Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumapili, 31 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu I” Sehemu ya Tano

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu I” Sehemu ya Tano

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio Mungu Pekee, Ambaye Anao Utambulisho wa Muumba, Anamiliki Mamlaka ya Kipekee Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hufai Kufuata lile Wazo la Imani ya Kuabudu Miungu Wengi Ingawaje Binadamu Amepotoka, Angali Anaishi Chini ya Ukuu wa Mamlaka ya Muumba
Mwenyezi Mungu alisema, Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho? La, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo! Hii ni kwa sababu vikao hivi vya ushirika vilitupa tu ufahamu wa sehemu ya tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho—na wala si kila kitu, au uzima Wake wote. Vikao hivi vya ushirika vilikuwezesha wewe kuelewa sehemu ya kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na kupitia kwa hayo uliweza kuielewa tabia ya Mungu, na kile Anacho, na alicho, pamoja na mtazamo na kufikiria kuliko kila kitu ambacho Amefanya. Hata hivyo huu ni ufahamu tu wa moja kwa moja, wa matamshi, na katika moyo wako, unabakia kutojua ni kiwango kipi haswa ambacho ni kweli. Ni nini hasa huamua kama kunao uhalisia wowote katika ufahamu wako wa mambo kama haya? Yanaamuliwa na kiwango kipi cha maneno na tabia ya Mungu ambayo kwa kweli umepitia kwenye yale yote ya kweli ambayo wewe umepitia, na kiwango kipi ambacho umeweza kuona na kujua kwenye hali hizi halisi ambazo ulipitia. “Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vilituruhusu kuelewa mambo yanayofanywa na Mungu, fikira za Mungu, na, zaidi ya yote, mtazamo wa Mungu kwa mwanadamu na msingi wa hatua Zake, pamoja na kanuni za vitendo Vyake. Na kwa hivyo tumekuja kuelewa tabia ya Mungu, na kujua Mungu kwa uzima Wake.” Je, kunaye aliyesema maneno haya? Ni sahihi kusema hivi? Kwa kweli ni wazi kwamba si sahihi. Na kwa nini Nasema kwamba si sahihi? Tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho, vyote vinaonyeshwa katika mambo ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye ametamka. Binadamu anaweza kuelewa kile Anacho na alicho kupitia kwa kazi ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye ameongea, lakini hii ni kusema tu kwamba ile kazi na maneno humwezesha binadamu kuelewa sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya kile Anacho na alicho. Kama binadamu atataka kufaidi ufahamu mwingi zaidi na ulio wazi kuhusu Mungu, basi binadamu lazima apitie maneno na kazi nyingi zaidi za Mungu. Ingawaje binadamu hufaidi tu ufahamu kiasi wa Mungu wakati anapokuwa akipitia sehemu ya maneno au kazi ya Mungu, je, ufahamu huu wa kiasi unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu? Je, unawakilisha hali halisi ya Mungu? Bila shaka unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu, na hali halisi ya Mungu, hapo hapana shaka. Haijalishi ni lini au wapi, au ni kwa njia gani ambayo Mungu hufanya kazi Yake, au ni umbo gani ambalo humwonekania binadamu, au ni kwa njia gani Anaonyesha mapenzi Yake, kila kitu Anachofichua na kuonyesha huwakilisha Mungu Mwenyewe, hali halisi ya Mungu na kile Anacho na alicho. Mungu hutekeleza kazi Yake na kile Anacho na alicho, na katika utambulisho Wake wa kweli; Huu ni ukweli mtupu. Ilhali, leo, watu wanao ufahamu kiasi tu wa Mungu kupitia maneno Yake, na kupitia kile wanachosikia wanaposikiliza mahubiri, na kwa hivyo hadi kufikia kiwango fulani, ufahamu huu unaweza kusemwa tu kuwa maarifa ya kinadharia. Kwa mtazamo wa hali zenu halisi, mnaweza kuthibitisha tu ufahamu au maarifa ya Mungu ambayo mmesikia, kuona, au kujua na kuelewa katika moyo wako leo kama kila mmoja wenu atashuhudia haya kupitia kwa yale yote halisi aliyoyapitia, na anakuja kuyajua kidogokidogo. Kama Singeweza kushiriki maneno haya na wewe, je, ungeweza kutimiza maarifa ya kweli ya Mungu ukiwa pekee kupitia kwa yale yote uliyoyapitia? Kufanya hivyo, Naogopa, kunaweza kuwa vigumu sana. Hiyo ni kwa sababu lazima watu wawe kwanza na maneno ya Mungu ili kujua namna ya kuyapitia. Hata hivyo wingi wa maneno ya Mungu ambayo watu hushiriki, hicho ndicho kiwango wanachoweza kupitia. Maneno ya Mungu huongoza njia iliyo mbele, na humpa binadamu mwongozo katika yale yote anayoyapitia. Kwa ufupi, kwa wale walio na baadhi ya mambo ya kweli waliyoyapitia, vikao hivi mbalimbali vya mwisho vitawasaidia kutimiza ufahamu wa kina wa kweli, na hali yenye uhalisia zaidi kuhusu maarifa ya Mungu. Lakini kwa wale wasiokuwa na hali yoyote ya kweli ya waliyoipitia, au ambao wameanza tu hali yao wanayopitia, au wameanza tu kugusia uhalisia wa mambo, huu ni mtihani mkubwa.
Yale maudhui makuu ya vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika yalihusu “tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe.” Ni nini ulichoona kwenye sehemu zile muhimu na kuu kati ya kila kitu Nilichoongea? Kupitia kwenye vikao hivi vya ushirika, unaweza kutambua kwamba Yule aliyefanya kazi, na Akaweza kufichua tabia hizi, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye na ukuu juu ya mambo yote? Kama jibu lako ni ndiyo, basi ni nini kinachokuongoza katika hitimisho kama hilo? Ni katika dhana zipi uliweza kufikia hitimisho hili? Je, kunaye yeyote anayeweza kuniambia Mimi? Ninajua kwamba vikao vya mwisho vya ushirika vilikuathiri kwa undani, na vilikupa mwanzo mpya katika moyo wako kwa minajili ya maarifa yako kwa Mungu, jambo ambalo ni kuu. Lakini ingawaje umeweza kuchukua hatua kubwa katika ufahamu wako wa Mungu ukilinganishwa na awali, ufafanuzi wako wa utambulisho wa Mungu bado unahitaji hatua zaidi ya majina ya Yehova Mungu wa Enzi ya Sheria, Bwana Yesu wa Enzi ya Neema, na Mwenyezi Mungu wa Enzi ya Ufalme. Hivi ni kusema kwamba, ingawaje vikao hivi vya ushirika kuhusu “tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” viliweza kukupa ufahamu fulani wa maneno yaliyowahi kuzungumzwa na Mungu, na kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na uwepo na vinavyomilikiwa vilivyowahi kufichuliwa na Mungu, huwezi kutoa ufafanuzi wa ukweli na mpangilio sahihi wa neno “Mungu.” Na wala huna mpangilio wa kweli na sahihi na maarifa ya hali na utambulisho wa Mungu Mwenyewe, hii ni kusema, katika hadhi ya Mungu miongoni mwa mambo yote na kotekote kwenye ulimwengu mzima. Hii ni kwa sababu, kwenye vikao vya ushirika vya awali kuhusu Mungu Mwenyewe na tabia ya Mungu, maudhui yote yalitokana na maonyesho na ufunuo mbalimbali wa awali kuhusu Mungu uliorekodiwa kwenye Biblia. Ilhali ni vigumu kwa binadamu kugundua uwepo na miliki ambazo zinamilikiwa na kuonyeshwa na Mungu wakati wa, au nje ya, usimamizi na wokovu Wake kwa mwanadamu. Kwa hivyo, hata kama utaelewa nafsi na miliki za Mungu ambazo zilifichuliwa kwenye kazi Aliyowahi kufanya, ufafanuzi wako wa utambulisho na hadhi ya Mungu ungali mbali sana na ule wa Mungu wa kipekee, Yule anayeshikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na ni tofauti na ule wa Muumba. Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vilifanya kila mmoja kuhisi kwa njia moja: Binadamu angejuaje fikira za Mungu? Kama kweli mtu angejua, basi mtu huyo bila shaka angekuwa Mungu, kwa maana Mungu Mwenyewe ndiye anayejua fikira Zake, na Mungu Mwenyewe tu ndiye anayejua msingi na mtazamo wa kila kitu Anachofanya. Yaonekana ya kueleweka na ya mantiki kwako wewe kutambua utambulisho wa Mungu kwa njia kama hiyo, lakini ni nani anayeweza kujua kutoka kwenye tabia na kazi ya Mungu kwamba kwa kweli hii ni kazi ya Mungu Mwenyewe, na wala si kazi ya binadamu, kazi ambayo haiwezi kufanywa kwa niaba ya Mungu na binadamu? Nani anayeweza kuona kwamba kazi hii inapatikana katika uongozi wa ukuu wa Yule aliye na hali halisi na nguvu za Mungu? Hii ni kusema kwamba, kupitia sifa au hali halisi gani ndipo unapotambua kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe, aliye na utambulisho wa Mungu, na Ndiye aliye na ukuu juu ya viumbe vyote? Umewahi kufikiria hivi? Kama hujawahi, basi hii inathibitisha hoja moja: Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vimeweza kukupa tu ufahamu fulani wa kipande cha historia ambapo Mungu alifanya kazi Yake, na mtazamo, maonyesho, na ufunuo wa Mungu kwenye kipindi cha kufanyika kwa kazi hiyo. Ingawaje ufahamu kama huo unafanya kila mmoja wenu kutambua bila ya shaka yoyote kwamba Yule aliyetekeleza awamu hizi mbili za kazi ni Mungu Mwenyewe ambaye tunamsadiki na kumfuata, na Ndiye lazima siku zote tumfuate, tungali hatuna uwezo wa kutambua kwamba Yeye ni Mungu aliyekuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, na Atakayeendelea kuwepo milele hadi milele, na wala hatuwezi kutambua kwamba Yeye Ndiye anayetuongoza na Anayeshikilia utawala juu ya wanadamu wote. Kwa kweli hujawahi kufikiria kuhusu tatizo hili. Awe ni Yehova Mungu au Bwana Yesu, ni kupitia kwa dhana zipi za hali halisi na maonyesho husika ndipo unaweza kutambua kwamba Yeye si Mungu tu ambaye lazima umfuate, lakini pia Ndiye anayeamuru mwanadamu na Anayeshikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu, ambaye, vilevile, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee anayeshikilia ukuu dhidi ya mbingu na ardhi na viumbe vyote? Ni kupitia kwenye njia gani ndipo unapotambua kwamba Yule unayemsadiki na kumfuata ni Mungu Mwenyewe anayeshikilia ukuu juu ya viumbe vyote? Ni kupitia kwenye njia gani ndipo unapounganisha Mungu unayemsadiki na Mungu anayeshikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu? Ni nini kinachokuruhusu kutambua kwamba Mungu unayemsadiki ndiye yule Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye mbinguni na ulimwenguni, na miongoni mwa viumbe vyote? Hili ndilo tatizo ambalo Nitatatua kwenye sehemu ijayo.
Matatizo ambayo hujawahi kufikiria kuhusu au huwezi kufikiria kuhusu ndiyo yayo hayo ambayo yanaweza kuwa muhimu zaidi kwa kumjua Mungu, na ambayo kwayo unaweza kutafuta ukweli usioweza kufikirika kwa mwanadamu. Wakati matatizo haya yanapokukumba, na lazima wewe ndiwe unayefaa kuyakabili, na unahitajika kufanya uamuzi, kama hutaweza kuyatatua kikamilifu kwa sababu ya ujinga au kutojua kwako, au kwa sababu yale yote uliyopitia wewe ni ya juujuu sana na unakosa maarifa ya kweli ya Mungu, basi yatakuwa kizuizi kikubwa zaidi na changamoto kubwa zaidi kwenye njia yako ya kumsadiki Mungu. Na kwa hivyo Nahisi kwamba tunahitajika kabisa kushiriki pamoja nanyi mada hii. Je, unajua tatizo lako ni nini sasa? Je, unatambua matatizo Ninayoyazungumzia? Je, matatizo haya ndiyo utakayokabiliana nayo? Je, haya ndiyo matatizo usiyoyaelewa? Je, haya ndiyo matatizo ambayo hayajawahi kukutokea? Je, matatizo haya ni muhimu kwako? Je, ni matatizo kweli? Suala hili ni chanzo cha mkanganyo mkuu kwako, na hivyo inaonekana kwamba huna ufahamu wa kweli wa Mungu unayemsadiki, na kwamba humchukulii Yeye kwa umakinifu. Baadhi ya watu husema, “Ninajua Yeye ni Mungu, na kwa hivyo ninamfuata Yeye kwa sababu maneno Yake ni maonyesho ya Mungu. Hayo yanatosha. Thibitisho lipi zaidi linahitajika? Kwa kweli hatuhitaji kuibua shaka kuhusu Mungu? Kwa kweli hatupaswi kumjaribu Mungu? Kwa kweli hatuhitaji kuulizia hali halisi ya Mungu na utambulisho wa Mungu Mwenyewe?” Bila kujali kama unafikiria kwa njia hii, huwa Siyaulizi maswali fulani ili kukukanganya kuhusu Mungu, au kukufanya umjaribu Mungu, na isitoshe ili kukupa shaka kuhusu utambulisho na hali halisi ya Mungu. Badala yake, Ninafanya hivi ili kuhimiza ndani yenu ufahamu mkubwa zaidi wa hali halisi ya Mungu, na uhakika na imani kubwa zaidi kuhusu hadhi ya Mungu, ili Mungu awe Ndiye wa pekee katika mioyo ya wale wote wanaomfuata Mungu, na ili ile hadhi ya asili ya Mungu—kama Muumba, Kiongozi wa viumbe vyote, Mungu Mwenyewe wa kipekee—iweze kurejeshwa katika mioyo ya kila kiumbe. Hii pia ndiyo mada itakayohusu ushirika wetu.

Jumamosi, 30 Machi 2019

Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kumpenda Mungu kwa Kweli

Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kumpenda Mungu kwa Kweli

Mwenyezi Mungu alisema, Je, ni jinsi gani mwanadamu anafaa kumpenda Mungu wakati wa usafishaji? Baada ya kupitia usafishaji, wakati wa usafishaji watu wanaweza kumsifu Mungu kwa kweli na kuona jinsi wanavyokosa kwa kiasi kikubwa. Kadiri usafishaji wako ulivyo mkubwa, ndivyo unaweza zaidi kukana mwili; kadiri usafishaji wao ulivyo mkubwa, ndivyo zaidi ulivyo upendo wa watu kwa Mungu, Hili ndilo mnapaswa kuelewa. Je, kwa nini ni lazima watu wasafishwe? Linalenga kutimiza matokeo gani? Je, umuhimu wa kazi ya Mungu ya usafishaji kwa mwanadamu ni gani? Ukimtafuta Mungu kwa kweli, basi baada ya kupitia usafishaji Wake hadi kiwango fulani utahisi kwamba ni mzuri sana, na ni wa umuhimu mkubwa kabisa. Je, mwanadamu anapaswa kumpenda Mungu jinsi gani wakati wa usafishaji? Kwa kutumia azimio la kumpenda Mungu kukubali usafishaji Wake: Wakati wa usafishaji, unateseka ndani, kana kwamba kisu kinasokotwa moyoni mwako, ilhali uko tayari kumridhisha Mungu kwa kutumia moyo wako, ambao unampenda, na hauko tayari kuutunza mwili. Hii ndiyo maana ya kutenda upendo wa Mungu. Unaumia ndani, na mateso yako yamefikia kiwango fulani, lakini bado uko tayari kuja mbele ya Mungu na kuomba ukisema: “Ee Mungu! Siwezi kukuacha. Ingawa kuna giza ndani yangu, ningependa kukuridhisha; Unaujua moyo wangu, na ningependa kwamba Uwekeze zaidi ya upendo Wako ndani yangu.” Huu ndio utendaji wakati wa usafishaji. Ukitumia upendo wa Mungu kama msingi, usafishaji unaweza kukuleta karibu zaidi na Mungu na kukufanya mwandani zaidi wa Mungu. Kwa kuwa unamwamini Mungu, ni lazima uukabidhi moyo wako mbele ya Mungu. Ukiutoa moyo wako na kuuweka mbele ya Mungu, basi wakati wa usafishaji, haitawezekana wewe kumkana Mungu, au kumwacha Mungu. Kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa karibu hata zaidi, na wa kawaida hata zaidi, na mawasiliano yako na Mungu yatakuwa ya mara kwa mara zaidi. Ikiwa wewe daima hutenda kwa jinsi hii, basi utashinda wakati zaidi katika mwanga wa Mungu, na wakati zaidi chini ya mwongozo wa maneno Yake, kutakuwa pia na mabadiliko zaidi na zaidi katika tabia yako, na ufahamu wako utaongezeka kila siku. Siku itakapokuja na majaribu ya Mungu yakufike kwa ghafla, hutaweza tu kusimama kando ya Mungu, bali pia utaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Wakati huo, utakuwa kama Ayubu, na Petro. Baada ya kuwa na ushuhuda kwa Mungu, utampenda kwa kweli, na utamtolea maisha yako kwa furaha; utakuwa shahidi wa Mungu, na yule ambaye ni mpendwa wa Mungu. Upendo ambao umepitia usafishaji ni wa nguvu, na sio dhaifu. Haijalishi ni lini au vipi Mungu anakufanya upatwe na majaribu Yake, unaweza kutojali ikiwa unaishi au unaangamia, kuachana na kila kitu kwa furaha kwa ajili ya Mungu, na kuvumilia chochote kwa furaha kwa ajili ya Mungu—na hivyo upendo wako utakuwa safi, na imani yako halisi. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu anayependwa na Mungu kwa kweli, na ambaye amefanywa kamili na Mungu kwa kweli.
Watu wakijipata chini ya ushawishi wa Shetani, basi hawana upendo kwa Mungu ndani yao, na maono, upendo na azimio yao ya awali yamepotea. Watu walikuwa wakihisi kwamba walifaa kuteseka kwa ajili ya Mungu, lakini leo wanafikiri kwamba ni aibu na hawakosi malalamiko. Hii ni kazi ya Shetani; inaonyesha kwamba mwanadamu amemilikiwa na Shetani. Ukikabiliwa na hali hii ni sharti uombe, na kugeukia upande ule mwingine haraka uwezavyo—hii itakulinda dhidi ya mashambulizi wa Shetani. Ni wakati wa usafishaji mkali ambapo mwanadamu anaweza kujipata chini ya ushawishi wa Shetani kwa urahisi zaidi—kwa hivyo ni jinsi gani unapaswa kumpenda Mungu wakati wa usafishaji kama huu? Unapaswa kuyaita mapenzi yako, kuuweka moyo wako mbele ya Mungu na kutenga muda wako wa mwisho Kwake. Haijalishi jinsi gani Mungu hukusafisha, unafaa kuwa na uwezo wa kutia ukweli katika vitendo kutimiza mapenzi ya Mungu, na unafaa kujitolea kumtafuta Mungu na kutafuta mawasiliano na Mungu. Nyakati kama hizi, zaidi unavyokaa tu, ndivyo utakuwa mtu hasi zaidi, na ndivyo itakuwa rahisi zaidi kwako kurudi nyuma. Wakati ambapo inakulazimu kutenda kazi yako, ingawa huitendi vyema, unafanya kila unachoweza, na unaifanya kwa kutumia tu upendo wako wa Mungu; bila kujali kile ambacho wengine husema—ikiwa wanasema umetenda vyema, au kwamba umetenda vibaya—motisha zako ni sahihi, na wewe sio wa kujidai, kwani unatenda kwa niaba ya Mungu. Wengine wanapokuelewa vibaya, unaweza kumwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Siombi kwamba wengine wanivumilie, wala kwamba wanisamehe. Naomba tu kwamba niweze kukupenda moyoni mwangu, kwamba niwe na uhakika moyoni mwangu, na kwamba dhamiri yangu ni safi. Siombi kwamba wengine wanisifu, au kuniheshimu, ninatafuta tu kukuridhisha kutoka moyoni mwangu, ninatenda wajibu wangu kwa kufanya kila ninachoweza, na ingawa mimi ni mpumbavu na mjinga, na mwenye ubora wa tabia duni, na kipofu, najua kwamba Unapendeza, na niko tayari kukutolea kila ninacho.” Punde tu unapoomba kwa jinsi hii, upendo wako kwa Mungu huibuka, na unahisi uhakika zaidi moyoni mwako. Hili ndilo linalomaanishwa na kutenda upendo wa Mungu. Unavyopata uzoefu, utashindwa mara mbili na kufaulu mara moja, au pia ushindwe mara tano na kufaulu mara mbili, na unavyopata uzoefu kwa jinsi hii, ni katikati ya kushindwa tu ndipo utaweza kuona uzuri wa Mungu na kugundua kinachokosa ndani yako. Unapopitia hali kama hizi tena, unafaa kujitahadharisha, kutuliza mwendo wako, na kuomba mara nyingi zaidi. Polepole utakuza uwezo wa kushinda katika hali kama hizi. Hilo linapofanyika, maombi yako ni yamekuwa yenye matokeo yanayotarajiwa. Unapoona umefanikiwa wakati huu, utafurahishwa ndani yako, na unapoomba utaweza kumhisi Mungu, na kuhisi kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu haujakutoka—na ni hapo tu ndipo utajua jinsi Mungu hufanya kazi ndani yako. Kutenda kwa njia hii kutakupa njia inayoelekea katika uzoefu. Usipoutia ukweli katika vitendo, basi utakuwa bila uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako. Lakini ukiutia katika vitendo, basi ingawa unaumia ndani, baadaye Roho Mtakatifu atakuwa nawe, utaweza kuhisi uwepo wa Mungu unapoomba, utakuwa na nguvu ya kutenda maneno ya Mungu, na wakati wa mawasiliano na ndugu zako, hakutakuwa na chochote kinachosumbua dhamiri yako, na utahisi amani, na kwa jinsi hii, utaweza kufunua yale ambayo umefanya. Bila kujali yale ambayo wengine husema, utaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, hutazuiliwa na wengine, hutashindwa na lolote—na katika hili, utaonyesha kwamba kutenda kwako maneno ya Mungu kumekuwa kwa matokeo yanayotarajiwa.
Kadiri usafishaji wa Mungu ulivyo mkubwa, ndivyo mioyo ya watu inaweza kumpenda Mungu zaidi. Mateso ndani ya mioyo yao ni ya manufaa kwa maisha yao, wanaweza zaidi kuwa na amani mbele ya Mungu, uhusiano wao na Mungu ni wa karibu zaidi, na wanaweza kuona vizuri zaidi upendo wa juu kabisa wa Mungu na wokovu Wake wa juu kabisa. Petro alipitia usafishaji mamia ya mara, na Ayubu alipitia majaribio kadhaa. Ikiwa mngependa kufanywa kamili na Mungu, nyinyi pia sharti mpitie usafishaji mamia ya mara; ni ikiwa tu lazima mpitie mchakato huu, na lazima mtegemee hatua hii, ndiyo mnaweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, na kufanywa kamili na Mungu. Usafishaji ndio njia bora zaidi ambayo Mungu hutumia kuwafanya watu kamili; usafishaji na majaribio makali pekee ndiyo yanaweza kusababisha kuonekana upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo ya watu. Bila taabu, watu hukosa upendo wa kweli kwa Mungu; ikiwa hawajaribiwi ndani, na hawapitii usafishaji kwa kweli, basi mioyo yao daima itakuwa ikielea katika dunia ya nje. Baada ya kusafishwa hadi kiwango fulani, utayaona mapungufu na matatizo yako mwenyewe, utaona kiasi ambacho unakosa na kwamba huwezi kuzishinda zile shida nyingi unazokabiliwa nazo, na utaona jinsi kutotii kwako kulivyo kukubwa. Ni katika majaribu pekee ndipo watu wataweza kujua kwa kweli hali zao halisi, na majaribu huwafanya watu waweze kufanywa kamili vyema zaidi.
Katika maisha yake, Petro alipitia usafishaji mamia ya mara na alipitia majaribu mengi ya uchungu. Usafishaji huu ukawa msingi wa upendo wake mkubwa kabisa kwa Mungu na ukawa uzoefu muhimu zaidi katika maisha yake yote. Kwamba aliweza kuwa na upendo mkubwa kabisa wa Mungu ilikuwa, kwa namna moja, kwa sababu ya uamuzi wake kumpenda Mungu; la muhimu zaidi, hata hivyo, ilikuwa kwa sababu ya usafishaji na mateso aliyopitia. Mateso haya yakawa mwongozo wake katika njia ya kumpenda Mungu, na yakawa jambo lililokumbukwa zaidi kwake. Ikiwa watu hawapitii uchungu wa usafishaji wanapompenda Mungu, basi upendo wao umejaa ukawaida na mapendeleo yao; upendo kama huu umejaa mawazo ya Shetani, na hauwezi hata kabisa kuridhisha mapenzi ya Mungu. Kuwa na azimio la kumpenda Mungu sio sawa na kumpenda Mungu kwa kweli. Hata ingawa yote wanayofikiria mioyoni mwao ni kwa ajili ya kumpenda Mungu, na kumridhisha Mungu, kana kwamba fikira zao hazina mawazo yoyote ya kibinadamu, kana kwamba zote ni kwa ajili ya Mungu, fikira zao zinapoletwa mbele ya Mungu, fikira kama hizi hazisifiwi wala kubarikiwa na Mungu. Hata wakati watu wameelewa kikamilifu ukweli wote—wakati wamekuja kuujua wote—hili haliwezi kusemwa kuwa ishara ya kumpenda Mungu, haiwezi kusemwa kwamba watu hawa hakika wanampenda Mungu. Licha ya kuelewa ukweli mwingi bila kupitia usafishaji, watu hawana uwezo wa kutia ukweli huu katika vitendo; ni wakati wa usafishaji tu ndipo watu wanaweza kuelewa maana halisi ya ukweli huu, hapo tu ndipo watu wanaweza kufahamu kwa kweli maana yao ya ndani. Wakati huo, wanapojaribu tena, wanaweza kutia ukweli katika vitendo kwa njia ya kufaa, na kulingana na mapenzi ya Mungu; wakati huo, mawazo yao ya kibinadamu yanafanywa kuwa kidogo, ukawaida wao wa kibinadamu unashushwa, na hisia zao za kibinadamu zinapunguzwa; ni wakati huo tu ndipo utendaji wao ni onyesho la ukweli la upendo wa Mungu. Athari ya ukweli wa upendo wa Mungu haitimizwi kupitia ufahamu wa kusemwa au kuwa tayari kiakili, wala haiwezi kutimizwa kwa kueleweka tu. Inahitaji kwamba watu walipe gharama, na kwamba wapitie uchungu mwingi wakati wa usafishaji, na hapo tu ndipo upendo wao utakuwa safi, na wa kuupendeza moyo wa Mungu. Katika hitaji Lake kwamba mwanadamu ampende, Mungu hadai kwamba mwanadamu ampende kwa kutumia mapenzi makali, au ukawaida; kwa uaminifu tu na utumiaji wa ukweli kumtumikia ndipo mwanadamu anaweza kumpenda kwa kweli. Lakini mwanadamu huishi katikati ya ukawaida, na hivyo hana uwezo wa kutumia ukweli na uaminifu kumtumikia Mungu. Yeye ama ni mwenye kutekwa na hisia kali kumhusu Mungu au hana hisia zozote na hajali, au anampenda Mungu kwa kiwango cha juu zaidi au anamchukia kabisa. Wale ambao huishi katikati ya ukawaida daima huishi katikati ya vipeo hivi viwili, na wao daima huishi katika hali isiyo na ukweli, na huamini kwamba wako sahihi. Ingawa Nimetaja hili mara kwa mara, watu hawana uwezo wa kulichukulia kwa uzito, hawawezi kutambua kikamilifu umuhimu wake, na hivyo wanaishi katikati ya imani ya kujidanganya na katika madanganyo ya upendo kwa Mungu usio na ukweli. Kotekote katika historia, kadiri mwanadamu ameendelea na enzi zimepita, mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu yamekuwa ya juu zaidi, na Amezidi kudai kwamba mwanadamu awe kamili Kwake. Ilhali ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu umekuwa usio yakini na wa dhahania zaidi na zaidi, na upendo wake wa Mungu kwa kufuatana umekuwa mchafu zaidi na zaidi. Hali ya mwanadamu na yote afanyayo yanazidi kubishana na mapenzi ya Mungu, kwa maana mwanadamu amepotoshwa kwa kina zaidi na Shetani. Hili linahitaji kwamba Mungu afanye kazi zaidi, na kazi kubwa zaidi, ya wokovu. Mwanadamu anazidi kulipisha kwa nguvu katika mahitaji yake kwa Mungu, na upendo wake wa Mungu unapunguka zaidi na zaidi. Watu wanaishi katika uasi, bila ukweli, na wanaishi maisha yasiyo na ubinadamu; hawana tu upendo hata kidogo kwa Mungu, lakini pia wamejaa tele uasi na upinzani. Ingawa wanafikiri kuwa tayari wana upendo mkubwa kabisa kwa Mungu, na hawawezi kuwa wa hisani zaidi Kwake, Mungu haamini hivyo. Ni dhahiri kabisa Kwake jinsi upendo wa mwanadamu Kwake umeoza, na Hawajawahi kubadilisha maoni Yake ya mwanadamu kwa sababu ya ushawishi wa mwanadamu, wala kuwahi kulipiza ukarimu wa mwanadamu kwa sababu ya kujitolea kwake. Tofauti na binadamu, Mungu anaweza kutofautisha: Anajua yule anayempenda kwa kweli na yule asiyempenda, na badala ya kujawa na ari na kupotea kwa sababu ya mvuto wa ghafla wa mwanadamu, Anamtendea mwanadamu kulingana na asili na tabia ya mwanadamu. Mungu, hata hivyo, ni Mungu, na Ana hadhi Yake na utambuzi Wake; mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu na Mungu hatapumbazwa na upendo wa mwanadamu ambao unazozana na ukweli. Kinyume chake, Anachukulia yote ambayo mwanadamu hufanya kwa jinsi ifaayo.
Anapokabiliwa na hali ya mwanadamu na mtazamo wake kwa Mungu, Mungu amefanya kazi mpya, Akimruhusu mwanadamu kuwa na ufahamu Wake na utiifu Kwake, na upendo pia na ushahidi. Hivyo, mwanadamu lazima apitie usafishaji wa Mungu kwake, na pia hukumu, ushughulikiaji na upogoaji Wake kwake, ambazo pasi nazo mwanadamu hangewahi kumjua Mungu, na hangewahi kuwa na uwezo wa kumpenda kwa kweli na kuwa na ushuhuda Kwake. Usafishaji wa Mungu kwa mwanadamu sio tu kwa ajili ya athari inayoegemea upande mmoja, bali kwa ajili ya athari inayogusia pande nyingi. Ni kwa jinsi hii tu ndiyo Mungu hufanya kazi ya usafishaji kwa wale ambao wako tayari kutafuta ukweli, ili upendo na uamuzi wa mwanadamu yafanywe timilifu na Mungu. Kwa wale walio tayari kuutafuta ukweli na wanaomtamani Mungu, hakuna kilicho cha maana zaidi, au cha usaidizi zaidi, kuliko usafishaji kama huu. Tabia ya Mungu haijulikani wala kueleweka kwa urahisi sana na mwanadamu, kwani Mungu, hatimaye, ni Mungu. Mwishowe, haiwezekani kwa Mungu kuwa na tabia sawa na mwanadamu, na hivyo si rahisi kwa mwanadamu kujua tabia Yake. Ukweli haumilikiwi kwa asili na mwanadamu, na hauleweki kwa urahisi na wale ambao wamepotoshwa na Shetani; mwanadamu hana ukweli na hana azimio la kutia ukweli katika vitendo, na asipoteseka, na asisafishwe au kuhukumiwa, basi uamuzi wake hautawahi kufanywa timilifu. Kwa watu wote, usafishaji ni wa kutesa sana na ni mgumu sana kukubali—ilhali ni katika usafishaji ndipo Mungu huweka wazi tabia Yake ya haki kwa mwanadamu, na Huweka hadharani mahitaji Yake kwa mwanadamu, na Hutoa nuru zaidi, na upogoaji na ushughulikiaji halisi zaidi; kwa kulinganisha mambo ya hakika na ukweli, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi kujihusu na ukweli, na Humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu, hivyo kumruhusu mwanadamu kuwa na upendo wa kweli zaidi na safi zaidi wa Mungu. Haya ndiyo malengo ya Mungu katika kutekeleza usafishaji. Kazi yote Afanyayo Mungu kwa mwanadamu ina malengo yake na maana yake; Mungu hafanyi kazi isiyo na maana, wala Hafanyi kazi isiyo na manufaa kwa mwanadamu. Usafishaji haumaanishi kuondoa watu kutoka mbele ya Mungu, wala haumaanishi kuwaangamiza katika kuzimu. Unamaanisha kubadilisha tabia ya mwanadamu wakati wa usafishaji, kubadilisha motisha zake, mitazamo yake ya kale, kubadilisha upendo wake kwa Mungu, na kubadilisha maisha yake yote. Usafishaji ni jaribio la kweli la mwanadamu, na aina ya mafunzo halisi na ni wakati wa usafishaji tu ndipo upendo wake unaweza kutimiza wajibu wake wa asili.

Ijumaa, 29 Machi 2019

Muujiza katika Msiba | Video ya Injili "Mungu Abariki"


Muujiza katika Msiba | Video ya Injili "Mungu Abariki"

Watu mara nyingi husema kwamba "Dhoruba hukusanyika bila tahadhari na balaa huwafika watu kwa ghafula sana." Katika enzi yetu iliyopo ya kupanua kwa haraka kwa sayansi, uchukuzi wa kisasa na utajiri wa mali, maafa yanayotokea pande zote zinazotuzunguka huongeza kila siku. Tunapoligeuza na kulifungua gazeti au kuwasha TV, tunayoyaona hasa ni: vita, matetemeko ya ardhi, sunami, tufani, moto, mafuriko, ajali za ndege, maafa ya kuchimba madini, msukosuko wa kijamii, mgongano mkali sana, mashambulizi ya kigaidi nk. Yote tunayoona ni maafa ya kiasili na maafa yaliyotengenezwa na mtu. Maafa haya yanatokea mara kwa mara na yanazidi kuwa makali zaidi. Shambulizi hili la maafa huleta mateso, damu, kulemazwa na kifo. Misiba hutokea pande zote zinazotuzunguka wakati wote, ikisisitiza ufupi na udhaifu wa maisha. Hatuna njia ya kutabiri ni aina gani ya maafa tutakayokutana nayo katika siku zijazo. Aidha, hatujui ni mkondo gani wa hatua tunaopaswa kuchukua. Kama wanajumuiya wa wanadamu, tunapaswa kufanya nini ili kuondokana na maafa haya? Katika programu hii, utapata jibu. Utapata njia ya pekee ya kupokea ulinzi wa Mungu ili kwamba uweze kunusurika maafa yanayokaribia.
Mwenyezi Mungu alisema, Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, wala njia inayoweza kukuongoza kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.
Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

Alhamisi, 28 Machi 2019

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao kwa Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na ukweli unaopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi unatii mipango ya Mungu katika mambo yote, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako. Ukifika mahali hapo utafurahia kujua imani katika Mungu ni nini, namna ya kumwamini Mungu vizuri, na kile unachopaswa kufanya ili kutenda mambo kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu. Hili litakufanya utii kikamilifu kazi ya Mungu, na hutakuwa na malalamiko, hutahukumu, au kuchambua, sembuse kutafiti. Zaidi ya hayo, nyote mtakuwa na uwezo wa kumtii Mungu hadi kifo, mkimruhusu Mungu awaongoze na kuwachinja kama kondoo, ili nyote muweze kuwa akina Petro wa miaka ya tisini, na muweze kumpenda Mungu kwa hali ya juu sana hata msalabani, bila malalamiko yoyote. Hivyo ndivyo mtakavyoweza kuishi kama akina Petro wa miaka ya tisini.
Kila mtu ambaye ameamua anaweza kumhudumia Mungu—lakini ni lazima iwe kwamba wale tu ambao wanayashughulikia kwa makini mapenzi ya Mungu na kuyafahamu mapenzi ya Mungu ndio wanaohitimu na walio na haki ya kumhudumia Mungu. Nimegundua hili kati yenu: Watu wengi wanaamini ya kuwa bora tu wanaeneza injili kwa bidii kwa ajili ya Mungu, waende barabarani kwa ajili ya Mungu, wajitumie na kuacha vitu kwa ajili ya Mungu, na kadhalika, basi huku ni kumhudumia Mungu; hata zaidi, watu wa kidini huamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kukimbia hapa na pale wakiwa na Biblia mikononi mwao, wakieneza injili ya ufalme wa mbinguni na kuwaokoa watu kwa kuwafanya watubu na kuungama; kuna wakuu wengi wa kidini wanaofikiri kwamba kumhudumia Mungu ni kuhubiri makanisani baada ya kusoma na kufunzwa katika chuo cha seminari, kuwafunza watu kwa kusoma sura za Biblia; pia kuna watu katika maeneo ya umaskini wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kupokea uponyaji na kufukuza mapepo, au kuwaombea ndugu, au kuwahudumia; miongoni mwenu, kunao wengi wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kula na kunywa maneno ya Mungu, kumwomba Mungu kila siku, na pia kutembelea na kufanya kazi katika makanisa kila mahali; kunao ndugu wengine wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kunamaanisha kutoolewa wala kulea familia kamwe, na kutoa nafsi zao zote kwa Mungu. Ilhali watu wachache wanajua maana ya kweli ya kumhudumia Mungu. Ingawa kunao wengi wanaomhudumia Mungu kama nyota angani, idadi ya wale wanaoweza kuhudumu moja kwa moja, na wanaoweza kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, ni hafifu—ndogo isiyo na maana. Kwa nini Ninasema hivi? Ninasema hivi kwa sababu wewe hufahamu kiini cha fungu la maneno “huduma kwa Mungu,” na unafahamu machache sana kuhusu jinsi ya kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu. Leo, tunawasiliana hasa jinsi ya kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu, jinsi ya kuhudumu ili kutosheleza mapenzi ya Mungu.
Ikiwa ungependa kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, ni lazima kwanza ufahamu ni watu wa aina gani wanapendwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanachukiwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanafanywa kuwa kamili na Mungu, na ni watu wa aina gani wana sifa zinazostahili kumhudumia Mungu. Hiki ni kiasi kidogo zaidi unachopaswa kujiandaa nacho. Isitoshe, unapaswa kujua malengo ya kazi ya Mungu, na kazi ambayo Mungu Ataitenda hapa na wakati huu. Baada ya kufahamu haya, na kupitia kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, kwanza unafaa kuingia, na kupokea agizo la Mungu kwanza. Unapopata uzoefu wa kweli kwa msingi wa maneno ya Mungu, na unapojua kweli kazi ya Mungu, utakuwa umehitimu kumhudumia Mungu. Na unapomhudumia ndipo Mungu hufungua macho yako ya kiroho, na kukuruhusu kuwa na ufahamu mkubwa zaidi wa kazi Yake na kuiona dhahiri zaidi. Ukiingia katika ukweli huu, uzoefu wako utakuwa wa kina zaidi na wa kweli, na wale wote ambao wamepata uzoefu wa aina hiyo wataweza kutembea miongoni mwa makanisa mengi na kuwatolea ndugu zako, ili muweze kutumia nguvu za kila mmoja kufidia upungufu wako na kupata maarifa mengi zaidi ndani ya roho zenu. Ni baada tu ya kutimiza matokeo haya ndipo utakapoweza kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu na kufanywa mkamilifu na Mungu wakati wa kufanya huduma yako.
Wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa marafiki wema wa Mungu, wanapaswa kupendwa na Mungu, na kuwa na uaminifu wa hali ya juu kwa Mungu. Bila kujali iwapo unatenda bila kuonekana na watu, au mbele ya watu, unaweza kupata furaha ya Mungu mbele za Mungu, unaweza kusimama imara mbele za Mungu, na bila kujali jinsi watu wengine wanavyokutendea, wewe huifuata njia yako mwenyewe kila mara, na kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu. Mtu wa aina hii pekee ndiye rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu wanaweza kumhudumia Yeye moja kwa moja kwa sababu wamepewa agizo kuu la Mungu, na mzigo wa Mungu, wao wanaweza kuuchukulia moyo wa Mungu kama moyo wao wenyewe, na mzigo wa Mungu kama mzigo wao wenyewe, na hawazingatii iwapo watafaidi au watapoteza matarajio: Hata wasipokuwa na matarajio, na hawatafaidi chochote, watamwamini Mungu daima kwa moyo wa upendo. Kwa hivyo, mtu wa aina hii ni rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu ni wasiri Wake pia; ni wasiri wa Mungu pekee ndio wanaoweza kushiriki katika kutotulia Kwake, matamanio Yake, na ingawa mwili wao una uchungu na ni mdhaifu, wanaweza kuvumilia uchungu na kuacha kile wanachokipenda ili kumridhisha Mungu. Mungu huwapa watu wa aina hii mizigo mingi, na kile ambacho Mungu atafanya hudhihirishwa kupitia kwa watu hawa. Yaani, watu hawa wanapendwa na Mungu, wao ni watumishi wa Mungu wanaoupendeza moyo Wake, na ni watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza kutawala pamoja na Mungu. Ukishakuwa rafiki mwema wa Mungu ndipo utakapoweza kabisa kutawala pamoja na Mungu.
Yesu aliweza kukamilisha agizo la Mungu—kazi ya ukombozi wa wanadamu wote—kwa sababu alikabidhi kila tatizo kwa mapenzi ya Mungu, bila kufuata mipango na fikira Zake binafsi. Basi pia, Yeye Alikuwa rafiki mwema wa Mungu—Mungu Mwenyewe, jambo ambalo nyote mnalielewa vizuri sana. (Kwa kweli, alikuwa Mungu Mwenyewe aliyetolewa ushahidi na Mungu; Ninataja jambo hili hapa kwa kuutumia ukweli wa Yesu ili kuonyesha mfano wa suala hili.) Aliweza kuuweka mpango wa usimamizi wa Mungu katika kiini cha mambo yote, na kila mara alimwomba Baba wa mbinguni na kuyatafuta mapenzi ya Baba wa mbinguni. Aliomba, na kusema: “Mungu Baba! Timiza kile ambacho ni mapenzi Yako, na usitende kulingana na nia Zangu; ingekwa heri ukitenda kulingana na mpango Wako. Mwanadamu anaweza kuwa dhaifu, lakini kwa nini unapaswa kumshughulikia? Ni vipi ambavyo mwanadamu aliweza kuwa mhusika wa shughuli Zako, mwanadamu ambaye ni kama chungu mkononi Mwako? Ndani ya moyo Wangu, Ninatamani tu kutimiza mapenzi Yako, na Ninatamani Utende Unachotaka kutenda ndani Yangu kulingana na makusudio Yako mwenyewe.” Alipokuwa njiani kuelekea Yerusalemu, Yesu alihisi maumivu makali, kama kwamba kisu kilikuwa kimedungwa ndani ya moyo Wake, ilhali hakuwa na nia yoyote ya kwenda kinyume cha Neno lake; kila mara kulikuwa na nguvu zenye uwezo mkuu zilizomvutia Yeye kuelekea mahali ambapo Angesulubiwa. Mwishowe, alipigiliwa misumari juu ya msalaba na akawa mfano wa mwili wenye dhambi, akiikamilisha kazi hiyo ya ukombozi wa wanadamu, na kufufuka kutoka kwa pingu za kifo na Kuzimu. Mbele Yake, kifo, jehanamu, na Kuzimu vilipoteza nguvu zao, na vilishindwa Naye. Aliishi miaka thelathini na tatu, na katika miaka hiyo yote daima Alifanya kila Alichoweza kutimiza mapenzi ya Mungu kulingana na kazi ya Mungu wakati huo, bila kuzingatia atakachofaidi au kupoteza Yeye binafsi, na kila mara akiwaza kuhusu mapenzi ya Mungu Baba. Hivyo, baada ya Yeye kubatizwa, Mungu alisema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Kwa sababu ya huduma Yake mbele ya Mungu, iliyokuwa na upatanifu na mapenzi ya Mungu, Mungu aliuweka mzigo mzito wa kuwakomboa wanadamu wote juu ya mabega yake na akamfanya ajitolee kuutimiza, na Alikuwa na ujuzi na ustahiki wa kuikamilisha kazi hii muhimu. Katika maisha Yake yote, alivumilia mateso yasiyokuwa na kipimo kwa ajili ya Mungu, na alijaribiwa na Shetani mara nyingi, lakini hakufa moyo. Mungu alimpa kazi ya aina hiyo kwa sababu Alimwamini Yeye, na kumpenda Yeye, na hivyo basi Mungu mwenyewe alisema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Wakati huo, ni Yesu pekee ambaye angeweza kutimiza agizo hili, na hii ilikuwa sehemu moja ya Mungu kutimiza kazi Yake ya kuwakomboa wanadamu wote katika Enzi ya Neema.
Ikiwa, kama Yesu, unaweza kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu, na kuyakataa mambo ya mwili wako, Mungu atakuaminia kazi Zake muhimu, ili uweze kufikia masharti ya kumhudumia Mungu. Ni katika hali hizo pekee ndipo utakapothubutu kusema kwamba unafanya mapenzi ya Mungu na kukamilisha agizo Lake, hapo ndipo utakapothubutu kusema unamhudumia Mungu kweli. Ukilinganishwa na mfano wa Yesu, unaweza kuthubutu kusema kwamba wewe ni mwandani wa Mungu? Je, unaweza kuthubutu kusema kwamba unatekeleza mapenzi ya Mungu? Je, unaweza kuthubutu kusema kwamba kweli unamhudumia Mungu? Iwapo, leo, hufahamu aina hii ya huduma kwa Mungu, unaweza kuthubutu kusema kwamba wewe ni rafiki mwema wa Mungu? Ukisema kwamba unamhudumia Mungu, humkufuru Yeye? Fikiria kuhusu hilo: Je, unamhudumia Mungu, au unajihudumia wewe mwenyewe? Unamhudumia Shetani, ilhali kwa ukaidi unasema kwamba unamhudumia Mungu—katika jambo hili humkufuru Mungu? Watu wengi walio nyuma Yangu wanatamani baraka ya cheo, wana ulafi wa chakula, wanapenda kulala na kuushughulikia mwili kwa makini, kila mara wakiogopa kwamba hakuna njia ya kuondoka ndani ya mwili. Hawaifanyi kazi yao ya kawaida kanisani, na kula chakula cha bure, au wanawaonya ndugu zao kwa maneno Yangu, wanasimama juu na kuwatawala wengine. Watu hawa huendelea kusema kwamba wanafanya mapenzi ya Mungu, wao husema kila mara kwamba ni marafiki wema wa Mungu—huu si upuuzi? Ikiwa una motisha iliyo sahihi, lakini huwezi kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, basi wewe unakuwa mpumbavu; lakini ikiwa motisha yako si sahihi, na bado unasema kwamba unamhudumia Mungu, basi wewe ni mtu anayempinga Mungu, na unastahili kuadhibiwa na Mungu! Sina huruma kwa watu wa aina hiyo! Wao hula chakula cha bure katika nyumba ya Mungu, na kila mara wao hutamani raha za mwili, na hawazingatii mambo ambayo Mungu anayapenda; kila mara wao hutafuta mambo yaliyo mazuri kwao, wala hawatilii maanani mapenzi ya Mungu, mambo yote wanayoyafanya hayaongozwi na Roho wa Mungu, kila mara wao hufanya hila na njama dhidi ya ndugu zao, na kuwa ndumakuwili, kama mbweha ndani ya shamba la mizabibu, akiiba mizabibu kila mara na kulikanyaga na kuliharibu shamba la mizabibu. Je, watu wa aina hiyo wanaweza kuwa marafiki wema wa Mungu? Je, unastahili kupokea baraka za Mungu? Wewe huwajibiki kuhusu maisha yako na kanisa, unastahili kupokea agizo la Mungu? Ni nani anayeweza kuthubutu kumwamini mtu kama wewe? Unapohudumu kwa njia hii, je, Mungu anaweza kuthubutu kukuaminia kazi kubwa zaidi? Je, si wewe unachelewesha mambo?
Nasema hivi ili uweze kujua masharti yanayohitajika kutimizwa ili kuhudumu kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu. Usipoutoa moyo wako kwa Mungu, usipoyashugulikia kwa makini mapenzi ya Mungu kama alivyofanya Yesu, basi huwezi kuaminiwa na Mungu, na mwishowe utahukumiwa na Mungu. Labda leo, katika huduma yako kwa Mungu, kila mara wewe huficha kusudi la kumdanganya Mungu—lakini bado Mungu atakugundua. Kwa kifupi, bila kujali mambo yote mengine, ukimdanganya Mungu hukumu isiyo na huruma itakujia. Unapaswa kutumia vizuri nafasi ya kuwa umeingia katika njia sahihi ya kumhudumia Mungu kwa kumpa Mungu moyo wako kwanza, bila kugawanya uaminifu wako. Bila kujali iwapo uko mbele za Mungu, au mbele ya watu wengine, moyo wako unapaswa kuelekezwa kwa Mungu kila wakati, na unapaswa kufanya uamuzi wa kumpenda Mungu kama Yesu. Kwa kufanya hivi, Mungu atakufanya uwe mkamilifu, ili uwe mtumishi wa Mungu anayempendeza Mungu. Ikiwa ungependa kweli kufanywa mkamilifu na Mungu, na huduma yako iwe katika upatanifu na mapenzi Yake, basi unapaswa kubadilisha maoni yako ya awali kuhusu imani kwa Mungu, na kubadilisha jinsi ulivyokuwa ukimhudumia Mungu, ili nafsi yako yote iweze kufanywa kuwa kamilifu na Mungu; kwa kufanya hivi, Mungu hatakuacha, na, kama Petro, utakuwa katika kikosi cha mbele cha wale wanaompenda Mungu. Ukibaki kuwa mtu asiyetubu, basi utakutana na mwisho kama wa Yuda. Hii inapaswa kufahamika na watu wote wanaomwamini Mungu.

Jumatano, 27 Machi 2019

Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yanayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake. Hayo ndiyo binadamu wote wanayaamini. Aina hii ya imani kwa Mungu haitaruhusu binadamu kupatwa na kukamilishwa Naye kwa uhakika. Kwa kweli, si kwamba neno la Mungu ni pungufu, badala yake uwezo wa binadamu wa kupokea neno Lake ni duni mno. Inaweza kusemwa karibu binadamu wote hutenda kulingana na nia za Mungu. Badala yake, imani yao kwa Mungu ni kwa mujibu wa nia zao wenyewe, fikra za kidini zilizowekwa, na desturi. Ni wachache wanaopitia mabadiliko baada ya kulikubali neno la Mungu na kuanza kutenda kwa mujibu wa mapenzi Yake. Badala yake, wanaendelea katika imani yao potovu. Wakati mwanadamu anaanza kuamini katika Mungu, anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za kawaida za dini, na anaishi na kuhusiana na wengine kwa misingi ya falsafa yake ya maisha. Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu tisa kati ya kila watu kumi. Ni wachache sana wanaounda mpango mwingine na kuanza mwanzo mpya baada ya kuanza kumwamini Mungu. Hakuna anayeona au kuweka katika vitendo neno la Mungu kama ukweli.
Chukua imani katika Yesu, kwa mfano. Kama mtu alikuwa mwanafunzi katika imani au alikuwa wa imani hiyo kwa muda mrefu, wote walitumia “vipaji” vyovyote walivyokuwa navyo na kuonyesha “ujuzi” wowote waliokuwa nao. Mwanadamu aliongeza tu “imani katika Mungu,” maneno haya matatu, katika maisha yake ya kawaida, bado hayakufanya mabadiliko katika tabia yake, na imani yao kwa Mungu haikukua hata kidogo. Ukimbizaji wa mwanadamu wa swala hili haukuwa baridi wala moto. Hakusema kwamba hakuamini, lakini pia hakujitoa kikamilifu kwa Mungu. Hakuwahi kumpenda Mungu kwa kweli wala kumtii Mungu. Imani yake kwa Mungu ilikuwa halali na ya kujifanya, na aligeuka na akapuuza na wala hakuwa na bidii kwa kutenda imani yake. Aliendelea katika hali kama hiyo ya kuchanganyikiwa tangu mwanzo hadi wakati wake wa kufa. Ni nini maana ya hili? Leo, lazima uwe katika njia sahihi kwani unaamini katika Mungu wa vitendo. Kwa kuwa una imani katika Mungu, hupaswi tu kutafuta baraka, lakini pia kutafuta kumpenda Mungu na kumjua Mungu. Kupitia kwa kupata nuru kutoka Kwake na harakati yako mwenyewe, unaweza kula na kunywa neno Lake, kukuza ufahamu wa kweli kuhusu Mungu, na kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu unaotoka moyoni mwako. Kwa maneno mengine, upendo wako kwa Mungu ni wa kweli zaidi, ambapo hakuna yeyote anayeweza kuharibu au kukuzuia kuonyesha upendo wako Kwake. Basi uko kwa njia ya kweli ya imani kwa Mungu. Inathibitisha kwamba wewe unamilikiwa na Mungu, kwani moyo wako umemilikiwa na Mungu na wala huwezi kumilikiwa na kitu kingine. Kutokana na tajriba yako, malipo uliyolipa, na kazi ya Mungu, wewe una uwezo wa kuendeleza upendo usioamriwa kwa Mungu. Kisha unawekwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa neno la Mungu. Ni wakati tu ambao umekuwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza ndipo unaweza kuchukuliwa kuwa umempata Mungu. Katika imani yako kwa Mungu, lazima utafute lengo hili. Huu ni wajibu wa kila mmoja wenu. Hakuna anayelazimika kutosheka na mambo jinsi yalivyo. Hamuwezi kuwa na fikira aina mbili kwa kazi ya Mungu au uichukulie kwa wepesi. Mnapaswa kumfikiria Mungu katika mambo yako yote na wakati wote, na kufanya mambo yote kwa ajili yake. Na wakati mnasema au kufanya mambo, mnapaswa kutilia maanani maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza. Ni hii tu ndio inayolingana na mapenzi ya Mungu.
Kosa kubwa sana la binadamu kuwa na imani katika Mungu ni kwamba imani yake ni ya maneno tu, na Mungu hayupo popote katika maisha yake ya utendaji. Watu wote, kwa kweli, wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini Mungu si sehemu ya maisha yao ya kila siku. Maombi mengi kwa Mungu hutoka katika kinywa cha mtu, lakini Mungu amepewa nafasi ndogo sana katika moyo wake, na hivyo Mungu humjaribu binadamu tena na tena. Kwa vile mtu ni mchafu, Mungu hana budi ila kumjaribu mtu, ili aweze kuona aibu na kisha aje kujitambua mwenyewe katika majaribu. La sivyo, mwanadamu atageuka mwana wa malaika mkuu, na kuzidi kuwa mpotovu. Wakati wa imani ya mtu katika Mungu, nia nyingi na malengo ya kibinafsi hutupwa mbali anavyotakaswa na Mungu bila kukoma. La sivyo, hakuna mwanadamu anayeweza kutumiwa na Mungu, na Mungu hana njia ya kufanya ndani ya mtu kazi anayopaswa kufanya. Mungu kwanza humtakasa mwanadamu. Katika mchakato huu, mtu anaweza kuja kujijua mwenyewe na Mungu huenda akambadilisha mwanadamu. Ni baada ya haya ndipo Mungu anaweza kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kwa njia hii pekee ndio moyo wa binadamu unaweza kumgeukia Mungu kwa ukamilifu. Kwa hivyo, kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Katika njia hii, wanadamu wengi wanaweza kusema wana maarifa mengi, lakini katika wakati wao wa kufa, macho yao hujawa machozi, nao hujichukia wenyewe kwa kuharibu maisha yao yote na kuishi maisha yasiyo na mazao hadi uzeeni. Wanaelewa tu mafundisho lakini hawawezi kutia ukweli katika vitendo na kushuhudia kwa Mungu, badala yake wakikimbia huku na kule, wakiwa na kazi kama nyuki; mara wanapochungulia kaburi wao hatimaye huona kwamba hawana ushuhuda wa kweli, kwamba hawamjui Mungu kamwe. Je, si huku ni kuchelewa mno? Kwa nini usichukue nafasi hii na kutafuta ukweli unaoupenda? Kwa nini usubiri hadi kesho? Iwapo katika maisha huwezi kuteseka kwa ajili ya ukweli au kutafuta kuupata, inaweza kuwa kwamba unataka kujuta katika saa yako ya kufa? Ikiwa hivyo, basi kwa nini umwamini Mungu? Kwa kweli, kuna mambo mengi ambayo mtu, iwapo ataweka juhudi kidogo tu, anaweza kuweka ukweli katika vitendo na hivyo kumridhisha Mungu. Moyo wa binadamu daima umepagawa na mapepo na kwa hivyo hawezi kutenda mambo kwa ajili ya Mungu. Badala yake, yeye daima yumo katika safari ya huku na kule kwa sababu ya mwili, na hafaidiki na chochote mwishowe. Ni kwa sababu hizi ndio mtu hupata matatizo ya mara kwa mara na mateso. Je, haya sio mateso ya Shetani? Je, huu sio ufisadi wa mwili? Hufai kumdanganya Mungu kwa maneno ya mdomo. Badala yake, lazima uchukue hatua inayoonekana. Usijidanganye; ni nini maana katika hilo? Ni faida gani utakayopata kutokana na kuishi kwa ajili ya mwili wako na kufanya bidii kwa ajili ya umaarufu na mali ya dunia?

Jumanne, 26 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawa Nimejazwa na hukumu na adabu kwa binadamu, kila ninachofanya bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, kwa ajili ya kueneza injili Yangu kwa njia bora zaidi na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili. Kwa hiyo leo, katika wakati ambapo watu wengi tayari wametamauka pakubwa, Naendelea na kazi Yangu, Nikiendeleza kazi ambayo lazima Nifanye ili kuhukumu na kuadibu binadamu. Licha ya ukweli kwamba binadamu amechoshwa na kile Ninachosema na licha ya ukweli kwamba hana tamanio la kujali kuhusu kazi Yangu, Ningali natekeleza wajibu Wangu kwa sababu kusudio la kazi Yangu halijabadilika na mpango Wangu asilia hautabadilika. Kazi ya hukumu Yangu ni kumfanya binadamu anitii Mimi kwa njia bora zaidi, na kazi ya kuadibu Kwangu ni kuruhusu binadamu awe na mabadiliko bora zaidi. Ingawa kile Ninachofanya ni kwa minajili ya usimamizi Wangu, Sijawahi kufanya chochote ambacho hakikufaidi binadamu. Hiyo ndiyo maana Nataka kufanya mataifa yote nje ya Israeli kuwa matiifu tu kama Waisraeli na kuwabadilisha kuwa binadamu halisi, ili Niwe na mahali pa usalama katika nchi zilizo nje ya Israeli. Huu ndio usimamizi Wangu; ndiyo kazi Ninayotimiza katika nchi za Mataifa. Hata sasa, watu wengi bado hawauelewi usimamizi Wangu kwa sababu hawajautilia maanani, badala yake wanafikiria tu kuhusu mustakabali na hatima zao. Haijalishi ni nini Ninachosema, watu hawajali kazi Yangu, badala yake wanalenga tu hatima zao za baadaye. Mambo yakiendelea kwa namna hii, kazi Yangu itapanuliwa vipi? Injili Yangu itaenezwa vipi kotekote ulimwenguni? Lazima mjue kwamba wakati kazi Yangu inapanuka, Nitawatawanya, Nitawaadhibu kama vile tu Yehova alivyoyaadhibu makabila ya Israeli. Haya yote yatafanywa ili injili Yangu iweze kuenea kotekote kwenye ulimwengu mzima, ili kazi Yangu iweze kuenezwa kwa Mataifa, ili kwamba jina Langu litukuzwe na watu wazima na watoto kwa pamoja na jina Langu takatifu litatukuzwa katika vinywa vya watu kutoka makabila na mataifa yote. Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.
Kazi ambayo Nimekuwa nikisimamia kwa maelfu ya miaka inafichuliwa kabisa tu kwa binadamu katika siku za mwisho. Ni sasa tu ndipo Nimelifumbua fumbo kamili la usimamizi Wangu kwa mwanadamu. Binadamu anajua kusudio la kazi Yangu na zaidi ya yote anapata uelewa wa mafumbo Yangu yote. Na Nimemwambia binadamu kila kitu kuhusu hatima ambayo amekuwa akijali kuhusu. Tayari Nimemfichulia binadamu mafumbo yote yaliyofichwa kwa zaidi ya miaka 5,900. Yehova ni nani? Masiha ni nani? Yesu ni nani? Mnafaa kuyajua haya yote. Mabadiliko makubwa ya kazi Yangu yamo katika majina haya. Je, mmeelewa haya? Jina Langu takatifu linafaa kutangazwa vipi? Jina Langu linafaa kuenezwaje katika taifa lolote ambalo limeniita kwa jina Langu lolote? Kazi Yangu tayari imeanza kupanuka, na Nitaeneza ukamilifu wake katika mataifa yote. Kwa sababu kazi Yangu imetekelezwa ndani yenu, Nitawapiga kama vile Yehova alivyowapiga wale wachungaji wa nyumba ya Daudi kule Israeli, na kuwasababisha kutawanyika miongoni mwa mataifa yote. Kwani katika siku za mwisho, Nitapondaponda mataifa yote kuwa vipande vidogo vidogo na kusababisha watu wao kuenezwa upya. Nitakaporudi tena, mataifa yatakuwa tayari yamegawanywa kwa mipaka iliyowekwa na mwako wa moto Wangu utakaokuwa ukichoma. Katika wakati huo, Nitajionyesha upya kwa binadamu kama jua linalochoma, Nikijionyesha kwao hadharani kwa taswira ya yule Aliye Mtakatifu ambaye hawajawahi kumwona, Nikitembea miongoni mwa mataifa yote, kama vile tu Mimi, Yehova, Nilivyotembea miongoni mwa makabila ya Wayahudi. Kuanzia hapo kuendelea, Nitawaongoza watu huku wakiishi ulimwenguni. Hakika watauona utukufu Wangu hapo na hakika wataona pia nguzo ya wingu hewani ili uwaongoze, kwani Nitaonekana katika sehemu takatifu. Binadamu ataiona siku Yangu ya haki na pia maonyesho Yangu ya utukufu. Hilo litafanyika Nitakapoutawala ulimwengu mzima na kuwaleta wana wengi katika utukufu. Kila pahali duniani, watu watainama, nalo hema Langu takatifu litaundwa miongoni mwao juu ya mwamba wa kazi ambayo Natekeleza sasa. Watu watanihudumia pia hekaluni. Madhabahu, yaliyojaa mambo machafu na ya kuchukiza, Nitayavunjavunja vipandevipande na Nitajenga upya mengine. Madhabahu matakatifu yatarundikwa wanakondoo na ndama waliozaliwa karibuni. Nitaangusha hekalu lililopo leo na kujenga jingine upya. Hekalu lililopo sasa na lililojaa watu wenye chuki litaporomoka na lile Nitakalojenga litajaa watumishi watiifu Kwangu. Kwa mara nyingine watasimama na kunihudumia Mimi kwa utukufu wa hekalu Langu. Kwa hakika mtaiona siku ambayo Nitapokea utukufu mkuu na hakika mtaiona siku ambayo Nitaliangusha hekalu na kujenga lingine upya. Pia, hakika mtaona siku ya kuletwa kwa hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu. Huku Nikilibomoa hekalu, ndivyo Nitakavyoleta hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu; itakuwa kama vile tu ambavyo watu wanavyoniona Nikishuka. Baada ya kuangamiza mataifa yote, Nitayakusanya pamoja upya, Nikilijenga hekalu Langu na kuandaa madhabahu Yangu, ili wote waweze kutoa kafara zao Kwangu, kunihudumia Mimi hapo, na kujitolea kwa uaminifu katika kazi Yangu kwenye mataifa mengineyo. Itafanywa namna tu ambavyo wana wa Israeli wanavyofanya sasa, na joho la kuhani na taji la mfalme, utukufu Wangu, Yehova, ukiwa miongoni mwao na uadhama Wangu ukivinjari juu yao na ukiwa nao. Kazi Yangu katika Mataifa itatekelezwa pia katika njia hiyo. Kama vile kazi Yangu kule Israeli ilivyokuwa, ndivyo kazi Yangu katika Mataifa itakavyokuwa kwa sababu Nitaongeza kazi Yangu kule Israeli na kuieneza katika mataifa yale mengine.
Sasa ndio wakati ambao Roho Wangu anafanya kazi pakubwa, na wakati Ninapofanya kazi miongoni mwa Mataifa. Hata zaidi, ndio wakati ambapo Naainisha viumbe wote na kuweka kila kiumbe katika kundi lenye uhusiano, ili kazi Yangu iweze kuendelea haraka zaidi na kwa njia ya kufaa zaidi. Kwa hiyo, bado Nahitaji kwamba mjitoe mzimamzima kwa minajili ya kazi Yangu yote; aidha, mnafaa kutambua waziwazi na kuwa na hakika ya kazi ile yote ambayo Nimefanya ndani yako, na kuweka nguvu zako zote katika kazi Yangu ili iweze kuwa ya matokeo bora zaidi. Hilo ndilo ambalo lazima uelewe. Msipigane tena wenyewe kwa wenyewe, kutafuta mbinu za usuluhishi, au kutafuta raha za mwili, mambo ambayo yanaweza kuchelewesha kazi Yangu na kuharibu mustakabali wako mzuri. Kufanya hivyo, mbali na kuweza kukupa ulinzi, litakuletea maangamizo. Je, si huu utakuwa ujinga kwa upande wako? Kile ambacho unafurahia leo kwa tamaa ndicho kile kile ambacho kinaharibu mustakabali wako, huku yale maumivu unayopitia leo ndiyo yaleyale ambayo yanakulinda. Lazima ufahamu waziwazi kuhusu jambo hilo, ili uepuke majaribio ambayo yatakuwa magumu kujinasua kutoka na kuepuka kuingia kwenye ukungu mzito unaozuia jua katika maisha yako. Wakati ukungu huu mzito utakapotoweka, utajipata katika hukumu ya siku kuu. Kufikia wakati huo, siku Yangu itakuwa imekaribia binadamu. Utatorokaje hukumu Yangu? Utawezaje kuvumilia joto kali la jua? Ninapompa binadamu wingi Wangu, haufurahii kwa dhati, lakini badala yake anautupa nje kwenye sehemu zisizotambulika. Wakati siku Yangu itawadia, binadamu hataweza tena kugundua wingi Wangu au kupata ukweli mkali Niliompa zamani sana. Ataomboleza na kulia, kwa sababu amepoteza mwangaza anaofuata na kuingia katika giza totoro. Kile mnachoona leo ni upanga tu mkali wa kinywa Changu. Bado hamjakiona kiboko kilicho katika mkono Wangu au moto Ninaotumia kumchoma binadamu, na ndiyo maana bado mna kiburi na msio na kadiri mbele Yangu. Ndiyo maana bado mnapigana na Mimi katika nyumba Yangu, huku mkipinga kwa ulimi wa mwanadamu kile ambacho Nimenena na kinywa Changu. Binadamu haniogopi Mimi. Akiwa bado katika uhasama na Mimi hadi leo, bado haniogopi kamwe. Mnao ulimi na meno ya wale wasio na haki vinywani mwenu. Maneno na matendo yenu ni kama yale ya yule nyoka aliyemshawishi Hawa na kumfanya kutenda dhambi. Mnadai nyinyi kwa nyinyi kulipiza kisasi, na mnashindana mbele Yangu kwa ajili ya nafasi, umaarufu, na faida kwa ajili yenu wenyewe, ilhali hamjui kwamba Natazama maneno na matendo yenu kwa siri. Kabla hata ya nyinyi kuja mbele Yangu, Nimejua vina vya nyoyo zenu kabisa. Siku zote binadamu hutamani kutoroka kutoka mfumbato Wangu na kuepuka uangalizi wa macho Yangu, lakini Sijawahi kuepuka maneno au matamshi yake. Badala yake, kwa kusudio kuu huwa Nayaruhusu maneno na matendo hayo yaingie katika macho Yangu, ili Niweze kuadibu udhalimu wake na kuhukumu uasi wake. Kwa hiyo, maneno na matendo fiche ya binadamu siku zote yanawekwa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na hukumu Yangu haijawahi kumtoka binadamu, kwa sababu uasi wake ni mwingi mno. Kazi Yangu ni kuteketeza na kusafisha maneno na matendo yote ya binadamu yaliyotamkwa na kufanywa mbele ya Roho Wangu. Kwa njia hiyo, baada ya Mimi kuondoka ulimwenguni, binadamu wataweza bado kuendeleza utiifu Kwangu, na bado watanihudumia kama vile watumishi Wangu watakatifu wanavyofanya katika kazi Yangu, wakiruhusu kazi Yangu hapa ulimwenguni iendelee mpaka siku itakapokamilika.

Jumatatu, 25 Machi 2019

Kumwamini Mungu Kunapaswa Kulenge Uhalisi, Si Kaida za Kidini

Kumwamini Mungu Kunapaswa Kulenge Uhalisi, Si Kaida za Kidini

Mwenyezi Mungu alisema, Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako? Ni mara ngapi umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, huku ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Vitendo kama hivi pekee ndivyo humridhisha Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli.
Wanadamu wengine wana upendeleo wa kujivutia nadhari. Mbele ya ndugu zao, wanasema kweli ni wadeni wa Mungu, lakini akiwapa kisogo, hawatendi ukweli ila wanafanya tofauti kabisa. Je, hawa si ni Mafarisayo wa dini? Mtu ambaye anampenda Mungu kwa kweli na ana ukweli ni yule ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, lakini bila ya hafichui kwa nje. Yeye yuko tayari kutenda ukweli wakati mambo yanapotokea wala hasemi au kutenda kinyume cha dhamiri yake. Anaonyesha hekima wakati mambo yanapotokea na ni mwenye maadili katika matendo yake, bila kujali hali. Mtu kama huyu ni mtu ambaye anahudumu kwa kweli. Kuna watu wengine ambao mara nyingi shukrani zao kwa kuwa wadeni wa Mungu ni kwa mdomo tu. Siku zao huisha wakiwa na nyuso za wasiwasi, kuonekana wameathiriwa, na kuvalia nyuso za huzuni. Hali ya kuchukiza kweli! Na kama ungewauliza, “Ni kwa njia zipi wewe ni mdeni wa Mungu? Tafadhali niambie!” Hawangeweza kutamka lolote. Kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi usizungumze kuhusu uaminifu wako hadharani, bali tumia matendo yako halisi ili kuonyesha upendo wako kwa Mungu, na kumwomba kwa moyo wa kweli. Wale wanaotumia maneno pekee kushughulika na Mungu ni wanafiki wote! Baadhi yao husema kuwa wao ni wadeni kwa Mungu katika kila sala, na kuanza kulia wakati wowote wanaposali, hata bila kuguswa na Roho Mtakatifu. Watu kama hawa wamepagawa na kaidi na fikira za kidini; wanaishi kulingana na hizo kaidi na fikra, daima wakiamini kwamba matendo kama hayo humpendeza Mungu, na kwamba kumcha Mungu kijuujuu au machozi ya huzuni ndivyo Mungu hupendelea. Ni kitu kipi kizuri kinachoweza kutoka kwa watu kama hao wa kushangaza? Ili kuonyesha unyenyekevu wao, baadhi yao huonyesha neema bandia wakati wanapozungumza mbele ya watu wengine. Baadhi yao kwa makusudi ni wanyonge mbele ya watu wengine, kama mwanakondoo asiye na nguvu yoyote. Je, hii ni tabia ya watu wa ufalme? Mtu wa ufalme sharti awe wa kusisimua na aliye huru, asiye na hatia na aliye na uwazi, mwaminifu na wa kupendeza; mtu aishiye katika hali ya uhuru. Ana tabia za kiajabu na heshima, na anaweza kushuhudia kokote aendako; yeye ni yule anayependwa na Mungu na wanadamu. Wale ambao ni wanafunzi katika imani huwa na matendo mengi ya nje; lazima kwanza wapitie kipindi cha ushughulikiaji na kuvunjwa. Wale ambao wana imani kwa Mungu katika nyoyo zao hawawezi kutofautishwa na wengine kwa nje, lakini vitendo na matendo yao ni ya kupongezwa kwa wengine. Watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza chukuliwa kuwa wanaishi kwa kudhihirisha neno la Mungu. Ukihubiri injili kila siku kwa mtu huyu na yule, ukiwaleta kwa wokovu, ilhali mwishowe, wewe bado unaishi katika sheria na mafundisho, basi wewe huwezi kuleta utukufu kwa Mungu. Watu wa aina hii ni watu wa dini, na wanafiki pia.
Kila mara watu wa kidini kama hao wanapokusanyika, wanauliza, “Dada, umeshinda vipi siku hizi?” Anajibu, “Nahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu na siwezi kuridhisha matakwa ya moyo Wake.” Mwingine anasema, “Mimi, pia, ni mdeni wa Mungu na nimeshindwa kumkidhi.” Sentensi na maneno haya machache pekee yanaonyesha mambo maovu yaliyo ndani ya nyoyo zao. Maneno kama hayo ni ya kuchukiza zaidi na yenye makosa sana. Asili ya watu kama hao inampinga Mungu. Wale ambao huzingatia uhalisi huwasilisha vyovyote vilivyomo katika nyoyo zao na kufungua mioyo yao katika mawasiliano. Hakuna shughuli hata moja ya uongo, hakuna heshima ama salamu na mazungumzo matupu. Wao daima huwa na uwazi na hawafuati sheria za duniani. Kuna wale ambao wako na upendeleo wa kujionyesha kwa nje, hata bila maana yoyote. Wakati mwingine anaimba, yeye anaanza kukatika, bila hata kugundua kuwa wali katika sufuria yake umeshaungua. Watu wa aina hii si wacha Mungu au waheshimiwa, bali ni watu wa kijinga kupindukia. Hizi zote ni maonyesho ya ukosefu wa ukweli! Wakati watu wengine wanawasiliana kuhusu masuala ya maisha katika roho, ingawa hawasemi kuhusu kuwa wadeni wa Mungu, wao hubaki na upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Kuwa kwako mdeni kwa Mungu hakuhusiani na watu wengine; wewe ni mdeni kwa Mungu, si kwa mwanadamu. Kwa hiyo ina maana gani wewe daima kuzungumzia haya kwa watu wengine? Lazima uweke umuhimu kwa kuingia katika uhalisi, si kwa bidii au maonyesho ya nje.
Je, matendo mazuri ya kijuujuu ya mwanadamu yanawakilisha nini? Hayo huwakilisha mwili, na hata matendo yaliyo bora zaidi ya nje hayawakilishi maisha, ila tabia yako tu mwenyewe. Matendo ya nje ya mwanadamu hayawezi kutimiza matakwa ya Mungu. Wewe daima huzungumza kuhusu udeni wako kwa Mungu, lakini huwezi kuyaruzuku maisha ya wengine au kuwafanya wengine kumpenda Mungu. Je, unaamini kwamba matendo kama hayo yatamridhisha Mungu? Unaamini kwamba hii ndiyo matakwa ya moyo wa Mungu, kwamba haya ni ya roho, lakini kwa kweli huu ni ujinga! Unaamini kwamba yale yanayokupendeza wewe na unayotaka ni yale yanayomfurahisha Mungu. Je, yanayokupendeza yanaweza kuwakilisha yanayompendeza Mungu? Je, tabia ya mwanadamu inaweza kumwakilisha Mungu? Yale yanayokupendeza wewe ndiyo hasa yale humchukiza Mungu, na mienendo yako ni ile ambayo Mungu huchukia na kukataa. Kama unahisi kuwa wewe ni mdeni, basi nenda na usali mbele za Mungu. Hakuna haja ya kuzungumzia jambo hilo kwa watu wengine. Usipoomba mbele za Mungu na badala yake mara kwa mara unajivuta nadhari kwako mbele ya wengine, jambo hili linaweza kutimiza matakwa ya moyo wa Mungu? Kama matendo yako daima yanaonekana tu, hii ina maana kuwa wewe ni mtu bure zaidi ya wote. Ni mtu wa aina gani yule aliye na matendo mazuri ya kijuujuu tu lakini hana uhalisi? Watu kama hao ni Mafarisayo wanafiki na watu wa dini! Msipoacha matendo yenu ya nje na hamuwezi kufanya mabadiliko, basi dalili za unafiki ndani yenu zitazidi kuimarika. Kadiri dalili za unafiki zinavyozidi, ndivyo upinzani kwa Mungu unavyozidi, na mwishowe, watu wa aina hii hakika watatupiliwa mbali!

Jumapili, 24 Machi 2019

Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, nyimbo za injili

Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

I
Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena. Wanajua ubaya wa Shetani, hivyo wanamkataa. Wanakuja mbele ya Mungu, wanakubali adabu na hukumu. Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu. Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani. Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena. Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu.
II
Katika usimamizi wa Mungu wa wakati huu, mwanadamu ni lengo la upotovu wa Shetani, yeye ni kasidi cha wokovu wa Mungu na kile ambacho Mungu na Shetani wanapigania. Wakati wa kazi ya Mungu, Anampata tena mwanadamu hatua kwa hatua kutoka Shetani. Kisha mwanadamu anakuwa karibu zaidi na Mungu ... Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu. Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani. Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena. Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu.
Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu. Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani. Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena. Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumamosi, 23 Machi 2019

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Mchezo mfupi Mipaka ya Meya wa Kijiji inaeleza hadithi ya kweli ya mume na mke Wakristo ambao wanalazimishwa kutoroka kwa sababu ya mateso ya serilaki ya CCP.
Mkristo Liu Ming'en anahukumiwa na CCP miaka saba gerezani kwa kuamini katika Mungu. Hata baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, anabakia kuwa wakulengwa na uchunguzi mkali wa CCP. Meya wa kijiji anatumia mfumo wa wajibu wa kaya-tano , kamera za usalama, ziara za nyumba, na njia nyingine kumzuia Liu Ming'en na mkewe kuamini katika Mungu, lakini hakuna inayoleta na matokeo yanayotakiwa. Wakati huu, meya anapokea taarifa za kipaumbele kutoka Kamati Kuu ya Chama, baada ya hapo anajaribu kutafuta njia za kumlazimisha Liu Ming'en na mkewe kuweka saini barua ya kuahidi kuacha kuamini katika Mungu. Baada ya hila yake kushindwa, polisi tena wanakuja kuwakamata waumini hawa wawili. Kuepuka kukamatwa na kuendelea kumfuata Mungu na kuamini katika Mungu, Liu Ming'en na mkewe wanalazimishwa kutoroka nyumbani kwao.
Mwenyezi Mungu alisema, Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kupotea kutoka kwa Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamwasi Mungu na kulaani Mbingu. Na hivyo, bila kujulikana kwa mwanadamu, majaliwa ya nchi yataletwa kwa uharibifu. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na anaweza hata kuzifuta kutoka uso wa dunia. Kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa kunategemea kama viongozi wao wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wao karibu na Mungu na kumwabudu. Lakini, kwa hii enzi ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli na kumwabudu wanazidi kuwa wachache, Mungu anaweka fadhili ya pekee juu ya nchi ambapo Ukristo ni dini ya serikali. Anazikusanya pamoja kuunda kambi ya haki kiasi ya dunia, wakati nchi zikanazo Mungu ama zile zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu mahali miongoni mwa wanadamu pa kufanyia kazi Yake, lakini pia Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, ili kulazimisha mipaka na vikwazo kwa nchi hizo zinazompinga Mungu. Lakini licha ya hayo, bado hakuna watu zaidi wanaokuja mbele kumwabudu Mungu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na Mungu hajakuwa kwa mawazo ya mwanadamu kwa muda mrefu. Kunabakia tu duniani nchi zinazotumia haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ni mbali na matakwa ya Mungu, kwani hakuna kiongozi wa nchi yoyote atamruhusu Mungu kuongoza watu wake, na hakuna chama cha kisiasa kitakachokusanya pamoja watu wake kumwabudu Mungu; Mungu amepoteza mahala Pake halali kwa mioyo ya nchi zote, taifa, chama tawala, na hata kwa moyo wa kila mtu. Ingawa nguvu za haki ziko kwa dunia hii, utawala ambapo Mungu hana mahali kwa moyo wa mwanadamu ni dhaifu. Bila baraka ya Mungu, uwanja wa kisiasa utaanguka katika vurugu na wenye kuweza kudhuriwa na mashambulizi. Kwa mwanadamu, kuwa bila baraka ya Mungu ni kama kukosa mwanga wa jua. Bila kujali jinsi viongozi wanafanya mchango kwa watu wao kwa uangalifu, bila kujali idadi ya mikutano ya haki wanadamu wanafanya pamoja, hakuna kati ya hii itakayorejesha mambo ama kubadilisha majaliwa ya mwanadamu. Mwanadamu anaamini kuwa nchi ambapo watu wanalishwa na kuvalishwa nguo, ambapo watu wanaishi kwa amani, ni nchi nzuri, na iliyo na uongozi mzuri. Lakini Mungu hafikirii hivyo. Anaamini kuwa nchi ambapo hakuna mtu anayemwabudu ndiyo Atakayoiangamiza. Njia ya mwanadamu ya kufikiria ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kwa hiyvo, kama mkuu wa nchi hamwabudu Mungu, basi majaliwa ya nchi hii itakuwa ya kutisha, na nchi haitakuwa na majaliwa.
Mungu hashiriki katika siasa za mwanadamu, lakini majaliwa ya nchi ama taifa inadhibitiwa na Mungu, Mungu anadhibiti dunia hii na ulimwengu mzima. Majaliwa ya mwanadamu na mpango wa Mungu yanashikamana kwa undani, na hakuna mwanadamu, nchi ama taifa limetolewa kwa mamlaka ya Mungu. Iwapo mwanadamu anatamani kujua majaliwa yake, basi lazima aje mbele ya Mungu. Mungu atawafanya wanaomfuata na kumwabudu kufanikiwa, na Atashusha na kuwaangamiza wale wanaompinga na kumkataa.
Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Loti alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma jinsi watu wa Ninawi walitubu dhambi zao kwa gunia na majivu, na kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.
Leo, Mungu amerudi duniani kufanya kazi Yake. Atasimama kwanza kwa mkutano mkubwa wa viongozi madikteta: Uchina, ngome kali ya ukanaji Mungu. Mungu amepata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Wakati huu, Anawindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso makubwa, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na kutoweza kupata makazi. Licha ya haya, Mungu bado anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Anatamka sauti Yake na kueneza injili. Hakuna anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu zaidi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu anafanya yote Awezayo kuokoa kila mshiriki wa ubinadamu. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo. Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama tu ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni.
Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.