Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Ijumaa, 2 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 2. Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

Xiaoxiao Jijini Xuzhou, Mkoani Jiangsu
Kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya kanisa, nilihamishwa mpaka mahali pengine ili kutimiza wajibu wangu. Wakati huo, kazi ya injili mahali pale ilikuwa katika hali duni, na hali ya akina kaka na dada kwa kawaida haikuwa nzuri.

Alhamisi, 1 Machi 2018

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (katika siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima. Hii ni kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho; Anazungumza tu ili dunia iwe ulimwengu wa maneno, ili kila mtu awe amepewa na kutiwa nuru maneno Yake, na ili roho ya mwanadamu iamshwe na aweze kuona vizuri kuhusu maono yake. Wakati wa siku za mwisho, Mungu katika mwili Amekuja duniani hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno. Yesu Alipokuja, Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni, na Akatimiza kazi ya wokovu wa msalaba. Alihitimisha Enzi ya Sheria, na Akakomesha mambo yote ya kale. Ujio wa Yesu ulihitimisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema. Ujio wa Mungu katika mwili wa siku za mwisho umehitimisha Enzi ya Neema. Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, kutumia maneno ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, kumwangazia na kumpa nuru mwanadamu, na kumwondoa Mungu asiye yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii sio hatua ya kazi ambayo Yesu Aliifanya Alipokuja. Yesu Alipokuja, Alifanya miujiza mingi, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alifanya kazi ya wokovu ya msalaba. Na matokeo yake ni kwamba, katika dhana za mwanadamu, mwanadamu anaamini kwamba hivi ndivyo Mungu Anapaswa kuwa. Maana Yesu Alipokuja, hakufanya kazi ya kuondoa taswira ya Mungu asiye yakini moyoni mwa mwanadamu; Alipokuja, Alisulubishwa, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni. Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho.
Kile unachopaswa kujua:
1. Kazi ya Mungu si ya kimiujiza, na hupaswi kuhifadhi dhana juu yake.
2. Unapaswa kuelewa kazi kuu ambayo Mungu katika mwili Amekuja kufanya wakati huu.
Hakuja kuponya wagonjwa, au kutoa mapepo, au kufanya miujiza, na Hajakuja kueneza injili ya toba, au kumpatia mwanadamu ukombozi. Hiyo ni kwa sababu Yesu Amekwishafanya kazi hii, na Mungu Harudii kazi ile ile. Leo, Mungu Amekuja kuhitimisha Enzi ya Neema, na kuzitupilia mbali desturi zote za Enzi ya Neema. Mungu wa vitendo Amekuja hasa kuonyesha kuwa Yeye ni halisi. Yesu Alipokuja Alizungumza maneno machache; hasa Alionyesha miujiza, Akafanya ishara na maajabu, na Akaponya wagonjwa na kutoa mapepo, au wakati mwingine Alizungumza unabii ili kumshawishi mwanadamu, na kumfanya mwanadamu aone kwamba ni kweli Alikuwa Mungu, na Alikuwa Mungu Asiyependelea. Hatimaye, Akakamilisha kazi ya msalaba. Mungu wa leo Haonyeshi ishara na maajabu, wala Haponyi wagonjwa na kutoa mapepo. Yesu Alipokuja, kazi Aliyoifanya iliwakilisha upande mmoja wa Mungu, lakini wakati huu Mungu Amekuja kufanya hatua ya kazi ambayo imetazamiwa, maana Mungu Harudii kazi ile ile; ni Mungu ambaye siku zote ni mpya na Hawezi kuzeeka kamwe, na hivyo yale yote unayoyaona leo ni maneno na kazi ya Mungu wa vitendo.
Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, ili kuelezea yale yote ambayo ni ya lazima katika maisha ya mwanadamu, kuonyesha yale ambayo mwanadamu anapaswa kuingia kwayo, kumwonesha mwanadamu matendo ya Mungu, na kumwonesha mwanadamu hekima, uweza na uajabu wa Mungu. Kupitia njia nyingi ambazo Mungu Anazungumza, mwanadamu anatazama ukuu wa Mungu, aidha, unyenyekevu na usiri wa Mungu. Mwanadamu anatazama kwamba Mungu ni mkuu, lakini ni mnyenyekevu na msiri, na Anaweza kuwa mdogo kuliko vitu vyote. Baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa Roho, baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu, na baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa kutoka kwa mtazamo wa nafsi ya tatu. Katika hili inaweza kuonekana kwamba namna ya kazi ya Mungu inatofautiana kwa kiasi kikubwa na ni kwa njia ya maneno ndipo Anamruhusu mwanadamu kuiona. Kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho ni ya kawaida na halisi, na hivyo kundi la watu wa siku za mwisho wanakumbwa na majaribu makubwa kuliko yote. Kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu, watu wote wameingia katika majaribu hayo; kwamba mwanadamu ameingia katika majaribu ya Mungu ni kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu. Wakati wa enzi ya Yesu, hakukuwa na dhana au majaribu. Kwa sababu kazi kubwa iliyofanywa na Yesu ilikuwa ni kulingana na dhana za mwanadamu, watu walimfuata, na hawakuwa na dhana juu Yake. Majaribu ya leo ni makubwa sana ambayo yamewahi kukabiliwa na mwanadamu, na inaposemwa kwamba watu hawa wametoka katika dhiki kuu, hii ndiyo dhiki inayoongelewa.
Leo, Mungu Ananena ili kusababisha imani, upendo, ustahimilivu na utii kwa watu hawa. Maneno yaliyozungumzwa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kutokana na hulka ya asili ya mwanadamu, kulingana na tabia ya mwanadamu, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia kwacho leo. Mbinu Yake ya kuzungumza[a] ni halisi na ya kawaida: Hazungumzi juu ya kesho, wala Haangalii nyuma, jana; Anazungumza kile tu ambacho kinapaswa kuingiwa kwacho, kuwekwa katika vitendo, na kueleweka leo. Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na ana uwezo wa kutoa mapepo, na kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine; mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Unapaswa kuelewa vizuri mambo haya. Kwa nini kazi ya Mungu leo ni tofauti na kazi ya Yesu? Kwa nini Mungu leo Haonyeshi ishara na maajabu, Hatoi mapepo, na Haponyi wagonjwa? Ikiwa kazi ya Yesu ingekuwa sawa na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Sheria, je, Angekuwa Amemwakilisha Mungu wa Enzi ya Neema? Je, Yesu Angekuwa Amemaliza kazi ya msalaba? Ikiwa, kama katika Enzi ya Sheria, Yesu Angeingia hekaluni na kuitunza Sabato, basi Asingeteswa na mtu yeyote na Angekumbatiwa na wote. Kama ingekuwa hivyo, je, Angesulubiwa? Je, Angekuwa Amemaliza kazi ya ukombozi? Je, ingekuwa na maana gani ikiwa Mungu katika mwili wa siku za mwisho Angeonyesha ishara na maajabu kama Yesu? Ikiwa tu Mungu Atafanya sehemu nyingine ya kazi Yake wakati wa siku za mwisho, kazi inayowakilisha sehemu ya mpango wa usimamizi Wake, ndipo mwanadamu anaweza kupata maarifa ya kina ya Mungu, na baada ya hapo tu ndipo mpango wa usimamizi wa Mungu unaweza kukamilika.
Wakati wa siku za mwisho Mungu Amekuja mahususi kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake. Anazungumza kutokana na mtazamo wa Roho, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu; Anazungumza kwa namna tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi fulani, na Anatumia njia za kuzungumza ili kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa taswira ya Mungu yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu iliyofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu Amekuja kuponya wagonjwa, kutoa mapepo, kufanya miujiza, na kumpatia mwanadamu baraka za vitu, Mungu Anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuweza kuondoa mambo hayo kutoka katika dhana za mwanadamu, ili mwanadamu aweze kuuelewa uhalisia na ukawaida wa Mungu, na ili kwamba taswira ya Yesu iweze kuondolewa moyoni mwake na kuwekwa taswira mpya ya Mungu. Mara tu taswira ya Mungu ndani ya mwanadamu inapozeeka, basi inakuwa sanamu. Yesu alipokuja na kutekeleza hatua hii ya kazi, Hakuwakilisha Mungu kikamilifu. Alifanya baadhi ya ishara na maajabu, Alizungumza maneno kadhaa, na hatimaye Akasulubishwa, na Aliwakilisha upande mmoja wa Mungu. Hakuweza kuwakilisha yale yote ambayo ni ya Mungu, bali Alimwakilisha Mungu katika kufanya upande mmoja wa kazi ya Mungu. Hiyo ni kwa sababu Mungu ni mkuu, na ni wa ajabu sana, na Haeleweki, na kwa sababu Mungu Anafanya upande mmoja tu wa kazi Yake katika kila enzi. Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Alimwongoza Musa kutoka Misri kwa maneno Yake, na Akazungumza maneno fulani kwa Wanaisraeli; wakati huo, sehemu ya matendo ya Mungu yaliwekwa wazi, lakini kwa sababu ubora wa tabia ya mwanadamu ulikuwa finyu na hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kufanya maarifa yake kukamilika, Mungu Aliendelea kuzungumza na kufanya kazi. Wakati wa Enzi ya Neema, mwanadamu aliweza kuona tena sehemu ya matendo ya Mungu. Yesu Aliweza kuonyesha ishara na maajabu, kuponya wagonjwa na kutoa mapepo, na kusulubishwa, siku tatu baadaye. Akafufuka na Akawatokea watu Akiwa katika mwili. Kumhusu Mungu, mwanadamu hakujua chochote zaidi ya hiki. Mwanadamu anajua tu kile ambacho Mungu Amemwonyesha, na kama Mungu Asingeonyesha chochote zaidi kwa mwanadamu, basi hicho kingekuwa kiwango cha mwanadamu kumwekea mipaka Mungu. Hivyo, Mungu Anaendelea kufanya kazi, ili maarifa ya mwanadamu juu Yake yaweze kuwa ya kina zaidi, na ili taratibu aweze kuijua hulka ya Mungu. Mungu anatumia maneno yake kumkamilisha mwanadamu. Tabia yako iliyoharibika imewekwa wazi kwa maneno ya Mungu, na dhana zako za kidini zinaondolewa na uhalisia wa Mungu. Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kutimiza maneno haya kwamba "Neno Lafanyika kuwa mwili, Neno Lakuwa mwili, na Neno Laonekana katika mwili," na kama huna maarifa ya kina kuhusu hili, basi hutaweza kusimama imara; wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya mpango wa Mungu wa usimamizi. Hivyo, maarifa yako yanapaswa kuwa wazi; bila kujali namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, Mungu Hamruhusu mwanadamu kumwekea mipaka. Ikiwa Mungu Asingefanya kazi hii wakati wa siku za mwisho, basi maarifa ya mwanadamu juu Yake yasingeweza kwenda popote. Ungeweza kujua tu kwamba Mungu Anaweza kusulubiwa na Anaweza kuiangamiza Sodoma, na kwamba Yesu Anaweza kufufuliwa kutoka katika wafu na kumtokea Petro.... Lakini usingeweza kusema kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutimiza yote, na yanaweza kumshinda mwanadamu. Ni kwa njia tu ya kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu ndipo unaweza kuzungumza juu ya maarifa hayo, na kadri unapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu zaidi, ndivyo maarifa yako yanavyokuwa ya kina zaidi kumhusu Yeye. Ni baada ya hapo tu ndipo utaacha kumwekea Mungu mipaka ndani ya dhana zako binafsi. Mwanadamu anakuja kumjua Mungu kwa kupitia kazi Yake, na hakuna njia nyingineyo sahihi ya kumjua Mungu. Leo, kuna watu wengi ambao hawafanyi chochote bali wanasubiri kuona ishara na maajabu na wakati wa maangamizi. Je, unamwamini Mungu, au unaamini katika maangamizi? Ukisubiri hadi wakati wa maangamizi utakuwa umechelewa sana, na ikiwa Mungu Hataleta maangamizi, basi Atakuwa si Mungu? Je, unaamini ishara na maajabu, au unamwamini Mungu Mwenyewe? Yesu Hakuonyesha ishara na maajabu wakati Alipobezwa na wengine; je, Hakuwa Mungu? Je, unaamini ishara na maajabu, au unaamini katika hulka ya Mungu? Mitazamo ya mwanadamu kuhusu imani kwa Mungu ni makosa! Yehova Alizungumza maneno mengi wakati wa Enzi ya Sheria, lakini hata leo baadhi yake bado hayajatimizwa. Je, unaweza kusema kwamba Yehova Hakuwa Mungu?
Leo, inapaswa kueleweka kwenu wote kwamba, katika siku za mwisho, ni kwa kiasi kikubwa ukweli wa "Neno linakuwa mwili" ambao unakamilishwa na Mungu. Kupitia kazi yake halisi duniani, Anafanya mwanadamu kumfahamu, na kushirikiana Naye, na kuona matendo Yake halisi. Anamsababisha mwanadamu kuona kwa wazi kwamba Yeye Anaweza kuonyesha ishara na maajabu na pia kuna nyakati ambapo Hawezi kufanya hivyo, na hii inategemea enzi. Kutokana na hili unaweza kuona kwamba Mungu sio kwamba Hawezi kuonyesha ishara na maajabu, lakini badala yake Anabadilisha kufanya kazi Kwake kulingana na kazi Yake, na kulingana na enzi. Katika hatua ya sasa ya kazi, Haonyeshi ishara na maajabu; kuonyesha kwake baadhi ya ishara na maajabu katika enzi ya Yesu, ilikuwa ni kwa sababu kazi Yake katika enzi hiyo ilikuwa tofauti. Mungu Hafanyi kazi hiyo leo, na baadhi ya watu wanaamini Hana uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, au wanafikiri kwamba kama Haonyeshi ishara na maajabu, basi Yeye si Mungu. Hii sio hoja ya uwongo? Mungu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, lakini Anafanya kazi katika enzi tofauti, na hivyo Hafanyi kazi hiyo. Kwa kuwa hii ni enzi tofauti, na kwa kuwa hii ni hatua tofauti ya kazi ya Mungu, matendo yaliyowekwa wazi na Mungu pia ni tofauti. Imani ya mwanadamu kwa Mungu sio imani katika ishara na maajabu, wala imani katika miujiza, bali ni imani katika kazi Yake halisi wakati wa enzi mpya. Mwanadamu anamjua Mungu kupitia namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, na maarifa haya yanamfanya mwanadamu amwamini Mungu, ambavyo ni kusema, imani katika kazi na matendo ya Mungu. Katika hatua hii ya kazi, Mungu Anazungumza hasa. Usisubiri kuona ishara na maajabu; hutayaona! Maana hukuzaliwa katika Enzi ya Neema. Kama ungezaliwa katika Enzi ya Neema, ungeweza kuona ishara na maajabu, lakini umezaliwa katika siku za mwisho, na hivyo unaweza kuona tu uhalisia na ukawaida wa Mungu. Usitarajie kumwona Yesu wa kimiujiza wakati wa siku za mwisho. Unaweza kumwona tu Mungu katika mwili wa vitendo, Ambaye si tofauti na mwanadamu yeyote wa kawaida. Katika kila enzi, Mungu Anaweka wazi matendo mbalimbali. Katika kila enzi Anaweka wazi sehemu ya matendo ya Mungu, na kazi ya kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu, na inawakilisha sehemu moja ya matendo ya Mungu. Matendo Anayoyaweka wazi yanatofautiana na enzi ambayo kwayo Anafanya kazi, lakini yote yanampatia mwanadamu maarifa ya Mungu ambayo ni ya kina, imani kwa Mungu ambayo ni yenye kuhusika na mambo halisi sana, na ambayo ni ya kweli zaidi. Mwanadamu anamwamini Mungu kwa sababu ya matendo yote ya Mungu, na kwa sababu Mungu ni wa ajabu ni mkuu sana, kwa sababu Yeye ni mwenyezi, na ambaye Hapimiki kina. Ikiwa unamwamini Mungu kwa kuwa Anaweza kufanya ishara na maajabu na Anaweza kuponya wagonjwa na kuwatoa mapepo, basi mtazamo wako si sahihi, na baadhi ya watu watakwambia, "Je, pepo wachafu pia hawawezi kufanya mambo hayo?" Je, hii sio kuielewa vibaya taswira ya Mungu kwa kuilinganisha na taswira ya Shetani? Leo, imani ya mwanadamu kwa Mungu ni kwa sababu ya matendo Yake mengi na njia nyingi ambazo kwazo Anafanya kazi na kuzungumza. Mungu Anatumia matamshi yake kumshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu. Mwanadamu anamwamini Mungu, kwa sababu ya matendo Yake mengi, na si kwa sababu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, na wanadamu wanamwelewa tu kwa sababu wanaona matendo Yake, Ni kwa kujua tu matendo halisi ya Mungu, namna Anavyofanya kazi, njia ambazo Anaonyesha hekima Yake, vile Anavyozungumza, na jinsi Anavyomfanya mwanadamu kuwa mkamilifu—ni kwa kujua tu vipengele hivi—ndipo unaweza kufahamu uhalisia wa Mungu na kuelewa tabia Yake. Kile Anachopenda, kile Anachochukia, namna Anavyomfanyia kazi mwanadamu—kwa kuelewa yale ambayo Mungu Anayapenda na Asiyoyapenda, unaweza kutofautisha kati ya kile ambacho ni chanya na kile ambacho ni hasi, na kupitia maarifa yako juu ya Mungu kunakuwa na maendeleo katika maisha yako. Kwa ufupi unapaswa kuwa na maarifa ya kazi ya Mungu, na unapaswa kuweka sahihi mitazamo yako kuhusu kuwa na imani kwa Mungu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.

Jumatano, 28 Februari 2018

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno;

Jumanne, 27 Februari 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni ili kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufichua ubovu wa Shetani usiovumilika. Aidha, ni ili kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kujua, kwa uhakika kabisa tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, kilicho kikuu na kilicho cha aibu. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wataweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Bwana wa viumbe—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Ninayeweza kumpa mwanadamu vitu kwa ajili ya raha yake; na atapata kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni mmoja tu wa viumbe niliowaumba na ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kuelewa mapenzi Yangu, na wajue kwamba Mimi Ndimi ukweli. Hivyo, wakati wa awamu ya kwanza ya kazi ya katika Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita, Nilifanya kazi ya sheria, ambayo ilikuwa ndiyo kazi ambayo kwayo Yehova aliwaongoza watu Wake. Hatua ya pili ilianzisha kazi ya Enzi ya Neema katika vijiji vya Yudea. Yesu Anawakilisha kazi yote ya Enzi ya Neema; Alipata mwili na kusulubiwa, na pia Akazindua Enzi ya Neema. Alisulubiwa ili kukamilisha kazi ya ukombozi, ili kumaliza Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema, na hivyo Yeye Aliitwa “Kamanda Mkuu”, “Sadaka ya Dhambi,” “Mkombozi.” Kwa hiyo kazi ya Yesu ilitofautiana katika maudhui na kazi ya Yehova, ingawa zilikuwa sawa katika kanuni. Yehova Alianzisha Enzi ya Sheria, Akaunda msingi wa nyumbani, yaani, mahali pa asili, pa kazi Yake hapa duniani, na Akatoa amri; haya yalikuwa mafanikio Yake mawili, yanayowakilisha Enzi ya Sheria. Kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema haikuwa kutoa amri bali kutimiza Amri, na hivyo kukaribisha Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria ambayo ilidumu kwa miaka elfu mbili. Alikuwa mwanzilishi, aliyekuja ili kuianzisha Enzi ya Neema, ilhali ukombozi ulibakia msingi wa kazi Yake. Na hivyo mafanikio Yake yalikuwa pia mara mbili: kufungua enzi mpya, na kukamilisha kazi ya ukombozi kupitia kusulubiwa Kwake. Kisha Akaondoka. Katika hatua hiyo, Enzi ya Sheria ilifikia mwisho wake na wanadamu waliingia katika Enzi ya Neema.

Kazi ambayo Yesu alifanyika ililingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Kazi Yake ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu, kuwasamehe dhambi zao, na kwa hivyo tabia Yake yote ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, ucha Mungu, ustahamilivu, huruma na wema. Aliwabariki wanadamu kwa wingi na kuwaletea neema nyingi, na mambo yote ambayo wangeweza kufurahia, Aliwapa kwa ajili ya furaha yao: amani na furaha, uvumilivu Wake na upendo, huruma Yake na wema. Katika siku hizo, chote alichokutana nacho mwanadamu kilikuwa wingi wa vitu vya kufurahia tu: Moyo wake ulikuwa na amani na uhakikisho, roho yake ilifarijika, na alikuwa anaruzukiwa na Mwokozi Yesu. Sababu iliyomfanya mwanadamu aweze kufaidi mambo haya ni matokeo ya enzi alimoishi. Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa tayari na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji neema nyingi, ustahimili na uvumilivu usio na mwisho, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu walichoona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya kulipia dhambi za binadamu, yaani, Yesu. Yote waliyojua ni kwamba Mungu angeweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na yote waliyoona ni huruma ya Yesu na wema Wake. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu wao waliishi katika Enzi ya Neema. Na hivyo, kabla ya kuweza kukombolewa, walilazimika kufurahia neema za aina nyingi ambazo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo lilikuwa la manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na pia wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia ustahimili wa Yesu na uvumilivu. Ni kwa njia ya ustahimili wa Yesu na uvumilivu pekee ndio walipata haki ya wa kupokea msamaha na kufurahia neema nyingi kutoka kwa Yesu—kama vile Yesu alivyosema, “Sijakuja kuwakomboa wenye haki, ila wenye dhambi, kukubali dhambi zao zisamehewe.” Kama Yesu angepata mwili wa tabia ya hukumu, laana, na kutovumilia makosa ya mwanadamu, basi mwanadamu kamwe hangeweza kupata nafasi ya kukombolewa, na daima yeye angebaki mwenye dhambi. Hali ingekuwa hivi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Sheria ingeendelea kwa miaka elfu sita. Dhambi za mwanadamu zingeongezeka zaidi na kuwa mbaya zaidi tu, na uumbaji wa binadamu ungekuwa wa bure. Wanadamu wangeweza tu kumtumikia Yehova chini ya sheria, bali dhambi zao zingezidi za wanadamu wa kwanza kuumbwa. Jinsi Yesu alivyowapenda wanadamu zaidi, Akisamehe dhambi zao na kuwapa huruma na wema wa kutosha, ndivyo wanadamu walizidi kuwa na uwezo wa kuokolewa, wa kuitwa wanakondoo waliopotea ambao Yesu Aliwanunua tena kwa gharama kubwa. Shetani hakuweza kuingilia katika kazi hii, kwa sababu Yesu Aliwatunza wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anavyotunza mtoto mchanga aliye kifuani pake. Yeye hakuwa na hasira nao au kuwadharau, bali Alikuwa Amejaa faraja; Yeye kamwe hakuwa na ghadhabu miongoni mwao, lakini alistahimili dhambi zao na Akapuuza upumbavu wao na kutofahamu, hata kusema, “Uwasamehe wengine mara sabini mara saba.” Kwa hiyo moyo Wake ulirekebisha mioyo ya wengine. Ilikuwa ni kwa njia hii ndiyo watu walipokea msamaha wa dhambi kupitia uvumilivu Wake.

Ingawa Yesu katika mwili Wake hakuwa na hisia kabisa, Yeye daima Aliwafariji wanafunzi Wake, Aliwapa mahitaji yao, Akawasaidia, na Akawaruzuku. Bila kujali kiwango cha kazi Alichofanya au kiasi gani cha mateso Alivumilia, Yeye kamwe hakuwa na matarajio ya kupita kiasi kwa mwanadamu, lakini kila mara Alikuwa mwenye subira na kuvumilia dhambi zao, kiasi kwamba katika Enzi ya Neema kwa upendo watu walimwita “Mwokozi Yesu anayependeka.” Kwa watu wa wakati huo—kwa watu wote—kile Yesu Alikuwa nacho na kile Alichokuwa, kilikuwa huruma na wema. Yeye kamwe hakukumbuka dhambi za, na hakuwatendea kulingana na dhambi zao. Kwa sababu hiyo ilikuwa enzi tofauti, mara nyingi Alitoa chakula na vinywaji kwa watu ili waweze kula hadi washibe. Yeye Aliwatendea wafuasi Wake wote kwa ukarimu, akaponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kufufua wafu. Ili kwamba watu waweze kumwamini na kuona kwamba yote Aliyofanya yalifanyika kwa bidii na kwa dhati, Yeye Alifika kiwango cha kufufua maiti iliyooza, kuwaonyesha kwamba mikononi Mwake hata wafu wanaweza kuwa hai tena. Kwa njia hii Alivumilia kwa kimya na kufanya kazi Yake ya ukombozi kati yao. Hata kabla Asulubiwe, Yesu Alikuwa tayari Amebeba dhambi za binadamu na kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya wanadamu. Hata kabla Asulubiwe, Alikuwa tayari Amefungua njia ya msalaba ili kuwakomboa wanadamu. Mwishowe Aligongwa misumari msalabani, Alijitoa sadaka Yeye Mwenyewe kwa ajili ya msalaba, na Alitoa huruma Yake yote, wema Wake, na utakatifu kwa wanadamu. Kwa wanadamu daima alikuwa mvumilivu, kamwe Hakutafuta kulipiza kisasi, lakini Aliwasamehe dhambi zao, Akiwasihi watubu, na kuwafundisha kuwa na subira, uvumilivu na upendo, kufuata nyayo Zake na kujitoa wenyewe kwa ajili ya msalaba. Upendo Wake kwa ndugu ulizidi upendo Wake kwa Maria. Kanuni ya kazi Aliyofanya ilikuwa kuwaponya watu na kutoa mapepo, yote kwa ajili ya ukombozi Wake. Haijalishi Alikoenda, Yeye Aliwatendea wote waliomfuata kwa neema. Aliwafanya maskini kuwa tajiri, viwete watembee, vipofu waone na viziwi wasikie; Yeye hata Aliwaalika watu wa hadhi ya chini kabisa, maskini zaidi, wenye dhambi, kula pamoja naye, Akikosa kuwaepuka kamwe ila daima Alikuwa na subira, hata kusema, “Wakati mchungaji anampoteza kondoo mmoja kati ya mia, yeye ataondoka na kuwaacha nyuma wale tisini na tisa ili amtafute kondoo mmoja aliyepotea, na anapompata yeye atafurahia sana.” Yeye Aliwapenda wafuasi Wake kama kondoo anavyopenda wanakondoo wake. Ingawa walikuwa wajinga na wasio na ufahamu, na walikuwa wenye dhambi katika macho Yake, na zaidi walikuwa washirika wa chini zaidi katika jamii, Aliona hawa wenye dhambi—waliodharauliwa na wengine—kama vipenzi Vyake. Kwa kuwa Aliwapendelea, Alitoa uhai Wake kwa ajili yao, kama mwana kondoo alitolewa madhabahuni. Alitembea kati yao kama mtumishi wao, Akiwaruhusu kumtumia na kumchinja, Alijinyenyekeza kwao bila masharti. Kwa wafuasi Wake Alikuwa Mwokozi Yesu aliyependeka, lakini kwa Mafarisayo, ambao waliwahubiria watu kutoka viweko virefu vya mnara, Hakuonyesha huruma na wema, bali chuki na maudhi. Hakufanya kazi nyingi miongoni mwa Mafarisayo, Akiwahubiria na kuwakemea mara chache tu; Yeye hakutembea miongoni mwao akifanya kazi ya ukombozi, au kufanya ishara na maajabu. Alitoa huruma Yake na wema Wake wote kwa wafuasi Wake, akivumilia kwa ajili ya hawa wenye dhambi mpaka mwisho kabisa, wakati Alipigwa misumari msalabani na akastahimili kila udhalilishaji mpaka Alivyowakomboa wanadamu wote kikamilifu. Hii ndiyo ilikuwa kazi Yake yote.

Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, dunia yote ingekuwa mahali pa kulala pa Shetani, maskani yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji kuonyesha huruma na wema kwa wanadamu; kupitia kwa njia hiyo tu ndio wanadamu wangeweza kupokea msamaha na mwishowe kupata haki ya kukamilishwa na kumilikiwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Katika miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alitumia kufanya kazi Yake hapa duniani alikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha, kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa yule mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaendesha majaaliwa ya wanadamu. Baada ya Yeye kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo alipowakomboa wanadamu. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Akidhihakiwa, kukashifiwa, na kuachwa, kiasi cha Yeye kukosa mahali pa kulaza kichwa chake, mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, huku nafsi Yake yote—mwili safi kabisa na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani, na akapitia kila namna ya mateso. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na maaskari hata wakamtemea mate usoni; ilhali Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa wanadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika. Kazi ambayo Yesu alifanya inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria wala si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo wanadamu wamepitia—Enzi ya Ukombozi.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 26 Februari 2018

Hymn of Christian Experience Swahili "Ni Furaha Kuu kuwa Mtu Mwaminifu" | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hymn of Christian Experience Swahili "Ni Furaha Kuu kuwa Mtu Mwaminifu" | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kuelewa ukweli huiachilia huru roho ya mtu na kumfanya mtu kuwa mwenye furaha. Nimejazwa na imani katika neno la Mungu na sina shaka. Mimi niko bila uhasi wowote, sirudi nyuma, na kamwe sikati tamaa. Ninauunga mkono wajibu wangu kwa moyo wangu wote na mawazo, na siujali moyo. Ingawa ubora wa tabia yangu ni wa chini, nina moyo wa uaminifu. Nimejitolea kikamilifu katika kila kitu ili kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ninatenda ukweli, namtii Mungu, na kujaribu kuwa mtu mwaminifu. Mimi ni wazi na mnyoofu, bila uongo, nikiishi kwenye mwanga. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu.
Kuelewa ukweli huiachilia huru roho ya mtu na kumfanya mtu kuwa mwenye furaha. Nimejazwa na imani katika neno la Mungu na sina shaka. Mimi niko bila uhasi wowote, sirudi nyuma, na kamwe sikati tamaa. Ninauunga mkono wajibu wangu kwa moyo wangu wote na mawazo, na siujali moyo. Ingawa ubora wa tabia yangu ni wa chini, nina moyo wa uaminifu. Nimejitolea kikamilifu katika kila kitu ili kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ninatenda ukweli, namtii Mungu, na kujaribu kuwa mtu mwaminifu. Mimi ni wazi na mnyoofu, bila uongo, nikiishi kwenye mwanga. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu.
Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu.
Kutoka kwa Fuata Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Sifa na Ibada
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Jumapili, 25 Februari 2018

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu.

Jumamosi, 24 Februari 2018

Swahili Gospel Movie "Ivunje Laana" | Mungu ni Wokovu Wangu

Swahili Gospel Movie "Ivunje Laana" | Mungu ni Wokovu Wangu

Fu Jinhua alikuwa mzee wa kanisa la nyumba nchini China. Kama Wakristo wengine wengi, alijitolea kwa Bwana kwa shauku kubwa, na alifanya kazi kwa bidii katika kazi yake kwa ajili Yake. Alikuwa hasa mwenye kujiamini, na alijiona kuwa mtu ambaye alimpenda Bwana kweli. Baada ya kumfuata Bwana kwa miaka mingi, aliamini kwa moyo wote kwamba Biblia ilikuwa imefunuliwa na Mungu, na kwamba maneno katika Biblia yote yalikuwa maneno ya Mungu. Kwa hivyo, akilini mwake, alilinganisha kuamini katika Bwana na kuamini katika Biblia. Alidhani kwamba wale walioachana na Biblia hawakuweza kuitwa wafuasi wa Bwana. Pia aliamini kwamba alihitaji tu kufuata Biblia ili kuchukuliwa kuenda katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaposhuka na mawingu.Hivyo wakati ambapo kikundi cha watu kilianza kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, Fu Jinhua aliamini katika dhana potovu za wachungaji na wazee wa kanisa wa kidini, na kamwe hakutafuta kuchunguza mambo zaidi. Siku moja, Fu Jinhua alimtembelea Dada He, mshiriki mwenza wa kanisa. Dada He alizungumza juu ya kiwewe chake mwenyewe: "Unabii wote juu ya kurudi kwa Bwana umetimia kimsingi, na Bwana anatakiwa kuwa amesharudi tayari. Hivyo kwa nini bado hatujamwona Bwana akishuka pamoja na mawingu?" Mfanyakazi mwenzake Fang Jianjie pia alisema: Miezi minne ya damu imeonekana, ambayo ina maana kwamba maafa makubwa yatatujia hivi karibuni. Kulingana na unabii kutoka katika vitabu vya manabii na Kitabu cha Ufunuo, Kanisa la Filadelfia litachukuliwa kwenda mbinguni kabla ya maafa makubwa,na Mungu atawastawisha watumishi na wajakazi Wake kwa Roho Wake ili kufanya kundi la washindi kabla ya maafa. Tusipochukuliwa kwenda mbinguni kabla ya majanga, huenda tutaangamia kati ya majanga haya makubwa. Lakini sasa, "Umeme wa Mashariki" limeshuhudia kwamba Bwana Yesu tayari amerejea, Ameonyesha ukweli, na kufanya kundi la washindi. Je, hili linatimiza unabii kutoka katika Biblia? Je, Umeme wa Mashariki ni onyesho la Bwana na kazi Yake? Baada ya kuwasikiliza wafanyakazi wenza, Fu Jinhua aliingia katika mawazo ya kina na akaanza kuyakadiria mambo haya … Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho.Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana. Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake.Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii. Maudhui ya video hii yametafsiriwa yote na wafasiri wataalam. Hata hivyo, kutokana na tofauti za lugha nk, makosa kadhaa yaliyofanywa hayawezi kuepukika. Ukigundua makosa yoyote kama hayo, tafadhali rejea kwa toleo la kwanza la Kichina. Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi. Injili ya Kushuka kwa Ufalme:Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi. Injili ya Kushuka kwa Ufalme:Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi. Injili ya Kushuka kwa

Ijumaa, 23 Februari 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Desturi ya Sala

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kusogea karibu na Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Desturi ya Sala

Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Katika sala zao hapo awali walikuwa wakifanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati na kufanya mchezo tu, na hakuna mtu aliyeupeana moyo wake kwa ukamilifu mbele ya Mungu na kumwomba Mungu kweli.

Alhamisi, 22 Februari 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Saba

Matawi yote ya magharibi yanapaswa kuisikiliza sauti Yangu:

Je, mmekuwa waaminifu Kwangu hapo awali? Je, mmeyatii maneno Yangu mazuri ya ushauri? Je, mna matumaini ambayo ni halisi na yasiyo na mashaka? Utiifu wa mwanadamu, upendo wake, imani yake—hamna kipatikanacho ila kutoka Kwangu, hamna hata kimoja ila kilichotolewa na Mimi. Enyi watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je, mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Hapo zamamni, mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda-shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwaokoa? Ni mara ngapi mmeanguka katika mitego ya Shetani? Ni mara ngapi mmejiingiza katika mitego ya wanadamu? Na tena, ni mara ngapi mmejikuta katika ugomvi usio na kikomo kati yenu kwa kukosa kuziachilia nafsi zenu? Ni mara ngapi miili yenu imekuwa katika nyumba Yangu ila roho zenu zikiwa kusikojulikana? Licha ya hayo, ni mara ngapi Nimewanyooshea mkono Wangu kuwainua; ni mara ngapi Nimewaonea huruma; ni mara ngapi Nimekosa uvumilivu wa kuziona hali zenu za kuhuzunisha za mateso? Ni mara ngapi … je, mnamfahamu?

Lakini leo kwa ulinzi Wangu, hatimaye mmezishinda shida zote na Nafurahia pamoja nanyi; hili ndilo dhihirisho la busara Yangu. Hata hivyo, likumbuke hili vyema! Ni nani kati yenu amewahi kuanguka na akaendelea kuwa thabiti? Ni nani kati yenu amewahi kuwa thabiti bila kuwa na nyakati za unyonge? Miongoni mwa wanadamu, ni nani amewahi kupokea baraka ambazo hazikutoka Kwangu? Ni nani amepitia misukosuko isiyotoka Kwangu? Inawezekana kuwa wale wote wanaonipenda hupokea baraka peke yake? Inawezekana kwamba misukosuko ilimpata Ayubu kwa sababu alikosa kunipenda ila alinikana Mimi? Inawezekana kwamba Paulo aliweza kunihudumia kwa utiifu mbele Yangu kwa sababu aliweza kunipenda kwa dhati? Ijapokuwa mnaweza kushikilia kwa uthabiti ushuhuda Wangu, lakini je, kuna mtu kati yenu aliye na ushuhuda safi kama dhahabu ambayo haijatiwa najisi? Je, mwanadamu anaweza kuwa na uaminifu halisi? Kwamba ushuhuda wenu huniletea furaha hakukinzani na “uaminfu” wenu kwa sababu Sijawahi kumtarajia mtu yeyote kutoa zaidi. Kwa kufuata dhamira asilia ya mpango Wangu, nyinyi nyote mngekuwa “bidhaa duni—zisizokidhi kiwango.” Je, huu sio ni mfano wa kile Nilichowaambia kuhusu “kuwaonea huruma”? Je, mnachoona sio wokovu Wangu?

Nyinyi nyote mnafaa kuvuta kumbukumbu zenu: Tangu mrejee katika nyumba Yangu, kuna yeyote kati yenu, bila kutafakari faida na hasara, amenifahamu sawa na Petro alivyonifahamu? Mmekariri Biblia kikamilifu, lakini je, mlijifunza chochote kuhusu kiini chake? Japo hivyo, bado mmeshikilia “mtaji” wenu, mkikataa kuziachilia nafsi zenu. Ninapotoa tamko, Nikiwazungumzia ana kwa ana, Ni nani kati yenu amewahi kuweka chini “nyaraka” zilizofunikwa kupokea maneno ya uzima ambayo Nimeyaweka wazi? Hamyajali maneno Yangu na wala hamyathamini. Badala yake, mnatumia maneno Yangu kama bombomu dhidi ya maadui wenu ili kudumisha nafasi zenu; hamjaribu hata kidogo kuyakubali maoni Yangu ili mnifahamu. Kila mmoja wenu anamwangazia sana mtu mwingine, nyinyi nyote ni “wasio bahili,” nyote “mnawajali wengine” katika kila hali; je, haya siyo hasa mliyokuwa mnafanya jana? Na leo je? “Utiifu” wenu umepanda juu kwa alama kidogo, nyote mmekuwa wazoefu kiasi, mmekomaa kidogo na kwa sababu ya haya, “heshima” yenu Kwangu imeongezeka kwa kiasi fulani, na hamna hata mmoja “anayethubutu kutenda kwa wepesi.” Kwa nini mnaishi katika hali ya ubaridi wa kudumu? Ni kwa nini sifa nzuri hazipatikani kabisa ndani yenu? Enyi watu Wangu! Ya zamani yalipita kitambo; msiendelee kuyashikilia zaidi. Zamani mlishikilia msimamo wenu, leo mnapaswa kunipa utiifu wenu wa dhati, na hata zaidi mnafaa kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu siku za usoni, na mtarithi baraka Zangu hapo baadaye. Hili ndilo mnapaswa kufahamu.

Ingawa Siko nanyi, Roho Wangu hakika ataleta neema juu yenu. Kwa kutegemea hili, Natumaini mtaienzi baraka Yangu na mtaweza kujitambua. Msichukulie hili kuwa mtaji wenu; badala yake, mnatakiwa kujaza kinachokosekana ndani yenu kutoka katika maneno Yangu, na kutoka humu mpate mambo mazuri mnayovihitaji. Huu ndio ujumbe Ninaowaachia.

Februari 28, 1992

Jumatano, 21 Februari 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko La Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko La Nne

Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote?

Jumanne, 20 Februari 2018

Maneno ya Mungu Yameniamsha

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, neno la Mungu

22. Maneno ya Mungu Yameniamsha

Miao Xiao Mji wa Jinan, Mkoa wa Shandong
Katika siku zilizopita, nilikuwa daima nikifikiri kuwa Mungu aliposema “ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi” Alikuwa anaashiria wale wanaoikubali hatua hii ya kazi lakini wanaishia kurudi nyuma kwa sababu hawako radhi kustahimili mateso ya kuadibu na hukumu Yake.

Jumatatu, 19 Februari 2018

Ninaona njia ya kumjua Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu

9. Ninaona njia ya kumjua Mungu

Xiaocao Mji wa Changzhi, Mkoa wa Shanxi
Siku moja, niliona kifungu hiki kifuatacho cha neno la Mungu kwa maandishi “Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu”: “Kwenye kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. …

Jumapili, 18 Februari 2018

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ufunuo wa Mungu

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Kwa imani yao, yote yanayohitajika kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kuhifadhi sheria, na iwapo watatubu na kukiri dhambi zao, moyo wa Mungu milele utaridhika. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?

Wakati huo, Yesu alisema kuwa kazi ya Yehova ilikuwa imebaki nyuma kwa Enzi ya Neema, kama Nisemavyo leo kwamba kazi ya Yesu imebaki nyuma. Kama kungekuwa tu na Enzi ya Sheria na siyo Enzi ya Neema, Yesu hangeweza kusulubiwa na hangeweza kuwakomboa wanadamu wote; kungekuwa tu na Enzi ya Sheria, kungekuwa na uwezekano wa mwanadamu kuendelea hadi siku ya leo? Historia inaendelea mbele; historia sio asili ya sheria ya kazi ya Mungu? Hii sio picha ya usimamizi Wake wa mwanadamu ndani ya ulimwengu mzima? Historia inaendelea mbele, na pia kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu yanaendelea kubadilika. Haingewezekana kwa Mungu kudumisha hatua moja ya kazi kwa miaka elfu sita, kwani kila mwanadamu anajua kwamba Yeye daima ni mpya na kamwe si mzee. Hangeweza kuendelea kuendeleza kazi sawa na kusulubiwa, na mara moja, mara mbili, mara tatu…. kupigwa misumari kwa msalaba. Huu ni mtazamo wa mwanadamu mjinga. Mungu haendelezi kazi sawa, na kazi Yake daima inabadilika na daima ni mpya, jinsi kila siku Nazungumza nanyi maneno mapya na kufanya kazi mpya. Hii ndiyo kazi Ninayofanya, umuhimu wake ukiwa kwa maneno “mpya” na “ajabu.” “Mungu habadiliki, na Mungu daima Atakuwa Mungu”; usemi huu hakika ni ukweli. Kiini cha Mungu hakibadiliki, Mungu daima ni Mungu, na Hawezi kamwe kuwa Shetani, lakini haya hayathibitishi kwamba kazi Yake ni ya daima na kabambe kama kiini Chake. Unatangaza kwamba Mungu yuko hivyo, lakini ni jinsi gani basi unaweza kueleza kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si mzee? Kazi ya Mungu inaendelea kuenea, na mapenzi ya Mungu yanaendelea kujitokeza na kufanywa kujulikana na mwanadamu. Wakati mwanadamu anakuwa na uzoefu wa kazi ya Mungu, tabia yake inaendelea kubadilika, na maarifa yake yanaendelea kubadilika. Basi mabadiliko haya yanatokea wapi? Siyo kwa kazi ya Mungu inayobadilika milele? Kama tabia ya mwanadamu inaweza kubadilika, mbona mwanadamu hawezi kuruhusu kazi Yangu na maneno Yangu pia kuendelea kubadilika? Ni lazima Nikabiliwe na vikwazo vya mwanadamu? Hutegemei tu maneno ya hila?

Kufuata kufufuka kwake, Yesu alijitokeza kwa mitume na kusema, “Na, tazameni, Nawatumieni ahadi ya Babangu kwenu: lakini ngojeni katika mji wa Yerusalemu, mpaka mjaliwe uwezo kutoka juu.” Je, wajua jinsi maneno haya yalielezwa? Umepewa sasa nguvu Zake? Umeelewa sasa kile kinachoitwa nguvu? Yesu alitangaza kwamba wanadamu wangepewa Roho wa ukweli katika siku za mwisho. Sasa ni siku za mwisho, umemiliki Roho wa ukweli? Yuko wapi Roho wa ukweli? Hizo roho chafu na roho ovu ni Roho wa ukweli? Hazina haki, wala hata utoaji wa uhai, na huifadhi sheria za zamani bila kufanya kazi yoyote mpya. Hizo ni Roho wa ukweli? Zina uhai, ukweli, na njia? Ziliibuka tofauti kwa dunia? Wale wanaojiweka imara kwa Biblia na kumshikilia kabisa Yesu—mmefuata kazi ya Yesu na maneno Yake? Ni jinsi gani mlivyo waaminifu kwa Yesu? Kitabu kikuu zaidi cha unabii cha Isaya kwa Agano la Kale hakikutaja kwamba mtoto anayeitwa Yesu angezaliwa kwa enzi ya Agano Jipya, bali tu mtoto mchanga wa kiume angezaliwa kwa jina Imanueli. Mbona hakutaja jina Yesu? Hakuna pahali popote kwa Agano la Kale panapotokea jina hili, hivyo mbona basi mnamwanini Yesu? Hakika hamkumwona Yesu kwa macho yenu kabla kuja kumwamini? Ama mlianza kuamini mlipopata ufunuo? Mungu kweli angewaonyesha neema kama hiyo? Na kuwapa baraka kubwa kama hiyo? Je, ni kwa msingi gani mlimwamini Mungu? Mbona basi hamwamini kwamba Mungu amekuwa mwili siku hii? Mbona mnasema kwamba kukosekana kwa ufunuo kutoka kwa Mungu kunathibitisha kwamba Hajakuwa mwili? Ni lazima Mungu amweleze mwanadamu kabla ya kuanza kazi Yake? Ni lazima apate idhini kutoka kwa mwanadamu? Isaya alitangaza tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini lakini hakutabiri kwamba Maria angejifungua Yesu. Mbona basi mlimwamini Yesu aliyezaliwa na Maria? Hakika imani yenu siyo isiyokuwa na uhakika na mkanganyiko! Wengine wanasema kwamba jina la Mungu halibadiliki, hivyo, mbona basi jina la Yehova likawa Yesu? Ilitabiriwa kuja kwa Masihi, hivyo mbona basi mwanadamu kwa jina Yesu alikuja? Mbona jina la Mungu lilibadilika? Kazi kama hiyo haikufanyika muda mrefu uliopita? Hawezi Mungu leo kufanya kazi mpya? Kazi ya jana inaweza kubadilishwa, na kazi ya Yesu inaweza kufuata baada ya hiyo ya Yehova. Haiwezi kazi ya Yesu kurithiwa na kazi ingine? Ikiwa jina la Yehova linaweza kubadilishwa kuwa Yesu, basi jina la Yesu haliwezi kubadilishwa pia? Hii si ya ajabu, na watu wanafikiria hivyo[a] tu kwa sababu ya akili zao rahisi. Mungu daima atakuwa Mungu. Bila kujali mabadiliko ya kazi Yake na jina Lake, tabia na maarifa Yake hayabadiliki milele. Ikiwa unaamini kwamba Mungu anaweza tu kuitwa na jina Yesu, basi unajua machache sana. Unathubutu kudai kwamba Yesu milele ni jina la Mungu, kwamba Mungu milele na daima atajulikana kwa jina Yesu, na kwamba haya hayatabadilika? Unathubutu kudai kwa uhakika ni jina la Yesu lililohitimisha Enzi ya Sheria na pia kuhitimisha enzi ya mwisho? Nani anaweza kusema kwamba neema ya Yesu inaweza kuhitimisha enzi? Kama sasa huwezi kujua kweli hizi wazi, hutaweza tu kuhubiri injili, lakini pia wewe mwenyewe huwezi kubaki umesimama. Itakapofika siku ambayo utatatua matatizo yote ya hao watu wa kidini na kukanusha imani zao za uwongo, hiyo itakuwa thibitisho kwamba una hakika kabisa ya hatua hii ya kazi na huna shaka hata kidogo. Ikiwa huwezi kukanusha imani zao za uwongo, basi watakushitaki na kukukashifu. Hii sio aibu?

Wayahudi wa wakati huo wote walisoma kutoka Agano la Kale na walijua unabii wa Isaya kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini. Mbona basi, na maarifa haya, bado walimtesa Yesu? Hii siyo kwa sababu ya asili yao ya kuasi na kutojua kazi ya Roho Mtakatifu? Wakati huo, Mafarisayo waliamini kwamba kazi ya Jesu ilikuwa tofauti na ile waliyoijua ya mtoto mchanga wa kiume aliyetabiriwa; mwanadamu wa leo anamkataa Mungu kwa sababu kazi ya Mungu mwenye mwili haikubaliani na Biblia. Si kiini cha uasi wao dhidi ya Mungu ni moja na sawa? Unaweza kuwa yule ambaye anakubali tu bila swali kazi yote ya Roho Mtakatifu? Kama ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi ni “mkondo” sawa. Unapaswa kuikubali bila wasiwasi hata kidogo, badala ya kuokota na kuchagua nini cha kukubali. Ukipata maarifa kiasi kutoka kwa Mungu na kujitahadhari dhidi Yake, hili silo tendo lisilohitajika? Unachopaswa kufanya ni kukubali, bila haja ya kuthibitisha zaidi kutoka kwa Biblia, kazi yoyote iwapo tu ni ya Roho Mtakatifu, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushuhuda zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu. Hata kama umegundua ushuhuda usiopingika ndani ya Biblia, haiwezi kukuleta kikamilifu mbele Yangu. Wewe ndiye mmoja anayeishi ndani ya mipaka ya Biblia, na sio mbele Yangu; Biblia haiwezi kukusaidia kunijua, wala haiwezi kuimarisha upendo wako Kwangu. Ingawa Biblia ilitabiri kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa, hakuna yeyote angeweza kuelewa kupitia nani unabii ungetimia, kwani mwanadamu hakujua kazi ya Mungu, na hii ndiyo ilisababisha Mafarisayo kusimama dhidi ya Yesu. Wengine wanajua kwamba kazi Yangu iko katika maslahi ya mwanadamu, lakini bado wanaendelea kuamini kwamba Yesu na Mimi ni viumbe tofauti kabisa visivyopatana. Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri kwa Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. Wakati Yehova aliandika sheria ya Agano la Kale kwa Enzi ya Sheria, mbona basi hakufanya kazi ya Enzi ya Neema? Mbona hakueleza wazi mapema kazi ya Enzi ya Neema? Hii haingekuwa ya manufaa kwa kukubali kwa mwanadamu? Alitabiri tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa na kuja mamlakani, lakini Hakutekeleza mapema kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu nini mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu. Hasa, haingekuwa tendo la imani ya uwongo kutafuta ndani ya Biblia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Nini unaweza kupambanua tu kwa kushika Biblia kwa mikono yako? Uwe mkalimani wa Biblia ama mhubiri, nani anaweza kujua mbeleni kazi ya leo?

“Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo makanisa yaliambiwa na Roho.” Umeyasikia sasa maneno ya Roho Mtakatifu? Maneno ya Mungu yamekuja juu yako. Unayasikia? Mungu anafanya kazi ya neno katika siku za mwisho, na maneno haya ni yale ya Roho Mtakatifu, kwani Mungu ni Roho Mtakatifu na Anaweza pia kuwa mwili; kwa hivyo, maneno ya Roho Mtakatifu, yalivyosemwa zamani, ni maneno ya Mungu mwenye mwili wa leo. Kuna wanadamu wajinga wanaoamini kwamba maneno ya Roho Mtakatifu yanapaswa kuja chini kutoka mbinguni hadi kwa masikio ya mwanadamu. Yeyote anayefikiria hivi hajui kazi ya Mungu. Kwa kweli, matamshi yaliyosemwa na Roho Mtakatifu ni yale yaliyosemwa na Mungu aliyekuwa mwili. Roho Mtakatifu hawezi kuongea moja kwa moja na mwanadamu, na Yehova hakuongea moja kwa moja na watu, hata kwa Enzi ya Sheria. Si ungekuwa uwezekano wa chini zaidi kwamba Angefanya hivyo kwa enzi ya leo? Kwa Mungu kunena matamshi ili kutekeleza kazi, lazima Awe mwili, la sivyo kazi yake haiwezi kukamilisha malengo Yake. Wanaomkataa Mungu ni wale wasiojua Roho ama kanuni ambazo Mungu hufanya kazi. Wanaoamini kwamba sasa ni enzi ya Roho Mtakatifu lakini bado hawakubali kazi Yake mpya ni wale wanaoishi kwa imani isiyo dhahiri. Wanadamu kama hawa hawatapokea kamwe kazi ya Roho Mtakatifu. Wale wanaotaka tu Roho Mtakatifu azungumze moja kwa moja na kutekeleza kazi Yake, lakini bado hawakubali maneno ama kazi ya Mungu mwenye mwili, kamwe hawataweza kuchukua hatua katika enzi mpya ama kupokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu!

Jumamosi, 17 Februari 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Uaminifu wa Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?

Je, unaweza kuonyesha tabia ya Mungu ya nyakati kwa lugha inayofaa iliyo na umuhimu wa nyakati? Kupitia uzoefu wako wa kazi ya Mungu, unaweza kueleza kwa undani tabia ya Mungu? Utaielezaje vizuri, kikamilifu?