Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumamosi, 17 Novemba 2018

Swahili Christian Video "Mazungumzo"(3): Upingaji wa Wakristo wa Kushangaza kwa Uvumi na Kashfa za CCP

Swahili Christian Video "Mazungumzo"(3): Upingaji wa Wakristo wa Kushangaza kwa Uvumi na Kashfa za CCP

Ili kuwadanganya Wakristo kumsaliti Mungu na kuiacha imani yao, CCP kimemsaliti Kristo wa siku za mwisho na Bwana Yesu hadharani, kikisema kuwa wote wawili ni watu wa kawaida na sio Mungu mwenye mwili. CCP kimewakashifu Wakristo kama wanaomwamini mtu tu na sio Mungu. Pia kimeeneza uvumi kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu liliundwa na mtu kwa kuwa tu mtu ambaye hutumiwa na Mungu ndiye anayeyaendesha mambo yote ya utawala ya kanisa. Kupata mwili kwa kweli ni nini? Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzwaje, na ni nani aliyelianzisha? Wakristo wanautumiaje ukweli na mambo ya hakika kukanusha uvumi na kashfa za umma ambazo CCP kinaeneza kuhusu Kristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Ijumaa, 16 Novemba 2018

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (2): Jinsi Wakristo Wanavyoukabili Utiaji Kasumba wa Ukanaji Mungu wa CCP

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (2): Jinsi Wakristo Wanavyoukabili Utiaji Kasumba wa Ukanaji Mungu wa CCP

Ili kuwalazimisha Wakristo kumtelekeza Mungu na kuiacha imani yao, CCP haijawaashawishi Wakristo kwa umaarufu na hadhi tu, lakini imewatia kasumba ya ukanaji Mungu, uyakinifu, kuamini mageuko, na maarifa ya kisayansi. Kwa hiyo Wakristo wamepokeaje utiaji kasumba na ubadilishaji wa CCP? Kwa nini wanaendelea kufuatilia kwa ukaidi njia ya kumwamini Mungu na kumfuata Mungu? Video hii fupi ya ajabu umetayarishiwiwa ili kuyajibu maswali haya.
Mwenyezi Mungu alisema, Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu

Alhamisi, 15 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unajua Nini Kuhusu Imani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unajua Nini Kuhusu Imani?

Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamumwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo. Kwani kazi Ninayoifanya ni yake binadamu kunijia Mimi na kunijia Mimi, wala si kwa binadamu kuvutiwa na kuniangalia Mimi kwa njia mpya kwa sababu ya kazi Yangu. Awali Nilijionyesha katika ishara na maajabu mengi na kufanya miujiza mingi. Waisraeli wakati huo waliniangalia Mimi kwa tamanio kuu na walistahi pakubwa uwezo Wangu wa kipekee wa kuponya wagonjwa na kupunga mapepo. Wakati huo, Wayahudi walifikiri nguvu Zangu za uponyaji zilikuwa za kistadi na zisizo za kawaida. Kwa matendo Yangu mengi kama hayo, wote walinichukulia Mimi kwa heshima; waliweza kuhisi tamanio kuu katika nguvu Zangu zote. Kwa hiyo yeyote aliyeniona Mimi nikifanya miujiza alinifuatilia Mimi kwa karibu kiasi kwamba maelfu ya watu walinizunguka ili kunitazama nikiwaponya wagonjwa. Nilionyesha ishara na maajabu mengi, ilhali binadamu alinichukulia Mimi kama daktari stadi; Niliongea maneno mengi ya mafunzo kwa watu hao wakati huo, ilhali wote walinichukulia Mimi tu kama mwalimu aliyekuwa na mamlaka zaidi kwa wanafunzi wake! Hadi siku ya leo, baada ya binadamu kuona rekodi za kihistoria za kazi Yangu, ufasiri wao unaendelea kuwa kwamba Mimi ni daktari mkuu anayeponya wagonjwa na mwalimu kwa wasiojua. Na wameniita Mimi Bwana Yesu Kristo Mwenye huruma. Wale wanaofasiri maandiko huenda walizidi mbinu Zangu katika uponyaji, au huenda pengine wakawa wanafunzi ambao tayari wamempita mwalimu wao, ilhali binadamu kama hao wanaofahamika sana ambao majina yao yanajulikana kote ulimwenguni wananichukulia Mimi kwa kiwango cha chini sana cha kuwa daktari tu! Matendo Yangu ni mengi zaidi kwa kuhesabiwa kuliko chembechembe za changarawe kwenye ufuo na hekima Yangu kubwa zaidi kuliko ile ya watoto wote wa kiume wa Suleimani, ilhali binadamu wanafikiria kwamba Mimi ni daktari tu asiye na mengi kumhusu na mwalimu wa binadamu asiyejulikana! Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupata uponyaji? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu niweze kutumia nguvu Zangu kupunga roho chafu kutoka kwenye miili yao? Na ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu waweze kupokea amani na furaha kutoka Kwangu? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili kuhitaji kutoka Kwangu utajiri mwingi zaidi wa dunia, na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuishi maisha hayo kwa usalama na kuwa salama salimini katika maisha yajayo? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuepuka tu mateso ya kuzimu na kupokea baraka za mbinguni? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili wapate tulizo lakini hawatafuti kupata chochote kutoka kwa ulimwengu ujao? Niliposhushia hasira Zangu binadamu na kuchukua furaha na amani yote aliyokuwa nayo mwanzo, binadamu akaanza kuwa na shaka. Nilipomkabidhi binadamu mateso ya kuzimu na kuchukua tena baraka za mbinguni, aibu ya binadamu iligeuka na kuwa hasira. Wakati binadamu aliponiomba Mimi kumponya, bado Sikumtambua na vilevile nilimchukia pakubwa, binadamu alienda mbali sana na Mimi na akatafuta njia za waganga na wachawi. Nilipochukua kila kitu ambacho binadamu alitaka kutoka Kwangu, kisha kila kitu kilitoweka bila kuonekana tena. Kwa hivyo, Ninasema kwamba binadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata. Wayahudi waliniamini Mimi kwa neema Yangu, na wakanifuata Mimi popote Nilipoenda. Binadamu hawa wasiojua wenye maarifa na uzoefu finyu walitafuta tu kuona ishara na maajabu ambayo nilionyesha. Walinichukulia Mimi kuwa mkuu wa nyumba ya Wayahudi ambaye angeweza kutekeleza miujiza mikubwa zaidi. Kwa hivyo, Nilipopunga mapepo kutoka kwa binadamu walijizungumzia miongoni mwao kwa mkanganyo mkubwa wakisema Mimi ni Eliya, kwamba Mimi ni Musa, kwamba Mimi ndimi nabii wa kale zaidi kati ya wote, kwamba Mimi ndimi daktari mkuu zaidi kuliko wote. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Mimi ndimi maisha, njia na ukweli, hakuna yeyote angejua uwepo Wangu au utambulisho Wangu. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba mbingu ndipo ambapo Baba Yangu anapoishi, hakuna aliyejua kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu, na tena Mungu Mwenyewe. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Nitaleta ukombozi kwa wanadamu wote na kulipia mwanadamu fidia, hakuna aliyejua Mimi ni Mkombozi wa mwanadamu; binadamu alinijua tu Mimi kama mtu mkarimu na mwenye huruma. Na mbali na Mimi Mwenyewe kuweza kufafanua kila kitu kuhusu Mimi, hakuna aliyeweza kunitambua Mimi, hakuna aliyeamini kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai. Binadamu pia anayo imani kama hii Kwangu Mimi, na ananidanganya Mimi kwa njia hii. Binadamu anawezaje kunitolea Mimi ushuhuda wakati anayo mitazamo kama hii kunihusu Mimi?
Binadamu anayo imani Kwangu Mimi lakini hawezi kunitolea ushuhuda Mimi; kabla ya Mimi Mwenyewe kujitambulisha, binadamu hawezi kunitolea ushuhuda Mimi. Binadamu anaona tu kwamba Mimi ninazidi viumbe na binadamu wote wengine watakatifu, na anaona kwamba kazi ninayofanya haiwezi kufanywa na binadamu wengine. Kwa hivyo, kuanzia kwaWayahudi hadi kwa binadamu wa siku ya leo, yeyote ambaye ameyaona matendo Yangu yenye utukufu anajawa tu na uchu wa kudadisi mengi kuhusu Mimi, ilhali hakuna kinywa cha kiumbe kimoja ambacho kingeweza kunitolea ushuhuda. Baba Yangu tu ndiye Aliyenitolea ushuhuda Mimi; Alinitengenezea njia Mimi miongoni mwa viumbe vyote. Kwani, haijalishi ni namna gani Nilivyofanya kazi, binadamu asingewahi kujua Mimi ndimi Bwana wa viumbe, binadamu anajua tu kuchukua, na hajui kuwa na imani ndani Yangu Mimi kwa sababu ya kazi Yangu Mimi. Binadamu ananijua Mimi tu kwa sababu Mimi sina hatia wala si mtenda dhambi kwa vyovyote vile, kwa sababu Ninaweza kufafanua mafumbo mengi, kwa sababu Mimi niko juu ya wengine wote, au kwa sababu binadamu amefaidi pakubwa kutoka Kwangu. Ilhali wachache ndio wanaoamini kwamba Mimi ndimi Bwana wa viumbe. Hii ndiyo maana Ninasema ya kwamba binadamu hajui ni kwa nini anayo imani Kwangu mimi; hajui kusudio au umuhimu wa kuwa na imani Kwangu mimi. Uhalisia wa binadamu umekosekana, kiasi cha kwamba karibu hana thamani tena ya kuweza kunitolea ushuhuda Mimi. Unayo imani ya kweli ndogo sana na umefaidi kidogo sana, kwa hivyo una ushuhuda mdogo. Aidha, unaelewa mambo machache sana na unapungukiwa na mambo mengi sana kiasi kwamba hufai kushuhudia matendo Yangu. Azimio lako kwa hakika linaeleweka, lakini je una hakika kwamba utaweza kunitolea ushuhuda kwa ufanisi kuhusu hali halisi ya Mungu? Kile ambacho umepitia na kuona kinazidi kile ambacho watakatifu na manabii wengine wa awali walivyoshuhudia, lakini je unaweza kutoa ushuhuda mkubwa zaidi kuliko maneno ya hawa watakatifu na manabii waliotangulia? Kile Ninachokupa wewe sasa kinazidi kile Nilichompa Musa na ni kikubwa zaidi kuliko kile nilichompa Daudi, kwa hivyo vilevile Ninakuomba ushuhuda wako uzidi ule wa Musa na kwamba maneno yako yawe makubwa zaidi kuliko yale ya Daudi. Ninakupa vyote hivi mara mia moja, kwa hivyo vilevile ninakuomba nawe unilipe tena vivyo hivyo. Lazima ujue kwamba Mimi Ndimi ninayempa maisha mwanadamu, na kwamba wewe ndiwe unayepokea maisha kutoka Kwangu na lazima unitolee ushuhuda Mimi. Huu ndio wajibu wako, ambao Ninashusha kwako na ambao unastahili kunifanyia Mimi. Nimekupa utukufu Wangu wote, na kukupatia maisha ambayo watu wateule, Waisraeli, hawakuwahi kupokea. Bila kukosea, unastahili kunitolea ushuhuda, na kuutoa ujana wako kwa ajili Yangu na kuyatoa maisha yako. Yeyote yule ninayempa Mimi utukufu Wangu ataweza kunitolea Mimi ushuhuda na kunipatia maisha yake. Haya yote yametabiriwa mapema. Ni utajiri wako wewe ambao Ninawekea utukufu Wangu kwako wewe na wajibu wako ni kuutolea ushuhuda utukufu Wangu. Kama unaniamini tu Mimi ili kupata utajiri, basi kazi Yangu haitakuwa yenye umuhimu, na hutakuwa unatimiza wajibu wako. Waisraeli waliona tu huruma Yangu, upendo Wangu na ukubwa Wangu nao Wayahudi walitoa tu ushuhuda wa subira Yangu na ukombozi Wangu. Waliona kazi kidogo sana ya Roho Yangu; huenda ikawa kwamba kiwango chao cha uelewa kilikuwa sehemu ndogo sana ya ile ambayo wewe umesikia na kuona. Kile ulichoona kinazidi hata kile ambacho makuhani wakuu waliona miongoni mwao. Siku hii, ukweli ambao umeelewa umezidi wao; kile ambacho umeona siku hii kinazidi kile kilichoonwa kwenye Enzi ya Sheria pamoja na Enzi ya Neema na kile ambacho umepitia kinazidi hata kile ambacho Musa na Eliya walipitia. Kile ambacho Waisraeli walielewa kilikuwa tu sheria ya Yehova na kile ambacho waliona kilikuwa tu ni mgongo wake Yehova; kile ambacho Wayahudi walielewa kilikuwa tu ukombozi wa Yesu, kile walichopokea kilikuwa neema waliyowekewa na Yesu, na kile walichoona kilikuwa ni taswira ya Yesu ndani ya nyumba ya Wayahudi. Kile utakachoona siku hii ni utukufu wa Yehova, ukombozi wa Yesu na matendo Yangu yote ya siku hii. Umesikia pia maneno ya Roho Yangu, hekima Yangu teule, na ukaja kujua kuhusu maajabu Yangu, na umeweza kujifunza kuhusu tabia Yangu. Nimeweza pia kukuambia kuhusu mpango Wangu wa usimamizi. Kile ambacho umeona si tu Mungu mwenye upendo na huruma, lakini yule aliyejawa na haki. Umeiona kazi Yangu ya maajabu na kujua kwamba Nimejawa na hasira na adhama. Aidha, umejua kwamba Niliwahi kuzishusha hasira Zangu katika nyumba ya Israeli, na kwamba leo hii, umeshushiwa wewe. Umeelewa zaidi kuhusu mafumbo Yangu kule mbinguni kuliko vile alivyoelewa Isaya pamoja na Yohana; unajua zaidi kuhusu uzuri Wangu na kustahiwa Kwangu kuliko watakatifu wote wa vizazi viilivyotangulia. Kile ulichopokea si ukweli Wangu tu, njia Yangu, maisha Yangu, lakini maono na ufunuo ambavyo ni vikubwa zaidi kuliko vile vya Yohana. Umeelewa mafumbo mengine mengi zaidi na pia umeona sura Yangu kamili; umekubali mengi kuhusu hukumu Yangu na tabia Yangu ya haki. Kwa hivyo, ingawaje ulizaliwa kwenye siku za mwisho, uelewa wako ni ule wa siku za awali na za kale; umeweza pia kupitia ni nini kilichomo kwenye siku hii, na kile kilichotimizwa na mkono Wangu. Kile Ninachokuomba kinawezekana, kwani kile Nilichokupa ni kingi mno na ni mengi ambayo umeona Kwangu mimi. Kwa hivyo, Ninakuomba kunishuhudia Mimi kama vile watakatifu wa awali walivyofanya na hili ndilo tamanio tu la moyo Wangu.
Ni Baba Yangu ambaye amekuwa akinishuhudia Mimi, lakini Natafuta kupokea utukufu mkubwa zaidi na kwa maneno ya ushuhuda kutoka kwenye vinywa vya viumbe. Kwa hiyo Ninakupa kila kitu chote Changu kwa kusudi la wewe kuweza kutimiza wajibu wako na kuhitimisha kazi Yangu miongoni mwa binadamu. Unastahili kuelewa ni kwa nini una imani Kwangu Mimi. Ukinifuata Mimi tu ili uwe mwanafunzi Wangu au mgonjwa Wangu, au kuwa mojawapo wa watakatifu Wangu mbinguni, basi jitihada zako zitakuwa bure. Kunifuata Mimi kwa njia kama hiyo ni sawa tu na kuharibu jitihada zako; kuwa na imani kama hiyo Kwangu mimi ni kuishi tu ukiharibu siku zako na kutomakinikia ujana wako. Na mwisho hutapokea chochote. Huku si ni kufanya kazi bure? Ni muda mrefu tangu Nimetoka miongoni mwa Wayahudi na mimi si daktari tena wa binadamu au dawa ya binadamu. Mimi si mnyama tena wa kumbebea mizigo binadamu ili aniendeshe au kunichinja akipenda; badala yake Nimekuja miongoni mwa binadamu ili kuhukumu na kuadibu binadamu, na kwa binadamu kunijua Mimi. Unafaa kujua kwamba Niliwahi kufanya kazi ya ukombozi; Niliwahi kuwa Yesu, lakini Nisingebakia kuwa Yesu milele, licha ya kwamba Niliwahi kuwa Yehova lakini baadaye nikawa Yesu. Mimi ndimi Mungu wa mwanadamu, Bwana wa viumbe, lakini Siwezi kubakia Yesu milele au kubakia Yehova milele. Nimekuwa kile ambacho binadamu aliona ni daktari, lakini haiwezi kusemekana kwamba Mungu ni daktari tu wa mwanadamu. Kwa hiyo kama utakuwa na mtazamo huo wa kale katika imani yako Kwangu mimi, basi hutapata chochote. Haijalishi ni vipi utakavyonisifu siku hii: “Tazama Mungu alivyo na upendo kwa binadamu; Ananiponya mimi na kunipa baraka, amani na furaha. Ni vipi ambavyo Mungu atakavyokuwa mzuri kwa binadamu; kama tutakuwa na imani tu Kwake Yeye, basi hatutahitajika kuwa na wasiwasi wa pesa na utajiri…,” Siwezi bado kutatiza kazi Yangu asilia. Kama utaniamini Mimi siku hii, utapokea tu utukufu Wangu na kustahili kunitolea ushuhuda, na kila kitu kingine kitafuata. Hili lazima ulijue wazi.
Sasa unajua kweli ni kwa nini unaniamini Mimi? Kweli unajua kusudi na umuhimu wa kazi Yangu? Kweli unajua wajibu wako? Kweli unaujua ushuhuda Wangu? Kama unaniamini Mimi tu, ilhali si utukufu Wangu wala ushuhuda Wangu vinaweza kuonekana ndani yako, basi Nimekutupa nje kitambo kirefu. Kwa wale wanaoona wanajua kila kitu, wao ni miiba zaidi katika macho Yangu, na katika nyumba Yangu, wao ni vizuizi tu Kwangu. Wao ndio magugu yanayopaswa kupepetwa kabisa na kuondolewa kwenye kazi Yangu, bila ya jitihada hata kidogo na bila ya uzito wowote; Nimevichukia kitambo kirefu. Na kwa wale bila ya ushuhuda, hasira Yangu siku zote iko juu yao, na kiboko Changu hakijawahi kutoka kwao. Kitambo kirefu Nimewakabidhi kwenye mikono ya yule mwovu, na hawana tena baraka Zangu zozote. Na siku hiyo ikifika, adhabu yao itakuwa mbaya zaidi kuliko ile ya wanawake wajinga. Sasa hivi Ninafanya kazi ile ambayo ndiyo wajibu Wangu kufanya; Nitakusanya pamoja ngano yote, pamoja na magugu. Hii ndiyo kazi Yangu sasa. Magugu haya yataweza kupepetwa na kuondolewa wakati wa kupepeta Kwangu, kisha nafaka za ngano zitakusanywa kwenye ghala, na magugu ambayo yatakuwa yamepepetwa yatawekwa motoni na kuchomwa hadi kugeuka jivu. Kazi Yangu sasa ni kuwaweka tu binadamu wote kwa pamoja, yani, kuweza kuwashinda wote kabisa. Kisha Nitaanza upepetaji wa kufichua mwisho wa binadamu wote. Kwa hiyo unastahili kujua namna ya kunitosheleza Mimi sasa na namna unavyostahili kuwa kwenye njia iliyo sawa katika imani yako Kwangu. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako. Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. Wajibu wa imani Yako Kwangu mimi ni kunishuhudia Mimi, kuwa mwaminifu Kwangu mimi na si mwengine yeyote, na kuwa mtiifu hadi mwisho. Kabla Sijaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu, utawezaje kunishuhudia Mimi? Utawezaje kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi? Je, unajitolea uaminifu wako wote katika utendakazi au utakata tamaa tu? Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa? Ninakuadibu ili uweze kunishuhudia Mimi, na kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi. Pia, kuadibu huku kwa sasa kunalenga katika kufichua hatua inayofuata ya kazi Yangu na kuruhusu kazi hiyo kuendelea bila kutatizwa. Hivyo basi Nakushawishi wewe kuwa mwenye hekima na kutochukulia maisha yako au umuhimu wa kuwepo kwako kuwa ule ambao hauna manufaa kamwe. Unaweza kujua haswa kazi Yangu ijayo itakuwa ipi? Je, unajua namna Nitakavyofanya kazi katika siku zijazo na namna ambavyo kazi Yangu itakavyobadilika? Unafaa kujua umuhimu wa kile ambacho umepitia katika kazi Yangu, na zaidi, umuhimu wa imani yako Kwangu mimi. Nimefanya mengi kweli; iweje Nikate tamaa Nikiwa katikati kama unavyofikiria? Nimefanya kazi kubwa kweli; ninawezaje kuiharibu? Kwa hakika, Nimekuja kuhitimisha enzi hii. Hii ni kweli, lakini zaidi, lazima ujue kwamba Ninafaa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na, zaidi ya yote, kueneza injili ya ufalme. Kwa hivyo unafaa kujua kwamba kazi ya sasa inalenga katika kuanzisha tu enzi mpya, na kuweka msingi wa kueneza injili na kuihitimisha enzi ya sasa katika wakati ujao. Kazi Yangu si rahisi sana kama unavyofikiria, wala si kwamba haina manufaa au maana kama unavyoweza kutaka kuamini. Kwa hivyo, Ninakuambia kama awali: Unastahili kujitolea maisha Yako katika kazi Yangu, na zaidi, unastahili kujitolea wewe mwenyewe katika utukufu Wangu. Aidha, wewe kunishuhudia ndicho kile kitu ambacho Nimetamani kwa muda mrefu, na kingine ambacho Nimetamani hata zaidi ni wewe kueneza injili Yangu. Unastahili kuelewa kile kilichomo ndani ya moyo Wangu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.

Jumatano, 14 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Tatu

Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Uyahudi na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai juu yao, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi. Kwa hakika Mungu atawahukumu hao, na kwa hakika Atakuwa mwenye hasira nao na mle uadhama wa Mungu utafichuliwa. Hukumu ya aina hiyo itakuwa papo hapo na kuwasilishwa bila kuchelewa. Ghadhabu kali ya Mungu itawachoma hao wote kwa ajili ya makosa yao ya kuchukiza na janga kubwa litawafikia wakati wowote; wao hawatajua njia ya kutoroka na hawatakuwa na mahali pa kujificha, wao watalia na kusaga meno yao kwa ajili ya uharibifu ambao wamejiletea wenyewe.
Wana wa ushindi wapendwa wa Mungu kwa hakika watakaa katika Uyahudi, kamwe wasiiache. Umati utasikiliza sauti Yake kwa makini, watatilia maanani kwa ungalifu matendo Yake, na sauti zao za sifa Kwake kamwe hazitakoma. Mungu mmoja wa kweli Ameonekana! Tutakuwa na uhakika juu Yake katika roho na kumfuata kwa karibu na kukazana kusonga mbele bila kusita. Mwisho wa dunia unajitokeza mbele yetu; maisha sahihi ya kanisa pamoja na watu, shughuli, na mambo ambayo yanatuzunguka yanaongeza mafunzo yetu. Kwa haraka chukua tena mioyo yetu ambayo inapenda dunia sana! Kwa haraka rudisha maono yetu yaliyovurugwa! Hatutasonga mbele zaidi tusije tukazidi mipaka na tutashikilia ndimi zetu ili tuweze kuishi kwa kufuata neno la Mungu, na tena hatutazozona juu ya faida zetu wenyewe na hasara. Acha upendo wako wa utajiri wa dunia ya kawaida! Jiweke huru kutoka kwa upendo wa mume wako na mabinti na wana wako! Acha maoni yako na upendeleo! Amka, kwa sababu muda ni mfupi! Iruhusu roho yako iangalie juu, angalia juu na umruhusu Mungu Achukue uongozi. Usijiruhusu kuwa kama mke wa Lutu. Kutelekezwa ni jambo la kusikitisha sana! Ni la kusikitisha kweli! Amka!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.

Jumanne, 13 Novemba 2018

Wimbo za Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation

Wimbo za Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation

Mpendwa Mwenyezi Mungu, ni Wewe ndiye Unayenipenda, uliniinua kutoka kwa rundo la kinyesi hadi kwa mazoezi ya ufalme. Maneno Yako yamenitakasa, yakanifanya nianze kuishi maisha ya furaha. Moyoni mwangu nahisi, kwa kweli, ni upendo Wako mkuu. Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu! Maneno Yako yote ni ukweli. Unastahili upendo wa binadamu. Ee Mungu! Ukipuuza uasi wangu wa zamani, Unanijali na kufanya kazi kuniokoa. Unaniongoza katika njia ya kweli, Ukitazama kila wakati katika upande wangu, natarajia tu nitakua na kuwa mtu mpya. Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu! Nitafuatilia kukupenda Wewe, mwaminifu kwa wajibu ili kukufurahisha Wewe.
Ee Mwenyezi Mungu, maneno Yako yamenitakasa. Neema Yako ya wokovu sitasahu kamwe. Nitakupenda Wewe maisha yangu yote, nikiuridhisha moyo Wako. Uliacha mengi sana ili kuniokoa, na sitakukosea Wewe kamwe. Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu! Nitakupenda Wewe maisha yangu yote, mwaminifu katika wajibu, katika wajibu. Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu! Nitakupenda Wewe maisha yangu yote, mwaminifu katika wajibu, katika wajibu.
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Jumatatu, 12 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini

Mungu aliwaumba wanadamu wote, na amewaongoza wanadamu wote mpaka leo. Hivyo, Mungu anajua yote yafanyikayo miongoni mwa wanadamu: Anajua uchungu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, Anaelewa utamu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, na kwa hiyo kila siku Yeye hufafanua hali za maisha za wanadamu wote, na, zaidi ya hayo, hushughulikia udhaifu na upotovu wa wanadamu wote. Si mapenzi ya Mungu kwamba wanadamu wote watupwe jahanamu, au kwamba wanadamu wote waokolewe. Kila mara huwa kuna kanuni kwa matendo ya Mungu, lakini hakuna anayeweza kuelewa sheria za yote Afanyayo. Watu wanapofahamu uadhama na ghadhabu ya Mungu, Mungu hubadilisha sauti mara moja kuwa ya huruma na upendo, lakini watu wanapokuja kujua huruma na upendo wa Mungu, Anaibadilisha sauti mara moja tena, Akiyafanya maneno Yake kuwa magumu kula kana kwamba ni kuku aliye hai. Katika maneno yote ya Mungu, mwanzo haujawahi kurudiwa kamwe, na maneno Yake yoyote hayajawahi kamwe kuzungumziwa kulingana na kanuni za matamko ya jana; hata sauti haifanani, wala hakuna uhusiano wowote katika maudhui—haya yote huwafanya watu wahisi wamekanganywa hata zaidi. Hii ni hekima ya Mungu, na ufichuzi wa tabia Yake. Yeye hutumia sauti na mtindo wa kunena Kwake kutawanya dhana za watu, ili kumtatiza Shetani, Akimnyang'anya Shetani nafasi ya kutia sumu matendo ya Mungu. Ajabu ya matendo ya Mungu husababisha akili za watu kuachwa zikiwa zimeshtushwa na maneno ya Mungu. Wanaweza kuupata mlango wao wa mbele kwa shida, au hata hawajui wakati wanaotarajiwa kula au kupumzika, hivyo wanatimiza kweli "kuacha kulala na kula ili kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu." Lakini hata wakati huu, Mungu bado haridhiki na hali za sasa, na kila mara huwa Amemkasirikia mwanadamu, Akimlazimisha kuonyesha moyo wake halisi. La sivyo, watu "wangetii" mara moja na kuwa wazembe, wakionyeshwa huruma kidogo tu na Mungu. Huu ni uduni wa mwanadamu; hawezi kubembelezwa, lakini lazima apigwe au alazimishwe ili asonge. "Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakiwafuata watu wengi, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kustawisha maisha yao." Hivyo ndivyo hali za wote walio duniani zilivyo. Hivyo, bila kazi ya mitume au viongozi, watu wote wangekuwa wametawanyika kitambo sana, na kwa hiyo, kotekote katika enzi, hakujakuwa na ukosefu wa mitume na manabii.
Katika matamko haya, Mungu anazingatia kwa hali maalum kufanya muhtasari wa hali za maisha za wanadamu wote. Maneno kama "Maisha ya mwanadamu hayana joto hata kidogo, na hayana ladha wala mwanga wowote wa binadamu—lakini hajawahi kujizoeza nayo, akivumilia maisha yasiyo ya thamani ambayo yeye huenda hapa na pale akiharakisha kufanya mambo bila kufikia kitu chochote. Kwa haraka sana, siku ya kufa inakaribia, na mtu anakufa kifo cha uchungu." yote ni ya aina hii. Ni kwa nini Mungu ameongoza kuishi kwa wanadamu mpaka leo, na bado pia Anafichua utupu wa maisha katika ulimwengu wa mwanadamu? Na kwa nini Anafafanua maisha yote ya watu wote kama "kufika kwa haraka na kuondoka kwa haraka"? Huu, inaweza kusemwa, wote ni mpango wa Mungu, wote umeamuliwa na Mungu, na kwa hivyo, kwa namna moja unaashiria jinsi Mungu anadharau yote isipokuwa maisha katika uungu. Ingawa Mungu aliwaumba wanadamu wote, Hajawahi kamwe kufurahishwa na maisha ya wanadamu wote, na kwa hiyo Yeye huwaruhusu tu wanadamu waishi chini ya upotovu wa Shetani. Baada ya wanadamu kupitia mchakato huu, Atawaangamiza au kuwaokoa wanadamu, na hivyo mwanadamu atatimiza maisha duniani ambayo si matupu. Yote haya ni sehemu ya mpango wa Mungu. Na kwa hiyo, huwa kila mara kuna matamanio ndani ya fahamu ya mwanadamu, jambo ambalo limesababisha kutokuwa na mtu anayekufa kifo maasumu kwa furaha—lakini wale ambao tu hutimiza matamanio haya ni watu wa siku za mwisho. Leo, bado watu huishi katikati ya utupu usiogeuka na bado wanangoja matamanio haya yasiyoonekana: "Ninapoufunika uso Wangu kwa mikono Yangu, na kuwasukuma watu chini ya ardhi, mara moja wao hupungukiwa na pumzi, na ni vigumu waweze kuishi. Wao wote hunililia, wakiwa wenye hofu kwamba Nitawaangamiza, kwa maana wote wanatamani kutazama siku ambayo Nitatukuzwa." Hivyo ndivyo hali za watu zilivyo leo. Wote huishi katika "ombwe," bila "oksijeni," ambalo huwafanya kuwa na ugumu kupumua. Mungu hutumia matamanio ndani ya fahamu ya mwanadamu ili kuwasaidia wanadamu wote kuendelea kuishi; la sivyo, wote "wangeondoka nyumbani ili kuwa watawa wa kiume," kwa sababu hiyo wanadamu wote wangetoweka, na wangemalizika. Hivyo, ni kwa sababu ya ahadi ambayo Mungu alimpa mwanadamu ndio mwanadamu ameendelea kuishi mpaka leo. Huu ni ukweli, lakini mwanadamu hajawahi kugundua sheria hii, na kwa hiyo hajui ni kwa nini yeye "anahofu sana kwamba kifo kitamjia mara ya pili." Kwa kuwa ni binadamu, hakuna yeyote ambaye ana ujasiri wa kuendelea kuishi, wala hakuna yeyote ambaye amewahi kuwa na ujasiri wa kufa, na hivyo Mungu asema kwamba watu "hufa kifo cha uchungu." Hivyo ndivyo hali halisi miongoni mwa wanadamu ilivyo. Labda, katika matarajio yao, watu wengine wamekumbana na vizuizi na wakawaza juu ya kifo, lakini mawazo haya hayajawahi kufaulu; labda, wengine wamewaza juu ya kifo kwa sababu ya ugomvi wa familia, lakini wanawajali wapendwa wao, na wanabaki kutoweza kutimiza matamanio yao; na labda, wengine wamewaza juu ya kifo kwa sababu ya mapigo kwa ndoa yao, lakini hawako radhi kupitia hilo. Hivyo, watu hufa wakiwa na majonzi au majuto ya milele ndani ya mioyo yao. Hivyo ndivyo hali mbalimbali za watu wote zilivyo. Nikitazama juu ya ulimwengu mpana wa mwanadamu, watu huja na kwenda katika mkondo usiokuwa na mwisho, na ingawa wanahisi kwamba wangekuwa na raha zaidi kama wangekufa kuliko kuishi huku wakiendelea kusema maneno matupu, kamwe hakuna yeyote ambaye amewahi kuonyesha mfano kwa kufa na kufufuka, akawaambia walio hai namna ya kufurahia furaha ya kifo. Watu ni mafidhuli duni: Hawana haya wala kujiheshimu, nao daima hukosa kutimiza ahadi zao. Katika mpango Wake, Mungu alijaalia kikundi cha watu ambao wangefurahia ahadi Zake, na hivyo Mungu asema, "wengi wameishi katika mwili, na wengi wamekufa na wamezaliwa upya duniani. Hata hivyo kamwe hakuna yeyote kati yao aliyepata nafasi ya kufurahia baraka za ufalme leo." Wote ambao wanafurahia baraka za ufalme leo wamejaaliwa na Mungu tangu Alipouumba ulimwengu. Mungu alipanga ili roho hizi ziishi ndani ya mwili katika siku za mwisho, na hatimaye, Mungu atalipata kundi hili la watu, na kuwapangia kuwa Sinim. Kwa sababu, hususa, roho za watu hawa ni malaika, Mungu asema "Je, Nimetoweka kabisa katika roho ya mwanadamu?" Kwa kweli, watu wanapoishi katika mwili, wanabaki kutojua mambo ya ulimwengu wa kiroho. Kutokana na maneno haya rahisi hali ya moyo wa Mungu inaweza kuonekana: Maneno rahisi ya "mwanadamu kunipiga macho ya hadhari" yanaonyesha saikolojia ya Mungu isiyoelezeka kwa urahisi. Tangu wakati wa uumbaji mpaka leo, ndani ya moyo wa Mungu daima kumekuwa na majonzi yanayoandamana na ghadhabu na hukumu, kwani watu walio duniani hawana uwezo wa kuyajali mapenzi ya Mungu, kama tu asemavyo Mungu, "Mwanadamu ni kama kiumbe katili cha mlimani." Lakini Mungu asema pia, "Siku itawadia ambapo mwanadamu ataogelea kuja upande Wangu kutoka katikati ya bahari kuu, ili aweze kufurahia mali yote ya dunia na kuacha hatari ya kumezwa na bahari." Huu ndio ufanikishaji wa mapenzi ya Mungu, na pia unaweza kuelezwa kama mwelekeo usioepukika, na unaashiria ufanikishaji wa kazi ya Mungu.
Ufalme utakaposhuka duniani kabisa, watu wote watapata tena mfano wao wa asili. Hivyo, Mungu asema, "Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida." Hili linaonyesha kwamba siku ambayo Mungu atapata utukufu kamili ndiyo siku ambayo mwanadamu atafurahia pumziko lake; watu hawakimbii huku na huko tena kutokana na usumbufu wa Shetani, dunia inaacha kuendelea mbele, na watu wanaishi katika pumziko—kwa kuwa idadi kubwa mno ya nyota angani zinafanywa upya, na jua, mwezi, na nyota, na kadhalika, na milima na mito yote iliyo mbinguni na duniani, vyote vinabadilishwa. Na kwa kuwa mwanadamu amebadilika, na Mungu amebadilika, kwa hiyo, pia, vitu vyote vinabadilika. Hili ndilo lengo la msingi la mpango wa usimamizi wa Mungu, na ule ambao utatimizwa hatimaye. Lengo la Mungu katika kuzungumza maneno haya yote ni hasa kwa mwanadamu kumjua Yeye. Watu hawaelewi amri za utawala za Mungu. Yote ambayo Mungu hufanya yametungwa na kupangwa na Mungu Mwenyewe, na Mungu hayuko radhi kumwacha mtu yeyote aingilie; badala yake, Yeye huwaruhusu watu kuona kwamba yote yamepangwa na Yeye na hayawezi kutimizwa na mwanadamu. Ingawa mwanadamu anaweza kuliona, au kuliona kuwa gumu kuwaza, yote yanadhibitiwa na Mungu pekee, na Mungu hatamani litiwe doa na wazo hata kidogo la mwanadamu. Mungu kwa kweli Hatawasamehe wowote wanaoshiriki, hata kwa kiasi kidogo; Mungu ni Mungu anayemwonea mwanadamu wivu, na inaonekana Roho wa Mungu hasa ni mwepesi wa kuhisi katika suala hili. Hivyo, yeyote aliye na nia hata kidogo ya kuingilia atazongwa mara moja na miale ya moto ya Mungu ya kuangamiza, ikimgeuza kuwa majivu ndani ya moto. Mungu hawaruhusu watu kuonyesha vipaji vyao jinsi wapendavyo, kwani wote walio na vipaji hawana uzima; hivi vipaji vya kudhaniwa humhudumia Mungu tu, na vinatokana na Shetani, na hivyo vinadharauliwa hasa na Mungu, Asiyeruhusu hili. Hata hivyo mara nyingi ni watu wasio na uhai ndio wanaweza kushiriki katika kazi ya Mungu, na, hata zaidi, kushiriki kwao huwa hakugunduliwi, kwani kunafichwa na vipaji vyao. Kotekote katika enzi, wale ambao wana vipawa hawajawahi kusimama imara, kwani hawana uzima, na hivyo wanakosa nguvu zozote za kupinga. Hivyo, Mungu asema, "Kama Sizungumzi waziwazi, mwanadamu kamwe hataacha kufanya upumbavu kamwe, na ataanguka katika kuadibu Kwangu bila kujua—kwa kuwa mwanadamu hanijui katika nafsi ya mwili Wangu." Wote ambao ni wa mwili na damu wanaongozwa na Mungu, lakini pia wanaishia katika kifungo cha Shetani, na kwa hiyo watu hawajawahi kuwa na uhusiano wa kawaida kati yao, kama ni kwa sababu ya tamaa, au kuabudu, au utaratibu wa mazingira yao. Mahusiano yasiyo ya kawaida kama hayo ndiyo Mungu anayachukua zaidi ya yote, na hivyo ni kwa sababu ya mahusiano kama hayo ndiyo maneno kama "Kile Ninachotaka ni viumbe vilivyo hai ambavyo vimejawa na uzima, si maiti ambazo zimegubika katika kifo. Kwa kuwa Ninaketi mezani pa ufalme, Nitatoa amri kwa watu wote duniani ili wapate ukaguzi Wangu" yanatoka kinywani mwa Mungu. Mungu anapokuwa juu ya ulimwengu mzima, kila siku Yeye huangalia kwa makini kila kitendo cha wale wa mwili na damu, na Hajawahi kumpuuza hata mmoja wao. Haya ni matendo ya Mungu. Na kwa hiyo, Nawasihi watu wote wachunguze fikira, mawazo, na matendo yao wenyewe. Siwataki muwe ishara ya aibu kwa Mungu, bali dhihirisho la utukufu wa Mungu, kwamba katika matendo, maneno, na maisha yenu yote, msiwe shabaha ya mizaha ya Shetani Haya ni matakwa ya Mungu kwa watu wote.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.

Jumapili, 11 Novemba 2018

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (1) : Kwa nini CCP Huwafuatia na Kuwakandamiza Wakristo Sana?

Swahili Christian Video "Mazungumzo" (1) : Kwa nini CCP Huwafuatia na Kuwakandamiza Wakristo Sana?

Katiba ya China hutamka kwa dhahiri uhuru wa dini, lakini kisirisiri, serikali hutumia rasilimali nyingi mno za binadamu na za kifedha kwa kuikandamiza imani ya dini na kuwatesa Wakristo kikatili. Hata hawajaacha kununua vifaa vya hali ya juu zaidi kuwafuatia, kuwafuma, na kuwakamata Wakristo. Serikali ya China imewanyang'anya raia wake haki ya uhuru wa imani na imewanyima kwa utundu haki ya kuishi. Kwa hiyo kwa kweli ni nini sababu na lengo la CCP kufanya yote haya?
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumamosi, 10 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Sita

Ni nani ameshinda nyumbani Kwangu? Ni nani amesimama kwa ajili Yangu? Ni nani ameteseka kwa ajili Yangu? Ni nani ameweka ahadi yake mbele Zangu? Ni nani amenifuata hadi leo lakini hajakuwa wa kutojali? Mbona wanadamu wote wana ubaridi na hawana hisia? Mbona binadamu ameniacha? Mbona mwanadamu amechoka na Mimi? Mbona hakuna joto katika ulimwengu wa mwanadamu? Nikiwa Zayuni, Nimeonja joto lililo mbinguni, na Nikiwa Zayuni Nimefurahia baraka iliyoko mbinguni. Tena, Nimeishi miongoni mwa binadamu, Nimeuhisi uchungu ulioko katika ulimwengu wa binadamu, Nimeona kwa macho Yangu hali zote tofauti zilizopo miongoni mwa wanadamu. Bila kujua, mwanadamu amebadilika pamoja na mabadiliko Yangu, na ni katika njia hii pekee ndio amepata kufika siku ya leo. Sihitaji kwamba mwanadamu aweze kufanya chochote kwa ajili Yangu, wala Sihitaji kwamba aongeze chochote kwa mujibu Wangu. Nataka tu aweze kukubaliana na mpango Wangu, bila kutonitii ama kuwa kigezo cha aibu Kwangu, na kuwa na ushuhuda unaovuma kwa sababu Yangu. Miongoni mwa wanadamu, kumekuwa na wale ambao Wamenitolea ushuhuda mzuri na kulipa jina Langu utukufu, lakini matendo ya mwanadamu, tabia ya mwanadamu vitawezaje kuutosheleza moyo Wangu? Atawezaje kufikia matakwa Yangu ama kutimiza mapenzi Yangu? Kwa milima yote na maji katika dunia, na maua, nyasi, na miti iliyo duniani, hapana hata moja isiyoonyesha kazi ya mikono Yangu, hakuna hata moja isiyokuwepo kwa ajili ya jina Langu. Ilhali mbona mwanadamu hawezi kufikia kiwango kile Ninachohitaji? Je, inaweza kuwa kwa sababu ya hali yake ya chini mno? Je, inaweza kuwa ni kwa sababu Yangu kumwinua? Je, inaweza kuwa ni kwa sababu Mimi ni mkatili kwake? Mbona kila wakati mwanadamu ana hofu kwa sababu ya mahitaji Yangu? Leo, miongoni mwa wengi katika ufalme, ni kwa nini mnasikia tu sauti Yangu lakini hamtaki kuuona uso Wangu? Mbona mnayaangalia tu maneno Yangu bila kujaribu kuyalinganisha na Roho Wangu? Mbona mnanitofautisha juu mbinguni na chini duniani? Je, yawezekana kwamba Mimi, Nikiwa duniani, Siko sawa na Mimi niliye mbinguni? Je, yawezekana kwambaMimi, Ninapokuwa mbinguni, Siwezi kushuka chini duniani? Je, yawezekana kwamba Mimi, Nikiwa duniani, Sistahili kuwa wa mbinguni? Ni kana kwamba Mimi, Ninapokuwa duniani, Mimi ni kiumbe duni, kana kwamba Mimi, Ninapokuwa mbinguni, Mimi ni kiumbe Aliyetukuzwa, na kama kwamba kuna shimo kubwa lisilopitika kati ya mbinguni na dunia. Lakini katika dunia ya wanadamu wanaonekana kutojua kitu chochote kuhusu asili ya vitu hivi, lakini wakati huo wote wamekuwa wakienda kinyume na Mimi, kana kwamba maneno Yangu yana sauti tu na hayana maana. Wanadamu wote wanaweka bidii kwa maneno Yangu, wakifanya uchunguzi wao kuhusu sura Yangu ya nje, lakini wote wanapata kushindwa, bila matokeo yoyote ya kuonyesha, badala yake, wanapigwa chini na maneno Yangu na hawawezi thubutu kusimama tena.
Nikiiweka imani ya binadamu katika majaribu, hakuna hata mwanadamu mmoja aliye na uwezo wa kuwa na ushuhuda wa kweli, hakuna hata mmoja anayeweza kujitoa kikamilifu; badala yake, mwanadamu anashinda akijificha na kukataa kujifungua na kuwa wazi, kana kwamba Ninaenda kuupora moyo wake. Hata Ayubu hakustahimili majaribu, wala hakufurahia katika mateso. Yote ambayo binadamu anaweza kufanya ni kutoa dokezo iliyofifia ya kijani kibichi katika joto la majira ya kuchipua; hajawahi kusalia kijani kibichi kila wakati chini ya mlipuko wa baridi wa majira ya baridi. Akiwa mkonde na gofu kwa kimo, mwanadamu hawezi kutimiza nia Zangu. Katika binadamu wote, hakuna hata mmoja anayeweza kutumika kuwa mfano kwa wengine, kwa sababu wanadamu ni sawa tu, bila tofauti kati yao, na kuna kidogo kinachowatofautisha mmoja na mwingine. Kwa sababu hii, hata leo wanadamu bado hawana uwezo wa kuijua kazi Yangu. Ni wakati ambao kuadibu Kwangu kutawashukia wanadamu ndipo wanadamu, bila kujua, wataifahamu kazi Yangu, na bila Mimi kufanya lolote ama kumlazimisha yeyote, wanadamu watakuja kunijua, na hivyo kupata kuiona kazi Yangu. Huu ni mpango Wangu, ni kipengele cha kazi Yangu ambayo ni wazi, na ni kile mwanadamu lazima afahamu. Katika ufalme, vitu vingi visivyohesabika vya uumbaji vinaanza kufufuka na kupata nguvu ya maisha yao. Kwa sababu ya mabadiliko katika hali ya dunia, mipaka kati ya nchi moja na nyingine pia inaanza kusonga. Hapo awali, Nimetabiri: Wakati ardhi itagawanywa kutoka kwa ardhi, na ardhi kujiunga na ardhi, huu ndio utakuwa wakati ambao Nitayapasua mataifa kuwa vipande vidogo. Katika wakati huu, Nitafanya upya uumbaji wote na kuugawa tena ulimwengu mzima, hivyo kuweka ulimwengu katika mpangilio, Nikibadilisha hali yake ya awali kuwa mpya. Huu ndio mpango Wangu. Hizi ni kazi Zangu. Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikipitisha wazi amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayeyakiuka:
Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa viwango tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.
Sauti Yangu inapoimarika kwa uzito, pia Ninaichunguza hali ya ulimwengu. Kupitia kwa maneno Yangu, vitu visivyohesabika vya uumbaji vyote vinafanywa upya. Mbingu inabadilika, na dunia pia inabadilika. Wanadamu wanafichuliwa katika hali yao halisi na, polepole, kila mmoja kulingana na aina yake, wanadamu bila kujua wanajipata wakirejea katika ngome za familia zao. Kwa sababu ya hili, Nitafurahishwa sana. Niko huru kutokana na vurugu, na kazi Yangu kuu inakamilika, bila kujua, vitu visivyohesabika vya uumbaji vinabadilishwa, bila kujua. Nilipoumba ulimwengu, Niliunda kila kitu kulingana na aina yake, Nikifanya kila kitu kilicho na umbo la kuonekana vikusanyike pamoja na aina zao. Wakati mpango wa usimamizi Wangu unapokaribia tamati, Nitarejesha hali ya awali ya uumbaji, Nitarejesha kila kitu kiwe katika hali ya awali, Nikibadilisha kila kitu kwa namna kubwa, ili kila kitu kirudi ndani ya mpango Wangu. Muda umewadia! Hatua ya mwisho katika mpango Wangu iko karibu kutimika. Ah, dunia ya kitambo yenye uchafu! Kwa hakika mtaanguka chini kwa maneno Yangu! Kwa hakika mtafanywa kuwa bure kwa mujibu wa mpango Wangu! Ah, vitu visivyo hesabika vya uumbaji! Wote mtapata maisha mapya katika maneno Yangu, sasa mko na Bwana Mkuu! Ah, dunia mpya, safi isiyo na uchafu! Kwa kweli mtafufuka katika utukufu Wangu! Ah Mlima Zayuni! Usiwe kimya tena. Nimerudi kwa ushindi! Kutoka miongoni mwa uumbaji, Ninaichunguza dunia nzima. Duniani, wanadamu wameanza maisha mapya, wameshinda tumaini mpya. Ah, watu Wangu! Mtakosaje kurudi kwa maisha ndani ya mwanga Wangu? Mtakosaje kuruka kwa furaha chini ya uongozi Wangu? Ardhi zinapiga kelele kwa furaha, maji yanapiga kelele na vicheko vya furaha! Ah, Israeli iliyofufuka! Mtakosaje kuhisi fahari kwa mujibu wa maajaliwa Yangu? Ni nani amelia? Ni nani ameomboleza? Israeli ya kitambo haiko tena, na Israeli ya leo imeamka, imara na kama mnara, katika dunia, imesimama katika mioyo ya binadamu wote. Israeli ya leo kwa hakika itapata chanzo cha uwepo kupitia kwa watu Wangu! Ah, Misri yenye chuki! Hakika, bado hamsimama dhidi Yangu? Mnawezaje kuichukulia huruma Yangu kimzaha na kujaribu kuepuka kuadibu Kwangu? Mtakosaje kuwa katika kuadibu Kwangu? Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, ghadhabu, na kuadibu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!
Machi 29, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Ijumaa, 9 Novemba 2018

2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Ulimwengu" (Swahili Subtitles)

2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Ulimwengu" (Swahili Subtitles)

Ulimwengu ni mkubwa sana na usio na kikomo, na una nyota nyingi mno zisizohesabika katika mzunguko sahihi…. Unatamani kujua aliyeziumba sayari za juu za ulimwengu, na yule ambaye huamuru tao la mtupo angani? Dondoo ya kustaajabisha ya filamu ya Kikristo ya Mungu Kuutawala Ulimwengu itakuonyesha nguvu yenye uwezo ya Muumba.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Alhamisi, 8 Novemba 2018

Muziki wa Injili "Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu" | God Is Salvation to Man

Muziki wa Injili "Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu" | God Is Salvation to Man

Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena. Wanajua ubaya wa Shetani, hivyo wanamkataa. Wanakuja mbele ya Mungu, wanakubali adabu na hukumu. Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu. Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani. Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena. Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu.
Katika usimamizi wa Mungu wa wakati huu, mwanadamu ni lengo la upotovu wa Shetani, yeye ni kasidi cha wokovu wa Mungu na kile ambacho Mungu na Shetani wanapigania. Wakati wa kazi ya Mungu, Anampata tena mwanadamu hatua kwa hatua kutoka Shetani. Kisha mwanadamu anakuwa karibu zaidi na Mungu … Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu. Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani. Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena. Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu. Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu. Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani. Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena. Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video

Jumatano, 7 Novemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo; lazima mle na mnywe maneno Yangu zaidi na, muhimu zaidi, lazima mweze kuyala na kuyanywa nyinyi wenyewe. Jiandaeni wenyewe na ukweli wote, njooni mbele Yangu ili nifungue macho yenu ya kiroho na kuwaruhusu kuona siri zote zilizo rohoni.... Wakati kanisa linaingia awamu yake ya ujenzi, vita vya watakatifu dhidi ya Shetani[a] vinaanza. Vipengele mbalimbali vya Shetani vya kutisha Vinawekwa mbele yenu; je, mnaacha na kurudi nyuma au mnainuka na kuendelea mkinitegemea Mimi? Weka hadharani vipengele vya Shetani vyenye upotovu na viovu, bila hisia wala huruma! Pambana na Shetani hadi kifo! Mimi ni msaada wenu na ni lazima muwe na roho ya mwana wa kiume! Shetani yuko katika hekaheka zake za kifo cha mwisho lakini bado hataweza kuhepa hukumu Yangu. Shetani yuko chini ya miguu Yangu na pia anakanyagwa chini ya miguu yenu—ni ukweli!
Wale wapinga dini wote na wale ambao hubomoa ujenzi wa kanisa hawafai kuvumiliwa hata kidogo na nitawahukumu mara moja. Weka Shetani hadharani, mkanyagie chini ya miguu, muangamize kabisa na usimuachie pa kujificha. Kila aina ya mapepo na vizuka hakika wataonyesha maumbile yao ya kweli mbele Yangu na Nitawatupa wote kuzimu ambamo hawatawahi kuwa huru; wote wako chini ya miguu yetu. Kama unataka kupigana vita vizuri kwa ajili ya ukweli, basi kwanza kabisa, usimpe Shetani nafasi ya kufanya kazi, na ili kufanya hivi mtastahili kuwa na nia moja na muweze kutumika katika kushirikiana, acheni dhana zenu za kibinafsi, maoni, mitazamo na njia za kufanya mambo, tuliza moyo wako ndani Yangu, zingatia sauti ya Roho Mtakatifu, kuwa makini na kazi ya Roho Mtakatifu na uwe na uzoefu wa maneno ya Mungu kwa kina. Lazima uwe na nia moja tu, ambayo ni kwamba mapenzi Yangu yaweze kutendeka. Hupaswi kuwa na nia nyingine. Lazima uangalie Kwangu kwa moyo wako wote, angalia hatua Zangu na Ninavyotenda mambo kwa karibu, na wala usiwe mzembe kabisa. Roho yako lazima iwe amilifu, macho yako yakiwa wazi. Kwa kawaida, wale ambao nia na malengo yao si sahihi, wale ambao wanapenda kuonekana na wengine, wenye hamu ya kutenda mambo, wenye tabia ya kukatiza, walio imara katika mafundisho ya dini, watumishi wa Shetani, nk., watu hawa wanapoinuka wanakuwa ugumu kwa kanisa na kula na kunywa kwa ndugu kunakuwa si kitu; unapompata mtu wa aina hii jifanye kisha mpige marufuku mara moja. Kama muda baada ya muda hawabadiliki basi watateseka sana. Kama wale wanaoendelea katika njia zao kwa ukaidi wanajitetea na kujaribu kufunika dhambi zao, kanisa linapaswa kuwaondoa mara moja na kutowaachia nafasi ya kuendelea. Usipoteze mengi kwa kujaribu kuokoa machache, na uzingatie makubwa.
Macho yako ya kiroho lazima sasa yafunguke, na kutofautisha aina kadhaa za watu kanisani:
Je, ni mtu wa ina gani anaelewa masuala ya kiroho na anajua roho?
Je, ni mtu wa ina gani haelewi masuala ya kiroho?
Je, ni mtu wa ina gani ana roho waovu ndani yake?
Je, ni mtu wa ina gani ana Shetani anafanya kazi juu yake?
Je, ni mtu wa ina gani ambaye ana tabia ya kukatiza?
Je, ni mtu wa ina gani ambaye Roho Mtakatifu anatenda kazi kwake?
Je, ni mtu wa ina gani huonyesha kuzingatia kuelekea mzigo wa Mungu?
Je, ni mtu wa ina gani anaweza kutenda mapenzi Yangu?
Je, ni nani shahidi Wangu mwaminifu?
Jua ya kwamba nuru ambayo Roho mtakatifu hupatia makanisa yote ni maono ya leo ya juu zaidi. Msichanganyikiwe kuhusu mambo haya, lakini badala yake lazima mchukuwe muda wa kuyafikiria kabisa—hii ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya maisha yenu! Kama huelewi mambo haya yaliyo machoni pako basi hutakuwa na uwezo wa kusonga mbele, utakuwa katika hatari ya majaribu na ufungwa wakati wowote, na huenda ukavamiwa. Jambo kuu sasa ni kuzingatia kuweza kuwa karibu na Mimi moyoni mwako, kufanya ushirika zaidi na Mimi, na chochote unachokosa au kutafuta utafidiwa kupitia kuwa karibu na Mimi na kufanya ushirika na Mimi. Maisha yako hakika yatashughulikiwa na utakuwa na nuru mpya. Mimi kamwe siangalii jinsi mlikuwa wajinga awali na siyakumbuki makosa yenu. Mimi huangalia jinsi mnavyonipenda: Je, mnaweza kunipenda zaidi ya mambo mengine yote? Naangalia kuona iwapo mnaweza kugeuka nyuma na kunitegemea kuondoa ujinga wenu au la. Baadhi ya watu husimama Kwangu, kunipinga hadharani, na kuhukumu watu wengine; hawajui maneno Yangu, na hata uwezekano wao wa kuona uso Wangu uko chini. Wote wale walio mbele Yangu ambao hunifuata kwa dhati, ambao wana mioyo yenye njaa na kiu cha haki, Nitawapa nuru, kuwafichulia, kuwaruhusu kuniona kwa macho yenu na kugusa mapenzi Yangu wenyewe; hakika moyo Wangu utafichuliwa kwenu, ili mpate kuelewa. Lazima muweze kutenda yale ambayo naangaza ndani yenu kulingana na maneno Yangu, vinginevyo mtahukumiwa. Fuata mapenzi Yangu na hamtapotea
Kwa wote wale wanaotafuta kuingia ndani ya maneno Yangu, neema na baraka vitaongezeka mara mbili juu yenu, mtapata nuru mpya kila siku, ufahamu mpya kila siku na kujisikia mpya katika kula na kunywa maneno Yangu kila siku; utayaonja kwa kinywa chako mwenyewe: Ni tamu jinsi gani! … Lazima uwe makini, na usitosheke unapokuwa na ufahamu kiasi na ladha kiasi ya utamu—cha msingi ni kuendelea kutafuta mbele! Baadhi ya watu hufikiria ya kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kweli ajabu na halisi—huyu kweli ni mtu wa Mwenyezi Mungu anafichuliwa wazi, na ishara na maajabu kubwa zaidi viko mbele. Kuwa makini na macho wakati wote, angalia kabisa kwenye chanzo, kuwa mtulivu mbele Yangu, zingatia na usikilize kwa makini, na kuwa na uhakika kuhusu maneno Yangu. Haiwezekani kuwa na utata; kama una shaka hata kidogo basi Nina hofu kuwa utapotea zaidi ya malango. Kuwa na maono wazi, simama kwenye sakafu ngumu, fuata mkondo huu wa maisha na uufuate popote ufikapo; usisite hata kidogo kabisa. Kula, kunywa na kutoa sifa tu, tafuta kwa moyo mtakatifu na usikate tamaa. Leta chochote usichokielewa mbele Yangu zaidi na hakikisha usiwe na moyo wa mashaka ili uepuke kupata hasara kubwa. Endelea! Endelea! Kaa karibu! Jikwamue kutoka kwa vizuizi na usijichafue. Endelea kwa moyo wote na usirudi nyuma. Lazima utoe moyo wako wakati wote na kamwe usiwahi kuupoteze muda wowote. Roho Mtakatifu daima ana kazi mpya ya kutenda, hutenda mambo mapya na ana nuru mpya kila siku; “kugeuka sura mlimani”—mwili mtakatifu wa kiroho wa Mungu umeonekana! Jua lenye haki hutoa nuru na huangaza, mataifa yote na watu wote wameona uso Wako mtakatifu. Nuru Yangu itaangaza juu ya wale wote wanaokuja mbele Yangu. Maneno yangu ni nuru, yakiwaongoza mbele. Hamtageuka kushoto au kulia mnapotembea lakini mtatembea ndani ya nuru Yangu, na kukimbia kwenu hakutakuwa kazi isiyo na matunda. Lazima muone kazi ya Roho Mtakatifu kwa uwazi na mapenzi Yangu yako pale ndani yake. Siri zote zimefichwa na zitafunuliwa kwenu hatua kwa hatua. Wekeni maneno Yangu akilini wakati wote na mje mbele Yangu kufanya ushirika zaidi na Mimi. Kazi ya Roho Mtakatifu huendelea. Tembeeni katika nyayo Zangu; maajabu makuu yako mbele na yatafunuliwa kwenu moja baada ya lingine. Ni wale tu ambao wanajali, wanaosubiri na ambao wako macho watayaona. Hakikisha usiwe mlegevu. Mpango wa usimamizi wa Mungu unakaribia hatua yake ya mwisho, ujenzi wa kanisa utafanikiwa, idadi ya washindi tayari imewekwa, mwana wa kiume mshindi atafanyika na wataingia katika ufalme na Mimi, kuchukua ufalme Nami, kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kuwa katika utukufu pamoja!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 6 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utangulizi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utangulizi

Mnamo Februari 11, mwaka wa 1991, Mungu alitoa tamko Lake la kwanza katika kanisa ambalo lilikuwa na athari isiyo ya kawaida kwa kila mmoja wa watu walioishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu wakati huo. Tamko hili lilitaja yafuatayo: “Makazi ya Mungu yameonekana” na “Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—Yeye ni Jua linalong’aa.” Kwa maneno haya ya maana sana, watu hawa wote waliletwa katika ulimwengu mpya. Wale wote waliosoma tamko hili walihisi maelezo ya kazi mpya, kazi kuu ambayo Mungu alikuwa karibu kuanzisha. Lilikuwa ni tamko hili zuri, laini, na lenye habari nyingi katika maelezo machache lililoleta binadamu wote katika kazi mpya ya Mungu na katika enzi mpya, na ambalo liliweka msingi na kuanzisha kazi ya Mungu katika kupata mwili huku. Mtu anaweza kusema kwamba tamko ambalo Mungu alitoa wakati huu ni lile ambalo linaunganisha enzi; kwamba ni wakati wa kwanza tangu mwanzo wa Enzi ya Neema ambapo Mungu amezungumza wazi kwa jamii ya binadamu; zaidi, kwamba ni wakati wa kwanza Amezungumza baada ya kujificha kwa miaka elfu mbili; na, zaidi ya hayo, kwamba ni utangulizi, sehemu muhimu ya kuanzia, kwa kazi ambayo Mungu yuko karibu kufanya katika Enzi ya Ufalme.
Wakati wa kwanza Mungu alitoa tamko, Alifanya hivyo kwa jinsi ya sifa kutoka kwa mtazamo wa nafsi ya tatu, kwa lugha ambayo wakati mmoja ilikuwa ya sanaa na ya ustaarabu na wazi na ya nyumbani, na vile vile ruzuku ya maisha ambayo ingeeleweka kwa urahisi na bila shida. Akiwa na hili, Alichukua kundi hili dogo la watu, waliojua tu jinsi ya kufurahia neema Yake wakingoja kurudi kwa Bwana Yesu kwa hamu, na kuwaleta kwa kimya katika hatua nyingine ya kazi katika mpango wa Mungu wa usimamizi. Katika hali hizi, binadamu hawakujua, sembuse kuthubutu kufikiri, ni aina gani ya kazi Mungu angefanya hatimaye, ama kilichokuwa njiani mbele. Baadaye, Mungu aliendelea kutoa matamko zaidi kuwaleta binadamu katika enzi mpya hatua kwa hatua. La kushangaza, kila tamko la Mungu ni tofauti katika maudhui na aidha hutumia aina tofauti za sifa na njia za maonyesho. Matamko haya, yaliyo sawa kwa sauti lakini ya namna mbalimbali katika maudhui, yamejazwa kila wakati na hisia za Mungu za utunzaji na kujali, na karibu kila moja lina ruzuku za maisha na maudhui tofauti na vile vile maneno ya kukumbusha, kushawishi, na kufariji kutoka kwa Mungu hadi kwa mwanadamu. Katika matamko haya, mafungu kama hili yanaonekana mara kwa mara: “Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote”; “Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu”; “Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake”; na mengineo. Ujumbe unapitishwa katika mafungu haya, ama mtu anaweza kusema kwamba mafungu haya yanapitisha ujumbe kwa jamii ya binadamu: Mungu tayari amekuja katika dunia ya binadamu, Mungu ataanzisha kazi kubwa hata zaidi, ufalme wa Mungu tayari umeshuka katika kundi fulani la watu, na Mungu tayari amepata utukufu na kushinda maadui Wake wengi. Kila tamko la Mungu linaushika moyo wa kila binadamu. Wanadamu wote wanamsubiri Mungu ayape sauti hata maneno mengi zaidi, kwa sababu kila wakati Mungu huzungumza, Anatikisa moyo wa binadamu hadi kwa kina chake, na zaidi Anaongoza na kuweka sawa kila mwendo na kila hisia ya mwanadamu, ili kwamba binadamu waanze kuyategemea na hata zaidi kuyaheshimu maneno ya Mungu…. Kwa njia hii, pasipo kujua, watu wengi sana walikuwa wameisahau Biblia kimsingi, na kuyasikiliza shingo upande mahubiri ya kale na maandishi ya watu wa kiroho, kwa sababu hawakuweza kupata katika maandishi ya zamani msingi wowote wa maneno haya ya Mungu, wala hawakuweza kugundua mahali popote makusudi ya Mungu katika kutoa matamko haya. Kwa sababu hiyo, ilimpasa kwa kiasi gani binadamu kukiri kwamba matamko haya ni sauti ya Mungu ambayo hayajaonwa wala kusikika tangu mwanzo wa wakati, kwamba yako mbali ya uwezo wa mtu yeyote anayemwamini Mungu, na kwamba yanapita matamko yote yaliyotolewa na mtu yeyote wa roho anayeishi katika enzi za zamani au na Mungu zamani. Wakihimizwa na kila moja ya matamko haya, binadamu waliingia bila kujua katika hali ya kuashiria wema wa kazi ya Roho Mtakatifu, kuingia katika maisha kwa safu ya mbele ya enzi mpya. Wakihimizwa na maneno ya Mungu, binadamu, wakiwa wamejawa na matarajio, walionja utamu wa kuongozwa binafsi na maneno ya Mungu. Naamini muda huu mfupi kuwa wakati ambapo kila binadamu ataangalia nyuma kwa kumbukumbu ya kuvumilia, wakati ambapo kwa kweli kile ambacho binadamu walifurahia wakati huu hakikuwa zaidi ya hali ya kuashiria wema wa kazi ya Roho Mtakatifu, au mtu anaweza kukiita ladha tamu ya kudanganya. Hii ni kwa sababu, kutoka hatua hii kuendelea, bado chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, bado katika hali ya kuashiria wema wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, binadamu waliongozwa katika awamu nyingine ya maneno ya Mungu pasipo kujua, ambayo ilikuwa hatua ya kwanza iliyohemshwa na tamko la Mungu katika Enzi ya Ufalme—jaribio la watendaji huduma.
Maneno yaliyotamkwa kabla ya jaribio la watendaji huduma yalikuwa hasa kwa jinsi ya maagizo, ushawishi, lawama, na kufundisha nidhamu, na katika sehemu nyingine yalitumia jinsi nzee ya utambulisho iliyotumiwa katika Enzi ya Neema—kutumia “Wanangu” kwa wale waliomfuata Mungu ili kufanya iwe rahisi kwa binadamu kumkaribia Mungu, au ili binadamu waweze kuchukulia uhusiano wao na Mungu kuwa wa karibu. Kwa njia hii, bila kujali hukumu ambayo Mungu alitoa kwa kujiona, majivuno na tabia nyingine potovu za binadamu, mwanadamu angeweza kushughulikia na kulikubali katika utambulisho wake wa “mwana,” bila kuwa na uhasama kwa matamko ya “Mungu Baba,” ambayo kwa kuongezea ahadi ambayo “Mungu Baba” alitoa kwa “wana” Wake haikuwa ya shaka kamwe. Katika kipindi hiki, binadamu wote walifurahia uwepo ulio huru kutokana na taabu kama wa mtoto mchanga, na hili lilitimiza makusudi ya Mungu, ambayo ni, walipoingia katika utu uzima, Angeanza kutekeleza hukumu kwao. Hili pia liliweka msingi wa kazi ya kuhukumu jamii ya binadamu ambayo Mungu anaanzisha rasmi katika Enzi ya Ufalme. Kwa sababu kazi ya Mungu katika kupata mwili huku hasa ni kuhukumu na kushinda jamii nzima ya binadamu, punde tu mwanadamu alipoweka miguu yake chini kwa uthabiti, Mungu aliingia katika mtindo wa kazi Yake mara moja—katika kazi ambamo kwayo Anamhukumu mwanadamu na kumwadibu. Kwa uwazi, matamko yote kabla ya jaribio la watendaji huduma yalitolewa kwa ajili ya kupitia mageuzi, lengo la kweli likiwa tofauti na lile lilioonekana kuwa. Nia ya hamu ya Mungu ilikuwa kwamba Aweze kuzindua rasmi kazi Yake katika Enzi ya Ufalme punde iwezekanavyo. Hakutaka kwa vyovyote vile kuendelea kumbembeleza binadamu mbele kwa kumpa maneno madogo madanganyifu; badala yake, Alikuwa na hamu kuona uso wa kweli wa kila mwanadamu kabla ya kiti Chake cha hukumu, na hata kwa hamu zaidi Alitaka kuona mtazamo wa kweli ambao binadamu wote wangekuwa nao kuelekea Kwake baada ya kupoteza neema Yake. Alitaka tu kuona matokeo, sio mchakato. Lakini wakati huo hakukuwa na mtu aliyeelewa nia ya Mungu yenye hamu, kwa sababu moyo wa binadamu ulishughulika tu na hatima yake na matarajio yake ya baadaye. Sio ajabu kwamba hukumu ya Mungu ilikuwa imeelekezwa, mara kwa mara, kwa jamii nzima ya binadamu. Ilikuwa tu wakati binadamu, chini ya mwongozo wa Mungu, walianza kuishi maisha ya kawaida ya binadamu ambapo mtazamo wa Mungu kwa binadamu ulibadilika.
Mwaka wa 1991 haukuwa wa kawaida: hebu tuuite mwaka huu “mwaka wa ustawi.” Mungu alianzisha kazi mpya ya Enzi ya Ufalme na kuelekeza matamko Yake kwa jamii yote ya binadamu. Wakati huo huo, binadamu walifurahia wema wa pekee na, hata zaidi, kupitia uchungu unaofuata hukumu ya Mungu ya pekee kwa mwanadamu. Jamii ya binadamu ilionja utamu usiojulikana mpaka sasa na kuhisi pia hukumu na hali ya kutupwa isiyojulikana mpaka sasa kana kwamba ilikuwa imempata Mungu na tena kana kwamba ilikuwa imempoteza Mungu. Kuteseka katika umiliki na kuteseka katika ufukara—hisia hizi zinajulikana tu na wale wanaozipitia wao wenyewe; ni kitu ambacho mwanadamu hana uwezo wala njia ya kueleza. Majeraha ya aina hii ni yale Mungu alimpa kila mtu kama aina ya uzoefu usioshikika na mali. Maudhui ya matamko yaliyotolewa na Mungu katika mwaka huu kweli yamo katika sehemu mbili kuu: Ya kwanza ni sehemu ambapo Mungu alishuka katika dunia ya wanadamu kuwaalika binadamu kuja mbele ya kiti Chake cha enzi kama wageni; ya pili, sehemu ambapo binadamu, baada ya kula na kunywa hadi kushiba, walitumiwa na Mungu kama watendaji huduma. Bila shaka ni dhahiri kwamba sehemu ya kwanza ni matakwa ya binadamu ya thamani nyingi na ari zaidi, hasa kwa kuwa wanadamu wamezoea tangu zamani kufanya kufurahia kila kitu cha Mungu kuwa lengo la imani yao Kwake. Hii ndiyo maana, punde Mungu alipoanza kuyapa matamko Yake sauti, binadamu wote walikuwa tayari kuingia katika ufalme na walisubiri hapo ili Mungu awape thawabu tofauti. Watu katika hali hizi hawakulipa gharama ya kufaa kabisa kwa kubadilisha tabia zao, kutafuta kumridhisha Mungu, kufikiria mapenzi ya Mungu na kadhalika. Kwa mtazamo wa haraka wa juu juu, wanadamu walionekana kushughulika huku na kule siku zote huku wakijitumia na kufanya kazi kwa ajili ya Mungu, wakati kwa kweli walikuwa wakifanya hesabu, katika mahala pa siri zaidi pa vina vya mioyo yao, hatua ifuatayo wanayopaswa kuchukua kupata baraka au kutawala kama wafalme. Mtu anaweza kusema kwamba, wakati moyo wa mwanadamu ulipokuwa ukimfurahia Mungu, ulikuwa ukifanya hila dhidi ya Mungu wakati huo huo. Wanadamu katika hali hii hukutana na chuki ya kina zaidi ya Mungu na karaha; tabia ya Mungu haivumilii binadamu yeyote kumdanganya au kumtumia. Lakini hekima ya Mungu haifikiki kwa mwanadamu yeyote. Ilikuwa katikati ya kuvumilia mateso haya yote ambapo Alisema sehemu ya kwanza ya matamko Yake. Kiasi cha mateso ambayo Mungu alivumilia, na ni kiasi gani cha kujali na fikira Alitumia wakati huu, hakuna mwanadamu anayeweza kuwaza. Lengo la sehemu ya kwanza ya haya matamko ni kufichua aina tofauti za ubaya ambazo mwanadamu huonyesha anapokabiliwa na cheo na faida, na kufichua ulafi na kustahili dharau kwa mwanadamu. Hata ingawa, katika kuzungumza, Mungu huyafuma maneno Yake kwa sauti ya kweli na ya moyo ya mama anayependa, ghadhabu katika kina zaidi ya moyo Wake huwaka kama jua la mchana ambalo Anaelekeza dhidi ya adui Zake. Mungu hataki katika hali yoyote kuzungumza kwa kundi la watu wasio na usawa wa kawaida wa jamii ya binadamu, na hivyo, wakati wowote Anapozungumza, Anazuia ghadhabu iliyo ndani ya moyo Wake ilhali wakati huo huo Akijizuia ili kuonyesha tamko Lake. Zaidi ya hayo Anazungumza kwa jamii ya binadamu isiyo na ubinadamu wa kawaida, isiyo na mantiki, potovu kabisa, na ulafi kugeuka kuwa asili ya pili, na isiyotii na inayomwasi Mungu hadi mwisho kabisa. Vina ambavyo jamii ya mwanadamu imeanguka vinaweza kufikiriwa kwa urahisi, na hata zaidi chuki na karaha ya Mungu kwa jamii ya mwanadamu inaweza kufikiriwa kwa urahisi, lakini jamii ya binadamu ina ugumu kufikiri kwamba maumivu waliyompa Mungu hayawezi kuelezwa na maneno. Lakini ilikuwa hasa katika usuli huu—ambapo hakuna mtu aliweza kugundua jinsi moyo wa Mungu unavyoteseka, na aidha hakuna mtu aliyegundua jinsi jamii ya binadamu isivyo ya akili na isiyorekebishika—kwamba kila mtu, bila aibu yoyote au haya hata kidogo, aliona kuwa jambo la kawaida kwamba alikuwa na haki kama wana wa Mungu kupokea thawabu zote ambazo Alikuwa amemtayarishia mwanadamu, hata kwa kiwango cha kugombana, kusiwe na mtu aliyetaka kubaki nyuma na wote wakiogopa sana kupoteza. Kufikia sasa unapaswa kujua ni nafasi ya aina gani ambayo watu wakati huo walimiliki machoni pa Mungu. Jamii ya wanadamu kama hii inawezaje kupata thawabu za Mungu? Lakini kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa Mungu ni hazina ya thamani sana nyakati zote, na kinyume chake kile ambacho Mungu hupokea kutoka kwa mwanadamu ni uchungu mkubwa kabisa. Tangu mwanzoni mwa uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, hiki ndicho mwanadamu amepokea daima kutoka kwa Mungu na kile ambacho amempa Mungu daima kama malipo.
Hata ingawa Mungu alijaa wasiwasi, Alipoona jamii hii ya binadamu, iliyo potovu kwa kina sana, Hakuwa na chaguo ila kuitupa ndani ya jahanamu ili iweze kusafishwa. Hii ni sehemu ya pili ya tamko la Mungu, ambapo Mungu aliwatumia binadamu kama watendaji huduma Wake. Katika sehemu hii, Mungu alitoka kuwa mpole hadi kuwa mkali, na kutoka machache hadi mengi, kuhusu mbinu na urefu, akitumia nafasi ya “nafsi ya Mungu” kama ubembe kufichua asili potovu ya mwanadamu ilhali wakati huo huo kuweka mbele vikundi tofauti vya[a] watendaji huduma, watu, na wana kwa watu kuchagua kutoka hapo. Bila shaka, kama vile Mungu alivyokuwa ametabiri, hakuna mtu aliyechagua kuwa mtendaji huduma kwa ajili ya Mungu, na badala yake wote walijitahidi kuwa nafsi ya Mungu. Hata ingawa, katika kipindi hiki, ukali ambao kwao Mungu alizungumza kilikuwa kitu ambacho binadamu hawakuwahi kutarajia na sembuse kusikia, hata hivyo, kujali sana kuhusu hadhi, na juu ya hili, kushughulika kwa msisimko mkubwa na kupata baraka, hawakuwa na wakati wa kuunda fikira kuhusu sauti ya Mungu ya kuzungumza na njia Yake ya kuzungumza, badala yake wakinuia kutenda bila hadhari hadhi zao na kile kilichowangoja baadaye. Kwa njia hii, binadamu waliletwa, bila kujua, na tamko la Mungu ndani ya matata mengi Aliyokuwa amewawekea. Wakiwa wameshawishiwa, bila hiari, na mvuto wa siku za mbele na kudura yao, binadamu walijijua hawafai kuwa nafsi ya Mungu, na bado walikuwa wakisita kutenda kama watendaji huduma Wake. Wakiwa wamechanganyikiwa kati ya fikira hizi zinazopingana, bila kujijua walikubali hukumu ya pekee na kuadibu ambako Mungu alikuwa amewapa binadamu. Kwa kawaida, aina hii ya hukumu na usafishaji kilikuwa kitu ambacho binadamu hawakuwa tayari kukubali hata kidogo. Hata hivyo, Mungu tu ndiye aliye na hekima, na ni Yeye tu aliye na uwezo, kutoza unyenyekevu mpole kutoka kwa jamii hii potovu ya wanadamu, ili kwamba, watake au wasitake, wote walikubali mwishowe. Binadamu hawakuwa na mbadala kuchagua kutoka. Ni Mungu tu aliye na uamuzi wa mwisho, na ni Mungu tu anaweza kutumia mbinu kama hii kumpa mwanadamu ukweli na uhai na kumwonyesha mwelekeo. Mbinu hii ni kutoepukika kwa kazi ya Mungu kwa mwanadamu, na pia, bila shaka au ugomvi, ni haja ya lazima ya mwanadamu. Mungu hutumia mbinu kama hii kwa ajili ya kunena na kufanya kazi kupitisha ukweli huu kwa binadamu: Katika kumwokoa binadamu, Mungu hufanya hivyo kutokana na upendo na huruma Yake na kwa ajili ya usimamizi Wake; katika kupokea wokovu wa Mungu, jamii ya binadamu inafanya hivyo kwa sababu imeanguka hadi kwa hatua ambapo Mungu huzungumza Yeye binafsi tu. Mwanadamu anapopokea wokovu wa Mungu, hii ndiyo neema ya juu zaidi, na pia ni fadhila ya pekee, yaani, isingekuwa Mungu kulipa tamko Lake sauti Yeye binafsi, majaliwa ya jamii ya binadamu ingekuwa kutoweka. Wakati huo huo ambapo Anakirihi jamii ya binadamu, Mungu bado yuko tayari na mwenye radhi kulipa gharama yoyote kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Wakati huo, mwanadamu huzungumza kwa kurudiarudia juu ya upendo wake kwa Mungu na jinsi anavyoweka yote wakfu kwa Mungu, anaasi dhidi ya Mungu na kupokonya kila aina ya neema kutoka kwa Mungu, na hata, wakati huo huo, akimwumiza Mungu na kuumiza moyo Wake kwa uchungu mbaya. Hivyo ndivyo ilivyo tofauti dhahiri kati ya asiye na ubinafsi na aliye na ubinafsi katika uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu!
Katika kufanya kazi na kuzungumza, Mungu halazimiki kufuata mbinu yoyote maalum, ila hufanya kufikia matokeo katika upande Wake. Kwa sababu hii, katika “maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa,” Amehakikisha kutoonyesha utambulisho Wake kwa dhahiri, ila tu kufichua maneno machache kama “Kristo wa siku za mwisho,” “Mkuu wa ulimwengu,” na mengineyo. Hili haliathiri hata kidogo huduma ya Kristo au ufahamu wa binadamu wa Mungu, hasa kwa kuwa binadamu katika siku hizo za awali walikuwa wajinga kabisa kuhusu dhana ya “Kristo” na “kupata mwili,” kiasi kwamba Mungu alilazimika kujinyenyekeza Mwenyewe kuwa mtu na “kazi maalum” kuonyesha tamko Lake. Huu ni mfano wa nia ya juhudi ya Mungu, kwa sababu watu wakati huo wangeweza tu kukubali aina hii ya utambulisho. Bila kujali aina ya utambulisho ambao Mungu hutumia, matokeo ya kazi Yake hayaathiriwi, kwa sababu katika yote Anayofanya Mungu hunuia kumwezesha mwanadamu kubadilika, kumwezesha mwanadamu kupata wokovu wa Mungu. Bila kujali Anachokifanya, Mungu daima hufikiria mahitaji ya mwanadamu. Hii ndiyo nia ya Mungu kufanya kazi na kuzungumza. Hata ingawa Mungu yuko mwangalifu kikamilifu katika kufikiria vipengele vyote vya binadamu, na ni mwenye busara kikamilifu katika yote Anayofanya, Naweza kusema hili: Kama Mungu hangejishuhudia Yeye Mwenyewe, hakungekuwa na mmoja miongoni mwa jamii ya binadamu walioumbwa ambaye anayeweza kumtambua Mungu Mwenyewe au kusimama kumshuhudia Mungu Mwenyewe. Kama Mungu angeendelea kutumia “mtu na kazi maalum” kama aina ya utambulisho katika kazi Yake, hakungekuwa na binadamu hata mmoja ambaye angemchukulia Mungu kama Mungu—huu ni huzuni wa binadamu. Yaani, miongoni mwa jamii ya binadamu walioumbwa hakuna mtu anayeweza kumjua Mungu, hakuna wa kumpenda Mungu, kumjali Mungu na kumkaribia Mungu. Imani ya mwanadamu ni kwa ajili ya kupata baraka pekee. Utambulisho wa Mungu kama mtu aliye na kazi maalum imetoa dokezo kwa kila binadamu: Binadamu anaona ikiwa rahisi kumchukulia Mungu kama mmoja miongoni mwa jamii ya wanadamu walioumbwa; uchungu na fedheha ya juu kabisa ambayo binadamu anamwumiza nayo Mungu ni hiyo hasa, Anapoonekana na kufanya kazi kwa wazi, Mungu bado anakataliwa na mwanadamu na hata kusahaulika na yeye. Mungu huvumilia fedheha ya juu zaidi ili kuiokoa jamii ya binadamu; katika kutoa kila kitu, lengo Lake ni kumwokoa binadamu, kupata utambuzi wa binadamu. Gharama ambayo Mungu amelipa kwa ajili ya haya yote ni kitu ambacho kila mtu aliye na dhamiri anapaswa kuweza kuthamini. Jamii ya binadamu imepata kuzungumza na kufanya kazi kwa Mungu, na kupata wokovu wa Mungu. Wakati uo huo, hakuna mtu ambaye amefikiria kuuliza hili: Na ni nini ambacho Mungu amepata kutoka kwa binadamu? Kutoka katika kila tamko la Mungu, binadamu wamepata ukweli, wamefanikiwa kubadilika, wamepata mwelekeo katika maisha; lakini kile ambacho Mungu amekipata si zaidi ya maneno Anayowia na minong’ono dhaifu za sifa. Hakika hii siyo fidia ambayo Mungu anadai kutoka kwa mwanadamu?
Ingawa matamko mengi ya Mungu sasa yameonyeshwa, watu wengi bado wamepumzika kidogo katika hatua inayowakilishwa na “maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa” katika ufahamu na maarifa yao ya Mungu, ambapo kwayo hawajaendelea mbele—hii kweli ni mada chungu. Sehemu hii ya “maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa” ni ufunguo tu wa kufungua moyo wa binadamu; kupumzika kidogo hapa ni kutotimiza nia ya Mungu kabisa. Lengo la Mungu katika kuzungumza sehemu hii ya matamko Yake ni kumleta binadamu kutoka kwa Enzi ya Neema tu hadi katika Enzi ya Ufalme; Hataki hata kidogo binadamu wabaki wakisimama katika sehemu hii ya matamko Yake au hata kuchukua sehemu hii ya matamko Yake kama mwongozo, vinginevyo matamko ya baadaye ya Mungu hayatakuwa muhimu au ya maana. Iwapo kuna yeyote ambaye bado hawezi kuingia katika kile ambacho Mungu anadai kwamba mwanadamu apate katika sehemu hii ya matamko Yake, basi kuingia kwa mtu huyo kunabaki kusikojulikana. Sehemu hii ya matamko ya Mungu inajumuisha mahitaji ya msingi kabisa ambayo Mungu hutaka kutoka kwa mwanadamu katika Enzi ya Ufalme, na ndiyo njia ya pekee ambayo kwayo binadamu ataingia katika njia sahihi. Iwapo wewe ni mtu asiyeelewa chochote, basi ni bora uanze kwa kusoma maneno katika sehemu hii!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?