafu, hivyo alikuwa tofauti na Hamu. Hakukubali na alipinga, aliasi dhidi ya Yehova, ndiyo sababu alianguka katika maeneo yenye giza zaidi. Kufanya kazi sasa kwa uzao wa Moabu ni kuwaokoa wale ambao wameanguka katika giza zaidi. Ingawa walikuwa wamelaaniwa, Mungu yuko tayari kupata utukufu kutoka kwao. Hii ni kwa sababu hapo awali, wote walikuwa watu waliomkosa Mungu mioyoni mwao—kuwafanya tu kuwa wale wanaomtii na kumpenda Yeye ni ushindi wa kweli, na matunda hayo ya kazi ni ya thamani sana na yenye kuridhisha zaidi. Huku tu ni kupata utukufu—huu ndio utukufu ambao Mungu anataka kuupata katika siku za mwisho. Ingawa watu hawa ni wa nafasi ya chini, sasa wanaweza kupata wokovu mkubwa mno, ambao kwa kweli ni kupandishwa hadhi na Mungu. Kazi hii ni ya maana sana, na ni kwa njia ya hukumu ndipo Anawapata watu hawa. Yeye hawaadhibu kwa makusudi, lakini Amekuja kuwaokoa. Kama bado angekuwa Anafanya kazi ya kushinda katika Israeli wakati wa siku za mwisho ingekuwa ni bure; hata kama ingezaa matunda, haingekuwa na thamani yoyote au umuhimu wowote mkubwa, na Yeye hangeweza kupata utukufu wote. Anafanya kazi kwenu, yaani, wale ambao wameanguka katika maeneo yenye giza zaidi, wao walio nyuma zaidi kimaendeleo. Watu hawa hawakiri kuwa kuna Mungu na kamwe hawajapata kujua kwamba kuna Mungu. Viumbe hawa wamepotoshwa na Shetani hadi kiwango ambapo wamemsahau Mungu. Wamepofushwa na Shetani na hawajui kabisa kwamba kuna Mungu mbinguni. Katika mioyo yenu nyote mnaabudu sanamu, mnamwabudu Shetani—je, si ninyi ni watu wa hali ya chini zaidi, watu walio nyuma zaidi kimaendeleo? Ninyi ni wa hali ya chini kabisa ya mwili, mnakosa uhuru wowote wa kibinafsi, na mnapitia shida pia. Ninyi pia ni watu mlio katika ngazi ya chini kabisa katika jamii hii, bila hata uhuru wa imani. Huu ni umuhimu wa kufanya kazi kwenu. Kufanya kazi kwenu sasa, uzao wa Moabu, sio kuwafedhehesha kwa makusudi, lakini ni kufichua umuhimu wa kazi. Ni kuwainua sana. Ikiwa mtu ana mantiki na utambuzi, atasema: “Mimi ni uzao wa Moabu. Kweli sistahili kuinuliwa kukuu huku na Mungu ambako nimepokea sasa, au baraka hizi nyingi. Kwa mujibu wa yale ninayofanya na kusema, na kulingana na hali na thamani yangu—sistahili kabisa hizo baraka nyingi kutoka kwa Mungu. Waisraeli wana upendo mkubwa kwa Mungu, na neema wanayoifurahia imefadhiliwa kwao na Yeye, lakini hali yao ni ya juu zaidi kuliko yetu. Abrahamu alijitolea sana kwa Yehova, na Petro alijitolea sana kwa Yesu—ibada yao ilishinda yetu kwa mara mia, na kwa msingi wa matendo yetu hatufai kabisa kufurahia neema ya Mungu.” Huduma ya watu hawa nchini China haiwezi kuletwa mbele za Mungu hata kidogo. Ni fujo kamili tu, na kwamba sasa mnafurahia neema nyingi za Mungu ni kuinuliwa na Mungu kabisa! Je, ni wakati upi mmeitafuta kazi ya Mungu? Je, mmeyatoa maisha yenu kwa Mungu lini? Ni wakati gani mmeiacha familia yako kwa urahisi, wazazi wenu, na watoto wenu? Hakuna hata mmoja wenu aliyelipa gharama kubwa! Kama haingekuwa kwa Roho Mtakatifu kukufanya uonekane, wangapi wenu wangeweza kutoa dhabihu kila kitu? Ni kwa sababu tu mmelazimishwa na kushurutishwa ndipo mmefuata hadi leo. Upendo wenu uko wapi? Utiifu wenu uko wapi? Kulingana na matendo vyenu, mngepaswa kuangamizwa muda mrefu uliopita—kufagiliwa mbali kungepaswa kufanywa kwenu. Mna haki gani ya kufurahia baraka nyingi mno—ninyi hamstahili kabisa! Nani kati yenu amebuni njia yake mwenyewe? Ni nani kati yenu ameipata njia ya ukweli mwenyewe? Ninyi nyote ni wavivu na walafi, fidhuli msio na maana ambao mnasherehekea katika faraja kwa tamaa! Mnafikiri ninyi ni wakubwa sana? Je, nini mlicho nacho cha kujivunia? Hata kama Singesema ninyi ni uzao wa Moabu, je, asili yenu, mahali penu pa kuzaliwa ni ya fahari sana? Hata kama Singesema ninyi ni uzao wake, je, si ninyi nyote ni uzao wa Moabu kwa kweli? Ukweli wa mambo unaweza kubadilishwa? Je, kufichua asili yenu sasa kunaenda dhidi ya ukweli wa mambo? Angalieni jinsi mlivyo wanyonge, maisha yenu, na tabia—je, hamjui kwamba ninyi ni wa chini kabisa kati ya walio chini miongoni mwa wanadamu? Nini mlicho nacho cha kujisifia? Angalia nafasi yenu katika jamii. Je, si mko katika kiwango cha chini kabisa? Je, mnadhani kwamba Nimenena vibaya? Ibrahimu alimtoa Isaka. Nini ambacho mmetoa? Ayubu ilitoa kila kitu. Nini ambacho mmetoa? Watu wengi sana wameyatoa maisha yao, wakafa, wakamwaga damu yao ili kutafuta njia ya kweli. Je, mmelipa gharama hiyo? Kwa kulinganisha, hamna sifa zinazostahili hata kidogo kufurahia neema hiyo kubwa, kwa hivyo ni sawa kusema leo kwamba ninyi ni uzao wa Moabu? Msijione kuwa wakuu sana. Huna chochote cha kujisifia. Wokovu mkubwa kama huo, neema hiyo kubwa imepewa kwenu bure. Hamjatoa chochote, lakini mmeifurahia neema bure. Je, hamuoni haya? Je, njia hii ya ukweli ni jambo ambalo ninyi wenyewe mlipata kupitia kutafuta? Je, si ni Roho Mtakatifu aliyewalazimisha kuikubali? Kamwe humkuwa na moyo wa kutafuta na hasa hamkuwa na mioyo ya kuutafuta ukweli, ya kuutamani ukweli. Mmekuwa tu mkistarehe na kuufurahia, na mmeupata ukweli huu bila jitihada kwa upande wenu. Mna haki gani ya kulalamika? Je, unadhani kuwa wewe ni wa thamani kubwa zaidi? Ikilinganishwa na wale ambao walitoa dhabihu maisha yao na kumwaga damu yao, nini mnachopaswa kulalamikia? Kuwaangamiza hivi sasa litakuwa ni jambo linalotarajiwa! Kando na kutii na kufuata, hamna chaguzi zingine. Ninyi hasa hamstahili! Wengi wa wale kati yenu waliitwa, lakini kama mazingira hayangewalazimisha au kama hamngeitwa, hamngekuwa tayari kabisa kutokea wazi. Nani yuko tayari kutelekeza mambo kwa namna hii? Ni nani yuko tayari kuacha anasa za mwili? Ninyi nyote ni watu ambao husherehekea kwa ulafi katika faraja na kutafuta maisha ya anasa! Mmepata baraka nyingi mno—nini kingine mnacho cha kusema? Mna malalamiko yapi? Mmefurahia baraka nyingi mno na neema kuu mno mbinguni, na kazi sasa imefichuliwa kwenu ambayo haikuwahi kufanywa duniani awali. Je, si hii ni baraka? Kwa sababu mmempinga na kuasi dhidi ya Mungu, sasa mmepitia kuadibu kiasi hiki. Kwa sababu ya kuadibu huku mmeziona rehema na upendo wa Mungu, na hata zaidi mmeziona haki na utakatifu Wake. Kwa sababu ya kuadibu huku na kwa sababu ya uchafu wa wanadamu, mmeiona nguvu kuu ya Mungu, na mmeuona utakatifu na ukuu Wake. Je, si huu ni ukweli adimu mno? Je! Si haya ni maisha yenye maana? Kazi ambayo Mungu hufanya ina maana tele! Hivyo nafasi yenu ilivyo chini zaidi, ndivyo inavyoonyesha zaidi kuinuliwa na Mungu, na ndivyo inavyothibitisha zaidi jinsi kazi Yake ilivyo na thamani kwenu leo. Ni hazina yenye thamani mno hasa! Haiwezi kupatikana popote pengine, na kwa muda mrefu hakuna mtu aliyefurahia wokovu mkubwa hivi. Ukweli kwamba nafasi yenu ni ya chini inaonyesha jinsi wokovu wa Mungu ulivyo mkuu, na inaonyesha kwamba Mungu ni mwaminifu kwa wanadamu—Yeye huokoa, sio kuangamiza.
Watu wa Uchina hawajawahi kumwamini Mungu na hawajawahi kumhudumia Yehova, hawajawahi kumhudumia Yesu. Yote wanayofanya ni kusujudu, kufukiza uvumba, kuchoma sanamu ya Mungu ya karatasi, na kumwabudu Buddha. Wao wanaabudu sanamu tu—wote ni waasi mno, hivyo jinsi nafasi ya watu ilivyo ya chini zaidi, ndivyo inavyoonyesha zaidi kwamba kile Mungu hupata kutoka kwenu ni utukufu hata zaidi. Kutoka kwa mtazamo wa watu fulani, wangesema: “Mungu, ni kazi gani Unayofanya? Wewe, Mungu mwenye fahari sana, Mungu mtakatifu mno, ulikuja katika nchi yenye uchafu? Je, Unajidharau sana hivyo? Sisi ni wachafu sana, lakini Uko radhi kuwa pamoja nasi? Uko tayari kuishi kati yetu? Sisi ni wa cheo cha chini sana, lakini Uko radhi kutufanya kuwa kamili? Na Ungetutumia sisi kama mifano na vielelezo? “Ninasema: Huelewi mapenzi Yangu! Huelewi kazi ambayo Nataka kufanya wala huelewi tabia Yangu. Huwezi kufikia umuhimu wa kazi ambayo Ninaenda kufanya. Je, kazi Yangu ingepatana na mawazo ya kibinadamu? Kulingana na mawazo ya kibinadamu, Ningelazimika kuzaliwa katika nchi nzuri ili kuonyesha kwamba mimi ni wa hali ya juu, kuonyesha kwamba Mimi ni wa thamani kubwa, na kuonyesha uheshimiwa, utakatifu, na ukuu Wangu. Kama Ningezaliwa mahali ambapo pananitambua, katika familia ya ngazi ya juu, na kama Ningekuwa wa cheo na hadhi ya juu, basi Ningetendewa vizuri sana. Hiyo haingekuwa na manufaa kwa kazi Yangu, hivyo je, wokovu mkuu mno bado ungeweza kufichuliwa? Wote wanaoniona Mimi wangenitii, na hawangenajisiwa na uchafu. Nilipaswa kuzaliwa katika mahali pa aina hii. Hivyo ndivyo ninyi mnaamini. Lakini litafakari: Je! Mungu alikuja duniani kwa ajili ya raha, au kwa ajili ya kazi? Kama Ningefanya kazi katika aina ya mahali hapo rahisi, mahali penye starehe, je, Ningepata utukufu Wangu kamili? Je, Ningeweza kuvishinda viumbe Vyangu vyote? Mungu alipokuja duniani Yeye hakuwa wa ulimwengu na Yeye hakuwa mwili ili apate kuufurahia ulimwengu. Mahali ambapo kufanya kazi kungefichua tabia Yake vizuri sana na pawe mahali pa maana zaidi ni mahali Alipozaliwa. Kama ni nchi takatifu au yenye uchafu, na bila kujali Anapofanya kazi, Yeye ni mtakatifu. Kila kitu duniani kiliumbwa na Yeye; Ni kwamba tu kila kitu kimepotoshwa na Shetani. Hata hivyo, vitu vyote bado ni Vyake; vyote viko mikononi Mwake. Kuja Kwake katika nchi yenye uchafu kufanya kazi ni kufichua utakatifu Wake; Yeye hufanya hivi kwa ajili ya kazi Yake, yaani, Yeye huvumilia aibu kubwa kufanya kazi kwa njia hii ili kuwaokoa watu wa nchi hii yenye uchafu. Hii ni kwa ajili ya ushuhuda na ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kile aina hii ya kazi inawaruhusu watu kuona ni haki ya Mungu, na ina uwezo zaidi wa kuonyesha mamlaka ya juu kabisa ya Mungu. Ukuu na uadilifu Wake vinaonyeshwa kupitia wokovu wa kundi la watu wa hali ya chini ambao hakuna mtu anayewapenda. Kuzaliwa katika nchi yenye uchafu haimaanishi kabisa kuwa Yeye ni duni; inawaruhusu tu viumbe vyote kuuona utukufu Wake na upendo wake wa kweli kwa wanadamu. Zaidi Anavyofanya kwa njia hii, zaidi inavyofichua upendo Wake safi zaidi kwa mwanadamu, upendo wake usio na dosari. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Hata ingawa Alizaliwa katika nchi yenye uchafu, na ingawa Anaishi na watu hao ambao wamejawa uchafu, kama vile Yesu alivyoishi na wenye dhambi katika Enzi ya Neema, si kazi Yake yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote? Je, si yote ni ili mwanadamu aweze kuupata wokovu mkuu? Miaka elfu mbili iliyopita Aliishi na wenye dhambi kwa miaka kadhaa. Hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya ukombozi. Leo, Anaishi na kikundi cha watu wachafu, wa hali ya chini. Hii ni kwa ajili ya wokovu. Je, si kazi Yake yote ni kwa ajili yenu, wanadamu hawa? Kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeishi na kuteswa pamoja na wenye dhambi kwa miaka mingi sana baada ya kuzaliwa horini? Na kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeurudia mwili kwa mara ya pili, kuzaliwa katika nchi hii ambako mapepo hukusanyika, na kuishi na watu hawa ambao wamepotoshwa kwa kina na Shetani? Je, si Mungu ni mwaminifu? Ni aina gani ya kazi Yake ambayo haijakuwa kwa ajili ya wanadamu? Ni aina gani ambayo haijakuwa kwa ajili ya kudura yako? Mungu ni mtakatifu! Hili haliwezi kubadilika. Yeye hanajisiwi na uchafu, ingawa Amekuja katika nchi yenye uchafu; yote haya yanamaanisha tu kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wenye kuwajali wengine sana, mateso na aibu Anayoyavumilia ni makubwa sana! Kwa ajili yenu nyote, na kwa ajili ya kudura yenu, Yeye hupitia aibu kubwa sana. Je, hamjui hivyo? Yeye hawaokoi watu wakuu au wana wa familia tajiri na zenye uwezo, lakini Yeye huwaokoa hasa wale ambao ni wa hali za chini na wanaodharauliwa na wengine. Je, si haya yote ni utakatifu Wake? Je, si haya yote ni haki Yake? Afadhali Azaliwe katika nchi yenye uchafu na kuteseka aibu yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote. Mungu ni halisi sana—Hafanyi kazi ya uwongo. Je, si kila hatua ya kazi Yake imefanyika kwa utendaji hivi? Ingawa watu wote wanamkashifu na kusema kuwa Anakaa mezani pamoja na wenye dhambi, ingawa watu wote wanamdhihaki na kusema kuwa Anaishi na wana wa uchafu, na watu wa hali ya chini sana, bado Anajitolea bila ubinafsi, na bado Anakataliwa kwa njia hii kati ya wanadamu. Je, si mateso Anayoyahimili ni makubwa zaidi kuliko yenu? Je, si kazi Yake ni zaidi ya gharama ambayo mmelipa? Mlizaliwa katika nchi ya uchafu lakini mmepata utakatifu wa Mungu. Mlizaliwa katika nchi ambako mapepo hukusanyika lakini mmepokea ulinzi mkubwa. Je, mna uchaguzi gani mwingine? Ni malalamiko yapi mliyo nayo? Je, si mateso ambayo Amevumilia ni makubwa zaidi kuliko mateso ambayo mmevumilia? Amekuja duniani na hajawahi kufaidi furaha za ulimwengu wa kibinadamu. Anayachukia mambo hayo. Mungu hakuja duniani kufurahia manufaa ya kibinadamu kutoka kwa mwanadamu, wala haikuwa kufurahia mambo mazuri ya wanadamu kula na kuvalia. Hazingatii mambo haya; Alikuja duniani kuteseka kwa ajili ya mwanadamu, si kufurahia mambo mazuri ya kidunia. Alikuja kuteseka, Alikuja kufanya kazi, na kukamilisha mpango Wake wa usimamizi. Hakuchagua mahali pazuri, kuishi katika ubalozi au hoteli ghali mno, wala Hana watumishi kadhaa kumtumikia. Kutokana na kile mmeona, hamjui kama Alikuja kufanya kazi au kufurahia? Je, macho yenu hayafanyi kazi? Amewapa kiasi gani? Kama Angezaliwa katika mahali pazuri Angeweza kuupata utukufu? Je, Angeweza kufanya kazi? Je! Huko kungekuwa na umuhimu wowote? Angeweza kuwashinda kabisa wanadamu? Angeweza kuwaokoa watu kutoka katika nchi ya uchafu? Kulingana na mawazo ya kibinadamu, “Mungu, kwa kuwa Wewe ni mtakatifu, kwa nini Ulizaliwa katika mahali penye uchafu mno kama hapa? Unatuchukia na kutukirihi sisi wanadamu wachafu; Unachukia upinzani wetu na uasi wetu, hivyo kwa nini Unaishi nasi? Wewe ni Mungu mkuu sana—hungeweza kuzaliwa tu popote, lakini ilibidi uzaliwe katika nchi hii yenye uchafu? Unatuadibu na kutuhukumu kila siku na Unajua wazi kwamba sisi ni uzao wa Moabu, basi kwa nini bado Unaishi kati yetu? Kwa nini Ulizaliwa katika familia ya uzao wa Moabu? Kwa nini Ulifanya hivyo? “Aina hii ya ufahamu wenu inakosa mantiki! Ni aina hii ya kazi tu ambayo inawaruhusu watu kuuona ukuu Wake, unyenyekevu na kujificha Kwake. Yuko tayari kutoa kila kitu kwa ajili ya kazi Yake, na Amevumilia mateso yote kwa ajili ya kazi Yake. Anafanya kwa ajili ya wanadamu, na hata zaidi kumshinda Shetani ili viumbe vyote viweze kutii chini ya utawala Wake. Hii tu ni kazi ya maana, yenye thamani. Kama uzao wa Yakobo ungezaliwa nchini China, katika kipande hiki cha ardhi, na wote walikuwa ninyi nyote, basi umuhimu wa kazi iliyofanyika kwenu ingekuwa nini? Shetani angesema nini? Shetani angesema: “Walikuwa wakikuogopa Wewe, lakini hakuna mtu aliyeirithisha kwa muda mrefu. Hata hivyo, mababu zao walikuogopa; Walikutii tangu mwanzo na hawana historia ya kukusaliti. Ni kwamba tu baada ya kipindi cha muda hiyo haikurithishwa tena. Wao si wenye giza kabisa, wa hali ya chini kabisa, au walio nyuma zaidi kimaendeleo kati ya wanadamu. Walikukiri tangu mwanzo. Hakuna umuhimu wa kuifanya kwa njia hiyo! Ikiwa inafanyika hivi kwa kweli, nani atakayeridhishwa na kazi hii? “Kati ya ulimwengu wote, watu wa Kichina ni watu walio nyuma zaidi kimaendeleo. Wamezaliwa na hali ya chini na uadilifu duni, ni wapumbavu na wenye ganzi, nao ni watovu wa adabu na waliofifia. Wameloweshwa na tabia za kishetani, wachafu na waasherati. Mnayo haya yote. Kwa mintarafu ya tabia hizi potovu, baada ya kazi hii kukamilika watu watazitupilia mbali na wataweza kutii kikamilifu na kufanywa kuwa kamili. Tunda tu kutoka kwa aina hii ya kazi ndilo huitwa ushuhuda kati ya viumbe! Je, unaelewa kile kinachoitwa ushuhuda? Je, ushuhuda unapaswa kutolewaje? Aina hii ya kazi imewafanya kuwa foili[a] pamoja na vyombo vya huduma, na hata zaidi, mmekuwa vyombo vya wokovu. Leo ninyi ni watu wa Mungu na baadaye mtakuwa mifano na vielelezo. Katika kazi hii, mnajitwisha majukumu mbalimbali, na hatimaye mtakuwa vyombo vya wokovu. Watu wengi ni hasi kwa sababu ya hili; Je, si wao ni vipofu kabisa? Huwezi kuona chochote waziwazi! Je, cheo hiki tu kinakuzidi? Je, unaelewa kile kinachotajwa kama tabia ya Mungu yenye haki? Je, unaelewa wokovu ni nini? Je, unaelewa upendo wa Mungu ni nini? Huna uaminifu! Unapoona jina zuri unafurahi. Usipoona jina zuri hukubali nawe unarudi nyuma. Wewe ni nini? Hufuati njia ya kweli! Afadhali uache kutafuta mara moja. Ni jambo la aibu! Jambo dogo sana linakuzidi. Je, si hii ni ishara ya aibu?
Afadhali uweze kujijua kiasi. Usijione kuwa mkuu sana, wala usiwazie kwenda mbinguni. Tafuta tu kushindwa hapa duniani kwa kufanya wajibu ipasavyo! Usifikiri kuhusu ndoto hizo zisizo halisi ambazo hazipo. Mtu akisema jambo kama: “Ingawa mimi ni wa uzao wa Moabu, niko tayari kujitahidi kumpata Mungu, na katika siku zijazo nitamkana babu yangu wa zamani! Alinizaa na pia alinikandamiza, na hadi sasa nimekuwa nikiishi tu katika giza. Leo Mungu ameniachilia na hatimaye nimeiona mbingu. Kupitia kwa ufunuo wa Mungu hatimaye nimeona kwamba mimi ni wa uzao wa Moabu. Awali nilikuwa gizani, na sikujua kwamba Mungu amefanya kazi nyingi sana; yote ni kwa sababu nimepofushwa na Shetani huyu wa zamani. Nitamkana na kumuaibisha kabisa.” Haya ni maneno kutoka kwa mtu mwenye hamu ya kupata, mwenye ujasiri. Hivyo mna ujasiri? Licha ya ukweli kwamba mna mfano wa mwanadamu, mnashindwa kustahimili kasi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, nanyi ni wepesi zaidi wa kuathirika kuhusiana na suala hili. Mara tu inapotajwa kwamba ninyi ni uzao wa Moabu, midomo yenu inapinda kwa kuibibidua. Je! Si hii ni tabia ya nguruwe? Haina maana. Mko tayari kutoa dhabihu maisha yenu kwa ajili ya umaarufu na bahati yenu! Huko tayari kuwa uzao wa Moabu, lakini sivyo ulivyo? Ninasema leo kwamba wewe uko hivyo, na lazima ukiri jambo hilo. Siendi kinyume na ukweli. Watu wengine ni hasi kwa sababu ya jambo hili, lakini wewe ni hasi kuhusu nini? Je, si wewe pia ndiye mtoto wa joka kubwa jekundu? Je, ni udhalimu kusema kwamba wewe ni uzao wa Moabu? Angalia kile unachoishi kwa kudhihirisha, ndani na nje. Kutoka kichwani hadi mguuni, hakuna kitu cha kujisifia. Uasherati, uchafu, upofu, upinzani, uasi—si haya yote ni sehemu ya tabia yako? Daima wewe huishi ndani ya nchi ya uasherati nawe hufanya uovu wote. Unadhani kuwa wewe ni mtakatifu wa ajabu sana, lakini hebu yalinganishe mambo ambayo umeyafanya. Unafurahishwa sana na matokeo yako—nini ulicho nacho cha kujisifia? wewe ni kama wanyama, huna ubinadamu! Mnaafikiana na wanyama, mnaishi ndani ya uovu, dhana za kiasherati. Je! Mnakosa kiasi gani? Mnakubali kwamba ninyi ni watoto wa joka kubwa jekundu, na mko tayari kufanya huduma, lakini baadaye inaposemekana kuwa wewe ni uzao wa Moabu unakuwa hasi. Je! Si huu ni ukweli? Sawasawa na ulivyozaliwa na mama na baba yako, haijalishi jinsi walivyo wabaya, bado ulizaliwa na wao. Hata ukipata mama wa kambo na kuondoka katika nyumba hiyo, je, si wewe bado ni mtoto wa wazazi wako wa mwanzo? Je! Ukweli huo unaweza kubadilishwa? Je, nimekupachika tu jina kwa kubahatisha? Watu wengine wanasema: "Je! Si ungenipa tu jina lingine?” Ninasema: “Je, unaonaje Nikikupa jina la foili[a]?" Hawataki kuwa foili[a] pia. Basi unataka kuwa nini? Foili[a], watendaji huduma—si ninyi mko hivi? Ungechagua nini kingine? Je, si wewe ni mtu aliyezaliwa katika nchi ya joka kubwa jekundu? Haijalishi ni kiasi gani unasema kuwa wewe ni mwana wa Daudi, haikubaliani na ukweli. Je, hili ni jambo ambalo wewe mwenyewe ulichagua? Je, unaweza tu kutumia jina zuri kujitaja kwa kubahatisha? Je! Si watoto wa joka kubwa jekundu waliozungumziwa zamani ni nyinyi, kundi hili la watu waliopotoshwa? Watendaji huduma waliotajwa—je, si wao pia ni nyinyi, watu hawa waliopotoshwa? Vielelezo vilivyoshindwa, mifano iliyotajwa— si hivi pia ni nyinyi, watu hawa? Njia ya kukamilishwa—si hilo linasemwa kwa ajili yenu? Wale ambao wanaadibiwa na kuhukumiwa ni nyinyi, na si wale wanaokamilishwa baadaye watakuwa baadhi ya wale miongoni mwenu? Je, jina hili lina maana? Ninyi ni wapumbavu sana kiasi kwamba hamuwezi hata kuona kitu hicho kidogo kwa dhahiri? Hujui nani ni uzao wa nani, lakini Niko dhahiri kulihusu. Nawaambieni. Ikiwa unaweza kulitambua leo hivyo ni vizuri. Usijidhalilishe kila wakati. Zaidi unavyokuwa hasi na kurudi nyuma, ndivyo inavyoonyesha zaidi kwamba wewe ni uzao wa Shetani. Kuna mtu ambaye, unapomtaka asikilize wimbo, anasema: “Je, uzao wa Moabu hutumia vinasasauti? Sitausikiliza; Mimi sistahili!” Ukimtaka aimbe, anasema: “Ikiwa uzao wa Moabu unaimba, Je, Mungu yuko radhi kusikiliza? Mungu ananichukia. Nina aibu sana kwenda mbele za Mungu na siwezi kushuhudia Kwake. Sitaimba kabisa, Mungu asije akakasirika Anapousikia.” Je! Si hii ni njia hasi ya kulishughulikia? Kama mmoja wa viumbe, ulizaliwa katika nchi ya uasherati na wewe ni mtoto wa joka kubwa jekundu, uzao wa Moabu; unapaswa kumkana babu yako wa zamani na kumkana Shetani wa zamani. Huyu tu ndiye mtu anayemtaka Mungu kwa kweli.
Mwanzoni nilipowapa nafasi ya watu wa Mungu mlikuwa mnaruka juu chini—mliruka kwa furaha zaidi kuliko mtu yeyote. Lakini ilikuwaje mara Niliposema kuwa ninyi ni uzao wa Moabu? Ninyi nyote mlishindwa kustahimili! Ungesema kimo chenu kipo wapi? Dhana yenu ya nafasi ni nzito sana! Wengi hawawezi kujiinua. Wengine huenda kufanya biashara, na wengine huenda kazini. Mara tu Ninaposema kwamba ninyi ni uzao wa Moabu nyote mnataka kukimbia. Je, huku ndiko kushuhudia kwa Mungu ambako huwa mnapigia kelele wakati wote? Je! Shetani ataridhishwa kwa njia hii? Si hii ni alama ya aibu? Ni faida gani kuwa na nyinyi? Ninyi nyote ni taka! Ni mateso ya namna gani ambayo mmestahimili, lakini mnahisi kuwa mmetendewa mabaya sana? Mnafikiri kwamba mara tu Mungu amewatesa hadi kiwango fulani Atafurahi, kana kwamba Mungu alikuja kuwahukumu kimakusudi, na baada ya kuwahukumu na kuwaangamiza, kazi Yake itakuwa imekamilika. Je, ni hivyo ndivyo Nimesema? Je, si hii ni kwa sababu ya upofu wenu? Je! Ni kwamba ninyi wenyewe hamjitahidi kufanya vizuri au kwamba Ninawahukumu kwa makusudi? Sijawahi kufanya hivyo—hilo ni jambo ambalo mlilifikiria wenyewe. Sijafanya kazi kwa njia hiyo kabisa, wala Sina nia hiyo. Kama Ningetaka kuwaangamiza kwa kweli, je, Ningehitaji kuteseka sana hivyo? Ningetaka kuwaangamiza kwa kweli, Ningehitaji kuzungumza nanyi kwa dhati? Mapenzi Yangu ni haya: wakati ambapo Nimewaokoa ndipo Nitakapoweza kupumzika. Zaidi mtu alivyo wa hali ya chini, ndivyo alivyo chombo cha wokovu wangu zaidi. Zaidi mwezavyo kuingia kiutendaji, ndivyo Nitakavyofurahia zaidi. Zaidi mnavyoshindwa kustahimili ndivyo Ninavyofadhaika zaidi. Daima mnataka kuingia kwa mwendo wa furaha kuelekea kiti cha enzi, lakini Nitawaambieni, hiyo sio njia ya kuwaokoa kutokana na uchafu. Njozi ya kukaa kwa kiti cha enzi haiwezi kukufanya kuwa mkamilifu; hiyo si kweli. Nasema kuwa wewe ni uzao wa Moabu, kisha unakuwa na huzuni. Unasema: “Unataka niende kuzimu. Sitakuwa na ushuhuda Kwako au kuteswa kwa ajili Yako.” Je, si kufanya kwako hivi ni kunipinga Mimi? Je, hili ni la manufaa kwako? Nimekupa neema nyingi sana—umesahau? Moyo wa Mungu ambao ni kama tu mama mwenye upendo umegeuka kuwa maji baridi kwa sababu yako na kuwa barafu. Je! Shetani atakuachilia huru? Ikiwa hushuhudii Kwangu Sitakuhimiza lakini unapaswa kujua kwamba hatimaye utakuwa lengo la maangamizo. Ikiwa Siwezi kupata ushuhuda ndani yako, Nitaupata kwa watu wengine. Hilo halina maana Kwangu, lakini mwishowe utalijutia, na wakati huo utakuwa umeanguka gizani muda mrefu uliopita. Basi nani atakayeweza kukuokoa? Usifikiri kwamba kazi haiwezi kufanyika bila wewe. Hakungekuwa na wengi sana pamoja na wewe, na hakungekuwa na wachache sana bila wewe. Usijione kuwa mheshimiwa sana. Ikiwa hutaki kunifuata, hiyo inaonyesha tu kwamba wewe ni muasi, na hakuna kitu cha kutamanisha ndani yako. Ikiwa wewe ni msemaji mzuri, si hivyo ni kwa sababu tu umejiandaa na maneno Niliyoyaleta kupitia kwa kazi Yangu? Nini ulicho nacho cha kujisifia? Usiruhusu mawazo yako yafikie hitimisho lisilo la msingi! Ikiwa Siwezi kupata utukufu kutoka kwenu, uzao huu wa Moabu, Nitachagua kikundi cha pili, na cha tatu cha uzao wa Moabu kufanya kazi mpaka Nipate utukufu. Ikiwa huko radhi kuwa na ushuhuda Wangu, basi toka nje! Sitakulazimisha! Usifikiri kwamba Nitashindwa kusonga hatua bila ninyi. Kupata vyombo vinavyofaa kwa kazi Yangu katika nchi hii ya China hakuhitaji jitihada. Hakuna kitu kingine chochote kinachoweza kupatikana katika nchi hii—watu wachafu, wapotovu bila shaka wako kila mahali na kazi Yangu inaweza kufanyika popote. Usiwe na kiburi sana! Bila kujali wewe ni mwenye kiburi vipi, je, si bado wewe ni mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi? Angalia thamani yako, na ni chaguo gani lingine ulilo nalo? Kukukubali tu kuishi ni kuinuliwa kukubwa, kwa hivyo ni nini unajivunia? Kama haingekuwa kwa ajili ya kazi Yangu kukomesha enzi, je, si ungekuwa umeanguka katika majanga ya kawaida na maafa ya kibinadamu zamani sana? Je! Unaweza bado kuishi kwa raha sana? Bado daima unabishana kuhusu suala hili. Tangu Niliponena kuhusu uzao wa Moabu umekuwa ukibibidua midomo wakati wote. Hufanyi uchunguzi, husomi, na unamchukia kila mtu. Unapowaona watu wengine wakifanya uchunguzi unawavuruga na kusema mambo ya kuwavunja moyo. Una ujasiri! Unasema: “Uzao wa Moabu unajifunza nini? Sitajifunza kwa ajili Yake. "Je, si hili ni jambo ambalo mnyama angesema? Je, hata unafikiriwa kuwa mwanadamu? Nimesema mambo mengi kwako, lakini haijafanikisha chochote. Je, Nimefanya kazi hii yote bure? Je, Nimesema maneno haya yote bure? Kama ungekuwa mbwa bado ungeutikisa mkia wako; mtu wa aina hiyo siye hata sawa na mbwa! Wakati mwingine unabibidua midomo, wakati mwingine unatazama kwa shaka—je, kazi hii yote iliyofanyika kwako ilikuwa ya bure? Mara tu Ninaponena kuhusu uzao wa Moabu, watu wengine hujishusha hadhi kimakusudi. Wanavaa tofauti kuliko hapo awali nao ni wachafu sana kisai kwamba hawaonekani kama watu, nao hunung’unika: “Mimi ni uzao wa Moabu, sifai kitu. Hata hivyo hakuna kitu kizuri ndani yangu na sitaki kupata baraka zozote. Kwa vyovyote, hivi ndivyo ilivyo. Je, uzao wa Moabu unaweza kufanywa kuwa mkamilifu? "Mara tu Ninaponena kuhusu uzao wa Moabu, watu wengi hawana matumaini tena, na kusema: “Mungu anasema kwamba sisi ni uzao wa Moabu—hii inaonyesha nini? Kwa kuchunguza toni ya sauti Yake, hakuna uwezekano wa ukombozi! Hakuna upendo katika maneno Yake. Je! Si sisi ni malengo ya maangamizo? “Je! Umesahau kile kilichosemwa hapo awali? Leo neno “uzao wa Moabu” ni jambo pekee ambalo umekumbuka? Kwa kweli, maneno mengi ni kwa ajili ya kufikia kitu, lakini pia yanafichua ukweli wa mambo. Watu wengi hawaliamini. Huko tayari kuteseka kwa njia hiyo kwa ajili Yangu. Unaogopa kifo na daima unataka kutoroka. Ikiwa unataka kwenda Sitakulazimisha kukaa, lakini ni lazima Nikweleze wazi jambo moja: Usiishi maisha yote bure, na usisahau mambo yote Nilivyokwambia zamani. Kama mmoja wa viumbe unapaswa kutekeleza wajibu wa mmoja wa viumbe. Usifanye mambo dhidi ya dhamiri yako; unachopaswa kufanya ni kujitolea kwa Bwana wa uumbaji. Uzao wa Moabu pia ni sehemu tu ya uumbaji, ni kwamba tu wamelaaniwa. Chochote kitokeacho, bado wewe ni mmoja wa viumbe. Ikiwa unasema: “Ingawa mimi ni uzao wa Moabu, nimefurahia neema nyingi ya Mungu mbeleni, hivyo ni lazima niwe na dhamiri. Nitakiri tu lakini sitafikiri sana kulihusu. Hata kama nitateseka ndani ya mkondo huu, nitateseka mpaka mwisho. Kama mimi ni wa uzao wa Moabu basi iwe hivyo! Bado nitafuata hadi mwisho. “Ikiwa unasema hivi, basi huko mbali sana. Lazima ufuate mpaka mwisho. Ukikimbia kwa kweli huna matumaini ya baadaye — umeingia kwenye barabara ya maangamizo.
Ni vizuri kuwafanya muelewe asili yenu, na kuwafanya muuelewe ukweli wa mambo ni wenye manufaa kwa kazi. Vinginevyo, matokeo ambayo yanapaswa kufanikishwa hayatafanikishwa. Hii ni sehemu ya kazi ya kushinda, na ni hatua muhimu katika kazi. Huo ni ukweli. Kufanya kazi hii ni kuziamsha roho za watu, kuamsha hisia za dhamiri zao na kuwaruhusu watu kupata wokovu huu mkubwa. Ikiwa mtu ana dhamiri, anapoona kwamba yeye ni wa hali ya chini anapaswa hasa kumshukuru Mungu. Anayashika maneno Yake kwa nguvu, anaishika kwa nguvu neema ambayo Amempa, na hata kulia kwa uchungu na kusema: “Nafasi yetu ni ya chini sana na hatujapata chochote duniani. Hakuna mtu kutuheshimu, watu hawa wa hali ya chini. Tunateswa katika mazingira yetu ya nyumbani, waume zetu hutukana, wake zetu hutushutumu, watoto wetu hutudharau, na tunapokuwa wazee, binti zetu wakwe pia hututesa. Hakika hatujateseka kidogo, na kwamba sasa tunafurahia upendo mkuu wa Mungu ni furaha sana! Kama haungekuwa wokovu wa Mungu kwetu, tungewezaje kung’amua mateso ya kibinadamu? Je, si bado tungekuwa tumepakazwa matope katika dhambi hii? Je, huku si Mungu kutuinua? Mimi ni mmoja wa watu duni kabisa na Mungu ameniinua juu sana. Hata kama nitaangamia bado lazima niulipize upendo Wake. Mungu anaweza kutuheshimu na kunena uso kwa uso nasi, watu duni mno, na hata kama Yeye huniadibu—ninaweza kusema nini? Je, si kuadibu pia ni kuinua Kwake? Hata ikiwa ninaadibiwa bado naweza kuiona nguvu Yake kuu. Siwezi kuwa bila dhamiri—lazima niulipize upendo Wake. Siwezi kuwa muasi sana dhidi ya Mungu. Yeye hunena nami uso kwa uso na Hunifundisha kwa kuushika mkono wangu. Yeye huniandalia kila kitu, Huishi pamoja nami, na Huteseka pamoja nami.” Nafasi ya Mungu na hadhi Yake si sawa na ya watu, lakini mateso Yake ni sawa, na kile Anachokula na kuvaa ni sawa, ni watu wote tu humheshimu—hii ndiyo tofauti pekee. Je, si kila kitu kingine ambacho kinafurahiwa ni sawa? Hivyo mna haki gani kuwa na mengi ya kusema kulihusu? Mungu amevumilia mateso makubwa mno na kufanya kazi kubwa sana, na nyinyi—mlio chini kuliko mchwa, kuliko wadudu—mmepata kuinuliwa pakubwa leo. Ikiwa huwezi kuulipiza upendo wa Mungu, dhamiri yako iko wapi? Watu wengine hunena kutoka mioyoni mwao na kusema: “Kila wakati nikifikiri kuondoka kutoka kwa Mungu macho yangu yanajawa na machozi nami nahisi kuhukumiwa na dhamiri yangu. Mimi ni mwenye kuwiwa kwa Mungu. Siwezi kufanya hivi. Siwezi kuwa namna hiyo Kwake. Ningekufa na kufa kwangu kuipe kazi Yake utukufu, nitaridhika kupita kiasi. Vinginevyo, hata nikiishi sitahisi amani. “Sikiliza maneno haya—huu ndio wajibu ambao kiumbe anapaswa kutimiza. Ikiwa mtu anakuwa na maono haya ndani yake kila mara, atahisi kuwa dhahiri na starehe ndani yake; atakuwa na uhakika wa mambo haya. Utasema: “Mungu haniumizi na Hanifedheheshi kimakusudi wala Haniaibishi. Ingawa Ananena kwa ukali kwa kiasi fulani na huuchoma moyo, ni kwa ajili yangu mwenyewe. Ingawa Ananena kwa ukali namna hiyo, bado Ananiokoa, na Yeye bado ni mwenye huruma kwa udhaifu wangu. Hanihukumu na ukweli. Naamini kwamba Mungu ni wokovu.” Ikiwa kweli una maono haya, hutafikia kiwango cha kukimbia. Katika dhamiri yako, unaweza kuhisi kuwa umekosea, unaweza kuhisi shutuma, kwamba hupaswi kumtendea Mungu kwa namna hiyo. Unafikiri kuhusu neema yote uliyoipata, maneno yote ambayo umeyasikia—je, unaweza kuyasikiliza bure? Haijalishi ni nani anakimbia, wewe huwezi. Watu wengine hawaamini, lakini lazima wewe uamini. Watu wengine wanamtelekeza Mungu, lakini lazima wewe umtetee Mungu na kushuhudia Kwake. Wengine humkashifu Mungu, lakini wewe huwezi. Haijalishi jinsi Mungu asivyo na huruma kwako, bado unapaswa kumtendea vyema. Unapaswa kuulipiza upendo Wake na lazima uwe na dhamiri, kwa sababu Mungu hana hatia. Kuja Kwake duniani kutoka mbinguni kufanya kazi miongoni mwa wanadamu kulikuwa aibu kubwa tayari. Yeye ni mtakatifu bila uchafu hata kidogo. Kuja kwenye nchi ya uchafu—ni fedheha kiasi gani ambayo Amevumilia? Kufanya kazi ndani yenu ni kwa ajili yenu. Ikiwa huna dhamiri katika kumtendea Yeye, ingekuwa bora kufa kifo cha mapema!
Hivi sasa, watu wengi wanakosa kipengele hiki cha maono na hawawezi kabisa kuielewa kazi hii na hawajui nini Mungu anataka hasa kukamilisha kupitia kazi hii. Hasa wale waliokanganyika—ni kama wameingia katika matata mengi na kutunduwazwa baada ya zamu chache. Ukifafanua kikamilifu lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu kwao, basi hiyo haingekuwa hivyo. Watu wengi hawawezi kulielewa, na wanaamini kwamba kazi ya Mungu ni kuwatesa watu. Hawaelewi hekima na maajabu ya kazi Yake, na hawaelewi kwamba kazi Yake ni kufichua nguvu Yake kuu, na hata zaidi ni kuwaokoa wanadamu. Hawaoni yote hayo, wao huona tu kama wana matumaini yoyote, na kama wataweza kuingia mbinguni. Wanasema: Kazi ya Mungu daima ni ya mzunguko; kama ungetufanya tu tuione hekima Yako moja kwa moja hiyo ingekuwa vizuri. Hupaswi kututesa kwa njia hii. Tunakosa sana katika ubora wa tabia na hatuyafahamu mapenzi Yako. Ingekuwa vizuri sana kama Ungenena na kutenda tu moja kwa moja. Unatufanya tukisie, lakini hatuwezi. Ingekuwa vizuri kama Ungeharakisha na kuturuhusu tuuone utukufu Wako. Nini haja ya kufanya mambo kwa njia ya mzunguko? “Kile mnachokosa sana sasa ni dhamiri. Zingatieni hili zaidi na fungueni macho yenu wazi kabisa ili muone nani hasa anayefanya hatua kwa hatua kwa kazi. Msifikie uamuzi upesi bila kutafakari. Sasa umeelewa zaidi kwa juujuu njia ya maisha unayopaswa kupitia. Bado kuna kiasi kikubwa cha ukweli ambacho unapaswa kupitia, na siku inapokuja ambapo unaweza kuuelewa kikamilifu, hutasema hivyo tena, wala hutalalamika. Wala hutaufafanua bila uzito. Utasema: "Mungu ni mwenye busara sana, mtakatifu sana. Yeye ni mwenye nguvu sana!"
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 24 Februari 2019

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Mwenyezi Mungu alisema, Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi. Watu, ambao wamepotoshwa, wote huishi katika mtego wa Shetani, wao kuishi katika mwili, kuishi katika tamaa za ubinafsi, na hakuna hata mmoja kati yao anayelingana na Mimi. Kuna wale ambao wanasema kwamba wao wanalingana na Mimi, lakini ambao wote huabudu sanamu zisizo yakini. Ingawa wanakubali jina Langu kama takatifu, wao hutembea kwenye njia ambazo huenda kinyume na Yangu, na maneno yao yamejaa kiburi na kujiamini, kwa sababu, katika mizizi, wote wananipinga na hawalingani Nami. Kila siku wao hutafuta dalili Yangu katika Biblia, na kupata vifungu "vinavyofaa" hapa na pale wanavyovisoma bila kukoma, na ambavyo wao hukariri kama maandiko. Hawajui jinsi ya kulingana na Mimi, hawajui maana ya kuwa katika uadui na Mimi, na wanasoma tu maandiko kwa upofu. Wao huzuia ndani ya Biblia na Mungu asiye yakini ambaye hawajawahi kumwona, na hawana uwezo wa kumwona, na wao huitoa tu na kuiangazia wakati wao wa ziada. Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswikufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo? Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu waliofuata maneno ya Maandiko kwa uimara; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?
Na je watu leo? Kristo amekuja kutoa ukweli, lakini wanaona ni afadhali wao kumfukuza Yeye kutoka kati ya wanadamu ili wapate kuingia mbinguni na kupokea neema. Wanaona ni afadhali kabisa kukataa kuja kwa ukweli, ili kulinda maslahi ya Biblia, na ni afadhali kumtundika Kristo ambaye Alirudi kwa mwili kwa misumari msalabani tena ili kuhakikisha kuwepo kwa Biblia milele. Jinsi gani mwanadamu anaweza kupokea wokovu Wangu, wakati moyo wake una nia mbaya namna hiyo, na asili yake inanipinga Mimi? Mimi huishi miongoni mwa wanadamu, ilhali bado wanadamu hawajui kuhusu kuwepo Kwangu. Ninapoangaza mwanga Wangu juu ya wanadamu, bado yeye hana ufahamu kuhusu kuwepo Kwangu. Wakati Ninatoa ghadhabu Yangu juu ya wanadamu, wao hukanusha kuwepo Kwangu kwa nguvu kubwa zaidi. Binadamu hutafuta uwiano na maneno, na Biblia, ilhali bado hakuna mwanadamu hata mmoja huja Kwangu kutafuta njia ya uwiano na ukweli. Binadamu huniheshimu sana Nikiwa mbinguni, na kujishughulisha hasa na kuwepo Kwangu mbinguni, ilhali hakuna anayenijali Nikiwa katika mwili, kwa maana Mimi Ninayeishi miongoni mwa wanadamu sina umuhimu kwao hata kidogo. Wale ambao hutafuta tu uwiano na maneno ya Biblia, na ambao hutafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, mbele Yangu ni fidhuli. Hiyo ni kwa sababu wanachokiabudu ni maneno yaliyokufa, na Mungu Aliye na uwezo wa kuwapa hazina isiyoambilika. Wanachoabudu ni mungu anayedhibitiwa na mtu, na ambaye hayuko. Ni nini, basi, ambacho watu wa namna hiyo wanaweza kupokea kutoka Kwangu? Mwanadamu ni kiumbe duni sana kiasi kwamba maneno hayawezi kueleza hali yake. Wale wanaonipinga, wanaofanya madai yasiyo na kipimo dhidi Yangu, wasio na upendo kwa ukweli, wanaoniasi—wangewezaje kulingana na Mimi?
Wale wanaonipinga ni wale ambao hawalingani na Mimi. Vile vile wale wasiopenda ukweli, na wale wanaoniasi ndio walio wapinzani Wangu zaidi na hawalingani na Mimi. Wale wote ambao hawalingani na Mimi Nawawasilisha mikononi mwa yule mwovu. Ninawaacha wao kwa upotovu wa yule mwovu, Nawaachilia huru ili wafichue maovu yao, na hatimaye kuwakabidhi kwa yule mwovu ili waliwe. Mimi Sijali ni watu wangapi wananiabudu, ambayo ni kusema, Sijali ni watu wangapi wanaamini ndani Yangu. Kinachonijalisha ni watu wangapi wanalingana na Mimi. Hiyo ni kwa sababu wote wasiolingana na Mimi ni wale waovu wanaonisaliti; wao ni adui Zangu, Nami "Sitawatunza" adui Zangu katika nyumba Yangu. Wale ambao wanalingana na Mimi watanitumikia milele katika nyumba Yangu, na wale wanaojiweka katika uadui na Mimi watateseka milele katika adhabu Yangu. Wale wanaojali tu kuhusu maneno ya Biblia, wasiojali kuhusu ukweli au kutafuta nyayo Zangu—wao wananipinga, kwa kuwa wao wananizuilia Mimi kulingana na Biblia, na kuniwekea vizuizi ndani ya na Biblia, na hivyo ni wa kukufuru pakubwa dhidi Yangu. Jinsi gani watu wa aina hii wanaweza kuja mbele Zangu? Wao hawatilii maanani matendo Yangu, au mapenzi Yangu, au ukweli, badala yake wanashikilia maneno, maneno yanayoua. Jinsi gani watu kama hao wanaweza kulingana na Mimi?
Nimeeleza maneno mengi sana, na pia nimeeleza mapenzi Yangu na tabia, lakini hata hivyo, bado watu hawana uwezo wa kunijua Mimi na kuniamini. Au, inaweza kusemwa, bado hawana uwezo wa kunitii. Wale wanaoishi katika Biblia, wale wanaoishi katika sheria, wale wanaoishi juu ya msalaba, wale ambao wanaishi kwa mujibu wa mafundisho, wale wanaoishi miongoni mwa kazi Ninayofanya leo—yupi kati yao analingana na Mimi? Ninyi mnafikiria tu kupokea baraka na tuzo, na hamjawahi kamwe kufikiria jinsi ya kulingana na Mimi, au jinsi ya kujizuia wenyewe kutoka katika uadui na Mimi. Nimeaibishwa sana na nyinyi, kwa kuwa Nimewapa mengi sana, ilhali Mimi Nimepokea kidogo sana kutoka kwenu. Udanganyifu wenu, kiburi chenu, tamaa yenu, tamaa yenu yenye fujo, usaliti wenu, kuasi—lipi kati ya haya linaweza kujificha kutoka kwa macho Yangu? Mnafanya mzaha na Mimi, mnanidanganya Mimi, mnanitusi, mnanilaghai, mnanilazimisha, mnapata sadaka kutoka Kwangu kwa nguvu—ni jinsi gani tabia ya kudhuru kama hii itaepuka ghadhabu Yangu? Udhalimu wenu ni thibitisho la uadui wako Kwangu, na ni thibitisho la uwiano wenu na Mimi. Kila mmoja wenu anaamini mwenyewe akilingana na Mimi, lakini ikiwa ni hivyo, basi ni kwa nani ushahidi huu dhahiri unatumika? Mnaamini wenyewe kwamba mnao ukweli wa juu sana na uaminifu Kwangu. Mnafikiri kwamba nyinyi ni wema sana, wenye huruma sana, na mmetoa sana Kwangu. Mnafikiri kwamba mmefanya vya kutosha kwa ajili Yangu. Bado hamjawahi kulinganisha imani hizi dhidi ya tabia zenu wenyewe? Nasema mmejaa mengi ya kiburi, tamaa nyingi, wingi wa uzembe; hila mnayotumia kunidanganya ni janja sana, na mna mengi ya nia ya kudharau na mbinu ya kudharau. Uaminifu wenu pia ni mdogo, bidii yenu pia ni ndogo, na dhamiri yako hata haipo zaidi. Kuna mabaya mengi sana katika nyoyo zenu, na hakuna mtu atakayesamehewa kutoka kwa hayo, hata Mimi mwenyewe. Mnanifungia nje kwa ajili ya watoto wenu, au waume wenu, au kwa ajili ya hifadhi zenu wenyewe. Badala ya kunijali, mnajali familia zenu, watoto wenu, hali yenu, maisha yenu ya baadaye, na kujitosheleza wenyewe. Ni lini mmewahi kuniwaza Mimi mnapozungumza au kutenda? Wakati hali ya hewa ni baridi, mawazo yenu hurejea kwa watoto wenu, waume wenu, wake wenu, au wazazi wenu. Wakati hali ya hewa ni ya joto, hata Siwezi kupata nafasi katika mawazo yenu pia. Unapotekeleza wajibu wako, wewe huwaza tu kuhusu maslahi yako mwenyewe, ya usalama wako mwenyewe binafsi, ya watu wa familia yako. Ni nini umewahi kufanya kwa ajili Yangu? Ni lini umeweza kuwaza kunihusu Mimi? Ni lini umewahi kujitoa mwenyewe, kwa gharama yoyote, kwa ajili Yangu na kazi Yangu? Uko wapi ushahidi wa uwiano wako na Mimi? Uko wapi ukweli wa uaminifu wako kwa ajili Yangu? Uko wapi ukweli wa utiifu wako Kwangu? Ni lini mujibu wako hujakuwa kwa sababu ya kupokea baraka Zangu? Mnanilaghai na kunidanganya Mimi, mnacheza na ukweli na kuficha kuwepo kwa kweli, na kuisaliti dutu ya ukweli, na mnajiweka wenyewe kwa uadui kama huu na Mimi. Basi, ni nini kinawangoja katika siku za usoni? Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Wakati uo huo, mtagundua kuwa hakuna mtu yeyote asiyelingana na Kristo atakayeepuka siku ya ghadhabu, na mtagundua ni aina gani ya adhabu italetwa juu ya wale walio katika uadui na Kristo. Siku hiyo itakapofika, ndoto yenu ya kubarikiwa kwa imani yenu katika Mungu na kupata kuingia mbinguni, yote itakatizwa. Lakini, hata hivyo, si hivyo kwa wale ambao wanalingana na Kristo. Ingawa wao wamepoteza sana, ingawa wamekabiliwa na mengi ya ugumu wa maisha, watapokea urithi wote ambao Nimeutoa kwa ajili ya mwanadamu. Hatimaye, mtaelewa kwamba Mimi tu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba ni Mimi tu Niliye na uwezo wa kuwachukua binadamu mpaka kwenye hatima yao yenye kupendeza.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumamosi, 23 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" Sehemu ya Pili

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Kuhusu Ayubu Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake Maonyesho ya Ubinadamu wa Ayubu Wakati wa Majaribio Yake (Kuelewa Utimilifu wa Ayubu, Unyofu, Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu Wakati wa Majaribio Yake) Urazini wa Ayubu Asili Halisi ya Ayubu: Mkweli, Aliyetakaswa, na Asiye na Uongo Utenganisho wa Ayubu kati ya Upendo na Chuki Ukarimu na Uaminifu wa Ayubu Uhusiano Kati ya Mungu kumpa Shetani Ayubu na Malengo ya Kazi ya Mungu Kubali Mitihani ya Mungu, Shinda Majaribio ya Shetani, na Mruhusu Mungu Kupata Nafsi Yako Nzima Onyo na Nuru Iliyotolewa kwa Vizazi vya Baadaye Na Ushuhuda wa Ayubu
Mwenyezi Mungu alisema, Maudhui ya ushirika wetu wa mwisho kuhusu kazi ya Mungu yaliweza kuangazia mambo yaliyofanyika kitambo kwenye Biblia. Maudhui hayo yote yalikuwa hadithi kuhusu binadamu na Mungu, na yalimfanyikia binadamu na wakati huohuo yakahusisha kushiriki na maonyesho ya Mungu, hivyo basi hadithi hizi zinashikilia thamani na umuhimu mkubwa katika kujua Mungu. Baada tu ya kuumba ubinadamu, Mungu Alianza kujihusisha na binadamu na kuzungumza na binadamu, na tabia yake ikaanza kuonyeshwa kwa binadamu. Kwa maneno mengine, tangu Mungu alipojihusisha kwanza na mwanadamu, Alianza kuujuza umma kuhusu binadamu, bila kusita, kiini Chake halisi na kile Anacho na alicho. Licha ya kama watu wa awali au watu wa leo wanaweza kuona au kuelewa kiini hicho, kwa ufupi Mungu anamzungumzia mwanadamu na kufanya kazi miongoni mwa binadamu, Akifichua tabia Yake na Akionyesha kiini Chake—jambo ambalo ni ukweli, na lisilopingika na mtu yeyote. Hii inamaanisha pia kwamba tabia ya Mungu, kiini cha Mungu, na kile Anacho na alicho vyote vinatolewa daima na kufichuliwa huku naye Akifanya kazi na kujihusisha na binadamu. Hajawahi kusetiri au kumfichia binadamu chochote, lakini badala yake anatangaza kwa umma na kuachilia tabia Yake binafsi bila ya kuficha chochote. Hivyo basi, Mungu anatumai kwamba binadamu anaweza kumjua Yeye na kuielewa tabia Yake na kiini chake. Hapendi binadamu kuchukulia tabia Yake na kiini Chake kuwa mafumbo ya milele, wala Hataki mwanadamu kumchukulia Mungu kama fumbo lisiloweza kutatuliwa. Mpaka tu pale ambapo mwanadamu atakapomjua Mungu ndipo binadamu atakapojua njia ya kufuata na kuweza kuukubali mwongozo wa Mungu, na mwanadamu tu kama huyu ndiye anayeweza kuishi kwa kweli katika utawala wa Mungu, na kuishi katika mwangaza, na kuishi katikati ya baraka za Mungu.
Maneno na tabia iliyowasilishwa mbele na kufichuliwa na Mungu inawakilisha mapenzi Yake, na pia inawakilisha kiini Chake halisi. Wakati Mungu anapojihusisha na binadamu, haijalishi ni nini Anachosema au kufanya, au tabia gani Anayofichua, na haijalishi ni nini binadamu anaona kuhusu kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho, vyote vinawasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Licha ya kiwango ambacho binadamu anaweza kutambua, kufahamu, au kuelewa, vyote hivi vinawakilisha mapenzi ya Mungu—mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Hii ni zaidi ya shaka! Mapenzi ya Mungu kwa binadamu ni vile Anavyohitaji watu kuwa, kile Anachohitaji wao kufanya, namna Anavyohitaji wao kuishi, na vile Anavyowahitaji kuweza kukamilisha kutimia kwa mapenzi ya Mungu. Je, mambo haya hayawezi kutenganishwa na kiini cha Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu huwasilisha mbele tabia Yake na vyote Alivyo navyo na kile ambacho Mungu ni wakati huohuo Akimtolea madai binadamu. Hakuna uongo, hakuna kusingizia, hakuna ufichaji, na wala hakuna kupiga chuku. Ilhali kwa nini binadamu hawezi kujua na kwa nini hajawahi kuweza kutambua waziwazi tabia ya Mungu? Na kwa nini hajawahi kutambua mapenzi ya Mungu? Kile ambacho kimefichuliwa na kuwasilishwa mbele na Mungu ndicho kile Mungu anacho Mwenyewe na maana yake, na kinaonyesha kila kipengele cha tabia Yake ya kweli—hivyo kwa nini binadamu hawezi kuona? Kwa nini binadamu hana uwezo wa kuwa na maarifa ya kina? Kunayo sababu muhimu ya haya. Na sababu yenyewe ni ipi? Tangu wakati wa uumbaji, binadamu hajawahi kumchukulia Mungu kama Mungu. Kwenye nyakati zile za mwanzo kabisa, haikujalisha ni nini Mungu alifanya kuhusiana na binadamu, yule binadamu ambaye ndiye tu alikuwa ameumbwa, binadamu alimchukulia yeye kuwa mwandani wake tu na wala si zaidi ya hapo, kama mtu wa kutegemewa, na hakuwa na maarifa yoyote wala uelewa wa Mungu. Hivi ni kusema, hakujua kwamba kile kilichowasilishwa mbele na Kiumbe huyu—Kiumbe huyu ambaye yeye alitegemea na kumwona kuwa mwandani wake—alikuwa kiini cha Mungu, na wala hakujua kwamba Kiumbe huyu ndiye anayetawala viumbe wote. Nikisema kwa urahisi, watu wa wakati huo hawakuwa na maarifa hata kidogo kumhusu Mungu. Hawakujua kwamba mbingu na nchi na mambo yote yalikuwa yameumbwa na Yeye na wala hawakujua ni wapi Alipotokea, na, zaidi hawakujua Yeye Alikuwa nani. Bila shaka, wakati huo Mungu hakumhitaji binadamu kumjua Yeye au kumfahamu Yeye au kuelewa kila kitu Alichofanya, au kufahamishwa kuhusu mapenzi Yake, kwani hizi zilikuwa nyakati za mapema zaidi baada ya uumbwaji wa mwanadamu. Wakati Mungu alipoanza matayarisho ya kazi ya Enzi ya Sheria, Mungu alifanya mambo fulani kwa binadamu na pia Akaanza kutolea binadamu madai fulani, Akimwambia namna ya kutolea Mungu sadaka na namna ya kumwabudu. Ni wakati huo ndipo binadamu alipopata mawazo machache mepesi kuhusu Mungu, ni hapo tu ndipo alipojua tofauti kati ya binadamu na Mungu na kwamba Mungu Ndiye aliyewaumba wanadamu. Wakati binadamu alipojua kwamba Mungu alikuwa Mungu na binadamu alikuwa binadamu kukawa umbali fulani kati ya Yeye na Mungu, bado Mungu hakuhitaji kwamba binadamu awe na maarifa makuu au uelewa wa kina kumhusu Yeye. Hivyo basi, Mungu anayatoa mahitaji tofauti kwa binadamu kutokana na awamu na hali za kazi Yake. Mnaona nini katika haya? Ni kipengele kipi cha tabia ya Mungu unayoitambua? Je, Mungu ni wa kweli? Yale mahitaji ambayo Mungu anampa binadamu yanastahili? Kwenye nyakati za mapema kabisa kufuatia uumbaji wa wanadamu na Mungu, wakati ambao Mungu alikuwa bado hajatekeleza kazi ya ushindi na utimilifu wa binadamu, na Alikuwa hata bado hajaongea yale maneno mengi sana kwake, Alihitaji kidogo sana kutoka kwa binadamu. Licha ya kile ambacho binadamu alifanya na namna alivyotenda—hata kama alifanya mambo fulani yaliyomkosea Mungu—Mungu alimsamehe hayo yote, na akayapuuza. Kwa sababu Mungu Alijua kile Alichokuwa Amempa binadamu, na Alijua kile kilichokuwa ndani ya binadamu, basi Alijua kiwango cha mahitaji ambayo anafaa kudai kutoka kwa binadamu. Ingawaje kiwango cha mahitaji Yake kilikuwa cha chini sana wakati huo, hii haimaanishi kwamba tabia Yake haikuwa kuu, au kwamba hekima na uweza Wake yalikuwa si yoyote ila maneno matupu. Kwa binadamu, kunayo njia moja tu ya kujua tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe: kwa kufuata hatua za kazi ya usimamizi ya Mungu na wokovu wa mwanadamu, na kuyakubali maneno ambayo Mungu anaongea akiyaelekeza kwa mwanadamu. Kujua kile Mungu anacho na alicho, na kujua tabia ya Mungu, bado binadamu angemuuliza Mungu kumwonyesha ubinafsi Wake halisi? Binadamu hatafanya hivyo, na hathubutu kufanya hivyo, kwa kuweza kuifahamu tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho, tayari binadamu atakuwa amemwona Mungu Mwenyewe wa kweli, na atakuwa tayari ameona ubinafsi Wake halisi. Haya ndiyo matokeo yasiyoepukika.
Kazi na mpango wa Mungu ulipokuwa ukiendelea mbele bila kusia, na baada ya Mungu kuanzisha agano la upinde wa mvua na binadamu kama ishara kwamba Hangewahi tena kuuangamiza ulimwengu kwa kutumia gharika, Mungu alikuwa na tamanio lililokuwa likiongezeka na kumsukuma kuwapata wale ambao wangeweza kuwa katika akili moja na Yeye. Hivyo, pia, Alikuwa na tamanio lenye udharura zaidi wa kupata wale waliokuwa na uwezo wa kutekeleza mapenzi Yake duniani, na, isitoshe, kupata kundi la watu ambao wangeweza kuwa huru dhidi ya nguvu za giza, na kutoweza kuwa watumwa wa Shetani, na kuweza kuwa na ushuhuda kwake Yeye duniani. Kupata kundi la watu kama hawa kulikuwa ni tamanio la Mungu kwa muda mrefu, Alichokuwa akisubiria tangu wakati wa uumbaji. Hivyo basi, licha ya matumizi ya gharika na Mungu ili kuuangamiza ulimwengu, au agano Lake na binadamu, mapenzi ya Mungu, hali yake ya akili, mpango, na matumaini yote yalibakia yaleyale. Kile Alichotaka kufanya, ambacho Alikuwa ametamani kwa muda mrefu kabla ya uumbaji, kilikuwa kupata wale walio miongoni mwa wanadamu ambao Alitamani kuwapata—Kupata watu wa kundi hili ambao walioweza kufahamu na kujua tabia Yake, na kuyaelewa mapenzi Yake, kundi ambalo lingeweza kumwabudu Yeye. Watu kwenye kundi kama hili wanaweza kweli kuwa na ushuhuda kwake, na wao ndio, yaweza kusemekana, wasiri Wake.

Ijumaa, 22 Februari 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu”

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Ikiwa ungependa kutumikia mapenzi ya Mungu, ni lazima kwanza ufahamu ni watu wa aina gani wanapendwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanachukiwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanafanywa kuwa kamili na Mungu, na ni watu wa aina gani wana sifa zinazostahili kumhudumia Mungu. Hiki ni kiasi kidogo zaidi unachopaswa kujiandaa nacho. Isitoshe, unapaswa kujua malengo ya kazi ya Mungu, na kazi ambayo Mungu Ataitenda hapa na wakati huu. Baada ya kufahamu haya, na kupitia kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, kwanza utaingia, na kupokea agizo la Mungu kwanza. Unapopata uzoefu wa kweli kwa msingi wa maneno ya Mungu, na unapojua kweli kazi ya Mungu, utakuwa umehitimu kumhudumia Mungu. Na unapomhudumia ndipo Mungu atayapa nuru macho yako ya kiroho, na kukuruhusu kuwa na ufahamu mkubwa zaidi wa kazi Yake na kuiona dhahiri zaidi. Ukiingia katika ukweli huu, uzoefu wako utakuwa wa kina zaidi na wa kweli, na wale wote ambao wamepata uzoefu wa aina hiyo wataweza kutembea miongoni mwa makanisa mengi na kuwatolea ndugu zao, kila upande ukipokea kutoka kwa uwezo wa wengine ili upungufu wao wenyewe, na kupata maarifa mengi zaidi ndani ya roho zao. Ni baada tu ya kutimiza matokeo haya ndipo utakapoweza kutumikia mapenzi ya Mungu na kufanywa mkamilifu na Mungu wakati wa kufanya huduma yako.”