Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumapili, 8 Julai 2018

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo za Neno la Mungu

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

I
Kwa kuwa Mungu alimuumba mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfikisha katika hatima sahihi. Kwa kuwa Alimuumba mwanadamu na Anamsimamia, ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu. Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu, mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.
II
Kwa sababu ni Mungu anayemfanyia mwanadamu kazi, mwanadamu ana hatima na hatima yake hivyo inahakikishwa, hatima yake inahakikishwa. Yale ambayo mwanadamu hufuatilia na kutamani ni matarajio aliyo nayo anapofuata tamaa badhirifu za kimwili, badala ya hatima, hatima inayotazamiwa na mwanadamu. Yale ambayo Mungu amemwandalia mwanadamu, kwa upande mwingine, ni baraka na ahadi zinazomngoja mwanadamu atakapotakaswa, ambayo Mungu alimwandalia baada ya kuiumba dunia. Hizo baraka na ahadi hazichafuliwi na fikira
ya mwanadamu na mawazo, au chaguo lake au mwili. Hii hatima haijaandaliwa kwa mtu mahsusi, mtu mahsusi, lakini ni mahali pa mapumziko kwa kila mwanadamu. Hii ndiyo hatima inayofaa, hatima inayofaa kwa mwanadamu.
III
Ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu. Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu, mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia. Ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu. Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu, mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ijumaa, 6 Julai 2018

Roho Mtakatifu Hufanya Kazi kwa Njia yenye Maadili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

26. Roho Mtakatifu Hufanya Kazi kwa Njia yenye Maadili

Qin Shuting Jijini Linyi, Mkoani Shandong
Kwa muda fulani, ingawa sikuwa nimeacha kula na kunywa manen0 ya Mungu, sikuhisi mwanga kamwe. Nilikuwa nimeomba kwa Mungu kwa ajili ya hili lakini, baadaye, bado sikuwa nimepata nuru. Hivyo niliwaza, “Nimekula na kunywa kile ambacho nilipaswa na Mungu hanipi nuru. Hakuna kile ninachoweza kufanya, na sina uwezo wa kupokea maneno ya Mungu. Kuna wakati wa Mungu kumpa kila mwanadamu nuru, kwa hivyo hakuna maana ya kuiharakisha.” Baadaye, nilishika amri na kula na kunywa maneno ya Mungu bila wasiwasi, nikingoja kwa “subira” kutoa nuru kwa Mungu.
Mpaka siku moja, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Ni kama tu moyo wako uko na amani mbele za Mungu ndio kutafuta kwako ukweli na mabadiliko katika tabia yako kutazaa matunda. Kwa sababu unakuja ukiwa na mizigo mbele za Mungu na huwa unahisi kila mara kuwa unapungukiwa kiasi kikubwa, kwamba kuna ukweli mwingi ambao unahitaji kujua, uhalisi mwingi unaohitaji kupitia, na kwamba unapaswa kujali kikamilifu kuhusu mapenzi ya Mungu—mambo haya kila mara huwa mawazoni mwako, ni kana kwamba yamekufinyia chini sana kiasi kwamba huwezi kupumua, na hivyo unahisi mzito wa moyo (lakini sio kwa hali hasi). Ni watu wa aina hii pekee ndio wanastahili kukubali kupata nuru ya maneno ya Mungu na kuguswa na Roho wa Mungu. Ni kwa sababu ya mzigo wao, kwa sababu ni wenye moyo mzito, na, inaweza kusemwa, kwa sababu ya gharama ambayo wamelipa na mateso ambayo wamepitia mbele ya Mungu ndio wanapata nuru na mwangaza wa Mungu, kwa kuwa Mungu hamtendei yeyote kwa upendeleo. Yeye huwa mwenye haki kila mara katika kuwatendea watu, lakini Yeye sio holela katika kuwakimu watu, na hawapi bila masharti. Huu ni upande mmoja wa tabia Yake yenye haki” (“Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kufaa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Katika kutafakari maneno haya ya Mungu, nilielewa: Mungu ni Mungu wa haki. Kamwe yeye Hayuko holela katika kumkidhi mwanadamu, na Hamtolei mwanadamu bila masharti. Kwa watu kupata nuru na mwangaza wa Mungu, lazima watulize mioyo yao mbele ya Mungu na wawe na moyo ambao unayatamani sana na kutafuta maneno ya Mungu. Lazima wabebe mzigo kwa ajili ya maisha yao wenyewe na kutafuta mapungufu yao wenyewe ndani ya maneno ya Mungu. Wakibeba mzigo wao, lazima kwa makusudi wale na kunywa maneno ya Mungu kujali mapenzi Yake na kwenda kwa kina zaidi katika ukweli. Ni kwa kulipa gharama kama hiyo kwa vitendo tu kufanya kazi na Mungu ndiyo mtu anaweza kupata nuru ya Mungu. Kwa kufikiria ya zamani, sikuwa nabeba mzigo wowote wala kuwa na moyo wowote wa kutamani sana hata kidogo kula na kunywa maneno ya Mungu. Kila mara nilipochukua kitabu cha neno la Mungu, ningepitia kwa haraka na kuona kwamba nilikuwa nimesoma kifungu hiki na kusoma kifungu kile, nikifikiri kuwa nilikuwa na wazo la juu juu kuhusu kila kifungu. Kisha ningepata chochote cha zamani, nikisome kwa haraka, na kisha ningekuwa nimemaliza. Nilipokula na kunywa maneno ya Mungu, ilikuwa inatosha tu kwangu kuelewa maana halisi ya maneno hayo, nikilenga tu kushika masharti machache na matendo. Bila shaka sikuona ukweli mwingi ambao nilipaswa kuingia ndani yake, wala sikuwa nauridhisha moyo wa Mungu. Sikuwa nabeba mzigo kwa ajili ya maisha yangu hata kidogo, wala sikuwa na wasiwasi kuhusu kutojiandaa na ukweli wa kutosha; nilikuwa nachukulia kula na kunywa kwangu maneno ya Mungu kwa kutojali tu. Na mwelekeo wa kifidhuli kwa maneno ya Mungu hivyo, ningewezaje kupata nuru na mwangaza Wake? Kwa kweli sikuwa nafanya kazi na Mungu, na nilikuwa natumia “Kuna wakati wa Mungu kumpa nuru kila mwanadamu” kama kisingizio kungoja kwa upofu kutoa nuru kwa Mungu. Kwa kweli nilikuwa mpumbavu sana! Ni sasa tu ndiyo natambua kwamba, ingawa kuna wakati wa Mungu kumpa nuru kila mwanadamu, hili ni kweli, kuna kanuni katika kazi ya Roho Mtakatifu kwa mwanadamu. Mwanadamu mwenyewe lazima awe na moyo wa tamaa kubwa, ya kutafuta ili kuweza kufanya kazi na Mungu kwa vitendo na kwa utendaji. Ni hapo tu ndipo Roho Mtakatifu anaweza kufanya kazi kwa mwanadamu na kutia nuru na kuangazia kuelewa kwa mwanadamu kwa mapenzi ya Mungu, kumfanya kuelewa ukweli katika maneno Yake.
Ee Mungu! Ninatoa shukrani kwa sababu ya kutoa nuru Kwako kwa muda ufaao ambako kuliniruhusu kuona mkengeuko katika uzoefu wangu mwenyewe. Sasa ninatamani kurudi katika kufanya kazi kwa moyo mwema na kiutendaji pamoja na Wewe, kuweka moyo unaotafuta na kutamani sana, kubeba mzigo wangu wa kula na kunywa maneno Yako, kufuatilia kupata nuru zaidi kunakopatikana kupitia katika maneno Yako, kujifanya kupenyeza zaidi katika ukweli, na kwa maisha yangu kua hata zaidi. Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Alhamisi, 5 Julai 2018

New Swahili Gospel Choir Full Album Documentary 2018 | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu"

New Swahili Gospel Choir Full Album Documentary 2018 | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu"

Throughout the vast universe, all celestial bodies move precisely within their own orbits. Under the heavens, mountains, rivers, and lakes all have their boundaries, and all creatures live and reproduce throughout the four seasons in accordance with the laws of life…. This is all so exquisitely designed—is there a Mighty One ruling and arranging all this? Since coming into this world crying we have begun playing different roles in life. We move from birth to old age to illness to death, we go between joy and sorrow…. Where does mankind really come from, and where will we really go? Who is ruling our fates? From ancient times to modern days, great nations have risen up, dynasties have come and gone, and countries and peoples have flourished and perished in the tides of history…. Just like the laws of nature, the laws of humanity's development contain infinite mysteries. Would you like to know the answers to them? The documentary The One Who Holds Sovereignty Over Everything will guide you to get to the root of this, to unveil all of these mysteries!

Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Jumatano, 4 Julai 2018

Swahili Christian Video 2018 | "Ni Vizuri Sana Kutupa Mbali Pingu za Hadhi" | Wokovu wa Mungu

Swahili Christian Video 2018 | "Ni Vizuri Sana Kutupa Mbali Pingu za Hadhi" | Wokovu wa Mungu

Baada ya Liang Zhi kumwamini Mungu, bila kukoma alitafuta kwa shauku, na kujitosa katika kutimiza wajibu wake. Baada ya miaka kadhaa, alichaguliwa kama kiongozi wa kanisa. Wakati alipokuwa akitekeleza wajibu wake kama kiongozi wa kanisa, aligundua kwamba baadhi ya ndugu walikuwa na uwezo zaidi kumliko, ambayo ilimfanya asiwe na furaha kwa kiasi kwamba alikuwa na wivu kwao. Ili kuokoa uso na kulinda hali yake, alishindana nao kwa siri ili kuona ni nani aliyekuwa bora, na alikimbilia umaarufu na hadhi. Umaarufu na hadhi vilionekana kama pingu zisizoonekana zilizomfunga sana, kumnyima uhuru, kumsababisha afanye mambo kinyume na ukweli na kupinga Mungu. Kwa sababu kutekeleza wajibu wake kulikuwa tu kwa ajili ya umaarufu na hadhi, na si kwa kufuatilia ukweli, matokeo yake ni kwamba alipoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Hakuweza kufanya kazi ya vitendo, na aliondolewa kwenye kazi zake za uongozi na kubadilishwa. Aliteseka sana kama matokeo, na akaja mbele ya Mungu kutafakari juu yake mwenyewe. Baada ya kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, alikuja kutambua kwamba ufuatiliaji wa umaarufu na hadhi uliletwa kabisa na tabia yake ya kishetani ya kiburi na majivuno, na kuabudu mamlaka na ushawishi na hadhi. Alifahamu kuwa kiini cha kutafuta umaarufu na hadhi kilikuwa kufuata njia ya mpinga Kristo. Kama hangetubu na kurekebisha njia zake kote, matokeo ya mwisho yalikuwa kwamba alikusudiwa kuzama ndani ya utupu. Wakati huo huo aliona wazi kwamba imani katika Mungu ilihitaji kutembea kwenye njia ya ufuatiliaji wa ukweli na kutekeleza wajibu wake kwa kujitolea. Baada ya hapo, katika kutekeleza wajibu wake aliambatanisha umuhimu katika ufuatiliaji wa ukweli na kutenda ukweli. Kila wakati ambapo tabia potovu ya kukimbilia umaarufu na hadhi ilitokea, hapo basi alimwomba Mungu akitafuta ukweli na, akikubali hukumu na adabu ya maneno ya Mungu, kulingana na neno la Mungu alifanya mazoezi ya kuutelekeza mwili, na kuweka kwa mpangilio nia yake kutimiza wajibu wake mwenyewe. Bila kujali kama alikuwa na hadhi au la, aliweza kabisa kutekeleza majukumu yake. Pole pole alitupa mbali pingu za hadhi ambazo zilimfunga na hakufuatilia tena umaarufu na hadhi, baada ya kutembea kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu ya kutafuta ukweli na kupokea wokovu.

Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wafuasi wa Kristo

Jumanne, 3 Julai 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Zhang Jin, Beijing
Agosti 16, 2012
Mimi ni dada mzee mwenye miguu miwili yenye kasoro. Hata wakati hali ya hewa ni nzuri nje, nina shida kutembea, lakini wakati maji ya mafuriko yalipokuwa karibu kunimeza, Mungu aliniruhusu kutoroka hatari kimiujiza.
Ilikuwa Julai 21, mwaka wa 2012. Siku hiyo mvua ya mfoko ilinyesha, na nilikuwa tu nje nikitimiza wajibu wangu. Baada ya saa 10:00 mchana, mvua ilikuwa bado haijaisha. Wakati mkutano wetu ulipomalizika, niliikabili mvua bila woga na kupanda basi kwelekea nyumbani. Wakati nikisafiri, mvua ikawa nzito zaidi na zaidi, na wakati basi lilipofika kituo cha basi kabla ya changu, dereva alituambia sisi sote abiria, "Basi hili haliwezi kwendelea zaidi; barabara imeporomoka huko mbele." Hakukuwa na kitu ambacho kingeweza kufanywa, kwa hivyo sikukuwa na chaguo ila kushuka kutoka kwenye basi na kutembea njia yote. Bila kudhubutu kumwacha Mungu, nilikuwa ninaendelea kuomba moyoni mwangu. Kutokana na nguvu ya gharika, maji yalikuwa yamemeza barabara kabisa. Nilijaribu kuendelea kwa kushikilia nguzo za saruji zilizosimama kwa safu kando ya barabara, nikisonga mbele hatua kwa hatua. Wakati huo, nikasikia mtu akipiga ukelele nyuma yangu, "Acha kusonga mbele! Haraka; geuka na kurudi! Huwezi kupita; maji hayo yana uketo na mkondo una kasi sana. Ukikusomba, sitaweza kukuokoa!" Wakati huo, hata hivyo, singesonga mbele wala kurudi nyuma, kwa sababu maji yalikuwa tayari yamefika kifuani mwangu. Sikudhubutu kutembea zaidi, hivyo yote niliyoweza kufanya ni kumwomba Mungu na kumsihi Yeye afungue njia yangu kupitia: "Mungu! Umeyaruhusu mazingira haya kunifika, na ikiwa nitaishi au kufa iko mikononi Mwako sasa. Kama kiwango cha maji kingeshuka kwa nusu futi tu, ningeendelea kutembea mbele. Mungu, fanya Unavyotaka; Niko tayari kuaminisha maisha yangu Kwako!" Baada ya kufanya sala hii, nilijihisi mnyamavu na mtulivu. Nilikumbuka mojawapo ya maneno ya Mungu: "Mbingu na ardhi na vitu vyote vimeasisiwa na kukamilishwa na maneno ya kinywa Changu na na Mimi chochote kinaweza kufanikishwa" (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). Maneno ya Mungu yalinipa imani na ujasiri. Kwa kuwa mbingu na ardhi na vitu vyote viko mikononi mwa Mungu, nilijua kwamba bila kujali jinsi gharika hiyo ilivyokuwa katili, haingeepuka mpango wa Mungu. Hakuna yeyote ambaye angetegemewa tena; mwanangu wa kiume, binti yangu … hakuna yeyote ambaye angeweza kumtunza mwenzake. Niliamini kuwa mradi nilimtegemea Mungu, hakukuwa na shida ambayo singeweza kuipita. Wakati ule ule, muujiza ukafanyika. Mkondo ukapungua zaidi na zaidi mpaka haukuwa tena mkali kama ilivyokuwa wakati mfupi awali, na nguzo za saruji zilizosimama kwa safu kando ya barabara zimefichuliwa hatua kwa hatua. Kwa hakika, kiwango cha maji kilishuka kwa nusu futi kutoka kiwango cha kifua changu. Na hivyo tu, niliondoka mahali hapo, hatua kwa hatua, chini ya uongozi wa Mungu. Isingekuwa kwa sababu ya huruma na ulinzi wa Mungu, sijui ambako gharika ingenipeleka. Kutoka kwa kina cha moyo wangu, nilionyesha shukrani yangu na sifa, nikimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa ya pili katika maisha.
Baadaye, nikasikia maelezo ya mtoto wangu kuhusu mvua hiyo: Siku hiyo, baada ya kurudi nyumbani kutoka kutimiza wajibu wake, alikwenda msalani kwanza. Mara tu alipotoka chooni na kurudi kwenye chumba chake alisikia sauti kubwa nje. Alipotoka nje kwenda kuangalia, aliona kwamba jengo zima la choo lilikuwa limeanguka kabisa chini ya maji. Isingekuwa kwa ulinzi wa Mungu, angekufa. Ilikuwa hasa kama Mungu alivyosema katika mojawapo ya maneno Yake: "vitu vyote, vilivyo hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, vitafanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu" ("Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili). Msisimko wa kuzidi kiasi niliouhisi ndani ya moyo wangu hakika hauwezi kuelezwa kwa maneno.
Kupitia matukio haya mawili, imani yangu imekuwa imara hata zaidi. Siku hiyo, Mungu alikuwa ameniruhusu kuokoka maafa hasa kuniruhusu mimi kutoa ushahidi kwa ajili Yake. Siwezi kupuuza dhamiri yangu. Ninapoangalia nyuma juu ya jinsi nilivyokuwa na ubinafsi, ukatili, na hali ya kujidai nilivyokuwa awali kwa kawaida nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, ninatambua kuwa sikuhisi kamwe busara ya Mungu ya umuhimu au kushiriki mawazo ya Mungu. Kuanzia sasa kwendelea, napenda kutubu na kubadilika. Nitatumia uzoefu wangu binafsi kuwaleta watu zaidi mbele ya Mungu, na kufanya wajibu wangu katika kazi ya kueneza injili.
kutoka kwa Vita Baina ya Haki na Uovu

Jumatatu, 2 Julai 2018

Swahili Worship Song "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu" | Seeing the Love of God

Swahili Worship Song "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu" | Seeing the Love of God

Wakati hamumwelewi Mungu na hamjui asili Yake, mioyo yenu haiwezi kamwe kufunguka, kufunguka kwa Mungu. Mara utakapomwelewa Mungu wako, utaelewa kile kilicho moyoni Mwake, na kufurahia kile kilicho ndani Yake kwa imani na usikivu wako wote. Unapofurahia kile kilicho ndani ya moyo wa Mungu, kidogo kidogo, siku baada ya siku, unapofurahia kile kilicho ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utakuwa wazi Kwake. Moyo wako unapokuwa wazi kwa kweli, moyo wako unapokuwa wazi kwa kweli, utaona madharau, utaiona aibu ya maombi yako ya kupita kiasi na yenye ubinafsi. Moyo wako unapokuwa wazi kwa kweli, moyo wako unapokuwa wazi kwa kweli, utaona dunia isiyo na mwisho moyoni mwa Mungu, na kuwa katika ulimwengu wa maajabu yasiyosimuliwa. Katika ulimwengu huu hakuna uongo, hakuna udanganyifu, hakuna giza na hakuna uovu. Kuna ukweli na uaminifu tu; haki na ukarimu pekee. Yeye ni upendo, Yeye anajali, ana huruma isiyo na mwisho. Maishani mwako, unahisi furaha, Unapoufungua moyo wako kwa Mungu. Hekima na nguvu Zake vinajaza ulimwengu huu, na vile vile mamlaka na upendo Wake. Unaweza kuona kile Mungu alicho na Alicho nacho, kinachomletea furaha, kinachomletea matatizo, kinachomletea huzuni na hasira, vyote viko wazi kwa kila mmoja kuona, unapoufungua moyo wako kwa Mungu na kumwalika aingie ndani.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, nyimbo-za-injili,

Jumapili, 1 Julai 2018

Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia

Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia

Feng Jiahui na wazazi wake waliamini katika Bwana tangu alipokuwa mdogo. Alipokuwa na umri wa miaka 18 aliingia katika shule ya seminari, na katika miaka yake ya 30 akawa mhubiri katika kanisa la nyumba huko Shanxi, Uchina. Kwa miaka mingi, Feng Jiahui alidumisha imani madhubuti ya kuwa Biblia ilitiwa msukumo na Mungu, na kwamba lazima tuamini katika Mungu kwa mujibu wa Biblia. Aliamini kuwa hakukuwa na maneno yaliyonenwa na Mungu nje ya Biblia, na kwamba kuondoka kutoka kwa Biblia kutakuwa uzushi. Biblia ilikuwa imepata nafasi takatifu moyoni mwake, mahali pa mamlaka ya juu na isiyoweza kushindwa. Hata hivyo, katika kipindi cha miaka michache iliyopita, kanisa lake lilianza kuwa tupu siku baada ya siku, na Feng Jiahui na wafanyakazi wenzake walianza kuhisi giza likiingia ndani ya roho zao, na hawakuweza kuhisi uwepo wa Bwana miongoni mwao.... Aliwaalika wahubiri kutoka katika makanisa mengine ili kusaidia kurejesha kanisa, lakini bila mafanikio …
Wakati mmoja, Ndugu Yuan, mfanyakazi mwenzake Feng Jiahui alimwalika shahidi kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu aje kanisani. Shahidi alipokuwa akifanya ushirika juu ya ukweli kuhusu Biblia, kila kitu alichosema kilikuwa cha utendaji, wazi sana, na waumini waliona kuwa ya faida sana kwao. Hata hivyo, Feng Jiahui aliendelea kushikilia Biblia, akisisitiza kwa uthabiti kwamba imani katika Mungu lazima iwe na msingi katika Biblia, na kuondoka kwa Biblia kulikuwa uzushi. Baadaye, baada ya kuwa na mjadala mkubwa, Feng Jiahui hatimaye alielewa... undani wa Biblia na kiini cha kweli cha Biblia: Biblia ni kumbukumbu tu ya hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu, na Biblia haiwezi kumwakilisha Mungu, sembuse kufanya kazi ya Mungu ya wokovu kwa ajili Yake. Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima kwa mwanadamu, na Mungu pekee ndiye anaweza kufanya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, sisi ambao tunamwamini Mungu lazima tufuate nyayo za Mungu, na wakati huo tu ndiyo tutaweza kufikia njia ya uzima wa milele. Hatimaye, Feng Jiahui aliweza kwenda zaidi ya Biblia, kukubali kazi ya Mungu ya siku zile za mwisho, na kuwaongoza waumini katika kanisa lake kurudi kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Filamu za Injili  

Jumamosi, 30 Juni 2018

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu"

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu"

Mwenyezi Mungu alisema, "Ukuu na nguvu ya uhai wa Mungu hauwezi kueleweka na kiumbe chochote. Hii ilikuwa hivyo awali, iko hivyo wakati huu, na itakuwa hivyo wakati ujao. Siri ya pili Nitakayotoa ni hii: chanzo cha uhai hutoka kwa Mungu, kwa viumbe vyote, haijalishi tofauti katika maumbile au muundo. Hata uwe kiumbe hai cha aina gani, huwezi kwenda kinyume na njia ya maisha ambayo Mungu ameweka. Katika hali yoyote, kile Napenda ni kuwa mwanadamu aelewe kwamba bila huduma, utunzaji, na utoaji wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, haijalishi juhudi au mapambano yake. Bila ruzuku ya uhai kutoka kwa Mungu, mwanadamu hupoteza maana ya thamani katika maisha na kupoteza madhumuni ya kusudi katika maisha."
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Ijumaa, 29 Juni 2018

Swahili Christian Movie | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Kukaribia Hatari na Kurudi"

Swahili Christian Movie | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Kukaribia Hatari na Kurudi"

Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.
Filamu hii ni masimulizi ya uzoefu wa kweli wa mateso katika mikono ya Chama Cha Kikomunisti cha China yaliyopitiwa na Chen Wenzhong, Mkristo wa Kichina. Chen Wenzhong alikuwa na mafanikio katika kazi yake na alikuwa na familia nzuri na yenye furaha, lakini kwa sababu alimwamini Mungu na kutekeleza wajibu wake, akawa mtu aliyetakiwa na CCP. Alilazimika kuondoka nyumbani na alikuwa mkimbizi kwa zaidi ya miaka kumi. Ili kupata habari za mahali alikokuwa, polisi wa CCP daima waliifuatia, kuitishia, na kuiogofya familia yake, na hata hawangemhurumia mwanawe mdogo wa kiume, Xiaoyu. Hatimaye, walimlazimisha Xiaoyu kutenda kitendo ambacho hangekiepuka …
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, sinema za Kikristo

Alhamisi, 28 Juni 2018

Neno la Mungu "Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni"

Neno la Mungu "Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni"

Mwenyezi Mungu alisema, "Wakati nuru ya Mashariki inapong’aa polepole tu ndipo giza kote duniani litaanza kugeuka na kuwa nuru, na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba Nilishatoka Israeli zamani na Nimeanza kuchomoza upya Mashariki. Niliwahi kushuka Israeli na baadaye Niliondoka kutoka huko, Siwezi tena kuzaliwa Israeli kwa mara nyingine, kwa kuwa kazi Yangu inauongoza ulimwengu mzima na, zaidi ya hilo, umeme unamulika moja kwa moja kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hii ndiyo sababu Nimeshuka Mashariki na kuwaletea watu wa Mashariki Kanaani. Ningependa kuwaleta watu kutoka dunia nzima waje katika nchi ya Kanaani, na kwa hiyo Naendelea kutoa maneno Yangu katika nchi ya Kanaani ili kuudhibiti ulimwengu mzima. Kwa wakati huu, hakuna nuru katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani, na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi. Niliipa Israeli utukufu Wangu kisha Nikauchukua na baadaye Nikawaleta Waisraeli Mashariki, na vilevile ubinadamu wote Mashariki. Nimewaleta wote kwenye nuru ili waweze kuungana tena nayo, na kushirikiana na nuru, na wasilazimike kuitafuta tena."
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Jumatano, 27 Juni 2018

Gospel Video Swahili (2018) | "Nuru ya Mapambazuko"

Gospel Video Swahili (2018) | "Nuru ya Mapambazuko"

Kama mtoto, Yangwang aliwafuata wazazi wake katika imani yao kwa Bwana, na kama mtu mzima alihudumia Bwana kanisani. Mnamo 2013, kanisa lake lilijiunga na Baraza la Makanisa Ulimwenguni ambalo hutetea uunganishwaji wa kanisa kote ulimwenguni na wingi wa dini. Akisadiki kwamba kusisitiza kwa wachungaji na baraza la wazee wake katika kujiunga na Baraza kulikuwa kuondoka kwa njia ya Bwana na hakuwiani na moyo wa Bwana, hatimaye aliliacha dhehebu lake na kuanza kulitafuta kanisa lililo na kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini, baada ya kuyatembelea makanisa mbalimbali, aligundua kwamba madhehebu yote yalikuwa na ukiwa, na kwamba hakukuwa na nuru katika mahubiri ya wachungaji na mabaraza yao ya wazee. Hakuweza kupata utoaji wa uzima, na roho yake ilikuwa ikinyauka na kugeuka kuwa giza. Kwa maumivu yake, mara nyingi angemuita Bwana, akimwomba Bwana arudiharaka. … Siku moja, alienda mtandaoni kutafutataarifa kuhusu kurudi kwa Bwana, pale alipoiona video ambayo maneno ya Mwenyezi Mungu yalisomwa. Maneno ya Mwenyezi Mungu yaliishtua nafsi yake. Alihisi yalikuwa na mamlaka na nguvu na yalionekana kama sauti ya Mungu. Ili kuamua kama Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, alianza kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kupitia kwa kulisoma neno la Mwenyezi Mungu na kusikia ushirika wa watoaji ushuhuda, aliutatua mkanganyo wake. Aligundua kwamba neno lote la Mwenyezi Mungu ni la ukweli, kwamba kwa hakika ni sauti ya Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu ambaye kurudi kwake alikuwa akisubiri kwa miaka mingi akiutamani. Kwa kuwa, amelisoma neno la Mungu kila siku, hivyo basi kuilisha nafsi yake yenye kiu, na kupokea kwa kweli maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Maisha ya Kanisa

Jumanne, 26 Juni 2018

New Swahili Gospel Choir Full Album Documentary 2018 | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu"

New Swahili Gospel Choir Full Album Documentary 2018 | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu"

Throughout the vast universe, all celestial bodies move precisely within their own orbits. Under the heavens, mountains, rivers, and lakes all have their boundaries, and all creatures live and reproduce throughout the four seasons in accordance with the laws of life…. This is all so exquisitely designed—is there a Mighty One ruling and arranging all this? Since coming into this world crying we have begun playing different roles in life. We move from birth to old age to illness to death, we go between joy and sorrow…. Where does mankind really come from, and where will we really go? Who is ruling our fates? From ancient times to modern days, great nations have risen up, dynasties have come and gone, and countries and peoples have flourished and perished in the tides of history…. Just like the laws of nature, the laws of humanity's development contain infinite mysteries. Would you like to know the answers to them? The documentary The One Who Holds Sovereignty Over Everything will guide you to get to the root of this, to unveil all of these mysteries!
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Jumamosi, 23 Juni 2018

Upendo wa Mungu na wokovu | "Kutanafusi kwa Mwenye Uweza" Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Upendo wa Mungu na wokovu | "Kutanafusi kwa Mwenye Uweza" Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Mwenyezi Mungu alisema, "Mwanadamu, ambaye aliacha kupokea uzima wake kutoka kwa Mwenye Uweza, hajui ni kwa nini anaishi, na bado anaogopa kifo. Hukuna usaidizi, wala msaada, lakini mwanadamu bado anasita kufumba macho yake, akiyakabili yote bila woga, kuishi katika maisha yasiyokuwa na maana katika ulimwengu ndani ya miili isiyokuwa na utambuzi wa roho. Unaishi hivyo, pasipo tumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na malengo. Kuna Mmoja tu aliye Mtakatifu katika hadithi hii ambaye atakuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa kuumia na wanasubiri kwa shauku kubwa kuja Kwake. Imani hii haiwezi kutambulika kufikia sasa kwa watu ambao hawana utambuzi. Hata hivyo, watu watu bado wanaitaka sana. Mwenye Uweza ana rehema kwa watu hawa wanaoteseka sana. Wakati huo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na utambuzi, maana lazima Asubiri sana jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kuchunguza, kuuchunguza moyo na roho yako. Anataka kukuletea chakula na maji na kukuamsha, ili usipate kiu na kupata njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote."
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Ijumaa, 22 Juni 2018

Latest Swahili Christian Video "Nuru ya Kweli Yaonekana" | The Good News From God

Latest Swahili Christian Video "Nuru ya Kweli Yaonekana" | The Good News From God

Gangqiang ni Mkristo. Aliona namna upendo wa Bwana na huruma Yake kwa binadamu vilivyo vikubwa, na akaamua mara nyingi kwamba angempenda Bwana, kumridhisha Bwana, kutekeleza neno la Bwana, na kuwa na mwenendo wake binafsi kama mtu anayesifiwa na Bwana. Lakini alipotoa athari ya kimatendo kwa neno la Bwana, aligundua kwamba kwake yeye mwenyewe kulikuwa na mambo mengi potovu na ya uasi-ubinafsi, kiburi, udanganifu, na ulaghai na kadhalika. Tabia hizi potovu zilikuwa zinamrudisha nyuma, na hakuwa na nguvu kamwe za kuyatekeleza maneno ya Bwana. Kwa sababu hii, alikuwa na mfadhaiko kabisa, na mara nyingi alimwita Bwana kwa usadizi. Gangqiang baadaye alienda Marekani kufanya kazi na huko akafahamiana na Dada Zhao wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kupitia kwa mawasiliano ya Dada Zhao na kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na kwa kuyasoma baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu, Gangqiang alipata kujua kwamba Bwana Yesu alikuwa tayari Amerudi, na kwamba Alikuwa ametekeleza kazi ya kuhukumu na kutakasa binadamu, Akimwelekeza binadamu katika njia ya kuitatua asili yake yenye dhambi. Moyo wa Gangqiang ulikuwa umepata nuru, na alikubali kwa furaha kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na akaja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kwa kulisoma neno la Mwenyezi Mungu, aliuelewa ukweli fulani, na maisha yake ya huzuni yaliangazwa na maneno ya Mungu …
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kuonekana kwa Mungu
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.