Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatano, 7 Machi 2018

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

Mwenyezi Mungu alisema, Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake?

Jumanne, 6 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Jinsi ya Kufuatilia Ili Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Jinsi ya Kufuatilia Ili Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni (1)

Waumini wengi wa Bwana wanahisi kwamba almradi tukiyafuata maneno ya Bwana, tukitenda unyenyekevu na uvumilivu, na kufuata mfano wa Paulo kwa kujitolea, kutumia rasilmali na kufanya kazi kwa ajili ya Bwana, tutayaridhisha mapenzi ya Mungu. Na tutaletwa katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Hata hivyo, je, tumewahi kufikiria iwapo jitihada kama hizi kweli zitastahili sifa za Bwana na ruhusa ya kuingia katika ufalme wa mbinguni? Kama sivyo, tunapaswa kufuatilia kupata sifa ya Bwana na kuletwa katika ufalme wa mbinguni vipi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Sinema za Injili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Jumatatu, 5 Machi 2018

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu. Ingawa ni uamuzi wa watu kama hawa kumfuata Mungu, hawafaidi chochote. Wale wote wasiopata chochote kwenye mkondo huu ndio watakaoondolewa—wao wote hawana kazi. Haijalishi ni hatua gani ya kazi ya Mungu unayopitia, lazima uandamane na maono makuu. Bila maono kama haya, itakuwa vigumu kwako kukubali kila hatua ya kazi mpya, kwa maana mwanadamu hana uwezo wa kuwaza kuhusu kazi mpya ya Mungu, ni kuu kushinda mawazo ya mwanadamu. Kwa hivyo bila mchungaji kumlinda mwanadamu, bila mchungaji kushirikiana na mwanadamu kuhusu maono hayo, mwanadamu hana uwezo kukubali kazi hii mpya. Iwapo mwanadamu hawezi kupokea maono haya, basi hawezi kupata kazi mpya ya Mungu, na iwapo mwanadamu hawezi kutii kazi mpya ya Mungu, basi mwanadamu hana uwezo wa kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na hivyo ufahamu wake wa Mungu ni bure. Kabla mwanadamu atimilize maneno ya Mungu, lazima ayajue maneno ya Mungu, hivyo ni kusema, aelewe mapenzi ya Mungu; ni kwa njia hii tu ndiyo maneno ya Mungu yanaweza kutekelezwa kwa usahihi na kulingana na moyo wa Mungu. Hili lazima liwe na kila mmoja anayetafuta ukweli, na ndiyo njia ambayo lazima kila mmoja anayejaribu kumjua Mungu aipitie. Njia ya kuyajua maneno ya Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na pia njia ya kuijua kazi ya Mungu. Na hivyo, kujua maono hakuashirii tu kuujua ubinadamu wa Mungu mwenye mwili, lakini pia kunajumuisha kujua maneno na kazi ya Mungu. Kutokana na maneno ya Mungu wanadamu wanapata kuelewa mapenzi ya Mungu, na kutokana na maneno ya Mungu wanapata kuelewa tabia ya Mungu na pia kujua kile Mungu alicho. Imani katika Mungu ndiyo hatua ya kwanza katika kumjua Mungu. Harakati ya kusonga kutoka katika imani ya mwanzo katika Mungu mpaka imani kuu kwa Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na harakati ya kuipitia kazi ya Mungu. Iwapo unaamini kwa Mungu kwa ajili tu ya kuamini kwa Mungu, na huamini kwa Mungu kwa ajili ya kumjua Mungu, basi hakuna ukweli katika imani yako, na haiwezi kuwa safi—kuhusu hili hakuna tashwishi. Iwapo, wakati wa harakati anapopata kumuonja Mungu, mwanadamu anapata kumjua Mungu polepole, basi hatua kwa hatua tabia yake itabadilika pia, na imani yake itaongezeka kuwa ya kweli zaidi. Kwa njia hii, wakati mwanadamu anafaulu katika imani yake kwa Mungu, ataweza kumpata Mungu kwa ukamilifu. Mungu alijitoa pakubwa kuingia katika mwili mara ya pili na kufanya kazi Yake binafsi ili mwanadamu apate kumjua Yeye, na ili mwanadamu aweze kumwona. Kumjua Mungu[a] ndiyo matokeo ya mwisho yanayofikiwa katika mwisho wa kazi ya Mungu; ndilo hitaji la mwisho la Mungu kwa mwanadamu. Anafanya hili kwa ajili ya ushuhuda Wake wa mwisho, na ili kwamba mwanadamu mwishowe na kwa kikamilifu aweze kumgeukia Yeye. Mwanadamu anaweza tu kumpenda Mungu kwa kumjua Mungu, na ili ampende Mungu lazima amjue Mungu. Haijalishi vile anavyotafuta, au kile anachotafuta kupata, lazima aweze kupata ufahamu wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumridhisha Mungu. Ni kwa kumjua Mungu tu ndio mwanadamu anaweza kumwamini Mungu kwa ukweli, na ni kwa kumjua Mungu tu ndio anaweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Wale wasiomjua Mungu hawataweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Kumjua Mungu kunahusisha kujua tabia ya Mungu, kuelewa mapenzi ya Mungu, na kujua kile Mungu alicho. Na haijalishi ni kipengee gani cha kumjua Mungu, kila mojawapo kinamhitaji mwanadamu alipe gharama, na kinahitaji nia ya kutii, ambapo bila hivi hakuna atakayeweza kufuata mpaka mwisho. Kazi ya Mungu hailingani na mawazo ya mwanadamu hata kidogo, tabia ya Mungu na kile Mungu alicho ni vitu vigumu sana kwa mwanadamu kufahamu, na yote Anayosema na kufanya Mungu ni makuu sana yasiyoeleweka na mwanadamu; iwapo mwanadamu anatamani kumfuata Mungu, na hana nia ya kumtii Mungu, basi mwanadamu hatafaidi chochote. Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa, Mungu Amefanya kazi nyingi ambayo haieleweki na mwanadamu na ambayo mwanadamu amepata ugumu kuikubali, na Mungu amesema mengi yanayofanya mawazo ya mwanadamu magumu kupona. Ilhali Hajawahi kukomesha kazi Yake kwa sababu mwanadamu ana ugumu mwingi; Ameendelea kufanya kazi na kuzungumza, na hata ingawa idadi kubwa ya “wanajeshi” wameangamia njiani, Yeye bado Anaendelea na kazi Yake, na bado anateua kundi baada ya kundi la watu walio tayari kukubali kazi Yake mpya. Yeye hawahurumii wale “mashujaa” walioangamia, na badala yake anawathamini wale wanaoikubali kazi Yake mpya na maneno. Lakini ni kwa sababu gani ndiyo Anafanya kazi kwa njia hii, hatua kwa hatua? Ni kwa nini Yeye kila mara huwaondoa na kuchagua watu wengine? Ni kwa nini Yeye hutumia mbinu za aina hii kila mara? Kusudi la kazi Yake ni ile wanadamu wapate kumjua, na ili waweze kutwaliwa na Yeye. Kanuni ya kazi Yake ni kufanya kazi kwa wale wanaoweza kutii kazi Anayofanya leo, na sio kufanya kazi kwa wale wanaotii kazi Yake ya zamani, na wanaipinga kazi Yake ya leo. Hii ndiyo sababu hasa Amewafuta na kuwaangamiza watu wengi.

Matokeo ya funzo la kumjua Mungu haliwezi kufikiwa kwa siku moja au mbili:; Mwanadamu lazima apate uzoefu wa matukio mengi, apitie mateso, na awe na utiifu wa kweli. Kwanza kabisa, anza na kazi na maneno ya Mungu. Lazima uelewe kumjua Mungu kunajumuisha nini, jinsi ya kupata maarifa kuhusu Mungu, na jinsi ya kumwona Mungu katika matukio yako. Hili ndilo kila mtu lazima afanye wakiwa bado hawajamjua Mungu. Hakuna anayeweza kushika kazi na maneno ya Mungu kwa mara moja, na hakuna anayeweza kupata maarifa ya ukamilifu wa Mungu kwa muda mfupi. Kinachohitajika ni harakati mahususi ya matukio, na bila haya hakuna mwanadamu atakayeweza kumjua au kumfuata Mungu kwa kweli. Mungu Anapofanya kazi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kumjua. Zaidi kazi ya Mungu inavyokinzana na mawazo ya mwanadamu, ndivyo ufahamu wa mwanadamu Kwake unavyofanywa upya na wenye kina kirefu. Iwapo kazi ya Mungu ingebaki milele bila kubadilika, basi mwanadamu angekuwa tu na ufahamu mdogo wa Mungu. Kati ya uumbaji na wakati wa sasa, vitu ambavyo Mungu alifanya wakati wa Enzi ya Sheria, Alichofanya wakati wa Enzi ya Neema, na kile Afanyacho wakati wa Enzi ya Ufalme: lazima ujue vizuri sana maono haya. Lazima mjue kazi ya Mungu. Ni baada tu ya kumfuata Yesu ndio Petro alipata kujua polepole kuhusu kazi ambayo Roho alifanya ndani ya Yesu. Alisema, “Kutegemea matukio ya mwanadamu hakutoshi kufukia ufahamu kamili wa Mungu; Lazima kuwe na mambo mengi kutoka kwa kazi ya Mungu ya kutusaidia kumjua Mungu.” Mwanzoni, Petro aliamini kuwa Yesu alitumwa na Mungu, kama mtume, na hakumwona Yesu kama Kristo. Wakati Petro aliitwa kumfuata[b] Yesu, Yesu Alimuuliza, “Simoni, mwana wa Yona, je, utanifuata?” Petro alisema, “Ni lazima nimfuate yule aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu. Nitakufuata Wewe.” Kutoka kwa maneno Yake, inaonekana wazi kuwa Petro hakuwa na ufahamu kumhusu Yesu; alikuwa ameyapitia maneno ya Mungu, alikuwa amejikabili mwenyewe, na pia alikuwa amepitia ugumu kwa ajili ya Mungu, ilhali hakujua kazi ya Mungu. Baada ya muda wa uzoefu, Petro aliona ndani ya Yesu matendo mengi ya Mungu, aliona vile Mungu anavyopendeza, na aliona uwepo wa Mungu ndani ya Yesu. Vilevile, aliona kuwa maneno ya Yesu hayangeweza kuzungumzwa na mwanadamu, na kwamba kazi Aliyofanya Yesu haingefanyika na mwanadamu. Katika maneno ya Yesu na matendo Yake, zaidi ya hayo, Petro aliona wingi wa hekima ya Mungu, na kazi nyingi ya uungu. Wakati wa matukio yake, hakupata kujijua mwenyewe tu, ila alitilia maanani matendo ya Yesu, ambayo kutokana nayo aligundua mambo mengi mapya; kama vile, kwamba kulikuwa na maonyesho mengi ya Mungu wa matendo katika kazi ya Aliyofanya Mungu kupitia kwa Yesu, na kwamba maneno ya Yesu, matendo Yake, na jinsi Alivyoyachunga makanisa na kazi Aliyofanya ilitofautiana kabisa na mwanadamu wa kawaida. Hivyo, kutoka kwa Yesu alijifunza mafunzo mengi aliyopaswa kusoma, na kufikia wakati Yesu Alikuwa karibu kusulubiwa, alikuwa amepata ufahamu kiasi kuhusu Yesu—ufahamu ambao ulikuwa msingi wa uaminifu wake wa maisha katika Yesu, na kusulubiwa kwake kichwa chini kwa ajili ya Yesu. Yeye alikuwa na mawazo kadhaa, na hakuwa na ufahamu kamili kuhusu Yesu mwanzoni, lakini mambo kama haya bila shaka yanapatikana ndani ya wanadamu wapotovu. Alipokuwa karibu Anaondoka, Yesu Alimwambia Petro kwamba kusulubiwa Kwake ndiyo kazi Aliyokuja kufanya; Lazima Akataliwe na enzi hiyo, enzi hii nzee yenye uchafu lazima imsulubishe msalabani, na Alikuwa Amekuja kukamilisha kazi ya ukombozi, na, kwa kuwa Alikuwa ameikamilisha kazi hii, huduma Yake ilikuwa imekamilika. Aliposikia haya, Petro alipatwa na huzuni, na akampenda Yesu sana hata zaidi. Yesu Aliposulubiwa msalabani, Petro alilia kwa uchungu akiwa peke yake. Kabla ya hili, alikuwa amemuuliza Yesu, “Ee Bwana! Unasema kwamba unaenda kusulubiwa. Baada ya Wewe kwenda, tutakuona tena lini?” Je, hakuna mchanganyiko katika maneno Aliyozungumza? Je, hakuna mawazo yake pale ndani? Moyoni mwake, alijua kuwa Yesu Alikuja kukamilisha sehemu ya kazi ya Mungu, na kwamba baada ya Yesu kuondoka, Roho angekuwa pamoja naye; ingawa Angesulubiwa na Apae mbinguni, Roho wa Mungu Angekuwa pamoja naye. Wakati huo, alikuwa na ufahamu kiasi kumhusu Yesu, na kujua kwamba Alitumwa na Roho wa Mungu, kwamba Roho wa Mungu Alikuwa ndani Yake, na kwamba Yesu Alikuwa Mungu Mwenyewe, Alikuwa Kristo. Lakini kwa sababu ya upendo wake kwa Yesu, na kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu, bado Petro alisema maneno hayo. Ikiwa unaweza kutilia maanani na kupitia matukio ya hali ya juu katika kila hatua ya kazi ya Mungu, basi utaweza kuutambua uzuri wa Mungu hatua kwa hatua. Na maono ya Paulo yalikuwa yapi? Yesu Alipomwonekania, Paulo alisema, “Ee Bwana! Wewe ni nani?” Yesu Akasema, “Mimi ndimi Yesu, ambaye wewe unamtesa.” Haya ndiyo yalikuwa maono ya Paulo. Petro alitumia kufufuka kwa Yesu na kuonekana Kwake kwa siku arubaini, na mafunzo ya Yesu wakati wa maisha Yake, kama maono yake mpaka alipofika mwisho wa safari yake.

