Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Ijumaa, 22 Machi 2019

Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna yeyote anayemchukua Kristo kama binadamu wa nyama na mwili aliye na kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao hufanya wanavyopenda wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa "Kristo wa kweli." Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.
Kabla ya kuwasiliana na Kristo, unaweza kuamini kwamba tabia yako imebadilishwa kabisa, kwamba wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo, na kwamba wewe unastahili kupokea baraka za Kristo zaidi. Pia kwamba, kwa kuwa umesafiri njia nyingi, umefanya kazi nyingi, na kuleta matunda mengi, hivyo ni lazima utakuwa mtu anayepata taji mwishowe. Hata hivyo kuna ukweli ambao hujui: Tabia potovu na uasi na upinzani wa mwanadamu huonekana wazi mara tu anapomwona Kristo, na uasi na upinzani unaoonekana wakati huu kwa hakika na kamilifu kuliko wakati mwingine wote. Ni kwa sababu Kristo ni Mwana wa Adamu—Mwana wa Adamu aliye na ubinadamu wa kawaida—kwamba mwanadamu hamwogopi wala kumheshimu. Ni kwa sababu Mungu anaishi katika mwili ndio maana uasi wa mwanadamu hufichuliwa kikamilifu na kwa uwazi sana. Kwa hivyo Nasema kwamba kuja kwake Kristo kumechimbua uasi wote wa wanadamu na kutupa asili ya mwanadamu katika afueni ya ghafla. Huku kunaitwa "kumvuta chui mkubwa kutoka mlimani" na "kumvuta mbwa mwitu kutoka pangoni pake." Je, unathubutu kusema kwamba wewe ni mwaminifu kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe huonyesha utiifu kamili kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe si muasi? Wengine watasema: Kila wakati ambao Mungu ananiweka katika mazingira mapya, mimi daima hutii na silalamiki na aidha siweki fikra zozote juu ya Mungu. Wengine watasema: Kazi zozote nilizopewa na Mungu mimi hufanya kadri ya uwezo wangu na kamwe mimi si mvivu. Kama ndivyo hali, Nawauliza hivi: Je, mnaweza kulingana na Kristo wakati mnaishi pamoja naye? Na ni kwa muda gani nyinyi mnaweza kulingana na Yeye? Siku moja? Siku mbili? Saa moja? Saa mbili? Imani yenu inaweza kuwa ya kustahili sifa, lakini hamna uthabiti wa kutosha. Wakati unaishi na Kristo kwa kweli, kujidai kwako na kujigamba kwako kutawekwa wazi kwa maneno na matendo yako kidogo kidogo, na hivyo ndivyo tamaa yako ya kupindukia na uasi na kutoridhika kwako kutafichuka kwa kawaida. Mwishowe, kiburi chako kitakuwa kikubwa zaidi, hadi wakati wewe utazozana sana na Kristo kama maji na moto, na basi asili yako itawekwa wazi kabisa. Wakati huo, fikra zako haziwezi kufichika tena, malalamiko yako, pia, yataonekana kwa ghafla, na ubinadamu wako duni utakuwa wazi kabisa. Hata hivyo, hata wakati huo, utaendelea kukana uasi wako mwenyewe, ukiamini kwamba badala yake kwamba Kristo kama huyu si rahisi kukubaliwa na mwanadamu, ni mwingi wa madai kwa binadamu, na ungetii kikamilifu kwake kama yeye angekuwa tu Kristo mwenye huruma zaidi. Mnaamini kwamba daima kuna sababu ya haki ya uasi wenu, na kwamba nyinyi mnamwasi tu baada ya Kristo amewafikisha hatua fulani. Kamwe hamjawahi kufikiri kwamba mmekosa kumchukulia Kristo kama Mungu na katika nia ya kumtii. Badala yake, wewe kwa ukaidi unasisitiza Kristo afanye kazi Yake kulingana na matakwa yako, na punde ambapo kuna jambo lolote ambamo Hafanyi hivyo, basi unaamini kwamba Yeye si Mungu bali ni mwanadamu. Je, si kuna wengi kati yenu ambao wameridhika na Yeye katika hali hii? Ni nani huyo mnayemwamini hata hivyo? Na ni jinsi gani mnatafuta?
Kila mara mnataka kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijipandishe hadhi hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, wakati unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa. Ushirika wako na ndugu (au dada) huenda usionyeshe mengi kukuhusu wewe, lakini si rahisi hivyo unaposhiriki na Kristo. Wakati wowote, fikira zako zinaweza kukita mizizi, kiburi chako kianze kuchipuka, na uasi wako kuzaa mitini. Unawezaje kufaa kushiriki na Kristo na ubinadamu kama huo? Je, kweli unaweza kumchukua Yeye kama Mungu kila wakati wa kila siku? Je, kweli utakuwa na hali halisi ya utiifu kwa Mungu? Mnamuabudu Mungu mkubwa ndani ya mioyo yenu kama Yehova wakati mnamchukua Kristo anayeonekana kama mwanadamu. Hisia zenu ni duni mno na ubinadamu wenu ni wa hali ya chini! Hamwezi kumfikiria Kristo kama Mungu milele; ni mara chache tu, mnapotaka, ndio mnamshika na kumwabudu kama Mungu. Hii ndiyo sababu Ninasema nyinyi si waumini wa Mungu, lakini kikundi cha washirika ambao wanapigana dhidi ya Kristo. Hata watu ambao huonyesha wema kwa wengine hulipwa, lakini Kristo, ambaye amefanya kazi ya namna hiyo kati yenu, hajapokea upendo wa Mungu au fidia na utii wake. Je, hili si ni jambo la kusikitisha mno?
Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kufanya tendo mbaya, lakini katika ushirika wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kwa uaminifu, au kutii neno la Kristo; basi, Ninasema kwamba wewe ni mtu mbaya na mwovu zaidi katika dunia. Unaweza kuwa mkunjufu na mwaminifu mno kwa jamaa zako, marafiki, mke (au mume), wanao na mabinti, na wazazi, na kamwe huwatumii wengine vibaya, lakini kama huwezi kulingana na kupatana na Kristo, basi hata ukitumia vitu vyako vyote kuwasaidia majirani zako au kulinda vizuri baba yako, mama, na wanakaya, Ningesema kwamba wewe bado ni mwovu, na zidi ya hayo aliyejaa hila za ujanja. Usifikiri, kwamba wewe unalingana na Kristo kwa sababu tu unapatana na wengine au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unafikiri kwamba nia yako ya huruma inaweza kupata baraka kutoka Mbinguni kwa udanganyifu? Je, unafikiri kwamba matendo machache mema yanaweza kubadilishwa na utii wako? Hakuna hata mmoja yenu anaweza kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, na wote wanaona vigumu kukubali ubinadamu wa kawaida wa Kristo, hata hivyo siku zote mnatangaza utiifu wenu kwa Mungu. Imani kama yenu italeta adhabu ya kufaa. Wacheni kujihusisha katika ndoto za ajabu na kutaka kumwona Kristo, kwa maana nyinyi ni wadogo sana katika kimo, kiasi kwamba nyinyi hata hamstahili kumwona. Wakati umeuwacha kabisa uasi wako na unaweza kupatana na Kristo, wakati huo Mungu Atakuonekania kwa kawaida. Iwapo utaenda kumwona Mungu kabla ya kupogolewa au kupitia hukumu, basi bila shaka utakuwa mpinzani wa Mungu na utakuwa katika njia ya kuangamizwa. Asili ya mwanadamu kwa kawaida ina uhasama kwa Mungu, kwa kuwa watu wote wamepotoshwa kabisa na shetani. Hakuna kizuri kinachoweza kupatikana kwa mtu kujaribu kushirikiana na Mungu kutokana na upotovu wake, vitendo na maneno yake kwa hakika vitafichua upotovu wake kila wakati; na katika kushirikiana na Mungu, uasi wake utafichuka katika vipengele vyote. Binadamu, kwa kutojua anakuja anampinga Kristo, kumdanganya Kristo, na kumtelekeza Kristo; hili litakapofanyika, mwanadamu atakuwa katika hali ya hatari zaidi na, hili likiendelea, atapata adhabu.
Baadhi ya watu wanaweza kuamini kwamba, kama kushirikiana na Mungu ni hatari sana, basi huenda likawa jambo la busara zaidi kukaa mbali na Mungu. Ni nini watu kama hawa wanaweza kupokea? Je, wanaweza kuwa waaminifu kwa Mungu? Hakika, kushirikiana na Mungu ni kugumu sana, lakini hiyo hasa ni kwa sababu mwanadamu amepotoka na si kwa sababu Mungu hawezi kushiriki naye. Ingekuwa bora kwenu kuweka juhudi zaidi kwa ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata fadhili kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu ni chukizo sana Kwake? Kwa nini maneno yenu yanachochea chuki Yake? Punde ambapo mmeonyesha uaminifu kidogo, nyinyi mnajisifu wenyewe, na mnadai malipo kwa ajili ya mchango mdogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kumdharau Mungu baada ya kufanya kazi ndogo. Mnataka utajiri, zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kutendewa kwa heshima. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Kuna chochote kinachostahili sifa katika maneno na matendo yenu? Wale ambao wanatekeleza wajibu wao na wale wasiofanya; wale ambao huongoza na wale ambao hufuata; wale wanaompokea Mungu na wale wasiompokea; wale wanaotoa na wale wasiotoa; wale wanaohubiri na wale ambao hupokea neno, na kadhalika; watu wote kama hawa hujisifu wenyewe. Je, hamuoni hili likiwa la kuchekesha? Mkijua vyema kwamba mnamwamini Mungu, hata hivyo ninyi hamwezi kulingana na Mungu. Mkijua vyema kutostahili kwenu, mnaendelea bado kujigamba. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imepunguka kiasi kwamba hamwezi tena kujizuia? Na hisia kama hii, mnastahili vipi kushirikiana na Mungu? Je, kufikia hapa nyinyi hamjionei hofu? Tabia yenu tayari imepunguka kiasi kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Hali ikiwa hivi, je, imani yenu si ya kuchekesha? Imani yenu si ya kipuuzi? Ni jinsi gani utashughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kutembelea?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu,

Alhamisi, 21 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”

Mwenyezi Mungu anasema, “Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu.” “Kila siku Naona vitendo vyote vya watu wengi, na kila siku Nachunguza mioyo na akili za watu wengi; hakuna aliyewahi kutoroka hukumu Yangu, na hakuna aliyewahi kuachana na uhalisi wa hukumu Yangu.”
Mwenyezi Mungu anasema, Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu. Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani? Wakati Wanangu na watu Wangu wanarudi katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Ambayo ni kusema, Nianzapo binafsi kazi Yangu duniani, na wakati enzi ya hukumu inakaribia tamati yake, Naanza kuelekeza maneno Yangu kwa ulimwengu mzima, na kutoa sauti ya Roho Wangu kwa dunia nzima. Kupitia maneno Yangu, Nitasafisha wanadamu na mambo yote miongoni mwa yote yaliyo mbinguni na duniani, ili nchi si chafu na fisadi tena, lakini ni ufalme takatifu. Nitatengeneza upya mambo yote, ili yatolewe kwa matumizi Yangu, na yasiwe na pumzi ya dunia tena, na yasichafuliwe na ladha ya ardhi tena. Duniani, mwanadamu ametafuta malengo na asili ya maneno Yangu, na amechunguza matendo Yangu, lakini bado hakuna aliyewahi kujua kwa kweli asili ya maneno Yangu, na hakuna aliyewahi kuona kwa kweli matendo Yangu ya ajabu. Ni leo tu, Nikujapo binafsi miongoni mwa wanadamu na kuongea maneno Yangu, ndipo mwanadamu anapata maarifa kidogo kunihusu, kutoa nafasi “Yangu” ndani ya mawazo yao, badala yake kutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya fahamu zake. Mwanadamu ana dhana na amejawa na udadisi; ni nani ambaye hangetaka kumwona Mungu? Ni nani ambaye hangetamani kukutana na Mungu? Lakini bado kitu pekee kilicho na nafasi ya uhakika ndani ya moyo wa mwanadamu ni Mungu ambaye mwanadamu anahisi kuwa dhahania na asiye dhahiri. Nani angetambua haya kama Singewaeleza wazi? Nani angeamini kwa kweli Mimi nipo? Kwa hakika bila shaka yoyote? Kuna tofauti kubwa kati ya “Mimi” aliye ndani ya mwanadamu na “Mimi” wa ukweli, na hakuna anayeweza kuwalinganisha. Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi Nijua, na hata angekuja kunijua, je, maarifa kama hayo bado hayangekuwa dhana? Kila siku Natembea miongoni mwa watu wengi, na kila siku Nafanya kazi ndani ya kila mtu. Wakati mwanadamu kweli ananiona, ataweza kunijua kwa maneno Yangu, na kuelewa njia Ninazotumia kuzungumza na pia nia Zangu.
Ufalme ufikapo rasmi duniani, ni nini, kati ya mambo yote, sio kimya? Nani, kati ya watu wote, hana hofu? Natembea kila mahali katika ulimwengu dunia wote, na kila kitu kinapangwa na Mimi binafsi. Wakati huu, nani asiyejua vitendo Vyangu ni vya ajabu? Mikono Yangu inashikilia mambo yote, lakini bado Niko juu ya mambo yote. Leo, si kupata mwili Kwangu na kuwepo Kwangu binafsi miongoni mwa wanadamu maana ya ukweli ya unyenyekevu na kujificha Kwangu? Kwa nje, watu wengi wananipongeza kama mzuri, wananisifu kama mzuri, lakini ni nani anayenijua kweli? Leo, mbona Nauliza kuwa mnijue? Lengo Langu sio kuaibisha joka kubwa jekundu? Sitaki kumlazimisha mwanadamu kunisifu, lakini kumfanya anijue kupitia hapo atakuja kunipenda, na hivyo kunisifu. Sifa kama hiyo inastahili jina lake, na si mazungumzo yasiyokuwepo; ni sifa tu kama hii inaweza kufikia kiti Changu cha enzi na kupaa angani. Kwa sababu mwanadamu amejaribiwa na kupotoshwa na Shetani, kwa sababu amechukuliwa na kufikiria kwa dhana, Nimekuwa mwili ili kuwashinda binafsi wanadamu wote, kufichua dhana zote za mwanadamu, na kupasua mawazo ya mwanadamu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu hajionyeshi mbele Yangu tena, na hanitumikii tena akitumia dhana zake mwenyewe, na hivyo, “Mimi” katika dhana za mwanadamu ameondoka kabisa. Ufalme ufikapo, Naanza kwanza hatua hii ya kazi, na Nafanya hivyo miongoni mwa watu Wangu. Sababu nyinyi ni watu Wangu waliozaliwa kwa nchi ya joka kubwa jekundu, kwa hakika hakuna tu hata kidogo, ama kipimo cha sumu ya joka kubwa jekundu ndani yenu. Hivyo, hatua hii ya kazi Yangu hasa inawaangazia, na hiki ni kipengele kimoja cha umuhimu wa kupata mwili Kwangu Uchina. Watu wengi hawawezi kuelewa hata chembe cha maneno Ninayoyasema, na wanapoweza, uelewa wao ni wenye ukungu na ovyo. Hii ni mojawapo ya sehemu muhimu ya mbinu Ninayozungumzia. Iwapo watu wote wangeweza kusoma maneno Yangu na kuelewa maana yao, basi nani miongoni mwa wanadamu angeweza okolewa, na kutupwa kuzimu? Mwanadamu anijuapo na kunitii ndio wakati Nitakapopumzika, na itakuwa wakati hasa ambapo mwanadamu ataweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Leo, kimo chenu ni kidogo sana, karibu kiwe kiwango cha kusikitisha, na hakistahili hata kuinuliwa—sembuse ujuzi wenu kunihusu.
Ingawa Nasema malaika wameanza kutumwa mbele kuchunga wana na watu Wangu, hakuna anayeweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Nikujapo binafsi miongoni mwa binadamu, malaika wanaanza wakati huo huo kazi ya uchungaji, na wakati huo wa uchungaji wa malaika, wana na watu wote hawapati tu majaribio na uchungaji, lakini wanaweza pia kuona, na macho yao, tukio la kila aina ya maono. Kwa sababu Nafanya kazi moja kwa moja kwa uungu, kila kitu kinaingia katika mwanzo mpya, na kwa sababu uungu huu unafanya kazi moja kwa moja, hauzuiliwi hata kidogo na ubinadamu, na unaonekana kwa binadamu kufanya kazi huru chini ya hali isiyo ya kawaida. Lakini bado, Kwangu, yote ni kawaida (mwanadamu anaamini si ya kawaida kwa sababu hajawahi kukutana na uungu moja kwa moja); hauna dhana zozote za mwanadamu, na haujachafuliwa na maana ya binadamu. Watu wataona haya wakati tu wote wataingia katika njia sawa; kwa sababu sasa ndio mwanzo, inapokuja suala la kuingia kwake, mwanadamu ana mapungufu mengi, na makosa kama haya na upofu huwezi ukaepukwa kwa urahisi. Leo, sababu Nimewaongoza hadi hapa, Nimefanya mipango ya kufaa, na Nina malengo Yangu Mwenyewe. Ningewaeleza kuyahusu leo, mngeweza kweli kuyajua? Nayajua vizuri mawazo ya akili ya mwanadamu na matakwa ya moyo wa mwanadamu: Nani hajawahi kutafuta njia ya kujitoa mwenyewe? Nani hajawahi fikiria matarajio yake mwenyewe? Lakini hata kama mwanadamu ana akili tajiri na wa mche nani aliweza kutabiri kwamba, kufuatia enzi, sasa kungekuwa kulivyo? Hili kweli ni tunda la juhudi zako binafsi? Haya ni malipo ya kazi yako ya bidii? Hii ndiyo picha nzuri iliyoonwa na akili yako? Nisingewaongoza wanadamu wote, nani angeweza kujitenga na mipango Yangu na kupata njia nyingine ya kutoka? Ni mawazo na matakwa ya mwanadamu ambayo yamemleta hadi leo? Watu wengi wanaishi maisha yao yote bila kutimiziwa kwa matakwa yao. Kweli hili ni kwa sababu ya kosa katika fikira zao? Maisha ya watu wengi yamejawa na furaha na ridhaa isiyotarajiwa. Kweli ni kwa sababu wanatarajia kidogo sana? Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu. Ingawa Sijitokezi binafsi kumruhusu mwanadamu kunitazama vizuri, watu wengi wanaogopa kuona uso Wangu, wanaogopa sana Nitawapiga chini, kwamba Nitawaangamiza. Mwanadamu kweli ananijua Mimi ama hanijui? Hakuna anayeweza kusema kwa hakika. Sivyo? Mnaniogopa na pia kuadibu Kwangu, lakini bado mnasimama na kunipinga wazi na kunihukumu hadharani. Sivyo? Kwamba mwanadamu hajawahi kunijua ni kwa sababu hajawahi kuuona uso Wangu ama kuisikia sauti Yangu. Hivyo, hata kama Niko ndani ya moyo wa mwanadamu, je, kuna wale ambao Sionekani mwenye ukungu na asiye dhahiri katika mioyo yao? Kuna wale Ninaoonekana vizuri ndani ya mioyo yao? Sitamani wale walio watu Wangu pia kutoniona vizuri, na hivyo Naanza kazi hii kubwa.Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu. Ingawa Sijitokezi binafsi kumruhusu mwanadamu kunitazama vizuri, watu wengi wanaogopa kuona uso Wangu, wanaogopa sana Nitawapiga chini, kwamba Nitawaangamiza. Mwanadamu kweli ananijua Mimi ama hanijui? Hakuna anayeweza kusema kwa hakika. Sivyo? Mnaniogopa na pia kuadibu Kwangu, lakini bado mnasimama na kunipinga wazi na kunihukumu hadharani. Sivyo? Kwamba mwanadamu hajawahi kunijua ni kwa sababu hajawahi kuuona uso Wangu ama kuisikia sauti Yangu. Hivyo, hata kama Niko ndani ya moyo wa mwanadamu, je, kuna wale ambao Sionekani mwenye ukungu na asiye dhahiri katika mioyo yao? Kuna wale Ninaoonekana vizuri ndani ya mioyo yao? Sitamani wale walio watu Wangu pia kutoniona vizuri, na hivyo Naanza kazi hii kubwa.
Nakuja polepole miongoni mwa wanadamu, na Naondoka taratibu. Kuna aliyewahi kuniona? Jua linaweza kuniona kwa sababu ya moto wake unaochoma? Mwezi unaweza kuniona kwa sababu ya uwazi wake unaong’aa? Kundinyota zinaweza kuniona kwa sababu ya mahali zipo angani? Nikujapo, mwanadamu hajui, na mambo yote yanabakia gizani, na Niondokapo, bado mwanadamu hafahamu. Nani anaweza kuwa na ushuhuda Kwangu? Inaweza kuwa sifa ya watu wa dunia? Inaweza kuwa mayungiyungi yanayochanua porini? Inaweza kuwa ndege wanaoruka angani? Inaweza kuwa simba wanaonguruma milimani? Hakuna anayeweza kunishuhudia kikamilifu. Hakuna anayeweza kufanya kazi Nitakayoifanya! Hata kama wangefanya kazi hii, ingekuwa na athari gani? Kila siku Naona vitendo vyote vya watu wengi, na kila siku Nachunguza mioyo na akili za watu wengi; hakuna aliyewahi kutoroka hukumu Yangu, na hakuna aliyewahi kuachana na uhalisi wa hukumu Yangu. Nasimama juu ya mawingu na kuangalia kwa umbali: Nimewaangamiza watu wengi, lakini pia watu wengi wanaishi katika huruma, na wema Wangu. Nyinyi pia hamuishi chini ya hali kama hizi?
Machi 5, 1992
Chanzo: Sura ya 11

Jumatano, 20 Machi 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Mungu Huweka Mipaka kwa ajili ya Vitu Vyote ili Kuwalea Binadamu Wote
Mwenyezi Mungu alisema, Mungu alipoumba vitu vyote, alitumia aina zote za mbinu na njia za kuziwekea uwiano, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya milima na maziwa, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya mimea na aina zote za wanyama, ndege, wadudu—lengo Lake lilikuwa ni kuruhusu aina zote za viumbe hai kuishi na kuongezeka ndani ya sheria ambazo alikuwa Amezianzisha. Viumbe vyote haviwezi kwenda nje ya sheria hizi na haziwezi kuvunjwa. Ni ndani ya aina hii tu ya mazingira ya msingi ndipo binadamu wanaweza kuendelea kuishi kwa usalama na kuongezeka, kizazi baada ya kizazi. Ikiwa kiumbe yeyote anakwenda zaidi ya ukubwa au mawanda yaliyoanzishwa na Mungu, au ikiwa anazidi kiwango cha ukuaji, ujirudiaji, au idadi chini ya utawala Wake, mazingira ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yangepata uharibifu wa viwango vinavyotofautiana. Na wakati uo huo, kuendelea kuishi kwa binadamu kungetishiwa. Ikiwa aina moja ya kiumbe hai ni kubwa sana kwa idadi, itawanyang'anya watu chakula chao, kuharibu vyanzo vya maji ya watu, na kuharibu makazi yao. Kwa njia hiyo, kuzaliana kwa binadamu au hali ya kuendelea kuishi ingeathiriwa mara moja. Kwa mfano, maji ni muhimu sana kwa vitu vyote. Ikiwa kuna wanyama wengi sana—ikiwa idadi ya panya, siafu, nzige, na vyura ni kubwa sana na wanahitaji kunywa maji—kunapokuwa na idadi iliyozidi ya wanyama, kiwango cha maji wanayokunywa pia kitaongezeka. Kadri kiwango cha maji wanachokunywa kinaongezeka, ndani ya mawanda haya yasiyobadilika ya vyanzo vya maji ya kunywa na maeneo ya majimaji, maji ya kunywa ya watu na vyanzo vya maji vitapungua, na watapungukiwa maji. Ikiwa maji ya kunywa ya watu yataharibiwa, kuchafuliwa au kuangamizwa kwa sababu aina zote za wanyama zimeongezeka kwa idadi, chini ya aina hiyo ya mazingira katili kwa ajili ya kuendelea kuishi, kuendelea kuishi kwa binadamu hakika kutakuwa kumetishiwa vikali. Ikiwa kuna aina moja au aina kadhaa za viumbe hai ambavyo vinazidi idadi yao inayofaa, hewa, halijoto, unyevunyevu, na hata vijenzi vya hewa ndani ya eneo la binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi litakuwa na sumu na kuharibiwa kwa viwango vinavyotofautiana. Hali kadhalika, chini ya mazingira haya, kuendelea kuishi kwa binadamu na hatma bado vitakuwa chini ya tishio la aina hiyo ya mazingira. Kwa hiyo, ikiwa watu watapoteza uwiano huu, hewa wanayovuta itaharibiwa, maji wanayokunywa yatachafuliwa, na halijoto ambayo wanahitaji pia itabadilika, itaathiriwa kwa viwango tofautitofauti. Ikiwa hiyo itatokea, mazingira asilia ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yataandamwa na madhara na changamoto kubwa. Chini ya aina hii ya mazingira ambapo mazingira ya msingi ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yameharibiwa, hatma na matarajio ya binadamu yatakuwa ni nini? Ni tatizo kubwa sana!
Kwa sababu Mungu anajua vitu vyote ni nini kwa binadamu, wajibu wa kila aina ya kitu, aina gani ya athari kinacho kwa watu, na faida kubwa kiasi gani kinaleta kwa binadamu—katika moyo wa Mungu kuna mpango kwa ajili ya haya yote na Anasimamia kila kipengele cha vitu vyote alivyoviumba, kwa hiyo kwa binadamu, kila kitu Anachofanya ni muhimu sana—vyote ni lazima. Kwa hiyo ama unaona baadhi ya matukio ya kiikolojia miongoni mwa vitu vyote, au baadhi ya sheria za asili miongoni mwa vitu vyote, hutashuku tena ulazima wa kila kitu ambacho kiliumbwa na Mungu. Hutatumia tena maneno ya kijinga kufanya hukumu zisizokuwa na msingi juu ya mipangilio ya Mungu juu ya vitu vyote na njia zake mbalimbali za kuwakimu binadamu. Pia hutafanya mahitimisho yasiyokuwa na msingi juu ya sheria za Mungu kwa ajili ya vitu vyote ambavyo Aliviumba. Je, hii haiko hivyo?
Je, haya yote tuliyoyazungumza ni nini? Yafikirie. Mungu ana nia Yake katika kila kitu anachofanya. Ingawa binadamu hawawezi kuona nia hiyo, siku zote inahusiana na kuendelea kuishi kwa binadamu. Inahusiana bila kutenganishwa nayo—ni ya lazima. Hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kufanya kitu ambacho hakina manufaa. Kwa kila kitu ambacho Anafanya, mpango Wake upo ndani ya nadharia na kanuni zake, ambazo zinajumuisha hekima Yake. Lengo la mpango na nia hiyo ni kwa ajili ya ulinzi wa binadamu, kumsaidia binadamu kuzuia janga, uvamizi wa kiumbe chochote hai, na aina yoyote ya madhara kwa binadamu yasababishwayo na vitu vyote. Kwa hiyo kutokana na matendo ya Mungu ambayo tumeyaona kutoka katika mada hii ambayo tunaijadili, tungeweza kusema kwamba Mungu anawakimu binadamu kwa njia nyingine? Je, tungeweza kusema kwamba Mungu anawalisha na kuwachunga binadamu kwa njia hii? Hakika ungeweza kusema hilo. Sasa mnapaswa kuelewa, je, kuna uhusiano mkubwa kati ya mada hii na anwani ya ushirika wetu, "Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote"? (Ndiyo.) Kuna uhusiano mkubwa, na mada hii ni kipengele kimoja chake. Kabla ya kuzungumza kuhusu mada hizi, watu walikuwa tu na fikra zisizo dhahiri juu ya Mungu, Mungu Mwenyewe na matendo Yake—hawakuwa na uelewa wa kweli juu ya vitu hivi. Hata hivyo, watu wanapoambiwa kuhusu matendo Yake na vitu ambavyo Amefanya, wanaweza kuelewa na kufahamu kanuni za kile ambacho Mungu anafanya na wanaweza kupata uelewa juu yake, sio? (Ndiyo.) Ingawa katika moyo wa Mungu, nadharia Zake, kanuni Zake, na Sheria Zake zinatatiza sana Anapokuwa anafanya kitu chochote, Alipotengeneza vitu vyote, na Anapotawala vitu vyote, ikiwa kitu kimoja kimechukuliwa kushiriki na nyinyi katika ushirika, je, hamtaweza kuelewa mioyoni mwenu kwamba haya ni matendo ya Mungu, na yapo thabiti sana? (Ndiyo.) Basi ni kwa jinsi gani uelewa wenu wa sasa juu ya Mungu ni tofauti na ulivyokuwa kabla? Ni tofauti kwa asili yake. Mlichokielewa kabla kilikuwa tupu, kisicho dhahiri sana, na kila mnachokielewa sasa kinajumuisha kiasi kikubwa cha ushahidi thabiti kushikilia matendo ya Mungu, kulinganisha na kile Mungu anacho na alicho. Kwa hiyo, yote ambayo nimeyasema ni nyenzo nzuri sana kwa ajili ya uelewa wa Mungu.
Februari 9, 2014
kutoka kwa Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)

Jumanne, 19 Machi 2019

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Mwenyezi Mungu alisema, Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewazia hili: Mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. Nyote mmetazamia kufika kwa wakati huo, na uaminifu wenu ni wa kusifika, imani yenu kweli ni ya kuleta wivu, lakini mnatambua kuwa mmefanya kosa kuu? Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: Wingu hili jeupe linaashiria nini? Na kwa kuwa wafuasi wengi wa Yesu wanangoja kurejea Kwake, Atashuka miongoni mwa watu wapi? Iwapo ninyi ni wa kwanza kati ya wale ambao Yesu Atawashukia, Je, wengine hawataona jambo hili kama lisilo la haki sana? Najua kuwa nyinyi mna ukweli mkubwa na utiifu kwa Yesu, lakini mmewahi kukutana na Yesu? Mnajua tabia Yake? Mmewahi kuishi na Yeye? Mnaelewa kiasi gani kumhusu kwa kweli? Wengine watasema kuwa maneno haya yanawaweka katika tatizo gumu. Watasema, “Nimesoma Biblia kuanzia mwanzo hadi mwisho mara nyingi sana. Nitakosaje kumwelewa Yesu? Usijali kuhusu tabia ya Yesu—najua hata rangi ya nguo Alizopenda kuvaa. Je, haushushi hadhi yangu ukisema simwelewi?” Napendekeza kuwa usiyapinge masuala haya; ni heri utulie na kufanya ushirika juu ya maswali yafuatayo: Kwanza, unajua uhalisi ni nini, na nadharia ni nini? Pili, unajua dhana ni nini, na ukweli ni nini? Tatu, unajua kile kinachowazwa na kile kilicho halisi?
Watu wengine wanakataa ukweli kuwa hawamwelewi Yesu. Ilhali Nasema hammwelewi hata kidogo, na hamwelewi hata neno moja la Yesu. Hiyo ni kwa sababu kila mmoja wenu anamfuata Yeye kwa sababu ya matukio ya Biblia, kwa sababu ya yale yaliyosemwa na wengine. Hamjawahi kumwona Yesu, sembuse kuishi na Yeye, na hata hamjapata kushinda na Yeye hata kwa muda mfupi. Hivyo, je, kuelewa kwenu kuhusu Yesu sio nadharia pekee? Je, si kuelewa kwenu kunakosa uhakika? Labda watu wengine wameiona picha ya Yesu, ama wengine wametembea nyumbani kwa Yesu kibinafsi. Labda wengine wamegusa mavazi ya Yesu. Ilhali kuelewa kwako kumhusu bado ni kwa nadharia na ila si kwa vitendo, hata kama umeonja chakula kilicholiwa na Yesu binafsi. Haijalishi ni hali ipi, hujawahi kumwona Yesu, na hujawahi kuwa pamoja na Yeye katika hali ya kimwili, na hivyo, kuelewa kwako kumhusu Yesu kutabaki kuwa nadharia tupu daima ambako hakuna ukweli. Pengine maneno Yangu yana uvutio mdogo kwako, lakini Nakuuliza hivi: Ingawa labda umesoma maandishi mengi yaliyoandikwa na mwandishi unayempenda, je, unaweza kumwelewa kikamilifu bila kuwahi kukaa na yeye kwa muda? Je, unajua tabia yake ilivyo? Je, unajua ni maisha ya aina gani anayoishi? Unajua chochote kuhusu hali ya hisia zake? Huwezi hata kumwelewa kikamilifu mwanadamu unayempenda, sasa utawezaje kumwelewa Yesu Kristo? Kila kitu unachoelewa kumhusu Yesu kimejaa mawazo na dhana, na hakina ukweli wowote wala uhalisi. Kinanuka, na kimejaa mwili. Kuelewa kwa aina hii kutakuwezesha vipi kustahili kukaribisha kurejea kwa Yesu? Yesu hatawakaribisha wale waliojawa na mawazo na dhana za mwili. Wale wasiomwelewa watafaa vipi kuwa waumini Wake?
Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?
Uaminifu wenu uko kwa maneno pekee, maarifa yenu ni ya kiakili tu na ya dhana, kazi yenu ni kwa sababu ya kupata baraka za mbinguni, na kwa hivyo imani yenu inafaa kuwa vipi? Hata leo, bado mnapuuza kila neno la ukweli. Hamjui Mungu ni nini, hamjui Kristo ni nini, hamjui jinsi ya kumcha Yehova, hamjui jinsi ya kuingia katika kazi ya Roho Mtakatifu, na hamjui jinsi ya kutofautisha kati ya kazi ya Mungu Mwenyewe na uongo wa mwanadamu. Unajua tu kukashifu neno lolote la ukweli linaloelezwa na Mungu lisilolingana na mawazo yako. Unyenyekevu wako uko wapi? Utiifu wako uko wapi? Uaminifu wako uko wapi? Tamaa yako ya kupata ukweli iko wapi? Uchaji Mungu wako uko wapi? Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeidaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Utaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe kawaida na wenye kutojali katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 18 Machi 2019

Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii moyoni mwake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni zozote, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi Anayofanya daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya utendaji kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake. Maarifa ya mwanadamu ya maisha yanakua hata juu zaidi, na vivyo hivyo kazi ya Mungu pia inakuwa juu zaidi. Mwanadamu anaweza kufikia ukamilifu kwa njia hii tu na kufaa kwa matumizi ya Mungu. Kwa upande mmoja, Mungu anafanya kazi hivi ili kupinga na kubadilisha fikira za mwanadamu, na kwa upande mwingine, kumwongoza mwanadamu katika hali ya juu zaidi na kweli zaidi, hadi katika ulimwengu wa juu zaidi wa imani katika Mungu, ili mwishowe, mapenzi ya Mungu yaweze kufanyika. Wote walio na asili isiyotii wanaopinga kwa kusudi wataachwa nyuma na hatua hii ya kazi ya Mungu ya haraka na yenye kusonga mbele kwa nguvu; wale tu walio na moyo mtiifu na wako tayari kuwa wanyonge wataendelea hadi mwisho wa njia. Katika kazi kama hii, nyote mnapaswa kujua jinsi ya kutii na kuweka kando fikira zenu. Mnapaswa kuwa waangalifu katika kila hatua mnayochukua. Kama wewe ni mzembe, hakika utakuwa mmoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na yule anayemkatiza Mungu katika kazi Yake. Kabla ya kufanyiwa hatua hii ya kazi, kanuni na sheria za mwanadamu za zamani zilikuwa nyingi sana hadi akawa na msisimko zaidi, na mwishowe, akawa mwenye majivuno na kujisahau. Hivi vyote ni vikwazo vinavyomzuia mwanadamu kuikubali kazi mpya ya Mungu; vinakuwa pingamizi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Iwapo mwanadamu hana utii katika moyo wake wala tamaa ya ukweli, basi atakuwa hatarini. Ukitii tu kazi na maneno yaliyo rahisi, na huwezi kukubali yoyote yaliyo na ugumu zaidi, basi wewe ni yule anayeendelea na njia za zamani na hawezi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa katika awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu ambaye ni mtiifu kwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima katika utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haikubaliki na Mungu. Kama huwezi kwenda sambamba na kazi mpya Ninayoshiriki na uendelee kuyashikilia maneno ya zamani, basi kutakuaje na ukuaji katika maisha yako? Kazi ya Mungu ni kukuruzuku kupitia neno Lake. Unapotii na kulikubali neno Lake, basi Roho Mtakatifu hakika atafanya kazi ndani yako. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa njia Ninayozungumza kabisa. Fanya Nilivyosema, na Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako mara moja. Natoa mwangaza mpya ili muweze kuona na kuwaleta kwa mwangaza wa wakati wa sasa. Unapotembea katika mwangaza huu, Roho Mtakatifu ataanza kazi ndani yako mara moja. Kuna wengine wanaoweza kuwa wakaidi na kusema, “Sitafanya tu usemavyo.” Basi Nakwambia kwamba sasa umefika mwisho wa njia umenyauka na huna maisha zaidi. Hivyo, kwa kupitia mabadiliko ya tabia yako, ni muhimu kabisa kwenda sambamba na mwangaza wa sasa. Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi ndani ya mtu mwingine ajaye. Fanya hima ufuate; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndivyo maisha yako yanaweza kuzidi kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Kwa kufanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu kwa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui ni kupitia kwa mtu wa aina gani ndiyo Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo ndiyo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani. Ukiweza kutembea kwenye njia hii sawa, hii inaonyesha kwamba kuna matumaini makubwa kwako kukamilishwa na Mungu. Kama huwezi kufanya hivyo, inaonyesha kwamba maisha yako ya baadaye ni ya dhalili na giza. Mara unapoendenda kwenye njia iliyo sahihi, utapata ufunuo katika mambo yote. Bila kujali yale ambayo Roho Mtakatifu atafichua kwa wengine, ukiendelea kupitia mambo wewe mwenyewe kwa msingi wa maarifa yao, basi uzoefu huu utakuwa sehemu ya maisha yako, na utaweza kuwakimu wengine kwa sababu ya huu uzoefu. Wale wanaowakimu wengine kwa kuyarudia maneno ni wale wasio na uzoefu wowote; lazima ujifunze kupata, kupitia mwangaza na nuru ya wengine, njia ya kutenda kabla ya kuzungumza kuhusu uzoefu na maarifa yako halisi. Hii itakuwa ya manufaa zaidi kwa maisha yako binafsi. Unapaswa kuwa na uzoefu kwa njia hii, kutii yote yatokayo kwa Mungu. Unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu katika vitu vyote na kujifunza masomo katika vitu vyote, ukijenga ukuaji kwa maisha yako. Vitendo vya aina hii huleta ukuaji wa haraka zaidi.
Roho Mtakatifu anakupa nuru kupitia uzoefu wa vitendo vyako na kukukamilisha kupitia imani yako. Uko tayari kweli kukamilishwa? Kama kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu, basi utakuwa na ujasiri kuweka kando mwili wako, na utaweza kutekeleza maneno ya Mungu na kutokuwa mtu anayekaa tu ama mnyonge. Utaweza kutii yote yatokayo kwa Mungu, na vitendo vyako vyote, viwe vimefanywa hadharani au faraghani, vitastahiki kwa Mungu. Kama wewe ni mtu mwaminifu, na unatenda ukweli katika mambo yote, basi utakamilishwa. Wale wanadamu wadanganyifu wanaotenda njia moja mbele ya wengine na nyingine nyuma yao hawako tayari kukamilishwa. Wote ni wana wa maangamizo na uharibifu; wao si wa Mungu lakini ni wa Shetani. Hao si aina ya wanadamu waliochaguliwa na Mungu! Kama vitendo na tabia yako haviwezi kustahiki mbele ya Mungu ama kufikiriwa na Roho wa Mungu, hii ni thibitisho kwamba wewe una shida. Ukikubali tu hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kuweka umuhimu katika mabadiliko ya tabia yako ndipo utafika kwenye njia ya kukamilishwa. Ikiwa kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu na kufanya mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kutii kazi yote ya Mungu na kutotoa neno lolote la kulalamika, wala hupaswi kutathmini ama kuhukumu kazi ya Mungu utakavyo. Haya ni masharti ya msingi kabisa ya kukamilishwa na Mungu. Mahitaji ya lazima kwa wale wanaotaka kukamilishwa na Mungu ni haya: fanya mambo yote kwa moyo unaompenda Mungu. Inamaanisha nini “kufanya mambo kwa moyo unaompenda Mungu”? Inamaanisha kwamba vitendo na tabia yako yote inaweza kuletwa mbele ya Mungu. Kwa sababu una nia sawa, iwapo vitendo vyako ni sawa ama vibaya, huogopi vikionyeshwa kwa Mungu ama kwa ndugu zako; unathubutu kuapa mbele ya Mungu. Kwamba kila nia, fikra, na wazo lako linaweza kufaa kuchunguzwa mbele ya Mungu: ukitenda na kuingia kwa njia hii, basi maendeleo katika maisha yako yatakuwa mepesi.
Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu? Hata wale walio tu na moyo nusu wa utii hawawezi kutembea hadi mwisho, sembuse hawa wadhalimu wasio na utii hata kidogo kwa mioyo yao. Kazi ya Mungu haipatwi virahisi na mwanadamu. Hata mwanadamu akitumia nguvu yake yote, ataweza kupata kipande tu na kufikia ukamilifu mwishowe. Na vipi basi kuhusu watoto wa malaika mkuu wanaotaka kuharibu kazi ya Mungu? Je, hawana hata matumaini madogo zaidi ya kupatwa na Mungu? Madhumuni Yangu katika kufanya kazi ya ushindi si tu kushinda kwa sababu ya ushindi, lakini kushinda ili kufichua haki na udhalimu, kupata ushahidi kwa ajili ya adhabu ya mwanadamu, kulaani waovu, na hata zaidi, kushinda kwa sababu ya kuwakamilisha wale walio radhi kutii. Mwishowe, wote watatengwa kulingana na aina, na mawazo ya wale wote waliokamilishwa yatajazwa na utii. Hii ndiyo kazi itakayokamilishwa mwishowe. Lakini waliojawa na uasi wataadhibiwa, kutumwa kuchomeka motoni na milele kulaaniwa. Wakati huo utakapofika, wale “mashujaa wakubwa wasioshindwa” wa awali watakuwa “waoga wanyonge na wasio na maana” wa chini zaidi na wanaoepukwa zaidi. Hii tu ndiyo inaweza kuonyesha kila kipengele cha haki ya Mungu na kufichua tabia Yake ambayo hairuhusu kosa lolote. Hili tu ndilo linaloweza kutuliza chuki iliyo moyoni Mwangu. Je, hamkubali kwamba hili ni la busara sana?
Sio wote walio na uzoefu wa kazi ya Roho Mtakatifu wanaweza kupata uzima, na sio wote katika mkondo huu wanaweza kupata uzima. Uzima sio mali ya kawaida inayoshirikisha binadamu wote, na mabadiliko ya tabia ni kitu ambacho hakifikiwi na wote kwa urahisi. Kujisalimisha kwa kazi ya Mungu lazima kugusike na kuishi kwa kudhihirishwa. Kujisalimisha kwa kiwango cha juu juu hakuwezi kupokea idhini ya Mungu, na kutii tu vipengele vya juujuu vya neno la Mungu bila kutaka mgeuzo wa tabia ya mtu, hakutaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Utiifu kwa Mungu na kujinyenyekeza kwa kazi ya Mungu ni kitu kimoja. Wale wanaomtii Mungu tu lakini hawatii kazi Yake hawawezi kudhaniwa kuwa watiifu, sembuse wale wasiotii kwa kweli na kwa nje hao ni wa kujipendekeza. Wale ambao kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu wote wanaweza kufaidika kutokana na kazi na kupata ufahamu wa tabia na kazi ya Mungu. Wanadamu kama hawa tu ndio kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu. Wanadamu kama hawa wanaweza kupata maarifa mapya kutokana na kazi mpya na kuwa na uzoefu wa mabadiliko mapya kutoka hayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wana idhini ya Mungu; mwanadamu wa aina hii tu ndiye amekamilishwa, ndiye amepitia mabadiliko ya tabia yake. Wale wanaopokea idhini ya Mungu ni wale wanaojisalimisha kwa Mungu kwa furaha, na pia kwa neno na kazi Yake. Mwanadamu wa aina hii tu ndiye yuko sahihi; mwanadamu wa aina hii tu ndiye kweli anamtamani Mungu, na anamtafuta Mungu kwa dhati. Na kwa wale wanaozungumzia tu imani yao kwa Mungu kwa vinywa vyao lakini kwa hakika wanamlaani, ni wanadamu waliovaa barakoa, walio na sumu ya nyoka, ni wanadamu wasaliti zaidi. Siku moja hawa waovu watavuliwa barakoa zao mbovu. Je, hiyo si kazi inayofanywa leo? Wanadamu waovu daima watakuwa waovu na hawataepuka kamwe siku ya adhabu. Wanadamu wazuri daima watakuwa wazuri na watafichuliwa kazi itakapoisha. Hakuna hata mmoja wa waovu atakayedhaniwa kuwa wenye haki, wala yeyote mwenye haki atakayedhaniwa kuwa mwovu. Je, Ningemruhusu yeyote ashtakiwe kimakosa?
Maisha yako yanapoendelea, lazima daima uwe na kiingilio kipya na ufahamu mpya na wa juu zaidi, unaokua kwa kina na kila hatua. Hiki ndicho wanadamu wote wanapaswa kuingia ndani. Kupitia kuwasiliana, kusikiliza ujumbe, kusoma neno la Mungu, ama kushughulikia suala, utapata ufahamu mpya na kupata nuru upya. Huishi ndani ya kanuni za zamani na nyakati za zamani. Unaishi daima ndani ya mwangaza mpya, na hupotei mbali na neno la Mungu. Huku ndiko kunaitwa kwenda katika njia sahihi. Kulipa tu gharama ya juu juu hakutakubalika. Siku baada ya siku, neno la Mungu linaingia katika ulimwengu wa juu zaidi na mambo mapya yanajitokeza kila siku. Ni muhimu pia kwa mwanadamu kuingia upya kila siku. Mungu anavyozungumza, ndivyo Anavyotimiza yote ambayo Amezungumza; kama huwezi kwenda sambamba, basi unabaki nyuma. Lazima uende kwa kina zaidi katika maombi yako; kula na kunywa neno la Mungu hakuwezikuwa kunakosa mfululizo. Imarisha nuru na mwangaza unayopokea, ufunuo unaopokea, na dhana zako na fikira zako lazima zipungue hatua kwa hatua. Lazima pia uimarishe hekima yako, na chochote unachopitia, lazima uwe na mawazo yako kukihusu na uwe na mtazamo wako.Kwa kuelewa mambo fulani katika roho, lazima upate ufahamu wa mambo ya nje na kuelewa kiini cha suala lolote. Kama hujajiandaa na mambo haya, utawezaje kuliongoza kanisa? Iwapo unazungumzia tu barua na mafundisho ya dini bila uhalisi wowote na bila njia ya kutenda, unaweza tu kuendelea kwa muda mfupi. Inaweza kukubalika kidogo kwa waumini wapya, lakini baada ya muda, wakati waumini wapya wanapata tajriba halisi, basi hutaweza tena kuwakimu. Basi unafaa vipi kwa matumizi ya Mungu? Bila kupata nuru upya, huwezi kufanya kazi. Walio bila nuru upya ni wale wasiojua jinsi ya kuwa na uzoefu, na wanadamu kama hao kamwe hawapati maarifa mapya ama tajriba. Na katika suala la kuleta maisha, hawawezi kamwe kufanya jukumu lao la kusambaza uhai, wala hawawezi kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu. Mwanadamu kama huyu ni dhaifu na hana maana. Kwa kweli, wanadamu kama hawa hawawezi kufanya jukumu lao kabisa kwa kazi na wote hawana faida. Wanashindwa kufanya jukumu lao na pia kwa kweli wanaweka mzigo mwingi usiohitajika juu ya kanisa. Nawahimiza hawa “wanaume wazee” kuharakisha na kuondoka kanisani ili wengine wasilazimishwe kuwaona tena. Wanadamu kama hawa hawaelewi kazi mpya lakini wamejawa na fikira zisizokoma. Hawafanyi chochote kanisani; badala yake, wanachochea na kusambaza uhasi kila pahali, hata kushiriki katika kila namna ya utovu wa nidhamu na vurugu kanisani, na hivyo kuwarusha wale wasiobagua katika vurugu na machafuko. Haya ibilisi wanaoishi, hawa mapepo mabaya wanapaswa kuondoka kanisani haraka iwezekanavyo, kanisa lisije likaharibiwa kwa sababu yako. Labda huogopi kazi ya leo, lakini huogopi adhabu ya haki ya kesho? Kuna idadi kubwa ya watu kanisani ambao ni vimelea, na pia kuna idadi kubwa ya mbwa mwitu wanaotafuta kuvuruga kazi ya kawaida ya Mungu. Vitu hivi vyote ni mapepo yaliyotumwa na Ibilisi, ni mbwa mwitu wakali wanaotafuta kuwala kondoo wasio na hatia. Iwapo wanadamu kama hawa hawatafukuzwa, basi wanakuwa vimelea kwa kanisa na nondo wanaokula sadaka. Hawa mabuu wenye kudharauliwa wajinga, duni, na wenye kuchukiza wataadhibiwa siku moja karibuni!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 17 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Siku hizi watu wengi hawatilii maanani mafunzo yapi yanayopaswa kusomwa wakati wa upatano na wengine. Nimegundua kuwa wengi wenu hawawezi kujifunza mafunzo hata kidogo wakati wa ushirikiano na wengine. Wengi wenu mnashikilia maoni yenu mwenyewe, na wakati mnafanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na yeye anatoa yake, moja uhusiano na mingine, bila kushirikiana kabisa. Mnajihusisha tu katika kutoa umaizi wenu wenyewe wa ndani, unaingia tu katika kuachilia huru “mizigo” ndani yenu, si kutafuta uzima hata kidogo. Inaonekana kwamba unafanya tu kazi hiyo kwa kutimiza wajibu, daima ukiamini kwamba unapaswa kufuata njia yako mwenyewe bila kujali jinsi watu wengine walivyo, na kwamba unapaswa kushiriki jinsi Roho Mtakatifu anavyokuongoza, bila kujali jinsi watu wengine walivyo. Hamna uwezo wa kugundua uwezo wa wengine, na hamuwezi kujichunguza. Njia yenu ya kupokea vitu ni yenye makosa sana. Inaweza kusemwa kwamba hata sasa bado mnaonyesha kujidai kwingi, kana kwamba ugonjwa huo wa zamani umerejea tena. Hamuwasiliani nyinyi kwa nyinyi ili kufikia uwazi kamili, kama ni matokeo gani yaliyopatikana kwa kuzuru kanisa hilo, au jinsi hali yako ya ndani ilivyokuwa wakati wa hivi karibuni, na kadhalika—ninyi hamuwasiliani tu kwa namna hii. Nyinyi kimsingi hamna mazoea kama vile kuacha dhana zenu wenyewe au kujitelekeza. Wale walio katika uongozi wanafikiri tu kuhusu kuwachangamsha ndugu na dada katika makanisa ya chini kwa njia ya ushirika wao, na wale wanaofuata wanajua tu kufuatilia peke yao. Kimsingi hamuelewi huduma ni nini au ushirikiano ni nini, na mnadhani tu kuhusu kuwa na dhamira nyinyi wenyewe kuulipiza upendo wa Mungu, wa kuwa na dhamira ya nyinyi wenyewe kuishi kwa kudhihirisha mtindo wa Petro, na si kuhusu kitu kingine chochote. Hata unasema, bila kujali jinsi watu wengine walivyo, hamtatii kwa upofu hata hivyo, na bila kujali watu wengine walivyo, ninyi wenyewe unatafuta ukamilifu na Mungu, na hiyo itatosha. Kwa kweli, dhamira yako hayajapata maonyesho thabiti katika uhalisi hata kidogo. Je! Hii sio aina yote ya tabia mnayoonyesha siku hizi. Kila mmoja wenu anashikilia imara utambuzi wenu wenyewe, na ninyi nyote mnataka kufanywa wakamilifu. Ninaona kwamba mmetumikia kwa muda mrefu sana na hamjaendelea sana, hasa katika somo hili la kufanya kazi pamoja kwa maelewano hamjaendelea kabisa! Kuenda kwenye makanisa unawasiliana kwa njia yako, na yeye anafanya ushirika kwa njia yake. Kuna uratibu wa upatanifu kwa nadra sana. Na watu walio chini ambao wanafuata wako namna hii hata zaidi. Ambayo ni kusema kwamba ni watu wachache sana miongoni mwenu wanaelewa kumtumikia Mungu ni nini, au jinsi mtu anapaswa kumtumikia Mungu. Mmechanganyikiwa, na kuchukulia masomo ya aina hii kama suala dogo sana, kwa kiasi kwamba watu wengi hawatekelezi tu kipengele hiki cha ukweli, wanafanya mabaya kwa kujua. Hata watu ambao wametumikia kwa miaka mingi kwa kweli wanapigana na kugombana. Je! Hiki si kimo chako halisi? Ninyi watu mnaohudumu pamoja kila siku ni kama Waisraeli ambao walimtumikia Mungu Mwenyewe katika hekalu kila siku. Inawezekanaje kuwa ninyi watu ambao ni kama makuhani hamjui jinsi ya kushirikiana na jinsi ya kutumikia?
Wakati ule, Waisraeli walimtumikia Yehova moja kwa moja hekaluni. Utambulisho wao ulikuwa ule wa kuhani. (Bila shaka si kila mtu alikuwa kuhani. Ni baadhi tu waliomtumikia Yehova katika hekalu ndio walikuwa na utambulisho wa makuhani). Wangevalia taji ambazo Yehova aliwapa (ambayo inamaanisha walifanya taji kulingana na matakwa ya Yehova, sio kwamba Yehova aliwapa taji moja kwa moja) na wakiwa wamevalia mavazi yao ya kikuhani ambayo Yehova aliwapa wangeingia katika hekalu wakiwa miguu mitupu kumtumikia Yehova moja kwa moja, tangu asubuhi hadi usiku. Utumishi wao kwa Yehova haukuwa usio na mipangalio au wa kutenda makosawapendavyo; yote ilikuwa kulingana na sheria, ambazo hakuna mtu aliyemtumikia Yehova moja kwa moja angeweza kukiuka. Wote walipaswa kufuata sheria hizi; vinginevyo, kuingia hekaluni kulikatazwa. Ikiwa yeyote kati yao alivunja sheria za hekalu, yaani, kama mtu yeyote aliasi amri za Yehova, ilikuwa lazima apate kutendewa kulingana na sheria zilizotolewa na Yehova, na hakuna mtu aliyeruhusiwa kupinga, na hakuna mtu aliyeruhusiwa kumtetea. Haijalishi ni miaka mingapi ambayo mtu huyo alimtumikia Mungu, wote walipaswa kufuata sheria. Hii ndio sababu makuhani wengi walivalia nguo za kikuhani kila wakati na kumtumikia Yehova kwa njia hii mwaka mzima, ingawa Yehova hakuwatendea kwa njia yoyote maalum, na hata walikwenda mbele ya madhabahu au hekalu maisha yao yote. Hivyo ndivyo ulivyokuwa uaminifu wao na utii wao. Haishangazi kwamba Yehova aliwabariki kwa njia hii; ilikuwa yote kutokana na uaminifu wao kwamba walipata kibali na kuyaona matendo yote ya Yehova. Wakati ule ambapo Yehova alifanya kazi katika Israeli, watu Wake waliochaguliwa, matakwa Yake juu yao yalikuwa makali sana. Wote walikuwa watiifu sana na walizuiliwa na sheria, ambazo zilitumika kuwalinda ili kwamba wamheshimu Yehova. Hizi zote zilikuwa amri za utawala za Yehova. Ikiwa miongoni mwa wale makuhani kulikuwa na yeyote ambaye hakuishika Sabato au ambaye alikiuka amri za Yehova na aligunduliwa na watu wa kawaida, huyo mtu angeletwa mara moja mbele ya madhabahu na kupigwa kwa mawe hadi kufa, na hivyo kutolewa kama dhabihu mbele ya “madhabahu ya mtu wa kawaida” ambayo Yehova alikuwa Ameanzisha. Haikuruhusiwa kuweka maiti zao katika hekalu au karibu na hekalu. Yehova hakukubali hilo. Ikiwa mtu alifanya hivyo, angetendewa kama wale ambao hutoa “dhabihu za kawaida,” na kutupwa katika shimo kubwa na kuuawa. Bila shaka, watu wote kama hao wangepoteza maisha yao, hakuna aliyeachwa hai. Kulikuwa hata na wale ambao walitoa “moto wa kawaida,” kwa maneno mengine, wale watu ambao hawakutoa dhabihu katika siku zilizotolewa na Yehova wangeteketezwa na moto wa Yehova pamoja na vitu vyao vya dhabihu, hawaruhusiwa kubaki juu ya madhabahu. Mahitaji kwa makuhani yalikuwa: Hawakuruhusiwa kuingia hekaluni, na hata ua wa nje wa hekalu, bila ya kwanza kuosha miguu yao; hakuna kuingia hekaluni ikiwa hujavalia vazi za kikuhani; hakuna kuingia hekaluni ikiwa hujavalia taji za kikuhani; hakuna kuingia hekaluni ikiwa umechafuliwa na maiti; hakuna kuingia hekaluni baada ya kuugusa mkono wa mtu asiye haki bila ya kwanza kuosha mikono yake mwenyewe; hakuna kuingia hekaluni baada ya mahusiano ya ngono na wanawake (hii haikuwa milele, kwa muda wa miezi mitatu tu), hawakuruhusiwa kuuona uso wa Yehova, wakati ulipokuwa umeisha, ikimaanisha kwamba ni baada ya miezi mitatu tu ndio wangeweza kuruhusiwa kuvaa mavazi safi ya kikuhani, na kuhudumu katika ua wa nje kwa siku saba kabla ya kuweza kuingia katika hekalu ili kuuona uso wa Yehova; waliruhusiwa kuvaa mavazi yote ya kikuhani ndani ya hekalu tu na hawaruhusiwa kuyavaa nje ya hekalu, ili kuepuka kulichafua hekalu la Yehova; iliwapasa wote waliokuwa makuhani kuwaleta wahalifu ambao wamekiuka sheria za Yehova mbele ya madhabahu ya Yehova ambako wangeuawa na watu wa kawaida, vinginevyo moto ungeanguka juu ya kuhani ambaye alishuhudia. Kwa hiyo walikuwa waaminifu kwa Yehova daima, kwa sababu sheria za Yehova zilikuwa kali juu yao, na hawangeweza kabisa kuthubutu kukiuka kikawaida amri Zake za utawala. Waisraeli walikuwa waaminifu kwa Yehova kwa sababu walikuwa wameuona moto Wake, walikuwa wameuona mkono ambao Yehova alitumia kuwaadibu watu, na pia kwa sababu hapo awali walimheshimu Yehova mioyoni mwao. Kwa hivyo kile walichopata sio moto wa Yehova tu; pia walipata utunzaji na ulinzi kutoka kwa Yehova, na kupata baraka za Yehova. Uaminifu wao ni kwamba walifuata maneno ya Yehova katika yale waliyofanya, bila mtu yeyote kuasi. Ikiwa mtu yeyote angekosa kutii, watu bado wangetekeleza maneno ya Yehova, na kuwaua wale wote waliokwenda kinyume na Yehova, bila njia yoyote ya kuficha. Hasa wale ambao walikiuka Sabato, wale waliokuwa na hatia ya uasherati, na wale walioiba sadaka kwa Yehova wangeadhibiwa vikali zaidi. Wale ambao walikiuka Sabato waliuawa kwa mawe nao (watu wa kawaida), au walipigwa viboko hadi kufa, bila yeyote kuachwa. Wale waliofanya vitendo vya uasherati, hata wale waliomtamani mwanamke mzuri, au wale waliokuwa na mawazo ya kiasherati baada ya kumwona mwanamke mwovu, au waliokuwa na tamaa ya kimapenzi baada ya kumwona mwanamke mwenye umri mdogo—kila mtu wa aina hii angeuawa. Ikiwa mwanamke mdogo yeyote ambaye hakuvaa nguo ya kufunika au utaji alimjaribu mwanaume katika kitendo cha tabia mbaya, mwanamke huyo angeuawa. Ikiwa ilikuwa ni kuhani (wale watu ambao walihudumu katika hekalu) ndiye aliyekiuka sheria za aina hii, angesulubiwa au kunyongwa. Hakuna mtu wa aina hii angeweza kuruhusiwa kuishi, na hakuna hata mtu mmoja angeweza kupata kibali mbele za Yehova. Jamaa za mtu wa aina hii hawangeruhusiwa kutoa dhabihu kwa Yehova mbele ya madhabahu kwa miaka mitatu baada ya kifo chake, na hawangeruhusiwa kugawana dhabihu ambazo Yehova aliwapa watu wa kawaida. Wakati tu ulipopita ndio wangeweka ng’ombe au kondoo wa daraja la juu kwenye madhabahu ya Yehova. Ikiwa kulikuwa na kosa lingine lolote, walipaswa kufunga kwa siku tatu mbele za Yehova, wakiomba neema Yake. Kuabudu kwao Yehova hakukuwa tu kwa sababu sheria za Yehova zilikuwa kali sana na za shuruti sana; badala yake ilikuwa ni kwa sababu ya neema ya Yehova, na pia ilikuwa kwa sababu walikuwa waaminifu kwa Yehova. Hivyo, huduma yao hadi leo imekuwa ya uaminifu vilevile, na hawajawahi kuvunja maombi yao mbele ya Yehova. Katika siku hizi watu wa Israeli bado wanapata utunzaji na ulinzi wa Yehova, na hata leo Yehova bado ni neema kati yao, na daima hukaa nao. Wote wanajua jinsi wanapaswa kumheshimu Yehova, na jinsi wanapaswa kumtumikia Yehova, na wote wanajua jinsi wanapaswa kuwa ili kupokea na kulindwa na Yehova, kwa sababu wote wanamcha Yehova mioyoni mwao. Siri ya mafanikio ya huduma yao yote si nyingine isipokuwa uchaji. Lakini nyinyi nyote mko namna gani leo? Je! Mnafanana na watu wa Israeli kwa vyovyote? Je! unafikiri kwamba huduma ya leo ni kama kufuata uongozi wa kielelezo mkubwa wa kiroho? Hamna tu uaminifu na uchaji wowote. Mnapokea neema nyingi, nyinyi ni sawa na makuhani wa Israeli, kwa sababu nyote mnamtumikia Mungu moja kwa moja. Ingawa hamuingii hekaluni, yale mnayopokea na mnayoona ni mengi zaidi kuliko kile ambacho makuhani waliomtumikia Yehova katika hekalu