Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumatano, 25 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (6) - Je, Bado Tunaweza Kupata Uzima Tukiondoka Kwa Biblia?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (6) - Je, Bado Tunaweza Kupata Uzima Tukiondoka Kwa Biblia?

Mara kwa mara wachungaji na wazee huwafundisha watu kuwa hawawezi kuitwa waumini wakiondoka kwenye Biblia, na kwamba kwa kushikilia Biblia pekee ndiyo wanaweza kupata uzima na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hivyo, je, kweli hatuwezi kupata uzima tukiondoka kwenye Biblia? Je, ni Biblia ambayo inaweza kutupa uzima, au ni Mungu ambaye anaweza kutupa uzima? Bwana Yesu alisema, "Tafuta katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnadhani kuwa mna uzima wa milele: na hayo ndiyo yananishuhudia. Nanyi hamtakuja Kwangu, kwamba mpate uhai" (Yohana 5:38-40). Mwenyezi Mungu asema, "Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atajua Mungu na kuidhinishwa na Mungu" (Neno Laonekana katika Mwili). Kwa hivyo, uzima una chanzo chake katika Kristo wala sio katika Biblia. Kristo pekee ndiye chanzo cha uzima na Yeye ndiye Bwana wa Biblia. Video hii itakusaidia kupata ufahamu mpya wa Biblia!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kukamilishwa na Mungu

Jumanne, 24 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (5) - Ni Vipi Kuna Makosa Ndani ya Biblia?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (5) - Ni Vipi Kuna Makosa Ndani ya Biblia?

Watu wengi wanaamini kwamba Biblia yote imetiwa msukumo na Mungu, kwamba imetoka kabisa kwa Roho Mtakatifu, na kwamba hakuna hata neno moja lililo na kosa. Je, mtazamo wa aina hii unawiana na ukweli? Biblia iliandikwa na waandishi zaidi ya 40, yaliyomo yaliandikwa na kupangwa na mwanadamu, na haikufunuliwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu. Ilikuwa vigumu kuepuka kuingiza mawazo na makosa ya mwanadamu wakati ambapo ilikuwa ikiandikwa na kupangwa na mwanadamu.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu

Jumatatu, 23 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (4) - Je, Biblia Nzima Imetiwa Msukumo na Mungu Kweli?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (4) - Je, Biblia Nzima Imetiwa Msukumo na Mungu Kweli?

Watu wengi katika ulimwengu wa dini wanaamini kwamba "Kila andiko limetolewa kwa msukumo wa Mungu," yote katika Biblia ni neno la Mungu. Je, kauli ya aina hii inakubaliana na ukweli? Biblia ni ushahidi wa Mungu pekee, rekodi ya kazi ya Mungu tu, na haijaundwa kwa matamshi ya Mungu kikamilifu. Ndani ya Biblia, ni maneno yaliyonenwa na Yehova Mungu, maneno ya Bwana Yesu, unabii wa Ufunuo na maneno ya manabii yaliyotolewa kwa msukumo wa Mungu pekee, ndiyo neno la Mungu. Mbali na hayo, mengi ya yaliyosalia yanahusiana na rekodi za kihistoria na ushuhuda wa uzoefu wa mwanadamu. Ikiwa ungependa kujua undani wa Biblia, basi tafadhali angalia video hii!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Dondoo za Video ,

Jumapili, 22 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (3) - Je, Inamaanisha Nini katika Ufunuo Inaposema Mtu Asiongeze kwa Unabii?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (3) - Je, Inamaanisha Nini katika Ufunuo Inaposema Mtu Asiongeze kwa Unabii?

Ufunuo sura ya 22, mstari wa 18 "Kwa kuwa namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Iwapo mtu yeyote ataongeza kwa mambo haya, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki." Je, ungependa kujua maana halisi ya maneno haya? Video hii itakuonyesha jibu.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maandiko ya Biblia

Jumamosi, 21 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (2) - Imefichuliwa: Uhusiano Kati ya Mungu na Biblia

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (2) - Imefichuliwa: Uhusiano Kati ya Mungu na Biblia

Wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini wanaamini kuwa maneno na kazi zote za Mungu yamo ndani ya Biblia, kwamba wokovu wa Mungu katika Biblia ni mkamilifu na mradi watu waweke msingi wa imani yao katika Bwana katika Bibilia na washikilie Bibilia, basi wanaweza kunyakuliwa na wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Je, kweli ukweli uko namna hii? Je, ni Mungu ambaye anaweza kufanya kazi kutuokoa, au Biblia? Je, ni Mungu ambaye anaweza kuonyesha ukweli, au Biblia? Ili kujifunza zaidi, tafadhali angalia video hii!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hekima ya Mungu

Ijumaa, 20 Julai 2018

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (1) - Imefichuliwa: Je, Kuna Maneno Yoyote au Kazi ya Mungu Mbali na Yaliyo katika Biblia?

"Fichua Siri Kuhusu Biblia" (1) - Imefichuliwa: Je, Kuna Maneno Yoyote au Kazi ya Mungu Mbali na Yaliyo katika Biblia?

Wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini mara nyingi huwafundisha watu kwamba hakuna maneno na kazi ya Mungu nje ya Biblia, na hivyo kwenda zaidi ya Biblia ni uzushi. Je, wazo hili linastahili kuchunguzwa? Je, linalingana na ukweli wa kazi ya Mungu? Kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema haijaandikwa tu katika Agano la Kale na inakwenda zaidi ya Agano la Kale. Ikiwa kwenda zaidi ya Biblia ni uzushi, je, si basi sisi pia tunahukumu kazi ya Bwana? Hivyo kuna maneno au kazi ya Mungu isipokuwa yale yaliyo katika Biblia, au hakuna? Video hii itakufichulia jibu.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Dondoo za Video ,

Jumanne, 17 Julai 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Je, Umekuwa Hai Tena?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Je, Umekuwa Hai Tena?

Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya kutimiza kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, na umefanywa mkamilifu, ingawa utakuwa huwezi kunena unabii, wala siri zozote, utakuwa unaishi kulingana na kufichua taswira ya mwanadamu. Mungu alimuumba mwanadamu, baada ya hapo mwanadamu akaharibiwa na Shetani, na uharibifu huu umewafanya watu wawe maiti—na hivyo, baada ya kuwa umebadilika, utakuwa tofauti na maiti hizi. Ni maneno ya Mungu ndiyo yanatoa uzima kwa roho za watu na kuwasababisha kuzaliwa upya, na roho za watu zinapozaliwa upya, watakuwa hai tena. Neno "wafu" linarejelea maiti ambazo hazina roho, kwa watu ambao roho zao zimekufa. Roho za watu zinapowekewa uhai, wanakuwa hai tena. Watakatifu waliozungumziwa awali huashiria watu ambao wamekuwa hai, wale ambao walikuwa chini ya ushawishi wa Shetani lakini wakamshinda Shetani. Wateule wa China wamestahimili ukatili na mateso na ulaghai wa joka kuu jekundu, ambalo limewaacha wakiwa wameharibika kiakili na kuwachwa wakiwa hawana hata ujasiri wa kuishi. Hivyo, kuamsha roho zao kunapaswa kuanza na hulka zao. Kidogo kidogo, katika hulka yao roho yao itaamshwa. Siku moja, watakapokuwa hai tena, hakutakuwa na vizuizi zaidi, na vyote vitasonga mbele bila tatizo. Kwa sasa, hii inabakia kuwa bado haijafanikiwa. Kuishi kwa kudhihirisha kwa watu wengi kunajumuisha mazingira ya kifo, wamezungukwa na hali ya kifo, na wamepungukiwa sana. Maneno ya baadhi ya watu yanabeba kifo, matendo yao yanabeba kifo, na takribani kila kitu wanachoishi kwa kudhihirisha ni kifo. Ikiwa leo, watu wanamshuhudia Mungu waziwazi, basi kazi hii itashindwa, maana bado hawajakuwa hai tena kikamilifu, na kuna wafu wengi sana miongoni mwenu. Leo, baadhi ya watu wanauliza kwa nini Mungu haonyeshi ishara na maajabu ili kwamba aweze kusambaza kazi Yake miongoni mwa nchi za Wamataifa. Wafu hawawezi kuwa na ushuhuda wa Mungu; walio hai wanaweza, lakini watu wengi leo ni wafu, wengi wao wanaishi katika kifungo cha kifo, wanaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hawawezi kupata ushindi—na hivyo wanawezaje kuchukua ushuhuda wa Mungu? Wanawezaje kueneza kazi ya injili?
Wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, ni wale ambao wanaishi katikati ya kifo, ni wale ambao wametawaliwa na Shetani. Bila kuokolewa na Mungu, na kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, watu wanakuwa hawana uwezo kukwepa athari ya kifo, hawawezi kuwa hai. Wafu hawa hawawezi kuwa ushuhuda kwa Mungu, wala hawawezi kutumiwa na Mungu, wala kuingia katika ufalme. Mungu anahitaji ushuhuda wa walio hai, na sio wafu, na Anaomba kwamba walio hai wafanye kazi kwa ajili Yake, na sio wafu. "Wafu" ni wale ambao wanampinga na kumwasi Mungu, ni wale ambao ni mbumbumbu katika roho na hawaelewi maneno ya Mungu, ni wale ambao hawaweki ukweli katika matendo na hawana utii hata kidogo kwa Mungu, na ni wale wamemilikiwa na Shetani na kunyanyaswa na Shetani. Wafu wanajionyesha wenyewe kwa kusimama kwa kuupinga ukweli, kwa kumwasi Mungu, na kwa kuwa duni, wa kudharaulika, kuwa waovu, katili, wadanganyifu, na kudhuru kwa siri. Ingawa watu wa namna hiyo wanakula na kunywa maneno ya Mungu, hawana uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu; wanaishi, lakini ni wafu wanaotembea, ni maiti zinazopumua. Wafu hawawezi kabisa kumridhisha Mungu, wala kumtii kikamilifu. Wanaweza tu kumdanganya, kusema maneno ya makufuru juu Yake, na kumsaliti, na yote wanayoyaishi kwa kudhihirisha hufichua asili ya Shetani. Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Baada ya hapo ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi. Mwanadamu wa asili aliyeumbwa na Mungu alikuwa hai, lakini kwa sababu ya uharibifu wa Shetani maisha ya mwanadamu yapo katikati ya kifo, na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo watu hawa wamekuwa wafu ambao hawana roho, wamekuwa ni maadui ambao wanampinga Mungu, wamekuwa nyenzo ya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu wote walio hai ambao wameumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda wake, na Amempoteza mwanadamu, ambaye Alimuumba na ndiye kiumbe pekee aliye na pumzi Yake. Ikiwa Mungu ataamua kurejesha ushuhuda Wake, na kuwarejesha wale ambao waliumbwa kwa mkono wake lakini ambao wamechukuliwa mateka na Shetani, basi ni lazima awafufue ili waweze kuwa viumbe hai, na ni lazima awaongoe ili kwamba waweze kuishi katika nuru Yake. Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake. Mungu anawaokoa wale ambao wanaweza kuwa hai tena, ambao wanaweza kuuona wokovu wa Mungu, ambao wanaweza kuwa watii kwa Mungu, na wapo tayari kumtafuta Mungu. Anawaokoa wale ambao wanamwamini Mungu aliyepata mwili, na wanaamini katika kuonekana Kwake. Baadhi ya watu wanaweza kuwa hai tena, na baadhi hawawezi; inategemea na asili yao kama inaweza kuokolewa au la. Watu wengi wamesikia sana kuhusu maneno ya Mungu lakini bado hawaelewi mapenzi ya Mungu, wameyasikia maneno mengi sana ya Mungu lakini bado hawawezi kuyaweka katika vitendo, hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ukweli wowote na pia kwa kukusudia kabisa wanaingilia kazi ya Mungu. Hawawezi kufanya kazi yoyote kwa ajili ya Mungu, hawawezi kujitolea chochote Kwake, na pia wanatumia kwa siri pesa za kanisa, na kula katika nyumba ya Mungu bure. Watu hawa ni wafu, na hawataokolewa. Mungu anawaokoa wale ambao wapo katika kazi Yake. Lakini kuna sehemu ya watu hao ambao hawawezi kupokea wokovu Wake; ni idadi ndogo tu ndiyo inaweza kupokea wokovu Wake, maana watu wengi ni wafu sana, ni wafu sana kiasi kwamba hawawezi kuokolewa, wameharibiwa kabisa na Shetani, na kwa asili, wamekuwa hatari sana. Wala idadi ndogo hiyo ya watu haikuweza kumtii Mungu kikamilifu. Hawakuwa wale ambao walikuwa waaminifu kabisa kwa Mungu tangu mwanzo, au wale ambao walikuwa na upendo wa hali ya juu kabisa kwa Mungu toka mwanzo; badala yake, wamekuwa watiifu kwa Mungu kwa sababu ya kazi Yake ya ushindi, wanamwona Mungu kwa sababu ya upendo wake mkuu, kuna mabadiliko katika tabia zao kwa sababu ya tabia ya Mungu ya haki, na wanamjua Mungu kwa sababu ya kazi Yake, ambayo ni halisi na ya kawaida. Bila kazi hii ya Mungu, haijalishi watu hawa ni wazuri kiasi gani bado wangebaki kuwa wa Shetani, bado wangekuwa ni wa kifo, bado wangekuwa wafu. Kwamba, leo, watu hawa wanaweza kupokea wokovu wa Mungu ni kwa sababu kabisa wanaweza kushirikiana na Mungu.
Kwa sababu ya utiifu wao kwa Mungu, walio hai wanaweza kuchukuliwa na Mungu na kuishi katika ahadi Zake, na kwa sababu ya upinzani wao kwa Mungu, wafu watachukiwa zaidi na kukataliwa na Mungu na kuishi katikati ya adhabu na laana Zake. Hiyo ndiyo tabia ya haki ya Mungu, na haiwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Kwa sababu ya utafutaji wao wenyewe, watu wanapokea kibali cha Mungu na kuishi katika nuru; kwa sababu ya hila zao za kutisha, watu wanalaaniwa na Mungu, na kushuka chini katika adhabu; kwa sababu ya matendo yao maovu, watu wanaadhibiwa na Mungu; na kwa sababu ya kutamani kwao sana na utii wao, watu wanapokea baraka za Mungu. Mungu ni mwenye haki: Anawabariki walio hai, na kuwalaani waovu, ili kwamba siku zote wanakuwa katikati ya kifo, na kamwe hawataishi katika nuru ya Mungu. Mungu atawachukua walio hai kwenda katika ufalme Wake, Atawachukua walio hai kwenda katika baraka Zake milele. Wafu Atawaangusha katika kifo cha milele; wao ni wahusika wa uharibifu Wake, na siku zote watakuwa kwa Shetani. Mungu hamtendei mtu yeyote bila haki. Wale wote ambao kweli wanamtafuta Mungu hakika watabaki katika nyumba ya Mungu, na wale wote ambao hawamtii Mungu, na wale ambao hawana ulinganifu Naye hakika wataishi katika adhabu Yake. Pengine huna uhakika kuhusu kazi ya Mungu katika mwili—lakini siku moja mwili wa Mungu hautapangilia hatima ya mwanadamu moja kwa moja; badala yake, Roho Wake, atapanga mwisho wa mwanadamu, na wakati huo watu watajua kwamba mwili wa Mungu na Roho Wake ni kitu kimoja, kwamba mwili Wake hauwezi kufanya kosa, na hata Roho Wake hawezi kabisa kufanya kosa. Na hatimaye, hakika atawachukua wale ambao watakuwa hai tena na kuwapeleka katika ufalme Wake, hakuna zaidi, wala pungufu, na wale wafu ambao hawakutoka wakiwa hai watatupwa katika shimo la Shetani.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 16 Julai 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Watu! Furahini!

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, utukufu kwa Mungu,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Watu! Furahini!

Mwenyezi Mungu alisema, Katika nuru Yangu, watu wanaona nuru tena. Katika neno Langu, watu wanapata vitu vya raha. Nimekuja kutoka Mashariki nami Natoka huko. Wakati ambapo utukufu Wangu unang'aa, mataifa yote yanaangaziwa, vitu vyote vinaletwa katika nuru, hakuna kitu kinachobaki katika giza. Katika ufalme, maisha ya watu wa Mungu pamoja na Mungu ni ya furaha isiyolinganishwa. Maji yanacheza kwa ajili ya maisha ya watu yaliyobarikiwa, milima inafurahia utele Wangu pamoja na watu. Wanadamu wote wanajitahidi, wakifanya kazi kwa bidii, wakionyesha uaminifu wao katika ufalme Wangu. Katika ufalme, hakuna uasi tena, hakuna upinzani tena; mbingu na dunia vinategemeana, Mimi na mwanadamu tuko karibu nasi tunahisi kwa kina, kupitia furaha kuu za maisha, tukiegemeana.... Wakati huu, Naanza rasmi maisha ya mbinguni. Kuingilia kwa Shetani hakuko tena, na watu wanaingia katika pumziko. Kotekote katika ulimwengu, wateule Wangu wanaishi katika utukufu Wangu, wamebarikiwa kwa kiwango kisichonganishika, si kama watu wanaoishi kati ya watu, bali kama watu wanaoishi na Mungu. Kila mtu amepitia upotovu wa Shetani, ameonja uchungu na utamu wa maisha. Sasa akiishi katika nuru Yangu, mtu anawezaje kukosa kushangilia? Mtu anawezaje kuuacha tu wakati huu mzuri na kuuacha upite? Watu! Sasa imbeni nyimbo zilizo ndani ya mioyo yenu na mnichezee! Sasa inueni mioyo yenu ya kweli na kuipeana Kwangu! Sasa pigeni ngoma zenu na kunichezea! Naangaza furaha juu ya ulimwengu wote! Nawaonyesha watu uso Wangu wa utukufu! Nitanguruma! Nitaupita sana ulimwengu! Tayari Natawala kati ya watu! Nainuliwa na watu! Nachukuliwa katika mbingu za samawati na watu wanaenda na Mimi. Natembea kati ya watu na watu Wangu wananizunguka! Mioyo ya watu ni yenye furaha, nyimbo zao zatetemesha ulimwengu, Nikifanya upenyu katika mbingu! Ulimwengu haujafunikwa kwa ukungu tena; hakuna matope tena, hakuna mkusanyiko wa maji taka tena. Watu watakatifu wa ulimwengu! Chini ya ukaguzi Wangu uso wenu halisi unafichuliwa. Ninyi sio watu waliofunikwa na uchafu, bali watakatifu safi kama jiwe la thamani, wapendwa Wangu wote, wote wanaonifurahisha! Vitu vyote vinafufuka! Watakatifu wote wamerudi mbinguni wakinihudumia, wakiingia katika kumbatio Langu la joto, hawalii tena, hawana wasiwasi tena, wakijitoa Kwangu, wakirudi nyumbani Kwangu, na katika nchi yao watanipenda milele! Hawabadiliki! Huzuni uko wapi! Machozi yako wapi! Mwili uko wapi! Dunia haipo tena; mbingu ni za milele. Ninaonekana kwa watu wote, na watu wote wananisifu. Uzima huu, uzuri huu, tangu wakati wa zamani na hata milele, havitabadilika. Huu ndio uzima katika ufalme.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 15 Julai 2018

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(6): Kurudi

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(6): Kurudi

Mwenyezi Mungu anasema, "Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yupo pembeni mwako Anakuangalia, anakusubiri uweze kumrudia. Anasubiri siku ambayo kumbukumbu zako zitarejea" (Neno Laonekana katika Mwili) Jinsi tu Xiaozhen aliachwa akiwa ameviliwa na kupigwa na ulimwengu huu na alijitoa mwenyewe kwa kukata tamaa, upendo wa Mwenyezi Mungu ulimjia na moyo wake ukaamshwa …
Soma Zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu

Jumamosi, 14 Julai 2018

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(5): Maisha katika Bwalo la Dansi

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(5): Maisha katika Bwalo la Dansi

Akiishi nyuma ya kinyago, Xiaozhen alisimilishwa na kumezwa polepole na ulimwengu huu. Alipoteza heshima yake miongoni mwa njia potovu za ulimwengu mbaya …
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kutenda ukweli

Ijumaa, 13 Julai 2018

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(4): Upotovu

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(4): Upotovu

Akiwa amekumbwa na ulimwengu mbaya na ukweli mkali, katika huzuni, Xiaozhen aliacha uaminifu wake na kung’ang’ana kuvaa kinyago. Kutoka wakati huo na kuendelea, alipotea …
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu

Alhamisi, 12 Julai 2018

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(3): Wakiacha Wema na Kufuata Uovu

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(3): Wakiacha Wema na Kufuata Uovu

Katika ulimwengu huu wa mioyo mibaya ambapo pesa ni mfalme, ni machaguo yapi ambayo Xiaozhen aliye safi na mzuri aliyafanya, ya maisha na ya kuendelea kuishi …
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wafuasi wa Kristo

Jumatano, 11 Julai 2018

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(2): Kupigania Dhahabu

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(2): Kupigania Dhahabu

Xiaozhen alipopata kipande kikubwa cha dhahabu, aliwaita marafiki wake ili wagawane. Kile ambacho hakutambua ni kwamba mara tu watu wanapoona dhahabu, asili nzuri na mbaya ya mwanadamu hujiweka wazi …
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kwaya za Injili

Jumanne, 10 Julai 2018

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(1): Jiwe, Karatasi, Makasi

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(1): Jiwe, Karatasi, Makasi

Kikundi cha watoto wachangamfu, wanaopendeza kilikuwa kikicheza mchezo wakati, bila kufikiri, waliuliza swali lenye cha kali: "Wanadamu hutoka wapi?" Je, unalijua jibu la swali hili?
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, watu wa Mungu