Mwanadamu humtambua Mungu, anapata kujijua mwenyewe, anajitoa katika tabia yake potovu, na kutafuta kukua katika maisha yote kwa ajili ya kumjua Mungu. Ukitafuta kujijua mwenyewe tu na kujishughulisha tu na tabia yako potovu, na huna ufahamu ni kazi gani Mungu Anafanya kwa mwanadamu, kuhusu jinsi wokovu Wake ulivyo mkuu, au jinsi unavyomjua Mungu na kushuhudia matendo ya Mungu, basi matukio yako hayana maana. Iwapo unafikiri kuwa kuweza kuuweka ukweli katika matendo, na kuwa na uwezo wa kuvumilia kunamaanisha maisha ya mtu yamekua, basi hii ina maana kuwa bado huelewi maana kamili ya maisha, na huelewi kusudi la Mungu la Kufanya kazi kwa mwanadamu. Siku moja, ukiwa katika makanisa ya kidini, miongoni mwa wanachama wa Kanisa la Toba au Kanisa la Uzima, utakutana na watu wengi wenye imani ambao maombi yao yana maono, na wanaohisi kuguzwa na walio na maneno ya kuwaongoza katika kuendelea kwao na maisha. La ziada, kwa mambo mengi wanaweza kuvumilia, na kujitelekeza wenyewe, bila kuongozwa na mwili. Wakati huo, huwezi kujua tofauti: Utaamini kuwa kila wanachofanya ni sawa, kuwa ni udhihirisho wa kawaida wa maisha, lakini ni jambo la kusikitisha kweli kuwa jina wanaloamini si sahihi. Je imani kama hizi si pumbavu? Ni kwa nini inasemekana kuwa watu wengi hawana maisha? Ni kwa sababu hawamjui Mungu, na hivyo inasemekana kuwa hawana Mungu, na hawana uhai. Iwapo imani yako kwa Mungu imefikia kiwango fulani ambapo unaweza kwa kikamilifu kuyafahamu matendo ya Mungu, ukweli wa Mungu, na kila hatua ya kazi ya Mungu, basi umejawa na ukweli. Iwapo hujui kazi na tabia ya Mungu, basi uzoefu wako bado ni wa chini. Jinsi Yesu Aliifanya hatua ile ya kazi Yake, jinsi hatua hii inavyoendelezwa, jinsi Mungu Alifanya kazi Yake katika enzi ya Neema na ni kazi ipi iliyofanywa, ni kazi ipi inafanyika katika hatua hii—iwapo huna ufahamu kamilifu wa mambo haya, basi hutawahi kuondokewa na wasiwasi na utakuwa na shaka. Iwapo, baada ya kipindi cha uzoefu, wewe unaweza kujua kazi inayofanywa na Mungu na kila hatua ya kazi ya Mungu, na unao ufahamu mkuu wa malengo ya maneno ya Mungu, na ni kwa nini maneno mengi yaliyozungumzwa na Yeye hayajatimika bado, basi unaweza kutulia na kuendelea katika safari iliyo mbele yako, ukiwa huru kutokana na wasiwasi na kusafishwa. Mnapaswa kuona kile Mungu anatumia wingi wa kazi Yake. Yeye hutumia maneno Anayozungumza, akimsafisha mwanadamu na kuyabadilisha mawazo ya mwanadamu kupitia maneno mengi tofauti. Mateso yote ambayo mmestahimili, kusafishwa kote ambako mmepitia, kushughulikiwa ambako mmekukubali ndani yenu, kupata nuru ambako mmeona—yote yamefanikishwa kutumia maneno Aliyozungumza Mungu. Ni kwa sababu ya nini ndio mwanadamu anamfuata Mungu. Ni kwa sababu ya maneno ya Mungu! Maneno ya Mungu ni yenye mafumbo makuu, na yanaweza kuuguza moyo wa mwanadamu, kufunua vitu vilivyo ndani ya moyo wa mwanadamu, yanaweza kumfanya ajue vitu vilivyotendeka zamani, na kumruhusu kuona katika siku za usoni. Na kwa hivyo mwanadamu anavumilia mateso kwa sababu ya maneno ya Mungu, na anafanywa mkamilifu kwa sababu ya maneno ya Mungu, na ni baada ya hapo tu ndipo mwanadamu anamfuata Mungu. Anachostahili kufanya mwanadamu katika hatua hii ni kukubali maneno ya Mungu, na haijalishi kama amefanywa mkamilifu, au kusafishwa, kilicho cha muhimu ni maneno ya Mungu; hii ni kazi ya Mungu, na ni maono ambayo mwanadamu lazima ayajue leo hii.
Mungu Anamfanyaje mwanadamu kuwa mkamilifu? Tabia ya Mungu ni gani? Na ni nini kilicho ndani ya tabia Yake? Haya yote lazima yaeleweke; hii ni kusambaza jina la Mungu, ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na kumtukuza na kumsifu Mungu, na bila shaka mwanadamu atafikia mabadiliko katika tabia ya maisha yake kwa msingi wa kumjua Mungu. Zaidi mwanadamu anavyopitia kushughulikiwa na kusafishwa, ndivyo nguvu yake inavyoongezeka, na hatua za Mungu zinavyozidi kuwa nyingi, ndivyo mwanadamu anavyofanywa mkamilifu. Leo, katika uzoefu wa mwanadamu, kila hatua ya kazi ya Mungu inayagonga mawazo ya mwanadamu, na kila hatua haiwezi kuwazwa na akili ya mwanadamu, na kuzidi matarajio ya mwanadamu. Mungu Anakimu mahitaji yote ya mwanadamu, na kwa kila njia yote huwa yanakinzana na mawazo ya mwanadamu, na ukiwa mdhaifu, Mungu Ananena maneno Yake. Ni kwa njia hii tu ndio Anaweza kukupa uhai wako. Kwa kuzigonga fikira zako, unakuja kukubali kazi ya Mungu, na kwa njia hii pekee ndio unaweza kuondoa upotovu wako. Leo hii, kwa upande mmoja Mungu mwenye mwili Anafanya kazi katika uungu, na kwa upande mwingine Anafanya kazi katika ubinadamu wa kawaida. Unapoacha kuweza kukana kazi yoyote ya Mungu, unapoweza kutii bila kujali lolote Analosema Mungu au kufanya katika hali ya ubinadamu wa kawaida, unapoweza kutii na kuelewa bila kujali ni ukawaida wa aina gani Anadhihirisha: ni wakati huo tu ndio unaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye ni Mungu, na ni hapo tu utakoma kuwa na dhana, na ni hapo tu ndio utaweza kumfuata mpaka mwisho. Kuna hekima katika kazi ya Mungu, na Anajua jinsi mwanadamu Anaweza kuwa na ushuhuda Kwake. Anajua pale ambapo udhaifu wa uhai wa mwanadamu upo, na maneno Anayozungumza yanaweza kukugonga pale penye udhaifu wako upo, lakini pia Anatumia maneno Yake makuu na yenye busara kukufanya uwe na ushuhuda Kwake. Hayo ndiyo matendo ya kimiujiza ya Mungu. Kazi inayofanywa na Mungu haiwezi kufikiriwa na akili ya mwanadamu. Hukumu ya Mungu inafunua aina za upotovu ambazo mwanadamu, kwa kuwa ni mwili, amejawa nao, na vitu vipi ndivyo umuhimu wa mwanadamu, na humwacha mwanadamu bila mahali pa kujificha aibu yake.
Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu. Mungu Anawatumia wale waliomjua baada ya kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Anawatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda, na vilevile Anawatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale basi ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hana haja na mwanadamu kumsifu kwa maneno tu, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa namna ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaohitimu kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanaofaa kumshuhudia Mungu, na Mungu hatamruhusu mwanadamu kwa makusudi aliletee jina Lake aibu.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 4 Machi 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sitisha Huduma ya Kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sitisha Huduma ya Kidini

Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia.

Jumamosi, 3 Machi 2018

Watiifu wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Watiifu wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote.

Ijumaa, 2 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 2. Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

Xiaoxiao Jijini Xuzhou, Mkoani Jiangsu
Kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya kanisa, nilihamishwa mpaka mahali pengine ili kutimiza wajibu wangu. Wakati huo, kazi ya injili mahali pale ilikuwa katika hali duni, na hali ya akina kaka na dada kwa kawaida haikuwa nzuri.

Alhamisi, 1 Machi 2018

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (katika siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima. Hii ni kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho; Anazungumza tu ili dunia iwe ulimwengu wa maneno, ili kila mtu awe amepewa na kutiwa nuru maneno Yake, na ili roho ya mwanadamu iamshwe na aweze kuona vizuri kuhusu maono yake. Wakati wa siku za mwisho, Mungu katika mwili Amekuja duniani hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno. Yesu Alipokuja, Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni, na Akatimiza kazi ya wokovu wa msalaba. Alihitimisha Enzi ya Sheria, na Akakomesha mambo yote ya kale. Ujio wa Yesu ulihitimisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema. Ujio wa Mungu katika mwili wa siku za mwisho umehitimisha Enzi ya Neema. Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, kutumia maneno ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, kumwangazia na kumpa nuru mwanadamu, na kumwondoa Mungu asiye yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii sio hatua ya kazi ambayo Yesu Aliifanya Alipokuja. Yesu Alipokuja, Alifanya miujiza mingi, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alifanya kazi ya wokovu ya msalaba. Na matokeo yake ni kwamba, katika dhana za mwanadamu, mwanadamu anaamini kwamba hivi ndivyo Mungu Anapaswa kuwa. Maana Yesu Alipokuja, hakufanya kazi ya kuondoa taswira ya Mungu asiye yakini moyoni mwa mwanadamu; Alipokuja, Alisulubishwa, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni. Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho.
Kile unachopaswa kujua:
1. Kazi ya Mungu si ya kimiujiza, na hupaswi kuhifadhi dhana juu yake.
2. Unapaswa kuelewa kazi kuu ambayo Mungu katika mwili Amekuja kufanya wakati huu.
Hakuja kuponya wagonjwa, au kutoa mapepo, au kufanya miujiza, na Hajakuja kueneza injili ya toba, au kumpatia mwanadamu ukombozi. Hiyo ni kwa sababu Yesu Amekwishafanya kazi hii, na Mungu Harudii kazi ile ile. Leo, Mungu Amekuja kuhitimisha Enzi ya Neema, na kuzitupilia mbali desturi zote za Enzi ya Neema. Mungu wa vitendo Amekuja hasa kuonyesha kuwa Yeye ni halisi. Yesu Alipokuja Alizungumza maneno machache; hasa Alionyesha miujiza, Akafanya ishara na maajabu, na Akaponya wagonjwa na kutoa mapepo, au wakati mwingine Alizungumza unabii ili kumshawishi mwanadamu, na kumfanya mwanadamu aone kwamba ni kweli Alikuwa Mungu, na Alikuwa Mungu Asiyependelea. Hatimaye, Akakamilisha kazi ya msalaba. Mungu wa leo Haonyeshi ishara na maajabu, wala Haponyi wagonjwa na kutoa mapepo. Yesu Alipokuja, kazi Aliyoifanya iliwakilisha upande mmoja wa Mungu, lakini wakati huu Mungu Amekuja kufanya hatua ya kazi ambayo imetazamiwa, maana Mungu Harudii kazi ile ile; ni Mungu ambaye siku zote ni mpya na Hawezi kuzeeka kamwe, na hivyo yale yote unayoyaona leo ni maneno na kazi ya Mungu wa vitendo.
Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, ili kuelezea yale yote ambayo ni ya lazima katika maisha ya mwanadamu, kuonyesha yale ambayo mwanadamu anapaswa kuingia kwayo, kumwonesha mwanadamu matendo ya Mungu, na kumwonesha mwanadamu hekima, uweza na uajabu wa Mungu. Kupitia njia nyingi ambazo Mungu Anazungumza, mwanadamu anatazama ukuu wa Mungu, aidha, unyenyekevu na usiri wa Mungu. Mwanadamu anatazama kwamba Mungu ni mkuu, lakini ni mnyenyekevu na msiri, na Anaweza kuwa mdogo kuliko vitu vyote. Baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa Roho, baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu, na baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa kutoka kwa mtazamo wa nafsi ya tatu. Katika hili inaweza kuonekana kwamba namna ya kazi ya Mungu inatofautiana kwa kiasi kikubwa na ni kwa njia ya maneno ndipo Anamruhusu mwanadamu kuiona. Kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho ni ya kawaida na halisi, na hivyo kundi la watu wa siku za mwisho wanakumbwa na majaribu makubwa kuliko yote. Kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu, watu wote wameingia katika majaribu hayo; kwamba mwanadamu ameingia katika majaribu ya Mungu ni kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu. Wakati wa enzi ya Yesu, hakukuwa na dhana au majaribu. Kwa sababu kazi kubwa iliyofanywa na Yesu ilikuwa ni kulingana na dhana za mwanadamu, watu walimfuata, na hawakuwa na dhana juu Yake. Majaribu ya leo ni makubwa sana ambayo yamewahi kukabiliwa na mwanadamu, na inaposemwa kwamba watu hawa wametoka katika dhiki kuu, hii ndiyo dhiki inayoongelewa.
Leo, Mungu Ananena ili kusababisha imani, upendo, ustahimilivu na utii kwa watu hawa. Maneno yaliyozungumzwa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kutokana na hulka ya asili ya mwanadamu, kulingana na tabia ya mwanadamu, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia kwacho leo. Mbinu Yake ya kuzungumza[a] ni halisi na ya kawaida: Hazungumzi juu ya kesho, wala Haangalii nyuma, jana; Anazungumza kile tu ambacho kinapaswa kuingiwa kwacho, kuwekwa katika vitendo, na kueleweka leo. Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na ana uwezo wa kutoa mapepo, na kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine; mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Unapaswa kuelewa vizuri mambo haya. Kwa nini kazi ya Mungu leo ni tofauti na kazi ya Yesu? Kwa nini Mungu leo Haonyeshi ishara na maajabu, Hatoi mapepo, na Haponyi wagonjwa? Ikiwa kazi ya Yesu ingekuwa sawa na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Sheria, je, Angekuwa Amemwakilisha Mungu wa Enzi ya Neema? Je, Yesu Angekuwa Amemaliza kazi ya msalaba? Ikiwa, kama katika Enzi ya Sheria, Yesu Angeingia hekaluni na kuitunza Sabato, basi Asingeteswa na mtu yeyote na Angekumbatiwa na wote. Kama ingekuwa hivyo, je, Angesulubiwa? Je, Angekuwa Amemaliza kazi ya ukombozi? Je, ingekuwa na maana gani ikiwa Mungu katika mwili wa siku za mwisho Angeonyesha ishara na maajabu kama Yesu? Ikiwa tu Mungu Atafanya sehemu nyingine ya kazi Yake wakati wa siku za mwisho, kazi inayowakilisha sehemu ya mpango wa usimamizi Wake, ndipo mwanadamu anaweza kupata maarifa ya kina ya Mungu, na baada ya hapo tu ndipo mpango wa usimamizi wa Mungu unaweza kukamilika.
Wakati wa siku za mwisho Mungu Amekuja mahususi kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake. Anazungumza kutokana na mtazamo wa Roho, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu; Anazungumza kwa namna tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi fulani, na Anatumia njia za kuzungumza ili kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa taswira ya Mungu yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu iliyofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu Amekuja kuponya wagonjwa, kutoa mapepo, kufanya miujiza, na kumpatia mwanadamu baraka za vitu, Mungu Anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuweza kuondoa mambo hayo kutoka katika dhana za mwanadamu, ili mwanadamu aweze kuuelewa uhalisia na ukawaida wa Mungu, na ili kwamba taswira ya Yesu iweze kuondolewa moyoni mwake na kuwekwa taswira mpya ya Mungu. Mara tu taswira ya Mungu ndani ya mwanadamu inapozeeka, basi inakuwa sanamu. Yesu alipokuja na kutekeleza hatua hii ya kazi, Hakuwakilisha Mungu kikamilifu. Alifanya baadhi ya ishara na maajabu, Alizungumza maneno kadhaa, na hatimaye Akasulubishwa, na Aliwakilisha upande mmoja wa Mungu. Hakuweza kuwakilisha yale yote ambayo ni ya Mungu, bali Alimwakilisha Mungu katika kufanya upande mmoja wa kazi ya Mungu. Hiyo ni kwa sababu Mungu ni mkuu, na ni wa ajabu sana, na Haeleweki, na kwa sababu Mungu Anafanya upande mmoja tu wa kazi Yake katika kila enzi. Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Alimwongoza Musa kutoka Misri kwa maneno Yake, na Akazungumza maneno fulani kwa Wanaisraeli; wakati huo, sehemu ya matendo ya Mungu yaliwekwa wazi, lakini kwa sababu ubora wa tabia ya mwanadamu ulikuwa finyu na hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kufanya maarifa yake kukamilika, Mungu Aliendelea kuzungumza na kufanya kazi. Wakati wa Enzi ya Neema, mwanadamu aliweza kuona tena sehemu ya matendo ya Mungu. Yesu Aliweza kuonyesha ishara na maajabu, kuponya wagonjwa na kutoa mapepo, na kusulubishwa, siku tatu baadaye. Akafufuka na Akawatokea watu Akiwa katika mwili. Kumhusu Mungu, mwanadamu hakujua chochote zaidi ya hiki. Mwanadamu anajua tu kile ambacho Mungu Amemwonyesha, na kama Mungu Asingeonyesha chochote zaidi kwa mwanadamu, basi hicho kingekuwa kiwango cha mwanadamu kumwekea mipaka Mungu. Hivyo, Mungu Anaendelea kufanya kazi, ili maarifa ya mwanadamu juu Yake yaweze kuwa ya kina zaidi, na ili taratibu aweze kuijua hulka ya Mungu. Mungu anatumia maneno yake kumkamilisha mwanadamu. Tabia yako iliyoharibika imewekwa wazi kwa maneno ya Mungu, na dhana zako za kidini zinaondolewa na uhalisia wa Mungu. Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kutimiza maneno haya kwamba "Neno Lafanyika kuwa mwili, Neno Lakuwa mwili, na Neno Laonekana katika mwili," na kama huna maarifa ya kina kuhusu hili, basi hutaweza kusimama imara; wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya mpango wa Mungu wa usimamizi. Hivyo, maarifa yako yanapaswa kuwa wazi; bila kujali namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, Mungu Hamruhusu mwanadamu kumwekea mipaka. Ikiwa Mungu Asingefanya kazi hii wakati wa siku za mwisho, basi maarifa ya mwanadamu juu Yake yasingeweza kwenda popote. Ungeweza kujua tu kwamba Mungu Anaweza kusulubiwa na Anaweza kuiangamiza Sodoma, na kwamba Yesu Anaweza kufufuliwa kutoka katika wafu na kumtokea Petro.... Lakini usingeweza kusema kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutimiza yote, na yanaweza kumshinda mwanadamu. Ni kwa njia tu ya kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu ndipo unaweza kuzungumza juu ya maarifa hayo, na kadri unapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu zaidi, ndivyo maarifa yako yanavyokuwa ya kina zaidi kumhusu Yeye. Ni baada ya hapo tu ndipo utaacha kumwekea Mungu mipaka ndani ya dhana zako binafsi. Mwanadamu anakuja kumjua Mungu kwa kupitia kazi Yake, na hakuna njia nyingineyo sahihi ya kumjua Mungu. Leo, kuna watu wengi ambao hawafanyi chochote bali wanasubiri kuona ishara na maajabu na wakati wa maangamizi. Je, unamwamini Mungu, au unaamini katika maangamizi? Ukisubiri hadi wakati wa maangamizi utakuwa umechelewa sana, na ikiwa Mungu Hataleta maangamizi, basi Atakuwa si Mungu? Je, unaamini ishara na maajabu, au unamwamini Mungu Mwenyewe? Yesu Hakuonyesha ishara na maajabu wakati Alipobezwa na wengine; je, Hakuwa Mungu? Je, unaamini ishara na maajabu, au unaamini katika hulka ya Mungu? Mitazamo ya mwanadamu kuhusu imani kwa Mungu ni makosa! Yehova Alizungumza maneno mengi wakati wa Enzi ya Sheria, lakini hata leo baadhi yake bado hayajatimizwa. Je, unaweza kusema kwamba Yehova Hakuwa Mungu?
Leo, inapaswa kueleweka kwenu wote kwamba, katika siku za mwisho, ni kwa kiasi kikubwa ukweli wa "Neno linakuwa mwili" ambao unakamilishwa na Mungu. Kupitia kazi yake halisi duniani, Anafanya mwanadamu kumfahamu, na kushirikiana Naye, na kuona matendo Yake halisi. Anamsababisha mwanadamu kuona kwa wazi kwamba Yeye Anaweza kuonyesha ishara na maajabu na pia kuna nyakati ambapo Hawezi kufanya hivyo, na hii inategemea enzi. Kutokana na hili unaweza kuona kwamba Mungu sio kwamba Hawezi kuonyesha ishara na maajabu, lakini badala yake Anabadilisha kufanya kazi Kwake kulingana na kazi Yake, na kulingana na enzi. Katika hatua ya sasa ya kazi, Haonyeshi ishara na maajabu; kuonyesha kwake baadhi ya ishara na maajabu katika enzi ya Yesu, ilikuwa ni kwa sababu kazi Yake katika enzi hiyo ilikuwa tofauti. Mungu Hafanyi kazi hiyo leo, na baadhi ya watu wanaamini Hana uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, au wanafikiri kwamba kama Haonyeshi ishara na maajabu, basi Yeye si Mungu. Hii sio hoja ya uwongo? Mungu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, lakini Anafanya kazi katika enzi tofauti, na hivyo Hafanyi kazi hiyo. Kwa kuwa hii ni enzi tofauti, na kwa kuwa hii ni hatua tofauti ya kazi ya Mungu, matendo yaliyowekwa wazi na Mungu pia ni tofauti. Imani ya mwanadamu kwa Mungu sio imani katika ishara na maajabu, wala imani katika miujiza, bali ni imani katika kazi Yake halisi wakati wa enzi mpya. Mwanadamu anamjua Mungu kupitia namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, na maarifa haya yanamfanya mwanadamu amwamini Mungu, ambavyo ni kusema, imani katika kazi na matendo ya Mungu. Katika hatua hii ya kazi, Mungu Anazungumza hasa. Usisubiri kuona ishara na maajabu; hutayaona! Maana hukuzaliwa katika Enzi ya Neema. Kama ungezaliwa katika Enzi ya Neema, ungeweza kuona ishara na maajabu, lakini umezaliwa katika siku za mwisho, na hivyo unaweza kuona tu uhalisia na ukawaida wa Mungu. Usitarajie kumwona Yesu wa kimiujiza wakati wa siku za mwisho. Unaweza kumwona tu Mungu katika mwili wa vitendo, Ambaye si tofauti na mwanadamu yeyote wa kawaida. Katika kila enzi, Mungu Anaweka wazi matendo mbalimbali. Katika kila enzi Anaweka wazi sehemu ya matendo ya Mungu, na kazi ya kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu, na inawakilisha sehemu moja ya matendo ya Mungu. Matendo Anayoyaweka wazi yanatofautiana na enzi ambayo kwayo Anafanya kazi, lakini yote yanampatia mwanadamu maarifa ya Mungu ambayo ni ya kina, imani kwa Mungu ambayo ni yenye kuhusika na mambo halisi sana, na ambayo ni ya kweli zaidi. Mwanadamu anamwamini Mungu kwa sababu ya matendo yote ya Mungu, na kwa sababu Mungu ni wa ajabu ni mkuu sana, kwa sababu Yeye ni mwenyezi, na ambaye Hapimiki kina. Ikiwa unamwamini Mungu kwa kuwa Anaweza kufanya ishara na maajabu na Anaweza kuponya wagonjwa na kuwatoa mapepo, basi mtazamo wako si sahihi, na baadhi ya watu watakwambia, "Je, pepo wachafu pia hawawezi kufanya mambo hayo?" Je, hii sio kuielewa vibaya taswira ya Mungu kwa kuilinganisha na taswira ya Shetani? Leo, imani ya mwanadamu kwa Mungu ni kwa sababu ya matendo Yake mengi na njia nyingi ambazo kwazo Anafanya kazi na kuzungumza. Mungu Anatumia matamshi yake kumshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu. Mwanadamu anamwamini Mungu, kwa sababu ya matendo Yake mengi, na si kwa sababu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, na wanadamu wanamwelewa tu kwa sababu wanaona matendo Yake, Ni kwa kujua tu matendo halisi ya Mungu, namna Anavyofanya kazi, njia ambazo Anaonyesha hekima Yake, vile Anavyozungumza, na jinsi Anavyomfanya mwanadamu kuwa mkamilifu—ni kwa kujua tu vipengele hivi—ndipo unaweza kufahamu uhalisia wa Mungu na kuelewa tabia Yake. Kile Anachopenda, kile Anachochukia, namna Anavyomfanyia kazi mwanadamu—kwa kuelewa yale ambayo Mungu Anayapenda na Asiyoyapenda, unaweza kutofautisha kati ya kile ambacho ni chanya na kile ambacho ni hasi, na kupitia maarifa yako juu ya Mungu kunakuwa na maendeleo katika maisha yako. Kwa ufupi unapaswa kuwa na maarifa ya kazi ya Mungu, na unapaswa kuweka sahihi mitazamo yako kuhusu kuwa na imani kwa Mungu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.

Jumatano, 28 Februari 2018

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno;

Jumanne, 27 Februari 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni ili kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufichua ubovu wa Shetani usiovumilika. Aidha, ni ili kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kujua, kwa uhakika kabisa tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, kilicho kikuu na kilicho cha aibu. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wataweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Bwana wa viumbe—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Ninayeweza kumpa mwanadamu vitu kwa ajili ya raha yake; na atapata kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni mmoja tu wa viumbe niliowaumba na ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kuelewa mapenzi Yangu, na wajue kwamba Mimi Ndimi ukweli. Hivyo, wakati wa awamu ya kwanza ya kazi ya katika Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita, Nilifanya kazi ya sheria, ambayo ilikuwa ndiyo kazi ambayo kwayo Yehova aliwaongoza watu Wake. Hatua ya pili ilianzisha kazi ya Enzi ya Neema katika vijiji vya Yudea. Yesu Anawakilisha kazi yote ya Enzi ya Neema; Alipata mwili na kusulubiwa, na pia Akazindua Enzi ya Neema. Alisulubiwa ili kukamilisha kazi ya ukombozi, ili kumaliza Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema, na hivyo Yeye Aliitwa “Kamanda Mkuu”, “Sadaka ya Dhambi,” “Mkombozi.” Kwa hiyo kazi ya Yesu ilitofautiana katika maudhui na kazi ya Yehova, ingawa zilikuwa sawa katika kanuni. Yehova Alianzisha Enzi ya Sheria, Akaunda msingi wa nyumbani, yaani, mahali pa asili, pa kazi Yake hapa duniani, na Akatoa amri; haya yalikuwa mafanikio Yake mawili, yanayowakilisha Enzi ya Sheria. Kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema haikuwa kutoa amri bali kutimiza Amri, na hivyo kukaribisha Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria ambayo ilidumu kwa miaka elfu mbili. Alikuwa mwanzilishi, aliyekuja ili kuianzisha Enzi ya Neema, ilhali ukombozi ulibakia msingi wa kazi Yake. Na hivyo mafanikio Yake yalikuwa pia mara mbili: kufungua enzi mpya, na kukamilisha kazi ya ukombozi kupitia kusulubiwa Kwake. Kisha Akaondoka. Katika hatua hiyo, Enzi ya Sheria ilifikia mwisho wake na wanadamu waliingia katika Enzi ya Neema.

Kazi ambayo Yesu alifanyika ililingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Kazi Yake ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu, kuwasamehe dhambi zao, na kwa hivyo tabia Yake yote ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, ucha Mungu, ustahamilivu, huruma na wema. Aliwabariki wanadamu kwa wingi na kuwaletea neema nyingi, na mambo yote ambayo wangeweza kufurahia, Aliwapa kwa ajili ya furaha yao: amani na furaha, uvumilivu Wake na upendo, huruma Yake na wema. Katika siku hizo, chote alichokutana nacho mwanadamu kilikuwa wingi wa vitu vya kufurahia tu: Moyo wake ulikuwa na amani na uhakikisho, roho yake ilifarijika, na alikuwa anaruzukiwa na Mwokozi Yesu. Sababu iliyomfanya mwanadamu aweze kufaidi mambo haya ni matokeo ya enzi alimoishi. Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa tayari na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji neema nyingi, ustahimili na uvumilivu usio na mwisho, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu walichoona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya kulipia dhambi za binadamu, yaani, Yesu. Yote waliyojua ni kwamba Mungu angeweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na yote waliyoona ni huruma ya Yesu na wema Wake. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu wao waliishi katika Enzi ya Neema. Na hivyo, kabla ya kuweza kukombolewa, walilazimika kufurahia neema za aina nyingi ambazo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo lilikuwa la manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na pia wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia ustahimili wa Yesu na uvumilivu. Ni kwa njia ya ustahimili wa Yesu na uvumilivu pekee ndio walipata haki ya wa kupokea msamaha na kufurahia neema nyingi kutoka kwa Yesu—kama vile Yesu alivyosema, “Sijakuja kuwakomboa wenye haki, ila wenye dhambi, kukubali dhambi zao zisamehewe.” Kama Yesu angepata mwili wa tabia ya hukumu, laana, na kutovumilia makosa ya mwanadamu, basi mwanadamu kamwe hangeweza kupata nafasi ya kukombolewa, na daima yeye angebaki mwenye dhambi. Hali ingekuwa hivi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Sheria ingeendelea kwa miaka elfu sita. Dhambi za mwanadamu zingeongezeka zaidi na kuwa mbaya zaidi tu, na uumbaji wa binadamu ungekuwa wa bure. Wanadamu wangeweza tu kumtumikia Yehova chini ya sheria, bali dhambi zao zingezidi za wanadamu wa kwanza kuumbwa. Jinsi Yesu alivyowapenda wanadamu zaidi, Akisamehe dhambi zao na kuwapa huruma na wema wa kutosha, ndivyo wanadamu walizidi kuwa na uwezo wa kuokolewa, wa kuitwa wanakondoo waliopotea ambao Yesu Aliwanunua tena kwa gharama kubwa. Shetani hakuweza kuingilia katika kazi hii, kwa sababu Yesu Aliwatunza wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anavyotunza mtoto mchanga aliye kifuani pake. Yeye hakuwa na hasira nao au kuwadharau, bali Alikuwa Amejaa faraja; Yeye kamwe hakuwa na ghadhabu miongoni mwao, lakini alistahimili dhambi zao na Akapuuza upumbavu wao na kutofahamu, hata kusema, “Uwasamehe wengine mara sabini mara saba.” Kwa hiyo moyo Wake ulirekebisha mioyo ya wengine. Ilikuwa ni kwa njia hii ndiyo watu walipokea msamaha wa dhambi kupitia uvumilivu Wake.

Ingawa Yesu katika mwili Wake hakuwa na hisia kabisa, Yeye daima Aliwafariji wanafunzi Wake, Aliwapa mahitaji yao, Akawasaidia, na Akawaruzuku. Bila kujali kiwango cha kazi Alichofanya au kiasi gani cha mateso Alivumilia, Yeye kamwe hakuwa na matarajio ya kupita kiasi kwa mwanadamu, lakini kila mara Alikuwa mwenye subira na kuvumilia dhambi zao, kiasi kwamba katika Enzi ya Neema kwa upendo watu walimwita “Mwokozi Yesu anayependeka.” Kwa watu wa wakati huo—kwa watu wote—kile Yesu Alikuwa nacho na kile Alichokuwa, kilikuwa huruma na wema. Yeye kamwe hakukumbuka dhambi za, na hakuwatendea kulingana na dhambi zao. Kwa sababu hiyo ilikuwa enzi tofauti, mara nyingi Alitoa chakula na vinywaji kwa watu ili waweze kula hadi washibe. Yeye Aliwatendea wafuasi Wake wote kwa ukarimu, akaponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kufufua wafu. Ili kwamba watu waweze kumwamini na kuona kwamba yote Aliyofanya yalifanyika kwa bidii na kwa dhati, Yeye Alifika kiwango cha kufufua maiti iliyooza, kuwaonyesha kwamba mikononi Mwake hata wafu wanaweza kuwa hai tena. Kwa njia hii Alivumilia kwa kimya na kufanya kazi Yake ya ukombozi kati yao. Hata kabla Asulubiwe, Yesu Alikuwa tayari Amebeba dhambi za binadamu na kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya wanadamu. Hata kabla Asulubiwe, Alikuwa tayari Amefungua njia ya msalaba ili kuwakomboa wanadamu. Mwishowe Aligongwa misumari msalabani, Alijitoa sadaka Yeye Mwenyewe kwa ajili ya msalaba, na Alitoa huruma Yake yote, wema Wake, na utakatifu kwa wanadamu. Kwa wanadamu daima alikuwa mvumilivu, kamwe Hakutafuta kulipiza kisasi, lakini Aliwasamehe dhambi zao, Akiwasihi watubu, na kuwafundisha kuwa na subira, uvumilivu na upendo, kufuata nyayo Zake na kujitoa wenyewe kwa ajili ya msalaba. Upendo Wake kwa ndugu ulizidi upendo Wake kwa Maria. Kanuni ya kazi Aliyofanya ilikuwa kuwaponya watu na kutoa mapepo, yote kwa ajili ya ukombozi Wake. Haijalishi Alikoenda, Yeye Aliwatendea wote waliomfuata kwa neema. Aliwafanya maskini kuwa tajiri, viwete watembee, vipofu waone na viziwi wasikie; Yeye hata Aliwaalika watu wa hadhi ya chini kabisa, maskini zaidi, wenye dhambi, kula pamoja naye, Akikosa kuwaepuka kamwe ila daima Alikuwa na subira, hata kusema, “Wakati mchungaji anampoteza kondoo mmoja kati ya mia, yeye ataondoka na kuwaacha nyuma wale tisini na tisa ili amtafute kondoo mmoja aliyepotea, na anapompata yeye atafurahia sana.” Yeye Aliwapenda wafuasi Wake kama kondoo anavyopenda wanakondoo wake. Ingawa walikuwa wajinga na wasio na ufahamu, na walikuwa wenye dhambi katika macho Yake, na zaidi walikuwa washirika wa chini zaidi katika jamii, Aliona hawa wenye dhambi—waliodharauliwa na wengine—kama vipenzi Vyake. Kwa kuwa Aliwapendelea, Alitoa uhai Wake kwa ajili yao, kama mwana kondoo alitolewa madhabahuni. Alitembea kati yao kama mtumishi wao, Akiwaruhusu kumtumia na kumchinja, Alijinyenyekeza kwao bila masharti. Kwa wafuasi Wake Alikuwa Mwokozi Yesu aliyependeka, lakini kwa Mafarisayo, ambao waliwahubiria watu kutoka viweko virefu vya mnara, Hakuonyesha huruma na wema, bali chuki na maudhi. Hakufanya kazi nyingi miongoni mwa Mafarisayo, Akiwahubiria na kuwakemea mara chache tu; Yeye hakutembea miongoni mwao akifanya kazi ya ukombozi, au kufanya ishara na maajabu. Alitoa huruma Yake na wema Wake wote kwa wafuasi Wake, akivumilia kwa ajili ya hawa wenye dhambi mpaka mwisho kabisa, wakati Alipigwa misumari msalabani na akastahimili kila udhalilishaji mpaka Alivyowakomboa wanadamu wote kikamilifu. Hii ndiyo ilikuwa kazi Yake yote.

Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, dunia yote ingekuwa mahali pa kulala pa Shetani, maskani yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji kuonyesha huruma na wema kwa wanadamu; kupitia kwa njia hiyo tu ndio wanadamu wangeweza kupokea msamaha na mwishowe kupata haki ya kukamilishwa na kumilikiwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Katika miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alitumia kufanya kazi Yake hapa duniani alikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha, kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa yule mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaendesha majaaliwa ya wanadamu. Baada ya Yeye kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo alipowakomboa wanadamu. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Akidhihakiwa, kukashifiwa, na kuachwa, kiasi cha Yeye kukosa mahali pa kulaza kichwa chake, mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, huku nafsi Yake yote—mwili safi kabisa na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani, na akapitia kila namna ya mateso. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na maaskari hata wakamtemea mate usoni; ilhali Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa wanadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika. Kazi ambayo Yesu alifanya inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria wala si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo wanadamu wamepitia—Enzi ya Ukombozi.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 26 Februari 2018

Hymn of Christian Experience Swahili "Ni Furaha Kuu kuwa Mtu Mwaminifu" | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hymn of Christian Experience Swahili "Ni Furaha Kuu kuwa Mtu Mwaminifu" | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kuelewa ukweli huiachilia huru roho ya mtu na kumfanya mtu kuwa mwenye furaha. Nimejazwa na imani katika neno la Mungu na sina shaka. Mimi niko bila uhasi wowote, sirudi nyuma, na kamwe sikati tamaa. Ninauunga mkono wajibu wangu kwa moyo wangu wote na mawazo, na siujali moyo. Ingawa ubora wa tabia yangu ni wa chini, nina moyo wa uaminifu. Nimejitolea kikamilifu katika kila kitu ili kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ninatenda ukweli, namtii Mungu, na kujaribu kuwa mtu mwaminifu. Mimi ni wazi na mnyoofu, bila uongo, nikiishi kwenye mwanga. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu.
Kuelewa ukweli huiachilia huru roho ya mtu na kumfanya mtu kuwa mwenye furaha. Nimejazwa na imani katika neno la Mungu na sina shaka. Mimi niko bila uhasi wowote, sirudi nyuma, na kamwe sikati tamaa. Ninauunga mkono wajibu wangu kwa moyo wangu wote na mawazo, na siujali moyo. Ingawa ubora wa tabia yangu ni wa chini, nina moyo wa uaminifu. Nimejitolea kikamilifu katika kila kitu ili kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ninatenda ukweli, namtii Mungu, na kujaribu kuwa mtu mwaminifu. Mimi ni wazi na mnyoofu, bila uongo, nikiishi kwenye mwanga. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu.
Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu. Watu waaminifu, kuja haraka, hebu tuongee kwa dhati. Watu wote wampendao Mungu, njooni mkusanyike na kuungana kama marafiki wazuri. Watu wote wenye kupenda ukweli ni ndugu. Ee watu wenye furaha, njooni muimbe na kucheza katika sifa kwa Mungu.
Kutoka kwa Fuata Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Sifa na Ibada
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Jumapili, 25 Februari 2018

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu.

Jumamosi, 24 Februari 2018

Swahili Gospel Movie "Ivunje Laana" | Mungu ni Wokovu Wangu

Swahili Gospel Movie "Ivunje Laana" | Mungu ni Wokovu Wangu

Fu Jinhua alikuwa mzee wa kanisa la nyumba nchini China. Kama Wakristo wengine wengi, alijitolea kwa Bwana kwa shauku kubwa, na alifanya kazi kwa bidii katika kazi yake kwa ajili Yake. Alikuwa hasa mwenye kujiamini, na alijiona kuwa mtu ambaye alimpenda Bwana kweli. Baada ya kumfuata Bwana kwa miaka mingi, aliamini kwa moyo wote kwamba Biblia ilikuwa imefunuliwa na Mungu, na kwamba maneno katika Biblia yote yalikuwa maneno ya Mungu. Kwa hivyo, akilini mwake, alilinganisha kuamini katika Bwana na kuamini katika Biblia. Alidhani kwamba wale walioachana na Biblia hawakuweza kuitwa wafuasi wa Bwana. Pia aliamini kwamba alihitaji tu kufuata Biblia ili kuchukuliwa kuenda katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaposhuka na mawingu.Hivyo wakati ambapo kikundi cha watu kilianza kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, Fu Jinhua aliamini katika dhana potovu za wachungaji na wazee wa kanisa wa kidini, na kamwe hakutafuta kuchunguza mambo zaidi. Siku moja, Fu Jinhua alimtembelea Dada He, mshiriki mwenza wa kanisa. Dada He alizungumza juu ya kiwewe chake mwenyewe: "Unabii wote juu ya kurudi kwa Bwana umetimia kimsingi, na Bwana anatakiwa kuwa amesharudi tayari. Hivyo kwa nini bado hatujamwona Bwana akishuka pamoja na mawingu?" Mfanyakazi mwenzake Fang Jianjie pia alisema: Miezi minne ya damu imeonekana, ambayo ina maana kwamba maafa makubwa yatatujia hivi karibuni. Kulingana na unabii kutoka katika vitabu vya manabii na Kitabu cha Ufunuo, Kanisa la Filadelfia litachukuliwa kwenda mbinguni kabla ya maafa makubwa,na Mungu atawastawisha watumishi na wajakazi Wake kwa Roho Wake ili kufanya kundi la washindi kabla ya maafa. Tusipochukuliwa kwenda mbinguni kabla ya majanga, huenda tutaangamia kati ya majanga haya makubwa. Lakini sasa, "Umeme wa Mashariki" limeshuhudia kwamba Bwana Yesu tayari amerejea, Ameonyesha ukweli, na kufanya kundi la washindi. Je, hili linatimiza unabii kutoka katika Biblia? Je, Umeme wa Mashariki ni onyesho la Bwana na kazi Yake? Baada ya kuwasikiliza wafanyakazi wenza, Fu Jinhua aliingia katika mawazo ya kina na akaanza kuyakadiria mambo haya … Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho.Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana. Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake.Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii. Maudhui ya video hii yametafsiriwa yote na wafasiri wataalam. Hata hivyo, kutokana na tofauti za lugha nk, makosa kadhaa yaliyofanywa hayawezi kuepukika. Ukigundua makosa yoyote kama hayo, tafadhali rejea kwa toleo la kwanza la Kichina. Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi. Injili ya Kushuka kwa Ufalme:Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi. Injili ya Kushuka kwa Ufalme:Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi. Injili ya Kushuka kwa

Ijumaa, 23 Februari 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Desturi ya Sala

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kusogea karibu na Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Desturi ya Sala

Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Katika sala zao hapo awali walikuwa wakifanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati na kufanya mchezo tu, na hakuna mtu aliyeupeana moyo wake kwa ukamilifu mbele ya Mungu na kumwomba Mungu kweli.

Alhamisi, 22 Februari 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Saba

Matawi yote ya magharibi yanapaswa kuisikiliza sauti Yangu:

Je, mmekuwa waaminifu Kwangu hapo awali? Je, mmeyatii maneno Yangu mazuri ya ushauri? Je, mna matumaini ambayo ni halisi na yasiyo na mashaka? Utiifu wa mwanadamu, upendo wake, imani yake—hamna kipatikanacho ila kutoka Kwangu, hamna hata kimoja ila kilichotolewa na Mimi. Enyi watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je, mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Hapo zamamni, mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda-shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwaokoa? Ni mara ngapi mmeanguka katika mitego ya Shetani? Ni mara ngapi mmejiingiza katika mitego ya wanadamu? Na tena, ni mara ngapi mmejikuta katika ugomvi usio na kikomo kati yenu kwa kukosa kuziachilia nafsi zenu? Ni mara ngapi miili yenu imekuwa katika nyumba Yangu ila roho zenu zikiwa kusikojulikana? Licha ya hayo, ni mara ngapi Nimewanyooshea mkono Wangu kuwainua; ni mara ngapi Nimewaonea huruma; ni mara ngapi Nimekosa uvumilivu wa kuziona hali zenu za kuhuzunisha za mateso? Ni mara ngapi … je, mnamfahamu?

Lakini leo kwa ulinzi Wangu, hatimaye mmezishinda shida zote na Nafurahia pamoja nanyi; hili ndilo dhihirisho la busara Yangu. Hata hivyo, likumbuke hili vyema! Ni nani kati yenu amewahi kuanguka na akaendelea kuwa thabiti? Ni nani kati yenu amewahi kuwa thabiti bila kuwa na nyakati za unyonge? Miongoni mwa wanadamu, ni nani amewahi kupokea baraka ambazo hazikutoka Kwangu? Ni nani amepitia misukosuko isiyotoka Kwangu? Inawezekana kuwa wale wote wanaonipenda hupokea baraka peke yake? Inawezekana kwamba misukosuko ilimpata Ayubu kwa sababu alikosa kunipenda ila alinikana Mimi? Inawezekana kwamba Paulo aliweza kunihudumia kwa utiifu mbele Yangu kwa sababu aliweza kunipenda kwa dhati? Ijapokuwa mnaweza kushikilia kwa uthabiti ushuhuda Wangu, lakini je, kuna mtu kati yenu aliye na ushuhuda safi kama dhahabu ambayo haijatiwa najisi? Je, mwanadamu anaweza kuwa na uaminifu halisi? Kwamba ushuhuda wenu huniletea furaha hakukinzani na “uaminfu” wenu kwa sababu Sijawahi kumtarajia mtu yeyote kutoa zaidi. Kwa kufuata dhamira asilia ya mpango Wangu, nyinyi nyote mngekuwa “bidhaa duni—zisizokidhi kiwango.” Je, huu sio ni mfano wa kile Nilichowaambia kuhusu “kuwaonea huruma”? Je, mnachoona sio wokovu Wangu?

Nyinyi nyote mnafaa kuvuta kumbukumbu zenu: Tangu mrejee katika nyumba Yangu, kuna yeyote kati yenu, bila kutafakari faida na hasara, amenifahamu sawa na Petro alivyonifahamu? Mmekariri Biblia kikamilifu, lakini je, mlijifunza chochote kuhusu kiini chake? Japo hivyo, bado mmeshikilia “mtaji” wenu, mkikataa kuziachilia nafsi zenu. Ninapotoa tamko, Nikiwazungumzia ana kwa ana, Ni nani kati yenu amewahi kuweka chini “nyaraka” zilizofunikwa kupokea maneno ya uzima ambayo Nimeyaweka wazi? Hamyajali maneno Yangu na wala hamyathamini. Badala yake, mnatumia maneno Yangu kama bombomu dhidi ya maadui wenu ili kudumisha nafasi zenu; hamjaribu hata kidogo kuyakubali maoni Yangu ili mnifahamu. Kila mmoja wenu anamwangazia sana mtu mwingine, nyinyi nyote ni “wasio bahili,” nyote “mnawajali wengine” katika kila hali; je, haya siyo hasa mliyokuwa mnafanya jana? Na leo je? “Utiifu” wenu umepanda juu kwa alama kidogo, nyote mmekuwa wazoefu kiasi, mmekomaa kidogo na kwa sababu ya haya, “heshima” yenu Kwangu imeongezeka kwa kiasi fulani, na hamna hata mmoja “anayethubutu kutenda kwa wepesi.” Kwa nini mnaishi katika hali ya ubaridi wa kudumu? Ni kwa nini sifa nzuri hazipatikani kabisa ndani yenu? Enyi watu Wangu! Ya zamani yalipita kitambo; msiendelee kuyashikilia zaidi. Zamani mlishikilia msimamo wenu, leo mnapaswa kunipa utiifu wenu wa dhati, na hata zaidi mnafaa kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu siku za usoni, na mtarithi baraka Zangu hapo baadaye. Hili ndilo mnapaswa kufahamu.

Ingawa Siko nanyi, Roho Wangu hakika ataleta neema juu yenu. Kwa kutegemea hili, Natumaini mtaienzi baraka Yangu na mtaweza kujitambua. Msichukulie hili kuwa mtaji wenu; badala yake, mnatakiwa kujaza kinachokosekana ndani yenu kutoka katika maneno Yangu, na kutoka humu mpate mambo mazuri mnayovihitaji. Huu ndio ujumbe Ninaowaachia.

Februari 28, 1992