walipokea. Lakini bado mnaasi na mnapinga mara nyingi kuliko walivyofanya. Uchaji wenu ni mdogo sana, na hivyo mnapokea neema ndogo sana. Ingawa mnajitolea kidogo sana, mmepata mengi zaidi kuliko Waisraeli hao. Je! Huku sio kuwatendea nyinyi kwa wema? Wakati wa kazi katika Israeli, hakuna mtu angethubutu kumhukumu Yehova kama alivyotaka. Na nyinyi je? Kama si kwa sababu kazi Ninayofanya miongoni mwenu ni kuwashinda, Ningewezeje kuvumilia kutenda kwenu ovyo ovyo kuliaibisha kwa jina Langu? Ikiwa enzi mnayoishi ingekuwa Enzi ya Sheria, hakuna hata mmoja wenu angekuwa hai, kutokana na matendo yenu na maneno yenu. Uchaji wenu ni mdogo sana! Nyinyi daima mnanilaumu kwa kutowapa kibali kikubwa, na hata kusema kuwa sikuwapa maneno ya baraka ya kutosha, kwamba Nina laana tu kwenu. Je, hamjui kwamba kwa uchaji mdogo hivyo haiwezekani kwenu kukubali baraka Zangu? Je! Hamjui kwamba Mimi huwalaani mara kwa mara na kuwahukumu kwa sababu ya hali mbovu ya huduma yenu? Je, ninyi nyote mnajihisi kuwa mmekosewa? Ninawezaje kuwapa baraka Zangu kikundi cha watu ambao ni waasi na hawatii? Ninawezaje kutoa neema Yangu kwa watu ambao huleta aibu kwa jina Langu? Matendo kwa nyinyi watu tayari ni yenye huruma sana. Ikiwa Waisraeli wangekuwa waasi kama mlivyo leo, Ningalikuwa Nimewaangamiza muda mrefu uliopita. Ilhali Mimi siwatendei kwa vyovyote ila kwa huruma. Je! Huu sio wema? Je! Mnataka baraka nyingi zaidi kuliko hii? Wale pekee ambao Yehova anawabariki ni wale wanaomheshimu Yeye. Yeye huwaadibu wale wanaoasi dhidi Yake, Hamsamehei mtu yeyote kamwe. Je, si ninyi watu wa leo ambao hamjui jinsi ya kutumikia mko na haja zaidi ya kuadibiwa na hukumu, ili mioyo yenu iweze kurekebishwa kikamilifu? Je, kuadibiwa na hukumu ya aina hii sio baraka bora zaidi kwenu? Je! Sio ulinzi wenu bora? Bila hiyo, je, yeyote kati yenu angeweza kuvumilia moto wa Yehova unaochoma? Ikiwa kweli mngetumikia kwa uaminifu kama watu wa Israeli, je, hamngekuwa pia na neema kama rafiki yenu daima? Je, hangekuwa pia na furaha na neema ya kutosha? Je, nyote mnajua jinsi mnapaswa kutumikia?
Leo mahitaji ya nyinyi kufanya kazi pamoja kwa upatanifu ni sawa na jinsi Yehova alivyowataka Waisraeli kumtumikia. Vinginevyo, tamatisha tu huduma yenu. Kwa sababu nyinyi ni watu wanaomtumikia Mungu moja kwa moja, kwa kiwango cha chini zaidi mnapaswa kuweza kuwa waaminifu na watiifu katika huduma yenu, na lazima muweze wa kujifunza masomo kwa njia ya vitendo. Hasa wale wanaofanya kazi kanisani, je, yeyote kati ya ndugu na dada walio chini angethubutu kushughulika na nyinyi? Je, mtu yeyote angethubutu kuwaambia makosa yenu uso kwa uso? Mko juu ya yote, nyinyi kweli mnatawala kama wafalme! Hata hamjifunzi au kuingia katika somo la matendo kama hilo, na bado mnazungumza juu ya kumtumikia Mungu! Kwa sasa unaulizwa kuongoza makanisa kadhaa, na sio tu kwamba unakata tamaa mwenyewe, hata unashikilia mawazo na maoni yako, na kusema mambo kama “Nadhani jambo hili linafaa lifanyike kwa njia hii, kwani Mungu amesema kuwa hatupaswi kuzuiwa na wengine, na kwamba siku hizi hatupaswi kutii kwa upofu.” Kwa hiyo kila mmoja anashikilia maoni yake mwenyewe, na hakuna mtu anayemtii mwingine. Ingawa unafahamu wazi kwamba huduma yako iko katika shida kubwa, bado unasema, “Vile ninavyoona, yangu haiko mbali sana. Kwa hali yoyote sisi kila mmoja ana upande mmoja; unazungumza kuhusu yako, na mimi kuhusu yangu; unashiriki kuhusu maono yako na ninazungumza juu ya kuingia kwangu.” Huchukui jukumu kwa vitu vingi ambavyo vinapaswa kushughulikiwa, au unamudu tu, kila mtu akieleza maoni yake mwenyewe, kwa busara akilinda hali yake mwenyewe, sifa na uso wake. Hakuna mtu aliye tayari kujinyenyekesha, hakuna mtu atakayejitoa kwa ari kumrekebisha mwingine na kurekebishwa ili maisha yaendelee kwa haraka zaidi. Mara chache sana wakati mnafanya kazi pamoja hakuna yeyote kati yenu atasema, Ningependa kukusikia ukishiriki na mimi kuhusu kipengele hiki cha ukweli, kwa sababu bado nina tashwishi kukihusu. Au kusema: una uzoefu zaidi kuliko mimi juu ya jambo hili; unaweza kunipa mwelekeo fulani, tafadhali? Je, si hii ingekuwa njia nzuri ya kufanya hivyo? Nyinyi mlio kwenye viwango vya juu husikia ukweli mwingi, na kuelewa mengi kuhusu huduma. Ikiwa ninyi watu ambao mnaratibu kufanya kazi katika makanisa hamjifunzi kutoka kwa kila mmoja, na kuwasiliana, kufidia mapungufu ya kila mmoja, mnaweza kujifunza masomo kutoka wapi? Mnapokutana na chochote, mnapaswa kushirikiana na kila mmoja, ili maisha yenu yaweze kufaidika. Na mnapaswa kushirikiana kwa makini kuhusu mambo ya aina yoyote kabla ya kufanya maamuzi. Ni kwa kufanya hivyo tu ndio mnakuwa na jukumu kwa kanisa na si kuwa wazembe. Baada ya kutembelea makanisa yote, mnapaswa kukutana na kushiriki juu ya masuala yote mnayotambua na matatizo mnayokabiliwa nayo kazini, na kuwasiliana kuhusu nuru na mwanga ambao mmepokea—huu ni utaratibu wa lazima wa huduma. Lazima mfikie ushirikiano wa upatanifu kwa kusudi la kazi ya Mungu, kwa manufaa ya kanisa, na kwa kuwachochea ndugu na dada kuendelea. Unashirikiana pamoja naye na anashirikiana na wewe, kila mmoja akimbadilisha mwingine, mkifikia matokeo bora ya kazi, ili kutunza mapenzi ya Mungu. Huu tu ndio ushirikiano wa kweli, na watu kama hao tu ndio wana kuingia kwa kweli. Kunaweza kuwa na hotuba fulani isiyofaa wakati wa ushirikiano, lakini hiyo haijalishi. Shirikiana juu yake baadaye, na mpate ufahamu wa wazi kulihusu; msipuuze suala hilo. Baada ya aina hii ya ushirika unaweza kufidia mapungufu kwa ndugu na dada. Ni kwa kuenda kwa kina zaidi tu kwa namna hii katika kazi yako ndio unaweza kufikia matokeo bora. Kila mmoja wenu, kama watu wanaohudumu, lazima muweze kulinda maslahi ya kanisa katika yote mnayofanya, badala ya kuwa macho kwa maslahi yako mwenyewe. Haikubaliki kufanya pekee yako, pale ambapo unamdharau naye anakudharau. Watu wanaotenda kwa njia hii hawafai kumhudumia Mungu! Tabia ya mtu wa aina hii ni mbaya sana; hakuna hata kiasi kidogo cha ubinadamu bado kimebaki ndani yake. Yeye ni Shetani asilimia mia moja! Yeye ni mnyama! Hata sasa mambo kama haya bado yanatokea kati yenu, kwenda mpaka kushambuliana wakati wa ushirika, kutafuta visingizio kwa makusudi, kukasirika mkibishana juu ya jambo fulani dogo, hakuna mtu aliye radhi kujitenga, kila mtu akificha kilicho ndani kutoka kwa mwingine, akimwangalia mwingine na makini na kuwa macho. Je! Tabia ya aina hii ni huduma inayofaa kwa Mungu? Je, kazi kama hiyo yenu inaweza kuwakimu ndugu na dada? Sio tu kuwa huwezi kuwaongoza watu kwenye njia sahihi ya maisha, kwa kweli unaingiza tabia zako za upotovu ndani ya ndugu na dada. Je! Huwaumizi wengine? Dhamiri yako ni mbaya sana, iliyooza kabisa! Huingii katika ukweli, na huutii ukweli katika vitendo. Zaidi ya hayo, bila haya unaonyesha hadharani asili yako ya mbovu sana kwa watu wengine, huoni aibu hata kidogo! Ndugu na dada wamekabidhiwa kwako, lakini unawapeleka kuzimu. Je, si wewe ni mtu ambaye dhamiri yake imeoza? Huna aibu kabisa!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumamosi, 16 Machi 2019

Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

Mwenyezi Mungu alisema, Mnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu. Ikiwa unamwamini tu Mungu lakini humpendi, hujapata ufahamu wa Mungu, na hujawahi kumpenda Mungu kwa upendo wa kweli utokao moyoni mwako, basi imani yako kwa Mungu ni bure; kama katika imani yako kwa Mungu humpendi Mungu, basi unaishi bure, na maisha yako yote ndiyo ya duni zaidi kwa maisha yote. Ikiwa katika maisha yako yote hujawahi kumpenda au kumtosheleza Mungu, basi kuna haja gani ya kuishi? Kuna haja gani ya imani yako kwa Mungu? Huku si kuharibu nguvu? Hii ni kusema, kama watu wanataka kuamini na kumpenda Mungu, ni sharti wagharamike. Badala ya kujaribu kuenenda kwa namna fulani kwa nje tu, wanapaswa watafute utambuzi wa kweli kutoka ndani ya mioyo yao. Ikiwa unapenda sana kuimba na kucheza lakini huwezi kuonyesha ukweli katika vitendo, unaweza kusemekana kwamba unampenda Mungu? Kumpenda Mungu kunahitaji utafutaji wa mapenzi ya Mungu katika mambo yote, na kwamba ujisaili wewe mwenyewe kwa kina jambo lolote likikutokea, kujaribu kujua mapenzi ya Mungu na kujaribu kuona mapenzi ya Mungu ni yapi katika suala hili, Anataka ufanikishe nini, na ni jinsi gani utayajali mapenzi Yake? Kwa mfano: jambo fulani linafanyika linalokutaka uvumilie hali ngumu, wakati huo unapaswa ufahamu ni nini mapenzi ya Mungu, na ni jinsi gani unapaswa kuyajali mapenzi ya Mungu. Usijiridhishe mwenyewe: Jiweke kando kwanza. Hakuna kitu kilicho duni kuliko mwili. Ni lazima udhamirie kumridhisha Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako. Katika mawazo kama hayo, Mungu atakupa nuru ya kipekee katika jambo hili, na moyo wako pia utapata faraja. Jambo lolote likikutendekea, liwe dogo au kubwa, ni sharti kwanza ujiweke pembeni na kuuona mwili kama kitu duni zaidi kuliko vitu vyote. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo unavyochukua uhuru zaidi; ukiuridhisha mara hii, wakati mwingine utataka zaidi, na jinsi hili linaendelea, ndivyo unapata kuupenda mwili hata zaidi. Mwili mara zote una tamaa kupita kiasi, mara zote mwili unakutaka uuridhishe, na kwamba uutosheleze kwa ndani, iwe ni katika chakula unachokula, unachokivaa, au kuwa na hasira katika matendo yako, au kuushawishi udhaifu na uzembe wako… Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo tamaa yake inaongezeka, na jinsi mwili unavyopotoka zaidi, hadi kufikia kiwango ambacho miili ya watu inahodhi dhana nzito, na kutomtii Mungu, na kujiinua, na kuanza kuishuku kazi ya Mungu. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo udhaifu wa mwili unavyokuwa mkubwa; daima utahisi kuwa hakuna anayekuonea huruma kwa udhaifu wako, daima utaamini kuwa Mungu amezidi sana, na utasema: Mungu anawezaje kuwa mkali namna hii? Ni kwa nini Hawezi kuwapa watu nafasi? Watu wakiudekeza sana mwili, na kuupenda kupindukia, basi watajiponza wao wenyewe. Ikiwa unampenda Mungu kwa dhati, na huuridhishi mwili, basi utaona kuwa kila anachokifanya Mungu ni chenye haki sana, na kizuri sana, na kwamba laana Yake kwa uasi wako na hukumu ya udhalimu wako ni haki. Zitakuwepo nyakati ambapo Mungu atakurudi na kukufundisha nidhamu, na kuanzisha mazingira ya kukukasirisha, na kukushurutisha uje mbele Zake—na daima utahisi kuwa anachokifanya Mungu ni cha ajabu. Hivyo utahisi kana kwamba hakuna uchungu mwingi, na kwamba Mungu anapendeza. Ukifuata udhaifu wa mwili, na kusema kwamba Mungu amezidi, basi daima utahisi uchungu na daima utahuzunika, na utakosa uwazi kuhusu kazi yote ya Mungu na itaonekana kana kwamba Mungu hana huruma kwa udhaifu wa mwanadamu, na Hatambui shida za mwanadamu. Hivyo utajihisi mnyonge na mpweke, kana kwamba umekumbwa na dhuluma kubwa, na wakati huo utaanza kulalama. Kadiri unavyoutosheleza udhaifu wa mwili, ndivyo unavyohisi kuwa Mungu anazidi, hadi inakuwa mbaya kiasi kwamba unaikana kazi ya Mungu, na kuanza kumpinga Mungu na kujaa uasi. Hivyo unafaa kuuasi mwili na usiutosheleze: “Mume wangu(mke), watoto, matarajio, ndoa, familia—hakuna hata moja kati ya haya ambalo ni la thamani! Moyoni mwangu mna Mungu pekee na nitajaribu kumridhisha Mungu kadiri ya uwezo wangu, na si kuuridhisha mwili.” Lazima uwe na azimio hili. Daima ukiwa na azimio hili, basi ukiuweka ukweli katika vitendo, na kujiweka kando, utaweza kufanya hivyo kwa juhudi kidogo. Inasemekana kuwa kulikuwepo na mkulima aliyeona nyoka barabarani aliyekuwa ameganda. Huyu mkulima alimchukua yule nyoka na kumweka kifuani mwake, na baada ya yule nyoka kuamka alimuuma yule mkulima hadi akafa. Miili ya wanadamu ni kama yule nyoka: asili yake ni kuyadhuru maisha yao—na ikipata mbinu yake kikamilifu, maisha yako yanapotea. Mwili ni wa Shetani. Kuna tamaa kupita kiasi ndani yake, hujithamini wenyewe, unafurahia faraja, na kushangilia burudani, kujiachilia katika uvivu na uzembe, na baada ya kuuridhisha kwa kiwango fulani mwishowe utakuangamiza. Hivi ni kusema, ukiuridhisha sasa, wakati mwingine utakuomba zaidi. Daima mwili una tamaa na matakwa kupita kiasi, na unajinufaisha kutokana na wewe kuutosheleza mwili na kukufanya uufurahie hata zaidi na kuishi katika starehe zake—na ikiwa hutaushinda, mwishowe utajipotosha. Iwapo utapata uzima mbele za Mungu, na namna hatima yako itakavyokuwa, inategemea uasi wako dhidi ya mwili utakuwa wa namna gani. Mungu amekuokoa, na kukuteua na kukuamulia kabla, bado ikiwa leo hauko radhi kumridhisha, hauko radhi kuuweka ukweli katika vitendo, hauko radhi kuuasi mwili wako kwa moyo umpendao Mungu kwa dhati, hatimaye utajiangamiza mwenyewe, na kwa hivyo utapitia mateso mengi. Ikiwa mara zote unautosheleza mwili, Shetani atakumeza hatua kwa hatua, na kukuacha bila uzima, au upako wa Roho, hadi siku itafika ambayo ndani utakuwa giza. Ukiishi katika giza, utakuwa umetekwa nyara na Shetani, hutakuwa na Mungu tena moyoni mwako, na wakati ule utaukataa uwepo wa Mungu na kumwacha. Kwa hivyo, ikiwa unataka kumpenda Mungu, ni lazima ulipe gharama ya uchungu na kupitia shida. Hakuna haja ya hamasa za nje na shida, kusoma zaidi na kuzungukazunguka zaidi; badala yake, unafaa kuweka kando vitu vilivyomo ndani yako: mawazo kupita kiasi, maslahi ya kibinafsi, na masuala yako binafsi, dhana, na motisha. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.
Ushughulikiaji wa Mungu juu ya tabia za nje za watu ni sehemu moja ya kazi Yake; kwa mfano, kushughulikia ubinadamu wa watu wa nje, usiokuwa wa kawaida, au maisha na tabia zao, njia na desturi zao, na vilevile vitendo vyao vya nje, na hamasa zao. Lakini Anapowataka watu wauweke ukweli katika vitendo na wabadilishe tabia zao, kimsingi kinachoshughulikiwa hapa ni motisha na mawazo yaliyo ndani yao. Kushughulikia tabia zako za nje tu si kugumu; ni sawa na kukukataza kula vitu uvipendavyo, jambo ambalo ni rahisi. Kinachogusia dhana zilizo ndani yako, hata hivyo, si rahisi kukiachia: inakuhitaji uuasi mwili wako, na kulipa gharama, na kuteseka mbele za Mungu. Hii ndiyo hali hasa katika motisha za watu. Tangu wakati wa imani yao kwa Mungu mpaka leo, watu wamekuwa na motisha ambazo si sahihi. Wakati ambapo huweki ukweli katika vitendo, unahisi kuwa motisha zako ni sahihi, lakini jambo likikutokea, utaona kuwa kuna motisha nyingi ndani zisizo sahihi. Hivyo, Mungu akiwafanya watu kuwa wakamilifu, Anawafanya kugundua kuwa kuna dhana nyingi ndani yao ambazo zinawazuia kumfahamu Mungu. Ukitambua kuwa motisha zako zina makosa, kama unaweza kuacha kutenda kulingana na motisha na dhana zako, na unaweza kuwa na ushuhuda wa Mungu na kusimama imara katika msimamo wako kwa kila lifanyikalo kwako, hili linathibitisha kuwa umeuasi mwili wako. Ukiasi dhidi ya mwili wako, bila shaka kutakuwa na vita ndani yako. Shetani atajaribu kufanya watu kuifuata, atajaribu kuwafanya wafuate dhana za kimwili na kutekeleza maslahi ya kimwili—ila maneno ya Mungu yatawapa nuru watu na kuwaangazia kwa ndani, na wakati huu itakuwa juu yako ikiwa utamfuata Mungu au utamfuata Shetani. Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu huwagusa watu ndani ya mioyo yao, na kuwapa nuru na mwangaza. Kwa hivyo katika tukio lolote katika vita: Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie. Kwa sababu motisha nyingi ndani ya watu zina makosa, ama kwa sababu kazi kubwa ya Mungu inakinzana na dhana zao, watu wakiuweka ukweli katika vitendo vita vikali huzuka kisirisiri. Baada ya kuuweka huu ukweli katika vitendo, kisirisiri watu watakuwa wamemwaga machozi mengi sana ya huzuni kabla ya kuamua kumridhisha Mungu. Ni kwa sababu ya vita hivi watu huvumilia shida na usafishaji; huku ni kuteseka kwa kweli. Vita vikikukabili, kama unaweza kusimama kweli upande wa Mungu, utaweza kumridhisha. Kuteseka katika harakati ya kutenda ukweli hakuepukiki; ikiwa, wanapoweka ukweli katika vitendo, kila kitu ndani yao kingekuwa sawa, basi wasingehitaji kufanywa wakamilifu na Mungu, na kusingekuwa na vita, na hawangeteseka. Ni kwa sababu kuna mambo mengi ndani ya watu ndipo hawafai kutumiwa na Mungu, na tabia nyingi za uasi wa mwili, ndipo watu wanapaswa kujifunza funzo la kuasi dhidi ya mwili kwa kina zaidi. Huku ndiko Mungu anaita kuteseka ambako Alimtaka mwanadamu kushiriki Naye. Ukikumbana na shida, fanya hima na umwombe Mungu: Ee Mungu! Ninataka kukuridhisha, ninataka kustahimili mateso ya mwisho ili kuuridhisha moyo Wako, na bila kujali kuwa vikwazo ninavyokumbana navyo ni vikubwa kiasi gani, bado ni sharti nikuridhishe. Hata ikiwa ni kuyatoa maisha yangu yote, bado ni sharti nikuridhishe! Ukiomba na hili azimio utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako. Kila wawekapo ukweli katika vitendo, kila wapitiapo usafishaji, kila wanapojaribiwa, na kila wakati kazi ya Mungu inapowashukia, watu wanapitia mateso makubwa. Haya yote ni mtihani wa watu, na kwa hivyo ndani yao wote mna vita. Hii ndiyo gharama hasa wanayolipa. Kusoma zaidi neno la Mungu na kuzungukazunguka zaidi, kwa namna fulani ni gharama. Ndiyo watu wanapaswa kufanya, ndio wajibu wao, na jukumu ambalo ni sharti walitimize, lakini ni lazima watu waweke kando yale yanayofaa kuwekwa kando. Ikiwa hamwezi, basi haijalishi mateso yako yatakuwa makubwa kiasi gani, na utazunguka kiasi gani, yote yatakuwa bure! Hivi ni kusema, ni mabadiliko ndani yako tu yanaweza kuamua iwapo mateso yako ya nje yana thamani. Tabia yako ya ndani ikibadilika na ikiwa umeweka ukweli katika vitendo, basi mateso yako yote ya nje yatapata kibali cha Mungu; ikiwa hakujakuwa na mabadiliko katika tabia yako ya ndani, basi haijalishi unateseka kiasi gani au unazungukazunguka kiasi gani nje, hakutakuwa na kibali kutoka kwa Mungu—na mateso ambayo hayajaidhinishwa na Mungu ni bure! Hivyo, kama gharama ambayo umelipa imedhinishwa na Mungu inaamuliwa na kama umekuwa na mabadiliko ndani yako au la, na kama unatia ukweli katika vitendo na kuasi dhidi ya motisha na dhana zako mwenyewe ili kupata ridhaa ya mapenzi ya Mungu, ufahamu wa Mungu, na uaminifu kwa Mungu. Haijalishi unazungukazunguka kiasi gani, ikiwa hujawahi kujua kuasi dhidi ya motisha zako, unatafuta tu matendo na hamasa za nje, na usitilie maanani maisha yako, basi taabu zako zitakuwa zimepita bure. Ikiwa una kitu unachotaka kusema katika mazingira fulani, ila kwa ndani huhisi ni sawa, kwamba hakina faida kwa ndugu na dada zako, na kinaweza kuwadhuru, basi na usikiseme, uchague kuumia kwa ndani, kwa kuwa haya maneno hayawezi kuridhisha mapenzi ya Mungu. Wakati huu, kutakuwa na vita ndani yako, lakini utakuwa tayari kuumia na kuviacha uvipendavyo, utakuwa radhi kustahimili haya mateso ili kumridhisha Mungu na ingawa utaumia kwa ndani, hutautosheleza mwili, na moyo wa Mungu utakuwa umeridhishwa, hivyo utafarijika kwa ndani. Kwa hakika huku ni kulipa gharama, na ndiyo gharama inayotakiwa na Mungu. Ukitenda kwa njia hii, kwa hakika Mungu atakubariki; ikiwa huwezi kulifanikisha hili, basi haijalishi unaelewa kiasi gani, au unaweza kunena vyema kiasi gani, yote haya hayatafaa kitu! Katika njia ya kumpenda Mungu, ikiwa unaweza kusimama upande wa Mungu anapopigana na Shetani, na usimgeukie Shetani, basi utakuwa umefanikisha mapenzi ya Mungu, na utakuwa umesimama imara katika ushuhuda wako.
Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. Kwa mfano, ikiwa unawabagua ndugu na dada zako, utakuwa na maneno ambayo unataka kusema—maneno unayohisi huenda yasimpendeze Mungu—lakini usipoyasema, utahisi kutoridhika ndani, na kwa wakati huu vita vitazuka ndani yako: “Niseme au nisiseme?” Hivi ndivyo vita. Kwa hivyo, katika kila jambo unalopitia kuna vita, na wakati kuna vita ndani yako, kutokana na ushirikiano wako na kuteseka kwako, Mungu anafanya kazi ndani yako. Hatimaye unaweza kuliweka kando jambo lenyewe na ghadhabu yako inazimika. Hiyo ndiyo athari ya ushirika wako na Mungu. Kila kitu wafanyacho watu kinawahitaji kulipa gharama fulani katika juhudi zao. Bila taabu ya kweli, hawawezi kumridhisha Mungu, hata hawakaribii kumridhisha Mungu, na wanarusha tu maneno matupu! Je, haya maneno matupu yaweza kumridhisha Mungu? Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda. Kwa nje yataonekana kama mambo madogo; lakini haya mambo yakitendeka huonyesha kama unampenda Mungu au la. Ikiwa unampenda, utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako Kwake, na ikiwa hujaweka upendo Wake katika vitendo, hili linaonyesha kuwa wewe si Mtu ambaye anapenda kuuweka ukweli katika vitendo, kwamba huna ukweli, huna uzima, kuwa wewe ni makapi! Mambo huwatokea watu wakati Mungu anawataka wasimame imara katika ushuhuda wao Kwake. Hakuna kubwa lililokutendekea kwa sasa, na huna ushuhuda mkubwa, lakini kila chembe ya maisha yako ya kila siku inahusiana na ushuhuda kwa Mungu. Ikiwa utawavutia ndugu na dada zako, wanafamilia, na kila aliye karibu nawe; ikiwa siku moja wasioamini watakuja na wavutiwe na yote unenayo na utendayo, na kuona kuwa yote afanyayo Mungu ni ya ajabu, basi utakuwa umekuwa na ushuhuda. Ijapokuwa huna ufahamu na wewe si mwerevu sasa, kupitia kwa kufanywa mkamilifu na Mungu, unaweza kumridhisha na kuzingatia mapenzi Yake. Wengine wataona kazi Yake kubwa miongoni mwa wasio werevu. Watu huja kumjua Mungu na huwa washindi mbele ya Shetani na waaminifu kwa Mungu kwa kiwango fulani. Hakuna atakayekuwa na uthabiti kuliko hili kundi la watu. Huu utakuwa ushuhuda mkubwa zaidi. Ijapokuwa huwezi kufanya kazi kubwa, unaweza kumridhisha Mungu. Wengine hawawezi kuyaacha mawazo yao, ila wewe unaweza; wengine hawawezi kuwa na ushuhuda kwa Mungu wakati wa mapito yao ya kweli, ila unaweza kutumia hadhi na matendo yako ya kweli kulipia mapenzi ya Mungu na kuwa na ushuhuda mkubwa Kwake. Hili ndilo huhesabika kama mapenzi ya kweli kwa Mungu. Ikiwa huliwezi hili, basi hutoi ushuhuda miongoni mwa jamaa zako, miongoni mwa ndugu zako, miongoni mwa dada zako, au mbele ya walimwengu. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda mbele ya Shetani, Shetani atakucheka, atakuchukulia kama mzaha, mwanasesere, mara kwa mara atakuchezea na kukughadhibisha. Majaribu mengi yatakupata siku za usoni—lakini ikiwa leo unampenda Mungu kwa moyo wa dhati, na ikiwa haijalishi ukubwa wa majaribu yaliyo mbele, bila kujali unachokipitia, unaweza kusimama imara katika ushuhuda wako, na kuweza kumridhisha Mungu, basi moyo wako utafarijiwa, na utakuwa jasiri hata majaribu utakayokabiliana nayo siku za usoni yawe makubwa kiasi gani. Hamwezi kuona ni nini kitatendeka siku za usoni; mnaweza tu kuridhisha Mungu katika hali ya leo. Hamwezi kufanya kazi yoyote kubwa, na unafaa kulenga kumridhisha Mungu kwa kuyapitia maneno yake katika maisha halisi, na kuwa na ushuhuda thabiti na mzito ambao unamtia aibu Shetani. Japo mwili wako hautaridhishwa na utateseka, utakuwa umemridhisha Mungu na kumletea aibu Shetani. Ikiwa daima unatenda hivi, Mungu atakufungulia njia mbele yako. Na siku moja, jaribio kubwa likija, wengine wataanguka chini, ila utaweza kuendelea kusimama imara: kwa sababu ya gharama uliyolipa, Mungu atakulinda ili usimame imara na usianguke. Kwa kawaida, ikiwa unaweza kuweka ukweli katika vitendo na kumridhisha Mungu kwa moyo ambao unampenda kweli, kwa hakika Mungu atakulinda wakati wa majaribu ya siku zijazo. Japokuwa wewe ni mpumbavu na mwenye kimo cha chini na usiye mwerevu, Mungu hatakubagua. Inategemea iwapo motisha zako ni za haki. Unaweza kumridhisha Mungu leo, iwapo uko makini na masuala madogo, unamridhisha Mungu kwa mambo yote, una moyo unaompenda Mungu kwa dhati, unampa Mungu moyo wa dhati, na japokuwa kuna baadhi ya mambo ambayo huwezi kuelewa, unaweza kwenda mbele za Mungu kurekebisha motisha zako, na kuyafuata mapenzi ya Mungu, na kufanya kila lipaswalo kumridhisha Mungu. Pengine ndugu na dada zako wataachana nawe, lakini moyo wako utakuwa unamridhisha Mungu, na hutatamani raha za mwili. Ikiwa daima unatenda kwa namna hii, utalindwa majaribu yakikusibu.
Majaribu haya yanailenga hali gani ya ndani ya watu? Yanalenga tabia ya uasi ndani ya watu ambayo haiwezi kumridhisha Mungu. Kuna mengi ambayo ni machafu ndani ya watu, na mengi ambayo ni ya unafiki, na kwa hivyo Mungu anawatia katika majaribu ili kuwasafisha. Lakini, ikiwa leo unaweza kumridhisha, basi majaribu ya siku zijazo yatakuwa ukamilifu kwako. Ikiwa leo, huwezi kumridhisha Mungu, basi majaribu ya siku za usoni yatakushawishi, na utaanguka bila kujua, na wakati huo hutaweza kujisaidia mwenyewe, kwani huendani na kazi ya Mungu, na huna kimo halisi. Na kwa hivyo, kama unataka kuweza kusimama imara katika siku za usoni, kumridhisha vyema Mungu, na kumfuata hadi mwisho, unapaswa kujenga msingi thabiti leo, unafaa kumridhisha Mungu kwa kutia ukweli katika vitendo kwa kila jambo, na kuzingatia mapenzi Yake. Iwapo daima unatenda kwa namna hii, kutakuwa na msingi ndani yako, na Mungu atahamasisha ndani yako moyo unaompenda, na Atakupa imani. Siku moja ambapo majaribu yatakuwa yamekukumba kwa kweli, ijapo utaumia, na kuhisi umedhulumiwa kwa kiwango fulani, na kuwa na huzuni kubwa, kana kwamba ulikuwa umekufa—ila mapenzi yako kwa Mungu hayatabadilika, na yataongezeka zaidi. Hizo ni baraka za Mungu. Ikiwa unaweza kumkubali Mungu na yote asemayo na atendayo leo kwa moyo mtiifu, basi kwa hakika utabarikiwa na Mungu, na kwa hivyo utakuwa mtu aliyebarikiwa na Mungu, na anayepokea ahadi Yake. Ikiwa leo hutendi, siku ambayo majaribu yatakukumba utakosa imani au moyo wenye mapenzi, na wakati huo jaribu litakuwa kishawishi; utatoswa ndani ya kishawishi cha Shetani na hutapata namna ya kuponyoka. Leo, unaweza kusimama imara jaribio dogo likikukabili, ila huenda usiweze kusimama imara siku ambayo jaribio kubwa litakukumba. Baadhi ya watu hujivuna, na kufikiri kwamba wako karibu na ukamilifu. Ikiwa huzami zaidi wakati huo, na kuridhika, basi utakuwa hatarini. Leo, Mungu hafanyi kazi ya majaribu makubwa, kwa kuonekana, kila kitu kiko salama, ila Mungu atakapokujaribu, utagundua kuwa umepungukiwa sana, kwani kimo chako ni kidogo mno, na huna uwezo wa kustahimili majaribu mazito. Ikiwa leo, hutasonga mbele, ukibaki katika hatua ile ile, basi dhoruba nzito ikija utaanguka. Mara nyingi inafaa mtazame udogo wa kimo chenu; mtapiga hatua kwa njia hii tu. Ikiwa unauona udogo wa ukomavu wako wakati wa majaribu tu, kwamba kimo chako ni dhaifu, kwamba kuna kidogo sana ndani yako ambacho ni halisi, na kwamba hutoshi kwa mapenzi ya Mungu—na kama utagundua haya wakati wa majaribu tu, utakuwa umechelewa mno.
Ikiwa hujui tabia ya Mungu, bila shaka utaanguka wakati wa majaribu, kwa kuwa hufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu kuwa wakamilifu, na ni kwa njia gani Huwafanya wakamilifu, na majaribu ya Mungu yakikushukia na yasilingane na mawazo yako, utashindwa kusimama imara. Upendo wa kweli wa Mungu ni tabia Yake kamili, na tabia kamili ya Mungu ikionyeshwa kwako, hili linakuletea nini mwilini mwako? Tabia ya haki ya Mungu ikionyeshwa kwako, bila shaka mwili wako utapata uchungu mkubwa. Iwapo hutapata haya maumivu, basi huwezi kufanywa mkamilifu na Mungu, wala huwezi kumpa Mungu mapenzi ya kweli. Mungu akikufanya mkamilifu kwa hakika atakuonyesha tabia Yake kamili. Tangu uumbaji hadi leo, Mungu hajawahi kuonyesha tabia Yake kamili—ila katika siku za mwisho Anaifichua kwa hili kundi la watu ambao Aliwateua awali na kuwachagua, na kwa kuwafanya watu wakamilifu, Anaiweka wazi tabia Yake, na kupitia kwayo Analifanya kamili kundi la watu. Huo ndio upendo wa kweli wa Mungu kwa watu. Kuyapitia mapenzi ya kweli ya Mungu kunawapasa watu wastahimili uchungu mkali, na kulipa gharama kubwa. Ni baada tu ya hili ndipo watapatikana na Mungu na waweze kutoa tena mapenzi ya kweli kwa Mungu, na ni hapo tu ndipo Moyo wa Mungu utaridhishwa. Ikiwa watu wanataka wafanywe wakamilifu na Mungu, na kama wanataka kufanya na mapenzi Yake, na kumpa Mungu mapenzi yao ya dhati kikamilifu, ni sharti wapitie mateso mengi na maumivu makali kutokana na hali hizo, kupata uchungu mkali kuliko mauti, hatimaye watashurutishwa kuirejesha mioyo yao ya kweli kwa Mungu. Ikiwa mtu anampenda Mungu kwa dhati au la, itafichuliwa wakati wa shida na usafishaji. Mungu hutakasa mapenzi ya watu, na hili vilevile hupatikana tu ndani ya shida na usafishaji.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili