Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatano, 1 Agosti 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Sita

Miongoni mwa maneno haya yote, hakuna yasiyoweza kusahaulika zaidi kama yale ya leo. Awali maneno ya Mungu yalifichua hali za mwanadamu au siri za mbinguni, lakini tamko hili halifanani na yale ya wakati uliopita. Halidhihaki wala kufanya mzaha, lakini ni kitu kisichotarajiwa kabisa: Mungu aliketi chini na Akazungumza na watu kwa utulivu. Kusudi Lake ni gani? Unaona nini Mungu anaposema, “Leo, Nimeanza kazi mpya juu ya ulimwengu. Nimewapa watu walio duniani mwanzo mpya, na Nimewaambia wote watoke nyumbani Mwangu. Na kwa kuwa kila mara watu hupenda kujideka, Nawashauri wajijue, na wasiisumbue kazi Yangu kila mara”? Ni huu "mwanzo mpya" ambao Mungu anazungumzia ni upi? Hapo awali Mungu alishawashauri watu waondoke, lakini kusudi la Mungu wakati huo lilikuwa kupima imani yao. Kwa hiyo leo, Anaponena na sauti tofauti—Anakuwa halisi au mwongo? Awali, watu hawakujua Mungu alikuwa Akizungumza kuhusu majaribio gani. Ilikuwa tu kupitia hatua ya kazi ya watendaji-huduma ndipo macho yao yaliona, na wakapitia binafsi majaribio ya Mungu. Hivyo, tangu wakati huo na kuendelea, kwa msaada wa mifano ya mamia ya majaribio ya Petro, mara nyingi watu walifanya kosa la kuamini kwamba "Yalikuwa majaribio ya Mungu." Zaidi ya hayo, katika maneno ya Mungu ukweli ulijitokeza lakini kwa nadra. Kwa hivyo, watu wakawa wa ushirikina kuhusu majaribio ya Mungu, na kwa hiyo katika maneno yote yaliyonenwa na Mungu, hawakuliamini hili kuwa kazi ya ukweli uliotekelezwa na Mungu; badala yake, waliamini kwamba Mungu, kwa sababu hakuwa na lingine la kufanya, Alikuwa hasa Anatumia maneno kuwapima watu. Ilikuwa katikati ya majaribio kama hayo, ambayo hayakuwa na tumaini lakini yalionekana kuleta tumaini, ndipo watu walifuata, na kwa hiyo Mungu aliposema “wote ambao watabaki wataelekea kupitia msiba na ukosefu kidogo mwishowe.” watu bado walijitolea kuzingatia kufuata, na hivyo hawakuwa na nia ya kuondoka. Watu walifuata katikati ya njozi kama hizo, na hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kuwa na hakika kwamba hakukuwa na tumaini—ambayo ni sehemu ya thibitisho la ushindi wa Mungu. Mtazamo wa Mungu unaonyesha kwamba Yeye hukishawishi kila kitu kimhudumie. Njozi za watu huwahimiza kutomwacha Mungu, bila kujali wakati au mahali, na kwa hiyo wakati wa hatua hii Mungu hutumia motisha za watu zenye dosari kuwafanya wawe na ushuhuda Kwake, ambao ni umuhimu mkuu wa wakati ambao Mungu asema, “Nimepata sehemu ya watu.” Shetani hutumia motisha za mwanadamu kusababisha ghasia, ilhali Mungu hutumia motisha za mwandamu kumfanya ahudumu—ambayo ni maana halisi ya maneno ya Mungu kwamba "Wanafikiri kwamba wanaweza kuingia ndani kwa hila, lakini wanaponipa pasi zao za kuingia zisizo halisi, Nazitupa ndani ya shimo la moto papo hapo—na, wanapoona 'juhudi zao za kujitahidi' zikiteketea moto, wanakata tamaa." Mungu huvishawishi vitu vyote kuvifanya vihudumu, na kwa hiyo Haepuki maoni mbalimbali ya mwanadamu, bali huwaambia watu kwa ujasiri waondoke; hii ndiyo ajabu na hekima ya kazi ya Mungu, ikichanganya maneno ya kweli na mbinu kuwa kitu kimoja, ikiwaacha watu wakiwa wenye kuchanganyikiwa na waliokanganywa. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba Mungu kweli anawataka watu watoke nyumbani Kwake, kwamba haya si aina fulani ya majaribio, na Mungu anachukua nafasi hii kusema, "Hata hivyo Mimi pia huwaambia watu kwamba wanapokosa kupata baraka, mtu yeyote asilalamike kunihusu." Hakuna anayeweza kuelewa kama maneno ya Mungu ni halisi au ya uwongo, lakini Mungu hutumia nafasi hii kuwaimarisha watu, kuwanyanganya hamu yao ya kuondoka. Hivyo, kama siku moja watalaaniwa, watakuwa wameonywa mapema kwa maneno ya Mungu, kama wasemavyo watu kwamba "Maneno yasiyovutia ndiyo mazuri." Leo, upendo wa watu kwa Mungu ni wenye ari na wa kweli, na kwa hiyo katika maneno ambayo hawangeweza kufahamu kama yalikuwa halisi au ya uwongo, walishindwa na wakaja kumpenda Mungu, ndiyo maana Mungu alisema "Tayari nimefanikisha kazi Yangu kuu." Mungu anaposema "Natumaini watapata njia yao wenyewe ya kuendelea kuishi, nami Sina mamlaka katika hili," huu ni uhalisi wa tamko la Mungu kuhusu maneno haya yote—hata hivyo watu hawafikiri hivyo; badala yake, kila mara wamefuata bila kutilia maanani maneno ya Mungu hata kidogo. Kwa hivyo, Mungu anaposema "katika siku za baadaye, hakutakuwa tena na maneno yoyote kati yetu, hatutakuwa tena na jambo la kuzungumzia, hatutaingiliana, kila mmoja wetu atashika njia yake," maneno haya ni ukweli, na hayajatiwa doa hata kidogo. Chochote ambacho watu hufikiria, hivyo ndivyo kutokuwa na urazini kwa Mungu kulivyo. Tayari Mungu amekuwa na ushuhuda mbele ya Shetani, na Mungu alisema kwamba Atawafanya watu wote wasimwache haijalishi wakati au mahali—kwa hivyo hatua hii ya kazi imeshakamilishwa, na Mungu hayasikilizi malalamiko ya mwanadamu. Hata hivyo Mungu amelifafanua hili tangu mwanzo, kwa hivyo watu wanaachwa wakiwa wadhaifu, wanalazimika kuomba radhi. Vita kati ya Mungu na Shetani vinategemea mwanadamu kikamilifu. Watu hawawezi kujidhibiti, wao ni makaragosi kweli, huku Mungu na Shetani ndio wanaovuta kamba bila kuonekana. Mungu anapowatumia watu kuwa na ushuhuda Kwake, Yeye hufanya kila Awezalo kufikiri, Hufanya chochote kiwezekanacho, kuwatumia watu kumfanyia huduma, Akiwasababisha watu kutawaliwa na Shetani, na, zaidi ya hayo, kuongozwa na Mungu. Na wakati ambapo ushuhuda ambao Mungu anataka utolewe umemalizika, Yeye huwatupa watu upande mmoja na kuwaacha wakiteseka, huku Mungu anajifanya kwamba Hana shughuli nao. Wakati ambapo Anataka tena kuwatumia watu, Yeye huwaokota kwa mara nyingine na kuwatumia—na watu hawana ufahamu wa hili hata kidogo. Wao ni kama tu ng'ombe au farasi anayetumiwa jinsi atakavyo bwana wake, hakuna kati yao aliye na mamlaka juu yake mwenyewe. Hili linaweza kuonekana kuwa la kusikitisha kidogo, lakini haijalishi kama watu wana mamlaka juu yao wenyewe au la, kumfanyia Mungu huduma ni heshima, si kitu cha kumfadhaisha mtu. Ni kana kwamba Mungu anapaswa kutenda hivi. Je, kuweza kuridhisa hitaji la Mwenye Uweza si jambo la kujivunia? Kwa hiyo unaonaje? Je, umewahi kufanya azimio lako kutoa huduma kwa Mungu? Yawezekana kwamba bado unataka kushikilia haki yako ya kutafuta uhuru wako mwenyewe?
Hata hivyo, yote afanyayo Mungu ni mazuri, na yanastahili kuigwa, na mwanadamu na Mungu ni, hata hivyo, tofauti. Kwa msingi huu, unapaswa kumpenda Mungu kwa moyo wa utu bila kujali kama Mungu anastahi upendo wako au la. Maneno ya Mungu yanaonyesha kwamba pia kuna huzuni nyingi ndani ya moyo wa Mungu. Ni kwa ajili ya maneno ya Mungu tu ndio watu wanasafishwa. Lakini kazi hii, hata hivyo, ilifanyika jana—na kwa hiyo ni nini hasa ambacho Mungu atafanya kufuatia? Mpaka sasa, hii inabaki kuwa siri, na hivyo watu hawana uwezo wa kuielewea au kuifahamu, na wanaweza tu kufuata mkondo wa Mungu. Hata hivyo, yote ambayo Mungu asema ni kweli, yote hutimia—hili halina shaka!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumanne, 31 Julai 2018

Wimbo wa Injili 2018 | "Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" Sifa kwa matendo ya Mungu ya ajabu


Wimbo wa Injili 2018 | "Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" Sifa kwa matendo ya Mungu ya ajabu

I
Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu, na Anatawala vitu vyote kutoka juu. Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia. Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati, kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya. Mungu anamjua mwanadamu kama kiganja cha mkono Wake. Mahali pa siri ni makao ya Mungu, anga ndicho kitanda Mungu akilaliacho. Nguvu ya Shetani haiwezi kumfikia Mungu, kwani Yeye amejawa na utukufu, haki, na hukumu.
II
Mungu amekanyaga vitu vyote na miguu Yake, Yeye ananyosha mtazamo Wake juu ya ulimwengu. Na Mungu ametembea kati ya wanadamu, ameonja utamu na uchungu, ladha zote za dunia ya mwanadamu; lakini wanadamu, kamwe hawakumtambua Mungu kweli, wala hawakumwona Mungu alipokuwa akitembea ughaibuni. Kwa sababu Mungu alikuwa kimya, na hakufanya matendo yasiyo ya kawaida, hivyo, hakuna aliyemwona kweli. Vitu haviko vilivyokuwa awali: Mungu anaenda kufanya vitu ambavyo, katika enzi zote, ulimwengu haujawahi kuona, Mungu anaenda kunena maneno ambayo, katika enzi zote, wanadamu hawajawahi kusikia, kwa sababu Yeye anawataka binadamu wote waje kumjua Mungu katika mwili.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kuonekana kwa Mungu

Jumatatu, 30 Julai 2018

Video ya Injili 2018 | "Kutoka Kinywani mwa Mauti" | Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Video ya Injili 2018 | "Kutoka Kinywani mwa Mauti" | Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Liu Zhen, mwenye umri wa miaka 78, ni mke wa nyumbani wa kawaida wa mashambani. Baada ya kumwamini Mungu, alihisi furaha isiyo na kisawe na kusoma maneno Yake na kuimba nyimbo za kumsifu siku zote, na mara nyingi kukusanyika pamoja na ndugu zake kushirikiana juu ya ukweli. ... Hata hivyo, mambo mazuri hayadumu. Anakamatwa na kuteswa na serikali ya Kikomunisti ya China, ikimtia katika shida mbaya sana. Polisi wanampeleka kwenye kituo cha polisi kwa ajili ya kuhojiwa mara tatu, na kumwonya asimwamini Mungu tena. Wanamchunguza na kwenda nyumbani kwake ili kumtisha. Chini ya shinikizo la serikali ya Kikomunisti ya China, mumewe, mwanawe, na mkwe wake pia wanapinga na kuzuia imani yake kwa Mungu. Kupitia maumivu haya, anamtegemea na kumtazamia Mungu kwa kweli, na maneno Yake yanampa imani na nguvu, yakimruhusu kusimama imara kati ya mateso na dhiki. Katika kilele cha mateso yake wakati hajiwezi kabisa, anamlilia Mungu kwa dharura. Anasikia sala yake na kumfungulia njia. Jioni moja, ghafla anapoteza fahamu na hawezi kuamshwa. Daktari anasema kuwa hawezi kuokolewa na anaiambia familia yake ijiandae kwa ajili ya kuaga kwake, lakini baada ya masaa 18, kimiujiza anaamka. Muujiza huu wa Mwenyezi Mungu unawashangaza wale walio karibu na yeye na kumfungulia njia mpya. ... Baada ya uzoefu huu, Liu Zhen anakuja kuelewa kwa undani kwamba maisha ya watu hayana uhakika, na hakuna yeyote kati yetu anayeweza kuyadhibiti—ni Mungu pekee ndiye Anayetawala jaala ya watu na ana maisha yetu, mauti, mafanikio, na bahati mbaya mikononi Mwake. Pia anakuja kupata uzoefu kwamba ni Mungu pekee ndiye ambaye Aliyepo kwa ajili yetu, daima Yuko karibu kutusaidia, na ni Yeye tu tunayeweza kumwamini na kumtegemea!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Video ya Injili

Jumapili, 29 Julai 2018

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen" | Mungu ni upendo

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen" | Mungu ni upendo

Xiaozhen alikuwa Mkristo mwenye moyo safi, ulio na huruma, ambaye kila wakati alikuwa akiwashughulikia wenzake kwa uaminifu. Hata hivyo, ilipokuwa ni kwa manufaa yao, marafiki wake wa awali waligeuka na kuwa maadui wake. Baada ya kuteseka kutokana na msiba huu, Xiaozhen alilazimika kuuacha moyo wake wa kweli na kanuni zake za awali. Alianza kuisaliti dhamiri yake mwenyewe iliyo nzuri na roho safi, na kugaagaa katika kinamasi cha ulimwengu mbaya. … Huku akianguka kutoka kwa rehema na kutembea katika njia ya upotovu, alikanyagwa na ulimwengu na kukung’utwa na makovu na vilio. Alikuwa amefika mwisho kabisa, na katika wakati wa kukata tamaa wakati alikuwa amepoteza matumaini yote, mwishowe mwito wa kuaminika wa Mwenyezi Mungu ukauamsha moyo na roho ya Xiaozhen …
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wafuasi wa Kristo

Jumamosi, 28 Julai 2018

Wimbo za wokovu | “Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa” | Wema wa Mungu

Wimbo za wokovu | “Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa” | Wema wa Mungu

I
Kwa kuwa Mungu alimuumba mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfikisha katika hatima sahihi. Kwa kuwa Alimuumba mwanadamu na Anamsimamia, ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu. Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu, mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.
II
Kwa sababu ni Mungu anayemfanyia mwanadamu kazi, mwanadamu ana hatima na hatima yake hivyo inahakikishwa, hatima yake inahakikishwa. Yale ambayo mwanadamu hufuatilia na kutamani ni matarajio aliyo nayo anapofuata tamaa badhirifu za kimwili, badala ya hatima, hatima inayotazamiwa na mwanadamu. Yale ambayo Mungu amemwandalia mwanadamu, kwa upande mwingine, ni baraka na ahadi zinazomngoja mwanadamu atakapotakaswa, ambayo Mungu alimwandalia baada ya kuiumba dunia. Hizo baraka na ahadi hazichafuliwi na fikira ya mwanadamu na mawazo, au chaguo lake au mwili. Hii hatima haijaandaliwa kwa mtu mahsusi, mtu mahsusi, lakini ni mahali pa mapumziko kwa kila mwanadamu. Hii ndiyo hatima inayofaa, hatima inayofaa kwa mwanadamu.
III
Ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu. Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu, mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia. Ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu. Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu, mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Ijumaa, 27 Julai 2018

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote"

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote"

I
Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safari ya maisha. Vyovyote vilivyo msingi wako ama safari iliyo mbele yako, hakuna anayeweza kuepuka utaratibu na mpango ambao Mbingu imeweka, na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake, kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote ndiye ana uwezo wa kazi kama hii.
II
Tangu siku ambayo mwanadamu alikuja kuwepo Mungu amekuwa imara katika kazi Yake, Akisimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na kusonga kwa vitu vyote. Kama vitu vyote, mwanadamu kwa kimya na bila kujua anapokea uboreshaji wa utamu, mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya utaratibu wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu viko mkononi mwa Mungu, na maisha yote ya mwanadamu yanatazamwa machoni mwa Mungu. Bila kujali kama unaamini katika hili ua la, chochote na vitu vyote, viishivyo au vilivyokufa, vitageuka, vibadilike, vifanywe upya, na kupotea kulingana na fikira za Mungu. Hivi ndivyo Mungu hutawala juu ya vitu vyote.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Tabia ya Mungu,

Alhamisi, 26 Julai 2018

Wimbo wa Injili 2018 | "Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" Sifa kwa matendo ya Mungu ya ajabu

Wimbo wa Injili 2018 | "Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" Sifa kwa matendo ya Mungu ya ajabu

I
Tangu uhusiano wa kwanza wa Mungu na mwanadamu, Amekuwa akifichua kwao Kiini Chake na vile Alivyo na Alicho nacho, bila kukoma, kila wakati. Kama watu katika enzi wanaweza kuona au kuelewa, Mungu huzungumza na kufanya kazi ili kuonyesha tabia Yake na kiini. Havijawahi kufunikwa wala kufichwa kamwe, vimeachiliwa bila kusita, Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake, vinafichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu.
II
Mungu anatumaini mwanadamu aweza kumwelewa, ajue kiini Chake, na tabia, ambavyo Hataki vichukuliwe kama siri za milele. Wala Hataki mwanadamu amwone Yeye kama kitendawili ambacho hakiwezi kutatuliwa. Havijawahi kufunikwa wala kufichwa kamwe, vimeachiliwa bila kusita, Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake, vinafichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu.
III
Ni wakati tu binadamu amemjua Mungu ndipo anaweza kujua njia ya kwendelea, kustahili kuongozwa na Mungu. Ataishi chini ya mamlaka Yake na kuishi katika mwanga na baraka Zake. Havijawahi kufunikwa wala kufichwa kamwe, vimeachiliwa bila kusita, Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake. Havijawahi kufunikwa wala kufichwa kamwe, vimeachiliwa bila kusita, Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake, vinafichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo za Injili

Jumatano, 25 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (6) - Je, Bado Tunaweza Kupata Uzima Tukiondoka Kwa Biblia?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (6) - Je, Bado Tunaweza Kupata Uzima Tukiondoka Kwa Biblia?

Mara kwa mara wachungaji na wazee huwafundisha watu kuwa hawawezi kuitwa waumini wakiondoka kwenye Biblia, na kwamba kwa kushikilia Biblia pekee ndiyo wanaweza kupata uzima na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hivyo, je, kweli hatuwezi kupata uzima tukiondoka kwenye Biblia? Je, ni Biblia ambayo inaweza kutupa uzima, au ni Mungu ambaye anaweza kutupa uzima? Bwana Yesu alisema, "Tafuta katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnadhani kuwa mna uzima wa milele: na hayo ndiyo yananishuhudia. Nanyi hamtakuja Kwangu, kwamba mpate uhai" (Yohana 5:38-40). Mwenyezi Mungu asema, "Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atajua Mungu na kuidhinishwa na Mungu" (Neno Laonekana katika Mwili). Kwa hivyo, uzima una chanzo chake katika Kristo wala sio katika Biblia. Kristo pekee ndiye chanzo cha uzima na Yeye ndiye Bwana wa Biblia. Video hii itakusaidia kupata ufahamu mpya wa Biblia!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kukamilishwa na Mungu

Jumanne, 24 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (5) - Ni Vipi Kuna Makosa Ndani ya Biblia?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (5) - Ni Vipi Kuna Makosa Ndani ya Biblia?

Watu wengi wanaamini kwamba Biblia yote imetiwa msukumo na Mungu, kwamba imetoka kabisa kwa Roho Mtakatifu, na kwamba hakuna hata neno moja lililo na kosa. Je, mtazamo wa aina hii unawiana na ukweli? Biblia iliandikwa na waandishi zaidi ya 40, yaliyomo yaliandikwa na kupangwa na mwanadamu, na haikufunuliwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu. Ilikuwa vigumu kuepuka kuingiza mawazo na makosa ya mwanadamu wakati ambapo ilikuwa ikiandikwa na kupangwa na mwanadamu.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu

Jumatatu, 23 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (4) - Je, Biblia Nzima Imetiwa Msukumo na Mungu Kweli?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (4) - Je, Biblia Nzima Imetiwa Msukumo na Mungu Kweli?

Watu wengi katika ulimwengu wa dini wanaamini kwamba "Kila andiko limetolewa kwa msukumo wa Mungu," yote katika Biblia ni neno la Mungu. Je, kauli ya aina hii inakubaliana na ukweli? Biblia ni ushahidi wa Mungu pekee, rekodi ya kazi ya Mungu tu, na haijaundwa kwa matamshi ya Mungu kikamilifu. Ndani ya Biblia, ni maneno yaliyonenwa na Yehova Mungu, maneno ya Bwana Yesu, unabii wa Ufunuo na maneno ya manabii yaliyotolewa kwa msukumo wa Mungu pekee, ndiyo neno la Mungu. Mbali na hayo, mengi ya yaliyosalia yanahusiana na rekodi za kihistoria na ushuhuda wa uzoefu wa mwanadamu. Ikiwa ungependa kujua undani wa Biblia, basi tafadhali angalia video hii!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Dondoo za Video ,

Jumapili, 22 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (3) - Je, Inamaanisha Nini katika Ufunuo Inaposema Mtu Asiongeze kwa Unabii?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (3) - Je, Inamaanisha Nini katika Ufunuo Inaposema Mtu Asiongeze kwa Unabii?

Ufunuo sura ya 22, mstari wa 18 "Kwa kuwa namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Iwapo mtu yeyote ataongeza kwa mambo haya, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki." Je, ungependa kujua maana halisi ya maneno haya? Video hii itakuonyesha jibu.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maandiko ya Biblia

Jumamosi, 21 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (2) - Imefichuliwa: Uhusiano Kati ya Mungu na Biblia

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (2) - Imefichuliwa: Uhusiano Kati ya Mungu na Biblia

Wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini wanaamini kuwa maneno na kazi zote za Mungu yamo ndani ya Biblia, kwamba wokovu wa Mungu katika Biblia ni mkamilifu na mradi watu waweke msingi wa imani yao katika Bwana katika Bibilia na washikilie Bibilia, basi wanaweza kunyakuliwa na wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Je, kweli ukweli uko namna hii? Je, ni Mungu ambaye anaweza kufanya kazi kutuokoa, au Biblia? Je, ni Mungu ambaye anaweza kuonyesha ukweli, au Biblia? Ili kujifunza zaidi, tafadhali angalia video hii!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hekima ya Mungu

Ijumaa, 20 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (1) - Imefichuliwa: Je, Kuna Maneno Yoyote au Kazi ya Mungu Mbali na Yaliyo katika Biblia?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (1) - Imefichuliwa: Je, Kuna Maneno Yoyote au Kazi ya Mungu Mbali na Yaliyo katika Biblia?

Wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini mara nyingi huwafundisha watu kwamba hakuna maneno na kazi ya Mungu nje ya Biblia, na hivyo kwenda zaidi ya Biblia ni uzushi. Je, wazo hili linastahili kuchunguzwa? Je, linalingana na ukweli wa kazi ya Mungu? Kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema haijaandikwa tu katika Agano la Kale na inakwenda zaidi ya Agano la Kale. Ikiwa kwenda zaidi ya Biblia ni uzushi, je, si basi sisi pia tunahukumu kazi ya Bwana? Hivyo kuna maneno au kazi ya Mungu isipokuwa yale yaliyo katika Biblia, au hakuna? Video hii itakufichulia jibu.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Dondoo za Video ,

Jumanne, 17 Julai 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Je, Umekuwa Hai Tena?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Je, Umekuwa Hai Tena?

Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya kutimiza kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, na umefanywa mkamilifu, ingawa utakuwa huwezi kunena unabii, wala siri zozote, utakuwa unaishi kulingana na kufichua taswira ya mwanadamu. Mungu alimuumba mwanadamu, baada ya hapo mwanadamu akaharibiwa na Shetani, na uharibifu huu umewafanya watu wawe maiti—na hivyo, baada ya kuwa umebadilika, utakuwa tofauti na maiti hizi. Ni maneno ya Mungu ndiyo yanatoa uzima kwa roho za watu na kuwasababisha kuzaliwa upya, na roho za watu zinapozaliwa upya, watakuwa hai tena. Neno "wafu" linarejelea maiti ambazo hazina roho, kwa watu ambao roho zao zimekufa. Roho za watu zinapowekewa uhai, wanakuwa hai tena. Watakatifu waliozungumziwa awali huashiria watu ambao wamekuwa hai, wale ambao walikuwa chini ya ushawishi wa Shetani lakini wakamshinda Shetani. Wateule wa China wamestahimili ukatili na mateso na ulaghai wa joka kuu jekundu, ambalo limewaacha wakiwa wameharibika kiakili na kuwachwa wakiwa hawana hata ujasiri wa kuishi. Hivyo, kuamsha roho zao kunapaswa kuanza na hulka zao. Kidogo kidogo, katika hulka yao roho yao itaamshwa. Siku moja, watakapokuwa hai tena, hakutakuwa na vizuizi zaidi, na vyote vitasonga mbele bila tatizo. Kwa sasa, hii inabakia kuwa bado haijafanikiwa. Kuishi kwa kudhihirisha kwa watu wengi kunajumuisha mazingira ya kifo, wamezungukwa na hali ya kifo, na wamepungukiwa sana. Maneno ya baadhi ya watu yanabeba kifo, matendo yao yanabeba kifo, na takribani kila kitu wanachoishi kwa kudhihirisha ni kifo. Ikiwa leo, watu wanamshuhudia Mungu waziwazi, basi kazi hii itashindwa, maana bado hawajakuwa hai tena kikamilifu, na kuna wafu wengi sana miongoni mwenu. Leo, baadhi ya watu wanauliza kwa nini Mungu haonyeshi ishara na maajabu ili kwamba aweze kusambaza kazi Yake miongoni mwa nchi za Wamataifa. Wafu hawawezi kuwa na ushuhuda wa Mungu; walio hai wanaweza, lakini watu wengi leo ni wafu, wengi wao wanaishi katika kifungo cha kifo, wanaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hawawezi kupata ushindi—na hivyo wanawezaje kuchukua ushuhuda wa Mungu? Wanawezaje kueneza kazi ya injili?
Wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, ni wale ambao wanaishi katikati ya kifo, ni wale ambao wametawaliwa na Shetani. Bila kuokolewa na Mungu, na kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, watu wanakuwa hawana uwezo kukwepa athari ya kifo, hawawezi kuwa hai. Wafu hawa hawawezi kuwa ushuhuda kwa Mungu, wala hawawezi kutumiwa na Mungu, wala kuingia katika ufalme. Mungu anahitaji ushuhuda wa walio hai, na sio wafu, na Anaomba kwamba walio hai wafanye kazi kwa ajili Yake, na sio wafu. "Wafu" ni wale ambao wanampinga na kumwasi Mungu, ni wale ambao ni mbumbumbu katika roho na hawaelewi maneno ya Mungu, ni wale ambao hawaweki ukweli katika matendo na hawana utii hata kidogo kwa Mungu, na ni wale wamemilikiwa na Shetani na kunyanyaswa na Shetani. Wafu wanajionyesha wenyewe kwa kusimama kwa kuupinga ukweli, kwa kumwasi Mungu, na kwa kuwa duni, wa kudharaulika, kuwa waovu, katili, wadanganyifu, na kudhuru kwa siri. Ingawa watu wa namna hiyo wanakula na kunywa maneno ya Mungu, hawana uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu; wanaishi, lakini ni wafu wanaotembea, ni maiti zinazopumua. Wafu hawawezi kabisa kumridhisha Mungu, wala kumtii kikamilifu. Wanaweza tu kumdanganya, kusema maneno ya makufuru juu Yake, na kumsaliti, na yote wanayoyaishi kwa kudhihirisha hufichua asili ya Shetani. Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Baada ya hapo ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi. Mwanadamu wa asili aliyeumbwa na Mungu alikuwa hai, lakini kwa sababu ya uharibifu wa Shetani maisha ya mwanadamu yapo katikati ya kifo, na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo watu hawa wamekuwa wafu ambao hawana roho, wamekuwa ni maadui ambao wanampinga Mungu, wamekuwa nyenzo ya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu wote walio hai ambao wameumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda wake, na Amempoteza mwanadamu, ambaye Alimuumba na ndiye kiumbe pekee aliye na pumzi Yake. Ikiwa Mungu ataamua kurejesha ushuhuda Wake, na kuwarejesha wale ambao waliumbwa kwa mkono wake lakini ambao wamechukuliwa mateka na Shetani, basi ni lazima awafufue ili waweze kuwa viumbe hai, na ni lazima awaongoe ili kwamba waweze kuishi katika nuru Yake. Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake. Mungu anawaokoa wale ambao wanaweza kuwa hai tena, ambao wanaweza kuuona wokovu wa Mungu, ambao wanaweza kuwa watii kwa Mungu, na wapo tayari kumtafuta Mungu. Anawaokoa wale ambao wanamwamini Mungu aliyepata mwili, na wanaamini katika kuonekana Kwake. Baadhi ya watu wanaweza kuwa hai tena, na baadhi hawawezi; inategemea na asili yao kama inaweza kuokolewa au la. Watu wengi wamesikia sana kuhusu maneno ya Mungu lakini bado hawaelewi mapenzi ya Mungu, wameyasikia maneno mengi sana ya Mungu lakini bado hawawezi kuyaweka katika vitendo, hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ukweli wowote na pia kwa kukusudia kabisa wanaingilia kazi ya Mungu. Hawawezi kufanya kazi yoyote kwa ajili ya Mungu, hawawezi kujitolea chochote Kwake, na pia wanatumia kwa siri pesa za kanisa, na kula katika nyumba ya Mungu bure. Watu hawa ni wafu, na hawataokolewa. Mungu anawaokoa wale ambao wapo katika kazi Yake. Lakini kuna sehemu ya watu hao ambao hawawezi kupokea wokovu Wake; ni idadi ndogo tu ndiyo inaweza kupokea wokovu Wake, maana watu wengi ni wafu sana, ni wafu sana kiasi kwamba hawawezi kuokolewa, wameharibiwa kabisa na Shetani, na kwa asili, wamekuwa hatari sana. Wala idadi ndogo hiyo ya watu haikuweza kumtii Mungu kikamilifu. Hawakuwa wale ambao walikuwa waaminifu kabisa kwa Mungu tangu mwanzo, au wale ambao walikuwa na upendo wa hali ya juu kabisa kwa Mungu toka mwanzo; badala yake, wamekuwa watiifu kwa Mungu kwa sababu ya kazi Yake ya ushindi, wanamwona Mungu kwa sababu ya upendo wake mkuu, kuna mabadiliko katika tabia zao kwa sababu ya tabia ya Mungu ya haki, na wanamjua Mungu kwa sababu ya kazi Yake, ambayo ni halisi na ya kawaida. Bila kazi hii ya Mungu, haijalishi watu hawa ni wazuri kiasi gani bado wangebaki kuwa wa Shetani, bado wangekuwa ni wa kifo, bado wangekuwa wafu. Kwamba, leo, watu hawa wanaweza kupokea wokovu wa Mungu ni kwa sababu kabisa wanaweza kushirikiana na Mungu.
Kwa sababu ya utiifu wao kwa Mungu, walio hai wanaweza kuchukuliwa na Mungu na kuishi katika ahadi Zake, na kwa sababu ya upinzani wao kwa Mungu, wafu watachukiwa zaidi na kukataliwa na Mungu na kuishi katikati ya adhabu na laana Zake. Hiyo ndiyo tabia ya haki ya Mungu, na haiwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Kwa sababu ya utafutaji wao wenyewe, watu wanapokea kibali cha Mungu na kuishi katika nuru; kwa sababu ya hila zao za kutisha, watu wanalaaniwa na Mungu, na kushuka chini katika adhabu; kwa sababu ya matendo yao maovu, watu wanaadhibiwa na Mungu; na kwa sababu ya kutamani kwao sana na utii wao, watu wanapokea baraka za Mungu. Mungu ni mwenye haki: Anawabariki walio hai, na kuwalaani waovu, ili kwamba siku zote wanakuwa katikati ya kifo, na kamwe hawataishi katika nuru ya Mungu. Mungu atawachukua walio hai kwenda katika ufalme Wake, Atawachukua walio hai kwenda katika baraka Zake milele. Wafu Atawaangusha katika kifo cha milele; wao ni wahusika wa uharibifu Wake, na siku zote watakuwa kwa Shetani. Mungu hamtendei mtu yeyote bila haki. Wale wote ambao kweli wanamtafuta Mungu hakika watabaki katika nyumba ya Mungu, na wale wote ambao hawamtii Mungu, na wale ambao hawana ulinganifu Naye hakika wataishi katika adhabu Yake. Pengine huna uhakika kuhusu kazi ya Mungu katika mwili—lakini siku moja mwili wa Mungu hautapangilia hatima ya mwanadamu moja kwa moja; badala yake, Roho Wake, atapanga mwisho wa mwanadamu, na wakati huo watu watajua kwamba mwili wa Mungu na Roho Wake ni kitu kimoja, kwamba mwili Wake hauwezi kufanya kosa, na hata Roho Wake hawezi kabisa kufanya kosa. Na hatimaye, hakika atawachukua wale ambao watakuwa hai tena na kuwapeleka katika ufalme Wake, hakuna zaidi, wala pungufu, na wale wafu ambao hawakutoka wakiwa hai watatupwa katika shimo la Shetani.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili