Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatano, 6 Machi 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote”

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote”

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Waisraeli pekee, na Yeye si Mungu wa Wayahudi pekee; Yeye ni Mungu wa viumbe vyote. … Kazi Yake ya awali ilifanywa Yudea, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uzinduzi wa enzi hata kidogo. Hatua ya mwisho ya kazi Yake haifanywi tu miongoni mwa watu wa mataifa yasiyo ya Kiyahudi; hata zaidi ya hayo, inafanywa miongoni mwa watu waliolaaniwa. Jambo hili moja ndio ushahidi unaoweza zaidi kumwaibisha Shetani; hivyo, Mungu “anakuwa” Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni na kuwa Bwana wa vitu vyote, Anayeabudiwa na kila kiumbe mwenye uhai.”
Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Yudea. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyoondoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Waisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Waisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Yudea, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi pekee, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Waisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaowakomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Waisraeli pekee, na Yeye si Mungu wa Wayahudi pekee; Yeye ni Mungu wa viumbe vyote. Hatua mbili za awali za kazi Yake zilifanyika Israeli, na kwa njia hii, dhana zingine zimejitokeza ndani ya watu. Watu wanafikiri kuwa Yehova alikuwa akifanya kazi Israeli na Yesu Mwenyewe alitekeleza kazi Yake Yudea—zaidi ya hayo, ilikuwa kupitia kupata mwili ambapo Alikuwa akifanya kazi Yudea—na kwa vyovyote, kazi hii haikuenea zaidi ya Israeli. Hakuwa akifanya kazi na Wamisri; Hakuwa akifanya kazi na Wahindi; Alikuwa tu akifanya kazi na Waisraeli. Watu basi wanaunda dhana mbalimbali; aidha, wanapanga kazi ya Mungu ndani ya eneo fulani. Wanasema kwamba wakati Mungu anafanya kazi, ni lazima ifanywe miongoni mwa wateule na ndani ya Israeli; mbali na Waisraeli, Mungu hana mpokeaji mwingine wa kazi Yake, wala Hana eneo lingine la kazi Yake; ni wakali hasa katika “kumfundisha nidhamu” Mungu mwenye mwili, kutomruhusu kuenda zaidi ya eneo la Israeli. Je, hizi zote si dhana za binadamu? Mungu aliunda mbingu na dunia yote na vitu vyote, na kuumba viumbe vyote; Angewezaje kuzuia kazi Yake ndani ya Israeli peke yake? Katika hali hiyo, kungekuwa na haja gani ya Yeye kuumba viumbe Vyake vyote? Aliiumba dunia nzima; Ametekeleza mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita sio tu ndani ya Israeli lakini pia na kila mtu ulimwenguni. Bila kujali kama anaishi Uchina, Amerika, Uingereza ama Urusi, kila mtu ni wa ukoo wa Adamu; wote wameumbwa na Mungu. Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuondoka katika mawanda ya viumbe wa Mungu, na hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuepuka utambulisho wa “ukoo wa Adamu.” Wote ni viumbe wa Mungu, na wote ni wa ukoo wa Adamu; pia ni wazawa wapotovu wa Adamu na Hawa. Sio tu Waisraeli ambao ni viumbe wa Mungu, lakini ni watu wote; hata hivyo, wengine miongoni mwa viumbe wamelaaniwa, na wengine wamebarikiwa. Kuna mambo mengi ya kupendeza kuwahusu Waisraeli; Mungu awali alikuwa akifanya kazi nao kwa sababu walikuwa watu wapotovu kwa kiasi kidogo zaidi. Wachina ni dhaifu wakilinganishwa nao, na hawawezi hata kutumaini kulingana nao; hivyo, Mungu awali alifanya kazi miongoni mwa watu wa Israeli, na hatua ya pili ya kazi Yake ilifanywa tu Yudea. Kwa sababu hii, watu huunda dhana nyingi na kanuni nyingi. Kwa kweli, iwapo Angetenda kulingana na dhana za binadamu, Mungu angekuwa tu Mungu wa Waisraeli; kwa njia hii Asingeweza kupanua kazi Yake katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, kwa sababu Angekuwa tu Mungu wa Waisraeli badala ya Mungu wa viumbe vyote. Unabii ulisema kuwa jina la Yehova lingekuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na kuwa jina la Yehova lingeenezwa kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi—mbona ulisema hivi? Iwapo Mungu angekuwa Mungu wa Waisraeli tu, basi Angefanya kazi tu Israeli. Zaidi ya hayo, Asingepanua kazi hii, na Asingefanya huu unabii. Kwa sababu Alifanya huu unabii, Angehitaji kuipanua kazi Yake hadi mataifa yasiyo ya Kiyahudi na hadi kila taifa na mahali. Kwa sababu Alisema hili, basi Angefanya hivyo. Huu ndio mpango Wake, kwani Yeye ndiye Bwana aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote, na Mungu wa viumbe vyote. Bila kujali iwapo Anafanya kazi na Waisraeli ama katika Yudea nzima, kazi Anayoifanya ni kazi ya ulimwengu mzima na kazi ya binadamu wote. Kazi Anayoifanya leo katika taifa la joka kubwa jekundu—katika taifa lisilo la Kiyahudi—bado ni kazi ya binadamu wote. Israeli inaweza kuwa kituo cha kazi Yake duniani; vivyo hivyo, Uchina pia inaweza kuwa kituo cha kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Je, sasa Hajatimiza unabii kwamba “jina la Yehova litakuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi”? Hatua ya kwanza ya kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi inahusu kazi hii Anayoifanya katika taifa la joka kuu jekundu. Kwa Mungu mwenye mwili kufanya kazi katika nchi hii na kufanya kazi miongoni mwa hawa watu waliolaaniwa hasa inaenda kinyume na dhana za binadamu; hawa watu ni wa chini zaidi na wasio na thamani yoyote. Hawa wote ni watu ambao Yehova alikuwa amewaacha mwanzoni. Watu wanaweza kuachwa na watu wengine, lakini wakiachwa na Mungu, hawa watu hawatakuwa na hadhi, na watakuwa na thamani ya kiwango cha chini zaidi. Kama sehemu ya viumbe, kumilikiwa na Shetani ama kuachwa na watu wengine yote mawili ni mambo machungu, lakini sehemu ya viumbe ikiachwa na Bwana wa viumbe, hii inaashiria kwamba hadhi yake iko katika kiwango cha chini kabisa. Wazawa wa Moabu walilaaniwa, na walizaliwa ndani ya nchi hii isiyo na maendeleo; bila shaka, wazawa wa Moabu ni watu walio na hadhi ya chini zaidi chini ya ushawishi wa giza. Kwa sababu hawa watu walimiliki hadhi ya chini zaidi zamani, kazi inayofanywa miongoni mwao inaweza kabisa kuzivunja dhana za binadamu, na pia ni kazi yenye faida kubwa zaidi kwa mpango Wake mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita. Ili Afanye kazi miongoni mwa watu hawa ni kitendo kinachoweza zaidi kuzivunja dhana za binadamu; Akiwa na hili Anazindua enzi; na hili Anavunja dhana zote za binadamu; Akiwa na hili Anatamatisha kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kazi Yake ya awali ilifanywa Yudea, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uzinduzi wa enzi hata kidogo. Hatua ya mwisho ya kazi Yake haifanywi tu miongoni mwa watu wa mataifa yasiyo ya Kiyahudi; hata zaidi ya hayo, inafanywa miongoni mwa watu waliolaaniwa. Jambo hili moja ndio ushahidi unaoweza zaidi kumwaibisha Shetani; hivyo, Mungu “anakuwa” Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni na kuwa Bwana wa vitu vyote, Anayeabudiwa na kila kiumbe mwenye uhai.
Kwa sasa bado kuna watu wengine wasioelewa ni aina gani ya kazi mpya ambayo Mungu amezindua. Mungu amefanya mwanzo mpya katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na Ameanza enzi nyingine na kuzindua kazi nyingine, na Anafanya kazi miongoni mwa ukoo wa Moabu. Je, hii si kazi Yake mpya kabisa? Hakuna yeyote katika enzi zote aliyeipitia kazi hii, wala hakuna aliyeisikia, sembuse kuithamini. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, kutoeleweka kwa Mungu, ukubwa wa Mungu, utakatifu wa Mungu vinategemea hatua hii ya kazi katika siku za mwisho, ili kuibuka wazi. Je, hii si kazi mpya inayovunja dhana za binadamu? Bado kuna wale wanaofikiria hivi: “Kwa sababu Mungu alimlaani Moabu na kusema kuwa Angewaacha wazawa wa Moabu, Angeweza kuwaokoaje sasa?” Hao ni wale watu kutoka mataifa yasiyo ya Kiyahudi waliolaaniwa na kulazimishwa nje ya Israeli; Waisraeli waliwaita “mbwa wasio wa Kiyahudi.” Kwa mtazamo wa kila mtu, wao sio mbwa wasio wa Kiyahudi pekee, lakini mbaya hata zaidi, ni wana wa maangamizi; kwa maneno mengine, wao si wateule wa Mungu. Ingawa awali walikuwa wamezaliwa ndani ya eneo la Israeli, wao siyo sehemu ya watu wa Israeli; wao pia walifukuzwa kwenda kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Wao ndio watu wa chini zaidi. Ni kwa sababu hasa wao ni watu wa chini zaidi miongoni mwa binadamu ndio Mungu anatekeleza kazi Yake ya kuzindua enzi mpya miongoni mwao. Kwa sababu wao ni wawakilishi wa binadamu wapotovu na kazi ya Mungu haikosi uchaguzi ama madhumuni, kazi Anayoifanya miongoni mwa watu hawa leo pia ni kazi inayofanywa miongoni mwa viumbe. Nuhu alikuwa sehemu ya viumbe, kama walivyo wazawa wake. Yeyote duniani aliye na mwili na damu ni sehemu ya viumbe. Kazi ya Mungu imeelekezwa kwa viumbe wote; haitekelezwi kulingana na kama mtu amelaaniwa baada ya kuumbwa. Kazi Yake ya usimamizi imeelekezwa kwa viumbe wote, sio wale wateule wasiolaaniwa. Kwa sababu Mungu anataka kutekeleza kazi Yake miongoni mwa viumbe Vyake, kwa hakika Ataifanya hadi kukamilika kwa mafanikio; Atafanya kazi miongoni mwa hao watu walio na manufaa kwa kazi Yake. Kwa hivyo, Anavunja mikataba yote ya kufanya kazi miongoni mwa watu; Kwake, maneno “kulaaniwa,” “kuadibu” na “kubarikiwa” hayana maana! Wayahudi ni wazuri hasa, na wateule wa Israeli sio wabaya pia; ni watu wenye ubora mzuri wa tabia na ubinadamu mzuri. Awali Yehova alizindua kazi Yake miongoni mwao na Akafanya kazi Yake ya awali, lakini ingekuwa bila maana kama Angewatumia kama wapokeaji wa kazi Yake ya ushindi sasa. Ingawa wao pia ni sehemu ya viumbe na wana vipengele vingi vyema, ingekuwa bila maana kutekeleza hatua hii ya kazi miongoni mwao. Asingeweza kumshinda yeyote, wala Asingeweza kushawishi viumbe wote. Huu ndio umuhimu wa uhamisho wa kazi Yake kwa watu hawa wa taifa la joka kubwa jekundu. Maana ya ndani zaidi hapa ni ya uzinduzi Wake wa enzi, ya kuvunja Kwake kwa kanuni zote na dhana zote za mwanadamu na pia kwa kumaliza Kwake kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kama kazi Yake ya sasa ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, ikifika wakati ambao mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilika, kila mtu angeamini kuwa Mungu ni Mungu tu wa Waisraeli, kuwa Waisraeli tu ndio wateule wa Mungu, kuwa Waisraeli tu ndio wanaostahili kurithi baraka na ahadi za Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anapata mwili katika taifa lisilo la Kiyahudi la joka kubwa jekundu; Ametimiza kazi ya Mungu kama Mungu wa viumbe wote; Amekamilisha kazi Yake yote ya usimamizi, na Atamaliza sehemu kuu ya kazi Yake kwa taifa la joka kubwa jekundu. Kiini cha hatua hizi tatu za kazi ni wokovu wa mwanadamu—ambao ni, kufanya viumbe wote vimwabudu Bwana wa viumbe. Hivyo basi, kila hatua ya kazi hii ni muhimu sana; Mungu hatafanya chochote kisicho na maana ama thamani. Kwa upande mmoja, hatua hii ya kazi inajumuisha kuzindua enzi na kukamilisha enzi mbili za awali; kwa upande mwingine inajumuisha kuvunja dhana zote za mwanadamu na njia ya zamani ya imani ya mwanadamu na maarifa. Kazi ya enzi mbili za awali ilifanywa kulingana na dhana tofauti za binadamu; hatua hii, hata hivyo, inafuta kabisa dhana za binadamu, na hivyo kuwashinda binadamu kikamilifu. Kwa kutumia ushindi wa ukoo wa Moabu na kutumia kazi iliyotekelezwa miongoni mwa ukoo wa Moabu, Mungu atawashinda binadamu wote katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa kina zaidi wa hatua hii ya kazi Yake, na ndicho kipengele cha thamani ya hatua hii ya kazi Yake. Hata kama sasa unajua kuwa hadhi yako ni ya chini na kuwa una thamani ya chini, bado utahisi kwamba umekutana na jambo linalofurahisha sana: Umerithi baraka kubwa, ukapata ahadi kubwa, na unaweza kamilisha hii kazi kubwa ya Mungu, na unaweza kuuona uso wa kweli wa Mungu, kujua tabia Yake ya asili, na kufanya mapenzi ya Mungu. Hatua mbili za awali za kazi ya Mungu zilifanywa Israeli. Iwapo hatua hii ya kazi Yake katika siku za mwisho bado ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, viumbe wote havingeamini kwamba Waisraeli tu ndio waliokuwa wateule, lakini pia mpango wa usimamizi wa Mungu wote haungefikia athari iliyotaka. Wakati ambapo hatua hizi mbili za kazi Yake zilifanywa Israeli, hakuna kazi yoyote mpya iliyokuwa imefanywa na hakuna kazi yoyote ya Mungu ya kuzindua enzi ilikuwa imewahi kufanywa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hatua hii ya kazi ya kuzindua enzi inafanywa kwanza katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, na zaidi ya hayo, inafanywa kwanza miongoni mwa ukoo wa Moabu; hii imezindua enzi mpya. Mungu amevunja maarifa yoyote yaliyo ndani ya dhana za binadamu na hajaruhusu yoyote yaendelee kuwa hai. Katika kazi Yake ya kushinda Amevunja dhana za binadamu, hiyo njia ya zamani, ya maarifa ya binadamu, Anaruhusu watu waone kuwa kwa Mungu hakuna kanuni, kwamba hakuna kitu kizee kumhusu Mungu, kwamba kazi Anayoifanya ni ya uhuru kabisa, ni huru kabisa, kwamba Yeye yuko sahihi katika chochote Anachofanya. Ni lazima utii kikamilifu kazi yoyote Anayoifanya miongoni mwa viumbe. Kazi yoyote Anayoifanya ni ya maana na inafanywa kulingana na mtazamo Wake na maarifa Yake na sio kulingana na chaguo za watu na dhana za watu. Anafanya yale mambo yaliyo na manufaa kwa kazi Yake; kama kitu hakina manufaa kwa kazi Yake, Hatakifanya, hata kiwe kizuri vipi! Anafanya kazi na kuchagua mpokeaji na eneo la kazi Yake kulingana na maana na madhumuni ya kazi Yake. Hafuati kanuni za zamani, wala Hafuati fomula nzee; badala yake, Anapanga kazi Yake kulingana na umuhimu wa kazi; mwishowe, Anataka kufikia matokeo yake ya kweli na madhumuni yanayotarajiwa. Iwapo huelewi mambo haya sasa, kazi hii haitatimiza matokeo yoyote kwako.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 5 Machi 2019

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wafuasi wa Kristo

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje

Mwenyezi Mungu alisema, Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu. Una uwezo wa kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu kila unapofanya chochote; hata kama huelewi mapenzi ya Mungu, bado ni lazima utimize wajibu na majukumu yako kadri ya uwezo wako. Hujachelewa sana kusubiri mapenzi ya Mungu yafichuliwe kwako na kisha kuyaweka katika vitendo. Wakati uhusiano wako na Mungu umekuwa wa kawaida, basi pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu. Kila kitu kimejengwa juu ya msingi wa maneno ya Mungu. Kupitia katika kula na kunywa maneno ya Mungu, tenda kulingana na mahitaji ya Mungu, weka sawa maoni yako, usitende mambo yanayompinga Mungu au kuingilia kati mambo ya kanisa. Usifanye vitu visivyo na manufaa kwa maisha ya ndugu, usiseme maneno yasiyosaidia wengine, usifanye vitu vya kufedhehesha. Kuwa mwadilifu na mwenye heshima unapofanya mambo yote na kuyafanya ya kupendeza mbele ya Mungu. Hata ingawa kutakuwa na nyakati ambazo mwili ni dhaifu, unaweza kushikiza umuhimu mkubwa kabisa kwa kufaidi familia ya Mungu, kutotamani faida yako mwenyewe, na kutekeleza haki. Ikiwa unaweza kutenda kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.
Kila unapofanya chochote, lazima uchunguze iwapo motisha yako ni sahihi. Ikiwa unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, basi uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida. Hiki ndicho kigezo cha chini zaidi. Iwapo, unapochunguza motisha yako, kunatokea zile zisizo sahihi, na iwapo unaweza kuzikwepa na kutenda kulingana na maneno ya Mungu, basi utakuwa mtu ambaye ni mwema mbele ya Mungu, kitu ambacho kitaonyesha kuwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, na kwamba kila unachofanya ni kwa ajili ya Mungu, na sio kwa sababu yako binafsi. Ni lazima uuweke moyo wako sawa kila unapofanya ama kusema chochote, uwe mwenye haki katika matendo yako, na usiongozwe na hisia zako, au utende kulingana na mapenzi yako: Haya ndiyo maadili ambayo wale wanaoamini katika Mungu wanatenda kulingana nayo. Motisha za mtu na kimo chake vinaweza kufichuliwa katika kitu kidogo, na hivyo, kwa watu kuingia kwa njia ya kufanywa wakamilifu na Mungu, ni lazima kwanza wasuluhishe motisha yao wenyewe na uhusiano wao na Mungu. Ni pale ambapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utaweza kufanywa mkamilifu na Mungu, na ni hapo tu ndipo ushughulikiaji, upogoaji, nidhamu, na usafishaji wa Mungu kwako utaweza kupata matokeo yanayotakiwa. Hiyo kusema, watu wanaweza kuwa na Mungu mioyoni mwao, wasitafute maslahi binafsi, wasifikirie kuhusu maisha yao binafsi ya baadaye (ikirejelea kufikiri juu ya mwili), lakini badala yake wanabeba mzigo wa kuingia katika maisha, wanajitahidi wawezavyo kutafuta ukweli, na kuitii kazi ya Mungu. Kwa namna hii, makusudi unayoyatafuta ni sahihi, na uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Inaweza kusemwa kwamba kuutengeneza uhusiano wako na Mungu ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia katika safari yako ya kiroho. Ingawa kudura ya mtu iko mikononi mwa Mungu, na imeshaamuliwa kabla na Mungu, na haiwezi kubadilishwa na yeye mwenyewe, kwamba unaweza au huwezi kufanywa mkamilifu au kupatwa na Mungu kunategemea na kama uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au la. Pengine kuna sehemu yako ambazo ni dhaifu au zenye kutotii—lakini bora tu mtazamo wako ni sawa na motisha zako ni sahihi, na bora tu umeuweka uhusiano wako na Mungu sawa na kuufanya wa kawaida, basi utastahili kufanywa mkamilifu na Mungu. Iwapo huna uhusiano sahihi na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili, au familia yako, basi haijalishi unafanya kazi kwa bidii vipi, itakuwa bure. Iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii chochote kingine, bali Anaangalia tu iwapo mitazamo yako kuhusu kuamini kwa Mungu ni sawa: unayemwamini, ni kwa ajili ya nani unaamini, na ni kwa nini unaamini. Iwapo unaweza kuona vitu hivi kwa udhahiri, na unaweza kuweka mitazamo yako na matendo, basi maisha yako yatapiga hatua, na una uhakika wa kuweza kuingia kwa njia sahihi. Iwapo uhusiano wako na Mungu sio wa kawaida, na mitazamo yako kuhusu kuamini katika Mungu inaacha maadili, basi haya yatazuia mengine yote. Haijalishi jinsi unavyoamini katika Mungu, hutafaidi chochote. Iwapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utasifiwa na Mungu unapokwepa mwili, unapoomba, unapoteseka, unapostahimili, unapotii, unapowasaidia ndugu zako, unaweka juhudi zaidi kwa Mungu, na kadhalika. Hiyo kusema, watu wanaweza kuwa na Mungu mioyoni mwao, wasitafute maslahi binafsi, wasifikirie kuhusu maisha yao binafsi ya baadaye (ikirejelea kufikiri juu ya mwili), lakini badala yake wanabeba mzigo wa kuingia katika maisha, wanajitahidi wawezavyo kutafuta ukweli, na kuitii kazi ya Mungu. Kwa namna hii, makusudi unayoyatafuta ni sahihi, na uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Inaweza kusemwa kwamba kuutengeneza uhusiano wako na Mungu ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia kwako katika safari ya kiroho. Ingawa hatima yako iko mikononi mwa Mungu, na imeshaamuliwa kabla na Mungu, na haiwezi kubadilishwa na wewe mwenyewe, kwamba unaweza au huwezi kufanywa mkamilifu au kupatwa na Mungu kunategemea na kama uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au la. Pengine kuna sehemu ndani yako ambazo ni dhaifu au zenye kutotii—lakini bora tu mtazamo wako wa nje ni sawa na motisha yako ni sahihi, na bora tu umeuweka uhusiano wako na Mungu sawa na kuufanya wa kawaida, basi utafuzu kufanywa mkamilifu na Mungu. Iwapo huna uhusiano sahihi na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili, au familia yako, basi haijalishi kiwango cha kazi unayofanya kwa bidii, itakuwa bure. Iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii chochote kingine, bali anaangalia tu iwapo mitazamo yako kwa kuamini kwa Mungu ni sawa: unayemwamini, ni kwa ajili ya nani unaamini, na ni kwa nini unaamini. Iwapo unaweza kuona vitu hivi kwa udhahiri, na unaweza kuweka mitazamo yako iwe sawa na kuweza kutenda, basi maisha yako yatapiga hatua, na una uhakika wa kuweza kuingia kwenye njia sahihi. Iwapo uhusiano wako na Mungu sio wa kawaida, na mitazamo yako kwa kuamini katika Mungu inakiuka maadili, basi haya yatazuia mengine yote. Haijalishi jinsi unavyoamini katika Mungu, hutafaidi chochote. Iwapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utasifiwa na Mungu unapoupa mwili kisogo, unapoomba, unapoteseka, unapostahimili, unapotii, unapowasaidia ndugu na dada zako, unaweka juhudi zaidi kwa Mungu, na kadhalika. Iwe kitu unachofanya kina thamani na umuhimu au hakina hutegemea iwapo makusudi yako ni sahihi na iwapo mitazamo yako ni sahihi. Siku hizi, imani ya watu wengi kwa Mungu ni kama kutazama saa kubwa huku vichwa vyao vikiwa vimeelekezwa upande mmoja—mitazamo yao imekengeuka. Kila kitu kitakuwa kizuri ikiwa mwelekeo mpya unaweza kufanyika hapa, kila kitu kitakuwa sawa ikiwa hili litatatuliwa, wakati hakutafanyika kitu ikiwa hili halitatatuliwa. Baadhi ya watu wanakuwa na tabia nzuri katika uwepo Wangu, lakini nyuma Yangu kile wanachofanya ni kupinga. Haya ni maonyesho yaliyopotoka na ya udanganyifu na aina hii ya mtu ni mtumwa wa Shetani, ni mfano halisi wa namna ile ile ya Shetani kumjaribu Mungu. Wewe ni mtu sahihi tu ikiwa unaweza kuitii kazi Yangu na maneno Yangu. Ilimradi unaweza kula na kunywa maneno ya Mungu, ilimradi kila kitu unachofanya kinapendeza mbele ya Mungu, ilimradi hufanyi mambo ya aibu, usifanye mambo ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya watu, ilimradi unaishi katika mwanga, hunyonywi na Shetani, basi uhusiano wako na Mungu utawekwa sawa.
Katika kumwamini Mungu, makusudi na mitazamo yako yanapaswa kuwekwa sawa; unapaswa kuwa na ufahamu sahihi na utendeaji sahihi wa maneno ya Mungu, kazi ya Mungu, mazingira yaliyopangwa na Mungu, mtu aliyeshuhudiwa na Mungu, na wa Mungu wa vitendo. Hupaswi kutenda kulingana na mawazo yako binafsi, au kufanya mipango yako midogo mwenyewe. Unapaswa kuweza kutafuta ukweli katika kila kitu na kusimama katika sehemu yako kama uumbaji wa Mungu na kuzitii kazi zote za Mungu. Kama unataka kutafuta kukamilishwa na Mungu na kuingia katika njia sahihi ya maisha, basi moyo wako siku zote unapaswa kuishi katika uwepo wa Mungu, usiwe fisadi, usimfuate Shetani, usimwachie Shetani fursa yoyote kufanya kazi yake, na usimruhusu Shetani kukutumia. Unapaswa kujitoa kikamilifu kwa Mungu na kumwacha Mungu akutawale.
Upo radhi kuwa mtumishi wa Shetani? Upo radhi kunyonywa na Shetani? Je, unamwamini Mungu na kumtafuta Mungu ili kwamba uweze kukamilishwa na Yeye, au ni ili uwe foili[a] katika kazi ya Mungu? Je, upo radhi kupatwa na Mungu na kuishi maisha ya maana, au upo radhi kuishi maisha tupu na yasiyo na thamani? Upo radhi kutumiwa na Mungu, au kunyonywa na Shetani? Upo radhi kuacha maneno ya Mungu na ukweli kukujaza, au kuacha dhambi na Shetani kukujaza? Litafakari na kulipima hili. Katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kuyaelewa maneno hayo uyasemayo na mambo hayo uyafanyayo ambayo yatasababisha uhusiano wako na Mungu kuwa usio wa kawaida, halafu ujirekebishe na kuingia katika tabia sahihi. Yachunguze maneno yako, vitendo vyako, kila mwenendo wako, na fikra zako na mawazo wakati wote. Ielewe hali yako ya kweli na ingia katika njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwa njia hii tu ndipo unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Kwa kupima iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kurekebisha makusudi yako, kuielewa asili ya mwanadamu, na kujielewa mwenyewe; kupitia hili, utaweza kuingia katika uzoefu halisi, na kujinyima kwa kweli, na kupata utiifu wa makusudi. Katika masuala hayo kama unapokuwa unapitia iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kupata fursa za kukamilishwa na Mungu, utaweza kuelewa hali nyingi, ambazo kwazo Roho Mtakatifu Anafanya kazi, na utaweza kubaini mengi ya udanganyifu na njama za Shetani. Ni kupitia njia hii tu ndipo unaweza kukamilishwa na Mungu. Unaweka uhusiano wako na Mungu sawa ili kwamba ujisalimishe mwenyewe mipangilio yote ya Mungu. Ni ili utaingia kwa kina zaidi katika uzoefu halisi, na kupata kazi zaidi ya Roho Mtakatifu. Unafanya mazoezi ya kuwa na uhusianao wa kawaida na Mungu, muda mwingi, utapata huu kupitia kuunyima mwili na kupitia ushirikiano wako wa kweli na Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba "bila moyo wa ushirikiano, ni vigumu kupokea kazi ya Mungu; ikiwa mwili haupati mateso, hakuna baraka kutoka kwa Mungu; ikiwa roho haihangaiki, Shetani hataaibishwa." Ikiwa unazitenda na kuzielewa vizuri kanuni hizi, mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu itawekwa sawa. Katika matendo yenu ya sasa, mnapaswa kuacha mtazamo wa "kutafuta mkate ili kutuliza njaa," mnapaswa kuacha mtazamo wa "kila kitu kinafanywa na Roho Mtakatifu na watu hawawezi kuingilia." Watu wanaozungumza namna hii wote wanafikiri, "Watu wanaweza kufanya chochote kile ambacho wako radhi kukifanya, na muda utakapofika Roho Mtakatifu atafanya kazi na watu hawatakuwa na haja ya kuushinda mwili, hawatakuwa na haja ya kushirikiana, watakuwa wanahitaji tu Roho Mtakatifu kuwashawishi." Mitazamo hii yote ni ya kipuuzi. Katika mazingira haya, Roho Mtakatifu hawezi kufanya kazi. Ni mtazamo wa aina hii ndio unakuwa kizuizi kikubwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Mara nyingi, kazi ya Roho Mtakatifu inapatikana kupitia ushirikiano wa watu. Bila ushirikiano na kudhamiria, basi kutaka kubadilisha tabia ya mtu, kupata kazi ya Roho Mtakatifu, na kupata mwangaza na nuru kutoka kwa Mungu zote ni fikra za kupita kiasi; hii inaitwa "kujifurahisha mwenyewe na kumsamehe Shetani." Watu kama hawa hawana uhusiano wa kawaida na Mungu. Umepata dalili nyingi za Shetani ndani yako, na katika matendo yako ya zamani, kuna mambo mengi ambayo yamepingana na matakwa ya sasa ya Mungu. Je, unaweza kuyatelekeza sasa? Pata uhusiano wa kawaida na Mungu, fanya kulingana na makusudi ya Mungu, kuwa mtu mpya na kuwa na maisha mapya, usitazame dhambi zako za zamani, usiwe mwenye majuto kupita kiasi, kuwa na uwezo wa kusimama na kushirikiana na Mungu, na kutimiza majukumu ambayo unapaswa kufanya. Kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.
Ikiwa unakubali tu maneno haya kwa mdomo baada ya kuyasoma lakini hayajaingia moyoni mwako, na huko makini kuhusu kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi inathibitisha kwamba huweki umuhimu mkubwa kwenye uhusiano wako na Mungu, mitazamo yako bado haijawekwa sawa, makusudi yako bado hayajaelekezwa kwa kumruhusu Mungu akupate, na kumkubalia Mungu utukufu, badala yake yameelekezwa kwa kuruhusu njama za Shetani kushinda na kwa kupata malengo yako binafsi. Watu wa aina hii wote wana makusudi na mitazamo isiyo sahihi. Bila kujali kile ambacho Mungu amesema au namna kilivyosemwa, hawajali na hakuna mabadiliko yanayoweza kuonekana. Mioyo yao haihisi woga wowote na hawaoni aibu. Mtu wa aina hii ni mtu aliyekanganyikiwa bila roho. Kwa kila tamshi la Mungu, baada ya kulisoma na kupata ufahamu, utaliweka katika vitendo. Bila kujali ulivyokuwa ukitenda kabla—pengine huko nyuma mwili wako ulikuwa dhaifu, ulikuwa muasi, na ulipinga—hili silo jambo kubwa, na haliwezi kuzuia maisha yako yasikue leo. Ilimradi unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu leo, basi kuna tumaini. Ikiwa kwa kila wakati unaposoma maneno ya Mungu, unakuwa na mbadiliko na kuruhusu watu wengine kuona kwamba maisha yako yamebadilika kuwa mazuri, inaonyesha kwamba una uhusiano wa kawaida na Mungu na kwamba umewekwa sawa. Mungu hashughulikii watu kulingana na dhambi zao. Ilimradi unaweza kutoasi tena na hupingi tena baada ya wewe kuelewa na kufahamu, basi Mungu atakuwa bado Ana huruma na wewe. Unapokuwa na ufahamu huu na nia ya kutafuta kukamilishwa na Mungu, basi hali yako katika uwepo wa Mungu itakuwa ya kawaida. Bila kujali unachofanya, zingatia: Mungu atafikiri nini ikiwa nitafanya hiki? Kitawaathiri vipi ndugu? Chunguza makusudi yako katika maombi, ushirika, usemi, kazi na kuhusiana na watu, na chunguza endapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au si wa kawaida. Ikiwa huwezi kutofautisha makusudi yako na fikra zako, basi huna ubaguzi, kitu ambacho kinathibitisha kwamba unaelewa kidogo sana kuhusu ukweli. Kuwa na ufahamu ulio wazi wa kila kitu ambacho Mungu hufanya, vitazame vitu kulingana na neno la Mungu na vitazame vitu kwa kusimama katika upande wa Mungu. Kwa njia hii mitazamo yako itakuwa sahihi. Kwa hiyo, kujenga uhusiano mzuri na Mungu ni kipaumbele cha juu kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuichukulia kama kazi muhimu na kama tukio lao kubwa la maisha. Kila kitu unachofanya kinapaswa kipimwe dhidi ya iwapo una uhusiano wa kawaida na Mungu au la. Ikiwa uhusianao wako na Mungu ni wa kawaida na makusudi yako ni sahihi, basi kifanye. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupoteza maslahi binafsi, hupaswi kumruhusu Shetani kushinda, hupaswi kumruhusu Shetani kupata kitu dhidi yako, na hupaswi kumruhusu Shetani kukufanya uwe kichekesho. Kusudi kama hili ni udhihirisho kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Si kwa ajili ya mwili, badala yake ni kwa ajili ya amani ya roho, ni kwa ajili ya kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali sahihi, unapaswa kujenga uhusiano mzuri na Mungu, unapaswa kuweka sawa mtazamo wako wa imani kwa Mungu. Ni kumruhusu Mungu kukupata, kumruhusu Mungu kufichua matunda ya maneno Yake kwako na kukuangazia na kukupatia nuru zaidi. Kwa namna hii utaingia katika tabia nzuri. Endelea kula na kunywa maneno ya Mungu ya sasa, ingia katika njia ya sasa ya kazi ya Roho Mtakatifu, fanya kulingana na matakwa ya Mungu ya sasa, usifuate mazoea ya kale, using'ang'anie njia za zamani za kufanya mambo, na haraka ingia katika namna ya kazi ya leo. Kwa njia hii uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida kabisa na utaingia katika njia sahihi ya kumwamini Mungu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 4 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Mwenyezi Mungu anasema, “Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka shtaka rasmi lililoandikwa; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika enzi zote, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga. Na wale wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu pekee watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya wanadamu na kuchukia matendo yao maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu, Nikisubiri tu nafasi kutoa adhabu kwa hao na kufurahia kuona hilo. Siku Yangu hatimaye imefika na siwezi kusubiri zaidi!”
Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimetamka mengi pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele katika mpango Wangu mpya, katika kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya katika kazi Yangu ili wale ambao wanaoniona watajipiga kifuani na kuulilia na kuombolezea uwepo Wangu bila kukoma. Kwani Ninaleta mwisho wa wanadamu duniani, na baada ya hapo kuendelea, Ninaweka wazi tabia Yangu yote mbele ya wanadamu, ili wote wanijuao na wasionijua watayashibisha macho yao na kuona kwamba kweli, nimekuja ulimwenguni, nimekuja duniani ambapo vitu vyote vinazidi kuongezeka. Huu ni mpango Wangu, ni “kukiri” Kwangu kwa pekee tangu Niwaumbe wanadamu. Matilaba yangu ni kuona mnafuatilia kwa moyo wenu wote kila Ninachokifanya, maana kiboko Changu kinamkaribia wanadamu tena, karibu na wale wote wanaonipinga. Pamoja na mbingu, Ninaanza kazi ambayo ni lazima Niifanye. Kwa hivyo Mimi husafiri kati ya misururu ya watu na kupita kati ya mbingu na ardhi, bila ya yeyote kutambua mienendo Yangu au kuyatambua maneno Yangu. Kwa hivyo, mpango Wangu bado unaendelea kwa urahisi. Ni vile tu hisia zenu zote zimekuwa nzito kiasi kwamba hamjui hatua za kazi Yangu hata kidogo. Hata hivyo, siku moja hakika mtakuja kutambua kusudio Langu. Leo hii, Ninaishi miongoni mwenu na Ninasumbuka pamoja nanyi. Kwa muda mrefu Nimeelewa mtazamo walio nao wanadamu juu Yangu. Nisingependa kueleza wazi zaidi, sembuse kutoa mifano zaidi ya kile kinachoniumiza ili kuwaaibisha. Ombi Langu la pekee ni kwamba myaweke moyoni yale yote mliyoyafanya kwa ajili ya kulinganisha maelezo yetu siku tutakapokutana tena. Nisingependa kumshutumu yeyote miongoni mwenu kwa njia isiyo ya kweli, kwa sababu daima Nimekuwa Nikifanya mambo kwa njia ya haki, bila upendeleo, na kwa heshima. Bila shaka, Ningependa pia kwamba nyinyi mngeweza kuwa wazi na wakarimu na kutofanya lolote lililo kinyume na mbingu na ardhi na dhamiri yenu. Haya pekee ndiyo Ninayowauliza. Watu wengi huhisi kusumbuka na hawana amani kwa sababu wametenda makosa mabaya, na wengi wanaona aibu kwa sababu hawajawahi kutenda tendo lolote zuri. Tena wapo pia wengi ambao, mbali na kutahayari kutokana na dhambi zao, wanakuwa wabaya zaidi, wakizitoa kabisa barakoa inayoficha sura zao mbaya—ambayo ilikuwa bado haijaonyeshwa kikamilifu—ili kujaribu tabia Yangu. Huwa Sijali wala sitilii maanani sana matendo ya mtu yeyote. Badala yake, Mimi hufanya kazi Ninayopaswa kufanya, iwe kukusanya habari, kuzungukazunguka katika nchi au kufanya lile ambalo linanipendeza. Katika nyakati muhimu, Mimi nitaendelea na kazi Yangu miongoni mwa wanadamu kama Nilivyopanga awali, bila kuchelewa au kuwa mapema hata kidogo, na kwa urahisi na kwa makini. Hata hivyo, kuna watu wengine ambao wanawekwa pembeni kwa kila hatua katika kazi Yangu, kwa sababu Ninadharau hali yao ya kujipendekeza na hali ya kujifanya wanyenyekevu. Wale wanaochukiza Kwangu hakika watatelekezwa, iwe ni kwa kupenda au kwa kutopenda. Kwa ufupi, Ninataka wale wote Ninaowadharau kuwa mbali sana Nami. Ni dhahiri kwamba, Sitawahurumia wale waovu ambao wamebaki katika makao Yangu. Kwa kuwa siku ya adhabu ya mwanadamu inakaribia, Sina haraka ya kuzitupa nje zile nyoyo zote zinazostahili dharau, kwa kuwa Nina mpango Wangu Mwenyewe. Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, wala si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo yote ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya nyingine, na vilevile njia zao katika kunifuata, sifa zao asilia, na utendakazi wao wa mwisho. Kwa njia hii, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu na kila mmoja atakuwa wa aina yake kama Nilivyowaweka. Ninaamua hatima ya kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu. Sijafanya mabadiliko yoyote katika mpango Wangu tangu kuuanzisha. Ni vile tu, kwa binadamu, wale ambao kwao Mimi huelekeza maneno Yangu wanaonekana kupungua kwa idadi, na vile vile wale Ninaowakubali kwa kweli. Hata hivyo, Ninasisitiza kwamba mpango Wangu haujawahi kubadilika; badala yake, ni imani na upendo wa mwanadamu ambao hubadilika daima, kufifia daima, kiasi kwamba upo uwezekano wa kila mwanadamu kubadilika kutoka kujipendekeza Kwangu hadi kufikia hali ya kunidharau au hata kunitupa nje. Mtazamo Wangu kwenu hautakuwa baridi wala moto, hadi pale Nitakapohisi kuchukizwa na kuchafuliwa moyo, na hatimaye kutoa adhabu. Hata hivyo, katika siku ya adhabu yenu, bado Nitawaona lakini nyinyi hamtaweza kuniona tena. Tayari Kwa kuwa maisha miongoni mwenu yamekuwa ya kuchosha na ya taabu tayari Kwangu, kwa hivyo ni wazi kuwa, Nimechagua mazingira tofauti Yangu kuishi, ili Niepuke vizuri kuumizwa na maneno yenu mabovu na kuwa mbali na tabia zenu hafifu sana, ili msinipumbaze au kunitendea kwa namna ya uzembe. Kabla Sijawaacha, lazima bado Ninawasihi mjiepushe kufanya yale ambayo hayaambatani na ukweli. Badala yake, mnafaa kufanya yale ambayo yanawapendeza watu wote, na yale ambayo yana manufaa kwa binadamu wote, na yale yanayofaidi hatima yenu wenyewe, la sivyo, yule atakayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe.
kutoka kwa Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Ijumaa, 1 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa

Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa. Ingawa Yeye huvumilia shida ambazo watu wanaweza kupata ugumu kuvumilia, ingawa Yeye kama Mungu mkuu ana unyenyekevu wa kuwa mtu wa kawaida, hakuna kipengele cha kazi Yake kimecheleweshwa, na mpango Wake haujatupwa katika mchafuko hata kidogo. Anafanya kazi kulingana na mpango Wake wa awali. Mojawapo ya madhumuni ya kupata mwili huku ni kuwashinda watu. Mengine ni kuwakamilisha watu Anaowapenda. Yeye hutamani kuwaona kwa macho Yake mwenyewe watu Anaowakamilisha, na Yeye hutaka kujionea Mwenyewe jinsi watu Anaowakamilisha humshuhudia. Sio mtu mmoja ambaye hukamilishwa, na sio wawili. Hata hivyo, ni kikundi cha watu wachache sana. Kikundi hiki cha watu huja kutoka nchi mbalimbali za dunia, na kutoka kwa makabila mbalimbali ya ulimwengu. Kusudi la kufanya kazi hii nyingi ni kukipata kikundi hiki cha watu, kupata ushuhuda ambao kikundi hiki cha watu humtolea, na kupata utukufu ambao Yeye hupata kupitia kwa kikundi hiki cha watu. Yeye hafanyi kazi ambayo haina umuhimu, wala hafanyi kazi ambayo haina thamani. Inaweza kusemwa kuwa, kwa kufanya kazi nyingi sana, lengo la Mungu ni kuwakamilisha watu wote ambao Yeye anataka kuwakamilisha. Katika wakati wowote wa ziada Alio nao nje ya hili, Atawaondosha wale walio waovu. Jua kwamba Haifanyi kazi hii kubwa kwa sababu ya wale walio waovu; kwa kinyume, Yeye hufanya kadri Awezavyo kwa sababu ya idadi hiyo ndogo ya watu ambao hawana budi kukamilishwa na Yeye. Kazi ambayo Yeye hufanya, maneno ambayo Yeye hunena, siri ambayo Yeye hufichua, na hukumu Yake na adhabu zote ni kwa ajili ya idadi hiyo ndogo ya watu. Yeye hakupata mwili kwa sababu ya wale walio waovu, sembuse wao kuchochea ghadhabu kubwa ndani Yake. Yeye husema ukweli, na huzungumzia kuingia, kwa sababu ya wale watakaokamilishwa, Alipata mwili kwa sababu yao, na ni kwa sababu yao Yeye hutoa ahadi na baraka Zake. Ukweli, kuingia, na maisha katika ubinadamu ambayo Yeye huzungumzia si kwa ajili ya wale walio waovu. Yeye hutaka kuepuka kuzungumza na wale walio waovu, na hutaka kuwapa wale ambao watakamilishwa ukweli wote. Lakini kazi Yake inahitaji kwamba, kwa sasa, wale walio waovu waruhusiwe kufurahia baadhi ya utajiri Wake. Wale ambao hawatekelezi ukweli, ambao hawamridhishi Mungu, na ambao hukatiza kazi Yake wote ni waovu. Hawawezi kukamilishwa, na wanachukiwa kabisa na kukataliwa na Mungu. Kwa kinyume, watu ambao hutia ukweli katika vitendo na wanaweza kumridhisha Mungu na ambao hujitolea wenyewe kabisa katika kazi ya Mungu ndio watu ambao watakamilishwa na Mungu. Wale ambao Mungu hutaka kuwakamilisha sio wengine bali ni kikundi hiki cha watu, na kazi ambayo Mungu hufanya ni kwa ajili ya watu hawa. Ukweli ambao Yeye huzungumzia unaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kuutia katika vitendo. Yeye huwa hazungumzi na watu ambao hawatii ukweli katika vitendo. Ongezeko la umaizi na ukuaji wa utambuzi ambao Yeye huzungumzia umelengwa kwa watu ambao wanaweza kutekeleza ukweli. Anapozungumza juu ya wale ambao watakamilishwa Yeye anazungumzia watu hawa. Kazi ya Roho Mtakatifu inaelekezwa kwa watu ambao wanaweza kutenda ukweli. Mambo kama kumiliki hekima na kuwa na ubinadamu yanaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kutia ukweli katika vitendo. Wale ambao hawatekelezi ukweli wanaweza kuusikia ukweli mwingi na wanaweza kuuelewa ukweli mwingi, lakini kwa sababu wao ni miongoni mwa watu waovu, ukweli ambao wao huuelewa huja kuwa tu mafundisho na maneno, na hauna umuhimu kwa mabadiliko yao ya tabia au kwa maisha yao. Hakuna hata mmoja wao aliye mwaminifu kwa Mungu; wao wote ni watu wanaomwona Mungu lakini hawawezi kumpata, na wote wamehukumiwa na Mungu.
Roho Mtakatifu ana njia ya kutembea katika kila mtu, na humpa kila mtu fursa za kukamilishwa. Kupitia uhasi wako unajulishwa upotovu wako mwenyewe, na kisha kwa njia ya kuacha uhasi utapata njia ya kutenda, na huku ndiko kukamilishwa kwako. Aidha, kwa njia ya mwongozo na mwangaza wa siku zote wa mambo fulani chanya ndani yako, utatimiza shughuli yako kwa kuamili na kukua katika umaizi na kupata utambuzi. Wakati hali zako ni nzuri, uko tayari hasa kusoma neno la Mungu, na hasa tayari kumwomba Mungu, na unaweza kuyahusisha mahubiri unayoyasikia na hali zako mwenyewe. Kwa nyakati kama hizo Mungu hukupatia nuru na kukuangaza ndani, na kukufanya utambue mambo fulani ya kipengele chanya. Huku ni kukamilishwa kwako katika kipengele chanya. Katika hali hasi, wewe ni dhaifu na hasi, na huhisi kuwa huna Mungu, lakini Mungu hukuangaza, akikusaidia kupata njia ya kutenda. Kutoka nje ya hili ni kupata ukamilisho katika hali chanya. Mungu anaweza kumkamilisha mwanadamu katika vipengele hasi na chanya. Inategemea kama unaweza kupata uzoefu, na kama wewe hufuatilia kukamilishwa na Mungu. Kama kwa hakika unatafuta kukamilishwa na Mungu, basi kilicho hasi hakiwezi kukufanya upoteze, lakini kinaweza kukuletea mambo ambayo ni halisi zaidi, na kinaweza kukufanya uweze zaidi kujua kile kilichopunguka ndani yako, uweze zaidi kufahamu sana hali zako halisi, na kuona kwamba mtu hana kitu, wala si kitu; kama hupitii majaribio, hujui, na daima utahisi kuwa wewe ni wa hadhi ya juu kuliko wengine na bora kuliko kila mtu mwingine. Kwa njia hii yote utaona kwamba yote yaliyotangulia yalifanywa na Mungu na kulindwa na Mungu. Kuingia katika majaribio hukuacha bila upendo au imani, huna sala, na huwezi kuimba nyimbo—na, bila kulitambua, katikati ya hili unakuja kujijua. Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua “siri” katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo.
Ni nini mnachokitafuta sasa? Labda ni kukamilishwa na Mungu, kumjua Mungu, kumpata Mungu, au ni mtindo wa Petro wa miaka ya tisini, ama kuwa na imani kubwa zaidi ya ile ya Ayubu. Mnaweza kutafuta mengi, iwe ni kutafuta kuitwa wenye haki na Mungu na kufika mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, au kuweza kumdhihirisha Mungu duniani na kuwa na ushuhuda wa nguvu na mkubwa sana kwa Mungu. Bila kujali mnachokitafuta, kwa jumla, ni kwa ajili ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Haijalishi kama unatafuta kuwa mtu mwenye haki, au unatafuta mtindo wa Petro, ama imani ya Ayubu, au kukamilishwa na Mungu, chochote unachokitafuta, kwa muhtasari, yote ni kazi ya Mungu. Hivyo ni kusema, bila kujali unachokitafuta, yote ni kwa ajili ya kukamilishwa na Mungu, yote ni kwa ajili ya kupitia neno la Mungu, ili kuuridhisha moyo wa Mungu; yote ni kwa ajili ya kugundua uzuri wa Mungu, yote ni kwa ajili ya kutafuta njia ya kutenda katika uzoefu halisi kwa lengo la kuweza kuiacha tabia yako ya uasi, kufanikisha hali ya kawaida ndani yako mwenyewe, kuweza kufuata kabisa mapenzi ya Mungu, kuwa mtu sahihi, na kuwa na nia sahihi katika kila kitu unachokifanya. Sababu ya wewe kupitia vitu hivi vyote ni kufikia kumjua Mungu na kufanikisha ukuaji wa maisha. Ingawa kile unachokipitia ni neno la Mungu, na kile unachokipitia ni matukio halisi, watu, mambo, na vitu katika mazingira yako, hatimaye unaweza kumjua Mungu na kukamilishwa na Mungu. Kutafuta kuitembea njia ya mtu mwenye haki au kutafuta kutia neno la Mungu katika vitendo, hizi ndizo njia. Kumjua Mungu na kukamilishwa na Mungu ndiyo hatima. Kama unatafuta sasa kukamilishwa na Mungu, au kumshuhudia Mungu, kwa ujumla, hatimaye ni ili kumjua Mungu; ni ili kwamba kazi Anayoifanya ndani yako sio ya bure, ili hatimaye uje kuujua uhalisi wa Mungu, kujua ukuu Wake, vivyo hivyo hata zaidi kuujua unyenyekevu wa Mungu na hali Yake ya kutoonekana, na kujua kazi nyingi ambazo Mungu hufanya ndani yako. Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani, kufanya kazi Yake katika watu hawa wachafu na wapotovu, na kukikamilisha kikundi hiki cha watu. Mungu hakupata mwili tu ili kuishi na kula kati ya watu, kuwalisha watu, kutoa wanachohitaji watu. Jambo muhimu zaidi ni kwamba Yeye hufanya kazi Yake kubwa ya wokovu na ushindi kwa watu hawa walio na upotovu usiovumilika. Alikuja katika kiini cha joka kubwa jekundu ili kuwafanyia kazi watu hawa wapotovu mno, ili watu wote waweze kubadilishwa na kufanywa wapya. Tatizo kubwa ambalo Mungu huvumilia siyo tu shida ambayo Mungu mwenye mwili huvumilia, lakini hasa ni kwamba Roho wa Mungu hupitia udhalilishaji uliokithiri—Yeye hujinyenyekeza na kujificha Mwenyewe sana kiasi kwamba Yeye huwa mtu wa kawaida. Mungu alipata mwili na kuchukua mfano wa mwili ili watu waone kwamba Ana maisha ya kawaida ya binadamu, na kwamba ana mahitaji ya kawaida ya binadamu. Hili linatosha kuthibitisha kwamba Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani. Roho wa Mungu hufanyika katika mwili. Roho Wake ni wa juu sana na mkuu, lakini Yeye huchukua mfano wa mwanadamu wa kawaida, wa mwanadamu asiye muhimu ili kufanya kazi ya Roho Wake. Ubora wa tabia, umaizi, hisi, ubinadamu, na maisha ya kila mmoja wenu vinaonyesha kwamba hamfai kweli kupokea kazi ya Mungu ya aina hii. Hakika hamfai kumruhusu Mungu kuvumilia shida kama hiyo kwa ajili yenu. Mungu ni mkubwa sana. Yeye ni mkuu sana, na watu ni duni sana na wa hali ya chini, lakini Yeye bado huwafanyia kazi. Yeye hakupata mwili tu ili kuwaruzuku watu, kuzungumza na watu, Yeye hata huishi pamoja na watu. Mungu ni mnyenyekevu sana, wa hupendeka sana. Ikiwa punde upendo wa Mungu unapotajwa, mara tu neema ya Mungu inapotajwa, unatoa machozi unapotamka sifa kubwa, ukifika katika hali hii, basi una maarifa ya kweli ya Mungu.
Kuna kuchepuka katika kutafuta kwa watu siku hizi; wao hutafuta tu kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu, lakini hawana maarifa yoyote juu ya Mungu, na wametelekeza nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu ndani yao. Hawana maarifa ya kweli ya Mungu kama msingi. Kwa njia hii wanapoteza nguvu wakati uzoefu wao unapoendelea. Wale wote wanaotafuta kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu, ingawa wakati wa zamani hawakuwa katika hali nzuri, walielekea kwa uhasi na udhaifu, na mara nyingi walitoa machozi, wakaingia katika kukata tamaa, na wakavunjika moyo; sasa hali zao zinakuwa bora kwa kukithiri wanapopata uzoefu zaidi. Baada ya uzoefu wa kushughulikiwa na kuvunjwa, au kupitia kisa cha kusafishwa, wamekuwa na maendeleo makubwa. Hali kama hizo hazionekani zikiwafika tena, tabia zao zimebadilika, na upendo wa Mungu unaishi kwa kudhihirika ndani yao. Kuna kanuni kwa kukamilishwa kwa watu na Mungu, ambayo ni kwamba Yeye hukupa nuru kwa kutumia sehemu yako inayofaa ili uwe na njia ya kutenda na unaweza kujitenga na hali zote hasi, ikisaidia roho yako kupata uhuru, na ikikufanya uweze kumpenda zaidi. Kwa njia hii, unaweza kuiacha tabia potovu ya Shetani. Wewe huna hila na uko wazi, ukiwa tayari kujijua, na ukiwa tayari kutia ukweli katika vitendo. Mungu huona kwamba uko tayari kujijua na uko tayari kutia ukweli katika vitendo, kwa hiyo unapokuwa dhaifu na hasi, Yeye hukupa nuru maradufu, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa tayari kujitubia, na kuweza zaidi kutenda mambo ambayo unapaswa kuyatenda. Ni kwa njia hii tu ambapo moyo wako unahisi amani na utulivu. Mtu ambaye kwa kawaida huzingatia kumjua Mungu, ambaye huzingatia kujijua, ambaye huzingatia vitendo vyake mwenyewe ataweza kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, mara kwa mara kupokea mwongozo na nuru kutoka kwa Mungu. Hata ingawa yuko katika hali hasi, anaweza kugeuka mara moja, iwe ni kwa sababu ya matendo ya dhamiri au kwa sababu ya nuru kutoka kwa neno la Mungu. Mabadiliko ya tabia ya mtu hufanikishwa daima anapojua hali yake mwenyewe halisi na kujua tabia na kazi ya Mungu. Mtu ambaye yuko tayari kujijua na yuko tayari kuwasiliana ataweza kutekeleza ukweli. Aina hii ya mtu ni mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, na mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu ana ufahamu wa Mungu, uwe ni wa kina au wa juu juu, haba au maridhawa. Hii ni haki ya Mungu, na ni kitu ambacho watu hupata, ni faida yao wenyewe. Mtu ambaye ana maarifa ya Mungu ni yule ambaye ana msingi, ambaye ana maono. Mtu wa aina hii ana hakika kuhusu mwili wa Mungu, ana hakika kuhusu neno la Mungu, na ana hakika kuhusu kazi ya Mungu. Bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi au kuzungumza, au jinsi watu wengine husababisha vurugu, anaweza kushikilia msimamo wake, na kuwa shahidi kwa Mungu. Kadiri mtu alivyo katika njia hii ndivyo anavyoweza kutekeleza zaidi ukweli anaouelewa. Kwa sababu daima anatenda neno la Mungu, yeye hupata ufahamu zaidi wa Mungu, na analo azimio la kuwa shahidi kwa Mungu milele.
Kuwa na utambuzi, kuwa na utii, na kuwa na uwezo wa kubaini mambo ili uwe hodari katika roho ina maana kuwa maneno ya Mungu yanakuangaza na kukupa nuru ndani mara tu unapokabiliwa na kitu fulani. Huku ni kuwa hodari katika roho. Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya kusaidia kufufua roho za watu. Kwa nini Mungu daima husema kuwa watu ni wa kujijali na wajinga? Ni kwa sababu roho za watu zimekufa, na wamekuwa wa kutojali kiasi kwamba hawajui kabisa mambo ya roho. Kazi ya Mungu ni kuyafanya maisha ya watu yaendelee na ni kusaidia roho za watu zichangamke, ili waweze kubaini mambo ya roho, na daima waweze kumpenda Mungu, kumridhisha Mungu. Ufikaji mahali hapa huonyesha kwamba roho ya mtu imefufuliwa, na wakati mwingine atakapokabiliwa na kitu fulani, anaweza kuonyesha hisia mara moja. Yeye huitikia mahubiri, na kuonyesha hisia haraka kwa hali mbalimbali. Huku ndiko kufanikisha uhodari wa roho. Kuna watu wengi ambao wana majibizo ya haraka kwa tukio la nje, lakini mara tu kuingia katika uhalisi au mambo kinaganaga ya roho yanapotajwa, wao huwa wa kutojali na wajinga. Wao huelewa kitu tu kikiwa ni dhahiri. Hizi zote ni ishara za kuwa wa kutojali kiroho na mjinga, za kuwa na uzoefu kidogo wa mambo ya roho. Watu wengine ni hodari wa roho na wana utambuzi. Mara tu wanaposikia kitu kinachoelekezwa kwa hali zao hawapotezi muda kukiandika. Wanakitumia kwa uzoefu wao wa baadaye, na kwa kujibadilisha. Huyu ni mtu ambaye ni hodari katika roho. Na kwa nini anaweza kuonyesha hisia haraka sana? Kwa sababu yeye hulenga vipengele hivi katika maisha ya kila siku, na mara tu mojawapo ya vipengele hivi kinapotajwa, kinatokea kufanana na hali yake ya ndani, na anaweza kukipokea mara moja. Ni sawa na kumpa mtu mwenye njaa chakula; anaweza kula mara moja. Ukimpa chakula mtu asiye na njaa, hana haraka kuonyesha hisia. Daima wewe humwomba Mungu, na kisha unaweza kuonyesha hisia mara moja unapokabiliwa na kitu fulani: kile Mungu huhitaji katika jambo hili, na jinsi unavyopaswa kutenda. Mungu alikuongoza juu ya suala hili mara ya mwisho; unapokabiliwa na kitu cha aina hii leo unajua jinsi ya kuingia katika hali hii, kuuridhisha moyo wa Mungu. Daima ukitenda kwa njia hii na daima upate uzoefu kwa njia hii, wakati fulani utakuwa stadi kwayo. Wakati unasoma neno la Mungu unajua ni mtu wa aina gani Mungu anamzungumzia, unajua ni aina gani ya hali za roho Anayozungumzia, na unaweza kuelewa jambo muhimu na kulitia katika vitendo; hii inaonyesha kuwa unaweza kupata uzoefu. Kwa nini watu wengine hawana jambo hili? Ni kwa sababu hawaweki jitihada nyingi katika kipengele cha kutenda. Ingawa wako tayari kutia ukweli katika vitendo, hawana umaizi wa kweli katika utondoti wa huduma, katika utondoti wa ukweli katika maisha yao. Wanachanganyikiwa jambo linapotokea. Kwa njia hii, unaweza kupotoshwa nabii wa uongo au mtume wa uongo anapokuja. Haikubaliki kupuuza utambuzi. Ni lazima uzingatie mambo ya roho daima: jinsi Mungu hufanya kazi, kile Mungu husema, yale yaliyo matakwa Yake kwa watu, ni watu wa namna gani unapaswa kuwasiliana nao, na ni watu wa aina gani unapaswa kuwaepuka. Ni lazima usisitize mambo haya wakati wa kula na kunywa neno la Mungu na wakati wa uzoefu. Daima ukiwa na uzoefu wa mambo kwa njia hii, utaelewa vizuri vitu vingi, na utakuwa na utambuzi pia. Ni nini kufundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu, ni nini lawama inayotokana na nia ya mwanadamu, ni nini mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini mpango wa mazingira, ni nini maneno ya Mungu yanatolea nuru ndani, kama huna uhakika juu ya mambo haya, hutakuwa na utambuzi. Unapaswa kujua kile ambacho huja kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini tabia ya uasi, jinsi ya kulitii neno la Mungu, na jinsi ya kuacha uasi wa mtu mwenyewe; unapaswa kuelewa utondoti wa ukweli huu wote, ili jambo linapotukia, una ukweli unaofaa wa kulinganisha nalo, una maono yanayofaa kama msingi, una kanuni katika kila jambo na unaweza kutenda kulingana na ukweli. Halafu maisha yako yatajazwa na nuru ya Mungu, yatajazwa na baraka za Mungu. Mungu hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye humtafuta kwa kweli. Hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye huishi kwa kumdhihirisha na ambaye hushuhudia kwa ajili Yake, na hatamlaani mtu yeyote ambaye kwa kweli anaweza kuona kiu ya ukweli. Ikiwa, unapokula na kunywa maneno ya Mungu, unaweza kuzingatia hali yako mwenyewe ya kweli, kuzingatia vitendo vyako mwenyewe, na kuzingatia ufahamu wako mwenyewe, basi, unapokabiliwa na tatizo, utapokea nuru na utapata ufahamu wa utendaji. Kisha utakuwa na njia ya kutenda na utakuwa na utambuzi kwa kila kitu. Mtu aliye na ukweli si rahisi kudanganywa, na rahisi kutenda kwa vurugu au kutenda kwa kupita kiasi. Kwa sababu ya ukweli amelindwa, na pia kwa sababu ya ukweli yeye hupata ufahamu zaidi. Kwa sababu ya ukweli ana njia zaidi za kutenda, hupata fursa zaidi za Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yake, na hupata fursa zaidi za kukamilishwa.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Alhamisi, 28 Februari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya "Wingu Jeupe"

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya "Wingu Jeupe"

Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe katika siku za mwisho (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho.”
Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani aweze kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamemtamani sana na kumwonea shauku kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, kwa Yesu Mwokozi kuwarudia watu ambao Amekuwa mbali nao kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumai kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atazisamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Anatamani Yesu Mwokozi awe jinsi Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi ambaye anapendeka, mwema na wa heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe katika siku za mwisho (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu hafahamu jambo hili: Ingawa Mwokozi Yesu mtakatifu Amejawa na upendo na mapenzi kwa mwanadamu, Angewezaje kufanya kazi katika “mahekalu” yaliyomilikiwa na uchafu na pepo wachafu? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Angewezaje kuwaonekania wale wanaokula mwili wa wasio na haki, kunywa damu ya wasio na haki, kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini lakini hawamfahamu, na wanaompokonya kila wakati? Mwanadamu anajua tu kuwa Yesu Mwokozi amejawa na upendo na huruma, naye ni sadaka ya dhambi iliyojawa na ukombozi. Lakini mwanadamu hana habari kwamba Yeye pia ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, uadhama, ghadhabu, na hukumu, na Aliye na mamlaka na kujawa na hadhi. Kwa hiyo ingawa mwanadamu anazamia kwa hamu na kuonea shauku kurudi kwa Mkombozi, na hata Mbingu inaguswa kwa maombi ya mwanadamu, Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.
“Yehova” ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. “Yesu” ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Uyahudi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa Wayahudi wote. Na hivyo katika enzi ya sasa, Wayahudi wote isipokuwa kabila la Yuda wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu, na kumtumikia wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani katika hekalu. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, nalo lilikuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataitamatisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka katika miisho ya dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.
Mwokozi atakapofika katika siku za mwisho, kama bado angeitwa Yesu, na kuzaliwa mara nyingine katika Uyahudi, na kufanya kazi Yake katika Uyahudi, basi hii ingethibitisha kuwa Niliumba Wayahudi peke yao na kuwakomboa Wayahudi peke yao, na kuwa Sina uhusiano wowote na Mataifa. Je, hii haitakuwa kinyume cha maneno Yangu kwamba “Mimi ni Bwana aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote”? Nilitoka Uyahudi nami Nafanya kazi Yangu kati ya Mataifa kwa sababu Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, ila Mungu wa viumbe vyote. Ninaonekana kati ya Mataifa katika siku za mwisho kwa sababu Mimi si Yehova, Mungu wa Wayahudi tu, lakini, zaidi ya hayo, kwa sababu Mimi ni Muumba wa wateule Wangu wote kati ya Mataifa. Sikuumba Uyahudi, Misri, na Lebanoni pekee, bali pia Niliumba Mataifa yote mbali na Israeli. Na kwa sababu hiyo, Mimi ni Bwana wa viumbe vyote. Nilitumia Uyahudi tu kama hatua ya kwanza ya kazi Yangu, Nikayatumia Uyahudi na Galilaya kama ngome za kazi Yangu ya ukombozi, nami Natumia Mataifa kama msingi ambao Nitatumia kuitamatisha enzi nzima. Nilifanya hatua mbili za kazi katika Uyahudi (hatua mbili za kazi ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema), nami Nimekuwa Nikitekeleza hatua mbili zaidi za kazi (Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme) katika nchi nyingine zote zaidi ya Uyahudi. Nitafanya kazi ya kushinda kati ya Mataifa, na hivyo kuikamilisha enzi. Mwanadamu akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa Nimeianza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa shauku kuwasili kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao wale wasioniamini. Wao ni watu ambao hawanijui, na imani yao Kwangu ni ya bandia. Je, watu kama hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja si kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani maangamizo Yangu ya dunia hii nzee yenye uchafu, lakini badala yake wanatamani kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili, ndipo watakapokombolewa; wanamtazamia Yesu kuwakomboa wanadamu wote mara nyingine kutoka nchi hii iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu kama hao watawezaje kuwa wale wanaoikamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Matamanio ya mwanadamu hayawezi kufikia mapenzi Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu hutamani au kuthamini tu kazi ambayo Nimeifanya hapo awali, naye hajui kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya siku zote na si mzee kamwe. Mwanadamu anajua tu kuwa Mimi ni Yehova, na Yesu, naye hana fununu kuwa Mimi ni Mwisho, Yule ambaye Atawaangamiza wanadamu. Mwanadamu anachotamani na kujua tu ni kuhusu dhana yake mwenyewe, nayo ni yale tu ambayo anaweza kuyaona kwa macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayoifanya, bali hayatangamani nayo. Kama kazi Yangu ingefanywa kulingana na mawazo ya mwanadamu, basi ingeisha lini? Mwanadamu angeingia katika pumziko lini? Nami Ningewezaje kuingia katika siku ya saba, Sabato? Nafanya kazi kulingana na mpango Wangu, kulingana na lengo Langu, na sio kulingana na nia ya mwanadamu.

Jumatano, 27 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Ikiwa watu wanaweza kweli kuielewa kikamilifu njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Wasingetamani tena kuwatumikia wazazi wao ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Je, mategemeo ya baadaye na majaliwa ya mwanadamu si kabisa kile kinachodaiwa nyakati za sasa kuwa “wazazi” wa Petro? Yamekuwa kama tu mwili na damu ya mwanadamu. Je, hatima, mategemeo ya baadaye ya mwili yatakuwa ni kumwona Mungu wakati ukiwa hai, au kwa roho kukutana na Mungu baada ya kifo? Je, mwili kesho utaishia katika tanuu kubwa kama katika taabu, au utakuwa katika kuteketezwa kwa moto? Je, maswali kama haya yanayohusu iwapo mwili wa mwanadamu utahimili taabu au mateso ni habari kubwa sana ambayo kila mtu sasa katika mkondo huu ambaye ana ubongo na akili yake iko sawa anahangaika zaidi nayo? (Hapa, kuhimili mateso hurejelea kupokea baraka; kuteseka humaanisha kwamba majaribu ya siku zijazo ni yenye manufaa kwa hatima ya mwanadamu. Taabu hurejelea kushindwa kusimama imara, au kudanganywa; au, humaanisha kwamba mtu anakabiliana na hali ya hatari ya bahati mbaya katikati ya majanga na maisha yake yanakuwa magumu kuendelea nayo, na kwamba hakuna hatima nzuri kwa roho.) Watu wanajitayarisha na mantiki timamu lakini pengine kile wanachofikiri hakifanani kabisa na kile ambacho mantiki yao inapaswa kutayarishwa nayo. Hii ni kwa sababu ni wajinga kiasi na wanafuata vitu bila kufikiri. Wote wanapaswa kuwa na uelewe wa kina wa kile ambacho wanapaswa kuingia kwacho, na kwa mahususi wanapaswa kutatua kile wanachopaswa kuingia kwacho wakati wa mateso (yaani, wakati wa utakasaji wa tanuu), na kile wanachopaswa kutayarishwa nacho katika jaribu la moto. Usiwatumikie wazazi wako siku zote (kumaanisha mwili) ambao ni sawa na nguruwe na mbwa, na ni wabaya zaidi kuliko chungu na wadudu. Kuna haja gani ya kuteseka juu ya hilo, kufikiri sana, kuutesa ubongo wako? Mwili si wako, bali upo katika mikono ya Mungu ambaye Hakudhibiti wewe pekee bali pia Anamwamuru Shetani. (Kwa asili ilimaanisha kuwa ulikuwa wa Shetani. Kwa kuwa Shetani pia yupo mikononi mwa Mungu, ingeweza kuwekwa hivyo tu. Maana inashawishi zaidi kusema namna hiyo—inamaanisha kuwa wanadamu hawapo chini ya miliki ya Shetani kabisa, bali wapo mikononi mwa Mungu.) Unaishi chini ya mateso ya mwili, lakini je, mwili ni wako? Upo chini ya udhibiti wako? Kwa nini usumbuke kufikiri sana juu ya hilo? Kwa nini usumbuke sana kumsihi Mungu kwa ajili ya mwili wako uliooza ambao umeshahukumiwa zamani sana na kulaaniwa, vilevile kutiwa najisi na roho wachafu? Kwa nini usumbuke siku zote kwa kushikilia washirika wa Shetani karibu na moyo wako? Huna wasiwasi kwamba mwili unaweza kuharibu mategemeo yako halisi ya baadaye, matumaini mazuri, na hatima ya kweli ya maisha yako?
Njia ya leo si rahisi kuitembea. Mtu anaweza kusema kwamba ni vigumu kuipitia na ni adimu sana katika enzi zote. Hata hivyo, nani angeweza kufikiri kuwa mwili wa mwanadamu pekee unatosha kumwangamiza mara moja? Kazi leo hakika ni ya thamani kama vile mvua wakati wa majira ya kuchipua na ni ya thamani kama wema wa Mungu kwa mwanadamu. Hata hivyo, ikiwa mwanadamu hajui kusudi la kazi Yake leo au kuelewa kiini cha mwanadamu, inawezekanaje tunu na thamani yake vizungumziwe? Mwili si wa wanadamu wenyewe, hivyo kwa kweli hakuna mtu anayeweza kuona waziwazi hatima yake itakuwa wapi. Hata hivyo, unapaswa kujua vizuri kwamba Mungu wa uumbaji Atawarudisha binadamu, ambao waliumbwa, katika nafasi yao ya asili, na kurejesha sura yao ya asili kutoka wakati wa kuumbwa kwao. Atachukua tena kikamilifu pumzi Aliyompuliza ndani ya binadamu, na kuchukua tena mifupa na mwili wake na kurudisha vyote kwa Bwana wa viumbe. Atabadilisha na kufanya upya binadamu kikamilifu, na kuchukua tena kutoka binadamu urithi wote ambao kwa asili haukuwa wa binadamu, bali ulikuwa wa Mungu. Hatamkabidhi tena binadamu urithi huo. Maana hakuna hata kitu kimoja kati ya hivyo vilikuwa vya binadamu kwa asili. Atavichukua vyote tena—huu si uporaji usio wa haki, bali unakusudiwa kuirejesha mbingu na dunia katika hali yake ya asili, na kubadilisha na kumfanya upya binadamu. Hii ni hatima inayofaa kwa mwanadamu, ingawa pengine si kuichukua tena baada ya kuuadibu mwili kama watu wanavyofikiri. Mungu hataki mifupa ya mwili baada ya maangamizi yake, bali vitu vya asili katika mwanadamu ambavyo mwanzo vilikuwa vya Mungu. Hivyo, hatawaangamiza binadamu au kuuondoa kabisa mwili wa binadamu, maana mwili wa binadamu si mali binafsi ya mwanadamu. Badala yake, ni kiungo cha Mungu, ambaye anasimamia binadamu. Angewezaje kuuangamiza mwili wa binadamu ili Yeye “afurahi”? Je, wakati huu, kwa kweli umeachana na kila kitu cha huo mwili wako ambao hauna thamani hata ya senti moja? Kama ungeweza kuelewa asilimia thelathini ya kazi ya siku za mwisho (asilimia thelathini tu, yaani, kuifahamu kazi ya Roho Mtakatifu leo, vilevile kazi ya neno Mungu hufanya katika siku za mwisho), basi usingeweza kuendelea “kuutumikia” au “kuwa” na upendo kwa mwili wako kama unavyofanya leo, ambao umepotoka kwa miaka mingi. Unapaswa kuelewa kwa kina kwamba binadamu sasa wameendelea kwa hali ambayo haijawahi kutokea na hawataendelea tena kusonga mbele kama magurudumu ya historia. Mwili wako wa udongo umeshafunikwa na nzi tangu zamani, hivyo unawezaje kuwa na nguvu ya kurudisha nyuma magurudumu ya historia ambayo Mungu ameyawezesha kuendelea hadi siku hii ya leo? Unawezaje kufanya saa ya siku za mwisho ambayo ni kama bubu ipige tena na kuendelea kusogeza mikono yake kwa upande wa kulia? Unawezaje kuubadilisha upya ulimwengu ambao unaonekana kama umefunikwa na ukungu mzito? Je, mwili wako unaweza kufufua milima na mito? Je, mwili wako, ambao una kazi ndogo tu, unaweza kweli kurejesha ulimwengu wa binadamu ambao umekuwa ukiutamani? Unaweza kweli kuwaelimisha wadhuria wako kuwa “binadamu”? Unaelewa sasa? Mwili wako unamilikiwa na nini hasa? Makusudi halisi ya Mungu ya kumfinyanga mwanadamu, ya kumkamilisha mwanadamu, na ya kumbadilisha mwanadamu hayakuwa kukupatia nchi nzuri ya asili au kuleta pumziko la amani kwa mwili wa mwanadamu. Badala yake, ilikuwa ni kwa ajili ya utukufu Wake na ushuhuda Wake, kwa furaha bora ya binadamu hapo baadaye, na ili kwamba hivi karibuni waweze kufurahia pumziko. Bado, si kwa ajili ya mwili wako, maana mwanadamu ni mtaji wa usimamizi wa Mungu na mwili wa mwanadamu ni kiungo tu. (Mwanadamu ni kitu chenye roho na mwili, wakati mwili ni kitu kiharibikacho tu. Hii humaanisha kwamba mwili ni chombo kwa ajili ya mpango wa usimamizi.) Unapaswa kujua kwamba kuwakamilisha wanadamu, kuwatimiza wanadamu, na kuwapata wanadamu hakujaleta kitu chochote zaidi ya mapanga na maangamizi kwa mwili wao, na kumeleta mateso yasiyokoma, kuungua kwa moto, hukumu zisizokuwa na huruma, kuadibu, na laana, na vilevile majaribu yasiyokuwa na mipaka. Hicho ni kisa cha ndani na ukweli wa kazi ya kumsimamia binadamu. Hata hivyo, vitu hivi vyote vimelengwa dhidi ya mwili wa binadamu, na mikuki yote ya uhasama bila huruma inaelekezwa kwenye mwili wa binadamu (maana kwa asili binadamu hakuwa na hatia). Hayo yote ni kwa ajili ya utukufu na ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake. Hii ni kwa sababu kazi Yake si tu kwa ajili ya binadamu, bali ni kwa ajili ya mpango wote na kutimiza mapenzi Yake ya asili Alipomuumba binadamu. Kwa hiyo, pengine asilimia tisini ya kile ambacho watu wanapitia ni mateso na majaribu ya moto, lakini kuna siku chache sana tamu na za furaha au hata hakuna kabisa ambazo mwili wa mwanadamu umekuwa ukitamani, na hata hawawezi kufurahia nyakati za furaha katika mwili wakishinda jioni nzuri pamoja na Mungu. Mwili ni mchafu, hivyo kile ambacho mwili wa mwanadamu unakiona au unakifurahia si chochote bali ni adabu ya Mungu ambayo haipendwi na mwanadamu, na ni kana kwamba ulikuwa unakosa mantiki ya kawaida. Hii ni kwa sababu Atadhihirisha tabia Yake ya haki ambayo haipendwi na mwanadamu, haivumilii makosa ya mwanadamu, na huchukia kabisa maadui. Mungu hufichua waziwazi tabia Yake yote kupitia njia yoyote iwezekanayo, na hivyo Akihitimisha kazi ya vita Vyake na Shetani vya miaka elfu sita—kazi ya wokovu wa binadamu wote na maangamizi ya Shetani wa zamani!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumanne, 26 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili. Kwa hivyo ingawa wale Waisraeli walinipigilia misumari msalabani hadharani, wao, ambao wamekuwa wanamngoja Masiha na Yehova na kumtamani sana Mwokozi Yesu, hawajasahau ahadi Yangu. Hii ni kwa sababu Sijawatelekeza. Hata hivyo, Nilikuwa nimechukua damu kama ushahidi wa agano Nililoanzisha na mwanadamu. Ukweli huu umekuwa "damu ya agano" lililoandikwa katika mioyo ya watu wachanga na wasio na hatia, kana kwamba lilichapiliwa, na kama kuishi kwa pamoja kwa amani kwa mbingu na dunia milele. Sijawahi kuzidanganya nafsi hizo za huzuni Nilizoziokoa, kuzipata, na ambazo hunipenda zaidi ya yule mwovu baada ya Mimi kuzijaalia na kuzichagua. Kwa hiyo, kwa shauku zinatazamia kurudi Kwangu na kwa hamu zinatarajia kukutana na Mimi. Kwa kuwa Sijawahi kufuta agano Nililoanzisha nazo kwa damu, si ajabu kwamba zimekuwa zikisubiri kwa hamu. Nitawateka tena wanakondoo hawa ambao wamepotea kwa miaka, kwa maana siku zote Nimewapenda mwanadamu. Ni kwamba tu dalili za uovu zimeongezwa kwa wema katika wanadamu. Nitazipata zile nafsi hafifu ambazo zinanipenda na ambazo Nimezipenda tayari, lakini Nawezaje kuwaleta wale waovu ambao hawajawahi kunipenda na wametenda kama adui ndani ya nyumba Yangu? Sitawaleta wazawa wa Shetani na nyoka mwenye sumu kali ambao hunichukia, hunipinga, hunikataa, hunishambulia, na kunilaani ndani ya ufalme Wangu, hata ingawa Nimeanzisha agano la damu na mwanadamu. Unapaswa kujua kwa nini na kwa ajili ya nani Ninatekeleza kazi hiyo. Je, ni wema au uovu katika upendo wako? Je, kwa kweli unanijua kama vile walivyonijua Daudi na Musa? Je, kwa kweli unanihudumia kama vile alivyonihudumia Ibrahimu? Ni kweli kwamba unafanywa kamili na Mimi, lakini unapaswa kujua hili: Ni nani utakayemwakilisha? Utakuwa na matokeo sawa na nani? Katika maisha yako, una mavuno ya furaha na mengi katika kupata uzoefu kunihusu? Je, ni mengi na yenye matokeo mazuri? Unapaswa kujichunguza mwenyewe. Kwa miaka umefanya kazi kwa bidii kwa ajili Yangu, lakini umewahi kupata chochote? Umebadili au kupata kitu chochote? Badala ya uzoefu wako katika shida, je, unakuwa kama Petro ambaye alisulubiwa, au kama Paulo ambaye alibwagwa na kupokea mwanga mkubwa? Unapaswa kuwa na ufahamu wa haya. Mimi sizungumzi siku zote juu ya, na kufikiria kuhusu maisha yako ambayo ni madogo kuliko mbegu ya haradali, ambayo ni ukubwa wa punje ya mchanga. Kusema kweli, ni mwanadamu ambaye Ninasimamia. Hata hivyo, Sifikirii maisha ya mwanadamu, ambaye wakati mmoja Nilimchukia lakini baadaye Nikamwinua tena, kama sehemu muhimu ya usimamizi Wangu. Unapaswa kuwa mwenye uhakika juu ya utambulisho wako wa zamani kwa kweli ulikuwa upi, na ni nani mliyemtumikia kama watumwa. Kwa hiyo, Situmii nyuso za wanadamu kama ya Shetani kama mali ghafi kuwasimamia, kwa kuwa wanadamu si vitu vya thamani. Mnapaswa kukumbuka mtazamo Wangu kwenu hapo mwanzoni, na hotuba Yangu kwenu wakati huo ambayo haikuwa bila umuhimu wa utendaji. Unapaswa kujua kwamba zile "kofia" juu ya vichwa vyenu zina msingi. Ninadhani kwamba nyote mnajua kwamba hamkuwa wa Mungu kwa asili, lakini mlikamatwa na Shetani zamani na kutumikia nyumbani kwake kama watumishi waaminifu. Mmenisahau kwa muda mrefu, kwani kwa muda mrefu mmekuwa nje ya nyumba Yangu lakini mikononi mwa yule mwovu. Wale ambao Mimi huokoa ni wale ambao Nimewaamulia kabla zamani na wamekombolewa na Mimi, wakati ninyi ni nafsi hafifu ambazo zimewekwa kati ya wanadamu kama jambo la pekee. Mnapaswa kujua kwamba nyinyi si wa nyumba ya Daudi au Yakobo, lakini ni wa nyumba ya Moabu, ambao ni wanachama wa kabila la Mataifa. Kwa maana Sikuanzisha agano na nyinyi, lakini Nilitekeleza tu kazi na kunena kati yenu, na kuwaongoza. Damu Yangu haikumwagika kwa ajili yenu. Nilitekeleza tu kazi kati yenu kwa ajili ya ushuhuda Wangu. Je, hamjajua hilo? Je, kazi Yangu kweli ni kama Yesu kumwaga damu hadi kufa kwa niaba yenu? Haikuwa na thamani kwamba Nilivumilia fedheha kubwa kwa ajili yenu. Mungu, ambaye hana dhambi kabisa, kwa kweli Alikuja pahali ambapo ni kama pahali pa mbwa na nguruwe, ambapo panachukiza kabisa na kukirihi, na hapawezi kukalika na mwanadamu. Hata hivyo, Nilivumilia hii aibu yote ya ukatili kwa ajili ya utukufu wa Baba Yangu na kwa ajili ya ushuhuda wa milele. Mnapaswa kujua mienendo yenu na kuona kwamba nyinyi si watoto waliozaliwa katika "familia tajiri na yenye nguvu" bali watoto fukara tu wa Shetani. Nyinyi si waanzilishi kati ya wanadamu, na hamna haki za kibinadamu au uhuru. Kwa asili, hamkuwa na mgao wowote kabisa la baraka kutoka kwa binadamu au ufalme wa mbinguni. Hili ni kwa sababu mko chini kabisa ya binadamu katika wanadamu, na Sijawahi kufikiria kuhusu wakati wenu ujao. Kwa hivyo, ingawa ilikuwa sehemu ya asili ya mpango Wangu kwamba leo Ningekuwa na imani kuwakamilisha, ni kazi ya pekee, kwa sababu hadhi yenu ni ya chini sana na kiasili hamkuwa na mgawo katika binadamu. Je, hii si baraka kwa wanadamu?
Wale Ninaowaokoa ni nafsi ambazo Nilizitoa kutoka toharani zamani, na waliochaguliwa ambao Nilitembelea zamani, kwa kuwa wametamani sana kuonekana Kwangu tena kati yao. Wamenipenda, na wameandika agano Langu ambalo Nilianzisha kwa damu katika mioyo yao, kwa sababu Nimewapenda. Wao ni kama kondoo waliopotea ambao wamekuwa wakinitafuta kwa miaka mingi, na wao ni wazuri, na kwa hivyo Ninawaita Waisraeli wazuri na malaika wadogo wanaopendeza. Singepitia aibu kama hii iwapo Ningekuwa miongoni mwao. Ni kwa sababu wananipenda zaidi kuliko wanavyopenda maisha yao wenyewe, na Ninawapenda kama kile ambacho ni kirembo zaidi kati ya vitu vyote. Ni kwa sababu waliumbwa na Mimi na ni Wangu; hawajawahi kunisahau. Upendo wao unazidi upendo wenu, na wananipenda kwa upendo mkubwa zaidi kuliko mnavyopenda maisha yenu wenyewe. Wananitii Mimi kama vile njiwa wadogo weupe hufanyia anga, na kwa upendo mkubwa zaidi kuliko mnavyonifanyia. Na ni kwa sababu wao ni wazawa wa Yakobo, watoto wa Adamu, na ni miongoni mwa wateule Wangu, kwa kuwa Nimewapenda zamani, na hata zaidi kuliko Ninavyowapenda, na kwa sababu nyinyi ni waasi sana, upinzani wenu ni mkubwa sana, mnaniangalia kwa dharau sana, hamnithamini hata kidogo Kwangu, mnanipenda kidogo sana, na mnanichukia sana. Mnadharau kazi Yangu, na kutweza vitendo Vyangu sana. Tofauti na wao, hamjawahi kuona matendo Yangu kuwa kitu cha thamani. Badala yake, mnayadharau na macho mekundu ya wasiwasi, kama tu Shetani. Utiifu wenu uko wapi? Tabia zenu ziko wapi? Upendo wenu uko wapi? Ni lini mmeonyesha wazi dalili ya upendo ndani yenu? Ni lini mmechukua kazi Yangu kwa uzito kabisa? Hurumia wale malaika wa kupendeza ambao kwa wasiwasi wananitazamia na kuteseka sana wakati wanaponisubiri kwa wasiwasi, kwani Ninawapenda kwa dhati. Hata hivyo, kile Ninachokiona leo ni ulimwengu usio wa kibinadamu sana ambao hauhusiani nao. Je, hamfikirii kuwa dhamiri zenu zilikuwa zisizojali na zisizo na huruma muda mrefu uliopita? Je, hamfikirii kuwa nyinyi ndio watu duni mnaozuia kurudiana Kwangu na malaika wa kupendeza? Ni lini hawajakuwa wakisubiri kurudi Kwangu? Ni lini hawajakuwa wakisubiri kuungana tena na Mimi? Je, ni lini hawajatarajia kushinda kwa siku nzuri na kula pamoja na Mimi? Je, mliwahi kutambua kwamba kile mfanyacho leo—yaani, kufanya ghasia ulimwenguni, kupanga njama dhidi ya nyinyi kwa nyinyi, kudanganyana, kutenda kwa uongo, kwa siri na kwa ukavu wa macho, kutojua ukweli, kuwa wasio waaminifu na wadanganyifu, kutenda ubembelezaji, nyinyi kujiona daima kuwa waadilifu na bora zaidi kuliko wengine, kuwa wenye kiburi, na kutenda kikatili kama wanyama wa mwitu milimani na kwa fujo kama mfalme wa wanyama—uko wapi mfano wa mwanadamu? Nyinyi ni fidhuli na wasio na busara. Hamjawahi kuliona neno Langu kuwa hazina, lakini badala yake mmechukua mtazamo wa dharau. Kwa njia hii, mafanikio, maisha ya kweli ya binadamu, na matumaini mazuri yangetoka wapi? Je, wazo lako badhirifu litakuokoa kwa kweli kutoka kwa kinywa cha chui? Kweli litakuokoa kutoka kwa moto unaowaka? Je, ungekuwa umeanguka hadi hapa iwapo kwa kweli ungeiona kazi Yangu kuwa kitu cha thamani kubwa mno? Inaweza kuwa kwamba majaliwa yako kweli hayawezi kubadilishwa? Je, uko tayari kufa na majuto kama haya?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili